· 2013-04-12 · utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa mtihani...

137
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA 4 MWAKA 2010 Dar Es Salaam Juni, 2011 www.JamiiForums.com

Upload: others

Post on 10-Jul-2020

32 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TAARIFA YA UTAFITI

KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO

CHA 4 MWAKA 2010

Dar Es SalaamJuni, 2011

www.JamiiF

orums.com

Page 2:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

i

SHUKRANI

Utafiti huu umehusisha wataalamu mbalimbali katika hatua za kubuni, kutayarisha,

kukusanya, kuchambua takwimu na kuandika ripoti. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya

Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

kwa pamoja zinawashukuru wataalamu wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine

katika hatua mbalimbali za utafiti huu. Pia tunawashukuru wadau wote wa elimu

waliohusika katika kutoa taarifa za utafiti. Aidha shukrani za pekee ziiendee Wizara ya

Fedha kwa kufanikisha mchakato mzima wa utafiti.

Shukrani pia zimwendee Bwana Jumanne Abdallah Sagini, Naibu Katibu Mkuu -

TAMISEMI kwa kuwa msimamizi mkuu wa kazi hii. Aidha, shukrani za dhati ziwaendee

wajumbe wa kikundi kazi kilichohusika katika utafiti huu kuanzia hatua za awali hadi

mwisho. Wajumbe hao ni:

JINA TAASISI WADHIFA

1. Francis M. Liboy OWM-TAMISEMI - Mwenyekiti

2. Lawrence John Sanga WEMU - Katibu

3. Fred Davidson Sichizya WEMU - Mjumbe

4. Abdallah Shaban Ngodu WEMU - Mjumbe

5. Hadija Mchatta Maggid WEMU - Mjumbe

6. Paulina Jackson Mkoma WEMU - Mjumbe

7. Elia Kalonzo Kibga WEMU - Mjumbe

8. Paulina Mbena Nkwama OWM-TAMISEMI - Mjumbe

9. Makoye J.N. Wangeleja TET - Mjumbe

10.Edward Simon Haule NECTA - Mjumbe

Aidha shukrani zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa TET kwa kugharamia vikao vya kikundi

kazi kupitia huduma ya ukumbi na chakula wakati kikiwa Dar-es-salaam.

Prof. Hamisi O. DihengaKatibu Mkuu

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

www.JamiiF

orums.com

Page 3:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

ii

DIBAJIRipoti hii ya utafiti inahusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato

cha 4 mwaka 2010. Utafiti huu umefanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu-

Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo

ya Ufundi (WEMU) ikihusisha Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani la

Tanzania.

Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa

Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri kwa

wadau wa elimu Serikali iliamua kufanya utafiti ili kuweza kubaini chanzo na ukubwa wa

tatizo. Utafiti huu unatoa mapendekezo kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu na ubora wa

elimu ya sekondari.

Ripoti hii inaonesha kwamba yapo masuala ya kimfumo, mfano mapungufu katika

usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini ambayo yanaweza kutatuliwa na serikali moja

kwa moja. Aidha, yapo masuala yanayohusu kujenga uwezo kwa wasimamizi na

watekelezaji wa mitaala, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora na vya kutosha vya

kufundishia na kujifunzia na uboreshaji wa majengo na miundombinu ambayo

yanahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wabia wake.

Matokeo ya utafiti huu ni muhimu kwa serikali, washirika wa maendeleo na wadau

mbalimbali wa elimu kwani inaonesha chanzo na ukubwa wa matatizo na changamoto

zinazojitokeza na inatoa mapendekezo ya namna ya kuyatatua na kukabiliana na

changamoto za kielimu. Hivyo sote kwa pamoja yatupasa tujipange na kuelekeza nguvu

zetu kupitia mipango yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili tuweze

kuyamaliza matatizo haya na kuinua ubora wa elimu nchini.

Ninawaomba wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza

kupiga hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo

nia ya dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu

ya sekondari nchini.

Mh. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

www.JamiiF

orums.com

Page 4:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

iii

YALIYOMO

SHUKRANI............................................................................................................................................. i

DIBAJI.................................................................................................................................................... ii

VIFUPISHO............................................................................................................................................ v

MUHTASARI PEMBUZI ..................................................................................................................... vi

SURA YA KWANZA: UTANGULIZI................................................................................................ 15

1.1. Usuli ....................................................................................................................................... 151.2. Hoja ya Kufanya Utafiti ....................................................................................................... 181.3. Malengo ya Utafiti................................................................................................................ 191.4. Maswali ya Utafiti................................................................................................................. 191.5. Muundo wa Ripoti ................................................................................................................ 20

SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO.................................................................................... 21

2.1 Sera na Mipango ya Elimu.................................................................................................. 212.2 Mipango na Mikakati ya Elimu ........................................................................................... 222.3 Uongozi katika Elimu ........................................................................................................... 232.4 Usimamizi na Uendeshaji.................................................................................................... 242.5 Ugharamiaji wa Elimu ......................................................................................................... 252.6 Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu........................................................................................ 27

SURA YA TATU: MWONGOZO WA UTAFITI............................................................................... 55

3.1. Utangulizi .............................................................................................................................. 553.2. Mbinu ya Utafiti .................................................................................................................... 553.3. Eneo la Utafiti ....................................................................................................................... 563.4. Uchaguzi wa Sampuli .......................................................................................................... 563.5. Zana za Utafiti ...................................................................................................................... 573.6. Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti ................................................................................ 58

3.6.1. Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya Taifa ................................................................ 583.6.2. Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na Halmashauri .......................... 583.6.3. Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika Jamii ................................................. 59

3.7. Uchambuzi wa Data............................................................................................................. 593.8. Maadili ya Kufanya Utafiti ................................................................................................... 59

SURA YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA DATA................................... 61

4.1. Utangulizi .............................................................................................................................. 614.2. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu .................................................................................. 63

4.2.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali................................. 634.2.2. Mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii...................................................................... 684.2.3. Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu ........................................................................ 694.2.4. Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya Kielimu....................................................... 694.2.5. Ufinyu wa Bajeti ya Elimu ........................................................................................... 704.2.6. Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................. 714.2.7. Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka 2010 75

4.3. Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala ............................................................................. 764.3.1. Utayarishaji wa Mitaala................................................................................................ 76

www.JamiiF

orums.com

Page 5:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

iv

4.3.2. Uwepo wa Mihtasari Shuleni na Vyuoni .................................................................... 774.3.3. Utekelezaji wa Mtaala .................................................................................................. 784.3.4. Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala Ulioboreshwa ............................................... 794.3.5. Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala ........................................................................ 79

4.4. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa........................................................................... 804.4.1. Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 ....................................................... 804.4.2. Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4.......................... 824.4.3. Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4 .................................................. 834.4.4. Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-CA) Katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4................................................................................ 854.4.5. Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTA ....................................................... 864.4.6. Matumizi ya Miongozo na Nyaraka Mitihani ............................................................. 884.4.7. Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2............................................................ 884.4.8. Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa ......................................... 90

4.5. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ................................................... 934.6. Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu............................................................... 97

4.6.1. Mfumo wa Utayarishaji wa Walimu............................................................................... 974.6.2. Ajira na Upangaji wa Walimu ..................................................................................... 984.6.3. Uwepo wa Walimu katika Shule .................................................................................. 1004.6.4. Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa Walimu .............................................. 106

4.7. Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia ........................................................ 108

SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO .................................................................. 115

5.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................................................ 1155.2. Utekelezaji wa mitaala ...................................................................................................... 1185.3. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa......................................................................... 1195.4. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ................................................. 1215.5. Mfumo wa utayarishaji wa walimu.................................................................................. 1215.6. Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia .......................................................................... 124

REJEA ................................................................................................................................................ 126

VIAMBATISHO ................................................................................................................................ 130

Kiambatisho Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti ...................................................... 130Kiambatisho 3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa ........................................... 132Kiambatisho 4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika Halmashauri zilizofanyiwa utafiti....................................................................................................................... 133

www.JamiiF

orums.com

Page 6:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

v

VIFUPISHOBEST Basic Education Statistics in Tanzania CA Continuous Assessment (Mazoezi Endelezi) CG Capitation Grant CDTI Community Development Training InstituteCWT Chama cha Walimu Tanzania EFA Education for All EMAC Educational Materials Approval Committee ETP Education and Training Policy FDC Folk Development CollegeFTC Full Technician Certificate GBS General Budget Support GDP Gross Domestic Product GER Gross Enrolment Rate MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania MMES Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari MEMK-WSM Mkakati wa Elimu ya Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za Msingi MMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi MMEMWA Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu MoEVT Ministry of Education and Vocational Training MWAKEM Mafunzo ya Walimu Kazini Elimu ya Msingi MTEF Medium Term Expenditure Framework MDGs Milemium Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Milenia) MUCE Mkwawa University College of Education NCDF National Curriculum Development Framework NECTA National Examinations Council of Tanzania OC Other Charges OUT Open University of Tanzania OWM-TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa PETS Public Expenditure Tracking System SEDP Secondary Education Development Programme TAMONGSCO Tanzania Association of Managers of Non Government Schools and Colleges TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TET Taasisi ya Elimu Tanzania TEN/MET Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania TES Tanzania Elimu Supplies TIE Tanzania Institute of Education TSD Teachers Service Department (Idara ya Huduma kwa Walimu) UKIMWI Ukosefu wa Kinga Mwilini URT United Republic of Tanzania TRC Teachers Resource Centre UPE Universal Primary Education (Elimu ya Msingi kwa Wote) WEMU Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

www.JamiiF

orums.com

Page 7:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

vi

MUHTASARI PEMBUZI

Utoaji wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo (ETP) ya

mwaka 1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya

Taifa 2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya

Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu

ilianzishwa. Aidha, Programu za Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na

Sekondari (MMES) zilianzishwa kutekeleza program ya sekta. Mafanikio ya MMEM

yameongeza mahitaji ya upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu la

kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-

2014) imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari.

Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila

mwaka kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na

2010 (50.4%). Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kufanya utafiti ili kubaini sababu

za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo

hilo.

Utafiti huu ulifanyika katika mikoa 11, ikiwa ni mmoja kwa kila Kanda ya Elimu. Aidha,

jumla ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa ikiwa moja iliyofanya

vizuri na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Kwa kila

Halmashauri jumla ya shule sita zikiwemo nne za serikali na mbili zisizo za serikali

zilihusika katika utafiti huu. Jumla ya shule 132 ambapo 88 ni za Serikali na 44 ni

shule zisizo za Serikali zilihusishwa. Pia, ofisi za elimu na ukaguzi wa shule, Taasisi ya

Elimu Tanzania (TET), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), pamoja na baadhi ya

asasi za serikali na zisizo za serikali zilihusishwa. Jumla ya wajibuji 3,894 walilengwa

katika utafiti ambapo washiriki 3,037 sawa na asilimia 80.0% walifikiwa.

Taarifa na takwimu za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Madodoso, Majadiliano ya

Pamoja, Hojaji, maandiko na makala mbalimbali. Uchambuzi wa takwimu umefanyika

kwa kuwasilisha hoja za wajibuji katika namba (asilimia), majedwali na chati ili kuleta

www.JamiiF

orums.com

Page 8:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

vii

taarifa zenye mantiki kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti kuhusu

kushuka kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 2010

yamewasilishwa kama ifuatavyo:-

a) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu

Utafiti umedhihirisha kuwa matatizo yanayohusu usimamizi na uendeshaji

yameathiri ufanisi katika utoaji wa elimu bora nchini. Baadhi ya viongozi wa

elimu huteuliwa bila kuzingatia utaalamu, taaluma, uwajibikaji, uwezo na

uadilifu. Aidha, maamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa elimu hufanyika

kisiasa bila kuzingatia utaalamu na tafiti. Vile vile ufinyu wa bajeti ya Wizara ya

Elimu na TAMISEMI (Elimu) unafanya usimamizi na uendeshaji wa elimu

kutokuwa fanisi.

Utekelezaji wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada na ziada umekuwa na

changamoto ambazo zimeathiri uchapishaji, usambazaji na upatikanaji wa vitabu

vyenye ithibati katika shule na vyuo. Aidha, kuna uelewa mdogo kwa wanafunzi

na walimu katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia na kujifunzia

katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu.

Utafiti umebaini kuwa, mmomonyoko wa maadili kama vile matumizi ya lugha

mbaya; matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),

kutozingatia mafundisho ya dini, matumizi ya dawa za kulevya na kujiingiza

katika masuala ya mapenzi ni masuala yaliyobainishwa kuchangia kumeathiri

maendeleo ya taaluma shuleni.

b) Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala

Utafiti umeonesha kuwepo kwa changamoto za utayarishaji na utekelezaji wa

mtaala kwa miaka mitano iliyopita. Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005

umetekelezwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Aidha, utafiti umebaini kuwa

kwa miaka mitatu iliyopita (2008 hadi 2010), jumla ya walimu 588 (1.5%)

walipata mafunzo kabilishi. Taarifa hii inaonesha kuwa walimu wengi hawana

maarifa na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari uliboreshwa.

www.JamiiF

orums.com

Page 9:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

viii

Ni muhimu watekelezaji mitaala kupatiwa mafunzo kabilishi ili kuimarisha

utendaji kazi wao na kuwawezesha kupata fursa ya mabadiliko ya mtaala, dhana

na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji.

Pia, utafiti umebaini upungufu wa mihtasari ya mtaala ulioboreshwa katika shule

za sekondari. Katika shule zilizofanyiwa utafiti, takwimu zinaonesha kuwa kuna

upungufu wa mihtasari kwa wastani wa asilimia 45.4 ambapo masomo ya

Mathematics na Geography yameongoza kwa kuwa na upungufu wa zaidi ya

asilimia 50. Vilevile, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka

TET kwenda shuleni.

c) Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu

Utafiti huu ulilenga Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya

utoaji wa elimu, utekelezaji wa mtaala na ukaguzi wa shule.

Utafiti ulibaini kuwa asilimia 49 ya wakuu wa shule hawafuatilii kikamilifu utoaji

wa taaluma shuleni, hali hii inapunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.

Hivyo inapaswa wakuu wa shule wasimamie kikamilifu majukumu yao kama

ilivyoainishwa katika Mwongozo wa Usimamizi wa Shule.

Aidha, ilibainika kuwa hakuna ufuatiliaji wala tathmini iliyofanyika tangu mtaala

wa elimu ya sekondari ulioboreshwa uanze kutumika mwaka 2005 na kwamba

mitaala hiyo haikufanyiwa majaribio kabla ya utekelezaji wake. Kutofanya

tathmini kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa serikali na

wadau wa elimu kubaini matatizo na changamoto za utoaji elimu na kuyapatia

ufumbuzi kwa wakati na hivyo kupunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji

Pia utafiti umebaini kuwa, katika shule 132 zilizotembelewa, shule 18 (13.53%)

zilikaguliwa mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Hali kadhalika

shule 6 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na shule 46 (34.59%)

hazikukaguliwa kabisa. Aidha, taarifa za ukaguzi wa shule hazifanyiwi kazi

ipasavyo. Kutokaguliwa kwa shule hizo za sekondari kumepunguza ufanisi wa

usimamizi na utoaji wa elimu bora.

www.JamiiF

orums.com

Page 10:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

ix

d) Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu

Ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa huchangiwa na sababu mbalimbali.

Uwepo wa walimu wenye sifa stahiki shuleni ni moja ya sababu muhimu.

Utafiti umebaini kuwa, sifa za udahili kwa walimu tarajali wa stashahada ni za

ufaulu wa kiwango cha chini (1Principal na 1Subsdiary) katika masomo ya

kufundishia na baadhi yao hawana wito wa kazi ya ualimu. Aidha utafiti umebaini

kuwa kuna changamoto katika matayarisho ya walimu tarajali unaosababishwa

na upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu

kimasomo hususani katika masomo ya sayansi na Mathematics unaosababishwa

pia na upangaji usiozingatia mahitaji hususan katika sehemu zenye mazingira

magumu. Katika shule zilizofanyiwa utafiti imebainika kuwa somo la

Mathematics, lina mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo

kuna upungufu wa walimu 264 sawa na asilimia 60.6. Tatizo la upungufu wa

walimu ni changamoto katika utoaji wa elimu.

e) Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa

Matokeo mbalimbali yahusuyo mfumo wa mitihani yamebainishwa ikiwa ni

pamoja na muundo wa maswali yatolewayo shuleni kutokidhi viwango

vinavyotumika na NECTA.

Aidha, Miundo ya mitihani ya Taifa haiwafikii baadhi ya walimu na wanafunzi na

hivyo kutoielewa. Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi

hawapati fursa ya kuiona na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika

shule za sekondari. Uwepo wa Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani

katika shule ni muhimu katika kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote

wanapaswa kupata na kutumia machapisho hayo.

Utafiti umebaini kuwa, uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule haufanywi

kwa makini. Aidha, utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’

walizosahihisha badala ya posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji

www.JamiiF

orums.com

Page 11:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

x

kwa siku ni baadhi ya masuala yanaweza kuchangia kupungua kwa umakini wa

usahihishaji.

Aidha utafiti umebaini kuwa, mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45%

majaribio na mazoezi na 5% projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au

mchakato wake katika matokeo ya mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu.

Hata hivyo NECTA wanatumia vigezo vingine vya ulinganifu sanifu ambavyo

mchakato wake wa kuvitumia haueleweki kwa wadau. Aidha utafiti umebaini

kuwa, gredi zinazotumika shuleni kwa uzoefu wa miaka mingi ni A (81-100), B

(61-80), C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa

alama za gredi zinazotumika kwa Mtihani wa Taifa wa K4 huamuliwa na Kamati

ya Kutunuku ambapo gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si chini ya alama

70. Hali hii ya kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu baina ya shule

na NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama za gredi. Vilevile, kuna

mapungufu ya kuadhibu watahiniwa kwa kuteremshwa daraja la I au la II kuwa

la III kutokana na kufeli baadhi ya masomo ya msingi na ya mchepuo.

f) Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

Utafiti umebaini kuwa katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti, kuna upungufu mkubwa

wa miundombinu, samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni ikijumuisha

maabara ya Chemistry (79.6%), Biology (66%) na Physics (65.2%) nyumba za

walimu (72%), na maktaba (80.6%). Aidha, baadhi ya shule zimepata usajili bila

kutimiza vigezo na nyingine kujengwa mbali na makazi ya jamii husika. Vilevile

utafiti umebaini upungufu wa vifaa vya kufundishia ikiwa ni pamoja na vitabu vya

kiada na ziada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa kwa baadhi ya masomo

kwa wastani wa 75.5% katika shule zilizofanyiwa utafiti.

Matokeo ya utafiti pia yamebaini kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa

wanafunzi katika shule za kutwa, na hivyo kuathiri mahudhurio na umakini wa

wanafunzi katika ujifunzaji.

Hali hii ya upungufu wa miundombinu, upatikanaji wa vitabu vinavyoendana na

mihtasari iliyoboreshwa na kutokuwepo kwa chakula cha mchana ni changamoto

ambazo zinaathiri utekelezaji wa mitaala shuleni.

www.JamiiF

orums.com

Page 12:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

xi

Mapendekezo

Kutokana na taarifa za utafiti kuna mapungufu na changamoto mbalimbali zilizoathiri

kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 mwaka 2010. Mapendekezo

muhimu yametolewa ambayo yanaweza kutekelezwa kwa muda mfupi, kati na mrefu.

1. Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,

uadilifu na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na

zisikaimishwe kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;

2. Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,

tathmini na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya

utoaji wa elimu;

3. Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili kutatua

changamoto zilizopo;

4. Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)

kianzishwe kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji

na haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa

inakidhi malengo yaliyokusudiwa; Utaratibu wa motisha kwa walimu

unaoendana na uzito wa kazi, wadhifa na ugumu wa mazingira anapofanyia kazi

uandaliwe na utekelezwe ipasavyo;

5. Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya

mitihani ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza

kitaaluma na kitaalamu;

6. Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA vipanuliwe ili kuwawezesha wahitimu wa

kidato cha 4 wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na

stadi za kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri;

7. Walimu wenye sifa wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji katika shule

zote. Pia, Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule

ziandaliwe;

www.JamiiF

orums.com

Page 13:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

xii

8. Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa

ufundishaji na ujifunzaji yaimarishwe.

9. Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo

vinavyotakiwa;

10.Walimu wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia

pia alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kama

ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi;

11.Utungaji na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala

inayotekelezwa

12.Adhabu katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III

baada ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila

mtahiniwa apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake;

13.Hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja

wanafunzi. Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada

(Remedial)

14.Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika

kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki

kwa watahiniwa;

15.Wasahihishaji wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu kwa sababu ni

haki ya mwajiriwa wa serikali;

16.Mafunzo kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na

kutekelezwa kwa walimu na wakaguzi wote. Aidha Mafunzo maalumu kuhusu

dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na kutekelezwa kwa maafisa

mitaala na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo;

17.Mihtasari ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft

copy) ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na

Mafunzo ya Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi;

www.JamiiF

orums.com

Page 14:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

xiii

18.Jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili

kubaini dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki;

19.Taratibu za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya

utafiti, tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake.

20.Fedha za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na

kujifunzia shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo. Vilevile, Hosteli/mabweni na

nyumba za walimu zijengwe kwenye shule za sekondari zilizo mbali na makazi

ya watu, na wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha

mchana;

21.Sifa za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada

zipandishwe kuwa Principal mbili za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha

mwalimu kuwa mahiri kitaaluma;

22.Vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa

miundombinu ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na

ongezo la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa. Wakufunzi na wahadhiri

wapewe mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi (Competence Based

Curriculum);

23.Maabara ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na

kuimarishwa katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali

watatumia kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na

kuandika. Pia Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa

walimu wa masomo yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za

sekondari;

24.Utaratibu maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post

Graduate Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili

kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi;

25.Ukaguzi wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa

kupatiwa nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia;

www.JamiiF

orums.com

Page 15:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

xiv

26.Ufuatialiaji wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada

pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe;

27.Sheria ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo

na ithibati katika shule nchini.

www.JamiiF

orums.com

Page 16:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

15

SURA YA KWANZA: UTANGULIZI1.1. Usuli

Utoaji wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka

1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya Taifa

2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya

Maendeleo ya Milenia (MDGs). Aidha, utekelezaji wa será hiyo unaenda sambamba na

utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama ya Mapinduzi ya mwaka 2010.

Katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya

Elimu ilianzishwa 1997 na kuhuhishwa 2001 na 2008. Aidha, Programu za Mipango ya

Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Sekondari (MMES) zilianzishwa kutekeleza

program ya sekta. Mafanikio ya MMEM (2002-2006) na MMEM II (2007-2011)

yameongeza mahitaji ya upanuzi wa Elimu ya Sekondari, ambapo Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu

la kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-

2014) imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari. Mafanikio

hayo yalihitaji dhamira kubwa ya uwekezaji katika elimu ambapo Serikali imetoa

mgawo mkubwa wa fedha za umma. Aidha, wazazi, jamii, na wahisani wana mchango

mkubwa katika utoaji wa elimu nchini na kuifanya Tanzania iwe mbele ya muda wa

kuyatekeleza na kuyafikia malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yanayohusu

upatikanaji wa elimu kwa usawa wa kijinsia.

Mantiki ya elimu ni kumsaidia kila mtoto kukuza maarifa, stadi na mielekeo ili aweze

kuishi maisha yenye ustawi duniani kwa kumsaidia kuanza kujua kusoma na kufanya

hesabu na stadi ambazo zinaweka msingi wa uwezo wa kudadisi, kufikiri, kusikiliza,

kuuliza maswali, kuchambua, kupambanua na kuwasiliana kwa kujiamini (UWEZO,

2010). Stadi hizi na maendeleo ya mwanafunzi yanapimwa wakati wa mchakato wa

ufundishaji na ujifunzaji wa somo husika ambapo mazoezi na mitihani anuai hutolewa

na walimu. Wakati mwingine, upimaji hufanyika baada ya mchakato wa ufundishaji na

ujifunzaji nje ya darasa.

www.JamiiF

orums.com

Page 17:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

16

Mitihani ni nyenzo mojawapo inayotumika katika upimaji ambayo hufanyika kwa

nyakati mbalimbali kama vile robo, nusu au mwisho wa muhula na wakati wa kuhitimu

ngazi ya elimu husika. Mitihani ya ndani katika ngazi ya Elimu ya Msingi, Sekondari na

Vyuo vya ualimu hutolewa na taasisi husika. Aidha ipo mitihani ya kitaifa ambayo ni

Mitihani ya Darasa la IV na VII (Msingi), Mitihani ya Kidato cha 2, 4 na 6 (Sekondari)

na Mitihani ya Cheti na Stashahada (Vyuo vya Ualimu). Mitihani ya Darasa la IV

huendeshwa na Idara ya Elimu ya Msingi ya WEMU na ya kidato cha 2 huendeshwa

na Idara ya Ukaguzi wa Shule. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) inahusika na

uendeshaji wa Mitihani ya Darasa la VII (Msingi), Kidato cha 4 na 6 (Sekondari) na

Mitihani ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada.

Mtihani wa Taifa wa Darasa la IV ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi

katika kupima ufahamu na kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Mtihani huu hutumiwa kutathmini maendeleo ya mwanafunzi kwa kipindi cha miaka

minne ya kwanza ya Elimu ya Msingi. Aidha, Mtihani wa Darasa la VII hutumika

kuthibitisha kuhitimu kwa mwanafunzi katika ngazi ya Elimu ya Msingi na hutumiwa

kufanya maamuzi ya uchaguzi wa mwanafunzi kuendelea na Elimu ya Sekondari na

mafunzo ya fani mbalimbali.

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya

mwanafunzi. Mtihani huu hutumiwa kutathimini maendeleo ya mwanafunzi kwa

kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya elimu ya sekondari. Aidha, mtihani huu ni

sehemu ya mazoezi endelezi (Continuous Assessment-CA), hivyo huchangia katika

matokeo ya mwanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 (Waraka wa Elimu

Na. 5, 1999).

Mitihani ya Taifa ya Kidato cha 4 na 6 inathibitisha kuhitimu kwa mwanafunzi katika

ngazi za elimu ya sekondari ya kawaida (Ordinary Level) na juu (Advanced Level).

Matokeo ya mitihani hii hutumiwa kufanya maamuzi ya uchaguzi wa wanafunzi

kuendelea na mfumo rasmi wa elimu kwa ngazi inayofuata, mafunzo ya fani

mbalimbali na ajira. Mitihani hii inalenga katika kupima ubora wa elimu itolewayo na

matokeo yake ni kiashiria cha ubora huo.

www.JamiiF

orums.com

Page 18:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

17

Mwaka 2005 na 2007 mtaala wa elimu ya sekondari uliboreshwa kutoka mtaala

unaozingatia maudhui (Content Based Curriculum) na kuwa mtaala unaozingatia ujuzi

(Competence Based Curriculum). Tofauti na mtaala unaozingatia maudhui, mtaala

unaozingatia ujuzi upimaji wake ni wenye kumjali mwanafunzi kwa kuzingatia usawia

katika maeneo makuu matatu ambayo ni maarifa (knowledge), mwelekeo (attitudes)

na stadi (skills). Aidha, upimaji huu pia huzingatia uelewa wa wanafunzi katika dhana

(nadharia), vitendo na mtazamo.

Zana zinazotumika wakati wa upimaji ni pamoja na mazoezi ya darasani, majaribio,

mitihani, vitendo (practicals) na projekti. Mwongozo wa NECTA wa Mazoezi Endelezi

(NECTA: 1990) unafafanua kuwa ufaulu wa mwanafunzi utapimwa kwa kutumia

alama za mazoezi endelezi na alama za Projekti ambazo zitajumuishwa kuchangia

asilimia 50 kwenye alama ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4.

Kiwango cha ufaulu kwa Mitihani ya Taifa ya Darasa la VII, Kidato cha 2 na 4

kinaonesha kuendelea kushuka katika ngazi za Elimu ya Msingi na Sekondari tangu

mwaka 2007 toka asilimia 70.48 mwaka 2006 hadi 53.55 mwaka 2010 kwa ngazi ya

elimu ya msingi, asilimia 91.9 mwaka 2007 hadi asilimia 61.8 mwaka 2010 kwa

Mtihani wa Kidato cha 2 na asilimia 90.3 mwaka 2007 hadi asilimia 50.4 mwaka 2010

Mtihani wa Kidato cha 4 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na.1.1.

Jedwali Na. 1.1 Kiwango cha Ufaulu Mitihani wa Darasa la VII, Kidato cha 2 na Kidato cha 4 (%) Mwaka 2006 – 2010

Mtihani 2006 2007 2008 2009 2010

Darasa la VII 70.48 54.18 52.73 49.41 53.55

Kidato cha 2 76.2 91.9 73.5 65.3 61.8

Kidato cha 4 89.12 90.3 83.6 72.5 50.4

Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results Statistics 2007-2010, WEMU, 2010.

Pamoja na kushuka kwa ufaulu wa jumla katika Mtihani wa Taifa ya Kidato cha 4, vile

vile ufaulu umeshuka katika baadhi ya masomo kama vile Mathematics na English

Language kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.2.

www.JamiiF

orums.com

Page 19:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

18

Jedwali Na. 1.2: Kiwango cha Ufaulu (%) Kidato cha 4 kwa Masomo ya Mathematics na English Language 2006 – 2010

Somo 2006 2007 2008 2009 2010

Mathematics 23.67 31.32 24.33 17.78 16.09

English 80.98 75.54 63.23 60.03 30.33

Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results Statistics 2007-2010

Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 yameonesha kuwa

kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 39.9 toka mwaka 2007. Matokeo hayo

pia yanaonesha idadi ya watahiniwa ambao hawakufaulu ni asilimia 49.60.

1.2. Hoja ya Kufanya Utafiti

Kitaalamu, mitihani ni nyenzo itumikayo kupima kiwango cha ujuzi ambacho

mwanafunzi amekipata. Mtihani unalenga katika kupima uelewa wa wanafunzi kwa

elimu itolewayo na matokeo yake ni kiashiria cha ubora huo. Kiwango cha ufaulu wa

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka mfululizo kwa miaka minne

tangu 2007 (Jedwali Na.1.1). Hali hii imejitokeza pia kwa matokeo ya mitihani ya

Darasa la IV, Kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la VII) na ile ya Elimu ya Sekondari ya

Kidato cha 2. Athari ya matokeo mabaya katika mitihani ya kuhitimu ni kuwa na jamii

ambayo haina elimu ya kiwango kilichokusudiwa kitaifa.

Kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 kumekuwa

tofauti na matarajio ya Serikali na wadau wengine wa elimu na hivyo kuibua hoja

mbalimbali juu ya sababu zilizochangia hali hiyo. Jamii ya Watanzania kwa ujumla

ingependa kujua hali halisi kuhusu kushuka kwa ufaulu. Hivyo, Serikali kwa kupitia

WEMU na OWM-TAMISEMI ikaona ni muhimu kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini

kiini cha tatizo.

Utafiti huu umefanyika kwa matarajio ya kuibua mambo yaliyosababisha kushuka kwa

ufaulu ikiwa ni pamoja na kubaini uzito na upeo wa matatizo yaliyojitokeza. Matokeo

ya utafiti huu yatatumiwa na Serikali na wadau wa elimu katika kufanya maamuzi na

kuchukua hatua stahiki za kuinua kiwango cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa

www.JamiiF

orums.com

Page 20:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

19

Kidato cha 4. Utafiti huu unatoa mwelekeo sahihi kwa Serikali ili kupata ufumbuzi wa

changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu.

1.3. Malengo ya Utafiti

1.3.1.Lengo Kuu

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu ili

kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo la kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa

Kidato cha 4 na hatimaye kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari nchini.

1.3.2. Malengo Mahsusi

Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa:

(i). Kufanya uchambuzi wa kiwango cha ufaulu wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa

wa Kidato cha 4 mwaka 2010;

(ii). Kubaini utoshelevu wa walimu katika shule za sekondari;

(iii). Kuchunguza hali ya mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji;

(iv). Kukusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu wa

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4;

(v). Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu;

(vi). Kuchambua mfumo wa uendeshaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4;

(vii). Kubaini michango ya wadau wa elimu katika usimamizi na uendeshaji wa Elimu

ya Sekondari; na

(viii). Kuchambua mfumo wa utayarishaji wa walimu wa sekondari.

1.4. Maswali ya Utafiti

a) Nini sababu za kushuka kwa ufaulu wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4 mwaka 2010?

b) Je shule zina walimu wenye sifa na wa kutosha katika kutekeleza mtaala?

c) Hali halisi ya mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikoje?

d) Nini maoni ya wadau wa elimu kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu wa Mtihani

wa Taifa wa Kidato cha 4?

e) Nini kifanyike kwa wahitimu waliofeli Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka

2011?

www.JamiiF

orums.com

Page 21:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

20

f) Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu ni wa namna gani?

g) Mfumo wa uendeshaji (utungaji, usambazaji, usimamizi, usahihishaji na

upangaji wa madaraja) Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 ukoje?

h) Alama za mazoezi endelezi (CA) zina mchango gani katika Mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4?

i) Wadau wa elimu wana mchango gani katika usimamizi na uendeshaji wa Elimu

ya Sekondari?

j) Walimu katika Shule za Sekondari wanaandaliwaje?

1.5. Muundo wa Ripoti

Ripoti ya utafiti kuhusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4 mwaka 2010, ina sura tano ambazo zimepangiliwa katika mtiririko

unaoanza na tatizo la utafiti mpaka hitimisho. Kila sura imebeba dhima moja ili

kujenga mtiririko wenye mantiki katika kujibu hoja na maswali ya utafiti.

Sura ya kwanza ya ripoti, imebeba utangulizi wa tatizo la utafiti ambapo usuli wa

tatizo, hoja ya kufanya utafiti, malengo na maswali ya utafiti yameainishwa. Sura ya

pili imeeleza mapitio ya maandiko kuhusu Sera na Mipango ya Elimu, usimamizi na

uendeshaji, ufuatiliaji na tathmini ya elimu, mitaala na utekelezaji, mitihani,

upatikanaji na usambazaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, mazingira ya

kufundishia na kujifunzia na uandaaji na upatikanaji wa walimu.

Mwongozo wa utafiti (Methodolojia) umetolewa katika sura ya tatu na unajumuisha

eneo la utafiti, walengwa wa utafiti, uchaguzi wa sampuli, zana za utafiti, utaratibu wa

kufanya utafiti na uchambuzi wa takwimu. Matokeo ya utafiti na uchambuzi wa

takwimu kulingana na malengo na maswali ya utafiti yamejadiliwa katika sura ya nne.

Taarifa ya utafiti imehitimishwa katika sura ya tano ambapo hitimisho na

mapendekezo muhimu kutokana na matokeo ya utafiti yameainishwa.

www.JamiiF

orums.com

Page 22:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

21

SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO

2.1 Sera na Mipango ya Elimu

Kama ilivyo kwa mataifa yote, Tanzania ina mfumo wake wa elimu tangu ilipopata

uhuru mwaka 1961. Mfumo huo umepitia katika mabadiliko anuai ikiwa ni pamoja na

utoaji wa elimu, mitaala na tathmini na upimaji. Serikali ilifuta Sheria ya Elimu ya

mwaka 1927 na kupitisha Sheria ya Elimu ya mwaka 1962 ili kurekebisha utoaji wa

elimu kwa kuleta usawa na kutoa ubaguzi wa rangi na dini uliokuwepo wakati wa

ukoloni (Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995).

Mwaka 1967, falsafa ya Elimu ya Kujitegemea (Education for Self Reliance) ilianzishwa

ambapo msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye ujenzi wa maarifa, ujuzi na mwelekeo

unaotakiwa katika kujenga jamii inayojitegemea (Nyerere, 1967). Pamoja na mambo

mengine falsafa hiyo ilisisitiza utoaji wa elimu utakaowasaidia wahitimu kushiriki

ipasavyo katika kujenga na kuiletea maendeleo jamii ya Watanzania juu ya masuala

yahusuyo ujenzi wa ari, udadisi na kufanya uchunguzi wa kisayansi, ubunifu, uwezo

wa kutatua matatizo ya kijamii na uwezo wa kujiamini na ushirikiano. Mitaala ya

Tanzania huandaliwa kwa kuzingatia dhana ya falsafa ya elimu ya kujitegemea.

Kati ya mwaka 1967 na 1978, Serikali ilichukua hatua kadhaa na ilitunga sheria

mbalimbali ili kuhalalisha hatua zilizochukuliwa wakati wa azimio la Arusha na Elimu

ya Kujitegemea. Sheria na hatua hizi zilijumuishwa na sheria za elimu za 1969 na

1978; Mpango wa Madaraka Mikoani wa 1972; Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa

Na. 21 ya 1973; Elimu ya Msingi kwa Wote (UPE) na Azimio la Musoma la mwaka

1974; Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Na. 12 ya 1975 na Sheria ya Taasisi

ya Elimu Tanzania Na. 13 ya 1975.

Mwaka 1981, Tume ya Rais ya Elimu iliundwa ili kuchunguza mfumo wa elimu

uliokuwepo na kutoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya lazima yaliyohitajiwa

kufanyika nchini ifikapo mwaka 2000. Mapendekezo mengi yaliyowasilishwa na Tume

mwaka 1982 yalitekelezwa na Serikali ikiwemo upanuzi wa elimu ya sekondari.

www.JamiiF

orums.com

Page 23:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

22

Mwaka 1990, Serikali iliunda Tume Maalumu ya Elimu kuangalia upya mfumo wa

elimu kwa ajili ya Karne ya 21. Mwaka 1992 Tume hii iliwasilisha taarifa serikalini

ambapo mapendekezo yake yalizingatiwa katika kuunda Sera ya Elimu na Mafunzo,

1995.

Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ambayo ipo katika mchakato wa kuhuishwa

ndiyo inayotumika katika utoaji wa elimu nchini. Sera hiyo inatekelezwa na Wizara

zote lakini zilizo muhimu kwa elimu rasmi na elimu ya nje ya mfumo rasmi ni Wizara

ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU), Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na

Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na

Watoto. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo pia unaenda sambamba na Dira ya

Taifa ya Maendeleo 2025, MKUKUTA, Malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo

ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ambapo Serikali imeridhia Mikataba hiyo (SEDP II,

2010).

Elimu ya Sekondari ni kiungo muhimu kati ya Elimu ya Msingi na Elimu ya Juu. Moja

ya malengo ya elimu ya sekondari ni kumwandaa mwanafunzi kwa ajili ya elimu ya

kati, ya juu, ya ufundi na ufundi stadi na kujiunga na ulimwengu wa kazi (Sera ya

Elimu na Mafunzo, 1995).

2.2 Mipango na Mikakati ya Elimu

Serikali ilianzisha Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu mwaka 1997 na

kuifanyia marekebisho mwaka 2001 na 2008 ili kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo

nchini. Ili kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo, ilianzishwa mipango na mikakati

mbalimbali kama vile Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM, 2002-2006)

na awamu ya pili ya MMEM (2007-2011). MMEM ilianzishwa ili kuboresha elimu ya

msingi na kutoa fursa sawa ya elimu kwa watoto wote.

Mafanikio ya MMEM yamesababisha upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango

wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari - MMES awamu ya kwanza, 2004-2009 na

awamu ya pili (2010-2014) unatekelezwa ili kuongeza uandikishaji wa wanafunzi

katika shule za sekondari kwa kuzingatia fursa na usawa. Aidha, MMES II imetoa

kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari, ambapo mpango huu

www.JamiiF

orums.com

Page 24:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

23

umeharakisha utekelezaji wa ibara ya 5.4.2 ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka

1995 inayosisitiza kujenga na angalau shule moja ya sekondari kwa kila Kata nchini.

Idadi ya shule za sekondari (za serikali na zisizo za serikali) imefikia 4,266 mwaka

2010 ukilinganisha na shule 1,745 zilizokuwepo mwaka 2005, ongezeko hili ni sawa

na asilimia 144.5. Mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi

(Kidato cha 1-4) walioandikishwa katika shule za sekondari za kawaida kutoka

wanafunzi 489,942 mwaka 2005 hadi kufikia 1,566,685 mwaka 2010. Vilevile,

kumeimarika kwa vigezo vya kupimia maendeleo ya Elimu kama Gross Enrolment

Ratio (GER) na Net Enrolment Ratio (NER) kutoka asilimia 15.9 na 10.3 mwaka 2005

kufikia asilimia 47.3 na 30.8 mwaka 2010. Mafanikio haya makubwa yamepatikana

kutokana na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, Serikali, Wafadhili pamoja na

wadau wengine mbalimbali wa elimu.

Katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari, MMES awamu ya kwanza ilikuwa na lengo

la kuboresha mtaala ili uendane na mahitaji ya soko la ajira. Maboresho ya mtaala

yalifanyika katika ngazi ya Elimu ya Msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu mwaka

2005 na 2007. MMES pia ilikuwa na lengo la kuongeza ubora wa elimu ya sekondari

kwa kutatua tatizo la upungufu wa walimu na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya

ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia (Updated SEDP, 2007 ).

2.3 Uongozi katika Elimu

Mfumo wowote wa elimu unategemea uongozi na utawala bora ili kufikia malengo

yaliyowekwa. Mbinu nzuri za uongozi ni muhimu kwa ufanisi wa mfumo wa elimu na

mafunzo na asasi zake. Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inabainisha kuwa uongozi

wa Elimu na mafunzo unafanywa na Wizara kadhaa, mashirika ya Umma na mashirika

yasiyo ya kiserikali.

Sheria mbalimbali zilizowezesha wizara na taasisi kubeba wajibu wa elimu na mafunzo

zina uhusiano mdogo na sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978. (Ripoti ya Tume ya

Rais ya Elimu, 1982) Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 1995 ili kujumuisha

maeneo mengine ya elimu na mafunzo, pamoja na uongozi, utawala na fedha.

www.JamiiF

orums.com

Page 25:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

24

Ibara ya 4.3 katika Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa madaraka na

utoaji uamuzi katika uongozi na utawala wa elimu na mafunzo vimebaki kwenye ngazi

ya wizara. Mwaka, 2009 usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari ulihamishiwa

katika serikali za Mitaa. (Waraka wa Elimu Na. 13 wa Mwaka 2009). Usimamizi huu

unaendana na Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) kwamba

‘Wizara zinazo wajibika na elimu na mafunzo zitakasimu madaraka yao ya uongozi na

utawala wa elimu na mafunzo kwa vyombo vya chini vya jamii’.

Viongozi na watawala wa elimu kwenye ngazi za taifa, Mkoa, Halmashauri na asasi

wawe na uzoefu na sifa za juu kitaaluma na kitaalamu na wawe na ujuzi katika

uongozi na utawala wa kielimu. Katika kuimarisha usimamizi na uongozi katika elimu,

utoaji wa mafunzo ya kujenga uwezo umetiliwa mkazo kwa kila ngazi ya elimu

(Updated SEDP, 2007).

2.4 Usimamizi na Uendeshaji

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inashughulika na masuala ya uandaaji wa sera,

mitaala, kuweka viwango, usimamizi wa ubora wa elimu, itolewayo na kufanya

ufuatiliaji na tathmini. Serikali iliamua kugatua majukumu ya usimamizi na uendeshaji

wa shule za sekondari kwenda katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na utekelezaji

wake ulianza rasmi tarehe 1 Julai, 2009. Lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha

huduma ya utoaji wa elimu na kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na wananchi.

Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) imeeleza katika ibara ya 4.3.6 kuwa

‘Bodi na Kamati za asasi za elimu na mafunzo zitawajibika katika uendeshaji, kupanga

maendeleo, nidhamu na fedha za asasi zilizochini ya mamlaka yao’.

Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari (1997) kinaeleza kuwa ‘Bodi ya shule ni

chombo muhimu ambacho kila shule inapaswa kuwa nacho ili kufanikisha lengo la

elimu ya Sekondari nchini. Kwa mujibu wa sheria ya Elimu Na 25 ya mwaka 1978 na

rekebisho lake Na.10 la mwaka 1995. Bodi ya Shule imepewa mamlaka ya kusimamia

uongozi na uendeshaji wa mipango yote ya maendeleo ya shule; kusimamia nidhamu

ya walimu, wanafunzi na masuala ya fedha za shule.

www.JamiiF

orums.com

Page 26:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

25

Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari (1997) kinaelekeza kuwa uongozi na

utawala unaopaswa kuwepo katika kila shule ya sekondari ni Mkuu wa shule, Makamu

Mkuu wa Shule na Mwalimu Mwandamizi Taaluma. Chini ya Mwalimu mwandamizi

Taaluma watakuwepo viongozi wafuatao: Mwalimu Mshauri Mafunzo na Kazi, Wakuu

wa idara za Masomo, Walimu wa Masomo Walimu wa Madarasa na Mwalimu

Mwandamizi Malezi na Utamaduni. Aidha, chini ya Mwalimu Mwandamizi Malezi na

Utamaduni watakuwepo viongozi wafuatao: Mwalimu Mlezi wa nyumba/Hosteli,

Mratibu wa Michezo. Pia shule zitakuwa na Mwalimu Mwandamizi Uzalishaji Mali na

Mwalimu wa Zamu

2.5 Ugharamiaji wa Elimu

Ugharamiaji wa Elimu na Mafunzo nchini kwa ujumla ni jukumu la Serikali. Aidha,

jamii, wazazi/walezi, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wa elimu

huhusishwa katika kugharamia elimu. Serikali pia inapata fedha za nje kwa Washirika

wa Maendeleo kwa ajili ya kugharamia elimu kupitia njia tatu zifuatazo; misaada ya

bajeti (General Budget Support- GBS), Mifuko ya pamoja (Basket funds) na Misaada

ya miradi ya Maendeleo (Direct Project Funds) (Andiko la MMES, 2004). Kwa ajili ya

kupima ufanisi na athari kutokana na rasilimali na matumizi ya fedha za umma,

serikali inatumia mfumo wa matumizi wa muda wa kati (Medium – Term Expenditure

Framework -MTEF).

Ugharamiaji wa elimu umeendelea kuwa mojawapo ya vipaumbele vya serikali.

Asilimia ya Bajeti ya sekta ya elimu kutoka kwenye bajeti kuu ya Taifa imeendelea

kupanda na kushuka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, 2000/01 hadi 2010/11 kama

ilivyobainishwa katika Jedwali Na. 2.1

Jedwali Na 2.1 Mgawo wa Bajeti ya Sekta ya Elimu 2000/01 -2010/11Mwaka wa Fedha

2000

/200

1

2001

/200

2

2002

/200

3

2003

/200

4

2004

/200

5

2005

/200

6

2006

/200

7

2007

/200

8

2008

/200

9

2009

/201

0

2010

/201

1www.Ja

miiForums.c

om

Page 27:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

26

% Sekta ya Elimu katika Bajeti kuu ya Taifa

16.7 22.1 18.8 18.7 15.1 18.8 18.3 18.3 19.8 18.3 18.9

% Sekta ya Elimu katika GDP 2.7 3.6 3.8 4.0 3.6 4.2 5.3 5.3 5.8 6.2 -

Chanzo; URT, 2010 (Basic Education Statistics in Tanzania)-Takwimu za Elimu

Katika kipindi hicho kiwango cha juu cha mgawo wa bajeti ya sekta ya elimu kilifikia

22.1% mwaka wa fedha 2001/02 na kimeendelea kushuka na kufikia 17.6% mwaka

wa fedha 2010/11. Aidha, kiwango kinachotengwa kwenye sekta ya elimu kutoka

kwenye Pato la Taifa (GDP) kimeendelea kuongeza kutoka 2.7% mwaka 2000/2001

na kufikia 6.2%, mwaka 2009/2010 ( (BEST 2010, PETS 2010).

Hata hivyo, mwenendo wa mgawo wa fedha katika sekta ya elimu tangu mwaka wa

fedha 2000/01 hadi 2010/11 unaonesha kuwa asilimia kubwa inaelekezwa kwenye

Elimu ya Msingi, Elimu ya Mfumo usio rasmi na Taasisi nyingine za Elimu na Huduma

Saidizi (62.2%) na kufuatiwa na Ufundi na Elimu ya Juu (26.5%) na kwa upande wa

elimu ya sekondari ni (9.8%) kwa mwaka 2010/11 (BEST 2010).

2.5.1 Upelekaji na Matumizi ya Fedha Shuleni

Shule zote za serikali za msingi na sekondari zinapaswa kupelekewa fedha kupitia

mfumo wa ugawaji fedha za serikali (Government Grants System). Fedha

zinazopokelewa shuleni zimegawanyika katika mafungu mawili; fedha za ruzuku

(Capitation Grants) na fedha za maendeleo (Development Grants). Halmashauri

zinapeleka fedha shuleni kupitia kwenye akaunti za shule yaani Akaunti ya Maendeleo

na Akaunti ya matumizi ya kawaida (School Development and Recurrent Accounts)

ambapo kila shule inapaswa kufungua akaunti hizo kama ilivyoelekezwa katika

Waraka wa Elimu Na 13 wa mwaka, 2009.

Akaunti ya maendeleo inahifadhi fedha zote za maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa

madarasa na maabara; ujenzi wa nyumba za walimu; na vifaa vya kudumu. Akaunti

hii pia inapokea fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali. Akaunti ya matumizi ya

kawaida ni kwa ajili kukusanyia fedha zote zinazohusika na matumizi ya kawaida

(Other Chargies) ya kila siku ya shule pamoja na makusanyo ya ada za wanafunzi.

www.JamiiF

orums.com

Page 28:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

27

Katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES I & II) serikali

inapeleka fedha katika shule za sekondari kutoka Hazina kwa kupitia katika

Halmashauri husika. Miongozo ya fedha za MMES II, 2010 inaelekeza kuwa,

Halmashauri zinapaswa kupeleka fedha za ruzuku katika kila shule ya sekondari kwa

kiwango cha sh. 25,000/= kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Taarifa ya OWM-

TAMISEMI (April, 2011), inafahamisha kuwa mgawo wa fedha za ruzuku zilizopelekwa

kwenye shule za sekondari za Serikali ni Sh. 10,883/= kwa kila mwanafunzi kwa

mwaka.

Mwongozo kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku (SEDP II, 2010), unaeleza kuwa

jumla ya fedha za ruzuku zitakazopelekwa kwenye kila shule, 50% itatumika

kununulia vitabu vya kiada na 50% itatumika kununua vifaa vingine vya kufundishia

na kujifunzia. Matumizi ya fedha hizo yanaidhinishwa na Bodi za shule kutokana na

mpango kazi wa shule uliothibitishwa.

2.6 Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu

2.6.1 Ngazi ya Kitaifa (Wizara na Taasisi zake)

Lengo la ufuatiliaji na tathimini ni kubaini mafanikio na udhaifu na kufanya

marekebisho ili malengo ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo yaliyowekwa

yaweze kufikiwa. Ufuatiliaji na tathimini ya mara kwa mara huimarisha majadiliano

kati ya wadau na kuinua ubora wa matokeo tarajiwa na kuharakisha ukamilishaji wa

shughuli zote zilizokusudiwa katika kutekeleza programu na miradi ya elimu (SEDP II

June, 2010).

Katika mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ya elimu, ipo Seksheni ya Ufuatiliaji na

Tathmini chini ya Idara ya Sera na Mipango ya WEMU. Seksheni ya Ufuatiliaji na

Tathmini inahusika na utoaji wa utaalamu na huduma katika utekelezaji, ufuatiliaji na

tathimini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.

www.JamiiF

orums.com

Page 29:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

28

Programme ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP 2008 - 17) inaeleza ufuatiliaji na

tathimini itafanyika ili kuhakiki utekelezaji wa shughuli kulingana uwepo wa thamani

ya fedha iliyotumika. Aidha, imeelezwa kuwa ufuatiliaji utajikita katika kuweka mkazo

kuangalia ubora wa taarifa za utekelezaji zitakazokusanywa, kuhifadhiwa na

kuchambuliwa. Katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari

(MMES) awamu ya kwanza na awamu ya pili, ufuatiliaji na tathimini ya utekelezji wa

mpango huu unapaswa kufanyika kwa kufuata muundo wa utawala wa WEMU na

OWM-TAMISEMI ili kuzuia mapungufu yoyote yanayoweza kujitokeza wakati wote wa

utekelezaji wake (SEDP II, 2010).

Taarifa za ufuatiliaji na tathmini katika ngazi ya taifa zinathibitisha kuwa ufuatiliaji

umefanyika kikamilifu katika ngazi ya elimu ya msingi, hususan katika utekelezaji wa

MMEM (Education Sector Performance Report, 2008).

2.6.2 Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa

Majukumu ya Sekretariati za Mikoa ni kufuatilia na kutoa ushauri wa kitaalamu na

kusimamia utekelezaji wa MMES katika Halmashuri na shule zote katika mkoa husika.

Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji hushiriki katika kuanzisha shule mpya

pamoja na ufuatiliaji wa usimamizi na uendeshaji wa shule katika Mamlaka zao.

Halmashauri huandaa mipango ya shule ambapo mikoa huratibu mipango hiyo.

Jukumu la Uongozi wa elimu ngazi ya kata ni kuhamasisha jamii katika kuchangia

rasilimali za uendelezaji wa elimu katika maeneo yao. Kwa ujumla Mamlaka hizi,

pamoja na kusimamia uendeshaji wa shule katika maeneo yao, hutakiwa kufuatilia na

kuandaa taarifa za utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo na kuwasilisha taarifa

hizo kwenye OWM-TAMISEMI na WEMU.

2.6.3 Ukaguzi wa Shule

Ukaguzi wa utekelezaji wa mtaala ni jukumu la Idara ya Ukaguzi wa shule. Idara ya

ukaguzi wa shule ipo chini ya WEMU na ilianzishwa rasmi mwaka 1978 (Kiongozi cha

Mkaguzi wa shule, 2006-MoEVT). Majukumu ya Idara ya ukaguzi wa shule ni

kuhakikisha kuwa sera, sheria, kanuni na viwango vya utoaji elimu vilivyowekwa

kitaifa vinatekelezwa na vinazingatiwa ipasavyo katika shule za awali, msingi,

www.JamiiF

orums.com

Page 30:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

29

sekondari na vitengo vya elimu maalumu, vituo vya ufundi stadi, elimu ya watu

wazima na vyuo vya Ualimu (Hotuba ya bajeti ya WEMU 2009/2010 p.43). Imeelezwa

katika Kiongozi cha Mkaguzi wa shule (2006), kuwa Ukaguzi wa shule umegawanyika

katika aina tatu, nazo ni ukaguzi wa jumla wa shule, ukaguzi wa kufuatilia na ukaguzi

maalumu.

Ukaguzi wa jumla ni wa mambo yote yanayohusu shule kama sehemu ya kufundishia

na kujifunzia kulingana na mpango wa jumla wa maendeleo ya shule. Inategemewa

kuwa kila shule itakaguliwa walau mara moja katika kipindi cha miaka mitatu. Katika

ukaguzi wa jumla wa shule kila mkaguzi anatarajiwa kukagua shule 30 (za

sekondari/vyuo au msingi) kwa kila mwaka. Aidha ukaguzi wa kufuatilia una lengo la

kuona kiwango cha utekelezaji wa ushauri uliotolewa katika ukaguzi uliopita na

ukaguzi maalumu unalenga katika kupata taarifa mahsusi kuhusu mambo mbalimbali

ya kielimu. Baada ya ukaguzi, wakaguzi wa shule hujadiliana na walimu kuhusu

mazuri na mapungufu yaliyojitokeza. Ukaguzi wa shule unafuatiwa na uandishi wa

taarifa ambayo inatumwa kwa wadau wa shule husika (Kiongozi cha Mkaguzi wa

Shule, 2006).

Huduma za ukaguzi wa shule hazijatolewa kwa ukamilifu kutokana na upungufu wa

nyenzo za kufanyia kazi pamoja na ufinyu wa rasilimali nyinginezo (Tume ya Rais ya

Elimu, Februari, 1982). Kimsingi imedhihirika kuwa taasisi za elimu ambazo

hukaguliwa mara kwa mara zimekuwa na maendeleo mazuri kitaaluma, kiuongozi,

kinidhamu na kimazingira (Waraka wa Elimu Na. 1 wa mwaka 1998). Aidha, ongezeko

la idadi ya shule za msingi na za sekondari limeongeza mahitaji ya rasilimali watu,

fedha na nyenzo nyingine za kufanyia kazi. Kutokana na hali hiyo, katika taarifa

mbalimbali zikiwemo za Tume ya Kero ya rushwa, Sekta ya Elimu ya Mei, 1997, vikao

vya viongozi wa Wizara ya Elimu na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, ilionekana

kuwa upo umuhimu wa kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule ili iweze kufanya kazi

zake ipasavyo (Waraka wa Elimu Na. 1 wa mwaka 1998).

Kumekuwepo kiwango kidogo cha ukaguzi wa shule na kutotekelezwa maoni ya

taarifa za ukaguzi wa shule. Matokeo ya utafiti kuhusu kushuka kwa kiwango cha

ufaulu wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ya mwaka 2008 (WEMU, 2008)

yamebainisha kuwa Ofisi za Ukaguzi wa Shule zimeshindwa kukagua idadi ya shule

www.JamiiF

orums.com

Page 31:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

30

zilizopangwa kwa kila mwaka. Hali isiyoridhisha ya Ukaguzi wa Jumla wa Shule

(Whole school Inspection) inaoneshwa katika jedwali Na. 2.1

Jedwali Na 2.2 Idadi ya Shule/Taasisi zilizokaguliwa mwaka 2009/10Aina ya Shule/Taasisi Idadi ya

shule/Taasisi (2009)

Maoteo ya idadi ya shule za

kukaguliwa

Idadi ya Shule/Taasisi zilizokaguliwa

Asilimia ya ukaguzi

Shule/Madarasa ya Awali41,154 5,137 2,570 50.0

Shule za Msingi 15,727 6763 3,406 50.4Vituo vya Ufundi 352 151 55 36.4Shule/Madarasa ya Elimu Maalumu 284 115 56 48.7

Vituo vya EWW 15,500 6,187 2,588 41.8Shule za Sekondari 4,102 1,664 1,258 75.6Vyuo vya Ualimu 75 77 27 35.1Chanzo: BEST, 2010

Takwimu za WEMU zinaonesha kuwa kuna jumla ya wakaguzi wa shule za sekondari

116 waliopo katika Kanda na makao makuu, ambapo wanahitajika 252 hivyo kuna

upungufu wa wakaguzi 136 sawa na asilimia 54 (BEST, 2010). Zipo sababu

mbalimbali zinazosababisha Idara ya Ukaguzi wa Shule kushindwa kutekeleza

majukumu yake. Sababu zifuatazo zimebainika kuchangia hali hiyo: Kiasi cha fedha

zinazotengwa/zinazotolewa hazitoshelezi na kutokuwepo kwa vitendeakazi hasa

vyombo vya usafiri. Aidha, imebainika kuwa kuna ufuatiliaji mdogo wa taaluma ngazi

ya Halmashauri na kutotekeleza taarifa za ukaguzi wa shule hali iliyosababisha

kushuka kwa ufaulu katika Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi na sekondari. Sababu

za kutokufuatilia kwa ukamilifu ni pamoja na kukosekana kwa usafiri wa uhakika

(Taarifa ya Utafiti Kuhusu Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Kuhitimu

Elimu ya Msingi, Mwaka 2008: uk. 26).

Idara ya ukaguzi wa shule inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi, ingawa

Serikali imendeelea na jitihada za kuhakikisha kuwa wakaguzi wa shule wanatekeleza

majukumu yao kwa ufanisi. Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali imeanzisha

utaratibu wa ukaguzi wa shule kwa kuzingatia makundi ya ubora ambapo shule zilizo

chini ya kiwango zitakaguliwa mara nyingi zaidi ili kuinua kiwango chake cha ubora.

Kwa mantiki hiyo Idara hii inatakiwa iimarishwe zaidi ili iweze kufuatilia na kuimarisha

www.JamiiF

orums.com

Page 32:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

31

viwango vya ubora wa elimu inayotolewa katika zekta nzima ya elimu. (Taarifa ya

Utafiti Kuhusu Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya

Msingi, Mwaka 2008)

2.6.4 Ngazi ya Shule

Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 na

Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 zinaeleza kuwa shule zote za sekondari

zinatakiwa kusimamiwa na Bodi za Shule ambapo wajumbe wake huteuliwa kwa

kuzingatia kanuni za uteuzi wa Bodi za Shule (The School Board Establishment Order,

1979 na GN. Na. 137 ya 1979). Aidha, kila shule ya sekondari inayo Timu ya

Menejimenti ambayo inaundwa na Mkuu wa Shule, Makamu wa Mkuu wa shule,

Mhasibu wa Shule, Mwalimu Mwandamizi Taaluma na Mwalimu Mwandamizi Nidhamu.

Tafiti za kielimu kuhusu ufaulu wa wanafunzi zinadhihirisha kuwepo uhusiano wa

ufuatiliaji kwa upande mmoja na mafanikio ya shule na kiwango cha ufaulu wa

wanafunzi kwa upande mwingine. Shule zenye mafanikio ni zile ambazo Wakuu wa

shule hufuatilia na kusimamia kwa karibu taaluma na mchakato wa ufundishaji na

ujifunzaji (Taarifa ya Utafiti Kuhusu Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa

Kuhitimu Elimu ya Msingi, Mwaka 2008: uk. 26). Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa, shule

zenye kiwango kidogo cha ufaulu ni zile ambazo kuna kiwango Kidogo cha Ukaguzi

wa Shule na kutotekelezwa maoni ya Taarifa za Ukaguzi wa Shule, kutokuwapo kwa

ufuatiliaji wa mara kwa mara kutoka ngazi ya Halmashauri na pale ambapo jamii

hazijahamasishwa kushiriki kikamilifu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao

shuleni.

Kutokana na changamoto nyingi zinazoikabili Idara ya ukaguzi wa shule, WEMU katika

utaratibu wake wa kuimarisha ukaguzi wa shule, imeandaa Mwongozo wa Usimamizi

wa shule kwa lengo la kuwawezesha wakuu wa shule na waratibu elimu kata, kama

wakaguzi wa ndani na wa karibu na shule, kuzisimamia ziweze kujiletea maendeleo

kitaaluma. Aidha, Wakuu wa Shule wanalo jukumu pia la kufuatilia ufundishaji na

ujifunzaji ndani ya shule kwa kufanya ukaguzi wa ndani wakati wote wa shule. Zaidi

ya hayo, katika ngazi ya shule, Timu za Menejimenti hutoa ushauri kwenye Kamati za

Maendeleo za Kata kuhusu Maendeleo ya ujenzi wa shule. Hivyo, Timu za Menejimenti

www.JamiiF

orums.com

Page 33:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

32

za shule, kwa kushirikiana na Bodi za Shule zina jukumu la kuhakikisha utekelezaji wa

Sera ya Elimu na Mafunzo inatekelezwa kwa ukamilifu na kuandaa taarifa za

utekelezaji za shule na kuziwasilisha kwenye Halmashauri zao (SEDP II, 2010)

2.7 Mtaala na Utekelezaji

Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa kila mfumo wa elimu ni lazima uwe

na mitaala ya shule kukidhi mahitaji ya kielimu katika taifa husika. Mtaala

umegawanyika katika maeneo manne muhimu ambayo ni malengo na madhumuni ya

mtaala; maudhui au mada; vitendo vya kufundishia na kujifunzia; na upimaji au njia

za kupima mafanikio. Aidha, Taasisi ya Elimu ya Tanzania itawajibika kwa maandalizi,

maendeleo, utoaji, ufuatiliaji na tathmini ya mitaala ya elimu ya awali, msingi,

sekondari na ualimu (Sera ya Elimu na Mafunzo 1995, uk. 38-42).

2.7.1: Utayarishaji wa Mitaala

Mitaala huandaliwa na kuendelezwa ili kufikia malengo ya elimu katika ngazi zote na

kuboreshwa ili kukidhi mabadiliko na mahitaji mbalimbali ya jamii husika (TIE, 2008).

Osaki (1996) anaeleza kwamba tokea 1968 hadi 1996, kulikuwa na jitihada ndogo

kwa Taasisi ya Elimu kutafsiri falsafa ya Elimu ya Kujitegemea ya 1967 kwenye

masomo kama Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Pia, maudhui ya msingi katika

mitaala ilibakia ni ile ile bila kuzingatia ubunifu, umakinifu (critical thinking), na udadisi

ambayo imeonesha katika maandiko yaliyotayarishwa na kuanza kutumika bila hata

kupitia katika hatua ya kujaribiwa.

Mwaka 2003, Taasisi ya Elimu Tanzania ilitayarisha Mwongozo wa Ukuzaji Mitaala

(National Curriculum Development Framework-NCDF) (TIE, 2003) kuhusu namna

ambavyo mitaala ya Tanzania inavyotayarishwa na kutekelezwa. Mwongozo huu

ulitayarishwa ili kutumiwa na serikali na wadau wote wa elimu katika utekelezaji wa

mitaala. Aidha kwa elimu ya sekondari, maeneo ya ufundishaji na ujifunzaji katika

mitaala ni Lugha, Maarifa ya jamii, Sayansi, Teknolojia na Hisabati. Pia mwongozo

(NCDF, 2003) umeonesha mchakato/hatua za kufuata wakati wa kuboresha mtaala

ambazo zinajumuisha:-

Kufanya tathmini ya awali (assessment) ya mtaala uliopo;

www.JamiiF

orums.com

Page 34:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

33

Kubadilisha mtaala kwa kuboresha mihtasari, vitabu (kiada na ziada), vifaa;

zana na vifaaa vya masikizi maono;

Kujaribisha mtaala na vifaa vya kufundishia na kufanya maboresho;

Utekelezaji wa mtaala mpya katika shule; na

Ufuatiliaji na tathmini ya mtaala ulioboreshwa.

Mchakato wa kurekebisha mtaala nchini Tanzania hujumuisha kazi ya kufanya utafiti

kwa kushirikisha wataalamu na wadau mbalimbali. Kulingana na maelezo ya Waziri

wa Elimu na Utamaduni (Juni, 2005) na utafiti wa TET wa mwaka 2003-2004,

mchakato wa kurekebisha mtaala ulihusisha washiriki katika ngazi mbalimbali kama

vile: Viongozi wakuu wa kielimu kitaifa; Wanasiasa na watumishi wa serikali;

Wahadhiri wa vyuo vikuu; Wakaguzi wa shule; maafisa mitihani; Walimu wa

sekondari, Wanafunzi; Wanapaneli wa masomo yote; Wakufunzi wa vyuo vya ualimu;

wakuu wa wilaya; Maafisa Elimu wilaya; Wakurugenzi watendaji wa wilaya, manispaa

na majiji; Viongozi wa madhehebu na mashirika ya dini; Viongozi wa mashirika yasiyo

ya kiserikali; na Viongozi wa Taasisi za wenye ulemavu. Wahusika na wadau hawa au

baadhi yao hutumika pia wakati wa kufanya tathmini ya mtaala ili kubaini mapungufu

na mikakati ya kuuboresha.

2.7.2: Uboreshaji wa Mitaala

Mwongozo wa ukuzaji mitaala (NCDF, 2003) unaonesha kwamba kuna mzunguko wa

mtaala (curriculum circle) kwa kila ngazi ya elimu. NCDF Uk.20 unaeleza kwamba

urefu wa mzunguko wa mtaala ni sawa na idadi ya miaka ya kukamilisha ngazi husika

ya elimu, mfano kwa sekondari ni miaka sita. Muda zaidi ya huu unapaswa kupita

kabla ya mtaala husika haujafanyiwa maboresho. Lengo la kubadilisha mitaala ni

kuingiza maarifa mapya ya kielimu na kiteknolojia, kuondoa maudhui na njia za

kufundishia zilizopitwa na wakati ili kukidhi mahitaji ya kitaifa.

Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE, 1991) ilifanya tathmini ya kitaifa kuhusu ubora wa

mitaala ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Ualimu mwaka 1991. Matokeo yalionesha

kwamba mitaala ya masomo ilikuwa na mapungufu katika ngazi za elimu ya msingi,

sekondari na vyuo vya ualimu. Mapungufu yalitokana na kutofikiwa kwa malengo kwa

www.JamiiF

orums.com

Page 35:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

34

sababu ya walimu kutumia njia ya mhadhara katika ufundishaji, kuwepo kwa mada

nyingi za mitaala, upungufu wa walimu, miundombinu, vifaa, vitabu na maabara.

Kufuatana na moduli ya Mtaala wa Sekondari wa Tanzania Bara (Secondary

Education Curriculum for Tanzania Mainland) (TIE, 2008), mitaala ya Tanzania

imebadilishwa na kuboreshwa kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.3

Jedwali Na. 2.3 Miaka ya mabadiriko ya mtaala na sababu zake

Na Mwaka Sababu ya Mabadiliko

1 1963 Kuingiza historia za kimila na fasihi katika elimu.

2 1976 Kukidhi utekelezaji wa dhana ya Elimu ya Kujitegemea

iliyoainishwa katika Azimio la Arusha mwaka 1967.

3 1979 Kuanzisha masomo ya michepuo.

4 1984 Kuingiza masuala ya kijamii

5 1996/1997 Kuingiza elimu ya mazingira na mahitaji ya Taifa na kimataifa

6 2005 na

2007

Mtaala uliboreshwa kwa sababu zifuatazo:

(i) Mtaala wa mwaka 1997 ulikamilisha mzunguko wake wa

kutumika kwa kipindi cha miaka 6 na zaidi;

(ii) Kuzingatia matakwa ya sera na programu za kielimu;

(iii) Kuzingatia matakwa ya soko huria kama vile ajira

katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi;

(iv) Mapendekezo ya tafiti za kielimu;

(v) Mahitaji ya Sayansi na Teknolojia;

(vi) Mahitaji na matakwa ya jamii kwa sasa; na

(vii) Kuingiza masuala Mtambuko.

Chanzo: Unit One: The revised O-level and A-level secondary education Curriculum

(TIE, 2008).

Maeneo yaliyoboreshwa katika mtaala wa shule za sekondari mwaka 2005 na 2007

yamezingatia Ujuzi (competences) katika ufundishaji na ujifunzaji; Njia na mbinu

shirikishi zinazomjali mwanafunzi na zinazomjengea ujuzi; Upimaji wenye kumjali

mwanafunzi; Kutorudia mada/maudhui yanayofanana katika masomo tofauti;

www.JamiiF

orums.com

Page 36:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

35

Kuanzishwa kwa somo jipya la TEHAMA; na kuongezwa mada za masuala mtambuko;

Mpangilio na mtiririko wa maudhui katika ngazi tofauti na ufaraguzi (improvisation) wa

zana za kufundishia na kujifunzia.

2.7.3: Mafunzo Kabilishi (Orientation) ya Mtaala

Mafunzo kabilishi ya mitaala iliyoboreshwa hutolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa

walimu na wadau wengine ili kufanikisha utekelezaji wa mitaala katika shule na vyuo.

(TET, Februari, 2011). Taarifa ya TET, (2011) katika kipindi cha mwaka 2007 hadi

2010 inaonesha kuwa mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa yalitolewa kwa

walimu 833 wa shule za sekondari zisizo za serikali katika mikoa ya Dar es Salaam,

Tanga na Dodoma. Aidha taarifa hiyo inaeleza TET ilitoa mafunzo kabilishi kwa

walimu 40 wa shule za sekondari za serikali mwezi Februari 2011 katika mikoa ya

Mwanza, Mtwara, Iringa, na Arusha ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo

ya Sayansi, Hisabati na Lugha.

Aidha, mwaka 2010, mafunzo ya wakufunzi wa vyuo vya ualimu wa ngazi ya

stashahada yalitolewa kwa wakufunzi 72 juu ya utekelezaji wa mitaala iliyorekebishwa

na matumizi ya mbinu shirikishi. Pia, mwaka 2010, kulikuwa na mafunzo kwa washiriki

12 (wakuza mitaala saba, Afisa wa WEMU mmoja, ADEM wawili, na TEWW wawili),

yaliyohusu matumizi ya TEHAMA katika kujenga ujuzi wa kutengeneza maudhui ya

kielektroniki kwa masomo ya sekondari. Utafiti uliofanywa na Meena (2009),

unathibitisha kuwa mafunzo kabilishi yanapewa umuhimu mdogo kwa kusema

“Serikali imeweka uzito mdogo kwenye elimu ya mafunzo kabilishi ya walimu

na kwamba walimu wanahitaji kujifunza kuhusu mitaala wakiwa kazini kwa

kuzifanya shule ziwe ‘taasisi za kujifunzia’”

2.7.4: Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji Mitaala

2.7.4.1: Tathmini ya Utekelezaji Mitaala

Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE- Secondary Education Curriculum for Tanzania

Mainland, 2008) inaeleza misingi na taratibu ambazo tathmini ya mitaala hufanyika

nchini Tanzania. TET inaeleza kwamba mitaala inatakiwa kufanyiwa tathmini katika

hatua mbalimbali wakati wa utekelezaji ili kubainisha mafanikio, mapungufu na

www.JamiiF

orums.com

Page 37:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

36

changamoto. Inasisitizwa kwamba ni muhimu TET ikafanya ufuatiliaji na tathmini ya

utekelezaji wa mtaala ipasavyo kwa nia ya kubaini matatizo yanayojitokeza.

Tathmini ya mtaala imeelezwa kuwa ni mchakato wa kufanya uchunguzi wa mtaala ili

kupata mrejesho utakaosaidia kutoa maamuzi yatakayopelekea kufanya marekebisho,

maboresho ya mtaala kulingana na malengo ya taifa. Aidha, wanaopaswa kushiriki

katika tathmini ya mtaala ni WEMU, TET, Mashirika yasiyo ya kiserikali,

Asasi/Mashirika ya elimu na wadau wengine. TET (2008) inaeleza zaidi kuwa kuna

aina tatu za tathmini za mitaala. Tathmini ya awali (Situational Evaluation) ambayo

hufanyika kabla ya utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa. Tathmini hii inalenga

kutambua mahitaji yanayohitajika kabla ya kuanza kutekeleza mtaala shuleni.

