wasifu kwa kifupi, prof sospeter muhongo) 20 machi 2015

2
1 Uongozi wenye Dira, Ubunifu na Ugunduzi – Uaminifu, Uadilifu na Kujituma – Stadi Bulibuli za Usimamizi na Uzoefu katika Uongozi – Uwazi na Ufanisi – Matokeo Yenye Tija na Ubora wa Hali ya Juu Prof Dkt Sospeter Muhongo, mwanazuoni maarufu, mwanajiolojia mbobevu na Mbunge wa Kuteuliwa, amewahi kuwa Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (April 2012- Januari 2015). Serikali ya Ufaransa ilimtunukia Cheo cha Afisa Mwenyetunu ya Kitaaluma Iliyotukuka - Ordre des Palmes Académiques (Iliyoanzishwa na Mfalme Napoléon Mwaka 1808) na ni mtu wa kwanza kupokea Tuzo (Mwaka 2004) inayoheshimika sana kwa Jamii ya Wanajiolojia wa Afrika ya Prof Robert Shackleton (UK) (Geological Society of Africa’s prestigious Prof Robert Shackleton Award), kwa ajili ya utafiti wa kipekee kuhusu Jiolojia ya Afrika ya miamba yenye umri wa zaidi ya miaka Milioni 500 (Precambrian Geology of Africa). Kwa kutambua mchango wake mkubwa wa kimataifa katika Sayansi na Ustawi wa Jamii ulimwenguni, Prof Muhongo amepewa nafasi nyingi zenye kuheshimiwa na wasomi na wataalamu maarufu Duniani, pamoja na kutambulika kwa ngazi za juu kabisa na Vyama na Taasisi zao za kitaaluma, kwa mfano: An Honorary Fellow of the Geological Society of London (Ilianzishwa Mwaka 1807), Honorary Fellow of the Geological Society of America (Ilianzishwa Mwaka 1888), an Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (Ilianzishwa Mwaka 1956). Ni Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Nchi Zinazoendelea (FTWAS), Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Chama cha Wanajiolojia wa Afrika (FGSAf) , Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Afrika (FAAS) na Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Tanzania (FTAAS) na nyingine kadhaa. Ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Tume ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW) na pia Mhariri Mkuu Mstaafu wa Jarida la Afrika la Sayansi za Miamba na Madini (The Journal of African Earth Sciences, Elsevier). Prof Muhongo ni Mshindi wa Mwaka 2014 wa Tuzo ya Heshima ya Jamii ya Wanasayansi wa Jiolojia na Uchimbaji Petroli na Gesi Asilia ya Nigeria (NMGS)/AMNI ya Prof M.O. Oyawaye. Prof Muhongo aliongoza na kusimamia mabadiliko endelevu ya ubunifu na ugunduzi katika Sekta za Nishati na Madini nchini mwetu kwa kuingiza sera mpya na kutengeneza nyaraka za kisheria, ameongeza idadi kwa wingi ya rasilimali watu iliyopata mafunzo mazuri ya kitaaluma katika Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia. Amesimamia ongezeko la kasi kubwa ya kampeni ya usambazaji umeme vijijini, na amesimamia usambazaji wa haraka na wa uhakika wa umeme mijini. Amesimamia punguzo kubwa la gharama za kuunganishiwa umeme vijijini na mijini. Amesimamia ongezeko la mapato katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kutokana na kodi na tozo mbalimbali kwenye madini yetu. Baadhi ya wachimbaji wadogo wamepatiwa mafunzo na ruzuku ya kuboresha uchimbaji wao. Tarehe 28.02.2015, Chama cha Wachimbaji Wadogo nchini (FEMATA) kilimteua, kwa kauli moja, Prof Muhongo kuwa Mshauri Mkuu wao. Prof Muhongo alisimamia utayarishaji wa mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Umeme nchini, ikiwemo TANESCO, na Juni 2014 Wizara ya Nishati na Madini ilitangaza mipango na miradi itakayotekelezwa kuhakikisha Taifa linapata umeme mwingi wa kutosha mahitaji yake, umeme unaopatikana kwa urahisi na kwa uhakika, umeme wa bei nafuu na umeme wa ziada (biashara) kwa manufaa ya uchumi wetu – Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap 2014-2025, Powering Vision 2025.

