al hikma vol 28

40

Upload: al-hikma-magazines

Post on 07-Apr-2016

330 views

Category:

Documents


4 download

DESCRIPTION

 

TRANSCRIPT

Page 1: Al hikma vol 28
Page 2: Al hikma vol 28

'' DAHE FAJR''Kwa Hakika kuna mengi ya kuzungumza kuhusiana

na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo kubwa zaidi ni kipindi mapinduzi hayo yalipopata ushindi bila kusahau uongozi wa busara wa Imam Khomeini (quddisa sirruh) kwa upande mmoja na jinsi utawala wa Mfalme Shah ulivyokuwa ukipata

himaya ya hali na mali. Alfajiri 10 au Dahe Fajr ni neno mashuhuri mno baina ya Wairani na wafuatiliaji wa harakati za Mapinduzi ya

Kiislamu ya Iran. Itakumbukwa kuwa tarehe Mosi Februari mwaka 1979, Imam Khomeini (quddisa sirruh), Mwasisi na Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alirejea

nchini Iran akitokea ubaidishoni nchini Ufaransa.

Siku 10 baadaye, Mapinduzi ya Kiislamu yalipata ushindi hapa na kipindi hicho

cha siku 10 za baina ya kurejea Imam Khomeini na kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni maarufu kwa jina la Dahe Fajr yaani Alfajiri 10. Kwa muktadha huo, sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu huanza tarehe Mosi Februari na kufikia

kileleni tarehe 22 mwezi wa Bahman kwa mwaka wa Kiirani

yaani tarehe 11 Februari kila mwaka. Mapinduzi ya

Kiislamu ya Iran ni harakati iliyotokana na mtazamo

wa kupigania uadilifu na inayofuatilia kuhuisha malengo ya Mtume Mtukufu (SAW).

Page 3: Al hikma vol 28

MKURUGENZI MKUUMorteza Sabouri

MHARIRI Maulidi Saidi Sengi

WAANDISHI NA WATARJUMIFatma Ali Othmani

Mohammed BandalyMSANIFU WA KURASA

Maulidi Saidi Sengi

KUMBUKUMBUUshindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran......................................3

Mapinduzi ya Kiislamu na kuchanua thaman................................6

Nabii wa Rehma, Mtume Muhammadi (SAWW).............................8

HOTUBA Umoja ndiyo suala muhimu zaidi..............................................11

SHEREHE / MAULIDUN NABIIBashiru na Nadhiru Mtume Muhammad......................................16

TA'ZIYAMaombolezo ya Sheikh Ansary..............................................18 – 19

JAMII / AFYAKomamanga huzuia kusambaa Kansa ya Matiti ........................20

JAMII / MALEZIMalezi ya watoto katika Uislamu....................................................23

JAMII / MWANAMKEMwanamke ni Muhimili wa Maendeleo katika jamii....................27

JIKONIMapishi..............................................................................................30

MALENGA WETUMashairi.............................................................................................31

KAZIUmuhimu wa kazi katika Uislamu..................................................32

MCHAPISHAJI

Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran

FEHERESI

MTAYARISHAJI

Kitengo cha Uhariri na Usanifu

ANUANI:Al-Hikma Jarida Maridhawa

Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran

S.L.P. 7898Dar es Salaam

Tanzania

'' DAHE FAJR''

Jarida la Maarifa ya Kiislamu ni kwa ajili ya nchi za Afrika Mashariki na kati, ni Jarida ambalo linakupa mwangaza wa kielimu, kijamii na kiutamaduni.Wewe ukiwa kama mmoja wa wadau wa Jarida hili Maridhawa tunachukua nafasi hii kukaribisha maoni au mapendekezo yako ili Jarida hili liendelee kuwa Bora katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na sehemu zingine za Dunia.

Muhammad Bandaly - Mwandishi, Al-hikma

Page 4: Al hikma vol 28

2

KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

Page 5: Al hikma vol 28

3

Moja ya matukio muhimu na makubwa katika karne ya 20 Miladia, lilikuwa

tukio la ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Ilikuwa tarehe 11 Februari 1979 wakati harakati za wananchi wanamapinduzi wa Iran walipopata ushindi dhidi ya utawala wa Mfalme Shah.

Kwa hakika kuna mengi ya kuzungumza kuhusiana na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo kubwa zaidi ni kipindi mapinduzi hayo yalipopata ushindi bila kusahau uongozi wa busara wa Imam Khomeini (quddisa sirruh) kwa upande mmoja na jinsi utawala wa Mfalme Shah ulivyokuwa ukipata himaya ya hali na mali.

Alfajiri 10 au Dahe Fajr ni neno mashuhuri mno baina ya Wairani na wafuatiliaji wa harakati za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Itakumbukwa kuwa tarehe Mosi Februari mwaka 1979, Imam Khomeini (quddisa sirruh), Mwasisi na Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alirejea nchini Iran akitokea ubaidishoni nchini Ufaransa. Siku 10 baadaye, Mapinduzi ya Kiislamu yalipata ushindi

hapa na kipindi hicho cha siku 10 za baina ya kurejea Imam Khomeini na kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni maarufu kwa jina la Dahe Fajr yaani Alfajiri 10. Kwa muktadha h u o , sherehe za Mapinduzi y a Kiislamu h u a n z a t a r e h e M o s i Februar i na kufikia k i l e l e n i tarehe 22 mwezi wa

Bahman kwa mwaka wa Kiirani yaani tarehe 11 Februari kila mwaka. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni harakati iliyotokana na mtazamo wa kupigania uadilifu na inayofuatilia kuhuisha malengo ya Mtume Mtukufu (SAW). Mapinduzi

ya Kiislamu ilikuwa harakati kubwa ya wananchi waliosimama kwa ajili ya kuhuisha thamani za kiutu kupitia mafundisho ya Mtukufu Mtume (SAW).

Harakati hiyo adhimu iliyodhihiri kupitia mapinduzi makubwa

iliwaathiri wanadamu wengine katika pembe zote za dunia. Ni

kawaida kwa Mapinduzi yoyote yale kuathiri

watu walio p e m b e n i

yake iwapo

Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, tukio kubwa la karne ya 20 Miladia

Na: Salum Bendera

Kila harakati huwa na siri ya mafanikio yake. Wengi wanajiuliza siri hasa ya ushindi na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni nini? Kwa nini Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameweza kudumu na kupata mafanikio makubwa licha ya kuweko mashinikizo ya kila uchao dhidi yake ya madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani?....

KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

Page 6: Al hikma vol 28

4

yatasimamishwa na kuendeshwa katika misingi iliyo sahihi. Kwa kudhihiri Mapinduzi ya Kiislamu wananchi wa Iran waliamua kuzingatia na kurejelea sira na sharia za dini tukufu ya Kiislamu.

Kwa ushindi wa mapinduzi hayo ya Kiislamu na kutekelezwa sheria za Kiislamu nchini Iran kwa mara nyingine tena ulimwengu ulihisi harufu nzuri na ya kuvutia ya manukato ya thamani za Kiislamu.Utukufu na utambulisho halisi wa umma wa Kiislamu ulidhihiri wazi kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Hii ni kwa sababu ujumbe wa Imam Khomeini, ni ujumbe uliouhusu umma mzima wa Kiislamu na uliosimama juu ya msingi wa mafundisho ya Mtukufu Mtume (SAW) aliyekuwa akiamini kwamba, utukufu na heshima ni msingi muhimu katika uwepo wa mwanadamu anayepigania haki.

Kwa ibara nyingine ni kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yalileta mwamko na uhai mpya katika umma

wa Kiislamu na hivyo kuhuisha utambulisho halisi wa Kiislamu katika maisha ya kijamii na kisiasa ya Waislamu wote duniani. Kupitia mafundisho yake ya kiutu na kidini, Mtume Muhammad SAW alifanikiwa kuwarudishia wanadamu, na hasa wanawake, heshima yao ya kiutu, kijamii na kisheri. Alizungumzia kwa kina utukufu na heshima ya mwanamke na kutambua rasmi haki yake ya kumiliki mali na kujiamulia masuala muhimu maishani. Mafundisho ya Mtume yalinyanyua nafasi ya mwanamke katika jamii na kuomuondoa katika hali ya

utumwa, udhalilifu na kutokuwa na utambulisho maalumu.

Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa ni marejeo kwenye utamaduni wa Mtume Mtume (SAW) na kuhuishwa heshima ya kiutu na kijamii ya mwanamke. Mwenendo unaozidi kukua wa mwanamke wa Kiirani kushirikishwa kwenye majukumu mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kielimu ni jambo linalotokana na mafundisho hayo ya Mtume Mtukufu (SAW).

Siri ya ushindi na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Kila harakati huwa na siri ya mafanikio yake. Wengi wanajiuliza siri hasa ya ushindi na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni nini? Kwa nini Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameweza kudumu na kupata mafanikio makubwa licha ya kuweko mashinikizo ya kila uchao dhidi yake ya madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani?

Kwa hakika siri kubwa ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni uongozi uliokuwa na busara wa Imam Khomeini (quddissa sirruh).Kusimama kidete na imara mbele ya njama za madola ya kibeberu ni siri nyingine kubwa ya mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

4

KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

Page 7: Al hikma vol 28

5

yalitokea katika kipindi cha kupamba moto vita baridi na kuongezeka ushindani baina ya kambi mbili za Magharibi na Mashariki. Kwa hakika Mpainduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuja na ujumbe na risala mpya ambayo ilikuwa tofauti kabisa na thamani pamoja na nara na sha’ari za ukomonisti na uliberali katika eneo la kiistratejia la Mashariki ya Kati.

Marekani na madola shirika na waitifaki wake ya Magharibi yalikuwa yakiunga mkono moja ya mfumo na tawala za kidikteta zaidi katika Mashariki ya Kati. Muhammad Reza Pahlavi, Mfalme wa Iran alikuwa ameiweka nchi yake katika nafasi

ya kutumikia maslahi ya Marekani na madola ya Magharibi; na nchini Iran kulikuwa na washauri takribani elfu 50 wa masuala ya kijeshi ambao walikuwa ni Wamarekani. Masuuliya muhimu ya Mfalme Shah yalikuwa ni kuwakandamiza wanamapinduzi na wapigania uhuru.

Jela zilikuwa zimejaa wafungwa wa kisiasa ambao walikuwa wametiwa mbaroni na kutupwa katika jela hizo za kuogofya kutokana na kujihusisha na harakati za kisiasa za kupigania uhuru. Madola ya Magharibi yakiwa na lengo la

kuendeleza njama na uadui wao dhidi ya taifa la Kimapinduzi la Iran, yalikuwa tayari kukanyaga na kufumbia macho madai yao yote ya demokrasia, haki za binaadamu na haki ya kupigania uhuru.

Kuyasadia makundi ya kigaidi na ya kupigania kujitenga, vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran na kuyafanyia njama mapinduzi ni sehemu moja tu ya faharasa ndefu ya hatua na mikakati ya Marekani na waitifaki wake iliyokuwa na lengo la kuikwamisha na kuiangusha serikali ya mpya ya Mapinduzi ya Kiislamu katika Iran. Marekani na waitifaki wake waliuunga mkono utawala wa dikteta Saddam Hussein katika

mashambulio na vita vyake vya kichokozi dhidi ya Iran mwaka 1980. Wananchi wa Iran walisimama kidete katika vita hivyo vya kujihami kutakatifu na kumfanya adui ashindwe kufikia malengo yake. Licha ya Marekani na waitifaki wake wa Kimagharibi kutumia mbinu na mikakati yote ya kisiasa, kiuchumi na kijeshi ili kutoa pigo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Waitifaki hao hawakughafilika pia na kutumia mbinu ya vita vya kisaikolojia na propaganda chafu dhidi ya taifa hili. Baada ya kupita zama na kupatikana maendeleo katika uga

wa teknolojia ya mawasiliano, vita laini (soft war) vikaanza kuzingatiwa. Vita laini inajumuisha kila hatua ya kisaikolojia na kipropaganda ya vyombo vya habari ambayo inalenga jamii au kundi maalumu katika jamii na hilo hufanyika bila ya kutumia vita vya silaha.

Vita laini huendeshwa kwa kutumia nyenzo na suhula mbalimbali kama kompyuta, intaneti, redio, kanali za televisheni, satalaiti, magazeti, michezo ya kompyuta na kadhalika. Katika vita hivi laini Marekani imekuwa ikilenga mambo makuu matatu. Mosi, kueneza uvumi kwamba, utawala wa Iran sio wa wananchi na kwamba eti

hauna ridhaa ya wananchi. Pili, viongozi wa Iran hawana uwezo wa kuongoza; na tatu ni kuwa kuna vita vya kuwania madaraka baina ya viongozi katika mfumo wa Kiislamu wa Iran. Hata hivyo njama zote hizo za maadui zimeshindwa kutokana na Iran kusimama kidete.

Leo hii Iran imepiga hatua kubwa katika nyuga mbalimbali za kielimu, kitiba, kisayanasi, kiteknolojia na kadhalika; na Iran imo katika faharasa ya nchi kumi duniani zilizopiga hatua katika mambo mengi tu ya kielimu. Wassalaam.

