mahusiano ya walimu na wazazi katika malezi ya...

14
Utafiti kuhusu Mazingira ya Kazi na Maisha ya Walimu Tafiti Namba 3 3 Mahusiano ya Walimu na Wazazi katika Malezi ya Watoto

Upload: hadan

Post on 21-Apr-2018

471 views

Category:

Documents


16 download

TRANSCRIPT

Utafiti kuhusu Mazingira ya Kazi na Maisha ya Walimu

Tafiti Namba 3

3

Mahusiano ya Walimuna Wazazi katikaMalezi ya Watoto

Covers for All 20/11/04 10:04 Page 5

1

Utangulizi

“… Mwenyekiti wa umoja wa walimu wakuu Dar es Salaam,Mwalimu Mwantumu Mahinza alisema …. Matokeo mazuri yamiaka iliyotangulia hayakutokana na hila zilizokuwa zikifanyika,bali ni utendaji mzuri, uwezo wa wanafunzi na ushirikiano bainaya wazazi na walimu … hali yakuwapa nafasi na uhuru walimuwa kupanga na kujituma pasipo kikomo na ushirikiano wa hali namali kwa wazazi pia vilichangia mafanikio hayo …” na Mwandishiwetu, gazeti la Mtanzania, 17 January 2004 Kichwa cha Habari“Walimu: Hizi ndizo sababu za kushuka kwa elimu Dar”

Mara tu ilipopata uhuru, Tanzania iliweka mikakati ya kufuta ujinga, umasikini namaradhi. Ili kuchochea kasi ya maendeleo, walimu walipewa nafasi muhimu sana katikamaendeleo ya taifa letu. Pamoja na umuhimu wao, mchango wa walimu umekuwahawatambuliwi katika jamii. Walimu wamekuwa wakiishi na kufanya kazi katikamazingira magumu sana. Nyumba za kuishi zenye hadhi duni kabisa, ufinyu wamishahara yao, kutopewa maslahi yao stahiki kisheria kama vile malipo ya uhamishona likizo, na hata posho nyingine mbali mbali.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya walimu ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi yawanafunzi waliopo mashuleni. Hali hii imekuwa inawaongezea walimu mzigo mzito wakazi ya ufundishaji, ufuatiliaji na uratibu wa maendeleo ya wanafunzi. Hali inazidi kuwambaya karibu kila mwaka kutokana na mwamko uliojitokeza miongoni mwa wazazi,hususani baada ya kuanzishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi(MMEM) nchini ambapo idadi ya wanafunzi waliosajiliwa darasa la kwanza mwaka2002 na 2003 imeongezeka maradufu kwa zaidi ya asilimia 500% wakati idadi yawalimu imeogezeka kwa kiwango kidogo tu.Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 1997,uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ulikuwa 1:37 wastani wa taifa, ambapo kufikiamwaka 2002, uwiano ulikuwa kwa 1:53 wastani wa taifa, japo katika sehemu nyingihususan mijini wastani uko juu zaidi ya 1:87 (Ripoti ya Tathmini ya MMEM, 2003).

Pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na walimu katika kukabiliana na mabadiliko hayo,bado wanakosa ushirikiano wa dhati kutoka kwa baadhi ya wazazi. Hali hii imedidimizamotisha kwa walimu katika kuleta mabadiliko ndani ya shule na kijiji kwa ujumla.

Mahusiano na Wazazi

MAHUSIANO YA WALIMUNA WAZAZI KATIKAMALEZI YA WATOTO

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na HakiElimu, wamefanya utafitikuanzia Septemba 2003 hadi Desemba 2003 juu ya maisha na mazingira ya kazi yawalimu katika wilaya saba nchini ili kuweza kupata mawazo na mtazamo ya walimu juuya hali ya maisha na kazi ya ualimu. Matokeo ya utafiti huo, yanalenga kuchangia katikamijadala mbali mbali ya serikali juu ya kuboresha hali ya walimu kwa lengo la kuinuakiwango cha ubora wa elimu inayotolewa nchini. Utafiti umekusanya takwimu zamahojiano yaliyohusisha watu 298, dodoso 1385 na ‘case study’ 10 katika wilaya saba,wilaya moja katika kila kanda ya Elimu yaani kanda ya kati, kanda ya nyanda za juukusini, kanda ya kaskazini, kanda ya kusini, kanda ya mashariki, kanda ya ziwa na kandaya magharibi.

