muongozo wa elimu ya masoko tanzania...umuhimu zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara...

28
Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania

Upload: others

Post on 08-Feb-2020

33 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

1

Muongozo wa Elimu ya Masoko

Tanzania

Page 2: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

2

Mradi: Wekeza kwa wanawake wa kimaasai

DCI-HUM/2014/341-127

Utangulizi

Karibu kwenye programu ya elimu ya masoko. Kuanzia sasa naamini tutakuwa pamoja

kuelimishana muongozo huu wenye ujuzi wa biashara na wateja,

Muongozo huu utakusaidia katika kufundisha elimu ya masoko. Muongozo huu utakuongoza

kwa vipindi 5, vitakavyochukua siku tano. Kila Kipindi kitakuwa na shughuli mbalimbali

yanayoendana. Utakaposoma programu hii utaona kuwa ina muswada na mambo elekezi kwako

wewe mwezeshaji kama ilivyoelezewa kwa maandishi meusi.

Utakapoanza kufundisha hii program tunakushauri utumie mswada huu wakati wote na uusome

mpaka utakapojiridhisha kuwa maelezo yote ni sahihi. Ukishajirizisha tunakushauri ukubaliane

na programu hii na kutumia maelezo, shughuli na mahojiano pale unapoona inafaa.

Asante kwa ushiriki wenu nawatakia kila la kheri katika ufundishaji.

Page 3: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

3

Sehemu ya 1

Zoezi:

Utangulizi/kuweka vipaombele sehemu za biashara

Muongozo:

Anza kwa kuwasalimia watu wote na kuwaomba wajitambulishe, ujitambulishe na

kuutambulisha muongozo.

Karibu kwenye kipindi chako cha kwanza cha elimu ya biashara na masoko. Mimi ni

mwezeshaji wa vipindi vijavyo. Wengi wenu imewabidi kuacha shughuli zenu muhimu ili

kuhudhuria kwenye darasa hili, Inawezekana una shughuli nyingi nyumbani. Wengine mme

tembea umbali mrefu kuwa hapa. Hata hivyo, kila mmoja wenu yupo hapa kwasababu ana nia ya

kuboresha maisha yake, na familia yake.

Inaweza ukawa unaogopa kuwa hauna elimu ya kutosha, au unaweza kuogopa kuwa huna vifaa

au ujuzi wa kutosha kuweza kuendesha biashara kwa mafanikio. Pamoja na kwamba wote tupo

makini katika kutunza nyumba na kuangalia familia zetu. Tunakabiliana na matatizo kama vile

kutokuwa na fedha za kununua vitu tunavyo hitaji au hatuna namna ya kupata bidhaa hizo. Hata

tukiwa na fedha bidhaa tunazohitaji hazipo. Wakati mwingine tunakabiliana na matatizo ya

kutokuwa na kazi kwa muda mfupi au muda mrefu, na hata tukipata ajira,mishahara ni midogo

sana na haitoshi.

Hapa darasani, hatutajibu tu maswali yenu bali kuwafundisha mambo unayotakiwa kuyajua ili

usipoteze fedha kama mteja na pia kuwafundisha maswala ya msingi anayotakiwa kuyajua mtu

mwenye mtazamo wa kibiashara. Kwa mtazamo wetu kuhifadhi fedha ni sawa na kutengeneza

pesa, na ndio sababu mafunzo haya ni ya muhimu. Dhumuni la mafunzo haya ni kukuwezesha

wewe kama mteja namna ya kufikiri kama mfanyabiashara.

Mafunzo haya yanaitwa Elimu ya Biashara na masoko. Mafunzo haya yametumika

kuwawezesha na kuwasaidia wanawake 1,000 wa India na sehemu nyingine za dunia.

Tumekuwa sasa tukifundisha mafunzo haya Tanzania kwa mwaka mmoja, na tumeona

yalivyoboresha maisha ya watu tuliowafundisha. Sio kila mmoja atayepata mafunzo haya

atakuwa mfanyabiashara, lakini kila mmoja atajifunza kuwa mteja mzuri ambaye itapelekea

kuwa na hela zaidi kutokana na kuhifadhi.

Unaweza kuuliza ina maana gani kuwa mteja. Sisi wote ni wateja kwa namna moja au

nyingine. Nimegundua kuwa mteja mzuri ni jambo la muhimu sana, kwa sababu ni hatua ya

kwanza inayopelekea kuwa mfanyabiashara na kupanua mawazo.

Page 4: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

4

Masomo haya yameandaliwa baada ya kuwasoma wateja kwenye mazingira yenu na

mazingira mengine yanayofanana na haya ya kwenu. Na matokeo yake ni kwamba tuna

programu ambayo inawahudumia maelfu ya watu duniani. Kuwasaidia kuwa wateja na

wafanyabiashara wazuri.

Wakati wote wa mafunzo haya tutashiriki kwenye mazungumzo kwenye makundi ambapo

utahamasishwa kuongea. Pale utakapochangia zaidi ndipo wote waliopo hapa kwenye mafunzo

haya mtaweza kunufaika na mafunzo haya. Kumbuka kuwa utajijengea ujasiri wa kuongea

mbele ya kundi dogo, utaweza pia kuzungumza na mteja ambaye haumfahamu sokoni. Kama

mtapenda, wale wenye ujasiri wa juu waje huku mbele na kuonyesha njia kwenye hili darasa la

kwanza; na kwenye madarasa ya mbeleni utawashawishi wengine kwenye kikundi chako

kwenda mbele na kuongea!

Mafunzo haya yatakuwa pia na mazoezi marahisi ya kupeleka nyumbani ambayo

yatakuandaa kwa wiki inayofuata. Tunakushauri uchukulie uzito mazoezi haya ya kupeleka

nyumbani na uyafikirie na kuyaongelea utakapoenda nyumbani. Hii itapelekea wewe kuelewa

zaidi mazungumgunzo haya na kusababisha uzoefu ulioupata uwe wa manufaa zaidi kwako na

wote waliokuzunguka.

Kabla ya shughuli yetu ya kwanza, ningependa kuuliza kama kuna mtu ana swali na pia

niwaulize maswali.

Unafikiri mafunzo haya yanahusu nini?

Utapenda kupata nini kwenye mafunzo haya?

Kwakuwa kila mtu anaonekana yupo tayari, nitawaomba sasa mkae kwenye makundi ya watu

wane au watano kwa ajili ya shughuli yetu ya kwanza.

Makundi yamzunguke mwalimu kwa mduara. Ikienda vizuri, labda uwaruhusu watu wakutane

kwa makundi halafu warudi tena kuongea kuwawezesha watu kusogea na kuwa na nguvu zaidi..

Hapa unaweza kuona picha zinazoendana zinazoonyesha vipengele mbalimbali vya

biashara. Kwa shughuli hii mahususi tunatumia picha za biashara za shanga ili itusaidie kuelezea

dhana hii kwa uwazi zaidi. Sehemu tofauti za biashara kama tulivyoonyesha ni: Pesa, Usafiri,

Mali ghafi (shanga), duka, mteja na bidhaa iliyokamilika.

Tunakuomba usome na kuelewa vipengele hivi sita vya biashara na kutueleza kuwa ni

kipengele gani kilicho cha muhimu sana kati ya hivi sita, kinachohitajika katika kuanza biashara,

tutakaporudi kipindi cha pili na cha tatu. Na utueleze ni kwa nini umechagua kila kipengele na ni

sababu ipi imepelekea kuchagua umuhimu wake. Kwa mfano, naweza kuamua na kikundi

changu kuwa kipengele muhimu kwenye biashara ni uzalishaji halafu nielezee ni kwa nini

nafikiri hivyo.

Sasa tutakupa dakika 15 kuzungumza na kikundi chako na kuamua kutoa majibu. Baada

ya muda huu kisha mtu mmoja wa kikundi chako ataombwa kuja na kujadili jibu lenu. Kwa hiyo

kwa mara nyingine tena, unafikiri ni sababu zipi za muhimu zinazopelekea kuanzisha biashara?

Page 5: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

5

Kabla hatujaanza kuzungumza kwenye vikundi, kuna mtu yeyote mwenye maswali kuhusiana na

zoezi hili.

Zunguka na kuonyesha picha za vipengele sita muhimu kwenye kila kikundi, kusaidia kila kundi

kuelewa. Waeleze wote waanze kwanza kuzungumza halafu utembelee kila kikundi na picha.

Kila kundi litakuja na kuonyesha

Baada ya kila kikundi kuonyesha, washukuru na kuwauliza kama kuna mtu yeyote mwenye

jambo la kuongeza au kujadili kuhusu yale yote yalioyoelezewa na kila kikundi.

Jibu kwa haya yafuatayo

Napendekeza kwenu kuwa sehemu ya muhimu zaidi kwenye biashara ni mteja. Bila mteja,

hakuna chochote kitakachosababisha uwe na biashara. Kati ya mambo yote tulioyazungumza,

mteja ndo sehemu pekee ambayo haitaweza kuondolewa na bado tukaweza kuwa na biashara.

Kwa mfano, tuna mteja aliyekuja kutembelea duka na kuulizia mchele. Kama muuza

duka akisema hana mchele dukani na mteja akaondoka, jambo gani litatokea? Biashara

itaendeleaje kama haitaweza kuwahudumia wateja.

Wengi wenu mmesema pesa, lakini naamini hicho sio cha muhimu kwenye kuanzisha

biashara. Labda unaweza kunipa kitu kama chakula au mbuzi kwa mabadilishano ya kitu kwa

kitu kwahiyo pesa haitahisika hapa. Labda hata biashara yangu haihusiani na bidhaa

inayoonekana au kushikika. Mwalimu kwa mfano anatumia ujuzi alionao kufanya biashara.

Thamani inaweza kuchukua sura mbalimbali na inaweza kuruhusu kupata ubunifu wa aina

mbalimbali wa kuanzisha biashara. Tutazungumzia zaidi kuhusu umuhimu wa thamani kwenye

vipindi vijavyo.

Sasa mchukulie mtu mwenye wazo la kuanzisha biashara ya chakula, na ana banda la

kuuza chakula kijijini lakini hakuna mauzo. Unafikiri ni kwa nini hakuna mauzo? Ni mambo

gani yanasababisha?

Nitawapa wote dakika 5 za kuzungumza mawazo yenu na wanakikundi. Mara mtakapomaliza

kuzungumza, nitaalika kila kikundi kije mbele na kueleza darasa wamejifunza nini na jambo gani

ndio la muhimu kwenye biashara ili iweze kufanikiwa.

Vikundi vinaonyesha tena.

Kwa mara nyingine tena nasisitiza kuwa mteja ndio jambo la muhimu sana kwenye biashara.

Nawashawishi wote mzungumze na kuchangia.

Zoezi la nyumbani

Majibu mazuri kutoka kwenu wote? Sasa katika maandalizi ya kipindi chetu kinachofuata, tuna

zoezi dogo la kufanyia nyumbani. Nawaomba mfikirie uzoefu wenu katika manunuzi. Fikiria

unachonunua ukienda dukani. Unafanyaje manunuzi? Umewahi kudanganywa? Kw nini unanua

Page 6: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

6

vitu pale unaponunua? Kwa nini unanua kile unachonunua? Tabia zipi kati ya hizi ni nzuri na

zipi ni mbaya? Uje ukiwa tayari kutueleza kwenye kipindi kinachofuata. Rudia zoezi hili mara

mbili. Mteja

Pesa/Mtaji

Page 7: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

7

Uzalishaji

Mali ghafi

Page 8: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

8

Usafiri

Duka/Sehemu

Page 9: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

9

Sehemu ya 2

Zoezi

Igizo la duka la rejareja

Dhumuni

Kujifunza changamoto za kuwa mteja

Umuhimu

Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi

na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu ya mteja.

Muongozo

Leo tutaanza kwa kuwaita baadhi ya watu ili waweze kutueleza kuhusu lile zoezi la kupeleka

nyumbani. Kama sehemu ya kujikumbushia kwenye kipindi kilichopita kufikiria kuhusu

unachonunua ukienda kufanya manunuzi. Unafanyaje manunuzi? Umewahi kudanganywa?

Kwanini unanua vitu pale unaponunua? Kwa nini unanunua unachonunua? Tabia zipi kati ya hizi

ni nzuri na zipi ni mbaya? Kama hukutumia muda wowote kufikiria kuhusu zoezi hili la

nyumbani. Nakushauri sana ufanye hivyo baada ya kipindi hiki, kuna thamani ya kuendelea

kufikiri shughuli/mazoezi haya.

Wachukue watu watano watakaojitolea kutoa mawazo yao, jaribu kuchagua watu ambao bado

hawajasimama mbele ya darasa kuzungumza, mruhusu yeyote anayetaka kushiriki ashiriki.

Vizuri, sasa tumetambua kidogo kuhusu namna ya kufanya manunuzi na kuangalia kidogo

tunachofanaya kwa sasa, tunaenda kufanya zoezi kidogo. Katika hili zoezi nitaenda kuandaa

duka na mtakuja kununua bidhaa kutoka kwangu, ni rahisi sana. Nitahitaji watu watatu watakao

kuwa wanunuzi na watatu watako kuwa watazamaji wakati wanunuzi wanakuja huku mbele.

kutakuwepo na duka ambalo litatengeneza na kusisimua uzoefu wa manunuzi kwa mtoa

huduma. Viwepo vitu mbalimbali vichache kama sabuni ya kuoga, na ya kufulia kuwakilisha

bidhaa zingine.

Orodhesha bidhaa tulizonazo na bei

Chapa kubwa (chapa x) ya dawa ya meno (inakuwa na mswaki wa bure mswaki

umeondolewa na kuuzwa tofauti) = ugx2500

Dawa ya meno = ugx1000

Sabuni kubwa

Chapa Y dawa ya meno (100g) – MRP = Tsh. 1600

Chapa kuu (chapa Z) sabuni ya kuoga (100g) – MRP = Tsh. 1200

Chapa Z sabuni za kuoga (100g; 3 nos. ndani ya pakiti)- MRP= Tsh. 3600 + (zawadi ya

bure ya kuweza kwenda kununua kifaa).

Page 10: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

10

Hii ni mifano inayoonyesha, na bidhaa zilizochaguliwa, hasa ambazo zinaonyesha uhalisia wa

mazingira ya hapa. Walimu au msaidizi anapaswa kuwa na jukumu la kawaida ya duka la

rejareja/ mtunza fedha na mtoa huduma wawepo katika duka la rejareja. Wanapaswa kuuza na

bidhaa na kuangalia huduma ya biashara kwa ujumla ikiwepo madeni, kukusanya malipo, na

kusambaza bidhaa. Wauzaji wanapaswa kutumia zote mbili kukusudia na inaonekana katika

makosa ya kawaida katika masoko ya ndani, kama vile suala zisizo za muswada wa bidhaa

kununuliwa, makosa ya jumla, utoaji wa bidhaa vibaya, au uuzaji wa bidhaa feki, na usambazaji

wa bidhaa zilizoisha muda wake. Washiriki kumi wanaweza kuambiwa waonyeshe jukumu la

wanunuzi na wanaobaki waangalie zoezi linavyofanyika.

Washiriki ambao walijitolea kwa jukumu la wanunuzi waelimishwe kwamba wanapaswa kuwa

na mahitaji ya familia zao katika akili, wachague bidhaa zao wanazopendelea, na kununua

bidhaa kama wangekuwa katika shughuli zao za kila siku.

Muuzaji lazima kufanya baadhi ya makosa ya kukusudia na kutumia mazoea ya udanganyifu,

kama vile utofauti katika bili na jumla na katika bidhaa zinazotolewa, na katika utoaji huwa

inatoa na zawadi pia inaweza kufanyika makosa katika bidhaa zinazotolewa. Baadhi ya

wanunuzi wanaweza kulipa kiasi baada ya kupokea bili, au wanaweza kudai muswada huo.

Baadhi ya wanunuzi wanaweza kuthibitisha muswada huo na jumla, ambapo wengine wanaweza

kuangalia muswada huo, na wangeweza kufanya hivyo ili kuweza kulipa bidhaa na kulipa kiasi

kwa kuulizwa na muuza duka. Baadhi ya wanunuzi wanaweza kuthibitisha MRP, tarehe ya

kumalizika, na kutoa maelezo ya bidhaa hiyo. Baadhi ya wanunuzi wapate kurejea tena dukani

na kumjulisha muuza duka makosa yake kupewa haki yao na kuelewana vizuri na muuzaji japo

wengine wanaweza kupuuza makosa yao. Baadhi ya wateja wanaweza ugomvi na wenye

maduka.

Baada ya washiriki kukamilisha ununuzi wa masharti (groceries), mwalimu lazima kukaribisha

watu wawili au watatu na kueleza kuwa wataenda kuagizwa dawa chache, ambayo wanapaswa

kununua dukani kama wanavyofanya katika maisha ya kawaida. Mwalimu lazima kuandika

majina ya dawa moja au mbili ambazo hazipatikani katika duka. Muuzaji lazima kutenda makosa

katika bei, hesabu na kusambaza madawa sahihi.

Matokeo

Baada ya kukamilisha zoezi, mwalimu lazima awaulize washiriki kushiriki uchunguzi wao.

Mwalimu lazima kuwezesha majadiliano kwa kutambua uwezo na udhaifu wa mazoea ya wateja

kwamba kuna vitu hawakuzingatia katika zoezi na ziorodheshwe majibu. Haya majibu yanaweza

kufafanuliwa na iwekwe kama haki na wajibu wa wanunuzi, na lazima ieleweke kwenye chati

kwa majadiliano zaidi.

Page 11: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

11

Washiriki wanaweza kuorodhesha yafuatayo

Wanunuzi wanapaswa kuwa na maarifa kuhusu bidhaa za kununuliwa, kwa mfano,

viungo na matumizi

Wanunuzi wanapaswa kuuliza katika maduka mbalimbali kabla ya kuamua juu ya duka

gani la kununulia

Wanunuzi wanapaswa kutathmini thamani kwa kulinganisha bei na ubora na sifa ya

bidhaa mbalimbali

Wanunuzi wanapaswa kulinganisha bei na kiasi au ukubwa wa furushi ili kuamua

ukubwa wa bidhaa za kununua

Wanunuzi wanapaswa kuamua kama kununua, au kufanya bidhaa fulani kutoka viungo,

kwa mfano, pilipili tayari mchanganyiko unga dhidi viungo kama vile pilipili,

kachumbari dhidi limao na vitunguu, na nguo iliyoshonwa tayari dhidi ya nguo ambayo

bado haijashonwa.

Wanunuzi unapaswa kuona haja halisi kwa bidhaa na kwa kiasi fulani cha bidhaa kabla

ya kununua (kwa mfano, kama wanapaswa kununua mashine ya maji au kutumia huduma

ya viwanda vya kusaga, kama wanapaswa kununua bidhaa zaidi kabla ya kuharibika

kuliko wangeweza kutumia kabla kuharibika, na kama wanapaswa kununua kiasi

kikubwa zaidi ya matumizi yao ya kawaida kwa sababu ya bei nafuu)

Wanunuzi wanapaswa kuangalia uzito na udogo na kuwa macho kuhusu mbinu ya uzito.

Wanunuzi wanapaswa kupanga mapema kwa ajili ya ununuzi na kuepuka kupoteza

muda.

Wanunuzi wanapaswa kuzuia matumizi ya fedha zao na wakati usiofaa kusafiri maeneo

ya mbali ili kufanya manunuzi

Wanunuzi wanapaswa kuomba, kama ni lazima, mahitaji, gharama kutoka kwa muuzaji

kwa bidhaa za kununuliwa

Wanunuzi wanapaswa kuthibitisha kiasi cha gharama kwa jumla, na bidhaa hutolewa,

kabla ya kuondoka dukani

Wanunuzi wanapaswa kuthibitisha tarehe ya kutengenezwa, uzito, na tarehe ya

kumalizika matumizi ya bidhaa

Wanunuzi wanapaswa kuwa macho kuhusu bidhaa bandia

Wanunuzi wanaweza kutafuta taarifa kuhusu bidhaa kutoka kwa muuzaji au msambazaji

Mnunuzi anaweza kutafuta msaada wa wengine ili kupata ushauri wa kiufundi au

ufafanuzi au maelezo kabla au baada ya kununua (kwa mfano, wanunuzi wanaweza

kutafuta msaada wa daktari wao kuhusu kipimo na majina ya madawa, na kutafuta

msaada wa wauzaji au huduma wanayotoa kuhusu kazi na bidhaa za elektroniki)

Wanunuzi wanapaswa kuangalia dhamira ya kampuni ya juu ya dhamana, vipindi

udhamini wa bidhaa, na baada ya mauzo ya huduma nyingine

Page 12: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

12

Ufupisho

mwalimu anaweza kurejea masomo muhimu waliojifunza kutokana na vikao vya mwanzo na

kukusanya masomo yao kama inavyoonyeshwa hapo chini na kuelekeza washiriki kwenye haki

na wajibu wa walaji:

Wateja wanapaswa kupanga manunuzi kwa makini

Wateja wanapaswa kutafuta, na kujifunza kuhusu, bidhaa, bei, na maduka, pia wateja

waombe gharama hizo, risiti kwa malipo, na kadi ya udhamini

Wateja wanapaswa kuangalia bidhaa kabla ya kupokea, ikiwa ni pamoja na tarehe ya

kumalizika muda

Wateja wanapaswa kutumia haki zao wakati wa kujadiliana au mazungumzo na wenye

maduka

Wateja lazima wakatishe tamaa tabia ambazo sio nzuri

Wateja wanapaswa kuwa na uwezo na tayari kulipia gharama za bidhaa na huduma

wanazopokea kutoka kwa muuzaji au mtoa huduma. Mwalimu anaweza kuuliza maswali

yafuatayo katika muhtasari wa majadiliano:

Nani mtazamo wake umefanikiwa leo?

Mwalimu lazima kuwezesha mjadala na kuhimiza washiriki kushiriki matatizo yao, kama vile

usalama, huduma kwa wakati, maeneo inapopatikana, au bei nafuu, na kuwakumbusha kuwa

mteja lazima kutathmini faida anayopata kwa bidhaa pamoja na kutangaza na kuangalia uwiano

wa fedha anazolipa, gharama anazotumia na hata kwa wateja. Ni lazima kuwepo na dhana ya

majumuisho na majadiliano na thamani, umakini wa kutathmini thamani ya fedha; mwalimu

anaweza kutumia Kielelezo 1 kuelezea dhana ya thamani, k.v., biashara ili kujua anachopata

mteja kama ina thamani na alichopewa.

Kazi ya nyumbani/zoezi la nyumbani

Wiki hii nina baadhi ya kazi rahisi ya ninyi kufanya nyumbani. Mimi nataka wewe uende na

kufikiri maeneo matatu ambayo mabadilishano ya thamani yanatokea na kwanini. Kwa mfano

unaweza kusema wewe kusafishwa nyumba yako na kwamba wewe kubadilishana muda na

nishati uliyotumia kusafisha mazingira vizuri zaidi kwamba ni bora kwa afya yako.

Unaweza kusema umesafisha nyumba yako na umebadilishana muda na nguvu uliotumia

kusafisha nyumba kuwa katika mazingira mazuri zaidi kwa afya yako.

Page 13: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

13

Sehemu ya 3

Kuwashukuru washiriki wote kwa kuja, jambo la kwanza tunalotaka kufanya kwa leo ni kurejea

masomo tuliyojifunza katika kipindi kilichopita ambayo ni tabia za kufanya manunuzi.kwa

hakika na kwa haraka nataka nirudie maeneo muhimu.

Wateja ni lazima waweke mipango ya kufanya manunuzi kwsa uwangalifu

Wateja ni lazima watafute, wajifunze kuhusu, bidhaa, bei na uhifadhi.

Wateja ni lazima waulize wanachodaiwa (bili zao), risiti za manunuzi,kadi ya

kudhibitisha ubora kwa muda maalum.

Wateja ni lazima wakague bidhaa bidhaa kabla ya kuinunua, na ni pamoja na muda wa

kutumika kuisha.

Wateja ni lazima kuonyesha na kusimamia haki zao wakati wa kuanza mazunguzo na

wauzaji wa madukani.

Wateja ni lazima wakatae tabia na mazoea mabaya ya wafanyibiashara.

Wateja ni lazima wawe na uwezo na utashi wa kulipa bidhaa na huduma kutoka kwa

muuzaji au mtoa huduma

Kwa hiyo tumalizie zoezi la kufanya nyumbani tuliyopeana wiki iliyopita. Ngoja niwakumbushe

kama mtakuwa mmesahau, Niwaeleza kwenda kuangalia sehemu tatu na kuona kama thamani

ya mabadilishano yanatokea. Nitawapa dakika tano mzungumze katika vikundi vyenu na

mjadiliane na mtu mmoja aje kuwasilisha mawazo yenu hapo mbele. Kama itawezekana, nahitaji

mtu ambaye hajaongea mbele ya kikundi kuja mbele na kuwasilisha.

Mawasilisho ya watu binafsi. Baada ya hapo ruhusu kujadili majibu yaliyotolewa na kuwasaidia

kuwe na mjadala mkali..

Nawashukuruni, namshukuru kila mmoja kwa mawazo au maoni yake aliyotoa.Kama

mnavyoona katika maoni yaliyotolewa, yapo maeneo katika maisha yenu ambapo thamani ya

mabadilishano.Ongezeko la thamani katika mabadilishano yanatokea kote kunakotuzunguka.

Kama tukienda kuokota kuni kwa mfano, tunafanya mabadilishano na muda ili kuokota kuni.

Hapa muda ndiyo kitu ambacho tunachofanya mabadilishano kwa kuni ambayo ndiyo ya

thamnai kwetu.

Ngoja tuchukue mfano mwingine.sema katika hali hii tunaenda kwenye stoo na kununua sabuni.

Katika mabadilishano ya ongezeko la thamani tunabadilishana na pesa ambayo ina thamani kwa

muuza duka, na badala yake kupata sabuni ambayo ina thamani kwetu. Kama tunahitaji kwenda

ndani zaidi, tunaweza kujiuliza kwanini sabuni ina thamani kwetu.

Uliza kama kila mmoja ataweza kujibu swali hili, anza majadiliano katika mada iliopo.

Page 14: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

14

kama hakuna maoni: tunathamini sabuni kwa sababu inatufanya kuwa wasafi na kutuzuia kuwa

wagonjwa. Tunatumia thamani ya pesa kusimamia thamini ya bidhaa ambayo itafanyakazi ya

kutuletea faida ya afya. Mfano mwingine wa mabadilishano ya thamani inaweza kuwa ni

uchaguzi wa mteja kwa masoko mawili, moja linaweza kuwa ni soko lililoko mbali na inauza

kwa bei ndogo na nyingine lipo karibu linauza vitu kwa bei ya juu. Mtu anapaswa kulinganisha

kati ya muda, nguvu na pesa zitakazotumika kukamilisha shughuli na achague ni njia ipi inaweza

kuwa nzuri kwao.

Kwa sasa naenda kuwaonyesha picha mbili za watu wanaofanyakazi ya mabadilishano ya

thamani na nahitaji wewe unieleze kuwa ni ni ipi thamani na zipi ambazo ni mabadilishano.

Onyesha picha za mwanamke anyefanya maamuzi kati ya stovu nyingi.

Mjadala.

Moja linuzwa kwa bei ya juu lakini haisababishi kukohoa na adha zingine na nyepesi kutumia.

Moja ni rahisi lakini inaumiza mapafu

Onyesha picha za mtu akifikiri

Mjadala.

Kwa ipande mmoja anaona muda atakayotumia kujifunza na hatua atakazochukua.

Kwa upande mwingine anjiona mwenyewe kama anapanda kiwango katika kufikia hatima.

Onyesha picha ya mtu anavyofikiri kuhusu umbali na vitu hapo kwenye duka.

Mjadala.

Kwa mbali, atapata vitu anavyotaka kwa gharama nafuu kwa gharama yake ya muda.

Je, atanunua ndogo au kubwa, ndogo itagharimu bei kidogo,lakini inaweza isiwe nzuri na kufaa.

Lile kubwa litakuwa na changamoto ya kuisafirisha nk.

Jitahidi kuelezea kila mabadilishano ya thamani ya kila mmoja wakati ukifundisha, lakini weka

mkazo zaidi katika kuwafanya waweze kufikiri zaidi na kuja na majibu wao wenyewe.

Zoezi la mnyororo wa thamani.

Sasa tunaenda kuvumbua seti nyingine ya mabadilishano, ambayo ina wajibu mkubwa katika

biashara.zoezi hili linalenga kwenye mnyororo wa thamani na kuelewa thamani iliongezwa

katika kila hatua za kutengeneza bidhaa na kwanini.katika mfano wa mwanzo naenda kuwaeleza

kwenda katika hatua zote za ujasiriamali katika kutengeneza wa jewe la thamani. Tumeweka

misingi ya mnyororo wa thamani kwa ajili yako katika picha ili kukuwezesha kuona kwa usahihi

njia mbalimbali ambao ni nzuri kidogo.

Page 15: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

15

Onyesha picha ya jiwe la thamani na mnyororo wa thamani, elezea kila hatua katika picha.

Anza na mpangilio wa mchoro wa jiwe la thamani

Halafu nenda kwenye uzalishaji unaofanywa na watu wa kawaida

Uza jiwe la thamani kwa mtu binafsi

Halafu rudisha katika mazingira yake.

Watauza au kuwapa madini hayo kwa watu wengine

.Mahitaji ya wateja itaendesha mzunguko kuanza tena.

Majadilianno yawe katika makundi kwanza na wawezeshe kuweza kuieleza ongezeko la thamani

katika kila hatua kadri iwezekanavyo. Kilakikundi kiwe na mwakilishi na afike mbele na

kuiwakilisha.

Baada ya sasa kupitia huu mnyororo wa thamani, tumeelewa kwanini mtu anapaswa kushiriki

katika sehemu za kila biashara kwa kuchukua sehemu ya kila hatua kwa kuongeza thamani

katika bidhaa zetukila iwezekanavyo,lakini kama mabadilishano katika thamani itafanyakazi

kwa manufaa yetu kwa muda mrefu. Hebu tuangalie mfano mwingine wa mnyororo wa thamani

wakati huu tutaangalia ni wakati gapi thamani inaongezwa katika uzalishaji wa ndizi.

Onyesha na jadili picha ya ndizi.

Mgomba unachukua fursa ya uwekezaji wa

Muda

Rasilimali

Nguvu

Ardhi

Mmea hukua na kuuzwa kwa wasafirishaji.

Wasafirishaji wanapata bidhaa

Wakulima wanpata pesa

Urahisi wa kuweka mahesabu (usiwe na chombo cha usafiri binafsi au tafuta

masoko mengine)

Mkulima anaweza kupata faida kubwa ya pesa kama wangesafirisha vitu/bidhaa

hivyo wao wenyewe?

Wasafirishaji wataleta kwa muuza duka.

Watapunguza muda wa muuza duka na rasilimali katika kustawisha mimea yako

mwenyewe.

Awapatia pesa wasafirishaji

Utapata ndizinzuri za kuuza

Muuza duka atauza bidhaa

Atapata faida kwa mauzo

Mauzo yanaweza kuongeza bei ya kununulia na kuleta kwa wateja

Muuzaji atapata pesa

Wateja watapata kwa urahisi chakula, hawahitaji kuzalisha chakula chao au

kusafiri kwenda shamba.

Wateja watapata chakula kwa mabadilishano kwa pesa.

Thamani ya kuonja

Thamani ya ubora wa bidhaa

Page 16: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

16

Kwa sasa tumeenda kuonyesha hatua mbili za mnyororo wa thamani tunaweza kuwa katika

uwelewa mzuri wa mabadilishano ya thamani na mchakato mwingine unaongeza thamani ya

bidhaa zetu, huduma nk. Wakati tunapangilia uzalishaji wa bidhaa tulitazama maamuzi Fulani,

kila kitu katika bidhaa lazima inalenga katika kuongeza thamini au sio ya muhimu kuongeza

katika bidhaa yetu. Hebu tuchambue picha hii inayoonyesha hatua mbalimbali katika

utengenezaji wa mkate kama bidhaa. Nahitaji uongee na vikundi vyako kwamba ni kwanini kila

bidhaa katika picha hapa chini zimeongezwa na ni thamani gani inaongeza katika mkate.

Majadiliano haalafu mawasilisho.

Mayai na ngano inakupa nguvu

Sukari, chumvi, na maziwa inaongeza ladha

Hamira na ikichangwa na hivyo hapo juu inaipa bidhaa muundo na ulani wake.

Nawashukuru kila mmoja. Hebu tutafakari umuhimu wa thamani na mabadilishano katika vitu

tunavyovifanya . Tumeona kila siku ya maisha yetu na mabadilishano haya ni ya lazima na ni ya

wajibu mkubwa katika kutubadilisha maisha yetu ya baadaye. Kwa kuzingatia faida na

mabaddilishano katika thamani ya bidhaa tumeweza kuwa wateja wazuri, wajasiriamali, na watu.

Zaidi.

Kazi za nyumbani.

Kwa kazi za nyumbani kwa wiki hii. Nahitaji kila mmoja wenu kufikiri zaidi kuhusu mnyororo

wa thamani.nahitaji kila mtu afikiri kuhusu biashara laakini siyo ya kutengeneza mkate.ni namna

gani watu wanapata bidhaa, usambazaji,usafiri wake nk. Tafadhali njoo na mnyororo wa thamani

katika bidhaa hiyo na ni namna gani thamani ilivyoongezwa katika matunda kama ilivyoelezwa

mapema katika vipindi. Je, kuna mtu mwenye swali/ maswali kuhusu kazi za nyumbai.

Page 17: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

17

Picha kwa ajili ya kipindi cha tatu (3)

Mifano ya mbadilishano wa thamani

Page 18: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

18

Page 19: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

19

Page 20: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

20

Page 21: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

21

Sehemu ya 4

Habari za leo kila mtu. Ninafurahi kwa kuwa kila mtu ameweza kufika katika kipindi chetu hiki

cha nne, lakini nahitaji kuanza kipindi hiki kwa kupita kazi niliyowapa ya nyumbani wiki

iliyopita. Kama mtakumbuka vema, niliwauliza mfikiri /kufikiri juu ya biashara ambayo siyo ya

kutengeneza shanga. Nilipotoka niliwataka mnieleze watu wanapataje bidhaa, usambazaji,

usafirishaji wake n.k.? nikataka tena mje na mnyororo wa thamani kwa bidhaaa hiyo au huduma

na mnieleze ni namna gani thamani ya kitu inaongezwa kwa kial hatua kama ilivyo katika hatua

ya kuongeza mnyororo wa thamani wa tunda uliofanyakatika kipindi cha awali. Kwa mfano

naweza kuja na wazo labiashara ya simu ya samasa katika biashara hii nauza samosa na kikapu

ili kuweza kuleta bidhaa yangu kwa wateeja.In this business hii inaongeza thamani kwa samosa

ya awali kwa kurahisisha upatikanaji wake kwa wateja.Nitawapa dakika kumi kujadili katika

vikundi vyenu ili kuona mlichofikiri kaatika kiipindi kilichopita na nitawahitaji watu watatu wa

kujitolea waje watueleze ni walichofikiria. Kama hakuna wakaojittolea nitawauliza watu watatu

kwa kuwachagua sehemu mbalimbali..

Ruhusu dakika kumi za mjadala na fafanua kama tena itahijika..

