sera za uchumi za chama cha mapinduzi

23
  0 CHAMA CHA MAPINDUZI SERA ZA UCHUMI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI Imetolewa na Idara ya Itikadi Na Uenezi kwa ajili ya Semina za Halmashauri Kuu za Taifa, Miko a na Wilaya. Inapatikana pia katika kitabu cha  Sera za Msingi za CCM Makao Makuu ya CCM Dodoma, 2004

Upload: shafii-muhudi

Post on 06-Oct-2015

372 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

SERA ZA UCHUMI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

TRANSCRIPT

  • 0

    CHAMA CHA MAPINDUZI

    SERA ZA UCHUMI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI

    Imetolewa na Idara ya Itikadi Na Uenezi kwa ajili ya Semina za Halmashauri Kuu za Taifa, Mikoa na Wilaya. Inapatikana pia katika kitabu cha Sera za Msingi za CCM Makao Makuu ya CCM Dodoma, 2004

  • 1

    SERA ZA UCHUMI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI 1.0 UTANGULIZI Kinyume na madai potofu ya wapinzani wetu, ukweli ni kwamba Chama cha Mapinduzi kina sera zake kuhusu uchumi. Sera zenyewe ni zipi? Kwanza tuelewane kwamba tunapozungumzia sera za uchumi, tunamaanisha mtazamo, mikakati na malengo ya kiutekelezaji ambayo Chama kinajiwekea kuhusu aina ya uchumi inaotaka kuujenga. Kimsingi imani na madhumuni ya Chama yaliyopo kwenye Katiba yake ndiyo dira ya sera za Chama zikiwemo za uchumi. Hivyo kwa falsafa na itikadi, kwa WanaCCM maendeleo, yakiwemo ya uchumi, msingi na lengo lake ni WATU na si vinginevyo. Aidha, kwa lengo la kujibu mahitaji ya umma, sera hubadilika au hudumu (kwa muda mrefu) kutegemea mazingira ya ndani na ya nje. Ndiyo maana, kwa kukiri kanuni hii, CCM imekuwa inachambua na kubainisha mabadiliko yanayotokea na kuyawekea sera na mikakati muafaka kulingana na mahitaji halisi ya wakati pasipo kupoteza misingi muhimu. Yafaa ieleweke kuwa Sera hizi za uchumi za sasa zinabidi kuyakinisha dira iliyomo kwenye Katiba ya CCM, na usasa hapa unajitokeza zaidi katika mikakati na mbinu zinazoendana na wakati. 2.0 CHIMBUKO LA SERA ZA CCM ZA UCHUMI ZA SASA Sera za uchumi ambazo Chama cha Mapinduzi inazitekeleza sasa chimbuko lake ni Mkutano Mkuu wa Nne wa Kawaida wa Chama cha Mapinduzi 1992 kama inavyoelezwa katika sura ya kwanza ya Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini (ukurasa 1- 8). Aidha Chama kimeendelea kuainisha zaidi sera zake katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2000-2005 na pia katika Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya 2000 Hadi 2010. Katika Mkutano Mkuu huo wa Nne, Chama kilizingatia hali halisi ya uchumi na kusisitiza kuwa:

    CCM itaendelea kuzitekeleza sera zinazojenga umoja, udugu, na mshikamano miongoni mwa Watanzania ulisisitiza kuwa Siasa ya Msingi ya Chama cha Mapinduzi itaendelea kuwa Ujamaa na Kujitegemea na kwamba lengo la Ujamaa na Kujitegemea katika miaka ya tisini litakuwa kuhakikisha kwamba wananchi wnyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu, mmoja mmoja kwa kupitia vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali, kwa kupitia makampuni ya wananchi na ya ubia ambamo maelfu ya wananchi watanunua hisa, na kwa kupitia umilikaji wa dola kwa mashirika yale yatakayoendelea kuwa mikononi mwake Na kwa maana hiyo sehemu kubwa ya uchumi wa nchi inakusudiwa umilikiwe na wananchi wenyewe ili kuinua

  • 2

    hali ya maisha yao na kujitosheleza mahitaji yao ya msingi (Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya Tisini, 1992 uk. 4-5).

    3.0 MALENGO MAKUU YA SERA ZA UCHUMI ZA CCM ZILIZOPO

    3.1 Malengo Makuu ya Sera za Uchumi za CCM yameainishwa vyema katika nyaraka za Msingi za CCM zikiwemo Mwelekeo wa Sera za Msingi za CCM katika Miaka ya Tisini na Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya 2000 Hadi 2010.

    3.2 Malengo Makuu mawili yaliyoainishwa Katika Mwelekeo

    wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini: (i) Lengo la Ujamaa na Kujitegemea ni

    kuhakikisha kuwa uchumi wa Tanzania unamilikiwa na kuendeshwa na wananchi wenyewe kwa njia mbalimbali. (Inasisitizwa kwamba hii ni sera ya msingi ambayo utekelezaji wake ni wa muda mrefu unaohitaji mipango na mikakati thabiti).

    (ii) Kuinua kiwango cha nguvu za uzalishaji mali

    ili kuinua uchumi wa Taifa. Katika lengo hili inasisitizwa kwamba nguvu na uwezo wetu uelekezwe katika kuinua kiwango hicho ambacho kiko chini sana, kwani raslimali watu inatumia maarifa kidogo sana katika uzalishaji, yaani vitendea kazi bado ni duni (jembe la mkono, panga n.k.) miundo mbinu iko nyuma. Jukumu kubwa linalokabili kuwajenga wananchi (watenda kazi) kwa elimu na maarifa ya kisasa, kueneza matumizi ya zana za kisasa (vitendea kazi) na kujenga miundo mbinu ya uchumi wa kisasa

    3.2 MAJUKUMU MAKUU kutokana na malengo makuu yaliyoainishwa katika mwelekeo wa sera za CCM za miaka 2000 hadi 2010 Kazi ni kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea na uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi. Majukumu Makuu hayo ili kutoa msukumo wa kuendeleza malengo makuu mawili Malengo Makuu yaliyoainishwa katika Mwelekeo wa Sera za CCM za Miaka ya Tisini, ikiwa ni kuzingatia thatmini ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 1995 inayodhihirisha mafanikio ya Serikali zote mbili SMT na SMZ katika kutekeleza ahadi nyingi zilizotolewa na Ilani

  • 3

    hiyo. Aidha, uwezo na uzoefu uliopatikana katika jitihada za kusukuma maendeleo, ukiwemo uwezo wa kifedha wa Serikali ulioongezeka toka wastani wa Tshs. 27bn/= kwa mwezi 1995 hadi zaidi ya wastani Tsh. 100bn/= kwa mwezi 2003 vimezingatiwa.

    Ikumbukwe pia kuwa jukumu hili limezingatia uchambuzi yakinifu uliofanywa na Chama wa hali ya uchumi wa Tanzania, ambao wamebainisha sifa kuu mbili, ambazo ni (i) Uchumi ulio nyuma na (ii) Uchumi tegemezi.

    4.0 Mkakati wa Kujenga Msingi wa Uchumi wa Kisasa wa Taifa

    linalojitegemea

    3.2 Udadisi makini juu ya Uchumi wetu unabainisha hali ya mgongano wa kimsingi, ambao ni kwamba matumizi yetu na mahitaji yetu mengi ni ya kisasa (mavazi, usafiri, huduma za jamii k.v. elimu, afya, mahakama, ulinzi, usalama, barabara, mawasiliano na miundo mbinu mingine) wakati vyote hivyo vinahimiliwa na sekta ya jadi (yaani kilimo, ufugaji na uvuvi) ambayo ni ya kujikimu, kwani vitendea kazi vyake vikuu ni duni vikiwemo jembe la mkono na zana nyingine za jadi. Mgongano huu bila shaka unadai suluhisho tena la haraka, kwani uchumi ulio nyuma (wa kujikimu) ni chimbuko la umaskini, ujinga na maradhi. Njia ya kuondokana ili kujikomboa/kujikwamua, tunahitaji kujenga uchumi wa kisasa ambao utaondosha mgongano huo, kwa vile uchumi huo wa kisasa ndio utakaohimili huduma za kisasa za kiuchumi (miundo mbinu) na za kujamii ambazo mahitaji yake yanazidi kukua na kupanuka wakati wote.

    3.3 Mkakati wa modenaizesheni ndio unaotegemewa katika

    kutekeleza na kufikia azma ya kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea. Huu ni mkakakti wa jumla. Mkazo au msukumo hapana budi uelekezwe katika maeneo ya elimu (ya kisasa), ngazi zote, kilimo, ufugaji na Uvuvi wa Kisasa (soma mada husika), sekta ya viwanda (chimbuko la sekta ya kisasa), Madini, Utalii, Miundo mbinu ya Kiuchumi (ya kisasa), sera Muafaka za Fedha na Biashara, Kazi, Maarifa, Nidhamu, Idadi ya Watu na Maendeleo ya Uchumi.

    3.4 Sambamba na eneo hili la uchumi, maeneo mengine ya kisiasa

    na kijamii uchumi yanahitaji kuzatitiwa barabara na kudhibitiwa ili kuhakikisha nchi yetu inapata mafanikio yanayokusudiwa. Haya yameainishwa vizuri katika Mwelekeo wa Sera za CCM za Miaka ya 2000 hadi 2010, Katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2000-2005, Katiba ya CCM, na katika nyaraka mbali mbali za CCM na hotuba za viongozi husasan za Mwenyekiti wa CCM Rais

  • 4

    Benjamin W. Mkapa. Inashauriwa wanaCCM wakati wote wafanye marejeo ya nyaraka hizi zenye utajiri mwingi wa elimu, maarifa na ujuzi.

    5.0 MSINGI WA MAAMUZI YA CHAMA JUU YA SERA ZA UCHUMI Chama Cha Mapinduzi kimeendelea wakati wote kushikilia vyema kanuni ya wakati na mahali, na kamwe hakijawa na utamaduni wa kuganda kifikra, kisera na hata kimtindo. Maamuzi ya Chama cha Mapinduzi kutilia mkazo sera hizi za uchumi yalitokana na sababu ambazo zimeainishwa wazi na Chama. Imeelezwa katika Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini kuwa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Mapinduzi wa Oktoba 1987 ulipitisha programmu ya CCM ya 1987 2002 na kwamba mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa programmu hiyo yalikilazimisha Chama kufanya uchambuzi mpya wa kimsingi na tathmini ya hali mpya iliyojitokeza. Maelezo hayo yameainishwa pia katika Tathmini ya Miaka 20 ya CCM 1977-1997 (uk. 23-24; 42-50). Kimsingi Chama cha Mapinduzi kilizingatia mabadiliko na hali ya dunia. Hali ya kisiasa iliyoambatana na kuanguka dola ya Kisovieti mwaka 1991 ilibadilisha sura ya kisiasa ya dunia. Aidha hali ya uchumi na mabadiliko yaliyoletwa na uchumi wa soko, maendeleo ya kiteknolojia na utandawazi kwa pamoja yalijenga mazingira mapya ya kisiasa na kiuchumi. Chama cha Mapinduzi kilizingatia suala la wakati na mazingira. Mwalimu J.K.Nyerere katika hotuba yake Ujamaa Una Njia Nyingi aliyoitoa Chuo Kikuu cha Cairo, April 10, 1967 aliasa kuzingatia mazingira ya wakati katika utekelezaji wa siasa ya ujamaa. Mwalimu alisema kuwa;

    Lazima wale wanaojiita mabingwa wa ujamaa wawe mabingwa kweli! Na wakiwa mabingwa watakataa au watakubali mawazo na maarifa ya kiujamaa kutokana na mazingira ya wakati na mahali. Wale hawatafungwa au kuzuiliwa na mawazo yasiyofanana na hali inayozungumzwa yaliyomo katika Elimu Ujamaa. Lakini hata hivyo sisemi kwamba Ujamaa ni kitu kisichokuwa na misingi, ambacho kina maana nyingi tofauti, na ambacho kila mtu anaweza kukieleza kwa namna yake Lakini misingi inakuwa na faida iwapo tu misingi hiyo itatumiwa katika maisha (J.K. Nyerere, Ujamaa Dar es Salaam: OUP,1970, uk. 74-75)

    Kwa kuzingatia mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi Chama kilitafakari na kufanya maamuzi ya msingi ya kuwa na sera sahihi za uchumi kulingana na wakati. Mazingira ya uchumi tunayokabiliana nayo, yaani uchumi wa soko na utandawazi ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya uchumi katiku siku za usoni. Ni muhimu kwa wanachama na viongozi kuielewa hali hiyo inayovuma sasa hivi inayoitwa Utandawazi kwani tusipojizatiti ipasavyo iko hatari ya kujikuta ni abiria tu ndani ya safari tusiyoelewa mwelekeo wake ama hata

  • 5

    kubaini fursa na vikwazo vyake na tufanyeje kuweka mkakati sahihi (sera na vitendo) ili tuvuke kiuchumi. 6.0 UTANDAWAZI NA NCHI ZA KUSINI 6.1 Dhana ya Utandawazi Utandawazi ni dhana au neno linalowakilisha mfumo au utaratibu wa mahusiano ya kiuchumi ya mataifa mbalimbali katika dunia katika wakati huu tulio nao. Ni dhana inayomaanisha ushirikiano wa kimataifa unaovuka mipaka ya kitaifa. Pia utandawazi unahusishwa na mabadiliko ya mzunguko wa habari, mzunguko wa fedha, fikra, wafanyakazi na teknolojia mpya na ya kisasa kwa haraka na kasi kubwa. Utandawazi pia unajumuisha mchakato mpana wa kuunganika kwa uchumi wa dunia, mfumo wa fedha, utamaduni na imani na fikra za kisiasa. Kwa maana pana utandawazi ni muunganiko na mahusiano ya dunia ambayo yameifanya dunia kuwa kijiji. Utandawazi umeambatana na kukua kwa haraka kwa teknolojia, ushindani na biashara ya dunia.

    6.2 Historia ya utandawazi Utandawazi ulichipua karne ya kumi na tano, miaka miatano iliyopita na umekua taratibu hadi kufikia hatua ya kukomaa tunayoiona sasa. Wafanyibiashara wa Ulaya waliunganisha dunia kuwa kitu kimoja. Mapinduzi ya viwanda Ulaya 1750 1850 na 1870 1890, na kupanuka kwa ubepari karne ya ishirini kuliunganisha dunia. Utandawazi ulikomaa ilipofika miaka ya 1980 hususan kutokana na uchumi wa soko na maendeleo ya kiteknolojia. Nchi na watu wanashiriki zaidi katika uchumi wa dunia. Mashirika hupeleka fedha zao, viwanda na bidhaa duniani kwa wepesi na haraka. Kimsingi utandawazi umeambatana na matumizi ya fedha za kimataifa; kuanzishwa kwa mashirika makubwa ya kimataifa; ongezeko kubwa la biashara kati ya mataifa na matumizi ya teknolojia mpya hasa kompyuta na teknolojia za mawasiliano. Teknolojia mpya ni muhimili wa utandawazi kwa sababu teknolojia zimepunguza gharama ya mawasiliano, usafirishaji na gharama za kuendeshea mipango ya uzalishaji. Kimsingi teknolojia mpya husababisha ongezeko la bidhaa za kibiashara, huduma na ubora wa bidhaa. Utandawazi pia umejiimarisha katika mahusiano ya kibiashara ambapo mitaji, bidhaa, watu, elimu, ujuzi na teknolojia husafiri kwa urahisi kutoka sehemu moja ya dunia au nchi na kwenda sehemu nyingine. Hali hii hulazimisha watu katika mataifa mbalimbali kuamka, kuchangamka na kubuni mkakati wa kujipenyeza katika mtandao wa mawasiliano hayo ya utandawazi. Nchi za ulimwengu zimekaribiana zaidi kisiasa, kiutamaduni, kijiografia kiteknolojia na kiuchumi kutokana na utandawazi. Hali hiyo hutoa nafasi kubwa ya kuboresha maisha ya watu wa dunia inayotegemeana. Lakini ni kweli pia kuwa kwa vile soko ndicho chombo kinachotawala mchakato huo basi kila nchi au watu

  • 6

    huingia kwa nafasi zisizo sawa kwenye soko hilo la ulimwengu. Hiyo ndiyo changamoto kwa nchi zote za dunia katika kuukabili utandawazi.

    Ili kukabiliana na utandawazi Chama Cha Mapinduzi na Serikali vimefanya jitihada na kubuni mikakati na mbinu za kiuchumi za kukabiliana na athari za utandawazi. Kimsingi Chama Cha Mapinduzi kimebaini kuwa:-

    1. Utandawazi ni mahusiano ya kihistoria ya kiuchumi na kijamii ya mataifa ya dunia ambayo hayaepukiki.

    2. Utandawazi ni dhana pana ambayo hujumuisha mchakato wa

    kuunganika kwa uchumi wa dunia, mfumo wa fedha, utamaduni, imani na fikra za kisasa, na kwamba utandawazi huimarika kutokana na teknolojia ya habari na mawasiliano, nguvu za soko na mawakala mbalimbali wa kimataifa.

