204152705 hotuba ya mheshimiwa jakaya mrisho kikwete rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania na...

Upload: haki-ngowi

Post on 04-Jun-2018

398 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    1/12

    1

    HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAISWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI

    WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA KATIKA SHEREHE ZAKUTIMIZA MIAKA 37 YA UHAI WA CCM KWENYE UWANJA WA

    SOKOINE, MBEYA, TAREHE 2 FEBRUARI, 2014

    Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndugu Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya na NaibuWaziri wa Kilimo, Chakula na !hirika"

    Ndugu #bdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM $aifa" Ndugu Wa%umbe wa Kamati Kuu na &alma!hauri Kuu ya $aifa" Ndugu Makatibu wa 'ekretarieti ya &alma!hauri Kuu ya $aifa Mliopo"Watenda%i Wakuu wa 'erikali na (iongozi wa CCM wa Ngazi Mbalimbali"Wana)hama Wenzangu wa CCM"

    Mabibi na Mabwana" Ndugu Wanan)hi"

    Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema,kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana siku ya leo hapa Mbeya,kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Nawashukurusana viongozi, wanaCCM na wakazi wote wa Mbeya kwa mapokezi mazuri naukarimu wenu kwangu na wageni wenzangu tangu tulipowasili jijini hapa janampaka sasa. akika tutaondoka Mbeya tukiwa na kumbukumbu nzuri yaukarimu na upendo wenu kwetu.

    !hukrani nyingine nazitoa kwa viongozi na wanachama wenzetu waMbeya kwa kukubali kuwa mwenyeji wa sherehe hizi. Na"ahamu "ika kwambakuandaa sherehe kubwa kama hii si jambo jepesi. #akini, ina"urahisha nakuleta "araja kwamba, kutokana na moyo wenu wa kujitolea, umahiri naumakini wenu, mambo yame"ana sana. Matembezi ya mshikamano yali"anasana na hapa kiwanjani mambo ni mazuri sana. ongereni sana.

    Niruhusuni, kupitia hadhara hii, niwapongeze kwa dhati viongozi,wanachama, makada, wapenzi na washabiki wote wa CCM kote nchini kwakuadhimisha miaka 37 ya uhai wa Chama chetu. $una"anya sherehe hizi leokwa vile tarehe % &ebruari, '()* ni siku ya kazi. !i vyema kuwatoa watukazini. Ndiyo maana tuna"anya madhimisho haya leo. $unayo kila sababu yakusherehekea siku hii kwa vi"ijo na nderemo kama tu"anyavyo siku zote. ii nikutokana na ukweli kuwa CCM ina historia iliyotukuka, kuvutia na kusisimua.Chama chetu kimepata ma"anikio makubwa tangu kuasisiwa kwake tarehe %

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    2/12

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    3/12

    3

    wa sababu ya 6chaguzi wa !erikali za Mitaa mwaka huu na 6chaguziMkuu mwakani kazi ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ina umuhimu wakipekee. #azima tupate ma"anikio katika jambo hilo kwani yanakipa Chamachetu nguvu ya kutuwezesha kupambana na kupata ushindi katika chaguzi hizo.

    azi nzuri tuliyo"anya katika utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Chama miakailiyopita ndiyo iliyotupa ma"anikio makubwa ya '((+ na '()( tunayojivuniasasa. ivyo basi tuki"anya vizuri mwaka huu tutapata ushindi kama ule au hatazaidi.

    /ila shaka sote tunatambua kuwa kazi ya kuimarisha Chama inahusishamambo matatu wanza, kujenga na kuimarisha Chama kama taasisi. iliku"anya kazi ya Chama ndani ya umma. Na tatu ni ku"anya kazi ya ku"uatiliautekelezaji wa 8lani ya 6chaguzi ya Chama, sera na maamuzi ya Chamaunao"anywa na !erikali na vyombo vyake. Naamini wote mnajua kuwasizungumzii mambo mapya. Mambo yote matatu tunayajua kwani tumekuwatunaya"anya kwa miaka mingi. Ninachoki"anya leo ni kukumbushana juu yaumuhimu wa kuendelea ku"anya kazi hiyo ila tui"anye kwa u"anisi zaidi, kwanguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi.(iongozi Wenzangu na Wana)hama Wenzangu"

    /ahati nzuri mwezi Novemba, '()' tulikamilisha 6chaguzi ndani yaChama, hivyo tunayo sa"u mpya madhubuti ya viongozi wa Chama chetu na9umuiya zake ya kuongoza mpaka mwaka '()7. ama ilivyokuwa miaka yanyuma, viongozi hao ndiyo watu wenye jukumu la kihistoria la kuongoza CCMna wanachama wake kuta"uta na kupata ushindi katika chaguzi zijazo mwakahuu na mwaka ujao. ivyo basi, viongozi tuliochaguliwa hatuna budikuitambua dhamana hiyo kubwa tuliyopewa na wanachama wenzetu. #azimakuhakikisha kuwa tunatimiza ipasavyo wajibu wetu huo. $usiwaangushewanachama wenzetu. wa ajili hiyo lazima tujipange vizuri, tuelekeze akilizetu, nguvu zetu na muda wetu kwenye kuhakikisha kuwa Chama chaMapinduzi kina uwezo na si"a ya kukiwezesha kupata ushindi mnono.

    Ndugu (iongozi Wenzangu"9ambo la kwanza muhimu kwetu ku"anya ni kuona kuwa viungo vyote

    vya Chama chetu viko kamili"u na vina"anya kazi vizuri. Chama kiwe nawanachama wengi ambao wanatimiza ipasavyo wajibu wao kwa Chama chao.1iongozi wa Chama wawe hodari ku"anya kazi ndani ya Chama na ndani yaumma. -asiwe mangimeza bali watoke waende kwa wanachama kuimarishauhai wa Chama. -aende kwa wananchi kukisemea Chama, kusikiliza shidazao na kusaidia kuta"uta u"umbuzi. #azima Chama kiwe mlezi na kimbilio lawananchi. $uki"anya hivyo watu wetu watakuwa na imani na mapenzi naCCM hivyo watakiunga mkono katika chaguzi za dola. $uhakikishe kuwa

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    4/12

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    5/12

    5

    yashughulikiwe ipasavyo tena kwa wakati mua"aka. jizi nyumba ya njaa.6sipoziba u"a utajenga ukuta.

    Ndugu Zangu, WanaCCM Wenzangu" Nawasihi sana tulipe uzito unaostahili suala la uadili"u wa viongozi wetu

    na wanachama. /ila ya hivyo Chama kinaweza kuwa imara na !erikali yakeikatekeleza majukumu yake ipasavyo, lakini kikakosa kuungwa mkono nakupoteza ushindi kwa sababu ya tabia na mwenendo usio"aa wa viongozi nawanachama. Ndiyo maana Chama kikaunda amati za 6salama na Maadiliku"anya kazi ya kuwabana wanaokiuka maadili. Naomba amati hizo zi"anyekazi zake ipasavyo. utoku"anya hivyo kunaathiri sana hadhira ya kukubalikakwa CCM katika jamii. ususan nawataka tu"anye kila linalowezekanatuondokane na tabia ya kutoa na kupokea rushwa katika kuchagua viongozi namchakato wa uteuzi wa wagombea.

    $usikubali uovu huu ikageuka kuwa mila na desturi ndani ya Chamakikubwa na chenye historia iliyotukuka kama CCM. 1itendo hivi lazimatuvikatae na tuvipige vita kwa nguvu zetu zote. $usiwaache watu wachachewanaotaka uongozi kwa gharama yo yote waharibu si"a nzuri ya Chama chaMapinduzi. $usiache ikajengeka dhana poto"u kwamba ukitaka uongozi ndaniya Chama uwe kupitia CCM na uwezo wa ki"edha kuhonga watu ndani yaChama na nje ya Chama. $usikubali kuacha Chama chetu ki"ikishwe hapo.$unakitoa thamani mbele ya watu na kuhatarisha uhai wake. $uchukue hatuastahiki sasa kwa mujibu wa atiba na anuni za Maadili za Chama chetu.-ale wote wanao"anya vitendo hivyo na mawakala wao wadhibitiwe.

    Ndugu Zangu"(iongozi Wenzangu na WanaCCM Wenzangu"

    ama nilivyokwishadokeza awali, kuimarisha Chama cha Mapinduzi ni pamoja na ku"anya kazi ya Chama ndani ya umma. 1iongozi wa Chama lazimawatoke kwenda kuwatembelea wananchi, kuzungumza nao, kuona au hatakushiriki katika shughuli zao. uwajulia hali na kutambua "araja zao namatatizo yao. :aliyo mema yaimarishwe na matatizo yapatiwe u"umbuzi./ahati nzuri CCM ndiyo yenye !erikali, hivyo viongozi wakiyakuta matatizo nakutoa taari"a kwa mamlaka za !erikali katika ngazi husika yatashughulikiwa.

    !ina budi kumpongeza sana atibu Mkuu wa CCM, Ndugu bdulrahmaninana kwa kuonesha njia na kutoa m"ano kuhusu ku"anya kazi ya Chama

    ndani ya umma. atika ziara zake Mikoani aki"uatana na baadhi ya Makatibuwa !ekretarieti na viongozi wengine wa CCM amekuwa ana"anya kazi kubwana nzuri sana. ;iara zake zinakijenga Chama cha Mapinduzi na kutoa taswiranzuri ya Chama chetu katika jamii. ;inahuisha uhai wa CCM. Ndugu inanaamekuwa ana"anya mambo ambayo hayajazoeleka ku"anywa. metembelea

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    6/12

    6

    maeneo ambayo si viongozi wengi hu"ika. -akati mwingine amekuwaanatumia njia za usa"iri zinazoogopesha wengi. ukaa na wananchi, anakulanao na ku"anya kazi nao. Na kubwa zaidi amekuwa anatoa "ursa kwa wananchikuelezea matatizo yanayowasibu, manungu

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    7/12

    7

    kujielimisha kuhusu 8lani ya 6chaguzi ya CCM. $ujue kwa undaniinazungumzia nini na kisha tuwa"uatilie viongozi na watendaji wa !erikaliwaitekeleze.

    Ndugu Wanan)hi"wa jumla utekelezaji wa 8lani na !era za CCM na ahadi za !erikali

    unaenda vizuri. !i yote yamekamilika na kwamba huenda tusiyamalize yotetuliyokusudia kuya"anya. iyo haitatokana na uzembe au kupuuzia bali kwasababu ya kutopata "edha zote tunazohitaji. imsingi mambo mengi mazuriyameya"anyika na tunaendelea kuya"anya. atika maeneo yote kuna ma"anikioya wazi kwa kila mtu kuona. 8we kwenye elimu, maji, a"ya, barabara, umemena mengineyo.

    wa upande wa elimu, kwa m"ano, tumepanua sana na"asi za masomokwa vijana wetu katika ngazi zote kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vya juu.6panuzi huo umewezesha watoto na vijana wetu wengi kupata "ursa ya kupataelimu na ma"unzo. azi tunayo"anya sasa kwa nguvu na ari kubwa nikuboresha elimu inayotolewa. $unacho"anya sasa ni kuhakikisha walimu wapowa kutosha na kila shule zinakuwa na vitabu na vi"aa vya ku"undishia nakuji"unzia vinavyokidhi mahitaji. ii ni pamoja na kuhakikisha kila shuleinakuwa na maabara za sayansi. 1ilevile, tunaboresha mazingira ya walimu yakuishi na ku"anyia kazi. azi hizo tunaendelea nazo vizuri.

    Ndugu Wanan)hi"Maji nayo tumeyapa umuhimu wa juu katika utekelezaji wa malengo ya

    8lani na !era za !erikali. #engo letu kuu ni kuona kuwa "$ & ! " '0 ya watu wamijini na "$ & ! " () ya watu wa vijijini wanapata maji sa"i na salama i"ikapo'()%. ama "edha zitapatikana kama ilivyopangwa tunatarajia kuwa katikamwaka '()3>)* watu milioni 7*1 watapata maji. atika mwaka ujao wa "edha'()*>)% tumepanga kuwapatia maji watu wengine ! & + 7 na mwakautao"uata ?'()%>)5@ tutaongeza tena huduma hiyo kwa watu ! & + 1*3* atuahizo zinatu"anya tu"ikie malengo kwa miji ambayo ni zaidi ya lengo.

    Ma"anikio pia yapo katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya a"ya kwawananchi wa $anzania. ;ahanati, vituo vya a"ya na hospitali zimeendeleakujengwa kote nchini. idha, hospitali za wilaya, mikoa, kanda na ospitali ya$ai"a Muhimbili zimeendelea kuboreshwa. wa ajili hiyo idadi ya -atanzaniawanaoweza kupata huduma ya a"ya iliyo bora inazidi kuongezeka. alikadhalika, wataalamu wa a"ya wa "ani mbalimbali wameongezeka na hali yaupatikanaji wa dawa na vi"aa tiba imezidi kuboreshwa.

    $umeendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya barabara, reli naumeme. wa upande wa barabara lengo letu la kuunganisha mikoa kwa

    barabara za lami linaendelea vizuri. Mwaka jana tulikamilisha ujenzi wa

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    8/12

    8

    - &+!./" 77 za barabara za lami na ujenzi wa nyingine unaendelea sehemumbalimbali nchini. uhusu reli, tunaendelea kuimarisha reli ya $ ; = nareli ya kati ili ziweze ku"anya kazi kwa u"anisi zaidi. Mchakato wa kuboreshanjia ya reli na ununuzi wa mabehewa na injini unaendelea vizuri. wa upandewa $ ; = ni matumaini yetu kuwa masuala ya uendeshaji yatapatiwau"umbuzi na !erikali za nchi zetu mbili.

    idha, jitihada zetu za kuwapatia umeme -atanzania kwa "$ & ! " 30i"ikapo '()% zinaendelea vizuri. $ume"anikiwa kuongeza idadi ya -atanzaniawanaopata umeme kutoka "$ & ! " 10 mwaka '()% hadi "$ & ! " 24 mwaka'()3. wa kasi tunayoendelea nayo hivi sasa, naamini tutavuka lengo letu hilo.

    aya yote ni ma"anikio ya kujivunia. Ndugu wanan)hi"

    wa hapa Mkoani Mbeya, nawapongeza kwa kupiga hatua nzuri yamaendeleo katika maeneo mbalimbali. wa upande wa elimu mme"anikiwakupanua "ursa za elimu katika ngazo zote. Mkoa unao shule za msingi 1,0'4zenye wana"unzi )32,7(), shule za sekondari ni 310 zenye wana"unzi 1)2,2 'vyuo vikuu 3 na matawi kadhaa ya vyuo vikuu pamoja na vyuo ( vya ualimu.

    azi mliyonayo ni kuwasimamia na kuwaongoza vijana wetu watumie ipasavyo"ursa hizo.

    wa upande wa a"ya, upanuzi wa ospitali ya Mkoa unaendelea vizurina majengo ya hospitali pamoja na wodi yanaendelea kujengwa. atika mwakawa "edha '()3>'()* zaidi ya $% & ! & + 300 zimetengwa kwa ajili yakumalizia ujenzi wa wodi ya watoto na Mkandarasi wa kui"anya kazi hiyotayari ameshapatikana. !uala la ghala la M!A ndani ya hospitali tutalipatiau"umbuzi mapema iwezekanavyo.

    Ndugu Wanan)hi"uhusu maji, kwa mwaka '()3>'()* ! #" 0 ya maji inatekelezwa katika

    vijiji 112 ambapo kati ya hiyo miradi 1) imekamilika. Miradi hiyo ni Namkukwe ?Chunya@, Namtambalala ?Momba@, Masoko ? yela@, yimo?=ungwe@, Mbambo, ipapa na ikuba ?/usokelo@, 6baruku na Chimala?Mbarali@, Mbebe na #uswisi ?8leje@, 8kombe ? yela@, Maninga ?Mbozi@,8walanje na !hongo>8gale ?Mbeya@. idha, miradi mingine )) iko katika hatuambalimbali za ujenzi na mingine 10 iko katika hatua za zabuni. 9umla ya$% & & + 3 *14 zinategemewa kutumika katika ujenzi wa miradi hiyoitakayohudumia watu wapatao )0 ,0(4* 8takapokamilika ita"anya huduma yamaji vijijini ku"ikia "$ & ! " 73*). wa hapa mjini na"ahamu hali ya upatikanajiwa maji sa"i na salama inaridhisha. 4mbi langu kwenu, tunzeni vyanzo vyamaji ili upatikanaji wa maji uwe wa uhakika.

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    9/12

    9

    wa upande wa umeme, kuna miradi 12 ya umeme vijijini ambayoinatekelezwa na !erikali kupitia -akala wa 6meme 1ijijini ?=B @. Miradi hiiimeshakamilika kwa "$ & ! " '4 katika -ilaya za Mbeya 1ijijini miradi minne,Mbozi miradi mitatu, Chunya miradi mitatu na =ungwe miradi mwili. Miradihii imegharimu jumla ya S% & && + 7*( na wateja wanaendeleakuunganishwa. atika mwaka '()*, jumla ya vijiji 170 vitapatiwa umeme na

    jumla ya $% & & + 2*2( zimetengwa kwa madhumuni hayo. Mradi waumeme wa Matema -ilayani yela, ambao ni ahadi yangu sasa umekamilikana umeme unasambazwa kwa wananchi. atika 9iji la Mbeya kuna miradi yaumeme chini ya mpango wa utekelezaji wa Millenium Challenge ccount$anzania ?MC $@ ambayo imekamilika kwa "$ & ! " '' .

    /arabara ya Mbeya Chunya inaendelea kujengwa ?=i"t 1alley #wanjiloimekamilika kwa "$ & ! " 2) na #wanjilo D Chunya imekamilika kwa "$ & ! "7 5* asi ya ujenzi ni ndogo hasa kwa kipande cha Mbeya D #wanjilo kwasababu ya mkandarasi wa kwanza kushindwa kazi. Naamini -izara itachukuahatua stahiki kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo. 6jenzi wa barabara ya

    yela hadi Matema /each umeanza na mwaka huu kasi itaongezwa kwa kuanzamchakato wa kujenga kilometa 1 . 6sani"u wa barabara ya Mpemba D8songoleumekamilika kitakacho"uata ni kuta"uta "edha za ujenzi. $unazita"uta. ivyondivyo ilivyo kwa barabara ya Mpemba D 8tumba na barabara ya atumba D=uangwa D $ukuyu. wa upande mwingine inatia moyo kuona kuwa sasa

    barabara nyingi zaidi za vijijini zinapitika mwaka mzima. Ndugu Wanan)hi"

    idha, ujenzi wa 6wanja wa Ndege wa imatai"a !ongwe umekamilikakwa "$ & ! " ') na kuwezesha ndege kutua. 6jenzi wa jengo jipya la abiriaunaendelea na unategemewa kukamilika miezi miwili ijayo. azi za kuwekatabaka la mwisho la zege kwenye maegesho ya magari, kununua na ku"ungali"ti na ngazi ya umeme zinaendelea. ata hivyo ili mazao ya kilimo yawezekusa"irishwa, tumewashauri Mamlaka ya 1iwanja vya Ndege $anzania wajengeghala kwa ajili ya mazao yanayoharibika haraka. ia wa"unge taa kwenye njiaya kutua na kuruka ndege.

    Ndugu Wanan)hi"wa upande wa kilimo napenda kutoa pongezi kwa Mkoa wa Mbeya

    kuendelea kuwa ghala la chakula la kutumainiwa. Naomna mwaka huu mvua ninzuri hivyo endeleeni kudumisha kazi nzuri mui"anyayo. $utaendeleakuwaunga mkono na hasa kwa upande wa kurahisisha upatikanaji wa pembejeoza kilimo. 8natia moyo kuona mengi tulioahidi katika 8lani za '((% na '()(tumeyatekeleza na mengine tunaendelea kuyatekeleza. Naomba viongozimueleze ma"anikio hayo yaliyopatikana. azi hii siyo ya Mwenyekiti, Makamu

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    10/12

    10

    Mwenyekiti, atibu Mkuu na viongozi wengine wa kitai"a peke yao. Ni kazi yaviongozi wote waliopo katika ngazi mbalimbali za uongozi kuanzia kwenye!hina. Naomba tui"anye kwa bidii, bila kuchoka.

    wenye kui"anya kazi hiyo, hakuna kulala. :apo mambo mengi mazuriya kusema na hakuna mwingine wa kuyasemea zaidi yetu sisi wenyewe.$usiposema sisi wananchi waliotutuma hawata"ahamu tuliyowa"anyia na wakatimwingine watapotoshwa na watu wasiotutakia mema. Ni kazi inayotakiwaku"anywa na kila kiongozi wa CCM na wanachama wao pia. u"anya hivyotutatambuliwa na kuheshimiwa inavyostahiki. $uki"anya hayo sioni kwa niniCCM isiendelee kushika dola kwa miongo mingi ijayo.

    M6%"-"/+ " K"/ " Ndugu WanaCCM"

    Mchakato wa atiba Mpya unakwenda vizuri mpaka sasa. $arehe 3(Aesemba, '()3 nilipokea =asimu ya ili ya atibaMpya na $aari"a ya $ume ya

    atiba. $aari"a ya $ume imekusanya maoni ya wananchi kuhusu mambombalimbali ikiwa ni pamoja na kero zao, mapendekezo ya marekebisho ya serambalimbali na mambo mengi yanayohusu maisha yao. !erikali itayata"akarimapendekezo hayo nakuchukua hatua zipasazo. =asimu ya atiba ita"ikishwakatika /unge la atiba ambalo tunategemea litakutana katika wiki ya tatu yamwezi huu. /unge litaijadili =asimu na kuamua watakavyoona ina"aa.Mwishoni mwa mjadala /unge Maalum litakuwa limetupatia =asimu yaMwisho ya atiba ambayo ita"ikishwa kwa wananchi kwa uamuzi kupitia uraya Maoni.

    Ndugu Wanan)hi"inachosubiriwa kwa hamu hivi sasa ni uteuzi wa -ajumbe '() wa

    /unge Maalum la atiba na kutangazwa kwa siku ya /unge hilo kuanza. aziya uteuzi wa -ajumbe ime"ikia ukiongoni naamini ndani ya siku mbili zijazoorodha hiyo itatangazwa. #azima nikiri kuwa ilikuwa kazi ngumu sana.-aombaji ni wengi mno ukilinganisha na na"asi zilizopo. $umejitahidi kwakadiri ya uwezo wetu kupata uwakilishi mpana kwa mujibu wa sheria. ivyotunajua watakuwepo watu wengi waliotumaini kupata wao au watu waliotakawao wateuliwe lakini hawaku"anikiwa.

    uhusu siku ya kuanza nina imani kwa wiki ya tatu ya mwezi &ebruari,'()* /unge hilo linaweza kuanza. Nayasema hayo baada ya kutembeleaukumbi wa /unge Aodoma na kuelezwa maendeleo ya maandalizi ya ukumbi,majengo mengi muhimu na vi"aa vya kuwezesha kikao cha /unge ku"anyika.

    Nimeelezwa kuwa tarehe )( &ebruari, '()* matengenezo ya ukumbi yatakuwayamekamilika na majaribio ya vipaza sauti yata"anyika siku hiyo kuthibitishaubora wake. wa maoni yangu muda usiozidi siku % D 7 baada ya siku hiyo

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    11/12

    11

    utatosha. Ndani ya siku mbili zijazo tunaweza pia kutangaza siku ya /ungekuanza.

    Ndugu (iongozi, WanaCCM na Wanan)hi Wenzangu" Ni matumaini yangu kuwa -ajumbe wata"anya kazi yao kwa umakini na

    uadili"u ili kuipatia nchi yetu atiba nzuri inayotekelezeka, itakayoimarishaMuungano badala ya kuudhoo"osha. atiba itakayodumisha amani na utulivunchini na kuongeza zaidi kasi ya kuleta maendeleo. Najua muundo waMuungano litakuwa ndilo suala litakaloleta mvutano katika /unge Maalum la

    atiba. utakuwa na mjadala mkali kuhusu upi muundo bora, Muungano wa!erikali mbili kama ilivyo sasa au Muungano wa !erikali tatu unaopendekezwakwenye =asimu ya atiba.

    Ni matumaini yangu kuwa kila upande utatumia hoja zenye nguvukushawishi na ku"anikiwa kuungwa mkono na upande wa pili. Nimesikitishwana kauli ya Mwenyekiti wa C ABM Mheshimiwa &reeman Mbowe kuwawatatumia hata ngumi kupata kukubaliwa kwa m"umo wa !erikali tatu. !ijui nikukosa ukomavu wa kisiasa au ni kitu gani. 9ambo la wengi utalilazimishajekwa ngumi. 9awabu ni kujenga hoja zenye mashiko na kwa umahiri mkubwa iliwenzako wakuelewe na kukubalia. utumia nguvu hakutasaidia na wala siyonjia bora ya kutunga atiba.

    Napenda kutumia na"asi hii kumkumbusha Mheshimiwa Mbowekutambua kuwa ugomvi /ungeni hautaleta jawabu bali kuvuruga mambo.!iamini kuwa mambo kuvurugika kuna maslahi yoyote kwake. 6gomvihaujengi bali unabomoa.

    Ndugu Wanan)hi" Niliwahi kuelezea rai yangu kwa vyama vya siasa kukutana kuzungumzia

    namna bora ya kushirikiana na mahusiano wakati na baada ya /unge kuanza nakumaliza kazi yake. Nilitoa rai ile kwa kuamini kuwa ushindani na mivutano

    baina ya vyama unaweza kukwamisha mambo. /ahati nzuri baada yamashauriano, vyama vya siasa nchini vimekubaliana kukutana wakati wowotewiki ijayo. wa kweli, hii ni hatua muhimu sana ya maendeleo. 8naanza kuletamatumaini ya mchakato huu kuanza na kuisha kwa salama na amani.

    Ndugu (iongozi na Wana)hama Wenzangu"Mwisho napenda kuchukua na"asi hii kuwapongeza sana wenyeji wetu

    wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa na wale wote walioshirikikuandaa sherehe hizi ambazo zime"ana sana. Nawashukuru pia wanachama nawashabiki, wakereketwa na wapenzi wa CCM pamoja na wananchi wa Mbeyakwa kujitokeza kwa wingi kuja kujumuika katika kilele cha sherehe hizi hapauwanjani, santeni sana kwa mapenzi yenu makubwa kwa Chama chaMapinduzi.

  • 8/13/2019 204152705 Hotuba Ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Mweny

    12/12

    12

    Naomba viongozi wenzangu maadhimisho haya yawe kichocheo chakuwatumikia wananchi kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. -anatupenda,wanatuamini na wanatuthamini. $wendeni tukawatumikie, tusiwaangushe.

    i d u m u C h a m a c h a M a p i n d u z i !

    santeni sana kwa kunisikiliza.