Utafiti huu uliangalia nyanja mbali mbali zinazoweza kuchangia kuboresha aukudidimiza hali ya maisha na kazi ya walimu. Hii ilikuwa ni pamoja na: Mzigo wa kaziya ufundishaji, uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu mmoja, maendeleo ya walimukitaalamu, athari za UKIMWI katika kufundisha na kujifunza, maisha ya walimu pamojana maslahi ya walimu. Taarifa ifuatayo inachambua matokeo ya ‘case study’yaliyopatikana katika nyanja ihusuyo:

“Mahusiano ya Walimu na Wazazi katika maendeleo ya Elimu.”

Utafiti umeongozwa na Prof. Suleman Sumra na Prof. Verdiana Grace Masanja waHakiElimu ambapo Mr. Anthony Mtavangu wa CWT ameshughulikia maswala yote yakiutawala kwa upande wa CWT. Watafiti ni Edward Masanja na Mwalimu Finesta Savai(Ilala), Amina Mnenge na Mwalimu Shaibu Mohamedi (Lindi), Francis Mkwawa naMwalimu Isidory Mwangeni (Ludewa), Kemirembe L. Mukyanuzi na Mwalimu CeciliaTzahaki (Moshi Mjini), Shaaban Mtengeti na Mwalimu Abel P. Mwangalyagila Manyoni,Lembris Laanyuni na Mwalimu Oswald Rulatunya (Kibondo) na Dorothy Karoli naMwalimu Mafuni Yango (Mwanza). ‘Case Study’ hii imeandikwa na Bwana Peter Khalidna imehaririwa na Prof.Verdiana Grace Masanja.

Matokeo ya Utafiti

Uhusiano mzuri kati ya wazazi na walimu huimarisha na kujenga maendeleo mazuri yakazi za walimu na kuifanya kuwa rahisi zaidi. Kuwepo na mahusiano mazuri, hupelekeamwalimu kujiamini na kuwa na uhakika wa kila anachokifanya kwa kujua anaungwamkono na wazazi. Lakini iwapo uhusiano unakuwa si mzuri, mwalimu huishi kwawasiwasi na kutokujiamini katika kila jambo analofanya, haswa lile litakalohitajikuungwa mkono na wazazi.

Mahusiano na Wazazi2

3

“Jamii huwaona walimu ni waonezi”

Nafasi ya wazazi katika kuimarisha nidhamu ya wanafunzi ni kubwa sana. Shule inahitajisana ushirikiano mzuri kati yake na wazazi katika nyanja zote zinazohusukuwafundisha maadili mema watoto. Kumekuwepo na ushirikiano mdogo katika shulenyingi, na hii inatokana na muonekano wa jamii kuwa walimu ni waonezi, hupendakuwaadhibu watoto bila sababu, na wana chuki kutokana na kutopewa maslahi yakutosha.

Walimu walisema kuwa wao ni kama walezi na wanakuwa na jukumu kubwa lakuwalea watoto katika maadili mema yatakayowajenga. Lakini wamekuwa na wakatimgumu sana kwa kutokuwepo kwa ushirikiano wa wazazi katika kuangalia taratibu zakuwarekebisha watoto wao. Kwenye baadhi ya shule walimu walisema, iwapomwanafunzi anafanya makosa mara nyingi wanakuwa na taratibu wanazofuata ikiwemokumshirikisha mzazi mwenyewe ili aweze kujua kinachoendelea na kushiriki katikakutoa maamuzi.

Walisema, hatua ya kwanza ni kikao maalum cha walimu ambao huzungumzia matatizoya mwanafunzi husika na kuorodhesha matatizo yake yote, baadaye huitwa nakuelezwa utovu wake wa nidhamu na kuonywa. Iwapo mwanafunzi huyo ataendeleakutokuwa na nidhamu inayoridhisha, au kuendelea kuvunja taratibu za shule, ndipomzazi hushirikishwa kwa kuitwa kwenye kikao kingine na kuelezwa matatizo ambayowalimu wamekuwa wanayapata dhidi ya mtoto wake.Wote kwa pamoja hukubalianaaina ya adhabu ya kumpa mtoto wake kama hatua ya kumkumbusha wajibu wake.

Mahusiano na Wazazi

Walimu waliohojiwa wamesema ya kuwa wakati mwingine wanapata matatizo nakukwaruzana na wazazi pale wanapotoa adhabu kwa watoto. Walisema adhabu kwamwanafunzi ni sehemu ya kumkumbusha wajibu wake na sio kumuumiza.Walisema yakuwa wazazi waliojiingiza katika vyama vya siasa wao kila kitu huona sio haki na maranyingi wamekuwa hawataki watoto wao waonywe wala kuadhibiwa hata kamawametenda kosa. “Wamekuwa wanatuona sisi walimu kama tumewekwa na chamakilichopo madarakani, kitu ambacho si sahihi”.

