torati na amri ya tisa [262] -...

32
Makanisa ya Kikristo ya Mungu [262] Torati na Amri ya Tisa (Chapisho La 2.0 19981011-19990525-20120510-20120822) Imeandikwa: Usiseme uwongo. Jarida hili linaelezea muundo mzima wa Torati ya Mungu, na jinsi inavyowiana na Amri jinsi zilivyoelezewa na manabii na Maagano yatokanayo na agizo la usomaji wa Torati katika mwaka wa Sabato. Christian Churches of God PO Box 369, WODEN ACT 2606, AUSTRALIA Email: [email protected] (Hati Miliki 1998, 1999, 2012 Wade Cox) Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

Upload: doanhanh

Post on 19-Mar-2018

438 views

Category:

Documents


10 download

TRANSCRIPT

Makanisa ya Kikristo ya Mungu[262]

Torati na Amri ya Tisa (Chapisho La 2.0 19981011-19990525-20120510-20120822)

Imeandikwa: Usiseme uwongo. Jarida hili linaelezea muundo mzima wa Torati ya Mungu, na jinsi inavyowiana na Amri jinsi zilivyoelezewa na manabii na Maagano yatokanayo na agizo la usomaji wa Torati katika mwaka wa Sabato.

Christian Churches of GodPO Box 369, WODEN ACT 2606, AUSTRALIA

Email: [email protected]

(Hati Miliki 1998, 1999, 2012 Wade Cox)

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:http://www.logon.org au http://www.ccg.org

Page 2 Torati na Amri ya Tisa

Torati na Amri ya Tisa

Imeandikwa:Kutoka 20:16 Usimshuhudie jirani yako uongo

Kumbukumbu la Torati 5:20 Wala usimshuhudie jirani yako uongo

Amri ya Tisa inashughulika kumuelezea mwandamu kuwa ni kiumbe wa Mungu na Israeli kama mashahidi wa Mungu, na hawa wote wakiwa ni wawakilishi na mawakala wa Mungu ambaye ndiye aliyeweka na kuiamuru Sheria. Haki au wema (tsedek) wowote vinakubalika kwa kutegemea ushahidi wa kweli na ndiyo maana vitendo vyovyote vya uwongo vinaendana kinyume kabisa na Sheria au Torati ya Mungu. Shetani, ambaye ni mshitaki wetu ndiye baba wa huo uwongo (Yohana 8:44). Mambo yake yako kinyume kabisa na amri zilizo kwenye Sheria na amri za Mungu na hizi zake zimeegama kwenye uwongo tu.

Ushahidi wa Mungu na utaratibu wakeTaifa ni mwendelezo wa mfumo wa Mungu.

Isaya 43:1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.

Tumeitwa ili tufanyike kuwa mashahidi wa Mungu aliye Hai, yaani sisi sote, yaani wateule na taifa.

Isaya 43:10 Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine.

Kwa hiyo inatunapasa tuwe ni mashahidi tunaoishuhudia imani ya Mungu.

Umuhimu na ulazima wa sheria kwa ulimwengu wote Sheria ni jambo linalowahusu watu wote na inawahusu watu wote wanaoishi na walio sehemu ya taifa.

Hesabu 15:13-16 Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kuandama mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. 14 Tena kwamba mgeni amekaa kwenu, au mtu ye yote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye yuataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa Bwana; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo. 15 Katika huo mkutano, kutakuwa na amri

moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo mbele za Bwana. 16 Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.

Sheria inasimama kwa namna moja, yaani kwa taifa na kwa watu wote. Mwanadamu anaweza kutenda dhambi iwe ni kwa kutokujua au hata akiwa anajua kabisa sheria, bali hukumu hufanyika kwa kila mmoja peke yake kwa mujibu wa sheria hiyohiyo moja.

Hesabu 15:29-30 Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao. 30 Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.

Hukumu hiyohiyo hutolewa kwa wotel.Kumbukumbu la Torati 10:18-19 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19 Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

Utakaso chini ya sheriaTumekwisha takaswa sote kwa mujibu wa sheria za Mungu tukiwa kama taifa takatifu.

Kumbukumbu la Torati 7:6-11 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi. 7 Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; 8 bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. 9 Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; 10 naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake. 11 Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru leo, uzitende

Utakaso wetu unatokana na Agano letu na Mungu kupitia kwa Masihi. Kwa jinsi hii tumejengwa na kuwa watu wakatifu na tulio kwenye familia yake Mungu na tusio na waa wala kunyanzi (Mambo ya Walawi 19:2; 22:17-25; pia soma jarida la Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [ Law and the Fifth Commandment (No. 258)]. Kwa mujibu wa

Page 4 Torati na Amri ya Tisa

neno la Mungu ambalo ni ushahidi wa kweli, ndipo tunaongozwa na kweli (Zaburi 119:105)

Maongezi ya utani au mzaha Kwenye ushuhuda wa Mungu hakutakiwi kufanya mizaha, kwa kuwa kwenye mizaha kuna mazungumzo na ushahidi wa uwongo, na tutatoa hesabu kwa kila neno la lisilo na maana tulilolisema.

Shetani ndiye baba wa uwongo (Yohana 8:44) na wale wasio wa imani huwazonga wateule kwa uwongo na chuki na hupingana na sisi bila sababu (Zaburi 109:3). Wale wanaoiacha imani hufanyika kuwa wapiga porojo na wenye mahangaiko mengi (1Tim. 5:13). “Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa.” (Mithali 11:9)

Mathayo 12:35-37 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. 36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Maranyingi tumekuwa tukiwahukumu wengine kabla hatujajihukumu wenyewe na kwenye hukumu ile potofu tunafikia kiasi cha kusema uwongo.

Mathayo 7:1-5 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Tumaini letu linapaswa liwe ni kwa Mungu na kwenye kweli yake, na sio kwenye nguvu zetu sisi wenyewe.

Zaburi 52:1-5 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. 2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila 3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. 4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. 5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele;

Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

Tunatakiwa tuongee mambo yaliyo sawa na mafundisho yenye uzima yanavyosema.

Tito 2:1-3 Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; 2 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi. 3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;

Mashitaka na shutuma zote vinatoka kwa yule muovu, ambaye pia ni mshitaki wetu. Ufalme wa Mungu wetu unakuja pale ambapo mshitaki wandugu zetu ametupwa chini. Watakatifu – wale wazishikao amri za Mungu na “wasioyapenda maisha yao hata kufa” – walioshinda kwa damu ya mwana kondoo. Ni hivi punde tu mshitaki wetu atakamatwa na kufungwa kwa kipindi cha milenia moja ambacho pia kitakuwa ni cha utawala wa Masihi (Ufunuo 12:1-11; 22:14; 20:1-4).

Dhana potovu kuhusu uhuru na maisha yasiyozingatia sheriaUhuru wa mataifa yote ulimwenguni unatokana na sheria za Mungu ambazo ni ushahidi wa kweli. Uhuru usio na sheria ni uhuru mpotovu na uvunjifu wa sheria. Neema na kweli vinatoka kwa Yesu Kristo (Yohana 1:17)….waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu (Yohana 4:23, 24). Ni kweli tu ndiyo itakayotuweka huru (Yohana 8:32).

Ushuhuda dhidi ya mtu na kwa malaika walioasiTumetakiwa tufanye mambo yetu katika ukweli, kwa kuwa imeandikwa:

Kumbukumbu la Torati 6:16 Msimjaribu Bwana, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa

Tunapaswa kuishi kwa kila neno litokalo kwenye kinywa cha Mungu.

Mathayo 4:3-10 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. 4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. 5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu

Torati na Amri ya Tisa Page 5

jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. 10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

Kristo alimuabudu Mungu na alimkanusha Shetani kwa neno: “imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” Iwapo kama Kristo hakuwa na mwingine wa kumuabudu ila Mungu peke yake, basi tutawezaje kuwa ni mashahidi iwapo kama hatufanyi hivyo? Kitendo cha kumwabudu Kristo ni cha kushuhudia uwongo na ni uvunjaji wa amri zake ambazo hata yeye mwenyewe asingediriki kuzivunja.

Kumjaribu MunguUwongo wa kwanza aliutoa Shetani na kumuongopea Hawa na uwongo ule ulikuwa ni kuhusu dhana ya maisha ya umilele ambao alisema: “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, (Mwanzo 3:4).

Mwanzo 3:4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

Na kwa ushahidi huo wa uwongo wakajikuta wote wawili wakijaribu Mungu na wote wawili yaani mwanamke na huyu Aliyejifanywa kuwa Kerubi (yaani Shetani) ndpo wakajikuta wanahukumiwa kifo (Mwanzo 3:1-24; Isaya 14:12; Ezekieli 28:1-19).

Tunatakiwa pia kuchagua mtu ambaye tunajifunza mafundisho yake au kujifunza kweli kwake, kama tulivyoelekezwa na maandiko tutofanya kuwa “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala mtupe lulu zenu kwa nguruwe,” Kristo alinena kwa kutumia mifano kama ilivyotabiriwa (Isaya 6:9) ili watu wasiweze kuelewa na wakamrudia na kuongoka na kuponywa kabla ya kufika kipindi chao (Mathayo 7:6; 13:10-13; Marko 4:11-17). Siri za ufalme wa mbinguni tumepewa sisi ili tuzitunze, kakini sasa ni nyakati za mwisho za kutimilika kwa yote na ni kipindi cha kusema na kuyaweka yote wazi. Ni kwa kipindi cha mwongo unaofuatia tu ndipo mataifa na

mfumo wa ulimwenguni kote wa siku za mwisho utafanywa kuwa si kitu, na mapepo watashushwa kuzimuni ili wafungwe humo kwa kitambo hadi utakapofika ufufuo wa pili wa wafu.

Tunamwabudu Mungu kwa kweli na uwazi wa kuongea ama kushuhudia. Maombi yetu hayapaswi kuwa kama yaw a mataifa wapagani wanaoomba kwa kupayuka na pasipo na thawabu yoyote.

Mathayo 6:5-8 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

Mungu anatusik8ia sisi kwa kuomba kwetu kimyakimya na kusema kwa wazi na sio kwa mtindo wa kupayuka payuka ambao ulikuwa ikifanywa na desturi za makuhani wa Baali (1Wafalme 18:28). Tunakuwa mashahidi wake Mungu kwa njia ya matendo yetu kwa jinsi tunavyofuata na kuzitenda amri na sheria zake (Zaburi 2:1,2).

Unabii wa uwongoUnabii wa uwongo utaondolewa atakaporudi Masihi. Na manabii wake waliokuwa wanatabiri wataangamizwa katika kipindi hiki cha kuhumu ambacho kitafuatiwa na kipindi cha milenia na ufufuo wa pili wa wafu.

Kumbukumbu la Torati 18:15 Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye

Nabii aliyetajwa kwenye kumbukumbu la Torati 18:15 alikuwa ni huyu Masihi ambaye neno lake ni la kweli, na nabii yule aliyetajwa kuthubutu kulitaja jina la Bwana visivyostahili na hakuagizwa, “nabii yule hakika atauawa.” Kwa hiyo, manabii hawa wote watauawa na kuingia kwenye kundi la watakaohukumiwa kwenye ufufuo wa pili wa wafu.

Kumbukumbu la Torati 18:20-22 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena

Page 6 Torati na Amri ya Tisa

katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. 21 Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? 22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope

Iwapo kama tutamgundua nabii kuwa ni wa ueongo, hatopaswi kumuogopa, kwa kuwa Mungu atamshughulikia. Nabii hawezi kuzuiwa kuifanya kazi yake hadi pale Mungu atakapoona kuwa imekwisha.

Yeremia 11:21-23 Basi, kwa hiyo, Bwana asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la Bwana, usije ukafa kwa mkono wetu. 22 Kwa sababu hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa; 23 wala hapatakuwa na mtu atakayesalia kwao; maana nitaleta mabaya juu ya watu wa Anathothi, mwaka wa kujiliwa kwao.

Ishara au alama ya kumjua nabii wa kweli ni kwa vile anavyokuwa mwaminifu kwenye utunzaji na kufundishaji wa Sheria na amri za Mungu (Yeremia 23:9-40). Nabii mkuu kuliko wote alifanya miujiza kwa nguvu na uweza wa Bwana Mungu, kwa kuwa dunia yote ni mali ya Bwana Mungu ili ayafanye na kuyaonyesha mapenzi yake, na anakaribia kumponda kichwa Shetani na kumseta chini ya miguu yetu (Kutoka 9:29; Kumbukumbu la Torati 10:14; Warumi 16:20).

Manabii hawahawa kama alivyokuwa Balaamu ben Peori, waliotajwa ama wanaelezewa na neno la Mungu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu, na ingawaje wao sio wateule wake. Aliwatumia nab ado anaweza kuwatumia kwa makusudi au mazingira fulani ya aina yake. Kuna idadi fulani ya mifano ya aina hiyo kwenye Biblia ambayo kwamba mambo aina hii yalifanyika. Jambo muhimu na linaloangaliwa ni iwapo tu kama watasema kwa kuzifuata Sheria na amri za Mungu na Ushuhuda wake na iwapo kama hawataongea jinsi hoyo, hakuna nuru ndani yao (Isaya 8:20).

Ushuhuda wa Mungu kwa kupitia mabanii na MasihiMungu alinena kupitia manabii tangu siku za mababa na kuendelea. Na hafanyi kitu chochote pasipo kwana kuwafunulia watumishi wake manabii.

2Wafalme 17:23 hata Bwana akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo.

(sawa na Amosi 3:7}

Na ndivyo Mungu alivyoongea na Yuda kupitia kwa Masihi. Kuhani mkuu alirarua nguo zake na kusema “Je, tunataka nini zaidi ya kuwa mashahidi?” Ingawa hakuwa ameelewa kikamilifu maana ya kitendo alichokuwa anakifanya na kusema. Na kisha wakamhukumu Yoshua na Masihi hukumu ya kifo (Marko 14:63). Alikuwa ni shahidi mwaaminifu na mfalme wa wafalme wa duniani, na mwanzo wa uumbaji wa (Ufunuo 1:5-6; 3:14). Unabii kuhusu kurudi kwa Masihi umekuwa ukitolewa kwa kipindi kirefu sana sasa.

Kumbukumbu la Torati 18:16-19 Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. 17 Bwana akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. 18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. 19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.

Masihi alimshuhudia Baba yake aliye mbinguni. Hatumwiti mtu baba hapa duniani kwa kuwa tuna Baba mmoja tu aliyeko mbinguni (Mathayo 6:9; 23:9). Wala hakuna aliyewahi kumuona Mungu, basin a umtumikie yeye aliyewahi kuwa na Mungu. Kwa kupitia ushuhuda wa Kristo, yeye aliyezaliwa elohimu peke yake, na yule ambaye Baba alitufunua sisi (Mathayo 11:27; Yohana 1:18; 6:46; 10:15). Iwapo kama tutazifanya kazi za Mungu ndipo tutakuwa mashahidi wa kweli na tunaweza kuaminiwa (Yohana 10:34-38). “Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.” (Yohana 3:36). “Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.” (Yohana 5:21).

Hili ndilo lengo la kumshuhudia Masihi, alikuja kumdhihirisha Baba. Kwa hiyo

Torati na Amri ya Tisa Page 7

inafuatiwa, shahidi wa kweli anabakia kwenye imani.

Ushahidi wa uwongo kwenye jamii zetu

Ushuhuda wa uwongo na ulimi wa uwongoMungu anauchukia ushuhuda wa uwongo na ulimi wa uwongo, na haya yamesababisha magomvi na matengano yatokee kati ya ndugu hata miongoni mwa waaminio.

Mithali 6:16-19 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. 17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; 19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Mithali 12:22 Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake

Mithali 19:5 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka.

Hukumu kwa ajili ya kumdanganya Roho Mtakatofu ni kifo, na wakati mwingine inatokea happhapo na kwa mara moja na kwa dhahiri.

Matendo 5:3-5 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.

Mtume Paulo alituambia tusijidanyanye kwa kudhani tumeuvua utu wa kale na matendo yake (Wakolosai 3:9)

Kristo aliwashangaa Wayahudi wenzake kwa kutaka kwao kumuua. Walitaka kumuua kwa kuwa neno lake halikuwa na nafasi ndani yao. Yeye aliye wa Mungu hulisikia neno lake Mungu (Yohana 8:31-59). Hili lingeweza kuwa ni jaribu la kwanza kabisa kwa Adamu na Hawa, ambalo kwalo walikuwa hawajawahi kuganmganyika na wala hawakuwa na kisingizio au udhuru kwa kufanya kwao hivyo (soma Mwanzo 3:1-24).

