mtoto 15014 bure - k4health.org · wavulana wanapaswa kutambua kwamba kwa kuwa tohara haitoi kinga...

23
Kwa maaelezo zaidi tafadhali tuma neno MTOTO kwenda 15014, huduma hii ni bure Tohara ya watoto wachanga lazima ifanywe na wataalam wa afya katika kituo cha huduma ya afya kupunguza matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza. Madhara madogo madogo yanayoweza kutokea mara chache, madhara hayo ni: • Maumivu yasiyopungua baada ya kufanyiwa tohara • Kutokwa na damu nyingi • Maambukizi ya kidonda • Kupata mzio (aleji) ya dawa ya ganzi Kipeperushi hiki kimetengenezwa kwa ruhusa ya UNICEF na USAID Swaziland • Hospitali ya Tosamaganga (Jumatatu, Jumanne na Alhamis) • Hospitali ya Ilula (Jumatatu, Jumatano na Ijumaa) • Kituo cha Afya cha Ipogolo (Kila siku) • Hospitali ya Rufaa ya Iringa (Kila siku) Kwa sasa huduma hii inapatikana katika vituo vya afya vifuatavyo: “Uume wa mtoto mchanga hupona haraka baada ya tohara. Ni huduma rahisi na ya haraka.” Front Back Jumatatu mpaka Ijumaa, saa 2 asubui mpaka saa 2 usiku Jumamosi na Jumapili, saa 2 asubui mpaka saa 8 mchana.

Upload: others

Post on 29-Aug-2019

66 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Kwa maaelezo zaidi tafadhali

tuma neno MTOTO kwenda 15014,

huduma hii ni bure

Tohara ya watoto wachanga lazima ifanywe na wataalam wa afya katika kituo cha huduma ya afya kupunguza matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza.Madhara madogo madogo yanayoweza kutokeamara chache, madhara hayo ni:• Maumivu yasiyopungua baada ya

kufanyiwa tohara• Kutokwa na damu nyingi• Maambukizi ya kidonda• Kupata mzio (aleji) ya dawa ya ganzi

Kipeperushi hiki kimetengenezwa kwa ruhusa ya UNICEF na USAID Swaziland

• Hospitali ya Tosamaganga (Jumatatu, Jumanne na Alhamis)

• Hospitali ya Ilula (Jumatatu, Jumatano na Ijumaa)

• Kituo cha Afya cha Ipogolo (Kila siku)• Hospitali ya Rufaa ya Iringa (Kila siku)

Kwa sasa huduma hii inapatikana katikavituo vya afya vifuatavyo:

“Uume wa mtoto mchanga hupona haraka baada ya tohara. Ni huduma rahisi na ya haraka.”

FrontBack

Jumatatu mpaka Ijumaa, saa 2 asubui mpaka saa 2 usikuJumamosi na Jumapili, saa 2 asubui mpaka saa 8 mchana.

Kumtahiri mtoto mchanga wa kiumekuanzia saa 24 mpaka wiki 8 kuna faida zifuatazo:

Je tohara inafanywaje?

Jinsi ya kumtunza mtoto baada ya tohara

Mtoto mchanga wa kiume anawezakutahiriwa endapo;

• Kunazuia ngozi inayofunika kichwa cha uume kubana na kufanya isiweze kushuka

• Inapunguza athari za magonjwa ya njia ya mkojo

• Ni rahisi kuusafisha uume

• Ana umri kati ya masaa 24 mpaka wiki 8 tangu kuzaliwa

• Ana uzito wa kuanzia kg 2.5• Hasumbuliwi na maradhi yoyote

Kwa baadae, tohara itamsaidia: kupunguza hatari ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kupunguza hatari ya maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya zinaa na kupunguza hatari ya saratani ya uume.

“Nina furaha, nilichukua uamuzi wa busara wa kumtahiri mtoto wangu mara tu alipozaliwa. Sasa nina amani kwamba yuko salama”.

