katiba ya malengo - malengo saccos · f) kupewa taarifa ya maendeleo ya chama kupitia mikutano...

22
1 MASHARTI YA MALENGO SAVINGS & CREDIT COOPERATIVE SOCIETY LIMITED. SEHEMU YA KWANZA 1.0 JINA NA ANUANI a. Jina la chama litakuwa: MALENGO SAVINGS AND CREDIT CO-OPERATIVE SOCIETY LTD. b. Anuani ya Chama: S.L.P 34791, DAR ES SALAAM. c. Tarehe ya kuandikishwa 02 JUNE 2015. d. Namba ya kuandikishwa DSR 1522 e. Idadi ya Wanachama waliotuma maombi: 20 f. Eneo la shughuli za Chama litakuwa: WILAYA YA KINONDONI. g. Makao Makuu ya Chama yatakuwa: WILAYA YA KINONDONI MKOA WA DAR ES SALAAM. h. Fungamanisho (Common Bond) ni: WANATAALUMA WA WILAYA YA KINONDONI NA MAENEO MENGINE 2.0 MADHUMUNI YA CHAMA: Madhumuni makuu ya MALENGO SACCOS LTD ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya maisha ya wanachama ili waweze kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kufuata Masharti ya Chama, misingi na Sheria ya Vyama vya Ushirika. Ili kufikia matarajio ya wanachama, Chama kitafanya yafuatayo:- 2.1 Kupokea kiingilio, Hisa, Akiba na Amana kutoka kwa wanachama. 2.2 Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanachama wake. 2.3 Kuweka viwango vya faida na riba juu ya akiba, amana na riba juu ya mikopo ya wanachama vinavyokidhi gharama za uendeshaji wa MALENGO SACCOS LTD na kutoa manufaa kwa wanachama . 2.4 Kupanga utaratibu unaofaa wa kutunza na kuweka kinga ya fedha ya wanachama dhidi ya hasara. 2.5 Kuwahimiza wanachama kuongeza Hisa, Akiba na Amana zao mara kwa mara. 2.6 Kutoa elimu ya Ushirika na Ujasiriamali kwa wanachama wake. 2.7 Kuhifadhi ziada katika Taasisi za fedha au kununua dhamana za Serikali na kununua Hisa katika Kampuni/Mashirika mbali mbali baada ya kutoa huduma za Akiba na Mikopo kwa wanachama. 2.8 Kuinua na kustawisha pamoja na kukuza ushirikiano miongoni mwa wanachama. 2.9 Kuwahamasisha Wanataaluma wasio wanachama kujiunga na chama. 2.10 Kupitisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi kwa manufaa ya Wanachama kama itakavyoamriwa katika Mkutano Mkuu na Masharti haya. Mrajis wa vyama vya ushirika ataidhinisha maamuzi hayo kabla ya utekelezaji wake.

Upload: others

Post on 08-Jan-2020

37 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

1

MASHARTI YA MALENGO SAVINGS & CREDIT COOPERATIVE SOCIETY LIMITED.

SEHEMU YA KWANZA 1.0 JINA NA ANUANI

a. Jina la chama litakuwa: MALENGO SAVINGS AND CREDIT CO-OPERATIVE SOCIETY LTD. b. Anuani ya Chama: S.L.P 34791, DAR ES SALAAM. c. Tarehe ya kuandikishwa 02 JUNE 2015. d. Namba ya kuandikishwa DSR 1522 e. Idadi ya Wanachama waliotuma maombi: 20 f. Eneo la shughuli za Chama litakuwa: WILAYA YA KINONDONI. g. Makao Makuu ya Chama yatakuwa: WILAYA YA KINONDONI MKOA WA

DAR ES SALAAM. h. Fungamanisho (Common Bond) ni: WANATAALUMA WA WILAYA YA

KINONDONI NA MAENEO MENGINE

2.0 MADHUMUNI YA CHAMA: Madhumuni makuu ya MALENGO SACCOS LTD ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya maisha ya wanachama ili waweze kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kufuata Masharti ya Chama, misingi na Sheria ya Vyama vya Ushirika. Ili kufikia matarajio ya wanachama, Chama kitafanya yafuatayo:-

2.1 Kupokea kiingilio, Hisa, Akiba na Amana kutoka kwa wanachama. 2.2 Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanachama wake. 2.3 Kuweka viwango vya faida na riba juu ya akiba, amana na riba juu ya mikopo ya

wanachama vinavyokidhi gharama za uendeshaji wa MALENGO SACCOS LTD na kutoa manufaa kwa wanachama .

2.4 Kupanga utaratibu unaofaa wa kutunza na kuweka kinga ya fedha ya wanachama dhidi ya hasara.

2.5 Kuwahimiza wanachama kuongeza Hisa, Akiba na Amana zao mara kwa mara. 2.6 Kutoa elimu ya Ushirika na Ujasiriamali kwa wanachama wake. 2.7 Kuhifadhi ziada katika Taasisi za fedha au kununua dhamana za Serikali na kununua

Hisa katika Kampuni/Mashirika mbali mbali baada ya kutoa huduma za Akiba na Mikopo kwa wanachama.

2.8 Kuinua na kustawisha pamoja na kukuza ushirikiano miongoni mwa wanachama. 2.9 Kuwahamasisha Wanataaluma wasio wanachama kujiunga na chama. 2.10 Kupitisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi kwa manufaa ya Wanachama kama

itakavyoamriwa katika Mkutano Mkuu na Masharti haya. Mrajis wa vyama vya ushirika ataidhinisha maamuzi hayo kabla ya utekelezaji wake.

Page 2: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

2

3.0 WANACHAMA WATAKUWA HAWA:-

a) Wanachama wote waliojiandikisha katika kuomba kuandikishwa kwa Chama hiki katika daftari la Serikali (Waanzilishi).

b) Kikundi cha Kijamii au Kiuchumi cha Wanachama wa Chama hiki. c) Wanachama wapya watakaojiunga baada ya kutimiza Masharti ya kujiunga na Chama hiki wenye sifa zifuatazo:- 3.1 SIFA ZA MWANACHAMA: 3.1.1 Awe mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18) 3.1.2 Awe mwenye tabia nzuri, mwaminifu na akili timamu. 3.1.3 Awe amelipa Kiingilio, hisa na kuweka Akiba kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu

wa Masharti haya na awe tayari kushiriki kikamilifu shughuli za Chama zinazompasa. 3.1.4 Awe tayari kufuata Masharti ya Chama, Sheria ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya

mwaka 2013 na Kanuni zake wakati wowote. 3.1.5 Uanachama wake utokane na mojawapo ya sifa kama ilivyo hapo juu kwenye kifungu

na. 3.0 a hadi c

3.2 TARATIBU ZA KUJIUNGA KATIKA USHIRIKA HUU: 3.2.1 Maombi ya mwanachama yatafanywa kwa maandishi kwa Bodi ya Chama ambayo

itayajadili na akikubaliwa atathibitishwa na Mkutano Mkuu. 3.2.2 Maombi yakipokelewa ndani ya siku thelathini Bodi iwe imeshughulikia ombi/maombi

na kutoa jibu kwa mwombaji au waombaji. 3.2.3 Mwanachama atalipa kiingilio cha shilingi laki moja tu (100,000/=) na angalau Hisa tano

au zaidi kati ya Hisa Hamsini (50) zenye thamani ya shilingi elfu Kumi (10,000/=) kila moja anazotakiwa kununua ndani ya miezi kumi na mbili tangu kujiunga na Chama.