HISTORIA / GHADIR KHOM KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

Page 8: Al hikma vol 28

6

KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi wa Iran hawakuwa na nafasi yoyote katika kujiainishia mustakbali wao. Utawala wa Kipahlavi uliokuwa ukitawala nchini Iran, haukuzingatia kabisa nafasi ya wananchi si katika Katiba wala katika vitendo.

Ni matumaini yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasomaji na karibuni

kujiunga nami katika Makala hiii maalumu ambacho ni mfululizo wa vipindi maalumu tulivyokuandalieni kwa mnasaba wa maadhimisho ya Alfajiri Kumi za kusherekea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979 uliopatikana kwa ushujaa na ushupavu wa wananchi wa Iran kwa uongozi wa Imam Ruhullah al-Musawi al-Khomeini (MA).

Makala yetu ya leo itatupia jicho taathira ya mapinduzi hayo na jinsi thamani za kimaanawi zilivyochanua na kupata nguvu nchini Iran baada ya mapinduzi hayo ya Kiislamu.Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa uongozi wa Imam Khomeini (MA), yalifungua mlango na kuleta mwelekeo mpya kwa wananchi wa Iran na wa mataifa mengine ulimwenguni.

Kutokea mapinduzi hayo makubwa kulikuwa na taathira kubwa katika mtindo wa maisha ya wananchi wa Iran na hivyo yakawapeleka upande wa maanawi. Kutawala anga ya utamaduni na mtazamo wa kidini na kimapinduzi katika jamii ya Wairani, kulipelekea wananchi wa taifa hili la Kiislamu waelekee zaidi upande wa thamani za Kiislamu

kama vile taqwa, uchaji Mungu, kuwa watu wa dini, kutafuta elimu, kusaidiana wao kwa wao na kuishi maisha ya kawaida na yasiyo ya kujifakharisha. Kwa msingi huo, kubadilika thamani za Wairani, yalikuwa matunda makubwa kabisa ya Mapinduzi ya Kiislamu ambapo katika hili vijana walikuwa mstari wa mbele ikilinganishwa na watu wa matabaka mengine katika jamii.

Vijana wa Kiirani hawakusimama na kukabiliana tu na thamani zisizo na maana za kipindi cha utawala wa Kipahlavi, bali walibadilika mno na kuwa watu wema na walioshikamana na dini ambapo mambo kama umaanawi, kuwa tayari kufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kujitolea kwa mara nyingine yalipata maana katika jamii ya Iran.

Fasili na maana ya maneno hayo ilidhihirika dhahir shahir katika kipindi cha Kujihami Kutakatifu yaani wakati wa vita vya kulazimishwa vya miaka minane vilivyoanzishwa na dikteta wa wakati huo wa Iraq Saddam Hussein. Kwa hakika katika kipindi hicho wananchi wa Iran, wake kwa waume, vijana kwa wazee walijitolea kwa hali na mali na kuunda hamasa kubwa, kiasi kwamba, kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu, vijana wa Kiirani

wamegeuka na kuwa kigezo na ruwaza njema isiyo na mithili kwa wapigania uhuru wengine duniani. Katika zama za utawala wa kidhalimu wa Kipahlavi mipango na uandaaji sera kiujulma ulikuwa na mtindo wa Kimagharibi na usio wa kidini.

Kuanzia muongo wa 60 Miladia mtindo wa maisha wa Marekani ulianza kupigiwa upatu katika vyombo rasmi vya utawala wa Kifalme nchini Iran na kutangazwa kama ni kigezo bora cha maisha. Kwa hakika, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mbali na kubadilisha mfumo wa kisiasa ulibadilisha pia thamani za kiutamaduni na kijamii zilizokuwa zikitawala katika jamii ya Iran. Mageuzi katika nyuga za kiutamaduni na kijamii lilikuwa takwa la akthari ya wananchi wa Iran waliokuwa wakitaka kuhuishwa sheria za Mwenyezi Mungu katika nyanja hizo.

Kuleta moyo wa kujiamini kiutamaduni ni miongoni mwa matunda mengine ya Mapinduzi ya Kiislamu. Katika kivuli cha uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini, Mapinduzi ya Kiislamu yaliwapeleka wananchi wa Iran upande wa kujiamini kiutamaduni na kurejea katika thamani asili za Kiislamu na Kiirani. Kuhuisha moyo wa

KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

7

Page 9: Al hikma vol 28

7

kupigania mamlaka ya kujitawala na kutaka izza na heshima, ni matunda mengine ya Mapinduzi ya Kiislamu. Katika kipindi chake chote cha historia, Iran ilikuwa imeonja kidogo sana ladha ya mamlaka ya kujitawala kisiasa na kikawaida ilikuwa tegemezi kwa madola ya Kiistikbari hususan Uingereza na Marekani.

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi wa Iran walipata moyo wa muqawama na mapambano kwa ajili ya kujikomboa na kuondokana na utegemezi wa Magharibi. Kwa msingi huo basi, kukawa kumejitokleza tajiriba mpya.

Wananchi wa Iran wakiwa na lengo la kufikia uhuru na kuchagua utawala wa wananchi na wa Kiislamu, walionesha ushujaa wa hali ya juu. Wananchi wa Iran walijitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha kwamba, wanapata maisha ambayo yako katika njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu na kuhuisha sheria za Kiislamu.

Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi wa Iran hawakuwa na nafasi yoyote katika kujiainishia mustakbali wao. Utawala wa Kipahlavi uliokuwa ukitawala nchini Iran, haukuzingatia kabisa nafasi ya wananchi si katika Katiba wala katika vitendo.

Hata hivyo kwa baraka za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi wa Iran wakawa na nafasi kuu na ya asili katika kujiainishia mustakbali wao na katika kuunda mfumo wa utawala wanaotaka, kuweka sheria na hata kuongoza nchi. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni mali ya wananchi wa matabaka yote, wake kwa waume, wazee kwa vijana, watu wa vijiji na mijini na watu

wa matabaka yote ya wananchi. Wananchi wenye uwelewa na utambuzi wa Iran walishiriki kikamilifu katika mapinduzi na kwa mujibu wa taklifu na wajibu wao wa kisheria na kwa msingi huo wakawa wameingia kikamilifu katika uga wa jamii.

Himaya yao ya hali na mali katika kipindi cha vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu mkabala na jeshi la dikteta Saddam, ushiriki wao katika maandamano na chaguzi mbalimbali kimsingi kulikuwa ni kudhihirisha itikadi yao madhubuti ya kidini. Moja ya matatizo makubwa ya jamii zilizoko katika hali ya kustawi na kuendelea ni kutokuwa na uwelewa watu na kuwa na mghafala watu kuhusiana juu ya matukio ya nchi yao na yale yanayojiri ulimwenguni kwa ujumla.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambayo ni mlinganiaji wa umaanawi na uadilifu yaliandaa anga na mazingira mwafaka kwa ajili ya kuinua kiwango cha weledi na uwelewa wa jamii. Sanjari na hilo, Mapinduzi ya Kiislamu yaliinua kiwango cha mtazamo wa kisiasa na fursa ya kuingilia kwa utambuzi kamili mustakbali wa kisiasa na kijamii kwa ajili ya wananchi.

Moja ya matunda yenye thamani kubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu ni kuleta hali ya uwelewa na ufahamu wa kisiasa wa wananchi. Wananchi wanamapinduzi wa Iran baada ya kutambulika makundi potofu yaliyokuwa dhidi ya mapinduzi, walitangaza kujibari na kuwa nayo mbali na kwa muktadha huo kutoruhusu Mapinduzi ya Kiislamu yaondoke katika mkondo wake. Hii leo kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, wananchi wa nchi nyingine za Kiislamu nao

wana mwamko na wameamka na hivi sasa wanafanya harakati dhidi ya ubeberu, udikteta na siasa za kijuba na za kimabavu za madola ya Magharibi. Miongoni mwa athari za kiutamaduni za Mapinduzi ya Kiislamu kwa mtindo wa maisha ya wananchi, ni kubadilika namna ya kuishi wananchi ambapo wameelekea upande wa kuishi maisha ya kawaida, yaliyo mbali na ufakhari na wakati huo huo kupambana na maisha ya kifakhari na anasa.

Kabla ya Mapinduzi wananchi wa Iran walikuwa wameathirika na mtindo wa maisha wa Magharibi. Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, wananchi wengi walitoa vitu vyao vya mapambano na vya anasa na kuvitoa zawadi kwa taasisi za masuala ya kheri na hivyo kuamua kuchukua mkondo wa kuishi maisha ya kawaida kabisa na yaliyo mbali na anasa na mambo ya kujifakharisha.

Ni kwa kuzingatia uhakika huo ndio maana, halikuwa jambo la ajabu hata kidogo kuona sherehe za arusi zikifanyika katika misikiti na Husseiniya; na hilo lilihesabiwa kuwa jambo lenye thamani. Katika upande mwingine, vikao vya visomo vya Qur'ani na dua navyo viliongezeka mno na kuchukua mkondo mpana zaidi na wananchi wakawa wakishiriki ibada za Sala za Jamaa kwa vuguvugu na hamasa ya aina yake.

Aidha vijana wengi wakawa wanamiminika katika Vyuo Vikuu kwa ajili ya kusoma elimu na taaluma mbalimbali huku idadi nyingine kubwa nayo ikielekea katika Vyuo Vikuu vya Kidini (Hawza) kwa ajili ya kujifunza na maarifa ya Kiislamu. Kiu hiyo ya... Itaendelea Toleo lijalo

KUMBUKUMBU / MAPINDUZI

7

Page 10: Al hikma vol 28

8

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya kwamba: "Wakati tunapolitaja jina la Mtume Mtukufu, mfano wake huwa ni kama zimejumuika na kudhihiri kwa pamoja katika ujudi huo mtakatifu shakhsia za Ibrahim, Nuh, Musa, Isa, Luqman na waja wote wema na wateule".

8

Nabii wa Rehma, Mtume Muhammadi (SAWW)

SHEREHE / MAULIDUN NABII

Amani ya Allah, rehma na baraka zake ziwe juu yenu wapenzi wasomaji.

Kwa furaha na moyo mkunjufu nakukaribisheni kuwa nami katika kipindi hiki kipya ambacho kitadondoa baadhi tu kati ya mengi yaliyosemwa na wasomi, wanafikra, malenga na shakhsia mbalimbali wasio Waislamu lakini wenye adili na insafu kuhusu Mtume wa Mwisho wa Allah, mbora wa viumbe na Nabii wa rehma Muhammad SAW.

Nina imani na matumaini kwamba mimi na nyinyi tutafaidika na kunufaika na yale tutakayoyasikia katika kipindi hiki. Tafadhalini kuweni nami basi hadi tamati ya sehemu hii ya kwanza ambayo ni ya utangulizi

wa kipindi hiki. Katika eneo moja la dunia linaloyakutanisha na kuyaunganisha pamoja mabara ya Asia, Afrika na Ulaya, wamedhihiri Mitume kadha wa kadha ambao wote hao wamekuja kuwalingania wanadamu njia ya kheri, saada na fanaka. Mitume watano wateule wanaojulikana kwa anuani ya "Ulul-azm" walidhihiri katika kitovu cha eneo nyeti na la kistratijia la dunia linalojulikana leo hii kwa jina la Mashariki ya Kati, na wote hao, kwa kutumia njia na mbinu tofauti waliwafikishia wanadamu wito na ujumbe wa aina moja na uliokuwa na lengo moja. Ujumbe huo uliofikishwa kwa wanadamu na waja hao wateule ulikuwa ni wa kumwabudu na kumtii Mungu mmoja tu wa haki na

kusimamisha haki na uadilifu katika dunia hii iliyokuwa imeghiriki kwenye giza totoro la upotofu. Wakati jahazi la Nuhu AS lilipotia nanga kwenye jabali la Juudiy baada ya tufani na dhoruba kubwa ya gharika, Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu pamoja na wafuasi wake wachache waliamua kuijenga na kuistawisha upya dunia na kufungua tena ukurasa mwengine wa historia ya wanadamu.

Baada ya Nabii Nuh AS sauti ya wito wa Tauhidi wa kumwabudu Mola na Muumba mmoja wa haki ilisikika tena katika ardhi ya Babil kupitia kinywani mwa Nabii Ibrahim AS. Musa AS na fimbo yake ya muujiza alidhihiri katika ardhi ya Misri, akasimama kukabiliana na taghuti jabari wa ardhi

Page 11: Al hikma vol 28

9

hiyo yaani Firauni, ili kuikomboa na kuitoa kwenye minyororo ya madhila kaumu ya Bani Israil iliyokuwa ikidhikishwa na kunyongeshwa na taghuti huyo. Firauni alikuwa akijiita mungu na akawafanya Bani Israil watumwa na wahadimu wake. Baada ya Musa AS, na wakati zogo la mabwana waliolewa na kunogewa na raha za kutumikisha, na sauti za kuhuzunisha za kilio cha wanyonge wanaotumikishwa vilipokuwa vimehinikiza katika jamii ya wanadamu, Isa Masih AS alidhihiri na wito wa huruma, upendo na rehma zisizo na kikomo za Mwenyezi Mungu na akatoa bishara pia ya kudhihiri Mtume wa mwisho wa Allah ambaye atakuja baada yake.

Hatimaye katika zama ambapo watu wa mataifa na jamii tofauti duniani walikuwa wakiabudu anuai za miungu huku wingu la ujinga, ujahili na khurafa likiwa limetanda ulimwengu mzima, mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu Nabii Muhammad SAW alidhihiri huko Makka katika ardhi ya Bara Arabu. Alikuja na ujumbe bora, uliokamilika na uliotukuka zaidi kuhusu heshima ya mtu, uhuru na haki za binadamu.

Na kwa hakika alikuwa mwalimu wa walimu wote na muelimishaji mkuu wa mwanadamu katika kipindi chote cha historia ya kiumbe huyo. Nabii Muhammad SAW ni sahifa iliyokamilika ya sifa za fadhila na utukufu walizopambika nazo Mitume na mawalii wote wa Mwenyezi Mungu katika historia nzima ya wanadamu. Ni kama alivyosema Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya kwamba: "Wakati tunapolitaja jina la Mtume Mtukufu, mfano wake huwa ni kama zimejumuika na

kudhihiri kwa pamoja katika ujudi huo mtakatifu shakhsia za Ibrahim, Nuh, Musa, Isa, Luqman na waja wote wema na wateule". Katika ulimwengu huu wa ustaarabu wa zama zetu hizi sambamba na kuenea kwa Uislamu, kuna mkakati maalumu pia wa kuipiga vita dini hiyo ya mbinguni unaotekelezwa na watu wenye fikra mgando na mawazo yaliyopitwa na wakati.

Watu hao wanatumia njia na mbinu za maudhi na matusi kufikia lengo lao hilo. Vita dhidi ya Uislamu vilichukua muelekeo mpya mnamo mwaka 2006 kwa kitendo cha kifedhuli kilichofanywa na gazeti la Jyllands-Posten linalochapishwa nchini Denmark cha kumvunjia heshima Mtume wa rehma, Nabii Muhammad SAW. Mwaka uliopita wa 2011, Terry Jones, k a s i s i mjinga na m w e n y e taasubi wa Kimarekani aliendeleza mkakati huo wa chuki na uadui dhidi ya Uislamu alipotangaza nia yake ya kuzichoma moto hadharani nakala za Kitabu Kitukufu cha Qur'ani.

Na amma kitendo cha kishenzi kilichofanywa hivi karibuni cha kutengeneza filamu inayomtusi na kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW kimedhihirisha wazi kuwa azma ya maadui wa Uislamu ya kuzipiga vita thamani na matukufu ya dini hiyo ingali iko pale pale. Wapenzi wasomaji, bila ya shaka yoyote jina la Nabii huyo wa rehma lililopambwa na sifa zote bora za kiakhlaqi ni lenye kung'ara na kumeremeta kwa namna ambayo matusi ya watu hao wajinga na wasio na insafu hayawezi kutia

doa wala kupunguza hata chembe ndogo ya nuru ya mng'aro na mmeremeto huo. Historia na walimwengu wamethibitisha kwamba waliofanya ufidhuli na kejeli hizo ni watu waliokosa kuwa na hata chembe ndogo ya ujuzi na busara, na ambao taasubu, bughudha na chuki za kijahilia zimeyapofua macho na nyoyo zao. Abbas Lajawardi, mtengeneza filamu wa Kiirani za matukio halisi, kwa kimombo documentary kitambo si kirefu nyuma alifanya safari katika nchi za Magharibi kwa ajili ya kutengeneza filamu yake iitwayo "Uhuru Upi?" Katika safari yake hiyo alikutana na kufanya mahojiano na Kasisi Terry Jones wa Marekani na

Nabii wa Rehma, Mtume Muhammadi (SAWW)

SHEREHE / MAULIDUN NABII

Page 12: Al hikma vol 28

10

vilevile Kurt Westergaard, mchoraji katuni wa Denmark licha ya ulinzi maalumu wa askari usalama waliowekwa kuwalinda watu hao. Moja ya masuali aliyowauliza katika mahojiano hayo ni kama wamewahi kuisoma Qur'ani. Jibu la wote hao lilikuwa ni 'la' hawajawahi asilani kuisoma Qur'ani bali walikurupuka tu na kumshambulia Mtume na kitabu hicho alichoteremshiwa pasina kuelewa chochote kuhusu muhtawa na yaliyomo ndani yake.

Wapenzi wasomaji, katika kipindi hiki kinachokujieni chini ya anuani ya "Yaliyosemwa na Wenye Hekima Kuhusu Nabii wa Rehma", tumekusudia kudondoa baadhi ya yale yaliyoelezwa na wanafikra na watu wenye hekima na insafu kuhusu Mtume Mtukufu wa Uislamu, Nabii Muhammad SAW. Hakuna shaka yoyote kuwa msomi na mwanafikra yoyote yule mwenye insafu hawezi kuikana taathira isiyo na kifani ya shakhsia yenye kung'ara ya Bwana Mtume SAW. Kwani popote pale

atakapotupia jicho mtu, atashuhudia athari ya Mtume huyo adhimu katika kujenga akhlaqi tukufu na maadili aali ya kiutu sambamba na ustawi wa ustaarabu na utamaduni wa mwanadamu. Hata kama wasomi na wanazuoni hao wasio Waislamu wameandika na kueleza waliyoyaeleza kuhusu Bwana Mtume kulingana na misingi ya maarifa na maadili ya Ulimwengu wa Magharibi lakini ndani ya maneno yao unashuhudiwa ukweli unaotoa picha na taswira halisi ya Nabii huyo wa rehma, na hilo ni jambo la kusifiwa na kupongezwa.

Kwa Mnasaba huoWaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dakta Muhammad Jawad Zarif amesema kuwa Tuzo ya Mtume Mtukufu (saw) ina nafasi muhimu katika kusambaza elimu na teknolojia katika ulimwengu wa Kiislamu. Akizungumza pambizoni mwa duru ya pili ya kikao cha Baraza la Mkakati wa Tuzo ya Mtume (saw) mjini

Tehran, Dakta Zarif alisema kuwa moja kati ya malengo muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi zote za Kiislamu, ni kunyanyua juu nafasi ya kielimu katika ulimwengu wa Kiislamu. Ameongeza kuwa kushiriki kikamilifu wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu katika masuala ya elimu na teknolojia katika uga wa kimataifa kunaweza kunyanyua malengo aali na muhimu ya nchi za Kiislamu.

Tuzo hiyo ya Mtume (saw) itatolewa kwa wasomi watatu kutoka nchi za Kiislamu na msomi mwingine wa Kiislamu kutoka eneo lingine lolote. Washindi wa tuzo hizo watapewa zawadi ya nishani za dhahabu na dola laki tano.

Kikao hicho pia kilipitisha mpango wa kutolewa Tuzo ya Mtume (saw) katika duru ya kwanza kwa wasomi wa sayansi na teknolojia ya nano, sayansi na bioteknolojia na sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano.Allahumma swali ala Muhammad waali Muhamma, Wassalamu Alaykum.

10

SHEREHE / MAULIDUN NABII

Page 13: Al hikma vol 28

11

HOTUBA / KHAMENEI (RA)

Kiongozi Muadhamu wa Mapunduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei

katika siku ya Maulidi na sherehe za kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) na mjukuu wake Imam Ja'far Swadiq (sa) alikutana na viongozi wa Mfumo wa Kiislamu wa Iran, wageni wanaoshiriki mkutano wa 27 wa Umoja wa Kiislamu na matabaka mbalimbali ya wananchi.

Aliuhimiza Umma wa Kiislamu kutimiza matarajio ya Mtume Muhammad (saw) na kusema: Umoja ndiyo suala muhimu zaidi hii leo katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema kuwa licha ya njama zote zinazoshuhudiwa sasa mustakbali wa ulimwengu wa Kiislamu unatoa bishara njema chini ya kivuli cha mshikamano, kuwa macho na mwamko wa Kiislamu.

Ayatullah Khamenei alitoa mkono wa baraka kwa Waislamu wote mnasaba wa sikukuu hii adhimu ya kukumbuka kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW na kuzaliwa Imam Jafar Sadiq AS na kukutaja kujiweka mbali na ndoto na mawazo yasiyotegemea uhakika wa mambo na baadaye kufanya jitihada za

kujikomboa kutokana na dhulma na ukandamizaji wa tawala za kidikteta na kuunda serikali ya kiadilifu kuwa ni mbinu mbili zinazotumiwa na Uislamu kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu.

Ameongeza kuwa: Mataifa ya Waislamu yanapaswa kujikomboa kwa ndani na kifikra na kufanya jitihada za kuasisi utawala wa wananchi, kuanzisha demokrasia ya kidini na kufanya harakati kwa mujibu wa sheria za Kiislamu kupitia njia ya kujikomboa kisiasa. Vilevile amezitaja hatua zinazochukuliwa na maadui wa Uislamu kwa ajili ya kuzuia kupatikana umoja wa kweli na saada na ufanisi wa

Umma wa Kiislamu kuwa ni njama tata na zenye sura mbalimbali na kuongeza kuwa, kuzusha mizozo na mifarakano kati ya Waislamu ndiyo msingi mkuu unaotumiwa katika njama za mabeberu.

Ayatullah Ali Khamenei amezitaja njama za miaka 65 sasa za maadui wa Uislamu za kujaribu kuisahaulisha kadhia ya Palestina na kuwabebesha Waislamu utawala pandikizi na ghasibu wa Kizayuni ambao unafanya jinai za kila aina dhidi ya Waislamu kuwa ni mfano mwingine wa njama za kiukandamizaji za Marekani na mabeberu wengine duniani na kuongeza kuwa: Vita vya siku 33

Umoja ndiyo suala muhimu zaidila Ulimwengu wa Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka Maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu kuwatahadharisha Waislamu kuhusu hatari za hitilafu na mizozo ya kimadhehebu.

Page 14: Al hikma vol 28

12

huko Lebanon, vita vya siku 22 na vile vya siku nane vya huko Ghaza vimeonesha kuwa, ukitoa baadhi ya tawala ambazo kivitendo zimegeuka kuwa walinzi wa malengo ya mabeberu, mataifa ya Waislamu yako macho na yamelinda utambulisho na uwepo wa Palestina na yanaendelea kutoa vipigo hivi na vile kwa utawala wa Kizayuni na waungaji wake mkono.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, unapoyaangalia kwa upana masuala ya ulimwengu wa Kiislamu utaona kuwa, kukumbwa na mghafala Umma wa Kiislamu na kujaribu kuufanya usahau kadhia ya Palestina ni moja ya malengo makuu yanayowafanya maadui wa Uislamu wazushe vita vya ndani, wachochee mizozo na hitilafu na waeneze fikra za kuchupa mipaka na za kitakfiri za kuwaona Waislamu wengine ni makafiri.

Aidha ameelezea kusikitishwa sana na suala hilo na kuongeza kuwa, kuna baadhi ya watu wanashikilia fikra za kitakfiri za kuwakufurisha Waislamu wengine badala ya kuelekeza nguvu zao katika kupambana na utawala khabithi wa Kizayuni na wanatumia jina la

Uislamu na sharia za dini hiyo tukufu kuwahesabu Waislamu walio wengi kuwa ni makafiri na kuandaa uwanja wa kuzusha vita na machafuko na mizozo na ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kuwepo makundi ya aina hiyo kunawafurahisha mno maadui wa Uislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria aya ya 29 ya sura ya 48 ya al Fat'h ambayo sehemu yake moja inasema: "Wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao..." na kuongeza kuwa: Makundi na mirengo ya kitakfiri inadharau amri hiyo ya wazi ya Mwenyezi Mungu na yanawazozanisha Waislamu kwa kuwagawa baina ya makundi

mawili ya Waislamu na makafiri na kuwafanya Waislamu waingie vitani kupigana wao kwa wao.

Vilevile amehoji kwa kusema: Kwa kuzingatia hali hii kuna mtu yeyote mwenye shaka kwamba, kuwepo makundi hayo na uungaji mkono wa kifedha na kisilaha yanayopata makundi hayo ni kazi ya mashirika ya kiusalama na khabithi ya madola ya kibeberu na vibaraka wao?Ayatullah Khamenei kwa kuzingatia uhakika huo ameitaja mirengo na makundi ya kitakfiri kuwa ni hatari kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na ameziusia nchi za Kiislamu kuwa macho sana mbele ya makundi hayo. Ameongeza kwa kusema: Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya tawala za Waislamu hazishughulishwi na madhara ya kuyaunga mkono makundi hayo na hazielewi kuwa kuna siku moto waliouwasha utawageukia wao wenyewe na kuwateketeza.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezitaja njama za kuchochoa na kushadidisha mivutano na hitilafu kati ya Waislamu wa Kisuni na Kishia na kuchochea mapigano ya wenyewe kwa wenywe kwenye mataifa ya Waislamu katika kipindi cha miaka mitatu minne iliyopita, kuwa ni

Rais Rouhani ameutaja kufuata mwito wa umoja na mshikamano uliotolewa na Imam Khomeini kuwa ndiyo njia pekee ya kuuokoa Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Dini moja, Mtume mmoja, manufaa ya pamoja, maadui wa pamoja na malengo kama vile Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na Quds azizi ni mambo ambayo yanaweza kuwaunganisha Waislamu.