Tathmini endelezi (Formative Evaluation) hufanyika kwa mpangilio maalum wakati

mtaala unatekelezwa shuleni kwa lengo la kubaini mafanikio, matatizo na mapungufu.

Tathmni hii hufanyika katika ngazi ya taifa, wilaya/mkoa/kanda na katika ngazi ya

shule. Wahusika wakuu ni walimu, maafisa elimu, wakaguzi wa shule, asasi na

wataalamu binafsi.

Tathmini tamati (Summative Evaluation) hufanyika wakati wa mwisho wa mzunguko

wa mtaala (curriculum review circle). Kwa Tanzania tathmini hii inapaswa kufanyika

angalau baada ya miaka minne kwa sekondari ya kawaida (Secondary O-level) na

miaka miwili kwa sekondari ya juu (Secondary A-Level). Tathmini hii hufanyika pia

wakati wowote ikiwa kuna ulazima kutokana na mahitaji ya kijamii, kisiasa,

kimaendeleo, kushuka kwa kiwango kikubwa cha ubora wa elimu, pamoja na

mabadiliko katika Sera ya Elimu nchini.

TET, 2003 inaeleza kuwa katika ngazi ya shule walimu na wanafunzi wanapaswa

kufanyiwa tathmini. Tathmini hii inafanyika kwa mwalimu kujitathmini na kumtathmini

mwanafunzi wake, na pia mwanafunzi kujitathmini na kumtathmini mwalimu wake.

2.8 Mitihani

2.8.1: Mitihani Ngazi ya Shule

www.JamiiF

orums.com

Page 38:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

37

Kwenye kila ngazi ya elimu, hutolewa aina mbalimbali ya mazoezi na mitihani

inayotungwa na mwalimu ili kutosheleza makusudio mbalimbali ya kielimu (URT: ETP,

1995). Mwaka 1976 iliamuliwa kuanza kutumia mazoezi endelezi (Continuous

Assessment) ambapo kila shule huendesha mitihani na majaribio mbalimbali na

kuhifadhi alama za mwanafunzi kulingana na mwongozo wa mazoezi endelezi

uliotolewa na NECTA (NECTA: Guidelines on the Conduct and Administration of

Continuous assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, 1990).

Kulingana na mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi, kuanzia mwaka 1990,

majaribio yatatumika badala ya utaratibu wa awali wa kutumia mazoezi na majaribio

katika mchakato wa kutayarisha alama za mazoezi endelezi. Kwa madhumuni ya

mazoezi endelezi, mwongozo unaelekeza kuwa, kila shule itaandaa jaribio moja kwa

kila mwisho wa muhula, ambapo Baraza la Mitihani linaweza kuhitaji kupatiwa nakala

za majaribio hayo. Ili kukidhi matakwa ya mazoezi endelezi, mwongozo unaelekeza

kuwa kutakuwa na jumla ya majaribio manne katika shule za sekondari ambapo

mtihani wa Kidato cha 2 utakuwa sehemu ya mazoezi endelezi (WEMU: Waraka wa

Elimu Na. 5 1999).

Majaribio mengine ambayo yatakuwa sehemu ya mazoezi endelezi ni yale ya kila

mwisho wa muhula Kidato cha 3 na jaribio la mwisho wa muhula wa kwanza Kidato

cha nne (NECTA: Guidelines on the Conduct and Administration of Continuous

assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, 1990). Wakuu wa

shule wanatakiwa kutunza alama za kila mwanafunzi ambazo zitatakiwa kujazwa

kwenye fomu maalumu ya NECTA kwa madhumuni ya mazoezi endelezi. Imewekwa

wazi katika mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi kuwa, wakuu wa shule

watawasilisha NECTA alama za matokeo ya mtihani wa Kidato cha 2 na alama za

muhula wa kwanza na wa pili Kidato cha 3 na muhula wa kwanza Kidato cha 4 katika

kipindi cha miezi mitatu kabla ya mitihani husika kufanyika.

Katika ngazi ya shule kutakuwepo pia upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi kwa

kutumia Projekti. Kulingana na mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi,

ufundishaji na ujifunzaji pamoja na tathimini ya maendeleo ya taaluma kwa njia ya

projekti, hulazimika kufanyika kutokana na matakwa ya mfumo wa elimu na maamuzi

www.JamiiF

orums.com

Page 39:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

38

ya kisiasa ambayo yamekuwa msingi wa mabadiliko katika mitaala ya shule. NECTA

huhimiza upimaji kwa kutumia Projekti kama njia ya kuimarisha ujifunzaji na kupima

mafanikio katika ujenzi wa uwezo na ujuzi wa wanafunzi (NECTA: Guidelines on the

Conduct and Administration of Continuous assessment in Secondary Schools and

teacher Training Colleges, 1990).

2.8.2: Mitihani ya Taifa

Kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo (URT ETP, 1995 p. 44) sera zifuatazo

zitatumika kuongoza mitihani kwenye ngazi ya kanda na taifa: itakuwepo mitihani ya

kitaifa mwishoni mwa Darasa la VII, Kidato cha 4, Kidato cha 6 na kozi za mafunzo ya

Ualimu za Cheti na Stashahada. Aidha, mitihani ya Darasa la VII, Kidato cha 4 na

Kidato cha 6 itaashiria kuhitimu katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari na

matokeo ya mitihani hii yatatumika kwa uchaguzi wa wanafunzi watakaoendelea na

elimu ya juu na mafunzo zaidi, na pia kwa kutolea cheti cha kuhitimu elimu ya ngazi

inayohusika. Baraza la Mitihani la Tanzania litawajibika kutunga, kudhibiti, kuendesha

na kusimamia mitihani ya taifa ya Darasa la VII, Kidato cha 4 Kidato cha 6 na

mafunzo ya Ualimu ya Cheti na Stashahada (URT: ETP, 1995)

Sera ya Elimu na Mafunzo 1995 imeeleza kuwa, katika ngazi ya elimu ya sekondari,

upo Mtihani wa Taifa wa kidato cha pili ambao hutumiwa kwa kubashiri maendeleo

halisi na kwa ajili ya kupata upimaji wa kuendelea katika elimu ya sekondari ya ngazi

ya kawaida.

2.8.3: Muundo wa Mitihani

Waraka wa Elimu Na. 1 wa mwaka 2006 umefafanua masomo ya msingi na masomo

chaguzi ambayo wanafunzi wanatakiwa kusoma na kufanyia mitihani kwa Kidato cha

4. Aidha, Mwongozo kuhusu muundo wa mitihani, ambao unajumisha masomo yote

yanayotahiniwa unatoa msaada kwa watumiaji na walimu kuhusu taratibu za mitihani

hususani matumizi ya chati ya maelekezo (Table of Specifications) katika kuandaa

mitihani (NECTA, Certificate of secondary Education Examination Format, February,

2008).

www.JamiiF

orums.com

Page 40:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

39

NECTA hupeleka nakala ya mwongozo wa mitihani kwa wakuu wa shule na vituo

vyote vya mitihani ili kusaidia wanafunzi na walimu kujiandaa kwa mitihani. Kulingana

na mwongozo huo, Muundo wa mitihani umegawanyika katika sehemu tano ambazo

ni: utangulizi, malengo ya jumla, ujuzi wa jumla, utaratibu wa mitihani (examination

rubric) na maudhui ya mtihani. Unyeti wa muundo wa mitihani unasaidia watunzi

(examination setters) na warekebishaji (moderators) wa mitihani, walimu na

wanafunzi katika kukabili mahitaji na ukamilishaji wa mtaala pamoja na ufahamu wa

maarifa na ujuzi (NECTA, Certificate of secondary Education Examination Format,

February, 2008).

2.8.4: Uendeshaji wa mitihani

Sera ya Elimu na mafunzo 1995 inafafanua kuwa, Baraza la Mitaihani la Tanzania

litawajibika kutunga, kuthibiti, kuendesha na kusimamia Mitihani ya Taifa ya Darasa la

VII, Kidato cha 4, Kidato cha 6 na Mafunzo ya Ualimu ya Cheti na Stashahada (URT:

ETP, 1995). Aidha NECTA itahusika pia na kutunga, kudhibiti, kuendesha na

kusimamia Mtihani wa Maarifa (Qualifying Test) kwa watahiniwa walio nje ya mfumo

wa shule. NECTA huendesha mitihani katika misimu mitatu ambapo mwezi Oktoba

mitihani ya maarifa na ya Kidato cha 4, mwezi Februari mitihani ya Kidato cha 6 na

mwezi Mei mitihani ya Stashahada na Cheti cha ualimu, stashahada za juu za ufundi

na mwezi Septemba mtihani wa kuhitimu Darasa la VII (NECTA WEBSITE, May 2011,

NECTA: The Examinations Regulations, 2006).

2.8.5: Utungaji

Kulingana na NECTA WEBSITE, May 2001, watungaji wa mitihani wanatakiwa wawe

wamebobea kitaaluma katika masomo husika ambayo yanatahiniwa. Aidha,

wanatakiwa wawe wanafundisha na uzoefu wa kufundisha katika ngazi wanayotahini

kwa muda usiopungua miaka mitatu. Website hiyo inafafanua kuwa, kila mwaka,

Baraza la mitihani la Tanzania hupeleka fomu ya kupata orodha ya watungaji wa

mitihani katika shule zote ambapo wakuu wa shule hutakiwa kutuma taarifa za siri

kuhusu uwezo na uaminifu wa mwalimu katika kutunza siri na kuonesha namana

anavyojituma kazini. Baada ya kupata taarifa za siri za walimu, NECTA huteua walimu

wa kutunga mitihani ambao hutakiwa kuandaa jozi mbili za karatasi za mtihani. Aidha,

barua za uteuzi wa watungaji wa mitihani humwelekeza mtunzi mambo ya kuzingatia

www.JamiiF

orums.com

Page 41:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

40

wakati wa kutunga maswali ya mtihani na pia huambatanishwa na muundo wa

mtihani ili arejee ipasavyo.

Kimsingi watungaji wote ambao wanateuliwa kutunga mitihani wanatakiwa wapatiwe

mfunzo ya msingi na mbinu za uandaji wa maswali mazuri ya mitihni. Hata hivyo

imeonekana kuwa hali hiyo haifanyiki na watungaji wa mitihani hutegemea utaalamu

kama walimu na uzoefu wao kazini (NECTA WEBSITE, May 2011).

Baada ya kupokea karatasi za mitihani kutoka kwa watungaji karatasi hizo hufanyiwa

marekebisho (moderation). Kwa kawaida marekebisho ya karatasi za mitihani

hufanywa na paneli ya watu 2-3 kwa kila somo. Karatasi za mitihani zinaandaliwa

zikionesha maelekezo kwa watahiniwa kuhusu idadi ya maswali wanayotakiwa kujibu

kwa kila somo na alama zinazotolewa kwa kila swali. Kama ilivyo kwa watungaji wa

mitihani, NECTA huteua warekebishaji baada ya kupokea taarifa za siri za walimu hao.

Kwa kawaida, wajumbe wa paneli za kurekebisha masomo ni watunga mitaala,

wakaguzi wa shule, wahadhiri katika vyuo vikuu na au walimu wazoefu ambao

hawashiriki kufundisha watahiniwa kwa wakati huo. NECTA 2011, imeeleza kuwa

warekebishaji wa mitihani hutakiwa kuzingatia kuwa mitihani inalingana na mihtasari

na suala la kuaminika (Reliability) na uhalali (Validity) umezingatiwa wakati wa

kuandaa mitihani. Aidha, wakati wa kurekebisha mithihani, huwasilishwa jozi tatu za

karatasi za mitihani kwa kila somo (NECTA WEBSITE, May 2011).

Baada ya kukamilisha kazi ya kurekebisha karatasi za mitihani, NECTA hurudufisha na

kuiandaa kwa ajili ya kuisambaza kwenye vituo vya mitihani. Website ya NECTA

inaonesha kuwa kazi ya kurudufisha na kuandaa katarasi za mitihani husimamiwa na

Idara ya Chapa na Uchapishaji wa mitihani ambapo jukumu la kuisafirisha mitihani

hiyo kwenda mikoani ni la Idara ya Kusimamia na Kuendesha Mitihani (Departmend of

Examinatios Administration). Aidha, usambazaji wa mitihani hufanyika kwa kutumia

misafara inayotumia barabara, reli, bahari na ndege. Katika hatua hii suala la ulinzi na

usalama wa mitihani hupatiwa umuhimu wa kipekee ambapo vyombo vya usalama

vya serikali hushirikishwa. Misafara kwa njia ya barabara hushirikisha Afisa wa

Mitihani, Askari mwenye siraha, Afisa usalama na dereva kutoka NECTA.

www.JamiiF

orums.com

Page 42:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

41

Kulingana na Website NECTA, misafara ya kupeleka mitihani kutoka ofisi za NECTA

huishia katika makao makuu ya Mikoa ambapo Afisa Mitihani hukabidhi mitihani

kwenye Kamati ya Mitihani ya Mkoa. Mitihani hupokelewa na kuhifadhiwa katika

chumba madhubuti (Strong room) cha mkoa na kulindwa na askari mpaka

itakapopelekwa wilayani.

Kamati ya Mitihani ya Mkoa husafirisha na kukabidhi mitihani kwa Kamati ya Mitihani

ya Wilaya. Kama ilivyo katika mkoa, mitihani inahifadhiwa katika vyumba maalumu

vyenye usalama na vinalindwa na maaskari wenye silaha. Kutoka katika ngazi ya

wilaya, mitihani hukabidhiwa kwa wakuu wa shule na wasimamizi wa nje wa mitihani

(external supervisors) na kuhifadhiwa katika vyumba vyenye usalama katika maeneo

yao na italindwa na askari wenye silaha.

2.8.6: Usahihishaji na Utoaji wa Matokeo

Sera ya Elimu na Mafunzo imeeleza kuwa, kutokana na mitihani kuathiri maisha ya

watu, malalamiko hayatakosekana kuhusu utungaji, uendeshaji, usimamizi,

usahihishaji, uandaaji wa matokeo; upangaji wa madaraja, tuzo pamoja na utoaji

matokeo. Mchakato wa kusahihisha na kutoa matokeo ya watahiniwa umegawanyika

katika hatua tatu ambazo ni: kwenye vituo vya mitinani, kwenye vituo vya usahihishaji

na ofisi za NECTA (NECTA: Examinations Processing, July, 1986).

Karatasi za Mitihani za watahiniwa hupokelewa kutoka kwenye vituo vya mitihani na

kupelekwa kwenye vituo vya usahihishaji na alama za matokeo kupelekwa ofisi za

NECTA kwa maandalizi ya matokeo ya watahiniwa kwa madaraja mbalimbali ili kutoa

matokeo ya watahiniwa (NECTA: Examinations Processing, July, 1986).

Kulingana na taratibu za mitihani za NECTA, katika Vituo vya Mitihani, orodha za

watahiniwa huandaliwa, alama za mazoezi endelezi na projekti huingizwa kwenye

fomu za mazoezi endelezi na majumuisho ya alama za mazoezi hufanyika. Katika vituo

vya usahihishaji, usahihishaji wa karatasi za mitihani za watahiniwa hufanyika kwa

kutumia paneli za masomo na alama za mtihani wa mwisho hukokotolewa kwa

kiwango cha asilimia 50. Katika Ofisi za NECTA, kimsingi, alama za mazoezi endelezi

hukokotolewa na kujumishwa na alama za mtihani wa mwisho ili kupata alama za

matokeo kwa watahiniwa (NECTA: Examinations Processing, July, 1986).

www.JamiiF

orums.com

Page 43:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

42

Kulingana na taratibu za mitihani (NECTA, 1986), matokeo ya mwisho ya mtihani wa

Taifa wa Kidato cha 4 yanatolewa kwa kutumia viwango vya ufaulu (Gredis) A, B, C, D

na F ambapo A-Ubora uliotukuka, B-Vizuri sana, C-Vizuri, D-inaridhisha na F-feli.

Uzito wa ‘gredi’ hizo ni A – 1 (krediti), B – 2 (krediti), C – 3 (krediti), D – 4 (kufaulu),

F – 5 (feli). Uzoefu unaonyesha kuwa Gredi hizi zinatolewa kwa kuzingatia mlolongo

wa alama zifuatazo: A (81-100), B (61-80), C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo

rejea kutoka NECTA (Juni, 2011) zinaeleza kuwa Kamati ya Kutunuku ya NECTA

hubaini viwango vya ushindi katika mwaka husika baada ya kulinganisha viwango vya

ushindi kwa miaka mbalimbali iliyopita ilikilinganishwa na uwezo wa ufaulu wa

watahiniwa wa mwaka husika. Aidha, kulingana na kanuni za kutoa ushindi wa alama

kwa mtihani wowote unaoendeshwa na NECTA, hakuna mtahiniwa yeyote

atakayeweza kupata gredi A katika somo kama atapata alama chini ya 70. Vilevile

hakuna mtahiniwa atakayepata gredi D endapo atapata alama chini ya 30.

Aidha, matokeo yatatolewa kwa kutumia madaja ya ufaulu (Divisions) I, II, III IV na 0

kwa kuzingatia masomo saba yenye ufaulu wa juu ukijumuisha yale ya msingi (core

subjects). Daraja la I (alama 7 – 17), Daraja la II (alama 18 – 20), Daraja la III

(alama 21 – 25) na Daraja la IV (alama 26 – 32). Daraja la 0 (alama 33-35) inaashiria

kufeli.

2.8.7: Mchango wa CA na Project katika Mitihani ya Taifa

Kabla ya mwaka 1976, Tanzania ilitumia mitihani ya mwisho kama njia pekee ya

kupima na kutathimini watahiniwa. Aidha, mfumo uliokuwa unatumika wakati wa

kikoloni ulikosolewa na wadau wa elimu kutokana na kutokuwa thabiti katika kupima

mafanikio ya jumla ya kielimu ya mwanafunzi w Kitanzania. Kwa hiyo, mwaka 1976,

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) lilianzisha mfumo wa kutumia mazoezi

endelezi (Continuous Assessment) kama njia ya kutatua kasoro na mapungufu

yaliyokuwepo katika mfumo wa upimaji uliokuwa unatumia mtihani mmoja wa mwisho

pekee (NECTA: Guidelines on the Conduct and Administration of Continuous

assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, 1990, Lisu, H.S,

2008).

www.JamiiF

orums.com

Page 44:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

43

Kulingana na mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi (NECTA: 1990), ufaulu wa

mwanafunzi utapimwa kwa kutumia alama za mazoezi endelezi (CA) na alama za

Projekti ambazo zitajumuishwa kwenye mtihani wa mwisho Kidato cha 4. Aidha,

Mwongozo umeweka wazi kuwa mchango wa alama za mazoezi endelezi katika tuzo la

mwisho wa elimu ya sekondari Kidato cha 4 ni asilimia 45 na mchango wa Projekti

utakuwa asilimia 5 hivyo, kuwa na jumla ya alama asilimia 50 (NECTA: Examinations

Processing, July, 1986).

Mapitio ya machapisho yanaonesha kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa upimaji

wa kutumia CA, hakuna jitihada za kutosha zilizofanyika katika kuelimisha umma juu

ya mchango wa mazoezi endelezi (CA) katika matokeo ya mwisho ya mtahiniwa.

Aidha, mfumo huo hauoneshi njia zinazotumika katika kuandaa mazoezi hayo ya

darasani na namna gani mazoezi hayo yanasimamiwa na kuchambuliwa (Lisu, H.S,

2008). Taarifa ya utafiti uliofanywa na Lisu, H. S, 2008, inathibitisha kuwa wadau wa

elimu wakiwemo maafisa wa NECTA, walimu, wazazi, na wanafunzi hawajui

kiwango/mchango wa CA katika mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya sekondari.

Taarifa hiyo, pia imeonesha kuwa pamoja na juhudi za NECTA kupeleka vitabu vya

mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi katika kila shule, vijitabu hivyo vilibakia

katika ofisi za taaluma na kuhifadhiwa kama nyaraka za siri na kwa matumizi ya

viongozi wachache tu. Aidha imeoneshwa kuwa alama za mazoezi endelezi zilikuwa

zina tolewa kwa upendeleo kwa baadhi ya wanafunzi. Kutokana na mapitio ya

machapisho imebainika kuwa alama za mazoezi endelezi (CA marks) na alama za

mtihani wa mwisho Kidato cha 4 hazijumulishwi na kutafuta wastani. Mchakato wa

kupata alama ya mwisho ya mtahiniwa inahusisha ukokotoaji wa kiwango sanifu cha

alama (standardization of raw marks) kabla ya kupata alama ya mwisho.

2.9: Upatikanaji na Usambazaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

2.9.1: Vitabu vya Kiada na Ziada

Miaka ya 1980, Shirika la Vifaa vya Elimu yaani “Tanzania elimu Supplies (TES) “chini

ya Wizara ya Elimu na Utamaduni lilikuwa na jukumu la kusambaza vitabu na vifaa

vya shule nchini (Tume ya Rais ya Elimu, 1982). Kuanzia Januari mwaka 1992 Serikali

ilipitisha sera ya upatikanaji na usambazaji wa vitabu vya shule na vyuo nchini

www.JamiiF

orums.com

Page 45:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

44

ambayo ilifuta Waraka no. EDTT/8/184 wa mwaka 1970 uliohusu “Uuzaji wa Vitabu

vya Kiada vinavyotayarishwa na Wizara ya Elimu”. Sera hii ilianzisha utaratibu wa

upatikanaji na usambazaji wa vitabu vya kiada na ziada kufanyika na makampuni ya

kibiashara ya uchapishaji kwa mtindo wa ushindani. Taasisi ya Elimu ilielekezwa

kubaki na majukumu ya ukuzaji mitaala kama lengo la muda mrefu, hii ni pamoja na

serikali kubaki na jukumu la kupitisha vitabu kwa matumizi ya shule na vyuo vya

ualimu.

Utekelezaji wa sera hii uliendana na utayarishaji wa utaratibu wa kuhakiki na kupitisha

vitabu vya kiada vya shule na vyuo kwa kufuata Waraka wa Elimu Na. 2 wa Agosti

1998 uliojulikana kama “New Approval System for Educational Books”. Waraka huu

ulikuwa na lengo la kuhakikisha ubora wa vitabu vitumikavyo shuleni. Mwaka 1998,

Kamati ya kutathimini Machapisho ya Kielimu (Educational Materials Approval

Committee -EMAC) ilianzishwa na Wizara ya Elimu. EMAC ipo chini ya uenyekiti wa

Kamishna wa Elimu na inaundwa na Sekretariati na wataalamu/ walimu mahiri wa

masomo (Book Evaluators). Taarifa ya EMAC (2011) inaeleza kuwa kufikia Aprili 2011

EMAC imetoa idhibati kwa aina za vitabu 248 vya elimu ya sekondari katika lugha ya

Kiingereza, ambapo aina 218 vya kiada na 30 vya ziada. Aidha, ithibati ilitolewa kwa

aina 65 ya vitabu vya sekondari katika lugha ya Kiswahili ikiwa 20 vya kiada na 45 vya

ziada vilivyoandikwa na wandishi tofauti na wachapishaji mbalimbali.

Vitabu vyote vya kiada vilivyopitishwa na EMAC vimeandikwa kufuata mtaala

ulioboreshwa mwaka 2005 na 2007. Shule zinapaswa kununua na kutumia vitabu vya

kiada na ziada vilivyopewa ithibati na EMAC (Miongozo ya MMES II, 2010). Shule

huagiza na kuvinunua kutoka maduka ya vitabu au kampuni za wachapishaji vitabu

moja kwa moja au kwa kuletewa shuleni kutoka makao makuu ya Wizara ya Elimu

kwa kupitia kwa Maafisa Elimu wa mikoa na Wilaya. Mpango wa Elimu ya Sekondari

(SEDP II, June 2010) umeonesha kuwa katika kipindi cha 2004 – 2009 wadau

wamekuwa wakitoa msaada wa vitabu kwa ajili ya shule na maktaba nchini ikiwa ni

pamoja na shirika la USAID lililotoa msaada wa vitabu 456,830, vya shule za

sekondari.

www.JamiiF

orums.com

Page 46:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

45

Kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo 1995, ibara ya 5.4.6, kila shule inapaswa

kuwa na vitabu vya kutosha, maktaba na wakutubi wenye utaalamu. Hata hivyo hali

halisi inaonesha kuwa maktaba za shule ni chache kwani hadi mwaka 2009, ni

maktaba 57 tu zilikuwa zimejengwa kati ya maktaba 2,406 zilizokuwa zimepangwa

kujengwa chini ya mpango wa MMES (SEDP II, 2010).

2.9.2: Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

Ubora wa utoaji wa elimu unaimarishwa na upatikanaji na utumiaji wa zana na vifaa

vya kufundishia na kujifunzia. Vifaa hivi vinajumuisha machapisho (textual materials)

kama vitabu, ramani na chati. Aidha, vifaa vingine ni vile visivyochapishwa (non

textual materials) kama vile tufe, modeli na vifaa vya masikizi na maono.

Sera ya Elimu na Mafunzo (1995, Kifungu 4.5.3) inaelekeza kwamba shule zote za

sekondari zinapaswa kuwa na zana na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia

ambavyo vipo katika idadi inayotosha mahitaji ya shule. Changamoto katika mchakato

wa ufundishaji wa masomo shule za sekondari ni upungufu mkubwa wa vifaa vya

kufundishia na kujifunzia (SEDP II, 2010). Kulingana na Mtaala wa Sekondari kwa

Tanzania Bara uliotayarishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (2008), mwalimu

anatazamiwa kuwa mbunifu wa kutengeneza na kufaragua vifaa vya kufundishia na

kujifunzia kwa kutumia vitu vipatikanavyo katika mazingira ya shule.

2.9.3: Maabara, Vifaa na Madawa ya Maabara

Ufundishaji wa masomo ya Sayansi unazingatia sana vitendo ili wanafunzi wapate

maarifa, stadi na ujuzi unaotakiwa katika mitaala. Maabara za sayansi zilizosheheni

vifaa yakiwemo madawa ndiyo nyenzo muhimu katika kuwezesha ufanyaji wa vitendo

kwa wanafunzi na walimu. Umuhimu huo umesisitizwa katika Sera ya Elimu na

Mafunzo (1995) na Mpango wa Mkakati wa Kati (Medium Term Strategic Plan,

2007/08-2009/10) wa WEMU uliobainisha lengo la kuweka vifaa vya kutosha katika

maabara za sayansi katika shule za sekondari.

www.JamiiF

orums.com

Page 47:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

46

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari

(2008), mahitaji ya maabara za sayansi yalikuwa 9,420 kwa shule 3,140 za sekondari

za serikali. Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 77 ya shule za serikali hazina

maabara za sayansi kama ilivyooneshwa katika jedwali Na.2.4

Jedwali Na 2.4 Hali ya Maabara katika shule za Serikali Tanzani mwaka

2008

Aina ya shuleIdadi ya Shule

Shule zenye Maabara

Hali ya maabara katika shule

Zilizo na Hali nzuri

Zinazohitaji matengenezo Upungufu

Shule za Kitaifa 90 90 - 90 -Shule za Jamii 3,051 639 36 603 2,412Jumla 3,141 729 36 693 2,412Asilimia 100% 23% 1% 22% 77%

Chanzo: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari, Disemba 2008

Kila shule ya sekondari inatakiwa iwe na maabara za masomo ya sayansi. Taarifa za

WEMU kwa mwaka 2010 zinaonesha kuwa Katika shule za sekondari 4,266 za serikali

na zisizo za serikali, kulikuwa na maabara za Baiolojia 670, Kemia 804, Fizikia 760 na

Kompyuta 1,540 hali inayoashiria upungufu wa maabara.

2.10: Mazingira ya Shule

Mazingira ya shule yanahusu jumla ya vitu vyote vilivyopo na vinavyotendeka nje na

ndani ya darasa katika shule. Mazingira hayo, ni pamoja na miundo mbinu, samani

zake na huduma za jamii.

2.10.1: Miundombinu na Huduma za Kijamii

Tume ya Rais (1982) ilibaini ongezeko kubwa la shule bila kuwepo na miundombinu

iliyokamilika. Kutokana na hali hii, Tume hiyo ilipendekeza kuwepo kwa kitabu cha

Mwongozo kitakachosaidia viongozi kuwa na msimamo mmoja kuhusu aina ya

majengo, madarasa na vitu vingine vya lazima kwenye shule za msingi, sekondari na

vyuo vya ualimu.

www.JamiiF

orums.com

Page 48:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

47

Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inabaini pia ongezeko la shule kutokana na

misukumo ya kisiasa au kwa ushindani miongoni mwa wazazi, mashirika yasiyo ya

kiserikali au uongozi katika wilaya na kusajili shule bila kuzingatia mahitaji ya kiwango

cha chini kilichowekwa kwa ajili ya majengo ya shule za sekondari iliyotolewa kwenye

Mwongozo wa uanzishaji shule. Katika Ibara ya 5.4.3. Sera inaelekeza kuwa:

Wamiliki na viongozi wote wa shule za sekondari watahakikisha kuwa majengo, vifaa,

zana na vifaa vya kufundishia ambavyo ni vya lazima kwa kufundishia na kujifunzia

kwa ufanisi kwa kiwango cha juu na bora vinapatikana katika idadi inayotosheleza na

vinakarabatiwa mara kwa mara. (uk.31).

Mwaka 2001, Idara ya Sera na Mipango ilitoa Mwongozo wa Majengo na Samani

kuhusiana na ujenzi wa shule za sekondari. Majengo haya ni pamoja na: Jengo la

Utawala (unajumuisha ofisi ya Mkuu wa shule pamoja na msaidizi wake, ubao wa

matangazo ya shule, vyoo vya utawala, ofisi ya walimu), madarasa, nyumba za

wafanyakazi, vyoo, maabara, maktaba, mabweni, bwalo la kulia chakula, jiko na stoo,

chumba cha kupumzikia wagonjwa (sick bay), viwanja vya michezo na barabara

zinazopitika. Aidha vipimo vya ukubwa wa kila jengo viliainishwa.

Mwaka 2007, WEMU ilielekeza mambo ya kuzingatia katika kuanzisha shule za

sekondari za kutwa zinazojengwa kwa nguvu za wananchi kuhusiana na miundo

mbinu. Mwongozo ulielekeza Halmashauri kuzingatia mahitaji yafuatayo: madarasa

mawili, jengo la utawala moja, vyoo matundu mawili kwa watumishi, matundu

matano kwa ajili ya wanafunzi (wasichana matundu matatu na wavulana matundu

mawili), maabara ya sayansi moja, stoo mbili za vifaa na nyumba tatu za walimu. Hii

ilikuwa hatua ya muda mfupi iliyochukuliwa na Serikali kusaidia wananchi kuanzisha

shule katika maeneo yao, ili kukabili hitaji la kuwa na shule zaidi za sekondari. Pamoja

na kuchukua hatua hizi, mategemeo ya serikali ni kwamba shule zilizoanzishwa kwa

njia hii, zitajiimarisha kadri siku zinavyokwenda na kuhakikisha zinaendelea

kujitosheleza katika mahitaji yote yaliyoainishwa mwaka 2007.

2.10.2: Samani

Samani huenda sambamba na mahitaji ya wanafunzi na walimu. Samani hizi ni

pamoja na madawati na viti kwa ajili ya madarasa, meza, mbao za darasani, mbao za

www.JamiiF

orums.com

Page 49:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

48

matangazo, viti, makabati, meza za chai, na samani za majengo yote mengine katika

shule. Katika mwaka 2001, Idara ya Sera na Mipango (WEMU) ilitoa Mwongozo wa

Samani kuhusiana na ujenzi wa shule za sekondari. Mwongozo huo ulianisha samani

za kila jengo ambazo zinaendana na mahitaji ya wanafunzi pamoja na walimu wao.

Aidha, uchaguzi wa samani unatakiwa uzingatie umri, ulemavu pamoja na kiwango

cha elimu inayotolewa katika shule husika.

Mwaka 2007 WEMU ilielekeza samani (madawati 80 na viti 80, meza za darasani mbili

na viti viwili) kwa shule ya mikondo miwili zilizokuwa zinajengwa kwa nguvu za

wananchi.

2.11. Uandaaji na Upatikanaji wa Walimu

Walimu ni Nguvu Kazi muhimu katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Mafunzo

ya walimu humuandaa mwalimu kitaalamu na kitaaluma. Kada ya walimu nchini

Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu tatu: cheti, stashahada na shahada.

Mafunzo ya walimu yamegawanyika katika sehemu kuu mbili: Mafunzo Tarajali (Pre-

service) na Mafunzo Kazini (In-service).

2.11.1: Mafunzo Tarajali

Mafunzo tarajali ni mafunzo ya awali ambayo hutolewa kwa mwanachuo anaye

andaliwa kuwa mwalimu katika ngazi yoyote ya elimu kulingana na sifa alizonazo. Sifa

na muda wa mafunzo ya Ualimu katika ngazi zote za elimu zimekuwa zikitofautiana

kutoka kipindi kimoja hadi kingine kulingana na mahitaji ya wakati huo.

Mara baada ya uhuru, Wizara ya Elimu iliamua kupanua elimu ya sekondari, ili kuweza

kupata watumishi wa sekta mbali mbali za maendeleo ya uchumi. Kwa hali hiyo

Serikali ilihitaji walimu wa kutosha ili waweze kuwaandaa wataalamu hao katika

kiwango cha sekondari. Kutokana na ukosefu wa walimu wa kutosha, muda wa

mafunzo ya Ualimu katika ngazi ya Stashahada ulipunguzwa kutoka miaka miwili na

kuwa na mwaka mmoja chuoni na miezi sita ya mazoezi nje ya chuo. Waombaji wa

kozi hii walikuwa wahitimu wa Kidato cha 6. Aidha, wanafunzi wa Chuo Kikuu,

walishawishiwa kuchukua mafunzo ya Ualimu. (Tume ya Rais ya Elimu, 1982, 5.7 uk.

225).

www.JamiiF

orums.com

Page 50:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

49

Tume ya Rais ya Elimu ya mwaka 1982 ibara ya 3.116 ilipendekeza kwamba ’Walimu

wa sekondari na vyuo vya ufundi wawe na Stashahada na Shahada wakati wale wa

ufundi sadifu wawe wenye cheti cha elimu ufundi mchundo (Full Technician

Certificate’ F.T.C.) Lengo kwenye shule za sekondari kuwe na walimu wenye shahada.

uk. 147. Katika miaka ya 70, sifa za waliojiunga na Stashahada ilikuwa mhitimu wa

Kidato cha 6, na kupata ufaulu si chini ya ‘Subsidiary’ mbili. Muda wa mafunzo ulikuwa

miaka miwili. Kutokana na upanuzi wa shule za sekondari, mwishoni mwa miaka ya 80

hadi mwaka 1991, Wizara ya Elimu ilianzisha utaratibu ambao uliruhusu wanafunzi

waliofanya vizuri Kidato cha 4 kuingia Kidato cha 5 na na mafunzo ya Ualimu. Vyuo

hivyo vilikuwa Mkwawa, Korogwe, Shinyanga na Monduli. Mwanafunzi alisoma kwa

miaka mitatu na baada ya hapo alipata cheti ngazi ya Stashahada na kwenda

kufundisha shule za sekondari. Hii ilikuwa jitihada ya makusudi ya Serikali kuhakikisha

kwamba wanaandaa walimu wenye ubora kitaalamu na kitaaluma.

Mwaka 2005, WEMU ilielekeza uimarishaji wa sifa na muda wa waliotaka kujiunga na

Kozi ya Stashahada ya Ualimu kuwa na sifa zifuatavyo: awe amehitimu Kidato cha 6,

na kupata ‘Principal Pass’ 2 au zaidi. Muda wa mafunzo kuwa miaka miwili. (Facts

About Basic Education in Tanzania, Final draft 2005).

Hata hivyo, Maelekezo ya Kamishna katika barua kumb.Na TTDB/85/483/01/25

mwaka, 2009 inaelekeza sifa zinazokinzana na zile za awali za 2005. Sifa za

wanaojiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada kuanzia tarehe 1, Julai ni

‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika masomo yanayofundishwa shule za

sekondari. Waraka huo pia unaelekeza Sifa kwa wanaojiunga na mafunzo ya

Stashahada ya Ualimu kwenye fani ya Ufundi kuwa itaendelea kuwa cheti cha Elimu

ya ufundi mchundo (FTC). Kwa lengo la kutoa fursa kwa wahitimu wenye ufaulu mzuri

katika masomo ya Sayansi na Hisabati, wasio na cheti cha Elimu ya ufundi mchundo

wamepewa nafasi kujiunga na Stashahada ya ualimu wa kawaida. Utafiti uliofanyika

na WEMU, 2006 umeonesha umuhimu wa kuboresha sifa za chini za kuingia katika

vyuo vya ualimu na kuimarisha kipindi cha mafunzo (The Teacher Management

Development Strategy 2008 - 2013). Kati ya mwaka 2004 -2007, Wizara ya Elimu

iliandaa Walimu wa Leseni 10,000 waliohitimu kidato cha 6. Walimu hawa

www.JamiiF

orums.com

Page 51:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

50

waliandaliwa kwa kupewa mafunzo ya muda mfupi (induction course) ya wiki 4

ambayo yalilenga kuwapa kwa kiasi kidogo mbinu za kufundishia na kujifunzia na

uongozi katika elimu kabla ya kuruhusiwa kufundisha. Ngodu, 2007 anaielezea dhana

ya walimu wa leseni (Licensed Teachers) kuwa ni walimu ambao hawajasomea kozi ya

ualimu isipokuwa wanayo taaluma ya masomo kwa maana wamemaliza kidato cha

sita au wamesomea shahada zisizo za elimu. Uandaaji wa walimu hawa ni wa

dharura na ni njia mbadala ya kupata walimu kwa haraka kwa lengo la kupunguza

tatizo kubwa la walimu shuleni.