3.2.4 Kuchangia Akiba yake ya shilingi elfu Hamsini (50,000/=) au zaidi kila mwezi. 3.2.5 Chama kitakuwa na daftari ya wanachama lenye maelezo muhimu ya kila mwanachama

ambapo mwanachama ataweka saini yake.

3.3 .1 WAJIBU WA MWANACHAMA:

a) Kulipa kiingilio, kununua Hisa na kuweka Akiba mara kwa mara pamoja na kukopa kwa busara kwa mujibu wa Masharti haya.

b) Kulipa madeni yote kikamilifu katika muda uliopangwa. c) Kuheshimu Mikataba ikiwa ni pamoja na kulipa mkopo alioudhamini endapo

mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake kama alivyoahidi bila sababu za msingi. d) Kuwa mwaminifu kwa Chama na kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ili

kukiwezesha kutimiza malengo yake. e) Kubeba dhamana iwapo janga lolote litatokea kwa kikomo cha kiwango cha hisa

alizonazo mwanachama zilizolipwa ama zisizolipwa. f) Kutoa taarifa kwenye uongozi wa Chama iwapo mtumishi au kiongozi yeyote

anatoa huduma kwa upendeleo au anafanya jambo lolote linalohatarisha masilahi ya Chama na Wanachama.

g) Kuhudhuria na kushiriki kwenye mikutano Mikuu yote kwa mujibu wa Masharti. h) Kujielimisha kuhusu shughuli zote za Chama. i) Kuyaelewa Masharti ya Chama na kuyafuata.

Page 3: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

3

3.3.1 HAKI ZA MWANACHAMA:

a) Kushiriki katika shughuli zote za Chama kwa kufuata kanuni, Sheria ya vyama vya ushirika iliyopo, Kanuni, Masharti na maazimio yote ya Mikutano Mkuu.

b) Kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano mkuu ya Chama. c) Kuchagua au kuchaguliwa kuwa mjumbe / kiongozi. Kuchaguliwa

kutategemea kuwa na sifa za kugombea uongozi. d) Kuweka na kutoa akiba, amana na hisa zake kwa kufuata Masharti ya Chama. e) Kuwa mdhamini wa mikopo kwa mwanachama mwingine. f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

Mrajis wakati wa saa za kazi. h) Kupewa huduma ya mikopo kwa mujibu wa masharti ya Chama na Sera ya mikopo. i) Kuomba kuitishwa kwa Mkutano Mkuu Maalum kwa mujibu wa Masharti ya

Chama. j) Kupata Gawio kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu. k) Mwanachama ambaye uanachama wake umekoma, iwapo hadaiwi anahaki ya

kurudishiwa Hisa, Akiba, Amana na haki nyingine ndani ya siku 90 kupita tangu siku uanachama ulipokoma, isipokuwa mgao wa ziada utasubiri hadi pale ukaguzi wa hesabu utakapofanyika na mizania kutolewa na wakaguzi wa nje.

l) Kuteua mrithi/warithi. KUTEUA MRITHI:

a) Kila mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa na mafao yote anayostahili mwanachama anapofariki kwa kufuata Sheria ya Mirathi.

b) Mwanachama ana haki ya kubadilisha jina la mrithi na kila uteuzi utaandikwa katika daftari ya wanachama na mwanachama anayehusika atatia saini yake na dole gumba.

3.3.4. KUSIMAMISHWA NA KUKOMA UANACHAMA:

Mwanachama anaweza kusimamishwa au kukoma uanachama kwa ajili ya: a) Kushindwa kulipa Mkopo wake katika muda ulioruhusiwa na Chama pasipo kuwa

na sababu yeyote inayokubalika na Bodi ya Chama. b) Kufanya kitendo chochote ambacho Bodi itaridhika kuwa ni cha kutokuwa

mwaminifu au ambacho ni kinyume na madhumuni ya Chama. Kusimamishwa kwa sababu hii lazima kuthibitishwe na Mkutano Mkuu wowote utakaoitishwa mapema.

c) Kuacha kushiriki katika shughuli za Chama kama kuweka Akiba kwa muda uliopangwa.

d) Kufungwa jela kwa muda usiopungua miezi sita kwa kosa la jinai hususani la kutokuwa mwaminifu.

3.3.5. UANACHAMA UTAKOMA KUTOKANA NA :-

a) Kuchukua Hisa zake zote kwenye Chama. b) Ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari wa tiba anayetambulika.

Page 4: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

4

c) Kujiuzulu/Kuacha Uanachama mwenyewe baada ya kutoa taarifa ya siku 90 kwa maandishi na awe hadaiwi na Chama. Hata hivyo haki zake za Gawio hazitalipwa mpaka hesabu kwa kipindi hicho yawe yamekamilika na kukubaliwa na Mkutano Mkuu.

d) Kufukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu kwa kura ya wanachama wasiopungua theluthi mbili (2/3) ya waliohudhuria, baada ya kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na makosa ( kama yalivyo ainishwa kwenye Sheria ya vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013) ambayo yanasababisha kufukuzwa huko.

e) Kifo cha Mwanachama.

3.3.6. KUJIUNGA TENA:

Mwanachama aliyeacha kwa hiari yake mwenyewe anaweza kujiunga tena kwa kufuata taratibu zote za kujiunga.

SEHEMU YA NNE 4.0. VYANZO VYA FEDHA

4.1. FEDHA ZA CHAMA ZITATOKANA NA:- a) Viingilio b) Hisa, Akiba na Amana za wanachama c) Michango maalum, ruzuku na misaada . d) Ziada halisi. e) Akiba ya lazima na malimbikizo mengineyo. f) Mikopo kutoka benki na taasisi nyingine za fedha. g) Vitega uchumi vya Chama na h) Mapato mengine

4.2 MTAJI WA CHAMA:

a) Hisa za wanachama. b) Ziada halisi iliyobakizwa baada ya mgawanyo wa ziada. c) Akiba ya lazima na malimbikizo. d) Michango maalum, ruzuku na misaada.

4.3. KIINGILIO, HISA, AKIBA NA AMANA

Kiwango cha kiingilio, Hisa na Amana kitakuwa kinapangwa na Mkutano Mkuu kila inapobidi na kuidhinishwa na Mrajis kupitia marekebisho ya Masharti haya.

4.3.1. KIINGILIO:

Mwanachama lazima alipe kiingilio cha shilingi laki moja (100,000/=) anapokubaliwa uanachama. Kiingilio hakitarejeshwa kwa mwanachama akiacha uanachama au

Page 5: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

5

kusimamishwa uanachama na wala hakizai faida. Kiwango cha kiingilio kitapangwa kila mara na Mkutano Mkuu.

4.3.2. HISA:

a) Thamani ya hisa moja itakuwa shilingi elfu Kumi tu ( 10,000) b) Idadi ya chini ya Hisa ni Hamsini (50) zenye jumla ya thamani ya shilingi laki tano

500,000/=), ambazo zitalipwa ndani ya miezi Kumi na mbili (12) baada kujiunga c) Mwanachama atalazimika kununua angalau hisa tano wakati wa kujiunga na

atalazimika kukamilisha hisa zitakazobaki ndani ya miezi kumi na mbili. d) Mwanachama inabidi anunue Hisa nyingi kwa faida yake mwenyewe na ya Chama

lakini isizidi 1/5 au 20%/ya hisa zote zilizonunuliwa na wanachama au kisiwe kiasi pungufu ya kiasi cha chini cha Hisa kama ilivyowekwa na Masharti haya.

e) Kila mwanachama atapewa Hati ya hisa (share certificate) akikamilisha hisa hamsini

na kuendelea na kuingizwa kwenye daftari la wanachama. f) Mwanachama atakayeshindwa kununua Hisa kufikia kiwango cha chini cha Hisa,

katika muda uliopangwa, ataondolewa kwenye Chama. Kabla ya kuchukua hatua hiyo, mwanachama atapewa taarifa ili ajirekebishe au kutoa sababu za msingi ambazo Bodi itaridhika.

g) Faida ya Chama inayopatikana kwenye shughuli zake itagawiwa kwa wanachama kulingana na hisa zao na muda wa uanachama kwa mwaka husika. Mgao huo utafanyika baada ya hesabu kukaguliwa na Mizania kupokelewa na kupitishwa na mkutano mkuu wa mwaka na kuidhinishwa na Mrajis wa vyama vya Ushirika.

h) Mwanachama akiachishwa uanachama anaweza kurudishiwa hisa zake zote katika kipindi cha siku tisini (90) iwapo hadaiwi na Chama ikiwa ni mkopo wake au ule alioudhamini.

i) Iwapo mwanachama ana mkopo, Hisa na Akiba ya lazima zitachukuliwa kama dhamana ya kwanza ya mkopo wake.

4.3.3. KUUZA AU KUHAMISHWA HISA:

a) Hisa zinaweza kurithiwa, kuuzwa au kuhamishwa kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013.

b) Chama kitanunua Hisa za mwanachama ambaye uanachama wake umekoma; kwa ridhaa yake mwenyewe au vinginevyo.

4.3.4. AKIBA:

a) Kila mwanachama lazima ajenge tabia ya kuweka akiba mara kwa mara, kwa ajili ya mahitaji yake ya baadaye.

b) Ili kuongeza Akiba ndani ya Chama kila mwanachama atapewa faida ya asilimia itakayopangwa juu ya akiba kila mwaka kulingana na hali ya viwango vya Riba vitakavyokuwepo.

c) Akiba za mwanachama zitachukuliwa kama kigezo cha kupata mkopo si zaidi ya mara tatu na kadiri hali ya fedha ya Chama itakavyoruhusu.

d) Akiba inatakiwa iwekwe mfululizo zaidi ya miezi mitatu ili mwanachama apate mkopo.

Page 6: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

6

e) Kuweka akiba ni lazima katika chama na kiwango cha chini kitakachowekwa kila mwezi kisipungue shilingi elfu Hamsini (50,000/=) au kwa mkupuo kwa malipo ya awali ya kipindi kirefu. Akiba zaidi itawekwa kulingana na uwezo/matakwa ya mwanachama mwenyewe.

Mwanachama ambaye anaweka akiba Zaidi ya kima cha chini (50,000) anaweza kupunguza kiasi kisichozidi 20% ya akiba yake ya ziada kwa kutoa taarifa ya siku 90(miezi mitatu kwa Bodi ya chama.

4.3.5. AMANA:

Chama kitakuwa na kanuni za kuendesha Akaunti ya amana zitakazopitishwa na Mkutano Mkuu na kuidhinishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika. a) Mwanachama ama asiye mwanachama anaweza kuweka Amana katika Chama. b) Amana zitawekwa na kuchukuliwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa. c) Kima cha chini cha kubaki kwenye hesabu (account) kitakuwa kinapangwa na Bodi

kwa niaba ya mkutano mkuu na kitaainishwa kwenye sera ya amana. d) Amana zitakuwa zinapata faida na kiwango cha faida kitapangwa na Mkutano Mkuu

kila mara na kuidhinishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika.

SEHEMU YA TANO: 5.0. MIKOPO KUTOKA TAASISI ZA FEDHA. 5.1 Chama kinaweza kukopa baada ya kupitishwa na Mkutano Mkuu na kuidhinishwa na

Mrajis wa Vyama vya Ushirika ambaye atatoa Hati ya Ukomo wa madeni. 5.2 Kiasi cha kukopa kitakuwa kile kisichozidi robo (1/4) ya jumla ya kiwango kilichotolewa

kama Hisa pamoja na Akiba, Amana, kwa uamuzi wa robo tatu (¾) ya wajumbe wa Bodi.

5.3 Kiasi zaidi kinaweza kukopwa baada ya kupata uamuzi wa wanachama kwenye Mkutano Mkuu baada ya pendekezo la robo tatu (3/4) ya wajumbe wa Bodi, Lakini kiasi hicho kisizidi nusu ya rasilimali za Chama.

SEHEMU YA SITA 6.0 DHIMA YA MWACHAMA:

Dhima ya mwanachama kwa ajili ya madeni ya Chama haitazidi hisa zake, ziwe zimelipwa ama hazijalipwa.

Page 7: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

7

SEHEMU YA SABA 7.0 MATUMIZI YA FEDHA ZA CHAMA NA UWEKEZAJI 7.1 MATUMIZI YA FEDHA:

Fedha za Chama zitatumika kwa shughuli za maendeleo ya Chama ili kiweze kutimiza Madhumuni yake kulingana na Masharti haya.

7.2 UHIFADHI, UWEKEZAJI NA USIMAMIZI WA FEDHA: 7.2.1. Chama kitahifadhi fedha zake kwa kuweka akiba na amana benki na kununua dhamana

za Serikali na sekta binafsi. 7.2.2. Mahitaji ya mikopo ya wanachama yakitoshelezwa, fedha ya ziada itawekwa Benki

katika akaunti za Amana za Muda Mfupi au Mrefu ili ipate faida kubwa. 7.2.3. Fedha yote ya Chama isipokuwa ile inayohitajika kwa matumizi madogo madogo

itahifadhiwa Benki.Kiasi maalum cha fedha kitakachobaki kwa matumizi madogo madogo na kwa ajili ya malipo ya wenye Amana kitawekwa kwa mujibu wa Kanuni za fedha za chama hiki.

7.2.4. Kutoa mikopo kwa wanachama. 7.2.5. Kununua Hisa kwenye Taasisi za fedha na kampuni n.k. 7.2.6. Kujenga Nyumba na kununua mali isiyohamishika. Aina hii ya uwekezaji itatumia kwa

kiwango kikubwa fedha zitokanazo na Hisa na faida iliyobaki kwa kukuza mtaji wa Chama.

7.2.7. Kiasi kikubwa cha Fedha za Chama zitakazohitajika kuwa mikononi zitalazimika kuwekewa bima inayostahili.

SEHEMU YA NANE 8.0. HESABU ZA CHAMA: 8.1. Mwaka wa fedha wa chama utaanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba. 8.2. Chama kitaandika vitabu vya hesabu na kutunza kumbukumbu zote muhimu kulingana

na Sheria ya vyama vya Ushirika na kanuni zake,maelekezo ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Kanuni/viwango vya uhasibu vya Kitaifa na Kimataifa.

8.3. Urari Mizania ya Hesabu ya kila mwezi utatolewa. 8.4. Kamati ya Usimamizi itapitia Hesabu na utunzaji wa kumbukumbu za Chama kila baada

ya miezi mitatu (mara nne kwa mwaka) kwa kushirikiana na Mkaguzi wa ndani wa Chama.

8.5. Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi watachunguza vitabu na kumbukumbu za Chama wakati wowote kwa kushirikiana na wakaguzi walioidhinishwa na Sheria ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013.

8.6. Vitabu vya Chama vitakaguliwa kila mwaka kwa kuzingatia sheria ya Vyama vya Ushirika na viwango vya Uhasibu na mkaguzi wa nje yeyote atakayekubalika na wanachama kwenye Mkutano Mkuu kwa mujibu wa sheria ya vyama vya ushirika.

8.7. Gharama za ukaguzi zitalipwa na Chama chenyewe. 8.8. Chama kitakuwa na Kanuni za fedha (Financial regulations).

Page 8: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

8

SEHEMU YA TISA 9.0 MGAO WA ZIADA:

Mgao wa ziada utafanyika kwa mujibu wa Sheria na kanuni za vyama vya Ushirika. Mgao wa ziada utakuwa kama ifuatavyo:-

9.1. Kila mwaka Chama kitatenga 20% kutokana na ziada halisi kwa ajili ya akiba ya lazima. 9.2. Akiba ya lazima itabakia kuwa ni mali ya Chama na haitagawanywa isipokuwa kama

Chama kitavunjwa ambapo Sheria ya Vyama vya ushirika na kanuni yake itafutwa. 9.3. Asilimia kumi na tano (15%) itatengwa kwa ajili ya Mfuko wa kukombolea Hisa za

walioacha uanachama. Lakini kiasi hicho hakitazidi asilimia kumi na tano (15%) ya mtaji wote wa Chama.

9.4. Asilimia kumi na tano (15%) ya ziada halisi itatengwa kwa ajili ya kinga ya madeni mabaya. Lakini haitazidi 15% ya madeni yote chamani.

9.5. Asilimia tano (5%) zitatengwa kwa ajili ya mfuko wa elimu. 9.6. Baada ya matengo ya lazima kutolewa, ziada itakayobakia itagawiwa kwa wanachama au

kama ambavyo wanachama watakavyoamua katika mkutano Mkuu kwa kuzingatia Sheria ya vyama vya ushirika.

9.7. Kwa idhini ya Mkutano mkuu, Wajumbe wa Bodi,Kamati ya usimamizi,Mwakilishi wa Wanachama na Watendaji wengine wasiolipwa mshahara wanaweza kupewa tuzo (Honoraria) kwa kiwango kitakachokubaliwa mkutano mkuu.

SEHEMU YA KUMI 10.0. UONGOZI NA USIMAMIZI:

a) Madaraka makuu yanayohusu Chama hiki yatakuwa mikononi mwa wanachama katika mikutano Mkuu.

b) Kutakuwa na Mikutano Mikuu ya chama ifuatavyo:- i) Mikutano Mikuu ya mwaka

ii) Mikutano Mikuu ya kawaida. iii) Mkutano Mkuu maalum.

10.1 MKUTANO MKUU WA MWAKA:

a) Mkutano Mkuu wa mwaka utafanyika mara baada ya kufunga mwaka na isizidi miezi tisa baada ya mwisho wa mwaka wa fedha.

b) Mambo yafuatayo lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu wa mwaka.

i) Kuthibitisha akidi (quorum) kabla ya kuanza mkutano. ii) Kuthibitisha tangazo la mkutano.

iii) Kusoma na kuthibitisha mambo ya Mkutano Mkuu uliopita. iv) Yatokanayo v) Kujadili taarifa ya mwaka ya Bodi ya Chama.

vi) Kupokea na kujadili taarifa ya ukaguzi ya Mrajis, Kamati ya Usimamizi na ya Wakaguzi wa nje na kukubali au kukataa mizania ya mwaka husika inapokuwa na kasoro.

vii) Kufanya uchaguzi wa wajumbe wa kamati mbalimbali za Chama, kusimamisha na kufukuza baadhi yao ikibidi.

Page 9: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

9

viii) Kujadili na kuamua namna ya kugawana ziada kwa kuzingatia Masharti, Kanuni na Sheria ya Vyama vya Ushirika.

ix) Kujadili mapendekezo ya miradi na kutoa maamuzi. x) Kuidhinisha ununuzi au uuzaji wa mali za Chama zenye thamani isiyozidi kiasi

kilichowekwa na Sheria ya vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013. xi) Kufikiria na kuamua kiwango cha posho (Honoraria) kwa ajili ya Bodi.

xii) Kuweka kiwango cha riba juu ya mikopo na faida juu ya amana na akiba. Kuweka idadi ya Hisa na thamani ya hisa moja.

xiii) Kubadili au kufanya marekebisho yoyote katika Masharti haya kama ilivyo kwenye sheria ya Vyama vya Ushirika.

xiv) Kujadili na kuthibitisha juu ya mapendekezo ya sera/kanuni mbali mbali za Chama.

xv) Uteuzi wa Mkaguzi wa hesabu za Chama. xvi) Kujadili na kuamua juu ya wanachama wapya na wanaojitoa/kufukuzwa.

xvii) Kuzungumzia mambo mengine yanayohusu maelekezo ya utendaji kwa Bodi ya Chama.

10.2. MIKUTANO MIKUU YA KAWAIDA:

Kutakuwa na mikutano mikuu ya kawaida ambayo itafanyika wakati wowote katika mwaka,mkutano mmojawapo ni lazima ufanyika miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha wa Chama kumalizika.

Mambo yafuatayo yatajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa kawaida:-

i) Kuthibitisha akidi kabla ya kuanza mkutano.

ii) Kuthibitisha tangazo la Mkutano Mkuu

iii) Kusoma na kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita.

iv) Yatokanayo

v) Kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya utekelezaji kutoka kwa Bodi.

vi) Kuweka ukomo wa madeni chini ya Sheria ya vyama vya Ushirika.

vii) Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya Chama kwa mwaka unaoufuata.

viii) Kuthibitisha kuingizwa kwa wanachama wapya na kufukuzwa kwa wanachama ikibidi.

ix) Kufanya uchaguzi wa viongozi, kuwasimamisha/kuwafukuza wajumbe wa Bodi ikibidi.

x) Kuzungumizia mambo yote yanayohusu maendeleo ya chama kwa ujumla na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Bodi ya chama.

Mkutano utakaopangwa kufanyika angalau miezi miwili kabla ya kufunga hesabu za Chama utajadili mambo yaliyomo kwenye 10 .2 (v), (vi) & (vii).

Page 10: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

10

10.3. MKUTANO MKUU MAALUM:

a) Mkutano mkuu maalum utafanyika wakati wowote iwapo utaitishwa na Mrajis wa Vyama vya ushirika au mtu aliyeruhusiwa na Mrajis au kwa maombi ya maandishi ya wanachama wasiopungua theluthi moja (1/3).

b) Mkutano Mkuu Maalum unaweza kuitishwa na Bodi kujadili jambo la dharura.

c) Mkutano Mkuu Maalum ulioombwa na wanachama, maombi hayo ni lazima yataje sababu za kutaka mkutano huo ufanyike na waombaji lazima waweke saini zao na wapeleke maombi hayo kwa Mwenyekiti wa Chama na nakala kwa Afisa Ushirika wa Manispaa.

d) Mkutano Mkuu Maalum utazungumzia jambo moja mahsusi na hautazungumzia jambo zaidi ya lile lililotakiwa kuzungumzia katika mkutano huo.

10.4. TAARIFA ZA MIKUTANO:

a) Mkutano Mkuu wa mwaka utafanyika baada ya kutoa taarifa isiyopungua siku ishirini na moja (21).

b) Mkutano Mkuu wa kawaida utaitishwa baada ya kutoa taarifa isiyopungua siku ishirini na moja (21).

c) Mkutano Mkuu Maalum utafanyika baada ya kutoa taarifa ya si chini ya siku saba (7).

10.5. MAHUDHURIO:

a) Mahudhurio katika mikutano mikuu ya Chama yatabidi kuwa si chini ya nusu ya wanachama au 100 ukichukulia idadi yoyote iliyo ndogo.

b) Kwa mikutano mikuu ya mwaka, kawaida maalum na ulioitishwa na Bodi ikiwa mahudhurio hayatoshi baada ya kupita saa 1 ½ ya muda uliopangwa kuanza mkutano utaahirishwa kwa siku 7 na mambo yatakayozungumziwa yatakuwa ni yale yale ya mkutano ulioahirishwa. Iwapo mahudhurio yatakuwa hayatoshi. mkutano utafutwa na kutangazwa upya.

c) Kwa Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na wanachama, mkutano utafutwa kabisa iwapo mahudhurio yatakuwa hayatoshi baada ya kupita saa 1 ½ ya muda wa kuanza kikao uliopangwa.

d) Kwa Mkutano Mkuu ulioitishwa na Mrajis na Kamati ya usimamizi, mkutano utafanyika kwa mahudhurio ya idadi yoyote na maamuzi yatakuwa halali.

Page 11: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

11

10.6. MWENYEKITI WA MKUTANO:

a) Mwenyekiti wa Chama ataendesha mikutano yote isipokuwa Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na Mrajis na kamati ya usimamizi ambapo, Mrajis mwenyewe au mtu atakayemteua atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo.

b) Mwenyekiti ikiwa hayupo Makamu wake ataongoza mkutano na iwapo wote wawili hawapo mtu yeyote katika Wanachama waliohudhuria atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa muda na ataongoza mkutano huo.

10.7. BODI YA CHAMA, KAMATI YA USIMAMIZI NA WAWAKILISHI.

Mkutano mkuu utachagua wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi na wawakilishi wa wanachama kutoka miongoni mwa Wanachama walioomba nafasi hizo.

a) Wanachama wa Chama Hiki ambao ni viongozi wa Siasa au Viongozi wa Serikali wenye vyeo vilivyoainishwa katika Kifungu cha 132 cha Sheria ya vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013 Kifungu kidogo cha nne (4) hawatoruhusiwa kuchaguliwa kuwa Wajumbe wa Bodi, Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi au Uwakilishi wa Chama Hiki wakati wakishikilia nyadhifa zao za kisiasa au za Kiserikali.

b) Wajumbe wa Bodi, Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi na Mwakilishi wa wanachama watashika madaraka kwa Muda usiozidi miaka Sita (6) wenye vipindi viwili vya miaka mitatu (3) na baada ya hapo hawatakuwa na sifa ya kuchaguliwa hadi baada ya miaka mitatu kupita.

10.7.1. WAJUMBE WA BODI:

(a) Bodi itaundwa na wajumbe wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa (9) na miongoni mwao atakuwepo Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe (3) watatu wa Kamati ya Mikopo.

(b) Hakuna mjumbe wa Bodi atakayekuwa na haki ya kudai mshahara au posho isipokuwa kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu.

10.7.2. KAMATI YA USIMAMIZI

Kutakuwepo na Kamati ya Usimamizi yenye wajumbe wasiozidi watatu (3) ikizingatiwa kuwa wajumbe wa Kamati hii si wajumbe wa Bodi.

10.7.3. WAWAKILISHI Chama kitakuwa na wawakilishi wawili wa Chama watakaohudhuria kwenye Mikutano

itakayoalikwa Chama. Mwakilishi mmoja atatokana na wajumbe wa Bodi na mwingine atatokana na wanachama.

Page 12: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

12

10.8. KANUNI ZA KUZINGATIA WAKATI WA UCHAGUZI:-

i) Awe na umri usiopungua miaka 18

ii) Awe amelipa Kiingilio na Hisa zote

iii) Awe na elimu kuanzia Stashahada (Diploma) na kuendelea katika fani yeyote itakayomwezesha kuongoza Chama kiufanisi na rahisi kufundishika.

iv) Awe ni mwanachama aliyetimiza/kuhudhuria angalau mikutano mikuu miwili mfululizo kabla/nyuma ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.

v) Awe mchapa kazi na anashiriki kikamilifu shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuweka Akiba mara kwa mara na kukopa.

vi) Kwa ujumla awe anatimiza wajibu wake kama mwanachama wa SACCOS

vii) Awe mtiifu na mwaminifu

viii) Awe hajawahi kuenguliwa kwenye uongozi wa Ushirika katika Chama chochote.

ix) Awe na uwezo wa kuongoza shughuli za chama kulingana na mabadiliko ya hali ya uchumi wa nchi

10.9. UPIGAJI KURA:

i) Upigaji kura utakuwa ni siri (kuandika)

ii) Utafanyika kwa kila nafasi iliyotangazwa

10.10. VIKAO VYA BODI:

a) Bodi itakutana kila baada ya miezi mitatu, pia inaweza kukutana mara nne zaidi kwa mwaka endapo ni lazima kukutana.

b) Bodi itapokea na kujadili taarifa za maendeleo ya chama kutoka kwenye Kamati zote za Chama.

c) Katibu wa Vikao vya Bodi atakuwa Meneja wa Chama ambaye ataajiriwa.

