ukristo - ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza...

160
UKRISTO SAFARI KUTOKA HAKIKA KUELEKEA KWENYE UBUNIFU MWANDISHI: HADHRAT MIRZA TAHIR AHMAD MFASIRI: JAMIL R. RAFIQ i

Upload: others

Post on 19-Jan-2021

15 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

UKRISTOSAFARI KUTOKA HAKIKA

KUELEKEA KWENYE UBUNIFU

MWANDISHI:HADHRAT MIRZA TAHIR AHMAD

MFASIRI:JAMIL R. RAFIQ

i

Page 2: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye UbunifuMtunzi: Hadhrat Mirza Tahir Ahmad

Kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya katika Islam.

Chapa ya kwanza: 1994, UingerezaChapa ya pili: 1996, UingerezaChapa ya tatu: 1997, UingerezaTafsiri ya Kiswahili: Des. 1999, Tanzania - Nakala 3000

Idhini ya kunakili: Islam International Publications Ltd.

Kimeenezwa na:Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya TanzaniaS. L. P. 376Dar es Salaam

Kimechapwa na Ahmadiyya Printing PressS. L. P. 376Dar es Salaam.Tanzania

Haki zote zimehifadhiwa.Sehemu yoyote ya kitabu hiki hairuhusiwi kunukuliwa au kuhifadhiwakwa njia yoyote, mfano kivuli (photocopying) kanda za sauti au njiayoyote ile itakayotumiwa kwa kunakili au kuhifadhi bila ya ruhusa yawaenezaji.

ii

Page 3: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Habari za Mwandishi

HADHRAT MIRZA TAHIR AHMAD

Hadhrat Mirza Tahir Ahmad, alizaliwa tarehe 18 Desemba 1928huko Qadian, India. Yu Khalifa wa Nne wa Masihi Aliyeahidiwa.Yeye ni kiongozi wa kiroho na msimamizi wa shughuli zaJumuiya ya Waislamu Waahmadiyya, na mjukuu wa mwanzilishiwa Jumuiya, Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad, MasihiAliyeahidiwa a.s.

Wadhifa rasmi wa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya WaislamuWaahmadiyya ni: Hadhrat Khalifatul Masih IV - Khalifa wa nnewa Masihi Aliyeahidiwa.

iii

Page 4: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

NENO LA MFASIRI

Hadhrat Khalifatul-Masih IV, Kiongozi Mtukufu wa Jumuiya yaWaislam Waahmadiyya , aliniamuru kukifasiri kitabu chake chaKiingereza "CHRISTIANITY- A Journey from facts to fiction"kwa lugha ya Kiswahili. Kwa baraka za maombi yake MwenyeziMungu amenisaidia na ameniwezesha kutimiza kazi hii kubwasana. Kitabu hiki naona alikiandika Khalifa wetu Mtukufu kwamsaada maalum wa Allah. Ametumia kipawa chake alichojaaliwana Mwenyezi Mungu kwa njia iliyo bora sana. Ni kitabu cha ajabukinacholeta hoja imara sana kuhakikisha ukweli hadi kupenyarohoni. Sidhani kwamba mtu baada ya kukisoma kwa uangalifuanaweza kushindwa kutambua uhakika wa mambo kumhusuYesu. Ni kazi ya kitaalamu inayoonekana katika kurasa za kitabuhiki. Mungu na ampe Khalifa wetu malipo bora kabisa ya hudumahii njema.

Naweka mbele ya wasomaji wetu wajuao Kiswahili tafsiri hiikwa kutegemea ya kwamba wataisoma kwa makini na kunufaikanayo.

Jamil R. Rafiq

iv

Page 5: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

YALIYOMO

UTANGULIZI. . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1

1. UANA WA YESU KRISTO 7Msingi wa Kisayansi wa uzazi. . . . . . . . . . . 7Je, mwana halisi wa Mungu anawezekana . . . . . . 9Hermaphroditism . . . . . . . . . . . . . . . . 1 1Parthenogenesis. . . . . . . . . . . . . . . . . 1 1Miujiza ni nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . 1 2Je, Yesu yu Mwana wa Mungu? . . . . . . . . . 1 4

2. DHAMBI NA KAFARA 1 9Kafara kwa mwanadamu . . . . . . . . . . . . . 2 0Dhambi ya Adamu na Hawa . . . . . . . . . . . 2 1Mateso ya binadamu yaendelea . . . . . . . . . . 2 4Dhambi ya kurithiwa . . . . . . . . . . . . . . 2 6Kuhamishwa kwa dhambi . . . . . . . . . . . . 2 8Adhabu yaendelea kutolewa. . . . . . . . . . . . 3 0Uadilifu na Msamaha . . . . . . . . . . . . . . 3 6Yesu hawezi kuwa kafara . . . . . . . . . . . . . 4 0Kutoa dhabihu pasipo kupenda . . . . . . . . . . 4 1Nani alitolewa kuwa dhabihu?. . . . . . . . . . . 4 5Mashaka ya Yesu . . . . . . . . . . . . . . . . 4 6Je, Mungu Baba naye alisumbuka . . . . . . . . . 4 8Adhabu ya Motoni . . . . . . . . . . . . . . . 4 9Kujitoa na kufurahia kiroho . . . . . . . . . . . 5 0Maana ya kifo kulingana na Yesu . . . . . . . . . 5 1Adhabu ya kiasi kwa dhambi isiyo ya kiasi . . . . . 5 3Kafara ilileta badiliko gani? . . . . . . . . . . . . 5 4

3. KAZI YA ROHO MTAKATIFU 5 6Ushirikiano wa Roho Mtakatifu katika uumbaji. . . . 5 7Siri ama hitilafu . . . . . . . . . . . . . . . 6 0

v

Page 6: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

4. KUSULUBIWA 6 3Ishara ya Yona . . . . . . . . . . . . . . . . . 6 5Ahadi ya Yesu kwa nyumba ya Israeli . . . . . . . 67Mambo yahusuyo tukio la msalaba . . . . . . . . . 6 8

5. KUHUIKA AU KUFUFUKA 7 8Maneno makali dhidi ya Watukufu . . . . . . . . 8 7Kupaa kwake . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9 1Ilitendeka nini kwa mwili wa Yesu? . . . . . . . . 9 2Maoni ya Waislamu Waahmadiyya . . . . . . . . 9 6Mifano ya kuponea chupuchuppu . . . . . . . . . 9 8

6. UTATU 101Uhusiano wa nafasi tatu zenyewe kwa zenyewe. . . . 102Hali au jiha mbalimbali za nafsi moja . . . . . . . . 103Nafsi mbalimbali zikishirikiana katika umilele . . . . 104Nafsi mbalimbali zenye sifa tofauti kabisa . . . . . . 108Nafsi tofauti zenye sifa zifananazo zilizo sawa . . . . 113

7. MAGEUZI YENYE KUENDELEA YA UKRISTO 116Wafuasi wa kwanza wa Yesu . . . . . . . . . . . 116Kazi ya Mtakatifu Paulo . . . . . . . . . . . . . 119Uhakika wa Yesu . . . . . . . . . . . . . . . . 120Kuendelea Dini . . . . . . . . . . . . . . . . . 123Upeo wa mwisho wa maendeleo ya dini . . . . . . 124

8. UKRISTO KATIKA ZAMA HIZI . . . . . . . . . 127Ukristo na ukoloni. . . . . . . . . . . . . . . . 127Ujaji wa Yesu Kristo mara ya pili . . . . . . . . . 131Masihi Aliyeahidiwa. . . . . . . . . . . . . . . 137Mwisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 144

NYONGEZA I . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 149NYINGEZA II. . . . . . . . . . . . . . . . . . . 151

vi

Page 7: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

UTANGULIZI

Dhati ya Yesu ni ya muhimu sana kwa ulimwengu wa kisasa.Umuhimu wake haukomei ulimwengu wa Kikristo pekee, baliunaenea hadi kwa dini nyingi pia mashuhuri kama vile dini yaKiyahudi na Islam. Kama dini hizo zenye nguvu zikielewanakuhusu uhakika wa dhati ya Yesu, ujaji wake wa mara ya kwanzana ule wa mara ya pili, hapo bila shaka uelewano huo utatatuamatatizo mengi yanayowakabili wanadamu katika zama hizi. Kwabahati mbaya mambo ya msingi ya maisha ya Yesu, shabaha yake,nadharia na dhati yake vimeeleweka visivyo kabisa. Katikakufahamu mambo hayo, dini hizo zinazozana vikali sana zenyewekwa zenyewe hata kwamba ushindani mkali unazuka baina yao.Tunapochunguza hakika ya tukio la msalaba na kutafakari yaleyaliyotukia na kwa nini yalitukia na pia katika wokovu na hekimayake, tunapata maelezo yanayopinzana kutoka njia tofauti zazamani. Nimechagua kutumia mantiki pekee kwa kuzungumziaswala hilo. Naamini ya kwamba hilo ndilo jukwaa lililo sawakwa wote linaloweza kutumiwa kwa maongezi yafaayo. La sivyo,majadiliano yoyote juu ya msingi wa maandiko pamoja namaelezo ya aina tofauti yataelekeza kwenye mgogoro wamabishano ambao kutoka nje yake kutakuwa vigumu.Miaka elfu mbili imekwisha pita, hata hivyo kwa msingi wamaandiko peke yake hakuna suluhisho ambalo litakubaliwa nawote lililokwisha fikiwa hadi sasa. Kiini cha tatizo ni tegemeo labaadhi ya maandiko ambayo yanapinzana yenyewe kwa yenyewe.Pia matatizo makubwa yamejitokeza kwa kukua polepolekutokana na kutoelewana kulikoizunguka historia ya Yesu Kristo.Mtazamo wa picha ya kihistoria kama kawaida huelekea kutiwa

1

Page 8: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ukungu na hufifia. Kwa vyovyote muda wa miaka elfu mbilikupita si kikwazo cha kawaida kwa kufahamu matukio yaliyotukiazama za uhai wa Yesu. Mantiki ya binadamu na akili yakezikisaidiwa na mwanga wa ujuzi wa elimu ya sayansi hazitegemeiimani ama rangi au dini ya mtu. Bali ziko sawa kwa watu wotena dini zote. Ni mantiki peke yake inayoweza kutupatia msingikwa kuleta umoja wa fikra.Nitajaribu kutathmini tatizo hili kwa njia mbalimbali. Hebu nianzekwa kuuchunguza Ukristo jinsi wanavyoufahamu Wakristowenyewe na kisha kuuchanganua kwa kuuangalia na hadubini yakiakili na hoja. Lakini sina budi kusisitiza ya kwamba simaanishikwa vyovyote kutokuwa na heshima kwa Wakristo ama YesuKristo. Nikiwa Mwislam ni nguzo ya imani yangu kumwaminiYesu Kristo na kumkubali kwamba yu Nabii wa Mungu mwenyeshani na utukufu, aliyekuwa na daraja la pekee baina ya Manabiiwa Kiisraeli. Lakini pale ukweli unapoamuru kwa haki na busara,akili na fahamu ya binadamu, mtu hawezi kujizuia kusahihishafikra zake kuhusu Ukristo. Sina shabaha ya kuleta mfarakanobaina ya Wakristo na Kristo, bali napenda kuwasaidia Wakristokusogelea karibu zaidi uhakika kumhusu Yesu Kristo na kujitengambali na hadithi zilizobuniwa kumhusu yeye.Zama zinaweza kupotoa hakika na kuigeuza kuwa hadithi nangano zisizo za kweli. Athari ya hadithi hizo za kubuniwahumpeleka mtu mbali na hakika halisi za maisha. Matokeo yakeni kwamba imani inakuwa mawazo ya kubuni tu, yasiyo ya kweli,yasiyo sawa. Ambapo imani ya kweli inayo asili yake katikamambo na matukio ya kweli ya kihistoria, ni ya hakika halisi naina nguvu ya kutosha kuleta mabadiliko katika jamii ya binadamu.katika jitihada ya kufahamu imani ya kweli na mafunzo hasa yaYesu, ni jambo la muhimu kabisa kuchuja uhakika kutoka nangano za kubuniwa. Kutafuta ukweli ndiyo shabaha hasa ya zoezihili lote. Natumai mtaniwia radhi na kufahamu kwambasimaanishi kudharau imani ya mtu ama kuchochea hisia zake.

2

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 9: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Uchunguzi wa kina ni jambo la muhimu ili kuulinda ulimwenguwa Kikristo kutokana na bahati mbaya ya maanguko ya khulka,hali ambayo imekuwa vigumu kwa Ukristo kuibadili. Sawa nauchunguzi wangu, kijana wa zama hizi haraka sana anaendeleakupoteza imani yake juu ya Mungu. Kulikuwa na wakati ambapowanasayansi walianza kwenda mbali na Mungu kwani walifikiriya kwamba fikra za Kiyahudi na Kikristo kuhusu maumbile yaasili zilizoelezwa katika Agano la Kale na Agano Jipya hazikuwasahihi. Ujuzi wa ulimwengu na maumbo ya kimbingu na vilevilivyo mbali na hayo jinsi ulivyoelezwa katika Biblia ni kinyumekabisa na uvumbuzi wa kisayansi uliofanyika tangu kuanzia zamaza kufufuka Elimu na Maarifa Ulaya ( mwaka 1300- 1600 A.D ).Tofauti hizo zikaendelea kukua kati yao kadri sayansiilivyoendelea kusonga mbele na ujuzi wa mtu kutambua hali yaasili ya ulimwengu ulipopata mabadiliko ya kimapinduzi. Habarihiyo pamoja na sababu nyinginezo zikaanzisha miongoni mwavikundi vya wanataaluma maelekeo ya hatari ya kutomwaminiMungu. Baadae elimu ilipoenea huko na huko vyuo vikuu namakao ya wataalamu yakageuka kuwa mwahali mwa kuzalishaimani ya kuwa hakuna Mungu. Mashaka ya maarifa ya Kiyahudina ya Kikristo kuhusu ulimwengu yalikuwa ni kwamba Neno laMungu likapingana na kitendo cha Mungu. Hoja dhidi ya imaniya kuwepo kwa Mungu ikawa hivi: Ikiwa Mungu ndiyeMwumbaji wa ulimwengu na vyote vilivyomo humu na ikiwayeye ndiye Mtungaji na Mdumishaji wa kanuni za ulimwenguzilizogunduliwa na akili tafiti ya kibinadamu, imekuwaje YeyeMwenyewe yu mjinga kabisa asijue hakika hizo?Mtu anaposoma maelezo ya Biblia kuhusu jinsi mbingu na ardhizilivyoumbwa na jinsi ambavyo mtu alitengenezwa kutoka katikavumbi na jinsi Bi Hawa alivyochongwa kutoka katika ubavu waAdamu na kadhalika (Hiyo ni mifano miwili tu miongoni mwamingi zaidi ambapo Neno la Mungu na kitendo cha Munguvinapingana kwa hali ya kushtusha), mtu anastaajabu nakushangaa kwa kuona tofauti moja kwa moja baina ya mwanzo

3

Utangulizi

Page 10: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wa uhai juu ya ardhi na maelezo yaliyotolewa katika kitabu chaMwanzo.Tofauti kama hizo zikalifanya Kanisa Kutumia mabavu katikazama zile ambapo Kanisa lilikuwa na madaraka ya kisiasayasiyoweza kupingwa. Mfano mmoja mashuhuri ni wa kugonganabaina ya Kanisa na Mwanasayansi Galileo.Galileo (1564 - 1642) alipoeneza uvumbuzi wake kuhusu mfumowa jua, dunia na sayari, ya kwamba ni sayari zinazozunguka,habari hiyo ikalikasirisha Kanisa kwani uvumbuzi wake huoulipinzana na utambuzi wa Kanisa kuhusu utaratibu wa jamii yajua, ardhi na sayari nyingine. Alitishwa vikali na kulazimishwakukanusha uvumbuzi wake wa kisayansi. La sivyo angewezakuuawa kwa kuteswa vibaya mno. Hata hivyo alihukumiwakifungo cha nyumbani kwake mpaka mwisho wa maisha yake.Ni mnamo mwaka 1992 ambapo Kanisa likaamua kutanguahukumu iliyotolewa dhidi ya Galileo, baada ya kujadiliana kwamuda mrefu wa miaka kumi na miwili katika kamati iliyoundwana Papa John Paul II.Mwanzo athari ya hitilafu hizo haikupenya kwa watu wa kawaidakatika jamii na kwa muda fulani ikabakia baina ya eneo maalumla wataalamu pekee. Lakini kwa kutapakaa kwa mwanga wa elimuya kidunia, ule ulioitwa 'mwanga wa itikadi za kidini' ukafifiapolepole mpaka ukawa sawa na giza. Mnamo siku za mwanzo zazama za kufufuka Elimu na Maarifa Ulaya ( karne ya 15) shughuliza wanasayansi ziliishia miongoni mwao wenyewe walioelimika.Uhusiano wao na watu wa kawaida unaoonekana siku hizihaukuwepo wakati huo. Kwahiyo imani yao kwamba hakunaMungu haikuathiri jamii kwa jumla. Hata hivyo elimu ya duniailipotolewa kwa vijana wa mataifa yaliyoendelea mamboyakaanza kubadilika polepole kuelekea mwelekeo potofu dhidiya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezekaharaka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafaza kidunia zikichanganyika na maendeleo na fikara za kiduniazikaangamiza msingi wa dini yaani imani juu ya Mungu.

4

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 11: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Khulka siku zote huongozwa na kulindwa na imani ya mtu katikaMungu. kama imani hiyo ni dhaifu au pungufu ama kitu fulanikinakosekana humo, basi kwa kiasi hicho hicho khulka itaathirika.Kwa mfano, kama imani juu ya Mungu inapinganana ujuzi wa kanuni za asili za ulimwengu na jinsi akili na busarainavyoamuru, hapo polepole ubora wa imani juu ya Munguunaendelea kupungua na papo hapo khulka za watu zinaathirikavibaya. Ndipo jamii kwa vitendo hugeuka kuwa jamiiisiyomwamini Mungu, ijapokuwa kwa kiasi kikubwa watuwanaweza kuwa waumini juu ya Mungu. Si vigumu kabisakuhakikisha habari hii na kutambua usafi wa imani ya jamii juuya Mungu. Kadri imani inavyokuwa dhaifu ama pungufu ndivyoinavyodhoofika nguvu yake juu ya khulka za watu. Wakatiwowote hayo mawili yanapogongana, imani juu ya Munguhulegea kuziachia nafasi tamaa mbovuKwa kutumia kanuni hiyo kwa jamii yoyote ya kidini popoteduniani daima twaweza kufikia maamuzi sahihi ya kutegemewa.Kwa kuichunguza jamii ya Kikristo inayojidai kuwa na imani,mtu anaweza kuangalia tu ya kwamba khulka za Kikristozinapatikana katika jamii hiyo ama hapana. Kwa mfano je,wanawatendea majirani zao jinsi Amri kumi zinavyowaamuru?Je, wanawatendea maadui zao sawa na kanuni za Kikristo wakatiwa hatari za kitaifa katika hali ya vita na kadhalika? Je, wasio nakosa wakiteswa na kushambuliwa wanawageuzia maadui zaoshavu la pili kwa kupigwa? Swali ni kwamba ni kwa kiasi ganimatendo ya mtu yanaonesha imani yake? Kama matendohayaoneshi picha hasa ya imani yake, basi hiyo ndiyo tuliyosemakwamba hapo imani juu ya Mungu imegongana na matakwa yakibinadamu na mahitaji yake. Kama imani juu ya Mungu ni kitubora kuliko vyote na kama matakwa ya mtu na mahitaji yakeyanatolewa dhabihu juu ya madhabahu ya imani hiyo, hapo mtuanaweza kusema kweli ya kwamba imani hiyo hata ikiwa ya ainagani, kwa akali, ni halisi safi na imara.

5

Utangulizi

Page 12: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kuchunguza ulimwengu wa Kikristo ulivyo siku hizi, na kuutahiniili kutambua usafi wa imani yake juu ya Mungu, kunahuzunishana kunamtoa mtu katika dhana za uwongo na kumwonesha ukweli.Kinachoonekana kama kawaida ni uhalifu dhidi ya imani juu yaMungu moja kwa moja, na wakati mwingine ni maasi baridiyasiyodhihirisha kukanusha imani juu ya Mungu waziwazi.Pingamizi baina ya imani juu ya Mungu na vitendo vya watubinafsi unamdanganya mtu kufikiri kwamba ipo jamii ya kidiniya waumini, ilhali ukweli ndiyo tofauti kabisa. Vivyo hivyondivyo ilivyo kwa jamii zote za dini nyingine. Lakini kila marasiyo sababu moja inayoleta matokeo ya aina moja. Kila jamiiinastahili kuchunguzwa sawa na hali yake maalum. Ndiyo maanauchunguzi unaofanywa kwa ukweli na utulivu bila upendeleo juuya asili ya upinzani baina ya imani ya watu na matendo yaounakuwa wa muhimu sana.Ni muhimu kuzingatia ya kwamba wakati mwingine imaniyenyewe inapotoka na inakuwa siyo ya asili. Kwa mfano, sehemufulani ya mafunzo ya Talmud kuwahusu wasiokuwa Wayahudi,na mafundisho ya Wahindu yaliyomo katika Manu Samartikuwahusu Wasioguswa, bila shaka kutokutenda sawa nayo ndiyoafadhali sana kwa jamii hizo. (Wasioguswa ni watu wa jamii fulaniya Wahindu ambao wanahesabiwa duni sana hata kwamba mtuwa jamii nyingine akiwagusa ananajisika moja kwa moja). Napengine imani yenyewe ni nzuri na inafaa kama watu wanatendasawa nayo, lakini watu wanakuwa waovu na wanaachana nayokwa kuona ni vigumu kutenda sawa nayo na wanaipuuzilia mbali.Tukirejea kwenye suala la Ukristo, twasema ya kwamba itikadiza msingi za Kikristo zinagongana na kanuni za asili za ulimwenguwala hazitimizi matumaini ya mtu yanayotegemea akili na busara.Katika hali kama hiyo Wakristo hawana budi polepole kuzipuuzaitikadi zao na kutoziruhusu ziongoze maisha yao.

6

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 13: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

1 UANA WA YESU KRISTO

Uhusiano wa Baba na Mwana baina ya Mungu na Yesu Kristo niimani ya msingi katika Ukristo. Hebu tujaribu kwanza kuelewamuradi wa kuwa mwana halisi. Tunapofikiria sana maana hasaya kuwa mwana halisi wa baba tunalazimika kusahihisha maoniyetu kuhusu 'uana' wa Yesu. Mwana maana yake nini? Katikazama ambapo elimu ya sayansi ilikuwa haijaendelea mbele nailikuwa haijajulikana mtoto anazaliwaje, swali hilo liliwezakujibiwa kwa njia isiyokuwa ya yakini hasa. Watu wa kale walionakwamba inawezekana Mungu kupata mwana anayezaliwa na mtu.Imani hiyo ilienea pote duniani katika jamii ya kipagani.Maitholojia ya kigiriki imejaa hekaya za aina hiyo na maitholojiaya Kihindu nayo haikubakia nyuma pia. Kwani miungu kujipatiawana na mabinti wengi walivyopenda haikuhojiwa kwa makinina akili ya kibinadamu. Lakini siku hizi sayansi imekwisha patamaendeleo kiasi hiki kwamba njia ya kuzaliwa imefafanuliwamno kuliko zamani. Habari hii ya Mungu kupata mwana imekuwatata mno na wale ambao bado wanaamini kwamba wana namabinti halisi wa Mungu waweza kuzaliwa, basi wanakabiliwana tatizo kubwa la kutatua na baadhi ya maswali magumukuyajibu.

MSINGI WA KISAYANSI WA UZAZI:Kwanza kabisa ningependa kuwakumbusha ya kwamba mamana baba wanashiriki kwa usawa katika kuzaa mtoto. Chembehai(cell) za binadamu zina kromosom 46 ambazo zinakuwa na nyuzi-nyuzi zile za kumjaalia mtoto sifa mbalimbali. 'Yai' la mwanamkelina kromosom 23 pekee ambazo ni nusu nzima ya kromosom 46

7

Page 14: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kwa jumla zinazopatikana katika kila mwanamume namwanamke. 'Yai' la mwanamke linapokuwa tayari kwa kushikamimba, nusu nyingine ya kromosom zinazopungua humozinatimizwa na mbegu ya mwanamume inayoingia mle nakulirutubisha. Ndivyo alivyopanga Mwenyezi Mungu; la sivyo,idadi ya kromosom zingeongezeka mara mbili kila kizazi. Namatokeo ya kuongezeka huko maradufu ni kwamba kizazi chapili kingekuwa na krosom 92, na binadamu haraka sanawangegeuka kuwa majitu na mpango mzima wa ukuajiungelivurugika. Mungu amepanga vizuri kabisa mpango wakuokoa viumbe kwa kufanya idadi ya kromosom iwe nusu katikaseli wakati wa kuzaana. 'Yai' la mama lina kromosom 23, nakadhalika mbegu ya baba pia inazo kromosom 23. Hivyo basimtu anaweza kutazamia kwamba mtoto atapata nusu ya nyuzi-nyuzi za kumtilia sifa kadha kutoka kwa mama na nusu nzimakutoka kwa baba. Hiyo ndiyo maana hasa ya mwana halisi.Hakuna ufafanuzi mwingine wowote ule wa 'mwana halisi'anayezaliwa kwa sura ya binadamu. Ziko njia mbalimbali zakutunga mimba lakini hakuna tofauti katika kanuni iliyoelezwahapo juu.Tukichunguza vizuri kuzaliwa kwa Yesu, hebu tutafakari ninikinaweza kuwa kilitendeka. Uwezekano wa kwanza unaowezakufikiriwa kisayansi ni kwamba 'yai' la Mariamu lilitoa kromosom23 kwa kushika mimba. Kama ndivyo hivyo, hapo swali linazukakwamba 'yai' lilirutubishwaje na kromosom nyingine 23 za lazimazilitokea wapi? Haiwezekani asilani kusema kwamba chembehaiza Yesu zilikuwa na kromosom 23 tu. Hakuna mtoto wa kawaidawa kibinadamu anayeweza kuzaliwa akiwa hai hata kama anazokromosom 45. Kama mtu anakosa hata kromosom moja tumiongoni mwa 46 ambazo ni za lazima sana kwake kuumbika,kama kuna matokeo yake, basi hayatukuwa chochote ilamachafuko. Kisayansi Mariamu peke yake asingeweza kutoakromosom 46; ni lazima nyingine 23 zingetokea mahali fulani.Kama Mungu ndiye baba, hapo tena kuna chaguzi kadha.

8

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 15: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kwanza, Mungu pia anazo kromosom sawasawa na kromosomza kibinadamu. Kwahiyo hizo kromosom zikaingia katika mfukowa uzazi wa Mariamu kwa namna fulani. Lakini hiyo haiaminikiwala haikubaliki. Kama Mungu anazo kromosom za kibinadamu,Yeye hawezi kubaki kuwa Mungu. Hivyo matokeo ya imani katikaYesu kuwa mwana wa halisi wa Mungu ni kuhatarisha Uunguwa Baba pia.Uwezekano wa pili ni kuwa Mungu aliumba kromosom za ziadakwa njia isiyo ya kawaida ya uumbaji. Kwa usemi mwingine hizohazihusikani hasa na nafsi ya Mungu, isipokuwa ziliumbwakimwujiza. Hii itatuelekeza moja kwa moja kuukataa uhusianowa Yesu na Mungu kuwa ni wa mwana na Baba, na utatuongozakuukumbatia uhusiano ule ulio mkuu wa ulimwengu kwa Mungu,yaani uhusiano wa kila kilichoumbwa kwa Muumbaji wake.

JE, MWANA HALISI WA MUNGU ANAWEZEKANA?Ni dhahiri kwamba haiwezekani kupatikana mwana halisi waMungu, kwani hapana budi huyo mwana halisi apate kromosomzake nusu kutoka baba yake na nusu kutoka kwa mama yake.Hapa panazuka tatizo jingine: Mwana atakuwa nusu mtu na nusumungu. Lakini wale wanaomwamini Yesu kuwa mwana halisiwa Mungu wanadai na wanasisitiza kwamba yeye alikuwa mtumkamilifu na mungu mkamilifu.Na kama kromosom zilikuwa nusu tu ya idadi iliyotakiwa, hapohamna tatizo tena, kwani mtoto hawezi kuzaliwa abadan. Natukidhani alizaliwa na kromosom nusu, basi atakuwa nusu mtu.Achilia mbali kromosom 23 nzima nzima, hata kama 'nyuzi' mojapekee ya kromosom moja ina upungufu, hiyo italeta hatari kubwakabisa kwa mtoto atakayezaliwa akiwa na upungufu katika mwiliwake. Anaweza kuwa kipofu, hana mikono na miguu kiziwi nabubu. Hatari zitokanazo na bahati hiyo mbaya hazina kikomo.Mtu anapaswa kukubali uhakika; haiwezekani kuwaza kwamba

9

Uana wa Yesu Kristo

Page 16: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Mungu anazo kromosom za kibinadamu ama za aina yoyotenyingine. Hivyo, ushirikiano wa Mungu binafsi kwa njia yakiwiliwili unapofutiliwa mbali, endapo Mariamu angezaa mtotokutokana na vijine (genes) vya kumtilia mtoto sifa za kibinadamuvilivyokuwamo ndani ya 'yai' (ovum) lake (Mariamu), kwavyovyote itakavyokuwa mtoto huyo hatakuwa mwana wa Mungu.Sana sana unaweza kusema kwamba huyo kiumbe wa ajabuatakuwa nusu mtu tu, basi. Kama viungo vya uzazi vya Mariamuvilikuwa sawasawa na vile vya mwanamke yeyote wa kawaida,na hata hivyo kama 'yai' likashika mimba lenyewe, tunachowezakutazamia kuzaliwa kwa wingi ni kiumbe fulani chenye sifa nusuza kibinadamu. Itachukiza kukiita kitu hicho 'Mwana' wa Mungu.Alizaliwaje, basi, Yesu? Tunajua ya kwamba uchunguzi kuhusukuzaliwa mtoto kwa mama pasipo ushirikiano wa mwanamumeunaendelea katika nchi zilizoendelea. Lakini mpaka sasa utaalamuwa mtu upo mahali ambapo elimu yake ya sayansi haijaendeleakiasi cha kuweza kuhakikisha pasipo shaka kwamba mtoto wakibinadamu anaweza kuzaliwa kwa bikira bila kushirikiana namwanamume. Hata hivyo, upo uwezekano wa jambo hilo kutokeakatika hali mbalimbali.Katika uhai wa daraja la chini mambo mawili yamethibitikaKisayansi: Hermaphroditism (yaani kuwa huntha) naParthenogenesis. Kwahiyo kuzaliwa Yesu kimwujiza kwaMariamu kunaweza kusababishwa na kanuni fulani aina hiyoambayo ni ya nadra sana na mipaka yake haijapimwa na mtukwa ukamilifu.Hapa chini kuna maelezo mafupi ya Hermaphroditism naParthenogenesis. Wasomaji wanaopenda kujua hayo zaidikisayansi wanaweza kurejea kwenye Nyongeza II mwishoni mwakitabu hiki.

10

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 17: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

HERMAPHRODITISM:Hermaphroditism inapatikana wakati ambapo viungo vya kiumena kike vinapatikana katika mwanamke mmoja na kromosomzinaonesha sifa zote mbili za kike na kiume zilizojipanga mojakando ya nyingine. Majaribio katika maabara yamethibitisha yakwamba sungura mmoja huntha (Hermaphrodite) aliwapandasungura wengi majike ambao wakazaa watoto 250 ambamo kunamajike na madume. Lakini sungura huyo huntha wakati mwinginealitengwa peke yake na akashika mimba bila kupandwa na akazaasungura majike na madume saba kwa jumla. Alipochunguzwaalipatikana na vifuko viwili vya 'mayai' tumboni vilivyofanyakazi na pia makende mawili yasiyoweza kuzaa wakati alipokwishashika mimba. Uchunguzi wa siku za karibu umeeleza ya kwambajambo hili linawezekana kwa nadra katika wanadamu pia.

PARTHENOGENESIS:Parthenogenesis ndiyo 'yai' la jike kupata kukua pasipo kusaidiwana dume. Jambo hili linaonekana katika namna nyingi za uhai wadaraja la chini kama vile vijidudu na pia samaki . Kuna ushahidipia ya kwamba Parthenogenesis inaweza kutokea katika mijusiwanaoishi katika sehemu zenye mvua haba. Katika maabara,panya na sungura waliweza kushika mimba nusu-nusu kwa njiaya Parthenogenesis, lakini mimba hizo zikaharibika. Katikauchunguzi wa siku za karibu wanasayansi wamegundua yakwamba mara moja moja Parthenogenesis inaweza kupatikanakatika binadamu pia, na mwanamke anaweza kushika mimba bilamume kwa msaada wa Calcium Ionophore ambayo inawekwahumo pasipo kutumika isipokuwa tu kuwapo kwake kunaathiri.Uchunguzi huu unaelekeza kwenye matarajio ya kwambakuharibika mimba ya mwanadamu katika siku za mwanzonikunaweza kusababishwa na ukuaji wa mimba kwa njia yaParthenogenesis.

11

Uana wa Yesu Kristo

Page 18: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Sawa na uchunguzi wa hivi karibuni, imehakikishwa ya kwambakuzaa bila baba kunawezekana kisayansi. Taarifa mojailiyochapishwa katika gazeti la Nature genetics la Oktoba 1995inaeleza habari ya mvulana mmoja mwenye umri wa miaka mitatuambaye mwili wake kiasi fulani ulitokana na 'yai'lisilochanganyikana na mbegu ya mwanamume. Wachunguziwalikagua mifuatano yote ya DNA kuhusu X-Kromosom katikangozi na damu ya mvulana na wakagundua ya kuwa X-Kromosomkatika chembehai zake zote zilitokana na mama peke yake.Kadhalika sehemu zote mbili za kila Kromosom miongoni mwajozi 22 za Kromosom nyingine katika damu yake zilikuwa kabisazinafanana na zilitokana zote na mama yake.

MIUJIZA NI NINI ?Kwa kudhihirika uwezekano wa bikira kuzaa, hivyo jambo hilihaliwi tena lisilowezekana na kinyume cha kanuni ya asili yaulimwengu. Ipo wapi basi haja ya kutafuta maelezo ya Yesukuzaliwa nje ya kanuni za asili, ama kupita kiasi katika kuaminikuwa 'Mwana' halisi wa Mungu aliyezaliwa kwa uzazi wakibinadamu? Pale mambo mbali mbali kama yalivyoelezwa hapojuu yanapoonekana kwamba ni ukweli wa asili, unaoshuhudiwakatika ulimwengu, kwa nini basi iwe vigumu kuamini kuzaliwakwa Yesu kuwa sawa na kanuni fulani ya ulimwenguiliyofichikana, iliyofanya kazi sawa na mpango maalum waMungu? Hali fulani ikapatikana ndani ya Mariamu iliyosababishamtoto kuzaliwa kimwujiza bila mwanaume kumgusa. Hii ndiyoimani ya Waislamu Waahmadiyya kwamba ndivyo hasailivyotendeka. Imani yetu hiyo ni imara kwani hakunamwanasayansi anayeweza kuikanusha kwa kuihesabu kuwaupuuzi, wala imani yetu hiyo haiko kinyume cha kanuni ya asiliiliyopo ulimwenguni.Katika Islam miujuiza haihesabiwi kuwa matukio yaliyo dhidiya kanuni ya asili ya ulimwengu, bali sawasawa kabisa na kanuni

12

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 19: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ya ulimwengu iliyofichikana tu katika zama fulani wasiitambuewatu. La sivyo, hapo patazuka matatizo mengi dhidi ya hekimaya Mungu. Kama ni Mungu ndiye aliyeunda kanuni za asili zaulimwengu, bila shaka Yeye angeweka taratibu ambazo pasipokuzivunja angeweza kutoa ufumbuzi unaohitajika kwa kila tatizo.Siyo kwamba kanuni zote za ulimwengu zinajulikana kwa mtu.Ziko aina mbalimbali za kanuni zinazofanya kazi katika tabakatofauti na maeneo mbali mbali. Wakati mwingine kanuni hizozinajulikana kwa mtu katika eneo moja tu lakini uwezo wake wakuona unashindwa kupenya nje ya eneo hilo. Kadiri wakatiunavyopita ujuzi wa mtu unaongezeka, kadhalika na uwezo wakewa kuona unazidi kupenya zaidi ya eneo hilo na anawezakushuhudia zile kanuni ambazo hapo kabla alikuwa hazitambui.Elimu ya sayansi ikiendelea mbele, uvumbuzi wa aina ainaunazitilia mwanga kanuni hizo zinazoonekana kufanya kazi katikavikundi. Hivyo kazi zake na ushirikiano wake pamoja na kanuninyingine hujulikana vizuri zaidi.Mambo yale yaliyoonekana ni miujiza katika zama za kalehayahesabiwi kuwa miujiza katika zama hizi. Mamboyanahesabiwa kuwa miujiza kwa kulingana na ujuzi wa mtu katikanyakati maalum. Mungu anapodhihirisha nguvu yake maalum,huonekana kana kwamba kanuni fulani imevunjiliwa mbali.Lakini sivyo ilivyo bali kanuni nyingine iliyofichikana kwa machoya binadamu ilikuwapo hapo mapema ambayo sasa imefanya kazikwa amri ya Mungu . Watu wa zama hizo hawakuweza kutambuakanuni hiyo wala hawakuidhibiti. Kwa mfano, nguvu ya sumakuhaikujulikana kwa mtu miaka elfu chache iliyopita. Kama mtufulani angeliigundua nguvu hiyo kwa bahati na kisha kamaangefanya hila ya kuvifanya vitu viangame hewani kwa kutumianguvu hiyo ya sumaku pasipo watu kujua uhakika huo, yeye mtuhuyo angeliweza kuwashangaza watu kwa kusema: Lo, mwujizaumetendeka. Siku hizi hila kama hizo ni mambo ya kawaidayasiyotiwa maanani sana. Ujuzi wa mtu una kikomo, lakini ujuziwa Mungu hauna mwisho. Kama kanuni fulani isiyojulikana kwa

13

Uana wa Yesu Kristo

Page 20: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

mtu inafanya kazi, hiyo huonekana kama mwujiza. Lakini kwakuangalia mambo ya ajabu ya aina hiyo yaliyofanyika zamanibaada ya kwisha kupata ujuzi wake sasa twaweza kukanushakwamba kanuni za ulimwengu zilivunjika, bali hayo yalitendekasawasawa kabisa na kanuni ambazo hazikujulikana kwa watu wazama hizo. Ndiyo maana nilisema kwamba ni lazima ilikuwepokanuni fulani iliyosababisha Yesu kuzaliwa bila baba, ambayohaikujulikana kwa watu wa zamani zile; haijaeleweka vizuri hatasasa. Lakini sayansi inasonga mbele upande huo na mengiyanazidi kueleweka. Hivyo utawadia wakati ambapo mtu yeyotehataweza kudai ya kwamba kuzaliwa kwa Yesu pasipo babakulikuwa kinyume na kanuni ya ulimwengu.

JE, YESU YU MWANA WA MUNGU ?Kuna matatizo mengine mengi ya Wakristo kuhusu kumwelewaYesu asili yake na uhusiano wake na Mungu. Tukichunguza nakuchambua imani ya Kikristo kinachojitokeza ni kwamba kunaMwana wa Mungu ambaye anazo sifa za mtu mkamilifu na piazile za mungu mkamilifu. Hata hivyo kumbuka ya kwamba sawana imani ya Kikristo 'Baba' si sawa hasa na 'Mwana'. MunguBaba yu Mungu mkamilifu lakini si mtu mkamilifu, ambapo'Mwana' ni mtu mkamilifu na papo hapo ni mungu mkamilifupia. Ndiyo kusema kwamba hawa wawili ni dhati mbili tofautiwalio na sifa mbalimbali.Ieleweke ya kwamba sifa hizo haziwezi kubadilishwa. Ziko sifakatika baadhi ya vitu ambazo zaweza kubadilishwa. Kwa mfano,maji yaweza kugeuka kuwa theluji na pia mvuke pasipo kubadilikakitu chenyewe ama asili yake. Lakini tofauti zilizopo katika sifaza Mungu na Kristo, ambapo sifa kadha zinaongezwa kwa mmojawao, haziwezi kupatanishwa asilani. Haiwezekani kwa mmojawao kupata mabadiliko hayo na asipambanuliwe na mwenzake.Ni tatizo kubwa kabisa ya kwamba Yesu Kristo alikuwa mungumkamilifu na mtu mkamilifu. Kama alikuwa na sifa za aina hizo

14

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 21: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

mbili kwa pamoja, bila shaka yeye alikuwa tofauti na Babaambaye hakuwa mtu kamili wala mtu asiye kamili. Huo uhusianoulikuwa wa aina gani? Je, 'Mwana' alikuwa mkubwa kuliko Baba?Kama sifa yake hiyo ya ziada haimfanyi 'Mwana' kuwa mkubwakuliko Baba, hapo bila shaka sifa hiyo ina dosari. Kwa maanahii 'Mungu Mwana' mwenye kasoro si tu ni kinyume cha madaiya Ukristo bali pia ni kinyume kabisa na Mungu jinsianavyofahamiwa na watu wote ulimwenguni. Basi mtu anawezajekuelewa itikadi ya ajabu inayojipinga yenyewe, ambayo inatutakatuamini kwamba 'Mmoja katika Watatu' na 'Watatu katika Mmoja'ni sawa tu pasipo tofauti yoyote iwayo? Hiyo inaweza kutokeatu iwapo msingi wa imani hauwekwi juu ya hakika bali unawekwajuu ya mawazo ya kuzushwa.Isitoshe, kuna tatizo jingine tena linalopaswa kutatuliwa, nalo nihili: Kama Yesu alikuwa 'Mwana wa Mungu' kwa sababu yakuzaliwa kutoka katika tumbo la Mariamu, basi cheo chakekilikuwa kipi hapo kabla? Na kama yeye alikuwa 'Mwana' sikuzote hata bila ya kuzaliwa na Mariamu, ilikuwa haja gani basi,kwamba azaliwe kwa sura ya binadamu? Na kama ilikuwa lazima,hapo sifa ya kuwa Mwana haikuwa ya milele; bali ilipatikanakama sifa ya nyongeza baada ya yeye kuzaliwa na ikatowekaalipotengana na mwili na kurejea mbinguni. Hivyo kuna matatizomengi yazukayo kutokana na itikadi inayokanushwa na akili nabusara. Nawaalikeni kukubali jambo lililo na heshima tena lahakika, la kuzaliwa kwa Yesu aliyeumbwa na Mungu kwakutumia kanuni fulani za asili zilizofichika machoni mwa watu.Yesu alikuwa mwana wa Mungu kimithali aliyekuwa mpenzimaalum wa Mungu, lakini hata hivyo alikuwa mwanadamu kwavyovyote. Cheo cha kuwa 'Mwana' alipachikwa miaka mia tatutakriban baadaye ili kuendeleza hekaya yake jambo ambalolitajadiliwa baadaye.Hali ya uhusiano wa ndoa baina ya Mungu Baba na Mariamu niswala ambalo mtu anachukia kulijadili waziwazi. Hata hivyokatika jitihada za kuelewa ile kazi ya kati aliyoifanya Mariamu

15

Uana wa Yesu Kristo

Page 22: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

baina 'Baba' na 'Mwana', hilo linakuwa ni uovu usioepukika.Labda swali hilo hilo lilimuudhi sana Nietzsche hata kwambamwishowe akaeleza kutoridhika kwake kusikoelezeka kwamaneno yafuatayo:

16

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

"Si muda mrefu baada ya Zarathustra kujikomboa kutoka kwawachawi, ila alimwona tena mtu ameketi pembeni ya njiaaliyokuwa akipita: Mtu mrefu, mweusi mwenye uso uliopaukana kukonda; mtu huyu alimwudhi sana. "Ala", aliwaza moyonimwake "haya ni mateso yaliyojigeuza", anaonekana kama padrivile; wanataka nini toka himaya yangu? Akasema 'yeyote uwayeewe msafiri msaidie aliyepotea njia, mzee ambaye huendaamekuja kukudhuru!'Dunia hapa ni ngeni na inajitenga nami, ninasikia milio yawanyama wa mwitu na yule ambaye angeweza kunilinda yeyemwenyewe hayupo tena.Nilikuwa namtafuta mcha Mungu wa mwisho, mtakatifu namtawa aishiye peke yake msituni ambaye hajasikia yoteinayoyajua dunia siku hizi?Ni nini inachojua dunia sasa? Aliuliza Zarathustra. Ni hivi labda:Mungu yule wa zamani ambaye ulimwengu ulimwamini, hayukotena.Hivyo ndivyo ilivyo, alijibu mzee kwa huzuni. Na nilimtumikiayule Mungu wa zamani hadi saa yake ya mwisho.Sasa nimejiuzulu katika huduma, pasipo bwana, hata hivyo badosijawa huru, wala sina furaha hata kwa saa moja isipokuwa kwakukumbuka yaliyopita. Ndiyo maana nikapanda katika milimahii ili nisherehekee sikukuu mara nyingine, jinsi anavyokuwaPapa mzee na Padre: kwani jueni mimi ndimi Papa wa mwisho ---- sikukuu ya makumbusho matakatifu na ibada za Mungu.'Lakini sasa yeye mwenyewe amekufa, mtu aliyekuwa mwemasana, yule walii msituni aliyekuwa anamsifu Mungu wake daimakwa kuimba na kunung’unika.'Nilipokuta banda lake sikumkuta mle ndani, bali nikawakutahumo mbwa mwitu wawili wakimlilia kifo chake - kwaniwanyama wote walimpenda. Kisha nikaondoka hapo haraka.'