2.11.2: Mafunzo Kazini

Mafunzo kazini (In-service) ni mafunzo ambayo hutolewa kwa mwalimu aliyefuzu kozi

ya ualimu kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza utaalamu na taaluma yake. Katika

kuimarisha na kuendeleza utaalamu na taaluma yake, mwalimu hupata fursa ya

kujifunza mambo mapya yanayojitokeza kulingana na wakati, kwa mfano, mabadiliko

ya mtaala wa shule, dhana na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji, mabadiliko ya

jamii, sayansi na teknolojia. Aidha mafunzo kazini, humfanya mwalimu kwenda na

wakati. Tume ya Rais ya Elimu (uk. 232) inaelekeza mafunzo kazini huendeshwa kwa

mtindo wa kozi fupi au ndefu, semina, warsha na ziara za kielimu zenye malengo ya

kuinua viwango vya elimu, ujuzi na utaalamu wa walimu.

Sera ya Elimu (1995) katika ibara ya 5.5.10 inatamka ‘Mafunzo kazini na mafunzo

rejea yatakuwa ya lazima ili kuhakikisha ubora wa ualimu na utaalamu’. WEMU,

Februari 2006 katika utafiti wake kuhusu mfumo wa Elimu ya Ualimu katika Tanzania,

ilifanikiwa kuanzisha Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu (MMEMWA)

ambapo moja ya lengo lake kuu ni kuhakikisha uwepo wa mafunzo kazini endelevu na

weledi kulingana na mahitaji ya utaalamu wa walimu. Malengo ya MMEMWA

yanajumuisha utafiti kuhusu mahitaji ya mafunzo kazini kwa ajili ya walimu, wakufunzi

na viongozi wa elimu kufikia mwaka 2009.

Kwa kupitia MMEMWA, Wizara imefanikiwa kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Elimu

na Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za Msingi (MEMK – WSM), 2009 – 2013.

Madhumuni ya mkakati huu ni kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu

baada ya mafunzo tarajali kwa lengo la kuhakikisha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji

www.JamiiF

orums.com

Page 52:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

51

katika shule za msingi, pamoja na kukidhi mahitaji ya walimu kitaalamu na kitaaluma

(MWAKEM 2010).

Waraka Na.10 wa mwaka 2009 kuhusu mafunzo ya walimu kazini kwa walimu wa

shule za sekondari unaelezea umuhimu wa mafunzo kazini kama nyenzo muhimu ya

kumuongezea mwalimu maarifa, ujuzi na stadi za kumwezesha kufundisha kwa

umahiri. Aidha, waraka umeweka wazi mapungufu ya utaratibu wa mafunzo kazini

ambayo yamekuwa yanatolewa kwa baadhi ya maeneo na makundi ya walimu na

kutokuwa endelevu. Kutokana na hali hii, waraka unaelekeza mafunzo haya

kuendeshwa na Halmashauri husika kwa kuzingatia kuwa usimamizi na uendeshaji wa

shule za sekondari kwa sasa uko chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

2.11.3: Uwepo wa Walimu

Uwepo wa walimu wenye sifa ni moja ya kiashiria cha ubora wa elimu itolewayo.

Tume ya Rais ya Elimu (1982, uk. 230) inasema kwamba ubora wa walimu

hutegemea njia zinazotumika katika utayarishaji wao. Aidha, Tume inabaini kwamba

umuhimu wa kuwa na walimu bora haukuzingatiwa kikamilifu tangu nchi ilipojitawala.

Juhudi zilifanywa zaidi katika upanuzi wa elimu katika ngazi zote bila ya kuwa na

uwiano na ubora wa walimu wengi waliokuwa wanahitajika.

Utayarishaji na upungufu mkubwa wa walimu kwenye shule zilizoko vijijini na hasa

kwenye masomo ya ufundi, sayansi, hisabati, kiingereza na jiografia; kinyume na Sera

ya Elimu na Mafunzo, Ibara 5.4.5 inavyoelekeza: Wamiliki wa shule za sekondari

watahakikisha kwamba wanapata walimu wenye sifa zinazotakiwa, wanakuwa na

mazingira mazuri ya kufundishia, wanatoa mafunzo na wanawaendeleza walimu wao

kitaalamu. Sifa zinazostahili kama zilivyoanishwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ni

walimu wenye Shahada na Stashahada kwenye shule za serikali na zisizo za serikali.

Walimu wa Stashahada wanapangiwa kufundisha Kidato cha 1 na 2 na walimu wa

Shahada wafundishe kuanzia Kidato cha 3 – 6.

Mwaka 2004, Serikali kupitia SEDP iliamua kuongeza usajili wa wanafunzi katika shule

za sekondari na wakati huo huo kuchukua juhudi za makusudi za kuinua ubora.

Kutokana na upungufu wa walimu uliokuwepo na ongezeko la uandikishaji wa

www.JamiiF

orums.com

Page 53:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

52

wanafunzi, Serikali iliamua kuajiri walimu wa leseni. Taarifa ya utafiti uliofanywa na

Ngodu (2007) unaonesha kuwa idadi kubwa ya walimu hao wapatao 3,500

waliandaliwa mwaka 2006 na walisambazwa katika shule mbalimbali nchini. Utafiti

huo pia ulionesha kuwa wadau wengi walilalamikia ubora wa walimu hao kutokana na

muda mfupi wa mafunzo. Hata hivyo, kutokana na juhudi hizo Serikali iliweza

kufanikiwa kuongeza walimu 10,000 katika muda wa miaka minne kati ya mwaka

2004 – 2007.

Ili kuendelea kukabili ongezeko la shule za sekondari zikiwa na wanafunzi wengi bila

walimu wa kutosha, WEMU (2007) iliamua kuwa na mafunzo ya mfumo wa ‘two tier’

ambao uliruhusu wanachuo wa Stashahada kusoma mwaka mmoja chuoni na mwaka

wa pili kuwa shuleni.

Mmari (1979) anasema kuwa ubora wa ufundishaji wa shule za msingi unategemea

ubora wa mafunzo ya walimu waliyoyapata ambao pia hutegemea ubora wa

wakufunzi waliokuwa nao. Kigezo kimojawapo cha kujulisha ubora wao ni kujua sifa

ya mwalimu kitaaluma. Taarifa ya WEMU inaeleza kuwa kufikia mwaka 2010, kulikuwa

na jumla ya walimu 40,255 katika shule za sekondari za Serikali (30,256) na zisizo za

Serikali (10,269) BEST, 2010. Jedwali Na. 2.5 linaonesha sifa na idadi ya walimu wa

sekondari waliopo nchini.

Jedwali Na. 2.5 Idadi ya Walimu wa Sekondari kwa Sifa, Mwaka, 2010

Sifa za Walimu

Shule za Sekondari za Serikali

Shule za Sekondari Zisizo za Serikali

Jumla

Me Ke JML Me Ke JML Me Ke JML Shahada 3,418 2,360 5,778 3,248 884 4,132 6,666 3,244 9,910Stashahada 11,494 6,678 18,172 3,171 828 3,999 14,665 7,506 22,171Cheti 1 3 4 1 3 4 2 6 8Nyingine 4,754 1,548 6,302 1,736 398 2,134 6,490 1,946 8,436JUMLA KUU

19,667 10,589 30,256 8,156 2113 10,269 27,823 12,702 40,255

Chanzo: Basic Education Statistics in Tanzania (BEST, 2010) uk. 115

Takwimu za kitaifa zilizokusanywa na OWM-TAMISEMI mwezi Machi 2011 zinaonesha bado

kuna upungufu mkubwa wa walimu katika masomo ya Mathematics na sayansi kama

inavyoonekana katika Jedwali Na. 2.6.

www.JamiiF

orums.com

Page 54:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

53

Jedwali Na 2.6: Takwimu za Mahitaji, Uwepo na Upungufu wa Walimu

katika Shule Sekondari kwa Masomo ya Sayansi na Mathematics, 2011.

Masomo Biology Chemistry Mathematics PhysicsMahitaji 8,846 8,012 10,508 8,009Waliopo 2,558 2,429 2,544 1,915Upungufu 6,288 5,583 7,964 6,094Asilimia ya Upungufu 71.1 69.7 75.8 76.1

Chanzo: Takwimu za Mahitaji ya walimu, OWM-TAMISEMI Machi, 2011

Mafunzo ya Ualimu hadi sasa yanaendeshwa katika vyuo 68 vilivyosajiliwa. Kati ya

hivyo, 34 ni vya serikali na 34 visivyo vya serikali. Vyuo 19 vya serikali viko katika

ngazi ya Stashahada. Changamoto iliyopo kulingana na maoni ya Ngodu (2009) ni

kwamba vyuo vya ualimu vilivyopo vina uwezo mdogo wa kudahili walimu tarajali wa

kutosheleza mahitaji ya nchi na wenye sifa stahili ya kuweza kuinua ubora wa elimu.

Takwimu zinaonesha kuwa ongezeko la wahitimu wa shahada katika vyuo vya ualimu

haliendani sambamba na ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi katika shule za

sekondari.

Kielelezo Na.2.1 Idadi ya walimu wa Stashahada waliohitimu na kufaulu

Mwaka 2005 – 2009

Chanzo: Basic Education Statistics in Tanzania (BEST, 2010) uk. 89

2.11.4: Upanuzi wa Mafunzo ya Walimu Tarajali Katika Ngazi ya Shahada

Ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu, mwaka 2007 Serikali ilichukua hatua

za kuanzishwa Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kinadahili idadi kubwa ya walimu

www.JamiiF

orums.com

Page 55:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

54

tarajali. Sanjari na uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma, iliamuliwa kuanzishwa

kozi ya ualimu katika vyuo vikuu vingine vya umma kama vile Chuo Kikuu cha Kilimo

cha Sokoine na Chuo Kikuu cha Mzumbe. Pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilipanua

matawi ya vyuo vikuu viwili vya Elimu vya Mkwawa (MUCE) na Dar es Salaam

(DUCE). Taarifa ya utekelezaji WEMU inaeleza kuwa idadi ya walimu tarajali

watakaohitimu katika vyuo vikuu inakadiriwa kuwa 11,000 kwa mwaka (Hotuba ya

Bajeti, WEMU 2010/11).

www.JamiiF

orums.com

Page 56:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

55

SURA YA TATU: MWONGOZO WA UTAFITI

3.1. Utangulizi

Mwongozo wa utafiti unaonesha mchakato wa utafiti ulivyofanyika wakati wa

kukusanya data na taarifa za utafiti kutoka kwa wajibuji mbalimbali katika eneo la

utafiti. Sura hii inabainisha kuhusu eneo na walengwa wa utafiti, uchaguzi wa

sampuli, aina na matumizi ya zana za utafiti. Pia, imeainisha mchakato wa utafiti na

uchambuzi wa data na taarifa.

3.2. Mbinu ya Utafiti

Utafiti huu umetumia aina mbili za mbinu katika ukusanyaji na uchambuzi wa data

ambazo ni maelezo stahilifu ya wajibuji (qualitative) na takwimu (quantitative). Aidha,

dhana ya ufaulu wa Kidato cha 4 ilitafsiriwa kwa kuhusisha viashiria mbalimbali kama

vile mitaala, upimaji, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, usimamizi na uendeshaji,

ufuatiliaji na tathmini, uwepo wa walimu na mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji

kama inavyoonekana katika Kielelezo Na. 3.1. Viashiria hivyo vilitumika katika

kuandaa zana za utafiti

Kielelezo Na.3.1 Viashiria vya Kiwango cha Ufaulu

www.JamiiF

orums.com

Page 57:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

56

3.3. Eneo la Utafiti

Utafiti huu ulifanyika katika kanda zote 11 za elimu na kuhusisha mikoa ya Dar es

Salaam, Pwani, Singida, Ruvuma, Manyara, Shinyanga, Lindi, Mara, Kagera, Rukwa na

Tanga. Maeneo mengine yaliyohusika ni ofisi za Ukaguzi wa Shule Kanda pamoja na

ofisi ya elimu ya mkoa husika. Aidha, Taasisi ya Elimu (TET), Baraza la Mitihani la

Taifa (NECTA), Chuo Kikuu cha Dar na Chuo Kikuu Huria (OUT), TEN/MET na

TAMONGSCO zilihusika katika utafiti. Pia, utafiti ulihusisha vyuo vya ualimu, ofisi za

elimu za Halmashauri na ukaguzi wa shule wilaya, ofisi za Tume ya Utumishi (TSD) na

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya. Vilevile, ofisi za waheshimiwa Wabunge,

Madiwani, Mashirika yasiyo ya kiserikali katika Halmashauri na madhehebu ya dini

zilihusishwa.

3.4. Uchaguzi wa Sampuli

Jumla ya mikoa 11 ilihusishwa katika utafiti ili kupata uwakilishi kitaifa. Uchaguzi wa

Mikoa ulizingatia uwepo wa shule za sekondari zilizofanya vizuri na vibaya katika

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 zikijumuisha shule 88 za serikali na 44

zisizo za serikali. Jumla ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa, moja

iliyofanya vizuri na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa ya Kidato cha 4

mwaka 2010. Shule sita kutoka kila Halmashauri za utafiti zilichaguliwa na kuhusika

katika utafiti huu ambazo ni 4 za serikali na 2 zisizo za serikali.

Uchaguzi wa shule hizo kwa kila Halmashauri ulifanywa kwa kuzingatia kiwango cha

ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Shule za serikali

zilizochaguliwa zilijumuisha shule mbili zilizofanya vizuri na mbili zilizofanya vibaya

katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Vile vile, shule mbili zisizo za

serikali zilizochaguliwa moja iliyofanya vizuri na moja iliyofanya vibaya. Uchaguzi wa

shule ulifanywa kwa lengo la kupata uwakilishi wa shule zenye viwango tofauti vya

ufaulu. Jumla ya shule za sekondari zilizohusishwa katika utafiti ni 132, zikiwemo 12

kutoka katika kila Halmashauri.

Utafiti huu ulijumuisha wajibuji 3,037 kati ya 3,894 sawa na 80.0% kutoka kwenye

makundi 29. Walioshirikishwa katika utafiti huu walikuwa Wakaguzi wa shule wa

www.JamiiF

orums.com

Page 58:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

57

Kanda 41, Wakaguzi wa shule Wilaya 22, Maafisaelimu Mikoa 11, Maafisaelimu wa

Halmashauri wa Msingi 21 na Sekondari 21, Maafisa wa TAMONGSCO 8, TEN/MET 6,

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) 23, na Tume ya Utumishi wa Umma wilaya (TSD)

22. Aidha, wengine ni pamoja na Wajumbe wa Bodi za Shule 82, Wakuu wa Shule za

Sekondari 132, Walimu wa kawaida 613, Walimu waliosahihisha mtihani wa Taifa

mwaka 2010 ni 162, Wakufunzi wa vyuo vya ualimu 28, wahadhiri wa vyuo vikuu 4,

wanachuo wa vyuo vya ualimu 44 na vyuo vikuu 4, Waheshimiwa Wabunge 17,

Waheshimiwa Madiwani 43, Wazazi/Walezi 95, Wanafunzi wa kidato cha 3 na 4 ni

1140, wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2010 ni 401 na viongozi wa madhehebu ya

dini 40. Utafiti huu pia ulilenga kupata taarifa kutoka kwa maafisa mitihani wa Baraza

la Mitihani la Tanzania (NECTA) 12 na wakuza mitaala wa Taasisi ya Elimu Tanzania

14 (Rejea Kiambatisho Na.3.5). Uchaguzi wa sampuli ulikuwa wa makusudi ambapo

wajibuji katika kila kundi ulizingatia uzoefu, nafasi zao kazini na jinsia katika taasisi

husika.

3.5. Zana za Utafiti

Taarifa na data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Dodoso, Hojaji na Majadiliano ya

Pamoja. Pia, taarifa za data zilipatikana kwa kupitia Maandiko mbalimbali yakiwemo

ya kisera, Programu, Mipango, Nyaraka za kielimu na Ripoti za utafiti.

Dodoso za aina nne zilitumika kukusanya taarifa za utafiti toka kwa Wakaguzi wa

shule wa Kanda, Wakuu wa shule, Wakurugenzi wa TET na Wakuu wa Idara za

mitihani NECTA. Vilevile, Hojaji zilitumika kukusanya taarifa kutoka katika makundi

nane ya wahadhiri wa vyuo vikuu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu, wanachuo wa vyuo

vikuu na vyuo vya ualimu, Maafisa Elimu mkoa, Maafisa Elimu wa Halmashauri Msingi

na Sekondari, Wakaguzi wa shule wa wilaya, Tume ya Utumishi wa Umma, Chama

cha Walimu Tanzania, Madhehebu ya Dini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali,

Waheshimiwa Wabunge, Madiwani, Wazazi/Walezi, Wajumbe wa Bodi za Shule na

wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Aidha, Mahojiano ya Pamoja yalitumika

kupata taarifa kutoka katika makundi sita ya wakuza mitaala, maafisa mitihani,

TAMONGSCO, TEN/MET, walimu wa masomo, walimu walioshiriki kusahihisha Mtihani

wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 na wanafunzi wa Kidato cha 3 na 4 mwaka

www.JamiiF

orums.com

Page 59:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

58

2011. Kiambatisho Na.3.5 kimeainisha aina ya zana ya utafiti, idadi ya wajibuji

waliohusika katika kila eneo la utafiti.

3.6. Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti

Mchakato wa kufanya utafiti ulianza kwa kuteua Kikundi Kazi ambacho kiliandaa

hadidu za rejea na zana za utafiti zilizojaribiwa katika Manispaa ya Temeke. Kikundi

Kazi kiliwasilisha na kupokea maboresho ya hadidu za rajea na zana za utafiti kwenye

Menejimenti ya WEMU na OWM-TAMISEMI.

Jumla ya Watafiti 44 waliteuliwa kutoka WEMU na OWM-TAMISEMI kushiriki katika

semina elekezi ya maandalizi ya utafiti kabla ya kwenda kukusanya data katika

maeneo husika. Watafiti wanne walipangwa kukusanya data na taarifa katika kila

mkoa wakisaidiwa na mtafiti msaidizi mmoja kutoka kila Halmashauri iliyokuwa

kwenye sampuli. Mchakato wa kupata taarifa kutoka kwa wajibuji kutoka katika

maeneo mbalimbali ya utafiti unaelezwa kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo:-

3.6.1.Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya TaifaWatafiti walikusanya data kutoka katika taasisi na asasi mbalimbali za kiserikali na

zisizo za kiserikali zilizochaguliwa ili kupata tarifa zenye taswira ya kitaifa kuhusu

kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Watafiti

walikusanya taarifa kwa kuwahoji wahadhiri wanne na wanachuo wanne wa vyuo

vikuu. Pia mahojiano ya pamoja yalifanyika kwa wakuza mitaala kumi, maafisa

mitihani wanane, maafisa nane wa TAMONGSCO na maafisa sita wa TEN/MET. Aidha,

Wakurugenzi wanne wa TET na Wakuu wa Idara wanne wa NECTA walijaza dodoso.

Taarifa za kitaifa pia zilikusanywa kwa kupitia maandiko mbalimbali.

3.6.2.Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na HalmashauriZana zilizotumika kupata data na taarifa kutoka katika Kanda za elimu, mikoani na

Halmashauri zilikuwa ni dodoso na hojaji. Dodoso ziligawiwa kwa Wakaguzi wa shule

wa Kanda wanne kwa kila Kanda ya elimu na Wakuu wa shule za sekondari 12 zilizopo

katika mkoa, ambapo ni shule sita kwa kila Halmashauri. Katika ngazi ya mkoa,

watafiti walitumia hojaji kupata taarifa kutoka kwa Afisaelimu Mkoa, wakufunzi wawili

na walimu tarajali wanne wa vyuo vya ualimu.

www.JamiiF

orums.com

Page 60:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

59

Aidha, katika ngazi ya Wilaya na Halmashauri, waliohojiwa ni mkurugenzi wa

Halmashauri, Afisa Elimu Halmashauri (Sekondari), Afisa Elimu Halmashauri (Msingi),

Mkaguzi Mkuu wa Shule Wilaya, Afisa wa Tume ya Utumishi wa Umma (TSD), Afisa

wa CWT Wilaya, Viongozi wawili wa madhehebu ya dini, afisa wa shirika lisilo la

serikali, Mheshimiwa Mbunge na Diwani na wajumbe wawili wa Bodi za shule.

3.6.3.Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika JamiiKatika ngazi ya shule na jamii, watafiti walitumia hojaji kwa wahitimu wa watano wa

Kidato cha 4 kwa kila shule husika. Mkuu wa shule katika kila shule husika alijaza

dodoso na kutoa takwimu muhimu za shule. Aidha, mahojiano ya pamoja yalihusisha

walimu kutoka kila shule husika. Wanafunzi 10 wa kidato cha 3 na 4 mwaka 2011

walihusishwa kwenye mahojiano ya pamoja kwa kuzingatia ushiriki wa wanafunzi

wenye mahitaji maalumu na jinsi. Walimu walioshiriki kusahihisha Mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4 mwaka 2010 walihusishwa katika mahojiano ya pamoja.

3.7. Uchambuzi wa Data

Data na taarifa mbalimbali kutoka shuleni, halmashauri na mkoa ziliunganishwa na

kupata taarifa ya kila mkoa husika. Hatua zilizofuatwa katika mchakato wa uchambuzi

na uandishi wa ripoti ya utafiti zilihusisha kuunganisha majibu ya kila swali kwa kila

zana kitaifa. Pia, majibu ya maswali ya kila zana kwa kila lengo mahsusi yaliainishwa,

yaliwekwa pamoja na kupangwa katika mtiririko wa uandishi kwa kila lengo mahsusi.

Aidha, taarifa zilichambuliwa, zikapangwa na kisha kutafsiriwa na ripoti ya utafiti

kuandikwa. Ripoti imeandikwa kwa kujadili masuala yaliyojitokeza kwa kila suala

muhimu na kuwasilishwa kwa kutumia idadi halisi na asilimia. Katika ripoti baadhi ya

taarifa na takwimu zimeoneshwa katika grafu, mihimili na majedwali.

3.8. Maadili ya Kufanya Utafiti

Utafiti huu ulizingatia taratibu na maadili katika hatua zote za ukusanyaji wa data,

uchambuzi na uandishi wa ripoti. Maadili yote ya utafiti katika ofisi na taasisi zikiwemo

shule za sekondari zilizofanyiwa utafiti yalizingatiwa, ikiwa ni pamoja na uhuru wa mtu

kushiriki katika utafiti, kutunza siri na mambo ya faragha yanayowahusu washiriki

www.JamiiF

orums.com

Page 61:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

60

(wajibuji). Utayari wa wajibuji katika kufanya utafiti ulipatikana kupitia viongozi na

wao wenyewe.

www.JamiiF

orums.com

Page 62:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

61

SURA YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA DATA

4.1. Utangulizi

Sura hii inahusu uwasilishaji, uchambuzi na tafsiri ya data na taarifa zilizokusanywa

kutoka kwa wajibuji katika maeneo mbalimbali yaliyohusishwa katika utafiti.

Uwasilishaji wa data na taarifa umezingatia masuala yanayoendana na malengo

mahsusi na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti yamejadiliwa katika maeneo makuu

yafuatayo: Usimamizi na uendeshaji wa elimu; Utayarishaji na utekelezaji wa mitaala;

Mfumo na taratibu za Mitihani ya Taifa; Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa

elimu; Mfumo wa utayarishaji na uwepo wa walimu; na Mazingira na vifaa vya

kufundishia na kujifunzia.

Utafiti ulilenga kuchambua kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4

mwaka 2010. Mapitio ya maandiko na makala yameonesha kwamba kiwango cha

ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila mwaka tangu

mwaka 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na 2010 (50.4%) (BEST, 2010 &

NECTA, 2011). Kielelezo Na. 4.1 imeonesha mwenendo wa kushuka kwa ufaulu wa

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2006-2010.

Kielelezo Na. 4.1: Kiwango cha Ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4

Mwaka 2006-2010

Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results

Statistics 2007-2010

www.JamiiF

orums.com

Page 63:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

62

Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 yameonesha kuwa asilimia

49.6 ya watahiniwa wote hawakufaulu mtihani huo. Utafiti huu umeweza kubaini

sababu mbalimbali zinazochangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu ambapo wajibuji

walieleza kwa kutumia zana za Mahojiano ya pamoja, Hojaji na Dodoso. Kwa kupitia

zana za Hojaji na Dodoso, jumla ya wajibuji 1,092 walibainisha sababu za kushuka

kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4 mwaka 2010 kama

ilivyooneshwa kwenye Kielelezo 4.2. Aidha, kwa kutumia mahojiano ya pamoja

wajibuji 1,945 walibainisha sababu mbalimbali za kushuka kwa kiwango cha ufaulu

ambapo usimamizi na uendeshaji wa elimu ulitajwa kwa kiwango kikubwa kuwa ni

chanzo cha tatizo.

Utafiti huu pia ulilenga kupata maoni mbalimbali juu ya kuinua kiwango cha ufaulu

cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Maoni yaliyopatikana kwa wajibuji

yameainishwa katika kila eneo kuu lililojadiliwa kwa kuzingatia malengo mahususi na

maswali ya utafiti.

Kielelezo Na. 4.2: Sababu za kushuka kwa Ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4 Mwaka 2010

Chanzo: Data za Utafiti, 2011

Ufunguo:

A. Matatizo katika utekelezaji wa

mitaala

B. Upungufu wa walimu na

wafanyakazi wasio walimu

C. Matatizo ya usimamizi na

uendeshaji wa elimu

D. Mazingira yasiyoridhisha ya

ufundishaji na ujifunzaji

E. Mapungufu katika uendeshaji

wa mitihani ya kitaifa

www.JamiiF

orums.com

Page 64:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

63

4.2. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu

Usimamizi na uendeshaji wa elimu ni lazima uwe na mfumo mzuri wa utendaji na

mawasiliano katika ngazi zote ili kufikia malengo ya utoaji wa elimu. Kwa kawaida

usimamizi na uendeshaji unazingatia miundo na mifumo iliyo rasmi katika ngazi zote

za elimu. Aidha, jukumu la usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini inahusisha

mifumo isiyo rasmi ikijumuisha wazazi/walezi, jamii na wadau mbalimbali wa elimu.

4.2.1.Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali Utafiti huu umebaini kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini unakabiliwa na

matatizo na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na watendaji wenye dhamana

ya kutekeleza jukumu hilo kutowajibika na kukosa umakini katika utendaji. Hali hii

inajionesha katika ngazi mbalimbali za usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini.

Ngazi hizo ni shule, kata, Halmashauri, mikoa na kitaifa. Kutokana na matokeo ya

utafiti, usimamizi na uendeshaji wa elimu umejadiliwa kwa kuhusishwa na masuala ya

kisiasa katika elimu, mmomonyoko wa maadili, mwamko duni wa jamii na ugharamiaji

wa elimu.

a) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Shule na Kata

Uongozi wa shule unajumuisha wakuu wa shule, walimu, wajumbe wa bodi za shule

na serikali za vijiji/mtaa. Kila kundi lina wajibu wake katika kuhakikisha kuwa kanuni

na taratibu za uendeshaji shule zinazingatiwa ipasavyo. Aidha, ngazi hii ya usimamizi

inahusika na uhamasishaji wa wananchi katika kuchangia maendeleo ya shule na

elimu kwa ujumla (Kiongozi cha Mkuu wa shule: WEMU, 1997).

Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa yapo matatizo ya kiuwajibikaji kwa bodi za

Shule, wakuu wa shule na walimu wenyewe katika kutekeleza majukumu yao ya

msingi. Hali hii husababisha wanafunzi kutofundishwa kikamilifu kama ilivyopangwa

katika mihtasari na mihula ya shule. Aidha, utafiti umebaini kwamba kutokuwajibika

kwa bodi za shule kumezifanya baadhi ya shule kuwa na migogoro ya umiliki wa

maeneo ya shule kwa muda mrefu na hivyo kuingiza shule katika uhasama na jamii

inayoizunguka.

www.JamiiF

orums.com

Page 65:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

64

Aidha, utafiti umeonesha kuwa bodi za shule hazisimamii uendeshaji wa shule

ipasavyo ikiwa ni pamoja na; nidhamu ya walimu na wanafunzi, mapato na matumizi

ya fedha ya shule na kuhamasisha upatikanaji wa raslimali katika shule. Madhara ya

bodi ya shule kutowajibika kunasababisha matumizi mabaya ya fedha inayotengwa

kwa ajili ya maendeleo ya elimu; wakuu wa shule na walimu kutotulia vituoni na

kutofuatiliwa kwa walimu katika uteketekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji na

ujifunzaji wa wanafunzi. Hoja ya walimu kutotekeleza majukumu yao pia ilidhihirishwa

na majibu ya mmoja wa wanafunzi katika majadiliano ya pamoja kuwa

“.....walimu hawafundishi, hivyo hatuna budi kwenda bondeni kula matango

mwitu“

Usemi huu unamaanisha wanafunzi kwenda kupata masomo ya ziada ya kulipia

(tuition) ambayo hawana uhakika na maudhui yake.

Utafiti umebaini kuwa Wakuu wa Shule wameshindwa kufuatilia ipasavyo mahudhurio

na utendaji kazi wa walimu walio chini yao, hali inayosababisha wanafunzi

kutofundishwa ipasavyo na hivyo kushindwa kufaulu mitihani ya taifa. Aidha, wakati

wa mahojiano ya pamoja na wanafunzi, mmoja wa wanafunzi alilalamika kwa

kusema:

“Baadhi ya walimu hututumikisha kazi za nje wakati wa vipindi darasani na

wengine hugawa kazi za kufanya darasani bila kutoa mwongozo wa namna ya

kuifanya kazi hiyo“.

Huu ni uthibitisho wa usimamizi usioridhisha wa utekelezaji wa mitaala ambapo

wanafunzi hutumia muda wa masomo kufanya kazi ambazo hazihusiani na ujifunzaji.

Pia mikakati ya wakuu wa shule ya kutumia walimu wa muda (part-time teachers)

wenye elimu ya kidato cha nne au sita bila taaluma ya ualimu kunaibua maswali

yanayohusishwa na kushuka kwa ufaulu. Vilevile, matokeo ya utafiti yamebainisha

kwamba baadhi ya walimu hufanya biashara wakati wa saa za kazi badala ya kuandaa

na kufundisha vipindi ipasavyo. Hali kadhalika, majukumu ya Waratibu Elimu Kata ya

kusimamia na kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji hayatekelezwi ipasavyo.

Matokeo ya utafiti kuhusu usimamizi na uendeshaji wa elimu shuleni yanaonesha

kuwepo kwa usimamizi usioridhisha tofauti na ilivyoainishwa katika Sheria ya Elimu

www.JamiiF

orums.com

Page 66:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

65

Na. 25 ya Mwaka 1978 na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 na Kiongozi cha

Mkuu wa Shule (1997). Hali hii inaathiri uendeshaji wa shule, ufundishaji na ujifunzaji.

b) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu Katika Mkoa na Halmashauri

Usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri umeelezwa

kuwa umechangia katika kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Utafiti umebaini kuwa

ufaulu duni unachangiwa na mgawanyo wa walimu usiozingatia mahitaji katika shule;

shule kutokaguliwa mara kwa mara na kutofanyiwa kazi kwa mapendekezo na ushauri

unaotolewa katika taarifa za ukaguzi wa shule.

Hali kadhalika, wingi wa wanafunzi darasani usio na uwiano na idadi ya walimu

wanaohitajika (1:40) na upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na

kujifunzia husababisha ugumu wa ufundishaji na ujifunzaji hivyo baadhi ya shule

hulazimika kuendeshwa kwa mfumo wa awamu mbili (double session). Aidha, kuwepo

kwa mfumo wa awamu mbili hupunguza muda wa ufundishaji na ujifunzaji kwa vile

haiwezekani kuwa na vipindi 8 kwa siku kama ilivyoelekezwa katika Kiongozi cha

Mkuu wa Shule. Katika mfumo huo, wanafunzi hufundishwa vipindi 7 kwa siku na

hivyo kupoteza dakika 40 za kujifunza kwa kila siku za masomo sawa na vipindi 194

kwa mwaka.

Wanafunzi walieleza kwamba kutochanganywa kwa wanafunzi kutoka kata tofauti

katika shule moja kumesababisha kutokuwa na ushindani wa kitaaluma miongoni

mwao. Hali hii inasababisha wanafunzi kutobaini mabadiliko ya kimazingira kati ya

shule za msingi na sekondari hivyo kuathiri ujifunzaji wao.

c) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Wizara

Baada ya zoezi la ugatuaji 2008, WEMU imebaki na jukumu la kuandaa sera, mitaala,

uthibiti wa viwango vya ubora wa elimu, ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya elimu

ambapo jukumu la usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari umehamishiwa

OWM-TAMISEMI (WEMU, Hotuba ya Bajeti, 2010).

Wadau wa elimu waliohusishwa katika utafiti walibainisha sababu za kushuka kwa

ufaulu zinazotokana na usimamizi na uendeshaji wa elimu usioroidhisha; kusajiliwa

www.JamiiF

orums.com

Page 67:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

66

kwa shule zisizotimiza vigezo vinavyotakiwa; kuajiriwa kwa walimu wasio na sifa;

kutoshughulikiwa kwa matatizo ya walimu. Hali inaathiri utoaji wa elimu bora nchini.

Utafiti umeonesha pia kuna tatizo katika taratibu za uteuzi wa viongozi wa elimu

katika ngazi mbalimbali wakiwemo Maafisaelimu na Wakuu wa Shule ambapo baadhi

yao huteuliwa bila kuwa na sifa za kiuongozi na hivyo kuwa chanzo cha migogoro

shuleni kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya wanafunzi na walimu.

Usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi ya Wizara umeonekana kuwa na

mapungufu kwa kuajiri walimu wa leseni na kutowaendeleza kitaalamu. Hali hii ni

kinyume na Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 seksheni 49 inayosisitiza leseni

kutolewa kwa muda maalum. Aidha, Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa

walimu wa sekondari wawe wenye stashahada na shahada. Pia, imebainishwa kuwa

usajili wa shule na uteuzi wa viongozi wa elimu wakiwemo wakuu wa shule hauzingatii

vigezo vinavyotakiwa na hivyo kuathiri ubora wa elimu nchini.

d) Michango ya Wadau wa Elimu katika Usimamizi na Uendeshaji wa

Elimu ya Sekondari

Serikali imekuwa ikihamasisha watu binafsi, mashirika ya kidini, taasisi zisizo za

kiserikali na wadau wengine kutoa michango mbalimbali katika sekta ya elimu.

Mojawapo ya michango hiyo ni kuanzisha na kumiliki taasisi za utoaji wa elimu katika

ngazi zote. Utafiti umebaini kuwa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali zikiwemo

taasisi za kidini na watu binafsi wameanzisha na kumiliki shule za msingi, sekondari,

vyuo na vyuo vikuu hapa nchini.

Aidha, matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya shule

na jamii katika kuinua kiwango cha taaluma shuleni. Wazazi/walezi hufuatilia kwa

karibu taarifa ya maendeleo ya taaluma ya watoto wao na kuhudhuria vikao na vipindi

maalum ili kuzungumza na wanafunzi juu ya mahudhurio na nidhamu. Pia

wazazi/walezi wanachangia gharama za uendeshaji wa elimu kwa kulipa ada na

michango muhimu ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama za chakula. Vilevile, shule

hutuma taarifa za maendeleo ya watoto kwa wazazi/walezi na vikao vya bodi za shule

www.JamiiF

orums.com

Page 68:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

67

hushirikisha wazazi katika kusimamia taaluma na maadili shuleni. Michango ya

mashirika/taasisi zisizo za kiserikali na jamii imeoneshwa katika Kielelezo 4.3

Kielelezo Na. 4.3 Michango ya Wadau wa Elimu katika Asilimia

Chanzo: Data za Utafiti, 2011

Kielelezo Na 4.3 kinaonesha kuwa taasisi/mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii

wanachangia zaidi katika eneo la taaluma shuleni kwa asilimia 21.6, maadili shuleni

asilimia 18.3% na ushauri kuhusu bajeti ya elimu asilimia 16.1. Katika eneo la

taaluma, utafiti umebaini kuwa mchango wa wadau hao umejikita katika kuboresha

mazingira ya kujifunzia na kufundishia kama vile kununua vitabu, kuhamasisha

mafunzo kuhusu mitaala, elimu ya UKIMWI, mafunzo elekezi kuhusu sheria za kazi,

michango ya tafiti na ya kuendeleza taaluma shuleni. Pia, katika suala la maadili,

taasisi za kidini zinatoa mafundisho ya dini kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa lengo

la kurekebisha mienendo isiyokubali katika jamii.

