kijarida kwa mgonjwa wa kisukari - counsenuthcounsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/... ·...

4
Ugonjwa wa kisukari ni nini? Ugonjwa wa kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu iliyomo mwilini inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu. Kuna aina ngapi za kisukari? Kuna aina kuu mbili za kisukari ambazo ni: Kisukari kinachotegemea insulini - au “type one diabetesKisukari kisichotegemea insulini au - “type two diabetes” i) Kisukari kinachotegemea insulini hutokea wakati mwili unaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulini ambacho huuwezesha mwili kutumia sukari. Kisukari cha aina hii huweza kudhibitiwa kwa kutumia sindano za insulini pamoja na kurekebisha ulaji. ii) Kisukari kisichotegemea insulini husababishwa na mwili kushindwa kutumia sukari. Mwili wa mtu mwenye aina hii ya kisukari huweza kutengeneza insulini ya kutosha lakini haitumiki kuuwezesha mwili kutumia sukari na hivyo sukari katika damu huwa katika kiwango cha juu. Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji, au kwa kurekebisha ulaji pekee. Dalili za ugonjwa wa kisukari Kukojoa mara kwa mara - Kusikia kiu sana - Kusikia njaa sana - Kuchoka sana bila kufanya shughuli yoyote - Kukosa nguvu - Kupungua uzito kwa kiwango kikubwa bila kukusudia - Kizunguzun - gu Unapokuwa na ugonjwa wa kisukari ufanye nini? Kwanza kabisa kubali hali hiyo na utambue kuwa ugonjwa wa kisukari ni wa kudumu, hata hivyo hudhibitiwa kwa dawa na chakula. Unaweza kuishi vizuri na kufanya kazi zako zote iwapo utafuata maelekezo na masharti yote yanayotakiwa kwa makini. Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kwa mgonjwa wa kisukari: Kudhibiti ulaji wako Ulaji unaofaa ni ule unaokuwezesha kutosheleza mahitaji ya mwili wako kilishe, na kukuwezesha kuwa na uzito unaostahili, pamoja na kuhakikisha sukari mwilini inakuwa katika kiwango kinachokubalika kwa afya njema. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia aina na kiasi cha chakula unachokula. Pia ni vyema ukawa makini na njia zinazotumika kuandaa chakula. KIJARIDA KWA MGONJWA WA KISUKARI Ukiona dalili hizi tafuta ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya mapema Insulini ni kemikali inayosaidia mwili kutumia sukari iliyoko kwenye damu © COUNSENUTH 2008 Information Series No. 12, November 2008

Upload: others

Post on 25-Jun-2020

124 views

Category:

Documents


12 download

TRANSCRIPT

Ugonjwa wa kisukari ni nini? Ugonjwa wa kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu iliyomo mwilini inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu.

Kuna aina ngapi za kisukari?Kuna aina kuu mbili za kisukari ambazo ni:

Kisukari kinachotegemea insulini- au “type one diabetes” Kisukari kisichotegemea insulini au - “type two diabetes”

i) Kisukari kinachotegemea insulini hutokea wakati mwili unaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulini

ambacho huuwezesha mwili kutumia sukari. Kisukari cha aina hii huweza kudhibitiwa

kwa kutumia sindano za insulini pamoja na kurekebisha ulaji.

ii) Kisukari kisichotegemea insulini husababishwa na mwili kushindwa

kutumia sukari. Mwili wa mtu mwenye aina hii ya kisukari

huweza kutengeneza insulini ya kutosha lakini haitumiki

kuuwezesha mwili kutumia sukari na hivyo sukari katika damu huwa katika kiwango cha juu.

Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji, au kwa kurekebisha ulaji pekee.

Dalili za ugonjwa wa kisukari Kukojoa mara kwa mara- Kusikia kiu sana- Kusikia njaa sana- Kuchoka sana bila kufanya shughuli yoyote- Kukosa nguvu- Kupungua uzito kwa kiwango kikubwa bila kukusudia- Kizunguzun- gu

Unapokuwa na ugonjwa wa kisukari ufanye nini?Kwanza kabisa kubali hali hiyo na utambue kuwa ugonjwa wa kisukari ni wa kudumu, hata hivyo hudhibitiwa kwa dawa na chakula. Unaweza kuishi vizuri na kufanya kazi zako zote iwapo utafuata maelekezo na masharti yote yanayotakiwa kwa makini. Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kwa mgonjwa wa kisukari:

Kudhibiti ulaji wako•Ulaji unaofaa ni ule unaokuwezesha kutosheleza mahitaji ya mwili wako kilishe, na kukuwezesha kuwa na uzito unaostahili, pamoja na kuhakikisha sukari mwilini inakuwa katika kiwango kinachokubalika kwa afya njema. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia aina na kiasi cha chakula unachokula. Pia ni vyema ukawa makini na njia zinazotumika kuandaa chakula.

