spots 1-20 swahili transcripts€¦ · web view6 kama jamii ya kiasili, na inatoa mamlaka. kuwa...
TRANSCRIPT
1. Nini maana ya Kuafiki Kwanza, bila Shuruti, baada ya kupewa taarifa kamili?
Msemaji 1: 1 Unajua haki ya kupata ridhaa ya bure, kabla ya, and Informed
2 ni nini?
Msemaji 1: 3 Bila shaka! Ni haki iliyokuwa nayo jamii yetu
4 kujulishwa na Serikali
5 kuhusu uchimbaji madini, mafuta, maji na mengineo
6 miradi inayoweza kutekelezwa
7 ndani ya jamii zetu. Na zaidi,
8 Serikali ina jukumu la kusikiliza na kuthamini
9 maoni yetu, ili sote tuweze kufikia
10 makubaliano kabla ya mradi wowote haujaanza kutekelezwa.
11 Kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti ya cultural survival dot org slash [culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
2. Haki ya Asilia
Msemaji 1: 1 Kutoka kuzaliwa, kila binadamu ana haki fulani
2 ambazo haziwezi kuchukuliwa, na kama Watu
3 Asilia, tuna haki ya kuafiki kwanza
4 bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili.
Msemaji 4: 5 Haijalishi ni nchi gani unatokea,
6 hii haki inatuhusu sote na lazima itekelezwe
7 pale Serikali inapoazimia kuchimba
8 maliasili kwenye jamii zetu,
9 hasa kama miradi hii itasababisha
10 mathara kwa ardhi yetu.
11 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
3. Kuwajibisha Makampuni
Msemaji 1: 1 Kila majira, nina wasiwasi na upungufu
2 wa mavuno, hatuna ardhi ya kutosha tena
3 tangia kampuni ije kwenye jamii yetu.
Msemaji 2: 4 Ni kweli, wamechukua ardhi yetu bila kuafiki kwanza
5 bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili. Hii haki inatulinda sisi
6 kama jamii ya kiasili, na inatoa mamlaka kuwa hakuna kazi
7 ifanyike kwenye ardhi yetu bila kampuni
8 au Serikali kutujulisha sisi, kushauriana nasi, na
9 kutusikiliza. Tuchukue hatua ya
10 kujiwajibisha kampuni hii.
11 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
4. Viongozi
Msemaji 1: 1 Mimi ni Indigenous. Nina
2 nina haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa
kamili, lakini
3 serikali inatumia mikakati mingi kukwepa
4 kuzingatia haki hii . Moja ya mikakati hiyo ni
5 kuwajua viongozi katika jamii zetu na kuwashawishi
6 kwa kutumia hongo, ahadi za kazi, wengine wanahaidiwa
7 kufanyakazi moja kwa moja kwa niaba ya serikali au
8 kampuni ya maendeleo, badala ya kusimamia
9 maslahi ya jamii nzima wanayoiwakilisha. Kwa
10 sababu hii, ni muhimu sana kama Watu wa Asili, tu
11 chague viongozi wenye ari na nia ya
12 ustawi wa watu wetu na ardhi yetu, na tufanye kazi
13 .karibu na viongozi wetu kusonga mbele kwa umoja
14 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
5. Azimio la Umoja wa Mataifa, Ibara 10
Msemaji 1: 1 Kwa jamii za kiasili, haki ya
2 kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili inaungwa
mkono na
3 Ibara 10, cha Azimio la Umoja wa Mataifa kwenye
4 Haki za Watu wa Asili,
5 inayosema kwamba serikali zisilazimishe
6 kuhamisha jamii za asili kutoka kwenye ardhi zao
7 au mipaka, hata kuridhia mikataba ya
8 miradi kwenye ardhi ya watu asilia bila ridhaa yao
9 ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili..
10 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
6. Azimio la Umoja wa Mataifa, Ibara 19
Speaker 1: 1 (mwangwi wa sauti) ibara 19 ya Azimioa la Umoja wa Mataifa
2 kwenye Haki za Watu wa Asili
3 inasema:
4 (sauti ya kawaida) kuwa mataifa yashikilie/ obtain
5 kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili kutoka kwa
6 Watu wa asilia kabla ya kuchukua na kutumia
7 hatua za kisheria na kiutawala
8 zitakazo waathiri wao.
9 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
7. Jamii Salama
Msemaji 1: 1 Kama Watu wa asilia, tunahaki ya kuishi kwenye
2 jamii salama, na mabadiliko yanapofanywa
3 katika ardhi yetu lazima tuangalie ibara 29 ya Umoja wa Mataifa
4 kwenye Azimio katika Haki za Watu wa Asilia:
5 Ibara hii inathibitisha kuwa Watu wa Asilia
6 lazima watoe afiki yao kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa
7 kamili kabla vitu vya hatari havijahifadhiwa
8 au kutupwa kwenye ardhi yao.
9 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
8. Miradi ya Maendeleo
Msemaji 1: 1 (ongea kupitia kinasa sauti) Hakuna mabadiliko kufanyika
2 kwenye ardhi yetu kabla ya kwanza
3 kutumia ibara 32 ya Azimio la Umoja wa Mataifa
4 la haki za Watu wa Asili
5 linalodhibitisha kuwa mataifa ni lazima
6 yashikilie kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili
7 kabla ya kukubali mradi wowote wa maendeleo
8 utakao athiri ardhi na rasilimali za
9 Watu wa Asilia, hasa katika
10 maendeleo, matumizi, au uchimbaji wa
11 madini, maji, au rasiliamali zingine.
12 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
9. Msaada wa Kimataifa
Msemaji 1: 1 Kama Watu wa asilia tuna haki ya kuamua
2 ni mabadiliko gani yanayowenza kufanywa kwenye
3 ardhi yetu, kama ilivyoainishwa kwenye Azimio la Umojawa Mataifa
4 kwenye Haki za Watu wa Asilia, pamoja na kwenye
5 mkataba 169 wa Shirika la Kazi la Kimataifa
6 na hatua nyingine za kimataifa
7 zinazotambua haki za kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa
8 taarifa kamili. Hizi hatua zinatamka haki za watu
9 wa asilia na kulazimu mataifa kuheshimu hizi haki.
10 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
10. Haki Isiyoweza Kuondolewa
Msemaji 1: 1 Kwa Watu wa Asilia, haki ya
2 kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili ni haki ya
msingi
3 ya asili, na ni haki isiyopingika. Hii ina maana ni
4 kitu muhimu na cha lazima kwa maendelezo ya mpango
5 unaoa athiri watu wetu hivyo hatuwezi kunyimwa/ kataliwa
6 Kwamujibu wa sheria ya Kimataifa, kuafiki kwanza bila shuruti baada
7 ya kupewa taarifa kamili ina hakikisha kuwa jamii za
8 asili zina amua kwa uhuru ni miradi gani yenye faida
9 kwetu na vizazi vyetu vijavyo, kwa mujibu wa
10 tamaduni zetu, dunia nzima, na maadili.
11 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
11. Ukiukwaji wa Haki za Binadamu unatosha
Dhibiti: muziki wa asilia
Msemaji 1:
1 Habari ya asubuhi!
Msemaji 2:
2 Mambo yanakwendaje?
Msemaji 1:
3 Vizuri asante. Umesikia kuna
4 kampuni mpya mjini? Wameanza kuajiri wakazi wa hapa
5 kufanya kazi kwenye mradi mkubwa wa ujenzi, hapa
6 kijijini kwetu.
