walimu na ufundishaji tanzania sauti za marafiki wa...

36
i Walimu na Ufundishaji Tanzania Sauti za Marafiki wa Elimu

Upload: lenga

Post on 29-Aug-2019

248 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

i

Walimu na Ufundishaji TanzaniaSauti za Marafiki wa Elimu

ii

Waandishi: Betty Malaki, Finike GogomokaWachangiaji: Mary Nsemwa, Lilian R. Kallaghe, Godfrey Telli Mhariri: Rakesh RajaniMchoraji: Nathan Mpangala

HakiElimu, 2004SLP 79401, Dar es Salaam,TanzaniaAnwani pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

ISBN 9987 – 423 – 00 – 00

Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa minajili isiyo ya kibiashara;ilimradi chanzo cha sehemu iliyonakiliwa kinaonyeshwa na nakala kutumwa kwaHakiElimu.

c

iii

Yaliyomo

Utangulizi

1 Mafunzo kwa Walimu……………………………….………………………….. 3

2. Mbinu za Ufundishaji……………………………….…………………………... 7

3. Makazi ya Walimu……………………………….……………………………… 12

4. Mishahara ya Walimu……………………………….………………………….. 15

5. Ubora wa Elimu……………………………….……………………………….. 20

6. Hitimisho……………………………….……………………………………… 30

iv Sauti za Marafiki wa Elimu

v1

UtanguliziRafiki wa Elimu aliyeko Tabora alitembelea wananchi wasiotaka kuwapeleka watoto shule katikajamii yake.Alitembelea pia shule za msingi akaongea na wanafunzi na kuwaelimisha haki yao yakupata elimu.Aliwaeleza wanafunzi hao pia mbinu wanazoweza kutumia katika kuwasaidia walewasiofahamu maana ya elimu. Ziara ya Rafiki huyo ilizaa matunda pale ambapo baadhi ya wazaziwalikubali kuwapeleka watoto shule na wazazi wengine walijiunga na elimu ya watu wazima.

Mfano huu unatufundisha jinsi ambavyo Marafiki wa Elimu wanaweza kuleta mabadiliko katikaelimu na jamii kwa ujumla. Katika kitabu hiki ipo mifano mingine ya shughuli zilizofanywa naMarafiki katika kuleta mabadiliko ya elimu. Mifano hiyo itawasaidia kufahamu nini Marafikiwanachoweza kufanya katika Harakati za kuboresha elimu. Maoni hayo pia yanaweza kuchocheamijadala hatimaye kuleta mabadiliko ya elimu nchini.

Marafiki wa Elimu ni Harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuona haki ya kupata elimu yamsingi inakuwepo Tanzania. Madhumuni ya Harakati za Marafiki wa Elimu ni kutoa fursa kwawatu wanaojali elimu nchini kubadilishana mawazo na maoni yao kuhusu masuala ya elimu.Harakati za Marafiki wa Elimu zinachangia kubadilisha mfumo wa shule na kuzifanya ziwe borakwa wote. HakiElimu tumepokea barua nyingi kutoka kwa Marafiki wa Elimu zenye maoni tofautiyanayohusu mazingira ya kazi na maisha ya walimu.Tunawapongeza wote waliotumia muda waokutuma maoni yao kwetu.

Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu tano: mafunzo kwa walimu, mbinu za ufundishaji,makazi ya walimu,mishahara ya walimu na ubora wa elimu.Kila sehemu imejengwa kwa kutumianukuu kutoka katika barua tulizopokea. Pia tumeandika majina ya waandishi wa nukuu hizo kwakutumia vifupisho vya majina na namba za uanaharakati kwa vile hatukuwaomba ruhusa yakuweka wazi majina yao.

Serikali iko katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM)unaohakikisha kuwa kila mtoto anapata elimu bora. Katika hotuba yake ya mwezi Oktoba 2004Rais Benjamin Mkapa alisema:

“Shule zimeongezeka.Vyumba vya madarasa vimeongezeka.Walimu wengi zaidi wameajiriwa, na wengine wanasomeshwa. Idadi ya wanafunzi katika shule za msingi imeongezeka, kwa usawa wa kijinsia, na wengi zaidi wanafaulu kuliko huko nyuma. Changamoto iliyo mbele yetu ni kurekebisha penye kasoro, na kuzidi kuboresha pale ambapo mambo yamekwenda vizuri.Huo ndio mtazamo sahihi wa kimaendeleo”.

Ni dhahiri kuwa Serikali inatambua umuhimu wa walimu na hata kero zinazowazunguka. Ndiomaana katika miaka ya karibuni walimu wengi zaidi waliajiriwa. Hata hivyo, katika kila kona yanchi hukosi kusikia malalamiko ya walimu. Mara mishahara midogo na inacheleweshwa, marahawalipwi posho, mara hawana nyumba za kuishi na madai mengine mengi. Wengi wao wakiwana maswali tofauti kama vile je, kuna haja ya kupandishwa madaraja ikiwa mishahara haibadiliki?

Sauti za Marafiki wa Elimu

2

Utafiti uliofanywa na Chama cha Walimu Tanzania kwa kushirikiana na HakiElimu umegunduakuwa matatizo makubwa yanayowakabili walimu huwafanya wasiweze kufundisha kwa ufanisi.Walimu wamedai kuwa wanapata matatizo si katika mishahara tu ila hata wanapodai haki zaoza msingi zinazohusu fedha kama vile bima ya afya, kodi ya nyumba, fedha za uhamisho, nk.Serikali inajikuta inadaiwa malimbikizo makubwa ya pesa hizo za walimu.

Bila shaka mazingira ya kazi ya walimu yangekuwa bora, elimu kwa watoto wetu ingekuwa bora.Ingekuwa vizuri ikiwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) ungehakikisha walimuwana nyumba za kutosha hasa katika maeneo magumu.Vilevile ushiriki wa walimu katika uundajiwa sera ya elimu na mafunzo na mambo mengine mengi kama hayo ni muhimu.Tunaamini kuwakijitabu hiki kitaibua mijadala zaidi hatimaye kuleta mabadiliko katika elimu.

Sauti za Marafiki wa Elimu

3

1. Mafunzo kwa Walimu

Mafunzo kwa walimu ni kwa ajili ya maendeleo ya mwalimu, shule na nchi kwa ujumla. Piahumwezesha mwalimu kukabiliana na mabadiliko ya mitaala na kuongeza ujuzi wa kufundisha.Mafunzo yanaweza kuleta mabadiliko katika ufundishaji kwa mwalimu hatimaye katikamaendeleo ya mwanafunzi. Ujuzi na uwezo wa mwalimu katika ufundishaji una madharamakubwa kwa mwanafunzi katika kujifunza na kupata kitu anachotarajia kutoka kwa mwalimuhuyo. Mafunzo yakitolewa kwa uhakika huongeza ufanisi kwa mwalimu hatimaye kuletamafanikio kwa mwanafunzi.

Katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Serikali ina mikakati ya kuongezauandikishwaji wa watoto katika shule za msingi. Katika utekelezaji wa mkakati huo Serikali inampango wa kuwapatia walimu mafunzo ili waweze kuboresha kiwango cha ufundishaji.Waziriwa Elimu na Utamaduni katika hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu na Utamaduni ya 2004/2005alisema “Serikali itaboresha taaluma na utaalamu wa ufundishaji kwa walimu kwa kutoa mafunzokazini kwa kutumia njia na mbinu shirikishi”.

Sauti za Marafiki wa Elimu

4

Wasemavyo Marafiki wa Elimu

Umuhimu wa mafunzo kwa walimuMwalimu ambaye ndiyo chanzo cha uboreshaji elimu shuleni atasaidiwaje kama hamtachangiamafunzo ya walimu, kupandishwa madaraja,wala kuwalipia kozi yoyote na tukizingatia kuwa zipofaida za kujiendeleza kimasomo hasa kwa walimu. Tunafahamu kuwa msingi wa mwanafunziunategemea kujengwa na mwalimu. Ili mwalimu aongeze taaluma zaidi anahitaji kujisomea zaidi.Naamini kwamba taaluma ndogo kwa walimu inasababisha kushusha elimu mashuleni hivyo ilikuboresha elimu nchini tuzingatie taaluma kwa walimu

Mwl.A. S (Namba: 300528), Shinyanga

Walimu wahusishwe katika kuandaa mitaalaMMEM iangalie suala la kuwapeleka masomoni walimu. Hii ina maana kwamba walimuwapelekwe kozi fupi kwa ajili ya kujikumbusha mbinu mpya za kufundisha. Mfano masomo kamaHisabati, Kiswahili, English, Sayansi ili waendane namabadiliko yanayotokea katika mfumo wa elimu. Katikakubadilisha mitaala ya shule za msingi hakuna utaratibumaalum kwamba baada ya miaka kadhaa mtaalautabadilika ili kuwawezesha walimu kwenda sambambana mabadiliko hayo. Pia hakuna utaratibu wakuwashirikisha walimu wa shule za msingi kutokamaeneo mbalimbali ya nchi, mijini na vijijini katika kuandaa mitaala. Kumbuka kuwa walimu ndiowanaofanyia kazi mitaala na ndio wanaoweza kutambua mapungufu ya mitaala. Naomba walimuwahusishwe katika kuandaa mitaala hasa wale walioko mashuleni ambao ndio walioko katikamazingira ya kazi.

A.H. L (Namba: 305037), Mtwara

Somo la stadi za kazi lifundishwe kwa vitendoKatika shule zote za msingi hivi sasa kuna somo la stadi za kazi na Maarifa ya Jamii ambayo kamayatafundishwa kwa vitendo yatamwandaa kabisa mwanafunzi kujitegemea baada ya elimu yakeya msingi. Ili kufanikisha hili mambo muhimu ya kuzingatia ni kuwa na walimu wenye taaluma yasomo la stadi za kazi inayowawezesha wanafunzi kutenda.

J. K. C, Mwanza

Sauti za Marafiki wa Elimu

Kumbuka kuwa walimu ndiowanaofanyia kazi mitaala nandio wanaoweza kutambuamapungufu ya mitaala.

5

Rafiki wa Elimu Tabora aleta mabadiliko!

