tangazo la zabuni ya ununuzi wa kiwanja no. c/r 326/43 kijitonyama kilichoko karibu na shule ya...

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 09-Mar-2016

215 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA KIWANJA No. C/R 326/43 KIJITONYAMA KILICHOKO KARIBU NA SHULE YA MSINGI MWENGE BARABARA YA ALLY HASSAN MWINYI MKABALA NA TAASISI YA ELIMU.

TRANSCRIPT

TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA KIWANJA No. C/R 326/43 KIJITONYAMA KILICHOKO KARIBU NA SHULE YA MSINGI MWENGE BARABARA YA ALLY HASSAN MWINYI MKABALA NA TAASISI YA ELIMU.Chama cha ushirika cha Ujenziwa Nyumba Mwenge (Mwenge Housing Co-operative Society Ltd) Kinauza kiwanja chake Na. C/R 326/43 chenye mita za mraba 742.

Kutokana na kusudio hilo, Chama kinakaribisha maombi ya Zabuni ya kununua Kiwanja hicho.

MASHARTI YA ZABUNI

1. Mzabuni ahakikishe kwamba kiwango alichokitaja hakibadiliki (Fixed amount).

2. Chama cha Ushirika hakitawajibika kukubali ama kukataa bei ya juu au ya chini kama itakavyokuwa imetolewa na mzabuni.

3. Kila fomu ya zabuni inatolewa na ofisi kwa ajili ya ombi moja kwa gharama ya Tsh 100,000/= ambazo hazitarudishwa.

4. Fomu za zabuni zinapatikana katika ofisi ya Meneja wa Chama cha Ushirika wa Ujenzi wa Nyumba Mwenge makao makuu mahali lilipo duka la Afrika Sana, kwenye kona ya barabara ya Shekilango na barabaraya maghorofani iendayo kwenye ofisi ya T.R.A. (Mwenge)

5. Mwombaji zabuni aambatanishe vivuli vya usajili wa:(a) TIN No.

(b) VAT No.

6. Mzabuni anaruhusiwa kwenda kuangalia mahali kilipo kiwanja.

7. Mzabuni atakayeshinda atatakiwa kulipa malipo ya awali ya asilimia ishirini na tano (25%) ya bei ya kiwanja ndani ya siku saba(7) kuanzia tarehe ya kushinda zabuni. Atatakiwa akamilishe malipo yaliyosalia ya asilimia sabini na tano(75%) kwa mkupuo mmoja ndani ya siku ishirini na nane(28) kuanzia alipolipa malipo ya awali . Endapo mzabuni atashindwa kukamilisha malipo yaliyosalia ya asilimia sabini na tano(75%) ndani ya siku hizo ishirini na nane asilimia hamsini (50%) itakatwa kutoka malipo ya awali na atarejeshewa salio.

8. Muda wa kuchukua fomu ni kuanzia tarehe 01/02/2016 Saa2:00 asubuhi mpaka saa 9:00 alasiri, Jumatatu hadi Ijumaa. Na siku ya Jumamosi ni kuanzia saa 1: 30 Asubuhi hadi saa 7:00 mchama.Maombi ya zabuni yafungwe kwa lakiri na yawekwe kwenye sanduku la zabuni lililopo katika Ofisi ya Ushirika Mwenge ikiwa na anwani inayotaja ZABUNI YA UNUNUZI WAKIWANJA NA. C/R. 326/43 MWENGE KIJITONYAMA ikiwa na anwani ifuatayo:MENEJA,

MWENGE HOUSING CO-OPERATIVE SOCIETY LTD,

P.O.BOX 32311,

DAR ES SALAAM.Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha zabuni ni 24/02/2016 Saa 4:00 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa tarehe 24/02/2016 saa 4:30 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ushirika.Wazabuni au wawakilishi wao watakaribishwa katika kikao cha ufunguzi wa zabuni.MWENGE HOUSING CO-OPERATIVE SOCIETY LIMITED

(CHAMA CHA USHIRIKA CHA UJENZI WA NYUMBA MWENGE)

P.O. Box 32311, SIMU 2775327 DSM

Email:HYPERLINK "mailto:[email protected]"[email protected]