Twatu watatu au zaidi wa kuwakilisha: gawanya ongezeko la thamani na poteza katika hatua

mbalimbali za mnyororo wa thamani kama itahitajika waulize maswali mara nyingi ya kwanini

na jaribu watoe ufafanuzi kila inapowezekana.

Sasa tusonge mbele katika somo letu la leo. Kwa leo tutaenda kupanua uelewa wetu kuhusu

biashara ni nini. Hii itatuwezesha kuwa na uwanja mpana wa kufahamu na kuelewa biashara

zinazotufaa na kuangalia biashara na uwekaji binafsi wa kumbukumbu za hesabu kwa uwanja

mpana. Tutazungumzia pia kuhusu mahitaji ya mteja na kuona namna mahitaji ya mteja

inavyobadilisha mtizamo wa dunia inayotuzunguka na kuleta mabadiliko. Hadi mwisho wa wa

majadiliano haya ya leoo, natumaini mtakuwa na misingi wa namna ya kufikiri namna mahitaji

yanavyobadilisha maisha yako na namna ambavyo tutatumia mahitaji mbalimbali ya wateja

kubadili biashara yako.kufahamu mahitaji mbalimbali ya wateja itasaidia kukubadilisha tabia

yako ya kusimamia vema manunuzi yako na thamnai ya mabadilishano katika maisha yako. .

Wakati tukijadili katika kipindi cha kwanza, kuwa na mteja ni jambo la msingi na la muhimu

sana wakati kuanza biashara. Ili kuwapata wateja hawa, tunahitajika na muda wa kufanya utafiti

na kujifunza juu ya wateja na upatikanai wa soko.

Kwa kufahamu mahitaji ya mteja, tutaenda kuandaa vitu ambavyo biashara yetu itaviuza au

biashara ipi ya kufanya. Kama tutakuwa tutakuwa na biashara zetu tayari , na kufahamu mahitaji

ya wateja kama walengwa wetu na wapi wateja hawa wataturuhusu kufanya marekesbisho ya

wapi pazuri pa kuweka masoko ili kukidhi mahitaji yetu

Lakini biashara zetu zitafanya nini? Ili kupanua ufafanuzi wetu ya kuwa biashara ni nini

inatupasa tutofautishe aina mbalimbali za biashara. Ni muhimu kutofautisha baina ya bidhaa

katika huduma. Bidhaa ni kitu kinachoshikika wakati huduma ni kitu ambacho hakishikiki lakini

Page 22: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

22

inatoa huduma na inatosheleza mahitaji ya mteja. Kwa mfano, nyanya ni mfano wa bidhaa na

itakupeleka mahali ambapo utaona kama inakupa huduma. Kwa sasa nawaonyesha seti za picha

ambazo mtazijadili katika vikundi na kuona kama picha zipi zitakuwa zinaonyesha bidhaa na

zipi zinaonyesha huduma na mnieleze kwa nini. Weka akili mwako kuwa vitu vinaweza kuwa ni

huduma na pia bidhaa.

Jadili picha, hakikisha unajiuliza maswali ya kwanini mara kwa mara.

Page 23: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

23

Page 24: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

24

Nampongeza kila mtu kwa ushiriki, kwa kurudia jambo ambalo tulikwisha lijifunza, kuwa kuna

aina mbalimbali za biashara na shughuli zenye tija. Tunaweza kuweka katika makundi biashara

hizo, huduma, au kuchanganya pamoja kuwa ni bidhaa na huduma. Kutoka hapa tuanweza

kupanua mawazo yetu ni namna gani biashara yetu biashara yetu itakuwaje.

Tukiangalia kwa undani kuhusu bidhaa hizi na huduma zinatukumbusha tena kuwa zinakuja

kutoka kwa wateja na mahitaji yao. Tukizungumza kuhusu mahitaji ya mteja ni vema tukazigawa

mahitaji haya katika makundi kwasababu hii, tuzigawe mahitaji haya katika makundi ya asilia au

kuzaliwa nacho na mahitaji ya kimwili. Vitu ambavyo vinakidhi mahit mahitaji au mahitaji asilia

ni vitu ambavyo tunahitaji ili tuishi. Chakula na maji kwa mfano vinatupa mfano wa vitu vya

kukidhi mahitaji ya asilia. Mahitaji ya kimwili inajumuisha vitu tunavyovitaji kuimarisha akili

zetu. Kusikiliza muziki kwa mfano inatosheleza mahitaji ya kimwili na roho zetu ili

kuburudisha.

Kwa kuanza mjadala katika hili nawataka kwenda katika vikundi vyenu na kushiriki katika

zoezi.

Sambaza mawazo haya katika vikundi.

Kikundi cha kwanza kijadili mahitaji unayohitaji kutosheleza wakati wa kununua viatu.

Page 25: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

25

Kundi linalofuata litajadili mahitaji unayotegemea katika dawa ya mswaki

Kundi linalofuata, litazungumzia mahitaji yanayotimizwa katika mwili kwa kutengeneza chakula

na kukila.

Page 26: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

26

Nitarudia swali langu.Tafadhali jadili mahitaji inayohusiana na ununuzi wa viatu. Kikundi

kingine kijadili mahitaji yanyopatikana katika dawa ya meno.kikundi kingine kijadili mahitaji

assilia na mahitaji ya mwili na roho inayotoshelezwa kwa kwa kula katika mgahawa.

Rudia kile ambacho watu wamekisema na tafakari juu ya majibu yaliyotolewa ambazo ni mazuri.

Kama tulivyosikia katika majdiliano, kuwa kuna nambari za fursa kwa ajili ya biashara na

huduma ambayo inafanyakazi ya kutosheleza mahitaji ya mteja katika njia mbalimbali yawe ya

mahitaji ya kimwili na kiroho au za kiasili. Kwa mfano mgahawa ni mfano wa huduma kwa

kuwa mtu mmoja ataweza kupikia na kutoa huduma ya chakula, lakini inaweza pia kutupa

bidhaa kwa chakula tunachopewa. Chakula kinatulisha na kutoshelza mahitaji yetu ya kimwili

wakati ladha nzuri ya chakula inatosheleza mahitaji yetu kisaikolojia.

