015 elimu ya dini ya kiislamu coverf - necta...kuchuja hadithi za mtume (s.a.w) hivyo watahiniwa hao...
TRANSCRIPT
-
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
TAARIFA YA UCHAMBUZI WA MAJIBU YA WATAHINIWA KATIKA MTIHANI WA KIDATO
CHA NNE (CSEE) 2019
-
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
TAARIFA YA UCHAMBUZI WA MAJIBU
YA WATAHINIWA KATIKA MTIHANI
WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2019
015 – ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
-
ii
Kimechapishwa na
Baraza la Mitihani la Tanzania,
S.L.P. 2624,
Dar es salaam, Tanzania.
© Baraza la Mitihani la Tanzania, 2019
Haki zote zimehifadhiwa.
-
iii
YALIYOMO
YALIYOMO ............................................................................................................ iii
DIBAJI ..................................................................................................................... iv
1.0 UTANGULIZI ............................................................................................... 1
2.0 TATHMINI YA KILA SWALI KWA MADA ............................................. 2
2.1 SEHEMU (A) ............................................................................................. 2
2.1.1 Swali la 1: Kuchagua Majibu Sahihi. ................................................. 2
2.1.2 Swali la 2: Kuoanisha ......................................................................... 8
2.2 SEHEMU B: Maswali ya kujibu kwa ufupi ............................................. 10
2.2.1 Swali la 3: Familia ya kiislamu. ....................................................... 10
2.2.2 Swali la 4: Mfumo wa Jamii ya Kiislamu ........................................ 13
2.2.3 Swali la 5: Nguzo za Imani ............................................................... 15
2.2.4 Swali la 6: Nguzo za Uislamu .......................................................... 18
2.2.5 Swali la 7: Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa Kiislamu. .......... 20
2.2.6 Swali la 8: Qur`an ............................................................................. 23
2.2.7 Swali la 9: Sunnah na Hadithi .......................................................... 26
2.3 SEHEMU C: Maswali ya Insha ............................................................... 29
2.3.1 Swali la 10: Dola ya Kiislamu Madinah ........................................... 30
2.3.2 Swali la 11: Qur'an. .......................................................................... 36
2.3.3 Swali la 12: Nguzo za Uislamu ........................................................ 42
2.3.4 Swali la 13: Mfumo wa Jamii ya Kiislamu ...................................... 47
3.0 UCHAMBUZI WA KUFAULU KWA KILA MADA ............................... 54
4.0 HITIMISHO ................................................................................................ 55
5.0 MAPENDEKEZO ....................................................................................... 55
6.0 Kiambatisho ................................................................................................. 56
-
iv
DIBAJI
Taarifa hii ya Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha
Nne (CSEE) 2019 katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu imeandaliwa ili kutoa
mrejesho kwa wanafunzi, walimu, wazazi, watunga sera na wadau wa elimu kwa
ujumla kuhusu kufaulu kwa watahiniwa katika mtihani wa somo hili. Majibu ya
watahiniwa katika mtihani ni kiashiria kimojawapo kinachoonesha mambo ambayo
watahiniwa waliweza kujifunza kwa usahihi na yale ambayo hawakuweza
kujifunza katika kipindi cha miaka minne ya Elimu ya Sekondari.
Katika taarifa hii, uchambuzi wa kila swali umefanyika ambapo dosari mbalimbali
zilizojitokeza katika majibu ya maswali zimeainishwa kwa kuonesha watahiniwa
walioshindwa kujibu kwa usahihi. Pia uchambuzi huu umeonesha watahiniwa
waliopata alama za juu, wastani na chini katika kila swali na sampuli za majibu ya
watahiniwa waliofanya vizuri au vibaya zimeoneshwa. Aidha, sababu mbalimbali
ambazo zilichangia wanafunzi kuweza au kushindwa kujibu maswali kwa usahihi
zimeelezwa. Sababu zilizowafanya baadhi ya wanafunzi kuweza kujibu maswali
kwa usahihi ni kama vile uelewa wa matakwa ya maswali na kuwa na maarifa ya
kutosha juu ya mada mbalimbali za somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu. Aidha,
uchambuzi umeonesha kuwa baadhi ya wanafunzi walishindwa kujibu maswali
kwa usahihi kutokana na kutotambua matakwa ya maswali na kuwa na maarifa
finyu katika mada mbalimbali na hasa katika Mambo ya lazima kufanyiwa maiti ya
Kiislamu na Nguzo za Imani. Uchambuzi umebaini kuwepo kwa udhaifu katika
kujibu maswali ya kujibu kwa ufupi na yale ya kujieleza kwa insha.
Baraza la Mitihani la Tanzania lina imani kuwa mrejesho uliotolewa
utawawezesha wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mchakato
wa ufundishaji na ujifunzaji ili hatimaye kuondoa changamoto zilizoainishwa
katika taarifa hii. Endapo mapendekezo yaliyotolewa mwishoni mwa uchambuzi
huu yatafanyiwa kazi, ujuzi na maarifa watakaopewa wanafunzi wa kidato cha nne
katika somo hili utaongezeka na kiwango cha kufaulu katika somo hili
kitaongezeka.
Dkt. Charles E. Msonde
KATIBU MTENDAJI
-
1
1.0 UTANGULIZI
Taarifa hii inachambua kiwango cha kufaulu katika mtihani wa kidato cha
nne (CSEE) wa mwaka 2019, somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu. Mtihani
huo uliofanyika mwezi novemba 2019 uliandaliwa kwa kuzingatia
muhtasari wa somo hili kwa kidato cha I hadi IV wa mwaka 2012.
Mtihani huu ulikuwa na karatasi moja iliyokuwa na sehemu tatu: A, B na C
zenye jumla ya maswali kumi na tatu. Sehemu A ilikuwa na maswali
mawili. Swali la kwanza lilikuwa na vipengele kumi na tano (i-xv) ambapo
mtahiniwa alitakiwa kuchagua majibu sahihi, swali hili lilikuwa na jumla
ya alama 15. Swali la pili lilikuwa la kuoanisha lenye vipengele vitano (i-v)
nalo lilikuwa na jumla ya alama 5. Sehemu B ilikuwa na maswali saba (7)
ya kujibu kwa ufupi. Kila swali lilibeba alama 5 kwa hiyo sehemu hii
ilikuwa na jumla ya alama 35. Sehemu C ilikuwa na maswali manne (4) ya
insha ambapo mtahiniwa alitakiwa kujibu maswali matatu tu, kila swali
lilikuwa na alama 15 na kuifanya sehemu hii kuwa na jumla ya alama 45.
Jumla ya alama zote katika karatasi hii zilikuwa 100.
Idadi ya watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani wa Elimu ya Dini
ya Kiislamu mwaka 2019 ni 69,433 na waliofanya mtihani walikuwa
67,230. Hii ni sawa na ongezeko la watahiniwa 20,361 ikilinganishwa na
watahiniwa 46,869 waliofanya mtihani wa Elimu ya Dini ya Kiislamu
mwaka 2018. Aidha, watahiniwa 67,035 walipata matokeo ambapo
watahiniwa 36,565 sawa na 54.55% walifaulu. Kati ya hawa, watahiniwa
20 (0.05%) walipata gredi A, 407 (1.11%) walipata gredi B, 11,123
(30.42%) walipata gredi C na 25,015 (68.41%) walipata gredi D.
Watahiniwa 30,470 sawa na asilimia 45.45 walipata gredi F. Kwa ujumla
kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa kwa mwaka 2019 kilikuwa asilimia
54.55.
Taarifa hii inaonesha uchambuzi wa maswali ya mtihani na majibu
yaliyotolewa na watahiniwa. Sampuli za majibu ya watahiniwa zimewekwa
ili kuonesha kile kilichofanywa na watahiniwa. Kufaulu kwa watahiniwa
kuligawanyika katika mafungu matatu ambayo ni: vizuri, wastani na
dhaifu. Kufaulu kwa mada kulikuwa dhaifu kama kulikuwa kati ya asilimia
0 hadi 29. kufaulu kulikuwa wastani kama kulikuwa kati ya asilimia 30
hadi 64 na kufaulu kulikuwa vizuri kati ya asilimia 65 hadi 100.
-
2
2.0 TATHMINI YA KILA SWALI KWA MADA
2.1 SEHEMU (A)
Sehemu hii ilikuwa na maswali mawili na ilikuwa na jumla ya alama 20.
Swali la kwanza lilikuwa la kuchagua jibu sahihi ambapo mtahiniwa
alipewa sentensi yenye majibu matano ya kuchagua (A, B, C, D na E) na
kutakiwa kuchagua herufi moja ya jibu sahihi na kujaza katika karatasi
yake ya kujibia. Swali la pili lilikuwa la kuoanisha ambapo mtahiniwa
alitakiwa aoanishe matendo matano yaliyopo katika orodha A (i - v) na
majina ya matendo hayo katika orodha B (A hadi G) na kujaza katika
kitabu chake cha kujibia.
2.1.1 Swali la 1: Kuchagua Majibu Sahihi
Swali la kwanza lilikuwa na vipengele kumi na tano (i-xv). Miongoni mwa
mada zilizopimwa katika swali hili zilikuwa ni: (i) Dola ya Kiislamu
Madinah, (ii) Historia ya Uislamu Baada ya Kutawafu Mtume (s.a.w), (iii-
v) Sunnah na Hadithi, (vi-ix) Qur’an, (x) Mtazamo wa Uislamu juu ya
Dini, (xi - xii) Familia ya Kiislamu, (xiii) Sheria katika Uislamu na (xiv -
xv) Nguzo za Imani. Katika kila kipengele mtahiniwa alitakiwa kuchagua
jibu sahihi kati ya majibu matano (A-E) aliyopewa na kuandika herufi ya
jibu hilo katika kitabu chake cha kujibia. Kila kipengele kilikuwa na alama
1, hivyo swali lote lilikuwa na jumla ya alama 15.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 67,199 (99.84%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
64,122 (95.46%) walifaulu. Watahiniwa 38,304 (57.00%) walipata alama
za wastani (5 hadi 9), na watahiniwa 25,818 (38.42%) walipata alama za
juu (10 hadi 15), ambapo kati yao watahiniwa 181 walipata alama zote 15
za swali hili. Watahiniwa 3,077 (4.58%) walipata alama za chini (0 hadi 4)
ambapo miongoni mwao watahiniwa 47 walipata alama 0. Chati namba 1
inaonesha kufaulu kwa watahiniwa hawa kwa asilimia.
-
3
Chati ya 1: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 1
Uchambuzi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa,
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa kizuri kwani watahiniwa
64,122 (95.46%) kati ya 67,199 waliojibu swali hili walipata alama 5 hadi
15. Watahiniwa waliopata alama za wastani (5 hadi 9) waliweza kujibu
vizuri vipengele vitano hadi tisa vya swali na wale waliopata alama za juu
(10 hadi 15) walijibu vizuri vipengele kumi na zaidi kati ya vipengele
kumi na tano vya swali. Miongoni mwa vipengele vilivyojibiwa vizuri na
watahiniwa hawa ni; (iii, iv, v, vi, vii, ix, x, xi na xv) vilivyotoka katika
mada za: Sunnah na Hadithi, Qur`an, Mtazamo wa Uislamu juu ya Dini,
Familia ya Kiislamu na Nguzo za Imani. Hii inaonesha kuwa watahiniwa
hawa walielewa vema vipengele hivyo na walikuwa na maarifa ya kutosha
katika mada hizo, hivyo walifanya vizuri. Watahiniwa waliopata alama za
chini (0 hadi 4 ) walishindwa kuchagua majibu sahihi katika vipengele
vingi vya swali kutokana na sababu mbalimbali kama zinavyochambuliwa
katika aya zinazofuata;
Kipengele cha (i) kilitoka katika mada ya “Dola ya kiislamu Madinah”
katika mada ndogo ya “Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah”. Katika
kipengele hiki watahiniwa walitakiwa kuchagua kundi linaloonesha vyanzo
muhimu vya mapato katika serikali ya Kiislamu ambapo jibu sahihi
lilikuwa ni E (Zakat, Sadaka, Jizya, Al kharaj, Al-fay, Al-ghanimah na Al-
ushru). Watahiniwa wengi hawakuwa na ufahamu juu ya istilahi hizi, hivyo
4.6%
57.0%
38.4%
0.0 - 4.0
5.0 - 9.0
10.0 - 15.0
Alama
-
4
hawakuweza kuchagua jibu sahihi. Wengine hawakuweza kuchagua jibu
sahihi kutokana na kutokuwa na ufahamu juu ya mada husika kwa ujumla
na hatimae walishindwa kufanya vizuri.
Kipengele cha (ii) kilitoka katika mada ya Historia ya Uislamu baada ya
kutawafu Mtume (s.a.w) kipengele hiki kiliuliza sababu ya baadhi ya watu
kuasi Uislamu mara baada ya kutawafu kwa Mtume (s.a.w), jibu sahihi
lilikuwa ni B (uroho wa madaraka). Watahiniwa wengi walijibu kwa
usahihi. Watahiniwa waliokosa kipengele hiki walichagua jibu A (kukataa
kutoa zaka) jibu linaloonesha kuwa watahiniwa hawa walichanganya
majibu kutokana na kuwa na maarifa finyu. Kukataa kutoa Zaka ni
matokeo ya uasi. Watahiniwa wengine walichagua jibu C (ugumu wa
sharia za kiislamu) kwa sababu ya kutokuwa na maarifa ya kutosha.
Kipengele cha (iii) kilitoka katika mada ya “Sunnah na Hadithi”, katika
mada ndogo ya Uchambuzi wa Hadithi za Mtume (s.a.w). Kipengele hiki
kiliuliza kuhusu kanuni inayotumika kuchuja Hadithi za Mtume (s.a.w) na
jibu lake sahihi lilikuwa D (kwa kuangalia maisha ya wapokezi wa
Hadithi). Uchambuzi unaonesha watahiniwa wengi hawakuchagua herufi
sahihi na badala yake walichagua E (kuangalia matumizi ya hadithi hiyo
katika maisha) kwa sababu hawakuwa na uelewa wa kanuni zinazotumika
kuchuja Hadithi za Mtume (s.a.w) hivyo watahiniwa hao walibahatisha
majibu kwa kuuganisha mzizi wa swali na kila jibu lililopo ikizingatiwa
kuwa jibu E lilikuwa na muunganiko mzuri kilugha.
Kipengele cha (iv) kilitoka katika mada ya “Sunnah na Hadithi” katika
mada ndogo ya Tanzu za Hadithi. Kipengele hiki kilimtaka mtahiniwa
kuchagua kundi ambalo litawekwa Hadithi iliyosimuliwa na msimulizi
anayejulikana kuwa na uwezo mdogo wa kuhifadhi masimulizi. Jibu sahihi
lilikuwa ni A (dhaifu). Takwimu zinaonesha wengi walijibu kwa usahihi na
wachache waliokosa walichagua jibu C (Maudhuu). Waliokosa kipengele
hiki hawakuwa na maarifa ya kutosha katika uchambuzi wa Hadithi, hivyo
walishindwa kubaini vigezo vya Hadithi dhaifu.
Kipengele cha (v) pia kilitoka katika mada ya “Sunnah na Hadithi”.
Mtahiniwa alitakiwa kuainisha kundi la Hadithi linalotokana na Isnad
(msururu wa wapokezi) ya watu wema na waadilifu katika maisha yao. Jibu
sahihi lilikuwa ni E (sahihi). Watahiniwa wengi waliweza kuchagua jibu
-
5
hili kwa kuwa walikuwa na maarifa ya kutosha katika mada ya uchambuzi
wa Hadithi. Watahiniwa wengi waliokosa walichagua jibu A. Watahiniwa
hawa walionesha kuwa hawafahamu maana ya neno “Maudhuu” katika fani
ya Hadithi.
Kipengele cha (vi) kilitoka katika mada ya Qur`an na kilimtaka mtahiniwa
kuainisha mafunzo ya Suratul Fatiha endapo Muislamu anataka kuanza
kufanya jambo lolote lile. Jibu sahihi lilikuwa B (kusoma Bismillahi
Rahmani Rahiim. Watahiniwa wengi walijibu kwa usahihi kwakuwa
kusoma Bismillahi Rahmani Rahiim ni kitendo ambacho kimezoeleka
kufanywa na waumini wa Kiislamu katika maisha yao ya kila siku kabla ya
kufanya jambo lolote. Baadhi ya watahiniwa waliokosa kipengele hiki
walichagua jibu A. Hii ni kwa sababu ya mafundisho kuwa kabla ya kuanza
kusoma Qur’an msomaji anatakiwa kuanza kwa kumlaani shetani kwa
kutamka Audhubillah Mina Shaytwaanir Rajiim.
Kipengele cha (vii) kilihusiana na mada ya Qur`an katika mada ndogo ya
“Surah zilizochaguliwa”. Swali lilimtaka mtahiniwa ataje dhambi kubwa
inayotajwa katika suratul Humazah. Jibu sahihi lilikuwa ni B (kusengenya).
Watahiniwa wengi walifanya vizuri katika kipengele hiki. Inaonesha kuwa
watahiniwa hawa walikuwa na maarifa ya kutosha juu ya tafsiri ya suratul
Humazah. Watahiniwa waliokosa kipengele hiki walikuwa hawajui
maudhui ya Suratul Humazah, hivyo majibu yao yalikuwa ya kubahatisha.
Kipengele cha (viii) kilitoka kwenye mada ya Qur`an, mafunzo ya Surah
zilizoteuliwa “Suratul Bayyinah”. Mtahiniwa alitakiwa kubainisha tafsiri ya
aya ya saba ya sura hiyo. Jibu sahihi lilikuwa B (hakika wale walio amini
na kutenda mema basi hao ndio wema wa viumbe). Kufaulu katika
kipengele hiki kulikuwa ni kwa wastani. Watahiniwa waliochagua jibu
sahihi walikuwa wamehifadhi surat Bayyinah na walikuwa wanafahamu
vizuri tafsiri yake. Watahiniwa wengi waliokosa swali hili walichagua jibu
C (ndani yake kuna sharia madhubuti) na D (kisha kwa hakika mtaulizwa
siku hiyo juu ya neema {mlizopewa}). Watahiniwa hawa hawakuwa
wanafahamu “Suratul Bayyinah” katika matini na tafsiri yake.
-
6
Kipengele cha (ix) kilipima mada ya Qur`an katika kipengele cha adabu za
usomaji wa Qur`an. Mtahiniwa alitakiwa kubaini katika Orodha ya adabu
zilizoorodheshwa ni ipi haikuwa miongoni mwa adabu za usomaji wa
Qur`an. Jibu sahihi lilikuwa ni C (kuanza kwa sauti ya chini kisha kwa
sauti ya juu katika kusoma). Watahiniwa wengi walifanya vizuri katika
kipengele hiki. Hii inadhihirisha kuwa walikuwa na maarifa ya kutosha
kuhusu adabu za usomaji wa Qur`an. Waislamu wengi huzingatia adabu
mbalimbali za usomaji wa Qur’an katika usomaji wao wa kila siku. Hivyo
nyingi katika adabu hizi zimezoeleka na hufuatwa na wasomaji wa Qur’an.
Hata hivyo katika kipengele hiki wapo waliochagua majibu mengine
ambayo si sahihi. Watahiniwa hawa walionesha kutokuelewa swali na
kutokuwa na maarifa ya kutosha kuhusu Adabu za kuisoma Qur`an.
Kipengele cha (x) kilipima mada ya “Mtazamo wa Uislamu juu ya dini”.
Kwenye kipengele hiki mtahiniwa alitakiwa kuchagua jibu linaloonesha
kazi kuu ya dini kwa mtazamo wa Uislamu. Watahiniwa wengi walifanya
vizuri katika kipengele hiki kwa kuchagua jibu sahihi ambalo lilikuwa ni A
(kusimamia sheria na kumkomboa mwanadamu). Watahiniwa hao
walionesha kuwa na maarifa ya kutosha juu ya kazi ya dini kwa mtazamo
wa Uislamu. Hata hivyo majibu B, D na E hayakuchaguliwa kwa vile
yalitaja mambo ambayo yapo kinyume na Uislamu.
Kipengele cha (xi) kilitoka katika mada ya “Familia katika Uislamu”.
Mtahiniwa alitakiwa kubaini jinsi ndoa inavyomuhifadhi Muislamu
kutokana na zinaa. Jibu sahihi katika kipengele hiki lilikuwa ni C (imeweka
utaratibu madhubuti wa kukidhi haja). Watahiniwa wengi walimudu
kuchagua jibu sahihi katika kipengele hiki kwa sababu ndoa ni ibada
muhimu katika jamii. Watahiniwa walionesha kuwa na maarifa ya ziada
kuhusu mada hii. Baadhi ya watahiniwa ambao hawakulielewa swali
walijibu kipengele hiki kwa kubahatisha.
Kipengele cha (xii) kilitoka katika mada ya “Familia ya Kiislamu” katika
mada ndogo ya “Talaka na Eda”. Kipengele hiki kiliuliza kuhusu hukumu
ya mwanamke mjamzito aliyepewa talaka katika sheria ya kiislamu. Jibu
sahihi la kipengele hiki lilikuwa ni E (eda hadi pale atakapo jifungua).
Watahiniwa wengi walimudu kuchagua jibu sahihi katika kipengele hiki,
kutokana na kuwa na maarifa ya kutosha kuhusu Talaka na Eda. Baadhi ya
waliokosa kipengele hiki walichagua jibu D (eda hadi atakapo maliza
-
7
kunyonyesha) ambalo halikuwa jibu sahihi. Ama watahiniwa wengine
waliochagua majibu A, B na C wote walidhihirisha kutokuwa na marifa ya
kutosha juu ya mada ya talaka na eda.
Kipengele cha (xiii), kilitoka katika mada ya “Sheria katika Uislamu”
kipengele hiki kiliuliza kuhusu adhabu ya mlevi katika sharia ya Uislamu.
Jibu la swali hili lilikuwa ni D (kuchapwa viboko arobaini). Watahiniwa
wengi walimudu kuchagua jibu sahihi hali iliyoonesha kuwa watahiniwa
hawa walikuwa na maarifa ya kutosha juu ya mada hii ya Sheria katika
Uislamu. Hata hivyo wapo baadhi ya watahiniwa walichagua majibu
mengine kama vile A, C na E kwa sababu mbalimbali: Waliochagua A
(kuchapwa viboko mia moja) hawa walishindwa kutofautisha kati ya
adhabu ya mlevi na mzinifu, wale waliochagua C (kuchwapwa viboko
hamsini) na E (kuchapwa viboko ishirini na moja) walionesha kuwa
hawana maarifa yakutosha juu ya hukumu za kisheria zilizoainishwa katika
Uislamu kwa makosa ya ulevi hivyo walichagua majibu yao kwa
kubahatisha.
