kuelekea mvurugano na mgongano wa siasa za kimataifa? ambaye chini ya uon-gozi wake amelisimamia...

14
munyange ambaye chini ya uon- gozi wake amelisimamia Jeshi katika mabadiliko makubwa ya kiutendaji, mikakati, mifumo na miundo ili kuliingiza katika karne ya ishirini na moja likiwa ni jeshi dogo, jepesi na la kisasa. Mojawapo ya mabadiliko makubwa ambayo yametokea ndani ya JWTZ wakati wa Mwa- munyange ni kulisogeza jeshi hilo karibu kiteknolojia na kiufundi kwa nchi ya Marekani kinyume na ilivyokuwa kwa muda mrefu huko nyuma ambapo JWTZ ili- kuwa karibu zaidi kiufundi na kiutalaamu na Jeshi la China. ROS NOSTO ODIT LAN ULLA FACIN HENIM ..................................................................... 1 RAESEQCTET NIAM ......................................................................................................... 1 SCIEM INE VERIPIO NSULIN ............................................................................................ 1 ASTIUS PUBLIS ETRIDET .................................................................................................. 1 ACIDUISMODIO ...........................................................................................2 HENDION DUNT ............................................................................................................... 2 AT ATUE ........................................................................................................................... 2 GIAM VER......................................................................................................................... 2 TIO VERIUSC ILIQUAT ..................................................................................3 ENIM IUSTO OD DOLORE VELENT WIS ALIQUIS ............................................................... 3 RAESEQCTET NIAM ......................................................................................................... 3 RAESEQCTET NIAM ......................................................................................................... 3 CULLA REM TUS ..........................................................................................4 UNTERE EFFRE DIO SULTORUM ....................................................................................... 4 AXIMPL. DUCESCIEMUS................................................................................................... 4 TO VE, MORUDE ............................................................................................................... 4 UGAIT AUGUE TAT ........................................................................................................... 5 ALISMOD BLANDRE .....................................................................................6 LOR ILIQUIS ALIQUIPIT .................................................................................................... 6 HENDION DUNT ............................................................................................................... 6 ED DOLOBOR PERCILIS .................................................................................................... 6 AMCORPER UTAT .........................................................................................7 SIM DIT ACING ................................................................................................................ 7 VEL BLAM CONSENT ESTO .............................................................................................. 7 NITALATORUS PROX NUM ............................................................................................... 8 INT, CONSIMISQUAM FACTALABUS ................................................................................. 8 VIDIIS NONSULA RITAMPL .............................................................................................. 8 SUM ALISCIP ERCILLA .................................................................................9 EXER SUSCILIQUAT AD DOLORPE RATING EL ULLA FEUGUE ........................................... 9 LOREM ULLAOR ILIT EXERO ............................................................................................ 9 ALISMOD SECTE BLANDRE ......................................................................... 10 ET, CONSEQUIPIT NULLAM ALIS NUM IN UTAT .............................................................. 10 VEL DOLUPTAT . ............................................................................................................. 10 PUTE MOD EXMINIBH AUTEM ....................................................................................... 10 DO AUGAIT EUGAIT ................................................................................... 11 OSTO DOLORE VER IUSCI TAT VELIT AM NIT ................................................................... 11 FEU FACI ETUEROS NIM VOLOBOR ................................................................................ 11 ED ELIQUIP ISMODOL ................................................................................................... 12 LIT NIAM .................................................................................................. 13 SERATUAM IUS PRICA ................................................................................................... 13 SERES NORUM MED ECONSUS INAM ............................................................................. 13 TOLEO LA KILA WIKI ISNN: Toleo la MAJARIBIO FEBRUARI 10, 2017 BEI SH 800/- ZAMA MPYA! Gazeti la Utetezi wa Fikra Mpya! Unachokijali Ndicho Tunachokijali... MAGUFULI AMTEUA MABEYO KUWA MKUU MPYA MAJESHI YA ULINZI MHARIRI: “Kwa hili CCM inabeba Lawama zaidi” Kati ya Mambo Mengi hili moja ni la kuilaumu CCM zaidi Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuilaumu CCM. Lakini Bungeni: Mbowe Adai Rais Anataka Kufuta Upinzani Na. Zahara Mussa Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai Bw. Free- man Mbowe leo Alhamisi amedai kuwa kuna kila dalili zinazoone- sha kuwa Serikali ya awamu ya Tano inataka kuangamiza upinzani nchini. Ametoa madai hayo wakati akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Bw. Kassim Majaliwa katika kipindi cha maswali INDEX » Inaendelea UK. 6 » Inaendelea, UK. 2 Donald Trump: Rais wa 45 wa Marekani Kuelekea mvurugano na mgongano wa siasa za kimataifa? MIJADALA NA HOJA Uk. 6 MAKALA YA MWANAKIJIJI - “Bunge lisilojiheshimu haliwezi kuheshimiwa” Uk. 8 MICHEZO: Cameron Yanyakua Ubingwa AFCON’17 Uk. 14 MIKOANI: Madaktari wa Korea Wato Tiba SengeremaUk. 3 Anashika madaraka huku akiacha Wamarekani na dunia ikiwa na maswali mengi ya diplomasia IJUMAA tarehe 20 Januari, 2017 saa sita kamili mchana Rais Mteule wa Marekani Bw. Donald Trump aliapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani akimrithi Rais Barack H. Obama anayemaliza muhula wake wa pili unaoruhusiwa kikatiba. Rais Trump anaelekea kushika madaraka huku akibeba maswali mengi ya siasa za ndani za nchi yake lakini vile vile akibeba mas- wali ya wanadiplomasia wengi wa dunia ambao wanahofia utawala wa Trump kubadilisha siasa za kimataifa za Marekani kwa kiasi kikubwa na katika hilo kuelekea kubadilisha mwelekeo wa siasa za kimataifa za dunia. Siasa za kimataifa katika mwaka 2017 na kuendelea bado zinak- abiliwa na changamoto mbalim- bali; nyingi zikiwa ni za miaka mingi iliyopita na nyingine zikiwa ni mpya. Donald Trump anaingia katika Jumba Jeupe la Rais wa Marekani akiwa ni mtu ambaye muda wote wa kampeni alioneka- na kushabikia siasa za zile ambazo zitaiweka “Marekani Kwanza”. Michael J. Green mchambuzi wa masuala ya kimataifa ambaye amewahi kuwa kwenye Baraza la Usalama la Taifa la Rais George W. Bush na baadaye kufanya kazi Wiz- ara ya Ulinzi ya Marekani ameliam- bia gazeti la mrengo la kushoto la New York Times la Marekani kuwa “Nchi inaingia katika eneo ambalo hatujawahi kuingia kama Jamhuri. Hatujawahi kuwa na Rais mwenye himaya kubwa ya kibiashara ndani na nje ya Marekani”. Kusema Donald Trump ana hima- ya nje na ndani ya Marekani labda hakutoshi kuelezea jinsi gani Bw. Trump amepanua biashara zake karibu kila pembe ya dunia na hivyo kusababisha maswali kama mataifa ambako anafanya biasha- ra yatahusiana naye vipi wakati akiwa Rais wa Marekani. Donald Trump ana miradi mbalimbali ya HABARI ZILIZOMO Na. Mwandishi Wetu IKULU – DAR-ES-SALAAM – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan- zania John Pombe Magufuli leo amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu mpya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuchukua nafasi iliyoach- wa wazi na Jenerali Davis Mwamu- nyange ambaye amestaafu mwis- honi mwa Januari mwaka huu. Pamoja na kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa wa kijeshi Rais amempandisha cheo Lu- teni Jenerali Mabeyo kuwa Jenerali. Jen. Mwamunyange alikuwa astaafu mwaka jana Januari lakini Rais Magufuli al- imuongezea mwaka mmoja wa utumishi wakati akiendelea ku- panga safu yake ya viongozi. Katika taarifa iliyotolewa na Iku- lu jioni jana (Alhamisi) Rais Magu- fuli pia amtemteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnad- hibu Mkuu wa jeshi kuchukua na- fasi iliyoachwa na kuteuliwa kwa Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Pamoja na kuchukua nafasi hiyo Meja Jenerali Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Lu- teni Jenerali. Teuzi hizo zinaanza mara moja na wataapishwa katika wakati utakaotangazwa baadaye. Rais Magufuli hadi hivi sasa ameshapanga sehemu kubwa ya serikali yake na kuteua karibu viongozi wote wakuu wa nchi ambapo tayari alishafanya teuzi za wakuu wa TAKUKURU, na Usalama wa Taifa. Kwa kuteua mkuu mpya wa Jeshi la Polisi na- fasi ambayo inasubiriwa kujazwa ni ile ya Jaji Mkuu ambayo sasa hivi inakaimiwa na Jaji Ibrahim Hamisi Juma ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa Jaji Othman Chande. Mkuu huyo mpya wa majeshi anaingia kushika madaraka aki- pokea kutoka kwa Jenerali Mwa- Rais Donald Trump akila kiapo cha uaminifu kwa Katiba ya Marekani wakati akiapishwa kuwa Rais wa 45 wa Taifa hilo siku ya Ijumaa tarehe 20 Januari, 2017. Aliyeshikilia Biblia mbili ni mkewe Melania Trump. » inaendelea, UK. 3 Na. Ben Godfrey WASHINGTON, DC » Inaendelea, UK. 5 Rais Donald Trump ameapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani. Hii ina maana gani katika mahusiano ya Kima- taifa? MAWASILIANO MATANGAZO OZ Media House Gazeti la Zama Mpya P. O. Box 90159 Dar es Salaam, Tanzania +255 746 202 000

Upload: ngodieu

Post on 09-Mar-2018

776 views

Category:

Documents


6 download

TRANSCRIPT

munyange ambaye chini ya uon-gozi wake amelisimamia Jeshi katika mabadiliko makubwa ya kiutendaji, mikakati, mifumo na miundo ili kuliingiza katika karne ya ishirini na moja likiwa ni jeshi dogo, jepesi na la kisasa.

Mojawapo ya mabadiliko makubwa ambayo yametokea ndani ya JWTZ wakati wa Mwa-munyange ni kulisogeza jeshi hilo karibu kiteknolojia na kiufundi kwa nchi ya Marekani kinyume na ilivyokuwa kwa muda mrefu huko nyuma ambapo JWTZ ili-kuwa karibu zaidi kiufundi na kiutalaamu na Jeshi la China.

ROS NOSTO ODIT LAN ULLA FACIN HENIM .....................................................................1RAESEQCTET NIAM .........................................................................................................1SCIEM INE VERIPIO NSULIN ............................................................................................1ASTIUS PUBLIS ETRIDET ..................................................................................................1ACIDUISMODIO ...........................................................................................2HENDION DUNT ...............................................................................................................2AT ATUE ...........................................................................................................................2GIAM VER.........................................................................................................................2TIO VERIUSC ILIQUAT ..................................................................................3ENIM IUSTO OD DOLORE VELENT WIS ALIQUIS ...............................................................3RAESEQCTET NIAM .........................................................................................................3RAESEQCTET NIAM .........................................................................................................3CULLA REM TUS ..........................................................................................4UNTERE EFFRE DIO SULTORUM .......................................................................................4

AXIMPL. DUCESCIEMUS...................................................................................................4TO VE, MORUDE ...............................................................................................................4UGAIT AUGUE TAT ...........................................................................................................5ALISMOD BLANDRE .....................................................................................6LOR ILIQUIS ALIQUIPIT ....................................................................................................6HENDION DUNT ...............................................................................................................6ED DOLOBOR PERCILIS ....................................................................................................6AMCORPER UTAT .........................................................................................7SIM DIT ACING ................................................................................................................7VEL BLAM CONSENT ESTO ..............................................................................................7NITALATORUS PROX NUM ...............................................................................................8INT, CONSIMISQUAM FACTALABUS .................................................................................8VIDIIS NONSULA RITAMPL ..............................................................................................8SUM ALISCIP ERCILLA .................................................................................9

EXER SUSCILIQUAT AD DOLORPE RATING EL ULLA FEUGUE ...........................................9LOREM ULLAOR ILIT EXERO ............................................................................................9ALISMOD SECTE BLANDRE .........................................................................10ET, CONSEQUIPIT NULLAM ALIS NUM IN UTAT ..............................................................10VEL DOLUPTAT. .............................................................................................................10PUTE MOD EXMINIBH AUTEM .......................................................................................10DO AUGAIT EUGAIT ...................................................................................11OSTO DOLORE VER IUSCI TAT VELIT AM NIT ...................................................................11FEU FACI ETUEROS NIM VOLOBOR ................................................................................11ED ELIQUIP ISMODOL ...................................................................................................12LIT NIAM ..................................................................................................13SERATUAM IUS PRICA ...................................................................................................13SERES NORUM MED ECONSUS INAM .............................................................................13

TOLEO LA KILA WIKI ISNN: Toleo la MAJARIBIO FEBRUARI 10, 2017 BEI SH 800/-

ZAMAMPYA!Gazeti la Utetezi wa Fikra Mpya! Unachokijali Ndicho Tunachokijali...

MAGUFULI AMTEUA MABEYO KUWA MKUU MPYA MAJESHI YA ULINZI

MHARIRI: “Kwa hili CCM inabeba Lawama zaidi”Kati ya Mambo Mengi hili moja ni la kuilaumu CCM zaidi

Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuilaumu CCM. Lakini

Bungeni: Mbowe Adai Rais Anataka

Kufuta Upinzani

Na. Zahara Mussa

Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai Bw. Free-man Mbowe leo Alhamisi amedai kuwa kuna kila dalili zinazoone-sha kuwa Serikali ya awamu ya Tano inataka kuangamiza upinzani nchini.

Ametoa madai hayo wakati akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Bw. Kassim Majaliwa katika kipindi cha maswali

INDEX

» Inaendelea UK. 6

» Inaendelea, UK. 2

Donald Trump: Rais wa 45 wa MarekaniKuelekea mvurugano na mgongano wa siasa za kimataifa?

MIJADALA NA HOJA Uk. 6 MAKALA YA MWANAKIJIJI - “Bunge lisilojiheshimu haliwezi kuheshimiwa” Uk. 8

MICHEZO: Cameron Yanyakua Ubingwa AFCON’17 Uk. 14

MIKOANI: Madaktari wa Korea Wato Tiba SengeremaUk. 3

Anashika madaraka huku akiacha Wamarekani na dunia ikiwa na maswali mengi ya diplomasia

IJUMAA tarehe 20 Januari, 2017 saa sita kamili mchana Rais Mteule wa Marekani Bw. Donald Trump aliapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani akimrithi Rais Barack H. Obama anayemaliza muhula wake wa pili unaoruhusiwa kikatiba. Rais Trump anaelekea kushika madaraka huku akibeba maswali mengi ya siasa za ndani za nchi yake lakini vile vile akibeba mas-wali ya wanadiplomasia wengi wa dunia ambao wanahofia utawala wa Trump kubadilisha siasa za kimataifa za Marekani kwa kiasi kikubwa na katika hilo kuelekea kubadilisha mwelekeo wa siasa za kimataifa za dunia.

Siasa za kimataifa katika mwaka 2017 na kuendelea bado zinak-abiliwa na changamoto mbalim-bali; nyingi zikiwa ni za miaka mingi iliyopita na nyingine zikiwa ni mpya. Donald Trump anaingia katika Jumba Jeupe la Rais wa Marekani akiwa ni mtu ambaye muda wote wa kampeni alioneka-na kushabikia siasa za zile ambazo zitaiweka “Marekani Kwanza”.

Michael J. Green mchambuzi wa masuala ya kimataifa ambaye amewahi kuwa kwenye Baraza la Usalama la Taifa la Rais George W. Bush na baadaye kufanya kazi Wiz-ara ya Ulinzi ya Marekani ameliam-bia gazeti la mrengo la kushoto la New York Times la Marekani kuwa “Nchi inaingia katika eneo ambalo hatujawahi kuingia kama Jamhuri. Hatujawahi kuwa na Rais mwenye

himaya kubwa ya kibiashara ndani na nje ya Marekani”.

Kusema Donald Trump ana hima-ya nje na ndani ya Marekani labda

hakutoshi kuelezea jinsi gani Bw. Trump amepanua biashara zake karibu kila pembe ya dunia na hivyo kusababisha maswali kama mataifa ambako anafanya biasha-

ra yatahusiana naye vipi wakati akiwa Rais wa Marekani. Donald Trump ana miradi mbalimbali ya

HABARI ZILIZOMO

Na. Mwandishi Wetu

IKULU – DAR-ES-SALAAM – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan-zania John Pombe Magufuli leo amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu mpya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuchukua nafasi iliyoach-wa wazi na Jenerali Davis Mwamu-nyange ambaye amestaafu mwis-honi mwa Januari mwaka huu.

Pamoja na kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa wa kijeshi Rais amempandisha cheo Lu-teni Jenerali Mabeyo kuwa Jenerali. Jen. Mwamunyange alikuwa astaafu mwaka jana Januari lakini Rais Magufuli al-imuongezea mwaka mmoja wa utumishi wakati akiendelea ku-panga safu yake ya viongozi.

