radio tanzania media kit - swahili v2.pdf

22
Tanzania Heritage Project www.tanzaniaheritageproject.org [email protected] +255 717 615 273 Dar-es-Salaam, Tanzania

Upload: rebecca-yeong-ae-corey

Post on 31-Oct-2015

676 views

Category:

Documents


14 download

DESCRIPTION

Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

TRANSCRIPT

Page 1: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Tanzania Heritage Projectwww.tanzaniaheritageproject.org

[email protected]

+255 717 615 273

Dar-es-Salaam,

Tanzania

Page 2: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

“Nchi isiyokua na utamaduni ni sawa na mkusanyiko wa watu usiokua na roho unaowaunganisha kama Taifa” ! ! ! ! ! ! ! ! – Julius. K. Nyerere, ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! Baba wa Taifa

Page 3: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Kufufua Maktaba ya Redio Tanzania

Y A L I Y O M O

1. Mradi2. Kutoka kwa Mwanzilishi

3. Maktaba4. Muziki5. Watu6. Maadili ya Msingi7. Jamii8. Redio Tanzania kwenye Habari

9. Mafanikio10.Malengo11. Shiriki12. Shukrani

Page 4: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Redio Tanzania Dar-es-Salaam ni kituo cha redio kwanza na cha pekee nchini Tanzania kurekodi muziki kwa muda wa miaka ishirini na tano baada ya uhuru. Maktaba yake ambayo ina zaidi ya masaa 100,000 ya nyaraka za kipekee kama hotuba za siasa na miziki ya kiafrika – haijawahi badilishwa kutoka kwenye hali ya tepu alimaarufu kama reel-to-reel tapes kwenda mfumo wa kisasa (digital format).

Hali hii imewafanya watanzania washindwe kusikiliza muziki yao ya asili na wasanii kushindwa kufaidika na kazi zao za muziki. Hali ina hatarisha kupotea kabisa kwa historia ya muziki wa kitanzania.

Nyaraka hizi, ambazo zina historia nzima ya kuzaliwa kwa Taifa jipya – Tanzania, zimekua zikitunzwa kwa miaka mingi kwenye maktaba zenye joto kali na vumbi, zipo kwenye uwezakano mkubwa wa kuharibika. Hali halisi ni kwamba nyaraka zilizopo Redio Tanzania ni nakala za pekee zilizopo – na mpaka hivi sasa watu wachache sana wanaweza kutumia nyaraka hizi au hata kujua kuhusu uwepo wake.

Endapo ikitokea maktaba kuteketea kwa moto, mafuriko au kuharibika kwa kawaida kutakua na msiba mkubwa kwa wanafunzi, wanahistoria, wanamuziki, wapenzi wa muziki na watanzania wote kwa ujumla.

Tanzania Heritage Project ni mradi ambao lengo lake kuu ni kufufua maktaba hizi kwa kubadilisha na kuhifadhi nyaraka hizi kwenye mfumo uliobora zaidi.

Mradi

Page 5: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf
Page 6: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Tulipofika skuamini macho yangu kuona wazee wenye mvi kichwani wakitikisa jukwa kwa muziki mzuri. Tamasha lilijaa maelfu ya mashabiki. Mimi na rafiki yangu tulicheza sana na nlikumbuka miaka ya tisini nlipokwendana familia yangu hotelini na kumwona Kasheba.

Muziki uliopo Redio Tanzania unakumbusha watanzania walipotoka. Sisiti kusema muziki huu ni kitambulisho cha muziki wa asili wa Kitanzania. Kitu cha kusikitisha ni kwamba muziki huu wa Zilipendwa unasikika kwenye matamasha tu, ukipigwa na wazee hawa na sio wengi wapo hai. Kuna maelfu ya tepu za muziki huu kwenye mashelfu ya maktaba ya Redio Tanzania ambazo hazijawahi kuguswa kwa miaka mingi. Ni watu wachache wana uwezo wa kupata nakala hizi au hata kujua kuwa zipo.

Mimi na rafiki yangu Rebecca Corey tuliamua kuanzisha mradi ambao utatunza na kuboresha mfumo ambao hizi tepu zimehifadhiwa, hiki kitendo kitaalamu kinaitwa Digitization. Hii ni hatua ambayo itasaidia kutunza urithi wetu wa muziki kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa njia ya kisasa na kiteknolojia. Maktaba za Redio Tanzania zina nakala zenye masaa zaidi ya 100,000. Tepu hizi zinatunza miziki, hotuba za kisiasa na vipindi vizuri vya Redio. Tulianzisha mradi huu sio tu kukuza na kutambulisha muziki wa Kitanzania ulimwenguni bali kuwarudishia Watanzania na wanamuziki kwa ujumla hazina ya utamaduni walioupoteza kwa miaka mingi.

K wa pamoja tunaweza kuokoa muziki. Tafadhali jiunge nasi kufufua maktaba ya Redio Tanzania.

- Benson Rukantabula

Founder’s Story“Baada ya kisa, mkasa. Baada ya chanzo, kitendo.”

- Mithali ya Kiswahili

Naitwa Benson Rukantabula. Nakumbuka nilipokua na miaka saba nilikwenda na familia yangu Kilimanjaro Hoteli hapa jijini Dar es salaam kwa ajili ya chakula cha jioni. Ilikua mara yangu ya kwanza kwenda kwenye hoteli ya kifahari na nilikua mwenye furaha sana. Kabla hatujaanza kula nlisikia mziki mzuri sana kwa mbali. Nilikua nna uhakika unatoka kwenye gitaa ya Acoustic. Nilipokua nkishangaa huku na kule kuangalia nani anapiga muziki huo, nlimuona Ndala Kasheba ambae alikua mwanamuziki maarufu miaka ya tisini. Alikua akipiga wimbo niliokua nkiupenda sana, “Umbea.” Nlikua mwenye furaha ya kupindukia kwa sababu usiku ule ilikua mara yangu ya kwanza kushuhudia muziki ukipigwa. Nyimbo nyingi za Kasheba zilikua zikipigwa Redio Tanzania na hii ndio sababu iliyonifanya niipende Redio hii kipindi hicho.

Nilipokua kijana mdogo, nilipenda kusikiliza Redio Tanzania sio tu kwa sababu ya nyimbo nzuri walizokua wakipiga bali kwa ajili ya vipindi vyake vyenye kusisimua kama Mama na Mwana – ambacho kilikua kipindi cha hadithi zenye kusisimua na Twende na Wakati ambao ulikua mchezo wa Redio wenye kuhamasisha maendeleo ya jamii. Redio Tanzania ilikua ina vipindi vizuri visivyochosha kusikiliza hata siku nzima.

Mwaka 2002, nilipokua nasomea elimu ya sekondari, Vituo vingi binafsi vya Redio vilichipukia. Kwa sababu za kibiashara Redio hizi ziliipa changamoto Redio ya Taifa kwa kuanzisha vipindi vyenye kuchukua usikivu wa wasikilizaji wengi. Taratibu, Redio Tanzania ilianza kupoteza umaarufu wake. Hata mimi nilipenda kwenda na wakati kwa hiyo nikajikuta nakua mpenzi wa Redio hizi mpya.

Mwaka 2006, nilipokua mwanafunzi wa chuo,rafiki yangu alinishawishi niende nae kwenye tamasha la muziki wa Zilipendwa. Nilibisha bisha lakini mwisho wa siku nilijikuta naenda naye tamashani.

Page 7: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Kitunze kidumu.