Kipengele cha (xiv), kilitoka katika mada ya “Nguzo za Imani” katika
kipengele cha “kuamini siku ya mwisho”. Kipengele hiki kiliuliza kuhusu
maana sahihi ya kuamini siku ya mwisho ambapo jibu lake sahihi lilikuwa
ni B (kuna maisha ya milele baada ya kufufuliwa). Kufaulu kwa
watahiniwa katika kipengele hiki kulikuwa kuzuri kwani watahiniwa wengi
waliweza kuchagua jibu hilo kwa sababu walikuwa na maarifa ya kutosha
kuhusiana na mada ya Imani ya siku ya mwisho. Watahiniwa wachache
walichagua majibu ambayo hayakuwa sahihi kama vile C (unapokufa nchi
moja utafufuliwa nyingine) na wengine D (haiwezekani kufufuliwa tena
baada ya kufa). Watahiniwa hawa walionesha kuwa wameathiriwa na
imani kuwa mtu akifa sehemu moja ya dunia hufufuliwa kwa kuzaliwa tena
upya sehemu nyingine. Watahiniwa wengine walijibu kwa mtazamo wa
makafiri kuwa hakuna maisha baada ya kufa.
Kipengele cha (xv) kilitoka katika mada ya Nguzo za Imani katika
kipengele cha Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu. Katika kipengele
hiki watahiniwa walitakiwa kubaini sababu ya kuhitajika Mtume mwingine
baada ya Mtume wa kwanza kurejea kwa mola wake. Jibu sahihi lilikuwa
ni D (Mtume aliyetangulia alipelekwa kwa taifa maalum). Kufaulu kwa
watahiniwa katika kipengele hiki kulikuwa kwa wastani.
-
8
Baadhi ya watahiniwa walichagua jibu B (Mtume aliyefuata alikuwa na
mafundisho tofauti na aliyetangulia), watahiniwa hawa walishindwa
kuelewa kuwa misingi ya mafundisho ya mitume haitofautiana.
Watahiniwa wachache walichagua majibu A, C na E ambayo hayakuwa
majibu sahihi. Majibu haya yanaashiria kuwa watahiniwa hawa hawakuwa
na ufahamu kuhusu mada husika hivyo walikuwa wanabahatisha.
2.1.2 Swali la 2: Kuoanisha Swali hili lilitoka katika mada ya Nguzo za Uislamu, mada ndogo ya Hija
na Umrah. Mtahiniwa alitakiwa kuoanisha matendo ya Hija yaliyokuwa
katika orodha A (i-v) na majina ya matendo hayo kutoka orodha B (A-G)
na kisha kuandika herufi ya jibu sahihi kwa kila kipengele katika kitabu cha
kujibia.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 67,124 (99.70%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
30,672 (45.70%) walipata alama 0 hadi 1 katika swali hili. Watahiniwa
27,242 (40.58%) walipata alama 2 hadi 3 na watahiniwa 9,210 (13.72%)
walipata alama 4 hadi 5. Chati namba 2 inaonesha kufaulu kwa watahiniwa
hao kwa asilimia.
Chati ya 2: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 2
45.7 40.6
13.7
0
10
20
30
40
50
60
70
80
90
100
0.0 - 1.0 2 - 3.0 4.0 - 5.0
Asi
lim
ia y
a w
ata
hin
iwa
Alama
-
9
Uchambuzi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kiwango cha kufaulu katika swali hili ni cha wastani kwani watahiniwa
36,452 (54.31%) waliojibu swali hili walipata alama 2 hadi 5. Watahiniwa
hawa walionesha kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu ibada ya Hija na
Umra jambo ambalo liliwawezesha kuoanisha kwa usahihi vipengele vingi
na wengine vyote vya swali hili. Vipengele ambavyo kwa kiasi kikubwa
watahiniwa hawa walimudu kuvioanisha kwa usahihi ni: (i), (iii) na (v). Hii
ni kwa sababu Mahujaji huvirejea vitendo hivi kwa kuvitaja kwa majina
kila wanapoeleza namna walivyotekeleza ibada ya Hija.
Kipengele cha (i) chenye sentensi inayosema "mahujaji husimama, kuleta
dhikri na kuomba dua mchana kutwa " ni miongoni mwa vipengele
ambavyo watahiniwa walifanya vizuri. Jibu la kipengele hiki lilikuwa ni
herufi D (Arafa). Tukio la mahujaji kusimama Arafa linakumbukwa sana
na waumini ambao hawakwenda Makka kufanya ibada ya Hija ili waweze
kutekeleza Sunnah ya kufunga inayoambatana na siku hiyo. Watahiniwa
ambao hawakuoanisha kipengele hiki kwa usahihi, wengi walioanisha na
herufi G (miqaat) ambalo halikuwa jibu sahihi. Watahiniwa hawa
walihusisha neno miqaati na ''mahujaji kusimama" kwasababu miqaat ni
sehemu au vituo ambavyo mahujaji husimama kwa ajili ya kutia nia ya Hija
na kuvaa ihram ili kuendelea na hatua nyingine.
Katika kipengele cha (iii) chenye sentensi inayosema "mahujaji hutembea
mara saba baina ya safwa na marwa" pia ni miongoni mwa vipengele
ambavyo watahiniwa walifanya vizuri. Jibu la kipengele hiki lilikuwa ni F
(sa`i). Watahiniwa walioshindwa kuonanisha kipengele hiki kwa usahihi
waliweka majibu ya kubahatisha. Baadhi yao walioanisha na herufi C
(Tawafu) kwa sababu kitendo cha Tawafu hufanyika mara saba kama ilivyo
kitendo cha (sa`i), hivyo majibu yaliwachanganya.
Kipengele cha (v) chenye sentensi isemayo "mahujaji huzunguka al-kaaba
mara saba kuanzia jiwe jeusi" ni miongoni mwa vipengele ambavyo
watahiniwa wengi walimudu kuonanisha kwa usahihi. Jibu la kipengele
hiki lilikuwa ni C (Tawafu). Watahiniwa ambao hawakuonanisha kipengele
hiki kwa usahihi walichagua herufi E (Qiraan) na wengine A (ifraad) kwa
sababu hawakuwa na maarifa ya kutosha kufahamu kuwa hizo zilikuwa ni
aina za Hija.
-
10
Uchambuzi zaidi katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa vipengele
ambavyo watahiniwa wengi hawakufanya vizuri ni (ii na iv). Katika
kipengele cha (ii) kinachosema mahujaji hutia nia ya hija na kuvaa ihram,
jibu lake lilikuwa G (Miqaat). Watahiniwa wachache waliweza kuoanisha
kipengele hiki kwa usahihi. Watahiniwa wengine walioanisha kipengele
hiki na herufi A (Ifraad) kwa sababu kitendo hiki cha kutia nia na kuvaa
Ihram katika Miqaat hakipewi uzito mkubwa katika mafundisho ya ibada
ya Hija pia watahiniwa kutojua maana ya neno “infraad” hivyo
wakabahatisha ili kuona kama yanaendana.
Kipengele cha (iv) kiliwataka watahiniwa kubaini Hija iliyo nafuu kwa
mahujaji wanaotoka mbali na Makka. Jibu sahihi katika kipengele hiki
lilikuwa B (Tamattu). Watahiniwa wengi walishindwa kuonisha kwa
usahihi kwa sababu ya kutokuwa na maarifa ya kutosha kuhusu aina za
Hija na kukosa uzoefu kutoka kwa watu waliowahi kuhudhuria ibada hii.
2.2 SEHEMU B: Maswali ya kujibu kwa ufupi
Sehemu hii ilikuwa na maswali saba ya majibu mafupi ambayo mtahiniwa
alitakiwa kujibu maswali yote. Kila swali lilikuwa na alama tano (5) hivyo
jumla ya alama zote katika sehemu hii ilikuwa 35. Maswali katika sehemu
hii yalitoka katika mada zifuatazo: Familia ya kiislamu, Mfumo wa jamii
ya Kiislamu, Nguzo za Imani, Nguzo za Uislamu, Mambo ya lazima ya
kufanyiwa maiti Muislamu, Qur`an na Sunnah na Hadithi.
2.2.1 Swali la 3: Familia ya Kiislamu.
Swali hili lilitoka katika mada ya Familia katika Uislamu ambapo
mtahiniwa alitakiwa kufafanua kwa ufupi kwa nini mwanamke wa kiislamu
haruhusiwi kuolewa na mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Swali
lilijibiwa na watahiniwa 64,952 (96.50%) kati ya watahiniwa 67,309
waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa 42,737
(65.80%) walipata alama 0 hadi 1 za swali hili. Watahiniwa 20,206
(31.11%) walipata alama 1.5 hadi 2.5 na watahiniwa 2,009 (3.09%)
walipata alama 3.5 hadi 5. Chati namba 2 inaonesha kufaulu kwa
watahiniwa hawa katika asilimia.
-
11
Chati ya: 3: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 3
Uchambuzi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kufaulu kwa watahiniwa katika swali hili kulikuwa ni wastani, kwa kuwa
watahiniwa 22,215 (34.20%) kati ya 64,952 waliojibu swali hili walipata
alama 1.5 hadi 5. Watahiniwa 20,206 (31.11%) walipata alama za wastani
(1.5 hadi 3) na watahiniwa 2,009 (3.09%) walipata alama za juu (3.5 hadi
5). Watahiniwa 20,206 (31.11%) waliopata alama za wastani hawakuweza
kutoa ufafanuzi wa kutosha kwenye hoja walizozitoa kuelezea sababu za
Uislamu kukataza mwanamke kuolewa na mume zaidi ya mmoja kwa
wakati mmoja ingawa hoja zao zilikuwa sahihi.
Watahiniwa waliopata alama za juu (3.5 hadi 5) walionesha kuwa na
maarifa ya kutosha juu ya mada hii ya Familia ya Kiislamu. Vile vile
walielewa vema matakwa ya swali na waliweza kutoa hoja madhubuti na
kufafanua kwa usahihi kwanini mwanamke wa kiislamu haruhusiwi
kuolewa na mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ufafanuzi waotoa
ulijumuisha hoja kama vile: mwanamke atakapopata mimba mtoto
hatafahamika baba yake wa halali, Kwa hali hii mtoto atakoseshwa haki
zake za msingi ikiwemo nasaba, malezi ya baba na mirathi. Mtoto huyu
anaweza kuchukua mirathi isiyo haki yake. Itakuwa ni ngumu mwnamke
huyu kutekeleza majukumu ya mke kwa mume ikizingatiwa kuwa mume ni
kiongozi katika familia. Matokeo ya hali hii itakuwa ni migogoro katika
65.8%
31.1%
3.1%
0.0 - 1.0
1.5 - 3.0
4.0 - 5.0
Alama
-
12
jamii. Kielelezo namba 3.1 kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa
aliyejibu kwa kuzingatia matakwa ya swali.