Napenda kutoa taarifa ya matunda au mafanikio ya kazi ya Harakati za Marafiki niliyofanya.Nimepita sehemu mbalimbali mijini na vijijini nikiwaelimisha watu kuhusu faida ya elimu.Katika sehemu nilizopita nilikutana na watu mbalimbali. Wengine ni waelewa, wengine siwaelewa. Wengine walikubali kuwapeleka watoto wao shule, wengine hawakutaka hatakusikia neno elimu. Hadi kufikia sasa nimetembelea shule 4 za msingi. Nimekaa na wanafunzina kuongea nao na kuwahakikishia kuwa wana haki ya kupata elimu bora. Pia niliwapa mbinumbalimbali za kuweza kuwasadia wenzao ambao hawajafahamu maana ya elimu.Pamoja na hayo nilitembelea familia ambazo wazazi wanawanyima watoto wao haki elimu.Familia nilizotembelea ni 23, katika hizo ni familia 9 ambazo hawakutaka watoto waowasome. Tena katika hizo 9 ni familia 3 ambazo kuanzia baba, mama na watoto hakunaaliyesoma hata chekechea. Familia hizo nilizielewesha kuhusu suala zima la elimu.Walikubaliana kuwa watu wote wana haki ya kupata elimu bora. Hivyo walionyesha kwavitendo kwa kuwapeleka watoto wao kuwaandikisha darasa la 1. Watoto ambao walipelekwakuandikishwa ni 38.Wazazi ambao walijiunga na elimu ya watu wazima ni 3.

Y. D (Namba: 302648) Tabora

Semina kuhusu mitaala mipya zitoleweKama kweli kuna harakati za kuinua elimu Tanzania naomba kozi ya ualimu iwe ya miaka miwiliGrade III A na sio ya mwaka mmoja. Mwaka mmoja walimu wanakuwa hawajaiva sawasawa hatamuhtasari unakuwa haujaisha.Walimu pia tunaomba semina na kozi kila mitaala mipya inapoanzakutumiwa shuleni. Sisitizo liwe kwa wale wenye vipindi hivyo ili kuepuka kurudiarudia kwa kuwani gharama.

N. K. I (Namba: 304294), Pwani

Walimu wenye Diploma wafundishe shule za msingi piaSerikali iongeze bidii zaidi katika upanuzi wa elimu ya walimu ili kuongeza idadi ya walimu nakupunguza tatizo la upungufu wa walimu katika shule zetu.Walimu waliopata elimu zaidi kamavile kutoka daraja A kwenda Diploma au zaidi isiwe ni kikomo cha kutoa elimu katika shule zamsingi na mwanzo wa kuhamia katika shule za sekondari bali wabaki kufundisha shule za msingi.Kinachotakiwa ni wizara husika kuboresha maisha yao kiuchumi ili kuwatia moyo wawezekubakia katika mazingira yanayowakabili.

C. P. M (Namba: 307296), Mwanza

Sifa maalum zitumike kwa wanaojiunga na ualimuKatika miaka ya karibuni kumetokea wimbi la vijana wanaojiunga katika mafunzo ya ualimuwakiwa na matokeo mabaya hususan daraja la nne na sifuri katika masomo yao ya kidato channe na wengi wao wakiwa na historia isiyo nzuri. Hali hii inasababisha kuwepo kwa walimuwahuni, wasio na nidhamu kwa wanafunzi na wenye uwezo duni wa kufundisha hivyokuhatarisha mikakati ya kuinua ubora wa elimu ya msingi. Hivyo naishauri Serikali na wizarahusika kulimulika suala hili ambapo ingeweka vigezo au sifa maalum zitakazomwezesha mtukupata mafunzo ya ualimu akiwa na sifa husika. Kwa kupitia utaratibu huu mikakati ya kuwa naelimu bora ingefikiwa.

S. D (Namba: 304563), Dar es Salaam

Sauti za Marafiki wa Elimu

6

Wanahitajika walimu bora na si bora walimu Wananchi na wazazi tunahitaji mazingira bora ya kujifunzia vijana wetu ambao ndio viongozi wakesho. Kero yangu na nzito kwangu ni juu ya kupata walimu bora ili watunze hayo mazingirabora na safi. Katika kipindi hiki cha mpito walimuambao watapatikana hawatakuwa walimu bora ila borawalimu. Mtindo wa walimu wa vyuo kuchaguawanachuo kuingia vyuoni umekuwa ni mbaya sana nawa upendeleo na unatoa mianya ya rushwa. Vijanawengi ambao wanajiunga hawana sifa ya walimu walahawana wito ila wanaona bora tu kupata ajira. Vyetifeki ni vingi na wenye daraja la nne na sifuri pia wapovyuoni. Walimu hao kweli tunategemea kuboresha elimu ya watoto au kuharibu tu. Ninawasiwasi baada ya miaka mitatu tutakuwa na majengo bora sana na bora walimu na siyo walimubora. Naomba suala la kuelimisha walimu kwa ajili ya shule za msingi lipewe uzito wa pekee kwakuchagua watu wanaofaa kuwa walimu. Huwezi kutoa usichokuwa nacho.Watu wanaoshindwamitihani wasiruhusiwe kusomea ualimu hawana uwezo kitaaluma.

G. K (Namba: 306289),Tabora

Sauti za Marafiki wa Elimu

Naomba suala la kuelimishawalimu kwa ajili ya shule zamsingi lipewe uzito wa pekeekwa kuchagua watu wanaofaakuwa walimu.

7

2. Mbinu za Ufundishaji

Mbinu bora za ufundishaji ni zile zinazomwezesha mwanafunzi kuwa mdadisi, mbunifu naanayependa kujifunza. Mbinu hizi zinazingatia ushiriki wa wanafunzi katika mchakato wakujifunza. Pia matumizi ya zana mbalimbali na mifano humwezesha mwanafunzi kuelewa vizurina kwa haraka zaidi. Ufundishaji mzuri ni pamoja na kujenga uhusiano mzuri kati ya mwalimuna mwanafunzi. Hata hivyo ufundishaji katika shule nyingi hapa nchini umetawaliwa na adhabuya viboko kama njia ya kuleta nidhamu na kuwafanya wanafunzi waelewe wanachofundishwa.

Katika baadhi ya shule zetu hapa nchini bado walimu wanatoa adhabu kali kupita kiasi kwawanafunzi. Baadhi ya walimu huwachapa wanafunzi idadi yoyote ya viboko kwa kosa dogo tu.Hivi kwa kumchapa mwanafunzi walimu hawaoni kuwa wanaweza kumuumiza mwanafunzibadala ya kumjenga? Walimu hao hawafahamu kuwa wanakiuka haki za binadamu? Kwa niniwalimu hawafuati kanuni zilizowekwa na Wizara ya Elimu? Ni ukweli usiopingwa kuwa adhabuya viboko kwa mtoto haimsaidii badala yake humfanya awe sugu. Kwa mujibu wa sheria ya elimuNa. 25 ya mwaka 1978 kifungu cha 60(0) mtu pekee anayeruhusiwa kumchapa mtoto niMwalimu Mkuu na ni lazima aandike katika rejesta jina la mtoto anayechapwa na kosa alilotenda.Sheria pia inataka mwanafunzi wa kike achapwe na mwalimu wa kike au mwalimu aliyeteuliwana Mwalimu Mkuu na adhabu isizidi viboko vinne. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto(kifungu cha 2 na 37) unakataza unyanyasaji na adhabu kali kwa watoto.

Sauti za Marafiki wa Elimu

8

Wasemavyo Marafiki wa Elimu

Mwanafunzi aliyeumizwa kwa kibokoLeo nawatumia kisa cha kushangaza tena cha kusikitisha kilichotokea katika shule moja yamsingi. Mwanafunzi wa darasa la tatu alipigwa na mwalimu ambaye kwa jina sijaweza kulifahamukwa sababu ni mgeni na alikuwa na siku kama nne toka aliporipoti kuanza kazi katika shule hiyo.Mwalimu huyo alimpiga mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali sana katika mguu wakewa kushoto kiasi cha mguu huo kuvimba sana na kushindwa kutembea. Hadi leo hii ameshindwakwenda shule. Mtoto huyo alipelekwa hospitali na mwalimu aliyempiga. Alipigwa picha ya X- Rayna kuonekana amepata hitilafu kidogo. Nilijaribu kumwuliza mwenyekiti wa kamati ya shule juuya vitendo wanavyofanyiwa watoto wadogo katika shule yake, alisema hawezi kuwaingiliawalimu utendaji wao wa kazi kwa vile yeye muda mwingi anakuwa hayupo shuleni. Nilimwendeamwalimu mkuu wa shule. Mwalimu huyo alitoa jibu moja tu “wasukuma hamtaendelea maanamnajifanya mnajua kila kitu”. Jibu hili lilinifanya nishindwe kuelewa ni nani hasa anayefanyavitendo hivyo vibaya. Je, ni walimu kwa amri ya mkuu wao wa shule? Nilikosa jibu.

P. K. J (Namba: 301568), Shinyanga

Mwalimu anapotumia zana katika kufundishaWalimu wanapofundisha masomo yao kwa kutumia vifaa au zana hueleweka vizuri na piawanapendwa na watoto. Watoto hutuletea sifa za walimu hao hadi nyumbani kuwa mwalimufulani anafundisha vizuri akiwa na zana na mwalimu fulani hafundishi vizuri kwa kuwa hatumiizana. Ndio maana katika shule za sekondari mwalimu mwingine akiingia darasani watotowengine hutoka nje.

S.Y. S (Namba: 301283),Tanga

Madhara ya adhabu ya kibokoMaoni yangu ni kuhusu suala la adhabu yaviboko shuleni. Kwa nini tusipewe adhabunyingine? Adhabu ya viboko inawezakumdhuru mtoto kwa kuwa mwalimuanaweza kumpiga mwanafunzi kwa kiboko nakumuumiza mara nyingine hata kusababishakifo au kumtoa vidonda.

I. A. A, 7 years, (Namba: 300454), Dodoma

Nidhamu haipatikani bila vibokoHaiwezekani wanafunzi kuwa na nidhamu bila kuchapwa viboko kwa sababu baadhi yawanafunzi huiga tabia za wenzao wasiokuwa na nidhamu. Kwa hiyo mwanafunzi wa namna hiyoakipata kiboko ndio ananyoka na kuacha tabia mbaya ya kutokuwa na nidhamu.Wanafunzi wengihawapendelei adhabu ya viboko, hivyo basi viboko vikielekezwa shuleni wanafunzi watakuwa nanidhamu na kufuata sheria za shule.

M. M (Namba: 302931), Mtwara

Sauti za Marafiki wa Elimu

Adhabu ya viboko inaweza kumdhurumtoto kwa kuwa mwalimu anawezakumpiga mwanafunzi kwa kiboko nakumuumiza mara nyingine hatakusababisha kifo au kumtoa vidonda.

