uhunguzi juu ya sababu zinazoathiri ufundishaji na usomaji wa kiswahili kaika shule za sekondari

23
UCHUNGUZI JUU YA SABABU ZINAZOATHIRI UFUNDISHAJI NA USOMAJI WA KISWAHILI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI LUWERO NA KISITU SAMUEL HDM/KU/BAED/575/07 TASNIFU ILIYOWASILISHWA KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA KUHITIMU SHAHADA YA SANAA NA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA KAMPALA

Upload: raymonduganda

Post on 28-Jul-2015

2.043 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

UCHUNGUZI JUU YA SABABU ZINAZOATHIRI UFUNDISHAJI NA USOMAJI WA KISWAHILI

KATIKA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI LUWERO

NA

KISITU SAMUELHDM/KU/BAED/575/07

TASNIFU ILIYOWASILISHWA KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA KUHITIMU SHAHADA YA SANAA NA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA KAMPALA

DESEMBA 2010

Page 2: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

UNGAMO

Mimi kisitu samuel,ninaungama kuwa tasnifu hii ni kazi ilitokanayo na jitihada Zangu mwenyewe na haijawahi kuwasilishwa kwa mahitaji yashahada yoyote ile kaika chuo kikuu

Sahihi…………………………………………

KISITTU SAMUEL

Tarehe ………………………………………..

Page 3: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

IDHINI

Utafiti huu uliofanywa na Kisitu Samuel wenye mada “uchunguzi juu ya sababu zinazoathiri ufundishaji na usomaji wa Kiswahili katika shule za sekondari” umefanyiwe chini ya usimamizi na ushauri wangu na ninapendekeza kuwa tasnifu hii ikubaliwe na chuokikuu kwa ajili ya kutahiniwa

Sahihi…………………………………………..

JUMA KASSIM MUHINDO

Tarehe……………………………………….

Page 4: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

TABARUKU

Tasnifu hii ninaitabarukia mjomba wangu Bw,Mukiibi Wilson kwa kunifundisha lugha ya Kiswahili sanifu ,ninakuombea Subuhana akubariki sana maishani mwako.

Page 5: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

SHUKURANI

Ningependa kuwashukuru sana wazazi wangu Bwana Kisitu Moses na Bi,Najjuma Efrance kwa kunizaa na kunipa malezi mwafaka , Mungu awabariki sana.

Ninashukuru sana msimamizi tena akiwa mhadhiri wangu Bw. Juma Kassim Muhindo, kwa kunielekeza na kunikosoa hapa na pale katika utafiti huu.

Siwezi kuwahau kamwe wahadhiri wangu wengine katika idara ya Kiswahili chuoani, Bw. M.Mayende .na Bw.Kamihanda Ally.

Pia ningependa kumshukuru mwandani wangu Bi.Nabayonga Rebecca pamoja na dada yangu Nakku Aidah kwa kunihimiza na kunipa msaada wa hali na mali masomoni.

Mwishoni na zaidi ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia vipawa kadhaa pamoja na kunibariki maishani hadi kumaliza masomo yangu ya shahada ya kwanza. Alhamudullah!

Page 6: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

YALIYOMO

Ungamo…………………………………………………………iIdhini……………………………………………………………iiTabaruku………………………………………………………..iiiShukurani……………………………………………………….iv

SURA YA KWANZA

1.0 untangulizi wa utafiti…………………………………..11.1 usuli wa utafiti…………………………………………..21.2 suala la utafiti…………………………………………...21.3 Malengo ya utafiti……………………………………….21.3.1 lengo la Jumla…………………………………….……..21.3.2Nadharia tete…………………………………………….31.4 Malengo mahususi……………………………………...31.5 Somo la Nadharia………………………………….…....31.6 upeo wa utafiti…………………………………………...31.7 Umuhimu Wa Utafiti……………………….…………….41.8 Matatizo Ya Utafiti………………….…………………....5

SURA YA PILI

2.0 Utangulizi wa Utafiti…………………………………I 2.1 Mapitio Ya Maandishi………………………………...ii

Page 7: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

SURA YA TATU

3.0 Mbinu Za utafiti……………………………………….113.1 Utangulizi…………………………………………….113.2 UainishaJi Wa Utafiti…………………………………113.3 Uchaguzi Wa wahojiwa………………………………113.4 mahali Pa Utafiti……………………………………...113.5 Mbinu Za ukusanyanji data…………………………..123.5.1Utafiti Wa Maktabani………………………………...123.5.2Utafiti Wa Nyanjani…………………………………..123.5.2.1 Vidasi…………………………………………………133.5.2.2 Hojaji…………………………………………………133.5.3 Mayadiliano…………………………………………...133.5.4 Kuangalia……………………………………………...143.6 Uhifadhi Wa date……………………………………...14