Pamoja na kutumika kwa adhabu, bado walimu walisema isitumike kupita kiasi. Iwe tuni sehemu ya kutoa onyo na sio sehemu ya kukomoa mwanafunzi.Walisema ya kuwaikitumika vibaya inaweza kuleta madhara kwa mwanafunzi kama vile kuleta usugu nahivyo kumfanya awe jeuri zaidi, kusababisha nidhamu ya woga miongoni mwawanafunzi na hata kuleta athari kisaikolojia.

Adhabu ndogo kama hizi ni sehemu ya mafunzo kwa mtoto na mazoezi ya mwili.

“Walimu wapenda maendeleo huwa ni maadui wa wazazi”

Pamoja na kuwepo kwa juhudi nyingi miongoni mwa walimu, ilibainishwa kuwa wapowazazi ambao hawapendi walimu wapenda maendeleo. Mwalimu akiwa na juhudi zakuleta mabadiliko ya elimu katika shule yake anakuwa adui wa baadhi ya wazazi.Akitoa mfano Mwalimu Fidel Nderego (43) wa Shule ya Msingi Kabare, wilaya yaKibondo, anasema kuwa alijitahidi kuweza kubadili sura ya shule ya Kabare kuanziamazingira yake kwa kuhamasisha jamii na kuweza kupata majengo mazuri ikiwemonyumba za walimu za matofali na kuezekwa kwa bati. Pamoja na juhudi zake, amekuwa

Mahusiano na Wazazi4

5

anakutana na vitisho juu ya maisha yake kama alivyosema:

“Kitu ambacho kinanisikitisha ni mapambano ya kushughulika, nimekutana navikwazo vingi sana toka kwa wananchi wapinga maendeleo. Niliandikiwa baruazenye vitisho. Nilitishiwa kuwa nyumba yangu itachomwa na nimekuwanaviziwa njiani na kupigwa na mawe bila sababu, na watu hao sijawafahamuhadi leo.”

Akichangia juu ya mahusiano ya wazazi na walimu, Mwalimu Pancracia Mtawali (48)Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Magereza iliyopo Manispaa ya Moshi alisema, kutokanana kuwa na hadhi ya chini kwa walimu, wamekuwa wanadharaulika haswa na wazaziambao wamejaliwa kuwa na uwezo kidogo. Alisema ya kuwa tofauti hii inasababishakuwepo na pengo kubwa kati ya wazazi na walimu na hata miongoni mwa wanafunziwenyewe.Akielezea alisema;

“Inakuwa ni vigumu sana kuwazoea wazazi kwani wengi wanaonekanakutowathamini walimu. Niliwahi kukwaruzana na wazazi kwa sababu unakutamzazi anakuwa upande wa mtoto wake mara zote hata kama mtoto huyoanakosa. Unajua wazazi wengi ni matajiri. Uwezo huo walionao ndio unaowapakiburi. Iwapo mwalimu akimbana mwanafunzi mzazi anakuja juu na kutuonasisi walimu ni dhiki tu inatusumbua. Hii ni kutokana na uduni wa maisha tuliyonayo sisi walimu.”

Akiongezea juu ya matatizo aliyowahi kuyapata alisema kuwa, aliwahi kutoa adhabu yaviboko mbele ya wazazi kwa wanafunzi ambao walivunja sheria za shule kwa kupiganadarasani, pamoja na kuwashirikisha wazazi alijikuta yupo polisi.

“Wanafunzi wawili wa kiume walipigana hadi wakavunja madawati darasanimwao. Sikuwaadhibu kwanza niliwaelezea juu ya kosa lao na kuwa wamevunjasheria ya shule. Kila mmoja alitoa maelezo yake kisha nikachukua hatua yakuwaita wazazi wao. Wazazi waliitikia wito na kufika shuleni. Tukakubalianakuwa waadhibiwe kwa kuchapwa viboko ili kuwarudi. Mimi kama mkuu washule nilipewa jukumu la kutoa adhabu hiyo niliwachapa mbele ya wazazi waona kila mzazi alionekana kuridhishwa na uamuzi tuliouchukua pamoja. Kitucha ajabu ni pale nilipoitwa polisi kwa ajili ya kujibu shitaka la kumchapamwanafunzi baada ya mmoja wa wazazi kwenda kunishtaki. Kwa kweli nilipatamshituko kwani maamuzi tuliyachukua kwa pamoja halafu iweje anizungukena kunishtaki? Baada ya kutoa maelezo polisi ilionekana nilitimiza wajibu kamailivyotakiwa na kwa matakwa ya wazazi wenyewe. Kwa bahati nzuri hatukufikambali sana kwani baadaye tulisuluhusishwa. Sasa hali kama hii mimi kamabinadamu nitajisikiaje?”

Mahusiano na Wazazi

“Wazazi huvua jukumu la kudhibiti utoro wa watoto wao”.

Wakielezea zaidi walimu walisema katika shule zenye tatizo la utoro, mara nyingiwazazi hujivua jukumu la kumdhibiti mtoto wao na kuona kuwa mwenye wajibu wakuona kama mtoto anaenda shule ni mwalimu. Lakini ukiangalia kwa undani wotewawili wanatakiwa kushirikiana katika hilo. Akielezea zaidi juu ya majukumu ya wazazikatika maendeleo ya watoto wao, Mwalimu Hamisi Mapila (36) Mwalimu Mkuu waShule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo katika wilaya ya Lindi alikuwa na haya ya kusema:

“Jamii yenyewe haitambui sana umuhimu wa shule. Kwani wakati mwinginemtoto anaweza akachaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakiniwazazi wanasema hawana uwezo wa kumlipia kwa madai ya hali ngumu yauchumi, lakini kinakuwa ni kisingizio tu. Pia kwa watoto watoro shuleni, baadhiya wazazi huchangia kwani hawasaidii katika kukemea hilo. Watoto watoromara nyingi huwa nje ya darasa kwa siku nzima na hata zaidi na wazazihawajali.Wakati mwingine watoto hao wanakuwa katika biashara ndogondogokatika maeneo ya kituo cha basi.”

“Mazingira ya shule ilipo yanaathari kiutendaji”.

Aidha sehemu shule zilipo imeonekana kuwa ni tatizo na kikwazo kikubwa kwawalimu. Wakitolea mfano, wamesema shule ambazo zimo ndani ya taasisi hasa zile zakijeshi inatumika amri zaidi toka kwa wazazi kuliko majadiliano. Akitoa mfanoMwalimu Mwangilika Festo (35) anayefundisha Shule ya Msingi Magereza iliyopoManispaa ya Moshi ndani ya maeneo ya Jeshi la Magereza alisema

Mahusiano na Wazazi6

7

“Kutokana na eneo shule hii ilipo ndani ya gereza kumekuwepo na ugumusana katika kazi yetu. Kuna kutumia nguvu zaidi kuliko majadiliano. Mtotoakiadhibiwa hapa mzazi hukimbilia polisi haraka, labda kwa ajili ya uhusianouliopo. Hali hii inatufanya walimu tuwe waangalifu sana na matokeo yake nikushuka kwa vyote, nidhamu ya wanafunzi na maendeleo ya kitaaluma.”

Akizungumzia juu ya ushirikiano wa wazazi na walimu, Mratibu Elimu Kata, MwalimuAlex Mpombwe wa kata ya Nkonko iliyopo katika wilaya ya Manyoni, amesemamatatizo yakutokuwepo kuelewana kati ya walimu na wazazi yanatokana na utovu wanidhamu wa wanafunzi unaochangiwa na wazazi wenyewe.

Matokeo yake wanafunzi wanajenga chuki na walimu, inafikia hatua ya wanafunzikuwasingizia walimu wao kwa wazazi kwani wanajua kuwa wazazi wao watawasaidia.Na mara nyingi wazazi wamekuwa wanachukua maamuzi kwa jazba na kuwatolealugha chafu sana walimu.

Sasa sijui wazazi wanafikiri wanamjengea msingi gani mtoto wao? Aliuliza Mwalimu Alex.Akitolea mfano binafsi, Mwalimu Alex alisema kuwa alishawahi kusingiziwa na mwanafunzikuwa ni mbakaji wakati huo alipokuwa akifundisha.

“Misukosuko waipatayo walimu huathiri maendeleo ya watoto”

Wazazi wanasahau kuwa misukosuko ambayo wanawasababishia walimu huwa naathari kwa watoto wao pia. Mwalimu Gaudensia M. Shada (30) ni Mwalimu MkuuMsaidizi katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo Wilaya ya Lindi, shule ambayoamekuwa akifanya kazi tangu apate ajira mwaka 1996 mwezi wa 8. Mkasa uliomkumbayeye kutokana na kusingiziwa na mzazi ulileta usumbufu mkubwa hata kwa wanafunzipia.

Mwalimu Shada ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi na pia mwalimu wa nidhamu kwawanafunzi, mwezi Machi 2003 akiwa ofisini aliletewa taarifa kuwa wanafunzi wawili wakike wa darasa la sita (tutawaita Somoye na Bella lakini si majina yao halisi) walikuwawakipigana darasani, alichukua hatua ya kwenda darasani. Aliwakuta Somoye na Bellawakipigana, mara walipomuona walitahayari kwa kuwa walijua kuwa ni kosa kupiganashuleni.