9

Walimu wasituchape ovyoTunaomba ushirikiano wenu katika kuzuia walimu wasituchape miguuni, kwenye migongo nakutupatia adhabu kali, pia kutuchapa viboko zaidi ya kiwango kilichopangwa na Serikali.Walimu wasiwachape ovyo wanafunzi kwa sababu viboko havimjengi mwanafunzi ilavinakomaza.

M. R.C (Namba: 306488), Mara

Njia bora zaidi ya viboko ni ipi?Ni adhabu gani ambayo mtoto mtukutu anastahili kupata ikiwa adhabu ya viboko haitakiwi?Maoni yangu ni bora yawepo makongamano kwa ajili ya walimu wale ambao wanafundishadarasani na sio maofisini ili tuweze kupata ukweli wa njia bora pamoja na elimu bora.

Mwl. B. S. H (Namba: 302028),Tanga

Viboko viendelee, fimbo tatu tu!Maoni yangu ni kuwa viboko viendelee kuwepo mashuleni ili viweze kujenga nidhamu kwawatoto, kwamba mwanafunzi kama hachapwi basi shule na wanafunzi watakuwa hawana nidhamu.Angalau tupigwe fimbo tatu iwapo mwanafunzi anakosea.

J.M (Namba: 302984), Std IV, Mwanza

Bila viboko nidhamu itashukaAwali jamii ilidhani kuwa kiboko ndiyo njia pekee ya kumrekebisha mtoto kinidhamu. Ndiomaana hivi sasa jamii inasema nidhamu itashuka shuleni kufuatia mabadiliko hayo ya utekelezajiwa adhabu ya viboko kwa msisitizo.

J. S.T, Singida

Kwa maoni yangu naona viboko ni muhimu kwa mwanafunzi kwa malezi bora ikiwa tu utaratibumaalum unafuatwa kama kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Elimu na Utamaduni. Taratibuzilizowekwa katika kutoa adhabu ya viboko zifuatwe.Kama kuna walimu wanaokwenda kinyumecha utaratibu uliowekwa, mwalimu mkuu anapaswa kuwachukulia hatua. Nakubali kuwa wapowatoto wanaoweza kukanywa kwa maneno wakarekebishika, hawa ni wachache. Walio wengisharti wapate msukumo kwani punda haendi bila mjeledi.

J. K. A (Namba: 301287), Shinyanga

Kijitabu cha “Shule Nzuri ni Ipi?” chaibua mjadala

Njia ya kwanza ninayotumia ni kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki katika kusoma pamojana kufanya majadiliano juu ya mada zilizojitokeza katika kijitabu cha Shule Nzuri ni Ipi? Njiahii ni nzuri kwa sababu ni rahisi na inaweza kufanyika wakati wowote.

Pia mpaka sasa nimefanikisha kuwashirikisha baadhi ya walimu wa shule za msingi Njombemjini ili wafanye majadiliano na wanafunzi wao.

E L. K, Dar es Salaam

Sauti za Marafiki wa Elimu

10

Bila kiboko mtoto atamdharau mwalimuSasa tumefika mahali ambapo hatuwaendelezi watoto bali tunawadidimiza kinidhamu kwasababu mtoto ukimwambia hakuna kiboko atamdharau mwalimu na atafanya vitu anavyotakayeye. Mfano kuchelewa shuleni na kutotekeleza adhabu aliyopewa na mwalimu kwa kuwa anajuahachapwi! Lakini kama viboko vipo mtoto ataogopa. Hivyo mimi nashauri viboko viendeleekama kawaida ila tu visiwe viboko vya unyanyasaji yaani kupiga kama punda.Viwe viboko vyamatakoni tu kwa wanafunzi wote wawe wa kike au wa kiume na visizidi vinne.

J.M.L (Namba: 302142),Tabora

Wanafunzi wasinyanyasweMaoni yangu ni kuwa unyanyasaji wa wanafunzi uthibitiwe ili wanafunzi wawe na uhuru. Imefikiawakati wanafunzi hawaoni umuhimu wa shule kutokana na walimu kuwanyanyasa kwa vitendokama vile kuwapiga viboko vingi.

A.I.N. 30 years (Namba: 301916,) Iringa

Watoto hawapendi vibokoKatika kijiji ninachoishi kuna watoto wengi ambaohawajapata elimu ya msingi. Hii inatokana na adhabuzinazotolewa na walimu shuleni, zinawafanya watotowasipende kwenda shule. Watoto watajifunzajekukiwa na adhabu shuleni. Katika shule ninayosomawalimu wanapenda sana viboko kwani wanafunziwanachapwa viboko 12 kwa kosa la kuchelewashuleni tu. Je hiyo ni haki katika elimu?

J. S. 8 years (Namba: 307121), Singida

Adhabu isitolewe kwa hasiraMimi mtazamo wangu ni kuwa adhabu ya viboko ndiyo inayofaa kuliko nyingine kwani inaendanana ile kauli ya toa adhabu pindi kosa linapofanyika. Aidha nawashauri walimu wenzangu kuwatunapotumia adhabu ya viboko tusitoe kwa hasira kiasi cha kufumba macho na kuumanishamidomo. Kwa njia hiyo mtoto atamwogopa mwalimu, pia si kila kosa kutumia kiboko hatakukemea tu inatosha.

H. S. L (Namba: 304443), Lindi

Adhabu ilingane na kosaNaomba walimu waangalie sana suala hili la adhabu wanazopewa wanafunzi. Walimu watoeadhabu kulingana na kosa la mwanafunzi kwani adhabu kali humpotosha mtoto badala yakumnyosha.

A. M (Namba: 306595), Lindi

Sauti za Marafiki wa Elimu

Adhabu zinazotolewa nawalimu shuleni, zinawafanyawatoto wasipende kwendashule. Watoto watajifunzajekukiwa na adhabu shuleni.

11

Viboko vitumikeNidhamu bila viboko haiji kwa kuwa watoto ni sugu. Lazima viboko vitumike katika kuwawekawatoto sawa. Mwanafunzi anapopigwa anaona uchungu kwa sababu fimbo inauma. Mwenyeufahamu anaweza kuelewa kuwa akifanya kosa atachapwa na kujirekebisha.

J. R. 23 years (Namba: 301560), Zanzibar

Mwalimu akubali kukosolewaKuuliza maswali ni muhimu sana kwani kunamwezesha mwanafunzi kujiamini mbele ya mwalimuwake. Kukosoa ni muhimu sana kwa mwanafunzi. Si kila kitu afundishacho mwalimu ni sahihikwani mara nyingine mwalimu hupitiwa na kuchanganya mambo anayofundisha. Kwa hiyomwanafunzi anapogundua kuwa mwalimu amekosea ni lazima amkosoe kwani atasaidia nawenzake ambao hawajagundua kosa la mwalimu huyo. Mwalimu yeyote inabidi akubalikukosolewa.

A.O (Namba: 301578), Dar es Salaam

Michango shuleni bado ipo!Tunamshukuru Rais Benjamin W. Mkapa kwa kufuta ada ila bado kuna michango ya mara kwamara.Tulikuwa tunachapwa bila kosa.Tukishatoa hiyo michango kila mwalimu anashika fimbo nakuwaita wale ambao hawajatoa michango na kuwapa adhabu, wakishamaliza adhabu kila mmojaanachapwa fimbo tatu. Je, hiyo elimu bora tutaipataje kama tutafanyiwa hivyo?

A. M (Namba: 304201), Shinyanga

Adhabu ya viboko iangaliwe zaidiAdhabu ya viboko iangaliwe kwa mtazamo wa karibuzaidi. Imeonekana kuwa kuna uhusiano mkubwakatika jamii zetu kati ya adhabu ya viboko na elimubora. Bado watu wengi wanaamini kuwa elimu borahaiwezi kupatikana bila adhabu kali ya viboko. Hivyohali hii inaonyesha kuwa kuna haja ya kuiangaliaadhabu ya viboko katika mtazamo unaofaa ili elimubora ipatikane. Tusijidanganye kwa kusema kuwa sisitulichapwa sana ndio maana tumefikia hapa.Tuangalie

madhara ya adhabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuweza kupoteza viungo vya mwili.O. S. N (Namba: 302217), Ruvuma

Sauti za Marafiki wa Elimu

Tusijidanganye kwa kusemakuwa sisi tulichapwa sana ndiomaana tumefikia hapa.Tuangaliemadhara ya adhabu hiyo ikiwani pamoja na kuweza kupotezaviungo vya mwili.

12

3. Makazi ya Walimu

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) unazingatia ujenzi wa nyumba za walimukama njia mojawapo ya kuwapatia walimu motisha. Serikali inaendelea kusisitiza kujenga nyumbaza walimu za kutosha hasa kuanzia katika maeneo ya vijijini ili ziwe vivutio kwa walimuwanaopangiwa kwenda kufundisha katika maeneo hayo. Kutokana na kutokuwa na nyumba borawalimu wengi wanaacha kazi vijijini, hivyo kunakuwa na upungufu wa walimu.

Nyumba za walimu zikijengwa karibu na shule zitampunguzia mwalimu umbali wa kutembeakutoka nyumbani hadi shuleni na kurudi.Vilevile zitaboresha hali ya maisha na utendaji bora wawalimu. Kuwepo kwa nyumba za walimu karibu na shule ni kivutio kwa walimu kuipenda kaziyao na hatimaye kuboresha elimu. Pia uangalizi wa mali na mazingira ya shule utaboreshwa ikiwawalimu wataishi karibu na shule.Wakati umefika wa Serikali kuangalia na kubuni mbinu sahihizenye kutoa suluhisho la kudumu kwa matatizo ya walimu.

Wasemavyo Marafiki wa Elimu

Serikali itoe kipaumbele kwa walimuWalimu wanawezaje kuwajibika katika kazi? Walimu wanaweza kuwajibika katika kazi zao kwakupewa kipaumbele na Serikali. Kwa mfano vijijini, walimu wengi wanaishi mbali sana na eneo lashule. Hivyo Serikali ingejenga nyumba za walimu karibu na shule ili walimu wapate ari yakuwajibika zaidi.

B. N (Namba: 302204), Kilimanjaro

Sauti za Marafiki wa Elimu

13

Walimu wajengewe nyumba karibu na shuleIli kuboresha elimu ya msingi mazingira yanatakiwa yawe safi na pawepo nyumba za walimu.Kuna baadhi ya shule walimu hawana nyumba za kuishi, wanaishi mbali na shule matokeo yakehuchelewa kufika shuleni. Hii ina maana kuwa mwalimu huyo hataweza kufundisha vipindi vyotekwa kuwa atakuwa amechelewa. Nashauri Serikali kuwajengea walimu nyumba karibu na shuleili walimu hao wasipate usumbufu.

E.P (Namba: 303033), Shinyanga

Mikakati kabambe ya kuboresha elimu

Mimi pamoja na wazazi ambao ni wanaharakati watarajiwa tumekaa na kuzungumziayafuatayo:

1. Kuhakikisha kila mtoto anayestahili kwenda shule anaandikishwa na kuhudhuriadarasani

2. Mzazi/Mlezi atakayezorotesha azimio hilo atachukuliwa hatua kama vile kuelimishwakuhusu umuhimu wa kusomesha watoto, atakayekaidi atachukuliwa hatua za kinidhamu

3. Wanaharakati tutahakikisha kuwa shule yetu inakuwa na taaluma ya hali ya juu, kuwana vitendea kazi vya kutosha, majengo, vyoo, viwanja vya michezo,

4. Tukishirikiana na kamati ya shule, Mratibu Elimu Kata, tumefanikiwa kuomba walimuwilayani na tunao wa kutosha hatuna upungufu

5. Tumeshirikiana pia na uongozi wa shule pamoja na kamati ya shule kuhakikisha kuwafedha yote inayotolewa na MMEM pamoja na zile za Elimu ya Kujitegemea zinatumikakwa masuala yaliyolengwa.

P. M. M. C ( Namba: 302716) Iringa

Tumechoka kugharamia nyumba za kukodiWalimu tumechoshwa na kugharamia malipo ya shilingi 3000 – 5000 kwa ajili ya kulipia nyumbaza kukodi kila mwezi. Je fedha hiyo itatoka wapi kama idara husika imeshindwa kulipa madeniyetu ili tuweze kulipia kodi hizo? Si madeni ya uhamisho tu bali hata walimu wapya walioajiriwahawajalipwa. Idara inatudanganya kuwa tutume barua za madai ila cha kushangaza ni kuwa baruahizo hazipati majibu.

Walimu Karagwe

Uhaba wa nyumba za walimuUkweli nyumba za walimu hazitoshi kabisa. Ili mwalimu afurahie kazi yake tunaomba serikaliiboreshe makazi ya walimu.

Mwl. R.T, Singida

Sauti za Marafiki wa Elimu

14

Walimu hawana nyumba boraNingeomba Serikali iwafikirie walimu hasa wale wanofundisha vijijini kwa kuwa hawana nyumbabora za kuishi. Walimu hao wajengewe kota za walimu. Ningeomba wafadhili wa MMEMwawafikirie walimu wanaoishi vijijini.

I. K. L (Namba: 307444), Lindi

Nyumba za walimu karibu na shuleWalimu wanaweza kufundisha vizuri kama watawekewa mazingira mazuri ya kufundisha. Kwamfano kujengewa nyumba karibu na shule ili kuepuka uchovu wa safari ndefu hadi shuleni.

M. C. M (Namba: 300049), Dar es Salaam

Upungufu wa nyumba za walimuKama tujuavyo mwaka 2006 ni mwisho waMMEM kuwepo katika shule zetu. Bado Katayetu ina upungufu wa nyumba za kuishi walimuzipatazo 72 ambavyo mpaka sasa Kata hiyo inanyumba 6 tu ambazo nazo nyingi ni zilezilizojengwa miaka ya 40. Hali hii inaonyeshawazi katika mashule ya Kata hiyo na hata katikabaadhi ya shule hakuna nyumba hata moja. Je tutafika kwa mtindo huu wa kuweka mipangokwenye kikapu? Mwisho nawaambia amkeni kumekucha viongozi na wananchi.

V.T. M (Namba: 304629), Mwanza

MMEM imeangalia mwanafunzi bila mwalimuMpaka sasa hivi karibu kila shule ina wastani wa vyumba vinne vya madarasa pasipo nyumba hatamoja ya mwalimu. MMEM imeangalia zaidi mwanafunzi bila ya mwalimu. Maoni yangu ninaombauanzishwe utaratibu maalum wa kujenga katika kila shule angalau nyumba nne za walimu ilikuboresha mazingira ya kufanyia kazi walimu. Inatisha sana, mfano katika wilaya yetu hii ni shulechache mno zenye nyumba za walimu. Walimu husafiri umbali wa Kilomita 5 – 20 kwendakufundisha. Hivi kweli mwalimu atajiandaa lini? MMEM ijenge nyumba za walimu kwenyemashule yote.

M. J. M (Namba: 306570), Shinyanga

Sauti za Marafiki wa Elimu

Bado Kata yetu ina upungufu wanyumba za kuishi walimu zipatazo 72ambavyo mpaka sasa Kata hiyo inanyumba 6 tu ambazo nazo nyingi nizile zilizojengwa miaka ya 40.

15

4. Mishahara ya Walimu

Kumcheleweshea mwalimu mshahara ni kumwadhibu pasipo makosa. Mwalimu huyoatawezaje kumudu maisha yake ya kila siku? Atapata wapi fedha ya matibabu maraatakapougua? Hakuna sababu ya kuchelewa kulipa mishahara ya walimu ukizingatia kuwaviwango vya mishahara yao si vikubwa ukilinganisha na sekta nyingine.

Utafiti uliofanywa na Chama cha walimu Tanzania kwa ushirikiano na HakiElimu umebainikuwa, yapo matatizo yanayosababisha walimu kushindwa kufundisha ikiwemo mishaharamidogo wanayolipwa. Mishahara hiyo pamoja na kutoweza kukidhi mahitaji yao ya msingivilevile huchelewa kupatikana na haijulikani tarehe kamili ya kupata mishahara hiyo. Ifikapomwisho wa mwezi walimu wanalazimika kuacha kufundisha kwa ajili ya kufuatilia mishahara.

Wasemavyo Marafiki wa Elimu

Madai ya walimu yashughulikiweMwalimu anapodhulumiwa haki zake hafanyi kazi jinsi inavyotakiwa. Ni vema viongozi waelimu (W) wakalitambua hilo. Naomba nisaidiwe ili nipate madai yangu ya uhamisho maratatu. Inasikitisha na inakatisha tamaa.

E. M (Namba: 300014), Mtwara

Sauti za Marafiki wa Elimu

16

Wiki nzima kufuatilia mishahara!Napenda kutoa maoni yangu juu ya elimu. Katika wilaya yetu hasa ifikapo mwisho wa mweziwalimu huwachukuwa juma zima kufuatilia maslahi yao ili waweze kuendesha shughuli zao kwaukamilifu.Ajabu hupewa majibu ya ubabaishaji ‘mshahara labda kesho’ hivyo mwalimu huwajibikakulala kwa jamaa au nyumba za kulala wageni na kesho hivyo hivyo. Mishahara yao haielewekikila mwezi ni mabadiliko tu.Tatizo liko wapi? Watoto wetu hawapati taaluma kikamilifu kwa ajiliya walimu wao kufuata maslahi na kutafuta riziki ya familia zao.Walimu hao hata wanapopatalikizo hawapewi nauli ya kutosha kwenda kuwaona jamaa zao. Elimu bora iko wapi? Nashauriwalimu tuwathamini na kuwapatia huduma zao muhimu kama maslahi, nyumba bora za kuishina vitendea kazi, hapo elimu bora itatolewa kwa ukamilifu.

S. M (Namba: 300274), Morogoro

Mishahara ya walimu iongezwe na iwafikie mapemaNionavyo na tuonavyo katika taasisi yetu ni kwamba walimu wana mchango mkubwa sana katikakufanikisha ubora wa elimu nchini na ustawi wa wanafunzi kiakili, kimaono na kisaikologia. Kwahiyo hakuna ubishi katika swala la kuwajali walimu hawa kwa kuwapa motisha kama askari jeshiwanavyomotishwa kwa kupewa mishahara mizuri. Kadhalika walimu wanastahili nyongeza yamishahara ili kupunguza makali ya maisha ikibidi kila mwaka katika muda huu wa utekelezaji waMMEM. Hata hivyo ni vema mishahara ya walimu ifike kwa wakati muafaka (kati ya tarehe 25hadi 30 ya kila mwezi)

Z. P, Mara

Chanzo cha madai ya walimu kiangaliweIli kuboresha elimu yetu kwanza hatuna budi kulivalia njuga swala la walimu wetu ambao kilakukicha wanakuwa wakilalama kwa madai mbalimbali. Ni lazima tuangalie nini chanzo cha madaihayo. Kama Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kulipia madeni ya walimu ni vipi basi madeni hayohuongezeka kila kukicha? Ni nani mchawi katika hilo: kama si Serikali kuwaongopea walimuwake? Endapo ni kweli fungu hutolewa, kwa nini Serikali haijafuatilia aliyepewa fungu la kuwalipawalimu madai yao na kulitumia visivyo? Sijasikia kabisa hatua yoyote iliyochukuliwa. Serikali yetuhaina budi kulivalia mkanda hilo.

R.T (Namba: 300439), Dodoma

Tushirikiane kuleta mabadilikoKwa maoni yangu Serikali yetuimetengeneza sera na mielekeo mizuriambayo ikitekelezwa inaweza kutufikishakwenye ubora wa elimu tunaohitaji. Lakiniutekelezaji wa sera za elimu hauhusuWizara ya Elimu pekee bali Serikali iangaliesera na kanuni nyinginezo zilizo chini yawizara mbalimbali, ambazo zinawezakushusha ubora wa elimu. Kwa mfano, ngaziza mishahara, inasemekana kuna watumishi wa Serikali au wawakilishi wa umma wanaolipwaposho za vikao kati ya 50,000/= hadi 70,000/= lakini mwalimu pamoja na mazingira magumu yakazi yake analipwa mshahara kati ya elfu 40,000/= na 80,000/= bila muda wa ziada (over time)

Sauti za Marafiki wa Elimu

Kwa sisi wananchi tusipende kukaa nakuilaumu serikali au walimu ni vizuritufahamu kwamba shule hizi ni zetu natuna wajibu wa kuziboresha,tushirikiane pamoja ili tuweze kuletamabadiliko.

17

wakati anafanya kazi za shuleni hata akiwa nyumbani kwake. Kwa sisi wananchi tusipende kukaana kuilaumu serikali au walimu ni vizuri tufahamu kwamba shule hizi ni zetu na tuna wajibu wakuziboresha, tushirikiane pamoja ili tuweze kuleta mabadiliko.

S. H. M (Namba: 302009),Tanga

Mwalimu anaishi katika mazingira magumuSerikali imeangalia sana maswala ya kuboresha elimu na mazingira bila kuangalia mtoa elimu(mwalimu). Mwalimu anaishi katika mazingira magumu sana ambayo humfanya ashindwe kutoaelimu bora. Mojawapo ya mambo anayosumbuliwa mwalimu ni kama ifuatavyo:-

- Ngazi za mishahara hazilingani na mshahara anaopata mwalimu, kwa mfano mwalimu waTGTS4 anatakiwa alipwe sh. 120600 kwa ngazi yake ya kukaa na cheo hicho kwa miakaminne lakini analipwa sh 95,810 kama ngazi ya mwaka wa kwanza wa TGTS4. Na hilo nitatizo la walimu wote.

- Kutolipwa malimbikizo ya mishahara aliyopunjwa kwa ajili ya kumchelewesha daraja.

- Kutolipwa fedha za uhamisho yaani subsistence na disturbance hivyo tunahamishwakama ng’ombe. Mwalimu ni mnyonge muda wote.

Ili kuboresha elimu tunaomba Serikali iangalie hili kwa makini ili tufanye kazi kwa moyo wote.Mwl.A. M, Mbeya

Iweje choo kijengwe na matofali yasiyofaa?

Harakati za Marafiki wa Elimu zinazidi kupamba moto sehemu mbalimbali, jijini Dar esSalaam.Wanaharakati walifanya mkutano wa hadhara kati ya wazazi pamoja na Katibu Tarafakuchunguza ubora wa choo wanachokitumia watoto wao shuleni. Katika mkutano huowajumbe waliuliza tofali zilizotumika kujengea choo kile ni zile ambazo zilikataliwa kujengeamajengo ya shule kwa madai kuwa hazikufaa. Sasa iweje kama Serikali ilitenga pesa kwa ajiliya kujengea vyoo hivyo, kamati ichukue matofali yasiyofaa wajengee vyoo vile? Akahoji mmojawa wajumbe. Wazazi walidai kuwa kamati iliyoko madarakani imekula baadhi ya pesazilizotolewa na Manispaa kiasi cha shilingi millioni nne kwa ajili ya kujengea vyoo vyenyematundu kumi, kisha kujenga vyoo visivyo imara ambavyo havina usalama kwa wanafunzi hao.

Serikali imeifunga kamati ya shule hadi itakapoleta wahandisi kuchunguza ubora wa chookinachodaiwa na wananchi kuwa hakikujengwa kitaalamu.

Katibu Tarafa alikiambia kikao hicho baada ya kuifunga kamati hiyo na kuahidi kuwa matatizoyote ya wananchi hao yatapatiwa ufumbuzi ndani ya siku 14.

Huu ni mfano bora wa Marafiki wa Elimu. Na wewe Je?

M C T (Namba: 300222), Dar es Salaam

Sauti za Marafiki wa Elimu

18

Mishahara ya walimu wapya inachelewaVilevile nataka kuuliza kuhusu mishahara ya walimu wapya walioajiriwa mwaka huu. Ni kwa ninimishahara yao haijaanza kulipwa mpaka muda huu wakati takwimu inaonyesha idadi ya walimuwanaotakiwa kila mwaka? Kwa maana hiyo hata takwimu ya mishahara yao ipo wazi. Kwa ninimpaka sasa hawapewi mishahara yao? Au wana utaratibu gani kuhusu mishahara ya hawawalimu.

Emmanuel,Tabora

Matatizo ya walimu ni mengiWalimu ndio hufanya wanafunzi kupanda au kushuka kielimu. Kwa hiyo uwepo wao kwa wingishuleni na kulipwa mishahara yao kwa muda muafaka ndio njia itakayowawezesha wanafunzikupata elimu kiufasaha zaidi. Inasikitisha kuona jamii kubwa ya Kitanzania wanawadharau walimuhasa wa shule za msingi.Tunaposema shule ya msingi au elimu ya msingi tuna maana huo ndiomsingi mkuu wa maisha na msingi huo hutolewa na walimu. Nilifanya utafiti na Mwenyekiti wabaraza la watoto kuhusu matatizo mengi wanayopata walimu. Kwa kweli tuligundua ni matatizomengi sana ikiwa ni pamoja na mishahara yao kuwa ni chini, kutokuwa na usafiri kutokawanakoishi kwenda shuleni ukizingatia shule nyingi tulizofika hazina nyumba za walimu.Vilevilekuna swala la kuchelewesha mishahara yao. Mwalimu itamwia vigumu kufundisha au kutoa elimuiliyo bora katika mazingira ya matatizo kama haya.Maoni yangu napenda kuishauri jamii ya Kitanzania kuwajali walimu na Serikali kwa ujumlaihakikishe kuwa matatizo kama haya yanapungua kama sio kwisha kabisa. Vilevile napendakuwapa moyo walimu wafanye kazi kwa bidii ili kumtokomeza adui ambaye ni “Ujinga”. Pianapenda kutoa ushauri kuwa vyama mbali mbali vya walimu viwasaidie na Serikali iwasaidiekupitia vyama hivyo. Hata ukisikiliza wimbo uitwao walimu uliotungwa na msanii John Workerunaweza ukaelewa matatizo wanayopata walimu.

F. E (Namba: 302824), Mwanza

Urasimu katika kurekebishiwa mshaharaMimi ni mwalimu wa shule ya msingi. Harakati zangu zote za kuomba kurekebishiwa mshaharana kulipwa mapunjo zinagonga mwamba. Nilishapeleka tatizo hili ofisi ya T.S.C wilayani ambayondiyo ofisi yetu ya fedha. Wakalishughulikia vizuri na kuniambia nisubiri kwa muda wa miezimiwili. Lakini bado hakukuwa na badiliko lolote baada ya muda huo. Nilivyorudia tena kuuliziaofisi ya fedha, waliniambia shughuli yako tulishaifanya wanaokwamisha ni hazina makao makuu.Mimi binafsi nashindwa kuwasiliana na hazina. Hali hii inatia uchungu sana. Kwani kazi ninafanyatena katika mazingira magumu sana. Halafu haki yangu sitahili sipati. Naomba mnisaidiekuukemea urasimu na ubabaishaji uliopo kati ya ofisi ya fedha wilayani, vijijini na hazina makaomakuu ili labda na mimi siku moja nije nifaidi matunda ya jasho langu. Matatizo kama hayayasipotafutiwa ufumbuzi mapema, zoezi zima la kuboresha elimu haliwezi kufanikiwa maana niwalimu wengi wenye tatizo kama hili.

Mwl. J. M, Sumbawanga

Mishahara ya walimu haitoshiMMEM inaonaje suala la mazingira ya walimu? Mfano walimu wamekuwa wakidai muda mrefukuwa mishahara haitoshi kabisa ukilinganisha na hali ya uchumi wa nchi. Pia hakuna hatamarupurupu yanayotolewa kwa walimu. Je, hili MMEM imeliona? Ni vizuri tunapozungumzia

Sauti za Marafiki wa Elimu

19

kuhusu kuboresha elimu walimu wakapewa kipaumbele kwani wao ndiyo kikolezo muhimu sanakatika kuboresha elimu nchini. Ni sawa na mboga isiyo na chumvi ya kutosha tunaposahauwalimu.

M. J. M ( Namba: 306570), Shinyanga

Mishahara ya walimu ni midogo na hakuna marupurupuNashukuru Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Napenda kutoamaoni yangu yanayohusu sababu ya kushuka kwa elimu ya shule za msingi pamoja na juhudikubwa ya MMEM. Sababu kubwa ni walimu kulipwa mshahara mdogo/kidogo ukilinganisha nakazi kubwa wanayoifanya, pamoja na kunyimwa posho. Unakuta mwalimu anafundisha darasalenye wanafunzi 90 huku ana kipindi kimoja muda wa dakika 40. Katika kipindi hicho anatakiwaasahihishe daftari 90 na pia inabidi aende kufundisha darasa lingine lenye wanafunzi 70. Hivyobasi mwalimu anapofikiria hapewi posho pia mshahara wake ni kidogo basi juhudi ya kufundishaitakuwa ndogo.

Pili, ukija kulinganisha mshahara na posho zawafanyakazi wengine kama vile madaktari, wabunge,wakuu wa mabenki na wanajeshi wanalipwa mishaharamizuri, tena unakuta mshahara wa mwalimu unazidiwana posho ya wafanyakazi hao. Ukija kuchunguza bilakuwepo mwalimu basi watu hao wabunge, madaktari,

wanajeshi wakuu wa mabenki, posta, wasingepatikana. Hivyo naomba Serikali kupitia (MMEM)ishughulikie suala hili ndipo elimu ya shule ya msingi itaweza kuwa juu kwa kuwapatia poshowalimu na mishahara mizuri.

E.A (Namba: 304776), Bukoba

Gharama za maisha zimepanda, mshahara wa walimu je? Mwalimu ni chachu kwa kitengo cha elimu kwani ana uwezo wa kupandisha au kushusha elimumahali popote duniani. Kwa hiyo yeye ni wa kwanza kufikiriwa kwa upande wa mishahara namarupurupu. Sasa je? Mbona mishahara yao hucheleweshwa kutolewa na mishahara haiendi nawakati? Nasema haiendi na wakati kwa sababu gharama za maisha zimepanda kiasi kwambamshahara wa mwalimu bado unaonekana mdogo. Kwa kutoa mishahara inayoendana na wakatimwalimu anaweza kutumia muda mwingi darasani kwa kumwelimisha mtoto pasipo yeyekupoteza muda kwa kujitafutia riziki nje.

A. S. N, Morogoro

Kukatwa mishahara Mishahara yetu haieleweki, kila mwezi na mshahara wake ukipata salary slip utashangaaumekatwa pesa ambayo haikuhusu. Mfano unakatwa kwa ajili ya mahakama pesa nyingi tu ukidaiwanakwambia ungojee salary slip. Hiyo inavuruga sana bajeti zetu.

Mwalimu, Rungwe

Sauti za Marafiki wa Elimu

Bila kuwepo mwalimu basiwatu hao wabunge, madaktari,wanajeshi wakuu wa mabenki,posta, wasingepatikana.

20

5. Ubora wa Elimu

Sera ya Elimu na Mafunzo inasisitiza ubora katika elimu na inazingatia maeneo yafuatayo:Uboreshaji wa mbinu za ufundishaji kwa walimu, kuhakikisha upatikanaji wa zana bora zakufundishia na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji muhimu yanayolenga katika kuboreshakiwango cha elimu.Walimu darasani ni zana muhimu katika kuinua ubora wa elimu. Lengo hilihufikiwa panapokuwa na mazingira mazuri, mahali ambapo wanafunzi huweza pia kushirikikikamilifu katika kujifunza.

Wasemavyo Marafiki wa Elimu

Idadi ya walimu iendane na idadi ya wanafunziUhaba wa walimu katika baadhi ya shule unasababisha kudidimiza elimu kwa wote wanaoihitaji.Mfano shule moja ina walimu saba (7) na ina wanafunzi 240 ambao hao ni kuanzia darasa lakwanza hadi la saba. Isitoshe shule hii ni ya muda mrefu. Kutokana na hali hii wanafunziwanakosa masomo mengi. Kwa hiyo ninaomba Serikali ijaribu kuangalia shule hasa ambazo zikovijijini. Kwa kweli hali hii mimi hainifurahishi kabisa. Jambo jingine ni baadhi ya walimukutohudhuria vipindi na pia wengine kutoa adhabu kwa upendeleo kwa wanafunzi. Kutokana nahayo ninawaomba kujua kwamba tutasaidiwaje? shule za vijijini hazifuatiliwi kimaendeleo ilamijini ndio huwa na walimu wengi wa kutosha.

D. P (Namba: 301037),Tanga

Sauti za Marafiki wa Elimu

21

Vivutio katika shule za msingiMambo kadha yanaweza kuchangia utoro shuleni. Moja ni mazingira ya shule yenyewe. Katikashule nyingi kuna tatizo la ukosefu wa vivutio mbalimbali kama vile michezo, miti kwa ajili yakivuli na mengineyo. Kukosekana kwa vivutio hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzikukosa ari ya kwenda shule.

Jambo jingine ni kuwa ufundishaji wa walimu haujengi mazingira mazuri ya watoto kujifunza.Walimu bado wanatumia mbinu ambazo hazimshirikishi mwanafunzi na kumpa mvuto wakupenda kujifunza na hatimaye kupenda shule. Walimu wengi bado wanajiona kuwa wao nivisima vya maarifa na kuwaona wanafunzi hawajui chochote bali wao ni wapokeaji tu.Vilevilejambo jingine ambalo ni baya zaidi ni kuwa bado katika shule nyingi kwa wazi tu walimuwanatumia adhabu za viboko na kushindwa kujua kuwa viboko ni kichocheo hasi kinachowezakusababisha wanafunzi kukimbia shule.’

A. M (Namba: 302341), Kilimanjaro

Mwalimu boraMwalimu bora ni mwalimu yule ambaye ana vigezo vifuatavyo:

Kwanza, mwalimu bora awe amehitimu masomo yake ya ualimu na kufaulu vizuri.

Pili, mwalimu bora awe mwenye kuipenda kazi yake wakati huo huo akijua kwamba kazi yaualimu ni wito.

Tatu, mwalimu awe mwenye kuwapenda wanafunzi wake, kwani bila ya kuwapenda, wanafunziwatamchukia mwalimu pamoja na somo lake hatimaye kushindwa kulielewa somo lake.

Nne, mwalimu awe mwepesi kusikiliza wanafunzi wake kama ni njia gani ambazo mwalimuakizitumia kuwafundishia wanaweza wakaelewa vizuri zaidi.

Tano, mwalimu bora awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa wanafunzi wake na pia awezekukosolewa na wanafunzi wake pindi anapokosea.

A.A. O (Namba: 301578), Dar es Salaam

Uhusiano wa walimu katika shule za mijini na vijijiniMimi nina kero moja inayonikabili kama mwanajamii.Tunapopigania kuboresha elimu bado kunasuala sugu linalotukabili, nalo ni uhusiano wa walimu waliopo shule za mijini na vijijini. Utakutashule ya kijijini ina wanafunzi 600 na walimu wanne au watano, hivi kweli hawa walimuwatamudu kutoa elimu bora? Wakati huo huo shule za mijini zina walimu zaidi ya 20. Shule zavijijini hazina walimu wa kike, hivi kwa nini? Wakati shule za mijini zina walimu wa kike hata zaidiya kumi.

Mwl. R. D.A (Namba: 304076), Shinyanga

Sauti za Marafiki wa Elimu

22

Majadiliano kati ya walimu na kamati ya shuleWalimu wawe na siku yao katika shule wanayofundisha kwa ajili ya majadiliano na kamati yashule na kuzungumzia shule yao kwa ujumla kila mwalimu akitoa maoni kuhusu a) wanafunzi,b) vipindi vya shule c) matatizo ya walimu nk.

S. S (Namba: 302225),Tanga

Ushirikishwaji wa wanafunziMwanafunzi ili aweze kusoma vizuri na kwa makini zaidi, anahitaji mazingira mazuri, madarasamazuri na yenye samani zilizopangwa vizuri ili kumjengea mwanafunzi hisia na hamu yakuendelea kusoma kwa bidii zaidi. Wanafalsafa walisisitiza umuhimu wa mazingira mazuri yamwanafunzi kujifunza. Mazingira mazuri ni pamoja na madarasa mazuri, vyoo safi, mazingira safiya kuizunguka shule. Ili wanafunzi hawa waweze kuelewa vizuri zaidi, wanatakiwa washirikishwekikamilifu katika somo ambalo mwalimu anafundisha (participatory method). Mwalimuawasaidie wanafunzi kusoma kwa njia ya vitendo (learning by practice). Mwanafalsafa DrMontessori aliona umuhimu wa wanafunzi kushiriki somo kwa vitendo kuwa wanafunzi hawahuwa na uwezo zaidi wa kuelewa somo.

E. J (Namba: 302934), Morogoro

Uhamisho unapotumika kama adhabuWalimu walevi wakati wa masomo wachukuliwe hatua kali siyo kuhamishiwa katika shulenyingine kama ilivyo kwa sasa. Baadhi ya walimu wanapopatikana na kosa la kuwa walevi kazinibasi utakuta wanapata uhamisho wa kupelekwa shule nyingine.

W. M. Kagera

Wanafunzi mia moja mwalimu mmojaNapenda kuwapongeza MMEM kwa kuletamaendeleo katika elimu, lakini kwa mtazamowangu mimi naona ya kwamba itachua mudamrefu sana katika kuleta maendeleo. Maendeleosio kujenga tu shule bali ni kumwendelezamwanafunzi. Unaweza ukakuta darasa moja linawanafunzi mia moja badala ya 45 na mwalimuanayefundisha ni mmoja halafu unaweza ukakutavitabu ni viwili, sasa hapa inakuwa ni ngumu sanakwa wanafunzi wote kuelewa. Unakutawanaoelewa ni wachache sana. Mimi ningeshauri ili waleta maendeleo wangeongeza walimu,vitabu vikawa vingi na pia darasa moja lingekuwa na wanafunzi si zaidi ya 45 badala ya 100.

N. R (Namba: 302445), Mwanza

Uwiano kati ya walimu, wanafunzi na madarasaKuna shule nyingine bado zina wanafunzi zaidi ya 1000, nyingine zina walimu chini ya 5, nyinginezina walimu zaidi ya 30, nyingine zina madarasa chini ya 5 na wanafunzi zaidi ya 500. Kwa hiyoshule nyingi hadi sasa bado hazijatekeleza agizo la waraka Na. 4 na Na 5 kutokana na ukosefuwa vyumba vya madarasa na walimu. Kwa hali hii tunaomba wahusika wa kuboresha elimu

Sauti za Marafiki wa Elimu

Unaweza ukakuta darasa moja linawanafunzi mia moja badala ya 45na mwalimu anayefundisha nimmoja halafu unaweza ukakutavitabu ni viwili, sasa hapa inakuwani ngumu sana kwa wanafunziwote kuelewa.

23

waangalie mgawanyo wa madarasa na walimu kwa kufuata waraka Na 4 na Na 5. Piawazigawanye kwa kuzipunguzia mzigo shule zenye wanafunzi wengi. Vilevile wazipunguziewalimu shule zenye walimu wengi kwa kuzipa shule zenye walimu wachache ili ikama iende sawana maagizo ya waraka Na 4 na Na 5. Hii italeta changamoto ya kuboresha elimu katika shulezote hasa za vijijini.

K. K, Kigoma

Mazingira ya kufundishia na kujifunzia yaboreshweKwanza hivi sasa baadhi ya shule walimu hawafundishi ipasavyo kutokana na mlundikano wawanafunzi katika chumba kimoja. Uwiano unaotakiwa ni mwalimu mmoja wanafunzi 45, lakiniutakuta watoto wamezidi kuanzia 90 – 120, na tatizo ni upungufu wa vyumba vya madarasa. Pili,tatizo la upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia hasa vitabu vya kiada na rejea ni tatizoambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu. Utakuta darasa lenye wanafunzi 70-90 wanavitabu 4-10. Hapa elimu siyo rahisi kuboreshwa kwa haraka.

Tatizo lingine ni kuwa serikali au wakuu wa idara ya elimu wilayani na mikoani baadhi badowanalazimisha walimu kufundisha muda wa ziada hasa darasa la VII na IV eti kwa kuwawanajiandaa kwa mitihani ya taifa.Walimu wanalazimishwa kufanya hivyo pasipo malipo ya ziadamatokeo yake ni kuharibu mitihani kwani walimu watafundisha kwa kinyongo hivyowanafundisha vitu ambavyo havimsaidii mwanafunzi.

Kuna jambo linalonishangaza na kunisikitisha sana. Jambo hilo ni upatikanaji wa elimu boravijijini, ukweli ni kwamba elimu inayotolewa vijijini siyo bora kwa sababu walimu wengiwamekuwa walevi kupindukia, unakuta muda wa masomo walimu wanakuwa kwenye vilabu vyapombe. Je, atafundisha muda gani? Mwanafunzi ataelewa nini mwalimu anapofundisha akiwaamelewa? Jamani walimu badilikeni ili muweze kufundisha kwa ufanisi zaidi kwani watoto ndioviongozi wa baadaye na ndiyo tegemeo la taifa.

P. K. M (Namba: 300420), Rukwa

Wizara itilie mkazo maendeleo ya elimu vijijiniMaafisa wa elimu na walimu kuwepo kwa muda mrefu kwenye kituo kimoja cha kazi ni haliambayo inasababisha kuzorota kwa ufanisi wa kazi na kushuka kwa taaluma yao. Pia ongezekola vyumba vya madarasa lisilokuwa na uwiano na idadi ya walimu kwenye shule hasa vijijini.Mfano, shule moja ilikuwa na wanafunzi 750 wakati walimu wa shule hiyo walikuwa saba (7)ambapo uwiano unakuwa kila mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 108. Je, ongezeko lavyumba vya madarasa litachochea kupanda kwa elimu katika sehemu hiyo? Ongezeko lamadarasa kwenye shule hizo msaada wake ni upi wakati mwalimu analazimika kulundikamikondo yote ndani ya darasa moja ili kupunguza ugumu wa kufundisha? Mwalimu huyo huyoana vipindi zaidi ya vitano katika madarasa tofauti. Nasikitishwa sana na mipango ya Wizara yaElimu isiyotilia mkazo maendeleo ya elimu vijijini ambapo watu wengi makazi yao ni vijijini.

M. M (Namba: 306610), Mtwara

Sauti za Marafiki wa Elimu

24

Umuhimu wa vifaa vya kufundishiaVifaa vya kufundishia pamoja na walimu wa kutoshandio nguzo kuu ya kufanikisha mpango mzima wakuendeleza na kuleta ubora wa elimu hasa katikaelimu ya msingi ambayo ni haki ya kila mtanzaniakuipata. Shule inapokuwa na vifaa bora na vyakutosha huleta mabadiliko makubwa shuleni nakatika elimu kwa ujumla.

K .S (Namba: 302705), Mwanza

Nyenzo za kufundishia ziwepo ili kufanikisha somoBaadhi ya mambo yanayozorotesha elimu ni kutokuwa na nyezo za kufundishia. Hali kama hiihusababisha watoto kushindwa kwenda shule baada ya kuambiwa na mwalimu watoe fedha kwaajili ya kununulia vifaa ili kufanikisha somo. Watoto wanapopewa adhabu nzito huwafanyawaamue kukaa nyumbani kwa kuogopa adhabu.

J.W (Namba: 306374), Mwanza

Walimu wasiotimiza wajibu wafukuzweWalimu wanapokuwa shuleni wamekaa na kuanza kufuma vitambaa vya majumbani mwao: Hiindio elimu? Walimu utawaona mitaani wanazunguka wakati wa kazi wanatafuta pombe zakienyeji au utawaona wamelewa. Siku nyingine hafiki shuleni kwa kisingizio kuwa anauguliwa.Mimi naomba serikali iliangalie hili kwa makini sana ili kuwabana na kuwachukulia hatua kali aukufukuzwa kazi.

N. B (Namba: 302417), Shinyanga

Mgawanyo wa walimu uzingatie pia idadi ya wanafunzi Napenda kutoa maoni yangu jinsi uhaba wa walimu unavyoathiri utoaji elimu katika shule nyingihapa nchini. Katika maeneo mengi hapa Tanzania hasa vijijini utakuta shule ina msongamanomkubwa wa wanafunzi mathalani 520 na idadi ya walimu wanaofundisha shule hiyo ni 4 tu, yaaniukigawanya idadi ya watoto na walimu waliopo utakuta kila mwalimu anafundisha watoto 104.Je, watoto hawa watakaa darasa lenye ukubwa gani? Je mwalimu huyu atawezaje kuwasaidiawatoto hawa kwa dakika 40 za kipindi kimoja? Wizara iliagiza mgawanyo wa walimu lazimauzingatie idadi ya watoto yaani 40 kwa kila darasa mwalimu mmoja, lakini maeneo mengi hapanchini agizo hili halijapewa nafasi yake. Ni vema likapewa nafasi yake.

P. M, Iringa

Sauti za Marafiki wa Elimu

Vifaa vya kufundishia pamoja nawalimu wa kutosha ndio nguzokuu ya kufanikisha mpangomzima wa kuendeleza na kuletaubora wa elimu

25

Vitabu vya kufundishia viboreshweWizara ya Elimu kwa sasa hivi imetunga au kupitisha vitabu vya kufundishia mashuleni vyakiwango cha chini kabisa hususan vitabu ambavyo vimetolewa mwaka 2000. Mada zilizomo niza chini sana ukilinganisha na vitabu vile vya zamani. Hii ni kwa masomo yote. Utakuta wizarainatoa maelekezo kwa mfano maarifa ya Jamii ambayo imechukuwa masomo yote sasa.Walimunao hawakufundishwa namna ya kufundisha somo hilo kikamilifu. Mada zilizomo ni fupi sana.Kwa walimu wa sasa nasema siyo rahisi kabisa kutafuta vitabu vya ziada pamoja na vya rejeaingawaje kwenye maazimio wameyaandaa somo la stadi za kazi. Wizara inasema mwalimuachague mada anazoweza kufundisha. Sasa utakuta walimu wanakimbilia michezo na zile rahisi.

K. L, Lindi

Walimu na viongozi Ikimba wachangamka!

Harakati za Marafiki wa Elimu hapa Ikimba Area, Butelankuzi,Tarafa ya Rubale, zatia fora; hatawalimu wetu wamechangamka na wao wakachagua kuwa Marafiki wa Elimu kwania yakuboresha elimu. Walimu hawa wametiwa motisha na viongozi wapendao elimu bora-wakajadiliana na wazazi wa wanafunzi, wakakubaliana kuongeza saa za ziada ili kupanua elimuya watoto kwa kufundisha masomo ya ziada hadi saa 12.00 jioni kila siku, isipokuwa siku zaJumamosi, Jumapili na sikukuu tu kwa nafuu ya malipo kidogo ya masomo ya ziada (tuition).

Tumejenga miundo mbinu kama madarasa, nyumba za walimu pamoja na vyumba vya utawalabora na vyoo.

Semina za MMEM pamoja na udhibiti wa fedha zimeendeshwa mara mbili kwa walimu husikana kamati za shule hata ripoti ya mapato na matumizi ilianza kutundikwa kwenye ubao wataarifa za shule huku MEMKWA ikiendeshwa pembeni. Hata gazeti la SautiElimu limetumiwana kusomwa hapa shuleni hata vijijini tunapotembelea.

Pamoja na kuwapo mikondo ya madarasa kwenye shule za msingi na madarasa ya awali,viongozi wema kwa pamoja wameshirikiana na jamii, ikajengwa Sekondari ya Kata na sasamaandalizi ya nyumba za walimu wa sekondari yamekwishafanywa na ujenzi karibu utaanzakwa ajili ya kuboresha elimu.

Wakati ninapoandika, utawala wa elimu tayari unayo maktaba yenye vitabu vyenye tungo zakisasa kwa ajili ya watoto na jamii.

Mijadala mingine zaidi inaendelea kufanywa ili kuboresha elimu.

Na wengine je?A. K (Namba: 302439), Kagera

Sauti za Marafiki wa Elimu

26

Serikali inajitahidi kuboresha elimu vijijiniSasa hivi Serikali ya Tanzania inajitahidi kuboresha upatikanaji wa elimu ya msingi hasa sehemuza vijijini ambako kuna idadi kubwa ya wanafunzi, sehemu hizi zinahitaji sana uongozi ambaoutasaidia katika kuweka mazingira ya elimu yanayofaa kwa mwalimu na mwanafunzi kufanya kazizao ipasavyo.

A. M (Namba: 304460), Arusha

Watoto kufanya kazi kwa walimuKero zangu katika hii shule ni kuwa, watoto muda mwingi wanapoteza kufanya shughuli zawalimu kama kulima mashamba ya walimu na shughuli mbalimbali

1. Siku zingine wanakaa darasani siku nzima bila kufundishwa2. Wakati mwingine watoto wakiandika hawasahihishwi3. Ambalo ni kero kubwa katika hii shule watoto bado wanalipa karo. Kwa mwaka Sh. 1200

ambayo wanalipa kila mwezi, mtoto anapokosa karo anapigwa viboko na kufukuzwashule mpaka atakapoipata.

Je, hii shule watoto watasaidiwaje ili wapate haki yao ya elimu?E. J (Namba: 302511), Mwanza

Tuisheni zinaendelea!Siyo siku nyingi zilizopita Serikali kupitia wizara husika ilikataza waalimu kufundisha masomo yaziada, yaani “tuisheni”. Hii bila shaka ililenga katika maswala mazima ya kuboresha elimu nchini.Yaani ili mwalimu aweke roho na mawazo yake yote kwa mwanafunzi wake wa darasani tubadala ya kuyagawa mara mbili kwa kufikiria wale anaowafundisha masomo ya ziada.

Amri hii ilipokelewa kwa roho moja na walimu kwani baada ya muda mfupi tu masomo hayoyalikoma mashuleni mara moja. Ila kilichokuja kunishangaza ni kuona muda huo huo wanafunzihawakukoma kuomba fedha za masomo hayo. Kitu hiki kilizua maswali mengi kichwani mwangu,ambapo ili kupata majibu yake niliamua kufanya uchunguzi rahisi (usio na gharama). Na matokeoyake yalikuwa hivi:

Ni kuwa kilichofanyika ni kubadili mazingira tu ya kufundishia.Yaani badala ya kufundishia katikamadarasa ya shule zao, wamefungua “senta” (pembeni) mbali ya shule husika na wenginemajumbani mwao ambako ndiko wanakoyafundishia masomo hayo. Na kila Jumamosi wanafunzihuenda na kati ya sh. 500/= na 800/= ili kufanya mtihani wa kila wiki (weekly test) ukiachilia mbaligharama za kati ya sh. 2,000/= na 4,000/= kwa kila somo kwa mwezi. Hili ni tatizo kwa kwelikatika sekta ya elimu. Kwa mfano inatakiwa kujiuliza, je kwa nini mwalimu apende kufundishamasomo ya ziada? Na kama jibu ni kujiongezea kipato, basi utatuzi wa tatizo hili ungekuwa nikuwalipa vizuri walimu ikiwa ni pamoja na kupewa marupurupu mazuri ya kuridhisha.

E. M (Namba: 306855), Dar es Salaam

Sauti za Marafiki wa Elimu

27

Ajira kwa watoto zipigwe vitaJamii inapaswa kutambua kwamba kila mtoto anahaki ya kupata elimu bora na ndio changamotokubwa kwa maendeleo ya taifa endapo aduiujinga atakuwa ametokomezwa kabisa. Hivyowanaharakati wanapaswa kutoa mwamkomkubwa katika jamii ili kuweza kuleta mabadilikoya elimu katika jamii inayowazunguka.Kinachotakiwa ni kupiga vita ajira mbaya kwawatoto wanaopaswa kwenda shule na kwa

watoto wanaoachishwa shule kwa sababu zisizo za msingi na kufanya kazi za nyumbani.

Pia Serikali inapaswa kutoa adhabu kali kwa mzazi au mlezi yeyote atakayemzuia mtoto kwendashule kwa ajili ya kufanya kazi nyumbani kama vile kuchunga, kulima, kulinda nyumba na sababuzingine zisizo za msingi.

D. M (Namba: 301834), Dodoma

Walimu wapatiwe maslahi yaoElimu inajumlisha upatikanaji wa wanafunzi, vifaa vya kusomea na walimu. Hivyo ili elimu boraipatikane Serikali inatakiwa kuimarisha mazingira bora na mazuri ya walimu kama ilivyofanyakwa madarasa na vitabu. Si kwamba mishahara tu isipokuwa watendaji wa serikali kamawakurugenzi, maafisa utumishi na maafisa elimu hususani wa wilaya imekuwa ni chachu yakukwamisha maendeleo ya elimu, hii inatokana na matumizi mabaya ya fedha mbalimbalizinazotolewa kwa ajili ya malipo ya walimu aidha kwa maslahi yao binafsi au kuhamisha fedhahizo na kuzitumia katika shughuli nyingine za Halmashauri.

Naomba ufahamu inatokea mwalimu halipwi fedha za likizo au za uhamisho, bahati mbaya zaidihana transport allowance au house allowance. Unadhani atafanya nini ili apate fedha za nauli kwaajili ya likizo, hivyo itabidi afanye shughuli za ziada hali ambayo itamfanya akose morali yakufundisha na hivyo kujiingiza katika shughuli nyingine. Kwa hiyo serikali iwadhibiti maafisa hawawaache kutumia fedha kwa maslahi yao na wawajali walimu. Pia naomba nifahamishwe ni linitutalipwa fedha za kujikimu na mishahara/posho ambazo hatukulipwa, na fedha ya kujikimu nishilingi ngapi?

Mwl. K , Mwanza

Wazazi wapewe taarifa za maendeleo ya watotoNi muhimu kwa wazazi kushirikishwa katika maendeleo ya watoto wao shuleni. Njia moja rahisiya kuwashirikisha wazazi ni kuwapatia wazazi mmoja mmoja taarifa za maendeleo yamwanafunzi kwa kila muhula wa masomo. Kinachoshangaza ni kuwa baadhi ya wakuu wa shuleza msingi za Serikali huwanyima wazazi taarifa za watoto wao mpaka watoe fedha za michangoiliyoainishwa na shule vinginevyo hawapatiwi taarifa hizo. Naamini kuwa michango na maamuzikama hayo hayaleti maendeleo kielimu bali huwanyima wazazi au walezi haki ya msingi yakushiriki kujua maendeleo ya watoto wao.

Sauti za Marafiki wa Elimu

Kinachotakiwa ni kupiga vita ajirambaya kwa watoto wanaopaswakwenda shule na kwa watotowanaoachishwa shule kwa sababuzisizo za msingi na kufanya kazi zanyumbani.

28

Ni muhimu wazazi wapewe taarifa za maendeleo ya watoto wao bila masharti yeyote. Endapokuna michango basi itumiwe njia nyingine mbadala ambayo ni shirikishi ya kuwadai wazazi auwalezi wa watoto husika badala ya maamuzi ya kibabe yasiyosaidia elimu nchini.

L. M (Namba: 304302), Arusha

Serikali iboreshe taaluma ya walimuWalimu wengi wa shule za msingi wana hali ngumu sana ya kimaisha ukizingatia mishahara yawalimu iko chini sana. Pili, walimu wanafundisha katika mazingira magumu kwani darasa mojalinakuwa na wanafunzi wengi hivyo inakuwa vigumu kwa walimu kujua kwa undani mazingira yawanafunzi kama wanaelewa wanachofundishwa.Tunajua kwamba uwalimu ni wito lakini inafikakipindi walimu wanakata tamaa na maisha ya kiualimu badala yake wanafikiria kuingia katikataaluma nyingine mbali na ualimu. Kwa mtaji huo taaluma kwa kiasi fulani inadidimia.Mapendekezo yangu kwa serikali ni kuangalia kwa makini circular nzima ya ualimu na kuangaliauwezekano wa kuongeza mishahara ya walimu kwani kuna taasisi nyingine za Serikali waajiriwake wanapata mishahara ya juu zaidi, vile vile uboreshaji wa madarasa na kuongeza nyenzo zakufanyia kazi kwa walimu. Kuimarisha vyuo vya ualimu pamoja na kuongeza idadi yawanaosomea ualimu kwani walimu wanapata wakati mgumu kwenye kufundisha.

G. D. M (Namba: 307053), Dar es Salaam

Mwalimu bora ni yule anayeweza kutoa elimu boraHamu ya kujifunza huweza kuongezeka au kupungua kutokana na motisha. Katika hali yakawaida, motisha chanya hupandisha ari ya kujifunza wakati motisha hasi hupunguza (hushushaari hiyo). Mazingira mazuri ya kujifunzia humwezesha mwanafunzi kujifunza vizuri zaidi. Katikamazingira mazuri ya kujifunzia ‘child – friendly environment’ vipaji vya watoto hukua haraka.Mwalimu mwenye furaha itokayo moyoni huwa kiungo bora cha mazingira haya. Kama mwalimuhana furaha ya kweli hufanya kazi ya kufundisha ili kupitisha siku tu. Hata kama wakaguziwanaolingana na idadi ya wanafunzi wangekaa darasani mwake bado mwalimu huyohatafundisha ipasavyo. Mtoto hajifunzi masomo pekee toka kwa mwalimu wake. Hujifunza hatamwenendo mzuri au mbovu toka kwa mwalimu wake. Hujifunza hata kuthamini toka kwamwalimu wake. Mwalimu aliyeboreshwa mwenye nia ya kweli mwenye demokrasia ya kwelindiye anayeweza kutoa elimu bora. Kama hali za walimu hazitajaliwa lazima tutegemeeubabaishaji mwingi katika kutoa elimu. Vilevile uchaguaji na uandaaji wa walimu lazima uwemakini na siyo kila apatikanaye apewe kazi ya ualimu. Lazima mwalimu afikishwe mahali pakumweleza mtoto aliyeko mbele yake sentensi hii ‘ulivyo ndivyo nilivyokuwa, nilivyo ndiyoutakavyokuwa.

G. M (Namba: 304167), Kagera

Sauti za Marafiki wa Elimu

29

Anwani za vyombo vya habari

VYOMBO VYA HABARI FAKSI SIMU SLP

Alasiri 2773582 2700735/7 31042, Dar es SalaamBusiness Times 2130033 2118378/9 71439, Dar es SalaamDaily News 2112881 2110595 9033, Dar es SalaamDTV/CTN/Channel 10 2113112 2116342 14678, Dar es SalaamEast African Radio 2775915 2775916 21122, Dar es SalaamFinancial Times 2773583 2700735/7 31042, Dar es SalaamIkulu 2113425 2116913 31042, Dar es SalaamMaelezo Hall 2113814 2122771Majira 2118382 2118377 71439, Dar es SalaamMsanii Afrika 2500713 2503262 1732, MwanzaMtanzania 2461459 2461459 4793, Dar es SalaamMwananchi 2180183 2180647 19754, Dar es SalaamNipashe 2700146 2700735/7 31042, Dar es SalaamRadio Uhuru 2182369 2181700 9221, Dar es SalaamRadio Free Africa 2500713 2503262 1732, MwanzaRTD 2865569 2865563 4793, Dar es SalaamRTD 2865569 2865563 9191, Dar es SalaamStar TV 2773583 2700735/7 1732, MwanzaTaifa Letu 2773583 2700735/7 31042, Dar es SalaamTaifa Letu 2461459 2461459 31042, Dar es SalaamThe African 2773582 2461459 4793, Dar es SalaamTvT 2772603 2700464 31042, Dar es SalaamTvT 2182659 2182665 31519, Dar es SalaamThe Citizen 2120791 2120897 20588, Dar es SalaamThe Citizen 2461459 2461459 19754, Dar es SalaamUhuru/Mzalendo 2183780 2461459 4793, ArushaUhuru/Mzalendo 2183780 744-691490

744-308529 9221, Dar es SalaamVictoria FM 2622944 2622091 1102, MusomaVoice of Tabora 744-261761 84, Tabora

Sauti za Marafiki wa Elimu

30

HitimishoMaoni ya Marafiki wa Elimu na hatua wanazochukua zinadhihirisha kwamba Tanzania inawananchi makini na hodari. Wananchi wanaofikiri na wenye maoni thabiti. Wananchi ambaohawaogopi kutoa changamoto na kuwauliza maswali viongozi wao.

Wananchi wanaofahamu kuwa shule siyo majengo na madawati pekee bali pia ziwe mahalaambapo wanafunzi watajifunza kuheshimu utu wa kila binadamu, kufurahia elimu bora,kuchambua, kuuliza maswali na kuwa wabunifu.

Hakuna jumuiya wala demokrasia ambayo inaweza kupatikana bila wananchi. Wananchiwanaweza kuwa injini ya mabadiliko katika nchi yetu. Usisubiri viongozi pekee waletemaendeleo ya elimu nchini. Fanya hivyo wewe pia!

Leo hii yapo mambo makuu 5 ambayo unaweza kufanya kama mwanajamii:1. Tumia kitabu hiki kuanzisha mijadala juu ya namna jamii unavyoweza kushiriki katika

uendeshaji wa shule2. Waulize maswali viongozi wako na toa mapendekezo3. Waulize wanafunzi, wazazi na walimu kuhusu shule yao4. Tuma maoni yako kwenye vyombo vya habari5. Ungana na Marafiki na wananchi wengine kuboresha angalau kitu kimoja kwa

pamoja.

Mara nyingi tumezoea, kama wananchi wa kawaida, kusema mimi siwezi kuleta mabadiliko. Hiyoni kazi ya viongozi. Lakini si kweli.Tukumbuke Margret Mead - mwanafunzi wa jamii wa Marekanialisema “Tusiwe na shaka kwamba kikundi kidogo cha wananchi wenye fikra, wenye kujitumakinaweza kugeuza dunia” (imetafsiriwa).

Sauti za Marafiki wa Elimu

31Sauti za Marafiki wa Elimu

32 Sauti za Marafiki wa Elimu