1 i ya ajili a 5 onuru ya galilaya. isaya 9:1-5 mtoto aliyefanywa zawadi. isaya 9:6-7 fimbo ya...

9
Somo la 5 kwa ajili ya Januari 30, 2021

Upload: others

Post on 04-Feb-2021

39 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Som

    ola

    5 k

    wa

    ajili

    yaJa

    nu

    ari3

    0, 2

    02

    1

  • Nuru ya Galilaya. Isaya 9:1-5

    Mtoto aliyefanywa Zawadi. Isaya 9:6-7

    Fimbo ya adhabu. Isaya 9:8-10:34

    Shina la Yese. Isaya 11

    Mwokozi. Isaya 12

    Masihi anatambulishwa katika Isaya sura ya 9 hadi ya12 katika mazingira ya uasi wa Yuda na Israeli.

    Yesu ni Masihi. Alikuja kuilaani dhambi na kuwapaamani watu wa Mungu. Zaidi ya yote, pia alikujakuwapatia nuru, kuwafariji, na kuwaokoa watu Wake.

    Hebu tujifunze namna Isaya alivyomtambulisha Yesukatika sura hizi.

  • “Watu wake waliokwenda katika giza wameona nuru kuu; wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewaangaza.” (Isaya 9:2; Mathayo 4:16)

    ZEBULUN

    NAPHTALI

    Sea of Galilee

    Katika jibu kwenda kwa Ahazi juu ya ombi lake la msaada, Tiglath-pileseri III aliishambulia Israeli na kuitwaa miji ya Naftali, Zabuloni, na ng’ambo ya Yordani. Badae, Salmanasari V aliishinda mipaka iliyosalia ya Israeli na kuwafukuza watuwaliokuwa wamesalia.

    Nchi hii ndio ilikuwa ya kwanza kushindwa na kujazwa giza la upagani (Is. 8:22). Ilipaswa pia kuwa ya kwanza kuiona nuruambayo Masihi alikuwa akiileta.

    Yesu alitumia muda Wake mwingi wakati wa hudumaYake katika eneo hili kando yabahari ya Galilaya(tazama Mathayo 4:12-17).

    Capernaum

  • “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume, nauweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme waamani.” (Isaya 9:6)Mtot huyu anayetabiriwa anapaswa tu kuwa Masihi, Yesu:

    Mshauri waajabu: Mshauri mwenye hekima anayeongoza vyema. Ni jila hilohilo ambalo Malaika wa Bwana (Yesu Mwenyewe) alilitumia alipowatembelea

    wazazi wa Samsoni (Amu. 13:18)

    Mungu mwenye nguvu: Ni Mungu aliyefanyika mwili, mwenye nguvu nashujaa jasiri

    (Yoh, 1:1; 1Yoh. 5:20)

    Baba wa milele: Yesu ni wa milele, na ni Baba wa wanadamu wote, kwasababu aliwaumba wanadamu na ulimwengu wao

    (Yoh. 1:3; Kol. 1:16; 2Pt 3:18)

    Mfalme wa amani: Yeu ni mfalme wa haki aliyekuja duniani kuleta amni(Uf. 17:14; Yoh. 14:27; Yoh. 16:33)

  • FIMBO YA ADHABU“Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeuka mbali, lakini mkono

    Wake umenyoshwa hata sasa.” (Isaya 9:12, 17, 21; 10:4)

    Mungu aliweza kuwaadhibu watu Wake kwa fimbo kwasababu ya uovu wao (Is. 9:4). Hili linamaanisha kwambaaliwaacha waumie katika magumu ili watubu dhambi zaona kumrudia Yeye.

    Matatizo haya Magumu yalikuja katika hatua nne, kila mojani kali zaidi.

    [1] War on their land (9:8-12)

    [2] The wicked leaders fall (9:13-17)

    [3] The land is devastated, and famine (9:18-21)

    [4] The unjust judges fall (10:1-4)

    Kama watu walitubu, matatizo yangekoma (tazama Walawi26:14-39).

    Mungu aliwapa wana wa Israeli uhuru wa kuchagua aidhakumtii Yeye au hapana. Pia ametuachia na sisi kufanyauamuzi huu leo.

    Mungu huruhusu katika hekima Yake madhara ya kutotiikwetu pale yatakapotufanya kukumbuka na kurudi kwake.

  • “hukumu nzito ambazo zingewaangukia—vita, utumwa,

    ukandamizwaji, na kukosa nguvu na heshima miongoni

    mwa mataifa—haya yote yalikuwa yaje ili kwamba

    ndani ya hayo watambue mkono wa hasira wa Mungu

    mwenye nguvu ukiwaongoza katika toba. Kabila kumi

    za ufalme wa kaskazini ulikuwa unaenda kutawanywa

    kati ya mataifa, na miji yake kuachwa ukiwa; majeshi

    ya uangamizi ya mataifa adui yangefagia nchi yao tena

    na tena; hata Yerusalemu hatimaye ingeangushwa, na

    Yuda ingechukuliwa utumwani; lakini bado Nchi ya

    Ahadi isingeachwa ukiwa milele.”

    E.G.W. (Mtapokea Nguvu, Septemba 14)

  • “Shina la Yese” huwakilisha wazo kwambaMasihi atakuwa wa uzao wa Daudi (mwana waYese). Hii ndi maana Yesu alijiita Mwenyewe“Shina na Uzao wa Daudi” (Ufunuo 22:16).

    Moja ya malengo makuu ya Yesu ilikuwa ni kukomesha dhambi, na uasi, na kuanzisha amani ya milele. Hili lilianza na huduma Yake, kifo, ufufuo, na kuketi katika kiti cha enzi. Hata hivyo, haijaisha bado.

    Bado tunasubiria wakati ambapo “Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtotoaliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.” (Isaya 11:7-8)

  • Isaya 12 ni wimbo ambao Isaya aliuimba ili kumtukuza Mwokozi wake [na wetu]. Alitushauri nasi kwamba “yatangazeni matendo Yake katiya mataifa” (aya. 4), akikumbuka wimbo wa ushindi ambao Musa aliuimba baada ya kuvuka Bahari ya Shamu (Kutoka 15).

    “Tazama Mungu ndiye wokovu wangu; nitatumaini walasitaogopa; maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo

    wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.” (Isaya 12:2)

    Malaika aliwaambia Yusufu na Mariamu kuwa Masihi angeitwa“Yesu;” kwamba ni , “Bwana ni wokovu wangu” (Mt. 1:21; Lk. 1:31).

    Kuna wimbo wa ushindi pia katika Ufunua 15. kwasababu hiyo, wale 144,000 wanaimba wimbo kamahuo wa kushangaza.

    Yesu ndiye chanzo pekee cha wokovu. Atakuwawimbo wetu muda si mrefu, tutakapoimba pamoja“wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbowa Mwana Kondoo.” (Ufunuo 15:3)

  • “Kristo ndiye ‘Mfalme wa Amani’ (Isaya 9:6),

    na ni utume Wake kuirejesha duniani na

    mbinguni amani iliyovunjwa na dhambi. ‘Basi

    tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika

    imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa

    njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.’ Warumi 5:1.

    Ye yote anayekubali kuikataa dhmabi na

    kuufungua moyo wake katika pendo la

    Kristo, anakuwa mshirika wa amani hii ya

    kimbingu.”E.G.W. (Thoughts From the Mount of Blessing, cp. 2, p. 27)