muongozo wa waragbishi...chadema chama cha demokrasia na maendeleo cuf chama cha wananchi das katibu...

83
UWEZESHWAJI WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA MASUALA YA UONGOZI WA SIASA NA NGAZI ZA MAAMUZI MUONGOZO WA WARAGBISHI

Upload: others

Post on 06-Aug-2021

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

1

UWEZESHWAJI WANAWAKE KUSHIRIKIKATIKA MASUALA YA UONGOZI WA SIASA NA NGAZI ZA MAAMUZI

MUONGOZO WAWARAGBISHI

Page 2: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,
Page 3: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

MCHAPISHAJIShirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF)

Mikocheni “A”, S.L.P 76215, Mtaa wa WiLDAF, Kitalu F, Kiwanja Na. 635Dar es salaam-TanzaniaSimu: +255 22 270 1995,

Barua Pepe: [email protected] / [email protected]: www.wildaftanzania.or.tz

Facebook, Twitter, Instagram - @wildaftz

MTAYARISHAJI: Victoria Lihiru (PHD)

WAHARIRI: Anna Kulaya

Iddi Rajabu Mziray

Haki za kunakili sehemu yoyote ya mwongozo huu kwa madhumuni ya mafunzo zimetolewa pale tu Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) litanukuliwa

kama mwandishi na mchapishaji wa mwongozo huu.

Page 4: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

1

SHUKRANI

Mwongozo huu wa mafunzo ya uwezeshaji wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala ya uongozi wa siasa na ngazi za maamuzi ni kitabu cha waraghbishi wa maswala ya ushiriki wa wanawake katika vyama vya siasa kugombea nafasi za uongozi katika

ngazi za maamuzi. Lengo kuu la mwongozo huu ni kuwawezesha wanawake katika vyama vya siasa kuelewa mambo mbali mbali yanayohusiana na uchaguzi na ushiriki wa wanawake katika chaguzi. Vile vile mwongozo huu unalenga kuongeza uelewa wa wanawake juu ya mbinu mbali mbali za kuweza kushinda uchaguzi.

Mwongozo huu umeandaliwa kwa lugha nyepesi na kwa kutumia mifano pamoja na picha nyingi inayotokana na hali halisi za jamii za kitanzania ili kuwezesha walio wengi kuweza kukitumia katika kukidhi mahitaji yao mbali mbali ya kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.

Mwongozo huu umeandaliwa kwa kupitia mlolongo wa ushirikishaji wadau mbali mbali wa ndani na nje ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (WiLDAF) wanaohusika na maswala ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.

WiLDAF inapenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa michango yao ya hali na mali kipindi chote cha uandaaji, uandishi na uchapishaji wa mwongozo huu.

Shukrani za pekee zimwendee mshauri mwelekezi; Daktari Victoria Lihiru katika kuandika toleo la kwanza la mwongozo huu. Aidha, WiLDAF inatoa shukrani kubwa kwa mraghbishi wa vikao vya majaribio ya awali ya kitini hiki Bwana Idd Rajabu Mziray kwa mchango mkubwa katika kuhariri kitabu hiki. Wote wawili kwa kushirikiana na mkurugenzi wa WiLDAF Wakili msomi Anna Kulaya walitumia muda mwingi kukamilisha yale yaliyopo katika sura mbali mbali za mwongozo huu.

Vilevile, WiLDAF tunatambua mchango wa wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya siasa na taasisi mbali mbali walioshiriki katika zoezi la kuhakiki mwongozo huu.

Ni matumaini ya WiLDAF kwamba, mwongozo huu utatoa chachu na ari kubwa kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala ya uchaguzi ili kushiriki katika uongozi na ngazi za maamuzi.

Anna KulayaMratibu Wa Kitaifa (WiLDAF)

Page 5: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

2

ORODHA YA VIFUPISHO VYA MANENO

ACHPR Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu

AU Umoja wa Africa

CCM Chama Cha Mapinduzi

CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo

CUF Chama Cha Wananchi

DAS Katibu Tawala wa wilaya

SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika

SWOT Uwezo, Udhaifu, Fursa, Vitisho

UNDP Umoja wa Mataifa Kitengo cha Programu za Maendeleo

WiLDAF Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Africa

Page 6: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

3

YALIYOMO

UTANGULIZI 5MODULI YA KWANZA 8Jinsia na Dhana ya Mamlaka 8Somo la 1: Jinsi na Jinsia 8Somo la 2: Dhana za Jinsia 10Somo la 3: Dhana Potofu juu ya jinsia 12Somo la 4: Mamlaka 14MODULI YA PILI 16 Misingi na Haki za Wanawake Kugombea 16 Somo la 1: Mikataba ya Kimataifa na kikanda 16 Somo la 2: Sheria za Ndani ya Nchi 18Somo la 3: Wajibu wa Wadau Mbalimbali 19Somo la 4: Changamoto za Wanawake Kushiriki Uchaguzi 24MODULI YA TATU 26Kujitengenezea jina na mbinu za kuongea kwenye hadhara 26Somo la 1: Kujitengenezea Jina kisiasa 26Somo la 2: Kuongea mbele ya hadhara 28MODULI YA NNE 35 Uteuzi ndani ya Chama 35Somo la 1: Uteuzi wa Wagombea Ndani ya Chama 35MODULI YA TANO 40Kampeni za uchaguzi 40Somo la 1: Dhana ya kampeni 40Somo la 2: Utafiti 42Somo la 2: Timu ya kampeni 45Somo la 4: Sera na Jumbe za Kampeni 49Somo la 5: Kufikia wapiga Kura 55Somo la 6: Rasilimali za kampeni za uchaguzi 57Somo la 7: Siku ya uchaguzi 62MODULI YA SITA 65Ukatili wa kijinsia kwenye Uchaguzi 65Somo la 1: Zoezi: Kupiga kura kwa miguu yetu 65Somo la 2: Dhana ya Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake 66MODULI YA SABA 72Usalama Wa wagombea 72Somo la 1: Usalama wa Kidijitali 72

Page 7: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

4

VIAMBATANISHOKiambatanisho Na. 1: Mpango mkakati wa kampeniKiambatanisho Na. 2: Kuchambua sheria za uchaguziKiambatanisho Na. 3: Kupima Uwezo, Udhaifu, Fursa na VitishoKiambatanisho Na. 4: Fomu ya vifaa vya uchaguziKiambatanisho Na. 5: Fomu ya mpango wa kufikia wapiga kuraKiambatanisho Na. 6: Jinsi ya kutumia fedha zako za kampeni

Page 8: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

5

UTANGULIZI

Mwongozo huu wa uwezeshaji wanawake kushiriki katika masuala ya uongozi wa siasa na ngazi za maamuzi ni nyenzo ya kuwawezesha wanawake wagombea wa vyama vya kisiasa ili kupata ujuzi muhimu wakati wa mchakato wa kugombea nafasi mbali

mbali za uongozi kupita vyama vya siasa. Mwongozo huu umeandaliwa na shirika la Wanawake katika Sheria na Maendelea Barani Afrika (WiLDAF) kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Wanawake Sasa”. Mradi huu unalenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa siasa na ngazi za maamuzi. Hii ni pamoja na kuwajengea uwezo wanawake wanaojihusisha na vyama vya kisiasa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ili kuweza kushawishi ajenda ambazo zinalinda usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na maendeleo endelevu.

1.1. Malengo Ya Mwongozo Lengo kuu la mwongozo huu wa mafunzo ya uwezeshaji wanawake wanaojihusisha na vyama vya kisiasa ni kuwapatia waraghbishi/ wawezeshaji na wasomaji wengine mbinu na maudhui ya kuwezesha wanawake ili kuimarisha stadi na mbinu za kushiriki kikamilifu katika uchaguzi kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi .

1.1.1. Malengo Mahususi ya MwongozoMuongozo huu una malengo mahususi yafuatayo;

1. Kuwapatia wawezeshaji mbinu na maudhui mbalimbali ili waweze kutoa mafunzo kwa wanawake wanaojihusisha na vyama vya siasa waweze kuelewa na kueleza;

a) Dhana mbalimbali kama vile Jinsia na dhana ya mamlaka

b) Misingi na Vichocheo vya Wanawake Kugombea ngazi za uongozi

c) Kujitengenezea jina na mbinu mbali mbali za kuongea kwenye hadhara

d) Mbinu na mikakati ya Kushinda Uteuzi ndani ya Chama

e) Kampeni za uchaguzi

f) Ukatili wa kijinsia katika kipindi cha uchaguzi

g) Usalama wa Mgombea kipindi cha uchaguzi.

2. Kuwezesha wanawake watia nia kuchokoza mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa vyama vya siasa ili viweze kuzingatia masualala ya jinsia katika uongozi hasa wa ngazi za juu.

3. Kuongeza ushiriki wa wanawake wanaogombea wenye uwezo, sifa na vigezo vya kushinda uchaguzi kupitia vyama vya siasa.

1.2. Muundo na jinsi ya Kutumia Muongozo HuuMuongozo huu umechanganya maelezo na mazoezi kwa makusudi ili iweze kutumika katika njia kuu mbili;

a) Mtu ambaye sio mraghibishi akipenda kusoma na kujua zaidi juu ya maswala ya uwezeshaji wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi na ngazi za maamuzi kupitia vyama vya siasa anaweza soma na kufanya mazoezi mwenyewe

b) Kikundi, chama au shirika linalotaka kutoa mafunzo juu ya mambo yote yaliyopo katika muongozi huu waweze kufanya hivyo kwa kutumia maudhui na mazoezi yaliyotolewa ndani ya mwongozo huu.

Page 9: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

6

Zaidi ya yote mwongozo huu umegawanyika katika sura kuu Saba (7) ambazo Ni;

1. Dhana ya Jinsia na Mamlaka

2. Misingi na Haki za wanawake kugombea.

3. Kujitengenezea jina na jinsi kuongea kwenye hadhara:

4. Uteuzi ndani ya Chama:

5. Kampeni za uchaguzi:

6. Ukatili wa kijinsia katika uchaguzi:

7. Usalama wa Mgombea

1.3. Mwongozo kwa Mwezeshaji/ Angalizo kwa MwezeshajiMwezeshaji ana jukumu la kufuatilia na kusimamia mchakato wa kujifunza. Hii ni pamoja na kuepuka kuwaongoza washiriki kulingana na mawazo yako baadala yake uwape washiriki uhuru wa kushiriki na kujifunza na kuheshimu mawazo na uzoefu wa kila mmoja. Ni muhimu kuzingatia mawazo na michango ya kila mshiriki katika darasa. Angalia zaidi wanachokileta kwenye kundi baadala ya kujikita zaidi katika mapungufu kwenye uelewa wao. Onyesha kuheshimu imani zao, dini, na itikadi zao.

1.3.1. Jukumu la Mwezeshaji

Mwezeshaji anapaswa:

i. Kuwa na subira

ii. Onyesha kwamba wewe ni mwanafunzi pia

iii. Ongezea juu ya uzoefu wa mshiriki

iv. Kuwa mwangalifu kwa kile kinachotokea katika kundi

v. Kukabiliana na masuala yanayoibuliwa katika kundi

vi. Himiza ushiriki

vii. Tumia lugha rahisi

viii. Kua msikilizaji mzuri

1.3.1. Kanuni za Maadili Mema kwa Mwezeshaji i. Kuheshimu, kukuza na kulinda haki za binadamu

ii. Onyesha unyeti wa utamaduni au itikadi

iii. Kuheshima utofauti wa mawazo mbalimbali

iv. Kuhakikisha unahifadhi na kulinda siri

v. Epuka kukuza ubinafsi wako

vi. Chunguza mipaka ya ufichuzi wa mambo yako binafsi

vii. Toa taarifa sahihi na isiyo na upendeleo.

Page 10: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

7

1.4. Sehemu ya UtanguliziDakika 30:

Lengo la sehemu hii ni kuhakikisha kwamba washiriki wanajitambulisha, lakini pia washiriki kutambua timu yako uliyoambatana nayo kwenye warisha hiyo.Vilevile, kufahamu matarajio ya washiriki kwa kutumia mfumo uliopendekezwa na mafunzo.

Hatua ya 1: Mwezeshaji awaambie washiriki kuandika yafuatayo katika kipande cha karatasi;

i) Majina yao na mahali wanapotoka,

ii) Kile wanachotarajia kujifunza,

iii) Ni nini wanakitarajia kuchangia katika warsha

Hatua ya 2: Baada ya kuandika majibu ya maswali hapo juu kwenye karatasi waambie wabadilishane karatasi na majirani zao ambao watasimama na kuwatambulisha kwa darasa kwa kusoma majibu ya maswali yote.

Hatua ya 3: Wasilisha mpango mzima wa mafunzo kuanzia mwanzo mpaka mwisho na eleza siku za mafunzo huku ukioanisha na matarajio ya washiriki. Waeleze matarajio ambayo yanaweza kufikiwa ndani ya siku za mafunzo na ambayo hayawezi kufikiwa.

Hatua ya 4: Mkaribishe mtu ambaye atatoa utangulizi na ufunguzi wa warsha ya mafunzo.

Page 11: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

8

MODULI YAKWANZA

DHANA YA JINSIA NA MAMLAKA

UtanguliziModuli hii inatoa uelewa kwa washiriki juu ya dhana ya jinsia na mamlaka na jinsi dhana hizi zinavoweza kuathiri au kuongeza ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa na vyombo vya maamuzi. Moduli hii pia ina mazoezi ya hiari na shughuli ambazo zinaimarisha uelewa namna ambavyo jinsia na mamlaka vinaweza kuwa kikwazo kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi.

Muda: Dakika 180 (Masaa Matatu)

SOMO LA KWANZA: JINSI NA JINSIA

Malengo ya SomoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

• Kueleza maana ya dhana muhimu kama vile “Jinsi” na “Jinsia”

• Kueleza tofauti kati ya “Jinsi” na “Jinsia”

Muda: Dakika 40

Vifaa:Kitini Namba 1: “Jinsi” na “Jinsia”

Stendi ya bango kitita

Bango kitita

Kalamu rashasha

Ubao

Chokaa

Gundi utepe

Mbinu:

Majadiliano ya pamoja

Bungua bongo

Hatua: Hatua ya 1: Tambulisha malengo ya somo hili kwa washiriki. Elezea kwamba katika somo hili tutajadili na kufafanua tofauti kati ya jinsia na jinsia kama misamiati muhimu ambayo itatumiwa katika warsha, na umuhimu wa dhana hizi katika maisha yetu ya kila siku

Hatua ya 2: Waulize washiriki kuchukua dakika moja kufikiria ni neno gani moja linakuja akilini wakati wanaposikia maneno ‘ mwanaume ‘ na pia neno moja wanapoisikia neno ‘mwanamke ‘.

Page 12: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

9

Andika majibu ya kikundi katika safu mbili kwenye bango kititi zilizoandikwa: ‘ Mwanaume ‘ na ‘ mwanamke’.

Hatua ya 3: Zunguka chumba cha warsha huku ukiuliza kila mshiriki kutaja neno moja ambalo linaelezea neno “Mwanaume” na neno moja ambalo linaelezea neno “mwanawake” (Waambie washiriki kwamba kama neno tayari limetajwa wanapaswa kufikiria neno tofauti).

Hatua ya 4: Hakikisha kwamba, baadhi ya maneno yakuelezea sifa za kibaolojia (Kama vile ‘ uume ‘ kwa wanaume na ‘ matiti ‘ au ‘ hedhi ‘ kwa wanawake hutokea kwenye orodha

Hatua ya 5: Wakati orodha itakapokamilika, waulize washiriki kama kuna maneno waliyotaja yanayoweza kubadilishwa kutoka kwenye neno mwanaume kwenda kwenye neno mwanamke.

Je, kuna maneno yoyote ya ‘ Mwanaume’ yanaweza kumuelezea ‘mwanaume’?

Ni maneno gani ambayo yanamuhusu tu ‘mwanaume’ na maneno yapi yanamuhusu ‘mwanamke’ peke yake

Hatua ya 5: Hakikisha vipengele vinavyoonesha maneno yahusuyo baiolojia yanaandikwa kwa rangi tofauti ya kalamu rashasha kwenye orodha.

Hatua ya 6: Hitimisha kwa kuelezea kwamba orodha ya maneno inaonyesha tofauti kati ya neno Jinsi na jinsia. (Tumia Kitini 1 A: Jinsi na Jinsia ili kuhitimisha somo hili.)

KITINI NAMBA 1A: Jinsi na Jinsia

Katika hali ya kawaida tunapozungumzia kuhusu Jinsia, jamii huchanganya kati ya hizo mbili. Ni vema kuangazia jinsia katika muktadha wa usawa katika fursa zilizopo katika jamii zetu, ugawaji majukumu na unufaikaji wa rasilimali baina ya wanaume na wanawake katika jamii zetu badala ya tabia za kibaiolojia zinazobainisha utofauti kati ya wanaume na wanawake. Jinsia ni kuhusu nani anamiliki nini, anayefanya nini, na ni nani anafaidika na nini katika jamii.Jinsi: Hizi ni tabia za kibiaolojia (ikiwa ni pamoja na vinasaba, anatomia, na fiziolojia) ambayo kwa kawaida hufafanua wanadamu kama wanawake au wanaume. Kumbuka kwamba tabia hizi za kibaiolojia si za kipekee; hata hivyo, watu wengine wanamiliki tabia za kiume na kike. Hii inajumuisha sifa ambazo ni; Ni zakuzaliwa na za asili Hakuna tofauti kutoka utamaduni mmoja na utamaduni mwingine au nyakati kwa nyakati.Haiwezekani kuzibadilisha ila kwa mfumo wa upasuaji: Kwa mfano. Wanawake tu wanaweza kuzaa au kunyonyesha

Jinsia: Hii ni mgawanyo wa majukumu ya kijamii na majukumu yanayohusishwa na kuwa msichana na wavulana au wanawake na wanaume.Hizi ni sifa ambazo; Si zakuzaliwa nazo, Ni majukumu ya jinsia ya kujifunza na hutofautiana sana katika jamii mbalimbali, tamaduni na

vipindi vya kihistoria, na pia hutegemea masuala ya kijamii na kiuchumi, umri, elimu, ukabila, na dini,

Ingawa majukumu haya yana mizizi ya kina, yanaweza kubadilishwa baada ya muda, kwa kuwa viwango vya kijamii na kanuni sio tuli bali hubadilika,

Kwa mfano: Mwanaume ndio anaweza kuwa kiongozi mzuriHivyo hatuhitaji sifa za kijinsi ili kuwa kiongozi, tunahitaji kubadilisha mitazamo ya jamii kuhusu jinsia ili kuwapa fursa wanawake kugombea.

Page 13: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

10

SOMO LA PILI: DHANA ZA JINSIA

Malengo ya SomoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kutambua na kufafanua dhana mbali mbali ambazo mara nyingi hutumika kueleza dhana ya jinsia

Muda: Dakika 45

VIfaaKadi za manila

Kalamu Rashasha

Kitini Namba 1 B: Dhana za jinsia

Zawadi/Tuzo kwa washindi

MbinuMajadiliano ya Vikundi

Muhadhara

Mhadhara

Hatua:

Hatua ya 1: Wajulishe washiriki kuwa sasa ni wakati wa zoezi! Gawa darasa katika makundi matano, kila kikundi kipate kadi 14 za manila (kadi 7 zilizo na misamiati mbali mbali ya jinsia na kadi 7 zinazoelezea maana ya misamiati hiyo ya dhana muhimu ya kijinsia)

Hatua ya 2: Uliza kila kikundi kuchukua dakika 5 ili kusoma kadi hizo: Wajulishe washiriki masharti ya zoezi: kwamba sasa “Utasoma kwa sauti maelezo yanayoelezea maana ya kila msamiati na kila kundi linapaswa kuoanisha maana na neno kisha kubandika kadi mbili yaani kadi ya neno na maana pamoja. Kundi litakaloweza kupatia kuoanisha litapewa alama 1.

Hatua ya 3: Anza kusoma maana ya misamiati kwa sauti, huku ukinakili alama kwenye bango kitita kwa kila kikundi kilichoweza kupatia kuoanisha maneno na maana zake.

Hatua ya 4: .Mwisho hesabu alama na kutangaza mshindi, Wasilisha tuzo ya mshindi na kama wanaweza kushiriki tuzo hiyo kwa pamoja miongoni mwa washiriki wote: (Tumia kitini na 1B: Dhana za jinsia kuhitimisha majadiliano)

KITINI NAMBA. 1B: DHANA ZA JINSIA

Usawa wa kijinsia Ni hali ambapo watu wote huwa na haki sawa fursa sawa na malipo sawa bila kujali kama ni wa kike au wa kiume. Ni pamoja na haki sawa thamani sawa nafasi sawa uwezekano sawa wa kupata rasilimali na faida na ushirikishwaji sawa kwenye maamuzi ili kudai mahitaji na haki sawa

Fursa sawa za jinsia Humaanisha kuwatendea wanawake na wanaume sawasawa kutokana na mahitaji yao. Ni pamoja na kutambua kisicho sawa na kulenga usawa wa wanawake na wanaume.

Page 14: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

11

Mgawanyo wa kazi kijinsia:

Kazi, Wajibu au vitendo vinavyowahusu wanawake na wanaume kutokana na walivyolelewa. Matokeo yake ni kuwa na “kazi za wanawake” na “kazi za wanaume. Tabia, majukumu hayo kuhusishwa na wanawake na wanaume na jamii husika ambayo ni kuimarisha viwango mbalimbali vya jamii kupitia taasisi zake za kisiasa na elimu, mifumo ya ajira, mila na maadili, na kwa njia ya familia

Ubaguzi wa kijinsia: Ni mtazamo wa kawaida au mtazamo kuhusu sifa, au tabia ambazo ni au zinapaswa kuwa na maana ya wanawake na wanaume au majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na wanawake na wanaume

Majukumu ya jinsi: Haya ni majukumu ambayo hufanywa na wanawake au wanaume kwa nguvu au hali ya kibiolojia. Majukumu ya jinsi yanaweza kufanywa tu na moja tu ya jinsi na jinsi nyingine haiwezi kufanya.

Majukumu ya uzazi: Inahusisha shughuli kama vile kuzaa na kutunza watoto, kuosha vyombo, kupika, kusafisha nyumba, kunyonyesha/kuwatunza wagonjwa, uchotaji maji ukusanyaji kuni, ununuzi nk. Katika jamii nyingi za vijijini, kazi ya uzazi ni sehemu ya kazi za wanawake kuliko wanaume.

Majukumu ya uzalishaji:

Shughuli zote zinazohusu uchumi wa kaya na jamii. Ni pamoja na kilimo ufugaji ajira na ujasiliamali. Wote wanawake na wanaume waweza kuwa na nafasi za uzalishaji lakini mara nyingi wanafanya kazi tofauti kutokana na mgawanyo wa kazi kutokana na jinsia. Kazi za wanawake mara nyingi hazionekani na hazithaminiwa sawa na za wanaume

Dhana potofu juu ya jinsia:

Ni maoni yanayohusu tabia au wajibu wa wanawake au wanaume. Dhana potofu ya jinsia ni imani inayomfanya mtu kuwa na mtazamo fulani kuhusu wanawake au wanaume. Matumizi ya dhana potofu ni kitendo cha kumwangalia mtu kupitia imani hiyo.

Pengo la jinsia: Mafanikio yasiyo sawa ya wanawake na wanaume kwenye soko la ajira pamoja na kukosa haki na umiliki wa mali kwa wanawake duniani kote au kukosa uwakilishi katika ngazi za uongozi na maamuzi.

Upofu wa kijinsia: Ni hali ya kushindwa kutambua kwamba mahitaji ya mwanamke na mwanaume yanatofautiana. Na hiii huhusishwa mitazamo kwamba maswala ya kijinsia hayana umuhimu katika miradi , programu au sera (UNDP)

Mwamko wa jinsia Utambuzi wa ukweli kwamba uzoefu wa maisha, matarajio, na mahitaji ya wanawake na wanaume ni tofauti, kwamba mara nyingi kuhusisha usawa na ni chini ya mabadiliko

Mzani sawa wa kijinsia Kuwa na idadi sawa (au ya kutosha) ya wanawake na wanaume katika ngazi zote ndani ya shirika/taasisi nk ili kuhakikisha uwakilishi sawa na ushiriki katika maeneo yote ya shughuli na maslahi

Kuzingatia Jinsia Utaratibu wa kuzingatia mahitaji husika, maslahi na vipaumbele vya wanaume na wanawake katika sera na shughuli zote za shirika/taasisi. Hii inakataa wazo kwamba jinsia ni suala la tofauti

Ufeministi Niharakati za ukombozi zilizoanzishwa na wanawake ili kupinga mfumo dume ambao unawakandamiza wanawake katika nyanja mbalimbali kama; Kifikira, kiuchumi, Kisiasa, kijamii na kiutamaduni

Mahusiano ya kijinsia: Haya ni mahusiano kati ya wanawake na wanaume wakati fulani na muda fulani. Yafafanua tofauti ya mamlaka kati ya jinsia za kuzaliwa na yachambua sehemu ya mwanamke na mwanamume wakati wa kugawa rasilimali nyajibu faida haki nguvu na upendeleo

Page 15: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

12

SOMO LA TATU: DHANA POTOFU JUU YA JINSIA

Malengo ya SomoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kuelewa dhana potofu za jinsia na athari zake katika ushiriki wa wanawake katika siasa

• Kuelewa jinsi ya kuondokana na dhana potofu dhidi ya jinsia ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa.

Muda: Dakika 45

VifaaOrodha ya vifaa, majukumu na shughuli

Kitini cha mshiriki Namba 1C: Dhana Potofu Juu ya Jinsia

Hatua:

Hatua ya 1: Anza kwa kutambulisha somo kwamba sasa tutaenda kuangalia dhana potofu mbali mbali dhidi ya jinsia ambazo huathiri ushiriki kamilifu wa wanawake katika siasa na ngazi za maamuzi.

Hatua ya 2: Gawa karatasi yenye orodha ya vifaa, majukumu na shughuli mbali mbali kisha waambie washiriki kuandika neno “Me”’ kama wanafikiri jamii inafikiria kifaa, jukumu au shughuli hiyo ni ya mwanaume, na waandike herufi “Ke” kama wanafikiri jamii inafikiria kifaa, jukumu au shughuli hiyo ni ya mwanamke.

Hatua ya 3: Baada ya zoezi hilo kusanya karatasi zote na anzisha majadiliano kulingana na majibu ya washiriki kwa kufutwa maswali yafuatayo huku ukinakili maelezo muhimu kwenye bango kitita.

• Kwa nini tunahusisha vifaa/mali/shughuli majukumu fulani na wanawake au wanaume?

• Ni shughuli gani zilizo hapa juu zina misingi ya kibiolojia?

• Ni shughuli gani ambazo zina msingi wa kibiolojia na bado zinafanywa na ama wanaume au wanawake pekee?

• Ni nini kinatokea wakati vitu hivi vikiwa na thamani ya kiuchumi? Kupika, kulima nk

Hatua ya 4: Hitimisha kwa kusema kwamba nia ya zoezi hili ni kufafanua jinsi jamii inahusianisha mali/majukumu/ au shughuli flani na wanawake au wanaume. Na pia kuona jinsi gani kazi ikishakua na kipato hubadilika na kuhusianishwa na wanaume. Hii huathiri wanawake katika harakati za ushiriki katika siasa. (Unaweza kutumia Kitini Namba 2: Dhana Potofu Juu ya Jinsia kutoa maelezo zaidi)

Page 16: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

13

KITINI NAMBA 1 C: DHANA POTOFU JUU YA JINSIA

a) Katika maisha, wanaume na wanawake hupokea masharti kutoka kwa familia, vyombo vya habari, na jamii kuhusu jinsi wanapaswa kutenda kama wanaume au wanawake. Kama tulivyoona, utofauti huu unajengwa na jamii na si sehemu ya asili yetu au kibaiolojia

b) Kanuni hizi zinatofautiana kuanzia umiliki wa mali, shughuli ambazo tunafanya na majukumu tunayofanya katika jamii. Kwa mfano, kuna baadhi ya mali kama ardhi, magari makubwa, mazao ya biashara, na wanyama wa biashara ambao wanawake wanaonekana kama hawana uwezo wa kumiliki. Wanawake ni kuonekana kama maridadi na wanapaswa kuwa na mambo kama vile kumiliki vifaa vya jikoni , kuku, na mimea kwa ajili ya matumizi ya nyumbani tu. Pia, wanawake wanaonekana kama hawawezi kuwa viongozi imara kama wanaume.

c) Hata hivyo, wanawake wanaweza kufanya chochote hata kujihusisha na uongozi na vyama vya siasa. Dhana potofu juu ya jinsia zinaweza kuathiri maisha yako na jamii nzima, hivyo tunapaswa kuwa makini kuhusu jinsi ya kukuza mahusiano mazuri zaidi ya kijinsia katika vyama vya siasa.

Dhana potofu juu ya jinsia ni nini?

Dhana potofu juu ya jinsia ni mitazamo kuhusu sifa au tabia ambazo ni/au zinapaswa kuwa za wanawake au wanaume au majukumu ambayo ni yanapaswa kufanywa na wanaume na wanawake. Ubaguzi wa kijinsia unaweza kuwa chanya au hasi kwa mfano, “wanawake ni walezi” au “wanawake ni dhaifu (Mtazamo hasi).

Ubaguzi ni hasi kama unaweka mipaka ya uwezo wa wanawake au wanaume wa kuendeleza uwezo wao, kufuata kazi zao za kitaaluma, na kufanya uchaguzi kuhusu maisha yao na mipango ya maisha.

MIFANO YA DHANA POTOFU YA JINSIA

a) Tabia: wanawake ni waoga, wapole, wenye mpango na wasafi wanaume ni jasiri, wakali, watawala na hujiamini.

b) Tabia za nyumbani: wanawake hupika, hutunza nyumba, walezi bora wa watoto. Wanaume ni bora kwenye utengenezaji, hawajui kupika, kushona au kulea watoto wao.

c) Kazi: wanawake wana kazi safi kama walimu nesi karani na mtunza maktaba wao si wanasiasa. Wanaume hufanya kazi chafu kama fundi magari wajenzi fundi bomba wahandisi na ni wanasiasa bora

d) Mwonekano: wanawake wawe wembamba na wafupi wasio na nguvu wanaume wawe warefu. Hata hivyo dhana potofu zinazohusu mwonekano ni tofauti kutokana na mila husika.

Je, ni kwa jinsi gani dhana potofu juu ya jinsia zinaweza kuathiri haki za wanawake kujihu-sisha na siasa?

a) Wasichana wengi hasa wa vijijini wamekosa elimu bora kwa sababu ya ubaguzi wa kijinsia. Kwa mfano, ubaguzi kuhusu jukumu la wanawake kama vile katika majukumu ya ndani na familia unaweka vikwazo vyote kwa njia sawa za kupata elimu bora. Mara nyingi wasichana huwa wanaegemewa kwa majukumu ya ndani kwa dhana kwamba watakuwa wanategemea wanaume.

Page 17: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

14

b) Kutokuwa na uwakilishi mzuri wa wanawake katika uongozi na ushiriki wa kisiasa. Majukumu ya kijinsia ni sababu kubwa na mzizi kwa wanawake wachache kushiriki katika siasa. Wanawake wamewekwa nyumbani na kuonekana kwa umma na kufanya uamuzi kuachwa kwa wanaume. Wanawake wamesemwa kuwa mapambo na wanapaswa kukaa nyumbani ili kuepuka wao kuwa kivutio kwa watu wengine. Hii huathiri wanawake wengi kushiriki katika siasa.

c) Wanawake kukosa mamlaka: Katika jamii yetu, wanawake kwa kawaida wana mamlaka kidogo kuliko wanaume. Hii ni desturi ya kijamii — kitu ambacho huchukuliwa kawaida katika jamii yetu. Kutokuaw sawa katika mamlaka kati ya wanawake na wanaume ina maana kwamba wanawake wanakosa uamuzi juu ya maswala yanayoathiri maisha yao ya kila siku ikiwemo uamuzi wa kujiunga na chama cha siasa na kuwa kiongozi.

SOMO LA NNE: MAMLAKA

Malengo ya somoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kuelewa maana na aina za mamlaka

• Kufafanua na kueleza athari za kutokua na usawa juu ya mamlaka katika jamii

• Kutambua hatua zinazofaa za kukuza usawa wa mamlaka na kuheshimu haki na heshima ya mtu binafsi.

Muda: Dakika Vifaa:Kitabu cha mwongozo wa mwezeshaji

Bango kitita

Kalamu Rashasha (Rangi mbili tofauti)

Kitini cha mshiriki Namba 1 D: Mamlaka

Mbinu:Majadiliano ya pamoja

Bungua Bongo

HatuaHatua ya 1: Anza kwa kutambulisha somo kwa kusema sasa tutaenda kujifunza dhana ya mamlaka na athari za kukosa mamlaka katika kukuza usawa wa kijinsia.

Hatua ya 2: Bandika bango kitita mahali ambapo kila mtu anaweza kuona, kisha chora duara katikati ya karatasi hiyo ya bango kitita na kuandika neno “MAMLAKA” kati kati ya duara

Page 18: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

15

Hatua ya 3. Uliza mshiriki kutaja maneno yoyote wanafikiri yanahusiana na neno “MAMLAKA” wakati huo endelea kurekodi majibu yao kuzunguka neno “MAMLAKA” kwnye bango kitita

Hatua ya 4: Waulize washiriki kutokana na majibu ambayo wametoa,

• Kati ya wanaume na wanawake ni nani ana mamlaka zaidi katika jamii zetu?

• Waulize washiriki kuhusu jinsi wanafikiria ukosefu wa mamlaka huathri wanawake kuchukua nafasi za uongozi kupitia vyama vya kisiasa?

Hatua ya 5: Hitimisha majadiliano kwa kueleza maana ya mamlaka, aina na athari za wanawake kukosa mamlaka (Tumia Kitini Namba 1 D: Mamlaka, kutoa maelezo zaidi)

KITINI NAMBA 1 D: MAMLAKA

Mamlaka ni nini? Ni uwezo au nguvu ya kushawishi wengine kuamini, na kufanya kama unavyotaka. Mamlaka inaweza kuwa umiliki wa mali, rasilimali, akili na itikadi. Kuna aina tofauti za mamlaka ambazo zinaweza kutumika kwa njia chanya au hasi. Wote tuna nguvu ndani yetu ambapo tukizitumia vizuri tunaweza kuleta mabadiliko chanya katika upatikanaji wa fursa na umiliki wa rasimali. Kuna aina kuu nne za mamlaka–

i. Mamlaka juu ya: ni nguvu aliyonayo mtu kuweza kumtawala mtu ; au uwezo wa kikundi cha watu kuweza kuwatawala watu wengine. Utawala huu unaweza kutokana na ukiukwaji ulio au usio wa moja kwa moja kutoka katika imani na mienendo ya jamii ambayo inawaweka wanaume katika nafasi iliyobora zaidi kuliko wanawake.

ii. Mamlaka ya kufanya: Ni nguvu na vitendo ambayo mtu mmoja au vikundi wanatumia kuleta mabadiliko chanya. Ni mamlaka inayoendana na uwezeshaji.

iii. Mamlaka na: Ni nguvu inayotokana na mmoja au zaidi kuungana na mwingine au wengine na kutekeleza jambo ambalo peke yake au peke yao wasingeweza. Hi ni pamoja na kuunganisha nguvu ya pamoja kwa lengo la kutatua uvunjfu wa haki kwa kutumia nguvu chanya.

iv. Mamlaka ya ndani: Ni ile nguvu inayotoka ndani yetu au ndani ya mtu. Inajumuisha kutambua uwezo wetu tulio nao ndani yetu. Hii inapelekea kujiamini na kuweza kubadilisha maisha yetu sisi wenyewe na yale ya jamii inayotuzunguka. Kwa kutambua, nguvu ya chanya ndani yetu tunasukumwa kushughulikia matumizi mabaya ya nguvu yanayoondoa haki katika jamii na kuwaheshimu wengine kama watu wenye hadhi sawa.

Kuna hali ambayo mtu mmoja anaweza kuwa na uwezo zaidi ya mwingine. Kutumia nguvu yetu juu ya mtu mwingine ni kukiuka haki zay yule mtu (Mamlaka ya juu). Kukosekana kwa mamlaka sawa kati ya wanaume na wanawake katika jamii inaweza kuwa na mchango mkubwa katika ushiriki wa wanawake katika uongozi na maamuzi ya kujiunga na siasa. Kwa mfano, mwanamke mara nyingi katika jamii zetu hana uwezo wa kuamua kama kugombea nafasi tofauti za uongozi bila ya kutafuta kwanza ruhusa kutoka kwa mume wake. Katika visa vingine, mwanamke ambaye ni tegemezi kwa mpenzi wa kiume kuomba ruhusa kwa ajili ya msaada wa kifedha. Wanawake wengi wanaweza kuhisi kwamba si sawa kwao kugombea katika nafasi yoyote tofauti ikiwa ni pamoja na hata ndani ya vyama vya kisiasa kwa hofu ya ukosefu wa msaada wa kifedha wakati wa kampeniTunaweza kuunganisha mamlaka zetu na wengine ili kuhamasisha ushiriki wa wanawake hasa ukizingatia kwamba wote tuna “mamlaka ya kufanya” kitu na kuchukua hatua. Vilevile tunaweza kushawishi jamii, serikali, vyama vya siasa kwa kutumia nguvu ya pamoja na kuhakikisha wanawake wanapata fursa za uongozi kwa kushirikiana nao katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

Page 19: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

16

MIKATABA NA SHERIA ZINAZOWAPA WANAWAKE HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA NGAZI ZA MAAMUZI

UtanguliziMada hii inafundisha kuhusu mikataba muhimu inayompa mwanamke uhalali na haki ya kugombea katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa kidemokrasia. Mikataba hii ambayo imegawanyika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na sheria mbalimbali za nchi imeweka bayana vifungu vinavyoelezea ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.

Pia inafundisha wajibu wa serikali na vyama vya siasa katika kuhakikisha kuna ushiriki sawa wa wanawake na wanaume katika uongozi, kujifunza sababu muhimu za kwa nini ugombee katika mchakato wa uchaguzi, na kufahamu changamoto zinazowafanya wanawake wasishiriki katika mchakato wa uchaguzi.

Muda: Dakika 135

SOMO LA KWANZA: MIKATABA YA KIMATAIFA NA KIKANDA

Malengo ya SomoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kufafanua maana ya mikataba ya kimataifa na ya kikanda

• Kufafanua na kueleza muktadha wa sheria za kimataifa na za kikanda zinazomwezesha mwanamke kugombea nafasi za uongozi

Muda: Dakika 30

Vifaa: • Mwongozo wa mweseshaji

• Kitini cha mshiriki Namba 2 A: Mitataba ya kimataifa na kikanda

• Bango kitita

Mbinu:Bungua bongo

Muhadhara

Hatua: Hatua ya 1: Anza kwa kuwauliza washiriki kutumia dakika mbili kufikiria wanachoelewa kuhusu maneno haya “Mikataba ya Kimataifa” na “Mikataba ya kikanda” Chukua majibu machache na yanakili kwenye bango kitita.

MODULI YAPILI

Page 20: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

17

Hatua ya 2: Kwa njia ya muhadhara elezea kuhusu mikataba ya kimataifa na kikanda juu ya haki za wanawake kugombea nafasi mbali mbali za uongozi (Tumia Kitini Namba 2A: Mikataba ya Kimataifa na Kikanda kutoa maelezo zaidi)

KITINI NAMBA 2 A: Mikataba ya Kimataifa na Kikanda

Mikataba ya kimataifa au ya kikanda ni makubaliano au ahadi kati ya nchi mbili au zaidi katika jambo fulani ambapo nchi hizo hukubaliana kulifanya kwa pamoja, kuweka mikakati ya nchi kufikia makubaliano hayo au kuacha kulifanya kabisa. Mkataba huo unaweza kuwa wa haki za binadamu, usawa wa kijinsia, kutunza mazingira n.k

Tanzania imesaini na kuridhia mikataba ya kimataifa na kikanda inayowapa watu wote haki kugombea na kushiriki katika ngazi za maamuzi. Wanawake ni zaidi za asilimia 50 ya watu wote duniani na hata nchini Tanzania, hivyo mikataba hii inaitaka Tanzania kuhakikisha inawapa pia wanawake haki ya kushiriki katika uongozi na uchaguzi. Mikataba hii ni kama vile:

1. Tamko la Kimataifa la Haki za msingi za Binadamu, 1948.

2. Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa, 1966.

3. Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni 1966.

4. Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), uliopitishwa mwaka 1981 na kuanza kutumika rasmi 1986

5. Sheria ya Kuanzishwa Kwa Umoja wa AU, 2000.

6. Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1999.

7. Agenda ya Afrika ya 2063.

8. Maendeleo Endelevu ya Dunia ya 2030.

9. Tamko la Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Africa (SADC) juu ya jinsia na maendeleo la mwaka 1997.

Kwa lengo la kupata suluhisho katika tatizo la ushiriki mdogo wa wanawake katika nafasi za uongozi kwenye nyanja mbalimbali, kuna mikataba mahususi ya kimataifa na kikanda inayolenga kukuza na kulinda haki za wanawake ikiwemo ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi. Mikataba hiyo ni kama vile:

a) Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake 1979.

b) Mkataba wa Nyongeza katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu juu ya Haki za Wanawake Barani Afrika (Maputo Protocol), 2003.

c) Azimio la Beijing, 1995.

d) Azimio la Solemn Juu ya Usawa wa kijinsia Barani Afrika, 2004.

e) Itifika ya Jinsia na Maendeleo ya SADC 2008

f) Sera ya Jinsia ya Afrika Mashariki, 2018

Muhtasari (Mwezeshaji)Mikataba tajwa hapo juu inatambua kuwa haki za wanawake ni haki za binadamu na hivyo ni muhimu kwa nchi kuziheshimu na kuweka utaratibu thabiti wa kuzitekeleza kama zilivyo haki nyingine. Pia mikataba hii pamoja na tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa ushiriki finyu wa wanawake katika ngazi za uongozi ni kikwazo katika:

Page 21: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

18

a) Kufanikisha maendeleo endelevu.

b) Huathiri jitihada za nchi kukuza demokrasia yake.

SOMO LA PILI: SHERIA ZA NDANI YA NCHI Malengo ya SomoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kueleza sheria za ndani ya nchi zinazomruhusu mwanamke kugombea.

• Kueleza sheria mbali mbali za nchi zinazosimamia na kutoa muongozo wa shughuli zote zinazohusu mchakato wa uchaguzi

Muda: Dakika 30Vifaa:

• Kitini cha mshiriki Namba 2 B: Sheria za ndani ya nchi

• Kalamu rashasha

• Gundi utepe

• Kadi za manila na vip kadi

Mbinu:Majadiliano ya vikundi

Matembezi ya picha

Hatua: Hatua ya 1: Gawa washiriki katika vikundi 4 na gawa vip kadi zenye swali moja kwa kila kikundi kwa majadiliano ya dakika 10. Kila kundi lazima waandike majibu yao kwenye bango kitita na kubandika kwenye eneo lolote ndani ya chumba cha mkutano.

Kikundi cha 1 & 2: Orodhesha sheria za nchi zinazompa mwanamke haki ya kugombea?

Kikundi cha 3 & 4: Orodhesha sheria za nchi zinazotoa muongozo wa shughuli zote za uchaguzi?

Hatua ya 2: Uliza vikundi kutumia dakika mbili (2) kwenda kwenye majibu ya kila kikundi na kuongeza sheria yoyote ambayo kikundi kingine kimesahau kuiandika.

Hatua ya 3: Fafanua kuhusu sheria za nchi zinazompa mwanamke haki ya kugombea na uoneshe jinsi sheria hizo zinatoa muongozo wa shughili zote za uchaguzi kwa kutumia Kitini Namba 2 B: Sheria za Ndani ya Nchi

Page 22: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

19

KITINI NAMBA 2 B: Sheria za Ndani ya Nchi

Kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na usawa wa kijinsia, Tanzania imetunga sheria ambazo zinatoa haki kwa wanawake kugombea nafasi mbali mbali za uongozi. Sheria hizi pia hutoa muongozo na kuratibu shughuli zote zinazohusu mchakato wa uchaguzi: Sheria hizo ni kama zifuatazo:

1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara ya 13 (4) inakataza ubaguzi wa mtu yeyote kwa mtu mwingine au mamlaka yoyote. Kifungu cha 21 (1) kinatoa haki kwa kila mwananchi kushiriki katika masuala yanayohusu utawala wa nchi ama moja kwa moja au kupitia wawakilishi.

2. Sheria ya Uchaguzi (Sura ya 343), 2015. Sheria hii ndio sheria inayosimamia mambo yote yanayohusu uchaguzi wa wabunge na raisi Tanzania. Pia inatambua ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi ya kisiasa na uongozi. Mbali na hilo, mwaka 1995 mfumo wa viti maalumu vilianzishwa chini ya sheria hii kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi na uongozi na kuhakikisha usawa wa kijinsia katika bunge.

3. Sheria ya Vyama vya Siasa, 2019. Sheria hii pia inavitaka vyama vya siasa kuhakikisha inazingatia maswala ya jinsia katika kusajili chama na uongozi wa chama

4. Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010. Sheria hii ndio inasimamia maswala yote ya gharama za uchaguzi, kuanzia mchakato unapoanza mpaka unapomalizika. Ni sheria muhimu sana kuijua kwa sababu inaweza kukusababishia kuenguliwa katika kinyang’anyiro au ushindi wako kutenguliwa

SOMO LA TATU: WAJIBU WA WADAU KATIKA KUKUZA USHIRIKI WA WANAWAKE

Malengo ya somoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kutambua wadau mbali mbali ambao wanawajibu wa kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika siasa na vyombo vya maamuzi.

• Kueleza mchango wa wadau mbali mbali katika kukuza ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi.

Muda: Dakika 30.

Vifaa: • Kitini cha mshiriki namba 2 C: Wajibu wa Wadau Mbalimbali kuongeza ushiriki wa

wanawake katika siasa na uongozi

• Kisa mkasa (Ziara ya bi Mwema)

• Kiongozi cha mwezeshaji

MbinuKisa Mkasa

Maswali na Majibu

Kazi za vikundi

Page 23: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

20

Hatua: Hatua ya 1: Anza kwa kueleza kwamba katika somo hili tutajifunza wajibu wa wadau mbali mbali katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa na kisha orodhesha na jadili wadau mbali mbali ambao wanamchango kuhakikisha ushiriki kikamilifu wa wanawake katika siasa na uongozi

Hatua ya 2: Jadili mchango wa kila mdau (Serikali, Vyama vya siasa, Asasi za Kiraia, Wanawake na wanaume) katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa. (Unaweza kutumia kitini namba 2 C: Wajibu wa Wadau kutoa maelezo zaidi)

Hatua ya 3: Mualike mshiriki mmoja kusoma kwa sauti kisa mkasa cha “Ziara ya Bi mwema” na gawanya washiriki katika vikundi kujibu maswali yanayofuata.

Maswali

1. Serikali inawajibu gani kuhakikisha mji wa kusadikika unatambua haki za wanawake katika uongozi? (Kikundi Na. 1)

2. Nini wajibu wa vyama vya siasa katika kisa hichi cha ziara ya bi Mwema? (Kikundi Na. 2)

3. Nini wajibu wa Asasi za Kiraia katika kisa hiki.

4. Wewe kama mwanamke nini wajibu wako kuhakikisha mji wa kusadikika wanaheshimu haki ya mwanamke kuwa kiongozi? (Kikundi Na. 3)

5. Nini mchngo wa wadau wengine kama wanaume, viongozi wadini katika kisa hichi? Kikundi Na. 4)

KISA MKASA: ZIARA YA BI MWEMAMwaka 2015 Bi Mwema alipata fursa ya kutembelea mji wa kusadikika kusini mwa nchi ya ahadi. Alikutana na viongozi wengi wa kisiasa katika nchi hiyo. Mkuu wa mji huo alimpa nafasi Bi Mwema ya kuhutubia umma wa watu wengi waliojitokeza. Baada ya kupanda jukwaani Bi mwema alianza na salamu ya Wanawake na uongozi hoyeeee! lakini alishtushwa na ukimya wa hadhara hiyo kutoitikia salamu yake. Baada ya kumaliza kuhutubia Bi mwenda alitamani kujua kwa nini watu hawakuitikia salamu yake, hivyo akaamua kumuuliza mkuu wa mji huo kwa nini hilo lilijitokeza.

Mkuu akamjibu hapa hakuna utamaduni wa wanawake kuwa viongozi, sisi tunaamini mwanamke hana haki hiyo mpaka aruhusiwe na mume wake au familia yake. Hapa kwetu sio kama wanawake wa huko kwenu mjini na hata chama chochote hapa hakiamini wanawake kabisa. Hata wanawake wenyewe wanajua hilo hivyo hata hawajitokezi kabisa kuomba nafasi maana wanajua hawatachaguliwa

Hatua ya 4: Waambie washiriki kuchagua mwakilishi mmoja kuwasilisha majibu ya maswali hapo juu.Hatua ya 5: Hitimisha somo kwa kutumia maelezo yaliyotolewa katika Kitini Namba 2 C: Wajibu wa Wadau Mbalimbali

Page 24: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

21

KITINI NAMBA 2 C:WAJIBU WA WADAU MBALIMBALIIli kufikia ushiriki sawa baina ya wanawake na wanaume katika njanya za siasa na katika vyombo vya maamuzi, mikataba ya kitaifa na kikanda pamoja na tafiti mbalimbali zinaainisha jitihada zinazotakiwa kuchukuliwa na serikali, vyama vya siasa na wadau wengine kama ifuatavyo :

Serikali

i) Kuweka jitihada na kuhakikisha usawa wa kijinsia (50: 50 )unafikiwa katika ngazi zote za maamuzi ikiwemo nafasi zote za maamuzi ikiwemo nafasi zote za kuteuliwa na kuchaguliwa ndani na nje ya nchi maamuzi .

ii) Kuchukua jitihada na kukataza aina yoyote ya ubaguzi dhidi ya wanawake

iii) Kuchukua na kutekeleza hatua mahususi na za muda mfupi (Temporary Special Measures) ili kuharakisha kupatikana kwa usawa baina ya wanaume na wanawake katika kushiriki katika ngazi za maamuzi

iv) Kufanya mapitio ya athari ya mifumo ya uchaguzi kwenye uwakilishi wa kisiasa za wanawake na kuzingatia marekebisho ya mifumo hiyo kwa kupitisha mifumo ya uchaguzi inayohimiza vyama vya siasa kujumuisha wanawake katika kuwania nafasi za uongozi bila ubaguzi wowote.

Vyama vya kisiasa

i) Kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika ngazi za utengenezaji wa katiba, sera, kanuni na mikakati ya ndani ya chama cha siasa.

ii) Kuhakikisha aina zote za uongozi wa chama katika ngazi zote unazingatia ushiriki sawa wa wanawake na wanaume.

iii) Kuzingatia na kuhakikisha uteuzi wa wagombea katika chaguzi mbalimbali zinazingatia uwakilishi sawa wa wanawake na wanaume.

iv) Kuingiza ajenda ya usawa wa kijinsia katika ajenda kuu na masuala muhimu ya kisiasa ya vyama.

v) Kutoa mafunzo ya uongozi na kusaidia wanawake na wasichana, pamoja na wale wenye uhitaji maalum, wenye ulemavu na wanawake kutoka baadhi ya jamii au makabila ili kuwajengea uwezo na kuwahamasisha kuchukua nafasi za uongozi.

Wajibu wa wanawake

a) Kuhakikisha wanajiandikisha kupiga kura na kushawishi wanawake wengine kujiandikisha kupiga kura

b) Kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi nje na ndani ya chama, hii ni pamoja na kuchukua fomu ya kugombea uchaguzi

Page 25: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

22

c) Kuhakikisha wanatoa taarifa juu ya ukatili wowote wa kijinsia dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi

d) Kutoa hamasa kwa wanajamii kuwaamini, kuwaheshimu na kuwapa wanawake nafasi ya kuongoza.

e) Kuhamasisha wanawake kuungana katika kudai masuala yao ya msingi bila kujali dini, itikadi, kabila na vyama vyao.

f) Kuhakikisha wanabeba ajenda za wanawake na usawa wa kijinsia pale wanapopata fursa ya kuwakilisha na kuongoza.

g) Kuhakikisha wanasaidia wanawake wenzao wanaogombea ili kushinda uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kuwapigia kura na kutia hamasa kwa wanawake kuwapigia kura wenzao.

h) Kuhamasisha wanawake wenye ndoto za kuwa wanasiasa kujiandaa mapema kwa kutengeneza mtandao wa wafuasi, kujenga uwezo wa kushawishi na kuaminika katika jamii.

Kwa nini Ushiriki Wako Katika Uchaguzi na Ngazi za Uongozi ni Muhimu-Kwa nini Ugombee?

a) Ni haki ya wanawake kimsingi ambayo inatambulika na kulindwa katika ngazi za kimataifa, kikanda na kitaifa

b) Wanawake na wanaume wanakumbana na changamoto tofauti katika maisha, na wana maono na mbinu tofauti zilizojengeka kibaiolojia, kihisia na kijamii kuhusu mbinu za utatuzi wa changamoto zinazowakumba.

c) Uwakilishi sawa wa wanawake na wanaume hukuza demokrasia jumuishi, shirikishi na utawala bora. Nchi haiwezi kuwa ni ya kidemokrasia kama zaidi ya asilimia 50 ya watu wake hawashiriki katika kufanya maamuzi ya masuala muhimu yanayowahusu.

d) Uwakilishi wa wanawake ni muhimu ili kuunda sera rafiki za kijinsia ambazo tafiti zinaonesha kuwa sera hizo huwa zina manufaa kwa jamii yote.

e) Wanawake ni watu na ni sehemu ya jamii, hivyo ni lazima washiriki katika kutolea maamuzi masuala muhimu ya nchi yao na masuala yanayowahusu.

f) Idadi ya wanawake duniani na nchini ni zaidi ya asilimia 50 hivyo masilahi yao yanatakiwa kuwakilishwa na wao wenyewe.

g) Mfumo wa kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kimazingira umejengwa kuwabeba na kuwathamini watoto wa kiume na wanaume kuliko watoto wa kike na wanawake. Wanawake wanahitajika katika ngazi za maamuzi ili kujenga mfumo rafiki unaoleta faida kwa watu wote wasichana kwa wavulana, wanawake na wanaume, walio na wasio na ulemavu.

Page 26: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

23

1.5 Mchango wa Wanawake Katika Nafasi za Uongozi

Tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961, wanawake wamekuwa katika nyanja mbalimbali za uongozi. Kwa sasa kuna asilimia 37 ya wabunge wanawake katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Asilimia 7 wamechaguliwa majimboni na wengine wanatokana na Mfumo wa Viti Maalumu. Asilimia tano ya madiwani ni wanawake waliochaguliwa kutoka kwenye kata, na asilimia 10 walichaguliwa kupitia Mfumo wa viti maalumu.

Wanawake katika ngazi za uongozi wameweza kuchangia yafuatayo:

a) Mabadiliko na kupitishwa kwa Sheria na Sera rafiki kwa wanawake na jamii kwa ujumla. Mfano ni sheria zinazohusu masuala ya; umiliki ardhi; ndoa; mirathi; elimu; ajira na adhabu za makosa ya ubakaji.

b) Katika halmashauri na kata wanawake wamewezesha upatikanaji wa huduma muhimu mfano maji, umeme, barabara, na huduma za afya.

c) Ushiriki wa wanawake umewezesha kumpata Makamu wa Raisi na Spika wa Bunge wa Kwanza mwanamke.

d) Pia wanawake wameshika nyadhifa mbalimbali katika wizara, mikoa, serikali za mitaa na taasisi nyinginezo ndani ya nchi na kimataifa.

e) Kutokana na wanawake kuwa katika nafasi mbalimbali za maamuzi vijana wa kike wamekuwa na muamko na ari ya kushiriki katika masuala ya siasa na uongozi.

Kutokana na wanawake kuwa katika nafasi mbalimbali za maamuzi jamii zimeanza kuwaamini na kuwapigia kura wanawake. Kwa mfano katika uchaguzi wa mwaka 2015 majimbo 26 nchini yalichagua wabunge wanawake. Haya ni majimbo machache ukilinganisha na majimbo yote Tanzania, lakini ni hatua kubwa.

Page 27: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

24

SOMO LA NNE: CHANGAMOTO ZA WANAWAKE KUSHIRIKI UCHAGUZI

Malengo ya SomoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kufahamu changamoto zinazowakabili wanawake wakati wanapotamani au kushiriki katika siasa na uongozi

• Kutambua mikakati ya kukabiliana na vikwazo na kuwawezesha wanawake kwa ajili ya kushiriki kwa ufanisi katika siasa.

Muda: Dakika 45

Vifaa: • Vip kadi

• Bango kitita

• Kalamu

• Picha ya mti wa matatizo

MbinuMajadiliano

Maswali na majibu

Matembezi ya picha

Mti wa matatizo

HatuaHatua ya 1: Elezea kwamba somo hili litachunguza changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake katika harakati za kushiriki katika uchaguzi na ngazi za maamuzi pamoja na njia za kutatua changamoto hizo.

Hatua ya 2: Bandika picha ya mti wa tatizo unaoonesha matawi, shina na mizizi kwenye bango kitita au picha iliyotolewa fotocopi na bandika kwenye ukuta au kwenye msimbo wa bango litita. (Mwezeshaji anaweza kuchora mti huu kabla ya somo kuanza)

Hatua ya 3: Gawa VIP kadi za rangi tatu tofauti kwa washiriki na waeleze wafuate maelekezo yafuatayo hatua kwa hatua.

• Washiriki watumie dakika moja kufikiria mizizi ya matatizo yanayowakumba wanawake katika harakati za kujihusisha na siasa na kubandika vip kadi hizo kwenye eneo la mzizi wa mti katika bango kitita

• Washiriki watumie dakika moja kufikiria changamoto moja moja inayomkabili mwanamke katika harakati za kushiriki katika siasa na nafasi za uongozi na kuzinakili katika vip kadi na kisha kuzibandika katika sehemu ya shina la mti wa matatizo uliopo katika bango kitita

• Washiriki watumie dakika moja kufikiria jinsi gani changamoto hizo zinaweza kutokomezwa na kuzinakili katika vip kadi na kisha kuzibandika katika sehemu ya matawi ya mti wa matatizo uliopo kwenye bango kitita.

Hatua ya 4: Waalike washiriki wote kwenye mti wa matatizo uliopo kwenye bango kitita na ongoza majadiliano na washiriki wote ili kuchambua changamoto zinazowakabili wanawake katika jitihada za kushiriki katika siasa na uongozi.

Hatua ya 5: Malizia somo kwa kutoa muhtasari kwa kutumia Kitini Na 2 D Changamoto za Wanawake Kushiriki Katika Uchaguzi na Uongozi.

Page 28: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

25

KITINI NA 2 D: CHANGAMOTO ZA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI NA UONGOZI

Pamoja na kwamba serikali ya Tanzania imefanya jtihada kubwa kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika siasa na ngazi za maamuzi, kwa kuridhia mikataba ya kimataifa, kikanda na sheria za ndani ya nchi ambayo inatoa haki kwa wanawake kushiriki katika uongozi na ngazi za maamuzi, wanawake bado wanakumbana na changamoto mbalimbali. Changamoto hizi zinazochangia ushiriki duni wa wanawake katika uchaguzi na ngazi za uongozi kama ifuatavyo:

a) Ukosefu wa nguvu za kiuchumi/fedha za kufadhili mchakato wa kisiasa hususani kampeni za ndani na nje ya chama.

b) Majukumu ya nyumbani ambayo kutokana na mila na desturi yanategemewa kutekelezwa na mwanamke.

c) Mila na desturi zinazopelekea wananchi kuona kuwa hawawezi kuongozwa na wanawake.

d) Mapengo yaliyopo kwenye sheria za uchaguzi na zile zinazoangazia uendeshwaji wa vyama vya siasa.

e) Katiba, sera na mikakati ya vyama vya Siasa zisizozingatia masuala ya usawa wa kijinsia.

f) Baadhi ya mifumo ya sheria kutoweka mazingira rafiki kwa wanawake kugombea na kushinda uchaguzi. Mfano, mfumo wa uchaguzi unaotumika Tanzania yaani First Past the Post(kata/jimbo moja, mshindi mmoja mwenye kura nyingi) sio rafiki kwa wanawake. Halikadhalika, changamoto zinazotokana na utekelezaji wa viti maalumu.

Pamoja na changamoto hizo, wanawake pia wanapitia hofu mbalimbali ambazo zinapunguza ujasiri wao na mwamko wa kushiriki kugombea nafasi za uongozi. Hofu hizo ni pamoja na

i) Hofu ya kutokuwa na elimu ya kutosha licha ya kuwa, sifa ya kuwa kiongozi wa kisiasa ikiwemo udiwani na ubunge ni kusoma na kuandika.

ii) Hofu ya hali ya ulinzi na usalama wakati wa kampeni za ndani na nje ya chama

Hofu ya rushwa ya fedha na rushwa ya ngonoKumbuka: Kama mwananchi, mgombea na kiongozi unatakiwa ubebe changamoto hizi kama ajenda ili kuchochea mabadiliko na kuwezesha mazingira rafiki ya wanawake kushiriki katika uchaguzi.

Hitimisho kutoka kwa MuwezeshajiKatika sura hii tumejifunza kuhusu mikataba na sheria zinazowapa wanawake uhalali wa kugombea katika nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa kidemokrasia. Pia tumejifunza wajibu wa serikali na vyama vya siasa katika kuhakikisha kuna ushiriki sawa wa wanawake na wanaume katika uongozi. Tumepata fursa ya kujifunza sababu muhimu za kwa nini ugombee katika mchakato wa uchaguzi. Pia tumesoma mchango katika nyanja mbalimbali ambao umeshapatikana kutoka kwa wanawake waliowahi kushika nafasi za uongozi nchini na kufahamu changamoto zinazowafanya wanawake wasishiriki katika mchakato wa uchaguzi

Page 29: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

26

MODULI YATATU

KUJITENGENEZEA JINA NA KUONGEA KWENYE HADHARA

UtanguliziModuli hii inalenga kuongeza uelewa wa mshiriki kuhusiana na masuala ya kujitengenezea jina ili kuweza kuwa mwanasisa bora na anayetambulika na jamii. Lakini pia sura hii inalenga kuongeza uelewa wa washiriki juu ya kuongea kwenye hadhara. Kuongea mbele ya hadhara na kujitengenezea jina ni stadi ambazo kila mgombea anatakiwa kuwa nazo.

SOMO LA KWANZA: KUJITENGENEZEA JINA/CHAPA BINAFSI

Malengo ya somoMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kufahamu maana ya kujitengenezea chapa binafsi

• Kueleza faida ya kujitengenezea chapa binafsi

• Kuelewa jinsi ya kutengeneza chapa binafsi na kuweka malengo binafsi

Muda: Dakika 60

Vifaa: • Vip kadi

• Bango kitita

• Kalamu

• Picha ya mti wa matatizo

Mbinu

Bungua bongo

Muhadhara

Kazi za vikundi

HatuaHatua ya 1: Mwezeshaji anza kwa kuwasilisha malengo ya kujifunza ya somo hili

Hatua ya 2: Mwezeshaji: uliza washiriki kutumia dakika moja kufikiria na kuchangia mawazo yao juu ya uelewa wao kuhusiana na kujitengenezea jina (Nakili majibu yao kwenye bango kitita). Hatua ya 3: Mwezeshaji anaweza kutumia jedwali hapo chini kuweka uelewa wa pamoja juu ya dhana ya kujijengea jina binafsi kwa mgombea au mtu mwenye malengo ya kugombea nafasi ya uongozi.

Page 30: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

27

KUJIJENGEA JINA/CHAPA BINAFSI

Ukiwa kama kiongozi au mtu unayetarajia kuwa kiongozi dhana ya kujijengea jina au chapa binafsi pengine huwa kitu cha kawaida kwako. Jina/ chapa yako ni kile kinachokufautisha wewe na washindani wako

Hii inahusisha namna kiongozi mwanamke anavyotakiwa kuhakikisha anafahamika na anatengeneza jina lake kisiasa. Unapozungumzia kujitengenezea jina ina maana kuwa unatakiwa uwe na kitu au chapa ya kukutofautisha wewe na wengine yaani mtu akisikia mgombea wa chama fulani katika ngazi fulani aone au awaze jina lako.

Bila ya chapa binafsi ambayo huvutia wafuasi wako, unaweza kujikuta kuwa na shida ya kujenga maisha yako ya kisiasa yenye mafanikio.

Hatua ya 4: Mwezeshaji uliza washiriki kushiriki (kuchangia mawazo) juu ya uelewa wao kwa nini tunahitaji kujenga chapa binafsi kama wanasiasa? Orodhesha majibu ya washiriki kwenye bango kitita

Hatua ya 5: Jadili faida za mwanasiasa kujitengenezea jina/chapa, unaweza kutumia kijedwali hapo chini huku ukiongezea na mifano ya watu waliofanikiwa kwa kisiasa kwa sababu ya chapa zao.

Kwa nini unahitaji kujenga chapa (brand) binafsi kama mwanasiasaa) Kuwa na chapa binafsi itakujengea uaminifu: Kuwa na chapa binafsi husaidia

kukujengea imani kwa wafuasi wako, na kuweza kukuweka wewe kama kiongozi wao

b) Kupata nafasi/fursa katika vyombo vya habari: kuwa na chapa binafsi hufanya iwe rahisi kwako kutafutwa na vyombo vya habari (machapisho ya mtandaoni, magazeti, televisheni, redio, podcasts, nk). Vyombo vya habari mara nyingi hutafuta wataalamu ambao wanaweza kushiriki mada zao kwa ajili ya wasikilizaji. Hii itakusaidia wewe kuweza kutumia majukwaa haya kutangaza umahiri wako na kufanya wafuasi wako kukuamini zaidi.

c) Kutengeneza mtandao wako: Ukiwa na chapa binafsi ambayo inaeleza wazi wewe ni nani, nini unafanya, na jinsi unawasaidia wengine, inafanya iwe rahisi kwa wafuasi wako wa kisiasa kuona thamani katika kukuunga mkono. Inaweza kukusaidia kutengeneza mtandao wako kwa haraka kwa njia ya mitandao na kawaida pia.

d) Kuwavutia wafuasi zaidi wa kisiasa: Kujenga chapa binafsi ambayo inakutambulisha wewe kama mwanasiasa mahiri husaidia kuwavutia zaidi wafuasi wako. Wakati wewe ukionekana kama mtaalam, pia ni rahisi kwa watu kukuzungumzia kwa watu wengine hivyo kuongeza wafuasi wako .

Hatua ya 6: Kazi za vikundi. Waongoze washiriki kuingia katika makundi matano (5) na waambie kila kikundi kiandae mpango mkakati wao wa kukuza chapa binafsi. (Kila kundi lazima kimchague kiongozi wao atakayewasilisha mkakati wao wa kukuza chapa binafsi.)

Hatua ya 7: Alika muwasilishaji wa kila kundi na wape dakika zisizozidi 3 kwa kila kundi kuwasilisha mpango mkakati wao wa kukuza chapa binafsi.

Hatua ya 8: Hitimisha kwa kujadili namna ambazo mtu anaweza kujitengenezea jina/ chapa binafsi. Mwezeshaje anaweza kutumia kijendwali hapo chini kueleza hatua za kujenga chapa binafsi

Page 31: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

28

Namna ambazo mtu anaweza kujitengenezea jina/ chapa:• Tengeneza maneno au maandishi, picha za kipekee za kukutambulisha kwa watu /

umma.

• Tumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujitangaza na kujijengea umaarufu.

• Tumia ujuzi wako, maadili, utashi katika kujitambulisha au kuonesha taswira na uhalisia wako kwa walengwa unaowatarajia. Hakikisha una kitu unachokiamini na unachokisimamia na kukipigania

• Weka orodha ya vitu vinavokusababishia umaarufu, na utofauti na wenzako, kisha vifanyie kazi kukuza jina lako

• Chagua ajenda moja kati ya mambo mengi yanayowatatiza jamii yako na kujinickname (kujibatiza),

• Rudia rudia meseji au ajenda yako mara kwa mara ili walengwa waifahamu unaweza kutumia maneno ya mtaani ambayo ni mepesi kueleweka (jargon words)

• Tumia mavazi , staili za nywele na vitu vingine kujitofautisha nk

• Tengeneza namna yako ya kuongea inayokutofautisha na wengine

• Chagua staili ya kuongea, mfano kwa kutoa takwimu (data), uwasilishaji wa mada zako, kuimba etc

• Fanya mambo au kazi zinazokutofautisha na wengine.Mfano: Kutembelea vijiwe vya kahawa, kusaidia wazee, kuhudhuria misibani, kuongea na watu vizuri, kusaidia yatima nk.

SOMO LA PILI: KUONGEA KWENYE HADHARA

Malengo MahususiMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kuelewa nini maana ya kuzungumza kwenye hadhara

• Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuzungumza kwenye hadhara.

• Kueleza hatua za kuandaa hotuba

• Kuelewa namna ya kutoa hotuba kwenye hadhara

Muda: Dakika 60

Vifaa: • Kadi za manila

• Bango kitita

• Kalamu

MbinuKazi za vikundi

Majadiliano ya pamoja

Page 32: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

29

Hatua

Hatua ya 1: Shughuli za vikundi:

Waelekeze washiriki katika vikundi vya watu watatu watatu wachague mada ambayo wanataka kuzungumzia. Wanapaswa kuchukua pointi 3 muhimu watakazoziandikia katika hotuba yao. Waambie watayarishe hotuba isiyozidi dakika 5 na kuiandika kwenye kadi ya manila

Hatua ya 2: Baada ya zoezi hilo waeleze kuchagua mshiriki mmoja kutoka kwenye kundi ambaye atawasilisha hotuba hiyo mbele ya darasa. Wape wawasilishaji muda wa kuwasilisha usiozidi dakika tano (5).

Hatua ya 3: Toa mrejesho kwa darasa kila baada ya wasilisho moja huku ukionesha mafanikio na udhaifu wa hotuba pamoja na muwasilishaji na jinsi ya kuboresha ujuzi wa kuzungumza kwenye hadhara.

Hatua ya 4: Tumia muhadhara kuelezea kuzungumza kwenye hadhara (Unaweza tumia kitini Na: 3: Kuzungumza Kwenye Hadhara)

KITINI NAMBA 3 KUZUNGUMZA KWENYE HADHARAMoja kati ya vitu muhimu sana ambavyo mgombea anapaswa kufahamu ni jinsi ya kuongea vizuri na hadhira yako ili kuongeza umaarufu na mvuto wa watu kusikiliza hotuba yako. Kuzungumza vizuri kwenye hadhara kunajumuisha pamoja na sauti utavyoitoa, matumizi ya viungo vyako wakati wa ufafanuzi au kusisitiza jambo, mpangilio wa hotuba yako na jinsi unavotumia kipaji kushirikisha hadhira yako ili nao waone kuwa ni sehemu ya hotuba yako.

Kama mgombea utalazimika kuongea hadharani katika matukio yafuatayo: Mkutano wa Umma-Hotuba, Mkutano wa waandishi wa habari, mada kwenye vyombo vya habari.

Ni vema kufahamu kuwa kuzungumza vizuri kwenye hadhara, huongezeka kwa njia ya kujifunza na kufanya mazoezi. Pia ni muhimu kuzingatia maeneo makuu matatu ambayo ni ujumbe wako, wasikilizaji wako, na wewe mwenyewe wakati unajitayarisha kuzungumza na hadhara. Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanya wasilisho lolote

o Tambua hadhira unayoenda kuongea nayo na matarajio yao kupitia timu yako ya kampeni- mfano vijana, wanawake, wazee, wenye ulemavu na kadhalika

o Orodhesha na chambua maoni yako, kisha yapange kwenye mtiririko mzuri

o Tumia takwimu zilizo kwenye ripoti sahihi kama kutoka Idara ya Takwimu kuhakikisha ujumbe wako unabebwa na takwimu

o Soma ripoti tofauti tofauti kama Dira ya Taifa 2025, Ripoti za serikali na Idara ya takwimu, taasisi mbalimbali, mashirika ya umoja wa mataifa, na taasisi za ndani na nje ya nchi.

o Jipike Zaidi kwenye ripoti za afya, elimu, ajira, miundo mbinu, mazingira na kadhalika

o Andaa ujumbe mfupi na unaoeleweka. Jiulize unataka watu wakumbuke nini baada ya wasilisho lako.

o Hakikisha wasilisho lako limehaririwa

o Fanyia mazoezi unachotaka kukizungumza ili kujenga ujasiri, kujiamini na uwezo wa kushawishi wasikilizaji

o Jifunze namna ya kutumia kipaza sauti

Page 33: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

30

o Jifunza namna ya kutulia, kuongea kwa sauti na taratibu wakati unatoa wasilisho lako

o Jiandae kujibu maswali, kuwa mwenye heshima hata ikiwa umeulizwa swali ambalo hujalipenda

o Fanyia kazi hasira zako endapo ikijitokeza

Andaa nakala za wasilisho lako ili kuwagawiwa hadhara kadiri mazingira yanavyoruhusu Kuandaa na kutoa Hotuba

Kama mgombea itakulazimu kutoa hotuba katika maeneo mbalimbali. Hivyo ni lazima kujua mbinu za kutoa hotuba nzuri. Kwa kawaida hotuba huwa na sehemu nne ambazo ni: Maandalizi kabla ya hotuba, Utangulizi, kiini cha hotuba na hitimisho.

Maandalizi kabla ya hotuba:

• Tathmini hotuba yako: Angalia maudhui uliyoweka na muda utakao tumia katika uwasilishaji. Hotuba isiwe ndefu sana wala fupi sana. Hotuba iguse maswala ya muhimu ya jamii husika

• Fanya mazoezi mbele ya kioo, mbele ya familia au mtu unayemuamini. Hii itakusaidia kujua kile unachotaka kusema, wakati wa kukisema na kwa nani pia utapata mrejesho juu ya uwasilishaji wako.

• Zingatia lugha yako ya mwili na sauti yako (fanya mazoezi haya kwa kurudia rudia).

• Kama hujapenda kile unachokisikia na kukiona, basi inawezekana kabisa asitokee mwingine wa kupenda hiyo hotuba

• Fika kwenye ukumbi mapema zaidi na ukague eneo la ukumbi, jitahidi kulizoea eneo la mkutano. Inashauriwa kufika eneo la tukio nusu saa kabla ya kuanza kwa tukio.

• Angalia jukwaa na jinsi watu watakavyokaa.

• Dhibiti hasira na hisia zako

• Unaposimama kwenye mimbari, vuta pumzi ndani, utazame ukumbi (watu walioko ukumbini) na kisha tabasamu na kisha anza kuzungumza.

• Sio busara kufika tu kwenye mimbari kuchukua kipaza sauti na kuanza kuongea harakaharaka tu baada ya kupanda stejini.

Utangulizi wa hotuba: Hapa mgombea anapaswa kuanza kwa salamu na kujitambulisha. Ni vizuri mgombea akatoa salamu inayozingatia muktadha wa hadhira anayoihutubia. Mfano: salamu izingatie lugha inayozungumzwa na hadhira yake, izingatie dini zote, pia atoe salamu ya chama chake. Hii ni muhimu kwani hutengeneza umakini wa wajumbe au hadhira kusikiliza. Kisha kulingana na muktadha / hadhira mgombea anaweza kuanza kwa kusimulia hadithi inayomhusu au kufanya utani wa kuanzisha mazungumzo. Kwa mfano, ikiwa unatoa hotuba kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu unaweza kuwaambia hadithi ambayo ilitokea wakati wako ukiwa chuo hapo. Ikiwa unatoa hotuba kwa timu ya mpira wa miguu, waambie utani ambao unahusiana na mechi za mpira wa miguu ulizowahi kufurahiwa (NB: Usioneshe upande wa ushabiki wako katika timu hizo-Onesha kufurahishwa na timu zote). Kupitia mbinu hii utaweza kuhamasisha wasikilizaji kutoka mwanzo hadi mwisho wa hotuba.

Page 34: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

31

Kiini cha Hotuba: Baada ya utangulizi, elezea hadhira lengo la hotuba siku hiyo. (Kwa mfano: Leo ningependa kuzungumza juu ya suala la elimu katika jimbo au kata yetu).

Chagua mambo matatu ya kipaumbele ya kuzungumzia na hakikisha una takwimu, nukuu na ushuhuda. Mfano.

o Hoja ya kwanza: kiwango cha elimu kimekuwa kikidorora kila mwaka.

o Hoja ya pili: elimu kwa wasichana ni msingi wa ukombozi wa wanawake lakini kumekuwa na changamoto nyingi.

o Hoja ya tatu: tunahitaji kuongeza rasilimali kuboresha elimu, haswa kwa kulenga wasichana wajiunge na shule za sekondari na vyuo vikuu.

Jenga hoja zako zikihusiana na hisia zako na kile unachoamini kuwa utakifanyia kazi baada ya kupata uongozi.

NB: Hakikisha hotuba yako unaielewa na lazima uhakikishe inalenga kutatua kero na changamoto za sehemu husika. Kabla ya kuhitimisha hotuba yako ruhusu maswali yasiyozidi matatu ili uweze kufafanua pale pasipoeleweka vizuri. Hakikisha unatambua maswali yanayolenga hoja na yale yaliyojikita kwenye kuchafua haiba. Onesha kupokea swali na lijibu kwa heshima na uvumilivu hata kama linakukera ili usije ukaharibu hotuba yako yote ya siku hiyo.

Hitimisho: Tumia hitimisho la hotuba kwa kurudia hoja zako kuu: Wasikilizaji wengi watakumbuka kile kitakachosemwa katika hitimisho tofauti na sehemu ya utangulizi. Hakikisha unahitimisha kwa kurudia ujumbe mkuu wa hotuba yako. Pia hitimisha kwa kuwakumbusha wasikilizaji kujitokeza siku ya kupiga kura kwa sababu ni haki yao ya kikatiba. Pia, ishawishi hadhira ikupigie kura kusudi ushirikiane nao kutatua changamoto zinazoikabili kata au jimbo hilo. Shukuru umma kwa muda wao kuonesha unaheshimu muda wao.Mambo ya kutofanya

• Epuka kukariri hotuba badala yake ielewe ili uweze kujibu maswali.• Epuka kusoma neno kwa neno.• Usijione mjuaji sana. Onesha utafanya mambo kwa ushirikiano na wananchi. Kuwa

msikilizaji• Usiwe ni mtu wa kuomba msamaha bila mpangilio

Namna ya Uwasilishwaji wa HotubaTengeneza karatasi ndogo (kipeperushi) yenye vidokezi/dondoo muhimu, na hivyo kukusaidia kukumbuka masuala muhimu ya wasilisho lako bila kutakiwa kusoma neno kwa neno. Haishauriwi kabisa kutumia mbinu ya kusoma neno kwa neno ingawa kuna baadhi ya wagombea huitumia.

Kuna faida na hasara za njia yoyote utakayochagua kuwasilisha hotuba yako.

Page 35: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

32

Faida na Hasara za Njia za Kutoa Hotuba

Njia Faida HasaraKusoma mstari kwa mstari

Hii itakusaidia kuondoa hofu na kukupa nafasi ya kusoma maoni/mawazo yako kama yalivyoandikwa

Inakutenganisha na wasikilizaji wako kwa sababu muda mwingi unaangalia hotuba kwenye karatasi. Inakua vigumu kuelewa wasikilizaji wako kwa kutokuelewa kama wamechoka ama wanakufuatilia

Kipande cha karatasi chenye vidokezo

Unaweza kuongeza maneno na kubadili sentensi. Ni rahisi kutumia pale ambapo hakuna jukwaa, vidokezo vinasaidia kukumbushia hoja zako na kukuweka karibu na wasikilizaji

Mgombea, asiye na uzoefu kuongea sehemu zenye umati mkubwa atakuwa na wasiwasi wa kusahau baadhi ya vidokezo vyake

Jinsi ya kujenga ujasiri katika kutoa hotuba

i) Wakati ukitoa hotuba, weka macho yako kwa mtu uliyemchagua (rafiki au jamaa) atakayeongeza ujasiri wako. Kubaliana na mtu huyu kuwa atakuwa anakupa moyo kwa kukubali kwa kichwa yale unayotaka kuyasema na kutabasamu.

ii) Anza kutazama hadhira kwenye paji la uso kwenda juu, baadae utapata ujasiri wa kuwaangalia machoni.

iii) Jisikie na jione kama unaongea na watu wachache kwenye mazungumzo ya kawaida.

iv) Shirikisha wasikilizaji wako wote kwa kuangalia watu walioketi nyuma ya chumba. Hii itakusaidia kuongeza sauti unapoendelea kuongea.

v) Hakikisha umesimama kama hali ya afya ya mwili wako inaruhusu. Wagombea walemavu wanapaswa kuwasilisha hotuba kwa namna inayolingana na asili yao ya mwili.

vi) Kwa wanawake, usivae viatu vyenye visigino hasa wakati wa hotuba ndefu, hivi huweza kukufanya ushindwe kusimama kwa muda mrefu.

vii) Usikunje mikono yako kwa sababu wasikilizaji wataona umewapuuza.

viii) Ikiwa unataka kusisitiza jambo, badilisha sauti yako.

ix) Hakikisha umevaa mavazi rasmi au zile zinazoendana na jamii uliyopo.

x) Meneja wako wa mawasiliano ahakikishe vipasa sauti vinafanya kazi na nyenzo zote zinazohitajika wakati wa kusoma hotuba zipo sehemu husika.

xi) Zingatia kupanda na kushuka kwa sauti yako. Hakikisha una sauti inayolingana au inayofanana sehemu zote

Page 36: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

33

Majukumu ya Timu ya Kampeni

o Kutambua vyombo vya habari vilivo katika eneo lako. Mfano redio, magazeti na televisheni za kijamii.

o Kutambua programu ambazo unaweza kutumia katika kila chombo cha habari bila gharama yoyote au kwa gharama ndogo.

o Kuandaa ratiba ya kuongea ana kwa ana na vyombo vya habari. Mfano mikutano ya waandishi wa habari nk.

o Kuandaa andiko mahususi (media briefing) kwa ajili ya waandishi wa habari katika kila kampeni na mikutano ya waandishi wa habari.

o Kuainisha waandishi wa habari mahususi kwa ajili ya kutoa habari zinazohusiana na kampeni na siaza zako. Hakikisha ni mchanganyiko wa wanahabari kutoka kwenye runinga, redio, magazeti, na mitandao ya kijamii kwa kuwa wapiga kura hupokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali.

o Kuandaa ratiba ya utaratibu wako wa kuvihusisha vyombo vya habari: Tambua utafanya mikutano mingapi na waandishi wa habari; mahojiano ya ana kwa ana; mijadala ya kampeni; n.k

o Kumbuka kuwa kila mpigakura ana chaguo pendwa la chombo cha habari cha kutumia. Tumia vyombo vya habari tofauti zinazopatikana kufikia wapiga kura wengi.

o Kumbuka kuwa hakuna chumba chochote cha habari ambacho hakina itikadi. Fanya utambuzi wa kujua vyombo vya habari ambavyo vinakubaliana na itikadi yako na ujumbe wa kampeni ya uchaguzi.

Njia kadhaa za kufanya kazi na vyombo vya habari na waandishiHizi ni pamoja na: Mkutano na waandishi wa habari, vipindi vya redio au runinga makala kwenye magazeti, na kutumia wasanii wa mziki, waigizaji au wachoraji.a) Mkutano na waandishi wa habari: Lengo kubwa la mkutano na waandishi wa habari ni kushawishi vyombo vya habari kukusikiliza na kutoa habari ambazo hueneza ujumbe wa mgombea na sera zake kwa wapiga kura. Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia:

o Jitayarishe vizuri kabla ya kukutana na waandishi wa habari na hakikisha una malengo yaliyowazi.

o Katika wasilisho kwa vyombo vya habari, mawazo ya mgombea yanahitaji kuandaliwa vizuri kusudi waandishi wa habari waweze kuchagua hoja za kutoa katika vyombo vyao vya habari.

o Wasilisho liwe fupi na liende moja kwa moja kwenye ujumbe unaolenga uwafikie waandishi.

o Panga sehemu ambayo itafikika kirahisi na waandishi wa habari wengi.o Alika waandishi wa habari wengi kutoka runinga, redio, magazeti na blogi.o Heshimu tarehe na muda kwa hafla ilivyopangwa.o Gawa tamko lako kwa njia ambayo itawafikia waandishi wengi zaidio Onesha anwani kamili ikiwemo namba za simu, tovuti na sehemu ambayo unapatikana.

Hii itasaidia waandishi wa Habari kukufikia kirahisi ikiwa wana maswali ya ziada.

Page 37: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

34

b) Hotuba au Mahojiano kupitia Runinga au Redio

Matumizi ya Runinga hukuonesha mbele ya kamera na kutazamwa na umma wa wapiga kura ambao wapo katika eneo lako na wale wa mbali. Vivyo hivyo, hotuba kupitia redio inasikika na umma mkubwa.

Zingatia yafuatayo ili kufanikiwa kutoa hotuba yako kupitia runinga

o Jua mada yako na jitayarishe vyema kuitetea mbele ya wasikilizaji wako kwa usahihi ili kuwashawishi wakupigie kura.

o Hakikisha kuwa ujumbe wako muhimu unasikika ndani ya dakika 30 za kwanza, ili muda uliobaki uwe wa kufafanua ujumbe.

o Zingatia aina ya nguo utakazo vaa kulingana na kile utakayoshauriwa na eneo husika.

o Kuwa mwangalifu juu ya matumizi ya lugha. Fikiria kabla ya kuongea na kujibu maswali.

o Wakati wa mazungumzo ya redio au runinga, kuna watu ambao wanaweza kupiga simu na kukuuliza maswali. Hakikisha unajibu maswali kwa usahihi.

o Wakati wa kuzungumza na mhojiwa jifanye kuwa uko kwenye mazungumzo ya kawaida. Puuza uwepo wa kamera na epuka kuangalia kamera moja kwa moja wakati wote.

Kumbuka: kuzungumza hadharani sio swala ambalo unaweza kubobea kwa siku moja. Hivyo, ni vema kuendelea na mazoezi ya kuzungumza hadharani wakati wa kujiandaa kuelekea kampeni. Washiriki pia wanapaswa kushauriwa kuangalia na kusoma sampuli za hotuba za kampeni

Hatua ya 4: HitimishoKatika mada hii tumejifunza kuhusu mbinu za kufikisha sera na ujumbe kwa wapiga kura na mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kutoa wasilisho lolote. Pia tumejifunza mbinu za kufanya kazi na vyombo vya habari na jinsi ya kuongea kwenye kipaza sauti. Pia tumejifunza kuhusu hotuba, jinsi ya kujenga ujasiri katika kutoa hotuba, na njia za kutoa hotuba pamoja na faida na hasara ya kila njia. Kumbuka ni muhimu sana kujadili na timu yako ya kampeni njia sahihi mtakazotumia ili kufikisha sera na ujumbe kwa wapiga kura, kama mtaenda nyumba kwa nyumba je kwa siku mtatembelea nyumba ngapi? Ni aina gani ya shughuli za kijamii unazoweza kushiriki ili kuwafikia wapiga kura wako? Je mnauwezo wa kuchanganya njia zote ili kufikia wapiga kura wengi.

Page 38: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

35

UTEUZI NDANI YA CHAMA

UtanguliziKatika mada hii tutajifunza kuhusu uteuzi wa wagombea ndani ya chama, hatua za uteuzi wa wagombea ndani ya chama, masuala muhimu ya kuzingatia na vigezo vitakavyo kuongezea nafasi ya kupata uteuzi ndani ya chama. Pia utajifunza kuhusu mchakato wa viti maalumu-udiwani na ubunge na mbinu za kuzingatia katika kugombea na kushinda viti maalum.

Muda:

SOMO LA KWANZA: UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA

Malengo ya somoMwisho wa somo mshiriki aweze:

• Kuelewa hatua za Uteuzi wa Wagombea Ndani ya Chama

• Kueleza masuala muhimu ya kumuongezea fursa ya kushinda uteuzi wa ndani ya chama

• Kuelewa vigezo vitakavyo msaidia kushinda kura za maoni

• Mchakato wa Viti Maalumu-Udiwani na Ubunge.

Muda: 45 Minutes

Vifaa: • Bango kitita

• Kalamu Rashasha

Mbinu: • Kazi za vikundi (Kulingana na vyama)

• Matembezi ya picha.

• Maswali na majibu

HatuaHatua ya 1: Gawa washiriki katika vikundi kulingana na vyama vyao vya kisiasa. Katika hali ya washiriki ambao hawako kwa makundi ya vyama wagawe katika makundi ya kawaida matano tu,

Hatua ya 2: Uliza kila kikundi kufanya zoezi la kuandika hatua kwa hatua jinsi zoezi la uteuzi wa wagombea wa ubunge, uraisi na udiwani linavyofanyika katika vyama vyao. Wape kila kundi karatasi moja ya bango kitita kwa ajili ya kuandika majibu yao kisha kuyabandika katika maeneo tofauti ya chumba cha mkutano.

MODULI YANNE

Page 39: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

36

Hatua ya 3: Baada ya zoezi hilo waambie washiriki kwamba kila kundi litumie dakika mbili kutembelea majibu ya kila kundi na kuweza kuangalia mambo yafuatayo;

• Ni hatua zipi ambazo zinafanana kwa kila chama?

• Kulingana na hatua hizo muhimu ni mambo gani yatakusaidia kama mwanamke kushinda uteuzi?

• Kufuatia hatua hizo unafikiri ni mambo gani yanaweza kukukwamisha kupata uteuzi kama mwanamke?

Hatua ya 4: Baada ya kila kikundi kumaliza matembezi, walete washiriki pamoja, na uulize kila kikundi kufanya muhtasari juu walichojifunza kulingana na muongozo wa maswali ya hatua ya 3. Waongoze washiriki kujadiliana huku ukikazia kwenye majibu yao.

Hatua ya 5: Hitimisha kwa kusema kwamba kila chama kinautaratibu wake wa kuteua mgombea lakini taratibu hizi hazitofautiani sana kutoka chama kimoja hadi kingine. Ni muhimu kama mgombea kujua mambo muhimu ambayo yanaweza kukuwezesha kushinda au kukwamisha katika harakati za kutafuta uteuzi wa chama. Unaweza kutumia kitini Na 4 Uteuzi ndani ya Chama.

KITINI NA 4. UTEUZI NDANI YA CHAMAKama inavofahamika, vyama vya siasa ndio mlango mkubwa kwa wanasiasa kugombea nafasi za uongozi, aidha wawe wanawake au wanaume. Hivyo basi, vimeweka utaratibu wa uteuzi wa wagombea uraisi, ubunge (sambamba na ubunge wa viti maalum) na udiwani katika kipindi cha uchaguzi na hususani uchaguzi mkuu. Uteuzi huu unatakiwa kuwa ni wa kidemokrasia, wa wazi, wenye ushindani na unaoeleweka katika ngazi zote.

2.3. Hatua za Uteuzi wa Wagombea Ndani ya Chama:

i) Vyama huandaa waraka ambao hutoa vigezo vitakavyotumika katika uteuzi wa wagombea uraisi, ubunge na udiwani.

ii) Kutoa mwaliko kwa wanachama wenye nia ya kugombea, kuchukua fomu za uteuzi kutoka katika ofisi za chama katika ngazi husika.

iii) Majina ya watia nia huchujwa na kamati ya siasa au chombo mahususi katika ngazi ya chama husika.

iv) Mchakato wa kura za maoni hufanyika.

v) Majina ya waliopita hupelekwa kwenye Baraza la Taifa la chama au mkutano Mkuu wa Chama kwa maamuzi ya mwisho na upitishaji.

2.4. Masuala Muhimu ya Kukuongezea Fursa ya Kushinda Uteuzi wa Ndani ya Chama

i. Fahamu unagombea nafasi gani na kwa nini. Andaa sababu kuu tatu za kwa nini unagombea ambazo utazielezea kwa mtu yeyote atakaekuuliza swali la kwa nini unagombea.

ii. Fahamu waraka unaotolewa na chama chako wenye vigezo na sifa za wagombea. Jiridhishe na vigezo hivo ili kuhakikisha unakidhi vigezo vilivyowekwa.

iii. Fahamu utaratibu wa kura za maoni ndani ya chama chako, mfano kipindi/wakati/muda wa kuchukua fomu za kugombea, na masharti muhimu katika kila hatua za mchujo.

iv. Andaa wasifu wako (CV) ukionesha taarifa zako muhimu. Hakikisha unaainisha mchango na mafanikio yako katika kutekeleza shughuli za chama na kukikuza chama.

Page 40: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

37

v. Fahamu gharama zinazohusiana na uteuzi wa ndani, mfano:-

a) Gharama za fomu

b) Kampeni za ndani ya chama

c) Kama utatakiwa kuchangia fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kura za maoni.

vi. Jiridhishe kama utahitaji kudhaminiwa na wanachama na utafute wadhamini hao mapema. Fahamu kuwa mwanachama mmoja hawezi kuwadhamini wagombea zaidi ya wawili.

vii. Jaza na wasilisha fomu ya kugombea na timiza masharti yote muhimu mapema.

viii. Jiandae kwa usaili kama italazimika ufanye hivyo kama sehemu ya mchujo wa ndani ya chama kabla ya kamati ya maoni.

ix. Yasome, yaelewe na yaheshimu maadili ya uchaguzi ya ndani ya chama pamoja na miongozo ya uchaguzi ndani ya chama.

x. Jiepushe na rushwa ya aina yoyote ikiwemo rushwa ya ngono na fedha ili kupitishwa katika nafasi yoyote ile. Amini kuwa uwezo wako unatosha.

2.5. VigezoVitakavyo Kusaidia Kushinda Kura za Maoni

Uwe mwanachama hai katika tawi la chama chako.

Uelewe malengo, itikadi na falsafa ya chama.

Uwe na uzoefu wa uongozi ndani ya chama.

Jenga uhusiano mzuri na viongozi ndani ya chama.

Shiriki na toa mchango wako wa hali na mali katika kutekeleza shughuli za chama.

Uwe mwadilifu katika uongozi wa kisiasa na kijamii.

Ukubalike na wanajamii unaoomba ridhaa ya kuwaongoza.

Uwe na uwezo wa kumudu majukumu ya nafasi unayoomba.

Uwe na uwezo wa kushirikiana na wengine kutimiza majukumu husika.

Uwe na uwezo wa kusoma na kuandika kwa kiswahili au kiingereza.

Tambua Kuwa:

Kuongoza kwenye kura za maoni si kigezo pekee cha kuhalalisha kupitishwa kwa jina moja kwa moja. Masuala ya rushwa na uadilifu wakati wa kura za maoni vinaweza kukufanya usipitishwe.

Unaweza kukata rufaa kama hujaridhika na mchakato wa kura za maoni. Fuata utaratibu wa chama chako na ule wa kimahakama.

Mchakato wa Viti Maalumu-Udiwani na Ubunge.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imetamka bayana kuwa kutakua na viti maalum kwa ajili wanawake katika bunge (sura/Ibara ya 66 ).Chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi wa bunge kinatakiwa kupendekeza kwa Tume ya Uchaguzi majina ya wanawake kwenye viti maalum. Kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata wabunge na madiwani wanawake kwa ajili ya viti maalumu. Kwa vyama vyingi mchakato unaweza kuwa kama ifuatavyo:

Page 41: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

38

1. Mchakato huanzia katika kata/wilaya husika.2. Mtia nia anajaza fomu kuonyesha kusudio la kugombea viti maalumu. 3. Majina huchujwa na kamati tendaji ya chama husika au tawi la wanawake.4. Wagombea hupigiwa kura na wanawake katika tawi ya wanawake.5. Majina hupangwa kulingana na kura walizopata wagombea.6. Mkutano mkuu wa kata/wilaya hupitisha majina ya viti maalumu.7. Majina hupelekwa Baraza kuu la chama Taifa au Mkutano Mkuu kwa upitishaji.8. Baraza kuu la chama au Mkutano Mkuu hupeleka majina yaliyopitishwa kwa Tume

ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili hatua za utangazaji kulingana na kura ambazo chama kitakuwa kimepata.

9. Majina ya wanawake yanayopendekezwa kwenye viti maalumu kwenda Tume yatakuwa kwa mpangilio wa kipaumbele kwenye nafasi za viti maalumu.

10. Tume itatangaza majina ya wabunge wa viti maalumu wa kila chama kulingana na idadi ya kura ilichopata chama hicho.

11. Tume itatuma taarifa kwa Spika wa bunge juu ya uteuzi wa wanawake viti maalumu kutoka kwenye kila chama

12. Majina ya wanawake yatakayopendekezwa kwa Tume kutoka kila chama ndio yatakayotumika na Tume kujaza nafasi yoyote iliyoachwa wazi katika viti maalumu wakati wote wa Bunge.

Kumbuka:

Fuatilia utaratibu maalum wa kuwapata wanawake viti maalumu katika ngazi husika kwenye chama chako na ufuate utaratibu.

Ni vyama ambavyo vitapata asilimia 5 ya kura na kuendelea ndio vitapata fursa ya kupata mgawanyo wa viti maalumu kulingana na idadi ya kura walizopata katika uchaguzi mkuu.

2.7 Mbinu za Kuzingatia Katika Kugombea na Kushinda Viti Maalumu

1. Kuwa mwanachama hai wa chama husika hususani kwa muda mrefu.2. Shiriki kwenye shughuli za chama mfano kuhamasisha watu kujiunga kwenye chama.3. Saidia chama katika kufanya kampeni na kupata kura kwa wagombea wa chama chako

kwenye kata na jimboni wakati wa uchaguzi.4. Kuwa na ukaribu na jamii ya watu unaotaka kuwawakilisha, shiriki katika harusi na

msiba.5. Jenga mahusiano mazuri na watu na viongozi wako (kata, jimbo na Taifa) kwa kufanya

yafuatayo.Jiamini katika mawazo yako yenye lengo la kujenga chama.Kuwa msikivu kwa viongozi wa chama kwa kufuata maelekezo. Kama una

maoni tofauti au changamoto fuata taratibu za chama kutatua changamoto husika.

Tekeleza majukumu kwa muda uliopangwa.

Kuwa msaada kwenye shughuli mbali mbali kama unavyohitajiwa na chama.

Page 42: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

39

6. Onyesha matendo na mwenendo mwema katika chama na jamii yako.

7. Tumia mitandao ya kijamii kufanya kazi zako zionekane. Fanya kazi za chama na hakikisha unazituma kwenye makundi ya chama, whatsapp, facebook, Instagram na Twitter.

8. Ondoa hofu na chukua fomu-Ujazaji wa nafasi za viti maalumu wakati wa uchaguzi na pengo litakalojitokeza baada ya uchaguzi huzingatia orodha ya waliojaza fomu na kupitishwa na chama.

9. Usitoe rushwa ya aina yoyote ili kupata nafasi ya uongozi.

Kama mwanamke ndani ya chama cha siasa siku zote kumbuka kushawishi:

1. Chama chako kiweke utaratibu wa kuwezesha na kuwajengea wanawake kushiriki kama wagombea katika nafasi zote.

2. Utaratibu wa wazi na wenye haki wa kupata wanawake viti maalumu

3. Shawishi kamati za siasa ziwe na wachujaji wanawake na wanaume

4. Shawishi utaratibu wa kupata idadi sawa ya wagombea yaani wanawake na wanaume.

Hitimisho

Katika mada hii tumejifunza kuhusu uteuzi wa wagombea ndani ya chama, hatua za uteuzi wa wagombea ndani ya chama, masuala muhimu ya kuzingatia na vigezo vitakavyo kuongezea nafasi ya kupata uteuzi ndani ya chama. Pia tumejifunza kuhusu mchakato wa viti maalu-mu-udiwani na ubunge na mbinu za kuzingatia katika kugombea na kushinda viti maalum. Ni vyema kuzingatia masharti na vigezo vilivyoainishwa na chama chako. Hakikisha una vigezo vyote kabla ya kwenda kutafuta uteuzi ndani ya chama.

Page 43: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

40

KAMPENI ZA UCHAGUZI

UtanguliziKampeni ni sehemu muhimu sana wakati wa mchakato wa uchaguzi ambayo ina jukumu kubwa la kumfanya mtu kuwa kiongozi. Sehemu hii inatoa uelewa wa dhana ya kampeni na mikakati ya kampeni. Inatoa mwongozo wa jinsi ya kupanga kampeni yako na kueleza jinsi ya kuwasilisha ujumbe wako wa kampeni. Vidokezo vya kufanya kampeni kwa ufanisi na jinsi ya kulenga hadhira husika pia zimetolewa na somo hili.

Muda: Masaa 5

SOMO LA KWANZA: UELEWA WA DHANA YA KAMPENI

Malengo MahususiMwisho wa somo mshiriki ataweza:

• Kueleza maana, aina na vipengele vya kampeni • Kueleza dhana ya kampeni za uchaguzi wa kisiasa • Kutofautisha kati ya mkakati na mpango wa kampeni • Ajue hatua za kuandaa kampeni

Muda: Dakika 45

Vifaa: • Vip kadi • Bango kitita• Kalamu

MbinuBungua Bongo

Kazi za vikundi

HatuaHatua ya 1: Muwezeshaji: Tambulisha malengo ya somo hili kwa washiriki. Elezea kwamba somo hili litajadili na kulenga katika kuelewa maana ya kampeni za uchaguzi, mkakati wa kampeni na tofauti kati ya mkakati na mpango wa kampeni.

Hatua ya 2: Uliza washiriki kufikiria na kutoa mawazo yao wanaelewa nini juu ya;

• Kampeni ni nini?

• Kampeni ya uchaguzi ni nini?

• Kwa nini kampeni ni muhimu?

MODULI YATANO

Page 44: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

41

Hatua ya 3: Baada ya kuchukua majibu machache kutoka kwa washiriki, unaweza kutumia jedwali hapo chini kutoa muhtasari wa nini maana ya kampeni, kampeni za uchaguzi na umuhimu wa kufanya kampeni.

KAMPENI ZA UCHAGUZI

• Kampeni ni mtiririko wa shughuli ambazo watu wanafanya kwa kipindi cha muda ili kufikia kitu kama mabadiliko ya kijamii au kisiasa

• Kampeni ya uchaguzi ni mfululizo wa matukio ya kumnadi mgombea ili kupata nafasi ya ofisi ya kisiasa. Kampeni za uchaguzi zinakusudia kuongeza na kutangaza wasifu wa mgombea, kunyamazisha upinzani, na kuwaelimisha wapiga kura kuhusu uwezo wa kibinafsi wa mgombea huyo ambao utakuwa wa manufaa kwa jamii.

• Wakati wa uchaguzi ni muhimu kuwa na kampeni ili;Kuwaelimisha wapiga kura wako juu ya ajenda na sababu za kukupa kura weweKuleta mabadiliko ya mtazamo wa watu juu yakoKunyamazisha sera za wapinzani wako Kuongeza idadi ya wafuasi wako wa kisiasa

Hatua ya 4: Kazi ya kundi zima

Gawa VIP kadi kwa kila mshiriki na waambie kila mshiriki aandike vipengele muhimu zaidi vya kuzingatia wakati wa kuandaa kampeni na kuweka kwenye upande mmoja wa ukuta.

Hatua ya 5: Uliza kila mshiriki kusonga karibu na ukuta mahali kadi zilipobandikwa na kusoma majibu ya kila mmoja. Ruhusu dakika 5 kwa zoezi hili.

Hatua ya 6: Uliza kundi zima kutoa mrejesho: ‘Ni vipengele gani muhimu vimejitokeza katika zoezi hilo. Andika mapendekezo kwenye bango kitita, kisha ainisha vipaumbele kutoka kwenye majibu yao na endesha mjadala huku ukitoa mifano kwa kila hatua. Unawea kutumia kitini au jedwali lililopo hapo chini kutoa muhtasari wa zoezi hili.

MPANGO WA KAMPENI:

Mpango wa kampeni ni mchakato muhimu wa kuandaa shughuli na kuweka mikakati ili kuweza kufikia malengo unayotarajia. Kuandaa mpango wa kampeni ni muhimu kwa mafanikio ya mgombea kwani kunaimarisha uratibu shughuli za kampeni, matumizi ya rasilimali na kupunguza gharama ambazo sio za lazima.. Mpango wa kampeni huorodhesha kila hatua katika kampeni ya mgombea, tangu wakati anaamua kugombea mpaka siku vituo vya kupigiwa kura vinafungwa. Lengo la kuandaa mpango wa kampeni ni kutoa muhtasari wa jinsi mgombea anapanga kupata asilimia nyingi za kura siku ya uchaguzi.Hatua zifuatazo ni muhimu wakati wa kuandaa mpango madhubuti:

1. Fanya utafiti na upembuzi yakinifu2. Andaa timu ya kampeni3. Tambua masuala muhimu ambayo ni ya wasiwasi kwa wapiga kura4. Andaa mkakati wa kufikia wapiga kura5. Andaa Sera na Jumbe za Kampeni6. Andaa rasilimali za kampeni

NB: Unaweza kuonesha mfano wa Kiambatisho 1: Mpango wa kampeni

Page 45: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

42

Hatua ya 7: Toa hitimisho kwa kifupi kwamba mpango wa kampeni ni jinsi kampeni yako itaendeshwa na jinsi itafanya kazi. Hii inajumuisha habari kuhusu wilaya, bajeti, timu yako, kufikia wapiga kura, pamoja na sera na jumbe za kampeni

SOMO LA PILI: UTAFITI Malengo ya somoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

• Kuelewa jinsi ya kufanya utafiti na upembuzi yakinifu kuhusu masuala muhimu na yatayomsaidia katika harakati za kampeni ya uchaguzi.

• Kueleza maeneo ya kufanyia utafiti

• Kuelewa matumizi ya taarifa na tafiti, vyanzo vya taarifa za utafiti na kuweza kufahamu muhusika mkuu katika kukusanya taarifa za tafiti

Muda: Dakika 45

Vifaa: • Vip kadi

• Bango kitita

• Kalamu

HatuaHatua ya 1: Anzisha somo hili kwa kueleza kuwa tutakuwa tukijadili kuhusu kufanya tafiti kabla ya kuanza kampeni ya uchaguzi na mambo muhimu ya kuyafanyia tafiti kabla ya kuanza kampeni.

Hatua ya 2: Bandika bango kitita Saba (7) sehemu tofauti tofauti za ukumbi unaofanyia mkutano. Kila bango kitita liwe na swali tofauti kati ya maswali yafuatayo:

i. Unajua nini kuhusu sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi Tanzania

ii. Una taarifa gani kuhusu jimbo unalogombea?

iii. Unaelewaje wapiga kura wako?

iv. Unajua nini kuhusu chaguzi zilizopita?

v. Una uelewa gani kuhusu hali ya chama chako kukubalika?

vi. Ni upi uwezo wako na udhaifu wako?

vii. Unajua nini kuhusu mpinzani wako (uwezo wake na madhaifu yake)

Hatua ya 3: Gawa vip kadi 8 kwa kila mshiriki na waambie waandike jibu moja kwa kila swali na wabandike kwenye bango kitika wakioanisha jibu na swali husika.

Hatua ya 4: Waambie washiriki wasogee karibu na bango kitita kusikiliza huku ukisoma majibu yao na hakikisha unachambua majibu hayo kama ni taarifa mahimu au laa katika kufanya utafiti kabla ya kuanza kampeni. (Fanya hivyo kwa kila swali)

Hatua ya 5: Warudishe washiriki kwenye kundi kubwa na utoe hitimisho kwamba kama mgombea kuna maeneo muhimu anapaswa kuyafanyia tafiti kipindi chote cha kampeni. (Unaweza kutimua Kitini Namba 5 A: UTAFITI A kutoa hitimisho).

Page 46: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

43

KITINI NA. 5 A UTAFITI

Kama mgombea na timu ya kampeni mnatakiwa kuwa na taarifa za awali kuhusu masuala muhimu ya nchi, jimbo au kata unayogombea katika kipindi chote cha kampeni. Pale tu un-apopata wazo la kugombea katika uchaguzi anza kukusanya taarifa wewe mwenyewe au kwa kutumia wasaidizi utakaoona wanafaa. Baada ya kuwa umepata timu ya kampeni, hakikisha kila mmoja anatafuta taarifa za nyongeza kwenye eneo lake husika.

Maeneo Muhimu ya kufanyia utafiti1. Zijue sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi:

o Tambua masuala yanayokubaliwa na yasiyokubaliwa wakati wa uchaguzi. Kwa mfano miongozo ya matumizi ya fedha za kampeni na maadili ya uchaguzi kwa wagombea na vyama vya siasa.

o Tafuta ushauri au fanya utafiti wako mwenyewe kujifunza kuhusu sheria maalum ambazo zinasimamia uchaguzi. Fahamu kuwa kanuni za uchaguzi mwaka 2015 zin-aweza kuwa zisiwe sawa na na za mawaka 2020.

o Tumia Jedwali lililopo kwenye Kiambatanisho 2 kuorodhesha kanuni muhimu za uchaguzi ambazo wewe na timu yako ya kampeni lazima ujue na kamwe usizivunje

2. Fahamu sifa na aina ya wapiga kura wako:

o Tafuta orodha kamili ya wapiga kura kutoka kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Fanya tathmini ya wapiga kura kulingana na umri, jinsia, elimu na kiwango cha utaalam, mapato, na ulemavu.

o Angalia changamoto walizonazo makundi ya wapiga kura ya wanawake, wanaume, vijana na wenye ulemavu katika masuala ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiteknolo-jia. Nini kimefanywa na kiongozi aliyepita, changamoto zipi bado zipo.

o Tafiti masuala ya kipaumbele katika jamii husika (kwa mfano elimu, ukosefu wa aji-ra, afya, ukatili wa kijinsia, afya ya uzazi ya vijana n.k)? Pata taarifa kutoka mashirika ya kimataifa, kitaifa, taasisi za serikali na taasisi za elimu.

o Buni mbinu za kuwafikia wapiga kura. Watu wa jamii hiyo hupata wapi taarifa za kisiasa? Je ni kwenye magazeti, majarida, vipeperushi, redio, television, mitandao ya kijamii, taarifa kutoka mtu mmoja mmoja n.k.

o Tafiti kufahamu nani aliye na ushawishi zaidi juu ya tabia za wapigakura wako. Watu hawa lazima wawe washirika na wafuasi wako.

3. Taarifa Kuhusu Chaguzi Zilizopita.

o Fuatilia taarifa za chaguzi zilizopita ili kufahamu idadi ya wapiga kura, chama kipi kilishinda na kwa nini, masuala gani muhimu yalijitokeza na kutoa dira ya uchaguzi huo.

o Fuatilia daftari la wapiga kura kufahamu, je ni kina nani walipiga kura na nani hak-upiga kura. Je, wanawake , vijana na watu wenye ulemavu wamewahi kushinda ka-tika chaguzi zilizopita katika eneo unalogombea?

o Tafiti hali ya kukubalika kwa chama chako. Je, chama chako kinaungwa mkono na walio wengi. Je, chama chako kimeendelea kukubalika au kinadidimia? Na kwa nini? Je, wanachi wanakukubali wewe hata kama hawakubaliani na masuala Fulani Fulani ya chama chako?

Page 47: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

44

4. Muktadha wa nchi/jimbo/kata unalogombea.

o Kusanya taarifa zinazohusu ukubwa wa eneo unalogombea

o Kusanya takwimu na idadi ya wakazi wa eneo hilo (wanawake, wanaume, vijana, watu wenye ulemavu)

o Fahamu shughuli zao za kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiteknolojia.

5. Taarifa kuhusu watu, makundi na taasisi mashuhuri.

Tambua wataalamu, wafanyabiashara, viongozi wa kimila na kidini katika eneo husika wenye nguvu ya ushawishi.

o Tafuta ya jinsi ya kuwasiliana na kuwahusisha katika kampeni yako

o Tambua vyombo vya habari vilipo, haswa redio za jamii na zile zenye hadhira pana ili kuweza kuzitumia wakati wa kampeni

o Tambua vikundi mashuhuri mfano vikundi vya mpira, vikoba na jumuia

o Tambua namna dini au ukabila unavoweza kuathiri uchaguzi na hakikisha una-jiepusha na kufanya kampeni za udini na ukabila

6. Fahamu kuhusu wewe

o Fahamu uwezo na udhaifu wako. Hii itakusaidia kufanya kampeni kwa ufanisi zaidi.

o Fikiria utu wako, wasifu wako kwa umma, mtandao wako, na historia yako ya zama-ni.

o Fikiria kuhusu maarifa yako, mahusiano au ujuzi ambao unaweza kukusaidia kush-inda.

o Ikiwa unagombea kama mgombea wa chama cha kisiasa, tathmini utendaji na sifa za chama chako kuanzia ngazi za chini hadi kitaifa.

o Uelewa kuhusu uwezo na udhaifu wako utakusaidia kutambua fursa na vitisho.

o Fursa ni pamoja na mambo kama vile kuwa na uwezo wa kufikia mitandao uliyo-nayo kama makanisa, biashara, au harakati za wanawake kueneza ujumbe wako. Chama chako kina kubalika katika eneo lako na wanachama wa chama wanaweza kutoa msaada.

o Vitisho vinaweza kuwa kama tukio ulishawahi kufanya siku zako za nyuma ambalo mpinzani wako anaweza kutumia kukupunguzia uwezo wa kushinda au ukosefu wa ufahamu wa masuala katika jamii yako.

Tumia Kiambatanisho 3: Kupima uwezo, udhaifu, fursa na vitisho kwako

7. Tafiti kuhusu Mpinzani wako:

o Tafiti sera, hoja na mikakati ya wapinzani wako

o Angalia mapengo na udhaifu alionao, kamwe usitumie lugha za matusi

o Tafiti taarifa za wapinzani wako yaani uwezo wao, udhaifu, historia yao ya awali, shughuli za sasa, mitandao yao .

o Fanya uchambuzi wa Uwezo, Udhaifu, Fursa na Vitisho (SWOT).

Page 48: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

45

8. Taarifa za kila siku

o Hakikisha una vyanzo vya taarifa kuhusu masuala yanayojitokeza katika kata au jumbo unalogombea na jinsi yanavyoweza kuathiri kampeni yako

o Angalia mapengo na udhaifu alionao, kamwe usitumie lugha za matusi

o Tafiti taarifa za wapinzani wako yaani uwezo wao, udhaifu, historia yao ya awali, shughuli za sasa, mitandao yao .

o Fanya uchambuzi wa Uwezo, Udhaifu, Fursa na Vitisho (SWOT).

SOMO LA TATU: TIMU YA KAMPENI

Malengo Mahususi ya somoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

• Kuelewa kuhusu timu ya kampeni.

• Kutambua majukumu ya timu ya kampeni na namna wanavyoshiriki kufanikisha zoezi zima la kampeni.

• Kuelewa kuhusu changamoto za timu ya kampeni na njia za kutatua

Muda: Dakika 45

Vifaa: • Kitini cha mshiriki Na. 5 B

• Bango kitita

MbinuBungua Bongo

Maswali na Mjibu

Kushirikishana uzoefu

HatuaHatua ya 1: Anzisha somo hili kwa kueleza kuwa tutakuwa tukijadili kuhusu kuunda timu imara ya kampeni.

Hatua ya 2: Kabla ya kueleza nini maana ya timu ya kampeni, Waulize washiriki kutumia uzoefu wao kuelezea kazi zote katika kampeni ya uchaguzi. Au Waulize washiriki kuelezea uchaguzi ambao walisaidia, walikua na majukumu gani katika uchaguzi huo (Nakili majibu yao kwenye bango kitita)

Hatua ya 3: Ikiwa hakuna mtu katika kikundi amesaidia kampeni ya uchaguzi, mwalike mshiriki ambaye ana uzoefu huu ongee kuhusu kile alichojifunza kuhusu kazi zinazohusika na kampeni za uchaguzi. (Nakili pointi muhimu kwenye bango kitita)

Hatua ya 4: Baada ya zoezi la majukumu ya kipindi cha uchaguzu Waulize washiriki kuelezea uzoefu ambao wameupata kufanya kazi na timu kipindi cha kampeni za uchaguzi. Unaweza kutumia maswali yafuatayo::

Page 49: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

46

• Ni mambo gani yaliwasaidia kama washiriki wa timu kufanya kazi pamoja na kwa ufanisi?

• Ni njia gani nzuri walitumia kuweka timu pamoja kwa muda mrefu na kufanya kazi mpaka tarehe ya uchaguzi?

• Mliweza kukabiliana vipi na kutoelewana miongoni mwa washiriki wa timu?

Hatua ya 5: Toa hitimisho kwa kueleza washiriki umuhimu wa kuwa na timu nzuri ya kampeni, wahusika na viongozi wa timu za kampeni, majukumu ya timu ya kampeni na changamoto wanazoweza kukutana nazo kwa timu zao za kampeni. (Tumia jedwali hapo chini kueleza dhana nzima ya timu ya kampeni na gawa kitini Na: 5 B Kuandaa Timu ya kampeni.

KITINI NAMBA 5 B: KUANDAA TIMU YAKO YA KAMPENIKutengeneza timu ya imara ya kampeni ndio kiini cha mafanikio katika kampeni za uchaguzi. Kama mgombea unahitaji timu ya watu wabunifu, wenye kujituma, na wenye ari ya kufanya kazi kwa bidii. Timu inapaswa iwe na watu wenye ujuzi, maarifa na weledi na talanta za aina mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kuleta ufanisi na matokeo chanya katika kampeni.

Timu ya kampeni ni muhimu kwa mafanikio. Unahitaji timu ambayo ni ya watu waaminifu na wenye bidii. Ni lazima timu yako kuwa na mchanganyiko wa watu wenye vigezo, ujuzi na maarifa na iongozwe na meneja wa kampeni mwenye ufanisi na anayeheshimika.

Ni muhimu pia wewe kama mgombea kuelewa wajibu wako kwenye kampeni. Wewe ni kion-gozi wa timu – unahitaji kuhamasisha, kuhimiza na kuthamini timu yako ya kampeni na kuji-tolea kwa matendo na maneno yako yote. Kazi yako ya msingi ni kuwasiliana na wapigakura moja kwa moja, kuwashawishi wapiga kura ambao bado hawajaamua wanampigia nani kura kupiga kura kwa ajili yako na kuorodhesha watu wanaojitolea kukusaidia katika kampeni zako.

Pia kama mgombea unawajibu wa kujihusisha na vyombo vya habari ili ujumbe wako pia ufike kwa wapiga kura -hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hizi kwa ufanisi kama wewe

Timu yako ya kampeni inapaswa kuwa na washiriki wafuatao:

i) Msimamizi wa Kampeni: Ni mtu wa karibu sana na mgombea. Anatakiwa kuwa na uzoefu wa kusimamia kampeni, mwenye mipango thabiti na mtandao mkubwa kwa ajili ya manufaa ya mgombea. Hutoa ushauri wa kimkakati kuhusuiana na muelekeo wa kampeni. Chagua mtu unayemuamini na mwenye ujuzi wa kuendesha kampeni.

ii) Meneja wa Programu: Ana wajibika kupanga na kusimamia ratiba yote ya mgombea kwa ujumla. Mtu huyu anahakikisha ratiba za mgombea hazigongani. Inabidi awe ni mtu mwenye uwezo wa kwenda na muda na anaeweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

iii) Meneja wa Fedha/Mweka Hazina: Hushughulika na uchangishaji fedha na kuweka hes-abu za kampeni, pia hutunza kumbukumbu za matumizi yote ya kampeni.

iv) Meneja Mawasiliano: Ni kiungo muhimu baina ya mgombea na vyombo vya habari. Kazi yake kubwa ni kumuunganisha mgombea na media. Mgombea anatakiwa achague Meneja Mawasiliano mwenye uzoefu wa kutosha na anayeelewa siasa za vyombo vya habari. Huandaa mikutano na waandishi wa habari, taarifa kwa vyombo vya habari, makala au blogu kuhusu mgombea chini ya Mratibu wa kampeni.

Page 50: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

47

v) Mratibu wa kuzalisha na kusambaza vitendea kazi: Husaidia kuratibu uzalishaji na usambazaji wa vitendea kazi na pia husimamia usambazaji na usafirishaji wote wa machapisho.

vi) Waratibu wa siku ya kupiga kura: Hawa ni watu watakaotembelea vituo mbalimbali ili kufuatilia mchakato wa uchaguzi unavyoenda. Hupokea taarifa kuhusu masuala yan-ayojitokeza siku ya uchaguzi na kuzipeleka kwa meneja kampeni na mgombea. Ni watu wanaofahamu sheria, kanuni za mwenendo na taratibu za kupiga kura.

vii) Mwanasheria: Hushauri na kuhakikisha kuwa kampeni inazingatia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi.

viii) Msaidizi binafsi: Husaidia katika upatikanaji wa wafuasi kwa ajili ya mgombea; kuand-ika barua za kuomba kuungwa mkono au barua pepe; hufanya kazi kwa karibu na Mra-tibu katika utekelezaji wa ratiba za mgombea; husaidia katika maandalizi ya mikutano ya mgombea. Mtu huyu pia hufanya utafiti juu ya mwenendo wa kampeni kwa niaba ya mgombea na timu nzima ya kampeni. Msaidizi binafsi pia husaidia kuweka shughuli za kampeni katika mitandao ya kijamii, kumtangaza mgombea na kujibu baadhi ya maswa-li kuhusu mwenendo wa kampeni.

ix) Wawakilishi wa mgombea katika vituo vya kupigia kura: Huangazia uhalali wa zoezi la kupiga kura, kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo.

Kumbuka:o Unaweza kuongeza nafasi kadri unavyoona inafaa kulingana na uhitaji na uwezo wa

kifedha.

o Kumbuka kila mtu katika timu ya kampeni lazima awe na majukumu mahususi.

o Tambua kuwa mgombea anapaswa kuihamasisha, kuitia moyo na kuithamini timu ya uchaguzi kwa maneno na vitendo.

o Licha ya kuwa na timu ya kampeni, ni jukumu la msingi la mgombea kukutana na wa-piga kura, kushawishi wapiga kura, na kuongea na vyombo vya habari. Wengine ni wasaidizi tu. Kazi hii haiwezi kufanywa na mtu mwengine kwa niaba yako kwa ufanisi kama vile utakavyo ifanye wewe mwenyewe.

Page 51: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

48

Changamoto za Timu ya Kampeni na Njia za Kutatua

No. Changamoto Utatuzi Mhusika1 Kutokua na watu sahihi

kwenye timu yakoHakikisha unachagua watu sahihi, watu wa karibu na mgombea ni bora zaidi

Mgombea

2 Kushindwa kutengeneza jumbe na mada ambazo zitakubaliwa na wapiga kura

Andaa ujumbe wako mapema na omba ushauri kwa watu wako wa karibu na waliokwisha pitia mchakato wa uchaguzi

Mgombea na timu yake

3 Kushindwa kuchangisha fedha za kampeni

Tengeneza bajeti kwanza, kisha tambua kiasi ambacho unaweza kuchangia mwenyewe na chama chako kisha tafuta vyanzo vingine.

Mgombea na timu yake

4 Kutopata muda wa kutosha kwenye vyombo vya habari muhimu

Tumia njia tofauti kufikia wapiga kura wako zikiwemo nyumba kwa nyumba,mitandao ya kijamii, redio au vipeperushi.

Mgombea na timu yake

5 Ukubwa wa eneo la kufanya kampeni

Kama eneo la kufanya kampeni ni kubwa sana, panga mapema ratiba inayogusa maeneo yote.

Mgombea na timu yake

6 Kutokufanya utafiti wa kutosha kabla ya kampeni

Fanya utafiti mapema ujue idadi ya kura zilizopo, aina ya wapigakura wako, na mpinzani wako.

Mgombea na timu yake

HitimishoKatika somo hii tumejifunza kuhusu timu ya kampeni. Tumeweza kufahamu aina ya watu wanaounda timu ya kampeni ikiwemo majukumu wanayopaswa kuyatekeleza ili kufanikisha zoezi la kampeni. Tumejifunza kwamba timu ya kampeni inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na matakwa ya kampeni. Kwa kuwa timu ya kampeni ina watu wa tofauti tofauti changamoto katika utendaji kazi lazima zitatokea. Usikubali makosa madogo madogo yawarudishe nyuma, jadilini kwa uwazi, haraka na kwa namna ya kutafuta suluhu. Ruhusu kujifunza kutokana na makosa.

Page 52: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

49

SOMO LA NNE: SERA NA JUMBE ZA KAMPENI Malengo Mahususi ya somoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

• Kuandaa sera za kampeni kulingana na wapiga kura wao,

• Kujua na kueleza vyanzo vya sera ,

• Kujua jinsi ya kuandaa na kutoa ahadi kwa makundi tofauti tofauti katika jamii

• Kuelewa jinsi ya kuandaa kauli mbiu za uchaguzi.

Muda: Dakika 30

Vifaa: • Bango kitita

• Kitini cha Mshiriki Na 5 C.

MbinuMkundi (Kulingana na vyama vya siasa)

Kushirikishana uzoefu

HatuaHatua ya 1: Tambulisha somo hili kwa kutumia maelezo ya kijedwali hapo chini.

JUMBE ZA KAMPENI

Ujumbe wako wa kampeni unaweza kuchukua sura tofauti kulingana na wapi, jinsi na wakati unapaswa kuwasilisha ujumbe huo. Wakati ukizungumza katika mikutano au makundi madogo ingiza ujumbe wako katika hotuba yako kwa kutumia hadithi na mifano ya kibinafsi, na hakikisha unarudia rudia ujumbe huo kwa njia tofauti. Unapaswa pia kuwa na uwezo wa kutoa ujumbe wako ndani ya sekunde 90. Lengo lako kuu la kuwa na jumbe ni kushawishi wapiga kura kukupigia kura wewe badala ya wapinzani wako.

Ujumbe wako unatoa sababu za kwa nini wapigakura wanapaswa kusaidia kampeni yako na kukupigia kura wewe. Ujumbe mzuri na wenye ufanisi lazima uwe:

Wakuaminika

Wazi na mafupi

Wa muhimu na wenye maadili kulingana na jamii

Unaoshawishi

Wakitofauti

Unaorudiwa mara kwa mara,

Hatua ya 2: Kama washiriki wamehudhuria kulingana na vyama vyao vya kisiasa, gawa vikundi kulingana na vyama vyao vya siasa, waombe kila kikundi kujifanya kwamba wamesimamisha mgombea na wataenda kugombea katika uchaguzi ujao wa kata, Jimbo au Taifa.

Hatua ya 3: Uliza kila kikundi wachague kata, jimbo au nchi wanayoielewa vizuri na kuamua kwa pamoja

• Ni nini dira ya jumla na malengo ya kampeni yao?

Page 53: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

50

• Ni masuala gani ambayo watayaibua wakati wa kampeni?

• Ni suluhisho gani na mawazo gani watawasilisha kwa wapiga kura?

• Watengeneze jumbe zisizopungua tatu watakazotumia kipindi cha kampeni?

• Waorodheshe mahitaji ya vifaa vya kampeni watakavyo tumia kufikisha ujumbe

Hatua ya 4: Baada ya zoezi hilo waombe kila kikundi kuwasilisha ujumbe wao kwa darasa zima. Wale wanaosikiliza wanaweza kuuliza maswali. Ili kufanya zoezi hili kuwa halisia unaweza kuuliza kila kikundi kuchukua mtu atakayejifanya kuwa kama mgombea. Mtu huyo anaweza kuwasilisha ujumbe wa kikundi na kujibu maswali kutoka kwa washiriki wengine kuhusu jumbe hizo.

Hatua ya 5: Boresha majadiliano kwa kutumia maelezo yaliyotolewa kwenye kitini Na. 5 C Kuandaa Sera Na Jumbe Za Kampeni

KITINI NAMBA. 5 C: JINSI YA KUANDAA SERA ZA KAMPENI KULINGANA NA WAPIGA KURA WAKO

Sera zako zinawavutia wapiga kura kwa namna tofauti. Tambua kuwa haiwezekani kuvutia watu wote. Katika kunadi sera zako kumbuka kuwa; -

o Wako wanaokuunga mkono kwa asilimia mia (100)

o Wako wanaokuunga mkono kwa kiwango fulani (Mfuasi vuguvugu)

o Wako wanaokupinga kabisa

o Wako wanaokupinga kwa kiwango fulani (Mpinzani vuguvugu)

o Wako ambao hawajafanya maamuzi

Kumbuka:

Nguvu na rasilimali za mgombea zinapaswa kuelekezwa kutunza wafuasi ulionao na kuwaleta wapinzani au wafuasi vuguvugu katika kundi la wafuasi.

Je Sera Zako Unazitoa wapi

o Ilani ya chama chako

o Tafiti juu ya changamoto za makundi mbalimbali katika kata au jimbo unalotaka kugombea.

Page 54: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

51

Kwa hali ilivyo Tanzania changamoto kwa makundi tofauti tofauti huweza kuwa kama ifutavyo.

Na. Kundi Changamoto Ahadi Unazoweza Kuziweka Katika Sera Zako.

1 Vijana • Kukosa Elimu ya ujasiriamali na mitaji

• Elimu haiwaandai vijana kujiajiri na kujitegemea

• Vijana hawashirikishwi katika maamuzi ya masuala muhimu yanayowahusu

• Vijana wa kike kukatazwa kurudi shule wanapopata ujauzito

• Ujuzi wa teknolojia na matumizi yake ili kuendana na maendeleo ya dunia

• Changamoto kwenye kupata elimu

Kuweka Utaratibu wa

• Kuwaunganisha vijana na taasisi za mikopo.

• Kufadhili elimu ya ujasiriamali kwa makundi ya vijana kama nyenzo ya kuondoa umasikini.

• Kuwatafutia masoko vijana.

• Kupata taarifa mbalimbali kuhusu fursa za kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kiteknolojia na kisiasa ndani nan je ya nchi.

• Kushirikishwa katika uongozi wako na kutoa nafasi kwa vijana kuelezea na kutafuta ufumbuzi wa matatizo/changamoto zao kupitia wajumbe vijana

• Kufungua kituo cha maarifa ya vijana kwa njia ya teknolojia

• Kufungua maktaba ya jamii ili kuwaongezea vijana maarifa ya kuhimiza usomaji wa vitabu.

• Kuishawishi serikali kutoa fursa za kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia, na kiutamaduni kwa vijana.

• Kushawishi serikali kutoa elimu bora ya msingi, sekondari, na vyuo.

Page 55: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

52

2 Wanawake • Ushiriki finyu wa wanawake katika Nyanja za maamuzi na uongozi

• Mazingira duni kwa wanawake wajasiriamali

• Ukatili wa Kijinsia

• Sheria za kibaguzi za mirathi zinazonyima haki wanawake kumiliki ardhi.

• Mitaji kwa ajili ya shughuli za kichumi

• Tozo kwenye taulo za kike.

• Wasichana wanapopata ujauzito kutokuruhusiwa kurudi shuleni

• Kazi nyingi za nyumbani zisizo na malipo

Kufanya utaratibu wa:

• Kupatiwa mkopo yenye riba nafuu

• Kupata fursa za kiuchumi

• Kutafutiwa masoko

• Kutoa elimu ya ujasiliamari

• Kutoa elimu juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi

• Kupunguza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake

• Kuwapa nafasi wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi

• Kutoa Elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana

• Kuhakikisha wanawake wanapata haki zao za msingi

• Kuzingatiwa kwa hedhi salama na gharama nafuu za taulo za kike

• Kuhimiza mgawanyiko wa majukumu ya nyumbani kwa wanaume na wanawake

• Wasichana wanaopata ujauzito kurudi shule

Page 56: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

53

3 Wenye

Ulemavu

• Unyanyapaa

• Ajira

• Elimu isiyo jumuishi

• Ushiriki finyu katika Nyanja za uongozi

• Gharama za matibabu huwa juu Zaidi

• Sehemu nyingi (shule, hospitali benki) hazina mazingira rafiki kwa wenye ulemavu

Kufanya Utaratibu wa:

• Kuwezeshwa kiuchumi kwa kupatiwa mitaji

• Elimu ya ujasiliamali

• Kushawishi serikali kuweka miundo mbinu ya elimu jumuishi

• Kushawishi waajiri(serikali na sekta binafsi kuajiri watu wenye ulemavu.

• Kutoa elimu kuhusu haki za watu wenye ulemavu kwenye jamii ili kupunguza unyanyapaa

• Kushawishi uboreshaji wa mazingira ya majengo ya umma kukidhi mahitaji ya wenye ulemavu

• Kupatiwa bima za afya bure

• Kushawishi wenye ulemavu kuwa kwenye nafasi za uongozi.

• Kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wazazi watakaobainika kuficha watoto kisa wamezaliwa na ulemavu.

4 Wazee • Wengi hawana kipato endelevu

• Baadhi ya familia kuwaona kama mzigo

• Kukosa muwakilishi wa matatizo yao

• Kiinua mgongo kuchelewa

• Gharama za matibabu ni kubwa na wengi hawajapata bima za bure

Kufanya Utaratibu wa:

• Kuhakikisha wazee kupitia mifuko ya jamii wanapata mahitaji yote muhimu

• Kuhakikisha kiinua mgongo kinatoka kwa wakati

• Kutoa bima za afya ili ku-hakikisha usalama wa afya za wazee

• Kuhakikisha wazee wana-jumuishwa katika nafasi za uongozi

• Kutengeneza miradi ya wa-zee

Page 57: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

54

Kumbuka o Hii ni mifano tu ya changamoto na aina za ahadi unazoweza kutoa kwa makundi haya.

Fanya mazungumzo na wawakilishi wa makundi haya katika kata au jimbo unalogombea ili kufahamu changamoto zao kiundani na pia sikiliza maoni yao kuhusu namna ambayo changamoto zao zinaweza kutafutiwa suluhu.

o Hakikisha sera zako zinajikita kutatua changamoto za makundi haya na masuala mengine muhimu katika kata na jimbo unalogombea

o Hakikisha kutoa sera zako kwa makundi yote katika mikutano ya hadhara na vyombo vya habari. Pia tenga muda na makundi mahususi uwaelezee kuhusu sera zako kwao.

Kuandaa Kauli Mbiu ya Kampeni ya UchaguziKauli mbiu ni ujumbe mkuu au ujumbe wa jumla kutoka kwenye sera zako. Kauli mbiu hutaki-wa kukuelezea wewe ni nani, unasimamia nini ukilinganisha na wagombea wengine. Kauli mbiu ina umuhimu mkubwa katika kampeni kama vile:

Kukutambulisha kama mgombea pamoja na maono yako hata kama haupo

Kukuletea upekee na kutofautisha na wapinzani wako

Kuwavutia na kukunganisha na wapiga kura wako. Ujumbe hufaa uwaguse wapiga kura wako.

Kukupa dira ya kuhakikisha kila unachofanya wakati wa kampeni kinaendana na kauli mbiu na malengo ya kampeni yako.

Kusaidia katika utayarishaji wa mabango, vipeperushi na vifaa vingine vya kutumiwa wakati wa kampeni yako.

Kauli mbiu yako inapaswa kuwa na sifa zifuatazo:Fupi na inayoeleweka

Yenye kuleta hamasa

Yenye kuleta mtizamo mpya

Yenye kuleta tumaini jipya

Yenye kuweza kukumbukwa haraka

Rahisi kurudiwa mara kwa mara.

Yenye kuvutia watu wakupigie kura;

Kuwa na uwezo wa kujibu swali ni kwa nini unagombea

Mifano ya Kauli MbiuHapa kazi tu-Raisi John Pombe Magufuli

Ni wakati wa mabadiliko-Mgombea Uraisi CHADEMA-2015

Kuwepo Kazi, Mkate, Maji na Chumvi kwa Wote – Nelson Mandela

Ndio Tunaweza! Matumaini na Mabadiliko– Barack Obama

Page 58: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

55

Kuandaa vifaa vya KampeniKabla ya kutoa ujumbe wako wa kampeni, utahitaji baadhi ya vifaa vya kampeni. Kama wewe ni mgombea wa chama cha kisiasa, chama chako kikusaidie kuzalisha vifaa, wakati wengine utahitajika kutumia gharama zako mwenyewe kutengeneza vifaa hivyo. Muda ni kila kitu ka-tika siasa na katika kampeni hivyo hakikisha unatenga muda wa kutosha kupata vifaa vyote ambavyo hutolewa na kuhitajika. Gharama za vifaa zinapaswa kujumuishwa katika bajeti yako. Vifaa hivyo vinapaswa kujumuisha jina lako, nambari ya uchaguzi ya chama (ikiwa una namba) na kauli mbiu: Unaweza kutumia kiambatanisho Kiambatanisho Na. 4. Aina ya vifaa vinavyo-hitajika, Jinsi vifaa vitakavyozalishwa, na ambapo vitatumika.

HitimishoKatika mada hii tumejifunza jinsi ya kuandaa sera za kampeni kulingana na changamoto za wa-piga kura wako. Pia tumejifunza kuhusu vyanzo vya sera zako, mifano ya changamoto na ahadi unazoweza kutoa kwa makundi tofauti tofauti katika jamii na jinsi ya kuandaa kauli mbiu za uchaguzi. Kauli Mbiu yako inapaswa kuwa fupi, rahisi kueleweka na kuirudiarudia na iendane na sera za chama chako pamoja na ahadi unazotoa kama mgombea. Vile vile tumejifunza kuhu-su vifaa vya kampeni na kujua jinsi vitatumika.

SOMO LA TANO: KUFIKIA WAPIGA KURA Malengo Mahususi ya somoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

• Kujua kuhusu mbinu za kufikisha sera na ujumbe kwa wapiga kura

• Kutengeneza mpango mkakati wa kufikia wapiga kura

Muda: Dakika 45

Vifaa: • Bango kitita

MbinuMichezo ya kugiza

Kazi za vikundi

HatuaHatua ya 1: Tambulisha somo hili na waeleze washiriki kwamba ili kuweza kushinda uchaguzi wowote ni lazima uwe na mkakati madhubuti ya kufikia wapiga kura wako ili wapate ujumbe na sera zako.

Hatua ya 2: Omba washiriki wanne (4) wakujitolea kuja mbele ya darasa na wape majukumu yafuatayo:

• Mshiriki wa kwanza ni mgombea wa nafasi ya ubunge

• Mshiriki wa pili ni mwanachama wa chama cha mgombea

• Mshiriki wa tatu ni mwananchi asiye na chama

• Mshiriki wanne ni mwanachama wa chama pinzani

Hatua ya 3: Muelekeze mshiriki wa kwanza (Mgombea) atoe sera zake kwa nini achaguliwe

Page 59: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

56

kuwa mbunge huku mshiriki wa 2, 3 na 4 wakisikiliza sera za mgombea. Hatua ya 4: Waelekeze washiriki wa 2,3 na 4 kuchukua kipande cha karatasi na kupiga kura ya ndio au hapana huku wakiwa wameandika namba zao kama zilivyotolewa kwenye hatua ya 2:

Hatua ya 5: Soma majibu ya washiriki 2, 3 na 4 alafu uliza darasa zima wamejifunza nini kutokana na zoezi hilo? Unaweza kuuliza maswali yafuatayo?

• Mmejifunza nini kutoka kwa mshiriki namba 2?

• Mmejifunza nini kutoka kwa mshiriki namba 3?

• Mmejifunza nini kutoka kwa mshiriki namba 4?

Hatua y 6: Andaa muhtasari wa zoezi hili na hitimisha majadiliano kwa kutumia maelezo yaliyotolewa na kijedwali hapo chini.

KULENGA WAPIGA KURA

Muda wako ni wa thamani na kumbuka kwamba una rasilimali ndogo katika kampeni yako. Unaweza kuongeza kura zako kwa kuandaa mkakati wa kufikia wapiga kura wako

Kwa kawaida, wapiga kura wamegawanyika katika makundi matatu ya msingi:

a) Wapiga kura wako: Hawa ni watu ambao watapiga kura kwa kuzingatia sababu za kibinafsi, kiutamaduni au uhusiano wenu kisiasa. Hawa ni watu ambao unaweza kuwahesabia kwamba watapiga kura kwa ajili yako, mara nyingi huwa wanachama wa chama chako

b) Wapiga kura ambao hawajaamua: Watu ambao hawana uaminifu kwa mgombea yeyote au chama na ambao hawakuamua jinsi ya kupiga kura. Watu hawa ni wapiga kura ambao wanaweza kuwa na maana ya kupiga kura kwa ajili yenu.

c) Wapinzani na wafuasi wao: Hawa ni watu ambao kamwe hawatakupiga kura kwa kuzingatia sababu za kibinafsi, kitamaduni au kisiasa. Kazi yako ni kuwalenga wapiga kura wako na wapiga kura ambao hawajaamua. Wapiga kura wako unaweza kuwauliza kama wanaweza kuwa watu wa kujitolea katika kampeni yako.

Hivyo basi ni vyema kuelekeza nguvu zako kwa wapiga kura wako pamoja na wale ambao bado hawajaamua kuhusu nani watampigia kura. Unaweza kuwekeza nguvu nyingi kwa wapinzani na wafuasi wao ukajikuta umesahau kuwekeza kwa wapiga kura wako na wale ambao bado hawajaamua.

Hatua ya 7: Kazi za vikundi. Gawanya washiriki kulingana na vyama vyao vya siasa, waeleza kwamba wataenda kutengeneza mpango mkakati unaoeleza aina ya wapiga kura na mbinu watakazotumia kufikia wapiga kura hao. (Unaweza kugawa kiambatanisho Na. 5 watumie kujaza mikakati hiyo). Kisha kusanya majibu yao na toa muhtasari juu ya majibu yao

Hatua ya 8: Hitisha somo hili kwa kutumia majibu yaliyoainishwa kwenye kitini Na….

Page 60: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

57

KITINI NA 5 D: MBINU ZA KUFIKIA WAPIGA KURA

Tayari una sera na kauli mbiu yako ya uchaguzi. Je ni namna gani utawasilisha sera na kauli mbiu yako kwa wapiga kura wako? Ni muhimu sana kama mgombea kuwa na mpango kazi wa jinsi ya kuwafikia wapiga kura wako. Mbinu za kuwafikia wapiga kura wako ni kama zifuatavyo.

o Kampeni za nyumba kwa nyumba: Hii ndio njia rahisi, pia inakupa fursa ya kupata muda wa kuwafahamu wapiga kura wako na mawazo yao kwako.

o Kampeni ya kutumia simu: Wapigie simu wapiga kura wako ambao huwezi kuonana nao ana kwa ana. Pia andaa jumbe fupi fupi zenye sera za kampeni yako na watumie wapiga kura wako.

o Shiriki shughuli za kijamii kama michezo, misiba na harusi. Omba nafasi ya kuzungumza kama inawezekana.

o Andaa vipeperushi na mabango yenye sera na jumbe za kampeni yako

o Sanaa ya maonyesho na muziki zenye kubeba sera na jumbe za kampeni yako

o Tumia vyombo vya habari, mfano magazeti, redio na runinga kutangaza sera na jumbe za kampeni yako

o Matumizi ya mitandao ya kijamii, mfano Facebook, Twitter, Instagram, Youtube, Blogi. Mitandao hii mipya ya mawasiliano inapendwa na vijana lakini pia hata watu wa makamo wameanza kuitumia. Kila aina ya mtandao wa kijamii una namna ya kutumia na maudhui unayoweza kuweka.

o Timu ya kampeni iweke taarifa zako, jumbe zako za kampeni pamoja na matukio yote yahusuyo kampeni kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii pamoja. Ainisha wahamasishwaji wa mitandao ya kijaamii wanaoweza kuweka

SOMO LA SITA: RASILIMALI ZA KAMPENI ZA UCHAGUZI

Malengo Mahususi ya somoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza kufahamu:

• Sheria zinazosimamia gharama za uchaguzi

• Kuandaa bajeti ya kampeni

• Mbinu mbali mbali za kuweza kupata rasilimali za kampeni za uchaguzi

• Kuwasilisha taarifa za gharama za uchaguzi baada ya uchaguzi

• Makossa na adhabu ndani ya sharia ya gharama za uchaguzi

Muda: Dakika 50

Vifaa: • Vip kadi

• Bango kitita

Page 61: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

58

MbinuMichezo

Kazi za vikundi

Uhadhiri

HatuaHatua ya 1: Waambie washiriki kwamba katika somo hili watajifunza kuhusu Rasilimali za kampeni na mbinu mbali mbali za kuweza kupata rasilimali mbali mbali za kampeni

Hatua ya 2: Uliza washiriki wanaelewa nini kuhusu gharama za uchaguzi? Chukua majibu machache na kwa kutumia mifano toa ufafanuzi kwa kutumia jedwali hapo chini:

GHARAMA ZA UCHAGUZI

Kila kampeni inajumuisha matumizi ya fedha na rasilimali mbalimbali. Gharama hizi huitwa gharama za uchaguzi na husimamiwa chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2015.

Sheria hii imelenga kuratibu na kuzuia matumizi mabaya/haramu ya pesa wakati wa mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombea, wakati wa kampeni na kipindi cha kupiga kura ili kuweka mazingira ya haki kwa vyama vyote na wagombeaji.

Sheria ina vifungu ambavyo vinasimamia matumizi ya pesa wakati wa kampeni na inataka wagombeaji wote na vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi kuweka wazi kiasi na chanzo chao cha fedha kinachotumiwa katika uchaguzi.

Kwa upande wa Tanzania Bara Sheria ya Gharama za Uchaguzi inasimamia mienendo ya gharama za uchaguzi kwa wagombea Urais, Wabunge na Madiwani. Kwa upande wa Zanzibar Sheria hii inasimamia wagombea uraisi pamoja na Wabunge.

Msajili wa vyama vya siasa ana jukumu la kusimamia utekelezaji wa sharia ya gharama ya uchaguzi. Baada ya kutoa taarifa ya siku tano, sharia hii inampa msajili wa vyama vya siasa na wawakilishi wake haki ya kukagua vitabu , nyaraka za chama cha siasa, au mgombea kwa ajili ya uchunguzi au kujiridhisha na taarifa za gharama zilizotumika katika uchaguzi.

Kama mgombea unahitaji rasilimali ili kugharamia kampeni yako ya uchaguzi. Mapato haya yanaweza kuja kutokana na fedha zako binafsi, kutoka kwa michango au kutoka kwenye matukio ya kuchangisha fedha. Kabla ya kuanza kuongeza mapato haya, hakikisha umesoma sheria za gharama za uchaguzi ili kuthibitisha nani anaweza na hawezi kuchangia fedha katika kampeni yako. Katika nchi nyingi wagombea wanaweza kupata michango kutoka kwa watu binafsi (wote katika nchi na wanaoishi nje ya nchi), biashara na Azaki. Wagombea wa vyama vya siasa wanaweza pia kutarajia kupokea msaada wa aina mbali mbali kama magari nk, badala ya pesa kutoka kwa chama chao.

Hatua ya 3: Bandika karatasi tatu za bango kitita katika maeneo tofauti tofauti ya chumba cha warsha. Kila bango kitita liwe na kichwa cha habari kama ifuatavyo:

Vyanzo mbali mbali ambavyo mgombea anaweza kujipatia fedha za kampeni (kadi nyekundu)

Matumizi ya rasilimali za kampeni (Kadi ya kijani)

Mbinu za Kuchangisha Fedha (Kadi ya njano)

Page 62: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

59

Hatua ya 4: Gawa vip kadi tatu (3) za rangi tofauti kwa kila mshiriki: Waambie kwamba aandike angalau majibu mawili kwa kila swali hapo juu na kubandika jibu kwenye kila bango kitita yenye kichwa cha habari kinachoendana na rangi ya vip kadi na jibu husika.

Hatua ya 5: Agiza washiriki kusogea kwenye kila bango kitita huku ukisoma majibu pamoja huku ukiendesha majadiliano ya pamoja na washiriki kuboresha majibu waliyoyatoa.

Hatua ya 6: Warudishe washiriki kwenye kundi kubwa na toa hitimisho la mada kwa kutumia maelezo yaliyopo kwenye Kitini Namba 5 E: RASILIMALI ZA KAMPENI

KITINI NA. 5 E: RASILIMALI ZA KAMPENIVyanzo vya fedha za kampeni Fedha ni sehemu muhimu ya kampeni yoyote na fedha inaweza kuja kutoka vyanzo mbalim-bali. Hata hivyo utahitaji kuhakikisha kwamba unazingatia vigezo na sheria zote kuhusiana na wahisani na michango ya kampeni. Hii ina maana kuangalia kabisa unafuata sheria za uchaguzi na pia kuhakikisha una rekodi michango yote na vyanzo vya mapato yako ya kampeni huku ukiweka nakala ya risiti. Vyanzo vyako vya fedha na michango vinaweza kuwa kutoka kwa:

• Vyanzo binafsi

• Ndugu jamaa na marafiki

• Watu binafsi,

• Chama chako

• Wanachama wa chama chako

• Mashirika ya kibiashara na ya kiraia

• Matamasha ya kuchangisha pesa

Unaweza kutumia jedwali hapo chini kurekodi vyanzo vyako vya fedha na kiasi

Chanzo KiasiVyanzo binafsiNdugu jamaa na marafikiWatu binafsiChama chakoWanachama wa chama chakoMashirika ya kibiashara na ya kiraiaMatamasha ya kuchangisha pesa

Jumla

Matumizi ya rasilimali FedhaUtahitaji kutumia fedha ili kuendesha kampeni yako. Kwa kawaida mapato na matumizi yako yatakuwa sawa. Kabla ya kutumia fedha zozote kwenye kampeni yako, jadili bajeti yako ya kampeni na maafisa wa chama chako ili kwamba uwe wazi kabisa juu ya kile ambacho wataku-wa na uwezo kulipa au hawawezi kulipia.