Katika taarifa iliyotolewa na Iku-lu jioni jana (Alhamisi) Rais Magu-fuli pia amtemteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnad-hibu Mkuu wa jeshi kuchukua na-fasi iliyoachwa na kuteuliwa kwa Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Pamoja na kuchukua nafasi hiyo Meja Jenerali Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Lu-teni Jenerali. Teuzi hizo zinaanza

mara moja na wataapishwa katika wakati utakaotangazwa baadaye.

Rais Magufuli hadi hivi sasa ameshapanga sehemu kubwa ya serikali yake na kuteua karibu viongozi wote wakuu wa nchi ambapo tayari alishafanya teuzi za wakuu wa TAKUKURU, na Usalama wa Taifa. Kwa kuteua mkuu mpya wa Jeshi la Polisi na-fasi ambayo inasubiriwa kujazwa ni ile ya Jaji Mkuu ambayo sasa hivi inakaimiwa na Jaji Ibrahim Hamisi Juma ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa Jaji Othman Chande.

Mkuu huyo mpya wa majeshi anaingia kushika madaraka aki-pokea kutoka kwa Jenerali Mwa-

Rais Donald Trump akila kiapo cha uaminifu kwa Katiba ya Marekani wakati akiapishwa kuwa Rais wa 45 wa Taifa hilo siku ya Ijumaa tarehe 20 Januari, 2017. Aliyeshikilia Biblia mbili ni mkewe Melania Trump.

» inaendelea, UK. 3

Na. Ben Godfrey

WASHINGTON, DC

» Inaendelea, UK. 5

Rais Donald Trump

ameapishwa kuwa Rais

wa 45 wa Marekani. Hii

ina maana gani katika

mahusiano ya Kima-

taifa?

MAWASILIANO

MATANGAZO

OZ Media House

Gazeti la Zama Mpya

P. O. Box 90159

Dar es Salaam,

Tanzania

+255 746 202 000

2 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

MAMA ABWAGA MOYO MBELE

YA RAIS SIKU YA MAHAKAMA Mama abeba bango likiwa na madai mazito dhidi ya Polisi, DPP na taasisi nyingine; amlilia Rais amsaidie

Na. Mwandishi Wetu

DAR-ES-SALAAM, Mwanamama mmoja jana jijini Dar-es-Salaam alizua tafrani baada ya kui-buka na bango kubwa lenye madai mbalim-bali wakati wa sherehe za Siku ya Haki Duniani ambazo zilihudhuriwa na Rais John Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wa mahakama na vyombo vingine vya dola. Mama huyo Bi. Sobha Mohammed (pichani)alisubiri wakati muafaka pale ambapo wageni walikuwa wanajiandaa kumaliza shughuli na kuelekea kwenye tukio la kupiga picha. Mama huyo alifunua bango la kitambaa na kuanza kuelekea kwenye meza kuu. Walinzi walioku-wepo mara moja walianza kumzuia kwenda mbele na kujaribu kumuondoa mahali pale. Hata hivyo Rais Magufuli aliingilia kati na kutaka mama huyo aletwe mbele zake na ajieleze pasipo woga wowote juu ya masahibu yake. Sauti yake ikikatika katika kwa uchungu mama huyo alielezea ni jinsi gani amedhulumiwa mali mbalimbali za marehemu mmewe na juhudi zake zote za kutafuta msaada zimegonga mwamba. Alidai kuwa amefika karibu kwa viongozi wote bila mafanikio yeyote na ndio akaamua kuchukua uamuzi huo akiamini liwalo na liwe. Baada ya kumsikiliza kwa makini Rais Magu-fuli aliagiza vyombo mbalimbali vishughulikie madai ya mama huyo na kuhakikisha kuwa analindwa na asipatwe na tatizo lolote. Hili ni tukio la pili la aina yake ambapo wanawake wamekimbilia kwa Rais kuelezea shida zao baada ya kushindwa kusikilizwa katika vyombo vya chini. Tukio hilo limeacha maswali mengi kwa baadhi ya watu kama mifumo yetu inaweza kweli kuwasaidia watu wanyonge na wale ambao wanaamini hawana mtetezi. Hata hivyo siyo wote walioamini habari ya mama huyo na wapo wengine ambao walidai kuwa haina ukweli. Ni wazi uchunguzi wa kina unatakiwa kufanyika kwa mujibu wa maoni ya wengi ili kuhakikisha kuwa mama huyo ana-tendewa haki na ukweli wote unajulikana

MABEYO ATEULIWAMKUU WA MAJESHI

YA ULINZI TANZANIA

HABARI ZA KITAIFA

Mojawapo ya matokeo hayo ni kuongezeka kwa askari wa Tanza-nia ambao wanapewa mafunzo ya kijeshi huko Marekani miongoni mwao wakiwemo makomandoo na na makamanda wa ngazi mbalimbali.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ali-potembelea chuo kikuu cha kijeshi cha Marekani cha West Point alisema wazi kuwa uhusiano kati ya Tanza-nia na Marekani uko katika ubora wa hali juu zaidi kuliko huko nyuma.

Wamarekani waliombwa ku-toa mafunzo kwa wanajeshi wa Tanzania waliokuwa wanajiandaa kwenda kuungana na majeshi ya kulinda amani huko Darfur, Su-dan na Lebanon. Wamarekani pia walitoa msaada wa kiusafirishaji kwa wanajeshi wa Tanzania wakati wa Operesheni ya Kurejesha De-mokrasia katika visiwa vya Comorro.

Mabadiliko mengine makubwa ni ya zana mbalimbali za kivita am-bayo yamefanyika na yanaendelea kufanyika hadi sasa. Hii ni pamoja na kutumia vifaru vya kisasa ambavyo vinatumiwa sana na Jeshi la China vya aina ya 63A pamoja na ndege 14 za kivita za J-7G ambazo zilika-bidhiwa kwa Tanzania mwaka 2014.

Na. Mwandishi Wetu

UYUI, TABORA - Mkuu wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora Bw. Gabriel Mnyele (pichani kulia) ameamua kuachia ngazi ili aweze kuendelea na shughuli zake binafsi. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari na mitandao ya jamii Bw. Mnyele aliambia kikao cha madiwani huko Uyui kuwa amemuandikia barua Rais John Magufuli kuomba kujiuzulu na kuwa amekubaliwa ombi lake na hivyo alitumia nafasi hiyo kuwaaga.

Habari za kuachia ngazi kwa DC huyo ambaye ni wakili zimepokelewa kwa hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wa wachan-giaji wakimpongeza kwa kuchukua uamuzi huo na wengine wakiuliza hasa sababu za kuachia ngazi waka-ti huu ambapo kwenye baadhi ya wilaya kumekuwa na matatizo ya upungufu wa chakula na ukame.

Wilaya ya Uyui imekuwa ni mion-goni mwa wilaya chache nchini am-bapo karibu kila mwaka zimekuwa zikikabiliwa na upungufu wa chakula. Mwaka 2013 Uyui ilipewa msaada wa karibua tani 500 ili kusamba-zwa katika kata 13 kati ya 24 za wilaya hizo ambazo zilikuwa zinak-abiliwa na upungufu wa chakula.

Mwaka 2015 Uyui walikabili-wa na njaa tena hususan kwenye jimbo la Igalula. Kwa mara ny-ingine wilaya hiyo iliomba tena chakula cha msaada kupitia ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa.

Hata mwaka jana Uyui bado wa-likuwa wanakabiliwa na upungufu wa chakula lakini katika moja ya

watano ambao wamewafikisha kwenye vyom-bo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Hata hivyo alisema wapo madalali wakubwa wa madawa ya kulevya na wapo wasambazaji. Alitumia dakika chache kutaja baadhi ya majina ya watu aliowatuhumu kuwa wanahusika na biashara hiyo. ZAMA MPYA haitotaja majina hayo hadi watuhu-miwa hao watakapokuwa wamekamatwa au kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Makonda alisema pia kuwa wapo watu wen-gine ambao wao wanatuhumiwa kutumia madawa hayo. “Hawa nao ni vyema nikakuta-na nao kesho pale central” alisema Makonda akitaja majina ya baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakitajwa kuwa ama wamea-thirika na madawa hayo au bado wanatumia.

Pamoja na hilo Makonda alidai pia kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo watu wenye leseni za biashara lakini maeneo hayo yanatumika pia kupitishia madawa ya kulevya. “Hawa pia naomba kesho tu-kutane nao na wasipokuja nitawafuata mwenyewe” amesema Makonda bila ya kuelezea ni sheria gani inampa madaraka ya kutoa tuhuma na hata kufanya uchun-guzi wa masuala ya kihalifu dhidi ya raia.

Pamoja na hilo Makonda pia alitoa madai dhidi ya baadhi ya watu wenye dhamana mbalimbali za uongozi ambapo alisema kuwa baadhi yao pia wanahusika katika kuwezesha biashara hii kuendelea katika Jiji hilo kubwa kabisa nchini lenye wakazi wapatao milioni 5.

“Katika operesheni yangu niliyofanya nimekutana na taarifa zao kwani nimekuwa nikijiuliza kwanini madawa haya ya kulevya hayaishi?” alisema Makonda na kutoa jibu kuwa “polisi wanashirikiana na wafanya-biashara wa madawa ya kulevya na hivyo kufanya biashara hii kutokuwa rahisi kuto-komezwa ndani ya Jiji la Dar-es-Salaam”.

Makonda aliagiza kuwa baadhi ya maafisa wa polisi ambao alikuwa awata-je wanatakiwa wakamatwe na kuwekwa mahabusu ili kupisha uchunguzi zaidi.

Hata hivyo kitendo cha Makonda ku-toa tuhuma hizo na kuonekana kuingilia wajibu na kazi za vyombo vingine vya dola kimeacha maswali mengi kwa wata-laamu wa sheria na wananchi wa kawaida.

Baadhi ya wachangiaji kwenye mitan-dao mbalimbali ya kijamii wameshangaa ni kwanini Makonda ameenda kwenye vyom-bo vya habari badala ya kufuata taratibu za kawaida za kuweza kuwanasa watuhumiwa hao badala ya kuwapa muda mzima wa kuji-andaa au kuharibu ushahidi na hivyo kufanya kesi dhidi yao kuwa ngumu mahakamani.

Haijajulikana ni kwa kiasi gani hatua hii ya Makonda itachangia kufanikiwa au kudhoof-idha kwa jitihada za serikali kupambana na uuzwaji na matumizi ya madawa ya kulevya nchini.

mambo ya kushangaza baadhi ya wa-nanchi waligomea chakula cha msaada ati kuwa “hakitoshi” kulinganisha na njaa iliyokuwepo. Hilo lilitokea katika kijiji cha Ibiri huko Uyui ambapo wananchi waligo-mea magunia 24 ya mahindi ambayo

yalipelekwa kwa ajili ya msaada. Mwaka huo pia Uyui walikuwa wanapokea tani 400 za chakula cha msaada ili kisamba-zwe kwenye vijiji 156 wilayani humo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya ZAMA MPYA Mkuu huyo wa wilaya ame-amua kuachia ngazi pia kutokana na saba-bu hizi hizi za njaa. “Ameona hawezi kuen-delea kuwa mahali ambapo hawezi kutoa msaada wakati watu wanatabika na njaa” kimesema moja ya vyanzo vyetu. Chanzo kingine kimedokeza pia kuwa “nafasi ile ya UDC ilikuwa ngumu kwake kwani ilisa-babisha ‘njaa ifike hadi nyumbani’ kwa DC.”

“Unajua kama wakili alikuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake na famil-ia vizuri lakini inawezekana sasa hivi kama DC hali haikuwa hivyo na ame-ona badala ya kutafutana lawama ni bora aachie ngazi” ameongeza mmoja wa marafiki zake wa karibu huko Uyui kwa masharti ya kutotajwa jina lake.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa yeyote anayepewa kuongoza wilaya ya Uyui ni lazima awe mtu wa kujitoa na mwe-nye ubunifu wa kukabiliana na hali ya njaa inayokumba wilaya hiyo karibu kila mwaka. “Hadi hivi sasa inaonekana hajapatikana mtu hasa mwenye kuweza kutoa uongozi wa kuongoza wilaya hiyo ili iwe na usala-ma wa chakula kwani hata mvua zikinye-sha watu wanakabiliwa na njaa!” ame-sema mmoja wa wananchi wilaya hapo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu siku ya Ijumaa imesema kuwa Rais John Magufuli amer-idhia kujiuzulu kwa Mkuu wa wilaya huyo.

Na. Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Paul Makonda jana amezua mjada-la mkubwa pale alipojitokeza hadha-rani na kuzungumza na vyombo vya habari na kutoa madai ya kujua wa-husika mbalimbali wa biashara ya madawa ya kulevya katika Jiji la Dar.

Akizungumza akiwa amesimama ofisini kwake, Makonda alisema kuwa tatizo la madawa ya kulevya ni kubwa na wakati umefika yeye kujitokeza kupambana nalo. Amesema kuwa ameendesha operesheni kwa kushirikiana na vyombo vya usalama ambapo walifanikiwa kuwakamata watu

MKUU WA WILAYA UYUI

AACHIA NGAZI

RC MAKONDA ATOATUHUMA NZITOKUHUSIANA NA NA MADAWA YA

KULEVYA

HABARI KUU: DONALD TRUMP: UJIO WA MGONGANO WA SIASA ZA KIMATAIFA?Februari 10, 2017 ZAMAMPYA 3

kibiashara katika nchi zaidi ya 20 duniani ambako amefungua mahoteli, majengo ya kibiashara na viwanja vya mchezo wa golfu na kumbi za burudani kama makasi-no n.k. Hadi anaenda kuchaguliwa mwaka jana Trump alikuwa na makampuni zaidi ya 140.

Baadhi ya nchi ambazo Trump anaenesha biashara yake ni pamoja na India, Brazil, Indonesia, Misri, Canada, China, Uturuki, Ireland, Falme za Kiarabu (UAE) n.k.

Lakini kubwa linalohofiwa na baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa na wana-diplomasia siyo tu mgongano wa kimasla-hi unaoonekana kuwepo kati ya Serikali ya Trump na nchi mbalimbali ambazo makampuni yake yanafanya biashara bali zaidi ni matokeo ya uongozi wa Trump ka-tika siasa za Kimataifa katika nchi hizo.

Kutokana na kampeni yake mwaka jana ambapo kwa kiasi alifunua mawazo yake juu ya masuala mbalimbali nyeti ya kima-taifa ni wazi Donald Trump anakabiliwa na masuala mbalimbali ambayo yata-amua kwa kiasi gani Marekani inahusiana na mataifa mengine – yale ambayo ni marafiki, washirika wake na yale ambayo yanatazamana kwa shuku au kiuadui. Baa-dhi ya maeneo ambayo siasa za Marekani zinaweza kubadilika kwa kiasi kikubwa na kuwa na matokeo ya kudumu kwa muda mrefu katika siasa za Kimataifa ni haya ya-fuatayo.

Uhusiano wa Marekani na NATO

Donald Trump alijionesha kuwa siyo shabiki mkubwa wa mfumo uliopo sasa wa Ushirikiano wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO). Wakati wa kampeni Trump alikosoa ni kwa jinsi gani Marekani inatumia fedha nyingi kulipia majukumu mbalimbali ya NATO kulinganisha na nchi nyingine tajiri zilizomo ndani ya Umoja huo. Wakati huo Trump alisema wazi kuwa NATO imepigwa na wakati na kuwa wakati umefika nchi nyingine zianze kulipia seh-emu yao ya gharama kuliko kuitegemea Marekani.

Kauli zake hizi zilipokelewa na baadhi ya watu kama Trump ana mpango wa ku-vunja umoja huo. NATO ilianzishwa mwa-ka 1949 ikiwa na mataifa kumi ya Ulaya pamoja na Canada na Marekani yakiwa na lengo la kujihami na kuibuka kwa Urusi ya Kisovieti. Sasa hivi umoja huo una wana-chama 28 ambao ni Uturuki tu yenye wau-mini wengi wa Kiislamu kulinganisha na nchi nyingine jambo ambalo tayari lime-kuwa likizua mitizamo mikali ya kisiasa katika baadhi ya nchi za NATO.

Alipokuwa akizungumza na mwandishi wa CNN Wolf Blitzer Machi 21 mwaka jana wakati wa kuelekea kampeni za ndani za chama chake Trump akijibu swali la mtazamo wake kuhusu NATO Trump alise-ma “tunalipia fedha nyingi sana kwenye NATO; umoja ulianzishwa wakati wa to-fauti sana na sasa na wakati huo tulikuwa ni nchi tajiri sana lakini sasa hatuko hivyo. Tunachangia zaidi kuliko wengine na hili nataka libadilike”.

Ni kwa kiasi gani Trump ataelekea kulib-adilisha hili na maana yake kwa ushirikia-no wake nan chi za Ulaya Magharibi lina-subiriwa kuonekana.

Donald Trump na Israeli na Siasa za Mashariki ya Kati

Kama kuna eneo la kimataifa ambalo watu wanaangalia chini ya Trump litaku-waje ni eneo la Mashariki ya Kati ambapo mgogoro kati iya Wapalestina na Waisraeli umekuwa ukifukuta kwa zaidi ya miaka hamsini sasa. Uhusiano kati ya Marekani ni wa muda mrefu na ni wazi bila Marekani Israeli isingeweza kuwepo ilipo sasa wala kuwa na nguvu ya kijeshi kama ilivyo sasa. Kwa Wamarekani, Israeli ndiye rafiki yao mkubwa zaidi katika Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, siku chache kabla ya kuapish-wa kwa Donald Trump na wiki chache kab-la ya kuondoka kwa Barack Obama tofauti kati ya serikali ya Marekani na ya Israeli ilifunuliwa zaidi kufuatia Marekani kuji-toa kupiga kura kwenye azimio la Umoja wa Mataifa (Azimio 2334) ambalo lililaani

upanuzi wa makazi ya walowezi wa Kiis-raeli katika maeneo ambayo Wapalestina wanaamini yanapaswa kuwa sehemu ya ardhi yao yatakapofikiwa maamuzi ya kuwa na mataifa mawili (two states solu-tion).

Mara kadhaa huko nyuma Marekani ime-kuwa ikitumia kura yake ya turufu kuzuia maazimio kama hayo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na safari hii ilidhaniwa ingekuwa hivyo.

Kitendo cha Marekani kukaa pembeni na kuacha azimio hilo liende na kuwa rasmi kwenye Baraza kilichukuliwa kama kiten-do cha usaliti cha serikali ya Obama. Waziri Mkuu wa Israeli Bw. Benjamin Netanyahu alitoa kauli kali ya kupinga jambo hilo na kuona ni kama Obama amewashtukiza. Alirusha madongo kwa Obama kwa kuse-ma kuwa hali hii ya Marekani kutoiunga mkono Israeli inaeleka mwisho kwani Donald Trump atakuwa Rais Januari 20 na jambo kama hilo halitorudiwa tena.

Na kweli, Donald Trump akitumia mtan-dao wa twitter aliandika kulaani uamuzi huo wa Marekani na kuwapa moyo Wais-raeli kuwa hali itakuwa tofauti kuanzia Januari hiyo 20. Hofu iliyopo ni kuwa urafi-ki wa karibu wa Trump na Netanyahu un-aweza ukasababisha mlipo wa mgogoro mkubwa Mashariki ya Kati ambao hau-jawahi kuonekana kabla.

Baadhi ya mambo ambayo yanaweza ku-sababisha mgogoro mkubwa mbeleni ni kama yale yaliyoanishwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mashariki ya Kati kutoka taasisi ya Washington Institute Bw. David Makovsky siku chache zilizopita huko New York. Bw. Makovsky ambaye amewahi ku-fanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (State Department) ameanisha baadhi ya mambo ambayo yanaweza ku-leta mgogoro mbeleni kuwa ni pamoja na.

Kama Donald Trump ataunga mkono maamuzi ya Serikali ya Netanyahu kuen-delea kujenga makazi ya walowezi kwe-nye maeneo ya Wapalestina au ambayo yanaendelea kubishaniwa tangu vita ya 1967

Endapo Donald Trump atatimiza ahadi yake ya kuhamisha makao makuu ya Uba-lozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Yerusalemu ambapo ni “Makao Makuu ya Milele” ya Israeli. Hili linaweza kuzifanya nchi za Kiislamu kuona kuwa Marekani imeamua kuwa Yerusalemu yote (bila ku-jali kuwa ni mashariki au magharibi) ni mali ya Israeli.

Wapalestina ambao sehemu kubwa ya ile wanayoamini ni ardhi yao inakaliwa kimabavu na Israeli wanaweza kuamua kujiunga na taasisi za Kimataifa ambazo hivi sasa hawajajiunga nazo kama ma-jibu yao kwa Trump. Wakifanya hivyo na kwa sababu hawajatambuliwa kama na jamii kubwa ya kimataifa kunaweza kusa-babisha Marekani chini ya Trump kuamua kukata fedha inazofadhili kwenye taasisi hizo. Baadhi ya taasisi ambazo Wapales-tina wanaweza kuamua kujiunga nazo ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO). Litakuwa pigo kubwa kwa miradi mbalim-bali ya WHO endapo Marekani itakata au kupunguza mchango wake huko.

Endapo Trump ataamua kutengua makubaliano yaliyoingiwa na jumuiya ya kimataifa na Iran ambayo yalikuwa na lengo la kuizuia Iran kuendelea kuchakat-ua teknolojia ya nyuklia. Ni kwa kiasi gani Trump atafumua mkataba huo ambao umekubaliwa nan chi kadhaa za Ulaya na Urusi haijulikani. Lakini endapo ataut-engeua au kuiondoa Marekani katika ku-tumiza majukumu yake je nchi nyingine zitachukua msimamo gani kuhusu Iran? Na kutakuwa na matokeo gani kwa nchi rafiki au ambazo zitaamua kuendelea na wajibu wao kwenye mkataba huo? Je Iran itajibu vipi Marekani kama itajiondoa?

Donald Trump na China

Mojawapo ya mambo ambayo yanasu-biriwa kuonekana yatachukua mweleko gani ni uhusiano wa Donald Trump na China. Tayari kumeshakuwa na hali ya ku-

tofautiana katika mambo ya msingi sana kati ya Donald Trump na China na hivyo kuonesha kuwa japo Wamarekani wen-gi wanaifikiria Urusi kama hasimu wao mkubwa kwa Trump inaonekana ni China ndiyo ambayo inamsumbua sana na in-aweza kumjaribu ujasiri wake.

Tayari alishagongana na China pale alipopokea simu ya Rais wa Taiwan kumpongeza kwa ushindi wake. Jambo hilo liliikasirisha China ambayo inachu-kulia Taiwan kama Jimbo lake lililojitenga toka China. Lakini zaidi Trump tayari ame-shachukua msimamo wa kusema kuwa sera ya “China Moja” ambayo imeshikiliwa na watangulizi wake kwa muda mrefu in-ajadilika na hivyo kuikasirisha zaidi China.

Tayari China imezidi kujijenga kijeshi na kuchukua hatua mbalimbali za kujiimari-sha katika Bahari ya Kusini mwa China ka-tika maeneo ambayo yanabishaniwa kati yake na majirani zake. Hili linawezakana kuwa jambo moja linalomfanya Trump kufikiria kuimarisha majeshi ya Marekani kuweza kukabiliana na matishio hasa ya taifa kama China.

Hata hivyo China wiki iliyopita ilitangaza wazi kuwa sera ya “China Moja” haina mjadala. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang amesema katika taarifa yake mwishoni mwa juma lililo-pita kuwa “Serikali ya watu wa Jamhuri ya China ndio serikali halali inayoiwakili-sha China.. na jambo hilo linatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa na hakuna mtu anayeweza kulibadilisha.”

Donald Trump na Afrika

Kati ya maeneo ambayo Donald Trump hajazungumzia sana wala kufuatilia sana wakati wa kampeni ni sera yake kuhu-siana na Afrika. Ni wazi kuwa Donald Trump anaona Marekani inatoa fedha ny-ingi kwenda nje nay eye lengo lake ni kui-weka Marekani kwanza. Haijulikani kama serikali yake itaendelea na mipango yake ya kusaidia nchi za Kiafrika kupitia Mil-lenium Challenge Account au fedha za PEPFAR ambazo zimesaidia sana katika kupungumza maambukizi ya VVU na ku-fanya dawa za ugonjwa wa UKIMWI kuwa nafuu sana na kwa kiasi kikubwa za bure kabisa; au mipango mingine ambayo il-ianzishwa chini ya Obama.

Na kwa vile hili halijulikani sana, hakuna uhakika sera za Trump kwa Afrika zitaku-wa na mwelekeo gani na nchi za Kiafrika zitapokea vipi. Kama Trump ataamua ku-kaa pembeni na kutokuingilia sana nchi za Kiafrika kiutawala au kidiplomasia kinyuma na waliomtangulia je, siasa za Afrika zitakuwaje miaka hii minne ijayo?

Profesa Peter Vale kutoka Chuo Kikuu cha Johannesburg Afrika ya Kusini anasema kuwa “Kuna uwezekano wa Afrika kush-uka sana katika vipaumbele vya serikali ya Donald Trump”. Akiandika katika uku-rasa wa CNN mwezi Novemba mwaka jana, Profesa Vale anasema kuwa “Donald Trump hatofuatilia sana siasa za ndani za nchi za Afrika isipokuwa kama zinagusa maslahi ya kitaifa ya Marekani”. Ana-ongeza na kusema kuwa “sidhani kama atafuatilia nini kinaendelea Somalia au Ethiopia”.

Mark Anderson na Nicholas Norbrook wakiandika kwenye jarida la The Africa Re-port kuwa kwa jinsi ambavyo Trump ana-onekana kupendelea aina ya uongozi wa watu kama Sadam Hussein na Vladimir Putin basi anaweza kuonekana kuwapa moyo madikteta wa Afrika au viongozi wababe. “Rais Mteule wa Marekani tayari ameshapokea pongezi kutoka kwa Mara-is wa ‘muhula wa tatu’ kama Yoweri Mu-seveni na Pierre Nkurunziza” wanaandika waandishi hao.

Je, Afrika itakuwa na nafasi gani katika siasa za Marekani? Jawabu liko wazi; ita-kuwa na nafasi ile tu ambayo itaonekana kuinufaisha Marekani. Na ni wazi basi kwa nadharia hiyo Afrika haitaangaliwa kama bara; bali kama nchi moja moja.

Donald Trump na ISIS na Syria

Mojawapo ya mambo ambayo Donald

“Haijulikani kama Marekani itaendelea na

mipango ya kusaidia nchi za kiafrika.”

Trump atakabiliwa nayo na inawezekana ya-lichangia kuchaguliwa kwake ni suala la Dola ya Kiislamu maarufu kama Daesh au ISIS. Kikundi hiki cha wapiganaji wa Kiislamu we-nye utii wao kwa Abubakar al Baghdad am-baye wamemkubali kama ndiye kiongozi wa Umma wa Kiislamu (khalifa) duniani kiliweza kuingia na kuchukua maeneo mbalimbali ya Iraq na Syria na kupata utii kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wapiganaji wa Kiisl-amu duniani ikiwemo Boko Haram wa Nige-ria na wapiganaji mmoja mmoja au vikundi vidogovidogo Afrika ya Mashariki hadi Ulaya.

Hata hivyo sera ya Donald Trump kupamba-na na ughaidi wa vikundi vya wapiganaji wa Kiislamu haiko wazi sana na mpinzani wake wakati wa kampeni Bi. Hillary Clinton alidai kuwa hana sera yoyote ya maana. Wakati wa kampeni Trump hakutaka kuweka wazi mkakati wa kupambana na ISIS kwa kuhofia kuwa kuutangaza mkakati huo hadharani ni kuwajulisha ISIS jambo ambalo wanaenda kufanya. Mwezi Aprili mwaka jana Trump alidai kuwa “nikichaguliwa kuwa Rais, ISIS itatoweka na itatoweka kwa haraka sana.. si-tawaambia lini na sitawaambia vipi”.

Hata hivyo, mpango wake wa kuanzisha oro-dha ya Waislamu wote Marekani (karibu mil-ioni 3.3) unakutana na vikwazo mbalimbali vya kisheria na kikatiba. Newt Gingritch ali-yewahi kuwa Spika wa Marekani na mmoja wa watu waliomuunga mkono Trump mape-ma amenukuliwa na gazeti la Independence la Uingereza kusema kuwa Trump anaweza kufanya kama alivyofanya Abraham Lincoln wakati wa vita vya wenyewe huko Marekani ambapo alisitisha baadhi ya haki za kika-tiba kupambana na wananchi wa Kusini wa Marekani ambao walikuwa wanaunga mko-no kujitenga kwa majimbo ya Marekani ku-toka kwenye Muungano wa Marekani.

Trump ameingia na mojawapo ya maagizo ya kwanza ambayo ameyatoa kama Rais ni lile la kusitisha programu ya kupokea wakim-bizi kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na kusitisha kabisa uhamiaji kutoka katika nchi saba ambazo anaamini zinatishia zaidi usalama wa Marekani.

Uamuzi huo wa kutoa agizo la Rais ume-

chukuliwa na kusababisha manung’uniko makubwa kutoka sehemu mbalimbali hasa kwa vile mara baada ya agizo hilo kutiwa saini na Trump wahamiaji wengi walijikuta wanakataliwa kuingia Marekani na hivyo kusababisha mvurugano katika huduma ya usafiri wa anga hasa kutoka katika nchi saba ambazo alizitaja kuhusika na usimamisha wa visa.

Nchi ambazo zimeathirika tayari na uamuzi huo ni Sudan, Libya, Yemen, Iraq, Iran, Soma-lia na Syria.

Uamuzi huo umechukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni ubaguzi wa wazi dhidi ya jamii ya Kiislamu na baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa ulikuwa ni uamuzi dhidi ya Waislamu.

Hata hivyo, japo jambo hilo limewakwaza Waislamu wengi bado kuna baadhi ya vion-gozi wa nchi za Kiislamu ambao wamemte-tea Trump. Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan amesema kuwa agizo hilo siyo katazo dhidi ya Waislamu kwani kama lengo ingekuwa ni Waislamu basi agizo la Rais lingezuia waisl-amu kutoka nchi zote duniani na baadhi ya nchi za Kiislamu hazikuguswa na agizo hilo.

“Nchi zilizotajwa na Marekani zina matatizo ya kimfumo, na zinapaswa kutatua mata-tizo yao ya ndani kabla ya kulalamikia yale ya Marekani” amesema Waziri huyo ambaye anatarajiwa kuwa siku moja anaweza kuwa ndio mtawala wa Saudia.

» Inaendelea, UK. 7

4 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

Katibu Mkuu UM Aipongeza Afrika Kupokea Wakimbizi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres Aipongeza Afrika

Mwandishi Wetu

ADDIS ABABA, ETHIOPIA - Katibu Mkuu Mpya wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Gutteres amelipongeza bara la Afrika kwa kuwa wakarimu kwa wakimbizi. Bw. Gut-teres ametoa pongezi hizo siku ya Jumata-tu Jijini Addis Ababa alipozungumza na viongozi wa Afrika ambao walikuwa wana-kutana katika kikao cha kawaida cha Umoja wa Afrika (UA). Bw. Gutteres amesema kuwa mataifa ya Afrika yameendelea kuwa wakarimu wakubwa kwa wakimbizi na kuwa “mipaka ya mataifa ya Afrika imeendelea kuwa wazi kupokea wale weney mahitaji ya kulindwa wakati baadhi ya mipaka ikifungwa hata kwenye baadhi ya mataifa yaliyoende-lea”. Kauli yake hiyo imechukuliwa kama immlenga Rais wa Marekani Bw. Donald Trump ambaye ametoa agizo la Rais kufun-ga mipaka kwa baadhi ya nchi ambazo zinatoa wakimbizi wengi sasa hivi duniani. Donald Trump alitangaza kuwa wakim-bizi kutoka nchi saba ambazo zina Waisl-amu wengi hawatoruhusiwa kuingia nchini Marekani kwa muda na miongoni mwa hizo nchi saba tatu ni za Kiafrika - Libya, Somalia na Sudan. Nchi nyingine ambazo Trump amezuia kutolewa visa kwa waha-miaji wake kwa siku tisini zijazo ni pamoja na Syria, Iraq, Iran na Yemen. Afrika ina wakimbizi wapatao milioni 18 hivi sawa na robo ya wakimbizi wote duniani. Wengi wa wakimbizi hao wana-toka kwenye nchi zenye migogoro ya ndani ikiwemo wale wanaokimbia vurugu katika nchi zao. Nchi ambazo zimetoa wakimbizi wengi Afrika hadi hivi sasa ni pamoja na Nigeria ambapo wananchi wengi wanakim-bia kundi la Boko Haram, Somalia, Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Burundi. Hadi hivi sasa kambi kubwa ya wakim-bizi duniani iko huko Dadaab nchini Kenya ambapo wakimbizi wapatao 300,000 kutoka Somalia wanaishi. Kenya hata hivyo imetangaza kuwa ina mpango wa kuifunga kambi hiyo kwani inatishia usalama wa nchi hiyo. Katika kikao hicho cha Umoja wa Afrika viongozi wa Afrika waliridhia kuipokea Morocco tena katika Umoja huo baada ya nchi hiyo kujitoa kupinga kutambuliwa kwa Jamhuri ya Sahara Magharibi ambayo imekuwa ikipigania uhuru wake kwa karibu miaka hamsini sasa. Kukubaliwa kwa Morocco kurudi tena kwenye UA kumehiti-misha kampeni ya kubembeleza kuungwa mkono jambo hilo kulikofanywa na Mfalme wa Morocco ambaye alitembelea nchi kadhaa ili kupata kuungwa mkono. Mion-goni mwa nchi alizotembelea ni pamoja na Tanzania. Kikao cha AU kimempitisha Moussa Faki Mahmat kutoka Chad kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU wakati Rais wa Guinea Alpha Konde amechaguliwa kuwa Mwe-nyekiti wa Umoja huo kuchukua nafasi

ya Rais wa Afrika ya Kusini Bw. Jacob Zuma ambaye muda wake umemalizika.

Trump Amtimua Kaimu Mwanasheria MkuuAliagiza maafisa wa wizara wasitetee katazo la viza lililowekwa na Rais kwa Mataifa Saba

Mwandishi Wetu

WASHINGTON, DC. Rais Donald Trump wa Marekani usiku wa Jumatatu wiki hii amemfuta kazi Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani Bi. Sally Yates kwa kushindwa kutekeleza na kutetea agizo la Rais la kusiti-sha utoaji wa viza za uhamiaji kwa wakazi wa nchi saba na zuio la kupokea wakimbizi kwa siku tisini zijazo hadi utakapowekwa utara-tibu mkali wa kuwachuja wahamiaji kutoka nchi hizo. Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani usiku wa Jumatatu Rais Trump ameamua kumvua madaraka yake Bi. Yates baada ya Kaimu Mwanasheria huyo ambaye ni mteuliwa wa Rais aliyepita Bw. Barack Obama kuagiza wanasheria wa wizara yake kutokutetea agizo la Rais kuhusu usitishwaji wa visa. “Bi. Yates ameisaliti Wizara ya Haki kwa kute-tea kusimamia agizo halali lenye lengo la kuwalinda Wamarekani” amesema msemaji wa Ikulu Bw. Sean Spicer. Mapema siku ya Jumatatu Bi. Yates alian-dika memo kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo akidai kuwa agizo la Rais Trump haliwezi kutetewa kisheria na kuwa linaenda kinyume na wizara hiyo ambayo inajukumu la kusi-mamia haki nchi Marekani. Wakati huo huo, Rais Trump amemteua Mwanasheria wa Kanda ya Virginia Bi. Dana Boente kuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu kuchukua nafasi ya Bi. Yates. Bi. Boente ame-sema baada ya kuteuliwa kujaza nafasi hiyo kwa muda kuwa “niko tayari kusimamia na kutetea sheria za nchi yetu mpaka hapo Seneta Sessions atakapothibitishwa na Bunge kuwa Mwanasheria Mkuu.” Tangu kutangazwa kwa agizo hilo la Rais kumekuwa na mchanganyiko wa mawazo ndani ya serikali ya Marekani kuhusiana na uhalali wa agizo hilo kisheria na kesi mbalimbali zimeshafunguliwa na watu na taasisi mbalimbali kupinga agizo hilo na kutaka mahakama ilione kuwa ni kinyume na Katiba. Bi. Yates pichani chini.

HABARI ZA KIMATAIFAVijana 6 Wafa kwa Kuvuta Hewa Chafu Ujerumani Wavulana 5 na msichana 1 wamekufa baada ya tafrija kwenye kibanda bustanini

Mwandishi Wetu

BAVARIA, UJERUMANI, Vijana wapatao sita wakiwa kati ya umri wa miaka 18 na 19 wamekutwa wamekufa baada ya kuvuta hewa chafu ya Carbon Monoxide wakiwa kwenye kibanda kidogo karibu na nyumba ya wazazi wa vijana wawili kati yao.

Polisi kwenye mji mdogo wa Arnstein huko Bavaria Kusini nchini Ujerumani wamesema kuwa mwenye nyumba ambaye ni baba wa binti na mvulana miongoni mwa wale sita ndiye aliyegundua tukio hilo la kusikitisha.

Mzazi huyo aliamka siku ya Jumapili iliyopita na kukuta kuwa watoto wake hawajarudi nyumbani baada ya kwenda kwenye tafrija si mbali sana na nyumbani wakiwa na vijana wenzao. Aliamua kwenda

kuangalia na kuwakuwa wamekufa wakiwa kama wamelala.

Awali polisi walisema kuwa kulikuwa na wasiwasi kuwa labda kuna gesi chafu ilikuwa inavuja mahali lakini baadaye wal-igundua kuwa jiko lenye kutumia kuni lili-kuwa limewashwa na vijana hao ili kupata joto kwenye kibada hicho lakini wakati huo huo hakikuwa na sehemu nzuri za kupitisha hewa na hivyo kusababisha kujaa kwa hewa chafu inayosababishwa na moto kuungua.

Kitaalamu moto huwaka kwa sababu ya hewa ya oksijeni ambayo binadamu na wanyama huiitaji na unapoungua unaacha hewa chafu ya carbon monoxide ambayo ni sumu kwa binadamu na wanyama.

Uchunguzi wa miili ya vijana hao ume-fanyika na kuthibitisha kuwa wamekufa kwa kuvuta hewa chafu. Pichani juu polisi wakikusanya vielelezo mbalimbali eneo la tukio. Pamoja na taarifa za awali kuon-esha kuwa chanzo inawezekana ni moto wa kuni polisi wamesema pia wanaangalia kama kuna kitu kingine chochote ambacho kinaweza kusababisha gesi hiyo ya sumu kuingia kwenye kibanda kilichotumiwa.

Inasemekana vijana hao walikuwa wame-kusanyika kwa ajili ya kusherehekea miaka 18 ya yule msichana kwa mujibu wa maji-rani. Eneo la kanisa dogo katika mji huo ndio linatumiwa kwa ajili ya maombolezo na watu wengi wamejitokeza kutoa rambi-rambi na pole zao kwa wafiwa.

Februari 10, 2012 ZAMAMPYA 5

Wanawake Waache Utegemezi - Kigogo UWTKuelekea Miaka 40 ya Chama cha Mapinduzi Naibu Katibu Mkuu UWT (Bara) Awataka Wanawake Kujikomboa Kiuchumi

Na. Dotto Kwilasa DODOMA, Zikiwa zimebaki siku chache chama cha mapinduzi kutimiza miaka arobaini

tangu kuanzishwa kwake Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Tanzania Bara Bi. Eva Mwingizi amewataka wanawake kujiamini na kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume ili waweze kuondokana na umasikini.

Hayo aliyasema jana mjini Dodoma alipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima kinachoitwa Rahmani Orphanage Center kilichopo kata ya Chang’ombe kinachomilikiwa na kikundi kidogo cha wanawake. Naibu Katibu Mkuu huyo ambaye aliongozana na wabunge watatu wa viti maalumu alisema kuwa wanawake wanatakiwa kujiamini na kujichanganya na watu wengine kwani anaamini kuwa wanawake wanaweza bila kuwezeshwa.

“Wanawake tujishughulishe tuache kuwa tegemezi kwani wapo waliowezeshwa kifedha wakapewa na ukimwi”alisema Mwingizi. Aidha wabunge wa viti maalumu (CCM)ambao walimuunga mkono naibu katibu UWT bara kwa kutoa msaada wenye zaidi ya shilingi laki nne na nusu ni Zainabu Vullu mkoa wa Pwani, Ester Mahawe mkoa wa Manyara, na Bupe Mwakipesile wa mkoa wa Rukwa.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Pwani (CCM)Zinabu Vullu aliwaasa watoto wa kituo hicho na kuwataka kusoma kwa bidiii na kuwaheshimu walezi wao ili waweze kuwa na maadili mema. “Watoto wakike jitahidi kusoma na siyo kusomwa ingawa mnatakiwakujifunza wenyewe ili muweze kuwa mfano kwa watoto wengine”alisema Vulla.

Naye Katibu mlezi wa kituo hicho Rukia Hamisi alisema kuwa kituo hicho kinawatoto zaidi ya 75 ambapo baadhi yao wameweza kuwasomesha mpaka kidato cha sita. Alisema baadhi ya changamoto walizonazo ni pamoja na kukosa mradi wa kujiendesha kiuchumi ambao ungeweza kusaidia katika kukipatia kituo kipato cha kuweza kulipia maji,umeme,matibabu, chakula na vifaa vya ofisi kwani hawapati fungu lolote kutoka serikalini.

“Ingawa tunakabiliwa na changamoto hizo lakini bado tumeweza kumiliki jengo letu la kisasa ambalo limeweza kusaidia kupunguza gharama tulizokuwa tunatumia kulipia kodi.” alisema Rukia.

HABARI ZA UCHUMI

kwa Waziri Mkuu. “Tunaona namna serikali inavyotumia mawakala na

vibaraka wake, kukigawa na kukidhoofi-cha Chama cha Wananchi (CUF), ikiwemo kumtumia Msajili wa Vyama vya Siasa kudhoofisha upinzani” amesema Mbowe akishangiliwa na wabunge wa upinzani Bungeni.

Mbowe (pichani) alimuuliza Waziri Mkuu kama ilikuwa ni sera ya serikali ya Rais Magufuli kutaka kufuta upinzani nchini kwani “Rais alishatangaza kusudio lake la kufuta vyama vya upinzani nchini ifikapo mwaka 2020?”.

Kabla ya kuuliza swali lake Mbowe alitoa mfano wa kuendelea kushikiliwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema ambaye licha ya kushtakiwa kwa kosa linalodhaminika lakini bado kwa miezi mitatu sasa ameendelea kukaa rumande. Alitolea mfano pia Mbunge wa Kilombero Bw. Lijualikali ambaye naye anatumikia kifungo cha miezi sita jela baada ya kuku-twa na hatia ya kufanya vurugu.

Hata hivyo kabla ya kujibu swali hilo Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Mwansasu aliingilia kati na kudai kuwa maswali ya Mbowe yamechanganyika yale yanayohu-siana na sheria na yale yanayohusiana na sera.

Hata hivyo Waziri Mkuu aliposimama kujibu maswali alianza kwa kukanusha kuwa Rais hajawahi kutangaza kufuta vyama vya upinzani nchini. “Kuna mihimili mitatu ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuin-

« MBOWE AMVAA WAZIRI MKUU , kutoka Uk.1 gilia mhimili mwingine” amesema Majaliwa. Aliongeza pia kuwa “siwezi kuzungumzia mambo yote ambayo yapo au yanaendelea kuwepo mahakamani”.

Maelezo hayo hata hivyo hayakumridhisha Mbowe ambaye alisimama na kuomba kuuliza swali la nyongeza. Katika swali lake la Nyonge-za Mbowe alitaka kujua endapo upinzani uki-leta ushahidi wa kauli ya Rais kutaka kufuta upinzani nchini ifikapo 2020 je, Waziri Mkuu atakuwa tayari kuwajibika kwa kujiuzulu?

Hata hivyo, swali lake hilo lilimfanya Naibu Spika Ackson kuingilia kati tena na kudai kuwa swali la Mbowe halikuwa swali la kisera kitu kilichosababisha kurushwa kwa maneno kutoka kwa baadhi ya wabunge waliodai kuwa swali hilo ni swali linalohusiana na sera ya utawala bora. Mbowe alijaribu kufafanua swali lake tena lakini Naibu Spika hakutoa nafasi kwa Waziri Mkuu kujibu kama angekuwa tayari kuwajibika endapo ushahidi wa kauli ya Rais kutaka kufuta upinzani nchini ungeweza kuletwa Bungeni.

Hata hivyo wabunge wa upinzani walien-delea kupiga kelele kitu ambacho kilimfanya Naibu Spika aombe msaada wa Mbowe kuwat-uliza ili kipindi cha maswali na majibu kiweze kuendelea.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Bw. Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu upungufu wa bidhaa mbalimbali hasa sukari na nafaka na kuwa licha upungufu ambao umejitokeza huko nyuma bado nchi iko katika hali nzuri ya kuweza kuk-abiliana na adha yoyote ya huko mbeleni.

Waziri Mkuu amesema kuwa kuhusiana na upungufu wa sukari uliojitokeza mwaka jana serikali imejipanga vizuri zaidi mwaka huu kuhakikisha kuwa upungufu huo hau-tajitokeza tena. Amesema kuwa tayari wame-shakaa mara kwa mara na wazalishaji wa sukari nchini na kuwa tayari viwanda vya hapa nchini vinaelekea kukidhi mahitaji ya sukari nchini.

6 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

Na. Ebbie Mkandara

Kwanza yabidi nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma na mwenye kurehemu. Atujaalie sote katika mjadala huu tuwe na ustaarabu kwa hoja, tuwe wasikivu na wenye kutakiana kheri badala ya kulaani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi wa yote, Mwenye nguvu, Mwenye busara, mwenye hekima na mwenye kujua yote yaliyopo ardhini na Mbinguni. Nasi tu-naweza tu kutafakari na kufanya yalokuwa chini ya uwezo alotujaalia yeye.

Leo hii mjadala wetu utahusu kilio cha wananchi kuhusiana na Ukombozi wa Kiu-chumi. Tuliuaga mwaka pasipo tathimini na marejesho ya mwaka mzima ulopita kulingana na matumaini ya wananchi juu ya uongozi wa awamu hii ya tano. Ni kosa kubwa kuendelea kuweka matumaini am-bayo hayawezi kutekelezeka yote ndani ya mwaka mmoja.

Ni muhimu zaidi kuukaribisha mwaka huu kwa kutazama mbele, nini matumaini yetu kule tunakokwenda kulingana na mipango ya maendeleo ya nchi yetu kwa vipimo hal-isi vya Ukombozi na dhana ya UHURU tu-lopigania ambayo bado haijabadilika zaidi ya Kujikomboa Kiuchumi.

Hatuwezi kufuta Umaskini kwa dhana. Was-wahili wanasema kwa mja huenda neno kwa muungwana vitendo; hivyo Ukombozi wa mwananchi kiuchumi sio dhana tena, ni hali halisi inayotakiwa kufanyiwa kazi. Nao wazungu husema - Why monitor a problem if you don’t have answers?

Hiki ndio kiini cha mada hii kutokana na kilio cha wananchi kutopata majibu sahihi ya ukombozi wao kiuchumi ndani ya ar-dhi yao wakiwa huru japo wanasiasa wote wamejikita katika kufuatilia matatizo na udhaifu wa wananchi na kuyaanika pasipo kuwapatia suluhisho linalohusiana mahitaji yao.

Wana taaluma walisema ili azma ya uhuru wetu ufanikiwe tunahitaji kwanza sisi wa-nanchi kujikomboa toka katika akili ya ki-tumwa. Akili ambayo kwamba ni tegemezi ya bwana mithili ya mbwa alofugwa. Hata akiachiwa huru basi mbwa huyo atash-indwa kujikimu pekee hatimaye kugeuka kuwa mbwa koko akisaka mabaki ya chaku-la kwenye taka.

Na haijalishi tena kama ni mbwa, jibwa ama kijibwa maana akili za mfugwa hazina tofauti na mtumwa. Mtumwa aliyechwa huru lakini akaishi maisha ya mbwa koko ni hitimisho la mazoea alokuzwa nayo kifikra. Mazoea yakawa sharia na sehemu ya mai-

sha yake.

Binafsi yangu nimekuwa nikishiriki mi-jadala mingi sana ya mitandaoni toka mwaka 2002 na nadhani swala la Uhuru wa Kiuchumi kwa miaka mingi limelijadiliwa sana kuliko mada nyinginezo na halijawahi kupatikana ufumbuzi wa kudumu. Hivyo nachelea kusema kwamba muda wote tumekuwa tukitazama upande usokuwa tatizo, bali tatizo ni sisi wenyewe wala sii la kimfumo wala uongozi bali sisi wote bado tuna akili za kitumwa.

Baada ya nchi yetu kupata Uhuru, mare-hemu Mwalimu Nyerere aliweka misingi ya Mtanzania kuweza kujikomboa kifikra, kujikomboa kiuchumi lakini kabla ya ku-fikia Ukombozi huo alikutana na upinzani mkubwa kwa baadhi ya hatua alozichukua japo kimantiki zilimlenga mwananchi kuwa huru na aweze kujitegemea. Lakini madhali tulizoea kulishwa utumwani, hayumkiniki dhana ya kujitegemea ilikuwa suluhisho la watwana.

Ni vigumu sana kuzungumzia Uhuru na kujitegemea ikiwa wananchi tumeshindwa kutoka katika lindi la utumwa kifikra. Hadi leo hii wananchi wengi kwa Ujumla wetu hata wale wasomi hutegemea serikali yetu itatufanyia nini badala ya sisi tunaifanyia nini serikali maana serikali ni sisi wenyewe tukiongozana. Akili zetu bado zimefung-wa fahamu, zinaashiria bado tumefugwa na mfugaji ni rais na serikali yake waliopo madarakani badala ya chama hicho kuwa viongozi wetu.

Akili zinatutuma kuamini tofauti iliyopo baina ya kutawaliwa na kuongozwa ni ran-gi ya mtawala tu lakini bado tunatawaliwa. Na Manyapala wetu ni vyama vya Upinzani ambao ndani ya utumwa huo wa akili, hutuaminisha kuwa wao tofauti na mab-wana japo tunapenda UHESHIMIWA, sifa na hadhi ilokuwa sawa na mabwana. Na wanapenda kuitwa Waheshimiwa hadi kwa mienendo, maneno na hata madaha yao ya Unyapala.

Kilio cha wananchi kina mengi na kina mshindo mkubwa haswa katika maswala yanayohusu maisha yao. Ukombozi wa mwafrika hauwezi kuwa na maana ikiwa bado tumevikwa juba pasi kuvuta fikra za Utumwa maana asili ya utumwa ni mshind-wa. Hivyo kama tumeshindwa kujinasua katika fikra hizi basi bado tupo kati ya wale waloshindwa.

Na hapana siku wala wakati, ugumu wa maisha ya wananchi umepewa kipaumbele zaidi ili wajitawale kiuchumi aidha iwe kwa hoja za watawala ama Upinzani isipokuwa

siasa za kusadikika pasipo kutanguliza ku-tambua mapungufu yetu, hitilafu, changa-moto na vikwazo vinavyopo katika hatua za awali katika kumkomboa mwananchi kifikra.

Tutaweza vipi kuwakomboa wananchi Kifikra ikiwa viongozi wenyewe wanatoka baina yetu? Je, yawezekana umaskini wa mwafrika unatokana na uvivu wetu we-nyewe kufikiri nje ya Utumwa na kwamba ubwana tulojipachika si njia wala suluhisho la kujitawala kiuchumi bali tumebadilisha tu sura na rangi za watawala kuongoza wa-nanchi walovaa suti na mavazi ya ubwana lakini akili zao bado zipo utumwani? Kwa nini hadi leo twajivunia uraia zaidi ya Utaifa wetu kama sio kukubali Uhuru tulopiga-nia ni wa bendera tu! Uhuru wa mipaka na kusimika bendera.

Toka tumepata Uhuru ni mafunzo gani ya kujitegemea yaloandaliwa kwa wananchi toka majumbani hadi mashuleni kwa mi-taala inayowajenga imani na uwezo wa kutambua kwamba uhuru wao unaam-batana na uwezo wa kujitawala kiuchumi ili kukabiliana na maisha? Ni maandalizi gani yalokuwepo ama yanaendelea kitaifa yalomwezesha mwananchi kujitegemea kiuchumi?

Kwa nini basi leo nimeamkia Ukumbini na hoja hii? Ni kwa sababu yanishangaza sana kusikia ngamia akicheka nundu ya ng’ombe. Yanishangaza sana mimi kusikia wanasiasa, viongozi, wananchi wakilia na kuhaha juu ya baa la njaa. Kila mmoja wao akionyesha ujasiri wake wa kukejeli mzigo aloubeba mwenza wakati yeye mwenyewe kaubeba mzigo huo huo tena mara mbili.

Baa la njaa sii swala la kuchukulia mzaha hata kidogo. Ni hatari inayogopwa dunia nzima na huhitaji maandalizi mapema na sii kuzodoana. Nasema hii leo kwamba si-jawahi kuona wala kusikia mtu hata mmoja akizungumzia njia sahihi za kupambana na Baa la njaa. HAKUNA hata mmoja isipokuwa malumbano wakati wananchi wanateseka.

Na inashangaza sana kwa miaka 50 ilopita tukiacha miaka ya 70, hakuna mafunzo wala maandalizi yoyote kwa wananchi ku-jikomboa kwa chakula. Hakuna mfumo ulowahi kuwekwa kama maandalizi sahihi ya wananchi kwa ujumla kutotegemea mis-aada ya chakula. Yaani hadi leo Taifa letu halijitoshelezi kwa chakula hadi tumefikia kuanza kuilamu mvua na serikali? Kinacho-fuata nini basi kama sii kumlaumu Mungu?

Itaendelea wiki ijayo

« MHARIRI: Kwa Hili CCM Ibebe Lawama Kubwa Zaidikati ya hayo mengi hili ni kubwa zaidi - kutengeneza taifa la watu tegemezi.

Chama cha Mapinduzi na serikali zake zote tangu uhuru kina mambo mengi sana kimefanya ambayo tunaweza kusifia na kukosoa lakini hili la kulifanya taifa letu liwe na fikra za za utegemezi uliovuka mipaka.

Ni vizuri kukumbushana kuwa tangu mwanzo kabisa wa taifa letu zaidi ya miaka hamsini na mitano iliyopita hakuna kanuni iliyokuwa inatuhamasisha kama taifa kama kuwa taifa la watu “wanaojitegemea”. Kujitegemea huku siyo kutokuwa na ushirikiano na watu wengine au kutokupata msaada wa aina fulani bali ni kuwa katika hali ya kuweza

kufanikisha kile tunachoweza kufanikisha sisi wenyewe kwa kutumia uwezo wetu, akili zetu, raslimali zetu. Ya kwamba pale tunapoamua kuomba msaada kwa mtu, taasisi au kundi fulani la watu maana yake ni kuwa sisi wenyewe uwezo wetu wa ndani umeshindwa kabisa.

Ni kweli baada ya uhuru na hata muungano bado Tanzania ilikuwa ina mahitaji mengi ya vitu ambavyo hatukuweza kuvipata hapa ndani na hivyo tulihitaji msaada kutoka nje yetu sisi wenyewe. Hili lilikuwa kweli kwenye sekta mbalimbali, afya, elimu, sayansi n.k Hata hivyo miaka hamsini na mitano baadaye bado tumeendelea kuwa taifa la watu tegemezi na hatari kubwa zaidi

ni kuwa siyo tu tumekuwa ni tegemezi wa vitu; tumeanza na tunaendelea kutukuza utegemezi wa fikra. Kwamba, kati yetu sisi sote zaidi ya watu milioni hamsini - wasomi na wasio wasomi, matajiri kwa masikini, walio nacho na wanaotaka kuwa nacho hatujaweza kutafuta masuluhisho ya matatizo yetu ya msingi. Kuanzia elimu, afya n.k. Leo hii tumekuwa kama watu walioshikwa na madawa ya kulevya kwamba tukiambiwa wafadhili wanaacha kutusaidia tunaweza kujihisi kama tutakufa tunajiona.

Hakuna kubwa kama utegemezi katika masuala ya njaa. Kwenye taifa la watu ambao kila mwaka wanajaliwa mvua za

EBBIE MKANDARA - NGAMIA KUCHEKA NUNDU YA NG’OMBE NI VITUKO

» Inaendelea, UK. 7

Februari 10, 2017 ZAMAMPYA 7

utaimarika na kuwachukua Wamarekani karibu milioni 96 wasio na kazi ni wazi ata-jipatia nafasi nyingine ya kuendelea “Kui-fanya Marekani Bora Tena”.

Hata hivyo hili la Mexico nalo limeanza na matatizo. Mkutano wa kwanza kati ya Rais Trump na Rais wa Mexico Pena Nieto uli-lazimishwa kuahirishwa baada ya Trump kung’ang’ania kuwa ni lazima Mexico iili-pe Marekani katika gharama za kujenga ukuta wa mpaka wakati Mexico ikigoma kulipa gharama hiyo.

Hivi sasa ni muda tu utakaoamua kama Donald Trump ataifanya Marekani iwe rafiki kwa jumuiya ya kimataifa au itajiten-geneza maadui wapya huku ikiendelea kung’ang’aniwa na maadui wa zamani.

kutosha hadi mafuriko, taifa ambalo limezungukwa na mito na maziwa makubwa, taifa ambalo lina maji ardhini na kwenye mabonde ya kila namna ni kwa vipi taifa hilo linaweza kuwa na watu wasomi na wanaonekana wenye akili timamu ambao wanasimama na kulia “njaa, njaa” au “upungufu wa chakula”?

Ni kwa vipi taifa letu hadi leo hii pamoja na kuwa na vyuo vya kila namna na kikiwemo chuo kikuu cha Kilimo cha aina yake bado lina watu ambao hawajaweza kujihakikishia usalama wa chakula mvua zikichelewa kidogo tu?

Ni utegemezi gani huu tuliojijengea na kulijengea taifa? Ni wazi kuwa serikali ina beba lawama kubwa zaidi kwa kutengeneza taifa la watu ambao hawajiamini na ambao hadi fikra zao zinategemea kusaidiwa?

Hivi ni kweli kabisa kuwa kila mmoja wetu anaiangalia serikali kama baba yake na mama yake na kuwa hata chakula chake na cha familia yake kinaiangalia serikali? NI kweli hatuna watu wabunifu na ambao wanaweza kuangalia tatizo na kusema kuwa hili tatizo linaweza kutatulika? Watu hao wakaunganisha vichwa vyao pamoja na kukaa chini na kusema nini kifanyike kwa haraka?

Hivi ni lini tutakuwa na kongamano kubwa la usalama wa chakula ambalo halitatumia muda kutueleza tatizo bali litakutanisha vichwa vya wasomi wa kada mbalimbali kuja na suluhisho la kudumu ambalo linaweza kuwa zawadi yetu kwa Tanzania ijayo ya watoto na watoto wetu kuwa taifa lao lina uwezo wa kuwalisha watoto wake kwani limejelewa kila kitu kinachohitajika katika kuzalisha mazao ya kila namna?

Ni vipi basi tuna watu ambao wana akili timamu ambao wakiwa na mazao ya ziada kidogo tu wanaenda kuyauza wakitegemea kuwa “mvua” mwakani zitakuwa kama mwaka uliopita na hivyo hawaweki hata akiba ya chakula kwa ajili ya familia zao?

Ni vipi watu wazima na wanaume na nyumba zao wako tayari kwenda kuuza mazao yao yakiwa shambani huku wakitegemea kuwa hela kidogo watakayopata wataenda kununua mazao mengine bila kujali uwezekano wa hali mbaya ya chakula?

Huu ni utegemezi mbaya sana na kwa kweli Serikali inapokataa kutoa misaada ya chakula ni rahisi kuona kwanini watu wengine wanalia kwa sababu hawajawahi kufikiria kuwa hawatosaidiwa chakula. Kuna wakati wa kutoa misaada hii lakini wakati mwingine ni kuwalazimisha watu kuanza kutumia akili zao kutatua matatizo yanayoweza kuzuiwa.

Tatizo ni kuwa utegemezi huu siyo wa mtu mmoja mmoja; ni utegemezi ambao umeanzia kwenye serikali yenyewe. Serikali yenyewe ni tegemezi hata kwa vitu visivyopasa. Tuilaumu CCM!

Ni lazima tuilaumu CCM na serikali yake kwa sababu kwa miaka nenda rudi imewafanya watu wetu waendelee kuamini kabisa kuwa ili tuendelee tunahitaji kweli misaada. NI ukweli usiopingika kuwa kuondoka na lile wazo la Azimio la Arusha la Kujitegemea CCM imealiacha taifa liwe katika hali ya utegemezi mkubwa sana.

Ni matumaini yetu kuwa mojawapo ya mabadiliko makubwa ambayo Rais Magufuli anaweza kuyafanya mwaka huu na ambayo yatatuma ujumbe kuwa yeye kweli ni muumini wa kujitegemea na mtu anayeamini kuwa viongozi wanapaswa kuonesha mfano basi itakuwa ni kuhakikisha kuwa bajeti yetu ya mwaka huu inapoenda kuandaliwa sasa hivi itaweka mkazo mkubwa katika kujitegemea.

Bajeti yetu ni lazima itegemee kwa asilimia 100 mapato yetu ya ndani. Kama wafanyakazi wanatarajiwa kutegemea maisha yao kuendesha maisha yao vivyo hivyo Serikali itegemee mapato yake. Ifanye na kupanga vitu kwa kutegemea ukweli huo. Nje ya hapo tutaendelea kuwa ombaomba wa kudumu.

HABARI KUU: UJIO WA TRUMP

« MHARIRI: Kwa Hili CCM Ibebe Lawama Kubwa Zaidi

Donald Trump na Mexico

Hata hivyo kwa Wamarekani wenyewe ni uhusiano wa Marekani na jirani yake wa Kusini – Mexico – ndio utagusa maisha yao kwa karibu zaidi labda kuliko uhusiano mwingine wowote wa kimataifa. Marekani inapokea wahamiaji wengi haramu kupitia mpaka wake wa kusini. Wahamiaji hawa wengi ni wale ambao siyo wataalamu au wenye ujuzi wa hali ya juu bali wale am-bao wanatafuza kazi za vibarua Marekani.

Wanapoingia Marekani na kupata kazi hizi za vibarua wahamiaji hao wako tayari ku-lipwa kidogo kuliko Wamarekani na wako tayari kufanya kazi ambazo Wamarekani wengi hawapendi kuzifanya kama kwenye mashamba na vibarua wa ujenzi.

Donald Trump ameona hilo kuwa ni tishio kubwa la maslahi ya Marekani na hivyo ameahidi kuwa atajenga ukuta kulinda mpaka huo. Jambo hilo limeonekana ni la kibaguzi lakini Trump ameng’ang’ania na ameshaahidi kuanza ujenzi wa ukuta huo mwaka huu. Pamoja na hilo anapanga ku-waondoa nchini humu wahamiaji wote ambao wana rekodi za uhalifu (karibu watu milioni 3) na wakati huo huo kuweka utaratibu mkali zaidi wa kuwashughulikia watu wengine wote wanaoishi Marekani bila ya kujulikana (maarufu kama “kutoku-wa na makaratasi”).

Kati ya mambo yote ambayo yanaweza kuja kuamua baadaye kama Trump ata-pata awamu ya pili basi ni hili la Mexico. Akifanikiwa hata kwa asilimia 50 kupun-guza uhamiaji haramu ifikapo mwaka ujao wa uchaguzi 2020 basi Trump anaweza kurudi hata kama maeneo mengine ya kimataifa atapata shida. Na kama uchumi

8 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

Mchungaji Ashikwa Ugoni Marekani, Akimbia MtupuNi mhubiri mashuhuri huko Florida, Marekani

Na. Mwandishi Wetu

TALLAHASSEE, FLORIDA - Mchungaji maa-rufu huko Florida amejikuta akiabika na kuliabisha kanisa lake baada ya kufumwa akiwa katika tendo la ngono na mke wa

MAISHA NA JAMIImtu mwingine baada ya mwenye nyumba kurudi na kumkuta yuko na mkewe.

Mtumishi huyo Bw. O. Jermaine Simmons wa Kanisa la Kibaptisti la Jakob huko Florida alijikuta kwenye tukio hilo la aibu baada ya kutaka kujuana zaidi - kibiblia - na mke wa mtu siku ya tarehe 17 Januari mwaka huu.

Mume wa mtu alianza kupiga kelele na mchungaji aliamua kukimbia akiwa mtupu bila nguo huku akiacha nyuma vitu vyake ambayo mume wa mtu aliamua kuvitumia kama ushahidi na kuwaita polisi. Mchungaji aliamua kujibanza kwenye fensi ya majengo ya nyumba jirani na alipofumaniwa.

Mume wa mtu alilazimika kurudi nyum-bani mapema baada ya shuleni kumuita akamchukue mtoto wake wa kiume ali-yekuwa mgonjwa baada ya shule kushindwa kumpata mkewe kwa njia ya simu. Alipofika nyumbani ndio akamkuta mchungaji na mkewe wakiwa kwenye chumba cha binti yake wakivunja amri ya sita.

Baada ya kuwakuta katika hali hiyo ali-kimbia chumbani kwake kuchukua bastola yake na ndipo mchungaji alipoamua kukim-bia akiwa mtupu kuepusha maisha yake. Mke aliyefumwa akaamua kupiga simu polisi kuelezea kuwa mume wake anamtishia mtu bunduki na polisi walipokuja pande zote tatu ziliamua kutokuleta mashtaka yeyote.

Baada ya mashauriano na polisi Mume wa mtu aliamua kumrudishia vitu vyake mchungaji, na akaamua kukabidhi silaha yake kwa taasisi ya kupigania haki za weusi ya NAACP.

Mchungaji huyo alijikuta akisimama kanisani na kuomba msamaha waumini wake kwa kuwaangusha. “Ninaumia kwa sababu nimeawumiza” amesema Mchungaji huyo siku ya Jumapili ya tarehe 22 katika ibada mojawapo na kurekodiwa na mmoja wa waumini ambapo video hiyo ilipostiwa kwenye mtandao wa youtube.

“Siwezi kuzungumza na watu wa nje; mimi si mchungaji wa (mji) wa Tallahas-see, mimis iyo mchungaji wa Florida, mimi ni mchungaji wa Kanisa hili la Jakobo na nasikitika mnalazimika kunitetea. Hamuwezi kutetea dhambi” alisema mchungaji huyo akipigiwa makofi na waumini wake.

Mch. Simmons ni mume wa mtu vile vile na ana mtoto mmoja wa kiume na amekuwa maarufu kwa kuwasaidia watu mbalimbali wenye mahitaji. Tukio hilo limetokea wakati kanisa lake likiwa kwenye sherehe za miaka kumi na moja ya uongozi wake .

Mchungaji Simmons amesema kuwa hatojiuzulu wadhifa wake hapo kwani “nimemuomba Mungu msamaha naye ame-nisamahe na ninawaomba wenzangu hapa wanisamehe pia” amesema. Kanisa lake wali-simama na kumshangilia kwa dakika kadhaa kwa kile kilichotafrisiwa kama ni kumpa nafasi nyingine baada ya kutubu.

Tanzania Kudai Fidia ya Ukoloni toka Ujerumani na Uingereza Bunge laitaka Serikali kudai fidia kutoka Ujerumani

Mwandishi Wetu

BUNGENI, DODOMA - Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuandaa mashtaka dhidi ya Ujerumani ili kulailazi-misha Marekani kulipa fidia ya vitendo vya kikatili vilivyofanywa na Ujerumani katika

Madaktari Toka Korea Kusini Watoa Matibabu Bure Sengerema Wataalamu wa afya 40 toka Korea Kusini wapiga kambi Sengerema

Na. D. Madukwa

SENGEREMA, MWANZA Jopo la madak-tari na wauguzi 40 shirika la World mission frontier wakishirikiana na Asan Medical center kutoka kutoka Korea Kusini wame-fika Tanzania katika wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, jopo hilo limetoa mati-babu katika maeneo ya Isole na Katunguru wilayani Sengerema.

Zaidi ya watu 1400 kutoka maeneo mbalimbali ya Senger-

ema wamenufaika na matibabu hayo. Matibabu hayo yametolewa bure kwa

wagonjwa wote waliofika kupata huduma pia baadhi ya wagonjwa wameweza kufany-iwa upasuaji na Daktari wa upasuaji Kim. Diwani wa Kata ya Katunguru Bw. Mathew Lubongeja Ndalahwa amefurahishwa sana na kazi kubwa iliyofanywa na watu wa Korea kusini na amewaomba waendelee na moyo huo huo wa kujitolea kwa kutoa matibabu bure kwa watanzania,.

Pia amewashukuru wananchi kwa kuji-tokeza kwa wingi kuja kupata huduma hiyo ya kutatua matatizo mbalimbali ya afya zao amabyo mengine wamekuwa wakihangai-ka nayo kwa muda mrefu.

Madaktari na wauguzi wa Korea kusini kama vile: Dr Park Kyun, Dr Ra, Dr Kim, na manesi kama Kim Rahee, Kim Hyunji na wengine wengi wanawashukuru sana Watanzania wa wilaya ya Sengerema kwa ushirikiano waliouonesha katika muda wa matibabu kwenye maeneo ya Isole na Katunguru (pichani).

ardhi ya Tanganyika wakati ambao Ujerumani ilikuwa ni mtawala wa kikoloni.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi, mpango huo upo ili kufanya kile ambacho kimefanywa pia na nchi nyingine za Kiafrika kama Kenya na Namibia ambazo zote zimedai fidia Uje-rumani.

Kwa upande wa Ujerumani serikali inakusu-dia kudai fidia kutoka na vitendo mbalimbali vilivyofanywa na Ujerumani wakati huo katika kuzima harakati za kukataa ukoloni wakati wa vita vya Majimaji.

Ujerumani iliikalia ardhi ya Tanganyika kuanzia 1890 hadi 1919. Vita vya Majimaji vilitokea kati ya 1905-1907 ambapo makabila mbalimbali ya Tanganyika yaliunganisha na kuanzisha uasi dhidi ya utawala wa Mdachi. Ili kuzima uasi huo Ujerumani nguvu kubwa ikiwemo kuwanyonga na kuwapiga risasi viongozi mbalimbali wa vita hivyo na katika tukio ambalo limebakia kama dola kuteketeza mazao yaliyokuwa shambani na kusababisha baa la njaa kutokea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na kulazimisha ushindi.

Januari mwaka huu Ujerumani ilitangaza kuwa imelipa fidia kwa Serikali ya Namibia kufuatia mauaji makubwa ya zaidi ya Wana-mibia 65,000 na kufanya tukio hilo kuchuku-liwa na wanahistoria wengi kuwa ni mauaji ya kwanza ya halaiki katika karne ya ishirini.

Uingereza nayo imelipa fidia ya zaidi ya dola milioni 21 kwa Kenya mwaka 2013 kama sehemu ya kuwajibika kwake kwa vitendo vili-vyofanywa na serikali hiyo wakati wa utawala wa kikoloni.

Hata hivyo utaratibu gani utatumika kufiki-sha madai hayo haijawekwa wazi na hai-jaeleweka au kuelezwa kama huu ni uamuzi ambao una baraka za Barala la Mawaziri. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uje-rumani Deutsche Welle Dkt. Mwinyi amesema kuwa ataiandikia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ili kuona ni namna gani jambo hili litafiki-shwa kwa serikali ya Ujerumani.

Vita vya MajiMaji vilipokwisha kwa nguvu za kijeshi na matumizi ya njaa kama silaha ya vita wapiganaji 75,000 wa Kiafrika waliuawa na wananchi wengine kati ya 200,000-300,000 walikufa sababu ya njaa iliyotokana na vita. Gharama ya vita ilikuwa kubwa siyo kwa uhai tu lakini jamii kubwa iliondokewa na nguvu kazi kubwa kwa muda mfupi na kusababisha kuvunjika kujiamini miongoni mwa wananchi kilicho kilichosababisha kwa kiasi kikubwa kutafuta uhuru kwa njia ya amani wakati wa Mwalimu Nyerere nusu karne baadaye.

Pichani juu sehemu ya mashujaa wa vita vya Maji Maji baada ya vita wakinyongwa kwa amri ya Serikali ya Mjerumani ikiwa ni fundisho dhidi uasi.

Chini sehemu hiyo hiyo walionyongewa mashujaa wa Maji Maji inavyoonekana leo. Sehemu ya mti wa ku nyongewa bado upo umesimama pamoja na kamba zake.

Februari 10, 2017 ZAMAMPYA 9

Wabunge wamekuja juu wanadai wamedharauliwa na viongozi wa Mkoa na Wilaya. Ni kweli bunge linaheshima bado?

Katika Bunge letu hili la Muungano kuna watu ninawaheshimu kweli kweli. Siyo wengi, lakini wapo. Ninawaheshimu kwa sababu wao wenyewe wanajiheshimu na wanaheshimu wengine. Lakini kama taa-sisi mimi sina heshima na Bunge letu la Muungano. Heshima hiyo kwa wengine inaweza kuwa imepotea siku za karibuni lakini kwangu binafsi niliipoteza heshima hiyo miaka kadhaa nyuma. Bado sijaona sababu ya msingi ya kurudisha heshima hiyo.

Ndugu zangu, wabunge wamekarisika na wamedai kuwa wamedharauliwa na kuwa Mhimili huo umevunjiwa heshima na Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Aru-meru. Wabunge walilipuka juzi wakidai kuwa wamedharauliwa na kuona kuwa vi jana “hawa” wamelivunjia sana heshima Bunge na wanastahili kuitwa mbele ya Kamati ya Uongozi ya Bunge wajieleze.

Huu ni ubabe wa aina fulani ambao wabunge wanafikiria unawe-za kupita bila kuhojiwa au kupingwa na watu makini. Nieleze tu kwanza kwamba unapodai kuwa umevunjiwa heshima unadhania kwanza kabisa kuwa unayo heshima hiyo na pili labda unastahili heshima hiyo. Kama huna heshima au hustahili heshima hiyo kudai kuwa mtu anakuvunjia heshima ni kujip-inga. Kama mtu ni mchafu hawezi kudai kuwa ameambiwa mchafu ametukanwa!

Binafsi ningechukulia kwa umakini madai ya Bunge kudharauliwa kama kwanza wao wenyewe wangejiheshimu humo Bungeni. Cha kushangaza na kukera kwa wakati mmoja ni kuwa masaa machache kabla ya kudai kuwa wamedharauliwa humo humo Bungeni mmoja wa wabunge (Mlinga) alidai kuwa ndani ya Bunge hilo hilo kuna watu wanatumia madawa ya kulevya; na akadai kuwa wapo watumiaji madawa ya kulevya.

Lakini hilo ni moja tu. Heshima ya kweli iko katika kuendesha mijadala. Kwa wale ambao tumekuwa tukifuatilia mijadala ya Bunge tunajua vizuri jinsi gani wabunge wenyewe ndani ya Bunge hawaheshi-miani. Ni mara ngapi tumesikia wabunge wakirushiana maneno ya kejeli na hata matusi ya kiana kwa vile tu hawafurahii anachosema mwingine? Ni mara ngapi tumeona wabunge wakijibishana na kiti cha Spika wao wenyewe na wengine kufikia hata kuchukuliwa hatua na bunge hilo hilo? Sasa kama wao wenyewe hawawezi kuheshimiana na hawaheshimu mamlaka zao ni vipi wao wataheshimiwa?

Na kama suala ni kuheshima mihimili ni mara ngapi tumewasikia wabunge wakimsema Rais ambaye ni mkuu wa Mhi-mili mwingine kwa dharau na kejeli? Au wao peke yao wanastahili kuzungumzwa kwa kuheshimiwa lakini mkuu wa mhi-

mili mingine yeye hastahili heshima hiyo? Hivi waliomuita Rais ni “Dikteta uchwara” siyo wabunge? Hivi siyo wabunge ambao wamekuwa wakitumia lugha za kila namna za dhihaka dhidi ya mkuu wa Mhimili mwingine? Au kwa vile yeye hana Kamati ya Uongozi ambapo anaweza kuwaita wajibu mashtaka – zaidi ya kutumia vyombo vya dola kufanya hivyo (iwe kwa uzuri au kwa ubaya)?

Lakini ni heshima gani hii ambayo wabunge wanaidai? Hivi siyo hawa hawa juzi wabunge wenzao wamekamatwa na kusekwa lupango lakini hawakuungana pamoja kuilazimisha serikali kutenda haki? Siyo kwamba Mbunge mwenzao Godbless Lema anasota jela na wao wanaendelea kula na kunywa? Ni heshima gani wanayo-amini wanayo kama hawawezi kusimama pamoja kama walivyosimama dhidi ya Makonda kudai Serikali imuachilie Lema?

Lakini pamoja na hayo, si wao ndio watunga sheria? Hivi Rais na kina Makonda wapo kwa mujibu gani? Si kwa sababu Katiba na Sheria zimewapa madaraka mbalimbali na kuwaweka hapo walipo? Sasa kama Bunge na Wabunge w a n a o n a k w e l i watendaji mbalim-bali hawana heshima na hawastahili hata kuwepo si wao ndio watunga sheria? Kwanini wasitunge

sheria kusimamia nyadhifa na madaraka ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya?

Na tena hili ni la muhimu kwa sababu ni wabunge hawa waliodai kuwa viongozi hawa wanatumia madaraka yao vibaya; sasa kama ni kweli, watu pekee wenye uwezo wa kusahihisha hili ni wabunge kwani ni wao peke yao ambao wanaweza kuondoa au hata kupunguza madaraka ya wakuu wa mikoa! Sheria ndio imewafanya kina Makonda kuwa wakuu wa ulinzi na Usalama katika mikoa na wilaya zao. Sasa kama hatutaki hilo ni wao wabunge wenye uwezo wa kulibadilisha! Sasa Makonda aki-tekeleza majukumu yake – hata kwa ubaya kiasi gani - ni wao wabunge wanaoweza kusahihisha. J

Ninachotaka kusema ni kuwa heshima haiombwi; na hakuna mtu ambaye haji-heshimu ambaye anaweza kutaka aheshi-miwa na wengine. Kama mzazi ni mlevi na anafanya vituko kila mahali na mtaani pote wanajua ni mzee asiye na heshima; watoto wanachoweza kufanya ni kumsiriti tu kwa ajili ya aibu yake lakini kwa sababu wanam-heshimu. Sisi kama raia tunaweza kusitiri wakati mwingine aibu yetu ya Bunge lakini hatuwezi kufisha kutoheshimika kwao.

Ili waheshimiwa ni lazima wao wenyewe wajiheshimu; lakini pia wao wenyewe wawe wa kwanza kuonesha kuwa waneheshimu wengine. Kuwa na Kinga ya Bunge si kibali cha kuvunjiana wao wenyewe heshima au kumvunjia mtu mwigine heshima.

Swali langu la nyongeza ni kuwa, kama wao wanataka Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru wawajibishwe kwa kulidharau Bunge, je wao wenyewe wako tayari kuwajibika kwa kujivunjia heshima?

KAMA BUNGE HALIJIHESHIMU LISILALAMIKE LISIPOHESHIMIWA!

“Ili waheshimiwa ni lazima wao wenyewe wajiheshimu; lakini

pia wao wenyewe wawe wa kwanza

kuonesha kuwa wane-heshimu wengine”

SWALI LA NYONGEZA: M.M MWANAKIJIJIMakonda Amefunua Tunalolijua

10 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

PAUL MPAZI: Mteja anapokuwa si mfalme tena!Huduma kwa mteja inapokuwa in huruma kwa mteja!

Na. Paul Mpazi

HUDUMA KWA wateja ni mfululizo wa shu-ghuli iliyoundwa ili kuongeza kiwango cha mteja kuridhika - yaani, hisia kuwa bidhaa au huduma imekutana na matarajio ya mteja. Msisitizo hapa ni “mteja kuridhika” Katika ofisi mbalimbali hasa zenye mlengo wa kibiashara mara nyingi kuna

kitengo hiki kinachotakiwa kuhakikisha wateja wanapa-ta msaada wa maelekezo au ushauri. Maelekezo haya yamekuwa yakitole-wa katika namna ambayo mhudumu na mhudu-miwa wanazungumza kwa

lugha ya “kirafiki” zaidi ili kuweza kuleta ufanisi wa kile anachokitarajia mteja. Katika utafiti wa muda mfupi niliou-fanya nimegundua kuwa kumeanza kuwa na tofauti kubwa kati ya huduma kwa wateja katika maeneo mbambali. Huduma inayotolewa kwa mteja ambaye shughuli iliyompeleka pale ni kuweka fedha au kuli-pia huduma fulani imekuwa ni nzuri naya ukarimu wa hali ya juu sana kuliko yule anayefika ofisni hapo kufuatilia malipo yake. Kwa mfano, mteja anayeingia katika ofisi ya bima kulipia bima mali yake anapokele-wa vizuri sana na kwa ukarimu wa hali

ya juu kuliko mteja anayeingia katika ofisi hiyo hiyo kuomba kulipwa baada ya mali yake kuharibika katika mazingira yasiyozuilika (Mfano gari linapopata ajali). Hali hii, kama nilivyotoa mfano wa shirika la bima hapo juu; ipo kwa kiasi kikubwa sana katika mashirika ya mifuko ya kijamii kama NSSF, PSPF, LAPF n.k. Je, wateja kwao ni wale wanaokuja kuweka tu na sio wanaokuja kuchukua?. Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka huyo mteja ndicho kinachowafanya wao wawe hapo?. Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka mteja huyo ndicho anachokuja kuchukua? Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka huyo mteja ndicho kinachowafanya wao wawe hapo?. Kwa nini wanasahau kuwa alichokiweka mteja huyo ndicho ana-chokuja kuchukua? Kwanini wasimpe heshima na staha mteja ambaye anakuja kuchukua fedha ZAKE kama vile wanavyo-mchangamkia na kumfanya ajisikie kweli ni ‘mfalme’ wakati anapokuja na kuwekeza?

Kwanini wasiseme basi mteja ni “mfalme wakati wa kuweka fedha ili wakati wa kuchukua yeye ni kabwela?”

Najiuliza tu.

Alien army worms threatens African CropsNative to Latin America these army worms are now showing in AfricaSpecial Report (E360 Digest)

Scientists and government officials are growing increasingly concerned about the rapid spread of fall armyworm — an agricul-tural pest known to cause major damage to

staple crops such as maize — across Africa in recent months.

Native to North and South America, army-worm, a kind of caterpillar that burrows deep into corncobs and more than 100 other kinds of plants, was detected on the African conti-nent last year. It has already spread to seven nations, including Zambia, Malawi, Ghana, and South Africa, according to Reuters. Armyworms are difficult to control and can “cause extensive crop losses,” the UN’s Food and Agriculture Organization (FAO) warned

earlier this month. The outbreak could be disastrous for a region emerging from two years of El Nino-induced drought, it said.

Scientists with the Center for Agriculture and Biosciences International, a UK-based non-profit research organization, said Monday that the outbreak could “become a major threat to agricultural trade world-wide,” spreading to the limits of suitable African habitat within a few years and into Asia and the Mediterranean soon after.

It is now fully known how these army-worms reached Africa and how they are spreading. So far the army worms have not been reported in Tanzania but with recent rain shortages it is only a matter of time before the army worms (viwavi jeshi) would find their way in Tanzania and cause damage especially if the country will be unprepared for their eventual appearance.

(Special reporting with ZamaMpya)

NEWS HEADLINESNew engineered material for cooling structures with

zero energy consumptionCOLORADO UNIVERSITY NEWS

A team of University of Colorado Boulder engineers has developed a scalable manu-factured metamaterial — an engineered material with extraordinary properties not found in nature — to act as a kind of air conditioning system for structures. It has the ability to cool objects even under direct sunlight with zero energy and water con-sumption.

When applied to a surface, the metama-terial film cools the object underneath by efficiently reflecting incoming solar energy back into space while simultaneously allow-ing the surface to shed its own heat in the form of infrared thermal radiation.

The new material, which is described today in the journal Science, could provide an eco-friendly means of supplementary cooling for thermoelectric power plants, which currently require large amounts of water and electricity to maintain the operat-ing temperatures of their machinery.

The researchers’ glass-polymer hybrid material measures just 50 micrometers thick — slightly thicker than the aluminum foil found in a kitchen — and can be manu-factured economically on rolls, making it a potentially viable large-scale technology for

both residential and commercial applica-tions.

“We feel that this low-cost manufactur-ing process will be transformative for real-world applications of this radiative cooling technology,” said Xiaobo Yin, co-director of the research and an assistant professor who holds dual appointments in CU Boulder’s Department of Mechanical Engineering and the Materials Science and Engineering Pro-gram. Yin received DARPA’s Young Faculty Award in 2015.

The material takes advantage of passive radiative cooling, the process by which objects naturally shed heat in the form of infrared radiation, without consuming energy. Thermal radiation provides some natural nighttime cooling and is used for residential cooling in some areas, but day-time cooling has historically been more of a challenge. For a structure exposed to sunlight, even a small amount of directly-absorbed solar energy is enough to negate passive radiation.

The challenge for the CU Boulder research-ers, then, was to create a material that could provide a one-two punch: reflect any incom-ing solar rays back into the atmosphere while still providing a means of escape for infrared radiation. To solve this, the research-

ers embedded visibly-scatter-ing but infrared-radiant glass microspheres into a polymer film. They then added a thin silver coating underneath in order to achieve maximum spectral reflectance.

“Both the glass-polymer metamaterial formation and the silver coating are manu-factured at scale on roll-to-roll processes,” added Rong-gui Yang, also a professor of mechanical engineering and a Fellow of the American Soci-ety of Mechanical Engineers.

“Just 10 to 20 square meters of this material on the rooftop could nicely cool down a sin-gle-family house in summer,” said Gang Tan, an associate professor in the University of Wyoming’s Department of Civil and Architectural Engi-neering and a co-author of the paper.

In addition to being useful for cooling of buildings and power plants, the material could also help improve the efficiency and lifetime of solar panels. In direct sunlight, panels can overheat to temperatures that hamper their ability to convert solar rays into electricity.

“Just by applying this material to the surface of a solar panel, we can cool the panel and recover an additional one to two percent of solar efficiency,” said Yin. “That makes a big difference at scale.”

The engineers have applied for a patent for the technology and are working with CU Boulder’s Technology Transfer Office to explore potential commercial applications. They plan to create a 200-square-meter “cooling farm” prototype in Boulder in 2017.

The invention is the result of a $3 million grant awarded in 2015 to Yang, Yin and Tang by the Energy Department’s Advanced Research Projects Agency-Energy (ARPA-E).

“The key advantage of this technology is that it works 24/7 with no electricity or water usage,” said Yang “We’re excited about the opportunity to explore poten-tial uses in the power industry, aerospace, agriculture and more.”

Februari 10, 2017 ZAMAMPYA 11

Na. M. M. MwanakijijiSURA YA 1

Siku ya mkosi haiji na mmoja. Siku yangu ilianza kwa jina langu kuwa miongoni mwa majina yaliyotajwa kama waliotum-buliwa na Waziri mara baada ya serikali mpya kuingia madarakani. Nilipolala jana yake nilikuwa miongoni mwa watu wazito kwenye mojawapo ya taasisi nyeti zilizo chini ya Wizara ya Fedha; unaweza kuniita kuwa nilikuwa miongoni mwa ‘vigogo’ au ‘vingunge’. Usiku ule ulikuwa ni kama siku nyingine zilizopita; nilienda kulala nikiwa na mipango yangu mingine mingi tu ya kazi na ya kutumi nafasi mbalimbali zilizo-kuwa zinajitokeza pale kazini kuendeleza maisha yangu, ya ndugu zangu na rafiki zangu. Nililala nikiwa na furaha na maisha yangu yakiendelea kung’ara. Sikutarajia kuwa asubuhi yake na siku nzima iliyofuatia ingekuwa ni siku ya kukumbukwa katika maisha yangu.

Asubuhi ya siku ile ya Jumatatu ilian-za kwa dalili fulani hivi. Kwa vile sikuwa mtu wa kuamini sana katika mambo ya ushirikina baadhi ya dalili hizo nilizipuu-zia kwani niliona kama bahati mbaya tu. Kwanza, niliamka na kukuta jenereta la umeme linaunguruma kuashirikia kuwa umeme wa TANESCO ulikuwa umekatwa. Hilo halikunisumbua kwani pale nyumbani sikujali sana umeme huo. Ukiwepo nashu-kuru ukikosekana nasonga mbele.

Nilimuacha mchumba wangu Rita akiwa kitandani; alikuwa amechoka kwa kunicho-sha usiku uliopita. Nilijiona kama miongoni mwa watu wenye bahati sana duniani. Rita alikuwa ni mtoto wa Balozi wa Tanzania nchini China Dkt. Rose Kitangile Ericsson. Baba yake alikuwa ni Msweden aliyekuwa amefanya kazi Tanzania kama Mkurugenzi Mkazi wa SIDA miaka ya themanini na baadaye kuamua kuishi Tanzania baada ya mkataba wake kuisha. Walizaliwa wawili tu kwenye familia yake; yeye mkubwa na mdogo wake wa kike Marieta ambaye ali-kuwa anasoma huko Sweden.

Wakati naamka kitandani nilimuangalie Rita alivyolala na kujipongeza moyoni kuwa kwa hakika nilikuwa nimeopota kweli kweli. Mtoto alikuwa ameumbwa akaumbika na kama mbinguni kuna malaika basi nina uhakika mmoja wao alitupwa duniani kama zawadi kwangu. Alikuwa amelala akiwa mtupu kabisa kajifunika shuka nyepesi ambayo ilimfanya aonekane kama picha nzuri ya kuchora ambayo mtu angeweza kuitundika ukutani kwa fahari.

Kwa kawaida sikuwa napata chakula cha asubuhi nyumbani kwani muda nilio-kuwa ninatoka nyumbani kwenda kazini ni mapema sana; nikishapiga mswaki na kuoga na kuvaa kujiandaa kwenda kazini nilikuwa nachukua glasi ya maji ya moto na kunywa kushtua tumbo kidogo. Siku hiyo hata hivyo, nilipochukua glasi kabatini kabla sijaishika vizuri iliteleza mkononi na kuanguka sakafuni; tena sakafu ya maru-maru. Ilivunjika vipande vikubwa vitatu; na vipande vingine vidogo vidogo. Nilifyonza na kusikilizia kama nimemshtua Rita huko juu ghorofani. Sikusikia kitu. Nilichukua ufagio na kwa haraka nikafagia fagia na kuokota vipande vile vikubwa kuvitupa kwenye pipa dogo la takataka nikiwa nime-funga kwenye mfuko. Niliandika ujumbe mdogo na kuacha kwenye mlango wa jokofu kumtaarifu Rita kuwa ahakikisha anatumia mashine ya kuvuta vumbi kwani kulikuwa na vipande vidogo vidogo vya glasi pale chini.

Sikutaka kuchukua glasi nyingine; nili-chukua ufunguo wa gari langu na mkoba wangu wa kazini ambao ulikuwa na nyara-ka mbalimbali pamoja na Ipad yangu. Nili-

harakisha kutoka ndani ya nyumba yangu huku mawazoni nikianza kupanga siku yangu itakavyokuwa pindi nikifika kazini. Kabla sijavuka kabisa mlango nikakumbu-ka nimeacha simu yangu juu pembeni ya kitanda; nikaamua kuharakisha. Na kama vile kulikuwa na njama imepangwa katika haraka yangu nikashindwa kukanyaga vizuri ngazi ya kwanza; nikateleza na kama nis-ingekuwa makini ningevunja pua hivi hivi. Niliwahi kushika chini na kujizuia kuumia. Nikashika kingo za ngazi vizuri na kupanda kwa heshima zote; na hata wakati wa kurudi nilidhamiria kuwa makini zaidi.

Niliingia kwenye gari langu wakati mlinzi akifungua geti kuniruhusu nitoke nyumbani kwangu. Mawazo yangu yalihamia barabara-ni wakati nakanyaga mafuta kuelekea kazini. Nilikuwa naishi Masaki nyuma kidogo ya ofisi za Water Aid upande wa barabara ya Haile Selasie. Niliposhika barabara ya Haile Selasie sikufikiria kitu kingine chochote isipokuwa kusikiliza kipindi cha asubuhi kutoka EFM Radio.

>>>

Nilipofika ofisini sikuhisi jambo lolote baya au kuwa na hisia yoyote kuwa kuna jambo baya linakuja. Ukiondoa Mkurugenzi Mkuu mimi nilikuwa ni mtu wa pili kufika ofisini siku ile. Kwa kawaida nilikuwa mtu wa kwanza kufika ofisini kila asubuhi. Ukiondoa sababu ya kukwepa foleni ya magari nilipen-da kufika mapema ili kuweza kufanya kazi nyingi mapema ili mchana niweze kufanya mambo yangu mengine. Nilishakuwa na kawaida ya kutoka kazini majira ya saa nane hivi kuendelea na shughuli zangu; haku-kuwa na mtu wa kuniuliza kwani nilikuwa msaidizi mkubwa wa Mkurugenzi lakini pia nilikuwa na watu chini yangu ambao wali-kuwa wanatekeleza majukumu mbalimbali pale ofisini.

Nimesahau kusema; nilikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu kwenye moja nyeti chini ya Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango. Nilianza kupitia kazi mbalimbali ambazo nilikuwa nimeacha jana ikiwemo kupitia mafaili ya nidhamu ambayo yalihi-taji kufikishwa kwa Katibu Mkuu baada ya Mkurugenzi Mkuu kuyapitia. Kulikuwa na baadhi ya maombi ya kusafiri kwenda nje ambayo nayo yalihitaji kupitiwa ili hatimaye tuweze kuyaombea kibali Ikulu. Niliende-lea kuchambua na kuandika mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya Mkurugenzi Mkuu ili baadaye niweze kuyapitisha. Pamoja na hayo nilipitia taarifa mbalimbali za matumizi ya fedha kwa ajili ya hatimaye kuidhinisha madai mbalimbali ya watumishi ili wenye kustahili waweze kulipwa.

“Bosi, habari za asubuhi?” ilinishtua sauti ya Clara baada tu ya kufungua mlango. Japo nilikuwa natarajia wakati wowote angetokea lakini nilikuwa nimezama sana kwenye kazi zangu hata sikumsikia alipoingia ofisini. Clara alikuwa ni Katibu Muhtasi wangu na kabla ya mimi kuhamishiwa hapo kutoka Mwanza miaka mitatu nyuma alikuwa pia ni Katibu Muhtasi wa mtangulizi wangu.

“Nzuri tu Dada Clara” nilimjibu huku nami nikimjulia hali. Aliniambia tu kuwa amech-elewa kidogo sababu ya mvua barabarani na mimi nilimwambia kuwa na mimi ilipiga vizuri tu wakati naelekea kazini. Alitaka kujua kama nilihitaji chai au kahawa asubuhi ile. Nilimwambia kahawa itatosha maana nilikuwa nataka nichangamke kidogo. Alienda sehemu yenye birika la umeme la kutengenezea kahawa na kufanya vitu vyake. Dakika chache baadaye harufu ya kahawa ilimtangulia alipoileta ofisini. Nili-shukuru na nikampa maagizo kidogo ya vitu ambavyo nilitaka ashughulikie mapema kwani nilihitaji kumpatia Mkurugenzi ripoti

saa nne kamili asubuhi. Niliendelea na kazi huku nikinywa kahawa yangu kavu taratibu.

Muda haukupita kwani ilipofika saa mbili hivi ofisi ilikuwa imeshachangamka na karibu kila mtumishi alikuwa tayari ofisini; japo wachache walikuwa wameanza kazi. Wapo ambao walikuwa wanapiga soga kidogo huku wakiwa wamekaa kwenye sehemu zao na wengine wakiwa nao wanakunywa chai. Miezi michache nyuma ilikuwa ni kawaida kwa lundo la wafanyakazi baada ya kujio-nesha kuwa wamekuja kazini walikuwa wanakimbia chini ambapo kuna migahawa kununua ‘chochote’ kabla ya kurudi kazini. Kazi hasa ilikuwa inaanza karibu saa nne asubuhi. Wengine walitumia muda mwingi wakiwa kwenye mitandao ya kijamii. Lakini tangu serikali mpya iingie madarakani hali ilikuwa inaendelea kubadilika taratibu; watu walikuwa wanaonesha kuheshimu kazi zaidi na hata labda kujionesha wanaheshimu kazi.

Nilitoka kwenye ofisi yangu na kutembea kidogo kusalimia baadhi ya wafanyakazi na ikawa kama ishara kwao kwamba ni muda wa kazi. Kila aliyeniona alijifanya anajishu-ghulisha. Nilirudi ofisini kwangu. Kama saa tatu hivi na nusu Clara alichungulia kutoka kwenye ofisi yake ambayo inapakana moja kwa moja na yangu na kuniuliza kama nili-kuwa na mpango wa kutoka.

“Hapana sitoki saa hivi hadi mchana” nilim-uambia na kumuuliza “kwani vipi?”

“Hapana DG aliulizia tu”Hilo lilinishtua kidogo, haikuwa kawaida

kwa Mkurugenzi Mkuu kuniuliza kwani aki-taka kujua nipo au vipi aliweza kunipigia extension yangu ya simu moja kwa moja.

“Kwani vipi?” nilijaribu kudadisi. Clara alin-yanyua mabega yake juu kuashiria kuwa na yeye hajui.

Akili yangu ikaniambia labda ni kuhusiana na ripoti ambayo nilikuwa niwasilishe kwake au labda kuna kitu kingine maana wiki hizi tangu JPM aingie madarakani ofisi imekuwa hakukaliki. Niliangalia ripoti zangu zilikuwa safi, na mambo mengine ya mitkasi yangu nayo nilijua iko salama.

Hazikupita dakika chache simu yangu iliita na ilikuwa inaonesha ni kutoka ofisini kwa bosi.

“Vicent, acha yote unayofanya sasa hivi tunaitwa ofisini kwa Katibu Mkuu” alisema.

Moyo ulishtuka; kwa muda wote ambao nilikuwa pale ofisini nimekutana na Katibu Mkuu kama mara mbili hivi na mara zote hizo ilikuwa ni vikao vilivyopangwa. Lakini kuitwa moja kwa moja na Katibu Mkuu kulinifanya nishtuke.

“Sawa bosi, on my away” nilisema huku nikizungumza kwa sauti ambayo ilionesha kujiamini na kuwa sijali sana nani alikuwa ananiita. Nilifunga tai yangu vizuri na kuchu-kua jaketi langu nililokuwa nimeliweka nyuma ya kiti changu. Nilimuaga Clara kuwa nimeitwa kwa Katibu Mkuu pamoja na DG na Wakurugenzi wengine watatu. Moyo ulianza kunienda mbio.

SURA YA 2

Nilikuwa nimelowa jasho; mwili bado ulikuwa unatetemeka. Koo langu lilikuwa limekauka nikiwa na kiu ya pipa la maji. Nilikuwa nimetembea kwa mwendo wa haraka sana toka pale ofisini hadi maku-tano ya Barabara ya Maktaba na Bibi Titi Mohammed. Sikuwahi kutembea kwa haraka namna hiyo kama nilivyotembea hivyo tangu nilipokuwa shule ya Msingi Nyanguge miaka ile. Nilitamani kukaa chini kupumzika lakini sikuamini kama nilikuwa na muda wa kufanya hivyo. Toka ofisini barabara ya Madaraka hadi nilipokuwepo nilikuwa nimetembea kwa muda mfupi sana. Sikutaka kusimama pale; mfukoni nilikuwa na shilingi elfu ishirini tu. Nilikuwa na mamilioni benki na nikapata wazo la kwenda ATM yoyote iliyokuwa karibu

nichukue hela kidogo kabla mambo haya-jawa mabaya zaidi. Nilikata kushoto kue-lekea barabara ya Morogoro. Nilikuwa na akaunti yangu mojawapo kwenye benki ya Barclays na lilikuwa ni kusudio langu kufika pale mara moja. Kelele za magari yaliyokuwa yanaenda huku na kule sikuzi-jali; mara mbili hivi nilijikuta narushiwa matusi na makonda wa daladala kwa sababu walinikosakosa. Akili yangu ilikuwa inazunguka kuliko pia; bado nilikuwa katika hali ya kutoamini kwani yaliyotokea kama saa moja kabla niliona kama ni ndoto fulani ambayo ningeweza kuzin-duka. Kwa kadiri nilivyokuwa natembea ndivyo nilivyojua kuwa sikuwa ndotoni; nilikuwa kwenye tukio lililokuwa linaende-lea kutokea wakati ule.

Nilipoingia pale benki kitu cha kwanza niliomba chupa ya maji. Kabla sijaenda kwenye kaunta kujaribu kutoa hela kidogo. Nilitumia tai yangu iliyokuwa mfu-koni kujipangusa uso wakati nakunywa maji. Nilisogea mbele ya kaunta ya dada wa benki na kumkabidhi kitambulisho changu pamoja na fomu ya rangi ya njano ya kuchukulia fedha. Alichukua vyote hivyo na kuanza kuingia kwenye mtandao wao kuangalia akaunti yangu na kunipatia fedha zangu.

Nilikuwa nimezama kwenye mawazo hata sikumuuona dada yule alipoondoka pale dirishani. Niligundua kuwa hakuwepo wakati namuona akija pale dirisha la kuchukulia fedha na mtu ambaye nilim-tambua kuwa ni menewa wa tawi lile la benki.

“Vipi kuna tatizo” niliwawahi kabla hawajasema kitu

“Samahani Vicent, kuna tatizo kidogo katika kuifungua akaunti yako” alisema Meneja ambaye nilikuwa nafahamiana naye kwa muda mrefu tangu nifungue akaunti yangu pale.

“Iddi, kuna shida gani ni kwa akaunti zote au yangu tu?” niliuliza kwa udadisi.

“Sasa hivi ni akaunti yako tu” alisema Iddi Mchonde. Mchonde alikuwa ni mtu wa makamu ambaye alikuwa amenyoa nywele zake zote kipara. Alikuwa mfupi na mwenye kitambi kidogo ambacho kama kitaachwa kinaweza kuwa ni shida mbele ya safari. Alivyonipa jibu hilo niliuma midomo yangu kutafakari kwa sekunde chache. Kabla sijasema lolote aliniwahi.

“Naomba uje ofisini ili tuweze kufuatilia makao makuu kugundua kuna tatizo gani” alisema.

Nilipiga hesabu za haraka haraka nika-ona kuna mtego hapo. Nilishaona filamu nyingi ambazo zinatoa mafunzo ya vitu kama hivi; mara nyingi hakuna jema hapo. Mawazo yangu yalikatishwa ghafla baada ya kuona gari la polisi likiingia katika eneo la benki ile; meneja hakuweza kuona kwani ilikuwa upande ambao alikuwa ameupa mgongo.

Niliamua kumshukuru na kumwambia kuna mahali ninaenda nitarudi tena baa-daye labda tatizo litakuwa limetatuliwa. Sikutaka kupoteza muda nilibeba chupa yangu ya maji macho yangu yakiwa yanaelekea upande wa lile gari la polisi. Sikujua lilikuwa linafuata nini pale na sikutaka kujua lakini akili yangu yote ilikuwa inapiga ving’ora vya tahadhari. Nili-toka kwenye eneo la benki na mara moja kuchepukia upande mwingine wa jengo lile kuelekea barabarani ambako nilikuwa nimetokea. Nikashika tena barabara ya Bi Titi Mohammed kuelekea makutano yake na mtaa wa Uhuru.

Nilipofika kituo cha basi cha Baridi pale nikadandia kibajaji kuelekea mtaa wa Uhuru. Nilimuambia yule kijana anipeleke hadi tawi la NBC mtaa wa Samora.

ITAENDELEA WIKI IJAYO

RIWAYA: SIKU YA MKOSI

12 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

IJUE SIKUKUU YA VALENTINE’SWapo walioifanya kuwa ni siku ya michepuko na ngono; lakini historia inasema vingine

Na. Dotto Kwilasa Zimebaki siku chache kufikia siku ya

wapendanao iliyopewa umaarufu wa jina la “Valentine’s Day ”ni vizuri kutafakari kwa kina nakuyafahamu malengo na maana ya siku hii wakati unajiandaa kusherehekea siku hii ambayo kwa kawaida imeapishwa kufanyika kila mwaka February 14.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ,Neno Valentine lilitokana na jina ‘Valentino’ huyu alikuwa Mtakatifu wa Kiroma aliyeitwa Valentino,siku ya Valentino hufahamika kama Siku ya wapendanao na wengi wanaiita ‘Valentine Day’ ni maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka sehemu nyingi Duniani.

Watu wengi husherehekea siku hii kwa kuonyesha upendo, kuthaminiana pamoja na kujaliana kati ya watu wenye mahusiano mbalimbali ya karibu japo mara nyingi siku hii hutumiwa na walio kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Hata hivyo baadhi ya watu huitumia siku hii kufanya ibada ikiwa ni ishara ya kum-uenzi Mtakatifu Valentino ambaye histo-ria inamtaja kuwa ndiye chanzo cha siku hii. Asili ya Siku hii ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwa ajili ya kuupenda Ukristo na Kihistoria ambapo Mtakatifu Valentino

alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia II.

Mfalme Claudia II alimkamata na kum-funga, Mtakatifu Valentino na kumtesa kwa ajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa Febru-ary 14 Kwa ajili ya msimamo,imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo . Historia inaeleza kuwa Papa Gelasius aliitangaza February 14 kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mnamo mwaka 496 AD.

Historia inatupasha kuwa kipindi hicho, vijana wengi hawakupenda vita kwa kuog-opa kuziacha familia zao na hivyo kupin-gana na kiongozi wao Claudius ambaye alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana

wangejitolea na kujiunga na jeshi lake. Claudius akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana ambapo Kuanzia hapo akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwasababu ya familia zao.

Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha ndoa vijana hao kwa siri na kusisimua hasira za Claudius II ambapo aliposikia habari hizo aliamuru Valentine akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.

Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitem-belewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae ikiwa ni pamoja na kumpa moyo wa ushujaa na uvumilivu.

Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine kuongea nae mambo mbalimbali . Inasemekana kwamba Val-entine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa na kwamba muda mchache

UTAMADUNI SANAA BURUDANIkabla hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika

meseji yake ya kuaga akiweka sahihi iki-someka hivi “From Your Valentine” ( kutoka kwa Valentine wako ) akanyongwa tarehe 14 Februari mwaka 269 AD.

Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma walianza kumuiga Valen-tine na kuwaandikia na kuwatumia wan-awake waliowapenda salamu za mapenzi.

Tangu siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa na dini, urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi. Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila miaka inavyoenda huku huku makampuni na wafanyabiashara mbali mbali wakiigeuza siku hiyo kuwa ya biashara zaidi kwa kufanya kila kitu maalu-mu kwa siku ya wapendanao kionekane kiwe chekundu kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka nguo wavaazo wapendanao kuonyesha ishara ya upendo.

Rangi nyekundu hutafsiriwa na wengi kama ishara ya upendo japo kuwa kwa wakati mwingine rangi hiyo huashiria hatari. Kuna watu wengi pia ambao hawash-erehekei siku hii kwa kuhoji umuhimu wa kuonyesha kumjali umpendaye katika siku moja tu ya mwaka badala ya siku zote 365.

Mbali na hayo siku hii katika misingi ya dini hususani katika kanisa katoliki ina-lenga kuwafundisha watu kuwa na moyo wa mapendo na kutokukata tama. Padre mmoja wa kanisa katoliki, Deus Mulokozi anaizungumzia siku hii kama ni maalumu kwa wakristo kujifunza kuwa na moyo wa kutokata tamaa

ikiwa ni pamoja na kuwaurumia walio-katishwa tamaa na mambo ya kidunia.

Pia Padre huyu anasisitiza na kuwa-kumbusha wakristo kuitumia siku hii kwa kujumuika na watu wenye kukosa mahitaji muhimu au faraja kama watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu,Wagonjwa hata wazee wetu maana si lazima utoe pesa,lakini ushiriki wako kwa chakula au mavazi unaweza kuwapatia furaha .

“Siku ya wapendanao ni sikukuu ambayo huadhimishwa ifikapo Februari 14 kila mwaka historia yake imeanzia karne ya tatu nchini Italia, kuna watu wanaigeuza siku hii kwa kufanya ngono/uzinzi, wakifikiri kwamba ndiyo maana ya siku hii ya Val-entine Day, kitu ambacho si kweli. Usahihi ni kwamba siku hii imelenga kuhamasisha watu kupendana, ndiyo kusema kwamba unaweza kuonyesha upendo kwa mtu yeyote, si lazima awe mwenza wako”.ame-sema Mulokozi.

Mwandishi wa makala haya ,alijaribu kukusanya maoni ya watu tofauti kuhusi-ana na siku hii ya wapendanao ambapo baadhi ya watu wanaoihusudu siku hii huku wakiwa tayari wamejipanga katika kuiadhimisha waliweza kuzungumzia siku hii. Josephine Manase,anaizungumzia ssiku hii kuwa ni maalumu kwake kwani hum-kumbusha kuwajali wengine na kwamba siku hii inamkumbushwa kuwa

makini na watu wanaopotosha moyo. Hata hivyo anasema kuwa maadhimisho ya siku hii yalipoanza, ilionekana kama ni ya kidini zaidi, lakini baadaye ilipochun-guzwa mantiki ya uadhimishaji wenyewe, ikaonekana kuwa na maana kwa watu wa madhehebu yote.

“Kwa jinsi ninavyofahamu mtu aliy-etangaza rasmi kuadhimisha siku hii ya wapendanao ni Papa Gelasius, ambapo alisema ikumbukwe kama ishara ya kumuenzi mtetezi wa ndoa Mtakatifu Valentino”amesema.

Mmoja wa watu wanaopinga siku hii ambaye hakupenda kufahamika alithubu-tu kusema kuwa siku hii ni maalumu kwa wazinzi kwa kuwa inapofika siku hii watu

wengi huacha shughuli zao na kuanza kutu-miana

zawadi na wapenzi wao. “Siku hii haina umuhimu wowote,kwanza ingepigwa maru-fuku hapa nchini

kwa kuwa katika kipindi cha kuazimi-sha siku hii ndoa nyingi huvunjika na hata mahudhurio na ongezeko la watu katika nyumba za kulala wageni huwa mara dufu hii inamaanisha kwamba uzinzi hutendeka sana katika siku hii” amesema.

Hata hivyo siku hii bado amepewa hes-hima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake. Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa habari wa kimataifa Mt. Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 269 CE ndo ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine). Papa naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 269 CE kuwa ni sikukuu ya mapendo papa huyo alikuwa ni Askofu mkuu wa kanisa la Katoliki ambaye ni mrithi wa Mt. Petro.

Yapo pia masimulizi men-gine mbalimbali yanayo-tofatiana kuhusiana na historia ya maisha ya Mt. Valentino. Kati ya yote yanaokubaliwa ni kuwa aliuawa na Kaisari Claudius II mwaka 269 mwezi Feb-ruari 14.

Ili kuendana na maa-gizo ya Mwenyezi Mungu Ya kutenda mema siku zote tunapaswa kuienzi siku hii kwa nia moja ya mapendo na sio uzinzi . Kupeana zawadi mbalimbali sio dhambi,lakini tunapas-wa kufahamu zawadi hizo tunazitoa kwa maana ipi. Hata hivyo kuna watu huthubutu kuibadili maana ya siku hii kwa

K u b a d i l i s h a n a maneno ya mapen-zi na matamanio k a t i k a k a d i wanazopele -keana, yakiwa k a t i k a m f u m o wa kimas-h a i r i , tenzi n a sen-ten-s i f u p i f u p i . W a k a t i mwingine sherehe hii huambatana na kuchanganyika wanaume na wan-awake, kuimba, na kucheza dansi mpaka kupelekea kulewa na kushawishika kufanya mambo yasiyo faa katika jamii. Hivyo basi,Ndugu

zangu wakristo tunapaswa tutambue kuwa tunatakiwa

kuwa makini kwa kuangalia na kuyafanya yanayofaa ikiwa ni pamoja na kufuata kauli zile zilizo njema.

Imefikia wakati lazima ufikirie kufanya jambo kubwa, maalumu ambalo si tu hali-tasahaulika bali litatengeneza kitu kikubwa katika historia ya maisha yako kwa kutenda yaliyomema.

Inawezekana umeumiza kichwa sana ukijaribu kufikiria kitu cha kufanya kwa ajili ya kuwapendeza rafiki na jamaa zako, lakini uwezo wako wa kufikiri umefika mwisho na

hujapata cha kufan-ya. Hebu jaribu

kumshirikisha M w e n y e z i

Mungu siku zote katika m a a m u z i y a k o i l i uweze kuwa

mmoja wa watu wanao-

enzi maadili ambayo yana-

onekana Kuendelea kuharibika na kuporo-

moka nchini. Mwenyezi Mungu akuon-

goze katika kila jambo u n a l o -lif ik ir ia

k u l i -f a n -y a

k a t i k a s i k u y a

wapendanao nina imani utai-fanikisha kwa kufuata maagizo na mapenzi ya mungu,nakutakia sikukuu njema ya wapendanao.

Februari 10, 2017 ZAMAMPYA 13

14 ZAMAMPYA Februari 10, 2017

YAIBWAGA MISRI 2-1 FAINALI ZA AFCON 2017Misri yaambiwa kutangulia siyo kufika!Na. Mwandishi Wetu

BAADA YA kusubiria kwa miaka kumi na mitano, Cameron hatimaye wamenyakua kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 baada ya kuichabanga Misri magoli 2 kwa 1 katika kinyang’anyiro cha fainali kili-chofanyika huko Libreville, Gabon. Mpira ulianza kwa Misri kuonekana kuumiliki vizuri zaidi kuliko Cameron. Dakika ya 22 Mohammed Elneny msham-buliaji wa Arsenal aliipatia timu yake goli la kuongoza. Hata hivyo dakika ya 59 Cameron walisawazisha bao hilo kwa goli lililofungwa na Nikolas Nk’oulou na mchezo kuendelea kwa muda huku kila timu iki-cheza kwa kujihami zaidi.Kufika dakika ya 89 Vincent Aboubakar ali-pachika bao safi baada ya kumtoka mlinzi wa Misri na kuuchomeka mpira kimiani na kuipatia timu yake bao la ushindi. Abou-

bakar aliingia kuchukua nafasi ya mche-zaji mwingine na hivyo kuleta damu mpya katika mechi hiyo. Timu ya Cameron haikupewa nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano haya hasa baada ya baadhi ya wachezaji wake wa kimataifa kukataa kujiunga nayo na kumlazimisha kocha Hugo Broos kuita wachezaji wengi vijana ambao wengi hawa-

DAR-ES-SALAAM, MKUU wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Paul Makonda ameanzisha zogo jingine ambalo limezua mjadala mkubwa kitaifa pale alipoendelea kuwataja watu mbalimbali ambao amedai kuwa kwa namna moja au nyingine wanahusika au kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.

Kutajwa kwa Manji na Makonda kume-lirudisha tena jina la mmoja wa wafanya-biashara wakubwa nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga mbele ya wananchi. Hii si mara ya kwanza kwa Manji kutajwa na baadhi ya watu mashuhuri na mara zote amekuwa akijitetea vikali.

Safari hii vile vile Manji aliitisha kikao na waandishi wa habari akilaani vikali kutajwa na Makonda na kuwa yeye mwenyewe ata-jipeleka mwenyewe polisi bila kusubiri siku ambayo aliambiwa aende yaani Ijumaa. Manji alienda jana Alhamisi ambapo alitu-

mia muda wa karibu masaa sita akizung-umza au kuhojiwa na polisi.

Manji alilaani vikali kitendo cha Makonda kumuita aende polisi kwani amemvunjia heshima yake na jina lake. Akizungumza kwa hasira Manji alidai kuwa kuhusishwa kwake na masuala ya madawa ya kulevya kunaweza kumletea matatizo hasa ana-posafiri na timu yake ya Yanga.

“Huwezi kuniita mimi kama mbwa” alisema Manji.

Pamoja na Manji watu wengine mashuhuria mbao walitajwa katika awamu ya pili ya orodha ya Makonda ni pamoja na mhubiri na mchungaji maarufu nchini Askofu Joseph Gwajima ambaye naye ali-takiwa kujipeleka polisi.

Hadi hivi sasa ni wasanii kadhaa ambao Makonda aliwataja wiki iliyopita ambao tayari walienda kukutana naye polisi na baadhi yao kufikishwa mahakamani ambapo nane kati yao wamewekwa chini ya uangalizi maalum.

Haijulikani hata hivyo ni lini Manji atafun-gua kesi dhidi ya Makonda kwa kumchafua jina lake.

Makonda tayari ameshajiingiza kwenye kile kinachoonekana ni matatizo baada ya kuitwa na Bunge la Jamhuri ya Muun-gano kutokana na madai ya kulidhalilisha na hivyo Bunge kwa kauli moja bila kujali vyama likaamua kutoa wito wa kibunge (summons) ili Makonda aende kujieleza mbele ya Kamati ya Uongozi wa Bunge.

MANJI ATAJWA NA MAKONDA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amtaja Yusuf Manji katika harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya Mkoani Dar-es-Salaam

Na. Mwandishi Wetu

ZAMAMPYA michezoCAMERON BINGWA

kutegemea kama wangeweza hata kufika nusu fainali. Baadhi ya wachezaji wa kimataifa wa Cameron waliokataa mwaliko wa kocha huyo ni pamoja na Joel Maltip (Liverpool) na Allan Nyom (West Bromwich). Ushindi wa Cameron umeifanya timu ya nchi hiyo kushinda kombe la Mataifa ya Afrika kwa

mara ya tano na kuinyima Misri mara ya nane kushinda kombe hilo. Mengi yatasemwa kuhusu timu ya Cameron lakini kubwa ni kuwa wakati mwingine si majina makubwa yanayoleta ushindi ni kuji-amini na kuthubutu kuchezea kwa heshima ya taifa. Mashindano haya yanaweza kuwa yameona mwisho wa golikipa mashuhuri na aliye-dumu kwa muda mrefu Essam El-Haddary.

Vincent Aboubakar akishangilia bao la ushindi la Cameron dakika ya 89 ya mchezo.