Vilevile, utafiti umeonesha taasisi/mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii wanachangia

kwa kiasi kidogo katika maeneo ya uboreshaji wa miundombinu na huduma muhimu

shuleni kwa asilimia 6.5%, usimamizi wa utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya

serikali asilimia 4.5, usimamizi wa haki na maslahi ya walimu asilimia 3.1 na

kuhakikisha ikama ya walimu shuleni asilimia 2.8. Katika kuboresha miundombinu

ilifafanuliwa kuwa wadau hao hujenga na kuboresha majengo kama vile hosteli,

www.JamiiF

orums.com

Page 69:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

68

mabweni, maktaba, madarasa, ofisi za walimu, nyumba za walimu, umeme na samani

mbalimbali.

Hivyo, utafiti umebaini kuwa wadau wa elimu wana mchango mkubwa katika

usimamizi na uendeshaji wa elimu ya sekondari. Wadau wa elimu wamekuwa

wakifanya kazi kwa karibu sana na serikali kwa kusimamia na kulinda maadili,

kusimamia haki na maslahi ya walimu, taaluma na utekelezaji wa miongozo shuleni,

kuboresha miundombinu na huduma, kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi shuleni,

kuimarisha mahusiano baina ya shule na jamii, kuhakiki ikama ya walimu na kutoa

ushauri juu ya bajeti ya elimu.

Pamoja na ushirikiano huo, utafiti umebaini kuwa kuna changamoto zinazokwamisha

jitihada za wadau wa elimu ya sekondari nchini katika kufikia malengo ya utoaji wa

elimu bora. Changamoto hizo ni pamoja na Serikali kutoza kodi ya ongezeko la

thamani (Value Added Tax-VAT) kwa vyombo vya usafiri na vifaa vingine vya

uendeshaji wa shule na vyuo. Aidha, ilielezwa Serikali haiyafanyii kazi ipasavyo

mapendekezo ya tafiti yanayotolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

4.2.2.Mmomonyoko wa Maadili Katika JamiiMmomonyoko wa maadili katika jamii huathiri mwenendo wa nidhamu ya walimu na

wanafunzi shuleni. Utafiti umebaini kuwa mmomonyoko wa maadili kama vile

matumizi ya lugha mbaya kwa walimu, wanafunzi, wazazi/walezi na jamii; matumizi

mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kutozingatia

mafundisho ya dini yanaathiri maendeleo ya taaluma shuleni. Aidha, matumizi ya

dawa za kulevya, utoro, kujiingiza katika masuala ya mapenzi ni kati ya masuala

yaliyobainishwa kuchangia kushuka kwa maadili. Walimu walilalamikiwa kwa kutofuata

maadili ya kazi zao, mfano mmoja wa wanafunzi katika mahojiano ya pamoja alisema:

“…..walimu wanadiriki hata kuvuta sigara mbele ya wanafunzi……”

Uamuzi wa kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kwa makosa ya kawaida

umelalamikiwa pia kuwa umechangia kushuka kwa maadili kwa vile walimu hawana la

kufanya juu ya watoto wanaofanya makosa. Hali hii inamjengea mwanafunzi kiburi

kwa walimu.

www.JamiiF

orums.com

Page 70:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

69

Matokeo zaidi yameonesha kuwa miongoni mwa watendaji katika sekta ya elimu

wameweka mbele maslahi yao binafsi kwa kukosa uadilifu na hivyo kuathiri utekelezaji

wa malengo yaliyopangwa. Aidha, baadhi ya wazazi wamekuwa wakijihusisha na

ununuzi wa mitihani kwa ajili ya kuwapa watoto wao na hivyo kuwajengea hali ya

kutojisomea kwa kutegemea mitihani bandia (fake). Kulingana na matokeo ya utafiti

ni dhahiri kwamba kuna mmomonyoko wa maadili kuanzia ngazi za familia, shule na

jamii kwa ujumla kinyume na sheria na kanuni za shule za sekondari kama

ilivyoainishwa kwenye Kiongozi cha Mkuu wa Shule (1997) ukurasa 42-43 na

mafundisho ya dini.

4.2.3.Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu Katika utafiti huu, mwamko duni wa jamii ni mojawapo ya sababu iliyochangia

kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Aidha, jamii kutoshiriki kikamilifu katika harakati za

maendeleo shuleni; kutokutoa karo na michango halali ya kuboresha taaluma; pamoja

na imani potofu ya kuona kuwa mtoto wa kike hatakiwi kusoma bali kuozwa ni mifano

ya mwamko duni wa jamii katika elimu. Vilevile utafiti umebaini kuwa, wazazi wengi

huwatumikisha watoto kazi za nyumbani na kuwahusisha katika kazi za kujiongezea

kipato cha familia badala ya kwenda shule. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa jamii

haijaelewa ipasavyo umuhimu wa elimu kwa watoto hasa wa kike. Pamoja na juhudi

za serikali kuhamasisha jamii na kutoa fursa na usawa wa elimu kwa watoto kama

ilivyoainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, bado jamii inadhani

kuwa jukumu la kuelimisha umma ni la Serikali pekee. Hivyo, juhudi za pamoja katika

utoaji wa elimu bado ni changamoto.

4.2.4.Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya KielimuUtafiti ulibainisha kuwa maamuzi ya baadhi ya masuala ya kiataalam ya kielimu

hufanyika kisiasa na kusababisha kukiukwa kwa Mipango ya Elimu, kanuni na taratibu

za uendeshaji wa elimu kama vile matumizi ya fedha za shule. Wahojiwa walibainisha

kuwa uanzishaji wa shule nyingi za wananchi kwa mwaka 2006 usioendana na uwepo

wa walimu wenye sifa, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, huduma za jamii na baadhi

ya shule hizo kujengwa maeneo yaliyo mbali na makazi ya watu ni mojawapo ya

maamuzi yaliyotawaliwa zaidi na maamuzi ya kisiasa.

www.JamiiF

orums.com

Page 71:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

70

Aidha, kumekuwepo na shinikizo la kisiasa kuhusu kusajiliwa kwa baadhi ya shule

ambazo hazikidhi viwango vilivyowekwa na serikali. Sababu nyingine zilizotolewa na

wajibuji waliohojiwa ni pamoja na wanasiasa kuwatumia wanafunzi na walimu kwa

mambo ya kisiasa kama vile wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Aidha, imebainishwa kuwa baadhi ya Waheshimiwa Madiwani huwakataa na

kuwaondoa baadhi ya wakuu wa shule na walimu katika shule zilizo katika maeneo

yao bila sababu za msingi. Kutofanyika kwa utafiti wa kina wakati wa maboresho ya

mitaala na kubadilisha muundo wa masomo ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa

kufanywa kisiasa.

Matokeo haya yanaonesha kuwa yapo mapungufu ya kiuendeshaji katika elimu

yanayotokana na mgongano wa maamuzi kati ya wataalamu na wanasiasa.

Migongano hiyo imesababisha ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa

elimu nchini kama zilivyoainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sheria ya

Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Kiongozi cha Mkuu wa Shule (1997).

4.2.5.Ufinyu wa Bajeti ya ElimuBajeti ndogo inayotengwa na serikali kwa ajili ya elimu nchini na matumizi ya fedha

yasiyoendana na thamani ya kazi yanasababisha kutokamilika kwa mipango ya kuinua

taaluma shuleni. Ilibainishwa kwamba ufinyu wa ruzuku za uendeshaji (capitation

grant) na maendeleo (development grant) ya shule umesababisha matatizo katika

uendeshaji wa shule. Bajeti ya Elimu ya sekondari kama inavyoonesha katika Kielelezo

Na. 4.4 inapungua tofauti na ongezeko la wanafunzi toka 524,325 (2005) mpaka

1,638,699 (2010) ambalo linasababisha ongezeko la mahitaji ya uendeshaji wa elimu

ya sekondari. Hali hiyo imeathiri upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia

na uboreshaji wa miundombinu kama vile maabara, maji, umeme ambavyo

vinachangia katika utoaji wa elimu bora. Ufinyu wa bajeti na matumizi yasiyozingatia

thamani ya fedha inathibitisha usimamizi na uendeshaji wa elimu ya sekondari

usioridhisha.

www.JamiiF

orums.com

Page 72:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

71

Kielelezo 4.4: Asilimia ya Mgao wa Bajeti ya Elimu ya Sekondari katika

Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2004/05-2010/11

Chanzo: BEST, 2010

4.2.6.Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimua) Kuimarisha Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu

Ili kuleta ufanisi wa kitaaluma, ni muhimu kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa

elimu katika ngazi mbalimbali. Hii itawafanya walimu na viongozi wa elimu wawajibike

na kusimamia shughuli za utoaji wa elimu ipasavyo. Maoni mbalimbali yalitolewa na

Wakaguzi wa shule, Walimu, Wakuu wa shule, Wazazi/walezi, Wanafunzi, Wanasiasa

na wadau wengineo walioshirikishwa katika utafiti.

Katika kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu ilipendekezwa kwamba uteuzi wa

viongozi wa elimu wakiwemo Maafisaelimu na Wakuu wa Shule uzingatie sifa stahiki.

Aidha, ilishauriwa kuwa wakuu wa shule wawepo katika vituo vyao vya kazi na

wawajibike ipasavyo na wapewe mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa shule ili

kuleta ufanisi katika kazi. Pia, utaratibu wa kuwasimamisha masomo wanafunzi

wasiolipa ada au kushindwa kulipa michango mbalimbali uachwe, na michango

itolewe kwa kuzingatia waraka unaoongoza utoaji wa michango kwa shule za serikali.

Vilevile, Waratibu wa Elimu Kata wapewe mafunzo ya kusimamia elimu ya sekondari

ipasavyo na uteuzi wao lazima uzingatie taaluma na ujuzi.

www.JamiiF

orums.com

Page 73:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

72

Aidha, masomo ya ziada yatolewe kwa wasio na uwezo darasani. Kuhusu usafiri wa

wanafunzi ilibainishwa kwamba mpango wa kuwa na vyombo vya usafiri kwa kila

shule ubuniwe. Vilevile, michezo shuleni iimarishwe ili kuwafanya wanafunzi wawe na

afya njema na wakue kiakili. Pia ilishauriwa kuwa shule ziwe na mpango wa motisha

kwa walimu, kama vile kuwaendeleza kitaaluma hususan walimu wa leseni ili kuleta

ufanisi na kujenga ari na morali ya kazi. Walimu walipendekeza kuwa huduma za

ushauri nasaha kwa wanafunzi ziimarishwe shuleni ili kuwaepusha na majanga

yakiwemo UKIMWI, ulevi na mimba. Maoni yaliyotolewa na wadau yanaonesha kuwa

kuna udhaifu katika uteuzi na uwajibikaji wa uongozi katika ngazi ya shule.

Ilipendekezwa kwamba uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha 1 katika shule za

wananchi uzingatie kuchanganya wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali ndani

na nje ya kata husika ili kuleta changamoto za ushindani na kuongeza chachu ya

maendeleo kitaaluma kwa ajili ya mabadiliko chanya ya kimtazamo. Ilishauriwa pia,

uandikishaji wa wanafunzi kuingia kidato cha kwanza uzingatie uwiano wa darasa 1:

wanafunzi 45. Vilevile, ilishauriwa kuwa, fursa ya chaguo la pili iondolewe kwa sababu

inahusisha wanafunzi wenye ufaulu mdogo wakiwemo wasiojua kusoma na kuandika.

Maoni hayo yanaonesha kuwa utaratibu wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato

cha 1 una mapungufu ambayo yanachangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa

Mitihani ya Taifa.

Maoni yalitolewa kuwa, wajumbe wa bodi waelimishwe kuhusu majukumu yao ya kazi

na Afisaelimu Mkoa ahudhurie vikao vya bodi ili kuwa na maamuzi yanayofanana. Vile

vile bodi ya shule ichukue hatua za kinidhamu kwa walimu wanaobainika kwenda

kinyume na taratibu za shule kwa mfano, kuwachangisha fedha wanafunzi kwa ajili ya

masomo ya ziada. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa Bodi za shule hazitekelezi

majukumu yao ipasavyo.

Mapendekezo ya kisera pia yalitolewa kuwa mfumo wa elimu uangaliwe upya ili uweze

kumwandaa mhitimu kuwa mbunifu na mwenye kujitegemea. Hii ni pamoja na

kuimarisha masomo ya ufundi ili wahitimu waweze kujiajiri. Pia imeshauriwa kuwa

mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa yarudishwe kwa ajili ya kujenga uzalendo na utaifa

www.JamiiF

orums.com

Page 74:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

73

kwa wahitimu. Vilevile, ilipendekezwa kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

idhibiti ada katika shule binafsi na kusimamia matumizi ya mtaala mmoja ili kuzuia

matabaka yanayojengeka. Aidha, tafiti za nje pekee zisitumike kubadili mfumo wa

elimu nchini. Ilishauriwa kuwa Idara ya Utumishi ya Walimu iimarishwe kwa ajili ya

kutoa huduma na maslahi bora ya walimu. Vilevile imebainika kuwa Masomo ya Elimu

ya msingi yapunguzwe na mkazo uwekwe kwenye KKK katika madarasa ya kwanza

hadi la tatu. Aidha, Somo la English Language liimarishwe katika ngazi ya Elimu ya

msingi na sekondari. Pia ilipendekezwa kuwa lugha ya kufundishia na kujifunzia iwe

moja katika ngazi ya msingi na sekondari.

Ilishauriwa viongozi wa elimu wafanye ziara za mara kwa mara na za kushtukiza

shuleni ili kujionea uendeshaji wa elimu unavyoendelea, Serikali idhibiti ufundishaji

holela wa masomo ya ‘tuition’ . Aidha, kuwepo na mfumo wa wazi wa tathmini ya

utendaji kazi (OPRAS). Kuhusu wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito ilipendekezwa

kuwe na mfumo unaowaruhusu kuendelea na masomo na kanuni za utoaji wa adhabu

zinazoendana na makosa ziangaliwe upya. Pia ilipendekezwa kuwa viboko virudishwe

shuleni kwani kukataza viboko kumeshusha nidhamu ya wanafunzi. Utafiti umebaini

kwamba maeneo mbalimbali ya kisera kuhusu mfumo wa elimu, maslahi ya walimu

na uongozi na uendeshaji wa elimu zina mapungufu ya kiutendaji.

b) Kuimarisha Mwamko wa Jamii Katika Elimu

Katika kuimarisha mwamko wa elimu kwa jamii wadau wote wahamasishwe ili

waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya elimu nchini. Aidha, imependekezwa

kuwa jamii ihamasishwe kubaini vipaji vya watoto tangu wakiwa wadogo na

wahimizwe kusoma kwa bidii. Wazazi wahamasishwe kuchangia elimu ikiwa ni pamoja

na kulipa ada kwa wakati na jukumu lao kwa watoto wao hususani kuwasomesha

watoto wa kike na wale wenye mahitaji maalumu.

Maoni yaliyotolewa yanadhihirisha kuwepo kwa mwamko duni wa jamii katika

kuchangia maendeleo ya elimu. Aidha, suala la uhamasishaji wa jamii kuchangia

elimu linahitaji utayari na ushirikiano wa wanasiasa.

www.JamiiF

orums.com

Page 75:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

74

c) Kukabiliana na Mmomyoko wa Maadili ya Walimu na Wanafunzi Shuleni

Kuhusu mmomonyoko wa maadili wajibuji walishauri kwamba, walimu wazingatie

kanuni, taratibu na maadili ya kazi yao. Pia wazazi, walimu, mashirika ya dini na

mashirika yasiyo ya kiserikali wahimize nidhamu ya wanafunzi kwa maendeleo ya

taaluma. Aidha, wanafunzi wanasihiwe kuhusu madhara ya kutumia madawa ya

kulevya, kuvuta sigara, na kwenda katika sehemu za starehe. Zaidi ya hayo walitoa

maoni kwamba hatua kali zichukuliwe kwa walimu na jamii wanaojihusisha kimapenzi

na wanafunzi, pia kianzishwe kitengo cha ushauri nasaha na unasihi ili kuwasaidia

wanafunzi kuwa na maadili mema. Walishauri kuwa jamii iwaheshimu walimu na

kuthamini kazi yao. Vilevile, ilipendekezwa kwamba adhabu ya viboko irejeshwe

shuleni. Maoni haya yanaonesha kuwa suala la maadili halishughulikiwi kikamilifu

katika uendeshaji wa elimu nchini. Madhara ya wadau wa elimu kutotilia mkazo suala

la maadili katika usimamizi na uendeshaji wa elimu kunasababisha kuwepo kwa jamii

na viongozi wasio na uzalendo, uadilifu na uwajibikaji katika kuleta maendeleo nchini.

d) Kuboresha Bajeti ya Elimu

Maoni yalitolewa kuwa ufinyu wa Bajeti ya Elimu na matumizi yasiyoendana na

thamani ya fedha inayotolewa husababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa

Mtihani wa Taifa. Vilevile, ilielezwa kuwa ruzuku ya maendeleo na uendeshaji wa

shule za sekondari ni ndogo hivyo ilishauriwa kuwa bajeti iongezwe ili kuwepo na

vitendea kazi vya kutosha na mishahara mizuri ya walimu. Aidha, fedha ya ruzuku ya

uendeshaji itolewe yote na ipatikane kwa wakati kama miongozo inavyoelekeza (SEDP

II, 2010). Walishauri kuwa, maeneo yenye changamoto nyingi za kielimu yapewe

kipaumbele katika mgao wa rasilimali watu na fedha, pia imesisitizwa kuwepo

usimamizi wa matumizi ya fedha yanayoendana na thamani ya kazi. Upatikanaji,

mgawanyo kulingana na mahitaji na matumizi ya fedha za ruzuku bado ni

changamoto katika uendeshaji wa elimu nchini.

e) Kuitumia Siasa katika Maendeleo ya Elimu

Maoni yaliyotolewa yameonesha kuwa jamii inathamini mchango wa wanasiasa katika

kuchochea maendeleo ya elimu. Ilishauriwa kuwa, Walimu na wanafunzi watumie

www.JamiiF

orums.com

Page 76:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

75

muda mwingi katika kufundisha na kujifunza badala ya kujishughulisha na masuala ya

kisiasa. Pia walisema, mambo muhimu ya kitaalamu kuhusu elimu yatokane na

ushauri wa wataalamu. Hivyo, maamuzi yote ya mipango na utekelezaji wa elimu

yatokane na tafiti na ushauri wa kitaalam.

4.2.7.Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka 2010

Mapendekezo juu ya nini kifanyike kwa wanafunzi walioshindwa Mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4 mwaka 2010 yalitolewa na wadau wa elimu 2,636 kati ya 3,037

waliohusishwa katika utafiti huu. Mapendekezo yaliyotolewa yamelenga katika

maeneo manne yaani kurudia mtihani kama watahiniwa wa kujitegemea, kukariri

darasa na kufanya mtihani kama watahiniwa wa shule, mtihani usahihishwe upya na

wahitimu kupatiwa mafunzo stadi kama inavyooneshwa katika Kielelezo Na. 4.5

Kielelezo Na. 4.5 Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka 2010

Chanzo: Data za Utafiti, 2011

a) Kuwapa Mafunzo Stadi

Wadau waliohojiwa walipendekeza kuwa wahitimu wote walioshindwa wapatiwe

mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vinavyotambuliwa na VETA ikiwemo VETA

yenyewe. Mafunzo hayo yalenge stadi za maisha na ujasiriamali kama vile ufugaji,

uvuvi, useremala na stadi zingine za maisha ikiwemo elimu ya UKIMWI. Pia

ilipendekezwa kuwa serikali iimarishe vyuo hivyo na kugharamia mafunzo hayo.

b) Kupewa Fursa ya kurudia mtihani kama watahiniwa wa kujitegemea

www.JamiiF

orums.com

Page 77:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

76

Walipendekeza kwamba, wahitimu warudie mitihani kama watahiniwa wa kujitegemea

kulingana na utaratibu uliopo. Ilishauriwa kwamba miundombinu iboreshwe ili

watahiniwa waliopo katika mazingira magumu waweze kupata fursa ya kufanya

mtihani.

c) Kukariri Darasa na Kufanya Mtihani wa Taifa Kama Watahiniwa wa

Shule

Wadau walipendekeza kuwa watahiniwa waruhusiwe kukariri kuanzia kidato cha tatu

kama wanafunzi wa kawaida shuleni ili waweze kupata ujuzi wa kutosha kuweza

kufanya mitihani. Pia ilipendekezwa kuwa watakaokariri wasome masomo ya jioni

badala ya muda wa kawaida wa shule.

Suala la kukariri darasa katika mfumo wowote wa elimu linaonesha kutokuwepo kwa

ufanisi wa ndani (internal efficiency) katika ngazi husika ya elimu. Ili kuepuka kufeli

kwa watahiniwa wengi kama ilivyojitokeza katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4

mwaka 2010, kuna haja ya kuimarisha ufanisi wa ndani katika ngazi zote za elimu.

d) Kusahihisha Mitihani Upya

Mapendekezo yalitolewa kuwa zoezi la usahihishaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha

4 mwaka 2010 ilirudiwe kwa kuwa usahihishaji haukuwa makini. Aidha ilishauri

kwamba, uchunguzi wa usahihishaji wa mitihani hiyo ufanyike kubaini mapungufu

yaliyojitokeza.

4.3. Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala

4.3.1. Utayarishaji wa MitaalaMtaala ni orodha ya maarifa ambayo mwanafunzi anatarajiwa kuyapata na namna

yanavyopangiliwa ikiwa ni pamoja na fursa za kujifunza maarifa hayo (HakiElimu,

2011). Utayarishaji wa mtaala ni mchakato unaotakiwa kuwahusisha wadau wote wa

elimu. Vilevile, mabadiliko au maboresho ya mtaala yanatakiwa kuzingatia mahitaji ya

jamii husika. Aidha, Mihtasari ya masomo ni nyenzo muhimu ya mtaala katika

kupanga na kukamilisha mchakato wa kufundishia na kujifunzia na humsaidia

mwalimu kufahamu mada mbalimbali zinazotakiwa kufundishwa katika darasa na

somo husika.

www.JamiiF

orums.com

Page 78:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

77

Jukumu la kuandaa mitaala ni la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na hufanywa

kulingana na mzunguko kwa kila ngazi ya elimu ambapo elimu ya msingi ni miaka

saba na sekondari ni miaka sita. TET huandaa, huboresha na kuchapisha mitaala na

mihtasari ya masomo ya elimu ya sekondari na vyuo vya ualimu na huhakikisha

kwamba inakuwepo shuleni. Utafiti umebaini kutokuwepo kwa ushirikishwaji toshelevu

wa wadau katika maandalizi ya mtaala hususan katika hatua za utayarishaji na

ujaribishaji wa mitaala (piloting). Kutojaribishwa kwa mtaala unaotumika

kumesababisha kutobainika kwa mapungufu yaliyopo kwa wakati. Hivyo mtaala

unaotumika una changamoto za utekelezaji unaothiri mchakato wa ufundishaji na

ujifunzaji. Hii inathibitisha kutozingatia hatua za utayarishaji wa mtaala kama

ilivyoinishwa katika Mwongozo wa Ukuzaji Mitaala-NCDF (TIE, 2003).

4.3.2. Uwepo wa Mihtasari Shuleni na VyuoniMahitaji muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ni uwepo na upatikanaji

wa mihtasari ya masomo shuleni kwa ajili ya matumizi ya walimu na wanafunzi.

Utafiti umebaini kuwa jukumu la usambazaji wa mihtasari shuleni baada ya

kuchapishwa siyo la TET. Wakuza mitaala waliohojiwa walieleza kuwa TET haihusiki

na jukumu la usambazaji wa mihtasari ya masomo katika shule za sekondari nchini.

Aidha, waliongeza kuwa hakuna mwongozo unaobainisha msambazaji wa mihtasari

katika ngazi ya shule. Vilevile walithibitisha kuwa, mihtasari huwa inauzwa na TET

kwa wanaoihitaji na kwa shule pia.

Kielelezo Na.4.6: Upungufu wa Mihtasari

Chanzo: Data za Utafiti, 2011

www.JamiiF

orums.com

Page 79:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

78

Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa idadi ya mihtasari ya masomo iliyoboreshwa

mwaka 2005 na 2007 iliyopo katika shule za utafiti haitoshelezi mahitaji kama

inayooneshwa katika Kielelezo Na.4.6. Utafiti umebaini uwepo wa upungufu wa

mihtasari, ambapo masomo ya Mathematics na Geography yameongoza kwa kuwa na

upungufu kwa zaidi ya asilimia 50.

Aidha, katika vyuo vya ualimu, utafiti ulibaini kuwa asilimia 61.3 (62) ya waliohojiwa

juu ya uwepo na matumizi ya mihtasari iliyoboreshwa katika vyuo walisema, mihtasari

iliyoboreshwa ipo vyuoni lakini ni kwa ajili ya wakufunzi tu na asilimia 38.7 walisema

mihtasari haipo. Hata hivyo WEMU imeweka mihtasari ya mafunzo ya ualimu katika

tovuti (website). Hivyo utafiti umebaini kuwa, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa

mihtasari na miongozo ya mitaala (curriculum documents) kutoka kwa mtayarishaji

mpaka kwa mtumiaji katika shule za sekondari.

4.3.3. Utekelezaji wa MtaalaUtekelezaji wa mtaala ni jukumu la mwalimu shuleni. Matokeo ya utafiti yameonesha

kuwa wajibuji 152 kati ya 1,092 sawa na asilimia 14 wamebainisha kuwepo kwa

mapungufu katika utekelezaji wa mtaala na kwamba walimu wengi hawana maarifa

na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari ulioboreshwa. Aidha, utafiti umebaini

kuwa dhana ya mtaala unaozingatia ujuzi haijaeleweka vizuri kwa wadau mbalimbali

wakiwemo baadhi ya wakuza mitaala na maafisa mitihani.

Mapungufu yaliyoainishwa na wajibuji ambayo yanakwamisha utekelezaji wa mtaala

kwa ufanisi ni pamoja na maboresho ya mitaala kufanywa bila kuwa na maandalizi ya

kutosha; kufanyika kwa kiwango kidogo cha mafunzo kabilishi; upungufu wa vitabu;

ukosefu wa fedha kwa ajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu; ubovu wa

miundombinu na uelewa mdogo wa lugha ya Kiingereza kwa walimu na wanafunzi.

Mapungufu hayo yamesababishwa na kutokuwepo kwa maandalizi ya kutosha kama

ilivyofafanuliwa katika mwongozo wa ukuzaji mitaala (NCDF TIE, 2003). Hali

inayosababisha tofauti ya uelewa baina ya walimu kuhusu mahitaji ya mtaala, hali

inayosababisha baadhi yao kutoutekeleza ipasavyo na hivyo kuwa chanzo cha

kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

www.JamiiF

orums.com

Page 80:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

79

4.3.4. Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala UlioboreshwaUtafiti ulitaka kufahamu kuhusu mafunzo kabilishi yanayotolewa kwa walimu kwa ajili

ya mtaala ulioboreshwa na ulibaini kuwa, TET ndiyo yenye jukumu la kutoa mafunzo

hayo. Utafiti umebaini kuwa taarifa zilizotoka kwa wakaguzi wa kanda zote za elimu

kuhusu mafunzo kabilishi ni kwa walimu 1,088 ambao wametoka katika shule za

sekondari 192 tangu mwaka 2008 hadi 2010 na yalitolewa kwa walimu wa masomo

yote toka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Hii ni sawa na asilimia 2.7 ya idadi ya

walimu wote 40,517 kitaifa kwa mwaka 2010. Hali hii ilithibitishwa na walimu 613

(asilimia 92) ya waliohojiwa ambao hawakupata mafunzo kabilishi. Aidha, asilimia 8 ya

walimu waliopata mafunzo kabilishi walieleza kwamba mafunzo hayo yalitolewa

kupitia Chama cha Hisabati Tanzania, TAHOSSA na kutoka kwa walimu wenzao. Hii

iliungwa mkono na wakaguzi wa shule na wakuu wa shule waliobainisha kuwa

mafunzo kabilishi hayajafanyika kwa walimu wengi na kwamba walimu wana utayari

mdogo wa kutumia mihtasari iliyoboreshwa.

Taarifa ya TET, (2011) katika kipindi cha mwaka 2007 hadi 2010 inathibitisha kuwa

mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa yalitolewa ni ya kiwango kidogo kwa vile

ni walimu 833 tu waliopata mafunzo kabilishi kitaifa. Hali hii inaashiria ugumu wa

walimu kutekeleza kwa ufanisi mitaala ya sekondari ya 2005 na 2007 na hivyo

kuwafanya wanafunzi kutofaulu mitihani ya Taifa.

Hivyo basi watekelezaji mitaala kama vile walimu, wapewe mafunzo kabilishi ili

kuwaimarisha katika utendaji kazi wao. Hii ni pamoja na kupata fursa ya mabadiliko

ya mtaaala na kupata dhana na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji (Moduli ya Ujuzi

wa Kufundisha kwa Umahiri: WEMU, 2010).

4.3.5. Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala Ilipendekezwa kuwa mafunzo kabilishi yatolewe kwa walimu na wakufunzi wakati wa

mabadiliko au maboresho ya mtaala. Ilisisitizwa kuwa Mihtasari ya masomo

isambazwe shuleni mapema kila inapotokea maboresho na mabadiliko ya mtaala

yazingatie mahitaji ya jamii. Vilevile, ilielezwa ni muhimu kuwepo na muendelezo wa

mtaala wa shule za msingi na sekondari. Aidha, mahusiano kati ya wakuza mitaala,

maafisa mitihani na walimu yaimarishwe wakati wa maboresho na utekelezaji wa

www.JamiiF

orums.com

Page 81:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

80

mtaala ili kuleta ufanisi katika utoaji wa elimu. Pia ilipendekezwa kuwa mitaala ya

elimu ya ualimu iboreshwe hususan katika maeneo ya malezi na maadili. Waliongeza

kuwa mtaala wa elimu ya msingi uboreshwe hususan katika stadi za Kusoma,

Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Aidha, ilishauriwa kuwa mtaala wa ufundi utayarishwe kwa elimu ya msingi na

ufundishwe kwa wanafunzi wa shule za msingi ili kuwaongezea fursa za kuajiriwa,

kujiajiri au kuendelea na masomo.

4.4. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa

Mfumo na taratibu za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 unahusisha mchakato wa

utungaji, uhakiki, usambazaji, usimamizi, usahihishaji na upangaji wa madaraja.

Utafiti ulifanyika ili kuelewa ufahamu wa wadau juu ya mchakato na taratibu za

mtihani na athari zake katika ufaulu.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa taratibu za uendeshaji na usimamizi wa Mtihani

wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka 2010 ni mojawapo ya sababu zilizotajwa

kusababisha kushuka kwa ufaulu. Aidha ilibainishwa kuwa, utungaji wa mtihani,

usambazaji na usimamizi; usahihishaji, upangaji wa madaraja; matumizi ya miongozo

na nyaraka; Mchango wa alama za mazoezi endelezi (Continuous Assesssment-CA) na

athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni masuala yaliyoathiri kiwango cha ufaulu.

4.4.1. Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4Utungaji wa mtihani wa taifa unapaswa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na utaratibu

wa NECTA ulio kwenye mwongozo uitwao Certificate of Secondary Examination

Format, 2008. Aidha utungaji unapaswa kuzingatia mwongozo wa upimaji na utahini

wa mtaala ulioboreshwa.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa lugha ya Kiingereza inayotumika kufundishia

elimu ya sekondari ni kikwazo kwa wanafunzi katika kuelewa kwa kina maudhui ya

somo na maswali. Katika mahojiano na wahitimu wa kidato cha 4 mwaka 2010,

asilimia 46 ya wanafunzi waliohojiwa walieleza kuwa misamiati iliyotumika kwenye

www.JamiiF

orums.com

Page 82:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

81

mtihani wa taifa haikufanana na ile iliyotumika kwenye mitihani ya kawaida ya

darasani. Mwanafunzi mmoja alisisitiza:

“Suala la wingi wa misamiati migumu na maswali mengi yenye lugha ya

kuchenga na yenye maelezo marefu yanatuchanganya. Hata walimu

wanaingia darasani wanatufundisha somo la English kwa kiswahili”.

Uelewa mdogo wa lugha ya kufundishia ni changamoto kwa watahiniwa katika

kuelewa maswali ya mitihani ya taifa.

Katika majadiliano ya pamoja na walimu ilithibitishwa kuwa lugha ya kiingereza ni

tatizo kubwa kwa walimu na wanafunzi. Kutokana na majadiliano hayo ya pamoja

inadhihirisha kuwa lugha ya Kiingereza haitumiki ipasavyo katika mchakato wa

kufundishia na kujifunzia. Tatizo hili linasababisha wanafunzi kushindwa kuelewa

kinachoulizwa katika maswali ya mtihani, kushindwa kujieleza kwa ufasaha na

hatimaye kufanya vibaya katika mtihani. Wahitimu 131 (33%) kati ya 401 wa kidato

cha 4 mwaka 2010 walithibitisha kuwa mtihani ulizingatia vigezo vilivyoainishwa

kwenye miongozo ya mitihani (Examination Formats) iliyoandaliwa na NECTA. Aidha,

asilimia 12 walieleza kuwa maswali ya mtihani katika baadhi ya masomo yalifuata

muundo wa mtihani wa taifa wakati masomo ya Kiswahili, Kemia, Historia na Jiografia

hayakufuata muundo. Hali hii ilichangia wanafunzi kushindwa kujibu inavyostahili.

Walimu walioshiriki kwenye majadiliano ya pamoja walieleza kuwa mtihani ulilenga

kupima uwezo wa wanafunzi katika kufikiri na uelewa wa dhana, hii ni tofauti na jinsi

walivyofundishwa darasani ambapo ufundishaji ulizingatia wanafunzi kujibu maswali.

Mwalimu mmoja alisisitiza kwa kusema:

“Utungaji wa Mtihani ulizingatia mtaala ulioboreshwa tatizo ni maandalizi

mabovu ya wanafunzi kwa kuwa walimu wengi tunaowafundisha watoto

hatujaelewa vizuri ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana”.

Matokeo haya yanaonesha kuwa wanafunzi wengi hawakufanya vizuri katika mitihani

kwa sababu ulipima malengo ya mtaala unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana

(Competence Based Curriculum) badala ya ule unaozingatia maarifa (Content Based

Curriculum).

Baadhi ya walimu wakati wa majadiliano ya pamoja waliwalaumu watungaji wa

mitihani kwa kueleza kuwa baadhi ya maswali yalitungwa nje ya mihtasari

www.JamiiF

orums.com

Page 83:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

82

iliyoboreshwa. Masomo hayo ni History, Geography, Physics na Mathematics. Mwalimu

mmoja alinukuliwa kwa kusema:

“…mtihani wa Historia ulikuwa na swali lililoulizwa ambalo halikutokana na

mada zilizopo kwenye muhtasari. Mada hiyo ni “Factors contributing to the

rise of Oyo Empire.”

Hivyo, utungaji wa maswali katika mtihani nje ya muhtasari yanakiuka taratibu za

utahini.

TET na NECTA wana jukumu la kuhakikisha kuwa mitihani inayotungwa inaendana na

maudhui yaliyo katika mtaala husika. Maoni yaliyotolewa na TET na NECTA katika

utafiti yamethibitisha kwamba upo udhaifu katika utungaji wa mitihani na kwamba

utungaji hauendi sambamba na mtaala ulioboreshwa katika baadhi ya masomo.

Utafiti umebaini kuwepo kwa tatizo la utungaji wa mtihani wa taifa linalochangiwa na

matumizi ya lugha ya kufundishia na kujifunzia, walimu kutofahamu ufundishaji wa

mtaala ulioboreshwa na utunzi wa mtihani usioendana na mahitaji ya mihtasari.

4.4.2. Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4Usambazaji na usimamizi wa mitihani ni muhimu katika mchakato wa uendeshaji wa

mitihani na unahitaji maandalizi mazuri, uadilifu na umakini ili kuhakikisha kuwa

taratibu zinafuatwa na haki inatendeka kwa kila mtahiniwa. Matokeo ya utafiti

yamebainisha kuwepo kwa mazingira yasiyoridhisha ya usimamizi wa mitihani, uwepo

wa askari polisi wenye silaha na wasimamizi kutumia lugha ya vitisho au/na

kuwakaripia watahiniwa wakati wa mitihani. MaafisaElimu wilaya 32 (73%) kati ya 42

waliohojiwa walisema kuwa, utaratibu wa usambazaji na usimamizi wa mitihani uliopo

ni mzuri, hivyo umepunguza undanganyifu wa mitihani. Hata hivyo, imebainishwa

kuwa baadhi ya wanafunzi wanaotegemea uvujaji na wizi wa mitihani husababisha

wasijiandae ipasavyo kwa matarajio ya kufanya undanganyifu.