Unaweza kutumia fomu ifuatayo kuorodhesha matumizi ya fedha za kampeni: Kiambatanisho Na 6. Fomu ya kujaza mahitaji na matumizi ya kampeni

Page 63: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

60

Mbinu za Kuchangisha Fedhao Andaa orodha ya watu, vikundi na mashirika yanayoweza kukuchangia

o Fanya mikutano ya ana kwa ana na watu na makundi hayo

o Wapigie simu wale usioweza kuwaona ana kwa ana

o Waeleze malengo yako ya kugombea, unahitaji mchango wa aina gani kutoka kwao, kwa nini wakuchangie na wanaweza kukuchangia wa njia gani.

o Wasikilize na kuwa tayari kupokea ushauri wa aina yeyote ya mchango kutoka kwao

o Timu yako ya kuchangisha pesa za kampeni itume ujumbe wa simu au kupiga simu kufuatilia wale waliokubali kukuchangia

o Weka matangazo ya kuomba michango katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari

o Kuandaa matukio/hafla na harambee za kupata fedha: Huu ni mkakati wa kuandaa tukio kama chakula cha asubuhi, mchana au jioni kwa watu na makundi maalum yenye ushawishi na nguvu za kifedha. Kumbuka: kuwa makini na matukio haya usije ukatumia fedha nyingi kuliko utakazozichangisha

Aina ya Michango Unayoweza Kuomba na Kupokeao Fedha taslimu

o Ujuzi wa mtu/watu au taasisi

o Michango ya kujitolea kwa mfano ofisi kwa ajili ya kampeni, kutoa nakala za ilani, rafiki anayetoa gari kwa ajili ya kusafirisha timu ya kampeni, msaada wa kuchapa vipeperushi au fulana.

Kumbuka: o Kama mgombea tenga muda wa kuwashukuru wote waliochanga kwenye kampeni

yako wewe mwenyewe.

o Sheria inaruhusu kuweka kwenye matangazo yako ya kampeni utambuzi wa wadhamini waliokuchangia.

o Wapo watakao kataa kukuchangia, songa mbele.

o Hakikisha fedha za kampeni zinatumika kwa ajili ya kufikia malengo ya kampeni na si vinginevyo.

Taarifa muhimu zinazohitajika katika sheria ya uchaguziMajina ya timu ya kampeni lazima yapelekwe kwa ajili ya kupata idhini:

o Kwa mgombea wa kiti cha Urais, taarifa hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa

o Kwa Mbunge, taarifa hupelekwa kwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS)

o Kwa diwani, taarifa hupelekwa kwa Mtendaji wa Kata (WEO)

Page 64: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

61

Taarifa ya Gharama Tarajiwa ya Kampeni ya UchaguziKulingana Sheria ya Gharama za Uchaguzi, mgombea anatakiwa kupeleka ripoti ya gharama tarajiwa za uchaguzi ndani ya siku 7 baada ya kuteuliwa.

o Hakikisha malipo ya gharama zote za uchaguzi yana stakabadhi na Ankara inayoelezea taarifa za malipo kutoka mlipaji

o Andaa na peleka taarifa za ya matumizi ya fedha ulizopewa na chama chako ndani ya siku 60. Hii ni kwa wagombea waliopewa fedha na vyama zao za kujikimu kipindi cha uchaguzi.

o Fomu ya kujaza gharama husika hutolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Manispaa, Jiji ambao husambaza kwa makatibu wa vyama vya siasa vya Wilaya.

o Katibu Mkuu wa chama cha siasa (kwa wagombea wa urais), Katibu wa Chama cha siasa ngazi ya Wilaya (kwa wabunge na wagombea wa baraza la udiwani) atatoa vyeti vinavyoonyesha kuwa wagombea wamekamilisha taratibu za gharama za uchaguzi kulingana na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

5.3.8 Kiwango cha juu cha Gharama za Uchaguzi?

o Waziri anayehusika huweka kikomo cha juu cha matumizi ya pesa katika uchaguzi. Kiwango cha juu cha gharama za uchaguzi kitatolewa kwenye chapisho la serikali ikitegemea ukubwa wa jimbo, aina za wagombea, idadi ya watu, mazingira ya mawasiliano.

o Endapo Chama cha siasa au mgombea akitumia pesa za ziada kupita ukomo uliowekwa, atatakiwa kutoa ripoti kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kueleza sababu za matumizi ya fedha kupika ukomo.

o Kwa mwaka 2015 ukomo wa kiwango cha juu cha uchaguzi kilikuwa kama ifuatavyo

Page 65: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

62

Kuwasilisha Taarifa za Gharama za Uchaguzi Baada ya Uchaguzi

o Hakikisha malipo ya gharama zote za uchaguzi yana stakabadhi na ankara inayoelezea taarifa za malipo kutoka kwa mlipaji.

o Mgombea aliepokea fedha za kukimu gharama za uchaguzi kutoka katika chama chake, ndani ya siku 60 baada ya siku ya upigaji kura, anatakiwa kuandaa na kurejesha taarifa ya matumizi ya fedha hizo ndani ya chama chake.

o Kila chama cha siasa kilichodhamini mgombea, ndani ya siku 180 baada ya kupokea ripoti ya mgombea, kitapeleka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa taarifa ya fedha za kampeni ya mgombea.

o Chama kitakachoshindwa kupeleka taarifa za fedha kitatozwa faini na kuwekewa kikwazo kushiriki uchaguzi unaofuata.

Kumbuka: Haijalishi kama umeshinda au umepoteza uchaguzi, ripoti ya fedha ni lazima iandaliwe na iwasilishwe la sivyo sheria itachukua mkondo wake.

Makosa na Adhabu Ndani ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi

o Ni kosa kwa mtu yeyote kutoa rushwa kabla au wakati wa mchakato wa uteuzi mfano kutoa pesa au kulipia garama za chakula, vinywaji, burudani kwa ajili ya kushawishi kupiga kura au kutopiga kura.

o Usimtishie mtu yeyote atayetaka kumchangia mgombea yeyote: Mtu yoyote atakaetishia kutumia nguvu au vurugu, kuumiza, kudhuru au mtu yeyote ambaye ametoa au amekusudia kutoa fedha yoyote kwa mgombea, kwa familia atakuwa ametenda kosa.

o Mgombea au chama kikishiriki kwenye vitendo vilivyokatazwa na hii sheria kutapelekea chama kufungiwa kushiriki uchaguzi

o Kumbuka: Mgombea hatafungiwa kwa kosa lililofanywa na chama bila idhini yake au bila yeye kujua

HitimishoKatika mada hii tumejifunza kuhusu gharama za kampeni ya uchaguzi. Tumeona namna ambavyo Sheria ya Gharama za Uchaguzi 2010 kama ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2015 imelenga kuratibu na kuzuia matumizi mabaya ya fedha wakati wa mchakato wa uchaguzi pamoja na uteuzi wa wagombea, wakati wa kampeni na kipindi cha kupiga kura ili kuweka mazingira ya haki kwa vyama vyote na wagombeaji. Tumeweza kuona jinsi maandalizi ya bajeti yanavyofanyika, vyanzo vyake na kuyatambua makundi tofauti ambayo yanaweza kuchangia katika kampeni. Tumeangazia mbinu tofauti za kuchanga fedha na namna mgombea anahusika katika uchangishaji. Tumeweza kujifunza juu ya taarifa zinazohitajika katika sheria ya uchaguzi bila kusahau namna ya kuwasilisha taarifa hizo baada ya uchaguzi kumalizika.

SOMO LA SABA: SIKU YA UCHAGUZI

Lengo ya SomoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza;

• Kujua mambo muhimu yakuzingatia siku ya uchaguzi

Muda: Dakika 30

Page 66: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

63

VifaaKitini cha mshiriki namba 5 F: Siku ya uchaguzi

Kiongozi cha mwezeshaji

Mbinu Bungua bongo

Muhadhara

Hatua Hatua ya 1: Anza kwa kueleza kwamba kazi ya kampeni na uchaguzi haiishi siku moja kabla ya kupiga kura bali huenda hata mbele zaidi baada ya kupiga kura.

Hatua ya 2: Tumia kitini Na. 5 F kutoa muhadhara juu ya mambo muhimu ya kuzingatia siku ya uchaguzi

KITINI NA. 5 F SIKU YA UCHAGUZIKumbuka kwamba umeandaa siku hii kwa miezi, wakati mwingine kwa miaka. Ni siku ya uchaguzi, siku ambayo unajua kama umechaguliwa kuwakilisha watu wako walio kuamini au umeshindwa ili kujipanga kwa muda mwingine: Unaweza kufikiri kuwa huu ni mwisho wa barabara, lakini bado kuna mengi ya kufanywa siku ya uchaguzi na siku chache baada ya siku ya kupiga kura.

a) Kulinda Kura zakoWanasiasa wengi wamelalamikia mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania. Moja ya ukosoaji

ni kwamba haina usalama wa kura zilizopigwa na watu.

Ulifanya kazi ngumu sana kuwashawishi watu juu ya uwezo wako na kwa nini wakuchague hivyo unahitaji kulinda kura zako ili kupata picha kamili ni kipi ungeongeza zaidi au kipi umefanikiwa zaidi.

Ili kuwa na macho na masikio katika upigaji kura, unahitaji kutegemea “mawakala wa kura”

Mawakala wa kuraMawakala wa upigaji kura ni sehemu ya Tume ya uchaguzi ya jimbo lako kwa niaba ya

chama chako.

Jukumu lao ni kushiriki shughuli zote kwa niaba ya chama katika siku ya uchaguzi, na kuhakikisha kwamba upigaji kura unaendelea katika misingi ya sheria.

Kwa kawaida wanafanya kazi kwa misingi ya kujitolea, lakini unaweza kuhitajika kugharamia malipo ya chakula na usafiri katika siku ya uchaguzi.

Ili mawakala wako wanaokusimamia kura wawe na ufanisi katika uchaguzi unapaswa kuwapa mafunzo yafuatayo:

Kuwafahamisha sheria zinazosimamia uchaguzi Tanzania ili kuepuka wao kuvunja sheria na kutolewa kwenye vituo ikakusababishia kukosa ulinzi wa kura zako

Kuwafundisha wadau muhimu wakati wa uchaguzi ikiwemo viongozi wa uchaguzi eneo hilo ili kuepuka kurubuniwa na watu watakaojitambulisha kuwa viongozi wa uchaguzi bila wao kuwajua

Page 67: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

64

Kuwafundisha hatua za uchaguzi kuanzia siku inaanza mpaka matokeo yanatangazwa na pia wajue majukumu yao siku hiyo.

Kuwafundisha changamoto ambazo wanaweza kupitia na jinsi ya kuzitatua watakapokutana nazo.

Kuwafundisha jinsi ya kukusanya taarifa ya za uchaguzi, ili uweze kufuatilia na kuweka takwimu zako vizuri kuhusu uendeshaji wa zoezi katika eneo la uchaguzi. Hii inaweza pia kuwa njia nzuri ya kupima chama chako ili kuweza kuboresha baadae.

Kutoa taarifa iwapo kuna vitu utaona haviendi sawaNi vyema pia kama mgombea kuwaeleza mawakala wako kwamba kuna fomu maalumu za kutolea taarifa hata wakati mchakato wa kupiga kura unaendelea. Fomu hizi zinaweza zisiwepo za kutosha kwenye kituo cha kupigia kura. Hivyo, ni vyema kuzitafuta kabla ya siku ya kupiga kura kuwa nazo ili kuzitumia kutoa taarifa pale anapoona zoezi linaenda kinyume na sheria au taratibu zilizowekwa.

Baada ya siku ya uchaguziBaada ya uchaguzi, unahitaji kualika timu yako kwa zoezi la kutathmini. Hii itakusaidia wewe kutambua

Wapi mlifanya kazi vizuri?

Wapi hamkufanya kazi vizuri?

Tunaweza kufanya nini ili kufanya kazi vizuri na kuwa na matokeo bora zaidi katika miaka 5?

Pia ni fursa ya kuwashukuru kila mmoja wao kwa msaada wao.

Page 68: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

65

UKATILI WA DHIDI YA WANAWAKE KIPINDI CHA UCHAGUZI

Utangulizi Moduli hii inalenga kutoa elimu juu ya ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi. Ukatili wa kijinsia kwa miaka mingi umekua ni moja ya sababu kubwa ya wanawake kutoshiriki kikamilifu kwa kuhofia maswala mbali mbali ya ukatili yanayoweza kujitokeza kipindi cha uchaguzi. Hivyo moduli hii inalenga kuwapa washiriki uelewa juu ya maswala la ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi na jinsi ya kukabiliana nayo.

SOMO LA KWANZA: KUPIGA KURA KWA MIGUU YETU.

Lengo mahususi• Kuwawezesha washiriki kufikiria kuhusu ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi

kabla ya kujadili mada hii.

Muda: Dakika 15:

Vifaa: • Saini tatu zilizoandikwa Nakubali, Nakataa na Sina uhakika (Kitini Namba 6 A)

HatuaHatua ya 1: Anza kwa kuelezea kwamba katika moduli hii tutajifunza kuhusu ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi. Lakini kabla ya kuanza moduli, hebu tufanye zoezi fupi la kuchangamsha.

Hatua ya 2: Soma seti ya maelezo na uwaulize washiriki ikiwa anakubaliana, hakubaliani au hana uhakika. Waulize washiriki kusogea karibu. Ikiwa wanakubaliana na maelezo , wasogee na kusimama chini ya seti ya neno nakubaliana, ikiwa hawakubaliani na seti ya maelezo basi wasimame chini ya seti ya neno Sikubaliani, na kama hawana hakika basi wasimame chini ya seti ya neno sina hakika.

Seti ya maelezo ni:

• Wanaume wote husababisha ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi

• Ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi ni jambo dogo na la kawaida na haliathiri watu wengi

• Mila mbaya za mfumo dume zinahamasisha ukatili kama njia ya kuendelea kubakiza madaraka kwa wanaume?

• Wagombea wanawake, wapiga kura wanawake, wafuasi wa kisiasa wanawake, na wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kuwa waathirika wa ukatili wa kijinsia?

• Wanawake walio na madaraka ya kisiasa hawawezi kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia

MODULI YASITA

Page 69: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

66

• Watu katika timu yako ya kampeni wanaweza kuwa chanzo cha ukatili

• Unyanyasaji wa kingono wakati wa uchaguzi sio ukatili

• Wagombea wanawake hujisababishia wenyewe ukatili wa kijinsia

Hatua ya 4: Kwa kila seti ya maelezo Sitisha kidogo na kisha uliza washiriki kwa nini wanakubaliana, hawakubaliani, au hawana uhakika. Jikite zaidi kwa washiriki ambao majibu yao ni tofauti na wengi. Waulize kwa ufafanuzi kwa nini walichagua kusimama ambapo walifanya.

Hatua ya 3: Fanya muhtasari kwamba zoezi hili ni kwa ajili tu ya kuchangamsha washiriki ili kuanza kujifunza Ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi.

SOMO LA PILI: DHANA YA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE KWENYE UCHAGUZI

Malengo ya somoMwisho wa somo hili, washiriki wataweza

• Kuelewa aina za ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi

• Kuelewa uhusiano kati ya ukatili dhidi ya wanawake na ukosefu wa mamlaka

Muda: Dakika 60: Vifaa:

• Bango kitita

• Kalamu Rashasha

• Kitini cha mshiriki namba 6

Mbinu:• Bungua bongo

HatuaHatua ya 1: Waambie washiriki wafikirie kimya kwa muda kuhusu kile wanachoelewa kuhusu “Ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi” na kisha kuwaalika kushirikisha mawazo yao kwa darasa zima. Andika majibu kwenye bango kitita.

Hatua ya 2: Jadili baadhi ya pointi za kawaida na za kipekee katika majibu yao. Sema kwamba hakuna makubaliano bado kufafanua nini maana ya ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi. Umoja wa mataifa unatafsiri rasmi ya Ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi

Hatua ya 3: Soma maana ya ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi kama ilivyoelezwa kwenye jedwali hapo chini na iandike kwenye bango kitita na itundike au kuibandika ukutani

Ukatili Dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi: Ni aina ya ukatili dhidi ya wanawake ambao lengo ni kuathiri upatikanaji wa haki ya kisiasa kwa wanawake katika mazingira ya uchaguzi. Hii inajumuisha athari juu ya ushiriki wa wanawake kama wagombea, wapiga kura, wanaharakati, wafuasi wa vyama, waangalizi, wafanyakazi wa uchaguzi, au viongozi wa kisiasa.

Hatua ya 4: Waulize washiriki kama wana maswali kuhusu maelezo haya. Waulize washiriki ni aina ngapi za ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi wanazoweza kuzifikiria. Kisha majibu yanapaswa kuwa na muhtasari katika aina nne kama ifuatavyo:

Page 70: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

67

Ukatili wa kimwili

Ukatili za kisaikolojia

Ukatili wa kingono

Ukatili wa kiuchumi

Hatua ya 5: Waulize washiriki kuchangia mawazo yao katika mambo mawili: (a) Ni maeneo gani ukatili dhidi ya wanawake unaweza kutokea kwenye uchaguzi, na (b) Nani anaweza kufanya ukatili dhidi ya wanawake kipindi cha uchaguzi

Hatua ya 6: Tumia maelezo ya kitini Na 6: kutoa ufafanuzi na kuhitimisha somo hili.

KITINI NAMBA 6: UKATILI DHIDI YA WANAWAKE KIPINDI CHA UCHAGUZIWanawake wanaweza kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kipindi cha uchaguzi katika nafasi mbali mbali ikiwemo kama wagombea, wafuasi wa vyama, wapiga kura na wanafamilia wa wagombea. Wakosaji wanaweza kuwa ama kisiasa, jamii au mtu binafsi. Kila mojawapo ya vipimo hivi itashughulikiwa katika sehemu hii

Ni muhimu pia kutambua kwamba wakati wanawake na wanaume wanaweza kupata ukatili kwenye uchaguzi, ukatili huu unakua na athari kubwa kwa wanawake kwa sababu kwa miaka mingi wanawake wamekua katika nafasi za chini katika jamii na kuna uwezekano mkubwa wa mashambulizi ya matendo ya ukatili dhidi yao.

Ukatili wa jumla kwenye uchaguzi dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi

Wanaume na wanawake wanaweza kuwa waathirika wa ukatili kwenye uchaguzi kama vile mauaji, unyanyasaji, na kulazimishwa. Hata hivyo, ufafanuzi wa jadi haujabeba dhana za vitendo vya ziada na vitisho vinavyolenga wagombea wanawake, wanaharakati, wapiga kura, na wafanyakazi wa uchaguzi kwa sababu wao ni wanawake.

Kanuni za kijamii na za kimila kuhusu muundo wa jinsia, hutoa mwanya kwa nini wanawake ni walengwa wa ukatili kwenye uchaguzi, pamoja na aina gani za matendo ya kikatili ili kupunguza au kuathiri ushiriki wao. »

Tofauti na wanaume, wanawake wanapata vitisho toka ngazi ya kifamila au vitisho vya kijamii katika nafasi binafsi, kama vile nyumbani, vitisho kutoka kwa wanachama na viongozi wa chama chao cha kisiasa. Lengo la ukatili kama hizo linaweza kuwa na lengo moja katika kuimarisha wajibu wa wanawake wa kimila, kuharibu ufanisi wa wanawake katika siasa au kudhibiti ushiriki wao.

Mambo ambayo huchangia Ukatili dhidi ya wanawake

Mambo ambayo huchangia ukatili dhidi ya wanwake kwenye uchaguzi hutofautiana kati ya mikoa na nchi, lakini inaweza kujumuisha:

Kupinga uongozi kwa wanawake

Utegemezi wa kiuchumi wa wanawake

Kutojua kusoma na kuandika

Usaidizi wa familia au mzigo wao wa majukumu nyumbani

Ukosefu wa elimu au upatikanaji wa elimu duni

Ukosefu wa kupata habari sahihi kwa muda sahihi

Tabia za kijamii na kitamaduni, utamaduni wa jamii wa ukatili au kutoadhibiwa (hasa ukatili wa kisiasa)

Kukosekana kwa miundo saidizi ya utawala na mahakama , pamoja na utawala duni wa taasisi za sheria na utawala.

Page 71: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

68

Aina za Ukatili

Ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi unaweza kuwekwa katika makundi matano makuu: kimwili, kingono, kisaikolojia, vitisho na kulazimishwa, na kiuchumi. Jedwali lifuatalo linaonyesha njia ambazo ukatili unaweza kutokea katika maisha ya mwanamke kwa umma na binafsi, katika ngazi zote za jamii na kuathiri uwezo wa wanawake kushiriki katika uchaguzi kama wagombea, wapigakura, maafisa wa uchaguzi, waangalizi, walinzi wa uchaguzi au wanaharakati.

Aina za ukatili Wapi hutokea, Waathirika, Wahusika MalengoUkatili wa Kimwili:

(mauaji, mashambulizi, utekaji nyara)

Ngazi ya chini ya ardhi au nyumbani; katika jamii za kijamii na za kisiasa

viongozi wanawake na wanaharakati; wapiga kura wanawake, wagombea au maafisa wa uchaguzi

Upinzani au wanachama wa chama chako mwenyewe, mashirika, wanafamilia au jamii, vikosi vya usalama

Kushinda migogoro ya ndani ya chama, kuendeleza kudidimiza hali ya wajibu wa wanawake katika jamii

Ukatili wa kingono:

(ubakaji au unyanyasaji wa kingono), Rushwa ya ngono)

Faragha au katika hali ya siri.

Wakati ukiwa umebanwa kisiasa, nyumbani au katika chama cha siasa,

Wanaharakati wanawake, wapiga kura, wagombea au wanachama, Maofisa wa uchaguzi

vikosi vya usalama,

Vikosi vya wanajeshi, Wapinzani wa kiume,

wanandoa wakiume au wanafamilia

Kuzuia au kudhibiti ushiriki wa wanawake kisiasa kama kama wagombea au wasimamizi; kuwalazimisha wanawake kupiga kura kwa mgombea yeyote anayependelewa

Ukatili wa kisaikolojia: (Kashfa na matusi, mashambulizi ya tabia, unyanyasaji (ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari), matusi ya chuki, hotuba za chuki, kuhusisha wanawake viongozi na uasherati

Katika vyombo vya habari kitaifa au

Katika mitandao ya kijamii;

katika ngazi ya jamii; ndani ya nyumba au chama cha kisiasa katika mchakato wa uteuzi au kampeni

Wanawake wagombea, wapiga kura, wanaharakati au maofisa wa uchaguzi

Vyama vya upinzani

Wanachama wa chama chako

Viongozi wanaume, jamii, familia na wanahabari

Kuzuia na kudhibiti mwanamke asichaguliwe na kupunguza ushiriki wao kikamilifu kuendeleza mfumo dume

Ukatili wa vitisho na kulazimishwa (

Kwenye vituo vya polisi

Mabaraza ya vyama,

Kamati za maamuzi, ofisini, kwenye jamii

Wanawake wagombea, wapiga kura, wanaharakati au maofisa wa uchaguzi,

Viongozi wa chama na wanachama

Viongozi au wanachama wa vyama vya upinzani

Wanachama wa chama chako, polisi,

,jamii, familia na wanahabari

Ili kuzuia au kudhibiti wanawake kugombea kwenye uchaguzi, kuchukua ofisi, kupiga kura au kushiriki katika usimamizi wa uchaguzi,

Ukatili wa Kiuchumi

Kwa umma, Kwenye vyama, kipindi cha kuteua wagombea, kwenye kampeni, nyumbani

Wanawake wagombea, wapiga kura, wanaharakati au maofisa wa uchaguzi,

Viongozi wa chama na wanachama

Viongozi au wanachama wa chama chako, wasimamizi wa uchaguzi, familia au wanajamii

Kuzuia wanawake kutumia rasilimali zilizopo ili kuwazuia kushiriki katika siasa.

Page 72: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

69

Madhara ya Ukatili wa Kijinsia Kwenye Siasa

1. Ukatili wa dhidi ya wanawake kwenye siasa ni ukiukwaji wa haki za binadamu,

2. Unazuia na kuogopesha wanawake kushiriki kwenye siasa/kufurahia haki ya ushiriki kwenye siasa.

3. Unarudisha nyuma mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia sanasana ukatili dhidi ya wanawake.

4. Unadunisha utu na hadhi ya mwanamke-wale walioamua kushiriki kwenye siasa hutafsiriwa kama watu wasio na tabia njema.

5. Ukatili wakati wa uchaguzi hauathiri wanawake pekee bali unaathiri uhalali wa mchakato wa uchaguzi pamoja na nia ya serikali kuhakikisha uchaguzi shirikishi.

