mwongozo wa kifaa cha mwanafunzi...nyakati nyingine, utapata ujumbe wa hitilafu unaofuata ikiwa...

15
Mwongozo wa Kifaa cha Mwanafunzi Taarifa ya Kuingia Taarifa ya Usaidizi kwa Mwanafunzi/Familia Kutatua Matatizo ya Muunganisho wa Intaneti Maelekezo ya Microsoft Outlook Maelekezo ya Microsoft Teams Kufikia Canvas

Upload: others

Post on 21-Oct-2020

8 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Mwongozo wa Kifaa cha Mwanafunzi

    Taarifa ya Kuingia

    Taarifa ya Usaidizi kwa Mwanafunzi/Familia

    Kutatua Matatizo ya Muunganisho wa

    Intaneti

    Maelekezo ya Microsoft Outlook

    Maelekezo ya Microsoft Teams

    Kufikia Canvas

  • Ukurasa wa 3 kati ya 15

    Kuingia kwenye Kompyuta Yako ya DMPS Kabla ya kuingia kwenye kompyuta yako ya DMPS, unahitaji kuhakikisha kuwa una muunganisho wa Intaneti. Utahitaji kuunganisha kwenye Wi-Fi ya nyumbani kwako au kupitia kituo cha muunganisho wa mtandao ukifuata maelekezo yaliyo hapa chini.

    Kuunganisha kwenye Wi-Fi yako 1. Ikiwa unatumia kituo cha muunganisho, hakikisha unakiwasha na uhakikishe unajua

    jina/nenosiri la mtandao wako. 2. Washa kompyuta, kisha bofya CTRL-ALT-DEL ili kupata skrini ya kuingia. Mara unapofika kwenye

    skrini iliyoko hapa chini, bofya ikoni ya Wi-Fi (iliyozungukwa kwa mduara hapa chini).

  • Ukurasa wa 4 kati ya 15

    3. Chagua jina la mtandao wako (ama mtandao wako wa nyumbani au ikiwa unatumia kituo cha muunganisho, jina la mtandao wa kituo hicho), kisha bofya "Unganisha" na uweke nenosiri au nywila ya Wi-Fi yako. Ikiwa limewekwa ifaavyo,

    linapaswa kuunganisha kwenye Wi-Fi yako.

    Kuingia Mara ya Kwanza – Uingiaji wa Mwanzo Ikiwa hujawahi kuingia kwenye kompyuta hii, fuata maelekezo haya.

    1. Baada ya kuanzisha muunganisho wa Wi-Fi na kusubiri takribani dakika 5, bofya kitufe cha "Uingiaji wa Mwanzo" kwenye kona ya chini kulia ya skrini yako.

    KUMBUKA: Ni muhimu KUSUBIRI takribani dakika 5 baada ya kuunganisha kwenye Wi-Fi yako kabla ya kuendelea na hatua inayofuata. Ikiwa utaenda haraka sana, inaweza kusababisha "Hitilafu ya 800" na utalazimika kuwasha upya na kuanza tena.

  • Ukurasa wa 5 kati ya 15

    2. Weka jina lako la mtumiaji ([email protected]). 3. Weka nenosiri lako. 4. Bofya ENTER kwenye kicharazio chako, au ubofye kishale kilicho upande wa kulia wa nenosiri

    lako ili kuingia

    Kuingia baada ya Mara ya Kwanza Ikiwa umeingia kwenye kompyuta hii hapo awali, jina lako la mtumiaji linapaswa kuonekana kwenye skrini na unachohitaji tu kufanya ni kuweka nenosiri lako kisha ubofye ENTER.

    Always On VPN Ili kuhakikisha kuwa kompyuta yako inafanya kazi vizuri, unahitaji kuunganisha kwenye mtandao wa DMPS kupitia AlwaysOnVPN (AOVPN). Hii inapaswa kufanyika kiotomatiki, lakini ni vizuri kuangalia hii kila wakati unapoingia kwenye kompyuta yako. Fuata hatua hizi za haraka/rahisi ili kuthibitisha kuwa umeunganishwa kwenye AOVPN:

  • Ukurasa wa 6 kati ya 15

    1. Baada ya kuingia, bofya kwenye muunganisho wa Wi-Fi kwenye kona ya chini kulia ya skrini ya kompyuta yako.

    2. Kwenye sehemu ya juu ya skrini ambayo inaibuka, hakikisha kuwa DMPS AlwaysOnVPN inaonyesha muunganisho. Ikiwa haibofyi kitufe cha "Unganisha".

    Hitilafu ya AlwaysOn VPN

    Nyakati nyingine, utapata ujumbe wa hitilafu unaofuata ikiwa umeshindwa kuunganisha kwenye AOVPN. Mara nyingi hitilafu hii hutokea ikiwa unajaribu kuunganisha kwenye AOVPN haraka mno baada ya kuingia, au haraka mno baada ya kukatisha muunganisho wa AOVPN. Subiri dakika chache na ujaribu kuunganisha tena. Ikishindikana kuunganisha, unaweza kuhitaji kuzima na kuanzisha tena kompyuta yako

  • Ukurasa wa 7 kati ya 15

    Kituo cha Usaidizi cha Familia/Mwanafunzi Unahitaji msaada? Unaweza kupiga simu kwenye Kituo cha Usaidizi cha Familia/Mwanafunzi ili kupata msaada. Nambari hiyo ni 515-242-8221 na imefunguliwa M-F, saa 1:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni.

    Vidokezi vya Kutatua Matatizo ya Muunganisho wa Intaneti 1. Fungua kivinjari na uende kwenye tovuti mpya ambayo hujawahi kutembelea hapo awali ili

    kuhakikisha kuwa imeunganishwa kwenye Intaneti. Kwa Mfano: msnbc.com, cbs.com, nbc.com, google.com, imdb.com. Je, unaweza kuingia kwenye tovuti mpya? Ikiwa ndiyo, basi umeunganishwa kwenye Intaneti, ikiwa sivyo, basi huna Ufikiaji kwenye Intaneti.

    2. Ikiwa hujaunganishwa kwenye Intaneti, angalia ikoni ya mtandao wako upande wa chini karibu na saa (kona ya kulia upande wa chini wa skrini) na uone ikiwa umeunganishwa kwenye mtandao wako wa nyumbani (hasa Wi-Fi). Ikiwa hujaunganishwa, unahitaji kuunganisha (na ujue nenosiri lako la intaneti).

    3. Ikiwa huwezi kuunganishwa kwenye Wi-Fi, au unaonekana kuunganishwa lakini huwezi kuingia kwenye tovuti mpya, mtoa huduma wako wa intaneti huenda anakabiliwa na matatizo, au ruta yako inaweza kuhitaji kuzimwa/kuwashwa.

    4. Ikiwa una simu ya mkononi, unaweza kwenda kwenye https://downdetector.com/na uone ikiwa kuna kukatika kwa intaneti ya mtoa huduma wako. Ikiwa hakuna kukatika kulikoripotiwa, huenda una matatizo mahususi nyumbani kwako, tafadhali mpigie simu mtoa huduma wako ili akusaidie.

    5. Ikiwa una Wi-Fi lakini utendaji ni duni au intaneti inafifia, unaweza kuunganisha kebo ya Ethaneti (ikiwa unayo) kwenye tundu nyuma ya ruta /modemu na uipachike moja kwa moja kwenye kompyuta yako.

    6. Angalia kasi ya muunganisho wako kwa kwenda kwenye https://www.speedtest.net/. Unapobofya kitufe cha GO, itaangalia kasi ya kupakua na ya kupakia. Ikiwa kasi ya kupakua ni polepole, chini ya 10, utakuwa na matatizo ya utendaji na hutaweza kuunganisha kwenye Always-on-VPN (AOVPN). Muunganisho wa Ethaneti (ona hapo juu) unaweza kuwa suluhisho.

    7. Ikiwa una kasi nzuri sana ya kupakua, lakini bado haiwezi kuunganisha kwenye AOVPN, huenda ruta yako inazuia VPN. Utahitaji kuwasiliana na mtoa huduma wako, au ikiwa utasanikisha Wi-Fi yako mwenyewe, mtu mmoja katika nyumba yako anaweza kujua jinsi ya kusanidi ruta yako ili kuruhusu VPN.

    8. Ikiwa unaishi katika nyumba aina ya kondo au fleti ambapo Intaneti inatolewa na huna ruta au modemu, unaweza kuhitaji kuzungumza na wasimamizi wa jengo lako kuhusu machaguo yaliyopo.

  • Ukurasa wa 8 kati ya 15

    Barua pepe kwa kutumia Microsoft Outlook Kumbuka: Ikiwa maelekezo hayalingani na yale unayoona, pengine unatumia toleo la zamani la Outlook kwenye wavuti.

    Fungua Outlook kwenye wavuti. 1. Nenda kwenye https://www.dmschools.org/ 2. Bofya kichupo cha "Wanafunzi" kilicho sehemu ya juu ya skrini.

    Telezesha chini ya ukurasa na uchague "Barua Pepe ya Mwanafunzi"

  • Ukurasa wa 9 kati ya 15

    3. Ingia kwa kutumia hati tambulishi zako za Shule za Des Moines (anwani ya barua pepe).

    Badilisha Mipangilio ya Kikasha cha Barua Pepe Muhimu

    Kikasha cha Barua Pepe Muhimu hugawa kikasha chako katika vichupo viwili—Muhimu na Nyingine. Vichupo vya Muhimu na Nyingine vitaonekana juu ya kikasha chako cha barua. Utaarifiwa kuhusu barua pepe zinazoelekezwa kwenye Nyingine na unaweza kubadilisha kati ya vichupo wakati wowote ili uangalie haraka.

    Unahitaji kuangalia sehemu zote mbili ili usikose barua pepe muhimu.

    Ikiwa ungetaka kubadilisha mpangilio huu, fuata hatua hizi:

    1. Kwenye sehemu ya juu kulia ya Kikasha chako, chagua Mipangilio . 2. Chagua kitufe cha kutogoa karibu na Kikasha cha Barua Pepe Muhimu.

    Badilisha jinsi ujumbe wako unavyopangwa

    1. Kwenye kikasha chako, chagua kichupo cha Muhimu au Nyingine, kisha ubofye kulia kwenye ujumbe unaotaka kuhamisha.

    2. Ili kuhamisha ujumbe kutoka kwenye Muhimu kwenda Nyingine, chagua Hamisha > Hamisha kwenda kikasha cha Nyingine.> Chagua Nyakati zote hamishia kwenye kikasha cha Nyingine ikiwa

  • Ukurasa wa 10 kati ya 15

    ungependa ujumbe wote wa siku za usoni kutoka kwa mtumaji huyo uwasilishwe kwenye kichupo cha Nyingine.

    3. Ikiwa unahamisha ujumbe mmoja kutoka kwenye Nyingine kwenda Muhimu, chagua Hamisha > Hamisha kwenda kikasha cha Muhimu.> Chagua Nyakati zote hamisha kwenda kwenye kikasha cha Muhimu ikiwa ungependa ujumbe wote wa siku za usoni kutoka kwa mtumaji huyo uwasilishwe kwenye kichupo cha Muhimu.

    Maelekezo ya classic Outlook kwenye wavuti Ikiwa skrini yako haikuonekana kama zile zilizoko hapo juu, unaweza kuwa katika "Outlook ya Kipekee." Haya hapa ni maelekezo ya kiolesura hicho.

    Washa Kikasha cha Barua Pepe Muhimu

    1. Fungua Outlook kwenye wavuti.

    2. Chagua Mipangilio > Mipangilio ya onyesho> Kikasha Muhimu .>> 3. Chini ya Wakati barua pepe inapokelewa, chagua Panga ujumbe kwenda kwenye Muhimu na

    Nyingine. Vichupo vya Muhimu na Nyingine vitaonekana juu ya kikasha chako cha barua. Utaarifiwa kuhusu barua pepe zinazoelekezwa kwenye Nyingine na unaweza kubadilisha kati ya vichupo wakati wowote ili uangalie haraka.

  • Ukurasa wa 11 kati ya 15

    Microsoft Teams Mara tu unapoingia kwenye kompyuta yako, walimu wako wa darasa wanaweza kuwa wanatumia Microsoft Teams kuwasiliana na wewe. Tazama maelekezo hapa chini ya jinsi ya kufikia Microsoft Teams.

    Ikiwa uko kwenye kifaa cha Wilaya: Bofya kwenye ikoni ya Windows kutoka kwenye mwambaa wa kazi chini ya skrini yako.

    Andika "Teams" na ubofye kwenye "Microsoft Teams"

    Kutoka kwenye kivinjari: Nenda kwenye https://www.dmschools.org/

    Bofya kichupo cha "Wanafunzi" kilicho sehemu ya juu ya skrini.

  • Ukurasa wa 12 kati ya 15

    Biringiza chini na uchague "Barua pepe ya Mwanafunzi"

    Ingia kwa kutumia hati tambuzi zako za Shule za Des Moines.

    Mara unapoingia kwenye barua pepe, bofya Kizindua Programu kwenye kona ya juu upande wa kushoto. Chagua Teams.

  • Ukurasa wa 13 kati ya 15

    Kufikia Canvas Unaweza kufikia Canvas

    1. Nenda kwenye http://www.dmschools.org 2. Bofya kwenye kichupo cha "Wanafunzi" upande wa juu 3. Bofya kiunganishi cha "Canvas"

    Miongozo ya Kusafisha Kompyuta

    Huku kukiwa na wasiwasi ya afya ya umma kuhusu virusi vya SARS-CoV-2 na ugonjwa wa COVID-19, ambao pia unajulikana kama Virusi vya Korona, unaoenea ulimwenguni kote, HP inataka wateja wawe na taarifa wanayohitaji ili kusafisha vifaa vya HP kwa ufanisi na kuwasaidia wateja katika kudumisha mazingira ya kazi yenye afya .

    Kiuaviini kinachopendekezwa na CDC ambacho pia kiko ndani ya miongozo ya kusafisha ya HP ni mchanganyiko wa alkoholi unaojumuisha asilimia 70 ya alkoholi ya isopropyl na asilimia 30 ya maji. Tafadhali fuata hatua zilizo hapa chini ili kutumia mchanganyiko wa alkoholi unaopendekezwa na CDC katika kusafisha sehemu za nje ambazo zinaguswa mara nyingi kwenye bidhaa za HP:

    1. Vaa glavu za kutumia mara moja na kutupwa zilizotengenezwa kwa lateksi (au glavu za nitrili ikiwa unaathiriwa na lateksi) wakati wa kusafisha na kuua viini kwenye sehemu hizo.

    2. Zima kifaa na ukate umeme wa AC. Kamwe usisafishe bidhaa wakati imewashwa au plagi kuunganishwa.

    3. Tenganisha vifaa vyovyote vya nje. 4. Tia unyevu kwenye kitambaa kidogo kwa mchanganyiko wa asilimia 70 ya alkoholi ya

    isopropyl/asilimia 30 ya maji. Usitumie vifaa vyenye nyuzinyuzi, kama taulo za karatasi au karatasi ya choo. Kitambaa kinapaswa kuwa na unyevu, lakini kisiwe kimelowana.

    Alkoholi ya Isopropyl inauzwa katika maduka mengi, kwa kawaida katika asilimia 70 ya Alkoholi ya Isopropyl/asilimia 30 ya Maji. Inaweza pia kuuzwa kama alkoholi ya kusugua.

    5. Usinyunyize vioevu vyovyote moja kwa moja kwenye bidhaa. 6. Futa taratibu ukitumia kitambaa kilicho na unyevu kwenye sehemu za kusafishwa. Usiruhusu unyevu

    wowote udondoke katika maeneo kama kicharazio, paneli za kuonyesha au vituo vya USB, kwani unyevu unapoingia ndani ya bidhaa ya umeme unaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa bidhaa hiyo.

    7. Wakati wa kusafisha, futa kwa uangalifu kwa mwelekeo mmoja, kutoka sehemu ya juu ya onyesho hadi chini.

    8. Hakikisha sehemu zimekauka kabisa kabla ya kuwasha kifaa baada ya kusafisha. Hakuna unyevu unaopaswa kuonekana kwenye nyuso za bidhaa kabla ya kuwashwa.

    9. Glavu zinapaswa kutupwa baada ya kila usafishaji. Safisha mikono mara tu baada ya glavu kuondolewa.

  • Ukurasa wa 14 kati ya 15

  • Ukurasa wa 15 kati ya 15