tuzo za watu tanzania 2015

8
TUZO ZA WATU TANZANIA 2015 Tuzo za watu Tanzania ni tuzo za kwanza zinazoanzishwa mahususi kwaajili ya kuwapa mashabiki wa muziki, filamu, michezo na mambo mengine jukwaa huru kuelezea mapenzi yao. Tuzo hizi zinawapa nafasi mashabiki kuwatunza wawapendao kwenye tasnia mbalimbali kuanzia muziki , filamu, radio , televisheni nk. Tuzo hizi zilitambulishwa na kuratibiwa kwa mara ya kwanza Tanzania na kampuni ya Bongo5 Media Group, chini ya mkurugenzi mtendaji, Nancy Sumari, mnamo Aprili mwaka 2014 na kuhitimishwa mwezi Juni mwaka huo. Upekee wa tuzo hizi ni kwamba majina yote ya washiriki wanaowania tuzo, yatachaguliwa na wananchi wenyewe na sio kundi la watu wachache kwenye tasnia hizo. Wananchi wenyewe ndio watawachagua washindi na hivyo kuzitofautisha tuzo hizi na tuzo zingine. Tuzo za watu zinalenga kuanzisha mchakato wa wazi wa utambuzi wa watu wenye umuhimu na mchango mahsusi katika nyanja mbalimbali waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe. Tuzo hizi zitatumika kuanzisha urithi utakaoleta hatua mpya ya heshima kwenye jamii yetu. MCHAKATO WA KUWACHAGUA WASHIRIKI NA UPIGAJI KURA Upigaji kura utaanza tarehe 26, Machii, 2015 katika vipengele 14 ambapo wananchi wenyewe watachagua majina ya washiriki. Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki tatu kutoka siku ya uzinduzi wa tuzo na majina ya watu watano walioongoza kwa kura zaidi kutoka kwenye kila kipengele watatangazwa 1

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 17-Nov-2015

8.437 views

Category:

Documents


2 download

DESCRIPTION

TUZO ZA WATU TANZANIA 2015

TRANSCRIPT

TUZO ZA WATU TANZANIA 2015

Tuzo za watu Tanzania ni tuzo za kwanza zinazoanzishwa mahususi kwaajili ya kuwapa mashabiki wa muziki, filamu, michezo na mambo mengine jukwaa huru kuelezea mapenzi yao. Tuzo hizi zinawapa nafasi mashabiki kuwatunza wawapendao kwenye tasnia mbalimbali kuanzia muziki , filamu, radio , televisheni nk.Tuzo hizi zilitambulishwa na kuratibiwa kwa mara ya kwanza Tanzania na kampuni ya Bongo5 Media Group, chini ya mkurugenzi mtendaji, Nancy Sumari, mnamo Aprili mwaka 2014 na kuhitimishwa mwezi Juni mwaka huo. Upekee wa tuzo hizi ni kwamba majina yote ya washiriki wanaowania tuzo, yatachaguliwa na wananchi wenyewe na sio kundi la watu wachache kwenye tasnia hizo. Wananchi wenyewe ndio watawachagua washindi na hivyo kuzitofautisha tuzo hizi na tuzo zingine.

Tuzo za watu zinalenga kuanzisha mchakato wa wazi wa utambuzi wa watu wenye umuhimu na mchango mahsusi katika nyanja mbalimbali waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe. Tuzo hizi zitatumika kuanzisha urithi utakaoleta hatua mpya ya heshima kwenye jamii yetu.

MCHAKATO WA KUWACHAGUA WASHIRIKI NA UPIGAJI KURA

Upigaji kura utaanza tarehe 26, Machii, 2015 katika vipengele 14 ambapo wananchi wenyewe watachagua majina ya washiriki. Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki tatu kutoka siku ya uzinduzi wa tuzo na majina ya watu watano walioongoza kwa kura zaidi kutoka kwenye kila kipengele watatangazwa

Kuanzia hapo, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele yaliyotangazwa. Wiki moja baada ya majina ya washiriki kutangazwa, mchujo mwingine utafanyika katika kila kipengele ambapo jina moja litakalopelea kura, litaondolewa, na hivyo kubakiza washindani wane katika kila kipengele.Wiki moja baadaye, mchujo utafanyika tena na kuwabakiza washiriki watatu kwenye kila kipengele walioongoza kwa kura. Washiriki wote 42 (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa mwisho, watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki mbili baada ya mchujo huo wa mwisho kufanyika.

Katika hafla hiyo, washindi katika kila kipengele watatangazwa.Kila mshindi atapokea zawadi ya fedha taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tunzo ya kuambatana na ushindi wake.

VIPENGELE NA VIGEZO/MASHARTI VYA KUZINGATIWA.Tuzo za watu mwaka 2015 zitajumuisha vipengele 11 ambavyo ni pamoja nVIfuatavyo ni vigezo vya kuteuliwa/kuingia katika vipengele 14 vya mashindano.

No.KipengeleVigezo Vya Kuzingatia

1.Mtangazaji wa redio anayependwaa. Ni lazima awe Mtanzania

b. Awe amesikika kwenye kipindi cha redio kati ya tarehe 01 mwezi Jan hadi tarehe 31 mwezi Des, 2014

c. Awe na sauti ya upekee katika uwasilishaji

d. Awavutie watu wengi katika utangazaji wake

e. Atumie lugha kwa usahihi na kuzingatia matamshi

g. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii

2.Kipindi cha redio kinachopendwaa. Kiwe kimeruka kati ya tarehe 01 mwezi Jan na tarehe 31 mwezi Des, 2014

b. Kiwe kinaeleimisha, kiburudishe na kitoe taarifa

c. Kiwe chenye kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika katika jamii

d. Kiwe cha Kitanzania

3.Mtangazaji wa kipindi cha runinga anayependwaa. Awe ni Mtanzania

b. Ni lazima awe ameonekana kwenye kipindi cha runinga kuanzia tarehe 01 mwezi Januari hadi mwezi Desemba 30 mwaka Dec 2014

c. Aonyeshe unadhifu katika muonekano wake

d. Awe na upekee katika uwasilishaji

e. Atumie lugha kwa usahihi na kuzingatia matamshi

f. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii.

4. Kipindi cha runinga kinachopendwaa. Kiwe imeruka kati ya tarehe, 01 Januari 31 Desemba 2014

b. Kiwe kinaelimisha, kiburudishe na kitoe taarifa

c. Kionyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili yanayokubalika na jamii

d. Kiwe cha Kitanzania

5.Tovuti/Blogu inayopendwaa. Iwe yenye maudhui bora, maadili na ubunifu

b. Iwe na utofauti katika muonekano wake

c. Muundo wa blogu/tovuti iridhishe mahitaji ya wasomaji

d. Iburudishe, ielimishe na kuota taarifa kwa wasomaji

e. Iwe imehaririwa na kusanifiwa kwa usahihi

f. Muonekano wa picha lazima uwe na ubora wa hali ya juu

g. Ifuate maadili hususan ya kiuandishi wa habari

h. Ionyeshe ongezeko la idadi ya wasomaji kwa nyakati tofauti.

i. Iwe hai

j. Iwe na utaratibu wa kuwashirikisha wasomaji wake mara kwa mara na kutoa maoni.

6.Muongozaji wa video za Muziki anayependwaa. Ahusishe maandhari na maneno yaliyo ndani ya wimbo husika

b. Awe mbunifu katika uchukuaji wa picha na mtiririko mzuri katika kazi yake

c. Awe Mtanzania

d. Ateke soko la watazamaji

e. Kazi yake iwe imeonekana kati ya tarehe 01 Jan- 31 Des, 2014

7.Muongozaji filamu anayependwaa. Awe Mtanzania

b. Awe mbunifu katika uchukuaji wa picha na mtiririko mzuri katika kazi yake

c. Ateke soko la watazamaji

d. Aonyesha kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii kwenye kazi yake

e. Kazi yake iwe imeonekana kati ya tarehe 01 Jan- 31 Des, 2014

8.Mwigizaji wa kike anayependwaa. Awe Mtanzania

b. Auvae uhusika stahili

c. Achangie kuikuza tasnia kupitia umahiri wake wa kuigiza

d. Awe na ushawishi wa kuvutia mashabiki

e. Kazi yake iwe imeshuhudiwa kati ya tarehe 01 Jan- 31 Des, 2014

f. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii

9.Mwigizaji wa kiume anayependwa

a. Awe Mtanzania

b. Auvae Uhusika stahili

c. Awe na ushawishi wa kuvutia mashabiki

d. Achangie kuikuza tasnia kupitia umahiri wake wa kuigiza

e. Kazi yake iwe imeshuhudiwa kati ya tarehe 01 Jan- 31 Des, 2014

f. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii

10.Mwanamuziki wa kike anayependwaa. Awe Mtanzania

b. Achangie kuikuza tasnia kupitia umahiri wake kwenye muziki

c. Kazi yake iwe imesikika kati ya tarehe 01 Jan- 31 Des, 2014

d. Awe na ushawishi wa kuwavutia mashabiki

e. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii

11.Mwanamuziki wa kiume anayependwaa. Awe Mtanzania

b. Achangie kuikuza tasnia kupitia umahiri wake kwenye muziki

c. Awe na ushawishi wa kuwavutia mashabiki

d. Kazi yake iwe imesikika kati ya tarehe 01 Jan- 31 Des, 2014

e. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii

12.Filamu inayopendwaa. Iwe na urefu wa dakika 45 au zaidi ambayo imeonekana kati ya tarehe na 01 Jan 31 Dec 2014

b. Iwe imetengenezwa Tanzania

c. Ielimishe, iburudishe na itoe taarifa

d. Iwe na maudhui bora yenye maadili

e. Iwe imeliteka soko la watazamaji

f. Iwe imekaguliwa na kupitishwa na bodi ya filamu

13.Video ya Muziki inayopendwaa. Iwe na maudhui bora yenye maadili

b. Iwe imetoka kati ya tarehe 01 Jan-31 Des, 2014

c. Iwe Imeliteka soko la watazamaji

d. Ielimishe, iburudishe na itoe taarifa

e. Iwe imetengenezwa Tanzania

14.Mfadhili maarufua. Awe ni Mtanzania

b. Mchango wake awe ameutoa nchini Tanzania

c. Mchango huo lazima awe ameutoa kati ya tarehe na 01 Jan 31 Dec 2014

d. Aonyeshe kiwango cha hali ya juu cha maadili kinachokubalika na jamii.

JINSI YA YA KUPIGA KURA

Mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika kwa njia kuu mbili. Ya kwanza ni kwa kutumia tovuti ya tuzo ambayo ni www.tuzozetu.com ambapo mpiga kura atakutana na hatua rahisi ya kupendekeza majina katika vipengele vyote 14.

Njia ya pili ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ambapo utaandika neno TZW kwenda namba 15678. Ukishafanya hivyo utaletewa Menu yenye vipengele vyote 14 vikiwa na code number yake. Kutaja ama kupendekeza jina, tuma code husika na jina kwenye namba hiyo hiyo; kwa mfano TZW1 Oliver Mtukudz8