kushughulikia maamuzi mabaya inatupasa kumpenda mungu zaidi ya vitu vyote na kuutafuta kwanza ufalme...
TRANSCRIPT
Somo la 12 kwa ajili ya Decemba 21, 2019
KUSHUGHULIKIA MAAMUZI MABAYA
Ezra:
Mwitikio. Ezra 9
Hatua. Ezra 10
Nehemia:
Mwitikio. Nehemia 13:23-25
Hatua. Nehemia 13:26-27
Tatizo leo
Baada ya kurudi Yerusalemu, wana wa masalia wakajitia doa wao wenyewe kwa kuoana na watu waabuduo miungu.
Wote Ezra and Nehemia walipambana kuzuia hali hii.
Hebu tujifunze namna walivyofanya, ili tujue namna ya kupambana na matatizo kama haya leo.
Katikati ya wakati wa Zerubabeli na kuja kwa Ezra, wana wa Israeli walikuwa wakioana na Wakanaani.
Viongozi wakuu walitarifu juu ya hili. Hata makuhani na Walawi walihusishwa na mwingilianao huu wa ndoa jambo lililokuwa halikubaliki kisheria.
Ezra alifahamu kwamba hii ndiyo ilikuwa moja ya sababu kwanini ibada ya miungu na kushuka kwa maadili vilikuwa vimejaa kwa watu. Alisikitishwa sana.
Aliendelea kuwa katika hali ya mshangao hata wakati wa sadaka ya jioni. Badaye, aliomba na akatambua mbele za Mungu kuwa walikuwa wametenda dhambi kwa sababu hawakujitenga kutoka kati ya mataifa ya kipagani.
HATUA ALIYOCHUKUA EZRA
Neno “jitengeni mbali” halitumiki kama taraka, lakini ubatilisho wa ndoa. Ndoa hizo hazikuwa halali kwasababu zilikuwa kinyume cha sheria.
Mungu anatutaka kusalimisha ubinadamu wetu kwake. Dhamira yetu kwa Mungu lazima iwe imara na thabiti, daima tukimweka Yeye wa kwanza.
Uchunguzi wa tatizo hili ulichukua miezi kadhaa, japokuwa baadhi tu ya familia zilihusishwa (kiasi cha ndoa 4 kati ya ndoa 1000)
Ni wanawake wapi wa kigeni ambao wataonekana kuwa ni “wapagani”? Ni nini walichokuwa wakiwafundisha watoto wao? Ni upi ulikuwa ushawishi katika familia zao? Wanawake waliofukuzwa hawakutenganishwa na watoto wao wala kutelekezwa.
“Kwa uvumilivu na umahiri, na kwa kuangalia
kwa umakini haki na ustawi wa kila mmoja
anayehusika, Ezra na wasaidizi wake walitoa
uvumi wa kurudi kwa Mwenyezi Mungu wa
Israeli katika njia sahihi. Zaidi ya hayo yote,
Ezra alikuwa mwalimu wa sheria; na kama
alivyosimamia kila kipimo cha kila kesi,
alifikiri kuwavutia watu kwa utakatifu wa
sheria na mibaraka ipatikanayo kwa kuitii.”
E.G.W. (Manabii na Wafalme, sura. 51, p. 622)
“Na watoto wao wakanena nusu kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kunena kwa Kiyahudi, bali kwa lugha
ya watu hao mojawapo.” (Nehemia 13:24)
Watu walidhamiria kuacha kuoa wanawake wageni (Nehemia 10:30). Hata hivyo, hawakufanya hivyo pale Nehemia alipoondoka.
Yawezekana waliwaoa wanawake wale kama wake wa pili. Hii ndiyo maana nusu ya watoto wao waliongea lugha moja, na nusu wakaongea lugha nyingine.
Neno la Mungu liliandikwa kwa Kiebrania (lugha ya Yuda), hivyo wale wasioongea Kiebrania walifukuzwa kujitenga na imani.
Nehemia alionesha hasira yake kwa kutumia nguvu ya mamlaka yake kuwaadhibu baadhi ya watu.
“Je, Sulemani, mwana wa Daudi hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengine hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.” (Nehemia 13:26)
Nehemia alieleza kwanini hawapaswi kuwaoa wanawake wageni.
Baadhi ya Waisraeli walikuwa wamekwisha oa wanawake wageni kabla, pasipo kulioana hilo kama dhambi.
Musa alimuoa Ziporah,
Mmidiani
SalmonialimwoaRahab,
Mkaanani
Boazi alimuoa
Ruth, Mmoabi
Shida haikuwa utaifa, lakini shida ilikuwa dini. Tatizo au dhambi ilikuwa ni kuoa mtu mwenye imani tofauti au asiyeamini katika Mungu.
Kama tumedhamiria kuwa kwa Mungu, ni lazima tutafute mwenzi anayetushauri kuwa na ibada kamili kwa Mungu.
“Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?. Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?” (2 Wakorintho 6:14-15)
Inatupasa kumpenda Mungu zaidi ya vitu vyote na kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu(Marko 12:30; Mathayo 6:33). Ni lazima tumwombe Yeye kabala hatujafanya maamuzi ya muhimu kama ya ndoa
Ushauri wake ulikuwa wazi: mwenzi asiyeamini hawezi kutusaidia kukua kiroho lakini atatufanya tutoke katika imani yetu.
Hata hivyo, Paulo alitushauri kubaki kuwa waaminifu kwa wenzi wetu wasio waumini, na kutovunja ndoa zetu (1 Wakorintho 7:12-16).
Tunaweza kuwa na uhakika kwamba neema za Mungu daima zinapatikana kwa kila mmoja, bila kujali ni maamuzi gani mabaya tumefanya.
“Hakuna hata mmoja anaye mcha Mungu ambaye hatakuwa
hatarini kwa kujiungamanisha mwenyewe na asiye mcha
Mungu. ‘Je, watu wawili waweza kutembea pamoja ,
wasipokuwa wamepatana?’ Amos 3:3. Furaha na mafanikio
ya uhusiano wa ndoa unategemea umoja wa pande zote;
lakini kati ya muumini na asiyeamini kuna tofauti kubwa
ya radha, upendeleo na malengo. Wanatumikia mabwana
wawili, ambao hawawezi kupatana. Hata hivyo vyovyote
mtu anavyoweza kuwa mkweli na mwenye kanuni sahihi,
ushawishi wa asiyeamini utakuwa ukikuongoza mbali na
Mungu.”
E.G.W. (Wazee na Manabii, p. 174)