Kwa kuwa kupigana shuleni ni kinyume na sheria za shule hivyo hao wanafunziwalistahili kupata adhabu.

Mahusiano na Wazazi

“Niliwaita hao wanafunzi wawili waliokuwa wakipigana, na kuwaonya mbele yawanafunzi wenzao darasani. Kwa sababu walifanya kosa kinyume cha sheriaza shule walistahili adhabu, hivyo niliwachapa fimbo mbili mbili mikononi kilammoja. Adhabu kama hii ni ya kawaida hapa shuleni na hasa kwa makosakama haya, na wakati mwingine hata wazazi wanaweza kuitwa kuthibitishautovu wa nidhamu wa watoto wao na watoto huadhibiwa mbele ya wazaziwenyewe. Adhabu hii ilishuhudiwa na wanafunzi wa darasa la sita, kwaniilitolewa mbele yao na Somoye na Bella walionekana kujutia tendo lao lakupigana baada ya adhabu hiyo.”

Katika hali isiyo ya kawaida, adhabu ndogo aliyoitoa Mwalimu Shada, ilibadili maishayake na hata mtazamo aliokuwa nao juu ya utendaji kazi ya ualimu. Hali hii imemfanyakuathirika kisaikolojia, na kukata tamaa hata kuona kuwa maisha yake yapo hatarini.Akielezea kwa undani juu ya tukio kubwa lililomtokea ambalo limepelekea hali hiyo,mwalimu Shada alikuwa na haya ya kusema:

“Nikiwa shuleni nililetewa taarifa ya Polisi ya kutakiwa kufika kituoni kutoamaelezo ya kumjeruhi mwanafunzi Bella. Nilishtuka sana kwani sikutarajiakuwa itafikia hatua hiyo. Niliongozana na mwalimu mkuu, ambaye tayarialikuwa na taarifa ya kuadhibiwa kwa wanafunzi hao wawili.Tulipofika kituoni,nilielezea kwa kusaidiana na Mwalimu Mkuu tukio zima jinsi lilivyotokea nahatua zilizochukuliwa. Baada ya melezo hayo Polisi iliridhika na maelezo yanguna kuona nilikuwa natimiza wajibu kama ilivyostahili. Hivyo walichukua jukumula kutusuluhisha na mzazi wa Bella. Walijaribu kumueleza kuwa hayo nimambo ya kawaida shuleni. Walimuelimisha mzazi kuwa sisi walimu pia niwazazi na walezi hivyo hatuwezi kumuadhibu mtoto kwa lengo la kumuumiza,bali kumrekebisha ili afuate maadili mema. Na walitoa ushauri wa kuitishakikao cha kamati ya shule ili mzazi aitwe kuelezwa zaidi hali ile na penginekutafuta muafaka baina yangu na mzazi. Lakini bado mzazi hakuridhika nauamuzi huo, kwani alitarajia mimi niwekwe ndani. Mwalimu Mkuu ilibidianiwekee dhamana ili nisiwekwe mahabusu.

Mwalimu mkuu alifuata ushauri aliopewa Polisi na aliitisha kikao cha dharuracha Kamati ya shule na mzazi wa Bella alipelekewa taarifa ya kuhudhuriakikao hicho. Wanakamati waliitikia wito huo mara moja, walihudhuria kikaohicho, lakini mzazi wake Bella hakuhudhuria kabisa.Taarifa zilizopatikanabaadaye zilisema kuwa mzazi wa Bella hakuhudhuria kikao hicho kwa sababueti yeye hawezi kusuluhishwa na Kamati ya shule, na wala Kamati hiyo hainamamlaka yoyote juu yake. Kamati iliamua kumuacha mzazi afanye kileanachotaka.”

Mahusiano na Wazazi8

9

Lakini kwa upande wa wazazi wa Somoye, kuadhibiwa kwa mtoto wao waliona nikitendo sahihi kama hatua ya kumfundisha mtoto. Hawakuchukua hatua kama za mzaziwa Bella, bali walimuonya mtoto wao na kumtaka kuwa mtiifu kwa walimu wake nakufuata kanuni na sheria za shule.

Mzazi wa Bella baada ya kukataa suluhisho la polisi na kugoma kuhudhuria kikao chakamati ya shule alichukua uamuzi wa kufungua kesi ya madai katika mahakama yawilaya ya Lindi. Ili aweze kutimiza lengo alilolikusudia, alizunguka katika hospitalimbalimbali ili aweze kupatiwa cheti kitakachothibitisha kuwa mtoto wake ameumizwasana na pia amepata athari katika ubongo wake.