-Mi!ali ya K"wahili

Page 8: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

TANZANIA Mnamo mwaka 1961,Tanganyika i l i p a t a u h u r u k u t o k a k w a muingereza. Miaka mitatu baadae Tanganyika iliungana na visiwa vya Zanzibar kuunda Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tanzania ipo kwenye pwani ya Afrika mashariki na imepakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi , Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Zambia, Malawi na Msumbiji. Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti, ukanda mzuri wa pwani, Bonde kuu la ufa na kabila la wamasai – hivi vyote vinapatikana Tanzania. M b a l i y a h i f a d h i z a wanyamapori zenye kupendeza, historia na bahari nzuri ya hindi, nchi ya Tanzania ina historia ya kisiasa ya kustaajabisha na muziki mzuri ambao haujafiki sehemu nyingi ulimwenguni.

JULIUS NYERERE Tanzania ilipopata uhuru, nchi ilikua imejikomboa kutokana na miaka mingi yaukandamizaji na unyonyaji chini ya wafanyabiashara wa Kiarabu na Kireno, na ukoloni wa Ujerumani naUingereza. Julius K. Nyerere aliongoza amani kwa ajili ya mapambano ya uhuru, hatimaye kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo. Kuitwa Baba wa Taifa zaidi ya yote “Mwalimu”-Nyerere ni maarufu kwa kuwa waanzilishi wa Ujamaa, alimaarufu kama “African Socialism.” Nyerere a l iwahi kusema, “Nchini Tanzania, zaidi ya makabila mia mmoja yaliyopoteza uhuru wao,Ila ni Taifa moja lililourudisha uhuru.” Nyerere alijikita zaidi kwenye kuinua utamaduni kama njia ya kuwapa nafuu ya kisaikolojia wananchi wake kutokana na majeraha waliyoyapata kutokana na ukoloni. Alianzisha Redio Tanzania Dar es salaam kama kituo cha habari cha watu huru!

RADIO TANZANIA DAR-ES-SALAAM Kama kituo cha kwanza cha redio nchini,Redio Tanzania Dar es salaam ilikua ni studio ya pekee ya kurekodi kwa zaidi ya miaka 25 baada ya uhuru. Pia kilikua chombo cha serikali cha kukuza umoja wa kitaifa kwa njia ya muziki.

M a k a o m a k u u y a r e d i o yamekuwa kitovu cha utamaduni kwa muda mrefu yaikiwa na historia ya kuwarekodi wanamuziki wakongwe kama King Kiki , Remmy Ongala na DDC mlimani Park Orchestra. Pia kilirekodi miziki ya aina mbali mbali kama Taarab,ngoma za asili na bendi za miziki ya dansi/jazi alimaarufu kama Zilipendwa.

Katika uwanja wa kisiasa, Redio Tanzania imekua ikiunga mkono mapambano dhidi ya wazungu wachache kutawala na ukoloni katika Afrika. Pia kituo hiki kilitumika kuhamasisha na kusaidia kampeni ya kumpindua dikteta Idi Amin Dada wa Uganda.

Benson Rukantabula, mwanzilishi wa mradi, na Bruno Nanguka, mkutubi wa maktaba Meza ya Bruno

Maktaba“Sanaa sio kioo

kinchoonyesha ukweli, bali

nyundo inayotengeneza

ukweli.” - Bertholt Brecht

Page 9: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

"Dhambi kubwa ya ukoloni ni ile ya kujaribu kutufanya tuamini ya kwamba hatukua na

utamaduni wa maana, usio wa thamani na wa aibu badala ya kujivunia."

-Julius K. Nyerere

Page 10: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

TAARAB"Kuwa na Furaha na muziki" طرب

Taarab ni aina ya muziki ambapo mashairi huimbwa kwa melodi ya Kiarabu. Muziki huu unaozingatia maadili ulianzia pwani ya Afrika Mashariki na kusambaa sehemu mbali mbali. Mara nyingi hutumika kutumbuiza kwenye harusi au kwenye mikusanyiko mengine ya kijamii. Vyombo vya muziki vinavyotumika ni vyombo kutoka Afrika (percussion), Ulaya (gitaa), na Mashariki ya Kati (Oudquanun), na Mashariki ya Asia (taishokoto), na kuimba kwa lugha ya kiswahili na kwa Melodi ya Kiislamu.