Kwa upande mwingine, walishauri kuwa ulinzi wa mitihani uimarishwe na posho ya

wasimamizi iongezwe ili kuendelea kuzuia mianya ya uvujaji wa Mitihani. Pia,

ilipendekezwa kujenga vyumba imara vya kuhifadhia mitihani (strong rooms) na

kumbi za kufanyia mitihani ili watahiniwa wafanyie mitihani katika eneo moja kwa

lengo la kurahisisha usimamizi. Vilevile walisisitiza kuwa fedha za usambazaji na

www.JamiiF

orums.com

Page 84:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

83

usimamizi wa mitihani zipelekwe mapema kwenye Halmashauri husika ili kurahisisha

maandalizi.

Vilevile, katika majadiliano ya pamoja na maafisa mitihani ilibainishwa kuwa baadhi ya

wasimamizi hawana sifa na hawafuati maelekezo ya usimamizi wa mitihani hivyo

kusababisha usumbufu kwa watahiniwa. Aidha, maafisa mitihani waliendelea kusema

kuwa watahiniwa wanaochelewa kujisajili husababisha usumbufu wa mwingiliano wa

namba za mtihani wakati wa usimamizi.

4.4.3. Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4Usahihishaji unapaswa kufanywa kwa uadilifu, uaminifu na umakini mkubwa ili kutoa

matokeo sahihi na ya haki kwa kila mtahiniwa. Katika mahojiano ya pamoja na walimu

wasahihishaji ilielezwa kuwa kutokuwepo kwa umakini katika zoezi la usahihishaji wa

mitihani kunatokana na malipo kidogo na kutumia muda mrefu wa kusahihisha kwa

siku. Wakuu wa shule na walimu wasahihishaji wa mitihani ya taifa walibainisha kuwa

baadhi ya wasahihishaji hawana sifa ya kusahihisha mitihani hiyo. Hii inadhihirisha

kuwa zipo kasoro za uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule ambapo baadhi ya

wakuu wa shule huteua walimu wasio na sifa stahili. Mwalimu ambaye hajawahi

kusahihisha mtihani alisema:

“uteuzi unategemea maelewano kati ya mwalimu na mkuu wa shule au

kama unatoa pesa kwa mkuu wa shule unaweza kuchaguliwa hata kama

hilo somo unaloenda kusahihisha hulifundishi darasani. Baadhi ya wakuu

wa shule hujichagua wao wenyewe au kuchagua walimu kwa mazoea,

undugu na urafiki, pia kuna walimu wa kudumu kwenye usahihishaji”

Hali hii inathibitishwa na NECTA ambapo huwarudisha walimu wasio na sifa kutoka

katika vituo vya kusahihishia, hivyo kusababisha usumbufu na kuathiri mchakato wa

usahihishaji.

Walimu waliowahi kusahihisha mitihani, walibainisha changamoto ya utaratibu wa

malipo kwa wasahihishaji kuwa malipo ni madogo kiasi kwamba yanawavunja moyo

wasahihishaji na wakati mwingine kulazimika kusahihisha haraka ili wamalize karatasi

za watahiniwa kwa muda mfupi. Katika kutilia mkazo hoja hii mwalimu mmoja

alieleza:

www.JamiiF

orums.com

Page 85:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

84

“Malipo ya walimu wasahihishaji hufanywa kwa kuzingatia idadi ya

karatasi za watahiniwa zilizosahihishwa wakati tunapaswa kulipwa posho

ya siku nje ya kituo cha kazi (Per- diem)”.

Walimu wengine walieleza kuwa mazingira ya kazi ya usahihishaji ni magumu hususan

uchafu wa vyoo na malazi; na ubovu wa huduma za chakula zinazopelekea

kutokuwepo kwa utulivu unaohitajika katika kazi muhimu ya usahihishaji. Vilevile,

katika majadiliano ya pamoja walimu walionesha masikitiko yao kwa kusema kuwa

kuna vitisho na manyanyaso kutoka kwa maafisa wa NECTA. Hali hiyo hujenga hofu

kwa msahihishaji na wakati mwingine kumvunja moyo na kushindwa kufanya kazi

ipasavyo.

Pia, walimu waliosahihisha mitihani ya kidato cha 4 walionesha kutoridhishwa na hali

ya kutoruhusiwa kusahihisha mwongozo wa usahihishaji kabla ya kuanza kuutumia

hata kama una makosa. Vilevile ilielezwa kuwa, wakati mwingine hutokea mapungufu

katika mwongozo wa usahihishaji lakini fursa ya kurekebisha haitolewi ipasavyo kwa

wasahihishaji. Hata hivyo, Maafisa Mitihani walieleza kuwa miongozo ya usahihishaji

hujadiliwa na paneli za masomo husika kabla ya kuanza usahihishaji.

Matokeo ya utafiti yamebaini kwamba, NECTA huandaa miongozo ya usahihishaji

iliyosanifiwa ipasavyo na kupeleka kwenye vituo vya usahihishaji, viongozi wa vikundi

pamoja na wasahihishaji wote hupewa nafasi ya kupitia mwongozo wa somo husika ili

kuelewa swali na majibu stahiki kabla ya kufanya jaribio la usahihishaji (trial marking)

kwa lengo la kubaini uelewa wa kila msahihishaji. Baada ya majadiliano ya jaribio la

usahihishaji, wasahihishaji wote hupitia mwongozo wa usahihishaji na kupata

mwongozo wa usahihishaji ulioboreshwa (standardized marking scheme) ambayo

hutumika katika usahihishaji (NECTA, Juni 2011).

Hoja ya usahihishaji wa kutokuwa makini inatofautiana na hali halisi kuhusu umakini

wa usahihishaji kama ilivyoelezwa na wajibuji wa NECTA. Mkanganyiko huu unaweza

kutafsiriwa kwa kuzingatia mazingira yanayotawala zoezi la usahihishaji. Kwa mfano

utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’ walizosahihisha badala ya

www.JamiiF

orums.com

Page 86:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

85

posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji kwa siku ni baadhi ya masuala

yanayoweza kuathiri umakini wa usahihishaji.

Matokeo ya utafiti, yanathibitisha kuwa kuna kasoro na ukiukwaji wa vigezo vya uteuzi

wa walimu wasahihishaji na mazingira magumu ya usahihishaji unaosababisha

usahihishaji usiokuwa makini na kupoteza haki za watahiniwa. Kutofautiana kwa

uwepo wa fursa ya kutosha katika kujadili miongozo ya usahihishaji katika paneli za

masomo husika kunaweza kuwanyima haki baadhi ya watahiniwa.

4.4.4. Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-CA) Katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4

Kutokana na mwongozo wa NECTA, ufaulu wa mwanafunzi katika mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4 unapimwa kwa kutumia alama za mazoezi endelezi (45%), projekti (5%)

na alama za mtihani wa mwisho (50%).

Matokeo ya utafiti yamethibitisha kuwa CA zinazowasilishwa NECTA zinajumuisha

alama za mitihani ya mihula ya kidato cha 3 na kidato cha 4 muhula wa kwanza.

Walimu walieleza kuwa alama za CA zinazowasilishwa NECTA hazitumiki, iwapo

zingetumika kusingekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli (mass failure). Hata

hivyo mwalimu mmoja wakati wa mahaojiano ya pamoja alisema:

“Hakuna mwenye uhakika kama CA zinatumika, tunajiliuza kuwa ikiwa

zinatumika vizuri kwanini watoto wamefeli masomo na kupata daraja la zero”

Aidha, Maafisa Mitihani wa NECTA walithibisha kuwa mwongozo wa mchango wa CA

ni 50% (45% ni mazoezi ya darasani na mitihani ya mihula na wa taifa Kidato cha 2

na 5% ya kazi mradi/projecti) hautekelezwi ipasavyo kwa kuwa umebuniwa mfumo

mbadala ambao unazingatia vingezo vingine. Vigezo hivyo ni pamoja na kufanya

ulinganifu sanifu (standardization) kwa kutumia alama za mwisho za mtahiniwa

(Candidates’ Final Written Examination marks) kama ilivyofafanuliwa katika taarifa ya

Miaka 30 (1973-2003) ya NECTA (NECTA, 2004). Mchakato wa kuzitumia CA kwa

ulinganifu sanifu ni mgumu na haueleweki kwa wadau, hoja hii ilithibitishwa na

Maafisa Mitihani katika majadiliano ya pamoja kuwa hawaufahamu mfumo huo.

www.JamiiF

orums.com

Page 87:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

86

Matokeo ya utafiti yameonesha kuwepo kwa changamoto zinahusu upatikanaji na

matumizi ya CA kwenye matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4. Miongoni mwa

changamoto hizo ni pamoja na shule kuchelewa kuwasilisha CA kwenda NECTA, CA

zinazowasilishwa kutokuwa na uhusiano wa karibu na alama za mtahiniwa za Mtihani

wa Taifa wa Kidato cha 4 na uelewa mdogo wa wadau kuhusu mchango wa CA

katika mtihani wa Taifa.

Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa NECTA haitumii CA kama ilivyoelekezwa katika

mwongozo (Continuous Assessment Guidelines on the Conduct and Administration of

Continuous Assessment in Secondary Schools and Teacher Training Colleges-1990).

Aidha udanganyifu wa CA pamoja na uhusiano mdogo wa alama za CA na alama za

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 katika shule nyingi unaathiri ufaulu wa watahiniwa.

4.4.5. Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTAMatokeo ya mtihani yanatolewa kwa viwango vya ufaulu kwa kila somo na kwa kila

mtahiniwa. Viwango vya ufaulu hupangwa katika madaraja ya I, II, III, IV na 0. Ili

kupata maoni ya wadau wa elimu kuhusu namna upangaji wa madaraja katika

matokeo ya mitihani ya taifa ya kidato cha 4, wakuu wa shule, wahadhiri wa vyuo

vikuu na wanachuo wa vyuo vikuu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu tarajali,

walimu, wahitimu na wanafunzi walishirikishwa.

Jumla ya walimu 613 waliohusika katika majadiliano ya pamoja walieleza kuwa

upangaji wa madaraja unafaa na unawafanya watahiniwa kujitahidi ili waweze kupata

madaraja mazuri. Hoja hii pia iliafikiwa na wakufunzi na wanachuo kwa kushauri

yafanyike marekebisho kwa kupanua msambao wa madaraja na pia nafasi kati ya

daraja moja na jingine zifanane. Vilevile jumla ya wakuu wa shule 109 (82.6%) kati ya

132 walisema kwamba, upangaji wa madaraja unafaa na kwamba uendelee kama

ulivyo kwani madaraja yanaleta ushindani miongoni mwa watahiniwa na hata kujenga

nidhamu ya kusoma.

Aidha, wanafunzi 1140 wa kidato cha 3 na 4 walioshiriki katika mahojiano ya pamoja

walitofautiana kuhusu upangaji wa madaraja, baadhi yao waliafiki na wengine

kukataa utaratibu wa upangaji wa madaraja unaotumika. Wanafunzi ambao

hawakuafiki, walisema hawakubaliani na upangaji wa madaraja kwa sababu hautoi

www.JamiiF

orums.com

Page 88:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

87

haki kwa watahiniwa. Mfano kutoa adhabu kwa wale wanaofeli somo la Hisabati au

Kiswahili kwa kushushwa madaraja.

Utafiti pia umebaini kuwa kuna tofauti ya uelewa kuhusu alama za gredi zinazotolewa

kwa watahiniwa. Aidha, uzoefu wa miaka mingi unaonesha kuwa Gredi zinatolewa

kwa kuzingatia mlolongo wa alama zifuatazo: A (81-100), B (61-80), C (41-60), D (21-

40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa alama za gredi zinazotolewa kwa

watahiniwa huamuliwa na jopo la wasahihishaji wa somo husika kwa kuzingatia

kiwango cha ufaulu kwa mwaka husika na hivyo hakuna alama maalum zilizowekwa

kwa kila gredi. Pia NECTA ilibainisha kuwa gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si

chini ya alama 70.

Kutokana na matokeo ya utafiti huu, wadau wengi wamekubaliana na upangaji wa

madaraja uliopo sasa. Hata hivyo, kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu

baina ya shule na NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama na gredi,

hivyo kuathiri ufaulu wa watahiniwa. Aidha, wanafunzi na walimu wakati wa

majadiliano ya pamoja ya wamelalamikia utaratibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania

kutoa adhabu kwa walioshindwa kufaulu masomo ya Mathematics na Civics kwa vile

unalazimisha wanafunzi kusoma masomo wasiyoyapenda na wasiyokuwa na uwezo

nayo. Hali hiyo inaonesha kuwa kuna mapungufu ya kuadhibu watahiniwa kwa

kuwateremsha daraja la I au la II kuwa la III kutokana na kufeli baadhi ya masomo

ya msingi na ya mchepuo. Hata hivyo kulingana na kanuni za mitihani za mwaka 2006

za NECTA, hakuna kipengele chochote kinachobainisha adhabu hiyo.

Pamoja na juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia

kama ilivyobainishwa katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya

kwanza na ya pili, bado kuna changamoto za uwepo wa walimu wa kutosha na vifaa.

Hivyo, kuwaadhibu watahiniwa ni kinyume na uhalisia wa mazingira ya kufundishia na

kujifunzia yenye uhaba wa vifaa na walimu hususani kwa somo la mathematics.

Usimamizi na uendeshaji wa mitihani ya Taifa unaonesha mapungufu katika matumizi

ya CA na upangaji wa madaraja tofauti na ilivyoelekezwa na Sera ya Elimu na

Mafunzo, 1995 ibara ya 6.18 pamoja na Mwongozo wa NECTA wa Mazoezi Endelezi

wa 1990.

www.JamiiF

orums.com

Page 89:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

88

4.4.6. Matumizi ya Miongozo na Nyaraka MitihaniUtafiti huu ulilenga kubaini usambazaji na utekelezaji wa miongozo, nyaraka na

machapisho ya elimu na mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Ilibainishwa kwamba

nyaraka, miongozo na mihtasari ya masomo kutoka Wizara ya Elimu huwafikia wakuu

wa shule kupitia ofisi za maafisaelimu na mikutano ya TAHOSSA kwa ajili ya

utekelezaji. Aidha, jukumu la NECTA ni kusambaza shuleni miongozo na machapisho

yanayohusu uendeshaji wa mitihani ya Taifa kama vile muundo (format) na kanuni za

mitihani kupitia Maafisaelimu wa Mikoa.

Utafiti umebaini kuwa, asilimia 67 ya walimu 613 katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti

walieleza kuwa hupokea muundo na kanuni za mitihani na kuzitumia katika kutunga

mazoezi ya darasani na mitihani ya ndani. Hata hivyo asilimia 33 ya walimu walieleza

kuwa hawajawahi kuuona na kuutumia muundo wa mtihani wa Taifa kwa kuwa

machapisho na nyaraka zinazotoka NECTA zinakuwa na usiri mkubwa. Hayo

yalithibitishwa na mmoja wa maafisa mitihani wa NECTA kwa kusema:

“....Nimefundisha shule ya sekondari kwa muda wa miaka kumi na

sikuwahi kuiona format ya mtihani mpaka nilipofika NECTA......”

Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi hawapati fursa ya kuiona

na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika shule za sekondari. Uwepo wa

Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani katika shule ni muhimu katika

kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote wanapaswa kupata na kutumia

machapisho hayo.

4.4.7. Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 hutoa tathmini ya kati ya elimu ya

sekondari ya kawaida ili kupata picha ya maendeleo ya wanafunzi kitaifa kabla ya

mtihani wa kidato cha nne. Mojawapo ya malengo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha

2 ni kupata alama zenye uwiano wa kitaifa kwa ajili ya kupima maendeleo ya

wanafunzi ambazo zitatumiwa na NECTA ikiwa ni sehemu ya mazoezi endelezi ya

mwanafunzi (CA). Tangu mwaka 1999 hadi 2007, mtihani huu ulitumika kama kigezo

cha kuchuja wanafunzi kuingia kidato cha 3. Kuanzia 2008 mpaka sasa, Mtihani wa

www.JamiiF

orums.com

Page 90:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

89

Taifa wa Kidato cha 2 hautumiki kuchuja wanafunzi kuendelea na masomo ya kidato

cha 3. Utafiti umebaini kuwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 kutotumika kuchuja

wanafunzi kuingia kidato cha 3 umesababisha wanafunzi kutojishughulisha katika

kujifunza kwa kukosa changamoto na hatimaye wanafunzi wasio na uwezo kupata

fursa ya kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Hali hii pia inawafanya walimu

kutofundisha kwa bidii.

Aidha, kuna uhusiano wa kitakwimu wa viwango vya ufaulu kwa wanafunzi waliofanya

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 mwaka 2008 na baadaye kidato cha 4 mwaka 2010

kwa baadhi ya shule zilizofanyiwa utafiti. Mfano, katika shule ya sekondari Siera

iliyopo Manispaa ya Kinondoni, wanafunzi waliofanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha

2 mwaka 2008 walifaulu kwa asilimia 15.0 na walipofanya Mtihani wa Taifa wa Kidato

cha 4 mwaka 2010 walifaulu kwa asilimia 15.4. Hii inaonesha kiwango cha ufaulu wa

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 kinakaribiana na kile cha kidato cha 4 kama

inavyooneshwa katika Kielelezo Na. 4.7 na 4.8. Pia takwimu zinaonesha kuwa ufaulu

wa shule ya sekondari Maghang, Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 mwaka 2008 ni

asilimia 83.4 na asilimia 81.0 kwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kwa mwaka 2010.

Kielelezo Na. 4.7: Kiwango cha Ufaulu katika Shule Zilizofanya Vizuri katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 Mwaka 2008 na cha 4 Mwaka 2010

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

www.JamiiF

orums.com

Page 91:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

90

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 hubashiri matokeo

ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Mtihani huu hutumika kutoa tathmini ya kati kwa

shule na kwa mwanafunzi, pia huongeza ari ya ufundishaji na ujifunzaji. Upo uhusiano

kati ya kufundisha, kujifunza na mitihani.

Kielelezo Na. 4.8: Kiwango cha Ufaulu katika Shule Zilizofanya Vibaya

katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 Mwaka 2008 na cha 4 Mwaka 2010

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

Mitihani humfanya mwanafunzi ajitahidi kurudia kwa makini yale aliyofundishwa, na

mwalimu hufundisha kwa kuzingatia kile kinachotakiwa katika mtihani. Hivyo, mtihani

hutoa msukumo wa kufundisha na kujifunza. Kwa hiyo, kutotumika kwa Mtihani wa

Taifa wa Kidato cha 2 kuchuja wanafunzi kuingia kidato cha 3 kumechangia kuathiri

ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010.

4.4.8. Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya TaifaWadau mbalimbali waliohusishwa katika utafiti huu walitoa maoni kuhusu sifa za

kujiunga na kidato cha 1; kuboresha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2; Kuimarisha

mitihani ya majaribio ya kujipima shuleni na kuimarisha utungaji, usimamizi,

usahihishaji, upangaji wa madaraja, mchango wa alama za CA na matumizi ya miongo

na nyaraka.

www.JamiiF

orums.com

Page 92:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

91

a) Sifa za Kujiunga na Kidato cha 1

Ilipendekezwa kuwa alama za ufaulu katika kujiunga na kidato cha kwanza ziwe 125

(50%) badala ya kiwango kidogo cha ufaulu cha alama ya 100 (40%) kati ya 250 na

walioshindwa kupata alama za ufaulu wasiruhusiwe kujiunga na sekondari za binafsi.

Aidha, wanafunzi wa chaguo la pili wasichelewe kuandikishwa kwa kuwa ni moja ya

sababu zilizobainishwa kushusha kiwango cha ufaulu.

b) Kuboresha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2

Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 kutotumika

kama kigezo cha kuchuja wanafunzi kuendelea na kidato cha 3 huwafanya wanafunzi

wasiomudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kufikia hatua ya kufanya

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 na hatimaye kufeli.

Ushauri ulitolewa na wajibuji katika utafiti kwamba Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2

uendelee kutumika kama kigezo cha kumfanya mwanafunzi kuingia kidato cha 3 na

wastani wa kuimarisha alama hizo uwe 40 badala ya 30. Hali hii inaonesha kuwa

kuna umuhimu wa kuchuja wanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2. Pia

utafiti kati ya waliofeli Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 na cha 4 ufanyike ili kubaini

kwa kina uhusiano uliopo.

c) Kuimarisha Mitihani ya Majaribio ya Kujipima Shuleni

Utafiti umebaini kuwa kuna mapungufu katika uendeshaji na tathmini ya mitihani ya

majaribio katika kumwandaa mwanafunzi kufanya mitihani ya kitaifa. Maoni yalitolewa

kuhusu kuwepo na utaratibu mzuri wa uendeshaji wa mitihani ya majaribio shuleni

ikiwemo mitihani inayoshindanisha shule kiwilaya, kimkoa au kikanda. Vilevile

imependekezwa kuwa uendeshaji wa mitihani ya majaribio (Mock examinations)

iangaliwe upya kwa vile haikidhi viwango na taratibu za uendeshaji. Pia, kuwepo na

mitihani ya kuchuja kwa kila darasa na kidato ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata

stadi muhimu kwa kila ngazi.

www.JamiiF

orums.com

Page 93:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

92

d) Kuimarisha Utungaji, Usimamizi, Usahihishaji na Upangaji wa

Madaraja katika Mtihani wa Taifa

Wadau wa elimu waliohusika katika utafiti walitoa maoni kuwa mitihani itungwe

kutokana na mtaala ulioboreshwa ambao unalenga katika kupima ujuzi; Waliongeza

kwa kusema kuwa maelekezo na lugha inayotumika katika utunzi wa mitihani isiwe

ngumu ya kuwachanganya watahiniwa pia lugha rafiki itumike kwa wasimamizi wa

mtihani.

Sambamba na hilo, ilishauriwa kuwa muundo wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi

ubadilishwe ili kuruhusu maswali ya kujieleza kwa lengo la kuimarisha taaluma na

kupunguza udanganyifu. Aidha, kipimo kingine cha ufaulu wa Mtihani wa Kumaliza

Elimu ya Msingi kitumike badala ya kutumia mtihani wa mwisho tu. Vilevile, wanafunzi

wanapomaliza mtihani nakala za karatasi za maswali zibaki shuleni kwa ajili ya rejea.

Kuhusu mitihani ya taifa ilishauriwa kuwa isahihishwe kikanda na wasahihishaji wa

mtihani wa kidato cha 4 waongezwe na wapewe muda wa kutosha ili wasahihishe kwa

umakini. Vilevile, vigezo vya kuchagua wasahihishaji viwekwe bayana na posho zao

ziboreshwe. Serikali iendelee kudhibiti uvujaji wa mitihani ili kujenga ari ya kujifunza

kwa wanafunzi na tathimini ya matokeo ya mtihani ijadiliwe kwa ngazi zote.

Vilevile, alama za mazoezi endelezi (CA) zitumike kulingana na miongozo na

maelekezo ya mihtasari; Muundo wa mtihani (format) uzingatiwe na kusambazwa

shuleni kwa wakati. Aidha, uhakiki wa wanafunzi wanaotaka kufanya mtihani ufanyike

kwa wakati muafaka. Zaidi ya hayo, ilishauriwa kuwa mitihani ya ‘altenative to

practical’ iondolewe. Pia walisisitiza kuwa, watahiniwa waelimishwe juu ya masharti ya

mitihani na adhabu zinazoandamana na ukiukaji wa masharti hayo.

Maoni yaliyotolewa na wadau yanaonesha kuwa ipo haja ya kufanya marekebisho

katika mchakato wa utungaji, usimamizi, usahihishaji, mchango wa alama za CA,

upangaji wa madaraja katika mtihani wa Taifa, matumizi ya mongozo na nyaraka za

mitihani na Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 na sifa na mitihani ya majaribio ya

kujipima shuleni.

www.JamiiF

orums.com

Page 94:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

93

4.5. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu

Ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu ni muhimu ili kubaini ufanisi wake katika

kufanikisha na kutekeleza mtaala katika ngazi mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji.

Ufuatiliaji na tathmini ya mtaala wa elimu ya sekondari ulioboreshwa hufanyika katika

ngazi zote za usimamizi na utekelezaji kwa kuwahusisha wakuza mitaala, maafisa

mitihani, wakaguzi, walimu na wadau wengine wa elimu.

4.4.1 Ufuatiliaji na Tathmini ya Mtaala Ulioboreshwa

Ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa mitaala ni jukumu la Taasisi ya Elimu

Tanzania, chombo ambacho kisheria kina jukumu la kubuni na kutayarisha mitaala ya

elimu nchini. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba asilimia 100 ya wajibuji wanne

wa dodoso walieleza kuwa tathmini zilizofanywa na TET katika shule nchini ni mbili

kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi 2010. Tathmini ya kwanza ilifanyika

mwaka 2003 ambayo ilihusu tathmini ya utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Msingi na

tathmini ya pili mwaka 2004 ilihusu utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Sekondari.

Aidha, utafiti umebaini kuwa TET huwasilisha ripoti na taarifa za utekelezaji wa

mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa elimu kwa Wizara yenye

dhamana. Imeelezwa zaidi kuwa mapendekezo hayo ya wadau wa elimu hutumika

kuboresha Mitaala ya elimu nchini kama ilivyofanyika kwa mitaala ya sekondari ya

mwaka 2005 na 2007. Taarifa hii ya utafiti imeonesha wazi uchache wa tathmini za

mitaala zilizofanyika katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Kutofanyika tathmini kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa

serikali na wadau wa elimu kubaini changamoto na matatizo katika utoaji wa elimu na

kuyapatia ufumbuzi, hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mtaala.

4.4.2 Utaratibu wa Kufuatilia Maendeleo ya Ufundishaji na Ujifunzaji

Shuleni

Taarifa zilizotokana na dodoso lililojibiwa na wakuu wa shule za sekondari 132 zilieleza

kuhusu ufuatiliaji wa maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi pamoja na

utaratibu wa kufikisha taarifa kwa watahiniwa. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa

wakuu wa shule 68 (51%) kati ya waliohojiwa hufuatilia mchakato wa ufundishaji na

www.JamiiF

orums.com

Page 95:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

94

ujifunzaji kwa kukagua maandalio ya masomo, mpango wa kazi, matumizi ya zana,

mahudhurio ya walimu darasani, kukagua shajara na kuangalia kazi za wanafunzi

darasani. Pia wakuu wa shule hao walieleza kuwa wana utaratibu wa kuzungumza na

wazazi/walezi, walimu na wanafunzi kuhusu umuhimu wa maendeleo ya kitaaluma.

Aidha, asilimia 49 ya wakuu wa shule hawakueleza chochote namna wanavyofuatilia

maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi. Uchambuzi wa data hapo juu

umeonesha kwamba baadhi ya wakuu wa shule hawatekelezi kikamilifu usimamizi wa

taaluma shuleni.

Mkuu wa shule ni msimamizi mkuu wa taaluma shuleni, ana wajibu wa kuhakikisha

uendeshaji wa shughuli za kila siku za shule na kusimamia utekelezaji wa mitaala,

hivyo ni vema asimamie kikamilifu majukumu yake kama ilivyoainishwa katika

Mwongozo wa Usimamizi wa Shule (WEMU, 2010).

4.4.3 Ukaguzi wa Shule

Ukaguzi katika utekelezaji wa mtaala ni muhimu ili kubaini changamoto zake kwa

lengo la kuleta ufanisi na kuboresha elimu katika ngazi mbalimbali za ufundishaji na

ujifunzaji. Hivyo basi, jukumu la Ukaguzi wa Shule ni kusimamia na kuhakiki ubora wa

elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na vyuo vya Ualimu nchini. Ili

kufikia malengo ya utekelezaji wa majukumu yao, wakaguzi wa shule hufanya ukaguzi

wa jumla wa shule; ukaguzi wa kufuatilia na ukaguzi maalum (Kiongozi cha Mkaguzi

wa shule, 2006). Utafiti huu ulilenga kupata taarifa juu ya ukaguzi wa shule wa jumla.

Katika Kiongozi cha Mkaguzi wa shule imeelezwa kuwa kila shule itakaguliwa angalau

mara moja katika kipindi cha miaka mitatu. Katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti

imebainika kuwa shule 18 (13.53%) zilikaguliwa mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka

2006 hadi 2010. Hali kadhalika shule 69 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na

shule 46 (34.59%) hazikukaguliwa kabisa. Angalia jedwali katika Kiambatisho Na. 4.1

Aidha utafiti umebaini kuwa, takwimu za ukaguzi wa shule zilizopatikana katika

Halmashauri 22 zilizofanyiwa utafiti zinaonesha kati ya mwaka 2006 na 2010 kiwango

cha ukaguzi wa shule cha kuridhisha kilifanyika katika Halmashauri za Sumbawanga

(100%), Tanga Jiji (91.3%), Mpanda (84%), Kinondoni (78.26%) na Babati

(75.76%). Hata hivyo, Halmashauri za Kilwa (12.50%) na Lindi (15.38%) zilifanya

www.JamiiF

orums.com

Page 96:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

95

ukaguzi wa shule kwa kiwango cha chini, wakati shule za Halmashauri za Karagwe,

Muleba, Bagamoyo, Maswa, Singida Vijijini na Manyoni hazikukaguliwa. Vilevile,

katika Halmashauri za Ilala na Mbinga takwimu hazikupatikana kama inavyooneshwa

katika Jedwali Na 4.1.

Jedwali Na.4.1: Idadi ya Shule za Sekondari Zilizokaguliwa katika Halmashauri Zilizofanyiwa Utafiti, 2006 – 2010

Na. Kanda Halmashauri Idadi ya shule

zilizoripotiwa

Idadi ya shule zilizokaguliwa

Asilimia ya ukaguzi

1DAR ES SALAAM

Kinondoni 46 36 78.26Ilala 91 Hakuna takwimu -

2ZIWA MAGHARIBI

Karagwe 47 0 0Muleba 41 0 0

3KUSINI Kilwa 24 3 12.50

Lindi 26 4 15.38

4KASKAZINI MAGHARIBI

Babati 33 25 75.76Mbulu 34 10 29.41

5MARA Bunda 30 9 30.00

Musoma 24 10 41.67

6MASHARIKI Mkuranga 30 7 23.33

Bagamoyo 34 0 0

7NYANDA ZA JUU

Sumbawanga 34 34 100.00Mpanda 25 21 84.00

8NYANDA ZA JUU KUSINI

Songea[v] 28 6 21.43Mbinga 61 Hakuna takwimu -

9MAGHARIBI Bukombe 26 4 15.38

Maswa 38 0 0

10KATI Singida Vijijini 61 0 0

Manyoni DC 30 0 0

11KASKAZINI MASHARIKI

Tanga Jiji 46 42 91.30Lushoto 79 13 16.46JUMLA 888 224

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

Utafiti umebaini kuwepo kwa kiwango kidogo cha ukaguzi wa shule na kutotekelezwa

kikamilifu kwa mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule, hali inayosababisha

kutokuwepo kwa ufanisi wa usimamizi na utoaji wa elimu bora.

Vilevile, kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule asilimia

61.7 ya Maafisaelimu mikoa na Halmashauri pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri

waliohojiwa walithibitisha kuwa, maoni/mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule

hufanyiwa kazi kwa kufanya ufuatiliaji katika shule husika ili kubaini mapungufu na

www.JamiiF

orums.com

Page 97:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

96

kujiridhisha kama mapendekezo ya ukaguzi yanatekelezwa. Ilielezwa kuwa Bodi za

Shule zinahusika katika utekelezaji wa mapendekezo hayo na kuweka mpango

mkakati ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza. Aidha, kuhusu masuala ya nidhamu ya

walimu, Ofisi za Elimu hushirikiana na TSD kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa

katika taarifa za ukaguzi wa shule.

Asilimia 73.17 (30) ya wakaguzi wa shule kanda walitofautiana na Maafisaelimu wa

mikoa, Wakurugenzi na Maafisaelimu wa Halmashauri kwa kueleza kuwa

mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule hayatekelezwi au utekelezaji wake ni wa

kiwango cha chini.

Matokeo ya utafiti yameonesha kuwepo kwa changamoto zinazohusu ukaguzi wa

shule ambapo shule hazikaguliwi kama ilivyoainishwa katika Kiongozi cha Mkaguzi wa

Shule (2006). Vilevile imebainika kuwa kiwango kidogo cha ukaguzi wa shule za

sekondari hali ambayo imesababishwa na ongezeko la shule ambazo haikwenda

sambamba na ongezeko la idadi ya wakaguzi wa shule na vitendea kazi. Idadi kubwa

ya wanafunzi iliyobainishwa inatofautiana na Waraka wa Elimu Na 16 wa Mwaka 2002

ambayo inapaswa kuwa 1:40, hivyo kuathiri uendeshaji wa elimu.

4.4.4 Maoni Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu

Kutokana na matokeo ya utafiti, imebainika kuwa mfumo wa ukaguzi uliopo haukidhi

malengo tarajiwa. Hivyo, wajibuji walipendekeza kwamba ukaguzi wa shule

uimarishwe kwa kuwajengea uwezo wakaguzi na kuwapa raslimali za kutosha ili

wakague shule ipasavyo.

Mfumo wa Ukaguzi wa shule uliopo sasa ni kwamba ukaguzi wa shule za msingi upo

katika ngazi ya wilaya na wa sekondari katika ngazi ya kanda. Kutokana na upanuzi

wa shule za sekondari na uamuzi wa serikali kugatua usimamizi na uendeshaji wa

shule za sekondari kuwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, kuendelea na mfumo

uliopo wa ukaguzi wa shule za sekondari hauwezi kuwa wa ufanisi. Hivyo, Ukaguzi wa

Shule katika ngazi ya wilaya uimarishwe ili kuwawezesha wakaguzi kukagua shule za

sekondari. Aidha, kuwe na ofisi za ukaguzi katika ngazi ya mkoa badala ya kanda ili

kusimamia utekelezaji wa ukaguzi ngazi ya Wilaya.

www.JamiiF

orums.com

Page 98:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

97

4.6. Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu

Ufanisi katika elimu unazingatia uwepo wa raslimali watu wa kutosha na wenye sifa.

Uwepo wa walimu wa kutosha na wafanyakazi wengine wasio walimu kama vile

wahasibu, mafundi mchundo maabara (laboratory technicians) na wakutubi huchangia

katika utoaji wa elimu bora shuleni. Walimu bora na wenye sifa hutokana na mfumo

wa kuwaandaa tangu wakiwa katika mafunzo tarajali. Aidha, mafunzo kazini ni eneo

lingine linaloongeza ubora wa walimu hao kwa kuwaongezea stadi na ujuzi kulingana

na mahitaji ya mtaala.

4.6.1. Mfumo wa Utayarishaji wa WalimuUtafiti umebaini kuwa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa walimu tarajali

pamoja katika vyuo hivyo umeelezwa kutokuwa fanisi kutokana na changamoto

mbalimbali, ikiwemo sifa za chini kwa wahitimu wanaojiunga na mafunzo ya

stashahada, upungufu wa miundo mbinu, vitabu, mihtsari na idadi kubwa ya walimu

tarajali isiyoendana mahitaji.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa asilimia 70 (56) ya wahadhiri, wakufunzi na

wanachuo waliohojiwa walibainisha sifa zinazotakiwa kudahili walimu tarajali za

principal pass 1 na subsidiary 1 hazimfanyi mwalimu anayeandaliwa kuwa mahiri.

Barua ya Kamishna yenye Kumb.Na TTDB/85/483/01/25, ya mwaka 2009 inaeleza sifa

za wanaojiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni ‘Principal Pass’ moja na

‘Subsidiary’ moja katika masomo mawili yanayofundishwa shule za sekondari. Kwa sifa

hizo ni wazi kuwa mwalimu anaeandaliwa hatamudu kufundisha masomo mawili

katika ubora unaostahili.

Aidha, utafiti ulibaini kuwa baadhi ya wadahiliwa wamekuwa wakitumia vyeti vya

kughushi na wengine hawana wito wa kazi ya ualimu kwa kuwa wanajiunga katika

mafunzo ya ualimu baada ya kukosa fursa nyingine walizotarajia.

Vilevile, matokeo ya utafiti yamebaini uwepo wa maandalizi yasiyotosheleza ya walimu

katika vyuo vya ualimu unaosababisha walimu wengi kufundisha kwa njia ya maswali

badala ya kuzingatia ujenzi wa dhana na vitendo kama mtaala unaozingatia ujuzi

(competence based curriculum) unavyoelekeza. Asilimia 67(54) ya wahadhiri,

www.JamiiF

orums.com

Page 99:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

98

wakufunzi na wanachuo waliohojiwa walisema kwamba wingi wa wanafunzi katika

mkondo mmoja husababisha kutokuwa na makusano ya kutosha (limited interaction)

kati ya wakufunzi na walimu tarajali na kuwalazimu wakufunzi kutumia ufundishaji wa

kipurure (Lecturing ). Mmoja wa wahadhiri aliongeza kwa kusema,

“Walimu wanaoandaliwa kwa mfumo huu hawawezi kuwa mahiri kutekeleza

mtaala ulioboreshwa ambao unasisitiza njia shirikishi”.

Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, maandalizi ya walimu tarajali vyuoni hayafanyiki

ipasavyo kutokana na kukosekana kwa vitendea kazi na miundombinu na baadhi ya

wakufunzi kutokuwa makini katika kufundisha kwa kuzingatia mahitaji ya mtaala wa

ualimu ulioboreshwa. Hali hii inasababisha walimu wanaoandaliwa kutokuwa mahiri.

Utafiti pia umebaini kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia na

kujifunzia katika baadhi ya vyuo ambapo ilielezwa na wakufunzi na wanachuo

waliohojiwa kuwa vitabu havitoshelezi na hata vilivyopo haviendani na mtaala

ulioboreshwa. Wajibuji walibainisha kuwepo kwa upungufu wa mabweni kwa walimu

tarajali.

Aidha, kupungua kwa muda wa mazoezi kwa vitendo (Teaching Practice) kuwa wiki

nne kumeathiri kwa kiasi kikubwa ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, matokeo ya utafiti

yamebaini kuwa walimu tarajali wanaandaliwa kwa kiwango kidogo katika mada za

ufundishaji, namna ya kuandaa azimio la kazi, andalio la somo, namna ya kufanya

nukuu za somo na zana za kufundishia somo kwa kuzingatia mihtasari iliyoboreshwa.

Aidha, walieleza kuwa mitihani hutolewa kwa kutumia mihtasari ya zamani. Hali

kadhalika, ilielezwa kuwa hakuna moduli za mada za mafunzo ya ualimu zilizoandaliwa

na TET katika kukidhi mahitaji ya mihtasari mipya.

4.6.2. Ajira na Upangaji wa WalimuMatokeo ya utafiti yameonesha kuwa baadhi ya viongozi siyo waadilifu katika kupanga

walimu. Viongozi hao hupanga walimu bila ya kuzingatia mahitaji ya walimu katika

shule za mijini na vijijini. Hali hii inasababisha kutokuwepo kwa mgawanyo linganifu

wa walimu kati ya shule za mijini na zile za vijijini hivyo kusababisha sehemu zenye

mazingira magumu kuwa na upungufu wa walimu. Pia, katika baadhi ya Halmashauri

www.JamiiF

orums.com

Page 100:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

99

utafiti umebaini kuwa baadhi ya watendaji huwadai walimu rushwa ya ngono, hayo

yalidhihirishwa katika mahojiano ya pamoja na walimu, ambapo mwalimu mmoja wa

kike alibainisha:

“Baadhi ya watendaji wa Halmashauri wamekuwa na tabia ya kuwadhalilisha

walimu wa kike kwa kuwataka kimapenzi wanapotaka kupangwa katika shule

zenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi“.

Hali hii inaleta athari katika malezi bora ya wanafunzi kwa baadhi ya shule kukosa

walimu hususani wa kike, mfano shule ya sekondari Wariku katika Halmashauri ya

Bunda wanafunzi wasichana walilalamika kuwa wanakosa mwalimu wa kike wa

kumweleza matatizo yao.

Waraka wa Elimu Na. 4 wa mwaka 2001 unatoa maelekezo kwa watendaji wa

Halmashauri kuondoa mrundikano wa walimu kwa shule za mijini. Utafiti umebaini

kuwa bado hakuna uwiano linganifu wa ikama ya walimu katika Halmashauri hali

inayo athiri ufundishaji na ujifunzaji. Utafiti umebaini kuwa hakuna uwiano mzuri wa

mgawanyo wa walimu unaozingatia jinsi na idadi ya masomo yanayofundishwa

shuleni. Katika mahojiano ya pamoja na walimu walilalamika kuwa, baadhi ya shule

zina walimu wengi wa somo moja wakati shule zingine hazina walimu masomo hayo

kabisa.

Jedwali Na. 4.2 linaonesha mahitaji, uwepo, upungufu na ziada ya walimu katika

masomo ya msingi kwa baadhi ya shule za sekondari za serikali za Mkoa wa Dar Es

Salaam zilizofanyiwa utafiti. Hali hii inathibitisha mgao wa walimu usiozingatia ikama,

mfano kuna ziada ya walimu katika baadhi ya masomo (idadi katika mabano) ya

Biology (4) , English (2), Geography (3) na Physics (2) katika shule ya sekondari ya

Jangwani wakati shule ya Mkera ina upungufu wa masomo hayo katika Halmashauri

hiyo hiyo ya Ilala.

Hata hivyo Maafisaelimu Mikoa, Wakurugenzi na Maafisaelimu wa Halmashauri

waliohojiwa walitofautiana na walimu kwa kueleza kwamba upangaji wa walimu

unazingatia mahitaji ya shule kimasomo (87%), jinsi na sifa ya ndoa (9%), hali ya

afya na mahitaji maalum ya mwalimu (2%) na kipaumbele kwa shule za pembezoni

(2%).

www.JamiiF

orums.com

Page 101:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

100

Jedwali Na 4.2: Mahitaji, Uwepo na Upungufu/Ziada ya Walimu katika

Baadhi ya Shule Sekondari za Serikali za Mkoa wa Dar Es Salaam

Shule Ma

them

atc

s

En

glis

h

Kis

wa

hili

Bio

log

y

Ch

em

istr

y

Civ

ics

Ph

ysic

s

Geo

gra

ph

y

His

tory

Jum

la

Mkera

Mahitaji 4 4 4 4 4 4 4 4 4 36

Waliopo 3 2 3 3 2 2 2 2 2 21

Upungufu 1 2 1 1 2 2 2 2 2 15

Ziada 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0

Nyeburu

Mahitaji 4 4 4 4 4 4 4 4 4 36

Waliopo 1 6 5 4 7 4 3 6 4 40

Upungufu 3 0 0 0 0 0 1 0 0 4

Ziada 0 2 1 0 3 0 0 2 0 8

Jangwani

Mahitaji 12 10 7 9 9 6 6 10 8 77

Waliopo 11 12 8 13 10 7 8 13 7 89

Upungufu 1 0 0 0 0 0 0 0 1 2

Ziada 0 2 1 4 1 1 2 3 0 14

Azania

Mahitaji 13 11 8 8 8 8 9 8 9 82

Waliopo 11 8 12 9 10 7 9 9 7 82

Upungufu 2 3 0 0 0 1 0 0 2 8

Ziada 0 0 4 1 2 0 0 1 0 8

Kambangwa

Mahitaji 8 8 5 5 3 7 4 5 8 53

Waliopo 8 7 6 8 5 6 3 8 7 58

Upungufu 0 1 0 0 0 1 1 0 1 4

Ziada 0 0 1 3 2 0 0 3 0 9

Goba Mpakani

Mahitaji 4 4 2 3 2 2 2 3 2 24

Waliopo 2 2 2 2 2 0 2 2 0 14

Upungufu 2 2 0 1 0 2 0 1 2 10

Ziada 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0

manzese

Mahitaji 8 8 4 5 5 3 5 5 5 48

Waliopo 8 8 7 7 4 3 2 4 6 49

Upungufu 0 0 0 0 1 0 3 1 0 5

Ziada 0 0 3 2 0 0 0 0 1 6

Salma Kikwete

Mahitaji 6 5 4 4 4 4 4 4 4 39

Waliopo 3 4 4 1 1 1 1 5 5 25

Upungufu 3 1 0 3 3 3 3 0 0 16

Ziada 0 0 0 0 0 0 0 1 1 2

Chanzo: Takwimu za Utafiti 2011

4.6.3. Uwepo wa Walimu katika Shule Uwepo wa walimu katika shule siyo sababu pekee ya kuinua kiwango cha ufaulu wa

wanafunzi, bali hutegemea pia utayari na ubora wa walimu. Utayari wa walimu

hutokana na kujengewa fursa na mazingira ya kuvutia ya kazi. Pamoja na jitihada za

serikali katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kama ilivyobainishwa

katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya kwanza na ya pili,

www.JamiiF

orums.com

Page 102:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

101

bado kuna changamoto za uwepo wa walimu wa kutosha. Matokeo ya utafiti

yamebaini upungufu wa walimu katika shule za serikali na zisizo za serikali kama

ilivyooneshwa katika jedwali Na. 4.3.

Jedwali Na 4.3 Uwepo wa Walimu katika Baadhi ya Shule Zilizofanyiwa

Utafiti

Jina la Shule Aina ya Shule

Mkoa Wilaya Idadi ya

walimu

Idadi ya wanafun

zi

Uwiano wa mwalimu na mwanafunzi

Monica Mbega Serikali Ruvuma Mbinga 3 308 1:103Ughandi Serikali Singida Singida(V) 3 382 1:127Senani Serikali Shinyanga Maswa 3 178 1:59Majebele Serikali Shinyanga Maswa 3 219 1:73Iyogelo Serikali Shinyanga Maswa 4 362 1:91Kireti Serikali Tanga Lushoto 2 292 1:146Kisiju Serikali Pwani Mkuranga 4 501 1:125Ikola Serikali Rukwa Mpanda 3 334 1:111Mipingo Serikali Lindi Lindi (V) 2 59 1:30Mtanga Serikali Lindi Kilwa 4 244 1:61Chitengule Serikali Mara Bunda 6 853 1:142Upendo Binafsi Tanga Lushoto 9 193 1:21Mkwese Binafsi Singida Manyoni 7 83 1:12Madunga Binafsi Manyara Babati 9 184 1:20Rondo Seminary Binafsi Lindi Lindi (v) 8 168 1:21Victoria Binafsi Mara Musoma(V) 14 158 1:11Goldenland Binafsi Shinyanga Bukombe 10 376 1:38Kikodi Binafsi Ruvuma Mbinga 10 334 1:33Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

Jedwali Na.4.3 linaonesha kuwa baadhi ya shule za sekondari za serikali zilizofanyiwa

utafiti zina wastani wa uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi zaidi ya 100

(1:100). Wastani wa uwiano huu haulingani na 1:40 unaotakiwa kitaifa hali

inayodhihirisha upungufu wa walimu. Kwa upande wa shule zisizo za serikali wastani

wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:11-1:38 hali inayoonesha kutokuwa na tatizo la

walimu. Hata hivyo wastani wa uwiano wa mwalimu kwa idadi ya wanafunzi kitaifa

katika elimu ya sekondari unaonesha kuwa mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi

51 (BEST, 2010) hali ambayo inaonesha kuwepo kwa upungufu wa walimu hivyo

kuathiri ufundishaji na ujifunzaji.

www.JamiiF

orums.com

Page 103:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

102

Kuhusu sifa za walimu, matokeo ya utafiti yameonesha kwamba, katika shule 132

zilizofanyiwa utafiti kuna jumla ya walimu 1,917 wakiwemo 515 wenye shahada,

1,051 wa stashahada, 126 wenye cheti na 225 wa leseni. Hali ya uwepo wa walimu

wenye cheti na wa leseni katika shule za sekondari zilizofanyiwa utafiti inaonesha

tofauti kati ya matamko ya Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) na hali halisi kuhusu sifa

ya mwalimu wa sekondari ambayo inasisitiza kwamba, mwalimu wa stashahada

afundishe kidato cha 1-2. Kwa kawaida mwalimu wa shahada anatazamiwa

kufundisha kidato cha 3-6.

Jedwali Na 4.4 Jumla ya Mahitaji, Walimu Waliopo na Upungufu katika

Shule za Sekondari 132 Zilizofanyiwa Utafiti

Mah

itaj

i

Wal

iop

o

kat

ika

oro

dh

a

Wal

iop

o

Vit

uo

ni

Wal

io N

je k

wa

Ru

hu

sa

Wag

on

jwa

Mu

da

Mre

fu

Wat

oro

wa

Mu

da

Mre

fu

Wal

ioaz

imw

a

Up

un

gu

fu

Asi

limia

ya

up

un

gu

fu

2903 1917 1556 67 48 229 171347 46.40

Asilimia 81.17 3.50 2.50 11.95 0.89

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

Pia utafiti umebaini kuwa, kuna tofauti ya takwimu za walimu waliopo katika orodha

shuleni na idadi halisi ya waliopo. Jedwali 4.4 linaonesha walimu waliopo vituoni

katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti ni asilimia 81.17 (1556) kati ya walimu 1,917

waliopo katika orodha shuleni. Aidha, asilimia 11.95 (229) ya walimu hao ni watoro

wa muda mrefu na asilimia 46.4% (1347) ni upungufu wa walimu katika shule hizo.

Uwepo wa walimu watoro kwa muda mrefu unaashiria tatizo la usimamizi wa rasilimali

watu na hivyo kukwamisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.

Utafiti umebaini kuwa uhaba wa walimu umesababisha baadhi ya Walimu kufundisha

masomo wasio na ujuzi nayo. Mfano katika shule za sekondari za Mipingo yenye jumla

ya walimu 2 na Mtanga yenye walimu 4 katika Halmashauri za Lindi na Kilwa wa

masomo ya lugha na sanaa pia wanalazimika kufundisha masomo ya sayansi.

Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 katika shule

www.JamiiF

orums.com

Page 104:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

103

hizo ni wa kiwango cha chini, ambapo shule ya Mipingo watahiniwa wote 12 walifeli

na shule ya sekondari Mtanga alifaulu Mtahiniwa mmoja kati ya watahiniwa 37.

Hali hiyo pia imethibitika katika baadhi ya shule zenye kiwango kidogo cha ufaulu

zilizofanyiwa utafiti kama inavyoonekana katika Kielelezo Na. 4.11. Shule hizo zina

idadi ya walimu chini ya 5 kinyume na maelekezo yaliyo katika Kiongozi cha Mkuu wa

Shule na Waraka wa Elimu Na. 10 wa mwaka 2004.

Kielelezo Na 4.11: Baadhi ya Shule Zilizofanya Vibaya katika Mtihani wa

Kidato cha 4 Mwaka 2010 na Idadi ya Walimu Waliokuwepo katika Kila

Shule - 2010

Chanzo: Takwimu za utafiti 2011

Aidha, katika mahojiano na wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2010, mhitimu

mmoja alisema:

“tangu tulipoanza kidato cha kwanza mpaka cha nne, hatukuwahi kuwaona walimu wa baadhi ya masomo darasani hata mara moja.”

Hali hii inaonesha kuwa baadhi ya shule zina upungufu mkubwa wa walimu hivyo

husababisha wanafunzi kufanya mitihani ya taifa katika baadhi ya masomo bila

kufundishwa.

www.JamiiF

orums.com

Page 105:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

104

Utafiti umeonesha kuwa ni dhahiri kuwa upo uhusiano kati ya uwepo wa walimu na

kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika Mitihani ya Taifa ya elimu ya sekondari.

Vielelezo Na 4.11 na 4.12 vinathibitisha mahusiano hayo, ambapo Kielelezo Na 4.11

kinaonesha baadhi ya shule za sekondari zilizofanyiwa utafiti ambazo zina ufaulu wa

kiwango cha chini wakati Kielelezo 4.4 kinaonesha shule zenye ufaulu wa juu.

Kielelezo Na 4.12: Baadhi ya Shule Zilizofanya Vizuri katika Mtihani wa

Kidato cha 4 Mwaka 2010 na Idadi ya Walimu Waliokuwepo katika Kila

Shule - 2010

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

Matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu kimasomo

hususani katika masomo ya English Language, Chemistry, Physics na Mathematics.

Katika shule za sekondari 132 zilizofanyiwa utafiti, somo la Mathematics, lina

mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo kuna upungufu wa

walimu 264 sawa na asilimia 60.6 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 4.5.

www.JamiiF

orums.com

Page 106:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

105

Jedwali Na 4.5: Mahitaji, Uwepo na Upungufu wa Walimu Kimasomo katika Shule

za Sekondari Zilizofanyiwa Utafiti

MASOMO

Bio

log

y

Ch

em

istr

y

Civ

ics

En

glis

h

Geo

gra

ph

y

His

tory

Kis

wa

hili

Mat

hem

atic

s

Ph

ysic

s

Jum

la

Mahitaji 327 332 290 341 305 289 264 436 319 2903

Waliopo katika Orodha 210 183 203 234 255 228 202 219 183 1917

Waliopo Vituoni 175 153 178 182 185 189 172 172 150 1556

Walio Nje kwa Ruhusa 8 9 3 13 14 12 3 3 2 67

Watoro wa Muda Mrefu 23 17 13 27 47 19 18 39 26 229

Wagonjwa Muda Mrefu 2 3 9 7 9 7 8 1 2 48

Walioazimwa 2 1 0 5 0 1 1 4 3 17

Upungufu wa Walimu 152 179 112 159 120 100 92 264 169 1347

Asilimia ya Upungufu 46.5 53.9 38.6 46.6 39.3 34.6 34.8 60.6 53.0 46.4

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

Vilevile, upungufu huo wa walimu wa somo la Mathematics unathibitisha kiwango

kidogo cha ufaulu wa somo hilo kama inavyoonekana katika Kielezo Na. 4.13 ambapo

kiwango cha ufaulu kimeshuka kutoka asilimia 31.2 (2007) na kufikia asilimia 16.09

(2011).

Kielelezo Na 4.13: Ufaulu wa Somo la Mathematics katika Mtihani wa

Kidato cha 4 Mwaka 2006-2010

Chanzo: NECTA, Examinations Results Statistics 2007-2010

www.JamiiF

orums.com

Page 107:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

106

Upungufu wa walimu katika baadhi ya masomo hususan wa masomo ya sayansi na

Mathematics umesababisha ongezeko la idadi ya vipindi kwa walimu waliopo na

kupunguza ufanisi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuathiri

kiwango cha ufaulu

Utafiti umebaini sababu za upungufu wa walimu ni pamoja na walimu kutokwenda

katika maeneo waliyopangiwa, kuruhusiwa kiholela au kutoroka kwenda kujiendeleza

kimasomo, hususan walimu wa stashahada na wa leseni na upanuzi wa elimu ya

sekondari ambao haukwenda sambamba na utayarishaji wa walimu wa kutosha kama

ilivyoeleza na walimu katika mahojiano ya pamoja.

Aidha, utafiti umebaini pia baadhi ya shule hazina wataalamu wa maabara, wakutubi,

wahasibu, maafisa ugavi, makatibu muktasi na wahudumu. Hali hii imesababisha

baadhi ya walimu kufanya kazi za uendeshaji zaidi kuliko kufundisha na hivyo kuathiri

ufaulu wa wanafunzi. Hivyo, kuna upungufu wa walimu na wafanyakazi wasio walimu

tofauti na ilivyoainishwa katika Kiongozi cha Mkuu wa Shule ukurasa 52 na 54

mtawalia.

Kwa ujumla matokeo ya utafiti yameonesha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa

walimu hasa katika shule za serikali hali ambayo hailingani na kanuni ya ikama ya

walimu. Hali hii imesababisha walimu wasio na sifa kufundisha sekondari na hivyo

kuwanyima wanafunzi fursa ya kujifunza kikamilifu.

4.6.4. Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa WalimuWajibuji mbalimbali walitoa maoni ya kuimarisha ubora na uwepo wa walimu.

Mapendekezo hayo ni pamoja na:-

a. Uwepo wa Walimu

Uwepo mkakati maalum wa kuandaa walimu wa kutosha na wenye sifa hususan wa

masomo ya Sayansi na Mathematics na kuajiri wataalamu wa kusaidia uandaaji wa

masomo ya Sayansi kwa vitendo. Pia, ilishauriwa kuwa Halmashauri ziruhusiwe kuajiri

walimu hao ili kurahisisha mgawanyo mzuri wa walimu kulingana na mahitaji ya kila

somo. Suala la kuajiri walimu wenye sifa linahusisha vyuo vya ualimu na vyuo vikuu

www.JamiiF

orums.com

Page 108:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

107

hivyo kuna umuhimu wa kuwa na mkakati maalum wa kuandaa walimu wa kutosha na

wenye sifa katika ngazi zote. Pia ilipendekezwa kuwatumia Walimu na Maafisa wa Elimu

wastaafu katika shughuli mbalimbali za elimu ili kusaidia kupunguza athari za upungufu wa

wafanyakazi na kutumia uzoefu wao kujenga uwezo wa wafanyakazi kwa gharama nafuu

b. Kuimarisha Ubora wa Walimu

Kuhusu Mafunzo ya Walimu Kazini, ilipendekezwa kwamba Serikali iboreshe Vituo vya

Walimu (TRCs) ili vitumike kuendeleza walimu kwa gharama nafuu. Ilipendekezwa

kwamba Halmashauri zisaidie kusomesha walimu wanaopata nafasi ya kusoma elimu

ya juu. Aidha walimu wasiende masomoni kwa wakati mmoja na kusababisha

upungufu mkubwa shuleni. Maoni yalitolewa na wadau kuwa, CWT igharamie

mafunzo ya walimu kazini ili wajengewe uwezo wa mbinu za kufundishia na kujifunzia

zinazolenga kuimarisha ushirikishaji wa wanafunzi. Mafunzo hayo pia yatawajengea

ubunifu na ujuzi katika kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira wanayofanyia

kazi (ufaraguzi).

c. Kuboresha Utendaji Kazi wa Walimu

Ilipendekezwa kuwa walimu wasibakizwe kituo kimoja cha kazi kwa muda mrefu ili

kubadili mazingira na kuwa na uzoefu unaolingana kwa walimu wote. Pia, walimu

wanaobadilishana vituo vya kazi wapangwe katika shule walikotoka walimu hao ili

kuziba pengo na wanaokwenda kusoma warudishwe katika vituo vyao vya kazi baada

ya masomo. Ufuatiliaji ufanyike ili kubaini walimu ambao hawajaripoti vituo vya kazi

na ikama ipangwe kulingana na masomo ya walimu.

Aidha, Halmashauri ziweke utaratibu wa kuhudumia walimu wapya kabla ya kupata

mishahara yao. Maoni hayo yamebaini kuwa walimu hawaridhishwi na utaratibu wa

upangaji vituo vya kazi, mapokezi wakati wa kuanza kazi na kukaa katika kituo kimoja

cha kazi kwa muda mrefu. Hali kadhalika, ubadilishanaji wa vituo vya kazi usioziba

mapengo umeonesha kutowaridhisha. Ilishauriwa pia walimu wasio na uwezo, walevi

na watoro waondolewe na wasiruhusiwe kuajiriwa tena nchini. Vilevile wahitimu wa

chuo kikuu wajaze mkataba wa kufundisha muda fulani ili wasitoke vituoni na kwenda

kujiunga na kazi nyingine. Aidha, Serikali iunde Bodi ya Walimu Tanzania

www.JamiiF

orums.com

Page 109:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

108

itakayoshughulikia viwango vya taaluma, maadili na utendaji wa walimu kama

ilivyopendekezwa katika Mkakati wa Maendeleo ya Elimu ya Ualimu (TDMS, 2008).

d. Kuboresha Mafunzo ya Walimu Tarajali

Ilipendekezwa mafunzo ya walimu tarajali yasiwe chini ya miaka miwili na muda wa

kufanya mazoezi ya kufundisha BTP uwe miezi miwili kwa mwaka wa kwanza na miezi

mitatu kwa mwaka wa pili ili wanachuo waandaliwe ipasavyo. Aidha, kwa ufumbuzi

wa muda mfupi, kuwepo kwa programu ya miezi mitatu ya mafunzo ya walimu tarajali

ili kupata walimu wa kutosha na mfumo wa mafunzo ya ualimu unaojumuisha elimu

ya juu ya sekondari na ualimu urejeshwe ili kutoa walimu mahiri na wenye ari ya

ualimu. Vilevile, walionesha umuhimu wa kujifunza kutoka nchi nyingine zinazofanya

vizuri kielimu.

4.7. Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

Mazingira ya utendaji wa kazi ya walimu hutegemea mwamko wa jamii, uhusiano wa

walimu na ushirikiano na jamii inayozunguka shule. Miundombinu ya shule kama vile

maabara na madarasa, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu vya kiada

na ziada vinavyoendana na mitaala ni miongoni mwa mahitaji katika mazingira ya

kufundishia na kujifunzia.

4.6.1 Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia

Ubora wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji unahitaji walimu na wanafunzi kuwa

katika hali inayorahisisha kazi na majukumu yao. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa

baadhi ya walimu hupigwa na wanakijiji, hubakwa na kufanyiwa vitendo vya

kishirikina. Pia, imebainishwa kuwa walimu hawapewi mapokezi mazuri na nyumba

bora za kuishi wanaporipoti katika vituo vyao vya kazi.

Pia utafiti umebaini kuwa asilimia 61 ya wakuu wa shule 132 za sekondari

zilizofanyiwa utafiti wamesema kuwa mazingira mazuri ya kazi ni fursa inayowafanya

walimu waendelee kubaki kwenye vituo vyao. Aidha, asilimia 57 (12) ya Maafisa elimu

sekondari wa Halmashauri waliohojiwa walieleza kuwa mazingira mazuri yenye

huduma za kijamii kama maji, afya, usafiri, umeme, teknolojia ya habari na

www.JamiiF

orums.com

Page 110:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

109

mawasiliano ni fursa inayowafanya walimu kuwepo shuleni. Pia, matokeo ya utafiti

yanaonesha kuwa kati ya maafisa 44 wa ofisi za TSD waliohojiwa, asilimia 55 (24)

walieleza kuwa baadhi ya walimu hupoteza muda wa vipindi kufuatilia stahili zao ofisi

za TSD wilaya na wakati mwingine kukata tamaa na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Hali ambayo inayodhihirisha ugumu wa mazingira ya kazi ya mwalimu. Hivyo ili kuinua

kiwango cha ufaulu, mazingira vutivu yanapaswa kuandaliwa kwa walimu ili waweze

kutimiza wajibu wao katika vituo wanavyopangiwa.

Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa chakula cha mchana hakitolewi kwa wanafunzi

katika shule nyingi za kutwa. Pia, baadhi ya shule zimejengwa mbali na makazi ya

walimu na wanafunzi na hivyo kuleta matatizo ya usafiri wa wanafunzi na walimu

mijini na vijijini. Kufuatia shida ya usafiri, mwanafunzi mmoja katika mahojiano ya

pamoja alisema

”….huku hakuna mabasi tunapanda vitengo.”

Usemi huo ukiwa na maana malori ya mchanga au “landrover” za wazi kama

zinavyotumiwa na vitengo maalum vya polisi. Aidha, ukosefu wa mabweni

umesababisha wanafunzi kuishi katika nyumba za kupanga ‘geto’ kama

inavyofahamika na wanafunzi ambako huishi bila usimamizi wa wazazi au walimu.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, uwepo wa mazingira mazuri ya kazi ni motisha

inayoweza kuwafanya walimu kubaki katika vituo vyao na kutimiza majukumu yao

kikamilifu. Pia, baadhi ya walimu wanatumia muda mwingi katika kufuatilia stahili zao

badala ya kuwa kazini. Kwa ujumla, hali hii husababisha walimu kukata tamaa na

kukosa morali ya kufundisha.

Pia, utafiti umeonesha kuwa fedha za ruzuku ya uendeshaji (Capitation Grant)

ambazo shule hununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia hutolewa chini ya kiwango

kinachotakiwa. Vile vile, fedha hizi huchelewa kutolewa toka Hazina hali ambayo

huathiri mwenendo wa manunuzi ya vifaa.

Kukosekana kwa mazingira mazuri ya kazi husababisha walimu kukata tamaa na

kukosa morali ya kufundisha. Vile vile, kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa

wanafunzi katika shule za kutwa, kunaathiri umakini wa wanafunzi katika ujifunzaji.

www.JamiiF

orums.com

Page 111:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

110

Aidha, ni ukweli ulio dhahiri kuwa matatizo ya usafiri wa wanafunzi mijini na vijijini

yanawakosesha vipindi kila siku na hivyo kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

Pia kutokutolewa fedha za kutosha kwa wakati kwa ajili ya kununulia vifaa vya

kufundishia na kujifunzia kunaathari katika mchakato wa utoaji wa elimu kufikia

malengo yaliyowekwa.

4.6.2.2 Uwepo wa Samani na Majengo katika Shule

Miongoni mwa miundombinu muhimu katika utoaji wa elimu kwa ufanisi ni pamoja na

madarasa, maabara, samani, mabweni/hosteli, nyumba za walimu, majengo ya

utawala na viwanja vya michezo. Takwimu zilizotolewa na wakuu wa shule 132

zilizofanyiwa utafiti zimeonesha kuwa upo upungufu mkubwa wa maabara kwa masomo ya

sayansi, maktaba, samani na miundombinu mingine kama inavyoainishwa kwenye Jedwali Na

4.6 na Kielelezo 4.6.1

Jedwali 4.6: Samani na Majengo Katika Shule za Sekondari 132

Miundombinu Mahitaji Uwepo Upungufu % UpungufuSamani(Viti na Meza) 63,601 48,665 14,936 23.5Hosteli/Bweni 1,900 840 1,060 55.8Nyumba 3,150 881 2,269 72Majengo Utawala 1,138 516 622 54.7Madarasa 2,866 1,535 1,331 46.4Maktaba 1,183 230 953 80.6Maabara Kemia 1,128 229 898 79.6Maabara Fizikia 1,099 383 716 65.2Maabara Bayolojia 1,123 382 741 66

Kielelezo Na. 4.9: Asilimia ya Upungufu wa Miundombinu katika Shule Zilizofanyiwa Utafiti

Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011

www.JamiiF

orums.com

Page 112:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

111

Aidha, walimu katika hojaji walibainisha kuwepo kwa mlundikano wa wanafunzi katika

vyumba vya madarasa, maktaba na maabara hali inayothibitisha upungufu wa

miundombinu hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji. Vilevile, wanafunzi katika

mahojiano ya pamoja walibainisha athari ya ukosefu wa hosteli/mabweni shuleni

hupelekea wanafunzi kulazimika kutembea umbali mrefu kati ya shule na makazi yao.

Matokeo haya kwa ujumla yanaonesha hali isiyoridhisha katika suala la miundombinu

ya shule tofauti na ilivyoelekezwa na Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995 na Mwongozo

wa Samani wa Wizara ya Elimu (2001).

4.6.2.3 Uwepo wa Vitabu vya Kiada na ZiadaUtafiti umebaini kuwa kuna upungufu wa vitabu vya kiada vinavyoendana na mtaala

ulioboreshwa kama inavyooneshwa katika Kielelezo Na 4.10. Aidha, utekelezaji wa Sera ya

upatikanaji na usambazaji wa vitabu ya Mwaka 1992 imekuwa na changamoto ingawa

serikali imeendelea kukasimu majukumu ya kununua vitabu shuleni.

Kielelezo Na. 4.10: Asilimia ya Upungufu wa Vitabu katika Shule

Zilizofanyiwa Utafiti

Chanzo: Data za Utafiti, 2011

Kielelezo Na. 4.10 kinaonesha kuwa upungufu wa vitabu vya kiada na ziada kwa

wastani wa asilimia 75.5 kwa shule zote zilizofanyiwa utafiti. Aidha, wajibuji

walionesha kuwa ununuzi wa vitabu huathiriwa na wanafunzi kutolipa ada na bei

kubwa ya vitabu.

www.JamiiF

orums.com

Page 113:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

112

Wakuza mitaala waliohojiwa walieleza changamoto za ucheleweshaji wa uhakiki wa

vitabu na utoaji ithibati inayofanywa na Kamati ya kuhakiki ubora wa machapisho ya

kielimu (EMAC). Walimu wakuu walitoa changamoto ya upungufu wa vifaa vya

kufundishia pamoja na vitabu vya kiada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa

kwa baadhi ya masomo, na kuwepo baadhi ya mada katika vitabu vya kiada

vilivyopewa ithibati na EMAC kutoendana na mahitaji ya mihtasari iliyoboreshwa.

Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa pamoja na shule nyingi kuwa na vitabu vichache,

baadhi ya vitabu hivyo haviendani na mtaala ulioboreshwa. Aidha, kukosekana kwa

mamlaka rasmi ya kusambaza vitabu katika ngazi ya Halmashauri pia ilibainishwa

kuwa chanzo cha ukosefu wa vitabu vinavyoendana na mtaala. Pia, mahojiano ya

pamoja ya wanafunzi na walimu yameonesha kuwa shule nyingi hazina utaratibu

mzuri wa matumizi ya vitabu hata vile vichache vilivyopo. Kwa ujumla, utafiti

unaonesha upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada katika shule nchini na

matatizo katika upatikanaji, usambazaji na matumizi yake katika shule. Hali hii ina

athari kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa taaluma shuleni.

4.6.3 Maoni ya Kuboresha Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia

Kati ya wakuu wa shule 132 wa shule za sekondari waliohojiwa, asilimia 61

wameeleza kuwa mazingira mazuri ya kazi ni fursa inayowafanya walimu waendelee

kubaki kwenye vituo vyao. Aidha, asilimia 57 (12) ya Maafisaelimu sekondari wa

Halmashauri waliohojiwa wameeleza kuwa mazingira mazuri yenye huduma za kijamii

kama maji, afya, usafiri, umeme, teknolojia ya habari na mawasiliano ni fursa

inayowafanya walimu kuwepo shuleni. Uwepo wa mazingira mazuri ya kazi kwa

walimu ni motisha itakayowafanya walimu kubaki katika vituo vyao na kutimiza

majukumu yao ya kufundisha kwa ukamilifu.

Wajibuji wamependekeza kuwepo na vitabu vya kutosha shuleni ambavyo

vimeidhinishwa na utaratibu wa kupitia vitabu. Aidha, Kitengo cha Kamati ya

Kutathimini Machapisho ya Kielimu (EMAC) kiimarishwe ili kiwe na watendaji wenye

ujuzi. Serikali irudishe utaratibu wa kuwa na aina moja ya vitabu vya kiada

vitakavyotumika nchi nzima kwa kila somo (visiwe zaidi ya viwili). Wizara inunue na

www.JamiiF

orums.com

Page 114:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

113

kusambaza vitabu hivyo ili kuwezesha kuwepo kwa vitabu vya kutosha shuleni. Hali

kadhalika, matumizi ya TEHAMA shuleni yatiliwe mkazo ili kuwezesha wanafunzi

kupata maarifa kwa njia ya mtandao. Vilevile, imeshauriwa kuwa Serikali ithibiti

matumizi holela ya vitabu vya kugushi vya kufundishia na kujifunzia shuleni. Pia vifaa

vya maabara viongezwe katika kila shule na shule zilizo na maabara ziwezeshwe ili

shule za karibu zisizo na maabara zitumie maabara za shule hizo teule.

Kuhusu posho kwa walimu, ilipendekezwa kuwepo na posho maalum ya kufundishia

ambayo ni asilimia 50 ya mshahara, posho ya mazingira magumu, kupandishwa

madaraja, mafunzo kazini, kuboresha huduma za jamii kama vile umeme, maji,

usafiri na nyumba bora ili kutoa motisha kwa walimu. Vilevile serikali ianzishe mfuko

wa kuwakopesha walimu ili kuwavutia wadumu kufundisha katika mazingira magumu.

Serikali ilishauriwa kuhamasisha wadau mbalimbali wa elimu kuimarisha miundombinu

shuleni kwa kuziwezesha shule kuwa na maktaba, maabara na vifaa vyake ili mitihani

ya “alternative to practical” iondolewe, kuwepo kwa mabweni na vyumba vya kutosha

hasa kwenye shule zilizojengwa kwenye mazingira magumu. Pia, ilipendekezwa kuwa

shule zijengewe uzio ili kuimarisha ulinzi. Sambamba na hilo wadau walipendekeza

kuwe na utaratibu wa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wa shule za kutwa

ili wanafunzi hao waweze kujifunza kwa ufanisi zaidi.

Aidha, ilipendekezwa kuwe na ziara za mafunzo na kuimarisha vyama vya kimasomo

ili kuwajengea wanafunzi na walimu utamaduni wa kusoma vitabu ili kuwapatia na

uwezo wa kujitafutia maarifa wenyewe kwa mfumo wa kujitegemea.