Msemaji 2:
7 Nini? Nilikuwa sina habari… siamini
8 serikali yetu inaendelea kupuuza haki zetu za
9 kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili, ambazo
zinatuhusu sisi
10 kama watu wa asilia. Wanahitaji kutujulisha na
11 kusikiliza mawazo yetu kama tunakubali au kukataa
12 miradi hii. Hasa kwasababu hizi
13 haki zimeandikwa wazi kwenye sheria ya kitaifa
14 na kimataifa.
Msemaji 1:
15 Upo sahihi kabisa. Ni wazi serikali
16 haifanyi kazi yake ya kutosha kulazimisha hii . Kama hatuta
17 walazimisha waheshimu haki zetu za kuafika kwanza bila shuruti
18 baada ya kupewa taarifa kamili, hizi haki na sheria zitakuwa ni
19 kwenye karatasi tu zenye vumbi makabatini. Makampuni
20 yataendelea kuvunja haki zetu na kutunyonya
21 sisi watu wa asilia
Msemaji 3:
22 Hatuwezi na hatutakubali hili litokee.
23 Ukiukwaji wa haki za binadamu umetosha! Tusimame kwajili ya
24 haki zatu na kwa ulindaji wa mazingira!
Narrator:
25 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
12. Maana ya "Bila Shuruti"
Dhibiti: muziki
Msemaji 1:
1 Haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili ni
2 haki inayowahusu watu wote wa asilia
3 wanaokabiliana na miradi ya maendeleo kwenye jamii zetu.
Dhibiti: muziki unakata (sekunde 3)
Msemaji 2:
4 Kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili? Ina
5 maana gani kwa ridhaa kuwa huru?
Dhibiti: muziki unakata(sekunde 3)
Msemaji 1:
6 Sehemu kuhusu “bila shuruti” ina maana serikali
7 inakatazwa kujihusisha na udanganyifu kwa viongozi
8 na wana jamii kuhusu maamuzi yao
9 kuhusu kukubali au kukataa kuruhusuh mradi kwenye
10 jamii yetu. Wakati wa mchakato wa kutafuta muafaka
11 Watu wa Asili hawawezi kulazimishwa kwa namna yeyote
12 kufikia maamuzi ya namna fulani. Hii ina jumuisha vitisho vya moja
kwa moja
13 au visvyo vya moja kwa moja kwa wana jamii, vurugu
14 kurubuni, hongo, au blackmail. Ni kwa kuhakikisha kuwa
15 maafikiano ya miradi haiingiliwa na aina yoyote ya haya manyanyaso
16 ,ndio serikali itakuwa imeenzi
17 haki ya ukweli “bila shuruti” ya ridhaa
Msemaji 2:
18 Lazima tudai haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya
19 kupewa taarifa kamili, iwe bila shuruti kabisa.
msimuliaji:
20 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
13. Maana ya "kuafiki kwanza"
Dhibiti : <<sauti za umati wa watu kwenye maandamano >>
Msemaji 1:
1 Tusimame! Tuamke! Hakuna muda muafaka
2 zaidi ya sasa kudai serikali kutekeleza
3 haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili
4 ambayo inatuhakikishia sasa kama Watu wa Asilia!
Dhibiti: muziki unakata (sekunde 3)
Msemaji 2:
6 Unajua. Hiyo inaleta maana maana sana. Itakuwa
7 hatua kubwa mbele kama kweli serikali
8 itazingatia haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa
9 taarifa kamili kwa kiwango chote. Kitu ambacho hasa
10 kimekosekana ni wazo la kuafiki kwanza. Kufikiwa kwa ridhaa
11 kabla ya kuanza kwa mradi au
12 kuidhhinishwa na serikali ni muhimu. Ina maana kuwa tutakuwa
13 na muda wa kutosha kwa jamii yote ya watu wa asili
14 kutoa matazamo wao kuhusu na maamuzi.
