afya ya uzazi mama na mwana ya uzazi.pdf4. vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino...

14

Upload: others

Post on 05-Nov-2020

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe
Page 2: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ②

AFYA YA UZAZIAFYA YA UZAZI.......................................................................................................②

UTANGULIZI......................................................................................................③SIKU YA KUPATA UJAUZITO........................................................................③

SIKU YA KUPATA UJAUZITO KWAMWENYE SIKU SIDOGO........④MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)................................................④SIFA ZA UTEUTE WA UKENI (CERVICAL MUCUS)..................................⑤DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)...........................................................⑤FANGASI SEHEMU ZA SIRI............................................................................⑦DALILI ZA KUTOKA KWAMIMBA...............................................................⑧SABABU ZA KUTOKA KWAMIMBA............................................................⑨HAYA NI HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA).............................................⑨HAYA HAYASABABISHI MIMBA KUTOKA................................................⑩MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA................................................⑩SABABU ZA KUKOSA HAMU YA TENDO LANDOA................................. 11TATIZO LA NGUZU ZA KIUME NA SABABU ZAKE.................................. 11KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA...................................12VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA.................12KUVIMBA VYA MIGUU KWAWAJAWAZITO............................................ 13

Page 3: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ③

UTANGULIZIAfya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana. Maradhi na mtindo wamaisha wa mtu huweza kuchukuwa nafasi kubwa katika kuzungumzia afya ya uzazi.Wazazi wengi wamekuwa wakilalamika kkuhusu swala na kushika mimba, maradhiya kizazi pamoja na wanaume kulalamika kutokuwa na nguvu za kutosheleza haja zao.Afya ya uzazi imekuwa ikichukuwa kundi kubwa la watu pindi inapozungumziwa.Kizazi kilicho salama kinategemea ubora wa afya hii pamoja na malezi yaliyo borakutoka kwa wazazi.

Katika makala hizi tutakwenda kuona mengi katika hayo yanayohusiana na afyaya uzazi kwa wanaume, wanawake pamoja na watoto ambao ndio kwa kiasi kikubwaafya zao. Makala hii imeandikwa kwa kuangalia tafiti za kiafya zilizofanya katikamaeneo mbalimbali duniani.

Tunaheshibu na kuthamini afya ya mtu. Katu hatuthubuthu kuandika kitua bila yamarejeo, hivyo basi ukigundua chochote ambacho hakiposawa kwenye makala hiibasi wasiliana nami kwa haraka zaidi

SIKU YA KUPATA UJAUZITO

Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm)inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuunganakwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote.Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaidakitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yaikukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian.Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaakama matatu, kisha huanza kusafirishwa nakupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo hukulitabakia mpaka mtoto kuzaliwa.

Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakatimwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hililinaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa haimpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ilimimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.

Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizimbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi yambegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwakuungana na yai.

Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke.Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazomwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16.katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii.

Page 4: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ④

Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima piakufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.

Pia kuna dalili kadha za kuijua siku hii kama kuzidi kwa joto la mwanamke siku mojakabla na siku ile ya kutolewa kwa yai. Pia kuongezeka kwa utelezi kwenye shingo yauzazi. Pia mwanamke anapenda sana kukutana kimwili kukaribia siku hii. Vipo vifaapia vya kuitambua siku hii. Siku hizi huhesabiwa kutoka kupata hedhi na kuendelea.Pia siku hisi kutofautiana kwa wanawake.

SIKU YA KUPATA UJAUZITO KWAMWENYE SIKU SIDOGO.

Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapoambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo. Sasa ni ipi siku ya kutolewakwa yai kwa wanawake hawa?. makala ya hapo juu katu haikugusa kipengele hiki.

Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla yakupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12nyuma, kisha ongeza 2 mnyuma ndani ya siku mbili zizi ndizo yai hutolewa. siku hizindizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--

1. Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla yakuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa mbili nyuma (9-2=7) basi mwanamke huyuanaweza kutoa yai kati ya siku ya 9 na 7 katika siku zake.2. Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kablaya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku mbili tena nyuma (20-2=18) kwa hiyomwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 18 mpaka 20

MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)

Kuna mabadiliko yanayotokea kwenye mwili wa mwanamke katika mzunguruko wasiku zake. Cervical mucus ni majimaji yenye sifa tofauti tofauti yanayopatikanakwenye njia ya uzazi yaani uke. Majimaji haya yanabadilika kulingana na siku amamaradhi. Miongoni mwa sifa hizi ni kama kinata, kuteleza, kufutika, ukavu na rangiyake.

Majimaji haya yanasaidia katika kutujulisha siku ambazo ni mujarabu kwa waleambao wanatafuta ujauzito. Pia majimaji haya ni taarifa kuwa yai lipo karibu ktolewahivyo ni vyema kujiandaa. Majimaji haya pia yanaweza kutujulisha kama mimbaimeingia ama laa. Tofauti na kazi hizi majimaji haya yana kazi zifuatazo:-1. Kuzuia bakteria na wadudu wengine wasiingie ndani kwenye tumbo la uzazi2. Kusafirisha mbegu za kiume (sperm) kuelekea ndani3. Kulainisha njia ya uke na kuwa katika hali iliyo bora zaidi.

Majimaji haya huweza kutofautiana muonekano kutokana na mabadiliko ya siku. Sikuhizi huanza kuhesabiwa punde tu baada ya kumalizika kwa hedhi. Ili kuchunguzamajimaji haya inahitaji muda na ni vyema kutokukutana kimwili kama unataka

Page 5: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ⑤

kuchunguza mabadiliko haya katika mwezi wote hii husaidia kwani kukutana kimwilikunaweza kuathiri muonekano wa majimaji haya.

Kama unataka kuchunguza kwa baadhi ya siku tu kama kutaka kujua kama yailinakaribia basi unaweza kukaa mkao wowote ambao utafanya uke uwe wazi, kishatumia kitambaa laini cheupe na kiingize ndani na fanya kama unapangisa kitu kwandani ili kuweza kuyapata majimaji haya kwa wingi. Ia unaweza kutumia kidole,baada ya hapo chunguza vyema rangi na muinekano wa majimaji haya kama kuteleza,kunata, kuvutika na uzito.

SIFA ZA UTEUTEWA UKENI (CERVICAL MUCUS)

Baada ya hedhi uke huwa mkavu hivyo majimaji haya yanakuwa ni macgache na siyenye mtelezo wowote. Hayana rangi yeyote na wala huwezi kuyapata kwa wingi. Hiihuashiria kuwa muda huu mwanamke hawezi kupata ujauzito.

Siku chache baadaye majimaji yataanza kuonekana yakiwa na muonekano wa kuwezakunatanata, majimaji haya sio mepesi kabisa. Huu ni mwanzo wa kuandaliwamazingira ya kupevushwa kwa yai.

Baada ya siku chache tu yai linakaribia kutolewa, muda huu majimaji hayayanakuwa mepesi, laini, mengi na yenye rangi nyeupe. Haya maji ni kiashiria kuwasasa yai lipo njiani kutolewa. Huu ni muda muafaka zaidi kwa wanaotafuta mtoto.

Siku moja ama mbili kabla ya yao kutolewa majimaji haya yanafanana sana namajimaji ya weupe wa yai, yaani kama yale majmaji meupe yanayooekana pindilinapopasuliwa yai. Majimaji haya yanaweza kuvutika kwenye vidole na yanatelezasana. Hii ni ishara kuwa yai limekaribia kutolewa eidha kwa siku moja ama mbili.

Punde baada ya yai kutolewa majimaji haya yanaanza kuwa makavu na kupotezamtelezo. Ama uke unakauka na kuwa mkavu na kurudi katika hali ya kawaida. Nakama mimba ilitungwa majimaji haya yanakuwa na rangi ya maziwa. Hivyo ni vyemakuchunguza vizuri ili kujuwa kama mimba ilitungwa au laa.

Pia ijulikane kuwa kuna wanawake wengine hawana majimaji haya na pia kunawengine ambao majimaji haya ni mengi sana zaidi ya kawaida. Hivyo katikakuchunguza hali hizi wanawake wa aina hii ni ngumu sana kwao.

DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)

Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupoteabila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua. Wapo wengine wanakujakujitambuaujauzito ukiwa na miezi kadhaa. Sasa ni zipi hasa dalili za ujauzito?. huenda swali hilikwa wanawake walio wengi lisiwe na manufaa kwao kwani tajari ni wajuzi wa swalahili. Halikadhalika wanaume wengi wanaujuzi pia. Kwani wengi wanaelewa kuwadalili ya ujauzito ni kukosekana kwa siku za mwanamke yaani hedhi kwa vipindizaidi ya kipoja. Lakini itambulike kuwa hii sio dalili pekee, kwani siku zinaweza

Page 6: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ⑥

kukosekana na isiwe mimba. Katika makala hii tutakwenda kuonesha kwa utani dalilikadhaa za ujauzito.

Kabla ya kiziona dalili hizo ningependa kutumia muda kidogo kueleza tatizo lakukosa kwa hedhi. Hedhi ni muhimu kwa kila mwanmke ambaye amefikia umri wakupata ujauzito. Afya ya mwanmke huyu huwa salama kama hedhi yake ipo salama.Kwa kawaida hedhi huweza kukatika yaani kukata kutoka kabisa pindi umri wamwanamke unapokuwa mkubwa yaani kuanzia miaka ya 45 na kuendelea. Katikakipindi hiki mwanamke huyu kupata tatizo la kutokupata siku zake ni la kawaida sana,ama siku zake kutokuwa na mpangilio maalumu.

Kwa wanawake walio wadogo kukata kwa hedhi kuna sababi nyingi sana. Watuwengi wamezoea kuwa lamda kupata ujauzito ndio sababu ya kutokupata siku zake.Hii sio swa kabisa. Kukata kwa siku za mwanamke kunaweza kusababishwa namaradhi kama kisukari na baadhi ya maradhi yanayoipata ovari ya mwanamke. Ovarindio sehemu pekee ya mwanamke ambayo mayai huzaliwa. Hivyo sehemu hii ndioambayo inatoa homoni ambazo huchochea upatikanaji wa hedhi ama huzuia hedhiisipatikane kutokana na kupata ujauzito. Pia matumizi ya njia za uzazi wa mpangohuweza kusababisha tatizo hili la kutokuona siku zake mwanamke. Matumizi yavyakula, hali ya hewa na madawa ni katika visababishi vikuu vya kutokupata hedhikwa muda sahihi.

Baada ya kugusia kidogo kipengele hiko sasa tukaone baadhi ya dalili za ujauzito.Kwa hali ya kawaida dalili hizi huweza kuwa tofauti kwa mwanamke mmoja hadimwingine. Ijapokuwa hali ni kama hii pia zipo dalili ambazo huwapata karibiawanawake wote:-

Kuonekana kwa damu iliyo chache. Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa asilimia 25%(yaani robo) ya wanawake wote wanaopata ujauzito hutokwa na damu kidogo, narangi ya damu hii haikuiva kama ile ya hedhi. Damu hii hutokea siku 6 mpaka 12baada ya kutungwa kwa mimba. Ila kwa wanawake walio wengi huiona damu hiikwenye wiki 12 za mwanzo za ujauzito.

Kujaa au kuuma kwa chuchu; mwanzoni mwa wiki ya 1 mpaka ya 2 ya ujauzitomwanamke anaweza kuona kuwa matiti yake yanajaa ama kuwa mazito tofauti nakawaida. Wanawake wengine chuchu za matiti yao zinakuwa ngumu na huwa zinajaa.Wanawake wengine wanaona chuchu ama maziwa yao huwa kama na maumivuwakiyaminya.

Uchovu isio wa kawaida; karibia wanawake wote wanaopata ujauzito huhisi uchovuusio wa kawaida. Mara nyingi dalili hii hutokea mwanzoni mwa wiki ya kwanza toka

Page 7: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ⑦

kupata kwa ujauzito. Na hii ni kutokana na kuwa mwili unazalisha homoni za kuwezakuufanya mwili uweze kulea ujauzito, upatikanaji nwa maziwa kwa ajili ya mtoto ajae.Pia kwa kuwa mwili wa mama unaongeza kuwango cha usukumaji wa damu, hivyouchovu kutokea ni hali ya kawaida.

Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya ujaozito, mwanamke anaweza kupatwa namaumivu ya ghafla ya kichwa. Na hii ni kutokana kuwa mwili umeongeza kazi yauzalishaji wa homoni, hivyo ongezeko hili linaweza kusababisha maumivu ya kishwa.Hali si kwa siku nyingi hali hii itapotea.

Kutapika; kwa kawaida hii hali huwapata wanawake wenye ujauzito kuanzia wiki yapili mpaka wiki ya nane. Kitaalamu hali hii hutambulika kama “morning sickness”. nahuenda hali hii ikaendelea katika kipindi chote cha ujauzito.

Kukojoa mara kwa mara; hali hii hutokea kwa sababu mwili huzalisha homoniiitwayo human chorionic gonadotropin ambayo hii huongeza damu kupita maeneo yachini yaani kuzunguka sehemu za siri, hivyo hali hii hupelekea mwanamke kwendakukojoa mara kwa mara.

Kutokupenda baadhi ya vitu ama vyakula. Hii hutokea kwa ghafla mwanamkeanachukia baadhi ya vitu ama hususani vyakula bila ya sababu yotyote.

FANGASI SEHEMU ZA SIRI

Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi nihatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakilikama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathirimwili wa binadamu.

Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina zafangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Fangasi wanaweza kuathirimakwapa, vidole, sehemu za siri kwenye tumbo na maeneo mengine.

Fangasi wa sehemu za siri husababishwa na fangasi waitwao candida. Hawawanaweza kuathiri sehemu za siri kuzungukia uume ama uke. Kunatafiti zinaoneshakuwa fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi. Japo tafiti zaidizinahitajika ili kuthibitisha hili.

FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI DALILI ZAO KWAWANAUME1. Kuvimba kwa kichwa cha uume2. Kuwasha kwa sehemu za siri, hususan kichwa cha uume3. Uume kuwa mwekundu kwa kuchubuka ama kuvumba ama kwa mashambulizi yafangasi hawa.4. Kuota kwa mapele na maruturutu kwenye uume5. Kuwasha uume ama kuungua moto kwa uume.6. Kutokwa na majimaji meupe kwenye uume, majimaji haya huwa na harufu mbaya.7. Maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo la ndoa.

Page 8: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ⑧

DALILI ZA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI KWAWANAWAKE1. Maumivu na miwasho kwenye mashavu ya uke na sehemu ya juu ya uke2. Maumivu wakati wa kukojoa ama kufanya tendo la ndoa3. Uuke kuwaka moto kwa ndani4. Kuvimba kwa mashavu ya uke na kuwa mekundu5. Kuot mapele na maruturutu kwenye uke6. Kutokwa na majimaji kwenye uke7. Kutokwa na majimaji mazito meupe na yenye harufu mbaya kwenye uke.

WATUWALIO HATARINI KUPATA FANGASI HAWA1. Wachafu2. Kuwa na mikunjomikunjo kwenye ngozi kama kitambi3. Wenye kisukari4. Wenye HIV5. Wenye saratani6. Wenye kutumia baadhi ya madawa ya kuzuia mimba7. Wajawazito

NJIA ZA KUPAMBANA NA FANGASI HAWA1. Kuwacha kutumia madawa ya kusafishia ama kuunga uke2. Kutokuvaa nguo mbichi3. Kutokuvaa nguo za kubana hususani za mpira4. Kuwa msafi muda wowote5. Kuosha kichwa cha uume na ngozi ya govi mara kwa mara6. Kuosha uke mara kwa mara7. Kutumia pedi zilizo kavua na safi na kubadilisha mara kwa mara

DALILI ZA KUTOKA KWAMIMBA

Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopataujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka.Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupoteakwa ujauzito kabla ya wiki ya 20. karibia mimba nyingi hutoka ndani ya miezi mitatuya mwanzo. Mimba iliyotoka inakuwa na dalili kadhaa. Pia wakati mwingine dalilihizi huashiria kuwa ujauzito upo hatarini.

Dalili hizi ni kama;1. Kutokwa na damu nyingi ukeni. Mjamzito anaweza kuona damu ikitoka ikiwachache yaani matone kadhaa ama madoa hii ni kawaida. Lakini ikiwa nyingi huashiriahatari kwa ujauzito.2. Kupungua uzito kwa ghafla. Bila ya kujuwa sababu yeyote mjamzito anapunguauzito wake kwa ghafla sana.3. Kutokwa na uteute wa rangi ya pink iliyo pauka kwenye uke4. Kuondoka kwa dalili za ujauzito kwa ghafla5. Kutokwa na tishu yaani kama vipande vya nyama vinatoka ukeni6. Maumivu makali ya mgongo ama tumbo

Page 9: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ⑨

SABABU ZA KUTOKA KWAMIMBA

Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopataujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka.Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupoteakwa ujauzito kabla ya wiki ya 20.

Sababu za kutoka kwa mimba:1. Sababu za kurithi (genetics): hutokea mwanamke akarithi hizi sabau kutokakwenye familia yake. Sababu hizi huenda zikapelekea matatizo ambayo baadayehuchangia mimba kutoka. Matatizo haya ni kama Mtoto kutokuendelea kukuwa tumboni Kiini tete (embriyo) kutokutengenezwa Placenta kuwa kubwa zaidi tofauti na kawaida.

2. Afya ya mama; hutokea mwanamke mjamzito afya yake ikawa ni sababu yaujauzito wake kutoka. Mwanamke akiwa na maradhi yafuatayo ujauzito wakeunaweza kuwa hatarini: Kisukari Maradhi ya moyo Presha ya kupanda (hypertension) Maradhi ya figo

3. Maambukizi; mwanamke mjamzito anweza kuweka ujauzito wake hatarini kamaatakuwa na maambukizi ama mashambulizi ya maradhi kama: Chlamydia Gonoria Syphilis Malaria Ukimwi

4. Udhaifu wa cervix; cervics ni mlango wa nyumba ya mimba.5. PCOS (Polycystic Ovary Syndrome). hii hupelekea ovary kuwa kubwa tofauti nakawaida. Ovary ndio sehemu ambayo mayai ya mwanamke hutengenezwa.

HAYA NI HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA)

Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka,kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini. Mambohaya yenyewe hayawezi kusababisha ujauzito kutoka ila yanaweza kuongeza hatari yaujauzito kutoka pindi yakiambatana na mambo matani niliyotangulia kuyataja hapojuu. Mambo haya ni kama:1. Kuwa na umri mkubwa kuanzia miaka 35 mpaka 402. Kuzidi kwa uzito mwilini3. Uvutaji wa sigara4. Unywaji wa pombe5. Ulaji wa caffeine nyingi kupita kiasi. Caffein hupatikana kwenye chai.

Page 10: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA ⑩

6. Sumu za kwenye vyakula, kama kwenye nyama.7. Matumizi ya baadhi ya madawa kama Misoprostol Retinoids Methotrexate NSAIDs kama ibuprofen8. Maambukizi na mashabulizi ya HIV Cytomegalovirus Bacterial vaginosis Gonorrhea Chlamydia Malaria Syphilis9. Kisukari

HAYA HAYASABABISHI MIMBA KUTOKA

1. Kufanya mazoezi2. Kufanya kazi3. Kula vyakula vinavyowasha kama vyenye pilipili4. Kufanya tendo la ndoa5. Kupata msituko6. Kuwa na mawazo

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia. Maumivu hayahutokea kwa namna mbalimbali. Mara nyingi maumivu haya huwapata wanawake.Mara chache wanaume wanapokuwa na maradhi flani kama fangasi kwenye uumeama maradhi mengine ya ngono ndipo hupata maumivu haya.

Maumivu haya hutokea pundi:1. Pindi uume unapoingia ukeni kwa mara ya kwanza2. Kila wakati uume unapoingia ukeni3. Maumivu wakati wa kupushi na kutoka kwa uume4. Kuhisi kuungua ukeni5. Maumivu baada ya kufanya tendo la ndoa

Sababu za maumivu haya Kutokuwepo kwa uteute wa kutosha wa kulainisha uke Majeraha na makovu ukeni kama waliotahiriwa Kuvimba kwa uke ama kuwa na mashambulizi ya bakteria Matatizo ya saikolojia Kukaza kwa misuli ya uke Maumbile ya uuke kama kuwepo kwa utando unaozuia njia ya uke kuwa wazi

Page 11: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA 11

Kufanyiwa upasuaji kama hysterectomy ama matibabu ya saratani Kuwa na msongo wa mawazo

SABABU ZA KUKOSA HAMU YA TENDO LANDOA

Hii ni hali inayompata mtu kukosa hamu kabisa ya kushiriki kitendo chochotekinachohusiana na kufanya tendo landoa au bunyeto. Hali hii kitaalamu hufahamikakama hypoactive sexual desire disorder (HSDD). Pia kuna watu wengine wanakuwana hisia chache kuhusu kitendo hiki. Hali hii huwapata wanaume na wanawake.Sababu za kukosa kabisa hamu ya tendo la ndoa ama hamu kuwa ndogo, sababu zaowote hufanana.

Sababu za kutokea kwa hali mbili hizi:1. Mumivu wakati wa tendo la ndoa2. Matumizi ya baadhi ya madawa ya arthritis, saratani, kisukari, presha ya kupanda,maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa fahamu3. Namna ya mtu anavyoishi kwa mfao unywaji wa pombe kupitiliza4. Kama mtu alifanyiwa upasuaji maeneo ya nyeti kama matiti, kwenye uke5. Uchovu6. Matatizo katika homoni7. Afya ya akili8. Kuwa na msongo wa mawazo9. Kutokujiamini10. Mahusiano yasiyo mazuri na mwenza

TATIZO LA NGUZU ZA KIUME NA SABABU ZAKE

Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa. Hii huwendakuwa uume unashindwa kusimama (kutisa) kwa kwa muda mrefu, ama unashindwakabisa kusimama. Kitaalamu hali hii hufahamika kama erectile dysfunction. Hali hiihaihusishi wale wenye tatizo la kumaliza hamu mapema (premature ejaculation) yaaniwanaomaliza haja yao hata kabla ya mwenza kuridhika.

Sababu za tatizo hili1. Kuwa na maradhi ya moyo2. Kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis)3. Kuwa na mafuta mengi mwilini (high cholesterol)4. Kuwa na presha ya kupanda (high blood pressure)5. Kisukari6. Matumizi ya baadhi ya madawa7. Uvutaji wa sigara8. Maradhi kwenye uume kama peyronie9. Unywaji wa pombe10. Utumiaji wa madawa ya kulevya11. Matibabu ya saratani ya korodani12. Upasuaji katika maeneo nyeti au ugwe mgongo13. Kuwa na mdongo wa mawazo ama woga

Page 12: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA 12

14. Mahusiano yasiyo mazuri15. Kuwa na uzito kupitiliza

KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA

Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoamapema kabla ya mwenza kuridhika. Hii hutokea pale mwanaume anapomwagambegu mapema sekunde chache ama muda mchache baada ya kuingiza uume ukeni.Wengi wenye tatizo hili humwaga ndani ya dakika moja na tatizo huwa baya zaidikwa wengine ambao humwaga ndani ya sekunde 30 baada ya kuingi za uume. Hali hiikitaalamu hujulikana kama premature ejaculation.

Hali hii huweza kuambatana na mambo mengi hususani matatizo ya kisaikolojia,maradhi ama maumbile. Wakati mwingine hali hii humpata mwanaume yeyote hatakama sio muathirika wa tatizo hili. Ila hii huwa ni tatizo kama hali hii itakuwainajirudia rudia muda mwingi.

Sababu za tatizo hili:1. matatizo kwenye mfumo wa homoni2. Maradhi na kuwepo uvimbe kwenye korodani3. Kurithi tatizo hili kwenye familia4. Kuwa na msongo wa mawazo5. Kuwa na tatizo la uume kunywea mapema6. Uwoga na msongo wa mawazo7. Kutokupendezewa na umbo la mwenza8. Mahusiano yaliyo mabovu9. Kuogopa kumaliza tendo mapema

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA

NDOA

Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoakwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojiaya mtu. Ni vyema kujiweka tayari kisaikolojia kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwaupande wa vyakula ni vyema kuchaguwa vyakula vilivyo salama kwa afya. Vyakulavyenye mafuta kupitiliza vinaweza kuleta athari mbaya kwa afya ya nguvu za kiume.Katika makala hii nitakuletea vyakula vitano ambavyo husaidia katika kuongezahamu ya kushiriki tendo la ndoa:

Vyakula hivyo ni:1. Vyakula vyenye arginine . Vyakula hivi vina ni vyakula vyenye chembechembeitambulikayo kama arginine. Ndani ya miili yetu arginine huweza kubadilishwa kuwaoxide ya nitric (nitric oxide). Arginine ni chembechembe za asidi ya amono (amino

Page 13: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA 13

acid). vyakula vyenvye arginine ni kama maharage ya soya, mbegu za maboga,karanga, korosho, samaki, nyama, kuku na samaki.

Arginine imafaida nyingi sana mwilini. Chembechembe hii huweza kutibu tatizo lakusinyaa kwa uume kabla ya kumwaga, ama kusinyaa mapema, ama kugoma kabisakusiama. Kama tatizo hili linahusiana na mishipa ya damua kama kuziba kwa mishibaya damu basi arginine ni msaada mkubwa. Pia husaidia kuimarisha afya kwa wenyekisukari na wenye maradhi ya moyo hususani yanayohusiana na mishipa ya damukama kujaa mafuta ama kuziba.

2. Vyakula vyenye phytochemical: vyakula hivi ni kama maepo (apples),mboga zaapricots, broccoli, Brussels sprouts, kabichi (cabbage), karoto (carrots), cauliflower,kitunguu thaumu (garlic), mimea jamii ya kunde (legumes), kitunguu maji (onion),pilipili kali (red peppers), maharage ya soya (soybeans), viazi vitamu (sweet potatoes),na nyanya (tomatoes).

3. Vyakula vya fati iliyo salama kwa afya ya moyo. Afya ya moyo huchukuwa nafasikubwa katika tendo la ndoa. Uzima wa moyo huweza kufanya damu kutembea vyamamaeneo yote ya mwili hususani maeneo yanayohusika katika tendo la ndoa.

Miongoni mwa vyakula hivi ni palachichi. Ndani ya palachichi kuna fat, vitamini B6asidi ya folik (folic acid) kwa hamoja hizi husaidia kuongeza nishati mwilini nakuimarisha afya katika kushiriki tendo la ndoa. Vyakula vingine ni kama aina flani yasamaki, mayai, mbegu za chia, chokleti, bidhaa za maziwa kama siagi n.k

4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii nichembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilishachembechembe hii ni kuwa arginine. Faida za arginine tumeshaziona hapo juu.Chemikali hizi pia husaidia katika kuufanya mwili uweze kuwa shwari (relax) kamavile viagra inavyofanya kazi.

Miongoni mwa vyakula hivi ni tikitimaji. Tunda hili lina citrulline kwa wingi sanatofauti na matunda mengi. Vyakula vingine ni kama maboga, matang n.k. citrullinepia husaidia katika kutanua misuli na kuboresha mishipa ya damu kufanya kazi vyemahivyo ni nzuri kwa wanaofanya mazoezi. Kwa upande wa afya ya tendo la ndoahusaidia katika kupeleka damu kwenye maeneo nyeti.

5. Vyakula vyenye Indole-3-carbinol: hii husaidia katika kuboresha homoni hasa kwawanaume. Huweza kupatikana kwenye mboga za majani kama kabichi, broccoli namboga nyinginezo. Tofauti na faida hizi pia huweza kusaidia katika kuzuia nakupunguza athari za saratani ya matiti, tumbo, na nyinginezo.

KUVIMBA VYA MIGUU KWAWAJAWAZITO

Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito. Kitaalamu hali hiihutambulika kama odema. Wakati mwingine si miguu tu ndio huvimba bali mikono,nyayo na uso huweza kuvimba. Ijapouwa huku kukuvimba kwa ghafla kwa uso namikono ni dalili ya maradhi mengine kama preeclampsia.

Page 14: AFYA YA UZAZI MAMA NA MWANA YA UZAZI.pdf4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe

AFYA YA UZAZI: MAMA NA MWANA 14

Hali hii ya kuvimba kwa miguu huweza kuwapata wanawake katika kipindi chote chaujauzito, iwe wajauzito ulio mchanga, ama kipindi cha katikati cha ujauzito amakipindi cha mwisho cha ujauzito. Katika hali ya kawaida kuvimba kwa miguu kwawajawazito sio jambo la kusumbua kiafya yaani kusema kuwa ni tatizo kubwa.Hapana hii ni kawaida kwa wajawazito.

Kuvimba huku kunaweza kuwa ni tatizo kama kutaweza kuambatana na baadhi yamatatizo mengine ya kiafya kama maumivu makali ya kicha, kizunguzungu, kutokwana damu, kushinwa kuona kwa usahihi ama kushinwa kupumua ama kupumua kwataabu, hali hizi kuweza kuashiria hatari. Ni vyema mjamzito awahi kituo cha afyakama ana hali hizi.

Sababu za kutokea kwa vimbe hizi ni mabadiliko ya mwilini yanayopatikana wakatiwa ujauzito. Kuongezeka kwa damu mwilini na kuongezeka kwa mapigo ya moyohuweza kuchangia zaidi hali hii. Halikadhalika ongezeko la homoni maalumuzinazotolewa wakati wa ujauzito. Haya yote kwa pamoja huchangia kutokea hali hiziza kuvimba.

Tofauti na sababu hizi pia zipo nyingine kama mabadiliko ya hali ya hewa. Hapatunazungumzia joto, ambalo pia ni sababu ya kuvimba. Sababu nyingine nikutokunywa maji ya kutosha, matatizo ya homoni yaani homone imbalance.Kukaachini kwa muda mrefu ukaaji wa kukalia miguu. Ama kusimama kwa mudamefu.

Kupunguza ama kuepuka hali hii ni vyema kufanya mazoezi ya mara kwa mara,kukaa kivulini, kulalia upande kwa kushoto unapolala. Hakikisha unakula mlo kamili,hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutoka kwa siku. Na hata ukizidisha ni faidakwako. Epuka kusimama kwa muda mrefu ama kukaa kwa kukalia mguu. Epukakukaa kwa muda mrefu kwa staili moja.

ENDELEA NA DARASA HILI

Unaweza kuendelea na somo hili la afya ya uzani, mamana mwana. Kuendelea na darasa hili pata kitabu chetukizima kwa bei poa tu. Wasiliana nasi kwa mawasilianohapo chini.

Unaweza pia kupata mwendelezo wa darasa hili ukiwakwenye tovuti yetu www.bongoclass.com. bongoclassimejipanga vyema kukupatia elimu bure.

Mawasiliano:Phone: 0675255927Email: [email protected]: www.bongoclass.com

1

1 www.bongoclass.com