SURA YA NNE

4.0 Uchanganuzi na Uasilishayi wa matokeo ya utafiti……...154.1 utangulizi…………………………………………………15

SURA YA TANO

5.0 Hitimisho na mapendekezo…………………………….23 5.1 Utangulizi……………………………………………...23 5.2 Mapendekezo 5.3 Hitimisho

Marejeleo………………………. Vidadisi………………………...

Page 8: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

SURA YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI

1.1 USULI WA UTAFITI

Kiswahili ni lugha ya kiafrika ambayo inazungumziwa sana katika maeneo ya Afrika mashariki. chimbuko la lugha hii linaaminika kuwa pwani ya afrika mashariki ambako kiswahili kilitumika kwanza katika shughuli za kibiashara .baina ya waafrika na waarbu kutoka uarabuni. kwa hiyo,kiarabu ni lugha ambayo mwigiliano wake au mchango wake kwa lugha za kibantu hasa,pamoja na lugha nyiginezo ,zilipanua zaidi kiswahili .

kasambaa kwa kasi na ,kuenea vururu kwa lugha ya kiswahili kunanasibishwa na sababu chungu nzima kama vile; shughuli za kibiashara ,dini ,ukoloni na utawala ,uhamiaji ,elimu ,miongoni mwa sababu nyingine nyingi .Baada ya kiswahili kupitia usanifishaji wa kutosha ,matumizi yake yalikita mizizi sana .Hii ndiyo maana nchini kenya na Tanzania ni lugha ya kitaifa. Pia ni somo la thamani kubwa katika mitaala ya elimu katika nchi mbalimbali za janibu hizi za Afrika mashariki,licha ya kuwa chombo mahususi cha mawasiliano. kwa hivyo ,inadhihirika dhahiri shahiri kwamba kiswahili ni lugha ya kiafrika inayojulikana kwa kuzungumziwa na watu wengi zaidi barani Afrika hususa katika maeneo ya maziwa makuu.

Nchini uganda ,ingawaje matumizi ya kiswahili yalianza kitambo katika karne ya kumi na nane , wanauganda wengi katika utafiti hawajui na hawatilii maanani lugha hii kutokana mitazamo na hisia zao tofauti.

katika utafiti huu ,mtafiti alichungunza sababu zinazoathoari ufundishaji na usomaji wa kiswahili katika shule za sekondari nchini uganda hasa wilayani Luweero.kwa yakini,watu wangi wanakitazama Kiswahili kama lugha ngumu sana kujifunza. Watu hawa wakiwemo wale ambao waliikosa nafasi ya kuonja kisomo cha kutosha shuleni pamoja na wale ambao wameelimika vya kutosha na kuhitimu katika vyuo vikuu na asasi mbalimbali za masomo,wanakiona kiswahili kama kizungumkuti kwao. Ndiposa watu hawa wasipobadilisha hisia zao kama nilivyoshuhudia mwenyewe kipindi nikikaa wilayani Luweero, mtazamo hasi dhidi ya kiswahili utaendelelea daima dawamu.

Page 9: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

1.2 SUALA LA UTAFITI

''sababu zinazoathri ufundishaji na usamaji wa kiswahili katika shule za sekondari wilayani luwerro''Kwa kweli lazima kuwepo changamoto katika ufundhaji na usomaji wa Kiswahili nchini Uganda hasa wilayani Luweero. Kuna uhaba wa walimu wa Kiswahili; vilevile,ni wanafunzi wachache wanaojasilia kuchukua kiswahili katika vidato vya juu .kwa baadhiwale wanaojitokeza kukisoma, matokeo yao ya mitihani ya kiswahili hayatazamiki wala hayatamaniki - jambo linalojumuisha mambo mengine juu ya mtazamo hasi tayari uliopo miongoni mwa jamii. Ni kutokana na athari hizi ndipo mtafiti ameamwa kuchunguza sababu zinazoathiri ufundushaji na usomaji wa lugha ya kiswahili katika shule za sekondari wilayani Luweero

1.3 MALENGO YA UTAFITI

Utafiti huu ulikuwa na lengo la jumla na malengo mahsusi

1.3.1 LENGO LA JUMLA

Mfafiti alichunguza sababu zinazoathiri ufundushaji na usomaji wa kiswahili katika shule za sekondari wilayani Luweero

1.3.2 Malengo mahsusi

Utafiti huu ulijikita katika kuchunguza;-

Mtazamo wa walimu wakuu/walimu viongozi wa ngazi za juu katika shule za sekondari wilayni Luweero.