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 17-Jan-2016

12.184 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Wasifu Kwa Kifupi, Prof Sospeter Muhongo) 20 Machi 2015

TRANSCRIPT

Page 1: Wasifu Kwa Kifupi, Prof Sospeter Muhongo) 20 Machi 2015

1

Uongozi wenye Dira, Ubunifu na Ugunduzi – Uaminifu, Uadilifu na Kujituma –

Stadi Bulibuli za Usimamizi na Uzoefu katika Uongozi – Uwazi na Ufanisi –

Matokeo Yenye Tija na Ubora wa Hali ya Juu

Prof Dkt Sospeter Muhongo, mwanazuoni maarufu, mwanajiolojia

mbobevu na Mbunge wa Kuteuliwa, amewahi kuwa Waziri wa Wizara ya

Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (April 2012-

Januari 2015). Serikali ya Ufaransa ilimtunukia Cheo cha Afisa

Mwenyetunu ya Kitaaluma Iliyotukuka - Ordre des Palmes Académiques

(Iliyoanzishwa na Mfalme Napoléon Mwaka 1808) na ni mtu wa kwanza

kupokea Tuzo (Mwaka 2004) inayoheshimika sana kwa Jamii ya

Wanajiolojia wa Afrika ya Prof Robert Shackleton (UK) (Geological

Society of Africa’s prestigious Prof Robert Shackleton Award), kwa ajili ya

utafiti wa kipekee kuhusu Jiolojia ya Afrika ya miamba yenye umri wa

zaidi ya miaka Milioni 500 (Precambrian Geology of Africa).

Kwa kutambua mchango wake mkubwa wa kimataifa katika Sayansi na Ustawi wa Jamii

ulimwenguni, Prof Muhongo amepewa nafasi nyingi zenye kuheshimiwa na wasomi na wataalamu

maarufu Duniani, pamoja na kutambulika kwa ngazi za juu kabisa na Vyama na Taasisi zao za

kitaaluma, kwa mfano: An Honorary Fellow of the Geological Society of London (Ilianzishwa Mwaka

1807), Honorary Fellow of the Geological Society of America (Ilianzishwa Mwaka 1888), an Honorary

Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (Ilianzishwa Mwaka 1956).

Ni Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Nchi Zinazoendelea (FTWAS),

Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Chama cha Wanajiolojia wa Afrika (FGSAf) , Mshiriki wa Ngazi

ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Afrika (FAAS) na Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa

Akademia ya Sayansi ya Tanzania (FTAAS) na nyingine kadhaa. Ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Tume

ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW) na pia Mhariri Mkuu Mstaafu wa Jarida la Afrika la Sayansi za

Miamba na Madini (The Journal of African Earth Sciences, Elsevier). Prof Muhongo ni Mshindi wa

Mwaka 2014 wa Tuzo ya Heshima ya Jamii ya Wanasayansi wa Jiolojia na Uchimbaji Petroli na Gesi

Asilia ya Nigeria (NMGS)/AMNI ya Prof M.O. Oyawaye.

Prof Muhongo aliongoza na kusimamia mabadiliko endelevu ya ubunifu na ugunduzi katika Sekta za

Nishati na Madini nchini mwetu kwa kuingiza sera mpya na kutengeneza nyaraka za kisheria,

ameongeza idadi kwa wingi ya rasilimali watu iliyopata mafunzo mazuri ya kitaaluma katika Tasnia ya

Mafuta na Gesi Asilia. Amesimamia ongezeko la kasi kubwa ya kampeni ya usambazaji umeme

vijijini, na amesimamia usambazaji wa haraka na wa uhakika wa umeme mijini. Amesimamia

punguzo kubwa la gharama za kuunganishiwa umeme vijijini na mijini. Amesimamia ongezeko la

mapato katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kutokana na kodi na tozo mbalimbali kwenye madini

yetu. Baadhi ya wachimbaji wadogo wamepatiwa mafunzo na ruzuku ya kuboresha uchimbaji wao.

Tarehe 28.02.2015, Chama cha Wachimbaji Wadogo nchini (FEMATA) kilimteua, kwa kauli moja, Prof

Muhongo kuwa Mshauri Mkuu wao.

Prof Muhongo alisimamia utayarishaji wa mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Umeme nchini,

ikiwemo TANESCO, na Juni 2014 Wizara ya Nishati na Madini ilitangaza mipango na miradi

itakayotekelezwa kuhakikisha Taifa linapata umeme mwingi wa kutosha mahitaji yake, umeme

unaopatikana kwa urahisi na kwa uhakika, umeme wa bei nafuu na umeme wa ziada (biashara) kwa

manufaa ya uchumi wetu – Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap 2014-2025,

Powering Vision 2025.

Page 2: Wasifu Kwa Kifupi, Prof Sospeter Muhongo) 20 Machi 2015

2

Prof Muhongo amevutia uwekezaji mpya (kutoka ndani na nje ya nchi) wenye mitaji midogo na

mikubwa kwenye Sekta za Nishati, Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Haya yote yamechangia ukuaji

mzuri wa uchumi wetu.

