miaka 50 bk - assets.thalia.media

15
MIAKA HAMSINI KISWAHILI NCHINI KENYA WAHARIRI: Inyani Simala | Leonard Chacha | Miriam Osore YA

Upload: others

Post on 16-Oct-2021

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: miaka 50 bk - assets.thalia.media

MIAKA HAMSINI

MIAKA HAM

SINI

KISWAHILI NCHINI KENYA

KISWAH

ILI NCHINI KENYA

WAHARIRI: Inyani Simala | Leonard Chacha | Miriam Osore

Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya ni mkusanyiko wa makala yaliyowasilishwa katika kongamano la kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) mwaka 2013, na likafanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA). Makala chache zimetokana na kongamano la mwaka 2012 lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Kitabu hiki kinadhihirisha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali za jamii. Kwa hiyo, utapata humu ndani makala yanayoangazia ufundishaji wa lugha ya Kiswahili; Kiswahili kama nyenzo ya maendeleo ya uchumi wa taifa; mchango wa Kiswahili katika kuleta uwiano na utangamano wa kitaifa; utafiti wa Kiswahili katika lugha na fasihi; Kiswahili na ujenzi wa taswira ya mwanamke; fasihi ya watoto katika Kiswahili; na athari za Sheng kwa Kiswahili. Kwa ufupi makala yaliyomo humu yanashadidia maendeleo ya Kiswahili katika miaka hamsini iliyopita nchini Kenya.

Hiki ni kitabu muhimu sana kwa wanafunzi na walimu wa Kiswahili. Pia ni kitabu kitakachomnufaisha yeyote anayependa Kiswahili na anayetambua mchango wake katika jamii.

YA

YA

Page 2: miaka 50 bk - assets.thalia.media

MIAKA HAMSINI YA KISWAHILI

NCHINI KENYA

Page 3: miaka 50 bk - assets.thalia.media
Page 4: miaka 50 bk - assets.thalia.media

MIAKA HAMSINI YA KISWAHILI

NCHINI KENYA

WAHARIRI: Inyani Simala • Leonard Chacha • Miriam Osore

Page 5: miaka 50 bk - assets.thalia.media

Kimechapishwa na:

Twaweza CommunicationsJumba la Twaweza, Barabara ya ParklandsMpesi LaneS.L.P. 66872 - 00800Nairobi, KenyaSimu: +(254) 020 269 4409; 0729 427740Barua pepe: [email protected]: www.twawezacommunications.org

© Haki ya kunakili ni ya Twaweza Communications na CHAKITA-Kenya

Chapa ya kwanza 2014

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupiga chapa, kutafsiribila idhini ya Twaweza Communications na CHAKITA-Kenya.

ISBN 978 9966 028 48 8

Kimeruwazwa na Catherine BosireJalada limesanifiwa na Kolbe Press

Kimepigwa chapa na Franciscan Kolbe PressS.L.P. 468-00217 Limuru, KenyaBaruapepe: [email protected]

Page 6: miaka 50 bk - assets.thalia.media

YALIYOMO v

Yaliyomo

DIBAJI ............................................................................................................................ vii

SHUKRANI .................................................................................................................... ix

WAANDISHI WA MAKALA ......................................................................................... x

UTANGULIZI .............................................................................................................. xiii

SHAIRI ......................................................................................................................... xxii

SEHEMU 1: MIAKA HAMSINI YA LUGHA NCHINI KENYAMiaka Hamsini ya Ujenzi wa Taswira ya Mwanamke katikaUshairi wa Kiswahili Nchini Kenya ............................................................................. 3Clara Momanyi

Miaka Hamsini ya Fasihi ya Watoto katika KiswahiliNchini Kenya: Maendeleo na Changamoto ............................................................... 16Pamela Y.M. Ngugi

Kwa Miaka Hamsini Sheng Imekitunza Kiswahili au Imekiua? ........................... 34Peter Githinji

SEHEMU 2: UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA KISWAHILIUfundishaji wa Kiswahili Ughaibuni: Maendeleo na Changamoto ...................... 53Kiarie Njogu

Ufundishaji wa Kiswahili Sekondari: Nafasi na Changamoto zaVitabu vya Kiada ........................................................................................................... 71Ombito Elizabeth Khalili na Mamai Margaret Nasambu

Ufundishaji wa Kiswahili katika Nchi za Kigeni: Mfano waChuo Kikuu cha Syracuse ............................................................................................ 80Miriam Osore na Brenda Midika

Changamoto za Kujifunza Kirai Nomino cha Kiswahili Miongonimwa Wanafunzi: Mchango wa Vitabu vya Kozi Vilivyoidhinishwa .................... 93Leah Mwangi, Leonard Chacha Mwita na Jacktone O. Onyango

Page 7: miaka 50 bk - assets.thalia.media

SEHEMU 3: KISWAHILI KAMA NYENZO YA MAENDELEO YAUCHUMI WA TAIFAKiswahili kama Lugha ya Mawasiliano katika Shughuli za Benki:Changamoto za Tafsiri ................................................................................................ 107Jacktone O. Onyango

Nafasi ya Kiswahili katika Utekelezaji wa Rajua 2030:Tathmini ya Kipindi cha Awali 2008 – 2012............................................................. 113Sheila Ali Ryanga

SEHEMU 4: KISWAHILI, UWIANO WA KITAIFA NA UTANGAMANODhima ya Methali za Kiswahili katika Kuelimisha Jamii KuhusuUwiano na Utangamano wa Kitaifa ......................................................................... 133Joseph Nyehita Maitaria

Miziki ya Kiswahili kama Chombo cha Kuhimiza Uwajibikaji katika Jamii:Nyimbo za Mbaraka Mwaruka Mwinshehe ........................................................... 151Henry Indindi

Methali za Kiswahili kama Chombo cha Kusuluhisha Migogoro yaKijamii ........................................................................................................................... 163Joseph Nyehita Maitaria

SEHEMU 5: UTAFITI WA KISWAHILI: LUGHA NA FASIHINajivunia Kuwa Mkenya: Utosarufi, Mtindo au Mabadiliko ya Lugha? ........... 179Leonard Chacha Mwita

Je, Sheng ni Lahaja ya Kiswahili? Nadharia ya Utambulisho wa Maana ........... 188Ayub Mukhwana

Tathmini ya Tafsiri ya Pendekezo la Katiba ya Kenya 2010 .................................. 201Grace Wanja na Miriam Osore

Tafsiri ya Majina ya Pekee – Uchunguzi Kifani wa Majina ya Nchi .................... 220Leonard Chacha Mwita

Lugha –Ishara Nchini Kenya: Katiba na Mustakabali Wake Kisera .................... 242Inyani K. Simala

UHAKIKI WA KITABUSiri Sirini: Mshairi na Mfungwa. Kitabu cha 1 ........................................................ 261Ombito Elizabeth Khalili

vi miaka hamsini ya kiswahili nchini kenya

Page 8: miaka 50 bk - assets.thalia.media

dibaji vii

DIBAJI

Tangu taifa la Kenya kupata uhuru mnamo Disemba 12, 1963 kumekuwa nahatua nyingi zilizopigwa ili kuimarisha Kiswahili kama lugha yautambulisho wa utaifa na kujenga hisia za uzalendo. Baadhi ya hatua hizozinaonekana katika mfumo wa elimu ambapo Kiswahili hufundishwa nakutanihiwa shuleni na vyuoni. Kiswahili pia hutumiwa bungeni na katikabiashara mbalimbali. Umilisi wa lugha hii miongoni mwa umma unatiamoyo. Watu wengi wa makamo huongea Kiswahili kwa ufasaha kulikoilivyokuwa siku za nyuma na mielekeo hasi kuhusu lugha yetu ya taifainaendelea kupungua. Jambo la kutia moyo zaidi ni kwamba hivi majuzi,Katiba ya Kenya katika Ibara ya Saba imeipa lugha hii hadhi kubwa kamalugha ya taifa na rasmi. Hadhi hii inatoa fursa kwa umma kupata hudumukupitia lugha ya taifa. Lakini inabidi sasa pawekwe mikakati madhubuti yakutekeleza agizo hili la kikatiba. Watetezi wa Kiswahili, kwa ushirika naWizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa, wako mbioni kuhamasisha ummakuhusu umuhimu wa Sera ya Lugha za Kenya. Uti wa sera hiyo ni fursailiyopewa Kiswahili. Tunatumaini kwamba Wizara itakamilisha Sera yaLugha na kuhimiza bunge ipitishe Sheria ya utekelezaji wa sera hiyo.Tungetaka kuona lugha ya Kiswahili ikitumika serikalini, bungeni,mahakamani na katika shughuli za kijamii. Hii ndiyo lugha inayowezakujenga uwiano na utangamano wa kitaifa.

Ni kutokana na hisia hizi ambapo Chama cha Kiswahili cha Taifa (Kenya)kwa ushirika na Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha AfrikaMashariki, walijumuika kwa furaha katika Kongamano la kuadhimishamiaka 50 ya Kiswahili Nchini Kenya. Katika Kongamano hilo, tulifikiamaamuzi yaliyoonyesha namna tunavyoweza kuimarisha Kiswahili nchiniKenya na katika ukanda wa Afrika Mashariki. Penye nia pana njia. Tuna niaya kuifanya lugha ya Kiswahili nyenzo ya maendeleo katika ukanda huu.Uundaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki uliidhinishwa naBaraza la Mawaziri mnamo 2007. Hata hivyo baadhi ya mataifa yalichelewakutia saini itifaki ya Kamisheni. Jamhuri ya Tanzania ilitia saini mnamoJulai 19, 2010, Jamhuri ya Uganda mnamo Septemba 12, 2013 na Jamhuri ya

Page 9: miaka 50 bk - assets.thalia.media

Burundi ziliafiki itifaki zote zilizokuwa zimetiwa saini. Kamisheni itakuwana kikao chake Zanzibar na tunatarajia kwamba itaanza kufanya kazi mnamoJulai 2014.

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa baadhi ya makala zilizowasilishwa katikakongamano la 2013. Wahariri wamejitahidi kuzipanga mada hizo ilikuendeleza mada za msingi zilizojadiliwa. Sina shaka kwamba kitabu hikikitatoa ndaro kwa masuala mbalimbali na ufumbuzi wake.

Prof. Kimani Njogu, Ph.D.MwenyekitiChama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) – KenyaFebruari, 2014

viii miaka hamsini ya kiswahili nchini kenya

Page 10: miaka 50 bk - assets.thalia.media

shukrani ix

SHUKRANI

Kitabu hiki ni zao la makala zilizowasilishwa katika Kongamano la Kimataifala Kiswahili – CHAKITA lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki chaAfrika Mashariki Agosti 21 – 23, 2013. Upeo mkubwa wa ufanisi wakongamano hilo, ikiwa ni pamoja na kuchapishwa kwa kitabu hiki, ulitokanana msaada kutoka kwa mashirika mbalimbali kama Longhorn Publishers,Goethe Institute, Catholic University of Eastern Africa, Nation Media Group,Oxford University Press, Twaweza communications na Jomo KenyattaFoundation. Mbali na mashirika hayo, wanachama wa kamati andalizi,Kamati kuu ya CHAKITA na washiriki wote wa kongamano hilo wanahitajikutolewa shukrani kwa juhudi zao na pia mchango wao wa hali na mali.

Page 11: miaka 50 bk - assets.thalia.media

WAANDISHI WA MAKALA

Githinji, Peter: Profesa Mshirikishi wa Lugha za Kiafrika na Mkuuwa Idara ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Ohio,Marekani.

Maitaria, Joseph N.: Mhadhiri katika Idara ya Kiswahili na Lugha zaKiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Mamai, Margaret N.: Mwalimu mkuu wa Shule ya Wasichana ya Lugulu,Bungoma. Ana shahada ya Uzamili katika Taalumaya Elimu ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia cha Masinde Muliro.