• Kwanza daktari au muuguzi athibitishe kwamba mtoto wako anafaa kufanyiwa tohara ya watoto wachanga

• Halafu, atapewa ganzi katika uume wake kabla ya kufanyiwa tohara

• Ngozi inayofunika kichwa cha uume (govi) itaondolewa na uume utafungwa bandeji

• Baada ya muda mfupi utaruhusiwa kuondoka na mtoto wako

• Weka uume katika hali ya ukavu na usafi• Usipakae dawa yeyote au poda kwenye

kidonda cha tohara• Mrudishe mtoto kwenye kituo cha afya siku

ya pili baada ya tohara ili achunguzwe kidonda na kuondolewa bandeji

• Usiirudishie bandeji kwenye kidonda cha tohara iwapo bandeji itatoka

Watoto waliozaliwa na mama mwenye maambulizi ya Virusi vya Ukimwi pia watapata huduma hii ya tohara

Inside

NI RAHISI NA HARAKA, HUPONA NDANI YA SIKU CHACHE,

SI LAZIMA KIDONDA KUSHONWA

NI NJIA RAHISI YA UPASUAJI INAONDOA NGOZI INAYOFUNIKAKICHWA CHA UUME WA MTOTO MCHANGA (govi)

Front

JINA LA KITUO CHA AFYA: _____________________________________

JINA LA MTEJA ____________________________________________

NAMBA YA KADI:

Tarehe ya kuzaliwa __________________

KIJIJI ANACHOTOKA MTEJA ___________________________________

KATA ________________

TAREHE YA KUFANYIWA TOHARA _______________________ TAREHE YA KWANZA YA KURUDI _______________________

MUDA _________________

TAREHE YA PILI YA KURUDI ___________________________

MUDA ___________________

Tafadhali rudi katika kituo cha afya muda na wakati uliopangiwa. Kama unatatizo lolote unaweza kurudi katika kituo cha afya hata kabla ya siku uliyopangiwa haijafika au unaweza kupiga simu ya dharura

Mawasiliano ya dharura (Simu ya kituo cha afya ______________________________________

KADI YA MAUDHURIO YA TOHARAYA WATOTO WACHANGA

Siku Mwezi Mwaka

Siku Mwezi Mwaka

Siku Mwezi Mwaka

Tohara Card

Maelekezo baaya ya tohara ya watoto wachanga • Usiitoe bandeji mpaka itakapodondoka yenyewe • Rudi katika kituo cha afya baada ya masaa 48 tangu kufanyiwa tohara ili muhudumu wa afya aweze kutoa bandeji.( ni muhimu kurudi ili muhudumu wa afya akague kidonda cha mtoto wako hata kama bandeji imetoka yenyewe nyumbani • Inaweza kuchukua siku kadhaa hadi wiki moja ili kidonda cha tohara kupona. Katika kipindi hiki chote, unashauriwa kukisafisha taratibu na kukiweka katika hali ya usafi na ukavu. Kama inawezekana, unashauriwa kutumia nepi za kutumia na kutupa

• Nepi imetota na damu au doa la damu katika nepi ni kubwa zaidi ya sarafu ya shilingi 200 • Majimaji ya njano yenye harufu mbaya (usaha) • Wekundu na uvimbe unaongezeka • Mtoto ana homa, amelegea, au anaonekana kuna kitu kinamsumbua na hanyamazi hata akibembelezwa

Back

Kadi ya Maudhurio ya Toharaya Watoto Wachanga

HONGERA KWA MTOTO WAKO KUFANYIWA TOHARA

MRUDUSHE MTOTO KATIKA KITUO CHA AFYA HARAKA IWEZEKANAVYO PINDI UTAKAPOONA

Kama unaswali lolote, tafadhali piga simu au tuma ujumbe mfupi kwenda namba ya simu ya dharura iliyoandikwa upande wa pili wa kadi hii

Kipeperushi cha Wavulana na Walezi wao

Orodha ya hospitali na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya bure ya Tohara ya Mwanaume

Kwa walio chini ya umri wa miaka 18 ni lazima waambatanena wazazi au walezi wao.

Wanaume wenye umri wa miaka 20 na kuendelea watapewa kipaumbele.