12

HOTUBA / KHAMENEI (RA)

Page 15: Al hikma vol 28

13

radiamali ya mabeberu wa dunia ya kukabiliana na suala la kuongezeka mwamko wa Kiislamu katika baadhi ya nchi.

Ameongeza kuwa: Mabeberu wanafanya njama za kujaribu kufifiliza na kuufunika mwamko wa Kiislamu kwa kuwagombanisha Waislamu wa madhehebu tofauti na baadaye kuvikuza kupindukia vitendo viovu na vichafu vinavyofanywa na magenge ya kitakfiri kama vile kutafuna tafuna maini mabichi ya watu waliouawa ili kupotosha mafundisho matukufu na ya asili ya Kiislamu katika fikra za walimwengu, na kujaribu kuidhihirisha dini hii ya Mwenyezi Mungu kuwa inafundisha ukatili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Ni jambo lisilo na shaka hata kidogo kuwa, mambo haya hayakutokea kwa sadfa bali madola ya kibeberu duniani yamechukua muda mrefu kuyaandalia mazingira na mikakati ya kutokea kwake. Ayatullah Khamenei amelitaja suala la kupambana na jambo lolote lililo dhidi ya umoja na mshikamano wa Kiislamu kuwa ni wajibu mkubwa na mzito kwa Waislamu wote wa

Kishia na Kisuni na wa madhehebu myingine za Kiislamu na kusisitiza kwamba: Watu wenye ushawishi na vipaji vya kisiasa, kielimu na kidini wana jukumu zito la kuleta umoja na mshikamano katika jamii za Waislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka Maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu kuwatahadharisha Waislamu kuhusu hatari za hitilafu na mizozo ya kimadhehebu. Amewataka wasomi wa vyuo vikuu kubainisha umuhimu wa malengo ya Kiislamu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kama

ambavyo amewahimiza watu wenye ushawishi wa kisiasa katika Umma wa Kiislamu kutegemea uungaji mkono wa wananchi na kujiweka mbali na mabeberu na maadui wa Uislamu akisisitiza kuwa: Leo hii jambo muhimu zaidi kuliko yote katika ulimwengu wa Kiislamu ni mshikamano na kuwa kitu kimoja.

Vilevile ameashiria namna mataifa ya Waislamu yanavyotoka pole pole chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa wakoloni na kutahadharisha kuwa: Mabeberu wamekusudia kulinda manufaa yao ya kipindi cha ukoloni na ubeberu wa moja kwa moja kupitia ubeberu usio wa moja kwa moja wa kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi. Ayatullah Khamenei amekutaja kuwa macho na kuwa na welewa wa kina wa mambo kuwa ndiyo njia pekee ya kuweza kupata saada na ufanisi Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Kuwa na suhula nyingi, kuwa katika eneo bora la kijiografia, urithi mwingi wa kihistoria na wenye thamani kubwa sana pamoja na vyanzo visivyo na kifani vya kiuchumi vilivyoko katika nchi za Kiislamu vinaweza kutumiwa kuwaletea heshima, utukufu na hadhi ya kipekee Waislamu chini ya kivuli cha mshikamano na kuwa kitu

HOTUBA / KHAMENEI (RA)

Page 16: Al hikma vol 28

14

kimoja. Vilevile ameutaja ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuzidi kupata nguvu sifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuwa kigezo bora kwa mataifa mengine licha ya kupita miaka 35 ya njama mbalimbali za mabeberu kuwa ni katika dalili za bishara njema kwa Umma wa Kiislamu na kusisitiza kuwa: Kwa baraka na msaada wa Mwenyezi Mungu, taifa la Iran na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unazidi kupata nguvu siku baada ya siku, unazidi kuimarika na unazidi kuwa madhubuti.

Mwishoni mwa mkutano huo, Ayatullah Khamenei ameonana na kuzungumza kwa karibu na wageni waalikwa kwenye Mkutano wa 27 wa Kimataifa Umoja wa Kiislamu.Kabla ya hotuba hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Hasan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa

mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimishio ya Maulidi ya Mtume wa Mwisho SAW na Imam Ja'far Sadiq AS na ameashiria kiza totoro cha kiutamaduni, kijamii na kisiasa kilichokuwa kimetanda katika kipindi cha ujahilia na kuongeza kuwa: Ni katika kipindi hicho kilichojaa masaibu mengi ndipo Nabii wa rehma alipozaliwa na kuijaza historia ya mwanadamu nuru ya uongofu na usafi na ukweli.

Rais Rouhani amegusia pia matatizo na hitilafu zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema kuwa, ni jambo lisilo na shaka kuwa hivi sasa Mtume wa Uislamu anateseka kutokana na watu wapotofu na watu walioamua kufuata njia ya misimamo mikali ya kitakfiri ya kuwakufurisha Waislamu wengine na kwamba jamii za Kiislamu zinapaswa kwa mara nyingine kusimama imara

kumsaidia Nabii wao wa rehma. Rais Rouhani ameutaja kufuata mwito wa umoja na mshikamano uliotolewa na Imam Khomeini kuwa ndiyo njia pekee ya kuuokoa Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa:

Dini moja, Mtume mmoja, manufaa ya pamoja, maadui wa pamoja na malengo kama vile Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na Quds azizi ni mambo ambayo yanaweza kuwaunganisha Waislamu.

Rais Rouhani ameongeza kuwa: Umma wa Kiislamu unapaswa kushikamana na Qur'ani Tukufu chini ya kivuli cha tadbiri, busara, misimamo ya wastani, matumaini na kufanya juhudi bila ya kuchoka ili kuufufua tena ustaarabu wa Kiislamu.

Wassalaam Alaykum.

Baadhi ya picha za washiriki wa wiki ya umoja wa Kiislamu mjini Tehran - Iran

HOTUBA / KHAMENEI (RA)

14

Page 17: Al hikma vol 28

15

Page 18: Al hikma vol 28

16

SHEREHE / MAULIDUN NABII

Kipando chake kwa usiku mmoja kilimfikisha Masjidul Aqswa (palestina) kutokea

Masjidul haram, Mtume ambae dunia inashuhudia wazi wazi kuwa yeye ni Rahmatu lil alamiina. Pamoja na hayo imepokewa hadithi kwamba: “Siku moja Mtume (saw) alikuwa anachukua udhu kisha akaja paka, Mtume (saww) alipogundua kuwa paka huyo ana kiu alimpa kwanza maji kisha akaendelea na udhu”.

Naam huyu ni Mtume ambae kwa waumini ana huruma na ni mkali kwa makafiri, mwenye kusamehe juu ya haki yake hata kwa kafiri lakini katika swala la kutekeleza kanuni na hukumu za M/Mungu habadili msimamo wala kulegalega hata kama ni kwa mtu wa karibu yake au mtu wa familia yake.

Tuseme nini juu ya Mtume ambae katika maajabu yaliyotokea wakati wa kuzaliwa kwake; kuzima kwa moto wa Faris/majusi na kutetemesha Ikulu ya enzi ya Kisra (mfalme wa Iran), lakini anapoalikwa

na watu masikini, wanyonge hukaa nao na kula pamoja nao. Mtume anaepelekewa salaam na Malaika mtukufu Jibril lakini yeye binafsi husikia raha na faraja kuwa wa kwanza kuwatolea salam watoto kisha wao wanaitikia salaam hiyo. Anaposujudu katika swala (Kama tunavyojua kuwa sijda ni hali ya kuonyesha unyenyekevu kwa Mola) wakija na kumpandia mgongoni basi huwacha hadi waondoke kisha huinua kichwa na kuendelea na swala.

Majina Ya Mtume Ndani Ya Qur' an.Kama tunavyofahamu Mtume Muhammad amepambwa kwa sifa nyingi sana, hapa kwa uchache tutaangalia baadhi ya majina

ambayo yametajwa katika Qur-an na yanaashiria utukufu na fadhila alizonazo bwana Mtume:

Ahmad: “Na kumbuka aliposema Isaa bin Mariyam, enyi wana wa Israil hakika mimi ni Mtume wa M/mungu kwenu, ninae thibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kutoa habari njema za Mtume atakaekuja baada yangu, jina lake ni Ahmad, Lakini zama alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhahiri (surat swaf ;6).

Muhammad:“Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliepitiwa na Mitume kabla yake. M/mungu… Surat al imran: 144, Surat

“Hakika M/Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba ya Mtume na kukutakaseni sana sana”. Surat Ahzaab: 33.

Naam huyu ni Mtume ambae M/Mungu amempandisha Mbinguni, nyayo zake tukufu kukanyaga sehemu wanayokanyaga Malaika, na kutoa funzo kuwa mwanadamu anapoingia katika taqwa anakuwa na daraja la kuwazidi hata malaika, katika safari ya miraj bwana Mtume alifika sehemu ambayo hata malaika mtukufu Jibril hakuweza kukanyaga.

16

Page 19: Al hikma vol 28

17

SHEREHE / MAULIDUN NABII

fat-h: 29.

Abdallah:“Na kwa hakika mja wa M/mungu aliposimama kumuomba mola wake…. Suratul jinn: 19.

Khatamu Nnabiyyiin:“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenuu bali ni Mtume wa M/munguna wa mwisho wa Mitume wa M/mungu…..suratul ahzab;40

Bashiiru na Nadhiiru:“Ewe nabii hakika sisi tumekutuma ili uwe shahidi na mtoaji wa habari nzuri na muonyaji.Na muitaji wa watu kwa M/mungu kwa idhiniyake,na uwe taa itoayo nuru( surat ahzab;45-46)

Swahib kauthar:“kwa hakika sisi tumekupa kheri nyingi ……surat kauthar;1-3.

M a j u k u m u y a M t u m e (SAW)1- Kusomesha aya za M/mungu: “Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyeleta Mtume katika watu wasiojua kusoma, anayetokana nao, anawasomea aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hekima” Surat jumaa: 2

2- Kutoa watu gizani: Kuwatoa watu katika giza la dhulma, ujinga na kuwaingiza katika nuru:“Ili uwatoe watu katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa idhini ya Mola wao” surat ibrahim:1

3- Kujenga maisha:Kujenga maisha ya wasiojiweza kwa kuwapa zaka na kuhamasisha utoaji zaka:“chukua sadaka katika mali zao,uwasafishe na uwatakase

kwa hizo (sadaka zao) na uwaombee.hakika kuomba kwako ni utulivu kwao na M/Mungu ndiye asikiaye,ajuaye” surat tauba;103 4- Muombezi:Kuombea msamaha umati wake basi kwa sababu ya rehma ya M/Mungu umekuwa laini kwaona kama ungekuwa mkali, mshupavu wa moyo, wangekukimbia:“Basi wasamehe na uwaombee msamaha na ushauriane nao katika mambo, na unapoazimia basi mtegemee M/Mungu, hakika M/Mungu anawapenda wenye kumtegemea” Surat ali imran: 159.

5- Adalat Kusimamisha uadilifu:“Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu” Surat maida; 42

6- Amri na Nahyi:Kuamrisha mema na kukataza mabaya:“Ambao wanamfuata Mtume, nabii alioko Makka, ambaye wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, ambaye anawaamrisha mema na anwakataza yaliyo mabaya na kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia maovu” surat

aaraf: 157

7- Kuongoza jihad:Kupigana jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu:“Ewe Nabii! Pigana na makafiri na wanafiki na uwe mgumu kwao, na makazi yao ni jahannam, hayo ni marejeo mabaya” Surat tauba: 73.

Ni wazi kuwa sehemu kubwa ya qur-an inazungumzia juu ya Mtume.Miongoni mwa mambo aliyokuwa akiyafanya Mtume ni pamoja na kuwahurumia mateka, kuwatibu waliojeruhiwa katika vita, akitumia muda mwingi wa usiku kufanya ibada.

Mwanadamu lazima atambue kuwa sehemu kubwa ya Qur- an inamzungumzia bwana Mtume na mwenendo wake mzima wa maisha, zikiwemo sifa zake, wadhifa wake, matatizo yake pamoja na ya wafuasi wake, jinsi alivyokabiliana na marafiki na maadui zake. Basi ni kitabu gani zaidi ya Qur- an kitakachokukinaisha? Na ni uongofu gani utakaoufata badala ya qur-an kama si upotevu? Na je ni khasara iliyoje kwa kuacha muongozo na sheria za qur -an na kufuata sheria za wanadamu?

