utangulizi - hakielimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia...

8
HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016 HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016 Utangulizi HakiElimu ni shirika la kijamii ambalo lilianzishwa mwaka 2001. Dira yake ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra tunduizi. HakiElimu inatumia mbinu ya haki na usawa kwa binadamu katika elimu, na kusisitiza ubora katika kujifunza, usawa, utawala na ushiriki makini kwa wananchi katika kuboresha elimu na demokrasia. Mkakati wetu unazungumzia uwezeshwaji wa jamii katika kubadili mfumo wa shule na kuathiri utungaji wa sera na utekelezaji wake, kwa kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki, kuchochea midahalo yenye ubunifu na kushirikiana na wadau ili kuongeza ushiriki, uwajibikaji, uwazi na haki kwa jamii. HakiElimu inatambulika kwa mapana zaidi katika ufanisi wake wa kushiriki kitaifa katika masuala kuhusu demokrasia, utawala na elimu ubora. Shirika limewezesha kuanzishwa kwa mtandao wa Marafiki wa Elimu ambao wako zaidi ya 35,000, ambao wanachama wake ni mashirika ya kijamii na mtu mmoja mmoja ambao wanataka kuleta mabadiliko katika shule na jamii.

Upload: others

Post on 01-Feb-2020

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Utangulizi HakiElimu ni shirika la kijamii ambalo lilianzishwa mwaka 2001. Dira yake ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra tunduizi. HakiElimu inatumia mbinu ya haki na usawa kwa binadamu katika elimu, na kusisitiza ubora katika kujifunza, usawa, utawala na ushiriki makini kwa wananchi katika kuboresha elimu na demokrasia.

Mkakati wetu unazungumzia uwezeshwaji wa jamii katika kubadili mfumo wa shule na kuathiri utungaji wa sera na utekelezaji wake, kwa kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki, kuchochea midahalo yenye ubunifu na kushirikiana na wadau ili kuongeza ushiriki, uwajibikaji, uwazi na haki kwa jamii.

HakiElimu inatambulika kwa mapana zaidi katika ufanisi wake wa kushiriki kitaifa katika masuala kuhusu demokrasia, utawala na elimu ubora. Shirika limewezesha kuanzishwa kwa mtandao wa Marafiki wa Elimu ambao wako zaidi ya 35,000, ambao wanachama wake ni mashirika ya kijamii na mtu mmoja mmoja ambao wanataka kuleta mabadiliko katika shule na jamii.

Page 2: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

Tangu mwaka 2005, HakiElimu imefanya kampeni mbalimbali kuwahamasisha wananchi kuzingatia ubora wa elimu, uwazi na uwajibikaji katika elimu, utawala na demokrasia.

Tangu kuanzishwa kwake, HakiElimu imesaidia kuwawezesha watu, kuleta mabadiliko katika elimu na demokrasia nchini Tanzania. HakiElimu imewahabarisha wananchi, imechochea mijadala na kuleta uelewa ambao umechagiza ushiriki wa wananchi katika kuleta mabadiliko katika elimu na taswira ya kisiasa katika Tanzania.

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Page 3: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

Lengo la Mkakati wa HakiElimu 2012-2016

Mwelekeo na kipaumbele cha mkakati ni kuhamasisha ubora wa ujifunzaji katika shule au madarasa ya awali, msingi, na sekondari; na katika kujenga, uwezo wa kusoma na kuandika kwa watoto ambao hawako shuleni, vijana na watu wazima. Hii ni zaidi ya kutambua matatizo na changamoto. Juhudi mahsusi zitaelekezwa ili kutambua na kuhamasisha njia sahihi na bora za kutatua changamoto zilizopo. Katika kuyafanya haya, HakiElimu inalenga kuona matokeo matatu yafuatayo: watoto watakuwa wako shuleni na wanajifunza kikamilifu, wananchi wanaufahamu, wanajiamini na wanashirikishwa kikamilifu na Serikali iko wazi, na yenye kuwajibika. Vifuatavyo ni viashiria vya mafanikio yanayotokana na mkakati huu:

1. Watoto wako shule na wanajifunza kikamilifu.

• Fedha zinafika shule na zinatumika kwa ufanisi.

• Walimu wako shule na wanafundisha kikamilifu.

• Uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu unaongezeka

• Shule zinawaandaa watoto katika kufanya upembuzi yakinifu na ubunifu.

• Kuhamasisha kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia, na kuhakikisha mijadala juu ya kutumia lugha mama katika elimu ya shule ya msingi inafanyika.

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Page 4: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

2. Wananchi wanaufahamu, wanajiamini na wanashirikishwa kikamilifu.

• Wananchi wanapata taarifa vizuri, wanakuwa makini na wabunifu.

• Kuna mijadala yenye ubunifu na makini ambayo inaondoa imani potofu na kuzungumza ukweli.

• Nafasi nyingi zinapatikana kwa ajili ya wananchi kupaza sauti zao, na wananchi kujipanga katika kuleta mabadiliko katika jamii na shule.

• Wananchi wanachukua hatua (kufuatilia, kupaza sauti na kuiwajibisha serikali).

• Vikundi vya harakati na mitandao vinaanzishwa

• Serikali inawajibika kwa wananchi

3. Serikali iko wazi na yenye kuwajibika.• Takwimu, nyaraka na maamuzi ya kisera vinapatikana kwa kila

mwananchi.• Maamuzi ya kufanywa mara baada ya kushirikisha umma.• Mamlaka zinasikiliza umma na kutoa mrejesho kwa wakati muafaka.

• Mamlaka zinahuru wakupokea mawazo mbalimbali.

Programu za kimkakati zinatoa kipaumbele kwa kuipa uwezo HakiElimu kufanya utetezi na kuleta mabadiliko katika; ubora wa kujifunza, utawala bora, uwazi, demokrasia na uwajibikaji. Jitihada za kujenga uwezo zitafanyika katika masuala ya tafiti na tathmini makini ili kujifunza mambo gani yanaweza kusaidia jamii yetu kuboresha elimu na demokrasia; na kwa namna gani, na pia kusimamia matokeo ya kazi za shirika na mchakato wa kuandaa taarifa. Mkakati huu unalenga katika kuleta mabadiliko ya kudumu katika elimu na demokrasia katika Tanzania.

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Page 5: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

Utekelezaji wa Programu

HakiElimu inaamini kwamba mabadiliko endelevu katika maendeleo na elimu yatatokea endapo wananchi watashiriki kikamilifu katika kutambua changamoto na fursa; na kutafuta ufumbuzi wao wenyewe ili kuboresha huduma na mchakato wa utoaji wa huduma. Programu hii itahakikisha kwamba wananchi wanapata taarifa ili waweze kufanya uchambuzi katika masuala ya elimu na demokrasia, kuhamasisha ubunifu katika kutafuta ufumbuzi, kufuatilia shughuli za viongozi wa maeneo yao na wa kitaifa na kuwawajibisha. Shirika pia litasisitiza juu ya kujifunza na kuboresha kiwango cha kusoma na kuandika kwa wananchi, kuhamasisha mijadala makini na yenye ubunifu, kuwezesha wananchi kupaza sauti zao na kuwaleta wananchi pamoja katika kuchukua hatua sahihi kuboresha utawala, usawa, uwajibikaji na demokrasia.

Mkakati wa utekelezaji umeundwa chini ya programu tatu za kimkakati ambazo zitachangia katika kufikia malengo yaliyowekwa na matokeo yake. Programu hizo ni:

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Page 6: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

Habari na Utetezi (MA)Idara ya Habari na Utetezi inawezesha upatikanaji wa taarifa ambazo zimefanyiwa uchunguzi na za uhakika kupitia njia ya kielektroniki, mitandao ya kijamii, na machapisho na kuchochea mijadala kwa kuanzisha kampeni bunifu za utetezi, kuandaa machapisho na taarifa.

Ushiriki wa Jamii na Uwajibikaji (CEA)Idara ya Ushiriki wa Jamii na Uwajibikaji inawezesha makundi anuai katika jamii na Marafiki wa Elimu kupata taarifa, kudai uwazi na utawala bora; kufuatilia utekelezaji wa sera na programu za elimu, kuratibu ushirikishwaji kikamilifu na kuleta mabadiliko endelevu ya kidemokrasia na kielimu.

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Page 7: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

Utafiti na Uchambuzi wa Sera (RPA)Idara hii inafanya tafiti na pia uchambuzi yakinifu wa sera na bajeti. Idara inahakikisha masuala yote muhimu ya kisera na taratibu zake vinakuwa wazi kwa wananchi pamoja na kuhamasisha uwajibikaji na ushiriki wa wananchi na asasi za kiraia. Pia, idara inafanya utetezi katika ngazi ya juu ya Serikali na watunga sera ili kuboresha sera na utekelezaji wake.

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016

Page 8: Utangulizi - HakiElimu 2012... · 2014-05-04 · ni kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra

Rukwa

Dodoma

Pwani

Dar es Salaam

Tabora

Kigoma

Shinyanga

Mwanza

SingidaTanga

Lindi

Iring

a

Mbeya

Ruvuma Mtwara

Moro

goro

Arusha Kilimanjaro

MaraKagera

Maeneo ya Kimkakati wa HakiElimu 2012 – 2016

HakiElimu Mpango Mkakati 2012-2016