kuunganisha vizazi kupitia radio - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na...

63
KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Upload: lythuan

Post on 02-Mar-2019

275 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

KUUNGANISHA VIZAZIKUPITIA RADIO

MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Page 2: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipavituo vya radio vya barani Afrika, maarifa,nyenzo na stadi za kuwashirikisha vijana kwenyeuandaaji wa vipindi vya radio katika ngazi ya chini

Lengo lake ni kuboresha stadi za utangazaji na uandaaji wavipindi vya radio kwa vijana kushiriki kikamilifu na kuwapamwongozo utakaochochea ubunifu ili waweze kufanya kaziyenye tija

Mwongozo huu utawasaidia kuanzisha kipindi cha radio kinachoendana navijana ambacho kinaweza kuboreshwa kuendana na uwezo wa kituo chakocha radio na mahitaji ya wasikilizaji wa jamii yako

Inapaza sauti za vijana barani Afrika

KUWEZESHA za kijamii

Kutumia TehamaRadio

Page 3: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

Mwongozo kutoka Afrika Kwa Waandaaji wa Vipindi vya Redio Wanaofanyakazi na Watoto na Vijana

Kuunganisha Vizazi

Page 4: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

7, place de Fontenoy, 75352, Paris 07 SP, France

Imechapishwa mwaka 2013 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni

@ UNESCO 2013 Haki zote zimehifadhiwa ISBN 978-92-3-001189-5

Nyadhifa zilizotumika na mambo yaliyowasilishwa kwenye chapisho hili hayahusiani kwa namna yoyote na msimamo wa UNESCOkuhusiana na hadhi ya kisheria ya nchi, jimbo, jiji au eneo lolote au mamlaka yake, au kuhusiana na ukomo wa mipaka yake.

Maoni yaliyomo kwenye chapisho hili na yale ya wahariri wake, sio maoni ya UNESCO na hayahusiani na asasi hii

Ukurasa wa mbele umesanifiwa na:CLD/UNESCO

Kurasa za ndani zimesanifiwa na:Meghan Adams

Picha: @Steven Mukobeko

Usanifu kwa ajili ya kuchapisha umefanywa na:CLD/UNESCO

Imechapishwa na UNESCO, Ufaransa

Page 5: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

DIBAJI

Watoto na vijana ni zaidi ya theluthi moja ya watu wote duniani na idadi yao inaweza kubwa zaidi miaka ijayo. Kwenye nchi zinazoendelea, vijana ni karibu asilimia 70 ya watu wote. Vijana ambao hawana ajira na elimu inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya vijana ikijumuisha na wale walioacha shule.

Radio inaendelea kutoa fursa kubwa za mawasiliano kwa vijana na watoto. Kwanini radio ambayo, ni maarufu zaidi, imesambaa na njia yenye kuwafikia watu wengi, mara nyingi imeshindwa kuwakilisha sauti za vijana? Labda watangaza-ji wanaongea kwenye vipaza sauti kwa niaba ya vijana kuliko kuwaacha wajiongelee wenyewe, au kwa sababu kundi hili halichukuliwi kama soko – kitu ambacho kinapunguza uwezo wa radio kuonyesha utofauti.

Mwongozo huu unatoa fursa kwa watangazaji wa radio ndani na nje ya Afrika kuanza kutumia mbinu jumuishi na shirikishi ili kujumuisha uwepo na uwakilishi wa vijana kwenye utangazaji.

Afrika kusini mwa Sahara, radio inaweza kuingia kwenye maisha ya vijana kama mshauri, rafiki, mtoa taarifa, mwalimu na stadi, ikitoa fursa kwa vijana wa kike na kiume walio kwenye shinikizo kutokana na hali za kijamii na kiuchumi ambazo mara nyingi zinavuruga elimu yao. Kiwango cha juu cha kusoma na kuandika kwa watoto wenye miaka minane na tisa kwenye maeneo ya vijijini barani Afrika kimechangiwa na kufikiwa kwa kiasi kikubwa na radio za kijamii.

Vijana wa kiume wenye umri wa kupata watoto ni sehemu muhimu ya hadhira ya vyombo vya habari kote Afrika Kusini mwa Sahara. Ili kipindi chao cha mpito kutoka utotoni kuelekea ukubwani kiwe cha mafanikio, inategemea uwezo wao kutawala shughuli zao za kujiingizia kipato kwa kutumia kiwango kidogo cha maarifa walichonacho. Uwezo wao kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika na kwa usalama wa vizazi vijavyo.

Juhudi za jumuiya ya kimataifa yamepelekea kuanzishwa kwa vyombo vya kimataifa vya kuwasaidia watoto na utangazaji. Mkataba wa Afrika kuhusu Utangazaji unaowahusu watoto ni moja ya juhudi za kupongezwa ambazo zinastahili kupewa kipaumbele na watangazaji katika ngazi ya kitaifa na chini kabisa kote barani Afrika. Mikataba mingine ni Changamoto za Oslo (Oslo Challenge) na Ilani ya Dunia kuhusu Utangazaji (World Manifesto on Radio), ambayo ina hoja za nguvu kuhusu mipango jumuishi.

Siku hizi, teknolojia inatoa fursa zaidi kwa vijana kutoa maoni yao kuhusu masuala ya kijamii, ambayo yataathiri maisha yao kama watu wazima. Uwezo wao wa kurekodi na kutengeneza vipindi vyenye maudhui ya eneo husika ambavyo vinashughulikia mahitaji ya wenzao, umekuwa juu sana kuliko mwanzo. Runinga imebadilika kutoka rangi nyeupe na nyeusi na katuni hadi vipindi vya elimu vya watoto na vijana ambavyo ni 3D na vyenye mwingiliano, radio pia inaweza kuwa na vipindi vya muziki vinavyojirudia rudia kuendana na ratiba za vijana na kuongezeka kwa vipindi shirikishi vya radio vilivyoandaliwa kwa ajili ya vijana na vile vilivyoandaliwa na vijana wenyewe.

Ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (Sida), mwongozo huu ni marejeo ya msingi kwa waandaaji wa vipindi vya radio ambao wanapenda kufanya kazi na watoto na vijana katika namna ambayo ina heshima, inayoweza kusimamiwa na yenye tija. Umeandaliwa kwa ushirikiano na Children’s Radio Foundation (CFR) ili kuongeza kiwango cha ushiriki wa vijana hususani wa kike, kwenye uandaaji wa vipindi vya radio kwenye vituo vya radio 32 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Lesotho, Namibia, Afrika Kusina, Tanzania na Zambia.Watangazaji wa radio popote walipo wanatakiwa kubadilisha desturi za vituo vya ili kutumia fursa ya mwongozo huu kwa kuanzisha vipindi vya radio vya vijana, kuongeza maudhui tofauti na yenye ubora kwa vijana na kuyajumuisha kwenye utangazaji wa radio wa kisasa.

Janis KarklinsUNESCOMkurugenzi Mkuu MsaidiziIdara ya Mawasiliano na Habari

Page 6: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

5

YALIYOMO

SEHEMU YA KWANZA: JINSI YA KUANZA

UTANGULIZIKWANINI RADIO YA VIJANA?JINSI YA KUTUMIA MWONGOZO HUU

SEHEMU YA PILI KANUNI ZA MSINGI

SURA YA 1: KUWASHIRIKISHA VIJANASURA YA 2: KUFANYA KAZI NA VIJANA – KUWA MSHAURISURA YA 3: MAADILI NA IDHINI

SEHEMU YA TATU KUJUA KIWANGO CHA UWEZO NA KUPANGA

NGAZI YA 1: RADIO KWA AJILI YA VIJANANGAZI YA 2: RADIO PAMOJA NA VIJANANGAZI YA 3: RADIO YA VIJANANGAZI YA 4: KUWAFIKIA VIJANA

SEHEMU YA NNE MAREJEO MUHIMU NA VIAMBATISHO

6

46

7911

14

25

15

26

19

31

21

3543

Page 7: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

6

• UTANGULIZI

• KWANINI RADIO YA VIJANA?

• JINSI YA KUTUMIA MUONGOZO HUU

JINSI YA KUANZA

SEHEMU YA KWANZA

Page 8: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

7

‘Kupitia mafunzo ya utangazaji, nimejifunza kuwa mtangazaji mzuri, jinsi ya kuwauliza watu maswali ambayoyananipatia majibu mazuri na pia kutafuta habari nzuri ambazo zinaongeza ufahamu wangu kuhusu mambombalimbali. Nafikiri kipindi chetu cha radio kitabadilisha hali ya mambo; kipindi kitaigusa jamii, kitapanuafikrazao kuhusu mambo mbalimbali, kitawapa matumaini na kuwabadilisha kuwa na hali bora na hatimayekuibadilisha Tanzania nzima’

Fadhili (16), mwandishi wa habari kijana, Radio Pambazuko, Ifakara, Tanzania

Kwa zaidi ya miaka miwili, Radio Pambazuko imekuwa ikishirikiana na kikundi cha vijana 15 kama Fadhili kipindi cha radiocha vijana kinachotoka kila wiki. Kipindi hicho kinachorushwa moja kwa moja kinahusu haki za watoto na kujadili masualakama ajira, udhalilishaji na elimu ya watoto. Hata hivyo, kinahusisha pia masuala ya kawaida kama muziki na michezo, nakinasimulia hadithi za kutia moyo za watu waliofanikiwa. Kipindi kinatoa nafasi ambapo vijana kutoka eneo husika kutoamaoni yao na kuzungumza kwa uhuru masuala ambayo ni muhimu kwao. Kinaifanya jamii kuzungumza na kufikiri na kuwaweka vijana katika nafasi ya kushawishi ufanyaji wa maamuzi ambayo yanawaathiri

Kwa bahati mbaya Radio Pambazuko inabaki kuwa ya kipekee kwa radio zinazorusha matangazo yake barani Afrika. Radio ina uwezo wa kuboresha kwa kiwango kikubwa hali za maisha ya vijana, lakini katika sehemu nyingi, haitumiwi kikamilifu.

Radio inawafikia zaidi ya asilimia 95 ya watu wote duniani na vituo kadhaa vya radio barani Afrika kila kimoja kina zaidi ya wasikilizaji milioni moja. Afrika kusini mwa Sahara, idadi ya vituo vya radio za kijamii imeongezeka maradufu katika miaka ya karibuni. Kwa mfano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina zaidi ya vituo 250 vya radio za kijamii mwaka 2006 kulinganisha na 10 tu mwaka 2000.

Moja ya faida ya radio za jamii ni kwamba zinawafikia watu wa aina tofauti na kuelezea mambo mbalimbali ya maishayao. Iwekuwatangazia jamii za wafugaji wanaohamahama maeneo ya vijijini nchini Kenya, wachimbaji wa shaba nchini Zambia, wafanyabiashara wa sokoni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au wanafunzi wa sekondari ya sekond ari ya juu nchini Afrika Kusini, radio ya jamii mara nyingi inaoengea lugha inayodharauliwa na vyombo vikubwa vya habari na inawapatia habarimuhimu hadhira ambayo ni ngumu kuifikia. Watoto na vijana ni sehemu kubwa ya hadhira hii.

Lakini sauti za vijana hazisikiki mara kwa mara na hazitambuliki ingawa karibu nchi zote duniani zimeridhia Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto (UNCRC) na sheria nyingine zinazohimiza ushiriki wa watoto.

Hata hivyo, kama wafanyakazi kwenye vyombo vya habari, ni wajibu wenu kuhakikisha watoto na vijana wanaonekana,wanatumia na kutengeneza vipindi vya radio vya vijana wakati ushiriki kwenye miradi yenu ukizingatia sheria zakimataifa na kitaifa zinazohusiana na watoto

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Utangulizi

UTANGULIZI

Page 9: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

8

IBARA YA 2: BILA UBAGUZI

IBARA YA 12

IBARA YA 13

IBARA YA 14

IBARA YA 15

IBARA YA 16

IBARA YA 17

MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA WA HAKI ZA MTOTO UNCRC inatoa mwongozo wa kile serikali na watu binafsi wanapaswa kufanya ili kuhimiza na kulinda haki za msingi za watoto wote

Ulipitishwa kwa kauli moja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1989, toka hapo umeridhiwa na serikali zote dunianiisipokuwa Somalia na Marekani. Zinaporidhia Mkataba serikali zinajifunga kuhakikisha watoto wanakuwa katika mazingiramazuri na salama, huku wakipata elimu bora na huduma bora za afya na hali nzuri za maisha

Ibara za mkataba ambavyo ni mahususi kuhusiana na ushiriki wa watoto na vijana ni kama ifuatavyo:

Mkataba huu unawahusu watoto wote, bila kujali rangi, dini au uwezo, wanachofikiri au kusema, aina ya familia wanayotoka. Haijalishi watoto wanaishi wapi, wanaongea lugha gani, wazazi wao wanafanya kazi gani, kama ni wavulana au wasichana, ni wa utamaduni gani, kama wana ulemavu au kama ni matajiri au maskini. Kusiwe na mtoto anayetendewa vibaya kwa sababu yoyote ile.

MAONI YA MTOTO

UHURU WA KUJIELEZA

Watoto wana uhuru wa kupata na kutengeneza habari zao wenyewe na kutoa maoni yao, bila kuathiri haki za wengine

UHURU WA KUFIKIRI, DHAMIRi NA KUABUDU

Mtoto ana haki ya kufikiri, kujitambua na kuabudu, kutokana na mwongozo sahihi wa wazazi na sheria za nchi

UHURU WA KUJIUNGA NA CHAMAMtoto ana haki ya kukutana na watu wengine na kujiunga au kuunda vyama, bila kuathiri haki za wengine

KINGA YA MAISHA BINAFSIWatoto wana haki ya kulindwa dhidi ya kuingiliwa katika miasha yao binafsi, ya kifamilia, nyumbani na mawasiliano nadhidi ya kauli / vitendo vinavyoshusha hadhi

KUPATA TAARIFA SAHIHI Vyombo vya habari vina wajibu wa kusambaza habari kwa watoto ambazo ni za kijamii, kimaadili, zenye kuelimisha na zenye

manufaaya kiutamaduni kwao na ambazo zinaheshimu utamaduni wao. Serikali ihimize machapisho/habari zenye manufaa kwa watoto na kuwalinda dhidi ya machapisho/habari zenye athari kwao.

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Utangulizi

UNCRC inatoa viwango ambavyo kwavyo juhudi za kila nchi kuboresha hali za watoto zinaweza kupimwa. Kila baada ya miakamitano serikali zinatakiwa kutoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto

Kamati hukutana na wawakilishi wa serikali na kusikiliza maoni ya asasi zisizo za kiserikali (NGOs) kabla ya kutoa mapendekezo yake kuhusu hatua ambazo kila nchi inabidi kuchukua ili kutimiza wajibu wake. Hata hivyo katika sehemu nyingi za dunia haki ya watoto na vijana kushiriki (Kifungu cha 17 cha UNCRC) haiheshimiwi au inakiukwa.

Mara nyingi hii inatokana na kutoelewa nini cha kufanya ili kuwashirikisha vijana kwenye vituo vya radio vya kijamii na jinsi radio inavyoweza kutumika kuchochea mazungumzo, ushiriki na kuwa raia bora

(Muhtasari wa CRC uliotolewa kama kiambatisho 1)

Ibara ya 1 inaelezea maana ya neno mtoto kuwa ni mtu aliye chini ya miaka 18”

Mtoto ana haki ya kuelezea maoni yake na yafanyiwe kazi kwa kuzingatia masuala au mchakato unaomuathiri mtoto

Page 10: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

9

KWANINI RADIO YA VIJANA?

MAJADILIANO KWENYE JAMII

John Liveti, mtangazaji, Radio Tumaini, Dar es Salaam, Tanzania

Mwajuma (14), mwandishi wa habari kijana, Radio Tumaini, Dar es Salaam, Tanzania

KUJENGA UWEZO

“Kwa kuwekeza kwa vijana, ninapanda mbegu kwenye bustani yangu”

Paul Obakeng Mahlate, Meneja wa kituo, Aganang FM, Potchefstroom, Afrika Kusini

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Kwanini Radio ya Vijana?

Radio ya vijana inaweza kuwa katika miundo mbalimbali. Hakuna mkakati ulio sahihi au usio sahihi kwa kuwa yote ina uhusiano wa moja kwa moja na idadi ya wafanyakazi na rasilimali zilizopo na mali na matatizo ya vituo vya radio. Kwa hakika, miongoni mwa vituo vya radio vinavyofanya kazi barani Afrika, vina rasilimali chache na msaada mdogo wa kitaasisi. Matokeo yake kiwango cha ushiriki wa vijana kinatofautiana sana. Wakati mwingine vijana wanahojiwa kwenye vipindi maalum kwa watu wazima, na ushahidi mwingine wa vijana unajumuishwa kwenye vipindi vya watu wazima na mara chache vijana wanaandaa na kuongoza vipindi wao wenyewe.

Majadiliano ni hali ya kubadilishana kati ya pande mbili yaani kituo cha radio na jamii. Inahusisha kushirikishana taarifa, kutoa fursa sahihi ya kusikiliza maoni ya hadhira na kuyafanyia kazi. Mchakato huu unawaleta pamoja vijana ili kujadili masuala mbalimbali ambayo wanayapenda na ni muhimu kwao, kuanzia burudani hadi vipindi vinavyozungumzia mambo ya msingi, maigizo, ucheshi, midahalo na vipindi vya maswali na majibu. Zingatia tofauti za mahitaji kati ya wavulana na wasichana-fanyia kazi mahitaji yao kwa namna tofauti kama ni lazima. Vipindi vya radio vilivyoandaliwa vizuri vimeweza kujadili mambo ya msingi kama shinikizo la kundi rika au uonevu shuleni. Ngazi hiyo ya ushirikishaji inaviweka vituo vya radio katika nafasi muhimu kwenye masuala ya kijamii.

Hata hivyo, vituo kadhaa vya radio za kijamii vina vipindi vinavyochochea maendeleo ya watoto wadogo. Mara nyingi vina mtangazaji mtu mzima anayewafundisha wasikilizaji watoto nyimbo, anayesoma hadithi za watoto au kujenga stadi za lugha. Wakati mwingine kikundi cha watoto kinaalikwa studio ili kushiriki kwenye kipindi. Wakati vipindi hivi vinakidhi mahitaji ya jamii yao, tatizo ni kwamba muda si mrefu watoto wanaviona vimepit-wa na wakati, na kama vijana, wanalazimika kusikiliza vipindi vya watu wazima.

Matokeo yake, kuna haja ya kuziba pengo hilo, kuwasikiliza na kuwapa sauti vijana walio kati ya miaka 10 na 18. Hiki ni kipindi muhimu sana kwa maisha ya kijana ambapo mabadiliko mengi hutokea, maamuzi hufanywa na malengo ya maisha ya kiutu uzima huwekwa.

Vijana ni zaidi ya nusu ya watu wote barani Afrika, na kitu cha muhimu ni kwamba fursa yao kama washirika na hadhira muhimu inaendelezwa na haidharauliwi. Majadiliani kwenye jamii na kujenga uwezo ni mamba ya muda mrefu ya kuzingatia kwenye vipindi vya vijana, ambavyo vinaweza kuongeza usikivu wa vituo vya radio.

‘Kwenye vipindi, watangazaji vijana wanazungumzia masuala wanayoyapa kipaumbele, wasikilizaji wanapenda vipindi vya vijana na wanapenda kusikiliza zaidi, hivyo tumeongeza muda ili kuwapa wasikilizaji kile wanachotaka. Wanapen-da pia kusikia watoto wakielezea uzoefu wao’

‘Kila Jumamosi wote tunakusanyika kuizunguka radio ili kusikiliza kipindi, wote, kama jamii. Watu wanashangaa kwamba tupo radioni na tunaweza kufanya wenyewe kama watoto’

Kujenga uwezo mara nyingi kunachukuliwa kwa maana sawa na mafunzo. Ingawa, neno hilo lina maana pana zaidi na ni muhimu kwa maendeleo endevu ya kituo cha radio na ushirikiano wake na vijana. Kutoa stadi za msingi za uandaaji wa vipindi, ushauri, nafasi, vifaa na ukarabati ni baadhi ya mambo muhimu

Page 11: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

10

KWANINI RADIO YA VIJANA?

Kujifunza kutafiti, kufanya mahojiano na kutangaza vinaongeza hali ya kujiamini kwa vijana na kunajenga stadi zamawasiliano nakufikiri kwa kina. Uzoefu wa kutangaza radioni hugeuka kuwa stadi muhimu inayotumika katika nyanja mbalimbali za maisha, kutoka darasani hadi kazini kwa siku za baadaye.

‘Kipindi cha radio kimenisaidia kujenga hali ya kujiamini kwa kiwango kikubwa, hususani shuleni. Siku za nyuma,kama aliongea na kufafanua jambo darasani na sikuweza kuelewa, tungenyamaza kimya bila kusema kitu, lakinisasa kwa kuwa sehemu ya kipindi hiki cha radio, siogopi kuuliza maswali hadi nielewe.’

Cecilia (10), mwandishi wa habari kijana, Radio Sauti, Moshi, Tanzania

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Jinsi ya kutumia mwongozo huu

Page 12: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

11

JINSI YA KUTUMIA MWONGOZO HUU

JE, UNGEPENDA

• Kufanya sauti i za vijana zisikike zaid?

• Kuwashirikisha vijana kwenye kipindi chako?

• Kupata vidokezo na ushauri jinsi ya kufanya kazi na vijana?

BASI MWONGOZO HUU WA VIJANA NA RADIO UPO KWA AJILI YAKO.

Zingatia: Wasiliana na mamlaka za eneo lako ili kuhakikisha kwamba fomu ya idhini ya mfano iliyowekwa kwenye mwongozo huu (Kiambatisho 4) inakidhi mahitaji ya kisheria ya nchi yako.

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Jinsi ya kutumia mwongozo huu

Umeandaliwa kuwasaidia waandaaji na mameneja wa vipindi wanaofanya kazi na vijana na kuhimiza mbinu zinazowalenga vijana zinazotokana na mafunzo kutoka kwa wafanyakazi wa radio za jamii wenye uzoefu na vijana barani Afrika. Inahimiza mbinu zinazotumia teknolojia ya chini na bila uhariri kwa kutumia mada ambazo zinaonyesha vipindi ambavyo tayari vimerekodiwa tayari kwa kurushwa radioni

Vidokezo na mifano kwenye mwongozo huu itakusaidia kufanya kazi na vijana wanaotaka kutengeneza vipindi vya radio ambavyo vyenye utajiri wa maudhui, ujuzi na endelevu ambavyo vinaonyesha hali halisi ya jamii yao. Ongeza idadi ya masikio yanayosikiliza na sauti zinazoongea!

Ni jambo lenye faida kubwa kutumia muda kwa ajili ya vijana na radio, lakini usidharau moyo wa kijitolea. Ni vizuri kama kazi yako inajadiliwa na inaungwa mkono na mkuu wako na hivyo kupewa majukumu yanayotambulika ili kuyafanyia kazi kikamilifu.

Lengo la msingi ni kuvisaidia vituo vya radio kuanzisha na kuendeleza ushiriki wa vijana pamoja na kuwapa taarifa na kuimarisha vipindi kwa ujumla. Kanuni, motisha na baadhi ya vifaa vya msingi vya kurekodia ni muhimu. Maudhui ya mwon-gozo huu yanawasilishwa kielektroniki ambapo unaweza kuyapata na kuyatumia kwenye mtandao au kuyapakua kwa muda wa PDF. Unapotumia nakala ya kwenye mtandao, bonyeza kwenye viunganishi sahihi ili kupata marejeo zaidi na makala za kusikiliza. Sehemu mbili za kwanza za mwongozo zinakuwezesha kujua mahitaji ya msingi ambayo unapaswa uyatimize na uyatilie mkazo kwenye shughuli zako za radio ili kuwashirikisha vijana kikamilifu. Miongozo maalum inayofua-ta hatua kwa hatua yenye lengo la kuonyesha mbinu sahihi kwa ajili ya kufanya kazi na vijana na kuweka viwango ambavyo vinaweza kutumika kukidhi mahitaji yako, inatolewa katika Sehemu ya 3. Orodha ya marejeo muhimu na ya ziada yanapatikana Sehemu ya 4.

Page 13: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

12

1. NGAZI YA USHIRIKISHAJI

KIWANGO CHA USHIRIKISHAJI

NGAZI YA 1: RADIO KWA AJILI YA VIJANA Katika ngazi hii ya mwanzo wafanyakazi wa radio wanaandaa vipindi vinavyohusu mada za vijana.

Vijana wanashirikishwa katika maandalizi ya mwanzo na baada ya kutangazwa kwa kipindi.

Usimamizi /ushauri: Hauhitajiki

NGAZI YA 2: RADIO PAMOJA NA VIJANA

Usimamizi /ushauri: Ni muhimu

NGAZI YA 3: RADIO YA VIJANA

Usimamizi / ushauri: Ni muhimu (lakini unaweza kupungua kadri kikundi kinavyoweza kujitegemea)

NGAZI YA 4: KUWAFIKIA VIJANA ZAIDI

Usimamizi / ushauri: Ni muhimu (lakini unaweza kupungua zaidi kadri kikundi kinavyoweza kujitegemea)

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Jinsi ya kutumia mwongozo huu

Mwongozo huu umepangwa katika ngazi nne za ushirikishaji wa vijana kulingana na Ngazi ya ushiriki ya Roger Hart, mwongozo umeandaliwa na kutumika kupima ushiriki wa watoto.

Ngazi hizi zinafafanuliwa vizuri kwenye Sehemu ya 3 ya mwongozo huu na zimeorodheshwa kwa muhtasari hapa chini. Zinaweza kutumika kuonyesha uwezo wa kituo cha radio kuwashirikisha vijana kwenye vipindi, kupanga kikamilifu na kusimamia kazi stahiki. Stadi muhimu, shughuli zenye uhusiano na mfano wa vipindi vya radio vinavyoonyeshwa katika kila ngazi vinaendelea kwa kufuatana, hivyo inabidi ujue kuwa, kama unaamua watoto waendeshe mdahalo wa moja kwa moja radioni kama inavyoelezewa kwenye Ngazi ya 3, radio yako lazima iwe tayari ina stadi za msingi zinazoelezewa katika Ngazi ya 1.

Wafanyakazi wa radio bado wanaandaa vipindi lakini sasa wanajumuisha mawazo ya vijana. Wanashirikishwa zaidi kwenye maandalizi na baada ya kutangazwa kwa kipindi na wanaombwa watoe maoni yao au kuwahoji vijana wengine na watu wazima ili kupata maoni yao. Halafu rekodi hizi zinajumuishwa kwenye vipindi vya watu wazima.

Kikundi kinaandaa vipindi ambavyo vitawasaidia wafanyakazi wa kituo cha radio. Wanahusika kwenye maandalizi na utangazaji

Vijana kwa msaada wa wafanyakazi wa radio, waandae matukio ya kijamii kuhusiana na vipindi vyao na kukutana na vyombo vingine vya habari ili kupata uzoefu wa kazi zao. Hii itakipa kituo cha radio na kipindi chake cha vijana matokeo makubwa na kuongeza usikivu wake na kuongeza ufahamu wao wa mambo yanayowagusa vijana.

Page 14: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

13

MALENGO VIDOKEZO

Introduction to help you understand why this is important.

Stadi/sanduku la vidokezo

SAUTI MAZOEZI YA KUJIFUNZIA

Quote from youth and mentors that relates to this section / chapter.

Mada za vitendo

REJEA MAREJEO

Ngazi, inarejesha sura iliyotangulia

marejeo / viunganishi / mifano ya makala za kusikiliza

MIFANO

Mifano ya hali halisiili kukusaidia kuelewa

2. HATUA ZA UTENGENEZAJI WA KIPINDI

3. KUELEWA ALAMA

Sehemu ya kwanza | Jinsi ya kuanza | Jinsi ya kutumia mwongozo huu

MAADALIZI YA AWALI UTENGENEZAJI UTANGAZAJI MREJESHO

Hatua za utengenezaji wa kipindi zimeandaliwa ili kukusaidia kuona na kutambua hatua mbalimbali za utengenezaji ili kuamua wapi na jinsi ya kuwashirikisha vijana na kwa kiasi gani. Zitumie ili kujua kiwango cha ushirikishaji wa vijana ambacho kizuri kwa ajili yako.

Page 15: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

14

• SURA YA 1: KUWASHIRIKISHA VIJANA • SURA YA 2: KUFANYA KAZI NA VIJANA – KUWA MSHAURI • SURA YA 3: MAADILI NA IDHINI

KANUNI ZA MSINGI

SEHEMU YA PILI

Page 16: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

15

SURA YA 1: KUWASHIRIKISHA VIJANA

NGAZI YA USHIRIKISHAJI WA VIJANA

SURA YA 3: MAADILI NA IDHINI

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 1 | Kuwashirikisha vijana

Kuna namnna nyingi za kuwashirikisha vijana katika radio yako. Katika hatua ya mwanzo kabisa unaweza kuliita jopo la vijana kutoa mrejesho wa wiki kuhusu kipindi cha vijana na kuonyesha mitazamo ya vijana kwenye vipindi vya mazungumzo au unaweza kwenda mbali zaidi na kukialika kikundi cha vijana waandae kipindi chao wenyewe. Inabidi ujue kiwango cha ushirikishaji wa vijana ambacho ni stahiki na endelevu kwa ajili ya kituo chako cha radio ya kijamii.

Bila kijali kiwango cha ushirikishaji, tunashauri kuwe na ushirikishaji wa mara kwa mara na wa kina ambao utawasaidia vijana kujifunza na kuchochea mchakato wa uandaaji wa kipindi. Dhamira ya dhati itakuwa ni mchango mkubwa kutoka kwa vijana. Katika ngazi ya Hart ya ushirikishaji wa vijana , ngazi tatu za kwanza – udhibiti, mapambo na kuigiza kama kuna usawa – zinajulikana kama ngazi ‘zisizo shirikishi’ ambapo vijana wanatumiwa na watu wazima kwa malengo yao.

Ili kuepuka hili, inabadi ushauriane na vijana katika kikundi chako katika kila ngazi ya mchakato na kuhakikisha kwamba wanaelewa vizuri jinsi michango yao itavyotumika. Ni wajibu wako kuwa mwangalifu ili kikundi kisijiingize au kuwaingiza wengine katika hatari kutokana na maudhui wanayorekodi na kutangaza.

Hii ni pamoja na kuhakikisha kwamba wao na vipindi vyao havitumiki kwa malengo ya kisiasa na kiuchumi, kwa mfano kuunga mkono kampeni za kisiasa au kutangaza bidhaa.

Hakikisha kwamba malengo na madhumuni yako yanafafanuliwa vizuri kwa uongozi wa kituo chako cha radio, vijana na wazazi na walezi wao kabla kuanza mradi. Kuunga mkono kwao ni jambo muhimu kwa mafanikio ya mradi.

Ni wajibu wako kisheria na kimaadili kuhakikisha kwamba haki za vijana zinalindwa na hazikiukwi. Usichukulie hili kama jambo gumu bali lenye faida kwa kila mmoja.

Inabidi uhakikishe kwamba vijana wanashirikishwa kama wachangiaji wa mara kwa mara, wanakuja kutoa maoni yao na kujenga uwezo wao. Hakikisha kwamba hili linafahamika kwa utawala wa kituo chako cha radio, vijana washiriki na wazazi au walezi wao.

Masaa matano kwa wiki ni kiwango cha juu ambacho vijana wanaruhusiwa kufanya kazi katika kituo cha radio ili kuandaa kipindi chao cha radio cha kila wiki. Hii inajumuisha:• Kipindi cha masaa mawili cha mkutano wa maandalizi ili kuchanganua mada• Kipindi cha masaa mawili ambapo waandishi vijana wanaingia mitaani ili kurekodi makala zao• Saa moja kwa ajili ya kutangaza kipindi moja kwa moja radioni

Zingatia kwamba vijana hawachukuliwi kwa ajili ya ‘kufanya kazi’ bali kushiriki kwenye kipindi cha radio, hii itachangia kuonyesha uhalisia wake na kutumia fursa za maendeleo binafsi.

Shirika la Kazi Duniani (ILO) linaelezea maana ya ajira za watoto kama:‘Kazi yoyote ambayo kiakili, kimwili, kijamii au kimaadili ni hatari na mbaya kwa watoto na inavuruga masomo yao au kuwa-zuia wasiende shule’Child Labor: A textbook for university students, International Labor Organization, 2004

Lakini ILO inaunga mkono shughuli ambapo watoto au vijana wanashiriki kwenye shughuli zinazochochea ukuaji, za kujitolea au kazi ambazo haziaathiri afya zao na ukuaji wao au kuvuruga masomo yao na hii inafafanuliwa kupitia:‘mpango wa mwongozo ulioandaliwa ili kurahisisha uchaguzi wa kazi au aina ya mafunzo ambayo yanachukuliwa kama chanya’(Article 6 (C), ILO Minimum Age Convention, 1973, (N° 138))

Page 17: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

16

KUCHAGUA WASHIRIKI

1. KUTAFUTA WASHIRIKA SAHIHI

Kama unaamua kufanya kazi kwa ushirikiano na asasi nyingine, ni muhimu kwa asasi hiyo kuelewa vizuri na kuunga mkonomradi wako na malengo yake.

2. FIKIRIA KUHUSU MIUNDO MBINU

UKUBWA WA KIKUNDI

SURA YA 2: KUFANYA KAZI NA VIJANA – KUWA MSHAURI MAHALI NA VIFAA

ORODHA YA VIFAA MUHIMU KWA AJILI KUFANYIA SEMINA NA VIJANA

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 1 | Kuwashirikisha vijana

Kuna njia nyingi za kufanya mradi uweze kusimamiwa na vijana. Kwa mfani unaweza kuunda vikundi viwili ambavyo vinaweza kubadilishana kila wiki, ambapo kila kikundi kiwe kinakuja kwenye kituo cha radio kila wiki ya pili.

Kwa vijana kutoa mrejesho kuhusu kipindi au kuchangia mara kwa mara kama wahojiwa, muda unaotumiwa kwa wiki kwenye kituo cha radio usizidi masaa matano

Kuwa na washiriki sahihi ni jambo la muhimu kwa mafanikio ya kipindi chochote cha vijana, hususani wanaposhirikishwa katika namna ambayo ni endelevu. Iwe unachagua kikundi wewe mwenyewe au kwa msaada asasi mshirika, hakikisha kuwa huharakishi mchakato wa uchaguzi. Kikundi ambacho hatimaye utakichagua kitakuwa msingi wa kipndi chako cha radio cha vijana. Kutokuchukua muda wa kutosha na tahadhari kumechangia kuanguka kwa miradi mingi ya radio za vijana. Usisahau kuweka usawa kwenye idadi ya washiriki wa kike na kiume. Pia jiandae kwa kuwa sio washiriki wote watashiriki kwa usawa au wataendelea, heshimu sababu zao.

Unaweza kushirikiana na shule ya sekondari iliyo karibu na kituo chako cha radio. Omba kufanya mkutano na mkuu au mwalimu maarufu wa shule na elezea dira yako, vijana wangapi unapenda kuwashirikisha na jinsi itakavyowasaidia wao na shule yao. Ulizia kuhusu vijana wanaopenda uandishi wa habari na kuongea mbele za watu au labda walio kwenye klabu ya midahalo au uandishi wa habari ya shule. Sisitiza kwamba kushiriki kwenye mradi wako hakutaingiliana na masomo ya washiriki.

Vinginevyo unaweza kushirikiana na asasi ya kijamii ambayo inafanya kazi na vijana katika sekta mahususi kama (VVU na Ukimwi, mabadiliko ya tabia nchi, vijana walio katika mazingira hatarishi)

Asasi mshirika mara kwa mara itasaidia kwenye masuala ya miundo mbinu kama kupata usafiri au sehemu ya kukutana na kutoa mwongozo muhimu kuhusu kufanya kazi na vijana.

Toka mwanzo washirikishe wazazi wa washiriki. Waalike kwenye mkutano wa kwanza na waambie kwamba utapokea maswali yao na mrejesho kutoka kwao katika hatua yoyote. Mara tu mradi unapoanza na kuendelea, wape CD ya vipindi vilivyorekodiwa na watoto wao (au namna nyingine ya kusikiliza) mara kwa mara.

Kiwango unachotaka cha ushirikishaji wa vijana na rasilimali za kituo chako – miundombinu – wafanyakazi na teknolojia – itasaidia kujua ukubwa wa kikundi. Kama unataka vijana wasiwe wachangiaji wa mara kwa mara, itakuwa rahisi kufanya kazi na kundi kubwa la hadi watu 20. kama unataka watangaze wenyewe vipindi vyao mara kwa mara, kikundi cha watu 10 ni rahisi kukisimamia.

Tangu wakati ambapo kikundi kinaanza kushirikishwa kwenye mchakato wa uandaaji wa kipindi, utahitaji mshauri kwa kila kikundi cha vijana watano.

Utahitaji kuwa na chumba kiknachofaa chenye viti na choo kilicho karibu. Hakikisha vyoo vinakidhi hitaji la kujistiri kwa wanawake na hakikisha kuna nafasi nyingine ambayo unayoweza kuhitaji. Toa vifaa vya kuandikia kama penseli na madaft-ari, nyaraka na machapisho ya marejeo. Orodha ya vifaa unavyoweza kuhitaji kwa ajili ya kuandaa semina inapatikana kwenye Kiambatisho 2

Page 18: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

17

USAFIRI

3. WASHIRIKISHE VIJANA KUHUSU MRADI WAKO

4. USIFANYE MAAMUZI YA HARAKA

MIFANO YA MICHEZO YA KUVUNJA UKIMYA NA KUTIA NGUVU: KIAMBATISHO CHA 3

5. UWE NA MCHAKATO WA UCHAGUZI ULIO WAZI

Iwe unawaambia waandike utungaji au waje kwa ajili ya mahojiano, vijana lazima wajue na waelewe ngazi za mchakato wauchaguzi na mambo yanayohitajika

6. ZINGATIA TOFAUTI ZA UMRI

7. HAKIKISHA KUNA USAWA WA KIJINSIA

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 1 | Kuwashirikisha vijana

Kuwashirikisha vijana wa mijini na vijijini ni wazo zuri lakini kuchagua washiriki wanaoishi umbali wa kilomita kadhaa ambao hawana usafiri ili kufika kwenye kituo cha radio, hatimaye unaweza kukosa wa mtu kufanya kipindi. Usafiri unaweza kuwa ghali sana na hiyo itawafanya vijana wanaoishi maeneo ya mbali kutoshiriki kikamilifu. Uzoefu unaonyesha kwamba njia bora ya kufanya ushiriki wa vijana kuwa endelevu ni kuchagua wale wanaoishi au wanaosoma karibu na kituo cha radio.

Kama kusipokuwa na mchango wa vijana, inabidi ushauriane na kuawashirikisha vijana kwenye kupangilia mradi. Kuna uwezekano wataleta mawazo mapya kwenye mradi, lakini ushirikishaji katika hatua za mwanzo kwa kiasi kikubwa utawapa hali ya kujiona wamiliki.

Huko Khayelitsha, kitongoji kilicho nje ya Cape Town, Afrika Kusini, Children’s Radio Foundation inafanya kazi kwenye kliniki ya vijana wanaoishi na VVU ambao wanaandaa na kutangaza vipindi kwenye kituo cha radio kilicho kwenye eneo hilo.

Washauri walifikiria kwamba kipindi kiwe na makala zilizorekodiwa kwenye eneo hilo zinazohusiana moja kwa moja na VVU na Ukimwi, kama kupima na unyanyapaa. Kwenye mkutano wa kwanza, vijana walielezea kwamba walitaka kutengeneza kipindi cha majadiliano ya moja kwa moja kwa njia ya simu na ushauri rika. Kwa kujua vionjo na tabia za vijana wa Khayelit-sha, walishiriki walijua kwamba muundo huu ungefanya kazi vizuri, ambapo washauri walikuwa hawajui chochote kuhusu hilo. Kwa kuwa washauri walishaurina na vijana, kipindi kilipewa muundo mpya wenye kuvutia.

Vijana ambao wana aibu au wasio waongeaji wanaweza kuwa washiriki wazuri. Usiweke mkazo kwa vijana wachangamfu tu kwenye jamii husika. Utashangaa kuona nani ataibuka kiongozi kwenye kikundi. Anza kila mkutano kwa michezo ya kikundi na kujumuisha nyimbo na kucheza, ni njia nzuri ya kuvunja ukimya na kuwafanya vijana kujuana na kufanya kazi kwa ufanisi kama kikundi.

Fafanua moja kwa moja kwenye mkutano wako wa kwanza kwamba kuwa radioni hakumaanishi kuwa DJ. Radio inahitaji pia watafiti, watangazaji na waandaaji wa vipindi. Orodhesha kazi na maandalizi yanayopaswa kufanywa na kikundi cha watu ili mtu mmoja aweze kutangaza kipindi. Ni muhimu kwamba kikundi hicho kijue nini kinachohitajika kwenye mradi na kiwe tayari kwa kazi kitakachofanya.

Kama wanakikundi wote wana umri sawa, itabadilisha hali ya kikundi. Itaathiri pia mahitaji ya washiriki na jukumu lako kama mshauri. Zingatia tofauti za ukuaji, hususani kwenye vikundi vyenye mchanganyiko wa rika tofauti. Wakati mwingine ni vizuri kuwa na vijana wa umri tofauti kwenye kundi moja lakini inaweza kuwa tatizo kwenye baadhi ya miradi

Mara nyingi wavulana wanakuwa watu wenye kujiamini na wazungumzaji zaidi kuliko wasichana hivyo ni kazi yako kuhakik-isha wasichana wana nafasi sawa ya kushiriki. Hii ni kuanzia mwanzo wa mchakato wa uchaguzi hadi kwenye semina na utangazaji.

Page 19: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

18

8. KAMWE USIWALIPE VIJANA ILI WASHIRIKI

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 1 | Kuwashirikisha vijana

Weka wazi toka mwanzo kuwa huu ni mradi wa kujitolea na hakuna mtu atakayelipwa. Hata hivyo unaweza kuwapa vinywaji baridi na vitafunwa kabla au baada ya semina. Kama baadhi ya vijana au wazazi wao watauliza vijana watapata nini kutoka kwenye mradi huu, unaweza kujibu ‘Stadi muhimu za maisha na sauti na maoni yako kusikika radioni. Washiriki watajifunza kufanya utafiti, kufanya mahojiano na kutangaza. Hii itaimarisha hali yao ya kujiamini’.

Shauriana na wazazi na walezi unapoandaa ratiba na kumbuka kwamba, wewe kama mshauri wao, inabidi uendane na ratiba ya vijana, na si vinginevyo. Mara zote shule ipewe kipaumbele na hii inaweza kuzuia au kuathiri ushiriki wao wakati wa mitihani.

Page 20: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

19

SURA YA 2: KUFANYA KAZI NA VIJANA – KUWA MSHAURI

JUKUMU LA MSHAURI

MAMBO YA MUHIMU KWA AJILI YA USHAURI

1. ANDAA MAZINGIRA YA UAMINIFU NA USALAMA

2. UWE NA HESHIMA

3. USIWE POA SANA

Wachukulie vijana kwa heshima na upendo, lakini kumbuka wewe sio rafiki yao

4. HESHIMU TOFAUTI ZAO

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 2 | Kufanya kazi na vijana – Kuwa mshauri

Sababu ya kuitwa mshauri ni kwa sababu utakuwa unawaongoza vijana kadri wanavyopata stadi fulani. Wewe sio mwalimu na sio mkufunzi-uko hapo kwa ajili ya kuwasaidia kujieleza na kukuza stadi zao ili kuwa watangazaji vijana.