Kielelezo 3.1: Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 3
Uchambuzi zaidi unaonesha kuwa watahiniwa 42,737 (65.80%) walipata
alama za chini (0 hadi 1), miongoni mwao watahiniwa 32,235 (47.90%)
walipa alama 0. Watahiniwa hawa walijibu tofauti na matakwa ya swali
kwa sababu ya kutokuwa na maarifa ya kutosha juu ya kipengele
kilichoulizwa hivyo wakapata alama 0. Baadhi yao walikuwa wakirejea
msingi wa swali kuwa: Mwanamke wa kiislamu haruhusiwi kuolewa na
mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja kwa sababu dini ya kiislamu
hairuhusu, na majibu mengine yanayofanana na hayo kama vile: Dini yetu
ya kiislamu haijaeleza kuwa mwanamke wa kiislamu aolewe na mume zaidi
ya mmoja kwa wakati mmoja, mwanamke haruhusiwi kuolewa akiwa ndani
ya ndoa, dini ya Kiislamu hairuhusu, Qur'ani hairuhusu, kwa sababu hiyo
ni sheria ya Uislamu, kwa sababu Allah (s.w) amejaalia aolewe na mume
mmoja. Wengine walitoa hoja moja kuwa: Mwanamke hawezi kuwahimili
wala kuwatosheleza wanaume wawili kwa wakati mmoja wala kutekeleza
majukumu, mwanamke ameumbwa dhaifu hivyo hana uwezo wa kumudu
mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Kielelezo namba 3.2 kinaonesha
sampuli ya majibu ya mtahiniwa aliyeshindwa kujibu swali kama
ilivyotakiwa.
-
13
Kielelezo 3.2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 3
2.2.2 Swali la 4: Mfumo wa Jamii ya Kiislamu Swali hili lilitoka katika mada ya “Uchumi katika Uislamu” na
liligawanyika katika sehemu mbili; (a) na (b) ambapo katika sehemu (a)
mtahiniwa alitakiwa kuainisha madhara matatu ya riba na katika sehemu
(b) alitakiwa kutoa hoja mbili zinazoonesha jinsi gani atalitatua tatizo la
riba.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 65,330 (97.10%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
35,567 (54.40%) walipata alama 1 hadi 2, na miongoni mwao watahiniwa
17,345 (25.80%) walipata alama 0. Watahiniwa 25,151 (38.50%) walipata
alama 1.5 hadi 3, na watahiniwa 4,612 (7.06%) walipata alama 3.5 hadi 5
ambapo miongoni mwao watahiniwa 450 (0.70% ) walipata alama zote 5.
Chati namba 4 inaonesha kufaulu kwa wanafunzi hao kwa asilimia.
Chati no: 4: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 4
54.4% 38.5%
7.1%
0.0 - 1.0
1.5 - 3.0
3.5 - 5.0
Alama
-
14
Kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa katika swali hili kilikuwa cha
wastani, kwani watahiniwa 29,763 (45.56%) kati ya 65,330 waliojibu swali
hili walipata alama kati ya 1.5 hadi 5. Watahiniwa 25,151 (38.50%)
walipata alama za wastani (1.5 hadi 3) kwa sababu walitoa hoja pungufu
katika sehemu zote mbili na wengine walijibu sehemu moja na kuacha
nyingine. Baadhi yao walijibu sehemu zote mbili lakini maelezo yao
hayakutosheleza kupata alama za juu.
Watahiniwa 4,612 (7.06%) waliopata alama za juu (3.5 hadi 5) waliweza
kuainisha madhara ya riba kwa usahihi. Waliweza pia kutoa hoja
madhubuti kuonesha namna ya kuondokana na tatizo la riba. Watahiniwa
hawa walielezea madhara ya riba kuwa ni: Riba huchafua moyo wa tajiri,
riba inamkandamiza mnyonge na mwenye dhiki, riba inaharibu uchumi wa
jamii na maendeleo yake, riba ni mali ya dhuluma. Pia walielezea utatuzi
wa tatizo la riba kwa njia mbalimbali kama vile; Kukopesha bila riba,
kushirikiana katika mtaji na kugawana gharama za uendeshaji faida na
hasara na kuanzisha benki za Kiislam. Watahiniwa hawa vilevile
walielezea suala la kuielimisha jamii juu ya riba na madhara yake. Kwa
ujumla watahiniwa hawa walikuwa na maarifa ya kutosha kuhusu
kipengele cha Uchumi katika Uislamu hivyo waliweza kupata majibu
sahihi ya swali hili kwa kuzingatia matakwa ya swali na walipata alama za
juu. Kielelezo namba 4.1 kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa
aliyejibu vizuri.
Kielelezo 4.1 Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 4
-
15
Uchambuzi zaidi uliofanywa katika majibu ya wanafunzi unaonesha kuwa
watahiniwa 35,567 (54.40%) walipata alama za chini (0 hadi 1) ambapo
miongoni mwao watahiniwa 17,345 (25.80%) walipata alama 0.
Watahiniwa hawa walishindwa kuainisha madhara ya riba na kuonesha
ufumbuzi wa tatizo la riba. Baadhi yao walibainisha adhabu za Allah (s.w)
dhidi ya mtoaji na mpokeaji riba kama vile; Kuingia motoni, milango ya
pepo itafungwa, hataingia peponi, hupata madhambi na kupatiwa adhabu
na Mola. Baadhi ya watahiniwa hawakujibu kabisa swali hili kwakuwa
hawakuwa na ufahamu wowote kuhusu majibu ya swali hili. Kwa ujumla
watahiniwa hawa walipata alama hafifu na wengine alama 0 kwa sababu ya
kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mada iliyoulizwa na
kutokufahamu matakwa ya swali. Kielelezo 4.2 kinaonesha sampuli ya
majibu ya mtahiniwa aliyeshindwa kujibu swali la 4 kama linavyotakiwa.
Kielelezo 4.2 Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 4.
2.2.3 Swali la 5: Nguzo za Imani Swali hili lilitoka katika kipengele cha kuamini Qadar ya Mwenyezi
Mungu, ambapo mtahiniwa alitakiwa kutoa tofauti kati ya Qudra na Qadar
ya Mwenyezi Mungu. Watahiniwa 58,913 (87.50%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu walijibu swali hili. Takwimu zinaonesha
kuwa watahiniwa 41,608 (70.60%) walipata alama 0 hadi 1. Watahiniwa
15,592 (26.47%) walipata alama 1.5 hadi 3 na watahiniwa 1,713 (2.91%)
walipata alama 3.5 hadi 5. Chati namba 5 inaonesha kufaulu kwa
watahiniwa hawa kwa asilimia.
-
16
Chati ya: 5: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 5
Uchambuzi unaonesha kuwa kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa katika
swali hili ni dhaifu kwani watahiniwa 41,608 (70.60%) kati ya 58,913
waliojibu swali hili walipata alama 0 hadi 1 ambapo miongoni mwao
watahiniwa 37,122 (55.20%) walipata alama 0. Watahiniwa hawa
walishindwa kutofautisha kwa usahihi kati ya Qudra na Qadar ya
Mwenyezi Mungu. Hii ilisababishwa na watahiniwa hao kutokuwa na
maarifa ya kutosha juu ya nguzo hii ya sita ya Imani. Baadhi ya watahiniwa
waliielezea Qudra kuwa ni: Bahati aliyomjalia mja na Qadar ni makadirio
ya mwanadamu aliyokadiriwa, Qudra ni neema anazotoa Allah (s.w)
kwenda kwa mja wake na Qadar ni nguzo ya tano ya Uislamu. Watahiniwa
wengine walibuni majibu yao na kuonesha kuwa Qudra ni kinyume cha
Qadar. Miongoni mwa majibu hayo ni: Qudra ni kuamini tofauti na
maamrisho ya Allah (s.w) na Qadar ni kuamini kuwa hapana apasae
kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), Qudra ni maneno yanayosemwa na
watu bila kuyatekeleza maamrisho yake na Qadar ni hali ya kutekeleza
maamrisho ya Allah (s.w).Watahiniwa hawa hawakuwa na maarifa ya
kutosha katika kipengele hiki cha nguzo za imani hivyo walipata alama
hafifu na wengine walipata alama 0. Kielelezo 5.1 kinaonesha sampuli ya
majibu ya mtahiniwa aliyeshindwa kutoa majibu sahihi ya swali.
70.6%
26.5%
2.9%
0.0 - 1.0
1.5 - 3.0
3.5 - 5.0
Alama
-
17
Kielelezo 5.1: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 5
Watahiniwa 15,592 (26.47%) walipata alama za wastani kutokana na
kushindwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya tofauti iliyopo kati ya Qudra
na Qadar ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya watahiniwa waliweza kueleza
maana ya neno moja tu kati ya Qadar na Qudra kwa usahihi hivyo walipata
alama za wastani.
Uchambuzi zaidi unaonesha kuwa watahiniwa 1,713 (2.91%) walipata
alama za juu (3.5 hadi 5) miongoni mwao watahiniwa 213 (0.30%)
walipata alama zote 5. Watahiniwa hawa waliweza kuelezea kwa usahihi
tofauti iliyopo kati ya Qadar na Qudra ya Mwenyezi Mungu, kama vile:
Qudra ya Mwenyezi Mungu ni uwezo wake juu ya kila kitu usio na mipaka
na Qadar ya Mwenyezi Mungu ni mpango/mpangilio wa kuendesha mambo
yote. Watahiniwa hawa walionesha kuwa na maarifa ya kutosha kuhusu
mada ya Nguzo za Imani na walitumia maarifa yao vema kueleza dhana
hizo hivyo waliweza kupata alama za juu. Kielelezo namba 5.2 kinaonesha
sampuli ya majibu ya mtahiniwa aliyejibu vizuri.
Kielelezo 5.2 Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 5
-
18
2.2.4 Swali la 6: Nguzo za Uislamu Swali lilitoka katika mada ya Nguzo za Uislamu kipengele cha Swaumu ya
Ramadhani, na lilimtaka mtahiniwa aorodheshe mambo matano ambayo
yanaweza kubatilisha swaumu ya mume na mke katika mchana wa
Ramadhani. Watahiniwa 66,422 (98.70%) kati ya watahiniwa 67,309
waliofanya mtihani huu walijibu swali hili. Takwimu zinaonesha kuwa
watahiniwa 35,823 (53.93%) walipata alama 1.5 hadi 3. Watahiniwa
16,683 (25.10%) walipata alama 0 hadi 1 na watahiniwa 13,916 (20.95%)
walipata alama 3.5 hadi 5. Chati namba 6 inaonesha kufaulu kwa
wanafunzi hawa kwa asilimia.
Chati namba 6 Kufaulu kwa watahiniwa kwa asilimia katika swali la 6
Uchambuzi uliofanywa kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa kizuri kwani watahiniwa
49,739 (74.88%) waliojibu swali hili walipata alama kuanzia 1.5 hadi 5
ambazo ni alama za kufaulu kwenye swali hili. Watahiniwa 1,112 (1.70%)
walipata alama zote 5. Watahiniwa hawa walionesha kuwa na maarifa ya
kutosha kuhusiana na mada ya Funga ya Ramadhani na walielewa matakwa
ya swali. Watahiniwa hawa waliweza kubainisha mambo ambayo
yanaweza kubatilisha Funga ya mume na mke kwa pamoja katika mchana
wa mwezi wa Ramadhani kama vile: kula na kunywa mchana wa
Ramadhani kwa makusudi, kufanya tendo la ndoa, kujitapisha kwa
makusudi kujitoa manii na kunuia kuvunja swaumu.