• Hospitali ya Mkoa - Kitete

• Hospitali ya Wilaya - Nzega

• Hospitali ya Wilaya - Igunga

• Hospitali ya Nkinga

• Hospitali ya Wilaya - Urambo

• Kituo cha Afya Kaliua

Ili kujua zaidi kuhusu Tohara na faida zake tuma neno TOHARA kwenda 15014Ili kujua vituo vitoavyo huduma tuma neno TABORA kwenda 15014

Sikiliza radio ili kujuavituo vingine zaidi.

Maisha ni Sasa! Wahi Tohara!Kuwa Msafi. Pata Kinga.

Maisha ni Sasa! Wahi Tohara!Kuwa Msafi. Pata Kinga.

ni huduma

BILA

MALIPOni huduma

BILA

MALIPO

ukwelikuhusutoharayamwanaume:

Hii ni moja ya njia za zamani sana za upasuaji katika historia ya mwanadamu. Tohara hufanywa kwa sababu mbali mbali za kiutamaduni, kidini, kuboresha usafi na pia kwa sababu za kitabibu.

Hivi karibuni, watafiti wamegundua, tohara ya wanaume husaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya VVU. Hii ni kwa sababu ngozi ya govi ni laini na rahisi kupata michubuko na vidonda na pia inazo chembe chembe hai maalumu ambazo huvutia virusi vya UKIMWI (VVU) kuingia mwilini kwa urahisi. Hivyo tohara husaidia kupunguza hatari hizi. Sasa tohara ya wanaume inafanyika kwa wavulana na wanaume wenye nia ya kupunguza hatari ya uwezekano wa kupata VVU.

Wavulana wengi huelezea kuwa ni rahisi kujifanyia usafi iwapo wametahiriwa. Wengine pia hupenda kufanyiwa tohara kwa sababu ni mila yao na wenzao wengi wa rika moja tayari wametahiriwa.

Maelezo kwa wavulana na walezi wao

Kwa muda wa wiki sita baada ya tohara, MVULANA HATAKIWI KABISA KUFANYA NGONO AU KUPIGA PUNYETO.

Hii ni kwa sababu eneo lililofanyiwa upasuaji halijapona kikamilifu, hivyo anaweza kujitonesha au kujiingiza katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU.

Baada ya wiki sita kupita, ni muhimu kuendelea kuzingatia njia nyingine za kujikinga dhidi ya maambukizi ya VVU.

Tohara ya wanaume inasaidia wavulana kupunguza uwezekano wa kuambukizwa VVU kwa hadi asilimia 60.

Wavulana wanapaswa kutambua kwamba kwa kuwa Tohara haitoi kinga ya asilimia 100 dhidi ya maambukizi ya VVU, wanapaswa kuendelea kutumia njia nyingine kama vile kusubiri, kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na kutumia kondomu.

Faida nyingine za tohara ni kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa ya zinaa, saratani yauume na maambukizi ya njia ya mkojo.“Wavulana wanashauriwa kutofanya ngono kabisa kama njia salama ya kujikinga na maambukizi ya VVU”

Kama ilivyo kwa upasuaji wa aina yoyote, tohara ya wanaume inaweza kuambatana na matatizo madogo madogo kama kutokwa damu au jeraha na kupata maambukizi ya vijidudu kama bakteria.

Matatizo haya huweza kudhibitiwa kirahisi kwa kufuata vizuri maelekezo utakayopewa baada ya tohara, na pia kuwaona wahudumuwa afya pindi matatizo yanapojitokeza.

Wavulana walio na umri chini ya miaka 18 wanahitaji kibali cha maandishi kutoka kwa wazazi / walezi wao ili waweze kufanyiwa huduma ya tohara.

Kuchukua uamuzi wa kufanyiwa tohara ni hatua ya muhimu katika maisha ya mvulana.

Tafadhali tembelea kituo cha afya kinachotoa huduma hizi kama vile hospitali ya mkoa, hospitali ya wilaya au kituo chochote cha afya ili uweze kufaidika na huduma hizi. Kwa maelezo zaidi kuhusu kituo kinachotoa huduma hizi kilichopo karibu na wewe, tuma ujumbe mfupi wa maandishi au [piga simu kwenda namba zilizotajwa nyuma ya kipeperushi hiki].

Huduma ya tohara hutolewa katika hospitali za mikoa, wilaya, na baadhi ya vituo vya afya.