17

Page 20: Al hikma vol 28

18

Watu Mashuhuri wakiweka sahihi zao kwenye kitabu maalum cha Maombolezo ya SHAHIDI Sheikh Ibrahim Ansary katika Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi Jamhuri ya Kiislamu ya Irani - Dar es

Salaam.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akiongoza watu mbalimbli kuweka sahihi katika kitabu cha Maombolezo, wengine walioweka sahihi zao ni pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Mh. Mahdi Agha Ja'fari, Sheikh Ali Mayunga, Sheikh Musabah Mapinda, Sheikh Mulaba Swaleh, Mudiri wa Hawza Imam Ja'fari Swadiq (AS) Sheikh Hemed Jalala, Mwenyekiti wa TIC) Bregedia Jeneral Simba, Haji Abul Qasim (Rais wa Jumuiya ya Walebanoni wanaoishi nchini Tanzania) Dokt. Alidina Imam wa Msikiti wa Makhoja Dar es Salaam, Sheikh Abaswale Imam wa Msikiti wa Idrisa.Haj Aghaa Ansary alikuwa ni mwambata wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanoni. Alikufa shahidi kwa kulipuliwa na bomu tarehe 19 Octoba 2013 , Mwenyezi Amrehemu Amin

Page 21: Al hikma vol 28

19

Page 22: Al hikma vol 28

20

Komamanga huzuia kusambaaKansa ya Matiti

Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la

komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti kusambaa mwilini. Uchunguzi huo uliochapishwa katika Jarida la Utafiti la Kuzuia Kansa umeonesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia kimeng'enyo (enzyme) aina ya aromatase. Suala ambalo huzuia kukua kwa homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti. Shiuan Chen aliyeongoza uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti kuzaliana

mwilini pamoja na tezi la ugonjwa huo kukua. Aromatase ni kimeng'enyo ambacho hugeuza homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambuliwa kimeng'enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen.

Huko nyuma pia uchunguzi ulionesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na antioxidant nyingi na vitamini mbalimbali, ambazo hulifanya tunda hilo liweze kusaidia katika mapambano dhidi ya magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer. Antioxidant huzuia radikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili

yetu. Uwezo huo huufanya mwili uweze kukabiliana na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe. Hivyo kutokana na faida nyingi za tunda hili, kama huwezi kulipata sokoni, basi unaweza kutumia juisi yake na daima kuitunza afya yako. Faida nyinginezo za juisi ya komamanga ni kuzuia maendeleo ya saratani ya mapafu.

Kupambana na saratani ya matiti Kupunguza ukuaji wa saratani ya kibofu, kuzuia na kupunguza kasi ya ugonjwa wa Alzheimer kupunguza mafuta mwilini, kushusha shinikizo la damu, kulinda meno Inasemekana kwamba ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza

Inasemekana kwamba ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi.

JAMII / AFYA

Page 23: Al hikma vol 28

21

mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi. Utafiti huo mpya uliofanywa na timu ya Jamii ya Saratani ya Marekani umeonesha kuwa, kufanya mazoezi kama vile kutembea kwa miguu, kunaweza kupunguza hatari ya kupata kansa ya matiti kwa wanawake ambao hawapati tena hedhi. Utafiti huo umeonesha kuwa, kutembea kwa saa moja kila siku hupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kupata ugonjwa huo.

Timu hiyo ya watafiti i l i w a c h u n g u z a wanawake zaidi ya 73,000 walio na umri wa kuanzia miaka 50 hadi 74 na matokeo yameonesha kuwa, wanawake waliotembea kwa masaa yasiyopungua 7 kwa wiki walipunguza hatari ya kupata kansa ya matiti kwa asilimia 14 ikilinganishwa na wale waliotembea kwa masaa matatu au chini ya hapo.

Dakta Baroness Delyth Morgan Mkurugenzi Mkuu wa Kampeni ya Kupambana na Saratani ya Matiti amesema kuwa, kwa mara nyingine utafiti huo umesisitiza jinsi mfumo wa maisha ya mtu unavyoweza kuathiri hatari ya kupata ugonjwa wa kensa ya matiti.

Tunahitimisha mada kuhusiana na saratani ya matiti kwa kuangalia tafiti mbalimbali kuhusiana na ugonjwa huo.Wataalamu wamegundua

kuwa mada zinazotokana na tikitimaji ambazo ni mboga zinazopatikana sana India, China, Amerika ya Kusini na hata barani Afrika zinaweza kusaidia kuwaepusha wanawake na kansa ya matiti.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliochapishwa kwenye Jarida la Utafiti wa Kensa, majimaji (extract) yanayotolewa katika tikitimaji

chungu yanayojulikana kama 'karela' kwa lugha ya Kihindi yanaweza kupunguza kasi ya kukua kwa seli za kansa ya matiti au hata kuua kabisa seli hizo. Ratna Ray aliyeongoza uchunguzi huo anasema kwamba, tikitimaji chungu zina

uwezo wa kuzuia kansa na kuchelewesha kutokea ugonjwa huo wa saratani ya matiti,

lakini bado haijathibitika iwapo mboga hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo. Wanasayansi wanasema kuwa, uchunguzi zaidi unapaswa kufanywa ili kuhakikisha uwezo na usalama wa tikitimaji chungu kuhusiana na suala hilo.

Ratna Ray aidha anasema kuwa, kutumia lishe asilia ni suala linalopewa umuhimu mkubwa hivi sasa na sayansi katika kuzuia ugonjwa wa

saratani unaoongezeka kila siku duniani.

Mtaalamu huyo vilevile amesema, katika siku za usoni watafanya

u c h u n g u z i u takaowahusisha

watu wengi zaidi walio na hatari ya kupata kansa ili kuona iwapo tikitimaji chungu zitawazuia kupatwa na ugonjwa huo au la. Kwa muda mrefu tikitimaji chungu ambazo zina Vitamin C na mada ya flavonoid zimekuwa zikijulikana kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia kisukari na

kupunguza kiwango cha sukari katika damu. Hali kadhalika wataalamu wanatuambia

JAMII / AFYA

Page 24: Al hikma vol 28

22

kuwa mammography inaweza kuokoa maisha ya wanawake wengi. Japokuwa kumekuwepo na mjadala mkubwa kuhusu uwezo wa kutambua ugonjwa wa kipimo kinachotumiwa kugundua kansa ya matiti, lakini utafiti umethibitisha kwamba kipimo hicho kina faida kubwa. Uchunguzi huo umeonesha kuwa, kipimo cha mammography kina faida kubwa zaidi kuliko hasara zake, na kwamba kutumiwa kwake kunaokoa zaidi maisha ya wanawake yanayoweza kupotea kutokana na kansa ya matiti.

Ijapokuwa mammography ina uwezo wa kuonesha uvimbe (tumors), lakini pia kipimo hicho kinaweza kuonesha uvimbe ambao hauna madhara na kuwafanya baadhi ya wanawake wapate wasiwasi na kufanyiwa operesheni bila kuwa na tatizo.

Uchunguzi wa huko nyuma ulishauri kuwa, umri wa kufanyiwa

kipimo cha mammography ili kujua kama mtu ana saratani ya matiti au la usogezwe kutoka miaka 40 hadi 50 ili kupunguza uwezekano wa wanawake kufanyiwa kipimo hicho mara nyingi maishani. Vilevile imesisitiza kwamba, kwa kila wanawake 6 ambao hufanyiwa kipimo hicho bila ya kuwa na ulazima, kuna maisha ya mwanamke mmoja yanayonusuriwa kwa kufanyiwa mammography.

Kwa hivyo wataalamu wamewashauri wanawake wasizembee na kuwahimiza wafanyiwe kipimo hicho, kwani faida zake ni kubwa zaidi kuliko hasara. Si vibaya kujua kuwa, nchini Uingereza pekee zaidi ya wanawake 45,000 hugunduliwa kuwa na saratani ya matiti kila mwaka, na zaidi ya wanawake 12,000 hufariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Tunahitimisha Makal hii kwa utafiti unaotujuza kuwa, kuishi maisha mazuri na

kunyonyesha mtoto kunaweza kuzuia kesi 70, 000 za kansa ya matiti kila mwaka. Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Marekani ya Wataalamu wa Uchunguzi wa Saratani Duniani zamani kidogo imeonesha kuwa, ingawa ni kweli jeni zina uhusiano katika kusababisha kansa ya matiti, lakini jinsi mtu anavyoishi pia kunaweza kumzuia asipatwe na ugonjwa huo hatari kwa kiasi kikubwa.

Bi. Susan Higginbotham mmoja wa wataalamu hao anasema kuwa, inakadiriwa kwamba asilimia 40 ya kesi za ugonjwa wa kansa ya matiti au kesi 70, 000 za ugonjwa huo zinaweza kuzuiwa nchini Marekani, kwa kufanyika tu mabadiliko katika mifumo ya maisha ya watu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kula vyakula visivyokuwa na mafuta mengi, kuwa na uzito unaotakiwa kiafya, kufanya mazoezi pamoja na kuacha pombe bila kusahau kunyonyesha, kunaweza kusaidia sana watu wasipate ugonjwa wa saratani ya matiti.

Wanasayansi wanahitimisha kwa kusema kuwa, namna mtu anavyoishi ndilo suala muhimu sana linaloainisha iwapo mtu anaweza kupata ugonjwa huo au la. Kwa hivyo, tunashauriwa kufanya mazoezi kila siku kwa muda usiopungua nusu saa, huku wakinamama wakihusiwa kuacha kunywa pombe.

Shukrani kwa Idhaa ya Kiswahili Radio Teran kwa Makala Hii.

HISTORIA / RASULU

Page 25: Al hikma vol 28

23

Malezi ya Watotokatika Uislamu

Lugha ya Kiswahili ina misemo chungu tele ambayo hutumiwa

kufikisha ujumbe, kubainisha jambo, kuashiria kitu au kutaka kutoa funzo fulani lakini kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Hili sio jambo ambalo linapatikana katika Kiswahili tu, bali kila lugha inajivunia kwa methali na mafumbo ambayo kwa mwenye kuitambua lugha husika hustaladhi na kuburudika anaposikia methali hiyo, akawa ni mwenye kuifahamu na hasa pale methali hiyo inapotumiwa mahala pake.

Katika makala hii nitajaribu kwa tawfiki ya Allah kuzungumzia suala la malezi katika Uislamu. Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo, hii ni methali mashuhuri mno katika lugha ya Kiswahili na

baina ya Waswahili. Sitajisumbua kubainisha maana na fasili ya methali hii hasa kutokana na kuwa kwake wazi na wadhiha. Uislamu ndio dini kamili kabisa miongoni mwa dini za mbinguni. Wanazuoni wanasema, dini ni mfumo kamili wa maisha. Kwa muktadha huo, Uislamu ni dini ambayo imebeba kila hitajio la mwanadamu. Suala la malezi kwa watoto ni miongoni mwa mambo yaliyokokotezwa na kutiliwa mkazo mno katika Uislamu.

Hapana shaka kuwa, masuuliya na majukumu ya wazazi kwa watoto wao sio kuwalisha, kuwasomesha na kuwavisha tu, la hasha, bila shaka wana jukumu jingine muhimu na kubwa zaidi nalo ni kuwapa watoto malezi bora yatakayowawezesha kuondokea kuwa watu wema na ambao watainufaisha jamii ya

mwanadamu. Kipindi cha kuanza malezi ya mtoto Ni makosa kudhani kwamba, malezi ya mtoto huanza baada ya kuzaliwa mtoto, ukweli wa mambo ni kuwa malezi ya mtoto huanza tangu pale mimba inapotunga.

Ni wakati huo ambapo mama mja mzito anapaswa kuwa makini katika kila hatua anayochukua, katika kila jambo analofanya na katika kila kitu anachokisema kwani yote hayo huwa na taathira kwa kichanga kilichoko tumboni mwake. Hivyo basi naweza kujusuru kusema kwamba, malezi ni jambo linalohusu yale yote anayofanyiwa mtoto tangu akiwa tumboni mwa mama mpaka kufikia umri wa kujitegemea. Fauka ya hayo, hata anapojitegemea mtoto huyo, bado anahitajia miongozo ya wazazi.

JAMII / MALEZI

Hapana shaka kuwa, ''MAS'ULIYA'' na majukumu ya wazazi kwa watoto wao sio kuwalisha, kuwasomesha na kuwavisha tu, la hasha, bila shaka wana jukumu jingine muhimu na kubwa zaidi nalo ni kuwapa watoto malezi bora yatakayowawezesha kuondokea kuwa watu wema na ambao watainufaisha jamii ya mwanadamu.

23

Page 26: Al hikma vol 28

24

Suala la malezi linamhusu mama tu? Wanajamii wengi wamekuwa na fikra potofu kwa kudhani kwamba, suala la malezi na kumlea mtoto ni la mama tu na kwamba, baba yeye ana majukumu yake mengine katika kutafuta riziki, hawaiji na mahitaji mengine ya familia. Jambo lililo dhahir shahiri ni kwamba, wazazi wote wawili wanahusika kwa ukamilifu na kadhia ya malezi kwa mtoto au watoto wao. Malezi ya mtoto yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili.1. Malezi ya kimwili. 2. Malezi ya kiroho.

Malezi ya kimwili ni yale yote anayofanyiwa mtoto ili akue katika afya njema. Malezi haya huanza mara tu mama anapopata ujauzito. Baba ana wajibu wa kumtunza mkewe na kumpatia vyakula maalum ili mama na mtoto tumboni wawe na afya nzuri.

Jukumu la mama ni kufuata masharti ya kulea mimba anayopewa na Daktari sambamba na kufuata miongozo na mafundisho ya Uislamu kwa mama mja mzito. Unadhani kama mama mja mzito atakuwa mtu wa ibada na mwenye kusoma Qur'ani,

kusikiliza mawaidha na kufanya mambo ambayo yanaridhiwa na Mwenyezi Mungu mtoto wake atakayezaliwa atakuwa sawa na mtoto wa mama mja mzito ambaye ni mlevi, mwenye kusikiliza miziki na anayefanya mambo yasiyomrisha Allah? Bila shaka watoto hawa wawili katu hawawezi kulingana kinafsi, kisaikolojia na hata kitabia.

Baada ya Mtoto KuzaliwaQur'ani Tukufu inabainisha jukumu na wajibu wa baba na mama baada ya mtototo kuzaliwa. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake.

Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi

hapana ubaya kwenu mkitoa mlichoahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda." (al-Baqara 2:233)Mpenzi msomaji wa jarida hili maridhawa, aya hii inatubainishia wazi kuwa hata katika umri wa kunyonya mtoto, wazazi wote wawili wanawajibika, kila mmoja katika nafasi yake. Katika kipindi chote cha kumlea mtoto jukumu kubwa la baba ni kuilisha familia, kuivisha na kuiweka katika makazi mazuri kwa kadiri ya wasaa wake.

Mama naye kwa upande wake ana jukumu la kuwatunza watoto kwa kuhakikisha kuwa wanakula vizuri wanakuwa wasafi wa mwili na nguo na wanaishi katika mazingira masafi.

Haya ndiyo malezi ya kimwili ambayo humuwezesha mtoto kuwa na afya mzuri na kukua vyema. Malezi ya kimwili ni muhimu sana, lakini yenyewe tu hayatoshelezi kumuinua mtoto atakayekuwa raia mwema mwenye kuwajibika ipasavyo kwa wazazi wake na kwa jamii yake kwa ujumla. Hivyo, wazazi pamoja na kuwalea watoto wao

“Siku moja Bwana Mtume (s.a.w.) alikuwa juu ya mimbari akiwahutubia watu, (mara) akawaona Hassan na Hussein (a.s.) wanakimbia na huku wakijikwaa, akakatiza hotuba yake, akashuka kutoka juu ya mimbari na kwenda kuwapokea watoto hao wawili. Akawabeba, kisha akapanda tena juu ya mimbari akasema: “Enyi watu, hakika mali zenu na watoto wenu ni fitina, Wallahi nimewaona wajukuu zangu wawili wakikimbia na kujikwaa, basi sikuweza kujizuia mpaka nimeshuka nikawabeba.”

JAMII / MALEZI

Page 27: Al hikma vol 28

25

kimwili, hawana budi kuhakikisha kuwa wanawalea kimaadili kwa kuwafunza tabia na mwenendo mwema anaouridhia Mwenyezi Mungu. Mtoto aanze kufunzwa tabia ya Kiislamu tangu mwanzo, hasa pale anapoanza kuongea na kuelewa lile analoelekezwa na kuambiwa.

Mtoto afikapo umri wa miaka mitano, ahudhurishwe pamoja na watoto wenzake katika kituo cha malezi ya watoto (madrasa) ambapo watoto wa Kiislamu wanalelewa. Mzazi ahakikishe kuwa watoto wa umri wa miaka saba na kuendelea wanatekeleza ipasavyo ibada maalum kama vile Sala, Saumu, na kadhalika.

Na sio kuhadaika na baadhi ya watu wanaosema, mwache mtoto bado mdogo kwa nini unamshinikiza kusali na kufunga? Wanaghafilika kwamba, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hivi unadhani kama mtoto wa kiume hajazoea kufunga akiwa na miaka saba, minane, tisa na kumi, atakuja kufunga akisha baleghe akiwa na umri wa miaka kumi na tano?

Au unadhani kama binti wa miaka sita, saba na nane hajazoeshwa kuanza kufunga katika umri huo atakuja kuweza kufunga atakapofikisha umri wa kuvunja ungo? Kuna hadithi nyingi zinasisitiza juu ya kuwafunza watoto Sala wanapofikisha umri wa miaka saba.Hivyo ni wajibu wa kila mzazi Mwislamu kumlea mtoto wake

katika dini yake ya asili kwa jitihada zake zote mpaka amfikishe kwenye utu uzima. Hapana shaka kutekeleza wajibu huu wa kuwalea watoto wetu katika maadili ya Kiislamu ni jambo gumu linalohitajia msaada wa Mwenyezi Mungu. Muumini wa kweli pamoja na jitihada zake katika kutekeleza wajibu huu hana budi kuomba auni na msaada wa Mwenyezi Mungu. Daima tuombe dua hii:

Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayoyapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. (al-Ahqaaf 46:15)

Nasaha kwa watoto baada ya kukua. Hata mtoto anapokuwa na akawa mtu mzima licha ya kuwa hahitajii tena malezi ya wazazi wake, lakini bado ni mwenye kuhitajia nasaha za wazazi wake. Kwani hawezi kushinda

tajriba na uzowefu wa wazazi wake katika maisha. Kwani kama wanavyosema wahenga, wazazi wake wamekula chumvi nyingi. Katika hili nitatosheka kunukuu nasaha za Luqman mwenye hekima kwa mwanawe.Na (wakumbushe) Luqman alipomwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika shirki bila ya shaka ni dhulma

iliyokubwa. (Luqman 31:13).Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya Khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye khabari za yote. (Luqman 31:16)

Ewe Mwanangu! Simamisha Sala, na uamrishe mema, na ukataze mabaya, na usubiri juu ya yale yatakayokusibu. Hakika hayo ni katika mambo yanayostahiki kuazimiwa. Wala usiwatazame (watu kwa jeuri) kwa upande

JAMII / MALEZI

25

Page 28: Al hikma vol 28

26

mmoja wa uso, wala usiende katika ardhi kwa maringo; hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunae, ajifakharishaye. Na ushike mwenendo wa katikati, na uteremshe sauti yako, bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (mbele ya Mwenyezi Mungu. (Luqman 31:17-19).

Mpenzi msomaji, aya hizo zimejaa malezi na mafunzo makubwa mno. Malezi ya kidunia na akhera. Tukizama kwa makini aya hizo tunaona kuwa zimejaa mafunzo ya kiakhlaqi na kimaadili na kutuonesha kwamba, tabia kama ya kukunjia watu uso, kujivuna, kujifakharisha, kutembea kwa maringo, kuzungumza kwa sauti ya juu na kuwatazama watu kwa jeuri ni miongoni mwa tabia mbaya na zisizopendwa na Allah. Moja ya mambo muhimu katika malezi ya watoto ni kuwafunza adabu na tabia njema. Kuwapenda WatotoMiongoni mwa mambo yenye taathira kubwa kwa watoto ni wazazi kuwaonesha watoto wao mapenzi, huruma na huba. Mambo haya huwa na taathira katika roho ya mtoto na hata

katika fikra zake jambo ambalo huwa na nafasi muhimu katika malezi ya kiroho kwa mtoto. Mapenzi ya Mtume (s.a.w.) kwa watoto yalijaa ndani ya moyo wake mwema, imeelezwa katika Hadith kwamba: “Siku moja Bwana Mtume (s.a.w.) alikuwa juu ya mimbari akiwahutubia watu, (mara) akawaona Hassan na Hussein (a.s.) wanakimbia na huku wakijikwaa, akakatiza hotuba yake, akashuka kutoka juu ya mimbari na kwenda kuwapokea watoto hao wawili.

Akawabeba, kisha akapanda tena juu ya mimbari akasema: “Enyi watu, hakika mali zenu na watoto wenu ni fitina, Wallahi nimewaona wajukuu zangu wawili wakikimbia na kujikwaa, basi sikuweza kujizuia mpaka nimeshuka nikawabeba.”

Siku moja Mtume (s.a.w.) alikuwa anaswali, mara Hassan na Hussein (a.s.) wakaingia ndani na kumpanda mgongoni kwake wakati alipokuwa amesujudu, Mtume (s.a.w.) akaendelea kusujudu tu. Alichukia kuwaharakisha washuke, mpaka waliposhuka wao wenyewe. Kisha alipotoa salaam na

kumaliza Sala, akaulizwa na masahaba zake sababu zilizomfanya arefushe kusujudu; akawajibu: “Wajukuu zangu wawili walikuwa wamepanda juu ya mgongo wangu nami nilichukia kuwahimiza washuke kwa haraka.”

Mtume (s.a.w.) alizoea kuharakisha Sala yake pindi asikiapo mtoto analia, na husema: “Mimi huchukia kumchosha mama yake.” Siku moja alikuwa anapita nyumbani kwa Fatima (a.s.) (binti yake), akamsikia mjukuu wake Hussein (a.s.) akilia, aliingia ndani akasema kumwambia Fatima (as): “Je hujui kwamba, mimi nimsikiapo Hussein akilia huwa nakereka?”

Siku moja Mtume (s.a.w.) alitembelewa na Al-Akraa Ibn Habis, ambaye alimwona Mtume (s.a.w.) akiwabusu wajukuu zake, Al-Akraa akasema: “Unawabusu watoto wa binti yako? Naapa kwa Mungu nina watoto kumi, na sijawahi kumbusu hata mmoja.”Mtume (s.a.w.) akamjibu: “Je ni kosa langu kama Mwenyezi Mungu ameing’oa rehma kutoka moyoni mwako.”

Siku ya Jumanne Tarehe 14 mwezi wa Januari 2014 saa mbili za usiku Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran Dar es Salaam kilipata msiba mkubwa kwa kuondokewa na Mfanyakazi wake Bw. Ramadhani Rajabu Kigambo (pichani) ambaye alifariki ghafla akiwa anaelekea sehemu yake ya kazi. Mkurugenzi na Wafanyakazi kwa jumla wamehuzunishwa sana na kifo hiki, wanapenda kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bw. Ramadhani Rajab. Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake pahala pema Peponi Inshallah

JAMII / MALEZI / TAAZIYA

Inna lilahi wainna ilayhi rajiuun

Page 29: Al hikma vol 28

27

JAMII / MWANAMKE

Wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika huduma

mbali mbali za kijamii, kiutu na kimaadili. Ni watu wanaoguswa na mahangaiko ya jirani zao, kiasi cha kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya mafao ya wengi. Wanawake ni watu wa kwanza kujitolea na watunzaji wakuu wa zawadi ya maisha ambayo mwanadamu amekabidhiwa na Mwenyezi Mungu kuilinda na kuindeleza kama njia ya kushiriki katika mchakato wa kumwabudu Muumba na kuilea na kuitunza jamii katika miiko na utaratibu alioupanga Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mafanikio ya mwanadamu kimwili na kiroho.

Katika historia tunayo majina ya wanawake kadhaa ambao shakhasiya zao adhimu ni alama ya kudumu ya utu wa mwanamke, huduma zake na kujitolea kwake kwa ajili ya mafao ya jamii yake bali na hata jamii baki iliyo mbali na mazingira yake. Bi Asia binti Muzahim ni mmoja kati ya wanawake hao, huduma yake kuu katika kulingania ‘‘TAWHID’’ na ibada ya Mungu mmoja kwa lengo la kuikomboa jamii ya Wana wa Izrail ni alama ya kudumu ya kujitolea katika maendeleo ya jamii kiroho na kimwili. Aliishi

Mwanamke ni Muhimili wa Maendeleo katika jamii kiroho na kimwili

Bi Mariam naye alijenga mnara wa kiroho ulio madhubuti ambao kamwe kimbunga cha historia hakiwezi kuubomoa, alisifika kwa utawa wake ambao ni kielelezo tosha cha utu wake binafsi na utu wa familia yake na jamii nzima,

27

Na: Saadiyyah Said.

Page 30: Al hikma vol 28

28

JAMII / MWANAMKE

2828

ubavuni mwa katili na kiumbe muovu zaidi katika zama zake, lakini hilo halikumzuia kuitangaza haki na kuiokoa na kuitetea jamii ya wanyonge, hadi Mwenyezi Mungu akatambua huduma yake na kuithamini, akasema: “Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.” (Sura Tahrim: 11).

Bi Mariam naye alijenga mnara wa kiroho ulio madhubuti ambao kamwe kimbunga cha historia hakiwezi kuubomoa, alisifika kwa utawa wake ambao ni kielelezo tosha cha utu wake binafsi na utu wa familia yake na jamii nzima, na hata alipotokewa na Malaika Jibril (as) kwa lengo la mwendelezo wa huduma ya utume katika jamii yake alijitambulisha kwa kutaja utu wake ambao ni sifa muhimu katika jamii yenye utu. Akasema: Nitampataje

mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? (Mariam: 20). Na hata aliposhika ujauzito jamii ilijitambulisha mbele yake kwa kusema: Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. (Mariam: 28).

Ni kwa maadili haya aliinua na aliistawisha jamii yake katika njia ya kutaka radhi za Muumba wake. Utu wake ukatukuka na heshima yake ikawa na mfano wa kuigwa na kufuatwa, huduma yake katika kuhudumia ‘‘TAWHID’’ katika jamii ili kujenga jamii yenye utu na mafungamano na Muumba ilikuwa ndio tamaa yake ya kwanza na shauku yake kuu.

Na kwa mantiki hii utiifu wake kwa Muumba ulijenga shakhsiya na muhimili ndani ya jamii ya wanatauhidi, Mwenyezi Mungu anasema: “Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho

yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu.” (Sura Tahrim: 11). Naye Bi Khadija akaandika historia katika huduma ya kiroho kwa kuwa mwanamke aliyejitolea kwa hali na mali kuulinda Uislamu na kuuteta, tunu kubwa ya kumpokea Mtume (saww) na kumlewaza wakati wote wa misukosuko lazima iheshimiwe na ithaminiwe.

Ni wakati huo ambao mchango wa mwanamke katika jamii ile ulikuwa mkubwa na wa maana sana kuliko wa wanaume wengi, na kwa kujitolea kwake Uislamu ukastawi na nuru yake kusambaa. Maneno ya pongezi kutoka kwa Mtume (saww) juu ya Khadija ni kumbukumbu ya milele na medali ya kudumu ambayo daima itaendelea kumtambulisha katika jamii ya wanadamu hasa wanyonge ambao yeye aliweza kutumia mali yake katika njia ya kuihudumia. Mtume (saww) anasema: “Hakika

Page 31: Al hikma vol 28

29

Tunashuhudia adhamu na utukufu wa Uislamu katika sura ya wanawake wanamapinduzi wa Iran ambao wanatafuta elimu na maarifa sambamba na kulinda vazi la hijabu, utakasifu, kutunza nyumba na kulea watoto. Hii leo jamii ya Wairan ina madaktari wengi hodari wa kike, wanawake waliohitimu masomo katika fani mbalimbali za elimu na wanavyuo wa kike wenye juhudi kubwa na vipawa ambao ni fahari ya Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

JAMII / MWANAMKE

2929

Mwenyezi Mungu hajanipa mke bora kushinda Khadija.” Kwakweli amali na matendo ya mwanadamu yana taathira kubwa katika kupata sifa njema na thamani aali, na kwa sababu hiyo kiwango kikubwa cha elimu na maarifa ya Bibi Fatima Zahra (as) katika kipindi cha ujana wake kilifungamana kwa kiwango kikubwa na juhudi za kimatendo za mtukufu huyo.

Binti huyo mtukufu wa Mtume (saw) alikuwa pozo la huzuni za baba yake, mke mwenye kujitolea kwa mumuwe na mlezi mkubwa kwa watoto wake. Alilea watu adhimu kama Imam Hasan, Imam Husain na Bibi Zainab (as). Aliimarisha imani

na kujenga nafsi yake kwa kufanya ibada na akafungua njia ya maarifa na nuru ya Mwenyezi Mungu katika moyo wake. Alijiepusha na utajiri na anasa za dunia.

Alikuwa mfano mwanajihadi wa kuigwa katika kumtetea Mtume na Uimamu na kumhudumia mumewe ambaye alikuwa shujaa mkubwa zaidi wa Uislamu. Uthubutu wa Bi Zainab (as) na ujasiri wake mbele ya dikteta wa Kibani Umaiyyah Yazid maluuni ni hatua nyingine ya lazima iliyochukuliwa na Wanawake katika jamii ya wanadamu. Ni ukombozi utokanao na silaha ya mwanamke na ni alama ya utu wake katika

jamii. Muhimili huu adhimu na imara ulikataa dhulma na ufisadi na ukaacha ujumbe kwa walimwengu hasa kwa wanawake kuwa utu wao una nafasi muhimu katika kukemea maovu na ufisadi ulimwenguni, hata kama dikteta wa zama zako atakuwa ni Rais wa Marekani au dola za Magharibi au ni Mazayuni.

Ni katika mantiki hii mwanamke ataendelea kuwa muhimili wa jamii katika ustawi wa maisha ya mtu kimwili na kiroho. Mwanamke wa Kiislamu anapaswa kufanya juhudi kubwa katika njia ya kutafuta elimu na kujenga nafsi kiroho na kimaadili. Anapaswa kupuuza anasa na kujiweka mbali ya macho ya wageni

kwa kulinda usafi wa roho na utakasifu wake. Katika mazingira ya nyumba, anapaswa kuwa pozo la roho ya mume na wanawe na sababu ya maisha ya utulivu ndani ya familia.

Anapaswa kulea wanadamu safi, watanashati na wasiokuwa na matatizo ya kinafsi. Dhamana hii inapaswa kutekelezwa kwa umakini mkubwa, kwa kuwasaidia wengine kutambua kwamba, wanathaminiwa na kupendwa na Mwenyezi Mungu katika safari ya maisha yao hapa duniani. Licha ya kushughulikia mahitaji ya mwili, katika maboresho ya afya na huduma za uzazi, lakini

wanawake ni walimu wa kwanza wa imani, maadili na utu wema kwa watoto na jirani zao.

Watu wanaodai kutetea haki za mwanamke na haki za binadamu katika ulimwengu wa kijahili, ulioghafilika na kupotea wa ustaarabu wa Magharibi, kwa hakika ndio madhalimu wa haki za mwanamke, kwa sababu wamemfanya kiumbe huyo kuwa wenzo wa kujiburudishia na kukidhia matamanio ya wanaume asherati kwa kutumia kaulimbiu ya uhuru wa mwanamke. Kwa itikadi yetu, dhulma iliyofanywa dhidi ya mwanamke katika utamaduni ulioporomoka wa Magharibi na ufahamu usiokuwa

sahihi kuhusu mwanamke katika turathi za kiutamaduni na fasihi ya Magharibi, haina mfano katika vipindi vyote vya historia.

Dhulma kubwa dhidi ya mwanamke hususan katika kipindi cha hivi karibuni imetokana na ustaarabu wa Magharibi na tunaamini kwamba, kile kinachoitwa uhuru wa mwanamke huko Magharibi hii leo si uhuru wa mwanamke, bali kwa hakika unapaswa kuitwa uhuru wa wanaume wakware kwa ajili ya kuwatumia wanawake. Wamagharibi wamemdhulumu mwanamke si katika medani ya kazi na shughuli za viwanda

Page 32: Al hikma vol 28

30

pekee bali hata katika nyanja za sanaa na fasihi. Mtazamo wao kwa mwanamke katika athari za sanaa, visa, filamu na uchoraji wao unaakisi ukweli huu. Wamagharibi wanamuona mwanamke kuwa ni kiumbe cha kutumia tu, chenye mkono na moyo wa wazi na kibarua wa bei duni. Uislamu umeafiki suala la mwanamke kufanya kazi. Si hayo tu, bali umemuwajibisha kufanya kazi kama kazi hiyo haipingani na wadhifa wake wa kimsingi na muhimu wa kulea watoto na kulinda familia.

Hata hivyo kazi ya mwanamke haipaswi kupingana na utukufu na thamani zake za kiroho na kibinadamu. Wakati dunia inaendelea kushuhudia wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, waathirika wa biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo, wakati ubepari ukiendelea kuwaingiza vijana katika

biashara ya binadamu na ukahaba bila kusahau matumizi haramu ya dawa za kulevya. Ni wakati wa Wanawake kuendelea kujisikia kwamba, wana changamoto kubwa na wajibu mkubwa wa kuendelea kutoa huduma bora ya ulinzi wa zawadi ya maisha; kwa kuwasaidia jirani zao katika shida na mahangaiko yao ya ndani kama kielelezo cha kujitolea kwao, kama walivyofanya hapo kabla kupitia Mabibi watukufu.

Ni sehemu ya dhamana yao kama muhimili wa jamii kimwili na kiroho kuwalea na kuwahudumia watoto waliotelekezwa na wazazi wao kwa kuelemewa na ubinafsi na matatizo mengine ya kijamii na kiuchumi. Bila shaka Wanawake wakiendelea kujisikia na kuguswa kwa namna ya pekee na udororaji wa huduma za kijami hasa zinazowagusa jirani zao, bila shaka mawazo yao na mchango wao utawakumbusha

wanaume wajibu wao na kuondoa ulegevu wao. Wakati mwanamke wa Kiislamu anaporejea kwenye fitra na maumbile yake halisi, hujitokeza muujiza mkubwa wa uwezo adhimu wa mwanamke wa Kiislamu kama ule tulioushuhudia baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Tunashuhudia adhamu na utukufu wa Uislamu katika sura ya wanawake wanamapinduzi wa Iran ambao wanatafuta elimu na maarifa sambamba na kulinda vazi la hijabu, utakasifu, kutunza nyumba na kulea watoto.

Hii leo jamii ya Wairan ina madaktari wengi hodari wa kike, wanawake waliohitimu masomo katika fani mbalimbali za elimu na wanavyuo wa kike wenye juhudi kubwa na vipawa ambao ni fahari ya Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wassalaam alaykum.

Mahitaji

Mchele kilo 1Samaki kilo 1Vitunguu kilo 1Samli ¾ kiloThomu kiasiMdalasini kiasiHiliki kiasiNdimu kiasiNyanya kiasiChumvi kiasi

1 Mkate kate samaki umtie chumvi na ndimu umkaange. Menya vitunguu uvikate. Saga nyanya, thomu na viungo vyote vilivyobakia.

(Bakisha mdalasini nzima kidogo).2. Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange, vikianza kupiga wekundu tia nyanya na viungo kidogo. Acha vikaangike kwa muda mdogo halafu tia vipande vya samaki, chumvi na ndimu, pamoja na maji kidogo. Acha ichemke kwa muda mdogo. Likibaki rojorojo epua.

3. Chukua sufuria nyingine uitie maji na chumvi. Yakichemka osha mchele utie. Acha utokote. Angalia kiini cha wali, ukiona umeshaiva umimine uyachuje maji yote. Teleka tena sufuria utie samli kidogo, ikichemka

tia vitunguu kidogo pamoja na vile vilivyobakia.

Vyote vikaange kidogo halafu umimine wali wote ukoroge koroge ili upate kuchanganyika na viungo. Halafu uweke vizuri upalie moto.

Ukishakauka utaupakua. Kuupakua kwake kwanza utatia wali kwenye sahani, baadae ndio utatia samaki pamoja na rojo rojo lake lote kwa juu.

Asante na kwaherini mpaka toleo lijalo panapo majaliwa msikose makala nzuri za mapishi.

BIRIANI YA SAMAKI Na: Fatma Othmani

Mapishi

30

JAMII / MWANAMKE

Page 33: Al hikma vol 28

31

MASHAIRI

Nakuomba Maulana, Madhumuni rahisisha.Lengo ni kukumbushana, Sio kuleta rabsha.Niandike ya maana, Wakati ninakumbusha.Jina lake Muhammadi, Mbora wa manabii. Mazuri yanayofaa, Yote ametufundisha.Yamejaa manufaa, Yale alotuonesha.Kamulika kama taa, Kona zote za maisha.Jina lake Ahmadi, Wa mwisho wa manabii. Hakuna lilopungua, Mtume kakamilisha.Ametimiza sheria, Kidigi hakubakisha.Kila kitu katatua, Kabla Mola kumfisha.Jina lake Mahmudi, Mbora wa manabii. Bila chembe ya hiana, Ujumbe amefikisha.Alivyotunza amana, Kwetu sisi somo tosha.Amana kubwa dhamana, Kuihini inatisha.Jina lake Mujtaba', Wa mwisho wa manabii. Kwa kumpenda moyoni, Na sunnaze kuhuisha.Tunataraji auni, Shafaa' namaanisha. Siku hiyo ya huzuni, Tukikwama kutuvusha.Jina lake Murtadha', Mbora wa manabii.

Furaha kubwa hakika, Umejaa moyo wangu.Kwa kweli naburudika, Shahidi Mwenyezi Mungu.Kwa bashasha naandika, Mufurahi na wenzangu.Alizaliwa mtume, Rehema kwa ulimwengu. Habeebu Mtume wetu, Pokea zetu salamu.Katika kalenda yetu, Leo ni siku adhimu.Kuzaliwa kwako kwetu, Sherehe jambo muhimu.Alizaliwa mtume, Kipenzi cha moyo wangu. Alizaliwa mbora, Na leo tunamuenzi.Kipenzi chake Ghafura, Sio jana tangu enzi.Ni kubwa hii bishara, Astahiki mapenzi.Alizaliwa mtume, Rehema kwa ulimwengu. Ni haki kufurahiya, Siku uliyozaliwa.Kwenye nuru 'metutiya, Gizani umetutoa.'Mefuta ujahiliya, Rasuli 'metuongoa.Alizaliwa mtume, Kipenzi cha moyo wangu. Wasiojua wajue, Wazi tunawaambia.Tukitaka tutatue, Matatizo ya dunia.Qur'ani na Sunnaye, Tuelewe ndio njia.Alizaliwa mtume, Rehema kwa ulimwengu.

JINA LAKE MUHAMMAD S.A.W.W..... ALIZALIWA S.A.W.W.....