10.11. KAZI ZA BODI:

Bodi itakuwa na Mamlaka ya kusimamia shughuli za utendaji wa kawaida wa Chama. Bodi itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo:-

a) Kutengeneza Sera/Kanuni mbalimbali za Chama zinazohusu uendeshaji, fedha, watumishi, mikopo n.k.

Page 13: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

13

b) Kuhakikisha kwamba shughuli za Chama zinaendeshwa kulingana na Sheria, Kanuni, Masharti na maadili ya Chama.

c) Kuhakikisha kwamba Chama kinatunza kwa usahihi Hesabu ya Chama kuhusiana na fedha, mali, madeni, mapato na matumizi.

d) Kufikiria kiwango cha riba itakayotozwa kwenye mikopo ya wanachama.

e) Kuajiri, kusimamisha au kufukuzwa watumishi wa chama kwa kuzingatia Kanuni na sheria za utumishi na kuhakikisha kuwa waajiriwa wote wana wadhamini wawili, wenye mali zisizohamishika.

f) Kusimamisha uanachama mwanachama au Mjumbe yeyote wa, Kamati ya Mikopo, kutokana na tabia mbaya au kushindwa kutimiza wajibu wa kazi na kupeleka mapendekezo kwa Mkutano Mkuu unaofuata ili uamuzi wa mwisho utolewe.

g) Kujadili mikopo ya wajumbe wa Bodi bila muhusika kuwepo.

h) Kufanya mambo yote yatakayo agizwa na mikutano Mikuu ya Chama na Mrajis wa Vyama vya Ushirika.

10.12. KAMATI YA MIKOPO:

Kamati ya mikopo itakuwa na wajumbe wasiozidi watatu (3) ambao watakuwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi.

a) Wajumbe wa Kamati hii watamchagua Mwenyekiti na Katibu miongoni mwao. Kumbukumbu za mambo yote yanayojadiliwa zitatunzwa na Katibu wa Kamati.

b) Maombi yote ya mikopo yatafikiriwa na kamati hii isipokuwa ile ya wajumbe wa Bodi. Kamati itahakikisha kuwa mkopo unaoombwa ni wa manufaa kwa mkopaji.

c) Kamati hii itawajibika kufuatilia matumizi bora ya mikopo na kuhakikisha kwamba wakopaji wanatumia fedha kwa miradi au shughuli walioombea mikopo hiyo.

d) Kamati itafanya kikao angalau kimoja kila mwezi lakini inaweza kufanya kikao cha dharura wakati wowote. Idadi ya juu ya jumla ya wanakamati wote itatosha kuendesha shughuli katika kikao. Hakuna mkopo utakaotolewa pasipo kukubaliwa kwanza na wanakamati wote wa mkopo ambao wamehudhuria katika kikao kilichofikipitisha mkopo huo. Taarifa ya vikao hivyo itatolewa kwa Bodi.

e) Kamati ya mikopo itachunguza kwa uangalifu tabia na hali ya fedha ya kila mwombaji wa mkopo pamoja na dhamana na kuhakikisha uwezo wa kulipa deni kwa ukamilifu katika muda uliowekwa. Kamati ya mikopo itawashauri wakopaji utaratibu na njia nzuri za kuondoa matatizo yao ya kifedha.

f) Kamati inaweza kumchagua mjumbe mmoja kuwa Afisa Mikopo atakaye idhinisha mikopo ya chama kwa niaba ya kamati.

g) Kamati hii itafanya kazi nyingine kama itakavyo amriwa na Bodi.

Page 14: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

14

10.13. KAMATI YA USIMAMIZI:

a) Kamati ya Usimamizi itakuwa na wajumbe wasiozidi watatu watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu. Wajumbe wa Kamati hii lazima wawe wenye maadili mema, wapenda haki, wanaoweza kusimamia kazi na kuchukua hatua za kurekebisha dosari pasipo upendeleo.

b) Wajumbe wa Kamati hii hawatakuwa wajumbe wa Bodi, ni kamati inayojitegemea.

c) Wajumbe wa kamati hii watatengeneza utaratibu wa kukagua na kusimamia kazi za kamati mbalimbali zingine. Watachagua Mwenyekiti na Katibu mingoni mwao.

d) Kamati itafanya kazi zifuatazo:-

i) Kukagua na kuchunguza matumizi ya fedha na mali zote za chama kwa niaba ya wanachama kila baada ya miezi mitatu (Mara nne kwa mwaka).

ii) Kukagua utekelezaji wa shughuli zote za chama na kuhakikisha kuwa zinafanywa ipasavyo kwa kufuata taratibu za Ushirika.

iii) Kamati itafuatilia maendeleo ya miradi mikubwa ambayo imepatiwa mikopo na chama mpaka wahusika wanapomaliza marejesho.

iv) Kutayarisha na kutoa taarifa ya maandishi juu ya hali ya fedha na huduma zitolewazo kwenye Bodi na Mkutano Mkuu na nakala kwa Afisa Ushirika wa Wilaya na Mkoa, kila miezi mitatu ya mwaka wa fedha.

v) Kuhakikisha kuwa chama kinakaguliwa na Mkaguzi wa nje aliyepitishwa na wanachama kupitia Mkutano Mkuu na kutoa ushirikiano wa kutosha na mkaguzi huyo.

10.14. VIONGOZI WA CHAMA:

(A) MWENYEKITI:

Mwenyekiti atachaguliwa na wanachama wote katika mkutano Mkuu.

Kazi, wajibu na madaraka yake ni kama ifuatavyo:-

i) Kusimamia na kuongoza vikao vyote vya Bodi na mikutano mikuu. Isipokuwa ile maalum iliyopitishwa na Mrajis na kamati ya usimamizi.

ii) Kutia saini katika Hundi, hati za mikataba, mihutasari ya chama na sehemu nyingine yote ile kwa niaba ya chama hiki.

iii) Kusimamia kazi nyingine zitakazohitajika kusimamiwa na Mwenyekiti.

iv)Msemaji Mkuu wa Chama.

v) Kufanya shughuli nyingine zitakazopangwa na Bodi na Mikutano Mikuu.

Page 15: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

15

(B) MAKAMU MWENYEKITI:

Wajibu wa Makamu wa Mwenyekiti ni kufanyakazi kwa kusaidiana na Mwenyekiti. Endapo Mwenyekiti hatakuwupo, atafanya kazi zote za Mwenyekiti.

10.15. KUKOMA KUWA MJUMBE WA BODI:

Ujumbe wa Bodi utakoma iwapo:-

(a) Mjumbe atafariki dunia

(b) Kujiuzulu kwa kutoa taarifa ya siku thelathini (30)

(c) Kufukuzwa na Mkutano Mkuu kwa sababu zozote zile ikiwemo ya kutowajibika/uzembe n.k.

(d) Kupata hatia ya kufungwa gerezani zaidi ya miezi mitatu.

(e) Kutokana na sababu zozote zilizomo kwenye Sheria na Kanuni za vyama vya Ushirika.

(f) Kukosa sifa za uanachama.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA.

11.0. WATENDAJI WA CHAMA

Chama kitakuwa na watendaji waajiriwa kama itakavyoainishwa kwenye Kanuni ya watumishi ya Chama wakiwemo Meneja na Mhasibu.

11.1. MENEJA/KATIBU WA CHAMA:

a) Meneja atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama na mshauri mkuu wa Bodi ya chama katika mambo yote yanayohusu utaalamu katika uongozi na usimamizi wa shughuli na zote za chama na atawajibika katika shughuli za siku hadi siku.

b) Atahudhuria mikutano mikuu yote ya chama pamoja na vikao vya Bodi ya chama na ataitisha vikao vyote vya bodi kwa kadiri ya maelekezo ya Bodi na ataweka pia kumbukumbu za mikutano na vikao vya bodi yaani atafanya kazi zote za ukatibu wa chama.

c) Atatunza daftari la wanachama, kumbukumbu na mikataba mingine ya chama.

d) Atahusika na kazi za chama kila siku na hasa :-

i) Kuhakikisha kuwa shughuli za Chama zinaendeshwa kama inavyotakiwa kwa kuzingatia Masharti,Sera mbalimbali za chama,Sheria ya vyama vya Ushirika Na.6 ya Mwaka 2013 na Kanuni zake.

Page 16: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

16

ii) Kupokea barua zote na kuziwasilisha kwa wahusika kwa utekelezaji.

iii) Kujibu na kupeleka barua zote zitakiwazo baada ya maelezo ya wahusika.

iv) Kutunza majalada yote na nyaraka mbalimbali za shughuli za chama kufuatana na taratibu , mipangilio na mgawanyo wa kazi katika chama na kuzipanga vyema Katika majalada hayo.

v) Kushauri Bodi juu ya ajira ya watendaji kwa mujibu wa makisio yaliyoidhinishwa.

vi) Kutoa mapendekezo yake katika kikao cha Bodi ambacho kitaamua kuwathibitisha kazini au kuwasimamisha kwa muda au kuwafukuza watumishi wa chini yake.

vii) Kuwasimamia wafanyakazi kulingana na maelekezo ya Bodi na Kanuni za Utumishi.

viii) Kwa uangalizi wa Bodi ataidhinisha malipo yote yaliyoidhinishwa na Mrajis.

ix) Kutayarisha na kutoa taarifa ya shughuli itakavyoamuliwa na Bodi ikiwa ni pamoja na kutayarisha agenda za Mikutano na vikao.

x) Kutunza kumbukumbu zote za Mikutano na vikao vya Bodi.

xi) Kubuni/kuratibu mipango ya maendeleo ya Chama na Kufanya mipango yoyote mingine itakayohakikisha mafanikio ya chama.

xii) Kutekeleza maagizo kama atakavyoelekezwa na Bodi, Mikutano Mikuu ya chama na Sheria ya vyama vya Ushirika.

11.2. MHASIBU/MWEKA HAZINA WA CHAMA:

Chama kitalazimika kuwa na Mhasibu wa kuajiriwa/Mwekahazina wa kuteuliwa mapema iwezekanavyo mara baada ya kuandikishwa chama. Katika utendaji wa kazi zake Mhasibu/Mwekahazina atakuwa hana budi kufuata kanuni zote za fedha (financial regulations) za chama na kuzingatia taratibu zote za kitaaluma ya Uhasibu katika utunzaji na uandishi wa vitabu vya hesabu na kumbukumbu zote za fedha za chama pamoja na utoaji wa taarifa za fedha hata na uhamisho wa miamala ya Hesabu.

Page 17: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

17

KAZI ZA MHASIBU ZITAKUWA ZIFUATAZO

a) Atahakikisha kwamba hesabu za chama zitakuwa tayari kwa ukaguzi ndani ya majuma manne baada ya mwisho wa mwaka wa hesabu za chama, na mali zote zimetayarishwa na kutiwa sahihi kama inavyotakiwa na wakaguzi kila mwisho wa mwaka (Stock Taking and Cash Counting)

b) Atafanya mpango wa kupokea mapato mbalimbali na fedha zingine zinazodaiwa na

chama na atafanya mipango pia jinsi ya kupeleka fedha hizo benki. c) Atasimamia Hesabu ya malipo ya chama ambayo yataingizwa vitabuni mara kwa mara

kwa kadiri ya maelekezo ya bodi na meneja wa chama. d) Atatimiza kazi zingine zinazohusu kuishauri bodi juu ya matumizi yenye tija kwa

kuzingatia makisio ya mapato na matumizi na kanuni za fedha za chama. e) Kushirikiana na meneja wa chama kuandaa mapendekezo ya Makisio ya Mapato na

Matumizi na kuyawasilisha kwenye vikao vya bodi na hatimaye kwenye mkutano mkuu wa kawaida kwa kupitishwa.

f) Kuandaa taarifa ya fedha na takwimu (Financial and Stastical Report) kila mwezi na

kuiwasilisha kwa Bodi na nakala kwa Afisa Ushirika Wilayani, na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika.

g) Kuandika na kutunza vitabu vya Hesabu na kumbukumbu zote zinazohusu fedha. h) Kufanya malinganisho ya hesabu ya benki kila mwezi i) Kutayarisha orodha ya wadaiwa kila mwezi na kuiwasilisha kwenye kamati ya

mikopo, ambazo zitatoa uamuzi kuhusu hatua za kuwachukulia wanachama waliochelewesha madeni yao zaidi ya kipindi kitakachoelezwa kwenye sera ya mikopo.

j) Kusaidia wanachama katika kujaza fomu ya maombi ya mikopo na kuziwasilisha kwa

Bodi ya mikopo ili zifikiriwe na kuidhinishwa k) Kutia saini katika hundi za chama l) Kuishauri Bodi juu ya kanuni, taratibu na mifumo bora ya usimamizi wa fedha. m) Kufanya kazi nyingine kama atakavyokuwa anaagizwa na Meneja mkuu wa chama na

sheria ya vyama vya Ushirika.

Page 18: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

18

11.3 UDHAMINI

Ajira ya watendaji wa chama itabidi iende sambasamba na udhamini angalau wa watu wawili na maadili ya uongozi yazingatiwe ikiwa ni kwa mujibu wa maadili ya Viongozi ‘‘code of conduct“.

SEHEMU YA KUMI NA MBILI.

12.0. TARATIBU ZA UWEKAJI AKIBA:

12.1. Kila mwanachama atapatiwa kitabu cha akiba (Pass-Book) ambacho kitaonesha kiasi cha akiba, hisa, amana na mikopo, faida na adhabu.

12.2. Vitabu vya akiba vitakuwa na namba zinazofuatana na kutolewa kwa wanachama. Namba za vitabu hivi zitaandikwa katika daftari za wanachama na kadi/leja ya mwanachama.

12.3. Fedha zitakazowekwa kwenye chama zitaletwa na mwanachama kwa njia mojawapo kati ya njia zifuatazo au zote:-

a) Makato kutoka kwenye mshahara wa mwanachama kwa kuwasilishwa na mwajiri.

b) Kuleta fedha taslimu kwa Mhasibu wa chama wakati wa saa za kazi.

12.4. Fedha yote ya mwanachama inayopokelewa, itakatiwa stakabadhi ya fedha na kuingizwa katika kitabu chake (Pass-Book) na baadaye kutiwa saini na Mweka hazina au mtu mwingine aliyeidhinishwa kupokea fedha, kisha kitabu hicho atapewa mwanachama mwenyewe akitunze.

12.5. Ikiwa kitabu kitapotea mwanachama anayehusika atawajibika kutoa taarifa ya maandishi kwa Meneja ama Mhasibu ikiambatanisha taarifa ya Polisi. Bodi ya Chama inaweza kuidhinisha kitabu kingine kitolewe katika muda wa siku 30 baada ya taarifa kupokelewa na mwenye kitabu atalipa gharama ya kitabu kipya kadri itakavyoamuliwa na wajumbe wa Bodi. Kitabu kipya kitaingiziwa salio za hesabu zote za mwanachama kama zilivyo kwa tarehe anayopata kitabu kipya.

12.6. Kitabu cha akiba hakina budi kionyeshwe wakati wote wa kuweka fedha au wakati wa kupata mkopo, amana ili Mhasibu aweze kuingiza kiasi kilichowekwa au kuchukuliwa

Page 19: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

19

SEHEMU YA KUMI NA TATU

13.0 UTOAJI MIKOPO:

13.1 Mikopo itatolewa tu kwa wanachama walio na akiba inayoruhusu kukopa.

13.2 Maombi yote ya mikopo yataidhinishwa na kamati ya mikopo ambayo lazima ihakikishe kuwa taratibu na masharti ya utoaji mikopo yamezingatiwa na mkopaji. Mikopo kwa viongozi wa chama itajadiliwa na kuidhinishwa na kikao cha wajumbe wa Bodi. Fomu ya maombi iambatanishwe na Leja kadi yake.

13.3 Itatolewa mikopo kulingana na matakwa ya Sera ya Mikopo.

13.4 Fomu maalum ya maombi ya mkopo lazima ijazwe kila mwombaji. Mwombaji atatoa taarifa ya uwezo wa kulipa mikopo anayoomba.

13.5. Kamati ya mikopo itafikiria maombi ya mkopo ikizingatia dhamana ya mkopo kama inatosha na uwezo wa kulipa mkopo wa mwombaji.

13.6. Mwombaji lazima awe na hisa na akiba na adhaminiwe na wanachama wawili akiwemo mkopaji mwenye Hisa na Akiba za kutosha mwanachama haruhusiwi kudhamini zaidi ya mikopo miwili.

13.7. Mjumbe yeyote wa Bodi ya mikopo atapaswa kudhaminiwa na wanachama wengine kama mwanachama mwingine yeyote.

13.8. Urejeshwaji wa mikopo utafanyika kwa kukatwa moja kwa moja kwenye mishahara au kwa fedha taslimu.

13.9. Mkopo utatozwa riba ya kiwango kitakachoamuliwa na mkutano Mkuu kwa kuzingatia gharama muhimu za asasi kama vile gharama uendeshaji chama, gharama za mkopo na gharama nyinginezo ili kuifanya asasi iwe endelevu.

13.10. Baada ya mikopo kuidhinishwa mkopaji atajaza fomu maalum ya Mkataba (loan agreement form) ambayo itatiwa saini na wadhamini hao wawili.

13.11. Kama Chama kimepata fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake kutoka sehemu nyingine nje ya fedha za wanachama basi kitakopesha fedha hizo kulingana na masharti yatakayopendekezwana kamati ya mikopo na kuidhinishwa na Bodi.

11.12. Bodi itakuwa inaandaa sera za mikopo kulingana na mahitaji ya wakati huo na Sera hiyo itaanza kutumika baada ya kupitishwa na mkutano mkuu na kuidhinishwa na Mrajis wa vyama vya Ushirika.

Page 20: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

20

SEHEMU YA KUMI NA NNE

14.0 MENGINEYO:

14.1. UIDHISHAJI NA UWEKAJI SAINI KUMBUKUMBU ZA CHAMA:

Kumbukumbu zote za kudumu na mikataba ya chama itasainiwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti kama wote hawapo Meneja na Mjumbe mmoja wa Bodi watatia saini.

14.2. LAKIRI YA CHAMA (COMMON SEAL):

a) Chama kitakuwa na Lakiri (Common Seal) na lakiri hiyo itakuwa na jina kamili la Chama “MALENGO SAVINGS AND CREDIT CO-OPERATIVE SOCIETY LIMITED”.

b) Lakiri (Common Seal) itatunzwa na Katibu/Meneja mahali salama na kutumika na wahusika wakuu tu waliopewa mamlaka ya kuweka saini mikataba, kumbukumbu za kudumu na nyaraka zingine muhimu za Chama.

c) Chama kitakuwa na muhuri wa kawaida ukionyesha jina la chama na nambari ya kuandikishwa ya Chama na utatunzwa na Meneja au Mhasibu na utatumika katika kumbukumbu zote zinazofanywa na Chama.

14.3. UTATUZI WA MIGOGORO:

Migogoro yoyote kuhusu tafsiri ya Masharti haya kati ya wanachama na Chama au uongozi wa Chama au watu wengine ipelekwe kwa Mrajis wa vyama vya Ushirika kwa uamuzi.

14.4. MASHARTI YA CHAMA:

Masharti ya Chama hiki yanaweza kubadilishwa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya 2013 na kanuni zake.

14.5. SIRI ZA CHAMA:

Bodi ya Chama hiki watatunza siri kuhusu kumbukumbu za wanachama binafsi isipokuwa masuala ya utoaji na ukusanyaji wa mikopo ambayo inaweza kuchukua hatua zozote za lazima dhidi ya wakopaji wasiokuwa waaminifu.

Page 21: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

21

SEHEMU YA KUMI NA TANO

15.0. KUVUNJWA, KUFUTWA NA KUFUNGWA KWA CHAMA:

15.1. Kwa maombi ya wanachama wasiopungua ¾ ya wanachama wote kwa kuzingatia sheria ya vyama vya ushirika no.6 ya 2013.

15.2. Iwapo wanachama wamepungua na kuwa chini ya 20 ya idadi inayohitajika kisheria.

15.3. Kwa amri ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika na. 6 ya mwaka 2013 na kanuni zake.

Page 22: KATIBA YA MALENGO - Malengo Saccos · f) Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano Mikuu. g) Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za

22

MASHARTI HAYA YAMETIWA SAINI ZA WANACHAMA (20) KWA NIABA YA WANACHAMA WENGINE KAMA IFUATAVYO: S/N JINA SAHIHI 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20