uchambuzi wa bajeti ya serikali 2016/17

Upload: zitto-kabwe

Post on 02-Mar-2018

458 views

Category:

Documents


4 download

TRANSCRIPT

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    1/26

    UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (Mb)

    Kiongozi wa Chama

    12 Juni 2016

    Dar es Salaam

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    2/26

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    3/26

    01. Utangulizi

    Serikali ya Awamu ya Tano imewasilisha Bungeni Bajeti yake ya kwanza tangu

    iingie madarakani. Bajeti hii inapaswa kutafsiri maono, malengo, shabaha

    na ahadi kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikitolewa tangu wakatiwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katika uchambuzi wetu huu mfupi

    tutatazama kama Serikali, kupitia Bajeti yake ya kwanza, imeweza kuweka

    fedha kwenye maneno yake.

    Serikali imependekeza kutumia jumla ya shilingi 29.5 trilioni ambapo kati ya

    hizo shilingi 17.7 ni za matumizi ya kawaida na shilingi 11.8 ni za matumizi ya

    Maendeleo. Hata hivyo uwezo wa Serikali kukusanya mapato yake ya ndani(Mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi na mapato ya Halmashauri) na

    misaada kutoka nje ni shilingi 22.1 trilioni tu. Hivyo nakisi ya Bajeti

    ni shilingi 7.4 trilioni sawa na asilimia 4.5 ya Pato la Taifa. Nakisi hii ya Bajeti

    itazibwa kwa mikopo ya ndani na nje ya Nchi ambapo Serikali itakopa jumla

    ya shilingi 7.4 trilioni ili kuziba nakisi hiyo ya Bajeti.

    Serikali imependekeza kufanya marekebisho kadhaa kwenye kodi mbalimbaliili kuweza kufikia malengo ya makusanyo ya kodi. Tutachambua baadhi ya

    mapendekezo hayo na kuonyesha kama yatakidhi haja na kuwezesha kufikia

    malengo husika.

    Chama cha ACT Wazalendo kinafanya mapitio ya Bajeti ya

    Serikali kwa lengo la kuainisha maeneo ambayo tunaamini Serikali

    inafanya vizuri na maeneo ambayo yanahitaji kuangaliwa upya

    na tunatoa mapendekezo mbadala. Tumeanza utaratibu mwaka

    huu na utakuwa endelevu kila mwaka.

    01UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    4/26

    02. Dhana na misingi ya Bajeti ya Serikali

    Bajeti ya serikali ndiyo tafsiri ya matamko ya kisera yanayotolewa na viongozi

    wa serikali katika nyakati mbalimbali. Ni kupitia bajeti ambapo serikali huja-ribu kutekeleza kwa vitendo ahadi zake mbalimbali. Aidha, bajeti ni nyenzo

    muhimu kwa chama kilichoshinda uchaguzi kutafsiri ilani yake kwa vitendo.

    Bajeti hujengwa katika misingi mikuu mitatu.

    Mosi:bajeti ya serikali huanisha vyanzo vya mapato ya serikali, ikiwemo kodi

    inayokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali.

    Pili:Bajeti ya serikali huanishi maeneo ambayo serikali inakwenda kutumia

    makusanyo ya fedha. Matumizi haya hugawanywa katika makundi mawili:

    matumizi maendeleo na matumizi ya kawaida.

    Tatu:Bajeti ya serikali hutoa dira ya maendeleo ya nchi kwa kipindi cha mwaka

    mmoja wa fedha na miaka mingi ijayo. Katika uchambuzi huu tunaangalia

    maeneo ambayo serikali inakwenda kukusanya na kutumia mapato yake nakwa kiasi gani maeneo haya yanajibu changamoto za nchi kwa sasa na muda

    mrefu ujao.

    UTU. UZALENDO. UADILIFU02

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    5/26

    03. Taswira halisi ya Bajeti ya Mwaka 2016/2017

    Katika mwaka wa fedha wa2015/2016,Serikali ilipanga kukusanya na

    kutumiaShilingi 22.5 trilioni.Kama tulivyoona kwenye utangulizi, Serikali

    ya Awamu ya Tano imepanga kukusanya na kutumia shilingi 29.5 trilionikatika mwaka wake wa kwanza (2016/2017).

    Ndiyo kusema Bajeti ya Mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 31

    ukilinganisha na Bajeti ya Mwaka jana. Hata hivyo, tangu Bajeti ya

    mwaka jana thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani

    imeporomoka kwa takribani asilimia 10. Kwa kuwa manunuzi yetu mengi

    hasa kwenye miradi ya Maendeleo (ununuzi wa ndege, ujenzi wa Reli,mikataba ya wakandarasi wa barabara nk ) hufanywa kwa fedha za

    kigeni hususan dola ya Marekani, thamani halisi ya Bajeti itakuwa

    imeongezeka kwa asilimia 21.

    Aidha, mfumuko wa bei umeongezeka kwa takribani asilimia 5 kutoka

    mwaka 2015/16. Ndiyo kusema uwezo wa kimanunuzi wa Bajeti ya mwaka

    huu ni pungufu kwa uwezo wa Bajeti ya mwaka jana kwa asilimia 5. Hivyobasi, ongezeko halisi la Bajeti ya mwaka huu ni takribani asilmia 16.Hata

    hivyo tunaipongeza serikali kwa ongezeko hili, pamoja na kwamba, kama

    tutakavyoonyesha, na kama ambavyo wachumi mbalimbali wamekwisha-

    oonyesha, utekelezaji wake unatia shaka.

    03UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    6/26

    04. Bajeti inajibu Changamoto za Nchi?Changamoto kubwa ya nchi yetu hivi sasa ni ukosefu wa Ajira kwa maelfu

    ya Vijana wanaomaliza masomo na kuingia kwenye soko la Ajira. Ili kujibu

    changamoto hii hatuna budi kutazama sera za kibajeti kwenye maeneo

    yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira nyingi na kuona kama maamuzi yakibajeti yanapeleka rasilimali kwenye maeneo hayo.

    Sekta yenye kuajiri Watanzania wengi kwa sasa ni sekta kubwa ya Uchumi wa

    Vijijini (Kilimo, Mifugo na Uvuvi)ambapo kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya

    Uchumi ya mwaka 2015 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango tarehe 8

    Juni 2016, asilimia 65 ya Watanzania wanajihusisha na ajira vijijini. Ajira katika

    sekta rasmi ni 2.1 milioni chini ya 10% ya Watanzania wote wenye uwezo wakufanya kazi 22.3 milioni.

    Katika ajira rasmi sekta inayoongoza ni Viwanda kwa kuchangia asilimia 20

    ya ajira zote rasmi ikifuatiwa na Elimu 17% na Ulinzi na Utawala asilimia 15.

    Mchanganuo huu unaonyesha kuwa Watanzania wengi (zaidi ya theluthi

    mbili) wanaishi nje ya mfumo rasmi na hivyo juhudi kubwa inapaswa

    kuwekwa kwenye Uchumi wa Vijijini ili kuboresha maisha yao na kuongezaajira rasmi huko huko vijijini.

    Bajeti ya mwaka 2016/17 inajibu changamoto hii? Ili kujibu swali hili kwa

    uhakika inabidi kutazama kwa ufupi hali ya sekta ya Kilimo (inayojumuisha

    na Mazao, Misitu Ufugaji, Uvuvi nk) na kuona kama rasilimali za kutosha

    zimeelekezwa kuikwamua sekta hiyo. Kiwango cha ukuaji wa shughuli za kilimo

    umeporomoka mpaka asilimia 2.3 mwaka 2015. Sababu kubwa imeelezwa nitija ndogo, teknolojia duni, ukosefu wa masoko na uhaba wa viwanda vya

    kusindika mazao ya kilimo (agroprocessing industries).