Iwe unashauriana na vijana kuhusu mada wanazozipenda au unawaongoza wanapoandaa kipindi chenye maudhui yao wenyewe, mambo yafuatayo ni ya kuzingatia

Toka mwanzo onyesha kwamba unavutiwa na kila mmoja. Kwa namna hiyo, kila mmoja kwenye kikundi atajiona anatambuliwa na kutiwa moyo kujieleza kwa uwazi na uaminifu. Fafanua kwamba kila wanachosema kwenye vikao vyako kitakuwa siri, kwa mfano, unaweza kusema hakuna atakayemwambia mtu aliye nje ya kikundi kilichosemwa kwenye vikao. Fafanua kwamba hilo linakuhusu wewe pia.

Onyesha umuhimu wa usiri kwa kutumia mfano wa kijana aliyetoa siri kwa rafiki yake ambaye naye alimsimulia kila mtu shuleni. Wanaulize wana kikundi wangejisikiaje kama mmoja wa rafiki zao angevunja uaminifu wao kama hivyo.

Elezea tofauti kati ya faragha na usiri kwa kufafanua kwamba faragha inahusu mambo yote ya maisha ya mtu wakati usiri unahusiana na kile kinachosemwa na mtu. Faragha ambayo ni haki ya msingi ya watoto iliyotajwa kwenye kifun-gu cha 16 cha Mkataba wa Haki za Mtoto na usiri ni misingi ya uhusiano wenye uaminifu kati ya mshauri na vijana.

Tumia mwonekano wako na sauti yako kuonyesha heshima kwa vijana. Usijiweke kama kiongozi kwa kusimama mbele ya chumba kila wakati, huku ukiwaonyeshea vijana na kuwapa amri.

Historia yako na imani yako inaweza isiwe sawa na zile za vijana. Wanaweza kuwa wanatoka katika familia, tamaduni, jinsia na imani tofauti. Mara zote zikubali na kuziheshimu tofauti na kuhimiza mazungumzo.

Wasichana na wavulana wana vitu maalum wanavyovipenda na wanaweza kutofautiana kimtazamo. Mambo tofauti wanayoyapenda lazima yaheshimiwe na yasibezwe.

Page 21: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

20

5. KUWA MTU WA MSAADA

6. USIMLAZIMISHE MTU YEYOTE KUSHIRIKI

KUFANYA KAZI NA VIJANA

Kufanya kazi na vijana hakumaanishi kuwaambia jinsi ya kufanya kitu fulani. Bali ni kuwasaidia kutafuta namna ya kufanya waowenyewe.

VIDOKEZO VYA JINSI YA KUFANYA KAZI NA VIJANA

1. Jibu maswali yote lakini usitoe maelezo zaidi ya kile ulichoulizwa

2. Mara zote kubali kama kuna kitu hujui

3. Sikiliza. Ongea pale inapohitajika

4. Himiza kazi za kikundi na hakikisha maamuzi yanafanywa kwa pamoja

5. Changanya vikundi ili marafiki wasiwe kila mara wanafanya kazi pamoja

6. Waache vijana waongoze kadri iwezekanavyo

7. Kila mara toa mrejesho chanya

8. Hakikisha kikundi kinajifunza kwa kutenda

9. Mara zote watambulishe wana kikundi wapya na washirikishe kwenye mambo yanayoendelea. Hii inahusu hata wageni watuwazima

10. Tengeneza sheria na waache vijana watengeneze ‘sheria zao za ndani’ ili kutoa mwongozo wa kipi kinachokubalikana kipi hakikubaliki

NGAZI YA 1: RADIO KWA AJILI YA VIJANA Kamwe usitumie nguvu au matusi. Kama kijana anasumbua wakati wa kipindi rejea sheria za ndani na kiambie kikundi kiamue hatua ya kuchukua kutokana na tabia yake

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 2 | Kufanya kazi na vijana – Kuwa mshauri

Wakati mwingine wana kikundi watakuelezea mambo au matatizo usiyoyategemea kama kifo cha mzazi au mambo yanayo-watatiza. Sikiliza na uwe mtu wa msaada lakini kumbuka kuwa kikao hicho cha kikundi sio wakati wa kutoa majibu au unasi-hi na kwamba wewe sio mnasihi, tatibu wa akili au mtu wa ustawi wa jamii. Zungumzia suala hilo kwa faragha na mhimize mtu huyo aomba msaada au mwelekeze kwa mtu mwenye taaluma anayeweza kusaidia

Zingatia ukweli kwamba baadhi ya vijana wana aibu kuliko wengine. Kama mtu hapendi kushiriki kwenye kitendo, kamwe usimlazimishe. Usimweke kijana kwenye shinikizo. Badala yake fikiria namna nyingine za kuwafanya washiriki, kama kwa kuwaambia wakionyeshe kikundi zoezi la kuchangamsha mwili. Kiambatisho cha 3 kinaonyesha mazoezi ya kuchangamsha mwili.

Page 22: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

21

SURA YA 3: MAADILI NA IDHINI

MAADILI: KUFANYA KAZI NA VIJANA

KANUNI ZA MAADILI ZA MSHAURI

Kuwa makini na mambo ambayo yanaweza kuwa hatari kwa vijana – kimwili au kihisia – na yadhibiti

KWA UJUMLA NI MAKOSA:

• Kutumia muda mwingi peke yako na vijana wakiwa mbali na wenzao• Kumpeleka kijana mahali mtakapokuwa wawili tu wewe na yeye A MENTOR MUST NEVER:

• Kumweka kijana katika hatari kwa ajili ya kurekodi kipindi• Kumpiga au kumshambulia kimwili kijana • Kuwa na mahusiano ya kimwili au kimapenzi na kijana • Kuwa na mahusiano na kijana ambayo yanachukuliwa kama ya kinyonyaji, yasiyofaa au kudhalilisha• Kutenda kwa namna ya kudhalilisha au kumweka mtoto katika hatari ya kudhalilishwa • Kuwalipa vijana au kuwapa upendeleo kwa ajili ya kufanya kazi

MSHAURI LAZIMA AEPUKE VITENDO AMBAVYO VINAWEZA KUONEKANA KAMA VIOVU AU VYAKUDHALILISHA, KWA MFANO, KAMWE:

• Usitumie lugha, kutoa mapendekezo, kufanya ishara au kutoa ushauri usiofaa, kuudhi au kudhalilisha • Usiwe na tabia ambayo sio sahihi kimwili au inayodhalilisha kijinsia • Usiwaruhusu vijana kukaa hadi usiku wa manane kwe chumba cha watu wazima • Usiwafanyishe kazi vijana kwenye kituo cha radio kwa zaidi ya masaa matano kwa wiki

Je, unataka kushauriana na vijana? A Toolkit of Good Practice, Save The Children, 2003www.crin.org/docs/resources/publications/hrbap/childconsult_toolkit.pdf

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 3 | Maadili na Idhini

Kama mshauri unapaswa ujue haki za vijana kwa kuwa zinaathiri jinsi utakavyofanya kazi nao. Kwa maneno mengine, haki zao zitakuwa mwongozo wa taratibu zako. Kama mshauri, utaweza kushirikishana na vijana mapenzi yako kwa radio na kuchochea maisha yao na kuwasaidia kujieleza kikamilifu kuhusu mada ambazo ni muhimu kwao.

Unaweza kufanya kazi kwenye jamii ambayo haitoa fursa sawa kwa wasichana na wavulana. Kama mshauri una jukumu muhimu la kuhakikisha kuna haki sawa na kuonyesha fursa na namna mpya zenye faida kwa vijana kutoa maoni yao.

Wakati Brandon mwenye miaka 13 na Keith kutoka Manenberg, Afrika Kusini, waliamua kufanya mahojiano na mhalifu maarufu na mtumiaji wa madawa ya kulevya katika kitongoji chao, kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya , mshauri wao ilibidi awe mwangalifu

Walikubaliana kwamba wale vijana wangefanya mahojiano wenyewe lakini alipitia maswali pamoja nao ili kuhakikisha kwamba sio ya kuudhi. Halafu waliwasindikiza vijana pamoja na mkuu wa kituo cha eneo hili anayemjua vizuri mhojiwa. Walipofika nyumbani kwake, waliutambulisha mradi wa radio na vijana walitaka kumhoji kuhusiana na maudhui ya kipindi cha matumizi ya madawa ya kulevya. Walipitia kwa pamoja naye masuala ya idhini na kutotajwa jina. Vijana walifanya maho-jiano yao, wakiamini kuwa watu wazima watatu waliokuwepo wangeingilia kati kama mambo yangeenda ndivyo sivyo. Mahojiano yalirushwa hewani na mhojiwa aliridhishwa na matokeo yake.

Kama utaandaa michezo kwa ajili ya kufungua kipindi, zingatia kuna miiko fulani kuhusu kugusa kati ya wavulana na wasichana. Katika baadhi ya mazingira, hutakiwi kufanya michezo ambayo inahusisha ukaribu kama huo. Kama ni hivyo watenganishe vijana kulingana na jinsia kama utafanya michezo inayohusisha kugusana. Usisahau mila hizo zinakuhusu wewe na washiriki. Sio vizuri kwa mshauri wa kiume kumgusa mshiriki wa kike, hata kama ni sehemu isiyo na shida ya nyuma

Page 23: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

22

MAADILI: KUWAHOJI VIJANA

MAMBO MUHIMU ILI KUWA MSHAURI MZURI

1.

2.

IDHINI: KUWAHOJI VIJANA

3.

4. Kwa mfano masimulizi nyeti (udhalilishaji, ubaguzi), wahimize vijana watumie majina bandia

5.

6.

7.

8.

9.

10.

11.

12. Upitie na uboreshe mwongozi wako kila baada ya muda fulani, kwa mfano, mwanzo wa awamu mpya.

International Federation of Journalists Guidelines and Principles for Reporting on Issues Involving Children www.ifj.org/en/articles/childrens-rights-and-media-guidelines-and-principles-for-reporting-on-issues-involving-children

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 3 | Maadili na Idhini

Maadili ni kitu muhimu sana unapowahoji vijana walio chini ya miaka 18. Hakikisha kwamba unawalinda na haukiuki haki zao kwa kujifunza na kuzielewa kanuni za kimaadili na kuziimarisha kwa vitendo.

Unapowahoji vijana wanaweza kukushirikisha taarifa muhimu au kukuelezea matatizo wanayokumbana nayo. Unaweza kuwahoji vijana ambao wamekuwa wakinyanyapaliwa kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, jinsia au dini yao. Unaweza kukutana na vijana ambao wanafanya kazi au waathirika wa udhalilishaji. Wasichana kutokana kwenye mazingira magumu wako kwenye hatari zaidi ya haki zao kukiukwa kuliko makundi mengine.

Kufuata kanuni za kimaadili kutakusaidia kuhakikisha unaweka uwiano mzuri kati ya haki ya vijana kushiriki na haki yao ya kulindwa.

Wakati unafanya utafiti wako, hakikisha una taarifa za kutosha kuhusu hadhi ya kisheria na kijamii ya vijana unaowa-hoji. Hususani kama wanatoka kwenye kundi au jamii maalum au ya wachache (vijana wenye ulemavu, vijana wanao-fanya kazi, vijana wahalifu)

Hakikisha vijana unawaowahoji wanaelewa maana ya sauti zao zinazorekodiwa kurushwa hewani na watoe idhini kwa maandishi

Waelezee kwamba hawapaswi kuwataja watu wengine kwenye vipindi. Unapomtaja mtu kwenye habari, tumia majina ya jumla (rafiki, ndugu, mwalimu, n.k)

Hakikisha maswali yako hayakiuki haki ya vijana ya faragha, yanazingatia hali zao binafsi na yasiyoendeleza dhana potofu

Kamwe usimpe kijana upendeleo wowote kwa ajili ya kujibu maswali

Kamwe usimlipe kijana ili kuhojiwa

Hakikisha kwamba mwongozo wa kuwahoji vijana unapatikana katika lugha ya kienyeji kwa wafanyakazi wa radio na washirikishe wengine

Hakikisha wazazi au walezi wa vijana wanajua kwamba wanafanya mahojiano. Wafafanulie madhumuni ya mahojiano na matumizi yanayokusudiwa

Katika mazingira mengine yoyote, waambie vijana watumie majina yao ya kwanza na kusiwe na taarifa nyingine binafsi (jina la ukoo, anwani, jina la shule). Tofauti na runinga na magazeti, radio ni chombo cha habari kipofu, lakini sauti zinatambulika hivyo fikiria kama unaweza kubadilisha sauti.

Mara zote toa muktadha sahihi kwa ajili ya habari za vijana na hakikisha kwamba wanasimulia habari mambo halisi yaliyowatokea. Kama una shaka, ipitie habari pamoja na ndugu au mwalimu lakini hakikisha lakini hakikisha uhakiki unafanyika bila ya kuwaweka vijana kwenye hatari.

Page 24: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

Idhini iko pande mbili. Kama waandishi wa habari vijana wanavyoombwa idhini yao, kila wanaowahoji au kuzungumza nao lazima washauriane nao na kuomba idhini yao.

Ni muhimu sana kufafanua kikamilifu sababu ya kutangaza radioni kipindi kilichorekodiwa na kukishirikisha na jamii. Usisite kuelezea kwamba matangazo ya radio ni kurusha hewani taarifa kwa wasikilizaji wengi. Mara wanapokuwa wameelewa, inabid upate idhini ya mdomo ya waandaji wote wa vipindi vya radio na washiriki.

Tumia hadithi ili kikundi kielewe umuhimu wa idhini, kwa mfano, hadithi ya msichana aliyeadhibiwa shuleni, kwa kusimulia hadithi huku akitaja jina la mwalimu. Waulize vijana unaofanya kazi nao kingetokea nini kama hadithi hiyo ingerushwa hewani na kituo cha radio cha jamii na hivyo kila mtu kwenye jamii angesikia mwanafunzi akimkosoa mwalimu wake. Je, angepata madhara gani? Je, mwalimu angepata madhara gani? Je, mwanafunzi angekuwa tayari kukubali madhara hayo?

Vijana inabidi waelewe kwamba ingawa vipindi vinarekodiwa mbali na macho ya watu, vinaishi mara tu vinaporushwa hewani na kuwa na matokeo yasiyopendeza

Andika majina kamili, umri na mawasiliano ya wanaohojiwa. Fafanua kwamba taarifa hizo hazitarushwa hewani bali ni kwa ajili ya kuwajulisha kama michango yao imerushwa hewani. Pia hakikisha kwamba wanajua jinsi ya kuwasiliana na wewe iwapo wanabadilisha mawazo na hawataki michango yao kurushwa hewani

IDHINI: KUFANYA KAZI NA VIJANA

MFANO WA FOMU YA IDHINI: KIAMBATISHO 4

IDHINI: KUWAHOJI VIJANA

• • Hakikisha wewe na waandishi wa habari vijana wanawaambia wahojiwa maana ya mahojiano na kwamba

yanaweza kutangazwa radioni

Vijana watakaohojiwa inabidi kwanza watoe idhini ya mdomo

Kama mhojiwa ana miaka chini ya 18, anayehoji inabidi atumie jina la kwanza tu na kamwe asitumie jina la ukoo au eneo analoishi radioni. Wahimize vijana wanaohojiwa kufanya hivyo hivyo

“Habari, jina langu ni ............ na ningependa kuwauliza maswali machache kwa ajili ya kipindi kitakachorushwa hewani kwenye kituo chetu cha radio. Sawa?”

Sehemu ya Pili | Kanuni za Msingi | Sura ya 3 | Maadili na Idhini

23

Maana ya idhini ni kibali au makubaliano ambayo yamefikiwa katika ya kituo cha radio, vijana na wazazi au walezi ili washiriki wafanye kazi kwenye radio kwa usalama na kujiamini. Inamaanisha kuelewa kikamilifu, hususani kwa vijana wanaoshiriki kwenye mradi wako

Mwanzoni mwa mradi, vijana wote lazima waelewe idhini. Fomu zako za idhini lazima ziandikwe kwa lugha ambayo vijana wanaielewa. Epuka kutumia misamiati kama "haki miliki” au ‘hati miliki’. Unaweza kusoma kila mstari wa idhini pamoja na vijana na kuwauliza kama kuna kitu ambacho hawakielewi.

Lazima upate ruhusa na uungaji mkono wa wazazi, walezi na asasi washirika. Ni muhimu kwao kukuelewa na kujua kile utakachokuwa unafanya. Hii itakulinda na kukusaidia kuungwa mkono kwenye mradi wako. Kila fomu ya idhini ya mshiriki inabidi isainiwe pia na wazazi au walezi wake.

Kumbuka kwamba vijana wanaweza kubadilisha mawazo hata kama mwanzo walikupa idhini ya kusikiliza na kutangaza vipindi walivyorekodi.

Itabidi ujiandae kupambana na mazingira magumu ambapo wazazi wanaweza kukataa kutoa idhini. Kumbuka ni muhimu kuwashirikisha wazazi wakati wa mashauriano yako na jamii ili kuepuka vikwazo

Page 25: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

24

KABLA HUJAJIINGIZA KATIKA ULIMWENGU WA RADIO YA VIJANA, HAKIKISHA UNAKUMBUKA:

1. Umuhimu wa kuchagua kwa usahihi kikundi chako cha washiriki au vijana na kuwashirikisha toka mwanzo na mara kwa mara

2. Wajibu wako kama mshauri na inajumuisha kazi na majukumu yapi

3. Kwamba kila mmoja anayeshiriki atimize majukumu yake binafsi na idhini ya kila mmoja ni muhimu sana

KUWEKA VIZURI MALENGO NA MWONGOZO KUTARAHISISHA KIPINDI CHA MPITO KUTOKA KUPANGA MRADI WA RADIO YA VIJANA HADI KUIANZISHA

Page 26: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

25

• NGAZI YA 1: RADIO KWA AJILI YA VIJANA• NGAZI YA 2: RADIO PAMOJA NA VIJANA • NGAZI YA 3: RADIO YA VIJANA• NGAZI YA 4: KUWAFIKIA VIJANA

KUJUA KIWANGO CHA UWEZO NA KUPANGA

SEHEMU YA TATU

The levels will help you to assess your radio station’s capacity and include young people’s involvement in your planning at a manageable degree. The necessary skills, linked activities and model radio formats presented in each level advance progressively, so be aware that if you decide to have young people hosting a live audio debate as described in Level 3, your radio station will need to have met the foundation skills described in Level 1.

Page 27: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

26

Ngazi hii itakusaidia:• Kutangaza mahojiano na vijana kwenye kituo cha radio ya jamii• Kujumuisha zaidi maudhui ya vijana kwenye kipindi cha watoto• Kuboresha ubora wa kipindi chako cha sasa kwenye radio ya vijana

SURA YA 3: MAADILI NA IDHINI

TARATIBU (SAA 1)Weka taratibu ambazo zitafanyiwa kazi na wafanyakazi wenzako ambao wanafanyakazi na vijana au wapo kwenye mradi wa vijana

A Resource Kit for Journalists, Media Monitoring - Africa Codes of Practice (p19 to 24) www.mediamonitoringafrica.org/images/uploads/childrenmentoring.pdf

1. MAANDALIZI YA UTENGENEZAJI WA VIPINDI: VIKUNDI VYA MAJADILIANO

1.1 KUANDAA KIKUNDI CHA MAJADILIANO NA VIJANA (SAA 1) 1. Watambue vijana kwenye jamii au eneo lako ambao wanapenda uandishi wa habari na wakaribishe wahudhurie

majadiliano ya kikundi. Tumia ushirikiano ulio nao na shule na asasi za vijana

2. Usiwaite vijana wengi. Kumi ni idadi ya kutosha

3. Hakikisha kuna usawa kati ya wasichana na wavulana na kwamba umri wa washiriki unafaa kwa aina ya vipindi vya radio unavyoviandaa

4. Pitisha karatasi ya mahudhurio mwanzoni mwa kipindi ili kila mtu aandike mawasiliano yake

5. Endesha kipindi kwenye chumba au eneo ambalo linafikika kwa urahisi na vijana wote

6. Andaa mazingira rafiki na jumuishi. Ni vizuri kupanga viti kwa duara

7.

Kama inawezekana, tumia manila, karatasi na kalamu za kuandikia ubaoni au ubao ili kuandika kila kitu kinachosemwa na vijana ili wafanye marejeo kwa kuona na kurekodi

8. Kama unaweza andaa vinywaji na vitafunwa kwa ajili ya vijana kujifurahisha baada ya kipindi

9. Waruhusu vijana watembelee kituo chako cha radio baada ya majadiliano ya kikundi

10. Fanya kipindi kwa saa moja

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 1: Radio kwa Ajili ya Vijana

NGAZI YA 1: RADIO KWA AJILI VIJANA

Kumbuka kuwa vijana ni sehemu muhimu ya jamii na kwamba kama mfanyakazi wa chombo cha habari ni jukumu lako kuwawakilisha kwa usahihi na kwa heshima

Washirikishe vijana kwenye awamu ya maandalizi ya vipindi kwa ajili na kuhusu vijana kutoa maoni yao na kugundua mambo wanayoyapenda

Zingatia mambo tofauti yanayopendwa na wasichana na wavulana na yaheshimu. Umuhimu wa hili ni kugundua mambo ya kuyaingiza kwenye kipindi na kujenga imani ya washiriki

Page 28: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

27

1.2 KUENDESHA MAJADILIANO YA KIKUNDI KUHUSU MASUALA YA VIJANA (SAA 1)

1. Tengeneza sheria za ndani kuhusu mwenendo na tabia za washiriki wakati wa majadiliano ya kikundi. Waambie vijana wapendekeze sheria, ziandike na mwambie kila mmoja asaini

2. Vunja ukimya na wape muda vijana wa kujiweka vizuri kabla ya kuanza majadiliano kwa kucheza mchezo mmoja au miwili

3.

Waulize vijana mambo gani yanawaathiri vijana katika jamii yao na ambayo ni muhimu sana kwa maoni yao na waambie vijana watoe mapendekezo yao

4.

5. Unapokuwa na mambo kumi kwenye orodha yako, yapitie moja baada jingine na waulize vijana mambo gani yanahusiana.

Andika kwenye manila au ubaoni mambo yote yaliyosemwa

1.3 KUENDESHA MAJADILIANO YA KIKUNDI KWENYE RADIO (SAA 1) Tunga sheria za ndani kama mwanzo

Waulize vijana:

• Wakati gani wanasikiliza radio• Vituo gani vya radio wanavyosikiliza na kwanini• Vipindi gani wanasikiliza kwenye kituo chao cha radio ya jamii• Kama hawasikilizi kituo chao cha radio ya jamii, kwanini• Wangependa kusikia nini zaidi kwenye radio• Wangependa kipindi chao cha radio kiweje • Mambo gani yanapendwa sana na wasichana na wavulana

2. KUANDAA KIPINDI: MAKALA ZA RADIONI

2.1 KUANDAA KIPINDI: MAKALA ZA RADIONI

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 1: Radio kwa Ajili ya Vijana

Majibu yanaweza kuwa utapiamlo, kuishi na VVU na Ukimwi, na jinsi ya kupangilia mlo na kufanya mazoezi au jinsi ya kuweka uwiano kati ya masomo na michezo

Waandae vijana kabla ya kuanza majadiliano ya kikundi kwa kuwachezesha mchezo wa ‘kuwasha radio’ ambapo mshauri atazunguka kwenye chumba, atasimama mbele ya kila kijana na kujifanya anawasha radio ya kufikirika. Kila wakati, mtu afanye kitendo kulingana na anachokisia kwenye radio kwa wakati huo, kwa mfano, taarifa ya habari, taarifa ya hewa, kipindi cha mazungumzo au muziki.

Mmoja wa washauri aandike chini mambo muhimu yanayosemwa na vijana kwa ajili ya marejeo na mshauri mwingine aandike mambo yanayoweza kujumuishwa kwenye hatua inayofuata

Weka sanduku la maoni kwenye mlango wa kituo kama huna muda au uwezo wa kuendesha majadiliano ya kikundi. Ukweli ni kwamba ukiweza kutoa maoni bila kujulikana wakati mwingine ni vizuri kwa sababu vijana wanajisikia huru kuchangia katika namna yenye kujenga

Fafanua tofauti kati ya mahojiano na vox pop. Kwenye mahojiano, mtu mmoja anaulizwa maswali mengi. Kwenye vox pop, swali moja linaulizwa kwa watu wengi. Majibu kwenye vox pop inabidi yawe mafupi sana (sekunde 30 kwa kila moja).

Vox pops au ‘sauti za watu’ itakufanya ujue vijana wanafikiria nini kuhusu tatizo au suala fulani. Zinatoa fursa nzuri ya kurusha hewani mijadala pamoja ns wataalam wa mambo yanayohusiana na vijana. Itaimarisha vipindi vyako vya vijana na kupanua wigo wa mawazo.

Kila mwanajumuiya, awe maskini, aliyetengwa, makundi ya wenyeji, wasichana na wavulana lazima wapewe fursa ya kushiriki.

Page 29: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

28

2.2 KUWAHOJI VIJANA

• Kuwa makini na eneo. Kutegemeana na mada haitakuwa sahihi kuwahoji watoto wakiwa nyumbani au shuleni. Kwa mfano ikiwa wana familia au waalimu wapo, mhojiwa hawezi kuwa huru kuongea.

• Zingatia kimo chao. Usizungushe zungushe kipaza sauti juu kama wamekaa.

• Eleza kwa makini utawahoji kuhusu nini na mahojiano hayo yatatumika vipi.Unaweza pia kuwaonyesha jinsi ya kutumia kipaza sauti na wasikilize sauti zao.

• Usiwachunge sana.Wanajua zaidi ya unavyofikiri .

• Usitumie maneno magumu. Ongea kuendana na umri wao na tumia lugha wanayoielewa.

• Fafanua mambo. Msichana anayeishi kwenye eneo lenye uhalifu anasema kuwa kundi lake la muziki linamfanya awembali na mambo ya mtaani, kwa sababu ndicho alichosikia wengine wakisema au anafikiri kuwa ndicho unachotaka kusikia.Uliza kwa kutumia mifano hai kwa jinis gani mafunzo ya muziki yanamshughulisha sana, yanamfanya awe mwenye afya, kumuepusha na vishawishi vibaya.

• Watoto wanaweza kuzingatia kwa muda mchache sana. Kutokana na hali hiyo inashauriwa kuwa kiwango cha juu kabisa cha muda wa mahojiano kiwe dakika kumi.

• Wape fursa ya kujieleza kwa kutumia lugha waipendayo.

• Usiwahoji vijana wenye asili moja. Wahoji pia vijana waliotengwa na waliokosa fursa ya kujieleza, kwa mfano vijana wanaoishi mitaani au walio kwenye mazingira magumu au wakimbizi.

• Watie moyo wasichana na wavulana waoga au wenye aibu waweze kuchangia. Hakikisha kuna usawa wa kijinsia.

2.3 MAONI YA VIJANA Makala ya redio kabla hazirekodiwa zinaonyesha mtazamo wa kina wa maoni ya vijana. Pia unawahamasisha vijana kujieleza katika masuala fulani.

KUREKODI MAONI YA VIJANA (SAA 1)

1. Andaa sentensi nne zenye utata kuhusiana na mada ya kipindi chako kijacho cha redio

2. Waite vijana 15, kuwe na idadi sawa ya wasichana na wavulana (unaweza kuwaalika washiriki kwenye majadiliano ya kikundi).

Andika “KUBALI” na “KATAA” kwenye karatasi mbili na kuziweka sehemu tofauti za chumba.3.

4. Mwambie mshauri asome moja ya sentensi ulizoandika na kuwaambia washiriki wasimame kwenye alama ya “kubali” au “kataa” kulingana na mtazamo wao. Rudia sentensi hiyo mara mbili au tatu.

5. Mshauri aulize nani angependa kuelezea kwanini wengine wamekubali na wengine wamekataa. Pata maelezo ya vijana wanne.

6. Mshauri awaambie baadhi wajitolee kufanya yafuatayo: “Jitambulishe, rudia sentensi, kisha tuambie kama unakubali au kukataa. Halafu tuambie kwanini unakubali au kukataa. Wahimize waliojitolea wafafanue maoni yao yakiambatana na mifano au taarifa, na kusimulia hadithi zinazowahusu au mtu au mambo mengine yanayohusiana na suala hilo.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 1: Radio kwa Ajili ya Vijana

Kuwahoji vijana kuhusu mada wazipendazo kutaifanya programu yako kuzingatiwa na vijana zaidi kuliko watu wazima kuongea kwa niaba yao.

Vuta muda.Usiwapelekeshe vijana wala kuwahoji kama watu wazima.

Wafafanulie waandaaji vijana wa vipindi vya radio kuwa sentensi sio swalo na kwamba inaelezea maoni au suala fulani. Sentensi zifuatazo ziliandikwa na kijana aliyeshiriki kwenye program ya redio kuhusu unywaji pombe miongoni mwa vijana. ‘Vijana wanakunywa pombe kwa sababu hawajali maisha yao ya baaadae’. ‘Umasikini unachang-ia kwa kiasi kikubwa kuwafanya vijana kunywa pombe’. ‘Ulevi ni chanzo kikuu cha vurugu kwenye jamii yetu”.

Page 30: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

29

7. Tumia muda mchache na kila kijana ili kuendeleza hadithi yake.Wasaidie kuongeza taarifa kuhusu uzoefu wao binafsina kutengeneza sentensi nzuri za kuhitimisha

Rekodi maoni mapya ya vijana. Kila mchango usizidi dakika mbili.

8.

MFANO WA MAELEZO YALIYOREKODIWA: MAREJEO YA SAUTI 1

2.4 MAELEZO MAFUPI YA VIJANA

REKODI MAELEZO YA VIJANA (SAA 1)1.

2.

• Ajitambulishe na kutoa historia yake (umri,shule, hali halisi ya familia)

• Aeleze ni lini na kwanini alianzisha bustani ya mboga.

• Aeleze muda maalumu ambapo wazo hili lilimjia au lini aligundua anafanya kitu sahihi

• Washirikishe vijana ujumbe huo wa kuvutia.

3. Waelezee vijana wanaotakiwa kujieleza kuhusu umuhimu wa kutoa maelezo yaliyovuta hisia ili kuwagusa wasikilizaji. Andika pamoja nao mambo muhimu na fanyia mazoezi muundo kama ni muhimu.

4.

• Waeleze waandaaji vijana umuhimu wa kurekodi kabla ya kutangaza. Kwa kuwa hutauliza maswali, unahitaji kufanyia mazoezi kile ambacho atakisema

• Waambie vijana ni kama ushuhuda kwa kile hadithi yao binafsi au jambao wanalolipenda.

• Dakika mbili au tatu zinatosha. Ni vigumu kwa vijana kuongea kwa muda mrefu kama hawajaulizwa maswali.

MFANO WA MAELEZO YALIYOREKODIWA: MAREJEO YA SAUTI 2

3. MREJESHO

Ni muhimu kupata mrejesho kutoka kwa vijana ili kushauri nao ili kupata mawazo ya awali.

VITI VYENYE ALAMA YA CHANYA NA HASI.(DAKIKA 30)

1. Chora alama ya kujumlisha na ya kutoa kwenye karatasi mbili.

2. Weka viti viwili mbele ya nusu duara ya viti na kisha bandika alama “chanya” (kujumlisha) kwenye upande mmoja na alama “hasi” (kutoa) kwenye upande mwingine.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 1: Radio kwa Ajili ya Vijana

Makala hii imeandaliwa tayari kwa kurushwa hewani.Unatakiwa uwe na uwezo wa kurekodi mchango wa kila mtu utakao-tolewa kwa usahihi kuepuka masahihisho kwa kufuata hatua za hapo juu na kuwapa taarifa vijana kwa usahihi.

Rekodi kipindi cha redio kwa kumtambulisha kwa wasikilizaji wako kijana mwenye jambo zuri analolipenda, ambalo lina mchango kwa jamii yako au anayepitia kipindi kigumu. Iwe ni masimulizi ya kijana mwanamichezo au kijana aliyepoteza wazazi wake kwa ugonjwa wa Ukimwi. Itawafanya waguswe na maisha ya kijana na kuwavutia wengine.

Kama ujuavyo maelezo si sawa na mahojiano.Ni masimulizi ya mtu wa kwanza ambapo kijana anayeongea kuhusu yeye mwenyewe bila kuingiliwa. Inaweza kuwa njia nzuri ya kuwafanya wengine waguswe na maisha ya huyo mtu.

Tafuta kijana mwenye kisa sawa na mada yako unayofikiria kwa ajili ya kipindi, kisha panga siku ya kukutana ili kurekodi kisa chake

Andaa mambo ambayo unayotaka kuyazungumzia. Kwa mfano kama unaongea na kijana aliyeanzisha bustani ya mboga shuleni kwa ajili ya kulisha familia fukara kwenye

Rekodi maelezo ya sauti.

Page 31: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

30

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 1: Radio kwa Ajili ya Vijana

3. Waeleze kuwa hii ndio nafasi ambayo wanaweza kuelezea kwa uhuru kile wakipendacho na kile wasichokipenda kuhusu kipindi, na pia wanafikiri kipi hakikwenda vizuri na watoe mawazo zaidi.

4. Chezesha kipengele cha sauti walichochagua.

5. Waambie kwa zamu wanafunzi wakae kwenye viti “chanya” na kusema kipi walichopenda au kwenye viti ‘hasi” na kusema kipi hawakukipenda

6. Andika mambo muhimu waliyoongea kwenye daftari.

• Sisitiza kuwa washiriki wako sehemu salama kuzungumza kile wanachofikiri.

• Wakumbushe kuhusu sheria za ndani walizozitengeneza wenyewe, kwa mfano kuheshimiana, au kumpa kila mmoja nafasi ya kutoa maoni.Ni muhimu kufanya hivi ili kila mmoja awe huru kutoa maoni yake.

• Kama ni lazima, mwuulize maswali mtu aliyekaa kwenye kiti ‘chanya’ au hasi ili kuwasaidia washiriki kuelezea nini walikipenda na nini hawakukipenda, kwa mfano, ‘kwanini hukupendezwa na kipindi? au ‘nini kifanyike kuboresha zaidi?.

Andaa mkutano na wafanyakazi wa kituo cha radio walioshiriki kwenye kipindi ili kuwapa taarifa ulizokusanya na kuhakikisha zinakusaidia kwa ajili ya baadaye.

Hadi hapo utakuwa umepata njia za kujumuisha zaidi maoni na sauti za vijana katika kipindi chako katika namna ambayo ni endelevu. Sasa unaweza kuendelea kuwashirikisha zaidi vijana kwenye mchakato wa uandaaji wa vipindi. Hatua ya 2 imeandaliwa ili kukusaidia kufanya hivyo.

Page 32: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

31

• Andaa mazingira ya kujifunzia ambayo hayafanani na darasa• Anzisha semina zenye mambo ya kufurahisha au mazoezi ya viungo.• Andaa chumba bila kufuata sheria ili kila mtu ajisikie huru kushiriki. Kupanga viti kwa duara mara nyingi ni vizuri

kuliko kuvipanga katika safu.

Wasaidie washiriki waweze kuchagua au kutaja watu katika jamii wenye visa waweze kusimulia kwenye mada maalum

Chagua moja ya mada zilizotajwa kwenye majadiliano ya kikundi

1. KABLA YA KUANDAA KIPINDI: KUITAMBUA JAMII.

KUITAMBUA JAMII (SAA 1)

1.

HATUA YA 1: KUANDAA KIPINDI: MAJADILIANO YA KIKUNDI

2.

Chora maduara matatu kwenye chati au ubaoni. Andika mada yako ndani ya duara la kwanza, andika “sehemu” kwenye duara la pili na neno “watu” ndani ya duara la tatu.

3.

4.

5.

2. KUANDAA KIPINDI: MAKALA ZA RADIO

2.1 VOX POPS

KUTOKA MTAANI HADI STUDIO (SAA 1)1.

2. Wafundishe jinsi ya kutumia vifaa na kufanya mazoezi ya kurekodi kabla ya kwenda kwenye jamii.

HATUA YA PILI: RADIO PAMOJA NA VIJANA.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 2: Radio Pamoja na Vijana

Sasa umevielekeza vipindi vyako vya radio vya vijana katika mambo yapendwayo na vijana, unaweza kuupeleka ushiriki wa vijana kwenye hatua nyingine ya kutengeneza vipindi vya radio pamoja na vijana huku ukiendelea kusimamia mchakato wa uandaaji na utangazaji.

Waambie wana kikundi wafikirie kuhusu kile wanachotaka kuongea kuhusiana na mada na uwasaidie kutafuta sehemu. Kadri wanavyotoa mapendekezo, andika kwenye duara la mada. Kwa mfano kama mada inahusu ajira ya watoto, wape nafasi ya kutoa mawazo yao kuhusiana na wanachotaka kujadili au wanachojua kuhusiana na hilo (haki za mtoto, shinikizo la familia au kuacha shule). Halafu waamue moja ya maeneo haya, kwa mfano, msichana anayelazimishwa kuacha shule ili afanye kaze.

Waambie wataje sehemu wanayodhani inaendana na eneo walilochagua kwa mfano, shule, vituo vya ustawi wa watoto, kaya au idara za serikali.

Wasaidie vijana pindi wakifikiria swali moja rahisi kuhusiana na mada. Mara zote kumbuka eneo walichochagua.

Mwisho, waambie wana kikundi wataje watu wanaohusiana na eneo hilo kama walimu,wafanyakazi wa ustawi wa jamii, mwanafunzi aliye shuleni au aliyeacha shule na mshauri wa wanafunzi.

Kwa kuwa kikundi kimeshatambua eneo kwa ajili ya kipindi, mahali ambapo wanaweza kupata habari na nani wa kumhoji, unaweza kuwasaidia kuandaa makala zilizorekodiwa kwa ajili ya kuzijumuisha kwenye kipindi chako cha radio cha vijana.

Vox pops ni muundo mzuri wa kutumia ambapo vijana wanaandaa maudhui kwa mara ya kwanza. Ni njia nzuri ya kupata hamu ya kwenda kwenye jamii na kuuliza maswali.

Makala zifuatazo zimeandaliwa ili kurekodiwa moja kwa moja ili kuepuka marekebisho baadaye. Makala hizi zinahitaji muda wa kutosha na nguvu nyingi katika hatua ya maandalizi.

Page 33: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

32

3.

4. Nenda nao ili kuwasaidia kurekodi.

2.2 MAHOJIANO

KUJIFUNZA KUULIZA MASWALI MAZURI (DAKIKA 30)

1. Waambie washiriki kuwa wanaweza kukuuliza maswali kuhusu kazi ya radio.

2. Waache waulize maswali kama vile ni kipindi cha michezo.

Andika maswali kwenye chati au ubaoni.3.

4.

5. Baada ya kujibu kila swali, wasaidie waweze kujua ni jinsi gani wameweza kurekebisha kiwango cha maswali yao.

Unaweza kuwapa waandaji vipindi vijana mwongozo wa kuuliza maswali mazuri, kwa mfano:

• Uliza maswali yasiyohitaji majibu ya ndio au hapana. Na ikiwa mhojiwa akijibu “ndio” au “hapana” muulize ‘kwanini’?

• ikiliza kwa makini habari za kusisimua au usizozitarajia na kisha uulize swali.Usitegemee tu maswali yaliyoandaliwa. Mara nyingi maswali ya yanayofuata huleta majibu mazuri.

• Epuka maswali yanayotoa majibu ya kwa mfano “kuwa mtangazaji ni furaha, sawa?” Njia nzuri ya kuuliza swali kama hili ni “unajisikiaje kufanya kazi radioni?”

• Rahisisha.Usiulize maswali mawili kwa pamoja. Mara nyingi watu hujibu la pili na kusahau la kwanza

Himiza maswali kuhusu mambo yanayowaathiri wasichana. Jadili jinsi mada nyeti na miiko zinavyobidi kufanyiwa kazi.

KUIGIZA (DAKIKA 20)Hili ni igizo ambalo washiriki hujifanya wapo kwenye mahojiano mmoja akijifanya mhojaji na mwingine mhojiwa ili kufanyia mazoezi muundo wa mahojiano.

1. Tumia mada kama “Kukufahamu vizuri”

2. Mwambie mmoja ajitolee kuwa mwandishi

3. Mwambie mmoja ajitolee kuwa mhojiwa

4. Mwandishi toka mwanzo wa igizo aende kwa mhojiwa na ajitambulishe

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 2: Radio Pamoja na Vijana

Wasaidie kufanya mazoezi ya kujitambulisha na staili. Kwa mfano “Habari, jina langu ni Kondwani na leo ningependa kuwauliza wanajamii, ni sababu ipi inayowafanya wasichana kulazimika kuacha shule.Hii ni kutoka redio (jina)

Wafafanulie waandaaji vijana wa vipindi vya radio kuwa kuuliza maswali hutokea tu kwa wengi wetu. Ndivyo tunavyojifunza kuhusu ulimwengu unaotuzunguka. Pia fafanua kwamba kuna tofauti kati ya kuuliza maswali na kufanya mahojiano. Mahojiano yanawapa fursa zaidi ya kuuliza maswali yote kuhusu maisha, kazi, na mawazo yao. Kipaza sauti kinawaruhusu kuuliza maswali lakini wana wajibu wa kuuliza maswali yenye maana.

Wakimaliza kuuliza maswali ya kutosha (kiwango cha juu ni 10) yapitie na kisha jibu swali moja baada ya lingine. Kuwa makini na maneno yaliyotumika kwenye kila swali na pia jibu tu kile kilichoulizwa. Kisha yatumie maswali yao kama mfano na ueleze tofauti iliyopo kati ya maswali-wazi (ambayo huwezi kuyajibu kwa kutumia “ndio” au “hapana” na mara nyingi huanza na ni kwa jinsi gani, nini, lini, kwanini, au kuulizia kuhusu na kupelekea majibu mazuri) na maswali funge (ni yale ya “ndio” au “hapana” hayahitaji anayejibu kutoa maelezo).

Kama mmoja wa washiriki mmoja aliuliza “je ni jambo kufurahisha kuwa mtangazaji wa redio? “(swali funge), jibu lako lazima liwe “hapana” ni muhimu kujibu maswali kama yalivyoulizwa.kwa kufanya hivyo watajifunza jinsi ya kuuliza maswali mazuri na kupata majibu mazuri.

Tumia muda kuweleza waandaaji vijana wa vipindi vya radio kuwa badala ya kuuliza “je, ni inafurahisha kuwa mtan-gazaji wa radio? Swali wazi kama vile “Je, unaweza kueleza jinsi unavyojisikia unapotangaza kipindi? Ingekuwa njia nzuri zaidi ya kupata habari na maelezo.

Page 34: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

33

5. Waambie washiriki wengine waseme “tulia” wakiona sehemu mhojaji angeweza kufanya vizuri.Waulize wanafikiri wapi kuna makosa na watoe mawazo yao ili kuboresha mahojiano.

Sisitiza hatua za kufuata wakati wa kufanya mahojiano.

• Chagua mada.

KABLA YA KUANDAA KIPINDI: KUITAMBUA JAMII

Washauri waandaaji vipindi vijana yafuatayo:

• Kuchagua mtu wa kumhoji kama vile mtu atakayetoa ushauri wa kitaalamu au mwenye uzoefu na mada husika. Hakikisha unachagua mtu kutoka kwenye jamii husika anayeijua mada na atakayekuwa tayari kukupa taarifa unazozihitaji. Hakikisha huwasahau wanawake kwenye mahojiano.

• Kumjua vya kutosha mhojiwa kabla ya mahojiano

• Kujiandaa kwa mahojiano. Andika maswali machache, angalia kama vifaa vinafanya kazi vizuri na pia beba betri za ziada kwa ajili ya kinasa sauti

• Muombe mhojiwa ridhaa ya kurekodi na kutangaza mahojiano hayo.

• Mara zote wajitambulishe na watambulishe pia wahojiwa na utakachozungumzia mwanzoni mwa kipindi.

• Mara zote washikilie kipaza sauti mwenyewe. Kamwe wasimpe mhojiwa. Wawe makini na vifaa muda wote.

• Hakikisha kuna hali ya mazungumzo katika mahojiana isiwe tu unasoma maswali. Fuatilia masuala muhimu yanayosemwa na mhojiwa, hata kama hayakuwa sehemu ya maswali ya mwanzo

• Mshukuru mhojiwa na kuhitimisha mazungumzo

2.3 MAONI YA KUSIKIA

HATUA YA 1: KUANDAA KIPINDI: MAONI YA VIJANA Waeleze waandaaji vipindi vijana kinachofanya maoni mazuri ya kusikia kwa kusema, kwa mfano:

• Mtangazaji lazima aanze kwa kujitambulisha (Habari, jina langu ni Tina na leo nitazungumzia umuhimu wa ngono salama) ikifuatiwa na maelezo kuhusu masuala yatakayojadiliwa kwa mfano “kuna mambo mengi yanayozungumzwa kuhusiana na ngono salama katika jamii yangu, lakini tukifuatilia kwa makini, matendo yana nguvu kuliko maneno”.

• Mtanzaji lazima atoe maoni yake kwanza kwa mifano iliyo katika jamii au kuelezea kisa chochote kilichowakuta. Ambacho ni cha binafsi zaidi

• Malizia kwa mapendekezo ya jinsi ya kutatua tatizo kwa sentensi kama “ Sisi kama vijana tunatakiwa kujilinda wenyewe, tukijua jinsi ya kuwa na taarifa. Tukijua jinsi ya kufanya ngono salama, tutaishi kwa afya na maisha marefu. Wasikilizaji wanaweza kumwuliza mwalimu au kutembelea zahanati kupata maelezo zaidi”.

2.4 MAELEZO YA KUSIKIA

HATUA YA 1: KUANDAA KIPINDI: MAELEZO YA VIJANA

KUTAFUTA HABARI BINAFSI ZA WATU (DAKIKA 30)

1. Wagawanye washiriki katika makundi na kasha wachague mtu anayefaa kuhusiana na mada ya kipindi. Waulize kama wanajali masuala ya jinsia au wabaguzi

2. Wajadiliane katika makundi yao

• Kwa nini wamemchagua huyu

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 2: Radio Pamoja na Vijana

Katika hatua ya kwanza tumeona jinsi ya kurekodi maoni ya vijana yatakayo jumuishwa kwenye vipindi vyako. Kwenye hatua ya pili tumeonyesha jinsi ya kuwasaidia kurekodi maoni yao wenyewe au maoni ya kusikia.

Waongoze washiriki kurekodi uzoefu wao binafsi kuhusiana na mada au wasaidie kutengeneza maelezo ya sauti ya mtu mwenyewe uzoefu au utaalamu.

Page 35: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

34

• Watamhoji wapi

• Sauti zipi zinahusiana na habari yake na wapi pakuzipata

• Andika maswali watakayouliza

3. Kila kundi litaje mtu waliomchagua na wamepanga nini kwa ajili ya maelezo ya kusikiliza

4. Waruhusu washiriki watoe mrejesho na kutoa mapendekezo yao kuhusiana na mawasilisho ya kila kikundi

5. Jiandae kurekodi maelezo ya mtu huyo

1. Waanze kurekodi sauti inayoendana na kile kinachokifanywa na mhojiwa

2. Mhojiwa ajitambulishe na kujieleza au anafanya nini kwa kujibu maswali mliyofanyia mazoezi

3. Hitimisha mahojiano kwa kutoa shauri au kuwatia moyo wasikilizaji wanaoweza kuwa kwenye hali kama hiyo.

3. MREJESHO

HATUA YA 1: BAADA YA KUANDAA KIPINDI: MREJESHO

Hatua ya 3 imeandaliwa kukusaidia kuwajumuisha vijana hata kwenye kupata wazo, kuandika mwongozo na kutangaza vipindi vya radio

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 2: Radio Pamoja na Vijana

Hakikisha umefuata hatua za zilizotajwa kwenye ukurasa uliopita na kukikumbusha kikundi kuwa maelezo ya kusikiliza ni hali ya mtu kujieleza bila kuulizwa maswali na wanatakiwa kufanya mazoezi na mhojiw kabla ya kurekodi ili kuepuka makosa wakati wa kurekodi. Mara wanapomaliza inabidi:

Kama kwenye hatua ya 1, ulipopata mrejesho kutoka kwa vijana kuhusiana na kipindi ulichoandaa, fanya hivyo kwa vipindi vyote walivyokusaidia kuandaa. Siyo tu itaboresha vipindi vyako vya radio ya vijana na maudhui yake, bali pia itawafunza vijana jinsi ya kutafakari kwa kina mawazo yao. Mara nyingi kutumia taarifa ulizopata kwa njia hii unapoandaa vipindi vingine.

Iwe unaziweka pamoja au unazitumia kila moja peke yake, miundo ya uandaaji wa vipindi vya radio iliyojadiliwa katika katika hatua hii, itakusaidia kuibua sauti sauti na maoni tofauti ya vijana na kutengeneza vipindi vizuri ambavyo havih-itaji kufinyiwa kazi baada ya kuandaliwa

Page 36: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

35

HATUA YA TATU: RADIO YA VIJANA

SURA YA 1: KUWASHIRIKISHA VIJANA, SURA YA 2: KUFANYA KAZI NA VIJANA: KUWA MSHAURI

1. KABLA YA KUANDAA

1.1 DIRA YA KIPINDI CHA JARIDA LA VIJANA (SAA 1)

1. Jadili maswali yafuatayo pamoja na mshauri na vijana:Washiriki wote wataweza kupata stadi za kuandaa kipindi ndani ya miezi sita na kubeba majukumu yao?•

• Inawezekana kurusha kipindi cha radio kilichoandaliwa na vijana kila wiki?Ni wasikilizaji wapi waliokusudiwa kuongeza uelewa wao kuhusu masuala ya vijana katika jamii yako?•

2. Mara malengo ya kipindi yakishaeleweka, fikiria kuhusu mambo yafuatayo:• Elezea kuhusu kipindi chako na eleza unachotaka kufanya• Andika aya moja inayoelezea malengo ya kipindi• Kwa nini ni muhimu kuwa na kipindi cha vijana kwenye kituo chako cha radio ya jamii• Itasikikaje?• Lugha gani zitatumika? Kipindi kitachukua muda gani? Na mada itakuwa ipi?• Je kitakuwa ni kipindi cha makala zilizorekodiwa au kipindi cha mazungumzo ya moja kwa moja na wageni studio.• Je, mshauri atawasaidiaje vijana? Nani atafanya kipi?• Kwa jinsi jamii iliyotofauti itaathiri maudhui ya kipindi?

1.2 JINA LA KIPINDI NA KIBWAGIZO

Epukana mambo ya hatimiliki kwa kutumia kipande cha wimbo maarufu ambao hauna haki ya kuutumia.

MFANO KWA VIJANA-MILIO ILIYOTAYARISHWA: RASILIMALI SAUTI 3

UTAMBULISHO WA KIPINDI (SAA 1)

1.

2. Waambie wapige kura kuchagua jina wanalolipenda.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

Kwenye hatua hii, kituo chako cha radio kwa vijana kitakuwa kimejumuisha vijana na kitakuwa na uwezo wa kushu-ghulikia mambo yanayowaathiri vijana moja kwa moja kupitia vipindi ambavyo vinapaza sauti na kutoa maoni ya vijana. Sasa uko tayari kushauri na kuwaelekeza wanapotunga na kutangaza kipindi chao moja kwa moja radioni.

Ni muhimu kutambua wajibu wako kama mshauri. Badala ya kutengeneza maudhui kwa ajili ya vijana, sasa unawasaidia kutengeneza maudhui yao; hicho ndio kipindi cha radio cha vijana kwa ajili ya vijana. Kama ujuavyo kipindi cha radio, ni kipindi chenye mada, kinaweza kurushwa moja kwa moja au kurekodiwa na kuendeshwa na mtangazaji mmoja au wawili. Inaweza kuwa na makala ambazo zimerekodiwa kabla, mahojiano ya moja kwa moja, mdahalo na simu kutoka kwa wasikil-izaji. Vipindi vinaweza kwenda kuanzia dakika 10 hadi nusu saa.

Kabla vijana hawajaanza kuandaa kipindi unatakiwa ufanye nao kazi kwa pamoja ili kupata dira yenu kwa ajili ya kipindi cha vijana.

Kutunga jina la kipindi wao wenyewe kunasaidia vijana kujisikia wamiliki wa kipindi na kukipa utambulisho unaowaonyesha wao ni nani na watakuwa na watakuwa wanaongelea nini. Wakisha chagua jina, watengeneze kibwagizo kitakachowasaidia wasikilizaji kutambua kipindi

Kibwagizo kiwe na sekunde 30 na kitasikika mwanzoni mwa kipindi. Kijumuishe jina la kipindi na unaweza kuwa wimbo waliotunga na kuimba wenyewe.

Wambie washiriki wataje neno moja ambalo litakalotambulisha kipindi chao na wandike mapendekezo yao kwenye karatasi. Wasisitize wachague majina yenye mvuto yanayoendana na dira ya kipindi na watumie lugha za asili na istilahi za vijana kama ikiwezekana

Page 37: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

36

3.

Wakishachagua jina, waanze kufanyia kazi kibwagizo. Watafakari kuhusu maneno waliyotamka mwanzoni

4. Watafute mdundo, nyimbo au ghani

5. Wakiwa tayari, waambie wapige kibwagizo

6. Warekodi kibwagizo na kukipiga tena.

1.3 MAJUKUMU

Kabla vijana hawajaendelea, inabidi wapewe majukumu. Hii itawasaidia kuwajibika kwa baadhi ya mambo na kuwapa hali ya umiliki

Hakikisha wasichana wanapata fursa ya kushiriki kwenye uongozi. Hakikisha pia wanaungwa mkono vya kutosha na mshauri wao ili kutekeleza jukumu la uongozi.

KUGAWA MAJUKUMU (DAKIKA 15)

1. Anza shughuli kwa mchezo unaosisitiza kufanya kazi kwa pamoja

Orodhesha majukumu tofauti tofauti kwenye chati au ubaoni

Eleza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na kwamba kuandaa kipindi ni juhudi za pamoja ndio maana majukumu yanagawanywa kwa watu tofauti, kulingana na majukumu yao.

2.

3. • Watangazaji• Wahandisi wa sauti• Waandaaji kipindi• Watafiti• Waandishi wa habari (kufanya maandalizi kabla ya kureko sauti)• Wapokea simu (ikiwa umewakaribisha wasikilizaji kupiga simu)

4. Pitia majukumu moja baada ya jingine na kisha kiulize kikundi wanafikiri kila jukumu linahusisha nini. Andika mambo wanayosema pembeni ya kila jukumu

5. Wajichagulie majukumu lakini usisahau kueleza kuwa majukumu hayo yatabadilika na kila mmoja atapata fursa ya kuchukua moja kati ya majukumu hayo.

Kama ni kundi kubwa, itakuwa vizuri kuligawanya katika makundi mawili na wawe wanabadilishana. Kama ni kundi dogo, unaweza kugawa majukumu mawili kwa mtu mmoja kwa mfano mtafiti anaweza kuwa mpokea simu.

1.4 MUDA WA KIPINDI NA KIDOKEZO

ANDAA MUHTASARI WA KIPINDI (DAKIKA 30)

1. Wasaidie vijana kufanyia kazi kile wanachokitakaAndika mada na eneo kwenye chati au ubaoni, kwa mfano VVU na Ukimwi: jinsi ya kupima.Orodhesha chini yake miundo tofauti ya redio (Vox pops, mahojiano, maoni ya kusikiliza na maelezo ya kusikiliza) Rejea ramani ya jamii uliyotengeneza kwa ajili ya mada ya kipindi na kisha andika watu na sehemu zilizotajwa.

• • • • Mwambie mtu ajitolee kuchora mistari ili kuunganisha kila muundo na sehemu na mtu.

2.

Miundo yote ikishaunganishwa na watu na mahali palipotajwa kwenye zoezi la kuitambua , kikundi kiandike muhtasa wa kipindi kwenye karatasi.

3. Waelekeze kufanya yafuatayo • Kuwasiliana na watu wanaopenda kuwahoji• Wajitambulishe wao ni nani, wanafanya nini na kwa nini wangependa kuwahoji.• Panga siku ya kukutana nao.• enga hisia kwa mawazo ya wahojiwa yanahusiana na mada na kile unachotegemea kupata kutoka kwao.

Huu ni muda wa vijana kuona wanataka nini na kuanza kutengeneza muundo wa kipindi chao.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

Page 38: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

37

MFANO WA KARATASI YA KIDOKEZO

KIPENGELE INAHUSU NINI MUDA

KIBWAGIZO CHA KIPINDI Kibwagizo Sekunde 30

UTANGULIZI Kuwakaribisha kwenye kipindi(watangazaji wajitambulishe na kutambulisha kipindi)

Sekunde 30

KUTAMBULISHA MADA Watangazaji watambulishe mada ya kipindi na kuifafanua

Dakika 1

KUTAMBULISHA VOX POP Watangazaji watambulishe vox pop na kuwatambulisha pia vijana waliorekodi

Sekunde 30

VOX POP Vox pop Dakika 2

KUHITIMISHA VOX POP Watangazaji wawashukuru waandaaji, warudie kwa muhtasari kile kilichosemwa na kipi kilikuwa cha kufurahisha kwenye vox pop, warudie kwa muhtasari mada ya kipindi na kupiga wimbo

Sekunde 30

NYIMBO Wimbo Dakika 2

2. KUANDAA: MAKALA ZA RADIONI

2.1 MIDAHALO YA MOJA KWA MOJA RADIONI

KUELEWA MDAHALO WA RADIONI (DAKIKA 25)1. Waulize vijana kwenye kikundi wanafikiria nini kuhusu mdahalo• Angalia kwa kiasi gani wanajua kuhusu mdahalo • Waambie watoe mifano ya midahalo wanayoijua au ambayo waliwahi kusikia na kuona hapo kabla.

2. Vitu muhimu vya kupitia pamoja na kikundi:

• • Wakumbushe kuwa ingawa watakuwa wanatangaza kipindi, wajibu wao ni kuuliza maswali na kusikiliza hoja za

wasikilizaji wao, na hoja zao. Inabidi waulize maswali kwa niaba ya wasikilizaji pia

Wageni lazima wawe na uelewa wa kutosha kuhusu mada na kuwa na mitazamo tofauti.

3.

• Watangazaji watambulishe mada itakayojadiliwa

Halafu fafanua kwamba midahalo ya radioni ina muundo maalum, kama ifuatavyo:

• Watangazaji wawatambulishe wageni

• Wageni wapewe muda wa kuelezea mitazamo yao.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

Tambulisha miundo zaidi ya kusikiliza ambayo kundi linaweza kurekodi na kuitumia kwenye vipindi vyao pindi wanapohisi kuwa wameridhika na miundo ya kusikiliza waliyojifunza kwenye Hatua ya 2.

Midahalo ni njia nzuri ya kuwasaidia vijana kutoa mawazo ya vijana wengine na watu wazima kwenye jamii kuhusiana na mada fulani. Kwa sababu ya muundo wake, watu wenye mawazo tofauti wanaweza kushirikishana na kujadiliana maoni yao.

Waeleze kwa makini waandaaji vijana wa vipindi kuwa mdahalo wa moja kwa moja ni kipindi cha mjadala kuhusiana na jambo au mada fulani inayorushwa moja kwa moja kutoka studio. Inaweza kuwa na watangazaji mmoja au wawili na wageni wenye mawazo tofauti. Unaruhusu mchango kutoka kwa wasikilizaji kupitia simu, meseji au barua pepe.

Page 39: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

38

• Watangazaji wadhibiti mjadala• Wageni wapewe fursa ya kuhitimisha• Watangazaji wahitimishe mdahalo

IGIZO LA MDAHALO (DAKIKA 20)

1. Mwambie mmoja ajitolee aigize kama mtangazaji

2. Waambie wawili wajitolee waigize kama wageni

3. Watatu wajitolee waigize kama wapiga simu kwenye kipindi

4.

5. Waambie wahakikishe kuwa mdahalo una mambo yafuatayo:-• Mwanzo, ambapo mtangazaji anajitambulisha, kuwatambulisha wageni na pia kutambulisha mada.• atikati, ambapo wageni watatoa maoni yao na kutoa hitimisho.

Mwisho, ambapo mtangazaji atahitimisha mdahalo na kuwashukuru wageni.

Wakimaliza waambie wengine watoe maoni

Wape dakika tano za kuigiza kipindi chao.

6.

7. Watumie vifaa vya kurekodia na watumie fursa hiyo pia kutumia kipaza sauti na kiwango cha usikivu

8.

9.

MFANO WA MDAHALO WA RADIONI: MAREJEO YA KUSIKILIZA 4

2.2 MRADI WA RADIO WA MUDA MREFU: SHAJARA ZA KUSIKILIZA

MFANO WA SHAJARA YA KUSIKILIZA: MAREJEO YA KUSIKILIZA 4

Richman, J., The Teen Reporter Handbook, Radio Diaries, 2000www.radiodiaries.org/wp-content/uploads/TeenReporterHandbook.pdf

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

Waache vijana wachague mada ya kujadili. Kwa ajili ya igizo, hakikisha kuwa ni mada ambayo wanaweza kuijadili vizuri na kwa ufasaha. Kama ubora wa elimu kwenye shule yao. Wakumbukushe kuwa itakuwa siyo haki kuwataja kwa majina baadhi ya walimu kwa kuwa watu hawa hawapo studio kujibu. Wakati huo huo, majadiliano yasiwe ya jumla kwa kuwa yatapoteza taarifa mahsusi

Chora alama ya ‘Hewani’ na waache waendelee kuigiza mbele ya wenzao. Iwe kama kwenye kipindi kinachorushwa moja kwa moja hewani na hakikisha wanazingatia muda ili shinikizo la matangazo ya moja kwa moja liwapate wahusi-ka.

Shajara ya kusikiliza inajumuisha miundo yote ya kusikiliza na inaweza pia kujumuisha mahojiano, maelezo mafupi na maoni. Inaweza kuwa ni mlolongo wa mambo mafupi au makala ndefu. Sifa mojawapo ya shajara huwa ni masimulizi ya visa vya watu .

Kutengeneza shajara pamoja na vijana inahitaji ushauri wa mtu na mtu, kujitolea na muda. Ni muundo unaochukua miezi kuuweka pamoja na unahitaji kazi kubwa ya kuhariri baada ya kuandaa

Page 40: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

39

HATUA ZA KUTENGENEZA SHAJARA

1.

2. Hakikisha kuwa anajua jinsi ya kutumia kifaa hicho na kurekodi kipindi kwa ubora.

3. Mfundishe jinsi ya kuandika vipindi vilivyorekodiwa kitabuni.

Pitia mambo mbalimbali – mahojiano, maelezo na maoni ambayo yanaweza kujumuishwa kwenye shajara

4.

5.

6.

7.

8. Ukishasaidia kuchagua sehemu za kutumia, wasaidie kuhariri ili kutengeneza kazi nzuri.

9.

10.

3. KURUSHA KIPINDI HEWANI

3.1 KUANDAA MUONGOZO (SAA 1)

Wanapoandika kwa ajili ya radio inabidi :• Waandike kama wanavyoongea. Inabidi iwe kama maongezi• Wafanye iwe rahisi na fupi waeleze kuwa watatakiwa kutumia maneno waliyoyatumia kujadili mada na marafiki zao. • Wasome mwongozo wao kwa sauti.• Wakumbuke kwa wanaongea moja kwa moja na wasikilizaji wao kwa hiyo watumie maneno kama ‘wewe’,

‘mimi’, ‘sisi’.

• Chora picha ikiwa na maneno yao ili wasikilizaji wavute taswira na kuona kile wanachokiongea. Wanatakiwa kueleza

mambo na kutumia maelezo.

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

Kituo kimwazime kijana kinasa sauti kwa muda mrefu. Ni wajibu mwazimaji kukitunza kifaa hicho na inabidi kuwe na sheria iwapo kifaa hicho hakitarudishwa au kikiharibiwa

Sisitiza umuhimu wa sauti kwa wasikilizaji na jinsi inavyoweza kutumika kutengeneza picha kwenye akili za wasikilizaji. Sisitiza pia kuna umuhimu wa kurekodi sauti ya anayezungumza na kile afanyacho wakati anaongea. Kwa mfano kama “kisa kinahusu kijana anayeitunza familia, lazima wasikilizaji wasikie vitendo vya yule mtoto mkubwa akipika, akifanya usafi au akiwahudumia nduguze wadogo.

Wakijisikia kuwa wamesharekodi vya kutosha, kaa nao na kusikiliza kazi yao kwa makini kabla haujachagua vipande vya kutumia. Kumbuka kuwa shajara ni masimulizi ya kisa cha mtu kwa hiyo lazima kuwe na mtiririko wa mwanzo, kati na mwisho.

Shajara ikishahaririwa unaweza kuamua kutumia kama kipande kidogo kwenye vipindi vya vijana au kama makala inayojitegemea.