“Hawa walimu wamezoea tu kutuendesha, mwaka huu lazima niwafunge tu hata kamani kuuza mifungo yangu yote. Nitafunga mmoja mmoja hadi waishe, sababu nitakuwanazitafuta”

Alienda katika hospitali ya misheni ya Nyangao na hospitali ya mkoa, Sokoine ambakoaliomba mtoto wake apigwe picha ya mionzi (X-ray). Bahati mbaya au nzuri, hospitalizote matokeo yalionyesha kuwa mtoto hajaathirika sehemu yoyote zaidi yakuonekana na malaria. Mzazi wa Bella hakufurahia matokeo hayo, hivyo aliendeleakuwashawishi madaktari kuwa mtoto wake alipoteza fahamu baada ya kupewa adhabuna mwalimu, na kuwa ameathirika kichwani. Lakini daktari anayehusika na magonjwaya akili alithibitisha kuwa mtoto ni mzima kabisa wala hajawahi pata athari yoyotekichwani.

Mwalimu Shada pamoja na Mwalimu Mkuu, waliitwa mahakamani kujibu shitaka lakumjeruhi mwanafunzi.

Akiendelea kuelezea mwalimu Shada alisema:

“Nilihudhuria mahakamani pamoja na mwalimu mkuu ili kutoa utetezi wangu.Tulijieleza kwa kina juu ya tukio zima na taratibu zilizochukuliwa. Mahakamaikaamua kuita mashahidi ili kuthibitisha maelezo yetu na ya mzazianayenishitaki. Mashahidi walioitwa ni pamoja na Bella mwenyewe, Somoye nawanafunzi wa darasa la sita waliokuwepo siku ya tukio.

Wakati wa ushahidi ilionyesha wazi kuwa Bella alifundishwa maneno yakusema na mzazi wake, kwani alisema kuwa alichapwa na gongo kubwa sanaambalo lililetwa mahakamani kama ushahidi, na aliumizwa sana na kupotezafahamu. Alielezea kuwa mzazi wake alifika shuleni kumbeba baada ya kuwaamepoteza fahamu na kumrudisha nyumbani.

Kwa upande mwingine, wazazi wa mwenziwe, Somoye, walimuonya mtoto waojuu ya kusema uongo hata kama mzazi wa Bella atamtishia kwa hali yoyote

Mahusiano na Wazazi

ile. Hivyo alipotoa ushahidi wake alielezea kwa ufasaha kila kitu jinsikilivyotokea na hatua nilizozichukua dhidi yao wote wawili. Maelezo ya Bellayaliendana kabisa na ya wanafunzi wengine wa darasa la sita walipoitwa kutoaushahidi wao na pia yalifanana labisa na yangu. Mashahidi walidhibitisha kuwamaelezo ya Bella ni ya uongo, na kuwa hakuumizwa popote pale na piawaliondoka naye kurudi nyumbani akiwa anatembea mwenyewe.”

Kwa upande mwingine, mama yake Bella hakutaka kabisa kujihusisha na suala hili tanguawali. Kwani yeye alikiona kitendo kile kuwa ni sawa, na ni sehemu ya kumuadabishamtoto. Katika hatua zote hizo, hakuwahi kufika polisi na hata mahakamani. Hata palemahakama ilipotaka kujua kuhusu mama, baba alijibu kuwa yeye ndio anayeshughulikiasuala hilo kwa niaba ya familia. Labda alijua kuwa mama yake Bella ataweza kupinganana maelezo yake na ya mtoto wake.

Kesi hii ilichukua takribani miezi mitano hadi kutolewa kwa hukumu yake. Katikakipindi chote cha kuendesha kesi hii, Mwalimu Shada hakuwa akifundisha kwa uhuruna wakati wote alikuwa na wasiwasi sana juu ya usalama wa maisha yake na familiayake. Kwani mzazi wa Bella alikuwa akipita kijijini akijitapa kuwa lazima angelifanyalolote ikiwa ni pamoja na kumfunga gerezani au hata kumdhuru kwa namna yoyote.Akielezea juu ya muendelezo wa kesi na hukumu iliyotolewa Mwalimu Shada alisema:

“Uongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) ulinisaidia katika utoaji wahukumu. Kwani waliitafuta sheria ya adhabu kwa wanafunzi mashuleni yamwaka 1979 na kuileta mahakamani kama ushahidi wa hatua niliyoichukuailikuwa ndani ya sheria za nchi.

Kwa kutumia ushahidi uliotolewa na wanafunzi waliokuwa mashahidi na yangumwenyewe na uthibitisho wa matokeo ya vipimo vya hospitali na wa sheria yaelimu kuhusu adhabu kwa wanafunzi shuleni, mnamo tarehe 14 Julai 2003,mahakama iliniona sina kesi ya kujibu na hivyo kuniachia huru. Mahakamailimshauri mzazi wa Bella iwapo hakuridhika na hukumu hiyo, anaruhusiwakukataa rufaa kwenye mahakama ya juu zaidi. Hajafanya hivyo hadi leo, baliameendelea kunitishia maisha na kuwa atanitesa kwa namna nyingine yoyoteile.”

Wafanyakazi wenzake ikiwemo walimu wa shule mbalimbali ndani ya kata yake,viongozi wa elimu wilayani na viongozi wa Chama cha Walimu, walikuwa wakimfarijisana tangu kesi hiyo ilipoanza. Lakini alielezea kuwa msaada wao ulikuwa ni wamaneno ya faraja tu. Kwani mwenendo mzima wa kesi umemgharimu pesa nyingi,kwani alikuwa na jukumu la kuwasafirisha wanafunzi ambao walikuwa ndio mashahidiwake, pia kuhakikisha kuwa wanapata chakula wanapokuwa mahakamani. Kwanimakao makuu ya wilaya ambako kesi ilikokuwa inasikilizwa ni umbali wa kilometa 24toka hapo shuleni. Gharama zote hizo alikuwa anazitoa mfukoni mwake, si msaada

Mahusiano na Wazazi10

11

wowote toka kwa walimu wenzake, si chama cha walimu na wala muajiri wakealiyechangia angalau sehemu ndogo sana ya gharama katika kesi hii.

“Kesi hii imeniathiri sana kisaikolojia. Kwani nilikuwa natimiza wajibu wangukama mwalimu wa nidhamu, pili nilikuwa ndio mwalimu mkuu kwa wakati huo,kwani mwalimu mkuu alikuwa nje ya kituo, na tatu nilikuwa ni mwalimu wakike ambaye kisheria ndiye ninayetakiwa kuwaadhibu watoto wa kike. Badalaya wazazi kutambua wajibu wangu wananiadhibu kwa kunipelekamahakamani, hivi haki iko wapi?

Nilijaribu kuomba uhamisho ili nirudi nyumbani kwetu. Lakini nilipata farajatoka kwa maafisa elimu wilayani kuwa hiyo ni misukosuko ya kawaida kazini.Pia namshukuru mume wangu kwani alinipatia msaada mkubwa sana kipindichote cha kesi, ingawaje na yeye alikuwa tayari kulipiza kisasi. Tatizo kubwatunalolipata katika eneo hili sisi walimu, ni kwamba unapokuwa mchapa kazisana basi huchukiwa sana na wazazi kwa madai kuwa unawasumbua watotowao, na hii ni kero kubwa kwa shule. Lakini wale walimu ambao ni walevi,hupendwa sana na kuonekana ni wenzao.”

Kwa kipindi chote cha miezi mitano ya ufuatiliaji wa kesi hii, wanafunzi wamekuwawakiathirika pia. Mwalimu Shada amekuwa akifuatilia kesi yake, na hivyo kutohudhuriamadarasa, wanafunzi waliokuwa wanatoa ushahidi nao pia wamekuwa hawahudhuriimadarasa. Aidha walimu waliokuwa wanampa faraja Mwalimu Shada walikuwawanahudhuria mahakamani ili kuweza kuonyesha mshikamano na kutaka kujua hatimaya mwenzao na hivyo wanafunzi wa madarasa mengine nao walikosa masomo.

Akitoa maoni yake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mnazi Mmoja Mwalimu Hamisi Mapila(36) alisisitiza umuhimu wa kujua sheria na kanuni mbalimbali za sekta ya elimu.Alisema kutokujua sheria kunaweza kuwa na madhara makubwa katika utendaji wakazi za walimu. Akitoa mfano alisema, kama si msaada wa CWT kuleta sheria yaadhabu kwa wanafunzi mahakamani kama ushahidi labda Mwalimu Shadaangelionekana ametenda kosa, au kesi ingelichukua muda mrefu zaidi. Aidha MwalimuMapila alikitaka Chama cha Walimu kuwasaidia walimu ambao ndio wanachama wake,kwa namna yoyote ile kama kutoa pesa pale zinapohitajika au kuwatafutia wanasheriapale wanapopata kesi kama hizo za kiutendaji kwani wao huchangia chama hicho.

“Mwalimu Shada alikuwa anatakiwa kuwalipia wanafunzi nauli kilaanapokwenda mahakamani, ilifikia hatua aliishiwa kabisa. Lakini ilikuwa nibahati kuwa mume wake ni mfanyabiashara hivyo alisaidia katika hilo. Sasa siwote wenye uwezo kama huo. Hali kama hii inaonyesha wazi kuwa kama sihivyo, Mwalimu Shada angelishindwa kujitokeza katika kesi hiyo na madharayake wote tunayafahamu.”Alisema Mwalimu Mapila.

Mahusiano na Wazazi

Kwa upande mwingine walimu walitoa chagamoto kwa serikali hususani Wizara yaElimu, kuhakikisha kuwa wanajenga misingi mizuri ya mawasiliano kati ya wizara nashule.Walisema kuwa hawana muongozo ulio wazi na hivyo inawaweka mahali pabayakiutendaji kazi.Walisisitiza kutaarifiwa mabadiliko yoyote yanayotokea katika sekta yaelimu, na kusambaziwa machapisho yote ya sekta hii ili kuwaweka katika nafasi nzuriya kuelewa taratibu zilizopo.Aidha walisema kwa kauli moja kuwa, wao wataendeleakutimiza wajibu wao kama inavyopaswa na kufuata sheria na taratibu za nchi, na hatakama mtoto Bella atavunja tena taratibu za shule ataadhibiwa tu kufuata sheria, kamani viboko atachapwa. Kinyume na hapo labda mzazi wake amuhamishe katika shulenyingine ambayo anaona hatoweza kuadhibiwa iwapo atavunja sheria za shule.

Hivi sasa mtoto Bella hana amani wala furaha tena awapo shuleni. Kwani wanafunziwenzake wamekuwa wakimsumbua na kumuona kama mtu hatari na muongomkubwa.Wamekuwa wakimuambia kuwa baba yake alitaka kusababisha mwalimu waoafungwe, na wamekuwa wakimuuliza, je wangelipata faida gani?

Ilibainika kuwa mzazi wa Bella hakuwa na sababu za msingi za kufungua kesi ile, balialikuwa anajaribu kuchochea uhasama baina ya walimu na wazazi. Pia alikuwa anatafutanjia za kujikosha kwani alikuwa anakabiliwa na shutuma nyingi za kutowatendea hakiwatoto wake. Ilibainishwa kuwa huyu mzazi amewahi kumkosesha mtoto wakekuendelea na masomo ya sekondari kwa kutomlipia ada ndogo inayotakiwa katikashule za serikali pamoja na kuwa na uwezo wa kulipia. Matokeo yake huyo mtoto hivisasa yupo tu nyumbani pasipo shughuli yoyote.

Aidha ilibainishwa kuwa mzazi huyu hana historia nzuri ya kuishi kwa amani nawanakijiji wenziwe. Amekuwa ni mtu wa matatizo na mzushi wa mitafaruku mingikatika jamii. Hali hii inaweza ikawa na athari kwa wazazi wengine wenye mitazamokama yake na hivyo kujenga mizizi ya uhasama kati ya wazazi na walimu katikautekelezaji wa majukumu na taratibu zinazotakiwa.

Ushirikiano kati ya shule na wazazi ni wa muhimu sana katika kujenga misingi bora yamaendeleo kwa watoto.Walimu kama walezi hukaa na watoto kwa muda mrefu zaidipengine kuzidi hata wazazi wenyewe. Iwapo wazazi watatilia mkazo yale maadili nanidhamu wanayofundishwa mashuleni ni wazi kuwa watajenga jamii yenye nidhamu nakuheshimika. Muungano mzuri wa wazazi na walimu umeweza kukuza maendeleo yashule kitaaluma miongoni mwa shule zilizo na ushirikiano wa karibu na wazazi.Zile zenye wazazi wenye mtazamo tofauti zimekuwa zikilegalega nyuma kwa miakamingi.

Mahusiano na Wazazi12

Dhira

Dhira ya HakiElimu ni kuiona Tanzania ikiwa mahali ambapo watoto wanafurahia haki ya kupata elimu bora ya msingi,

pale ambapo shule zinaheshimu utu na haki za binadamu wote,na pale ambapo elimu inakuza usawa, ubunifu, udadisi na demokrasia

Dhamira

HakiElimu inafanya kazi kufikia usawa, ubora, haki za binadamu na demokrasia katika elimu kwakuwezesha jamii kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera za elimu,

kuchochea mijadala yenye ubunifu na kuleta mabadiliko,kufanya utafiti yakinifu, kudadisi, uchambuzi na utetezi na

kushirikiana na wadau kuendeleza manufaa ya pamoja na haki za jamii

HakiElimu TafitiPO Box 79401 • Dar es Salaam • Tanzania

Tel. (255 22) 2151852 / 3 • Fax (255 22) 2152449 [email protected] • www.hakielimu.org

HakiElimu

Covers for All 20/11/04 10:04 Page 6