Mtazamo wa walimu dhidi ya lugha ya kiswahili katika shule za sekondari wilayani luweero .

Mtazamo wa wanafunzi dhidi ya lugha ya kiswahili katika shule za sekondari wilayani Luweero.

Kuchunguza mwamko juu ya kiswahili miongoni mwa watu katika shule za sekondari wilayani luweero

Page 10: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

Matatizo au changamoto zinazowakumba walimu na wanafunzi wa Kiswahili shuleni za sekondari katika wilaya ya Luwero,

Nama ya kukabiliana na sababu zinazoathiri ufundishaji na usomaji wa kiswahili katika shule za sekondari wilayani Luweero.

1.4 NADHARIA TETE.

utafiti huu uliongozwa na makisio kwambamtazamo hasi dhidi ya kiswahili unaotokana na historia zinazonasibishwa na lugha hii ndio unaoathiri ufundishaji na usomaji wa kiswahili shuleni.

ukosefu wa lugha moja inayoleweka kwa kila mwananchi una athiri hasi chungu nzima katika elimu na jamii kwa ujumla.

1.5 SOMO LA NADHARIA

utafiti huu uliongozwa na nadharia ya isimu jamii kwani suala la mawasiliano linaihusu jamii kikamilifu .

1.6 UPEO WA UTAFITI

katika utafiti huu, mwandishi alishughulilikia sababu zinazoathiri ufundishaji, na usomaji wa kiswahili ,mtazamo pamoja na matatizo yanayowakabili walimu na wanafunzi wa kiswahili na namna ya kupunguza changamoto zinazokumba ufundishaji na usomaji wa kiswahili katika shule za sekondari wilayani Luweero nchini uganda .

mtafiti aliwahiji walimu wakuu, wakuu wa idara ,walemu ,wanafunzi na wazazi ili kupata matilabu ya utafiti.

shule ambazo mwandishi alifanyia uchunguzi ni tano zikiwa,Luweero SS ,MULUSA.S.S, Bombo.S.S, Ssaku.S.S.S na Ndejje.S.S

1.7 umuhimu wa utafiti

Utafiti huu una umuhimu kwa jamii kupitia njia zifuata zo;

Page 11: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

kwanza kabisa ,Mtafiti katambua changamoto zilizo katika ufundishaji na usomaji wa kiswahili shuleni ,hali itakayoiwezesha jamii kuepukana na changamoto hizo ili wajifunze lugha ya kiswahili bila kipingamizi chochote.

Matokeo ya utafiti huu yanaweza kusaidia kushinikiza serikali kuweka mikakati madhubuti itakayowahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kiswahili ndipo watokee kukipenda.

HalikandhaIika, utafiti huu unaweza kusaidia serikari kupitia wizara ya elimu na michezo juu ya jinsi ya kurekebisha na kuweka vivutio au vipengele natharia katika silabasi ya kiswahili kwa ajaili ya kuwavutia wasomaji.

utafiti huu unaweza kuweka mapinduzi kimasomo kwa kuleta mtazama mpya katika jamii juu ya manufaa ya Kiswahili katika suala zima la uhusiano na mawasiliano.

Isitoshe,kuwahamasisha wanafunzi kuipenda na kuisoma lugha ya kiswahili bila wasiwasi wala vizuizi vyovyote.

walimu pia wanaweza kupata motisha na mtazamo mpya wa kufundisha kiswahili katika shule za sekondari wilayani Luweero na nchini uganda kwa ujumla

Jamii nchini uganda inaweza kupata mwamko mpya wa kubadilisha ule mtazamo hasi dhidi ya kiswahili uanaotokana na historia mbaya na vijihadithi vinavyonasibishwa na lugha hii kuitia doa. kwa hivyo ,mwamko mpya katika utafiti huu utalitoa doa jeusi na badala yake kuing’arisha upya lugha ya kiswahili nchini kwa ujumla.

utafiti unapendekeza njia kadha wa kadha zinazoweza kukiendeleza na kukisabaza kiswahili na kuhimiza matumizi yake hadharani katika karne hii ya utenda wazi .

