ukaguzi wa kivuko mv dar es salaam

2
WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA DKT. JOHN MAGUFULI AKAGUA KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM. Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amekagua kivuko cha MV Dar es salaam kinachotarajia kutoa huduma zake kati ya Dar es salaam na Bagamoyo na kuahidi kuwa kivuko hicho kitaanza kazi siku chache zijazo mara baada ya kukamilika kwa vituo vya maegesho. Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Waziri Magufuli amewataka wakazi wa Dar es salaam na Bagamoyo kukitumia kivuko hicho ambacho kitawawezesha kufika katika maeneo yao kwa haraka na kuepuka usumbufu wa msongamano katikati ya jiji la Dar es salaam. “Tumieni kivuko hiki kwa uangalifu ili kidumu kwa muda mrefu, na sisi Serikali tutahakikisha tunaweka nauli nafuu ili kuwezesha wananchi wengi kumudu kutumia usafiri wa kivuko hiki, amesema Waziri Magufuli”. Waziri Magufuli amemtaka mkandarasi wa Ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho ambae ni Kamandi ya Wanamaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kukamilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho mapema iwezekanavyo ili huduma za usafirishaji zianze mara moja. Kwa upande wake Mkuu wa MKoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuwezesha kupatikana kwa kivuko cha MV Dar es salaam ambacho kitafungua fursa za kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi. Aidha, Eng. Ndikilo ameiomba Wizara ya Ujenzi kuiendeleza barabara ya Bagamoyo- Zinga hadi Mbegani na kuhakikisha kuwa na usafiri wa basi moja kutoka Bagamoyo kwenda Mbegani na kuwepo maegesho ya magari yenye usalama.

Upload: sasha-rogers

Post on 25-Dec-2015

2.649 views

Category:

Documents


8 download

DESCRIPTION

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amekagua kivuko cha MV Dar es salaam kinachotarajia kutoa huduma zake kati ya Dar es salaam na Bagamoyo na kuahidi kuwa kivuko hicho kitaanza kazi siku chache zijazo mara baada ya kukamilika kwa vituo vya maegesho.

TRANSCRIPT

Page 1: Ukaguzi Wa Kivuko Mv Dar Es Salaam

WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA DKT. JOHN MAGUFULI AKAGUA KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amekagua kivuko cha MV Dar es salaam kinachotarajia kutoa huduma zake kati ya Dar es salaam na Bagamoyo na kuahidi kuwa kivuko hicho kitaanza kazi siku chache zijazo mara baada ya kukamilika kwa vituo vya maegesho.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Waziri Magufuli amewataka wakazi wa Dar es salaam na Bagamoyo kukitumia kivuko hicho ambacho kitawawezesha kufika katika maeneo yao kwa haraka na kuepuka usumbufu wa msongamano katikati ya jiji la Dar es salaam.

“Tumieni kivuko hiki kwa uangalifu ili kidumu kwa muda mrefu, na sisi Serikali tutahakikisha tunaweka nauli nafuu ili kuwezesha wananchi wengi kumudu kutumia usafiri wa kivuko hiki, amesema Waziri Magufuli”.

Waziri Magufuli amemtaka mkandarasi wa Ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho ambae ni Kamandi ya Wanamaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kukamilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho mapema iwezekanavyo ili huduma za usafirishaji zianze mara moja.

Kwa upande wake Mkuu wa MKoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuwezesha kupatikana kwa kivuko cha MV Dar es salaam ambacho kitafungua fursa za kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aidha, Eng. Ndikilo ameiomba Wizara ya Ujenzi kuiendeleza barabara ya Bagamoyo- Zinga hadi Mbegani na kuhakikisha kuwa na usafiri wa basi moja kutoka Bagamoyo kwenda Mbegani na kuwepo maegesho ya magari yenye usalama.

Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng. Marceline Magessa, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya kuanza kazi kwa kivuko hicho yamekamilika ambapo tayari manahodha, mabaharia na mafundi watakaohudumia kwenye kivuko hicho wameshaajiriwa.

Aidha Eng. Magessa alibainisha kuwa Kivuko cha MV Dar es salaam kimetengenezwa na kampuni ya Western Marine Shipyard

Page 2: Ukaguzi Wa Kivuko Mv Dar Es Salaam

kutoka Denmark kwa takriban Shilingi bilioni 8 na kina uwezo wa kubeba abiria 300 wakiwa wamekaa.

Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ya JWTZ Meja Jenerali Rogasian Laswai, amemshukuru Waziri kwa kupewa kazi ya kujenga maegesho hayo na kuahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili wananchi wanufaike na huduma za kivuko hicho mapema.

Takriban vituo saba vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya maegesho ya kivuko hicho ikiwemo Magogoni, K awe, Jangwani, Rungwe Oceanic, Mbweni, Kaole na Mbegani.