25.1
53.9
21.0
0
10
20
30
40
50
60
70
80
90
100
0.0 - 1.0 1.5 - 3.0 3.5 - 5.0
Asi
lim
ia y
a w
ata
hin
iwa
Alama
-
19
Watahiniwa 35,823 (53.93%) waliopata alama za wastani waliezea majibu
pungufu kulingana na yaliyohitajika katika kujibu swali hili. Vile vile
watahiniwa hawa walichanganya majibu yaliyo sahihi na mengine yasiyo
sahihi, kama vile: Kuamka na janaba, kutokusimamisha swala, matendo
maovu, kutokwa na najisi, kusengenya, kutamani, kutooga janaba, kuvaa
nguo zinazoonesha, kutotii sharia za Ramadhani, kubusiana mke na mume
na kufuata nafsi matamanio. Kielelezo namba 6.1 kinaonesha sampuli ya
majibu ya mtahiniwa aliyejibu kwa kuzingatia matakwa ya swali.
Kielelezo namba 6.1 Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 6.
Uchambuzi zaidi wa majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa watahiniwa
16,683 (25.10%) walishindwa kujibu swali hili kwa usahihi hivyo walipata
alama hafifu (0 hadi 1) na miongoni mwao watahiniwa 3,786 (5.60%)
walipata alama 0. Hii ni kwa sababu ya kutozingatia matakwa ya swali na
kutokuwa na maarifa ya kutosha juu ya mambo ya jumla yanayo batilisha
Funga ya mume na mke kwa pamoja. Baadhi yao badala ya kuandika
yanayo batilisha Funga waliandika mambo ambayo yanadhaniwa kuwa
yanabatilisha Funga. Mambo hayo ni kama vile: kukumbatiana mke na
mume, kupigana busu mke na mume, kutamaniana mke na mume, kuamka
na janaba na kulia.
Watahiniwa wengine badala ya kuandika yanayobatilisha Funga,
waliandika mambo ambayo yanapunguza uzito au thamani ya Funga, kama
vile: Kusengenya, kutukana, kusema uongo, kuchonganisha, kugombana,
kudhulumu, kutosimamisha swala na kutovaa stara. Kutokana na majibu
haya watahiniwa hawa walipata alama hafifu au alama 0. Kielelezo namba
6.2 kinaonesha mfano wa majibu ya mtahiniwa aliyeshindwa kujibu kwa
kuzingatia matakwa ya swali.
-
20
Kielelezo 6.2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 6
2.2.5 Swali la 7: Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa Kiislamu
Swali hili lilitoka katika mada ya mambo ya lazima ya kufanyiwa maiti wa
kiislamu. Mtahiniwa alitakiwa kueleza hatua tano za kumkafini maiti wa
kiume. Watahiniwa 63,063 (93.70%) kati ya watahiniwa 67,309 waliofanya
mtihani huu walijibu swali hili. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
57,238 (90.8%) walipata alama 0 hadi 1. Watahiniwa 5,060 (8.02%)
walipata alama 1.5 hadi 3 na watahiniwa 765 (1.21%) walipata alama 3.5
hadi 5. Chati namba 7 inaonesha kufaulu kwa wanafunzi hao kwa asilimia.
Chati namba 7: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 7
Uchambuzi uliofanywa kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa dhaifu kwani watahiniwa
57,238 (90.8%) waliojibu swali hili walipata alama 0 hadi 1. Miongoni
90.8%
8.0%
1.2%
0.0 - 1.0
1.5 - 3.0
3.5 - 5.0
Alama
-
21
mwao watahiniwa 41,561 (61.70%) walipata alama 0, kwa sababu ya
kushindwa kuelewa matakwa ya swali na kutokuwa na maarifa ya kutosha
juu ya namna ya kukafini maiti wa kiislamu. Baadhi ya watahiniwa
hawakuelewa na kuandika mambo ya lazima ya kufanyiwa maiti Muislamu
badala ya hatua za kukafini maiti wa kiume. Majibu waliyo andika ni:
kuosha maiti, kuvika sanda maiti, kuswalia maiti na kuzika. Watahiniwa
wengine waliandika hatua za kuosha maiti Muislamu kama vile: Kumfunika
maiti kwa nguo yenye kupenyeza maji na kumwagia maji na kumsugua kwa
kumgeuzageuza, kumbinya kutoa uchafu tumboni, kumkalisha na kumbinya
tena, kumtilisha udhu maiti na kumvalisha sanda. Watahiniwa wengine
walieleza hatua za kumkafini maiti mwanamke badala ya hatua za kukafini
maiti wa kiume. Hivyo watahiniwa hawa hawakuelewa matakwa ya swali.
Kielelezo namba 7.1 kinaonesha mfano wa majibu ya mtahiniwa
aliyeshindwa kujibu kwa kuzingatia matakwa ya swali.
Kielelezo 7.1: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 10
Watahiniwa 5,060 (8.02% ) waliopata alama za wastani (1.5 hadi 2.5)
waliweza kutaja baadhi ya hatua bila maelezo ya kutosha juu ya hatua hizo
za kumkafini maiti wa kiume na wengine walielezea hatua pungufu ya
tano.
-
22
Uchambuzi zaidi kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa katika
watahiniwa 765 (1.21%) waliopata kuanzia alama 3.5 hadi 5 ni watahiniwa
102 (0.20%) tu walipata alama zote 5 za swali hili. Watahiniwa hawa
waliopata alama za juu walionesha kuwa na maarifa ya kutosha juu ya
namna ya kumkafini maiti wa kiislamu. Vile vile walielewa matakwa ya
swali, hivyo waliweza kueleza kwa usahihi hatua tano za kumkafini maiti
wa kiume kwa kuandika kama vile: kuweka pande la kwanza la sanda juu
ya jamvi, kisha la pili na la tatu, kutoa kamba katika pande zote za jamvi la
kwanza, Kamba nyingine zitolewe kwenye jamvi la tatu kwa ajili ya
kumfungia maiti ili sanda isije kumvuka akabakia uchi. Maiti alazwe juu ya
mapande yote matatu na kuzibwa kwa pamba zilizofukizwa manukato
katika matundu yote ya mwili, Maiti atatizwe (afunikwe) kwa mapande yote
matatu moja baada ya jingine na kamba zitumike kufunga vitanzi miguuni,
tumboni na kichwani. Kielelezo namba 7.2 kinaonesha sampuli ya majibu
ya mtahiniwa aliyejibu kwa kuzingatia matakwa ya swali na kueleza kwa
ufasaha hatua muhimu katika kukafini.
Kielelezo namba 7.2: Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 7
-
23
2.2.6 Swali la 8: Qur`an
Swali hili lilitoka katika mada ya Qur'an, katika mada ndogo ya kushuka na
kuhifadhiwa kwa Qur'an. Swali lilikuwa na vipengele viwili; (a) na (b).
Katika kipengele (a) mtahiniwa alitakiwa atoe sababu mbili kueleza
kwanini Qur'an ilishushwa kidogokidogo na katika kipengele (b)
mtahiniwa alitakiwa kuelezea njia kuu tatu zilizotumika katika kuihifadhi
Qur'an.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 64,957 (96.50%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Watahiniwa 31,101 (47.88%) walipata
alama 1.5 hadi 3. Watahiniwa 30,349 (46.70%) walipata alama 0 hadi 1 na
watahiniwa 3,507 (5.40%) walipata alama 3.5 hadi 5. Chati namba 8
inaonesha kufaulu kwa wanafunzi hawa kwa asilimia.
Chati namba 8: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 8
Uchambuzi uliofanywa kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa cha wastani kwa kuwa
watahiniwa 34,608 (53.28%) walipata alama 1.5 hadi 5. Watahiniwa
waliopata alama za juu walionesha kuwa na maarifa ya kutosha juu ya
mada ya Qur'an. Watahiniwa hawa walielewa matakwa ya swali hivyo
waliweza kuandika kwa usahihi sababu za kushuka Qur'an kidogo kidogo
na njia kuu tatu zilizotumika katika kuihifadhi Qur'an.
46.7%
47.9%
5.4%
0.0 - 1.0
1.5 - 3.0
3.5 - 5.0
Alama
-
24
Katika kipengele (a) waliandika sababu za kushushwa kidogo kidogo kwa
Qur’an kuwa ni: Ili uthibitishwe moyo wa Mtume (s.a.w) kwa aya mpya, ili
kuwa wepesi kwa Mtume (s.a.w) kufikisha ujumbe uliotangulia kwa
ukamilifu kabla ya ujumbe uliofuata na ili iwe wepesi kwa waumini wa
mwanzo kusoma na kuhifadhi Qur'an.
Katika kipengele (b) waliainisha njia kuu zilizotumika kuihifadhi Qur'an
kama vile: Kuhifadhishwa Mtume (s.a.w) na kuahidiwa kutosahau,
waislamu kuhifadhi Qur'an vifuani mwao baada ya kusomewa na Mtume
(s.a.w) na Qur'an kuhifadhiwa katika maandishi chini ya usimamizi wa
Mtume (s.a.w).
Watahiniwa 31,101 (47.88%) walipata alama za wastani kutokana na
sababu tofauti tofauti. Baadhi yao walijibu kipengele kimoja tu kati ya (a)
na (b) na kuacha kingine badala ya kujibu vipengele vyote viwili. Wengine
waliandika hoja pungufu katika kipengele kimoja au vyote viwili.
Sababu nyingine iliyosababisha watahiniwa hawa kupata alama za wastani
ni kuchanganya majibu sahihi na yasiyo sahihi katika vingele vya swali
kwa mfano katika kipengele (a) waliandika hoja kama vile: Hali aliyokuwa
nayo Mtume (s.a.w) wakati anapokea wahyi, kutokujua kusoma na
kuandika, watu waweze kusilimu, kuaminika Qur'an, kwa sababu Qur'an ni
tukufu. Pia katika kipengele (b) Mtume aliwaomba waandishi wake
wamsomee, kwenye juzuu, kanda, katika mapango na majabali. Kielelezo
namba 8.1 kinaonesha sampuli ya jibu la mtahiniwa aliyejibu kwa
kuzingatia matakwa ya swali.
Kielelezo namba 8.1: Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 8
-
25
Uchambuzi zaidi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
watahiniwa 30,349 (46.70%) walipata alama kuanzia 0 hadi 1, kati yao
watahiniwa 6,171 (9.20%) walipata alama 0. Watahiniwa hawa walijibu
kinyume na matakwa ya swali kutokana na kukosa maarifa ya kutosha juu
ya mada ya Qur'an. Baadhi yao hawakufanya kabisa swali hili katika
vipengele vyote viwili (a) na (b).
Watahiniwa wengine waliandika mahali au sehemu ambayo Mtume (s.a.w)
alishushiwa Qur'an badala ya kueleza kwa nini Qur’an ilishuka kidogo
kidogo kama ilivyoulizwa. Katika majibu yao walielezea: Qur'an
ilishushwa kidogo kidogo Mtume (s.a.w) alipokuwa Jabal Hiraa, Qur'an
ilishushwa kidogo kidogo Mtume (s.a.w) alipokuwa anaelekea Makka.
Kundi lingine la watahiniwa waliofanya vibaya katika swali hili walieleza
awamu ama hatua za kushuka kwa Qur’an (kutoka Lauhim mahfudh mpaka
wingu wa dunia na kuletwa duniani) badala ya kutoa sababu za Qur'an
kushuka kidogo kidogo kutoka wingu wa dunia kuja kwa Mtume (s.a.w).
Kundi lingine liliandika kuwa Qur'an kushushwa kidogo kidogo ni Qur'an
kushushwa Makka na Madinah.
Katika kipengele (b) kadhalika, baadhi ya watahiniwa badala ya kueleza
njia kuu zilizotumika kuhifadhi Qur'an walitoa maelezo kuwa: Qur'an
iliandikwa na kuhifadhiwa kwenye: Magome ya miti, mawe, mapangoni
katika mifupa na katika milima mirefu.
Aidha kuna watahiniwa wengine walijbu kipengele hiki cha (b) kwa
kuandika njia anazotumia Allah (s.w) kuwasiliana na waja wake, kama
vile: kutumia malaika, ndoto za kweli na kutumia vibao. Kielelezo namba
8.2 kinaonesha mfano wa majibu ya mtahiniwa aliyeshindwa kujibu kwa
kuzingatia matakwa ya swali.
-
26
Kielelezo 8.2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 10
2.2.7 Swali la 9: Sunnah na Hadithi
Swali hili lilitoka katika mada ya Sunnah na Hadithi, katika mada ndogo ya
uchambuzi wa hadithi za Mtume (s.a.w). Swali lilikuwa na vipengele viwili
(a) na (b). Katika kipengele (a) mtahiniwa alitakiwa aeleze tofauti kati ya
Hadithi Qudusy na Hadithi Nabawiyyah na katika kipengele (b) mtahiniwa
alitakiwa atofautishe Aljar-hi na Ata-adil.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 47,917 (71.20%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
32,412 (67.7%) walipata alama 0 hadi 1. Watahiniwa 14,772 (30.83%)
walipata alama 1.5 hadi 3 na watahiniwa 733 (1.53%) pekee ndio walipata
alama 3.5 hadi 5. Chati namba 8 inaonesha kufaulu kwa wanafunzi hao
kwa asilimia.
-
27
Chati no: 9: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 9.
Uchambuzi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa cha wastani ambapo
watahiniwa 15,505 (32.36%) kati ya 47,914 waliojibu swali hili walipata
alama 1.5 hadi 5. Watahiniwa hawa walionesha kuwa na maarifa ya
kutosha juu ya mada ya uchambuzi wa Hadithi za Mtume (s.a.w) hivyo
waliweza kutofautisha kwa usahihi baina ya Hadithi Qudusy na Hadithi
Nabawiyyah, vilevile Aljar’hi na Ata’adili kwa namna ambayo
iliwawezesha kupata alama za juu.
Miongoni mwa tofauti walizozitoa ni kuwa: (a) Hadithi Qudusyi ni habari
aliyoitoa Mtume (s.a.w) kama alivyoipokea kutoka kwa Allah (s.w) ilihali
Hadithi Nabawiyyah ni usemi au habari aliyoitoa Mtume (s.a.w) kwa watu
kwa maneno yake. Hadithi za aina hii zinaanza kwa maneno amesema
Mtume (s.a.w).
Kipengele (b) Aljar-hi ni kumtia dosari msimulizi kwa kukataa hadithi yake
kutokana na udhaifu aliokuwa nao ilihali Ata-adili ni kumkubali msimulizi
wa hadithi kutokana na sifa nzuri alizokuwa nazo. Kutokana na maelezo
haya waliyoyatoa, watahiniwa hawa waliweza kupata alama nzuri.
Watahiniwa 14,772 (30.83% ) walipata alama za wastani (1.5 hadi 3) kwa
sababu walijibu kipengele kimoja na kuacha kingine. Vile vile waliandika
67.7%
30.8%
1.5%
0.0 - 1.0
1.5 - 3.0
3.5 - 5.0
Alama
-
28
maelezo yasiyotosheleza kuhusu istilahi zilizoulizwa. Watahiniwa hawa
walipata alama za wastani. Kielelezo namba 9.1 kinaonesha mfano wa
majibu ya mtahiniwa aliyeweza kutofautisha vipengele hivyo vya Hadithi.
Kielelezo 9.1: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 9
Uchambuzi zaidi uliofanywa kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha
kuwa watahiniwa 32,412 (67.60%) waliopata alama hafifu (0 hadi 1)
walijibu kinyume na matakwa ya swali kutokana na kutokuwa na maarifa
ya kutosha juu ya mada ya uchambuzi wa Hadithi za Mtume Muhammad
(s.a.w). Watahiniwa hawa walishindwa kutofautisha istilahi walizopewa
kama ilivyotakiwa na wengine waliacha kabisa kujibu swali hili.
Baadhi ya watahiniwa hawa walitafsiri neno Aljar-hi na Ata-adil kama aina
au tanzu za Hadithi kama vile: Aljar-hi ni hadithi fupi fupi kutoka kwa
Mtume wetu (s.a.w) na Ata-adili ni hadithi ndefu ndefu zenye aya ndefu,
Aljar-hi ni hadithi ambayo imesimuliwa na nabii mussa wakati ata-adil ni
-
29
hadithi ambayo imesimuliwa na nabii Ibrahim na aljar-hi ni hadithi zenye
wapokezi wengi wakati at-adil ni hadithi zenye wapokezi kidogo.
Baadhi ya watahiniwa ambao hawakuwa na maarifa ya kutosha kuhusu
kipengele (a) walitoa majibu yafuatayo: Hadithi qudusy ni hadithi ambayo
imepokelewa Makka na mahujaji na nabawiyya ni hadithi ambayo
ilipokelewa Madina kwa lengo la kuendeleza uislamu, Qudusy ni hadithi
iliyoandikwa enzi za Mtume (s.a.w) na Nabawiyyi ni Hadithi
zilizopokelewa na Imamu muslim na Bukhar, Nabawiyya ni hadithi dhaifu
na Qudusy ni Hadidhi sahihi na Qudusy ni hadithi za kuhifadhiwa
vichwani na hadithi Nabawiyya ni hadithi za kuhifadhiwa kwenye misahafu
na juzuu.
Wengine katika kujibu kipengele (a) walifananisha Hadithi Qudusy na
Nabawiyah kama vile Hadithi Mutawatir na Ahad na kuzieleza kama;
hadithi qudusy ni hadithi ambayo imesimuliwa na watu wachache wakati
Nabawiyyah ni hadithi ambayo imesimuliana watu wengi. Kutokana na
majibu haya na mengine yanayofanana na hayo watahiniwa hawa walipata
alama hafifu au alama 0. Kielelezo namba 9.2 kinaonesha mfano wa majibu
ya mtahiniwa aliyeshindwa kujibu swali kwa usahihi.
Kielelezo 9.2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 10
2.3 SEHEMU C: Maswali ya Insha Sehemu hii ilikuwa na jumla ya maswali manne ya insha ambapo
mtahiniwa alitakiwa kujibu maswali matatu. Kila swali lilikuwa na alama
15. Jumla ya alama katika sehemu hii ilikuwa 45. Maswali katika sehemu
hii yalitoka katika mada za: Dola ya Kiislamu Madina, Qur an, Nguzo za
Uislamu na Mfumo wa jamii ya Kiislamu.
-
30
2.3.1 Swali la 10: Dola ya Kiislamu Madinah Swali hili lilitoka katika mada kuu ya Dola ya kiislamu Madinah katika
kipengele Kutawafu kwa Mtume (s.a.w). Watahiniwa walitakiwa kueleza
mafunzo manne wanayopata Waislamu kuanzia kuumwa hadi kutawafu
kwa Mtume Muhammad (s.a.w).
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 45,147 (67.10%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
27,210 (60.30%) walipata alama 0 hadi 4.5. Watahiniwa 16,501 (36.55%)
walipata alama 5 hadi 9.5 na watahiniwa 1,436 (3.18%) walipata alama 10
hadi 15 za swali hili. Chati namba 10 inaonesha kufaulu kwa wanafunzi
hao katika asilimia.
Chati 10: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 10
Kwa ujumla kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa katika swali hili
kilikuwa cha wastani kwani watahiniwa 17,937 (39.73%) kati ya
watahiniwa 45,147 waliojibu swali hili walipata alama 5 hadi 15.
Watahiniwa waliopata alama za juu waliweza kubainisha mafunzo sahihi
kutokana na kuugua hadi kutawafu kwa Mtume (s.a.w). mafunzo hayo ni
kama vile: Ugonjwa sio sababu ya mtu kuacha kufanya ibada na majukumu
mengine, kiongozi anapopata dharura sio sababu ya mambo kusimama bali
akabidhi mtu mwingine majukumu yake, tunafundishwa kuwa ni bora maiti
60.3%
36.5%
3.2%
0.0 - 4.5
5.0 - 9.5
10.0 - 15.0
Alama
-
31
ashughulikiwe na ndugu zake wa karibu kinasaba na uchungu wa umauti
utampata kila mtu akiwa mwema au muovu. Kielelezo namba 10.1
kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa aliyeweza kueleza kwa
usahihi mafunzo yatokanayo na kuugua hadi kutawafu kwa Mtume (s.a.w).
-
32
Kielelezo namba 10.1 Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 10
Watahiniwa 16,501 (%) walipata alama za wastani (5 hadi 9.5) kutokana na
kushindwa kutoa maelezo ya kutosha katika hoja walizozianisha ingawa
hoja zao zilikuwa sahihi. Wengine walitoa hoja pungufu ya nne ambazo
zilihitajika katika swali hili. Watahiniwa wengine walichanganya majibu
-
33
sahihi na yasiyo sahihi kama vile: Imani ya kweli, malipo mazuri ni kutoka
kwa Allah (S.W), kuamini qadar, tunajifunza kuwa Allah (S.W) ni Muweza
wa kila jambo na Allah (S.W) ndiye aliyemtuma Mtume (s.a.w).
Watahiniwa 27,210 (60.30%) walishindwa kujibu swali hili kwa usahihi
hivyo walipata alama hafifu (0 hadi 4.5) ambapo miongoni mwao
watahiniwa 3,246 (4.8%) walipata alama 0. Hii ni kwa sababu ya
kushindwa kujua matakwa ya swali na wengine kutokuwa na maarifa ya
kutosha juu ya historia ya kutawafu kwa Mtume (s.a.w).
Baadhi ya watahiniwa walionesha kuwa hawakuelewa kabisa matakwa ya
swali kwani waliorodhesha vitendo vya waja wema kama mafunzo
kutokana na tukio hili, mfano wa majibu hayo ni kama vile: uvumilivu,
uchamungu, subra, kufanya mambo mema kuutangaza Uislamu, kumuamini
Mwenyezi Mungu, kusoma Qur'an kiufasaha, kujua jinsi ya kuishi na jirani
na kujipamba na tabia njema.
Watahiniwa wengine walielezea sifa na uwezo wa Mwenyezi Mungu kama
mafunzo, mfano: Allah (s.w) ni Mola wa viumbe vyote humchukua
amtakaye, Allah (s.w) humnusuru amtakaye, Allah (s.w) ndiye mwenye
mamlaka ya kufanya chochote na Allah (s.w) humpa amtakaye na
kumnyima amtakaye.
Baadhi ya watahiniwa badala ya kuandika mafunzo ya tukio hili, walieleza
sifa za Mtume (s.a.w) kama ilivyozoeleka kwa jamii kumsifia kiongozi
anapofariki, kama vile: alikuwa na mapenzi makubwa na watu, alikuwa
mwaminifu, alikuwa mkarimu, alikuwa mchamungu na alikuwa akitoa
zakat sadaka. Kwa ujumla watahiniwa hawa hawakuwa na maarifa juu ya
mada hii na wengine hawakuelewa kabisa matakwa ya swali, hivyo baadhi
yao walipata chini ya alama tano (5) huku wengine wakipata alama 0.
Kielelezo namba 10.2 kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa
aliyeshindwa kujibu swali hili kama inavyostahili.
-
34
-
35
Kielelezo namba: 10.2 Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 10
-
36
2.3.2 Swali la 11: Qur'an. Swali hili lilitoka katika mada ya Qur'an, katika mada ndogo ya kushuka na
kuhifadhiwa kwa Qur'an. Swali lilimtaka mtahiniwa aeleze namna Mtume
(s.a.w) alivyoteremshiwa Qur'an kwa mara ya kwanza na kueleza mafunzo
manne yanayopaswa kufanyiwa kazi katika maisha ya kila siku kutokana
na tukio hilo.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 48,693 (72.30%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Watahiniwa 28,239 (58.00%) walipata
alama 0 hadi 4.5. Watahiniwa 18,973 (39.0%) walipata alama 5 hadi 9.5 na
watahiniwa 1,481 (3.04%) walipata alama 10 hadi 14.5. Chati namba 11
inaonesha kufaulu kwa watahiniwa hawa kwa asilimia.
Chati namba 11: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 11
Kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa katika swali hili kilikuwa cha
wastani kwani watahiniwa 20,454 (42.01%) kati ya 48,693 waliojibu swali
hili walipata alama 5 hadi 14.5. Watahiniwa waliopata alama za juu (10
hadi 14.5) waliweza kueleza kwa umahiri namna Mtume (s.a.w)
alivyoteremshiwa Qur'an kwa mara ya kwanza na kubainisha mafunzo
manne yanayopaswa kufanyiwa kazi katika maisha ya kila siku kutokana
na tukio hilo. Watahiniwa hawa walieleza kuwa: Mtume (s.a.w) alianza
kushushiwa Qur'an mwaka 610 A.D akiwa na umri wa mika 40 katika
pango la Jabal Hira katika usiku wa mwezi wa Ramadhani. Malaika Jibril
58.0%
39.0%
3.0%
0.0 - 4.5
5.0 - 9.5
10.0 - 14.5
Alama
-
37
alimuendea mtume pangoni hapo na kumuamuru asome. Mtume (s.a.w)
alijibu kuwa hajui kusoma. Jibril alimbana kwa nguvu na alipomuachia
alimsomea aya tano za mwanzo za suratul Alaq. Mtume alirejea nyumbani
na aya hizi huku akitetemeka kwa hofu na alimuhadithia mkewe Bi Khadija
yote yaliyompata. Mafunzo waliyoyatoa kutokana na tukio hili ni pamoja
na: Elimu ni amri ya kwanza aliyopewa mtume (s.a.w), kutafuta elimu sio
jambo jepesi bali tutakumbana na magumu mengi, utukufu wa Mwezi wa
Ramdhani unatokana na Qur'an kuanza kushuka mwezi huo hivyo tuzidishe
kusoma Qur'an katika mwezi huo na Qur'an ni kitabu cha Allah (s.w).
Watahiniwa 18,973 (38.96% ) walipata alama za wastani (5 hadi 9.5)
kwakuwa hawakutoa maelezo ya kutosha juu ya historia ya kushushwa kwa
Qur'an kwa mara ya kwanza na mafunzo tunayoyapata. Baadhi ya
watahiniwa waliandika hoja pungufu ya nne na walichanganya majibu
sahihi na yasiyo sahihi kama vile: Kutekeleza maamrisho na kuacha
makatazo, tunapaswa kufuata sharia na kanuni, tunapaswa kumuamini
Allah (s.w) na Mtume wake, Jibril ndiye aliyekuwa akishusha wahyi na
kutii amri Allah (S.w) ni sababu ya kupata radhi zake. Kielelezo namba
11.1 kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa aliyejibu kwa kuzingatia
matakwa ya swali.
-
38
-
39
Kielelezo namba 11.1: Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 11
Uchambuzi zaidi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
watahiniwa 28,239 (58.00%) walipata alama hafifu (0 hadi 4.5) ambapo
miongoni mwao watahiniwa 2,455 (3.60%) walipata alama 0. Watahiniwa
hawa walijibu kinyume na matakwa ya swali kutokana na kutokuwa na
maarifa ya kutosha juu ya historia ya kushushwa na kuhifadhiwa kwa
Qur'an.
Baadhi ya watahiniwa hawa badala ya kueleza namna Mtume (s.a.w)
alivyoshushiwa Qur'an kwa mara ya kwanza na mafunzo tunayoyapata
kutokana na tukio hilo waliandika majibu ya jumla yaliyokuwa kinyume na
matakwa ya swali kama vile, hali aliyokuwa nayo Mtume (s.a.w) baada
kupokea wahyi, kwamba: Alikuwa mwoga sana baada ya kumuona Jibril,
baada kushushiwa Qur'an alikuwa anatetemeka, Mtume (s.a.w) alibadilika
haiba, Mtume (s.a.w) alipewa jukumu la kufundisha Qur'an na alikuwa
hajui kusoma wala kuandika.
-
40
Watahiniwa wengine waliandika faida za kuisoma Qur'an na kuifuata kama
vile: Qur'an ni kinga kwa mwanadamu, Qur'an inamfanya Mtu kuwa
mchamungu, Qur'an humrahisishia mtu kufanya jambo, Qur'an inamfanya
mtu kuwa muadilifu, Qur'an inafanya waislamu kushirikiana, Qur'an
inapelekea watu kuwa na hofu juu ya Allah (S.W) na Qur'an imepelekea
kuvumbuliwa kwa Sunnah.
Kwa ujmla watahiniwa hawa hawakuwa na maarifa juu ya historia ya
kushushwa kwa Qur’an, hivyo baadhi yao walipata alama hafifu na
wengine walipata alama 0. Kielelezo 11.2 kinaonesha sampuli ya majibu ya
mtahiniwa aliyeshindwa kujibu swali hili kwa kuzingatia matakwa ya
swali.
-
41
Kielelezo namba 11.2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 11
-
42
2.3.3 Swali la 12: Nguzo za Uislamu
Swali hili lilitoka katika mada ya Nguzo za Uislamu katika mada ndogo ya
kusimamisha Swala za jamaa. Mtahiniwa alitakiwa kueleza mambo matano
ya kuzingatia wakati wa kuandaa Khutba ya Ijumaa.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 32,967 (49.00%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Watahiniwa 25,356 (76.90%) walipata
alama 0 hadi 4.5 za swali hili. Watahiniwa 4,988 (15.13%) walipata alama
5 hadi 9.5 na watahiniwa 2,623 (7.96%) walipata alama 10 hadi 15. Chati
namba 11 inaonesha kufaulu kwa watahiniwa hao katika asilimia.
Chati namba: 12: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 12
Uchambuzi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa dhaifu, kwakuwa
watahiniwa 25,356 (76.90%) kati ya 32,967 waliofanya swali hili walipata
alama 0 hadi 4.5 ambapo miongoni mwao watahiniwa 9,369 (13.90%)
walipata alama 0. Watahiniwa hawa walijibu kinyume na matakwa ya swali
kwa sababu ya kutokuwa na maarifa ya kutosha juu ya khutuba ya Swala
ya ijumaa, hususani nguzo zake, badala ya kueleza mambo ya kuzingatia
wakati wa kuandaa khutuba ya Ijumaa watahiniwa wakaelezea hatua za
76.9%
15.1%
8.0%
0.0 - 4.5
5.0 - 9.5
10.0 - 15.0
Alama
-
43
kufuata katika kufikisha khutuba ya Ijumaa, kama vile: salamu na
utangulizi, mwanzo wa hutuba, kiini au katikati ya khutuba na mwisho wa
khutuba au hitimisho. Watahiniwa wengine walifahamu kuwa mambo ya
kuzingatia kabla ya kuandaa khutuba ni namna khatibu anavyotakiwa kuwa
au sifa za khatibu na khutuba yenyewe, hivyo wakatoa sifa kama vile:
Khatibu awe na udhu, awe nadhifu, awe mnyenyekevu, awe amehifadhi
Qur'an na kuielewa, awe amehifadhi Hadithi na kuzielewa, awe anajua
tafsiri ya sura zote na awe amehifadhi tafsiri ya Hadithi zote.
Na katika sifa za khutuba wakaeleza kuwa: Khutuba iwe fupi nzuri na
yenye kueleweka, khutuba itumie lugha ya walengwa, khutuba ilenge jamii
husika, khutuba ilenge matatizo ya jamii, isiwe ya kusengenya mtu, isiwe
na utata na izingatie muda. Pamoja na kuwa baadhi ya mambo
waliyoyaeleza ni ya kweli lakini sio majibu sahihi kwa sababu sio nguzo za
khutuba ya Ijumaa, hivyo watahiniwa hawa walipata alama hafifu na
wengine alama 0. Kielelezo namba 12.1 kinaonesha sampuli ya majibu ya
mtahiniwa aliyeshindwa kujibu swali hili kwa kuzingatia matakwa ya
swali.
-
44
-
45
Kielelezo namba 12.1: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 12
Watahiniwa 4,988 (15.13%) waliopata alama za wastani (5 hadi 9.5)
walikuwa na mapungufu mbalimbali kama vile: Baadhi walitaja majibu
sahihi lakini hawakutoa maelezo kamili juu ya mambo hayo. Wengine
walieleza pungufu ya mambo matano yaliyohitajika na baadhi yao
waliochanganya majibu sahihi na yasiyo sahihi, kama vile: kutoa salamu
kwa waislamu, kuwaruhusu waislamu kuomba dua, kuweka kituo baina ya
khutuba mbili, kuwa na mfano wa aya na hadithi, lugha ya khutba ifanane
na wale wanaohutubiwa, mada iendane na jamii na khutuba iwe ni yenye
kuelimisha. Baadhi ya mambo haya ni kweli hufanyika wakati wa khutuba
ya Ijumaa lakini sio katika misingi ya kuandaa khutuba ya Ijumaa.
Uchambuzi zaidi uliofanywa kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha
kuwa watahiniwa 2,623 (7.96%) walipata alama za juu ambapo miongoni
mwao watahiniwa 7 walipata alama zote 15 za swali hili, watahiniwa hawa
walionesha kuelewa matakwa ya swali na walikuwa na maarifa ya kutosha
juu ya uandaaji wa khutba ya Swala ya Ijumaa.
Watahiniwa hawa waliweza kueleza kwa usahihi mambo matano ya
kuzingatia wakati wa kuandaa khutuba ya Ijumaa kuwa ni: Kuanza khutuba
ya Ijumaa kwa kumhimid au kumshukuru Allah (s.w,), kisha kumswalia au
kumtakia rehema na Amani Mtume (s.a.w), kuwausia waislamu juu ya
kumcha Allah (S.w), kusoma aya au sura yeyote katika Qur'an na
kuwaombea waislamu/waumini wote dua. Kielelezo namba 12.2
-
46
kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa aliyejibu kwa kuzingatia
matakwa ya swali.