1.8 matatizo ya utafiti

katika harakati za kufanya utafiti wake, mtafiti alikabiliana na matatizo chungu nzima;-

Page 12: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

Mtafiti hakuwa na pesa za kutosha kugharamia mahitaji yote ili kuzikamilisha shughuli zake za utafiti katika muda uliofaa.Hii ni kwasababu fedha zaidi katika kukusanya matilabu ya utafiti, kuchapisha na kuweka jalada. Kwa kusuluhisha tatizo hili, Mtafiti alijitolea na kujikusuru mengi matamu maishani kwa ajili ya kukamilisha utafiti.

Baadhi ya wahojiwa wapendwa hawakupatikana katika wakati mwafaka walipotegemewa na kwa hiyo ilimbidi mtafiti kuwasubiri na kufuata ratiba zao hasa wakati wa mapumzika.

Isitoshe, baadhi ya wahojiwa walishindwa kuzizuia hisia zao za huzuni punde tu walivyokuwa wakikumbuka enzi zile waliponyanyasika na kuteswa na watumiaji wa kiswahili(wajeshi na wezi)kipindi hicho vitani vilivyokuwepo kati ya 1970-1986 ambamo maelfu na maelfu ya watu waliuawa kikatili wilayani luwero.

Halikadhalika, baadhi ya wa hojiwa walikataa katakata kutoa habari ambazo mtafiti alizihitaji mno .Wahojiwa wengine walidai pesa ili kumtolea mtafiti habari zao. wengi wa wahojiwa wa aina hii hawakuwa watoto yakhe bali walikiwa ni watu wazima hasa wale ambao walikuwa na kisomo duni.

SURA YA PILI

2.o Mapitio ya maandishi

2.1 Utangulizi

Katika sura hii , mtafiti alipekua na kusoma vitabu na maandishi ya wataalamu mbalimbali ili kupata maoni yao kuhusu sababu zinazoathiri ufundishiji na usomaji wa kiswahili, matatizo yanayowawakumba wanafunzi na walimu wa Kiswahili na namna ya kupunguza changamoto hizo wilayani luweero nchini uganda.

Sababu zinazoathiri ufundishaji na usomaji wa kiswahili shuleni nchini;

Page 13: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

Mwandishi Hezron mogambi (2007), alisema kwamba ukosefu wa msimamo wazi kuhusu ufundishaji wa lugha ya kiswahili nchini. serikali haijajitokeza na msimamo madhubuti wa kushinikiza ufundishaji wa kiswahili katika shule za serikali na zile za kibinafsi. Hii hawafanya walimu wakuu wa shule nyingi kutojali kiswahili.

Mwalimu Milton Rwabushaija (2000),alibainisha kwamba, ukosefu wa uhamasishaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa Kiswahili ndicho chanzo cha sababu zinazoathiri ufundishaji na usomaji wa lugha hii. Wananchi, wazazi kwa wanafunzi hawajahamasishwa vya kutosha juuya umuhumu wa kiswahili Hii ndiyo maana kuna idadi ndogo sana ya wanafunzi wa kiswahili katika shule za sekondari.

Byakutaga (1998), Aliona kwamba mwanafunzi mwenyewe akiwa na mtazamo hasi juu lugha yoyote ile kama kiswahili, hata mwalimu wake akimfunza vya kutosha hataitumia lugha hiyo. Vile vile, mwanafunzi akiwa anatamani kijifunza lugha , atajitahidi juu chini ilimuradi aweze kuisoma na kuitumia upesi upesi.

Ssekamwa (1994), asema kwamba wanauganda wengi walichukia ufundishaji wa kiswahili kwani lugha hiyo walinasibisha na dini ya kiislamu. Kwa hivyo, wengi wao ambao hawakuwa waislmu nyakati hizo walipinga Kiswahili nah ii ndiyo maana ufundishaji na usomaji wa lugha hii ukawa na msingi mdhaifu shuleni nchini uganda

Government white paper (1992),ilipendekeza ufundishaji na usomaji wa lugha ya kiswahili katika shule za vijijini na mijini nchini uganda. Ilisisitiza umuhimu na kuhimiza ufundishaji wa kiswahili kwa madai kwamba ndiyo lugha ya kipekee ambayo ingeweza kuwaleta pamoja wananchi wa makabila mbalimbali na kuhakikisha umoja na amani, na kupanua maendeleo nchini.