Midika, Brenda: Mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika Idara yaKiswahili na Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuucha Kenyatta.

Momanyi, Clara: Profesa na Mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili katikaChuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki.

Mukhwana, Ayub: Mhadhiri katika Idara ya Isimu na Lugha za Kiafrikakatika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mwangi, Leah: Mwalimu katika Shule ya Upili ya Passenga, Kauntiya Nyandarua. Ana shahada ya uzamili kutoka ChuoKikuu cha Kenyatta.

Mwita, Leonard C.: Mhadhiri katika Idara ya Kiswahili na Lugha zaKiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Osore, Miriam: Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Kiswahili naLugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Ombito, Elizabeth K.: Mwalimu anayesomea shahada ya uzamifu katikaTaaluma ya Teknololojia ya Mawasiliano ya Kielimu,Chuo Kikuu cha Moi.

x miaka hamsini ya kiswahili nchini kenya

Page 12: miaka 50 bk - assets.thalia.media

Onyango, Jacktone: Mhadhiri katika Idara ya Kiswahili na Lugha zaKiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Ngugi, Pamela: Mhadhiri katika Idara ya Kiswahili na Lugha zaKiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Njogu, Kiarie: Profesa na mkuu wa Idara ya Kiswahili katika ChuoKikuu cha Yale, Marekani.

Ryanga, Sheila A.: Profesa na Mkurugenzi wa Bewa la Mombasa katikaChuo Kikuu cha Kenya Methodist.

Simala, Inyani K.: Profesa katika Idara ya Elimu ya Lugha na Fasihikatika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia chaMasinde Muliro.

Wanja, Grace: Mhadhiri katika Chuo cha Walimu cha Egoji. Anashahada ya uzamili (Kiswahili) kutoka Chuo Kikuucha Kenyatta.

waandishi wa makala xi

Page 13: miaka 50 bk - assets.thalia.media
Page 14: miaka 50 bk - assets.thalia.media

UTANGULIZI

Kitabu hiki ni zao la kongamano la kimataifa la Kiswahili – CHAKITAlililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki mnamoAgosti 21 – 23, 2013. Mada kuu ya kongamano ilikuwa Miaka Hamsini yaKiswahili Nchini Kenya: Tumejifunza Nini? Kwenye kongamano hilo, makalazenye mada ndogondogo anuwai zilitolewa. Baadhi ya makala hizo ndizozimeunda sehemu mbalimbali za kitabu hiki. Kwa jumla, kitabu hiki kinasehemu sita ambazo zinaingiliana na mada ndogo za kongamano hili.

Kwanza, kitabu kinaanza kwa shairi lenye anwani Tukipende Kiswahili.Shairi hili lilitungwa na Nuhu Bakari na lilitongolewa wakati wa ufunguziwa kongamano lenyewe. Shairi hili linawahimiza wanaCHAKITA naWakenya kwa ujumla kukipenda Kiswahili ili waangamize ukabila ambaoumeisakama nchi ya Kenya.

Sehemu ya kwanza inazo makala tatu ambazo zinaangazia miakahamsini ya lugha ya Kiswahili nchini Kenya. Makala ya kwanzainayozungumzia miaka hamsini ya taswira ya mwanamke katika ushairi waKiswahili nchini Kenya imeandikwa na Clara Momanyi. Anaonyesha kuwabaada ya Kenya kujipatia uhuru mnamo mwaka wa 1963, kumekuwa namaendeleo makubwa ya uandishi wa mashairi yanayosawiri hali namiktadha mbalimbali. Taswira ya mwanamke katika tungo hizi imeendeleakubadilika kutegemea mabadiliko ya kiitikadi yanayochochewa na hali halisiza kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na hata kisiasa. Matilaba ya makala hayani kujadili na kutathmini mitazamo na rai za baadhi ya washairi ili kubainishamchango wao ama katika utetezi au udunishaji wa mwanamke nchini Kenyatangu uhuru. Kutokana na upana wa mada yenyewe, wasilisho limejikitakatika uchunguzi wa baadhi tu ya tungo zinazomsawiri mwanamke. Hivyo,ni washairi wachache ambao kazi zao zimerejelewa ili kubaini vichocheoambavyo huenda vinachangia mabadiliko tuyapatayo katika tungo zawasanii hao. Waaidha, makala yameangazia kwa ufupi mustakabali wautanzu huu katika dahari hizi, hususan mchango wake katika maendeleo yamwanamke.

utangulizi xiii

Page 15: miaka 50 bk - assets.thalia.media

Naye Pamela Ngugi amejaribu kuonyesha kuwa mafanikioyanayobainika sasa katika fasihi ya watoto yanatokana na mifumo mitatumikuu ya kihistoria; mfumo wa kabla ya uhuru, wakati wa uhuru na baadaya uhuru. Mifumo hii imeathiri maendeleo ya fasihi ya watoto kwa njiambalimbali. Anaonyesha kuwa lengo la makala hii ni kuichanganua mifumohii kwa kubainisha jinsi ilivyoathiri maendeleo ya fasihi ya watoto katikaKiswahili nchini Kenya. Makala imejaribu kuonyesha namna kitengo hikicha fasihi kimepokelewa na jamii kupitia upatikanaji wa vitabu vya kusoma,ufunzaji wake katika viwango mbalimbali vya elimu pamoja na tafiti ambazozimefanywa katika eneo hili. Mwisho, makala imeangazia changamotozinazokumba utanzu huu wa fasihi na namna changamoto hizi zinavyoathirimaendeleo yake kwa ujumla.

Makala nyingine katika sehemu hii ya kwanza ni ile iliyoandikwa naPeter Githinji ambaye anatathmini mchango na athari za Sheng’ katikakukuza au ‘kukiua’ Kiswahili. Anasema kuwa kwa muda mrefu, wateteziwa Kiswahili wamekuwa wakilalamika kwamba msimbo wa Sheng nikikwazo kikubwa katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili, hasa katikamaeneo ya mijini ambako msimbo huu umetia fora. Katika makala hii, anadaikwamba kusambaa kwa Sheng hakukihatarishi Kiswahili, ila sera zetu naufundishaji wetu wa Kiswahili ndio wenye kasoro. Pia anajadili jinsi Shengimechangia katika kuendeleza matumizi ya Kiswahili katika mikatadhaambayo ingetwaliwa na Kiingereza au lugha za kiasili. Anarejelea historiaya chimbuko la msimbo huu iliyoanza wakati nchi ya Kenya ilipokuwaikijikomboa kutoka kwenye minyororo ya ukoloni, anazungumzia jinsi Shengilitumia muundo wa Kiswahili katika ubunifu wake na hivyo kupanuamatumizi ya Kiswahili mjini Nairobi wakati baadhi ya viongozi walikuwawakipigia debe Kiingereza badala ya Kiswahili. Anakubaliana na ChegeGithiora kwamba Sheng ni mojawapo ya lahaja chipukizi za Kiswahili nakama vile lahaja kongwe za Kiswahili hurutubisha Kiswahili badala yakukiua, Sheng imekirutibisha Kiswahili hasa katika ulimwengu wateknohama na utandawazi. Badala ya kuiona Sheng kama zimwi lililokujakukiangamiza Kiswahili, anawahimiza walimu na wadau wa Kiswahiliwabadilishe mtazamo wao na waelekeze juhudi zao katika kuunda mbinunzuri za ufundishaji wa Kiswahili sanifu. Anahitimisha kwa kusema kuwabadala ya kuipiga Sheng’ vita tunahitaji kuielewa lahaja hii mpya zaidi.

Sehemu ya pili ya kitabu hiki inahusu ufundishaji na ujifunzaji wa lughaya Kiswahili kama lugha ya pili. Kuna makala nne katika sehemu hii; mbili

xiv miaka hamsini ya kiswahili nchini kenya