Page 23: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

17

Uana wa Yesu Kristo

Je, nilifika katika misitu hiyo na milima hiyo bure? Ndipo moyowangu ukaamua kumtafuta mwingine aliye mwema kuliko walewote wasiomwamini Mungu - kumtafuta Zarathustra!''Ndipo akasema yule mzee na kumkazia macho aliyesimamambele yake; Zarathustra akaushika mkono wa papa mzee na kwakitambo kirefu akauheshimu kwa kuusifu.''Angalia, mheshimiwa,' kasema tena, mkono mrefu na mzuriulioje huu! Huu ni mkono wa yule ambaye daima aligawa baraka.Lakini sasa huu unamshika kwa nguvu yule unayemtafuta, mimi,Zarathustra.''Ndimi mimi, Zarathustra nisiye na Mungu, nisemaye: Ni naniasiye na mungu kuliko miye, ili niweze kufurahia mafundishoyake.'Ndivyo alivyosema Zarathustra na kutoboa kwa nadhari yakemawazo ya papa mzee na yaliyofichika moyoni mwake.Mwishowe mwingine akaanza:'Yule aliyempenda sana na kummiliki amemkosa sana pia!:'Angalia, je, mimi mwenyewe kati yetu si yule asiye na Munguhivi sasa. Lakini nani angefurahia hayo! Ulimtumikia mpakamwisho,' kauliza Zarathustra kwa makini, baada ya kiyma kirefu,je, wajua alikufaje? Je, ni kweli wasemayo ya kwamba hurumailimkwama!'Ya kwamba alimwona mtu alikitundikwa msalabani walahakustahamili, mapenzi yake kwa mtu yakawa Jahanamu yakena hatimaye kafa?'Papa mzee hakujibu, lakini akaangalia upande mwingine kwahaya na kwa uso wa huzuni na uchungu.'Wacha niende!, kasema Zarathustra baada ya kutafakari sana,na kwa muda huo wote aliendelea kumkodolea macho moja kwamoja mzee huyo.'Mwache aondoke, yeye amekwisha. Na ijapokuwa ni heshimakwako ya kwamba wewe useme vyema kuhusu mungu huyo mfu,hata hivyo wewe na pia mimi twajua huyo alikuwa nani; nakwamba yeye alifuata njia za ajabu.''Iwe siri yetu,' katamka papa mzee akichangamka, ama nisemechini ya macho (kwani alikuwa mwenyewe chongo) 'katikamambo ya roho mimi nina maarifa zaidi kuliko Zarathustra

Page 24: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

______________________

1Thus Spoke Zarathustra, utungo wa Friedrich Nietzsche. kurasa 271-273,Tafsiri ya kiingereza ilienezwa na Penguin Books 1969.

18

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

mwenyewe - na ningeweza kuwa hivyo!'Mapenzi yangu yalimhudumia kwa miaka mingi, takwa langulikalitii takwa lake. Mtumishi mwema anatambua kila kitu,na mambo mengi pia, ya kwamba bwana wake anajificha kwakemwenyewe.''Yeye alikuwa mungu aliyekuwa mafichoni, siri tupu. Kusemakweli, alikuja kwa njia ya mwana tena kisirisiri siyo dhahiri.Kizingitini mwa imani hiyo pana uzinzi.'Yeyote anayemheshimu kuwa mungu wa upendo hauthaminiupendo vya kutosha. Je, Mungu huyo hakupenda kuhukumiwa?Lakini apendaye hupenda pasipo kujali thawabu ama adhabu.''Mungu huyo wa mashariki alipokuwa kijana, alikuwa mkali namwenye kujilipiza kisasi na mwenyewe akatengeneza Jahanamukwa kuwafurahisha wapenzi wake.'Lakini mwishowe akazeeka na akawa mpole, laini na raufu zaidikama babu kuliko baba, zaidi kama bibi mkongwe.''Kisha akaketi akikunjamana kwenye kona ya dohani yake,akihuzunika kwa miguu yake isiyo na nguvu, aliyechoka na dunia,hata nia yake ya kutenda ikachoka, na siku moja akakosa hewakwa huruma yake iliyopita kiasi.'1

Page 25: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

2 DHAMBI NA KAFARA

Sasa twaelekea kwenye nguzo muhimu ya pili ya imani yaKikristo. Ningebainisha kwanza ya kwamba Wakristo wotehawaamini neno kwa neno yatakayofuata hapa chini. Hata baadhiya viongozi wa Kanisa wamekwenda upande na kuachana namsimamo mgumu wa fundisho la imani la Kanisa. Hata hivyofalsafa ya 'Dhambi na kafara' ni kanuni ya msingi ya imani yaKikristo inayokubalika kwa jumla.Sehemu ya kwanza ya maana ya Dhambi na Kafara ni kwambaMungu ni mwadilifu na anafanya uadilifu wa dhati. Yeyehasamehe dhambi pasipo kuadhibu; kwani kusamehe tu dhambihivi hivi kungekuwa kinyume cha uadilifu halisi. Sifa hiyo yaMungu inasababisha kafara ilivyoaminiwa na Wakristo kuwajambo la lazima.Sehemu ya pili ni kwamba mtu ni mwenye dhambi kwa sababuAdamu na Hawa walitenda dhambi. Matokeo yake ni kwambawazao wao wakaanza kurithi dhambi, kana kwamba hiyo dhambiikaingizwa katika vijine (genes) vyao na tangu hapo watoto wotewa Adamu huzaliwa wakiwa wenye dhambi.Sehemu ya tatu ya itikadi hiyo ni kwamba mwenye dhambi hawezikutoa kafara ya dhambi ya mwingine: mtu asiye na dhambi pekeendiye anayeweza kutoa kafara ya dhambi za wengine. Juu yamsingi huu, inakuwa wazi sawa na ufahamu wa Kikristo, yakwamba Nabii yeyote wa Mungu hata akiwa mwema namna ganiama akiwa karibu sana na ukamilifu hawezi kumtakasa mtu nakumwondolea dhambi na matokeo yake. Akiwa mwana waAdamu, asingeweza kuepukana na dhambi aliyorithi alipozaliwa.

19

Page 26: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Huo ndiyo muhtasari wa muradi wa imani nzima ya kafara. Hapachini pana maelezo yaliyotolewa na wataalamu wa dini yaKikristo.

KAFARA KWA MWANADAMU:Ili kutatua tatizo lisiloweza kutatulika kidhahiri, Mungu akawazampango wa akili sana. Haijulikani kwamba yeye alishauriana namwana ama hapana; ama wote wawili wakawaza mpango huuwakati mmoja; au uliwazwa na mwana peke yake lakiniukakubaliwa na Mungu Baba. Maelezo ya mpango huuyalifafanuliwa katika zama za Yesu kama ifuatavyo. Miaka elfumbili iliyopita 'Mwana wa Mungu' aliyeshirikiana na Mungukatika umilele barabara, alipata kuzaliwa tumboni mwa mamawa kibinadamu. Akiwa 'Mwana wa Mungu' yeye akajikusanyiandani yake sifa kamilifu za kibinadamu na pia za Mungu Baba.Tena tunaambiwa ya kwamba mama mmoja mwema na mtawa,jina lake Mariamu, akachaguliwa kuwa mzazi wa 'Mwana waMungu' Mama huyo akashika mimba ya Yesu kwa kushirikianana Mungu. Ndiyo kusema kwamba Yesu akiwa mwana halisi waMungu akazaliwa pasipo kuwa na dhambi, hata hivyo akachukuasifa na sura ya binadamu. Hivyo akajitolea kwa hiari yake kubebamzigo wote wa madhambi ya wale watu watakaomwamini nakumkubali kuwa mwokozi wao. Kwa njia ya mpango huo waakili, inadaiwa, Mungu akaepa kuhatarisha sifa yake ya uadilifuhalisi.Kumbukeni ya kwamba sawa na mpango huu pia mtuhatasamehewa dhambi pasipo kuadhibiwa. Bado Mungu atawezakumwadhibu mwenye dhambi bila ya kuepa sifa yake ya uadilifu.Tofauti yenyewe ni kwamba sasa Yesu ataadhibiwa, siyo walewana na mabinti wa Adamu waliotenda dhambi. Hiyo ni fidia yaYesu itakayosababisha kuwaondolea dhambi watoto wa Adamu.Mantiki hiyo hata ikionekana ya ajabu na ya kutatanisha namna

20

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 27: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

gani, lakini ndivyo ilivyokubaliwa hasa kwamba ilitendeka. Yesuakajitolea mweyewe na akaadhibiwa kwa ajili ya dhambi ambazohakuzitenda kabisa.

DHAMBI YA ADAMU NA HAWA:Hebu tuchunguze upya kisa cha Adamu tangu mwanzo. Sehemuyoyote ya itikadi hiyo hapo juu haiwezi kukubaliwa na dhamiriya mtu na mantiki.Kwanza, tunaambiwa ya kwamba kwa kuwa Adamu na Hawawalitenda dhambi, basi wazao wao wakachafuliwa kwa kudumuna dhambi waliyorithi wakati wa kuzaliwa. Lakini kinyume chake,sayansi ya tabia zirithishwazo inabainisha ya kwamba mawazona matendo ya mtu, yakiwa mazuri ama mabaya , hata mtu akiwanayo kwa kudumu maisha mazima, hayawezi kuhamishwa katikamfumo wa tabia za kurithishwa katika kuzaana. Muda wa maishaya mtu ni mdogo sana kwa kuleta mabadiliko hayo makubwa.Hata maovu ama mema ya taifa, kizazi baada ya kizazi, hayawezikuingizwa katika wazao yakiwa ni mienendo ya kurithiwa. Labdamamilioni ya miaka inahitajika kuingiza sifa mpya katika vijine(genes) vya mtu.Hata kama mtu angekubali kutukia jambo hilo la ajabu lakutatanisha kwa kapanua mawazo yake ya kipuuzi yasiyokubalikaakilini, basi na angekubali kilicho dhidi yake pia kwa kutumiamantiki kama hiyo. Hiyo itamaanisha ya kwamba kama mtumwenye dhambi akitubu na akatakasika mwishoni mwa siku, basihiyo nayo ingerekodiwa katika mfumo wa sifa zilezinazorithishwa na kufutilia mbali kabisa athari ya dhambi ile yazamani. Kisayansi hiyo haiwezi kutendeka, lakini kwa yakini kunamantiki zaidi katika picha hiyo inayoonesha pande mbili kwausawa kuliko kufikiria kwamba maelekeo kwa dhambi tuyanaandikwa katika utaratibu wa sifa za kurithishwa lakinimaelekeo ya mema hayaandikwi.

21

Dhambi na Kafara

Page 28: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Pili, kwa kujaribu kutatua tatizo la Adamu kwa kutoa shauri yakuwa dhambi inahamishwa kwa vizazi vijavyo ambavyo vinairithitangu kuzaliwa, msingi wenyewe unabomolewa ambao juu yakeimani ya 'Dhambi na kafara' imejengwa. Kama Mungu ndiyemwadilifu halisi, basi upo wapi uadilifu katika kuwahukumuwazao wote wa Adamu na Hawa kwa dhambi yao waliyotendamara mmoja tu na kisha wakatubu pia?Kwa vyovyote, hiyo ilikuwa dhambi ambayo waliadhibiwa vikalikwa sababu yake na wakafukuziliwa mbali katika Pepo kwafedheha kubwa . Ni aina gani ya uadilifu ya kwamba baada yakuwaadhibu Adamu na Hawa sana sana kupita kiasi kwa sababuya dhambi yao, bado hamaki ya kujilipiza kisasi haijapoa naakawahukumu wanadamu wote wapate fedheha ya kuzaliwa tayariwamerithi dhambi? Nafasi gani wanayo wazao wa Adamukuikwepa dhambi? Kama wazazi wanafanya kosa, kwa niniwatoto wao wasiokosea wasumbuke daima kwa sababu ya kosala wazazi wao?Kama ni hivyo, basi batilifu iliyoje maana ya uadilifu anayojidaiaMungu na kuifurahia ikiwa Yeye anawaadhibu watuwaliopangiwa kutenda dhambi hata wakichukia dhambi namnagani? Dhambi ikafanywa sehemu ya maana sana ya maumbileyao. Hamna kabisa sasa nafasi kwa mtoto wa Adamu kubakikatika hali ya kutokuwa na dhambi. Kama dhambi ndiyo jinaibasi ni jinai ya Mwumbaji siyo ya viumbe. Basi, uadilifu ganiungetaka kuwaadhibu wasiokosea kwa jinai za wengine?Tangazo la Kurani Tukufu ni tofauti kabisa na ufahamu waKikristo wa dhambi na matokeo yake. Kurani Tukufu inatangaza:

22

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Hakuna mbebaji atakayebeba mzigo wa mwingine. (35: 19)

Mungu haikalifishi nafsi yoyote zaidi ya uwezo wake. (2:287)

Page 29: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Tangazo hilo la Kurani kwa kulinganisha na imani ya Kikristokuhusu Dhambi na Kafara ndiyo taratibu halisi ya kuituliza roho.Sasa tugeukie maelezo ya Biblia kuhusu yaliyotendeka hasawakati Adamu na Hawa walipotenda dhambi, na matokeoyaliyofuata nyuma ya wao kuadhibiwa. Sawa na mafunzo yaMwanzo, Mungu alikubali nusu-nusu udhuru wao na wakapewaadhabu ya kudumu milele inavyoelezwa hapa chini:

Wanadamu walikuwapo muda mrefu sana kabla hawajazaliwaAdamu na Hawa. Wanasayansi wa magharibi wenyewewaligundua mabaki ya watu wengi waliokuwepo ardhini katikazama za kale sana na wakawapa majina mbali mbali yakupambanua. Neanderthal - mtu pengine ndiye anayejulikana zaidimiongoni mwa hao. Wa-Neanderthal waliishi zaidi katika Yoropa,Mashariki ya Karibu na Asia ya Kati, baina miaka 100,000 na35, 000 mpaka sasa. Maiti ya mtu mkamilifu imenguduliwaambaye mtu huyo aliishi ardhini miaka 29,000 kabla Adamu naHawa hawajaanza safari yao fupi huko Peponi. Katika zama hizowanadamu kimaumbile walikuwa kama sisi na waliishi katikaYoropa, Afrika na Asia, na baadaye mnamo zama za Theluji (IceAge) walienea hadi Marekani pia. Vilevile huko Australia historiathabiti ya utamaduni wa Waaborijini (Aborigines) inaoneshaulianza miaka 40,000 iliyopita kutoka leo. Waaborijini ni watuwa asili ya Australia.

23

Dhambi na Kafara

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako,na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto, na tamaa yakoitakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu,Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda yamti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwaajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maishayako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga zakondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hatautakapoirudia ardhi, ambayo kwa hiyo ulitwaliwa kwa maana umavumbi wewe nawe mavumbini utarudi (Mwanzo 3:16-19)

Page 30: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kwa kulinganisha na zama za hivi majuzi, mifupa yote ya mwiliikiwa pamoja, ya mwanamke, imepatikana huko Hedar katikaEthiopia ambayo mifupa hiyo ni ya tangu miaka milioni 2.9. Sasakwa kulingana na matukio ya historia yalivyoelezwa katika Biblia,Adamu na Hawa waliishi karibu miaka 6,000 tu tangu leo.Mtu aweza kuangalia nyuma kwa mshangao taarifa ya historiaya wanadamu, ama Homo Sapiens wanavyoitwa katika istilahiya Kisayansi.

MATESO YA BINADAMU YAENDELEA:Akiisha soma maelezo ya Biblia kuhusu walivyoadhibiwa Adamuna Hawa, mtu hana budi kustaajabu kama kweli uchungu wa kuzaahaukujulikana kwa mwanamke hadi zama za Adamu na Hawazilipoanza. Mwanasayansi yeyote hawezi kukurubia kuwazamawazo kama hayo yasiyo ya kweli. Isitoshe, tunao ushahidimwingi usiyoweza kukanushwa ya kwamba, muda mrefu hatakabla ya Adamu na Hawa hawajapatikana, wanadamu walikuwawanaishi katika mabara yote ya dunia, hata huko visiwa vya Bahariya Pasifiki vilivyo mbali kabisa, na daima walijibidiisha sana ilikupona katika hatari. Kwahiyo kusema kwamba Adamu na Hawawalikuwa watu wa kwanza kutenda dhambi kwa sababu hiyosheria ya kumwadhibu mwanamke kwa uchungu wa kuzaailiundwa, kumethibitika kwamba ni batili kabisa, hakuna msingiwake, tukitaali maisha ya binadamu. Hata wanyama wa daraja lachini zaidi wanajifungua kwa uchungu. Kama mtu akishuhudiang’ombe akimzaa ndama, ataona ya kwamba uchungu wakeunafanana na uchungu wa mwanamke akizaa. Wanyama wengisana mno wa aina hiyo twajua walipatikana juu ya uso wa ardhimamilioni ya miaka kabla ya Adamu na Hawa.Kuchuma riziki kwa taabu ni jambo la kawaida kwa mtu, lakinihaihusikani na wanaume pekee bali hata wanawake pia wanapatataabu kwa kuchuma riziki zao. Tangu zamani kila kiumbehujipatia riziki yake kwa kujibidiisha na kusumbuka. Hakika hiyo

24

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 31: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ndiyo iliyosababisha kuleta mabadiliko na maendeleo katika uhai.Kujibidiisha ili kubaki hai ndiyo pengine kipambanuzikinachopambanua baina ya kilicho hai na kisichokuwa na uhai.Hiyo ndiyo kanuni ya kawaida isiyohusikana na dhambi.Kama hiyo ndiyo adhabu iliyotolewa kwa sababu ya dhambiwaliyotenda Adamu na Hawa, basi mtu atashangaa itatokea ninibaada ya kafara yaani baada ya dhambi hiyo kufutiliwa mbali.Kama Yesu Kristo alikuwa amefutilia mbali dhambi za watuwenye dhambi, je, adhabu iliyotolewa kwa Dhambi ya Adamuna Hawa iliondolewa baada ya tukio la Msalaba? Je, walewanawake waliomwamini Yesu Kristo kuwa 'Mwana wa Mungu'hawasikii sasa uchungu wakati wa kuzaa? Na je, wanaumewaumini wameanza kuchuma riziki zao pasipo kujibidiishakufanya kazi kwa mikono? Je, tabia ya kutenda dhambi iliishiapapo hapo pasipo kuingia ndani ya vizazi vingine na watoto wasiona dhambi wakaanza kupata kuzaliwa? Kama majibu ya maswaliyote hayo ndiyo 'Naam', hapo bila shaka kuna sababu kiasi fulaniya kutafakari kwa makini falsafa ya Kikristo kuhusu Dhambi naKafara yake. Lakini, ole wako, majibu ya maswali hayo yote ni:Hapana, hapana tena hapana! Kama lolote halikupata kubadilikatangu tukio la Msalaba katika ulimwengu wa Wakristo na wasioWakristo, basi Kafara ina maana gani tena?Hata baada ya Yesu kusulibiwa, uadilifu unamtuma mtu dunianikote ya kwamba mtu yeyote akitenda dhambi, aadhibiwe yeyehuyo tu aliyefanya dhambi hiyo pasipo kuwaadhibu wengine.Wanaume na wanawake wote watasumbuka kwa sababu yadhambi zao wao wenyewe. Watoto huwa wanazaliwa bila yadhambi. Kama hiyo siyo sawa, basi uadilifu wa Munguunatupiliwa mbali.

Sisi tukiwa Waislamu tunaamini ya kwamba vitabu vyote vyaMungu vina msingi juu ya ukweli wa daima wala hakuna awezayekudai dhidi yake. Tunapoona hitilafu katika kitabu kimojawapomiongoni mwa vitabu vinavyodaiwa kuwa vya Mungu, hatukikani

25

Dhambi na Kafara

Page 32: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

moja kwa moja bali twashika njia ya kukichunguza kwa uangalifuna kwa upole. Maneno mengi ya Agano la Kale na Agano Jipyatunayoona ni dhidi ya ukweli wa kawaida, hapo kwanza twajaribukuyachukua hayo kimithali na kimafumbo, ama twayakataatukifahamu kwamba hiyo sehemu imeingizwa na watu humondani wala siyo maneno ya Mungu. Ukristo ukiwa dini ya kweliusingekuwa na upotevu, mambo na itikadi zisizokubalika zilizodhidi ya kanuni ya ulimwengu. Ndiyo sababu hatukuanzia nauchunguzi wa matini ya Biblia, bali tukaanzia na imani za kimsingiambazo imani hizo zilikubaliwa na ridhaa ya watu wote kuwasehemu za lazima za falsafa ya Kikristo. Kitu cha kwanza kabisakatika itikadi hizo ni muradi wa Kikristo wa Dhambi na Kafara.Mimi naamini kwamba mtu fulani wakati fulani katika historiaya Ukristo alielewa vibaya mambo na akajaribu kuyafafanua sawana ujuzi wake na akawa sababu ya kuvipoteza vizazi vijavyo.

DHAMBI YA KURITHIWA:Hebu tufikirie kwa shabaha ya kuhojiana ya kwamba Adamu naHawa walifanya dhambi hasa jinsi ilivyoelezwa katika Agano laKale. Adhabu yake, inavyoelezwa katika kisa, haikutolewa kwaopekee bali hata kwa wazao wao wote. Kama adhabu hiyo ilikwishaamuliwa na kutolewa tayari, ilikuwa haja gani tena ya adhabunyingine yoyote? Kama adhabu imekwisha tolewa kwa dhambimoja, basi habari ikaisha. Hukumu ikiisha tolewa tayari, mtuyeyote hana haki ya kuendelea kuongeza daima adhabunyinginezo. Katika kesi ya Adamu na Hawa siyo kwambawalilaumiwa tu vikali sana kana kwamba walitenda jambolililozidi kuliko dhambi inayotolewa adhabu, bali hata aina yaadhabu waliyotolewa ambayo iliendelea kwa wazao wao pia siyobarabara kabisa. Kuhusu hiyo tumekwisha eleza vya kutosha.Tunalojaribu kulidokeza ni uvunjaji wa uadilifu halisiunaochukiza sana sana. Kuadhibiwa kwa kudumu kwa dhambi

26

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 33: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

walizotenda babu zetu ni jambo tofauti lakini ni chukizo mojakwa moja kulazimishwa kuendelea kufanya dhambi kwa sababutu babu wa mtu aliwahi kufanya kosa fulani.Hebu tufikirie hakika tupu ya majaribio ya mtu na kujaribukuelewa falsafa ya Kikristo ya dhambi na adhabu kwa kulinganana yale tunayoshuhudia kila siku. Tufikirie hukumu aliyotolewamvunja sheria ambayo hukumu hiyo ni kali zaidi sana kulinganana dhambi iliyotendwa. Kila mtu mwenye akili atailaumu vikalisana hiyo hukumu isiyolingana kabisa na kosa lililotendwa. Kwahiyo, twaona ni vigumu kuamini ya kwamba adhabu aliyopewaAdamu kwa dhambi yake ilitolewa na Mungu mwadilifu. Hiyosiyo tu habari ya adhabu kutokulingana na dhambi. Hiyo ndiyoadhabu ambayo sawa na ufahamu wa Kikristo wa mwenendo waMungu ikaendelea hata baada ya Adamu na Hawa kufariki nakudumu kupatikana kwa wazao wao kizazi baada ya kizazi. Wazaokupata adhabu ya wazazi wao kwa hakika ni kuuvunjilia mbaliuadilifu kupita mipaka. Lakini hatuzungumzii hiyo pia. Kamakwa bahati mbaya tukishuhudia jaji mmoja wa zama hizi katoahukumu iliyowalazimisha watoto wajukuu na vilembwe nakadhalika wa mvunja sheria fulani na kuwashurutisha kisheriakuendelea na dhambi hiyo na kuhalifu na kuadhibiwa kadhalikadaima dawamu, itafanyaje jamii ya kisasa ambayo imekwishatambua maana hasa ya uadilifu kwa sababu ya utamaduni kupatamaendeleo?Msomaji anapaswa kukumbushwa hapa ya kwamba nadharia hiyoya dhambi ya kurithiwa imeletwa na Bwana Paulo aliyeelezavibaya sehemu fulani ya maandiko. Hiyo haiwezi kunasibishwakwa mafundisho ya Agano la Kale. Upo ushuhuda wa kuelemeakatika vitabu vingi vya Agano la Kale ulio kinyume chake kabisa.Mnamo karne ya tano, Augustine, Askofu wa Hippo, aliingiakatika mapambano na mwendeleo wa (Pelagian Movement)kuhusu majadiliano juu ya hakika ya Adamu na Hawa kuangukakwa kufanya dhambi. Bwana Askofu alitangaza ya kwambawafuasi wa mwendeleo wa Pelagius ndio wazushi kwa sababu

27

Dhambi na Kafara

Page 34: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wanafundisha ya kwamba dhambi ya Adamu ilimwathiri Adamutu pekee siyo kizazi kizima cha Adamu kwa ujumla, na kwambakila mmoja anazaliwa akiwa hana dhambi na anao uwezo wakuishi maisha yasiyo na dhambi na kwamba walikuwepo watuwaliofaulu kuishi pasipo dhambi.Waliokuwa sawa wakabandikwa jina 'wazushi' . Mchana ukaitwausiku na usiku ukaitwa mchana . Uzushi ukawa ukweli na ukweliukawa uzushi.

KUHAMISHWA KWA DHAMBI:Sasa tuchunguze upya habari hii ya kwamba Mungu hawasamehewenye dhambi bila kuwaadhibu kwani hiyo ni kinyume cha tabiayake ya uadilifu. Mtu anachukizwa kabisa kujua ya kwamba karnebaada karne Wakristo wameamini jambo lisiloeleweka kabisaakilini mwa mtu na ni kinyume cha dhamiri ya binadamu. Munguangewezaje juu ya uso wa ardhi ama huko mbinguni kumsamehemwenye dhambi kwa sababu tu asiye na dhambi amejitoleakuadhibiwa badala yake? Pindi Mungu afanyapo hilo papo hapoyeye anavunjilia mbali kanuni ya uadilifu. Mwenye dhambi hanabudi aadhibiwe kwa dhambi zake. Kwa kifupi matatizo chungumbovu ya kibinadamu yatazuka ikiwa adhabu itahamishiwa kwamwingine asiyetenda dhambi.Wataalamu wa dini ya Kikristo wameleta hoja ya kwambakuhamishwa dhambi kwa njia hii hakuvunji kanuni ya uadilifukwa sababu mtu asiye na dhambi amekubali kwa hiari yakekuadhibiwa badala ya mtu aliyetenda dhambi. Wanauliza,mtasemaje kuhusu habari ya mdeni aliyelemewa na deni kubwasana asiweze kulipa na mja fulani wa Mungu mfadhili anaamuakumwondolea mzigo wake kwa kumlipia deni lake lote? Jawabuletu ni kwamba tutamshangilia kwa kupaza sauti kwa sababu yatendo lake hilo la ukarimu, huruma na kujitolea sana. Itakuwajefikira ya mtu anayetukabili akiuliza kama deni linalotakiwakulipwa ni mamilioni milioni ya pauni za Kiingereza na paleanajitokeza mfadhili anayetoa mfukoni mwake peni moja akitaka

28

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 35: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ya kuwa deni lote lile analodaiwa mdeni lifutwe kwani anatoahiyo peni badala ya deni hilo lote. Habari ya Yesu Kristo kujitoaili kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi za wanadamu woteinachekesha kwani dhabihu yake hailingani kabisa kabisa nadhambi chungu mbovu za wanadamu wote. Isitoshe, hapa hamnamdeni mmoja ama wadeni wote wa kizazi kimoja, twazungumziamabilioni ya wakosefu waliokwisha zaliwa na wenginewasiozaliwa bado lakini watazaliwa mpaka siku ya kiama.Lakini hiyo siyo basi tu. Kufahamu dhambi kwa mfano waanayedaiwa fedha na mtu fulani ni kifafanuzi cha kijinga sanacha dhambi nilichowahi kuambiwa. Mithali hiyo tuliyoambiwainastahili tuifikirie zaidi kabla hatujashughulikia baadhi ya jihanyingine za dhambi na adhabu.Hebu tuchukue habari ya mdeni aitwaye 'A' ambaye anatakiwakumlipa mwingine 'B' pauni 100,000. Kama mfadhili fulani tajiriakiwa na akili timamu anataka kwelikweli kumwondolea mdenimzigo wa deni, sheria itamtaka amlipe B yote ile anayodaiwa A.Lakini ufikirie kwa mfano ya kwamba mfadhili huyo wa mithalianajitokeza akiomba ya kuwa ndugu A aondolewe wajibu wakumlipa B na badala yake yeye huyo mfadhili apigwe kidogoama atiwe kifungoni kwa siku tatu usiku na mchana kwa wingi.Kama hiyo ingetokea kweli katika maisha hasa ingekuwa tafrijakuona nyuso za jaji aliyeshikwa na butwaa na mdai Baliyefadhaika. Lakini mfadhili huyo bado anataka kutimizahuruma yake. Yeye angependa kuleta masharti akisema: Eebwanangu, hiyo siyo yote nitakayo badala ya kujitolea kwangu.Ninataka wadeni wote popote walipo katika ufalme walio haileo au watakaozaliwa baadaye mpaka siku ya kiama waondolewedeni zao kwa sababu ya mimi kusumbuka kwa siku tatu, usiku namchana hapo roho ya mtu inasita kwa kushikwa na butwaa.Mtu anawezaje kumshauri Mungu, Mungu mwadilifu, ya kwambawale walionyang’anywa mali yao waliyochuma kwa kutokwajasho ama wale walioibiwa akiba zao za maisha mazima, walipwe,kwa uchache, hasara zao kiasi fulani. Lakini yaonekana Mungu

29

Dhambi na Kafara

Page 36: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wa Kikristo yu mpole sana na mwenye huruma zaidi kwa wahalifukuliko kuwahurumia wasio na dhambi waliosumbuliwa nawahalifu. Hiyo ni maana ya ajabu ya uadilifu inayosababishakuwasamehe wezi, wanyang’anyi, wawatendeao vibaya watoto,wanaowaudhi wasio na dhambi na watendao maovu ya kinyamakinyume cha utu, sharti wapate kumwamini Yesu Kristo saa zakukata roho. Katika deni kubwa mno lisilohesabika, kiasi ganihao wanalazimika kuwalipa wale walioteswa? Je, dakika chacheza Yesu kukaa katika Jahanamu zaonekana zinatosha kuwatakasamaisha yao marefu ya maovu yachukizayo yanayoendelea kizazihata kizazi wala hawajaadhibiwa kwayo?

ADHABU YAENDELEA KUTOLEWA:Tufikirie sasa namna nyingine ya dhambi iliyo kubwa zaidiambayo tabia ya asili ya mtu haiwezi asilani kukubali ya kwambahiyo iweze kuhamishwa kwa mwingine. Kwa mfano, mtu fulanianamtendea mtoto bila kumhurumia, bali hata analala naye kwanguvu na kumwua. Hapo utu wa mtu unavunjiliwa mbali kiasicha juu sana kisichoweza kuvumiliwa. Fikiria kwa mfano yakwamba mtu huyo anaendelea kuwasumbua na kuwatesa wenginepembezoni mwake pasipo kukamatwa na kuaadhibiwa. Baadaya kuishi maisha yote ya dhambi bila kukamatwa anakurubiamauti lakini anaamua kuepa hata adhabu kubwa zaidi ya Siku yaHukumu na mwishowe anakata shauri ghafula na kumwaminiYesu kuwa mwokozi wake. Je, madhambi yake yote yatatowekamara moja naye ataingia katika akhera akiwa hana dhambi kamamtoto aliyezaliwa sasa hivi? Labda mtu huyo anayeahirishakumwamini Yesu mpaka wakati wa kifo chake ndiye mwenyebusara zaidi kuliko yule anayemwamini mapema katika maishayake. Kwani anayeamini mapema yuko katika hatari ya kutendadhambi baada ya kuamini na kuangukia hila za shetani nauchongezi wake. Kwa nini usingoje hadi mauti yakukurubie iliusimpe shetani nafasi ya kukunyang’anya imani yako katika

30

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 37: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Yesu? Maisha huru yenye dhambi na anasa juu ya ardhi, nakuzaliwa upya katika wokovu wa daima ni nafuu sana kwa hakika.Je, hiyo ndiyo hekima ya uadilifu wanayonasibisha Wakristo kwaMungu? Uadilifu wa aina hiyo au Mungu wa aina hiyo hakubaliwikabisa na dhamiri ya mtu ambayo yeye mwenyewe Akaiumbapasipo kupambanua baina ya sawa na isiyo sawa.Kwa kuangalia swala hilo katika mwanga wa maarifa ya binadamuna fahamu yake, mtu ana kila haki ya kulaumu hiyo falsafakwamba haina maana wala haina msingi. Hiyo haina hakika walanguvu. Maarifa ya binadamu yanatuambia ya kwamba ni haki yawanaosumbuliwa na wengine kuwasamehe amakutokuwasamehe. Wakati mwingine serikali kwa kusherehekeasiku ya taifa ama kwa sababu nyingine zinatangaza msamaha kwawaliozikosea serikali hizo pasipo kuwabagua. Lakini hiyohairuhusu kuwasamehe wale waliowadhuru wenzao wasio nahatia kwa madhara yasiyoweza kurekebishwa na kuwasumbuakwa kudumu. Kama serikali kutoa msamaha kwa wote pasipoubaguzi inajuzu kwa vyovyote na kama hiyo haihesabiwi nawataalamu wa dini ya Kikristo kuwa kinyume cha maana yauadilifu, kwa nini basi hawamwachilii Mungu haki ya kusamehejinsi apendavyo na wakati apendapo? Kwa vyovyote, Yeye ndiyeMfalme Mkuu, Mwumbaji na Bwana wa kila kitu. Kama Yeyeanasamehe yeyote uovu aliomfanyia mwanadamu mwenzake,Bwana Mkuu anao uwezo halisi wa kumlipia kwa wingi sanayule aliyekosewa hadi akaridhika barabara kwa uamuzi wake.Kama ndiyo hiyo, iko wapi basi haja ya kumtoa mwanaye asiyena dhambi kuwa dhabihu?. Hilo lenyewe ndilo kuudhihakiuadilifu. Sisi tumezaliwa tukilingana na sifa za Mungu.Yeyeanatangaza katika Biblia takatifu:

31

Dhambi na Kafara

Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu(Mwanzo 1:26).

Page 38: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kuhusu habari hiyohiyo Yeye anasema ndani ya Kurani Tukufu:

Itikadi hiyo iliyo sawa baina ya Wakristo na Waislamu inaitakadhamiri ya mtu kuwa picha bora ya tendo la Mungu katika halifulani. Tunaona kila siku ya kwamba tunasamehe mara nyingipasipo kuvunja maana ya uadilifu hata kidogo. Kama mtotoanawaudhi wazazi wake kwa kuwaasi, ama kwa kuharibu kitufulani chenye thamani cha nyumbani, ama kuwaharibia heshima,hapo yeye amewafanyia dhambi. Wazazi wake wanawezakumsamehe bila ya dhamiri yao kuwachoma au kuwalaumukwamba wamevunjilia mbali uadilifu halisi. Lakini kama mtotowao anaharibu mali ya jirani yao, au anamjeruhi mtoto wa mtumwingine, wazazi wa mtoto huyo mhalifu wanawezaje kuamuakumsamehe mtoto wao kwa kuwasumbua wengine? Hiyoitaonekana ni kitendo kilicho kinyume cha uadilifu hata sawa nadhamiri yao wenyewe kama watamsamehe hivyo.Dhambi na adhabu zinahusiana jinsi sababu na matokeovinavyohusiana, na zinalazimika kulingana kiasi fulani. Jiha hiyoya uhusiano baina ya dhambi na adhabu imekwisha elezwa kiasifulani kulingana na mtu mmoja kutumia vibaya mali ya mwingine.Ndivyo ilivyo hali ya dhambi nyingine, bali vibaya zaidi, kamavile kuwajeruhi wananchi wasiofanya dhambi au kuwavunjaviungo vyao ama kuwaua ama kuvunja heshima zao kwa namnayoyote. Kadiri itakavyokuwa kubwa dhambi, ndivyoitakavyotazamiwa kuwa kubwa adhabu na namna ya adhabu hiyo.Kama Mungu anaweza kuwasamehe watu wote, na ndivyoniaminivyo kwamba Yeye, tena Yeye peke yake anaweza, basihalizuki kabisa suala la kufutilia mbali dhambi kwa kumwadhibumtu asiyefanya dhambi. Na kama ni suala la kuhamisha adhabuya mhalifu kwa mtu asiyefanya dhambi aliyekubali kwa hiarikuadhibiwa, basi uadilifu utalazimisha ya kwamba adhabu nzima

32

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Fuateni sifa za Mungu ambazo yeye akawaumba watu juu yake(30: 31).

Page 39: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

nzima ihamishwe kwa huyo mwingine pasipo kupunguza kiasikiwacho chochote kile. Kuhusu habari hiyo tumekwisha elezatayari vya kutosha.Je, Wakristo wanaamini ya kwamba Mungu Baba alitimiza shartihiyo ya uadilifu kuhusu habari ya Yesu, Mungu Mwana? Kamani hivyo, basi itamaanisha ya kuwa adhabu zote za wahalifu wotewale waliokwisha zaliwa katika zama za Yesu na hata waliozaliwabaadaye hadi Siku ya Hukumu, zikarundikana pamoja, zikawanzito na kali sana sawasawa na Jahanamu hata kwamba taabu yaYesu Kristo aliyopata kwa siku tatu pekee, usiku na mchana,ikawa sawa na shida ya adhabu zote zile walizojichumia wahalifuwaliotajwa juu au walizotazamiwa kujichumia mpaka Siku yaMwisho. Kama ni hivyo, basi Mkristo yeyote hastahili dunianikuadhibiwa na Serikali ya Kikristo. La sivyo, hicho kitakuwa nikitendo kilicho kinyume kabisa cha uadilifu. Itakalofanyamahakama baada ya kwisha kumhukumu mhalifu Mkristokwamba amefanya hatia, ni kumwadhibu huyo mhalifu kwambaamwombe Yesu mwana wa Mungu kumwokoa. Na habari hiyoingemalizika na kuishia papo hapo. Hiyo itakuwa ni habari yakuhamisha hesabu ya mhalifu kwenye hesabu ya Yesu.

Ili kutoa mfano, hebu tuchunguze hali ya uhalifu ulioenea katikaAmerika. Uhalifu wa ujambazi na mauaji umezidi huko na kueneasana hata kwamba ni vigumu kuweka hesabu yake. Nakumbukasafari moja nilifungua redio nilipokuwa huko New York. Idhaaniliyofungua ilihusikana na kutoa taarifa ya uhalifu mkuu wamauaji na kadhalika. Taarifa hiyo ilitisha moja kwa moja. Ilikuwayenye kuudhi sana hata kwamba sikuweza kuvumilia zaidi yasaa moja. Katika kila dakika tano takriban mtu mmoja aliuliwakatika Amerika na kuripotiwa wakati mwingine pamoja namaelezo ya kuogofya mno na wale walioshuhudia mauajiyalipokuwa yanafanywa. Siyo nia yetu kutoa picha kamili yauhalifu Marekani, lakini wote wanajua ya kwamba siku hiziAmerika iko mbele katika orodha ya nchi ambamo uhalifu wa

33

Dhambi na Kafara

Page 40: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kila aina ni jambo la kawaida sana, hususan katika miji mikubwakama vile Chicago, New York na Washington. Katika New Yorkuharamia ni jambo la kawaida kama ilivyo kukata mikono, miguuama viungo vingine vya mwili wa wale wasio na hatia ambaowanajaribu kushindana na hao wahalifu ili kujilinda. Matukiohayo ya kila siku yanaleta picha chafu mno ya kulemaza na kuuakwa manufaa madogo.Achilia mbali kwa kitambo mwenendo unaoendelea kuzidi wakutenda maovu duniani kote, kuhusu habari ya Amerika pekeyake mtu anashangaa kuona jinsi imani ya Wakristo juu ya dhambina kafara inavyolingana na maovu yanayotendeka kila siku. Hatawakiweza kuwa mbali sana na khulka za Kikristo kwa kitendo,kwa akali wanayo sifa hii ya kwamba wanaiamini itikadi yaKikristo ya Dhambi na Wokovu na kwamba Yesu ndiye mwokoziwao, lakini nasikitika hiyo yote ni bure. Wahalifu wengi zaidikatika Amerika ndio wanaojiita Wakristo, ijapokuwa Waislamuna wengineo pia ndio hivyo hivyo. Lakini, je, kwa sababu tuwahalifu hao wanahusikana na Ukristo na wanaamini katika fidiainayosemekana aliitoa Yesu Kristo kwa hiari yake kwa ajili yawaumini wenye dhambi, watasamehewa wote hao na Mungu?Kama ndiyo, kwa njia gani? Mwishowe, asilimia kubwa ya haowanaweza kukamatwa na kuadhibiwa na sheria ya nchi. Lakinihata hivyo wengi zaidi hawatakamatwa ama wanaweza kupataadhabu kwa sehemu ya madhambi waliyotenda katika muda wamiaka mingi.Ukristo utawatolea nini hao wanaoadhibiwa na sheria, nautawaahidia nini wale ambao hawakuweza kushikwa hapaduniani? Je, hao wote wa aina mbili watapewa adhabu tofautiama wataadhibiwa namna moja pasipo tofauti?Hapa pana mashaka mengine tena kuhusu wokovu wa mhalifukwa sababu ya yeye kumwamini Yesu Kristo. Mashaka hayoyanasababishwa na hali isiyo wazi sana wala haikupambanuka.Kama, kwa mfano, Mkristo mmoja anamsumbua mtu asiyekosaambaye si Mkristo, hapo huyo Mkristo atasamehewa kwa sababu

34

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 41: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ya baraka za imani yake katika Yesu. Adhabu ya dhambi yakeitahamishwa na kuingizwa katika hesabu ya Yesu. Lakini itakuwanini hesabu ya faida na hasara ya yule maskini aliyekosewaambaye si Mkristo? Yesu maskini na yule maskini aliyesumbuliwawakaadhibiwa kwa dhambi wasiyotenda wao.Akili yetu inafadhaika kama tukijaribu kuwaza wingi ule wamadhambi yaliyokwisha tendwa na watu tangu Ukristo kufikaduniani na yataendelea kutendwa mpaka Siku ile ya Mwisho. Je,dhambi hizo zote huingizwa katika hesabu ya Yesu, amani nabaraka za Mungu ziwe kwake? Je, Yesu alikwisha adhibiwa tayaribarabara kwa madhambi hayo yote katika muda mfupi wa sikutatu, usiku na mchana, inavyosemekana kwamba Yesuakasumbuka kwa huo muda? Bado mtu anashangaa ya kwambanamna gani bahari kubwa kabisa ya wahalifu iliyofanywa kuwachungu moja kwa moja na sumu ya madhambi, ikawa tamu nakutakaswa kwa kuondolewa mbali matokeo ya madhambi yaokwa sababu tu ya wao kumwamini Yesu. Isitoshe, fikara ya mtuinampeleka nyuma sana katika zama ambapo maskini Adamu naHawa waliwahi kutenda dhambi yao ya kwanza kwa kukosakuamua vizuri kwa sababu walidanganywa kwa hila na kutegwana Shetani. Kwa nini dhambi yao haikuondolewa pia? Je,hawakuwa na imani katika Mungu? Je, ni wema hafifukumwamini Mungu Baba? Na je, ni kosa lao ya kwamba haohawakuambiwa habari ya Mwana kuwa na Mungu Baba milele?Kwa nini ‘Mungu Mwana’ hakuwahurumia hao na kumwombaMungu Baba amwadhibu yeye kwa dhambi zao badala yakuwaadhibu wao? Mtu anawezaje kupenda kilichotendeka, kwaniingekuwa rahisi zaidi kuadhibiwa kwa kosa lililofanywa kwadakika moja pekee na Adamu na Hawa. Kisa kingine kabisa chabinadamu kingepata kuandikwa katika kitabu cha bahati.Ingeumbwa ardhi ya kipeponi na Adamu na Hawawasingelifukuzwa kutoka Peponi kwa kudumu pamoja na wazaowao wenye majonzi wasiohesabika. Badala yao Yesuangeondoshwa kutoka Peponi kwa muda mfupi wa siku tatu, usiku

35

Dhambi na Kafara

Page 42: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

na mchana. Basi tu. Ni sikitiko kwamba Mungu Baba hakupatawazo hilo wala Yesu. Angalieni jinsi hakika tukufu ya kupendezaya Yesu imegeuzwa kuwa kisa cha kuchekesha na jambo lakubuniwa lisiloweza kuaminika.

UADILIFU NA MSAMAHA:Falsafa ya Kikristo ya Dhambi na Adhabu siyo tu inaibumbuazamoja kwa moja akili ya mtu mwadilifu asiyependelea, bali piainazusha maswali yanayohangaisha sana. Falsafa ya uhusianobaina ya uadilifu na msamaha, inavyothibitishwa na falsafa yaKikristo ya Kafara, inajaribu kueleza kwa nini Mungu Mwenyewehakuweza kusamehe. Hiyo inalitegemea wazo kosefu lisilofuatakanuni kuhusu uadilifu. Wazo hilo limechukuliwa kuwa kwelikabisa ya kwamba uadilifu na msamaha haviendi pamoja. Kamani hivyo, kwa nini, basi, Agano Jipya linasisitiza sana kusamehepindi uhusiano wa watu wao kwa wao unapozungumzwa?Sijasoma katu katika kitabu cho chote cha Mungu cha dini yoyoteduniani fundisho linaloelekea zaidi upande mmoja na kukazaniakupita kiasi kusamehe.Tofauti sana mno iliyoje hilo na ule mkazo juu ya uadilifuunaopatikana katika mafundisho ya Kiyahudi. Jicho kwa jicho;jino kwa jino. Huo ndiyo uadilifu - halisi, usiyo na matata,usiopunguzwa thamani. Ajabu iliyoje kuachana na fundisho hilona kushikilia fundisho la Kikristo la kugeuza shavu la pili kamashavu moja limepigwa kofi. Nani alifundisha fundisho la pili lililodhidi ya fundisho la zamani la Torati? Mtu anashikwa na butwaaya kwamba je, fundisho hilo la zamani lilifundishwa na MunguBaba lipingwalo moja kwa moja na fundisho la Agano Jipyalililofundishwa na 'Mwana wa Mungu'? Kama ndivyo hivyo, kwanini 'Mungu Mwana' akahitilafiana vikali sana na Mungu Baba?Je, kupingana huko kuchukuliwe kuwa dosari ya kuzaliwa amamageuzi ya maendeleo? Au mwenendo huu wa kusamehe moja

36

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 43: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kwa moja unaopingana vikali na mkazo wa kujilipiza kisasi sawana mafundisho ya Kiyahudi unahakikisha mabadiliko katikaMungu Baba? Yeye anaonekana amejuta sana kwa mafundishoaliyompa Musa na watu wa Kitabu na anaonekana kwambaamependa kurekebisha kosa alilowahi kulifanya. Sisi tukiwaWaislam, twashuhudia uhamisho wa huo mkazo, lakini hatuonitofauti, kwani tunamwamini Mungu ambaye amejikusanyia sifazote mbili za uadilifu na msamaha bila ya sifa hizo mbilikupingana zenyewe kwa zenyewe. Sisi tunaona kulihama fundishola Kiyahudi na kuhamia fundisho la Yesu Kristo siyo kwa shabahaya kulirekebisha fundisho lenyewe la kwanza, bali matumizi yakemabaya na Mayahudi. Kwetu sisi Mungu siye tu Mwadilifu baliYu Msamehevu, Mrehemevu na Mpaji pia. Kama Yeye akitakakusamehe hahitaji msaada wa nje ili kumsamehe mwenye dhambi.Lakini sawa na nadharia ya Kikristo hilo ni tatizo kubwa kabisa.Inaonekana kwamba Mungu wa Torati ndiye Mungu anayejuauadilifu pekee asiyetambua huruma na rehema. Kidhahiri yeyehakuwa na uwezo wa kusamehe hata akitaka sana namna ganikusamehe. Kumbe akaja tena Mungu Mwana kumsaidia nakumwokoa katika tatizo baya sana. Yaonekana 'Mungu Mwana'alikuwa mwenye huruma tupu kinyume cha Baba yake Mwenyekujilipiza kisasi siku zote. Huo siyo tu ubovu dhahiri wa busarahiyo ya 'Mwana' inayotatiza dhamiri ya mtu bali huo unazushamara nyingine swala la upingamizi katika mienendo yao. Yesuhaonekani kuwa mwana halisi wa Baba yake. Labda kosa fulanililiingia katika uzazi.Hapa pana suala jingine la muhimu kuhusu dini nyinginezo zaulimwengu ya kwamba dini hizo zinafikirije dhambi na matokeoyake. Bila shaka Ukristo peke yake siyo dini iliyofunuliwa naMungu. Wasio Wakristo wanawazidi Wakristo katika idadi.Maelfu ya miaka kabla ya historia ya binadamu inayojulikana,dini nyingi zilizalika na kuimarika baina ya watu katika sehemumbali mbali za dunia kabla hajaja Yesu Kristo duniani. Je, dinihizo zilizungumzia falsafa ya msamaha hata mara moja kwa

37

Dhambi na Kafara

Page 44: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kufungamanisha msamaha na itikadi ya Kikristo juu ya Kafara?Dini hizo zilifundisha imani gani kumhusu Mungu , ama miungukama ilivyoanza kuaminiwa sasa? Nini imani yao kuhusumwenendo wa Mungu kwa watu wenye dhambi ?Miongoni mwa dini mbalimbali, labda dini ya Kihindu ndiyokaribu kiasi fulani na Ukristo kuhusu habari hiyo. Wahindu piawanamwamini Mungu Mwadilifu Halisi ambaye uadilifu wakeunamlazimisha kumwadhibu mwenye kutenda dhambi kwa njiahii au ile. Lakini kulingana kunaishia hapo hapo. Hamna habariya Mungu Mwana mwenye kuchukua mabegani mizigo ya adhabuza ulimwengu mzima wa watendao dhambi. Hata habari hiyohaijadokezwa katika dini hiyo. Kinyume chake twaambiwa yakwamba mtu kwa sababu ya kutenda dhambi nyingi anaadhibiwakwa njia hii ya kwamba roho yake inarudishwa mara kwa maraduniani katika kiwiliwili cha wanyama mbali mbali. Yaani kwashabaha ya kuadhibiwa, mtu anapokufa anazalika tena dunianikwa mfano wa sura ya mbwa ama kuku au mbuzi na kadhalika.Hiyo inaitwa 'Tanasukhi' au kwa Kiingereza Reincarnation. Ndiyokusema kwamba mtu anatakasika katika dhambi alizowahikuzitenda kwa kuzalika mara nyingi sana duniani kwa sura yawanyama mbalimbali hadi hesabu yake ya dhambi inakamilika.Baadhi ya watu wanaweza kufadhaika na habari hiyo nakutatanika; lakini kwa vyovyote ndani ya falsafa hiyo mnauadilifu. Nadharia hiyo bila shaka inaafikiana na imani ya uadilifuhalisi.Kwa kuachilia mbali dini ya Kihindu na nyinginezo zinazoiteteafalsafa ya 'Tanasukhi' pamoja na matatizo ya 'sababu' na 'matokeo'yake, hebu tuone msamaha wa Mungu ukoje sawa na mafundishoya dini zingine kubwa ama ndogo za ulimwengu? Dini hizo zotepamwe na bilioni moja ya wafuasi wa dini hizo kama vile dini yaKihindu huonekana hawana habari kabisa ya wazo la kubuniwala Kafara. Hiyo kweli inabumbuaza sana. Alikuwa nani mahalipengine katika dini nyingine aliyewafunulia watu wahyi? Kamasiye Mungu Baba ilivyo katika imani ya Kikristo basi je viongozi

38

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 45: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wote wa dini zote isipokuwa Yesu Kristo walikuwa wanafunziwa shetani? Na Mungu Baba alikuwa wapi? Kwa nini hakujakuokoa wakati watu wengine walikuwa wanapotezwa na shetanikwa jina lake Yeye? Ama watu hao wote wengine waliumbwa namwingine minghairi ya Mungu Baba? Tena, kwa nini aliwatendeakama baba wa kambo na kuwaachilia wapotezwe na shetani?Sasa tugeukie suala hilo na kuliangalia sawa na majaribu yetu yakila siku. Inaweza kuhakikishwa ya kwamba uadilifu na msamahaviko sawasawa na vyaweza kukaa pamoja na kwamba havipinganisiku zote. Wakati mwingine uadilifu unataka msamaha utolewe,na pengine unadai kwamba msamaha ukataliwe. Kama mtotoakipata moyo wa kuhalifu zaidi pindi asamehewapo, hapomsamaha unaulanda uhalifu na kwa hiyo ni kinyume cha shabahaya uadilifu. Kama mhalifu anasamehewa na matokeo yake nikwamba yeye mhalifu huyo anazidi kufanya matendo ya uhalifuna kuwaudhi watu pembeni mwake na kuwadhulumu eti kwasababu atasamehewa tena, basi msamaha huo utakuwa dhidikabisa ya uadilifu na utakuwa sawa na kuwadhulumu raia wasiona hatia. Wako wahalifu wa aina hiyo wasiohesabikawanaositiriwa na kafara ya Yesu. Hiyo yenyewe ndiyo kinyumecha uadilifu. Lakini kama mtoto fulani anajuta, kwa mfano, namama yake ana hakika kwamba mwanaye hatarudia hilo kosatena, hapo kumwadhibu huyo mtoto itakuwa kinyume cha muradiwa uadilifu. Mtu mwenye kutubu anapojuta, majuto hayo yenyewehuwa adhabu kwake ambayo wakati mwingine ni kali zaidi kulikoile adhabu ambayo yeye angeweza kupewa. Wenye dhamiri haisiku zote husumbuka rohoni baada ya kufanya dhambi. Na mtuakijuta na kuudhika rohoni mara kwa mara kwa sababu ya makosayake na moyo wake unachomwa sana mno, aweza kufikia halifulani hata kwamba Mungu anamwonea huruma huyo mja wakemnyonge akoseaye siku zote na kutubu kila mara. Hilo ndilo somokatika uhusiano baina ya uadilifu na msamaha wanalopata wenyeakili nyingi na wale wenye fahamu ya kawaida kwa usawa kwakushuhudia yanavyofanyika maishani. Wakati umewadia sasa

39

Dhambi na Kafara

Page 46: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kwamba Wakristo wazinduke katika usingizi wa kuamini itikadiya Kikristo pasipo kuihoji hekima yake.Kama wakichunguza upya itikadi ya Kikristo kwa kutumia akilina hoja, bado wanaweza kubaki kuwa Wakristo wema lakini waaina nyingine na wapendao hakika zaidi. Hapo watakuwa na imanizaidi na mapenzi na kujitolea zaidi kwa Yesu akiwa binadamuhalisi kuliko Yesu wa kuzushwa na mawazo yao asiye zaidi yakitu cha kubuniwa. Adhama ya Yesu haimo katika kisa chakecha kubuniwa bali katika dhabihu yake kuu akiwa mwanadamuna Mtume. Dhabihu yake inaathiri moyo kwa nguvu sana mnokuliko kisa chake cha kubuniwa cha kufa msalabani na kufufukakatika wafu baada ya kukaa motoni kwa saa chache za kutisha.

YESU HAWEZI KUWA KAFARA :Jambo la mwisho lakini la maana ni kwamba Yesu angewezajekuzaliwa akiwa hana dhambi ilhali alikuwa na mama wakibinadamu? Kama dhambi ya Adamu na Hawa ilikwishakichafua kizazi cha hao wawili wenye bahati mbaya, basi matokeoyake ni kwamba wazao wao wote wa kiume na wa kike walirithimaelekeo ya kufanya dhambi katika kuzaliwa kwao. Labdawanawake wakarithi zaidi shauku ya kutenda dhambi kwa sababuHawa ndiye aliyetumiwa na shetani ili kumbembeleza Adamukutenda dhambi. Kwahiyo, Hawa anahusika na dhambi moja kwamoja kuliko pengine Adamu. Katika habari ya kuzaliwa Kristo,binti wa Hawa alihusikana zaidi. Swali linalozuka kwa nguvusana ni kwamba je, Yesu alirithi kromosom zenye vijine, (genes)kutoka kwa mamake binadamu ama hapana? Kama ndiyo, hapohaikuwezekana kwa Yesu kuepukana na dhambi ya lazima yakurithiwa. Kama hakuirithi kromosom yoyote kutoka kwamamake wala kwa Mungu Baba, hapo kuzaliwa kwake kutakuwamwujiza maradufu. Mwujiza pekee yake unaweza kuzalishamwana asiyehusikana na baba yake wala mamake. Jambo

40

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 47: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

lisiloeleweka ni kwamba kwa nini kromosom za Hawahazikumtilia mwanaye Yesu maelekeo ya kiasili ya kutendadhambi. Tukidhani kwamba ilikuwa hivyo kwa vyovyote na Yesualikuwa safi asiye na dhambi - jambo ambalo ni lazima ilikujichukulia dhambi za wanadamu sharti wamwamini, hapo swalijingine litazuka: Walikuwaje, mtu aweza kuuliza, waliokufamiongoni mwa wazao wa Adamu na Hawa kabla haujafikaUkristo? Mabilioni mangapi ya watu hao waliwahi kutawanyikaduniani kote katika mabara matano kizazi baada ya kizazi. Lazimawaliishi na wakafa pasipo kutumaini bali pasipo uwezekano wakusikia habari ya Kristo, Mwokozi wao, ambaye alikuwahajazaliwa. Kwa hakika wanadamu wote waliokuwapo baina yaAdamu na Kristo wanaonekana waliangamia kwa kudumu. Kwanini hao hawakupewa nafasi walau hafifu sana ya kusamehewa?Je, hao watasamehewa na Yesu Kristo kwa kutumia kanuni yakafara kwa waliopita kabla ya kanuni hiyo kuundwa? Kama ndiyo,kwa nini?Katika sehemu nyingine za dunia zilizo kubwa zaidi kulikoUyahudi ilivyo ndogo sana, haikupata kusikika habari za Ukristohata katika zama za uhai wa Yesu Kristo; watu hao watakuwaje?Maana hawakuamini 'Uana' wa Yesu Kristo wala hawangeweza.Je, wataadhibiwa kwa madhambi yao ama hapana na kwa hojagani? Walikuwa na nafasi gani kwa vyovyote? Walikuwa hoikabisa. Maana mbovu iliyoje hiyo ya Uadilifu!

KUTOA DHABIHU PASIPO KUPENDA :Sasa na tugeukie kuchunguza tukio la msalaba. Hapo twalikabilitatizo lisiloweza kutatulika. Tunavyoambiwa kwa kusisitiza nikwamba Yesu alijitolea kwa hiari yake mbele ya Mungu Baba naakasukumiziwa madhambi ya wanadamu wote sharti wamwaminikwanza. Lakini saa ya upendo wake kukubaliwa unaposogeleakaribu na mwanga wa tumaini la wanadamu wenye dhambi

41

Dhambi na Kafara

Page 48: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

unapoanza kumulika kama mapambazuko ya alfajiri, twamgeukiaYesu tukitazamia kushuhudia uchangamfu wake na furaha yakena shangwe yake ya hali ya juu sana katika wakati wa muhimukabisa katika historia ya binadamu, tunasikitikaje sana nakuvunjika moyo moja kwa moja! Badala ya kumkuta Yesuakingojea saa ya furaha kuu, twamwona akilia na kupaza sauti nakuomba na kumsihi Mungu Baba ili kimwepuke kikombe chamauti. Yeye akamkaripia vikali sana mwanafunzi wake mmojaalipomkuta akisinzia baada ya kupitisha mchana mrefu wa hatarina kusumbuka usiku wa majonzi ambao ukamchosha vibaya yeyena bwana wake. Biblia inasimulia habari hiyo kama ifuatavyo:

Ni masikitiko, kinavyotoboa kisa hiki cha Kikristo, ya kwambakurongaronga kwa Yesu wala kwa wanafunzi wake hakukubaliwana Mungu Baba, na japo akateta sana lakini akasulubishwa shingoupande. Je, huyo ndiye yule yule mfalme asiyekosa, na upeo wamwisho wa dhabihu, aliyejitolea mhanga sana ili kubeba mizigoya madhambi ya wanadamu wote mabegani pake, ama yu mtutofauti? Mwenendo wake, ilipowadia saa ya kutundikwa

42

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemaneakawaambia wanafunzi wake, ketini hapa hata niende kule nikaombe.Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanzakuhuzunika na kusononeka. Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuninyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. Akaendeleambele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akisema, Baba yangu,ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi,bali utakavyo wewe. Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala,akamwabia Petro: Je, hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakinimwili ni dhaifu. Akaendelea tena mara ya pili, akaomba, akisema, Babayangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa,mapenzi yako yatimizwe. Akaja tena akawakuta wamelala; maanamacho yao yamekuwa mazito. Akawaacha tena, akaenda, akaombamara ya tatu, akisema maneno yaleyale. (Mathayo 26: 36- 44).

Page 49: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

msalabani na wakati aliposulubishwa, unatia shaka sana kwambaaliyesulubishwa kweli alikuwa Yesu au kwamba kisa chenyewehicho kweli ni sawa kilichobuniwa kumhusu yeye. Lakini hilotutalijadili baadaye. Wakati huu tugeukie pale tulipoachauchunguzi wetu.Maswali mengine yanayozuka kutokana na kilio cha mwisho chaYesu katika hali ya kuteswa ndiyo haya: Ni nani aliyetamka hayomaneno ya kutia majonzi na kuhuzunisha? Alikwa Yesu-mtu amaYesu 'Mwana'?Kama huyo alikuwa ni Yesu mtu aliyeachwa (Mungu wangu,Mungu wangu mbona umeniacha) basi kaachwa na nani? Na kwanini? Kama alikuwa Yesu mtu, hakuna budi basi ya kwamba yeyealikuwa hadi mwisho nafsi ile ile moja inayojitegemea aliyewezakufikiria na kuhisi mwenyewe pasipo kizuizi chochote kiwacho.Je, yeye alikufa wakati roho ya Yesu Mwana wa Munguilipotengana na mwili wa aliokuwa ameuchukua yeye? Kamandiyo, kwa nini na kwa namna gani? Kama ni hivyo, na ilikuwani kiwiliwili cha mtu kilichokufa baada ya roho ya Mungukukitoka, basi swali linazuka hapo ya kwamba nani alifufukakatika wafu pindi roho ya Mungu ilipouingia mwili huo huobaadaye.Tena, habari hiyo itatuongoza kuamini ya kwamba siye Yesu'Mwana' aliyekuwa anasumbuka, bali ni Yesu mtu aliyepaza sautikatika hali ya kuteswa na ndiye aliyeudhika ilhali Yesu 'Mwana'aliangalia tu akitepetea asijali. Hapo anawezaje kudai ya kwambayeye akiwa 'Mwana' alisumbuka kwa ajili ya wanadamu walasiye yeye akiwa mtu?Naam, kama tukidhani ya kwamba alikuwa ni Yesu 'Mwana'aliyepaza sauti ya kilio ilhali 'mtu' ndani yake pengine akitumainikuanza maisha mapya akaangalia tu akitazamia pasipo hakika yakwamba pamoja na Yesu 'Mwana' kutoa dhabihu, yeye Yesu mtunaye atachinjwa, apende asipende, pamoja na mwenzakeasiyekosa. Uadilifu gani ulimhimiza Mungu kupata shabaha mbilikwa hila moja? Hiyo labda ni siri nyingine.

43

Dhambi na Kafara

Page 50: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kama huyo alikuwa Yesu 'Mwana', na kweli alikuwa huyo kwakulingana na maoni ya makanisa ya Kikristo, hapo litazuka swalijingine kutokana na jawabu la swali la kwanza ya kwamba alikuwanani ambaye Yesu alizungumza naye (Mathayo 26:39, 42).Twaweza kuchagua rai mojawapo katika rai mbili:Ya kwanza ni kwamba 'Mwana' alikuwa anaongea na Babaakilalamika kwamba ameachwa katika wakati wa haja. Hiyo hainabudi kutuongoza kuamini ya kwamba hao walikuwa wawili mbalimbali wasiokuwapo pamoja katika dhati moja wakishirikiana kwausawa katika sifa zote na kuzitumia kwa pamoja kwa usawa.Mmoja katika hao anaonekana kuwa mwamuzi mkuu, mweza,mwenye nguvu ya mwisho ya kutoa hukumu. Na mwingine yule'Mwana' maskini, anaonekana amenyimwa kabisa ama pengineakaondolewa kwa muda ile tabia ya kupiga ubwana aliyokuwanayo Baba. Kiini cha habari kinachotakiwa kuzingatiwa nikwamba matakwa yao na matilaba yao yanayopinganahayaonekani yakizozana na kuhitilafiana zaidi kuliko yalivyokuwawakati wa kitendo cha mwisho cha kisa cha msalaba.Swali la pili ni kwamba je, hao wawili mbalimbali, wakiwa namaoni tofauti, khulka tofauti na sifa tofauti wataona taabu na udhiawakiwa 'wawili katika mmoja' ama 'mmoja katika wawili'? Basiswali jingine litahitaji maongezi marefu baina ya wataalamu wadini ya kwamba je, upo uwezekano wa Mungu kupata kusumbukana kuadhibiwa? Hata kama upo uwezekano huo, Mungu nusu tuataudhika ilhali nusu nyingine ya Mungu hataweza kupata taabukwa sababu pengine kwa mpango maalum ama kwa sababu yakulazimika kwa tabia yake ya asili. Na tunaposogelea mbele katikaulimwengu huu wa wasiwasi wa falsafa hiyo iliyopotoka, mwangaunaanza kufifia zaidi na zaidi na tunakuta bumbuazi juu yabumbuazi.Lipo tatizo jingine tena. Kristo alikuwa anaongea na nani kamayeye mwenye alikuwa Mungu?. Alipoongea na Baba, yeyemwenyewe alikuwa sehemu isiyotenganishwa na Baba; ndivyotuambiwavyo. Basi alikuwa anasema nini na kumwambia nani?

44

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 51: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Swali hilo linatakiwa lijibiwe kwa dhamiri huru pasipokuikimbilia itikadi. Hiyo inakuwa itikadi hapo tu ambapohaiwezekani hiyo kufafanuliwa sawa na akili ya kibinadamu. Kwakulingana na usemi wa Biblia, Yesu alipokuwa atoe roho yakeakalia akimwambia Mungu Baba: Mbona umeniacha? Nanialimwacha nani? Je Mungu alimwacha Mungu?

NANI ALITOLEWA KUWA DHABIHU ?Tatizo jingine tunalokuta ni kwamba 'mtu' katika Yesuhakuadhibiwa wala asingeweza kuadhibiwa kwa mantiki yoyotekwani yeye hakujichagulia kubeba mzigo wa dhambi zawanadamu wote. Hiyo habari mpya kuingia katika mjadalainatuongoza kwenye hali maalum ambayo hatukuizungumziahapo kabla. Mtu analazimika kushangaa juu ya uhusiano wa 'mtu'katika Yesu akiwa na maelekeo ya kutenda dhambi tangu kuzaliwaambayo maelekeo hayo yanapatikana kwa kizazi chote cha Adamuna Hawa. Kwa wingi mtu anaweza kujielekeza kuamini yakwamba katika uwili wa 'Mungu Mwana' na 'mtu' wakiwa ndaniya kiwiliwili kimoja 'Mungu Mwana' peke yake ndiye asiyekuwana dhambi. Lakini ikoje hali ya 'mtu' aliyekuwepo pamoja naye?Je, yeye naye alizaliwa kutokana na vijine (genes) vya Mungu nasifa zake? Kama ndiyo, basi yeye analazimika kutenda kamaMungu katika Yesu na udhuru wowote hautakubalika kamaakilegea au akiwa ajizi asitende kama Mungu eti kwa sababualikuwa binadamu. Kama hakuwa na sifa yoyote ya Mungu, yaaniyule 'mtu' aliyekuwa ndani ya Yesu hakuwa na sifa yoyote yaMungu, basi hatuna budi kukiri ya kwamba yeye alikuwabinadamu wa kawaida tu, au labda binadamu nusu. Hata hivyo'mtu' huyo akiungamana na Yesu atalazimika kuwabinadamu wa kutosha kurithi tabia ya kutenda dhambi. Kamahapana, kwa nini hapana?

45

Dhambi na Kafara

Page 52: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Ni wazi ya kwamba haifai kusema kuwa yeye akiwa 'mtu' tofautina mwenzake Mungu, atakuwa amefanya dhambi kwakujitegemea akimtupia lawama yote huyo 'mtu' ndani yake.Mfululizo huo wa matukio hautakamilika pasipo kumwona Yesu'Mwana wa Mungu' akitoa roho siyo sana bila ubinafsi, wala siyokwa ajili ya wanadamu wote, bali shabaha yake kubwa penginendiyo nduguye mama mmoja, yule 'mtu' ndani yake.Hiyo yote ni vigumu kufahamu kama si haiwezekani kabisa.Lakini nadharia yetu haizushi matatizo ya aina hiyo. Kwani huyoalikuwa Yesu binadamu asiyekosa, pasipo kuwa na uwili ndaniyake, aliyepaza sauti kudhihirisha mshangao na udhia.

MASHAKA YA YESUNingeeleza tena ya kwamba simkatai Yesu bali ninamheshimusana akiwa Mtume wa Mungu aliyetoa dhabihu maalum.Namwamini Yesu kuwa mja mtakatifu aliyepatwa na jaribiokubwa. Lakini masimulizi ya tukio la Msalaba yanapoanzakufafanuka na yanapoishia, hapo tunakuwa hatuna njia yoyoteisipokuwa kuamini ya kwamba Yesu hakujitolea kwa furaha iliafe msalabani. Usiku wa kuamkia siku ambayo maadui zakewalijaribu kumwua msalabani twamkuta akiomba usiku kuchapamwe na wanafunzi wake, kwani ukweli wake ulikuwa hatarini.Imesemwa katika Agano la Kale ya kwamba yule mwongoanayemzushia Mungu maneno Asiyomwambia yeye, mwongohuyo atatundikwa mtini na kufa hapo kifo cha laana.

46

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalosikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine,nabii yule atakufa. (Kumbukumbu la Torati 18:20).

Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, naweukamtundika juu ya mti; mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti;lazima utamzika siku hiyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa naMungu. (Kumbukumbu la Torati 21:22-23).

Page 53: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Yesu alijua kwamba kama akifa Msalabani, Mayahudiwatafurahia kwa shangwe sana kifo chake na kudai yu mlaghaiambaye uwongo wake mwishowe umethibitika pasipo shakayoyote kulingana na hukumu ya Maandiko Matakatifu. Hiyondiyo sababu ya kwamba yeye alikuwa na kiherehere ya kuwakikombe hicho kichungu kimwepuke; si kwa sababu ya woga,bali kwa kuhofia isije watu wakapotoka na wakashindwakutambua ukweli wake akifa msalabani. Usiku kucha aliombakwa huzuni pasipo kujiweza hata kwamba kusoma jinsialivyoudhika na kusumbuka kunahuzunisha sana mno. Lakini kisahiki cha kweli kinapokurubia mwisho wake, upeo wa kuudhikakwa maono yake, majonzi yake na ushinde wake, vinaelezekakikamilifu katika kilio chake cha mwisho: Eloi, Eloi, lamasabakthani? yaani Mungu wangu, Mungu wangu, mbonaumeniacha? (Mathayo 27:46).Mtu anapaswa kuzingatia ya kwamba haukuwa udhia tuuliodhihirishwa katika kilio hicho bali huo ulichanganyikana namshangao uliopakana na hofu kubwa. Baada ya yeye kuzinduliwana kupata fahamu kwa kusaidiwa na baadhi ya wanafunzi wakehalisi waliojitolea kwake ambao walipaka marahamu juu yamajeraha yake ambayo marahamu hiyo walikuwa wameitayarishamapema kabla ya tukio la msalaba ambamo mlikuwa na dawa zakutuliza maumivu na kuponya jeraha, hakuna budi atakuwaameshangaa sana akifurahi na imani yake katika Mungu MpenziMkweli ikarejea na kuimarika upya kwa namna ambavyo mtuhakuwahi kushuhudia wingi wake na wasaa wake.Habari hii ya kwamba marahamu ilikuwa imetayarishwa mapemandiyo uhakikisho madhubuti wa kuthibitisha ya kwambawanafunzi wa Yesu walitazamia sana ya kuwa Yesu ataondolewamsalabani akiwa hai akihitaji sana kutibiwa.Kutokana na maelezo ya hapo juu, inabainika ya kwamba itikadiya Dhambi ya Asili na kusulubiwa inao msingi juu ya dhana nafikara ya kitamaa waliyozusha baadaye wataalamu wa dini yaKikristo. Inawezekana sana ya kwamba mawazo hayo yalizalika

47

Dhambi na Kafara

Page 54: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kutokana na visa vya kubuniwa vya kabla ya ujaji wa Ukristo,ambavyo visa hivyo vikawashawishi wataalamu hao Wakristokuona kwamba hivyo vinafanana-fanana na hali alizopata Yesubasi wakabuni itikadi hiyo. Kwa vyovyote, hiyo iwe siri amajambo linalojipinga lenyewe, tulionavyo, lakini hamna ushuhudawowote uwao wa kuhakikisha ya kwamba falsafa ya Dhambi naKafara inalitegemea lolote lililotamkwa na Yesu ama likatendwaau likafundishwa naye. Yeye asingeweza kuhubiri kilicho dhidiya akili ya mtu na kinachopingana na fahamu ya binadamu.

JE, MUNGU BABA NAYE ALISUMBUKA?Tukifikiria asili ya 'Mwana', hatuwezi kuamini kwamba yeyealitupwa motoni, kwani hiyo ingepingana kiundani naye yeyemwenyewe. Tukirejea kwenye imani ya msingi ya Kikristotunaona ya kwamba Mungu na 'Mwana' ni wawili lakini wenyetabia ya asili ile ile moja. Haiwezekani katu mmojawapo apitiehali fulani pasipo wa pili kushirikiana naye katika hali hiyo.Twawezaje kuamini ya kwamba nafsi moja ya Mungu, yaani,'Mwana' alisumbuliwa ilhali Mungu Baba akabaki pasipokuudhika? Kama yeye hakuudhika, basi hiyo itamaanisha kuvunjaUmoja wa Mungu. 'Watatu katika Mmoja' inazidi kutokufahamikakwani hali ilizopata kila nafsi mojawapo ya utatu ni tofauti kabisana mbali mbali hata kwamba inaonekana haiwezekani Nafsi mojaya Mungu iungue katika moto wa Jahanamu ilhali Nafsi zinginembili zibaki nje zisiguswe katu na moto. Hakuna hiari kwaWakristo wa leo isipokuwa watengane na imani katika Umojawa Mungu na waamini miungu watatu, kama wanavyoaminiMapagani wa kabla ya Ukristo kama vile Warumi na Wagiriki,ama wabaki waaminifu na kuamini Mungu ni Mmoja hivi kwambahali mbili za Mungu haziwezi kupinzana zenyewe kwa zenyewe.Mtoto anaposumbuka, mama hawezi kutulia na kukaa kimya.Lazima yeye naye atasumbuka, bali pengine zaidi kuliko mtotomwenyewe. Mungu Baba alikuwaje wakati yeye alipomsumbua

48

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 55: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

'Mwanaye' katika Jahanamu kwa siku tatu? Na nini ilimsibuMungu Mwana? Je aligawanyika katika wawili wenye hali naasili tofauti? Mmoja akiungua katika Jahanamu na mwingineakiwa nje kabisa asisumbuke asilani. Na kama Mungu Babaalikuwa anasumbuka, basi kulikuwa na haja gani ya kumwumba'Mwana'? Maana Mungu Baba mwenyewe angeweza kusumbuka.Basi hili ni suala hasa ya kwamba kwa nini Yeye mwenyewehakuchukua jukumu la kusumbuka? Kwa nini akaunda mpangohuo mgumu kwa kutatua tatizo la msamaha?

ADHABU YA MOTONI:Hapa suala la Jahanamu alimotiwa Yesu kulingana na imani yaKikristo linapaswa kuchunguzwa vizuri zaidi. Jahanamu hiyoilikuwa ya aina gani? Je, hiyo ilikuwa ile ile Jahanamu iliyoelezwakatika Agano Jipya kama hivi:

Kabla hatujaendelea mbele yatupasa kutambua ya kwamba AganoJipya linamaanisha nini lisemapo 'adhabu ya moto' ama 'adhabuya Jahanamu'? Je, huo ni moto unaounguza roho ama ni moto wakimwili unaoteketeza mwili na kwa njia hiyo unaitesa roho? JeWakristo wanaamini kwamba tutarejea kwa mwili huo huo ambaowakati wa kufa roho iliuacha ili kuchanganuka katika vumbi namajivu? Au je, kila roho itaumbiwa mwili mpya na mtualiyefufuliwa atapata maisha mapya?Kama huo ni moto wa kimwili na ni adhabu ya kuutesa mwili,basi mtu anaweza kufikiria sana hadi uwezo wake wa kufikiriauishe ya kwamba ilikuwa imetendeka nini kwa Yesu Kristo. Kabla

49

Dhambi na Kafara

Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutokakatika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, nakuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusagameno. (Mathayo 13:41-42).

Page 56: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ya kutupwa Motoni, je, roho yake iliingizwa tena katika mwiliwa 'mtu' ilimokaa muda wote katika maisha yake juu ya ardhi,ama ilitiwa kwa njia fulani ndani ya mwili wa kiroho? Kamaroho yake ilipewa mwili wa kiroho, hapo mwili huo wa kirohousingeliweza kufikiwa na moto wa kimwili wa Jahanamu ilikuumiza, kuuadhibu ama kuuangamiza. Na kama tukikubali yakwamba mwili ule ule wa 'mtu' alimokaa Yesu duniani utaundwaupya kwa ajili ya Yesu ili kwa njia ya mwili huo Yesu apatekuudhika katika Jahanamu, hapo hatuna budi kushuhudia msibamwingine kwa uadilifu wa Mungu. Mtu maskini kwanza alitiwanguvuni kwa maisha mazima na roho ngeni, tena kama malipoya 'ukarimu' wake aliolazimishwa kuonyesha aungue katikaJahanamu pasipo dhambi aliyotenda. Lakini heshima ya kutoafidia hiyo akajichukulia moja kwa moja huyo mgeni aliyekaandani ya huyo mtu. Tena ikoje hali ya roho ya mtu huyomwenyewe? Pengine alikuwa hana roho yake mwenyewe. Kamani hivyo, basi hapo mtu katika Yesu na Mungu katika Yesu ndiyeyule yule mmoja na kwa hiyo dai la kusema kwamba Yesu wakatimwingine akatenda kibinadamu na pengine ki-mungu litakuwani maneno ya kilinge. Kanuni ya pekee inayokubaliwa na akili nikwamba roho moja na mwili mmoja hufanya mtu mmoja. Rohombili na mwili mmoja ni wazo la upuuzi linaloweza kukubaliwana wale tu ambao wanaamini watu kupagawa na pepo na mizukana kadhalika.

KUJITOA NA KUFURAHIA KIROHO:Kama inakubalika zaidi kwa wataalamu wa dini ya Kikristo yakwamba roho pekee ya Yesu iliingia Jahanamu na Jahanamu hiyonayo ilikuwa ya kiroho, basi hapaonekani sababu yoyote yakuikatalia shauri hiyo kuwa upuuzi. Lakini jahanamu ya kirohohumaanisha kuudhika dhamiri na kuyajutia makosa. Na hayo yotemawili hayalingani na hali ya Yesu. Unapokubali kutozwa kwa

50

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 57: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ajili ya uhalifu wa mwingine, wewe mwenyewe ukiwa huna hatia,hapo dhamiri yako haiudhiki bali matokeo ni dhidi yake. Rohoya mtu huyo inapaswa kufurahia kujitoa kwake kwa fikara yawema na uungwana, jambo ambalo ni kama Pepo ya roho kulikokuwa kama Jahanamu.Sasa twageukia suala la mwili alimokaa Yesu na maana ya kifokulingana na mwili huo na kufufuliwa pia. Tujuavyo sana nikwamba mwili wa Yesu unalazimika kuwa sehemu isiyowezakutengwa na Yesu akiwa Mwana wa Mungu. La sivyo,hapatakuwa na nafasi ya uungu wake na ubinadamu wakekuunganika pamoja na kutenda matendo tofauti waziwazi katikahali mbalimbali. Wakati fulani tunamwona mtu akishika hatamuya mambo sharti akiwa na roho tofauti, na wakati mwinginetwashuhudia Mungu akijitokeza na kutawala fikara na maono yamtu. Twakazania hapo ya kwamba hayo yanaweza kutendekahapo tu ambapo dhati moja akiingiwa na nafsi mbili mbalimbali.

MAANA YA KIFO KULINGANA NA YESU:Baada ya kwisha kuzingatia vizuri hiari mbalimbali kuhusumatendo aliyotenda 'Mungu' na 'Mtu' ndani ya Yesu, twajaribusasa kuelewa matumizi ya neno 'kifo' na maana yake kamilifukumhusu yeye.Kama yeye alikufa kwa siku tatu, usiku na mchana, basi kifokitamaanisha roho kutengwa na mwili na kuuaga. Na maana yakendiyo kwamba roho haina budi kuuaga mwili na kukata kabisauhusiano wake na mwili hata kwamba mwili usio na roho unabakinyuma. Mpaka hapo, sawa. Yesu mwishowe akapata farajakutokana na kifungo chake katika mwili wa udongo wa mtu.Lakini kupata uhuru katika kifungo hicho kusichukuliwe katukuwa ni adhabu. Marejeo ya roho ya kiungu ya 'Mwana' kwenyehali tukufu ya kuwepo hayawezi kuhesabiwa kwa vyo vyote sawa

51

Dhambi na Kafara

Page 58: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

na kifo cha kawaida cha binadamu. Kifo cha mtu kinaogofya sikwa sababu roho inatengana na mwili na kukata uhusiano wakenao kwa kupata ufahamu mpya, bali hofu za kifo ni kwa sababuya mtu kutengwa kwa kudumu na wapenzi wake hapa ardhini nakuacha nyuma mali yake na mambo mengine anayopenda. Maranyingi twaona mtu ambaye hana kitu cha kuishia anapendeleakufa badala ya kuishi maisha matupu.Yesu asingeweza kujuta na kuhuzunika wakati wa kufa, kwanikifo kilimfungulia njia moja tu ya kupata faida siyo hasara. Kwanini kuugua mwili kuhesabiwe kuwa jambo la kuhuzunisha nakusumbua? Tena kama yeye alikufa hasa mara moja, siyokimfano, na kukata roho, wanavyotaka Wakristo kwamba tuamini,hapo kurejea tena katika mwili huo ni hatua isiyo na busara kabisainayonasibishwa kwake. Je, alizaliwa upya aliporejea katika mwilialiouacha pindi alipokufa? Na kama kurejea kwake katika mwilihuo kwamaanisha kwamba alihuika au kufufuka, hapo hata mwilihuo ungekuwa wa kukaa milele. Lakini tunayosoma katika Bibliani kisa kingine tofauti kabisa. Sawa na kisa hicho Yesu alifufuliwakwa kuingia katika mwili huo huo uliokuwa umesulubishwa nahiyo ikaitwa kuhuika. Kama ni hivi, kuuacha kwake mwili maranyingine kutamaanisha nini? Je, hiyo itakuwa ni sawa na mautiya pili?Kama kuuaga mwili mara ya kwanza ndiyo kifo, basi hakunabudi alipouacha mwili mara ya pili atangazwe alikufa kwakudumu. Roho inapouacha mwili mara ya kwanza, mwaita kifo,na roho inaporejea katika mwili huo, mwasema kuhuika baadaya kufa. Lakini mtaisemaje ikiwa roho inauacha mwili huo maranyingine pasipo kuurejea abadan? Je, hiyo itaiwa kifo cha mileleama uhai wa milele kwa kulingana na istilahi ngumu za Kikristo?Haikosi hiyo ndiyo kifo cha milele wala haina maana nyingine.Kujipinga juu ya kujipinga. Ni jambo la kuchosha na kuhuzunishakweli!Kama ifikiriwe kwamba mwili haukuachwa mara ya pili, hapotutakabili hali ya ajabu ambamo Mungu Baba huwepo akiwa nafsi

52

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 59: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

isiyo na mwili, isiyo na mipaka ilhali 'Mwana' hudumu kunaswakatika eneo fupi lenye kukabili mauti.

ADHABU YA KIASI KWA DHAMBI ISIYO YA KIASI :Yaweza kusemwa ya kwamba siyo kila mara maumivu ya dhamirindiyo yanayosababisha kusumbuka roho na moyo kwa walewasioweza kuvumilia makosa yao. Bali huruma nyingi kwa kuonataabu za wengine pia yaweza kumwudhi mtu ambaye hana dhambikabisa ama hana dhambi sana, lakini anayo tabia njema yakusumbuka kwa kuona mateso ya wengine. Hali hiyo nayoitazalisha namna ya jahanamu kimfano. Kina mama wazazihusumbuka kwa ajili ya watoto wao wanaougua. Imeshuhudiwaya kwamba wakati mwingine maisha mazima ya mama hugeukakuwa jahanamu kwa ajili ya mwanaye aliyelemaa kwa kudumu.Kwa nini basi tusikubali sifa hiyo njema kupatikana ndani yaYesu iliyomfanya asumbuke kwa ajili ya wengine? Bila shakatwapaswa kukubali. Lakini kwa nini kwa siku tatu, usiku namchana pekee? Kwa nini si kwa muda wote wa kukaa ardhinibali na hata kabla yake na baadaye pia? Waungwanahawasumbuki kwa muda mfupi sana wa saa ama siku chache.Nyoyo zao hazitulii hadi waone kwamba shida zimetulia amazimeondolewa kabisa. Ile jahanamu tunayozungumzia haimhusutu mzungupule asiye na dhambi, bali hata wanyama wa mwituninao wanashirikiana katika sifa hiyo njema na wanasumbuka kwaajili ya wanyama wenzao.Nikiisha sema maneno machache nitaiacha habari hiyokushughulikia, lakini ninalo jambo moja la muhimunitakaloligusia kidogo. Adhabu aliyohukumiwa Yesu kupatailidumu kwa siku tatu tu, mchana na usiku, ilhali wale wenyedhambi ambao yeye alisumbuka kwa ajili yao walitenda dhambichafu sana tena kwa muda mrefu kabisa na kulingana na Biblia

53

Dhambi na Kafara

Page 60: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

adhabu yao ilikuwa kuungua katika jahanamu milele. Mwadilifugani huyo Mungu ambaye alitaka kuwaadhibu viumbe wakewasiokuwa wana wake na mabinti zake kwa adhabu ya kudumumilele? Lakini alipotakiwa kumwadhibu mwanaye mwenyewekwa ajili ya dhambi alizojitolea kwa hiari yake kuadhibiwa, maraadhabu ikapunguzwa. Ikawa siku tatu tu, usiku na mchana.Adhabu hizo mbili hazilingani, hazifanani hata kidogo. Kamahuo ndio uadilifu, afadhali usiwepo tena. Mungu ataonajemwenendo wa wanadamu aliowaumba kwa mkono wake wakuume wakifanya uadilifu walivyojifunza kutoka kwake Yeyewakitumia vipimo mbalimbali kwa watoto wao wenyewe nawatoto wa watu wengine? Je, Mungu Baba ataangalia mwigo huomwaminifu kwa furaha kuu na hofu kubwa? Hakika ni vigumumno kujibu swali hilo.

KAFARA ILILETA BADILIKO GANI?Kuhusu matokeo ya Yesu Kristo kusulibishwa tumekwishahakikisha ya kwamba imani katika Yesu haikupunguza adhabuya dhambi kwa namna yoyote iliyotolewa na Mungu kwa Adamuna Hawa na wazao wao. Wanawake wote bado wanazaa kwauchungu na wanaume bado wanachuma riziki yao kwa jasho lauso wao. Twaweza kuliangalia jambo hilo kwa jiha nyingine,kwa kulinganisha ulimwengu wa Kikristo na ulimwengu wawasiokuwa Wakristo kuanzia zama za Yesu Kristo. Katika kipindichochote cha historia waumini wa Kikristo hawawezi kuoneshabadiliko lolote maalum kwa wanawake wao kwamba wanazaabila uchungu, wala kwa wanaume wao kwamba wanachuma rizikiyao bila kutokwa jasho. Hawawezi kuonesha tofauti yoyote iwayobaina ya Wakristo na Wasiokuwa Wakristo.

54

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 61: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kuhusu maelekeo ya kutenda dhambi twashuhudia ya kwambahayo hayakufutika kabisa baina ya waumini wa Kristo kwa athariya kafara ya Yesu. Aidha, mtu anashangaa kweli kwa nini imanikatika Mungu imehesabiwa kuwa hafifu kuliko imani katika'Mwanawe'. Hiyo inahusika hasa na zama kabla haijatobolewasiri hii kubwa ya kwamba Mungu anaye Mwana. Naam,walikuwapo watu zamani waliokuwa na imani katika Mungu naUmoja wake. Vilevile watu wengi wasiohesabika walizaliwatangu wakati wa Yesu katika dini mbalimbali na nchi mbalimbalihapa ardhini waliomwamini Mungu na Umoja wake. Mbona imanikatika Mungu haikuathiri dhambi za wanadamu na adhabu zao?Tena kwa nini Mungu Baba hakudhihirisha wema wake nakusumbuka kwa ajili ya wenye dhambi ambao wema huoukaoneshwa na 'Mwana' aliyekuwa na daraja dogo kuliko Baba?Kwa yakini 'Mwana' anaonekana anayo khulka bora zaidi (Munguapishe mbali) kuliko Baba asiye mstaarabu sana. Je, Uunguunakua na bado unaendelea kukua ili kufikia ukamilifu wake,mtu aweza kuuliza?