Lakini cha kushangaza ni kwamba, mapendekezo hayo ya utafiti yalibakia mlangoni mpaka sasa hayajatimizwa kikamilifu. kwanini ufundishaji wa kiswahili

Page 14: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

katika shule za sekondari umebaki kuwa kutaka au chaguo la walimu wakuu wachache mno? Na ni hatua gani ambazo zimechukuliwa kutimiza mapendekezo ya kanuni hii muhimu ya serikali?

Mutabiirwa (1990), asema kwamba ni watu wachache sana ambao wamejaribu kujifunza kiswahili sanifu wakiwa shuleni. Kwa mujibu wake ,aliendelea kusema kwamba wanauganda walio wengi sana wanaendelea kuzungumza kiswahili cha mitaani ambacho kimejaa makosa yasiyohesabika.

Halikadhalika, akaendelea kutaja kwamba wanajeshi katika tawala au serikali zilizopita waliwanyanyasa sana wananchi wasio na hatia yoyote huku wakitumia lugha ya Kiswahili. kwa hivyo, Kiswahili kikapata doa kubwa na kuwafanya wanauganda kukichukiaUfundishaji wa kiswahili shuleni nchini uganda unategemewa kuondoa mtazamo mbaya wa watu dhidi ya kiswahili kama lugha.

Ssekamwa (1994), Kwa mujibu wake, asema kwamba matumizi ya kiswahili nchini uganda yalianza mapema sana katika miaka ya 1930 kutokana na uundaji wa kamati mbalimbali za lugha ya kiswahili baina ya kaloni hizi za maziwa makuu yaani, Kenya, Tanzania, Uganda na Unguja. Lakini katika mwaka wa 1940, ufalme wa buganda ulipiga marufuku ufundishaji wa kiswahili kwa wanachi wa Buganda na katika shule zilizomo kwenye ufalme huo. kutokana na umuhimu wa Buganda wakati huo, Uganda ilijitoa moja kwa moja kwenye kamati hizo. Kwa upande mwingine wanachi walikiona kiswahili kama lugha ambayo ingeweza kudidimiza lugha zao asilia.

Mukama (1987), Julai 22-25 akiwa kwenye warsha mjini kampala, alisema kwamba kiswahili ni lugha iliyotakiwa kutumuka Afrika mashariki kote lakini ilizuiliwa na kukataliwa kwa madai kwamba ni lugha ya kigeni wakati lugha ya kitaifa lazima itoke kwenye lugha za kimama( lugha asiilia) zilizopo na isitoke ngambo kama kiswahili.

Mukama (1990), asema kwamba nchini nyingi barani Afrika hususa zile zilizo kusini mwa jangwa la sahara zinakumbwa na matatizo chungu nzima ya kiwemo; ukabila ubaguzi wa kirangi na kuwepo lugha tofautitofauti. Matokeo yake ni ukosefu wa mawasiliano mazuri baina ya wananchi nchini uganda ,mjadala juu ya lugha ya kiafrika ulipoanza,wakati huo kiswahili kilikuwa kinazungumziwa na watu takribani asilimia thelathini na tano (35%) ukilinganisha na kiingereza kilicho na asilimia ishirini na moja (21%) ya watu nchini. kutokana na ubaguzi wa kilugha nchini Uganda , kiingereza kinathaminiwa sana kuliko Kiswahili .Isitoshe ,katika miaka ya 1970,mjadala mwingine juu ya lugha ya kitaifa ulioitishwa na rais Idi Amin, lugha ya luganda na Kiswahili zilikataliwa katakata na waliohudhuria wakati huo .Hizo ndizo zilizokuwa lugha mashuhuri wakati huo na zilizungumziwa na idadiya watu wengi zaidi.

Kagaba (1998), aligudua na kusema kwamba mtazamo hasi dhidi ya Kiswahili

Page 15: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

ulisababishwa na wamisheni hasa ambao walipinga kinyama Kiswahili kwa madai kwamba ni lugha ngeni huku wakitaka kuendeleza matumizi ya lugha asilia pamoja na kukuza ufundishaji wa kiingereza.