Yeye ni Profesa Kamili (mstaafu) wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Profesa wa

Heshima wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini. Ni mjumbe wa bodi kadhaa za

uhariri wa majarida ya sayansi na vijarida vya sayansi, teknolojia na ubunifu. Yeye ni Mhariri

Mwandamizi wa Kitabu cha Mwaka 2009 kiitwacho: Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Maendeleo

ya Kiuchumi na Kijamii: Simulizi za Mafanikio kutoka Afrika (“Science, Technology and Innovation for

Socio-Economic Development: Success Stories from Africa”).

Prof Muhongo na watafiti wenzake wamechapisha ramani kwa kuzingatia dhana na maarifa ya kisasa

ya Jiolojia, kama vile: Jiolojia na Mashapo Makubwa ya Madini ya Afrika, Jiolojia na Mashapo ya Vito

vya Thamani vya Afrika Mashariki na Ramani ya Jiolojia na Madini ya Tanzania. Hakuna mikopo au

misaada ya fedha ilitumika kutengeneza ramani hizi. Ramani hizi zinatumika kupanua na kukuza

uwekezaji mpya katika Sekta ya Madini Barani Afrika.

Prof Muhongo alikuwa Rais wa Chama cha Wanajiolojia wa Afrika (1995-2001). Alikuwa Mkurugenzi

Mwanzilishi (2005-2010) wa ICSU Ofisi ya Sayansi ya Kanda ya Afrika, Pretoria, Afrika Kusini. Alikuwa

Mwenyekiti wa Bodi ya UNESCO-IUGS-IGCP Programu ya Kimataifa ya Sayansi ya Jiolojia (2004-

2008), na Mwenyekiti (2007-2010) wa Kamati ya Programu ya Kisayansi (SPC) ya Mwaka wa

Kimataifa wa Sayari ya Dunia uliotangazwa na Umoja wa Mataifa (UN-IYPE). Prof Muhongo aliteuliwa

na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea (2009) wa nafasi ya Mkurugenzi

Mkuu wa UNESCO.

Alikuwa Mwenyekiti (1999-2005) wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO),

Tanzania; na alikuwa Mkuu wa Idara ya Jiolojia, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (1997-2000). Prof

Muhongo alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi ya Serikali ya Tanzania kuhusu ajali mbaya ya

vifo katika migodi ya Mererani (2002). Prof Muhongo alisimamia kwa umakini mkubwa uboreshaji

wa rasilimali watu, majukumu, miradi na utendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Shirika

la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC).

Prof Muhongo amechapisha zaidi ya makala (publications) 200 za sayansi ya hadhi ya juu zikiwa ni za

kiutafiti zenye kukubaliwa na kurejelewa na watalaamu Duniani kote. Ametoa mihadhara ya

kisayansi zaidi ya 500 akiwa ndiye Mzungumzaji Mkuu (Keynote Speaker) katika Mikutano ya

Kimataifa na Kitaifa. Kwa zaidi ya miongo miwili, Prof. Muhongo ameandaa vikao zaidi ya 100 vya

mikutano ya vikundi vya wataalamu wa Kitaifa na Kimataifa vya sera, teknolojia na sayansi za nishati,

miamba, madini, maji, tabianchi na mazingira. Amekuwa Mwandishi Mkuu wa mikutano ya sera za

sayansi ikiwa ni pamoja na “Sayansi na Afrika” ambayo inadhaminiwa na Kamisheni ya Umoja wa

Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA), Kamisheni ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) na

washirika wake.

Prof. Muhongo amepata tuzo mbalimbali za kiuanazuoni na kitaalamu, ametambuliwa na kupata

hibafedha kwa kazi mbalimbali za kitaaluma pamoja na kutunukiwa fedha za utafiti. Ameshirikiana

na wanasayansi mabingwa wa Mabara yote kwenye tafiti za kisayansi. Alisomea Jiolojia katika Chuo

Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania) na Gӧttingen (Ujerumani). Alihitimu na kutunukiwa shahada ya

Dr.rer.nat. kutoka Technical University of Berlin, Ujerumani. Prof. Muhongo anaongea, na kuandika

kwa ufasaha na umahiri mkubwa Kiswahili, Kiingereza na Kijerumani, na kwa wastani kwa lugha ya

Kifaransa.

Baruapepe: [email protected] / [email protected]

Prof. Dr. Sospeter MUHONGO (Officier, Ordre des Palmes Académiques) 20 March 2015

FGSAf, FAAS, FASI, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FTWAS, HonFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol