maendeleo endelevu michezoni barani afrika...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada...

6
MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA Utafiti umefanywa na Mtandao wa Washikadau wa Kimataifa (INP): Dkt. Lain Lindsey (Chuo Kikuu cha Durham, Uingereza) Dkt. Emmanuel Owusu-Ansah, Dkt. Belaa Bello Bitugu (Chuo Kikuu cha Ghana) Dkt. Hamad Ndee (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania) Dkt. ABT Zakaria, Dkt. Seidu Alhassan, Dkt. Edward Sirleaf Makhama (Chuo Kikuu Cha Mafunzo ya Maendeleo, Ghana) Dkt. Jenes (Chuo Kikuu cha Monash, Australia) Wakisaidiwa na: Mohammed Abdul-Wahid, Tahiru Abdullahi, Gideon Adjorlolo, Abdul-Mumin Al Hassan, Jilala Arobert, Alfred Attieku, Sam Napoleon Bellua, Derrick O. Charuuay, Francis Fikili, Kassim Imoro, Yonnas Ngonyani, Charles Paul, Erick Sena Adjeyi, Ernest. B.Sylvester Funded by: The Leverhulme Trust (IN-050) Shaped by the past, creating the future School of Applied Social Sciences SASS Research Briefing no. 14

Upload: others

Post on 20-Jan-2021

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu

MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA

Utafiti umefanywa na Mtandao wa Washikadau wa Kimataifa (INP): Dkt. Lain Lindsey (Chuo Kikuu cha Durham, Uingereza) Dkt. Emmanuel Owusu-Ansah, Dkt. Belaa Bello Bitugu (Chuo Kikuu cha Ghana)Dkt. Hamad Ndee (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania) Dkt. ABT Zakaria, Dkt. Seidu Alhassan, Dkt. Edward Sirleaf Makhama (Chuo Kikuu Cha Mafunzo ya Maendeleo, Ghana) Dkt. Jenes (Chuo Kikuu cha Monash, Australia)

Wakisaidiwa na: Mohammed Abdul-Wahid, Tahiru Abdullahi, Gideon Adjorlolo, Abdul-Mumin Al Hassan, Jilala Arobert, Alfred Attieku, Sam Napoleon Bellua, Derrick O. Charuuay, Francis Fikili, Kassim Imoro, Yonnas Ngonyani, Charles Paul, Erick Sena Adjeyi, Ernest. B.Sylvester

Funded by: The Leverhulme Trust (IN-050)

Shaped by the past, creating the future

School of Applied Social Sciences

SASS Research Briefing no. 14

Page 2: MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu

Kumekuwako na ongezeko la matumizi ya michezo katika uchangiaji wa maendeleo barani Afrika na maeneo mengine katika kanda ya Kusini Katika mwongo uliopita. Michezo mingi yenye nia ya miradi ya maendeleo kwa sasa inalenga kuchangia katika maswala mengi kama vile ueneaji na kampeni za maswala ya afya, elimu rasmi na isiyo rasmi, uboreshaji wa maswala ya kijinsia na vijana, ujumulishaji wa kijamii na upunguzaji wa umaskini. Mipango kama hiyo imekuwa ikiendelezwa na afisi ya Michezo kwa Maendeleo na Amani katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) likishirikiana na mashirika ya kimataifa na kutekelezwa na mataifa tofauti tofauti pamoja na mashirika ya kijamii katika miktadha ya Afrika zikiwemo nchi ya Ghana na Tanzania.

Licha ya kuwepo kwa tafiti nyingi, kumekuwako na uhaba wa tafiti kuhusu michezo kama nyenzo ya kuleta maendeleo. Maswala yanayohusu uendelevu wa maendeleo kwa mfano, yamesemekana kuwa muhimu (Wallice & Lambert, 2014) lakini hayajahusishwa na uchunguzi wa takwimu. Zaidi, tafiti kuhusu michezo katika maendeleo zimekuwa zikijihusisha

na masuala katika ngazi za kimataifa na kupuuza yale masuala katika ngazi za mashinani kwa sababu zimekuwa zikifanywa na watafiti wanaofanya kazi katika vyuo vikuu vya mataifa yaliyoendelea kutoka bara Ulaya.

Msaada kutoka Wakfu wa Leverhulme uliwezesha changamoto hizo kushughulikiwa kikamilifu kupitia kwa utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Ushirika wa vyuo vikuu vitano kutoka Uingereza, Ghana, Tanzania na Australia. Mradi huo wa Maendeleo Endelevu Michezoni Barani Afrika: Utatuzi wa Ghana na Tanzania ulifanywa kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Utangulizi

Kwa vile swala la maendeleo endelevu huzua mijadala mikali na linalolezwa vibaya (Taylor, 2014), malengo matatu makuu yenye uketo yalibainishwa:

1. Kuelewa namna maendeleo endelevu yanavyoeleweka na mashirika ya kienyeji na kimataifa yanayoshirikiana na michezo nchini Ghana na Tanzania.

2. Kusoma kuhusu maswala yanayochangia au kutochangia katika uafikiaji wa maendeleo endelevu kupitia michezo kule Ghana na Tanzania.

3. Kupata ushahidi kuhusu uafikiaji (au utoafikiaji) wa matokeo ya maendeleo endelevu kupitia michezo kule Ghana na Tanzania.

Katika kushughulikia malengo haya, maswala yote ya mpanglio wa utafiti, ukusanyaji wa data na uchanganuzi wake yalifanywa kupitia mwelekeo wa ushirikiano kwa nia ya kujenga na kuendeleza ujuzi, tajriba na uwezo wa washika dau wote mtandaoni.

Sehemu mbili za uchanganuzi halisi wa data zilitumika;

• Sampuli kutoka shule za mataifa haya (Ghana na Tanzania) na mashirika ya kijamii katika nchi hizo ambazo zilitumika kuchunguza uendelevu wa michezo mahsusi katika kuleta maendeleo na uwezo wa athari ya muda mrefu kwa wanaolengwa na masuala haya. Mahojiano na mijadala ya makundi ya vijana, walimu, makocha na washirika wengine kutoka jamii hizo ilifanywa katika vituo 66 vya shule na mashirika ya kijamii kwa ujumla. Muhimu zaidi ni kwamba, data zilikusanywa na watafiti wasaidizi 16 wapya kutoka Ghana na Tanzania ambao tajriba zao zimefafanuliwa zaidi katika Sehemu ya 1.

• Mahojiano ya washikadau na wawakilishi mbalimbali kutoka mashirika ya kitaifa na kijamii ambayo yalichunguza matarajio, mbinu na maswala yanayoathiri maendeleo endelevu katika maendeleo kwa upana zaidi. Mahojiano haya yalijumuisha mashirika 17 na 11 kutoka Ghana na Tanzania mtawalia, na pia wahojiwa kutoka mashirika 11 ambayo yanatoa msaada au kuunga mkono kwa maswala ya michezo katika mipango ya maendeleo katika nchi hizi.

Uchanganuzi ulifanywa katika kiwango cha binafsi na katika makundi na Washikadau wa Kimtandao. Mijadala inayoendelea kati ya Washikadau wote wa Kimtandao na watafiti wasaidzi ilizua matokeo ambayo yalitokana na nyanja mahsusi zinazohitaji maarifa na tajriba na zenye kumakinikia maswala ya utamaduni. Uchanganuzi jumuishi huu ulifanywa kwa kutumia mbinu za kisasa za video kule ambako umbali wa kijiografia haungewezesha watafiti kuwafikia wahojiwa.

Malengo ya Utafiti na Methodolojia

02 Maendeleo Endelevu Michezoni Barani Afrika

Page 3: MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu

Uzingatiaji wa vikwazo katika maswala ya maendeleo ulifuatiwa kwa kuwahusisha watafiti wasaidizi katika ukusanyaji wa data uliofanywa na vyuo vikuu vitatu, vyote kutoka Afrika. Wengi wa watafiti wasaidizi hao walikuwa wamehusishwa awali katika tafiti kuhusu swala la utoaji wa maendeleo endelevu michezoni lakini walikuwa na ujuzi finyu katika utafiti wa aina hii. Kupitia kwa mafunzo na uungaji mkono unaoendelea kwa sasa na unaotolewa na Washikadau wa Kimtandao na hasa tajriba za ukusanyaji data, aina mbalimbali za ujuzi wa utafiti zilitambuliwa. Derrick Charway (Ghana) alibaini ujuzi huo kujumulisha:

“Utafiti huu ulinifanya nikaongeza ujasiri katika utekelezaji wa shughuli kama hizo (kupitia), kusoma mbinu tofauti za ukusanyaji data na mbinu zinazotumika kupenyeza katika majumba ya watu.”

Ufanyaji wa utafiti huu ulisababisha uchunguzi wa kina wa maswala yanayochangia katika ufanisi wa michezo na maendeleo. Kulingana na Mohammed Muvumagu

(Tanzania), ukosefu wa uendelevu uliogunduliwa kupitia kuzuru shule mbalimbali ulikuwa “tofauti kidogo’’ kutoka kwa matarajio yake ya awali na Erick Sena Adjeyi (Ghana) na kwa hivyo kuonyesha haja ya kuwepo kwa mipango ya michezo kwa maendeleo kufungamanishwa na “ufuatilizi wa mara kwa mara, uchunguzi wa maendeleo na mafunzo” ili hali hiyo idumishwe.

Maendeleo ya kibinafsi katika kiwango cha kibinafsi yalishuhudiwa na hivyo basi kuwa muhimu kwa vile watafiti wasaidizi wengi waliendelea kushiriki katika mipango ya michezo kwa minajili ya maendeleo na pia katika masomo yao baada ya kumaliza utafiti huu. Mazungumzo mengine ya tajriba na maendeleo ya kibinafsi ya watafiti wasaidizi yamenukuliwa katika video ya jumla iliyotolewa na utafiti huu.

Tanbihi: Kushiriki kwa watafiti wasaidizi kutoka Tanzania kulifaidika kutokana na msaada wa kuungwa mkono kutoka Shirika la Kimataifa la Michezo na Umotishaji kutoka Uingereza.

Sehemu ya 1: Tajriba za Watafiti wasaidizi kutoka Afrika

Kutokana na uchunguzi wa mashinani na hasa kesi stadi za shuleni, miradi ya maendeleo endelevu katika michezo mara nyingi ilijumuisha utekelezaji wa michezo miongoni mwa vijana pamoja na utoaji wa mafunzo kwa lengo la kuleta uendelevu huu. Ukusanyaji wa data uliofanywa katika mwaka wa kwanza baada ya mafunzo huku mipango ikiendelea ulibaini kuwa miradi hiyo:

• Ilichangia katika ukuzaji wa hadhi ya michezo, maswala ya elimu ya kata na maswala mengine yenye mafungamano na haya shuleni

• Iliunga mkono mafunzo ya walimu ambayo yanawezesha kuwa na ujasiri na kupenda kushirikishwa michezoni

• liwapa motisha walimu kuhusu mbinu za mafunzo hasa kwa kumulika zaidi katika kuwasaidia vijana kuwajibika kwa maswala ya michezo yanayotolewa shuleni

• Iliwezesha vijana kuwa na motisha na uwezo wa kuwaongoza watu hasa miongoni mwa wale waliopata nafasi ya kufunzwa kama viongozi wa vijana

• Iliboresha uwezo wa vijana kufanya kazi na watu wengine na mahusiano yao na walimu

Uchunguzi wa matokeo kama haya ya moja kwa moja katika maendeleo endelevu michezoni ni muhimu katika uzingatiaji wa udumishaji wa baadaye wa michezo na matokeo yake. Maswala makuu yaliyobainishwa ambayo yalichangia au kutochangia umuhimu tuliotaja hapo juu yalikuwa pamoja na:

• Uungwaji mkono kutoka usimamizi wa shule na walimu ambako wazo la kutumia michezo kwa malengo ya maendeleo mapana ilikuwa jipya kwao. Kwa hivyo, kulikuwa

na kiwango fulani cha upya katika utoaji wa mafunzo uliolenga hasa ukuzaji wa uongozi na ujuzi mwingine wa kijamii badala ya kujifunga tu katika maswala ya michezo. Katika hali nyingine, aghalabu ulengaji wa maendeleo kama hayo ulipata uungwaji mkono wa walimu wakuu na walimu wa kawaida.

• Kupata nafasi katika ratiba za shule kwa shughuli za michezo katika maendeleo ingawa upataji nafasi katika ratiba za shule kulitegemea uungwaji mkono wa walimu wakuu pia kulichangia katika mapenzi ya shughuli hiyo miongoni mwa vijana. Kwa kuhisi kuwa juhudi zao zilikuwa zikiungwa mkono na kuthaminiwa, vijana wangeshiriki sana katika uongozaji na ukuzaji wa mradi huu.

• Upatikanaji wa vifaa vya michezo na raslimali tulibainishwa kama elementi muhimu tena ya kimsingi katika udumishaji wa mradi mzima. Japo vijana na walimu walionyesha kupenda shughuli hii, wakati fulani kulikuwa na maoni kuwa ukosefu wa vifaa vya michezo na raslimali nyingine zingekuwa kikwazo.

• Urudiaji wa utoaji mafunzo kwa lengo la kushughulikia walimu wanaoondoka shuleni pamoja na vijana wanaotoka hatua fulani ya maisha hadi nyingine. Kulikuwa na haja ya mafunzo ya ziada kwa walimu waliobaki na vijana kwa lengo la kudumisha motisha wa kupenda mradi huu.

• Kwa upande wa vijana ambao walikuwa wamepewa mafunzo kama viongozi wa vijana, nafasi za kutumia ujuzi wa uongozi zinazoendelea zilikuwa muhimu katika kuhakikisha kwamba vijana wanakuza ujuzi wa aina hiyo na kutuumia baadaye katika hali nyingine za maisha yao.

Maendeleo Endelevu Michezoni: Matokeo kutoka kesi stadi za Mashinani

03 www.durham.ac.uk/sass/research/briefings

Page 4: MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu

Maendeleo Endelevu Michezoni: Matokeo kutoka kwa Mahojiano na Sekta pana za Washikadau

Washikadau wa Kimtandao wakiwa katika maeneo ya mijini na mashinani nchini Ghana, mradi uliweza kushughulikia tatizo la ukosefu wa ulinganishaji wa kijiografia na kimuktadha katika maendeleo enedelevu ya michezo. Maeneo ya mijini na mashinani ya Ghana yanaweza kuelezwa kimtawalia kama yaliyo na yasiyokuwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Japo utamaduni wa maeneo ya mijini ni ya kimchanganyiko, maeneo ya mashinani yana utamaduni mmoja. Upataji wa washiriki wa utafiti mijini ilikuwa kupitia viongozi wa vijana (kama njia kuu) ingawa watafiti walihitaji kuwafikia viongozi wa kijamii na watawala wa jadi katika maeneo ya mashinani.

Matokeo muhimu katika maeneo haya mawili yalikuwa kwamba vijana katika maeneo ya mijini waliona michezo kama shughuli zinazowasaidia kuwa na maadili na sifa

nzuri kama uaminifu, ujasiri-binafsi, ujuzi wa uongozi, upaji uwezo jinsia ya kike na kutoa nafasi kupitia mtandao mkubwa wa watu. Vijana wa mashinani, kando na faida hizo, waliona michezo kama njia za kupata pesa, ajira, kuvunjwa kwa kalautala au dhana hasi za kijinsia na kubakia shuleni kwa wanafunzi hasa wasichana wadogo. Kwa kurejela athari za jumla kwa jamii, wahojiwa wa mijini walisema kuwa mradi huu ulichangia umoja wa kijamii, ukuzaji wa ujuzi wa uongozi na hisia za kuwepo kundini huku jamii ya vijijini ikitaja kuwa athari za michezo ni kama kusuluhisha na kuzuia migogoro, uchangiaji umoja na amani, uboreshaji wa usafi, burudani na maendeleo ya kiuchumi. Kwa ujumla, athari za michezo kama chombo cha maendeleo na amani zilionekana dhahiri katika vijiji vya Ghana.

Sehemu ya pili: Mitazamo kutoka maeneo ya mijini na mashinani ya Ghana

04

Mahojiano na washikadau yalidhihirisha umuhimu mkubwa wa baadhi ya matokeo kutoka kwa tafiti za mashinani. Maendeleo endelevu michezoni mara nyingi ni wazo lililoeleweka kama udumishaji wa shughuli ambazo zilikuwa zikitekelezwa kupitia miradi maalum hapo awali. Utekelezaji huu wa michezo kwa lengo la maendeleo unaoendelea ulihitaji ujumulishaji wa raslimali za kifedha na huduma za kibinadamu. Data kutoka kwa utafiti huu pamoja na mapitio ya tafiti za kimaendeleo zilionyesha changamoto halisi za mwelekeo huu katika maendeleo endelevu michezoni kama ifuatavyo:

• Katika visa vingi, misaada ya kifedha inayotolewa na mashirika ya kimataifa na hata yaliyo katika nchi zilizofanyiwa utafiti ilikuwa ya muda mfupi na kulikuwa na uwezekano mdogo wa mashirika hayo kuendelea kutoa ufadhili. Badala yake, jukumu la kutafuta ufadhili liliachiwa mashirika ya Ghana na Tanzania ambayo yalihitaji ujuzi mahsusi na kujitolea kwa kiwango fulani kulikojikita kwa kipindi cha wakati. Licha ya kuwepo juhudi za kufanya ufadhili kutoka maeneo tofautitofauti, mifano mingi ya miradi iliyosimamishwa au kupunguzwa ilibainishwa.

• Utoaji wa mafunzo ya kukuza uwezo wa kuelewa mradi huu katika nchi husika na vilevile miongoni mwa wenyeji ilikuwa ni shughuli iliyokuwa imeenea sana hata nje ya maeneo yaliyochaguliwa kama kesi stadi. Utumiaji mbaya wa wataalamu waliopewa mafunzo hasa katika ule kama walivyobainishwa katika sehemu iliyotangulia lilibainishwa hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu michezoni lilimaanisha kuwa uzingatiaji wa kukuza uwezo wa kuelewa matatizo ya shughuli nzima ili kuelewa namna ya kuongoza mradi huu ulipewa makini ndogo ilhali hili lilikuwa muhimu katika udumishaji wa mradi huu.

• Mbali na changamoto hizi zilizokuwa wazi, kulikuwepo pia na matatizo mengine hasa ya kuelewa uendelezaji wa mradi huu kwa njia ya kuufanya kuwa mradi wa shughuli nyingine zilizokuwepo mwanzoni. Uelewa huu wa uendelevu ulichukuliwa kama muhimu miongoni mwa washikadau katika mradi wa maendeleo endelevu michezoni (japo kwa njia isiyo ya wazi) japo na chukulizi za ubora wa shughuli zilizokuwepo mwanzoni za kuyafikia matokeo ya kimaendeleo. Huku tathimini ikifanywa pia na watu wengi kama njia ya kutetea mradi huu badala ya kuuendeleza, kulikuwa na watu wachache sana waliouliza maswali, kuhusu “ni nini hasa kinachopaswa kudumishwa” (Walsh et al, 2011, p 2).

Hata hivyo, uwezekano na mifano michache ya mbinu mbadala ya maendeleo endelevu kupitia michezo inaweza kutambuliwa. Ujenzi wa maeneo ya kufanyia michezo yanayokusudiwa kuwafanya watu kujiendeleza kifedha na kusaidia juhudi zingine za maendeleo katika jamii nchini Ghana ulikuwa mojawapo wa mifano. Nchini Tanzania, kuwepo kwa mfumo rasmi wa kuwatambua makocha ungeendelezwa kwa raslimali chache na hivyo basi kuwa na athari ya kudumu. Mifano hii inaakisi michango ya tafiti za kimaendeleo katika mapitio ya maandishi ambayo yanaonyesha kuwa maendeleo endelevu yanaweza kuafikiwa kupitia kwa mbinu jumulishi zinazohusisha uletaji pamoja raslimali mbalimbali na kufungamanisha mabadiliko katika viwango mbalimbali (Mog, 2004). Kulingana na mtazamo huo, mradi wa michezo na uongozi wa vijana ulisababisha kuanza kwa shughuli mbalimbali zikiwemo kuanzishwa kwa vilabu vya mashindano ya michezo na usafishaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Ghana na Tanzania. Kuthamini mambo kama hayo ambayo hayakulengwa kimahsusi lakini ambayo kwa jamii yamethaminiwa na yamedumishwa, ni vyema basi matokeo kutiliwa maanani badala ya kufuata mwongozo fulani mahsusi katika maendeleo endelevu (Walsh et al., 2001).

SASS Research Briefing no. 14

Page 5: MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu

Uundaji wa mbinu bunifu za uenezaji wa utafiti ulikuwa muhimu katika uafikiaji wa malengo ya mradi huu kuweza kuwahusisha washikadau wa mashinani nchini Ghana. Kule Tanzania na kwingineko katika mataifa yaliyoendelea ya Ulaya pia huendeleza kwa njia chanya maswala ya michezo, sera na mapitio ya maandishi. Orodha kamili na ya kisasa ya machapisho na upataji wa njia za kueneza habari zinapatikana katika tovuti; http://bit.ly/sport4devresearchoutputs.

• Washikadau katika mradi huu wamepanga, kuchangia na kuwasilisha makala katika makongamano mengi, warsha na maeneo mengine ya mawasilisho. Nchini Ghana na Tanzania, jumla ya mikutano mitano iliyowahusisha wapangaji wa sera, watekelezaji wa sera hizo na wanaakademia ilipangwa kwa vipindi mbalimbali vya wakati wa mradi. Athari za mojawapo wa mikutano hiyo zimeelezwa katika sehemu ya 3. Warsha ya mwisho iliyoitwa,”Michezo katika Maendeleo: Uangaziaji wa Mustakabali wa Kitaifa na Kimataifa” uliopangwa na Shirika la Usimamizi wa Michezo barani ulaya (EASM) ilikuwa mojawapo wa michango kama hiyo katika makongamano ya kiakademia tokea mwanzo wa mradi.

• Uenezaji habari uliojikita kwenye mitandao na filamu umewezesha kupata habari kuhusu mafunzo na matokeo ya utafiti wa mradi. Katika maendeleo ya mwanzo kabisa, kongamano la EASM lilionyeshwa kwa mtandao kupitia ushirikiano na Ukumbi wa Kimataifa wa Michezo na Maendeleo (ISDP). Video za mawasilisho mengine katika kongamano na yanayopatikana katika mitandao.

• Kwa kipindi cha mradi na baadaye, Washikadau wa Kimtandao walichangia maswala mengi ya kiakedemia na maandishi mengineyo. Muhimu zaidi, kuna sura iitwayo “Beyond Sport for Development and Peace’ katika makala yaliyohaririwa, iliyowezesha Washikadau wa Kimtandao kushughulikia kimahsusi na tajriba katika usomaji kutokana na ushirikiano katika mradi wenyewe. Makala mengi katika majarida yanayohusu Maendeleo Endelevu Michezoni, maendeleo ya jamii kupitia michezo na utawala ya Shirika la Kimataifa la Michezo na Maendeleo yanaandaliwa. Makala haya yameambatana na makala mengine masaidizi yaliyoandikwa kwa lengo la kuhakiksha athari zaidi miongoni mwa wanasera and watekelezaji wa sera hizo.

Ujengaji wa Athari Kupitia Uenezaji wa Habari

Jumla ya wawakilishi 45 wa washikadau kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shirika la Kitaifa la Michezo la Tanzania, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na shule walihudhuria mkutano huu wa washikadau ulioandaliwa katika British Council kule Dar es Salaam, mwezi Juni mwaka 2014. Mawasilisho kutoka kwa madaktari Ndee na Lindsiy yalichangiwa na maoni kutoka kwa watafiti wasaidizi kutoka Tanzania na yakafuatwa na mijadala hai miongoni mwa waliohudhuria. Mshiriki mmoja wa kineji kutoka Kituo cha Vijana cha Buguruni kwa jina Sabrina Nafisa alitoa mwelekeo wake kuhusu mkutano huo kama ifuatavyo:

Kongamano hilo lilikuwa muhimu sana….Natumai kuwa tutaweza kubuni mbinu mwafaka za namna ya kushughulikia changamoto za kudumisha mradi huu kwa muda mrefu kwa mujibu wa utafiti.

Kwa njia nyingine, Dkt. Mwajuma Vudzo (Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo cha Elimu, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam), mkutano ulipongeza hatua yake ya kupongeza

ubunifu wa mradi huu kwa njia ifuatayo: Umoja wa elimu na sayansi ya michezo ( katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) inahusika katika utafiti muhimu wa aina hii….Umejumuisha watafiti wa kiakademia wenye ujuzi na wengine kutoka mashinani na mtandao wa utafiti ni wa kimataifa kwa hakika.

Sehemu ya 3 – Kongamano la Washikadau wa Dar es Salaam

05 Maendeleo Endelevu Michezoni Barani Afrika

Page 6: MAENDELEO ENDELEVU MICHEZONI BARANI AFRIKA...hasa kuwa tatizo kama ilivyokuwa katika mapitio ya mada ya utafiti huu (Mog,2004). Isitoshe, lengo finyu la kusititiza maendeleo endelevu

MarejeleoMog, J.M (2004) Struggling with sustainability – a comparative framework for evaluating sustainable development programs. World Development, 32(12), 2139-2160.

Robinson, J.(2004) Squaring the circle? Some thoughts on the idea of sustainable development. Ecological economics, 48(4), 369-384.

Taylor, B. (2014). Who wants to give forever? Giving meaning to sustainability in development. Journal of International Development, 26(8), 1181-1196.

Wallis, J. and Lambert, J. (2014) Reflections from the field: challenges in managing agendas and expectations In: Schulenkorf , N. and Adair, D. (eds) Global sport-for-development: critical perspectives. Basingstoke: Palgrave Macmillan.

Walsh, A., Mulambia, C., Brugha, R., & Hanefeld, J. (2011). “ The problem is ours, it is not CRAIDS’”. Evaluating sustainability of Community Based Organisations for HIV/AIDS in a rural district in Zambia. Globalization and health, 8 (40)Sehemu ya 3 – Kongamano la Washikadau wa Dar es Salaam

06

School of Applied Social Sciences

ALP

H/0

7/15

/185

www.durham.ac.uk/sass/research/briefings

ContactSchool of Applied social Sciences32 Old ElvetDurhamDH1 [email protected]