KIJARIDA KWA MGONJWA WA KISUKARI

Ukiona dalili hizi tafuta ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya mapema

Insulini ni kemikali inayosaidia mwili kutumia sukari

iliyoko kwenye damu

© CoUnsenUtH 2008Information series no. 12, november 2008

Ugonjwa wa KisUKariInashauriwa:

Kula chakula cha mchanganyiko, hata hivyo - zingatia kiasi na aina ya chakula kwa kuangalia hasa kiasi cha sukari na mafuta yaliyomo Kula milo kamili mitatu kwa siku na asusa zenye - virutubishi vingi muhimu kati ya mlo mmoja na mwingine Kula kiasi kidogo cha vyakula vya nafaka, mizizi na - ndizi kwa mfano wali, ugali, viazi, mihogo, ndizi, magimbi n.k. tumia nafaka isiyokobolewa kwa mfano dona na ngano Kula mbogamboga kwa wingi kwa mfano mchicha, - matembele, majani ya maboga, karoti, biringanya, kisamvu, mlenda n.k Kula vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi kama - vile maharagwe, njegere, mbaazi, kunde, choroko n.k (tumia kama kitoweo) Kula matunda kwa kiasi kwa mfano ndizi au - chungwa moja au kipande kidogo cha embe kubwa au papai katika kila mloKunywa maji kwa wingi- epuka kutumia vinywaji na vyakula vyenye sukari - nyingi kama jamu, asali, visheti, futari ya sukari, soda, chokoleti, pipi, bazoka, barafu na juisi bandia. epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi au - chumvi nyingi

Kufuata mtindo bora wa maisha• Fany- a mazoezi ya mwili mara kwa mara angalau kwa nusu saa kila siku, kwani husaidia mzunguko wa damu na kukufanya uwe na afya nzuri

epuka unywaji wa pombe kwani unaweza kukuletea - athari mwilini epuka uvutaji wa sigara na bidhaa za tumbaku na - madawa ya kulevya, kwani huathiri afya yako epuka msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi au - kushiriki katika matukio salama yanayokufurahisha

Kufuata kanuni za afya na usafi• Piga mswaki kila baada ya kula au angalau mara - mbili kwa siku Kuwa msafi wa mwili na mavazi- tunza miguu yako kwa makini kuzuia kupata - majerahaKausha vizuri maji katikati ya vidole vya miguuni- epuka kujiumiza mwilini- Vaa viatu na soksi zisizobana kila wakati- Inashauriwa kuvaa viatu vya wazi-

Kutimiza masharti ya dawa na ulaji •

Kuhudhuria kliniki za kisukari kwa kufuata ratiba •uliyopangiwa

Kumuona daktari mapema mara unapopata tatizo •lolote la kiafya

Kupata taarifa sahihi na elimu kuhusu kisukari •kutoka kwa wataalamu wa afya

KUmbUKa• IKIwA UnA UzIto MKUbwA nI MUHIMU

KUUPUngUzA• UsIACHe MAtIbAbU bIlA UsHAUrI wA dAKtArI• UsIKAe bIlA KUlA KwA MUdA MreFU

madhara ya muda mfupi ya ugonjwa wa kisukariKuna hali za aina mbili ambazo kila mgonjwa wa kisukari, familia

au waalimu wanapaswa kujua na kuchukua tahadhari kubwa

zinapojitokeza. Hali hizi ni pale kiwango cha sukari katika damu

kinaposhuka au kupanda kwa kiwango kikubwa. Hatua za

haraka inabidi zichukuliwe kumsaidia mgonjwa, kwani anaweza

kupoteza fahamu na hata maisha.

i) Kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu (Hypoglycaemia)

Hali hii hutokea wakati kiwango cha sukari kinapokuwa chini

kuliko kawaida. Hii inaweza kutokana na kutumia dawa kuzidi

kipimo, kunywa pombe, kufanya mazoezi bila kula, kufanya

mazoezi yanayotumia nguvu kwa muda mrefu, au kukaa bila

kula kwa muda mrefu.