    3. Wadau wa Utandawazi ni nchi zote za dunia na watu wote wa dunia

    hii. Aidha, nchi zinatofautiana katika mahusiano yao na utandawazi. Utandawazi ni mzigo katika baadhi ya nchi, na nchi nyingine hujinufaisha na huutumia kugandamiza nchi maskini.

    4. Nchi yetu imepita katika historia ya harakati, mikakati na mbinu

    mbalimbali zilizotuwezesha kujikimu, kujihami na kunufaika na changamoto mbalimbali. Ni vizuri tukaendelea kubuni mbinu mpya ambazo zitatuwezesha kushiriki na kufaidika na utandawazi ambao hatuwezi kuukwepa.

    Kimsingi Watanzania tujifunze kuishi katika dunia tandawazi. Serikali imefanya jitihada ili kuiwezesha nchi kukabiliana na changamoto za utandawazi. Utandawazi una faida kama tunajiandaa vizuri. Nchi za Kusini Mashariki ya Asia zimenufaika na kufaidika na utandawazi. Tusipojiandaa kuishi katika dunia ya utandawazi ni dhahiri kuwa tutasukumwa na matakwa ya nchi shindani za dunia. Uzoefu wa nchi za Asia unaonyesha kuwa nguzo sita zinazowezesha nchi kunufaika katika utandawazi ni; kujishirikisha na soko la Dunia; kuufanya uchumi uwe huru; kuondosha sheria zinazoleta vikwazo; kubinafsisha; kutilia mkazo teknolojia kwani ndiyo ufunguo wa maendeleo ya jamii na mwisho kufanya shughuli kwa ufanisi na ubora zaidi. Pamoja na fursa mbalimbali zinazotokana na utandawazi ni vema umakini utumike katika kubuni mkakati na mbinu sahihi ili kuepuka athari za utandawazi kama vile mmomonyoko wa maadili. 6.3 UTEKELEZAJI Ili kujiandaa na kuishi katika dunia ya utandawazi Chama cha Mapinduzi na Serikali zake kinaendelea kutekeleza mabadiliko ya sera za uchumi. Sera hizo zimelenga kukuza sekta binafsi, ubinafsishaji, ufanisi na ushindani wa soko, kungiza teknolojia mpya na pia diplomasia ya uchumi inayolenga kukuza

  • 7

    mahusiano na ushirikiano wa uchumi kama vile na nchi nyingine Afrika ya Kusini (SADC) au Afrika Mashariki (EAC) ili kuvuna faida na kupambana na utandawazi. Utekelezaji wa sera hizi ni maandalizi tosha ya kuishi na utandawazi na kujihakikishia uvunaji wa faida zitokanazo na utandawazi. Sera ya Sekta Binafsi na ubinafsishaji inalenga katika kuwahamasisha wananchi wote kushiriki kujenga uchumi wa nchi wakati huu ambapo dunia ni ya mfumo wa utandawazi. 7.0 SEKTA BINAFSI NA UBINAFSISHAJI

    Chama cha Mapinduzi kinatekeleza sera ya kuipa nafasi kubwa sekta binafsi na sera ya ubinafsishaji. Sera hizi kama ilivyoelezwa katika ilani zote za uchaguzi za mwaka 1995 na 2000 zinalenga katika kurekebishaji uchumi wa nchi. Jitihada hizo zimetekelezwa kwa kasi zaidi katika kipindi cha 1995 - 2000 na zinaendelezwa 2000 - 2005. Lengo ni kufufua uchumi kwa kuipa nguvu sekta binafsi ili iwe injini ya uchumi.

    7.1 Dhana ya Sekta Binafsi Dhana ya Sekta Binafsi ina maana pana zaidi kuliko ilivyo dhana ya ubinafsishaji. Kimsingi ni dhana inayomaanisha kuwapa watu binafsi, yaani wananchi walio wengi fursa ya kumiliki na kuendesha uchumi moja kwa moja badala ya kupitia sekta ya dola. Lengo la sera ya sekta binafsi limeainishwa vizuri katika Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini (uk. 4-5 na 12-13). Imeelezwa wazi kuwa msingi wa dhana hii ni kutoa nafasi kwa jamii, kwa maana ya mtu mmoja mmoja, kaya binafsi au vikundi vya watu au ushirika kushiriki zaidi katika shughuli za uchumi badala ya dola. Na kwa kufanya hivyo Serikali inapewa nafasi kuelekeza nguvu zake katika shughuli za huduma za jamii, miundo mbinu, ulinzi na usalama na utawala. Jukumu la Chama limebainishwa katika uk. 13 kuwa ...CCM itaona kwamba sekta binafsi ya wananchi inawekewa mazingira ya kuvutia ya kuongeza uzalishaji mali kwa ufanisi na tija... Kimsingi uchumi wa taifa unategemea sana uchangiaji wa mtu mmoja mmoja au kaya binafsi. Katika kuzungumzia suala mada ya Kujitegemea ni Jambo la Lazima, Mwl. J. K. Nyerere alisisitiza suala la sekta binafsi kama ifuatavyo;

    ...Kama nchi inahitaji kuwa na watu walio sawa, basi lazima kila mtu amiliki njia zake za uchumi. Mkulima lazima awe na vifaa vyake mwenyewe, jembe lake, ama plau lake. Seremala lazima awe na msumeno wake mwenyewe, wala asitegemee ardhi ya mtu mwingine kuupata na kuutumia msumeno huo. Na kadhalika. Vyombo vya uchumi lazima vimilikiwe na mtu, kikundi cha watu wanaovitegemea kupatia riziki zao ... (J.K. Nyerere Ujamaa uk. 78-79) Anaendelea kusema ... Lakini Ujamaa si ndoto. Wala Ujamaa haukatai kwamba uwezo wa mtu mmoja ni tofauti na uwezo wa mtu mwingine. Kinyume cha hivyo, Ujamaa umejengwa katika ukweli wa asili ya binadamu. Ni fikra zinazomkubali mwanadamu jinsi alivyo, na Ujamaa unataka uweko utaratibu ili tofauti za uwezo wa binadamu ziwreze kutumikia

  • 8

    usawa wa binadamu...J. K. Nyerere Ujamaa Uk. 76. Kwa maana nyingine ujamaa unatoa fursa ya ushiriki wa mtu binafsi, ila tofauti za uwezo wetu zisitumike kukiuka misingi ya usawa wa binadamu.

    Ushiriki wa wananchi katika uchumi siyo jambo geni. Kilimo chetu hutegemea wakulima wadogo wadogo. Historia yetu imetuonyesha kuwa Wakulima, wafugaji na wavuvi ndio wawekezaji katika uchumi wa nchi yetu. Jambo hili siyo geni kwa Watanzania. Uchumi wetu umetegemea sekta binafsi ya wazalishaji wetu wadogo wadogo. Ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi wa Taifa ndiyo umekuwa ukibadilika sambamba na sera za Chama za uchumi. Uchumi wa kijamaa msingi wake siyo uchumi wa dola, bali umilikaji wa njia za uzalishaji, mgawanyo wa haki na usawa wa binadamu. Ili kufikia Ujamaa kuna njia nyingi. Uchumi kumilikiwa na dola haitoshi kutufanya tuwe Wajamaa. Vivyo hivyo kutilia mkazo sekta binafsi pia hakutufanyi tusiwe Wajamaa. Mwalimu J. K. Nyerere alilielezea vizuri sana suala hili katika hotuba yake ya Shabaha ni Binadamu aliyoitoa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti 5, 1967. Mwalimu alisema hivi;

    Kwanza ni muhimu kuelewa kwamba kuchukuliwa kwa viwanda na biashara zilizopo na kuzifanya mali ya taifa ni sehemu ndogo sana ya ujamaa tulioukubali. Jambo la maana kwetu ni kiasi tutakacofanikiwa katika kumzuia mtu asimnyonye mwenzake, na katika kueneza mtindo wa kufanya kazi pamoja kwa faida ya wote badala ya kila mtu kushindania faida yake binafsi. Na kwa kweli ni kwamba uchumi wetu hivi sasa uko nyuma sana, hata mafanikio au kushindwa kwa ujamaa kutategemea maendeleo yetu. Kuchukua mabenki, kampuni za bima, na viwanda vile vichache, ni mambo ya muhimu, lakini lililo muhimu zaidi ni kuhakikisha kwamba tunapanua uchumi wetu bila kupanua nafasi za mirija ya kunyonya (J.K. Nyerere, Ujamaa uk. 99)

    7.2 Historia ya Sera ya Sekta binafsi na Ubinafsishaji

    Pamoja na ukweli kwamba sekta binafsi imekuwepo nchini Tanzania kwa muda mrefu, mwaka 1967 Watanzania tuliamua kupitia Azimio la Arusha kuwa na uchumi uliotegemea umiliki/usimamizi wa dola. Kulikuwapo na jitihada tokea awali za dola kusimamia uchumi baada ya uhuru wa Tanganyika 1961 na Mapinduzi ya Zanzibar 1964, hata hivyo uamuzi wa kuwa na mfumo wa dola kumiliki na kusimamia uchumi na mashirika ya umma kupewa jukumu kubwa ulikuja kwa kasi kubwa baada ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1967. Hali mbaya ya uchumi iliyojitokeza miaka ya 1980, na mabadiliko katika dunia hususan kuporomoka kwa dola ya Kisovieti na kujikita na kupanuka kwa utandawazi yalisababisha hali ya uchumi wetu uliosimamiwa na dola

  • 9

    na mashirika yake ya umma kuwa mbaya. Pamoja na mabadiliko hayo maadili ya ufanisi hayakuwepo katika menejimenti ya mashirika ya umma na hivyo kuyatia hasara kubwa makampuni ya umma na nchi. Hali hii ilihatarisha hali ya uchumi, na ilileta kiwango kidogo cha ukuaji uchumi, kudorora kwa uzalishaji katika kilimo na viwanda, mfumuko mkubwa wa bei na deni kubwa la Taifa. Kutokana na uzoefu wa miaka ile ya 1980 CCM ilibaini kuwa mfumo wa uchumi unaoifanya serikali kuhodhi nguvu zote na madaraka yote katika kumiliki uchumi wa nchi si mkakati endelevu na wa tija na hivyo ilianza kutekeleza taratibu za kutegemea sekta binafsi kushika hatamu katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu. Chama cha Mapinduzi kwa hiyo kililazimika kuanzisha kampeni ya kukuza uchumi kutegemea sekta binafsi. Sambamba na mkakati huo, Chama cha Mapinduzi baada ya kubaini uzito wa kubeba mzigo wa mashirika ya umma ulitoa Mwelekeo wa Sera za Uchumi mwaka 1992 ambao uliainisha urekebishaji wa mashirika ya umma. Serikali iliunda Tume ya kusimamia marekebisho ya Mashirika ya Umma (Presidential Parastatal Sector Reform Commission) ambayo pamoja na majukumu mengine ilikuwa na kazi ya kuona jinsi ya kuyauza baadhi ya mashirika na kuingia ubia na sekta binafsi.

    Pamoja na mazingira yaliyoelezwa hapo juu kulikuwa na sababu nyingine nyingi ambazo zilipelekea kufikia mkakati wa ubinafsisahaji. Chama cha Mapinduzi kiliamua mwaka 1992 kurekebisha mashirika ya umma, mpango ambao unaitwa ubinafsishaji. 7.2.1 Ubinafsishaji Dhana ya ubinafsishaji ina maana ya hatua ya mpito ya kurekebisha mashirika ya umma. Mkutano Mkuu wa Nne ulitoa msisitizo wa kurekebisha mashirika ya umma ili kuipunguzia dola mzigo wa kutoa ruzuku ya kuendesha mashirika hayo. Maana halisi ya ubinafsishaji imetolewa katika Tathmini ya Mika 20 ya CCM (uk. 47) kuwa;

    ... ubinafsishaji hauna maana ya serikali kukabidhi mali ya umma kwa watu au taasisi binafsi. Ubinafsishaji maana yake ni kuuza baadhi ya hisa za kampuni ya umma kwa wawekezaji binafsi, kuingia ubia na makampuni binafsi au watu binafsi wa ndani na nje ya nchi; kukodisha kampuni ya umma kwa taasisi au watu binafsi; kuingia mikataba ya uendeshaji na kampuni binafsi au kukabidhi kampuni ya umma kwa menejimenti na wafanyakazi wa kampuni inayohusika. Pia makampuni au viwanda ambavyo haviendesheki kibiashara wala kuuzika hufilisiwa na kufungwa. Muhimu ni kuchagua wa kumuuzia hisa kwa uangalifu ili awe mtu mwenye uwezo wa fedha na teknolojia; ujuzi wa biashara wa soko linalohusika; manufaa kwa Taifa na mipango ya baadaye kuendeleza kampuni inayohusika...

  • 10

    Mkutano Mkuu wa nne uliagiza pia kuwa urekebishaji mashirika uzingatie yafuatayo:-

    (i) Mashirika ambayo ni ya msingi na nyeti kwa maendeleo ya Taifa kama bandari, reli, posta na simu, nishati na mabenki ya umma yaliyopo, yanaendelea kumilikiwa na dola. Hata hivyo, wananchi wataweza kuuziwa sehemu ya hisa katika mashirika hayo, na mashirika haya kuweza kuingia ubia na makampuni binafsi mradi tu uwiano wa hisa unalifanya shirika kuendelea kuwa la dola.

    (ii) Mashirika ya umma ambayo yanaendeshwa kwa ufanisi yaendelee kuwa ya dola. Kwa lengo la kuwashirikisha wananchi katika umilikaji, mipango itaandaliwa ya kuwawezesha wananchi kununua hisa katika mashirika hayo. Pia mashirika ambayo yanahitaji mtaji mkubwa au kupenyeza sayansi na teknolojia ya kisasa yataweza kuingia katika ubia ili kufikia azma hiyo. Aidha, kwa mashirika ambayo serikali italazimika kuendelea kumiliki, mashirika haya itabidi yaendeshwe kibiashara.

    (iii) Kwa upande wa mashirika ambayo yanaweza kufanya shughuli zake kwa faida, lakini yana matatizo mbalimbali kama ukosefu wa mtaji, madeni makubwa katika mabenki, menejimenti mbovu, nk. Dola italazimika kuchukua hatua za kuyaondoa katika matatizo hayo. Hatua hizo ni pamoja na kuondoa menejimenti mbovu, kuimarisha mtaji kwa kuwauzia wananchi hisa na kuingia ubia na vyombo vingine vya uchumi au kuyakodisha kwa mteja mwenye uwezo wa kuyaendesha kwa faida.

    (iv) Mashirika yaliyo sugu kwa kufanya shughuli zake kwa hasara yatakodishwa,kuuzwa au kufungwa kwa kutilia maanani jawabu ambalo lina maslahi zaidi kwa Taifa (Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini Uk. 11-12.)

    Kimsingi ubinafsishaji ulibadilisha mkakati wa uendeshaji wa uchumi kutoka mfumo wa uchumi unaotilia mkazo mashirika ya umma ambao Chama kiliuendesha kuanzia baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967 na kuanzisha mfumo wa uendeshaji uchumi ambapo wananchi wenyewe wataendesha uchumi. Mashirika ya umma badala ya kuleta maendeleo ya uchumi kwa taifa yalikuwa yanakwamisha ukuaji wa uchumi. Na kwa hiyo Chama kilifanya uamuzi wa kujenga Ujamaa na Kujitegemea kwa kutegemea sekta binafsi na wananchi.

  • 11

    7.2.2 Lengo la Ubinafsishaji Ubinafsishaji ni njia inayotumika na nchi za kijamaa na kibepari kwa malengo makuu yafuatayo:

    Kuongeza ufanisi na mchango wa mashirika katika uchumi wa taifa. Kupunguza mzigo wa kutoa fedha kwa mashirika ya umma kwenye

    bajeti ya serikali.

    Kupanua mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa taifa ili serikali isimamie zaidi suala la usalama na kutoa huduma za msingi za jamii kama elimu na afya.

    Kuwawezesha wananchi wengi kumiliki na kuendesha shughuli za kibiashara.

    Mkutano Mkuu wa Nne ulibaini wazi malengo hayo. Dhamira ya Serikali ni kujenga uchumi imara, uchumi bora unaojitosheleza na utakaowawezesha wananchi kuishi maisha bora, kuinua ari ya kufanya kazi na moyo wa kujitegemea.