Mukama (1994), alisema kwamba mtazamo hasi dhidi ya ufundishaji na usomaji wa Kiswahili nchini Uganda unatokana na wanasiasa na viongozi serikalini .kwa mfano katika mwaka wa 1994 Mh.Samson Kisekka aliyekuwa makamu rais wa Uganda wakati huo,alisema waziwazi kwamba Kiswahili ni lugha isiyo na utaduni wowote na haileweki na kwa hiyo haifai kwamwe kutumika kama lugha ya kiafrika nhini Uganda.

Matatizo yanayowakumba wanafunzi na walimu wa Kiswahili shuleni,

Buuwa (1990), aligundua kwamba vifaa vya kufundishia ni muhimu sana katika ufundisaji na usomaji wa somo lolote shuleni kwa hivyo ,ukosefu wa vifaa vya kufundishia somo la lugha ya Kiswahili shuleni ni changamoto kubwa kwa walimu pamoja na wanafunzi

Adedeyi (1982), katika utafiti wake juu ya lgha silia za kiafrika ,alisema kwamba nchi nyingi za kiafrika zimezua mikakati ya fufua ufundishaji wa lugha asilia za kiafrika lakini Kiswahili hakifundishwi kwenye maderaja mbalimbali ya mfumo wa elimu .lugha hii ilitumika zaidi katika biashara ,siasa ,usambazaji wa dini ,redioni naruningani ,magazetini na pia katika michezo ya kuigiza .kwa hivyo, anawashutumu vikati na kubanisha kwamba kuna watu walio na kasumba za kikoloni wanaothamani lugha za kikoloni na kuzidharau lugha asilia .

Douglas (1989), aligundua kwamba ukosefu wa walimu wa kuitosha ni changamoto kubwa shuleni walimu waliohitimu kikamilifu katika lugha ya Kiswahili kutoka vyuo vikuu ni wachacha sana nchini wakati wao ndio wangekuwa wakuu au nguzo.muhimu katika usazaji Kiswahili sanifu kwenye shukle za sekondari nchini Uganda.

j.c Nsodkwa (1991), alisema kwamba wanafunzi wanakabiliwa na matatizo mengi katika usomaji wa Kiswahili kuna baadhi ya watu wanaowavunja wanafunzi mioyo wakiwaambia kwamba lugha ya Kiswahili ni ngumu sana ,haisomeki wakati wao wenyewe hawejawahi kujifunza Kiswahili hata kidogo .pia baadhi ya walimu wanaofundisha Kiswahili hawayahitimu katika somo hilo na huwa hawana maarifa ya kutosha na uwezo wa kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza na somo la Kiswahili katika vidato vya juu. Kwa hivyo ,hii inayengua hu jitihada za kweza Kiswahili.

Crookail (1972), alitoa maoni kwamba ukosefu wa maktaba nzuri yanye vitabu ,magazeti,majarida ya maana ni kipingamizi kikubwa katika ufundishaji na usomaji wa somo husika matokeo yakeni uvunjikayi wa mioyo ya wanafunzi.

Byakutanga (1995), aligundwa kwamba mbali na shule marejeo mengine ya lugha a Kiswahili ni vitabu ,majarida magazeti ,fasihi nakadhalika chanzo au marejeo hayo huasaidia sa walimu na wanafunzi katika kurahisha kazi wakati wa ufundishaji na usomaji vile vile wanafunzi hupata fursa ya kuhusika wenyewe katika utafiti na uchangunuzi wa vipengele vya lugha .kutokana na hali halisi nchini Uganda ,inashangaza sana kuona kwamba shule za upili hazina vitabu vya kufundishia na kujifunzia Kiswahili . na hata serikali yenyewe kupitia wizara ya elimu na michezo haijaweka sera na mikakati ya uzalifaji wa vitabu vya serufi na fsihi ambavyo vingesaidia sana kupanua ufundishaji na usomaji wa lugha ya Kiswahili.

Mukiibi Wilson (2003), alibainishia kwamba wanafunzi wa Kiswahili nchini Uganda,hawatumii lugha hii

Page 16: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

nyumbani kwao mbali na wanajeshi na walinzi pamoja na wale wanaoishi karibu na mipaka ya Kenya na Tanzania tu, kuna wazazi wachache wanaotgumia Kiswahili nyumbani kwao .hii ni kwa sababu familia nyingij zaidi zinatumia lugha zao za kimama kwa hivyo ,wanafunzi wanasoma Kiswahili shuleni hawajifunzi Kiswahili chochote nyumba=ni .hili ni tatgizo kubwa kwani hawapati mazoezi ya kutosha ya kuongea na kujieleza katika Kiswahili wakati lugha ya kimama ndio inayotumika zaidi.