6. Huwafanya wanawake kutegemea zaidi nafasi za kuteuliwa /viti maalumu kuliko nafasi za ushindani/kugombea.

7. Huwakatisha moyo wanawake na wasichana wengine kuingia katika siasa.

8. Huzuia watu kwenda kupiga kura. Nusu ya wapiga kura wanawake waliohojiwa baada ya uchaguzi (53%) kupitia utafiti wa TWCP walisema hawajapiga kura kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya kuhofia ukatili na kutokuamua kwenda kupiga kura kwa sababu za kiusalama.

Mbinu za Kuepuka Ukatili wa Kijinsia wakati wa Kampeni

1. Fuata utaratibu wa kugombea wa ndani ya chama chako kama zinavyo oneshwa katika kanuni za vyama. Usitegemee upendeleo

2. Usifanye mazoea na viongozi wa vyama na wafuasi zaidi ya mazoea yanayohitajika katika kutekeleza majukumu ya kiofisi.

3. Jinoe kimaarifa ili kuonesha uwezo usiokuwa na mashaka ili kujiweka mbali na mazingira ya rushwa na vitendo vya ukatili.

4. Jipambanue kimsimamo ili kutuma ujumbe wa wazi kwa wale wanaodhani utakuwa rahisi kuingia katika mitego ya rushwa ya ngono.

5. Kemea vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono ndani na nje ya chama na kuripoti kwenye mamlaka husika. Epuka Ukimya.

6. Toa elimu kwa wanawake wenzako ndani ya vyama vya siasa wasiweze kuvumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono. Watoe taarifa na kuhakisha washukiwa wanatiwa nguvuni

7. Tunza kama ushahidi viashiria vyote vya kuombwa rushwa ya fedha na ngono kutoka kwa viongozi wa vyama au vinginevyo-utavihitaji kama ukiamua kupeleka kesi mahakamani.

Kama mgombea shawishi chama chako kufanya yafuatayo ili kuzuia ukatili wa kijinsia /Rushwa ya ngono.

o Kuchukua hatua za kitaasisi na kuwa na sera zenye uvumilivu (SIFURI) katika vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani na nje ya chama, ikiwemo ukatili wa kingono sambamba na kudhibiti vitendo vya rushwa ya fedha na ngono.

Page 73: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

70

o Kutoa elimu kwa wafuasi wake kuhusu kutofanya vitendo vya ukatili kwa wagombea wa vyama vingine.

o Kutoa elimu kwa kamati inayohusika na kuchuja na kupitisha wagombea kubaini kama wagombea wamekiuka misingi ya kijinsia au wamejihusisha na rushwa za ngono au fedha.

o Kuwepo na utaratibu wa kuwezesha mazingira rafiki kwa wanawake katika vyama kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia /rushwa ya ngono kwa uongozi wa chama na katika vyombo vya usalama.

o Chama kutoa msaada wa huduma ya kisaikolojia kwa waathirika wa rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia katika siasa.

o Kuwafunza na kuwahamasisha wanawake kuvunja utamaduni wa kuwa kimya/ kushindwa kuzungumzia vitendo vya ukatili vinavyo wakabili hususani kwa ukatili unaoleta madhara yasiyoonekana.

Hitimisho

Kwenye mada hii tumejifunza nafasi ya mgombea katika kutekeleza jukumu la ulinzi na Usalama kipindii wa uchaguzi, tumeweza kuona majukumu ya vyombo Vya ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi. Pia tumeangalia suasa la ukatili wa kijinsia wakati wa Kampeni, madhara yake pamoja na mbinu za kuepuka.

Hatua ya 7: Mchezo wa Kuigiza: Wagawe washiriki katika vikundi vitano. Elezea kwamba kila kundi litaulizwa kuja na jukumu la kuonesha aina za ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi katika mazingira tofauti ya uchaguzi. Kila kundi litakuwa na dakika za 5 za kuonesha igizo lao. Hapa chini ni majukumu matano ya makundi kutengeneza igizo lao la ukatili dhidi ya wanawake.

i. Kikundi 1: Ukatili wa kingono ndani ya chama

ii. Kikindi 2: Ukatili wa kimwili wakati wa kampeni

iii. Kikundi 3: Ukatili wa kiuchumi nyumbani.

iv. Kikundi 4: Ukatili unaofanywa na vyombo vya dola na usalama

v. Kikundi 5: Ukatili unaofanywa na chama pinzani

Hatua ya 2: Wape dakika 20 kwa washiriki kuandaa igizo lao. Baada ya dakika 20, uliza kila kikundi, mmoja baada ya mwingine, kufanya kazi yao ya kuigiza.

Hatua ya 3: Baada ya kila jukumu la kuigiza, uliza maswali yafuatayo ya kundi zima:

• Ni aina gani ya ukatili mlizoonesha kwenye igizo, nani aliathirika na ukatili huo, nani aliyefanya ukatili huo?

• Ni aina gani ya haki ya mwanamke ya kisiasa imepokonywa kwenye igizo lenu?

• Unafikiri ni nini matokeo ya kunyima haki hiyo mwanamke kwenye igizo lenu?

• Nini kifanyike kutokomeza aina hii ya ukatili?

Hatua ya 4: Baada ya vikundi vyote kutekeleza jukumu lao la kuigiza na kujibu maswali, fanya muhtasari kwa kutumia jedwali hapo chini:

Page 74: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

71

Wasimamizi na waangalizi wa uchaguzi wanaweza kuwa na majukumu katika kuhakikisha wanarekodi, kupunguza na kutathmini athari za ukatili dhidi ya wanawake kwenye uchaguzi. Baadhi ya hatua muhimu na lazima wazingatie yaliyo orodheshwa hapa chini.

Kabla ya uchaguzi• Mamlaka za serikali, asasi za kiraia na wadau wengine wa uangalizi wa uchaguzi

wanapaswa kuwatambua na kutengeneza mtandao wa wadau kabla ya uchunguzi:

Baadhi ya wadau hawa wanapaswa kuwa watoa taarifa juu ya ushiriki wa wanawake katika siasa pamoja na ukatili dhidi ya wanawake, ambao utasaidia serikali kutengeneza miundo ya ulinzi wa mwanamke pamoja na mbinu za kutokomeza ukatili huo

Wadau wengine wanapaswa kulengwa hasa kwa uwezo wao wa kushughulikia na kutoa huduma katika maswala ya ukatili wa wanawake kipindi cha uchaguzi. Wadau hawa wanaweza kujumuisha mamlaka za eneo hilo au viongozi wa jamii hizo, na vikosi vya usalama kama vile polisi, vyama vya kisiasa au mashirika ya kusimamia uchaguzi

• Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na maswala ya wanawake na unyanyasaji wa kijinsia yanapaswa kuhusishwa ili kusaidia kutambua wadau muhimu ambao tayari wanashiriki katika maswala hayo ili kurahisisha ukusanyaji taarifa, mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili huo.

• Inaweza kuwa muhimu kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama, wafanyakazi wa uchaguzi au maofisa wa kuchaguliwa, au vikundi vinavyojikita katika huduma za waathirika au watoa huduma wengine wa jamii ili kuelewa na kushughulikia changamoto za usalama au hali kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake.

Wakati ya uchaguzi• Kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wanawake waathirika wa ukatili ikiwa ni pamoja

na kushtakiwa kwa uhalifu huo.

• Kuanzisha mbinu za kutoa taarifa za kesi za ukatili kwa usalama na kuripoti kwa siri.

Baada ya uchaguzi• Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na sera kupinga ukatili dhidi ya wanawake

• kuhakiki sheria na sera na kufanya marekebisho kama inavyohitajika ili kuzuia ukatili wa kijinsia kwenye chaguzi zinazofuata

• Kesi za ukatili wa kijinsia zilizotokea kipindi cha uchaguzi zitolewe hukumu mapema na haki ipatikane

• Kushtakiwa kwa wahusika wa ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wanawake katika siasa

Page 75: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

72

USALAMA WA KIDIJITALI NA MITANDAO KWA WAGOMBEA WANAWAKE

Utangulizi. Kwa miaka ya hivi karibuni matumizi ya vifaa vya elektronic kama kompyuta, simu na vifaa vingine umeongezeka, hivyo kuongeza matumizi ya mitandao ya kijamii kwa asilimia kubwa. Mara nyingi tumekutana na kesi nyingi za mtu kupoteza vifaa hivyo au kuibiwa au muda mwingine kuona mtu akichafuliwa kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo kama mgombea mwanamke unahitaji kujua usalama wako kwenye ulimwengu wa kidijitali. Moduli hii inafundisha usalama wa kidijitali na katika mitandao ya kijamii.

SOMO LA KWANZA: ULINZI WA KIDIJITALI NA KIMTANDAO

Malengo MahususiMwisho wa somo hili washiriki wataweza;

• Kutoa fasili ya usalama wa kidijitali na usalama wa taarifa muhimu • Kuelewa umuhimu wa kuchukua hatua za usalama kama wagombea wa kisiasa• Kutengeneza na kuhifadhi nywila thabiti kwa usalama wa taarifa zake za siri • Jinsi ya kujilinda kwenye mitandao ya kijamii

VifaaKitini cha mshirikiKaratasi zilizo na kisa mkasa Bango kititaKalamu rashasha

Mbinu• Kisa mkasa

• Mazoezi ya mtu moja moja

HatuaHatua ya 1: Anza kwa kueleza malengo ya somo hili la ulinzi wa kidijitali. Tumia kisanduku hapo chini kutambulisha somo hili.

Kila mtu anayetumia kompyuta au kifaa chochote cha kidijitali kama simu anahitaji kuelewa jinsi ya kuweka taarifa zake katika hali ya usalama. Hasa kwa wagombea wa kisiasa ambao mara nyingi wapinzani wako watatamani kupata taarifa zako za siri ili waweze kuzitumia dhidi yako wakati wa kampeni na hata wakati wa uteuzi ndani ya chama.

MODULI YASABA

Page 76: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

73

Hatua ya 2: Omba mshiriki mmoja kujitolea kusoma kisa mkasa cha Bi. Mujuni Mujuni Haikisha kwamba wakati mshiriki anasoma kisa mkasa umegawa kopi moja moja ya kisa hicho kwa kila mshiriki.

Hatua ya 3: Baada ya kumaliza kusoma kisa cha Bi. Mujuni Mujuni waelekeze washirki kutathimini kisa hicho huku wakijibu maswali yafuatayo: (Nakili majibu yao kwenye bango kitita)

• Je, umejifunza nini katika kisa hiki?

• Ni nini kinaweza kutokea kwenye vifaa vya Bi. Mujuni Mujuni wakati vilipokua kwenye mikono ya vyombo vya usalama.

• Kuna madhara gani kwa Bi. Mujuni Mujuni kwa maafisa wa usalama kukaa na vifaa hivyo hata kwa muda mfupi?

• Ni kwa nini unafikiri Bi: Mujuni Mujuni alipata wasiwasi?

• Je, angeweza kufanya nini kabla ya kusafiri ili kuhakikisha kama hali kama hii ikitokea hangeweza kuwa na wasiwasi sana?

Kisa cha Bi. Mujuni MujuniBi. Mujuni Mujuni ni kiongozi mwaandamizi wa chama cha siasa na pia ni mtetezi wa haki za wanawake hapa Tanzania. Bi. Mujuni Mujuni ni mgombea wa kiti cha ubunge katika jimbo la kusadikika. Siku moja Bi.Mujuni alipokea simu kutoka nje ya nchi kwamba kuna watu walitamani kumsaidia fedha kwa ajili ya ghrama za uchaguzi hivyo anapaswa kusafiri na ndege siku nne zijazo kwenda nchini Namtumbo huku barani ulaya. Anaenda kuwasilisha budget yake ya kampeni, majina na wasifu wa timu yake ya kampeni, taarifa zake binafsi pamoja na familia yake na ripoti ya utafiti juu ya hali ya wanawake nchini Tanzania. Bi. Mujuni mujuni aliondoka na baadhi ya vifaa vyake ikiwa ni pamoja na simu yake ya mkononi, kompyuta, na Flash ambayo ina nyaraka zote zilizotajwa hapo juu.

Bi. Mujuni Mujuni alikua akisafiri peke yake, na wakati anaelekea kwenye uwanja wa ndege alipofika karibu na wanakagulia mizigo walikuja maafisa wawili ambao hawakujitambulisha na kumuuliza kama anavifaa vyovyote vya kidijitali. Bi. Mujuni alishangazwa na tukio hilo na kwakua alikua hajui vifaa vya kidijitali ni nini aliwajibu hapana sina vifaa hivyo. Maafisa wakamuamuru kuweka mfuko wake kwa njia ya scanner x-ray na kugundua USB flash drive, simu ya mkononi na kompyuta katika mfuko wake kisha wakachukua vifaa hivyo

Baaada ya kuchukua vifaa hivyo wakamuomba asubiri, na wao kutoweka navyo ofisini kwa muda wa dakika kumi na tano, wakarudi na kumpatia vifaa vyake huku wakimtakia safari njema. Bi. Mujuni Mujuni ana hofu wakati yuko kwenye ndege, wasiwasi kuhusu kile kilichotokea kwa vifaa vyake na je vipi kuhusu taarifa zake.

Hatua ya 4: Toa muhtasari wa majadiliano, toa umuhimu wa haja ya wanawake wanaogombea na watetezi wa haki za wanawake kufahamu maswala ya usalama wao katika shughuli zao za kisiasa. (Unaweza kutumia kijedwali hapo chini)

Page 77: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

74

Ni muhimu kama mwanamke anayegombea kuwa na mpango wa usalama juu ya taarifa zako ambazo unahifadhi kwenye vifaa vyako kama kompyuta, simu ya mkononi, na hata vifaa kama flash nk.

• Uelewa bora wa maswala ya kidijitali unakuwezesha wewe kuweka mipango bora ya usalama wako

• Ufahamu mkubwa juu usalama wa kidijitali utakufanya uewele viashiria mbali mbali ambavyo vinaweza kusababisha hatari kwenye usalama wako

• Kuna madhara makubwa endapo mtu asiyepaswa kuwa na taarifa zako atazipata kwa mfano;

• Kuanza kutengeneza upya taarifa ulizopoteza • Taarifa zako zinaweza kupotezwa au kuharibiwa • Kupoteza wafanyakazi au kupoteza imani kwa umma kama taarifa zitakua hazifai

kutoka kwa umma • Unaweza kupata adhabu kutoka kwenye chama chako kama umevujisha siri za

chama • Taarifa zinaweza kukutia aibu, kukudhalilisha au hata kupoteza wafuasi kwenye

chama chako.

Hatua ya 5: Katika makundi ya watu wawili wawili waambie washiriki wafikirie sasa Bi. Mujuni Mjuni anataka kusafiri tena kwa mara ya pili miezi miwili baadae na amekuja kwao kuomba ushauri juu ya kuhakikisha usalama wake endepo vifaa vyake hivyo vitachukuliwa tena. Unaweza kutoa vidokezo Kama:

• Je, anapaswa kufikiria kufanya nini kuhusu vifaa vyake?

• Je, yeye anapaswa kufikiria nini ili kujiweka salama zaidi?

• Je, anapaswa kuzingatia nini kuhusu taarifa alizobeba?

Hatua ya 6: Kusanya vikaratasi hivyo na usome majibu yao mbele ya darasa huku ukiendeleza mjadala juu ya jinsi ya kuhakikisha usalama wa kidijitali kwa wagombea wanawake (Tumia Kitini Namba 7. Njia sahihi za kujilinda kidijidali)

KITINI NAMBA 7 NJIA SAHIHI ZA KUJILINDA KIDIJIDALI

Kabla ya kujua jinsi ya kulinda taarifa zako ni lazima kujua ni mazoea gani mazuri ya kutumia vifaa vyako kama kompyuta, simu na vifaa vingine vya kuhifadhia taarifa

a) Usiweke taarifa za siri kwenye vifaa vya kubebeka kama computer, simu na flash. Ni rahisi sana kujisahau na kumuazima mtu kifaa hicho na akapata taarifa izo bila wewe kujua (Hebu fikiria mpinzani wako apate taarifa zako za siri za mkakati wako wa kampeni, nini kitatokea?)

b) Hifadhi taarifa zako mahali tofauti tofauti. Fanya zoezi hili kuwa kazi ya kawaida, walau angalau mara moja kwa siku. Hifadhi taarifa hizi kwenye vifaa kama flash, CD nk na hakikisha vifaa hivi vinakaa mbali na ulipo. Usiweke taarifa zako sambamba na komputa yako. Data chelezo ya midia chomekezi kama vile diski kuu ya kubebeka.

Page 78: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

75

c) Tumia nywila (Neno la siri ) zenye nguvu ambazo haziwezi kubadilishwa au kuhisiwa kwa urahisi kuwakinga. Hakikisha unazilinda, hauziandiki popote na hamshirikishi mtu yoyote neno lako la siri.

d) Hakikisha kuwa kompyuta yako ina program za kupambana na virusi, kupambana na vitishio vingine vya kompyta.

e) Usisakinishe programu zisizojulikana au ambazo hazijulikani vyanzo vyake. f) Matumizi salama ya Barua pepe. Usifungue au kujibu barua pepe usizozijua chanzo

chake. Usifungue viambatisho vya barua pepe au kubofya kwenye anwani za tovuti inayotumwa kwenye barua pepe bila kujua chanzo chake.

Hatua ya 7: Zoezi: Anza kuwaambia washiriki kwamba tutaenda kutengeneza pamoja neno la siri lenye nguvu ambalo haliwezi kubadilishwa au kuhisiwa kwa urahisi ili kuhakikisha kwamba kama mgombea unalinda taarifa zako. Tumia maelezo kwenye jedwali hapo chini kuwaeleza sifa za neno la siri bora.

Neno la siri (Nywila) Ni namba au kikundi cha maneno ambacho mwenye nacho anakitumia ili kuweza kuingia na kutumia kifaa akaunti binafsi ya mtu. Imekua mazoea kwa watu wengi kutumia neno la siri kama miaka yao ya kuzaliwa, tarehe za kuzaliwa watoto wao au wazazi, au tarehe za harusi au ndoa zao. Ni rahisi sana kwa mtu mwenye nia ya kupata taarifa zako kuhisi neno la siri la aina hiyo. Wengine hutumia neno la siri moja kwenye kila kitu anachomiliki kwa mfano benki, barua pepe, mitandao ya kijamii, simu, nk. Ni rahisi sana endepo mtu atafanikiwa kupata neno lako la siri kuhatarisha usalama wako katika maeneo yote unayotumia neno hilo la siri. Zifuatazo ni dondoo za neno imara la siri:

Usitumie namba, neno au maneno yenye umuhimu maalum kwako — kama mwana wa kuzaliwa nk. Hiyo ni aina ya neno la siri ambalo linaweza kugunduliwa na mtu kufanya udukuzi: Unaweza kutumia maneno ya lugha ya kimila ambayo hamna mtu anaweza kulifikiria.

Usitumie neno la siri la chaguo-msingi, kwa kuwa ni rahisi mtu kulijua. Nywila za chaguo-msingi ni pamoja na nenosiri kama namba zinazofuatana mfano 123, 1234, nk

Unda mlolongo mgumu lakini wa kukumbukwa wa maneno Unaweza kutumia kifungo cha maneno chenye mchanganyiko wa namba, maneno ya herufi kubwa na ndogo pamoja na alama. Kwa mfano Machame#1©NDIZI

Kujilinda kwenye mitandao wa kijamii Mitandao ya kijamii ni miongoni mwa tovuti maarufu zaidi kwenye matumizi duniani. Kila mtu anatamani kuwa na akaunti yake ya mitandao ya kijamii ili aweze kutengeneza mtandao wake na jamii na wafuasi wake. Vile vile wagombea wa nafasi za uongozi wanapaswa kutengeneza majina pengine kupitia mitandao ya kijamii. Ipo mitandao mingi ya kijamii lakini ambayo inajulikana sana na kuwa na wafuasi wengi ni Facebook, Instagram na Twitter. Hii ina mamia ya mamilioni ya watumiaji kila mmoja.

• Mitandao ya kijamii kwa ujumla ilianza kwa lengo la kushirikisha makala, picha, na taarifa za kibinafsi za mtu. Lakini pia zipo hotuba zinatolewa kwa njia ya mitandao ya kijamii .

• Kwa hiyo, maswali yafuatayo ni muhimu kuzingatia wakati wa kutumia mitandao ya kijamii:

Page 79: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

76

• Jinsi gani unaweza kutumia mitandao hiyo wakati ukijilinda mwenyewe? • Faragha yangu ya msingi ni ipi kwenye mitandao hii ? Utambulisho wangu ni upi?

Nachangamana na watu gani kwenye mtandao? • Ni taarifa gani napaswa kuiweka kuwa binafsi toka kwa nani? Napaswa kuchapisha

mtandaoni au ninataka kuitunza binafsi?• Kabla ya kuweka taarifa yoyote jiulize inafaida gani kwangu, na madhara yake ya sasa

na baadae kama mtu mwenye malengo ya kisiasa?

Page 80: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

77

VIAMBATANISHO Kiambatanisho Na. 1 Mpango Mkakati wa kampeni

Jedwali hili limeandaliwa ili kukusaidie wewe kama mgombea kufikira vitu muhimu ambavyo unapaswa kuvifanya katika kampeni

Jina mgombea ………………………………………………………………………………….

Menaja wa kampeni …………………………………………………………………………..

Nafasi ……………………………………………………………………………………………Hatua ya 1: UtafitiMaelezo ya sheria zitakazohusu uchaguzi huuMambo yanayoweza kushawishi kwenye uchaguzi huuKuhusu mimi (Uwezo, udhaifu, fursa na Vitisho)Kuhusu Mpinzani wangu (Uwezo, udhaifu, fursa na Vitisho)Nahitaji kura ngapi Kushinda?Hatua ya 2: Timu ya kampeniJina Majukumu Mawasiliano

Hatua ya 3: Kufikia wapiga KuraWapiga kura wangu wanapatikana wapi zaidiWapiga kura gani napaswa kuwafikiaNjia gani ntatumia kuwafikia wapiga kuraHatua ya 4: Kutengeneza Jumbe na sera za kampeniUjumbe wangu (Usiozidi maneno 25)Sera zangu kwa wapiga kura

Hatua ya 5: Bajeti yangu ya kampeniKifaa Gharama

Jumla

Page 81: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

78

Hatua ya 6: Siku ya uchaguziVituo vingapi nitapigiwa kura

propppp

Mawalaka wangapi nahitaji na kuwapa mafunzoJinsi ya kukumbusha wapiga kura wangu wapi na siku ya kupiga kuraUsafiri kwa wapiga kura wangu wasio na uwezoJinsi ya kutoa taarifa kwenye vituo

Kiambatanisho Na. 2 Jinsi ya kuchambua sheria husika za uchaguziKifungu cha sheria/kanuni Maelezo ya kifungu

Kiambatanisho Na. 3 Kupima Uwezo, udhaifu, Fursa na Vitisho vyako pamoja na mpinzani wako

Uwezo Udhaifu

Fursa Vitisho

Kiambatanisho Na. 4 Vifaa vya kampeni ya uchaguziKifaa Kampuni ya

uzalishajiIdadi Tarehe kinapohita-

jikaWapi kitatumika

Page 82: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

79

Kiambatanisho Na. 5 Mkakati wa kufikia wapiga kuraAina ya mpiga kura Maelezo Wapi WanapatikanaFamilia na marafikiWanachama wa chama changuMitandao yangu ya elimu na kaziViongozi wa kijamiiMakundi maalumuWanaume/wanawakeWasio na vyama vya siasaMashirika mbali mbaliWengine

Kiambatanisho Na. 6 Matumizi ya Fedha za kampeniKifaa Idadi Gharama Gharama za uteuzi N/A

Vifaa

Vipeperushi

Mabango (uchapishaji na usambazaji)Barua (uchapishaji na usambazaji)

Kadi za mawasiliano

Vifaa vingine kwa ajili ya shughuli za mawasiliano ya wapigakura na matukio (T-shirt, kofia nk

Gharama za usimamizi kampeni

Kukodisha ofisi

Gharama za Simu/mtandao Posho kwa wafanyakazi, na wanaojitolea

Matangazo

FacebookMagazetiRedioRuninga

Gharama nyinginezo

Usafiri ViburudishoWawezeshaji kwenye warshaWarsha za kutafuta fedha

Ulinzi (Mgombe, masanduku ya kura, nk)Jumla

Page 83: MUONGOZO WA WARAGBISHI...CHADEMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo CUF Chama Cha Wananchi DAS Katibu Tawala wa wilaya SADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SWOT Uwezo, Udhaifu,

80

MCHAPISHAJIShirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF)

Mikocheni “A”, S.L.P 76215, Mtaa wa WiLDAF, Kitalu F, Kiwanja Na. 635Dar es salaam-TanzaniaSimu: +255 22 270 1995,

Barua Pepe: [email protected] / [email protected],Tovuti: www.wildaftanzania.org

Twitter, Instragram@wildaftz