    Dhana ya ubinafsishaji, inatokana na kwanza kuwepo kwa mali ya dola

    na pili kuwa mali hizo kutokana na sababu kadhaa zinabinafsishwa kwa maana ya ama kuuzwa au kwa njia nyingine toka umiliki wa dola na kuwa chini ya umiliki wa ama mtu binafsi, kaya binafsi au vikundi vya watu (washirika) kwa kuzingatia vigezo kadhaa kama vile soko, utaifa na uzalendo, na umuhimu wa chombo kinachouzwa. Kwa hiyo ni njia ya mpito na ya muda. Urekebishaji wa mashirika ukiisha sera hii itakuwa imekamilika.

    Kimsingi ubinafsishaji ni njia ya kufikia lengo na siyo lengo lenyewe. Ubinafsishaji kwa maana nyingine haulifanyi taifa kuwa la kijamaa au kibepari, bali ni mkakati au njia ambayo inatumika katika mazingira ya kihistoria tuliyonayo kufikia lengo letu la Ujamaa na Kujitegemea. Jambo la muhimu ni kuwa tushirikiane kusimamia ufikiaji wa lengo letu la Ujamaa. Katika hili ni vizuri tukajikumbusha usemi wa Mwalimu J. Nyerere kuhusu Ujamaa Una Njia Nyingi alioutoa Chuo Kikuu cha Cairo kwamba;

    Lakini ingawa utaalamu wa kisiasa ndio unaofanya njia za uchumi na za usafirishaji zistahili kuwa mikononi mwa umma, lakini jambo hili haliwezekani wakati wowote na mahali popote. Msingi wa watu kumiliki njia hizo hautoi jawabu la kila tatizo. Kama tulivyokwisha kuona katika Tanzania, inawezekana wakulima wakanyonywa hata na chama chao wenyewe cha wakulima, au na nchi yao wenyewe kama utaratibu wenyewe ni mbaya, au kama wakuu na watumishi si mahodari au si waaminifu. Na inawezekana vyombo hivyo kumilikiwa na watu wengi kukaharibu au kusimamisha maendeleo, hata mwishowe ikaonekana wakulima wangalipata faida kubwa zaidi kama mtu

  • 12

    mmoja angalipewa nafasi ya kunyonya . Kwa hiyo tunapata matatizo ya kuamua kitu gani kiwe mali ya umma au kimilikiwe na umma katika kila hatua ya maendeleo. Hata kwa vitu ambavyo ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi, si lazima kwamba kuvifanya vitu hivyo mali ya taifa kila mara ndiko kutakakotoa jawabu lifaalo kwa wapenda ujamaa. Hasa kama kumilikiwa kwa kitu hicho kutaharibu uchumi uliopo huenda ikafaa zaidi kufuata utaratibu mwingine. J.K. Nyerere Ujamaa una Njia Nyingi Ujamaa, op. cit. uk. 81-82.

    Uchaguzi wa njia hii ni sahihi kabisa na umetokana na sababu nyingi za ndani na nje, hali ya utandawazi na mapungufu katika mkakati wetu wa awali wa uchumi uliomilikiwa na dola katika ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea. Njia hii hailengi kujenga ubepari wala kuuza nchi, bali kuinua uchumi wa taifa ambao utatuwezesha kujitegemea na kudumisha usawa wa wananchi.

    7.2.3 Faida za Ubinafsishaji. Ubinafshaji ni njia inayotumiwa kwa lengo la kuboresha uchumi. Uzoefu unaonyesha kuwa ubinafsishaji una faida zifuatazo:

    Unapanua umilikaji na ushiriki wa wananchi katika uchumi wa taifa Unaongeza ushindani katika uchumi

    Uongeza ufanisi katika biashara na huduma Unapunguza mzigo wa gharama kifedha na kiutawala Unaingiza teknolojia mpya katika uchumi Unaongeza kodi na kurahisisha ukusanyaji wake Unaongeza ujuzi na mbinu za uendeshaji

    Unaongeza ubora wa bidhaa na huduma Unatoa nafasi zaidi za ajira Unaboresha maslahi ya wafanyakazi

    7.2.4 Utekelezaji Utekelezaji umeendelea kwa mfano tangu kuundwa kwake TIC Septemba 1990 -Juni 2002 kituo kimeidhinisha miradi 2008 itakayotoa nafasi za ajira 292,993. Miradi 904 (40%) inamilikiwa na wawekezaji wa ndani ya nchi, miradi 450 (21%) ni ya wawekezaji wa nje na miradi 654 (32%) ni ya ubia kati ya wawekezaji wa ndani na wa nje. Na katika Ubinafsishaji hatua zifuatazo zimetumika: 1. Kuuzwa kwa asilimia 100 mashirika yote yanayoendeshwa kwa hasara

    na ambayo hayawezi kutengamaa tena.

  • 13

    2. Mashirika yenye matatizo lakini yanahitaji kukwamuliwa kiuchumi yanatafutiwa mwekezaji binafsi ili anunue kiasi fulani cha hisa ili upatikane uwezo wa kujikwamua.

    3. Kukodisha kwa kipindi maalumu taasisi nyeti kama vile Mamlaka ya

    Bandari na Shirika la Reli. 4. Serikali kubakiza hisa katika baadhi ya mashirika yanayobinafsishwa

    kwa nia ya kuziuza kwa Watanzania kupitia soko la hisa baada ya mashirika hayo kujiendesha kwa faida mifano halisi hapa ni kama vile NBC, Mbeya Cement na Tanga Cement.

    Lengo ni kuona kuwa baadhi ya Mashirika yamilikishwe na kuendeshwa

    na wafanyakazi, chini ya utaratibu wa MEBO (Management and Employee Buy Out).

    Utekelezaji wa ubinafsishaji tokea uanze rasmi Januari 1993 hadi Juni 2002 ni kama ifuatavyo:

    Mashirika na mali 469 vimebinafsishwa, yaani kampuni 281 na mali 271.

    Idadi ya Kampuni zinazotakiwa kubinafsishwa ni 389.

    Kampuni 138 kati ya 259 zimenunuliwa na wawekezaji Watanzania kwa asilimia 100.

    Pia Watanzania wengine wameingia ubia na wageni katika mashirika 123 kati ya 266 yaliyobinafsishwa.

    Kampuni 14 zimenunuliwa na wawekezaji wa nje kwa asilimia 100.

    Zaidi ya mali 180 kati ya 210 zilizouzwa pia zimenunuliwa na

    Watanzania.

    7.2.5 Matatizo Yanayokwaza Utekelezaji Tatizo la msingi ni lile la baadhi ya wananchi, wanachama na viongozi kutoelewa bayana umuhimu wa mabadiliko haya ya mbinu. Shutuma zisizo sahihi kuhusu ubinafsishaji zimetolewa mara kwa mara, na hata pale ufafanuzi unapotolewa bado wapo wanaopotosha ukweli. Kama ilivyoelezwa, maamuzi ya Chama ni sahihi na utekelezaji wake haujakiuka misingi ya uamuzi wa Chama. Ubinafsishaji unalenga kujenga uchumi imara ambao utaliwezesha taifa kujenga Ujamaa kwa misingi ya usawa na kujitegemea.

  • 14

    Mara kadhaa kumekuwepo upotoshaji unaotokana na kuchanganya dhana ya ubinafsishaji na ile ya uwekezaji. Aidha, upotoshaji mwingine ni kuwa mashirika yaliyobinafsishwa yanauzwa bei poa kwa wageni hoja ambayo si sahihi. Ukweli ni kwamba yaliyonunuliwa na Watanzania thamani yake (bei) ni takriban Sh. 60 bilioni na waliyonunua wageni ni Sh. 23 bilions. Wengi wanatoa hoja hii wanazungumzia kiwanda au benki kwa maana ya majengo tu wala hawazingatii suala la aina ya teknolojia, madeni ya shirika na thamani halisi ya shirika katika soko wakati wa uuzaji. Pia kuna matatizo kadhaa ya kiutendaji. Baadhi ya mashirika yaliyobinafsishwa bado yanakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa mitaji mikubwa, ukosefu wa mbinu sahihi za kuendesha viwanda/mashirika hayo kisasa, pamoja na malimbikizo makubwa ya madeni. Tume ya Kusimamia Marekebisho ya Mashirika ya Umma (PSRC) imeorodhesha matatizo makubwa ya ubinafsishaji kama ifuatavyo:

    Mashirika mengi ya umma yaliajiri wafanyakazi wengi mno kuliko mahitaji halisi. Matokeo yake gharama za kuwapunguza ni za juu sana.

    Mashirika mengi yamekuwa na madeni makubwa kwa hiyo yameshindwa kuvutia wanunuzi au wawekezaji.

    Baadhi ya wawekezaji ni wababaishaji na matapeli wa kitaifa na kimataifa. Sheria zetu na vyombo vya usalama vinapaswa viwe macho zaidi na matapeli ili tusiruhusu kuhujumiwa.

    Wawekezaji wengi hasa wa nchini wanapata matatizo kulipa malipo

    waliyokubaliana na PSRC wakati wa uuzaji. Wengi wamegeuka kuwa wadaiwa sugu.

    Baadhi za menejiment na Bodi za Wakurugenzi zinapinga ubinafsishaji kwa hiyo zimewekea vikwazo shughuli za ubinafsishaji.

    Matatizo katika utekelezaji wa ubinafsishaji hutofautiana kutoka shirika moja hadi jingine. Moja ya tatizo sugu ni lile la upunguzaji wa wafanyakazi na maslahi yao. Kimsingi tatizo hili limetokana na udhaifu wa menejimenti za awali za mashirika ya umma hususan kutowasilisha makato ya mafao kwenye vyombo husika kama vile NSSF, LAPF. Mzigo huo wa deni unaachiwa serikali (hazina) wakati shirika linapobinafsishwa. 7.2.6 Mafanikio Yaliyopatikana Pamoja na matatizo yote haya ubinafsishaji umefanikiwa kuleta wawekezaji. Kampuni 138 zimenunuliwa na wawekezaji Watanzania kwa asilimia 100. Vile vile zaidi ya wananchi 98,000 wamenunua hisa katika mashirika

  • 15

    yaliyobinafsishwa na katika hawa wanawake wanaongoza (55%). Pia sera ya ubinafsishaji inakubalika sasa miongoni mwa Watanzania. Tumeshuhudia pia ongezeko la tija, uzalishaji na ongezeko la ajira kwa baadhi ya mashirika. Aidha, mashirika mengi yaliyobinafsishwa yanalipa kodi na gawio kwa Serikali, mishahara na marupurupu ya wafanyakazi yameongezeka. Mfumo mpya wa uongozi na teknolojia mpya pia vimepatikana. Kimsingi uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 6.2 na 7 na mapato ya Serikali yameongezeka kuanzia Sh. Bilioni 25 hadi kufikia bilioni 100 kwa mwezi hivi sasa. Kabla ya ubinafsishaji Serikali ilikuwa ikitoa ruzuku kuyabeba mashirika ya umma kwa kiasi cha dola milioni 100 kila mwaka na mashirika haya yalikwisha iingiza Serikali hasara ya dola 300 milioni. Hivi sasa baada ya kubinafsisha Serikali inalipwa kodi badala ya kutoa ruzuku. Mfano mzuri ni viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kilombero; Mbeya Cement, Tanga Cement, Tanzania Portland Cement, NBC, CRDB, Canvas Mill, TCC, DAHACO, Sabuni Detergents Ltd. Mtibwa ililipa VAT ya zaidi ya Sh. 800 milioni mwaka 2001. TBL mwaka 2002 ililipa kodi ya Sh. Bilioni 43.5, vivyo hivyo Blankets & Textile Manufactures Ltd inalipa wastani wa kodi ya Sh. 200 milioni kwa mwaka wakati kilipofungwa 1997 kilikuwa hakilipi kodi. NBC ililipa kodi ya Sh. 3.2 bilioni mwaka 2002 wakati 1999 ilikuwa inapata hasara ya Sh. 1.5 bilioni kila mwezi. Hali ya ulipaji kodi kwa Serikali ni mzuri pia kwa viwanda vya cement; Tanzania Portland Cement ililipa Sh. 1.9 bilioni na Mbeya Cement Sh. 847.5 milioni mwaka 2002. Hali ya uzalishaji pia imepanda kutokana na uwekezaji katika teknolojia ya kisasa na mbinu bora za uendeshaji. Kilombero uzalishaji wa sukari umepanda zaidi ya mara tatu, kutoka tani 29,000 wakati wa ubinafsishaji mwaka 1997 hadi tani 98,000 mwaka 2002/2003. Mtibwa kutoka tani 29,000 wakati wa ubinafsishaji mwaka 1998 hadi tani 49,700 sasa. Katumba kilo 1,402,000 mwaka 2001 hadi kilo 2,194,000 za chai mwaka 2002. Kabla ya ubinafsishaji ukulima wa chai ulisimama na viwanda vya Katumba na Mwakaleli kufungwa. Uzalishaji pia umeongezeka katika viwanda vya cement, sabuni (foma), katani na vya nguol kama Mwatex na Mutex ambavyo vilisimama kwa muda mrefu. Saruji yetu pia huuzwa nje; Malawi, Zambia, Rwanda na Burundi na maturubai ya Canvas Mill yanauzwa katika majeshi ya NATO na sabuni zetu zimepata soko DRC Kongo, Malawi, Msumbiji na Kenya. Ajira pia imeongezeka. Inakadiriwa kuwa maisha ya zaidi ya Watanzania 300,000 hutegemea usambazaji na ugawaji wa bidhaa za kampuni ya bia (TBL). Mishahara na maslahi pia yameboreshwa. Kabla ya kubinafsishwa kima cha chini pamoja na marupurupu Tanga cement kilikuwa Sh. 150,000/= kwa mwezi. Sasa ni zaidi ya Shs. 450,000/=. TBL ilikuwa inalipa kima cha chini Sh. 9,000/= kabla ya ubinafsishaji na sasa ni zaidi ya Sh. 120,000/= mbali na marupurupu yanayotolewa. Aidha kiwanda cha Tanga cement hutumia Sh. 100 milioni kwa mwaka kugharimia elimu kwa wafanyakazi. Hivi sasa kwa karibu asilimia 75 ya pamba yetu inasindikwa na viwanda vyetu.

  • 16

    7.2.7 HITIMISHO: Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya Taifa imetafakari kwa kina na imebaini kuwa ni kweli kabisa kwamba sera hii ni njia pekee kwa mazingira tuliyonayo kutusaidia kufika katika lengo letu la Ujamaa na Kujitegemea. Sera za CCM za Uchumi ni sahihi kabisa. Wananchi waelimishwe ili wabadili mtazamo ili wajenge fikra na uelewa sahihi kuhusu ubinafsishaji. Mapungufu yanayojitokeza ni ya mpito. Viongozi wa Chama na Serikali wawaeleze wananchi mafanikio, na pia sababu za mapungufu yanayojitokeza pale yanapojitokeza. Maeneo ambayo yameleta mabishano ni yale yanayohusu mikataba, maslahi ya wafanyakazi, nafasi ya wawekezaji wazalendo katika ubinafsishaji na suala la uvunaji wa maliasili na madini.

    Elimu na ushirikishwaji mara zote upewe mkazo. Upotoshwaji umelenga kulinda maslahi binafsi. Serikali imechukua hatua ya kuweka bayana taarifa za ubinafsishaji wa makampuni ya umma hususan malengo na faida ya kufanya hivyo. Uamuzi wa Chama na utekelezaji wake unapaswa kupongezwa na kuungwa mkono. Aidha, kwa kuwa zoezi la ubinafsishaji limeonyesha mafanikio mazuri katika utekelezaji wake, Viongozi wa Chama na Serikali waeleze mafanikio yake kwa wananchi kwa kujiamini.

    8.0 SERA YA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI NA KUPIGA

    VITA UMASKINI 8.1 Mikakati ya Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wananchi Ni vema turejee tena kwenye lengo la msingi la Sera za CCM (Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya Tisini) ambalo linatamka:

    Lengo la Ujamaa na Kujitegemea katika miaka ya tisini litakuwa kuhakikisha kwamba wananchi wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu, mmoja mmoja, kwa kupitia vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali kwa kupitia makampuni ya wananchi ya ubia ambamo maelfu ya wananchi watanunua hisa na kwa kupitia umilikaji wa dola kwa mashirk ayote yatakayoendelea kuwa mikononi mwake.

    Yafaa kuzingatia ukweli wa kihistoria kuwa tamko hili linakiri kuwa azma hiyo imekuja baada ya kubaini kwamba tangu kabla ya kupata Uhuru na hata baada ya kupata uhuru hadi sasa, uwezo wa Watanzania wa kumiliki na kuendesha uchumi umekuwa mdogo sana. Kauli hiyo hapo juu inaweka mtazamo wa CCM kuwa inakusudiwa sasa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi imilikiwe na wananchi wenyewe ili kuinua hali ya maisha yao na kutosheleza mahitaji yao. Hiyo pia ndiyo inaendelea kuwa sera na lengo kuu la CCM katika miaka ya 2000-2010.

  • 17

    8.1.1 Tatizo/Vikwazo ni Vipi?

    Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya 2000 hadi 2010 (Uk.34) unabainisha kwamba pamekuwepo na ugumu wa kuifanikisha sera hii kutokana na ukweli kwamba Watanzania Waafrika huko nyuma hawakupewa nafasi ya kushiriki katika uchumi wa kisasa wa kilimo, viwanda na biashara ya nje na ndani. Hali imebaki hivyo hadi leo kwa vile Waafrika hao waliachwa kwenye sekta ya uchumi wa jadi wa kilimo, ufugaji, na uvuvi, na kuwa vibarua na soko la sekta ya kisasa, hivyo kujikuta wanaendelea kuwa pembezoni mwa sekta ya kisasa ya uchumi wa nchi yetu. Kimsingi hawana uwezo wa kumiliki na kuendesha uchumi huo; wala mitaji na uzoefu.

    8.1.2 Dhana ya uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi ni njia

    ambayo imebuniwa na Chama na kutekelezwa na Serikali na vyombo vingine yenye lengo la kuwafanya Watanzania walio wengi nao waweze kumiliki na kuendesha uchumi katika nchi yao. Hivyo UWEZESHAJI kama dhana maana yake ni kuunda mazingira muafaka yatakayowapatia fursa kumiliki ardhi, viwanda na zana za kazi, kupata mitaji ya kwuekeza katika shguhuli za kiuchumi, kupata elimu na maarifa ya kuendesha biashara na miradi ya kiuchumi, n.k. Katika utekelezaji wa mikakati ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, vijana na wanawake wapeewe kipaumbele (Mwelekeo wa sera za CCM 2000-2010: 34)

    8.2 HALI YA UMASKINI NA JUHUDI ZA KUWAWEZESHA

    WANANCHI KUJIKWAMUA TANGU KUPATA UHURU

    8.2.1 Utangulizi Tangu taifa letu lilipopata uhuru katika mwaka 1961, umaskini uliainishwa kuwa miongoni mwa maadui watatu wakubwa. Umaskini ni pamoja na hali ya kutomudu kupata chakula bora na cha kutosha, tiba, nyumba, mavazi na huduma za msingi za jamii. Hali inaonyesha kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wanaishi katika umaskini. Kwa sababu hiyo mikakati mingi inaendelea kubuniwa na kutekelezwa ya kupambana na umaskini. Katika mazingira ya uchumi wetu hivi sasa suala la kuwawezesha wananchi waingie kwenye shughuli kuu za uchumi ni la muhimu wa pekee. Tangu awali wananchi binafsi wamekuwa wakishiriki. Hata hivyo, wananchi binafsi walishiriki chini ya mwavuli wa uchumi wa umma/ uchumi wa pamoja. Chini ya utaratibu huu, watu binafsi na haswa wananchi hawakupata fursa ya kuonyesha vipawa vyao binafsi vya ujasiriamali (entrepreneurship). Kwa mfano miradi ya uzalishajimali ilitolewa zaidi kwa Mashirika ya Maendeleo ya Wilaya na hakuna mtu binafsi aliyekopeshwa miradi hiyo. Hata taasisi zilizotoa huduma kwa miaka ya 1970 zilitoa kipaumbele kwa vijiji na vyama vya

  • 18

    ushirika. Pale ambapo mtu binafsi alibahatika kuhudumiwa, masharti yalikuwa magumu zaidi. Katika kipindi hicho wananchi wengi waliaojiriwa Serikalini na katika mashirika ya Umma, walizuiliwa kuwekeza katika uzalishaji mali au biashara. Miiko ya uongozi iliwabana sana wajasirimali na hasa Watanzania weusi. Hayo yote yaliinyima sekta binafsi hasa ya Watanzania Waafrika uzoefu wa kumiliki na kuendesha miradi na shughuli nyingine kubwa za kiuchumi. Pamoja na serikali kujiingiza katika shughuli za uzalishaji na biashara, uchumi wa nchi uliendelea kuzorota. Mashirika mengi yaliendeshwa kwa hasara kubwa na yaliendelea kuwa mzigo mkubwa kwa serikali. Kwa sababu hiyo, serikali iliona umuhimu wa kuyarekebisha na mengine kuyabinafsisha. Sambamba na hatua hiyo ya ubinafsishaji na urekebishaji wa mashirika ya umma, Tanzania ilifanya mabadiliko kadhaa katika mfumo wa uchumi wake, hii ikiwa ni pamoja na kuingia katika mfumo wa uchumi wa soko ambapo nguvu ya soko huamua masuala mengi ya kiuchumi na biashara. Lengo kuu ni kuandaa mikakati maalum na ya upendeleo ya kuwawezesha wazalendo au makundi maalum ya watanzania kushiriki katika shughuli za uchumi za nchi. 8.2.2 Tatizo la Umaskini Chama kinatekeleza pia sera ya kuwawezesha wananchi kiuchumi na kupiga vita umaskini. Sera hii ni ya muhimu sana hasa ukizingatia mabadiliko ya uchumi hasa baada ya mwaka 1986 ambapo wananchi walitakiwa kuchangia gharama mbali mbali. Kuanzishwa kwa soko huria nako pia kuliathiri maisha ya Mtanzania wa kawaida na kwa hiyo kulihitajika njia ya kusaidia kuwawezesha watanzania kumudu maisha yao. Umaskini bado ni tatizo kubwa kwa wananchi walio wengi. Umaskini wa kutokuwa na kipato cha kutosha unajidhihirisha katika baadhi ya wananchi kutokumudu kupata chakula bora na cha kutosha, tiba, nyumba, mavazi na huduma za jamii. Umaskini wa kipato unaonyesha kwamba Mtanzania anapata shilingi 650.80 kwa siku. Hali hii inahitaji mikakati ya kuwawezesha wananchi ili waondikane na umaskini. 8.2.3 Jitihada Zilizofanyika Jitihada zimefanyika kuwawezesha wazalendo kujiingiza katika uzalishaji mali, hususan: 8.2.3.1 Mitaji; Mwaka 1994 Serikali ilianzisha mifuko maalum ili

    kuwawezesha makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu. Mifuko hii ni pamoja na mfuko wa wafanya biashara (NEDF), Mfuko wa Vijana na Mfuko wa Wanawake. Kwa mfano, kati ya 1994 na Julai 2002, Mfuko wa Wafanyabiashara Wadogo (NEDF) uliweza kutoa mikopo 12,965 ya thamani ya shilingi 4.17 bilioni iliyotoa ajira kwa ajili ya watu 21,780. Serikali ilianzisha pia benki maalum ya kutoa mikopo midogo kwa ajili ya wananchi wa kipato cha chini, yaani National Micro-finance Bank (NMB). Kilio

  • 19

    cha wananchi wengi ni kuwa hawana owezo wa kutimiza masharti magumu yanayotolewa na taasisi zinazotoa mikopo, riba kubwa na masharti ya dhamana. Pia PRIDE Tanzania NGO, ilianzishwa kwa ajili ya mikopo ya biashara ndogo ndogo.

    8.2.3.2 Mafunzo; mafunzo ya kukuza teknolojia, biashara, uanzishaji,

    uendeshaji na uendelezaji wa miradi. Tasisi zinazotoa mafunzo ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), VETA na TAFOPA (Tanzania Food Processors Association). Lengo la mafunzo ya ujasirimali ni kuibua na kuendeleza vipawa vya kuthubutu, kubuni, kuanzisha na kuendesha miradi ya kiuchumi na kibiashara.

    Vikundi mbalimbali vya uzalishaji; Vikundi hivi ni muhimu ili kuunganisha nguvu za wazalishaji wadogo ili waweze kupata kwa pamoja teknolojia, masoko, mitaji na mahitaji mengine.

    Taasisi za kutoa huduma; Serikali ilianzisha taasisi kadhaa za

    kuwahudumia wazalishaji na wafanyabiashara ili kufanikisha upatikanaji wa miundombinu, mtaji, teknolojia, utaalam wa kiufundi, malighafi, utaalam wa kibiashara, masoko, nk. Taasisi zilizoanzishwa ni kama Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo-SIDO, VETA, CARMATEC, TIRDO, nk. Uko umuhimu wa kuimarisha taasisi hizo ili zitoe huduma bora zaidi.

    8.2.4 HALI YA UWEKEZAJI NCHINI

    Ili kuwezesha uchumi wa Taifa kukua na hivyo kipato na ajira kwa wananchi kuongezeka uwekezaji ni lazima ufanywe. Uwekezaji hufanywa kwa kutumia uwezo uliopo nchini (akiba ya wananchi) au kwa kutumia misaada, mikopo na mitaji ya wawekezaji kutoka nje. Hapa nchini uwekezaji umetumia wawekezaji kutoka ndani na wawekezaji kutoka nje. Wawekezaji kutoka ndani hutegemea uwezo wa wananchi wa kujiwekea akiba ambayo hatimaye huwekezwa. Kutokana na kukosekana kwa uwezo wa kutosha wa wananchi wa kujiwekea akiba, mashirika mengi ya umma na makampuni yaliyobinafsishwa yalichukuliwa na wageni. Kati ya mashirika/makampuni 395 yaliyokuwa katika orodha ya kubinafsishwa ni mashirika 122 tu ndiyo yaliyopata wawekezaji watanzania kwa asilimia 100. Wawekezaji kutoka nje, ndiyo wamekuwa chanzo kikubwa cha uwekezaji katika nchi yetu. Vivutio kadhaa vimewavutia wawekezaji hawa kuchagua kuanzisha miradi yao hapa nchini. Vivutio hivyo ni pamoja na gharama nafuu za uchukuzi, umeme, maji, malighafi, mishahara na mazingira ya amani, utulivu na hali ya utengemano wa uchumi. Kuanzishwa kwa kituo cha uwekezaji (Tanzania Investiment Centre-TIC) ambayo hutoa huduma kwa wawekezaji na marekebisho mengine ya kuboresha mazingira ya uwekezaji, kumevutia wawekezaji wengi kutoka nje.

  • 20

    8.3 UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI Kutokana na hali halisi ya kiuchumi na haja ya kufanyika kwa mabadiliko ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kidunia, Chama Cha Mapinduzi kiliona umuhimu wa kuwapa nafasi Watanzania ya kushiriki katika uchumi wa kisasa wa kilimo, viwanda na biashara ili kuweza kuondokana na uchumi wa jadi wa kilimo, ufugaji na uvuvi. CCM ilibuni mkakati wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ambao utawafanya Watanzania walio wengi waweze kumiliki na kuendesha uchumi katika nchi yao. Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inalenga katika kuwashirikisha na kuwamilikisha Watanzania katika sekta ya kisasa ya uchumi wa taifa. Uwezeshaji unaelezwa vema katika Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2000- ya Chama Cha Mapinduzi katika ukurasa wake wa tano kuwa ni kuunda mazingira mwafaka yatakayowapatia Watanzania fursa ya kumiliki na kuendesha uchumi wa nchi yao. Uwezeshaji unalenga kuhakikisha kuwa wananchi wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu (Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka 2000-2010, uk.33). 8.3.2 MATATIZO; Katika kutekeleza Sera hii ya uwezeshaji

    kumejitokeza ugumu wa kufanikisha kutokana na ukweli kwamba Watanzania Waafrika huko nyuma hawakupewa nafasi ya kushiriki katika uchumi wa kisasa katika kilimo, viwanda na biashara ya ndani na nje. Hii inapunguza uwezo wao wa kumiliki na kuendesha uchumi wa kisasa. Ili kurekebisha hali hii, mkakati wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi umebuniwa kama njia ya kuwafanya Watanzania walio wengi waweze kumiliki na kuendesha uchumi katika nchi yeo.

    8.3.3 MKAKATI

    Kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi yanayotoa fursa ya kufanya kazi za utoaji wa huduma na uzalishaji mali kwa mfano kuwa na sera bora za uchumi, mfumo wa sheria, kulinda haki za wawekezaji, amani na utulivu, kuwa na miundombinu bora, kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu.

    Kuwapa wananchi fursa ya kufanya kazi za utoaji wa huduma na

    uzalishaji mali kwa kuwapa uwezo wa kubuni na kuandaa miradi. Kuhimiza na kuhamasisha maendeleo vijijini. Kilimo chetu kiwe cha kisasa ili kiweze kuongeza tija na kutoa ziada kubwa.

    Kuendeleza harakati za kuondoa umaskini ule uaskini wa kipato na ule

    sio wa kipato. Uwezo wa kupata mapato unaweza kutokana na shughuli za uzalishaji mali; kilimo cha mazao ya biashara, ufugaji, uvunaji wa maliasili na miliki na ajira katia sekta za viwanda, biashara,

  • 21

    nishati na madini. Umaskini usio wa kipato utapigwa vita kwa kuongeza utoaji wa huduma za jamii(elimu, afya, maji, utoaji haki, ulinzi na usalama na utawala bora na uimarishaji wa misingi ya demokrasia). Kufanikiwa hili kunategemea kwa kiwango kikubwa uwezo wetu wa kuzalisha mali, kuunda na kuongeza utajiri wa taifa letu.

    Kuwawezesha wanawake kiuchumi; Ni dhahiri kuwa hakuna mafanikio

    katika vita vyetu dhidi ya umaskini bila kuwainua kwa wingi kiuchumi wanawake katika nchi yetu.

    Kuongeza ajira kwa vijana

    Kuongeza vyanzo vya mikopo kwa kuendeleza juhudi za sasa.

    Kuongeza masoko ya ndani na ya nje; kwa kukuza uwezo wa wananchi

    wa kununua bidhaa na kuongeza uwezo wa kuzalisha bidhaa bora za kuuza nje.

    8.3.4 MAFANIKIO: Pamoja na matatizo yaliyojitokeza kama wananchi kushindwa kupata mikopo kutoka mabenki kutokana sababu mbalimbali bado mafaniko yaliyopatikana katika kutekeleza ikiwa ni pamoja na:

    Hatua kadhaa zimekuwa zikichukuliwa kusahihisha kasoro hizo. Hii ni pamoja kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi yanayotoa fursa ya Mtanzania kufanya kazi za utoaji wa huduma na uzalishaji mali, kuongeza vyanzo vya mikopo na kuongeza masoko ndani na nje.

    Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kila wakati inahakikisha nchi yetu ina amani na utulivu.

    Mfumo wa sheria umehakikisha kulinda mali na haki za wawekezaji.

    Serikali ya CCM inaimarisha Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ili kuwapa wananchi uwezo wa kuweza kusanifu miradi.

    Mifuko maalum ya Wanawake na Vijana na wafanyabiashara ndogo ndogo imeanzishwa kuwawezesha kupata mikopo ya riba nafuu na dhamana kwa miradi wanayoanzisha.

    VETA chini ya Wizara ya Kazi, Mendeleo ya Vijana na Michezo imeendelea kutoa mafunzo ya ujuzi na stadi mbalimbali.

    Wananchi kuhamasishwa kuingia ubia na wageni na kuunda mazingira mwafaka ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji wa nje. Hii ni pamoja na hatua za makusudi za kujenga na kuimarisha tabaka la

  • 22

    wazalendo wenye uwezo wa kuwekeza na wa kuvutia na kujenga vivutio vya wawekezaji kutoka nje.

    Kuwepo kwa dhamira ya kitaifa ya kuboresha viwango vya ubora wa bidhaa tunazozalisha ili ziweze kukubaliwa katika viwango vya kimataifa na hivyo kuwa na uwezo wa kukabili ushindani wa masoko ya ndani na nje. Hii itasaidia kutuepusha na hali ya nchi yetu kugeuzwa dampo tu la bidhaa za wenzetu.

    8.4 HITIMISHO:

    Sera za Chama zinalenga kutekeleza kwa vitendo kuendelezwa na kuboreshwa kwa imani juu ya UTU na USAWA wa binadamu ambavyo ndiyo msingi mkuu unaoshikilia uhuru, umoja, amani na mshikamano wa kitaifa. Wananchi wakiwezeshwa kiuchumi wataweza kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi, kuongeza tija, kujitosheleza katika mahitaji ya msingi, kujitegemea na kuwa na hakika wa kuwepo kwa maisha bora na kupiga vita umaskini. Ushiriki wa mtu mmoja moja, kaya, familia, kijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa utawezesha ushiriki wa taifa. Mafanikio yake yataimarisha uhuru na maendeleo ya Taifa. Kuwashirikisha wananchi kiuchumi na kuwafanya wajitegemee ni nguzo muhimu katika kuwawezesha Watanzania kukabiliana na matatizo, majukumu na changamoto za maisha yao kiafya, kielimu, kiutamaduni na kijamii.