55

Dhambi na Kafara

Page 62: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

3 KAZI YA ROHO MTAKATIFU

Mpaka sasa tumezungumzia suala la Yesu, anayefanywa kuwaMwana, na suala la Mungu anayedhaniwa kuwa Baba halisi waYesu. Lakini bado kuna nafsi ya tatu, jina lake Roho Mtakatifu,ambaye japo anayo dhati tofauti peke yake lakini ameunganikakikamilifu daima na 'Baba' na 'Mwana' hata kwamba muunganowa hao watatu umezalisha umoja katika utatu. Sasa twageukiakuchunguza ya kwamba je, Roho Mtakatifu anajitambua kuwepokwake mbali na Mungu au Yesu, ama wote watatu wanashirikianakatika kujitambua kuwepo kwao kwa pamoja? Kujitambuakuwepo ama kujijua kuwepo kwa mtu kunamaanisha kuelewakwamba mtu anakuwepo peke yake pasipo kuwa sehemu yamwingine. Utambuzi huo wa mtu kwamba anayo dhati yakebinafsi mbali na dhati za wengine unazalisha 'mimi' na 'yangu' na'ya kwangu', na 'wewe'na 'yako'.Tukichunguza sehemu tatu za Mungu twalazimika kuamuakwamba je, kila mmoja anajitambua kuwepo kwake mbali nakuwepo kwa wengine wawili ama hapana. Kama kila mmoja waohana utambuzi wa kuwapo kwake mbali na utambuzi wa wenginekuhusu kuwapo kwao, hapo kunasibisha kwao dhati mbalimbalihakutafahamika. Kila mmojawapo hata akimkurubia mwenzakesana namna gani hana budi kujijua kwamba anakuwapo peke yakena anayo dhati yake mbali na wengine.Itikadi rasmi ya makanisa mengi iko wazi sana na imefafanuliwavizuri nayo ni kwamba kila nafsi katika nafsi tatu za Mungu nidhati halisi tofauti na nyingine mbili. Kwahiyo hapa hatuna 'Tatukatika moja' bali 'Watatu katika Mmoja'. Uchungu aliopata Yesu

56

Page 63: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

alipoyakabili mauti na matokeo yake ya hatari haikosi RohoMtakatifu pia alishirikiana katika hayo yote kwa usawa pamwena Yesu. Na vilevile hakuna budi yeye naye akashirikiana na Yesukatika kujitolea. Aidha lazima akasumbuka pia katika jahanamupamoja na Yesu na Mungu Baba. Kama hapana, hapo mtu hanabudi kuamua ya kwamba hao watatu siyo kwamba ni watatu mbalimbali tu bali hata maono yao, fikara zao na kadhalika, pia nimbalimbali.Tukijaribu kupata mwanga zaidi juu ya utatu, twapaswa kutambuauhakika wa watatu kuunganika pamoja ama kuwapo kwa haowatatu kama mmoja tu kwa sababu ya hao kufungamana pamojakwa kudumu milele. Mpaka sasa tumeshidwa kufahamu jinsi yakufungamana kwao katika maono na mawazo.Kilichobaki ni kufahamu ya kwamba waliunganika pamoja katikamwili tu mmoja. Hiyo yatukumbusha habari ya yule joka kuualiyetajwa katika hadithi za kubuniwa za Kigiriki, ambaye alikuwana vichwa vingi ambavyo vikikatwa vinaota tena. Ni sawa mtuhawezi kutambua hasa alivyo Mungu na jinsi sifa zakezinavyofanya kazi humo ndani, lakini ni rahisi sana kuamini katikadhati pamoja pasipo sehemu zake mbalimbali kama vile kichwa,moyo na figo na kadhalika. Lakini habari ya mawazo na maonomaalum ya mmoja inahitilafiana kulingana na hali iliyoelezwajuu ya dhati moja. Hiyo inatoa picha ya Mungu isiyowezakuaminiwa na kufahamika kwa binadamu ambao wengi waowaliishi muda mrefu wakiamini itikadi hiyo ya Kikristo bila yakuipinga na wakafumba macho yao wasiangalie yanayoipingaakili ya mtu ambayo iliumbwa na Mungu Mwenyewe.

USHIRIKIANO WA ROHO MTAKATIFU KATIKAUUMBAJI:Hatuoni kazi yoyote iliyoshughulikiwa na Roho mtakatifu au YesuKristo katika mpango wa uumbaji:

57

Kazi ya Roho Mtakatifu

Page 64: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. (Mwanzo 1:1)

Hakuna shaka kwamba katika Agano la Kale Mungu Baba ndiyeametajwa aliyeumba mbingu na nchi pasipo hata kudokeza habariya Kristo ama Roho mtakatifu. Zama zote za kabla ya Ukristo,miongoni mwa Mayahudi ,walioliamini Agano la Kale na bilashaka waliwahi kusikia mstari huo hapo juu mara malaki kwamalaki, hakuna hata mmoja aliyeweza kulisoma jina la Kristo aula Roho Mtakatifu katika kisa cha uumbaji wa ulimwengu. KatikaInjili ya Yohana Mtakatifu 'Neno' limetumika kwa ajili ya Yesu.Ni la ajabu ya kwamba habari ya muhimu kabisa imezungumzwana Injili moja peke yake; tena na yule ambaye hata hakuwamwanafunzi wa Yesu.1 Hata mtu akikubali usemi wake kuwaneno la Mungu, hata hivyo huo utamaanisha kuwa Takwa laMungu; hilo ni wazo linalopatikana katika dini nyingine vile vilekatika habari ya uumbaji.Ni mshangao mkubwa ya kwamba siri ya zamani sana ya Kristona Roho Mtakatifu kushirikiana pamoja katika uumbaji ikabakikuwa siri hata kwa Yesu mwenyewe. Hatusomi hata mara mojaya kwamba Yesu Kristo alidai kuwa Neno. Hivyo, Yesu walaRoho Mtakatifu hawakuwa na sehemu yoyote ya kazi ya kufanyakatika uumbaji. Tena twaambiwa ya kwamba alikuwa ni MunguBaba peke yake aliyemfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi kwamikono yake mwenyewe. Sijasoma kabisa katika maandikoyoyote ya Kikristo ya kwamba mikono hiyo miwili ilikuwa yaYesu na Roho Mtakatifu. Basi Mungu aliumba vitu vyote pasipokusaidiwa hata kidogo ama kushirikiana na Yesu ama RohoMtakatifu. Je, hao walikaa tu na kuangalia wakikubaliana kwajumla na aliyokuwa anafanya Mungu ama walishirikiana nayehasa? Kama wataalamu wa Kikristo wanapendelea kukubali ya

______________________________________________

1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Nenoalikuwa Mungu. (Yohana 1:1).

58

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 65: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kwamba hao wawili nao walishirikiana katika uumbaji, basiharaka swali litazuka ya kwamba je, kila mmoja kati yao alikuwana uwezo wa kuumba bila kusaidiwa na wengine, ama walikuwana uwezo huo wakiwa pamoja?Isitoshe, kama wote watatu walihitajika kutoa mchango wao kwakuumba, hapo je, wote wakatoa mchango kwa usawa ama mmojawao akalazimika kutoa sehemu kubwa zaidi katika mpango wauumbaji? Je, kila mmoja katika hao watatu alikuwa na namna nakiasi cha uwezo tofauti ama uwezo wa kila mmoja ulikuwa sawana uwezo wa mwenzake?Mtu hata akikiri hii au ile analazimika kukubali ya kwamba kilammoja katika Utatu hana uwezo wa kuumba chochote peke yake.Kama hoja hiyo itumiwe kwa kazi nyinginezo za Mungu, swalihilo hilo litawasumbua wataalamu wa Kikristo. Na mwishoweWakristo watalazimika kukiri ya kwamba wao hawaamini dhatimoja ya Mungu mwenye jiha na sura tatu za nguvu kuu na utukufu.Bali wanaamini sehemu tatu za Uungu zilizo mikato mitatu yamwili wa Mungu. Hapo swala la sehemu zote kuwa sawa ama sisawa halitakuwa na uzito zaidi.Kwa mfano, chukueni sifa ya uadilifu na msamaha. 'Mwana'anaonekana kuwa na huruma zaidi ilhali Mungu Baba anaonekanaMwadilifu kidogo kuliko Roho Mtakatifu ambaye hakushirikianana Mungu Baba katika dhuluma yake.Uwezekano wa pili tuliozungumzia ulikuwa kwamba pengineYesu na roho Mtakatifu walikaa tu pasipo kushirikiana kwakitendo katika shughuli za uumbaji na kuendesha kanuni zaulimwengu. Kama ni hivi, hapo yatazuka maswali mengi mengine.Kwanza kabisa, hao washiriki wawili wa Mungu walipewa kazigani katika kutekeleza wajibu wao wa Kiungu? Kama hao ndiowashiriki wa kukaa tu kimya kama washiriki katika biasharawanaokaa tu pasipo kushughulikia kazi kwa kitendo, hapowamekwisha punguziwa hadhi yao na kupewa daraja la piliambako wanakuwapo pamoja na Mungu lakini bila yakushirikiana naye hususan katika madaraka yake. Wazo hili la

59

Kazi ya Roho Mtakatifu

Page 66: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Mungu kuwa na nyongeza mbili zisizo na kazi ni jambo lakutatanisha kusema kwa uchache. Nashangaa, wazo hilo linawezakuwatuliza kina nani. Hiyo haiwezi kukubaliwa kiakili walahaiafikiani na imani ya Kikristo ya 'Watatu katika Mmoja' na'Mmoja katika Watatu'. Watatu hawawezi kuwa na Umoja walahaiwezekani kuwaza umoja huo pasipo hao watatu kuunganikakikamilifu katika nia, madaraka na mengine yote yanayowezakudhaniwa katika maisha ya mmoja.Ama Roho Mtakatifu akiwa dhati peke yake, asipofungamanakikamilifu kwa kudumu na wengine wawili akitengana na nafsiyake, hakuna tumaini kujitokeza kwa Mungu mwenye vichwavingi akiwa na fikara moja nia moja na mwili mmoja.

SIRI AMA HITILAFU:Inakubaliwa ya kwamba mtu aliamini jambo asilolifahamukikamilifu kwa sababu kuna ushuhuda usioweza kukataliwakulihakikisha hilo. Kwa mfano, wapo watu wengi wasioelewanamna zinavyofanya kazi radio na televisheni kwa kutuletea sautina picha kutoka mbali sana, lakini hata yule mtu asiyejua kabisakusoma na kuandika anaamini katika uhakika wa kuwepo kwaradio na televisheni. Kadhalika wengi kati yetu hawajui namnakompyuta zinavyofanya kazi, hata hivyo hakuna atakayekataakupatikana kwa kompyuta kwa sababu hiyo tu. Mambo hayoyanaweza kuhesabiwa katika fungu la 'siri', lakini hakuna swalala kuyakatalia kuwapo kwa hayo ama kuwadhihaki wanaoyaaminihayo sharti yanahakikishwa na ushahidi usioweza kukatalika.Pia tunakubali kulegeza kamba na kuamini siri nyingizinazohusikana na itikadi za kidini. Watu wengi sana wanaaminiitikadi kama hizo bila kuweza kufahamu ama kuweza kuzieleza.Wanaonekana wamerithi imani hizo kizazi hata kizazi nakuzichukua kuwa ni sawa hasa. Lakini mambo yanayojipinga na

60

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 67: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kuhitilafiana yanapojiingiza katika itikadi za kidini, hapo udhuruwowote haukubaliwi kuziamini eti kwa sababu siri za kushangazazinakubaliwa basi na hayo yanayojipinga na kuhitilafiana pia nayoyakubaliwe. Hapo ndipo swala linaleta matatizo. Nawezakuliamini nisilolifahamu, lakini siwezi kulikubali linalojipingalenyewe wala sitoamini kwamba mtu yeyote mwenye fahamuaweza kuliamini. Kwa mfano, sijui namna inavyotengenezwa saa.Mpaka hapo ni sawa. Lakini sina haki ya kuamini papo hapokwamba saa ni mbwa anayelia na kupiga mateke. Maana hiyohaitakuwa fumbo bali ni jambo linalojipinga lenyewe.Pindi unapokuwa upingamizi baina ya sifa mbili au zaidi zaMungu, ama maneno ya Mungu na matendo ya Munguyanapopinzana, hapo mipaka ya siri huwa imekwisha rukwa tayarisana na mtu anaondoka katika eneo la siri akaingia katikaulimwengu wa mawazo yasiyo na msingi. Ikithibitika hivyo, hapowaaminio katika yanayojipinga wanapaswa kurekebisha itikadizao na hatimaye kunyoosha imani yao. Lakini ni bahati mbayaya kwamba katika maongezi yetu twawakuta mapadrekushikamana na maoni ya kwamba hamna upingamizi katikakumwamini Yesu kuwa Mingu na binadamu wakati ule ulemmoja. Pia hawaoni hitilafu yoyote katika hili ya kwamba mtummoja anaweza kuwa watu watatu pasipo kutokea tofauti yoyotekatika mwenendo wao. Wanakazania ya kwamba ni fumbo tuwala hamna hitilafu katika kumwamini Mungu mmoja na papohapo kuamini Mungu mwenye jiha tatu aliyefanyika na Mungu,Roho Mtakatifu na 'Mwana' wanafumba macho yao wasionehitilafu katika dai lao ya kwamba Mungu anakuwa dhati moja tuingawaje ni hakika ya kwamba Mungu Baba ni tofauti kabisa naYesu,-'Mwana' na Roho Mtakatifu. Tunapowaashiria katikamshangao wetu ya kwamba twazungumzia watatu wala siyo jiha,hali na sifa za mmoja, na kwamba Mungu akiwa 'Mmoja katikaWatatu' na 'Watatu katika Mmoja' siyo fumbo bali ni hitilafu,wanatikisa kichwa kutuhurumia na kutuambia kwa upole tuingietu katika hitilafu zinazoonekana katika majadiliano yetu.

Kazi ya Roho Mtakatifu

61

Page 68: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Wanatutaka tuamini kwanza lisiloaminika na kisha kuanzakuendelea mbele kutoka hapo kuzoea kuyaamini yanayopinzana,ama yaliyo mafumbo kama wapendavyo kuyaita. Hivyo, asiyeMkristo hawezikutambua hitilafu za itikadi za Kikristo, na ili kufahamu asilowezakuliamini yeye analazimika kuamini bila kulielewa. Huo ndiyoulimwengu wa mawazo yasiyo na msingi tunamosihiwa kuingiasisi tusio Wakristo. Lakini zulia hilo la ki-uchawi lirukalolinakataa kuruka ikiwa analipanda asiye mwaminio.

62

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 69: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

4 KUSULUBIWA

Kabla sijaeleza matukio kuhusu Yesu na kusulibiwa kwake jinsiyalivyoelezwa ndani ya Biblia, ningeonelea kufafanua kwa kifupitunavyoelewa sisi Waislamu Waahmadiyya yale yaliyotendekawakati Yesu alipotundikwa msalabani na baadaye pia. Nitaigusiatu kidogo habari hii hapa kwa kifupi, maelezo zaidi yatafuatabaadaye.Tunaamini ya kwamba kumwamba Yesu msalabani kulikwa nijaribio la kumwua yeye jinsi ya kujaribu kumwua mtu yeyotemwingine. Kumwamba msalabani ilikuwa ni njia tu ya kutakakumwua. Lakini jaribio hilo la kumwua msalabani lilishindwa.Tusemapo hayo, twamaanisha kabisa jinsi tutakavyosema kuhusujaribio la kumwua mtu yeyote mwingine. Kama mtu fulanianafanyiwa njama ili akauawe, lakini jaribio hilo linashindwa,huwezi kusema kwamba aliyefanyiwa njama amekwisha uawatayari. Kwa mfano, kama mtu fulani ameshambuliwa kwa upangalakini jaribio hilo likashindwa, hapo hutaweza kusema kwambamtu huyo ameuawa na upanga. Basi sisi Waislam Waahmadiyyatunaamini ya kwamba Yesu alifanyiwa njama ili auawe, msalabaukawa njia tu ya kujaribu kumwua. Baada ya saa chache za taabukubwa sana juu ya msalaba, kabla hajafa, akaondolewa kutokamsalabani katika hali ya kuzimia sana ambako katika hali hiyoyeye akapona na kupata fahamu tena. Kwa kuwa serikali yoyotehaiwezi kumpa ulinzi mtu aliyehukumiwa kuuawa lakini akaponakwa njia hii au ile, na ndivyo ilivyokuwa pia katika sheria yaKirumi, kwahiyo Yesu asingeweza kuachiliwa baada ya kupona

63

Page 70: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

msalabani. Basi hiyo ilikuwa ni sababu ya kutosha sana kwa Yesukuukimbia utawala wa Kirumi na kuikimbilia nchi ya usalamana uhuru. Lakini yeye pia alitakiwa kutimiza wajibu wake fulanina kutimiza utabiri mmoja. Kulikuwa na kondoo wa nyumba yaIsraeli waliopotea, ambao baada ya kuvamiwa na Wababiloni naWarumi wakatoka nyumbani mwao na kutawanyika katika nchinyingi za mashariki. Hao walikuwa wanamngojea yeye. Na hiyoilikuwa sababu nyingine madhubuti kwa Yesu kuihama Uyahudina kuzikimbilia nchi nyingine ambako walikaa Wayahudi kwakarne nyingi. Kwa wakati huu kiasi hicho kinatosha kuelezwa.Ningependa kuwabainishia wale wanaotudaia uhakikisho wa Yesukufa ajali baada ya kupona juu ya msalaba, hao wanatusukumiamzigo wao pasipo sababu yoyote. Zipo kanuni za ulimwenguzijulikanazo kwa watu na zinaeleweka kikawaida. Tunajua yakwamba umri wa mtu juu ya ardhi hauzidi miaka mia na hamsinihivi; kwa vyovyote hauwi miaka elfu au zaidi. Ndivyotunavyoshuhudia kwa jumla kuhusu muda wa mtu kuishi juu yauso wa ardhi. Kama kuna mtu anayedhania kuwa kinyume chakanuni hiyo kimetendeka, hapo itakuwa wajibu wake kuhakikishatofauti hiyo iliyotendeka, wala katu si faradhi ya mwenzakeanayeamini katika kanuni ya kawaida ilivyo ahakikishe yakwamba haikutendeka kinyume chake. Hoja hiyo inapaswakutumiwa kuhusu habari ya uhai na mauti ya Yesu Kristo. Walewanaoamini ya kwamba yeye hakufa hawana budi kuletauhakikisho wa madai yao. Lakini wanaodai ya kwamba yeyelazima amekwisha kufa wanafuata tu kanuni za kawaida zaulimwengu, wala haina maana kuwadaia uhakikisho wa habarihiyo. La sivyo, mtu yeyote anaweza kudai ya kwamba babu wababu wa babu.... yake hajafa bado, na kama mtu anakataa habarihiyo alete hoja ya kuhakikisha kwamba mzee huyo kweli amekufa.Watu watamfikiriaje huyo mtu? Maana mtu anawezaje kuletauhakikisho ya kwamba mzee wa zamani sana aliyeishi miakamamia amekwisha kufa. Uhakikisho wenyewe ni kanuni yenyeweya kawaida ambayo inahusikana na kila mtu. Basi kama mtu fulani

64

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 71: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

anadai kinyume chake, mtu huyo analazimika kuthibitisha madaiyake hayo. Hilo ni jibu la kwanza, lakini nitajaribu kubainishahabari hiyo kwa jiha nyingine.Pasipo kujali uhusiano wake na Mungu, je, ilikuwa kinyumekabisa Yesu Kristo kufa? Wakristo wenyewe wanakubali yakwamba alikufa. Kama kufa ilikuwa kinyume cha tabia yake,hapo asingelikufa hata kidogo. Hata hivyo sote twakiri kwambakwa akali alikufa mara moja. Kilichobaki ni kuchunguza alikufalini. Je, alikufa msalabani ama baadaye wakati mwingine?

ISHARA YA YONA:Twaweza kuhakikisha kutoka katika Biblia ya kwamba Munguhakumwacha na akamlinda asife kifo cha laana juu ya msalaba.Habari hiyo inaweza kuchunguzwa kwa kutalii mambo kadhayaliyotukia kabla ya tukio la msalaba, na yaliyotukia alipokuwajuu ya msalaba na yale yaliyotukia baada ya tukio la msalaba,jinsi yalivyoelezwa katika Agano Jipya.Muda mrefu kabla ya tukio la msalaba, Yesu aliahidi ya kwambawatu hawataonyeshwa ishara yo yote isipokuwa ishara ya NabiiYona. Hebu someni:

65

Kusulubiwa

Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakisema,Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia: Kizazikibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila isharaya Nabii Yona. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchanana usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo mwana wa Adamuatakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. Watuwa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazihiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubukwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.(Mathayo 12: 38-41).

Page 72: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kwahiyo kabla hatujahakikisha yaliyotendeka kwa Yesutwalazimika kuelewa yaliyotendeka kwa Yona, kwani Yesu alidaiya kwamba mwujiza huo huo utarudiwa. Ilikuwa nini Ishara yaYona? Je, alikufa tumboni mwa nyangumi na kisha akafufukabaadaye? Wakristo, Wayahudi na Waislamu wote kwa neno zimawanakubali ya kwamba Yona hakufa tumboni mwanyangumi.Yeye alikaa katika hali ya hatari baina ya kufa nakupona na akaokolewa kimwujiza katika hali hiyo, ilhali mtuyeyote mwingine angekufa katika hali kama hiyo. Hata hivyobaadhi ya kanuni zisizoelezeka kwa urahisi zilifanya kazi chiniya amri ya Mungu ili kumwokoa katika mauti. Kumbukenihatuzungumzii habari hii ya kwamba jambo hilo linawezekanaama hapana. Tunaloashiria ni kwamba Yesu aliposema yakwamba yatatendeka kwake mfano wa yale yaliyotendeka kwaYona, alimaanisha ya kwamba yaliyotendeka kwa Yonayatatendeka kwake yeye pia. Katika ulimwengu mzima waWayahudi wakiwa katika Uyahudi ama popote walipo Wayahudiduniani walipokaa baada ya kutawanyika, hamna hata Myahudimmoja aliyefahamu maana tofauti ya usemi huo wa Yesu. Wotehao waliamini ya kwamba Yona kimwujiza ama kwa njia nyinginealipona katika hatari kwa siku tatu mchana na usiku katika tumbola nyangumi wala hakufia humo hata kwa dakika moja. Naam,sisi tunahitilafiana kidogo kuhusu habari hiyo. Kisa cha Yonakilivyoelezwa katika Kurani hakielezi popote ule muda wa sikutatu mchana na usiku aliokaa Yona katika tumbo la nyangumi.Lakini twaiachia habari hiyo hapa, bali twarejea tuliyokuwatwazungumzia na twajaribu kufafanua mambo yanayofananakatika visa vya Yona na Yesu jinsi alivyotabiri Yesu. Yafananayoni kupona katika hatari kubwa kabisa kwa muda wa siku tatumchana na usiku, wala siyo kufufuka baada ya kwisha kufa. Yesuanadai ya kwamba yatatendeka kwake hayo hayo.

66

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 73: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

AHADI YA YESU KWA NYUMBA YA ISRAELI:Ushuhuda muhimu wa pili ni kwamba Yesu aliwaambia watuwake ya kwamba kondoo wa nyumba ya Israeli wanaoishi katikaUyahudi na pembeni mwake siyo tu kondoo ambao yeye alitumwakwao, bali kuna kondoo wengine pia ambao si wa zizi hili ambaoninapaswa kuwaleta pia:

Sasa, tujuavyo ni kwamba katika muda ulio baina ya yeye kutoaahadi hiyo na kutundikwa msalabani, yeye hakuondoka Uyahudikuelekea mahali pengine. Hapa lazuka swali: Kama Yesu alipaambinguni, je, na kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea naowalipaa mbinguni mapema zaidi? Wakristo wanaamini yakwamba baada ya Yesu kuteremshwa kutoka msalabani akiwamfu akafufuka baada ya siku tatu hivi na kisha akaonekana akipaakatika mawingu na kupotea katika sehemu za ndani za mbingunina kufikia Kiti cha Enzi cha Baba yake na kuketi upande wakewa kuume daima. Kama hiyo ndiyo sawa, basi tunalikubali tatizokubwa kabisa kweli. Tutalazimika kuchagua jambo mojawapokatika mawili: Moja lililoshikwa na Yesu mwenyewe na jinginena wafuasi wake. Na hayo mawili yanapinzana kiasi hiki kwambakila moja linalifutilia mbali jingine. Kama Yesu alikuwa sawa,na twaamini alikuwa sawa, basi kabla hajapaa mbinguni alitakiwakukumbuka ahadi yake na kumwomba Mungu Baba muhula wakukaa zaidi hapa ardhini ili aende kwa nchi zile ambako makabilamengi ya Israeli yalikuwa yamehamia na kukaa huko. Yeyeasingalipaa mbinguni pasipo kuvunja ahadi yake na uaminifuwake, akitia dosari na kujiharibia picha yake ya kuwa mungumkamilifu, mtu mkamilifu. Na kama, kinyume chake tukikubaliwataalamu wa Kikristo kuwa sawa, na inakubaliwa ya kwambaYesu kwa hakika alisahau wajibu wake kuhusu nyumba ya Israeli

67

Kusulubiwa

Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasakuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja namchungaji mmoja. (Yohana 10:16)

Page 74: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

na akaenda mbinguni moja kwa moja, hapo basi tutakubali shingoupande kwamba watalaamu wa Kikristo wako sawa, lakini olewenu, Ukristo unathibitika kuwa wa uwongo.Kwani, kama Yesu akithibitika kuwa mwongo, basi Ukristohauwezi kuwa wa kweli.Sisi twakubali ya kwamba Yesu alikuwa Nabii mkweli wa Munguwala asingeweza kufanya ahadi ya uwongo. Alichomaanisha kwakauli yake ya kondoo waliopotea ni makabila kumi ya Israelambayo mapema yaliihama Uyahudi na kutawanyika huko katikanchi za mashariki. Basi ahadi yake ilikuwa kwamba yeyehatauawa msalabani bali atajaaliwa umri mrefu ili kuufuatiawajibu wake na kwamba yeye hakuwa nabii kwa makabila mawilitu yaliyoishi pembeni mwake, bali kwa ajili ya Waisraeli wotepopote walipo. Shuhuda mbili za hapo juu zikiwa pamojazinaashiria moja kwa moja nini kilitakiwa kutendeka kwa Yesubaada ya tukio la Msalaba.

MAMBO YAHUSUYO TUKIO LA MSALABA:Jambo jingine linalolingana na habari hiyo ni ule wakati maalumna tarehe iliyowekwa na Pilato kwa kuwambwa Msalabani. Hatakabla hajaweka tarehe na wakati twasoma habari za baadhi yamambo ambayo mtu asiwe na shaka ya kwamba yaliathiri uamuziwa mwisho. Kwanza kabisa twajua kutokana na Agano Jipya yakwamba mkewe Pilato hakupendezwa asilani na Pilatokumhukumu Yesu kwa sababu ya kuathirika na ndoto aliyoiotausiku wa kuamkia siku ya kusikilizwa kesi ya Yesu.Mama huyo alitishika sana na ndoto hiyo iliyomtia imani yakwamba Yesu hana kosa hata kwamba akaonelea kuingiliakusikilizwa kwa kesi na kumpelekea mumewe ujumbe wa ndotoyake (Mathayo 27:19). Labda ilikuwa ni utetezi huo wa mkeweuliomfanya Pilato ajitenge na kumhukumu Yesu:

68

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 75: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Hiyo inamaanisha ya kwamba yeye alikiri ya kuwa Yesu alikuwahana kosa na kwamba hukumu kali aliyotoa ilikuwa kwa sababuyeye alishurutishwa. Ni wazi kabisa kutokana na Agano Jipya yakwamba jamii ya Kiyahudi iliunganika pamoja dhidi ya Yesuikanuia kabisa kwamba Yesu lazima apate kuadhibiwa. Hivyo,hukumu yoyote kinyume cha matakwa ya Wayahudi ingewezakuchafua amani nchini. Hali hiyo ndiyo ilimbana asiweze kitu naakadhihirisha kulazimika kwake kwa njia ya kitendo chake chakunawa mikono yake.Pilato alifanya jaribio jingine tena ili kumwokoa Yesu. Yeyeakawapa hiari makutano hao wenye hasira kumwokoammojawapo kati ya Yesu au Barabbas, mhalifu mashuhuri. Nahiyo ndiyo dalili kubwa ya kuonesha hali ya moyo wa Pilato katikawakati huo. Ni dhahiri shahiri kwamba yeye hakuwa na wazo lakumhukumu Yesu. Katika hali hiyo ya kisaikolojia yeye aliwekakusulibiwa kwake siku ya Ijumaa saa za jioni. Hiyo inadokezauwazi kwa ya kwamba yeye alifanya kusudi, kwani Sabatohaikuwa mbali kutoka jioni ya Ijumaa, na Pilato akiwa msimamiziwa sheria alitambua habari hii zaidi kuliko mtu yeyote mwingineya kwamba kabla halijatua jua mwili wa Yesu unatakiwakuondolewa kutoka msalabani. Na ndivyo kabisa ilivyotendeka.Kwa kawaida muda wa siku tatu mchana na usiku ulitakiwakumwua mtu kwa kuteseka sana juu ya Msalaba, lakini Yesuakakaa saa chache tu juu ya Msalaba. Mtu hana budi kushangaaya kwamba mtu kama Yesu ambaye maisha magumu yalikuwayamemfanya kuwa mgumu kafa kweli katika muda huo mfupi.Je, huo siyo ufumbuzi wa siri ya tukio la Yona? Kwa kuwa mtualiyehukumiwa kwa hatia alikuwa kwa kawaida anatundikwa

69

Kusulubiwa

Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lolote, bali ghasia inazidi tu, akatwaamaji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sinahatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyiwenyewe. (Mathayo 27:24).

Page 76: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

msalabani kwa siku tatu mchana na usiku, basi hilolinamkumbusha mtu mithali ile ya Yesu kujifananisha na Yonaambayo imekwisha tajwa kabla. Yona pia anafikiriwa kukaakatika tumbo la nyangumi kwa siku tatu, mchana na usiku.Pengine yeye naye akatolewa katika saa tatu kwa mpangowa Mungu badala ya siku tatu. Basi kilichotendeka katika kisacha Yesu ndicho kioo cha kuonesha kilichotendeka kwa Yona.Sasa twageukia yaliyofanyika katika muda aliokaa YesuMsalabani. Hata katika dakika ya mwisho Yesu alikuwa imarakudakuliza: Eloi, Eloi, lama sabachtani? (Mungu wangu, Munguwangu, mbona umeniacha?) Huzuni kubwa iliyoje hiyo, na yenyekuumiza mno iliyoje hali hiyo ya kukata kwake tamaa! Kilio chakehicho chaashiria kwa uwazi kwenye ahadi ya zamani namatumaini ambayo pengine Mungu alikwisha mpa. La sivyo, kiliochake hicho hakina maana asilani. Hicho kinakataa katakata niayake na upendo wake wa kujitwisha kwa hiyari mzigo wa dhambiza watu wengine, na kinakanusha moja kwa moja wazo hili yakwamba yeye alitazamia kufikiwa na saa ya mauti wakati huo.Kwa nini kilio hicho cha maumivu ikiwa yeye mwenyewe alidaikuadhibiwa hivyo? Kwa nini kumlaumu Mungu ama kumwombaaokolewe? Maneno ya Yesu yanapaswa kuzingatiwa kutokanana yaliyofanyika hapo kabla. Yeye alikuwa akimwomba Munguwakati wote kwamba kikombe kichungu kimwepuke.Sisi Waislamu Waahmadiyya twaamini ya kuwa Yesu alivyokuwamwema na mtukufu akamfanya Mungu asikatae maombi yake.Bila shaka alikwisha ambiwa ya kuwa dua yake imepokelewatayari. Siamini katu ya kwamba yeye alitoa roho yake juu yamsalaba. Kwangu mimi hamna hapa hitilafu bali yote yanalinganana kuafikiana. Alihesabiwa kuwa mfu kwa sababu ya maoni yamtazamaji fulani ambaye hakuwa daktari wala hakupata nafasiya kumkagua. Mtazamaji tu mmoja aliyekuwa anamwangaliakutoka mbali akihangaika na kufadhaika isije Bwana wakempendwa akafa, akaona tu kichwa chake kilichochoka sanakikainama na kikaegemea kifuani pake, basi akapaza tu sauti:

70

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 77: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Lo, ametoa roho yake. Lakini tulivyosema mapema, hiki si kitabucha kujadili ukweli wa maelezo ya Biblia na kuchunguza yakwamba maandishi ya Biblia yanaweza kutegemewa ama hapana,au kubishana kuhusu maelezo yoyote yanayonasibishwa kwake.Hapa shabaha yetu ni kukagua tumantiki na busara ya falsafa na itikadi ya Kikristo. Jambo ambalolimethibitika barabara ni kuwa Yesu alizimia au alikufa lakinikwa vyovyote mshangao wake unahakikisha ya kuwa yeyealitazamia kinyume kabisa cha kilichotendeka. Kama ni kifoalichotaka, basi mshangao wake aliodhihirisha hauna maanakabisa. Maelezo yetu sisi Waislamu Waahmadiyya ni kwambaYesu alishangaa kwa sababu yeye aliahidiwa usiku mmoja kablaalipofanya maombi mbele ya Mungu ya kwamba ataokolewakatika kifo cha Msalabani. Lakini Mungu alitimiza ahadi yakekwa mpango wa kumfanya azirai ili walinzi waamini kwambaamekufa na wakamkabidhi Yusufu wa Arimathaya mwili wakeili kuwatolea jamaa zake. Mshangao wa Yesu tunaouona katikakauli yake ya mwisho, hata Pilato alishirikiana katika mshangaohuo. Maana alipopashwa habari ya kifo cha Yesu, Pilato akasemakwa mshangao: 'Amekwisha kufa' (Marko 15:44). Haikosi yeyePilato alitambua kwa sababu ya kazi yake hiyo ya kuwa Gavanawa Uyahudi kwa muda mrefu ya kwamba mtu hawezi kufa harakahivyo juu ya msalaba. Alielewa sana ya kwamba mtu kupata kufajuu ya msalaba katika muda mdogo wa saa chache ni kinyumecha kawaida. Hata hivyo akakubali ombi la kutoa mwili katikahali hiyo kwa siri. Ndiyo sababu yeye analaumiwa siku zotekwamba alifanya mpango wa kumwokoa Yesu. Inasemekana yakwamba kwa sababu ya kushawishiwa na mkewe alipangakumtundika msalabani katika wakati ulio karibu sana na Sabato.Pili aliruhusu kutoa mwili ilhali ripoti ya kifo cha Yesu ilikuwana shaka shaka. Uamuzi huo wa Pilato uliwahangaisha sanaWayahudi waliomlalamikia na kueleza shaka yao kuhusu kifocha Yesu. (Mathayo 27:62-66).

71

Kusulubiwa

Page 78: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Pia tunaona kutokana na Biblia ya kwamba mwili wakeulipoondolewa kutoka Msalabani, miguu yake haikuvunjwa, ilhalimiguu ya wale wevi wawili waliowambwa pamoja naye msalabaniilivunjwa ili kuhakikisha kwamba wamekwisha kufa (Yohana19:31-32). Kumwachilia Yesu hamna budi kulisaidia kumzinduakatika hali ya kuzirai. Haiwezekani kukanusha uwezekano mojakwa moja ya kwamba walinzi waliagizwa na baadhi ya wajumbewa Pilato wasimvunje Yesu Miguu yake. Pengine hiyo ilifanywakama alama ya kumheshimu yeye na jamii ya Kikristowasioelewa.Kulingana na Biblia ubavu wake ulipochomwa mkuki ikabubujikadamu na maji:

Kama yeye alikwisha kufa na moyo wake uliacha kufanya kazi,isingeweza kububujika damu kwa wingi, damu iliyovilia na majiyake vingetoka pole pole. Lakini hiyo siyo picha iliyotolewa naAgano Jipya; bali linasema ya kwamba damu na maji vikabubujika(vikatoka kwa nguvu), ama 'vikatoka damu na maji mara moja'.(Hasa soma Biblia ya Kiingereza). Msishangae kuhusu 'maji' piakutoka kwani Yesu alipata kuugua ugonjwa wa ngozi laini ya njeya mapafu kwa sababu ya kusumbuliwa na kuudhika katika saaza kuadhibiwa juu ya msalaba. Pia shida ya kuwambwa msalabaniinaweza kuleta maradhi hayo ya mapafu yanayoitwa kwaKiingereza Pleurisy ambamo majimaji yanakusanyika kamavifuko vya maji. Hali kama hiyo kwa hakika huwa ya hatari sanana ya kuumiza kweli, lakini inaonekana hiyo ikamfaa Yesu kwanialipochomwa mkuki vifuko hivyo vya majimaji vilifanya kazi yamto ili kumlinda sehemu zake muhimu za kifuani zisipate kuumiana mkuki. Maji yakichanganyika na damu yakatoka haraka kwasababu ya moyo kufanya kazi barabara.

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Lakini walipomjia Yesu na kuona kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwamkuki, na ikatoka damu na maji. (Yohana 19:33 -34)

72

Page 79: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kuna ushuhuda mwingine ninaoandika hapa chini. Sawa namaelezo ya Biblia, mara mwili ulipotolewa kwa Yusufu waArimathaya, ulipelekwa mahali pa siri ili kuzikwa katika kaburilililofukuliwa katika mwamba ambamo mlikuwa na nafasi yakutosha si kwa Yesu pekee bali na kwa wahudumu wawili pia ilikumwangalia na kumtunza:

Si hivyo tu basi, bali pia twaambiwa katika Agano Jipya yakwamba Yesu alipakwa juu ya majeraha yake marhamu iliyokuwaimetayarishwa mapema kwa kazi hiyo. Marhamu hiyoiliyotayarishwa na wanafunzi wa Yesu ilikuwa na dawa zakuponya jeraha na kutuliza maumivu na kadhalika. Mahangaikoya nini hayo kwa kushughulikia kazi ngumu ya kutafuta madawakumi na mawili yanayopatikana kwa nadra ili kutengenezamarhamu hiyo? Madawa hayo yametajwa katika vitabu vyazamani vya madawa kama vile kitabu mashuhuri cha kufundishaudaktari kiitwacho Al-Kanun kilichotungwa na Bu Ali Sina(Tazameni 'Nyongeza' kwa orodha ya vitabu vya aina hiyo).Kulikuwa na haja gani ya kupaka marhamu kwa maiti? Hiyoitakuwa na maana hapo tu ambapo wanafunzi walikuwa na sababuimara ya kuamini kwamba Yesu ataondolewa msalabani akiwahai. Yohana Mtakatifu ndiye mtume wa pekee aliyediriki kutoamaelezo kwa nini marhamu ilitengenezwa na kupakwa kwa mwiliwa Yesu. Hiyo inatia nguvu tena habari hii ya kwamba kupakamarhamu kwa mwili wa maiti ni kitendo kilicho kinyume kabisana kawaida, kisichoweza kueleweka kwa wale waliomwaminiYesu kuwa mfu wakati wa kupakwa marhamu. Ndiyo maanaYohana alichukua jukumu la kutoa maelezo yake. Anasemakwamba marhamu ilipakwa kwa sababu Mayahudi walikuwa na

73

Kusulubiwa

Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao. LakiniMariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basiakilia hivi aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. Akaona malaikawawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmojamiguuni, hapo ulipolazwa mwili wa Yesu. (Yohana 20:10-12)

Page 80: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

desturi ya kupaka marhamu ama dawa kwa maiti zao. Hapa panajambo la muhimu sana kuzingatia ya kwamba, wataalamu wotewa kisasa wana rai moja ya kwamba Mtakatifu Yohana hakuwawa asili ya Kiyahudi, na akisema hayo amehakikisha ukweli warai ya wataalamu hao. Inatambulikana pasipo shaka ya kwambaWayahudi ama wana wa Israeli katu hawapaki marhamu yoyotekwa miili ya maiti zao. Kutokana na hilo watalaamu wakashikiliakwamba Yohana hana asili ya Kiyahudi, la sivyo asingelikuwajahili asijue desturi za Kiyahudi. Basi kulikuwa na sababunyingine ya kupaka marhamu.Marhamu ilipakwa ili kumwokoa Yesu katika kifo. Sababu yapekee ndiyo hii ya kwamba Yesu hakutazamiwa na wanafunziwake kuwa atakufa wala kwa hakika hakufa juu ya msalaba. Mwiliulioteremshwa haikosi ulionesha alama halisi za uhai kabla yakupakwa marhamu, waila kitendo cha waliopaka marhamukitaonekana cha kipuuzi, kisicho cha akili na kisicho na maana.Haielekei ya kwamba waliotengeneza marhamu hiyo mapemasana wakafanya hivyo bila ya kuwa na ishara madhubuti yakwamba Yesu hatakufa msalabani, bali ataondolewa akiwa haiakiwa na majeraha ya hatari na atahitaji dawa yenye nguvu kubwaya kuponya.Itambulikane ya kwamba eneo la kaburi alimolazwa Yesuliliwekwa katika hali ya siri kubwa waliyojua wanafunzi wakewachache tu. Hiyo ilikuwa kwa sababu dhahiri ya kwamba yeyealikuwa hai na bado alikuwa katika hali ya hatari ya kushikwa.Ama yaliyofanyika humo kaburini, hilo ni jambo la kujadiliwakwa jiha nyingi; wala haliwezi kuthibitika kwa uchunguzi mkali,na pia haiwezekani kuhakikika ya kwamba yule mtu aliyetokakatika kaburi alikuwa kweli amekufa na akafufuka kutoka wafu.Tunao ushuhuda wa pekee wa imani ya Wakristo ya kuwa Yesualiyetoka humo kaburini alikuwa na mwili uleule uliokuwaumesulibiwa, ukiwa na alama zilezile na majeraha yaleyale. Kamaalionekana akitoka na mwili huo huo, basi natija ya kiakili ndiyotu ya kwamba yeye hakufa asilani.

74

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 81: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Ushuhuda mwingine wa kuhakikisha kuwa Yesu alikuwa badohai wala hakufa ndiyo ufuatao: Baada ya siku tatu, mchana nausiku, watu wa kawaida hawakumwona isipokuwa wanafunziwake tu. Au tuseme akijitokeza mbele ya wale tu aliowategemea.Yeye hakuonana nao katika mwanga wa mchana bali katika gizala usiku. Mtu anaweza kutambua kutokana na maelezo ya Bibliaya kuwa Yesu anataka kuondoka katika hali ya hatari haraka sanana kwa kujificha. Pana swali hapa: Kama yeye alikuwa amejaaliwauhai mpya wa milele baada ya kifo chake cha kwanza walaasingeweza kufa tena, kwa nini alijificha asionekane mbele yamaadui, yaani wajumbe wa serikali na watu wa kawaida? Ilimpasakujitokeza mbele ya wajumbe wa serikali ya Kirumi na Wayahudipia na kuwaambia: 'Nipo hapa nikiwa na uhai wa milele. Jaribunikuniua tena kama mtaweza, lakini hamtaweza kamwe'. Lakinialihitaji kujificha. Siyo kwamba rai ya kujitokeza hadharanihakupewa; bali kinyume chake alishauriwa waziwazi ajidhihirishekwa ulimwengu, lakini akakataa na akaendelea kwenda mbali yaUyahudi ili mtu yeyote asiweze kumsaka:

Hilo linahakikisha ya kwamba yeye alikuwa mtu mwenye kufaasiye mbali na kufikiwa na mauti ama majeraha. Hiyo inayoneshatu ya kwamba Yesu alikuwa hajafa katika maana hii ya kwambaakaondolewa ule ubinadamu uliokuwamo ndani yake, bali akabakikabisa kama alivyokuwa wala kifo hakikutokea kumtenganishana mwili wa zamani na kumpa mwili mpya. Ndiyo kusemakwamba aliendelea kuishi pasipo kufa.

75

Kusulubiwa

Yuda (siye Iskariote) akamwambia, Bwana imekuwaje ya kwambawataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? (Yohana 14:22)

Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kamaanataka kuendelea mbele. Wakamshawishi wakisema, kaa pamoja nasi,kwa kuwa kumekuchwa, na mchana umekwisha. Akaingia ndani kukaanao. (Luka 24:28-29).

Page 82: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Roho inayohusikana na ulimwengu mwingine kabisa haitendi jinsialivyotenda Yesu wakati alipokutana na marafiki na wafuasi wakekisiri saa za usiku katika giza.Suala la Yesu kuwa roho limekataliwa katakata na Yesumwenyewe. Yeye alipojidhihirisha kwa baadhi ya wanafunziwake, hao wanafunzi hawakuweza kuficha hofu yao kwaniwalimwamini kwamba huyo siye Yesu mwenyewe bali ni rohoyake. Yesu Kristo akitambua tatizo lao akafutilia mbali hofu yaokwa kukataa kwamba yeye siye roho bali yu Yesu yuleyulealiyekuwa amesulubiwa, hata akawakaribisha wachunguzewenyewe majeraha yake ambayo bado yalikuwa mabichi (Yohana20:19-27). Kudhihirika kwake kwa wanafunzi na wengineohakuhakikishi kwamwe ya kwamba yeye alifufuka katika wafu.Kilichothibitika ni kwamba yeye alipona katika uchungu wamauti.Yaonekana ili kuwaondolea shaka waliyokuwa nayo badonyoyoni mwao, yeye akawauliza walikuwa wanakula nini. Naalipoambiwa kwamba walikuwa wanakula mikate na samaki,akawaomba apewe yeye pia kwani alisikia njaa na akala (Yohana24:41-42). Hilo pasipo shaka yoyote ndilo hakikisho dhidi yayeye kufufuka katika wafu, yaani kurejea ile hali ya asili ya mtualiyekwisha kufa na kuhuika tena. Matatizo yazukayo kutokanana kuhuika huko yatakuwa mara dufu.Kama Yesu bado alikuwa kitu kama mungu-mtu, jinsiinavyodaiwa alikuwa kabla ya kusulubiwa, basi alikuwa badohajaepukana na 'mtu' ndani yake. Hilo linazusha hali ngumu yakutatanisha. Kifo kilimfanya nini ama kiliwafanya nini, yaani yule'mtu' ndani ya Yesu na yule 'mungu' ndani yake? Je, roho za wotewawili, 'mtu' na 'mungu', zilitoka na zikarejea ndani ya mwilihuo huo wa udongo, baada ya kukaa katika jahanamu ile ilepamoja, ama hiyo ilikuwa roho ya mungu ndani ya Yesu iliyorejeakatika mwili wa kibinadamu bila ya kufuatana na roho ya mtu?Roho hiyo ya mtu ilipotea wapi? Mtu anashangaa. Je, safari yakekwenda katika jahanamu iliishia mumo humo pasipo kurejea,

76

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 83: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ilhali roho ya mungu ndani yake ilikaa tu humo kwa siku tatumchana na usiku? Na Je, Mungu alikuwa baba wa Yesu-mtu amaYesu mwana? Suala hilo linapaswa kutatuliwa kwa kutupatiapicha safi. Je, mwili wa Yesu ulikuwa nusu wa Mungu na nusuwa mtu?Fikara kumhusu Mungu tunayopata kutokana na Agano la Kalena Agano Jipya ni kwamba hana mwili, tena ameenea mahalapote, dhati yake siyo ya kiwiliwili. Tukiisha zingatia hiyo, hebusasa tugeukie nyuma kumwangalia Yesu ambapo alikuwa anapitakatika hali mbalimbali za kukua akiwa mimba ndani ya tumbo lauzazi la Mariamu. Kitu alichoumbika nacho Yesu kilitolewa chotena mama wa kibinadamu, hata sehemu sawa na punje ya haridalihaikutolewa na Mungu Baba. Naam, Mungu angeliwezakumwumba kimuujiza. Lakini kulingana na maoni yangu, kiumbeni kiumbe tu hata akiumbwa kikawaida ama kimwujiza. Twawezakumkubali mtu kuwa baba wa mwanae hapo tu mwana huyoanapoumbika kutokana na mwili wa baba na mwili wa mamakwa usawa au kwa uchache sehemu walau ndogo sana wa mwiliwa baba ipatikane katika uumbaji wa mwana.Kutokana na maelezo hapo juu inapaswa kubainika kwa msomajiya kwamba Mungu hakufanya kazi yoyote ya baba kabisa katikamimba kushikwa. Na kiwiliwili kizima pamoja na taratibu kuhusumoyo, kupumua, na utaratibu wa mwanzo na kuhusu ufa katikaini, mpango wa seli na taratibu ya neva, vyote hivyo viliumbikakutokana na mama wa kibinadamu pekee bila ya kusaidiwa namwingine yeyote awaye. Basi iko wapi sehemu ya 'Uana' katikaYesu ambaye alikuwa ni chombo cha kuwekea roho iliyoumbwana Mungu tu? Ufahamu huo mpya wa uhusiano baina ya Munguna Yesu unaweza kuelezwa kiakili kwa namna lakini siyo kamauhusiano wa baba na mwana.

77

Kusulubiwa

Page 84: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

5 KUHUIKA AU KUFUFUKA

Habari ya Yesu kuhuika katika wafu inaleta matatizo mengi.Baadhi ya matatizo miongoni mwa hayo yamekwisha elezwakatika mlango uliopita. Sasa tunageukia baadhi ya sababunyingine na matatizo mengine.Tunachokusudia ni asili ya 'ubongo' wa Yesu kabla hajasulubiwana baada ya kufufuka katika wafu. Ubongo wake ukahuishwabaada ya kuacha kufanya kazi kwa siku tatu mchana na usiku.Swali lenyewe ni kwamba mtu anapokufa ubongo unakuwajehasa? Kuhusu jambo moja wataalamu wa matibabu walioWakristo na wasio Wakristo wanapatana. Na jambo lenyewe niya kwamba ubongo ukifa kwa zaidi ya dakika chache unakufakwa kudumu hauhuiki tena. Damu ikatikapo tu, ubongo huanzakuchanganua.Kama Yesu alikufa juu ya msalaba, hiyo inamaanisha kuwa moyowake ulikoma kufanya kazi na kuacha kupeleka damu kwenyeubongo wake na kwa hiyo ubongo wake ukafa haraka baadaye.Basi utaratibu mzima wa kusaidia uhai kubaki ukakoma kufanyakazi, la sivyo yeye asingeweza kuchukuliwa kwamba amekufa.Kama ni hivi, twakabiliwa na tatizo la kukanganya kuhusuufahamu wa uhai na mauti ya Yesu Kristo.Kifo cha Yesu Kristo, ilivyoelezwa nyuma, kinamaanishakuondoka mwili wa kiroho, ama roho, katika kizimba cha mwiliwa kibinadamu. Kama ni hivi, basi kuhuika kwake kutamaanishakurejea mwili huo huo wa kiwiliwili aliouacha siku tatu kabla.Kurudi roho hivyo kutaanzisha upya uhai wa kiwiliwili. Na ilikutendeka hilo hakuna budi seli zilizokufa za ubongo zihuikeghafla na hali ya kuchanganuka haraka irudishwe nyuma kabisa.

78

Page 85: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Habari hiyo italeta matatizo mengi ambayo yatawadaia milelewanakemia Wakristo kuyatatua. Kueleza kurudi nyuma kabisakuchanganuka na kuoza utaratibu wa kati wa ki-neva ni jambolisiloweza kuwazwa na mwanasayansi. Kama kwa vyovyoteilifanyika, basi itakuwa ni mwujiza tu ukigongana na Sayansi nakuzidhihaki kanuni zilizoundwa na Mungu Mwenyewe; lakiniitakuwa ni mwujiza ambao bado utashindwa kutatua tatizo lililokombele yetu.Kuhuika hivyo siyo tu kuhuika seli za utaratibu wa kati wa ki-neva, bali kwa hakika kuziunganisha pamoja hadi zikawa kitukimoja. Hata kama seli zilezile za zamani ziundwe tena nakuhuishwa kabisa zilivyokuwa hapo kabla, hata hivyo kwa hakikahuo utakuwa utaratibu mpya wa seli usiokuwa kabisa nakumbukumbu ya zamani. Hizo hazitakuwa na budi kuundwa maranyingine na kujazwa humo mambo yote yaliyolingana na maishaya Yesu ambayo yalifutiliwa mbali katika ubongo wake baadaya kufa kwake.Tujuavyo, uhai huwa na ufahamu unamojazwa taarifa mbalimbalizinazopatikana katika mabilioni ya neva zilizomo katika ubongo.Taarifa hiyo tena inagawanyika katika sehemu ndogondogongumu kufahamika zinazohusiana zenyewe kwa zenyewe zataarifa zilizohesabiwa ki-kompyuta zinazopokelewa kutoka katikakila nguvu miongoni mwa nguvu tano za kuona, kusikia, kunusa,kuonja na kugusa. Kama taarifa hizo zikifutika basi na uhaiwenyewe unafutika. Kwahiyo, kuhuika kwa ubongo wa Yesukunamaanisha kufanyiza kompyuta mpya ya ubongo pamoja nataarifa mpya kabisa na kadhalika humo ndani. Matatizo hayoyatahusika pia na kemia ya sehemu nyingine za mwili wa YesuKristo. Ili kuhuisha mwili kazi kubwa ya kufanyiza upyaitaanzishwa baada ya kukomboa vilivyokwisha oza na kupotea.Mwujiza huo wote ukisha fanyika tayari, swali zitazuka nanialihuika na matokeo yake ni nini? Je, ni 'mtu' ndani ya Yesualiyehuika, ama ni 'mungu' aliyekuwamo ndani yake? Ndiyomaana sisi tukasisitiza kuelewa vizuri uhakika wa dhati ya Yesu.

79

Kuhuika au Kufufuka

Page 86: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Wakati wowote Yesu anapoonekana amekosea na ameshindwakudhihirisha nguvu zake kubwa akiwa Mwana wa Mungu,Wakristo wanajikinga kwa kudai ya kwamba yeye alikosea akiwamtu siyo akiwa mungu. Kwahiyo tunayo kila haki ya kuuliza nakujua waziwazi sehemu gani ndani yake ilikuwa mtu na ipimungu. Kukaa kwa mtu ndani ya Yesu kunataka ubongo wa 'mtu'mbali na ubongo wa 'mungu' ndani yake. Ubongo ulipohuika basi'mtu' ndani ya Yesu alihuika, kwani Uungu wa Yesu hauhitajiubongo wa kiwiliwili ili kumsaidia. Ubongo huo wa kiwiliwiliuliingiwa tu na mungu alipokuwa ardhini mara ya kwanza, jinsiinavyokuwa katika mambo ya roho kwamba kitu fulani kinakuwachombo ama njia ya kudhihirisha onyesho la kiroho. Basi kuhuikaYesu kutamaanisha kuhuika mtu ndani ya Yesu, kwani pasipokuwa hivyo haiwezekani roho yake kurejea ndani ya mwili huo.Kama jambo hilo halikubaliwi, hapo tutalikabili tatizo jingine lakukubali kwamba Yesu alikuwa na bongo mbili mbalimbali zakujitegemea pindi alipokuwa duniani humu: Ubongo mmoja wa'mtu' na mwingine wa 'mungu', zote mbili zikikaa mahali pamoja,lakini hazikulingana bali kila mmoja unajitegemea. Kama nihivyo, basi suala la kuhuika lichunguzwe upya ili uhakika wakehasa utambulikane. Basi hamna haja tena ya kufikiria ubongo wakibinadamu kufanyizwa upya ili kuipatia dhamiri mahali pakukalia. Bali twahitaji kufikiria kwamba Yesu analitembelea tenafuvu la kichwa cha mtu aliyekuwa mwenyeji wake wa zamani,ambamo ndani ya fuvu hilo mna masazo ya ubongo yaliyooza.Kadiri tunavyochunguza kwa uangalifu zaidi suala hilo, ndivyoyanavyojitokeza matatizo zaidi katika kila daraja la uchunguzi.Mtu anahitaji ubongo kuwa chombo cha mfuatano wa fikira.Kuhusu kazi zinazofanywa na mwili wa kiwiliwili ni kwambakama tukiamini kuwa dhamiri inakuwapo peke yake na inaishikwa kujitegemea, basi hiyo itamaanisha kwamba dhamiri na rohoni kitu kilekile kimoja. Waweza kuita dhamiri ama roho lakiniinaishi peke yake hata kama uhusiano wake na ubongo wa mtuunakatika. Lakini kama dhamiri au roho inahitajika ili kuutawala

80

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 87: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

mwili wa mtu ama inaathirika na yanayotokea katika ufalme wakewa kiwiliwili, hapo bila shaka unahitajika ufungamano madhubutibaina ya dhamiri na ubongo ama roho na ubongo. La sivyo, hivyo(roho na ubongo) haviwezi kabisa kuathiri, kuhimiza au kutawalamafuatano ya kimwili na ya kiakili ama ya ki-maono katika mtu.Naona hilo halina haja ya kujadiliwa.Hilo linatuongoza kwenye tatizo jingine kubwa zaidi: Je,anayefanywa kuwa Mwana wa Mungu anahitaji kuutawala amakusimamia mwili kwa njia ya ubongo? Na je, yeye anautegemeaubongo wa kiwiliwili kwa mfuatano wa fikra zake? Kama yeyeanavuka mipaka yote ya kibinadamu, na kama yeye anao mfumowa kujitegemea wa mfuatano wa fikira ambao ni wa pekee kwakeusiyo na kifani katika ulimwengu mzima aliouumba, hapo kurejearoho ya Mungu katika mwili wa mtu pamoja na dhamiri ya mtukunaleta natija isiyolingana na akili yaani kupatikana kwa dhatiiliyo na mifuatano miwili ya fikra inayopingana, kwanihaiwezekani kwa dhamiri na roho ya mtu kulingana kikamilifuna dhamiri na dhati ya Mungu. Kutakuwa na upinzani wa kudumubaina ya mifuatano hiyo miwili utakaosababisha mapambano yakusumbua baina ya mawimbi ya ubongo. Mwenye shida hiyoanafaa kutibiwa na mtaalamu wa utibabu wa maradhi ya rohomwenye uwezo zaidi ya mtu. Huo pengine ndiyo ugonjwa mpyawa roho uitwao schizophrenia kwa Kiingereza.Baada ya kueleza hayo, tuliangalie jambo hilo kwa jiha nyingine.Nikiisha taali Ukristo mpaka undani wake kadiri fulani,nimetambua kwamba baadhi ya istilahi na matumizi yakehavikueleweka barabara wala hapakutambulikana matokeo yaistilahi hizo zisipotumika mahali panapofaa. Nadharia ya Kikristohaieleweki vizuri akilini kwa sababu ya matatizo hayo na kutumiaistilahi hizo pasipohusikana. 'Kuhuika upya' ni istilahi mojawapona 'kufufuka' ni nyingine, ambazo zina muradi tofauti. Mpakasasa tumetumia kusudi istilahi ya 'kuhuika' upya wakati wakuzungumzia Yesu kupata uhai mara ya pili. Tulivyokwisha onakutokana na maelezo ya hapo kabla, kuhuika upya kunamaanisha

81

Kuhuika au Kufufuka

Page 88: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kurejea kwa hali ambamo mwili wa kibinadamu unaanza kufanyakazi zote tena baada ya kufa. Lakini 'kufufuka' ni kitu kinginekabisa.Kwa bahati mbaya Kanisa duniani kote linahusika na kuletampasuo katika mioyo ya Wakristo kwa kutumia vibaya istilahihizo, kwa kuiweka mojawapo mahali pa ya pili, au kwa uchachekuinasibisha maana ya mojawapo kwa ile nyingine. Wakristowengi wanafahamu kufufuka Yesu ni kuhuika kwa mwili huohuo wa kiwiliwili aliouacha wakati alipokufa wanavyofikiri.Naam, sisi hatuafikiani nao bali tunayo haki ya kuieleza hali hiyokuwa kuzimia siyo kufa.Kama maneno 'kufufuka kwa Yesu' yakifahamika sawasawa nakutumika vizuri, hayo hayawezi kumaanisha roho yake kurejeandani ya mwili huo wa kibinadamu aliouacha wakati wa kufa.Kufufuka ndiyo istilahi ambayo inamaanisha tu kuumbika mwilimpya wa kiroho. Mwili huo asili yake ni ya kiroho na unafanyakazi kama chombo ambamo mna roho nyepesi zaidi. Huounaumbwa ili kuendeleza maisha baada ya kufa. Baadhi ya watuwanauita mwili huo mwili wa nyota au athma. Hata ukiupa jinagani maana yake ni hiyohiyo moja. Ufufuo unatumika kwauumbaji wa mwili mpya kimbinguni ama wa kiroho ambamo rohoinakaa, siyo, twarudia, siyo kurejea ndani ya mwili uleuleuliokwisha changanuka na kuoza ambao roho iliuondoka hapokabla.Mtakatifu Paulo amezungumzia ufufuo wa Yesu Kristo kabisakatika maana hiyo. Yeye aliamini katika ufufuo wa si Yesu tubali na ufufuo kwa ujumla wa wale wote wanaokufa naowanastahili machoni mwa Mungu kujaliwa kuwapo kupya nanamna mpya ya maisha. Roho inakuwa hiyohiyo lakini makaziyake yanabadilika. Sawa na usemi wa Paulo Mtakatifu, hiyo nikanuni ya kawaida ambayo haina budi ikubaliwe, la sivyo, Ukristoama dini haitakuwa na maana.Nyaraka za Paulo mtume kwa Wakarintho zinapaswa kusomwakwa makini kwani hizo zina maana sana kuhusu suala hilo.

82

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 89: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Hizo haziachi nafasi yoyote ya shaka, angalau kwangu mimi, yakwamba wakati wowote yeye alipozungumzia Yesu kuonekanahai baada ya kusulibiwa, alizungumza waziwazi pasipo shakakuhusu kufufuka tu kwa Yesu, wala haikupitia moyo wakekwamba roho ya Yesu imerejea katika mwili wake ule ule wenyekufa na akahuika kimwili baada ya kufa katika maana ya kawaida.Kama baadhi ya wataalamu wa Wakristo hawakubali nilivyoelewakuhusu Paulo Mtakatifu, basi hapo hawatakuwa na budi kukubaliya kwamba Mtakatifu Paulo alijipinga kwa uchache katika baadhiya maelezo kuhusu maisha mapya ya Yesu kuwa yeye alifufukawala siyo kwamba mwili wake ulihuika ambamo roho yakeinasemekana ilikuwa imefungwa.Hapa chini kuna baadhi ya maneno yake yanayolingana na swalahilo yanayojieleza yenyewe:

83

Kuhuika au Kufufuka

Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.(1Wakorintho 6:14).

Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika uharibifu, kufufuliwakatika kutokuharibika; hupandwa katika aibu, kufufuliwa katika fahari;kupandwa katika udhaifu, kufufuliwa katika nguvu; kupandwa mwiliwa asili, kufufuliwa mwili wa kiroho. Ikiwa uko mwili wa asili, na waroho pia uko. (1Wakorintho 15:42-44).

Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanada yamwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe nauharibifu, nasi tutakubalika. Maana sharti huu uharibikao uvaekutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikaoutakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapondipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, mauti imemezwa kwakushinda. (1 Wakorintho 15:52-54).

Lakini tunao moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katikamwili na kukaa pamoja na Bwana. (2 Wakorintho 5:8).

Page 90: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Suala linalobakia kutatuliwa linazuka kutokana na MtakatifuPaulo kutaja maelezo ya Wakristo wa kale kuhusu jinsialivyoonekana Yesu akiwa hai katika mwili wake mara baada yakusulibiwa. Kama Mtakatifu Paulo alifahamu ya kwamba Yesualifufuka, yeye anaweza kuwa sawa, na yeye kumwona Yesu aukuongea naye kwaweza kuelezwa kwa sura ya ufufuo jinsi rohoya mtu aliyekufa inavyokuja kutoka ulimwengu mwingineikijichukulia mzuka anayefanana sana na sura aliyokuwa nayokabla ya kufa. Lakini hapa panaonekana habari hiyo imevurugikakwa sababu ya kuchanganya ushuhuda wa aina mbili. Kwanzatwatakiwa kufikiria ushuhuda wa mwanzoni wa wanafunzi wakena wale waliompenda na kumheshimu ingawaje hawakuingiakatika Ukristo kama desturi. Ushuhuda huo haikosi MtakatifuPaulo akauelewa vibaya kwani huo unahakikisha kwamba Yesualionekana katika sura ya binadamu ndani ya mwili wake wakiwiliwili, jambo ambalo haliwezi kumaanisha ufufuo.Ili kuthibitisha jambo hilo, mtu anapaswa kurejea habari ya Yesukuwashangaza wanafunzi wake:

Tukio hilo linakanusha kabisa wazo la ufufuo na linaeleza yakwamba Yesu alikusudia waziwazi kuwa yeye alikuwa mtu yuleyule pamoja na mwili uleule wala hakuwa roho, wala siye mtuambaye sasa hahitaji chakula ili kuishi. Hiyo inaonesha tena kuwaWakristo wa kale walikuwa wakizungumzia mambo mawilitofauti. Kila walipozungumzia Yesu kuhuika na walipokabiliwa

84

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Wakashtuka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.Akawaambia, mbona mnafadhaika? na kwa nini mnaona shaka mioyonimwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimimwenyewe. Nishikeni-shikeni, muone; kwa kuwa roho haina mwili namifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayoaliwaonyesha mikono yake na miguu yake. Basi walipokuwahawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, mna chakulachochote hapa? Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa,akala mbele yao.(Luka 24:37-43).

Page 91: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

na mashaka kuhusu wazo hilo la kipuuzi, wakakimbilia wazo laufufuo ambalo wazo hilo linaweza kuelezwa kifalsafa nakimantiki. Waraka wa kwanza kwa Wakorintho hususan unatoanafasi nzuri ya kutaali mashaka ya kukanyaga katika mashua mbiliwakati mmoja.Hatimaye, tukirejea kwa ushuhuda wa Wakristo wa kale kukutanana Yesu Kristo, hatubakiwi na njia yoyote isipokuwa kuamini yakwamba yule Yesu aliyeonekana kwa wanafunzi wake wengi namarafiki zake mara baada ya kusulibiwa, na akaongea nao naakakaa nao na taratibu akaondoka kule alikosulibiwa zaidi katikagiza la usiku, hakuwa kabisa mtu aliyefufuka bali alikuwa mtuambaye pengine alihuika tu kimwili ama hakufa asilani baliakaokolewa kimwuujiza katika hali iliyokurubia sana kifo. Yeyealikuwa karibu kabisa na kifo hata kwamba hali yake inafananana hali ya Yona katika tumbo la Nyangumi. Hatuna shaka yakwamba kinachoweza kukubalika hasa ndiyo hali hiyo iliyoelezwamwishoni.Ili kuwarahisishia Wakristo kuelewa nadharia yetu ningeoneleakuweka mbele yao mfano mmoja wa kukisia. Mathalan, mtummoja anawambwa msalabani kwa shabaha ya kumwua pale naanachukuliwa kuwa alikufa msalabani. Baadaye mtu huyo huyoanaonekana akitembea pamoja na baadhi ya marafiki zake. Haowanashuhudia ya kwamba mwili wake unayo makovuyaliyosababishwa na majeraha aliyoyapata kwa ajili yakuwambwa msalabani. Yeye anakamatwa tena na serikali nakuletwa mbele ya mahakama kwa mashtaka ya kwamba kwa kuwayeye amepona katika mauti kwa sababu hii au ile hivyo asulubiwetena ili kutimiza alivyohukumiwa. Lakini mtu huyo anajiteteaakidai kwamba kwa kweli alikufa mara moja, kwahiyo shabahaya sheria imekwisha timia tayari, na sasa kwa kuwa yeye amehuikakwa amri maalum ya Mungu kwahiyo hukumu ile ya zamani yakumuua haiwezi kutekelezwa kwa mara ya pili, kwani sasa yeyeamepata muda mpya tena wa kuishi ambamo katika muda huuyeye hajafanya uhalifu wa sheria.

85

Kuhuika au Kufufuka

Page 92: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kama mahakama ikikubali hoja yake, ni dhahiri kwamba yeyehataadhibiwa mara nyingine kwa uhalifu ambao amekwishaadhibiwa.Kama tukio la namna hiyo likitukia katika mahakama katika nchiya Kikristo, jaji akiwa Mkristo, na baraza la Wakristo, msomajianafikiriaje kuhusu mtu huyo ya kwamba watamhukumuje amawanapaswa kumhukumuje? Kama hoja ya mtu anayechunguzwainakataliwa na anahukumiwa kunyongwa tena, hiyo itakuwa sawakwa msingi gani?Ni dhahiri ya kwamba jaji yeyote mwenye akili, akiwa Mkristoau si Mkristo, na pia baraza la watu wenye akili timamuhawatakubali hata kidogo ya kwamba mshtakiwa huyu amehuikabaada ya kwisha kufa. Hukumu ya aina hiyo haina upendeleo wakimtaa, dini, taifa, ama kabila. Bali inahusikana na watu wotewala hamna mtu mwenye akili yake timamu awezaye kuwazahukumu nyingine yoyote iwayo. Hivyo, shauri ya watu wotewenye akili na fahamu ni kukataa dai la kuhuika, bali kumhukumukwamba alipona tu kifo. Ndivyo ilivyotendeka katika habari yaYesu Kristo. Hakuhuika wala hakufufuka bali inavyoamua akilialipona mauti juu ya msalaba.Kuhuika Yesu kimwili ni jambo la muhimu kabisa kabisa kwaUkristo hata kwamba mtu anapaswa kuchunguza sababu zake.Kwa dhahiri hamna mantiki katika jambo hilo zima. Kwa ninianayehesabiwa kuwa Mwana wa Mungu akajichagulia kurejeatena katika kitundu cha mwili wa binadamu baada ya kwisha patauhuru katika hicho? Na habari hiyo inawezaje kuwa hoja pasiposhaka ya kwamba yeye alikufa hasa na kisha akahuika tena? Hiyohabari imekwisha elezwa kiasi kadhaa nyuma wala sina nia yakuikazania hapa tena, lakini ningependa kumwelekeza msomajimwenye swali jingine la muhimu linalolingana na habari hiyo.Kwa nini fikra hiyo ya kipuuzi ikaimarika katika dini ya Kikristoambayo polepole katika muda wa karne chache baada ya Yesuikawa nguzo mojawapo ya imani ya Kikristo ambayo pasiponguzo hiyo jengo zima la theolojia ya Kikristo linabomoka?

86

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 93: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Sisi tutajaribu kujitia katika dhamira za Wakristo wa kalewaliokabili tatizo lisiloweza kutatulika, na tutaanza kuleta halizile ambamo Ukristo ulipewa sura kinyume cha uhakika halisi.Kwa njia hiyo pengine itakuwa rahisi kufahamu hasa kuumbikana kuumbuka kwa Ukristo. Ukweli halisi unaotakiwa kuzingatiwasana ndio huu ya kwamba ikiwa Yesu, amani iwe kwake, kweliamekufa msalabani, hana budi ataonekana machoni mwaWayahudi kuwa nabii mwongo, mdanganyifu.

MANENO MAKALI DHIDI YA WATUKUFU:Ilivyoelezwa hapo kabla, maandiko yalitabiri kuwa mdai mwongoaliyenasibisha chochote kwa Mungu asichosema Yeye,atatundikwa mtini. Kwahiyo kifo cha Yesu msalabani ndiyosawasawa na kifo cha Ukristo. Ndiyo sababu maandikoyanayotegemewa ya dini ya Kiyahudi yanafurahia mno kifo chaYesu juu ya msalaba. Alihesabiwa kwamba alithibitishwa kuwamwongo pasipo shaka yoyote na maadui zake Wayahudi wa zamazake sawa na uamuzi huo maalum wa Biblia. Walikosa hatakumtaja kwa heshima na wakatumia maneno machafu mno yakumtukana hata kwamba kuyasoma hayo hawezi kuvumiliayeyote anayempenda Yesu kama vile sisi tumpendao akiwamtume mkweli mtukufu wa Mungu. Mtu anaweza kutambuakusumbuka na kuudhika mno kwa Wakristo wa kale waliomjuaYesu kuwa mtu mtukufu na Mjumbe mkweli wa Mungualiyejaaliwa heshima maalum ya kuwa Masihi. Wakristo haowangejiteteaje dhidi ya matusi hayo machafu ambayo yakisomwaleo katika mazingira ya siku hizi yanaleta moyoni picha chafu yakitabu kiovu cha Salman Rushdie kiitwacho 'Satanic Verses'?Kukosa adabu kabisa kwa wote hao inaonekana kumezuka kwasababu ya kudharau sana ubinadamu. Maneno yafuatayoyatamsaidia kidogo msomaji kuelewa kwamba hulka bora za mtuzinapoteaje ambapo maadui wenye wazimu wa watu watukufu

Kuhuika au Kufufuka

87

Page 94: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wanapochagua kuwafanya shabaha ya kichaa chao kipotofu pasipokuona haya.Talmudi kilicho kitabu cha dini kinachoeleza kikamilifu mambona imani za Wayahudi kilifundisha ya kwamba si tu ya kuwaYesu alizaliwa kwa njia ya haramu bali kuzaliwa huko ni kubayamara dufu kwa kusabibishwa na ndoa ya kishetani ya Mariamuiliyofungwa wakati yeye alipokuwa katika siku zake za hedhi.Kitabu hicho kilifafanua pia ya kuwa yeye alikuwa na roho yaEsau, na alikuwa mjinga, mpunga pepo, mtongozi na aliuawamsalabani na kuzikwa katika jahanamu na akafanywa sanamu yakuabudiwa na wafuasi wake tangu wakati huo. Maneno yafuatayoyamechaguliwa kutoka kitabu 'The Talmud Unmasked', utungowa Reverend I.B. Pranaitis.

88

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Yafuatayo yamesimuliwa katika Chuo Kallah, Ib (18b): "Safari mojawazee walipokuwa wameketi Langoni, vijana wawili waliwapitia,mmojawapo akifunika kichwa chake. Mwingine alikuwa kichwa wazi.Mwalimu Akibah akasema ya kwamba huyo mwenye kichwa wazindiye mwana haramu. Mwalimu Jehoschua akaongeza kusema kwambahuyo ndiye ben niddah, yaani mama yake alishika mimba yakealipokuwa mwezini. Mwalimu Akibah akasema tena kwamba huyoalikuwa na mabaya yote hayo mawili. Ndipo wengine wakamwuulizaMwalimu Akibah kwa nini yeye anajasiri kuwapinga wenzake. Akajibukuwa yeye anaweza kuthibitisha aliyosema. Basi akamwendea mamamzazi wa kijana huyo aliyekuwa ameketi akiuza mboga sokoni, naakamwambia: Binti yangu, kama ukinijibu sawasawa nitakayokuulizasasa hivi, ninakuahidi utaokoka katika Akhera. Mama huyo akamtakakwamba ale kiapo kwamba atatimiza ahadi, na Mwalimu Akibahakaitikia kwa kutikisa midomo tu, kwani moyoni alitangua kiapo. HapoMwalimu Akibah akamwuliza: 'Niambie mwanao huyu ni wa namnagani?' Mama akamjibu: 'Siku niliyoolewa nilikuwa mwezini, na kwasababu hiyo mume akaniacha. Lakini ikaja roho moja chafu ikalalanami na huyo mtoto ndiyo akazaliwa kwa sababu ya ile roho chafukuingiliana nami'. Basi ikathibitika ya kwamba kijana huyo hakuwa tumwanaharamu bali pia akazaliwa kwa sababu ya mama yake kuingiliwakatika siku zake za hedhi. Na waulizaji wake waliposikiliza hayowakatamka: 'Hakika Mwalimu Akibah ndiye mkuu alipowasahihishawazee wake!' Na wakapaliza sauti: Mwenye mibaraka ndiye Mungu

Page 95: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Uzuri wowote uliomo katika mtu unauchukia kabisa uchafuunukao uliorundikwa juu ya jina tukufu na heshima ya Yesu katikavitabu vya maadui zake wenye uhasama. Naam, mama mwemamtukufu Bi Mariamu alishika mimba ya Yesu wala hakunachochote kiwacho kilichoshughulikia mimba hiyo kushikwaisipokuwa uwezo wa Mungu wa kuumba usio mipaka. Wazo lakushikwa mimba kwa sababu ya shetani kuingiliana katika haliya hedhi inaafikiana zaidi na moyo uliodhania uovu huo wa kupitakiasi. Ole wao wapotevu ambao wake watukufu wa watu watukufuwala mama zao hawakuachiliwa na ndimi zao wala kalamu zaowanaotema sumu na ubaya kwa usawa. Haina tofauti kamamwenye wazimu wa aina hiyo kaishi miaka elfu mbili tangu leoama akazaliwa katika zama zetu hizi. Ni la kushangaza sana jambohili ya kwamba hata jamii zilizostaarabika mno za zama hizizinaweza kufumba macho zisione unyama huo bali penginezinatoa kibali kwa uhalifu mbaya sana eti kuna uhuru wa kusemana kuandika.Lugha aliyotumia Salman Rushdie, kwa mfano kuwakashifu wakewatukufu wa Mtume Mtukufu wa Islam siyo tofauti na lughailiyotumika kumkashifu mama mtukufu wa Kristo:Imesimuliwa pia katika Sanhedrin, 67a:'

________________1The Talmud Unmasked, by Rev I. B. Pranaitis, Chap. 1 P. 30

89

Kuhuika au Kufufuka

wa Israel aliyemfunulia siri Mwalimu Akibah mwana wa Yusufu!'"Jambo hili kwamba Wayahudi wanairejeza habari hiyo kwa Yesu namama yake Mariamu, inaonekana wazi katika kitabu chao ToldathJeschu - Uzazi wa Yesu - ambamo uzazi wa Mwokozi wetu umeelezwatakriban kwa maneno kama hayo.1

'Hayo ndiyo waliyotenda kwa mwana wa Stada katika Lud, nawakamsulubisha jioni ya Pasaka. Kwani mwana huyo wa Stada alikuwamwanaye Pandira. Maana Mwalimu Chasda anatuambia ya kuwaPandira alikuwa mume wa Stada aliyekuwa mamake, na yeye aliishikatika zama za Paphus mwana wa Jehuda.'

Page 96: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Mwandishi wa 'The Talmud unmasked', Rev I.B. Pranaitisakifafanua maneno hayo juu akasema:

Hicho ni kilio cha uchungu kilichotoka katika moyo wa aliyeteswaasiyejiweza ambaye amehuzunishwa kwa sababu ya Bwana wakempendwa kufanyiwa dhihaka kupita kiasi. Bila ya shaka Wakristowa kale walisumbuka zaidi sana na kuudhiwa mno kwa sababuya dhihaka ya Wayahudi wa zama hizo. Walilazimikakusumbuliwa na shutumu zilizotolewa dhidi ya yule ambaye sikwamba kumbukumbu lake lilisahaulika zamani, bali ukumbukowake wa kupendeza bado ulikuwa mpya, ambaye alipendwa sanasana na wale waliowahi kumwona na kukaa naye muda fulanikatika maisha. Haikosi hao waliudhika mara mbili, kwani haikuwadhihaka ovu sana tu iliyowahuzunisha, bali na Yesu Kristoaliposumbuliwa wakati wa kuhukumiwa na kutundikwamsalabani kwa nia ya kuuawa hilo likaongeza dharau katikajeraha.Mimi ningependa kwamba dhamiri ya nchi huru za Magharibikwa uchache ijaribu kuzingatia uchungu na udhia wa bilioni yaWaislam ambao bila shaka wanasumbuka na kuudhika hivyohivyo pindi lugha chafu ya kinyama inapotumika kumtukanaBwana wao mpendwa na Masahaba zake.Wakristo wa kale walilazimika kuudhika ijapokuwa walijua sanaya kuwa Yesu alikuwa hai na walikuwa na ushuhuda usiowezakukanushwa ya kuwa Yesu hakufia msalabani jinsi Wayahudiwalivyojigamba. Wao wenyewe walimtibu majeraha yake.Wakamwona akizinduka kimwujiza kutoka kwenye hali ya kuziraisana ambayo katika hali hiyo walikabidhiwa mwili wake, na

90

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

'Hayo yanamaanisha ya kwamba Mariamu ndiye aliyeitwa Stada, yaanimalaya, kwani sawa na ilivyofundishwa hapo Pumbadita yeyealimwacha mumewe na akafanya uzinzi. Hayo pia yameandikwa katikaJerusalem Talmud na Maimonides'.'Siwezi kusema ya kwamba wanaouamini uwongo huo wa kishetaniwanastahili kuchukiwa sana ama kuhurumiwa.'

Page 97: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wakamshuhudia wenyewe kwa macho yao siyo kwa sura yamzuka au roho, bali katika mwili huo huo dhaifu wa kibinadamuuliosumbuka kwa ajili ya ukweli na ukapona kifo kimwujiza.Waliongea naye, na wakamwona akitembea hatua kwa hatua,usiku hadi usiku, katika hali ya siri kupakimbia alipotundikwamsalabani.

KUPAA KWAKE:Habari ya Yesu Kristo kupaa haikutajwa na Mt. Mathayo na Mt.Yohana katika Injili zao. Kutokutaja habari hiyo ya muhimukabisa kunashangaza mtu.Katika Injili tatu zinazofanana katika kusimulia mambo, Injilimbili tu za Marko2 na Luka3 zinataja habari za kupaa kwa Yesu.Hata hivyo uchunguzi wa kisayansi na wa kitalaamu wa kisasaumethibitisha ya kuwa maneno ya kupaa kwa Yesu ndiyonyongeza ya baadaye iliyofanywa katika Injili hizo mbili. Mistarihiyo haikuwamo katika matini ya asili. Codex Sinaiticus ndiyoBiblia ya zamani zaidi, ya tangu karne ya 4, ambamo mna Aganola kale na Agano Jipya kikamilifu takriban.4 Biblia hiyoinashuhudia ya kwamba mistari kuhusu Yesu kupaa haimo katikaMarko na Luka, bali iliongezwa baadaye na mwandishi fulanikwa upendo wake. Katika Codex Sinaiticus, Injili ya Markoinaishia kwa mstari wa 8 wa Mlango wa 16. Uhakika huoumekwisha tambuliwa katika baadhi ya chapa za kisasa za Bibliapia.5

91

Kuhuika au Kufufuka

_____________________________2 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketimkono wa kuume wa Mungu. (Marko 16:19)3 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. (Luka 24: 51)4 Uk 18 wa Jesus the Evidence, mwandishi Ian Wison (1984)5 Uk 1024 wa The Holy Bible, New International Version (1984), Imeenezwa naInternational Bible Society.

Page 98: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Vile vile Injili ya Luka ya (24: 51) ndani ya Codex Sinaiticushamna maneno haya: 'akachukuliwa juu mbinguni' Sawa namchunguzi wa maneno yaliyopata kuandikwa hivi au hivi, jinalake C.S.C. Williams, kama kweli mistari hiyo inakosekana katikaCodex Sinaiticus, basi hamna tena habari ya Yesu kupaa katikamatini halisi ya Injili.6

Hata mashahidi wa Jehovah wanaoamini sana Yesu kuwa 'Mwana'na kwamba yeye alipaa kwa Mungu Baba wamekiri mwishoweya kwamba mistari hiyo ya Marko na Luka ndiyo nyongeza katikamatini ya asili bila msingi wowote 7

ILITENDEKA NINI KWA MWILI WA YESU ?Uchunguzi mkubwa zaidi kwa kutumia busara na akiliunadhihirisha mambo mengine tena yasiyo na maana yaliyomokatika tukio la Msalaba na kupaa jinsi Wakristo wa siku hiziwanavyoeleza. Ama kuhusu kurejea kwa Yesu katika mwili wakibinadamu, tumekwisha sema vya kutosha. Hapa twapendakuongeza kile kilichoweza kutokea kwa mwili huo ambapo Yesualipaa mwishowe, kama kwa vyovyote alipaa.Wakati wa kulikabili suala la kuwa mwili wa Yesu ulikuwaje,baadhi ya Wakristo wanasema yeye alipopaa kwa Babake wambinguni hapo kiwiliwili chake cha udongo kikachanganuka nakikapotea katika mwako. Habari hiyo inazusha swali la msingi:Kama kaondoka Yesu katika mwili wa kibinadamu kulikuwa nitukio la kulipuka hivyo, kwa nini halikufanyika hilo wakatialipokufa mara ya kwanza inavyosemekana?________________________

6 The Secret of Mount Sinai, the story of finding the world’s oldest Bible CodexSinaiticus; by James Bently uk 131.7 New World Translation.

92

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 99: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Habari ya kifo cha Yesu twasoma ndani ya Biblia mara tu wakatialipokuwa bado ametundikwa msalabani na Mt. Mathayoanaripoti akisema: Akaitoa roho yake. Ni dhahiri ya kwambahaikutendeka kitu isipokuwa tu roho yake ikatoka taratibu. Jetwatazamiwa kuamini ya kuwa yeye hakufa basi juu ya msalaba,kwani kama angeliuacha mwili, mwili huo ungelipuka vivyohivyo hata wakati huo? Kwa nini hiyo ilitendeka mara ya pili tuYesu alipouacha mwili wake? Katika hali kama hiyo njia mbilitu ziko wazi ili kuendelea mbele:

1. Ya kwamba Yesu hakubaki akifungwa ndani ya mwili wakibinadamu kwa kudumu baada ya roho yake kurejea mlendani yake na kwamba wakati alipokuwa akipaa mara yapili akauacha mwili wake wa kibinadamu na akapaa akiwaroho halisi ya Mungu.

Lakini hiyo hailingani na uhakika hasa wala haingii akilini, kwanihiyo itaongoza kwenye kichochoro kilichozibwa cha kuaminikwamba Yesu alikufa mara mbili, kwanza juu ya msalaba, na pilialipopaa.

2. Ya kwamba yeye alidumu milele akifungwa katika kiwiliwilicha kibinadamu.

Hiyo haiwezi kukubalika kwani inachukiza sana na ni kinyumekabisa cha heshima na utukufu wa Mungu.Upande mwingine sisi tunayo nadharia inayolingana na busara:'Itakuwa ni kosa kufahamu kupaa kwa Yesu kuwa safari ya kaleya angani, na mbingu kuwa mahali palipo nyuma ya jua, mwezina magalaksi.' Ukweli hauko hapa wala pale.8 Kisa hicho chakuchekesha kilibuniwa kwa hakika kwa sababu ya tatizolisilotatulika walilolikabili Wakristo wa zamani ambapo Ukristoulikuwa unachimbuka. Yesu alipotoweka machoni pa watu, bilashaka swali lilizuka kwamba imefanyika nini kwake._________________________

8 The lion Handbook of Christian Belief, Lion, London (1982) uk 120.

93

Kuhuika au Kufufuka

Page 100: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Wakristo wa kale wasingeweza kutatua tata hilo kwa kutangazahadharani ya kwamba kwa kuwa yeye hakufa asilani hivyo hakunatena suala la mwili wake kuachwa nyuma na kwamba kwa hakikamwili wake umekwenda pamoja naye alipohama. Kwa njia hiyosuala la kutoweka mwili lingeweza kutatuliwa kwa urahisi. Lakiniilikuwa haiwezekani kukiri hilo. Wale ambao wangejasirikukubali kwamba Yesu alionekana akiwa hai akiondoka taratibukisirisiri nchi ya Kiyahudi wangejitia katika hatari ya kuhukumiwana sheria ya Kirumi kwamba hao ndio waliomsaidia katika uhalifuwa kutoroka hukumu.Kukimbilia kisa cha kubuniwa cha kupaa kwa Yesu hata kikiwakinyume kabisa cha akili kulikubaliwa kwani kilikuwa chakuwaletea usalama zaidi. Lakini hata hivyo kilikuwa cha uwongo.Twalazimika kuwasifu wanafunzi wa kale kwa maadili yaoambayo juu ya kuwa katika hatari hawakujitafutia usalama katikamaneno ya kuongopa. Waandishi wote wa Injili walinyamaakuhusu habari hiyo kuliko kujificha nyuma ya wingu la moshi lakuongopa. Hamna shaka walisumbuka kwa kuchekwa na maaduizao, lakini walikubali kuudhika wakikaa kimya.Kimya kisichoelezeka cha hao waliojua habari hiyo kilisababishakupanda mbegu ya shaka katika nyoyo za vizazi vya baadayevya Wakristo. Hamna budi walishikwa na butwaa kwamba kwanini habari ya mwili wa Yesu aliouacha nyuma haikutajwa baadaya yeye kukata roho? Mwili huo ulipotea wapi na ulikuwaje?Kwa nini roho ya Yesu iliuerejea mwili huohuo kama ulirejea?Maswali hayo ya muhimu yawezekana yalizusha maswalimengine pia. Kama kuhuika kunamaanisha kurejea roho yakekatika mwili huohuo, ilifanyika nini kwa Yesu baada ya kipindichake cha pili kufungwa ndani ya kiwiliwili hicho? Je, alipatakufungwa katika hicho milele pasipo kuachiliwa tena?Upande mwingine, kama roho ya Yesu iliuwaga mwili huo maraya pili, je, kuhuika huko kulikuwa kwa muda ama kwa milele?Kama yeye hakudumu kuwamo humo, ulikuwaje mwili wakebaada ya kifo cha mara ya pili? Ulizikwa wapi na je, habari hiyo

94

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 101: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

imetajwa katika taarifa ama historia ya zamani ?Inaonekana kwamba maswali hayo, hata kama hayakuzukazamani zaidi, haikosi yalizuka katika karne za baadaye wakatiambapo wataalamu wa dini ya Kikristo walijishughulisha kwabidii zao zote kufikiria falsafa na hekima ya fumbo kuhusu Yesuna mengine yote kulingana na hiyo.Yaonekana kwambamwandishi fulani mpotofu alijaribu kujiokoa katika mushkili huoakaongeza mistari 12 ya mwisho katika Injili ya Mt. Marko naakanasibisha kwake kauli hii ya kwamba Yesu alionekana maraya mwisho akipaa mbinguni katika mwili huo huo.Mzushi huyo hakuiachilia mbali hata Injili ya Luka ambamonyongeza yake ya kiujanja ya maneno haya 'akachukuliwa juumbinguni' (24:51) yalimsaidia shabaha yake. Kwa njia hiyo yeyemwandishi huyo akaziba njia ya maulizo yoyote moja kwa moja.Kwa uchache tatizo moja la itikadi ya Kikristo likatatuliwa.Lakini, ole wao, kwa hasara gani? Kwa hasara ya kupotezamambo mema halisi yaliyohusikana na dhati tukufu ya YesuKristo. Uhakika halisi wa Yesu ulitolewa dhabihu juu madhabahuya uwongo na uzushi. Tangu hapo Ukristo uliendelea kusongambele katika safari ya kutoka kwenye hakika yake kuelekeakwenye ngano.Twajua sana ya kwamba Wayahudi hawakuwa na furaha nawalihangaika walipoukosa mwili wa Yesu Kristo.9 Walitakakuwa na hakika ya kwamba Yesu amekufa, na kwahiyo walihitajithibitisho la kifo linalokubaliwa na watu wote, yaani kuwapo kwamaiti yake. Malalamiko yao mbele ya Pilato yanadhihirishawaziwazi kwamba walikuwa na wasiwasi wa mwili wakekutokomea.10

Jawabu halisi la kawaida limo katika uhakika huu ya kwambakwa kuwa Kristo hakufa jinsi walivyoamini, hivyo swala la mwilikupotea halina maana, na tena sawa na ahadi yake yeye lazima__________________________9 Mathayo 28:11-1510 Mathayo 27:62-64

95

Kuhuika au Kufufuka

Page 102: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

angeondoka Judea kwenda kutafuta kondoo wa nyumba ya Israeliwaliopotea. Ni dhahiri yeye asingeweza kuonekana hapo tena.

MAONI YA WAISLAM WAAHMADIYYA:Maoni ya Waislam Waahmadiyya kuhusu mwili wa Yesu kwambaulikuwaje yako wazi, yanalingana na akili na ndiyo kweli kabisa.Jumuiya yetu inaeleza habari za Yesu na ilitendeka nini kwakekatika mwanga wa ukweli ukizingirwa na utukufu wake. Hakikahalisi ya Yesu Kristo ni nzuri sana kiasi hiki ya kwamba hainahaja ya kuipamba kwa kuizulia fumbo la aina hiyo. Uhakika wakeunazizingira taabu alizovumilia maisha yote kwa ajili yawanadamu wenye dhambi ambazo zilifikia upeo wakealipotundikwa msalabani; na kuokolewa katika kifo cha msalabaniilivyoahidiwa na Mungu Mrehemevu Mkarimu Mwenye uwezowote, na hatimaye akahama pale kwa kutafuta makabila kumiyaliyopotea ya Israeli.Hivyo basi, yeye si tu aliyafikishia ujumbe wa Mungu makabilamawili aliyozungumza nayo kabla hajatundikwa msalabani balina akayaendea vilevile makabila mengine ya Israeli na kwa njiahiyo akatimiza shabaha ya ujaji wake. Hapo ndipo akamaliziamatilaba ya kazi yake ya dini. Hizo ndizo hakika bora na tukufuza maisha ya Yesu.Mwanzilishi ya Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya, HadhratMirza Ghulam Ahmad wa Qadian alitangaza miaka mia mojatakriban hapo kabla ya kwamba Yesu, Nabii mkweli wa Mungu,alipona kifo juu ya msalaba jinsi ilivyoelezwa katika maongezihapo kabla. Mara ya kwanza katika historia ya Islam, HadhratMirza Ghulam Ahmad akiongozwa na Mwenyezi Munguakaondolea mbali pazia la mafumbo kwenye hakika zing’aazo zamaisha ya Yesu . Yeye ndiye aliyetangaza akikabili hasira yaWaislam wengi wakali wa kufuata desturi zao ya kwamba Yesu

96

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 103: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

hakufia msalabani wala hakupaa mbinguni, bali akaokolewakimwujiza akiwa hai pasipo kufia msalabani sawa na ahadi yaMungu. Ndipo yeye Yesu akahama hapo ili kuwatafuta kondoowa nyumba ya Israeli waliopotea jinsi alivyoahidi yeyemwenyewe.Kwa kufuata njia inayoelekea yaliyoipita makabila ya Israelimtu anaweza kukisia vizuri ya kuwa Yesu haikosi alisafiri nchiniAfghanistan akielekea Kashmir na sehemu nyingine za Indiaambako iliripotiwa Waisraeli wanakaa.Kuna ushuhuda madhubuti wa kihistoria ya kwambaWaafghanistani na Wakashimiri ndio vizazi vya makabila yaKiyahudi yaliyohamia nchi hizo. Hadhrat Mirza Ghulam Ahmadalifichua siri hii ya kuwa Yesu hatimaye alifariki na akazikwamjini Srinagar, Kashmir.Waahmadiyya, maelezo hayo ya kuvutia na ya kweli kwakufafanua kupotea kwa mwili wa Yesu katika nchi alimozaliwa,mara nyingine wanakataliwa ya kwamba hata kama Yesu hakufiamsalabani bali aliondolewa akiwa hai, hata hivyo ni kubahatishatu ya kwamba yeye alifunga safari ya hatari kutoka Judea kuelekeaKashmir. Wakisikia majibu hayo Waahmadiyya wanashangaakwamba safari ipi ni ndefu zaidi, ile ya kutoka Palestino kuelekeaKashmir ama ile ya kutoka ardhini kuelekea sehemu za mwishoza mbinguni. Isitoshe, Waahmadiyya wanashangaa ilikuwaje ileahadi ya Yesu Kristo ya kuwa yeye hana budi awaendee kondoowa nyumba ya Israeli waliopotea. Kama yeye aliondoka mojakwa moja Palestina kuelekea kule kukaa upande wa kuume waBaba yake, je alisahau wajibu wake ama haikuwezekana kwakekutimiza ahadi yake? Haikosi alisahau ahadi yake ama kamatulivyoshauri hapo kabla, je, yapasa kutazamiwa ya kuwa kondoowa nyumba ya Israeli waliopotea walikwisha tangulia mapemazaidi kupaa mbinguni ambako Yesu alikwenda kuwafuata?

97

Kuhuika au Kufufuka

Page 104: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

MIFANO YA KUPONEA CHUPUCHUPU:Kwa wale ambao bado wanaona ni mushkili kuamini kwambaYesu anaweza kupona kifo juu ya msalaba, twawaelekezakwenye mifano ya baadhi ya watu katika historia waliopona kifokatika hali ya hatari kabisa kabisa. Na kwa kuona mifano hiyo,habari ya Yesu jinsi tulivyofafanua siyo ya kipuuzi wala siyokwamba haiwezekani kuikubali. Kuna mifano mingi ya watuwaliothibitishwa baada ya uchunguzi wa kidaktari kuwa karibusana kufa, wakapona mauti katika hali ambamo mtu hawezikusalimika kwa kawaida.Mfano unaohakikishwa kwa maandiko ya kiserikali wa maharaja(sultani) wa eneo fulani katika India kabla ya kugawanyika BaraHindi unafaa utajwe hapa. Maharaja huyo alipatwa na shida kubwamno ambayo kwa kawaida ilikuwa haiwezekani kupona mauti.Maharaja huyo alilishwa sumu na mkewe na akaonekana amekufa.Sawa na desturi yao mwili wake ulipokuwa unachomwa motouliokuwa unawaka sana mara ikavuma dhoruba kali kabisa.Matokeo yake, yeye si tu akapona kifo bali baada ya kupiganiakesi yake katika mahakama ya sheria akarudishwa katika cheochake cha kuwa maharaja. Kisa chenyewe ni kama hivi:

98

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Ramendra Narayan Roy alikuwa mwanamfalme wa eneo la Bhowalambalo makao makuu ya Baraza yake ya hukumu yalikuwa Joydevpur.Ilidaiwa kwamba yeye alipewa sumu na akatangazwa kuwa maiti. Mwiliwake ukawekwa pale pachomwapo maiti panapowaka moto, mnamomei 1909. Mambo kadha yalielekeza kwamba mkewe ndiye alijaribukumwua. Mvua kubwa ya radi kabla haujakamilika mchomoikawafanya waliohusika kuchoma maiti kuondoka haraka pale nakuacha maiti. Mvua ilizima moto. Kundi moja la ma-Sadhu (watawawa dini ya Hindu) likapitia hapo ambapo walimkuta mtu akiwa hai.Hivyo yeye akaokolewa. Keshoye ilipogunduliwa na wale waliokuwawamekula njama kwamba mwili umetokomea pale wakachoma maitiya mtu mwingine ili kudhihirisha kwamba kweli mwanamfalmeamekwisha chomwa tayari.Masadhu hao waliomwokoa wakamchukua na kumpeleka mahali mbalimbali. Hiyo hali ya mwanamfalme kuwa karibu sana na mauti

Page 105: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Malaki ya mifano kama hiyo pengine ilitukia bila kuripotiwa.Twashukuru kwamba siku hizi zipo njia za kisasa za utibabu navyombo vya kueneza habari, basi mamia ya matukio ya aina hiyoyanapata kuripotiwa na kurekodiwa. Kama hiyo ndiyo kwelikuwahusu watu wa kawaida wa aina zote za jamii na kuhusu watuwa dini na khulka mbalimbali, kwa nini isiwezekane kumhusuYesu?Kama mtu yeyote ana nafasi ya kupona katika hali ya hatari kabisaambamo kwa dhahiri haiwezekani kusalimika, basi Yesu alikuwana nafasi hiyo zaidi kwa sababu ya ile hali maalum alimokuwamoyeye. Ni la kushangaza ya kwamba wenye mashakawanayakanusha maoni ya kwamba Yesu alipona kifo juu yamsalaba. Lakini mara moja wanakubali jambo lisilowezekanazaidi, la kipuuzi lisilo la kawaida kwamba yeye alipata kuhuikabaada ya kufa kabisa, na akaendelea kuwa maiti kwa siku tatumchana na usiku, waaminivyo.____________________________

11 The Bhowal Case, wakusanyaji: J.M.Mitra na R.C. Chakravarty, iliyoenezwana Peer & Sons, Calcutta.

99

Kuhuika au Kufufuka

ilimwondolea uwezo wa kukumbuka mambo, Lakini pole pole akaanzakupata uwezo na akatembelea mji wa Joydevpur baada ya kupita miakakumi na miwili. Mazingira ya mji wake yalimkumbusha mambo yotena akapata uwezo wa kukumbuka kikamilifu. Yeye alipodai katikamahakama ya kwamba yeye ndiye mrithi na mwenyewe wa BhowalEstate, mkewe na wengineo wakateta sana na kukaidi. Kila kundi katikahayo mawili lilipigania vikali kesi hiyo. Mashahidi zaidi ya elfu mojawalitoa ushahidi kwa ajili ya mwanamfalme na mia nne wakamtoleaushahidi mkewe. Tatizo hasa lilikuwa ni kuhakikisha kwamba bwanahuyo ndiye yuleyule mwanamfalme kwani watu wote walitambuakwamba huyo alikufa miaka kumi na miwili iliyopita.Mwanafalme akashinda kesi, kwani aliweza kueleza baadhi ya alamakatika mwili wa mkewe ambazo alama hizo asingeweza mtu kuzijuaisipokuwa mumewe tu. Basi akakabidhiwa usultani wake.11

Page 106: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Uchunguzi wa kitabibu pia umevutiwa na ile hali ya kuwa karibusana na mauti. Watu sabini na nane walichunguzwa waliosongakaribu sana mno na kifo. Wataalamu wa udaktari walikuwapowenyewe katika matukio asilimia themanini ama wakawasili palemara baada ya majaribu hayo. Ni la kuvutia ya kwamba asilimia41 katika hao walitoa taarifa ya kwamba walipokuwa karibu kufawalikuwa wamekwisha chukuliwa kuwa maiti 12

Kama wataalamu wa matibabu walio na vyombo vyote vyakuchunguza wanaweza kumtangaza mtu aliye hai kwambaamekwisha kufa tayari, unawezaje kutegemea ushuhuda wa mtualiyefadhaika ambaye akamwona Yesu akizirai na akamwaminikwamba amekufa? Isitoshe, alipomwona hai baadaye akafikirikwamba amehuika katika wafu; hiyo kabisa haiwezi kukubaliwa,ni kinyume cha uadilifu moja kwa moja.

_______________________

12 The Phenomenology of Near-Death Experiences, by Bruce Greyson M. D naIan Stevenson M.D., A.M. Psychiatry 137:10, Oktoba 1980

100

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 107: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

6 UTATU

Mpaka sasa tumechunguza mambo yaliyolazimisha kuzua imaniisiyo ya kweli ya kumfanya Yesu kuwa mungu na kazi yakeinavyosemekana katika Utatu akiwa Mwana wa Mungu. Lakininafsi ya tatu katika itikadi ya Kikristo ya Utatu, yaani RohoMtakatifu, ni vigumu kufahamika. Kwa nini 'Mbili katika Moja'isitoshe, na iko haja gani ya kuongeza nafsi hiyo ya tatu katikaitikadi ya kimsingi? Kiakili nafsi ya tatu kupewa nafasi katikaimani ya Kikristo ya kuwa mungu haiko sawa. Harnack,aliyefafanua suala hilo, anafikiri kwamba mwanzoni Ukristoulifahamika kuwa Umoja wa nafsi mbili za Mungu na Yesu.Baadaye kanisa likaongezwa humo likiitwa 'Roho' ili kulitiliamaana ya uungu ambao pasipo huo nyongeza hiyo ya tatuingeonekana tupu isiyovutia. Hiyo pia ikatenda kazi ya zana dhidiya dini ya kiyahudi.1 Kuhusu habari hiyo, Rev K.E. Kirk anasemakatika makala yake juu ya The Evolution of the Doctrine of Trinitykama ifuatavyo :

Yeye anaendelea kuainisha theolojia ya Kikristo kushindwa kabisakuleta hoja ya kiakili kuthibitisha itikadi ya Utatu, na kwambautatu wa Kikristo unaweza kuelezwa kuwa hasa itikadi katika___________________________1 Harnack, 'Constitution and Law of the church', E.T.uk 264

101

Kwa kawaida twawageukia waandishi wa zama hizo ili kujua wanayomisingi ipi ya itikadi yao. Twashangaa ya kwamba tunalazimika kukirikuwa hawana msingi wowote. Suala walilolikabili halikuwa ni kwanini ziwepo nafsi tatu, bali lilikuwa kwa nini zisiwepo?'

Page 108: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

uwili ambamo kiliongezwa kitu cha tatu kilicho tofauti kabisa ilikuchora picha kamilifu zaidi.2

Sisi tunaamini ya kwamba nafsi hiyo (Roho Mtakatifu) ilipatakukua hatua kwa hatua kwa kuathirika na falsafa na hadithi zakipagani zisizo na msingi ambazo zilijaa tele tele katika ufalmewa Kirumi. Kubadilishana mawazo na hao watu bila shakakuliwahimiza kumwamulia Roho Mtakatifu kiwango chake. Kwakuwa upo ushuhuda wa kutosha sana kwamba zipo imani namadhehebu zilizomfahamu Mungu kuwa ameungwa na dhati tatu,kwahiyo ni vugumu kutafuta chanzo hasa cha itikadi ya Kikristokatika Utatu. Kwani kama kwa vyovyote mbili zaweza kuwa moja,na moja kuwa mbili kwa nini tatu zisiweze kuwa moja pia? Nijuu ya wataalamu wa uchunguzi kugundua barabara kwamba linina namna gani nafsi ya tatu ya mungu wa Kikristo ilipatakuimarika katika mitholojia ya Kikristo. Lakini habari hiyo hivisasa haihusikani na mazungumzo yetu. Hapa twanuia kuchunguzaupuuzi wa madai kama hayo ambayo yanakataliwa na fahamu yabinadamu moja kwa moja. Tabia ya asili ya mtu inakataa katakatafikara zinazojipinga na zenye hitilafu.

UHUSIANO WA NAFSI TATU ZENYEWE KWAZENYEYWE:Mtu anapotaka kutambua namna zinavyohusiana nafsi hizo tatuzenyewe kwa zenyewe ndizo hizi zifuatazo:

a. Hizo ndizo jiha mbalimbali za dhati moja.b. Hizo ni dhati tatu mbalimbali zinazoshirikiana kwa

usawa daima milele.c. Hizo ni dhati tatu ambazo kila moja katika hizo ina

baadhi ya sifa za pekee ambamo nyingine hazishirikianinazo kikamilifu.

______________________2. 'Essays on the Trinity and the Incarnation', mkusanyaji A.E. J. Rawlinson,Longmans, London ( 1928 )

102

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 109: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

d. Hizo ni dhati tatu katika moja, na kila moja inazo sifazilezile na nguvu zilezile, na zote hizo zimeunganikapamoja, na kazi zao pia ni zilezile pasipo tofauti yoyoteile iwayo.

HALI AU JIHA MBALI MBALI ZA NAFSI MOJA:Kuhusu jambo la kwanza linalowezekana miongoni mwa hayomanne hapo juu hakuna haja ya kulijadili zaidi, kwani hamnasiku hizi Mkristo yeyote ambaye angemwamini Yesu kuwa haliama jiha moja ya Mungu kuliko kuwa nafsi moja maalum.Wanaouamini utatu wanasisitiza kuwepo kwa nafsi tatu tofautizilizounganika na zikawa moja.Pindi mtu anapokubali habari hiyo ya nafsi moja yenye hali mbalimbali zikidhihirika wakati mmoja, papo hapo itikadi ya Utatu,yaani miungu watatu katika mmoja, inatokomea, pasipo kubakiautatu wowote kabisa. Basi atakayebakia ni Mungu Baba ambayekwa kuona huruma atakufa kwa ajili ya madhambi ya watu. Nahiyo itakuwa ni hali ya kupita ya nafsi hiyohiyo. Hali mbalimbalisiyo nafsi, wala jiha mbalimbali hazimaanishi dhati tofauti. Mtuyeyote anaweza kupitia hali mbalimbali bila ya kugawanyikakatika wawili, watatu ama watu wengi. Hivyo, kama Munguakiamua kufa kwa ajili ya watu wenye dhambi, basi ni Mungumwenyewe atakayekufa siyo hali zake fulani tu zitakazokufa.Basi kuhusu habari tunayozungumzia, ile hali ya Mungu ambayoilifanya kazi kubwa sana ya kutoa dhabihu yake kwa ajili ya watuwenye dhambi inaweza kufahamika kuwa kazi ya sifa moja tuyake. Hivyo, kama huruma ya Mungu peke yake ikihesabiwakuwa 'nafsi' na nafsi hiyo ikapewa jina Yesu Kristo, hapo kilekilichokufa ni 'huruma' ya Mungu. Upingamizi mkubwa uliojehuu ya kwamba huruma ya Mungu ikiwahurumia watu wenyedhambi inajiua. Hiyo inamaanisha ya kwamba Munguhakubakiwa na huruma kwa siku tatu mchana na usiku.

103

Utatu

Page 110: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kumbukeni kwamba hapo Yesu hakuhesabiwa nafsi tofauti yakujitegemea, bali ni sifa ama hali ya huruma ya Mungu ambayohuruma hiyo ikadhihirika kwa sura ya mtu. Na mtu huyo kwavyovyote ndiye Mungu mmoja asiyeweza kugawanyika. Basikama chochote kilikufa katika kisa hicho, hicho ni MunguMwenyewe ama ni sifa yake ya Huruma iliyofanya kazi kubwasana katika tukio hilo. Basi hatuna hiari yoyote isipokuwa kuaminikwamba Huruma ya Mungu ilikufa ama Mungu Mwenye HurumaMwenyewe Alikufa.Matatizo mengi yatazuka kutokana na madai ya kwamba hali ausifa fulani inaweza kufutika kwa muda ama kwa kudumu. Habarihiyo inaweza kueleweka vizuri ikilinganishwa na majaribu yabinadamu. Mtu anaweza kupoteza nguvu yake ya kuona au kusikiakwa muda au daima, lakini mtu huyo bado atabaki kuwa yuleyule mtu aliye hai. Kifo cha nguvu moja ya mtu kwa hakika ninusu kifo cha mtu huyo. Hatimaye mwenye kupata hasara amakusumbuka anakuwa mtu yuleyule.

NAFSI MBALI MBALI ZIKISHIRIKIANA KATIKAUMILELE:Kama sehemu za mungu wa Kikristo ni nafsi tatu mbalimbalizikishirikiana pamoja milele, hapo swali litazuka kuhusu uhusianowa ndani wa nafsi hizo. Kama hizo ni tatu daima zikifanyizamungu mmoja, haikosi kila moja katika hizo tatu itakuwa na fikrayake na upendo wake binafsi hata kwamba taabu ya mmoja, kamaanaweza kutaabika, ni taabu yake tu. Nafsi nyingine mbilizinaweza kuihurumia tu bila ya kushirikiana katika shida yake.Naam, haiwezekani kuwaza namna Mungu anavyofikiri nakuamua, lakini madai haya ya kwamba yeye kwa hakika ni nafsitatu zilizounganika pamoja kufanyiza Mungu mmoja yanatupatiahaki ya kujaribu kutafuta uhusiano wa ndani baina ya mifumomitatu ya kujitegemea ya kufikiria.

104

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 111: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Mfano wa kwanza unaweza kuwa wa mtoto mmoja aliyezaliwana vichwa vitatu. Hali hiyo mbaya kupita kiasi inamaanisha yakwamba huyo ni mtu mmoja kwa sababu kuna kiwiliwili kimoja,mikono miwili na miguu miwili, lakini vichwa vitatu vinaletamatatizo yasiyoweza kuelezeka hakika hasa ya kila kichwa katikahivyo vitatu. Kama viumbe visivyo vya kawaida vikiishi mudawa kutosha mpaka viweze kusema na kujieleza, hapo tu ndipotwaweza kuwauliza yanayofanyika katika vichwa vyao vitatumbali mbali. Bila ya kuwa na ujuzi huo haiwezekani kuamuahuyo ndiye mtu mmoja ambaye anashirikiana katika mawazomatatu ama ni watu watatu wanaoshirikiana katika mwili mmoja.Ni la ajabu ya kwamba jiha hiyo ya muhimu sana ya itikadi yaKikristo haikuelezwa kabisa katika maandiko. Naam, kuhusuKristo na Roho Mtakatifu kuna ushuhuda mwingi wa kuhakikishaya kuwa hao ni wawili mbalimbali wasioshirikiana katika fikarawala katika maono. La sivyo, itakuwa vigumu kufahamumadhihirisho ya Roho Mtakatifu tofauti kabisa na Kristo, hususankatika kipindi ambamo Kristo alikuwa amefungwa katika mwiliwa mtu.Maswali ambayo yangezuka kuhusu kilichotendeka kwa Kristo,katika muda wa kusumbuka kwake, kwa kulinganishwa nasehemu mbili nyingine za Mungu wa Kikristo, ni haya yafuatayo:

1. Je, nafsi nyingine mbili, Mungu Baba na RohoMtakatifu, zilishirikiana kwa njia yoyote katika mwiliwa Yesu Kristo au katika majaribu yake kwa kulinganana mwili huo?

2. Je, Yesu peke yake alikuwa ndani ya mwili huo, nakwa hiyo yeye hakushirikiana na nafsi nyingine mbiliza Utatu katika majaribu yake kwa kulingana na mwilihuo?

Matokeo ya hilo la kwanza yamekwisha zungumzwa tayari. Nakuhusu hilo la pili tatizo jingine tena linazuka kuhusu uhusiano

105

Utatu

Page 112: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wa Yesu na nafsi nyingine mbili za utatu katika muda wa Yesukuwa katika mwili wa mtu. Je, katika muda huo wote Yesualitengwa kikamilifu na nafsi nyingine mbili na akajitegemea,ama bado alibaki kuwa sehemu isiyoweza kutengwa na nyinginembili isipokuwa tu yeye akashika makao yake katika mwili wamtu pasipo kushirikiana na wenzake wawili? Sasa tunalo swalijingine tena la kulijibu:

3. Je, uungu wake mzima-mzima ulikuwamo ndani yamwili wake wa kibinadamu, ama huo ulijitokeza tu njekutoka kwenye 'sura' ya Mungu Baba na Roho Mtakatifuambayo alishirikiana nao katika hiyo, kama kajidolekadogo kale kanakojitokeza nje ya mwili wa viduduvidogo vidogo mno visivyoonekana pasipo kutumiahadubini kali?

Jambo hilo litatufanya tuamini pia ya kwamba katika kipindi hichoYesu alikuwa mkubwa kuliko wenzake wawili, kwani yeyealishirikiana kwa usawa pamoja na Mungu Baba na RohoMtakatifu katika 'mwili' wa kiungu, lakini hao wawilihawakushirikiana naye katika 'kajidole' kale kalikojitokeza ka'mwili' wa mtu.Hivyo basi, ili kurahisisha kuelewa habari yenyewe twajaribukufafanua hitilafu zilizomo humo na mambo yasiyoelewekaakilini kwa kueleza hali mbalimbali za kukisia ili kutafuta ukweli.Naam, mifano hii isichukuliwe na wasomaji kuwa hasa ndivyoilivyotendeka.Suala lililoko mbele yetu ni kwamba je, yupo mtu mmojaanayedhihirisha sifa tatu ama anapitia hali tatu tofauti. Hiyoitazusha swali la kufikiria shauri ya 'Watatu katika Mmoja' na'Mmoja katika Watatu', hususan kwa jiha malimbali tofauti, nayule yule mmoja kudhihirisha mienendo na hali mbalimbali.Hali hiyo imekwisha elezwa kirefu katika mlango uliopita. Hapaiko haja ya kusisitiza tena habari hii ya kwamba ikiwa mtu mmoja

106

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 113: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ama dhati moja inadhihirisha hali mbalimbali, basi haiwezikuzidhihirisha hali hizo tofauti wakati huohuo mmoja bila yakujigawa katika sehemu mbalimbali.Kwa mfano, chukua maji kiasi fulani maalum. Maji hayoyanaweza kugeuzwa yote kuwa mvuke ama barafu pasipokubakiza sura ya maji. Kama kunahitajika kuyaona katika surazote tatu, hamna budi kuyagawa hayo maji katika sehemu tatu ilitheluthi moja igeuzwe kuwa barafu na theluthi nyingine kuwamvuke na theluthi moja ibakie kuwa maji. Kila sura itakuwatofauti na sura ya sehemu nyinginezo wala yoyote katika hizohaitashirikiana na nyingine mbili wakati uleule mmoja. Kiasihicho cha maji chaweza kugawanywa katika hali tatu, lakiniukubwa wa kila sehemu utakuwa mdogo kuliko yale maji kwajumla yaliyochukuliwa mwanzoni, wala hamna yeyote awayeawezaye kusema kwamba hayo ni 'moja katika tatu' na 'tatu katikamoja'. Kadhalika, basi, kudhihirika Kristo kwa sura ya binadamuya Yesu, ilhali aliendelea kuungika na Yesu-mtu na Mungu Baba,haiwezekani asilani kueleweka akilini.Wanadamu wote wameumbwa kwa vitu vilevile vimoja, lakinikufanana kwao wao kwa wao hakuwafanyi kuwa mtu mmojapekee. Sifa zao tofauti, dhati zao mbalimbali, na wote hao kuwepombalimbali vinawagawa na wakagawanyika kuishi kila mmojapeke yake, ijapokuwa wote hao wameumbwa kutokana na kitukilekile kimoja. Huwezi kuwaita 'mmoja katika bilioni tano' na'bilioni tano katika mmoja' juu ya wote hao kushirikiana katikauanadamu.Hebu sasa na tuchunguze suala hilo kwa jiha nyingine. Kamakwa muda fulani maalum Yesu alikuwa ametengana na MunguBaba upande mmoja na katengana na Roho Mtakatifu upandemwingine na akapambanuka mbali na hao wawili, basi ni sehemuzipi na maeneo yepi ambamo Yesu alikuwapo peke yake?Kumbukeni kwamba hapo Yesu anatakiwa kukaa peke yakepasipo kubaki kuunganika na Baba na Roho Mtakatifu, hatakwamba kujitolea kwake kwa nduguze wanadamu, ama tuseme

107

Utatu

Page 114: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

nusu-nduguze binadamu, kufikiriwe kuwa majaribu yake binafsitofauti kabisa na yale ya Mungu Baba na Roho Mtakatifu.Matokeo yake ni sisi kufikiria ya kwamba Kristo peke yakealihamisha nia yake ama fikra yake kutilia mwili wa udongo waYesu-mtu. Pia itafahamika kwamba yeye Kristo alipitia majaribupasipo kushirikiana na sehemu nyingine mbili za utatuwa Kikristo. Inakanganya, au sivyo ?

NAFSI MBALI MBALI ZENYE SIFA TOFAUTI KABISAKama Mungu Baba, Yesu na Roho Mtakatifu ni nafsi tatu zenyesifa mbali mbali kabisa ambazo katika hizo hazishirikiani zotetatu, hapo hizo tatu haziwezi kuhesabiwa kuwa 'Tatu katika moja'na 'Moja katika tatu'. Utatu unaweza kuunganika ukawa umojahasa hapo tu ambapo nafsi zote tatu zinakuwa na mienendo ileile na sifa zile zile na kazi zile zile na nguvu zile zile za aina mojawala hamna hata sifa moja maalum inayoitenga moja na nafsinyingine mbili.Hiyo inaweza kufananishwa kiasi fulani na watoto watatuwaliozaliwa kutokana na mimba moja ambao wanafanana sanasana kabisa, hata fikra zao, maono yao na kazi za viungo vyaovinaafikiana mno hata kwamba majaribu ya kila mmoja wao nimajaribu ya wote hao kikamilifu bila tofauti yoyote. Kama ndivyoilivyo, hapo Utatu wa Mungu, Mwana na Roho Mtakatifu utawezakueleweka zaidi. Lakini bado tatizo litabaki kuhusu miili mitatuyenye nafsi hizo tatu zinazofanana kwa kila jiha kikamilifu. Lakinihiyo haiafikiani na wazo la Kikristo juu ya Utatu. Mtu akiangaliamara ya pili analazimika kuwaza picha ya mwili mmoja wenyenafsi tatu mle ndani. Lakini umoja huo wa watatu unawezakuzingatiwa hapo tu ambapo mwili mmoja ukiweza kuwa na nafsitatu ndani yake, jambo ambalo linazua matatizo mengi. Naam,kwa kuwa Mungu hana mwili, kwahiyo mithali ya mwili wakibinadamu ilivyoshauriwa nyuma haifai. Twajua sana yakwamba Mungu hana mwili, lakini bado tatizo litabakia kuhusu

108

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 115: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

dhati tatu za kiroho zilizo kama wale watatu waliozaliwa kutokanana mimba moja wanaofanana, wanaokuwepo mbalimbali lakiniwanaungana katika mambo mengine yote.Tatizo jingine litakalowakabili hao watatu wa kukisiwa ni namnawanavyohusiana wao kwa wao katika habari ya ibada. Je, nafsizote tatu za 'Tatu katika Moja' zinaabudiana zenyewe kwazenyewe? Je, zote hizo zinapokea ibada za viumbe vyao, lakinihaziabudiani zenyewe kwa zenyewe?Ingawaje Yesu Kristo anatajwa mara kwa mara katika AganoJipya akimwabudu Mungu Baba na anawasihi wengine piakumwabudu Yeye. Lakini haikuelezwa kuhusu Roho Mtakatifuakimwabudu Mungu Baba. Tena hamna kabisa habari ya Yesukujaribu kuwaelekeza wengine kumwabudu yeye walakumwabudu Roho Mtakatifu sawa na taarifa ya Agano Jipya. Mtuanakanganywa na kutokutajwa kuabudiwa kwa Yesu na RohoMtakatifu katika Agano Jipya, lakini habari ya Mungu Babakuabudiwa imetajwa mara kwa mara.Ijapokuwa ni desturi ya kawaida ya Wakristo kumwabudu Yesukuwa 'Mwana wa Mungu' pamoja na kumwabudu Mungu Baba,hata hivyo hamna taarifa yoyote iliyohifadhiwa katika maandikoya kwamba mwanafunzi yeyote wa Yesu Kristo aliwahikumwabudu yeye, ama Yesu akawaelekeza kufanya hivyo katikamuda wote aliokaa ardhini. Hata kama yeye angelifanya hivyo,maswali mengi yasiyoweza kujibika yangezuka. Ndivyo ilivyohali ya Roho Mtakatifu, yeye naye hakumtaka yeyote kumwabuduyeye. Kwa nini?

Ile hali imekwisha chunguzwa tayari kiasi fulani ambako haowalikuwa 'Tatu katika Moja' katika maana hii ya kwambautambuzi wao wa kuwapo kwao ulikuwa mmoja juu yakugawanyika katika hali ama jiha tatu. Dhati ya aina hiyo haiwezikiakili kuhesabiwa kuwa 'watu watatu katika mmoja'. Aidha, haliama jiha haziabudiwi, wala hazijiabudu. Kwa kuwatambua kuwawatu watatu tofauti, wanalazimika kujijua wanakuwapo kwa

109

Utatu

Page 116: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kujitegemea. La sivyo, suala la kujitaja ama kuwataja wenginekwa kusema 'Mimi', 'Wewe' na 'Yeye' halizuki asilani.Utatu ukitumika kwa dhati moja humaanisha sifa tu basi. Na sifakwa kweli hazina kikomo, haziwezi kuwa tatu tu. Tujue tusijue,Mungu anazo sifa nyingi teletele.Kwa kumalizia mazungumzo haya, twasisitiza mara nyingine yakwamba suala la wao kuabudu wao kwa wao linaweza kuzukahapo tu ambapo hao wangekuwa watu watatu wenye madarakambalimbali na sifa tofauti.Katika shauri hiyo, mmoja tu ataabudiwa na wengine wawiliwakiwa wenye daraja dogo watatazamiwa kumwabudu yeye. Hilolakubaliwa, lakini ule 'Umoja katika utatu' utatoweka. Hamnanjia yoyote ya kuwa na 'Tatu katika Moja' na 'Moja katika Tatu',zote mbili hizo, wakati huohuo mmoja.Hiyo imenikumbusha kisa kimoja cha kuchekesha ambachoningependa kuwaambieni. Imesimuliwa ya kwamba wakatiTamerlane alipovamia mji wa Baghdad alifurahiwa na BwanaJoha, mcheshi wa mahakama, mpaka akaamua kumchukuapamoja naye kama mateka na akampa kazi maalum ya kuwamchekeshaji mkuu wa korti. Inasemekana safari moja Johaakajawa na shauku ya kula nyama akiwa peke yake bilakushirikiana na wengine. Akashikwa na kiherehere hicho sanahadi hakuweza kujizuia. Basi akanunua nyama kilo mbili nzurikabisa kutoka kwa muuza nyama. Alipomkabidhi mkewe nyamahiyo akaagiza kuichoma vizuri sana, lakini akamuambia hakunaatakayeila isipokuwa yeye peke yake, yaani Joha, hata mkewehawezi kuionja. Sasa kwa bahati mbaya, mkewe alipokwisha tukuichoma vizuri sana nyama hiyo, ghafula wakaja nduguze kadhakumtembelea. Hiyo ilikuwa furaha aliyopata ghafula, lakini ikawahabari mbaya ya kwa Joha. Harufu nzuri ya kuvutia iliwashindahao ndugu za mkewe, na matokeo ndiyo unaweza kukisia. Wakalana kumaliza mpaka kipande cha mwisho kisha wakamwaga dadayao ambaye sasa akaanza kuhangaika. Lakini akajituliza kablahajawasili nyumbani Bwana Joha, maana

110

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 117: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

alishawaza hila ama udhuru fulani ili kujiokoa katika hali hiyongumu. Joha alipoingia na akasikia harufu nzuri ya kuvutia yanyama iliyochomwa ambayo ilikwisha liwa tayari, akamwagizamkewe kuleta haraka hiyo nyama. Hapo mkewe akiashiria kwenyepaka wa Joha aliyekuwa amemfuga kwa shauku sana, akasema:Toa nyama yako kutoka katika paka huyu, ukiweza. Maananilipokuwa nimeshughulika, huyu akaila yote. Hapo haraka sanaJoha akamshika paka na kumpima katika mizani. Kumbe uzitowake ulikuwa kilo mbili barabara. Basi kamwelekea mkewe kwaupole na akamuuliza: Mke wangu mpenzi, hakika nimekubaliulivyosema, lakini kama hiyo ndiyo nyama yangu, basi yuko wapipaka wangu; na kama huyu ndiye paka wangu, basi nyama yanguiko wapi!Achilia mbali vichekesho, nisingependa kujadili suala hilo juuya msingi wa mafunzo halisi na ya kweli ya Yesu. Maandikohaya shabaha yake hasa ni kuchunguza itikadi za sasa hivi zaKikristo ambazo twaamini kwamba zimepotoka na kwenda mbalikabisa na mafunzo ya asili ya Yesu.Tukiisha kanusha habari ya Yesu kuabudiwa ndani ya Biblia,inatulazimu kufafanua sehemu ya pekee ndani ya Biblia, yaaniLuka 24:52 ambamo Yesu anaonekana aliabudiwa. Wenginewanasema ya kuwa mstari huo unatoa ushahidi ya kwamba Yesualiwahimiza kumwabudu. Wataalamu wa Kikristo wa zama hiziwanaelewa sana ya kwamba mistari hiyo imekwisha hakikishwakuwa ya uwongo iliyoongezwa baadaye wala hakuna haki yakuihesabu mistari hiyo kuwa sehemu halisi ya Injili ya Mt. Luka.Hebu sasa tugeukie kwa suala la desturi ya kawaida kwamba jehiyo inathibitika kwa ushuhuda uliomo katika Injili ama hapana.Sawa na desturi ya kawaida, Yesu anaabudiwa akiwa 'Mwanawa Mungu' katika madhehebu mengi ya Kikristo. Hata hivyo wotehao wanakiri ya kwamba Yesu huyohuyo mwenyewe alikuwaanamwabudu Mungu Baba peke yake.Bure kabisa nimewauliza mara nyingi wataalamu wa Kikristowenye ujuzi mwingi ya kwamba kwa nini Yesu alimwabudu

111

Utatu

Page 118: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Mungu Baba ikiwa yeye mwenyewe alikuwa sehemu ya Munguisiyoweza kutenguka na alikuwa ameunganika naye kabisakikamilifu kwa kuleta maana ya umoja japo nafsi tatu zilikuwepo?Je siku yoyote aliwahi kumwabudu Roho Mtakatifu pia aliye nafsiya tatu katika Utatu? Je, alijiabudu wakati wowote? Je, RohoMtakatifu alimwabudu Yesu siku yoyote? Na je, Baba aliwahisiku yoyote kumwabudu yeyote miongoni mwa wawili wenginewa Utatu? Kama hapana kwa nini? Pengine majibu ya suala hiloyatawalazimisha Wakristo kukiri ya kwamba Baba anacho cheokikubwa zaidi kuliko nafsi mbili nyingine za Utatu. Inathibitikakutokana na hiyo ya kwamba sehemu tatu za Utatu haziko sawakatika daraja. Hivyo, hao ndio 'Watatu katika Watatu' kama kwavyovyote wako watatu, lakini siyo kabisa 'Watatu katika Mmoja'.Wakati mwingine wataalamu wa Kikristo wanapokabiliwa naswali la Yesu, wanayemwamini kuwa Mwana wa Mungu,kumwabudu Mungu Baba, husema Yesu-mtu ndiyealiyemwabudu Mungu Baba, siye Yesu Mwana aliyemwabuduYeye. Hiyo inatupeleka nyuma tena kwenye mazungumzotuliyokwisha fafanua tayari. Je, mwili huohuo mmoja wa Yesuulikaliwa na nafsi mbili, moja yenye dhamira ya binadamu nanyingine ya Mwana wa Mungu?Aidha, kwa nini mtu ndani ya Yesu aliepa na kumpuzilia mbalikabisa Mwana wa Mungu aliyekuwemo ndani yake asimwabuduKristo hata mara moja? Huyo huyo Yesu-mtu alitakiwakumwabudu Roho Mtakatifu pia aliye nafsi ya tatu katika Utatu,lakini mbona hakufanya hivyo katu!Ibada ni tendo la moyo na roho ambalo pengine huoneshwa kwaalama za kimwili, lakini lina mizizi yake katika fahamu na maonoya dhamiri ya mtu. Hivyo inapaswa kungunduliwa nani aliabudupindi Yesu Kristo alipomwabudu Mungu. Tumekwisha elezajambo hilo hapo kabla pamoja na matatizo yake ya kwambaKristo, Mwana wa Mungu, ndiye aliyemwabudu Mungu.Kinyume chake, kama alikuwa ni mtu aliyemwabudu MunguBaba, na huyo mtu hakumwabudu Kristo, kwa nini basi Wakristo

112

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 119: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wanaukaidi mfano huo bora wa Yesu mwenyewe? Kwa niniwanaanza kumwabudu Kristo pamoja na Mungu, ilhali Yesu-mtuhakumwabudu mwenzake Kristo japo alikaa karibu yake mno.

NAFSI TOFAUTI ZENYE SIFA ZIFANANAZO ZILIZOSAWA:Hebu tuchunguze mara nyingine tena, lakini safari hii kwa jihatofauti kabisa, kanuni ya 'Tatu katika Moja' ndani ya Utatu,tukizichukua kuwa dhati tatu tofauti lakini zenye sifa zilezilezifananazo kabisa kikamilifu. Hapa hatuzungumzii dhati mojayenye sifa mbalimbali zilizounganika pamoja, bali twazungumziadhati tatu kama watoto watatu waliozaliwa katika mimba moja.Twazungumzia hao watatu ambao wanafanana wao kwa wao sanakabisa hata kwamba kufanana kwao hakuishii tu katika kufananaumbo na sura, bali hata fikara zao na maono yao pia ni ya ainamoja. Wanashirikiana katika fikira zao, maono yao na majaribuyao kwa namna moja kabisa. Hapo mtu hana budi kukiri yakwamba nafsi mbili katika utatu hazina kazi tena, ni bure kabisa.Kama hizo mbili zikiondolewa mbali, hazitaleta kasoro yoyoteile iwayo kwa nafsi iliyobaki ya Utatu ambayo nafsi hiyo itakuwakamilifu peke yake.Kurani Tukufu pia inauliza swali hilo inapodokeza ya kwambakama Mungu akiamua kumuangamiza na kumfutilia mbali kabisaYesu Kristo na Roho Mtakatifu, tofauti gani itatokea kwa utukufuwake, Umilele wake na Ukamilifu wake, na ni nani awezayekumzuia Yeye asifanye hivyo (5:18). Hiyo inamaanisha yakwamba sifa zote za Mungu zitaendelea kufanya kazi milele nakwa hivyo itikadi ya Utatu ilivyoelezwa hivi sasa haina maanawala haihitajiki.

113

Utatu

Page 120: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Lakini kama ifikiriwe ya kwamba dhati tatu hizo za utatuzinafanya kazi mbalimbali, hapo bila shaka sehemu zote tatu zautatu zitahitajika ili kufanyiza Mungu. Hata hivyo hapo patakuwana Miungu watatu tofauti wanaosaidiana wao kwa wao na kukaapamoja kwa amani kamilifu na hapo wanaweza kuhesabiwa'Miungu Watatu katika Watatu' wala hapana 'Miungu Watatukatika Mmoja'.

Na kama isemwe ya kuwa Utatu ndiyo kama mtu mmoja mwenyeviungo mbalimbali vinavyofanya kazi tofauti vikiunganika ndaniya mtu mmoja, hapo bila shaka Umoja utakuwepo lakini Utatuutatoweka. Lakini tukumbuke ya kwamba hatuzungumzii hapamtu mmoja mwenye viungo kadha vinavyofanya kazi, bali watuwatatu wanaofanana kabisa kwa kila hali na kila jiha, na kilammoja akifanya kazi hizohizo za aina moja na hata hivyo kilamoja anabaki kuwa mtu binafsi peke yake. Iliyojadiliwa ni haliya mtu mmoja mwenye viungo kadha. Mpaka hapo sawa, hamnakilicho kinyume cha akili. Lakini viungo vikihesabiwa kuwa watuna palepale watu hao wote wakiwa pamoja wanafanyiza mtummoja kwa jumla, hapo habari hiyo inakuwa kinyume cha akiliwala haiwezi kukubalika. Ni sawa kuwa kila kiungo kina kuwapokwake, lakini kuwapo huko ndiyo sehemu tu ya mtu ambaye situ kwamba anacho kiungo hicho tu kimoja bali anavyo viungovingine pia. Viungo hivyo vikiwa pamoja ndani ya mtu huitwa'mtu' kwa jumla. Naam, baadhi ya viungo vinafanya kazi yamuhimu zaidi na vingine vina kazi si ya muhimu sana, na mtuanabaki kuwa mtu bila ya viungo hivyo vyenye kazi isiyo muhimu,lakini mtu huyo atakuwa si mkamilifu, bali atakuwa na kasorofulani. Mtu mkamilifu hupaswa kuwa na viungo vyote vileanavyokuwa navyo mtu yeyote kikawaida, na jumla ya viungohivyo hufanyiza mtu mkamilifu.Tukichukua mfano wa mtu mmoja aitwaye Paulo, mtu hawezikusema ya kwamba kwa kuwa ini, moyo, mapafu na mafigo yaPaulo ni vitu maalum mbalimbali ambavyo vina kazi mbalimbali,

114

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 121: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

basi kwa hiyo hivyo ni nafsi mbalimbali zilizokamilika ambazokila nafsi katika hizo ni sawasawa na Paulo. Kila kiungo chawezakuwa Paulo hapo tu ambapo kwa mfano mafigo peke yake yafanyekazi zote kwa jumla anazofanya Paulo, na kadhalika kila kiungokiwe hivyo hivyo. Jambo hilo linamaanisha ya kwamba viungohivyo vikikosekana, hakuna badiliko litakalotokea katika Paulo.Au tuseme kwamba Paulo bado atabaki kuwa Paulo kikamilifukama viungo vyake yaani mapafu, moyo, mafigo na ubongo, kwahakika viungo vyote vikiondolewa mbali. Hiyo ni kwa sababukatika ukaguzi wa mwisho viungo hivyo vyote vinafanana, nadhati ya Paulo inabakia tu pale pasipo kujali viungo hivyo vipoama havipo.Kama hiyo ndiyo picha ya 'Tatu katika Moja', basi si sawa kujaribukuchambua itikadi za Kikristo kwa kutumia mantiki na akili. Hapoakili itakayotumika kuhusu itikadi ya Kikristo ya siku hizi ndiyoakili ya wanawake wachawi wa Macbeth wanaposema: 'Safindiyo chafu na chafu ndiyo safi'.

115

Utatu

Page 122: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

7 MAGEUZI YENYE KUENDELEA YA UKRISTO

Imani ya Utatu ambayo ndiyo sehemu ya muhimu kabisa yaUkristo haikuwepo katika Ukristo katika zama za uhai wa YesuKristo. Sana sana unaweza kuruhusu kukubali ya kwamba imanihiyo ilianzia kuzuka baada ya tukio la Msalaba. Ilichukua karnenyingi kufikia sura ya mwisho waziwazi lakini isiyowezakuelezeka. Hiyo ikapitia majadiliano machungu sana na ubishimkubwa baina ya wataalamu wa Kikristo na wana falsafa wadini mbalimbali, utamaduni tofauti na mafundisho yaliyotokeazamani.Dini ya Kikristo iliathirika na visa vya kubuniwa na simulizi zanchi zilizoupokea Ukristo katika zama za mwanzoni. Shina hasala Ukristo lililouhifadhi na kulea ukuaji wa itikadi za Kikristo nafalsafa yake katika zama za kale lilikuwa ni shina la Kiyahudi.Athari ya Kiyahudi ilikuwa kubwa zaidi katika muda wote wamwanzo wa historia ya Ukristo. Wanafunzi wa Yesu waliojifunzana kutambua Ukristo moja kwa moja kutoka kwa Yesu nawakaushuhudia katika sura ya maisha yake, walihusikana na asilihiyo ya Kiyahudi. Hao walikuwa wasimamizi wa kwanza waUkristo na waliimarika sana katika mwanga wa maagizo ya Yesuna namna alivyoishi. Ndio hao walioshuhudia tukio la msalabana wakajionea Yesu akipona jaribio hilo la mauaji.

WAFUASI WA KWANZA WA YESU:Wakristo wa kale wanaonekana waligawanyika kimsingi kuhusuasili ya Yesu na kwamba wafungamane na sheria ya Musa amahapana. Katika kipindi cha pili cha maendeleo ya Ukristo, Mt.Paulo akawa mtu muhimu kabisa kwa kuupatia Ukristo falsafa

116

Page 123: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

na fikira mpya. Kulikuwa hitilafu za kimsingi baina ya Paulo naJames Mnyofu. Wakati James aliposimamia Kanisa la Jerusalem,Paulo alikuwa anahubiri katika nchi za Magharibi hususan walewasiokuwa Wayahudi. Kanisa la Magharibi likapata mageuzi namaendeleo kulingana na maoni ya Paulo kuhusu itikadi, lakiniKanisa katika Jerusalemu likasonga mbele kushikamana namafundisho katika umoja wa Mungu.Natija moja ya mahubiri ya James ndiyo Waebioni, dhehebuambalo jina lake limechukuliwa kutoka kwa neno Ebionim laKiebrania, maana yake 'wapole' au 'maskini'. Hao walikuwaWakristo waliotokana na Wayahudi ambao kwa ajili yao Yesuakashika kazi ya kuwa Masihi wala siyo ile ya 'Mwana wa Mungu'.Hao jamaa walishikilia kwa jazba kubwa sheria ya Musa nawalikuwa na Injili yao wenyewe iitwayo kwa jina 'Injili yaWaebrania', 'Injili ya Waebioni' au 'Injili ya Wanazareti'. Hapachini twatoa picha ya Waebioni iliyochukuliwa kutoka katikavitabu mbali mbali.Katika 'The History of the Church' kilichoandikwa katika karneya 4 baada ya Yesu huko Ceasaraea, mwandishi Eusebiusanawataja Waebioni katika kitabu cha 3, Vespasian to Trajan.Yeye anawadhihaki maoni yao akisema kwamba hata jina laolinatokana na rai yao duni na 'maskini' kuhusu Yesu. Waebioniwalimwamini Yesu kuwa binadamu mfile na walimheshimu kuwamwema kwa ajili ya mienendo yake myema. Wakiwa Wayahudiwaliishika sabato na sheria kikamilifu, wala hawakukubali wazola Paulo kupata wokovu wa kutegemea imani tupu. Yeye analitajapia kundi jingine la Waebioni walioamini kuzaliwa Yesu bilababa, na Roho Mtakatifu vile vile, lakini wakakataa kukubalikwamba Yesu alikuwapo tangu na tangu akiwa 'Mungu - Nenona Hekima'. Waliifuata 'Injili ya Waebrania' ambayo penginendiyo Injili ya Mathayo. Hao waliishika Sabato na desturi yaKiyahudi, lakini waliusherehekea ufufuo1

________________1 'Eusebius: 'The History of the Church', uk 90-91 (Penguin 1989)

117

Mageuzi yenye kuendelea ya Ukristo

Page 124: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

R. Eisenman na M. Wise wakieleza habari za Waebioni katikakitabu chao The Dead Sea Scrolls Uncovered (1992) wanasemaya kwamba James (Zaddik au Zadok, maana yake mwema,mkweli) alikuwa kiongozi wa Kanisa la Jerusalemu katikati yakarne ya kwanza (40- 60 AD takriban). Tawi hilo kwa kuangaliamambo ya nyuma likaitwa Ukristo wa Kiyahudi katika Palestino.Waebioni wakazalika kutokana na tawi hilo.2

Jumuiya iliyomfuata James ilijulikana kwa jina 'Masikini'(Wagalatia 2:10, Waraka wa Yakobo 2:3-5), cheo cha heshimakilichoelezwa katika Hotuba ya Mlimani na katika Dead SeaScrolls. Kwa jiha nyingi Eisenman anafikiri ya kwamba Waebioniwalifanana na waandishi wa Dead Sea Scrolls. Haowalimuheshimu Yakobo Mwema na walimwamini Yesu kuwaMasiha wao mwenye kufa, ilhali Paulo akawa Mkufuru kwaSheria. Waliishika sheria na Sabato kwa jazba kubwa.Walimheshimu sana sana Yakobo lakini walimhesabu Paulo kuwa'Adui' (Mathayo 13:25-40)3.Sawa na maoni ya Baigent, Leigh na Lincoln katika 'TheMessianic Legacy', chanzo cha mafundisho ya asili ya Waebioni,Wagnosi, Wamaniki, Wasabi, Wamandai, Wanestori na Waelkasindicho falsafa ya Kinazareti. Hao wanaieleza fikara ya Kinazaretikuwa:'

_________________2 'The Dead Scrolls Uncovered', R. Eisenman na M. Wise, uk 186 (Element Books, 1992)3 'The dead sea Scrolls Uncoverd', kilichotajwa nyuma, uk 233 -34)

118

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Kuelekea kwa Yesu na Mafundisho yake yaliyochukuliwa kutokakwenye hali ya asili ya Nazareti yalivyoelezwa wazi wazi na Yesumwenyewe, kisha yakaenezwa na Yakobo, Jude au Judas Thomasna wafuasi wao wa mwanzoni'. Itikadi zao zilikuwa hizi:

1. Kushikamana sana na sheria ya Musa.2. Kumtambua Yesu kuwa Masihi.3. Kuamini kuzaliwa kwa Yesu kwa njia ya kawaida ya kibinadamu.4. Ukinzani kwa maoni ya Paulo.

Page 125: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Miongoni mwa itikadi mbali mbali zilizojitokeza katika kipindiambamo Ukristo ulikuwa unafanyika, itikadi za wale tu zinawezakuthaminiwa walioamini falsafa ya Kinazareti. Wakristo hao wakale walifundishwa Ukristo na Yesu mwenyewe.

KAZI YA MT. PAULO:Ni dhahiri ya kwamba Mt. Paulo na fikara zake hamna hapo.Kwa hakika kutokea zama za Paulo na kuendelea mbele, kwakuwa Ukristo ulienea katika nchi ngeni na itikadi za kipaganizikiwa ndani ya Ufalme wa Kirumi, hivyo Ukristo ukaathirikakwa nguvu sana na kupindika kwa utamaduni na simulizizilizopata kuenea katika nchi hizo na ukaenda mbali zaidi nauhalisi wake wa kale. Mt. Paulo kadiri alivyoweza akaathiri nakuiharibu fikira ya Kikristo kwa kuongeza humo mafundisho yamafumbo ya aina yake. Yeye hakutokana na Wayahudi5 walahakuonana na Yesu isipokuwa katika ndoto alivyodai. Inaonekanayeye alikuwa mapema chini ya athari kubwa sana ya utamaduniwa kigeni.______________________________________

4 'The Messianic Legacy', M. Baigent, R. Leigh, H. L:incoln, k 135 - 138 (CorgiBooks)5 'The Hiram Key'. Christopher Knight and Robert Lomas, p. 246 (Century 1996)

119

Mageuzi yenye kuendelea ya Ukristo

Kuna miswada mingi ya Kiarabu iliyowekwa katika maktaba ya Istanbulambayo ndani yake kuna maneno yaliyonakiliwa kutoka katika matiniya karne ya 5 au 6, yalionasibishwa kwa 'al-nasara'. Miswada hiyoimeandikwa katika lugha ya kishamu na ilipatikana katika nyumba yaWatawa huko Khuzistan katika kusini- magharibi ya Iran karibu nampaka wa Iraq. Hiyo inaeleza jamii ya mapadre wa Nazareti kutorokeaJerusalem baada ya maangamio ya mwaka 66 AD. Hiyo miswadainamtaja Yesu kuwa binadamu na inakazania sheria ya Kiyahudikufuatwa.Wafuasi wa Paulo waliachana na dini ya Kristo na wakaelekea kwenyeitikadi za kidini za Warumi'.4

Page 126: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kwa dhahiri Mt. Paulo alikuwa hana budi kuchagua njiamojawapo katika njia mbili. Ama angechagua kupigana vikalidhidi ya mawazo mabovu yasiyo ya msingi ya kiuchawi, vizimwina simulizi zilizotapakaa katika nchi za Ufalme wa Kirumi tanguzama za kale, au angelegea na kuuacha Ukristo kubadilika ilikuzifaa tamaa na falsafa za kupendwa na watu wengi katikaulimwengu usiokuwa wa Kiyahudi.Maarifa hayo yalifanya kazi vizuri katika maana hii ya kwambayalinyakuwa idadi kubwa ya wale walioikubali imani mpya ambaowasingeweza kupatikana kwa urahisi. Lakini kwa hasara gani?Kwa bahati mbaya hayo yaliishia katika mashindano mabayabaina ya khulka bora za Kikristo na mawazo ya kipagani yasiyona msingi. Aliyoyageuza Mt. Paulo yalikuwa ni majina tu yamiungu ya kipagani na badala yake akayaleta majina ya Yesu,Mungu Baba na Roho Mtakatifu. Kwa hakika si Paulo aliyezuawazo lisilo na msingi la Utatu na kuliingiza katika upagani kwajina la Ukristo, bali kinyume chake yeye aliiga fikira mbovu yaUtatu kutoka kwa mitholojia ya kipagani na akaiingiza katikaUkristo. Kutokea hapo huo ulikuwa ni upagani uleule wa zamanilakini ukapewa majina mapya na sura mpya.Kwahiyo, Ukristo wa Kipaulo haukufaulu kubadilisha itikadi,simulizi zisizo na msingi na mawazo mabovu yasiyo na hakikaya ulimwengu wa kipagani, bali akaishia kuugeuza Ukristo nakuusawazisha na upagani. Mlima usipomwendea alipouita, basiakaamua yeye auendee.

UHAKIKA WA YESUNaam, kila mmoja anayo haki ya kujichagulia Ukristommojawapo miongoni mwa Ukristo wa Kipaulo na Ukristo waYakobo Mwema na viongozi wengine wa kale wa Kikristowaliokuwa wanafunzi wa Yesu Kristo mwenyewe. Lakinitwapenda kuhakikisha hapa habari hii ya kwamba Ukristo halisi

120

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 127: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

uliendelea kusonga mbele kushikamana na imani katika Umojawa Mungu na ukajiweka kando kabisa na bidaa zilizozuka baadayezilizozalisha upayukaji na matatizo ya itikadi ya Kikristo kamavile Yesu kuwa Mwana wa Mungu, Utatu, Dhambi ya Asili,Wokovu, kuhuika Yesu kimwili baada ya kufa na kadhalika.Fikara za viongozi wa zamani wa Kanisa, Yakobo Mwemaakijulikana zaidi kati yao, zilikuwa nyofu na halisi zisizokuwana upingamizi wa ndani wala hitilafu zilizofichikana nyuma yawingu la moshi la siri. Mtaala wa historia ya Imani ya Umoja waMungu katika Ukristo unahakikisha pasipo shaka ya kwambaUmoja wa Mungu usiofanywa kuwa mgumu kueleweka na keleleza utatu, uliendelea kuwa imani safi na rasmi ya Kanisa halisi laKristo.Tafadhali kumbukeni ya kwamba kitabu hiki kidogo hakina lengola kuwaingiza Wakristo katika imani yoyote nyingine isipokuwatu kuwaongoza kwenye imani halisi ya Kristo mwenyewe. Hilini jaribio halisi la kuwakaribisha Wakristo warudi nyuma nakuiamini imani na amali safi ya Yesu isiyochanganyikana namambo mengine yasiyotakikana. Hili ni jaribio aminifu kwakuondoa yaliyobuniwa na kuleta mahali pake mambo ya kweliya Ukristo - mambo ya kweli ambayo kwa hakika ndiyo mazurikama yalivyo ya hakika na yanatuliza akili na moyo.Siyo hekaya za kubuniwa kumhusu Yesu Kristo zilizoubakizaUkristo tangu miaka karibuni elfu mbili na kuusaidia kupona miitoya akili na busara inayodumu ya kuzidi kwa sababu ya maendeleoya sayansi, wala haukubaki kwa sababu ya itikadi ya kubuniwaya Utatu. Kilichobakiza ukweli na kiini cha Ukristo ndiyo dhatina mafunzo ya Yesu Kristo. Sio uungu wa Yesu bali ni matendoyake bora matakatifu yanayovutia ili mtu afungamane nao. Utiwa mgongo wa Ukristo hasa ulikuwa ni yale masumbufu na subirana uvumilivu kwa ajili ya shabaha njema na kukataa kwa uaminifumajaribio yote ya kikatili ya kumlazimisha yeye kugeuza kanunizake. Bado ni mzuri na wakupendwa hata leo jinsi ulivyokuwahapo kabla. Huo umeziathiri kwa nguvu sana fikira na nyoyo za

121

Mageuzi yenye kuendelea ya Ukristo

Page 128: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Wakristo hata kwamba wamebakia kufungamana na Yesu nawanaonelea kufumba macho yao wasiangalie hitilafu za kiakilikatika Utatu na kadhalika ni afadhali kuliko kutengana na Yesu.Utukufu wake hasa umo katika hakika hii ya kwamba yeyeakazishinda nguvu za giza zilizokula njama kumtiisha ijapokuwayeye alikuwa mnyonge sana wala si zaidi ya kuwa binadamu.Ushindi wa Yesu ni kitu wanachopaswa watoto wa Adamukushirikiana katika hicho kwa fahari. Sawa na nadharia yaWaislamu, yeye alikuwa miongoni mwa kizazi bora sana chaAdamu. Yeye aliwafunza wanadamu kwa mfano wake wakuvumilia alipokabiliwa na usumbufu mkali na uchungu mwingisana. Ushindi mkuu wa Yesu ulikuwa kutokujisalimisha na kukaaimara katika hali ngumu sana ya majaribio makali. Ni maishayake ya uchungu na usumbufu yaliyookoa wanadamu nayalimfanya ayashinde mauti. Kama yeye angelichagua kufa kwahiari, kitendo chake hicho kingelikuwa sawa na kujaribukuyakimbia hayo mateso. Mtu anawezaje kulihesabu tendo hilokuwa ushujaa? Hata wale wanaojiua kwa kulazimika, kitendochao pia kinahesabika kuwa cha woga tu. Kushirikiana katikashida maishani ni afadhali kuliko kuzikimbia kwa njia ya kujiua.Hivyo wazo la dhabihu kuu ya Yesu kwa kukubali mauti kwaajili ya binadamu ndiyo maono matupu yasiyo na kiini mle ndani.Ubora wa Yesu, twasisitiza tena, ulikuwamo katika kujitoleakwake sana katika maisha mazima. Katika maisha yake yote yeyealishindana na vishawishi bila kulegea na kuyabadilisha maishaya uchungu kwa maisha ya raha. Kila siku aliyakabili mauti lakiniakakataa kulegea na akaishi ili awapatie wenye dhambi uzima.Aliyashinda mauti si kwa kujisalimisha kwa mauti bali kwakukataa kunyongea mbele yake. Aliyashinda waziwazi na akajitoakatika mamlaka yake ambapo mtu mdogo zaidi angewezakuangamia. Basi akahakikisha ukweli wake na ukweli wa manenoyake pasipo shaka yoyote. Ndivyo hivyo tumwonavyo Yesu nandiyo sababu twampenda sana. Sauti yake ilikuwa sauti ya Munguwala siyo sauti ya matakwa yake na tamaa zake. Alisema

122

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 129: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

aliyoamrishwa kusema, si zaidi wala si kidogo kulikoaliyoambiwa na Mungu kusema. Yeye alimwabudu Mungumaisha yake mazima, naam, alimwabudu Yeye peke yake, nahakumtaka yeyote mwenye kufa kuinama mbele yake wala mbeleya mamake au mbele ya Roho Mtakatifu. Hiyo ndiyo hakika yaYesu ambayo tunawakaribisha Wakristo wa madhehebu yote naimani zote kuirejea.

KUENDELEA DINI:Sisi twaziamini dini kuendelea na kupatikana kwa watu wotekatika ulimwengu mzima. Ndiyo maana Islam inasisitiza desturiya Unabii ndiyo kawaida kwa ulimwengu mzima, na inamaanishaya kwamba manabii wote kwa jumla wanapaswa kukubaliwa.Kumkataa mmojawapo ndiyo kuwakataa wote hao, kwani mtukwa hakika anawaamini wote kwa sababu wote hao wametokakatika chanzo kilekile kimoja. Basi neno 'kuendelea' dinilinamaanisha kufanana namna fulani na 'maendeleo' ya uhai lakinisiyo kabisa kama hayo. Tunaamini ujumbe kuendelea kusongambele pamoja na binadamu kupata maendeleo katika maeneombalimbali. Inaonekana kwamba sura za mwanzoni za dinizilizofunuliwa na Mungu ijapokuwa zilikuwa na mafundisho yaleyale ya asili lakini yalikuwa na maelezo mafupi zaidi. Yaanimaamrisho na makatazo yalikuwa machache zaidi. Kisha hayoyakapanuka na kuzidi katika idadi ya maamrisho na makatazoyaliyoenea katika maeneo makubwa zaidi ya shughuli zabinadamu. Pia inaonekana ya kwamba dini zilizohusikana nautamaduni wa kale zilikuwa kwa watu wachache zaidi wamakabila ama jamii au eneo fulani tu. Ujumbe wao ulilingana namahitaji yao machache katika zama hizo. Hizo zawezakuchukuliwa kuwa dini za kikabila, za kiukoo ama za kitaifa.Mfano mmoja ufaao wa jambo hilo ndiyo Wana wa Israeli namafundisho ya Kiyahudi.

123

Mageuzi yenye kuendelea ya Ukristo

Page 130: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Maelekeo ya kihistoria kwa maendeleo yaweza kuelezwa kwakifupi kwamba yalikuwa ya pande mbili:

1. Mafundisho yaliendelea kusonga mbele hatua kwa hatuakuelezwa zaidi na kukamilika zaidi na zaidi.

2. Maeneo ya dini yalizidi pole pole kupanuka.

Kuendelea dini siyo maana yake ya kwamba dini iliyofunuliwakwa Adamu dini hiyohiyo iliendelea kuongoza watu na ikaendeleakubadilika ikiongeza mafundisho na eneo lake. Bali twamaanishaya kwamba katika sehemu mbalimbali za dunia ambakoutamaduni wa aina mbali mbali uliimarika na kustawi, funuo zaMungu zikazalisha dini tofauti kwa kulingana na maendeleo yakijamii ya binadamu katika sehemu hizo za dunia. Lakini dinihizo zote zilikuwa zinasonga mbele katika njia hiyo kwa jumla.

UPEO WA MWISHO WA MAENDELEO YA DINI:Miongoni mwa madhehebu hayo ya dini, twaamini ya kwambamojawapo katika Mashariki ya Kati ilikuwa inalelewa ili kuzalishadini kubwa ambazo zingesaidia kuleta maendeleo ya kidini katikadunia nzima hadi kukamilika dini. Hiyo ndiyo wazi kabisakutokana na mtaala wa historia ya dini. Uyahudi kufuatwa naUkristo kufuatwa na Islam kunadokeza bayana upande yasongaomaendeleo ya mafundisho ya dini. Baina ya dini hizo, maendeleoya mafundisho yanaweza kutafutwa nyuma na mbele kwa urahisina itaonekana kwamba hayo yanalingana sana. Kwahiyo nimuhimu kabisa kufahamu mpango huo mkubwa ungesababisha,na ukasababisha, kutimiliza na kukamilisha mafundisho hayo kwasura ya dini moja kwa ajili ya watu wote yaani dini ya Kiislamu.Katika hali kama hiyo inafaa Wayahudi wakazanie kutambuaumuhimu wa Yesu bila chuki au upendeleo. Waliposhindwakumtambua yeye, mfano wa Wayahudi ni kama mfano wa aina

124

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 131: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

nyingi za wanyama ambao wamekwisha fukiwa katika historiaya mageuzi (evolusheni), ambao hawana kazi yoyote muhimu yakufanya katika uhai uliposogelea karibu na upeo wake. Hivyohali ya Wayahudi ndiyo kama mabaki ya historia tu lakini badowanaendelea kubaki katika eneo dogo la kuwepo.Aidha hali ya Wakristo ni kama hali ya Wayahudi, isipokuwawamesimama hatua moja mbele kuliko hao, karibu zaidi na Islamkatika utaratibu wa kihistoria. Naam, ni muhimu kuzingatia yakwamba walipoachana na njia ya Yesu na kuanza kuifuata njiambovu waliyotayarishiwa mwanzoni na Mt. Paulo, basi hiyo njiambovu iliwapeleka mbali zaidi na Islam kuliko Wayahudi. MaanaWayahudi baada ya zaidi ya miaka elfu nne tangu kuwapo kwaowamejifunza kwa uchache somo la Umoja wa Mungu ulio wamuhimu kabisa kwa ajili ya uhai wa dini yoyote. Lakini juu yakuwa karibu zaidi ya Islam katika imani za msingi, zipo sababunyingine zilizowafanya Wayahudi kuwa wagumu zaidi katikakukataa kukubali Islam kwa wingi.Mtaala huo unanifanya niamini ya kwamba Wayahudiwataendelea kuwa mbali na Islam kuliko Wakristo juu ya imanizao kufanana na imani za Kiislam, isipokuwa tu wakikuza ilehali ya moyo iliyo muhimu sana kumtambua Kristo. Wamekosakiungo cha muhimu sana yaani Yesu Kristo, kilicho baina yao naujaji wa Mtume Muhammad s.a.w. Kukanusha ukwelikuliwafanya wagumu kiasi cha juu sana hata kwamba kitabiahawako tayari kupokea ujumbe wowote mpya. Wanadumukumngojea Kristo, ilhali Kristo alikuja na kaondoka tayari.Wakiisha kosa kumtambua mara ya kwanza, haielekei waokumtambua tena katika ujaji wake wa mara ya pili.Yaonekanaimekadiriwa kwamba wataendelea kumngojea milele Kristo wamawazo yao.Ni Kristo aliyekuja kutengeneza njia ya kuongoza kwenye diniya daraja la juu zaidi ambayo ndiyo Islam. Maneno hayoyasichukuliwe kwa ukali zaidi. Hatuna maana kwamba Wayahudikwanza waukubali Ukristo ndipo wachukue hatua nyingine ya

125

Mageuzi yenye kuendelea ya Ukristo

Page 132: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kuingia katika Islam. Fikira hiyo ni kinyume kabisa na busara.Tunachojaribu kudokeza ni kwamba watu ambao wamemkataanabii ama mjumbe fulani ambaye hakuwa nabii wa kawaida tu,bali alikuja kufanya kazi muhimu kabisa ya kuwapatia mazoeziya kifikira na kiroho, wamekataa kwa sababu wanaugua kirohona kitabia. Mpaka maradhi hayo yaponywe na tabia yaoiliyopindamana isiyopokea ukweli irekebishwe, haielekei sanakwamba watamkubali nabii aliyewahi kuwapo baada ya kiungokile walichokwisha kosa kukitambua.Ama kuwahusu Wakristo ni hivi kwamba hao wanawezakuongozwa kwenye ukweli wa Mtume Muhammad s.a.w. hapotu ambapo wanarejea kwenye ukweli na uhakika wa Yesu Kristo.Yeye hakuwa njia ya kuongoza kwa Mungu tu, bali pia alikuwa,kama walivyokuwa manabii wengine vilevile, njia ya kuongozakwenye Nabii yule aliyekadiriwa kuja nyuma yake.Yesu alikuwa ni kiungo cha kati katika mfano wa shamba lamizabibu. Katika mfano huo, bado Bwana mwenyewe, yaaniMjumbe mkamilifu wa Mungu, alibaki kufika. Kwa hiyo, mpakaWakristo waachane na fikara mbovu ya mawazo yao yasiyo namsingi kumhusu Yesu Kristo, na kukubali uhakika hasa mtukufuwa Bwana wao Mtakatifu, hawawezi kuongozwa kwenye njiainayomwunganisha yeye na Mtume Muhammad, amani na barakaza Mungu ziwe kwake.Mtume Muhammad s.a.w. alikuwa hakika hasa wala siyo wakubuni na kwa kweli hakika huongoza kwenye hakika nyinginezo.Hivyo basi, siyo fikra za kubuni juu ya Yesu, bali ni uhakikawake hasa utakaowabariki Wakristo kutambua ukweli wa MtumeMuhammad s.a.w.

126

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 133: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

8 UKRISTO KATIKA ZAMA HIZI

Tatizo kubwa zaidi linaloukabili ulimwengu wa Kikristo siku hizisiyo kukosekana ufahamu kama kukosekana hamu na upendo wakupokea ukweli. Ukristo ukiwa wa kubuni ama wa uhakikaumekuwa sehemu ya utamaduni wa Magharibi isiyowezakutengwa, na umefanya kazi muhimu katika shabaha zao zakikoloni na kibepari. Huo unaitilia nguvu mifumo yao ya kisiasana kiuchumi na unawapatia nguvu ya kuwaunganishainayowaweka katika hali imara ya umoja. Umefanya kazi kubwasana katika kufuma na kuimarisha mfumo mgumu wa kijamii yakisiasa na kiuchumi wa Magharibi. Tunachoelewa kuhusuutamaduni wa Magharibi au ubepari wa Magharibi na utawalawake wa kiuchumi ni kwamba huo wote umekwisha ingiliwa naUkristo. Katika hali ya hivi sasa Ukristo unaonekana unaelekeakutumikia miradi ya kiwiliwili ya Magharibi vizuri zaidi kulikoile ya kiroho, ilhali katika zama zilizopita kazi ya Ukristo ilielekeazaidi kuimarisha imani za Kikristo na kustawisha khulka bora.Kazi kubwa zaidi ya kihistoria iliyofanywa na Ukristo ndiyokujenga na kukuza ubepari wa Magharibi. Mashariki ilitekwa kwamoyo wa bidii wa Kikristo, na hususan vita vilivyopiganwa naUfalme wa Kiislam vilisababishwa hasa na chuki ya Wakristodhidi ya Islam.

UKRISTO NA UKOLONI:Utawala wa kikoloni ulipotiisha karibu bara zima la Afrika nakuwafunga Waafrika katika minyororo ya siasa, Waafrikahawakukawia sana mpaka wakatiwa katika mikono yao na miguu

127

Page 134: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

yao minyororo ya utumwa wa kiuchumi pia. Kupata madarakaya kutawala hakuna maana pasipo kuwatiisha watu kiuchumi.Baada ya mabwana wa siasa na uchumi, hawakukawia zaidiMapadre wa Kikristo kuwasili nyuma yao haraka wakivaa majohoya unyenyekevu na kujitolea. Shabaha yao ya kuwasili Afrikailionekana kinyume kabisa na ujaji wa watangulizi wao wa kisiasana uchumi. Walikuja, walivyodai, si kuwatia utumwani balikuwatoa utumwani roho zao Waafrika. Inashangaza ya kwambaWaafrika hawakuonea mashaka nia hiyo njema ilivyodaiwa. Kwanini hawakuwauliza kwa adabu viongozi hao wakarimu waKanisa: Mbona mwazihurumia roho zetu tu pekee? Hamwoni miiliyetu imetiwa utumwani bila kuonewa huruma? Mbonatumenyang’anywa pasipo sababu uhuru wetu wa siasa, na kutiwaminyororo ya utumwa wa kiuchumi? Kwa nini hamkutuhurumiakatika hali yetu ya utumwa wa kimwili na kwa nini mwapendakuziachisha huru roho za watu waliotiwa utumwani?Hitilafu iliyomo humo iko wazi, lakini ni masikitiko ya kwambahaikuwa wazi sana kwa wale waliotegwa na hila za Kikristo.Afrika ni nyofu haina hila, na haina hila hata leo jinsi isivyokuwana hila miaka mia mbili kabla. Waafrika hata leo hawaoni kwambawametiwa katika utumwa wa kisiasa na kiuchumi kwa njia yamfumo usioonekana unaosimamiwa kutoka mbali na ukolonimamboleo. Bado hawajafahamu kwamba Ukristo kwao ndiyo njiaya kuwatiisha. Huo ni kama dawa ya kutuliza iliyowatia usingiziwa usahaulifu. Hiyo inawapatia ufahamu usio sawa kwamba wakochini ya mabwana zao kwa uchache katika kushirikiana nao katikakitu fulani kwa usawa.Ufahamu huo wa kuwa chini yao ndiyo uliowaongoza kuigamtindo ghali sana wa maisha ya Magharibi. Miti inabakikupandikizwa katika nchi za kigeni, lakini matunda yakehusafirishwa na kupelekwa kwa watu walioshindwa na mazoeaya ladha yake. Huo ni mfano mdogo wa kuonesha namna Ukristoulivyo kitu cha lazima kwa kuutawala kibepari na kiuchumiUlimwengu wa Tatu.

128

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 135: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Katika magharibi yenyewe mtu wa kawaida, bila kujali anafahamumatatizo ya itikadi ya Ukristo ama hapana, anauona Ukristo ndiyosehemu isiyoweza kutengwa ya ustaarabu na utamaduni wake.Yafaa ikumbukwe ya kwamba nguvu hasa ya khulka za Kikristopopote zinapobakia haimo katika imani za simulizi za Ukristo.Bali imo katika mkazo ule unaotiliwa katika upole, huruma,huduma katika shida na taabu, khulka nyinginezo ambazozimekuwa sawa na maana ya Ukristo. Ijapokuwa Khulka hizozinafundishwa katika dini zote za ulimwengu na zinaonekana nishabaha ambayo Mungu aliwawekea watu wote kuipata, hatahivyo propaganda yenye nguvu ya Kikristo inadumu kusisitizamambo hayo kuyanasibisha kwa Ukristo tu pekee, na imefaulukuwaaminisha watu habari hiyo mwishowe. Ujumbe wa huruma,upole, wema, na mwenendo mwanana unafanya kazi kama muzikimwororo wa kuvutia. Huo ndiyo ulimwengu wa hadithi za kubunina kupigwa chuku ambao kwa kawaida unavutia watu kuipokeaimani ya Kikristo. Hata hivyo, papo hapo kwa kutengana na habarihiyo, zipo hakika madhubuti za kisiasa na kiuchumi za maishaya Magharibi na hayo kuutisha ulimwengu uliosalia.Yaonekana hitilafu zilizomo katika imani wanazolazimikaWakristo kuwa nazo zimekwisha ingia kwa namna fulani katikamwenendo wao wa kidunia pia. Upole, huruma, uvumilivu,kujitoa na maneno mengine ya aina hiyo yanafuatana pamoja naukatili, ukandamizaji, dhuluma na kuwatiisha watu wengi sanawasioweza kujitetea. Kanuni ya sheria, Uadilifu nakutokupendelea ni mambo yanayotumika humo ndani yautamaduni wa Magharibi pekee. Lakini katika uwanja wauhusiano wa mataifa, hayo yanahesabiwa istilahi za kipuuzizisizofaa ambazo zinathaminiwa na wajinga tu.Siasa, maarifa ya ujumbe na uhusiano wa kiuchumi baina yamataifa havina uadilifu isipokuwa tu vikilinufaisha taifa. Khulkaza Kikristo hata zikiwa nzuri namna gani haziruhusiwi kuingiakatika uwanja wa siasa na uchumi wa Magharibi. Hiyo ndiyohitilafu ya hatari mno ya nyakati mamboleo.

129

Ukristo katika zama hizi

Page 136: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Linapokuja suala la kudhihirisha uzuri wa Ukristo, hapo Ukristounaoneshwa katika sura ya kuvutia ya ustaarbu na utamaduni waMagharibi, kwa kuziita nchi za mashariki kwenye maisha ya rahana uhuru yanayoruhusu kila ulipendalo dhidi ya kawaida ngumuza jamii zao chakavu za kidini. Ujumbe huo wa kupata uhuruulikosa sana kueleweka hasa na watu wa kawaida walioelimikakidogo katika Dunia ya Tatu na wakauchukua kuwa wa kuvutiasana. Ongeza katika hiyo ziada ya manufaa ya ki-saikolojia yaupataji wa fikara kuhusiana na ulimwengu ulioendelea mbele kwanjia ya dini moja, na hapo ndipo mtu anaaza kutambua kazi halisiya Ukristo ya kuwavutia idadi kubwa ya watu waliokuwawamekandamizwa, na mara nyingi watu mafukarawaliodhulumiwa ambao ni watu wa chini kabisa katika jamiizilizogawanywa watu katika madaraja mbalimbali. Kuifahamuimani ya Kikristo ni nje ya uwezo wa watu hao. Hiyo inanyanyuadaraja lao la kibinadamu, lakini siyo kwa hakika hasa.Ingebainika kabisa kutokana na hayo yaliyoelezwa juu ya kwambaUkristo tunaozungumzia uko mbali sana na Ukristo wa YesuKristo. Kuutambua utamaduni wa Magharibi kuwa Ukristo nikosa lililowazi sana. Kuunasibisha kwa Kristo Ukristo ulivyo sasakatika maeneo mbalimbali kwa hakika ni kumtukana Kristo.Lakini kuhusu kila kanuni kuna baadhi ya mambo yanayotengwambali. Hatuna kauli inayofaa moja kwa moja kundi lolote lenyeidadi kubwa. Hakuna shaka ya kwamba yapo matumaini kidogona uhai katika ulimwengu wa Kikristo ambako uaminifu waKikristo, upendo wa kujitoa vinashikwa kwa kitendo kwa niahalisi. Hivyo ni visiwa vya matumaini ambavyo pembezonimwake mna bahari zilizochafuka za maovu ambazozinamomonyoa sehemu za visiwa hivyo na kuziingiza katikabahari. Kama ulimwengu wa Kikristo usingelipambwa na mifanoing’aayo ya Ukristo unaofuatwa sawasawa na jazba ya YesuKristo, japo uko mbali sana na yeye, bila shaka giza totorolingelienea katika Magharibi hadi upeo wa macho. Pasipo Ukristohamna mwanga katika utamaduni wa Magharibi, lakini nasikitika

130

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 137: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

mwanga huo nao unaendelea haraka kufifia.Yaulazimu Ulimwengu wa Kikristo kurudi kwenye hakika yaKristo na kujitibu nafsi iliyogawanyika na unafiki uliofichikana.Kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kubuni na simulizi zisizona msingi kuna hatari ya kuangamia. Shabaha hasa ya majaribiohaya ni kuuamsha ulimwengu wa Kikristo ili utambue hatarizisizoonekana kwa dhahiri lakini zipo tu kwa hitilafu ziendeleazokuzidi zilizopo baina ya imani na matendo. Simulizi zisizo namsingi ni kitu kizuri maadamu zinasaidia shabaha ya kuwatiishawatu wenye hali ya chini sana katika jamii kwa Mapadrewanaohusikana na mfumo unaowatawala na kuwanyonya kwasababu ya ujinga wao kwa kuwaweka katika hali ya kipumbavu.Lakini linapokuja swala la imani kufanya kazi ili kuwahuishawafu wa roho na kurekebisha khulka zao zinazoendelea kuharibikaharaka, hapo ndipo simulizi hizo hazifai kabisa. Hayo kwa hakikani mawazo tu, na mawazo hayawezi kufanya kazi ya maana sanakatika mambo yanayomuhusu binadamu.

UJAJI WA YESU KRISTO MARA YA PILI:Tuliyonena hapo juu sasa yanaweza kuoneshwa kwa kitendo.Suala la muhimu la binadamu kuokoka leo linaitegemea pichahalisi ya Yesu Kristo. Kwahiyo, ni jambo la muhimu kabisakuutambua uhakika wake. Alikuwa nani hasa na akiwa Kristoalifanya kazi gani ya muhimu kwanza katika jamii iliyochakaaya Wayahudi? Kiasi gani cha uzito twaweza kutia katika ahadiyake ya kuja mara ya pili katika zama za mwisho? Hayo nimaswali muhimu ambayo hakuna budi kuyazungumzia.Kama fikira kuhusu Yesu siyo ya kweli bali ni matokeo yamawazo tu ya kibinadamu, hapo bila shaka haiwezekani kutambuaufikaji wake mara ya pili. Lakini Yesu hakuwa matokeo yamawazo. Yeye alikuwa mtu hasa na akiwa hivyo anaweza

131

Ukristo katika zama hizi

Page 138: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kuzaliwa tena akiwa mtoto wa binadamu wala hawezi kuteremkakama mzuka akiwatembelea mara nyingine wenye kufa. Mawazokama hayo hayahusikani na hakika za maisha ya binadamu. Aidha,watu wanaoishi wakitosheka na mawazo yao matupu na simuliziza kubuni wanadumu katika hali yao hiyo pasipo kupata nafasiya kumtambua mwokozi wao wakati afikapo.Kama Yesu alikuwa kweli Mwana wa Mungu, kama Wakristowanavyotutaka tuamini, hapo bila shaka yeye atakuja mara yapili katika utukufu akiweka mikono yake juu ya mabega yamalaika wa kweli. Lakini kama hayo ni mawazo ya kubuniyaliyopigwa chuku ya matumaini na matamanio ya Wakristo,hapo ujaji wake hautatokea katu. Abadan dunia haitalishuhudiatukio hili la kipuuzi la mungu fulani kuteremka kutoka mbingunikatika sura ya binadamu pamoja na jeshi la malaika kumbeba nakumwimbia nyimbo za dini.Fikira yenyewe hiyo inakataliwa na akili ya mtu na dhamira yabinadamu. Hiyo ni hekaya ya kizimwi ya kipuuzi zaidiiliyozushwa kwa kutumbuiza akili za watu fulani. Kinyume chake,kama fikira ya Kiahmadiyya ikubaliwe kumhusu Yesu Kristo,hapo picha hiyo ya ajabu itabadilika kuwa picha nyingine ambayosiyo tu kwamba inakubaliwa na akili ya mtu, bali inaungwa mkonokwa nguvu na historia nzima ya kidini ya binadamu. Na hapotutakuwa tunatizamia ujaji wa mwokozi asiye tofauti na Kristokatika ujaji wake wa mara ya kwanza. Tutakuwa twatazamia ujajiwa mtu mpole, mwenye kuzaliwa katika ukoo mpole kama YesuKristo alivyokuwa katika ujaji wake wa mara ya kwanza,atakayeanza kazi yake ya mahubiri kwa namna alivyofanya maraya kwanza. Atatokana na watu wa dini wafananao na Wayahudiwa Judea katika tabia na hali. Na hao si tu kwamba watamkataana kumtenga kwa sababu ya yeye kudai kuwa mwongozialiyeahidiwa waliyemtazamia kufika akiwa mwokozi kutoka kwaMungu, bali nao watafanya chini juu ili kumwangamiza. Ataishialivyoishi Kristo kwa jumla na atafanyiwa dhihaka, chuki na ujeurialivyofanyiwa Yesu. Atasumbuka mara nyingine, si kwa mikono

132

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 139: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ya watu wake, bali kwa mikono ya maadui zake wafananao nawale waliomsumbua hapo kabla. Yeye atasumbuliwa vile vile nanguvu kubwa kabisa ya utawala wa kigeni ambao chini ya utawalahuo atakuwa amezaliwa miongoni mwa watu waliofanywa kuwawatumwa.P.D. Ouspensky, mwandishi habari maarufu aliye Mrusi wamwanzo wa karne ya ishirini, akiandika juu ya kutokea kwa YesuKristo mara ya pili alishirikiana katika maoni ya aina hiyoAkaandika:

Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuletwa manabii na waongozi wadini. Nadharia yoyote nyingine ni tupu ya uwongo na isiyo namaana.Siku zote inakuwa hivi ya kwamba wakati ambapo bishara zamanabii kuhusu ujaji wa waongozi wa dini zinapokwisha timia,wale watu wanaoletewa mwongozi ili kuwaokoa wanashindwakumtambua. Katika kipindi hicho cha historia wanakuwawamekwisha geuza picha ya kweli ya mwongozi wao wa dini nakuchukua picha ya bandia ya mawazo yao yasiyo na msingi.Wanaanza kutazamia kutokea mawazo yao na kugeuka katikasura ya kiwiliwili, ilhali kinachotokea ni kufanyika mara nyingine_____________________________________________

1 P.D.Ouspensky, ‘A New Model of the Universe’, k. 149 -150, Kegan Paul ,Trench, Truberner & Co.,Ltd 1938

133

Ukristo katika zama hizi

Kwa vyovyote hii siyo fikira mpya ya kwamba Kristo akizaliwa ardhinibaadaye siyo kwamba hatakuwa kiongozi wa Kanisa la Kikristo, balipengine hatahusiana na hilo na katika zama nzuri sana za nguvu nauwezo wa Kanisa yeye kwa yakini atatangazwa kuwa mzushi nakuchomwa kufungiwa na mti. Hata katika zama zetu hizi za mwangaambapo makanisa ya Kikristo japo hayajaachana na mambo yake yaliyokinyume cha Ukristo lakini yameanza kuyaficha, Kristo ataweza kuishipasipo kupata kudhulumiwa na 'Waandishi na Mafarisayo', labda hukokatika nyumba ya watawa katika Urusi peke yake.1

Page 140: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

sawa na historia ya dini jinsi ilivyotendeka tangu alipokujaMwongozi wa kwanza wa dini. Waongozi wa dini siku zote hujawakiwa wanadamu wanyenyekevu waliozaliwa na mama wazaziwa kibinadamu na wanachukuliwa kuwa wanadamu siku zotekatika maisha yao. Ni baada ya muda mrefu sana wakiisha kufahabari ya kuwafanya miungu inaanza. Ndiyo maana kuwapokeamara moja wanapotokea tena kunakuwa hakuwezekani.Watu wa dini wa aina hiyo wanapozikabili hakika za Waongoziwa dini wanaoonekana watu wanyenyekevu, wanawakataa mojakwa moja. Mnapotazamia ujaji wa kizimwi ama kizuka,mwawezaje kukubali ujaji wa mtu wa kawaida badala yake?Ndiyo sababu dunia imeshindwa kumwona na kumtambua YesuKristo katika ujaji wake wa mara ya pili, ilhali amekwisha kujatayari mara ya pili.Hilo ni dai kubwa pengine ambalo yaelekea litakataliwa katakatana wasomaji. Yawezekanaje aje Yesu na aondoke pia pasipo duniakuitambua habari hii? Anawezaje kuondoka bila ya ulimwengumzima wa Ukrito na Islam kumjua? Nyakati mamboleozimewaona wadai wengi wa aina hiyo ambao walishtusha piakwa muda na kuleta msukosuko, Lakini hao wote wako wapileo?Hizi ni zama ambamo katika nchi nyingine madhehebu yanatokeaghafula kama uyoga na madai mabovu ya kurejea kwa Yesu amaYesu kumtuma mtangulizi wake yanafanywa huko na huko. Daihilo nililosema pengine ni mojawapo katika madai hayo. Kwanini mtu mtulivu apoteze nafasi yake hata kuifikiria kwa makinihabari hiyo? Shaka halisi zitazalika na mashaka makubwayatakabiliwa. Tungemwomba msomaji kuzingatia hali ya ujajihasa wa Yesu. Je, ujaji wake ndiyo wazo tu la uwongo ama yeyekweli anaweza kufika tena duniani yeye mwenyewe binafsi amakwa njia ya ujaji wa mtu mwingine badala yake anayefanana naye?Hilo ndilo swali linalopaswa kujibiwa kwanza kabla hatujawezakujaribu kutoa majibu kuhusu mashaka kadha yaliyodokezwa juu.Je, ulimwengu, ukiwa wa Kikristo au wa Kiislam, upo tayari kweli

134

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 141: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kiroho kukubali ujaji wa mara ya pili wa Yesu? Kama ndiyo,katika sura gani na kwa njia ipi? Tukiangali sawa na nadharia yaWaislamu na pia Wakristo, Yesu kama akija atakuja na shanikubwa na ishara zilizo wazi akiteremka kutoka mbinguni saa zamchana na malaika wa kumbeba, hata kwamba haitawezekanakwa hata mwenye mashaka sana kukataa kumpokea.Ni masikitiko ya kwamba zama za leo ziko tayari kumpokea Yesuwa mawazo tu matupu ambaye mfano wake haujatokea asilanihapo kabla katika historia ya binadamu. Kama historia ya diniizingatiwe kwa makini, mtu atakuta mifano mingi sana yawaanzilishi wa dini au watawa wengine waliosemekana walipaambinguni na miili yao. Madai hayo ni mengi sana na yametapakaahuko na huko hata kwamba inaonekana ni maelekeo ya mtukubuni hadithi za aina hiyo kuwakuza viongozi wa dini yake nakuwafanya kuwa zaidi kuliko binadamu. Swali lipo hapa yakwamba tunawezaje kukanusha taarifa hizo zote zinazokubaliwana kuaminiwa na pengine mabilioni ya watu leo katika dunia hii?Wakristo na Waislam pekee wanaoiamini hiyo na matukiomengine ya kipuuzi wapo zaidi ya bilioni mbili. Kwahiyo msomajianaweza kuuliza ya kuwa tuna haki gani au mtu yeyote dunianiana haki gani kukatalia mbali madai hayo yote kwa kusema kuwahayo siyo ya kweli, ni mawazo tu ya watu. Tunakubali ya kuwakuichunguza habari hiyo kwa jiha hiyo kutahitaji juhudi kubwaili kukanusha madai hayo kwani hayasaidiwi na maandiko yadini ambazo zinafanya madai hayo. Mtu akiisha ongozwa kuingiakatika mzingile huu wa maelezo haya au yale yanayowezekana,habari hiyo itaishia katika swali la kupendelea na kujichaguliamaelezo fulani. Hapo hiyo itakuwa ni mchezo wa mtu yeyotekutoa tafsiri ya maneno yalivyo katika maandiko au historia yadini ilivyoripotiwa au kuyaeleza kwa kuyafikiria kuwa mafumboau mithali. Kukanyaga katika bwawa la matope la maelezoyanayopinzana hakutasaidia kupata shabaha. Hata hivyo kuna njiamoja ya kutokea jambo hilo zito tunayoweza kuwaoneshawasomaji na kuwakaribisha kuifuata ama kuikataa

135

Ukristo katika zama hizi

Page 142: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

jinsi wapendavyo.Hebu tukubali, kwa shabaha ya kuhoji tu, madai yote hayo yaviongozi wa dini kupaa mbinguni na kuyahesabu jinsi yalivyokidhahiri. Kama kupaa Yesu mbinguni jinsi kulivyoripotiwakuchukuliwe katika maana ya dhahiri na ujaji wake wa mara yapili halikadhalika uhesabiwe kuwa ujaji wake hasa, hapohapatakuwa na sababu yoyote ya kukatalia madai ya aina hiyo yawafuasi wa dini nyingine kuhusu kupaa kwa viongozi waombinguni na kuteremka tena na kiwiliwili chao ardhini. Kwa ninituwatenge tena Eliya, Mfalme wa Salemu, Imamu wa Kumi nambili wa Mashia Ithna Ashariyya - dhehebu moja la Waislam,kupaa kwa miungu ya Wahindu na watukufu wengine na walewanaochukuliwa kuwa madhihirisho ya Mungu? Kwahiyo niafadhali zaidi kujiepusha na kubishana na wenye kuamini hivyokwani mabishano hayo hayataleta manufaa yoyote bali yatapoteabure kabisa. Mtu anaweza kuwauliza hao wenye kuamini harakasimulizi pasipo ushuhuda ya kuwa je wanaweza kutuonesha hatammojawapo miongoni mwa wanaoaminiwa walipaa hadi sehemuza mwisho za huko mbinguni kwamba aliwahi kurejea dunianimara ya pili yeye mwenyewe binafsi. Je, historia yote yabinadamu yaweza kutoa hata mfano mmoja wa mtu kurudi dunianimara ya pili aliyeripotiwa kupaa mbinguni pamoja na mwili wake?Tuonesheni basi kama upo mfano hata mmoja.Kwa kuangalia kwamba madai ya kurejea duniani mara ya pilihayakutimia abadan hata mara moja, mtu anabakiwa na kuchaguajambo mojawapo katika haya mawili: Ama kukataa katakatamadai hayo yakiwa ya udanganyifu, au kuyakubali hayo madaiyakiwa mafumbo ama mithali jinsi Yesu alivyofanya kuhusu ujajiwa Eliya mara ya pili. Hapo panabainika ya kwamba walewanaomngojea Yesu ateremke mwenyewe binafsi kutokambinguni wanajiwekea kinga baina yao na uhakika halisi wa Yesu.Kama Yesu akija tena, lazima atakuja akiwa mtu jinsiwalivyotazamiwa waongozi wote kabla yake. Ikiwa anadhihirikaleo akiwa mtu mnyenyekevu wa kawaida aliyezaliwa katika nchi

136

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 143: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ifananayo na Judea katika Palestino na akapewa kazi ya mahubirialivyofanya katika ujaji wake wa kwanza, je, wenyeji wa nchihiyo watamtendea tofauti na vile alivyotendewa hapo kabla?

MASIHI ALIYEAHIDIWAHivyo ndivyo ilivyo habari ya ujaji wa mara ya pili wa Masihitunayemwamini. Ilikuwa karibu miaka mia moja na kitu hiviiliyopita ya kwamba mja mnyenyekevu wa Mwenyezi Mungu,jina lake Mirza Ghulam Ahmad wa Qadian, alipashwa habari naMungu ya kuwa Yesu Mnazareti, Mwana wa Mariamu, ambayeujaji wake wa pili unangojewa na Wakristo na Waislamu kwausawa, alikuwa nabii maalum wa Mungu aliyekwisha kufa tayariwalivyokufa manabii wengine wote wa Mungu. Hadhrat MirzaGhulam Ahmad a.s. alitangaza ya kuwa Yesu hayuko hai kimwiliwala hakupaa mbinguni akisubiri huko kurejea tena kuitembeleaardhi. Alikwisha kufa kama manabii wengine wa Mungu walahakuwa zaidi ya nabii. Ujaji wa pili wa Yesu Kristo unaoaminiwana Wakristo na Waislamu kwa pamoja ulimaanisha kutokeakiroho siyo kimwili. Ndivyo alivyoambiwa Hadhrat MirzaGhulam Ahmad na Mungu. Na akapashwa habari pia ya kwambaMungu amemtuma yeye ili kutimiza bishara hiyo.

Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. alitokana na ukoo mmojawenye heshima wa Panjab. Shughuli kubwa zaidi za ukoo wakezilihusikana na kujijenga kiutajiri na heshima, lakini yeyealijitenga na shughuli za kidunia na akapitisha wakati wakemwingi katika ibada ya Mungu na kutaali vitabu vya dini. Alikuwamtu asiyejulikana katika dunia, hata katika kijiji alimozaliwahakujukana sana. Kisha akaanza kujitokeza katika ulimwenguwa kidini nchini India kama mtu thabiti mwaminifu na shujaamwenye kupigania miradi ya Kiislam. Akawa mwenye kujulikanakuwa mtu Mtakatifu sana hata kwamba si tu ya kuwa Waislamu

137

Ukristo katika zama hizi

Page 144: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

pekee walimheshimu bali hata wafuasi wa dini nyingine naowakampa heshima sana. Watu wakaanza kushuhudia ya kwambayeye anaongea na Mungu ambaye maombi yake yanapokelewana ambaye huruma yake kwa wanadamu na kusumbuka kwakekwa shida za watu ni jambo la hakika kabisa lisilo na shaka.Katika zama hizo, Islam katika India kwa bahati mbaya ilikuwana hali mbaya mno. Hiyo ililengwa na wamishionari wa Kikristoambao sawa na mfumo wa himaya ya Uingereza wakaanzishavikali shughuli za siyo kuyashambulia mafunzo ya Kiislamu tubali na Mwanzilishi Mtakatifu wa Islam pia. Isitoshe, katika diniya Kihindu, iliyo dini kubwa katika India, miendeleo iliyonuiakutaka makuu ilianza kuzalika iliyokuwa na mpango wenye nchambili: Kuhuisha utamaduni wa desturi za kihindu, na kufutiliambali Islam na Waislamu nchini India kwa kueneza ya kwambahao sio wananchi halisi bali ni wageni ambao hawana haki yakuimarika katika nchi hiyo. Miongoni mwa miendeleo hiyo, mkalizaidi ulikuwa ni Mwendeleo wa Arya Samaj ulioanzishwa naPandit Swami Dyanand Sarsvasti (1824-1883) mnamo mwaka1875. Huo pengine ulimhimiza zaidi Hadhrat Mirza GhulamAhmad a.s. kuanza kuchunguza sana mambo ya dini mbalimbalikwa shabaha ya kuitetea Islam.Mtaala wake huo wa dini mbalimbali ukaimarisha zaidi imaniyake katika ubora wa mafunzo ya Kiislam. Aliathirika mno naKur'ani Tukufu jinsi ilivyoshughulikia matatizo ya binadamu.Aligundua ya kwamba Kur'ani baada ya kufundisha khulka borahaikuishia tu hapo, bali iliendelea kuleta hoja madhubuti za kiakilizilizosaidiwa na ushuhuda ya kwamba mafundisho hayo ndiyoyanayofaa sana kufuatwa katika hali kadha wa kadha.

Mwishowe mtaala wake huo ukamwezesha kuishindisha Islamambayo katika zama hizo haikuwa na uwezo wa kujitetea. Hivyobasi, yeye alifanya kazi ya muhimu sana iliyohitajika kwa kuiteteaIslam katika India katika zama hizo. Alianza kujulikana baina yawatu alipoanza kufanya maongezi na mijadala na makundi ya

138

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 145: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

watu wachache kwanza lakini eneo lake likapanuka pole pole.Akaanza kujulikana kote kote kuwa msimamizi wa miradi yaKiislam aliye mwenye akili nyingi na mwenye kuogofya sana.Katika zama hizo yeye akaanza kutunga kitabu kikubwa sanakuhusu utaalamu wa kidini. Kitabu hicho, Barahine Ahmadiyya,alinuia kuandika majalada yake hamsini. Lakini alipokuwaamekwisha chapisha majalada manne tu akapatwa na mambokadha ambapo ikawa haikuwezekana kwake kuendelea na kaziya kitaalamu mpaka mwisho. Hata hivyo aliandika vitabu vingikwa kulingana na haja za wakati huo. Vitabu vyake vilieleza yoteyale aliyokuwa amenuia kuyaandika mwanzoni bali na zaidi pia.Kwa kweli akatimiza zaidi ya ahadi yake ingawaje siyo kwa jinahilo la Barahine Ahmadiyya. Inashangaza aliwezaje kuandikavitabu vingi hivyo peke yake bila kupata msaada sana wa kikarani.Vitabu, nyaraka na makala alivyowahi kuandika ni takriban miamoja na kumi hivi.Siyo tu maandiko yake ya kitaalamu yaliyompa umashuhuri sanakatika Bara Hindi zima, bali sifa zake za kiroho pia zilikuwa nisababu kubwa ya yeye kujulikana sana na kuheshimika.Katika hali hiyo ya yeye kuzidi kupata heshima Mungu akamtumaili kubeba wajibu mzito wa kuwa Mwongozi mrekebishaji wazama za mwisho aliyekuwa anatazamiwa na kungojewa na karibudini zote za dunia. Kwa kulingana na nadharia ya Waislamu yeyealikuwa Al-Mahdi, msuluhishi aliyeongozwa na Mungu. Nakulingana na itikadi ya Kikristo na Waislamu yeye aliinuliwakwa daraja la kuwa Masihi Aliyeahidiwa ili kutimiza bishara zaujaji wa mara ya pili wa Yesu Kristo. Lakini kutumwa hukukulisababisha yeye kupoteza umashuhuri wake na kupendwakwake na watu, hali aliyokuwa nayo hapo kabla. Papo hapoHadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. alitengwa na kukataliwa si tuna wafuasi wa dini nyingine bali vikali zaidi na Waislamuwenyewe wa India ambao yeye alikuwa anaitetea dini yao kwabidii kubwa mno.

139

Ukristo katika zama hizi

Page 146: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Tuseme yeye alizaliwa upya kiroho. Jinsi alivyokuja dunianiakiwa peke yake, ndivyo alivyoanzia uhai mpya akiwa peke yakekatika ulimwengu wa kidini, akiisha achwa kwa kitendo na watuwote waliokuwa pembeni mwake. Lakini Mungu hakumwacha.Akahakikisha mara kwa mara kupatiwa msaada wa Mungu kwanjia ya Wahyi aliofunuliwa katika muda alipofanyiwa uadui mkalisana. Wakati mwingine alifunuliwa yafuatayo:

Hizo ni baadhi ya funuo zake zilizomsaidia na kumpa nguvu katikahali alipokuwa peke yake na ambapo alikataliwa na wapinzaniwake. Sasa miaka zaidi ya mia moja imepita, na mamboyaliyodhihirika polepole na kwa mfululizo yanahakikisha ukweliwa madai yake na bishara zake na ukweli wa funuo zake.Mtu huyo aliyekuwa mmoja tu pekee sasa wafuasi wake waliozaidi ya milioni kumi wanapatikana katika nchi mia moja nathelathini na nne wakitawanyika katika mabara matano. Ujumbewake umekwisha fika hadi pembe za dunia, kutoka Magharibi yambali hadi Mashariki ya mbali. Anakubaliwa kuwa KiongoziMwongofu na Masihi Aliyekuwa Ameahidiwa kuja mara ya pili,katika Marekani, katika Yuropa, katika Afrika, katika Asia, hatakatika visiwa vilivyo mbali sana vya bahari ya Pasifiki ya kusini-mashariki, kama vile Fiji, Tuvalu, visiwa vya Soloman nakadhalika. Hata hivyo wafuasi wake wanaweza kufananishwa nakidimbwi kidogo kulingana na bahari kubwa ya ulimwengu waKikristo.Ufaulu wa Jumuiya ya Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.sunahitaji maelezo marefu lakini nafasi tuliyo nayo ni ndogo. Hatahivyo ni jambo la kuzingatia ya kwamba hakuna mwendeleowowote wa kidini katika zama hizi ulio imara, uliosonga mbele

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Mwonyaji mmoja alikuja duniani, lakini dunia haikumpokea; lakiniMungu atampokea na atadhihirisha ukweli wake kwa mashambuliomakali.

Mimi nitafikisha ujumbe wako hadi pembe za dunia.

140

Page 147: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

na kuenea haraka kwa hatua hii. Hiyo siyo dhehebu wala kitukinachotamaniwa sana lakini kwa muda. Huo ndiyo ujumbe wamaana sana - kazi ngumu inayohitaji bidii kubwa na maadili kwawale wanaothubutu kuufuata. Wanaoufuata, kwa hakika,wanafanya hivyo kwa kukubali wajibu mzito wanaotakiwakutimiza maisha yao mazima. Huo ni mgumu kama ilivyokuwajamii ya kale ya Waesseni. Kuupokea siyo kusuhubiana katikahali ya raha, bali ahadi ya kutimiza maisha mazima. Wanaoingiakatika Jumuiya hii wanalazimika kutengana na furaha zisizofaakatika maisha, siyo kama ulivyo mtindo wa wale wanaojinyimahata furaha za halali au wale wanaoitwa Watawa wanaokaa katikaupweke pasipo kuoa na kadhalika, bali kwa imani thabiti, kujitoleasana na utulivu wa moyo unawawezesha kutoa dhabihu nakuvumilia shida kwa wema wa hali ya juu sana katika njia hii.Yeye aliunda Jumuiya inayopatikana duniani kote ambayo hainakifani chake katika kutoa sadaka ya mali sana. Wanajumuiya wotewenye mapato wanajilazimisha kutoa kwa uchache sehemu yakumi na sita ya mapato yao katika njia hii njema. Roho ya kujitoleamhanga na kiasi cha bidii inayofanywa duniani kote inashangazamno. Hata hivyo hayo yote yanatendwa pasipo kushurutishwahata kidogo. Wale wanaoweza kutoa sehemu ya bidii yao nasadaka ya mali yao hujihesabu kuwa ni wenye bahati njema sana.Hiyo ni Jumuiya inayojitegemea kabisa katika mambo ya fedha.Mpango huo wa kuchanga mchango kwa hiari unaendelea kufanyakazi duniani kote tangu miaka mia moja iliyopita kwa uaminifuwa hali ya juu sana na wema mwingi kabisa. Humo ndimo imosiri ya ufaulu wake katika kujitegemea pasipo kuathirika na sababuza nje kwa zaidi ya karne moja. Lakini hiyo ndiyo jiha moja tu yakuiangalia Jumuiya hii. Kuangalia sifa za Wanajumuiya wakekwa jiha nyingine kunaleta picha ya kuvutia mno. Hii ndiyoJumuiya inayojulikana kwa khulka zake njema, kukaa kwa amani,kupendana na kuheshimu sana khulka za kibinadamu. Hii ndiyoJumuiya ya dini inayosifiwa sana duniani kote kwa sababuinaiheshimu sheria ya nchi na kuthamini

141

Ukristo katika zama hizi

Page 148: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kuhusiana na watu bila kujali dini, rangi na imani.Msomaji anaweza kufikiria pengine ya kwamba tumetoka nje nakuingia katika habari isiyohusikana na madhumuni yenyewetuliyokuwa twazungumzia. Hebu tumdokezee msomaji huyo kwaheshima ya kwamba yeye amekosa shabaha. Habari hiyoitaonekana inalingana na madhumuni tuliyokuwa twazungumziakama tukizingatia kauli hii ya Yesu Kristo ya kwamba mtihujulikana kwa matunda yake.2

Kama kuna mtu leo anayependa kweli kuhakikisha ukweli wamadai ya Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. hicho ni kipimokinachoweza kutegemewa kabisa. Sawa na kipimo hichoinawezekana kuamua ya kwamba yeye alikuwa kweli MasihiAliyeahidiwa ambaye ujaji wake ulitabiriwa si tu na Yesu Kristobali na Mwanzilishi Mtukufu wa Islam pia. Kugundua kwambayeye alizalisha wafuasi wa aina gani na karne moja iliyopitailiwatendeaje itakuwa ni kazi ya kufaa sana. Swali litazuka piaya kwamba je, wanatendewa na zama jinsi walivyotendewawafuasi wa Yesu Kristo katika karne ya kwanza ya Kikristo? Tenahakuna budi swali lizuke ya kwamba na Mungu AlimtendeajeHadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. wakati alipojaribiwakuangamizwa na kufutiliwa mbali yeye na Jumuiya yake? Je,Mungu aliitendea kwa upendo Jumuiya hiyo iliyokuwa inasakwaama akaitendea kinyume chake? Je, kama Wakristo wa kale,wafuasi wa Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. pia walipatakusaidiwa na Mungu katika shida? Ikiwa kila mara walipoteswana kusagwa kwa dhuluma badala ya kusagika tikitiki wakajitokezawakiwa wengi zaidi na wenye nguvu maradufu na heshima nyingikuliko

__________________________

2 Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwambaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mtihutambulikana. (Mathayo 12:33).

142

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 149: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

zamani, hapo bila shaka madai ya mdai kama huyo hayawezikupuuziliwa mbali kama jambo lisilo na maana. Hayo siyo madaimakubwa ya mwendawazimu, au mawazo ya kupendeza ya mtuazoeaye kuwaza mambo yasiyo ya kweli. Uahmadiyya umeishakuwa hakika inayotakiwa kutiwa maanani sana zaidi kulikoUkiristo ulivyoonekana mwishoni mwa karne yake ya kwanza.

Hapa pana habari ya Masihi aliyekuwa kweli ya historia walahakuwa mazao ya ngano, na hapa tena pana habari ya Masihiambaye ujaji wake mara nyingine ulikuwa hakika halisi jinsiulivyokuwa ujaji wake wa mara ya kwanza akiwa ametumwakuwa mwongozi wa dini. Sasa ni juu ya watu wa zama hizikujichagulia kuendelea kuishi katika ulimwengu wa simulizi namawazo yasiyo na msingi na kudumu kuwangojea viongoziwalioahidiwa na dini na imani zao au kuzikubali hakika halisi zamaisha haya. Jambo moja lazima tulikubali ya kwamba viongoziwengi wa dini wamekwisha pandishwa kutoka cheo cha kawaidacha binadamu hadi cheo cha kuwa miungu. Mara nyingi viongoziwa dini walifikiriwa kupaa mbinguni kusubiri huko katika konaza mbali sana angani ili kuja tena kuitembelea sayari ya Ardhi.Hakuna sababu kwamba mtu alikubali dai moja la aina hiyo nakuyakatalia mengine ya aina hiyohiyo, kwani ni madai matupupasipo uthibitisho halisi wowote wa kisayansi kuhakikisha ukweliwake. Basi hakuna hiari yoyote isipokwa tu kuyakubali yote hayoama kuyakataa yote kwa jumla. Hiyo itakuwa njia ya kutendauaminifu na uadilifu. Naam, lipo jambo moja la hakika sana yakwamba walipokwisha ondoka dunia hii, bila kujali waliaga kwanjia ipi sawa na imani ya wafuasi wao, kamwe hawakurejeaduniani humu hata mmoja wao katika historia nzima ya binadamu.Aidha, ni jambo la hakika kabisa pia ya kwamba watawa naviongozi wote wa dini walionyanyuliwa kwenye cheo cha kuwamiungu au washiriki wa Mungu walianzia maisha yao kama watuwa kawaida hadi walipokufa. Ni wafuasi wao tu waliowafanyakuwa miungu. Lakini kumbukeni hata mmoja kati yao hakuonesha

143

Ukristo katika zama hizi

Page 150: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

kuwa anashughulikia kazi ya kuendesha kanuni za asili zaulimwengu. Daima Yupo Mmoja tu anayeonekana anaendeshana kutawala kanuni za ulimwengu. Kioo cha mbingu na kanuniza asili za ulimwengu vinaonesha uso wa Mungu Mmoja tu pekee.Kurani Tukufu inasema:

MWISHO:Ama kuhusu swali hilo, twaona tumekwisha lieleza vya kutosha.Lakini kabla hatujamalizia habari hiyo, twapenda kuwasihiWakristo kwa jazba kubwa waachane na mawazo yao yakujifurahisha yasiyo na msingi na kukubali hakika ngumu zamaisha.Yesu Kristo alikuwa mtu mkamilifu kulingana na zama zake,lakini hakuwa zaidi ya binadamu. Alifikia ule upeo aliokuwaamekadiriwa kuufikia akiwa nabii maalum wa Mungu aitwayeMasihi. Jambo hilo likamfanya kuwa wa pekee kati ya manabiiwaliokuja baada ya Musa hadi alipokuja yeye.Kwa hakika kila nabii alikabidhiwa kazi ngumu kuitekeleza.Wanalazimika kuwarekebisha watu ambao wanageuka kuwawabaya moja kwa moja. Kwa Yesu, kazi yake hiyo ilikwa ngumuzaidi kwani si tu kwamba yeye alitakiwa kupigana na maovu yakawaida ya jamii, bali pia alipaswa kuleta mabadiliko yakimapinduzi katika mwendo wa Wayahudi.

144

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Nao husema: Rahmani Amejipangia mwana. Bila shaka mmeleta jambolichukizalo. Karibu mbingu zitatuke kwalo na ardhi ipasuke na milimaianguke vipande-vipande, kwa sababu wamemdaia Rahmani kuwa namwana. Wala haimpasi Rahmani kupanga mwana. (19:89-93)

Page 151: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Kama inavyofanyika kwa wafuasi wa kila dini ya kwambawanaanza kupotoka njia polepole wakiachana na ukweli nakuhangaika katika nyika za dhambi, ndivyo ilivyotendeka kwaWayahudi pia. Wakati alipodhihirika Yesu, hao walikuwa kwadhahiri wamekwisha kufa kiroho. Maji ya uhai wa dini yalikuwayamekupwa, kwa kuacha nyuma nyoyo ngumu kama mawezilizokwisha kufa. Kazi aliyokuwa amepewa Yesu ilikuwakuzigeuza hizo kuwa nyoyo za binadamu zinazodunda nakububujisha kutoka humo chemchem za huruma ya kibinadamu.Huo ulikuwa mwujiza alioutenda Yesu na humo mnapatikanaukuu wake.Sasa Waislamu na Wakristo wakiwa pamoja wanapomngojeaYesu Kristo aje mara ya pili duniani, wanapaswa wasisahau yakwamba Yesu aliyekusudiwa kuja analazimika kuwa Yesu yulekisifa na kikazi ya dini. Walakini sawa na bishara za Mwanzilishiwa dini ya Kiislamu, Mtume Muhammad s.a.w., Yesu huyualitakiwa kuja mara ya pili si katika ulimwengu wa Kikristo balikatika ulimwengu wa Kiislamu. Na safari hii ni nyoyo zaWaislamu wa zama za mwisho atakazopewa kuzigeuza nakuzirekebisha. Muradi huo wa ujaji wake wa mara ya piliunaungwa mkono na baadhi ya bishara nyingine za Mtume s.a.w.Yeye alitabiri ya kwamba hali za Waislamu katika zama zamwisho zitafanana kabisa na hali za Wayahudi walipokuwawamekwisha haribika, jinsi kiatu kimoja kinavyofanana sana nakiatu cha pili cha jozi hiyo moja.Hivyo kama maradhi ni yale yale, basi na tiba pia ni ile ile. Masihihana budi kurejea duniani akiwa mtu mnyenyekevu, siyo mtuyuleyule binafsi bali kiroho na kisifa, na ndivyo hivyoilivyofanyika kwa kitendo. Watu wa dini kama hao wanaokujakuleta mapinduzi ya kiroho daima huzaliwa katika hali yakutokujulikana na huwa watu wapole wanyenyekevu na wanaishimaisha kwa unyenyekevu. Hao wanarejea katika duniakuitembelea kabisa kwa njia hiyo na wanatendewa pia kikatili nakwa chuki na uadui mkali sana. Hawatambuliwi kwa urahisi kuwa

145

Ukristo katika zama hizi

Page 152: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

ni wajumbe wa wale walioahidi kurejea tena.Alivyotendewa Kristo mara ya kwanza na Wayahudi, ndivyohivyo alivyolazimika kutendewa mara ya pili lakini safari hii kwamikono ya Waislamu na Wakristo waliokuwa wakingojea kurejeakwake. Matumaini yaleyale yaliyopindama yasiyo ya kweli,shabaha zilezile za kuwaza zisizo za hakika alizotazamiwakuzifuata, nadharia zilezile zisizokuwa sawa za kazi zake na ufauluwake hapa ardhini, vyote hivyo jinsi vilivyodhihirishwa naWayahudi wa zama za Yesu Kristo, ndivyo vilivyotakiwakurudiwa na Waislamu katika zama za ujaji wake wa mara yapili. Na kwa njia hiyo historia ilitakiwa kujirudia mara nyingine.Kwa kuangalia nyuma, mtu anaweza kutambua vizuri zaidi sababuza Wayahudi kushindwa kumtambua Masihi wao. Twawezakuzingatia kwa urahisi shida yao na kujifunza kutokana na msibawao. Kuchukua maana ya dhahiri ya maandiko yao kuliwapoteza.Hayo yote yamekwisha zungumzwa tayari, lakini ili kusisitizahabari hiyo twaikumbusha tena. Siku zote inafanyika hivi katikahistoria ya viongozi wa dini wanaotazamiwa kuja ya kwambawatu wao wanaowangojea zaidi, mara nyingi wanashindwakuwatambua, kwani alama za utambuzi wao zinasomwa vibayana zinatambuliwa vibaya. Mambo ya hakika yanageuzwa kuwaya kubuni, na mafumbo na mithali huchukuliwa katika maana yadhahiri.Yote hayo takriban yamerudiwa wakati wa ujaji wa mara ya piliwa Masihi, Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. wa Qadian. Jinsialivyotazamiwa Eliya kuteremka kutoka mbinguni na Wayahudiwa zama za Yesu Kristo, ndivyo mtu fulani alivyokuwaanatazamiwa kushuka kutoka mbinguni mara nyingine tena, nayealikuwa Masihi Mwenyewe safari hii.Wayahudi walikuwa wanamtazamia Masihi kufika katika utukufuna kuwaongoza kwenye zama mpya za kupata utawala nakuwashinda mabwana zao wa Kirumi. Matumaini hayo yoteyalivunjika tikitiki alipofika Yesu wa Nazareti. Maana, kwa vyovyote alipofika, alionekana mbali sana na ile picha waliyokuwa

146

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

Page 153: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

wamechora katika mawazo yao tangu karne nyingi kuhusu ujajiwa Masihi.Ni jambo la kushtusha ya kwamba matukio kama hayo yametukiasasa ambapo amekuja Kristo kwa sura ya Hadhrat Mirza GhulamAhmad wa Qadian. Waliyotenda wapinzani wake ndiyo yale yaleisipokuwa majina ndiyo tofauti. Waislamu kwa jumla na Wakristokwa pamoja wameshikilia kazi ya Wayahudi wa zama za Yesu.Upinzani ni uleule. Hoja za kumkataa ndizo zilezile. Hata hivyoalimtendea mja wake huyu mnyenyekevu kwa kumpatia isharakubwa zaidi za kumsaidia kuliko Yesu wa zamani na kumsaidiayeye kueneza ujumbe wake haraka zaidi katika nchi nyingi zaidina katika mabara yote ya ardhi. Hayo ndiyo mambo ya kweliyaliyo dhahiri shahiri, lakini kwa wale wenye masikio ya kusikia.Hayo ndiyo mambo ya kweli ambayo yanaendelea kudhihirikawaziwazi pamoja na kupita wakati, lakini kwa wale tu wanaojalikuangalia.Isitoshe, kiini cha ujumbe wa Masihi kulingana na hali za sasa zaWaislamu na Wakristo siyo tofauti. Lakini wataufahamu waleambao hawatafumba macho yao.

Hebu mwishowe niwakumbushe Wakristo na Waislamuwanaongojea ujaji wa mara ya pili wa Kristo tangu karne nyingizilizopita, maneno aliyonena Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad waQadian, aliyefanywa na Mungu kuwa Masihi wa zama za mwisho,ambayo ndiyo yafuatayo:

147

Ukristo katika zama hizi

Kumbukeni ya kwamba hakuna atakayeshuka kutoka mbinguni.Wapinzani wetu wote walio hai wakati huu watakufa wote wala hamnakati yao yeyote atakayemwona Yesu mwana wa Mariamu akishukakutoka mbinguni. Kisha wazao wao watakaobaki nyuma yao naowatakufa, wala hamna kati yao vilevile yeyote atakayemwona Yesumwana wa Mariamu akiteremka kutoka mbinguni. Kisha wazao wawazao wao pia watakufa wala hawatamwona Yesu mwana wa Mariamuakishuka kutoka mbinguni. Ndipo Mungu atawatilia nyoyoni mwaofadhaa ya kwamba zama za utawala wa msalaba pia zimekwisha pita,na hali ya dunia imebadilika tayari, lakini mwana wa Mariamu

Page 154: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Basi mwaweza kusubiri hadi kizazi kipya kizaliwe. Hao naowatangojea mpaka mwisho na kizazi kingine kipya kitashikamahali pao. Hali hiyo ya kungojea yaweza kuendelea hadi sikuya mwisho, lakini hakuna Yesu atakayeteremka kimwili kutokambinguni. Fikara zao kuhusu ujaji wake binafsi kimwilihazitasadikika kamwe, hata wakitamani sana namna gani kurejeakwake. Wanaweza kujijengea ukuta wa vilio jinsi walivyofanyaWayahudi miaka elfu tatu iliyopita. Na wanaweza kugongavichwa vyao kwenye ukuta huo. Lakini jinsi ilivyotendeka kwaWayahudi, ndivyo itakavyotendeka tena. Hawatamwona Masihiyeyote kushuka juu ya maombolezo yao kizazi hata kizazi hatakizazi. Matumaini yao ya ujaji wa Kristo katika siku zijazohayatazalisha chochote ila patupu. Hayo ni matazamio matupukabisa.Ama kwa Wakristo wale wanaomchukua Kristo kuwa mwanawa Mungu katika maana ya dhahiri, twamaliza maelezo haya kwakutoa maonyo ya Kurani Tukufu ambayo ni kitabu cha Mungukilichofunuliwa kwa Mtume Mtukufu wa Islam. Hicho kinaelezashabaha ya ujaji wake kikisema:

__________________3 Ruhani Khazain, J 20: Tadhkiratush Shahadatain uk 67

148

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu

hajateremka kutoka mbinguni. Ndipo wenye busara watachoka maramoja na imani hiyo: Na haitapita karne ya tatu tangu leo hii hata kwambawamngojeao Yesu, wakiwa Waislamu na Wakristo, kwa kukata tamaana kudhania vibaya wataachana na imani hiyo mbovu.3

Yeye (Mtume Mtukufu wa Allah) awaonye wale wanaosema: MunguAmepanga Mwana. Wao hawana elimu ya jambo hili, wala babazao. Ni neno kubwa litokalo katika vinywa vyao; hawasemi ilauwongo tu. (18: 5-6)

Page 155: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

NYONGEZA I

Orodha ya baadhi ya vitabu vinavyotaja habari za Marhamu ya Yesu pamojana kueleza ya kuwa marhamu hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya Yesu, yaanikwa kumtibu majeraha yake. Tafadhali kumbukeni ya kuwa kwa jumla vitabuvinavyoeleza hayo ni zaidi ya elfu moja. Hapa chini twataja baadhi yake:

Qanun, na Shaikh-ul-Rais Bu Ali Sina, J 3, Uk 133.Sharha Qanun, na Allama Qutb-ud-Din Shirazi, J 3.Kamil-us-Sunnat, na Ali Bin Al-abbas Al-Majusi, J 3. Uk 602.Kitab Majmua-e-Baqai, Muhammad Ismail Mukhatif az Khaqan, na Khitab

pidar Muhammad Baqa Khan, J 2, uk 497.Tadhkirai Ulul-Albab, na Sheikh Dawud-ul-zarir-ul-Antaki, uk 303.Qarabadin-i-Rumi, kilichokusanywa katika zama zilizo karibu na Yesu na

kilifasiriwa katika enzi ya mamun al - Rashid katika Kiarabu, angaliahabari ya marahamu hiyo chini ya Skin Diseases.

Umdatul - Muhtaj, na Ahmad bin Hasan Al-Rashidi al-Hakim. Katika kitabuhiki Marhamu ya Yesu na dawa nyingine zimetajwa kutoka katika vitabumia bali zaidi ya mia. Vitabu hivyo vyote viko kwa kifaransa.

Shifaul-Asqam, J 2, uk 230.Mir’atush-Shifa, na Hakim Natho Shah - (Muswada) Skin Diseases.Zakhira-i-Khawarazm Shahi, Skin Diseases.Sharha Qanun Gilani, J 3.Sharha Qanun Qarshi, J 3.Qarabadin, na Ulwi Khan, Skin Diseases.Ilajul Amradh, na Hakim Muhammad Sharif Khan Sahib, uk 893.Qarabadin Unani, Skin Diseases.Tuhfatul - Muminin, kwenye hashiya ya Makhzanul - Adwiya, uk 713.Muhfit fi Tibb, uk 367.Aksir-i-A'dham, J 4, na Hakim Muhammad Adham Khan Sahib,

Al-Mukhtabba ba Nadhim-i-Jahan, uk 331.Qarabadin, na Masumi-ul-Masum bin Karamu-Din Al-Shustri Shiraz.Ijala-i-Nafiah, na Muhammad Sharif Dehlavi, uk 410.Tibbi-Shibri, yajulikana pia kwa jina Lawami Shibriyya, na Seyid HussainShibr Kazimi, uk 471.Makhzan-i-Sulaimani, tafsiri ya Iksir Arabi, uk 599, na Muhammad Shams-

ud-Din wa Bahawalpur.

149

Ukristo katika zama hizi

Page 156: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Shifa-ul-Amradh, tafsiri ya Maulana Al-Hakim Muhammad Nur Karim,uk 282.

Kitab Al-Tibb dara Shakohi, na Nur-ud-din Muhammad Abul Hakim, Ain-ul-Mulk Al Shiraz, uk 360.

Minhaju-ud-Dukhan ba Dastur-ul-A'yan fi Amal wa Takrib al - Nafiah lil-Abdan, na Aflatun-i-Zamana wa Rais-i-Awana Abdul Mina Ibn nasrul-Ataa

Al-Israili Al-Haruni (yaani Myahudi) uk 86.Zubdatul-Tibb, na Seyid Al-Imam Abu Ibrahim Ismail bin Hasan-ul-Husaini

Al-Jurjani, uk 182.Tibb-i-Akbar, na Muhammad Akbar Arzani. uk 242.Mizan-ul-Tibb, na Muhammad Akbar Arzani, uk 152.Sadidi, na Rais-ul-Mutakallimin Imamul Muhaqqiqin Al-Sadid-ul-Kaz-runi,

J 2, uk 283.Hadi Kabir, na Ibn Zakariyya, Skin Diseases.Qarabadin, na Ibn Tilmidh, Skin Diseases.

Orodha hiyo hapo juu imenakiliwa kutoka kwenye ‘Jesus in India’kilichoandikwa na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad wa Qadian, MasihiAliyeahidiwa, uk 56-57.

150

Page 157: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

NYONGEZA II

Parthenogenesis: Kuzaa bila ya kuingiliana, yaani 'yai' la kike kukua nakufanyika kiumbe pasipo kushika mimba kwa kuchanganyika na mbegu zakiume.Parthenogenisis ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa vijidudu na piakatika samaki, na ni desturi katika vijidudu vile kama nzi wa kijani kibichi(greenfly) wanaoharibu mimea. Miongoni mwa wanyama watambaazi, jambohili linaweza kufanyika kati ya mijusi katika mahali penye kunyesha kidogosana mvua pasipo kutabiriwa.1

Katika Lancet mnamo 1955 iliripotiwa ya kwamba mama mmoja alizaa bintiambako parthenogenesis haikuweza kukanushwa. Jambo hili limefanyizwakimajaribio katika wanyama wanaonyonyesha watoto wao. Lakini hatunataarifa ya uzazi katika wanyama wanyonyeshao kwa njia ya parthenogenesis.Kwa wingi, ufaulu umepatikana kiasi hiki ya kwamba panya na sungurawalishika mimba kwa njia hii na mimba ikapata kukua mpaka nusu yakelakini kisha mimba ikaharibika.Kati ya wanadamu hivi majuzi uchunguzi ulifanywa juu ya 'Parthnogenesiskufanyika na kuchunguzwa kimpango na ukuaji wa 'yai' la kibinadamumapema.' 2 Katika uchunguzi huo, 'mayai' ya mwanamke yalichukuliwa, lileliliokuwa limefanyika tu na lile lililogusana na mbegu za kuime lakinihalikushika mimba na yote mawili yalibenuliwa kwa ionophore ya dawa yaalcohol au calcium na yakachunguzwa kushuhudia yaliofanyika. Matokeoya uchunguzi huu yalikuwa ya kwamba upo uwezekano wa 'yai' la mwanamkekushika mimba kwa njia ya parthenogenesis kwa kutumia ionophore yacalcium, lakini kidogo zaidi kuliko inavyoshuhudiwa katika panya. Parthenoteza mwanamke zaweza kukamilisha mgawanyiko hadi hatua ya seli 8. Hayoyanaleta uwezekano ya kwamba mimba iliyoharibika mapema inaharibikakwa sababu ya 'mayai' yaliyoshika mimba ghafula kwa njia yaparthenogenesis.

Tukio moja la parthenogenesis nusu nusu liliripotiwa katika gazeti la NewScientist la tarehe 7 Oktoba 1995 chini ya kichwa cha maneno, 'The boywhose blood has no father'3 (Yaani mtoto ambaye damu yake haina babamzazi). Katika wanaume seli zote zinatakiwa kuwa na Y Kromosom moja,

_______________________

1 Genetics : 1991 September : 129 ( 1 ): 211-92 Fertility - Sterility - 1991 Novemba; 56 (5) : 904-12.

151

Nyongeza I

Page 158: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

lakini seli nyeupe za damu ya mvulana huyo zilingunduliwa kuwa na XXKromosom pekee. Mwenye kutoa ripoti anaeleza pia ya kwamba mara mojamoja kike cha kromosom kinakuwa na X kromosom moja iliyomo humo piakijine (gene) cha kiume, na wachunguzi kwanza walidhani ya kwamba mfanohuu wa mvulana ndiyo mfano wa alama zinazoashiria kwenye hali hiyo isiyoya kawaida. Lakini walipotumia ufundi mwepesi sana wa DNA hawakuwezakugundua hata Y kromosom moja katika seli nyeupe za damu ya mvulanahuyo. Hata hivyo ngozi ya mvulana iligunduliwa kuwa tofauti isiyolinganana damu yake, maana ilikuwa na kromosom X na Y pia.Uchunguzi zaidi wa X kromosom katika noizi na damu ya mvulana ulitoboaya kwamba X kromosom zake zote zilikuwa zinafanana kabisa na zilitokanana mamake peke yake. Kadhalika sehemu zote mbili za jozi nyingine 22 zakromosom pia zilikuwa zinafanana moja kwa moja, na zote zilitokana namamake. Maelezo yaliyotolewa na wachunguzi ni kwamba 'yai' lisiloshikamimba likaanza kujigawa katika seli zifananazo; kisha seli mojawapo ikapatwana mbegu ya baba mzazi, basi mchanganyiko wa seli hizo ukaanza kukuakama mimba ya kawaida. Jambo hili linahakikisha ya kwamba selizinafanyizwa kwa njia ya parthenogenesis katika wanyama wanyonyeshaosiyo kila mara zinalemaa. Katika mfano wa mvulana huyo hizo ziliwezakufanyiza utaratibu wa kawaida wa damu.

HERMAPHRODITISM:Mtu kinyume cha kawaida anakuwa na sehemu zote mbili za uzazi, ya kiumena ya kike pamoja. Sehemu zake za nje zina dalili za yeye kuwa wa kike nawa kiume, na kromosom zake zinaonyesha mchanganyiko wa kiume na kike(XX/XY).Katika uchunguzi mmoja huko Netherlands mnamo mwaka 1990 ulioitwa'Combined Hermaphroditism and Auto-fertilization in Domestic Rabbit',sungura mmoja aliyekuwa Hermaphrodite (huntha) kweli aliwapanda sungurawengi majike. Matokeo yake ni kwamba hao majike wakazaa watoto 250ambao kati yao walikuwapo majike na madume pia. Katika majira mengineya kuzaa, huyo sungura huntha ambaye alikuwa amewekwa upwekepasipoweza kugusana na sungura wengine, akatunga mimba na hatimaye

__________________________

3 Ripoti hii inahusiana na uchunguzi wa David Bonthron na wengineo na unarejezakwa toleo la Octoba 1995 la Nature Genetics ambamo ripoti hii inapatikana.

152

Page 159: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

akazaa sungura majike na madume saba kwa jumla. Mchanganyiko wakromosom ulionyesha idadi kubwa ya Autosomes na kromosom mbilizisizobainika vizuri kuwa ni za kuime ama za kike.Uchunguzi ulifanywa juu ya mtu-huntha katika idara ya Obstetrics andGynaecology, Chicago, Lying-in Hospital, Illinois. 4 Shabaha ya uchunguzihuo ilikuwa kuhakikisha matukio yanayosababisha huntha wa kweli mwenye46xx, 46xy kupatikana na kuripoti mimba ya kwanza katika huntha halisimwenye 46xx, 46xy aliye na sehemu za kike na kiume za uzazi.Mpango wa uchunguzi huu ulioshughulikia kuchunguza Kromosomuliofanywa juu ya Iymphocytes za mgonjwa, na antigenes za seli nyekundu,Ieucocytes antigene za binadamu na kuwepo kwa y-kromosomdeoxyribonucleic acid zilichanganuliwa. Matokeo yake yalilinganishwa navifungu vya damu ya baba mzazi na ndugu na dada zake.Natija ya uchunguzi huo ilihakikisha ya kwamba mgojwa wetu ni kitu chenyeuhai ambamo mna aina mbili kwa uchache za matengenezo ya seliyanayohitilafiana katika umbo la kiuzazi, na kwahiyo mgonjwa wetu huyoanatenda kazi mbili za baba na mama pamoja. Isitoshe, juu ya kuwa na sehemumbili, uke na uume, yeye alishika mimba na akazaa mtoto.

______________________________________________

4 Journal of Fertility and sterility - JC : evf 57(2) : 346 - 9 1992 Februari.

Nyongeza II

153

Page 160: UKRISTO - Ahmadiyya · 2012. 1. 17. · ya dini. Saikolojia mpya ya jamii na filosofia vikaanza kuongezeka haraka hususan mnamo karne ya kumi na tisa na ishirini. Falsafa za kidunia

Siyo kazi ya mwandishi au mhubiri wa Kikristo kufifisha Ukristoili uwafae watu wote walioelimika. Itikadi ya Mungu kuzaliwakwa sura ya mtu - Yesu ilikuwa kikwazo kwa Wayahudi naupumbavu kwa Wagiriki na ndivyo itakavyokuwa siku zote, kwaniitikadi hiyo si tu kwamba inaruka mipaka ya akili, hiyo ni fumbola hali ya juu sana na inaweza kuyakinishwa kwa imani tu kwaharara ya ndani na moyo wa kupenda. Kutia akili mahali pa imanikunamaanisha kifo cha Ukristo.

Keirkegaard

Ukristo - Safari kutoka Hakika kuelekea kwenye Ubunifu