Ni muhimu sana kujadili madhara kushirikishana kisa chao kwa ajili ya kurushwa hewani na mtengeneza shajara. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa muhimu kwenye kisa yanaweza kuachwa ili kumlinda mtu huyo. Waambie wafikiri kwa makini kuhusiana na kile wanachotaka kukishirikisha na kwa nini.

Kuandaa mwongozo na kutangaza ni vipengele viwili vya kuandaa kipindi cha radio ambavyo vijana wanaweza kushirikish-wa. Ushiriki wao utasaidia kutoa vionjo vya vijana kwenye kipindi ila ni vizuri kusubiri kwa wiki chache baada kuanza mradi hadi watakapokuwa tayari kuandaa miundo tofauti ya radio kabla ya kuwafundisha kuandaa mwongozo na kutangaza kipindi.

Sasa vijana wana mada gani ya kuifanyia kazi na tayari wana muhtasari sasa ni muda wa kuubadilisha muhtasari kuwa mwongozo. Mwongozo utawasaidia kutambulisha kipindi na wageni na utatumika hatua kwa hatua kama ramani ya mambo wanayotaka kujadili wakati wa kipindi. Ni muhimu kuwa na kipindi kilichoandaliwa vizuri. Itaunganisha mambo ya kawaida kwenye kipindi na nyongeza ya mambo yenye vionjo vya vijana

Baadhi ya watu wanaogopa kuandika na wanafikiri hawawezi kufanya hivyo. Kwa hiyo inabidi kukikumbusha kikundi kuwa kuandika kwa ajili ya radio kunahusu kujieleza kama vile kuhusiana na watu wengine katika maisha ya kila siku

Kama kwenye kuitambua jamii, fikiria kisa gani wanachopenda kusimulia. Inawezakuwa kuacha shule, uzoefu wao kama waandishi wa habari vijana au kinaweza kuwa kisa cha mtu mwingine.

Page 41: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

40

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

1. Fafanua kwamba mwongozo unatakiwa uwe na sehemu zifuatazo na kila moja inatakiwa uandikwe neno hadi neno(tumia karatasi ya muda wa kipindi au kidokezo kwa ajili ya mwongozo):

• Utangulizi• Hitimisho

Utambulisho wa makala kabla ya kurekodi.Hitimisho kwa makala ya kwanza kabla ya kurekodiwa baada ya kuchezwa. (kila makala kabla ya kurekodiwa lazima iwe na utangulizi na hitimisho).

• •

2. Wakishaandika mwongozo, wausome kwa sauti ili kuona kama uko kwenye mtiririko mzuri na unavutia.

3. Wakumbushe watambue kuwa• Kisa wanachosimulia kinatakiwa kuwa na mwanzo kati na mwisho.• Wasitoe maelezo mengi mwanzoni. Wachore picha kwa ajili ya wasikilizaji, na sio kuwalundikia wasikilizaji taarifa

kutoka mwanzo hadi mwisho

• Mwongozo uandikwe kwa lugha rahisi. Uwe kama maongezi.

4.

5. Hakikisha kuwa wanarudia rudia kutangaza jina la kipindi na kituo cha redio mara kwa mara.

MFANO WA MWONGOZO WA KIPINDI KUHUSU KUISHI KWA AFYA:KIAMBATISHO 5

3.2 KUTANGAZA

MAZOEZI NA KUTAMKA (DAKIKA 15)

Wafundishe watangazaji vijana:-

1.

2.

3.

4.

Wakati wanasoma kila kipengele kwa sauti, hakikisha wanatumia muda uliowekwa kwa ajili ya wasikiliza waliojiunga baada ya kuanza kwa kipindi.

Wakati waandishi na waandaaji kipindi wanaandaa makala za kabla kurekodiwa, watangazaji wanaweza kuandika mwon-gozo kwa msaada wa watafiti. Waandaaji waangalie kila kitu kuhakikisha kwamba kinaenda kama kilivyopangwa

Kufanyisha mazoezi misuli ya uso. Wazifanyie masaji nyuso zao, kwa kufunga na kufungua mdomo. Wafanyanye nyuso za kuchekesha na wawe na uraha.

Wawe makini na upumuaji pamoja na miili yao. Kukaa vibaya kutawafanya wapumue vibaya. Wajiachie na miguu yao ikanyage vizuri sakafuni

Kufanya mazoezi ya kuweka hisia kwenye sauti kwa kurudia baadhi ya mistari kwenye mwongozo na kuipa hisia tofau-ti tofauti kama vile (upendo, uoga, hasira, huzuni). Kutabasamu wakati wa kusoma mwongozo kutachangamsha sauti zao. Mwanzo na mwisho inabidi kuwe kwa sauti ya bashasha

Kufanya mazoezi ya kutamka kwa kusema sentensi hiyo hiyo kwa mwana kikundi aliyesimama umbali wa mita 10. Ni vizuri kutopiga kelele bali kutamka kwa ufasaha. Kutamka kunaanzia tumboni badala ya kwenye koo, ikiwa na maana ya kutumia dayafram badala ya visanduku vya sauti

Muongozo ukishaandikwa, hatua inayofuata ni kuutumia. Waeleze watangazaji kuwa wanatakiwa kufanya mazoezi kabla ya kusikika hewani. Hata ukiwa na mwongozo kutangaza moja kwa moja radioni sio kazi rahisi. Kasi na toni ni muhimu sana kwa ajili ya kutoa maana ya maneno na sentensi vya kuangalia. Wakishaelewa kile wanachosema na kujiamini hata wasikil-izaji watawaamini.

Page 42: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

Mpango kazi unaandaliwa ili kurahisisha mawasiliano. Baada ya kikao cha mwezi cha kupanga, inabidi uwasaidie vijana kupanga tarehe na muda kwa ajili ya vikao vya wiki ili hapo kituoni kila mtu awe na taarifa.

Kusoma utangulizi na hitimisho kwa wana kikundi wengine na kujifanya wanatangaza hewani. Ni muhimu kutowaida “ma DJ” waliowasikia kwenye radio, bali watafute sauti, kasi na toni zao wenyewe. Wakumbushe kuwa kipindi sio kwa ajili yao bali mada na ujumbe wao

Waambie watangazaji wajifanye wanaongea na mtu mmoja, kwa mfano rafiki au mwana familia. Wakumbushe kuwa nguvu ya redio inategemea na ukaribu. Msikilizaji anaweza kuwa, chumbani, sebuleni, jikoni au kwenye gari. Fafanua kwamba wakiwa hewani wahisi kuwa na msikilizaji yupo pamoja nao studio na vivyo hivyo wajue inabidi wawavutie wasikilizaji wengine ambao huenda hawaelewi au kuguswa kwa haraka.

Sasa, vijana wanatengeneza kipindi chao wenyewe, vipindi vya mrejesho ni muhimu sana kwa ajili ya kuendeleza na kukuza stadi zao pamoja na kuhakikisha kuwa wanatimiza malengo yao. Hata hivyo, kwa kuwa mshauri sio muhusika pekee anahusika kupanga na kuandaa vipindi, vijana wanatakiwa kusaidia kutengeneza mpango kazi ili kuendeleza vipindi.

41

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

KUWEKA SAUTI KWENYE MWONGOZO (SAA 1)

Waambie watangazaji vijana wafanye yafuatayo:-

1. Kuchagua utangulizi na hitimisho kutoka kwenye mwongozo

2. Kusoma kwa sauti kisha kuweka alama pumzi ilipoishia kwenye sentensi.

3. Kupigia mstari maneno ambayo ni muhimu na yanayohitaji msisitizo.

4.

4. MREJESHO NA MIPANGO YA MUDA MREFU

4.1 KIPINDI CHA MREJESHO

NGAZI YA 1: MREJESHO

4.2 MPANGO WA MUDA MREFU

MPANGILIO WA KAZI (SAA 1)

Chati iliyo kwenye ukurasa unaofuata ni mfano wa mpangilio wa kazi na unaweza kuigwa kulingana kikundi chako.

1. Kila muhula wa shule, kijana tofauti anaweza kuongoza na kusimamia uandaaji wa kipindi kwa muhula huo. Vivyo hivyo hata washauri wanaweza kubadilishana

2. Hii haina maana kuwa wanatakiwa kufanya kila kitu. Kila mtu ataendelea kuwa na wajibu pamoja na majukumu yake lakini watakuwa viongozi kwa mhula huo.

Page 43: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

42

KAZIINASIMAMIWA

NA WASHIRIKI MUDA MALENGO MATOKEO

KIKAO CHA KILA MWEZI CHA KUPANGA

Ataongoza mshauri na mtangazaji kijana (wabadilishwe kila mhula)

Washauri wote na watangazaji vijana

Wiki ya kwanza ya kila mwezi

kuamua malengo ya mwezi mgawanyo wa majukumu

Idadi ya vipindi vilivyotengenezwa

KIKAO CHAUANDAAJIVIPINDI

Ataongoza mshauri na mtangazaji kijana

Kwa wiki

Tathmini ya maendeleo ya wiki

KUTANGAZA

Vipindi vilivyorushwa hewani

Kutangaza vipindi kwenye kituo cha radio

MREJESHONA MPANGILIOWA KAZI

Ataongoza mshauri na mtangazaji kijana

Washauri na watangazaji vijana wote

Kila baada ya kipindi

Toa maoni kuhusu kipindi na pangilia kipindi kijacho

Tangaza kipindi redioni. Rekebisha maudhui na uwezo.

Panga kipindi kingine

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 3: Radio ya Vijana

MPANGILIO WA KAZI I (SAA 1)

Vijana waon-goze na wajisimamie wenyewe mshauri asaidie inapohitajika

Majukumu yanabadilika kila wiki/kipindi

Mhandisi wa sauti na waandishi kukutana ili kufanya kazi

Watafiti kukutana ili kufanya kazi

Waandaaji wasimamie

Waandaaji makala

Ataongoza mshauri na mtangazaji kijana

Washauri, watangazaji na wapiga simu

Inategemea idadi ya vipindi vitakavyotangaz-wa kwa mwezi

Majedwali na miundo ya radio iliyoonyeshwa hapo juu inabidi ikusaidie kuandaa vipindi tofauti vya radio kwa ajili ya vijana. Kwa msaada wa nyenzo hizi, jukumu lako inabidi libadilike kutoka mwezeshaji anayeshiriki kwenye kila hatua ya maandalizi hadi kuwa mshauri unayetoa ushauri na mwongozo kwa mwandishi kijana na kusimamia mchakato mzima wakati wanashu-ghulika na maandalizi ya awali, utengenezaji na utangazaji wa vipindi.

Kwa kuweka mkazo kwenye kupangilia na hatua ya maandalizi ya awali ya kipindi cha radio, utahakikisha uandaaji wa mara kwa mara wa vipindi ambao unasimamiwa kwa waandishi wa habari vijana na wafanyakazi wa kituo chako cha radio

Page 44: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

43

HATUA YA NNE: KUWAFIKIA VIJANA

1. KUWAFIKIA VIJANA KATIKA JAMII YAKO

1.1 MATANGAZO YA NJE

KUFANYA MDAHALO WA NJE.

1.

2.

Tafuta mada kuhusiana na shughuli maalum ya jamii husika au tukio la kidunia kama Siku ya Radio Duniani, terehe 13 Februari

3.

4.

5.

6. Funga mjadala kwa kuwakaribisha washiriki waweze kuuliza maswali.

1.2 MATUKIO YA KIJAMII NA KUIFIKIA JAMII

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 4: Kuwafikia Vijana

Hatua hii inahusu kuchanganyika na vijana nje ya kituo cha radio.Ili kuweza kujua matatizo, mambo na matukio yaliyomo kwenye jamii. Pia itakusaidia kuweza kujua miradi mingine kwa ajili ya kushirikiana. Aina hiyo ya ushirikiano itasaidia kuongeza uzoefu wa kituo chako cha radio na kuimarisha uwepo na mwonekano wake kwenye jamii.

Mtaalamu wa maendeleo ya radio Mary Myers anatoa maana ya “radio ya kijamii”, kuwa ni uwezo wa kuongea na uhuru wa watu kujieleza au kukuza utambulisho wao.

Umewafundisha wanahabari vijana jinsi ya kuandaa kipindi cha vijana kwa ajili ya vijana. Ni muhimu uendeleee kushauriana na vijana katika jamii yako. Kwa njia hiyo utakutana na wasikilizaji vijana na utaongeza kiwango cha usikilizwaji wako. Pia itawasaidia wanahabari vijana kubadilishana mawazo na vijana wengine katika jamii

Hata kama huna teknolojia kwa ajili ya matangazo ya nje, toka nje ya studio na waandishi wa habari vijana ili kwenda kupata habari zaidi.

Jadili mada husika kundini na uwakaribishe wageni wako kama vile viongozi wa kijamii, wanafunzi, na wanajamii. Hakikisha pia vijana wanashiriki.

Andaa utaratibu wa kutangaza jambo hilo. Kwa mfano vijana wanaweza kuandaa mabango au kutangaza tukio hilo radioni siku moja kabla

Andaa studio inayobebeka au meza yenye vipaza sauti vinavyobebeka. Kama huna kipaza sauti, hakikisha unatumia chumba au eneo ambalo wageni na wasikilizaji wataweza kusikilizana.Weka viti kwa ajili ya wasikilizaji.

Rusha hewani tukio hilo moja kwa moja au rekodi mjadala huo na uurushe hewani muda mwingine siku hiyo hiyo. Unaweza kuchukua baadhi ya vipande na kuvitumia kwenye vipindi vingine siku nyingine

Andaa mara kwa mara midahalo ya nje kuhusu mambo ya vijana pamoja na wana jamii yako. Kwa mfano, unaweza kupanga tukio la utetezi wa haki za mtoto ili kuchangia kwenye kufanya maamuzi katika jamii husika. Unaweza kufanya midahalo hii kwenye kituo cha kijamii, maktaba, au kliniki au kuurusha hewani baadaye

Tumetaja uwezekano wa kutangaza tukio fulani katika jamii lakini pia unaweza kuwahamasisha waandishi chipukizi kutun-ga tukio lao kupitia mada walizozitumia kwenye vipindi vyao.

Huko Zambia, kundi la wanahabari vijana ambao ni sehemu ya UNICEF Zambia’s Unite for Climate Programme walirusha vipindi kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na utunzaji wa mazingira na kuelekeza mada zao kwa shughuli za kijamii au za kielimu

Page 45: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

44

2. ITUMIE KAZI YAKO NJE YA KITUO CHA REDIO: VYOMBO VYA HABARI NA INTANETI

2.1 SHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

2.1.1 MAGAZETI YA KIJAMII

2.1.2 VITUO VYA REDIO

2.1.3 INTANETI

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 4: Kuwafikia Vijana

Katika mji wa Kabwe, wana habari vijana waliomba ruhusa ya kuandika kuta za shule. Walifikiria waandike nini na kushirikiana na vijana wengine kuchora picha ukutani zikionyesha watu wakikusanya uchafu na kutunza mazingira yao

Huko Ndola, wanahabari vijana walifanya kipindi kuhusu utunzaji wa mazingira, walipanda miti mashuleni na kufanya mjadala kuhusu mada hiyo.

Waamdishi wengi vijana wanaweza kuandika na kuchapisha makala kuhusu tukio au jambo la kufurahisha kwenye gazeti la shule

Waandishi vijana watakuwa katika nafasi nzuri kutoa mchango kwenye jamii yao na kuanzisha majadiliano kwa kujumuisha hatua na mikakati hii.Vile vile ushiriki huu utaisaidia radio kituo cha radio, kuchangia maendeleo yake na mafanikio na kukifanya kuwa muhusika muhimu ndani na nje ya jamii

Kuziendea asasi au vyombo vya habari ambavyo vinaweza kutumia maudhui ya kipindi chako cha vijana ni njia nzuri ya kukuza kipindi chako. Kwa njia hii maudhui yatasikika mbali na wasikilizaji au jamii yako.

Ni rahisi sana kubadili maudhui ya kipindi cha vijana kwenda kwenye makala ya magazeti ya kijamii. Magazeti ya kijamii yanahitaji maudhui mapya unaweza pia kupeleka matukio mapya yaweze kuchapishwa. Hii ndio nzuri ya kutangaza kituo na kipindi cha vijana

Kumbuka kuchukua kamera unapoenda kurekodi ili uweze kupiga picha kama kielelezo kitakachotumiwa kwenye makala.

Kunaweza kuwa na vituo vingine katika mji wako au chini ambavyo vinafanya kazi na vijana. Kwa nini usiungane nao na kubadilishana maudhui ya vipindi? Kwa njia hii mtatengeneza mtandao utakaosaidia kutoa maoni tofauti ya vijana nchini kote kupitia kituo chako

Kama una huduma ya Intaneti, moja ya njia rahisi ya kusambaza makala zako duniani kote ni kupitia mitandao ya kijamii kama vile “ Facebook” na “Twitter” ambayo vijana wengi wanatumia. Mitandao hii itasaidia kuvitangaza vipindi vyako vya radio kwa kuvifanya visikilizwe na watu wengi baada kuwa vimetangazwa. Kwa kuwa ni vigumu kutumia faili kubwa kwa njia ya barua pepe tunashauri pia kutumia tovuti (www.soundcloud.com) ambayo kila siku utakuwa unaweka yaliyojiri. Na ni njia rahisi kwa watu kuangalia, kusikiliza yale yaliyojiri na kuweza kushirikiana kwa face book au twitter na kutoa mchango wao wa mawazo. Hakikisha pia wasichana wana nafasi sawa na wavulana katika matumizi ya intaneti.

Washirikishe vijana kwenye kuendesha mitandao ya kijamii ya kituo cha radio ili iwe muhimu kukifanya kituo cha radio kifahamike duniani. Wanaweza kuitumia kuunda ushirikiano na mashirika ya kimataifa na kufanya urafiki na watu na asasi ili kuongeza uzoefu wa kituo na kuongeza thamani kwenye kazi zake. Mara nyingi kuna faida za ushirikiano, ufadhili na miradi ya pamoja, na wakati ambapo inabidi waongozwe kupitia mchakato huu, wanaweza kujenga jamii ya waungaji mkono kwa faida ya kituo cha radio

Page 46: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

45

Sehemu ya Tatu | Kujua Kiwango cha Uwezo na Kupanga | Ngazi ya 4: Kuwafikia Vijana

2.2 MASHIRIKA YA KIJAMII

Rekodi uzoefu wako, wekeza stadi zako na endeleza mkakati wako wa kuwashirikisha vijana

Shirikiana na kundi kutafuta mashirika, asasi na makundi yatakayowafaa. Tafuta asasi ambazo zinalinda ustawi wa vijana na makundi yenye ubunifu kama vile wasanii, wanawake na taasisi za watu wazima ndani na nje ya jamii. Wanaweza kuwa na gazeti, tovuti au vipindi vyao vya radio ambapo wanaweza kutangaza vipindi vya vijana .

Hatua hii ya mwisho itakusaidia kukuza kipindi chako baada ya kurushwa hewani na kukitumia kama njia ya kushirikiana na vijana kwenye jamii. Kushirikiana huku kukifanye kipindi chako kiwe muhimu wakati ukiongeza mwonekano wa kituo cha radio kwenye jamii

Tunategemea nyenzo, vidokezo na mifano kwenye Mwongozo vitakusaidia kutengeneza kipindi endelevu cha vijana ambacho kitaleta mawazo, mitazo na habari mpya kwa wasikilizaji vijana na watu wazima. Kwa namna ya pekee, tunatege-mea wasichana na wanawake na sauti zao watakuwa sehemu muhimu ya matangazo ya radio kwa upana wake.

Page 47: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

46

MAREJEO MUHIMU NA VIAMBATISHO

SEHEMU YA NNE

Page 48: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

47

VIAMBATISHO

KIAMBATISHO 1: MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA WA HAKI ZA MTOTO (MUHTASARI)

KIAMBATISHO 2: ORODHA MUHIMU YA VIFAA KWA AJILI YA KUENDESHEA SEMINA YA VIJANA

KIAMBATISHO 3: MIFANO YA MICHEZO YA KUVUNJA UKIMYA NA KUTIA NGUVU

KIAMBATISHO 4: MFANO WA FOMU YA IDHINI

KIAMBATISHO 5: MFANO WA MWONGOZO WA KIPINDI

MAREJEO YA KUSIKILIZA YANAYOPATIKANA KWENYE MTANDAO

MAREJEO YA KUSIKILIZA 1: MFANO WA MAONI YA KUSIKILIZA

MAREJEO YA KUSIKILIZA 2: MFANO WA MAELEZO MAFUPI YA KUSIKILIZA

MAREJEO YA KUSIKILIZA 3: MFANO WA KIBWAGIZO KILICHOTENGENEZWA NA VIJANA

MAREJEO YA KUSIKILIZA 4: MFANO WA MDAHALO WA KUSIKILIZA

MAREJEO YA KUSIKILIZA 5: MFANO WA SHAJARA YA KUSIKILIZA

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Page 49: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

48

KIAMBATISHO 1:

MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA WA HAKI ZA WATOTO (MUHTASARI)

IBARA YA 1 (MAANA YA NENO MTOTO)

IBARA YA 2: BILA UBAGUZI

IBARA YA 3 (MASLAHI YA MTOTO)

IBARA YA 4 (ULINZI WA HAKI ZA MTOTO)

IBARA YA 5 (MWONGOZO WA WAZAZI)

IBARA YA 6 (KUISHI NA KUKUA): Watoto wana haki ya kuishi. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa watoto wanaishi na kukua kwa afya

IBARA YA 7 (USAJILI, JINA, UTAIFA, MATUNZO):

IBARA YA 8 (HIFADHI YA UTAMBULISHO):

IBARA 9 (KUTENGANA NA WAZAZI):

IBARA YA 10 (KUUNGANA KWA FAMILIA):

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Mkataba unaelezea maana ya neno ‘mtoto’ kuwa ni mtu aliye chini ya miaka 18, isipokuwa kama sheria za nchi husika zinaweza umri wa mtoto. Kamati ya haki za mtoto, chombo cha kufuatilia utekelezaji w mkataba, imezihimiza nchi kupitia upya umri wa walio wengi kama umewekwa chini ya miaka 18 na kuongeza kiwango cha ulinzi kwa watoto waliochini ya miaka 18

Mkataba huu unawahusu watoto wote, bila kujali rangi, dini au uwezo, wanachofikiri au kusema, aina ya familia wanayoto-ka. Haijalishi watoto wanaishi wapi, wanaongea lugha gani, wazazi wao wanafanya kazi gani, kama ni wavulana au wasicha-na, ni wa utamaduni gani, kama wana ulemavu au kama ni matajiri au maskini. Kusiwe na mtoto anayetendewa vibaya kwa sababu yoyote ile.

Maslahi ya mtoto lazima yawe jambo la msingi katika kufanya maamuzi yanayoweza kuwaathiri. Watu wazima lazima wafanye kilicho bora kwa watoto. Watu wazima wanapofanya maamuzi lazima wafikirie jinsi maamuzi yao yatawaathiri watoto. Hii hususani inahusu bajeti, sera na watunga sheria

Watoto wote wana haki ya kuwa na jina lilosajiliwa kisheria, linalotambulika rasmi na serikali. Watoto wana haki ya utaifa (kuwa sehemu ya nchi). Watoto pia wana haki ya kujua, kadri iwezekanavyo, kutunzwa na wazazi wao.

Watoto wana haki ya utambulisho - rekodi rasmi ya wao ni nani. Serikali inapaswa kuheshimu haki za watoto kuwa na jina, utaifa na mahusiano ya kifamilia.

Watoto wana haki ya kuishi na wazazi wao, vingenevyo itakuwa mbaya kwao. Watoto ambao wazazi wao hawaishi pamoja na wana haki ya kuwasiliana na wazazi wote wawili, vingenevyo inaweza kumuumiza mtoto.

Familia ambazo baadhi ya wanafamilia wanaishi nchi tofauti, waruhusiwe kusafiri katika nchi hizo ili wazazi na watoto waendelee kuwasiliana, au kuishi pamoja kama familia

Serikali inabidi ziheshimu haki na wajibu wa familia kuwaongoza watoto wao ili kadri wanavyokuwa, wajifunze kutumia haki zao kwa usahihi. Kuwasaidia watoto kuzielewa haki zao hakumaanishi kuwalazimisha kufanya uchaguzi wenye matokeo ambayo wao bado ni wadogo sana kuyamudu. Ibara ya 5 inawahimiza wazazi kukabiliana na masuala ya haki "katika namna inayokwenda sambamba na mabadiliko ya uwezo ya mtoto". Mkataba hauondoi jukumu la wazazi kwa watoto wao na kuzipa mamlaka zaidi serikali. Mkataba unazipa serikali wajibu zaidi wa kulinda na kusaidia familia katika kutimiza wajibu wao muhimu kama walezi wa watoto.

Serikali zina wajibu wa kuchukua hatua zote ili kuhakikisha haki za watoto zinaheshimiwa, zinalindwa na kutekelezwa. Nchi zinaporidhia Mkataba, zinakubali kupitia sheria zao kuhusu watoto. Hii inajumuisha kufanya tathmini ya huduma zao za jamii, mifumo ya kisheria, afya na elimu, pamoja na viwango vya kugharamia huduma hizi. Serikali zinapaswa kuchukua hatua muhimu ili kuhakikisha viwango vilivyowekwa na mkataba vinafikiwa. Inabidi wazisaidie familia kulinda haki za mtoto na kutengeneza mazingira ambapo wanaweza kukua na kufikia malengo yao. Wakati mwingine hii inaweza kuhusi-sha kubadilisha sheria zilizopo au kutunga mpya. Mabadiliko haya hayalazimishwi, bali yanafuata mchakato ule ule ambao kwao sheria inatungwa au kurekebishwa katika nchi. Ibara ya 41 ya Mkataba inafafanua kwamba kama nchi tayari ina viwango vya juu vya sheria kuliko vile vilivyo kwenye Mkataba, viwango vya juu mara zote vinatumika

Page 50: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

49

IBARA YA 11 (UTEKAJI NYARA):

IBARA YA 12 (KUHESHIMU MAWAZO YA MTOTO):

IBARA YA 13 (UHURU WA KUJIELEZA):

IBARA YA 14 (UHURU WA MAWAZO, DHAMIRA NA DINI):

IBARA YA 15 ( UHURU WA KUJIUNGA NA CHAMA ):

IBARA YA 16 ( HAKI YA MAISHA BINAFSI ):

IBARA YA 17 ( KUPATA HABARI ; VYOMBO VYA HABARI ):

IBARA YA 18 (MAJUKUMU YA WAZAZI; MSAADA WA SERIKALI):

IBARA YA 19 (ULINZI DHIDi YA AINA ZOTE ZA UNYANYASAJI):

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Serikali inapaswa kuchukua hatua kuzuia watoto wasichukuliwe nje ya nchi yao kinyume cha sheria. Ibara hii inahusu kwa namna ya pekee utekaji wa wazazi. Itifaki ya Hiari ya Mkataba huu kuhusu uuzaji wa watoto, ukahaba na picha za ngono za watoto ina kipengele kinachohusu utekaji kwa ajili ya kupata fedha

Watoto wana haki ya kupata na kushirikishana habari, ili mradi kama habari hizo haziwaathiri wao na au wengine. Katika kutumia haki ya uhuru wa kujieleza, watoto wana wajibu wa kuheshimu haki, uhuru na heshima ya wengine. Uhuru wa kujieleza unajumuisha haki ya kushirikishana habari kwa njia yoyote ile wanayochagua, ikiwa ni pamoja na kuzungumza,kuchora au kuandika.

Watoto wana haki ya kukutana na kujiunga na vikundi na asasi, ili mradi hiyo hazuii watu wengine kutumia haki zao. Katika kutumia haki zao, watoto wana wajibu wa kuheshimu haki za binadamu, uhuru na heshima ya wengine.

Watoto wana haki ya kupata taarifa ambazo ni muhimu kwa afya na ustawi wao. Serikali inapaswa kuhimiza vyombo vya habari - redio, televisheni, magazeti na Internet - kutoa taarifa ambazo watoto wanaweza kuzielewa na kutochochea habari ambazo zinaweza kuwadhuru watoto. Vyombo vya habari vihimizwe kusambaza habari katika lugha ambayo makundi ya wachache na wazawa wanaweza kuielewa. Watoto wanapaswa pia kupata vitabu vya watoto.

Wazazi wote wawili wana wajibu wa kulea watoto wao, na lazima wafikirie maslahi bora kwa kila mtoto. Serikali lazima ziheshimu wajibu wa wazazi kwa kutoa mwongozo sahihi kwa watoto wao - Mkataba hauondoi jukumu la wazazi kwa watoto wao na kutoa mamlaka zaidi kwa serikali. Unahimiza serikali kubeba majukumu ya kutoa msaada kwa wazazi, hasa kama wazazi wote wawili wanafanya kazi nje ya nyumba yao.

Watoto wana haki ya kulindwa dhidi ya kuumizwa na kutendewa vibaya, kimwili au kiakili. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa watoto ni wanatunzwa ipasavyo na kuwalindwa dhidi ya unyanyasaji, dhuluma na kutelekezwa na wazazi wao, au mtu mwingine ambaye anawatunza. Katika suala la nidhamu, Mkataba hataji aina gani ya adhabu wazazi wanapaswa kutumia. Hata hivyo aina yoyote ya adhabu inayohusiana na unyanyasaji halikubaliki. Kuna njia za kuwaadhibu watoto ambazo zenye ufanisi katika kusaidia watoto wajifunze kuhusu matarajio ya familia na jamii kuhusu tabia zao - zile ambazo sio za vurugu, ni sahihi kwa kiwango cha maendeleo ya mtoto na kuzingatia maslahi ya mtoto. Katika

Watoto wana haki ya faragha. Sheria inapaswa kuwalinda dhidi ya mashambulizi ya mfumo wao wa maisha, jina lao zuri, familia zao na makazi yao.

Watu wazima wakifanya maamuzi yanayoathiri watoto, watoto wana haki ya kusema nini wanafikiri kifanyike na maoni yao yazingatiwe. Hii haimaanishi kwamba watoto sasa wanaweza kuwaambia wazazi wao nini cha kufanya.Mkataba huu unahimiza watu wazima kusikiliza maoni ya watoto na kuwashirikisha katika maamuzi – na sio kuwapa watoto mamlaka juu ya watu wazima. Ibara ya 12 haiondoi haki na wajibu wazazi wa kutoa maoni yao juu ya masuala yanayoathiri watoto wao. Hata hivyo, Mkataba huu unatambua kuwa kiwango cha ushiriki wa mtoto katika maamuzi lazima kiendane na kwa kiwan-go cha kukomaa kwa mtoto. Uwezo wa watoto kuunda na kutoa maoni yao unakuwa kulingana na umri na wazazi wengi watayapa uzito zaidi maoni ya vijana kuliko ya watoto ambao hawajaanza shule, iwe katika maamuzi ya familia, ya kisheria au kiutawala

Watoto wana haki ya kufikiri na kuamini wanachotaka na kuiishi dini yao, ili mradi hawazuii watu watu wengine kutumia haki zao. Wazazi wanapaswa kuwaongoza watoto wao katika mambo haya. Mkataba huu unaheshimu haki na wajibu wa wazazi katika kutoa mwongozo wa kidini na kimaadili kwa watoto wao. Vikundi vya kidini duniani kote vimeunga mkono Mkataba huu, ambapo inaonyesha kwamba hauzuii wazazi kwa namna yoyote kuwalea watoto wao kulingana na desturi za kidini. Vivyo hivyo, Mkataba unatambua kuwa kadri watoto wanavyokuwa wana uwezo wa kuwa na maoni yao wenyewe, baadhi wanaweza kuhoji desturi fulani za kidini au mila na desturi. Mkataba unaunga mkono haki ya watoto ya kuchunguza imani zao, lakini pia unasema kwamba haki yao ya kueleza imani yao inahusu kuheshimu haki na uhuru wa watu wengine.

Page 51: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

50

IBARA YA 20 (WATOTO KUNYIMWA MAZINGIRA YA KIFAMILIA):

IBARA YA 21 (KUASILI):

IBARA YA 22 (WATOTO WAKIMBIZI):

IBARA YA 23 (WATOTO WENYE ULEMAVU):

IBARA YA 24 (AFYA NA HUDUMA ZA AFYA):

IBARA YA 25 (MAPITIO YA MATIBABU NA HUDUMA):

KIFUNGU CHA 26 (HIFADHI YA JAMII):

IBARA YA 27 (HALI BORA YA MAISHA):

IBARA YA 28: (HAKI YA KUPATA ELIMU):

IBARA YA 29 (MALENGO YA ELIMU):

IBARA YA 30 (WATOTO WA JAMII ZA WACHACHE / VIKUNDI VYA WENYEJI):

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

nchi nyingi, tayari sheria zinafafanua aina za adhabu ni mbaya na zenye kudhalilisha. Ni juu ya kila serikali kupitia upya sheria hizi katika kuendana na Mkataba huu

Watoto ambao hawawezi kutunzwa na familia zao wana haki ya kupata huduma maalum na lazima watunzwe vizuri, na watu ambao wana heshimu kabila, dini, utamaduni na lugha yao.

Watoto wana haki ya kuhudumiwa na kulindwa kama wameasiliwa au wako katika malezi ya kimkataba. Kitu cha muhimu lazima kiwe kipi ni bora kwao. Sheria zile zile inabidi zitumike iwe wanaasiliwa ktika nchi yao ya kuzaliwa, au kama wanapel-ekwa kuishi katika nchi nyingine.

Watoto wana haki ya kupata huduma bora za afya - huduma bora za afya kadri iwezekanavyo - maji safi ya kunywa, chakula bora, mazingira safi na salama, na habari kwa ajili ya kuwasaidia kuwa na afya njema. Nchi tajiri lazima zisaidie nchi maskini kufakia lengo hili.

Watoto ambao wanatunzwa na serikali zao za mitaa, badala ya wazazi wao, wana haki ya huduma hizi kupitiwa mara kwa mara ili kuona kama ziko vizuri zaidi. Huduma na matibabu lazima ziwe kwa "maslahi bora ya mtoto". (angalia Kanuni Elekezi, Ibara ya 3)

Watoto wana haki ya ulinzi maalum na kuwasaidia kama wao ni wakimbizi (kama wamelazimika kuondoka nyumbani kwao na kuishi katika nchi nyingine), pamoja na haki zote katika Mkataba huu.

Watoto ambao na aina yoyote ya ulemavu wana haki ya kupata huduma maalum na msaada, pamoja na haki zote katika Mkataba huu, ili waweze kuishi maisha kamili na huru.

Watoto – iwe kupitia kwa walezi wao au moja kwa moja - wana haki ya kupata msaada kutoka kwa serikali kama ni maskini au wahitaji.

Watoto wana haki ya hali ya maisha ambayo ni nzuri kiasi cha kutosha kukidhi mahitaji yao ya kimwili na kiakili. Serikali zinapaswa kusaidia familia na walezi ambao hawawezi kumudu chakula, mavazi na malazi.

Watoto kutoka makundi ya wachache au wazawa wana haki ya kujifunza na kuuishi utamaduni wao, kuongea lugha na kuishika dini yao. Haki ya kuuishi utamaduni, kuongea lugha na kuishika dini inamuhusu kila mtu; Mkataba unaainisha haki hii katika mazingira ambapo mambo hayo hayashirikishi dadi kubwa ya watu katika nchi.

Watoto wote wana haki ya kupata elimu ya msingi, ambayo inapaswa kuwa bure. Nchi tajiri zinapaswa kusaidia nchi maski-ni kupata haki hii. Adhabu shuleni lazima ziheshimu utu wa watoto. Ili watoto wafaidike na elimu, shule lazima ziendeshwe kwa kufuata utaratibu - bila ya matumizi ya nguvu. Aina yoyote ya adhabu shuleni inapaswa kuzingatia utu wa mtoto. Kwa hiyo, serikali lazima zihakikishe kwamba viongozi wa shule wanapitia sera zao nidhamu na kuondoa adhabu zozote ambazo zinahusishwa unyanyasaji wa kimwili na kiakili na kudharauliwa. Mkataba huu unatoa kipaumbele kwa elimu. Vijana wanapaswa kuhimizwa kufikia kiwango cha juu cha elimu ambacho wana uwezo nacho.

Elimu ya watoto lazima ikuze kikamilifu haiba, vipaji na uwezo kila mtoto. Iwahimize watoto kuheshimu wengine, haki za binadamu na tamaduni zao wenyewe na za wengine. Pia itawasaidia kujifunza namna ya kuishi kwa amani, kulinda mazingi-ra na kuheshimu watu wengine. Watoto wana wajibu maalumu wa kuheshimu haki za wazazi wao, na elimu lazima iwe na lengo la kuongeza heshima kwa maadili na utamaduni wa wazazi wao. Mkataba haushughulikii masuala kama vile sare za shule, na taratibu za mavazi, kuimba wimbo wa taifa au sala katika shule. Ni jukumu la serikali na viongozi wa shule katika kila nchi kuamua kama, katika mazingira ya jamii yao na sheria zilizopo, mambo hayo hayakiuki haki zinazolindwa na Mkata-ba huu

Page 52: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

Serikali inapaswa kulinda watoto kutokana na aina zote za unyonyaji wa kingono na unyanyasaji. Kipingele hiki katika Mkataba huu kinaongezewa nguvu na Itifaki ya Hiari kuhusu uuzaji wa watoto, ukahaba wa watoto na picha za ngono za watoto.

Serikali inapaswa kuchukua hatua zote iwezekanavyo ili kuhakikisha kuwa watoto hawatekwi nyara, kuuzwa au kusafirish-wa. Kipengele hiki kwenye Mkataba kinaongezewa nguvu na Itifaki ya Hiari kuhusu uuzaji wa watoto, ukahaba wa watoto na picha za ngono za watoto.

Watoto ambao wamesahauliwa, wamenyanyaswa au kunyonywa wanapaswa kupewa msaada maalum wa kimwili na kisaikolojia ili wapate nafuu na kuwaunganisha katika jamii. Mkazo inabidi uwekwe kurejesha afya, heshima na hadhi ya mtoto.

Serikali inapaswa kuhakikisha Mkataba huu anajulikana kwa watu wazima na watoto. Watu wazima wanapaswa kuwa-saidia watoto kujifunza kuhusu haki zao, pia. (Angalia pia ibara ya 4).

Ibara hizi zinajadili jinsi ya serikali na mashirika ya kimataifa kama UNICEF yanapaswa kufanya kazi kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa.

Watoto ambao wanatuhumiwa kuvunja sheria wana haki ya kupata msaada wa kisheria na na kutendewa kwa haki katika mfumo wa sheria ambao unaheshimu haki zao. Serikali zinatakiwa kuweka umri wa chini ambao watoto hawawezi kuchukuliwa kama wahalifu na kuwahakikishia utatuzi wa haraka na wa haki wa masuala ya kisheria au mashtaka mbadala.

Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoa adhabu kwa watoto katika njia ya kikatili au yenye madhara. Watoto wanaovunja sheria haipaswi kutendewa kikatili. Hawapaswi kufungwa gereza moja na watu wazima, wanapaswa kuendelea kuwasiliana na familia zao, na hawapaswi kupewa adhabu ya kifo au kifungo cha maisha bila uwezekano wa kuachiwa huru.

Serikali lazima zichukue hatua kuwalinda na kuwatunza watoto walioathirika na vita. Watoto walio chini ya miaka 15 wasilazimishwe au wasiingizwe vitani au kujiunga na jeshi. Itifaki ya Hiari ya Mkataba huu kuhusu ushiriki wa watoto katika vita inakazia haki hii, kwa kuongeza umri kwa ajili ya kushiriki moja kwa moja katika vita hadi miaka 18 na kupiga marufuku kuwatumia watoto walio chini ya miaka 18.

51

IBARA YA 31 (BURUDANI, KUCHEZA NA UTAMADUNI):Watoto wana haki ya kupumzika na kucheza, na kushiriki katika shughuli mbalimbali za utamaduni, sanaa na burudani.

IBARA YA 32 (KAZI ZA WATOTO):

IBARA YA 33 (MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA):Serikali inapaswa kutumia njia zote kuwalinda watoto dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na madhara na kutumiwa katika biashara ya madawa ya kulevya.

IBARA YA 34 (UNYONYAJI WA KINGONO):

IBARA YA 35 (UTEKAJI NYARA, UUZAJI NA USAFIRISHAJI):

IBARA YA 36 (AINA NYINGINE ZA UNYONYAJI):Watoto wanapaswa kulindwa dhidi ya shughuli yoyote ambayo inachuma faida kutoka kwao au inayoweza kuathiri ustawi na maendeleo yao.

IBARA YA 37 (KUWEKA KIZUIZINI NA ADHABU):

IBARA YA 38 (VITA NA MIGOGORO YA KUTUMIA SILAHA):

IBARA YA 39 (MATIBABU KWA WAATHIRIKA WATOTO):

IBARA YA 40 (MFUMO WA KUTOA HAKI ZA WATOTO):

IBARA YA 41 (KUHESHIMU VIWANGO VYA JUU VYA KITAIFA): Kama sheria za nchi zinatoa ulinzi bora wa haki za watoto kuliko ibara za Mkataba huu, sheria hizo zinapaswa kutumika.

IBARA YA 42 (KUZIJUA HAKI):

IBARA ZA 43-54 (HATUA ZA UTEKELEZAJI):

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Serikali inapaswa kuwalinda watoto dhidi ya kazi ambazo ni hatari au zinaweza kudhuru afya zao au elimu yao. Wakati Mkataba huu unawalinda watoto dhidi ya kazi zenye madhara na za kinyonyaji, hakuna kinachowazuia wazazi kutegemea msaada kutoka kwa watoto wao kusaidia kazi za nyumbani ambazo ni salama na sahihi kwa umri wao. Kama watoto wana-saidia kazi katika shamba la familia au biashara, kazi hizo inabidi ziwe salama na zinazoendana na umri wao na kuzingatia sheria za kazi za nchi husika. Kazi za watoto hazipaswi kuhatarisha haki zao nyingine, ikiwa ni pamoja na haki ya kupata elimu, au haki ya mapumziko na kucheza.

Page 53: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

52

KIAMBATISHO CHA 2

ORODHA YA VIFAA MUHIMU KWA AJILI YA KUENDESHEA SEMINA PAMOJA NA VIJANA

NYARAKA

VIFAA VYA KUANDIKIA

VIFAA

Vifaa vya kurekodiaBetri

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Karatasi za mahudhurio ya kila siku zikiwa na taarifa ya mawasiliano ya washirikiFomu za idhiniRatiba ya siku ya Washauri

Chati mgeuzo na karatasiKalamu za kuandikia ubaoni Gundi ya nailoni (kwa ajili ya kugundishia karatasi ukutani)Mpira 1 wa tenisiManila/karatasi ya rangiPeni na penseli kwa ajili ya kikundi Madaftari kwa ajili ya kikundiVitabu vya kumbukumbu kwa ajili kuweka kumbukumbu ya vipindi vilivyorekodiwa

Page 54: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

53

KIAMBATISHO CHA 3

MIFANO YA MICHEZO YA KUVUNJA UKIMYA NA KUTIA NGUVU

KUJUANA – KUVUNJA UKIMYA

MAJINA NA VIVUMISHI

KUCHEZEA MPIRA

KUANGALIANA

VITATU VYA UKWELI NA KIMOJA CHA UONGO

TUNA VITU GANI VINAVYOFANANA?