Baada ya kufanyiwa tohara ni muhimu mvulana apumzike kwa muda wa siku mbili. Hii ina maana asifanye kazi ngumu kama kubeba vitu vizito au kuendesha baiskeli.

Anatakiwa kuvaa nguo zisizobana ili kuepuka kujitonesha na kupata uambukizowa vijidudu kwenye kidonda.

Baada ya siku mbili atatakiwa kurudi katika kituo cha afya alichofanyiwa ili mhudumu aweze kutoa bandeji na pia kukagua kidonda chake. Vilevile anashauriwa kurudi katika kituo cha afya baada ya siku saba kwa uchunguzi na ushauri nasaha zaidi.

Pia atapatiwa ushauri zaidi wa jinsi ya kukitunza kidonda chake baada ya tohara hususani katika kipindi cha wiki sita zinazofuata.

Kuna hatua kadhaa katika mchakato mzima wa kupatiwa huduma za tohara:

Hatua ya nne: Baada ya tohara, atapelekwa katika chumba cha mapumziko kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani, pia atapewa dawa za kumeza ili kupunguza maumivu.

Hatua ya kwanza: Mvulana na mzazi/mlezi watashiriki katika ushauri nasaha wa kundi ili waweze kufahamishwa kuhusu faida na matatizo madogo madogo yanayohusiana na tohara na hivyo kuwapa nafasi ya kufikia uamuzi iwapo mvulana atahitaji kupata huduma hii.

Hatua ya pili: Mvulana na mzazi/mlezi watapewa ushauri nasaha binafsi wakiwa ana kwa ana na mhudumu wa afya mwenye ujuzi. Hapa watapata nafasi ya kumuuliza mhudumu maswali yoyote ya ziada waliyonayo na pia mvulana atapewa nafasi ya kupima VVU iwapo wataridhia. Mvulana atafanyiwa uchunguzi wa afya yake ili kufahamu iwapo inafaa kumfanyia upasuaji.

Hatua ya tatu: Mvulana atafanyiwa tohara na wahudumu wa afya wenye ujuzi. Tohara huchukua takribani dakika 30. Kabla ya upasuaji, atachomwa sindano ya ganzi sehemu inayotahiliwa ili asipate maumivu wakati wa upasuaji. Baada ya tohara, kidonda kitafungwa vizuri kwa bandeji ili kukinga uambukizi wa vijidudu vya magonjwa.

3

1

2

4

Tohara ya mwanaume ina faida nyingi kijamii, kiafya na kwa usafi. Inaweza kupunguza uwezekano wa mwanaume kuambukizwa VVU kwa hadi asilimia 60.

Maisha ni Sasa! Wahi Tohara!Kuwa Msafi. Pata Kinga.

ni huduma

BILA

MALIPOni huduma

BILA

MALIPOKuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioniJumatatu hadi IjumaaMUDA WA KAZI NI:

JumamosiKuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 8 mchana

Tarehe 8 April hadi 4 Mei, 2013Huduma hii itaanzaTohara ya Mwanaume

Orodha ya hospitali na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya bure ya Tohara ya Mwanaume

Kwa walio chini ya umri wa miaka 18 ni lazima waambatanena wazazi au walezi wao.

Wanaume wenye umri wa miaka 20 na kuendelea watapewa kipaumbele.

Maisha ni Sasa! Wahi Tohara!Kuwa Msafi. Pata Kinga.

Ili kujua zaidi kuhusu Tohara na faida zake tuma neno TOHARA kwenda 15014Ili kujua vituo vitoavyo huduma tuma neno TABORA kwenda 15014

Sikiliza radio ili kujuavituo vingine zaidi.

Wilaya ya Igunga • Kituo Cha Afya Usongo• Kituo Cha Afya Nanga

Wilaya ya Nzega• Kituo Cha Afya Lusu• Kituo cha Afya Busondo• Kituo Cha Afya Itobo• Kituo cha Afya Bukene• Zahanati ya Mbutu

Wilaya ya Urambo• Hospitali ya Wilaya Urambo• Kituo Cha Afya Usoke• Kituo cha Afya Kaliua• Kituo Cha Afya Ulyankulu

HONGERA KWA

TOHARAKUFANYIWAHONGERA KWA

TOHARAKUFANYIWA

Maisha ni Sasa! Wahi Tohara!Kuwa Msafi. Pata Kinga.