Wasomi wamebainisha kuwa Taarab ina jukumu la muhimu hasa katika masuala ya kijamii ya maisha ya Kiswahili, kutoa fursa ya kuwa wamoja na kutatua migogoro. Redio Tanzania ina rekodi ya baadhi ya wanamuziki wengi wa taarab mashuhuri kama vile Bi Kidude na Siti Binti Saad.

MUZIKI WA DANSITucheze dansi! (Let's dance!)

Muziki wa dansi alimaarufu kama Zilipendwa ni mziki ambao ni maarufu sana nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Mziki huu ulianza kuchipukia miaka ya 1930 na hatimaye kupata umaarufu baada ya uhuru wa Tanzania. Mziki huu ulichipukia pale bendi zinazopiga miondoko ya Rumba kuchanganywa na vyombo vya muziki vya

asili.Upigwaji wa muziki huu pia ulitokana na mtindo wa upigaji wa bendi za brasi kipindi cha ukoloni wa Mjerumani.

Wakati wa kilele cha umaarufu wake, kutoka 1960 hadikatikati ya miaka ya 1980, bendi 25 hadi 30 zimekuwa zikifanya maonesho na kutoa burudani kila siku. Bendi hizi zimekuwa zikijizolea maelfu ya mashabiki kote Dar es Salaam. kila bendi ilikuwa ina mtindo wake wa muziki, utendaji na njia fulani ambapo watazamaji wao walicheza nyimbo zao.

Bendi zote za dansi zilikua zikifadhiliwa na asasi mbalimbali za serikali na mashirika binafsi. Wanamuziki walikua wafanyakazi wa mashirika haya kwa hiyo mashirika yalikua yakinunua vyombo vya muziki vya bendi na kutafuta sehemu za bendi ku fany ia mazoez i na ku fanya maonyesho. mfano,Uhamiaji Jazz ilikuwa ikiendeshwa na idara ya uhamiaji,Magereza Jazz iliendeshwa na Magereza, Mzinga Troupe iliendeshwa na jeshi la wanachi, Vijana Jazz iliendeshwa na chama tawala cha vijana cha ujamaa, na NUTA Jazz band iliendeshwa na muungano wafanyakazi wa Tanzania.

Mpaka leo muziki wa dansi bado ni hai sana. Wasanii wengi wa zamani wanaendelea kufanya maonyesho kwenye maeneo mbali mbali nchini. Mpaka hivi sasa muziki huu una mashabiki wengi ambao wanafurahia maonyesho na burudani ya Zilipendwa usiku kucha!

““Muziki huu ukawa maarafu kwa

kuchanganya mziki wa asili na ule wa kisasa...”

-JONATHAN KALAN, GLOBAL POST

Muziki

Page 11: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

MKUTUBIBruno Nanguka, anajulikana tu kama ‘Mkutubi’, alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1974. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka kumi na nane tu. Tangu muda huo amekua akifanya kazi kwenye maktaba mpaka alipofikia cheo cha Mkuu wa Huduma za Maktaba. Maarifa yake ya kutunza nyaraka na hazina hii ya Taifa yanaastahili pongezi. Bruno anadai kuwa anajua mahali ilipo tepu yoyote kwa kumbu kumbu tu! “Wenzangu niliokua nikifanya nao kazi wengine wamekwishafariki na wengine ni wastaafu,Nimebaki peke yangu sasa” anasema Bruno.Bruno imekuwa polepole akijaribu kubadili baadhi ya nyaraka mwenyewe, lakini kwa mtu mmoja kufanya digitization kwa seti moja ya mashine ni mchakato wa polepole sana. Kunakili masaa 100,000 ya nyaraka kutamchukua karibu Miaka 15 bila kusimamisha zoezi. Hata hivyo, Bruno anasema kuwa kitendo cha kubadilisha nyaraka ni muhimu kwa siku zijazo na kwa taifa.

Rebecca na Bruno wakiwa ofisini kwa Bruno, Tanzania Broadcasting Corporation

Watu

Page 12: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

MWANZILISHI WA MRADIKwa mara ya kwanza Rebecca Corey alitembelea Tanzania mwaka 2007, na amekuwa akirudi mara kwa mara kwa ajili ya Kufanya kazi, kusoma na kuishi. Amewahi kufanya kazi kwa kujitolea shule ya Bagamoyo, Kampuni ya utoaji mikopo midogo iitwayo Tujijenge Tanzania Ltd na  kuwa mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam akichukua shahada yake ya pili. Rebecca amekua mara zote akijifunza kuhusu Tanzania na kuwa sehemu ya jamii.

Kipindi alipokuwa kwenye wakati mgumu, akiugua kutokana majeraha aliyoyapata kwenye ajali Dar es salaam, amekua akisikiliza muziki wa Zilipendwa na ulimfariji sana. Hapo ndipo alipopata wazo la kuanzisha mradi wa Tanzania Heritage Project ili kurudisha fadhila kwa Taifa na utamaduni uliompa faraja kubwa mno.

MFALME WA RUMBAKing Kiki, au kama ajulikananvyo kwa jina la "Mzee wa Kitambaa Cheupe," — kwa sababu ya tabia yake ya kujifuta jasho kwenye paji la uso na leso nyeupe wakati akifanya maonyesho. Alizaliwa Congo lakini amekua akipaita Dar-es-Salaam nyumbani tangu miaka ya 1970. Yeye ni mmoja wa wakongwe waliowahi kurekodi Redio Tanzania, na bado anafanya maonyeshi jijini Dar-es-Salaam mara nne au tano kwa wiki. Mtindo wake wa rumba ya Kikongo imempa umaarufu mkubwa na imemsaidia kumpa jina kati ya mashabiki maelfu ambao wanapenda nyimbo zake.

Kiki alirekodi katika studio za Redio Tanzania kati ya miaka ya 70 na 80, kwasababu studio ya Redio Tanzania ilikuwa mahali pekee pa kurekodi muziki nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka ishirini. Anakadiria nyimbo alizorekodi zinaweza kuweza kutosha kutoa CD tano au sita. "Ninaona faraja kuona vijana ambao wanauthamini na kuupenda muziki huu, "anasema. "Nilidhani tumesahaulika kabisa!"

Page 13: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

MWANAHARAKATILicha ya kuwa mmoja wa wapiga gitaa mashuhuri Tanzania, John Kitime pia ni msemaji wa jumuiya ya wasanii wanaopigania haki za wanamuziki. Siku ambazo hafanyi maonyesho na bendi yake Kilimanjaro band, huwa anatoa msaada kwa wanamuziki wenzake kutokana na changamoto za kila siku na kuandika hadithi zao kwenye blog yake.

"Maisha kama mwanamuziki nchini Tanzania ni magumu sana," anasema John. "Ni vigumu mno kutafuta hela ya kukidhi mahitaji kwa njia hii- sisi bado tunaendelea kupiga muziki kwa sababu tuna upendo na muziki wa kitanzania. Uharamia ni tatizo kubwa, na watu hufanya bila kuheshimu sheria ya hati miliki ya nchi. Kitendo cha muziki uliopo maktaba ya Redio Tanzania kuboreshwa na kubadilishwa kuwa kwenye hali ya kisasa kitatunufaisha sisi wanamuziki ambao tuliwahikurekodi pale redioni." Mradi huu ukifanikiwa utaweza kuwasaidia wanamuziki kama John kuweza kunufaika na muziki wanoupenda.

MWANDAMIZILeo Mkanyia, ni mwanamuziki maarufu na nyota wa kizazi kipya ambaye mtindo wa muziki wake unaoonyesha wazi kuwa wamevutiwa na muziki wa zama za Zilipendwa. Leo ni mtoto wa Bwana Henry Mkanyia, aliyekuwa mpiga gitaa la bass kwenye bendi ya DDC Mlimani Park Orchestra. Leo, amekua akimsikiliza baba yake akipiga muziki huu na muziki wa dansi umekuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku. Mziki ni mchanganyiko wa mziki wa kiasili wa makabila ya kigogo na kizaramo ambayo ni makabila ya baba yake na marehemu bibi yake.

Inasikitisha sana wanamuziki wengi wa kizazi kipya wanashondwa kusikiliza na kuipata miziki ya zamani kwasababu nakala nyingi zipo kwenye tepu za reel-to-reel ambazo zimefungiwa kwenye makataba ya redio Tanzania.Nakala chache ambazo hazina ubora kutokana na kunakiliwa vibaya na maharamia zinapatikana mitaani kwenye CD na kanda. Kutokana na hali hii wanamuziki hawa wa kizazi kipya wamekua wakiiga mitindo ya muziki ya nchi za magharibi kama hip-hop, RnB na pop, lakini Leo Mkanyia amekua ushuhuda ya kwamba watanzania wengi wanapenda muziki wenye asili ya Tanzania kutokana na mashabik i lukuki aliojikusanyia.

Page 14: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Tupo...

PAMOJA KWA MUZIKI

Page 15: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Tunaamini...1) Muziki ni lugha ya Ulimwengu

Kuna mithali ya Kizimbwabwe asemayo, "kama unaweza kuongea, unaweza kuimba. Kama unaweza kusimama, unaweza kucheza." Mziki ni

lugha ipitayo mipaka na tofauti za kitamaduni. Hakuna kitu muhimu zaidi kwa binadamu kuliko sanaa..

2) Sanaa siku zote inabadilika na ni endelevu

Utamaduni kamwe haupo tuli. Siku zote unatuletea changamoto na kutuhamasisha. Hivyo kujua sanaa inapokwenda, hatuna budi kujua

ilipotoka.

3) Nyimbo hutoa hadithi. Hadithi huanzisha mazungumzo. Mazungumzo

husababisha ustahimilivu

The first step toward a more peaceful planet is communicating with each other. We can all learn something from a different culture & we all

have something to share from our own.

4) Tunahitaji kuhifadhi na kuendeleza utamaduni ambao upo hatarini kupotea

Ulimwenguni kote, kuna mktaba anbazo zipo katika hatari kubwa kupotea au kuharibiwa kutokana na hali ya hewa mbaya kwenye

naktaba (kama unyevu), migogoro isiyo ya lazima na kupuuzwa. Hatuna budi kuchukua hatua kabla hatujachelewa.

5) Utamaduni ni lazima urejeshwe & kukuzwa kwa kutumia teknolojia mpya na

ubunifu

Teknolojia ni kuboresha kwa kasi isiyokuwa ya kawaida, kufanya digitalisering nafuu zaidi na ufanisi zaidi kuliko milele. Kizazi mahitaji yetu

ya kuchukua faida ya mapinduzi ya kiteknolojia na kutunza urithi kwamba imekuwa kushoto kwa ajili yetu.

6) Uhifadhi wa utamaduni unapaswa kuwa shirikishi na bunifu

Muziki sio wa kukaa kwenye makaba zenye vumbi na zilizosahaulika. Miziki ni kwa ajili ya watu kusikiliza. Kwa kutumia njia mpya za uhifadhi

wa miziki, hatuna budi kuulinda na kuutunza muziki wetu kwa heshima na ushirikiano.

7) Kutunza utamaduni po hatarini kupotea, ni faida kwa jamii

Kitendo cha kutunza na kubadili muziki kuwa kwenye hali ya kisasa (digital format) hutoa ajira, mafunzo na kipato kwa watu. Digitisation

pia ni silaha mojawapo ya kupambana na uharamia. Utunzaji wa utamaduni huboresha maisha na huondoa umaskini.

8) Mradi huu ni jukwaa linalo paza sauti isiyosikika kwa kuwapa fursa wasanii

kufaidika na kazi zao za sanaa

Dhamira yetu ni kufanya ulimwengu kuwa mahali bora zaidi kwa kuokoa muziki ambao upo

hatarini kupotea na kuusambaza ulimwenguni kote.

Maadili ya Msingi

Page 16: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Jamii

13 Januari 2012

Nina kumbuka kipindi Redio Tanzania Dar-Es-Salaam ikiwa mashuhuri.Nakumbuka  wakati huo nilikuwa katika shule ya msingi, sekondari na chuo. Nakumbuka kusikiliza nyimbo hizo kwenye redio za mkulima. Nyimbo nnazokumbuka  kusikia ni kama "Ni Kinda Langu” , “Rangi ya Chungwa, "" kifo,"Unapenda Dezo Dezo," na "Asha" ya Tabora Jazz na nyimbo  nyingi nzurikutoka bendi mbalimbali ya Tanzania. Nakumbuka vipindi kama  "Mama RangiMwana", "Club Raha Leo Show”. Sio busara kuacha miziki na vipindi hivi vizuri vipotee. Hebu tuunge mkono mradi huu na tulinde historia yetu.

! ! ! ! -Shabaan Fundi

B a r u a k u t o k a kwa wanaotuunga mkono

"Muziki ulianza kwa upendo, umoja na kushikana mikono ili kujenga Taifa jipya. Ukiisikiliza muziki hata kipindi hiki ni faraja na inagusa sana”.-Benson Rukantabula,mwanzilishi wa mradi

“Kama mwanamuziki wa Tanzania, nina furaha sana kusikia kuhusu mradi wowote ambao ungeweza kuokoa maktaba ya TBC... Baadhi ya kanda hizo zimehifadhiwa hapo kwa takribani miaka 50 bila hata ya kuguswa. Ni vizuri hatua za lazima zichukuliwe kufufua muziki huu.” -John Kitime, Kilimanjaro Band

""Wote wenye upendo wa dhati na

utamaduni na muziki, ni kitu gani

chenye thamani na umuhimu kwa

binadamu kama sanaa? Ninawasihi

muunge mkono mradi.”-Nila Uthayakumar, Kickstarter

Page 17: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

RADIO TANZANIA

GOOD MAGAZINE: "[...] Masaa yote 100,000 yenye muziki wenye thamani na vipindi vya kuwa digitized, na maudhui yake kuzorota. Tepu hizi zinaweza kupotea kama haitachukuliwa hatua. Kwa bahati nzuri, mradi wa kitamaduni wa Tanzania Heritage Project una mpango madhubuti wa kuhifadhi na kuboresha maktaba hizi; na kuutangaza utamaduni wa kitanznaia ulimwenguni kote.” (2/3/2012)CHRISTIAN SCIENCE MONITOR:

  Tanzania Heritage Project [...] ni mradi wenye dhamira ya kuweka muziki huuhai,  kwa kutunisha mfuko ambao utasadia zoezi zima la kuhifadhi, kuboresha na kuweka nyaraka hizi kwenye hali ya kisasa ili ziweze kwa umma kwa urahisi zaidi.

"Kadri hizi kanda zinavyooendelea kukaa kwenye hali ya joto na unyevu ndipo ubora unapopungua" anasema Rebecca Corey.   “Kiziza cha wanamuziki hawa kikipita kutakuwa hakuna mtu atakaye endelea mila hizi kama hakutakuwa na uwezekano wa watu kusikiliza miziki hii tena.”(3/23/2012)WILLWORKFORMUSIC.ORG: “Muziki huu wa kipekee ambao umekua ukikaa kwenye maktaba za Tanzania bila kutumika, ni maelfu ya rekodi za kutoka miaka ya 1960 hadi 1980 na kuendelea. Historia  hii ya muziki wa Afrika mashariki imekua ikikaa bila kuguwa,tafadhali saidia Tanzania Heritage Project iiweke huru.” (Feb 2012)GAZETI LA MWANANCHI:

“Itakuwa ni kitu cha faraja kushuhudia huu mradi ukifanikiwa "Fu alisema."Kama ilivyo kuwa Redio India, Redio China au Redio Brazil. kimsingi huu mradi wa kitanzania utakuwa mfano wa kuigwa na ulimwengu utajifunza mbinu za uboreshaji na utunzaji wa muziki”(1/20/2012)

“Miaka hamsini baada ya uhuru wa Tanzania, mradi wa kibunifu na wa kijamii unafanya kazi kuhifadhi historia ya taifa na muziki [...] redio TBC, kama taasisi ya kiserikali ya Tanzania ina masaa zaidi ya 100,000 ya kanda ambazo hazijawahi kusikilizwa na umma zenye miziki ya afro-jazz , ngoma na hotuba za kisiasazilizotumika kutafuta msaada kwa ajili ya harakati za uhuru katika Afrika......” -Global Post, 16 February 2012

K W A M A E L E Z O Z A I D I F U A T I L I A :

TANZANIAHERITAGEPROJECT.ORG/

PRESSW A S I L I A N A N A S I K W A :

in fo@tanzaniaher i tageproject .org

au p iga +255 717 615 273

kwenye habari

“Afrika kwenye vyombo vya habari ni maarufu kwa habari kuhusu umaskini, magonjwa na maisha yasiyokuwa na matumaini. Ila mradi huu wa Kitanzania ni kuhusu biashara ya kijamii, ufumbuzi na matumaini." -Flagpole Magazine, 25 Jan 2012

“Nyaraka hizi ni za historia muziki wa Kitanzania Tanzania na mapambano ya uhuru na kuzaliwa kwa Taifa jipya barani Afrika. Digitisation ni tendo jema la utunzaji wa utamaduni, na litakuwa na faida kwa wanamuziki, wasomi na wapenzi wa muziki."-Filtre News, Jan 2012

No. 1

Page 18: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

Mafanikio

Usajili wa NGO

Kampeni ya Kickstarter

Page 19: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

4) Scale digitization: 10 digital audio workstations, 15 employees, digitization and preservation of full collection (~19,000 tapes).After we have proven the model and raised funds, we will establish the long-term digitization system. At this point, we will be providing consistent training and employment to a local Tanzanian staff.

5) Muda mrefu online uhifadhi wa vifaa digitized, mtandao jukwaa kuonyeshamusic.As the music is digitized, we will create access, sustainability, and a revenue stream online. Our web platform will enable users to engage with the material, bringing the music to life for old and new generations alike.

6) Modeli wa utunzaji shirikishi kufaidisha nyingine.Once we have successfully revived the Radio Tanzania archives, we will share our methods so that other projects can replicate our model for preservation in other locations.

Malengo

1) Tathmini ya maktaba ya Redio Tanzania Dar es Salaam.First, we will gain intellectual control of the collection, create a digital catalogue, plan the digitization workflow, and make long-term physical preservation recommendations.

2) Jaribio la digitization: 50 kanda, Kituo kimoja cha Digitisation.Next, we will train one technician trained, and digitize 25 hours of the best music. This will allow us to prove our model.

3) "Juu ya Redio Tanzania" CDremastered na iliyotolewa ikiwa ni pamoja namjengo maelezo, picha, nakihistoria.Then, we will continue to raise awareness and support, working toward sustainability.

Page 21: Radio Tanzania Media Kit - Swahili v2.pdf

DESIGN & CONTENT: Rebecca Corey“THE MUSIC”: Nils Von der Assen, Stephen Witt, & Rebecca Corey“THE PROJECT” & “PEOPLE”: Jonathan Kalan, Rebecca CoreyRADIO TANZANIA LOGO: Carlo EspirituTANZANIA HERITAGE PROJECT LOGO: Heather McMichenPHOTOGRAPHY: Jonathan Kalan, Rebecca Corey, Xiao Liu, John Kitime, Nitesh Gandhi, Helena Goldon