MAFUNDO

KUJENGA UAMINIFU

KUMSOGEZA MTU

KUONGOZA NA KUELEKEZA

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Huu mkusanyiko wa michezo ya kuvunja ukimya na kutia moyo ambayo imekusanywa kwa kutumia kitabu kinachoitwa ‘100 ways to energise groups: Games to use in workshops, meetings and the community’ kilichoandikwa na International HIV/AIDS Alliance

Washiriki wafikirie kivumishi ili kujielezea wanavyojisikia au walivyo. Kivumishi lazima kianzie herufi kama ya majina yao, kwa mfano, “Ninaitwa Henri na nina furaha” au “Ninaitwa Alice na ni wakushangaza”. Wanaposemwa hivyo wanaweza kuigiza kitendo ambacho kinaelezea kivumishi

Kila mmoja aandike jina lake pamoja mambo yenye kumhusu kwenye karatasi kubwa, kwa mfano “Alfonse anapenda kuimba, anapenda mpira, ana wake watano na anapenda PRA”. Halafu washiriki wazunguke na karatasi zao. Wakutane wawili wawili, waonyeshane karatasi zao halafu wakisie “taarifa” ipi ni ya uongo

Mwezeshaji ataje sifa zinazofanana kwa baadhi ya watu kwenye kikundi, kama kuwa na “rangi ya bluu kwenye fulana”. Wote wenye fulana zenye rangi ya bluu waende kwenye kona moja ya chumba. Mwezeshaji ataje sifa nyingine kama “anayependa soka” watu wenye sifa hiyo waende kwenye eneo linalioonyeshwa.

Kila mmoja asimame karibu kwenye duara. (Kama duara ni kubwa sana, linaweza kugawanywa katika maduara mawili). Mwezeshaji aanze kwa kurusha mpira kwa mtu mmoja aliye kwenye duara, amwite jina lake wakati akirusha mpira. Mpira uendelee kurushwa na kudakwa, ukitengeneza muundo wa kikundi. (Kila mtu akumbuke amepokea mpira kutoka kwa nani na amemrushia nani.) Kila mmoja anapokuwa amepokea mpira na muundo kuwa umetengenezwa, ongeza mpira mmoja au miwili zaidi, ili kila mara kuwe na mipira inayorushwa kwa wakati huo, kwa kufuata muundo uliotengenezwa

Washiriki wasimame kwenye duara. Kila mmoja amwangalie mwenzake kwenye duara. Wawili hao watembee kukatisha duara na kubadilishana nafasi, huku wakiwa wanaangaliana. Vikundi zaidi vinaweza kubadilishana nafasi wakati huo huo na kikundi kihakikishe kwamba kila mmoja aliye kwenye duara anahusika kwenye kubadilishana. Anza kwa kujaribu kimya kimya halafu kwa kusalimiana katikati ya duara

Washiriki wasimame kwenye duara na kuunganisha mikono. Wakiwa wameunganisha mikono, wasogee kwa namna yoyote wanayotaka, kupindapinda na kugeuka na kufanya “fundo”. Halafu wakunjue fundo hilo bila kuachiana mikono

Washiriki wasimame katika mistari miwili wakiangaliana. Kila mmoja ashike vizuri mikono ya mwenzake aliye mkabala naye. Mtu mmoja ajitolee kulala uso ukitazama juu akiwa mwanzoni mwa mstari. Wawili walioshikana wainue mikono juu na chini kumsogeza mtu aliyejitolea hadi kwa watu wengine wawili. Mchezo uendelee hadi huyo mtu anasogezwa hadi mwisho wa mstari.

Washiriki wagawanyike katika vikundi vya wawili wawili. Mtu mmoja kwenye kila kikundi ajifunike usoni ili asione. Mmoja amwongoze mwingine kwa uangalifu kuzunguka eneo huku akihakikisha hagongi kitu chochote. Baada ya muda, mwezeshaji awaambie washiriki kubadilishana nafasi. Mwishoni, washiriki wajadili walivyojisikia walipotakiwa kumwani mtu ili wawe salama

Huu mkusanyiko wa michezo ya kuvunja ukimya na kutia moyo ambayo imekusanywa kwa kutumia kitabu kinachoitwa ‘100 ways to energise groups: Games to use in workshops, meetings and the community’ kilichoandikwa na International HIV/AIDS Alliance

Page 55: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

54

KUPASHA MWILI MOTO

SANAMU ZA KIKUNDI

SOGEA HADI KWENYE ALAMA

KUSIKILIZA, KUANGALIA KWA MAKINI NA KUSIMULIA HADITHI

“PRRR” na “PUKUTU”

TIDE’S IN/TIDE’S OUT

MTAFUTE MTU ALIYEVAA...

NINI KIMEBADILIKA?

TASWIRA KWENYE KIOO

MFALME AMEKUFA

KUTIA NGUVU – KUJIACHIA

KUCHEZA KWENYE KARATASI

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Kiambie kikundi kizunguke kwenye chumba, kikichezesha mikono yao taratibu na kuzungusha taratibu vichwa na shingo. Baada ya muda mfupi, tamka neno. Kikundi kijitengeneze na kuwa kama sanamu inayoelezea neno hilo. Kwa mfano, kama mwezeshaji akitamka neno “amani” washiriki wote inabidi watengeneze umbo hilo mara moja, bila kuongea, wakiwa katika mkao unaoonyesha “amani” ina maana gani kwao. Rudia zoezi hilo mara kadhaa.

Mwambie kila mmoja achague alama fulani kwenye chumba. Waanze mchezo kwa kusimama kwenye “alama” yao. Waam-bie washiriki wazunguke kwenye chumba na kufanya kitendo fulani, kwa mfano, kurukaruka, na kumsalimia kila aliyevaa nguo ya bluu au kutembea kwa kurudi nyuma. Mwezeshaji anaposema “simama” kila mmoja akimbie kurudi kwenye alama yake. Mtu anayefika kwenye alama yake wa kwanza atakuwa kiongozi wa hatua inayofuata na anaweza kuwaambia wana kikundi wafanye kile anachotaka

Mwambie kila mmoja afikirie ndege wawili. Mmoja anaitwa “prrr” na mwingine “pukutu”. Kama ukimwita “prrr” washiriki wote inabidi wasimamie vidole na kuchezesha viwiko vyao kama ndege anakung’uta mabawa yake. Kama ukiita “pukutu”, kila mmoja asimame wima bila kuchezesha mabawa.

Chora mstari uwe kama ufukwe wa bahari na waambie washiriki wasimame nyuma ya mstari. Mwezeshaji anapotamka “Tide’s out”, kila mmoja aruke mbele na kuvuka mstari. Kiongozi anapotamka “Tide’s in”, aruke nyuma kuvuka mstari. Kama mwezeshaji akitamka “Tide’s out” mara mbili kwa mpigo, washiriki watakaoruka watatoka mchezoni

Washiriki wagawanyike katika vikundi vya wawili. Washiriki wachunguzane na kukumbuka mwonekano wa kila mmoja. Halafu mmoja ageuke wakati mwingine akibadilisha mambo matatu kwenye mwonekano wake, kwa mfano kuvaa saa kwenye mkono mwingine, kuvua miwani na kukunja mikono ya shati. Mchezaji mwingine ageuke na kugundua mabadiliko matatu. Halafu wachezaji wabadilishane nafasi

Washiriki wajigawe kwenye vikundi vya wawili wawili. Kila kikundi kiamue nani aatakuwa “kioo”. Halafu mtu huyo (kioo) aige vitendo vya mshirika wake. Baada ya muda, kiambie kikundi kibadilishane nafasi ili mtu mwingine awe “kioo”

Wawezeshaji waandae magazeti au nguo ambazo zina ukubwa sawa. Washiriki wagawanyike kwenye vikundi vya wawili. Kila kikundi kipewe kipande cha karatasi au nguo. Wacheze wakati

Mchezaji wa kwanza amgeukie jirani yake na kusema, “Mfalme amekufa”. Jirani aulize, “amekufaje?” na mchezaji wa kwanza ajibu, “Amekufa akifanya hivi” na aigize. Washiriki wote warudie ishara hiyo kwa mfululizo. Mchezaji wa pili arudie sentensi na watatu aulize, “amekufaje?” Aongeze ishara nyingine. Halafu kundi zima liige ishara hizo mbili. Mchezo uendelee kuzun-guka duara hadi kuwe na ishara nyingi za kukumbuka

Waambie washiriki watembee taratibu, wakitingisha miguu na wakiwa wamejiachia. Baada ya muda mfupi, mwezeshaji atamke “Mtafute mtu...” na kutaja sehemu ya nguo. Washiriki wakimbie na kusimama karibu ya mtu aliyeelezewa. Rudia zoezi hili mara kadhaa kwa kutumia aina tofauti za nguo. Gusa kitu cha bluu na waambie washiriki wasimame. Fafanua kwamba utawaambia watafute kitu cha bluu na kwamba wakifuate na kukigusa. Inaweza kuwa shati la bluu, peni ya bluu, kiatu cha bluu na kadhalika. Endelea na mchezo kama hivyo, ukiwaambia washiriki kutoa mapendekezo yao ya vitu vya kugusa

Page 56: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

mwezeshaji anapiga muziki au makofi. Wakati muziki na makofi yanaposimama, kila kikundi kisimame kwenye kipande chake cha gazeti. Mara nyingine muziki au makofi yanaposimama, kikundi kikunje marakatasi au nguo zao kwa nusu kabla kusimama juu. Baada ya raundi kadhaa, karatasi au nguo itakuwa ndogo sana kwa sababu ya kukunjwa mara nyingi. Itaku-wa ngumu kwa watu wawili kusimama juu yake. Vikundi ambavyo sehemu ya miili yao iko sakafuni, watatoka mchezoni. Mchezo uendelee hadi kuwe na kikundi kilichoshinda

Washiriki wasimame au kukaa kwenye duara, wakiwa wameshikana mikono kimya na kuwa makini. Mwezeshaji atume mfululizo wa “shoti” pande zote mbili za kikundi kwa kwa kukandamiza mikono kwa mtu aliye karibu naye. Washiriki watume shoti kuzunguka duara, kama kwenye mkondo wa umeme, kwa kukandamiza mikono kwa mtu aliye karibu na “kukipa nguvu” kikundi

Kiambie kikundi kigawanyike katika vikundi viwili na kufanya mistari miwili. Halafu waambie wana kikundi wote kuweka mikono kwenye kiuno cha mtu aliye mbele yao kutengeneza muundo wa joka. Chomeka kitambaa nyuma ya suruali, sketi au mkanda wa mtu wa mwisho kwenye kila mstari ili kufanya muundo wa mkia wa joka. Halafu vikundi inabidi vishike mkia wa joka jingine bila kupoteza mkia wao

Washiriki wasimame au wakae kwenye duara. Wapige makofi kuzunguka duara huku wakimtazama na kupiga makofi kwa pamoja na mtu aliye upande wa kulia, ambaye anayerudia kupiga makofi na mtu aliye kulia, na kuendelea. Fanya hivyo haraka iwezekanavyo. Piga makofi mara nyingi yenye midundo tofauti, kuzunguka duara wakati huo huo.

Washiriki wakae kwenye duara. Kwa zamu kila mmoja aonyeshe hisia fulani. Wengine wajaribu kukisia mtu huyo anajisikia-je. Mtu anayekisia kwa usahihi, awee anayefuatia kuonyesha hisia.

55

PASIA NGUVU

MKIA WA JOKA

KUPIGIANA MAKOFI

KUELEZEA UNAVYOJISIKIA

NINAJISIKIAJE?

RANGI – HISIAKwa zamu kila mmoja aseme jinsi anavyojisikia na kuhusianisha rangi na hisia

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Page 57: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

56

KIAMBATISHO CHA 4

MFANO WA FOMU YA IDHINI

Andika jina

Sahihi Tarehe

Jina la mzazi / mlezi

Saini ya mzazi / mlezi

Anwani

Simu Barua pepe

Jina langu kamili

Umri

Nashiriki kwenye mradi unaoendeshwa na (jina la kituo cha radio) kutoka (tarehe) hadi (tarehe).

Kwa kusaini fomu hii, natoa kwa ruhusa kwa (jina la kituo cha radio)

Kutumia kazi yangu kwenye kipindi chao.

Nafahamu kwamba sauti yangu iliyorekodiwa inaweza kuhaririwa na (jina la kituo cha radio)Nafahamu kwamba sauti yangu itarushwa hewani, nina uhuru wa kutumia jina langu la kwanza tu au kutojulikana

Kipindi kinaweza kurushwa hewani. Kinaweza pia kuwekwa kwenye mtandao au kusambazwa kwenye CD, mp3 au miundo mingine ya sauti

Pia naelewa kwamba kama kuna kitu chochote nisichotaka kushikishana na (jina la kituo cha radio)

nitawaambia na hakitatumika

Naelewa (jina la kituo cha radio) Naelewa (jina la kituo cha radio)

itaniheshimu mimi na familia yangu. Naelewa kwamba, kadri iwezekanavyo, watanipa nakala ya kazi yangu ili niweze kusikia jinsi ilivyotumika. Nakubali kuheshimu sheria za kituo cha radio. Naelewa kwamba ushiriki ni wa hiari na naweza kuusitisha kama nikitaka kwa kutoa taarifa ya maandishi kwamba sishiriki tena

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Page 58: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

57

KIAMBATISHO CHA 5

MADA YA KIPINDI: KUISHI KWA AFYA

Tumia makala za radio zilizorekodiwa, utafiti, mwongozo uliopendekezwa na swali kumsaidia mwandishi wa habari kijana kuandika mwongozo wa kipindi

UTANGULIZI

[(WEKA KIBWAGIZO)

MTANGAZAJI WA 1: Mambo mazuri kabisa na unasikiliza [JINA LA KIPINDI] hapa [KITUO CHA RADIO]My name is [JINA] .

MTANGAZAJI WA 2: Na mimi ninaitwa [JINA] . Leo tutazungumzia kuhusu kula kwa afya.

MTANGAZAJI WA 1:

Na hiyo haimaanishi kula milo mitatu kwa siku, tutaona tunahitaji kula nini ili kuifanya miili na akili zetu ziwe na afya na imara

MTANGAZAJI WA 2:

Tuna bahati kuzungumza na [JINA LA MWANAMICHEZO] na kusikia siku ya mwanamichezo

(WEKA SAUTI YENYE MAELEZO MAFUPI)

HITIMISHO

MTANGAZAJI WA 1: Wanasema tufaa moja kwa siku...

MTANGAZAJI WA 2: Ndio, kama tukila kwa afya, tutakuwa na afya na wenye nguvu, na hatutahitaji daktari mara kwa mara. [KITUO CHA RADIO] kwenye Kama ukitaka kujua mambo mengine mazuri zaidi, sikiliza [JINA LA KIPINDI] wiki ijayo [SIKU] saa Tutazungumza kuhusu [MUDA] [MADA YA KIPINDI CHA WIKI IJAYO]

MTANGAZAJI WA 1: Hadi siku hiyo, tunasema kwaheri !

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

inakuwaje

.

Page 59: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

58

MAREJEO YA ZIADA

All Sides of the Story. Reporting on Children: A Journalist’s Handbook, UNICEF and Media Monitoring Project, 2003http://www.unicef.org/uganda/allsidesofthestory.pdf

Children’s Rights and Media: Guidelines and Principles for Reporting on Issues Involving Childrenhttp://www.ifj.org/fr/articles/childrens-rights-and-media-guidelines-and-principles-for-reporting-on-issues involving-children

Editorial Guidelines and Principles for Reporting on Children in the Media 2008, A Snapshot of Children in Zambian News, Media Monitoring Project/Save the Childrenhttp://www.mediamonitoringafrica.org/images/uploads/zam_guidelinesBooklet.pdf

Gender-Sensitive Indicators for Media. Framework of indicators to gauge gender sensitivity in media operations and content, UNESCO, 2012http://unesdoc.unesco.org/images/0021/002178/217831e.pdf

Getting the balance right: Gender Equality in Journalism, International Federation of Journalists, 2009

Getting the Story and Telling it Right: HIV and TV, UNESCO, 2009http://unesdoc.unesco.org/images/0021/002178/217831e.pdf

http://www.ilo.org/wcmsp5/groups/public/---dgreports/---dcomm/documents/publication/wcms_180976.pdf

How to Start a Youth Radio Project in Your Community: Facilitator’s Handbook, Children’s Radio Foundation and UNICEF, 2011http://www.childrensradiofoundation.org

How to Make Your Own Radio Shows: Youth Radio Toolkit, Children’s Radio Foundation and UNICEF, 2011http://www.childrensradiofoundation.org

How to report on children in crisis (2006)http://www.mediawise.org.uk/wp-content/uploads/2011/03/How-to-report-on-children-in-crises.pdf

Lloyd F., Sakaza Mngani ! Kids Community Radio Project Handbook, Institute for the Advancement of Journalism, 2007

Media Development Indicators: a framework for assessing media development, UNESCO, 2008http://tinyurl.com/mx8nxqh

Media and Information Literacy Curriculum for Teachers, UNESCO, 2011http://unesdoc.unesco.org/images/0019/001929/192971e.pdf

Media as Partners in Education for Sustainable Development, UNESCO, 2008 http://tinyurl.com/3qdo8m5

New Questions, New Insights, New Approaches. Contributions to the Research Forum at the World Summit on Media For Children and Youth, 2010, The International Clearinghouse on Children, Youth and Media, NORDICOM, University of Gothenburghttp://www.nordicom.gu.se/common/publ_pdf/Yearbook_2011.pdf

Radio Manifesto, World Radio Forum, 2004http://www.worldradioforum.org/manifesto/RadioManifesto.pdf

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Page 60: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

59

MAREJEO YA ZIADA MWENDELEZO

Regional study of children’s participation in Southern Africa: South Africa, Swaziland and Zambia, Save the Children Sweden, 2010

Research Summary Report, BBC WST (World Service Trust), African Media Development Initiative (AMDI), 2006http://africanmediainitiative.org/wp-content/uploads/2013/01/AMDI-BBC-summary-report.pdf

Speaking Up and Talking Back? Media Empowerment and Civic Engagement Among East and Southern Africa Youth, NORDICOM, University of Gothenburg, 2013 Shout Out: A Kids Guide to Recording Stories, Urban Rangers and Neighborhood Stories, 2005http://transom.org/tools/basics/200501.shoutout.web.pdf?9d7bd4

The African Charter on the Rights & Welfare of the Child, Organization of African Unity, 1990http://acerwc.org/acrwc-charter-full-text/

The African Charter on Children’s Broadcastinghttp://www.planchildrenmedia.org/IMG/pdf/African_charter_on_children_s_broadcasting_eng.pdf

The Media and Children’s Rights’, MediaWise and UNICEF, 2005

The Media and Children’s Rights (2012)http://www.mediawise.org.uk/children/the-media-and-childrens-rights/

 

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Page 61: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

60

ORODHA YA VITABU VYA MAREJEO

Asthana S., Innovative Practices of Youth Participation in Media, UNESCO, 2006

Barry C. and Jempson M., The Media and Children’s Rights, UNICEF, 2005

Byerly C., Global Report on the Status of Women in the News Media, International Women’s Media Foundation, 2011

in the 21st century, Campbell- Kibler, Associates, Inc., 2001

Gigli S., Children, Youth and Media Around the World: An Overview of Trends and Issues, InterMedia Survey Institute for UNICEF, 2004

Hart R., Children’s Participation from Tokenism to Citizenship, UNICEF, 1992

Bank, 2011

Kinkade S. and Macy C., What Works in Youth Media: Case Studies from Around the World, International Youth Foundation, 2003

Myers M., Radio and Development in Africa, International Development Research Centre (IDRC), Canada, 2009

Myers M., Voices from Villages: Community Radio in the Developing World. Center for International Media Assistance (CIMA), Washington, 2011

and Open Society For Southern Africa (OSISA), 2012

Shipler M., Youth Radio for Peacebuilding, a guide, Search for Common Ground and Radio For Peace Building Africa, 2006

Population facts, UN Population Division, 2009

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

Page 62: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

61

Sehemu ya nne | Marejeo Muhimu na Viambatisho

SHUKRANI

Shukrani za ziada ziende kwa Meghan Adams, Kaitlin Parker, Erla Rabe, Elizabeth Sachs na Bill Siemering .

Mwongozo huu umekamilishwa kutokana na uzoefu na kujitoa kwa watu wengi sehemu mbalimbali duniani. UNESCO inatambua mchango mkubwa wa Children’s Radio Foundation na inawashukuru wafanyakazi na vijana kutoka vituo vya radio vya kijamii na asasi za kijamii katika nchi zifuatazo: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Lesotho, Liberia, Namibia, Afrika Kusini, Tanzania na Zambia

UNESCO inawashukuru kwa utaalam wa mapitio uliotolewa na Peter Frank Banda (Zambia), Alymana Bathily (Senegal), Steve Buckley (UK), Francesco Diasio (Italia), Njuiki Githethwa (Kenya), Daoud Kuttab (Jordan), Julius Mtemahanji (Namib-ia) na Olivier Pessot (France)

Ikiwa na makao yake Afrika Kusini, Children’s Radio Foundation ni asasi isiyo ya kiserikali inayoshughulika na kubuni, kuandaa, mafunzo na kusaidia miradi ya radio za vijana barani Afrika. Ikiwa na zaidi ya vituo vya radio za kijamii washirika na vijana 1000 waliopata mafunzo ya uandishi wa habari katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Liberia, Afrika Kusini, Tanzania na Zambia, Children’s Radio Foundation (CRF) inatoa fursa za mazungumzo, uongozi na ushiriki kwenye kazi za jamii kwa vijana. Kwa kupitia vipindi vya radio, vijana wanazungumzia matatizo yao na wanawafikia wenzao na wasikilizaji wengi zaidi kuhusiana na mambo yanakumbana nayo

Page 63: KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO - unesco.org · kushirikiana na wengine uvumilivu, maarifa na uzoefu wao kupitia radio inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo wa jamii husika

62

UNESCOMedia and Society SectionCommunication and Information Sector7, place de Fontenoy75352 Paris 07 SPFrance

Shirika la Umojawa Mataif la Elimu,

Sayansi na Utamaduni