Kristo ameitwa mwaminifu na mkweli kwa kuwa ni mwaminifu na mkweli. Anapanga vita kwa haki na kwa kweli (Ufunuo 19:11).

1Wafalme 22:18-28 ni kifungu cha maandiko kinachoshangaza, inapoonekana kuwa Mungu aliiagiza na kuielekeza roho ya uwongo iingie kwenye vinywa vya manabii. Jibu linalotolewa kwa tukio lile ni kumfanya mfalme aelewe kwamba manabii wa Israeli walikuwa wamepewa roho wa udanganyifu. Wakamdanganya mfalme na nabii wa kweli akaonekana kuwa ndiye nabii wa uwongo. Unabii ulikuwa unasema: “Nenda [Ramothi-Gileadi] kwa kuwa Yahova ataiokoa nchi hii ya mfalme” (1Wafalme 22:6). Tatizo lilikuwa ni kwamba mji huu ulikuwa unakwenda kukombolewa kutoka kwenye mikono ya mfalme wa Ashuru, na sio kwa mfalme wa Israeli.

Hata hivyo, Mungu alikuwa amempeleka nabii wake wa kweli Mikaya, na alipoulizwa aseme kweli alisema hiyo kweli (1Wafalme 22:19-23). Kitendo cha kuomba maelekezo pasipo kuzifuat sheria na amri za Mungu ni machukizo na kinakaribisha maafa. Kwenye andiko hili tunajionea kwamba Mungu anaijaribu roho pia kwa kupitia jambo hili.

Mapokeao kama ushuhuda wa uwongoKristo aliyakemea sana mapokeao ya Mafarisayo kwa kuwa yalikuwa yamefundishwa na kuingizwa katika imani yao Yuda kwa wakati ule, kama tunavyojionea kwenye Mathayo 15.

Mathayo 15:1-14 inasema: Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema, 2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. 3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. 5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, 6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. 7 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, 8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. 9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya

Page 8 Torati na Amri ya Tisa

wanadamu. 10 Akawaita makutano akawaambia 11 Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi. 12 Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa? 13 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa. 14 Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Mafarisayo na Waandishi walilifanya neno la Mungu lionekane kuwa sio la muhimu kwa ajili ya mapokeo yao; na kwa hiyo walipaswa wajaribiwe kwanza na sheria au amri (Isaya 8:20). Matokeo yake walipelekwa mbali utumwani mnamo mwaka wa 70 BK, ambayo ilikuwa ni miaka arobaini baada ya kufa kwake Masihi ambayo pia ilikuwa ni Ishara ya nabii Yona (soma majarida ya Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [ The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].

Kutoka 1:17-21 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. 18 Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? 19 Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. 20 Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. 21 Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.

Ulinzi wa watu wote unategemea na jinsi wanavyomcha Mungu. Wale walioitwa na kuchaguliwa wanafanyika wote kuwa ni nyumba au vyumba kwenye Hekalu la Mungu wetu.

Mambo ya Walawi 19:14; 17-18 Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. 17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. 18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana

Mfumo mzima wa haki umewekwa kwa kufuata kweli na pasipo kuwaogopa au kuwapendelea watu, nah ii ahaimaanishi kuwa kwenye ujinga.

Haitakiwi kuweka upendeleo kwa watu fulani inapotolewa hukumu (cf. Kumbukumbu la Torati 1:17).

Shahidi wa kweli anatakiwa atathminiwe na watu wa Mungu kwa kila jambo maishani mwake. Kunatakiwa kusiwe na shahidi wa uwongo kwa jambo lolote lihusulo utendaji kazi wake, wala kwa maongozi yake, au kwenye haki, au kwenye biashara kwenye matumizi ya mzani, au vipimo, au nakala.

Mambo ya Walawi 19:35-36 Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. 36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.

Udanganyifu Kudanganya (au uzushi) ni wizi kama tulivyofafanua kwenye jarida letu la Torati na Amri ya Nane (Na. 261) [ Law and the Eighth Commandment (No. 261)] .

Kwa tabia hii ya kudanganya au uzushi tunaiba tabia ya mwingine na kwa hiyo tunawaua. Maisha yao yanadhulumiwa na mioyo yao inatibuliwa na kuumizwa. Tumekuwa njia panda dhidi ya jambo hili hapo juu.

Waongo na wazushi wamekataliwa na Mungu.Yeremia 6:27-30 Nimekuweka uwe mnara na ngome kati ya watu wangu; upate kuijua njia yao na kuijaribu. 28 Ni waasi kupita kiasi wote pia, waendao huko na huko wakisingizia, ni shaba na chuma hao, hutenda dhuluma wote pia. 29 Mifuo inafukuta kwa nguvu; risasi tu inatoka katika moto huo; mfua fedha ameyeyusha bure tu; maana wabaya hawaondolewi mbali. 30 Watu watawaita taka za fedha, kwa sababu Bwana amewakataa.

Mungu anatuonyesha matokeo ya mwisho ya uvunjaji huu wa sheria kupitia kwa nabii Yeremia.

Yeremia 9:1-6 Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu! 2 Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana. 3 Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema Bwana. 4 Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu

Torati na Amri ya Tisa Page 9

awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huko na huko na kusingizia. 5 Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoeza ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu. 6 Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema Bwana.

Ushahidi wa uwongo unawazuia watu wasimjue Mungu. Watu wanabeba silaha ili wakamwage damu (Ezekieli 22:9).

Kutoka 23:6-7Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. 7 Jitenge mbali na neno uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu

Haki na isipimwe kwa kuangalia idadi au utajiri. Ukweli usipingwe au kukanushwa kwa kufuata mtazamo wa watu wengi.

Mambo ya Walawi 19:16 Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana.

Usengenyaji au utesi unaua watu na unaharibu familia. Ni ishara na alama ya taifa lisilo na maadili mema.

Uwongo na udanganifu kwenye familiaMwamaume anayejisingizia kuwa ni msafi na hajawahi kulala na mwanamke na kufanya ngono akimdanganya hivyo mkewake, anabidi afanyiwe uchunguzi na wazee wa mji ule, sawa na anavyofanyiwa mwanamke mjinga asiyeiheshimu ndoa yake (soma Kumbukumbu la Torati 22:13-21; na majarida ya Torati na Amri ya Tano (Na. 258) na Torati na Amri ya Saba (Na. 260) [ Law and the Fifth Commandment (No. 258) and Law and the Seventh Commandment (No. 260)].

Wanaume wote wanapaswa kuwapenda wake zao kama Kristo anavyolipenda Kanisa. Hakuna mtu mwenye tabia ya kuiganganya familia yake anayeruhusiwa kuwa kwenye familia ya Mungu (soma Waefeso 5:28-29). Wanawake wanapaswa wawe kwenye njia kama hii na ndipo wawapeheshima waume zao. Hali kadhalika, waume wanapaswa waishinao kwa akili, wakiwapa wake zao heshima wakiwa ni warithi pamojanao wa neema ya maisha, ili kwamba maombi yetu yasizuiwe (1Petro 3:1-7). Mungu hamsikilizi mtu mwongo na mdanganyifu, au mtu anayeipuuzia familia yake asiipe heshima yake

kwa Mungu. Na wala mwanaume asimnyenyekee wala kumdhalilishe mwanamke (Kumbukumbu la Torati 22:29; Kutoka 22:16,17).

Tabia ya udanganyifu kwenye familia ni jambo lililokatazwa kabisa.

Zaburi 50:19-20 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. 20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.

Ugndanganyifu unapofanana na wiziTumejionea kwamba tabia ya udanganyifu inaiba tabia ya mtu mwingine. Tunatakiwa kuuvua utu wa kale na kuuvaa utu upya, ambavyo ni kuzifanya upya nia yetu iliyo sawa na taswira ya Mungu (Wakolosai 3:9-10).

Wakolosai 3:9-10 Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; 10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba

Mtu mpya ni Roho Mtakatifu katika Yesu Kristo, ambaye ni “mfano wake yeye aliyemuumba.” Hii ni mojawapo ya nukuu rasmi tatu (soma Waebrania 3:2; Ufunuo 3:14) kwa kulinganisha na uumbaji wa Masihi na ni mmoja tu peke yake ambaye hajawahi kukasirika kama ilivyoonekana mara nyingi.

Inampaswa kila mtu achukie na kuiacha tabia ya udanganyifu na badala yake aanze kusema kweli kwa jirani yake (Waefeso 4:25; sawa na Mithali 11:9). Tunaonywa hivi:

Waefeso 4:29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia

Tito 3:1-3 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. 3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

Inatupasa kuziheshimu sheria na tusimnene mabaya mtu yeyote.

Yakobo 4:11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini

Page 10 Torati na Amri ya Tisa

ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.

Tusijihukumu wenyewe na kujidhania wajinga kwa kuzitumia ndimi zetu wenyewe.

Mithali 10:18 Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.

Mungu amesema kile atakachowafanyia wadanganyifu na wenye kujivuna.

Zaburi 101:5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamharibu. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitavumilia naye.

Sehemu ya IIMfumo wa Haki

Misingi ya sheria za asiliMambo ya Walawi 24:22 Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Kanuni za haki za asili zinamtaka kila mtu aijue sheria zilezile. Kila mtu anapswa kujua mashitaka yaliyo dhidi yake kwa kwandishi na anapaswa kupewa fursa kujua anachotakiwa kufanya. Mtuhumiwa au mdaiwa anatakiwa kupewa usikivu wa haki na asiwe na aina yoyote ya shinikizo, na hukumu yake iwe ya haki na sio ya kupindisha au ya kumpendelea mtu.

Kwa sababu hii ndiyo maana Mungu ametupatia sheria zake kwenye maandiko na mashitaka yanayofanywa dhidi yetu yanafanywa na manabii na yamewekwa kwenye maandiko. Tumepewa muda wa kutafakari mashitaka, na Mungu hafanyi haraka kutoa hukumu akikusudia kwamba asiwepo mtu wa kupotea. Utaratibu huo huo wa kisheria ulioko kwenye jamii yetu na ambao unafanya kazi zhini ya sheria au Torati ya Mungu, pamoja na aunzishwaji wa mahakama yanayofanya kazi kwa niaba ya Mungu mwenyewe.

Tumepewa namna nyingi za majaribu ambayo kwayo tunajaribiwa imani zetu. Wateule wako hukumuni sasa na hukumu inaanza kwenye myumba ya Mungu.

1Petro 4:17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?

Sehemu nyingine yote iliyobakia ya dunia haitahukumiwa sasa hadi kwenye ufufuo wa pili wa wafu, wakati watu wote watakapokuwa wamefufuka, na kisha kurekebishwa kwenye hukumu na kupewa fursa ya kuokolewa (Ufunuo 20:4-15).

Kutenda jambo kwa kuamrishwa na mwingineNi uvunjifu wa sheria asilia ya haki na Amri ya Mungu kuitendea kazi amri ya mtu mwingine kwa niaba ya mtu mwingine. Kristo alitekeleza hukumu kwa namna alivyokuwa amepewa mamlaka na Mungu. Hakuja hapa ulimwenguni kuhukumu bali kuja kuufundisha ulimwengu jinsi unavyopasa kuhukumu. Wale waliompokea na kumkubali na kuwa sehemu ya Nyumba ya Mungu wangehukumiwa tangia hapo hadi sasa na ufufuo wa kwanza wa wafu (1Petro 4:17). Wale ambao hawakumpokea watahukumiwa katika siku za mwisho, kwa ajili hii ambayo inamaanisha ufufuo wa pili wa wafu uliotajwa kwenye Ufunuo 20:11-15.

Yohana 12:46-48 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Masihi hakutumwa ili auhukumu ulimwengu, bali alitumwa ili auokoe. Siku za meisho ni kipindi cha miaka elfu tangu Marejeo ya Masihi na ufufuo wa pili wa wafu mwishoni mwa kipindi cha Milenia (soma Ufunuo 20:1-14; pia tazama jarida la Siku ya Bwana na Siku za Mwisho [ The Day of the Lord and the Last Days (No. 192)].

Kujaribiwa kwa matesoBwana ameanzisha utaratibu wa aina hiyohiyo wa kujaribiwa kwa mateso makali kwa sababu fulani maalumu za kisaikolojia kwenye nchi. Mambo haya yote yamefanywa ili kulinda familia isitatizwe.

Hesabu 5:11-31 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 12 Nena na wana wa israeli, uwaambie, kama mke wa mtu ye yote akikengeuka, na kumkosa mumewe, 13 na mtu mume akalala naye kwa uasherati, na jambo hilo likamfichamania mumewe, likawa jambo lisilojulikana, na huyo mwanamke akawa najisi, wala hapana shahidi aliyeshuhudia juu yake, wala hakufumaniwa; 14

Torati na Amri ya Tisa Page 11

kisha mumewe akashikwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye akawa najisi huyo mwanamke; au kama akiingiwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye hakuwa na unajisi huyo mke; 15 ndipo huyo mume atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri; asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu. 16 Basi kuhani atamleta mwanamke akaribie, na kumweka mbele za Bwana; 17 kisha kuhani atatwaa maji matakatifu katika chombo cha udongo; kisha kuhani atatwaa katika vumbi lililo pale chini ya maskani, na kulitia katika hayo maji; 18 kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za Bwana, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake; 19 tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena kwamba hukukengeuka kuandama uchafu, uli chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru; 20 lakini kwamba umekengeuka uli chini ya mumeo, na kwamba u hali ya unajisi, na mtu mume amelala nawe, asiyekuwa mumeo; 21 hapo ndipo kuhani atamwapisha mwanamke kwa kiapo cha kuapiza, kisha kuhani atamwambia huyo mwanamke maneno haya, Bwana na akufanye wewe uwe laana na kiapo kati ya watu wako, hapo Bwana akufanyapo paja lako kupooza, na tumbo lako kuvimba; 22 na maji yaletayo laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina. 23 Kisha kuhani ataziandika laana hizo ndani ya kitabu, na kuzifuta katika maji ya uchungu; 24 kisha atamnywesha mwanamke hayo maji ya uchungu yaletayo laana; nayo maji yaletayo laana yataingia ndani yake, nayo yatageuka kuwa uchungu. 25 Kisha kuhani ataitwaa hiyo sadaka ya unga ya wivu, kwa kuiondoa mkononi mwa huyo mwanamke, naye ataitikisa sadaka ya unga mbele ya Bwana, na kuisongeza pale madhabahuni; 26 kisha kuhani atatwaa konzi moja ya sadaka ya unga, kuwa ni ukumbusho wake, na kuuteketeza madhabahuni, baadaye atamnywesha mwanamke hayo maji. 27 Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji, ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosa mumewe, hayo maji yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu wake. 28 Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana. 29 Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi; 30 au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za Bwana, na kuhani atatenda juu yake sheria

hii yote. 31 Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.

Sheria hizi ni kwa ajili ya kuzilinda familia na kila mtu kutokana na vishawishi au matamanio ya watu walio kwenye nyumba husika. Tunajionea hilo kutoka kwenye Kumbukumbu la Torati 22:13-21.

Tabia ya udanganyifu au uzushi na uvuruga nyumba vinatozwa faini na hairuhusiwi kuchukuliwa kuwa ni jambo linalostahili kuwaachanisha watu kwa kipindi hicho na kwa siku za mbele, hata kama uamuzi huu wa kuachana utaonekana kama unafaa au watu wanaupendelea kwa kigezo cha kuwepo wa ushahidi wa dhahiri. Shahidi wa uwongo kwenye suala la lonaloathiri ushuhuda au sifanjema ya mtu kwa siku za usoni ndvyo ilivyo pia kwa suala la uaminifu wa mwanamke aliyeolewa.

Eheria hii inayohusika na ushahidi wa uwongo ina namna nyingi sana za kuitendea kazi pia. Iwapo kama ushahidi utakuwa umesababisha kupindishwa kwa hukumu kwa makusudi, au ikatolewa kimakosa, basi ushahidi huo ni lazima uondolewe kwenye orodha ya mambo yanayoandamana nayo. Kufanya hivyo wakati mwingine kunaitwa Fundisho la Mti Uliooza lakini inatakiwa ifanyiwe kazi kwa uangalifu na katika mazingira yake maalumu tu. (soma Kumbkumbu la Torati 22:13-21; na pia jarida la Torati na Amri ya Saba (Na. 260) [The Law and the Seventh Commandment (No. 260)].

Torati au sheria ya Mungu ni ushuhuda kwa ulimweng.

Warumi 3:9-23 inasema: Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; 10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. 11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. 12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 13 Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. 14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. 15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu. 16 Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. 17 Wala njia ya amani hawakuijua. 18 Kumcha Mungu hakupo machoni pao. 19 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; 20 kwa sababu hakuna mwenye mwili

Page 12 Torati na Amri ya Tisa

atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria. 21 Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; 22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

Hakuna mtu anayehesabiwa haki kwa sheria, bali ni kwa ushuhuda wa Totati na manabii na ndipo Mungu anaonekana kuwa ni mwenye haki. Uumbaji wenyewe unaonekana kwa ni jaribu lenye mateso, na wote wametenda dhambi na wote wamepugukiwa na utukufu wa Mungu.

Kuanzishwa kwa mfumo au utaratibu wa kimahama na mahakimu au waamuziMamlaka yote yamewekwa na Mungu. Maamuzi yote yanapaswa yafanyike kwa kulingana na maagizo ya Torati ya Mungu kama ilivyotanguliwa na asili yake (soma jarida la Amri za Mungu (Na. 174) [ The Government of God (No. 174)]. Torati yote na manabii imetuama kwenye Amri Kuu Mbili za Torati. Inasereresha matendo yake kinyume na Mapenzi ya Mungu.

Sheria zinatendakazi kwa kufuata sheria zilizo kwenye biblia zinapaswa zisiwadhuru watu wengine. Sheria ndogondogo zinapaswa zianzishwe ili itimiwe na jamii kama udhibiti umefanyika kwenye taifa kama maongozi yake.

Hakuna kinachoweza kuongezwa kwenye Ushuhuda au kuondolewa kutoka na vile ilivyo. (soma Ufunuo 22:18-19). Maana ya andiko hili imefungwa hadi kwenye nyakati za mwisho na sasa Roho Mtakatifu anaoweka wazi kwa wale watakao msikiliza. Hakuna sheria itakayoenda kinyume au kupunguzwa maana yake kwa ajili ya dhana hii ya uhuru na utaratibu uliowekwa kwenye hii Torati ya Mungu.

Sheria za dunia hii zinaweza kupingana na sheria zilizo kwenye Torati ya MunguHakuna taifa linalopitisha sheria ambayo uwepo wake unaenda kinyume au unapingana

na Torati ya Mungu. Wala hakuna kikundi kinachoanzisha mapokeo yanayogeuza au kubadili au kupuinguzia nguvu zake Torati ya Mungu. Hali kadhalika, hakuna Kanisa linaloweza kuipitisha sheria ambayo inaibadili au kuigeuza Torati ya Mungu au Kalenda yake ambayo kiini chake ni mpangilio wa kimbingu na maelekezo ya Biblia. Kanisa kuu la Kikristo la kidunia limekuwa likiwaua watu kinyume kabisa cha sheria hasa wale waliokataa au kupinga kuyatii mapokeo na maamrisho haya yaliyotungwa na kuwekwa na wanadamu na yaliyo kinyume na maandiko ya Torati ya Mungu, kuliko hata mfumo au dini yoyote ile hapa duniani. Kwa kweli wamelewa kwa damu za watakatifu na wafia dini (Ufunuo 17:4-6).

Matendo 5:29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

Mahakumu na wajibu waoKungu ameanzisha utaratibu wa mahakimu au waamuzi kwenye sheria (Kutoka 18:13-26). Umuhimu wa mahakimu umeandikwa na kuelezewa kwenye kumbukumbu la Torati 16:18.

Kumbukumbu la Torati 16:18 Weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo Bwana, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki.

Torati ilitolewa na kukabidhiwa wazee sabini wa Israeli ambao walipewa majukumu na uelewa wa Roho Mtakatifu wa Bwana.

Hesabu 11:16-17 Kisha Bwana akamwambia Musa, Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli, ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe. 17 Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako.

Jukumu la watu hawa lilikuwa ni kwenye umahiri wao wa kuitafsiri Torati, kazi ambayo walipewa watafsiri, Kuhani Mkuu na baraza la Wazee wa Israeli. Tangia hapo, waamuzi waliwekwa kwenye miji yote ya Israeli katika makabila yao yote.

2Mambo ya Nyakati 19:1-7 Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi Yerusalemu nyumbani kwake kwa amani. 2 Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao Bwana? Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa Bwana. 3

Torati na Amri ya Tisa Page 13

Walakini yameonekana mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu. 4 Na Yehoshafati akakaa Yerusalemu; akatoka tena kwenda kati ya watu toka Beer-sheba mpaka milima ya Efraimu, akawarudisha kwa Bwana, Mungu wa baba zao. 5 Akasimamisha makadhi katika nchi, katikati ya miji yote yenye maboma ya Yuda, mji kwa mji; 6 akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu. 7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.

Bwana yu pamoja na waamuzi wa Israeli na hakukutakiwa kuwa na upendeleo wa aina yoyote miongoni mwa watu au kupokea zawadi au kupokea rushwa nah ii ilikuwa sio kwa kuwaogopa wanadamu, bali ni kwa kumuogopa Mungu. Jambi hili limeagizwa kwenye Torati .

Kutoka 23:8 Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.

Mambo ya Walawi 19:15 Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.

Kumbukumbu la Torati 24:17-18 Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani; 18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.

Waamuzi waliwekwa kama ilivyoandikwa kwenye Kutoka 18:22-27.

Kutoka 18:22-27 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. 23 Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani. 24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. 25 Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi. 26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe. 27 Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe.

Musa ndiye aliyehusika kuwachagua waamuzi watakaowahukumu Israeli.

Kumbukumbu la Torati 1:12-17 Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na mateto yenu? 13 Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu. 14 Nanyi mkanijibu, mkaniambia, Jambo ulilonena ni jema la kufanya. 15 Basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu. 16 Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. 17 Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.

Hata hivyo, Israeli walikuwa na matatizo ya kiimani, hata walipokuwa chini ya waamuzi.

Waamuzi walipaswa kuilinda utu, siri na heshima ya mtu, kwa namna zote mbili, yaani kwa kipindi cha mchakato wa kushughulikia hatia ya mtu hadi huku yake.

Kumbukumbu la Torati 25:1-3 Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu; 2 na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu. 3 Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.

Sheria inataka kuweko na upepelezi wa kina kuchunguza makosa ya mtu na kupata uthibitisho au kithibiti, kama inavyoonekana kwenye mfano wa Kumbukumbu ka Torati 21:1-9.

Kumbukumbu la Torati 21:1-9 Aonekanapo mtu ameuawa katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, kuimiliki, amelala kondeni, wala haijulikani ni nani aliyempiga; 2 na watoke nje wazee wako na waamuzi wako, nao wapime hapo mpaka miji iliyomzunguka huyo aliyeuawa; 3 na iwe, mji ulio karibu na yule aliyeuawa, wale wazee wake mji huo watwae mtamba katika kundi la ng'ombe, ambaye hajafanya kazi, wala hajakokota jembe la nira; 4 wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule

Page 14 Torati na Amri ya Tisa

mtamba shingo yake humo bondeni; 5 nao makuhani wana wa Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua Bwana, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la Bwana na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao; 6 na wazee wote wa mji ule, ulio karibu sana na yule aliyeuawa, na waoshe mikono yao juu ya huyo mtamba aliyevunjwa shingo yake humo bondeni; 7 na wajibizane kwamba, Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuiona. 8 Ee Bwana, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao. 9 Ndivyo utakavyoondoa damu ya asiye makosa katikati yako, utakapofanya yaliyo sawa machoni pa Bwana.

Kwenye tukio hili kuna tuhumu ya makosa ya kubambikizwa kati ya pande mbili yaliyongojelewa huhukumiwa. Makosa ya kubambikiwa ni mwiba mkubwa katika utoaji haki inayoendeshwa kwa mujibu wa Torati ya Mungu na hasa inapotokea kwamba watu wote wana makosa mbele ya sheria (soma jarida la . Torati na Amri ya Sita (Na. 259) [Law and the Sixth Commandment (No. 259)].

Hata mshitaki wetu ambaye ni Ibilisi alitiwa hatiani mbele ya wakuu wa baraza kipindi ambacho Kristo alikuwa jangwani. Ni kwa damu ya Kristo ndiyo uliyotuondolea hatia yetu na kutuokoa na mauti na kutufanya tusamehewe kutoka kwenye kazi zetu mbovu na kustahili tumtumikie Mungu aliye Hai (Waebrania 9:13-14).

Wakati huhuku inapokuwa imetokewa na ushahidi kutolewa na ndipo fedha zote zinaweza kulipwa ili kufidia uhai uliopotezwa.

Kutoka 21:30-32 Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. 31 Akiwa ng'ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. 32 Ng'ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng'ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe.

Samweli akiwa ni mwamuzi mkuuSamweli alianzisha utaratibu wa kufanya kazi hii kwa kuzunguka kwenye maeneo yote ya Israeli na kwa hiyo inaruhusiwa kuweka mahakama za muda na kuhama hama kwa waamuzi.

1Samweli 7:16-17 Naye huenda mwaka kwa mwaka kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua Israeli mahali hapo pote. 17 Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhabahu.

Hukumu ilikuwa ni juu ya viongozi wa Israeli kama taifa. Hukumu zote zilitakiwa ziwe ni kwa mujibu wa maelekezo ya ibada kwa Mungu aliye Hai.

2Mambo ya Nyakati 6:23 basi, usikie mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimlipiza mwovu, kumpatilizia njia yake kichwani; ukamfanyie haki mwenye haki, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake.

Watu wote waliofanywa kuwa ni watumishi wanapaswa wakutwe wakiwa ni waaminifu.

1Wakorintho 4:2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

Klwa hiyo, ni kwa yule mtarajiwa tu miongoni mwa wawakilishi kwa mamlaka juu ya mashitaka magumu na wajibu wake.

Mahakama na mchakato wakeInafuatia na uwekaji wa waamuzi ambapo mahakama na mchakato zinapaswa pia ziamuliwe chini ya mamlaka iliyo chini ya sheria. Mchakato wa uchunguzi na upelelezi vinabidi kufanyika na kutolewa matokeo yake (soma Kumbukumbu la Torati. 21:1-9 above).

Mambo yote yanayotakiwa kusuluhishwa kati ya pande zote kwanza na yapelekwe mahakamani tu iwapo kama kuna mmoja wao atakayeonyesha kutoridhia na usuluhishi huo ulivyofanywa.

Mathayo 18:15-16 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.

Masuala magumu na yenye utata yanapaswa yapelekwe kwenye mahakama za juu. (cf. Kumbukumbu la Torati 17:8-11).

Wazee wa mji wanapaswa kuweka mahakama ya haki, ambazo zitachukuliwa ziwemo kwenye malango ya miji, ambazo hapo kale wazee waliketi na kutoa hukumu (Kumbukumbu la Torati 21:19; 22:15; 25:7; Amosi 5:12,15; Zekaria 8:16).

Torati na Amri ya Tisa Page 15

Mahakama yenye mamlaka ya Kuhukumu iliyoanzishwa na Sulemani ilitengenezwa kwa miti aina ya mkangazi au mshitana kiti cha kuhukumia kiliwekwa kwenye baraza iliyonakshiwa kwa mti wa mshita. Hii ilikuwa ni mbali na nyumba ya mfalme ambayo ilikuwa na baraza nyingine ndani ya baraza ya hukumu, ambayo ilikuwa sawa na ujenzi wa zile zingine (1Wafalme 7:7).

Mambo yote yanayolalamikiwa yanatakiwa wapunguzwe kwa maandishi (sawa na Ayubu 31:35)

Utaratibu wa mahakama yanapaswa yashughulikiwe kikamilifu na kwa heshima, kama yanavyokuja kutoka kwa Mungu ambaye ni elohimu wa Haki (soma Kutoka 22:28). Hakutakiwi kuweko na hali ya kuidharau mahakama au maamuzi (Kumbukumbu la Torati 17:9-13).

Mungu atamuondoa Roho wake Mtakatifu aliyekuwa akimtia nguvu Masihi na atawapa waamuzi na watawala wa Israeli sawasawa na maombi yao na utii wao kwake.

1Wafalme 3:5-15 Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. 6 Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. 7 Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 8 Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 9 Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? 10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. 11 Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. 13 Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika

wafalme kama wewe, siku zako zote. 14 Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi. 15 Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Bwana, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.

Hata Sulemani alianguka mbali na neema baada ya kupewa hekima yake yote na uweza, na kuruhusiwa kulijenga Hekalu. Na ndivyo ilivyo kwamba hata wateule wanaweza kupoteza nafasi zao kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu kwa ajili ya ibada za sanamu au uvunjaji wa Roho ya Torati.

Ushahidi Kuna utaratibu wa kukusanyika na kutathmini ushahidi ulioanzishwa (sawa na Kumbukumbu la Torati 19:3-13).

Hakuna mtu aliyeruhusiwa kuuawa kwa ushahidi wa mtu mmoja tu.

Hesabu 35:30 Mtu awaye yote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu hata akafa.

Shahidi mmoja hakuruhusiwa kuinuka na kumshuhudia mtu yeyote kwa dhambi yoyote.

Kumbukumbu la Torati 19:15 Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wo wote, wala kwa dhambi yo yote, katika makosa akosayo yo yote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.

Jambo hili linafanywa pia na wazee (1Timotheo 5:19).

Evidence should be disclosed in a hearing of both parties. There can be no withholding of evidence or of witnesses (cf. Mat. 18:15, 16).

Torati ailiyopewa nabii Musa ni kiini msingi wa sheria zote za Mungu. Ingawaje kuna Roho Mtakatifu, watu wote wanatakiwa waipokee neema.

Waebrania 10:28-29 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

Page 16 Torati na Amri ya Tisa

Katika siku za Waamuzi, kosa lilijulikana kwa kupigia kura na pia kwa mtu kukiri au kukubali kosa (sawa na Yoshua 7:14-26). Hakuna vitisho vilivyowahi kutumika ili kupata ushahidi chini ya mfumo wa sheria ya kibiblia. Neno lililotoka vinywani mwa manabii lilitumika mara nyingi na Mungu.

Kitendo cha kushindwa kupata ushahidi kwenye makosa yanayofanyiwa madai ni kukamililisha ukomo wa madai ya makosa (mambo ya Walawi 5:1; Zaburi 50:18).

Mambo ya Walawi 5:1 Na mtu awaye yote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe;

Ushahidi wa uwongo umekatazwa.Kutoka 23:1-3 Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. 2 Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; 3 wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake

Utaratibu wa Mungu ni mmoja ya kitu cha kutilia maanani kwa walio masikini na kwa kila mtu anatakiwa apewe fursa, lakini ni kwa juhudi zitokanazo na matendo yao.

Mambo ya Walawi 19:9-11 Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako; 10 wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako, wala usiyaokote matunda ya mizabibu yako yaliyopukutika; uyaache kwa ajili ya maskini na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 11 Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo.

Hakuna mtu anayetakiwa ashughulikiwe au atendewe vibaya na mwingine. Umuhimu huu unaendelea hadi kwenye biashara na viwanda kwa mambo yote.

Kumbukumbu la Torati 25:13-19 Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. 14 Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako. 15 Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 16 Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. 17 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; 18 jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia;

wala asimche Mungu. 19 Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.

Tendo la kutumia vipimo vya uzito na vya ujazo vya uwongo ni ushuhuda wa uwongo pia. Tendo la kuchukua fursa ya udhaifu katika kujaribu kuliharibia sifa kundi lingine au watu wengine kwa kuvunja kwao torati ya Mungu, isipokuwa kwa wakati ilipoamriwa hivyo kimahsusi na Mungu chini ya sheria yake.

Kuficha kwa kutoutoa ushahidiHatupaswi kuficha kutoutoa ushahidi. Inapotokea kughafilika na kutokuwepo kwa ushuhuda ndipo kamosa au hatia inaweza kugundukika. Hapo ndipo ushuhuda unabidi utolewe, hadi itakapokuwa imefanywa hivyo kwa sadaka ya dhambi kama tunavyojionea kwenye maandiko. Aina hii ya sadaka ya dhambi fidia yake haiwezi kupunguza umuhimu wa ushuhuda huu, ambao ulikuwa unajulikana na kuhitajika mapema kabla ya toba.

Mambo ya Walawi 5:4-13 au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo; 5 kisha itakuwa, hapo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo, ndipo atakapoliungama jambo hilo alilolikosa; 6 naye atamletea Bwana sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake. 7 Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea Bwana hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa. 8 Naye atawaleta kwa kuhani, atakayemsongeza kwanza yule wa sadaka ya dhambi, naye atamkongonyoa kichwa shingoni mwake, lakini asimpasue vipande viwili; 9 kisha baadhi ya damu ya hiyo sadaka ya dhambi atainyunyiza katika ubavu wa madhabahu; na damu iliyosalia itachuruzishwa hapo chini ya madhabahu; ni sadaka ya dhambi. 10 Kisha huyo ndege wa pili atamsongeza kuwa sadaka ya kuteketezwa, sawasawa na sheria; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa. 11 Lakini asipowaweza hua wawili, au makinda mawili ya

Torati na Amri ya Tisa Page 17

njiwa, ndipo hapo atakapoleta matoleo yake kwa ajili ya neno hilo alilolikosa, sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, kuwa sadaka yake ya dhambi; asitie mafuta juu yake, wala ubani usitiwe juu yake; maana, ni sadaka ya dhambi. 12 Naye atamletea kuhani, na kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi. 13 Na huyo kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake ambayo katika mambo hayo mojawapo amefanya dhambi, naye atasamehewa; na unga uliosalia utakuwa wa kuhani, kama hiyo sadaka ya unga ilivyokuwa.

Tendo la kuficha ukweli kwenye udhalimu pia linafanywa sana na waalimu wa uwongo na hutumika kwenye mafundisho yao. Haturuhusiwi kushuhudia uwongo au kuufundisha kwa kisingizio cha ufunuo wa Roho Mtakatifu tunapokuwa tunaifasiri au kuielezea Biblia. Watumisni wanaofundisha kinyume na kweli na hisia zao wanahukumia na kujisikia hatia kwa uovu huu.

Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

Hakuna Kanisa lililo na haki ya kuanzisha sheria au mafundisho yaliyo kinyume na Torati na ushuhuda wa Biblia. Kila baraza la kanisa na kila kanuni ya imani ya Kanisa zinazopingana na sheria za Biblia sio tu kwamba haziko sahihi bali pia ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu. Na kila mtu aliyewahi kufanya uovu huu, basi amejihukumu mwenyewe kwa hukumu itakayotolewa kwenye ufufuo wa pili wa wafu pamoja na wale wote waliowafuata. Kwa kweli, hakuna mateso makuu yatakayowahi kuumiza watu zaidi ya haya ya kwenye ufufuo wa pili wa wafu, wakati ambapo mamilioni yasiyohesabika ya watu watakapogundua kuwa walikuwa wanawafuata wahubiri shupavu waliokuwa wanawahubiria uwongo nay a ukengeufu na kwamba wamewapoteza na wanatakiwa kuanza upya tena. Sio suala la kukataliwa kwao kuuingia Ufalme wa Mungu kwa watu wa aina hii ambao viongozi wao ni watumishi na vifaa kamilifu vya Joka ambaye pia ni Shetani, aliyelishawishi Kanisa na kufanya vita na wale waliokuwa wanazishika amri za Mungu na ushuhuda wa imani ya Yesu Kristo (Ufunuo 6:9-11; 12:17; 14:12; 22:14).

Agizo la kusema na kuhubiri ukweli limetolewa kwa wote. Kitendo cha kusema uwongo kwa kutojali mamlaka iliyowekwa kisheria ni sawa na dhambi ya kushuhudia uwongo.

Kuvuapa kwa uwongoHairuhusiwi mtu kuapa kwa uwongo.

Mambo ya Walawi 19:12 Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana

Adabu au hukumu kwa mtu aliyeapa kwa uwongo ni ya muhimu (Mithali 19:5,9 sawa na 25:18). Mashahidi wote wa uwongo hawatakiwi waishi (Mathayo 19:17-19; Marko 10:18-19; Luka 18:19-20). Pia soma Warumi 13:8-10.

Luka 18:19-20 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu. 20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.

Kwa hiyo, kila mtu aliyeshindwa kuzishika amri za Mungu ameshindwa au kuanguka kiimani na anapaswa aondolewe kutoka kwenye ushirika wa waumini hadi atakapotubu.

Ni kama tulivyojionea kwamba kushuhudia uwongo ni dhambi mbele za Mungu.

Mambo ya Walawi 6:1-7 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya Bwana, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang'anya, au kumwonea mwenziwe; 3 au kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo; 4 ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang'anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokizumbua yeye, 5 au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia. 6 Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa Bwana, ni kondoo mume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani; 7 na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.

Page 18 Torati na Amri ya Tisa

Ushuhuda wote wa uwongo kuhusu dhambi iliyotendwa na ni uharibifu ambao kwamba unahitaji kufanyike marejesho.

Kumbukumbu la Torati 19:16-21 Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu ye yote na kushuhudia juu yake ya upotoe; 17 ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za Bwana, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo; 18 nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye; 19 ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. 20 Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. 21 Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Kwa hiyo hukumu kwa ajili ya kuvunja kiapo inandana na ile ya makusudi, na ni uhalifu ambao unabidi uhukumiwe.

Hukumu Mtume Yakobo anatuonyesha umuhimu wa Torati au Sheria.

Yakobo 2:8-13 8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. 9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji. 10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. 11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. 12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. 13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

Hukumu isiyozingatia rehema inakiuka misingi ya haki. Yeyote anayehukumu pasipo huruma atahukumiwa pasipo huruma (cf. Kumbukumbu la Torati 1:16).

Hakimu hauchukui upanga bure na anapata uweza wake kutoka kwa Mungu, haijalishi ni utaratibu gani.

Warumi 13:1-4 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa

kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu

Mungu huwahukumu wateule au elohimu wake (Zaburi 82:1).

Zaburi 82:8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote

Je, tutawezaje kuwahukumu malaika ikiwa tunashindwa kuhukumu maneno yetu wenyewe?

1Wakorintho 6:3-4 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? 4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?

Kwa kuitendea kazi hukumu wote wanafundishwa kwa kazi hiyo ambayo imewekwa juu yao kwa kiwango cha juu, na kwa amri au maagizo ya maandiko Matakatofu. Hakimu anatakiwa ahukumu kwa haki, kwa kuwa mahali pasipo haki hakuna utauwa – kuna neno la namna hiyohiyo kwenye Waebrania (tsedek), kama tulivyoona.

Haki ni tendo la kuishi maisha yasiyo na mawaa kwa kuwa haki ni dhabihu kwa Mungu ya utauwa.

Kumbukumbu la Torati 17:1-20 inasema: Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. 2 Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, 3 naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi; 4 ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli; 5 ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe. 6 Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. 7 Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo uovu katikati yako. 8 Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo

Torati na Amri ya Tisa Page 19

nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 9 uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonyesha hukumu ya maamuzi; 10 nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonyesha mahali hapo atakapochagua Bwana; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; 11 kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonyesha, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto. 12 Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia Bwana, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. 13 Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai. 14 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, itaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu; 15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako. 16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile. 17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno. 18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi; 19 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; 20 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli.

Mfumo wa haki unaendana na idadi dhana zilizotajwa mapema huko nyuma.

Kumbukumbu la Torati 16:19-20 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. 20 Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Hakuna mtawala aliyetawala huku akiwa hajajitengenezea nakala ya kitabu cha Torati na kujisomea, na kuiandika Torati hii na kuiteda. Tamko la hukumu ni la rehema na hukumu inapaswa ifanyike kwa kufuata maelekezo ya Torati ya Mungu, na inatakiwa ichukuliwe kikamilifu.

Jela au lokapuMtuhumiwa anaweza kuhukumuwa kifungo cha nje (Hesabu 15:32-36). Hukumu inatakiwa ifanyike haraka na hukumu ifanyike kulingana na kosa lenyewe lilivyofanyika.

Ezra 7:26 Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kwa bidii, kwamba ni kuuawa, au kwamba ni kuhamishwa, au kuondolewa mali yake, au kufungwa.

Kwa hiyo, mtu anatakiwa aletwe mbele ya mashitaka pasipo kumchelewesha. Kitendo cha kulaza mtu jela bila kumfikisha mahakamani ni kinyume na Torati au sheria za Mungu.

Kifungo kinakusudiwa kurekesha harasa au deni lililotokana na uhalifu uliofanyika, kwa kufanya kazi, sawa na jinsi alivyohukumiwa. Fedha zitakazopatikana zinatarajiwa kutumika kwa kulipa au kufanya ukombozi au fidia kwa uhalifu uliofanyika iwapo kama utaifishaji wa mali za mwalifu hautatosha kufidia hasara ya uhalifu huo. Inafuatia kwamba malipo kwa ajili ya kazi unatakiwa kuwa ni wa haki kama hivi na ndipo unamfanya akutwe na hatia na nchi yake au kwa kushikilia mashahara wa masikini na kuelekea katika kupunguza kiwango cha hukumu au adhabu. Kwa hiyo viwanda vya magerezani zinazotumia nguvukazi ndogo kama tunavyoona huko Uchina, vinapingana na maongozi ya Torati ya Mungu. Kila mtu anaweza kukatarufaa ya kupunguziwa kazi ngumu anapokuwa kwenye Mji wa Makimbilio ambao anakuwa huko kipindi chote cha uhai wa kuhani wa mji ule. Kazi zinazofanywa kwenye Mji wa Makimbilio hazitakiwi kuchukuliwa kuwa ni sawa na zile zinazofanywa kwa mtindo shuruti wa gerezani, ambazo zinaweza kuonekana kama za kikatili na za aina ya hukumu isiyo ya kawaida kwenye jamii. Kizuizi ni kwa ajili ya kumlinda kila mtu na kwa jamii yote kwa hukumu iliyopaswa kumkabili (pia soma jarida la Torati na Amri ya Nane (Na. 261) [ Law and the Eighth Commandment (No. 261)].

Hukumu ya mwili ilifanyika nje ya makao au kambi zao Israeli (Mambo ya Walawi 24:14).

Page 20 Torati na Amri ya Tisa

Sulemani alifanya dhambi na akafa kifo cha kimwlili asilia. Hata hivyo, thawabu yake haikuwa kama ile ya baba yake Daudi.

Marekebisho na malipiziKufuatia na makosa au mashitaka ya kumdhalilisha mtu au kumuaibisha, tunaendelea kwenye hukumu. Dhana au lengo la kwanza kuhusu kumhukumu mtu ni kumrekebisha. Makosa yote ni dhambi na dhambi ni uvunjifu wa sheria. Mungu anapenda kwamba kusiweko mtu yeyote atakayepotea bali wote waweze kumuona yeye, na ndio maana jambo la kwanza linalotiliwa maanani ni kutubu na marekebisho ni neema tu.

Israeli wote wanatakiwa wawe watakatifu kwa Bwana. Marekebisho ni kuhakikisha kwamba mtu emerudi kwenye jamii na anafaa kwenye taifa lake na kwamba yuko sawia. Kumbuka kwamba kwenye kila hukumu kunatakiwa kuonekane maongozi ya Roho wa Mungu.

Mathayo 5:3-13 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. 5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. 7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. 9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. 13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Ingwa wokovu wa Kristo umeendelea hadi kwa Wamataifa na utaratibu wa hukumu ulitolewa kwa watu wa mataifa yote. Wamoabu na Waamoni walitabiriwa kuwa watajumuishwa na Yuda na kwa hiyo wataingia kwenye imani katika siku za mwisho wakiwa ni sehemu ya Israeli. Wamisri watabakia wagumu. Mataifa yoye watakuwa ni sehemu ya hekalu la Mungu aliye.

Kumbukumbu la Torati 23:3-8 Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa Bwana milele; 4 kwa sababu hapo

mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize. 5 Lakini Bwana, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; Bwana, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda Bwana, Mungu wako. 6 Usitafute amani yao wala heri yao siku zako zote, milele. 7 Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake. 8 Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa Bwana.

Hapa tunaiona dhana ya udugu ilivyo kwenye Torati ya Mungu inavyoendelea mbali zaidi kwenye makabila ya Israeli kwa wana wa Ibrahimu na kwa watu mchanganyiko wa Kisyria na Kifoenike, ambao walijumuishwa kwa waedomu (Waidumea), na Wamisri, walio na msingi wa ukarimu kwa Waisraeli. Pia imeenelea hadi kwa Waashuru ambao walifanya kazi mkono kwa mkono na Israeli watakaotokea pande za kaskazini katika nyakati za mwisho. Wokovu uliendelea hadi kwa Wamataifa.

Mwisho wa sheria ni kumhakikishia pia usalama wa kila mtu. Pale ambapo ushahidi wa uwongo ulisababisha hasara kuliko kutokea kwa marejesho. Hata hivyo, kwenye sheria zote kuna asili fulani ya msamaha na huruma. Mahali pasipo na msamaha, hapawezi kuwa na marekebisho makamilifu. Kila mtu anapaswa kujua kwamba amepoteza kile wanachokitarajia kukipata. Ni vema kurejeshwa kwa ndugu yako kuliko kurejeshewa mali zako.

Uhalifu unaendana na adhabu, na sio kila mara kini aiwa kwa unaendana na toba. Pasipo toba laana ya Torati inafuatia. Laana hizi zinalitesa taifa zaidi kuliko zinavyomuathiri mtu binafsi.

Kumbukumbu la Torati 28:18-19 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,

Kila mara kuna dhambi, na ukosaji na malipizo, lakini hata hivyo, Mungu huhukumu moyo wa kila mmoja.

Hesabu 5:5-10 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 6 Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yo yote, ifanywayo na binadamu, kumwasi Bwana, na mtu huyo akawa na hatia; 7 ndipo watakapoungama

Torati na Amri ya Tisa Page 21

dhambi yao waliyoifanya; naye atarudisha kwa hatia yake, kwa utimilifu wake, tena ataongeza juu yake sehemu ya tano, na kumpa huyo aliyemkosa. 8 Lakini kwamba mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa Bwana kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo mume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake. 9 Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyosongeza kwa kuhani, itakuwa ni yake. 10 Tena vitu vilivyowekwa wakfu na mtu awaye yote, vitakuwa ni vya kuhani; kitu cho chote mtu atakachompa kuhani, kitakuwa chake.

Kila mmoja sasa anawajibika kwa dhambi zake mwenyewe na Mungu amesema kwa kupitia manabii wake kuhusu dhambi za.

Hesabu 14:18 Bwana ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.

Neema hii ya Mungu imetokana na Roho wake aliyemfanya akae na watu wote, ili kwamba kila mtu sasa awajibike kwa maovu yake au dhambi zake.

Ezekieli 18:19-24 Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi. 20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. 21 Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. 22 Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. 23 Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? 24 Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.

Kusomwa na Kukaziwa kwa Torati kila miaka sabaTorati inapaswa isomwe na kutangazwa kwa kuwekewa mkazo kila baada ya miaka saba na kwenye mwaka wa Sabato wa Yubile.

Kumbukumbu la Torati 31:10-13 Musa, akawaamuru, akasema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, 11 Israeli wote wafikapo ili kuonekana mbele za Bwana, Mungu wako, mahali pale atakapopachagua, uisome torati hii mbele ya Israeli wote masikioni mwao. 12 Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha Bwana, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii; 13 na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha Bwana, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.

Ukamilifu wa kila mmoja na wa mfumo mzimaMatokeo ya mwisho ya sheria na mpango wa Mungu ni ukamilifu wa Roho Mtakatifu.

Kumbukumbu la Torati 18:13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako

Tunatakiwa pia kuwapenda adui zetu, kwa kuwa kama tutawapenda marafiki zetu tu tatakuwa na tufauti gani na watu wa mataifa?

Mathayo 5:46-48 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Lengo hili linawezekana kulifikia wana wa Adamu. Tunapaswa kuwa wakamilifu kana Nuhu aliyokuwa mkamilifu na kama Henoko alivyokuwa mwenye haki na mkamilifu.

Mwanzo 6:9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.

Ingawa Mungu alimuamuru Abrahamu awe mkamilifu, ni sawa kama Kristo alivyotuamuru sisi tuwe.

Mwanzo 17:1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

Kwa hiyo, ukamilifu katika Roho Mtakatifu sio tu kwamba unawezekana, bali pia tumeamriwa kuwa hivyo. Tumeamriwa pia kuwapenda maadui zetu na kuwarekebisha wale wote walioanguka mbali na neema. Kwa hiyo, adhabu kali zilizo kwenye sheria zinapaswa ziruhusiwe pale tu inapotolewa fusra ya

Page 22 Torati na Amri ya Tisa

mkosaji kukiri nay eye akakiri lakini asitake kutubu kabisa.

Zaburi 37:37 Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.

Watu wote wanatakiwa kuenenda kwa Roho Mtakatifu kwa Sheria ya Kifalme ya Uhuru.