taarifa ya utendaji kazi 2013/2014 - tanzania · 2015. 11. 3. · dira kuwa mamlaka inayoongoza...

36
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

Upload: others

Post on 15-Feb-2021

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

  • Sera ya Utoaji Huduma Bora

    TFDA imejidhatiti katika utoaji huduma bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake. Mamlaka inajitahidi kuwaridhisha wateja wake wote huku ikihakikisha ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba unadumishwa.

    Tumedhamiria kufuata na kutekeleza kanuni za kimataifa za utoaji bora wa huduma kama zilivyoainishwa katika “ISO 9001:2008” na kuendelea kuboresha na kusimamia mfumo bora wa utoaji huduma (Quality Management System). Tutahakikisha na kusimamia upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika katika uboreshaji wa huduma zinazotolewa ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja.

  • i

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    Dhima Kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

    Dira Kuwa Mamlaka inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa wote.

    Falsafa Kutoa huduma bora za udhibiti katika kulinda afya ya jamii na mazingira kwa kutumia wafanyakazi wenye ujuzi na ari ya kazi.

    Misingi ya kazi Kufanya kazi kwa ushirikiano, Uaminifu,

    Kuzingatia mahitaji ya wateja,

    Ubora,

    Uwajibikaji.

  • ii

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

  • iii

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    Mhe. Dkt. Seif S. Rashid (Mb.),Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,6 Samora Machel,S. L. P 11478 Dar es Salaam, Tanzania.

    Dkt. Donan W. Mmbando,Katibu Mkuu,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,6 Samora Machel,S. L. P 11478Dar es Salaam, Tanzania.

    Mhe. Waziri,

    Ninayo heshima kuwasilisha kwako Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kipindi cha mwaka 2013/2014. Taarifa hii imeainisha hatua ya utekelezaji wa shughuli za udhibiti wa ubora na usalama wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa kipindi hicho, ikiwa ni pamoja na changamoto zilizopo na mbinu zinazotumika kukabiliana nazo.

    Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (MAB) kwa TFDA, imepitia na kutoa ushauri kwa mambo ya msingi yatokanayo na taarifa hii ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi zaidi na Wizara na Menejimenti ya TFDA. Hii ni katika kuhakikisha kuwa Wizara kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa inatimiza malengo yake ya kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.

    Ninawasilisha,

    Dkt. Donan W. Mmbando

    KATIBU MKUU

    BARUA YA KUWASILISHA

  • iv

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Huu ni mwaka wa 11 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) tarehe 1 Julai, 2003. Katika kipindi chote hicho, TFDA imeweza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mipango na mikakati iliyojiwekea. Lakini pia, Mamlaka imekumbana na changamoto mbalimbali na kubuni mbinu za kukabiliana nazo ili kufikia lengo lake kuu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini na hivyo kulinda afya ya jamii.

    Taarifa hii inaainisha kazi zilizotekelezwa na TFDA katika kipindi cha Julai 2013 hadi Juni 2014 na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa kazi hizo kwa kipindi tajwa. Katika kipindi hicho, Mamlaka ilikuwa katika mwaka wa pili wa kutekeleza Mpango Mkakati wa awamu ya tatu (3) wa miaka mitano (5) yaani 2012/13 – 2016/17. Mpango huu umeainisha malengo makuu ya kila mwaka kwa huduma zinazotolewa na TFDA na viashiria vya upimaji wake.

    Katika mwaka 2013/14, kumekuwa na ongezeko la maeneo ya biashara ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba yaliyofanyiwa tathmini, kukidhi vigezo na kusajiliwa na TFDA ukilinganisha na mwaka 2012/13. Aidha, 91% ya sampuli za bidhaa zilizokuwepo zilifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na kiwango cha kukidhi vigezo stahiki kuwa 97% ya sampuli zilizochunguzwa hivyo kuashiria ubora na usalama wa bidhaa zinazodhibitiwa katika soko la Tanzania. Pamoja na upungufu wa maombi ya usajili wa bidhaa yaliyofanyiwa tathmini na kusajiliwa na TFDA kwa kipindi hiki cha 2013/14 ikilinganishwa na 2012/13, kwa kiasi kikubwa TFDA imefikia malengo yaliyoainishwa kwa mwaka 2013/14 kama ilivyochanganuliwa kwenye taarifa kuu.

    Mafanikio ya TFDA kwa kipindi tajwa ni matokeo ya ushirikiano wa karibu na wadau wake mbalimbali ikiwa ni pamoja na wananchi, asasi za kijamii na washirika wa maendeleo pamoja na maelekezo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wajumbe wa Bodi ya Ushauri.

    Napenda kutoa pongezi kwa Menejimenti ya TFDA pamoja na wafanyakazi wote kwa ujumla kwa kufuata maelekezo, kufanya kazi kwa bidii na kuonesha mshikamano katika kusimamia shughuli za udhibiti wa usalama na ubora wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba. Niwaombe kuendeleza moyo huu wa kujituma na mahusiano ambayo tayari yamejengeka na wadau wote.

    Natoa wito kwa wadau wa TFDA kuendeleza ushirikiano katika kuhakikisha taratibu zinafuatwa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa pale inapohisiwa au kujulikana kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Mchango wa wadau wote wa TFDA ni muhimu katika kutimiza lengo lake la kulinda afya ya jamii.

    Balozi Dkt. Ben Moses

    MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI (MAB)

    MAELEZO YA MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI (MAB)

    “Mafanikio ya TFDA kwa kipindi tajwa ni matokeo ya ushirikiano wa karibu na wadau wake mbalimbali

  • v

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    “Huu ni mwaka wa pili wa kutekeleza Mpango Mkakati wa Mamlaka wa awamu ya tatu (3) wa miaka mitano (2012/13 – 2016/17), na umekuwa wa mafanikio…

    Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa mwaka 2013/14 inaainisha kazi na majukumu yaliyotekelezwa kwa kipindi husika, changamoto mbalimbali ambazo Mamlaka imekabiliana nazo pamoja na matarajio ya baadaye katika kutimiza malengo ya Taasisi.

    Huu ni mwaka wa pili wa kutekeleza Mpango Mkakati wa Mamlaka wa awamu ya tatu (3) wa miaka mitano (2012/13 – 2016/17), na umekuwa wa mafanikio makubwa kwa TFDA na wadau wake. Mafanikio hayo yanazingatia utekelezaji wa malengo mkakati sita (6) yafuatayo;

    i. Kuimarisha udhibiti wa usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba;

    ii. Kuimarisha utoaji elimu na shughuli za kutangaza huduma za Mamlaka;

    iii. Kuimarisha usimamizi wa rasilimali;

    iv. Kutoa huduma kwa waathirika na kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI;

    v. Kuimarisha na kutekeleza kwa ufanisi Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Rushwa; na

    vi. Kuboresha masuala ya Jinsia na Mazingira.

    Katika utekelezaji wa lengo la kuimarisha udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, Mamlaka ilitathmini maombi 5,130 ya usajili wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba pamoja na matangazo ya bidhaa husika. Hii ni sawa na 70% ya maombi yote yaliyokuwepo. Maombi 3,870 sawa na 75% ya maombi yaliyotathminiwa yaliidhinishwa. Vilevile, Mamlaka ilikuwa na jumla ya maombi 5,160 ya usajili wa maeneo ya kuendesha biashara za bidhaa inazozidhibiti ambapo maombi 4,934 (96%) yalifanyiwa tathmini na kati yake maombi 4,034 sawa na 82%, yalikidhi vigezo na hivyo kuidhinishwa.

    Ukaguzi wa majengo na bidhaa ulifanyika katika maeneo 5,785 yakijumuisha viwanda vya utengenezaji dawa na chakula vya ndani na nje ya nchi. Idadi hiyo ni zaidi ya majengo 1,869 (48%) ikilinganishwa na majengo 3,916 yaliyokaguliwa katika kipindi cha mwaka 2012/13. Jumla ya maeneo 4,000 sawa na 69% yalikidhi vigezo ambayo ni ongezeko la maeneo 1,397 (34%) ikilinganishwa na mwaka 2012/13. Ongezeko hili limechangiwa na juhudi katika kazi za udhibiti ikiwa ni pamoja na elimu kwa wadau na uhamasishaji.

    Vilevile, katika kipindi cha mwaka 2013/14, Mamlaka ilipokea sampuli 2,381 kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara na kufanya kuwa na jumla ya sampuli 2,686 zikiwa ni pamoja na baki ya sampuli 305 za mwaka 2012/13. Kati yake, sampuli 2,456 (91%) zilichunguzwa ambapo sampuli 2,379 sawa na 97% zilifaulu, hivyo kuashiria ubora na usalama wa bidhaa katika soko la Tanzania.

    MAELEZO YA MKURUGENZI MKUU

  • vi

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Katika kudhibiti usalama na ubora wa bidhaa zinazoingia na kutoka nchini, Mamlaka ilipokea maombi 11,887 ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ambapo maombi 10,394 (10,082 ya kuingiza bidhaa ndani ya nchi na 312 ya kutoa bidhaa nje ya nchi) sawa na 87% yaliidhinishwa. Maombi yaliyopokelewa katika mwaka huu ni ongezeko la maombi 4,333 (57%) ikilinganishwa na maombi yaliyopokelewa mwaka 2012/13.

    Sanjari na hilo, bidhaa za uzito wa tani 313.4 zenye thamani ya takriban TZS 961,883,633 ziliteketezwa baada ya kubainika kutofaa kwa matumizi ya binadamu na mifugo.

    Katika kufuatilia usalama wa dawa katika soko, jumla ya taarifa 123 za madhara ya dawa (Adverse Drug Reactions - ADRs) zilipokelewa kutoka sehemu mbalimbali nchini. Aidha, taarifa 20 za maendeleo ya usalama wa dawa zilizo katika soko yaani “Periodic Safety Update Reports - PSURs” zilipokelewa na zote zilifanyiwa tathmini. Katika ripoti zilizopatikana kutoka nje ya nchi, yaliripotiwa madhara kwenye ini yaliyohusiana na dawa ya vidonge ya kutibu ‘fungus’ iitwayo ‘Ketoconazole’ hivyo matumizi ya dawa hiyo yalisitishwa nchini. Vilevile, taarifa 198 za madhara ya majaribio ya dawa zilipokelewa kutoka katika majaribio ya dawa hapa nchini na taarifa 91 kutoka nje ya nchi. Tathmini ilionesha kuwa hapakuwa na athari za kiafya zilizotishia usalama wa washiriki katika majaribio ya dawa.

    Aidha, katika kuhakikisha kwamba majukumu ya TFDA yanaeleweka kwa wadau, elimu kwa umma imeendelea kutolewa, sanjari na kuitangaza Mamlaka kwa wadau kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuendesha vipindi vya Radio na TV, kutoa taarifa kwa umma na matangazo yenye ujumbe tofauti kuhusu huduma za TFDA, kufanya mikutano na wahariri na waandishi wa habari kwa lengo la kuwapa taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za udhibiti pamoja na kuandaa vipeperushi, mabango na machapisho yenye ujumbe kuhusu usalama na ubora wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

    Kwa upande wa usimamizi wa rasilimali, Mamlaka ilikusanya jumla ya TZS 17,911,067,896 kutoka vyanzo vilivyoainishwa katika Mpango Kazi wa 2013/14, sawa na 118% ya makadirio ya makusanyo ya TZS 15,224,495,434 kwa kipindi husika. Kati ya fedha hizo, TZS 15,054,913,000 ni kutokana na vyanzo vya ndani sawa na 127% ya lengo la kukusanya TZS 11,848,076,405.

    Hii ni ongezeko la 33% ikilinganishwa na kiasi cha TZS 11,327,961,785 kilichokusanywa mwaka 2012/13. Aidha, kiasi cha TZS 14,700,071,722 kilitumika katika kipindi husika cha 2013/14 kwa ajili ya shughuli za udhibiti, ununuzi wa vifaa vya maabara na huduma za uendeshaji ofisi.

    TFDA iliajiri watumishi wapya 25 wa ajira ya kudumu na malipo ya pensheni na watumishi 13 kwa mkataba wa muda mfupi ili kuongeza nguvu kazi katika idara zenye upungufu wa watumishi. Sanjari na hilo, mpango wa mafunzo wa Mamlaka ulitekelezwa ambapo watumishi 61 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi na hivyo kuboresha utendaji kazi. Utekelezaji huu ni kwa kiwango cha 94% ukilinganisha na idadi ya watumishi 65 waliopangwa kuhudhuria mafunzo kwa mwaka 2013/14.

    Pamoja na mafanikio hayo makubwa, TFDA imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali hususan uwezo mdogo wa kutathmini maombi ya usajili wa bidhaa kutokana na upungufu wa watumishi pamoja na viwanda vya ndani na machinjio kutokidhi matakwa ya Sheria. Matarajio ya baadaye katika kukabiliana na changamoto hii ni kushirikiana na mamlaka za ajira Serikalini na ofisi za Halmashauri katika kusimamia sheria.

    Nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wenzangu wa TFDA. Vilevile, natoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara (MAB) kwa TFDA na uongozi wa Wizara kwa maelekezo sahihi ambayo yameiwezesha TFDA kupata mafanikio makubwa.

    Ni matarajio yangu kwamba ushirikiano uliopo utaendelezwa katika mwaka 2014/2015.

    Hiiti B. Sillo

    MKURUGENZI MKUU

  • 1

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    1.0 UtanguliziMamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inaendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano (2012/13 - 2016/17) ambao unalenga kutimiza jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa kuzingatia Mpango wa kazi wa kila mwaka.

    Taarifa hii inaainisha kazi zilizotekelezwa na TFDA kwa mwaka wa pili (2) wa utekelezaji wa Mpango Mkakati kwa kuzingatia malengo mkakati yafuatayo:-

    i. Kuimarisha udhibiti wa usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba;

    ii. Kuimarisha utoaji elimu na shughuli za kutangaza huduma za Mamlaka;

    iii. Kuimarisha usimamizi wa rasilimali;

    iv. Kutoa huduma kwa waathirika na kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI; na

    v. Kuimarisha na kutekeleza kwa ufanisi Mkakati wa Taifa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa; na Kuboresha masuala ya jinsia na mazingira.

    TAARIFA KAMILI

  • 2

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    2.0 Kuimarisha ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba

    2.1 Tathmini na usajili wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na matangazoMamlaka ilikuwa na baki ya maombi ya usajili wa bidhaa 1,315 kwa mwaka 2012/13 na kupokea maombi 5,987, hivyo kufanya jumla ya maombi yote ya usajili wa bidhaa kwa 2013/14 kuwa 7,302. Jumla ya maombi 5,130 sawa na 70% yalifanyiwa tathmini ambapo maombi 3,870 sawa na 75% yaliidhinishwa.

    Aidha, maombi yaliyofanyiwa tathmini ni pungufu ya maombi 1,839 ikilinganishwa na maombi 6,969 yaliyofanyiwa tathmini katika pindi cha mwaka 2012/13. Tofauti hii imechangiwa na idadi ndogo ya maombi ya chakula yaliyotathminiwa (2,320) ikilinganishwa na maombi ya chakula yaliyotathminiwa mwaka uliopita (3,718). Hii inatokana na upungufu wa watathmini wa chakula pamoja na maboresho katika mfumo wa taarifa “Integrated Management Information System – IMIS” kuwa katika majaribio kwa kipindi husika.

    Mchanganuo wa maombi ya usajili wa bidhaa, utekelezaji wa lengo la usajili kwa mwaka pamoja na mchanganuo wa maombi ya usajili ambayo hayajafanyiwa tathmini kwa kuzingatia umri/tarehe ya kupokelewa TFDA umeainishwa katika jedwali Na. 1 (a) - 1 (c).

  • 3

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    Jedwali Na.1 (a): Mchanganuo wa Maombi ya Usajili wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba, matangazo na majaribio ya dawa

    Na Aina ya bidhaa Maelezo

    Maombi

    Bak

    i ya

    2012

    /13

    Poke

    lew

    a

    Jum

    la

    Tath

    min

    iwa

    Bak

    i

    Idhi

    nish

    wa

    1Chakula

    Mapya 393 2283 2676 1907 769 1292

    Huishwa 0 120 120 52 68 31

    Mabadiliko 0 18 18 18 0 18

    Hoja 0 343 343 343 0 309

    Jumla ndogo 393 2764 3157 2320 837 1650

    2 Dawa

    Binadamu

    Mapya 259 618 877 493 384 528

    Huishwa 308 647 955 460 495 450

    Mabadiliko 41 485 526 387 139 387

    Hoja 9 331 340 255 85 0*

    Jumla ndogo 617 2081 2698 1595 1103 1365

    Mifugo

    Mapya 20 34 54 27 27 18

    Huishwa 30 61 91 52 39 52

    Mabadiliko 7 13 20 17 3 17

    Hoja 1 25 26 10 16 0*

    Jumla ndogo 58 133 191 106 85 87

    Mitishamba

    Mapya 4 10 14 12 2 4

    Mabadiliko 2 2 4 4 0 4

    Hoja 0 2 2 2 0 0*

    Jumla ndogo 6 14 20 18 2 8

    3 Majaribio ya dawa Mapya 0 14 14 12 2 8

    Mabadiliko 0 4 4 4 0 4

    Jumla ndogo 0 18 18 16 2 12

    4 Vipodozi 224 615 839 745 94 617

    5 Vifaa tiba 15 203 218 173 45 15

    6 MatangazoChakula 0 7 7 3 4 2

    Dawa 2 112 114 114 0 114

    Jumla ndogo 241 977 1218 1075 143 748

    Jumla Kuu 1315 5987 7302 5130 2172 3870

    Nb: * Majibu ya hoja hayajaamuliwa. Hoja zinapofungwa dawa husajiliwa au kukataliwa usajili

  • 4

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Jedwali Na. 1 (b): Utekelezaji wa lengo la usajili wa bidhaa kwa mwaka

    Na. Maelezo

    Bidhaa

    Chakula Dawa

    Vipodozi Vifaa tiba Binadamu Mifugo

    1. Idadi ya maombi kwa ajili ya tathmini (A) 3157 2698 191 1063 233

    2. Lengo la Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) 80% 72% 72% 70% 39%

    3. Idadi ya maombi yanayopaswa kutathminiwa (B) 2 526 1 943 138 744 91

    4. Idadi ya maombi yaliyotathminiwa (C) 2320 1 595 106 745 173

    5. % ya maombi yaliyotathminiwa (C/A*100) 73% 59% 55% 70% 74%

    6. % ya utekelezaji wa lengo mkakati (C/B*100) 92% 82% 77% 100% 190%

    Kwa mujibu wa Jedwali Na. 1 (a) na 1(b), lengo lililowekwa la usajili wa vipodozi kwa kuzingatia Mpango Mkakati lilifikiwa na kwa upande wa vifaa tiba lengo lilivukwa. Pamoja na idadi ya maombi ya usajili wa dawa na chakula yaliyotathminiwa kuwa kubwa, malengo ya usajili hayakufikiwa kutokana na mfumo wa kufanya tathmini kwa bidhaa za chakula na dawa (IMIS) kuwa kwenye majaribio katika kipindi husika. Mkakati wa kufanya tathmini ya maombi yaliyobaki unaendelea kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuwa na mpango maalum wa kuwashirikisha watathmini wa ndani na nje ya TFDA kwa njia ya retreats.

    Jedwali Na. 1(c): Mchanganuo wa maombi mapya ya bidhaa ambayo hayajafanyiwa tathmini kulingana na tarehe ya kupokelewa (Age analysis)

    Aina ya Bidhaa

    Idadi ya siku kwa mujibu wa Mkataba

    wa Huduma kwa Wateja

    Muda uliopita tangu maombi husika kupokelewa(Siku)

    ≤30

    31-6

    5

    66-1

    30

    131-

    250

    251-

    360

    > 36

    0

    JUMLA

    1 Chakula 45 14 35 15 35 0 0 99

    2 Vyakula Nyongeza (Food supplements)

    60 0 1 0 0 0 0 1

    3 Dawa za binadamu zinazotengenezwa nchi za nje

    250 94 50 87 71 78 4 384

    4 Dawa za mifugo zinazotengenezwa nchi za nje

    250 12 4 9 0 2 0 27

    5 Dawa za mitishamba zinazotengenezwa nchi za nje

    250 1 0 0 1 0 0 2

    JUMLA KUU 513

    Nb: Hakukuwa na maombi ya usajili wa dawa za binadamu, mifugo na mitishamba zinazotengenezwa hapa nchini.

    Jedwali Na. 1(c) linaonesha kuwa maombi 50 ya usajili wa chakula kati ya 99 na maombi 82 ya dawa za binadamu kati ya 384 hayakutathminiwa kwa wakati kwa mujibu wa viwango vya Mkataba wa Huduma kwa Wateja (CSC) vya siku 45 na 250. Kushindwa kutathmini ndani ya muda kumetokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa kuhamisha taarifa za bidhaa kutoka kwenye mfumo wa taarifa wa awali (Management Information System - MIS) kwenda kwenye mfumo ulioboreshwa. Pia, kumechangiwa na idadi ndogo ya watathmini pamoja na baadhi ya wateja kutokidhi matakwa ya Miongozo ya Usajili wa bidhaa husika.

  • 5

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    2.2. Usajili wa maeneo na utoaji wa vibali vya biashara ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba

    Jumla ya maombi 4,920 (3,029 mapya na 1,891 ya kuhuisha) ya usajili wa maeneo ya biashara za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba yalipokelewa katika kipindi husika. Aidha, maombi 240 yalibaki katika kipindi cha mwaka 2012/13 hivyo kufanya jumla ya maombi 5,160. Maombi 4,934 sawa na 100.3% yalifanyiwa tathmini ikilinganishwa na lengo la kutathmini 100% ya maombi yote yanayopokelewa kwa mwaka. Jumla ya maombi 4,034 sawa na 82% ya maombi yaliyofanyiwa tathmini yalikidhi vigezo na kuidhinishwa. Mchanganuo wa maombi hayo ni kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.

    Jedwali Na. 2: Maombi ya Usajili wa Maeneo na Utoaji wa Vibali vya biashara ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba

    Aina ya jengo Baki Juni 2013

    Yaliyopokelewa Jumla

    Yaliy

    otat

    hmin

    iwa

    Yaliyosajiliwa

    Map

    ya

    Hui

    sha

    Idad

    i

    %

    Chakula Viwanda 59 314 289 662 603 450 75Maghala 4 89 73 166 161 158 98Hoteli 0 45 98 143 143 105 73Kuuzia chakula- jumla 23 933 221 1177 1154 1054 91Kuuzia chakula-reja reja 114 294 244 652 556 444 80Machinjio 0 2 1 3 3 2 67Magari 0 175 426 601 601 242 40

    Jumla ndogo 200 1852 1352 3404 3221 2455 76

    Dawa Viwanda vya ndani 0 2 6 8 8 5 63Maghala 0 8 10 18 18 18 100Duka la dawa-Binadamu 23 7 66 96 73 70 96Duka la dawa- Mifugo 5 46 30 81 77 67 87Magari 0 12 0 12 12 0 0

    Jumla ndogo 28 75 112 215 188 160 85Vipodozi Watengenezaji 0 7 4 11 9 8 89

    Wauzaji wa Jumla 12 116 42 170 158 148 94Wauzaji Rejareja 0 930 355 1285 1285 1202 94Maghala 0 7 5 12 10 10 100Magari 0 9 0 9 9 0 0

    Jumla ndogo 12 1069 406 1487 1471 1368 93Vifaa tiba Wauzaji wa jumla 0 33 21 54 54 51 94

    Jumla ndogo 0 33 21 54 54 51 94Jumla kuu 240 3029 1891 5160 4934 4034 82

    Idadi ya maombi yaliyofanyiwa tathmini kwa mwaka 2013/14 ni ongezeko la maombi 2,243 (83%) ikilinganishwa na maombi 2,691 yaliyofanyiwa tathmini mwaka 2012/13. Vilevile, idadi ya maeneo yaliyokidhi vigezo na kusajiliwa mwaka huu ni ongezeko la maombi 1,397 (34%) ikilinganishwa na mwaka uliopita.

    Ongezeko hili la idadi ya maombi yaliyotathminiwa na maeneo mengi kukidhi vigezo linatokana na juhudi zilizofanywa katika kazi za udhibiti ikiwemo elimu kwa wadau na wananchi kuwataka kutii sheria bila shuruti.

  • 6

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    2.3 Ukaguzi na ufuatiliaji wa usalama na ubora wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba

    Mamlaka iliendelea kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa majengo na bidhaa za vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba. Ukaguzi wa majengo na bidhaa ulifanyika katika maeneo 5,785.

    Idadi hiyo ni zaidi ya majengo 1,869 (48%) ikilinganishwa na majengo 3,916 yaliyokaguliwa katika kipindi cha mwaka 2012/13. Jumla ya maeneo 4,000 sawa na 69% yalikidhi vigezo.

    Aidha, Mamlaka ilikagua jumla ya viwanda 84 vya kutengenezea dawa vilivyoko nje na ndani ya nchi ambapo viwanda 62 sawa na 74% vilikidhi vigezo. Mchanganuo wa majengo yaliyokaguliwa umeainishwa kwenye Jedwali Na. 3.

    Jedwali Na. 3: Maeneo yaliyokaguliwa katika kipindi cha 2013/14

    Na. Aina ya biashara Yaliyokaguliwa Yaliyokidhi vigezoIdadi Idadi %

    1 Chakula Viwanda - ndani 1150 830 72Sehemu za kuuzia 1651 1175 71Maghala 173 132 76Machinjio 77 11 14

    Jumla ndogo 3051 2148 702 Dawa Famasi/DLDM -binadamu 838 620 74

    Famasi/DLDM- mifugo 237 164 69Viwanda vya dawa vya nje ya nchi 72 60 83Viwanda vya dawa vya ndani ya nchi 12 2 17Maghala 45 26 58

    Jumla ndogo 1204 872 72(1) Serikali 59 47 80(2) Binafsi 66 56 85(3) Mashirika ya Dini (FBO) 22 21 95(4) Hospitali 109 109 100(5) Zahanati 10 10 100

    Jumla ndogo 266 243 913 Vipodozi

    Maduka 1014 547 54Maghala 2 2 100Watengenezaji 10 9 90

    Vifaa Tiba Jumla/reja reja 238 179 75

    Jumla ndogo 1264 737 58

    Jumla kuu 5785 4000 69

    Kwa mujibu wa jedwali Na.3 hapo juu, 69% ya maeneo yaliyokaguliwa yalikidhi matakwa ya sheria ikilinganishwa na 59% kwa mwaka 2012/13. Changamoto ilikuwa kwa baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na machinjio ambayo kiwango cha kukidhi matakwa ya sheria bado ni kidogo.

    Uhamasishaji kwa wamiliki unaendelea kwa lengo la kuboresha maeneo yao ili yafikie vigezo vinavyokubalika kwa lengo la kuongeza kiwango cha usalama na ubora wa bidhaa zinazouzwa au kuzalishwa katika maeneo hayo.

    Maeneo yaliyoonesha kuongezeka kwa kiwango cha kukidhi matakwa ya sheria kwa mwaka huu ikilinganiswa na mwaka uliopita wa 2012/13 ni pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya, viwanda vya ndani vya chakula pamoja na viwanda vya dawa vya nje ya nchi.

  • 7

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    2.4 Udhibiti wa uingizaji na usafirishaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ndani na nje ya nchi.

    Mamlaka ilipokea jumla ya maombi 11,887 ya kuingiza nchini na kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Maombi 10,082 ya kuingiza bidhaa nchini na 312 ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi sawa na 87% ya maombi yote yaliyopokelewa yaliidhinishwa. Maombi yaliyopokelewa katika mwaka huu ni ongezeko la maombi 4,333 (57%) ikilinganishwa na maombi 7,504 yaliyopokelewa mwaka uliopita wa 2012/13.

    Mchanganuo wa maombi ya uingizaji na usafirishaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ndani na nje ya nchi umeainishwa kwenye Jedwali Na. 4.

    Jedwali Na. 4: Mchanganuo wa maombi ya vibali vya kuingiza na kusafirisha vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ndani na nje ya nchi

    Na.

    Aina ya bidhaa

    Maombi yaliyopokelewa Vibali vilivyotolewaVibali vilivyokaguliwa katika vituo vya forodha

    Kuingia Kutoka Kuingia Kutoka Kuingia kutoka

    1 Dawa 3272 79 2972 79 3286 22

    2 Vipodozi 854 56 809 56 744 2133 Vifaa tiba 2026 21 1611 21 128 6

    4 Chakula 5008 571 4690 156 6684 1224

    Jumla 11,160 727 10,082 312 10,842 1,465

    11,887 10,394 12,307Nb: Vibalivilivyokaguliwakatikavituovyaforodhanipamojanabaadhiyavilivyotolewamwaka2012/13namizigo

    husikakuingizwakatikamwaka2013/14

    2.5 Uchunguzi wa sampuli katika maabara ya MamlakaKatika kipindi cha 2013/14, Mamlaka ilipokea sampuli 2,381 na kufanya kuwa na jumla ya sampuli 2,686 zikiwa ni pamoja na baki ya sampuli 305 za mwaka 2012/13. Sampuli 2,456 ambazo ni sawa na (91%) ya sampuli zilizokuwepo, zilichunguzwa ambapo sampuli 2,379 sawa na 97% zilikidhi vigezo.

    Sampuli zilizochunguzwa mwaka huu ni pungufu ya sampuli 235 (8.7%) ikilinganishwa na sampuli zilizochunguzwa mwaka uliopita wa 2012/13 kutokana na kukosa vigezo vya ubora (reference standards) kwa uchunguzi wa sampuli za vipodozi. Aidha, sampuli zilizokidhi vigezo mwaka huu ni pungufu ya 64 (2.6%) ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mchanganuo wa sampuli za bidhaa zilizochunguzwa umeainishwa kwenye jedwali Na. 5 (a).

  • 8

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Jedwali Na. 5(a): Mchanganuo wa sampuli za bidhaa zilizochunguzwa

    Bidhaa

    Bak

    i ya

    mw

    aka

    2012

    /13

    (A)

    Poke

    lew

    a 20

    13/1

    4 (

    B)

    Jum

    la (

    C)

    Chu

    nguz

    wa

    (D)

    Asilimia ya zilizo chunguzwa (%)

    Zili

    zoki

    dhi (

    E)

    Zili

    zofe

    li (F

    )

    Bak

    i (G

    )

    Kiwango cha kukidhi% (E/D)

    Dawa za binadamu 292 1198 1490 1400 94 1379 21 90 99

    Dawa za mifugo 0 69 69 62 90 56 6 7 90

    Vipodozi 2 71 73 31 42* 31 0 42 100

    Vifaa Tiba 0 91 91 91 100 91 0 0 100

    Vyakula 11 952 963 872 91 822 50 91 96

    JUMLA 305 2,381 2,686 2,456 91 2,379 77 230** 97

    NB: *Sehemukubwayasampulizavipodozihazikuchunguzwakutokananakukosavigezovyaubora(CertifiedReferenceStandards-CRSna“HPLCcolumn”).

    Kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa Mamlaka, lengo ni kufanya uchunguzi wa 90% ya sampuli zote kwa mwaka husika. Kwa kuzingatia Jedwali Na. 5 (a), Mamlaka ilipaswa kuchunguza sampuli 2,417 ambazo ni 90% ya sampuli 2,686 zilizokuwepo kwa ajili ya uchunguzi. Mamlaka ilichunguza sampuli 2,456 (91%) na hivyo kuvuka lengo. Aidha, kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Wateja, Mamlaka ilijiwekea lengo la kutoa majibu ya uchunguzi ndani ya siku 15 za kazi. Jedwali Na 5(b) linaonesha mchanganuo wa siku za utoaji majibu ya uchunguzi.

  • 9

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    Jedwali Na. 5(b): Siku za majibu ya uchunguzi wa sampuli tangu kupokelewaBidhaa Chanzo cha sampuli Kiwango cha siku kwa

    mujibu wa Mkataba≤ 15 16-21 22-30 >30 Jumla

    Dawa Ukaguzi 15 10 0 20 7 37

    Usajili 15 241 96 66 586 989

    Wateja wa nje 15 3 2 0 43 48

    Ufuatiliaji wa bidhaa sokoni (PMS) 15 0 5 0 20 25

    Utafiti - 0 0 16 45 61

    Vipodozi Ufuatiliaji wa bidhaa sokoni 15 0 0 0 29 29

    Chakula Ukaguzi 15 124 329 59 39 551

    Usajili 15 33 190 13 4 229

    Wateja wa nje 15 58 - - - 58

    Ufuatiliaji wa bidhaa sokoni 15 - 130 - - 130

    Utafiti - 206 668 - 111 985

    Uchambuzi katika Jedwali Na 5(b) unaonesha kuwa 50% ya majibu ya uchunguzi wa sampuli yanatolewa kati ya siku 15 - 21 ukilinganisha na siku 15 ambazo ndio kiwango cha juu cha Mamlaka. Kushindwa kutoa majibu ndani ya muda kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja kumetokana na ongezeko la sampuli kwa kuzingatia kuwa Maabara ya Dawa ya TFDA imetambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia, Maabara za Chakula na Maikrobaiolojia zimepata cheti cha Ithibati kwa kiwango cha kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005. Sababu nyingine ya ucheleweshwaji wa kazi za kiuchunguzi ni upungufu wa watumishi na vitendea kazi hususan kukosekana kwa “reference standards’’ kwa wakati.

    2.6 Ufuatiliaji wa usalama wa chakula na dawaMamlaka katika kipindi hiki cha 2013/14, ilifanya uchanganuzi wa taarifa za bidhaa za chakula, kufuatilia madhara yatokanayo na matumizi ya chakula na kudhibiti uchafuzi wa sumu kuvu katika chakula. Aidha, katika kusimamia ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa zinazodhibitiwa, Mamlaka ilifanya ufuatiliaji wa madhara ya matumizi ya dawa, kudhibiti majaribio ya dawa na ufuatiliaji wa ubora wa dawa katika soko kama ilivyoainishwa kwenye vipengele 2.61 - 2.66.

    2.6.1 Uchanganuzi wa usalama wa bidhaa mbalimbali za chakula

    Uchanganuzi wa usalama wa chakula ulifanyika kwa lengo la kupata ushahidi wa kisayansi utakaosaidia katika tathmini na usajili wa chakula pamoja na kutoa elimu kwa umma na tahadhari juu ya usalama wa bidhaa. Taarifa ya bidhaa zilizofanyiwa uchanganuzi, matokeo na hatua zilizochukuliwa imeainishwa katika jedwali Na. 6.

  • 10

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Jedwali Na. 6: Taarifa ya bidhaa zilizofanyiwa uchanganuzi na hatua zilizochukuliwa

    Na. Jina la bidhaa Matokeo ya uchanganuzi Hatua iliyochukuliwa

    1. Mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu

    Taarifa za kisayansi zinaonesha kuwa mafuta ya ubuyu yasiyosafishwa (unrefined) yana kiwango cha juu cha kemikali aina ya“cyclopropenoicfattyacids(CPFA)”. Kemikali hii huweza kusababisha athari mbalimbali za kiafya kwa watumiaji pindi wanapotumia mafuta haya kama chakula.

    Hata hivyo mafuta haya yanaweza kutumika kama mali ghafi kwa bidhaa nyingine ambazo si chakula au kutumika kwenye chakula baada ya kusindikwa katika viwanda vinavyoweza kuyasafisha na kuondoa kemikali za CPFA.

    (i) Tahadhari ilitolewa kwa umma juu ya athari za matumizi ya mafuta hayo kama chakula. Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilitoa tamko kuwatahadharisha wananchi kujiepusha na matumizi ya mafuta ya mbegu za ubuyu yasiyosafishwa.

    (ii) TFDA kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela inaendelea kufanya utafiti wa mafuta hayo ili kubaini kiwango cha tindikali hiyo ya CPFA na kujua ukubwa wa matumizi ya mafuta hayo hapa nchini.

    2. Matumizi ya viambato vya ginseng,aloeveranaroyaljelly katika vinywaji

    Uchanganuzi ulibaini kuwa kiwango cha kitaifa cha bidhaa hizo(MaltDrink:Specifications) and Energydrinks hakiainishi matumizi ya viambato hivi katika bidhaa zote za aina hii.

    Aidha, uchanganuzi ulibaini kuwa viambato hivyo haviruhusiwi kutumiwa na watoto, wajawazito na wanaonyonyesha.

    Hata hivyo, mpaka sasa hakuna ripoti za kisayansi duniani zinazothibitisha juu ya usalama wa viambato hivyo vinapotumika kwa pamoja katika vinywaji.

    Mamlaka inaendelea kufanya ufuatiliaji wa hatua zinazochukuliwa na Taasisi ya Kimataifa ya viwango (FAO/WHO Codex Alimentarius Commission) ambapo kiwango cha vinywaji vyenye ginsengkinaandaliwa.

    2.6.2 Mpango wa ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na matumizi ya chakula

    Mpango wa ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na chakula na ukusanyaji wa takwimu uliendelea kutekelezwa katika Wilaya 17 za mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara pamoja na mkoa wa Kigoma ambapo watendaji wa afya katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote na Hospitali binafsi ya Kabanga walihamasishwa.

    Vilevile, mafunzo kuhusu mbinu za kutambua magonjwa yatokanayo na chakula, namna ya kuyatabiri, kuyakabili na kuyatolea taarifa, yalitolewa kwa waratibu 23 wa fani za Mafundi Sanifu Maabara, Maafisa Afya na Matabibu kutoka katika maeneo tajwa. Lengo la mpango ni kuweka na kujifunza namna bora ya kutekeleza mfumo wa ufuatiliaji na uchunguzi wa usalama wa chakula ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa takwimu na kudhibiti magonjwa yatokanayo na chakula hapa nchini.

    Mamlaka ilifanya mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula 450 kuhusu Kanuni Bora za Usindikaji wa Chakula.

  • 11

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    Mafunzo haya yalifanyika katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Morogoro, Pwani, Mtwara, Lindi na Dar es Salaam. Pia, mafunzo ya kutathmini chakula na mafunzo kuhusu utengenezaji bora na salama wa chakula ikiwa ni pamoja na mfumo unaotoa uhakika na usalama wa chakula kinachosindikwa/kuzalishwa (Hazard Analysis Critical Control Point - HACCP) yalifanyika. Mchanganuo wa taarifa za matukio ya magonjwa umeoneshwa katika Jedwali Na. 7.

    Jedwali Na. 7: Takwimu za magonjwa yatokanayo na chakula

    Aina ya ugonjwa Idadi ya wagonjwa

    Dodoma Singida Manyara JumlaKuharisha 8,825 791 264 9,880Kuhara damu 4,839 371 66 5,276Minyoo 714 0 55 769Homa ya matumbo 537 158 63 758Amiba 0 0 192 192Ugonjwa wa kutoa mimba (Brucelosis) 0 0 27 27Kimeta 0 0 14 14

    Jumla 14,915 1,320 681 16,916

    Kwa mujibu wa Jedwali Na. 7, mkoa wa Dodoma ndiyo uliotoa taarifa nyingi za magonjwa yatokanayo na matumizi ya chakula. Uhamasishaji zaidi juu ya umuhimu wa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa kama hizi sanjari na utoaji wa elimu ya kanuni za usafi vitaendelea kufanyika katika mwaka ujao wa fedha.

    2.6.3 Mkakati wa kudhibiti uchafuzi wa sumu kuvu katika chakula

    Mamlaka iliendelea kufanya utafiti wa usalama wa bidhaa za nafaka dhidi ya uchafuzi wa sumu kuvu (mycotoxins) hususan katika mahindi na mazao mengine jamii ya nafaka katika wilaya za Hanang na Kilosa.

    Jumla ya sampuli 470 za mahindi, 37 mtama, 8 ulezi, 24 ngano, 10 mchele na 82 za maziwa kutoka kwa akina mama wanaonyonyesha zilifanyiwa uchunguzi wa sumu kuvu aina ya aflatoxins na fumonisins. Matokeo ya uchunguzi yameainishwa katika jedwali Na 8

    Jedwali Na. 8: Matokeo ya uchunguzi wa sumu kuvu

    Wilaya Aina ya sampuli

    Idad

    i ya

    sam

    puli

    zi

    lizoc

    hung

    uzw

    a

    Ain

    a ya

    sum

    u ku

    vu

    iliyo

    chun

    guzw

    a

    Sam

    puli

    ziliz

    ocha

    fuliw

    a (%

    )

    Kia

    si c

    ha u

    chaf

    uzi

    (ran

    ge)

    (μg/

    kg)

    Sam

    puli

    ziliz

    ocha

    fuliw

    a kw

    a ki

    wan

    go

    kisi

    chor

    uhus

    iwa

    (%)

    Hanang Mtama 12 Aflatoxin B1 16 0.55 - 2.5 0Total aflatoxins 41 0.53 - 10.1 8Fumonisins 8 53 - 611 0

    Ulezi 8 Aflatoxin B1 25 0.55 - 0.58 0

    Total aflatoxins 36 0.53 - 2.25 0Fumonisins 50 53 - 201 0

    Ngano 24 Aflatoxin B1 8 0.56 - 0.57 0Total aflatoxins 45 0.52 - 2.2 0Fumonisins 63 92 - 302 0

    Mahindi 211Aflatoxin B1 10 0.58 - 74.0 2Total aflatoxins 14 0.45 - 91.0 6Fumonisins 64 51- 2507 5

  • 12

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Wilaya Aina ya sampuli

    Idad

    i ya

    sam

    puli

    zi

    lizoc

    hung

    uzw

    a

    Ain

    a ya

    sum

    u ku

    vu

    iliyo

    chun

    guzw

    a

    Sam

    puli

    ziliz

    ocha

    fuliw

    a (%

    )

    Kia

    si c

    ha u

    chaf

    uzi

    (ran

    ge)

    (μg/

    kg)

    Sam

    puli

    ziliz

    ocha

    fuliw

    a kw

    a ki

    wan

    go

    kisi

    chor

    uhus

    iwa

    (%)

    Kilosa Mtama 25 Aflatoxin B1 48 0.53 - 26. 7 8Total aflatoxins 56 0.52 - 41.6 8Fumonisins 44 75 - 929 0

    Mchele 10 Aflatoxin B1 60 0.55 - 2.0 0Total aflatoxins 70 0.58 - 2.64 0Fumonisins 90 163 - 445 0

    Mahindi 259Aflatoxins B1 61 0.55 - 247 30Total aflatoxins 69 0.45 - 313.5 28Fumonisins 76 54 - 6564 6

    Maziwa ya akina mama wanaonyonyesha

    82Aflatoxin M1 90 0.007 - 0.252 22

    Jedwali Na. 8 linaonyesha kiwango cha uchafuzi kwenye zao la mahindi kuwa ni kikubwa kuliko kwenye nafaka nyingine. Aidha, uchafuzi kwenye mahindi katika wilaya ya Kilosa ni wa kiwango cha juu ikilinganishwa na wilaya ya Hanang. Maziwa ya akina mama wanaonyonyesha yalionesha kuchafuliwa na sumu kuvu aina ya AflatoxinM1.

    Kiwango kinachovumilika ni kile kisichozidi 5μg/kg kwa AflatoxinB1, 0.025 μg/l AflatoxinM1, 10μg/kg kwa TotalAflatoxin na 1000 μg/kg kwa Fumonisins. Matokeo haya yanakusudiwa kutumika katika kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa sumu kuvu kwa wadau wanaohusika katika hatua mbalimbali za mnyororo wa chakula (food chain). Pia Mamlaka iliratibu na kushiriki katika mkutano wa Kamati Endeshaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Sumu Kuvu - National Steering Committee on Mycotoxins Control ambayo TFDA ni sekretarieti.

    Kamati ilijadili na kutoa mapendekezo mbalimbali ya udhibiti wa uchafuzi wa sumu kuvu nchini. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na viwango vya sumu kuvu aina ya AflatoxinM1 katika maziwa na bidhaa zake na udhibiti wa sumu kuvu katika vyakula vya mifugo ili kuepuka uchafuzi kwenye bidhaa za mifugo kama vile maziwa, nyama na mayai.

    2.6.4. Ufuatiliaji wa Madhara ya Matumizi ya dawa

    Jumla ya taarifa 123 za madhara yanayohisiwa kusababishwa na matumizi ya dawa (AdverseDrugReactions–ADRs) zilipokelewa na kufanyiwa tathmini na baadaye kuingizwa kwenye kanzidata (vigiflow database). Aidha taarifa tano (5) za madhara yaliyotokana na matumizi ya dawa ya sindano aina ya ‘Chloramphenicol’ inayotengenezwa na kiwanda chaLincolnPharmaceuticalsLtd. zilipokelewa na kutathminiwa na hivyo TFDA ilisitisha matumizi ya dawa hiyo wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.

    Vilevile, taarifa 20 za maendeleo ya usalama wa dawa zilizoko katika soko yaani “Periodic Safety Update Reports - PSURs” zilipokelewa kutoka nje ya nchi na kufanyiwa tathmini. Katika taarifa hizo, yaliripotiwa madhara kwenye ini yaliyohusiana na dawa ya “Ketoconazole” ya vidonge na hivyo Mamlaka kusitisha matumizi ya dawa hiyo nchini.

    Kazi ya ufuatiliaji wa karibu wa usalama wa dawa za UKIMWI aina ya Zidovudine, Lamivudine na Nevirapine/ Efavirenz iliendelea katika mikoa nane (8) ya Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Mbeya, Tanga, Arusha, Mwanza na Mara. Jumla ya wagonjwa 1,228 walishiriki katika mpango huo na taarifa za usalama wa dawa hizo kwa wagonjwa wote zilirekodiwa na kuingizwa kwenye kanzidata ya “CEMflow” iliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Tathmini ya taarifa hizo ilifanyika na kubainisha kuwa hapakuwa na madhara mapya ya kiafya yaliyotokea kwa

  • 13

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    watumiaji wa dawa hizi. Madhara yaliyotokea ni yale yaliyokwisha tolewa taarifa zake katika tafiti mbalimbali za dawa hizo wakati wa utengenezaji na yameambatishwa katika vielelezo vilivyomo katika vifungashio vya dawa.

    2.6.5 Udhibiti wa Majaribio ya Dawa

    Katika kipindi cha 2013/14, jumla ya maombi 14 ya majaribio ya dawa yalipokelewa, ambapo kati yake maombi 12 (86%) yalifanyiwa tathmini na maombi nane (8) kati yake yaliidhinishwa. Vilevile maombi manne (4) ya mabadiliko katika majaribio ya dawa yalipokelewa na yote kufanyiwa tathmini na kuidhinishwa.

    Taarifa 198 za matukio makubwa katika majaribio ya dawa (Serious Adverse Events – SAEs) kutoka ndani ya nchi na 91 kutoka nje ya nchi zilipokelewa. Tathmini ilionesha kuwa matukio hayo hayakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na dawa za majaribio na hivyo kutokuwa na athari za kiafya zilizotishia usalama wa washiriki katika majaribio ya dawa.

    Majaribio mawili (2) ya dawa yalisimamishwa baada ya kubainika kuwa yanakiuka matakwa ya sheria. Watoa huduma za afya 21 walipewa mafunzo kuhusu utoaji wa taarifa zitokanazo na madhara ya matumizi ya dawa.

    2.6.6 Ufuatiliaji wa dawa katika Soko

    Kazi ya kufuatilia usalama na ubora wa dawa kwenye soko ilifanyika kulingana na mpango ulioidhinishwa wa ufuatiliaji wa bidhaa na ukusanyaji wa sampuli (Post Marketing Survailance). Hata hivyo, ufuatiliaji wa dharura na uchukuaji wa sampuli ambao haukuwepo kwenye mpango ulifanyika pia pale ilipohitajika.

    Aidha, Mamlaka ilishiriki kwenye mafunzo ya ukaguzi wa viwanda yaliyoendeshwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) nchini Kenya, mafunzo ya mawasiliano na utoaji wa taarifa kuhusu dawa duni na bandia pamoja na mafunzo ya utambuzi na uchukuaji vielelezo wakati wa kukamata dawa bandia.

    Jumla ya sampuli 570 zilikusanywa zikiwemo sampuli za dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs), dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria, dawa za Kifua Kikuu, viuavijasumu aina ya “Cloxacillin” pamoja na dawa ya Sindano aina ya ‘Chloramphenicol’ inayotengenezwa na kiwanda cha LincolnPharmaceuticalsLtd. kilichopo nchini India.

    Dawa ya ‘Chloramphenicol’ haikuwepo kwenye mpango ila ilifuatiliwa baada ya kupata taarifa kuwa dawa hiyo husababisha vifo miongoni mwa watumiaji. Sampuli zote za dawa zilifanyiwa uchunguzi na majibu/matokeo yake yameainishwa kwenye jedwali Na. 9.

    Jedwali Na. 9: Sampuli za dawa zilizokusanywa na kufanyiwa uchunguzi Na. Mpango kazi Aina ya dawa Maelezo1. Mpango wa

    kufuatilia ubora wa dawa katika soko 2011 - 2013

    Cloxacillin,SP’s&Sulphamethoxazole/Trimethoprime

    Uchunguzi hakiki (confirmatory test) wa jumla ya sampuli 66 (dawa za malaria jamii ya SP- 34, dawa zenye mchanganyiko wa Trimethoprim+Sulphamethoxazole- 11 na dawa zenye kiambato cha Cloxacillin zilionesha - 21 kati ya 154 (40/54/60) zilizokusanywa. Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa dawa za jamii ya Cloxacillin kupungua kiwango cha kiambata hai kabla ya muda wake matumizi kumalizika, hivyo kusababisha Mamlaka kufuta usajili wa dawa hizo.

    2. PMS phase IV&V Dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV’s), Dawa za mifugo, DuocotexinErythromycin&Azithromycin.

    Uchunguzi hakiki wa jumla ya sampuli 30 (7Erythromycin,4Azithromycin,2Duo-cotexin, 11 ARVs na 6 Dawa za mifugo) ulifanywa kati ya sampuli 280 (85Erythromycin,43Azithromycin,24Duo-cotexin,72ARVs na 56 Dawa za mifugo) zilizokusanywa. Sampuli zote zilifaulu na kukidhi viwango vya ubora

  • 14

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Na. Mpango kazi Aina ya dawa Maelezo3. PMS phase VI &

    VIIParacetamol,ARVs na dawa zenye mchanganyiko wa viambata vya Ampicillin+Cloxacllin.

    Jumla ya sampuli 120 (32 dawa zenye mchanganyiko wa Ampicillin + Cloxacllin, 48 Paracetamol na 40 ARVs) zilikusanywa na kufanyiwa uchunguzi wa awali ambapo sampuli zote zilifaulu na kukidhi viwango vya ubora.

    4. - Dawa ya sindano ya Chloramphenicol

    Sampuli zilikusanywa katika miji ya Mwanza na Moshi, Wilaya za Kyela, na Igunga, pamoja na Bohari ya Dawa Dar es Salaam baada ya kuhisiwa kusababisha madhara kwa watumiaji na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara. Sampuli zote zilifaulu. Hata hivyo, kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo Mamlaka ilisimamisha uingizaji, usambazaji na matumizi ya dawa hii kwa ajili ya ufuatiliaji na uchunguzi zaidi wa kimaabara kubaini kiwango cha uchafuzi (impurity levels).

    5. - ThermotolerantNewcastleDiseaseVaccineStrainI-2 iliyotengenezwa na TVI

    Sampuli zilikusanywa na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara baada ya kuhisiwa kuwa bandia. Uchunguzi ulionesha chanjo hiyo kutokuwa na kiambato hai. Mamlaka ilisimamisha utengenezaji na usambazaji wa chanjo hiyo na kutoa taarifa kwa umma.

    6. - Dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria, Kifua Kikuu na za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI

    Sampuli 358 (145 za kutibu Malaria, 61 Kifua Kikuu na 152 za kufubaza virusi vya UKIMWI) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia (GF) zilikusanywa kutoka mikoa mitano (5) ya Geita, Iringa, Manyara, Pwani na Singida na kufanyiwa uchunguzi wa awali (Screening). Uchunguzi hakiki (confirmatorytest) bado unaendelea na majibu yatatolewa ndani ya robo ya kwanza ya 2014/15.

    Aidha, Mamlaka ilikusanya sampuli 476 za vifaa tiba kwa ajili ya kuthibitisha ubora wake ambapo kati yake 40 ni za kupima virusi vya UKIMWI, 20 kupima vimelea vya malaria, 280 nyuzi za kushona baada ya upasuaji na 136 ni givingsets. Matokeo ya uchunguzi yalionesha kwamba sampuli zote zilifaulu na kukidhi viwango vya ubora. Vilevile, taarifa 276 za vifaa tiba vilivyoko sokoni zilikusanywa na baada ya kuhakikiwa ziliingizwa kwenye benki ya takwimu.

    Vilevile, operesheni maalum iliyoitwa “GIBOIA” ilifanyika nchi nzima kwa ajili ya kubaini dawa duni na bandia katika soko. Dawa mbalimbali 273 zenye thamani ya takriban TZS 49,000,000/= zisizoruhusiwa na TFDA zilipatikana na kuzuiwa matumizi yake. Sababu za kuzuiwa dawa hizi ni kutokana na kuhisiwa kuwa duni au bandia, kuisha muda wa matumizi, kutosajiliwa au usajili wake kuwa umefutwa pamoja na dawa za Serikali zenye nembo ya MSD.

    2.7 Maadhimisho ya Wiki ya Chakula SalamaMaadhimisho ya Wiki ya Chakula Salama yaliyosimamiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yalifanyika nchini mnamo tarehe 18 - 22 Desemba, 2013. Maadhimisho yalihusisha Wizara, Taasisi za Serikali na Sekta binafsi ambazo ni wadau katika masuala ya usalama wa chakula.

    Lengo la maadhimisho haya yaliyobeba kauli mbiu “Chakula Salama kwa Afya ya Jamii na Uchumi wa Taifa Letu” ni kuhamasisha na kuelimisha wadau mbalimbali juu ya umuhimu wa chakula salama katika kulinda afya ya jamii na kukuza uchumi wa taifa. Shughuli mbalimbali zilifanyika wakati wa maadhisho kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kupitia vipeperushi, makala katika magazeti, vipindi vya redio na runinga.

    Aidha, wananchi walipata fursa ya kutembelea maonesho yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuuliza maswali pamoja na kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalam juu ya masuala ya usalama wa chakula.

  • 15

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    Maadhamisho haya yamekuwa na mchango mkubwa katika kufikisha ujumbe wa kuhamasisha jamii kutambua na kutumia chakula salama na faida zake kiafya na kiuchumi.

    Mamlaka iliratibu na kushiriki katika warsha ya wadau wa usalama wa chakula iliyohusisha wadau kutoka katika Taasisi, Idara na Wizara zenye mchango katika usalama wa chakula. Warsha hiyo iliratibiwa kwa ushirikiano kati ya TFDA na Mpango wa EDES kwa lengo la kuainisha vipaumbele na mikakati mbalimbali ya kuboresha mfumo wa usalama wa chakula nchini.

    2.8 Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Chakula Salama

    Rasimu ya mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Chakula Salama iliandaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zinazofuata za uandaaji na uidhinishwaji wa Sera. Mkakati huo ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa matamko ya Sera ili kuweza kufikia malengo yaliyoainishwa kwa muda uliokusudiwa. Mkakati ulijadiliwa na wadau ikiwa ni uzingatiaji wa taratibu za uandaaji wa Sera.

    2.9 Mpango wa Maduka ya Dawa Muhimu Ukaguzi wa maduka 31 ya dawa za mifugo yaliyopo katika mkoa wa Dar es Salaam na 15 yaliyopo mkoa wa Ruvuma ulifanyika kwa ajili ya kuyatambua ili hatimaye baada ya kukidhi vigezo yasajiliwe kama Maduka ya Dawa Muhimu za Mifugo. Jumla ya maduka ya mifugo manne (4) yaliyopo katika mkoa wa Dar es Salaam yalipandishwa hadhi na kuwa Maduka ya Dawa Muhimu baada ya kukidhi vigezo. Maduka mengine 27 (Dar es Salaam) na 15 Ruvuma yalielekezwa kufanya marekebisho ili kukidhi vigezo vya Duka la Dawa Muhimu la Mifugo.

    2.10 Uboreshaji wa Huduma za Maabara 2.10.1 Ukarabati na ugezi wa vifaa vya uchunguzi

    Vifaa 34 vilifanyiwa ugezi na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati vifaa saba (7) aina ya Thermohygrometer na Tachometer moja (1) vilifanyiwa ugezi katika Maabara ya Archemedesiliyoko Afrika ya Kusini. Aidha, maabara ilipokea vifaa vifuatavyo:-

    i. Mashine mbili (2) aina ya PCR, moja kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na nyingine ilinunuliwa na Mamlaka. Mashine hizi bado hazijafungwa na kukabidhiwa;

    ii. HighPerformanceLiquidChromatography(HPLC) aina ya ‘Waters’;

    iii. HighPerformanceLiquidChromatographycolumn tano (5);

    iv. Mashine ya kusafisha hewa (Fumehood); na

    v. Mashine ya kuosha vyombo vya maabara (Glassware washer).

    2.10.2 Kushikilia Ithibati na Kutambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)

    Maabara mbili za uchunguzi wa chakula za Maikrobailojia na Kemia zilikaguliwa na wataalamu wa mashirika ya Ithibati ya SADCAS/SANAS ya Afrika Kusini tarehe 25 - 26 Julai 2013. Ukaguzi huu ulikuwa ni kwa ajili ya kupanua wigo wa ithibati kwa njia za uchunguzi wa CalciumnaManganese katika maji na Totalplatecount na vimelea vya Salmonella katika samaki. Maabara hizi zimeendelea kushikilia cheti cha ithibati baada ya kukidhi vigezo.

    Aidha, Maabara ya uchunguzi wa Dawa na Vipodozi ilikaguliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) tarehe 28 - 29 Januari, 2014. Upungufu uliobainishwa ulifanyiwa kazi na kuridhiwa na wakaguzi, hivyo Maabara kuendelea kushikilia cheti cha kutambuliwa na WHO kwa miaka mingine mitatu (3) kuanzia Januari, 2014.

  • 16

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    2.10.3 Upimaji wa Umahiri katika Uchunguzi wa Sampuli (Proficiency Testing Scheme)

    Maabara ilishiriki katika majaribio 22 ya kupima umahiri wa wachunguzi (Proficiency Testing-PT). Kwa wastani matokeo yalikuwa mazuri (Z score < 2).

    2.11 Uteketezaji wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na usalama

    Katika mwaka 2013/14, jumla ya bidhaa za chakula, dawa na vipodozi zenye uzito wa tani 313.4 na thamani ya takriban TZS 961,883,633 zilikamatwa baada ya kubainika kutokidhi viwango vya ubora na usalama na hivyo kuteketezwa kwa kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

    Mchanganuo wa bidhaa husika kwa uzito na thamani ni kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali Na. 10 hapa chini.

    Jedwali Na. 10: Mchanganuo wa bidhaa zilizoteketezwa na thamani yake kwa TZS

    Na Aina ya Bidhaa Uzito (Tani) Thamani (TZS)1. Vyakula 69.6 148,798,941

    2. Dawa 189.9 459,474,518

    3. Vipodozi 53.8 353,610,174

    Jumla 313.4 961,883,633

    2.12 Sheria, Kanuni na MiongozoKanuni tano (5) ziliandaliwa chini ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura 219. Kanuni hizo zinaweka masharti ya usajili wa dawa; usafirishaji dawa nje na uingizaji wake hapa nchini; majengo na makundi ya dawa; udhibiti wa vifaa tiba na uondoaji wa dawa zisizofaa katika soko.

    Kesi 77 zilifunguliwa kwa kukiuka Sheria tajwa. Aidha, kesi tatu (3) za madai zilizofunguliwa dhidi ya TFDA katika Mahakama Kuu zimeendelea kusimamiwa. Vilevile, Mamlaka imeendelea na usimamiazi wa karibu wa kesi zote za jinai ambazo zinakiuka sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini. Kesi hizo zipo katika mikoa mbalimbali.

  • 17

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    3.0 Kuimarisha utoaji elimu kwa umma na shughuli za kutangaza huduma za Mamlaka

    Elimu kwa umma imeendelea kutolewa kwa jamii pamoja na kuitangaza Mamlaka kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na uandaaji wa programu na matangazo mafupi ya radio na televisheni, uandaaji na usambazaji wa machapisho yenye ujumbe mbalimbali kuhusu huduma za TFDA kama ilivyoainishwa katika Jedwali Na. 11.

    Jedwali Na. 11: Njia zilizotumika kutoa elimu na kurusha matangazo ya TFDA Na Njia ya uelimishaji na kuitangaza TFDA Idadi

    1 Vipindi vya radio 182 Vipindi vya TV 103 Taarifa kwa umma 144 Matangazo 335 Matangazo mafupi ya Radio na TV 66 Mikutano na waandishi wa habari 97 Habari fupi 118 Mabango 69 Vitabu vya kumbukumbu (Diaries) na kalenda za 2014 4,38010 Kitabu cha Miaka 10 ya TFDA 50011 Vipeperushi 15,000

    Vilevile, Mamlaka iliendesha mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari 94 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhusu wajibu wao katika utekelezaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 hususan katika udhibiti wa matangazo ya bidhaa.

  • 18

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Pia ulifanyika mkutano wa wazi (outreach campaign) kuhusu madhara ya matumizi ya vipodozi vyenye viambato sumu vilivyopigwa marufuku. Mkutano huu ulifanyika eneo la kituo cha forodha cha Tunduma kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuepuka kuvitumia vipodozi hivyo ili kulinda afya zao.

    Mamlaka ilishiriki kwenye maonesho mbalimbali saba (7) ambapo elimu kuhusu shughuli za udhibiti ilitolewa kwa washiriki ikiwa ni pamoja na ufafanuzi wa moja kwa moja wa maswali kutoka kwa wadau. Hii ni pamoja na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) na Wiki ya Chakula Salama. Maonesho mengine ni pamoja na yale ya Juakali/Nguvukazi yaliyoratibiwa na kujumuisha wajasiriamali kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na yale yaliyoratibiwa na Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) na Baraza la Famasi. Kupitia maonyesho hayo, wadau wengi wamepata kuifahamu TFDA na huduma zake na mategemeo ni kutoa ushirikiano katika kutekeleza matakwa ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219.

    Katika mwaka 2013/14, TFDA ilihudumia wateja 31,750 kupitia dawati la huduma kwa wateja na wengine 3,124 kupitia Maktaba. Sambamba na hilo, hoja 17 za wateja ikiwa ni pamoja na malalamiko, taarifa, maombi na mapendekezo ya kuboresha huduma zilipokelewa na kufanyiwa kazi ambapo 15 kati yake zimekamilika na wahusika kupewa mrejesho.

  • 19

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    4.0 Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za Mamlaka

    4.1 Usimamizi wa Mapato Mamlaka ilikusanya jumla ya TZS 17,911,067,896 kutoka vyanzo mbalimbali vilivyoainishwa katika Mpango Kazi na Bajeti ya mwaka 2013/14. Kiasi hiki ni sawa na 118% ya makadirio ya makusanyo ya TZS 15,224,495,434. Kati ya fedha hizo, TZS 15,054,913,000 ni kutokana na vyanzo vya ndani sawa na 127% ya lengo la makusanyo kwa mwaka na hii ni sawa na ongezeko la 33% ikilinganishwa na kiasi cha TZS 11,327,961,785 kilichokusanywa kutokana na vyanzo vya ndani kwa mwaka 2012/13.

    Jedwali Na. 12 linaonesha mchanganuo wa makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2013/14.

    Jedwali Na. 12: Mapato katika kipindi cha Julai 2013-Juni 2014Na. VYANZO VYA MAPATO BAJETI KIASI

    KILICHOKUSANYWA% MAELEZO

    1 Vyanzo vya ndani (ada na tozo)

    11,948,076,405.0 15,054,913,000.72 127 Kuimarika kwa shughuli za udhibiti

    2 Serikali Kuu- Fedha za matumizi ya kawaida

    800,000,000.00 221,591,500.00 27 Makadirio yalikuwa juu

    3 Serikali Kuu - mishahara 2,376,379,029.00 2,375,363,404.00 100 Makusanyo yalikwenda vizuri

    4 Serikali Kuu-Maendeleo (HSPS –PMS)

    100,040,000.00 75,000,000.00 75 Kiasi pungufu kilipokelewa

    5 Washirika wa maendeleo - 90,722,035.00 -JUMLA KUU 15,224,495,434 17,911,067,896.72 118

    4.2 MatumiziKatika kipindi hiki, jumla ya TZS 14,700,071,722 zilitumika kwa kazi mbalimbali zilizokuwa zimepangwa ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji. Aidha, kiasi cha TZS 271,421,155 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kilitumika kuendeleza kazi zilizokuwa za mwaka 2012/13.

    4.3 Ukaguzi wa Hesabu na Rasilimali Katika mwaka 2013/14, hesabu za Mamlaka kwa kipindi kinachoishia Juni 2013 zilikaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na Mamlaka kupata hati safi za utunzaji wa hesabu na rasilimali. Huu ni mwaka wa 10 mfululizo kwa TFDA kupata hati safi kutoka kwa CAG na nakala ya taarifa yake imeambatishwa. Aidha, hesabu za kipindi cha 2013/14 zimeandaliwa na kuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya ukaguzi.

    4.4 Rasilimali Watu

    4.4.1 Ajira

    Jumla ya watumishi wapya 25 kati ya 26 wa ajira ya kudumu na malipo ya pensheni waliajiriwa na Mamlaka. Vilevile, jumla ya watumishi 13 waliajiriwa kwa mikataba ya muda mfupi ili kuongeza nguvu kazi katika idara zenye upungufu wa watumishi.

    4.4.2 Tathmini ya kazi, Mapitio ya ngazi za Mishahara na Miundo ya Utumishi (Job Evaluation, Salary Grading Review and Scheme of Service)

    Rasimu ya Mwisho ya kazi ya Mapitio ya Tathmini ya Kazi, Ngazi za Mishahara, na Miundo ya Utumishi iliandaliwa na kukamilika. Rasimu husika inasubiri kujadiliwa na Baraza la Wafanyakazi kabla ya kuwasilishwa MAB na baadaye kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa idhini.

  • 20

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    4.4.3 Ushughulikiaji wa masuala ya kiutumishi, Maadili na Nidhamu

    Watumishi 13 walipandishwa vyeo katika mwaka wa fedha 2013/14. Aidha, watumishi hao waliingizwa katika mfumo wa kiutumishi (Lawson) na kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili kuboresha taarifa za TFDA.

    Mamlaka iliandaa ikama ya mishahara kwa mwaka wa fedha 2014/15. Katika ikama hiyo jumla ya watumishi wanaotarajiwa kuajiriwa ni 15 na watumishi 14 walipendekezwa kupandishwa cheo. Mapendekezo haya yaliingizwa katika mfumo wa Lawson kwa ajili ya idhini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2014 bado kibali cha ajira kilikuwa hakijatolewa.

    Katika mwaka 2013/14 Kamati ya Maadili ilifanya kikao kimoja kwa ajili ya ushughulikiaji masuala ya maadili kwa baadhi ya watumishi waliobainika kukiuka maadili ya utumishi wa umma. Vile vile, mtumishi mmoja aliachishwa kazi kutokana na kukiuka taratibu za kazi.

    4.4.5 Mafunzo, mikutano na warsha

    Utekelezaji wa Mpango wa Mafunzo

    Mpango wa Mafunzo wa Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2013/14 ulitekelezwa ambapo jumla ya watumishi 65 walipangwa kuhudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi ambapo kati yao watumishi 61 walihudhuria na kufanya utekelezaji kuwa sawa na 94%.

    Mchanganuo wa utekelezaji wa Mpango wa Mafunzo ni kama ilivyoainishwa katika jedwali Na. 13 hapa chini:-

    Jedwali Na.13: Watumishi waliohudhuria mafunzo katika mwaka wa fedha 2013/14

    Aina ya mafunzo Muda mrefu Muda mfupi Jumla

    Kurugenzi Ndani Nje Ndani Nje

    Ofisi ya DG 2 1 2 6 11

    DLS 4 1 0 4 9

    DFS 2 3 0 3 8

    DMC 0 1 5 8 14

    DBS 2 0 6 11 19

    Jumla 10 6 13 32 61

    4.5 Uhakiki Mifumo Mfumo wa utoaji na ufuatiliaji wa vibali vya kuingiza na kutoa bidhaa nchini ulifanyiwa mapitio ambapo mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia vibali umeandaliwa na upo katika hatua za majaribio. Vilevile, mafunzo ya kuhamasisha wafanyakazi juu ya utekelezaji wa mfumo wa kuhakiki ubora wa huduma (QMS) yalitolewa na wakufunzi kutoka Shirika la Viwango la Kenya (KEBS).

    Aidha, nyaraka mbalimbali zilifanyiwa mapitio kwa lengo la kuboresha shuguli za utoaji huduma. Hizi ni pamoja na Mwongozo wa usajili wa dawa za tiba asili, Miongozo ya usajili wa chakula na dawa, taratibu sanifu (SOPs) na michakato tisa (9) kutoka Idara mbalimbali.

  • 21

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    4.6 Mifumo ya taarifa Mamlaka ilifanya maboresho katika mifumo ya taarifa (MIS) ambapo mfumo mpya (Intergrated Management Information Systerm-IMIS) ulianza kutumika rasmi tarehe 07/04/2014. Mfumo huu mpya wa taarifa umetengenezwa kwa teknolojia inayoruhusu kupatikana popote penye mtandao (internet) ikiwa ni pamoja na Ofisi za Kanda. Kwa kuanzia, Kanda ya Kaskazini imeanza kutumia mfumo mpya wa kutoa vibali vya majengo na pia vya kuingiza/kutoa bidhaa nchini.

    Mfumo huu ambao umeboresha usalama wa kanzidata na unatunza kumbukumbu ya miamala inayofanywa na watumiaji mbalimbali kwa kuchukua majina na taarifa za kompyuta zinazotumika, utasaidia kurahisisha utoaji huduma za TFDA kwa wadau na hivyo kufikia viwango vya Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa 2012. Vilevile, katika kuboresha ulinzi wa mali za TFDA na wadau wake, Mamlaka imefunga “CCTV cameras” na kudhibiti uingiaji hovyo katika vyumba vya ofisi (access door control system).

    5.0 Uwianisho wa Taratibu za Udhibiti wa bidhaa

    5.1 Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)Katika kipindi cha mwaka 2013/14, kamati tatu (3) kati ya tano (5) za kitaalamu zilizoundwa chini ya Mradi wa Uwianishaji wa Taratibu za Udhibiti wa Dawa zilikamilisha miongozo, taratibu sanifu za utendaji kazi na viwango vya tathmini na usajili, ukaguzi wa viwanda vya dawa na uhakiki ubora wa mifumo baada ya kupitiwa na wadau mbalimbali katika ngazi za kitaifa na kikanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nyaraka zote hizi ziliidhinishwa na kikao cha kisekta cha Baraza la Mawaziri wa Afya kilichofanyika Zanzibar tarehe 17 Aprili, 2014.

    Aidha, katika mwaka 2013/14, Mamlaka imeshiriki katika mafunzo mbalimbali na tathmini ya pamoja na Shirika la Afya Duniani kwa dawa tano (5) zilizoombewa usajili kwenye nchi zote za EAC. Malengo ya mafunzo na tathmini ya pamoja ni kuendelea kujenga uwezo wa wataalam kwenye maeneo ya tathmini, ukaguzi wa viwanda vya dawa na uhakiki ubora wa mifumo na kuharakisha usajili wa dawa kwenye nchi wanachama wa Jumuiya baada ya tathmini ya pamoja kukamilika.

    Vilevile, Mamlaka ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya na Tiba (MUHAS) Shule ya Famasi iliandaa andiko kwenda taasisi ya kimataifa ya ‘New Patnership for Africa’s Development (NEPAD)’ ili kuanzisha Kituo cha Kikanda cha Tathmini na Usajili wa dawa (Regional Centre of Regulatory Excellence in Medicines Evaluation and Registration - RCORE) kitakachotoa mafunzo kwa wataalam wa tathmini za dawa barani Afrika ambapo tarehe 6 Mei, 2014 kituo hiki kiliteuliwa rasmi kuendesha mafunzo hayo.

    Katika kipindi hiki pia, tathmini ya mradi ilifanyika ili kuangalia maendeleo yake na kubaini changamoto mbalimbali zinazoathiri utekelezaji wake na kuzitafutia ufumbuzi. Katika tathmini hii iliyoongozwa na wataalam kutoka ‘WHO’ na Benki ya Dunia, mradi ulipata alama ya kuridhisha kuhusu maendeleo na kupendekezwa kuendelea na hatua ya pili (Second Phase).

    5.2 Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)Katika kipindi cha mwaka 2013/14, kikao cha Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afya na UKIMWI kwa nchi wanachama wa SADC kilichofanyika tarehe 7 Novemba, 2013 Lilongwe Malawi, kilipitisha pendekezo la kufanya kazi ya maboresho ya miongozo ya usajili wa dawa iliyokuwepo na kuiweka sanjari na miongozo inayotumika sehemu nyingine duniani kwa sasa. Azimio hili lililenga kuifanya miongozo hii kuwa kiwacho cha nchi za ICH, pamoja na miongozo ya Shirika la Afya Duniani. Vilevile miongozo hiyo ilitakiwa iwekwe katika mfumo wa CTD.

    Katika kipindi hiki Mamlaka ilishiriki katika kikao cha kwanza cha kuboresha miongozo ya usajili wa dawa uliofanyika Gaborone Botswana. Katika kikao hicho rasimu za miongozo mbalimbali ziliandaliwa. Hizi ni pamoja na muundo wa mwongozo wa CTD kwa nchi za SADC, mwongozo wa namna ya kuandaa maombi ya usajili katika mfumo wa CTD, mwongozo wa kuwasilisha taarifa za ubora wa dawa, mwongozo wa kuwasilisha taarifa za ulinganifu hai kwa dawa pamoja na mwongozo wa kuwasilisha taarifa za uthabiti wa dawa (Stability studies).

  • 22

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Mamlaka ilishiriki katika kikao cha Wakuu wa Taasisi za Udhibiti wa Dawa kutoka nchi za SADC cha kujadili na kuboresha andiko la pendekezo la Mradi wa Uwianisho wa Taratibu za udhibiti wa dawa kwa nchi husika. Rasimu ya andiko la mradi huo iliandaliwa tayari kwa kuboreshwa na kuwasilishwa kwa ajili ya idhini katika ngazi za juu. Aidha, ndani ya kipindi hicho, Mamlaka ilishiriki katika kazi ya tathmini ya pamoja ya maombi ya usajili wa dawa ya kutibu Malaria ya Coartem 80/480 mg ya kampuni ya Novartis ambayo ilikuwa imewasilisha maombi hayo kwa nchi za Jumuiya wanachama wa SADC. Kazi hii ilifanywa na maafisa wa tathmini wa dawa kutoka katika nchi zote za SADC.

    6.0 Changamoto na Mbinu za kuzikabili

    6.1 ChangamotoMamlaka imeendelea kukabiliwa na changamoto zifuatazo:-

    (a) Uwezo mdogo wa kutathmini maombi ya usajili wa bidhaa;

    (b) Viwanda vya ndani vya dawa na machinjio kutokidhi matakwa ya sheria;

    (c) Halmashauri nyingi kutokukusanya na kuwasilisha mapato ya TFDA.

    6.2 Mbinu za Kupambana na ChangamotoHatua zifuatazo zimeendelea kuchukuliwa katika kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utendaji:-

    (a) Kuendelea kuwatumia watathmini wa nje ya Mamlaka ikiwa ni pamoja na kuendelea na kufanya tathmini ya bidhaa kwa njia ya “retreat”;

    (b) Kuwa na mikutano ya pamoja na kuweka makubaliano kati ya wamiliki wa viwanda na machinjio ili kukidhi matakwa ya sheria; na

    (c) Kuendelea kuhamasisha Halmashauri kuzingatia matakwa ya sheria na makubaliano yaliyofikiwa.

    7.0 HitimishoKatika kipindi cha mwaka 2013/14, viashiria vya tathmini vinaonesha kuwapo ufanisi katika udhibiti wa ubora na usalama wa bidhaa. Aidha, kulikuwa na makosa machache ya uvunjaji wa sheria ikilinganishwa na mwaka 2012/13. Hiki ni kiashiria kuwa kuna ongezeko la uelewa wa wadau na wananchi kwa ujumla juu ya matakwa ya Sheria Chakula, Dawa na Vipodozi,Sura 219.

    Vilevile, kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu wa sampuli za bidhaa kupitia chunguzi za kimaabara kikilinganishwa na kiwango cha mwaka 2012/13, kunaashiria kuwepo na ubora wa bidhaa katika soko.

    Mamlaka itaendelea kushirikiana na wadau ikiwa ni pamoja na Halmashauri ili kuendelea kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa lengo la kulinda afya ya jamii.

  • 23

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    INDEPENDENT AUDITORS’ REPORT ON THE FINANCIAL STATEMENTS

    To: Ambassador Dr. Ben Moses, Chairman of the Ministerial Advisory Board, Tanzania Food and Drugs Authority, P. O. Box 11750, Dar es Salaam.

    RE: REPORT OF THE CONTROLLER AND AUDITOR GENERAL ON THE FINANCIAL STATEMENTS OF TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY FOR THE YEAR ENDED 30TH JUNE, 2014.

    Introduction

    I have audited the accompanying financial statements of Tanzania Food and Drugs Authority which comprise the Statement of Financial Position as at 30th June, 2014, Statement of Comprehensive Income, Statement of Changes in Equity and Statement of Cash Flows for the year then ended, and a Summary of Significant Accounting Policies and other Explanatory Notes set out on pages 16 to 33 of this report.

    Ministerial Advisory Boards’ Responsibility for the financial statements

    The Ministerial Advisory Board of Tanzania Food and Drugs Authority is responsible for the preparation and fair presentation of these financial statements in accordance with International Financial Reporting Standards. This responsibility includes designing, implementing and maintaining internal control relevant to the preparation and fair presentation of financial statements that are free from material misstatement, whether due to fraud or error, selecting and applying appropriate accounting policies and making accounting estimates that are reasonable in the circumstances.

    Responsibility of the Controller and Auditor General

    My responsibility as auditor is to express an independent opinion on the financial statements based on the audit. The audit was conducted in accordance with International Standards on Auditing (ISA) and such other audit procedures I considered necessary in the circumstances. These standards require that I comply with ethical requirements and plan and perform the audit to obtain reasonable assurance about whether the financial statements are free from material misstatement.

    An audit involves performing procedures to obtain audit evidence about the amounts and disclosures in the financial statements. The procedures selected depend on the auditor’s judgment, including the assessment of the risks of material misstatement of the financial statements, whether due to fraud or error. In making those risk assessments, I considered the internal controls relevant to the Authority’s preparation and fair presentation of the financial statements in order to design audit procedures that are appropriate in the circumstances, but not for the purpose of expressing an opinion on the effectiveness of the Authority’s internal control. An audit also includes evaluating the appropriateness of accounting policies used and the reasonableness of accounting estimates made by management, as well as evaluating the overall presentation of the financial statements.

    In addition, Sect. 10 (2) of the PAA No. 11 of 2008 requires me to satisfy myself that the accounts have been prepared in accordance with the appropriate accounting standards and that; reasonable precautions have been taken to safeguard the collection of revenue, receipt, custody, disposal, issue and proper use of public property, and that the law, directions and instructions applicable thereto have been dully observed and expenditures of public monies have been properly authorized.

  • 24

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Furthermore, Sect. 48 (3) of the Public Procurement Act No. 7 of 2011 and the Public Procurement (Goods, Works, Non-consultant services and Disposal of Public Assets by Tender) Regulations of 2013 requires me to state in my annual audit report whether or not the auditee has complied with the provisions of the Law and its Regulations.

    I believe that the audit evidence I have obtained is sufficient and appropriate to provide a basis for my audit opinion.

    Unqualified Opinion

    In my opinion, the financial statements present fairly, in all material respects, the financial position of Tanzania Food and Drugs Authority as at 30th June, 2014, and its financial performance and its cash flows for the year then ended in accordance with International Public Sector Accounting Standards and comply with Tanzania Food, Drugs and Cosmetics Act Cap 219.

    Report on other Legal and Regulatory Requirements

    Compliance with Public Procurement Act

    In view of my responsibility on the procurement legislation, and taking into consideration the procurement transactions and processes I have reviewed as part of this audit, I state that Tanzania Food and Drugs Authority has procurement processes have generally complied with the Public Procurement Act No. 7 of 2011 and its related Regulations of 2013.

    Francis MwakapalilaAg. CONTROLLER AND AUDITOR GENERAL

    National Audit Office,Dar es Salaam. 13th February, 2014

  • 25

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    STATEMENT OF FINANCIAL POSITION AS AT 30TH JUNE, 2014

    2014 2013

    Note TZS TZS

    NON CURRENT ASSETS

    Property, Plant and Equipment 2 3,273,244,232 2,865,262,909

    CURRENT ASSETS

    Inventories 3 197,111,167 0

    Accounts Receivable 4 455,570,666 910,715,810

    Cash and Cash equivalent 5 9,122,331,217 7,121,799,783

    Total Current Assets 9,775,013,050 8,032,515,593

    Total Assets 13,048,257,282 10,897,778,502

    EQUITY AND LIABILITIES

    Equity

    Capital 1,139,932,800 1,139,932,800

    Retained Surplus 11,771,289,406 9,570,348,232

    12,911,222,206 10,710,281,032

    Current Liabilities

    Accounts payable 6 137,035,076 187,497,470

    Total Equity and Liabilities 13,048,257,282 10,897,778,502 Note 1 to 15 form part of the Accounts

    ______________________ ____________________Chairperson of the Board Director General

    Date 13-02-2015 Date 13-02-2015

  • 26

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    STATEMENT OF FINANCIAL PERFORMANCE FOR THE YEAR ENDED 30TH JUNE, 2014

    2014 2013 Note TZS TZS

    REVENUE

    Fees and Licenses 7 17,946,970,127 11,324,224,148

    Government Grants 8 2,331,783,046 3,087,096,757

    Donors Grants 9 216,818,170 790,485,346

    Revenue from exchange transactions 0 148,552,354

    Other income 10 205,140,094 45,240,219

    Sub Total 20,700,711,437 15,395,598,824

    Prior year adjustment 14 22,593,148,374 -

    TOTAL REVENUE 43,293,859,811 15,395,598,824

    EXPENSES

    Administrative expenses 11 40,254,567,759 13,361,588,644

    Finance costs 12 27,392,779 136,920,800

    Audit fee expenses 51,855,000 -

    Depreciation & amortization 2 668,381,064 640,581,578

    Total Expenses 41,002,196,602 14,139,091,022

    Surplus for the year 2,291,663,209 1,256,507,802

    Surplus/(Deficit) B/F 9,570,348,232 8,313,840,430

    Pre year Adjustment (90,722,035) -

    Accumulated Surplus C/F 11,771,289,406 9,570,348,232

    Note 1 to 15 form part of the Accounts

    ______________________ ____________________Chairperson of the Board Director General

    Date 13-02-2015 Date 13-02-2015

  • 27

    MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA - TFDA

    STATEMENT OF CASH FLOWS FOR THE YEAR ENDED 30TH JUNE, 2014

    2014 2013TZS TZS

    Surplus/(deficit) 2,291,663,209 1,256,507,802

    Add: Non Cash expenses

    Depreciation Expenses 668,381,064 640,581,578

    Adjustment of Machines 16,200,000 0

    2,976,244,273 1,897,089,380

    CHANGE IN WORKING CAPITAL

    (Increase)/Decrease in Receivables 455,145,144

    (Increase)/decrease in inventories (197,111,167) 143,901,758

    Increase/(decrease in payables) (50,462,394) (708,596,684)

    Net cash flow from operating activities 3,183,815,856 1,332,394,454

    INVESTMENT ACTIVITIES

    Proceeds from sale of assets - -

    Purchase of fixed assets (1,092,562,387) (498,445,375)

    Net cash used in investing activities (1,092,562,387) (498,445,375)

    FINANCING ACTIVITIES

    Capital grants (90,722,035) -

    Net cash used in financing activities (90,722,035) -

    Net cash flow for the year 2,000,531,434 833,949,079

    Add: Cash at the beginning of the year 7,121,799,783 6,287,850,704

    Net cash and cash equivalent at the end of the year 9,122,331,217 7,121,799,783

    Note 1 to 15 form part of the Accounts

    ______________________ ____________________Chairperson of the Board Director General

    Date 13-02-2015 Date 13-02-2015

  • 28

    TAARIFA YA UTENDAJI KAZI 2013/2014

    Mkurugenzi MkuuMamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

    Makao MakuuBarabara ya Mandela, External - Mabibo

    S. L. P. 77150, Dar es SalaamSimu: +255 22 2450512 / 2450751 / 2452108

    +255 658 445 222 / 685 701 735 / 777 700 002Nukushi: +255 22 2450793

    Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.tfda.or.tz

    Kanda ya Ziwa,Mtaa wa Nkurumah,S. L. P. 543, Mwanza

    Simu: +255 282 500733. Nukushi: +255 282 541484

    Barua pepe: [email protected]

    Nyanda za Juu Kusini,Jengo la Ofisi ya Mifugo (Mkoa),

    S. L. P. 6171, MbeyaSimu: +255 25 2504425.

    Nukushi: +255 25 2504425Barua pepe: [email protected]

    Kanda ya Kaskazini,Mtaa wa Sakina,

    S. L. P. 16609, ArushaSimu: +255 27 254 7097.

    Nukushi: +255 27 254 7098Barua pepe: [email protected]

    Kanda ya Mashariki,Jengo la GEPFBarabara ya Ali Hassan Mwinyi,S. L. P. 77150, Dar es SalaamSimu: +255 737 226 328 / 766 368 412Nukushi: +255 22 2450793Barua pepe: [email protected]

    Kanda ya Kusini,Jengo la Chuo cha WagangaBarabara ya Ligula,S. L. P. 1447, MtwaraSimu: +255 23 2334655Barua pepe: [email protected]

    Kanda ya Kati,Jengo la Hospitali ya Rufaa ya MkoaS. L. P. 1253, DodomaSimu: +255 26 2320156 Nukushi: +255 26 2320156Barua pepe: [email protected]

    Imechapwa Juni, 2015