Jinsi ya kupunguza sababu zinathoari ufundishaji na usomaji wa Kiswahili katika shule nchini Uganda.

Mutabiirwa (1990), alisema kwamba kuna idadi fulani ya watu ambao wanejifunza Kiswahili shuleni kupitia mfumo wa elimu uliopo,na endapo shule nyingi nchini zitajitokeza kuanzisha na kuhimiza ufundishaji wa Kiswahili , bila shaka idadi ya watu wanaogea Kiswahili sanifu itaongezeka mno.

Jon.C.Nsookwa (2004), aliandika kwamba kutokana na ukolsefu wa vitabu ,majarida na makala mengine ya kiswahilik ,inawabidi walimu,wataalamu na wakereketwa wa lugha ya Kiswahili wenyeye kijitolea kua hali na mali kuchangia katika wadishi na uchapishayi wa vitabu na makala mengine muhimu ya Kiswahili sanifu.

Kwa mujibu wa mwalimu Mukiibi Wilson na Mugabe Robert (2003), wakiwa katika mdahalo ,walisisitiza kwamba serikali ya uganda ikipitia wizara ya elimu ,kuwajiriwalimu wa Kiswahili na kuwagawa katika shule za upili na asasi mbalimbali za elimu ya juu nchini kwa kupitia mkakati huu huenda katika siku za mbeleni uhaba wa walimu utapungua kwa asilimia Fulani.

Mwandishi Hezron mogombi (2007), alishauri kwamba kwa ajili ya kupunguza matatizo yanayokabili ufundishaji na usomaji wa Kiswahili ,serikali pamoja na wabunge inawabidi wapitishe sera nziri kuhusu Kiswahili Bungeni, kuhimiza kuwepo kwa idara za Kiswahili katika taasisi zote nchinio na kufanya utafiti kuhusu sarufina fasihi ya kiswahili.

Mwandishi Ashton(1970), alisema kwamba wasomi ambao wajiendeleza na kufuzu katika somo la Kiswahili yawabidi wawe kwenye mstari wa mbele katika kueneza njiri ya Kiswahili . halikadhalika ,kawaita wana Uganda wote wakiwemo wanafunzi, wajivunie ufundishaji na usomaji wa Kiswahili kama ilivyo desturi katika masomo mengine yanayotahiniwa na kupitika kwa urahisi kwenye shule za upili.

Kwa mujibu wa mwandishi Ssekamwa(1994) alibainisha waziwazi kwamba ,Kiswahili ni lugha ilioudwa kutokana na mwingiliano wa maneno ya kiarabu na kibantu sarufi ya Kiswahili imesheheni misamiati mingi na maneno kutoka lugha nyingi za kibantu na kiarabu pia .lakini Kiswahili ni lugha ya kiafrika na si kiarabu .kwa hivyo ,Kiswahili ni lugha inayotazamiwa na watu wengi zaidi kuwa ni lugha ya kipekee inayoweza kuleta umoja wa kiafrika na kimataifa barani afrika .

Mwandishi Douglas(1989), alidhirisha kwamba vifaa vya kufundishia ni vyombo muhimu sana katika ufundishaji na usomaji wa somo lolote lugha ya Kiswahili ikiwemo vifaa hivi kama vile ,vitabu miogoni mwa vingine vinasaidia sana katika kuleta maelewano namasikilizano baina ya mwalimu na wanafunzi wake.

Byakutanga (1995), alimuunga mkono mwandishi Douglas (1989) aliposema kwamba shuleni ni pahali ambapo mtu anaweeza kujifunzia lugha husika kwa urahisi mbali na mazungumuzo baina ya wanafunzi kwa wanafunzi pamoja na walimu wao, shuleni pia kuna vifaa au vyanzo vingine vya Kiswahili.kwa mfano,maktabani mtafitiau mwanafunzi ndipo anapopota fursa ya kubukua vitabu,majarida, magazeti, kamusi ,pamoja na makala mengine ya lugha kama Kiswahili .hii hupungunza sababu zinatoari ufundishaji na usomaji wa Kiswahili katika shule za sekondari nchini Uganda.

SURA YA TATU

3.0 MBINU ZA UTAFITI

3.1 utangulizi.

Page 17: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari

Mtafiti alitambua na kueleza mbinu mbalimbali za utafiti alizotumia kukusanya nabari za utafiti maktabani na nyanjani . mbinu hizi zilikuwa ;uainishaji wa utafiti uchaguzi wa wahojiwa ,mahali pa utafiti mbinu za ukusanyaji data maktabani kama kuchagua vitabu ,kusoma na kunakili. Mtafiti alizitumia mbinu za ukasayaji data nyanjani za vidadisi, hojaji, majadiliano na kuangalia.

3.2 uainishaji wa utafiti.

Utafiti huu ulikuwa wa maktabani na nyanjani mtabani mtafitialitumia mbinu ya ukadiriayi bora kuchunguza data nyanjani mtafiti alitumia minu ya ukadiriaji kiasi.

3.3 mahali pa utafit.

Mtafiti alifanyia utafiti wake katika shule tan zilizoteuliwa wilayani luweero nchini Uganda .miogoni mwa shule hizi ni pamoja na.Shule ya pili ya Luwero ,shule ya upili ya mulusa, shule ya upili ya Bombo ,shule ya upili ya Ssaku na shule ya upili ya Ndejje .Mtafiti alizichaagua shule hizo kutokana na sababu zifuatazo;

i. katika shule hizo Kiswahili ni mojawapo ya masomo yanayofundishwa Kiswahili kinafundishwa na kutahiniwa kutoka kidato cha kwanza hadi kidato cha sita .

ii. shule zote hizo ni z mchanganyiko yaani kuna wanafunzi wa kike na wanafunzi wa kuime kwa hivyo mtafiti alfadika sana kapata mawazo na maoni kutoka kwa watu wa jinsia tofauti

iii. kimawasiliano ,shule hizi zote zinafilika kwa urahisi kwani zilijegwa karibu na miundombinu kama vile ,barabara nzuri ,karibu na mijiikwa hivyo kuna mawasiliano mazuri.

iv. Shule ya sekondari ya Ssaku ipo kijijini Nsawo, shule ya sekondari ya Luwero ipo njini Luwero ,shule ya sekondari ya Ndejje ipo kijijini Ndejje na sekondari ya mulusa ipo njini wobulenzi na shule ya sekondari ya Bombo ambayo ipo mjini Bombo kwa hivyo mtafiti aliweza kupata mawazo na maoni kutoka vijijini na mijini wilayani luwero.

3.4 uchaguzi wa wahijiwa.

Katika harakati za kuwa chagua wahojiwa, mtafiti alitumia mbinu ya uteuzi mpango .hii ilikuwa ni kuhakikisha kwamba mtafiti anachagua wahojiwa ambao wangeweze kutoa maoni na habari mwafaka juu ya suala la utafitit.mtafiti aliwahusha wahojiwa wa marika na jinsia zote ,hususa wale wahusika halisi walio ndani ya mfumo huu wa elimu kwa mfano; walimu wakuu ,walimu wanafunzi pamoja na wadau, wasomi na wale wasiosoma.

Kielelezo cha utafiti kimesheni walimu wa Kiswahili tisa(9) tu pamoja na walimu wengine arobani na watani(45) waliofikiwa na kuhojiwa na mtafiti katika shule hizo tano za sekondari .pia walimu. Viongozi walikuwa kumi na saba (17) ,wakati miongoni mwao watano(5) wakiwa walimu wakuu kwenye shule za sekondari hizo tano (5) zilizoteuliwa na mtafiti.

Kielelezo kwa upande wa wanafunzi jumila yake ni mia tatu sabini na watatu (373) ambao wanachukua lugha Kiswahili.somo la Kiswahili ni lazima katika kidato cha kwanza na pili kwenye shule hizo kwa hivyo mtafiti aliwateua wanafunzi angalau kumi kutoka kila darasa kwenye kidato cha kwanza mpaka kidato cha nee sitini (60) katika kila mojawapo ya shule hizo kwa ujumla walikuwa mia tatu (300)

Katika vidato vya yaani kidato cha tano na sita mtafiti aliwajumuisha wanafunzi wowote wale wanaochukua Kiswahili na kuwahoji katika kila mojawapu ya shule hizo .kwa ujumla walikuwa sabini na watatu (73)

Nanbari na vikundi vya wahojiwa katika kielelezo ch uatfiti vimefupishwa kwenye jedwali lifuatalo.

Page 18: Uhunguzi Juu Ya Sababu Zinazoathiri Ufundishaji Na Usomaji Wa Kiswahili Kaika Shule Za Sekondari