Kutokana na maoni hayo imeonekana kuna upungufu wa vifaa vya kufundishia na

kujifunzia, miundombinu ya kutosha, ziara za mafunzo na vyama vya masomo. Aidha,

ukosefu wa fedha, ubovu wa miundombinu, uchapaji na usambazaji mbaya wa vitabu

vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa, na uelewa mdogo wa lugha ya Kiingereza

kwa walimu na wanafunzi, ni changamoto ambazo zinaathiri utekelezaji wa mitaala

shuleni.

www.JamiiF

orums.com

Page 115:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

114

Pamoja na juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia

kama ilivyobainishwa katika MMES I na II, bado kuna changamoto za uwepo wa vifaa

vya kutosha. Aidha, zinahitajika juhudi za makusudi kuhamasisha wanafunzi

kupenda masomo ya Sayansi na Mathematics kwa kuhakikisha kuwepo kwa vifaa

toshelevu vya kufundishia na kujifunzia kwa sababu Taifa linahitaji wataalam ili

kuhimili ushindani wa kisayansi na kiteknolojia.

www.JamiiF

orums.com

Page 116:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

115

SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

Sura hii inaainisha hitimisho la matokeo ya utafiti kwa kuzingatia masuala

yanayoendana na malengo mahsusi na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu

yameonesha sababu mbalimbali za kushuka kwa ufaulu zilizobainishwa na kujadiliwa

katika sura ya nne. Sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu zimegawanyika katika

sehemu mbili ambazo ni chanzo (cause) cha tatizo na athari (effects). Matokeo ya

utafiti yameonesha kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi zote ni

chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4

mwaka 2010. Usimamizi na uendeshaji wenye mapungufu umeathiri utayarishaji na

utekelezaji wa mitaala, mfumo wa utayarishaji na uwepo wa walimu, mfumo na

taratibu za mitihani ya taifa, mazingira na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na

mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu.

Aidha, mapendekezo yamewasilishwa kwa kila suala na kubainishwa kwa kuzingatia

muda wa utekelezaji ambao ni mfupi, wa kati na mrefu. Muda mfupi (MF) ni kipindi

chini ya mwaka mmoja, muda wa kati (MK) ni mwaka mmoja hadi mitatu na muda

mrefu (MR) ni zaidi ya miaka mitatu.

5.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimui) Baadhi ya viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali wanateuliwa bila kuzingatia

vigezo vya utaalamu, uzoefu na uadilifu. Hali hii imepelekea kuwa na usimamizi na

uendeshaji usioridhisha na kuwepo na uwajibikaji mdogo katika ngazi mbalimbali

za kielimu;

ii) Maamuzi ya kitaalamu yahusuyo elimu pamoja na uendeshaji wake hufanyika

kisiasa na hivyo kuleta athari katika utekelezaji wa mipango ya utoaji wa elimu

bora nchini;

iii) Kuna ufinyu wa bajeti ya Wizara ya Elimu, TAMISEMI na Halmashauri, hivyo

usimamiaji na uendeshaji wa elimu kutokuwa na ufanisi unaotakiwa kulingana na

malengo ya elimu;

www.JamiiF

orums.com

Page 117:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

116

iv) Utekelezaji wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada hauendani na

upatikanaji wa vitabu vyenye ithibati na hivyo kusababisha kuwepo kwa vitabu vya

kughushi na kupenyezwa kwa vitabu visivyo na ubora; na

v) Kuna matatizo makubwa katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia

na kujifunzia katika elimu ya sekondari, na hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji.

vi) Kutokuwepo kwa uadilifu katika usimamizi na matumizi ya fedha zilizotengwa licha

ya ufinyu wa bajeti hali inayokwamisha kufikia malengo ya utoaji wa elimu bora;

na

vii) Kumekuwepo na ongezeko kubwa la wahitimu waliofeli katika mtihani wa Taifa wa

Kidato cha 4, hivyo kuwanyima fursa ya kuendelea na masomo ya juu na fani

mbalimbali.

Mapendekezo

a) Uendeshaji, usimamizi, mawasiliano na mahusiano baina ya asasi za kielimu,

Taasisi, ofisi za elimu mikoa, Halmashauri, na mashirika yasiyo ya kiserikali

uimarishwe katika utoaji wa elimu kwa ngazi zote; (MF)

b) Uadilifu katika usimamizi na matumizi ya fedha zilizotengwa uimarishwe; (MF)

c) Mchakato wa kutoa ithibati ufanyike kwa ukamilifu ili kupata vitabu vyenye ubora

unaotakiwa; (MF)

d) Ufuatialiaji wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada

pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe; (MF)

e) Ufundishaji na ujifunzaji wa somo la English kwa shule za Awali, Msingi na

Sekondari uimarishwe; (MF)

f) Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,

uadilifu na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na

zisikaimishwe kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;

(MK)

www.JamiiF

orums.com

Page 118:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

117

g) Klabu za masomo kama vile “English, Mathematics, Science na Geography clubs”

vianzishwe na kuimarishwa; (MF)

h) Mfumo wa kuandaa viongozi katika kuachiana madaraka (succession plan)

uanzishwe/kuimarishwa na kutumika; (MK)

i) Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,

tathmini na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya

utoaji wa elimu; (MF)

j) Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili kutatua

changamoto zilizopo; (MK)

k) Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)

kianzishwe kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji na

haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa inakidhi

malengo yaliyokusudiwa; (MK)

l) Utaratibu wa motisha kwa walimu unaoendana na uzito wa kazi, wadhifa na

ugumu wa mazingira anapofanyia kazi uandaliwe na utekelezwe ipasavyo; (MK)

m) Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya

mitihani ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza

kitaaluma na kitaalamu; (MK)

n) Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa walimu wa masomo

yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za sekondari; (MK) na

o) Sheria ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo na

ithibati katika shule nchini. (MR) na

p) Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC),

Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (CDTI) vipanuliwe ili kuwawezesha wanafunzi

wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na stadi za

kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri. (MR)

www.JamiiF

orums.com

Page 119:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

118

5.2. Utekelezaji wa mitaala

i) Mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa mwaka 2005 na 2007 ambao

unazingatia ujuzi yametolewa kwa kiwango kidogo kwa walimu, wakaguzi na

Maafisa Mitihani na hivyo kutotekeleza mtaala ipasavyo;

ii) Dhana ya mtaala unaozingatia ujuzi (competence Based Curriculum) haieleweki

kwa wadau wengi wakiwemo maafisa mitaala, maafisa mitihani, wakaguzi wa

shule na walimu;

iii) Upungufu wa mihtasari ya masomo na vitabu vya kiada na ziada vinavyoendana

na mtaala ulioboreshwa katika shule na vyuo vya ualimu umeathiri mchakato wa

ufundishaji na ujifunzaji;

iv) Mitaala inatayarishwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Kutojaribisha mitaala

wakati wa utayarishaji wake kunasababisha kutekeleza mitaala yenye mapungufu

na isiyokidhi mahitaji ya jamii; na

v) Kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka TET kwenda shuleni,

aidha TET huuza mihtasari na kusababisha upungufu shuleni.

Mapendekezo

a) Mafunzo maalumu kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na

kutekelezwa kwa maafisa mitaala na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo; (MF)

b) Mafunzo kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na

kutekelezwa kwa walimu na wakaguzi wote; (MF)

c) Mihtasari ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft copy)

ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya

Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi; (MF)

d) Ithibati ya vitabu vyenye kukidhi mahitaji ya mtaala iharakishwe. Aidha mafunzo

elekezi yatolewe kwa waandishi na wachapishaji ili wachapishe vitabu

vinavyoendana na mtaala ulioboreshwa; (MK) na

www.JamiiF

orums.com

Page 120:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

119

e) Taratibu za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti,

tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake. (MR)

5.3. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa

i) Muundo na aina ya maswali yanayotolewa na walimu katika ngazi ya shule kwa

kiasi kikubwa haufanani na ule wa mitihani ya Taifa. Hivyo upimaji wa wanafunzi

shuleni kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa katika mitihani ya Taifa;

ii) Wanafunzi wana uelewa mdogo wa lugha ya kufundishia (Kiingereza) na hivyo

kushindwa kujibu maswali ya mitihani ipasavyo;

iii) Kuna mianya ya uvujaji wa mitihani unaotokana na kutokuwa na vyumba vya

kuhifadhia mitihani (strong room) katika ngazi ya Halmashauri na shule;

iv) Uteuzi wa wasahihishaji unafanyika kwa upendeleo na hivyo kupoteza umakini

katika usahihishaji;

v) Wasahihishaji wa mitihani ya Taifa hulipwa kwa kiwango kidogo cha pesa na

kufanya kazi kwa muda mrefu kwa siku, na hivyo kushusha ari na kupoteza

umakini katika usahihishaji;

vi) Miongozo ya usahihishaji (marking scheme) ya baadhi ya masomo yenye

mapungufu na makosa katika baadhi ya maswali hutumika wakati wa usahihishaji

wa mitihani ya taifa, hivyo kuwanyima haki watahiniwa;

vii) Muundo wa mitihani (Format) kutowafikia baadhi ya walimu na hivyo kutopata

fursa ya kuutumia katika kuwaandaa wanafunzi;

viii) Mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45% majaribio na mazoezi na 5%

projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au mchakato wake katika matokeo ya

mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu. Hii inatoa matokeo ambayo siyo

halisia, pia ni kinyume na mwongozo wa mazoezi endelezi (CA) wa NECTA;

ix) Baadhi ya shule huwasilisha NECTA alama za CA zisizo na uhalisia na hivyo

kusababisha NECTA kukosa imani na alama hizo;

www.JamiiF

orums.com

Page 121:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

120

x) Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 una athari katika ufaulu wa Mtihani

wa Taifa wa Kidato cha 4;

xi) Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni sehemu ya mazoezi endelezi (CA) na

hautumiki kuchuja wanafunzi kuendelea na Kidato cha 3. Hali hii imepunguza ari

ya ufundishaji na ujifunzaji;

xii) Utoaji wa adhabu ya kumshusha mtahiniwa daraja kutokana na kufeli kwa baadhi

ya masomo ya msingi na ya mchepuo hakuleti usawa katika ufaulu pia ni kinyume

na alama za madaraja husika; na

xiii) Kuna tofauti ya taratibu zinazotumika kupata gredi katika mitihani ya Taifa na

zile zinazotumika kupata gredi hizo katika mitihani ya shule. Hali hii inasababisha

watahiniwa kutopata gredi stahiki, hivyo kuathiri ufaulu.

Mapendekezo

a) Walimu wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia

(authentic) pia alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4

kama ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi; (MF)

b) Uteuzi wa wasahihishaji uzingatie sifa na usawa kutoka shule za kitaifa, jamii na

zisizo za serikali; (MF)

c) Utungaji na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala

inayotekelezwa; (MF)

d) Adhabu katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III

baada ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila

mtahiniwa apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake; (MF)

e) Fomati ya mitihani ya Taifa isambazwe katika shule zote na ufuatiliaji ufanyike

kuhakikisha kwamba kila mwalimu anaitumia; (MF)

f) Utaratibu wa kuweka kwenye mtandao (website) taarifa muhimu zinazohusu

taratibu na maelekezo mbalimbali ya uendeshaji wa mitihani ya Taifa na utoaji

matokeo uimarishwe. Kwa mfano ziwekwe fomati za mitihani, ripoti za tathmini za

mitihani, taratibu za mitihani; (MF)

www.JamiiF

orums.com

Page 122:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

121

g) Hadhi ya Mtihani wa taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja

wanafunzi. Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada

(Remedial); (MF)

h) Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika

kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki kwa

watahiniwa; (MF) na

i) Wasahihishaji wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu (perdiem) kwa

sababu ni haki ya mwajiriwa wa serikali. (MK)

5.4. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimui) Mfumo wa ukaguzi wa shule za sekondari kuwa katika ya ngazi ya kanda hauleti

ufanisi katika ufuatiliaji na tathmini ya elimu; na

ii) Ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mtaala umefanyika kwa kiwango kidogo

hivyo kutobainika kwa dosari za utekelezaji wake;

Mapendekezo

a) Ukaguzi wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa kupatiwa

nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia; (MF)

b) Viongozi wa elimu wafanye ziara za mara kwa mara na za kushtukiza shuleni ili

kufuatilia uendeshaji wa elimu; (MF)

c) Jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili

kubaini dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki; (MF) na

d) Ukaguzi wa shule ngazi ya elimu ya sekondari uwe katika ngazi ya Mkoa na

Halmashauri ili kusogeza huduma karibu na walengwa na kuimarisha usimamizi na

uendeshaji; (MK)

5.5. Mfumo wa utayarishaji wa walimu

i) Sifa za udahili wa mwalimu tarajali anayeandaliwa kufundisha elimu ya sekondari

ngazi ya stashahada (1 Principal, and 1 Subsidiary passes) hazitoshelezi kumfanya

mwalimu anayeandaliwa kuwa mahiri;

www.JamiiF

orums.com

Page 123:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

122

ii) Baadhi ya wadahiliwa katika vyuo vya ualimu kutokuwa na wito wa kazi ya ualimu

hivyo kusababisha walimu hao kutokuwa na maadili ya kazi ya ualimu na

kutodumu katika ajira;

iii) Matayarisho hafifu ya walimu tarajali yanatokana na wingi wa wanachuo darasani,

upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kutotumika

kwa mbinu shirikishi. Hali hii inasababisha kutopata walimu mahiri wa kutekeleza

mtaala ulioboreshwa;

iv) Baadhi ya wanachuo wanaomaliza shahada ya elimu huajiriwa kuwa wakufunzi

katika vyuo vya ualimu moja kwa moja, utaratibu ambao unawafanya wanachuo

watayarishwe na wakufunzi wasio na uzoefu wa kufundisha; na

v) Wanachuo wengi wana tatizo la kutumia lugha ya kiingereza katika kuandika na

kujieleza, hivyo wanapohitimu hushindwa kutumia lugha hiyo katika kufundisha

katika shule za sekondari.

i) Kuna upungufu mkubwa wa walimu pamoja na usambazaji wa walimu usiofuata

uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kati ya shule na shule, mijini na vijijini. Hali hii

inasababisha wanafunzi kutofundishwa ipasavyo;

ii) Kuna walimu wasio na sifa kufundisha sekondari ambao wapo katika shule za

sekondari wakifundisha bila utaalamu wa ualimu;

iii) Kuna upungufu mkubwa wa walimu unaosababishwa na walimu wa shule moja

kwenda masomoni kwa wakati mmoja hususan wa leseni, na hivyo kuathiri

ufundishaji na ujifunzaji shuleni; na

vi) Baadhi ya shule huwatumia wahitimu wa kidato cha 6 na 4 na wasiokuwa na

taaluma na maadili ya ualimu. Hii inasababisha wanafunzi kutopata fursa ya elimu

na malezi bora.

Mapendekezo

a) Walimu wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji (ikama) katika shule

zote; (MF)

www.JamiiF

orums.com

Page 124:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

123

b) Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule ziandaliwe;

(MF)

c) Uanzishwe utaratibu wa kuwatumia walimu kufundisha shule zaidi ya moja kwa

masomo yenye ukosefu au upungufu wa walimu; (MF)

d) Sifa za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada

zipandishwe kuwa Principal 2 za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha

mwalimu kuwa mahiri kitaaluma; (MK)

e) Vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa

miundombinu ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na

ongezo la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa; (MK)

f) Wakufunzi na wahadhiri wapewe mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi

(Competence Based Curriculum) ; (MK)

g) Wakufunzi mahiri na wenye uzoefu wa kufundisha katika shule za sekondari

waajiriwe. Aidha wahitimu wa vyuo vikuu wanaoajiriwa moja kwa moja waanzie

kazi katika shule za sekondari za mazoezi; (MK)

h) Uhamasishaji ufanyike kwa wahitimu wa kidato cha 6 na vyuo vikuu kuelewa fursa

za kazi ya ualimu ili waweze kuijiunga na kuifanya kazi hiyo; (MK)

i) Maabara ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na kuimarishwa

katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali watatumia

kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na kuandika; (MR)

j) Udahili wa walimu tarajali uzingatie mahitaji ya walimu kimasomo ili kukabiliana na

upungufu walimu katika baadhi ya masomo; (MK)

k) Udahili wa walimu tarajali ngazi ya stashahada ufanyike kwa wahitimu wa Kidato

cha 4 waliojaza “Sel Form” na mafunzo yawe miaka mitatu yakijumuisha masomo

ya taaluma (Kidato cha 5-6) na ualimu ili kupata walimu mahiri na wenye wito;

(MK)

www.JamiiF

orums.com

Page 125:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

124

l) Utaratibu maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post Graduate

Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili kukabiliana na

tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi; (MK)

m) Utaratibu wa kutumia/kuajiri watu ambao sio walimu kufundishaji katika shule za

sekondari uachwe; (MK)

n) Utaratibu uandaliwe wa kuwaendeleza walimu wanaofundisha katika shule za

sekondari ambao hawana utaalam wa ualimu ili kuwajengea uwezo walimu hao;

(MK)

o) Utaratibu uanzishwe wa kuwatumia Walimu na Maafisa wa Elimu wastaafu ili kutumia

uzoefu wao katika kufanikisha shughuli mbalimbali za elimu; (MK)

p) Wahitimu wa kidato cha 6, 4 na vyuo vikuu wanaofundisha katika shule za

sekondari wajiendeleze kwa kusomea taaluma ya ualimu; (MK) na

q) Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa

ufundishaji na ujifunzaji yaimarishwe. (MK)

5.6. Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia

i) Kuna upungufu mkubwa wa samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.

Hali hii inasababisha wanafunzi kutoshiriki kikamilifu katika mchakato wa

ufundishaji na ujifunzaji;

ii) Baadhi ya shule zimepata usajili bila kutimiza vigezo vinavyohitajika kama vile

maabara za Sayansi, maktaba, ofisi na nyumba za walimu na hivyo shule hizo

kuendeshwa kwa mapungufu;

iii) Baadhi ya shule zimejengwa mbali na makazi ya wanafunzi na walimu. Hali hii

inawasababisha walimu na wanafunzi kutumia muda mrefu wa kwenda na kurudi

shuleni na hivyo kupunguza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji; na

iv) Kutokuwepo kwa chakula cha mchana katika shule za kutwa, hivyo kuathiri

mahudhurio na umakini wa wanafunzi katika ujifunzaji.

www.JamiiF

orums.com

Page 126:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

125

Mapendekezo

j) Jamii na wadau wengine wa elimu wahamasishwe kugharamia elimu nchini; (MF)

k) Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo

vinavyotakiwa; (MF)

l) Fedha za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na

kujifunzia shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo; (MK)

m) Utaratibu wa usafiri wa wanafunzi na walimu kwenda na kurudi shuleni uandaliwe

kwa shule ambazo ziko mbali na makazi ya walimu na wanafunzi; (MK)

n) Hosteli/mabweni na nyumba za walimu zijengwe kwenye shule zilizo mbali na

makazi ya wanafunzi na ya walimu; (MR) na

o) Wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha mchana ili kuimarisha

ufundishaji na ujifunzaji. (MR)

www.JamiiF

orums.com

Page 127:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

126

REJEA1.0 Lissu H. S (2008). Public Perception On The Use Of Continuous Assessment

Marks In Grading O-Level Secondary, M.Ed. (Science Education) Dissertation(Unpublished), Faculty of Education, University of Dar es Salaam.

2.0 Natinal Examinations Council of Tanzania: Examinations Processing, Dar es Salaam, July, 1986

3.0 National Examinations Council of Tanzania: NECTA WEBSITE, Dar es Salaam, May 2001

4.0 National Examinations Council of Tanzania: The Examinations Regulations, Dar es Salaam, 2006.

5.0 NECTA, 2004. Thirty Years of National Examinations Council of Tanzania (1973-2003). Dar es Salaam.

6.0 National Examinations Council of Tanzania: Certificate of Secondary Eeducation Examination, Paper on Literature in English, Dar es Salaam, Oktober, 2010

7.0 National Examinations Council of Tanzania: Certificate of secondary Education Examination Format, Dar es Salaam, February, 2008

8.0 National Examinations Counci of Tanzania: Guidelines on the Conduct and Administration of Continuous assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, Dar es Salaam,

9.0 United Republic of Tanzania: Education and Traininng Poplicy, Ministry of Education, Dar es Salaam, 1995.

10.0 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi: Waraka wa Elimu Na. 1 wa Mwaka 2006, WEMU, 2006

11.0 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi: Waraka wa Elimu Na. 5 wa Mwaka 1999, Mtihani wa kidato cha Pili katika Shule za Sekondari, WEMU, 1999.

12.0 Babyegeya E (2006) Teacher Education in Tanzania: developments and prospects, Journal of Issues and practice in Education (pg.32-46).

www.JamiiF

orums.com

Page 128:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

127

13.0 TIE (1991) A Summary Report on baseline Survey on primary, secondary and Teacher Education Curriculum Reform in Tanzania Mainland, MOEVT, Dsm.

14.0 Meena W.E. (2009) Curriculum Innovation in Teacher Education. Abo Academy University Press.

15.0 Osaki K.M. (1996) “Changing Forms of Curriculum in Tanzania” in Papers in Education and Development No. 17, DSM.

16.0 IBE/UNESCO (Dec 2000) Capacity Building for Curriculum Specialists in East & South East Asia and The Pacific, Bangkok, Thailand.

17.0 WEU (1995) Sera ya Elimu na Mafunzo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dar es Salaam.

18.0 TIE (2003) National Curriculum Development Framework (NCDF), TIE, Dar es Salaam.

19.0 TIE, (2008) Secondary Education Curriculum for Tanzania Mainland. Dar es Salaam.

20.0 TET ( Februari 2011) Taarifa ya Utekelezaji wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Elimu na Walimu kwa miaka 2005-2010, TET Dar es Salaam.

21.0 WEU (Juni 2005) Marekebisho ya Mtaala wa sekondari na Kuunganishwa kwa Masomo, Wizara ya Elimu na Utamaduni, Dar es Salaam.

22.0 MOEVT (2007) Teacher Development Management Strategy (TDMS), Ministry of Education & Vocational Training, Dar es Salaam.

23.0 MoEVT (2001) Practices and Possibilities in Teacher Education in Tanzania, edited by Mhando et al., Ministry of Education and Vocational Training , Dsm

24.0 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Februari 1982), Mfumo wa Elimu ya Tanzania 1981-2000:Ripoti na Mapendekezo ya Tume ya Rais ya Elimu, Juzuu la Kwanza, JMT, Dsm.

25.0 MoEVT (May 2004) A Deliberate Support to Licensed Teachers-Facilitator and Mentor’s Guide, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm

26.0 WEMU (2006), Kiongozi cha Mkaguzi wa shule. Dar es Salaam

27.0 WEMU (2009), Hotuba ya bajeti ya WEMU 2009/2010 p.43). Dar es Salaam

www.JamiiF

orums.com

Page 129:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

128

28.0 Ngodu, A. S . (2007), Licensed Teachers’ Professional Develepment and the Fate of Teaching Science and Mathematics in Secondary Schools. M.Ed. (Science Education) Dissertation. (Published), Faculty of Education, University of Dar es Salaam.

29.0 WEMU (2009), Mihtasari ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada iliyorekebishwa, na Utaratibu wa Kutahini (Barua ya Kamshina), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm

30.0 MoEVT (2010) Basic Education Statistics in Tanzania, 2006 – 2010, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm

31.0 WEMU (2010) Moduli ya Ujuzi wa Kufundisha kwa Umahiri, MWAKEM, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, DSM

32.0 MoEVT (2005) Facts About Basic Education in Tanzania, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm

33.0 MoEVT (2001), Construction of Secondary Schools, Guidelines for Buildings and Furniture., Ministry of Education and Vocational Training , Dsm

34.0 WEMU (2007), Utaratibu wa kuzingatia katika kuanzisha Shule za Serikali za kutwa zinazojengwa kwa nguvu za wananchi (Barua ya Kamshina), wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm

35.0 WEMU (2005), Nyaraka za Elimu za mwaka 1998 – 2005, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm

36.0 MoEVT( 2008), Education Sector Development Program(EDSP) (2008 – 17), Ministry of Education and Vocational Training, Dsm

37.0 MoEVT (2004), Secondary Education Development Program(SEDP) (2004 –2009), Ministry of Education and Vocational Training, Dsm

38.0 MoEVT (2010), Education Sector Review Aide Memoire. Ministry of Education and Vocational Training, Dsm

39.0 MoEVT, The Teacher Management Development Strategy 2008 – 2013

40.0 Wizara ya elimu na Utamaduni (1997 ) Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari . Dar es Salaam

www.JamiiF

orums.com

Page 130:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

129

41.0 MOEVT (2010), Secondary Education Development Program II (SEDP II) 2010 – 2014, MOEVT, Dsm

42.0 Nyerere (1967), Education for Self Reliance ……………………………………………

43.0 MOEVT (2002), Primary Education Development Program I (PEDP I) 2002 -2006, MOEVT, Dsm

44.0 MOEVT (2017), Updated Secondary Education Development Program I (SEDP I) 2007, MOEVT, Dsm

45.0 MOEVT (2007), Primary Education Development Program I (PEDP I) 2002 -2006, MOEVT, Dsm

46.0 WEMU (2009), Waraka wa Elimu Na.13 wa mwaka 2009, WEMU, Dsm

47.0 MOEVT (2010), Public Expenditure Tracking Survey, MOEVT, Dsm

48.0 OWM-TAMISEMI (2011), Taarifa ya OWM-TAMISEMI……………………………

49.0 MOEVT (2008), Education Sector Performance report, MOEVT, Dsm

50.0 WEMU (1998), Waraka wa Elimu Na.1 wa mwaka 1998, WEMU, Dsm

51.0 WEMU (2009), Taarifa ya Utafiti Kuhusu kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2008, WEMU, Dsm

52.0 TIE (2008), Secondary Education Curriculum for Tanzania Mainland,

53.0 Maelezo ya Waziri (Juni, 2005),………………………………………..

54.0 UWEZO (2010), Uwezo Assessment Project

www.JamiiF

orums.com

Page 131:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

130

VIAMBATISHOKiambatisho Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti(a) Kanda za Elimu, Mikoa, Halmashauri na Shule zilizohusika:Na Kanda ya

ElimuMkoa Halmashauri Shule

1 Dar es Salaam Dar es Salaam Kinondoni Kambangwa, Salma Kikwete, Manzese, Goba Mpakani, Canosa, Sierra

Ilala Azania, Jangwani, Mkera, Nyeburu, Tusiime, Sandy Valley

2 Mashariki Pwani Bagamoyo Bagamoyo, Chalinze, Zinga, Ubena, Marian girls, Kaole

Mkuranga Mwinyi, Lukanga, Kisiju, Mkungilo, Mwandege Boys, Mseru

3 Nyanda za Juu Kusini

Ruvuma Mbinga Kigonsela, Kitura, Monica Mbega, Mkoha, St Luise Mbinga Girls, Kikodi

Songea (V) Matimira, Daraja mbili, Ndongosi, Sili, Peramiho, Wilima

4 Nyanda za Juu

Rukwa Sumbawanga Mzindakaya, Msanzi, Mbizi, Kaoze, Kaengesa, Laela

Mpanda Katumba, Kanoge, Kabungu, Ikola, FPC-Tumaini, Milala

5 Kusini Lindi Lindi (V) Mchinga, Mnara, Chikonji, Mipingo, Namupa Sem, Nyangao

Kilwa Kilwa, Mitole, Pande, Mtanga

6 Magharibi Shinyanga Bukombe Iyogelo, Ushirombo, Nyakasaluma, Uyovu, Queen

Maswa Senani, Majebele, Mwakaleka, Mwamanenge, Ng’wanza, Lalago

7 Ziwa Magharibi

Kagera Muleba Kimwani, Izigo, Kibanga, Biirabo, Rubya Sem., Humura

Karagwe Rwambaizi, Mukiri, Morongo, Nono, Karagwe, Rumanyika

8 Ziwa Mara Musoma Mara, Musoma, Nyasho, Nyabisare, Makoko Sem, Victoria

Bunda Chitengule, Bunda, Sizaki, Nyeruma, Ikizu, Wariku

9 Kati Singida Singida (V) Ughandi, Mungaa, Siuyu, Minyughe, Dungunyi Sem, Ihanja

Manyoni Ipamuda, Idodyandole, Makuru, Kinangali, Amani Girls, Mkwese

10 Kaskazini Mashariki

Tanga Tanga Jiji Galanos, Tanga Tech, Mabokweni, Chongoleani, Rosmini, Sahare

Lushoto Mgwashi, Soni, Mdando, Kireti, Kifungiro Girls, Upendo

11 Kaskazini Magharibi

Manyara Mbulu Maghang, Tlawi, Siday, Haydom, Sanu Sem, Dongobeshi

Babati Dareda, Duru, Gorowa, Ndeki, Madunga, Joshua

www.JamiiF

orums.com

Page 132:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

131

(b) Maeneo Mengine Yaliyohusika katika Utafiti

Na. Eneo la Utafiti Ngazi1 Taasisi ya Elimu Tanzania Taifa2 Baraza la Mitihani la taifa Taifa3 Vyuo Vikuu Mkoa/Taifa4 Vyuo vya Ualimu Mkoa5 Uk aguzi wa Shule Kanda Kanda6 Ukaguzi wa Shule Wilaya Wilaya7 Elimu Mkoa Mkoa8 Elimu – Halmashauri(M) na (S) Wilaya9 Tume ya Utumishi wa Umma (TSD) Wilaya10 Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Wilaya11 Madhehebu ya Dini Wilaya12 Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilaya13 TAMONGSCO Taifa14 TEN/MET Taifa15 Ofisi ya Mh. Mbunge Wilaya16 Ofisi ya Mh. Diwani Kata

www.JamiiF

orums.com

Page 133:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

132

Kiambatisho 3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa

Na AINA YA ZANA WAJIBUJI

MALENGO IDADI YA WAJIBUJI WALIOPATIKANA KITAIFA NA KIMKOA

JUMLA

KIM

KO

A

KIT

AIF

A

KIT

AIF

A

RU

VU

MA

RU

KW

A

SH

INY

AN

GA

SIN

GID

A

DS

M

PW

AN

I

KA

GE

RA

MA

RA

LIN

DI

MA

NY

AR

A

TA

NG

A

1 Dodoso A Wakaguzi wa Shule Kanda 4 44 4 4 4 4 4 4 1 4 4 4 4 412 Dodoso B Mkuu wa Shule 12 132 12 12 12 12 12 12 12 12 13 12 12 1323 Dodoso C Wakurugenzi TET 4 4 44 Dodoso D Wakuu wa Idara za Mitihani NECTA 5 4 45 Hojaji A Wahadhiri - Vyuo Vikuu 2 4 46 Hojaji A Wanachuo- vyuo Vikuu vya Elimu 2 4 47 Hojaji A Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu 2 22 2 2 2 4 2 2 8 2 2 2 288 Hojaji A Wanachuo- vyuo vya Ualimu 4 44 4 4 4 8 4 4 6 4 4 2 449 Hojaji B Afisa Elimu Mkoa 1 11 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1110 Hojaji B Wakurugenzi Halmashauri 2 22 2 1 2 2 2 1 2 1 2 1511 Hojaji B Afisa Elimu Halmashauri (S) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 1 2 2 2 2112 Hojaji C Afisa Elimu Halmashauri (M) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 1 2 2 2 2113 Hojaji C Mkaguzi Mkuu wa Shule(W) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2214 Hojaji D Maafisa Tume ya Utumishi wa

Umma TSD (W)2 22 2

2 2 2 2 2 2 2 2 2 222

15 Hojaji E Afisa CWT (W) 2 22 2 2 3 2 2 2 2 2 2 2 2 2316 Hojaji E Viongozi wa Dini 4 22 4 4 2 4 4 4 4 2 4 4 4 4017 Hojaji E Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2 22 2 1 2 2 2 1 1 2 2 2 1718 Hojaji F Wabunge 2 22 1 2 2 2 2 1 3 1 2 1 1719 Hojaji F Madiwani 2 22 2 2 5 11 2 2 2 11 2 2 2 4320 Hojaji F Wazazi/Walezi 4 44 4 4 35 21 4 4 4 5 4 6 4 9521 Hojaji G Wajumbe wa Bodi ya Shule 4 44 4 4 18 17 4 4 4 16 4 3 4 8222 Hojaji H Wahitimu wa Kidato cha 4 - 2010 60 660 39 48 23 30 24 60 15 73 17 12 60 40123 Mahojiano ya Pamoja A Wakuza Mitaala 5 10 1024 Mahojiano ya Pamoja B Maafisa Mitihani (NECTA) 5 8 825 Mahojiano ya Pamoja C TAMONGSCO 5 6 626 Mahojiano ya Pamoja C TENMET 5 6 627 Mahojiano ya Pamoja D Walimu 60 660 43 67 67 43 72 60 50 48 51 52 60 61328 Mahojiano ya Pamoja E Walimu Wasahihishaji Mitihani

Kidato cha 460 660 8

4 9 7 30 24 5 4 3 8 60 162

29 Mahojiano ya Pamoja F Wanafunzi Kidato cha 3-4 120 1320 108 109 106 115 120 116 100 112 130 4 120 1140

JUMLA 353 3894 46 246 275 301 287 305 313 217 316 252 129 350 3037

www.JamiiF

orums.com

Page 134:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

133

Kiambatisho 4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika Halmashauri zilizofanyiwa utafiti.

MKOA HALMASHAURI SHULEUKAGUZI UMEFANYIKA

MARA NGAPID

AR

ES

SA

LAA

MILALA MKERA 2

NYEBURU 3Jangwani 4Azania 3

KINONDONI Kambangwa 2Goba Mapakani 1Manzese 1Salma Kikwete 1

Zisizo za serikaliILALA Siera 1

Canossa 3MAGNUS 4Tusiime 0

KA

GER

A

KARAGWE RWAMBAIZI 0NONO 0MUKIRE 1MURONGO 0

MULEBA BIIRABO 2KIBANGA 0KIMWANI 1IZIGO 0

Zisizo za serikaliKARAGWE KARAGWE 0

RUMANYIKA 0MULEBA RUBYA SEMINARI 1

HUMURA 0

LIN

DI

KILWA MITOLEKIVINJE 1KIRANJERANJE 1MTANGAMPUNYUREKILWA 1

LINDI (V) Chikonji Mnara sekondari 1Mchinga sekondari 1Mipingo Sekondari

Zisizo za serikaliLINDI (V) Nyangao sekondari

Khairaat Islamic ss 1Rondo seminari

MA

NY

AR

A

MBULU HAYDOM 2MAGHANG 1SIDAY 1TLAWI 2

Babati(HW) GOROWA 1DURU 2NDEKI

www.JamiiF

orums.com

Page 135:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

134

MKOA HALMASHAURI SHULEUKAGUZI UMEFANYIKA

MARA NGAPIDAREDA 4

Zisizo za serikaliMBULU Dongobesh 2

Sanu sem 3Babati(HW) Madunga 1

Joshua 1

MA

RA

BUNDA CHITENGULE 1BUNDA 1WARIKUNYERUMA 2SIZAKI 1

MUSOMA (M) MUSOMA 1NYABISARE 3MARA 2NYASNHIO 1

Zisizo za serikaliBUNDA IKIZU 2MUSOMA (M) Victoria 2

Makoko sem

PW

AN

I

BAGAMOYO Bagamoyo 2ChalinzeZinga 2Ubena 2

MKURANGA Kisiju 2Mwinyi 2Mkugilo 1Vikindu 2

Zisizo za serikaliBAGAMOYO Kaole 1

Marian Girls 2MKURANGA Mseru Seminary

Mwandege Boys 1

RU

KW

A

SUMBAWANGA –V Mzindakaya 3

Msanzi 2SUMBAWANGA –M Mbizi 1

Kaoze 3MPANDA IKOLA

KABUNGUKANOGEKATUMBA

Zisizo za serikaliSUMBAWANGA –V Laela

Kaegesa Seminary 1MPANDA MILALA

FPCT TUMAINI

www.JamiiF

orums.com

Page 136:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

135

MKOA HALMASHAURI SHULEUKAGUZI UMEFANYIKA

MARA NGAPI

RU

VU

MA

MBINGA KIGONSERA 2KITURAM.MBEGAMKOHA 4

MBINGA Daraja MbiliMatimiraNdongosiSili 2

Zisizo za serikaliMBINGA St. Luise 1

Kikodi 2MBINGA Peramiho 2

Wilima

SH

INY

AN

GA

BUKOMBE IYOGELO 3USHIROMBO 3NYAKASALUMAUYOVU

MASWA SENANIMAJEBELEMWAKALEKA 1MWAMANENGE 1

Zisizo za serikaliBUKOMBE Queen 2

Goldenland 3MASWA Ng'wanza 2

Lalago

SIN

GID

A

SINGIDA -V MUNGAA 3SIUYU 1UGHANDI 1MINYUGHE 1

MANYONI IPAMUDAIDODYANDOLE 1MAKURU 1KINANGALI

Zisizo za serikaliSINGIDA -V Ihanja

Dung'unyi Seminary 2

MANYONI Amani girls 3Mkwese 1

TAN

GA

MABOKWENI 1GALANOSI 1CHONGOLEANITANGA UFUNDIKIRETIMDANDOMGWASHI 2

SONI3

www.JamiiF

orums.com

Page 137:  · 2013-04-12 · Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri

Rasimu 2

136

MKOA HALMASHAURI SHULEUKAGUZI UMEFANYIKA

MARA NGAPIZisizo za serikali

Sahare 4Rosmin 1Kifungilo 1Upendo 3

TANBIHIJumla ya shule 132

Jumla ya shule ambazo hazikukaguliwa 46Jumla ya shule zilizokazguliwa mara 1 mau 269Jumla ya shule zilizokaguliwa mara 2 au zaidi 18

Ukaguzi uliofanyika ulikuwa wa jumla, kufuatilia au maalum

www.JamiiF

orums.com