Al-Akh.Alhaaj Osan Omari Ngulangwa.

(LILENGANE).(DIWANI YA ALHAAJ OSAN).

Nyaminywili, Rufiji.19 Rabi -Ul- Awwal 1435/ 21 Januari 2014

Na: Fatma Othmani

Page 34: Al hikma vol 28

32

Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi bila ya kutegemea kiegemeo cha

dhahiri. Ardhi na milima vimeishikilia mbingu na kuifanya kuwa imara na madhubuti. Mwezi na jua viko kwa ajili ya kuimulikia ardhi. Nyota nazo zinaipamba mbingu na kuipendezesha. Na katika kila kona ya ulimwengu zipo ishara za wazi zilizozagaa za kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Miongoni mwa hizi, ni hivi kufanywa jua na mwezi na nyota kunyenyekea kwa faida ya binaadamu. Na kadhalika kupishana zamu usiku na mchana, na kuwa mchana unaingilia kiza cha mbingu. Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kwa maji na udongo, kisha akampulizia roho na kumtaka afanye hima na bidii pamoja na amali njema ili aweze kuwa khalifa na kiongozi Wake katika ardhi. Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya 29 ya Surat ar-Rahman:

"Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo." Hivyo basi kukaa bure, kutofanya kazi na kutokuwa na malengo ni mambo ambayo hayana nafasi katika ulimwengu huu na Uislamu unayapiga vita haya. Kila kilichomo katika ulimwengu huu, yaani viumbe wote, miti na mimea vinafanya kazi

zao kwa mipango na utaratibu maalumu. Viumbe vyote vinafanya harakati kwa nidhamu na mpango maalumu na makini kuelekea katika lengo maalumu. Kwa muktadha huo, mwanaadamu naye akiwa kiumbe bora kabisa wa Mwenyezi Mungu katika mgongo wa ardhi anapaswa kwenda sambamba na nidhamu na mipango hii. Kwa

Ulimwengu ni majimui yenye mpangilio na utaratibu maalumu. Kiuhakika ni kuwa, kila kitu katika ulimwengu huu, kinafanya kazi kwa mujibu wa mpango na utaratibu maalumu. Ulimwengu, vilivyomo pamoja na mpangilio maalumu wa mambo kama vile mawio na machweo ya jua ni mambo yananyoonyesha adhama, uwezo na qudra ya Muumba wa ulimwengu huu yaani Mwenyezi Mungu.

Na: Salum Bendera

Umuhimu wa Kazi Katika Uislamu -1

JAMII / KAZI

Page 35: Al hikma vol 28

33

Umuhimu wa Kazi Katika Uislamu -1

mtazamo huu, kazi, hima na kujituma ni mambo yanayohesabiwa kuwa sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu na wakati huo huo, kukaa bure na kubweteka kunahesabiwa kuwa ni kuachwa nyuma na kafila pamoja na msafara wa maisha na ulimwengu. Maendeleo, ustawi pamoja na mabadiliko ya daima ni uhakika na ukweli ambao haukanushiki na kimsingi ni muhimu katika maisha ya mwanaadamu. Katika jamii ya mwanaadamu wa leo yenye maendeleo, nafasi ya kazi, kujituma na kujishughulisha na kazi ni mambo ambayo yanashuhudiwa katika kona zote za maisha ya watu.

Hata inawezekana kusema kuwa, kazi ni jambo ambalo lina taathira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja katika hali ya kiroho, kifikra na thamani za mwanaadamu. Ili mwanaadamu aweze kuendelea na maisha na hata aweze kuboresha maisha yake sambamba na kukidhi mahitaji yake ya kila siku ya kimaisha anahitajia kufanya kazi na kujituma katika kutafuta maisha. Hakuna matumaini na ndoto alizonazo mwanaadamu ambazo zinaweza kufikiwa pasina ya kuweko hima, idili na juhudi mtawalia katika maisha.

Kila mtu au taifa ambalo linataka kufikia katika vilele vya maendeleo na mafanikio na hivyo kuvuka vizingiti na vikwazo vyote vilivyoko katika njia hiyo na kuyafikia mafanikio, ni lazima lijiepusha na uvivu na kutaka kupata mambo bure bure na kirahisi rahisi . Kuna wanaadamu wengi ambao hutaka kufikia malengo fulani lakini wakati huo huo, hawako tayari kujishughulisha au kufanya bidii kwa ajili ya kulifikia lengo alilokusudia.

Tamaduni na staarabu nyingi na adhimu za mwanaadamu ziliweza kung'ara na kutakata kutokana na juhudi zisizochoka zilizofanywa na watu katika kipindi chote cha historia; watu ambao walikuwa na vipaji na kwa msingi huo wakajitokeza na kuwa na nafasi muhimu katika ulimwengu huu. Kujengwa majengo makubwa na ya kudumu kama majumba ya kihistoria ya Takhte Jamshid nchini Iran, mapiramidi makubwa ya Misri na ukuta mrefu wa China ni vitu ambavyo vilipatikana kutokana na hima na juhudi kubwa ya mwanaadamu tena katika kipindi

ambacho, mwanadamu alikuwa hajapiga hatua kubwa kama leo katika uga wa sayansi na teknolojia. Ni dhahir shahir kwamba, maendeleo makubwa yaliyofikiwa na mwanadamu wa leo kama ya kutuma satalaiti katika anga za mbali, kutibu magonjwa sugu, kujenga barabara na njia za chini kwa chini na maendeleo makubwa katika uga wa teknolojia ya mawasiliano na vyombo vya usafiri kama ndege na kadhalika, ni mambo ambayo yamefikiwa kutokana na fikra, hima, bidii na kujituma mwanaadamu.

Kwa baraka za kazi na kufanya hima, mti wa maisha ya mwanaadamu umeneemeka kwa matunda ya furaha na uchangamfu na kuwa mbali na hali ya udhaifu na msononeko. Endapo harakati ya kazi katika maisha ya mwanaadamu itasimama, mwenendo wa kudorora nao utaanza. Will Durant mwandishi wa Kimagharibi wa kitabu cha Historia ya Ustaarabu anasema kuwa: "Afya na uzima vipo katika kufanya kazi. Kufanya kazi ni moja ya mambo ya nembo za furaha ya mwanaadamu katika maisha. Kwa mtazamo wangu, ni bora tumuombe Mwenyezi Mungu tawfiki ya kufanya kazi badala ya kuomba mali na utajiri."

Kuwa na hima na kufanya, udharura na umuhimu wake ni kama vile maji na chakula katika maisha ya mwanaadamu. Kimsingi, dhati ya mwanaadamu huelekea katika hima na kufanya kazi. Hata hivyo swali la kimsingi na la kujiuliza ni kuwa, mwanaadamu anafanya kazi kwa ajili ya lengo gani? Je mwanaadamu

anafanya kazi kwa ajili ya kukidhi mahitaji na hawaiji zake za kimaada na kwa ajili ya kuboresha maisha yake? Je mwanaadamu anakula na kunywa ili apate nguvu ya kufanya kazi? Au anafanya kazi ili aweze kula vizuri na kuwa na maisha mazuri na bora? Ukweli wa mambo ni kuwa, kazi na kufanya hima katika jamii

Nukta ya kuzingatia kuhusiana na mafundisho ya Uislamu ni kuwa, dini hii ya Mwenyezi Mungu imekokoteza na kuusia mno juu ya kufanya kufanya kazi na kuwa na hima sambamba na kuwa na taqwa na uchaji Mungu. Kwa maana kwamba, wakati mtu anapofanya kazi ya kutafuta riziki yake halali anapaswa kutomsahau Mwenyezi Mungu na kutoacha kushikamana na taqwa na uchaji Mungu.

JAMII / KAZI

Page 36: Al hikma vol 28

34

yoyote ile na katika mtazamo wa dini na maktaba na pote lolote lile la kifikra ina maana na nafasi maalumu. Baadhi ya mitazamo ya upande mmoja inaona kuwa, kufanya hima na kujitahidi ni mambo ambayo yanaishia tu katika kukidhi mahitaji ya kidunia na maisha ya kimaada ya mwanaadamu na baadhi ya maktaba zingine za kifikra zina mitazamo tofauti.

Kazi ni taklifu na jukumu ambalo mfumo wa ulimwengu umeliweka katika mabega na dhima ya mwanadamu ili mja huyu aweze kudhamini mahitaji yake ya kimaisha kupitia hima na idili yake. Hima na jitihada na harakati za maisha zilianza tangu mwanzo tu wakati Nabii Adam AS alipoumbwa na Mwenyezi Mungu na kuwekwa katika mgongo wa ardhi.

Hata hivyo suala hilo halihusiani na mwanadamu tu bali viumbe wote wamo katika hali ya harakati ha hima ili waweze kudhamini chakula na mahitaji yao kimaumbile na hivyo kuweza kubakia hai. Hata mnyama wa porini hana budi kutembea huku na huko msituni ili kutafuta nyasi au kitoweo. Kama tulivyosema, hima na kufanya kazi katika mtazamo wa Uislamu ni jambo ambalo lina nafasi maalumu.

Hii inatokana na kuwa, jambo hili lina sudi na faida nyingi za kimaada na kimaanawi kwa mwanadamu. Kupitia aya za Qur'ani Tukufu na mafundisho ya dini inapatikana natija hii kwamba, mwanadamu anapaswa kupiga hatua katika njia ya ustawi na kukwea kimaada na kimaanawi katika kivuli cha akili, tadbiri, mipango, hima na idili. Kufanya kazi na kuwa na hima na juhudi kwa ajili ya kutafuta riziki ya

halali mbali na kufukuza uvivu na hali ya kukata tamaa katika ujudi wa mtu, hatua hiyo huleta nishati na uchagamfu. Kazi ni wenzo bora kabisa kwa ajili ya kuishughulisha kwa salama fikra na mwili wa mwanadamu.

Wataalamu wa mambo wanaamini kwamba, chimbuko kuu la ushindi ni hima na juhudi za wanadamu na watu ambao wanafanya hima na juhudi zaidi huwa ni wenye saada na mafanikio zaidi na wale ambao wana uvivu na ambao hawafanyi hima hukosa mafanikio na hivyo kutofikia saada na ufanisi. Ndio maana wahenga wakasema, uvivu ni adui mkubwa wa maendeleo.

Akili inahukumu kwamba, ili mwanadamu ajikomboe na kuondokana na umasikini anahitajia kufanya kazi na hivyo kuweza kudhamini hawaiji na mahitaji yake ya maisha kwa njia ya izza na heshima; badala ya kujidhalilisha na kujidunisha kwa kuwa ombaomba mbele za watu.

Nukta ya kuzingatia kuhusiana na mafundisho ya Uislamu ni kuwa, dini hii ya Mwenyezi Mungu imekokoteza na kuusia mno juu ya kufanya kufanya kazi na kuwa na hima sambamba na kuwa na taqwa na uchaji Mungu.

Kwa maana kwamba, wakati mtu anapofanya kazi ya kutafuta riziki yake halali anapaswa kutomsahau Mwenyezi Mungu na kutoacha kushikamana na taqwa na uchaji Mungu. Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya 37 ya Surat Nur kwamba: Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka.

Katika aya hii Allah anataka kuonyesha kuwa, watu ambao ni wa Mwenyezi Mungu yaani watu ambao wameshikamana na taqwa na uchaji Mungu, kujihusisha kwao na biashara na kazi za kutafuta riziki kwa ajili ya kudhamini mahitaji yao ya maisha huwa hakuwashughulishi kiasi cha kuwafanya waghafilike na suala la kumtaja na kumdhukuru Mwenyezi Mungu.

Kwa maneno mengine ni kuwa, watu hao humfanya Mwenyezi Mungu kuwa mhimili mkuu katika maisha yao ambapo juhudi za kimaada na kiuchumi hazipaswi kumfanya mtu amsahau Mwenyezi Mungu bali anapaswa kumtanguliza Allah katika kazi zake hizo.

Kwa muktadha huo kazi ya kiuchumi na hima ya kutafuta riziki inapaswa kuathiriwa na kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kuchunga taqwa. Kwa maana kwamba, mtu anapokuwa katika pirika pirika za kutafuta riziki hapaswi kumuasi Mwenyezi Mungu.

Kama anga ya kiuchumi inayotawala katika jamii itakuwa ni kujiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, kufanya mambo kwa usahihi na ushirikiano, bila shaka jamii kama hiyo itakuwa na mahusiano salama baina ya wanajamii. Kwa upande mwingine, wakati wanadamu wanapomuogopa Mwenyezi Mungu na kuchunga taqwa, hujiepusha na kazi za haramu na zile ambazo haziko katika ridhaa ya Mwenyezi Mungu. Hatua hiyo hupelekea kushuka zaidi rehema na baraka za Mwenyezi Mungu. Allah anasema katika aya za 2 na 3 za Surat Talaq;"...Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyotazamia...."

34

JAMII / KAZI

Page 37: Al hikma vol 28

35

JAMII / KAZI

Page 38: Al hikma vol 28

36

JAMII / KAZI

Page 39: Al hikma vol 28
Page 40: Al hikma vol 28