tathmini ya mahusiano baina ya watu na tembo karibu na … · 2020. 3. 6. · 2 muhtasari tulifanya...
TRANSCRIPT
Tathmini ya Mahusiano Baina ya Watu na Tembo karibu na Uwanda wa Magharibi wa Mapori ya Akiba ya Rungwa-Kizigo-Muhesi
Septemba 2016
1
Mawasiliano Southern Tanzania Elephant Program S.L.P 2494, Iringa www.stzelephants.org [email protected] Waandishi Josephine Smit Dr. Trevor Jones Rehema John
Uchoraji ramani Frank Lihwa Rehema John
Ukusanyaji wa takwimu Kephania Mwaviko Rehema John
Nakala ya ripoti hii Ripoti hii kwa lugha ya kiswahili na kiingereza linapatikana katika tovuti: www.stzelephants.org/publications-news/articles-reports. Nukuu Southern Tanzania Elephant Program. 2016. Tathmini ya mahusiano baina ya watu na tembo karibu na uwanda wa Magharibi wa Mapori ya Akiba ya Rungwa-Kizigo-Muhesi. Ripoti ya kiufundi. Ufadhili Ripoti hii inawezeshwa kwa msaada mkubwa wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), kupitia ufadhili mdogo kutoka Wildlife Conservation Society’s Southern Highlands and Ruaha-Katavi Protection Program (SHARPP). Yaliyomo ni wajibu wa waandishi na si lazima kutafakari maoni ya USAID au Serikali ya Marekani. Shukrani Tunaishukuru taasisi ya utafiti ya Tanzania (Tanzania Wildlife Research Institute-TAWIRI) na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ajili ya kutoa ruhusa ya kufanya utafiti huu, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kwa ushirikiano wao. Tunawashukuru viongozi wote wa vijiji na wakulima walioshiriki katika utafiti huu, na tunatarajia kupitia ripoti hii itawafaidisha wale wanaoishi na tembo. Kuhusu Southern Tanzania Elephant Program STEP ni taasisi isiyo ya kiserikali inayohusika na uhifadhi wa tembo iliyosajiliwa mwaka 2014 na makao makuu yake yapo kusisni mwa Tanzania. Kazi za STEP zimegawanyika katika makundi makuu manne: Ulinzi wa tembo, utafiti na ufuatiliaji, kuimarisha mahusiano baina ya tembo na watu kupitia miradi ya uhifadhi ya jamii, na utetezi na elimu.
Kuhusu Southern Highlands na Ruaha-Katavi Protection Program (SHARP)
SHARPP ni programu ya miaka mitano inayofadhiliwa na Shirika la Marekani kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ambao unatekelezwa na Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori (Wildlife Conservation Society – WCS)kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, taasisi binafsi za ndani, na wanajamii. SHARPP inalenga maeneo makuu manne, ambayo ni: maeneo ya usimamizi wa wanyamapori (WMAs); maisha; usimamizi wa mazingira; na ufuatiliaji na ulinzi wa tembo. Tathmini hii ya muingiliano baina ya tembo na watu kuzunguka Mapori ya Akiba ya Rungwa, Kizigo na Muhesi ina lengo la kuwajulisha jitihada za kuongeza mshikamano baina ya tembo na watu kuzunguka hifadhi hizi muhimu.
2
Muhtasari Tulifanya utafiti juu ya mahusiano baina ya watu na tembo katika vijiji tisa vinavyopakana na Mapori la Akiba ya Rungwa, Kizigo na Muhesi kati ya Agosti na Septemba 2016. Aina kuu za madhara ya tembo ilikuwa ni upotevu wa mazao, na mazao makuu yaliyolioathiriwa yalikuwa ni mahindi, viazi, na mtama. Pia, tembo ilisemekana kuvunjwa kwa maghala ya vyakula, paa za nyumba, na vyanzo vya maji, na kusababisha ushindani wa maji na chakula kwa mifugo. Maeneo makuu yenye athari za tembo ni vijiji vya Rungwa na Dorotto, na kwa kiwango cha chini Kintanula na Itagata. Juhudi za kukabiliana na athari hizo kwa sasa zipo kwa kiwango kidogo hadi cha kati, na huhusisha mbinu za jadi kama vile kelele, moto, na kulinda mashamba. Kwa mitazamo ya wahojiwa, Wizara ya Maliasili na Utalii, Serikali Kuu, na Mamlaka ya Mapori ya Akiba (katika mfuatano huo) zilionekana kuwa na majukumu yaa kusimamia kukubaliana na athari za tembo. Mitazamo ya wahojiwa ilionyesha utendaji wa mashirika hayo katika kusimamia athari za tembo kwa ujumla ilionekana kutokidhi. Wengi wa wahojiwa walidhani ilikuwa ni muhimu sana kuboresha mahusiano baina ya jamii na tembo. Mahusiano baina ya jamii na mamlaka ya Mapori ya Akiba kwa ujumla ilionekana kuwa mazuri sana.
1. Utangulizi Mshikamano baina ya watu na tembo ni changamoto kubwa katika uhifadhi nchini Tanzania, na katika maeneo mengi ya Tembo wa Afrika. Tembo ni aina ya viumbe vyenye kipaumbele katika uhifadhi nchini Tanzania, hutambuliwa kwa mchango wao katika uchumi wa Taifa kupitia utalii wa wanyamapori,na wamekuwa hatarini kutoweka kutokana na ujangili kwa ajili ya meno yao ambao umepunguza idadi ya tembo kitaifa kutoka 109,000 mwaka 2009 hadi kufikia takribani tembo 50,0001 mwaka 2015. Hata hivyo, tembo wanaweza pia kuwa na athari juu ya watu na maisha, hasa katika jamii ambazo hushirikiana na tembo katika maeneo na rasilimali. Hivyo, kuhakikisha mshikamano wa muda mrefu baina ya tembo na watu, Tanzania inahitaji hatua za kukabiliana na athari za tembo kwa watu na kuongeza msaada kwa jamii mzima kuhusiana na uhifadhi wa tembo.
Lengo la tathimini hii ilikuwa ni kuelewa muingiliano baina ya tembo na watu katika mwambao wa Magharibi wa Mapori ya Akiba ya Rungwa-Kizigo-Muhesi, na kuwapatia wadau taarifa na mapendekezo kwa ajili ya kusaidia kusimamia migogoro baina ya watu na tembo.
Utafiti uliopita (Wilbright 2016) wa muingiliano baina ya tembo na watu katika vijiji sita karibu na Pori la Akiba la Rungwa ulionyesha kuwa umbali wa eneo la hifadhi ulikuwa ishara kubwa ya upotevu wa mazao, ambapo vijiji vilivyokuwa karibu na hifadhi viliathirika zaidi kuliko vijiji vilivyoko mbali na hifadhi. Utafiti huu pia uliweza kutambua uhamiaji wa wafugaji wa kabila la wasukuma kama moja ya sababu zinazopelekea migogoro baina ya watu na tembo, kwa sababu wahamiaji (ambao walikuwa wakilima jirani na mipaka ya Mapori ya Akiba) walikuwa katika hatari zaidi ya mazao yao kuliwa na tembo kuliko wenyeji (Wilbright 2016).
Tathmini hii hujenga juu ya kazi ya awali ya kutoa ufahamu zaidi juu ya madhara ya tembo katika vijiji vinavyopakana na mipaka ya Pori la Akiba ili kuwajulisha mikakati ya kupunguza athari zinazosababishwa na tembo. Ni matumaini yetu kuwa ripoti hii itahamasisha kwa kiasi kikubwa ushirikiano kati ya jamii zinazoishi kando ya Mapori ya Akiba ya Rungwa, Kizigo na Muhesi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori, Serikali ya Wilaya na ya Mkoa, na mashirika ya uhifadhi katika kufanya kazi ili kufanikisha mshikamano baina ya watu na tembo katika mazingira ya Rungwa.
1.1 Malengo
1. Kutambua aina na mgawanyo wa muingiliano baina ya watu na tembo 2. Kutambua maeneo yanayopata migogoro kwa kiasi kikubwa 3. Kuelewa jinsi uongozi wa kijiji na wakulima wanavyosimamia muingiliano baina ya tembo na watu. 4. Kukusanya taarifa kuhusu shoroba na mapito ya tembo. 5. Kupata ufahamu juu ya maoni ya jamii kuhusu tembo na mamlaka ya mapori ya akiba. 6. Kutoa mapendekezo juu ya usimamizi wa muingiliano baina ya watu na tembo
3
1.2 Maeneo yaliyofanyiwa utafiti
Utafiti huu ulifanywa katika vijiji tisa ndani ya wilaya ya Manyoni (mkoa wa Singida) vilivyoko kando ya mpaka wa magharibi wa Mapori ya Akiba ya Rungwa, Kizigo na Muhesi (Jedwali 1). Hifadhi hizi ni sehemu ya eneo la mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa (wenye eneo lipatalo 45,000 km2), ambapo mwaka 2015 iliofanyika sensa ya Tembo na kupata idadi inayookadiriwa kuwa 15,000, na hii ni kufuatia kushuka kwa idadi hiyo kutoka Tembo 36,000 mwaka 2006 kutokana na ujangili kwaajili ya meno ya Tembo (TAWIRI 2015). Pori la Akiba la Rungwa lilianzishwa mwaka 1951 na lina ukubwa wa kilomita za mraba 9,000. Hifadhi hii inaundwa na vilima vilivyochanganyikana na maeneo machache ya misitu kandokando ya mito katika bonde la Mto Mpera. Pori la Akiba la Kizigo lilianzishwa mwaka 1982 na lina ukubwa wa kilomita za mraba 4,000. Pori la Akiba la Muhesi lina ukubwa wa kilomita za mraba 2000 na lilianzishwa mwaka 1994. Mapori ya Akiba ya Kizigo na Muhesi yana uoto wa miombo, pamoja na nyasi, miamba iliyojitokeza, na mabonde ya kandokando ya mito. Mapori ya Akiba ya Rungwa, Kizigo na Muhesi yanasimamiwa na Idara ya Wanyamapori (Wildlife Division). Vikwazo vikuu katika hifadhi hizi ni pamoja na kuvamiwa na watu, matumizi mabaya ya maji, moto usiosimamiwa, malisho yasiyokuwa na udhibiti, uwindaji haramu na migogoro baina ya watu na wanyamapori (Coppolillo 2004, Wilbright 2016).
Ramani ya vijiji vilivyofanyiwa tafiti
4
Sensa ya Tanzania ya mwaka 2012 ilionyesha kuwa wilaya ya Manyoni ilikuwa na idadi ya watu 296,763
kutoka katika kabila sita tofauti ikiwa ni pamoja na Nyiramba, Nyaturu, Sukuma, Mang'ati, Barabaig na
Hadzabe. Utafiti wetu juu ya viongozi wa vijiji ulionyesha kuwa vijiji vingi vinajikita katika kilimo na
ufugaji, pamoja na ukusanyaji wa asali. Mazao makuu yanayolimwa ni pamoja na mahindi, alizeti,
tumbaku, karanga, viazi, mchele, karanga, tikiti maji na mtama (Singida Region Socio-economic Profile
1997). Asilimia ya kaya wanazoishi chini ya kiwango cha umaskini katika mkoa wa Singida ni asilimia 49
(URT 2005).
Jedwali 1. Idadi ya watu katika vijiji mbalimbali vilivyofanyiwa utafiti kuzunguka Mapori ya Akiba ya
Rungwa-Kizigo-Muhesi (chanzo: mahojiano na viongozi wa vijijii)
Jina la kijiji Idadi ya watu
mwaka 2016
Kayui 17560
Makale 3077
Dorotto 12849
Itagata 4916
Mitundu 23000
Kalangali 2050
Rungwa 6300/6400
Kintanula 3089
Mwamagembe 17568
2. Mbinu Zilizotumika Dodoso za tafiti zilifanyika ndani ya vijiji tisa mnamo tarehe 25 mwezi wa nane hadi tarehe 2 mwezi wa
tisa mwaka 2016 (Jedwali 2). Chaguzi za vijiji zilitolewa taarifa na Meneja Mkuu wa Pori la Akiba ya
Rungwa Bwana S. Kabanda ambaye aliainisha sehemu hatarishi zenye migogoro baina ya watu na tembo.
Barua ya ruhusa ya kufanya tafiti za dodoso ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Kutoka Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni. Kopi ilitolewa kwa viongozi wa vijiji.
Jedwali 2. Vijiji vilivyofanyiwa tafiti
Kijiji Tarehe ya Tafiti Pori la Akiba la jirani Idadi ya Dodoso
Dorotto 26/08/2016 Muhesi 11
Itagata 27/08/2016 Muhesi 9
Kayui 25/08/2016 Muhesi 6
Makale 25/08/2016 Muhesi 7
Mitundu 27/08/2016 Muhesi 8
Kalangali 01/09/2016 Kizigo 8
Mwamagembe 31/08/2016 Kizigo/Rungwa 11
Kintanula 30/08/2016 Rungwa 12
Rungwa 29/08/2016, 02/09/2016
Rungwa 23
5
Aina mbili za dodoso zilitumika, moja kwa viongozi wa vijiji na ya pili kwa wakulima. Jumla ya wahojiwa
95 walihojiwa, ikiwemo viongozi wa vijiji 12 (wenyeviti wa vijiji, vitongoji na watendaji wa vijiji) na
wakulima 83 ndani ya vijiji tisa (kiiambatinisho 1). Angalau kiongozi mmoja wa kijiji na wakulima sita
walihojiwa kila kijiji. Kwa wastani wa dodoso kumi zilifanyika kwa kila kijiji.
Dodoso (ambazo zinapatikana kwa maombi) zilizofanyika kutadhimini muingiliano baina ya watu na
tembo na mitazamo ya watu kuhusu mahusiano baina ya watu na tembo. Wahojiwa waliulizwa maswali
kuainisha aina tofauti za madhara ya tembo yanayotokea. Dodoso pia zilijumuishwa maswali kuhusu ni
kwa namna gani kwa sasa viongozi wa vijiji na wakulima wanadhibiti madhara ya tembo. Pia dodoso
ilikuwa na maswali kuhusu ufugaji wa nyuki na masoko ya asali. Vipengele vingine vya dodoso ni pamoja
na maswali kuhusu misafara ya tembo na maeneo ya mapito ya tembo, na mawazo ya jamii kuhusu
tembo na maeneo ya uhifadhi.
Dodoso zilifanyika na watafiati wawili kutoka STEP: Bwana Kephania Mwaviko na Bi. Rehema John. Timu
hii inauzoefu mzuri wa tafiti za kijamii na ujuzi wakufanya mahojiano, pamoja na jinsi ya kuhakikisha
ridhaa ya watu, kuhudhulia bila malipo na kufanya mahojiano bila Kuchukua majina ya wahojiwa,
kuelezea malengo ya tafiti, kuongeza dodoso. Wahojiwa walichaguliwa kwa kufanya matembezi kwa
kutumia taratibu za sampuli, wahojiwa kuanzia mwisho mwa kijiji na kutembea kurudi nyuma, na
kuchagua kila baada ya nyumba ya tatu kwa mahojiano. Mahojiano yote yalifanyika kwa Kiswahili na
majibu yaliandikwa kwenye karatasi ya dodoso. Uingizaji taarifa na uchambuzi ulifanywa kwakutumia
mfumo wa takwimu wa Sayansi ya Jamii (SPSS-21) Software na Microsoft Excel. Watafiti walipima
kiwango cha ushiriki na uelewa wa dodoso kwa wahojiwa katika vipimo vya 1 mpaka 5 (1 ikiwa kiwango
kidogo cha kushiriki/kuelewa, na 5 ikiwa ni kiwango kikubwa cha kushiriki). Kiwango cha ushiriki kutoka
kwa viongozi wa kijiji na wakulima kilifika wastani wa 4 na 3.8, na ilikuwa ni kiwango kizuri. Kiwango cha
uelewa cha wastani wa 4.1 kwa viongozi wa kijiji na 3.7 kwa wakulima, pia kilikuwa ni kizuri.
3. Matokeo 3.1 Mgawanyiko na Aina Mbalimbali za Athari za Tembo
Vijiji vitatu (Rungwa, Dorotto, na Kintanula) viliripotiwa kuwa na kiwango kikubwa cha upotevu wa
mazao kutokana na wanyamapori (Jedwali 3) na athari za mara kwa mara za tembo (Jedwali 4). Kijiji
kimoja (Itagata) kililipotiwa kuwa na athari za tembo za kiwango cha chini. Vijiji vitano viliripotiwa kuwa
kiasi cha wanyamapori kusababisha upotevu wa mazao na athari za tembo ambazo zilionekana kwa kiasi
kidogo. Vijiji vya Rungwa na Dorotto vilitoa ripoti ya namba kubwa ya matukio ya upotevu wa mazao na
misafara ya mara kwa mara ya tembo (Jedwali 5). Kuvunjwa kwa maghala ya kuhifadhi mazao iliripotiwa
kwa kijiji cha Rungwa pekee. Watu kujeruhiwa na vifo vitokanavyo na tembo iliripotiwa na vijiji viwili
(Itagata na Dorotto), lakini ilitokea mara chache. Hakuna kijiji kilitoa taarifa ya matukio ya mauaji ya
mifugo inayosababishwa na tembo, wala tembo kuuawa. Viongozi wa vijiji Dorotto, Rungwa na Itagata
walitoa taarifa za athari za tembo kwa wafugaji ndani ya vijiji vyao. Walielezea kwamba watu na tembo
wanashindania malisho ya mifugo na vyanzo vya maji ndani ya eneo la kijiji (visima). Wafugaji pia
wameripotiwa kuwa wamehamisha makazi yao kwa kuofia kuathiriwa na tembo.
6
Jedwali 3. Ni kwa kiasi gani upotevu wa mazao unatokea kutoka na wanyama pori ndani ya kijiji?
Kijiji Hakuna tatizo
Kwa kiasi kidogo
Sifahamu Kwa kiasi kikubwa
Kwa kiasi kikubwa sana
Makale 0 75 0 25 0
Mitundu 0 75 0 25 0
Kalangali 0 75 13 0 13
Itagata 0 44 0 33 22
Mwamagembe 0 45 0 27 27
Kayui 17 33 0 17 33
Dorotto 9 0 0 18 73
Kintanula 0 0 0 25 75
Rungwa 0 0 0 0 100
Jedwali 4. Ni kwa jinsi gani migogoro ya watu na tembo ipo ndani ya kijiji? (majibu kwa %)
Kijiji Hakuna tatizo
Kwa kiasi kidogo
Sifahamu Kwa kiasi kikubwa
Kwa kiasi kikubwa sana
Kalangali 50 50 0 0 0
Kayui 50 33 0 17 0
Makale 0 88 0 13 0
Mitundu 0 88 0 13 0
Mwamagembe 36 45 0 9 9
Itagata 0 33 0 33 33
Kintanula 0 33 0 17 50
Dorotto 0 0 0 9 91
Rungwa 0 0 0 0 100
Jedwali 5. Aina za madhara ya tembo na mzunguko wake (majibu yaliyotolewa na wahojiwa wengi)
Kijiji Misafara ya tembo
Upotevu wa mazao
Kuvunjwa kwa maghala ya chakula
Watu kujeruhiwa/ vifo
Mauaji ya mifugo
Tembo kuuawa/ kujeruhiwa
Rungwa > Mara 5 kwa mwaka
> Mara 5 kwa mwaka
> Mara 5 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Dorotto > Mara 5 kwa mwaka
> Mara 5 kwa mwaka
Mara 5 kwa mwaka
<Mara 1 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Kintanula Mara 1-5 kwa mwaka
Mara 1-5 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Itagata Mara 1-5 kwa mwaka
> Mara 5 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
< Mara 1 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijulikani
Mwamagembe Mara 1-5 kwa mwaka
< Mara 1 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Mitundu < Mara 1 kwa mwaka
< Mara 1 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Kayui Mara1-5 kwa mwaka
Mara 1-5 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
7
Kijiji Misafara ya tembo
Upotevu wa mazao
Upotevu wa maghala ya chakula
Watu kujeruhiwa/ vifo
Mauaji ya mifugo
Tembo kuuawa/ kujeruhiwa
Kalangali < Mara 1 kwa mwaka
< Mara 1 kwa mwaka
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Makale Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Haijawahi kutokea
Upotevu wa tembo kwenye maghala ya kuhifadhi mazao na kuvunjwa kwa paa za nyumba ndani ya kijiji
cha Rungwa, mwezi wa tisa 2016 (Picha na K. Mwaviko)
3.2 Kiwango cha Upotevu wa Mazao Unaosababishwa na Tembo na Misafara ya Tembo
Aina ya wanyamapori wanne wakuu waliainishwa kuhusika na upotevu wa mazao katika eneo la utafiti ni tembo, nguruwe pori, nyani na tumbili. Jumla ya spishi 14 yaliainishwa kusababisha upotevu wa mazao. Upotevu wa mazao kutokana na tembo ilionekana kuathiri zaidi zao la mahindi, ikifuatiwa na viazi pamoja na ulezi. Katika eneo la utafiti, asilimia 56% ya wahojiwa walitoa taarifa kuwa upotevu wa mazao kutokana na tembo unatokea kipindi cha masika na kipindi cha mavuno, wakati asilimia 36% ya wahojiwa walitoa taarifa kuwa upotevu wa mazao unatokea kipindi cha kiangazi na masika. Vijiji vya Rungwa na Dorotto vilionekana kuwa tembo ni mnyama namba moja anayesababisha upotevu wa mazao, uzoefu unaonesha watu wanakutana na tembo mara nyingi. Wahojiwa walitoa taarifa kuwa upotevu wa mazao kutokana na tembo ulianza miaka kumi iliyopita, na kiwango cha upotevu kinazidi kuongezeka. Vijiji hivi vilitoa taarifa ya upotevu wa mazao unaosababishwa na tembo kutoka 2015 na 2016, na ni zaidi ya matukio matano ya upotevu wa mazao na ndani ya kijiji kwa mwaka (Jedwali 5). Kiukweli, wahojiwa wengi ndani ya kijiji walitoa taarifa kuwa upotevu wa mazao kutokana na tembo yanatokea mara nyingi kwa mwaka (Jedwali 8). Vijiji vya Kintanula na Itagata pia vilimuweka tembo kama ni aina la wanyama linalosababisha upotevu wa mazao, lakini uzoefu unaonesha sio mara nyingi ukilinganisha vijiji vya Rungwa na Dorotto. Vijiji hivi pia vilitoa taarifa ya upotevu wa mazao kuanza kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, na matukio ya upotevu wa mazao kati ya mwaka 2015 na 2016. Wahojiwa wengi walitoa taarifa kuwa idadi ya matukio ya upotevu wa mazao inaongezeka. Wahojiwa walikadilria kuwa na misafara ya tembo 4.3 (Kintanula) na 3 (Itagata) kwa mwaka, inachukuliwa ni ndogo kuliko Rungwa na Dorotto. Mwamagembe, Mitundi na
8
Kayui walimuweka tembo kama ni mnyama namba tatu au ya nne yanayosababisha upotevu wa mazao. Mitundi na Kayui havikutoa taarifa yeyote ya misafara ya tembo ndani ya mwaka 2016, na kilitoa taarifa ya wastani ya misafara mmoja kwa mwaka. Mwamagembe kilitoa taarifa ya upotevu wa mazao ndani ya mwaka 2016 (misafara 1.3) na mwaka 2015 (1.7), na wastani mdogo isiyozidi misafara tatu ya tembo kwa mwaka. Vijiji vya Kalangali na Makale kwaujumla havijazulika na tembo na havikuambatanishwa kwenye Jedwali 8. Jedwali 6. Kwa jinsi gani Tembo amewekwa kiwango tofauti na wanyama wengine wanayosababisha upotevu wa mazao (kwa eneo lote la utafiti)
Kiwango Aina la mnyama
1 Tembo
2 Nguruwe pori
3 Tumbili
4 Kudu
5 Pofu
6 Ndege
7 Pundamilia
8 Nungunungu
9 Kicheche
10 Kakakuona
11 Nyati
12 Ngiri
13 Swala pala
14 Ngiri
Jedwali 7. Mazao makuu yanayoathiriwa na tembo (kwa eneo lote la utafiti)
Kiwango Mazao
1 Mahindi
2 Viazi
3 Ulezi
4 Karanga
5 Alizeti
6 Miwa
7 Maboga
8 Mpunga
9 Mihogo
10 Nyanya
11 Tikiti
12 Dengu
13 Ndizi
14 Mtama
15 Nyanya
9
Jedwali 8. Kiwango cha mfululizo wa tembo kusababisha upotevu wa mazao
1. Kiwango cha upotevu wa mazao kinachosababishwa na tembo tofauti na aina nyingine ya wanyamapori
Kijiji Kiwango cha tembo1
Lini upotevu wa mazao ulianza
Misafara ya mwisho ya tembo
Kipindi cha upotevu wa mazao
Kiwango cha upotevu wa mazao
Idadi ya misafara ya tembo kwa mwaka (wastani)
Misafara ya tembo 2016 (wastani)
Misafara ya tembo 2015 (wastani)
chanzo
Rungwa 1 > Miaka 10 iliyopita 2016 Kipindi cha mavuno
Imeongezeka sana Kila siku Kila siku Kila siku Pori la Akiba
Dorotto 1 > Miaka 10 iliyopita 2016 Kipindi cha mavuno
Imeongezeka kidogo Kila siku Kila siku Kila siku Pori la Akiba
Kintanula 1 > Miaka 10 iliyopita 2016
Kipindi cha masika na mavuno
Imeongezeka sana 4.3 3.25 3.7 Pori la Akiba
Itagata 1 > Miaka 10 iliyopita 2016 Kipindi cha masika Haijulikani 3.4 2.2 2.9 Pori la Akiba
Mwamagembe 4 > Miaka 10 iliyopita 2016 Kipindi cha masika
Imeongezeka kidogo 2.9 1.3 1.7 Pori la Akiba
Mitundu 3 Miaka 0-10 iliyopita 2015 Kipindi cha masika
Imepungua sana 1 0 1
Pori la Akiba Sikonge-Tabora
Kayui 3 Miaka 0-5 iliyopita Haijulikani Kipindi cha masika
Imepungua sana 1.3 0 4 Pori la Akiba
10
Ramani inayoonyesha vijiji ambavyo vinahitaji kipaumbele kwenye jitihada za kukabaliana na athari za
tembo
3.3 Usimamizi na Uzuiaji
Kwa ujumla, mitazamo ya wahojiwa ni kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii, Serikali Kuu na Mapori ya
Akiba wanawajibika na tembo na kuzuia madhara hasi ya tembo (Jedwali 9). Ni wahojiwa wachache
waliona Serikali za vijiji na jamii wanawajibu wa kuwalinda tembo na kuzuia madhara hasi yatokanayo na
tembo. Miongoni mwa wahojiwa wengi waliona vitengo hivi havikuwajibika vizuri zaidi (Jedwali 10)
katika kuwasimamia tembo na madhara yao. Hata hivyo, wahojiwa walitoa taarifa kwamba mahusiano
kati ya jamii na Pori la akiba yalikuwa mazuri sana (Jedwali 11)
Jedwali 9. Ni akina nani wanawajibika na tembo?
Kiwango Wakala
1 Wizara ya Maliasili na Utalii
2 Serikali Kuu
3 Mapori ya Akiba
4 Wanakijiji
5 Serikali ya Kijiji
11
Jedwali 10. Ni kwa jinsi gani Mamlaka zinazohusika zinafanya kazi?
Kiwango cha utendaji kwa mamlaka % Mwitikio
Mbaya sana 32
Mbaya 43
Kotekote 5
Mzuri 18
Mzuri sana 1
Jedwali 11. Mitazamo juu ya mahusiano kati ya Kijiji na Mamlaka ya Pori la Akiba
Mahusiano na Pori la Akiba % Mwitikio
Mabaya sana 17
Mabaya 4
kotekote 5
Mazuri 14
Mazuri sana 57
Sifahamu 2
Wahojiwa wengi (64%) walionyesha kuwa juhudi za kuzuia zililenga kupunguza upotevu wa mazao, kwa wakulima kuanzia chini kwenda kati (Jedwali 12). Pia kwenye vijiji hivyo kuna vijiji vilivyoathiriwa na migogoro ya watu na tembo (Rungwa na Dorotto) mawazo juu ya kiwango cha jiitihada ziligawanywa, kwa makadirio sawa ya idadi ya wahojiwa walitoa taarifa ya juhudi hafifu kama walivotoa taarifa za kati kwenda jiitihada za juu. Sababu kuu mbili kwa jiitihada za chini za kuzuia upotevu wa mazao, ni mkwamva watu walikuwa na hofu juu ya tembo na ufahamu kidogo kuhusiana na njia sahihi za uzuiaji. Njia kuu zinazotumika kwa sasa ni kupiga kelele, moto na ulinzi wakati wa usiku (Jedwali 13). Jedwali 12. Juhudi za wakulima za kuzuia upotevu wa mazao
Juhudi za kuzuia % Mwitikio
Hakuna jitihada 26
Jiitihada kidogo 32
Jiitihada za kati 32
Jiitihada kubwa 11
Jedwali 13. Njia zinazotumika na wakulima kukabiliana na tembo
Njia % Mwitikio
Kelele 84
Moto 56
Kulinda mashamba 56
Kutoa taarifa kwa mamlaka 11
Fensi 4
12
Wengi wao wa wahojiwa (66%) waliona kuna umuhimu mkubwa kuboresha mahusiano kati ya watu na tembo ndani ya kijiji chao (Jedwali 14). Wazo hili lilitamkwa kwa mkazo mkubwa vijiji vya Rungwa, Dorotto, na Itagata. Kwa ujumla, kuna hisia chanya kwamba migogoro ya watu na tembo inaweza kushughulikiwa (Jedwali 15), na 62% ya wahojiwa walisema kwamba kuzuia migogoro ya tembo na watu inawezekana. Mawazo yaliyojirudia kwaajili ya njia za uzuiaji miongoni mwao wahojiwa ilikuwa ni ulinzi wa mashamba na mipaka ya Mapori ya Akiba, kuwatumia maaskari kuwafukuza tembo, kujenga fensi na vizuizi vingine kunzunguka mashamba, na Serikali kuchukua hatua (Jedwali 16). Jedwali 14. Maoni juu ya kama migogoro dhidi ya watu na tembo inaweza kushughulikiwa
Je ni muhimu kushughulikia migogoro ya tembo na watu? % Mwitikio
Sio muhimu 4
Muhimu kidogo 3
Sifahamu 3
Muhimu 25
Muhimu sana 66
Jedwali 15. Imani juu ya uwezekano wa kukabiliana na migogoro kati ya watu na tembo
Je inawezekana kukabiliana na migogoro baina ya tembo na watu? % Mwitikio
Haiwezekani kabisa 22
Inawezekani kwa kiasi 7
Sifahamu 9
Mara nyingi inawezekana 13
Inawezekana sana 49
Jedwali 16. Njia zilizo pendekezwa kutumika kukabiliana na tatizo
Njia za kukabiliana % Mwitikio
Kulinda mashamba na Mipaka ya Mapori ya Akiba 23
Askari kuwafukuzia tembo 19
Fensi na vizingiti vingine 18
Serikali kuchukua hatua 11
Elimu ya uhifadhi 9
Sifahamu 9
Askari kuwaua tembo 4
Kutoa taarifa kwenye mamlaka husika 3
Kuwapa uwezo wanakijiji kuwafukuzia mbali tembo 3
Shoroba ya tembo kuachwa wazi 1
13
3.4 Maoni Juu ya Tembo na Mwingiliano Baina ya Watu na Tembo
Wahojiwa waliulizwa kuhusu ukubwa wa madhara tofauti ya tembo (Jedwali 17). Wahojiwa wengi (60%)
walisema misafara ya tembo ndani ya kijiji mbali na makazi halikuwa tatizo. Zaidi ya theluthi mbili ya
wahojiwa walisema upotevu wa mazao unaosababishwa na tembo, kuvunjwa kwa maghala ya chakula,
na misafara ya tembo kupita karibu na makazi ya watu lilikuwa ni tatizo kubwa sana. Kwa kuongezea,
73% ya wahojiwa walifikiri kwamba kuwaua tembo kwa ajili ya upotevu wa mazao lilikuwa ni tatizo
kubwa sana.
Jedwali 17. Mtazamo juu ya ukubwa wa athari za tembo
Sio tatizo
Ni tatizo kidogo Kotekote
Ni tatizo kubwa
Ni tatizo kubwa sana Sifahamu
Tembo kupita ndani ya kijiji mbali na makazi ya watu 60 5 1 12 22 0 Tembo kupita ndani ya kijiji jirani na makazi ya watu 2 4 0 24 67 1
Tembo kuharibu mazao 1 1 0 20 77 0 Tembo kuharibu maghala ya chakula 2 1 0 21 69 5 Kuuwa tembo wakati wanapovamia mazao 5 2 7 26 47 11
Kwa ujumla, wahojiwa wengi walidhani kwa sasa idadi ya tembo kwenye aridhi ya kijiji inazidi kuongezeka, wakati wahojiwa waliowengi hawakuwa na ufahamu wa idadi ya tembo kwenye Mapori ya Akiba na Tanzania kwa ujumla. Waliulizwa kuhusu idadi inayohitajika ya tembo, na 73% ya wahojiwa walisema wangehitaji tembo wapungue kwa kiasi kikubwa kwenye aridhi ya kijiji. Kwa heshima ya Mapori ya Akiba na nchi nzima kwa ujumla, 78% na 83% ya wahojiwa walihitaji namba ya tembo kuongezeka.
Jedwali 18. Mtazamo juu ya idadi ya sasa ya tembo
Mwenendo wa idadi ya tembo
Aridhi ya Kijiji
Pori la Akiba
Nchi
Inapungua sana 21 11 25
Inapungua kidogo 6 5 1
Imara 16 2 0
Inaongezeka kidogo 11 2 4
Inaongezeka sana 38 34 20
Sifahamu 8 46 48
Jedwali 19. Mtazamo juu ya idadi ya tembo inayotakiwa
Idadi inayohitajika Aridhi ya kijiji
Pori la Akiba
Nchi
Ipungue sana 73 12 6
Ipungue kidogo 1 2 0
Ibaki iliyopo 6 0 1
Iongezeke kidogo 4 1 1
Iongezeke sana 11 77 82
Sifahamu 5 7 8
14
Japokuwa kuna wastani wa juu wa migogoro kati ya watu na tembo, mitazamo ya jamii kuhusu tembo
bado ni mtazamo chanya. Karibia ya theluthi mbili ya wahojiwa walikubali kuwa tembo ni mnyama mzuri.
Pia 56% ya wahojiwa walikubali kwa kuunga mkono kuwa tembo ni wa muhimu kwenye mazingira, na
93% walikubali na kuunga mkono kuwa tembo wanaongeza pato la Taifa kwa kupitia utalii. Utafiti wa
vijiji sita vinavyokaribiana na Pori la Akiba la Rungwa (Wilbright 2016) vilevile ilionyesha kwamba watu
wengi walikuwa na uelewa wa faida za uhifadhi, hasa mapato yatokanayo na utalii wa kuwinda
yanayofanyika kwenye Mapori ya Akiba. Kati ya mwaka wa fedha 2011/2012 na 2014/2015, Wilaya ya
Manyoni imeweza kupata Shilingi za Kitanzania 324,962,413 (ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani
147,710) kutoka kwenye mapato ya uwindaji kwenda kufadhili mahitaji ya jamii (Wilbright 2016). Kwa
kuongezea, 87% ya wahojiwa walikubali kuwa kuna umuhimu wa kuwahifadhi tembo. Hata hivyo, 71% ya
wahojiwa walikubali kuunga mkono kuwa tembo wanawapa watu gharama, wakati 55% walikubaliana
kuwa tembo wanawapa watu binafsi faida. Zaidi ya nusu ya wahojiwa walikataa kuwa mahusiano kati ya
tembo na watu kuwa ni mazuri ndani ya kijiji.
Jedwali 20. Mitazamo juu ya kauli mbalimbali kuhusu tembo na mshikamano
Haikubaliki kabisa
Haikubaliki Sifungamani na upande wowote
Inakubalika Inakubalika sana
Sifahamu
Tembo ni mnyama mzuri 24 3 1 31 33 7
Tembo wananipa hasara 17 7 0 25 46 3
Tembo wananipa faida 32 4 0 29 26 7 Tembo ni muhimu kwa uhifadhi wa mazingira 23 2 0 28 38 7 Tembo wana faida kwa watu kwasababu ni kivutio cha utalii 1 0 0 38 55 2 Ni muhimu kuwahifadhi tembo 4 2 0 42 45 5 Mahusiano kati ya tembo na watu ndani ya kijiji ni mazuri 49 5 3 13 17 11
3.5 Shoroba na Misafara ya Tembo
Kulingana na wahojiwa 71%, tembo wanaokuja mara kwa mara kwenye kijiji chao wanatoka Mapori ya Akiba ya Rungwa, Kizigo na Muhesi. Kiasi kidogo cha wahojiwa walisema kwamba tembo walikuwa wakitoka upande wa Tabora (Wilaya ya Sikonge, vijiji vya Kilumbi na Kihombe).
Jedwali 21. Mahali ambapo tembo ilisemekana wanatoka
Chanzo % Wahojiwa
Pori la Akiba la Rungwa-Kizigo-Muhesi 71
Vijiji vya jirani 3
Wilaya ya Sikonge, Tabora 1
Vijiji vya Kilumbi na Kihombo (Tabora) 1
Rungwa North Open Area 1
15
Ndani ya vijiji saba, zaidi ya nusu ya wahojiwa wanafahamu eneo la shoroba au njia za tembo, na wanafikiri kwa sasa bado zinatumika na tembo (Jedwali 22-23). Wahojiwa ndani ya vijiji vitano vinaonyesha kwamba matumizi ya hivi karibuni ya nji za tembo ni mwaka 2016, na ndani ya mwaka 2015 ndani ya vijiji viwili (Jedwali 24). Kila kijiji kilitoa maelezo ya mdomo ya njia za tembo na shoroba (Jedwali 25). Jedwali 22. Je unafahamu njia zinazotumika na tembo karibu na kijiji chako? (% majibu)
Kijiji namba Ndiyo Sifahamu
Dorotto 0 91 9
Itagata 33 44 22
Kalangali 50 50 0
Kayui 33 67 0
Kintanula 25 67 8
Makale 71 29 0
Mitundu 25 75 0
Mwamagembe 36 55 9
Rungwa 9 74 17
Jedwali 23. Njia hizi kwa sasa bado zinatumika na tembo?
Kijiji Namba Ndiyo Sifahamu
Dorotto 0 100 0
Itagata 0 100 0
Kalangali 0 50 50
Kayui 0 50 50
Kintanula 0 100 0
Makale 0 100 0
Mitundu 0 83 17
Mwamagembe 0 100 0
Rungwa 0 100 0
Jedwali 24. Ni lini ilikuwa mara ya mwisho misafara ya tembo kupita katika njia hizi?
Kijiji 2014 2015 2016
Dorotto 0 0 100
Itagata 0 25 75
Kalangali 50 0 50
Kayui 0 67 33
Kintanula 0 0 100
Makale 0 0 100
Mitundu 17 50 33
Mwamagembe 17 17 67
Rungwa 0 0 100
16
Jedwali 25. Maelezo kuhusu njia na shoroba za tembo
Dorotto
Legeza mwendo, charcoaling camp (kambi ya mkaa)
Dalabeta-Msimbehe-Mkwegi-Ipunguli
Damweru-Kahomwe-Dorotto katikati-Msisi-Mwakitanda-Mkwegi-Ipunguli
Ipunguli, Mwakitanda
Ipunguli, Kenyekenye, Dorotto
Misisi, Kahomwee
Simbanguru-Chikola-Kiula-Mugandu-Dorotto katikati mwa upande wa kaskazini
Itagata
Italia-Mwakita-Muhesi
Mkwegi, charcoaling camp (kambi ya mkaa)
Pori la Akiba-Itagata-Tabora Reserve
Pori la Akiba Muhesi-Itagata-Ukimbu
Kalangali
Balabala ya Salada
Kati ya Kintanula na Tandamilomo
Tabora -Kalangali
Kayui
Isanzu na Mihama
Njarumono-Lulanga-Chaya
Njarumono -Chang'ombe-Kigoma-Mkwira
Njarumono-Itagata-Chaya
Kintanula
Itaga-mabonde-Miungu
Mwinuko wa Mkolole, Matumaini
Mpanda, Miungu, Kintanulayazamani
Pori la akiba -Mkolole (kanda)- Sehemu ya wazi kusini mwa Rungwa
Pori la Akiba -Mwabhuki-Kintanula
Pori la akiba-Mwauki (Kanda)- Sehemu ya wazi Kusini mwa Rungwa
Makale
Kaselya, Misonge
Matagata-Misiu-pori la akiba
Mitundu
Makale, Ipanduka
Pori la akiba-Mahinya-Makuga-Mitundu-Nzinge – Hifadhi
Pori la akiba-Itandamilo-Mitundu
Kati ya Makale na Mitundu
Mwamagembe
Pori la Akiba - Mikese (Shoroba) – Mwamagembe
17
Rungwa
Pori la akiba- Cemetery (Makaburini) – Kijiji cha Rungwa
Pori la Akiba- Daraja la mkola A – Kijiji cha Rungwa
Itaga –Shule ya sekondari mkola
Itaga, Itangalala
Karibu na kanisa, Mkola B
Mimalaupene-Mansega
Msufini
Mkola A, Mahikwi
Station Useli
Njia ya tembo, kijiji cha Rungwa
18
4. Mapendekezo
4.1 Maeneo ya Kipawombele Kufanyiwa Jitihada
Uchaguzi wa maeneo sahihi ya kukabiliana nayo na mbinu ni sanjari na historia ya hivi karibuni na ukubwa wa athari za tembo, ukaribu wa njia za tembo, upokeaji wa jamii kushirikiana kama wahojiwa kufanya kazi ya uhifadhi ni mzuri. Kwa kuzingatia uchunguzi wa upotevu wa mazao unaosababishwa na tembo na misafara ya tembo, tunapendekeza vijiji vinne ambavyo ni muhimu kukabiliana na migogoro ya watu na tembo:
Kipawombele namba 1: Rungwa na Dorotto
Kipawombele namba 2: Kintanula na Itagata
4.2 Mwingiliano Baina ya Watu na Tembo Kijiji cha Rungwa
Kulingana na matokeo ya tafiti hii na majadiliano yaliyofanyika kati ya WCS pamoja na uongozi wa Pori la
Akiba la Rungwa, STEP ilipendekeza kuelekeza jitihada zakupunguza athari za tembo ndani ya kijiji cha
Rungwa, ambacho kimepakana na Makao Makuu ya Pori la Akiba la Rungwa.
Rungwa ni kijiji kilichopo kwenye uwanda wa magharibi mwa mipaka ya Pori la Akiba la Rungwa. Baada
ya kumaliza tathimini, STEP walifanya mikutano na wananchi wa vitongoji vya Mkola, Stesheni na Itaga
mnamo tarehe 15 mpaka tarehe 17 ya mwezi wa kumi mwaka 2016. Lengo kuu la mikutano hiyo ilikuwa
ni kuwasilisha majibu ya tathimini iliyofanyika na kujifunza zaidi juu ya kiwango cha mwingiliano baina ya
watu na tembo ndani ya vitongoji hivyo vinavyo pakana na Pori la Akiba la Rungwa. Kijiji cha Rungwa kina
jumla ya idadi ya wakazi wapatao elfu sita, na idadi ya kaya ikiwa ni 1200. Upotevu wa mazao na upotevu
wa maghala kutokana na tembo ulitolewa taarifa ndani ya kijiji wakati wa mikutano. Mazao makuu
yakiwa ni mahindi, viazi vitamu, karanga, na ulezi. Tembo pia waliripotiwa kuvunjwa maghala ya chakula
na kuvunjwa paa za nyumba, na kushindania malisho na maji pamoja na mifugo. Kwa sasa, juhudi dhidi
ya uhifadhi wa mazao dhidi ya tembo ni kubwa, na wakulima wanatumia njia kama vile kupiga kelele,
moto, na wakulima kuyalinda mashamba yao nyakati za usiku, na kupiga mayowe. Hata hivyo, njia hizo
zimeonekana kushindwa kuzuia na kumaliza tatizo la tembo, na sababu kubwa ikiwa watu kuogopa
tembo, na ukosefu wa elimu juu ya njia sahihi za kumzuia tembo kuharibu mazao. Japokuwa Rungwa
kuna ukosefu na uhaba mkubwa wa maji, lakini ni sehemu muhimu sana ya ufugaji wa nyuki, na hii
inaonyesha kwamba njia ya utumiaji wa fensi ya mizinga ya nyuki kutumika kuzuia upotevu wa mazao na
maghala inaweza kuwa njia sahii, kama mizinga itakuwa na nyuki na fensi kutunzwa na kuhifadhiwa
vizuri.
19
Chemchem na visima vya maji vinavyotumiwa na binadamu pamoja na tembo
Kitongoji cha Mkola
Kitongoji hiki kipo jirani sana na Pori la Akiba la Rungwa. Kitongoji kilitoa taarifa ya kiwango kikubwa cha
upotevu wa mazao, misafara mingi ya tembo kwa mwaka, upotevu wa maghala ya chakula na upotevu
wa paa za nyumba. Upotevu wa mazao unaosababishwa na tembo unatokea mwanzoni mwa kipindi cha
masika na kipindi cha kiangazi. Ndani ya mwaka 2016 zaidi ya kaya 30 waliathiriwa na upotevu wa
mazao, na maghala tisa kuvunjwa na tembo. Kukiwa hakuna matukio ya binadamu kujeruhiwa wala vifo
vya mifugo vinavyosababishwa na tembo. Sababu kuu ya misafara ya tembo kutoka kwenye Pori la Akiba
na kuingia kwenye aridhi ya kijiji ni uhaba ya maji na chakula kipindi cha kiangazi. Njia za kuzuia upotevu
zilizopendekeezwa na jamii wakati wa mikutano ni kama vile kuendelea kulinda mashamba, kuendlea
kupata msaada kwa maaskari wa Rungwa kufukuza tembo, pamoja na matumizi ya fensi.
Kitongoji cha Stesheni
Ndani ya Kitongoji hiki mwingiliano baina ya tembo na binadamu inazidi kuongezeka kutokana na ukaribu
wa Kitongoji na Pori la akiba la Rungwa, na kwa sababu hii inaonyesha umbali wa kiuhifadhi eneo
limekuwa ni tatizo la kuzuia upotevu wa mazao na uhaharibifu wa maghala ya chakula ndani ya kijiji
kutokana na ukaribu na watu wanaathiriwa zaidi ukilinganisha na watu wanaoishi mbali zaidi. Washiriki
walielezea kuwa upotevu wa mazao unatokea zaidi kipindi cha masika mpaka kipindi cha kiangazi kipindi
cha mavuno, na zaidi ya familia 37 ziliathiriwa na upotevu wa mazao. Ndani ya mwaka 2016 maghala
matatu yalivunjwa na tembo. Kukiwa hakuna matukio ya kujeruhiwa binadamu wala vifo
vilivyosababishwa na pasipo mifugo kupotea uhai kwa kusababishwa na tembo. Kwa sasa jitihada za
kuzuia upotevu wa mazao ni hafifu zinazojihusishwa na utumiaji wa njia za kimila zisizofanya kazi
kiusahihi kama vile kupiga kelele, moto na kuyalinda mashamba nyakati za usiku. Sababu kubwa ni watu
wanahofu juu ya tembo na ukosefu wa elimu kuhusu njia sahihi za kuzuia upotevu wa mazao.
Kitongoji cha Itaga
Kitongoji hiki kina sifa ya kuwa na makazi zilizoachana umbali mpaka kaya nyingine kutokana na kabila
kuu la Wasukuma ambao ni wafugaji na ni jamii inayohamahama. Katika Kitongoji hiki pia taarifa
zimeripotiwa kuwa na kiwango kikubwa cha upotevu wa mazao unaosababishwa na wanyama pori
akiwemo tembo na migogoro mingi kati ya binadamu na tembo ilianza mnamo mwaka 2012 mpaka sasa.
Familia zipatazo 15 zimeathiriwa na tembo kwa kuharibiwa mazao, kaya 3 kubomolewa, na maghala 9
kuvunjwa kabisa na mazao kuliwa mwaka 2016. Miitikio hii ilijionyesha dhahiri wakati wa mikutano
20
iliyofanyika ndani ya Kitongoji, athari za mara kwa mara na kijiji kutoa taarifa ya namba kubwa ya
upotevu wa wa mazao na misafara ya tembo kwa mwaka, kuvunjwa kwa maghala na paa. Ikiwa hakuna
taarifa za binadamu kuuawa au kujeruhiwa na tembo, na hakuna vifo vilivyosababishwa na tembo na
wala hakuna mifugo iliyopotea kwa kusababishwa na tembo. Pia viongozi wa vijiji walitoa taarifa ya watu
na tembo kugombania maji (visima) na malisho ya mifugo. Wafugaji wamekuwa wakihamisha makazi yao
kwa hofu ya kukutana na tembo. Kwa kawaida upotevu wa mazao unaanza kutokea kipindi cha masika
mwezi wa pili mpaka kipindi cha kiangazi muda wa mavuno (kati ya mwezi wa pili na mwezi wa tatu
mpaka mwezi wa kumi na moja).
4.3 Mbinu za Kukabiliana na Athari za Tembo
Vizuuizi vya tembo vyenye msingi yake mashambani na nyumbani Kwenye maeneo yenye matukio mengi ya upotevu wa mazao, tunashauuri kuwawezesha wakulima kuzuia upotevu wa mazao kwa kutumia njia zenye misingi yake mashambani kama fensi za mizinga ya nyuki, ambapo kwa uzoefu wa STEP ni njia yenye ufanisi mkubwa wa kupunguza upotevu wa mazao ambapo mizinga itakuwa na nyuki na fensi kutunzwa vizuri.Fensi ya mizinga ya nyuki inafaida zaidi na kipato kinachotokana na asali,na ushiriki wa wakulima kwenye miradi ya fensi ya mizinga ya nyuki inaweza kuongeza Uvumilivu dhidi ya tembo.Mazingira ya Rugwa yenye misitu aina ya miombo ni bora kwa ufugaji wa nyuki ,na vijiji vingi vilivyofanyiwa tafiti Rungwa ikiwemo tayari kuna sekta za ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kienyeji.Ufugaji wa nyuki pia unahamasisha ulinzi wa mazingira na vyanzo vya maji,kwakuwa nyuki wanahitaji maji na chakula ili kujiimarisha na kustawi.
Fensi ya mizinga ya nyuki Mang’ula, Udzungwa (kushoto); Mizinga ya kienyeji kijiji cha Rungwa (kulia)
Njia nyingine ya kawaida ya kuzuia tembo ni fensi ya pilipili. Kufuatana na Semina zilizotolewa na Pori la Akiba la Rungwa kuhusu matumizi ya fensi ya pilipili, fensi ya pilipili mwanzoni ilifanyiwa majaribio na wakulima wachache ndani ya kijiji cha Rungwa. Fensi hiyo ya pilipili haikuweza kuzuia tembo kuingia mashambani, na wakulima walisitisha kuitumia.
Mashamba na nyumba zinaweza kulindwa dhidi ya madhara ya tembo kwa kutumia kinyesi cha tembo kilichochanganywa na pilipili na kisha kukaushwa na kuchomwa ambapo huweza kuzalisha moshi ndani ya masaa 8 na kuzuia tembo kwa moshi unaozalishwa wenye pilipili. Matofali haya ya pilipili na kinyesi cha tembo kwa sasa yamefanyiwa majaribio na mradi wa Eco-Exit nchini Botswana. Pia, uvunjwaji wa maghala ya chakula unaweza kupunguzwa kwa kujenga maghala ya kuzuia tembo kwenye kaya. Maghala haya yanamuundo imara ambapo tembo hawataweza kuyafikia mazao kiurahisi, na pia inapunguza harufu ya chakula kutoka nnje ambayo itawavutia tembo. Maghala haya yakuzuia tembo kwasasa yamefanyiwa majaribio na Mradi wa South Luangwa Conservation Society nchini Zambia na kunaonyesha kiasi kikubwa cha mafanikio andapo maghala yatatunzwa vizuri.
21
Ghara la kuzuia tembo (kushoto); matofali ya kutengenezwa na pilipili pamoja na kinyesi cha tembo
(kulia)
Ufuatiliaji wa tembo kwa jamii
Utaratibu wa utoaji taarifa za misafara ya tembo na upotevu wa mazao utatathimiwa kwa kufuatilia
mwingiliano wa watu na tembo kwa muda mrefu, na pia kwa ajili ya kuamua maeneo ambayo ni muhimu
kuchukuliwa hatua zaidi.
Njia mbadala ya Tembo kuwapa Maji
Ukosefu wa maji kipindi cha kiangazi ndani ya eneo la Pori la Akiba la Rungwa karibu na kijiji cha Rungwa
(iliripotiwa kuwa chanzo cha maji kilicho jirani ilikuwa ni umbali wa kilometa 40) inawezekana ikawa
sababu inayopelekea tembo kutoka ndani ya hifadhi, na kwakuwa tembo wanahitaji maji kilasiku.
Kuwepo kwa njia mbadala ya vyanzo vya maji kwaajili ya tembo kupata maji ndani ya Pori la Akiba
inaweza kupunguza misafara ya tembo kwenda kwenye chem chem na visima vya kijiji kwaajili ya
kujipatia maji. Bwawa au sdimbwi la maji lakutengenezwa linaweza kujengwa ndani ya Pori la Akiba
kwamadhumuni hayo. Bwawa la maji mwanzoni lilikuwepo karibu na makao makuu ya poli mnamo
mwaka 1990 na iliripotiwa kuwa lilitumika na tembo pamoja na wanyamapori wengine, lakini bwawa hili
lilikauka baada ya mto Rungwa kubadili mkondo wake (mazungumzo binafsi na S. Kabanda). Mradi huu
utakuwa wamafanikio zaidi kama utafanikiwa kusambaza maji ya kuaminika ndani ya kijiji cha Rungwa.
Matumizi ya aridhi na mipango ya kuunganishwa na kujenga uhusiano Aidha, tunaamini kwamba mshikamano wa mda mrefu baina ya watu na tembo unapaswa kushirikisha
zaidi mipango ya matumizi ya aridhi na uudwaji wa shoroba za wanyama pori. Kusimamia misafara ya
tembo nje ya maeneo ya uhifadhi ili kupunguza upotevu wa mazao utokanao na kusambaa kwa tembo
na uhamiaji, vijiji vinaweza kuzingatia kuacha sehemu ya aridhi inayotenganisha maeneo ya uhifadhi na
maeneo ya kijiji kwaajili ya misafara ya tembo katika maeneo ambayo yako mbali na makazi ya watu na
mashamba ya watu.
22
5. Marejeo
Coppolillo, P. (2004). A preliminary situation analysis for the Rungwa-Ruaha landscape, Tanzania. A
report to WWF International “Improving Conservation and Development within Ecoregions Programme.”
<http://www.coppolillo.com/uploads/1/1/2/3/11231708/wwf-report-situationanalysis30sep04.pdf>
Accessed 01/10/2016.
The Planning Commission of Dar es Salaam and Regional Commissioner’s Office Singida (1997) Socio-
Economic Profile of Singida Region http://www.tzonline.org/pdf/singida1.pdf Accessed 04/10/2016.
Research and Analysis Working Group (2005). Poverty and Human Development Report 2005. Poverty
Monitoring System of the Government of Tanzania. Dar es Salaam, Tanzania.
<http://www.repoa.or.tz/documents/PHDR_2005_Prelim.pdf> Accessed 01/10/2016.
Thouless CR, Dublin HT, Blanc JJ, Skinner DP, Daniel TE, Taylor RD, Maisels F, Frederick HL, Bouché PJC.
(2016). African Elephant Status Report 2016: an Update from the African Elephant Database. Occasional
Paper Series of the IUCN Species Survival Commission, No. 60 IUCN/SSC Africa Elephant Specialist Group,
IUCN, Gland, Switzerland. Vs + 309 pp.
Munuo, W. (2016) Distribution Patterns of Human Elephant Conflict in Areas Adjacent to Rungwa Game
Reserve, Tanzania. MSc Thesis submitted to the Norwegian University of Science and Technology,
Norway.