Utajuaje kiwango cha sukari katika damu kimeshuka?Utafahamu kwa kuona dalili zifuatazo:

Moyo kwenda mbio- Mwili kutetemeka- Kusikia njaa- Kizunguzungu- Kuona mbilimbili (double vision)- Kuchanganyikiwa- Kutokwa jasho kwa wingi- Kuchoka sana-

Hali hii ikizidi mgonjwa huweza kupoteza fahamu. Mgonjwa

akipatwa na hali hii apewe kitu chenye sukari kama vile sukari,

glukosi, soda au juisi.

Kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu ii) (hyperglycaemia)

Hali hii hutokea wakati kiwango cha sukari kinapokuwa juu kuliko

kawaida. Hii inaweza kutokea wakati mgonjwa anapoacha kutumia

dawa, anapoacha kufuata masharti ya ulaji unaotakiwa, anapopata

maambukizo au maradhi mfano, malaria, flu, nimonia n.k

Utajuaje kiwango cha sukari katika damu kimepanda?Utafahamu kwa kuona dalili zifuatazo:

Kupumua haraka haraka- Kuongezeka mapigo ya moyo-

Hali hii ikizidi mgonjwa hupoteza fahamu na hatimaye maisha

kama hatapata matibabu mapema.

KUmbUKaMgonjwA AlIYePotezA FAHAMU AsIPewe CHoCHote bAlI AwAHIsHwe KAtIKA KItUo

CHA KUtoA HUdUMA zA AFYA MAPeMA IwezeKAnAVYo

KUmbUKa• Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe kinywaji au

chakula chochote kwani huweza kumpalia • Anaweza kuwekewa sukari au glukosi kwenye fizi • Awahishwe katika kituo cha kutoa huduma za afya

Ugonjwa wa KisUKari

Ugonjwa wa KisUKarimadhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari

Kupungua kwa uwezo wa kuona na hata upofu•Figo kutofanya kazi zake sawasawa• Vidonda vya miguuni kutopona na hata kusababisha kukatwa •kidole au mguuMaradhi ya moyo•Kufa ganzi na kupoteza hisia hasa mikononi na miguuni•Kiharusi•

• Kupungua kwa nguvu za kiume

angalIzoMtoto anayetumia insulini• Inabidi awe makini na ulaji wake, hususan akiwa shuleni• Aelimishwe kuhusu dalili za mwanzo za kushuka au kupanda

kwa kiwango cha sukari katika damu • Azingatie na aoanishe muda wa kupata sindano ya insulini na

muda wa kula

• Waalimu washirikiane na wazazi au walezi kuhakikisha mtoto anapata asusa zenye virutubishi muhimu anapokuwa shuleni

• Asaidiwe kuepuka vyakula visivyo na ubora kama vile vyenye sukari nyingi, chumvi nyingi au mafuta mengi

• Afikiriwe wakati wa michezo, mazoezi na kazi za kutumia nguvu ili kiwango cha sukari mwilini kisishuke kupita kiasi

• Aangaliwe ili aweze kuzingatia masharti ya kula na kutumia dawa

MAMBO MUHIMU YA KUKUMBUKA NA KUZINGATIA UKIWA NA KISUKARI

Wewe ni nguzo muhimu katika kumudu kisukari•Ikubali hali yako na tafuta ushauri wa kitaalam•Jikinge na madhara yaletwayo na kisukari• Fuata ushauri unaopewa na wataalam wakati wote • Endapo una swali au mashaka muulize daktari wako•

KUmbUKaIlI KUPUngUzA MAdHArA HAYo nI MUHIMU KUzIngAtIA UsHAUrI wA dAKtArI, UlAjI nA

Mwenendo borA wA MAIsHA

KUmbUKa• AFYA nI YAKo, UHAI nI wAKo nA CHAgUo nI lAKo• IsHI VYeMA IlI KUFUrAHIA KesHo

mgonjwa wa Kisukari: Hakikisha unatembea na kitambulisho kinachoonesha kuwa wewe ni mgonjwa wa kisukari. Kumbuka kutembea na sukari au glukosi kidogo wakati wote.

Kituo cha Ushauri Nasaha Lishe na Afya (COUNSENUTH)S.L.P 8218, Dar es SalaamSimu/Faksi: +255 22 2152705 Barua pepe: [email protected]

The Association of Private HealthFacilities in Tanzania (APHFTA)

S.L. P 13234, Dar es Salaam, TanzaniaSimu/Faksi: +255 22 2184508/2184667

Barua pepe: [email protected]

Kijarida hiki kimetolewa na: