matokeo ya mtihani wa kidato cha nne

12
Matokeo ya Mhani wa Kidato cha Nne Wananchi wazungumzia changamoto wa kujifunza Tanzania 1. Utangulizi Mnamo tarehe 18 Februari 2013, Serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba wanafunzi 240,903 ka ya 397,126 waliofanya mhani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 walifeli, kufeli huko kukiwa sawa na asilimia 61 (kutoka asilimia 46 za mwaka 2011). Asilimia nyingine 34 walipata Daraja la IV, ikiwa na maana kwamba ni asilimia 6 tu walipata Daraja la I, II na III kwa pamoja. Matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 yalitajwa kuwa “janga” na ya “kushtusha” na yamemsukuma Waziri Mkuu kuunda Tume kuchunguza kilichosababisha matokeo mabaya na kutoa mapendekezo kuhusu nini kifanyike. Kaka muhtasari huu, Uwazi iliyopo Twaweza inatoa mchango kaka mjadala huu, ikionyesha takwimu zenye sura ya kitaifa za hivi karibuni kabisa kuhusu elimu. Takwimu hizi zimekusanywa na utafi wa kwanza wa njia ya simu za mkononi nchini Tanzania ujulikanao kama Sau za Wananchi, ambao pia ni utafi wa kwanza wa aina yake barani Afrika. Takwimu zilizotumika kwenye Muhtasari huu zilikusanywa ka ya tarehe 18 Machi hadi 3 Aprili, 2013. Vilevile, muhtasari huu unaonyesha matokeo kutoka kwenye utafi wa msingi wa Sau za Wananchi (ambao mahojiano yalifanyika ana kwa ana) uliofanyika ka ya Oktoba na Desemba, 2012. Utafi wa msingi uliendeshwa kwenye kaya 2,000 Tanzania Bara, waka utafi wa awamu ya kwanza kwa njia ya simu za mkononi ulifanikiwa kuzifikia kaya 1,774 (asilimia 89 ya sampuli ya utafi wa msingi). Muhtasari huu pia unaonyesha ushahidi kwa kutumia takwimu za BEST (Basic Educaon Stascs of Tanzania) , ka ya 1998 na 2012, kama zilivyochapishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (MOEVT). Mani hii iliandikwa na kutayarishwa na Uwazi iliyopo Twaweza, ambayo inatumia ofisi ya Hivos Tanzania. Imetolewa mwezi Mei 2013. S.L.P. 38342, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 266 4301 Nukushi: +255 22 266 4308. [email protected] www.twaweza.org/sau 1 Mai 2013 Muhtasari Na. 2 Wakati muhtasari huu ukichapishwa, Serikali ilitangaza Bungeni kwamba matokeo ya Kidato cha Nne 2012 yatasahihishwa upya kwa kutumia vigezo vya alama vilivyokuwa vikitumika miaka ya nyuma.

Upload: dothuan

Post on 09-Dec-2016

673 views

Category:

Documents


17 download

TRANSCRIPT

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne Wananchi wazungumzia changamoto wa kujifunza Tanzania

1. UtanguliziMnamo tarehe 18 Februari 2013, Serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba wanafunzi 240,903 kati ya 397,126 waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 walifeli, kufeli huko kukiwa sawa na asilimia 61 (kutoka asilimia 46 za mwaka 2011). Asilimia nyingine 34 walipata Daraja la IV, ikiwa na maana kwamba ni asilimia 6 tu walipata Daraja la I, II na III kwa pamoja.

Matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 yalitajwa kuwa “janga” na ya “kushtusha” na yamemsukuma Waziri Mkuu kuunda Tume kuchunguza kilichosababisha matokeo mabaya na kutoa mapendekezo kuhusu nini kifanyike. Katika muhtasari huu, Uwazi iliyopo Twaweza inatoa mchango katika mjadala huu, ikionyesha takwimu zenye sura ya kitaifa za hivi karibuni kabisa kuhusu elimu. Takwimu hizi zimekusanywa na utafiti wa kwanza wa njia ya simu za mkononi nchini Tanzania ujulikanao kama Sauti za Wananchi, ambao pia ni utafiti wa kwanza wa aina yake barani Afrika.

Takwimu zilizotumika kwenye Muhtasari huu zilikusanywa kati ya tarehe 18 Machi hadi 3 Aprili, 2013. Vilevile, muhtasari huu unaonyesha matokeo kutoka kwenye utafiti wa msingi wa Sauti za Wananchi (ambao mahojiano yalifanyika ana kwa ana) uliofanyika kati ya Oktoba na Desemba, 2012. Utafiti wa msingi uliendeshwa kwenye kaya 2,000 Tanzania Bara, wakati utafiti wa awamu ya kwanza kwa njia ya simu za mkononi ulifanikiwa kuzifikia kaya 1,774 (asilimia 89 ya sampuli ya utafiti wa msingi). Muhtasari huu pia unaonyesha ushahidi kwa kutumia takwimu za BEST (Basic Education Statistics of Tanzania) , kati ya 1998 na 2012, kama zilivyochapishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (MOEVT).

Matini hii iliandikwa na kutayarishwa na Uwazi iliyopo Twaweza,ambayo inatumia ofisi ya Hivos Tanzania. Imetolewa mwezi Mei 2013.

S.L.P. 38342, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 266 4301 Nukushi: +255 22 266 [email protected] www.twaweza.org/sauti

1

Mai 2013Muhtasari Na. 2

Wakati muhtasari huu ukichapishwa, Serikali ilitangaza Bungeni kwamba matokeo ya Kidato cha Nne 2012 yatasahihishwa upya kwa kutumia vigezo vya alama vilivyokuwa vikitumika miaka ya nyuma.

Mambo ya msingi yaliyogunduliwa na muhtasari huu ni:

• Wananchi 7 kati ya 10 wana habari kuhusu uchapishaji wa Matokeo ya Kidato cha Nne ya 2012 na 8 kati ya 10 wanaona kuna kuporomoka kwa viwango vya ubora wa elimu ya sekondari

• Viwango vya umahiri katika Hisabati na Kiingereza viko chini, hii ni katika ngazi zote za shule za msingi na sekondari

• Wanafunzi wanaeleza kwamba mara kwa mara walimu hawahudhurii vipindi, na pindi wanapohudhuria kuna uwezekano mkubwa wakatoa kazi kisha kuondoka

• Walipotakiwa kueleza sababu za kiasi kikubwa cha wanafunzi kufeli katika mitihani, wazazi wanataja upungufu wa walimu kama tatizo na kuitaka serikali kuwapunguzia mzigo mzito walimu; na vilevile, wazazi wanabainisha ari ndogo miongoni mwa walimu na sifa duni miongoni mwa baadhi ya walimu kama sehemu ya sababu ya kushuka kwa viwango vya ujifunzaji.

2. Mambo makuu kumi kuhusu kujifunza TanzaniaJambo la 1 : Matokeo ya 2012 yanaendana na mwenendo wakushuka kwa matokeo ya mitahani ambao umekuwa ukitokeaMatokeo ya mitihani ya taifa ya Kidato cha Nne (yanayojulikana pia kama Cheti cha Kuhitimu Elimu ya Sekondari au CSSE) yanaonyesha mwendelezo wa kuanguka tangu 2007.

Kielelezo cha 1 kinaonyesha matokeo ya Kidato cha Nne kwa makundi ya matokeo kati ya 1998 na 2012 (yaliyochapishwa na MOEVT). Kipindi hiki kinaweza kugawanywa katika awamu mbili, huku mwaka 2007 ukiwa wa mwaka wa mabadiliko . Katika awamu ya toka 1998 hadi mwaka 2007, kulikuwa na ongezeko dogo la viwango vya ufaulu kwa madaraja ya I-III hadi kiwango cha juu cha asilimia 38, huku viwango vya darala la 0 vikishuka. Mwaka 2007 (mwaka wa mabadiliko), viwango vya daraja la 0 vilikuwa asilimia 10. Baada ya mwaka 2007, viwango vya Daraja la 0 vilianza kuongezeka kwa kasi hadi kufikia asilimia 61 ya sasa ndani ya miaka mitano.

Mabadiliko haya katika mwenendo wa matokeo yameambatana na upanuzi mkubwa wa sekta ya elimu. Idadi ya watahiniwa wa mitihani ya Kidato cha Nne imeongezeka kwa kigawe cha tisa, kutoka watahiniwa 42,887 mwaka 1998 hadi watahiniwa 397,126 mwaka 2012.

2

Kielelezo cha 1: Matokeo ya Mitihani ya Cheti cha Sekondari Kuanzia 1998 hadi 2012

Chanzo cha takwimu: Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Basic Education Statistics in Tanzania (BEST), 1998-2012.

Sehemu iliyobaki ya muhtasari huu inaripoti takwimu zilizo kusanywa kwa njia ya simu miongoni mwa wahojiwa wa utafiti wa Sauti za Wananchi.

Jambo la 2: Wananchi wana habari kuhusu uchapishaji wa matokeo ya mitihani Mnamo tarehe 18 Februari 2013, Serikali ya Tanzania ilitangaza matokeo ya mtihani ya Kidato cha Nne ya 2012. Utafiti wa Sauti za Wananchi ulianza kuwapiga simu kwa wahojiwa wake mwezi mmoja kamili baadaye, tarehe 18 Machi 2013, ukiwauliza kama walijua kuhusu kuchapishwa kwa matokeo hayo. Jumla ya wahojiwa 68 walijibu kuwa walikuwa na habari.

Hata hivyo, walipoulizwa kuhusu undani wa matokeo hayo, asilimia 71 hawakuweza kubainisha idadi wala asilimia ya waliopata Daraja la 0. Miongoni mwa wale asilimia 29 waliobaki, wengi waliweza kutoa makisio yaliyo karibu na ukweli kwamba waliopata Daraja 0 (kati ya asilimia 50 na 74 ya watahiniwa).

3

29%

38% 36%

6%

47%50%

55%

26%24%

12% 10%

61%

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

70%

80%

1998 2000 2002 2004 2006 2008 2010 2012

Daraja la 1-3

Daraja la 4

Daraja la 0

Kielelezo cha 2: Mhojiwa ana habari kwamba matokeo ya Kidato cha Nne yalichapishwa?

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti kwa Njia ya Simu – Awamu ya 1, Aprili 2013.

Jambo la 3: Wananchi wanatambua kuanguka kwa elimu Utafiti wa Sauti za Wananchi uliwauliza wahojiwa kueleza walichokielewa kuhusu mwenendo wa ubora wa elimu ya sekondari katika miaka 10 iliyopita. Sanjari na viwango vya ufaulu vilivyochapishwa, wananchi wengi wanaona kuwa mwenendo wa ubora wa elimu umekuwa ukiporomoka.

Kielelezo cha 3: Maono ya mwenendo wa ubora wa elimu ya sekondari katika miaka 10 iliyopita

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti kwa Njia ya Simu – Awamu ya 1, Aprili 2013.

4

5%

12%

83%

Haina mabadiliko

Imeongezeka ubora

Ubora umeshuka

32%

68%

Ndiyo

Hapana

Maoni ya wananchi, kwa hiyo, yanawiana na takwimu zilizochapishwa kuhusu mgogoro wa matokeo ya kujifunza nchini Tanzania. Hatua ya kwanza katika kubadili mwelekeo huu ni kuelewa sababu na vichochezi vya matokeo ya kujifunza. Muhtasari huu unachunguza vitabu, walimu na wazazi. Katika kupata mitazamo ya wazazi kuhusu hali za shule, Sauti za Wananchi kwanza iliwauliza wahojiwa endapo walikuwa na watoto wa umri wa kwenda shule. Ni wale tu waliokuwa na watoto wanaosoma shule za msingi au sekondari au wale ambao watoto wao wameacha shule ndani ya mwaka mmoja uliopita ndio waliulizwa kuzungumzia hali za shule.

Jambo la 4: Wazazi waliripoti upungufu wa vitabu vya kiada Moja ya masuala yanayohitaji kutazamwa kwa ukaribu ni upatikanaji wa vitabu Kama hakuna vitabu, wanafunzi wanategemea njia moja tuu ya kujifunza, nayo ni kupitia kwa mwalimu darasani huku wakinakili matini kwenye madaftari yao. Pale vitabu vinapokuwapo, njia nyingine za kujifunza hufunguka; kwa mfano, wanafunzi wanajisomea wenyewe au walimu wanatoa kazi za ziada kwa kutumia vitabu vya kiada ili wanafunzi waendelee kujifunza hata baada ya vipindi.

Kama Kielelezo cha 4 kinavyoonyesha, asilimia 55 ya wazazi walio na wanafunzi shule za msingi wanaripoti kwamba watoto wao hawana kabisa vitabu vya kiada. Matokeo yanaonyesha kwamba hali ni nafuu kidogo ingawa bado si ya kuridhisha katika shule za sekondari. Miongoni mwa wazazi wenye watoto wanaosoma sekondari, asilimia 32 wanaripoti kwamba watoto wao hawana vitabu vyovyote vya kiada; hata hivyo, asilimia 54 wanaripoti kwamba watoto wao wana vitabu viwili au zaidi vya kiada. Ni muhimu kuzingatia pia kwamba miongoni mwa wazazi wenye watoto katika shule za sekondari, asilimia 10 ya wazazi walieleza kuwa hawajui kabisa kuhusu upatikanaji vitabu. Mwanafunzi wa kawaida wa shule ya sekondari husoma kati ya masomo sita mpaka tisa, na anatarajiwa walau awe na kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo.

Kielelezo cha 4: Umiliki wa vitabu vya kiada miongoni mwa wanafunzi katika shule za Msingi na Sekondari

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti kwa Njia ya Simu – Awamu ya 1, Aprili 2013.

5

55%

32%36%

11%

4%9%

31%

54%

44%

2%

10% 10%

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

Watoto shuleza msingi

Watoto shuleza sekondari

Watoto katika shuleza msingi na secondary

Hakuna kitabu cha kiada

Kitabu kimoja cha kiada

Vitabu viwili au zaidi vya kiada

Sijui

Jambo la 5: Wanafunzi wanaripoti kwamba walimu wanaingia kwenye baadhi tu ya vipindi Wakati wa Utafiti wa msingi wa Sauti za Wananchi (mahojiano ya ana kwa ana, Novemba 2012) katika kila kaya iliyokuwa na mtoto au watoto wanaosoma shule ya msingi au sekondari, mtoto mmoja alichaguliwa kwa nasibu ili kuelezea kuhusu shule yake. Tuliwauliza wanafunzi hawa ikiwa walimu waliingia kwenye vipindi vyote katika siku ya mwisho waliyohudhuria masomo.

Kama Kielelezo cha 5 kinavyoonyesha, tuliona kwamba zaidi kidogo ya asilimia 30 ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari waliripoti kwamba kila kipindi cha somo walichohudhuria mara ya mwisho walipokuwa shule mwalimu aliingia kufundisha.

Kielelezo cha 5: Mahudhurio ya walimu katika shule za Msingi na Sekondari

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti wa Msingi, Oktoba 2012.

Kwa wastani, asilimia 59 ya wanafunzi waliripoti kwamba baadhi ya walimu waliingia na wengine hawakuingia kufundisha. Mwisho, kwa wastani, asilimia 10 ya mwanafunzi katika shule za msingi na sekondari waliripoti kwamba hakuna mwalimu kabisa aliyeingia katika siku ya mwisho walipohudhuria shule.

Izingatiwe kwamba wanafunzi wengi zaidi wanaripoti kwamba zaidi ya mwalimu mmoja anawajibika kuwafundisha. Kundi la jibu “Mwalimu aliingia kwa baadhi ya vipindi” kwa hiyo, inahusisha kesi zile ambapo mwalimu mmoja hakuwapo na mwingine alikuwapo darasani, na hii inaweza kuficha viwango vya juu vya utoro wa walimu. Hii inawiana na matokeo ya utafiti wa Sauti za Wananchi pale shule 156 za msingi zilizo kwenye sampuli zilipotembelewa. Kwa mujibu wa kumbukumbu za shule, shule ya kawaida huajiri jumla ya walimu 11 lakini wakati zilipotembelewa, watendaji wa Sauti za Wananchi waligundua kwamba, katika shule ya kawaida, kulikuwa na walimu 4 tu wakifanya kazi ya kufundisha.

6

32% 31%

60%57%

8%12%

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

70%

Msingi Sekondari

Walimu waliingia vipindivyote

Walimu waliingia baadhi yavipindi

Hakuna mwalimu aliyeingiakwenye kipindi

Hii inaonyeshwa pia na majibu ya wanafunzi. Ni asilimia 30 ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari wanaoripoti kufundishwa katika vipindi vyote. Majibu mengi zaidi yapo katika kundi la mchanganyiko, ambapo walimu walikuwa wakifundisha sehemu ya vipindi na waliacha kazi ya kufanya na kisha kuondoka zao.

Kielelezo cha 6: Wanafunzi wanaripoti kuhusu kazi ya walimu darasani

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti wa Msingi, Oktoba 2012

Jambo la 6: Wazazi wanahusika na kujifunza kwa mwanafunzi Wazazi ni wadau wa muhimu katika mchakato wa kujifunza kwa mtoto. Kuna walau njia mbili ambazo mzazi anaweza kufuatilia kama mtoto wake anajifunza shuleni au la. Njia moja ni kwa kukagua madaftari (kuona kama walimu wanapitia kazi za wanafunzi na kujaribu kubaini maeneo ambayo mtoto anahitaji msaada). Njia ya pili ni kumsaidia mtoto wake kufanya kazi ya masomo ya ziada nyumbani. Katika Awamu ya 1 ya Utafiti wa Sauti za Wananchi wazazi waliulizwa endapo waliwasaidia watoto wao kwa njia hizi na wakati gani. Wazazi walioripoti kukagua madaftari ya watoto wao katika siku hiyo (asilimia 29) au wiki moja kabla ya mahojiano (asilimia 35) . Asilimia 25 walifanya hivyo muda mrefu uliopita au hawajafanya kabisa. Zaidi ya hayo, asilimia 41 ya wazazi waliripoti kuwasaidia watoto wao kufanya kazi zao za ziada za masomo walau wiki moja iliyopita; asilimia 44 walisema kwamba hawajawahi au walifanya hivyo zamani sana.

7

Kielelezo cha 7: Ushiriki wa Wazazi katika Kujifunza

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti kwa Njia ya Simu – Awamu ya 1, Aprili 2013.

Jambo la 7: Wanafunzi wanajua udhaifu wao Kufuatia matokeo mabaya ya mitihani, wanafunzi wote walielezwa kubaini masomo yale wanayoona kuwa ni magumu. Wanafunzi waliripoti kwamba Kiingereza na Hisabati ndiyo masomo magumu zaidi katika shule za msingi na sekondari. Zaidi ya hilo, Kielelezo cha 8 kinaonyesha kwamba masomo ya sayansi ni magumu pia kuelewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Kielelezo cha 8: Wanafunzi waripoti masomo magumu zaidi katika shule za Msingi na Sekondari

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti wa Msingi, Oktoba 2012

8

12%

29%

16%

44%

29%

35%

12%

25%

0% 5% 10% 15% 20% 25% 30% 35% 40% 45% 50%

Jana

Wiki iliyopita

Ndani ya miezi 6iliyopita

Zamani sana/Kamwe

Walikagua madaftari (%) Walisaidia kazi ya ziada ya masomo (%)

1%

2%

3%

3%

23%

64%

5%

20%

3%

5%

34%

16%

0% 10% 20% 30% 40% 50% 60% 70%

Historia

Sayansi

Kiswahili

Masomo mengine

Hisabati

Kiingereza

Secondari

Msingi

Jambo la 8: Viwango vya kujifunza viko chini Ili kuthibitisha uwezo mzuri na udhaifu ulioripotiwa na wanafunzi wenyewe hapo juu, watendaji wa Sauti za Wananchi waliendesha tathmini rahisi ya kujifunza inayofahamika kama jaribio la Uwezo. Jaribio hili ni la ngazi ya Darasa la 2 kwa masamo ya Kiswahili, Kiingereza na Kuhesabu. Ili kupata sampuli za majaribio na taarifa zaidi kuhusu mbinu zinazohusika tembelea www.uwezo.net.

Kielelezo cha 9 hapo chini kinaonyesha matokeo ya jaribio la Uwezo miongoni mwa wanafunzi waliopimwa. Ni muhimu kukumbuka kwamba majaribio hayo ya Darasa la 2 ndio yaliyotumika kupima uwezo wa kujifunza kwa wanafunzi wa ngazi zote waliokuwa kwenye sampuli yetu, wawe wameandikishwa shule za msingi au sekondari.

Kielelezo cha 9: Tathmini ya kiwango cha kujifunza ya Darasa la 2

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti wa Msingi, Oktoba 2012

Matokeo ya kupima uwezo wa wanafunzi kujifunza yanayonyesha viwango vya chini vya kujifunza kwa shule za msingi na sekondari. Kwa mfano, asilimia 72 ya wanafunzi wa shule za msingi na asilimia 66 ya wanafunzi wa sekondari hawawezi kuzidisha. Zaidi ya hilo, wanafunzi walio wengi katika shule za msingi hawakumudu kujibu maswali ya ufahamu ya hadithi ya Kiingereza au ile ya Kiswahili (mfano wa hadithi na maswali yaliyotumika uko hapa juu). Uwezo wa wanafunzi katika shule za sekondari kuelewa hadithi ya Kiingereza ya Kiwango cha Darasa la Pili, ambapo Kiingereza ndio lugha ya kufundishia, ni jambo linalofadhaisha.

9

72%81%

93%

66%

43%

70%

0%

20%

40%

60%

80%

100%

Hawawezikuzidisha

Hawezi kuelewaHadithi yaKiswahili

Hawezi kuelewaHadithi yaKiingereza

Shule za Msingi

Shule za Sekondari

Example story: Zuberi is our class teacher. He loves our parents. We love our teacher too. He gives his pupils books. The pupils write in the books. Our books are red. We use pencils to write.

Question: 1. What do the pupils write in? 2. Who gives his pupils books?

Jambo la 9: Wazazi wanailaumu serikali na walimu Utafiti wa Sauti za Wananchi uliwauliza wazazi kuhusu yule wanaemfikiria kuwa anahusika na matokeo mabaya ya wanafunzi wa Kidato cha Nne ya mwaka 2012. Kwa mujibu wa maoni ya wananchi wengi, Serikali ya Tanzania na walimu ndio wanaohusika, kwa pamoja wana zaidi ya asilimia 70 ya majibu kwa swali hili. Shutuma zaidi zinaelekezwa na wananchi kwao wenyewe (kama wazazi), watoto wao (wanafunzi) lakini pia kwa Wizara na Waziri mwenye dhamana ya elimu.

Kielelezo cha 10: Wazazi waitupia Serikali lawama kwa matokeo mabaya ya mitihani ya Kidato cha Nne

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti kwa Njia ya Simu – Awamu ya 1, Aprili 2013.

Jambo la 10: Wazazi wanaeleza kwamba idadi na ari ya walimu kuwa ni baadhi ya vikwazo vikuu Utafiti wa Sauti za Wananchi uliwauliza wazazi wenye watoto wa umri wa kwenda shule kuhusu vikwazo vikuu viwili vinavyowafanya wanafunzi kwenye jamii zao kushindwa kufaulu mitihani.

Majibu makuu yamejikita katika idadi ya walimu, ubora wao na motisha, kama inavyoonyeshwa kwenye Kielelezo cha 11. Kwanza, kwa wastani asilimia 22 ya wazazi wenye watoto shule ya msingi na sekondari wanaeleza kwamba shule zina walimu wachache sana. Idadi isiyotafautiana sana hiyohiyo ya wazazi (asimilia 18) wanaripoti kwamba walimu katika jamii zao hawana motisha. Kujazana madarasani ni jambo lililozungumziwa na asilimia 12 ya wazazi kwa wastani.

10

1%

1%

1%

1%

1%

3%

7%

8%

34%

38%

0% 5% 10% 15% 20% 25% 30% 35% 40%

Rais

Wanafunzi kuendelea na masomolicha ya matokeo ya kidato cha pili

Viongozi wa serikali

Jamii

Baraza la Mitihani

Wazazi

Waziri/Wizara ya Elimu

Wanafunzi

Walimu

Serikali (Kwa Ujumla)

Wazazi pia waliombwa kueleza serikali ifanye nini ili kuongeza ubora wa elimu katika shule za sekondari.

Mapendekezo ya wazazi kuhusu namna ya kuongeza ubora wa elimu kama yalivyoainishwa hapo juu yanawiana vema na vikwazo vilivyowakabili wanafunzi kufaulu mitihani iliyobainishwa na wazazi (Kielelezo cha 11).

Kielelezo cha 11: Wazazi waainisha vikwazo vikuu kwa watoto kufaulu mitihani

Chanzo cha takwimu: Sauti za Wananchi, Utafiti kwa Njia ya Simu – Awamu ya 1, Aprili 2013.

Hitimisho Moja ya matokeo chanya na matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 yaliyochapishwa hivi karibuni ni kwamba yameibua mjadala wa kitaifa, miongoni mwa wananchi, kwenye magazeti, na kwenye duru za kutunga sera, kuhusu hali ya elimu nchini. Mambo makuu kumi yaliyoripotiwa katika muhtasari huu wa utafiti wa Sauti za Wananchi yanachangia takwimu za hivi karibuni kabisa zenye sura ya kitaifa kuhusu elimu katika mjadala huu. Makusudi ya Sauti za Wananchi ni kuupeleka mjadala kwa watu wanaohusika na takwimu hizi na kuwafanya wazungumze.

Wazazi na watoto wa umri wa kwenda shule kutoka katika kila jamii Tanzania Bara wanatoa maoni yaliyo wazi kuhusu elimu. Kwa ufupi, wananchi hawa wanaripoti kwamba wana taarifa kuhusu matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 yaliyochapishwa na wanaona kwamba kuna kushuka kwa ubora wa elimu ya sekondari; kwamba mara nyingi watoto wao hawana vitabu vya kujifunzia, hasa katika shule za msingi; kwamba mara nyingi walimu hawaingii kwenye vipindi vyao vyote na pale wanapofanya hivyo, sana sana ni kutoa tu kazi na kisha kuondoka zao; na kwamba kwa wastani wazazi wanafanya jitihada kuwasaidia watoto wao kujifunza.

11

 

3%  

5%  

5%  

7%  

8%  

11%  

18%  

11%  

23%  

3%  

3%  

5%  

7%  

7%  

13%  

17%  

17%  

21%  

0%   10%   20%   30%  

Shule  zina  rasilimali  kidogo  (Viingizishi)  

Wanafunzi  wanaghasiwa  na  mambo  mengine  

Wanafunzi  hawajisomei  nyumbani  

Shule  ziko  mbali  

Wanafunzi  hawana  moCsha  

Madarasa  yamefurika  wanafunzi  shuleni  

Walimu  hawana  moCsha  

Walimu  hawana  sifa  

Shule  zina  walimu  wachache  sana  

Shule  za  Msingi  

Shule  za  Sekondari  

• Asilimia 24 walishauri serikali iongeze idadi ya walimu mashuleni• Asilimia 17 walishauri serikali kujikita katika kukuza ubora wa walimu• Asilimia 13 walishauri serikali kuongeza mishahara na kuwalipa walimu kwa wakati• Asilimia 5 walishauri serikali kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa shule za serikali

Tathmini ya kujifunza kwa wanafunzi iliyo katika takwimu za utafiti wa Sauti za Wananchi inaonyesha kwamba viwango vya umahiri katika Hisabati na kusoma Kiingereza viko chini kwa namna ya kukera, vikithibitisha kabisa matokeo ya mitihani ya kitaifa. Mwisho, walipoulizwa na watendaji wa Sauti za Wananchi kuhusu sababu za kufeli kwingi katika mitihani, wazazi wanakazia dhima ya walimu. Wazazi wanaona kuna upungufu wa walimu na wanaitaka serikali kuwapunguzia wazazi mzigo; kwa upande mwingine, wazazi wanabainisha kuwa motisha ndogo miongoni mwa walimu na viwango vya chini vya sifa ni baadhi ya matatizo.

Matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne yanaonyesha viwango vya chini kabisa vya kupata elimu katika elimu ya msingi nchini Tanzania leo. Uwekezaji mkubwa uliofanyika katika muongo uliopita bado haujaonekana katika kukua kwa viwango vya kujifunza miongoni mwa wanafunzi. Katika kusukuma mambo mbele, serikali italazimika kutazama upya ushahidi wa nini hasa huleta msukumo katika kujifunza na hivyo kurekebisha sera, programu na malengo yake kwa namna inayostahili. Kukuza ari ya walimu, ufanisi na uwajibikaji ndio kiini cha changamoto hii.

12