    Kwa sisi wachumi tunatambua kuwa ili kupunguza umasikini wa Tanzania

    kwa zaidi ya nusu ilihitajika sekta ya Kilimo kukua kwa kati ya asilimia 8 na

    10 kwa mwaka. Kwa ukuaji huu tulionao sasa, maana yake itachukua miaka

    mingi sana watanzania kuondoka kwenye dimbwi la umasikini. Baadhi yamazao yanayotarajiwa kuzalisha malighafi za viwanda uzalishaji wake

    umeporomoka kwa kiwango cha kutisha.

    UTU. UZALENDO. UADILIFU04

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    7/26

    Kwa mfano Zao la Pamba, uzalishaji na mauzo ya nje ya zao hili yameshuka

    kwa asilimia 45 kwa mujibu wa Taarifa ya hali ya Uchumi iliyosomwa na

    Serikali bungeni tarehe 8 Juni 2016.

    Hata hivyo, katika Bajeti yote ya Maendeleo ya Tshs 11.8 trilioni, ni shilingi100 bilioni tu zimetengwa kwa ajili ya sekta ya Kilimo sawa na asilimia 1

    ya Bajeti nzima ya Maendeleo. Ni dhahiri kwamba ili kujenga uchumi

    shirikishi ni muhimu kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha kwamba

    kilimo kinaanza kuchangia vya kutosha katika kasi ya ukuaji wa Uchumi.

    Kwa Uchumi wa Tanzania, ujenzi wa Sekta ya Viwanda hauwezi kufanikiwa

    bila kukua kwa sekta ya kilimo. Kilimo ndio sekta Kiongozi katika kutokomezaumasikini kwani inachangia theluthi moja ya Pato la Taifa na kuajiri theluthi

    mbili ya Watanzania wote. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano

    imeshindwa kufungamanisha Sekta ya Kilimo na ndoto ya maendeleo ya

    Viwanda. Ushahidi wa kisayansi unaotokana na Taarifa za Serikali yenyewe

    unaonyesha kuwa hakuna mahusiano kati ya mipango ya maendeleo ya

    viwanda na mipango ya maendeleo ya wananchi.

    Maeneo mengine ambayo yanaweza kuzalisha ajira za kutosha ni Sekta ya

    Utalii ambayo kwa kiasi kikubwa inazalisha ajira kwenye sekta za usafirishaji,

    malazi na huduma za vyakula. Sekta ya Utalii ililiingizia Taifa Mapato ya kigeni ya

    Dola za Kimarekani 2.3 bilioni. Ikumbukwe kuwa kila Mtalii anayeingia nchini

    anatarajiwa kula, kulala na kusafiri na yote hayo ni huduma zinazotolewa na

    Watanzania wanaoajiriwa kwenye mahoteli na magari ya Watalii.

    Hata hivyo Serikali katika hotuba yake ya kwanza kabisa ya Bajeti imeamua

    kurudisha nyuma juhudi zote za kukuza Sekta ya Utalii kwa kuanzisha kodi

    ya VAT kwenye huduma zote za Utalii. Kodi hii itaifanya Tanzania kuwa ghali

    kuliko washindani wake kama Kenya ambayo imeifuta kodi hii na kuongeza

    Bajeti ya kutangaza Utalii. Utalii ndio sekta inayoongoza kwa kuingiza

    mapato mengi ya fedha za kigeni na kawaida inapaswa kuangaliwa

    kama sekta ya nje (export sector). Sekta za nje hazina kodi ya Ongezeko laThamani yaani VAT lakini cha kushangaza ni kwamba Serikali imeweka kodi

    hii kwa sekta ya Utalii.

    05UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    8/26

    Vile vile maamuzi ya Serikali kubana matumizi kwa kufanya mikutano yake

    kwenye majengo ya Serikali yatapelekea mahoteli mengi nchini kufunga

    shughuli zao na kuachisha kazi mamia ya Watanzania wanaofanya kazi

    kwenye mahoteli hayo. Hatua hii itakosesha Serikali mapato yatonayo na

    Kodi na PAYE ambayo hulipwa na Wafanyakazi.

    Kwa Ujumla Bajeti ya mwaka 2016/17 haitaweza kutatua kero ya ajira

    nchini na badala yake itapelekea Watanzania wengi zaidi kukosa ajira kwa

    waajiri kupunguza wafanyakazi ili kubana matumizi. Tumeanza kusikia

    waajiri mbalimbali wakipunguza wafanyakazi. Hali itakuwa mbaya zaidi

    kwa wenye mahoteli na miji kama Arusha itaumia zaidi kwani inategemea

    sana Biashara ya Utalii. Kuanguka kwa sekta ya Utalii ni kuanguka kwauchumi wa nchi kwa ujumla.

    UTU. UZALENDO. UADILIFU06

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    9/26

    05. Viwanda Vitajengwa?Kauli mbiu ya Bajeti ya mwaka 2016/17 ni kuongeza uzalishaji viwandani ili

    kupanua fursa za ajira. Kama tulivyoainisha hapo juu, Viwanda vinachangia

    asilimia 20 ya ajira zote rasmi nchini na kwamba thuluthi mbili ya Watanzania

    wameajirwa na sekta isiyo rasmi. Hivyo juhudi za kuongeza uzalishaji viwandanini muhimu sana ili kuwaondoa Watanzania wengi kutoka sekta isiyo rasmi na

    kuwaingiza kwenye sekta rasmi. Ili kupima nia hii ya Serikali inabidi kutazama

    hatua mbalimbali za kisera kuwezesha sekta binafsi kufungua viwanda vingi

    zaidi nchini na kuajiri watu wengi.

    Moja ni jambo la kupongeza sanakwamba Bajeti ya mwaka 2016/17 imelenga

    kuondoa changamoto ya miundombinu kwa kiwango kikubwa sana. Wenyeviwanda wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kutokuwepo kwa

    umeme wa uhakika, gharama kubwa za usafirishaji wa malighafi na

    bidhaa na mawasiliano ya intaneti yasiyo na kasi ya kutosha. Katika

    Bajeti ya mwaka 2016/17 Serikali imeelekeza rasilimali nyingi sana kujibu

    changamoto hizo. Kwa mfano, Bajeti za Miundombinu ya Usafirishaji na

    Umeme zimechukua asilimia 53 ya Bajeti yote ya Maendeleo. Jumla ya

    shilingi 6.2 trilioni ya Bajeti imetengwa kwa ajili ya miradi ya miundom-binu na umeme. Huu ni mwelekeo mzuri katika kujibu changamoto hizo.

    Hata hivyo inawezekana kabisa kuwa uwekezaji kwenye Viwanda ukakumbwa

    na changamoto ya soko maana katika Bajeti ya Mwaka huu Serikali imebana

    matumizi na hivyo watu hawatakuwa na fedha za kutumia kununua bidhaa

    na huduma. Miundombinu inaweza kujengwa lakini ikawa haina watu

    wa kuitumia wala bidhaa za kusafirisha kwa sababu hakuna vivutio vyakuanzisha viwanda pia. Ikumbukwe kuwa Serikali haianzishi viwanda bali

    inajenga mazingira mazuri ya wawekezaji kuanzisha viwanda. Bajeti ya

    mwaka 2016/17 haijaweka hivyo vivutio vya kaunzisha viwanda na ime-

    minya uwezo wa walaji kutumia kwa kudhibiti matumizi na pia kutoza

    kodi nyingi zinazopunguza uwezo wa kutumia bidhaa na huduma.

    Ni vema kukumbusha kuwa kasi ya ukuaji wa shughuli za uzalishaji viwandani nindogo kwa kiwango cha asilimia 6.5 na mchango wake katika Pato la Taifa

    ni mdogo sana, wa asilimia 5.2 tu.

    07UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    10/26

    Serikali ilipaswa kuja na Sera mahususi za kufikisha asilimia 10 au zaidi ukuaji

    wa uzalishaji viwandani. Hii maana yake ni kwamba matamshi mengi kuhusu

    viwanda hayaendani na hali halisi ya viwanda nchini. Serikali haina budi ku-

    kaa na wenye viwanda na kupata mwafaka wa namna bora ya kuweka sera

    mahususi zitazopelekea uwekezaji mkubwa wa wenye mitaji katika viwandana kuongeza uzalishaji. Vinginevyo, ahadi za Serikali hazitaweza kutekelezwa

    kwa wakati. Vile vile viwanda vitahitaji muda mpaka kuanza uzalishaji, hivyo

    juhudi kubwa ilipaswa kuwekwa kwenye uzalishaji wa malighafi za viwanda

    ili wakati viwanda vinaanza kazi vikutane na malighafi.

    5.1 Mapendekezo

    Katika sekta hizi tatu nyeti kwa uchumi wa Tanzania, Chama cha ACT Wazalendotunapendekeza hatua zifuatazo kuchukuliwa

    Serikali itunge mfumo wa kodi unaoeleweka na usiotetereka (stable

    fiscal regime) kwa sekta ya kilimo ili kumwezesha mkulima kubakia na

    sehemu kubwa ya mapato yake na kuvutia wananchi wengi kujishu-

    ghulisha na uzalishaji katika kilimo.

    Serikali iharakishe kuanza kufanya kazi kwa soko la bidhaa (commoditiesexchange) ili kupuguza watu wa kati katika sekta ya Kilimo

    Serikali ianzishe mfumo wa hifadhi ya jamiikwa wakulima kwa kuanzisha

    pia Fao la Bei ili kuhakikisha kuwa mkulima anarudisha gharama zake za

    uzalishaji pindi bei katika soko zinapoterereka.

    Serikali ifute kodi zote za mazao (produce cess) na kuondoa vizuizi vya

    aina yeyote ile ili kuhakikisha mkulima anauza bidhaa zake anapotaka

    mwenyewe.Serikali ifanye maamuzi ya kisera ili kuhakikisha kuwa Viwanda vya ku-

    ongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi (agroprocessing

    industries) vinapewa vivutio vya kikodi.

    Serikali iweke utaratibu kurahisisha taratibu za kufungua viwanda na

    kuweka mfumo wa kisheria wa kufidia baadhi ya gharama za uzalishaji

    kwa viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotumiwa na wananchi wengi

    zaidiSerikali iondoe msururu wa kodi katika sekta ya Utalii ikiwemo

    kuondoa kabisa wazo la kuweka VATkwenye huduma za Utalii katika

    UTU. UZALENDO. UADILIFU08

    I.

    II.

    III.

    IV.

    V.

    VI.

    VII.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    11/26

    Bajeti ya 2016/17

    Serikali itunge mfumo rahisi wa kikodi katika sekta ya utalii kwani ni

    sekta inayoweza kuajiri vijana wengi sana na kupunguza kwa kiwango

    kikubwa tatizo la ajira nchini.

    06. Bajeti ina maana gani kwa Wananchi?Tunapotazama maana ya Bajeti kwa wananchi hatuna budi kuangalia mam-

    bo ya msingi kama bei za bidhaa za huduma. Iwapo shilingi 1000 aliyonayo

    mwananchi leo itanunua bidhaa nyingi zaidi kuanzia Mwezi Julai mwaka

    2016, tutasema hali ya maisha ya mwananchi imeboreka. Iwapo shilingi

    1000 aliyonayo mwananchi leo itanunua bidhaa chache zaidi kuanzia mwaka

    mpya wa fedha tutasema hali ya wananchi imeporomoka.

    Serikali imepandisha kodi mbalimbali kwenye bidhaa zinazoagizwa

    kutoka nje na ushuru wa bidhaa mbalimbali. Hii itapelekea bei ya bid-

    haa na huduma kupanda na kusababisha mfumuko wa bei tofauti na

    malengo ya Serikali. Serikali inatarajia mfumuko wa bei kuwa katika

    tarakimu moja. Hata hivyo uchumi wetu unategemea sana uchumi wa

    dunia kwa sababu tunaagiza zaidi ya uwezo wetu wa kuuza nje. Bei ya

    Mafuta katika soko la dunia imeanza kupanda taratibu na sasa imefikia

    $50 kwa pipa moja kutoka chini ya $30. Uzalishaji wa kilimo umeku-

    wa hauridhishi kwani chakula ni sehemu kubwa ya mfumuko wa bei

    (huchangia takribani asilimia 52 ya kapu la bidhaa na huduma). Kuna

    mwelekeo mkubwa kwamba mfumuko wa bei utaongezeka mpaka

    kwenye taratimu mbili na hivyo kupelekea hali za wananchi kuwa mbaya.

    Kodi za miamala ya kutuma fedha kwenye mabenki au simu za mkononi

    inabidi zitazamwe upya ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya

    kuwaingiza wananchi wengi katika mfumo wa kibenki yanafanikiwa.

    Serikali imeamua kubana matumizi kwenye baadhi ya maeneo, ni jam-

    bo jema sana. Hata hivyo uamuzi huo utaendana na biashara nyingi

    kufungwa na watu wengi kupoteza ajira na kuingia mtaani. Hii inaweza

    kuongeza ugumu maisha kwa wananchi wengi wa kawaida.

    09UTU. UZALENDO. UADILIFU

    VIII.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    12/26

    Serikali inabidi kuaianisha hatua inazochukua na madhara yake katika

    kuhakikisha jamii inabaki salama. Ni vizuri Serikali ikatazama ni maeneo

    gani ambayo matumizi yake yanachochea ukuaji wa sekta binafsi na

    kuyaachia badala ya kubana na kukumbatia fedha zote. Madhara yake

    ni kwamba uchumi hautapata multiplier effect na hivyo kuendeleakudumaa badala ya kukua mpaka kufikia tarakimu mbili.

    Kwa ujumla, Bajeti ya mwaka 2016/17 itapelekea maisha ya mwananchi

    wa kawaida kuwa magumu zaidi kwa sababu gharama za maisha

    zitapanda na kipato kupungua. Sera za Bajeti zimeshindwa kutazama

    Bajeti kama Sera (policy instrument) na badala yake imekuwa nyenzo

    tu ya kukusanya mapato na kuyatumia.

    07. Mambo ya Kushangaza katika Bajeti 2016/17Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya Tano imeshindwa kutoka na jambo

    kubwa la kisera ambalo lingeamsha ari ya wananchi ya kufanya kazi na kujenga

    Taifa lao. Jambo kubwa la kushangaza ni kwamba Bajeti hii ni ya kawaida

    mno na haina tofauti kubwa na Bajeti zilizopita. Tofauti na matamko makali

    makali ya Serikali kabla ya Bajeti, kimsingi Bajeti hii inathibitisha kauli

    kwamba watawala ni wale wale na inaonyesha kuwa Utawala wa Awamu

    ya 5 utachoka mapema sana kabla hata kazi haijaanza. Hii inathibitishwa

    na ukweli kwamba hakuna ubunifu katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

    Yafuatayo ni mambo ambayo yanashangaza katika Bajeti ya mwaka 2016/17

    Serikali imeamua kupandisha nakisi ya Bajeti mpaka 4.5% ya Pato la

    Taifa na kuziba nakisi hiyo kwa kukopa kutoka ndani na nje. Mwaka

    2016/17 Serikali itakopa shilingi 7.5 trilioni ambapo kati ya hizo mikopo

    ya masharti ya kibiashara itakuwa shilingi 2.1 trilioni. Mikopo ya ndani

    itapelekea Serikali kugombania vyanzo hivyo na wafanyabishara wa

    ndani na kupelekea wafanyabiashara kupata tabu kubwa kupata fedha

    za kuendesha biashara (crowd out effect). Mikopo ya nje nayo itaongeza

    gharama za kuhudumia Deni la Taifa ambapo hivi sasa nusu ya mapato

    yote ya Serikali itakwenda kulipa madeni (Wakati Mapato yote ya Ndani

    ya Serikali ni shilingi 17.7 trilioni, mwaka Huu Serikali italipa madeni

    UTU. UZALENDO. UADILIFU10

    i.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    13/26

    shilingi 8 trilioni). Hata hivyo, Serikali haina uhakika wa kupata mikopo

    hii kwa sababu inategemea na jamii ya kimataifa ya mabenki yao yan-

    aonaje Serikali yetu. Mwaka 2015/16 Serikali ilipanga kukopa shilingi

    2.1 trilioni na ikaambulia shilingi 1.1 trilioni tu. Kwa namna Serikali ya

    awamu ya tano inavyohusiana na mataifa ya nje na hatua mbalimbaliza kuonekana kuvunja mikataba ya kibiashara na kampuni za uwekez-

    aji za nje, inawezekana Serikali isipate hata theluthi ya mikopo hii ku-

    toka nje. Jambo la kushangaza ni kwamba matamko ya Viongozi wa

    Serikali yalionyesha kuwa Tanzania haitahitaji misaada kutoka nje lakini

    Bajeti kwa kiwango kikubwa inategemea fedha kutoka nje (Misaada na

    Mikopo shilingi 3.6 trilioni na mikopo ya kibishara kutoka nje shilingi

    2.1 trilioni kufanya jumla ya shilingi 5.7 trilioni).

    Serikali inategemea kukusanya shilingi 17.8 trilioni kutokana na kodi na

    mapato yasiyo ya kikodi. Hata hivyo, Serikali inatarajia kutumia shilingi

    8 trilioni kulipia deni la Taifa na shilingi 6.6 trilioni kulipia mishahara ya

    wafanyakazi. Jumla ya Matumizi haya shilingi 14.6 trilioni sawa na

    asilimia 82 ya mapato yote ya Serikali. Hii maana yake ni kwamba

    katika kila shilingi 100 ambayo Serikali inakusanya, shilingi 82 zinalipiadeni na mishahara na hivyo Serikali kubakia na shilingi 18 tu kwa ajili

    ya matumizi mengineyo na matumizi ya maendeleo. Uamuzi wa Seri-

    kali kutenga shilingi 11.82 trilioni kwa ajili ya Maendeleo unategemea

    misaada ya wafadhili na mikopo ya ndani na nje jambo ambalo Seri-

    kali haijawaambia wananchi kwani inajua ni jambo gumu kutekelezeka.

    Kutenga asilimia 40 ya Bajeti kwenye maendeleo ni jambo jema lakini ni

    siasa zaidi kuliko uhalisia kwani hakuna fedha za uhakika kwenye Bajetikuweza kulipia miradi hiyo ya maendeleo.

    Serikali imeamua kutoza kodi ya asilimia5 kwenye Kiinua Mgongo cha

    Wabunge wanapomaliza miaka yao mitano. Kwanza, ni jambo jema

    sana kuwa Serikali inataka kuwaweka wabunge sawa na wafanyakazi

    wengine wowote ambao kiinua mgongo hutozwa kodi. Hata hivyo

    jambo la kushangaza ni kwamba kodi hii haina nyongeza yeyote yamapato katika mwaka wa fedha 2016/17. Chama cha ACT Wazalendo

    tulitarajia Serikali ama kufuta posho za vikao katika mfumo mzima wa

    11UTU. UZALENDO. UADILIFU

    ii.

    iii.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    14/26

    utumishi wa umma au kutoza kodi posho hizi angalau kwa kiwango cha

    kodi zuio ya asilimia 10. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba Mapato

    ya Viongozi wakuu wa Serikali kama Rais, Makamu wa Rais nk hayapo

    wazi na hayatozwi kodi yeyote ile. Serikali ingeanza kwa kutoza kodi

    mishahara ya viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Rais ili kuonyeshamfano wa uzalendo kwa wananchi.

    Serikali imeamua kushusha kiwango cha chini cha kodi ya mapato

    (PAYE) kutoka asilimia 11 mpaka asilimia 9. Nafuu anayopata mfanyaka-

    zi ni tshs 3800 tu. Jambo la kushangaza ni kwamba Serikali imebakiza

    kiwango cha kutozwa kodi kuwa kile kile cha zaidi ya shilingi 170,000.

    Tulitaraji kuwa kipato cha chini ya shilingi 360,000 kisingetozwa kodina kiwango cha juu kingeongezwa mpaka kufikia zaidi ya shilingi 15

    milioni. Rais mara kwa mara amekuwa akizungumza kuhusu dhamira

    ya kupunguza malipo makubwa wanayopata watu (wanaoishi kama

    malaika kuwashusha waishi kama mashetani). Serikali inapaswa ku-

    rekebisha tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasio nacho kwa

    kupitia sera za kodi. Tulitarajia Serikali ingetumia Bajeti yake ya kwanza

    kurekebisha tofauti hizo. Chama cha ACT Wazalendo kinapendekezamfumo mbadala wa kodi ya Mapato katika majumuisho ya mada hii

    (Angalia kiambatanisho namba 1).

    Serikali haikugusia mabadiliko ya mfumo wa kodi kwa kampuni za

    kimataifa zinazowekeza nchini (Multinational Corporations). Jambo la

    kushangaza ni kwamba Serikali imeshiriki katika mkutano wa kimataifa

    wa rushwa uliofanyika nchini Uingereza ambapo ajenda yake kubwailikuwa kuzuia makampuni makubwa kukwepa kodi katika nchi wa-

    nazozalisha faida. Serikali ya awamu ya tano imeshindwa kabisa kuja

    na sera za kibajeti kuzuia ukwepaji huu mkubwa wa kodi ambao kwa

    hapa Tanzania ni zaidi ya asilimia 5 ya Pato la Taifa (yaani zaidi ya nakisi

    ya Bajeti ya mwaka huu).

    UTU. UZALENDO. UADILIFU12

    iv.

    v.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    15/26

    ACT Wazalendo ingefanya nini katika mwaka wake wa Kwanza?

    Chama cha ACT Wazalendo kinapendekeza mabadiliko makubwa ya mfumo

    wa kodi kufanyika ikiwemo kuwa na mtazamo kuwa Kodi sio tu ni sera ya

    mapato bali ni sera ya kuchochea ukuaji uchumi wa sekta teule. Bajeti ya

    kwanza ya Serikali ya awamu ya Tano haipelekei kujenga Tanzania ambayohakuna unyonyaji wala kujenga Uchumi Imara, shirikishi na unaosimamiwa na

    Dola. Serikali ya awamu ya tano inaendeleza vikundi vya kinyonyaji (cartels)

    ama kwa kuziimarisha cartels zilizopo au kujenga vicartel vipya kwa faida za

    watawala. Kwa mfano, Serikali imeshindwa kuvunja vikundi maslahi kwenye

    sekta ya Sukari na bidhaa zingine zinazoagizwa kutoka nje ikiwemo mafuta

    ya kula na mchele licha ya kelele ambazo zimepelekea bei ya sukari kupanda

    maradufu na kuwapa wananchi ugumu wa maisha. Wakulima wa mpunganchini hivi sasa wanapata ushindani mkubwa kutoka mchele unaotoka nje ya

    nchi kama Vietnam na Pakistani na hivyo kupelekea bei ya wakulima kuporo-

    moka na kushindwa kulipa mikopo waliyochukua kuendesha kilimo.

    Tunapendekeza Wabunge wazingatie masuala machache yafuatayo kwenye

    mjadala wa Bajeti na hatimaye kuweza kuifanya Serikali kuepuka madeni

    makubwa inayokwenda kuchukua na kuanza kujitegemea.

    Katika sheria ya Fedha ya mwaka 2016, kuwe na kifungu cha Sheria

    kinachoweka ukomo wa misamaha ya kodi mpaka asilimia 1 ya Pato

    la Taifa. Misamaha ikaguliwe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu

    za Serikali, na misamaha yenyewe na taarifa ya ukaguzi viwekwe wazi

    kwa umma. Mfumo ambao Serikali imependekeza sasa unaweza kuwa

    na madhara makubwa sana kwa kuongeza urasimu na hasa ukizinga-tia kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania haina utamaduni wa kurudisha

    fedha (tax refunds). Uamuzi wa kutunga sheria tunayopendekeza un-

    aweza kuwezesha Serikali kukusanya shilingi trilioni 1.8 ya kodi.

    Serikali irekebishe sheria ya Kodi ya Mapato na kuweka vifungu vina-

    vyohakikisha kuwa kila Mtanzania anajaza Tax Returns kila mwaka. Hii

    itawezesha kila Mtanzania kuwa na wajibu wa kujaza fomu inayoonye-sha kipato chake na TRA kutambua walipa kodi. Rais aongoze hili kwa

    kujaza Tax Returns kila mwaka na kuweka wazi. Fomu zaweza kutolewa

    13UTU. UZALENDO. UADILIFU

    I.

    II.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    16/26

    kupitia mfumo wa Serikali za Mitaa kwa Watendaji wa Mitaa na Vijiji.

    Serikali ifanye marekebisho ya sheria mbalimbali za kodi zinazohusisha

    makampuni ya kimataifa (MNCs) ili kuzuia kumomonyoa wigo wa kodi

    (Base Erosion and Profit Shifting) kunakofanywa na kampuni hizi. Hililinawezekana kwa Serikali kuchukua hatua ya kupitia mikataba ya kiko-

    di (double taxation treaties) ambayo Tanzania iliingia na nchi nyingine

    duniani. Tafiti mbalimbali katika eneo hili zinaonyesha kuwa Tanzania

    hupoteza asilimia 5 ya Pato la Taifa kutokana na vitendo vya kampuni

    kubwa kukwepa kodi kwa kutumia mbinu za kihasibu (tax planning

    measures). Iwapo Serikali ikichukua hatua kwenye eneo hili haitahitaji

    kukopa kabisa shilingi 7.5 trilioni inazopanga kukopa mwaka 2016/17,ama itakopa kidogo sana kwa sababu hatua hizi zitaingiza fedha nyingi

    kwa mara moja.

    Kodi za Majengo ziendelee kukusanywa na Mamlaka za Serikali za Mi-

    taa kwa kuziwezesha kuwa na mfumo wa kielektroniki wa kukusanya

    kodi hizi kupitia kwa Watendaji wa Mitaa. Mamlaka ya Mapato Tanzania

    haina uwezo wala nyenzo za kukusanya kodi hii kwa ufanisi.

    Michango ya Hifadhi ya Jamii ishushwe mpaka asilimia 14 kwa Waajiri

    kuchangia asilimia 7 na Waajiriwa kuchangia asilimia 7 ya mishahara

    yao. Hii itasaidia kupunguza gharama za kuajiri kwa Waajiri. Tozo ya

    SDL ishushwe mpaka asilimia 3 pia. Eneo hili ni muhimu liangaliwe kwa

    muktadha wa kukuza ajira nchini hivyo ajira zinapoongezeka mapato

    kwenye maeneo haya yanaongezeka pia.

    Fedha za uwezeshaji wananchi ( 50m kila kijiji) zitumike kujenga mfumo

    wa hifadhi ya jamii wa taifa kwa kuchangia nusu ya michango ya wa-

    nanchi watakaokuwa tayari kuingia kwenye hifadhi ya jamii kupitia vi-

    kundi vya uzalishaji mali. Hii itawezesha wananchi wengi kuwa na bima

    ya afya na usimamizi wa mikopo kwneye vikundi kuwa mkubwa maana

    utatokana na mfumo wa hifadhi ya jamii badala ya mpango ulivyo hivisasa. Kuna hatari kubwa ya fedha hizi kutumika vibaya kwa kuzigawa

    kwa watu watakaozichezea tu kama ilivyokuwa kwa mabilioni ya JK.

    UTU. UZALENDO. UADILIFU14

    III.

    IV.

    V.

    VI.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    17/2615UTU. UZALENDO. UADILIFU

    Msamaha wa kodi kwenye maduka ya Majeshi na Taasisi za Dini ien-

    delee kama ilivyo sasa kwani misamaha hii ni chini ya asilimia 1 ya misa-

    maha yote inayotolewa nchini. Taasisi za Dini zinatoa huduma nyingi

    kwa jamii hasa maeneo ambayo Serikali imeshindwa kutoa huduma

    kama vile Elimu, Afya nk. Kuwapa posho wanajeshi ili wanunue bidhaakunaweza kuwaweka wanajeshi katika hatari ya kununua bidhaa zisizo

    na ubora na hata kuwaweka kwenye hatari ya kudhuriwa. Vikosi vyetu

    vya ulinzi na usalama havipewi misamaha kwa ajili ya mapato tu bali ni

    kwa ajili ya kuimarisha usalama na ustawi wao kijamii.

    Pendekezo la kodi ya VAT kwa huduma za utalii liondolewe ili Tanzania

    iendelee kuwa shindani kwenye sekta ya utalii.

    Pendekezo la kodi kwenye karatasi kutoka nje litazamwe upya kwani

    litaongeza gharama za uzalishaji wa vitabu nchini. Tanzania haina vi-

    wanda vya karatasi vya kulinda ukiachana na Mgololo ambacho kara-

    tasi zake hazitumiki hapa nchini kwa kiasi kikubwa.

    Pendekezo la tozo kwenye miamala ya simu za mkononi na ile ya kiben-ki iondolewe ili kuhakikisha Watanzania wanaendelea kutumia mifumo

    ya kifedha ya nchi.

    VII.

    VIII.

    IX.

    X.

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    18/26

    08. HitimishoTanzania isiyo na unyonyaji na yenye uchumi shirikishi unaozalisha ajira ny-

    ingi haitajengwa kwa Bajeti ya mwaka mmoja. Hata hivyo ni muhimu juhudi

    zianze kuonekana katika hatua za mwanzo kabisa.

    Serikali ya awamu ya Tano ina maono ya kujenga Tanzania ya Viwanda. Hata

    hivyo, Bajeti yake ya kwanza kabisa imeshindwa kuonyesha sera mahususi

    ambazo zinaweza kupelekea watu wenye mitaji kuleta mitaji yao Tanzania

    na kujenga viwanda. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya Tano imekosa

    ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato na sera zitakazopelekea nchi yetu ku-

    songa mbele kiuchumi. Maamuzi ya kibajeti yaliyotangazwa na Serikali ku-

    pitia kwa Waziri wa Fedha na Mipango hayana mvuto unaoonyesha nia yakujenga uchumi wa viwanda.

    Chama cha ACT Wazalendo kimejaribu kuonyesha mapungufu kadhaa yali-

    yomo kwenye mfumo wa Bajeti ya mwaka 2016/17 na kutoa mapendekezo ya

    namna ya kuboresha. Ni dhahiri kuwa mwaka unaoanzia Julai 2016 utakuwa

    ni mwaka mgumu sana kwa Watanzania wa kawaida kwani Bajeti haijawapa

    unafuu wa maisha na badala yake imeongeza machungu. Ni kweli kwambaili kupata maendeleo ni lazima kuumia katika mchakato, lakini kuumia huko

    ni lazima kueleweke na umma. Hivi sasa Umma umebakia bumbuwazi bila

    kuelewa. Bajeti na Serikali imekosa uwezo wa kuwasiliana na umma vizuri.

    Chama cha ACT Wazalendo kinahimiza wananchi kufuatilia kwa kina

    utekelezaji wa Bajeti ya Serikali na kupaza sauti pale wanapoumia ili Serikali

    ipate kusikia na kurekebisha mapungufu. Tunaamini kuwa tunao uwezo wakujenga Uchumi shirikishi na usio na unyonyaji wa kidola au sekta binafsi.

    Tuna uwezo wa kujenga Tanzania lenye Ujamaa wa Kidemokrasia yaani Taifa

    lisilo na unyonyaji na lenye uchumi unaowashirikisha wananchi wengi.

    Mungu ibariki Afrika,

    Mungu ibariki Tanzania.

    Ahsanteni kwa kunisikiliza na kunisoma!

    UTU. UZALENDO. UADILIFU16

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    19/2617UTU. UZALENDO. UADILIFU

    Kiambatanisho namba 1

    09. Viambatanisho

    Mapendekezo ya ACT Wazalendo ya Viwango vipya vya Kodi ya Mapato (PAYE)

    Asilimia sifuri 0%Mapato ya Jumla kwa mwezi yasiyozidi Shilingi 360,000/=

    Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 360,000/= lakini hayazidishilingi 720,000

    Mapato ya jumla yanayozidi shilingi 720,000/= lakini hayazidishilingi 1,440,000

    Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi 1,440,000/= lakini hayazidi

    shilingi 2,880,000

    Mapato ya jumla yanayozidi shilingi 2,880,000/= lakini hayazidishilingi 15,000,000

    Mapato ya jumla yanayozidi shilingi 15,000,000/=

    Shilingi 36,000 + 11% ya kiasikinachozidi shilingi 360,000/=

    Shilingi 72,000 + 20% ya kiasikinachozidi shilingi 720,000/=

    Shilingi 144,000 + 25% ya kiasi

    kinachozidi shilingi 1,440,000/=

    Shilingi 288,000 + 30% ya kiasikinachozidi shilingi 2,880,000/=

    Shilingi 3,000,000 + 40% ya kiasikinachozidi shilingi 15,000,000/=

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    20/26

    Mchango wa Ndg. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mbunge wa Kigoma Mjini

    akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara 2016/17

    Mheshimiwa Spika, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji amewasilisha

    maombi ya Fedha ili Bunge lako Tukufu limuidhinishie Jumla ya Tshs 82 Bilioni

    (Tshs 42 Bilioni za Matumizi ya Kawaida na Tshs 40 Bilioni za Maendeleo). Waziri

    anaomba tumpe idhini kutumia Fedha hizi ili aanze kutekeleza Mpango wa Pili

    wa Miaka Mitano ambao lengo lake kubwa ni kuwezesha Tanzania ya Viwanda.

    Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni sawa na 0.3% ya Bajeti

    nzima ya Serikali ya mwaka 2016/17.

    Mheshimiwa Spika, Waziri Kivuli wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ameibua

    hoja nzito sana kwenye hotuba yake ambazo naamini Serikali hainabudi kuz-

    ipatia majibu yanayostahili. Hoja kubwa ni ile inayohusu kuwepo kwa matamko

    3 tofauti, yenye tarakimu tofauti kutoka Serikali moja. Mfano uliotolewa ni kufu-

    fua Kiwanda cha General Tyre ambapo Vitabu vya Bajeti vinaonyesha kutengwa

    tshs 150 milioni, randama za Wizara zinaonyesha tshs 500 milioni na mpango

    wa Maendeleo unaonyesha tshs 2 bilioni zimetengwa. Kisheria za Bajeti, kilicho-

    mo kwenye vitabu vya Bajeti ndio kitakachoidhinishwa na Bunge. Kwamba Seri-

    kali inataka kufufua Kiwanda cha General Tyre kwa kutenga tshs 150 milioni, ni

    kichekesho cha karne. Mambo haya yanadhihirisha kuwa Serikali hii haitembei

    kwenye maneno yake. Wananchi wapatiwe majibu ya uhakika kuhusu masuala

    haya. Ni muhimu sana Serikali kuhakikisha kuna uratibu miongoni mwa Wizara

    za Serikali ili kuwa na sauti moja inayokwenda kwa wananchi.

    Kufungamanisha Sekta ya Viwanda na Sekta ya Kilimo

    Mheshimiwa Spika, adhma ya nchi yetu kuwa ya Viwanda ni adhma yetu sote.

    Jambo hili ni jambo la Maendeleo na halina ushabiki wa kivyama. Tumepitisha

    Mpango wa Maendeleo katika Bunge hili na kwa hiyo ni Mpango wa Nchi sio

    mpango wa vyama tena. Hivyo sote kwa pamoja tunafanya kazi ya kuhakikisha

    tunafikia malengo. Sisi tulio kwenye upinzani jicho letu pamoja na kushauri na

    UTU. UZALENDO. UADILIFU18

    Kiambatanisho namba 2

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    21/26

    kupendekeza ni kukosoa pale ambapo walio kwenye Serikali wanakosea. Kuko-

    soa ni tendo la kizalendo na walio Serikalini wawe tayari kukubali kukosolewa

    ili kuboresha zaidi. Kwa maoni yangu, kama tusipofanya marekebisho ya kimka-

    kati mapinduzi ya Viwanda itakuwa ni nyimbo na ngonjera za kisiasa. Wataka-

    oumia ni Wananchi ambao hawatapata ajira na Serikali yenyewe itakosa kodikuweza kutoa huduma kwa wananchi. Kama nilivyosema hapo awali Serikali

    inahitaji kufanya uratibu ili kufikia malengo. Sekta ya Viwanda au Maendeleo

    ya Viwanda yanapaswa kufungamanishwa na sekta nyengine za uchumi kwa

    sababu kuna kutegemeana. Kwa Tanzania unahitaji Sekta ya Kilimo inayokua

    kwa kasi ili kuzalisha malighafi kwenye viwanda. Sekta nyingine kama Elimu,

    Afya, Nishati, Mazingira nk zinahusiana na Viwanda pia. Kwa leo tutazame

    Sekta Kilimo na Viwanda kwa muktadha wa Hotuba ya Waziri wa Viwanda nakulinganisha na Hotuba ya Waziri wa Kilimo.

    Mheshimiwa Spika, Sekta ya Viwanda na Sekta ya Kilimo kwa pamoja zinachan-

    gia nusu ya Pato la Taifa ( GDP) na nusu nyingine ni sekta ya Huduma. Nadharia

    za Uchumi zinatuambia kuwa Tija ikiongezeka kwenye ya Kilimo inawezesha

    sekta ya Viwanda kukua na kisha sekta ya Huduma. Hapa Tanzania na nchi

    nyengine nyingi za Afrika, sekta ya huduma iliruka hatua hizi na hivyo kuchan-gia kwa kiasi kikubwa sana kwenye Pato la Taifa. Ndio maana tuna Kitendawili

    nchini kwetu kuwa Uchumi unakua lakini umasikini haupungui; ni kwa sababu

    sekta ya huduma haijiri watu wengi kama sekta ya Kilimo na hivyo uchumi una-

    okuzwa na sekta ya huduma ni nadra kuondoa umasikini. Tanzania bado ina-

    pambana na umasikini. Juhudi zote tunazofanya lengo lake ni kuondoa uma-

    sikini kwa watu wetu. Sekta za kuondoa umasikini ni Kilimo na Viwanda hivyo

    lazima mikakati ya Serikali iendane na kufungamanisha haya. Ndio Maana Nchinyengine Wizara ya Kilimo hujumuisha uongezaji thamani ( Ministry of Agricul-

    ture and Agro-processing ). Hatuhitaji kufanya hivyo, tunachohitaji ni kufun-

    gamanisha. Hata hivyo Serikali imeshindwa kufanya hivyo katika mwaka wake

    wa kwanza tu wa Bajeti. Nitaeleza kwa kutumia changamoto tuliyonayo kuhusu

    Sukari, Mafuta ya Kula na Nguo.

    Mheshimiwa Spika, Malengo ya Serikali kwenye Viwanda yapo uk.140 ibara ya191 ya Hotuba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Serikali imepanga

    kutekeleza mambo 9 na katika mambo yote hayo hakuna hata moja linalohu-

    19UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    22/26

    siana na Viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazohudumiwa na wananchi wengi

    zaidi kama Sukari na Mafuta ya kula. Bidhaa hizi ni bidhaa zinazoleta maneno

    ya kisiasa ndani ya nje ya Bunge. Nadhani baada ya madawa ya kulevya, bidhaa

    zenye mizengwe mingi zaidi katika duru za kisiasa ni Sukari na Mafuta ya kula.

    Sukari na Mafuta ya kula imeangusha Mawaziri kadhaa hapa nchini katika kip-indi cha miaka 20 iliyopita. Hata hivyo Wizara ya Viwanda na Biashara haina

    mkakati kabisa kushughulika na Bidhaa hizi licha ya uwezo wake wa kutene-

    genza ajira na kuokoa fedha za kigeni kuziagiza. Wizara imezungumza kuhusu

    viwanda vya nguo lakini haijafafanua changamoto kubwa zinazoikabili sekta

    ya nguo nchini na hasusan biashara haramu ya magendo ya Nguo inayoathiri

    sana ukuaji wa sekta ya nguo nchini.

    Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ukitazama hotuba ya Waziri wa Kilimo ambayo

    Bunge lako tukufu limeshapitisha bajeti yake kuna mikakati ya kulima Miwa

    kwa ajili ya Sukari. Ukurasa wa 44 ibara ya 107 ya Hotuba ya Wizara ya Kilimo na

    ukurasa wa 25 ibara za 63 na 64 zinaeleza mikakati ya kukabiliana na uhaba

    wa Sukari nchini. Kiambatanisho namba 6 cha Hotuba hiyo kimeeleza kwa kina

    changamoto nzima ya Sukari na miradi inayopaswa kutekelezwa ili kumaliza

    kabisa suala la uhaba wa Sukari nchini. Nimejumlisha miradi ile kutoka konambalimbali za nchi na nimekuta ni takribani Hekta 300,000 za kulima Miwa.

    Kwa Hesabu ya chini ya wastani wa kuzalisha Sukari kwa kila Hekta, miradi hii

    ikitekelezwa Tanzania itaweza kuzalisha Tani 1.5 milioni za Sukari. Ukiondoa Su-

    kari tunayotumia nchini, ziada itakayouzwa nje inaweza kuliingizia Taifa Fedha

    za Kigeni USD 500 milioni, sawa na 30% ya malengo ya Mpango wa Maendeleo

    kwa sekta ya Viwanda katika mapato ya Fedha za kigeni ya USD 3bn. Hapo si-

    jaeleza kiwango cha Ajira kitakachopatikana, ukuaji wa biashara kwenye sektanyengine na Umeme utakaozalishwa ( Multiplier effect ).

    Mheshimiwa Spika, swali la kujiuliza, chukulia Wizara ya Kilimo inalima hiyo

    miwa hekta 300,000 halafu Wizara ya Viwanda haina mpango wa hivyo viwan-

    da, hii miwa itakwenda wapi? Sio kwamba inapaswa kufungaminisha Kilimo

    cha Miwa na Viwanda vya Sukari? Ni kwa nini Wizara 2 zilizo chini ya Serikali

    moja zinashindwa kusomana? Baraza la Mawaziri linajadili nini? Ndio maanaRais anajikuta akitoa matamshi ya Mawaziri barabarani. Suala la Rais kutoa

    matamko kuhusu Sukari sio sawa, hii ni Kazi ya Mawaziri maana mnamuexpose

    UTU. UZALENDO. UADILIFU20

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    23/26

    Rais. Rais sio mtu wa kuhangaika na masuala ya kunywa Chai na Uji.

    Mheshimiwa Spika, nashauri Bunge lako tukufu leo lisipitishe Bajeti ya Wizara

    ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili Wizara hii ikakae na Wizara ya Kilimo

    wawianishe mipango hii na kisha walete hapa Bungeni ndio tupitishe. Sukari nimfano mmoja tu katika suala hili. Hebu tumuunge mkono Rais kwa kuwareje-

    sha mezani Wizara hizi mbili.

    Mheshimiwa Spika, kwenye sukari kuna suala la low hanging fruits. Hivi tuna-

    vyozungumza kila Mwaka miwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 50,000 ya Su-

    kari huoza hapa nchini uko Kilombero na Mtibwa. Wakulima wanalima miwa

    mingi kuliko uwezo wa Viwanda kununua. Bodi ya Sukari inapaswa kutoa leseniili vikundi vya wakulima au wawekezaji wadogo wazalishe Sukari. Bodi ya Sukari

    haijatoa leseni na wala Serikali haijahamasisha Watanzania kuwekeza kwenye

    viwanda vidogo vya Sukari ili kuwezesha miwa yote inayozalishwa kutoa Sukari.

    Kama hili lingefanyika, leo tusingekuwa na ukali huu wa uhaba wa Sukari. Wa-

    ziri wa Viwanda, hii ni low hanging fruits.

    Mheshimiwa Spika, uwekezaji wa bidhaa kama Sukari unahitaji vivutio maalu-mu kutoka Serikalini. Kule Uganda, Rais Museveni tangu aingie madarakani

    aliweka vivutio maalumu kwa Viwanda kama Kakira Sugar ili wazalishe Sukari

    ya kutosha. Viwanda vya Sukari Uganda hata umeme hulipiwa na Serikali kwa

    Asilimia 50 ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuokoa kutokana na ushin-

    dani wa Sukari kutoka nje inayotupwa nchini ( dumping). Subsidies kwa ajili ya

    kupunguza gharama za uzalishaji ili kuwezesha kuzalisha Sukari, kutengeneza

    ajira na kupata faida nyengine ni jambo ambalo Lazima Serikali ianze kulifikiria.Sisi Kigoma kuna mtu anataka kuzalisha Sukari tani milioni 1 kwa mwaka. Wiz-

    ara ya Fedha na Wizara ya Viwanda wanabishana kuhusu vivutio. Rais anahan-

    gaika na kuwafanya Watanzania wanywe Chai na Uji kwa bei rahisi, Mawaziri

    wake wanabishana kuhusu vivutio vya mitambo ya kupanda miwa nakuzalisha

    Sukari na kuzalisha Umeme. Serikali, hebu mtawale. Hebu muongoze. Utawala

    sio kutoa matamshi ya barabarani. Uongozi ni kufanya maamuzi yanayomaliza

    shida za wananchi kwa muda mrefu zaidi na sio matamko ya kupata Kurasa zaMbele za magazeti ya siku moja au mbili.

    21UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    24/26

    Mheshimiwa Spika, suala la Mafuta ya Kula halina tofauti na suala la Sukari.

    Ukipanda gari ukapita njia ya Singida unaona wananchi wamepanga madumu

    ya mafuta ya Alizeti wanauza. Nguvu kazi hii ya Wananchi inapotea kwa sababu

    Serikali imetoa unafuu mkubwa wa kodi kwa wanaoagiza mafuta ya kula kuto-

    ka nje ya Nchi. Leo kodi kwenye mafuta ya kula kutoka nje ni 18% tu. Tukiendeleahivi tutaendelea kuwaona wananchi wetu wanapigwa na jua kuuza mafuta ya

    Alizeti. Tunaposema mapinduzi ya Viwanda tunataka kumsaidia nani kama sio

    huyu Mwananchi anayeshinda juani? Kama tunataka kubadilisha hali ya Wa-

    nanchi ni lazima tuwawekee mazingira mazuri. Ni Aibu kubwa nchi hii kuagiza

    mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. Tunatumia USD 340 milioni kila mwaka kua-

    giza mafuta ya kula kutoka nje. Leo hii bei ya lita ya mafuta ya Alizeti ni kubwa

    kuliko bei ya lita ya petroli kwenye soko la dunia. Lakini wazalishaji wetu, wa-nanchi wetu masikini tunawatazama tu tukipita na mashangingi yetu baraba-

    rani. Hali hii lazima ibadilike. Serikali ndio yenye wajibu wa kubadili hali hii kwa

    kuweka kodi kubwa zaidi dhidi ya Mafuta ya kula kutoka nje na kuwekeza kwe-

    nye viwanda vya kukamua Mafuta kwa kutumia Alizeti na Mawese.

    Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kigoma kuna Mradi tunaotaka kuanza wa kupan-

    da Michikichi ili kuzalisha Mafuta ya Mawese. Tuna mpango wa kila familia 1 ku-panda hekta 1 ya michikichi kwa lengo la kufikia familia 100,000. Uzalishaji huu

    wa Mawese unaweza kuondoa kabisa suala la Tanzania kuagiza mawese kutoka

    nje maana tutaweza kuzalisha Tani 200,000 za Crude Palm Oil (CPO) kwa mwa-

    ka, kuzalisha ajira nyingi, kupandisha hali ya maisha ya wananchi wakulima na

    kukuza biashara nyengine. Tunahitaji watu watakaowekeza kwenye Viwanda

    vya kuzalisha mawese. Wizara ya Viwanda ishirikiane na Uongozi wa Mkoa wa

    Kigoma kuhakikisha tunazalisha mafuta ya Kula ya kutosha ili kuondokana nauagizaji huu. Mawese na Alizeti ndio suluhisho la kudumu la suala la Mafuta

    ya kula. Bunge liitake Serikali ikae upya kuandaa Bajeti ya Wizara ya Viwanda,

    Biashara na Uwekezaji ili kuifungamanisha na Bajeti ya Wizara ya Kilimo.

    Mheshimiwa Spika, Suala la Mwisho ni sekta ya Nguo. Nchi nyingi duniani am-

    bazo zimefanikiwa kuondokana na umasikini zimetumia sekta ya nguo ( textile

    industry). Mnyororo wa thamani wa Sekta ya Nguo ni mrefu kuanzia kwa Mku-lima mpaka kwenye nguo tunazovaa. Hii inapaswa kuwa sekta ongozi kwenye

    suala zima la uchumi wa viwanda. Hata hivyo tuna tatizo la Pamba.

    UTU. UZALENDO. UADILIFU22

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    25/26

    Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa Pamba umeporomoka kwa asilimia 47. Tut-

    apata wapi Pamba ya kulisha viwanda vya nguo? Wizara ya Kilimo na Wizaara

    ya Viwanda lazima zikae pamoja ili kuhakikisha kuwa tunafufua zao la Pamba.

    Vinginevyo nchi hii itaishia kuagiza pamba kutoka nje au tutajikuta tunaungan-isha nguo za kutoka China tu.

    Mheshimiwa Spika, Viwanda vya Nguo nchini vinapata shida kubwa sana ku-

    tokana na magendo ya nguo. Kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi kwenye

    bidhaa za nguo zinazoingizwa hapa nchini na hivyo kuua viwanda vya ndani.

    Viwanda vinapata shida kubwa ya matumizi ya Umeme maana umeme hauna

    uhakika na ni bei kubwa. Matokeo yake viwanda vingi vinafungwa na watuwetu kukosa ajira. Serikali lazima ifanye kazi ya ziada ya kuzuia magendo ya

    nguo vinginevyo viwanda vilivyopo vitakufa na hakuna atakayekubali kujenga

    kiwanda hapa nchini kwani atajua kuwa Serikali haifanyi ziada kuhakikisha

    tunalinda viwanda.

    Mheshimiwa Spika, hakuna nchi duniani isiyolinda viwanda vyake. Leo Taifa

    kubwa kama Uingereza linahangaika na kiwanda cha Chuma na kutaka hatakuingiza mtaji wake ili kulinda ajira za Wanananchi wake. Tujifunze kwa wen-

    zetu. Kama tunataka kupata ajira kwa watu wetu ni lazima kulinda viwanda

    vyetu. Viwanda vya nguo nchini vipo kwenye tishio kubwa sana kutokana na

    magendo ya nguo. Serikali ichukue hatua stahiki. Nguo zitatutoa kuanzia kwa

    mkulima mpaka kwa wenye viwanda.

    Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja kwamba Tuahirishe mjadala wa Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili kuiruhusu Serikali kuwianisha mipango

    ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda. Wakiwa tayari ndio Bunge lije kupi-

    tisha Bajeti ya Wizara hiyo.

    Zitto Zubeir Ruyagwa Kabwe

    Mbunge Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)

    Mei 9, 2016

    23UTU. UZALENDO. UADILIFU

  • 7/26/2019 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17

    26/26