nakala mtandao(online document) bunge la tanzania ...parliament.go.tz › polis › uploads ›...

170
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ BUNGE LA KUMI NA MOJA MKUTANO WA SABA Kikao cha Arobaini na Nane – Tarehe 15 Juni, 2017 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI KWA WAZIRI MKUU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali kwa Waziri Mkuu tunaanza na Mheshimiwa Daniel Nicodemus Nsanzugwanko. MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mheshimiwa Waziri Mkuu, nina swali la ufafanuzi nataka kujua sisi tunaokaa katika Mikoa ya mipakani hususan Kigoma, Kagera, recently nimeambiwa na Mtwara limekuwepo tatizo kubwa la wananchi wetu kuambiwa siyo raia linapokuja suala la uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wananchi hawa wako Tanzania na kama unavyofahamu nchi yetu wananchi wake wengi wako mipakani mwa nchi yetu.

Upload: others

Post on 10-Jun-2020

32 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

BUNGE LA KUMI NA MOJA

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Arobaini na Nane – Tarehe 15 Juni, 2017

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

MASWALI KWA WAZIRI MKUU

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali kwaWaziri Mkuu tunaanza na Mheshimiwa Daniel NicodemusNsanzugwanko.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, nina swali la ufafanuzinataka kujua sisi tunaokaa katika Mikoa ya mipakani hususanKigoma, Kagera, recently nimeambiwa na Mtwaralimekuwepo tatizo kubwa la wananchi wetu kuambiwa siyoraia linapokuja suala la uandikishwaji wa vitambulisho vyaTaifa. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wananchi hawa wakoTanzania na kama unavyofahamu nchi yetu wananchi wakewengi wako mipakani mwa nchi yetu.

Page 2: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Nini tamko la Serikali kuhusu hali hii na namna ganiSerikali yako itajipanga kuhakikisha kuwa wananchi hawawanapewa haki sawa kama wananchi wengine wote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombanitumie nafasi hii kujibu swali la Mheshimiwa Nsanzugwanko,Mbunge wa Kasulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kuna mambo mawili,uandikishaji na utaratibu wake pia vikwazo vya uandikishajikwenye mikoa ya pembezoni, hasa kwenye mikoa ambayoumeitaja, Kigoma ambapo Mheshimiwa unatoka, Kagera,Mtwara, Kilimanjaro pia hata Arusha kwa Wilaya za Loliondo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Taasisi yetu ya NIDAinaendelea kufanya kazi ya uandikishaji wa kutoavitambulisho vya Kitaifa, kitambulisho ambacho ni muhimusana kwa Mtanzania kukipata, lakini katika utoaji wakelazima tuwe makini kwa sababu ni kitambulisho ambachotukifanya makosa tunaweza kujikuta tunakabidhivitambulisho vya Utaifa kwa watu wa Mataifa mengine. Kwahiyo, NIDA tumewataka wawe makini sana na kazi hiyowanaifanya kwa umakini ukubwa na zoezi hili la utoajivitambulisho linaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa takwimuzinaonesha zaidi ya mikoa tisa imeishakamilika ingawawalikuwa wanaenda mkoa mmoja mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo umelieleza lamkanganyiko wa raia wa Tanzania na wageni na hasakwenye mikoa ya pembezoni Kigoma ikiwemo maeneo hayalazima tuwe makini sana katika uandikishaji, tumeonamakundi mengi ya Mataifa ya nje wakiingia nchini na hasanchi jirani, kwa nafasi ile ya kwamba wao wanazungumzalugha yetu, wakijifunza kidogo wanaingia huku halafu

Page 3: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

wanaleta mkanganyiko wa namna ya kutumia lughaakishamudu kuzungumza lugha inakuwa tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano Kigoma,Kigoma ni mpakani mwa Tanzania na Burundi na Warundiwengi wanazungumza Kiswahili na wananchi wa Kigomakwa Kabila lao wanazungumza lugha moja na Burundi, kwahiyo ni ngumu sana ukifanya jambo hili kwa haraka unawezakukuta unatoa vitambulisho kwa Warundi walioko nchiniTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunatakiwa kuwamakini na Serikali tumejipanga kuwa makini kupitia Taasisiyetu ya NIDA. Wananchi walioko kwenye Mikoa hii wasioneusumbufu pale tunapohoji na kutumia njia zetu za kiintelijensiakujua huyu kama ni Mtanzania au laa na wakaonawanachelewa, wengi wanaolalamika kwambatunachelewesha ni hao wanaotaka uraia kwa haraka, kwahiyo tuko makini sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungezoezi hili ni lazima mtuvumilie hasa kwa mikoa ya pembezonikwa sababu lazima tuwe makini. Kule Mtwara, Watanzaniawanaokaa Mtwara ni Wamakonde, lakini kule Msumbijiwalioko mpakani ni Wamakonde pia na wanazungumzalugha moja, kwa hiyo lazima tuwe makini. Halafu kuleLoliondo, mimi nimeenda Loliondo wananchi wengi niWamasai lakini mpakani Kenya wanaoishi kule ni Wamasai,kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuwa makini. Kwa hiyo, hatatunapofanya shughuli zetu za Kiserikali tunakuwa makini sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie kwamba,zoezi la uandikishaji linaendelea, lakini kwa umakini mkubwaili vitambulisho viende kwa Watanzania tu na sio raia wa njeili kupunguza idadi kubwa ya watu wa nje kuingia ndani nakufanya idadi ya wanaokaa nchini kuwa wengi, mwishoSerikali tutakuwa tunalaumiwa kwa kutomudu kutoahuduma, kumbe sisi tumepanga bajeti ya Watanzania walemilioni 50, lakini tunajikuta tuko milioni 55 kwa sababu yakuwaachia wananchi wa kutoka nchi nyingine kuingia hapa

Page 4: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

nchini. Hivyo, tutaendelea kutoa vitambulisho katika mikoayote. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nsanzugwanko.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu, nashukuru kwaufafanuzi huo nina swali moja dogo tu nalo la ufahamuvilevile. Maafisa wa Uhamiaji wamekuwa na tabia yakuvamia watu kwenye disco usiku, wamekuwa na tabia yakuvamia watu kwenye masoko, kwenye magulio, etiwanasaka watu ambao sio raia. Je, mnaweza mkaelekezavizuri ili Maafisa Uhamiaji wetu hasa katika Mkoa wa Kigomawatumie weledi zaidi wanapokuwa wanajiridhisha na uraiawa wananchi walioko mipakani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, upo ukwelikwamba maeneo hayo aliyoyataja kwenye masoko, kwenyeminada, kwenye disco ni maeneo ya mikusanyiko ambayoni rahisi sana wageni kutoka nje kwenda kujichanganyawakijua kwamba ni ngumu kwa taasisi kama yetu kuingiapale kwenda kufanya ukaguzi. Tunachofanya ni kwambakutumia utaratibu wetu tulionao wa ndani wa kujua nani ninani, tukijua huyo mtu kama yuko kwenye disco yuko sokonitutamfuata hapo hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na msisitizo wakwamba tunapofanya kazi watumishi wa Serikali tufanye kazikwa weledi mkubwa, lakini lazima tutakwenda popote alipoendapo tutagundua kama huyo hajafanya matendoyanayokwenda sambamba na sheria ya nchi na taratibu zanchi, bado tumesisitiza weredi katika kufanya kazi yetu,hakuna haja ya kusumbua wananchi badala yake nendakwa unayemtaka mchukue, mwambie kwa nininimekuchukua ili ajue na aweze kupata nafasi ya kujitetea,huo ndio utaratibu ambao tumeusisitiza Serikalini. (Makofi)

Page 5: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri Mkuu.Mheshimiwa Mbatia.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Jamii yoyote maendeleo yake yanatokana namfumo wake wa elimu, ni tunda la mfumo wake wa elimu,Sera ya Mafunzo ya Elimu ya mwaka 2014 inaelezeakuwawezesha rasilimali watu kuwekeza kwenye akili zamwanadamu ili waweze kuendana na karne hii ya sayansina teknolojia katika nyanja zote. Je, ni nini nguvu ya Sera hiiya Elimu ya 2014 ukilinganisha na Sera ya Elimu ya 1995 katikakudhibiti ubora wa vitabu vya kiada na ziada. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakujibu swali la Mheshimiwa Mbatia, Mbunge wa Vunjo, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera yaElimu na Sera hii ya Elimu ndiyo ambayo tunaifuata katikakuendesha shughuli zote za elimu kuanzia ngazi ya Awali,Msingi, Sekondari hata Elimu ya Juu. Ni mwongozo ambaotunatakiwa tuufuate ili kufikia malengo tunayoyataka. Sasanini nguvu ya Sera ya Elimu ya sasa na ile ya miaka iliyopita nikwamba nguvu yake ni pale ambapo Sera inakwendainakidhi matakwa ya sasa kulingana na mabadiliko ya Sayansina Teknolojia katika kupata rasilimali watu yenye uwezo wakutekeleza shughuli ambazo sasa tumejipangia ili ziwezekuleta matokeo mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya mwaka 1995ambayo ameieleza pamoja na uzuri uliokuwepo katikautekelezaji wake na malengo yake kwa miaka hiyo na hii yasasa nikiri kwamba tunayo mabadiliko ya kisera, ndani yanchi ambayo yanataka Sera iweze kukidhi matakwa yawakati huo, wakati huu sasa msisitizo wa elimu yetu ni wasayansi na teknolojia ili tuweze kwenda sambamba namabadiliko yetu.

Page 6: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nguvu ya sera ni paleambapo inatoa matokeo tunayoyatarajia na kamaambavyo nimesema sasa matarajio yetu ni kuzalishawanasayansi wengi. Leo hii Tanzania Serikali yetu imesematunataka kuendeleza viwanda, kwa hiyo Sera yetu ni lazimaijielekeze kwenda mashuleni kuwaandaa vijana,kuwaandaa wasomi ambao wataweza kuingia kwenyeulimwengu huu wa sayansi na teknolojia pia kuendeshaviwanda mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wetu ni kufanyamaboresho ya sera, kufanya mapitio ya kupitia wataalamwetu walioko Vyuo Vikuu, Walimu ambao wako kazini, lakinina wadau wengine ili tuone kama je, sera tuliyonayo inakidhimahitaji ya sasa na mabadiliko hayo ndiyo ambayoyanaweza kuleta nguvu ya kuleta rasilimali watu ambayokweli itakidhi mahitaji ya sasa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru.

Mheshimiwa Waziri Mkuu kutokana na majibu yakoya nguvu ya sera hii, nikikwambia kwamba sera hii ndiyoimezalisha vitabu vibovu ambavyo havijawahi kuonekanakatika historia ya Tanzania, ambavyo vimegharimu zaidi yabilioni 108. Je, ni nini wajibu wa Serikali kwenye ubovu wavitabu hivi vya sasa viondoke kwenye mzunguko kwa sababuni sumu inayolishwa Taifa la Tanzania na kuua nguvu yasayansi na teknolojia katika Taifa la Tanzania? (Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, natakanimjulishe Mheshimiwa Mbatia kwamba sera ni kitu kinginena kitabu ni kitu kingine, ingawa vitabu vinaandaliwakutokana na sera. Kwanza lazima uwe na sera, seraitakwenda kuandaa mtaala, mtaala ndio ambao unaandaasyllabus, syllabus ndiyo inapendekeza somo hili liandaliwevitabu gani vya kiada na ziada.

Page 7: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitabu vya kiada ni vilevitabu vya msingi na vya ziada ni vile ambavyo vinasaidiakatika pia katika kuelimisha somo hilo. Kwa hiyo, sasa syllabusi l iyotokana na mtaala na hiyo Sera, syllabus ndiyoinayopendekeza somo fulani liandaliwe kitabu gani kwenyemada zipi ili zitoe matokeo gani. Kwa hiyo, ile syllabusambayo inapendekeza kitabu sasa ndiyo unakusanyawataalam wanaandaa kitabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ubovu wa kitabu ukohuku kwenye maandalizi, huyu anayeandaa kitabu kile ndiyeanayeweza kuleta ubovu. Wito wangu ni kwamba ndani yaSerikali tunayo Taasisi ya Elimu Tanzania ndiyo ambayo inaowajibu sasa wa kuandaa vitabu, nataka nikujulishe tukwamba awali suala la uandaaji vitabu tuliwaachia watummoja mmoja kutunga vitabu na sisi tunavichukua, tulionavitabu hapa vya Mheshimiwa Mbunge aliyemaliza mudaMheshimiwa Nyangwine alikuwa na Waandishi wengine, kwahiyo kila mmoja alikuwa anaandika kitabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukagundua liko tatizokidogo, ndiyo yake tumeamua kurudisha katika Taasisi yetuya Elimu ambayo yenyewe imekusanya wataalam wengi tuwasomi wa kila fani ambao sasa wanatakiwa watengenezevitabu kutokana na matakwa ya syllabus ya somo hilo iliviweze kutumika mashuleni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama liko tatizo, tatizolitakuwa ni la mtengenezaji, yule ambaye anatunga, ile panelambayo inatunga, labda kwenye uchapishaji, ndiyo kunatoahayo matokeo ya mwisho. Kwa hiyo, nimwahidi MheshimiwaMbunge tu kwamba tutafanya marekebisho makubwakwenye Taasisi yetu ya Elimu na Waziri wa Elimu amefanyamarekebisho hapa baada ya kumwajibisha Mtendaji Mkuuwa Taasisi, tunataka Taasisi iwe makini kwa kujua matakwaya somo na kitabu ambacho kimependekezwa na uborawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaamua sasa kutumiawasomi wetu wa Vyuo Vikuu waliojikita kwenye fani,

Page 8: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

tuwapeleka Taasisi ya Elimu ili wao watutengenezee vitabuvinavyotosha kufundisha kwa mujibu wa mtaala nakutosheleza sera ya nchi. Huo ndio mkakati wetu kwa hiyonimhakikishie tu kwamba tutafanya marekebisho namarekebisho yameendelea kufanyika. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri Mkuu.Mheshimiwa Kuchauka.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali kwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, Tanzania ni nchi ambayoina mifugo mingi sana na wafugaji wetu wengi ni walewafugaji wa kuhamahama. Jambo hili limetuletea migogorosana ya ardhi mpaka kusababisha mauaji. Sasa kumezukamtindo wa mikoa ile ya wafugaji tayari watu wanahamasasa wanaenda katika mikoa ambayo sio ya wafugaji kwaasili, maana yake ni kwamba hapa sasa migogoro sasa yamauaji haya ya wafugaji na wakulima tunayahamishiakwenye hiyo mikoa ambayo siyo ya wafugaji. Je, ni nini kauliya Serikali juu ya kusambaza haya mauaji ya wakulima nawafugaji katika mikoa ambayo siyo ya wafugaji? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakujibu swali la Mheshimiwa Kuchauka, Mbunge wa Liwale,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali linataka nini mpangowa Serikali wa kupunguza mauaji yanayotokana namigogoro ya wakulima na wafugaji kwenye maeneo kadhaa.Jambo hili Serikali tumekuwa tukifanya utaratibu wa kuonanamna nzuri ya kundi hili la wafugaji na mifugo yao, piawakulima waendelee na shughuli zao za kilimo kwa kuanzazoezi la uandikishaji wa mifugo tuweze kuitambua, kijiji gani,kina nani, ana mifugo kiasi gani ya aina gani, ili tuweze kuonakama je, mifugo hiyo inatosha kukaa kwenye eneo hilo,

Page 9: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

baada ya kuwa vijiji vyetu vyote vimefanyiwa mpango wamatumizi bora ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri leo nimeitaMaafisa Mifugo wa nchi nzima wako hapa na Saa Tanonitakutana nao pale Chuo cha Mipango. WaheshimiwaWabunge, Wafugaji na Wakulima yapo mambo ambayolazima watuvumilie, Serikali sasa lazima tuchukue mkondowetu. Tunahitaji sasa tuanze kujua utaratibu mzuri wa ufugajina kwamba Taifa hili tunataka tupate wafugaji ambao kwelini wafugaji wanaofuga, ambao wako serious kwenye ufugaji,ufugaji huu lazima uendane na maeneo ya kulisha ili kuondoamigogoro kati ya wakulima na wafugaji yanayopelekeakwenye mauaji ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyaeleza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kikao changu naMaafisa Mifugo ambao watakaa leo na kesho kujadili namnabora, tutatoka na azimio ambalo nchi nzima lazimalitatakiwa lifuatwe kwa namna bora ya kufuga mifugo yetu.Tunataka sasa Maafisa Mifugo washiriki kikamilifu kwakuwasaidia wafugaji namna bora ya kufuga mifugo yao ilitupate mifugo ambayo ina tija kwa yeye mfugaji binafsi lakinipia hata kwa mapato ya Kitaifa. Hatuwezi kuwatunajilinganisha na nchi ya Botswana ambayo ina ng’ombewachache kuliko Tanzania, lakini wenzetu wana mapatomakubwa ya Kitaifa, Tanzania tuna mapato kidogo ingawatuna ng’ombe wengi, maana yake hatufugi kwa utaalam.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kikao changu chaleo na Maafisa Mifugo nitatoka na maazimio ambayonitakuja kuyatamka hapa siku ya mwisho ya Bunge ili Taifatwende na utaratibu ambao kweli mifugo hii itakuwainaweza kuratibiwa vizuri na kufugwa vizuri ili itoe matokeoambayo tunayatarajia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kuchauka.

Page 10: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Pia namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamajibu mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa utaratibu huoumefanywa, mfano ipo mikoa ambayo siyo ya wafugaji kwaasili na utaratibu huu unaosema kutenga maeneo kwa mfanokama Halmashauri yetu ya Liwale tumetenga yale maeneo,lakini kutokana na hawa wafugaji kuwa na pesa nyingiwamekuwa wakiwahonga Viongozi wenye mamlaka,matokeo yake kijiji ambacho kimepangiwa idadi fulani yamifugo utakuta idadi ile inaongezeka.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, unawaeleza nini hawa watuwenye mamlaka mbalimbali kwanza, kwa Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na hata Wenyeviti wa Vijiji ili wafuate ilesheria kama kijiji kimepangiwa mifugo 200 basi iwe ni 200 nakama ni 1,000 basi iwepo 1,000. Je, nini kauli yako juu yahawa wenye mamlaka za kuwaruhusu hawa wafugaji?(Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapaumuhimu ni kuweka utaratibu na kila mmoja mwenyedhamana kutekeleza wajibu kwa dhamana ambayoamepewa. Baada ya kikao chetu nitatoa maelekezo kwaWakuu wa Mikoa walioko kwenye maeneo yetu, Wakuu waWilaya, Wakurugenzi, Maafisa wenyewe ambaowanashughulikia sekta hii ya mifugo kila mmoja lazimaawajibike inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelekezo yaletutawashirikisha Waheshimiwa Wabunge kwenye maeneoyenu, tuone kwamba matamko yetu ya Serikali yanakwendakwa Watendaji ili kusaidia kuondoa migogoro, migonganoambayo sio muhimu tuweze kuifuatilia ili nayo pia itusaidiekatika kuona kwamba sekta hii nayo pia inaweza kutoamwelekeo ambao tunautarajia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kufanya haya yote nayale ambayo tutayapata baada ya mjadala ambao

Page 11: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

tutauweka, tunafikiria pia kama ambavyo Wizaraimependekeza kuandaa zone za shughuli za mifugotukitambua Mikoa ambayo imejikita katika ufugaji tuwapenguvu zaidi ya kufuga zaidi ili na Serikali tuongeze nguvu yakuwasaidia wafugaji kwenye maeneo ambayo tunadhaniyanafaa zaidi kuimarisha mifugo. Yale maeneo ambayohayana mifugo hatuwezi kum-limit mtu ambaye anatakakuweka ng’ombe wake watano, sita. Muhimu zaidi, lazimauwe na idadi ya ng’ombe wanaotosha kwenye eneoulilonalo la kuwalisha.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu, ahsante.Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana.

Mheshimiwa Waziri Mkuu ni sera ya Serikali kuhakikishakwamba miundombinu katika maeneo mengine mengi yanchi hii inapitika, lakini unafahamu kwamba Mkoa wa Dares Salaam tuna mradi mkubwa wa DMDP ambao ni dolamilioni 75, takriban bilioni 158. Fedha hizi zinatakiwa zifanyekazi ya kusaidia miundombinu katika Manispaa zote tanoMkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Jimbo la Ukonga na Ilalaambalo tunaweza kupata bilioni 43.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, mradi huu umekuwaukisuasua sana, Jimbo langu la Ukonga lina Kata mbili Kataya Ukonga mitaa yote minne na Kata ya Gongo la Mbotobarabara zile zimeshindwa kutengenezwa kwa sababu fedhaimechelewa kutolewa.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa sababu unafahamuhali mbaya ya miundombinu baada ya mvua kubwa Dar esSalaam ikoje, nini kauli ya Serikali juu ya kuwezesha miradi hiimikubwa iendelezwe na fedha kupatikana ili kupunguzaadha kwa wananchi wa Dar es Salaam?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

Page 12: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakujibu swali la Mheshimiwa Mwita Waitara, Mbunge waUkonga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo kumbukumbukwamba tuliwahi kukutana Wabunge wote wa Mkoa waDar es Salaam, moja kati ya mambo ambayotuliyazungumzia ni huu mradi wa Dar es Salaam Metropolitankitu kama hicho, ambao pia unanufaisha Manispaa zetu zotetatu za Kinondoni, Ilala pamoja na Temeke kwa ujenzi wamiundombinu iliyoko kwa fedha ambayo tumeipata kutokaBenki ya Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tulishatoamaelekezo kwa Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam,tulitoa maelekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar esSalaam kuhakikisha kwamba fedha hii ambayo tumeipatakutoka Benki ya Dunia itumike kikamilifu. Nilihakikishiwakwamba usimamizi huo utafanywa na utekelezaji wa miradihiyo utafanywa ni vile sikujua kama swali hili litakuja hapaningeweza kufanya mawasiliano ya haraka ili kujua namnaambavyo wanatekeleza sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwahidi kwamba baadaya hapa nitawapigia simu kujua utekelezaji ukoje, kwasababu fedha tunayo, maeneo yaliyoharibika yapo namahitaji ya matengenezo ni muhimu kwa barabara zetu nahasa kwenye Jimbo lake la Ukonga na maeneo mengine,Mheshimiwa Mwenyekiti pia ni mnufaika wa mradi huu waDMDP ambao pia tungehitaji pia naye aweze kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu kwamba,baada ya kikao hiki nitapiga tena kwa Katibu Tawala anipemrejesho wa namna hiyo. Pia Waziri wa TAMISEMI yuko hapa,ataanza kuwahi kupiga simu kule kujua nini kinafanyika,halafu atanipa mrejesho hapa Bungeni. Kama jambo hilohalijakamilika, basi tutafanyia kazi. (Makofi)

Page 13: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru sana kwamajibu hayo na nafikiri watu wa Dar es Salaam watakuwawamefurahi kusikia kwamba umetoa maelekezo sasamaalum ya kufuatil ia mradi utekelezwe mapemaiwezekanavyo. Nina swali moja la nyongeza. MheshimiwaWaziri Mkuu, Ukonga ni Jimbo jipya na ni Majimbo ya MjiniVijijini, lakini barabara yangu ya Kitunda, Kivule, Msongolaimekuwa na hadi zaidi ya miaka 25 sasa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, naomba ukae.Hilo swali lako sio la kisera lakini vile vile katika pesa hizo hizoza DMDP zipelekwe huko huko kwenye barabara hiyo.

Ahsante, naomba ukae, maana hata hizo DMDP namimi nimo humo. Tunaendelea na Mheshimiwa Gulamali.(Makofi/Kicheko)

MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi kumuuliza swali MheshimiwaWaziri Mkuu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, kumekuwa na matukio yaukamataji katika maeneo mbalimbali hasa Wilaya ya Igungana maeneo mengineyo ya nchi hasa kukamatwa kwamifugo, mifugo hii inapokuwa inakamatwa wakati mwinginekatika hifadhi huwa inapigwa minada pasi na kuwashirikishawale ambao ng’ombe wao wamekamatwa, tayarikunakuwa na watu tayari ambao wanatoka Dar es Salaamkuja kununua ile mifugo katika yale maeneo, wale ambaong’ombe wao wamekamatwa wakienda kutaka kununuawale ng’ombe hawaruhusiwi na watu wa hifadhi. Je, Serikaliinatoa tamko gani juu ya ukamataji hovyo wa ng’ombekatika maeneo haya yetu pia juu ya kauli tata ya MheshimiwaWaziri wa Maliasili kwa wafugaji?

Page 14: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakujibu swali la Mheshimiwa Gulamali, Mbunge wa Manonga,kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake eneo ambalonimeweza kulipata vizuri ni pale ambapo anataka Serikaliitoe tamko juu ya ukamataji wa mifugo. Suala la mifugolinafanana na swali ambalo limeulizwa hapa awali nanimetoa maelekezo kwamba leo hii nakutana na MaafisaMifugo wote nchini kufanya mapitio ya udhaifu na upungufu.Pia kuimarisha utaratibu ambao tutaweza kuutoa kwa sektaya mifugo nchini ambayo imeweza kupelekea matatizomengi, kuwa na migongano ya wakulima na wafugaji,migongano ya wafugaji na maeneo yetu yaliyohifadhiwakisheria, lakini tuna migongano tu ya wafugaji wenyewe kwakuchanganya ng’ombe na vitu vya namna hii na ikomigogoro mingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbungeanataka kujua Serikali inasema nini juu ya ukamaji wa hovyo.Kimsingi iko sheria inayoelekeza mifugo, shughuli za kilimozifanywe kwenye maeneo gani. Kwa hiyo, kama kunakuwana ukiukwaji lazima kutakuwa na ukamatwaji. Kwa hiyo, hilowalijue kwamba maeneo yote haya tumeyaratibu natumeyawekea sheria ya namna kila mmoja anatakiwakuyatumia, unapokwenda kinyume lazima utakamatwa.Kwa hiyo, hilo ndilo jibu la msingi la kwamba lazima kutakuwana kukamatwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni udhaifu ganiumejitokeza katika ukamataji kama ambavyo nimeshaurijambo hili niachiwe kwa sababu leo nakutana na Maafisawanaoshughulikia mifugo kwenye Halmashauri zote ikiwemona Halmashauri yake ya Igunga ambayo pia ina wafugaji,ina wakulima ili tuweze kuondoa matatizo hayo.

Page 15: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi hatuhitaji kuwa namigogoro kati ya makundi yetu huko ya wafugaji, wakulimana watumishi wetu wa hifadhi pale ambako kila mmojaangehitaji kupata huduma. Sasa tunataka tuweke utaratibuwa nani, wakati gani na kwa namna gani, unaweza kupatahuduma kutokana na shughuli unayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge, mudawetu umekwisha na Mheshimiwa Waziri Mkuu maswaliyamekwisha. Nakupongeza, Wazungu wanasema man of allseasons, hongera sana Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Katibu.

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Maswali ya kawaida, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mheshimiwa Omari Shekilindi.

Na. 394

Huduma za Afya kwa Makundi Maalum

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza:-

Wilaya ya Lushoto ni Kongwe na ina wananchiwapatao 550,000; kati ya hao kuna wenye ulemavumbalimbali, wajane na wazee na wengi wao wapo vijijinina hawajawahi kupata huduma za msingi:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia makundihayo ili nao waweze kupata huduma muhimu kama watuwengine?

Page 16: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Shabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utambuzi wa watu wenyeulemavu wapatao 699 umefanyika, watoto wanaoishi katikamazingira hatarishi 3,471 wametambuliwa na wazee 8,511wametambuliwa. Zoezi hili ni endelevu kwa Halmashauri zotekwa ajili ya kutumia takwimu hizo katika mipango na bajetikila mwaka wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wa seraya utoaji huduma bure kwa makundi maalum, Halmashauriya Wilaya ya Lushoto hivi sasa imefanikiwa kutoa kadi zaCHF kwa wazee 3,991 na watoto wanaoishi katika mazingiramagumu 1,619 wamepewa kadi za msamaha wa gharamaza matibabu. Aidha, dirisha maalum limefunguliwa kwa ajiliya huduma za wazee katika vituo vyote vya afya vya kutoleahuduma za afya. Serikali itaendelea kuboresha hudumazinazotolewa kwa makundi maalum yenye msamaha wamatibabu kwa kutenga bajeti kila mwaka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Shekilindi.

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kuniona ili niweze kuuliza maswalimadogo mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, Ilani ya Chamacha Mapinduzi inasema kila Kata kitajengwa kituo cha afya;je, Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga vituo vya afyavinne kwenye vituo hivyo 150 ambavyo Serikali itavijenga nchinzima hasa katika Kata ya Ngwelo, Makanya, Malibwi naKata ya Gare. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mimi kamaMwakilishi wao naomba nimhakikishie Mheshimiwa NaibuWaziri kwamba makundi haya hayapati huduma

Page 17: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

aliyoiongelea hapo pamoja na kwamba majibu yakeameyajibu kitaalam. Je, yupo tayari kwenda au kutuma timuyake ili ikapate uhalisia wa kuwa makundi hayo hayapatihuduma hiyo ipasavyo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza katikampango mkakati wa ujenzi wa vituo vya afya jambo hilitumelipa kipaumbele zaidi. Mheshimiwa Mbunge Shekilindianafahamu hata tulivyokwenda pale tuliangalia Halmashauriya Lushoto na ndiyo maana tukaona kwamba kwa sababuLushoto ina changamoto kubwa sana aliyoizungumza hapakatika ujenzi wa hivi vituo vipya tunavyoenda kuvijenga, lakinisasa hivi tunaenda kufanya ukarabati mkubwa katika kituohicho cha Mtao katika Halmashauri ya Lushoto japokuwakiko katika Jimbo la Mheshimiwa Shangazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishiekwamba ni mpango wa Serikali na hasa Lushoto ukiangaliachangamoto yake, ile barabara kwanza hata mvua ikinyeshahuduma inakuwa ni changamoto kubwa. Naombanimhakikishie kwamba tutaipa kipaumbele kwa kushirikiananaye na Halmashauri yake, kuhakikisha kwamba Lushotoinapata huduma nzuri za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima lakwamba watu hawapati huduma hii inayokusudiwa naameniomba niweze kufika tena. Naomba nimhakikishiekwamba nina zoezi la Q and A’s (questions and answers),mara baada ya kuwapatia Watendaji mbalimbali waHalmashauri maelekezo, zoezi la pili ni kwenda kufanyaverification, jinsi gani wamefanya compliance ya yale ambayotumeelekezana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishiekwamba tutafika Lushoto, hata hivyo, nilivyofika katikahospitali ambayo iko pale nimekuta dirisha la wazee lipo.

Page 18: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Namhakikishia tutakwenda mimi mwenyewe natutashirikiana na yeye kufanya verification kuona jinsi ganisasa wananchi hawa wanapata huduma hiyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Susan Kiwanga.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Suala la walemavu nchi hii limekuwa sugu kwamiaka mingi lakini Serikali bado haijaweka mpango mkakatiwa kuwasaidia walemavu wao. Kwa mfano, ndani ya Jimbolangu la Mlimba kila siku napata maombi ya walemavuwakiomba vifaa na wengine watoto wadogo hawanauwezo kabisa wa kwenda kwenye shule maalum zawalemavu. Je, Waziri yuko tayari sasa kutoa mpangomkakati wa kusaidia walemavu hawa, kuorodheshaHalmashauri zote ili wasaidiwe kwa mpango maalum?Maana tatizo hilo limekuwa sugu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, MheshimiwaKiwanga ni kweli inawezekana huko nyuma tulikuwahatufanyi vizuri zaidi, lakini katika Serikali ya Awamu ya Tanotumefanya mambo makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wiki iliyopita tulishuhudiaWaziri Mkuu akipokea vifaa maalum kwa ajili ya kundi hili lawatu wenye ulemavu ambapo vifaa vile tutavipelekasehemu mbalimbali, lengo kubwa ni kuwasaidia watu wenyeulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, sasa hivi kunadatabase maalum inaandaliwa katika zoezi hilo. Kwa hiyonaomba nimtoe shaka, Serikali imejipanga, tutafanya kilaliwezekanalo, lengo letu kubwa ni kuhakikisha kundi hili lawatu walemavu linapata huduma. Vile vile kwa sababutulikubaliana baada ya Bunge hili tutafika kule katika Jimbolake, katika haya nayo tutaangalia katika muktadha mpana

Page 19: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

sana, katika eneo gani na jinsi gani tufanye, kama kunajambo specific katika eneo hilo. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na Wizara hiyo hiyo, Mheshimiwa Tendega.

Na. 395

Kuboresha Maslahi ya Walimu Nchini

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:-

Miaka ya 1980 kulikuwa na ushindani mkubwauliojitokeza kati ya shule binafsi na za Serikali ambapo Walimubora wote walipatikana katika shule za Serikali kutokana namaslahi bora ikiwemo posho zaidi nje ya mshahara kamavile posho ya ufundishaji, posho ya kupanga, posho ya usafirina posho ya mazingira magumu:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuboreshamaslahi ya Walimu kama ilivyokuwa miaka ya 1980 ilikuendana na dhana ya elimu bure lakini bora?

(b) Je, Serikali ina mpango mkakati gani wakuboresha zana za kufundishia ili kwenda sambamba naukuzaji wa ujuzi wa stadi za taaluma wanazosoma?

(c) Kwa kuwaombea Walimu wapande mabasibure kwenda kazini kama ombaomba kama ilivyotokea Dares Salaam; je, huku sio kuwadhalilisha?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha

Page 20: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

elimu nchini, Serikali imeanza kutoa posho kila mwezi kamamotisha kwa Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na WaratibuElimu Kata ili kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu.Aidha, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishiwa Umma na Utawala Bora inafanya mapitio ya majukumuya watumishi wote wakiwemo Walimu ili kuboresha maslahiya watumishi wote kwa kuzingatia uzito wa kazi.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechapishana kusambaza vitabu, chati na miongozo mbalimbali yakufundishia na kujifunza zipatazo 8,359,868 kwa ajili ya darasala kwanza na la pili na tayari vimeshasambazwa katika shulezote za msingi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usambazaji wa vitabuhivyo, umeboresha uwiano wa kitabu kwa mwanafunzikutoka uwiano wa 1:3 hadi 1:2, lengo likiwa ni kufikia uwianowa 1:1 kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka2015. Vile vile, Serikali imefanikisha kununua na kusambazavifaa vya maabara vyenye thamani ya shilingi bilioni 16 ilikuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa vitendo.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwawekeautaratibu Walimu kupanda mabasi bila kulipia siyo azma yaSerikali kuwadharau Walimu na kuwafanya kuwaombaomba, bali ni njia ya kuthamini kazi nzuriinayotekelezwa na Walimu hapa nchini. Naomba kutoa raikwa viongozi wote wakiwemo Waheshimiwa Wabungekatika maeneo yetu kubuni utaratibu wa kuwapatia motishawatumishi ili kuwapa ari ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tendega.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali ya nyongeza.Mheshimiwa Waziri amesema katika majibu yake kwambaSerikali imechapisha vitabu na kusambaza vitabu milioni8,359,868, Je, katika vitabu hivi ndivyo vitabu ambavyo Bungeletu lilishuhudia ni vitabu vile ambavyo vina upungufu wa

Page 21: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

kisarufi pamoja na kimaudhui? Je, hawaoni kama wanaendakulisha sumu watoto wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika majibuya Mheshimiwa Waziri amesema Wabunge twende tukafanyeutaratibu wa kuwapa motisha watumishi katika maeneoyetu. Ikumbukwe kwamba Mbunge ni Diwani katikaHalmashauri zetu na hivi majuzi tu Wizara ya Fedhawamesoma bajeti yao na tumeona katika bajeti ile vyanzovya mapato katika Halmashauri vimechukuliwa na SerikaliKuu. Je, Serikali iko tayari kurudisha vyanzo vya mapatokatika Halmashauri zetu ili tuweze kuipanga bajeti na kuwana posho za ziada kwa watumishi wetu? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi,mengine tumia uzoefu wako tu. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanaomba nimshukuru dada yangu kwa swali zuri ambaloukizungumza suala la elimu na bahati nzuri hapa kuna swalilingine ameuliza Mheshimiwa Mbatia liligusa suala zima laelimu. Naomba nikiri wazi kwamba ndiyo maana Bunge hilililifanya maazimio maalum kuhusu vile vitabu ambavyovilikuwa na changamoto na ndiyo maana hivi sasa Wizaraya Elimu imeshaunda timu kufanya verification ya yalemakosa ilimradi mwisho wa siku tuje kufika katika sehemumuafaka ambako Taifa letu hili linakwenda. Kwa hiyo,naomba aondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, Serikali sualahili iko katika kulifanyia kazi kwa kina kwa maslahi mapanaya elimu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la vyanzovya mapato ambapo Waziri wa Fedha alizungumza hapakwamba vyanzo hivi sasa vingine vimerudi Serikali Kuu.Naomba niwaambie, leo hii hapa ninapozungumza kwasababu sisi ni Serikali za Mitaa kuna baadhi ya Halmashaurizingine uwezo wake ni mdogo zaidi. Kwa hiyo, ni jukumu laSerikali kufanya tathmini pana lengo ni kukusanya mapatokwa kiwango kikubwa halafu kuyarudisha katika Halmashauri.

Page 22: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni commitment ya Serikalihivi sasa na Waziri wa Fedha atakapohitimisha hapaatazungumza wazi kwamba fedha hizi zitakapokusanywahata zile property tax, fedha hizi naomba niwahakikishieWabunge kwamba zitarudi katika Halmashauri zetu ilimipango yetu ya bajeti ambayo imepangwa iwezekutekelezeka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chatanda, MheshimiwaSusan Lyimo na Mheshimiwa Mboni Mhita.

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza, IliWalimu waweze kufanya vizuri kwa kutulia, wanahitajiwasikil izwe kero mbalimbali ndogo ndogo ambazozinawakabili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo baadhi ya Walimuambao wake zao au waume zao wako mbali na wao,wameomba uhamisho kwa muda mrefu hawajafanikiwawenzi wao kwenda kwenye maeneo yale ambayowanatakiwa kufanya kazi. Kwa mfano, kule Korogwe kunaMwalimu ambaye yupo Korogwe lakini mke wake yukoMtwara. Je, Serikali, ili kupunguza kero ndogondogowatakuwa tayari sasa kuwasaidia Walimu ili kuwahamishawake zao waende kwenye maeneo ambayo wapo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili najuakwamba lina maslahi mapana kwa sababu ndoa za watuni maisha ya watu. Zoezi hili la uhamisho limekuwa tofautina miaka mingine lilisimama kwa sababu tulikuwa na zoezikubwa sana la kufanya verification hapa ambapo ninyimmebaini wazi kwamba suala la watumishi hewa, suala lavyeti feki, jambo hili ndio lilisababisha maeneo mengi sanahasa suala zima la uhamisho liweze kusitishwa.

Page 23: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuhakikishieMheshimiwa Mbunge jambo hili lipo katika utaratibu wamwisho, litakamilika, baadaye tutatoa maelekezo rasmi sasaya jinsi gani uhamisho huu utaanza, kwa sasa lilisimama kwamaslahi mapana ya nchi yetu, litaendelea mara baada yazoezi zima la uhakiki wa vyeti feki.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Susan Lyimo,jiandae Mheshimiwa Mboni.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Kwanza nimesikitishwa sana na majibuya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Sera ya Elimu ni kitu kingine navitabu ni kitu kingine, naomba niulize swali sasa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa uliza swali lako achamambo mengine.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Sawa nauliza swaliMheshimiwa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Utakaa chini sasa hivi hapo.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimuulize swali Mheshimiwa Naibu Waziri hasa lavitabu, pamoja na kwamba Kamati imeundwa naMheshimiwa Waziri wa Elimu, lakini nimepita kwenye shulembalimbali bado vitabu vilevile vyenye makosa ndivyovinavyotumika. Nilitegemea Wizara ingevitoa waendeleekutumia vitabu vya zamani. Je, sasa hawaoni kwambakuendelea kutumika kwa vitabu hivyo, ni makosa makubwana wanapanda sumu kwa watoto wetu na ni l iniwataviondoa vitabu hivyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Elimu, limejibiwana Waziri Mkuu hapa vilevile, endelea.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Bahati nzuri wakatiwa bajeti yetu wewe ulikuwa una-chair na suala la vitabu

Page 24: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

tulilijadili na Bunge likawa limetoa maelekezo kwambabaada ya Serikali kukamilisha, taarifa tutaiwasilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kufanyiakazi na niwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba kwasasa hivi wanafunzi wapo likizo, suala la kusemawanaendelea kutumia vitabu kwa sasa hivi wapo likizo. Hatahivyo, si vitabu vyote ambavyo vina makosa na kama Serikalii l ivyokwishasema baada ya Kamati za Wataalamkukamilisha, maamuzi ya Serikali yatawasilishwa kamaambavyo tayari Kiti chako kilikuwa kimeelekeza. Kwa hiyo,ningeomba Waheshimiwa Wabunge wavute subira,waiachie Serikali ifanye suala hili kwa umakini unaotakiwana muda unaotakiwa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mboni.

MHE. MBONI M. MHITA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kuna uhaba mkubwa sana wa nyumba zawatumishi katika Jimbo la Handeni vijijini, japo Halmashauri,wananchi pamoja na Mbunge wamejitahidi sana kwa halina mali kuweza kupunguza changamoto hii. Je, Serikali inampango gani ya kuweza kupunguza au kumaliza kabisachangamoto hii ya nyumba za Walimu katika maeneo yavijijini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunachangamoto hizi za nyumba za Walimu na nawashukurukwanza Waheshimiwa Wabunge tulivyokuwa tunajenga zilenyumba karibuni 229 ambazo ni six unit in one nilipataushirikiano wa kutosha sana katika ofisi yetu kuhakikishakwamba tunatoa maelekezo na mpaka nilivyofika mweziwa 12 tulifanikisha kujenga zile nyumba zote ndani ya MMESII ambazo ni kwa ajili ya Walimu wetu wa sekondari.

Page 25: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo katika mpangowa sasa tunaendelea katika bajeti ya mwaka huu, tutajenganyumba kadhaa katika maeneo mbalimbali. Naomba nikiriwazi kwamba ni kweli Jimbo lake lina changamoto yanyumba, naomba nimhakikishie kwamba Serikali tutaangalianini tufanye, tutafanya kila liwezekanalo nipende kuwaombahasa Wakuu wa Wilaya mbalimbali tuweze kuiga Mkuu waWilaya ya Lushoto anavyofanya kazi katika maeneo yake.Nimepita kule Lushoto kuna mambo mengi sana ya mfanoyanafanyika, naamini tukifanya haya tutaweza kupatamafanikio makubwa sana katika miundombinu hasa katikasekta ya elimu na sekta ya afya.

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaendelea, Wizara nahiyohiyo, Mheshimiwa Mussa Ntimizi kwa niaba yakeMheshimiwa Almasi.

Na. 396

Kujenga Mabwawa ya Maji Jimboni Igalula

MHE. ALMAS A. MAIGE (K.n.y. MHE. MUSA R. NTIMIZI)aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga mabwawaya maji katika Jimbo la Igalula hasa ikizingatiwa kuwa Jimbohili lina maeneo mazuri ya kutega mabwawa ya maji?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Musa Rashid Ntimizi, Mbunge wa Igalula, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka wafedha 2016/2017, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradiwa bwawa katika Kijiji cha Igalula unaohusisha ujenzi wamiundombinu ya maji. Utekelezaji wa mradi huu wenye

Page 26: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

thamani ya shilingi milioni 365.47 unaendelea na mkandarasianakamilisha kazi hiyo ifikapo tarehe 23 Agosti, 2017 ikiwa nimkataba wa miezi minne (4).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kufanyajuhudi kubwa kwa kuangalia fursa mbalimbali za miradi yamaji ili kupunguza shida ya maji katika Jimbo la Igalula naHalmashauri ya Wilaya ya Uyui kwa ujumla.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Almasi.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kwa niaba yaMheshimiwa Musa Ntimizi na wananchi wa Jimbo la Igalula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa vile,Jimbo la Igalula halitapatiwa kabisa maji ya Ziwa Victoria;je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza mradi wakuchimba mabwawa katika Vijiji vya Igalula, Goweko naLoya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa vile Wilayanzima ya Uyui haina maji chini; je, Serikali ina mpango ganitena wa kuchimba mabwawa katika vijiji vya Jimbo laTabora Kaskazini vya Kanyenye, Majengo na Izugawima.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hilianalozungumza Mheshimiwa Mbunge kweli kunachangamoto hii ya maji, ndiyo maana pale kuna miradi yamabwawa. Kuna moja ambalo inafanyika design pale lakinikuna mradi mwingine upo katika maandalizi ya hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa sababuinaonekana kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Uyui naMbunge anafahamu siku ile tulipokuwa kwenye vikao vyaHalmashauri miongoni mwa shida kubwa aliyozungumzapale kwa niaba ya wananchi wake ni shida ya maji katika

Page 27: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Wilaya nzima ya Uyui. Serikali katika mpango wake hivi sasa,licha ya masuala ya mabwawa imefanya uwekezaji mkubwasasa wa kutenga fedha nyingi za kutosha na hasa zinginekutoka wahisani wetu kutoka India, sasa fedha nyingizinapelekwa katika suala zima la mradi wa Ziwa Victoria nabahati nzuri mnafahamu mradi ule umezinduliwa rasmi.Naomba nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba mradiule kupitia Wizara ya maji utatekelezwa kusaidia Halmashauriya Wilaya ya Uyui na Mkoa mzima wa Tabora kamaulivyokusudiwa wakati wa uzinduzi wa mradi ule.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleamuda wetu umekwisha, tumebakiwa na dakika 10 tu nabado tuna maswali. Wizara ya Maliasili, Mheshimiwa YussufSalim Hussein.

Na. 397

Ulinzi na Udhibiti wa Misitu Nchini

MHE: YUSSUF SALIM HUSSEIN aliuliza:-

Kuongezeka kwa idadi ya watu na ukosefu wa ajirakwenye sekta nyingine kumechangia sana jamii kubwa yawatu kujikuta kwenye shughuli zinazosababisha uharibifu wamisitu kwa ajili ya kumudu maisha yao:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza udhibiti naulinzi pamoja na upandaji miti nchini?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kumekuwana ongezeko la vitendo vya baadhi ya wananchi kuvamiana kutumia maeneo ya hifadhi za misitu na wanyamaporikinyume cha sheria na kufanya shughuli za kibinadamu kamavile kulima, kufuga, kuchimba madini na kuvuna mazao yamisitu kama vile mbao na magogo kwa visingizio mbalimbaliikiwemo ukosefu wa maeneo ya kufanya shughuli hizo.

Page 28: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kwa kutumiaSheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 imekuwa ikichukuahatua mbalimbali kudhibiti hali hiyo ikiwa ni pamoja nakufanya doria za mara kwa mara, kukamata wakiukaji washeria na kuwachukulia hatua mbalimbali za kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kwakushirikiana na wadau wengine inaendelea kuboreshausimamizi wa misitu na kusisitiza kuhusu mipango ya matumizibora ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini. Aidha,Wizara inaendelea kuboresha utekelezaji wa jukumu hili kwakuongeza idadi na umahiri wa watenda kazi wa uhifadhi,kuongeza vitendea kazi na kuboresha mazingira ya kazi kwawatumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada hizo zaSerikali za kuimarisha ulinzi kwa kutumia Askari wa Uhifadhi,Wizara inasisitiza kuwa njia bora zaidi ya kuhakikisha uhifadhina matumizi endelevu ya misitu na bidhaa za misitu ni kwawananchi kushiriki katika vita hii kwa utaratibu wa uhifadhishirikishi. Hivyo, Wizara itaendelea kutoa elimu kwa jamii nakutoa wito kwa wananchi wote kushiriki katika vita hiimuhimu kwa mustakabali wa Taifa kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la upandajimiti, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira), imeandaa mkakati wa kuhifadhi mazingira nakupanda miti ambao utashirikisha wadau wote nchini. Serikaliitaendelea kuhimiza utekelezaji wa agizo la kupanda mitikwa Halmshauri za Wilaya kote nchini.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Yussuf Salim.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake, lakininina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati ya upandaji mitikatika nchi hii imeanza miaka mingi sana iliyopita, tokeamiaka ya 1980 kwa miradi mikubwa ya wafadhili ambayo

Page 29: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

ilikuwa ni miradi ya HASHI na HADO lakini bado nchi yetuinaendelea kuwa jangwa. Hebu Mheshimiwa Waziriatuambie, hiyo mikakati hasa ni ipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, suala la malezibora kutoka utotoni sio kwa wanadamu tu, lakini hata kwamiti na pale miti, katika miaka mitatu ya mwanzoinapopandwa ndio inahitaji hasa kulelewa na utalaamunahitajika pale, leo Chuo cha kutoa wataalam wa Misitucha Olmotonyi kimetelekezwa mpaka inafikia hatuamwanafunzi anajil ipia mwenyewe ndio asome. Je,Mheshimiwa Waziri hii miti inayopandwa ni asilimia ngapiambayo ina-survive ili nchi yetu isiendelee kuwa jangwa?Nashukuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza ni kweli kabisa kwamba kasi ya uharibifuwa mazingira kwa maana ya uharibifu wa misitu ni kubwasana. Takwimu zinaonesha kwamba kiasi cha hekari 372,000cha misitu kinaangamia kila mwaka na kutokana natakwimu hizo za uharibifu wa kiasi hicho ili tuweze kurudikatika hali ya kawaida, ili tuweze kwenda sambamba katikamkakati wa kukabiliana na hali hii tunapaswa kuwatumepanda jumla ya hekari 185,000 za miti, hii ni sawa namiti milioni 280 kwa kila mwaka, kwa sababu zile hekari185,000 kwa muda wa miaka 17.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mikakati hiyo ni ipi.Mkakati una mambo mengi, lakini kwa sababu ya muda huunilionao kwa majibu ningeweza kusema kwamba utekelezajiwa mkakati huo utafanyika katika Mamlaka za Serikali zaMitaa zote 181, kwenye vijiji vyote 3,692 na mitaa 6,538.Mahali ambako kinachofanyika ni uhamasishaji, lakini piakutoa elimu na kuwezesha kwa namna mbalimbali ili zoezihili liweze kufanyika kwa ushirikiano wa wananchi wote kwaujumla nchi nzima, tuweze kufikia viwango hivyo vya kuwezakurudisha misitu katika hali yake ya kawaida baada yauharibifu ambao nimeuzungumza hapo awali.

Page 30: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la piliambalo anazungumzia malezi bora ya tangu awali, kwambaanazungumzia miti inavyopandwa iweze kupandwa nakusimamiwa mpaka iweze kukamilika. Hoja yake ya msingini kwamba unaweza kupanda miti, lakini ukisha pandausipoitunza humo katikati miti mingi inapotea na ili uwezekufikia malengo hayo unahitaji kuwa na wataalamwatakaoweza kusimamia, pamoja na kushirikisha wananchilakini lazima uwe na wataalam wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba kwa sasahivi Serikali kwa namna ilivyojipanga kwanza tunatambuagap hiyo ya wataalam ni kubwa kiasi gani, kutokana naukubwa wa misitu tuliyonayo tungepaswa kuwa na jumlaya wataalam 9,600 na ukiangalia idadi ya wataalamtulionao tuna gap kama 3,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimfahamishe MheshimiwaMbunge tu kwamba tutatumia Vyuo vyetu kikiwemo hichocha Olmotonyi, kwamba tunakiboresha Chuo cha Olmotonyiili kiweze kuchukua wanafunzi wengi zaidi, pia kuboreshamazingira ambayo yatawawezesha kujifunza wawezekuhitimu wakiwa na huo ujuzi na si suala la kujaza idadi tu.Kama nilivyosema kwenye jambo langu la msingi tunatakwawawe wengi, lakini tunataka pia wawe na ujuzi ambaotunaohitaji ili waweze kwenda kushiriki katika kukamilishamalengo tunayokusudia.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleamuda wetu umekwisha kabisa Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia, Mheshimiwa Josephine Tabitha Chagula, Mbungewa Viti Maalum.

Na. 398

Hitaji la Chuo cha VETA Geita

MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA aliuliza:-

Mkoa wa Geita hauna Chuo cha Ufundi (VETA):-

Page 31: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Chuo chaVETA katika Mkoa wa Geita?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Josephine Tabitha Chagula, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu Swali Na.48 tarehe 4 Novemba, 2016 kuhusiana na ujenzi wa Chuohiki, Serikali inaendelea na maandalizi ya ujenzi wa Chuohiki kwa Mkopo wa Fedha toka Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB).

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chagula.

MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Nampongeza Mheshimiwa NaibuWaziri kwa majibu yake mazuri na ya kututia moyo wananchiwa Mkoa wa Geita, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru sana Serikali kwakuliona hilo tatizo letu la kutokuwa na Chuo cha VETA Mkoawa Geita na kuweza kupanga na kuanza kujenga, sasa niulizeni lini sasa utekelezaji wake ili Chuo hicho kiweze kukamilikakwa wakati ili wananchi na watoto wetu walio wengi, vijanawaweze kupata ujuzi na kujiajiri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mkoa wa Geitahauna kabisa Chuo chochote cha Serikali, je, Serikali inampango gani wa kuweza kujenga vyuo vyote kwa pamojakikiwemo Chuo cha Madini na ikizingatiwa kwamba Mkoawa Geita ni wadau wakubwa wa madini? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

Page 32: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nashukuru kwa shukranializotupa kwa niaba ya Waziri wangu. Vilevile katika swalilake niseme tu kwamba utekelezaji huu unategemeana sanana masharti ambayo yanaendana na mtoa mkopo huoambaye ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kamanilivyosema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hatua mbalimbalizinaendelea sasa hivi tupo kwenye hatua za mwisho zakumpata Mshauri Elekezi. Hata hivyo, lazima niseme kwaniaba ya Mheshimiwa Waziri wangu kwamba sisihatujaridhishwa na namna ambavyo taratibu za ujenzi wavyuo hivi hususani vinne vya Kimkoa unavyoendelea, tunaonahatua zimekuwa ni za taratibu sana. Kwa hiyo, tayaritumeshawaita wenzetu ili tukae tujadiliane ili tuone namnabora ya kushughulikia suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusianana kutokuwa na chuo, nafahamu kwamba Geita tunachoChuo Kikuu Huria. Pia katika suala la madini hii VETAtunayotegemea kuijenga Geita sehemu kubwa ya fani zakeitakuwa ni kushughulikia masuala ya madini kwa kuwamaeneo hayo ndio chimbuko kubwa la madini katika nchiyetu kwa sasa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulembo.

MHE. ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Kwa sababu suala la msingi laGeita linafanana na suala ambalo nauliza katika Mkoa waKagera. Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao una Wilaya zaidiya saba, Majimbo nane hakuna hata dalili za kuwa na Chuocha VETA. Je, Serikali inatuambiaje kuhusu Mkoa wa Kagera?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Mzazi

Page 33: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

ni kweli tunahitaji kuwa na chuo kikubwa cha VETA chuomahiri, lakini kwa sasa tunayo VETA pale Bukoba Mjini. Piakuna chuo cha KVTC ambacho kipo Karagwe nachotunakifanyia ukarabati mkubwa il i kiweze kuchukuawanafunzi wengi zaidi, vilevile kuna mkakati wa kujengachuo cha Kimkoa pale Muhengele ambapo tuna tatizo labarabara pamoja na miundombinu ya umeme, wafadhiliwapo tayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwambaMheshimiwa Mbunge Rweikiza ambaye anafuatilia amesemakwamba ameahidiwa kuondolewa hizo changamoto ili nasisi tuanze ujenzi mara moja. Vilevile kuna Gera ambayo piasasa hivi imeshafanyiwa ukarabati Chuo cha Wananchi nakinaendelea kutoa mafunzo ya ufundi.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwisha. Jana wachangiaji watatu hawakupata nafasikwa sababu ya muda.

Waheshimiwa Wabunge, wageni waliopo Ukumbini,mpaka sasa hivi orodha kamili sijaipata, lakini ipo orodhaya Mheshimiwa Oran Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini anawageni wake wanakwaya 35 kutoka Mbalizi Mbeya nawanachuo kumi wa UDOM wa kutoka Wilaya ya Mbeya,karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Katibu.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba mwongozo wakokwa mujibu wa Kanuni ya 64 inayosema:

“Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katibayanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadilianokatika Bunge.”

Page 34: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiunganisha Kanuni ya 68inayohusu jambo lililotokea mapema ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Bunge lako Tukufu lilitoamaagizo kwamba tusiwajadili Viongozi Wastaafu, lakini kwamujibu wa Sheria ya The Parliamentary Immunities Powers andPrivilege, sisi kama Wabunge tuna immune ambazo zinatupamamlaka tukiwa ndani ya Bunge ku-dialog na kujadilimambo mbalimbali yanayolihusu Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Ibara ya 100 inazungumza uhuru wamawazo ndani ya Bunge. Kwa hiyo sisi kama Wabunge, uhuruwa mawazo ndani ya Bunge hili siyo powers ambazotunapewa na mtu, tunanyang’anywa halafu tunarudishiwani powes za Kikatiba, ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania inatupa hizo powers. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni zetu zinasema hivyokwamba tunaruhusiwa kujadiliana, Katiba inaruhusu na hiziimmune tunazo na majadiliano tunayoyafanya haya,hatuamui kuwaondoa watu madarakani ni kushaurianaili kuliongoza Taifa tuangalie tulikosea wapi, twendewapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wakokwamba kwa kutuzuia tusiwajadili baadhi ya watu je,Wabunge tunanyang’anywa hizo powers na immunitiesambazo tumepewa kwa mujibu wa sheria na kwa mujibuwa kanuni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako.(Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hili sualalinajirudia sana. Ruling niliyotoa jana ndio final. Kwa lughaya Kibunge ruling niliyotoa jana ndio final na haina mjadalandani ya Bunge, isipokuwa unaweza vilevile kurudi kwenyehiyo Katiba Ibara ya 100, ambayo inatoa fursa hiyo ukishukachini, Katiba hiyo hiyo imetoa fursa kwa Bunge kujitungia

Page 35: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Kanuni zake za kuendesha Bunge na Kanuni za kuendeshaBunge tumezipitisha hapa na Mheshimiwa Msigwa na weweulikuwa ni mmoja wa Wabunge waliopitisha Kanuni zetundani ya Bunge. Kwa hiyo, the ruling stands. Nakushukurusana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, orodha wa wageniimekuja. Tunao wageni 50 wa Mheshimiwa Dunstan Kitandulaambao ni wanafunzi na Walimu kutoka shule ya Msingi St.Joseph Millenium ya Mkoani Dar es Salaam, karibuni. (Makofi)

Wageni waliokuja Bungeni kwa ajili ya mafunzo niwanafunzi 62 na Walimu Sita kutoka Shule ya Msingi MaranguHills, iliyopo Wilaya ya Marangu, Mkoani Kilimanjaro. (Makofi

Vile vile wapo wanafunzi 50 na Walimu watanokutoka Shule ya Msingi Mazengo iliyopo Mkoani Dodoma,karibuni. (Makofi)

Pia kuna wanafunzi 75 kutoka Chama cha Wanafunziwa Kiswahili wa Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Tawi la ChuoKikuu cha St. John kilichopo Mkoani Dodoma, karibuni.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na hoja zaSerikali, ni Waziri wa Fedha na Mipango. Katibu.

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

na

Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato namatumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

(Majadiliano yanaendelea)

Page 36: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

MWENYEKITI: Sasa namwita mchangiaji wetu wakwanza, Mheshimiwa Riziki Said Lulida.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Bismillah Rahman Rahim.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru kwakunipa nafasi ya kuwa mchangiaji wa kwanza na MwenyeziMungu anijalie hilo nitakalolizungumza liwe ni haki na ukweli.Tukisimamia haki tutafikia mahali ambapo nchi hiitutaitendea haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge inabidi turudiMajimboni kwetu tukawaombe radhi wananchi wetu. Bungehili ndilo tulipitisha haya mambo, lakini leo wanaichukulia hiihoja kuwa ni hoja ya sehemu moja, kuona wao ndio wanahoja hii, haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikwambie kitu naWabunge wote wanielewe, tuliapa kwa kushika Quran,tuliapa kwa kushika Biblia, hivi vitabu ni vya Mwenyezi Munguna vitabu hivi havitakiwi kudanganya na kuvifanyia uwongo,mbele yetu kuna Mwenyezi Mungu. Unapoishika Bibliaukasema naapa na kumtanguliza Mungu katika Biblia halafuukaja hapa ukazungumza uwongo ni dhambi kubwa, inabiditukaombe radhi hiyo kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unashika Quran, ukasemanaishika Quran kwa kuahidi na kuilinda kwa mujibu wa Sheriana Katiba halafu baadaye ukaja kuibadilisha kwakuzungumza vingine hii ni laana kubwa. Kila siku unasematumerogwa na nani? Imeturoga Quran, imeturoga Biblia.Mara nyingi ukiwa mkweli, unakuwa hukubaliki mahalipopote pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni shahidi niMwenyekiti kipindi cha tatu hapa ndani na baadhi yaWabunge tupo ndani kwa muda mrefu tunayaona haya.

Page 37: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

Hata hivyo, kuna wakereketwa na wanaharakatiwalionyesha hii hali kuwa hali ya madini ni ngumu, natakaniwataje kwa majina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla Ubunge wake ulikuwa wa tabu kwa vilealiyasimamia kwa dhati kuhakikisha madini hayahayaharibiwi wala hayachakachuliwi, alipigwa mabomu,akadhalilishwa inabidi aombwe radhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kafuli laalisimamia kwa dhati akaitwa tumbili humu ndani.Mheshimiwa Zitto Kabwe alikuja na hoja nzito ambazo zinamashiko lakini siku ya mwisho ndio inakuwa hapana nahapana inakuwa ndiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mheshimiwa Raisameonesha ushujaa kwa kukubali maamuzi na matakwaya Wanaharakati hawa na akayafanyia kazi ndiyo hayounayoyaona maamuzi mazuri yanakuja sasa hivi. Hivyo siyohoja ambayo imeletwa na upande mmoja, hii ni dhambi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa Mjumbe waKamati ya Nishati na Madini, jina nililopewa ni jina la surapana, mnalikumbuka au hamlikumbuki Wabunge? Maanayake nil ikuwa nasema kuna baadhi ya Wachinawalikamatwa Arusha na madini ya Tanzanite ikasemekanahawajui Kiswahili na Kiingereza, wakaachiwa yale madini.Tulikuja kuhoji hapa ndani mwisho wa siku tukasema ndioakapita Mchina akaenda zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, walikamatwa Wachina napembe za ndovu Rukwa, shahidi ni Mheshimiwa JenistaMhagama nilikuwa naye katika ziara. Lori la pembealilokamatwa nalo yule Mchina ikasemekana hajui Kiswahilina Kiingereza, Mheshimiwa Jenista ni shahidi na tulikuwa naMheshimiwa Lekule Laizer, lakini mwisho wa siku tukasemandio na hapana ikawa hapana. (Makofi)

Page 38: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

Mheshimiwa Mwenyekiti, ifikie mahali, juzi nilitoataarifa nikasema mtakuwa tayari wenzetu penye ndiokusema hapana? Maana yake msiburuzwe kwa ndiyo wakatikuna hapana ndani yake. Kulikuwa na baadhi ya Wabungewalikuwa wanaona hiki kama tunachokifanya hiki ni dhambikwa wananchi, sasa leo mnailetaje hoja hii ikawa ni hoja yaupande mmoja? Haikubaliki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hoja ni ya Magufuli nawanaharakati na msiichukulie kama hoja ya kisiasa Wabungewote iwe wa Upinzani, iwe wa CCM tushirikiane kwa hili.Unapoleta uchumi bora, huleti kwa upande mmoja ni kwaWatanzania wote, leo tunaiona Bulyankhulu watu ni maskini,unaiona Geita watu ni maskini, lakini umaskini huuumesababishwa na mikataba yetu mibovu na sisi wenyewekusema ndio wakati ni hapana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge tumeumbuka,kwa aibu hii hatuna haja ya kufumba macho na kupepesamacho, tuwaombe radhi wananchi. Narudia tena Wabungetumeumbuka kwa hili, hakuna haja ya kupepesa macho,wala kumwambia mwenzako kumkodolea kwamba ni hojaya CCM au hoja ya CUF au hoja ya CHADEMA, ni hoja yaWabunge wote tumekosea humu ndani. Watu wengiwalikuwa wanaangalia conflict of interest na conflict ofinterest ikajengea hoja tunaitana pembeni jamani tukubali,wakati unajua kabisa hiki ni hapana, hizi ni dhambi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa idhini ya Sheriaza Bunge tutoe hii Kanuni ya kushika Quran na Biblia itatulaanihumu ndani. Tunashika Biblia wakati Biblia haitamki uwongo,tunashika Quran haitamki uwongo, leo tunatamka uongohalafu baadaye tunakula matapishi, tunageuza leo,tunabeza na kukebehi na kuona wenzetu hawana hoja. Nanihumu ndani atamwomba radhi Mheshimiwa Kafulila?Nauliza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba radhi Kafulilakwa vile Mheshimiwa Kafulila ameonewa wakati alikuwaanaleta hoja ya kuisadia nchi hii. Tulikuja na hoja ya Tanzanite,

Page 39: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Tanzanite inatoka Tanzania, mimi nilikuwa New York palekaribu na UN nje kuna maduka ambayo yanauza madini,Wallah Tanzanite hiyo inaonekana inatoka Kenya, inatokaIndia, inatoka South Africa, niliuliza kwani hakuna Interpol?Jibu halipatikani, lakini leo hapa watu wanataka kufumuamapafu kuzungumza uwongo, dhambi kubwa sana naitatulaani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nimshukuru na nimpongeze Rais Magufuli kwa vileamethubutu na sisi wote tuungane kwa pamoja bila unafikikumpongeza kwa kazi anayoifanya kubwa na inahatarishamaisha yake. Hivyo kila Mtanzania amwombee huruma kwahilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haponakuja katika hoja iliyopo mezani. Leo tunasema tunatakauwekezaji wa viwanda, katika viwanda tumeona A to Zimekuja kufanya semina ngapi hapa ndani? Wanakujawageni wanaingiza vyandarua bure, hawana tozo, yeyeanalipa bilioni 17 wale watu wameachiwa vilevile waingizevyandarua hakuna mahali palipobadilishwa hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naibu Waziri wa Fedhatulikuwa naye katika semina ,akasema atalifanyia kazi, lakininimeangalia katika vitabu hawa A to Z wameachwa hivihivi, kiwanda chao kinakufa, wanalipa kodi, wana madenina marekebisho hayajafanywa. Naomba Serikali hii kamatunavyosema ni Serikali sikivu iangalieni A to Z ili angalauyale maombi yao yasikilizwe yafanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niko humu ndani yaBunge miaka mingi tumezungumzia suala la Dinosaur.Dinosaur yupo Ujerumani sisi hatutaki mjusi aje Tanzania lakinije, hata mrabaha haiwezekani? Tunakimbizana na mamalishe, tunakimbizana na watu wa mitumba, leo kuingia ndaniya exhibition unatoa Euro 24 kwa watu wazima na Euro 12kwa vijana lakini watu wa ndani…

Page 40: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kuna orodhaya wageni ambayo tumeipata sasa hivi, Mheshimiwa JanuaryMakamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anawageni wake kutoka Tanga ambao ni Al-madrasatulShamsiya au TAMTA Tanga wako ukumbini. Karibuni sanaDodoma. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naMheshimiwa Gekul ajiandae Mheshimiwa Ngeleja.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nami nichangie machache katika bajeti yaSerikali ambayo ipo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, Wabungetunapokaa katika ukumbi huu kazi yetu ni kuisimamia nakuishauri Serikali, lakini kwa bajeti hii ambayo iko mbele yetuni vizuri Serikali ikawa wazi ili tuishauri na tuisimamie. Hatahivyo, kama mtaleta vitu kwa mafungu na bila kufanyaanalysis ya kina maana yake hamtupi nafasi ya kuwashauri ilimfanye vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti hii ambayotunaitumia sasa ni wazi kwamba Serikali imefikia malengokwa asilimia 70 ya makusanyo, lakini kwenye makusanyo hayoambayo mlikuwa mnategemea tri l ioni 29, tri l ioni 11mmekusanya ya kodi lakini leo mnaleta trilioni 31 wakatimakusanyo yetu yako asilimia 70. Mngetuambia tu ukweli,kwamba ni wapi mmekwama? Kwa sababu gani namnarekebishaje? Kwa haya mnayotuletea kwamba kilamwaka mnakuza bajeti ambayo haitekelezekimnawadanganya Watanzania siyo kweli. Ni bora mseme niwapi mmekwama na tuishi according to bajeti ambayotunaweza tukakusanya na tukapeleka kwenye miradi yamaendeleo, lakini kama mnataka tufanye biashara kamabiashara mtapitisha bajeti hii lakini utekelezaji haupo. (Makofi)

Page 41: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalisema hili kwa sababu nibahati mbaya sana leo Serikali mnawaza kuzimisha kabisaSerikali za Mitaa. Makusanyo yenu yote mmekusanya hukommeshindwa, mnakwenda kuchukua vyanzo vyaHalmashauri zetu sasa ni kitu kinachosikitisha na nilishawahikusema kwenye Bunge hili. Mwaka 1980 Baba wa Taifa alijutasuala zima la kufuta Serikali za Mitaa na kuondoa nguvu zaSerikali za Mitaa. Wakati huo barabara zilikwama, zahanatizetu zilikwama kwa sababu fedha zilikuwa haziendi baadaya Serikali Kuu kukusanya. Hii bajeti mnayotuletea leo ni yakuua Serikali zetu za Mitaa kwa asilimia mia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalisema hili mwaka janamlitufukuza hapa mkapitisha bajeti, lakini mkaondoa chanzocha kodi ya majengo. Mpaka hivi tunavyoongea mpakaleo Serikali haijakusanya, TRA haijakusanya kodi ya majengoni bora mngetuachia Halmashauri tukakusanya. Kama hilohalikutosha hamkufanya tathmini ndiyo maana nasemamnaleta bajeti kama biashara tu kwamba muda wa kuletabajeti umefika mnaleta bajeti hamjafanya tathmini. LeoSerikali mngekiri tu kwamba mlishindwa kukusanya namlifanya maamuzi mabaya kuondoa chanzo hiki katikaHalmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hilo haitoshi kodi yaardhi mmechukua, kodi ya mabango mmechukua, ukokwenye minada mmefuta. Naomba Waziri wa Fedhaaniambie ukweli wakati anajibu hivi wana mpango gani naHalmashauri zetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyoongea mimiHalmashauri ya Mji wa Babati, nitoe tu mfano, wametuachiavyanzo viwili tu, ushuru wa soko na ushuru wa stendi. Wakatihuohuo wanasema kwamba, Halmashauri zetu tuorodhesheidadi ya wazee, tuwalipie bima ya afya, wauna watutunawalipa mishahara madereva na ma-secretary palewasaidizi zile kada ambazo Halmashauri zetu zinaajiri, lakinihakuna chanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya sana hizi

Page 42: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

fedha tunazoambiwa kwamba, leo naomba tu nichangiehii sehemu ya Serikali za Mitaa. Hizi fedha ambazo Serikalimnasema mtakusanya mtatuletea ni uwongo mtupu.Ninavyoongea hivi Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nilikwendanikamwona pale kwenye Kiti nikamweleza hata OChawatuletei kwenye Halmashauri zetu, hivi ninavyoongeatangu bajeti hii imeanza ya trilioni 29 Halmashauri ya Mji waBabati wametuletea OC ya milioni 26 tena ya mitihani! Helaya Walimu wanaoenda kusimamia mitihani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Halmashauri ukiendawatu wanaandamana hakuna fedha, hatuna makusanyo,fedha zote wamechukua. Ile asilimia 30 ya kodi ya ardhiambayo tunakusanya hata hawarudishi tena kwa Wizara yaArdhi hawatuletei tena! Halafu wao watu wa Mungubinadamu wanasema kwamba, kila kitu kifanyike kwenyeHalmashauri, miradi ya maendeleo hawaleti fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele chaMheshimiwa Waziri kwenye hiki kitabu, fedha zotewamepeleka zaidi ya milioni 500 kwa Jeshi. OCwanazopeleka ni za Jeshi, Polisi, ndiyo hela wanazolipa, lakinihuku hawapeleki! Hakuna hela ambazo wanatuletea, leotutawaaminije kwamba, wao tukiwaachia hivi vyanzowataturudishia kwenye halmashari zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu wajitafakari, nibora wakaacha Halmashauri zikakusanya kwa sababu, waovipaumbele vyao ni tofauti na walivyoviahidi. KwenyeUchaguzi Mkuu wakaja wakatuahidi wakasema milioni 50kwa kila kijiji, hakuna chochote huku Mheshimiwa Waziri. Tenahajaongelea chochote! Mwaka jana wakatenga mikoa sijuimingapi kama bilioni 59, hawakupeleka kabisa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekaa Wabungetunaulizwa, Serikali imeahidi milioni 50 kwa kila kijiji ziko wapi?Hata kuzisema tu wamekwepa, hata kuziandika tu, mwakajana walithubutu kuandika, mwaka huu hawajathubutu hatakuandika kutaja. Wanavyoviahidi tofauti nawanavyotekeleza! Ni nini kinawaroga? Ni nini

Page 43: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

kinawasahaulisha? Ni kitu gani ambacho kinawafanyawasifikirie waliyoyaahidi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri zetuwametuachia kitu cha ajabu sana, wamepandisha faini zamtu ambaye ametupa takataka, labda kimfuko cha malboroamekidondosha chini, kutoka Sh.50,000/=, wamepandishampaka Sh.200,000/= mpaka Sh.1,000,000/=! Eti ndio chanzowanachotuachia Halmashauri. Ni aibu kwa Serikali ambayoinawaza eti fine ndiyo iendeshe Halmashauri. Yaaniwamepandisha eti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ile ni By Laws yaHalmashauri zetu, to be honest, tuwe wa kweli, walahakiwahusu hicho chanzo, halafu Serikali wanakaawanafikiria, halafu kingine, ada ya uchafu unapozolewasokoni wamefuta, hata kuzoa uchafu hawataki tu-charge.Halafu wanaweka faini kwa kitu gani, wakati hata hizo adaza kuondoa tu huo uchafu wameondoa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana nasema wakaewafikirie. Waheshimiwa Wabunge kila mmoja hapa anaHalmashauri yake, Wabunge wa Majimbo, Wabunge wa VitiMaalum tunaingia, hii bajeti wale wanaosema ni bajeti yakarne, wanajidanganya na watapiga makofi watapitisha,lakini kwa upande wa Halmashauri, Serikali Kuu imeamuakunyonga Halmashauri zetu, kuchukua vyanzo vyote,wanatuachia eti tukakimbizane na wananchi, mtu ametokahospitali kawekewa drip ameenda haja ndogo hapo tukam-charge laki mbili! Nani anaweza kufanya hayo? Hatuwezikufanya hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri akaechini afikirie, ushauri wangu kwa Serikali na kwa bajeti hii,wakae chini wafikirie warudishe vyanzo vyote vyaHalmashauri, ili tuwasaidie kufanya maendeleo kwa sababubarabara zetu hazipitiki, tunavyoongea hatuwezi kuchongahizo barabara wala kukarabati. Tulishauri katika Bunge hilikwamba, asilimia 70 wanazopeleka TANROAD wapelekekwenye Halmashauri, 30 iwe viceversa kwa sababu barabara

Page 44: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

nyingi za mikoa wameshaunganisha kwa lami. Sasa hiviwaturudishie hivyo vyanzo, wabadilishe, hawakutaka.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kinachotokea sasakwa sababu wameona kwamba, hawakusanyi huku juumambo hayaendi, wakaunda task force ile ya TRA ambayowameweka Usalama wa Taifa, wameweka Polisi hukowanakimbizana na madeni ya nyuma huko, wakati walisemahawatafufua makaburi, leo wanafufua makaburi!Wanaenda wanadai kodi ya 2011 hata wao hawakuwepokwenye hizo nafasi! (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ngeleja,atafuatiwa na Mheshimiwa Mbene, Mheshimiwa Musukumana Mheshimiwa Serukamba wajiandae.

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kunipa fursa hii. Naanza kwa kuwashukurusana viongozi wa Wizara yetu hapa, Mheshimiwa Dkt.Mpango kama Waziri, Naibu Waziri wake Dkt. Kijaji, KatibuMkuu pia Doto James, Naibu Katibu Mkuu, Wataalam wotewanaoongoza Tume ya Mipango na Watendaji wote katikaWizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapojadili bajeti hii sisi niwawakilishi kutoka maeneo mbalimbali. Mojawapo yamambo yanayotuongoza kutafakari na hatimaye amakuikubali ama kutoikubali bajeti hii ni pamoja na kuonamambo ambayo yamezingatiwa katika maeneo yetu ya kazitunakotoka pamoja na mambo ya Kitaifa. Naanza kwakusema naungana na wale wote ambao wanaiunga mkonobajeti hii asilimia mia moja kwa sababu, kule Jimbo laSengerema ambako mimi nawakilisha, yako mamboambayo yamejitokeza moja kwa moja kwenye bajeti hii nanitasema kwa ufupi sana. (Makofi)

Page 45: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kwa nini naiungamkono bajeti kwa sababu, naona sekta ya maji.Nampongeza sana Mheshimiwa Injinia Lwenge na Msaidiziwake kule Sengerema ule mradi mkubwa kabisa ambaounaongoza kwa ngazi ya Halmashauri na Wilaya Tanzaniaumeshakamilika sasa uko hatua za mwisho mno. Baada yahapa nina hakika kwamba Viongozi Wakuu wa Serikaliwatakwenda kuuzindua na mimi nawakaribisha sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi ule sasaunapokamilika tunaanza kuufungua kuwafikishia majiwananchi wanaozunguka Mji wa Sengerema na maeneomengine. Sio hivyo tu, kuna miradi kadhaa imebuniwainayotokana na chanzo cha Ziwa Victoria. Kwa hiyo, hivitunavyozungumza bajeti hii naiona Sengerema imezingatiwavizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kufika Sengeremaunapotokea Mwanza lazima uvuke Ziwa. Tuna barabara yaLami ya Kamanga – Sengerema pale, nimezungumza naTANROADS wametuahidi kwamba, mwaka huu wa bajetiunaokuja, mwaka mpya wa fedha, wataanza kushughulikiaujenzi wa lami. Pia, tuna vivuko, kutoka Mwanza kwendaSengerema unavuka kwa kutumia njia mbili, kuna Kamangapale kwenda Sengerema, lakini pia kuna njia ya Busisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa pale Busisi kunamambo mawili yanafanyika kuanzia Kigongo, Jimbo laMisungwi; kwanza kuna ununuzi wa kivuko kipya, naipongezasana Serikali, lakini pia kuna ferry tatu zinafanya kazi pale,zinafanyiwa matengenezo na bajeti imeonesha hivyo. Ndiomaana nasema katika mazingira hayo hakuna namnanyingine, isipokuwa kuiunga mkono bajeti hii kwa asilimiamia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maandalizi ya ujenziwa daraja kubwa, kilometa 3.5 unafanyika pale kwenyekivuko kati ya Kigongo kwenda Busisi ambako ni Jimbo laSengerema. Yote haya ni maandalizi yanayofanywa kupitia

Page 46: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

bajeti hii ya fedha. Kwa nini wananchi wa Sengerema tusiungemkono? Tuiunge mkono kwa sababu tunaona tunafaidika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ina mambo mengi,lakini lingine mojawapo ambalo ni baadhi ya mambomachache ambayo yamenifurahisha na mimi naungana nawenzangu ni kuwatambua rasmi wafanyabiasharandogondogo, maarufu kama Machinga, lakini wanaofanyakazi za kujiendeleza wenyewe na kuchangia uchumi wa Taifa.Ni jambo muhimu na lazima tuliheshimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii imepunguza ushuruwa mazao, kwa sisi tulioko kule vij i j ini tunafahamu.Inawezekana tukaongea katika lugha tofauti kwa sababutunatoka maeneo tofauti, watu wa mjini watatuulizamambo ya mjini, lakini sisi tunaotoka Majimbo ya vijijinitunafahamu kero ambazo zimekuwa zikiwagusa wananchieneo hili. Kushusha ushuru wa mazao mpaka mzigo uzidi tanimoja ni jambo kubwa sana. Tunasema mazao ya biasharani asilimia tatu na mazao ya chakula asilimia mbili, hili nijambo kubwa tunaishukuru sana Serikali kwa kuja namapendekezo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Sh.40/= pale,tumesema kwenye utaratibu wa Road License sasa ziendekwenye maji. Nasema tufanye uamuzi mgumu, lakini kwasababu naiona neema inakuja labda tusifike huko, nasemahivyo kwa sababu Mheshimiwa Shabiby juzi aliongea vizurisana hapa, kwamba zile Sh.40/= tunazoziongeza zilikuwakwenye utaratibu wa kawaida, lakini tumekuwa na kilio chakuongeza Sh.50/= kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Maji kule.Sasa kwa sababu naiona neema inakuja saa nyingine tusifikehuko, lakini ukiniuliza mimi ningesema ushauri wangu nikwamba, hata ile Sh.50/= ambayo tulikuwa tumeikusudia,tuliyoichangia sana kabla ya bajeti hii tuiongeze kule ziendezote kwenye maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia na dunia nzimainafahamu, Bunge jana tumetoa pongezi kwa Mheshimiwa

Page 47: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kudhibiti na kuisimamiavilivyo bora zaidi sekta ya madini. Naungana na Watanzaniawenzangu kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazialiyofikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wiki iliyopita nilichangiahapa nikasema kwa hali tuliyofikia sasa hivi tunahitaji tumaamuzi ya usimamizi wa sheria na sera tulizonazo. Mojaya jambo nililozungumza kupitia kile Kifungu cha 11 cha Sheriaya Madini kinaruhusu kabisa kuipitia mikataba hii, lakininikasema hata ushiriki wa Serikali kuwa na hisa katikamakampuni haya kupitia Kifungu cha 10 tunaweza kabisakuwa nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mambo haya nanazungumza mimi nikiwa na Kiapo cha Bunge, lakini pia nikochini ya Kiapo cha Serikali, nilishawahi kuwa Waziri wa Nishatina Madini kwa miaka mitano na nusu. Nazungumzanikifahamu michakato, tungefuata utaratibu wa kawaidawa kuanza mchakato wa kuwaalika wawekezaji tushaurianenamna ya kuboresha mikataba hii, ingetuchukua miaka.Mheshimiwa Rais ameturahisishia, jana tumesikia wote nadunia imeelewa kwamba, ndani ya wiki mbili hizimazungumzo yataanza na upo uelekeo wa kuelewanakatika hali ya kuwa na win-win situation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana tumepitisha Azimio lakumpongeza Mheshimiwa Rais JPM, lakini ilikuwa ni kabla yaTaarifa ya Mheshimiwa Rais. Kuna utamaduni umezoelekaduniani kwamba mambo makubwa yakifanywa na ViongoziWakuu wa nchi kwa pamoja, kuna utaratibu na hasa kamahili Bunge, tunaweza sisi, sisi ndio wawakilishi wa wananchiTanzania nzima. Wapo Wabunge hapa wana simu zakumpigia Mheshimiwa Rais moja kwa moja kumpa pongezikwa kazi anayofanya, lakini wengine hata namba yakehawana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaowakil ishawawakilishi wa Watanzania, nilikuwa naliomba Bunge lakodakika moja, tumpe standing ovation Mheshimiwa Rais kwa

Page 48: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

wale tunaoguswa kuonesha sisi kuguswa kwetu kwa namnaambavyo tumeunga mkono na tumhakikishie kwamba, tukopamoja. Tumuunge mkono Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwaaliyoifanya, tumuunge mkono kwa niaba ya Watanzaniawote tunaoguswa na jambo hili, tumhakikishie kwamba vitahii sio ya kwake peke yake ni ya Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa hilo.Kwa kufanya hivyo, hatufanyi kwa sababu ya favour, lakinikwa sababu ya kutambua kazi kubwa anayoifanya.Kupambana katika sekta hii na mmeona katika mitandaoinasemekana zipo familia mbili ambazo zimeamua kudhibitimadini yote duniani, lakini Mheshimiwa Rais anaungana nakundi la viongozi duniani ambao wana uthubutu nawanafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si jambo la kwanza,tunafahamu historia ya Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyererealivyopigana katika mawimbi mazito sana akaifikisha nchihii hapa, lakini ukienda Marekani kuna Rais yule mnafahamu,Rais Franklin Roosevelt aliikamata ile nchi akaongoza hatazaidi ya kile kipindi ambacho yeye kwa taratibu za Kimarekanikilikuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Franklin aliichukua nchiikiwa katika hali ngumu sana na akaanzia pale ambapoMarais waliokuwa wamemtangulia, akaivusha Marekanimpaka kifo kilipomkumba. Mheshimiwa Rais Dkt. JohnPombe Magufuli amejitoa muhanga kwa niaba yetuWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda China, Mao Tse Tungkuanzia mwaka 1949 walivyofanya mapinduzi Chinaaliongoza lile Taifa mpaka mwaka 1978 akaja kiongozi,Mwanamapinduzi, akaanzia pale alipokuwa ameishia MaoTse Tung akaichukua ile nchi, anaitwa Deng Xiao Ping,aliichukua ile nchi ni miaka ishirini na kitu tu, China ikabadilikasana kuanzia mwaka 1978 mpaka 1989 alipokuwa anaachia

Page 49: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

nafasi. Kwa hivyo, duniani kunawezekana. Nenda Singaporekuna yule Li Kuyan Yew ameichukua ile nchi akaibeba kutokailipokuwa ikafika hapa ilipokuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachosema nikwamba, mambo haya yanawezekana. Mheshimiwa RaisDokta John Magufuli…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Raisanaichukua nchi akijenga msingi kuwa…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa!

MWENYEKITI: Taarifa!

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndio maana nikasema ni muhimu sana kutambua mchangowake na…

MWEYEKITI: Mheshimiwa Ngeleja subiri kidogo.

TAARIFA

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Naomba kumpa Taarifa mzungumzajikwamba yeye ni miongoni mwa Wabunge waliotajwa katikakashfa hii ya makinikia. Sasa atuambie anapokuwaanachangia kidogo atoe ufafanuzi uhusika wake katika hilila makinikia kwa sababu amewahi kuwa Waziri. Naombatu aweze kutoa ufafanuzi ili Watanzania waweze kujua.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Kaa chini. Mheshimiwa Ngeleja hiyo siyotaarifa, endelea. (Kicheko)

Page 50: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Mdogo wangu Mheshimiwa Haongaanafahamu kutuhumiwa siyo kupatikana na hatia, maishayanaendelea na kazi inaendelea, tunazungumzia maslahi yaTaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini suala la standingovation na interception ya Taarifa ya Mheshimiwa Haongainalinda muda wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasema kwa hii,hatua tulipofikia hapa ni nzuri sana. Pamoja na kwamba,hatujajua tutapata kiasi gani, lakini tunakoelekea ni kuzurina Mheshimiwa Rais amethubutu na sote tunaungana kamaTaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye bajeti.Tunapozungumzia Tanzania ya Viwanda tunazungumzia yakomambo ambayo lazima yafanyike. Huwezi kuzungumzia nchiya viwanda bila kuwa na umeme wa uhakika. Natakaniseme ninachokifahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu sasa linakwendakufumuka kwa maendeleo. Unasikia sasa hivi MheshimiwaRais jana ametuambia akiwa na Mwekezaji ambaye ni Raisna Mwenyekiti wa Barrick amesema kwamba, pamoja namambo mengine ambayo tutayajadili ni pamoja na ujenziwa smelter, kunahitajika umeme mkubwa sana, lakininimesikia reli itakayojengwa itatumia treni inayoendeshwakwa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumemsikia Mheshimiwa Raiswa Rwanda kule amesema wanaisubiri reli hii inakwenda,unahitajika umeme mwingi sana. Unapozungumzia viwandaunazungumzia umeme mwingi, ushauri wangu kwa Serikali,lazima sasa kama ambavyo tumeji-commit kwenye bajetihii, tuishirikishe sekta binafsi tusaidiane na Serikali kuwekezakatika vyanzo vya kuzalisha umeme, kwa sababu vinginevyohatutaweza kuhimili hiyo kasi inayokuja. (Makofi)

Page 51: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba,hapa sasa hivi kuna miradi inatekelezwa pale Kinyerezi Onempaka Kinyerezi Six. Naomba, kama inawezekana kwasababu, wapo Wakandarasi kwa mfano wanaomalizia ileKinyerezi One, Serikali imeingia nao utaratibu wanajenga,naishauri Serikali wakati tunaishirikisha sekta binafsi pia,inaweza kuwa-engage hawa Wakandarasi kwa utaratibukwa sababu, ndani ya miaka mitatu tunaweza kufanikiwakumaliza mradi mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bomba la gesi ambalolimejengwa miaka michache iliyopita na mimi ambayenilisimamia katika eneo hilo nafahamu, sasa hivi wamesemalimetumika asilimia sita tu asilimia 90 haijatumika, inahitajivyanzo vingi vya kuzalisha huo umeme ili uwafikie wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania hii tuna vyanzovingi vya nishati, tusitegemee gesi peke yake kwa sababu,kwanza gesi ina bei juu kidogo kuliko vyanzo vya maji. Leohapa tuna Bonde la Rufiji inafahamika, kuna mradi mkubwawa Stiegler’s Gorge. Nakumbuka mpaka mwaka 2012tulikuwa tumeshaanzisha mazungumzo na Wabrazilwalikuwa tayari kuja kuungana na sisi, una uwezo wakuzalisha megawatt 2,100. Nchi hii kwa potential tuliyonayokwenye sekta ya umeme unaoweza kuzalishwa kutokana namaporomoko ya maji ni zaidi ya megawatt 4,600. NaombaSerikali ifunguke kote kule twende tukatumie vyanzo vyotekuhakikisha kwamba, nchi hii inafikia lengo lililokusudiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nirudie tena kusema umuhimu wa sekta binafsiulivyojionesha, Mheshimiwa Waziri ameonesha utayari huo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante. MheshimiwaMbene, ajiandae Mheshimiwa Musukuma.

Page 52: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono na ahsantesana. (Makofi)

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naminakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuongea. Nianzekwanza kwa kuunga mkono hoja asilimia mia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sana kumpongezaWaziri wa Fedha, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na NaibuMakatibu Wakuu wote kwa bajeti nzuri ambayo inaelekeasana katika mfumo mzima wa kuboresha viwanda katikanchi yetu. Napenda vilevile kumpongeza Rais wetu waTanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli,kwa hatua na ujasiri aliouchukua kusimamia rasilimali za nchiyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha kuwa watuwalewale ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipigiakelele suala hili mara wamegeuka sasa wanaona kuwa nivibaya lakini tuyaache hayo, wale wenye macho wameona,wenye masikio wanasikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitishiwa hapa kamaambavyo Viongozi wa Afrika huwa wanatishiwawanapojitokeza kupigania rasilimali za nchi zao kuwa,watashitakiwa, hii ni mikataba mikubwa sana, haya niMataifa makubwa sana, hamuwezi kuwachezea hawa,wanaweza wakawafanya hivi, wakawafanya vile!

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yake tumeona,huyo Rais wa Barrick Gold badala ya kutushtaki kajamwenyewe, nginja-nginja na ndege yake mwenyewe kajahapa anasema tuongee na hatujaambiwa, tumemsikiakwenye youtube anaongea! Tuongee tuangalietunachotakiwa kuwalipa tuwalipe, sasa kiko wapi chakushtakiana? Hatuwezi kuwa tunaishi kwa uwoga wakatirasilimali ni zetu wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Magufuli endelea baba,

Page 53: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

sisi wananchi wako tuko nyuma yako, tunakuamini na tunajuaunalolifanya ni kwa ajili yetu sio kwa ajili ya binafsi yako nafamilia yako. Endelea kutetea maslahi hayo kwa sababu huundio wakati muafaka, hukuwekwa pale kwa bahati mbaya,Mungu kakuweka hapo akijua makusudi gani anayo juu yakowewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wanaosematunaendela kuibiwa, sijui kama wametambua kuwa katikayale mapendekezo ya Kamati ya Profesa Osoro kuna sualala kuzuia sasa madini yasisafirishwe nje moja kwa moja.Zinaenda kutengenezwa clearing houses na kilayanapoondolewa madini yatafanyiwa ukaguzi na asilimiamoja itatozwa palepale kwa ajili ya ukaguzi huo kwathamani ya madini yanayotoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachotaka kuiombaSerikali ni kuwa mfanye haraka hizo clearing houses ziwekwena tayari hili zoezi lianze kusudi madini yasiendelee kutoka.Siamini hawa jamaa wana ujasiri wa kuendelea kutuibiaharakaharaka baada ya kuona eti kuwa sisi tunawadhibiti.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nirudi sasa kwenyemasuala mazima ya hotuba yetu. Miradi ya kimkakati nimiradi ambayo imekuwa ikizungumzwa kwa miaka mingisana. Hebu sasa Serikali amueni jambo moja, malizeni ziletaratibu zote zilizobakia ambazo ni chache sana za mikatabaya uwekezaji, za maeneo ya uwekezaji, taratibu za ulipajiwa fidia, ili sasa hii miradi ya kimkakati ianze kufanya kazikwa sababu moja kubwa, miradi hii ikianza kufanya kazi sualazima la uchumi wa viwanda litakuwa dhahiri zaidi, maanahivi ndio viwanda mama vitakavyozalisha input za kuingiakatika viwanda vyetu tunavyovitegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme tayari tunao wakutosha, miundombinu ya barabara imeshatengenezwa yakutosha, reli imeshaanza, tunachongojea sasa ni hii miradimingine ya kimkakati ambayo sasa itashirikiana katikakuhakikisha kuwa viwanda vyetu vinawezekana.

Page 54: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la maeneomaalum ya kiuchumi. Serikali ilituanishia maeneo maalumya kiuchumi karibu nchi nzima, ilikuwa ni jambo jema sana,yenyewe pia yamesimama kwa muda mrefu. Hebu Serikaliwaje sasa na bajeti hata kama watakwenda kukopa,wamalize masuala ya fidia na miundombinu muhimu katikamaeneo haya, halafu wayatangaze kwa sekta binafsi yandani na ya nje waje wawekeze ili wananchi kwanza wapateajira lakini vilevile wapate mapato na nchi yetu iendelee.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna suala la PPP,najua kuwa PPP labda ni dhana ambayo haijatambulikavizuri au haieleweki vizuri kwetu. Hebu tutafute jinsi yakuboresha uelewa wetu wa PPP tupate mafunzo Serikalinina sisi Wabunge vilevile tupate mafunzo ya kutosha, tujuejinsi gani ya kushauriana na hawa wawekezaji wanaokujakuingia mikataba hiyo na sisi ili tupate mikataba ambayoitatunufaisha sisi wote. Kwa hiyo naomba PPP isitupwepembeni tu kwa sababu hatuifahamu vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna suala zimala ukusanyaji wa mapato hasa kwenye Halmashauri.Tunashukuru sana Serikali kwa hatua ambazo wameziainishaambazo wanaenda kupunguza tozo mbalimbali. Vileviletunaomba sana kwa yale maeneo ambayo wamepunguziaHalmashauri uwezo wa kukusanya wenyewe, hebuwatuhakikishie watakuwa wanaturudishia hizo fedha kwamuda mfupi kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama wanavyofahamuhata sasa hivi Halmashauri zetu nyingi zinajiendesha kwashida sana kwa sababu vyanzo vingi vilikuwa vimechukuliwana Serikali Kuu. Wafanye hima watakapokusanya tuwaturudishie, kama vile ambavyo kila mwezi wanatangazawamekusanya kiasi gani basi mwezi huo huo watuambie naHalmashauri wanapeleka kiasi gani. Mambo yote sasa hivini kielektroniki, sioni kama kutakuwa kuna ugumu katikakurudisha hizo fedha kwa wakati. (Makofi)

Page 55: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni juu yakupunguza kwa tozo, crop cess. Nafikiri katika Kamati yaBajeti tulipendekeza kuwa kusema kuwa wanapunguza tozopeke yake na kuainisha kuwa mazao yawe ni chakula namazao yawe ni biashara inaweza ikaleta mkanganyiko navilevile ikatumika vibaya. Waweke tozo moja na kwa vyoteili ijulikane kuwa whether inatumika kwa chakula whetherinatumika kwa biashara tozo ni hiyo moja. Wasitoe mwanyakwa watu kuanza kucheza na hiyo dhana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala zima la ufuatiliajiwa mapato na tathmini zake. Tumekuwa mara nyingitukikadiria mapato tutapata kiasi gani kwa vyanzombalimbali, lakini je tunafanya tathmini labda ya miakamiwili, mitatu kuona kuwa pamoja na kuwa tulikuwatumeweka maoteo fulani tumekuwa tumefikia kiwango hikitu, ili itusaidie tunapopanga tupange kwa uhakika zaidi kwauhalisia zaidi tusipange kwa vitu ambavyo penginehatutaweza kufikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuzungumziamasuala ya elimu ya walipakodi na hasa kwenye masualaya sekta isiyokuwa rasmi. Sekta isiyokuwa rasmi ni kubwa naitaendelea kukua na itaendelea kuwepo. Ni muhimu sasakuhakikisha kuwa pamoja na hil i suala la kuanzakuwaorodhesha au kuwa-register basi tuanze kutoa na elimuya kulipa kodi, tuanze kuwaelekeza kodi zitakuwa za namnagani, watazilipa kwa mfumo upi, watazilipia sehemu zipi.Maana kodi zilizopo ni nyingi na zina sehemu nyingimbalimbali za kwenda kulipia. Huu kwanza ni usumbufu lakinivilevile inaleta hali ya mkanganyiko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sanawatakapokuwa wakitoa elimu ya kulipa kodi wahakikishekuwa wajasiriamali hasa wadogowadogo wanatambuakwanza wajibu wao wa kulipa kodi lakini kuwa watalipakodi za aina gani wapi na kwa mtindo upi. Hii inatuhakikishiakuwa watu wengi watalipa kodi wakijua kuwa ni wajibuwao na siyo za usumbufu. (Makofi)

Page 56: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata kwa walipa kodiwa kawaida kwa wengine bado elimu hii haijaenea ndiomaana bado kuna resistance, lakini nafikiri kwa kuongezajuhudi za TRA za kutoa elimu badala ya kujikita kwenye rediona kwenye TV peke yake itasaidia zaidi. Ningependa vilevile,kupendekeza hata mashuleni sasa suala la elimu ya kulipakodi lianze kuwekwa ili watoto wakue wakiamini kuwa kulipakodi ni sehemu ya kuchangia maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia sanakuzungumzia suala la Ileje. Ileje ni Wilaya au hata Mkoa nzimawa Songwe ni mkoa ambao unazalisha sana mazaombalimbali ya biashara na ya chakula. Mungu ametujaliakuwa na hali ya hewa nzuri sana, lakini hatuna masoko yauhakika kwa mfano kahawa. Kahawa yetu lazima ipelekweikaweke kwenye mnada wa Kilimanjaro. Hiyo inatuletea…….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Musukuma,ajiandae Mheshimiwa Serukamba.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niwezekuchangia. Kwanza kabisa nimshukuru sana Mheshimiwa Raiskwa kazi nzuri aliyoifanya. Sisi wananchi tulioteseka namachimbo na wawekezaji wakubwa wa migoditunamwomba aendelee kukaza buti, sisi tuko nyuma yake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatake Watanzaniakuuona Upinzani wetu ulioko Tanzania kuwa ni kamamaigizo. Watu wanaingia humu ni kwa sababu tu pengineya kutafuta maisha, lakini hawana nia thabiti ya kulikomboaTaifa hil i. Lingine wajiulize hawa ndio Wabungewanaowatuma kuja kuwawakilisha, badala ya kushughulikana matatizo yaliyoko kwenye Majimbo yao wanahangaikana kutetea wezi. (Makofi)

Page 57: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niliwahi kusema kwenyemchango wangu kwamba tunafahamu na wenginetumeshuhudia sikupata nafasi na kuwataja na wakigunanaweza kutaja, kwamba watu walivuna mpunga sasampunga ule jinsi ya kuurudisha inakuwa ni vigumu, kwa hiyowanataka kufa na tai shingoni. (Makofi_

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niseme tu kwambaMheshimiwa Rais kazi aliyoifanya ni fundisho hata kwaUpinzani. Namshukuru Mama mmoja kule nyuma amesemasuala hili liwe la wote. Hata mimi nakubaliana na tumekuwatukiomba sana sisi Wabunge wa CCM kwamba, tumuungemkono Rais kwa jitihada aliyoifanya wakawa wanatupinga.Toka mwanzo nilimsifu sana Mheshimiwa Ole-Millya yeyealiunga mkono. Wengine wote humu mlitolewa naMheshimiwa Ester Bulaya kama watoto wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kwa sababuimeonekana na Wazungu wamekubali kutulipa wanakujahumu kupiga makofi na kung’ang’ana na miongozo. Miminiwaombe tu Wapinzani wa Tanzania mjifunze kwa kuonamfano kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri pia kwambapamoja na kuhusiana na kodi za makinikia na sisi watu waGeita GGM imetunyonya vitu vingi sana, tumepiga kelelemuda mrefu, tunakosa support na bahati nzuri MheshimiwaRais anatoka kwenye Mkoa wetu. Ukiambiwa fedhatulizokwisha kulipwa kwa Geita dola milioni tatu kwa miakamiwili ukiangalia makorongo yaliyoko pale tunahitaji Serikaliiunde timu ya uchunguzi kwenye mgodi pia wa GGM ambaoupo Geita na watu wa Geita tunasema hatujafaidika kabisana mgodi ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababugani tulikuwa hatuna uwezo kama Halmashauri wa kuwezakupiga hesabu na Wawekezaji hawa. Tumekuwa tukilalamikasana, tunapewa pesa kama hisani na mtu anayetupa hesabundiyo TMAA ambao ni wezi wameshikwa na Mheshimiwa Raiskwamba hawafai. Kwa hiyo, tunamwomba pia Mheshimiwa

Page 58: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Rais aunde Tume ambayo itaenda kwenye migodi ilekuangalia kwa sababu wale tuliokuwa tunategemewawanatupa hesabu sahihi ndiyo hao wameonekana kwenyeripoti ya Osoro kwamba hawafai, kwa hiyo, turudie hatamgodi wa GGM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie tu ninyi ambaohamuelewi migodini baada ya kauli za Rais na yule mkubwawa Barrick kuja, jana watu wa GGM Geita walituita tukutanewanataka kutupa bomba la maji kwa mpango wa haraka.Tumekataa kwa nini mtupe bomba la maji, tunataka tupigiwehesabu, haiwezekani Rais anachachamaa kushika wezi sisitunapewa maji. Tutajitwisha ndoo kichwani tutabanana naWaziri humu, lakini Serikali iunde Tume kwenda kuchunguzamgodi mkubwa wa GGM ambao una mapato makubwana una dhahabu nyingi kuliko hata Kahama. Kwa hiyo,naomba sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, nampongezasana Mheshimiwa Rais na Profesa Osoro amekuwa jasiri,amewataja wezi, amewataja watu waliosababisha matatizomengine tunao CCM. Tufike mahali tuambizane ukwelituache mizaha. Ripoti imesomwa tumeangalia watu wotewenye Degree ma- Professor na wengine ambao hatukusomana wananchi wetu kule vijijini. Halafu watu waliotajwa Bungekutoka CCM wanaanza kuweka kwenye twitter wanasemamimi sihojiwi mpaka nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kweli wezi wana kingagani? Kama wametajwa ni wezi haiwezekani hata kamayuko CCM. Hili siyo suala ya mzaha kuna maisha ya watu nawatu tumeumia. Watu mmetajwa Wabunge wenzangu waCCM humu halafu mtu anaanza na heshima zake,tunamheshimu kabisa Mzee wetu humu ndani ana-twittkwenye twitter anasema mimi siwezi kuhojiwa mpakanipelekwe Mahakamani, yeye ni nani? Kama tunatakakumaliza matatizo haya sisi wengine tuliburuzwa sana,tuliburuzwa sana miaka iliyopita watu wakafunga mikatabawakafungia Ulaya wakagawana hela na bado wanakujakutuletea upinzani kule kwetu.

Page 59: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kama kunauwezekano wa hawa watu kama ni Mbunge kama ni naniwakamatwe. Wanaotusumbua humu ni hawa ni hao haowametajwa kwa professa Osoro, katajwa MheshimiwaKafumu, katajwa Mheshimiwa Ngeleja, Mheshimiwa Chenge,wana kinga gani kama wezi? Kwani Magereza yamewekwaya akina Babu Seya peke yake.Tufike mahali tulipiganie Taifahili, CCM siyo kichaka cha kuja kujificha wezi. Kila mwakamtu anatajwa, kila tuhuma, yeye ni nani. Tufike mahalituweserious na suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nimesomakwenye kitabu cha Waziri, ukurasa wa 55, ukisoma palekipengele kinasema atatoza kodi ya asimilia tano kwenyedhahabu kwa wachimbaji wadogo. Halafu MheshimiwaWaziri akasema mwishoni, anategemea kukusanya milioni88. Hivi anaendaje kufanya pressure ya kuhangaika nawachimbaji wadogo ambao kimsingi huwezi kuishika iledhahabu. Akiweka haya masharti kuna asilimia nne ya TMAAkuna asilimia tano ya kwake na kuna asilimia moja yakusafirisha dhahabu, karibia asilimia 10 wakati ukiendaKampala ni one percent. Sasa kwa nini Waziri, Wizara yaFedha wasiondoe kodi zote za kuingiza dhahabu ili tukapatana watu wanaotoka Malawi, Congo, Zambia, Uganda naBurundi wakaleta dhahabu Tanzania kwa sababu hakunaushuru, tuka-deal na asilimia moja tu ya kusafirisha tukapatahela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Mheshimiwa Waziriaking’ang’ana na hizo kodi zake nilishasema humu ndani,hawezi kumshika msafirisha dhahabu tunajua tunavyobeba,kwa nini asilegeze masharti tukaweka zero halafu hii onepercent atapata hela nyingi kuliko hizi milioni 88. Kwa hiyo,nashauri sana Mheshimiwa Waziri ajaribu kufikiria na alionehili suala kwa macho mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sanaMheshimiwa Rais na nimekuwa nikifuatilia taarifa zote hataalivyomtumbua Mheshimiwa Profesa Muhongo, sijui kamayumo humu ndani nina hamu naye kweli, alisema niliamini

Page 60: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

vyeti, vyeti vimeniangusha! Juzi tena kasema mara tatu PhD17. BOT hii ndiyo return yake Ma-PhD?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali tuangalieuwezo wa mtu na ikiwezekana hata Mawaziri hawa wawewanafanyiwa hata interview, haiwezekani unakuwa na watuwana PhD za kutisha, wanapogundua wezi hao wenye PhDwanaanza kututishia sisi ambao hatuna PhD. Hata hivyo,suala hili ni halali, ziko wapi degree tunazozitegemea hapa?Watu wamebeba Dokta, PhD sijui nini, halafu mwisho wasiku tunapopata matatizo wanatutisha wanatupelekaMahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Rais na walewawekezaji wamekaa, watu wamekaa kimya, PhD tenazimerudi kwetu sisi wajinga kusema tumuunge mkono. Miminafikiria tufanye kitu cha msingi kama Wabunge. Hata kamani kubadilisha sheria tusiamini hizi degree. Kuamini degreehizi... (Maneo Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge)

T A A R I F A

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: MheshimiwaMwenyekiti, nataka nimpe taarifa mzungumzaji kwambaatumie angalau lugha ya staha, asiseme kwamba sasa zilePhD zimerudi kwetu wajinga. Sisi siyo wajinga humu ndani.Kila mmoja ana uelewa wake, kila mmoja yuko vizuri, kwahiyo sisi siyo wajinga naomba awe na lugha ya kiasi. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Musukuma endelea nalugha za Kibunge na hilo neno wajinga linatoka kwenyeHansard.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nalitoa, lakini namshangaa kwanza yeye ana shule, amesomaana Degree, niliyesema sikusoma ni mimi, sasa anawashwakitu gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

Page 61: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Taifa hili,watu wengi hawana vyeti na watu wengi hawana elimukwa kuwa Katiba ilisema watu kupata vyeo fulani inatakaelimu kubwa wamefoji hizo digrii ambazo input yaketunaiona leo hapa. Kwa nini tusijifunze kwenye nchizilizoendelea? Kuna nchi ambazo zimeweka watu ambaohawana hizo digrii na zinafanya vizuri. Tuking’ang’ana nahizo degree ndugu zangu tutakuja kupata matatizo, uwezoni mdogo makaratasi ni makubwa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nataka kushaurikuhusiana na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano, hatakwenye ushauri wangu nilipochangia mwanzo nilisema…..

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Serukamba.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nianze kukushukuru kwa kunipa nafasi. NaipongezaWizara ya Fedha, nimpongeze Waziri, Naibu Waziri, KatibuMkuu na wenzake kwa bajeti nzuri sana. Kwa kweli ukiangaliabajeti ya mwaka jana na bajeti ya mwaka huu tofauti naionani kubwa. Bajeti hii wametusikiliza vizuri sana, hongereni sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, China wameanza miakamingi sana, maendeleo unayoyaona leo China yameanzamwaka 1978 baada ya Deng kuchukua ile nchi. Dengamechukua nchi lakini kwenye Serikali zilizopita alikuwamo.Brazil unayoiona leo maendeleo yameanza mwaka 1998baada la Lula kuchukua ile nchi, kabla ya hapo alikuwa niKiongozi. Malaysia unayoina leo maendeleo yameanzamwaka 1980 baada ya Mahathir Mohamad ambaye kulenyuma alikuwa ni kiongozi alipochukua nchi. Sohat waIndonesia baada ya kuchukua nchi ndio tuameanza kuonamaendeleo makubwa ya Indonesia. Ethiopia unayoina yaleo yameanza mwaka 1992 baada ya Meles Zenawi kuchukuanchi, naweza nikataja Mataifa mengi sana.

Page 62: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na hili kwa sababugani Waheshimiwa Wabunge. Lazima Taifa lolote yuko mtuambaye atakuja ndio atasababisha Taifa hilo liendelee. Naminaomba leo niseme kwamba ninayo hakika Rais Dkt. Magufuliatatupeleka kwenye uchumi wa kati.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Marais wote hawanimewataja ambao wamefanya vizuri sana kwenye Mataifayao wana sifa kubwa tatu, wote kwa maana ya SingaporeMalaysia, Indonesia kote, kazi ya kwanza walifanyawaliwekeza kwenye elimu, unaona Rais Magufuli ameingiakazi ya kwanza aliwekeza kwenye elimu. Wote kazi ya pili nikusimamia nidhamu ya utekelezaji wa kazi, tunaona leoSerikalini kuna nidhamu kubwa sana. Sifa ya tatu ya Maraishao waliobadilisha nchi zao ni suala la kusimamia mapatona rasilimali za nchi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Dkt. Magufuli ameamuakusimamia kwa uthabiti kabisa rasilimali na mapato ya nchiyetu kwa sababu naamini Rais anatupeleka kwenye Taifa lamaendeleo. Hata hili la makinikia, hili la madini ni katika ulemwendelezo wa kusimamia mapato na kusimamia rasilimaliza Tanzania. Nilisema siku ile Rais Magufuli, anaendakubadilisha namna ambavyo uchimbaji wa madini dunianiutakavyofanyika. Kwa hiyo, yeye ndio atakuwa chachualichofanya Rais Magufuli atazisaidia Kenya, Mali, Guineaatasaidia nchi zote kwa sababu sasa wote wanakwendakwa kuamka na ninayo hakika sasa tutapata share yetu natutaendelea kama nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nimewasilikiza sanaWapinzani. Hakuna hata Mpinzani mmoja ambayeamesema Rais Magufuli anakosea, hakuna! Hata hivyo,Wapinzani kama walivyo Wapinzani wao wameamua kuwaThomaso. Wanataka waone yatapotokea. Kwa hiyo,nawaelewa, mashaka yao nayaelewa ni mashaka yaThomaso. Yesu amefufuka, Thomaso anamwambia Yesunaomba niangalie mahali palipochomwa mkuki.

Page 63: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaelewawenzetu na ndiyo maana nasema, wao wanaoneshawasiwasi lakini hawasemi kama tumekosea. Nami naaminikazi anayofanya Mheshimiwa Rais, Dkt. Magufuli, anafanyakazi nzuri sana na Rais Mheshimiwa Magufuli anaendelezapale walipoacha wenzake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema kule nyuma kila Raisataandika kitabu chake, Rais Dkt. Magufuli anaandika kitabuchake na kitabu cha Mheshimiwa Dkt. Magufuli kitakuwakitabu ambacho nina hakika kwenye historia ya nchi yetundio Rais tutakayesema alitutoa third world kutupelekakwenye uchumi wa kati kama Taifa. Jukumu letu kamawanasiasa, tumuunge mkono ili aweze kufanya vizuri zaidihuko anakokwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, sasanirudi kwenye bajeti. Naipongeza sana Serikali kwenyekubadili mfumo wa kukusanya Road License. Wako watuwanasema Road License imeondolewa; hapana,haijaondolewa. Road License imeletwa il i iwe rahisikuikusanya na iwe rahisi kwa sisi tunaochangia lakini piaitozwe kwa magari yanayofanya kazi. Naipongeza sanaSerikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo naiombaSerikali tulikazanie, ni suala la deni la ndani. Leo hii ukiendanchini, malalamiko ni kwamba pesa hazipo, wanasemaliquidity haiko kwenye market. Liquidity haipo kwa sababuwatu wengi ambao wamefanya biashara na Serikaliwanatudai. Naiomba Serikali ije na mkakati wa kulipamadeni ya ndani. Tukifanya hivyo, uchumi wetu utaanzakukua kwa kasi kubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza kwa suala laasilimia 18 ya VAT kwenye auxiliary. Sasa mnaisaidia bandariyetu, lakini naomba suala la single custom na DRC tuliondoeili single custom itusaidie na watu wengi watumie Bandariza Tanzania. (Makofi)

Page 64: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine Mheshimiwa Raisameamua kwa dhati kufufua Shirika la Ndege la Tanzaniana amenunua ndege kubwa. Zile ndege kubwa zitakuwazinasafiri kwenda kwenye Mataifa makubwa duniani. Mojaya gharama kubwa ya ndege ni mafuta ya ndege. Tumeamuawenyewe kama Serikali; kama Afrika Mashariki, mafuta yandege yasitozwe kodi yoyote na yasitozwe RDL. Sisi badotunang’ang’ania kuweka tozo hiyo. Tukiweka tozo hiyo,tunaongeza gharama za ndege. Tukiongeza gharama zandege, tunaiumiza tourism yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho naomba leoniseme, shirika ambalo linatoa mafuta haya ya ndege niPuma. Puma, Serikali ina asilima 50. Ukiliongezea gharamamaana yake ni nini? Maana yake, profit and loss yao inakuwakubwa, maana yake dividend itapungua, corporate taxitapungua na yote haya yatapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali; na bahatinzuri Kamati ya Bajeti kwenye ukurasa wa 41 mmeliandikahili jambo; nawaombeni sana mwende kwenye Finance Bill.Hii ni element ndogo sana, tukaliondoe ili nasi tuweze kuwacompetitive na sisi ndege nyingi ziweze kuja kunywa mafutahapa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuikumbusha Serikali,kila wanapoongelea reli ya kati wanaongelea Dar es Salaam– Mwanza. Naombeni mkumbuke ni Dar es Salaam – Kigomana matawi yake ya Mpanda na Mwanza lakini central line nikwenda Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la maji ni kubwa sana,naombeni sana tuweke bajeti kubwa ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la soko ladhahabu. Musukuma amelisema hapa, tulisema mwaka 2016na Bwana Kishimba, naombeni tuweke soko la dhahabu,halafu kwenye soko lile tuwaambie kila atakayeleta dhahabumsimwulize ameitoa wapi? Isipokuwa watakaokuja kununuandio tuweke export levy. Tutakusanya pesa nyingi sana kama

Page 65: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Taifa. Wala siyo hii asilimia tano ya wachimbaji wadogo.Wachimbaji wadogo watakwepa, hatutoikusanya hii hela;lakini tukiwafanya waje kwenye soko, wanunuzi wakaja,tutapata fedha nyingi sana kama Taifa. Naombeni mwendemkalifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la ten percentya crude oil. Jamani, Kenya na Uganda hawana crude oil.Kitakachotokea, sisi tutakuwa soko la Kenya na Uganda, nasihatuna mafuta mengi sana nchini jamani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Kigoma tunamichikichi, lakini angalia mafuta ya michikichi yanayozaliwaKigoma, huwezi kutumia hata kwa mwezi mmoja, nimachache. Nawaombeni sana tuwekeze kwenye mbegu nautafiti ili tuweze kuzalisha michikichi mingi na tuweze kuzalishaalizeti nyingi sana. Bila hivyo… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,muda umekwisha?

MWENYEKITI: Umekwisha. Hoja zako ni nzito na mudaumekwisha. Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Jasmine halafuMheshimiwa Juma Hamad jiandae.

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami niwezekuchangia katika bajeti yetu hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napendakumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kweli kwa tukio hiliambalo linaendelea katika harakati zile zile za kutetea nakulinda maslahi ya Watanzania ili maslahi haya, rasilimali zetuziweze kuwatetea na kuwasaidia hawa wanyonge hasa

Page 66: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

akinamama ambao tuna shida ya afya na maji. Munguambariki sana Mheshimiwa Rais wetu achape kazi, tupopamoja naye. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, napendakumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Naibuwake kwa bajeti ambayo inatoa mwanga katikakumkomboa Mtanzania. Mambo hayawezi yakaja maramoja, ni taratibu, kwa hiyo, tuwape muda wawezekutusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kwanza nijikitekwa kuondoa upotoshaji. Nimesikiliza michango mingi,upotoshaji ni mkubwa kwa kusema kwamba Marais waliopitana awamu hii wanaendeleza umaskini, kwambawamechangia kulipeleka Taifa hili kwenye umaskini naChama cha Mapinduzi ndiyo kinachangia katika kuleteaumaskini Taifa hili. Siyo kweli, huu ni upotoshaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombaniwaambie wananchi, maendeleo yetu hadi yanafikia hapa,bajeti zetu hazitekezwi; mara asilimia 38, mara asilimia 40 nikutokana na matatizo mbalimbali ambayo yamelikumbaTaifa hili tangu tumepata uhuru hadi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi tu napendanieleze kwamba viongozi hawa, tukimchukulia Baba wa Taifaamejitahidi sana kulitoa Taifa hili katika umasikini; juhudi zakewote tunazifahamu, lakini amekumbana na vikwazo vingi;vikwazo vya nje na vikwazo vya ndani. Kwa mfano, wakatitulipoanzisha Azimio la Arusha tumeona wafadhili wengi sanawaki-withdraw misaada kwa sababu ya sera zetu.Wajerumani walitoa misaada na Waingereza walitoamisaada. Kwa hiyo, bajeti iliyumba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya 1970, suala la oilbei yake ilikuwa kubwa sana. Export tulizotegemea zilishuka;kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, vita ya Kagerana mambo mengine yote hayo yameyumbisha uchumi.Wakoloni nao hawakutuacha huru, wakaendeleza ukoloni

Page 67: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

mambo leo; kila tunavyojitahidi kujikwamua na wenyewewanatukwamisha. Kwa hiyo, haya yote yanachangia katikakufanya bajeti zetu zisiwe za kutekelezwa kiurahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya 1980 tukaachanana sera zetu, tukayumbishwa tena; tukaletewa zile sera zastructure adjustment policies, tulikuwa hatutajiandaa ndiyomasuala ya ubinafsishaji, uwekezaji na hii mikataba mibovuilipoanzia. Kwa hiyo, siyo kwamba ni mtu mmoja, ni timu yawataalam mbalimbali. Wataalam hawa wanatoka wapi?Wanatoka kwenye vyama mbalimbali. Kwa hiyo,tusilaumiane, tuangalie tatizo ni nini? What is the root causeambayo imetufikisha hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuangalie tutawezajekujikwamua kwa haya Mataifa makubwa na sera zake? Sasahivi tunashindwa kutekeleza malengo yetu, tunatekelezamalengo haya ya kidunia; ile Millennium Development Goals,sijui kuna ile 2030, yote haya yanaharibu. Tunashindwa ku-concentrate kuwaletea watu wetu mahitaji ya msingi,tunafanya mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zote hizi ni propaganda zaKizungu, lazima tuzitambue ili tuweze kuleta mshikamanokatika Taifa letu. Wameshatugawanya na mambo ya vyamavingi, mambo ya NGOs na nini; yote hii ni divide and rule iliwaweze kutuharibia. Kwa hiyo, Serikali inapopanga, huyuanakataa, huyu anafanya hivi, kunakuwa na mvutano.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni matatizo ya ndani.Tumeona mambo ni mengi lakini rushwa na ufisadi ndiyoimetupelekea Taifa hili kufikia bajeti ambayo tunashindwakuitekeleza. Pesa zinatolewa, miradi haitekelezwi, miradihewa na Watumishi hewa, kwa hiyo, mambo yanakuwamazito. Je, fisadi huyu ni nani? Fisadi huyu siyo wa Chamacha Mapinduzi peke yake; sio Rais wala siyo nani; ni sisiWatanzania hasa viongozi ambao tumepewa dhamana yakuongoza Taifa hili kwa umoja wetu ndio tumefikisha hili tatizokatika mkanganyiko huu. (Makofi)

Page 68: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tufike mahalitujitambue. Hata kama wewe unakuwa kwenye Upinzani,hata kama wewe ni mwanaharakati, lakini kitu cha kwanzasimamia maslahi ya Taifa hili, wasitugawanye. Kwa mfano,nilitegemea tungepongeza, maana wale wengine mnasemawalikuwa wapole, walikuwa hivi; sasa tumempataMheshimiwa Rais huyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka Bunge la Katibakila mtu aliyesimama alisema tunataka Rais atakayethubutu,Rais sio mwoga, Rais mzalendo na anayesimamia watu nawengine mpaka wakatumia Rais mwenye kichwa chamwendawazimu, maana yake haogopi; Rais huyotumempata, ndio Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.Anafanya kazi kutetea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilitegemea kwamfano, juzi wakati anapambana na hili suala la madiniambalo limechukua trillions of money kwenda huko nje,nilitegemea Watanzania wote bila kujali itikadi zetutungemuunga mkono. Hapa tunashuhudia Wabungewengine wanaunga mkono na wengine wanakataa. Kwanini? Kwa sababu tumeshagawanywa. Kwa hiyo, hali hiiikiendelea haitatuletea tija katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitegemea wanasheria wanchi hii wangeungana kumsaidia Mheshimiwa Rais ili kuwezakuiangalia upya hii mikataba. Hivi kama Mwanasheriaanaweza akaungaunga aka-forge akamtetea yule muuajikwa kutumia hizo sijui technical nini, kwa nini wasiungane ilikumsaidia Mheshimiwa Rais kutengeneza na kutetea haki zetuambazo zimepotea na tunazidai? Badala yake tunaanzakubeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili Taifa miminasema tukifikia mgawanyiko huu kwamba kwa sababuSerikali hii labda ni ya Chama cha Mapinduzi, mimi niko huku,hatutafika na hizi ni mbinu na propaganda za mabeberu iliwatugawanye waendelee kutunyanyasa na kuchukuarasilimali zetu. (Makofi)

Page 69: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wenzangu,tuamke tujitambue sasa ili tuweze kuhakikisha rasilimali zetutunazilinda. Tanzania kwanza mambo mengine baadaye.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi sasa kwa upande wabajeti. Bajeti yetu ni nzuri, kwa mfano suala la kumkomboamkulima na tozo mbalimbali. Mimi nitazungumzia suala lakodi ya majengo. Nia ni kuondoa umaskini, lakini sasa kidogonina wasiwasi pale ambapo malipo yamewekwa kwa flatrate ya Sh.10,000/= na Sh.50,000/= kwa nyumba ambazohazijathaminiwa. Naomba kuuliza, je, hizi zikithaminiwa inamaana kodi itakuwa juu zaidi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kuhusunyumba za kuishi; leo mtu yupo kazini au amefanya biasharaau leo ni Mbunge umepata mkopo ukatengeneza nyumbanzuri, baada ya hapo huna kazi, biashara ilikufa halafunyumba ile sasa imethaminiwa ulipe labda Sh.300,000/=auSh.400,000/=. Hii itaishia kwamba huyu mtuatanyang’anywa ile nyumba kwa sababu ile nyumbahaizalishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali,nyumba za kuishi zote, contribution ni lazima katika kuletamaendeleo; iwepo labda hata kati ya Sh.2,000/= kwa zileambazo vigezo vyake ni vya chini, labda mwisho iwe niSh.50,000/= ili watu waweze ku-afford. Otherwise tutaendatu kuuza nyumba za hawa wananchi ambao sasa hivi kazihakuna. Unasema huyu ana mtoto, watoto wenyewe kazihawana, tunao majumbani. Kwa hiyo, tutaishia kuendelezaumaskini. Bora mtu awe na nyumba yake, asubuhi anajuaakagange vipi. Kwa hiyo, naishauri Serikali hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala maji ni muhimu sanakatika ku-stimulate maendeleo, kwa hiyo, tunaomba sana,akinamama na watoto wetu wa kike wananyanyasika,wanapigwa, wanabakwa na ndoa zinavunjika kwa sababuya maji. Kwa hiyo, naiomba Serikali, bajeti ya maji hii nanawaunga mkono wenzangu kwamba ile Sh.50/= iongezwe

Page 70: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

ili akinamama waondolewe hii adha, kwa sababu piawatapunguziwa muda. Time factor ni muhimu sana katikasuala la maendeleo. Watapata maji jirani, lakini watafanyana shughuli nyingine za uzalishaji na mambo mengine.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la mazingira.Suala la mazingira linatu-cost sana katika nchi yetu hii. Wotetunashuhudia mazingira sasa hivi yanaharibiwa mno.Tunaiomba Serikali ihakikishe kwamba… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Juma Hamad,halafu Mheshimiwa Kubenea jiandae.

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naomba kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwakunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna siku nilifarijikasana katika Bunge hili ka Kumi na Moja ni siku ambapo KatibuMkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad alituita kwenda kutuasasisi Wabunge. Hiyo aliifanya baada ya kile kikao cha kuapa.Naomba ninukuu; alitueleza hivi:

“Mnapokuwa Bungeni jaribuni kuikosoa Serikali iliifanye vizuri na mnapoikosoa, basi mkosoe kwa maana yaconstructive criticisms kwamba muwashauri, kama hilihalikufanyika vizuri, basi wafanye nini?” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pil i akasema,“mnapokuwa Bungeni pale ambapo Serikali inafanya vizuri,basi muisifu.” Huo ndiyo ulikuwa wasia wa Maalim Seif SharifHamad. Wenzangu wa CUF kama nasema uongowanisimamishe hapa wanipe utaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, MamaLulida amesema, tuliapa na sisi wote ni waumini wa Mwenyezi

Page 71: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mungu. Tuliapa kwa kutumia Biblia na Quran kwambatutaitumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahiya wananchi wetu ambao tumewawakilisha hapa. Kamahiyo haitoshi, kila siku hapa asubuhi tunasoma Dua yakuliombea Bunge na kumwombea Rais wa Jamhuri yaMuungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Dua zetu za kila siku,maana nataka ninukuu kipande kidogo tu: “Ewe MwenyeziMungu, Muumba Mbingu na Ardhi, umeweka katika duniayako hii au katika Ardhi yako hii Mabunge au Mabaraza yakutunga sheria na Serikali za wanadamu ili haki itendekekama upendavyo wewe Mwenyezi Mungu. Tunakuomba sisiWajumbe wako utupe hekima na busara ili kujadili mamboyetu kadhaa, kadhaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka nijadili hii bajetiya mwaka 2017/2018 kwa mustakabali huu. Nafikiri ni vizurikabla ya kujadili bajeti ya mwaka 2017/2018, tufanye tathminiya bajeti iliyopita ili tujue what went wrong in the 2016/2017budget, what are the challenges that we faced? Tukifanyahivyo tutakuwa tunaitendea mema bajeti ya 2017/2018. Bilahivyo, no, hatuitendei haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kubwa la bajeti yamwaka 2016/2017 ni kuelekeza matumizi in such a waykwamba development budget tuitengee asilimia 40 narecurrent budget tuitengee asilimia 60. Sisi tulimpongeza sanaMheshimiwa Dkt. Magufuli kwa sababu kwa mara ya kwanzaanazungumzia maendeleo ya watu na huko nyuma ilikuwachini ya asilimia 40. Sasa tuje kwenye ukurasa wa 30 wabudget speech ya Mheshimiwa Waziri. Naomba sana kamamna vitabu mfungue ukurasa wa 30. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 30 kwenyeparagraph ya 41, sitaki nisome ile paragraph yote, lakini kwaufupi anachosema hapa ni kwamba up to April, 2017tumekusanya 20.03 trillion. Sasa hivyo kwamba tumewezakutekeleza recurrent expenditure kwa asilimia 87.4 natumetekeleza development expenditure kwa asilimia 38.5.

Page 72: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Sasa Mheshimiwa Waziri waambie wataalam wako kulekwamba huku usifikiri Wabunge hawakusoma; sisi wenginetumeichambua neno kwa neno hotuba hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa if you add those twoingetufanya tupate 100 percent au tupate less than 100percent kwa sababu hii ni mpaka Aprili lakini uki-add 87.4percent na uka-add na 38.5 percent unapata 125.9 percent.Maana yake nini? Ni kwamba kile kilichokuwa kadiriokutumika katika bajeti hii, kimetumika na tumeongeza fedhanyingine. This is absolutely rubbish. (Makofi) (Maneno HayaSiyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hamad hilo neno lako“rubbish” lifute. Lifute!

MHE. JUMA HAMAD OMAR: Nimeshafuta, lakini hiitakwimu siyo sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye real na nominalterms; maana kuna wakati nilisema hapa, kuna vitu viwili;kuna kitu kinaitwa real terms and nominal terms. Is this budgetreal, ya 2016/2017? Is this real? Sasa nafikiri bajeti ya mwkaa2016/2017 is not realistic. Angalau hii ya 2017/2018 now it isreal, lakini angalau ni nzuri, it is healthier. Uki-compare bajetimbili hizi; ya 2016/2017 na 2017/2018, hii bajeti ya sasa nihealthier kwa sababu imewalenga wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niishukuru sanaSerikali kwa kubana matumizi, hilo wame-achieve vizuri,lazima tuwashukuru; lakini kwa maana ya mapato ambapondiyo msingi wa bajeti yote, bado tuna kazi kubwa. Natakaniwaambie, hakuna Serikali yoyote duniani inayoweza ku-survive bila tax revenue. Marekani imefika stage kwambaikiwa wewe ni mgombea wa Urais kama ume-evade taxes,basi wanasema hufai kuwa Rais wa nchi hiyo. Kwa hiyo,naelewa umuhimu wa kukusanya kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka niseme, katikahili suala la kukusanya kodi kuna siri tatu; moja, collect taxes

Page 73: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

with minimum inconvenience to the tax payers; ya pili,kusanya kodi hizi rates za kodi ziwe affordable to the taxpayers; lakini la tatu, kusanya kodi ili yule mlipa kodi aonekuna good returns katika maisha yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niipongeze Serikali;kwa maana ya minimum inconvenience to the tax payersSerikali imefanya vizuri sana. Tuna mifumo mbalimbali yakielektroniki ambayo sasa hivi tunaitumia; juzi Kamati ya Bajetitulikwenda kukagua ule mtambo wa TTMS ambao kwa kweliutawezesha kujua kodi za operators wa simu hawa on timelybasis, lakini pia tuna mfumo pale katika Idara ya Forodhaambao unaitwa TANCIS; ni mfumo wa kielektroniki wa kujuani nani aliyelipa kodi na wakati gani na kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni kwamba ule Mfumowa TANCIS bado ni TRA ndiyo imekuwa nao, lakini kunawadau wengine ambao wanapaswa kukusanya kodi kwaniaba ya TRA, ule mfumo hawana. Nadhani ni vizuri tuishauriSerikali hapa kwamba wale wadau wengine nao wa-adhereto that TANCIS system.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niende harakaharaka. Kama kuna kitu ambacho kimesahaulika katikabajeti hii ya 2017/2018 ni suala la utalii. Mapato yatokanayona utalii sasa hivi ndiyo mapato makubwa kwa maana yaforeign exchange tunayo-earn. Nafikiri kama sikosei, asilimia17.5 ya mapato yetu ya nje yanatokana na utalii. Wenzetuwa Kenya wamechukua comperative advantage; wakati sisitulikubaliana wote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwambatutoze VAT, wao hawakutoza. Kwa hiyo, bei ya mtalii kujaTanzania sasa hivi imekuwa ghali sana kuliko kwenda Hija.Tunakosa watalii wengi na huenda baada ya muda mdogosana tukakuta mapato yetu yana-decline kabisa katika Sektahii ya Utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tuna comperativeadvantage ukilinganisha na Kenya. Over the years kuanzia2011 mpaka sasa hivi namba ya watalii in Kenya inapungua,sisi huku inaongezeka na inategemewa kwamba mwaka

Page 74: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

unaokuja namba ya watalii itakuwa kama milioni moja nakitu in Kenya na milioni moja na kitu hapa kwetu. Kwa hiyo,kama tutajipanga vizuri, tutaondoa kodi hii VAT on tourism,basi nina uhakika tuna uwezo wa kukusanya mapato zaidiya Kenya. Kwa hiyo, naiomba Serikali inapokuja na FinanceBill iliangalie suala… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kubenea, halafuMheshimiwa Cosato Chumi jiandae.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imekuwepo hoja ndani yaBunge na tokea jana na leo Waheshimiwa Wabungewamekuwa wanazungumza mambo mengi juu yetu sisiupande wa pili ambao tunaambiwa hatuungi mkono juhudiza Serikali au za Rais za kutetea rasilimali za Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya msingi ni kwambasisi hatuhusiki kwa namna yoyote ile na mikataba yote yamadini iliyofungwa na Serikali hii. Hatujawahi kuwa kwenyeSerikali hiyo na hatujawahi kuingia katika hiyo Serikali na kwahiyo, hatujawahi kusaini mkataba wowote ule. Kwa hiyo,hiyo mikataba yote iliyofungwa ni ya Chama cha Mapinduzina Serikali yao. Wasichukue kesi isiyotuhusu wakatutupia sisi.Hiyo ni kesi yao, hilo ni dudu lao, wameliamsha, wamalizanenalo wenyewe. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imekuwepo hoja ya msingisana kwamba eti tumeibiwa katika rasilimali zetu, kwambatumeibiwa na watu waliokuja kuwekeza. Mikatabailiyofungwa imefungwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.Waliofunga mikataba na ambao bahati njema mmoja waoamezungumza hakamatiki, anasema, mikataba hiyoimefungwa baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kukutana

Page 75: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

na kuwepo minutes za vikao hivyo. Hatuwezi kusematumeibiwa wakati tumeruhusu mali yetu wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningewaelewa sana kamatungesema mikataba iliyofungwa ni ya kinyonyaji, mimi hiyoningewaelewa. Siyo wizi, hapa hakuna wizi! Wizi ni mtuanayeondoka ndani ya nchi yako, anagonga stempu,analipa ushuru, anakulipa hela yako, anaondoka unasemaanakuibia! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana kuthibitishakwamba hakuna wizi, Rais amekaa na aliyemwita mwizi janaIkulu. Mlango wa Ikulu jana ulifunguliwa ukawa wazi, mwiziakaingia Ikulu, Rais mwenye vyombo vya dola… (Makofi)

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

TAARIFA

MWENYEKITI: Taarifa. Mheshimiwa Kubenea, taarifa.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda, kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7), kumpa taarifamsemaji anayeendelea kuzungumza kwamba MheshimiwaRais jana amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni yaBarrick Gold, sio Mkurugenzi Mkuu wa Acacia. Natakanimrekebishe tu hapo.

MWENYEKITI: Hiyo ndiyo taarifa sahihi.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,lakini huyo ndio mwizi aliyeitwa na Mheshimiwa Rais kwambakampuni hii haikusajiliwa nchini, inatudhulumu, wamekaanaye Ikulu wakazungumza naye. Nilitegemea MheshimiwaRais angeenda kumweka ndani huyu mtu na akamzuiaasizungumze.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

Page 76: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kubenea…

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Musukuma hebu kaa.

Mheshimiwa Kubenea, jenga hoja yako na sentimentsambazo unataka kuzitumia sasa hivi hazitasaidia hoja yako.Kwa hiyo, nakuomba elekeza hoja yako kwenye masualamuhimu ya uchumi na masuala muhimu ya mambo ambayoyako mbele yako leo. Sasa haya mambo yaliyopitatulishasema yamepita, tunakwenda mbele. (Kicheko)

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima yako, naomba niliache hilo jambo, lakini messageimefika. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangukwenye Wizara ya Nishati na Madini nilizungumza juu yakuwepo mgongano wa maslahi kwa baadhi ya viongoziwetu waandamizi kwenye Serikali. Bahati njema au bahatimbaya nilimtaja kaka yangu, rafiki yangu Mheshimiwa VictorMwambalaswa, Mbunge wa Lupa. Naye juzi akajibu hapa,akanieleza mimi binafsi nilivyo na akasema amenichangiamatibabu, akasema ameninunulia kompyuta yeye na rafikizake. Kwa kweli kama nisingelelewa katika misingi ya Uislamuningerejesha fedha ya Mheshimiwa Mwambalaswaaliyonichangia matibabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sikumwombaMheshimiwa Mwambalaswa anichangie, nilikuwa kitandanininaumwa, watu wakaomba mchango wakanichangia,lakini nimesikitika kwamba mchango alioutoa sirini amekujakuusema hadharani ndani ya Bunge hili. Ni masikitikomakubwa sana, kwamba ukiwa na kiongozi wa namna hiisiku akikuchangia maziko atakuja kukudai sanda au kujakukudai jeneza.

Page 77: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe onyo kwaWaheshimiwa Wabunge mnaochangisha michango ya harusihumu ndani ya Bunge, mkimchangisha MheshimiwaMwambalaswa, kuna siku atakuja kuwadai wake mnaooa.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwambalaswaamesema kwenye Bunge,…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kubenea, tuendelee nabajeti, hayo ameyasema…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: No, no, no, Waheshimiwa Wabunge,Kanuni zetu ziko very clear, kama MheshimiwaMwambalaswa ameyasema, kayasema yameshapita, nawekama unavyosema ni Muislamu, huna haja tena ya kutakakusema, atakulipia Mungu yako. Kwa hiyo, huna haja sasaya kuanza ku-throw back yale ambayo amekutuhumu.Tuendelee na bajeti.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mgongano wa maslahi upo katika viongozi wetu wakubwakatika nchi hii. Mheshimiwa Ame Mpungwe alikuwa Baloziwetu wa Afrika Kusini, akawa dalali katika makampuni yaMakaburu yaliyonunua NBC, yaliyochimba Tanzanite namagazeti yaliandika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gazeti la Rai lilihoji BaloziMpungwe ni Balozi mzalendo au muuza nchi? Mara baadaya Balozi Mpungwe kustaafu akawa mmoja wa wamiliki wamakampuni makubwa ya uwekezaji wa madini katika nchihii, AFGEM ya Tanzanite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Daniel Yonaaliyekuwa Waziri wetu wa Nishati na Madini alichukuadokezo akapeleka kwenye Baraza la Mawaziri la kuuza Kiwira.Kiwira ikauzwa akaanzisha Kampuni inaitwa TanPower, nayoikaingia ubia na Kampuni nyingine inaitwa ANBEN Limited

Page 78: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

wakauziana Kiwira. Ilivyoenda Kiwira, mnaijua. Leo tunakaahapa tunazungumza kana kwamba hayo mambo hayapo!Eti tusijadili watu waliohusika kuiingiza nchi hii katikamigogoro ya kifisadi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwambalaswaamesema kwenye Bunge hili kwamba yeye hakuwa namaslahi binafsi na mradi wa umeme wa upepo wa Singida,akiwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, mimi natoaushahidi hapa, alikuwa na mgongano wa maslahi. Mwaka2011 kuna invitation letter, hii hapa, inatoka China inamwalikaMheshimiwa Victor Mwambalaswa mwenye Passport numberAD002021 iliyotolewa Januari, aliyezaliwa tarehe 08, issuedJanuari, 2006. Hii hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaliko huuanakwenda China akifuatana na William Mhando ambayealikuwa Mkurugenzi wa TANESCO; na wengine ni TimothyNjunjua Kalinjuna na Machwa Kangoswe, hii hapa.Wanasema wanakwenda kufunga mkataba kati ya TANESCOna Kampuni ya China na Kampuni ya Power East AfricaLimited ambayo ni yake. Anasafiri kwa fedha za Tanzania,anasafiri kwa passport ya Tanzania, analipwa posho yaTANESCO, anakwenda kufunga mkataba wa kampuni yake,halafu anakuja hapa anasema lile lilikuwa wazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hapa taarifa ya NDCinasema Mradi wa Umeme wa Upepo wa Singida PT 33162,mradi umeanza mwaka 2010. Maelekezo ya mradi; mradiunatekelezwa kwa Kampuni ya Seawind Power Limited naNDC; na hiyo Power Pool East Africa Limited, ya kwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2010 MrindokoBashiru anakuja kutoa barua hii ya kuipa kazi kampuni yaakina Mheshimiwa Mwambalaswa. Mwaka 2010, MheshimiwaSitta anafunga mjadala wa Richmond Bungeni kwa ubabetu. Mwaka 2011 Mheshimiwa Mwambalaswa anakuwaMwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, mwaka 2010Mheshimiwa Mwambalaswa anakuwa Makamu Mwenyekitiwa Bodi ya TANESCO. Jamani…

Page 79: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

MBUNGE FULANI: Ayayayayaaah!

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hayamambo, tunapozungumza mgongano wa maslahi ndiyohuu. Mnazungumza vitu gani humu ndani? Halafu watuwanasema hapa mnafukua makaburi, fukueni haya.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mgongano mkubwawa maslahi. Nina orodha ndefu ya viongozi wa Serikali hiiambao mikataba iliyofungwa nyuma yao wana mgonganowa maslahi. Hatuwezi kukaa hapa tunadanganyanakwamba Taifa hili ni letu wote wakati wengine wananufaika,wengine wanaliibia Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mtu mmoja hapaamesimama asubuhi anasema nampongeza MheshimiwaRais. Namwomba Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli akaangaliefedha iliyotumika kulipa Kampuni ya IPTL; na Waziri wa Fedhana Mipango akaangalie. Mwaka 2010 kuelekea kipindi chaUchaguzi Mkuu, shilingi bilioni 46 kulipia mafuta IPTL; kwamwezi shilingi bilioni 15, Mheshimiwa Ngeleja akiwa Waziriwa Nishati na Madini na ndiye aliyesaini hiyo hoja; yule,Mheshimiwa William Ngeleja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyaraka zipo, ushahidi upo!Aende, Mheshimiwa Rais ana faili huko Ikulu afungue faili laIPTL aangalie mwaka 2010 kipindi ambacho tunaelekeakwenye Uchaguzi Mkuu. IPTL imelipwa shilingi bilioni 15 kwamwezi kuwasha mitambo ya IPTL. Halafu mnakaa hapatunadanganyana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima kabisa,naviomba vyombo vya ulinzi na usalama viwachunguzehawa watu, hatuna maslahi binafsi, tunatetea maslahi yaTaifa letu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chumi, halafuMheshimiwa Elias Kwandikwa na Mheshimiwa Ester Mahawe.(Makofi)

Page 80: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

MBUNGE FULANI: Yatosha kwa leo. (Makofi)

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru nami kwa kupata nafasi. Napenda kuipongezaWizara ya Fedha na Mipango kwa jinsi ambavyo tulishirikianawakati watu wa Halmashauri wa Mji wa Mafinga tulipopatamsaada kutoka Ubalozi wa Japan. Kulikuwa na somecomplications, lakini kwa ushirikiano mkubwa tuliwezakufanikiwa kiasi kwamba tukafanikiwa kupata huo msaadabaada ya Wizara kufanya marekebisho ya kanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nichangie katika bajetihii kwa kuanza kusema yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema ni wizi katikaSekta ya Madini, nil ikuwa najaribu kupitia nyarakambalimbali, mojawapo, ni hii inasema protecting yourcommunity against mining companies. Katika document hiiimeeleza kwa ufasaha namna gani makampuni makubwaya madini yanavyofanya mbinu mbalimbali ambayohitimisho lake ndiyo tunaita wizi. Katika utangulizi wadocument hii anasema:

“The company may deliberately try to disrupt andweaken a community’s ability to organize effectively againstthem.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maana yake ni nini?makampuni yanaweza yakatumia mbinu mbalimbaliyakatugawa sisi ili tusiweze kushikamana katika kukabilianana wizi mbalimbali ambao wanaufanya. Wizi huuunafanyikaje? Kwa sababu wenzetu wako mbali kwateknolojia na mbinu mbalimbali za kufanya internationaltrading. Moja, wanafanya kitu tunaita trade mispricing. Ndiyoile wakileta machinery wanakuza bei baadaye wanadai taxrefund. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, wanafanya kitukinaitwa payment between parent companies and their

Page 81: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

subsidiaries, ndiyo maana tulikuwa tunagombana na Acacialakini amekuja kuibuka Mwenyekiti wa Barrick ambayo ndiyoKampuni Kuu. Pia wanafanya wizi huo kwa kutumia profitshifting mechanism ambayo imekuwa designed ku-hiderevenue, ndiyo maana tunaita wizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nil ivyosema,watatumia mbinu nyingi kutu-divide. Gazeti la The East Africanla wiki hii limeandika, “Magufuli Fight for Mineral RevenueSplits Parliament.” Hiki siyo kitu kizuri kwetu kama Taifa. Lazimasisi tubaki kitu kama kimoja. Kama Bunge, kama Taifa, lazimatuwe nyuma ya Mheshimiwa Rais ambaye ameamuakuthubutu kukabiliana na huu wizi mkubwa wa Kimataifa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Director wa Global Justiceanasema kuwa Afrika siyo maskini na ukipitia ripotimbalimbali za Taasisi za Kimataifa, zinasema kwamba kupitiamakampuni haya, fedha inayoondoka ni zaidi ya mara kumiya fedha wanayotupa sisi kama misaada. Maana yake ninini? Ukienda kwenye bajeti yetu, karibu shilingi trilioni sabani mikopo, misaada na fedha kutoka kwa wahisani; lakiniinayoondoka kupitia wizi huu niliousema, maana yake nimara kumi ya shilingi trilioni saba. Kwa hiyo, zinazoondokahapa nchini kwetu ni shilingi trilioni 70, ndiyo maana tunasemawizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa hizi zinazoondokakwa mbinu hizi mbalimbali ambazo Mheshimiwa Raisameamua kuwa na uthubutu ili tuweze kukabiliana namultinational companies, lazima sisi kama Taifa na kamaBunge tuwe united, tusigawanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais kwa niniameweza kuwa na uthubutu? Ukisoma gazeti la SundayNation la Jumapili linasema, “Uhuru tycoons raise millions intwo hours” kwa ajili ya kampeni, lakini we are lucky Rais wetuameingia pale hakuwa na backing ya watu wenye helachafu, ndiyo maana…

Page 82: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chumi subiri kidogo.Mheshimiwa Kubenea, tunaomba documents zote ulizozitajazije Mezani sasa hivi.

Endelea Mheshimiwa Chumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ihope utanilindia huo muda wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunapopatakiongozi wa namna hii, lazima tuwe united kumuungamkono, kwa sababu tunachozungumzia ni upotevu wamapato ambayo yakipatikana wote tutafaidika. Wote hapatunalia, nami nalia kuhusu kukosekana maji, umeme, hudumabora za afya, kuanzia Lumwago, Bumilanyinga, Isalavanumpaka Itimbo na Mafinga kwa ujumla. Sasa anapotokeakiongozi mwenye uthubutu ni lazima sisi tushikamanekumuunga mkono kukabiliana na multinational companies.Haya madude ni hatari sana, nitawaambia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hugo Chaves alipoingiamadarakani tarehe 11 Aprili, 2002, alifurumua mikataba kamaanavyojaribu kufanya Mheshimiwa Rais. Madude haya(multinational companies) yaliji-organise yakafanya hujumakumwondoa madarakani lakini kwa sababu Bunge nawananchi wa Venezuela walikuwa united, baada ya masaa47 alirudi Ofisini. Ndiyo maana nasisitiza ndugu zangu tuwekitu kimoja kukabiliana na madude haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu siyo wakati wa kutafutapersonal recognition. Kila mtu kwa nafasi yake alipaza sautikuhusiana na hujuma na wizi huu. Wapo waliokuwawanaharakati wakati huo kama Mheshimiwa Tundu Lissu,wapo waliokuwa Wabunge kama Mheshimiwa PeterSerukamba na Mheshimiwa Kigwangalla ametajwa hapa,wapo akina Rugemeleza na Nshema wale wa LEAT wotewalipaza sauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mwaka 2008 Mawaziriwanaohusika na Sekta ya Madini walikutana kujadili katika

Page 83: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

Afrika namna gani tutanufaika kutokana na madini. AUSummit 2009 ilipitisha azimio ni kwa namna gani tutaendeleakunufaika na madini na kuachana na wizi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2011 Mawaziri wamadini katika Afrika walikutana na kujadili na kuja kitukinaitwa “From Mission to Vision”; na hiki ndicho MheshimiwaRais anachofanya. Ametoka from mission to vision to action.Sasa ameingia kwenye action. Anapoingia kwenye action,sisi tuna kila sababu ya kumuunga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitaka ujue wizi huu, nendakasome kitabu hiki cha Nicolaus Shakson; (Treasure Island),“Uncovering the Damage of Offshore Banking and TaxHavens.” Yote haya ni wizi unatumika. Vile vile kasome kitabucha Mwandishi the same; “Poisoned Worse; The Dirty Politicsof African Oil.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nenda kaangalie documentinaitwa “Stealing Africa.” Why is Africa so rich in resources, yetso poor? Ni kwa sababu ya wizi wa namna hii ambao lazimatukubaliane tuwe united kama Taifa, tuwe pamoja kamaBunge na kwa maana hiyo, tutaweza sana kufanikiwa.Vinginevyo tukitafuta muda wa recognition, kila mtu playedhis/her own part. Viongozi wa dini walisema, wananchi wakawaida walisema, wanaharakati walisema, Wabungewalisema. Kwa hiyo, ni wakati ambao tunatakiwa tukwepesana kugawanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia, wakatianaapishwa Commisioner wa TRA, Mheshimiwa Makamu waRais alisema, “Maafisa wako na Mameneja wa Mikoawaache kutoa kauli za kuigombanisha Serikali nawafanyabiashara, wakusanye kodi kwa kufuata sheria nataratibu na pia wawe na lugha nzuri.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu kinaitwaMawakala wa TRA, lugha yao na operation namnawanafanya, ni kuigombanisha Serikali na wananchi.Naiomba TRA, pamoja na kutoa elimu ya mlipa kodi, ijaribu

Page 84: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

kukaa na hawa Mawakala wao iwe inawapa hata trainingya namna gani ya kufanya customer care. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mudaumeniishia naona unanikimbia; katika makinikia haya, yakomengi. Sisi kule Mufindi suala la misitu, nimeshaandika hatakatika mchango wangu; MPM wanauziwa magogo mpakaleo nusu ya bei pasipo sababu. Hayo nayo ni makinikia. Kwahiyo, naiomba Serikali, kama ilivyoanza katika dhahabu, kunamakinikia kwenye misitu, kuna makinikia kwenye fishingindustry kutoka bahari kuu, kuna makinikia kwenye mambomengi, hata kwenye mchezo wetu wa soka kuna makinikia.(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Elias Kwandikwana Mheshimiwa Esther Mahawe jiandae.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

MHE. ELIAS J. KWANDIKWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangiakwenye hoja muhimu hii ya bajeti ya Serikali. Kwanza nianzekumshukuru sana Mungu kwa yote kwa afya na haya yoteyanayoendelea, naamini mkono wa Mungu unaonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kupongezahotuba nzuri ya Mheshimiwa Waziri. Napongeza kwa dhatikabisa na wakati hotuba hii inasomwa, WaheshimiwaWabunge wengi tulishangilia na yale tuliyokuwatunayashangilia, naipongeza pia Kamati kwambaimeyazungumza. Sehemu ya tano ukisoma utaona namnaKamati imejaribu kuchambua na kuweka kielelezo namnabajeti hii ilivyoweza kukidhi mambo kadha wa kadha. Hii nipamoja na kuiangalia hii sura ya bajeti. Kwa hiyo,naipongeza sana Serikali.

Page 85: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami niseme kwambaunaweza ukaangalia mafanikio ya bajeti hii na hususani bajetiiliyopita kwa kuangalia yale matokeo (outcomes) kwenyemaeneo yetu. Kwa hiyo, lazima nishukuru sana kwa sababuJimbo la kwetu ni jipya, Halmashauri ya kwetu ni mpya; hivisasa tunaendelea kujenga Ofisi kwa kasi; fedha tunazo;tumejenga mashule; kuna maeneo ya maji, tunaendeleakupata huduma za maji na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mambo mengi siwezikuyasema yote, nashukuru kwamba hii hotuba ni nzuri kwasababu ukiangalia bajeti zilizopita ukilinganisha na bajeti hii,utakubaliana nami kwamba kwa kweli hii ni hatua nzuri.Nami naipongeza Serikali iendelee na mwendo huu, tutafikambali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nizungumze hili sualamuhimu la madini. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais wetukwa sababu tulikuwa na kiu ya kuyaona mengi na yakomengi ambayo pia yanakwenda kugusa Halmashauri zetu.Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa sababu kamaambavyo nilisema wakati uliopita nilipokuwa nachangiahapa, kwamba ile dhamira nzuri ya Mheshimiwa Rais ndiyohasa itaweza kuleta msukumo huku chini ili tuweze kufikapale tunapotaka kwenda. Nina uhakika tunakwenda kwenyeuchumi wa kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa najaribu kuangaliabaadhi ya figures za report hizi zilizotoka, nikawa najaribukuona sisi kwenye Halmashauri zetu za Kahama tukiwa naMajimbo matatu ya Msalala, Kahama Mjini na Ushetu, utaonahapa service levy ambayo nikiitaja utajua tulikuwatumepoteza mapato mengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naangalia kwenyedhahabu peke yake kwa report hii, kwa kile kiwango chachini cha upotevu wa mapato, tumepoteza service levy yashilingi bilioni 324 kwenye dhahabu peke yake; lakini tukawana shilingi bilioni 549 kwa kiwango cha juu kwenye dhahabupeke yake. Ukiangalia kwenye madini mengine 13

Page 86: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

yaliyoorodheshwa na Tume, utaona kabisa tulikuwatumepoteza yapata kama shilingi bilioni 397 kwa upandewa madini yote na kwa kiwango cha chini; na kiwango chajuu tunakwenda kwenye shilingi bilioni 689. Nazungumza kwaupande wa hili zoezi lililofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda kuangalia kwenyeupande wa service levy tulizopoteza kwa wale waliotoahuduma kwenye migodi wakiwemo wale waliofanyainsurance, wale waliofanya consultation, waliouza mafuta;naomba sasa hapa Mheshimiwa Waziri atusaidie kwa sababutulikuwa na shida ya kupata information.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutaweza kupatafinancial statement tangu migodi hii ilivyoanza itatusaidianasi kwenye Halmashauri zetu kuona wale waliotoa hudumakwenye migodi kama tulipoteza. Tulishaanza hilo zoezikutafuta hizo information. Tunajua kuna kiasi kikubwaambacho kingeweza kusaidia Halmashauri zetu. Kuna kiasikikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, uone kabisakwamba Mheshimiwa Rais ameanza nasi huku tunaendeleakupigana. Hata alipotembelea Shinyanga wakati ule,nakumbuka ndugu yangu Mheshimiwa Kishimba, Mbunge waKahama Mjini alizungumza, tumwombe Mheshimiwa Raisatusaidie kwa sababu tunaona tumepoteza service levynyingi. Kwa hiyo, kwa upande wa Serikali mnawezakutusaidia ili tuweze kukomboa na kupeleka maendeleo kwawatu wetu. Sura ya Kahama ilivyo, sivyo inavyotakiwa kuwakwa fedha nyingi ambazo tunatakiwa kuzipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonataka nizungumze kwa ufupi ni kuhusu hizi takwimu.Namwomba Mheshimiwa Waziri, hata bajeti iliyopita nilikuwanimeomba kwamba Ofisi ya Takwimu tuisaidie sana iwe nawatu wa kutosha, iwe na vifaa vya kutosha ili tuweze kupatadata muhimu za kutusaidia kuweza kufanya mambombalimbali, kwa sababu ukija kuona hapa, data nyingiambazo tunazitumia kwenye records zetu za bajeti na

Page 87: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

kadhalika, nyingi tunatumia ambazo ni wastani, tunatumiaaverage, lakini sasa tukitumia average tunaacha groupkubwa la watu nje ya hizo data ambazo tunazipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wakati mwinginetunahitaji wataalam wasaidie Ofisi yako kwenda kwenyemeasures nyingine. Waangalie measures of dispersion ilituweze kuona tunavyozungumza kwamba wastani wakipato ni shilingi milioni mbili, lakini tumewaacha watuwangapi nje ya msitari?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiria kwambaOfisi hii iboreshwe, itatusaidia pia kuweza kufanya decisionnyingi, tuweze kuona pia tuna income gap ya namna gani?Bajeti iliyotangulia, tuliona pia hata Mikoa ambayo iliyokuwachini ya mstari wa umaskini. Kwa hiyo, nashauri tu MheshimiwaWaziri, hii Ofisi ni muhimu sana kuiangalia kwa jicho lakipekee itusaidie kupata information za kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze kidogo suala lakodi kwenye assessment. Nataka nizungumze tu kwa sababuCommissioner naamini anaweza kuwa yuko hapa. Kwamiaka mingi tumechukua hii kwa kutumia band, tunachukuablanket tu kwenye maeneo fulani. Sasa nafikiri tuendeleekufanya analysis ili mlipa kodi alipe fair kodi kulingana nakipato chake. Kwa sababu utakuja kuona kuna maeneomengi tunatoza kodi kutokana na eneo, hatuendi kutozakutokana na uhalisi wa mtu anavyopata kipato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, twende zaidikuboresha taarifa zetu ili tutoze kwa usahihi. Kwa hiyo,utaona maeneo mengine kwa mfano, kwenye Mji tunasemalabda wafanyabiashara wanaofanana kwenye Mji fulaniwatozwe kiasi hiki kwenye kodi ya mapato. Kwa hiyo, nafikiritwende zaidi ili tuweze kuboresha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hili kwenye zoezi lautozaji wa kodi ya majengo, tukisema tunakwenda kumtozamtu mwenye ghorofa la Sh.50,000/=, lakini mwenye ghorofakuna mwingine anaweza akawa ametengeneza kwa leisure

Page 88: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

tu. Kwa mfano, ndugu zangu Wangoni kule nilikuwa nikiendanaona wana maghorofa ambayo wameezeka kwa nyasi.Nilikuwa nakwenda Mbinga, nil ishuhudia kuna watuwametengeza maghorofa hayo. Kwa hiyo, tuangalie ilitutoze kutokana na thamani. Vile vile wako watu wenginewana nyumba zao wamepangisha; tukitazama vizuri,tutaona kuna watu ambao wanaweza wakatupa kodinyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa sababuya muda, nataka nizungumzie juu ya sura ya bajeti. Naonakabisa kwamba upande wa madeni hasa deni la Taifa, tuki-manage vizuri hili deni, utaona kabisa kwamba makusanyoyetu ukiwianisha na hali halisi ya matumizi, kidogo kunauwiano mzuri. Kwa hiyo, tunakusanya shilingi trilioni 19.2kwenye mapato ya TRA, kwenye non-tax revenue pamojana Halmashauri, lakini matumizi yake bila kutoa madeniambayo tunakwenda kulipa, tuko kwenye shilingi trilioni 22.Kwa hiyo, kuna gap kidogo la shilingi trilioni kama 2.9 hivi.Kwa hiyo, tunahitaji ku-manage vizuri hili deni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona sasa hivi tunakwendakulipa deni lakini utaona tunakopa shilingi trilioni 11 mkopowa ndani na nje, lakini tunakwenda kulipa shilingi trilioni tisa.Kwa hiyo, hili gap la deni litaendelea kuzidi. Kwa hiyo, naombatufanye effort kupunguza hili deni ili siku za usoni tukopekidogo, tulipe kidogo ili tuweze kujenga uwezo mkubwa wakupeleka fedha nyingi kwenye eneo la maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu kwakuzungumzia juu ya upande huu wa nakisi ya bajeti. Nilikuwanajaribu kuangalia hapa kwamba tumepata nakisi ya bajetiya 3.8 lakini hapa tumezingatia mapato ya mikopo nafuukutoka nje, tumewianisha na GDP. Tumeacha pia hii mikopomingine ya ndani na nje yenye masharti ya kibiashara ambayoukijumlisha na mikopo ya ndani tunakuwa na shilingi trilioni11. Sasa nikiwianisha na pato la Taifa, tunaona kwamba uleuwezo wetu wa ku-deal na government spending unakuwauko short kwa asilimia 11.3.

Page 89: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiria lazimatutazame yote kwamba tuna uwezo wa kukusanya kodi, tunauwezo wa kukusanya mapato ya ndani mengine yale pamojana Halmashauri zetu, lakini ule uwezo wa sisi kupata fedhakutoka nje ya makusanyo yetu tunapungukiwa asilimia 11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri tulitazamekwa sababu tukitazama upande huu wa mapato ya mikoponafuu kutoka nje pake yake ya shilingi trilioni tatu, nafikiri siyosahihi kuweza kuiona hii nakisi ya bajeti. Kwa sababu nilikuwanajaribu kuangalia nchi mbalimbali, nimeona Uholanzi wana-shoot kutoka 2.8 hadi 2.5, Marekani wana 3 - 3.5. Ukionarange, iko within lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mahawe,atafuatiwa na Mheshimiwa Kadutu na Mheshimiwa Massare.

MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi iliniweze kuchangia bajeti hii iliyoko mbele yetu. Ni ukweliusiopingika kwamba haiwezekani mtu mwenye nia ya dhatina mzalendo kwenye Bunge hili ukasimama bila kuanzakumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais JohnPombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nil ipokuwanatazama kitabu cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri waFedha, niliona jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais hakukurupukakwenda kuzuia madini yetu kusafirishwa kwenda nje ya nchi.Ilikua ni sehemu ya vipaumbele ambavyo Mheshimiwa Raisalivizungumza alipokuwa hapa Bungeni akihutubia tarehe20 Novemba, 2015 na habari ya madini ilikuwa kipaumbelechake Namba nne (4).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nampongeza sanaMheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzurialiyoifanya. Hawa wanaosema jana amemkaribisha mwizi

Page 90: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Ikulu, yaani tunasema hiyo ni danganya toto, maanaMheshimiwa Rais alisema anakaribisha wahusika kwenyemeza ya majadiliano, wala hakuandika invitation letter yakumleta yule Mwenyekiti hapa. Watu walijipima wenyewe,wakaona jinsi gani tumetiwa hasara na Makampuni yaohayo, wakaona wabebe mzigo huo wa kuja ku-negotiatemambo yaliyofanyika ya kutia nchi hii hasara na Rais wetuna mambo haya yamefanyika hadharani. Kwa hiyo, hawandugu zetu wakikosa la kusema, ni bora wakati mwinginewakanyamaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niseme, watu hawamara nyingi wanawasumbua hawa Waheshimiwa Mawazirikwa maswali na vitu vingine vya namna hiyo na michangoBungeni humu wakihitaji Serikali kupeleka mahitaji kwenyeMajimbo yao; wanahitaji elimu, maji na afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa, kama siyoMheshimiwa Rais ameamua kuchukua jukumu hili zito lakujitoa muhanga akaamua kutetea rasilimali kwa ajili yawananchi wa nchi hii, hivi hawa watu hayo mahitaji muhimuya watu wao watayatoa wapi? Kwa hiyo, nampongezasana Mheshimiwa Rais na tunaendelea kumwombea Munguaendelee kumpa maisha marefu, maana ana mpango wakututoa mahali tulipo kwenda mahali pengine. Ni sawa naMusa alivyowatoa wana wa Israel kwenye nchi ya utumwaya Misri na kuwapeleka Kanaani. Ndicho anachokifanyaMheshimiwa Rais kwa sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nimpongezesana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa bajeti nzuri sanaambayo imekuja mbele yetu. Tunafahamu kwamba kazikubwa inafanyika. Naipongeza na timu nzima ambayo ikochini ya Wizara hii ya Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza habari hiiya bajeti, naomba nianze na suala la makusanyo ya mapato.Naipongeza pia Serikali kwa sababu sasa imechukua hatuaya kuweza kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ilikudhibiti upotevu wa fedha hasa katika Halmashauri na

Page 91: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

maeneo mengine mbalimbali nchini. Ninachokiomba nakuishauri Serikali yangu ni kwamba, katika mgawanyo huusasa wa ile Keki ya Taifa baada ya makusanyo haya kufanyika,basi mgawanyo wa Keki ya Taifa uweze kwenda sawia kwanchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nikizungumza hili,naomba nizunguzie suala zima la elimu. NampongezaMheshimiwa Rais kwa kukubali kupeleka katika shule zetushilingi bilioni 18 kila mwezi kwa ajili ya elimu bila malipo. Nikweli na ni dhahiri kwamba watoto sasa wanasomamashuleni na changamoto zilizokuwepo huko nyuma hazipotena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nazungumza hivi,karatasi niliyoibeba mkononi mwangu inaeleza orodha yashule ambazo zitakarabatiwa katika maeneo mbalimbalinchini kwa ile bajeti ya 2016/2017. Nitoe masikitiko yangukwamba Mkoa wa Manyara shule inayokwendakukarabatiwa ni moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetazama Mikoa mingi;Dar es salaam na Mikoa mingine, kila mtu aliiona hii karatasi.Kuna mikoa imepata bahati ya kukarabatiwa shule saba,sita, nane au nne lakini Mkoa wa Manyara tunakarabatiwashule moja tu ya Nangwa iliyoko Wilayani Hanang. Naonakidogo hapa haijakaa sawa sawa. Namwomba sanaMheshimiwa Waziri Ndalichako katika hili nalo atuangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna shule kongwe, tunashule inaitwa Endagikoti ambayo iko Wilayani Mbulu,ilianzishwa mwaka 1929, tuna shule iko Mbulu inaitwa Dawi,imeanzishwa mwaka 1917; hizi shule ni kongwe. Masikitikomengine ni kwamba, hatuna high schools kwenye Mkoa waManyara. Tuna high schools chache mno, mfano Wilaya yaSimanjiro haina high school hata moja; Hanang haina highschool hata moja; Wilaya ya Mbulu ina high school mbili.Kwa hiyo, naomba, kwa sababu kipaumbele cha kwanzacha Mtanzania ni elimu na tukimkamata huyu elimu tukaacha

Page 92: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

kumwacha aende zake, watoto wetu watakombolewa.Naomba sana kwa hili tukumbukwe katika Mkoa waManyara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru na kuipongezabajeti hii kwa kuwa inatambua akinamama; Mama Lishe,akinamama wanaofanya biashara zao ndogo ndogo navijana hawa Wamachinga, hili ni jambo kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sanaMheshimiwa Waziri pamoja na Naibu kutambua hili. Wakatihaya ya kurasimisha biashara zao yanafanyika, naiombaSerikali iangalie namna gani itakusanya kodi kwenyeMakampuni makubwa ambayo hayakusanyi kodiinavyotakiwa ili ikiwezekana hawa watu wapewe baadaya kutambuliwa na kupewa maeneo ya kufanyia biasharazao, waweze kupatiwa muda wa kutosha ili kwamba sasaifikie mahali nao waweze kuchangia kodi. Siyo kwambawanapewa maeneo na wakati huo huo basi wanaanza tenakutozwa kodi wakati wanakuwa hawajaji jenga vileinavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasema badotuna vyanzo vingi vya kodi vinavyoendelea kupotea; kunaMakampuni makubwa ambayo yanakwepa kodi.Namshukuru sana Mheshimiwa Rais, juzi hapa alizindua datacenter kwa ajili ya collection ya mapato yote yanayotakiwakukusanywa katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya Makampuni makubwakama ya simu, Makampuni ya uchimbaji ambayo yamehodhivitalu vikubwa kwa ajili ya uchimbaji lakini hawachimbi,vitalu hivyo vimekaa tu. Naomba Serikali ifanye tathmini yakutosha waone kwamba Serikali inakwenda kufaidika na nini.Najua Mheshimiwa Rais ameshaanza hili na nina hakikatunakwenda kufanikiwa siku zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusisahau pia kwamba tatizokubwa la maji bado lipo pale pale. Hatukuona ile Sh.50/=ambayo Waheshimiwa Wabunge wengi wameipigia kelele

Page 93: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

humu ndani ya kuongezwa kwenye mafuta ili kwambatuweze kumtua mama wa Kitanzania ndoo kichwani. Badonaendelea kuililia na kuiomba Serikali yangu itazame hili kwajicho la tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, akinamama wengi ambaoni wazalishaji na wachangiaji wa uchumi wa mapato yanchi hii, wanapoteza muda mwingi kwenye kutafuta maji.Tunaomba ile Sh.50/= iongezwe kwenye mafuta ili kwambatuweze kumtua mama ndoo kichwani. Wakati huo huo,Mkoa wa Manyara ni Mkoa wa wafugaji; tuna Kata kama zaNdedo kule Kiteto; kata nyingi tu za pale Kiteto, Simanjiro,Kata za Dongo, Kijungu, Lolera, Olboloti; Kata hizi hazinamaji kabisa ya bomba wala mabwawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba ikiwezekanawatu hawa wapate kuchimbiwa mabwawa. Juzi tulikuwana mafuriko ya kutosha hapa nchini. Naiomba Serikali yangukupitia hizi Halmashauri zetu, wahakikishe hawa watuwanachimbiwa mabwawa wakati ambapo mvuaimesimama kama hivi, ili nyakati za mvua tuweze ku-trackyale maji yaende kwenye hayo mabwawa kupunguza hiichangamoto ya maji. Mbona ni rahisi! Kwa hiyo, naombahasa maeneo ya Kiteto na Simanjiro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Wilaya ya Hanang’tunahitaji mabwawa pia, maana nako katika zile Kata tunawafugaji wengi tu. Tukiweza kuwawekea wafugaji hawa majikupitia mabwawa, wataacha kuhamahama, watakaakwenye maeneo yao, maana rasilimali za kutosha zitakuwepopale, maji pamoja na mambo mengine wanayoyahitaji.Naomba sana Mkoa wa Manyara ukumbukwe katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna matatizo yamawasiliano baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kiteto, tunashida katika Kata za Ndedo pamoja na Makame. Bado watuhawa wanaishi ile karne ya kupanda juu ya miti ili uwezekuzungumza na ndugu yako aliyeko upande mwingine. Kwahiyo, namwomba sana Waziri husika ama Mheshimiwa Waziri

Page 94: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

katika bajeti hii aikumbuke Wilaya ya Kiteto na maeneomengine mengi tu ya Mkoa wa Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze pia masualamazima ya mazingira ya ulipaji kodi. Naishauri sana TRA;naishauri Wizara ya Fedha waweze…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa. MheshimiwaKadutu atafuatiwa na Mheshimiwa Massare.

MHE. JOHN P. KADUTU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nikushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii kuchangiahoja iliyoko mbele yetu, hoja muhimu kwa maisha ya Serikaliyetu pamoja na wananchi wetu, wakati huutunapohangaika na maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nachukua fursa hiikuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziripamoja na timu ya uongozi wote wa Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko tofauti ya bajeti yamwaka unaokwisha na hii iliyoletwa mwaka 2016 na mwakahuu wa 2017 kuna tofauti kubwa, kuna maboresho, lakinibado yapo mambo ambayo tunapaswa kuyatilia mkazo ilimaisha ya wananchi wetu yaende vizuri na yawe bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo hudumatunazozingumzia hasa barabara. Toka mwaka 2016tumekuwa tunazungumzia barabara inayotoka Mpandakupitia Kaliua, Uliyankulu hadi Kahama. Barabara hii nimuhimu sana kwa sababu itakuwa inaunganisha mikoakaribu mitatu au minne.

Page 95: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama azma ya Serikali yetukuunganisha mikoa kwa lami, basi baada ya kipande chaChaya na Nyahuwa kupata pesa, basi naomba Wizara yaFedha na Wizara ya Ujenzi mwelekeze sasa nguvu zote kwenyebarabara hii inayotoka Mpanda kupitia Uliyankulu mpakaKahama. Ni kilomita 428 na nina imani wakipatiwaWakandarasi kama watatu, kazi inaweza kwenda vizuri,badala ya kila mwaka kuizungumza kwenye Ilani lakiniutekelezaji wake hakuna. Tunataka pia tupate performanceya utekelezaji wa mradi huu umefikia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo moja ambalotunalizungumza hapa, lakini Serikali bado inakuwa ipo kimya.Suala la Mfuko wa Maji; tumezungumza sana lakini Serikaliije basi na kauli, tunakubaliana au hatukubaliani? Maanaunapozungumza halafu mwenzako kakaa kimya, maanayake labda unachozungumza ni msamiati wa Kichina auKijapani, maneno ambayo ni michoro michoro ambayohuwezi kuielewa. Serikali i je hapa na majibu: Je,tumekubaliana juu ya mfuko wa maji? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu, tatizo la majivijijini ni kubwa kuliko tunavyodhani. Mpo wengine hapandani mkienda vijijini kwenu mnabeba maboksi ya maji.Hakuna mtu anayekwenda kunywa maji ya kij i j ini.Yawezekana mkaona hakuna haja kwa sababu huku ndanimjini mnaoga vizuri, mnakunywa vizuri, maji ya kupikiamazuri, hakuna anayejali. Kwa nini Serikali isije na majibu basi!Toka mwaka 2016 tunazungumzia Mfuko wa Maji, lakinitunaona kama vile mmeziba masikio. Njooni na ufumbuziwa tatizo la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi wiki nzima nilikuwaJimboni, kila eneo ukienda ni shida ya maji, lakini humuBungeni kila mmoja akiulizwa swali la maji, maswali yanyongeza Bunge zima linasimama, hata wewe Mwenyekitiunapata tabu sasa nani aulize na nani aache kuuliza? Hiyoni kuonesha ni jinsi gani ambavyo suala la maji lina umuhimu.(Makofi)

Page 96: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ukamilishaji wamradi wa umeme; tunakwenda tumeshaanzisha REA III.Naiomba sana Serikali, sasa tusiichie njiani, maana yakeshida ni kwamba watu wote tunaelekea kenye madini; wotemazungumzo yamekuwa ni madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kukamilisha REA IIIliende kweli likatatue matatizo yaishe. Siyo tena tujetuambiwe kuna REA IV na V. Itafika wakati hata pesahatutapeleka kwenye umeme, kwa sababu umemeutaonekana siyo tena jambo la umuhimu. Kwa hiyo, nashaurihilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala lingine juu ya sualala ujenzi wa Zahanati pamoja Vituo vya Afya. Jambo hilikama tunawaachia wananchi zaidi, hatuwezi kulikamilisha.Lazima Serikali ielekeze nguvu huko. Sasa tulisema kila Kataijenge Kituo cha Afya; mabadiliko yamekuja, kila Kata mbilizijenge Kituo cha Afya; tunaanzisha tena migogoro kituohicho kijengwe wapi? Kila Kata inapiga chepuo kujenga eneolake. Kwa hiyo, nadhani Serikali kwa makusudi kabisatuelekeze nguvu huko kwenye ujenzi wa Vituo vya Afyapamoja na Dispensary.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningumzie hili suala lamadini, migodi na kodi; mimi kabla ya kuingia hapa Bungeni,nimekuwa mfanyakazi huko kwenye migodi. Mwaka 2008wakati issue ya Buzwagi inaletwa hapa, mimi nilikuwamgodini. Sisi wafanyakazi wa kule tumekuwa tukipaza sautisana juu ya matatizo haya ya uibiwaji wa mali hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaziona ndege,tunasema, lakini watu walikuwa hawasikii. Tumezungumzasana juu ya mambo haya! Kule mgodini pia kuna mambo yaunyanyasaji, kuna ubaguzi mkubwa na hasa raia hawa waKizungu wanaotoka South Africa, wananyanyasa. Sasa wakatiwafanyakazi mgodini wanaponyanyaswa, wanapaza sautijuu ya wizi wa mali hii, lakini hakuna aliyesikia. Leo hatatukisema, hao wanaokuja kufanya kazi migodini, hawanaelimu.

Page 97: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule nimeshuhudia watuwana vyeti vya semina ya siku tatu; na wenzetu wapo makinisana. Ukipiga semina hata ya siku moja, unapata cheti.Ukipiga semina ya siku mbili, unapata cheti; ndizo CVwalizonazo. Ukienda Idara ya kazi, vibali vinatoka kila sikuwatu wafanye kazi, ambapo masharti yanataka mtu mwenyeelimu zaidi, lakini awe na mpango wa kufundisha wazawa.Hakuna anayejali. Watu wapo migodini wanakamatwa nabangi, wanafikishwa Mahakamani, lakini kesho yake mtu huyohuyo anaomba kibali anaruhusiwa kufanya kazi ndani yaardhi ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie ukwepaji kodi.Wote hapa akili sasa ipo kwenye Barrick na Acacia, lakinimigodini, Mheshimiwa Waziri wa Fedha anisikie vizuri, zipoKampuni nyingi zaidi kuliko kampuni tunayoizungumza, lakinihawa watu wanaiba, wanakwepa kodi kwa njia mbalimbali.Pesa zao wao wanalipana juu kwa juu, hakuna malipo yamoja kwa moja. Maana yake hata kodi haijulikani ni kiasigani. Hata mifuko ya jamii hii hawachangii, kwa sababu waowanarekodi mishahara midogo kuliko mishaharawanayolipwa kule nje. Mimi ni shahidi na niko tayari kuelezajinsi kodi inavyoibiwa kwa sababu nimekuwepo kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziriwa Fedha ajaribu kuangalia sana, tusijikite kwenye Kampunimoja tu kubwa, wakati mle mgodini kuna kampuni nyingizinafanya shughuli hiyo. Kwa hiyo, nashauri, kuchunguza kwamakini zaidi wizi au ukwepaji wa kodi wa kampuni zile ndogondogo ambazo zimepewa kazi na makampuni ya migodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la shilingi milioni50. Imekuwa ni msumari huu, kila ukizunguka kwenyemajimbo swali kubwa ni shilingi milioni 50, hatuna majibu!Serikali ije na majibu hapa. Siyo dhambi kusema kwambatumeahirisha au tutafanya mara nyingine. Tuondokane najambo hili au liletwe katika mpango mwingine kulikokung’anga’na tutatoa shilingi milioni 50; huu ni mwaka wapili sasa hatujatekeleza. Hatujafanya hata majaribio. (Makofi)

Page 98: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabla hatakengele haijanil i l ia kama kawaida yangu, fedha zamaendeleo zinazopelekwa kwenye Halmashauri zetu, hatamwaka 2016 nil isema, lazima tuhakikishe fedhazinazokwenda kwenye Halmashauri ziende kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama fedha…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. JOHN P. KADUTU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Massare na MheshimiwaMipata ajiandae.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami nichangie kwamuhtasari tu hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha naMipango Mheshimiwa Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongezasana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwana za dhati na za makusudi katika kuhakikisha nchi hii inafikiamalengo yake ya kujitegemea kama nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuomeona hotuba yaMheshimiwa Waziri wa Fedha ilivyoainisha na kuoneshamakusudio mazima na dhamira nzuri ya Serikali ya Awamuya Tano kwa kutaka kufanya nchi hii wananchi wakewaendelee kukiamini Chama kinachotawala sasa, Chamacha Mapinduzi kwa maana ya CCM. Ndiyo chama ambachohuwezi kuacha kuihusisha nchi hii na chama hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sanaMheshimiwa Waziri na timu yake ya Wizara ya Fedha kwa

Page 99: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

kuona na kutambua wananchi wanyonge ambao walikuwawananyanyasika kwa kusumbuliwa sana na hususan katikakodi mbalimbali hizi ndogo ndogo, ikiwemo ya kusafirishamazao kidogo chini ya tani moja, kutoka Halmashauri mojakwenda Halmashauri nyingine, lakini kutambua sekta isiyorasmi ya akinamama Lishe na wajasiriamali wadogo wadogoili nao wawe na mchango katika uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nianzekuishauri Serikali kidogo hasa katika kuhakikisha nchiinajitegemea katika suala zima la chakula. Ni vizuri sasatukaanza kufikiria na kuondokana na utegemezi huu wakil imo kinachotegemea mvua. Nchi hii tumekuwatunategemea sana kilimo kinachotegemea mvua. Skimu zaUmwagiliaji ziko kidogo sana na ziko maeneo ambayo yanauasilia wa mito labda na maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri sasa tukatengenezamiundombinu ya makusudi, yakiwemo mabwawa madogomadogo kwa maana ya malambo, kuhakikisha wananchisasa wanalima kilimo cha umwagiliaji kutokana na hali yahewa ambayo inabadilika badilika. Kumekuwa nachangamoto ya tabia ya nchi, wananchi wetu na maeneoyetu mengi, ikiwemo mwaka huu maeneo mengi ya hali yachakula siyo nzuri sana, ikiwemo Mikoa ya Kati, hata Mikoaya Kaskazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna haja ya juhudi zamakusudi za Serikali kuwekeza katika kilimo hiki chaumwagiliaji. Ni vizuri sasa na sisi tutoke tukajifunze kwabaadhi ya nchi zilizofanikiwa nchi ambazo zilikuwa maskiniwenzetu lakini sasa wametoka kabisa huku ambako tupo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kusaidia wakulima ambaondio wengi katika nchi hii, lazima tuhakikishe mbolea yetuinawekewa ruzuku. Kulikuwa na mpango hapa wa Waziriwa Kilimo aliyekuwa ametoka kwenye nafasi yake sasaamepewa Wizara nyingine ya kulinda watu wetu na malizao; ni kwamba kulikuwa na mpango wa kuhakikisha

Page 100: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

mbolea yote ambayo inaingia katika soko inawekewaruzuku. Hii itaondoa kufuatanafuatana; kazi kubwa itakuwaya kudhibiti kwamba hii mbolea sasa badala ya kutumikandani isitoke tu nje ya mipaka yetu, iuzwe kama bidhaanyingine ambazo mkulima anaweza kununua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuwe na ruzuku yambegu iwe wazi iingie masokoni ili mkulima akienda kwenyeduka, mbegu iwe tayari ina ruzuku. Kama Serikalihaitathubutu bado wakulima wa nchi hii wataendeleakusumbuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado nchi hii tuna tatizo lamaji. Naomba Serikali ifanye juhudi za makusudi mazimakuhakikisha upatikanaji wa maji vijijini. Tumediriki sana katikamiji yetu mingi, tumeona juhudi kubwa za Serikali kupitiaWizara ya Maji kuhakikisha miji inapata maji, lakini vijiji vingivina tatizo kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sasa Serikali ifikemahali ione na ichukue mawazo ya Waheshimiwa Wabunge.Wameongeza Sh.40/= katika kuhakikisha tunaziba mapengoambayo yatatokana na misamaha ambayo wametoa.Naomba basi iongezeke hata Sh.10/= tu ambayo itasaidiakuongeza katika Mfuko wa Maji ili miaka hii iliyobaki tuwezekutekeleza vizuri ilani ya chama chetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina dhamira njemaya kuunganisha Mikoa yote kwa lami, ukiwemo Mkoa waSingida ambao natoka mimi. Tuna nia ya kuunganisha Mkoawa Singida na Mbeya, kunabaki kilomita 413. Kilomita hizi ninyingi. Naishukuru Serikali kwa kuanza kutaka kujenga sasakilomita 56.9 kutoka Mkiwa, Itigi hadi Noranga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwakumbusheWaheshimiwa Mawaziri wa Wizara hii ya Ujenzi, kwambaukijenga kilomita 57 hizi takriban, bado utakuwa umebakizakilomita 300 na zaidi. Ikiwezekana, ni vizuri basi speedikaongezeka, lakini Waziri wa Fedha aone, awasaidie. UleMradi Mkandarasi hadi sasa hajafika, hatumjui mpaka sasa

Page 101: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

hivi, lakini tunaambiwa tunajengewa kilomita 56.9 takribankilomita 57.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuunganisha Mkoa waSingida na Mkoa wa Simiyu kupitia daraja la Simbiti ni jamboambalo tunataka tuone sasa wananchi wa Mikoa hiiwanasafiri lakini wanapita katika barabara kama wenzaowanaotoka maeneo mengine. Napongeza kwa sasakumalizia kipande cha barabara ya kutoka pale Chayampakani kwenye Mkoa wa Tabora maeneo ya Nyahuwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naipongeze Serikali piakwa kusimamia kutaka kujenga reli hii ya Kati, kutoka Dar esSalaam hadi Morogoro, lakini dhamira ni kufika Makutuporakatika Mkoa wetu wa Singida. Vile vile kuna reli hii ya Katiambayo ni kutoka Dar es Salaam, Kigoma na Mwanza, inatawi lililoanzishwa na Mheshimiwa Mwalimu Nyerere Rais waAwamu ya Kwanza, Baba wa Taifa hili kutoka Manyonikwenda Singida, haizungumzwi hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli hii ilikuwa na msaadamkubwa katika uchumi wa nchi hii. Sisi ni wakulima nakulikuwa na mashamba ya NAFCO. Kule Basutu yalikuwayakipita pale inarahisisha kufika kwa walaji wengi ambao nimiji mikubwa lakini kwenye viwanda kule Dar es Salaam. Nivizuri sasa mkaanza kufikiria reli hii ya Manyoni – Singida nayoiwe katika kiwango kizuri; lakini wameanza kung’oa hadimataruma. Sasa sijui uwekezaji ule nchi inaenda namna gani?Naiomba Serikali iangalie kipande hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie kidogokuhusu suala zima la hifadhi ya chakula. NFRA wametengewahela mwaka huu, lakini hapa nyuma tumeshuhudia maeneomengi yanapata upungufu wa chakula lakini msaada nanamna ya kuwahami wananchi wetu unachelewa sana. Leohii tumeanza kutoa eti chakula cha bei nafuu wakati tayariwatu wameshavuna. Naiomba Serikali kwa makusudimazima, panapokuwa na upungufu wa chakula, basi

Page 102: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

zichukuliwe hatua za makusudi kusaidia watu wetu wawezekulima na kurudi tena mwaka mwingine usiwe na njaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anapokutana na haliya uhaba wa chakula, hawezi hata kufanya kazi zake za kilasiku. Kwa hiyo, tunatengeneza mazingira ya janga kubwazaidi kama hatutaweza kutumia akiba ya chakula ya Taifakuwanusuru wananchi wanaokutana na tatizo hili. Hiiimetokea sana miaka hii miwili ambapo nami nimeonanikiwa Mbunge kwamba hazichukuliwi hatua za haraka,wanaposaidia wananchi, wanapewa chakula kile wakatitayari wameshaumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nataka nisemeekuhusu ujenzi wa Zahanati kila kijiji na ujenzi wa Kituo chaAfya kila Kata; ni ahadi yetu ya uchaguzi. Sasa sijui tukiruditutakuja kusema nini? Naomba sasa juhudi za makusudiangalau tufikie nusu ya yale ambayo tuliahidi.

(Hapa kengele ilia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mipata na MheshimiwaYussuf Kaiza Makame, ajiandae.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi. Niungane na wenzangukumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia uzima, lakini pianimpongeze Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Wazirikwa kuja na hotuba nzuri sana. Hotuba hii ni nzuri sana, tofautina wenzangu wanaosema ina matatizo. Mimi niko hapaBungeni kwa muda wa kutosha, miaka sita, nasema hotubahii ni nzuri sana.

Page 103: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea,nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanyiaTanzania. Rais huyu ni wa pekee! Waswahili wanasema, “Kilazama na kitabu chake.” Kitabu cha Mheshimiwa Rais Magufulikitaandikwa kwa wino wa dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utendaji huu ni message kwawanasiasa wengine wanaotafuta nafasi kama ya kwake.Una kiatu cha kujaa hapo? Una mguu? Kiatu chakokinatosha? Mguu wako unatosha hicho kiatu? Ni messagekwa Watendaji Serikalini, huyu Rais anataka Watendaji wanamna gani kwenye Serikali yake? Ni message kwa wananchiwote. Tumuunge mkono kwa sababu dhamira yakeameiweka wazi, ni ya kizalendo kupita kiasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ni message kwa nchinyingine kwamba Tanzania kuna viongozi wana macho nawanajua kulinda nchi yao. Nampongeza sana MheshimiwaRais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye bajeti. Bajeti hiini nzuri, imekonga mioyo ya Watanzania wengi. Imefuta adaya motor vehicle licence, imepunguza ushuru wa mazao yabiashara kwa wakulima wadogo wadogo nawafanyabiashara wadogo wadogo ambao mara nyingiwako kwenye wigo wa gunia 10 hizo hizo. Imemfanyamkulima sasa ajisikie kwamba kile anacholima kina thamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri pia tuone kwenyeushuru kama dagaa na samaki na zenyewe tunaziachaje?Isiwe kimya namna hii, ili kama ni ushuru, basi tuwapunguziewale wafanyabiashara wa samaki na dagaa katika kiwangokidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii inaenda kutekelezaahadi za Mheshimiwa Rais alizoziweka. Tena aliweka ahadiya kwanza kabisa kwamba anataka nchi yetu iende kwenyeuchumi wa kati. Bajeti hii imeweka mipango mizuri kabisaya kuboresha ujenzi wa barabara zetu, ujenzi wa reli katikastandard gauge, ujenzi wa mifumo ya usafiri wa anga, majini

Page 104: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

lakini vile vile mfumo wa uendelezaji umeme ambao nimuhimu sana katika uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoweza kushauri nikwamba utendaji lazima uwe makini; tutumie fursatulizonazo hasa za kijiografia kuhakikisha kwamba hayamazingira tunayoyaweka tunafanya uzalishaji mzuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Mkoa wetu waRukwa ni wa kilimo. Leo hii hali ya hewa ni nzuri sana Mkoawa Rukwa, lakini bado kilimo siyo kizuri sana vile tunavyotaka.Bado hatujaingia kwenye kilimo cha kutumia matrekta, kilimocha kibiashara ambacho kinaweza kikatukomboa na lazimawatumishi waangalie, Mawaziri mjue kwamba kilimokinabeba watu wengi; kinaajiri watu wengi. Ukiimarishakilimo, kwa vyovyote vile unakuwa na wigo mpana wakubadilisha uchumi wa nchi na kusaidia watu wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba bajeti hii ambayonaiunga sana mkono inisaidie mambo yafuatayo katikaJimbo langu. Vipo vijiji ambavyo vilisahaulika kupelekewaumeme na sikuviona kwenye orodha na niliweza kupatanafasi ya kumwona Mheshimiwa Waziri lakini na MtendajiMkuu wa REA. Vijiji hivi ni vijiji vya Katani, Malongwe, Nkana,Sintali, Ifundwa, Nkomachindo na Nchenje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba umeme pia uendeKata ya Ninde iliyo na vijiji saba; Kata ya Kala ina vijiji saba,Kata ya Wampembe ambayo Waziri alitembelea mwenyeweina vijiji vitano na hawa ni wavuvi wamekuwa wakivuasamaki zao wanapeleka Zambia. Akiwapelekea umemehawa amewakomboa na bajeti hii ni ya ukombozi. Kwa hiyo,naomba umeme ufike katika Kata hizi za mwambao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia bajetininayoiunga mkono sana iniunge mkono katika juhudi ya majikatika Jimbo langu la Nkasi Kusini. Tuna tatizo la maji katikaKata ya Nkhandasi ambayo ina Vijiji vya Kasu, Milundikwa,Malongwe, Katani na Kisula. Vijiji hivi vimekuwa na shida yamaji muda mrefu sana na juzi tumehamisha Shule ya

Page 105: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Milundikwa tukapeleka kwenye Kata hii hapa. Kwa hiyo,naomba…

TAARIFA

MHE. KANGI A. N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. KANGI A. N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa mchangiaji kwamba miongoni mwavijiji ambavyo vina kero kubwa ya maji katika Jimbo lake nipamoja na Chonga, Katani, Talatila pamoja na Miyula. Kwahiyo, nataka tu nimpe hiyo taarifa mchangiaji anayeongea.

MWENYEKITI: Mchangiaji, taarifa!

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naikubali sana taarifa yake na nilikuwa naendelea huko. Kwahiyo, Vijiji vya Chonga, Makupa, Talatila na Miyula vina shidakubwa ya maji na ina mitambo na mtandao wa maji unafikapale. Kwa hiyo, ni suala la kufufua na kuanzisha. Namshukurusana Mheshimiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado ipo miradi ya majikatika Vijiji vya Nkundi na Kalundi. Vijiji hivi vina bwawa laKawa ambalo tumekuwa tukilizungumza muda mrefu. Hatuazake ni nzuri, naomba Serikali ikamilishe ili wananchi wawezekupata matunda ya jasho la Serikali yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi mwingine ni mradi wamaji wa Zuma, Isale ambao utahudumia vijiji vya Ntemba,Kitosi na Ntuhuchi. Mradi huu uko katika hatua za mwanzo.Naomba Watendaji waharakishe il i pesa ambazotulitengewa kwenye bajeti ya mwaka 2016 zisirudi kwa sababuzipo za kutekeleza mradi huu. Kwa taarifa nilizozipata sasahivi, karibu utekelezaji uanze.

Page 106: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, bajeti hii inisaidiekutenga pesa kwa ajili ya Vituo vya Afya. Kipo Kituo cha Afyacha Kandasi, wananchi wameamua kujenga wenyewe,tunachohitaji hapa ni nguvu za Serikali, mtusaide. Kipo Kituocha Afya cha King’ombe, Kata ya Kala. Kata ya Kala iko naumbali wa zaidi ya kilometa 150 kutoka Makao Makuu yaWilaya. Akinamama na Watoto wamepoteza maisha yaokwa sababu ya umbali wa barabara isiyofikika. Bajeti hiininayoiunga mkono leo ikawe mkombozi kwa vifo vyaakinamama na watoto kutoka Kata ya Kala na Kituo chaAfya cha King’ombe kiweze kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia Kituo cha Afyakijengwe Kate na Ninde na wananchi tumewahimiza nawako na utayari wa kutosha katika kuanza kujenga majengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ninayoiungamkono, naomba ikawe mkombozi wa kuleta uchumi kwawafanyabiashara wadogo waliotambuliwa leo,wasinyanyaswe tena ili pamoja na kutambuliwa kwao, basiSerikali ione namna ambavyo inaweza ikatumia vyombovya fedha kuwasaidia watu hawa kwa kutoa mikopomidogo midogo ili waweze kupata mitaji na kuchangiakatika uchumi wa Taifa pamoja na uchumi wa familia zao.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini nimiongoni mwa Jimbo ambalo liko kwenye maeneo ambayoyana changamoto nyingi. Zipo barabara za Kitosi -Wampembe; barabara ya Kana - Kala; na barabara yaNamanyere – Ninde. Barabara hizi zimekuwa na changamotokubwa sana, ukiziachia Halmashauri peke yake haiwezikumudu kuwasaidia wananchi. Nomba bajeti hii ninayoiungamkono sana, mtutengee pesa pia ya kuweza kuhakikishakwamba barabara zetu zinapitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii naomba itusaidiepia kuhakikisha kwamba mazao ambayo tumelima sisi watuwa Rukwa yanapata ununuzi kwa bei nzuri kidogo. Sasa hivibei siyo nzuri sana, lakini gharama ya uzalishaji imekuwa

Page 107: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

kubwa. Mkipandisha bei mnatusaidia zaidi katika kuwekabei elekezi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Yussuf Makame.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naunga mkono hoja yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusiana na hili jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nataka niweke sawarecord au Hansard kwamba wakati jana Mheshimiwa AliSalim akichangia, alipewa taarifa na Mbunge mmojakwamba kwenye Taifa hili haikumbukwi Tanganyika. Hili nijambo la upotoshaji na tunajua kwamba Muungano wetuhuu ni wa Watanganyika na Wazanzibari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Tanganyika ipo.Hapa pia tukiwa Bungeni tunasema kuna mambo ambayosiyo ya Muungano. Hayo siyo mambo ya sehemu nyingine, nimambo ya Tanganyika na hakuna jambo ambalo ni laTanzania Bara. Hakuna Taifa lililozaliwa Tanzania Bara nahakuna uhuru tunaousherehekea ukawa wa Tanzania Bara,ni uhuru wa Tanganyika. Kwa hiyo, naomba tuweke recordsawa katika hili. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Kweli kabisa.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, la pili ambalo nilitaka niliseme leo hii ni hili sualala mchanga. Suala la mchanga kidogo limetutoa kwenyeajenda kuu ya bajeti kwa Bunge zima. Sizungumzii Wapinzaniwala sizungumzii watawala; nasema kwamba limetutoa napengine ni mkakati maalum, uliotengenezwa ututoe katikaajenda ya msingi ya bajeti. Watu wengi kwa asilimia 70 bajetihii, wanazungumzia makinikia ya mchanga, hawazungumziibajeti. (Makofi)

Page 108: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema kwenye kuchangiahotuba ya Wizara ya Nishati na Madini na nasema tena.Katika jambo ambalo linahitaji mshikamano na umoja waKitaifa ni hili, lakini mshikamano huo hauwezi kupatikana kwamaneno tu, tunahitaji kubadilisha sheria zetu na ikibidi twendejuu zaidi kwenye Katiba yetu ya nchi kufanyia yalemapendekezo yaliyoletwa na Tume ya Jaji Warioba, yaletwetena basi tuyapitie na tupitishe Katiba mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili mnadhani kanakwamba linaongelewa kijuujuu. Kama neno alilolitumiaMheshimiwa Bilago, kama kuna watu wanaoenda namaandamano ya mioyo ni Wazanzibari. Suala la Muunganosiyo suala la mchezo mchezo la kuangaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumziamikataba ya madini na tunazungumzia tume zilizoundwa.Leo tumempongeza Mheshimiwa Rais lakini tume zilizoundwakuangalia masuala ya madini ni nyingi na findings zakezilisomwa, lakini utekelezaji wake haukufanyika. LeoMheshimiwa Rais kaja, kazungumza aliyoyazungumza, kawana ujasiri kafanya alichokifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mungu katika Taifahili kwamba aje Mheshimiwa Rais azione tume zilizopitiamasuala ya Muungano au jambo hili la Muungano namapendekezo yao, aje aseme kwamba sasa ipo haja yakuunda Serikali tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu jambo hili lipona tume zote zaidi ya nane zilizoundwa kwenye nchi hii tokakipindi cha Mwalimu Nyerere mpaka leo zote zimependekezaSerikali tatu. Leo tukizungumzia suala la Muungano humundani ni kana kwamba unazungumzia kitu cha ajabu. Wapowaliozungumzia madini tunayoibiwa mkawaona wa ajabu;leo ndiyo mnaona hili jambo ni jema zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la utawala wa sheria,haki na demokrasia; hatuwezi kuendesha bajeti zetu hizikama hakuna haki, hakuna demokrasia ya kweli katika nchi

Page 109: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

yetu. Hili jambo mnaweza mkaliona nila mchezo mchezosana. Leo Babu Ally anaendesha Serikali Zanzibar, lakiniamewakosesha Watanzania walio wengi ….(Maneno HayaSiyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge)

MBUNGE FULANI: Babu Ally gani?

MBUNGE FULANI: Shein.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, wamekosa maji, wamekosa umeme, wamekosana huduma nyingine muhimu kutoka misaada ya nje……(Kicheko)

TAARIFA

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa!(Kicheko)

MWENYEKITI: Taarifa.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpetaarifa mzungumzaji ambaye anazunguza, Zanzibar hakunamtu anaitwa Babu Ali na Zanzibar kuna Rais wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar ambaye anaitwa Dkt. Ali MohamedShein, ni Rais halali na yuko Kikatiba halali na amechaguliwakihalali. Kwa hiyo, nimpe taarifa ndugu yangu aweke manenoyake sawa, afahamu kama Zanzibar kuna Rais makiniambaye amechaguliwa kihalali. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Yussuf, hebu kaa kwanza.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru...

MWENYEKITI: Mheshimiwa, kaa kwanza!

Waheshimiwa Wabunge, nafikiri humu ndani kunawatu ni viongozi. Ninyi ni viongozi, wote sisi ni viongozi. Tunaviapo ndani ya Bunge ambavyo tumekula. Majina ya kuitana

Page 110: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

mitaani siyo humu ndani. Sasa nakuomba futa jina hilo laBabu Ally na utam-address Rais wa Zanzibar kwa jina lakesahihi.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, kwa heshima ya Kiti chako mimi sina shida yakufuta. Nimefuta hilo neno…

MWENYEKITI: Siyo shida, nakupa amri ufute. (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Safi.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: MheshimiwaMwenyekiti, nimefuta hayo maneno. Nasema kwambautawala wa sheria ambao unafuata haki na demokrasia,sawa sawa! Hapa tunachokizungumza hasa ni uchaguzi ulewa Zanzibar; na hapa mimi sizungumzii nini kinachoendeleaZanzibar, nazungumzia impact ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano kutokana na uchaguzi wa Zanzibar kwakulazimisha viongozi ambao hawakuchaguliwa nawananchi kukaa katika madaraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania sasa hivi nikaribu milioni 50. Sisi Wazanzibari hatufaidiki na REA, lakiniwanaoathirika ni Majimbo yenu hayo mnayopigia kelele. Kwahiyo, ili utekelezaji wa bajeti uende vizuri, ni lazima Serikaliikubali utawala wa sheria, haki na demokrasia katika nchiyetu kwa sababu tumekubali mfumo wa vyama vingi vyasiasa nchini. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mfuko wa UKIMWI;ninachotaka kuzungumza hapa kuna Watanzania wenzetuwanaoishi na virusi vya UKIMWI, wengi sana. Donorswamejitoa au wengi wamejitoa kutoa misaada katikamasuala haya ya UKIMWI. Pengine huko tunakoenda haliitakuwa mbaya zaidi. Sasa ninachotaka kushauri kwa Serikalihii, tuwa-serve Watanzania wenzetu kwa pesa zetu za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetengeneza percent yakuingia kwenye REA, basi tutengeneze percent ya kuingia

Page 111: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

kwenye mfuko wa UKIMWI kwa ajil i ya kuwa-serveWatanzania wenzetu wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Mfano,tumeweka tozo ya Sh.40/= kwa kila lita ya mafuta, tunawezaaidha, kupandisha ikawa Sh.42/= ama kwa hiyo hiyoiliyowekwa tukaweka Sh.2/= kwa kila lita ikaingia kwenyeMfuko wa UKIMWI ili waweze kujiendesha wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wa Zimbabwetumeambiwa hawategemei misaada kwenye suala hili.Kwenye suala la UKIMWI Wazimbabwe pamoja na kasorozao walizonazo, suala la UKIMWI wanategemea fedha zaoza ndani. Kwa hiyo, nasi tujitathmini katika hili, linapotezanguvu kazi kubwa ya Taifa. Kwa hiyo, tuweke tozo japo yaSh.2/= kwenye lita ya mafuta ama kwenye bia. Kwenye biatumeongeza Sh.765/= kutoka Sh.729/=. Sasa hapa kwenyeSh.765/= tunaweza tukatoa Sh.5/= tukaingiza moja kwa mojakwenye Mfuko wa UKIMWI kwa ajili ya kwenda ku-serveWatanzania wenzetu. Hii itaenda na yale malengo yakwamba 2030 UKIMWI uwe haupo tena Tanzania au katikadunia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la ajirakwa vijana, bajeti hii haikuzungumza kabisa suala la ajira naSerikali hii haijazungumza kabisa toka iingie madarakani sualala ajira. Wanafunzi wanaomaliza vyuo ni numbers...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namwita MheshimiwaPascal Haonga.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kabla sijaanza kuchangia naomba nimshauri MheshimiwaRais kwamba afanye uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madinipamoja na hii nafasi ya Mheshimiwa Dkt. Possi, kwa sababunimeona kuna baadhi ya Wabunge wa Chama chaMapinduzi wanashindana kutafuta nafasi hizo kwakushambulia upande huu. Kwa hiyo, naomba niseme tukwamba afanye uteuzi huo haraka... (Makofi)

Page 112: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

MWENYEKITI: Wewe changia Bajeti, acha hayamambo! (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Wewe Haonga (Kicheko/Makofi)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,baada ya ushauri huo, naomba niendelee sasa kuchangiabajeti ambayo iko mbele yetu. Naomba niseme tu kwambakatika bajeti hii, yako baadhi ya mambo ambayo nimeyaonakwa kweli hayatawasaidia Watanzania, naona tunaendakuwaongezea Watanzania mzigo wa umaskini. Kwa mfano,liko jambo hili la ada ya leseni ya magari. Ada ya leseni yamagari kwenda kuihamisha kupeleka kwa wale watuwanaotumia mafuta ya taa, kupeleka kwa wanaotumiapetrol na diesel, hapa hatujatatua tatizo tumeruka majivuna kukanyaga moto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme tu kwambaWatanzania walio wengi wanaoishi mijini na vij i j ini,wanatumia mafuta ya taa na ndio wengi hao maskini. Leotumeamua kuwatwisha magunia ya mawe kwakuwaongezea bei kwenye nishati hii ya mafuta ya taa.Umeme mmewanyima, hali ni mbaya kweli kweli! Hali ningumu huko vijijini, lakini leo unaenda kumpandishia Sh.40/= kwenye mafuta ya taa. Hii siyo sahihi hata kidogo! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii alipokuwaanaingia madarakani Mheshimiwa Rais alisema kwamba yeyeanawaonea huruma maskini. Alizungumza akasema yeye nirafiki wa maskini. Sasa urafiki na maskini, huyu unayemtwishamzigo huu wa kumwongezea Sh.40/= kwenye mafuta ya taa,ni masikini wa namna gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake ni nini? Tafsiri nikwamba leo Tanzania wanaotumia magari hata asilimia 20hawafiki. Unachukua asilimia 20 ya Watanzania wanaotumiamagari unaenda kuwatwisha mzigo Watanzania zaidi yaasilimia 80 ambao hawana magari eti walipie hii motorvehicle. Hii siyo sahihi hata kidogo.

Page 113: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu niwaambieWatanzania, najua tu japokuwa hawanisikilizi, lakini najuatu watasikia hata kwa njia nyingine, kwamba ile Serikali yaAwamu ya Tano waliyotegemea kwamba ingewezakuwasaidia sasa imeshawasaliti haina msaada tena kwaona hapo waangalie mbadala mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni jambo laushuru wa Sh.10,000/= kwa nyumba ambazo hazifanyiwauthamini. Yaani leo Watanzania walio wengi wanaoishikwenye nyumba ambazo siyo bora, ukienda Mkoa huu waDodoma, ukienda huko Mtera kwa Mheshimiwa Lusinde,ukienda huko Chemba na maeneo mengine; na mikoamingine; nimetoa mfano Dodoma tu, lakini yako na maeneomengine pia, utakuta nyumba ni ya nyasi, juu wamewekaudongo, wamejengea miti, leo huyu mwananchi etiunamwambia eti akatoe Sh.10,000/=, kwa kweli naombatafadhali atakapokuwa anahitimisha, Mheshimiwa Wazirinaomba mwombe Watanzania msamaha kwambatulikosea, tuliteleza kidogo tulikuwa hatumaanishi hivyo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo unaposema walipeSh.10,000/= kwa kila nyumba, ni kuwatwisha mzigo mzito sanamaskini hawa. Hofu yangu kubwa sana ni kwamba ipo sikututaambiwa tuanze kulipia pumzi tunayoivuta. Kama leomnasema tuanze kulipia vibanda vyetu vidogo vidogoambavyo tunavyo, leo vifaa vya ujenzi ni gharama, kila kituni gharama, lakini wanaopata shida zaidi ni watu maskinizaidi hawa wa vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali naomba kamamimi labda sikuelewa vizuri, naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja kuhitimisha, atoe tamko kwambahatukumaanisha tuichokiandika hapa, au wafute kabisa hikikitu, kwa kweli watakuwa wamefanya jambo baya sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala laukuaji wa uchumi usiopunguza umaskini. Leo tunasema

Page 114: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

kwamba uchumi wa Taifa letu unakuwa kwa asilimia saba.Uchumi huu ambao tunasema unakuwa kwa asilimia saba,lakini uchumi huu haupunguzi umaskini wa Watanzania wetu.Ni kwa nini uchumi haupunguzi umaskini wa Watanzania?Uchumi umebaki kukua kwenye makaratasi kwa sababusekta ambazo zinachangia katika ukuaji wa uchumi ni sektazile za utalii, sekta za mawasiliano, madini na fedha. Kwahiyo, sekta hizi haziwagusi Watanzania walio wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungekuza uchumi wetukupitia kilimo, naamini Watanzania wengi tungekuwatumewasaidia kwa kiasi kikubwa sana. Mheshimiwa Wazirininakuomba hii hotuba ya Upinzani tafadhali naomba uisomevizuri. Siku za nyuma mlikuwa mnasema hawa Wapinzaniwanakuja na vihotuba vyao vidogo vidogo, makaratasimawili, matatu; wengine wakaiita toilet paper, wenginewakafanya mambo ya ajabu ajabu; leo tumekuja na hii bajetiya Upinzani mbadala. Mnasema mbona mmeweka kubwasana? Mnaandika thesis, sijui mnafanya nini? Ninyi watuhamwaminiki! Naomba Waziri tafadhali, tumia hii hotubaya Upinzani, hii ina vitu vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamechukua takwimu; kwamfano takwimu zile za utafiti uliofanywa na REPOA. Ule utafitiunasema kwamba tukikuza kilimo kuanzia asilimia nane hadikumi tutakuwa tumekata umaskini kwa asilimia 50 ndani yamiaka mitatu. Yaani ndani ya miaka mitatu tukikuza Sektaya Kilimo kwa asilimia nane hadi asilimia kumi, ndani yamiaka mitatu tutakuwa tumeondoa umaskini kwa Tanzaniazaidi ya asilimia 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli Serikali hii inania njema naomba tafadhali chukueni bajeti hii ya Upinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, naombakwa kuwa kuna watu wamezungumza, nami naombanichangie kidogo kuhusu suala hili la makinikia suala lamadini. Naomba tujiulize adui yetu ni nani? Adui yetu nimwekezaji? Adui yetu ni sheria zetu? Adui yetu ni nani?

Page 115: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

MBUNGE FULANI: Wewe hapo!

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,adui yetu ni sheria tulizozitunga; Sheria za Madini na Sheriaza raslimali zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui namba mbili ni yulealiyetunga sheria hizi ambaye ni Serikali yetu hii ya Chamacha Mapinduzi. Hii ndiyo iliyotunga sheria hizi. Huyu ndiyo adui.Leo ziko sheria mbalimbali na kuna watu hawasomi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwambakuna watu ambao hawasomi. Ziko Sheria za Madini; ninayoSheria ya Madini hapa ya mwaka 1997. Mwaka 1997 kulikuwana sheria mbili ambazo zilifanyiwa marekebisho. Iko Sheriaya mwaka 1997 ya Madini ambayo ni ya Uwekezaji kwenyeMadini, lakini kuna Sheria nyingine ya Madini ya mwaka 1997ambayo hii Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali zaFedha ambayo ilifuta kodi kwa wawekezaji wa madini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Serikali imeamua kufutakodi kwa wawekezaji wa madini inawatwisha mzigoWatanzania maskini. Hii siyo sahihi kabisa. Leo madini yetutunapata mrabaha wa asilimia nne, kuna watu walishangiliaSheria hizi mbaya zinapotungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa hata kuonaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walealiowaita wezi, anawaita Ikulu, anasema hawa jamaa nijasiri sana. Leo wale wezi wamekuwa jasiri, anasema niwanaume, lakini kuna wenzetu Wabunge wako humu ndaniakina Mheshimiwa Ngeleja na wengine akina Chenge nawengine amesema wasisafiri, hawa watu wamezuiliwapassport zao kusafiri. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Ulikuwepo!

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,leo anakuja mtu ambaye ulisema ni mwizi, unasema ni

Page 116: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

mwanaume. Kumbe ukiliibia Taifa hili kama wewe niMwekezaji kutoka nje wewe ni mwanaume. Naomba nisemetu kwamba...

TAARIFA

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nataka kumpa taarifa mzungumzaji kwambaMheshimiwa Rais Magufuli hakumwita Mwenye Barrick baadaya Rais kushikilia utaratibu, wao wamekuja kukaa mezanikuzungumza na ndiyo ilikuwa concern ya Tanzania. Kwa hiyo,nampa taarifa kwamba Mheshimiwa Rais hakumwitaMwekezaji. (Makofi)

MWENYEKITI: Taarifa hiyo na ndiyo sahihi.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niseme tu kwamba huyu bwana nadhani maranyingi sana vyombo vya habari hafuatilii; taarifa ya habarihasikilizi, magazeti hasomi, WhatsApp haangalii. Kwa hiyo,naikataa taarifa yake ambayo ni ya kijinga kabisa na yakitoto. Siwezi kuipokea taarifa kama hiyo. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme tu kwambanchi yetu ilipofika...

MWENYEKITI: Mheshimiwa hebu subiri. Chief Whip!

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NAUFUNDI (KAIMU MNADHIMU MKUU): Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa mujibu wa Kanuni ya 64, naomba tu nimfahamisheMheshimiwa Mbunge kuendelea lugha ya staha. Hiyo nipamoja na masuala anayomzungumzia Mheshimiwa Raiskwa misingi ifuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Tanzania ni kuonakwaba rasilimali ambazo tumezipoteza kwa kipindi hichotunazipata. Hiyo ndiyo iwe spirit yetu kuwa–encourage wale

Page 117: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

waweze kukubali na kutupa rasilimali iliyokuwa imepotea.Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge achangie lakini kwakweli awe na staha, tuheshimiane na asitumie maneno kamahayo “kijinga” na vitu gani, siyo lugha sahihi. (Makofi)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,hivi leo, naomba niseme...

MWENYEKITI: Subiri kwanza.

Waheshimiwa Wabunge, sishangai, mimi ndiyo Kiti.Mimi nasimama, nakaa ninapopenda. (Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Rais aliwekawazi kabisa wale wote waliohusika waje wakubali wenyewena biashara. Sikilizeni, subirini. Nawe Ruge umeanza? Mamausifuate mkumbo, Bunge gumu hili! Unaweza ukakaa mwezimmoja ukaondoka hapa. (Kicheko/Makofi)

Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais alitoa kauli, watu wotewanaohusika ambao wanaona wamefanya makosa, wajewaungame. Aliyekuja sio mtu wa Acacia, ni mtu wa Barrickambaye ndiye majority shareholders wa hiyo kampuni.Msinijibu kitu, kaeni kimya, tulieni kimya hapo.

Jana nilitoa tangazo hapa, kama kuna mtu anamatatizo ya ugonjwa wa kusikia, wako Wauguzi palewanapima masikio. Nendeni mkatibiwe, pande zote siyoupande huu tu, pande zote nendeni mkatibiwe ili msikie vizuri.

Endelea sasa Mheshimiwa Pascal . (Makofi/Kicheko)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nasikitika kwamba Mwenyekiti wangu hata wewe hujuikwamba Barrick ndiyo hawa wana hisa zaidi ya asilimia 60kwenye Acacia. Nasikitika kwamba hata hili pia hulifahamu.Sasa kama kuna mtu...

MWENYEKITI: Ndiyo maana nikasema kama watuwana matatizo ya masikio, nimesema Barrick ndiyo

Page 118: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

shareholders; Acacia ni minority ndani ya Barrick. Sasanakushauri baadaye upitie kule Dispensary kidogoukajitizame. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Hao ndiyo Walimu wetuTanzania. Hao ndiyo Walimu wetu hao!

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba pia tujaribu kupitia Dispensary wote hata ambaohawajui kwamba Acacia na Barrick wame-share hisa.Naomba niendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hili nil iacheniendelee sasa kwenye mambo mengine.

MBUNGE FULANI: Wewe hujui!

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,wako Watanzania wengi waliofungwa kwa kuiba kuku,ng’ombe na vitu vingine, tukawaite wale tufanye naonegotiation pia basi. Tuwaite Watanzania walioba tufanyenao negotiation. Kama tunasema huyu ni mwizi ,tukaemezani tufanye negotiation, tuwachukue na walioiba nawengine. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tu,kwamba haya mambo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Haya, muda wako umekwisha,nakuongezea sekunde 30.

(Hapa Waheshimiwa Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mnaona! Namwongezea muda,mnapiga makelele. Ndiyo maana nimewaambia mkatibiwejamani! Nakuongezea muda sekunde 30. (Kicheko)

Page 119: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nizungumze suala la mwisho; hilo la madini nadhanina wengine pia wamezungumza nitazungumza baadaye.Niseme tu kwamba kwa kweli bajeti hii imewasahauwafanyakazi wa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri waUtumishi alisema kwamba mwaka huu anaajiri 56,000 lakinihatujaambiwa tarehe ya kuajiri ni lini? Nataka niseme tukwamba msaliti namba moja wa Watumishi wa Umma niMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu ndio mtumishi namba moja. (Makofi) [Maneno HayaSiyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, akiwa Mtumishi nambamoja, leo hajaajiri, watu wamehitimu vyuo, hawaajiri kwanini?

MWENYEKITI: Hebu kaa chini Mheshimiwa Pascal.Mheshimiwa Pascal, jamani hebu tufuate hizi Kanuni.Sikuombi, nakuagiza, futa hilo neno msaliti namba moja sasahivi. Sasa hivi futa hilo neno. (Makofi)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niseme nimefuta hii, lakini niseme amewasahauWatumishi hajawaajiri. Nimefuta hii kauli ya... (Makofi)

MWENYEKITI: Futa, kaa chini. Umeshafuta kaa chinina muda wako umekwisha. (Kicheko/Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, jioni tutakaporudi saa 10.00,mchangiaji wetu wa kwanza atakuwa ni Mheshimiwa WilfredLwakatare, Gibson Meiseyeki, Salum Rehani na MashimbaNdaki.

Nasitisha shughuli za Bunge mpaka saa 10.00 jioni.

(Saa 7.00 mchana Bunge lilisitishwa hadi saa 10.00 jioni)

Page 120: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

(Saa 10.00 Jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae.Tunaanza na majina tuliyoyatangaza asubuhi, MheshimiwaWilfred Lwakatare, atafuatiwa na Mheshimiwa GibsonMeiseyeki, wajiandae Mheshimiwa Salum Rehani naMashimba Ndaki. Mheshimiwa Lwakatare.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Nianze kwa kuipongezahotuba iliyowasilishwa na Kambi ya Upinzani hapa Bungeni.Kwa bahati mbaya Mheshimiwa Waziri hata leo hayupo nawakati hotuba ile inawasilishwa hakuwepo lakini bahati nzurikipindi chote Naibu Waziri amekuwepo. Kwa manufaa yaTaifa hili, naomba hiyo hotuba pamoja na kwamba inakurasa nyingi hebu wajaribuni kuisoma, itawasaidia sana naitasaidia Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujisema mimimwenyewe kwamba miaka ya 2000 niliwahi kuwa Kiongoziwa Kambi ya Upinzani ndani ya Bunge hili nikiongoza vyamavitano. Kwa hiyo, bajeti zote ambazo zilipita wakati wakipindi changu nikiwa Kiongozi (KUB) ni bajeti ambazo hatatukienda kutafuta kwenye Hansard, hakuna bajeti hata mojaambayo Wabunge wa CCM hawakuipitisha mia kwa mia,hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia hata nilipokuwagerezani kwenye kesi feki ya ugaidi kwa kipindi cha miezikama minne hivi, nampongeza Kamishna wa Magerezaaliruhusu nika-own radio nikiwa gerezani na kipindi cha bajetizilipitishwa kwa maneno matamu kweli na Wabunge waCCM. Yale maneno haijawahi kutokea, hii ni bajeti yakihistoria, hii ni bajeti ya kizazi kipya, kwangu mimi ambayenina experience na Bunge hili chini ya Chama cha Mapinduzina Serikali yake ni maneno ambayo mimi nayaona ni swagaza kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nadanganya twendetu huko mbele, hakuchi, kutakucha hata hii bajeti utasikia

Page 121: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

inapigwa mapiku hata bajeti zingine zijazo. Kwa hiyo,kwangu mimi nafikiri mvinyo ni ule ule kinachobadilika nichupa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka Waziri atakapokujaku-wind up na najua atatanguliwa na baadhi ya Mawaziriambao wako Serikalini kujibu katika maeneo yao, hebutuambieni wananchi wa Kagera, Bukoba, Kanda ya Ziwa meliambayo tumekuwa tunaahidiwa tangu MV Bukoba izamena watu wengine bado wamo humo humo ndani ya melihiyo mpaka leo, inaonekana wapi katika nyaraka hizi, hotubahii na bajeti hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wametaja meli za Nyasa,viwanja vya ndege ambavyo vimekuja baada ya tukio laMV Bukoba na hata lugha ya kuizungumziazungumzia hii melimpya ambayo tumekuwa tunaahidiwa na Awamu zote zauongozi wa nchi hii chini ya Chama cha Mapinduzi inaanzakueleaelea au kufutikafutika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua, badala yakuelezwa kijuujuu tuelezeni maandalizi ya hiyo meli yakowapi, inakuwa designed wapi, nchi gani na imetengewahela kutoka wapi? Taarifa hizi zitasaidia wananchi waKagera, Bukoba na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kufahamumoja nini kinachoendelea. Kama wametupotezea tu kijuujuuni bora wakatamka bayana kwamba hamna hela na walahamna nia ya kutupa meli mpya. Sasa hivi dunia ni kijiji,mimi naamini kuna watu wako nchi nyingine wanawezakujitolea kutuletea meli wananchi wa Kagera, Bukobaambao wanatambua mateso tunayoyapata kulikokuendelea kuuziwa mbuzi kwenye gunia (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kahawa, tumesikiahapa kodi zimeondolewa. Nataka Waziri atakapokuja ku-wind up na kwa kuwa nafahamu hata Waziri wa Kilimoanaweza akachangia katika ku-wind up kwa upande waSerikali atueleze maana sehemu kubwa ya kodizilizoondolewa zinawazungumzia watu wa kati na wale ma-processor. Watu wa Kagera na Bukoba Town ambao tuna

Page 122: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

vijiji vinavyolima kahawa pale greenbelt vijiji vya Kata zaKibete, Kitendagulo, Iduganyongo, Nyanga wanauzakahawa, wawaeleze kilo moja kwa kodi hizi zilizopunguainakwenda kupanda kwa kiasi gani? Hicho ndicho mkulimaanachohitaji siyo maneno maneno haya ya jumla jumla.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, nakubalianana nawaunga mkono Waheshimiwa Wabungewaliochangia sana hapa kwamba katika suala la madinina vita ya rasilimali inayoendelea inahitaji uzalendo namshikamano wetu wote. Hilo naliunga mkono na nawezanikalipigania mimi kama Lwakatare. Hata hivyo, uzalendoni lazima utengenezewe mazingira. Huwezi kutoka hewaniunazungumzia tuwe wazalendo, tuwe na mshikamano,lazima tutengeneze mazingira ambayo yatawezesha, kwanzatuheshimiane humu ndani, tutambuane umuhimu natuheshimu hoja ambazo ni kinzani kwa nia ya kujifunza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi binafsi maana natokaKagera mimi Mlangira mimi, sili chakula ambacho ni halfcooked, ni kwamba mambo ya kubebeshana maiti ambapohatujui marehemu kafia wapi tunakuja kubebeshana tu,mimi siko tayari kuibeba hiyo maiti. Tungetaka kutokea kwaviongozi wetu wakuu wawe consistency maana kiongozianakwenda mahali fulani anasema mimi kwa capacity yangusiwezi kumteua Mpinzani kwenye Serikali yangu, haijapitakipindi anateua Wapinzani. Jamani dunia ni kijiji kunawenzetu wanatushangaa kwa matamko tunayoyatoa. Hiyoinafanya tunashindwa kuwa na consistency ya matamko yaviongozi wetu na dunia wanashindwa kuelewa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ninalotaka kumalizianalo, naomba bajeti hii Mheshimiwa Waziri leo yuko NaibuWaziri lakini Serikali iko pale pale, wamwongezee pesa Msajiliwa Vyama vya Siasa na iende purposely kwa ajili ya kujengacapacity kwenye vyama vyetu, vyama vinapaswakujengewa capacity. Chama cha kwanza ambacho kwa

Page 123: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

kweli kutokana na michango na yale yanayoendelea naonakijengewe capacity ni Chama cha Mapinduzi. Haiwezekanikwa miaka 56 ya Uhuru tunaendesha Serikali kwa individualcapacity badala ya taasisi. Matokeo yake Mheshimiwa Raiswamemuachia mzigo ndiye anaendesha Serikali wakati tunaBaraza la Mawaziri hewa, viongozi wa taasisi hewa,Wakurugenzi hewa kwa sababu wote wanakwenda kwamtindo wa ndiyo mzee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani yanayoonekana sasahivi na mimi namkubalia Ndugu yangu Mheshimiwa Bwegealisema sasa hivi inayoendesha Serikali ni Serikali ya Magufulialiyoisema yeye mwenyewe, Watanzania chagueni Serikaliya Magufuli, hakuna Serikali ya CCM hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo ya hili inazaa sualala watu kujipendekeza, kila mmoja anajipendekeza kwa mtummoja anayeendesha Serikali. Msajili akijengee Chama chaMapinduzi capacity ya kuendesha Serikali kitaasisi. Matokeoyake huyu Rais jamani tutamuua bure, kubeba mizigo yaWizara zote, taasisi zote, makontena ya madini anatembeleayeye, yeye ndiyo anapanga bajeti, akiamua sijui… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Gibson,wajiandae Mheshimiwa Salum Rehani na MheshimiwaMashimba Ndaki.

MHE. GIBSON B. MEISEYEKI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotubaya Waziri wa Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianze kwa kuungamkono maoni ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizarahii. Kama alivyosema mwenzangu, Waziri achukue mudakwenda kupitia mapendekezo hayo kutoka Kambi hii,

Page 124: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

wataalam wetu wamepitia na kuja na mapendekezoambayo yangeweza kumsaidia sana kuweza kutekelezamajukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuiasa Serikalikutekeleza majukumu yake kwa kufuata utawala wa sheria.Tutapona sana na itakuwa na manufaa makubwa sana kwanchi yetu kama tutaongozwa kisheria. Hivi karibuni tumekuwatukiongelea sana masuala ya Sheria zetu za Madini,kumekuwa na maneno ya ajabu ajabu kupinga wengineambao wanatoa mapendekezo lakini tunashukuru kwambakwa namna fulani Serikali imechukua mapendekezo yabaadhi ya watu ambao wanaitwa waropokaji na sasatunaona kwamba sheria hiyo inataka kuletwa hapa Bungenikufanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba wataalam wetuwa sheria, Waziri wetu wa Sheria asisite kutumiarasil imaliwatu walioko upande huu katika kuletamarekebisho ya Sheria hiyo ya Madini ili tuweze kupata sheriaambayo italinusuru Taifa hili katika kutokupoteza rasilimalimadini tuliyonayo katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile sitasita kumshukuruMheshimiwa Lissu kwa uelewa wake katika eneo hili.Ningependa kama inawezekana Serikali bila kuona aibuisisite kuchukua maarifa ambayo wataalam au kwa watuambao wamebobea kwenye maeneo hayowakatengenezea kitu ambacho tukija hapa kama ilivyodesturi yetu tutapitisha tu kwa ‘ndiyo’ tupitishe kitu ambachokimefanyiwa kazi vizuri na kiko balanced ili tuweze kunufaika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Maazimio yalikuja hapaya kumpongeza Rais, lakini mimi niseme kwa uelewa wangumsingi mkubwa wa hasara ambayo tumeipata kwenyemadini na matatizo yote haya yamejikita kwenye Katiba yetu,ni sheria lakini na Katiba pia. Ningekuwa mtu wa kwanzakabisa, tena na kubeba mabango ikiwezekana nitaingiahuku na vuvuzela kumpongeza Rais kama angetuletea

Page 125: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mapendekezo ya Warioba, ile Rasimu ya Pili ya Wariobaikaletwa hapa Bungeni tukapitisha kama Katiba yetu.Tutakuwa tumelitatua hili tatizo pale kwenye kiini chake lakinihaya mazingaombwe ambayo naona yanataka kufanyikahapa katikati hayatatufikisha popote kwa sababu msingi wamakosa yote umejikita sehemu ambayo hatutaki kuigusa.Kwa hiyo, mimi ningeomba tukali-attempt hili maanaWazungu wanasema you can not solve a problem with thesame mind that created it. Nasema kwamba tuilete Katiba,tuibadilishe hapa, tutakuwa tumetatua kwa kiasi kikubwasana mlolongo wa haya matatizo ambayo yako kwenyesheria zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niseme hivi karibunikumekuwa na kulipukalipuka kwa watu kutekelezamapendekezo au tuseme sheria mbalimbali zilizopo. Hivimajuzi nimeona watu wakiingilia kwenye mashamba yawawekezaji tena moja la Mwenyekiti wetu, wakaendawakafanya uharibifu mkubwa. Nasema huko ni kukurupukana tukikurupuka tutaipeleka nchi hii kama walivyosemawenzangu, wataipeleka kama ilivyo Zimbabwe sasa hiviambako wote tunafahamu kwamba Zimbabwe haitumiicurrency yake sasa hivi kwa sababu, kwa bahati mbaya nenoambalo lilikuwa linakuja sio zuri, wamejiharibia wenyewe.Ilifika wakati wanaenda kununua kilo ya sukari kwa mfukowa fedha na sasa hivi wanatumia fedha za kigeni kama billof exchange kwenye nchi yao. Sasa tukikurupuka kurupukana sisi kwenda kuvamiavamia watu nadhani tutaishiapabaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashamba ambayo yanasifa kama alilokuwa nalo Mheshimiwa Mbowe yako mengisana na kama Wakuu wengine wa Wilaya waohawatatekeleza kama alivyotekeleza yule pengine siku mojawendawazimu wengine kama sisi au mimi tutaendakuwasaidia kuharibu. Maana katika Wilaya yetu ya Arumeruwawekezaji wenye mashamba ya maua ambayo yamekaapembezoni mwa maji au mito ni karibu mashamba yote lakinisijui ni nani huyo na akili zake ziko vipi amekurupuka ameendakuvunja shamba la Mwenyekiti wetu.

Page 126: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

Mheshimiwa Mwenyekiti, mienendo kama hiihaitatupeleka pazuri. Kama ni operesheni ya kuondoamashamba ambayo yako pembezoni mwa mito basimashamba mengine yote ya maua, miwa, mpunga nafikirini vyema yakahakikiwa na yenyewe ili hii kama ni sheria basiile pande zote lakini tuwe na tahadhari, tusije tukaipelekanchi yetu kwa akina Zimbabwe na Venezuela. Nilitaka nisemehivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitaka kwenda kwenyebajeti nianze kwa usemi wa mwanamuziki hayati Bob Marleymaarufu kwa taste ile ya reggae, aliwahi kuimba kwenyewimbo wake wa get up, stand up akasema, you can foolsome people sometimes but you can not fool all the peopleall the time. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii bajeti iliyoletwa hapainataka kututegatega. Watanzania wa sasa hivi ni werevusana, tusidhani ni kama wale watu wa miaka ya 60, 70, watuwamezidi kujanjaruka kwa hiyo huwezi kutudanganya.Nimwombe tu Waziri wa Fedha hili suala mnalosema elimubure kwa bajeti hii tuanze kulifuta kwa sababu umedanganyakwa upande huu halafu sasa kwa upande huu unakuja ku-balance. Watoto wengi ambao wanasoma kwenye shulezetu za msingi ni zile familia ambazo kiukweli hata umemewanausikia tu hawajawahi kuuona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo unapowawekea hiziSh.40/= kwa kila lita moja ya mafuta hao ni kwambaunaenda kuwatoza zile hela zako ulizosema elimu bure, kwahiyo tuifute. Utapitisha bajeti yako hii kwa Sh.40/= kwa kilalita moja ya mafuta ya taa, nazungumzia mafuta ya taa,petroli na dizeli tutajua huko mbele lakini mafuta ya taa,maana yake ni kwamba unakwenda kuwatoza Watanzaniaile pesa ya ada ya shule waliyokwenda kuilipa, ndiyo maanayake na wajanja wameshajanjaruka. Kwa hiyo, hapa hamnaelimu bure, you are charging us. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia Mheshimiwa Wazirimwaka jana tulizungumza mengi kuhusiana na bandari.

Page 127: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Walikwenda pale wakasema hata zikiingia meli mbili kamazile nyingine haziingii, sasa kule kumetetereka amekuja hapaanatuambia kwamba uchumi wa dunia umeyumba, siokweli! Siku hizi tunakaa na simu zetu hapa, tunaangalia Beira,Mombasa, Tanzania sasa hivi Bandari yetu ya Dar es Salaaminakaribiana na Kismayo Somalia kule kwenye ma-pirates kwajinsi ambavyo hakuna meli sasa hivi. Sasa wasituambiekwamba uchumi umetetereka, hapana! Walizinyima hizo melijana kuja na tuliwaambia wakakataa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumewaambia tenakuhusiana na VAT kwenye utalii, wameleta ndege sijui naniatazipanda hizo Bombadier ambayo tunajua moja tayari ikogrounded na ilikuwa mpya. Hawawezi wakaleta ndege,apande nani wakati utalii huku kwao wana-discourage?Wenzetu wa nchi za jirani wamefuta VAT, wao wamekomalia.Sasa utalii utaanguka halafu mwakani atakuja kutudanganyakwamba kuna mtikisiko wa kiuchumi. Hii tunai-note namwakani sijui atatuambiaje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti hii naombatunapo-set priorities tuzisimamie. Rais alipokuwa anaombakura hata na sisi wote tatizo la maji tuliliona tumeli-addressna akasema anaenda kuleta suluhu ya shida ya maji nchini.Hata hivyo, wameingia madarakani cha ajabu ni kwambahela nyingi wamezipeleka kwenye kuleta ndege mpyaukilinganisha na walizozipeleka kwenye maji. Pesa za kununuandege zimezidi karibia bilioni 50 pesa walizopeleka kwenyemaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna shida ya maji, Arumeruyangu tuna kiu sana ya maji tuangalie priority zetu,tunapopata fedha tusikengeuke, twende kwenye zile areasambazo tulisema kwamba tunaenda ku-accomplish. Kwahiyo, naomba tu-stick kwenye bajeti kama tulivyokuwatumeipendekeza ili tuweze kumaliza kero nyingi ambazowananchi wanazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna shida sana, tunahitajibarabara, mwaka jana swali langu moja lilijibiwa na Naibu

Page 128: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Waziri, nafikiri ni wa Ujenzi, akasema kwamba barabara yetuinayounganisha Arusha na Simanjiro inafanyiwa upembuziyakinifu. Walisema shilingi milioni 600 imeshapelekwa paleisije ikawa tena miaka mitano. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. GIBSON B. MEISEYEKI: Mheshimiwa Mwenyekiti,siungi mkono hoja. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Salum Rehani kama hayupoMheshimiwa Ndaki na ajiandae Mheshimiwa Stephen Masele.

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kutoamchango wangu kwenye bajeti hii ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwakuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwakutuletea bajeti nzuri lakini pia niwashukuru sana watendajiwao wakuu, Katibu Mkuu pamoja na timu yao hiyo nyingineiliyopo ofisini. Wamefanya kazi nzuri na wametuletea bajetiambayo kila Mtanzania aliposikia alifurahia na alipongeza.Kwa hiyo, nawapongeza sana sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niwapongeze pia TRAkwa makusanyo yao mazuri ambayo kupitia hayoyametusaidia kufanya mambo makubwa kwa mwaka huuunaoisha na naamini hata kwa mwaka ujao tunawezakuendelea kufanya mambo makubwa zaidi. Tumelipamishahara sisi wenyewe, tumelipia reli sisi wenyewe, tumelipiaulinzi na usalama wa nchi yetu sisi wenyewe, tumelipia ndegeingawa watu wanazidharau lakini tumelipa sisi wenyewe,kwa hiyo imetusaidia kujitegemea kama nchi kwa kiasikikubwa. (Makofi)

Page 129: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu kwa watu wa TRAni kwamba waweze tu kuongeza kujenga mazingira mazurikwa walipa kodi wetu ili makusanyo yao yaweze kuongezeka.Wafanye juu chini kuwafanya walipa kodi wetu wajisike faharikulipa kodi yao, waone kwamba wanastahili kulipa,waelewe kwamba kulipa kodi ni ustaarabu lakini wataonahivyo baada ya wao TRA pia kujenga mazingira mazuri kwaajili yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia naomba kodi zaTRA zieleweke, mtu akitaka kuanza biashara fulani ajue kabisaatatakiwa kulipa kodi zipi. Kuwe na namna za kodi elekeziambazo TRA wanakuwa nazo ili mimi nikitaka kufanyabiashara nijue TRA watachukua hela yao kiasi gani hapa.Unajua wafanyabiashara wanataka mambo yao yajulikane,yawe wazi na wanataka uhakika ili atakapoingia kwenyebiashara aweze kupata faida anayoitarajia. Uchumi wetuunakua, kwa hiyo lazima pia TRA wajenge mazingira yabiashara kukua, ya kilimo kukua na uchumi wetu kuendeleakupanda vinginevyo makusanyo yao yanaweza yasiweendelevu sana kama biashara na kilimo havikui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie piaupande wa ajira pamoja na mzunguko wa fedha, hivi vituvina uhusianao sana. Fedha au pesa inazo tabia nyingi lakinitabia mojawapo ni kwamba pesa ni adimu, money must bescarce or limited in supply na pesa inazunguka kwa mtuambaye anafanya kazi, pesa haizunguki tu kwa zamukwamba ni zamu yako imefika, inazunguka kwa mtu ambayeanafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naisihi Serikaliitengeneza mazingira ya watu kufanya kazi ili kwambawaweze kupata pesa. Naiomba Serikali waanze kufikiriamiradi ambayo itazalisha au itatoa mazao kwa haraka,inatoa faida kwa haraka, hiyo nayo watie nguvu hapo ilikwamba watu wafanye miradi kama hiyo waweze kupatapesa. Miradi ambayo tunaita ni quick wins au low hangingfruits ili watu waweze kujiingiza huko na kupata helamzunguko wa pesa uweze kuongezeka. (Makofi)

Page 130: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi kama hiyo ni kamawachimbaji wadogo, viwanda vidogo vidogo vikitiwanguvu na moyo vinaweza vikafanya mzunguko wa fedhaukawa mkubwa kwa sababu wengi wataingia huko. Piamiradi mikubwa ya kielelezo ambayo nchi yetuimekwishakuianza iajiri Watanzania. Najua kandarasi kubwawamepewa watu wa nje lakini tuwe na utaratibu ambaohata nadhani sheria zetu unaukubali kwamba Watanzaniawaajiriwe wengi kwenye miradi hii, wanaweza kuajiriwa walewatu wakubwa wakubwa kule juu kidogo lakini hapa katikatina huku chini waajiriwe Watanzania ili waweze kupata pesaiweze kuzunguka hapa nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia NGO’s zilizokokwenye nchi yetu hii walazimishwe waajiri Watanzania. HiziNGO’s nazo wanapokuja hapa wanalazimisha kuleta watuwao kutoka nje. Nafikiri umefika wakati sasa kazi hizozinazofanywa kwenye NGO’s zifanywe na Watanzania kwasababu tuna ujuzi na weledi wa kutosha kufanya kazi hizi ilipesa zinazokuja kwa sababu wanazileta kwa lengo lakusaidia umaskini wetu, basi umaskini wetu uwe ni fursa isiweni kitu ambacho ni balaa au kinatupita pembeni.Watanzania wengi waajiriwe kwenye hizi NGO’s kuanzia chini,katikati na hata juu ili pesa zinazokuja zizunguke hapa nazitusaidie kweli kama wanataka kuondoa umaskini kwenyenchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kazi za makampunimakubwa ya hapa nchini pia yapewe kazi kubwa kubwa.Nimesikia juzi Mheshimiwa Makamu wa Rais anasemawakandarasi wanaweza wakapata kazi isiyozidi shilingi bilioni10, nadhani hili ni jambo zuri kwa sababu hawa wakandarasiwa ndani wakipewa pesa kama hiyo itafanya izunguke hapandani na kufanya mazunguko wa fedha uwe mkubwa hapanchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la kukuzaviwanda kwenye nchi yetu. Kwanza nipongeze kabisahotuba ya Mheshimiwa Waziri hasa kwa upande wa viwandavinavyozalisha mafuta ya kula kwamba wameweka tozo/

Page 131: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

ushuru kwenye mafuta ghafi yanayoingia kutoka nje hasayanayotokana na mawese. Hongera sana kwa jambo hilikwa sababu tozo hii ilikuwa imeondolewa hapo nyuma.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kwamba tozo hiiiongezwe badala ya asilimia 10 aliyoiweka Mheshimiwa Waziriiwe asilimia 15 ili kulinda viwanda vyetu vya mafuta ya kulahapa ndani lakini pia kulinda wafanyabiashara wetu. Kwasababu hata hayo mafuta wanayosema wanaingiza mafutaghafi lakini ukiyachunguza asilimia ya mafuta ghafi ni kama10 tu, asilimia 90 ya mafuta haya yako kamili kabisa. Kwahiyo, ili tuweze kujenga viwanda vyetu, ushuru kwa bidhaazinazotoka nje lazima uongezeke ili tuweze kulinda viwandavyetu hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nizungumzie sualala wastaafu hasa wale wanaopata pesa zao kupitia Hazina,walio na account zao Benki ya Posta. Hawa wana dirisha lakupata mikopo huko Benki ya Posta lakini wanapoombamikopo yao nyaraka zinachelewa sana kutoka Hazina tofautina nyaraka au na wale ambao walikuwa kwenye Mifuko yaPSPF na LAPF.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana MheshimiwaWaziri awafikirie hawa wastaafu maana na wenyewe badomaisha yanaendelea, kwa hiyo tuwasaidie wale wanaopatahela zao kutoka Hazina wakiomba mikopo kupitia Benki hiiya Posta wapewe mikopo yao mapema, hiki kisingizio chanyaraka zinachelewa nadhani hakina sababu ya kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kamamuda wangu pia utakuwa haujaisha niongelee suala la …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante muda wako umekwisha.Mheshimiwa Rehani umerudi, baada ya Mheshimiwa Rehanijiandae Mheshimiwa Shaabani Shekilindi.

Page 132: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kunipa nafasi yangu. Nami nashukurukupata fursa ya kuchangia kwenye bajeti hii kuu nikiwanataka kujielekeza kwenye mambo manne ambayo nahisiyanaweza kuisaidia Serikali lakini kumsaidia Waziri sasakuweza kujipanga zaidi katika kuhakikisha anapata mapatoya kutosha kutokana na vyanzo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwanzo ninalotakakuzungumza ni suala zima la bandari bubu na magendoyanayofanyika kwa bandari zetu kutoka Zanzibar kujaTanzania Bara. Biashara kubwa inayofanyika hapa ni mafutaya kupikia. Hii biashara imekuwa ni kubwa na kama nchihakujawa na utaratibu mzuri wa kudhibiti hizi bandari lakinikudhibiti zi le bidhaa zinazoingia pale Zanzibar nakutawanywa katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara hii inafanyikakupitia bandari ndogo ndogo mbalimbali na kushushwakatika bandari ndogo ndogo hapa Dar es Salaam na bidhaanyingi zinazosafirishwa ni mchele, mafuta, sukari, mafriji yaleused, redio, mipira used kitu ambacho kwa kiasi kikubwakinaikosesha Serikali mapato. Hii imetokana na mfumo mzimaule wa ukusanyaji mapato kule Zanzibar, double tax, ndichokitu kinachosababisha wafanyabiashara kukimbia kulipa kodimara mbili katika bandari yetu ya Dar es Salaam. Kwa sababuwao wanaleta bidhaa pale Zanzibar wakishashusha kwenyemakontena wanalipishwa ushuru, TRA wanachukua chao naZRB wanachukua chao, lakini mtu yule yule akisafirisha mzigoule kuuleta bandari ya Dar es Salaam analipa tena kodi marambili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie waziMheshimiwa Waziri, kiwango kikubwa cha bidhaa zile aumafuta yanayoingia Tanzania Bara asilimia 80 yanapitiaZanzibar. Hiyo ni taarifa rasmi naomba aifanyie kazi na si hivyotu, mipira used na vifaa vingine used vinavyoletwa kutokanje vinashushwa tu Zanzibar lakini vinaishia Tanzania Bara namaeneo mengine kwa njia za panya. (Makofi)

Page 133: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni jukumu laSerikali kujipanga sasa kuhakikisha hii kero inayotajwa kilasiku kwamba tumemaliza tatizo la tozo ya ushuru wa marambili kwa biashara au kwa bidhaa zil izoko Zanzibarzinazoingia Bara bado halijamalizika na imekuwa manenoya kila siku. Hili nimwombe Waziri ulifanyie kazi na tufikemahali iwe mwisho wa hili suala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia eneolingine ambalo Serikali bado ina nafasi kubwa ya kuwekezana kuweza kujipatia mapato mengi. Nimeangalia bajeti vyakutosha lakini bado wito wetu tunaoutoa na kulia kila kwenyesuala zima la uvuvi wa bahari kuu na uanzishwaji wa viwandavya kuchakata samaki halina kipaumbele. Nimwombe Wazirihesabu za haraka haraka, sasa hivi duniani mpaka juzinilivyokuwa natembea kwenye mitandao ndani ya soko ladunia kuna mahitaji ya tani 271,000 kwa mwezi za samakiambazo zinahitajika zikiwa processed ambao ni cane fish.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kama nchi ingewezakuwa na hii tunaita pot fish moja tu au mbili zinawezakutengeneza ajira zaidi ya watu 30,000 kwa kila meli inayo-land kwa kipindi cha miezi mitatu watu wale wanafanyakazi lakini pato linalopatikana kwa meli mojatumeshawaeleza mara nyingi pale ile process nzima ya melimoja ni zaidi ya dola 85,000, pesa zile zinakuwepo ndani yanchi, zinasaidia Watanzania na watu wengine. Vilevile bahariyetu tumeshaeleza mara nyingi jamani, hivi sasa pamoja namazingira mengine yaliyoko katika maeneo mengine currentya maji katika maeneo yetu ni very conducive kuliko maeneomengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Namibia current imechafuka,Mozambique current imechafuka, Tanzania current niconducive. Kwa hiyo, stock kubwa ya samaki imekusanyikakatika maeneo yetu na ndiyo maana meli nyingi za njezinakimbilia kuvua katika maeneo yetu kwa sababu kunamazingira rafiki ya kuishi. Si hivyo tu, wenzetu wa Philippinena Mataifa mengine ya nje yanakuja kumwaga vyakula

Page 134: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

katika maeneo ya Tanzania ili kuwavuta samaki kuwepo kwawingi na kuvuna samaki wale kwa njia ya kirahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu nyinginetuendeleze uvuvi mpya unaoingia hivi sasa wa kutengenezauvuvi wa kutumia cadge. Utafiti tayari umeshafanyika nacadge fishing imeonekana kuwa na mafanikio makubwa.Leo hii wavuvi wetu wengi walikuwa wanavua majongookwa kutumia gesi lakini leo baada ya kufanyika utafiti, wavuvihawa wanaweza kuvua kwa kutega cadge tu ndani ya deepsea na cadge moja ina uwezo wa kuingiza mpaka milioni 24kwa mvuo mmoja tu wa kipindi ambacho utaweza kufugawale samaki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini kusiwe na mipangomahsusi kuwawezesha wananchi hawa, wakawa navyombo vya kisasa wakaweza kwenda kuweka cadge zaokatika deep sea, wakavua kwenye deep sea na tukawezakupata samaki wa kutosha lakini tukaanzisha viwanda vyakuchakata samaki na kufunga na kusafirisha nje, wakati sokosasa hivi linatafuta bidhaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo natakakulisema ni kwamba bado tuna tatizo kwenye kilimo.Tunasema kilimo tumekipa kipaumbele lakini bado sijaonamikakati halisi ya kusaidia kilimo cha Tanzania kikawezakuonesha mafanikio na kuwasaidia wakulima wengi katikanchi yetu. Nitoe mfano mmoja wa kahawa bado kunaurasimu katika soko la kahawa, soko la kahawa lazimauende Moshi, lakini tuna kiwanda kipo Mbinga kilianzakuchakata na kutengeneza Mbinga Instant, kahawa ile ikawaimepata soko kubwa tu katika nchi mbalimbali zikiwemoUlaya hata Zanzibar na maeneo mengine lakini bado Serikalihaikutoa msukumo wa kufanya eneo lile likaweza kuzalishana kufanya canning ile kahawa iliyoko katika maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeweza kukianzisha kilekiwanda cha Mbinga kingehamasisha kilimo cha kahawakatika maeneo yote yale ya Mikoa ya Ruvuma lakini hatamaeneo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara yale ambayo

Page 135: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

yanakubali kahawa ingeweza kuzalishwa, lakini Njombeingepata fursa kubwa zaidi ya kuzalisha kahawa na ikaingiakatika ramani ya maeneo ambayo yana uzalishaji mkubwawa kahawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe vitu kama hiviSerikali itie mkono wake si tu kuiachia pengine kampuni auHalmashauri na wananchi wenyewe wakaweza kufanya kitukama kile, lakini ile ile ingesaidia urasimu wa kutoa kahawaMbinga kuipeleka sokoni Moshi. Vilevile ungesaidia urasimuwa kutoa kahawa Mbozi ukaipeleka Moshi, tunapotezagharama kubwa ya uzalishaji bila ya sababu wakati hukutunasema Serikali inaondoa tozo lakini tunaanzisha tozonyingine ambazo tunaweza kuzipunguza na... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa ShaabaniShekilindi, ajiandae Mheshimiwa Mussa Sima na MheshimiwaAmina Mollel.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza kabisa nimshukuruMwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha mimi kusimamakwenye Bunge lako Tukufu ili niweze kuchangia hoja ambayoipo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nianze kumpongezaWaziri wa Fedha na Naibu wake kwa hotuba nzuri ambayosiku ile ya kusoma hotuba Watanzania wote naaminiwalikuwa kwenye luninga na kwenye redio kusikiliza hotubana walifurahi mno. Kwa hiyo, hotuba hii kwa kweli imejibukiu ya Watanzania hususan wale wa hali ya chini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Rais wangu,Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli kwa kazianayoifanya kwani sisi katika upande wetu wa dini unasemakwamba Mwenyezi Mungu anapomchagua mtu wakeanamtuma Jibril. Jibril anapeleka majibu kwa Mwenyezi

Page 136: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mungu kwamba Mwenyezi Mungu nimeleta jina la JosephJohn Pombe Magufuli kwamba huyu ndiyo anakubalika kwawatu, Mwenyezi Mungu anaidhinisha. Mwenyezi Munguanapoidhinisha anatuma malaika, malaika wanakuja kwetusasa kusambaza kwenye mioyo ya wananchi kwambamchagueni John Pombe Magufuli huyu ndiyo Rais wa kweli.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii ni tunu ambayotumepewa na Mwenyezi Mungu ambaye hamuungi mkonoRais wetu kwa juhudi hizi anazozifanya, basi apimwe akilikwa sababu naamini kabisa huu ni ujumbe wa MwenyeziMungu, ameletwa na Mungu huyu. Kwa hiyo, kama mtuhatamuunga mkono tunaita ni kizazi cha shetani. Mara nyingiviongozi wazuri wanapofanya kazi vizuri basi wale ambaoni mlolongo wa shetani huwa wanapinga. Kwa hiyo, usionewatu wanapinga ujue ni mlolongo wa shetani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niendelee kuchangia,kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mpango na timu yake kwaujumla hasa kwa kutoa hii tozo ya Road Licence. Hata hivyo,nimuombe tu sasa kwamba amekula ng’ombe mzimaamebakisha mkia, kuna hii fire extinguisher na sticker zake nikodi kandamizi ambayo kwa kweli naomba aiangalie naikiwezekana nayo iondoke. Kwa sababu yeye mwenyewenaamini anakiri kwamba gari ikipata ajali ule mtungi weweabiria, dereva au turnboy huwezi kuamka na kuzima gari ileau hao watu wanaokata sticker hizi za fire extinguisherhawawezi kuzunguka barabarani na kukuta gari inaunguana wakazima sijawahi kuwaona. Kwa hiyo, naona hii ni kodikandamizi itolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, kunahawa vijana wetu wa bodaboda wameamua kujiajiri nahili ni kundi kubwa sana, nao ikiwezekana hii SUMATRA itoke.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, sasaniende kwenye suala zima la viwanda. Nashukuru kwenyehotuba ya Waziri ameainisha mikoa ya viwanda ikiwemo

Page 137: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Tanga lakini cha kushangaza Mheshimiwa Mpango kwenyehotuba yake anasema atatengeneza viwanda vipya wakatiTanga kuna viwanda vimekufa mfano Kiwanda cha Chuma,Kiwanda cha Afritex na Kiwanda cha Foma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu kuna Kiwanda chaChai cha Mponde hakifanyi kazi na hapa lazima niseme,tumeongea vya kutosha, kiwanda kile hakina tatizo loloteni kizima kabisa, kinaendelea tu kulipiwa bili za umeme.Wananchi, wakulima wa Mponde wanapata tabu sana.Imefikia hatua sasa hata ule mlo mmoja kwa siku hawaupati,hawapeleki watoto wao shule, hawana ada, hata bili yaumeme wameshindwa kulipa. Kwa hiyo, nimwombe WaziriMpango kwa unyenyekevu na heshima kubwa aliyokuwanayo atenge hata shilingi bilioni nne akafungue kiwanda kileili tuweze kuokoa maisha ya wananchi wale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala zimala maji. MWewe ni shahidi wakati unaniona nimevaa mabutiniko kwenye barabara ya Soni – Mombo - Lushoto,kumenyesha mvua nyingi mno. Nashindwa kuelewanimeshaongea sana mbele ya Bunge lako Tukufu kwambaWizara sasa ipeleke wataalam wa kutujengea mabwawa iliyatumike kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji cha mbogamboga na kuwapa wananchi maji. Vilevile mabwawa hayayatazuia uharibifu wakati wa mafuriko hata kama yatashuka,yatashuka kidogo sana. Niiombe Serikali hebu itenge fedhaza kutosha ili ipeleke vijijini ili wananchi wa vijijini wawezekupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, hizi fedhazinazoenda Halmashauri kwa ajili ya maji naomba sasamfumo ubadilishwe. Kuna watu wanaitwa DCCA wapewekazi hawa au kuundwe Mamlaka ya Maji Vijijini, naaminihawa wataenda sawia kabisa na kuboresha huduma nakwenda kwa kasi zaidi ili wananchi waweze kupata maji.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara zanguzimeharibika mno. Nimeomba kwa muda mrefu sana

Page 138: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

barabara ya kutoka Mlalo - Ngwelo – Mlola – Makanya -Milingano - Mashewa ipandishwe hadhi lakini mpaka sasahivi bado haijapandishwa. Nimwombe Waziri MheshimiwaMpango ikiwezekana barabara ile sasa ipandishwe hadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyojua barabarayetu ile inashuka matope na mawe, inafunikwa kutokanana mafuriko, kwa hiyo, ningeomba sasa tupate barabarambadala. Kuna barabara inaanzia Dochi - Ngulwi - Mombokilometa 16 tu, niiombe Serikali yangu tukufu, sikivu iwezekunisaidia barabara ile ili wananchi wangu wa Lushotowasiishi kisiwani. Pamoja na hayo, Rais wa Awamu ya Nnealiahidi kilometa nne, nizikumbushie kwa Waziri MheshimiwaMpango aweze kutupa hizo kilometa ili tuweze kutengenezaMji wetu wa Lushoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la vituo vya afya,wananchi wangu nimewahamasisha wamejenga vituo vyaafya zaidi ya vinne, vimefikia hatua ya lenta lakini kama ilivyoada Serikali imesema kwamba wananchi wakijenga ikifikiahatua ya lenta basi Serikali inachukua. Kwa hiyo, niombeSerikali sasa nimeshafikisha hatua ya lenta hebu wanipe pesaili niweze kumalizia vituo vile ili wananchi wangu wawezekupata huduma ya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, usambazaji umeme vijijini.Nishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ina kasi sana yakusambaza umeme vijini lakini imetoa vijiji vichache sana.Niiombe sasa Serikali yangu, sisi tumeshaahidi kule kwambajamani umeme unakuja kama Ilani ya chama inavyosema,sasa unapopata vijiji hata 10 havizidi sijui tutawajibu niniwananchi wale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, milioni 50…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

Page 139: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante na naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nina wageni15 wa Mheshimiwa Rashid Shangazi ambao ni Wataalamwa Afya ya Sikio kutoka Tanzania Society for the Deaf (uziwi),wakiongozwa na Mkurugenzi Yassin Mawe. Hawa ndiyowataalam wetu wa kuchunguza masikio ya WaheshimiwaWabunge, karibuni sana. Baadaye mtanipa taarifa mmepatawagonjwa wangapi na matatizo ambayo wanayo. (Makofi/Kicheko)

Sasa tunaendelea na Mheshimiwa Mussa Sima,ajiandae Mheshimiwa Stephen Masele

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naminichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu lakininipongeze sana Wizara, Waziri na Naibu wake kwa kutuleteabajeti nzuri ambayo inajali maisha ya Watanzania wa haliya chini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nichukue fursa hiikumshukuru sana Mheshimiwa Rais, kwa kweli ameoneshadhamira yake ya dhati ya kuwatumikia Watanzania. Nimpemoyo tu hata Mitume nao wakati wanakuja walitokea watuambao hawakuwaunga mkono lakini leo bado tunaendeleakuwaabudu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti yetu ni nzuri sana, kwakweli inatufanya tutembee kifua mbele. Yako mambomachache ambayo nami napenda niyazungumzie. Nianzena eneo ambalo bajeti imelizungumzia na nipongeze sanaWizara kwa kuondoa kodi kwenye mazao ya biashara nakilimo. Kwenye eneo hili yametajwa mazao hapa kama vilechai, pamba na mengine lakini alizeti halijaangaliwa naMkoa wa Singida sisi ni maarufu sana na ndiyo waasisi wazao hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumza ninihapa? Takwimu inatuambia Tanzania tunatumia karibu tani

Page 140: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

laki nne za mafuta, lakini tani laki mbili na themanini ni(importation) yanatoka nje, palm oil zinazobaki ndizo taniambazo sisi tunatumia kama laki moja na ishirini. Serikali leotunazungumza kuwekeza katika viwanda vyetu vya ndanina lazima tujikite katika kuwakomboa wakulima wetu na nilazima tuhakikishe kwamba mazao ya kwetu tunayapakipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mkulima akilima alizetiyake akishaisindika tu maana yake analipa VAT asilimia 18.Huyo huyo mkulima tunamtarajia aende akaongeze angalauheka moja, mbili hawezi, matokeo yake wakulima wote waalizeti wanaiuza alizeti ikiwa shambani, ndiyo maanauzalishaji unakuwa mdogo. Mafuta ya alizeti tukiyaangaliana ndiyo mafuta bora yana cholesterol ndogo ya asilimia 17kulinganisha na mafuta mengine yote ambayo yana zaidiya cholesterol asilimia 60. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafuta yanayoagizwa njeni asilimia 70, yanayobaki ni asilimia 30 mafuta yetu ya ndani.Sasa kama Serikali ina lengo la ku-promote tuweze kutumiamafuta yetu ya ndani hasa alizeti tulikuwa na kila sababu yakuhakikisha tunaondoa hii kodi ya VAT. Serikali imeongezaasilimia 10 kwenye importation ya mafuta yanayotoka nje,mwenzangu aliyepita amesema iongezwe iwekwe hataasilimia 15 na mimi namuunga mkono kwenye hilo, kwasababu kama tuna lengo la kulinda viwanda vyetu vyandani basi niiombe Serikali iondoe kodi hii ya asilimia kumina nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwomb sana MheshimiwaWaziri, sisi tunaotoka kwenye maeneo haya alizeti ndiyo zaokuu Mkoa wa Singida ambalo uzalishaji wake unashuka kilakukicha, kwa sababu wametuwekea VAT bila sababu yamsingi. Mwaka 2010 tulikuwa na zero rate lakini tumekwendamwaka 2014 wametuwekea VAT lakini hakuna sababu yamsingi. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri awajaliwakulima hawa wa zao hili la alizeti ili tuweze kuwasaidiaWatanzania. (Makofi)

Page 141: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pale Singida tunalimasana kitunguu na kitunguu bora kinatoka Singida. Wakatinauliza swali mwanzoni Serikali i l i j i-commit kwambaitakwenda kutujengea soko la kisasa la vitunguu. Sisitumekwishatenga eneo na Mheshimiwa Rais alianza ziarayake ya kwanza Mkoa wa Singida namshukuru sana na katikaziara ile aliwaahidi Wanasingida kwamba sasa anahitaji vilevitunguu tuweze kufanya packing pale pale Mkoani Singidabadala ya kubeba kitunguu kikiwa raw kiende kufanyiwapacking Kenya na maeneo mengine. Sasa nimwombeMheshimiwa Waziri, tumeshaandaa eneo, tuna vitunguu vyakutosha, waje mtusaidie kujenga lile soko liwe soko la kisasa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze sana Serikaliimewatambua wafanyabiashara wadogo wadogo, mamalishe, Wamachinga na wengine. Hata hivyo, nilikuwanajaribu kuangalia hawa bodaboda na bajaji niwafanyabiashara wa namna gani? Mkoa wa Singida hususanSingida Mjini tunao vijana wengi sana na eneo hili lausafirishaji wameturahisishia sana sisi, lakini jambo lakushangaza, Mheshimiwa Waziri vijana wangu leowanatozwa (income tax) kodi ya mapato ya Sh.150,000/=kwa mwaka bila sababu ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati naanza kulalamikakwa nini wanatozwa nilimwandikia barua Meneja wa TRA,nashukuru sana kijana yule ni msikivu, lakini ananijibu kwapikipiki moja bwana tutaacha lakini mmiliki wa pikipiki mbiliatalipa Sh.150,000, tunakwenda wapi? Tunataka vijana haowajiajiri na ajira Serikalini hamna, sasa leo kama watalipaincome tax maana yake vijana wale watafanya kazi usiku,madhara ya usiku tunayajua, akishindwa kupata fedha yakununua mafuta maana yake ataanza kufanya shughulinyingine. Naomba tusiwaweke kwenye majaribu,Mheshimiwa Waziri hili ni eneo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Sheria ya Mapato mwaka2014 ya kukusanya kila mahali sidhani kama ina tija kwavijana wa bodaboda. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri

Page 142: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

vijana wangu pale mjini wako wengi, wamejiajiri na mimi nisehemu ya shughuli zao na mimi ni mlezi wa eneo lao,niombe sana hili eneo kwa kweli kwangu wanatozwaSh.150,000/= bodaboda na bajaji, hebu tuiondoe kodi hii.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie eneo lingine lamaji. Nami niungane na wenzangu kwa kuongeza Sh.50/=kwenye maji lakini tunayo miradi ya vijiji 10 ambayo imekujaSingida lakini utekelezaji wake ni hafifu sana. Niombe eneohili pia mtaenda kuliangalia kwa sababu ya muda nisielezesana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kwenye milioni50, kila Mbunge anasimama na vitabu vinaandika milioni 50kila kijiji. Mheshimiwa Waziri hebu tuliweke vizuri hili sisiwengine tuna mitaa, sasa ukizungumza milioni 50 kila kijiji,mimi naenda kusimama naambiwa naletewa milioni 50 nasheria imekuja inasema milioni 50 kila kijiji, mitaa haipo.Naomba tuiweke vizuri wala hapa hakuna mgogoro, tuwekemilioni 50 kila kijiji na kila mtaa ili wananchi wangu kotewapate, kwa sababu hii categorization ya vijiji na mtaa niya Kiserikali wala siyo ya kwetu, Watanzania ni wale wale tu.Nimwombe Mheshimiwa Waziri hili pia nalo aliangalie.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la REA,tunazungumzia umeme vijijini. Sisi tunaoishi mjini maana yakeni kama unaambiwa wewe unaishi mjini umeme hauwezikuja. Mimi nina vijiji 20 na mitaa havina umeme, MheshimiwaWaziri hebu na jambo hili tuliangalie, tutazungumza lughagani? Kama tunasema Serikali inaleta umeme lakini umemeunakwenda vijijini sisi tunaishi mjini, hatukuzaliwa kuishi mjiniili tukose hizi fursa ambazo Serikali inazitoa, wote tunaishimaisha sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni lazima Wizarailiangalie vizuri ituletee umeme, tusiwe watu wa kulalamikakwenye maeneo haya. Kama wenzetu wanapata umemena sisi tupate umeme bila kujali vijijini wala mjini. (Makofi)

Page 143: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Singida unarasilimali ya madini, eneo la Singida Mashariki, SingidaMagharibi hali kadhalika Iramba kuna madini. Wakowawekezaji wanaitwa Shanta Gold Mine, wananchi kwaridhaa yao wamepisha eneo lakini hawajalipwa fidia. Bahatimbaya sana kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu hilihakuliona lakini naomba mimi niliseme kwa sababu miminaishi mjini nahitaji waje wawekeze mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe sanaMheshimiwa Waziri wale wawekezaji, Shanta Gold Mine sasawana miaka mingi, wananchi wangu sasa wamebakikuvamia kuanza kuchimbachimba kidogo kidogo yalemadini yako ya kutosha, wanahitaji kulipwa fidia na uleuchimbaji uweze kuonekana. Mheshimiwa Raiskeshatuonyesha njia sasa hatuna sababu ya kurudi nyuma.(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Amina Mollel, ajiandaeMheshimwa Stephen Masele.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia.Awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaliakuwepo hapa tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwakuwapongeza Mawaziri na hasa nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake.Nimpongeze sana pia Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kuwamshauri mzuri kwa Waziri na hatimaye kutuletea bajeti yenyetija na inayojali maslahi ya wananchi. (Makofi)

Page 144: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Kondoa wana msemousemao kwamba mwana wa mukiva amanyire michungiro.Usemi huu una maana kubwa sana na ndiyo maananikampongeza Naibu Waziri kwa sababu ya ushauri wakemzuri na kuweza kumsaidia majukumu Mheshimiwa Wazirina hatimaye tumeletewa bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niipongeze sana Serikalikwa hatua zake katika kujali maslahi ya kundi la watu wenyeulemavu. Kubwa zaidi niipongeze Serikali, kuondoa kodikatika vifaa vya watu wenye ulemavu, ukurasa wa 71. Vifaahivi ni muhimu sana. Vifaa hivi ndivyo vinavyowasaidia watuwenye ulemavu kuweza kutekeleza majukumu yao lakini piani sawa na miguu au mikono ya watu wengine ambayowamepewa na Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, kwa kitendo hikicha kuondoa kodi katika vifaa vya watu wenye ulemavu nifaraja kubwa sana kwa sababu hivi sasa vifaa hivi vitakuwana bei angalau afadhali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, calipersambazo zimekuwa zikitumiwa na watu wenye ulemavuzinafika kwenye Sh.400,000/= mpaka Sh.500,000/= lakini ninamatarajio makubwa sana kwamba baada ya kuondolewaushuru wa kodi kwa vifaa hivi, basi vitapungua na walemavuwengi wataweza ku-afford vifaa hivi. (Makofi)

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

TAARIFA

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa mzungumzaji anayeendeleakuchangia, calipers sasa hivi zinauzwa kwa Sh.1,500,000/=mpaka Sh.1,900,000/= bei ambayo nilipewa mwezi February.Ni hilo tu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mollel, taarifa hiyo.

Page 145: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,naipokea taarifa hiyo kwa mikono miwili na kwa sababumwenzangu amekuwa akitumia sana vifaa hivi, kwa hiyo,anachokizungumza anakifahamu kwa undani zaidi. Kwahiyo, niungane naye tu katika kuipongeza Serikali kwa maanakwamba sasa hiyo gharama ambayo imekuwa ikitozwaitapungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda katika Hospitali yaCCBRT, Hospitali ya KCMC lakini pia Hospitali ya Selianiambazo zimekuwa zikihudumia sana watu wenye ulemavu,naamini kabisa kwamba msamaha huu wa kodiuwatawasaidia. Kwa maana hiyo pia tutaweza kuboreshahospitali yetu ya Muhimbili ili basi na wenyewe wawezekuboresha zaidi kitengo hiki cha huduma ya vifaa saidizi kwawatu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naipongeza kwamoyo wa dhati kabisa Serikali na niendelee tu kuipongezaWizara, Mama yangu Ndalichako, Mheshimiwa Waziri Mkuuambaye pia hivi karibuni alipokea vifaa vya watu wenyeulemavu ambavyo vimesambazwa katika shule na vyuombalimbali. Kwa hiyo, naamini kabisa kwamba Serikali hiiimekuwa ikijali maslahi na kuangalia kundi hili la watu wenyeulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizi nakuishukuru Serikali, nitoe tu pia ushauri kwa Serikali kwa sababukuhusu Kitabu hiki cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka2016. Pamoja na kwamba tumepunguza kodi lakini badokuna mahitaji mengi ya watu wenye ulemavu. Kwa hiyo, nivyema katika bajeti ijayo tuone ni kwa jinsi gani tutasaidiazaidi kundi hili. Kwa mfano, maisha ya watu wenye ulemavuni ya chini sana na hasa maeneo mengi ya vijijini hali zao zakiuchumi ni mbaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunapokuja nabajeti tuone kundi hili tunaliangalia vipi? Kwa mfano, kwahivi sasa tulipo katika Sera ya Serikali katika kuhakikisha

Page 146: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

kwamba inajikita zaidi katika viwanda, pia tuangalie hivyoviwanda ni kwa jinsi gani vitaweza kutoa ajira kwa watuwenye ulemavu, kuwasaidia na hali ngumu au maishamagumu waliyonayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze pia Serikali nanimpongeze sana Mheshimiwa Rais ambapo nilizungumzakwa undani zaidi na nimekuwa nikilipigia sana kelele sualala TBC kutokana na uchakavu wa mitambo. Kwa sababu niSerikali sikivu Mheshimiwa Rais alifanya ziara katika shirika hilina kujionea hali jinsi ilivyo lakini pia akaweza kutatua baadhiya changamoto zilizopo katika shirika hili, nampongeza sanaMheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na yote haya, sasani wakati muafaka kabisa kwa wafanyakazi na watumishiwote wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoa ushirikiano,kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha kwamba shirika hililinarudi katika hali yake iliyokuwepo hapo awali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzurialiyoifanya ambayo hivi sasa Afrika inafahamu kwambaTanzania inaye Rais anayeitwa Dokta John Pombe Magufuli.Kitendo alichokifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania ni kitendo cha kuungwa mkono na Watanzaniawote, ni kitendo cha kuungwa mkono na wale wotewapenda maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababumimi katika kundi ninaloliwakilisha na naomba nijikitekulizungumzia hili, ni watu wenye maisha duni sana. Rasilimalihizi zikitumika ipasavyo ni dhahiri kabisa kwamba tutatatuachangamoto nyingi za watu wenye ulemavu na kupunguzaukali wa maisha waliyonayo. Kwa maana hiyo, naomba sananimpongeze Rais. Pia naamini kwanza ni fundisho ambalotumejifunza lakini pia tutakuwa makini katika kupitishamikataba ili mikataba hiyo isije ikatufunga sisi na ikatuumiza.(Makofi)

Page 147: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali ya hivyo pia, ni wakatimuafaka sasa na ningemwomba Mheshimiwa Rais aangaliemkataba na mwekezaji wa Pori la Loliondo ambao kwamuda mrefu umekuwa ni mgogoro unaoumiza ndugu zanguwa jamii ya Kimasai. Kwa hiyo, namwomba pia kuangaliani kwa jinsi gani watapitia mkataba huu ili kama kunavipengele ambavyo vinawabana au vinawaumiza wananchivifanyiwe marekebisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine pia ambalo napendakuishauri Serikali, kwanza nampongeza Mheshimiwa Spikakwa kuunda Kamati kupitia Mkataba wa Sky Associatepamoja na State Mining Companies Limited (STAMICO) ilikuweza kurekebisha upungufu uliopo. Kabla Mkoa waManyara haujagawanywa madini haya yalikuwa ndani yaMkoa wa Arusha na nafahamu kabisa ni kwa jinsi ganiyamekuwa yakisaidia wakazi wa Arusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa ukienda hali ningumu sana kwa vijana wengi ambao walizoea kuchimbamadini haya na kujipatia kipato, hali imekuwa tofauti. Kwahiyo, kwa kitendo hiki cha Mheshimiwa Spika kuunda hiiKamati kupitia mkataba huu, ni faraja kubwa na naaminikabisa sasa mikataba hii itaangalia ni kwa jinsi ganiitakwenda kuwanufaisha wananchi hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naishauri Serikali katikaHalmashauri na Mikoa yetu kuangalia kwa mfano, ndiyo,tumepunguza kodi katika vifaa saidizi kwa watu wenyeulemavu lakini tunawaandalia mazingira gani mazuri yakuwawezesha watu hawa kufanya…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga hoja mkono. (Makofi)

Page 148: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

MWENYEKITI: Mheshimiwa Stephen Masele, ajiandaeMheshimiwa Dokta Christine Ishengoma.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nianze kwa kukushukuru kwa kunipa nafasi hii yakuchangia bajeti hii ya Serikali. Nianze kwa kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri, Dokta Mpango, ama kweli ameoneshauwezo wake kwamba yeye ni mchumi aliyebobea kwakutuletea bajeti ambayo kwa kweli imeandaliwa kisayansisana. Pia nipongeze sana timu yake yote ya watendaji,ikiongozwa na Katibu Mkuu Ndugu Dotto James na timunzima ya Wizara ya Fedha kwa kazi nzuri ya kutengenezabajeti ambayo inatoa majawabu ya matatizo ya wananchiwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasiasa na watumbalimbali wamekuwa wakisema Serikali haisikilizi ushauri,Serikali haishauriwi, lakini nimesoma bajeti hii mambo mengiambayo wananchi na Wabunge wamekuwa wakishauriyamezingatiwa. Kwa kweli, naomba sasa MheshimiwaMpango na timu yake waharakishe utekelezaji wa maamuziya kisera waliyoyafanya. Wamepunguza ushuru kwenyebaadhi ya maeneo hasa kwenye mazao kwenye Halmashaurina wametoa maelekezo kwa TRA ifanye kazi bila kubughudhiwafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Shinyanga,Shinyanga tuna wafanyabiashara wadogowadogo nawakubwa, wafanyabiashara wanasumbuliwa, wanafuatwana Polisi, wanafuatwa na PCCB. Maelekezo aheshimiwaMpango naomba ayapeleke kule chini na ayasimamiekuhakikisha wafanyabiashara wanapewa mazingira wezeshiili waweze kuzalisha na hatimaye Serikali iweze kupata kodi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia huu ushuru wamama-ntilie, mama-lishe, wakulima wadogo wadogo wabustani, yote ambayo wamepunguza maelekezo yaendekwenye Halmashauri zetu. Hatuwezi kujenga Taifa hili kwakutegemea ushuru wa mama-lishe au wa mama anayeuza

Page 149: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

mboga. Kwa hiyo, nina imani na kazi yake, nina imani nauwezo wake, naamini atayazingatia haya na atapelekamaelekezo kwenye ngazi za chini za wananchi ili wasiwezekusumbuliwa na wananchi wangu wa Soko la Nguzo Nanekule Kambarage, Soko Kuu la Shinyanga waweze kufanyabiashara zao bila kusumbuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wiki nzima hii nchi yetuimekuwa inazungumzia suala la mchanga wa dhahabu.Mimi nimewahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati naMadini, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge kamakuna vita yoyote duniani hivi leo ni vita ya uchumi. Yale yotemnayoyaona yanatokea Syria, watu wengi hawaelewi Syriani nini kinatokea, pale kuna gesi ya Qatar inazalishwa naWamarekani wanataka kusafirisha kwenda Ulaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Urusi ndiye muuzaji wa gesimkubwa Ulaya, Marekani na Qatar wanataka wajengebomba la gesi lipite Syria liende Ulaya, Urusi hataki lijengwelitaharibu soko lake, anamwambia Assad weka ngumu,hakuna bomba kupita mimi nitakusaidia. Marekani nayenyewe inaingiza nguvu zake kumng’oa Assad. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kuwaambiaWaheshimiwa Wabunge, tunapozungumzia masuala yauchumi ni mazito na yanaingilia hadi na Mataifa. Leo hiiTanzania tumetoa maamuzi haya, Mataifa ya kibeberu nakibepari yatataka kutuingilia ndani. Nataka niwaambieWaheshimiwa Wabunge na Watanzania wote tumuungemkono Mheshimiwa Rais kwa maamuzi aliyoyafanya kwasababu atakumbana na vikwazo mbalimbali vingi na ili Taifaletu liendelee ni lazima tuwe na utulivu wa kisiasa, lazimawananchi tutulie na tuelewe nini tunataka kupata.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine unapatatabu Watanzania wanalalamika tunanyonywa, tunaibiwa,unapochukua maamuzi ya kudhibiti kunyonywa na kuibiwandipo watu wanaanza kugeuka tena. Mtu anaanza kusemaooh, kwa nini mnafanya hivyo? (Makofi)

Page 150: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nikiwa Naibu Waziriniliwahi kutoa tamko hapa Bungeni, nilitegemea Watanzaniawenzangu na Wabunge wenzangu asilimia kubwa waungemkono unyonyaji na unyanyasaji tuliokuwa tunafanyiwa naMataifa ya kibeberu, lakini Wabunge wengine humuwakasimama kuanza kutetea mabeberu. Tulikuwa tunajengabomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar-es-Salaam kuongezauwezo…

TAARIFA

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba hili jambo liwe clear kwenye statement hapaambazo watu wanatoa, hakuna Mbunge anayepinga walaanayesema tuendelee kuibiwa. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Wapo.

MHE. JOHN W. HECHE: Sisi wengine tunatoka kwenyemaeneo yenye migodi na waliohusika wengine ndiyo haowanaozungumza hapa.

WABUNGE FULANI: Kweli kabisa.

MHE. JOHN W. HECHE: Watu wetu wameuawa, kwahiyo, wasitu-provoke hapa. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa, nimeruhusu taarifa mojatu. Mheshimiwa Masele, unaikubali taarifa?

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nataka nimsaidie rafiki yangu Mheshimiwa Heche. Chakwanza jana kuna mtu amesema hapa ripoti ile ni rubbish.

Page 151: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

MBUNGE FULANI: Ndiyo.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,hauwezi ukapinga ripoti ya kitaalam na ya kisayansi kwamaneno, unaipinga ripoti ya kisayansi kwa kuja na ripoti ku-counter ripoti iliyotolewa. (Makofi)

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Mwenykiti,taarifa.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,lakini nataka nimwambie…

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuuliobaki ni mdogo sana, taarifa nimemruhusu MheshimiwaHeche, sasa Mheshimiwa Masele endelea. (Makofi)

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sisiwengine humu tumeshakuwa wakongwe. Natakanimwambie mimi nikiwa Naibu Waziri, Halmashauri zotezenye migodi Tanzania zilikuwa zinalipwa dola laki moja, dolalaki mbili. Nilisimamia kuhakikisha kwamba tunafuata sheriaza nchi ambapo Halmashauri zetu zinapata asilimia 0.3 yaturn over ya migodi hii, leo Halmashauri ya Geita inapatazaidi ya bilioni tatu kwa mwaka, ilikuwa inapata dola lakimbili tu. Haya mambo yanawezekana, tukiwabanawawekezaji wanaonyonya kwa mikataba nyonyaji tunawezakufanikiwa kupata mapato zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tufanye radicaldecisions, hatuwezi tukakaa mezani tunachekeana tukitakakupata mapato zaidi. Nchi za Afrika zinatia huruma, ukiendaKongo pale, leo Kongo…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Wewe endelea tu.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ukienda Kongo pale thamani ya madini ya Kongo kwa

Page 152: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

takwimu inaonesha ina thamani zaidi ya GDP ya EuropeanUnion lakini Kongo inaibiwa, watu wamekaa, wananchiwana shida. Leo Tanzania tumeweka mfano, Tanzania tume-set standard na wote tunatakiwa tumuunge mkonoMheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimetoka kwenyeVikao vya Bunge la Afrika, nchi nyingine za Afrika zinatuuliza,zinatusifia, zinamsifia Rais wetu na zina hamu aende akashirikikwenye mikutano ya kimataifa ili waweze kujifunza ninianafanya Tanzania. Kwa hiyo, ndugu zangu natakaniwaambie muda wa kunyosheana vidole huyu kafanya nini,kafanya nini, utatupotezea muda kama WaheshimiwaWabunge, ni vyema Waheshimiwa Wabunge tuanze kufikiriamapendekezo, maoni ambayo yataboresha ile task forceiliyoundwa na Mheshimiwa Rais ya kuboresha mikataba hii.Kama una maoni mazuri yaandike yapeleke kwa MheshimiwaProfesa Kabudi ili aweze kuyaingiza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mikoa yote yenyerasilimali haipati chochote, pelekeni mapendekezo angalauasilimia moja kinachovunwa kibaki kwenye mikoa husika ilimaisha ya wananchi yafanane na rasilimali zao. Leo ukiendaGeita maisha ya wananchi hayafanani na rasilimali zao.Ukienda Shinyanga almasi ile, maisha ya watu wa Kishapuna Shinyanga hayafanani. Ni lazima Serikali iamue kwamakusudi asilimia moja ama asilimia yoyote ambayoitaonekana kitaalam ibaki kwenye maeneo ya wananchi ilikuboresha maisha yao yafanane na rasilimali zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba na nimshukuruMheshimiwa Rais amelianzisha jambo, amelisimamia,amelifikisha mwisho. Kitendo cha watu wa ACACIA kujakukaa naye mezani maana yake sasa tunapata muafakawa matatizo tuliyokuwanayo. Unaweza ukalianzisha jambona usiweze kulisimamia, unaweza ukalianzisha jambo nausiweze kulifikisha mwisho, lakini tuna Rais ambaye nimtendaji, mtekelezaji, analianzisha jambo, analisimamia naanalifikisha mwisho. (Makofi)

Page 153: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoombaWaheshimiwa Wabunge na Watanzania wote tumuungemkono na tusimamie na tutambue kwamba hii vitatunayopigana siyo vita ndogo. Siyo vita ndogo kuanzia kwamakampuni, siyo vita ndogo kuanzia kwa Mataifa ya kibeberukwa sababu kazi yao iliyobakia ni kunyonya rasilimali za Afrika.Wanakuja na mbinu mbalimbali lakini Waafrika lazimatusimame tuoneshe mfano na Tanzania imeonesha mfano.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ishengoma,ajiandae Mheshimiwa Dkt. Getrude Rwakatare.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii yakuchangia bajeti ya Serikali. Nichukue nafasi hii kumshukuruMwenyezi Mungu aliyenipatia afya na kuweza kuchangiakwenye bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufulikwa kazi kubwa sana anayoifanya. Kwa kweli, ni mtuanayestahili kufanya mambo anayoyafanya. MheshimiwaRais akisema anatenda, Mheshimiwa Rais amefanya mambomengi kwa muda wa miezi 18 tu. Mheshimiwa Rais kwa kweli,kila mmoja anastahili kumpongeza kwa mambo yoteanayowafanyia Watanzania. Amejitoa yeye mwenyewena siyo yeye mwenyewe ni mkono wa Mwenyezi Mungu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana nanamwombea Mwenyezi Mungu azidi kumlinda na azidikumwongoza aweze kuishi maisha marefu. Hasa tendo hilila makinikia na kweli amelifanyia mambo mazuri, wenginewameanzisha lakini yeye mwenyewe nadhani atamalizia.Sasa hivi akikaa hivi karibuni mezani na hawa watu, fedha

Page 154: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

zitakuja, kila mmoja atatamani kuzitumia kwenye miradiyake. Kwa hiyo, naomba wote tuwe kitu kimoja, nchi yetu ninzuri, nchi yetu ya Tanzania ina amani, naomba tuwe kitukimoja hasa kushughulikia mambo haya yaliyo mbele yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri wa Fedhapamoja na Makatibu wa Fedha na Manaibu wake. Kwa kweli,bajeti hii ni nzuri sana, inawajali Watanzania, inawajaliwakulima…

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu ndani ya Bunge, please.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Inawajali watuwote kwa wastani. Kwa hiyo, tunashukuru kwa bajeti hii nzuriambayo mmetueletea ya shilingi trilioni 31.7 na kati ya hizowamesema asilimia 38 ni fedha za maendeleo. Naombahizi fedha za maendeleo ziweze kuja zote kamawalivyozipanga kusudi miradi ya maendeleo ile ambayo niviporo na ile ambayo bado iweze kutekelezeka. Kwa hiyo,naomba kitu kama hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya kati kwa ujenzi wastandard gauge, tunashukuru sana imeanza na wakandarasiwako tayari pale na itajengwa kwani tayari mkatabaumeshawekwa saini ya kutoka Dar-es-Salaam mpakaMorogoro. Wamesema bado mnatafuta wafadhili kwa relikuanzia Morogoro – Makutupora – Kigoma - Mwanza,naomba wafanye bidii sana kwa sababu reli hii inawasaidiawatu wote. Reli hii haitachagua chama gani itawabebawatu wote wa kanda hizo hizo, kwa hiyo, naomba Serikaliwaifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalopendakuliongelea ni tatizo la maji, kila mmoja humu anazungumziatatizo la maji.

Page 155: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

TAARIFA

MHE. KANGI A.N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. KANGI A.N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge ambayeanaongea ambaye amesema kwamba anampongeza Raiskwa kazi kubwa aliyoifanya takriban miezi kumi na naneambayo ni sawa na miaka miwili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimpe taarifakwamba Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambayealikuwa Rais wa Awamu ya Pili alikiri kwa kinywa chakekwamba kazi ambayo Mheshimiwa Magufuli ameifanya kwamwaka mmoja ni sawasawa na miaka 30. Kwa kuwa mudaalioutaja Mheshimiwa Mbunge ni takriban miaka miwilimaana yake kwa kauli ya Mheshimiwa Mwinyi ni sawasawana miaka 60. Kwa hiyo, naomba nimpe taarifa hiyo. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa endelea.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba unilindie muda wangu hata MheshimwaLowassa na yeye amemkubali Mheshimiwa Rais kwa kazikubwa anayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumzia tatizola maji, uwe Mbunge wa chama chochote kila mmojaanakiri kuwa ana tatizo la maji. Ilani yetu ya Chama chaMapinduzi inasema kuja kufikia mwaka 2020 asilimia 85 vijijiniwawe wamepata maji safi na salama na asilimia 95 mijininao wawe wamepata maji safi na salama ili kusudi tuwezekuwatua ndoo kichwani wanawake. Kwa hiyo, naombasana tena sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha hii ahadi iwezekutimilika maji yaweze kwenda vijijini. (Makofi)

Page 156: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana kwakufuta leseni ya magari. Hii bajeti imepokelewa na watuwengi…

TAARIFA

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, taarifa hii niya mwisho.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kwanza nimpe taarifa mama pale kwasababu…

MWENYEKITI: Hapana, hapana utamwita jina lake laKibunge.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Ishengomakwamba Mheshimiwa Lowassa hajamkubali Magufuli ilaalichokifanya ametoa taarifa kwamba Serikali ya CCM nasera zake ndizo zilizouza madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Kicheko)

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, siikubali hiyo taarifa, kama hajui kusoma aendeakasome aangalie ni kitu gani kinatendeka huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumziakufutwa kwa leseni ya magari. Nendeni kwenye mitandaoongea na watu wote, ongea na wasomi, ongea na kilammoja, hii kweli anaiunga mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu kutoaushuru wa Sh.40/= kwa kila lita ya mafuta…

Page 157: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tena upandehuu, naona zogo limezidi huku na nitaanza kutaja majina.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, nashauri Mheshimiwa Waziri wa Fedha hizi helaziweze kwenda kwenye Mfuko wa Maji. Nikiwa mwanamkenasisitiza hilo kwa sababu najua shida ya wanawake ambaowanatafuta maji pamoja na watoto wao, hizi hela ziwezekwenda kwenye Mfuko wa Maji. Nasisitiza kuwa asilimia 30ya hizi fedha ziweze kwenda mjini pamoja na asilimia 70ziende vijiji. Nasema hivi kwa sababu mjini inaweza kutokeataasisi zingine zikasaidia kugharamia maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo,asilimia 65 ya wananchi wanategemea kilimo na malighafinyingi zinatoka kwenye kilimo. Kwa hiyo, namwomba sanasana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, fedha zilizotengwakwenye kilimo ahakikishe zote zinakwenda kwenye kilimo kwasababu bila ya kilimo hakuna viwanda, chakula na lishe niduni. Kwa hiyo, naomba sana hizi hela ziweze kutoka zotetuweze kuinua pato la familia pamoja na pato la Taifa nahasa tukazanie kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa sababuwameweza kutoa tozo mbalimbali kwenye pembejeo naushuru wa mazao asilimia tatu kwa bidhaa za biashara naasilimia tatu kwa bidhaa za chakula. Hata hivyo, katikamikoa mingine, kwa mfano, Morogoro tunalima mahindi,mpunga na viazi yote yanafanana ni biashara pamoja nachakula. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri tozo iwemoja kwa zao moja, iweze kufanana kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo tani moja ambayowamesema kuwa kama unasafirisha kutoka Halmashaurimoja kwenda Halmashauri nyingine ushuru umefutwa.Mheshimiwa Waziri akija kuwa-wind up hapo awezekulifafanua kwa sababu kuna wakulima wengine kwa mfanonakaa Manispaa ya Morogoro lakini nalima Halmashauri yaMorogoro Vijijini na ukisema tani ni magunia kumi, maguniakumi kwa wakulima wa kisasa wanavuna mpaka magunia

Page 158: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

ishirini, je, tozo itakuwaje na mimi ni mkulima siyomfanyabiashara, nimevuna magunia yangu ishirini utanitozaushuru? Naomba sana Mheshimiwa Waziri aliangalie kusudiaweze kutushauri vizuri kama ushuru utakuwepo au hapana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakwenda kwenye ufugaji,wafugaji kusamehewa malighafi ambayo inatengenezachakula cha kuku, naishukuru sana Serikali na naipa pongezi.Wananchi wote ambao wanafuga kuku na hasa wanawakeitawasaidia sana katika kufuga kuku na itasaidia kuongezakipato, lishe pamoja na ajira hasa kwa vijana ambaowanamaliza shule na hawana kazi. Ushauri wangu, naombawaangalie mazingira mazuri ya kukopa na hasa Benki yaKilimo pamoja na Dirisha la TIB, hela zote hizo walizozitengaziweze kutolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, msamaha wa Kodi yaOngezeko la Thamani kwenye mayai yanayototoleshwa nayenyewe inasaidia sana wafugaji. Wale wafugaji vifarangavilikuwa bei ya juu sasa kwa kufanya hivyo bei ya vifarangaitapungua na gharama pia itapungua, pato litapanda nalishe pia litapanda. Ushauri wangu ni kama huo huowaangalie mazingira mazuri ya ukopaji na hasa Benki yaKilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naongelea kuhusu shambala kilimo Mkulazi na Mbigiri ambayo tayari yako kwenyemchakato wa kujenga viwanda vya sukari na kilimo chasukari. Nashauri waangalie out growers, hawa wakulimawetu wa Morogoro ambao wanazunguka mashamba hayowatafaidikaje? Naomba waangalie kusudi na wenyewewaweze kuwa kwenye mpango wa kupata na ajira itaongezekwa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mapato, kwa kwelinashukuru kuwa Sh.10,000/= ambayo wameiweka kwenyenyumba ambayo haijathaminishwa pamoja na Sh.50,000/=kwa nyumba ya ghorofa itasaidia kuongeza mapato yetuna hasa mapato ya ndani ambapo itasaidia kufanyamipango yetu ya maendeleo. Ila Mheshimiwa Waziri kama

Page 159: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

maswali yalivyokuwa yanaulizwa akija ku-wind-up aelezeekuwa tumeanza na hizi za Manispaa na Halmashauri ni linina ni nyumba ya aina gani ambayo itatozwa Sh.10,000/=kama Wabunge wenzangu walivyouliza.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Rwakatare,ajiandae Bhagwanji Meisuria.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kuniona. Pia nashukuru kwa kaziyako nzuri sana ya kiwango unayoifanya, Mungu akubariki.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napendanimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa zawadi adimu yaRais wetu wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli. Kwa kweli Rais Magufuli anastahili pongezi za dhati.Kama mtu haoni alichokifanya basi hana macho, huyu nikipofu. Kama kweli yeye ni Mtanzania anasimama hapa sikuzote anapinga ufisadi, anapinga mambo mabaya, halafutena haoni alichokifanya, basi huyu mtu siyo Mtanzania halisianajifanya tu. Inabidi tumwombee Rais wetu kwa hali namali. Katika Isaya 54:17, unasema; kila silaha itakayoinukajuu yake isifanikiwe kwa Jina la Yesu. Kila ulimi utakaosimamakumpinga, tunaupinga wenyewe kwa Jina la Yesu.

WABUNGE FULANI: Ameen, Haleluya.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, kwa taarifa fupi Jumapili ni Ibada Maalum yakumwombea Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli, kuombea

Page 160: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Taifa letu na Bunge letu. Tutakuwa Mikocheni B, Kanisa laMlima wa Moto, njooni jamani tukutane na Mungu aliye hai.

WABUNGE FULANI: Ameen.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, kuna watu wanabisha, wanapinga…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

WABUNGE FULANI: Aaaaaa.

MWENYEKITI: Kaa chini, kaa chini, kaa chini.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: Hata kamaunabisha lakini Mzungu si mmemwona, Mzungu si amekuja,amekuja mwenyewe… (Makofi)

MBUNGE FULANI: Bila kuitwa.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: Ndiyo, bilakuitwa kwa tiketi yake. Amesema amekuja na ndege yakemwenyewe.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Taarifa tafadhali Mheshimiwa.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: Sasa kamaamekuja kukubali yaishe kuna ubaya gani?

WABUNGE FULANI: Hakuna. (Makofi)

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: Si lazimatujipongeze. Hata kwa yale mazuri jamani pia tunapinganakwa vipi? Amekutana Ikulu, kumbe ulitaka akutane naye wapiFeri, Kariakoo au Buguruni au wapi? Nyumbani kwake si Ikuluamekutana naye, ni vizuri na wote tunashukuru, Munguamejibu maombi.

WABUNGE FULANI: Ameen. (Makofi)

Page 161: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: Wasemewasiseme lakini hata nchi j irani wote wanasema,wanatupigia simu hongereni Tanzania, hongereni kwa kazinzuri, hongereni kwa Rais mzuri. Kwa hiyo, lazimatumpongeze sana, amejitahidi kwa muda mfupi kaondoawafanyakazi hewa, amegundua makontena ya mafisadi,amenunua ndege, amejenga barabara na kadhalika, silazima tumshukuru. Mnataka nini jamani gunia la chawa auawabebe mgongoni? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ametoa vifaa tiba Wilayazote na ambulance amejitahidi kama mwanadamu. Elimubure, jamani kazi alizofanya ni kama miaka 60, miminaongeza na 30 kama miaka 90, Mungu ambariki sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye bajeti yetu,napenda kuipongeza bajeti kuu ya Wizara ya Fedha chini yaMheshimiwa Dkt. Mpango na Naibu Waziri wake, kwa kwelini bajeti ya kihistoria iliyoacha simulizi mitaani. Ni bajetiiliyomjali hata mtu wa chini, mnyonge hadi mama lishe hadimfanyakabiashara ndogo ndogo, wote wameguswa. Njewenzetu wanafurahia lakini hapa ndani watu wanabisha.Sasa walengwa wamefurahia lakini wewe kwa sababu siyomlengwa ndiyo maana hata wala huoni umuhimu wake,pole. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tazama jinsi alivyowezakufuta road licence, tazama jinsi ilivyoweza kupunguza kodimbalimbali yaani ili mradi wamefanya walichoweza. Jamanikuna mabadiliko mabwa mwaka huu. Watu wanasema nimwaka wa neema, ni bajeti ya neema wamefanya kileambacho walichoweza kufanya, lazima tuwapongeze.Mheshimiwa Dkt. Mpango hongera sana, pongezi nyingina mama pale, pongezi nyingi na Wizara nzima kwakazi nzuri na mabadiliko makubwa waliyoyaleta.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie jambomoja ambalo ni kodi kwa ajili ya shule binafsi nikisema

Page 162: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

kwamba mimi pia ni mdau mmojawapo, na- declare interest.Mheshimiwa Waziri Dokta Mpango kodi katika shule binafsizimezidi. Kuna kodi zaidi ya 25, mpaka unashangaa sisi nasitunachima madini au nini, wakati sisi tunafundisha watotowenu. Waangalieni sana kodi ni nyingi hata akikaa na timuyake ingetakiwa wafute kodi zote katika shule kwa sababushule ni huduma siyo biashara na huduma tunazofanya nikwa faida ya Taifa zima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto hawa walikuwawanakwenda Kenya, Uganda na nchi nyingine za jirani lakinisisi tumefanya hawa watoto wasome Tanzania, wawezekujifunza historia yao, wajifunze jiografia yao, wajue viongoziwao, lakini zamani walivyokuwa wanakwenda nchi jiraniutakuta akiulizwa wewe Rais wako nani, inabidi aseme UhuruKenyatta. Kwa sababu akisema mimi Rais wangu Dokta JohnPombe Magufuli atakoseshwa, japo yeye ni Mtanzania yukonchi ya kigeni, lakini sisi tumeleta fikra za watotokubadilika kwa kusoma wakiwa wadogo ndani yanchi baadaye wakiwa wakubwa ndiyo waende siyo mbaya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi mtusaidieyaani jamani tunachajiwa hata majengo, tunaambiwaproperty tax, hasa yale majengo si ya shule, si watoto wenundiyo wanasoma? Mbona shule za Serikali hawatozi kwa ninisisi tu ndiyo mtutoze? Unaambiwa hata vile viwanjatumejenga shule wanakuambia bwana lazima ulipe kodikama vile kiwanja cha biashara yaani kama kiwanjaumefanyia biashara kubwa fulani. Hakika wakitusaidia katikahilo itakuwa ni unafuu kwa ajili yetu na hata kwa ajili yawatoto wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakiangalia wenyewe ilekaro tunayotoa ni ndogo mno. Watoto hawa wanakunywachai asubuhi, saa nne wanakunywa tena na wenzao wa dayscholars, mchana wanakula chakula, jioni wale boarderswanakula mlo kamili, sasa hivi vyakula vyote ni gharama.Vilevile wanapewa magodoro na vitanda, wana matron napatron wanaowalinda, kuna daktari na manesi

Page 163: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

wanaowatunza watoto wetu ili wakae vizuri. Waangaliewatuhurumie, watusaidie tufanye kazi pamoja kwa sababuhapa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. MCH. DKT. GETRUDE J. RWAKATARE: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja mia kwa mia. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaBhagwanji Meisuria, ajiandae Mheshimiwa LolesiaBukwimba.

MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana, Mungu akuweke. Nimepatanafasi hii kuzungumzia bajeti yetu ya Serikali. Nataka nisemesisi Wabunge wote hakuna ubaguzi wa rangi wala Kabilatunaunga mkono bajeti ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza MheshimiwaWaziri pamoja na Naibu wake. Hicho kitabu alichoandikacha bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango, namuungamkono, Mungu amweke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana sanaMheshimiwa Rais wetu Dokta John Pombe Magufuli,amefanya kazi nzuri, kwa sababu tulikuwa tunadhulumiwamadini yetu yanakwenda nje. Mungu ameweka neema yakeawamu yake akafanya vizuri na anasaidia kuondoa umaskini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wetuMagufuli amefanya mambo mengi, ujenzi wa barabara,uwanja wa ndege na ameleta ndege mbili na analeta ndegenyingine nne. Hayo yote yatasaidia kuondoa umaskini kwasababu itaongeza mapato. (Makofi)

Page 164: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Mheshimiwa Mwenyekiti, akinamama wa Zanzibarpamoja na Watanzania wote wamechoka kubeba mizigoya maji, pesa hizo zitasaidia wananchi wetu wa Tanzaniatutoke kwenye umaskini twende katika hali nzuri. Inshallah,Mwenyezi Mungu atampa nguvu Rais wetu MheshimiwaMagufuli na ataondoa shida zetu zote na maji yatapatikanakwa kila mmoja wetu, Zanzibar pamoja na Bara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia Halmashauri,Halmashauri zetu wanakusanya pesa, tuwasimamie vizurilakini naomba Serikali zile pesa milioni 50 tuzipeleke kwenyeHalmashauri. Wananchi wanangoja kwa hamu pesa zilekwani zitasaidia kuondosha umaskini na tutasaidia wale watuwaliokuwa na shida kwenye ushirika, asilimia nne au tanowalikuwa wanapata na kukopeshwa basi Serikali isaidie.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pamoja na Rais wetuamefanya kazi nzuri kwa kuanzisha mabasi ya mwendokasi,Watanzania wamekuwa wakifaidika. Pia tunaingiza pesachungu nzima na pesa hizo tutaziweka katika kilimo, majipamoja na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni viwanda, kwelinasema Serikali inajitahidi kusimamia viwanda. Kwa kuwana viwanda itasaidia sana wananchi na vijana wetu kupataajira na ajira ni muhimu kwa Tanzania yetu. Kwa kuanzishaviwanda mbalimbali mapato ya Taifa yataongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TRA yetu lazima isimamieukusanyaji wa mapato. Mapato yapo kwenye viwanda, sektaya utalii na bandari, haya yote tuyasimamie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine naomba Serikaliyangu ya Muungano tuwasaidie watu wa Zanzibar.Mwenzangu Mheshimiwa Rehani amesema lakini mimi nazidikusema sisi wote ni ndugu moja, hakuna upinzani walaubaguzi. Wale watu wanyonge kutoka Zanzibar wanaletabiashara ndogo ndogo, wanatoa ushuru kule lakini ikifikahapa wanahangaishwa, basi tuwatazame na tuwaachie.

Page 165: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Wazanzibar tuwaache wafaidike kwa sababu kule Zanzibarunalipa ushuru namna mbili, ZRB pamoja na TRA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri tuboreshe biashara za viwanda. Kama tutasimamiakweli Tanzania yetu tutapata mapato mengi sana, asidharau.Vilevile tunataka tufufue viwanda vyetu, wale watuwanakuja kutoka nchi za nje wanataka kuanzisha viwandatuwapokee. Hii ni kwa sababu vijana wetu watapata ajirana kuondokana na umaskini. Vijana wakifanya kazi nanyumbani akipeleka chochote itasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kitu kimoja,sisi Zanzibar pamoja na Tanzania yetu tuna mambo mengisana ya kusaidia kuingiza pesa. Tanzania tunazalisha mazaokama kunde, choroko na dengu, tunao watu kutoka nchiza nje kama India wanakuja kununua tuwakaribishe. Sisitunataka maendeleo na mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru MheshimiwaWaziri ameondoa kodi katika mazao ya kilimo kwa tanimoja. Vilevile ameondoa kodi kwenye magari, tunamshukurusana Mungu amweke. Serikali yetu inataka kufanya mambo,tumuunge mkono Rais wetu Mheshimiwa Dokta John PombeMagufuli kwa sababu Mheshimiwa Waziri… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bhaghwanji, mudawako umekwisha. Tunaendelea na Mheshimiwa Lolesia.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kwa kunipa nafasi ili na mimi niwezekuchangia katika bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongezasana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kazi kubwaambayo ameendelea kuifanya ndani ya Taifa letu hasa katikasekta ya madini, ameanza kuonyesha mfano. Kwa kipindi

Page 166: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

kirefu sana kumekuwepo na malalamiko mengi kwawananchi na watu mbalimbali na NGOs kuhusiana na sualala madini. Kwa kweli Mheshimiwa Rais amefanya kitu kikubwacha ujasiri kuweza kuchukua hatua thabiti na kuweza kuonanamna ya kukwamua mambo ya rasilimali katika Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ambao tunatokamaeneo ya madini tunaona jinsi ambavyo tunaachiwamashimo. Ukienda kwa mfano GGM watu wanachimbamadini kwa kiwango kikubwa lakini wananchi waliopo jiranina maeneo hayo hatuoni faida zaidi katika madini hayo.Kwa hiyo, kwa hatua ambazo Mheshimiwa Rais amechukuamimi binafsi pamoja na wananchi tunampongeza sanaMheshimiwa Rais kwa kazi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mwimbaji mmojaalisema kwamba niseme nini Bwana. Kwa kweli hata miminasimama hapa leo kuimba kusema niseme nini Bwana kwakazi kubwa ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya katika Taifaletu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niendelee sasakuomba kwamba mikataba iendelee kuletwa hapa Bungeniili tuweze kuipitia kuona namna ya kuwezesha zaidi rasilimaliza Taifa hili ili tuweze kufaidika sisi wananchi wa Taifa laTanzania. Sambamba na mikataba lakini pia ziangaliwesheria ambazo zipo pamoja na sera, kama hazitupelekimahali ambapo tunastahili, tuweze kuzifanyia kazi nakuzirekebisha ili wananchi tuendelee kufaidika zaidi narasilimali ambazo Mungu ametupatia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kutoamsisitizo pia kwenye usimamizi wa maliasili zetu. MheshimiwaRais ametuonesha mfano na viongozi wengine tuendeleekuonyesha mfano, tuwe wazalendo kwa Taifa letu. Kwa hiyo,niombe tu kwa ujumla sisi sote kwa pamoja wananchi naWabunge tusimame imara tukiendelea kumuunga mkonoMheshimiwa Rais lakini pia hata sisi wenyewe tuwezekusimamia kwa dhati rasilimali za Taifa letu. (Makofi)

Page 167: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri kwa uwasilishaji mzuriwa bajeti ya mwaka huu 2017/2018. Kama ambavyowenzangu wametangulia kusema ni bajeti ya mfano. Ni bajetiambayo kwa kweli ukiisoma inafurahisha na wananchi wengitumeifurahia bajeti hii. Mimi nasimama kwa niaba yawananchi wa Jimbo la Busanda kumpongeza MheshimiwaWaziri kwa bajeti nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu gani?Wananchi walio wengi hasa vijijini walikuwa wanatesekasana na vikodi vidogo vidogo lakini bajeti hii imewezakuondoa hizi kero. Mwananchi alikuwa anaenda kuuza gunialake la mahindi analipa kodi, lakini kwa jinsi ambavyo bajetihii imeweza kuondoa kodi ndogo ndogo, kwa kweli nichukuenafasi hii kwa niaba ya wananchi kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri pamoja na Wizara kwa ujumla kwamambo makubwa ambayo ameyafanya kwa wananchiwetu na kwa Taifa zima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika bajeti tunaonajinsi ambavyo imejikita katika kuangalia miundombinumuhimu kwa ajili ya kujenga uchumi kuelekea kwenyeviwanda. Tanzania ya viwanda inahitajika tuwe na reli natayari kwenye bajeti imo, tunaenda kujenga reli ya standardgauge. Kwa hiyo, nipongeze kwa kweli kwa jinsi ambavyoameangalia mifumo ya kiuchumi ikiwepo reli, maji naumeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tu msisitizo zaidi katikasuala la maji. Katika bajeti mmeonyesha jinsi ambavyomtaangalia vyanzo vya maji kwa mfano kwenye maziwamakubwa kama Ziwa Viktoria, Tanganyika na maziwamengine. Kwa hiyo, niombe sasa katika utekelezaji wa bajetituhakikishe wananchi walio kandokando ya maziwa, kwamfano, mimi Jimbo langu la Busanda lipo kandokando yaZiwa Viktoria lakini hatuna maji. Kwa hiyo, nitumie fursa hiikuomba sasa utekelezaji, wananchi waweze kupewa majiya kutosha na ya uhakika. (Makofi)

Page 168: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iweke utaratibu mzuriwa kuweza kutenga hizi fedha ikiwezekana tuwe na MfukoMaalum wa Maji, kama jinsi ambavyo REA iko katika sualala umeme, inapeleka umeme vijijini, hata katika suala la majituangalie kuwa na Mfuko Maalum kwa ajili ya kusaidiaupelekaji wa maji vijijini. Vijijini ndiyo kuna changamotokubwa sana ya suala la maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia kumtuandoo mwanamke ni hasa wanawake waliopo vijijini. Kwahiyo, niiombe Serikali sasa ituwezeshe kuwa na Mfuko Maalumkwa ajili ya maji ili utuwezeshe kutekeleza miradi ya majikatika vijiji vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa umeme,mimi napenda kuishukuru Serikali kwa mipango thabiti nandiyo maana nasema nitaiunga mkono bajeti hii ya Serikali.Hii ni kwa sababu katika upande wa umeme Serikaliimejipanga vizuri kupeleka umeme vij i j ini na tayaritumeshapata wale wakandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoomba sasa umemehuu tunapofikisha kwenye vijiji vyetu, tuhakikishe unafikakwenye taasisi muhimu za umma zikiwepo shule za sekondari,shule za msingi, vituo vya afya na zahanati ili kuwezeshawananchi kupata huduma vizuri kwa sababu kuna hudumamuhimu ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika suala laumeme, naomba Serikali iangalie uwezekano miradi hii ianzemara moja, kwa sababu wananchi wamesubiri umeme kwamuda mrefu na wanahitaji umeme ili waweze kuwa naviwanda vidogo vidogo. Vilevile wachimbaji wa madini nawafanyabiashara wanahitaji umeme. Kwa hiyo, naombasana utekelezaji mara tutakapopitisha hii bajeti uanze maramoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika bajetitumezungumzia suala la elimu kwamba tutatoa mikopo kwawatoto wetu kwa masomo ya elimu ya juu. Napenda

Page 169: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

kuipongeza sana Serikali, tunaomba utekelezaji huo ufanyikeili watoto waweze kupata mikopo na waweze kuendeleana masomo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, ni vizurikuwa na Vyuo vya VETA. Kwa mfano, kwenye Mkoa wa Geitahatuna Chuo hata kimoja cha VETA. Nitumie fursa hii kuiombaSerikali kupitia Wizara ya Elimu, hebu hakikisheni basi tunakuwana Chuo cha VETA katika Mkoa wa Geita. Wilaya zote tanohatuna VETA hata sehemu moja na pia katika mkoa hatunahata VETA moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe sasaSerikali iangalie kutoa kipaumbele kwa mikoa na sehemuambazo hawana kabisa huduma ya VETA. Hapotutawazesha vijana wetu ambao ni wengi wanamalizasekondari kupata ujuzi na hatimaye kuweza kuanzishabiashara zao na kujimudu katika maisha yao ya kila siku.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la zahanatipamoja na vituo vya afya, ni Sera ya Taifa inasema kwambakila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya.Ninachoomba sasa Serikali iangalie uwezekano wakuendelea kutimiza, kweli imetenga fedha, lakini tuhakikishezinafika kwa wananchi kwa wakati hasa katika Halmashaurizetu ili kazi iweze kufanyika, wananchi tuweze kujengazahanati kwenye kila kijiji kama ambavyo Sera ya Taifainasema, lakini vilevile kuwa na kituo cha afya kwenye kilakata na hospitali kwenye kila wilaya. Vilevile kuboreshahuduma zote ambazo ni za muhimu ili wananchi wetuwaweze kuwa na huduma bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kodi kwawachimbaji wadogo wa madini. Napenda tu kuombaWizara ya Fedha hebu tuiangalie hii kodi, haiwezekani hawawachimbaji wetu wadogo tuanze kuwatoza kodi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

Page 170: NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ...parliament.go.tz › polis › uploads › documents › 1522158880... · Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tunayo Sera ya Elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, orodha yavyama vyote iliyokuja mezani imekwisha na muda wetuumekwisha, niwashukuru kwa kazi nzuri. Sasa naahirishashughuli za Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.

(Saa 11.54 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Ijumaa,Tarehe 16 Juni, Saa Tatu Asubuhi)