15 Hasa! Lazima tuwe na habari kamili na yenye maelezo yote
16 KABLA hii miradi haijaanza, hivyo
17 tuweze kuchambua na kufanya maamuzi yetu kama
18 watu. Nal la zaidi, lazima watushirikishe sisi
19 kabla ya kila awamu mpya ya mchakato kuanza, kwa mfano
20 katika utafutaji, uchimabji, ufungaji na usafishaji wa
21 miradi ya uchimbaji madini.
Msimuliaji:
22 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
14. Maana ya "Kupewa taarifa kamili"
Dhibiti: muziki
Msemaji 1:
1 Wewe na mimi, kama wakazi wa jamii ya asilia,
2 tume hakikishiwa haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya
3 kupewa taarifa kamili.
Dhibiti: muziki unakata (sekunde 3)
4 Hii ni haki ya msingi kwajili ya uendelevu
5 wa maendeleo ya jamii yeyote. Ndiyo maana ni lazima
6 kutekelezwa. Ngoja tuangalie ina maana gani kutoa
7 afiki baada ya kupewa taarifa kamili.
8 “taarifa kamili” ina maana tuna haki ya kupata habari
9 yote na timilifu kuhusu maendeleo ya
10 mradi uliopendekezwa kwenye jamii yetu. Hii
11 inajumuisha habari kuhusu athari za
12 miradi hiyo kwenye mazingira, pamoja na athari
13 kwetu sisi watu binafsi na jamii yetu. Tafiti
14 zilizofanywa katika kukusanya habari hizi zinajulikana kama
15 Tathmini ya Athari za Kimazingira na Kijamii, au
16 ESIA, ambayo inatakiwa kufanywa na makundi
17 huru yasiyofungamana na kampuni.
18 Habari zote zitolewazo lazima ziwe kamili,
19 kueleweka, na katika lugha yetu mama,
20 na kwa mujibu wa maadili ya tamaduni zetu
21 na kwa namna tunayofanya maamuzi. Ni jukumu letu
22 kuhakikisha tunaelewa kwa kina kabla maamuzi hayajafanyika
23 ambayo yata athiri watu wetu na ardhi yetu.
Msimuliaji:
24 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
15. Ni wapi inatumika?
Msemaji 1:
1 Habari za asubuhi, unaendeleaje?
Msemaji 2:
2 Vizuri asante. Mkutano wa jana ulikuaje? Mlizungumzia nini?
Msemaji 1:
3 Ulikuwa mzuri sana. Tulijadili haki ya kuafiki kwanza bila shuruti
baada ya kupewa taarifa kamili.
Msemaji 2:
4 Lakini ni nini hiyo? Unaweza kunifafanulia zaidi?
Msemaji 1:
5 Inahusu haki tuliyokuwa nayo kama Watu wa Asili kutetea ardhi yetu
Na mipaka yetu,
6 haki iliyoainishwa katika sheria za kitaifa na kimataifa.
Msemaji 2:
7 Sawa, lakini tutaitumiaje? Katika hali gani?
Msemaji 1:
8 Tunaweza na tuitumie wakati mradi wowote unapopangwa kwenye
ardhi yetu
9 hasa kama kuna hatari ya uharibifu wa mazingira. Kwani nini ndio
tunaoishi kwenye
10 ardhi hizi, na ndio tutakaokumbana na athari, hivyo ni juu yetu
kuamua kama miradi hii
11 iendelee. Haki ya kuafiki kwanza, bila shuruti baada ya kupewa
taarifa kamili inaweka wazi kuwa makampuni
12 zinahitaji kushauriana na sisi na kuheshimu maamuzi yetu kabla
hawajaanzisha mradi. Tujifunze
13 zaidi kuihusu, inaonyesha ni kitu muhimu sana kwa jamii yetu!
Msimuliaji:
14 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
16. Wajibu
Dhibiti: rekebisha sauti ya redio ikitafuta matangazo (sekunde 3)
Msemaji 1:
1 Haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili
2 ni haki tuliyokuwa nayo kama Watu wa Asilia
3 tukiendelea kutetea ardhi yetu. Lazima tudai
4 haki zetu kuheshimiwa.
Dhibiti: muziki unakata (sekunde 3)
Msemaji 2:
5 Babu; sikiliza wanachosema kwenye redio
6 kweli unadhani kuna tija kwa watu wetu
7 kupigania haki ya ridhaa?
Msemaji 3:
8 Bila shaka, mjukuu wangu! Hii haki
9 inalinda maadili yetu; italeta
10 faida kubwa kwa watu wetu na dunia nzima. Ngoja
11 nikuelezee: Kutumia haki hii, tunaweza kulinda
12 mazingira na kujihakikishia maji safi na hewa safi,
13 kuwa watu wetu wataendelea kuishi katika
14 mazingira bora. Tunaweza kuhakikisha tunaongoza
15 miradi ya maendeleo na kuwa mabadiliko yeyote yatakayofanyika
16 ardhi yetu itafaidika, badala ya
17 watu wetu kudhurika.
Msemaji 2:
18 Sasa naelewa, Babu! Hii ni muhimu. Asante
19 kwa kizazi chenu, nina sehemu nzuri ya kuishi. Nitatimiza
20 wajibu wangu wa kulinda mazingira ili niweze
21 kuacha ardhi nzuri kwa watoto wangu
22 wajukuu, pia.
Msimuliaji:
23 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
17. Kugawanya and Kutawala
Msemaji 1:
1 Kugawanya na kutawala:
2 hii imekuwa mbinu ya makampuni na
3 serikali ili kuendelea na maendeleo
4 ya miradi kwenye jamii za asili. Ni moja ya mifano mingi
5 jinsi wanavyoshindwa kutekeleza
6 haki ya watu ku kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa
kamili.
7 Sheria za Kimataifa zimeweka dhahiri kuwa serikali
8 isitulazimishe kubadilisha mawazo yetu, maadili yetu, au
9 au mbinu zetu za kitamaduni za kufanya maamuzi. Wakati mwingi
10 makampuni hujaribu kuzunguka mchakato wa kupata
11 kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili
kwasababu wanajua
12 hatutaweza kukubali miradi, hatari, yenye athari za kimaendeleo
13 ambayo haitatuacha na mabadiliko chanya. Badala yake,
14 wanajaribu kujionyesha kama wana idhini ya watu wengi
15 kwa kuvutia watu wenye ushawishi kama walimu,
16 viongozi wa dini, au viongozi wa siasa kwa kutumia
17 habari za uwongo au hongo. Hatuwezi kuvumilia haya.
18 Ni sisi wenyewe kuhakikisha haki ya kuafiki kwanza bila shuruti
19 baada ya kupewa taarifa kamili inatekelezwa. Hatuwezi
20 kuruhusu amani, usawa, na ustawi wa
21 jamii yetu na mazingira kuwekwa hatarini na
22 mgawanyiko na rushwa.
Msimuliaji:
23 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
18. Mikutano ya Kijiji
Msemaji 1:
1 (Masikitiko) Habari, mambo yanakwendaje…
Msemaji 2:
2 Vizuri asante! Lakini unaonyesha ulie na huzuni, nini kinaendelea?
Msemaji 1:
3 Nina wasiwasi sana, nimekuwa nikisikia minong’ono kuhusu
4 mradi wa madini kuwa tayari umeshapangwa kufanyika
5 kijijini kwetu. Siyo sahihi kuwa watu walio na mamlaka
6 hata hawakutuambia kinachoendelea. Hawafuati
7 haki ya kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili,
8 ambayo tunayo
9 kama Watu Asilia. Nimejifunza kuwa nchi
10 ina wajibu wa kuzingatia hizi haki
11 wakati miradi ya maendeleo kama huu hapa
12 unapofanyika.
Msemaji 2:
13 Upo sahihi kabisa. Lazima tuhakikishe wanaheshimu
14 haki zetu, kwa kutujulisha, na kupata ridhaa yetu kabla ya kuanza
16 mradi kama huu.
17 Kwa mfano, mradi unaofanana kama huu
18 ulikuja katika jamii yetu, tukafanya mikutano
19 kujua kila kitu kilichokuwa kinaendelea, na
20 bila shaka, lazima tuwe macho katika uwajibikaji wa kampuni
kwenye ahadi zake na
21 kuhakikisha wanatekeleza
22 mradi vile vile kama tulivyo kubaliana
23 kwenye majadiliano yetu. Itakuwa ni mbinu nzuri kutumia
24 kwenye kijiji chako- hatuwezi kuachia miradi iendelee
25 bila ridhaa yetu.
Msimuliaji:
26 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
19. FPIC Inahusisha nini?
Msemaji 1:
1 Unajua kuafiki kwanza bila shuruti baada ya kupewa taarifa kamili
2 ina maana gani?
Msemaji 2:
3 Ndiyo! Ni haki tuliyokuwa nayo sisi kama watu wa asili
4 Ni watu ndiyo wa kuamnua ni nini kifanyike kwenye ardhi yetu.
Msemaji 1:
5 Na unajua ni jinsi tunavyoweza kuitumia haki hii
6 kwa usahihi kwenye jamii yetu?
Msemaji 2:
7 Hmm sio sana.
Msemaji 1:
8 Kama mwana jamii wa jamii ya asili ni
9 jukumu letu kutafuta habari za kina kuhusu hii
10 haki, hivyo wasilaghaiwe na
11 serikali au makampuni. Ili kufanya hii haki iwe
12 halisi, lazima tuelewe kuwa
13 inaweza kutumiwa na watu wote wa asili, ikiwa ina maana
14 serikali na makampuni lazima waheshimu
15 jinsi tunavyo wasiliana na tunavyofanya maamuzi. Ina
16 maana kuwa mwakilishi wa serikali, wa
17 kampuni na wa jamii lazima wakae pamoja
18 na kukubaliana vipengele vya mradi na kuwa
19 sisi tuna kauli ya mwisho ili kukubaliana na mpango utakao
20 nufaisha jamii yetu.
Msimuliaji:
21 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]
20. Vidokezo
Dhibiti: muziki wa asilia nyuma
Msemaji 1:
1 Unajua hatua zinatakiwa kuchukuliwa ili kuweza
2 haki ya kuafiki kwanza bila shuruti
3 baada ya kupewa taarifa kamili kwa watu wa asili inafanywa kwa
usahihi?
Dhibiti: muziki unakata (sekunde 3)
Msemaji 2:
4 Ili kuweza kutambua haki hii kwa idadi yote ya
5 watu, lazima tufikirie hivi vielelezo tunapokabiliana na
6 mradi wa maendeleo katika ardhi yetu. Watu wa asili
7 lazima wafahamishwe kuanzia mwanzo
8 wa hatua za upangani. Muda wa kutosha
9 utolewe kwa jamii nzima kuweza kupata
10 habari zote muhimu kuhusu mradi na
11 athari zake, na kuruhusu mazungumzo na majadiliano ya
12 masuala haya. Habari itolewa
13 kwa mujibu na namna ya tamaduni yetu.
14 Maamuzi yafikiwe bila
15 udanganyifu wowote au shinikizo kutoka kwa wenye mamlaka
16 na mradi. Miafaka yote itakayofikiwa na jamii
17 iandikwe kwa undani. Kama haki yoyote kati ya hii
18 imekiukwa, kumbuka kuna njia
19 tunazoweza kutafutia msaada na kukemea ukiukwaji huu
20 wa haki za binadamu, kwenye taasisi za kimataifa kama
21 Umoja wa Mataifa.
Msimuliaji:
22 Kwa taarifa zaidi, tembelea cultural survival dot org slash consent[culturalsurvival.org/consent or cs.org/consent]