-
47
Kielelezo namba 12.2: Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 12
2.3.4 Swali la 13: Mfumo wa Jamii ya Kiislamu Swali hili lilitoka katika mada ya Mfumo wa jamii ya Kiislamu katika
mada ndogo ya Sheria katika Uislamu. Mtahiniwa alitakiwa afafanue kazi
tano za sheria ya Kiislamu katika jamii.
Swali hili lilijibiwa na watahiniwa 56,876 (84.50%) kati ya watahiniwa
67,309 waliofanya mtihani huu. Takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa
34,211 (60.20%) walipata alama 0 hadi 4.5 za swali hili. Watahiniwa
19,454 (34.20%) walipata alama 5 hadi 9.5 na watahiniwa 3,211 (5.65%)
walipata alama 10 hadi 15. Chati namba 13 inaonesha kufaulu kwa
watahiniwa hawa katika asilimia.
-
48
Chati namba 13: Alama za watahiniwa kwa asilimia katika swali la 13
Uchambuzi uliofanywa katika majibu ya watahiniwa unaonesha kuwa,
kiwango cha kufaulu katika swali hili kilikuwa cha wastani kwani
watahiniwa 22,665 (39.85%) kati ya 56,876 waliofanya swali hili walipata
kuanzia alama 5 hadi 15.
Watahiniwa waliopata alama za juu (10 hadi 15) walielewa vema matakwa
ya swali na walionesha kuwa na maarifa ya kutosha juu ya mada ya sheria
katika Uislamu. Watahiniwa hawa waliweza kubainisha kazi za sheria ya
kiislamu katika jamii kama vile: Kumlinda mwanadamu dhidi ya madhara
yanayoweza kusababishwa na mwenendo wake mbaya, kulinda watu na
mali zao, kuhifadhi maadili ya jamii, kuhifadhi amani na usalama, kupanga
utaratibu namna ya kuendesha shughuli mbalimbali zenye maingiliano ya
kijamii na kulinda na kuhifadhi dini.
Watahiniwa 19,454 (34.20%) waliopata alama za wastani (5 hadi 9.5)
hawakutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu kazi tano za sheria ya kiislamu
ingawa walizitaja kazi hizo kwa usahihi. Baadhi ya walitaja walitaja kazi
pungufu ya zile zilizohitajika katika swali na wengine waliandika kazi tano
za sheria za Kiislamu huku wakizirejea hoja zao kwa maneno mbadala na
kuziandika kama hoja mpya.
60.2%
34.2%
5.6%
0.0 - 4.5
5.0 - 9.5
10.0 - 15.0
Alama
-
49
Watahiniwa wengine waliachanganya majibu sahihi na yasiyo sahihi ndani
ya insha moja, kama vile: kujenga jamii mpya, kutoa hukumu ya mambo
mbalimbali, kutatua juu ya migogoro na kuwaongoza waumini katika lengo
la kuumbwa. Kutokana na sababu hizi, watahiniwa hawa walipata alama za
wastani. Kielelezo namba 13.1 kinaonesha sampuli ya majibu ya mtahiniwa
aliyejibu kwa kuzingatia matakwa ya swali.
-
50
Kielelezo 13.1: Sampuli ya majibu sahihi ya mtahiniwa katika swali la 13
-
51
Uchambuzi zaidi uliofanywa kwenye majibu ya watahiniwa unaonesha
kuwa watahiniwa 34,211 (60.20%) walipata alama hafifu (0 hadi 4.5) kati
yao watahiniwa 6,860 (10.20%) walipata alama 0. Watahiniwa hawa
walijibu kinyume na matakwa ya swali, kutokana na kutokuwa na maarifa
ya kutosha juu ya mada ya sheria katika Uislamu na kazi zake katika jamii.
Watahiniwa hawa badala ya kuandika kazi ya sheria ya Kiislamu katika
jamii waliandika makatazo mbalimbali ya sheria ya Kiislamu kama vile:
sheria inakataza kuiiba, sheria inakataza kuzini, sheria inakataza kuuwa,
sheria inakataza riba, sheria inakataza kufanya maovu. Kwa ujumla
watahiniwa hawa walishindwa kuelewa kazi za msingi za sheria ya
Kiislamu katika jamii. Watahiniwa wengine walieleza maamrisho ya sheria
ya Kiislamu kama vile: kusoma Qur'an, kufunga ramadhani, kusimamisha
swala, kutenda mema na kuwa mtiifu kwa kazi yeyote.
Baadhi ya watahiniwa walibadilisha maudhui ya swali kutoka kazi tano za
sheria ya Kiislamu na kuelezea kama nguzo tano za Uislamu, kwa hiyo
walifafanua nguzo tano za Uislamu badala ya kazi za sheria ya Kiislamu
katika jamii. Watahiniwa wengine katika kundi hili walijitunga majibu
yasiyohusiana na mada ya sheria katika Uislamu kama vile masharti ya
utoaji Zakat na Sadakat wakichanganya ndani yake nguzo za Uislamu, kwa
mfano: kuwapa wanaostahiki, kutoa vilivyo halali, kwenda kuhiji makka,
kutoa zakat na kufunga ramadhani. Kielelezo namba 13.2 kinaonesha
sampuli ya majibu ya mtahiniwa aliyeshindwa kujibu swali hili kama
ilivyotakiwa.
-
52
-
53
Kielelezo 13.2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi ya mtahiniwa katika swali la 13
-
54
3.0 UCHAMBUZI WA KUFAULU KWA KILA MADA
Mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa mwaka 2019 ulikuwa
na jumla ya maswali 13 ambayo yalitungwa kutoka katika mada kumi na
moja (11) ambazo ni: Dola ya kiislamu Madinah, Historia ya Uislamu
Baada ya Kutawafu Mtume (s.a.w), Sunnah na Hadithi, Qur’an, Mtazamo
wa Uislamu juu ya Dini, Familia ya Kiislamu, Mfumo wa Jamii ya
Kiislamu, Nguzo za Uislamu, Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa
Kiislamu, Sheria katika Uislamu na Nguzo za Imani.
Mada zilizotahiniwa katika swali la kwanza ni: Dola ya Kiislamu Madinah,
Historia ya Uislamu baada ya Kutawafu Mtume (s.a.w), Sunnah na
Hadithi, Qur’an, Mtazamo wa Uislamu juu ya Dini, Familia ya Kiislamu,
Sheria katika Uislamu na Nguzo za Imani ambazo kwa ujumla watahiniwa
walifanya vizuri na kufaulu kwa asilimia 95.42.
Uchambuzi wa takwimu wa matokeo ya watahiniwa katika mada
mbalimbali unaonesha kuwa na kiwango cha wastani cha kufaulu katika
mada zifuatazo: Nguzo za Uislamu (50.76%), Qur’an (47.64%), Mfumo wa
Jamii ya Kiislamu (42.71%), Dola ya Kiislamu Madinah (36.55%), Familia
katika Uislamu (34.20%) na Sunna na Hadithi (32.36%). Kiwango hiki cha
kufaulu kilitokana na: Watahiniwa kujibu maswali kwa maelezo
yasiyojitosheleza, kutotimiza idadi ya vipengele vilivyotakiwa kujibiwa
kwenye maswali na kuchanganya majibu sahihi na yasiyo sahihi katika
majibu yao.
Aidha mada zilizokuwa na kiwango cha chini cha kufaulu ni: Nguzo za
Imani (29.37%) na Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa Kiislamu
(9.24%). Uchambuzi uliofanywa umebaini kuwa sababu kubwa za mada
hizi kuwa na kiwango cha chini cha kufaulu ni watahiniwa kutokuwa na
maarifa ya kutosha na kushindwa kuelewa matakwa ya maswali.
Muhtasari wa uchambuzi wa kufaulu kwa watahiniwa kwa mada
umeoneshwa kwenye kiambatisho ambapo rangi nyekundu inaonesha
kiwango hafifu cha kufaulu, rangi ya njano inaonesha kufaulu kwa wastani
na rangi kijani inaonesha kiwango kizuri cha kufaulu katika swali husika.
-
55
4.0 HITIMISHO
Kwa ujumla kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa wa Elimu ya Dini ya
Kiislaamu kidato cha nne mwaka 2019 ni cha wastani (43.29%).
Uchambuzi huu umeonesha changamoto mbalimbali ambazo hazina budi
kutatuliwa ili kuboresha kiwango cha kufaulu. Aidha changamoto
zilizobainika ni kama vile: Watahiniwa kutofuata maelekezo ya swali hivyo
kushindwa kutoa majibu yanayojitosheleza; Kuchanganya majibu sahihi na
yasiyo sahihi; Kutoa maelezo yasiyojitosheleza kwa hoja sahihi walizozitoa
na uelewa mdogo wa mada mbalimbali.
Ili kuinua zaidi kiwango cha kufaulu kwenye mada zote katika mitihani
ijayo jitihada zinahitajika katika ufundishaji na ujifunzaji ili kuwajengea
watahiniwa uwezo wa kuelewa matakwa ya maswali, namna ya kuyajibu
kwa usahihi, na kuboresha namna ya kuwasilisha hoja kwa maandishi
katika muundo wa insha au majibu mafupi.
5.0 MAPENDEKEZO
Ili kuinua kiwango cha kufaulu katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu,
mambo yafuatayo yanapendekezwa:
(a) Walimu waboreshe ufundishaji wa mada kwa kuwaongoza wanafunzi
katika vikundi kueleza namna ya kutekeleza haki za maiti Muislamu.
(b) Walimu waboreshe ufundishaji wa mada kwa kuwaongoza wanafunzi
kivitendo au kwa kutumia igizo kuonesha namna ya kutekeleza haki za
maiti Muislamu.
(c) Walimu waboreshe ufundishaji kwa kuwaongoza wanafunzi kwa
kutumia mbinu ya maswali na majibu kueleza dhana (istilahi)
mbalimbali za kiitikadi na kubainisha umuhimu wake.
-
56
6.0 Kiambatisho
UCHAMBUZI WA KUFAULU KWA WATAHINIWA KWA MADA
Na. Mada
Kufaulu wa Kila
Swali Asilimia ya wanafunzi
waliopata wastani wa
alama 30 au zaidi
Maoni Nambari
ya
Swali
Asilimia
ya
Kufaulu
1
Dola ya Kiislamu
Madinah, Historia ya
Uislamu baada ya
Kutawafu Mtume
(s.a.w), Sunnah na
Hadithi, Qur’an,
Mtazamo wa Uislamu
juu ya Dini, Familia
ya Kiislamu, Sheria
katika Uislamu,
Nguzo za Imani.
1 95.42
95.42
Vizuri
2 Nguzo za Uislamu
2
6
12
50.76 58.46 Wastani
3 Qur’an 8
11 47.64 48.12 Wastani
4 Mfumo wa Jamii ya
Kiislamu.
4
13 42.71 42.71 Wastani
5 Dola ya Kiislamu
Madinah 10 39.73 39.73 Wastani
6 Familia katika
Uislamu 3 34.20 34.20 Wastani
7 Sunnah na Hadithi 9 32.36 32.36 Wastani
8 Nguzo za Imani 5 29.37 29.37 Dhaifu
9
Mambo ya lazima
kufanyiwa maiti
Muislamu.
7 9.24 9.24 Dhaif
Wastani wa Jumla wa Kufaulu 43.29 Wastani