nakala 14 – nambari 1 – 2006 matendo / 3 mag swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi...

40

Upload: others

Post on 21-Jan-2021

2 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi
Page 2: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

2 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Je Wewe Ni Mwinjilisti?Usomapo andiko hili utajiuliza wewe mwenyewe ikiwa

kama wewe ni mwinjilisti. Haya ni maswali machacheyakukusaidia katika sala yako ufanyayo ili kuweza kuamuakama Mungu ndiye anayekuita kuwa mwinjilisti:

1. Je, nina uhakika Bwana amesema nami kwa kuniita aukatika roho yangu kwamba nina wito wa kuwamwinjilisti?

2. Je, ninahisi uzito wa maumivu na hali ya kukuzamatumaini iwapatayo watu waliotengana na Kristo?

3. Je, nina mawazo maishani mwangu kuhusu watuwanaoishi bila Kristo?

4. Je, nina mwamko wa kuwaeleza watu wengine kuhusumaisha ya Yesu Kristo, kifo chake na kufufuka kwake?

5. Je, nina njaa ya kusoma Neno la Mungu ili kupatauelewa mpana wa Injili?

6. Je, mawazo ya wanaume na wanawake wanaoishiumilele wa Jehanamu mbali na Mungu una madharamakubwa kwangu?

7. Je, ninajisikia kuona kuwa ninahitaji kuhubiri waleambao bado hawajaokoka?

8. Je, nimekuwa na ndoto au maono ya kujikutaninawahubiri waliopotea na kunihimiza kutakakueneza Injili?

9. Je, ninaona maeneo yanayonihitaji mimi kutakakusaidia wengine ili kuwaleta kwa Yesu Kristo?

10. Je, ninajisikia kubeba mzigo wowote ninapokutana na

Wakristo wengine ambao hawataki kufikiri au kujalihabari za kuwafikia wasiokoka na ujumbe wa Yesu?

11. Je, kuonesha wengine njia ya kwenda kwa Yesu Kristoni kitu muhimu kwangu?

12. Je, nimeandaa mipango yoyote ya kuhubiri aukushirikiana na wengine Habari Nzuri za wokovupekee wa Yesu Kristo?

Unaweza kuwa na majibu ya “Ndiyo” katika sehemu yamaswali haya. Kama ndivyo ilivyo ni kuwa upo uwezekanohalisi kuwa Mungu anakuita katika kazi ya uinjilisti. Katikagazeti hili utasoma kuhusu mambo yanayofuata:

• Mwinjilisti ni nani?• Jadili tabia za kazi ya uinjilisti• Gundua mwinjilisti na wale wenye wito wa uinjilisti• Tia moyo, changamoto na fundisha mwinjilisti• Saidia wachungaji kuwatambua na kuwatia moyo

wainjilisti, kusimama imara katika uinjilisti waowenyewe, na pia kusaidia kanisa likue kwa kuwa nawaumini wapya.

• Kutoa msaada wa kimatendo kwa kusaidia uinjilisti waviongozi na makanisa yao

MUHIMUAndiko hili litazungumzia wainjilisti wote wawili,

mwanaume na mwanamke. Sasa na katika historia nzima,ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti napia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti.

Utangulizi Wa Mhariri:Yesu aliwaambia wanafunzi Wake, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”

(Marko 16:15). Maandiko yanaonesha kuwa wote wanaomwamini Yesu Kristo wameitwa kushiriki HabariZake Njema na wengine (Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Hata hao ambao wameitwa na kukirimiwakama wachungaji katika kanisa la mahali wanaangalizwa kuwa tayari kuhubiri katika nafasi mbalimbaliwanazokutana nazo (2 Timotheo 4:5).

Hata hivyo wapo wale ambao wameitwa kipekee na kuchaguliwa na Mungu kwa kipawa na hudumakuwa “Wainjilisti” (Waefeso 4:11). Toleo hili la Gazeti la MATENDO litasaidia kueleza wito na kazi zamwinjilisti kama Maandiko Matakatifu yasemavyo.

Mafundisho haya yatakuwa ya msaada kwa kiongozi yeyote wa kanisa au waumini wa Kristo, kwaniyana mikazo yenye kutia mtu nguvu, kufundisha na pia kukuwezesha wewe na wale unaowaongozakuwapata waliopotea ili waje kwa Yesu Kristo.

Sehemu Ya Kwanza

Mwinjilisti NiNani?

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Page 3: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3

Mwinjilisti Ni Nani?Mwinjilisti ni mwanaume au mwanamke aliye-

chaguliwa na Mungu kueneza Habari Njema (Injili) zawokovu wa Yesu Kristo. Mwinjilisti ni mnenaji waMungu. Mwinjilisti hueleza watu habari za Yesu Kristo,Mwana wa Mungu, Mkombozi. Mwinjilisti huzungumzakwa maneno habari za Kristo na shabaha ya maishaYake, kufa Kwake, na kufufuka.

Mwinjilisti, kwa maneno mengine huhubiri Injili.Hakuna ujumbe mwingine mkubwa wa kuhubiri“…Injili … ni uweza wa Mungu uletao wokovu”(Warumi 1:16).

Habari za Yesu Kristo zimebeba mambo yafuatayo:alivyokuja duniani; alivyoishi maisha adilifu, hakuwana dhambi katika maisha yake; alivyokufa msalabani;alivyotoka kaburini; na pia anavyoishi milele.Shabaha ya kifo cha Kristo ilikuwa ni kuchukuwahukumu ya Mungu kwa dhambi za watu wote, na piakuangamiza nguvu za dhambi. Yesu alishinda mautina pia alimshinda ibilisi na nguvu zote za uovu.Maisha ya Yesu Kristo, kufa, na kufufuka kwakekunaleta matumaini kwa watu wote na pia kuondoawoga.

Kama wewe ni mwinjilisti, wewe ni mjumbe waMungu mwenye habari muhimu kuliko habari zoteduniani!

Mwinjilisti Ni Yule Ambaye AmetumwaMwinjilisti ni mjumbe - mtu aliyetumwa kutoa

tangazo. Kama Yohana Mbatizaji, mwinjilistianamtangaza Yesu kwa watu. “Injili” ni neno lenyemaana “habari njema”. Kwa hiyo mwinjilisti anabebaujumbe wa habari njema kwa watu ambao wanatakakuusikia. Ni habari bora kwa dunia nzima zinazohusukifo cha Yesu Msalabani na jinsi alivyojitoa kubebaghadhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu nakutupatia msamaha wa dhambi, na pia kutupa uzima wamilele.

Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu Mto Yordanikatika jangwa (Mathayo 3:1-12; Yohana 1:6-8,19-34).Mara nyingi mwinjilisti atatumwa kwenda mahaliambapo watu hawajui au hawajawahi kusikia habari zaYesu.

Neno “mwinjilisti” linamaanisha “mtu ambayeametumwa mwenye ujumbe”. Mungu aliwachaguawainjilisti kwenda na ujumbe wa Yesu na kuwaambiawengine. Uinjilisti ni kazi ngumu - ikiwa ni pamoja nakulisoma Neno la Mungu, kujitoa dhabihu, kufanyamipango, kujitia moyo, kusali, na kufunga.

Uinjilisti Ni KipawaSoma Waefeso 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa

mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwawainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu;kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi yahuduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”.

Mistari hii inatuambia kuwa Yesu amejalia Kanisakipawa cha wainjilisti. Zawadi maana yake ni kupokea

kwa shukrani na kuikubali. Mara nyingine wainjilistihawakubaliki na wachungaji au na kanisa. Lakini walewanaokuja kwa Kristo kupitia katika kazi za mwinjilistihushukuru Mungu zaidi na zaidi kwa vipawaalivyowapa - yeye aliyewaambia habari za Yesu nakuwaambia namna ya kupata wokovu na maisha mapyakatika Kristo.

Uinjilisti ni mojawapo ya huduma kuu tano zakiongozi-mtumishi alizotoa Kristo (Waefeso 4:11).Mwinjilisti ni kipawa kwa Kanisa maana anawaletawatu kwa Kristo. Watu waliookoka ukweli wanaendakanisani na kujifunza namna ya kumfuata nakumtumikia Mungu.

Mwinjilisti pia ni kipawa kwa watu waliopoduniani. Mwinjilisti anawaambia watu habari mpya zamaajabu ya Mwokozi Yesu, yeye aliyekufa nakufufuka tena. Kwa njia ya kuhubiri Injili, watuhusikia namna ya kusameheka kwa dhambi zao nakuupata uzima wa milele. Kuhubiri Injili ni kiini chahuduma ya uinjilisti

Wajibu Au OfisiKila huduma katika Waefeso 4:11 inakamilishwa na

watu ambao wameitwa kuifanya kazi ya Mungu.Mwingine ni mchungaji, mwingine ni mwinjilisti, namwingine anaweza akawa mtume.

Baadhi ya watu wanafundisha kuwa vipawavilivyopo katika kifungu hiki (Waefeso 4:11) ni kamaofisi au nafasi za mamlaka. Wanadai eti kipawa hikikinawapa wachungaji na wainjilisti ruhusa yakuwaamrisha wengine katika Kanisa.

Biblia haitufundishi hivyo. Uchungaji au uinjilistisiyo kuwa na mfalme juu ya watu wa Mungu. LakiniBiblia inaweka bayana kuwa mchungaji na mwinjilistini viongozi ambao wanafundisha wengine, kamaPaulo alivyoandika, “kwa kusudi la kuwakamilishawatakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili waKristo ujengwe” (Waefeso 4:12).

Njia ya Yesu Kristo katika huduma na pia mfanoWake kwetu sisi ni kuhudumia wengine. “Kwa maanaMwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, balikutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”(Marko 10:45).

Viongozi Ni WatumishiYesu alikuwa na mawazo na matendo ya kiutumishi

(Wafilipi 2:4-12). Kuwa kiongozi wa kimungu katikaKanisa, maana yake ni kuchukuwa njia ya Msalaba,kutokuwa na tamaa na mipango ya binafsi (soma Luka9:23; Wagalatia 5:16-25; Wafilipi 2:3-11). Viongoziwanaofanana na Kristo huishi kama watumishi waMungu kuwatumikia wengine, pamoja na unyenyekevuwa kweli.

Wachungaji, wainjilisti, waalimu, mitume, namanabii lazima waoneshe maisha yaliyotengwa ilikuwatumikia watu. Huduma kuu tano ni kuwa viongozi-watumishi - ambao wanatumikia wengine kama Yesualivyotumika.

Page 4: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

4 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Wito, Na Siyo CheoHuduma kuu tano zinazoorodheshwa katika Waefeso

sura ya 4 zinabeba matendo na kazi za hao walioitwana si vyeo. Wameitwa kuongoza na kuwafundishawafuasi wengine wa Kristo.

Kwa mfano, mchungaji atatunza waumini, kuwalishaNeno la Mungu, na pia kuwashauri. Wachungajiwanakirimiwa na kuitwa na Yesu kufanya hivyo.Mchungaji atajibu kwa Mungu jinsi alivyotunza nakufundisha ‘kondoo’ wa Mungu.

Mwinjilisti naye ana kazi. Wito wake na hudumayake vilevile zinatoka kwa Yesu. Ni watu wake ambaowamechaguliwa kuhubiri habari za Yesu Kristo naMsalaba wa Yesu. Kila mtumishi-kiongozi awe wa kikeau wa kiume amekirimiwa katika huduma yake kwenyeeneo la huduma. Mchungaji anashughulika na matatizona pia mahusiano katika kanisa. Ni lazima ahakikishekuwa watu wanakua na pia wawe na afya zao za kiroho.Anaweza kuwafundisha nidhamu, kama mchungakondoo anavyosaidia kundi lake. Hatatumia nafasi yakevibaya ili kuwa na amri juu ya watu au kufaidika nao iliatosheleze tamaa zake.

Kwa kawaida wainjilisti wamekirimiwa kuwa navipaji vya kupambanua roho na pia ujasiri wa kupinganana mapepo na roho wabaya zenye kupinga kazi ya Injilipale ambapo mwinjilisti ametumwa kuhubiri. Wanauwezo wa kuhubiri Habari Njema kwa nguvu, pamojana ishara zitokazo mbinguni huwapa uhakika wa ujumbewao. Siku zote wainjilisti hutarajia mafanikio palewanapokuwa wanahubiri kwa usikivu kwa Mungukwani wanavyofanya hivyo wanakuwa wanafanya kaziya wito wao na pia wananena kweli ya Injili (Warumi1:16).

Siyo CheoWatu wanaopenda cheo husisitiza kuheshimika kwa

vyeo vyao. Muda si mrefu wanadhani kuwa wao ni borazaidi ya wengine. Lakini Yesu alisema, “Basi, ye yoteajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyondiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo18:4). Soma zaidi kuhusu Yesu alivyosema kwawafanyakazi na wafuasi wake kuhusu kuwa na utumishimnyenyekevu katika Marko 9:33-35 na Yohana 13:3-15.

Wengi wanadhani kwamba kupata cheo kunawa-stahilisha kuwaongoza wengine; lakini sivyo. Wenginewanadhani ni lazima waoneshwe heshima kubwa kamawana cheo cha “Uinjilisti”. Hata hivyo, wapo wanaumena wanawake ambao wanampenda Yesu na piahushirikisha watu habari za Kristo katika miji na vijijivingi. Hawana cheo au kukubalika zaidi, walakini waoni wainjilisti wa kweli ambao wanafanya kaziiliyotakiwa.

Paulo aliwaleta watu wengi Korintho kwa uwezo wakuelewa wokovu wa Yesu. Paulo aliwaambia kuwa waoni barua yake iliyokubalika. Kazi yake na wito wakevilioneshwa na watu wengi ambao walimwamini YesuKristo (soma 2 Wakorintho 2:14 - 3:3 na pia1 Wathesalonike 2:19-20).

Nakala 14 / Nambari 1TOLEO LA KISWAHILI

YALIYOMO

Mwinjilisti Na Uinjilisti -Kupeleka Injili Duniani Kote!

Sehemu Ya Kwanza Mwinjilisti Ni Nani? ................... 2Sehemu Ya Pili Msingi Wa Uinjilisti ....................... 8Sehemu Ya Tatu Ujumbe Wa Mwinjilisti ................ 14Sehemu Ya Nne Kazi Ya Mwinjilisti ...................... 17Sehemu Ya Tano Mfano Wa Mwinjilisti Filipo ....... 19Sehemu Ya Sita Ishara & Miujiza Na Mwinjilisti .. 22Sehemu Ya Saba Kuhubiri Ujumbe Ulio Wazi

Wa Injili ........................................ 25Sehemu Ya Nane Mungu Anavyomuandaa

Mwinjilisti ................................. 32

Wahariri: ...............................................Frank na Wendy ParrishWahariri Kimataifa: ................................................ Gayla DeaseMfasiri wa Kiswahili: .............................................. Anna MakyaoWahariri wa Kiswahili: .................. Sig Feser & Godson LoshetieMhakiki wa Kiswahili: ............................................. Ndelilio Nnko

Gharama za Posta zimelipwaChennai - 600 010 India

MAONO NA UTUMEWA GAZETI LA MATENDO

Kuwapatia bure mafundisho ya Bibliana mafunzo yahuduma viongozi wa makanisa wa nchi za Asia, Afrika, naLatini Amerika ambao wanafundisha au kuhubiri neon laMungu (Biblia) kwa kundi la watu 20 au zaidi angalaumara moja kwa wiki.

MATENDO (ISSN 0744-1789) hutolewa mara nne kwamwaka na World MAP, 1419 North San Fernando Blvd.,Burbank, CA 91504-4194, U.S.A. Gharama za Posta zagazeti zimelipwa kule Arcadia, California na katika ofisinyingine za Posta. Maswali hupokelewa kwa anwani ya hapojuu pamoja na Box 4142, Manila, Philippines; Box 942,White River 1240, South Africa; Box 1037, Kilpauk,Chennai, 600 010, India.

MKUU WA POSTA: Tafadhali utume mabadiliko yaanwani kwa ACTS, World MAP, 1419 North SanFernando Blvd., Burbank CA 91504-4194, U.S.A.MATENDO ni gazeti linalotolewa bure, ambalohuchapishwa na kutumwa kwa viongozi wa makanisa.

MATENDO

Page 5: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 5

Waraka wa Yakobo unatufundisha kuonesha imaniyetu kwa kazi zetu, na siyo kwa maneno tu (Yakobo2:14-20). Ni kosa kufikiri kuwa cheo pekee ndichokinachokufanya uwe mwinjilisti.

Huduma ambayo Yesu aliitoa siyo cheo. Utumishi nihuduma. Inamaanisha kufanya kazi ngumu,kuudhamini wito wako na pia kujitoa kwa Mungu.Utumishi siyo kupokea cheo ili uheshimike mbele zawatu. Kazi inayofanywa na mwinjilisti ni kazi yakumpendeza Mungu na pia inaleta heshima mbele zaMungu Mwenyewe.

Biblia inafundisha, “Mwingine na akusifu wala sikinywa chako mwenyewe...” (Mithali 27:2). Acha watuwakubali kipawa chako kwa kazi yako na matunda yakona siyo wewe mwenyewe ujipe cheo.

Yesu alisema, “Utawatambua kwa matunda yao”(Mathayo 7:16). Mchungaji anafahamika kwa utunzajina mafundisho yake mazuri kwa kondoo wake;anaongoza na kulinda watu wa Mungu. Mwinjilistianafahamika kwa kuwaongoza watenda dhambi kujakwa Kristo na pia kuwaleta katika Kanisa.

Mojawapo Ya Karama Tano Za UongoziUinjilisti ni kazi kubwa na nzuri ya wito. Lakini

hakuna mtu atakiwaye kujivuna kwa wito wake kwaniYesu ndiye anayetoa kipawa hiki.

Uinjilisti ni mojawapo ya karama tano za uongoziiliyopewa Kanisa, zikiwa na mpango maalum wa utendaji.Wachungaji na waumini ni lazima wakubali mwinjilisti nikama zawadi, na pia waishi naye vizuri. Wainjilisti, kamawalivyo wachungaji, wapewe heshima na pia wawezeshwekifedha (1 Wakorintho 9:14; 1 Timotheo 5:17). Kwaupande wake mwinjilisti anategemewa awe kiongozi nakutumika katika nafasi ya uinjilisti.

Wakristo na viongozi ni lazima wakubali kuwa kilaMkristo ni kiungo muhimu sana katika Mwili wa Kristo(1 Wakorintho sura ya 12 & 14; Warumi 12:3-8). KilaMkristo ni muhimu na pia ana kazi ya kumfanyiaMungu katika ulimwengu huu.

Ni vizuri kufikiria huduma kuu tano katika kanisa(Waefeso 4:11-12) kama ni watu wanaofanya kazi kwabidii kuitimiliza kazi ya Mungu na mipango yake.Wanatumika kwa kipawa maalumu maana wanamtiiYesu. Wanafikia malengo maana wamechaguliwa naYesu. Ni vema kuwafikiria hawa viongozi, badala yaofisi zao na vyeo vyao na mamlaka yao kueleza wengineya kufanya.

Matunda Katika UtumishiWachungaji, waalimu, wainjilisti, mitume, na

manabii wanaofanya kazi kwa bidii kutimiliza wito waona pia kumfurahisha Mungu watalifanya Kanisa imarana hai. Ni vizuri kutumika kwa uadilifu na moyo zaidibadala ya kukumbatia vyeo na kuamini ubembelezaji wawatu. Yakobo 3:16 anasema, “Maana hapo palipo wivuna ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendobaya”. Ni mpango wa Mungu kwa walio nao witomiongoni mwa huduma kuu tano wafanye kazi

pamoja; kila mmoja kwa wito wake, na pia hupatamatunda kwa Mungu.

Tafuta kuzipata roho zinazopotea na pia fanya kazina watu wengine, na kila mtu ataelewa kuwa wewe nimwinjilisti wa kweli. Kazi yako itatoa ushuhuda wako.

Wachungaji Na Wainjilisti WanatakiwaWasaidiane

Wachungaji na wainjilisti wana kazi tofauti na wanawito tofauti, lakini wote ni wafanyakazi kwa pamojahapa duniani kwa Yesu Kristo. Wachungaji na wainjilistini lazima wathaminiane na kuheshimiana kwa vipawavyao na pia wito wao. Wito wa mtu mmoja siyo borazaidi ya wito wa mwenzake; wote ni muhimu.

Wachungaji na wainjilisti wana kazi tofauti. Nilazima wajitahidi kusaidiana katika kazi ya Injili.Wengine wamesema mchungaji ni kiongozi muhimuzaidi katika Kanisa. Hii siyo kweli. Viongozi wote waAgano Jipya ni muhimu na pia wana thamani kwaMungu na kwa malengo Yake. Kumbuka Yesuamewaita na kuupa ulimwengu wanawake na wanaumewenye vipawa vya kiroho. Wakati Yesu akiwa hapaduniani, alitumika kama mtume, mwinjilisti, mchungaji,mwalimu, na pia nabii. Na sasa kazi hizo ameziachakwa wengine (Waefeso 4:11-12).

Mwinjilisti anamsaidia mchungaji kuwaleta Wakristowapya katika Kanisa. Kanisa linaongezeka. Mwinjilistianajua kuwa mchungaji atamfundisha muumini mpya nakumsaidia kuwa imara katika Kristo. Mchungajianamsaidia mwinjilisti kwa kumwombea, kuwatia moyowatu kumsaidia mwinjilisti katika kazi yake, nakumsaidia kwa msaada wa fedha na mali.

Mchungaji na mwinjilisti ni watu wanaoishi pamojatena wanahitajiana tena wanapendana (Warumi 12:10;Waefeso 4:1-6). Hakuna anayemwambia mwenzakeafanye nini; wote wapo chini ya mamlaka ya Mungu.

Wengine Ni Wachungaji–WainjilistiMaeneo mengi watu wanaokolewa kwa muda mfupi.

Wanatakiwa wafundishwe na wakue katika maisha yaona Yesu. Mwinjilisti anayehubiri ujumbe wa Kristo nakuwapata waumini anatakiwa kuwatunza hawa kondookatika kundi lake Mungu hadi mchungaji apatikane napia awatunze hawa waumini wapya.

Wapo wanaume na wanawake ambao “wana miito yaaina mbili” - kuwaongoza watenda dhambi kwa Yesu napia kuwafundisha kama waumini wapya. Ni witowaliojitia kuwafanya watu wawe waumini wa Kristo.

Unaweza ukawa wewe ni mchungaji ambaye unawito wa uinjilisti. Kama saa zote wewe unatafutawaliopotea kwa Yesu, unatunza yale mtume Pauloaliosema kwa Timotheo kama mchungaji, “Fanya kaziya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako” (2 Timotheo4:5). Mungu amekuweka wewe hapo mahali ulipo iliutunze kondoo, na pia unaweza ukafanya uinjilisti hapoulipo. Pengine Mungu anataka uanzishe kanisa linginekatika mji au jiji lingine. Karama yako ya uinjilistiitakusaidia kuwapata watu waokoke. Lakini angalia

Page 6: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

6 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

usijaribu kuwafundisha wale ambao wana wito wawainjilisti wawe wachungaji.

Mwinjilisti Ni MtaalamuMungu amezungumza na wanaume au wanawake

maalumu kuhubiri na pia kueleza ujumbe wa wokovu.Mwinjilisti atasema “Ndio” kumtumikia Mungu katikanjia hii.

Kila Mkristo ameamriwa kushiriki imani yake katikaYesu Kristo na wengine(Mathayo 28:18-20; Marko16:15; Luka 24:46-48;Matendo 1:8). Kila Mkristoanatakiwa kwa furaha aelezeKristo ni nani naamemfanyia nini? Wakristowote wanatakiwa wawaletewengine kwa Yesu Kristo!

Lakini mwinjilisti ana witomaalumu katika kufanya hivyo.Mwinjilisti amefundishwa na kuwezeshwa kuwavutawaliopotea kuja kwa Yesu. Mwinjilisti akapewa wito wamaisha kuvua wanaume na wanawake kwa Kristo Yesu.Yesu alimwambia Petro “Njoni mnifuate, naminitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Marko 1:17).

Uinjilisti Ni KaramaMungu amewapa wainjilisti karama na vifaa vya

kazi. Mwinjilisti atahubiri kwa mamlaka na nguvu kwakuwa ni sehemu ya kipawa chao toka kwa Mungu.Miujiza hutokea wakati mwinjilisti anahudumu - lakinini Injili pekee na siyo miujiza inayookoa (Warumi 1:16;1 Wakorintho 1:21-24).

Mungu anaweza kumfundisha mwinjilisti namna yakuhubiri ili watu waelewe Injili na kuiamini. Kamawewe ni mwinjilisti, unaweza kumuuliza Mungu akupedhana na uelewa wa kuifanya kazi yako vizuri.

Mwinjilisti Ni MuhimuKatika nchi yetu pasingekuwepo na Mkristo kama

hakuna mtu aliyekuja kuhubiri Injili. Mtume Tomasondiye wa kwanza aliyesafiri kwenda nchi ya Indiakueneza Habari Njema. Towashi wa Kushi katikaMatendo ya Mitume sura ya 8 alipeleka Injili Afrika.Wainjilisti waliweza wakawepo maaskari wa Kirumi naWafanyabiashara waliopeleka habari za Yesu Ulaya naUingereza.

Watu waliopotea hawawezi kuokolewa pasipokufahamu habari za Injili ya wokovu katika Yesu Kristo(Warumi 10:14-15).

Mwinjilisti Awezeshwe Na Atiwe MoyoMwinjilisti ni mtu, mwanaume na mwanamke,

aliyepewa ari ya kueneza ukweli wa wokovu kwa watuwengi inavyowezekana. Hii inaweza kuleta ugumu kwamwinjilisti. Mara nyingi Mungu anatuma mwinjilistimaeneo ya vijijini au maeneo ambayo Injili inapingwa.

Ibilisi anapingana na kazi ya mwinjilisti wa kweli.

Shetani anapinga uinjilisti kwa sababu anajua nguvukubwa ya Injili iwaokoavyo watu kutoka kuzimu,inabadilisha maisha na kuwaweka huru kutoka dhambina nguvu za mapepo.

Mwinjilisti anaombea walio wagonjwa na walewaliopagawa na pepo na kuwaweka huru. Mwinjilistianawaita watu watubu kutoka dhambi na kumtumikiaMungu aishiye na wa kweli. Wainjilisti wanakwendamahali na kuwaleta wengine kwa Yesu na hivyo

kuwawezesha kuanzishakanisa.

Wachungaji na makanisa nimuhimu wawathaminiwainjilisti na kuwawezeshakufanya kazi yao kwa maombina kifedha. Hatutegemei watuwasiookoka wamlipemwinjilisti kwa kuwaleta nakufahamu Habari Njema yaYesu. Ni wajibu wa Wakristo

na makanisa kuwawezesha na kuwatia moyo wainjilisti.Kanisa linahitaji wainjilisti!

Hata hivyo, kila mhudumu apende kufanya kazi iliaweze kujisaidia mwenyewe. Mtume Paulo alifanya hivikwa kutengeneza mahema (Matendo 18:1-3; 20:34;1 Wakorintho 4:12). Paulo anaeleza kuwa ni vemakupokea msaada kutoka kwa wengine kama mhudumu(1 Wakorintho 9:1-23). Lakini Paulo anasisitiza kuwahakutegemea hali hii, “Basi thawabu yangu ni nini? Nihii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama,bali kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katikaInjili” (1 Wakorintho 9:18). Mwinjilisti, na wahudumuwote, watumie hekima na waongoze kwa RohoMtakatifu katika mambo haya, ili wasipate malalamikoau changamoto kwa ajili yao au Injili ya Yesu Kristo.

Yesu Alihubiri InjiliYesu aliposafiri kando kando ya miji ya Galilaya,

watu walikuja katoka maeneo mbalimbali ili waponywena kumsikiliza akihubiri na kufundisha.

“Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwonawakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Akawaambia,Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu,nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea”(Marko 1:36-38).

Yesu alikuwa anahubiri nini? La msingi ni Injili!Yesu alihubiri Habari Njema: “Hata baada ya Yohanakutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiriHabari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, naufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiaminiInjili” (Marko 1:14-15). Yesu alikuwa akihubiri kamamwinjilisti!

Mwishoni mwa huduma ya Yesu, alikuwaakifundisha watu na kuhubiri habari kwamba watuwatubu na kumwamini (Yesu) ili waokolewe “Ikawasiku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, nakuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani nawaandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula”

Kazi ya kwanza yamwinjilisti ni kueleza

watu matendo ya ajabuya Yesu Kristo.

Page 7: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 7

(Luka 20:1). Mstari huuunaonesha kuwa Yesualikuwa akihubiri kwawatu wasioamini karibuna muda wake wakwenda Msalabani. Kwakuwa Yesu alihubiri Injilitugundue kwambahuduma ya uinjilisti nimuhimu sana.

Mitume WalihubiriInjili

Yesu alituma mitumekupeleka Injili “Akawekawatu kumi na wawili,wapate kuwa pamojanaye, na kwambaawatume kuhubiri”(Marko 3:14). BaadayeYesu aliwatuma 70 zaidikwa kazi hii yakuwaambia HabariNjema (Luka 10:1,9).

Paulo AlihubiriInjili

Safari za MtumePaulo zilimpeleka kwawatu wengi ambao walikuwa hawajasikia habari zaYesu. Katika safari yake ya pili, Paulo na kundi lakewalikwenda Makedonia kwa sababu ya ndoto aliyompaMungu (Matendo 16:9). Katika miji hiyo, alihubirikama mwinjilisti kwa watu wasio Wayahudi.

Baadaye, waumini walikusanyika pamoja na Pauloaliwafundisha kama mchungaji. Kazi yake ya kwanza nikuhubiri Kristo kwa wote ambao hawakumjua. Baadayemakanisa yalikua katika miji hii.

Paulo alikwenda katika miji ya karibu na alihubiritena kama mwinjilisti. Hata hivyo Paulo alimtumaTimotheo, Tito au mtu mwingine katika kundi lakekufundisha na kuwasaidia wafuasi wapya.

Katika Makedonia, Paulo alikwenda Filipi,Thesalonike, Beroya, Athene na hatimaye Korintho(angalia Matendo 16:9 - 18:7). Kila mara, jambo lakwanza alihubiri kama mwinjilisti. Kitabu cha Matendoya Mitume kinaeleza kuwa Paulo alikaa Korintho kwamiezi 18 kwa amri ya Bwana. Alitenda yote mawili yakuhubiri kama mwinjilisti na kufundisha na kuongozawatu kama mchungaji.

Wanafunzi Wengi Walihubiri InjiliMariamu Magdalene alitumwa na Yesu kama

mwinjilisti wa kwanza kuwaambia wanafunzi kuwaamefufuka kutoka kwa wafu (Yohana 20:17-18). Filipoaliitwa “mwinjilisti” (Matendo 21:8). Wenginewalifanya kama wainjilisti kabla ya kuwa wachungaji.

Petro alihubiri kama mwinjilisti siku ya Pentekoste

Safari za Mtume Paulo zilimkutanisha na watu wengiambao bado hawajamsikia Yesu.

(Matendo 2:14-36). Aliwahubiria watu ambao walijuaMungu wa kweli lakini ambao walikuwahawajamwamini Yesu. Mahubiri yake katika Matendo yaMitume sura ya 2 yatatupa ukweli wa Yesu na maelezoya ukweli kuwa - wakati Yesu alipokufa, ilikuwa namaana muhimu. Petro aliwaambia watu pia kuhusumambo ya kufanya, sasa wanapojua kazi ya Mungu kwanjia ya Yesu Kristo (Matendo 2:37-39).

Waandishi wanne wa Injili katika Agano Jipyawana ujumbe ulio wazi wa uinjilisti na makusudi(Mathayo 28:18-20; Marko 1:1; Luka 1:1-4; Yohana20:31; 1 Yohana 1:1-4). Mathayo, Marko, Luka, naYohana wanatimiza kazi ya uinjilisti kwa sababuwameandika habari za Yesu ili kila mtu apate kusoma.Wameandika vitabu vinne vya kwanza vya AganoJipya. Wanaeleza jinsi Yesu alivyoteswa,alivyomwaga damu yake Msalabani, na kufa kwa ajiliya dhambi za mwanadamu. Injili pia inauambiaulimwengu jinsi Yesu alivyofufuka kutoka kaburini nakushinda kifo.

Waandishi wa nyaraka za Agano Jipya wanatimizakazi ya uinjilisti. Paulo, Petro, Yakobo, Yohana, Yuda, namwandishi wa Kitabu cha Waebrania wanaelezaumuhimu wa ukweli wa Injili. Kila mwinjilisti (na kilamwamini) anapaswa ajifunze nyaraka na kupataufahamu wa kweli wa Habari Njema za wokovu katikaYesu Kristo. Maandiko yana nguvu, yasiyo na makosana vyanzo muhimu ambavyo Mungu ametoa kwa kilamtu.

Page 8: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

8 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Sehemu Ya Pili

Msingi Wa Uinjilisti

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Hii ni sehemu muhimu kwa wachungaji na wainjilistikuisoma. Hii itawasaidia katika kufundisha uinjilistikwa wengine.

Kila nyumba inahitaji msingi imara. Kama msingihaujasimama wima, siyo imara, au umejengwa kwavifaa vibaya, nyumba inaweza kuanguka, hasa wakatiwa dhoruba (Mathayo 7:24-27). Habari za nyumbambili, uliyoelezwa na Yesu inafanyika kwa loloteufanyalo kwa Mungu. Huduma, familia, na maisha yakobinafsi lazima ujengwe katika msingi imara ambaohautatia ufa na hautaoza. Ndiyo ilivyo kazi ya uinjilisti.

Uinjilisti haufahamiki vema kwa viongozi wengi waKanisa. Wengine wanafikiria uinjilisti ni kuwa namkutano ya kanisa na kutegemea wasiookoka wajekanisani na kuitikia Injili.

Wengine wanafanya makosa kwa kuwaambia watuwafuate taratibu fulani za Kikristo, badala yakuwaonesha hitaji la kumpokea na kumfuata Kristo.Kuwapata watu na kuwaingiza katika hali fulani nakuwafanya kufuata taratibu zao siyo kuwaleta kwawokovu katika Kristo!

Kuwa Mkristo maana yake ni kuwa mmoja anayepokeana kumfuata Kristo na kuwekwa katika uhusiano mzuri waMungu Baba. Huokolewi kwa kujiunga na kanisa aukufuata mapokeo ya kidini. Kuokolewa ni kupokea Yesualiyefufuka, kutoa maisha yako kwa Yesu, kumtegemeaYeye na kazi Yake ya kutuokoa Msalabani, na kumfanyaYeye kuwa Bwana na Mwokozi wako.

Ni lazima kuwakilisha ukweli wote wa Injili ya YesuKristo. Hii ndiyo sababu ni vema kujifunza yale ambayoBiblia inatufundisha kuhusu uinjilisti na ukweli wa ujumbewa Injili. Ujumbe wa uinjilisti usifanywe kuwa ni kitukigumu. Uwekwe wazi, uwekwe sawa na rahisi kuelewekakatika kuwakilisha Ukweli wa Yesu kama Maandikoyasemavyo. Ni muhimu utolewe katika hali itakayomfanyamsikilizaji aelewe. Hii ndiyo kazi ya mwinjilisti.

Injili Ni Kuhusu Mtu – YesuPaulo anatoa ujumbe kwa Injili rahisi katika

1 Wakorintho 15:1-5: Yesu Kristo alikufa kama dhabihu

kwa dhambi zetu, alizikwa, na alifufuka toka kwa wafuna kutupa wokovu na kufanya tuwe na uhusiano naMungu. Hii ndiyo Injili iokoayo.

Uinjilisti Ni Kutangaza InjiliKuwashirikisha Injili maana yake kuwaambia

matendo makuu Yesu aliyotenda. Yesu anawapenda watusana hata akafa badala yao na kuchukua mwenyeweadhabu ya dhambi zao. Wakati Yesu alipofufuka toka kwawafu, alishinda dhambi, kifo, kuzimu, na nguvu zote zauovu. Hii ni habari njema kwa kila mtu dunia yote!

Mambo Yaoneshayo UinjilistiKuelewa na kutumia maneno haya kutakusaidia

kuwakilisha Injili kwa njia iliyo wazi ili kila mtu apatekuelewa mpango wa Mungu wa wokovu.

Upendo: Mungu anakupenda na alimtoa mwanayeafe na kuchukua adhabu ya dhambi yako. Upendo waMungu ni upendo wa milele, upendo usio na mipaka aumasharti. Mungu anakupenda pamoja na kuwa unadhambi na unamchukiza. Hakuna kitu wala yeyoteawezaye kubadilisha upendo wa Mungu kwa ajili yako(Yohana 3:16; Warumi 5:18; 8:31-39).

Kutubu: Ina maana kubadilisha mawazo,inayotokana na kubadilisha kusudi na maamuzi. Hivyo,kutubu ni kuamua kubadilisha dira/mwelekeo - kugeukakutoka ubaya na njia ya uovu na kumgeukia Mungu. Tobasi kusema tu samahani; inahusisha kubadili tabia(Mathayo 3:8). Kutubu ni kukubali kuwa mwenyedhambi na kuchagua njia ya Mungu badala ya njia zakomwenyewe (Marko 1:15; Luka 7:44-49; Matendo 26:20).

Kusamehewa: Kila mtu amefanya dhambi naanahitaji kusamehewa. Kila mmoja anahitaji kujua kuwaaibu na hatia ya dhambi zinaweza kuondolewa.Msamaha wa Mungu maana yake Mungu amekuondoleamzigo wa lile baya lililokuumiza. Amechukua naamesahau dhambi zako (Warumi 4:6-8; Waefeso 1:7).

Uzima Mpya (Uzima wa Milele): Yesu anatoa uhaimpya kwa wote wanaomwamini. Unakuwa kiumbe kipya(2 Wakorintho 5:17). Unapokea maisha mapya, msamaha

Page 9: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NUMBARI 1 – 2006 MATENDO / 9

wa dhambi zako, amani ya moyo wako, upendo waMungu kwa ajili yako na wengine, na kuishi maishamapya. Pia utaishi maisha ya milele na Yesu Kristombinguni (Yohana 3:1-6; 10:27-29; 1 Yohana 5:11-12).

Uhusiano: Uhusiano kati ya Mungu na mtuunawezekana kwa njia ya Yesu Kristo tu. Dhambi zetuzinatutenga na Mungu Mtakatifu, lakini wakatitunapokea dhabihu ya Kristo kwa ajili ya dhambi zetuna msamaha wake, Mungu hatuhesabii tena dhambikinyume chetu (soma Warumi 4:4-8). Munguanatuhesabia “wenye haki” kwa sababu ya kazi yaKristo, na tunaweza kuwa na uhusiano na Mungu nakumkaribia (Warumi 3:23-24; 5:18-19; 1 Wakorintho1:30; 2 Wakorintho 5:21).

Wokovu na uhusiano wetu na Mungu hauji kwakutunza orodha za sheria “usifanye hiki” na “fanyahivi”. Ni ukweli kuwa kama tutampenda Mungu,tutatimiza amri zake (Yohana 14:15). Lakini kazi zetuhaziwezi kutuokoa (Waefeso 2:8-10).

Yesu alimfunua Mungu kwetu sisi kama Baba yetu(Mathayo 6:9; Yohana 14:7-9). Tunaweza kumfahamuMungu na anaweza kutujua sisi (Yohana 17:3;2 Timotheo 2:19). Ndiyo maisha ya Mkristo - siyomatambiko matupu, kuishi kwa woga au kutenda memakiasi cha kukubaliwa na Mungu.

Kuamini: “Kuamini” ni kuweka tumaini, kuwa naimani, kushawishiwa kabisa, kutegemea. Kuamini Yesuni kuweka tumaini lote kwake na kuwa mfuasi wake.Hili si jambo la kukubali tu kiakili; ina maana kuyatoamaisha yako kabisa kwa Yesu (Yohana 1:12). Kuaminini kushawishika kuwa utakiri kwa maneno imani yakokwa Kristo (Warumi 10:9-10).

Kuzimu/Jehanum: Biblia inatoa maelezo ya ziwa lamoto lililopo kwa ajili ya Shetani na malaika zake(Mathayo 25:41). Yesu alisema kuwa kuzimu kuna “gizala nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”(Mathayo 8:12).

Wote wanaomkataa Yesu Kristo na kazi zake palepalewanaamua kutenda dhambi na kufuata njia zao. Mbayazaidi, watamfuata Shetani mpaka mahali pa adhabu yamilele, kuzimu/Jehanum. Mungu hakukusudia hili kwawatu wake na si kusudi lake yeyote aangamie nakuteseka milele (1 Timotheo 2:4; 2 Petro 3:9). Lakinikila mtu ni lazima achague Yesu kuwa mwokozi wakena kuishi na Mungu au kuteseka milele na kutengwa naMungu huko kuzimu.

Mambo Manne Ya Msingi Wa InjiliInjili ina mambo makubwa manne. Wakati wowote

unapohubiri ujumbe, au unapomshirikisha mwingine,kuandika barua, au kuzungumza na kundi la wanaumeau wanawake, ujumbe muhimu unafanana.

Mambo haya ni: Mpango wa Mungu - Kuasi kwaMwanadamu - Kazi ya Yesu ya Kutokoa – Itikio laMwanadamu. Jifunze Maandiko yaliyoko chini iliupate kujifunza zaidi katika kila jambo. [Wachungaji:Uwafundishe watu wa kanisa lako ili waweze kuwa-shirikisha wengine Injili!]

1. Mpango wa Mungu• Mungu anakupenda (Yohana 3:16; Warumi

8:35-39)• Mungu amekusudia kukupa maisha tele ya milele

na kuwa na faragha naye (Yohana 10:10; Ufunuo3:20)

• Mungu amekusudia mema kwa ajili ya maishayako (Yeremia 29:11; Warumi 8:28)

• Mungu amekusudia wewe umfahamu (Yohana7:3)

2. Dhambi ya Mwanadamu• Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu na njia zake

(Yohana 3:19-20; Warumi 5:10)• Dhambi inatutenga na Mungu (Waefeso 2:12;

4:18)• Kila mtu ametenda dhambi, imeleta maumivu

makubwa, mateso na kifo katika ulimwengu(Warumi 3:23; 5:12)

• Haki ya kweli ya Mungu inaleta hukumu kwadhambi ya Mwanadamu (Warumi 6:23)

3. Kazi ya Yesu Kristo ya Kutuokoa• Yesu alikufa Msalabani badala yetu kutulipia

gharama ya dhambi zetu (Wakolosai 2:13-15;1 Petro 2:24)

• Yesu aliweka njia pekee kwa ajili yetu ili tuwezekumrudia Mungu (Yohana 14:1-6; Matendo 4:12)

• Yesu alishinda dhambi na kifo na alifufuka tokakwa wafu (Warumi 1:3-4, 1 Wakorintho 15:20-23)

• Yesu anatupa msamaha wa dhambi, anatupaamani, upendo, na maisha mapya (Yohana 10:10;Warumi 5:1)

• Yesu anaishi leo kama Mfalme wa wafalme(Ufunuo 1:17-18; 19:16)

4. Itikio la Mwanadamu• Ni lazima niitike lile ambalo Yesu amesema na

kufanya (2 Wakorintho 6:1-2)• Nikubali dhabihu ya Kristo kwa ajili yangu na

dhambi yangu (Matendo 2:37-41; 16:30-34)• Nimwambie Yesu anisamehe dhambi zangu na

awe Bwana na Mwokozi wangu (Yohana 3:15-16;Waefeso 1:7)

• Nigeuke kutoka maisha ya dhambi na kuishi kwaNeno la Mungu na mpango wake (Warumi sura ya6; Waefeso 4:17-32)

• Nimfuate Kristo kila siku (Luka 9:23-26;1 Yohana 1:7)

• Niwashirikishe wengine imani yangu kwa Yesu(Mathayo 28:19; Marko 16:15)

Kutoa ujumbe mzuri wa Injili – kwa kutumia mambohaya manne - inaweza kuwa hivi:

“Kuna mmoja mwenye nguvu kuliko wote, Mungu,ambaye ameumba ulimwengu wote. Yeye ni mkamilifumtakatifu na wa haki; mkubwa kuliko chochote auyeyote. Hakuna kinachoweza kulinganishwa na ukubwa

Page 10: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

10 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

na nguvu za Mungu mwenye enzi. Mungu huyuanakupenda. Amekuumba ili uwe naye. Amekusudiakuwa na uhusiano na wewe.

“Lakini kuna jambo ambalo limetokea kati yetu naMungu. Kuna jambo linakuzuia usiwe na uhusiano naMungu na kujua upendo wake na kusudi lake kwa ajiliyako katika maisha haya. Hili linaitwa dhambi. Dhambiimekuja kati yako na Mungu. Dhambi inaleta shidanyingi na matatizo katika ulimwengu. Dhambi ni kamakusema uongo, kudanganya, chuki, kuiba, mawazomabaya, mauaji. Biblia inatuambia kuwa moyo wa kilamwanadamu umejaa dhambi (Yeremia 17:9). TanguAdamu na Hawa (Eva)(wanadamu wa kwanza)hawakumtii Mungu katikabustani ya Edeni, kila mtuamezaliwa na asili yadhambi (Zaburi 51:5).Dhambi ni kama ukuta,unaokufanya ujitenge naMungu. Kwa sababu yadhambi ya asili, tunatakatuishi tutakavyo kulikokuishi katika njia yaMungu. Watu wotewamefanya dhambi(1 Wafalme 8:46; Warumi3:23). Haki ya Munguiliyo timilifu inatakatuadhibiwe kwa dhambizetu.

“Mungu anajua tu wafundani yetu kwa sababu yadhambi zetu (Waefeso 2:1;Wakolosai 2:13).Amemtuma mwanaye,Yesu Kristo, achukueadhabu tuliyopaswa sisikwa ajili ya dhambi zetuna afe badala yetuMsalabani. Yesu alivunjaukuta wa dhambi nakufanya njia yetu yakumrudia Mungu. Yesualifufuka toka wafukuonesha kuwa Yesu niMungu (Warumi 1:4).Yesu Kristo anaishi milelekama Mfalme aliye Mkuukuliko mfalme yeyoteyule.

“Unaweza kuamini kuwa hii ni kweli kwa kukubalidhabihu ya Kristo. Unaweza kukubali kuwa wewe nimwenye dhambi, mwambie Mungu kuwa najutiamakosa yangu, na kupokea msamaha wa Kristo, nakuishi kwa amani na Mungu. Uchaguzi ni wakomwenyewe: Mwamini Kristo na kupokea msamaha,au kuendelea katika dhambi zako na kuishi katika

uharibifu sasa na hata milele. Je, unachaguakumwamini Yesu Kristo?”Kuna njia nyingi za kuzungumza juu ya mambo haya

manne. Kuelezea mambo haya manne ya Injili kutakuwarahisi unavyojizoesha kufanya mara kwa mara. Unawezakuanza kwa kuyasema kwa sauti mwenyewe; baadayejizoeze na Wakristo wenzako; na hatimaye anzakuwaelezea wasioamini.

Jozi Katika Kupeleka InjiliHapa kuna “jozi” ambayo inafanya kazi pamoja

wakati wa kupeleka Injili. Jifunze kuitumia; itakusaidiakatika kushirikisha Injiliwazi na kuwaongoza watukatika kumkubali Kristo.

Jozi Ya Kwanza -Habari ZakoMwenyewe & NenoLa Mungu

Waeleze habari zakoau shuhuda au jinsiulivyoanza kuamini Yesuinasaidia watu kumwonaMungu na kwambaanapenda kuwasaidia waobinafsi pia. Ni vema kutoaneno la shukrani nakuwaambia wenginemambo ambayo Munguamekutendea (Luka 8:39).

Wakati mwingineinasaidia unapowaambiahabari za watu wengine.Ushuhuda wa mamboayatendayo Mungukugeuza maisha ya watuni ushuhuda wenye nguvukuhusu uwezo wa Kristokubadilisha maisha yamtu.

Ushuhuda mzuri unamaeneo matatu:

1) Maisha yanguyalikuwaje kabla ya mimikukutana na Yesu?

2) Ilikuwajenikakutana na Yesu (nimazingira yapiyaliyonileta kwa Kristo)?

3) Maisha yangu yana tofauti gani tangu nikutane naYesu?

Kama utajibu maswali haya matatu utatoa ushuhudamzuri unapozungumza. Usiwaambie kila kitu, lakinichagua yale mambo muhimu. Usiweke mkazo sanakatika mambo mabaya uliyotenda zamani, lakini elezauzuri wa Yesu na jinsi alivyobadilisha maisha yako. Nivema ukaandika ushuhuda wako. Siyo lazima ushuhuda

Kuhadithia au kutoa ushuhuda wakojuu ya jinsi ulivyoweza kumuamini Yesu

Kristo kutasaidia watu waone kuwaMungu anajishughulisha nao pia.

Page 11: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NUMBARI 1 – 2006 MATENDO / 11

wako ukawa mrefusana. Unaletamafanikio mazurikama utaelezwa kwahabari fupi.

Neno la Biblia linauhai na lina nguvu.Hakuna neno jingineambalo ni muhimuzaidi. Washirikishemaneno ya Biblia,kwani Neno la Mungulina nguvu kuokoawenye dhambi:

“Kwa kuwanimezaliwa mara yapili; si kwa mbeguiharibikayo, bali kwaile isiyoharibika; kwaneno la Mungu lenyeuzima, lidumulo hatamilele…. Neno laBwana hudumu hatamilele. Na neno hili nineno lile jema lililo-hubiriwa kwenu”(1 Petro 1:23-25;angalia pia Yakobo1:18).

Biblia ndiyo zanayetu muhimu. Shuhudazetu pia zaweza kuwazana muhimu. Tumia zana hizi mbili (jozi) pamojawakati unaposhuhudia Yesu au wakati wa kuhubiri.

Jozi Ya Pili – Neno & RohoWakati unaposhuhudia au kuhubiri kwa ajili ya

Kristo, tumia maneno ya Biblia. Katika baadhi yatamaduni, wana ufahamu mdogo wa elimu. Wanawezawakawa hawajui hata kusoma. Maneno uyatumiayoyawe na mpaka na yawe marahisi. Kama ikilazimu, kwauangalifu, chukua neno la Mungu na kulifanya rahisikwa wengine kulielewa.

Kwa mfano, unaweza kusema, “Watu wotewamefanya mambo mabaya na kutokumtii Mungu;tunapaswa tuadhibiwe, lakini Mungu ametoa msamahakwa njia ya Kristo”. Hii ndiyo ukweli unaopatikanakatika Biblia katika Warumi 3:23 na Warumi 6:23,kwamba umeweka katika maneno marahisi. Lakini uwemwangalifu sana usibadilishe kamwe maana ya yaleBiblia inasema.

Roho Mtakatifu ni sehemu ya pili ya jozi hii. Yeyeameahidi kuwa atakusaidia kuelewa na kukumbuka yaleambayo alifundisha Yesu (Yohana 14:26; 15:26; 16:13).Ni Roho Mtakatifu anayemfanya mwenye dhambikushawishika na kuongoza wengi wamwamini Yesu(Yohana 16:8). Pasipo kazi ya Roho Mtakatifu huwezikuwaleta watu katika wokovu.

Roho wa Munguameahidi kutupauwezo wa kuwamashahidi (angalizi:“Ujazwe na RohoMtakatifu” katikaSehemu ya Saba). Nivema umwambieRoho Mtakatifu akupenguvu na ujasiri.Hubiri kwa kutumiaNeno la Mungu naamini Roho Mtakatifukuleta moyo wakupokea. Ni mapenziya Mungu kwa watuwote waokolewe nakujua ukweli(1 Timotheo 2:4);hivyo Munguatakusaidia!

Jozi Ya Tatu –Maombi &Maandalizi

Unaweza kupatamafanikio makubwakatika kuwaleta watukwa Yesu kwa kadriutakavyokuwaunawaombea waleutakaowaendea kuwa-

shirikisha Injili. Ni muhimu kuwaombea watu na maeneoambayo utakwenda kuhubiri. Inawezekana Munguatakupa mzigo katika mawazo yako kwa mtu fulani.Utapaswa kuomba mara kwa mara kwa ajili ya mtu huyu.

Unapaswa pia uwe na maandalio. Maandalio nipamoja na:

• kusoma na kujifunza Neno la Mungu• andaa ujumbe (angalia Sehemu ya Saba katika

gazeti hili)• jizoeze katika lile utakalosema• tumia muda mwingi na Mungu katika maombiChukua muda na ujiulize, “Nichukue habari ipi ya

kumwendea mtu huyu au kikundi?” Kariri mistari katikaBiblia. Mwombe Yesu akuoneshe njia nzuri ya kuwa-shirikisha watu wengine. Kama utachukua tahadharinzuri, Mungu atakusaidia ili watu wengi waje nakumfahamu Kristo.

Jozi Ya Nne – Nenda Mkiwa WawiliWawili

Yesu aliona ni muhimu watumishi wake wasiendemmoja mmoja, bali “wawili wawili”. Kamaunashuhudia katika maeneo ya barabarani, chukua mtumwingine atakayekuombea kimya kimya wakatiunazungumza. Hili ni jambo zuri. Kufanya wawiliwawili kunatoa nafasi ya kuelimisha wengine katika

Neno la Biblia ni hai nalina nguvu.

Page 12: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

12 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

kazi ya kushuhudia na uinjilisti. Mnaweza pia kutianamoyo na kusaidiana.

Katika Nchi ya Afrika Kusini kuna wanaume vijana nawanawake wanaompenda Yesu Kristo na wanafanya kazikila siku kuleta roho za watu kwa Yesu. Wengine niwanafunzi na wengine ni wafanyakazi. Hawafanyi kazi yauchungaji ya kanisa bali ni wavuvi wa roho za watu. Kilajuma wanatoka na kwenda barabarani au katika nyumbakuwaambia wengine habari za Yesu. Wamejifunzamambo manne ya kueneza Injili na wangeelewa zanamuhimu (hii jozi) za kutumia. Wanaomba na kujiandaawenyewe ili kuwashuhudia. Mwanamke analeta watuwawili hadi wanne kila juma anapotembelea mjini wakatiwa chakula cha mchana na kuongea na watu.Anawaongoza watu kwa Yesu na kuwaleta kanisani.

Haya Ni Mpaenzi Ya Mungu Kwa Kila Mkristo:Uufahamu ujumbe wa Injili, ujue jinsi ya kupelekaujumbe na jinsi ya kuzungumza pasipo woga au aibu.Kila Mkristo ni muhimu ajifunze jinsi ya kuwashirikishawengine Injili kwa njia bora ili upate mafanikio mengi.

Uwe Wazi Wakati UnapoongeaBiblia inasema, “Basi wamwiteje yeye

wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeyewasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?”(Warumi 10:14). Watu wanawezaje kuokolewa pasipokuelewa ujumbe wa neno?

Ni muhimu kujifunza jinsi ya kupeleka Injili kwanjia iliyo rahisi na iliyo wazi ili watu waelewe uamuziambao wanaitwa kuufanya na wauamini katika ukweliwake. (Angalia Sehemu ya Tatu, Ujumbe WaMwinjilisti.) Wakati mwingine maneno ya kidinitunayotumia yanaeleweka kwetu, hata hivyo yanasikikakama lugha mpya kwa mtu asiyeelewa. Epuka kutumiamaneno yasiyoeleweka kwa watu ambao hawanaufahamu wa Kikristo.

Tumia maneno ya kawaida katika kueneza Injili.Kama utatumia maneno ya Kikristo uwe na uhakika wakuyaelezea na mawazo ya Injili wasiyoyajua. Zaidi yahayo yote, hakikisha maneno uyatumiayo yanaelezaukweli wa Injili nzima.

Mifano

VigumuKueleweka

“Ni muhimu uokolewe, jiachie kwa Yesu.”

“Haleluya, ndugu maisha ya milele ni kwaajili yako.”

“Nimeokolewa na kukombolewa.”

“Nilikuwa mwenye dhambi lakini sasanimeokolewa.”

“Ngoja nikuambie ushuhuda wangu.”

RahisiKueleweka

“Unalo hitaji. Kristo alikufa kwa ajili yakona kuchukua dhambi zako. Mpe maishayako.”

“Rafiki yangu, Yesu anataka uwe na maisha- sasa na milele!”

“Yesu amechukua dhambi zangu nakuniweka huru.”

“Maisha yangu yalitawaliwa na dhambi.Baadaye nilikutana na Yesu naakanisamehe dhambi zangu. Amenipamaisha yanayonifanya nitake kuishi.”

“Ngoja nikuambie habari zangu jinsiYesu alivyoniokoa.”

Page 13: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NUMBARI 1 – 2006 MATENDO / 13

Njia nzuri ya kufuata: Weka maneno yako kuwamarahisi kueleweka bila kubadilisha ukweli wa Injili.

Njia ya pili: Jaribu kuelewa mazingira ya watuunaotaka kuzungumza nao. Ukiwaelewa, itakuwa rahisikuzungumza nao.

Ni muhimu kwako –kama mchungaji,mwinjilisti, au kiongoziwa kanisa - uelewe jinsiya kutoa ujumbe wa Injili.Ni vema ukajua jinsi yakuwakilisha Injili kwawazi na kwa njia yaukamilifu. Mara unapojuanjia hii, unawezakuzungumza habari zaYesu Kristo kila mahali,na kwa kila mtu na kwanjia itakayohitajika wakatihuo.

Mungu anatutaka tutoeukweli wa kazi, uhakika,na kwa uangalifu(2 Timotheo 2:15). Hii inamaana zaidi kuliko kuelezea Biblia kwa Wakristo. Hiiina maana pia tuweze kuleta Injili ya Yesu Kristo kwawanaume na wanawake wasiookoka.

Njia Za Kushirikisha Injili1. Katika uhusiano: Mara nyingine hii inaitwa

“uinjilisti kirafiki”. Kuwa rafiki na mtu fulani. Upatenafasi ya kumjua mtu huyo kabla ya kumshirikishahabari za Yesu. Jenga daraja la kuaminika nakutunzana. Mtu atakuwa tayari kufungua moyo wakekusikia habari za Kristo kwa kadri unavyopenda nakuishi maisha yako yawe mfano wa imani mbele yawengine.

Katika hali nyingine (kwa mfano, Waislamu), upateruhusa ya kuzungumza nao. Watu wanahitaji muda wakuona kuwa wewe ni mkweli na mwaminifu.

Njia hii ya uinjilisti inachukua muda. Huu ndiomwenendo. Ina maana utahusika na maisha ya mtu huyuna uangalizi wake na furaha, mahangaiko na matumainiyake, familia na kazi yake.

2. Nafasi moja tu na kuzungumza: Njia hii yauinjilisti ni ya haraka na yenye nguvu. Ni kile ambachounaweza kushirikisha wakati unakaa katika gari moshiau basi karibu na mtu, au wakati umekutana na mtukando ya barabara. Mara nyingi ni mtu mgeni ambayehujabahatika kukutana naye. Hii ni kama kukabiliana.Waambie mambo manne ya Injili na kama panauwezekano muulize kama unaweza kuomba naye iliampokee Kristo. Wakati mwingine unaweza kumwachiaBiblia au kipande cha maandiko au tract (vipeperushi).Unaweza kumwonesha upendo wa Mungu. MwombeMungu akupe ujasiri wa kumshirikisha Injili wakatiukiwa na nafasi.

3. Tendo la huduma: Hali ya upole au kujitoakunazungumza kwa ukubwa zaidi. Kufanya jambo lakumsaidia mtu kunafungua moyo wa kusikiliza Injiliya Yesu. Omba na angalia nafasi ya kumshirikisha

habari za Yesu kwa njiahii. Hili ndilo ambaloMungu ametutendea.Alionesha upendo wakekwetu kwa kumtumaYesu kuja kwa ajili yetu(Warumi 5:8).

4.Kutamkahadharani: Aina hii yauinjilisti ni kuzungumzakatika mhadhara wawatu. Wakati mwingineunahitaji kuwakusanyawatu pamoja iliuzungumze nao. Nyimbo,waimbaji, wachezaji, autendo ambalo linawezakuwavuta watu, nahatimaye kuwahubiria

habari njema za Yesu.Huu siyo wakati wa kuhubiri mahubiri marefu. Utoe

Injili kwa muda wa dakika tano au sita. Watuhawatangoja ili wakusikilize kama utahubiri mudamrefu. Kumbuka huu si mkutano wa Kanisa! Una mudamfupi tu kushirikisha habari iliyo muhimu kwa watuwanaosikiliza. Huu ni muda wa kuwaita watu waombenawe ili kumpokea Yesu.

5. Tukio maalum: Kanisa lako na huduma inawezakukuwezesha katika tukio au wajibu wa kukusanyawatu. Makanisa mengi katika nchi mbalimbaliwamefanya hivi. Wamekuwa na tamasha la muziki, ausikukuu, kualika wahubiri maalum, kutoa maigizo,kuonesha sinema ya Injili, au tamasha la kwaya. Baadhiya makanisa wameandaa chakula na kualika wageniambao hawajaokoka.

Watu katika kanisa lako wanaweza kwenda kutoahuduma katika shule au katika hospitali. Hii inawezakutoa nafasi ya kuwashirikisha Injili kwa kundi lawatu.

Unatakiwa uweze kuwafanya watu wajisikiekukaribishwa na wasifungwe katika mipaka ya desturiza kanisa fulani. Kama unataka kuwafanya wawewaumini wa kanisa lako, wataweza kuona motisha waubinafsi. Lakini kama unataka kuwatambulisha kwaMwokozi Yesu, watapenda kumpokea Kristo. (nawanaweza kuja katika kanisa lako).

Kuna njia nyingi za kuwafikia watu. Mungu atakupahekima ya kujua jinsi ya kuwashirikisha wengine Injilina kuwaelimisha wengine jinsi ya kufanya hivyo.Jifunze na kumbuka mambo manne ya Injili. Hivyoutaweza kufundisha wengine jinsi ya kuwashirikishahabari za Yesu.

Mungu anatutaka tutoeukweli wa kazi, uhakika, nakwa uangalifu (2 Timotheo2:15). Hii ina maana zaidikuliko kuelezea Biblia kwaWakristo. Hii ina maana piatuweze kuleta Injili ya Yesu

Kristo kwa wanaume nawanawake wasiookoka.

Page 14: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

14 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Sehemu Ya Tatu

Ujumbe WaMwinjilisti

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Ujumbe Muhimu Wa InjiliKuhubiri Injili ni kueneza habari ya Yesu. Ujumbe

wa mwinjilisti unahusika na maisha, kifo na kufufukakwa Yesu.

Kuwa na ufahamu wa ujumbe wa Maandiko ya Injili,inakupasa usome na ujifunze kwa uangalifu vifunguvifuatavyo vya Biblia.

Yesu Kristo AlitabiriwaMwanzo 3:15Kumbukumbu 18:15Zaburi 16:10; 22:1-31; 41:9Isaya 7:14, 9:6-7; 53:1-12; sura ya 61Zekaria 11:12-13

Kuja Kwa Yesu Kristo Na Ujumbe WakeMathayo 1:21; 7:13-14; 18:11Marko 1:15; 10:27,45; 16:16Luka 2:10-11; 9:56; 19:10; 23:33Yohana 1:12-13; 3:16; 10:10,28; 14:1-7; 20:31Matendo 2:17-39; 3:19; 4:12Warumi 3:9-26; 5:1-21; 6:17-23; 8:1-11,15-171 Wakorintho 15:1-42 Wakorintho 5:18-21Wagalatia 2:16; 3:13,21-26; 4:4-7; 5:16-24Waefeso 1:1-14; 2:1-18Wakolosai 1:13-141 Timotheo 2:5-61 Petro 1:1-5; 3:182 Petro 3:91 Yohana 4:9-10

Kurudi Kwa Yesu KristoMathayo sura ya 24Yohana 14:1-3Matendo 1:10-111 Wathesalonike 4:15-182 Wathesalonike 2:1-2Tito 2:13Ufunuo wa Yohana 22:1-5,20

Kuhubiri vizuri kwa mwinjilisti ni lazima aeleze habariza Yesu, kueleza jinsi Biblia isemavyo kuhusu Yesu, nakuwaita watu ili watubu na kumwamini Yesu.

Soma Matendo sura ya 2. Hapa Petro alihubiri na watu3,000 walimwamini Yesu Kristo. Petro aliwaambia ukwelikuhusu Yesu na aliwaelezea watu. Hatimaye Petroaliwaambia makutano waliosikiliza mambo ya kufanyakwa kuwa sasa wamepata kuelewa ukweli. Aliwaambiawatubu na kumrudia Mungu na kuamini Yesu na kumfuata.

Hubiri UkweliWewe pia unaweza kuwaona watu wakija kwa Yesu

Kristo; wakati unapohubiri ujumbe wa Injili ya Yesu. KamaPaulo aandikavyo katika 1 Wakorintho 15:1-4: “Basi, nduguzangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiria; ambayo ndiyomliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyomnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri;isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo

Kwa mwinjilisti na kuwaitawatu ili watubu na

kumwamini Yesu... Petroaliwaambia makutano

waliosikiliza mambo yakufanya kwa kuwa sasa

wamepata kuelewa ukweli.Aliwaambia watubu na

kumrudia Mungu nakuamini Yesu na kumfuata.

Page 15: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 15

mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristoalikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kamayanenavyo maandiko”. Huu ni ujumbe rahisi: Yesu aliishi,alikufa Msalabani, alizikwa na alifufuka kwa nguvu yaMungu (angalia Warumi 1:4).

Eleza UkweliEleza kuwa Yesu alikuja ili kurudisha uhusiano wetu na

Mungu anayetupenda (Warumi 5:1; 2 Wakorintho 5:18-20;Waefeso 2:11-18; 1 Yohana 4:9-10). Yesu alikuja ilikutusamehe dhambi zetu (Waefeso 1:7; Wakolosai 1:13-14)na kutuweka huru kutoka kongwa la dhambi (Warumi6:17-23). Yesu Kristo alikuja kutupa maisha mapya na safi(Waefeso 1:3-4; 2:10; Tito 2:13-14). Amemtuma RohoMtakatifu wake kutupa nguvu ya kuishi maisha ya haki nakumpendeza Mungu (Warumi 8:1-11; Wagalatia 5:16-23).Kwa sababu ya Yesu, tunawezeshwa kustahimili kama wanawa Mungu Aishiye milele, tuwe warithi pamoja na Yesu(Yohana 1:12-13; Warumi 8:15-17; Wagalatia 4:4-7). Nasiku moja, wajibu wetu tuliopewa duniani utakapotimilika,tutakaa katika uwepo wa Mungu milele, kumfurahia Mungumilele (Yohana 17:3; Ufunuo wa Yohana 22:1-5).

Mara Zote Uwaite WaitikieYesu anataka wanaume na wanawake kumwitikia Yeye.

Baada ya Yesu kumponya kipofu, Yesu alimtafuta nakumtaka amwamini Yeye (Yohana 9:35-38). Katika Injiliya Yohana mlango wa 4, Yesu alitumia muda kwa kuongeana mwanamke Msamaria kisimani na kumwita amwaminiYeye Mwenyewe - kama Mwana wa Mungu.

Mwinjilisti anapenda kuomba itikio la watu maraupatapo nafasi (isipokuwa, labda kwa sababu maalumuwanadhani wasingeweza kufanya). Watu wanahitajikuusikia ukweli wa Injili na hivyo wafanye jambo fulanikwa lile walilolisikia.

Katika mji fulani nchini India, kikundi cha Injiliwalitembelea gereza kila juma na kuwashirikisha Injili ya

Yesu, lakini hawakutoa nafasi kabisa ya watu kumpokeaKristo. Mwishoni mwinjilisti mgeni alikuja nakuzungumza habari za Kristo na kuwaambia watuumuhimu wa wao kumpokea Kristo. Alisema, “Ni wangapikati yetu wanapenda kuomba nami kumpokea Yesu Kristokama Mungu wako na Bwana wako?” Wengi wawasikilizaji waliitikia na kumpokea Yesu.

Ni muhimu wakaonesha itikio lao wakati wanaposikiaHabari Njema kuhusu mambo ambayo Mungu amefanyakatika Yesu Kristo. Waambie watu jinsi ya kuitikia. Nilazima watubu dhambi zao; ni lazima wamrudie Mungu nakumwomba awasamehe. Ni lazima wapokee kazi ya kafaraya Kristo na kumkubali kuwa Bwana na Mwokozi wao.Kumtaka Yesu awe ndani ya mioyo yao, ni muhimuwakajitoa kumfuata Kristo aliye Bwana.

Ujumbe Wenye NguvuNi muhimu kuamini kuwa Mungu ameagiza, anawapa

nguvu, na kubariki mahubiri ya Neno Lake kuhusu Yesu(Isaya 55:10-11; Warumi 10:14-17; 1 Wathesalonike 2:13;2 Timotheo 4:1-5). Amini hivi kwa sababu Yesu alisemambegu ya Neno huzaa mavuno na watu wataokolewa(Marko 4:26-29).

Mungu anaeleza jinsi ujumbe wa neno kuhusu Kristoulivyo na nguvu: “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwambegu, iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno laMungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Maana, mwili woteni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani.Majani hukauka na ua lake huanguka; bali Neno la Bwanahudumu milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwakwenu” (1 Petro 1:23-25; angalia pia Yakobo 1:18).

Ujumbe wa Injili ni habari yenye nguvu kubwakatika dunia. Linaweza kubadilisha moyo wa mwanaumeau mwanamke; linaweza kubadili familia, mji, au taifa.Unapohubiri na kushirikisha ujumbe wa Injili wenyenguvu, unaweza kuvuna roho nyingi kwa Mungu.

Uinjilisti unafafanua kazi ya Yesu,unaelezea ni nini maana yake kwa

watu leo hii.

Ujumbe waInjili ni

ujumbe wenyehabari nzuri

duniani.

Page 16: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

16 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

MASIMULIZI YA MAMBO YA WOKOVUmsalabani - na kuchukua hukumu ya Mungu kwaajili ya dhambi zetu

• Aliharibu nguvu ya dhambi• Alifufuka toka wafu kuonesha kuwa Yeye ni

Mungu• Anaishi na kutawala milele kama Mfalme wa

wafalmeJambo ambalo Yesu alilifanya ni kwa

ajili ya wanadamu wote. Kila mtuamefanya dhambi na anahitajikuokolewa kutoka matokeo yadhambi zake. Hili linawezakufanyika wakati mtu anapoaminikuwa Yesu Kristo alikuja na kufakwa ajili yetu na akafufuka tokakwa wafu. Kila mtu ni lazimaatubu dhambi zake na kukubalikafara ambayo Yesu alifanyaili kutuokoa kutoka kifo.Wanapofanya hivi, Munguanasamehe dhambi zao nakuondoa adhabu ya kifo kwaajili yao. Kwa njia hii

wanaweza kuwa na uhusianona Mungu, aliye Baba yetu wa

mbinguni, sasa na mpaka milele.Watu hawawezi kufanya mema wenyewe kiasi cha

kumrudia Mungu au kupata wokovu. Hata nguvu zetubora ni kama takataka ukilinganisha na utimilifu waMungu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Munguisipokuwa kukubali malipo ya Yesu aliyolipia madeniyetu ya dhambi.

Tunapomwamini Kristo kama Mwokozi na Bwanawetu, Roho wa Mungu anakuja katika maisha yetu. RohoMtakatifu anatusaidia ili tupate kumjua Mungu nakufikiri, kuamini na kuishi katika njia ya Mungu. Kwakuwa Mungu anataka kila mtu aokolewe, RohoMatakatifu anatupa nguvu ili tuwe na ujasiri wa kuwa-shirikisha wengine Habari Njema za wokovu upatikanaokatika Yesu Kristo.

Mungu amejifunua Mwenyewe katika nafsi ya YesuKristo. Pia amejifunua Mwenyewe katika njia na mpangowa wokovu kwa ajili yetu katika Biblia. Biblia ni manenoya Mungu ambayo Mungu aliwafunulia watu kuandikakwa kadri walivyoongozwa na Roho. Bibliainatufundisha lile lililo kweli. Tunaweza kuliamini nakulitumaini. Ni lazima tulisome na kujifunza Biblia maranyingi kwa kadri inavyowezekana.

Kila mtu atakufa kifo cha mwili. Lakini tunapoaminiYesu Kristo na wokovu wake, tutakaa katika maisha yamilele mbinguni na Mungu. Wale wote wanaokataamwaliko wa Mungu wa msamaha watatengwa na Munguna kuingia Kuzimuni.

Mungu ni wa milele - Yeye hana mwanzo walahana mwisho. Yeye ni Mungu Pekee wa kweli,Mwenye enzi na Ajuaye kila kitu. Anao upendo

mkamilifu, ana huruma, ana samehe, mvumilivu, nampole. Mungu ni wa rehema; tena ni Mungu wa haki.Mungu amejifunua mwenyewe kwetu kama Baba,Mwana, na Roho Mtakatifu - ni nafsi tatu za MunguMmoja.

Mungu aliumba mbingu na nchi. Katika mfano wakealiwaumba Adamu na Hawa (Eva). Aliwaweka iliwatawale vilivyoko duniani, na kuwapa Bustani nzuri yaEdeni kuishi. Mungu aliwaambia wazae na kuongezeka.Mungu aliwapenda, aliwatembelea na kuzungumza nao.

Shetani alimjia Hawa na Adamu katika mfano wanyoka, na kuwashawishikuwa kuna mambo mengikatika maisha kuliko yaleambayo Mungu aliwajalia.Huyu muongo, mwizi, namharibifu alileta changamotokwa Mungu na Neno lake, kamaalivyofanya wakati alipoleta uasimbinguni na akafukuzwa na wafuasiwake. Shetani na mapepo yake badowanafanya kazi ya kuwajaribu watuwamwache Mungu.

Adamu na Hawa wakachaguakuasi agizo la Mungu la utunzajiwake na kutokula katika mti ambaomatunda yake yangeweza kuwafanya kuona uovu.Kutokutii kwao kulifanya dhambi iingie katikawanadamu. Dhambi ni mawazo, maneno, na matendoyaliyo kinyume na sheria ya Mungu na kusudi lake laupendo kwa binadamu. Dhambi inaleta uharibifu namaumivu kwa binadamu. Dhambi inatutenga na Munguna mpango wa Mungu wa maisha yetu sasa na hatamilele.

Haki ya Mungu iliyo kamilifu inatutaka tufahamumatokeo ya dhambi, ambayo ni kifo – kimwili na kiroho.Lakini Mungu, katika upendo wake mkamilifu, amewekampango wa kumwokoa mwanadamu kutoka dhambi namauti na kutufanya tuwe na uhusiano kati ya Mungu namwanadamu ambao dhambi iliharibu.

Katika muda mwafaka katika historia yamwanadamu, Mungu alimtuma Mwana Wake wa pekee,Yesu Kristo, kutimiliza mpango wake wa wokovu kwamwanadamu.

Yesu Kristo, alikuwa na ambaye ni Mungu:• Alizaliwa na bikira, aliishi maisha yasiyo na

dhambi• Alimfunua Mungu na mpango wake wa

kumwokoa mwanadamu• Alitoa maisha yake badala ya mwanadamu - akafa

Page 17: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 17

Sehemu Ya Nne

Kazi YaMwinjilisti

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Wajibu Wa Mwinjilisti

1) Kazi muhimu za mwinjilisti ni:• kueleza habari za Yesu (Yesu ni nani na Amefanya

nini?)• kuwaita watu watubu dhambi zao.• kuwataka wamwamini Kristo• kuwaambia watu wampokee Kristo kwani ndiyo

njia pekee ya kuwa na uhusiano na MunguWainjilisti wa kweli wengi wanajisikia mzigo kwa

ajili ya giza la kiroho ambalo limewapofusha wanaumena wanawake wanaowazunguka, na ambao wamepoteana wanakwenda Kuzimu pasipo Kristo.

Wainjilisti hawajisikii kutosheka kwa kuhudhuriakanisani. Wanafahamu kuwa Mungu huwatumia ilikuwaokoa watu kutoka giza walilo nalo sasa, na kutokakatika maisha ya kuzimu milele, ambayo yameandaliwakwa wale waliomkataa Kristo (Wagalatia 1:4; Wakolosai1:13; 1 Wathesalonike 1:10).

Wainjilisti wanajisikia kusukumwa kuwaombea nakuwataka watu waliopotea (wanaweza kuwa wa taifa la

mwinjilisti au kutoka maeneo mengine ya dunia). Tenawatakuwa na hamu kubwa kuwaendea watu hawa nakuwaambia ukweli ili waokolewe. Watu wenginewanaweza kuwakatisha tamaa wasiende, kuwatia wogaau changamoto nyingine. Lakini pamoja na hayowainjilisti watakwenda, kwa sababu wanajua kuwaMungu amezungumza nao na wanalazimika kutii. Hizini baadhi ya ishara za wale walio na wito wa uinjilisti.

Mwinjilisti ni lazima ajifunze kuonesha matokeo yakuita watu wampokee Yesu na kuwasaidia wawezekuweka maisha yao yote katika kumfuata Kristo. Nilazima ajifunze jinsi ya kutoa mwaliko wa Mungu kwawatu waliopotea ili wapokee msamaha. Ni lazimawaweze kuwaongoza katika maombi ya kukiri dhambizao na kutaka Kristo awe Bwana wa maisha yao.

2) Mwinjilisti aelimishe wainjilisti wengine.Wainjilisti wengi wameonesha mafanikio makubwakatika huduma zao. Pamoja na hayo, wameshindwakupeleka elimu, ujuzi na uzoefu wao kwa wengine.Mwinjilisti anaweza kuleta maelfu ya watu, hatamakumi ya maelfu kwa Kristo. Lakini wainjilistiwatakuwa hawajatimiza utume wao kama hawatawezakuelimisha wainjilisti wapya.

Mpango wa Mungu mara zote kwa viongozi (ambaoni pamoja na wainjilisti, wachungaji, waalimu, nawengine) ni muhimu kuelimisha wengine na kuwainuawaweze kuendeleza kazi ya Mungu (Waefeso 4:11-12;2 Timotheo 2:2). Kwa njia hii kazi ya hudumainaongezeka kizazi hata kizazi.

Kama wewe ni mwinjilisti, ni yupi unamwinuakatika huduma ya uinjilisti? Ni nani atakufuata katikakazi yako? Paulo anamwandikia Timotheo, “Na mamboyale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi,hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaakuwafundisha na wengine” (2 Timotheo 2:2). Kilakiongozi anawiwa kufundisha kizazi kinachofuata nakuwarithisha hekima na uzoefu wao. Hawa walio-elimishwa, wanaume na wanawake, ni muhimuwaelimishe wengine wawe wainjilisti pia.

Uzoefu wako una thamani kwa vijana. Mwongozo

Mwinjilisti anawaandaa wainjilistiwengine.

Page 18: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

18 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

wako, ufahamu wako, na ujuzi vinasaidia kuepukamakosa na matatizo. Tumia muda wako kuelimishawainjilisti ambao Mungu amewaleta ili uwaelimishe.Nenda nao katika huduma zako. Wape masomo yauinjilisti. Wafundishe toka Biblia. Waelimishe jinsi yakufanya huduma ya uinjilisti. Kwa njia hii Ufalme waMungu unakua!

Kuna mtu huko Ulaya ambaye ni mchungaji namwinjilisti mwenye kazi nyingi. Ana kanisa lenyewaumini maelfu. Bado anatumia siku moja kila jumakuelimisha watu 12 kwa ajili ya huduma ya Injili.Anatumia masaa kuongea, kushauri, kusikia, na kuombapamoja nao. Anawapa kazi kumsaidia na hata kutoahuduma, wakati anapowafundisha. Baada ya mwaka aumiaka miwili wanakuwa tayari, anawaacha wakafanyehuduma zao. Kila mmoja kati ya hawa 12 anaanzakuelimisha 12 wengine. Baada ya miaka 2 tu watakuwawameelimishwa watu 144 ili kutumikia Mungu kamaviongozi wa Kikristo. Baada ya miaka miwili minginekutakuwa na watu 1728 ambao watakuwawameelimishwa na kuendelea! Na inaendelea hivyo.

Hii ndiyo njia ambayo Yesu aliwaelimisha wanafunziwake. Ni lazima utumie muda kukaa na wale wanaotakakuwa wainjilisti. Wachungaji, ni muhimu utafutemwinjilisti mwenye uzoefu ambaye ataweza kuelimishawengine. Ni vema akawa ni mtumishi mwenzi na rafikiwako. Wainjilisti wanaweza kuwa baraka kwa kanisalako na kwa Ufalme wa Mungu.

3) Mwinjilisti anafundisha waumini jinsi yakueneza Injili. Kazi ya tatu ya mwinjilisti ni kuelezeayaliyoko kwa Waefeso 4:11-12: “Naye alitoa wenginekuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wenginekuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji nawaalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hatakazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujenge”.

Elewa kuwa katika mistari hii viongozi wa Mungu,ni pamoja na wainjilisti, wanafundisha watu katikaMwili wa Kristo ili watende kazi ya kumtumikia Mungukatika ulimwengu. Mwinjilisti anaitwa kufundisha nakuandaa watu kwa kazi hii.

Uinjilisti ni kazi ya kila Mkristo. Mungu amewaitawainjilisti watoe maisha yao ili kuwashirikisha wengineInjili. Lakini kila muumini ajitahidi kuwaambiawengine habari za Kristo na mambo aliowatendea. Nijambo linalohitajika kuwa kila Mkristo aelimishwekushirikisha imani yake kwa wengine.

Mwinjilisti anawafundisha wengine jinsi yakuwaleta watu kwa Yesu na jinsi ya kuwashirikishawengine imani ili watu wengi waje katika mpangowa wokovu wa Yesu Kristo.

Hii ni kazi muhimu kwa mwinjilisti. Mwinjilistianaleta mwamko wa imani na kuwafanya wenginewapate hamu kutangaza habari za Kristo.Kuwafundisha wengine jinsi ya kushirikisha imaniya Kristo inasaidia wengi kukua na kuimarika. Imanikatika Kristo ni kuwashirikisha wengine.

Ni lazima uchukuemuda na wale ambaowanataka kujifunza

kuwa wainjilisti.Hayo ndiyo Yesu

aliyofanya.

Page 19: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 19

Sehemu Ya Tano

Mfano WaMwinjilisti Filipo

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Chukua dakika chache na usome mlango wa 8 waKitabu cha Matendo ya Mitume. Utaelewa kuwa Filipoalikuwa mtu wa Mungu na mwenye tabia njema. Ndiyepeke yake katika Biblia anaitwa “mhubiri wa Injili”, yaanimwinjilisti (Matendo 21:8).

Mtu Aliyewatumikia WengineMara ya kwanza tumesoma habari za Filipo katika

Matendo sura ya 6. Ni miongoni wa wahudumu saba walio-chaguliwa na kanisa la Yerusalemu kusaidia watu wenyemahitaji mbalimbali. Filipo alianza kumtumikia Mungu kwakuwasaidia maskini na wajane. Alitumika kwa sababu kanisana viongozi walimtakaafanye kazi hiyo. Filipohakukataa kufanya hudumahii ya ushemasi kwasababu, labda, hakujifikiriakuwa mkuu kuliko hudumaya shemasi. Alikuwa tayarikujinyenyekeza nakutumika pamoja nakujifunza.

Kama unataka Munguakubariki anzia paleMungu alipokuweka.Biblia inaeleza kuwaFilipo alikuwa miongonimwa wahudumu sabawaliokuwa na sifa nzurikwa ajili ya imani yao,hekima zao, na nguvu zakiroho katika Roho Mtakatifu (Matendo 6:1-6). Sifa hizonzuri za kiroho zilimstahilisha kuwapa wajane chakulamezani!

Filipo alifanya kazi yake kwa bidii, akiwatimiziamahitaji yao ya kimwili na ya kiroho pia. Tafuta kufanyakazi kwa uangalifu katika kanisa au katika hudumamahali ambapo Mungu amekuweka. Uwe macho sanakuona mahitaji ya watu wanaokuzunguka. Watumikiewanawake na wanaume ambao Mungu amekuweka juu

yao, kama Filipo alivyotumikia mitume, na viongozi wakanisa la Yerusalemu. Jitahidi kujituma mwenyewe nakuwa mtumishi mwaminifu, na wakati unafanya hivi,Mungu atakuongezea na kukupeleka maeneo menginekatika wajibu mkubwa zaidi (Mathayo 25:21; Luka 16:10).

Filipo: Mtu wa MaombiKatika Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaeleza

kuwa Filipo alikwenda kaskazini mpaka Samaria. Kwanini Filipo aende mji mgeni? Biblia inatueleza kuwaalikwenda kwa sababu ya mateso makubwa yaliyoanzaYerusalemu. Filipo angeweza kutumia muda wake

kuomba na kumsikilizaMungu na kumtakaMungu amueleze mahaliatakapokwendakuhubiri. Filipo piaangeliweza kuombeawaliokuwa wagonjwakwa sababu Bibliainatuambia kuwa wengiwaliponywa.

Fikira YaKimungu KwaAjili YaWaliopotea

Filipo alijisikiakutumwa na Mungukuhubiri Wasamaria.Hawa walikuwa tofauti

kuliko Wayahudi ambao Filipo aliwafahamu. Filipoalikwenda kwa watu wageni, ambao waliwachukiaWayahudi, kuwaambia habari za Yesu. Filipo alikuwa namzigo kwa Wasamaria ambao hawakumjua Yesu.Walimhitaji Kristo pia. Alikwenda kwa sababu Yesualimtuma. Alikwenda kuwaambia wengine habari za YesuKristo. Alikwenda kwa sababu alijua fikira ya Mungu kwawatu waliopotea. Kile ambacho Mungu alikijali, pia Filipoalikijali. Filipo alianza kuwa na moyo uliofanana na ule wa

Filipo alienda kwawatu wageni, walewaliochukua watuwake, kuwaambia

habari za Yesu.

Page 20: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

20 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Yesu, pengine kwa njia ya maombi na kumsikiliza Mungukatika maombi. Lakini Filipo hakuomba tu; bali alifanyakwa vitendo. Alikwenda kuhubiri.

Ujumbe Aliohubiri Filipo Ulikuwa MrahisiWa Kueleweka

Injili yenyewe ni wazi, ujumbe wa kueleweka. Mungualituumba sisi na anatupenda sisi. Tumetengwa na Mungukwa sababu ya dhambi. Yesu, Mwana wa Mungu, alikujaduniani katika hali ya mtu; alikufa Msalabani ilitusamehewe dhambi zetu na kutuwezesha kumrudiaMungu. Kristo alizikwa na alifufuka kutoka kwa wafu nakaburi. Dhambi na nguvu za Shetani ziliharibiwa. YesuKristo anaishi leo na ana nguvu zote. Yesu anakutakaumwamini Yeye na kumpa maisha yako. Hukumuinawangoja wale wote waliomkataa Mwana wa Mungu;baraka zisizo na mwisho zipo kwa wale waliofuata Yesu.

Huu ni ujumbe wenye nguvu na ambao unafanya kaziya kugeuza watu. Unagusa mioyo migumu na unaletatumaini kwa wale walio gizani. Kuwaambia watuinatakiwa wawe wazuri siyo Injili. Wanaume nawanawake hawawezi kuwa wazuri wao wenyewe;wanahitaji nguvu ya Yesu katika maisha yao ili wawezekushinda uovu na kuishi katika haki.

Ni muhimu kuwaambia watu kuwa Yesu anayo nguvuna anaweza kuondoa dhambi zao zote, aibu yao kwa ajiliya dhambi zao. Yesu anaweza kufanya mtu mpya kutokamfanya dhambi (2 Wakorintho 5:17). Yeye anaweza kuletatumaini kwa waliokata tamaa na nguvu kwa waliowadhaifu (Isaya 40:29; Warumi 15:13). Anaponya waliowagonjwa na kutupa mahitaji yetu yote tunayohitaji katikamaisha yetu kwa ajili ya Mungu.

Injili ni ujumbe mzuri, uliojaa matumaini na ahadi!Kama mwinjilisti mwema, Filipo alijua jinsi ya kuhubiriujumbe mwepesi ulioleta maana kwa wasikilizaji – nawengi waliokolewa.

Filipo Alipewa MiujizaMiujiza, ishara, na maajabu ni sehemu ya huduma ya

mwinjilisti. Biblia inatuambia kwamba miujiza mikubwailifanyika wakati Filipo alipohubiri (Matendo 8:6-7,13).Watu waliona miujiza na ishara zilizowafanya wavutiwekusikia maneno ya Filipo. “Na makutano kwa nia mojawakasikiliza maneno yake yaliyosemwa na Filipowalipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya”(Matendo 8:6).

Ishara ni matendo ambayo si ya kawaida kutoka kwaMungu yanayomfunua kuwa wa kweli na mwenye nguvu.Ishara na miujiza imeahidiwa kwa kila amwaminiyeKristo; wainjilisti kwa upekee wa mara nyingi wana isharana maajabu wakati wakihubiri Injili (soma Marko16:15-18).

Siku za karibuni mwinjilisti alikuwa akihubiri katikakijiji msituni. Aliwaambia watu kuwa Mungu amemtumakwao na ujumbe. Aliwaambia jinsi Yesu alivyoteswa nakufa na kufufuka siku ya tatu; na kuwa Yesu anatoamsamaha wa dhambi. Hatimaye mwinjilisti akasema, “Ilikuwahakikishia niliyoyasema kwenu ni kweli,

tutawaombea watu wote wagonjwa, na nitamwomba Yesuawaponye.” Alianza kuwaombea wagonjwa na wakapona.Mchawi alitubu na alianguka ardhini wakati mapepoyalipoamriwa kutoka katika Jina la Yesu. Watu walipoonamambo haya, walimwamini Yesu. Zaidi ya watu ishirinikatika kijiji kile walimpokea Yesu Kristo siku hiyo!

Ipo mifano mingi ya ishara na miujiza. Katika Afrika,katika kijiji cha Waislamu, kikundi cha wanawakewalipewa ruhusa ya kuwaambia watu habari za Injili.Kulikuwa na ukame mkubwa kwa muda mrefu. Kila maramwinjilisti alipozungumza na mvua ikaanza kunyesha!Kila mmoja katika kijiji, hata kiongozi wa kijiji, alikubalikuwa Mungu alikuwa anatuma baraka kwa sababu mvuainanyesha.

Wainjilisti wanatoa ujumbe wa Injili na miujizainatokea wakati wakiomba na kuzungumza. Yesu alisema,“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio...” (Marko16:17).

Kama mwinjilisti, unaweza kumuomba Mungumiujiza, na kuomba mpaka miujiza itokee. Ombeawagonjwa katika jina la Yesu wakati unapohubiri na aminikuwa Mungu atawaponya watu.

Hivyo miujiza na ishara nyingi zilifanyika Samaria namji mzima ukataharuki na kufahamu jambo hilo. Bibliainatuambia kuwa mji wote ukajaa furaha (Matendo 8:8).Mahali popote ambapo Injili inakwenda panakuwa nafuraha na shauku njema. Injili inapohubiriwa nakuaminiwa, dhambi zinasamehewa na maisha mapyayanapatikana; na hiyo ndiyo miujiza ya Mungu ikitendakazi! Mara nyingi, kuna mambo ya nyongeza kamamagonjwa yanapona, mapepo yanatolewa, na watuwanafunguliwa na kufanywa upya. Injili ina nguvu!

Siyo muda mrefu uliopita, mwinjilisti alikuwaanahubiri katika mji mmoja na mvulana mdogo ambayealikuwa kiziwi na bubu aliponywa wakati wakimwombea.

Ujumbe wa matumaini na ahadi ambaoFilipo alihubiri ulikuwa wazi na

mwepesi. Mungu ametuumba sisi naanatupenda sisi... Kristo alikufa kwa

ajili yetu... Huu ni ujumbe mzito ambaohufanya kazi ya kubadili watu.

Page 21: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 21

Mama yake akaenda kwamajirani, marafiki, nafamilia na wote wakaonakuwa aliweza kusikia naalianza kuzungumza.Usiku uliofuata watuwaliongezeka na mamaalisimama mbele nakuwaambia watu jinsimtoto wake alivyoponywa.Usiku ule watu wengiwaliyatoa maisha yao kwaYesu, pamoja na mamayake yule mwana. Baadaya ujumbe wa Injili,Bwana Mungu anatoauponyaji wa aina nyingi.Watu wengi waliamini kwasababu waliona jinsi mtotoalivyoponywa, na kundi liliendelea kuongezeka kilamara. Mamia ya watu waliokolewa kwa siku tatu. Ndivyoilivyotokea wakati Filipo alipokwenda Samaria!

Filipo Alikuwa Mwepesi KutiiYesu anajua mahali ambapo watu wako tayari kusikia

Injili. Alimtuma Filipo Samaria. Baadaye Yesu alimtumaFilipo kutoka kazi ya uinjilisti yenye mafanikio makubwakwenda kuzungumza na mtu mmoja katikati ya jangwa.

Matendo 8:26: “Malaika wa Bwana akasema na Filipo,akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njiaile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo nijangwa.”

Mwinjilisti ni lazima atumie muda wake kuendeleakujifunza kufahamu kusudi na mapenzi ya Mungu, na kutiiMungu anapomwongoza. Mipango mizuri ingaliwezakumhimiza Filipo akae Samaria, ambapo alikuwa amepatamafanikio mazuri, na watu wengi walikuwa wakimpokeaYesu Kristo. Lakini Mungu alizungumza na Filipo kwendana kuzungumza na mtu mmoja.

Tunaweza kujifunza jambo muhimu sana katika habarihii. Ni lazima kumtii Mungu. Yeye anajua zaidi mipangoyake. Mungu alijua kuwa mtu wa Kushi aliyekutana naFilipo angeamini na kuchukua ujumbe wa Injili katikanchi yake katika Afrika. Alikuwa mtu mashuhuri (alikuwana mamlaka chini ya Kandake Malkia wa Kushi). Mtuhuyu mmoja alikuwa muhimu kwa Mungu. KupelekewaInjili ulikuwa ni mpango kamili. Mtu wa Kushi angewezakuongea na taifa, na Mungu alimtuma mwinjilistikuzungumza naye.

Mwinjilisti ni lazima awe mnyenyekevu, awe tayarikuzungumza na mtu mmoja sawa na kuzungumza na kundikubwa. Azungumze na watu waliokataliwa, ambaowanaonekana hawana umuhimu, hata kwa mtu mmoja.Mtu mmoja ambaye hathaminiwi na watu wa duniaanaweza kuwa muhimu sana mbele zake Mungu.Inawezekana Mungu anachagua kiongozi mmoja ambayeanaweza kushawishi watu wengi na Mungu anawezakukutumia kwake.

Utii amri ya Munguakikutuma kwenda na

kuhubiri hata wakati watuwanazungumza mabayakuhusu wewe, au hatawakati wewe binafsi

huelewi ni kwa nini. Munguamejaa hekima na uwezo na

anawabariki wote

Wainjilisti ni lazimawawe watiifu katika witowao ambao Munguameuweka maishani mwaohata wakati ambao nimgumu au wakatimwingine watuhawaelewi. Kutii amri yaMungu ni muhimu mnokwa mwinjilisti. Utii amriya Mungu akikutumakwenda na kuhubiri hatawakati watuwanazungumza mabayakuhusu wewe, au hatawakati wewe binafsihuelewi ni kwa nini.Mungu amejaa hekima nauwezo na anawabariki

wote wanaomtii.

Uwe Tayari KwendaMwinjilisti ni lazima awe tayari kwenda mahali popote

ambapo Mungu anamtuma. Mungu anaweza kumtumamahali pageni na mahali papya. Mungu anaweza maranyingi hututuma kwa watu ambao hawatufanani.Wasamaria walikuwa hawako sawa na Filipo.Ingewezekana kuwa ni jambo geni na mahali ambapoasingejisikia kupapenda yeye mwenyewe. Hata mtu waKushi hakuwa sawa na Filipo. Lakini Filipo alikuwa tayarikwenda mahali pale Mungu alipomwita. Mwinjilisti nilazima wawe tayari kujitoa mwenyewe na kwenda mahalipale ambapo Mungu anawatuma.

Mwinjilisti mmoja ameeleza jinsi alivyokwenda vijijivingi kuhubiri Injili. Katika baadhi ya vijiji alipigwa;mahali pengine alifungiwa nje ya nyumba. Lakini hatahivyo alikwenda. Watu wengi walichagua kumwaminiYesu. Angesema nini kwa Yesu kama hakuwa amekwendakatika vijiji na watu wangekuwa hawajasikiliza ujumbe?Watu wengi katika dunia wanaangamia bila kufahamuhabari za Mungu kwa sababu hakuna mtu wa kuwapelekeaHabari Njema za Yesu.

Mwinjilisti huyo alimsifu Bwana kwani Mungualimkubali afikwe na mateso kwa ajili ya Yesu - na alimsifuMungu kwani wengi watakuwa mbinguni!

Mateso, kukataliwa, maisha magumu, na uovu kamaitikio la watu ni sehemu ya wito wa mwinjilisti. Kilamwamini ni lazima akutane na mateso wakati anapotakakuishi maisha ya kumpendeza Mungu ya kumtii(2 Timotheo 3:12). Lakini Mungu atakusaidia, atakulindana kukuongoza, na kukupa utoshelevu na tuzo katikati yamateso na maisha magumu.

Filipo alikuwa na mafanikio ya kweli.Kwa sababu Filipo alimtii Mungu na alihubiri Injili

kamili, watu wengi waliokolewa. Kila Mkristo ni lazimaamtii Mungu. Usiangalie tu mafanikio mbele ya machoya watu; badala yake kila mara jaribu kumfurahishaMungu.

Page 22: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

22 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Sehemu Ya Sita

Ishara & MaajabuNa Mwinjilisti

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Sababu Za Kumuuliza Mungu AkupeIshara Na Miujiza

1. Yesu aliwaahidi wote wamwaminio (Marko16:17-20; 1 Wakorintho 12:8-11; 13:2-8).

2. Yesu alisema wote wamwaminio watapewakufanya mambo makubwa kuliko alivyofanya (Yohana14:12-13).

3. Kristo aliondoa kazi zote za giza na mapepokatika Msalaba (Wakolosai 2:15). Aliwapa waaminiomamlaka juu ya nguvu za giza (Marko 16:17; Yohana14:12-13). Wakati mwinjilisti anapotumia mamlaka yaKristo kutoa mapepo, nguvu za mapepo zinazomtawalamtu zinavunjika na mtu anafunguliwa. Watu wengiwamefungwa na nguvu za mapepo na wanahitajikuwekwa huru kwa nguvu za Yesu. Wale wotewanaojikuta katika nguvu za mapepo wanapaswa kujuakuwa kama Mkristo, hawako chini ya nguvu za giza nahawapaswi kuishi kwa hofu.

4. Ishara na miujiza inaonesha nguvu ya kweli namamlaka ya Yesu Kristo.

5. Ishara na miujiza inasaidia kuifanya Injili iwe nanguvu pale inapohubiriwa.

6. Paulo aliona miujiza mingi wakati wa hudumayake (Warumi 15:18-19; 2 Wakorintho 12:12), kamaalivyofanya Filipo. Petro naye aliona miujiza ikifanyikawakati alipokuwa anahubiri habari za Yesu. Wainjilistiwengi na wahudumu wa Neno mahali pote dunianinyakati zote hata siku hizi wanaona Mungu akitendamiujiza wakati wanapoombea watu. Kama mwanafunzina mhudumu wa Kristo, ni vema ukafahamu na kuaminiMungu kwa ishara na miujiza kama sehemu mojawapoya huduma.

Miujiza Yaweza Kuleta MatatizoMiujiza inawafanya watu wawe na sababu ya

kufurahia na kuamini Injili. Yohana 20:30-31 inaeleza,“Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesumbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu

hiki. Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini yakwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu; na kwakuamini mwe na uzima kwa jina lake.”

Lakini miujiza inayofanywa kwa jina la Yesuinaweza isilete kila mara itikio lenye mwelekeo mwema.Yesu alipingwa wakati alipokuwa akifanya miujiza(Mathayo 12:9-14). Paulo alikutana na shida nyingiwakati akihubiri Injili na miujiza ikatokea (somaMatendo 19:9-12,23-41). Shetani anapinga Injili na kilakitu ambacho kinamtukuza Yesu aliyefufuka; watuambao hawajakombolewa hufanya hivyo pia.

Omba na kutaka ulinzi wa Mungu. Munguatakusaidia kila mara unapohubiri na kuwaombeawagonjwa na kukabiliana na mapepo. Kila maramsikilize Roho Mtakatifu na fanya kwa hakika lileambalo Roho Mtakatifu anakueleza ufanye. Usijaribukufanya kama watu wengine wafanyavyo au mitindo yahuduma za wengine. Wewe huna huduma zao. Weweuna huduma ambayo Mungu amekupa, na inaweza kuwana nguvu kwa njia ya Kristo. Fanya kwa imani lileambalo Bwana anakuonesha.

Jinsi Ya Kuanza Kuona MiujizaMoja: Mtii Mungu. Hubiri Injili pale ambapo

Mungu amekutuma. Waambie watu kuwa Yesu anawezakuwaponya na wawekee mikono na kuwaombea katikajina la Yesu; wapake mafuta walio wagonjwa, kulinganana Maandiko Matakatifu (Marko 6:13; Yakobo 5:14).Kumbuka, si wewe au karama yako inayowaponeshawatu. Ni nguvu ya Mungu inayoponesha wakati unatiikuongozwa na Roho Mtakatifu.

Mbili: Neno la Mungu lina nguvu na li hai(Waebrania 4:12) na linabebwa na mamlaka ya Mungu.Kariri mistari au milango kadha ya Biblia mara nyingikama sehemu ya tabia yako ya Kikristo. Hatimaye,wakati unapowaombea wengine, nukuu mistari yaMaandiko ambayo Roho Mtakatifu anaileta katikamawazo yako.

Page 23: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 23

Kwa mfano, kama unamwombea mtu aliye mgonjwa,unaweza kusema, “Yesu, Neno Lako linatuambia kuwa,maombi ya imani yataokoa walio wagonjwa, na Bwanautawainua wewe. Hivyo, sasa hivi, tunakubali manenoyako na tunakutaka wewe umponye na kumuinua mtuhuyu!” Kuna nguvu wakati Neno la Mungu linapo-zungumzwa.

Tatu: Uwe na imani katika Yesu Kristo kwambaYeye ndiye ambaye Biblia inasema wazi kuwa ni YeyeMwenye mamlaka YOTE, na nguvu ZOTE! Wakatitunatembea katika utii wa kuongozwa na RohoMtakatifu na Neno la Mungu, Kristo atafanya kazikwa njia yetu katika nguvu zake za mamlaka yakutenda mapenzi yake. (Mathayo 18:18-20; Marko16:17).

Nne: Ni vema ukataka sana karama ya maarifa naya hekima na ya utambuzi. (1 Wakorintho 12:8-11). Je,mtu ni mgonjwa kwa sababu amepagawa na mapepo,magonjwa ya kimwili au yote mawili? Je, kuna dhambikatika maisha yake ambayo inasababisha magonjwa?Je, mtu huyo au familia yake imeshajihusisha namambo ya ushirikina? Tegemea zaidi Roho Mtakatifukukusaidia katika kutambua sababu za ugonjwa aumatatizo, ili uweze kusema ukweli wa shida katikamaombi. Usiwe na haraka. Katika hali nyingine,kufunga na maombi ya ziada yatahitajika (Mathayo17:21).

Tano: Katika muda wako wa maombi, umwombeBwana upate kutiwa moyo ili uwe tayari kuona ishara na

miujiza. Omba kwa lugha na jieleze mwenyewe, jengaimani yako (Yuda 20).

Sita: Mwambie Roho Mtakatifu akufundishe kuhusumiujiza unaposoma Biblia. Mwambie Mungu akupewatu wengine ambao watakufundisha na kukusaidiakukua katika maeneo hayo.

Wakati unapohubiri au kuwashirikisha HabariNjema wengine, uulize kama kuna mtu mgonjwa katiyao. Waulize ruhusa kama unaweza kuwaombea.Waambie kuwa Yesu anaweza kuponya waliowagonjwa. Omba na amini kuwa Mungu atafanyamiujiza. Hatimaye washirikishe Injili na kuomba naoili wampokee Kristo.

Wakati unapoombea wagonjwa, uwe makini katikaRoho Mtakatifu. Msikilize wakati unapohudumu. Nijambo muhimu sana kumleta mgonjwa au waliopagawana pepo ili waokolewe katika Kristo kwa sababu wanayonguvu ya kupinga mipango yote ya kipepo kwa njia yaKristo tu (Mathayo 12:43-45; Waefeso 6:10-18; Yakobo4:7; 1 Petro 5:8-9).

Ishara, Maajabu, Na Miujiza Mara NyingiVinatendwa Na Wainjilisti

Katika masomo yaliyotangulia, tumejifunza kuwaFilipo alihubiri na aliomba kwa jina la Yesu. Marohomachafu yaliondoka; watu waliokuwa wagonjwawalipona.

Haya yote ni ishara zenye nguvu zinazoonesha watukuwa Filipo aliwaambia ukweli. Hivyo watu

Omba na mwambie Mungu akupe ulinzi wake. Munguatakusaidia kila mara unapohubiri na omba kwa ajili yawagonjwa na pia kemea mapepo. Siku zote sikiliza Roho

Mtakatifu na fanya kile ambacho Roho Mtakatifuamekuambia ufanye.

Page 24: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

24 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

walishangaa na kufurahia (Matendo 8:5-13).Soma tena Matendo 8:5-13, mwambie Bwana

akufundishe. Kama wewe ni mwinjilisti ambaye anamtiiMungu na anahubiri ujumbe kamili wa Injili, aminikuwa Mungu atakupa miujiza na ishara zitafuata!

Kundi la wainjilisti katika bara la Afrika waliombana walijisikia kuongozwa na Mungu kwenda katika vijijiviwili kuhubiri Injili. Walikwenda pale na kuhubiriInjili; watu wengi wakamkubali Yesu Kristo. Wanakijijiwaliwataka wainjilisti waombe mvua, kwanihapakuwepo na mvua kwa miezi mingi. Baada ya kundihili kuondoka na kwenda kijiji kingine, mvua ilinyeshakwa masaa matatu na nusu! Wanakijiji waliwatuma watuwafuate kundi hilo na kuwaambia habari hizo. Mungualiwapa ishara kijiji kizima kwamba nguvu za Mungu niza kweli na kwamba yale ambayo wainjilisti waliyasemani kweli.

Miujiza ilifanyika kila mahali Yesu alipokuwa.Miujiza ilifanyika mahali wanafunzi walipokwenda.(Warumi 15:19; Matendo 6:8). Filipo alikuwa nimwanafunzi na wewe ni mwanafunzi pia. Duniaimebadilika lakini Mungu habadiliki (Waebrania13:8). Mwambie Mungu kwa imani akupe karama yamiujiza ili kuthibitisha nguvu za Mungu na ujumbewa Injili.

Sababu Miujiza Isiweze KufanyikaMoja: Kutokuwa na imani au unashindana na

kutokuamini. Ni muhimu kuwa na imani katika Yesu nakwamba Yeye ni nani ili nguvu za miujiza ziwezekuonekana (Mathayo 17:14-20; Waebrania 11:6).

Mbili: Kama huamini kuwa Mungu anafanyamiujiza, au anaweza kukutumia kuwa wewe uombe kwamiujiza. Mungu hakuahidi nguvu zake kwa watu waliona elimu, matajiri, wasomi, au kwa watu wasemaji bora.Yesu aliahidi nguvu zake kwa watu wote, “haowaaminio” (Marko 16:16-17).

Tatu: Kama maisha yako si safi. Hukumtii Munguau unatenda dhambi. Au unakuwa na malengo ambayosi sawa, kutaka kufanya miujiza ya Mungu ili kujitukuzamwenyewe na siyo Yesu Kristo (Matendo 8:14-23). Nilazima utubu nenda kwa kaka au dada na kukirimadhaifu yako na waombe kwa ajili yako nakukuombea (Yakobo 5:16; 1 Yohana 1:9). Wahudumuwote wa Injili ni lazima waishi maisha maadilifu.(1 Timotheo 3:2; Tito 1:6).

Nne: Mtu fulani amekufundisha kuwa miujizahaifanyiki siku hizi. Una habari ambazo si za kweli.Amua kusoma Neno la Mungu na jifunze ukweli kuhusumambo ambayo Yesu alifanya na alivyosema kuhusumiujiza. Inahitaji imani kuamini Mungu na Neno Lake.Kumbuka, tunamtumikia Mwokozi aliyefufuka naasiyebadilika, “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo nahata milele” (Waebrania 13:8).

Yesu Mwenyewe alisema, “Na ishara hizizitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoapepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka;hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;

wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, naowatapata afya” (Marko 16:17-18).

Kuhusu Paulo na Barnaba, inasemekana, “Basiwakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaakatika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake,akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikonoyao” (Matendo 14:3). Mwambie Mungu akupe hayomatendo ya nguvu kwa ajili ya huduma yako iliMungu apate kutukuzwa na Ufalme wa Mungu upatekukua.

Tano: Ingewezekana umekosa taratibu au unakiburi. Huchukui muda wa kusoma na kujifunzaBiblia au kuijenga imani yako kwa Mungu. Ni marachache unahubiri au kuwaambia wengine habari zaYesu Kristo. Unataka mialiko maalum kwa ajili yakuhubiri.

Katika mambo haya yote unatakiwa utubu! Ni lazimauamue kuwa mwanafunzi mwaminifu, kuomba nakujifunza. Ni muhimu ukawa tayari kukubali kwendamahali ambapo Mungu anakutuma ukahubiri - na kwayeyote ambaye hajapata kusikia Habari Njema! Wakatitunapokuwa waaminifu katika madogo au vitu dhaifu,ndipo Mungu anatoa zaidi (Mathayo 25:23).

Inachukua muda kwa imani yako kukua katika haliitakayokufanya uamini Mungu kwa miujiza. SomaBiblia yako ili ujifunze vizuri ujumbe wa Injili. Somasehemu hii ya ujumbe mara nyingi, na masomo mengineyanayoonesha miujiza. Anza kuamini Neno la Mungu namwambie Mungu, “Ninakuamini.” Mungu anapokupanafasi kuwashirikisha wengine Injili, omba kwa ajili yamahitaji ya mtu au watu wale unaowashirikisha.Mwombe Mungu akuongoze na kukuelekeza nakukufundisha. Muda si mrefu utaanza kuona mambo yamiujiza yakifanyika. Uwe mtii katika yale yote Munguanayokuonesha, na hivyo utakua katika ufahamu naBwana Yesu atakutumia.

Vifungu Vya Biblia Vioneshavyo Ishara,Maajabu, Na Miujiza

Chukua muda kusoma, kujifunza, na kuomba kwaajili ya mistari kutoka Maandiko ambayo yanakuambiakuhusu nguvu za Mungu na miujiza, ishara, namaajabu:

Ayubu 5:9Yeremia 32:21Mika 7:15Mathayo 12:28Marko 16:16-17,20Luka 5:17; 10:18-20Yohana 4:54; 6:14; 12:9-11; 14:12Matendo 3:16; 4:7-10,16,22; 4:29-30; 8:5-13; 10:38;14:3; 15:12; 19:11-12Warumi 15:191 Wakorintho 4:20; 12:9,10,282 Wakorintho 12:12Waefeso 1:18-191 Wathesalonike 1:5Waebrania 2:2-4

Page 25: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 25

Sehemu Ya Saba

Kuhubiri UjumbeUlio Wazi Wa Injili

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Ni Mungu, kwa njia ya Roho Mtakatifu Wake,huwaita watu waje kwake Mwenyewe (Yohana 6:44). Nilazima tuombe sana, kumwambia Mungu awalete wotekwa wokovu wale ambao hawajamjua Yesu.

Lakini tutakuwa tumefanya makosa kamahatutatambua ushauri mzima wa Neno la Mungu namaagizo ya Kristo: Pamoja na kuwa Mungu atawavutawatu, ni lazima sisi tumtii Mungu na kwenda kuhubiriInjili na kuwaambia watu Habari Njema!

“Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tenawamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikiejepasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa?Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yaowahubirio habari ya mema!” (Warumi 10:14-15).

Ndiyo, Roho Mtakatifu atawavuta watu kwa wokovu.Lakini kama kifungu hiki kinavyoeleza kwa uwazikabisa, watu ni lazima wasikie habari za Yesu kabla yawao kumuamini.

Yesu aliwaagiza wanafunzi wake, “Basi, enendeni,mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatizakwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu”(Mathayo 28:19-20); “Enendeni ulimwenguni mwote,mkahubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15).

Kama jambo hili halikuwa muhimu mno kwa watukupokea wokovu, hivyo ingekuwa ni zoezi ambalohalina maana. Ni lazima tuende; ni lazima tutangaze!Watu wanaangamia kila siku ambao hawajasikia Injili.Ni kusudi la Mungu kwamba HATA MMOJAasiangamie, lakini WOTE waje na kutubu (2 Petro 3:9).Wakristo ni lazima wamtii Kristo, wafuate mfano wake–waite watu wapate kutubu na kuamini, wahubiri Injilikwa kila kiumbe kama Kristo alivyotuagiza tufanye!

Na wakati tunapohubiri ujumbe wa Injili, ni muhimuukawa rahisi na kueleweka. Tena ujumbe huo uletemaana kwa wasikilizaji. Ujumbe wa Injili ni lazimaueleweke ili watu wawe na uhakika na uamuzi ambaowatafanya.

Ujumbe mzuri wa uinjilisti ni wa kipekee kwani nikuhusu Yesu ni nani – na siyo jinsi ya kuomba, kusaidiawengine, au jinsi ya kufanya mambo mema (yale

mafundisho siyo ujumbe wa uinjilisti). Wakatimwinjilisti anapohubiri, anawaambia watu habari zaYesu Kristo na kuwaita watu kwa Yesu Kristo kwa toba.Wahubiri wengi hawajui jinsi ya kuhubiri ujumbe wauinjilisti. Ujumbe wa kiinjili ni lazima uwe juu ya Yesuna kwa nini watu wanahitaji kumpokea Yesu awe Bwanana Mwokozi wa maisha yao.

Chagua Somo La Biblia Lenye UmuhimuWake

Chagua somo la kuhubiri ambalo litaleta maana kwawatakaolisikia. Hapa ipo mifano michache kutoka Bibliaya kuhubiri ili kuwafanya watu wamfahamu Yesu Kristona wokovu ambao anatoa kwa ajili yao:

• Kondoo aliyepotea (Luka 15:4-7)• Shilingi iliyopotea (Luka 15:8-10)• Mtu ambaye Yesu alimfungua kutoka nguvu za

mapepo (Marko 5:1-15)• Mwanamke aliyemwendea Yesu kwa hitaji lake

(Luka 8:43-48)• Mwaliko uliokataliwa (Mathayo 22:1-10)• Je, jina lako liko katika Kitabu cha Uzima cha

Mwanakondoo? (Ufunuo 20:12-15)• Yesu atakuwa Mchungaji Wako (Yohana

10:2-4,26-29)• Njia mbili za maisha (Mathayo 7:13-14)• Kumwita Yesu wakati wa shida (Warumi 10:13)Kuna vifungu vya Maandiko vingi ambavyo

vitakuwa msingi jinsi ya kutoa ujumbe ulio wazi waInjili. Mwambie Mungu akupe mwelekeo wa Biblia namaisha ya watu ili unapohubiri ueleweke.

Kutoa Injili Ya UpendoBaadhi ya wainjilisti wanaanza kutoa ujumbe wao

kwa kusema, “Ni lazima uokoke! Utakwenda Jehanam!”Wanarudia maneno haya tena na tena. Hali hii yakuhubiri inawafanya watu wajione hawafai na kujengakujihukumu. Baada ya muda, wataacha kusikiliza nawakaondoka.

Maneno yako ni lazima yawavute watu. Biblia

Page 26: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

26 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

inatufundisha ni wema wa Mungu unaotuongozatufikie toba (Warumi 2:4). Je, unaweza kuwaambiawatu kwa nini ni lazima waokoke? Je, unawezakuwaambia upendo mkubwa wa Mungu, na kafarakubwa ya Yesu aliotoa kwa ajili yao? Je, unawezakuwaambia furaha iliyopo kwa kumjua Yesu? Waambiemambo watakayokosa kwa kumkataa Yesu. Waambiemambo ambayo watapata wakimpokea Yesu Kristo!

Hapa kuna mifano michache itakayokusudiakuelewa mahubiri mazuri ya kiuinjilisti:

Baadhi Wanahubiri...

“Wote ni watenda dhambi na mtakufa!”

“Ni lazima uokoke!”

“Ni lazima uwe Mkristo!”

“Usiwe mdhambi, njoo kanisani.”

“Utakwenda Jehanam!”

“Ni lazima uwe mzuri!”

“Ni lazima ubadilishe maisha yako!”

“Ninajua mengi kuhusu Mungu!”

“Sikiliza mtu mwenye nguvu zaMungu!”

Mahubiri Mazuri...

“Wote tumefanya dhambi. Hukumu ya Mungu kwa dhambi ni kifo.Yesu alichukua hukumu hii Mwenyewe. Kama utampokea Kristo nadhabihu yake kwa ajili yako, Yeye atakusamehe dhambi na kukupauzima.”

“Dhambi inatutenga na Mungu na upendo wake. Ndiyo sababuunamhitaji Yesu - alikufa na kulipia dhambi zako.”

“Unaweza kumfahamu Mungu kwa kumpokea Yesu awe Mwokoziwako.”

“Je, umechoka na dhambi na kutengwa na Mungu? Yesu peke yakeanasamehe dhambi na kukusafisha na mambo yote yasiyo haki, nakukuponya madhara yote ya dhambi.”

“Wote wanaompokea Yesu Kristo watafanywa kuwa wa Mungu nakukaa naye milele. Wale wote wanaomkataa Kristo watatengwa naMungu milele, pale Jehanam. Mungu anapenda ukae naye lakini niuamue mwenyewe.”

“Wote tumefanya dhambi mbele za Mungu. Lakini Yesu alikufaMsalabani ili tupate kusamehewa dhambi. Hatuwezi kuwa wema pasipomsaada wa Kristo.”

“Wengi wetu tunapenda kubadilika, lakini hatuna nguvu kujibadilishawenyewe. Yesu anatupa nguvu ya kubadilika, kushinda dhambi, kukataaubaya na kuwapenda wengine badala ya kuwachukia.”

“Uwezo wa kumfahamu kiakili tu Mungu au Yesu hauwezi kutuokoa.Ni lazima upokee msamaha wa Kristo na kumkubali awe Bwana naMwokozi.”

“Mimi si mzuri zaidi yako. Mimi ni mkosaji. Lakini nimempokeaYesu Kristo. Yeye amenisamehe na amenipa Uzima na Roho Wake,na sasa ninamfahamu Mungu. Niko hapa kukuwezesha nawe upatenafasi hii.”

Elewa Watu Ambao UnawahubiriaNi watu gani ambao unapenda kuwashirikisha

Injili? Je, ni wafanyabiashara? Wanawake? Wafanya-kazi? Wanafunzi? Watu muhimu? Waislamu?Wahindu? Wabudaa? Jitahidi ufahamu desturi zao,mawazo yao, na imani yao. Jitahidi kuwaelewa nakwa nini wako kama walivyo.

Unaweza kufanya hivi kwa njia mbili. Moja,jifunze kila uwezalo kuhusiana na watu hawa.Wanaishije? Nini kinawaogopesha? Wanaamini nini?

Page 27: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 27

Wana wasiwasi na mambo gani? Wana matumainigani?

Ya pili, omba na kutaka Mungu akufunulie mahitajiyao. Mngojee Mungu naye atakuelekeza kwa njia yamaneno, mitazamo, au kwa njia ya picha katika mawazoyako. Tayari Roho Mtakatifu anajua maisha yao naatakusaidia jinsi ya kuzungumza nao. Atakusaidia.Kuhubiri mahitaji muhimu ya binadamu ni njia yenyenguvu katika mahubiri ya kiuinjilisti.

Wathamini Watu Ambao UnawahubiriaMara nyingi utawahubiria wanaume, wanawake na

watoto pamoja. (Hata watoto wadogo sana wanawezakuelewa Injili na kumpokea Yesu!) Ni lazima usemekwa kuheshimu na ukweli (1 Petro 3:15). Wainjilistihawakuitwa kuwahukumu watu (Yohana 3:17). Nilazima kuwa wanyenyekevu na kukumbuka kuwa kilamtu (pamoja na sisi) tumefanya dhambi na tunamhitajiYesu - kwani hakuna aliye bora zaidi ya mwingine.Wasaidie watu watambue upendo wa Mungu kwa ajiliyao; waite katika tumaini lipatikanalo kwa Yesu Kristo.Kama ukiwaonesha watu upendo wa kweli na heshima,kwa vyovyote watapenda kusikiliza ujumbe ulio nao.

Kuzungumza Kwa KujiaminiWewe kama mtu binafsi huna lolote unaloweza

kusema ili kubadilisha maisha. Lakini ni muhimukukumbuka kuwa ni Yesu anayekutuma. Wewe nimtumishi wa kusema ujumbe wa Mtu Mwingineambaye ni Mkubwa kuliko wewe mwenyewe. Wewe nimtumishi kufanya mapenzi ya Bwana wako. Ameahidikukusaidia. Jinsi utakavyohubiri zaidi, ndivyo utakavyo-jijenga katika kujiamini. Kila mwinjilisti anafanyamakosa, lakini unaweza kujifunza kutokana na makosaili kufikia mhubiri bora. Wakati ambapo hujafanyavizuri, omba na mwambie Yesu akufundishe jinsi yakufanya vizuri. Kwa njia ya mazoezi mengi utakuwamhubiri wa Injili vizuri.

Ujazwe Na RohoYesu alikuwa mfano wa aliyejazwa Roho, Roho

alimtia nguvu (Matendo 10:38). Yesu alihubiri kwamamlaka, akitoa pepo, akiponesha walio wagonjwa, nakuwafungua waliofungwa na kuwaacha huru (Mathayo4:23; Luka 4:14-19). Yesu alikuwa mkamilifu, Mwanawa Mungu asiye na dhambi. Hata hivyo kuna wakatikabla ya kuanza huduma yake ambapo Roho Mtakatifualikuja na kumjaza (Luka 4:1; Yohana 1:32-33).

Yesu aliweka wazi kuwa wanafunzi wake – waleambao walikuwa tayari wanamwamini – walihitaji piaRoho Mtakatifu kuwajaza ili waweze kuwa mashahidiwenye nguvu (Luka 24:45-49; Matendo 1:5,8).

Ubatizo wa Roho Mtakatifu umetolewa na Yesu(Mathayo 3:11). Ubatizo huu wa Roho Mtakatifuunatenda mambo makuu katika mahubiri ya Petro nawanafunzi wengine. (Matendo 2:14-47; 3:11-26;4:23-31), na utakusaidia wewe pia kuhubiri Injili kwaujasiri zaidi.

Wakati mtu anampokea Kristo, anazaliwa upya kwakazi ya Roho Mtakatifu. (Yohana 3:5-6). RohoMtakatifu anakuja na kuishi ndani yake (Warumi8:9-11). Hata hivyo, Kristo anajua kuwa tunahitajinguvu Yake ili tuweze kukamilisha mapenzi Yake katikadunia hii. Hivyo, Yesu ametuahidi kujazwa na RohoMtakatifu na kufurika (Yohana 7:38-39) ili tuwezekupakwa mafuta katika huduma (Luka 24:49; Matendo1:8).

Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulitokea kwa wauminiwale waliokwisha kumwamini Kristo kama Mwokoziwao (Matendo 2:1-4). Haya yalitokea baadaye kwawengine pia, ambao walimpokea Kristo na kubatizwakwa maji, lakini walikuwa bado Roho Mtakatifuhajawajilia juu yao. “Na mitume waliokuwakoYerusalemu, waliposikia ya kwamba Samariaimelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro naYohana; ambao waliposhuka, wakawaombeawampokee Roho Mtakatifu; kwa maana badohajawashukia mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwajina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juuyao, nao wakampokea Roho Mtakatifu” (Matendo8:14-17).

Je, Roho Mtakatifu amekushukia kwa nguvu? Je,unataka kuwa na ujasiri zaidi wakati unapohubiri nakuzungumza juu ya Yesu? Kama Yesu Kristo ni Bwanana Mwokozi wako, hivyo karama ya Roho Mtakatifu ikokwako (Matendo 2:37-41). Nguvu ikuwezeshayo kuwana ushuhuda ufaao wa Yesu inakuja wakati unapokeaubatizo wa Roho.

Kupokea Roho MtakatifuUnapokeaje Roho Mtakatifu? Kwanza, hakikisha

kuwa maisha yako ni safi mbele za Mungu. Kiri dhambiyoyote inayofahamika na kutubu mbele za Mungu.Mwombe Mungu akuchunguze, na kwa njia ya maombiyakiri mambo yote aliyokuonesha.

Baadaye mwambie Yesu akujie kwa njia ya RohoMtakatifu na kwa nguvu. Anza kumsifu Yesu Kristo.Biblia inatufundisha kuwa unaweza kuanza kwakusema kwa lugha nyingine ambayo hujapatakujifunza, kama ilivyotokea kwa wanafunzi (Matendo2:1-4; 10:44-46). Usikatishwe tamaa kama itatokeakuwa huanzi kusema mara moja. Chukua mudaumwabudu Bwana Yesu na mwambie akupe RohoWake Mtakatifu.

Kama unamjua mtu ambaye ameshajazwa na RohoMtakatifu, mwambie mtu huyu aweke mikono juu yakona kukuombea (Matendo 8:14-17). Mungu anajibumaombi! Ni Yesu alituambia kuwa tunahitaji kupewa -hivyo omba nawe utapokea kama Yeye Mwenyewealivyoagiza.

Uendelee Kujazwa Na Roho MtakatifuTunahitaji kujazwa Roho Mtakatifu kila mara na

kwa upya. Biblia inaelekeza waumini kuwa, “...balimjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi nanyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia

Page 28: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

28 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Babasikuzote…” (Waefeso 5:18-20). Ni wazi kwambamaelekezo haya siyo jambo la wakati mmoja, lakini nijambo la wakati wote. Ni lazima liwe linatokea marakwa mara. Neno la asili la Kiyunani (Kigriki) la“kujazwa” limetafsiriwa “kuendelea kujazwa” - jambolinaloendelea na kufanywa upya kwa njia ya RohoMtakatifu na Mungu.

Tunahitaji RohoMtakatifu akae ndaniyetu kama Wakristo -ili atupe faraja,atuongoze, nakutufundisha.Tunahitaji pia RohoMtakatifu atujie nakutupa nguvu katikahuduma yetu. Natunataka RohoMtakatifu kuendeleakutujaza - ili kutupaupya na kutusaidiakuiwezesha mioyoyetu na midomokujazwa na sifa,nyimbo, na shukrani!

Kuamini Mungu– TumiaKarama Zako

Mwinjilisti mzurianategemea nguvu zaMungu na hekimazitende kazi ndaniyake. Matokeomazuri ya uinjilistihayatokani na uwezoau kipawa chetu chakiasili. Munguanatumia mamboyetu ya kawaida,lakini Mungu anataka umwamini Yeye - kwani ni RohoMtakatifu peke yake awezaye kuleta ushawishi kwawatu (Yohana 16:8). Wajibu wa mwinjilisti ni kuwamwaminifu kuwashirikisha Injili, hivyo atalazimikakumwamini Bwana kwa matokeo yake.

Mungu anatoa karama na vipawa kwa watu nawahubiri wenye hekima wanaovitumia kwa utukufu waMungu (1 Wakorintho 10:31). Mungu anatutazamatutumie vipawa kwa uwezo tulio nao (Mathayo25:14-28). Mungu amefanya kila mtu na upekee wake.Analo kusudi la kutuumba sisi kwa jinsi tulivyo nahakuna anayeweza kufanya kama tufanyavyo. Siyojambo la hekima kuiga wahubiri wengine; wanao wajibuwao wenyewe wa kutimiza. Hata hivyo, unaweza kupatamawazo kutoka kwa wahubiri wengine na kuyatumiakatika ujumbe wako, utumie njia zako, unapowa-shirikisha ukweli wa Yesu.

Hubiri Kwa Ajili Ya TobaNi muhimu kwa mwinjilisti kuwaambia wanaume na

wanawake kwamba ni lazima wabadilishe mwelekeo wamaisha yao. Wanatembea katika njia ya uharibifu; nilazima wageuke na kumfuata Yesu (Mathayo 7:13-14).Waite watu wabadilishe mwelekeo (watubu), kutokakufuata njia zao wenyewe na kufuata njia za Mungu.Hubiri na kuweka ujumbe wazi kwa watu kwamba ni

lazima waamue ninani wanatakawamfuate. Kunauchaguzi wa ainambili tu: kumpokeaYesu Kristo nakutembea katika njiazake; au kuchaguaubinafsi wao ambaoutawafikisha katikauharibifu wa milele.

Hubiri IliKugusa MioyoYao

Maisha nimagumu, makatilikwa watu wengi.Ujumbe wa Injili unatumaini la kweli nala amani na Mungu,ana msamaha wadhambi. Watuwanahitaji kufahamukuwa Munguatatembea nao katikamaisha yote kama tuwatamgeukia Yeyekwa wokovu. Hubirina kutoa upendo waMungu, wokovu waKristo, na faraja yaRoho Mtakatifu.

Hubiri ukiwaambia watu jinsi ya kumfuata Kristo.Watu wanahitaji kujua pia kuwa kuna hukumu na

adhabu kwa ajili ya dhambi. Elezea kifo cha Yesu chaMsalaba, misumari iliyopigiliwa katika miguu namikono yake, damu ilivyochuruzika katika mwili wake,Waambie jinsi Yesu alivyotundikwa juu ya Msalaba kwamasaa akiwa katika maumivu makali, jinsi alivyoteseka- kwa ajili ya kafara ya dhambi zetu, akachukua adhabuyetu juu yake mwenyewe. Elezea matukio yote; chorapicha kwa maneno yako mwenyewe. Waangalize kuwahii siyo hadithi - ni Ukweli! Waambie Yesu alifufukatoka kwa wafu kwa nguvu ya Mungu na Yeye ni haisasa. Watie moyo wafikie uamuzi wa kumchagua Kristo!

Hubiri Kuendana Na Wasikilizaji WakoNjia nyingine ya kuhubiri ni kuwakilisha hoja

yenye kufikirisha na kuitikisha hadi mwisho. Mtume

Shiriki ukweli wa Yesu!

Page 29: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 29

Paulo alifundisha hivi wakati mwingine (Matendo suraya 17).

Unataka kuwashawishi watu waone mpango sahihiwa Kristo (2 Timotheo 4:2) na ukweli wa uamuzi wakumfuata Kristo. Unafikiri na wao na kuwaleta kwauamuzi ulio sahihi.

Unaweza kuwaambia habari za faida za rohoni(lakini watu wasije wakaambiwa kumfuata Kristo kwabaraka zake tu). Kuna sababu nzuri ya kuogopa hukumuya mwisho; ni uamuzi mzuri kumfuata Kristo. Mtuanaweza kumfuata Kristo ili aondolewe aibu na hatiayake kwa sababu ya dhambi zake huko nyuma na piakuondoa dhamiri kujishtaki. Kumwamini Yesu kwakutubu kunaondoa dhambi, na hii ndiyo sababu nzuri yakumfuata Kristo.

Kwa mfano nikijua mtu ambaye anaingia katikasafari ya hatari na pengine kufa, ningependa kufikirinaye kuhusu uamuzi wake. Nitampa sababu kwa niniasiende: mvua itanyesha sana na kuosha barabaranzima; kuna wanyama wakali; kuna wezi na silaha kilamahali - kuna hatari. Nitamwambia yote ambayoyatampoteza katika safari yake; jinsi ambavyo familiayake itakavyoteseka, na mengineyo. Na huu ni ujumbemuhimu.

Ni sawa na wakati ambao unahubiri habari zakumkubali Kristo. Safari ya maisha ni hatari na inauangalifu mdogo sana. Maovu na mabaya hutokea paleambapo mwanadamu anachagua njia ya dhambi.Mwanadamu anaweza kupoteza kitu muhimu sanakatika maisha yake na tena anaweza kupoteza nafsiyake. Je? Unaona jinsi ambavyo sababu hii inasaidiamwanadamu kuweza kuona wazi maisha yake yalivyokama jinsi ambavyo hakumfuata Mungu na njia Zake.

Kwa mahubiri aina hii utakuwa umeweka wazimawazo ya uongo yanayofanya watu wafikiri kuwawanaweza kuishi bila Kristo. Unatakiwa ueleze usalamawa kitambo tu wa maisha yao, pengine ipo katika fedha,familia, mafanikio, au tambiko fulani katika dini.Sisitiza kuwa kila mtu ana uwezo wa kuchagua juu yamaisha yake, na pia kuwa matokeo ya milele katikachaguo afanyalo. Kama wanakataa kuchukua uamuzi nikuwa wamekwisha kumkataa Kristo kwa kutokupokeawokovu anaoutoa.

Tumia Picha Na Hadithi Katika MahubiriUnapohubiri unaweza ukatumia picha za maneno za

maisha ya kila siku zenye kuhusiana na watuunaozungumza nao. Yesu alifanya hivyo alipokuaanazungumza katika mifano na mafundisho yake. Neno“mfano” maana yake ni “kulinganisha”, kuchukua kitukimoja mbele ya kingine na kuonesha jinsivilivyofanana.

Yesu alizungumzia mashamba, wanyama, fedha,kula chakula, kazi za shambani, watoto wakicheza(Mathayo 11:16-19; 13:1-32; 20:1-16; 22:1-14;25:14-30; Luka 15:4-7). Wakati Yesu anasema, “Mimindimi mlango” (Yohana 10:9), kila mmoja alimuelewaana maana gani. Waliweza kuona mlango katika

mawazo yao. Yesu alitumia vitu vinavyoeleweka kamapicha kuonesha kuwa alikuwa Yeye ni njia pekeekumfikia Mungu.

Kuna mifano mingi, habari, na picha katika Bibliazinaweza kuchora ujumbe kwa wasikilizaji wako, zenyekuonesha upendo wa Mungu, hali ya watu kupotea, naukweli wa wokovu:

• Shilingi iliyopotea (Luka 15:8-10)• Msamaria Mwema (Luka 10:30-37)• Nyumba mbili (Mathayo7:24-27)• Njia nyembamba na njia pana (Mathayo 7:13-14)• Mwanamke aliyefumaniwa (Yohana 8:3-11)• Mwizi aliyetubu akiwa msalabani (Luka

23:39-43)Mifano hii na mingine mingi itakusaidia kuhubiri

kwa picha na hadithi. Itawasaidia wasikilizaji wakowaelewe upendo wa Mungu na matumaini yake yakuwaokoa watu.

Hubiri Kwa Huruma NA JuhudiVipo vitu vitatu ambavyo Mwinjilisti anahitaji.Kwanza, ni jambo la muhimu kutambua upendo

mkubwa wa Mungu kwa watu wake. Munguanawapenda watu unaowahubiria! Amewafanya YeyeMwenyewe kwa ajili Yake, na kuchagua kuwapendawote. Hapendi watu hawa waishi katika dhambi, kuishikatika maisha ya giza na maumivu, kuitumikia miunguya uongo, na kutengwa na Yeye katika maisha haya hatamilele. Siyo mapenzi Yake hata mmoja aangamie(2 Petro3:9).

Upendo wa Mungu kwa wasikilizaji wako uujazemoyo wako. Mungu aliangalia umati kwa huruma kwasababu aliona jinsi walivyopotea na hali waliyo nayo(Mathayo 9:36-38). Hii ndiyo huruma ya Mungu.Huruma ni pale mhubiri anapoguswa kwenda katikakina kumsaidia aliyepotea. Ni zaidi ya kusikia huruma.Ni hali ya kuona kuwa rehema za Mungu zinapatikanakwa ajili yetu ambao hatukustahili. Unatakiwa uwe naupendo wa namna hiyo kwa watu waliopotea nawanaoangamia.

Pili, unahitaji mawazo ya Kristo (1 Wakorintho2:11-16). Yesu anajua nini kuhusu watu hawa? Yeyeanajua wanachohitaji, jinsi ya kuwasaidia ili wawezekumjua Yeye. Yesu alizungumza kuhusu mambo yandani kabisa moyoni mwa mwanamke kisimani.Alijieleza hali yake na akamwambia yale anayohitajikuyasikia ili kumleta katika wokovu (Yohana 4:7-42).Yesu atakusaidia ujue unayohitaji kuyasema. Anajuamahitaji ya watu na wanachotaka, madhaifu yao na hofuzao. Muulize Mungu akupe hekima kwa sababu anatoakwa wote wanaotaka (Yakobo 1:5).

Tatu, kila mwinjilisti anahitaji nguvu na juhudi zaRoho Mtakatifu (angalia “Kujazwa na Roho Mtakatifu”hapo juu). Wanahitaji nguvu na juhudi ya Mungu rohoniili kuhubiri Habari Njema.

Juhudi ni kujisikia kwa uzito, kuwa na mzigo,upendo usio na mpaka, na matakwa makali. Kuwa najuhudi kwa ajili ya mambo ya Mungu kunamfanya

Page 30: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

30 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

muumini amfuate Mungu na awe tayari kutendamakusudi ya Mungu. Hali hii ni kama moto wakatimwinjilisti anatumia muda wake kuomba na kuwakatika uwepo wa Mungu, na anapojifunza Neno laMungu.

Unapokuwa na juhudi kwa Injili, unakuwa na ujasiriwa kueneza ukweli kuhusu Yesu na mambo yaliyopoyanaouzunguka ulimwengu. Unashawishika kuwa lileulisemalo ni kweli na muhimu.

Roho Mtakatifu atakupa nguvu na uhai katikakuhubiri kwako, na kukujaza na mzigo wa huduma kwaajili ya waliopotea. Tafuta huruma za Mungu kwa ajiliya watu na hii itakusaidia kuwa mnyenyekevu na kuwatayari mbele za Bwana.

Wakati mwingine mwinjilisti lazima aongee kwaushujaa na bila woga kuwatangazia watu kwambawamepotea katika dhambi. Lakini kila wakati kumbukakwamba huruma na upendo wa Mungu umekugusa nakukuokoa wakati ulipokuwa mdhambi. Neema niupendeleo wa Mungu ambao haupatikani au hatustahili.Tunapewa bure. Toa neema na huruma hiyo kwawasikilizaji wengine wa Habari Njema. Uwe shujaa, bilawoga katika Mungu, na mwombe Mungu akujazehuruma kwa ajili ya wanaokusikiliza.

Toa MwalikoMwinjilisti huhubiri Injili, akiwaita watu watubu na

kumfuata Yesu. Kila wakati maliza mahubiri kwakuwatia moyo wanaokusikiliza ili wafanye uamuzi juuya wanachosikia. Huu ni mwaliko wa wasikilizajikuitikia katika ujumbe wa Injili.

Mwitikio unaweza usiwezekane; lakini kamaunaweza, uwaombe wasikilizaji kuamua kamawatakaomkubali Kristo. Wakati unahubiri umati wawatu au katika chumba kilichojaa watu, mwinjilistiaweza akasema:

• Ni wangapi wameelewa ujumbe wa Mungu?• Ni wangapi kati yenu wanataka kuomba Yesu

msamaha wa dhambi zao?• Wapo watakaotoa maisha yao kwa Yesu na kuishi

naye?• Nani atatubu dhambi na kumkubali Yesu Kristo?• Nani anataka kumpokea Yesu Kristo kama Bwana

na Mwokozi wake?• Ni nani atachagua kumfuata Yesu?Waweza kuwaambia kuonesha matumaini yao kwa

kunyoosha mikono, kusimama, kuja mbele, au kutoamaamuzi yao kwa waliokaa karibu. Waambie wachukuehatua ya kuonesha wanajitoa kwa Yesu. Nenohuwashauri wanaoamini kutokuwa na aibu kukiri wazina kumfuata Yesu Kristo (Mathayo 10:32-33; Warumi10:9-13).

Waume na wake lazima wajue kwamba wanafanyamaamuzi; lazima wapaswa kujua wafanye nini. Uwewazi kabisa, hivyo hawatachanganyikiwa na kufikirikwamba labda wanajiunga tu na kanisa au wanatoasadaka aina fulani za kidini. Elezea wazi nini maana yakumpokea Kristo kama Mwokozi wao.

Wakati Wote Omba Na Wale WanaoitikaWakati watu wanaonesha kutamani kumpokea Yesu,

kumkubali Yesu kama Mwokozi na Bwana, waombewasali pamoja nawe. Ni vizuri wasali kwa sauti,wakirudia sala yako. Hii yaweza kuwa ngumu kwawengine, lakini watie moyo kushiriki. Ni rahisi kwakokusali kwanza na kuwaambia warudie maneno yako.Tumia sentensi rahisi na ufanye sala zako kwa kifupi.

Huu ni mfano wa sala unayoweza kusali na walewanaoitikia ujumbe wa Injili:

“Mpendwa Bwana Yesu, naamini wewe ni Mwanawa Mungu. Naamini ulikufa Msalabani kwa ajili yangu,ili uondoe dhambi zangu. Naamini ulifufuka katikawafu. Mimi ni mdhambi. Natubu dhambi zangu zote.Natubu kwa kuishi maisha yangu kwa mapenzi yangumwenyewe. Naomba unisamehe na uondoe dhambizangu zote. Nioshe na unitakase. Niokoe, Yesu Kristo,na unipe maisha mapya. Ingia moyoni mwangu, naunifanye niwe Wako. Asante kwa kuniokoa. Nakuchaguauwe Bwana wangu, nikufuate Wewe siku zote za maishayangu. Nashukuru kwa uwezo wa kumjua Mungu.Asante kwa kunipa Roho Mtakatifu Yako. Niwezesheniishi kila siku kukupendeza Wewe. Amina.”

Baada Ya Watu Kumkubali KristoTumia muda kuwasaidia watu kuelewa walichofanya

kwa kumkubali Kristo. Waambie, “Sasa mmekuwa waYesu. Mmekuwa sehemu ya familia ya Mungu. Yesuatawawezesha kuishi maisha hayo. Yesu yupo karibunawe kila wakati. Unaweza kuongea naye kwa sala namaombi, kama tulivyofanya hapa. Hakikisha kwambaunapata Biblia na kuisoma kila siku. Hii itakusaidiakujifunza juu ya Mungu na jinsi ya kuishi naye.”

Katika mikutano mengine au makanisa, baada yawatu kumpokea Yesu kama Mwokozi na Bwana wao, nivizuri kuchukua muda kidogo na kuwaombea. Watubukwa maneno yao wenyewe. Wakatae uhusiano namambo maovu, vitendo, au watu - kama uchawi,kuabudu mashetani, au kujihusisha na dini za uongo.Kukataa maana yake ni kuacha kutii au kuacha kufuatajambo. Wakati watu wamekataa maovu katika maishayao, unaweza kuwaombea na kuamrisha nguvu za gizakutoka, katika Jina la Yesu. Ombea ulinzi wa Mungukatika maisha yao.

Mifano ya sala hizo:Muumini Mpya: “Yesu Mpendwa, nakataa dhambi

ya ____________ (uchawi au dhambi zingine). Nakataakushiriki katika nguvu za giza na nachagua kukutumikiaWewe kama Mwokozi na Bwana wangu. Tafadhalinifanye huru katika maovu sasa nikikuita. Asante Yesu.”

Mwinjilisti: “Baba Mungu, natumia mamlaka yakokupitia Yesu kuamrisha kila nguvu ya kuzimu na rohowachafu kumwacha mtu huyu na nyumbani kwake,familia yake na maisha yake yote. Nasema kwambadamu ya Yesu Kristo imemfanya huru. Nakuombauwalinde katika njia zote. Asante, Baba, katika Jina kuula Yesu. Amina.”

Baada ya watu kumpokea Yesu ni vizuri kuwaombea

Page 31: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 31

kujazwa na Roho Mtakatifu (angalia “Kujazwa naRoho” hapo juu). Kama tulivyojifunza, Roho Mtakatifuhuja na kukaa kwa kila mmoja anayekiri Yesu Kristokama Bwana naMwokozi wake.Lakini Yesu ametoakwa kila anayeaminikipawa cha RohoMtakatifukuwashukia na kuwamashahidi wake.Waombee wapokeehiki kipawa.Wanaweza wakasalikatika lughawasizozijua.Waelekeze waeleweni vizuri kusemakatika lugha mpya.

Ubatizo WaMaji

Bibliainamwamuru kilamuumini katikaKristo abatizwekatika maji (Mathayo28:19; Matendo2:38). Mtie moyokila anayekubalikumpokea Kristoabatizwe katika maji.Hii inawezakufanyika kanisaniau mahali popotepenye maji (mtoni,baharini, bwawanin.k.). Unawezaukawabatiza auukamtumiamchungaji aukiongozi wa kanisa unayemwamini kuwa anawezakuwabatiza waumini wapya katika maji.

Kanisa Kama FamiliaMwisho, utawaongoza watu hawa katika kanisa

ambalo litawafundisha na kuwatunza. Kama hakunauwezekano unatakiwa uwafundishe hadi mchungaji aumwalimu aje. Paulo alifanya hivi katika Matendo14:20-23. Watakuwa pia wanahitaji Biblia kusoma nakujifunza kwayo. Jitahidi uwape waumini wapya Bibliayao wenyewe, angalau Agano Jipya.

Mtumaini Mungu Katika MatokeoAmini kuwa Mungu atawaleta watenda dhambi kwa

Yesu. Bwana alisema kwa Paulo, “...Usiogope, balinena, wala usinyamaze …kwa maana mimi nina watuwengi katika mji huu” (Matendo 18:9-10). Amini nguvu

Chukua muda kumgojea Bwana!

za Roho Mtakatifu aliyeko ndani. Uamini ukweli nauhakika wa Neno la Mungu na Injili ya Yesu Kristo. Nineno lililo hai na lenye nguvu! Kumbuka kuwa ni

Mungu pekee ndiyeanayeokoa; wewe nimhudumu unayebebaujumbe wake katikamaagizo ya YesuKristo. Munguanatamani watu wotewaokoke na piawamwamini Yesuzaidi ya jinsi weweunavyotamani(2 Petro 3:9).

Kunapokuwa namatokeo kidogounaweza kufanyamambo mawili.Kwanza kabisa, nendakwa Mungu kwamaombi na zungumzanaye kwa haliuliyonayo. Chukuamuda wa kusubiriMungu. Mwacheakushtue kama kunajambo ambaloanatamani weweulielewe. Pili,mwambie Munguakufundishe, jinsianavyopenda weweuhubiri Injili yake.Mungu atakaponenanawe, uitikie! Munguatakufundisha, na piaatakupa waalimu.Unapofanya mapenziya Mungu kwa uwezawako wote, mtumaini

kwa mafanikio. Wakati mbegu zinapoingia ardhini zinazaamatunda. Unaweza au usiweze kuyaona mafanikio yake.Jambo muhimu ni kumwamini Mungu na Neno Lake.

Haimaanishi matokeo uyaonayo, msifu Mungu nakumpa shukrani. Mungu anastahili sifa zetu zote naheshima yako, muda wote, kila mara. Watu wataitikiaujumbe wako, mpe Mungu sifa. Ni Mungu anawakarimuwainjilisti; ni Neno la Mungu linaloleta uzima; ni Rohowa Mungu ndiye analeta watu kutubu. Mwinjilisti nikama mhudumu mtiifu kwa kazi hii kubwa ya Mungu!Ni heshima gani ambayo Mungu ametuitia kuihubiriInjili na kushiriki kuleta ukweli wa Yesu Kristo kwawengine. Wale wanaojitwika utukufu (kujisifu) waowenyewe ni wanyonge na pia ni wajinga ambaowamekumbatia dhambi ya majivuno. Ni Mungu pekeeambaye anamwokoa mwanadamu. Hivyo mpe Mungusifa ZOTE (Zaburi 115:1)!

Page 32: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

32 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Sehemu Ya Nane

MunguAnavyomuandaaMwinjilisti

Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!

Mungu Anataka Ujitoe Moja Kwa MojaWakati Yesu anapokuwa Bwana wa maisha yako,

anakuwa Bwana wa kila kitu. Mipango yako, vipawavyako na ujuzi, mawazo yako, kujisikia kwako, familiayako, mwili wako, maisha yako - vyote hivi ni vya YesuKristo na si vyako. Kama hujampa Yeye mambo yote nakila kitu, kutoka katika moyo wako, afanye kamaatakavyo, fanya hivyo leo. Mwambie Mungu kwa njiaya maombi.

Hivyo kila siku omba Roho Mtakatifu akuchunguze

na aletaye kukusadikisha.Mwache Mungu akuoneshemambo unayoyahitaji kupata aukuacha ili uweze kujiachia kwaMungu kikamilifu. Ukiri nakutubu pale unapotambua kuwaumefanya dhambi au makosa,ubinafsi au tamaa za mwili.Uwe na nidhamu na mwili wakoili uweze kuwa mwanafunzi waYesu mwenye nguvu. Bibliainatuambia, “Basi nyenyekeenichini ya mkono wa Mungu uliohodari...” (1 Petro 5:6).

Mambo yafuatayoyatakusaidia kujipima katikamaisha yako. Hizi si sheria aumambo ya nje ya kujihakiki. Hiini njia ya uaminifu yakujitathimini maisha na hudumayako kutoka katika moyo.Maswali haya yana lengo lakukusaidia ukue katika maishayako na kuwa chombo kizurikatika mikono ya Mungu. Uwemwaminifu mwenyewe; na zaidisana, uwe mwaminifu kwaMungu. Hatuwezi kumdanganyaMungu. Anajua yaliyomo

moyoni na anaona kila kitu katika maisha yetu. Ni vemakila wakati kumkaribia Mungu kwa unyenyekevu,kumtaka akusaidie kwa neema ili tuweze kukua na kuwaimara na kuwa mtumishi mwaminifu Kwake.

Kama baadhi ya mambo hayo si ya kweli kwako,lakini unataka yawe yako, mtake Mungu akusaidie. Nachukua hatua ya kuyatenda! Inasemekana kuwainatupasa tutoe muda kwa mambo yenye umuhimu.Kama mambo haya ni muhimu kwako, ni lazima uanzekutoa muda kwa ajili hiyo.

Page 33: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 33

Mambo Yamfanyayo Mwinjilisti Kukua• Je, mnatumia muda muafaka kwa maombi nakujifunza somo la Biblia kila siku?• Je, ninachukua muda wa kumsikiliza Mungu,kungoja ili azungumze na kuyafunua mawazo yakena mpango kwa ajili yangu?• Je, ninamwomba Roho Mtakatifu achunguzemaisha yangu? Je, ninakiri dhambi zangu kilamara?• Je, ninajifunza Biblia na kupanga vizuri hubiriambalo nitalifanya?• Je, ninajaribu kusahihisha mazungumzo,muonekano, elimu ya Biblia, na ujuzi wangu?• Je, nitakapokwenda kuhubiri, nina wauminiwengine pamoja nami?• Je, nimemwomba Mungu aongeze hudumaaliyonipa kwa upako na nguvu?• Je, nimejazwa na uwezo wa Roho Mtakatifukama ilivyo katika Matendo ya Mitume sura ya 2?• Je, ninao watu wanaoniombea kila siku katikahuduma yangu na kwa ajili yangu, kipekee wakatininapokwenda kuhubiri au kuwashirikisha wengineInjili?• Je, ninaomba kwa ujasiri ili kuwa mhubiri mzuriwa Kristo?• Je, mmefunga na kuomba kwa mwezi huu?• Je, ninajua Biblia isemavyo kuhusu kuomba nakumwamini Mungu kifedha, ili Mungu awezekutoa mahitaji kwa familia yangu NA hudumayangu?• Je, ninaye mshauri kunisaidia? Je,nimemwambia Mungu anipe mtu wa kunifundisha?• Je, kuna mwanaume au mwanamke ambayenaweza kumwomba anisaidie kwa muda wake nakunisaidia katika huduma yangu?• Je, nimeomba na kumwambia Mungu anioneshemwanaume au mwanamke ambaye nawezakumuandaa na kumsaidia katika uinjilisti? Kamandivyo, ilivyo je, ninafanya nini katika hilo?• Je, nina nidhamu nzuri katika njia zangu aumimi ni mvivu?• Je, ninatumia muda wangu vizuri na mwenziwangu na watoto?• Je, ninachelewesha kuanza kazi au ninafanyakazi kwa bidii, kutunza wito wangu na kuheshimuneno langu?• Je, mawazo yangu ni mazuri? Je, mawazo yanguyapo kwa Mungu?• Je, ninasoma Biblia na vitabu vingine vyaKikristo kunisaidia mimi kukua?• Je, ninafanya kazi na wachungaji, kuwasaidiakulijaza kanisa au kuanzisha kanisa lingine?• Je, nimesoma na kuelewa - na pia ninafuata -yasemayo Maandiko kuhusu wale walioitwa katikauongozi katika kanisa la Kikristo (1 Timotheo3:1-13; Tito 1:5-9)?Tumia mistari hii kujisaidia wewe - na wainjilisti

wengine - jikumbushe na pia kutia moyo.

Dhamani Ya Kuwa Mwinjilisti MzuriSiyo rahisi kuwa katika huduma, bali zawadi ya utii

wa wito wa Yesu Kristo ina thamani kuliko dhiki.Kuwaona watu wanakuja kwa Kristo ni zawadi kubwatunayoweza kuwa nayo duniani. Biblia inatufundishakuwa “mwenye hekima huvuta roho za watu” (Mithali11:30).

Zipo zawadi za kipekee za milele zinazowasubiriwalio watiifu na wenye imani katika Kristo. Kwa walewanaowashawishi wengine kwa ajili ya haki, Daniel12:3 anasema, “Na walio na hekima watang’aa kamamwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutendahaki watang’aa kama nyota milele na milele.”

Tunda la Injili na kuwaambia wengine habari zaKristo ni tunda la milele ambalo litadumu milele.Mungu siku zote atawafariji na kuwazawadia walewanaomtumikia na imani na utiifu wa moyo.

Yesu anaelewa vizuri, na zaidi ya wengine wote,majaribu na vikwazo ambavyo tunakutana navyo katikamaisha tukiwa wafuasi Wake. Lakini tuna mfano Wakemzuri na tutashinda, “tukimtazama Yesu, mwenyekuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwaajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimilimsalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wakuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2).Furaha ya Kristo inajumuisha uelewa kuwa kifo chakekitaturudisha katika uhusiano wa Mungu, aliye Baba –Baba yetu wa mbinguni! Sisi waumini ni furaha kwaKristo, ni Bibi Arusi mtarajiwa kwa hamu kubwa(Waefeso 5:25-27; Ufunuo 19:7-9). Kuwaleta wenginekwa Yesu ili waokoke kupitia Yesu Kristo kutuleteefuraha pia.

Kukamilisha wito wa Mungu maishani mwakokutakugharimu sana. Kila muumini ana gharama zake:kuacha utajiri, uchoyo, na matendo ya mwili - nakubadilishwa tufanane na Yesu.

Unapotoa maisha yako kuishi maisha ya sadaka kwaajili ya Kristo, utafanya zaidi ya yale ambayo Babaanafanya. Utaona nguvu zaidi za Mungu na uwepo wakekwako. Unapoendelea kuwa mwenye nidhamu namwenye imani, utakuwa mwenye ujuzi wa kuziokoaroho zinazopotea na kuwa mvuvi wa watu (Mathayo4:19). Utakua katika hekima, na kuwa tajiri katikamambo ya Mungu. Kumtumikia Mungu kwa maishayako kuna thamani kuliko gharama yoyote(1 Wakorintho 9:19-22)!

Maisha Ya Binafsi Ya MwinjilistiMwinjilisti – kama muumini yeyote, anajitahidi

kuishi maisha safi na yenye mwelekeo mbele zakeMungu. Ni lazima awe na uhusiano mwema na familiayake na jamii yake. Matunda ya mwili kama hasira aukuhukumu, itaonesha vibaya wakati unapohubiri.Kumtendea mkeo au watoto mambo yasiyo memahalimfurahishi Mungu, na linaathiri ushuhuda wako kwawengine. Kudanganya mtu kunatoa jina mbaya kwa ajiliya Kristo, ambaye unamwakilisha. Kusema nitafanyajambo fulani na hatimaye usifanye si jambo la uaminifu

Page 34: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

34 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

na si la Kimungu. Tabia yako ya kutenda dhambi nilazima ishughulikiwe ili uweze kumwakilisha Kristokama alivyo na mambo yatendwayo na nguvu yake yakukomboa!

Mwinjilisti apende Biblia na aisome na kujifunza.Atafute nafasi itakayo-mwezesha kuwa-shirikisha ukweli waBwana, lakini asiachewajibu wake wa kutunzafamilia au kazi yake yaasili. Mwinjilistianaomba sana - katikabasi, anapotembea, akiwakatika jumuia ya watu,au akiwa peke yake,daima ni vema kuombana kumsikiliza Mungu.

Moyo wa mwinjilistini lazima uwe laini na wakufundishika. Wakatiunapomngojea Mungu,atakusaidia umfahamuzaidi. Wakati unapokuakatika kumjua zaidi,utakuwa mwinjilistimzuri kwa sababuunamfahamu Baba yako.Yesu alifanya tu yalealiyofanya Baba; alisematu yale Baba aliyosema(Yohana 5:19; 8:26).Shabaha yetu kama wahudumu ni kumjua Mungu kwakaribu ili tuweze kuongozwa kwa sauti yake na kujuamapenzi yake.

Kama umeolewa ni lazima umwangalie mwenziwako kama ambavyo Yesu angemwangalia, nakuwapenda kama alivyolipenda Kanisa (Waefeso 5:25).Mtunze mkeo kwa upole na kwa ufahamu (1 Petro 3:7)Mjali mumeo kwa heshima na utii (Waefeso 5:33).

Kama hujaolewa lazima uwe na mawazo mazuri namwili safi (1 Wathesalonike 4:3-5). Bwana anajua yoteuyatendayo kwa siri zaidi ya masikio na macho ya watuwengine. Mhudumu ambaye hajaoa au kuolewaanapaswa kuwa na mawazo na matendo maadilifu. Nilazima wakiri makosa yao na kujiweka mbali na vifungovya tabia ya dhambi.

Katika mahusiano ya kibiashara, kifamilia, kikanisa,au kirafiki ni lazima yasiwe na lawama ili kazi ya Yesuisiwe na kipingamizi au isemwe vibaya. Wengi wetutumesikia watu wakipinga wokovu wa Yesu kwa sababuya muumini wanayemfahamu hakuwa mpole, haaminiki,au si mwaminifu. Wamekuwa “kikwazo” kwa sababu yamatendo ya dhambi ya waumini (1 Wakorintho10:32-33).

Kama mhudumu unamwakilisha Mfalme wawafalme. Maneno yako lazima yawe kweli; ni lazimautende yale yote uliyoyaahidi. Kama huwezi kwa

maneno yako, na badala yake unatoa udhuru, inawezakuwa kikwazo kwa wengine, na kuwafanya wampingeKristo. Mnawakilisha Yesu kila dakika katika kila siku,siyo tu wakati unahubiri, lakini katika kila tendo.Maneno yako yawe ya kutia moyo, na siyo yaliyojaa

lawama (Waefeso4:15,29; Wakolosai 4:6).

Mungu anatamanituwe vyombo vyaheshima (2 Timotheo2:21). Huwezikuwaandalia wageniwako katika vyombovichafu. Ungependauwape chakula katikavyombo safi. Munguanapokea heshimawakati wewe ni msafikiroho na kuwa tayarikuwa chombo chake.Kama dhambi, kusemamabaya, au tabia mbayaya maisha yakohautakuwa unafaa kwakazi ya Mungu.Chukua muda sasa wakumtaka RohoMtakatifu achunguzemoyo wako. Wakatianapozungumza nawe,ukiri, utubu kwa njia yamaombi, na umruhusu

Yesu aondoe mambo yote machafu. Utakuwa huru nautatumika kwa Bwana wako. Tubu mbele za Mungumara kwa mara. Chukua hali ya chini ili Mungu apatekukuinua na kukuweka katika makusudi makubwa.Katika maombi yako, toba na kukiri iwe sehemu ya kilasiku: Mtake Mungu akuchunguze; mwombe akusamehe,mwombe Mungu akupe uzima.

Ni Lazima Ujifunze Neno La Mungu,Yaani, Biblia

Biblia ni chanzo chako cha Ukweli. Ni lazimauisome kila siku, jifunze na kukariri mistari ili uwezekukua na kukomaa na ufundishe na kuhubiri vizuri.Usihubiri jambo lolote ambalo haliwezeshwi naMaandiko yote. Mafundisho ya uongo yamekuweposana siku hizi. Biblia inatuonya juu ya waalimu wauongo na mafundisho ya uongo yatatokea siku zamwisho na wengi watapotoka. Wakati unapojifunza,chunguza Maandiko kila siku ili kuhakikisha kuwa lileunalolisikia ni kutoka kwa Neno la Mungu (Matendo17:11).

Mtu ambaye hajui maneno ya Mungu hawezi kutoaushauri mzima wa Kimungu kwa watu. Bwanaanaelekeza, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa naMungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari,ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15).

Chukua muda sasa hivi kumwombaRoho Mtakatifu kuupeleleza moyowako. Wakati anapozungumza na

wewe, ungama, tubu katika sala, namruhusu Yesu aondoe uchafu wote.

Utakuwa huru na pia utatumika zaidikwa Bwana wako.

Page 35: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 35

Kuna mwinjilisti nchini India alikuwa anakaririmistari ya Biblia kila juma. Watoto wake nao piawalikariri mistari kila juma. Alikariri maelfu ya mistari.Alipohitajiwa kuhubiri au kushauri au alipohitajihekima, alikuwa ameweka maneno ya Mungu katikamoyo wake. Mtu huyu aliye na nguvu ya Neno laMungu ambalo laweza kugeuza watu na kumlindamwenyewe kutoka nguvu za uovu (Zaburi 119:11).

Ni Lazima Uwe Ni Mtu Wa MaombiMaombi katika maisha ya mhudumu au mwanafunzi

wa Yesu hayana uchaguzi - ni agizo la msingi, nalinapatikana katika Maandiko yote! Uwe ni mtu wamaombi.

Anzisha tabia nzuri ya maombi. Omba katika mudauliojipangia kila siku. Omba wakati unapotembea auunapokaa. Omba kila wakati wa usiku na mchana(1 Wathesalonike 5:17). Omba kwa roho na ufahamu(1 Wakorintho 14:15). Kufunga na kuomba kunavunjavifungo vyote walivyofungwa navyo watu na maeneo.

Mwinjilisti mmoja katika Afrika aliyataka makanisambalimbali kufunga na kuomba pamoja. Mikutano hiiiliwasaidia kuunganisha makanisa kwa kusudi maalumna kuzidisha matokeo ya kiroho. Kazi ya ibilisiimezuiliwa wakati watu wanapokutana pamoja.Makanisa yamebadilika na watu wengi wamekuja kwaKristo kwa sababu makanisa na wainjilisti wameombana kufanya kazi pamoja.

Huwezi kuwa mhudumu au mwinjilisti ambayeMungu amekusudia pasipo kuwa ni mtu wa maombi.Katika maombi unapata uhuru, msamaha, nguvu, namwongozo unaoutaka.

Chukua muda wako wa kuomba na timu yako au nakiongozi mwingine. Tafuta mwombezi na kuwatakawakuombee kila siku. Chukua muda uombe kila siku nawenzako na pia omba peke yako, ombea nchi na watuambao utawahubiria.

Endelea Kuwa MwanafunziInaweza kutokea kuwa hakuna uwezekano wa

kujiunga na Chuo cha Biblia au Seminari. Tafutamapenzi ya Mungu katika jambo hilo na kulifuata kwaimani. Kama pana uwezekanao, hudhuria mafundishoyatolewayo katika semina au masomo ya Biblia katikaeneo lako.

Chukua nafasi uongee na wahudumu wengine nawainjilisti. Jifunze kutoka kwao, na jitolee utumike nao.Wako tayari, kutenga muda wa kuwauliza maswali.Nenda uwasikie wakihubiri. Wasikilize, watathimini, najifunze.

Baadhi ya wanaume na wanawake waliofanikiwahawakupata elimu ya masomo ya Biblia, hata hivyowalifanya mambo makubwa kwa Mungu. Wahudumuwazuri sana ni wale wanaojifunza Biblia kwa uaminifuna kuendelea kujifunza kwa kadri iwezekanavyo, nakuyaweka kwa vitendo yale waliyojifunza. Kujifunza nizaidi ya kuingia darasani. Kujifunza ni jambo ambalolinafanyika kwa maisha yote.

Tafuta Mshauri Katika Kristo; UweMshauri Kwa Wengine

Omba na kumtaka Mungu akupe mwalimu, mshaurikatika Bwana. Huyu ni mtu ambaye amekomaa katikaMungu, atakayekusaidia kukua. Mshauri anatoaushauri wakati anakuangalia katika maisha yako.Katika nchi nyingi, mtu ambaye ni mchanga kiimanianamtaka mtu aliyekomaa awe “baba wa kiroho” wake.Hii inafanyika pia kwa wanawake wanaohitaji “mamawa kiroho”.

Wajibu wa mtu aliyekomaa ni kumwongoza nakumfundisha yule aliye mchanga kiimani, awe nimsaidizi atakayempa hekima. Paulo alikuwa nauhusiano na Timotheo (1 Timotheo 1; 2 Timotheo 1:2).Ni jambo la uhakika kuwa Paulo alimpenda Timotheona alimtaka Timotheo mzuri. Paulo alikuwa tayarikujitoa na kuchukua muda kumsaidia na kumfundishaTimotheo.

Walio wachanga kiimani ni lazima waheshimuwazima na uzoefu wa wale waliokomaa kiimani. Ni kwanjia hii hawa wachanga wanapata ujuzi muhimu kwanjia ya uzoefu na hekima ambayo wengine wamejifunzakwa miaka mingi. Ni njia ya Mungu kuelimishaviongozi wa vizazi vijavyo.

Ni lazima uanze kuangalia mtu au watu wawili wakuelimisha, ambao watapata faida kutokana na uzoefuna mafunzo yako (2 Timotheo 2:2). Omba na Munguatakuonesha ni nani umwelimishe na kumshauri.

Kukataliwa Na KujaribiwaKazi ya mwinjilisti inamweka katika hali ya

kukutana na watu ambao watakubali au watamkataaKristo. Wale watakaomkataa Kristo watamkataamwinjilisti pia.

Siyo kila mtu alimkubali Yesu na ujumbe Wakewakati alipohubiri. Baadhi ya watu watakuwa na hasiranawe na kukuchukia kwa sababu unaleta Habari Njema.Baadhi ya wainjilisti watapigwa na kutishiwa maishayao kwa kumhubiri Kristo. Hata baadhi ya wanafamiliawanaweza kuwa kinyume nawe. Yesu alituambiatutateswa kwa sababu Yake (Mathayo 10:16-20).

Watu watazungumza yasiyofaa na pia kutoa hukumuza uongo. Ni muhimu usifanye moyo wako kujishitakiau kukua katika uchungu, kwani utajichafua wewe nawengine (Zaburi 37:38; Waebrania 12:15). Usijeukawalaumu watu wengine wanapokushitaki. Usijeukapenda kulipiza kisasi. Huu siyo mpango wa Munguwa kushughulika na majeruhi ya rohoni (Warumi12:17-21). Hasira ya mwanadamu siku zote haitengenezihaki ya Mungu (Yakobo 1:20).

Ni lazima kusamehe wale ambao wamekukosea nakukuudhi (Mathayo 18:21-35). Njoo kwa Mungu kamaungemjia Baba mpendwa ambaye anakujali nakukukubali (Warumi 15:7; Waefeso 1:6). Unawezakuyatoa majeruhi yako kwa Mungu na pia kumwambiaakuponye (Zaburi 42:4; 62:8). Acha Baba yako wambinguni akufariji, akutengeneze na pia kukujengakatika majaribu.

Page 36: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

36 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

Kama hupendi Mungu ayachukue majeraha yako yakukataliwa, ibilisi atayatumia majeraha yako kukuumizawakati unahubiri Injili. Utajaribiwa kubadili ujumbewako ili upate kushawishi watu wakunje mkono. Bibliainaita mtego huu kuwa ni “kuwaogopa wanadamu”(Mithali 29:25).

Kuwa makini pia namtego wa mafanikio.Mafanikio katika uinjilistiyatakufanya uanzekujihesabia ushindi nakuanza kujitwalia utukufu.Unaweza ukaangukakatika dhambi ya kujivunana kuanza kuhudumukimwili. Angalia sanamajivuno (Mithali 11:2;16:18; 1 Petro 5:5-9).

Lazima tuwe wapolekwa Mungu pamoja namajeraha tuliyonayo, tubukwa uchoyo na kiburi,samehe waliokukosea naumwombe Mungu kwauponyaji katika maishayetu.

Unapomruhusu Munguakuponye utakuwa nauhakika wa Mungu zaidina upendo. Utagunduakuwa anakupenda na piawewe ni muhimu Kwake.Baadaye utakuwa na uwezo wa kuwapendawanaokukataa na kuchukia, katika nafasi uliyonayokatika Kristo - ambapo ni mahali pa nguvu ya kushindana kukubaliwa bila sharti lolote.

Kuwa Na Mpangilio Na Huduma1) Maono (Dira) Kwa Ajili Ya HudumaJe, unajua huduma yako inaenda wapi? Je, unayo dira

kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kazi yako maishani?Kama huna, unaweza kumwambia Mungu akupe dira namwelekeo katika maisha yako. Kama amekuita nakukupa kazi ya huduma yake, anapenda kukuoneshaufanye nini ili kufanikisha hilo!

Katika maono ya pekee, Isaya aliyaona maono yaBwana (Isaya sura ya 6). Isaya alikubali hali yake yadhambi na alitubu na alibadilishwa. Mungu alimwitakuwa nabii na kufunua njia na shabaha katika maisha yaIsaya. Maono kama hayo siyo ya kawaida, na yametokeakwa watu maalum katika Maandiko ambao Mungualiwapa mwito wa pekee (kama Isaya; na Sauli [Paulo]katika Matendo 9:1-19).

Lakini Mungu amekuita katika huduma yako. Anampango maalum kwako ili uutimilize. Kamaunavyomtafuta kwa bidii na kutumia muda katika sala,Mungu atakusaidia uweze kuona mapenzi yake katikamaisha yako. Atakupa ndoto au maono. Tena

atazionesha njia zako unavyomtegemea na kumkubalisiku hadi siku (Mithali 3:5-6; Mathayo 6:33).

Yesu alifanya tu yale ambayo Mungu alimfunulia.Alisema, “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ilalile ambalo anamwona Baba analitenda; kwa maanayote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile

vile” (Yohana 5:19-20).Yesu alifanya yaliyomapenzi ya Baba.Hakufanya wala kusemakila kitu isipokuwa lileambalo Baba alimfunulia.Yesu amekuwa ndiyeametuonesha mfano wakumtegemea Baba kabisa.

Mungu amejifunuaMwenyewe na makusudiyake katika Biblia nzima.Njia mojawapo nzuri sanaya kumtambua Mungu namakusudi Yake, ni kusomaNeno la Mungu maranyingi uwezavyo. Biblia ni“mwanga wa njia yangu”(Zaburi 119:105). Mwangaunatuangaza njia zetu,unatusaidia kuona jinsi yakutembea. MruhusuMungu akuoneshe kwaupya ukweli mtimilifu waMaandiko ili akuongozekatika njia zake.

Mungu aweza pia kukupa mwelekeo maalum,kuhusu majukumu ya huduma. Je, unataka kuufikia mjifulani ili watu wapate kumjua Kristo? Je, umeomba nakumtaka Mungu akupe mpango wake? Je, umetakaMungu kama anayo njia ambayo ingewezesha uinjilistikufanyika? Au jinsi ya kuanzisha kanisa? Wakatimwingine Mungu anakupa hatua za wazi kabisa zakufuata ili kuyafanya mapenzi yake.

Mruhusu Roho Mtakatifu azungumze nawe nakukuongoza katika kufanya maamuzi – kama ni mahaligani pa kuhubiri, ni jambo gani la kusema, ni naniatafanya kazi nawe? Usiwe na hamu ya kujengayafuatayo au kuwa na sifa uwe mkuu. Usiwe na hamuya kujenga huduma yako au kuwa na “mafanikio”.Tunafanya kazi kwa matunda ya milele (Yohana 15:16),si ili tupate thawabu hapa duniani (Mathayo 6:1-4).

Uwe na utayari wa kwenda na kufanya kazi - wakatina mahali pale Roho akuelekeza, kwa utukufu waMungu. Kila mji au jinsi ni tofauti; hivyo njia ya kufikiamahali au kundi la watu inaweza kutofautiana.

Mtume Paulo alipewa jinsi ya kufikisha utume wake.Aliwahubiri Wayahudi kwanza; ndipo akaenda kwawasio Wayahudi. Katika safari yake ya pili ya misheni,alitaka kwenda kaskazini na mashariki; lakini Munguakamkataza. Alipata ndoto ambayo mtu kutokaMakedonia (Ulaya) alikuwa anamwita aende na

Je unajua mtazamo wahuduma yako?

DIRADIRADIRADIRADIRA

Page 37: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 37

kuwasaidia (Matendo 16:9-10). Paulo alikuwa anatakakuyafanya mapenzi ya Mungu, lakini alikuwa karibu nakwenda mwelekeo mbaya. Mungu alitaka Paulo na timuyake kwenda magharibi, Ulaya na kuipeleka Injili.

Paulo, alipofika Makedonia, alimkuta Lidia ambayendiye wa kwanza kuongoka Ulaya (Matendo 16:12-15).Lidia alikuwa mfanyabiashara, alimpa Paulo nyumbayake aitumie kwa kazi yake, na kuwa ndilo kanisa lakwanza Ulaya. Nyumba hii ikawa pia msingi wauinjilisti maeneo ya Ulaya. Lidia na wenzakewalimsaidia Paulo katika kueneza Injili. Mungu alikuwana mpangilio ulio wazi, lakini Paulo alihitaji kufahamumpangilio utakaomsaidia kutimiza kusudi la Mungu.

Mngoje Bwana, mwombe na kujitoa mbele Zake.Mwimbie Yesu; msifu; mwaga moyo wako wote Kwake;na hatimaye ngoja umsikie Yeye. Mungu ataachiliakusudi lake kwako. Mungu anaweza kukupa maonomaalum au mpangilio, au kuyafunua mapenzi yakekatika picha za kiakili au kwa maneno na kuziwekakatika mawazo yako. Yaandike yote, pamoja na tarehe,Mungu aliyokuambia na kukuonesha. Yaombee hayayote na yaweke yote mbele ya watu wa kiroho ambaounawaamini. Anza sasa kuchukua hatua ya imanikufanya yale ambayo Mungu amekuonesha uyafanye!

2) Maelezo Ya TaswiraMara unapoanza kuona mwelekeo na dira, inasaidia,

ukiandika maelezo ya taswira. Maelezo ya taswirayanakueleza kwa kifupi lile ambalo umeitwa kwalo.Maelezo haya yanasaidia sana kama yatatolewa kwaujumla kuliko kuwa na mambo madogo madogo. Kwamfano, badala ya kuandika “Tutaanzisha makanisamatano na nyumba za yatima mbili na kuwa namikutano mwaka huu”, ingekuwa vizuri kamaungeandika, “Tutaeneza Injili kwa kuanzisha makanisana kufanya kazi za kijamii kama Mungu atakavyo-tuelekeza, ili Yesu atukuzwe.”

Tenganisha maeneo ya kazi na kuyawekea malengomaalum na yaandike yote. Kwa mfano, kama Munguamekupa wito wa kuanza shule, iweke kwenye maelezoyako pia.

3) MalengoBaada ya kuandika maelezo kwa njia ya maombi,

elezea kimaandishi jinsi ya kufikia dira na taswira ilizifanyike. Je, una mpango wa kuifanya? Andikamalengo yote ambayo unakusudia kukamilisha. Huondiyo wakati wa kuwa na mambo madogo madogozaidi.

Kwa mfano: “Baada ya muda wa miaka miwilitutaelimisha wachungaji wawili na kuanzisha makanisamawili katika eneo hili; baada ya miaka mitanotutakuwa na makanisa matano zaidi.” Au, “Kundi letulitahubiri Injili kwa kila kijiji katika eneo hili - katikakijiji kimoja kwa mwezi, kwa miaka mitatu inayofuata.”Au, “Tutasambaza vipeperushi 10,000 katika miji kwamiezi sita ifuatayo. Pia tutakuwa na mikutano yauinjilisti katika maeneo yote manne ya mji kila juma.”

Kuwa na utaratibu mzuri unasaidia kuwezesha kazikufanyika kwa vizuri. Kwa njia ya maombi nakumsikiliza Bwana, utajua mpango wake kwa ajiliyako. Mungu atakupa njia ya kusaidia makanisawaweze kufanya kazi ya uinjilisti kwa pamoja.

Maelezo ya taswira yako na malengo yako nimuhimu yaeleweke kwako, katika mawazo yako, na uwetayari kumwambia mtu yeyote atakayekuuliza. Nimuhimu kuombea maandiko haya mara kwa mara nakuwa na nia ya kubadilisha au kurekebisha ifanyikehivyo kama ni lazima.

Kumsikia Mungu na kufanya mambo yote kwa imaniitakufanya uwe na mafanikio katika kukamilisha kusudila Mungu kwako. Wengine wataona ni rahisi kuelewa nakukuwezesha na kazi yako.

Kujenga Timu Ya UinjilistiYesu alijenga kundi la watu kumi na wawili. Yesu

aliwatuma watende kazi yake wawili wawili nao;walikuja tena kutaka maelekezo na mahusiano, nakwenda tena. Mtume Paulo alijenga pia timu zake.Wakati mwingine alikwenda mwenyewe, lakinialipendelea kufanya kazi kwa timu.

Kila mtu katika timu yake atakuwa na karama tofautina wewe. Hii itaongeza mafanikio zaidi katika huduma.

Mwinjilisti mmoja alikuwa na mwanamke katikatimu yake aliyekuwa na karama ya kuponya. Mtu huyumara nyingi aliona nguvu ya Yesu na kutenda miujiza yakuponya katika mikutano yao. Watu wengiwanafunguliwa katika Injili wakati wanapomuona Yesuakiponya watu kwa njia ya huduma ya mwanamke huyu.Mwanamume mwingine katika timu alikuwa na uwezowa kuandaa mikutano mikubwa ya kiroho katika miji.

Mwinjilisti huyu aliwaelimisha wainjilisti wenginekatika timu yake. Kulikuwa na wainjilisti watatu katikatimu hii ambao walikuwa wakihubiri katika magulio,wanaotembelea wafungwa vifungoni au hospitali, auwalifanya mambo ambayo yalihitajika katika kuwa-shirikisha wengine ujumbe wa wokovu.

Kuwainua na kuwatia moyo wafanyakazi inasaidiakuiwezesha Injili kufikia wengi na kuwa na mafanikiomakubwa. Timu inakuwa kama familia ambako mahitajiyote yatumike na malengo ya taswira yanatimilizwa.

Kuwa Mtumishi Wa UfalmeMungu hamuiti mtu yeyote awaye yote kujenga

huduma yake mwenyewe. Mungu amekuita kwamakusudi yake, na amekuruhusu wewe kuwa mbia wakekama Yesu anavyojenga Ufalme wa Mungu!

Viongozi wengi wa kanisa wanataka kumtumikiaMungu, lakini wanataka watengeneze jina kubwa kwawao wenyewe. Wanadharau na kukatisha tamaa viongoziwengine na wahudumu. Ni wachoyo na hawatakikuwatumikia wahudumu wengine kama mbia.Wanafikiri utumishi wao ni mzuri zaidi, na kazi yaondiyo kazi pekee muhimu. Na hii ni chukizo kwa duniana Kanisa! Kiongozi wa namna hii hulenga zaidimaslahi yake mwenyewe na siyo mahitaji ya wengine,

Page 38: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

38 / MATENDO NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006

na pia siyo kwa Ufalme wa kweli wa Mungu. Hii siyoRoho ya Kristo.

Kushiriki na watu wengine na wahudumu wenginekunaleta utukufu mkubwa kwa Mungu na ufanisi mzurizaidi katika kazi. Kutia moyo na kuwasaidia wahudumuwengine kunaleta baraka kubwa za Mungu katikautumishi wako. Unapotoa, unapokea (Luka 6:38).Wakati unapopoteza maisha yako (na matakwa yako)kwa ajili ya Kristo, utapata maisha ya kweli (Mathayo16:25). Wakati unapochukua “nafasi ndogo” yakutumikia wahudumuwengine na hudumazingine, Munguatakupandisha cheo (Luka14:10-11).

Maono yako yanatakiwayawe na uwezo wa kufanyakazi na makundi mengine,makanisa, na hudumambalimbali. Hii ni kujengaUfalme mkubwa waMungu na siyo kanisamoja, dhehebu au hudumamoja. Wakati wahudumuwanapofanya kazi pamoja,watu wanaona umoja waMwili wa Kristo na barakaza Mungu zinakuja (Zaburi133:1-3). Wainjilistiwanajikusanya pamoja nakufanya kazi katikamakanisa yaliyo mengikatika miji na kuleta barakanyingi katika mji huo.

Tenga MudaKupumzika

Wafanyakazi wengi wamechoka kama ukuni katikamoto maana hawakuchukua muda wa kupumzika. Miiliyao huugua; mawazo yao huchoka; roho zao hufifia; napia kushindwa kuhimili majaribu. Mungu ameamurukuwa tupumzike siku moja kwa juma. Sote tunahitajimapumziko.

Kila muhudumu - na kila mtu - anahitaji mapumzikoangalao mara moja kwa juma kujirudisha upya kwaMungu na kupumzisha mwili wake, mawazo yake naroho yake.

Kuna wakati ratiba yako inahitajika sana zaidi yakawaida. Utumike lakini ni lazima utenge muda wakupumzika na utafute matendo ambayo yanaburudishamwili wako.

Wakati Yesu na wanafunzi wake walipohudumu,watu wengi walikuwa wanaingia na kutoka hata wakatimwingine Yesu na wanafunzi wake hawakuwa na mudawa kula. Yesu aliwambia, “Njooni ninyi peke yenu kwafaragha, mahali pasipokua na watu, mkapumzikekidogo” (Marko 6:31).

Mara kwa mara Yesu alikuwa na muda wa

Shirikiana na watu pia wahudumuwengine kuleta utukufu mkubwa kwa

Mungu na ufanisi mzuri wa kazi.

kupumzika na pia kufanya sala. Yeye ni mfano kwetukuwa hakuna asiyeruhusiwa na Mungu kupumzika.

Chombo Cha HeshimaKumbuka kuwa watu watapokea zaidi uyasemayo

endapo watakuheshimu wewe kama ulivyo naunavyoishi katika maisha yako. Kujiweka chini yamaongozi ya Ufalme wa Mungu ni jambo la mudamrefu. Unatakiwa siku zote ukue, ujifunze, na pia ujitoekwa kazi ya Mungu inayolenga kwako.

Mwinjilisti, Munguamekuita kuubeba ujumbeWake wa ukombozi kwawatu wengine. Unawezaukawa mfano hai wamabadiliko mazuriambayo ujumbe waMungu unaweza kufanyakatika maisha ya mtu.Chunga sana maisha yakoyawe safi na pia angaliamwelekeo na tabia yako.

Mungu anajishughulishana mabadiliko ya maishayako kwa jinsi ambavyowewe unajishughulisha nakutafuta msaada Wake.Atakupenda nakukuwezesha wewe nakazi yako kwakukubadilisha wewekutoka ndani. Ni lazimautii na kulifuata NenoLake. Jipe muda wakutosha kujichunguzambele za Mungu nakuitikia maneno Yake na

kuyaacha yafanye kazi katika maisha yako na familiayako. Kwa kufanya hivyo utakuwa mwinjilisti namhudumu mzuri wa Injili aliye chombo cha heshima naamfaaye Bwana wake!

Mambo Yaliyo Muhimu ZaidiTabia yako – itakavyokuwa ni kitu muhimu sana

mbele za Mungu zaidi ya kitu chochote ungefanya kwaajili yake. Mungu anajali zaidi jinsi ulivyobadilishwakufanana na Yesu zaidi, kuliko kiasi cha kaziunachoweza kumfanyia.

Utii na kujitoa kwako kwa Mungu ni kitu muhimusana kwake zaidi ya mikutano mingi yenye mafanikio nawingi wa watu. Mwamko wa kumwonesha Yesu katikautukufu wake, nguvu, uweza wake ni muhimu kulikokujitengenezea sifa. Yaweke mawazo hayo akilinimwako kila siku katika huduma yako. Miongozo hii namafundisho haya yanalenga kukusaidia wewe uwe mtumwenye uwezo kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Tumiawewe mafundisho haya na umwamini Mungu akutumiekwa malengo na utukufu wake!

Page 39: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

Unahitaji Kufanya Upya Kibali Chako Cha MATENDO?

Hapa ni maelezo ya kujua:

Angalia katika kibandiko kilicho juu ya bahasha ya MATENDO. Juu kabisa upande wa kulia wa

kibandiko ni TAREHE (mwezi/mwaka) wa kumalizika baada ya neno "EXPIR".

Ikiwa tarehe hiyo ni CHINI YA MIEZI SITA tangu sasa, basi, huu ni wakati wa kufanya upya!

Hupaswi kuandika kila mara unapopokea toleo la MATENDO; unatakiwa kujaza tu IWAPO kibali

chako cha miaka miwili kitaishia katika miezi sita ijayo.

Jinsi ya kufanya upya kibali chako cha MATENDO cha miaka 2:• Kata kipande cha "Fomu Ya Kuomba Kuendelea Kupokea Gazeti La Matendo" hapo chini

(au nakili kwenye karatasi nyingine);

• Fuata maelekezo YOTE katika hiyo fomu (zungushia duara majibu ya NDIYO au HAPANA);

• Jibu maswali YOTE yaliyomo kwenye fomu - andika vizuri kwa herufi kubwa; na

• Utume bila kuchelewa fomu uliyojaza kwa ofisi ya World MAP.

ANGALIZO:

Gazeti la MATENDO sio "Masomo kwa njia ya Posta".

Hutapokea "cheti" au "stashahada" baada ya kusoma

MATENDO. Ni tumaini na maombi yetu kuwa unapokea

kilicho bora zaidi. Mafundisho yaliyo ya kiBiblia namafunzo ya huduma kivitendo! Hili litakutayarisha

wewe kuwa na ufundishaji ulio mzuri, kuhudumia na

kuwahubiria wengine. MATENDO hutumwa bure kwa

viongozi wa kanisa wanaoomba kulipokea katika Asia,

Afrika na Latini Amerika. Viongozi wa kanisa watapokea

MATENDO kwa miaka miwili; kisha wanatakiwa kujaza

upya kibali chao ili kuendelea kupokea MATENDO kwa

miaka miwili zaidi.

1. Kwa kuwa kibali changu cha gazeti la MATENDO kitamalizika katika muda wa miezi sita ijayo, ninahitaji kuomba upya

kibali changu: (Zungushia duara kwenye jibu lako.) NDIYO HAPANA

2. Namba yangu ya kibandiko cha MATENDO ni LABL NO: _____ _____ _____ _____ _____ _____

(Namba hii inapatikana sehemu ya juu, upande wa kushoto wa kibandiko kilichoko juu ya bahasha ya MATENDO, baada ya "LABL NO".)

Tarehe ya kumalizika kwa muda wa kupokea gazeti la MATENDO ni: EXPIR ______ / ______

(Tarehe hii inapatikana sehemu ya juu, upande wa kulia , baada ya "EXPIR".) mwezi mwaka

3. Mimi ni kiongozi wa kanisa katika Afrika na ninahubiri au kufundisha neno la Mungu kutoka kwenye Biblia kwa kundi la

watu wapatao 20 au zaidi kila wiki. (Hii ni LAZIMA iwe ni kweli ndipo uweze kupokea Gazeti la MATENDO au kitabu

cha Fimbo ya Mchungaji.) (Zungushia duara kwenye jibu lako.) NDIYO HAPANA

4. Je, unayo nakala ya (kitabu cha) Fimbo ya Mchungaji katika lugha yoyote? (Zungushia duara kwenye jibu

lako.) NDIYO HAPANA

5. Unaomba nakala ya (kitabu cha) Fimbo ya Mchungaji? (Zungushia duara kwenye jibu lako) NDIYO HAPANA

6. TAFADHALI ANDIKA JINA NA ANWANI YAKO HAPA CHINI. ANDIKA ISOMEKE VIZURI, KWA HERUFI KUBWA.

Jina:

__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __

Anwani:

__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __

__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __

Mkoa/Jimbo:

__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ Nchi: __ __ __ __ __ __ __ __

Wadhifa (au wajibu) wangu katika kanisa ni:__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __

Sahihi/saini yangu:: ________________________________________ Tarehe ya leo: _________________________

7. Nakala hii ya MATENDO ilikuwa: ___rahisi kueleweka ____ngumu kueleweka ___inasaidial ___ haisaidii

Tuma fomu yako kwa: WORLD MAP, PO BOX 721, ARUSHA, TANZANIA

Hakikisha umeomba

upya kibali chako

mara moja baada ya

kila miaka miwili ili

usikae na kungojea na

kujiuliza: "Nakala

yangu ya gazeti la

Matendo iko wapi?"

FOMU YA KUOMBA KUENDELEA KUPOKEA GAZETI LA MATENDO / FIMBO YA MCHUNGAJI - zungushia duara NDIYO/HAPANA

SW 14/1

Page 40: NAKALA 14 – NAMBARI 1 – 2006 MATENDO / 3 Mag Swahili...ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Utangulizi

Omba kupatiwa nakala

yako ya zana ya mafunzo

yenye uwezo kutoka

World MAP!Fimbo ya Mchungaji - yenye

kujulikana kwa wengine kama

"Shule ya Biblia katika

Kitabu" -- ni kitabu chenye

kurasa 1000 kilichotayarishwa

kwa kusudi la kuwafunza na

kuwaandaa viongozi wa kanisa.

Kimejaa maandiko ya waan-

dishi wengi yaliyojaa upako wa

Roho, na yenye msingi wa

kiBiblia. Kitabu hiki kime-

andikwa kwa kusudi la kukidhi

mahitaji maalum ya viongozi

wa kanisa wafanyao kazi Asia,

Afrika na Latini Amerika.

NDANI ya kitabu hiki kimoja, yaani Fimbo ya Mchungaji, utapata:

[1] Kitabu Kidogo Cha Malezi Ya Waamini Wapya ambacho kinakupatia masomo yote ambayo inapasa

uwafundishe watu wote wapya wanaookoka.

[2] Mwandani Wa Biblia wenye maelfu ya rejea za Biblia zinazoshughulikia masomo makuu 200 katika

Biblia. Sehemu hii katika Fimbo Ya Mchungaji, itakusaidia katika kufundisha wengine Biblia.

[3] Mwongozo Wa Kufunza Viongozi chenye masomo mazuri mno ya kufunza viongozi yaliyochapishwa

na World MAP kwa zaidi ya miaka thelathini.

Yote hayo na zaidi yamo katika kitabu kiitwacho Fimbo Ya Mchungaji.Ili kuweza kupokea nakala yako ya kitabu hiki cha mafunzo ya uongozi yenye uwezo, yaani Fimbo YaMchungaji, soma kwa makini na ujaze Fomu ya Maombi iliyoko nyuma ya ukurasa huu wa mwisho (au

andika vizuri kwa HERUFI KUBWA maswali hayo yote katika karatasi ya pembeni iwapo hutaki kukata

gazeti lako).

Mara baada ya kujibu kila swali, na kuandika mwitikio wako kwa wazi kama iwezekanavyo, tuma fomu

hii kwa ofisi ya World MAP iliyo karibu. (Anuani imeoneshwa kwenye Fomu ya Maombi.) Utapokea

nakala yako ya Fimbo Ya Mchungaji upesi iwezekanavyo (lakini kwa kuwa wakati mwingine usafirishaji

ni wa polepole, tafadhali ruhusu kama miezi 6 hivi ili Fimbo Ya Mchungaji ikufikie.) Asante sana.

For private circulation