pastoralist integrated support programme · pdf fileshirika la pisp lilisajili mnamo 1996 ili...

10
Kenya PASTORALIST INTEGRATED SUPPORT PROGRAMME (PISP) Empowered lives. Resilient nations. Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

Upload: vannhi

Post on 31-Jan-2018

289 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Kenya

PASTORALIST INTEGRATED SUPPORT PROGRAMME (PISP)

Empowered lives. Resilient nations. Empowered lives. Resilient nations.

Miradi ya EquatorWanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

WahaririMhariri Mkuu : Joseph CorcoranMuhariri Meneja : Oliver HughesWahariri Waliochangia : Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniEquator ingependa kuwashukuru wanachama wa Pastoralist Integrated Support Programme (PISP) na haswa mwongozo na mchango wa Ali Doti. Picha ni za PISP, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa kwa Kiswahili na Dr. Ken Ramani.

Nukuu ZiadaUnited Nations Development Programme. 2012. Pastoralist Integrated Support Programme (PISP), Kenya. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

MAELEZO KUHUSU MRADI HUUKatika sehemu kame ya Marsabit iliyomo kaskazini mwa Kenya, maisha ya wafugaji wa kuhamahama yametishiwa na ulishaji uloikithiri, ulimaji, uhasama wa kikabila na mabadiliko ya hali ya hewa. Shirika Mseto la Kuwasaidia Wafugaji wa kuhamahama (Pastoralist Integrated Support Programme- PISP) ambalo ni shirika lisilo la kiserikali, limefanya kazi tangia mwaka 1996 ili kuongeza vituo vya maji safi na ya kutegemewa kwa wanyama na binadamu, pamoja na kupiga jeki uhifadhi wa wanyama pori katika mbuga ya kitaifa ya Marsabit na maeneo ya karibu.Juhudi hizi za kuimarisha ulishaji mifugo pamoja na kuwatafutia mbinu mbadala wa kujipatia riziki wafugaji zimesaidia dhidi ya wao kutotegemea rasilimali ya ardhi jambo ambalo limepunguza uhasama wa kikabila. Isitoshe, jamii tofauti zimeanzisha mazungumzo baina yao ili kupata mwafaka wautumiaji wa rasilimali ya maji na namna ya kuepuka vizingiti vya maisha yao ya kawaida.

MUHTASARIMSHINDI WA TUZO YA EQUATOR: 2004

ULIANZISHWA: Mwaka 1996

ENEO: Marsabi, Kaskazini mwa Kenya

WANAOFAIDI: Zaidi ya wafugaji 11,000

MAZINGIRA: Uhifadhi wa Malisho

3

PASTORALIST INTEGRATED SUPPORT PROGRAMME (PISP) Kenya

YALIYOMOHistoria na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 6

Matokeo ya Kimazingira 8

Matokeo ya Kijamii 8

Matokeo ya Kisera 8

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 9

Maono 9

Wahisani 9

4

PISP ni shirika lisilo la kiserikali ambalo ufanya kazi katika eneo kubwa la Marsabit Kaskazini mwa Kenya. PISP linajaribu kupunguza umasikini unaosababishwa na makali ya kiangazi miongoni mwa jamii za kuhamahama ambazo zinaishi maeneo haya yaliyotengwa nchini Kenya. PISP hutafuta mbinu za kuwapa maji, kazi ndogo ndogo za kujichumia riziki, kuunga mkono juhudi za elimu na kupunguza uhasama kati ya makabila tofauti katika eneo hili. PISP hufanya kazi katika maeneo ya kati na kaskazini ya Marsabit, Laismis na Chalbi ambapo asilimia 97 ya ardhi inatumika kama malisho. Sehemu hii ni kame, isiyo na rotuba, tambalale, iliyo na vichaka vilivyo tapakaa, majabali yaliyobomoka na vijilima vya kivolikano kama; Mlima Kulal (mita 2230) mlima Marsabit (mita 1700) na Harri hills (mita 1310).

Maeneo mengi ya sehemu hii hupata mvua takribani milimita 300 kwa mwaka ilihali maeneo ya miinuko hupata mvua mara dufu. Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, kumekuapo na upungufu wa mvua, lakini kiwango cha unyevunyevu ubadilika mwaka hadi mwaka. Mabadiliko ya hali ya hewa yamechangia mafuriko na kiangazi cha mara kwa mara katika eneo hili. Maji ya ardhini na yale ya juu ya ardhi huelekea mashariki ya mto Jubba, magharibi kuelekea Ziwa Turkana na kaskazini kuelekea jangwa la Chalbi.

Maisha ya wafugaji wa kuhamahama

Makabila ya Waburji na Warendile hujishughulisha na kilimo kwa kiwango kidogo katika maeneo ya mlima Marsabit. Hata hivyo jamii nyingi katika eneo hili hujishughulisha na ufugaji wa kuhamahama ili kupata riziki na vilevile kama desturi yao. Jamii hizo ni kama; Gabra, Konso, Wata na Borana. Ufugaji wa kuhamahama ulizuka katika eneo hili kwa sababu ya kiangazi – ni mifugo tu wanaoweza kufanya vyema katika eneo hili. Baadhi ya taabu na mwenendo wa wafugaji huwasaidia kuhimili mishtuko na mahangaiko yanayosababishwa na ukame. Jamii nyingi hutunza maji na huweka nyasi ili kuokoa mifugo wakati wa kiangazi. Tangu zamani, jamii ya Waherega walikua wakitunza sehemu za chemichemi ndiposa kutumiwa na mifugo wakati wa ukame. Wafugaji vilevile hufuga mchanganyiko

wa mifugo kulingana na mahitaji yao ya maji; Ng’ombe huitaji maji baada ya siku mbili, mbuzi na kondoo wanaweza kwenda bila maji kwa siku nane na ngamia huvumilia bila maji hadi siku kumi na kumi na moja. Ngamia anaweza kuvumilia ukame zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote – anaweza kutembea mwendo wa kilomita 50 akila nyasi huku akitafuta maji.

Ingawaje wafugaji huhitaji maji , mifugo ndo muhimu kwao kwa sababu wao hutegemea maziwa kwa asilimia 60 kama chakula chao. Wakati maziwa yanapopungua, wao huchanganya maziwa na damu. Aidha, mifugo changa huchinjwa, huuzwa au kubadilishwa na bidhaa kama vile mahindi, sukari na majani. Wafugaji huwa na mifugo wanaolishwa nyumbani na wengine hupelekwa mbali malishoni ndiposa wahifadhi nyasi iliyo karibu na nyumbani , wapate wakati wa kufanya kazi za nyumbani na kuepukana na kisirani cha kuangamia kwa mifugo wote kutokana na hulka hiyo ya kuhamahama. Ili kuhimili ukame, kwa sasa jamii za eneo la Marsabit wana idadi ya watu na mifugo inayokisiwa kuwa; watu 144,739, ng’ombe 150,000, kondoo 460,000, mbuzi 360,000, ngamia 100,000, punda 20,000 na kuku 20,000.

Ruwala na vipindi tofauti tofauti vya uhamaji huipa nyasi na majani kuota na kukua. Wafugaji hulisha mifugo yao milimani wakati kuna mvua nyingi na hulazimika kupeleka mifugo chini milimani mahali pana mkusanyiko wa maji. Wafugaji wanapohamia sehemu tambalale, mifugo wao hutegemea nyasi na matawi ambayo aidha hung’ang’aniwa na wanyama pori ambao hufuata mkondo kama wa wafugaji. Wafugaji na mifugo wao huhatarisha maisha ya wanyama pori kama vile; punda milia,chui, twiga na kadhalika.Ndovu, hata hivyo, ndiye huzua mtafaruko kwa kuharibu mimea na kuua watu na wanyama.

Katika miaka ya hive karibuni, hali katika eneo la kaskazini mwa Kenya imetikizwa kutokana muongezeko wa shughuli za kibinadamu pamoja na misukosuko ya kimazingira. Matatize sugu ni pamoja na; ukosefu wa usalama, ongezeko la idadi ya watu, magonjwa na

Historia na Mandhari

55

wizi wa mifugo. Ukosefu wa mvua na nyasi kutokana na ukame, hususanule wa miaka ya 1997, 1999, 2000, 2005, 2006 na 2011, umechangia kuathirika kwa desturi na taasisi za wafugaji. Aidha, ukosefu wa sera mwafaka kutoka kwa serikali kuhusu mazingira na uchumi, umewalazimisha wafugaji kuhamia sehemu tambarare ili waweze kunufaika kutokana na kupatikana kwa maiji, msaada wa chakula,elimu ya msingi na huduma za kimatibabu. Aidha, watu huhamia sehemu tambarare kuepuka kuibwa kwa mifugo wao na majangili wenye bunduki kubwa kubwa wakitokea mataifa jirani.

Shirika la PISP linafanya kazi kwenye eneo lenye umasikini mkubwa. Idadi ya vifo vya watoto iko juu mno. Katika idadi ya watoto 1000, 62 hufa kabla ya kufikia miaka mitano. Aidha, watoto wengi kati wenye umri wa miaka tano na sita hukosa kukua sababu ya utapiamlo.Mpango wa maendeleo ya wilaya ya Marsabit ya 2005-2015 unaonyesha kwamba asilimiia 86 ya wakaazi huko hutegemea chakula cha msaada na asilimia 73 husafiri kwa muda mrefu wakitafuta maji na kazi nyingi hufanywa na akina mama. Asilimia kubwa ya watu hawapati maji safi ya kunywa na watu wengi hawana vyoo na hivyo hulazimika kutumia misitu kujisaidia.

Changamoto za wafugaji zimechangiwa na serikali isiyotilia maanani maisha magumu yao. Mfano ni asilimia 62 ya watoto ambao uhudhuria shule za msingi lakini wanapohitimu kuingia shule za sekondarihe ambao hupata nafasi. Idadi hiyo ndogo yaonyesha kuwa mfumo wa elimu haujali kamwe maisha na hulka ya wafugaji. Vilevile, kampuni nyingi hazijabuni huduma za kifedha zinazoana na maisha ya ya wafugaji. Benki nyingi hazikubari wafugaji kutumia wanyama kama dhamana ili kupata mikopo. Miundo msingi mibaya imesababisha bidhaa za wafugaji kutofika sokoni; vilevile wafugaji huuza mifugo wao kwa hasara wakati wanatishiwa na kiangazi. Eneo lote la Marsabit huwa halina barabara nzuri wala huduma za usafiri za kuridhisha.

Shirika la PISP lilisajili mnamo 1996 ili kushughulikia tatizo la huhifadhi na usambazaji wa maji lakini kwa sasa, PISP imeanza kushughulikia matukio mengine yanayoathiri jamii za wafugaji kama; kubadilika kwa hali ya hewa, kupunguza umasikini na utunzi wa mazingira.

6

Majukumu Makuu na Ubunifu

Mwanzoni PISP ilinuia kutambua matatizo ya wafugaji na kuwapelekea maji lakini kufikia mwishoni mwa 1997, wazee waanzilishi wa PISP walitembea sehemu fulani nchini wakidadisi ujuzi wa kuwapelekea maji wakaazi wa Marsabit. Walirudi nyumbani wakiwa wamesoma namna ya kujenga mabwawa au tanki ardhini na namna ya kuteka maji ya mvua. Kwa sasa, PISP inajishughulisha na kujenga, kukarabati na kuimarisha utekaji maji.

Kukabiliana na uhaba wa maji

Licha ya kujenga vianzo vya maji, PISP huwafunza mafundi namna ya kukarabati na kuifadhi vianzo hivyo vya maji. Nao wazee kutoka koo mbali mbali hufunzwa umuhimu wa kuishi na kutumia maji pamoja. Makundi ya utunzaji wa maji yameundwa ili kuwafunza watu umuhimu wa usafi. Wakati wa kiangazi wa miaka ya 1997, 2000 na 2005 na 2006, PISP waliwapatia wanakijiji takriban tanki 120. Aidha, PISP ilinunua wanyama kutoka wafugaji wale walioonekana wamelemewa na ukame na kuwachinja kisha kuwagawia nyama wafugaji. Kwa kufanya hivi, PISP iliweza kupunguza mahitaji ya malisho na maji kwa wanyama katika eneo hilo.

Kupunguza umasikini

Kwa miaka ya hivi karibuni,shirika la PISP limepanua mbinu zake za kupunguza umasikini miongoni mwa wafugaji. PISP imeazinsha mikakati ya kudumu ya kuzuia majanga moingoni mwa wafugaji kuliko ile mbinu ya kitambo ya kuzima janga pindi litokeapo. Shirika hili husaidia wafugaji kwa kuimarisha ufugaji wao, kukuza malisho na kuwawezesha kupata mikopo midogo midogo. PISP limewasaidia wafugaji kwa kuwafunza namna ya kuepukana na magonjwa ya mifugo pamoja na kuwatafutia masoko ya kuuza mifugo wao. Mafunzo ya wafugaji hujumuisha kutunza malisho pamoja na mazingira yao. PISP vilevile huwahimiza wafugaji kutafuta mbinu mbadala za kujikimu kimaisha licha ya kutegemea mifugo wanoweza kuangamizwa na ukame. Kuanzia mwaka wa 2006 jamii zilizoathiriwa na ukame zimepokea ngamia kutoka kwa PISP ili kujikimu kimaisha ikizingatiwa kwamba ngamia hana mahitaji makubwa ya maji. Aidha, PISP limewasaidia wafugaji kunufaika na huduma za benki kama vile mikopo ya riba ya chini.

7

Kupunguza uhasama na kukuza amani

PISP ilipanua juhudi zake kwa kukuza amani na udugu kati ya jamii za ufugaji. Hii ni muhimu katika kuhakikisha matumizi ya sehemu zenye rotuba ambazo zinakaa bila kulimwa kutokana na utovu wa usalama. PISP uhimiza wafugaji kutumia malisho na maji kwa pamoja, na mara kwa mara wazee hukutana na kuongea iwapo kuna utata wowote.

Kuekeza katika elimu

Katika kutimiza malengo makuu katika eneo hili, PISP limeanzisha shule mbili ambazo huwaleta pamoja watoto wa jamii tofauti za Marsabit. PISP huwafadhili wanafunzi kwa kuwapa vifaa vya masomo, kulipia karo za sekondari na kujenga shule nzuri kwa jumla. Aidha, PISP imeanzisha vituo vya masomo kwa watoto wa wafugaji wanaohamahama bila kutulia kwenye makao maalum. Kwa kuanzisha shule, PISP inanuia kukuza viongozi wa kesho kutoka eneo hili.

Uongozi

Tangu kuanzishwa mwaka 1996, PISP imekuwa likitegemea jamii ya mashinani kwa uongozi hususan kamati ya Yaa Galbo ambayo ni kati ya kamati tano za Gabra ambao walikuwa waanzilishi wa shirika hili. Hapo awali wafanyikazi walikuwa wa kujitolea hadi shirika likaanza kupata ufadhili. Hapo awali bodi ya uongozi ilikua imetawaliwa

na wazee Kijiji cha Yaa Gaibo ambao baadaye waliamua kuwa na uakilishaji kutoka kwa makabila mengine kumi yanayoishi kwenye sehemu hii ndiposa makabila yote yanufaike kutokana na huduma ya PISP. Mara kwa mara bodi na wafanyakazi hujadiliana ili kupata mwafaka na njia nzuri ya kutumia maji na malisho baina ya makabila yote. Shirika hili la PISP huakikisha kuwa bodi na wafanyakazi wamepewa mafunzo kuhusu mbinu za kisasa za usimamizi ndiposa kutimiza malengo na wafugaji kwa jumla. Shirika hili la PISP hufanya kazi sako Kwa bako na mashirika mengine yenye malengo sawa. Juzi juzi, PISP imejiunga na kundi la dunia la wafugaji wa kuhamahama ili kuboresha maisha yao na kutunza mazingira ndiposa wawe na makao ya kudumu.

Kujumuisha mbinu za kitamaduni na za kisasa

PISP imefaulu katika kujumuisha mbinu za matumizi ya rasilimali mema ya mazingira. PISP inatumia ya kuhifadhi maji ya mvua kwa kujenga mabwawa kwa changarawe na mawe katika eneo la Marsabit. Haya maji ya mvua hukusanywa na kutumiwa baadae na mifugo pamoja na wanyama pori. Mabwawa hayo huwa rahisi kutumiwa na hudumu kwa miaka mingi bila kukarabatiwa. Hayo mabwawa huzuia mmomonyoko wa udongo na pia huchangia katika kuifadhi mazingira.

8

Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRAMajaribio ya maendeleo kuwafanya wafugaji wa kuhamahama wawe na makao ya kudumu yamewaathiri kutokana na makali ya ukame. Wafugaji wameanza kubadilisha mbinu zao za matumizi ya ardhi. Mifugo huchangia pakubwa kwa kusambaza samadi inayotumiwa kwa ukuaji wa haraka wa nyasi. Aidha, kuhamaha huzuia ulishaji uliokithiri na kuipa nyasi wakati mwafaka wa kukua. PISP linadhamiria kukuza mazingira Kwa kuhimiza uhamaji wa mara kwa mara ndiposa malisho yapate ukuaji wa nyasi na miti. PISP linadhamiria kufungua sehemu zilizopiganiwa hapo awali kwa wafugaji wote. Hayo yote yatapunguza mirundiko ya watu na wanyama wao mahali pamoja. PISP inanuia kuimarisha ujuzi wa kale wa uhifadhi wa raslimali ya malisho. Mfano, kamati ya wazee ya Warendile (Bano) uhakikisha kuwa malisho ufuata mkondo fulani na vilevile wanahakikisha kuwa mito na misitu imehifadhiwa kikamilifu. PISP huhakikisha kuwa jamii zinazopewa maji zimehifadhi chemichemi zao za maji pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira. Isitoshe, PISP inashughulika na utekaji wa maji ya mvua ili yaweze kutumiwa na kupunguza ushindani wa maji. Maji ya ardhini jambo hili limesaidia kuhifadhi mvuke ardhini ambao hutumika na miti, wanyama pori, binadamu na mifugo. PISP huzuia mmomonyoko wa udongo kwa kutumia gunia.

MATOKEO YA KIJAMIIUhifadhi wa vianzo vya maji na shirika hili la PISP umewafaidi mno watu wa eneo hili. Ripoti ya shirika hili inaonyesha kwamba kufikia mwaka 2008, lilikuwa limekarabati visima 100 na kujenga tanki 63 ardhini, silanga 2, kununulia shule tanki 25 na kujenga mabwawa 50 kwa kutumia mchanga na kujenga mabwawa juu ya majabali. Uhifadhi huu wa maji umesaidia na kuboresha kiwango cha mifugo. Aidha, maji haya huwasaidia wenyeji kupata chakula cha kutosha. Vianzo hivi vingi vya maji vimesaidia Sana wanawake ambao kwa sasa wanaweza kushughulikia kazi zingine kuliko kwenda mbali kusaka maji. Wanaume vilevile hawambuliwi kukarabati visima mara Kwa mara. Magonjwa vilevile yamepungua kwa vile maji hayachafuki Kwa urahisi. PISP limehimiza kubuniwa bodi za kijiji za kushughulikia uhifadhi maji.

PISP linadhamira kuwa utunzaji huu wa maji hutasaidia katika kupata chakula cha kutosha, kupunguza uhasama wa kikabila na kukaza amani. Mfano ni mauaji ya halaiki ya Turbi ya 2006 yaliyosababisha vifo 96, kupoteza mifugo takriban mbuzi na kondoo 10,000, ng’ombe 2,000, ngamia 1,200 – haya yote yalisababishwa na wezi wa mifugo. Wengi waliopoteza mifugo wao walisaidiwa na shirika la PISP kwa kupewa ngamia 900 wa kike ndo waanze maisha upya. Isitoshe, wafugaji 800 walioathirika na ukame pamoja na vita vya kikabila walitunukiwa ngamia ambao hufanya vyema sehemu hii. Ngamia husaidia kuwabebea mifugo wengine maji wakati wa kiangazi na misukosuko nyingineo. Isitoshe, ngamia ukamuliwa wakati wa ukame na kusaidia wenyeji kinyume na mifugo wengine ambao huathirika na ukame. PISP huwasaidia wenyeji masikini ngamia moja au kubadilishana na mbuzi 30 hadi 40 kwa ngamia mmoja.

Aidha shirika la PISP huwapa mikopo vikundi 13 vya wahamaji. Mikopo hii huwasaidia kujishughulisha na biashara vidogovidogo ili kujichumia riziki ndiposa wasitegemee ufugaji. Wafugaji hao hunufaika na kitita cha shilingi million nne ambazo huzunguka miongoni mwao. (4m ksh) au USD 40,000.

Licha ya kujenga shule mbili, PISP imeenda mbele na kusaidia shule za sekondari na za msingi 17 kwa kuzijengea paa zinazoteka maji. Haya yoteyamefanywa kwanzia mwaka 1998. Shule hizi zimenufaika na maji yanayowasaidia wanafunzi wakati wa ukame. Isitoshe, PISP imewafadhili wanafunzi werevu 100 na kujenga shule kwa watoto wa wafugaji wanaohamahama.

MATOKEO YA KISERAPISP hujumuika na mashirika ya serikali;yasiyo yakiserikali na yakimataifa ili kuunda sera zinazoongoza uhifadhi wa maji pamoja na rasilimali zingine za wafugaji wa kuhamahama.

9

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUUu mwanzo, PISP imetegemea pakubwa wafadhili katika kuendeleza majukumu yake. Ufadhili wa kigeni unaendelea kupanuka yafuatayo yameingia kwenye hiyo orodha; Kitengo cha Msaada cha Kimataifa cha Uingereza(DfID), SNV WORLD, Shirika la Katoliki la Misaada na Maendeleo ya Kitekinolojia (ITDG)- ambalo kwa sasa laitwa Practical Action , Ubalozi wa Japan nchini Kenya na mashirika mengine yanayojishughulisha na misaada ya maji. Ufadhili huu umewezesha PISP kutimiza malengo yake bila kutegemea mfadhili mmoja. Shirika la PISP kwa sasa lina wafanyakazi 21, nyumba na offisi zake, mtandao, tarakilishi kadhaa, pikipiki kadhaa, gari aina ya Land Cruiser na simu ya satellite.

PISP huwapa mafunzo watu mbalimbali ili wajue namna ya kuhifadhi na kutumia maji na kuna mafundi wa maji takribani 21. Mafundi hawa hujenga na kukarabati vianzo vya maji.

Namna ya kuzuia msongamano

PISP inajaribu kusambaza vianzo vya kudumu vya maji ndiposa watu watapakaa kuliko kusongamana mahali pamoja pamoja na kuchafua mazingira lakini kuna changamoto kuwazuia wafugaji kurudikana mahali pana maji na malisho.

MAONOTangu kuundwa kwa shirika hili mwaka wa 1996, linadhamiria kufungua ofisi katika eneo la Horr-kaskazini ndiposa waweze

kuinua maisha ya wafugaji wengi. Shirika hili linapoendelea kupanua mabawa yake kwingineko, linaamini fika kwamba njia mwafaka ya kuinua maisha ya wafugaji ni kuwahimiza waendelee kauahamahama ili kuhakikisha matumizi mema ya rasilimali za mazingira kama malisho na maji.

WAHISANI• Serikali ya Kenya• The European Commission Humanitarian Organization • The Food and Agriculture Organization of the United Nations

(UN FAO)• The Catholic Organization for Relief and Development Aid• Community Development Trust Fund• United Nations International Children’s Education Fund (UNICEF)• The UK’s Department for International Aid (DFID)• Oxfam GB• Canadian International Development Agency• Caritas Austria• The Japanese Embassy in Kenya• The International Institute for Rural Reconstruction• United Nations Office for the Coordination of Humanitarian

Affairs (UNOCHA)• United Nations Development Programme (UNDP)• Netherlands Development Organization (SNV)• HelpAge International• Africa Oil Corporation• Kenya Community Development Foundation• Maji Na Ufanisi (MNU)

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa:

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781 4023www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator

MAREJELEO YA ZIADA

• Ministry of State for Development of Northern Kenya and other Arid Regions. 2009. Arid Lands Resource Management Project II http://www.aridland.go.ke/index.php

• Pastoralist Integrated Support Programme website http://www.pisp.org/ • Kenya National Bureau of Statistics. 2008. Kenya Eastern Province: Monitoring the situation of women and children. Multiple Indicator

Cluster Survey http://www.childinfo.org/files/Marsabit_Report.pdf• Haro, G.O., Doyo, G.J. and Mc Peak, J.G. 2003. Linkages between Community, Environmental and Conflict Management: Experiences

from Northern Kenya. Prepared for the conference ‘Reconciling Rural Poverty Reduction with Renewable Resource Conservation: Iden-tifying Relationships and Remedies’, Cornell University, Ithaca, NY, May 1-3, 2003.

• Marsabit District Vision and Strategy, 2005. http://www.aridland.go.ke/NRM_Strategy/marsabit.pdf• World Initiative for Sustainable Pastoralism (WISP): a program of IUCN. 2010. Building climate change resilience for African livestock in

sub-Saharan Africa. http://data.iucn.org/dbtw-wpd/edocs/2010-103.pdf