tamko la tef - kufutwa kwa mawio2.pdf

2
 Tanzania Editors Forum Zanaki Street Plot No. 2285/7, Opp. CCM Office Mtendeni Branch P.O.Box 75206 Dar es Salaam, Tanzania Tel: +255 22 123236 Mob: +255 715 339090, +255 713 488269 TAMKO LA JUKWAA LA WA HARIRI TANZANIA TEF) KUHUSU KUFUTWA KWA GAZETI LA MAWIO UTANGULIZI 1. JUKWAA la Wahariri Tanzania (TE F) limeshtushwa na kusononeshwa na hatua ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye KULIFUTA katika daftari la Msajili wa Magazeti, Gazeti la Mawio. 2. TEF inaichukulia hatua hii kama aina mpya ya ukandamizaji wa uhuru vyombo vya habari nchini. Kwa serikali zilizopita, tulikuwa tukipambana na vitendo vya kufungiwa kwa magazeti kwa muda maalum, wakati adhabu kubwa iliyowahi kutolewa ilikuwa ni i le ya kufungiwa kwa muda usiojulikana kwa Gazeti la Mwanahalisi, kabla gazeti hilo kurejeshwa kwa umma na Mahakama. 3. Uamuzi wa kulifuta Mawio (hata kama lilifanya makosa) umetufikirisha sana. Tumetafakari kwa kina na kujiuliza kwamba pengine habari ambazo ziliandikwa na gazeti hili, zilikuwa hatari kwa kiasi gani kwa nchi kiasi cha kufikiwa uamuzi huo? Ni magazeti mangapi yatafuata kufutwa baada ya Mawio ikiwa serikali itaendelea na ubabe wa aina hii? 4. Ndiyo maana tunaiona hatua ya Serikali kulifuta Mawio kama aina mpya ya ukandamizaji wa uhuru wa habari ambayo imeasisiwa na Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli. Tunajiuliza ikiwa kwa miezi takriban mitatu tu tangu kuanza kazi kwa serikali mpya tayari imefuta gazeti, itakuwaje katika safari ya miaka mitano (miezi 60) ambayo atakuwa madarakani? MSIMAMO WA TEF TEF inapinga uamuzi wa serikali kulifuta Mawio kutokana na sababu zifuatazo: 1. Zipo kasoro nyingi za kimfumo z inazosababis ha uamuzi wa Serikali kutokubalika. Hii haimaanishi kwamba vyombo vya habari havifanyi makosa, la hasha; lakini hata pale vyombo hivyo vinapofanya makosa yoyote yale, taratibu za kuyashughulikia ni kinyume kabisa cha misingi ya utawala bora, haki na demokrasia. 2. Mfumo wa sasa wa kushughulikia matatizo au kasoro za kitaaluma katika vyombo vya habari ni kandamizi kwani unamfanya Waziri kuwa “Mhariri Mkuu” na ana mamlaka ya kutoa adhabu kwa kuzingatia mtizamo wake, hata kama mtizamo huo unakinzana na misingi ya taaluma.

Upload: imma

Post on 10-Mar-2016

130 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

7/21/2019 TAMKO LA TEF - KUFUTWA KWA MAWIO2.pdf

http://slidepdf.com/reader/full/tamko-la-tef-kufutwa-kwa-mawio2pdf 1/2

Tanzania Editors Forum

Zanaki Street Plot No. 2285/7, Opp. CCM Office Mtendeni BranchP.O.Box 75206 Dar es Salaam, Tanzania

Tel: +255 22 123236 Mob: +255 715 339090, +255 713 488269

TAMKO LA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA TEF)KUHUSU KUFUTWA KWA GAZETI LA MAWIO

UTANGULIZI1. JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limeshtushwa na kusononeshwa na hatua

ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Nape Nnauye KULIFUTA katika daftari la Msajili wa Magazeti, Gazeti laMawio.

2. TEF inaichukulia hatua hii kama aina mpya ya ukandamizaji wa uhuru vyombovya habari nchini. Kwa serikali zilizopita, tulikuwa tukipambana na vitendovya kufungiwa kwa magazeti kwa muda maalum, wakati adhabu kubwailiyowahi kutolewa ilikuwa ni ile ya kufungiwa kwa muda usiojulikana kwaGazeti la Mwanahalisi, kabla gazeti hilo kurejeshwa kwa umma na Mahakama.

3. Uamuzi wa kulifuta Mawio (hata kama lilifanya makosa) umetufikirisha sana.Tumetafakari kwa kina na kujiuliza kwamba pengine habari ambazoziliandikwa na gazeti hili, zilikuwa hatari kwa kiasi gani kwa nchi kiasi cha

kufikiwa uamuzi huo? Ni magazeti mangapi yatafuata kufutwa baada yaMawio ikiwa serikali itaendelea na ubabe wa aina hii?

4. Ndiyo maana tunaiona hatua ya Serikali kulifuta Mawio kama aina mpya yaukandamizaji wa uhuru wa habari ambayo imeasisiwa na Serikali ya Awamuya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli. Tunajiuliza ikiwa kwa miezitakriban mitatu tu tangu kuanza kazi kwa serikali mpya tayari imefuta gazeti,itakuwaje katika safari ya miaka mitano (miezi 60) ambayo atakuwamadarakani?

MSIMAMO WA TEF

TEF inapinga uamuzi wa serikali kulifuta Mawio kutokana na sababu zifuatazo:

1. Zipo kasoro nyingi za kimfumo zinazosababisha uamuzi wa Serikalikutokubalika. Hii haimaanishi kwamba vyombo vya habari havifanyi makosa,la hasha; lakini hata pale vyombo hivyo vinapofanya makosa yoyote yale,taratibu za kuyashughulikia ni kinyume kabisa cha misingi ya utawala bora,haki na demokrasia.

2. Mfumo wa sasa wa kushughulikia matatizo au kasoro za kitaaluma katikavyombo vya habari ni kandamizi kwani unamfanya Waziri kuwa “MhaririMkuu” na ana mamlaka ya kutoa adhabu kwa kuzingatia mtizamo wake, hatakama mtizamo huo unakinzana na misingi ya taaluma.

7/21/2019 TAMKO LA TEF - KUFUTWA KWA MAWIO2.pdf

http://slidepdf.com/reader/full/tamko-la-tef-kufutwa-kwa-mawio2pdf 2/2

3. Tunauona uamuzi wa serikali kuwa na nia mbaya kwani hata katika taarifayake kwa umma, haikuweka wazi habari ambazo zimesababisha kufutwa kwaMawio. Badala yake taarifa ya serikali inatoa kauli ya jumla kwamba wahaririwa gazeti hilo “wameonywa mara nyingi lakini wamekuwa hawabadiliki”.Hakuna anayefahamu walionywa lini wala kuhusu nini?

4. Utaratibu uliotumika kulifuta Mawio ni uleule wa matumizi ya Sheriakandamizi ya Magazeti ya 1976 ambayo takriban kwa miaka 20 imekuwaikipigiwa kelele kutokana na kumpa mtu mmoja (Waziri) mamlaka ya kuamuasuala kubwa la kuwanyima watu wengi (kwa idadi yoyote) haki ya kupatahabari. Hii ni tofauti na taaluma nyingine ambazo Serikali inaziheshimu kwakupeleka masuala husika katika vyombo vya sheria au mabaraza ya uamuzi.

5. Kwa taaluma ya habari, Serikali bado imeendelea kujipa mamlaka ya“kukamata, kushtaki, kusikiliza kesi, kuhukumu na kufunga” Maana kamailikuwa ni kesi iliyozaa hukumu ya kufutwa, basi uendeshaji wake ulifanyikakatika “mahakama ya siri”, na usiri huu matokeo yake ni hukumu ya siriambayo haikuwapa wahusuka kutoa utetezi wa kile kilichokuwa kikilalamikiwadhidi yao. Hakuna anayefahamu nani alikuwa mlalamikaji katika kesi hiyo,utetezi wa washtakiwa ni upi na chombo gani kilichopima uzito wa mashtakadhidi ya utetezi na kutoa uamuzi!.

6. Mfumo wa aina hii ni kichaka ambacho Serikali imekuwa ikikitumia kufanyakile ambacho kimeandikwa katika taarifa ya Waziri kwamba Wahariri waMawio walionywa mara kadhaa! Hivi walionywa na nani, wapi na kwasababu zipi? Kama kile kinacholalamikiwa kingekuwa kimefikishwa katika

chombo rasmi cha utoaji haki, kila kitu kingekuwa wazi kwa umma kwambamashtaka ni yapi na utetezi wa washtakiwa ni upi.

7. Mwenendo wa aina hii wa kufuta magazeti iwe ni kwa muda siyo tu kwambainaathiri dhana nzima ya utawala bora, bali inaliweka Taifa katika hatari yakutumbukia katika uovu, hasa pale wenye dhamana watakapofanyawapendavyo kwa kuwa tu vyombo vya habari vitakuwa vimezibwa midomo.

8. Kwa kuwa hii inaonekana kuwa dhamira rasmi ya Serikali kutumia sheriakandamizi kudhibiti demokrasia na uhuru wa habari, tunatoa mwito kwawatawala wetu kutafakari upya suala hili na kuachana kabisa na dhamira hiyoisiyokuwa na tija kwa nchi yetu.

IMETOLEWA NAJUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA TEF)

DAR ES SALAAM