taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa vyombo vya habari “press release” tarehe 18.03.2015

3
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA. RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260, Fax - +255252503734 MBEYA. E-mail:- [email protected] [email protected] KIJANA MMOJA MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI BAADA YA KUTOKEA UGOMVI. JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI. JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA SIMBALIVE WILAYANI CHUNYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI, POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU. KATIKA TUKIO LA KWANZA: KIJANA MMOJA MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HODAR JOHN (22) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GILBERT MWASIMA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU. TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 17.03.2015 HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KILICHOPO KATIKA KITONGOJI CHA ITIMBO, KIJIJI CHA ISALE, KATA YA LUTEBA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA ULEVI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 03-Oct-2015

10.695 views

Category:

Documents


5 download

DESCRIPTION

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.03.2015.

TRANSCRIPT

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHIJESHI LA POLISI TANZANIA.

RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,Fax - +255252503734 MBEYA.E-mail:- [email protected] [email protected]

KIJANA MMOJA MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI BAADA YA KUTOKEA UGOMVI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA SIMBALIVE WILAYANI CHUNYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI, POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

KIJANA MMOJA MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HODAR JOHN (22) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GILBERT MWASIMA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 17.03.2015 HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KILICHOPO KATIKA KITONGOJI CHA ITIMBO, KIJIJI CHA ISALE, KATA YA LUTEBA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA ULEVI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA KUWEZESHA KUMPATA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

TAARIFA YA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA KISEPE ALPHONCE (28) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA KASUMULU-KYELA PAMOJA NA NSAJIGWA MWAKALONGE (39) DEREVA NA MKAZI WA KYELA WAKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] KUTOKA NCHINI MALAWI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA DOUBLE PUNCH KATONI 70, BOSS KATONI 18, CHARGER KATONI 14 NA RIDDER KATONI 08.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2015 MAJIRA YA SAA 03:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA WAKIWA WANASAFIRISHA BIDHAA HIZO KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.479 CJM TOYOTA IPSUM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA NSAJIGWA MWAKALONGE WAKITOKEA KASUMULU KUELEKEA MBEYA MJINI.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA SIMBALIVE WILAYANI CHUNYA AITWAYE ELIZA KISUNGA (33) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA SIMBALIVE AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NNE NA NUSU PAMOJA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA RIDDER PAKETI 03 NA VIPODOZI AINA YA EPIDEMIC PAKETI 02.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SIMBALIVE, KIJIJI CHA ITUMBA, KATA YA CHALANGWA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BIDHAA HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Imesainiwa na:[AHMED Z. MSANGI SACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.