mchungaji afanyaye watu kuwa wanafunzihebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano...

21
www.shepherdserve.org Unaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza haya kwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukata chochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Haki zote zimehifadhiwa 2006 David Servant Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi David Servant Sura Ya Sita Huduma Ya Kufundisha Katika sura hii tutatazama sehemu nyingi za huduma ya kufundisha. Kufundisha ni wajibu wa mitume, manabii, wainjilisti, 1 wachungaji/wazee/waangalizi, waalimu (ndiyo kabisa!), na kwa kiwango fulani, wafuasi wote wa Kristo. Maana sisi sote tunatakiwa kuwa katika kufanya watu kuwa wanafunzi, tukiwafundisha wanafunzi wetu kutii yote aliyoagiza Kristo. 2 Kama nilivyokwisha kazia hapo nyuma, mchungaji – au mtumishi - anayefanya watu kuwa wanafunzi kwanza hufundisha kwa mfano wa maisha yake, kisha kwa maneno. Anahubiri anachokitenda. Mtume Paulo ambaye alifaulu sana katika kufanya watu kuwa wanafunzi, aliandika hivi: Niigeni mimi, kama na mimi ninavyomwiga Kristo (1Wakor. 11:1 – TLR). Hilo linapaswa kuwa lengo la kila mtumishi – kuweza kusema ukweli kwa wale anaowaongoza: “Fanyeni kama mimi. Mkitaka kujua jinsi mfuasi wa Kristo anavyoishi, nitazameni mimi.” Nikitazama nyuma, nakumbuka nikiwaambia washirika wangu zamani: “Msinifuate mimi … mfuateni Kristo!” Japo halikuniingia wakati huo, nilichofanya ni kukiri kwamba mimi sikuwa mfano mzuri wa kufuata. Ukweli ni kwamba, nilikuwa nakiri kwamba sikuwa namfuata Kristo inavyotakiwa, kisha ninawaambia wengine wote kufanya kitu ambacho mimi sikuwa nakifanya! Hiyo ilikuwa tofauti kabisa na jinsi Paulo alivyosema. Ni hivi: Kama hatuwezi kuwaambia watu watuige kwa sababu na sisi tunamwiga Kristo, hatupaswi kuwa katika huduma. Kwa sababu, watu huwatumia watumishi kama mifano ya kuiga katika maisha yao. Kanisa ni onyesho la viongozi wake. 1 Mahubiri ya Injili yanayofanywa na wainjilisti yahesabiwe kuwa ni aina ya kufundisha. Wainjilisti wanatakiwa kutangaza Injili iliyo sahihi KiBiblia. 2 Si waamini wote waliopewa wajibu wa kufundisha makundi ya watu, ila wote wana wajibu wa kufundisha mtu kwa mtu, wanapowafanya watu kuwa wanafunzi (taszama Mathayo 5:19; 28:19-20; Wakolosai 3:16; Waebrania 5:12).

Upload: others

Post on 02-Feb-2020

66 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

www.shepherdserve.orgUnaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza hayakwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukatachochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Hakizote zimehifadhiwa 2006 David Servant

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziDavid Servant

Sura Ya SitaHuduma Ya Kufundisha

Katika sura hii tutatazama sehemu nyingi za huduma ya kufundisha. Kufundisha niwajibu wa mitume, manabii, wainjilisti,1 wachungaji/wazee/waangalizi, waalimu (ndiyokabisa!), na kwa kiwango fulani, wafuasi wote wa Kristo. Maana sisi sote tunatakiwakuwa katika kufanya watu kuwa wanafunzi, tukiwafundisha wanafunzi wetu kutii yotealiyoagiza Kristo.2

Kama nilivyokwisha kazia hapo nyuma, mchungaji – au mtumishi - anayefanya watukuwa wanafunzi kwanza hufundisha kwa mfano wa maisha yake, kisha kwa maneno.Anahubiri anachokitenda. Mtume Paulo ambaye alifaulu sana katika kufanya watu kuwawanafunzi, aliandika hivi:

Niigeni mimi, kama na mimi ninavyomwiga Kristo (1Wakor. 11:1 –TLR).

Hilo linapaswa kuwa lengo la kila mtumishi – kuweza kusema ukweli kwa waleanaowaongoza: “Fanyeni kama mimi. Mkitaka kujua jinsi mfuasi wa Kristo anavyoishi,nitazameni mimi.”

Nikitazama nyuma, nakumbuka nikiwaambia washirika wangu zamani: “Msinifuatemimi … mfuateni Kristo!” Japo halikuniingia wakati huo, nilichofanya ni kukiri kwambamimi sikuwa mfano mzuri wa kufuata. Ukweli ni kwamba, nilikuwa nakiri kwambasikuwa namfuata Kristo inavyotakiwa, kisha ninawaambia wengine wote kufanya kituambacho mimi sikuwa nakifanya! Hiyo ilikuwa tofauti kabisa na jinsi Paulo alivyosema.Ni hivi: Kama hatuwezi kuwaambia watu watuige kwa sababu na sisi tunamwiga Kristo,hatupaswi kuwa katika huduma. Kwa sababu, watu huwatumia watumishi kama mifanoya kuiga katika maisha yao. Kanisa ni onyesho la viongozi wake.

1 Mahubiri ya Injili yanayofanywa na wainjilisti yahesabiwe kuwa ni aina ya kufundisha. Wainjilistiwanatakiwa kutangaza Injili iliyo sahihi KiBiblia.2 Si waamini wote waliopewa wajibu wa kufundisha makundi ya watu, ila wote wana wajibu wakufundisha mtu kwa mtu, wanapowafanya watu kuwa wanafunzi (taszama Mathayo 5:19; 28:19-20;Wakolosai 3:16; Waebrania 5:12).

Page 2: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Kufundisha Umoja Kwa Njia Ya Mfano

Hebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada mojamuhimu sana: umoja. Wachungaji wote au wazee au waangalizi wanatamani kwambamakundi wanayoyaongoza yawe na umoja. Wanachukia migawanyiko katika makundiyao. Wanajua kwamba migawanyiko inamchukiza Bwana. Yesu alituamuru tupendanesisi kwa sisi kama Yeye alivyotupenda (ona Yohana 13:34-35). Kupendana kwetu sisikwa sisi ndicho kinachotujulisha kuwa wanafunzi Wake kwa dunia inayotutazama. Kwakuwa ni hivyo, viongozi wengi wa makundi huwashauri kondoo wao kupendana, nakutafuta sana umoja.

Lakini – kama watumishi tunaopaswa kufundisha kwanza kwa mfano wetu wenyewe,sisi mara nyingi tunapungua sana katika mafundisho yetu kuhusu upendo na umoja, kwajinsi tunavyoishi. Kwa mfano: Wakati sisi tunapo-onyesha kutokuwa na upendo na umojana wachungaji wengine, tunapeleka ujumbe ambao ni kinyume cha kile tunachohubirikwa washirika wetu. Tunawatazamia wafanye kitu ambacho sisi hatufanyi.

Ukweli ni kwamba: Maneno muhimu sana ambayo Yesu alizungumza kuhusu umoja,aliyasema kwa viongozi juu ya mahusiano yao na viongozi wengine. Mfano: Wakati waChakula cha Mwisho baada ya kuwanawisha wanafunzi Wake miguu, Yesu aliwaambiahivi:

Mnaniita Mwalimu na Bwana. Ni sawa, maana ndivyo nilivyo. Kamamimi, Bwana na Mwalimu, nimewasafisha miguu yenu, ninyi piamnatakiwa kusafishana miguu. Maana nimewapa mfano ili mfanye kamanilivyowafanyia (Yohana 13:13-15. TLR) [Hebu jionee mwenyewe: Yesualifundisha kwa mfano.]

Mara nyingi wachungaji hutumia mstari huo kuwafundisha watu wao juu yakupendana. Ni sawa kabisa. Ila, maneno ya fungu hili yalitolewa kwa viongozi – walemitume kumi na mbili. Yesu alijua kwamba kanisa Lake la baadaye lisingekuwa namatumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama viongozi wake wangekuwawamegawanyika, au kama wangeshindana wao kwa wao. Basi akaweka wazi kabisakwamba anatazamia viongozi Wake wahudumiane kwa unyenyekevu.

Kulingana na utamaduni wa siku alizokuwa hapa duniani, Yesu alionyeshaunyenyekevu katika huduma kwa kufanya kazi ya chini sana iliyofanywa na mtumishi wanyumbani – kunawisha watu miguu. Kama angetembelea utamaduni mwingine katikawakati tofauti kihistoria, pengine angechimba vyoo au kusafisha mapipa ya takataka yawanafunzi Wake. Je, ni wangapi katika viongozi Wake wa kisasa walio tayari kuonyeshaaina hiyo ya upendo na unyenyekevu kwa wenzao?

Baada ya muda usiozidi saa moja, Yesu alirudia kutilia mkazo ujumbe huo muhimusana. Dakika chache tu baada ya kuwanawisha miguu yao, Yesu aliwaambia hiviviongozi Wake wa kanisa la baadaye:

Nawapa amri mpya kwamba mpendane. Kama mimi nilivyowapendaninyi, ninyi nanyi pendaneni. Kwa hilo, watu wote watajua kwamba ninyini wanafunzi wangu, mkipendana (Yohana 13:34-35. TLR).

Page 3: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Hayo maneno kweli yanawafaa wanafunzi wote wa Kristo, lakini yalizungumzwahasa kwa viongozi kwa habari ya mahusiano yao na viongozi wenzao.

Dakika chache baadaye, Yesu akasema tena, hivi:

Amri yangu ni hii, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi, kama ambavyomimi nimewapenda. Hakuna mwenye upendo mkuu kuliko huu, kwambamtu atoe uhai wake kwa ajili ya rafiki zake (Yohana 15:12-13. TLR).

Ona tena kwamba Yesu alikuwa anazungumza na viongozi.Baada ya nukta chache alisema hivi tena:

Ninawaamuru hivi: pendaneni ninyi kwa ninyi (Yohana 15:17).

Dakika chache baadaye, wanafunzi wa Yesu wakamsikia akiwaombea.

Mimi siko tena duniani, ila wao wapo, nami nakuja kwako. BabaMtakatifu, walinde katika jina Lako, jina lile ulilonipa, ili wawe na umoja,kama sisi tulivyo (Yohana 17:11, TLR. Maneno mepesi kukazia).

Mwishowe, nukta chache tu baadaye alipoendelea na maombi Yake, wanafunziwalimsikia Yesu akisema hivi:

Siombi kwa ajili ya hawa tu, bali hata kwa ajili ya watakaoniaminikupitia neno lao. Kwamba wote wawe na umoja; kama ambavyo WeweBaba, ulivyo ndani Yangu, nami ndani Yako, na wao wawe ndani Yetu, ilidunia ipate kuamini kwamba ulinituma. Na utukufu ule ulionipa,nimewapa wao, ili wawe na umoja, kama sisi tulivyo. Mimi ndani yao, naWewe ndani Yangu, wapate kukamilishwa katika umoja, ili dunia ijuekwamba ulinituma, na kwamba unawapenda, kama ulivyonipenda mimi(Yohana 17:20-23. TLR – maneno mepesi kukazia).

Basi – katika kipindi kisichozidi saa moja, Yesu mara sita alikazia kwa viongoziWake wa baadaye umuhimu wa wao kuwa na umoja na kuonyesha umoja wao kwakupendana na kuhudumiana kwa unyenyekevu sana. Bila shaka jambo hili lilikuwa lamuhimu sana kwa Yesu. Umoja wao ulikuwa kitu cha msingi katika dunia kumwaminiYeye.

Tunaendeleaje Mpaka Sasa?

Kwa bahati mbaya sana – tunapotazamia makundi yetu yaungane kwa upendo –wengi wetu tunashindana na kutumia njia ambazo si halali kuyakuza makanisa yetu kwagharama ya mengine. Wengi wetu tunaepuka kushirikiana na wachungaji wowote ambaomafundisho yao ni tofauti na yetu. Hata tunatangaza kutokuwa na umoja kwetu kwa njiaya vibao tunavyoweka mbele ya makanisa yetu ili dunia ivione, tukipeleka ujumbe huukwa kila mtu: “Sisi si kama wale Wakristo wengine katika makanisa mengine”. (Na

Page 4: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

tumefaulu sana kuelimisha dunia kuhusu kutokuwa na umoja kwetu, maana wasioaminiwengi wanajua Ukristo ni dini iliyogawanyika sana.)

Kwa kifupi ni hivi: hatutendi tunayohubiri, na mifano ya maisha yetu huwafundishawatu wetu mengi kuliko mahubiri yetu ya umoja. Ni upumbavu kufikiri kwambaWakristo wa kawaida wataungana na kupendana wakati viongozi wao wanafanyakinyume.

Ufumbuzi wa pekee ni toba. Lazima tutubu kwa kuwa mifano mibaya mbele yawaamini na mbele ya dunia. Lazima tuondoe kuta zinazotugawa na tuanze kupendanakama Yesu alivyoagiza.

Maana yake ni kwamba – kwanza kabisa: Tukutane na wachungaji wengine nawatumishi ambao wanafuata mafundisho tofauti na yetu. Hapa sisemi tuwe na ushirika nawachungaji ambao hawajaokoka, ambao hawana juhudi yoyote katika kumtii Yesu, auambao wanafanya huduma kwa faida zao binafsi. Hao ni mbwa mwitu waliovaa ngozi yakondoo, na Yesu alituambia jinsi ya kuwagundua. Wanajulikana kwa matunda yao.

Ila ninazungumza juu ya wachungaji na watumishi wanaojitahidi kushika amri zaYesu – ndugu na dada kweli katika Kristo. Kama wewe ni mchungaji, unatakiwa kujitoakuwapenda wachungaji wengine, na kuonyesha upendo huo kwa njia za vitendo mbele yakundi lako. Njia moja ni kwa kuanza kuwaendea wachungaji wengine katika eneo lako nakuwaomba msamaha kwa kutowapenda kama inavyotakiwa. Tendo hilo litavunja kuta.Kisha, jitoe kukutana nao mara kwa mara ili kula chakula pamoja, kutiana moyo,kushauriana na kuomba pamoja. Hayo yatakapotokea, itawezekana hata kuzungumza nakujadili kwa upendo yale mafundisho yanayowatenganisha, na hatimaye kutafuta kuwana umoja – mwe mmekubaliana au bado juu ya kila mtakachozungumza. Maisha yanguna huduma vilitajirishwa sana nilipokuwa tayari kuwasikiliza wachungaji waliokuwa naitikadi tofauti na kambi yetu. Kwa kujifungia nilikuwa nakosa baraka nyingi sana kwamiaka mingi sana.

Unaweza pia kuonyesha upendo wako na umoja kwa kuwakaribisha wachungajiwengine waje kuhubiri kanisani kwako au katika makanisa ya nyumbani, au mnawezakuunganisha ibada na hayo makanisa, mkafanya ibada ya pamoja.

Unaweza pia kubadilisha jina la kanisa lako ili lisitangazie dunia kwamba huna umojana wengine katika mwili wa Kristo. Unaweza kutoka katika dhehebu lako au shirikaunalohusiana nalo na ukajitambulisha na mwili wa Kristo tu, kwa njia hiyo kutumaujumbe kwa kila mtu kwamba unaamini kwamba Yesu anajenga kanisa moja tu, siomakanisa mengi tofauti yasiyoweza kushirikiana.

Najua hilo linasikika kuwa gumu. Lakini, kwa nini ufanye kitu chochote kuendelezayale ambayo Yesu hakukusudia? Mbona kujihusisha na kitu chochote kinachomchukiza?Hakuna madhehebu wala miungano maalum inayotajwa katika Maandiko. Wakorinthowalipogawanyika juu ya waalimu waliowapenda, Paulo aliwakemea sana, akisemamigawanyiko yao ilidhihirisha kwamba wao ni watu wa kimwili na ni wachanga kiroho(ona 1Wakor. 3:1-7). Je, migawanyiko yetu sisi inadhihirisha kitu kingine tofauti nahicho?

Chochote kinachotutenganisha kiepukwe. Makanisa ya nyumbani yanatakiwakujiepusha kujipa majina au kujiunga na mashirika yoyote yenye majina. KatikaMaandiko, makanisa yalijulikana kwa nyumba waliyokutania. Muungano wa makanisamahali ulijulikana kwa miji yaliyokuwemo. Yote yalijihesabu kuwa sehemu ya kanisamoja tu – Mwili wa Kristo.

Page 5: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Kuna Mfalme mmoja tu na ufalme mmoja tu. Yeyote ajiinuaye ili waamini aumakanisa yajitambulishe naye anajenga ufalme wake mwenyewe ndani ya ufalme waMungu. Ni afadhali awe tayari kusimama mbele za Mfalme anayesema hivi: “Sitampamwingine utukufu wangu” (Isaya 48:11).

Hayo yote ni ili tuseme hivi: Watumishi wanatakiwa kuonyesha mfano mzuri wakumtii Kristo mbele ya watu wote, kwa sababu watu watafuata mfano wao. Jinsiwanavyoishi mbele ya wengine ndiyo njia kuu yenye ushawishi ya kufundisha. Pauloaliwaandikia hivi waamini wa Filipi:-

Ndugu, jiungeni katika kufuata mfano wangu, na mwatazame kwamakini wale wanaoenenda kulingana na mfano mlioona kwetu (Wafilipi3:17 – TLR. Maneno mepesi kukazia).

Cha Kufundisha

Mtumishi mwenye kufanya wengine kuwa wanafunzi ana lengo, sawa tu na Paulo.Lengo hilo ni “kumfikisha kila mmoja akiwa mkamilifu katika Kristo” (Wakolosai1:28b). Basi, yeye naye, sawa na Paulo, ata”mwonya kila mtu na kumfundisha kwahekima yote” (Wakolosai 1:28a – TLR. Maneno mepesi kukazia). Ona kwamba Paulohakufundisha ili kuwaelimisha watu tu au kuwastarehesha.

Mtumishi mwenye kufanya wengine kuwa wanafunzi anaweza kusema na Paulo:-“Lengo la mafundisho yetu ni upendo utokao katika moyo wa kweli, na dhamiri safi, naimani ya dhati” (1Timo. 1:5 – TLR). Yaani, anachotaka ni kusababisha hali ya kufananakweli na Kristo, na utakatifu katika maisha ya watu anaowahudumia. Ndiyo sababuanawafundisha waamini kuzitii amri zote za Kristo. Anafundisha ukweli, akiwashauriwasikilizaji wake kutafuta “kwa bidii amani na watu wote, na utakaso [au utakatifu]ambao bila huo hakuna mtu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14 – TLR).

Mtumishi mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi anajua kwamba Yesu aliwaagizawanafunzi Wake wawafundishe wanafunzi wao kutii yote, wala si sehemu tu ya maagizoYake (tazama Mathayo 28:19-20). Anataka kuhakikisha kwamba hataacha kufundishachochote kilichoagizwa na Kristo, kwa hiyo, anafundisha Injili na Nyaraka zote mstarikwa mstari, mara kwa mara. Maagizo ya Yesu yameandikwa humo na kutilia mkazo pia.

Mafundisho hayo ya kufafanua pia huhakikisha kwamba yatakuwa na mlingano.Tunapofundisha jumbe zenye kulenga mada fulani tu, inakuwa rahisi kujali madazinazopendwa na watu na kupuuza zile zisizopendwa sana. Mwalimu anayefundishamstari kwa mstari hatafundisha juu ya pendo la Mungu tu, bali pia juu ya adhabu nahasira Yake. Hatafundisha tu juu ya baraka za kuwa Mkristo, bali pia juu ya wajibu aumajukumu ya Mkristo. Hatatilia mkazo mambo madogo na kupuuza mambo ya muhimuzaidi. (Hilo ndilo kosa walilofanya Mafarisayo, kulingana na Yesu – ona Mathayo 23:23-24).

Kushinda Hofu Za Mafundisho Ya Kufafanua

Wachungaji wengi wanaogopa kufundisha mstari kwa mstari kwa sababu kuna mengiwasiyoelewa katika Maandiko, na hawataki washirika wao wajue kwamba hawajui! Hayoni majivuno. Hakuna mtu yeyote duniani anayeelewa kikamilifu kabisa kila kitu katika

Page 6: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Maandiko. Hata Petro alisema kwamba baadhi ya mambo aliyoandika Paulo yalikuwamagumu kuelewa (ona 2Petro 3:16).

Mchungaji anayefundisha mstari kwa mstari anapofikia mstari au fungu la Maandikoambalo haelewi, anatakiwa kuwaambia washirika wake kwamba haelewi sehemuinayofuata, na kuiacha. Pia anaweza kuwaomba washirika wamwombee ili RohoMtakatifu amsaidie kuelewa. Unyenyekevu wake utakuwa mfano mzuri mbele ya kundilake, na kuwa ujumbe kamili kabisa.

Mchungaji au mzee au mwangalizi wa kanisa la nyumbani ana ziada nyingine yakufundisha kundi dogo katika mazingira yasiyo rasmi, kwa sababu maswali yanawezakuulizwa wakati wa mafundisho yake. Hili pia hutoa nafasi ya uwezekano wa RohoMtakatifu kuwapa wengine katika kikundi hicho ufahamu kuhusu maandikoyanayochunguzwa. Matokeo ni kwamba kila mtu anaweza kujifunza kwa uzuri zaidi.

Mahali pazuri pa kuanza kufundisha amri za Kristo ni kwenye Mahubiri Yakealiyotoa mlimani, katika Mathayo sura ya 5 hadi ya 7. Yesu alitoa amri nyingi sana hapo,na aliwasaidia wafuasi Wake Wayahudi kuelewa vizuri zile sheria zilizotolewa kwa njiaya Musa. Baadaye katika kitabu hiki nitafundisha kutoka Mahubiri ya Mlimani mstarikwa mstari ili uone inavyoweza kuwa.

Kuandaa Mahubiri

Hakuna ushahidi wowote katika Agano Jipya kwamba mchungaji yeyote, au mzee, aumwangalizi aliandaa mahubiri au hotuba ya kila juma, ikiwa na mada zilizoandaliwavizuri na vielelezo au mifano iliyoandikwa kwa muhtasari, kama ilivyo kawaida yawatumishi wengi wa kisasa. Nadhani hatuwezi kufikiria Yesu akifanya hivyo! Katikakanisa la kwanza, mafundisho yalifanyika kimatendo na kila mmoja alihusika, kwakufuata mtindo wa Kiyahudi badala ya kuwa mihadhara au hotuba, kama ilivyokuwadesturi ya Wayunani na Warumi. Desturi hii ilikuja kuingizwa katika kanisa mwishoni,lilipokuja kuwa kama lilivyo leo. Ikiwa Yesu aliwaambia wanafunzi Wake wasitayarishejinsi watakavyojitetea wakiitwa mahakamani, akiahidi kwamba Roho Mtakatifuangewapa pale pale maneno ya kusema ambayo yasingekuwa rahisi kupingwa, ni vizuritutazamie kwamba Mungu ataweza kuwasaidia wachungaji katika mikutano ya kanisakwa kiwango fulani!

Hii si kusema kwamba watumishi wasijiandae wenyewe kwa kuomba na kujisomea.Paulo alimshauri Timoteo hivi:

Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu kama mtendakaziasiyehitaji kuaibika, anayetumia sawasawa neno la kweli (2Timo. 2:15 –TLR).

Watumishi wanaofuata mashauri ya Paulo kwamba “Neno la Kristo likae kwa wingindani yenu” (Wakolosai 3:16 – TLR) watajawa na Neno la Mungu kiasi cha kwambawataweza kulifundisha kutokana na “kufurika” kwao. Basi mchungaji mpendwa: Chamuhimu ni kwamba, zama ndani ya Biblia. Ukijua vizuri mada yako, na ukiwa na motojuu ya mada yako, hakuna matayarisho mengine unayohitaji ili uweze kuwasilisha kweliya Mungu kwa wasikilizaji wako. Tena, kama unafundisha mstari kwa mstari, unawezakutumia mstari unaofuata kama muhtasari wako. Basi, maandalizi yako yawe ni

Page 7: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

kutafakari kwa hali ya maombi mistari ile utakayofundisha juu yake. Kama wewe nimchungaji wa kanisa la nyumbani, ile hali ya kushirikiana katika kufundisha itapunguzasana hitaji la kuwa na muhtasari wa mahubiri.

Mtumishi mwenye imani kwamba Mungu atamsaidia wakati anapofundisha,atazawadiwa msaada wa Mungu. Basi, usijiamini wewe sana, wala matayarisho yako auvidokezo ulivyuoandika. Mtumaini Mungu zaidi. Kadri utakavyopata imani na kujiamini,punguza vidokezo unavyoandaa mpaka uweze kufundisha ukitumia vidokezo kidogo aubila muhtasari wenye vidokezo kabisa.

Mwenye kujifikiria mbele ya wengine ndiye atakayetegemea vidokezo alivyoandaakwa sababu anaogopa kufanya makosa mbele ya watu. Anahitaji kujua kwamba hofuyake inatokana na kutojiamini, na kiburi. Afadhali asijali jinsi anavyo-onekana machonipa watu, ajali zaidi jinsi yeye na wasikilizaji wake wanavyoonekana mbele za Mungu.Hakuna hotuba iliyoandaliwa inayhoweza kuwagusa wasikilizaji kama mafundisho tokamoyoni, yenye upako wa Roho Mtakatifu. Hebu fikiri jinsi ambavyo mawasilianoyangekwamishwa kama kila mtu angetumia vidokezo vilivyoandikwa katikamazungumzo yake yote! Kuzungumza kungekoma! Mtindo wa mazungumzoyasiyoandaliwa husikika kuwa kweli kuliko mhadhara ulioandaliwa. Kufundisha sikuigiza. Ni kutoa ukweli. Wote tunajua wakati tunaposikiliza hotuba, na inapokuwahivyo, tunajua jinsi ya kufunga “mawazo” yetu tusisikie chochote.

Mawazo Mengine Manne

(1) Watumishi wengine ni kama kasuku. Wao hupata vitu vya kuhubiri kutokakwenye vitabu vilivyoandikwa na wengine. Wanapoteza baraka kubwa sana yakufundishwa na Roho Mtakatifu, na kuna uwezekano mkubwa sana kwao kuendelezamakosa ya waandishi wanaowanakili.

(2) Wachungaji wengi huiga mitindo ya kuhubiri na kufundisha ya watu wengine – yakimapokeo. Kwa mfano: Inaaminika kwamba mahubiri yamevuviwa kama yatakuwa kwaharaka na kwa sauti kubwa. Basi, wahudhuriaji wanaketi kusikiliza mahubiri ambayo nikelele tupu tangu mwanzo hadi mwisho. Ukweli ni kwamba watu huacha kusikilizakelele zisizo na maana, kama wanavyofanya wakati mtu anapozungumza kwa sauti mojatu isiyobadilika. Sauti yenye kubadilika-badilika inavutia zadi. Tena, mahubiri huwa yasauti kubwa kidogo kwa sababu ni kama mawaidha, ila mafundisho hufanywa kwa sautikama ya kuzungumza maana ni kama ushauri.

(3) Nimeona wasikilizaji mahubiri wengi sana katika makanisa mengi sana, namisijaacha kushangaa jinsi ambavyo wahubiri wengi na waalimu wasivyoweza kuona isharanyingi kwamba wasikilizaji wao wamechoka na hawasikilizi. Mchungaji, ni hivi: Watuwanao-onekana wamechoka ni kweli wamechoka! Wale wasiokutazama ni kwambahawaskilizi. Watu ambao hawasikilizi hawapati msaada hata kidogo. Kama watu wenyekumaanisha wamechoshwa na hawasikilizi, unahitaji kurekebisha mahubiri yako. Toamifano zaidi. Eleza visa vyenye maana na msaada kwao. Tunga mithali. Rahisishamambo. Fundisha Neno la Mungu kutoka moyoni. Maanisha unachosema. Usiige mtu.Badilisha sauti yako. Jaribu kuwatazama watu wengi iwezekanavyo machoni. Simuliakisa chako kwa maigizo. Tumia mikono. Usisimame mahali pamoja – tembea tembea.Usizungumze kwa muda mrefu. Kama kundi ni dogo, ruhusu watu waulize maswali kwawakati unaofaa.

Page 8: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

(4) Wazo kwamba kila mahubiri yanatakiwa kuwa na mambo makuu matatu ni lakibinadamu. Lengo ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi, siyo kufuata nadharia za kisasaza kutayarisha mahubiri. Yesu alisema hivi: “Lisha kondoo wangu”. Hakusema:“Babaisha kondoo wangu”.

Wa Kufundishwa

Anapofuata mfano wa Yesu, mtumishi mwenye kufanya watu kuwa wanafunzihuchagua atakayefundishwa. Pengine litakushangaza hilo, lakini ndiyo ukweli. Maranyingi Yesu alizungumza na makundi ya watu kwa mifano, na alikuwa na sababu yakufanya hivyo. Hakutaka kila mtu aelewe alichokuwa anasema. Maandiko yanaweka hilowazi, kama ifuatavyo:

Wakaja wanafunzi wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwamifano? Akajibu akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wambinguni, bali wao hawakujaliwa. Kwa maana yeyote mwenye kituatapewa, naye atazidishiwa tele; lakini yeyote asiye na kitu, hata kilealicho nacho atanyang’anywa. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano;kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa(Mathayo 13:10-13).

Fursa au nafasi ya kuelewa mifano ya Kristo ilitolewa kwa wale tu waliokuwawametubu na kuamua kumfuata. Wale waliopuuza nafasi ya kutubu na kupinga mapenziya Mungu kwa ajili ya maisha yao, walikataliwa na Mungu na kupingwa Naye pia.Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa neema wanyenyekevu (ona 1Petro 5:5).

Vile vile Yesu aliwaagiza wafuasi wake hivi: “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu,wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao,wakageuka na kuwararua” (Mathayo 7:6). Hapa, Yesu alizungumza kwa lugha ya mfano.Alimaanisha hivi: “Msitoe kitu cha thamani kwa watu wasiothamini thamani yake.”Nguruwe hawatambui kwamba lulu zina thamani. Vivyo hivyo, nguruwe wa kirohohawatambui thamani ya Neno la Mungu wanapolisikia. Wangeamini kwamba wanasikiaNeno la Mungu, wangelisikiliza kwa makini sana na kulitii.

Utajuaje mtu ni nguruwe kiroho? Wewe mtupie lulu moja uone atakachofanya.Akiipuuza, utajua kwamba yeye ni nguruwe kiroho. Akiitii, utajua kwamba si nguruwekiroho.

Cha kusikitisha ni kwamba wachungaji wengi hufanya kile ambacho Yesuamewakataza kufanya. Wanaendelea kutupa lulu zao mbele ya nguruwe, wakiwafundishawatu ambao wanapinga au waliokataa Neno la Mungu. Watumishi hao wanapoteza mudawao waliopewa na Mungu. Wangepaswa kukung’uta mavumbi ya miguuni pao nakwenda mahali pengine zamani, kama Yesu alivyoagiza.

Kondoo, Mbuzi Na Nguruwe

Ukweli ni huu: Huwezi kumfanya mtu kuwa mwanafunzi ambaye hataki hivyo,yaani, mtu asiyetaka kumtii Yesu. Makanisa mengi yamejaa watu wa aina hiyo, watuambao wana mila ya Kikristo. Wengi hufikiri kwamba wamezaliwa mara ya pili kwa

Page 9: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

sababu tu wamekubaliana na kweli fulani za kitheolojia kuhusu Yesu au Ukristo. Wao ninguruwe na mbuzi – si kondoo. Lakini, wachungaji wengi hutumia asilimia 90 ya wakatiwao wakijaribu kufurahisha hao nguruwe na mbuzi, huku wanapuuzia wale ambaowangeweza kuwasaidia kiroho na wanaotakiwa kuhudumiwa – yaani, kondoo wa kweli!Ewe mchungaji: Yesu anataka ulishe kondoo Zake, si mbuzi au nguruwe! (Ona Yohana21:17)

Lakini sasa, utajuaje nani kondoo? Ni wale wanaokuja kanisani mapema, nakuondoka wa mwisho. Hao wana njaa ya kujifunza ukweli, kwa sababu Yesu ni Bwanawao, na wanataka kumpendeza. Wanakuja kanisani – si Jumapili tu – bali sikuzotekunapokuwa na mkutano. Wanajiunga na vikundi vidogo. Mara nyingi wanaulizamaswali. Wana msisimko kuhusu Bwana. Wanatafuta nafasi za kutumika.

Mchungaji: Tumia muda wako mwingi kwa watu hawa. Hao ndiyo wanafunzi.Kuhusu mbuzi na kondoo wanaohudhuria kanisani kwako: Wewe hubiri Injili muda wotewatakaoweza kuvumilia. Lakini ukihubiri Injili ya kweli, hawataweza kuvumilia kwamuda mrefu. Wtaondoka kanisani – au kama wana uwezo – watajaribu kukuondoa.Wakifanikiwa, kung’uta mavumbi miguuni pako unapo-ondoka. (Lakini: Katika kanisa lanyumbani, jambo hilo haliwezi kutokea, hasa kama kanisa lenyewe linakutania nyumbanimwako!)

Wainjilisti nao wasijisikie wajibu wa kuendelea kuhubiri Injili kwa watu wale waleambao wameikataa mara kadhaa. Waache wafu wazike wafu wenzao (ona Luka 9:60).Wewe ni balozi wa Kristo, mwenye ujumbe wa maana sana kutoka kwa Mfalme wawafalme! Nafasi yako ni ya juu sana katika ufalme wa Mungu, na wajibu wako nimkubwa! Usipoteze wakati kumwambia mtu Injili mara mbili kabla wengine hawajasikiahata mara moja.

Basi: Kama utakuwa mtumishi mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi, unatakiwakuchagua sana wale utakaowafundisha, ili usipoteze wakati wako wa thamani sana kwawatu wasiotaka kumtii Yesu. Paulo alimwandikia Timotheo hivi:-

Mambo yale uliyosikia kutoka kwangu mbele ya mashahidi wengi,wewe wakabidhi watu waaminifu, watakaoweza kuwafundisha na wenginepia (2Timo. 2:2 – TLR. Maneno mepesi kukazia).

Kulifikia Lengo

Hebu fikiri kidogo juu ya kitu ambacho kisingetokea katika huduma ya Yesu,kinachotokea kila mara katika makanisa ya kisasa. Tufikiri kwamba, baada ya kufufukaKwake, Yesu alibaki duniani na kuanzisha kanisa kama haya tuliyo nayo, na kulichungakwa miaka thelathini. Hebu fikiri kwamba kila Jumapili aliwahubiria watu wale wale.Fikiri kwamba Petro, Yakobo na Yohana wanaketi kiti cha mbele katika mahubiri hayo,mahali ambapo wameketi kila Jumapili kwa miaka ishirini. Jaribu kupiga picha umwonePetro akimwinamia Yohana na kusema sikioni mwake, “Aa! Tumesikia mahubiri hayahaya mara kumi.”

Tunajua kwamba ni kitu kisichowezekana, maana wote tunafahamu kwambaasingejiweka katika hali kama hiyo, wala kuwaweka mitume Wake. Yesu alikuja kufanyawatu kuwa wanafunzi, kwa namna fulani na katika kipindi fulani. Kwa kipindi cha miakamitatu, alimfundisha Petro, Yakobo na Yohana, na wengine pia. Hakufanya kwa

Page 10: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

kuwahubiria mara moja kila Jumapili katika jengo la kanisa. Alifanya kwa kuishi maishaYake mbele yao, kwa kujibu maswali yao, na kwa kuwapa nafasi ya kutumika. Alimalizakazi Yake akasonga mbele.

Sawa. Sasa, mbona sisi tunafanya kitu ambacho Yesu asingekifanya? Kwa ninitunajaribu kukamilisha kile ambacho Mungu anataka kwa kuwahubiria watu wale walemiaka na miaka? Tutakamilisha lini kazi yetu? Kwa nini wanafunzi wetu – baada yamiaka fulani – hawako tayari kutoka na kuwafanya wengine kuwa wanafunzi wao pia?

Ninachosema ni hiki: Kama tunafanya kazi zetu sawasawa, wakati utafika ambapowanafunzi wetu watakua kiasi cha kutosha kutohitaji huduma yetu. Ikifikia hapo,waruhusiwe kwenda kufanya wengine kuwa wanafunzi. Tunatakiwa kulifikia lengoambalo Mungu ameweka mbele yetu, na Yesu alituonyesha jinsi ya kulifikia. Katikakanisa la nyumbani linalokua, lipo hitaji la kudumu la kuwafanya watu kuwa wanafunzi,na kuzaa viongozi. Kanisa la nyumbani lenye afya halitaingia katika mzunguko wamhubiri huyo huyo kuwahubiria watu hao hao kwa miaka na miaka.

Makusudi Sahihi Ya Moyo

Makusudi sahihi ya moyo ni muhimu sana katika kufanikiwa kufundisha kwa njiaitakayopelekea watu kufanywa kuwa wanafunzi. Mtu anapokuwa katika huduma kwasababu zisizofaa atafanya makosa. Hii ndiyo sababu ya msingi ya kuwepo na mafundishomengi ya uongo na yasiyo na maana katika kanisa siku hizi. Wakati makusudi yamtumishi ni kupata umaarufu, kufanikiwa machoni pa watu, au kujipatia fedha nyingi,anaelekea kwenye kushindwa mbele za Mungu. Cha kusikitisha ni kwamba anawezakufanikiwa kufikia lengo lake la kupata umaarufu, kufanikiwa machoni pa watu, aukutengeneza fedha nyingi tu, lakini siku itafika ambapo makusudi yake mabayayatafunuliwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, naye hatapata thawabu yoyote kwaajili ya kazi yake. Kama ataruhusiwa kuingia katika ufalme wa mbinguni,3 kila mtuatakayekuwepo atajua ukweli juu yake, maana kukosa thawabu kwake na nafasi yake yachini katika ufalme vitadhihirisha hayo. Bila shaka kuna nafasi tofauti tofauti mbinguni.Yesu alionya hivi:-

Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo nakuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wambinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwakatika ufalme wa mbinguni (Mathayo 5:19).

Watumishi wale wanaotii na kufundisha amri za Kristo watateseka kidogo hapaduniani kwa sababu hiyo. Yesu aliahidi mateso kwa watakaomtii (ona Mathayo 5:10-12);Yohana 16:33). Hawataweza kufanikiwa duniani, au kuwa maarufu au kupata mali.Wanachopata ni thawabu za baadaye na sifa kutoka kwa Mungu. Je, wewe ungependakipi? Paulo aliandika hivi kuhusu jambo hili:-

3 Nasema “kama” kwa sababu walio mbwa mwitu waliovaa mavazi ya kondoo ni “watumishi” wenyemakusudi ya ubinafsi. Hao watatupwa jehanamu. Nadhani kinachowatenganisha na watumishi wa kweliwenye makusudi yasiyo sahihi ni kiwango cha kinachowasukuma.

Page 11: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwaomliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apoloakatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, walaatiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye na yeye atiaye majini wamoja, lakini kil amtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa nataabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu;ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wawajenzi mwenye hekima naliuweka msingi, na mtu mwingine anajengajuu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maanamsingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni uleuliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juuya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majaniau manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ileitaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyeweutaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juuyake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ilayeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto (1Wakor. 3:5-15).

Paulo alijilinganisha na mjenzi bingwa mwenye kuweka msingi. Apolo ambaye nimwalimu aliyekuja Korintho baada ya Paulo kuanzisha kanisa hapo analinganishwa namtu ambaye anajenga juu ya msingi uliokwisha wekwa.

Ona kwamba Paulo na Apolo wangepata thawabu mwishowe, kutokana na sifa yakazi yao, siyo wingi wa kazi yao (ona 3:13).

Kimfano ni kwamba Paulo na Apolo wangeweza kujenga jengo la Mungu kwakutumia aina sita tofauti za vifaa – vitatu vya kawaida kabisa na ambavyo si ghali, tenavyepesi kuungua. Vitatu si vya kawaida sana, ni ghali sana, na haviungui kwa urahisi.Siku moja, vitu vyao vya kujengea vingepitia hukumu ya moto wa Mungu, na zile mbao,majani na manyasi vingeteketezwa kwa moto na kudhihirisha sifa yake isiyo ya thamanina ya muda sana. Lakini dhahabu, fedha na mawe ya thamani ambavyo ni mfano wakaziza thamani na za milele mbele za Mungu, vingeshinda kipimocha moto.

Tuwe na uhakika kabisa kwamba mafundisho yasiyo ya KiBiblia yatachomwa nakuteketea kabisa wakati wa hukumu mbele ya Kristo. Hata vitu vingine vyotevitakavyofanywa kwa nguvu, mbinu au hekima ya mwili, pamojana chochotekitakachofanywa kwa makusudi yasiyo mazuri. Yesu alionya kwamba chochotetunachoweza kufanya kitakachotokana na kutaka sifa ya watu hakitapata thawabu(tazama Mathayuo 6:1-6, 16-18). Matendo hayo ambayo si kitu yanaweza yasiwe dhahirimachoni pa watu wakati huu, lakini hakika yatadhihirishwa kwa wote siku za baadaye,kama alivyosema Paulo. Kibinafsi – kama matendo yangu ni miti, majani na manyasi –ningependa kujua sasa kuliko baadaye. Kwa sasa iko nafasi ya kutubu; wakati huohaitakuwepo!

Page 12: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Kukagua Makusudi Yetu

Ni rahisi sasa kujidanganya kwa habari ya makusudi yetu. Hata mimi nimewahikudanganyika. Je, tutajuaje ikiwa makusudi yetu ni safi?

Njia iliyo bora zaidi ni kumwomba Mungu atufunulie ikiwa makusudi yetu nimabaya, kisha kuendelea kufuatilia mawazo yetu na matendo yetu. Yesu alituambiatutende mema kama vile kuomba na kuwasaidia maskini kwa siri. Hiyo ni njia moja yakujihakikishia kwamba tunatenda vema kwa sababu tunatafuta sifa ya Mungu badala yasifa za watu. Kama tutamtii Mungu wakati watu wanapotuona tu, hiyo ni ishara kwambakuna kitu kisicho sawa. Au – kama tutaepuka dhambi mbaya ambazo zitaharibu sifa yetutukigunduliwa, hukmu tunajihusisha na dhambi ndogo ambazo hakuna mtu anayewezakufahamu, hilo linaonyesha kwamba makusudi yetu si mazuri. Ikiwa kweli tunajaribukumpendeza Mungu – anayejua kila wazo letu, neno na tendo – basi tutajitahidi kumtiikila wakati katika mambo makubwa na madogo, mambo yajulikanayo na yasiyojulikanakwa wengine.

Pia, kama makusidi yetu ni sahihi, hatutafuata mitindo ya ukuaji wa kanisa ambayolengo lake ni kuongeza wahudhuriaji tu huku ikipuuza kuwafanya watu kuwa wanafunziwatakaotii maagizo yote ya Kristo.

Tutalifundisha Neno kamili la Mungu badala ya kulenga mada zinazopendwa tu,zenye kuwavutia watu wa kidunia, wasio wa kiroho.

Hatutalibadili Neno la Mungu au kufundisha Maandiko kwa njia yenye kuhalifumantiki yake katika Biblia.

Hatutafuta majina makubwa au nafasi za heshima kwa ajili yetu wenyewe.Hatutatafuta kujulikana.

Hatutawahudumia matajiri tu (au wenye mali) na kujali maslahi yao.Hatutajiwekea hazina duniani, bali tutaishi kwa hali ya kawaida na kutoa kiasi

tunachoweza, na kuwa mfano wa uwakili mwema mbele ya kondoo wetu.Tutajali zaidi Mungu anasema nini juu ya mahubiri yetu kuliko mawazo ya watu.Vipi basi: Makusudi yako yakoje?

Fundisho Lenye Kuharibu Mpango Wa Kufanya Watu Kuwa Wanafunzi

Mtumishi mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi hafundishi chochotekitakachopingana na lengo la kuwafanya watu kuwa wanafunzi. Hivyo, hasemi kituchochote kitakachowafanya watu wajisikie vizuri kuacha kumtii Bwana Yesu. Haelezi juuya neema ya Mungu kama ruhusa ya watu kufanya dhambi bila kuogopa hukumu. Yeyehuelezea juu ya neema ya Mungu kwamba ni njia ya kutubu dhambi na kusaidia kuishimaisha ya ushindi. Kama tujuavyo, Maandiko yanasema kwamba ni washindaji tu ndiyowatakaourithi ufalme wa Mungu. Tazama Ufunuo 2:11; 3:5; 21:7.

Kwa bahati mbaya sana, kuna watumishi wa kisasa ambao wanashikilia mafundishoyasiyo ya KiBiblia, yenye kudhuru sana lengo la kuwafanya watu kuwa wanafunzi.Fundisho moja ambalo limekuwa maarufu sana Marekani ni lile la usalama wa mileleusio na masharti, yaani, “ukiisha okoka, umeokoka milele”. Hili fundisho linasemakwamba watu waliozaliwa mara ya pili hawawezi kupoteza wokovu wao hata kamawataishi maisha ya aina gani. Kwa kuwa wokovu ni kwa neema, neema ile ile yenyekuwaokoa watu wenye kuomba sala ya kupokea wokovu, ndiyo itakayowadumisha.

Page 13: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Wanasema kwamba wazo la namna nyingine ni sawa na kusema watu huokolewa kwamatendo yao.

Msimamo wa aina hiyo ni kikwazo kikubwa sana kwa utakatifu. Kwa kuwa kumtiiKristo si kitu cha lazima kwa mtu kuingia mbinguni, hakuwi na hamasa yoyote ya kumtiiYesu, hasa utii unapokuwa na gharama.

Kama nilivyokwisha kusema mapema, neema ambayo Mungu anawapa wanadamuhaiwaondolei wajibu wa kumtii. Maandiko yanasema kwamba wokovu si kwa neema tu,bali pia kwa imani (tazama Waefeso 2:8). Neema na imani ni vya lazima ili wokovuupatikane. Imani ndiyo itikio sahihi kwa neema ya Mungu, na imani ya kweli sikuzotehusababisha toba na kutii. Imani isiyo na matendo imekufa, haifai, na haiwezi kuokoa.Hayo ni maneno ya Yakobo (ona sura ya 2:14-26).

Hii ndiyo sababu Maandiko yanarudia kusema kwamba kuendelea katika wokovuhutegemea kuendelea katika imani na utii. Yapo Maandiko mengi sana yenye kuwekawazi jambo hilo. Mfano: Paulo anawaambia hivi waamini wa Kolosai:-

Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa tena adui katika niazenu kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa katika mwili wanyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu,wasio na mawaa wala lawama, mkidumu tu katika ile imani, halimmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliachatumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyotevilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake(Wakolosai 1:21-23. Maneno mepesi kukazia).

Yaani – ni wazi mno. Anayeweza kukosa kuelewa maana ya Paulo au kuigeuza nimwana-theolojia tu. Yesu atatuthibitisha bila lawama ikiwa tutaendelea katika imani.Kweli hiyo hiyo inarudiwa katika Warumi 11:13-24; 1Wakor. 15:1-2 na Waebrania 3:12-14; 10:38-39. Inatamkwa waziwazi hapo kwamba wokovu wa mwisho unategemeana nakudumu katika imani. Mafungu hayo yote ya Maandiko yanalo neno ikiwa au kama.

Umuhimu Wa Utakatifu

Je, mwamini anaweza kupoteza wokovu wa milele kwa kutenda dhambi? Jibulinapatikana katika Maandiko mengi sana, kama haya yafuatayo, yenye kuthibitishakwamba wale watendao dhambi fulani fulani hawataurithi ufalme wa Mungu. Kamamwamini atarudia kutenda dhambi zile katika orodha zifuatazo za Paulo, basi anawezakupoteza wokovu.

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme waMungu?Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, walawaabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi,wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi(1Wakor. 6:9-10. Maneno mepesi kukazia).

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya: uasherati, uchafu,ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina,

Page 14: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo kama hayo, katika hayonawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watuwatendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu (Wagalatia5:19-21. Maneno mepesi kukazia).

Maana neno hili mnalijua hakika ya kwamba hakuna mwasherati walamchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithikatika ufalme wa Kristo na Mungu. Mtu asiwadanganye kwa manenoyasiyo na maana; kwa kuwa kuwa sababu ya hayo hasira ya Munguhuwajia wana wa uasi (Waefeso 5:5, 6. Maneno mepesi kukazia).

Ona kwamba katika kila sehemu, Paulo alikuwa anawaandikia waamini, akiwaonya.Mara mbili aliwaonya wasidanganywe, kuonyesha kwamba alijali maana waaminiwengine wangeweza kudhani kwamba mtu anaweza kutenda dhambi zilizotajwa na badoakaurithi ufalme wa Mungu.

Yesu aliwaonya wafuasi wake wa karibu sana – Petro, Yakobo, Yohana na Andrea –juu ya uwezekano wao kutupwa jehanamu kwa sababu yakutokuwa tayari kwa ajili yakurudi Kwake. Ona kwamba wao ndiyo walioambiwa maneno yafuatayo (ktk Marko13:1-4), sio kundi la wasioamini.

Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.Lakini fahamuni neno hili: kama mwenye nyumba angaliijua ile zamumwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliicha nyumba yakekuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi [Petro, Yakobo, Yohana naAndrea] jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani [ninyi akinaPetro, Yakobo, Yohana na Andrea] Mwana wa Adamu yuaja.

Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwanawake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakatiwake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanyahivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakinimtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;akaanza kuwapiga wajoli wake na kula na kunywa pamoja na walevi;bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,atamkata vipande viwili, na kumweka fungu lake pamoja na wanafiki;ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno (Mathayo 24:42-51. Manenomepesi kukazia).

Fundisho la habari hii ni nini? Ni hili: “Petro, Yakobo, Yohana na Andrea – msiwekama mtumwa asiyekuwa mwaminifu katika mfano huu.”4

4 Cha kushangaza ni hiki: Kuna waalimu wengine wanaofundisha kwamba pale kwenye kilio na kusagameno ni eneo fulani nje kidogo ya mbinguni. Wanasema kwamba hapo, waamini wasiokuwa waaminifuwatapewa nafasi ya kuomboleza – kwa muda fulani – kupoteza thawabu kwao, mpaka Yesu atakapowafutamachozi, kisha awakaribishe mbinguni! Wanafundisha hivyo kwa sababu ya kushindwa kuepuka ukwelikwamba Yesu alikuwa anawaonya wanafunzi Wake wa karibu sana, na kwamba mtumwa asiyekuwamwaminifu ni mwamini.

Page 15: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Ili kutilia mkazo kile alichowaambia wanafunzi Wake wa karibu sana, Yesualiendelea kutoa mfano wa Wasichana Wanawali Kumi. Hao wote walikuwa tayari kwaajili ya kuja kwa bwana arusi, lakini watano wakawa hawakujiandaa vizuri, basiwakaikosa ile karamu. Yesu alimalizia mfano wake kwa maneno haya: “Basi kesheni[Petro, Yakobo, Yohana na Andrea]; kwa sababu hamwijui siku wala saa (Mathayo25:13). Yaani, “Petro! Yakobo! Yohana! Andrea! Msiwe kama wale wanawali watanowapumbavu.” Ni hivi: Kama usingekuwepo uwezekano wa Petro, Yakobo, Yohana naAndrea kutokuwa tayari, Yesu asingekuwa na haja ya kuwaonya.

Ndipo Yesu akasimulia mara hiyo hiyo Mfano wa talanta. Ujumbe ulikuwa ni ule ule– “Msiwe kama yule mtumishi wa talanta moja, ambaye hakuwa na kitu chakumwonyesha bwana wake kutokana na mali aliyokabidhiwa, wakati aliporudi.” Mwishowa mfano huo, yule bwana alitamka hivi, “Mtupeni mbali katika giza la nje; ndikokutakuwako kilio na kusaga meno” (Mathayo 25:30). Yesu aliweka wazi kabisa ujumbeWake – hauwezi kuwa wazi kuliko hapo. Anayeweza kubadilisha maana ya ujumbe huoni mwana-theolojia tu – ndiye haelewi! Ni hivi: Ilikuwepo hatari ya Petro, Yakobho,Yohana na Andrea kutupwa jehanamu mwishoni kama wasingekuwa watiifu wakati wakurudi kwa Yesu. Sasa – kama uwezekano huo ulikuwepo kwa ajili ya Petro, Yakobo,Yohana na Andrea, ni kwamba upo hata kwetu wote. Kama alivyoahidi Yesu ni kwamba,wale tu watendao mapenzi ya Baba Yake ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni(ona Mathayo 7:21). 5

Wale wanaofundisha uongo kwamba ukiokoka unalindwa milele bila masharti yoyoteni wafanya kazi kinyume cha Kristo. Wanamsaidia Shetani, wakifundisha kinyume nayale aliyofundisha Yesu na mitume. Wao wanabatilisha kabisa agizo la Yesu kwambawatu wafanye wengine kuwa wanafunzi, watakaoitii yote aliyoamuru. Wanaiziba njia ilenyembamba iendayo mbinguni, na wanaipanua ile njia pana iendayo upotevuni.6

5 Ieleweke kwamba Wakristo watendao dhambi moja hawapotezi wokovu wao saa hiyo hiyo. Walewanaotubu dhambi zao wanasamehewa na Mungu (kama nao watawasamehe wenye kuwakosea). Walewasiomwomba Mungu msamaha wanajiweka katika hatari ya kuadhibiwa na Mungu. Waamini wanawezakupoteza wokovu wao kama wataifanya mioyo yao kuwa migumu, katika kipindi cha kuadhibiwa naMungu.6 Kama bado kuna wasioamini kwamba Mkristo anaweza kupoteza wokovu wake, hebu watazamemaandiko yote yafuatayo katika Agano Jipya: Mathayo 18:21-35; 24:4-5, 11-13, 23-26, 42-51; 25:1-30;Luka 8:11-15; 11:24-28; 12:42-46; Yohana 6:66-71; 8:31-32, 51; 15:1-6; Matendo 11:21-23; 14:21-22;Warumi 6:11-23; 8:12-14, 17; 11:20-22; 1Wakor. 9:23-27; 10:1-21; 11:29-32; 15:1-2; 2Wakor. 1:24; 11:2-4; 12:21 – 13:5; Wagalatia 5:1-4; 6:7-9; Wafilipi 2:12-16; 3:17 – 4:1; Wakolosai 1:21-23; 2:4-8, 18-19;1Wathes. 3:1-8; 1Timo. 1:3-7, 18-20; 4:1-16; 5:5-6, 11-15; 6:9-12, 17-19, 20-21; 2Timo. 2:11-18; 3:13-15;Waebrania 2:1-3; 3:6-19; 4:1-16; 5:8-9; 6:4-9, 10-20; 10:19-39; 12:1-17, 25-29; Yakobo 1:12-16; 4:4-10;5:19-20; 2Petro 1:5-11; 2:1-22; 3:16-17; 1Yohana 2:15-28; 5:16; 2Yohana 6-9; Yuda 20-21; Ufunuo 2:7,10-11, 17-26; 3:4-5, 8-12, 14-22; 21:7-8; 22:18-19. Maandiko “ya kuthibitisha” yatolewayo na wale wenyekufundisha usalama wa milele wa wokovu bila masharti ni yenye kutilia mkazo uaminifu wa Mungu katikawokovu, na wala hayasemi chochote juu ya wajibu wa mwanadamu. Kwa hiyo, lazima yafasiriwe nakulingana na hayo maandiko mengi niliyoorodhesha hapo juu. Ahadi ya Mungu kwamba ni mwaminifu siuhakikisho kwamba na mwingine ni mwaminifu kama Yeye. Kumwahidi mke wangu kwamba sitamwacha,na kuitunza ahadi yangu, si uhakikisho kwamba yeye hataniacha!

Page 16: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Fundisho Lingine La Kisasa Linalopingana Na Mpango Wa Kufanya WatuKuwa Wanafunzi

Si mafundisho ya usalama wa wokovu wa milele bila masharti yoyote tuyanayowadanganya watu kufikiri kwamba utakatifu si muhimu kwa ajili ya wokovu.Upendo wa Mungu mara nyingi unaelezwa kwa njia yenye kubatilisha shughuli yakuwafanya watu kuwa wanafunzi. Mara nyingi wahubiri watasikika wakisema hivi:“Mungu anakupenda bila masharti yoyote.” Watu hutafsiri maneno hayo kuwayanamaanisha hivi: “Mungu ananikubali na kunipokea bila kujali kama ninamtii ausimtii.” Lakini huo si ukweli.

Wahubiri wengi wa aina hiyo pia wanaamini kwamba Mungu huwatupa jehanamuwatu ambao hawajaokoka. Ni sawa kabisa. Sasa hebu tufikiri kidogo juu ya hilo. Ni wazikwamba Mungu hakubaliani na watu anaowatupa jehanamu. Sasa, inawezekanaje basikwamba anawapenda tena? Je, watu wanaotupwa jehanamu wanapendwa na Mungu? Je,unadhani watakwambia kwamba Mungu anawapenda? Hapana. Je, Mungu atasemaanawapenda? Hapana! Wanamchukiza, ndiyo sababu anawaadhibu jehanamu. Nikwamba hakubaliani nao wala hawapendi.

Kama ni hivyo basi, ni kwamba upendo wa Mungu kwa watenda dhambi wa hapaduniani ni wa rehema ambao ni wa muda tu. Si upendo wenye kukubali mtu.Anawarehemu kwa kuchelewesha hukumu Yake na kuwapa nafasi ya kutubu. Yesualikufa kwa ajili yao na kutengeneza njia ya wao kusamehewa. Kwa hali hiyo na njiahiyo tunaweza kusema Mungu anawapenda. Lakini hakubaliani na hali yao. Hajisikiiupendo kwao kama baba anavyojisikia kwa mtoto wake. Maandiko yanatangaza hivi juuya jambo hili: “Kama baba anavyowahurumia watoto wake, ndivyo na Bwana alivyo nahuruma kwa wale wamchao” (Zaburi 103:13 – maneno mepesi kukazia). Basi, tunawezakusema kwamba Mungu hana huruma ile ile kwa watu wasiomcha Yeye. Upendo waMungu kwa wenye dhambi unalingana na huruma ambayo hakimu anaweza kuonyeshakwa mwuaji anayehukumiwa kifungo cha maisha badala ya kunyongwa.

Hatusomi popote katika Matendo ya Mitume kwamba mhubiri alihubiri Injili nakusema kwa watu wasio-okoka kwamba Mungu anawapenda. Wahubiri wa KiBibliamara nyingi walionya wasikilizaji wao kuhusu ghadhabu ya Mungu na kuwataka watubu,na kuwajulisha kwamba Mungu hakuwa anakubaliana na hali zao, na kwamba walikuwahatarini, na kwamba walihitaji kufanya mabadiliko makubwa sana maishani mwao. Kamawangewaambia wasikilizaji wao kwamba Mungu aliwapenda (kama ambavyo wahubiriwengi wa siku hizi wanavyofanya), wangewapotosha wasikilizaji wao kufikiri kwambahawako katika hatari aina yoyote, kwamba hawakuwa wanajikusanyia ghadhabu, nakwamba hawakuwa na haja ya kutubu.

Mungu Anavyowachukia Wenye Dhambi

Tofauti na jinsi inavyotangazwa siku hizi kwamba Mungu anawapenda wenyedhambi, Maandiko yanasema mara nyingi sana kwamba Mungu anachukia wenyedhambi.

Page 17: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; unawachukia wotewatendao ubatili. Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humziramwuaji na mwenye hila (Zaburi 5:5-6. Maneno mepesi kukazia).

BWANA humjaribu mwenye haki; bali nafsi yake humchukia asiyehaki, na mwenye kupenda udhalimu (Zaburi 11:5. Maneno mepesikukazia).

Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenziwangu katika mikono ya adui zake. Urithi wangu umekuwa kwangu kamasimba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyonimemchukia (Yeremia 12:7-8. Maneno mepesi kukazia).

Uovu wao wote u katika Gilgali; maana huko naliwachukia; kwasababu ya uovu wa matendo yao nitawafukuza watoke katika nyumbayangu; sitawapenda tena; wakuu wao wote ni waasi (Hosea 9:15. Manenomepesi kukazia).

Angalia mistari yote hiyo – haisemi kwamba Mungu anachukia matendo ya watu tu.Inasema anawachukia hata watu wenyewe. Hii inaweka wazi ule usemi wa kisasakwamba Mungu anampenda mwenye dhambi bali anachukia dhambi yake. Hatuwezikumtengansiha mtu na kile anachofanya. Anachofanya hudhirisha alivyo. Kwa hiyo,Mungu anawachukia watu watendao dhambi, si dhambi tu watu wanazotenda. KamaMungua nawakubali watu wanaofanya kile anachochukia, basi hana msimamo. Katikamahakama za kibinadamu watu hufikishwa mbele ya sheria kwa ajili ya makosa yao, naowanapokea ijara inayostahili. Hatuchukii uhalifu na kuwakubali wanaoufanya.

Watu Ambao Mungu Anawazira

Maandiko yanafundisha kwamba Mungu anawachukia watu fulani. Pia, yanatangazakwamba Mungu anawazira wenye dhambi wa aina fulani – yaani, ni chukizo Kwake.Angalia tena maandiko yafuatayo, uone kwamba hayasemi yanayotendwa na watu haokuwa ni chukizo kwa Mungu, bali kwamba wao wenyewe ni chukizo kwa Mungu.Hayasemi kwamba Mungu anazira dhambi zao, bali kwamba Mungu anawazira wao.7

Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, walamwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyayemambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako (Kumbu. 22:5.Maneno mepesi kukazia).

7 Hoja inaweza kutolewa kwamba maandiko hayo yote yenye kuonyesha chuki na Mungu kuwazira wenyedhambi yanatoka katika Agano la Kale. Ni sawa, lakini hali ya moyo ya Mungu kuhusu wenye dhambihaitofautiani katika Agano la Kale na katika Agano Jipya. Yesu alipokutana na mwanamke Mkanaanikatika Mathayo 15:22-28 ni mfano mzuri katika Agano Jipya. Mwanzoni, Yesu alikataa hata kujibu kiliochake, akamwita mbwa. Imani yake isiyokata tamaa ilisababisha Yeye kumwonyesha rehema kiasi fulani.Hali ya moyo aliyokuwa nayo Yesu kuhusu waandishi na Mafarisayo haiwezi kuhesabiwa kwamba ilikuwaupendo wenye kuwakubali (ona Mathayo 23).

Page 18: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendaoyasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako (Kumbu. 25:16.Maneno mepesi kukazia).

Nanyi mtakula nyama ya miili ya wana wenu, na nyama ya miili yabinti zenu mtaila. Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, nakuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu yamizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia (Walawi 26:29-30.Maneno mepesi kukazia).

Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; unawachukia wotewatendao ubatili. Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humziramwuaji na mwenye hila (Zaburi 5:5-6. Maneno mepesi kukazia).

Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA, bali siri yake ni pamojana wanyofu (Mithali 3:32. Maneno mepesi kukazia).

Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA; walio wakamilifukatika njia zao humpendeza (Mithali 11:20. Maneno mepesi kukazia).

Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; hakikahatakosa adhabu (Mithali 16:5. Maneno mepesi kukazia).

Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemay ekwambamwenye haki hana haki; hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA(Mithali 17:15. Maneno mepesi kukazia).

Sasa, tuowanisheje maandiko kama hayo na yale yanayosema kuhusu upendo waMungu kwa wenye dhambi? Inawezekanaje kusema kwamba Mungu anawachukia nakuwazira wenye dhambi, lakini tena anawapenda?

Lazima tutambue kwamba upendo haufanani. Kuna upendo ambao hauna masharti.Huo unaweza kuitwa “upendo wenye rehema”. Ni upendo unaosema hivi: “Nakupendalicha ya”. Unawapenda watu licha ya matendo yao. Upendo aina hiyo ndiyo Mungu anaokwa wenye dhambi.

Kinyume cha huo ni ule mwingine – upendo wa masharti. Huu unaweza kuitwa“upendo unaokubali”. Ni upendo unaopatikana kwa kazi au matendo. Ni upendounaosema hivi: “Ninakupenda kwa sababu ya.”

Kuna wanaodhani kwamba upendo ukiwa wa masharti, si upendo. Au, wanaupuuzia,wakisema kwamba ni wa kibinafsi sana – kichoyo – tena, haulingani na upendo waMungu.

Lakini, ukweli ni kwamba Mungu ana upendo wa masharti, kama tutakavyoona hivikaribuni tu katika Maandiko. Basi, upendo unaokubali usipuuzwe. Upendo unaokubalindiyo upendo wa msingi ambao Mungu anao kwa watoto Wake wa kweli. Tunatakiwakutamani zaidi upendo unaokubali wa Mungu kuliko ule wa rehema.

Page 19: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Je, Upendo Unaokubali Ni Upendo Wa Hali Ya Chini?

Hebu jiulize swali hili: “Ningependa watu wanipende upendo aina gani – wa hurumaau wa kukubali?” Nina hakika ungependa watu wakupende “kwa sababu ya,” badala yakukupenda “licha ya”.

Je, ungefurahia kusikia mwenzako akisema hivi: “Sina sababu ya kukupenda, nahakuna chochote kwako kinachonihamasisha nionyeshe kukujali”? Au ungependa kusikiahivi: “Ninakupenda kwa sababu nyingi sana, maana kuna mambo mengi juu yakoninayofurahia”? Nadhani tungependa wenzetu watupende kwa upendo unaokubali. Huondio upendo wa msingi unaowavutia wenzi kuwa pamoja, na kuwafanya waendelee kuwapamoja. Wakati kinapokosekana chochote ambacho mtu anakipenda kwa mwenzake,wakati upendo unaokubali unapomalizika, ndoa hazidumu. Zikidumu, ni kwa sababu yaupendo wa rehema, ambao unatokana na asili ya utauwa ya yule mwenye kuutoa upendohuo.

Basi, mambo ni hayo. Tunaona kwamba upendo unaokubali – au, wenye masharti, siupendo wa hali ya chini hata kidogo. Japo upendo wa kurehemu ndiyo unaosifika naunaopaswa kutolewa, upendo unaokubali ndiyo unaostahili kupatikana. Tena, ukwelikwamba upendo unaokubalika ndiyo upendo pekee ambao Baba alikuwa nao kwa Yesu,unaufanya uwe na nafasi yake ya kipekee na ya heshima. Mungu Baba hakuwahi kuwana tone la upendo wa rehema kwa Yesu, kwa sababu hakukuwa na chochote kibaya ndaniya Kristo. Yesu alishuhudia mwenyewe, hivi:

Kwa sababu hii, Baba ananipenda, kwa kuwa nautoa uhai wangu,kisha naweza kuutwaa tena (Yohana 10:17 – TLR. Maneno mepesikukazia).

Basi tunaona kwamba Baba alimpenda Yesu kwa sababu ya utii wake kukubali kufa.Upendo unaokubali unadai kila kitu kiwe sawa. Yesu alipata na kustahili upendo waBaba Yake.

Pia, Yesu alitamka kwamba alikaa katika pendo la Baba Yake kwa kuzishika amri zaBaba Yake.

Kama Baba alivyonipenda mimi, mimi nami nimewapenda ninyi.Kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendolangu; kama mimi nilivyoshika amri za Baba yangu na kukaa katika pendoLake (Yohana 15:9-10, TLR. Maneno mepesi kukazia).

Tena, kama tunavyoona katika mstari huu, tunatakiwa kufuata mfano wa Yesu nakukaa katika pendo Lake kwa kuzishika amri Zake. Anazungumza kuhusu upendounaokubali katika fungu hili, na anatuambia kwamba tunaweza na tunapaswa kupataupendo Wake. Tena, kwamba tunaweza kujiondoa katika pendo Lake kwa kutokutii amriZake. Tunadumu katika upendo Wake kama tutashika amri Zake tu. Kitu kama hichohakifundishwi sana siku hizi, lakini kinapaswa kufundishwa, maana ndiyo aliyosemaYesu.

Yesu alithibitisha upendo unaokubali wa Mungu kwa wale tu wanaozishika amriZake, hivi:

Page 20: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

Kwa sababu Baba Mwenyewe anawapenda, kwa kuwa mmenipendaMimi na kuamini kwamba nilitoka kwa Baba (Yohana 16:27, TLR.Maneno mepesi kukazia).

Yeye aliye na amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye; nayeanipendaye atapendwa na Baba yangu. Mimi pia nitampenda nakujidhihirisha kwake … Mtu yeyote akinipenda, atashika maneno Yangu;na Baba Yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetupamoja naye (Yohana 14:21, 23, TLR. Maneno mepesi kukazia).

Ona katika fungu la pili kwamba Yesu hakuwa anatoa ahadi kwa waaminiwasiojitolea Kwake, kwamba, kama wangeanza kuyashika maneno Yake, angewakaribiakwa njia ya kipekee sana. Hapana! Yesu alikuwa anaahidi kwamba kama mtu yeyoteangeanza kumpenda Yeye na kuyashika maneno Yake, basi Baba Yake angempenda mtuhuyo, na wote wawili – Yeye na Baba – wangekuja kukaa katika mtu huyo, ambayo ninjia nyingine ya kusema kwamba amezaliwa mara ya pili. Kila mtu aliyezaliwa mara yapili anaye Baba na Mwana ndani yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu (tazama Warumi8:9). Basi, hapo tena tunaona kwamba wale waliozaliwa upya kweli kweli ni wale wenyekutubu na kuanza kumtii Yesu, nao ndiyo watakaoweza kupata ule upendo unaokubali,wa Baba.

Bado Yesu anao ule upendo wa rehema kwa ajili ya watakaomwamini. Wanapoachakumtii, Yeye yuko tayari kuwasamehe kama watakiri dhambi zao na kuwasamehewengine.

Hitimisho

Kinachosemwa ni hiki: Mungu hawapendi watoto Wake watiifu kwa namna ile ileanayowapenda wenye dhambi. Anawapenda wenye dhambi kwa upendo wa rehema tu,na upendo huo ni wa muda, unaodumu mpaka wanapokufa. Wakati huo huoanapowapenda kwa upendo wa rehema, anawachukia kwa chuki itokanayo na kutokubalitabia na mwenendo wao. Hayo ndiyo mafundisho ya Maandiko.

Kwa upande mwingine ni kwamba, Mungu anawapenda watoto Wake zaidi kulikowale ambao hawajazaliwa mara ya pili. Kimsingi, anawapenda kwa upendo unaokubalikwa sababu wametubu na wanajitahidi kutii amri Zake. Wanapokua katika utakatifu,sababu ya kuwapenda kwa upendo wa rehema zinapungua, na sababu za kuwapenda kwaupendo unaokubali zinaongezeka, na ndicho wanachotaka.

Vile vile tunachoona hapa ni kwamba jinsi wahubiri wengi wa kisasa na waalimuwanavyoonyesha upendo wa Mungu si sahihi. Kulingana na kinachosemwa na Maandiko,hebu tafakari kidogo semi hizi za kawaida kuhusu upendo wa Mungu.

1) Hakuna chochote unachoweza kufanya kitakachomfanya Mungu akupendezaidi au pungufu ya anavyokupenda sasa hivi.2) Hakuna chochote unachoweza kufanya kitakachomfanya Mungu aache

kukupenda.3) Upendo wa Mungu hauna masharti.

Page 21: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziHebu tuonyeshe kanuni hii ya kufundisha kwa njia ya mfano kuhusu mada moja muhimu sana: umoja. ... matumaini ya kufanikiwa katika utume wake kama

4) Mungu anampenda kila mtu sawasawa.5) Mungu anampenda mwenye dhambi, lakini anachukia dhambi yake.6) Hakuna chochote unachoweza kufanya ili upate au kustahili upendo wa

Mungu.7) Upendo wa Mungu kwetu hautegemei tunavyotenda.

Hayo yote yaliyosemwa hapo juu yanaweza kukupotosha au ni uongo kabisa, maanasehemu kubwa inakataa moja kwa moja upendo wa kukubali wa Mungu, na mengiyanaeleza vibaya upendo wa rehema wa Mungu.

Kuhusu la kwanza – Kuna kitu waamini wanachoweza kufanya kitakachomfanyaMungu awapende na kuwakubali zaidi: wawe watiifu zaidi. Na kuna kitu wanachowezakufanya ili kumfanya Mungu asiwapende sana na kuwakubali: waache kutii. Kwa wenyedhambi, kuna kitu wanachoweza kufanya kitakachomfanya Mungu awapende zaidi:watubu. Kisha wangejipatia upendo wa kukubalika wa Mungu. Na kuna kituwanachoweza kufanya kitakachomfanya Mungu asiwapende zaidi: kufa. Hapo watakuwawamepoteza upendo wa pekee ambao Mungu alikuwa nao kwa ajili yao – yaani, upendowa rehema.

Kuhusu la pili – Mkristo anaweza kupoteza upendo wa kukubalika na Mungu kwakurudia dhambi – kujiweka katika nafasi ya kupokea upendo wa rehema tu wa Mungu.Tena, asiyeamini angeweza kufa, na hilo lingekomesha upendo wa rehema wa Mungu,ambao ndiyo pekee alikuwa nao kwa ajili yake.

Kuhusu la tatu – Upendo wa kukubalika wa Mungu ni wa masharti. Na hata upendowa rehema wa Mungu ni wa masharti kwamba mtu awe hai kimwili. Baada ya kifo,upendo wa rehema wa Mungu unakoma. Basi, ni wa masharti kwa sababu ni wa muda tu.

Kuhusu la nne – Ni kweli kwamba Mungu hawapendi wote kwa kiwangokinachofanana, kwa sababu wote – wenye dhambi na watauwa – anawakubali aukuwakataa kwa kiwango fulani. Ni kweli kwamba upendo wa Mungu haufanani kwawenye dhambi na watakatifu.

Kuhusu la tano – Mungu anawachukia wenye dhambi pamoja na dhambi zao.Ingekuwa afadhali kusema kwamba anawapenda wenye dhambi kwa upendo wa rehemana anachukia dhambi zao. Kwa habari ya upendo wa kukubali, anawachukia.

Kuhusu la sita – Mtu yeyote anaweza na anapaswa kupata upendo wa kukubalika naMungu. Ila, hakuna awezaye kuupata upendo wa rehema, maana wenyewe haunamasharti.

Kuhusu la saba – Upendo wa rehema wa Mungu hautokani na matendo, bali ule wakukubalika unategemea matendo.

Yote hayo ni kwa sababu hii: Mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi anapaswakueleza upendo wa Mungu kwa usahihi, kama unavyoelezwa katika Biblia, kwa sababuhataki mtu yeyote adanganywe. Ni watu ambao Mungu anawapenda kwa kuwakubali tundiyo watakaoingia mbinguni, na Mungu anawapenda na kuwaubali wale waliozaliwamara ya pili, na wenye kumtii Yesu. Mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzikamwe asifundishe kitu kinachoweza kuwafanya watu waondoke kwenye utakatifu.Lengo lake ni sawa na lile la Mungu – kuwafanya wanafunzi watakaotii amri zote zaKristo.