rais kikwete aenda rwanda leo

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 05-Oct-2015

13.481 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

RAIS KIKWETE AENDA RWANDA LEO

TRANSCRIPT

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: [email protected]: www.ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE, STATE HOUSE,

1 BARACK OBAMA ROAD,

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, kwenda Kigali, Rwanda kwa ziara ya siku moja nchini humo kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame.Wakati akiwa Kigali, miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini - Northern Corridor Integration Projects unaofanyika leo katika Hoteli ya Serena mjini Kigali.

Mkutano wa leo unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zimealikwa kuhudhuria mkutano huo.

Lengo la mkutano huo ni kujadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.

Rais Kikwete atarejea nchini jioni ya leo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

7 Machi, 2015