Pumzika hapa uone kama kuna mtu mwenye maswali au anayehitaji ufafanuzi.

Kama katika vitu vingi vilivyo, mahitaji ya mteja inayobadilika kila wakati na hivyo hivyo kwa

biashara kwa ajili ya kufikia mahitaji hayo. Kwa ajili ya kufikia hali ya mabadiliko ya mahitaji

ya wateja, biashara inaweza kubakia yenye faida na inayojiendeleza yenyewe kila wakati. Kwa

mfano, kuhitajika kwa ufanisi na mawasiliano ya haraka kulingana na umbali imepelekea

kugundulika kwa simu ambazo kulingana na muda itafanya kuwepo kwa hatua za miundo

mbalimbali ili kufikia mahitaji ya mteja kwa ufanisi zaidi katika uzalishaji wa bidhaa. Kwa

wakati huu tunazo simu zilizoboreshwa kwa aina tofauti tofauti kwa kuzifanya kuwa ndogo,

inayochukulika, na inayofanya shughuli nyingi.

*kujadiliana katika vikundi na kuziwasilisha, na kuendelea kuhamasisha*.

Kazi za nyumbani:

Jaribu nenda kila kipndi ambazo kulizimaliza wiki iliyopita na jikumbushe umejifunza nini.

Wote ninyi mtaulizwa wiki ijayo kitu ulichojifunza na kila mmoja atakiwa kusema kitu fulani

ambacho ni tofauti na kile kilichosemwa na mwenzake na kuendela hadi kumalizika kwa

kukisema kitu halisi ulichokijifunza.

Page 27: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

27

Sehemu ya 5

Napenda kuwashukuru wote mliohudhuria kwenye kipindi hiki cha mwisho cha mafunzo ya

biashara na masoko. Kipindi cha leo kitalenga zaidi kurejea tulichojifunza na baadae

kuzungumzia mazoea endelevu. Tutaanza na mazoezi ya kufanyia nyumbani ya wiki iliyopita.

Wiki iliyopita niliwaambia mpitie mambo yote mliojifunza kwenye hivi vipindi, na niliwaambia

kuwa kila mmoja atapaswa kueleza alichojifunza. Kwa hiyo nitakupa dakika ya kufikiria hili

tena na nitaanza kuzunguka nikimuuliza kila mmoja alieleze jambo.

Zunguka ukimuuliza kila mmoja akueleze jambo. Jadili na kufafanua mada inapowezekana. Hii

sehemu itachukua muda.

Mmefanya kazi nzuri, inaonekana kuwa kila mmoja wetu amejifunza sana kwenye vipindi hivi.

Sasa naomba mnivumilie na kuniruhusu nirudie baadhi ya mambo tuliojifunza wiki zilizopita.

Kwenye kipindi cha kwanza tumejifunza kuhusu vipengele tofauti vya biasharana zoezi ambalo

tulifanya kupanga vipengele muhimu katika kuanzisha biashara. Kwenye majadiliano haya

tulikubaliana kuwa kipengele cha muhimu sana kwenye biashara ni mteja. Hivyo basi tulitambua

umuhimu wa kutafuta mteja wako na tulifafanua baadae na kujadiliana namna ya kutafiti

mahitaji ya mteja inavyoweza kusaidia katika kuanzisha biashara.

Tulia kidogo nakuuliza kama kuna mtu ana swali au jambo la kuongeza kuhusiana na siku ya

kwanza au kujadiliana zaidi kuhusu walichojifunza.

Baada ya hapo tutaenda kwenye kipindi cha mwisho ambapo tulilenga kwenye ujuzi tulionao

kwa kuwa wateja wazuri. Tulipanga duka na mkanunua kutoka kwangu. Niliwadanganya baadhi

yenu na kwa ujumla nilikuwa muuza duka mbaya. Kwa hiyo hili lilikufundisha kuwa makini

tunapoenda dukani/sokoni na kuwa makini na kuangalia kila kitu. Kwenye majadiliano tulitaja

mambo kadhaa kama vile

Wateja wanapaswa kupanga manunuzi yao kwa uangalifu

Wateja wanapaswa kutafuta na kujifunza kuhusu bidhaa, bei na maduka?

Wateja wanapaswa kuulizia risiti ya malipo na kadi ya uthibitisho.

Wateja wanapaswa kuangalia bidhaa na tarehe ya mwisho wa matumizi kabla ya kupokea,

Wateja wanapaswa kutumia haki yao kudai punguzo au katika mazungumzo na mwenye

duka

Wateja wasiendekeze mazoea yasiofaa

Wateja wawe tayari na kukubali kulipa gharama ya bidhaa na huduma kutoka kwa muuzaji

au mtoa huduma.

Kuna mtu yeyote mwenye jambo lingine ambalo tumejifunza analotaka kuongezea. Waombe

watu wawili waongezee kama kuna mtu atapenda kujitolea.

Page 28: Muongozo wa Elimu ya Masoko Tanzania...Umuhimu Zoezi hili linatoa fursa ya kuonyesha faida na hasara ya mazoea ya wateja wakati wa wanunuzi na kuwaelimisha kuhusu haki na majukumu

28

Mwisho wa kipindi chetu cha pili, tutajiimarisha katika sehemu yetu kama wateja na

kujiunganisha kuwa wateja wazuri kama sehemu ya kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio.

Kwa kuwa wateja wenye uelewa, kwa upande mwingine tunajifunza zaidi na kuelewa maswala

ya biashara na masoko.

Uendelevu

Swali hili la uendelevu ni la nini?

Lenga uendelevu kwenye….

Biashara

Kuheshimu wateja

Kujenga mahusiano

Kutengeneza mikataba

Jiboreshe na tafuta maoni

Dunia

Heshimu mali

Epuka mafuta yalioganda ukiweza

Panda mbogamboga

Ufugaji usio endelevu kwenye eneo moja

Kilimo cha kuhama hama

Madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi

Kama tupo makini, tutaboresha mambo. Kama tutachukua hatua kwenda mbele pamoja,

tutafanya jambo. Dunia ina changamoto lakini tunaweza kupata yalio mazuri.