Maisha ni Sasa! Wahi Tohara!Kuwa Msafi. Pata Kinga.

1. Zitakapopita wiki sita ambapo kidonda chako kitakuwa kimepona kabisa hadi ndani unaweza kufanya ngono na mpenzi wako. Hakikisha unatumia kondomu iwapo haufahamu hali ya maambukizi ya mpenzi wako.

2. KUMBUKA: Tohara inatumika kama njia ya ziada ya kuzuia maambukizi ya VVU, lakini haikupi ulinzi wa asilimia 100(%). Baada ya tohara ni muhimu kutumia njia nyingine kujikinga na maambukizi ya VVU kama vile, kutofanya ngono kabisa, kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu aliyepima afya yake na kutumia kondomu kwa kila tendo la ngono.

• Baada ya wiki sita ya TOHARA:

Maelekezo muhimu ya kuzingatia baada ya kufanyiwa TOHARA

Kwa kupata ushauri zaidi au ukiwa na dharura piga: 0686 884 233 (Tabora), 0686 884 737 (Iringa na Njombe) ni huduma

BILA

MALIPOni huduma

BILA

MALIPO

Ili kupata ujumbe kuhusu kujitunza baada ya Tohara tuma neno BAADA kwenda namba 15014

• Siku za mwanzo baada ya TOHARA:

• Siku ya pili baada ya TOHARA:

1. Mara nyingi watu huweza kuendelea na shughuli zao mara baada ya tohara.

2. Siku za mwanzo baada ya tohara ni vizuri upumzike ili upone vizuri. Hii ina maana ya kwamba usifanye kazi ngumu, kubeba vitu vizito au kuendesha baiskeli. Uonapo dalili yoyote kati ya hizi zifuatazo, pata ushauri wa mhudumu wa afya mara moja: • Kutoka damu nyingi (kulowanisha bandeji) • Kuvimba kwa uume pamoja na korodani/pumbu • Maumivu makali yasiyoisha • Kushindwa kukojoa

3. Ni kawaida kwa uume kusimama wakati wa usiku; na inaweza kusababisha maumivu katika siku chache za kwanza baada ya tohara. Unapokojoa, uume hulala, hivyo jitahidi kunywa maji mengi kupunguza uume kusimama mara kwa mara.

4. Ni muhimu kutambua pia kusimama kwa uume hakusababishi kukatika kwa nyuzi zilizotumika katika mshono.

1. Ni muhimu kuoga kila siku kwa maji sa� na sabuni. 2. USITIE DAWA yoyote kwenye kidonda pasipo ushauri wa Mhudumu wa afya. 3. Endelea kutunza kidonda katika hali ya usa� na hakikisha unajikausha vizuri unapomaliza kuoga.4. Rudi katika kituo cha afya ulichofanyiwa tohara siku ya saba kwa uchunguzi wa kidonda. 5. Epuka shughuli zinazoweza kutonesha jeraha.

1. Unapaswa kurudi siku ya pili katika kituo cha afya ulichofanyiwa tohara ili kuondoa bandeji na kuchunguza maendeleo ya kidonda.

1. Kidonda kinaweza kuonyesha kukauka baada ya wiki moja, lakini kinakuwa bado ni kibichi kabisa kwa ndani hadi zitimie wiki sita tangu kufanyiwa tohara. Usifanye ngono kabisa wala kupiga punyeto katika kipindi hiki.

2. Kushiriki tendo la NGONO kabla ya kupona kabisa huchelewesha kupona na pia kuongeza hatari ya kupata MAAMBUKIZI ya VVU au magonjwa ya ngono.

3. Utakaporudi nyumbani mkumbushe mwenzi wako kuhusu umuhimu wa kutofanya ngono kwa muda wa wiki sita baada ya tohara. Pia upange nae mikakati ya jinsi ya kuepuka kufanya ngono katika kipindi hiki. Kwa mfano mnaweza kuamua kulala katika vyumba tofauti kwa muda huo.

• Kufikia wiki moja baada ya TOHARA:

• Kufikia wiki sita baada ya TOHARA: