kuongeza msamiati wa kiswahili · lugha ya kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa...
Post on 13-Feb-2020
575 Views
Preview:
TRANSCRIPT
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1
MADA YA 1
KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI
Uundaji wa Maneno
Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo
kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili
msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.
Njia za Uundaji Maneno
Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:
1. Kubadili mpangilio wa herufi.
2. Kuambatanisha maneno.
3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine.
4. Uambishaji wa maneno.
5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura.
Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi
Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza
kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine
Mfano
Neno lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama
mali, kumi,imla, mila.
Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:-
tatu, tua, viatu, tatua.
Njia ya kuambatanisha maneno
Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno
Njia ya kurudufisha au kukariri neno
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2
Mfano; barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.
Njia ya uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti
Nomino na Nomino
Punda + mlia unapata Pundamilia
Bibi + Shamba unapata Bibishamba
Afisa + Elimu unapata Afisaelimu
Mwana + Siasa unapata Mwanasiasa
Bata + maji unapata Batamaji
Kuunganisha kitenzi na Nomino/Jina
Changa + moto changamoto
Chemsha + bongo chemshabongo
Piga + mbizi pigambizi
Zima + moto zimamoto
Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi
Mfano
Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA
Mzaliwa wa mahali Fulani MZAWA
Chama cha Mapinduzi CCM
Nyamamfu NYAMAFU
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3
Kutohoa maneno kutoka lugha nyingine
Kila lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya
Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa
kimatamshiili ya fuate kanuniza Kiswahili.
Maneno yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya
Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.
Mfano
Neno la Kiswahili Lugha ya Mwanzo Neno Lililotoholewa
Kijerumani Schule
Salama Kiarabu Salaam
Duka Kihindi Dukan
Karoti Kiingereza Carrot
Shati Kiingereza Shirt
Picha Kiingereza Picture
Papai Kihispania Papaya
Meza Kireno Mezi
Shukrani Kiarabu Shukran
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4
Ngeli Kihaya Engeli
Ikulu Kinyamwezi Ikulu
Ng'atuka Kizanaki Ng'atuka
Ndafu Kichaga Ndafu
Namba
Kuunda maneno kwa njia ya uambishaji wa maneno
Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa
maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina
husiana.
Mfano mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama
lima, analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.
Kufananisha sauti, sura au tabia
Mfano
Kengele - utokana na sauti ya kengele inapo pigwa
Pikipiki - hutokana na muungurumo wa pikipiki
Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama
tembo
Chubwi - Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.
ZOEZI
Maana ya pili ya neno komba ni mtu mlevi sana iliyopatikana kwa kuhamisha
maana ya neno, maana yake halisi ni___.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5
A Aina ya ndege
B Aina ya mdudu
C Aina ya mnyama
D Aina ya samaki
Bainisha njia ya uundaji wa maneno iliyotumika kuunda neno \"MKURABITA\":
A Njia ya urudifishaji
B Njia ya uhulutishaji
C Njia ya kuangalia kazi ya kitu
D Njia ya kufupisha maneno
___ ni mfano wa neno lililoundwa kutokana na kufananisha sauti.
A BAKITA
B Kengele
C Shule
D Analima
___siyo neno lililoundwa kwa kufananisha sauti, sura au tabia.
A Beberu
B Kengele
C Kifaru
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6
D Mfuniko
___ ni mfano wa neno lililotoholewa kutoka katika lugha ya Kinyamwezi.
A Ikulu
B Ng‟atuka
C Ndafu
D Ngeli
Mazingira yanayoelezea Kuhitaji Maneno Mapya
Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha-
mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia. Katika mazingira kama
haya, watu watahitaji kuwasiliana, lugha itahitaji kuunda maneno ili kuwasilisha
dhana mpya zilizoibuka. Kwa mfano, maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi,
puku, talakirishi n.k yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknoljia kwa
Kiswahili.
ZOEZI
Faida za kuongeza msamiati ni pamoja na hizi zifuatazo isipokuwa___.
A kuwasiliana bila tatizo
B taaluma kujitosheleza kimsamiati
C kujitosheleza kimawasiliano
D kuongeza watumiaji
Msamiati mpya unaundwa kwa lengo la___.
A Kusanifisha lugha
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7
B Kuimarisha lugha
C Kuwasilisha dhana mpya
D Kuongeza msamiati katika lugha
Mabadiliko ya ___yamesababisha uhitaji wa neno 'nywila'.
A Utamaduni
B Uchumi
C Siasa
D Sayansi na teknolojia
Uundwaji wa maneno kama vile plasta, vidonge na asprini yametokana na
mabadiliko katika fani ya___.
A Sheria
B Tiba
C Sanaa
D Uandishi
Mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na kiutawala yamesababisha kuundwa kwa
neno___.
A Sidii
B Kiotomotela
C Mafisadi
D Tarakilishi
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8
Undaji wa Maneno katika Miktadha mbalimbali
Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na
kutumiwa na jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno
hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali, kama vile sayansi na teknolojia,
siasa, utamaduni na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo. Mfano wa
msamiati ni kama vile fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali n.k
ZOEZI
Neno pembejeo linapatikana katika muktadha wa___.
A Sayansi na teknolojia
B Kijamii
C Kisiasa
D Kiuchumi
___ ni neno linalopatikana katika muktadha wa kisiasa ambalo hutambulisha cheo
cha kiongozi wa juu kabisa Tanzania.
A Luteni
B Mfalme
C Rais
D Kanali
Maneno yafuatayo yameundwa kutokana na maendeleo katika muktadha ya
kiutamaduni, isipokuwa:
A Suruali
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9
B Uma
C Dansi
D Walalahoi
___ni mfano wa neno lililotoholewa kutoka katika lugha ya Kihindi.
A shule
B bajia
C beseni
D hisani
Ifuatayo ni mifano ya maneno yaliyoundwa katika muktadha wa sayansi na
teknolojia sipokuwa___.
A bunduki, nyukilia
B umeme, bunduki
C zahanati, asprini
D kikokotozi, redio
MADA YA 2
UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI ENZI YA WAINGEREZA NA
BAADA YA UHURU
Ukuaji na ueneaji wa Kiswahili katika enzi ya Waingereza
Mambo waliyochangia Waingereza katika Ukuaji wa Kiswahili nchini Tanzania
Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta
Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Kwa kuwa
nao walihitaji kutawala hawakupuuzia matumizi ya Kiswahili katika utawala wao
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10
japo hawakutumia Kiswahili kwa lengo la kukikuza lakini walijikuta wanakieneza
na kukikuza bila ya wao kukusudia.
Waingereza walitumia Kiswahili kama nyenzo ya kusaidia shughuli zao za
kiutawala. Hata hivyo kuna mambo waliyofanya waingereza yaliyosaidia kukua na
kuenea kwa Kiswahili, mambo hayo ni kama yafuatayo:
Shuguli za kiuchumi
Shuguli za kiuchumi wakati wa Waingereza zilihusisha kilimo na biashara. Kwa
upande wa klimo, Waingereza waliendesha kilimo cha mazao mbalimbali, na
walitumia mfumo wa kuajiri vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Vibarua
hao walijulikana kwa jina la manamba.
Katika mkusanyiko wa vibarua hawa waliokuwa na usuli wa makabila
tofautitofauti, lugha pekee iliyoweza kuwaunganisha ni Kiswahili ikizingatiwa
kwamba Kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha rasimi katika mawasiliano ya kiutawala.
Walilazimika kuzungumza Kiswahili kwani bila hivyo mawasiliano yasingeweza
kufanyika kwa urahisi.
Hata hivyo kupitia shuguli za kilimo maneno mapya ya Kiswahili yaliweza
kuzaliwa, kwa mfano: yadi, belo, belingi, bani, mtama n.k, kwa hiyo kupitia
shughuli hizi Kiswahili kilizidi kukua.
Shuguli za kiutamaduni
Shughuli hizi ni kama vile uigizaji wa tamthiliya za kigeni, uchezaji wa mziki wa
kigeni hususani twisti. Tamthiliya za kigeni zilikuwa zikiigizwa majukwaani kwa
lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili.
Shughuli za kidini
Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio wa wamishonari
waliokuwa na lengo la kueneza dini ya kikristo.
Katika harakati hizi walitumia lugha ya Kiswahili ili kufanikisha malengo yao
ikizingatiwa kwamba Kiswahili kilikuwa kimeshaenea vya kutosha wakati wa
utawala wa Mjerumani, kwa hiyo wamishonari wa Kiingereza waliendelea
kukiimarisha zaidi.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11
Pia shughuli za kidini zilipelekea kutafsiriwa kwa vitabu mbalimbali vya kidini
kama vile Biblia na vitabu vingine. Tafsiri ya vitabu hivi ilikuwa ni kutoka katika
lugha ya kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili. kwa kufanya hivi Kiswahili
kiliweza kuingiza msamiati mwingi sana na hivyo kukuza lugha ya Kiswahili.
Wamishonari walilazimika kujifunza Kiswahili hukohuko kwao ili wanapokuja
huku Afrika Mashariki wasipate tabu ya kujifunza Kiswahili. Kwa sababu hii
wamishonari waliokuwa wamekwishajifunza lugha ya Kiswahili walitunga kamusi
za Kiswahili – Kiingereza ili kuwasaidia wenzao pia kujifunza Kiswahili; kwa njia
hii waliweza kukikuza Kiswahili.
Shughuli za kisiasa
Shughuli za kisiasa hasa katika uanzishwaji wa vyombo mbalimbali vya kiutawala,
jeshi, polisi, mahakama, boma n.k. Kufuatia uanzishwaji wa vyombo hivi msamiati
mwingi wa Kiswahili uliweza kuzuka na hivyo kukuza Kiswahili.
Shughuli za kiutawala
Makampuni ya uchapishaji yalianzishwa (East African literature Bureau), na
kamati ya lugha iliundwa (Interterritorian language committee). Hatua hii
iliimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili hali iliyosaidia kukua kwa lugha ya
Kiswahili.
Shuguli za ujenzi wa reli na barabara
Shughuli hizi pia zilisaidia kuibuka kwa msamiati mpya kama vile, reli, stesheni,
tiketi n.k.
Usanifishaji wa Kiswahili
Usanifishaji wa lugha ya Kiswahili pia lilikua ni jambo jingine muhimu sana
lililosaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Lengo la usanifishaji wa Kiswahili
lilikuwa ni kuleta ulinganifu wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda wa
Afrika Mashariki.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12
UENEAJI WA KISWAHILI
Ukuaji na Ueneaji ni maneno mawili yenye maana zinazokaribiana lakini
zinazotofautiana. Ukuaji humaanisha ongezeko la msamiati katika lugha na ueneaji
ni uongezekaji wa matumizi ya lugha kieneo. Kwa hiyo hapa tutaangalia yale
mambo yaliyosababisha Kiswahili kitumike katika eneo kubwa. Mambo hayo ni
haya yafuatayo:
Vyombo vya habari
Vyombo vya habari vilivyokuwepo kwa wakati huo ni redio, magazeti na majarida
mbalimbali. Kwa upande wa redio kulikuwepo na redio Tanganyika iliyoanza
kurusha matangazo yake kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Na magazeti
yaliyokuwa yakichapishwa wakati huo ni pamoja na: Mambo leo, Sauti ya Pwani,
Kiongozi na Habari za leo. Magazeti haya yote yalikuwa yakichapishwa kwa lugha
ya Kiswahili. Kwa hiyo kwa kutumia vyombo vya habari (redio na magazeti)
kiswahili kiliweza kuenea.
Kilimo
Kupitia kilimo watu waliweza kukutana pamoja, watu wa makabila tofautitofauti.
Kwa hiyo katika kipindi chote walichokaa kwenye makambi ya mashambani
waliweza kujifunza Kiswahili na walipomaliza muda wao walirudi nyumbani
wakiwa wamejifunza lugha mpya na hivo kwa njia hii waliweza kuieneza lugha ya
Kiswahili.
Muundo wa jeshi la kikoloni (KAR)
Jeshi la KAR liliundwa na watu kutoka makabila mablimbali, na lugha iliyokuwa
ikitumika jeshini ni Kiswahili, askari hawa walisaidia kueneza lugha ya Kiswahili
ndani na nje ya nchi kwani kila walipokwenda walikuwa wakizungumza Kiswahili.
Mfumo wa elimu
Chini ya utawala wa Waingereza Kiswahili kilitumika katika masomo yote kwa
ngazi ya shule ya msingi, na pia kilitumika kama somo kwa ngazi ya shule za
sekondari. Kwa hiyo hii pia ilichangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili
Harakati za kudai uhuru
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13
Chama cha TANU kilianzisha harakati za kudai uhuru, harakati hizo ziliendeshwa
kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kupitia harakati hizo Kiswahili kiliweza kuenea
kwa kiwango kikubwa.
Tathimini ya maendeleo ya Kiswahili wakati wa Waingereza
Licha ya maendeleo ya lugha ya Kiswahili katika utawala wa Waingereza, pia
kulikuwa na changamoto zilizoikabili lugha ya Kiswahili katika kupiga hatua ya
maendeleo. Changamoto hizo ni kama zifuatazo:
Kutofundishwa kwa Kiswahili shule zote nchini
Wakati wa utawala wa Waingereza Kiswahili kilifundishwa katika shule za watoto
wa kiafrika tu, wakati katika shule za watoto wa kizungu Kiswahili
hakikufundishwa. Kwa hiyo suala hili lilifanya Kiswahili kipewe msukumo mdogo
sana na hivyo kuhafifisha ukuaji wake.
Kutotumika kwa Kiswahili kama lugha ya kufundishia
Lugha ya Kiswahili ilitumika kufundishia katika shule za msingi pekee ilihali
lugha ya kiingereza ilitumika kuanzia shule za sekondari hadi elimu ya juu. Hali
hii ilisababisha watu kujitahidi sana kujifunza kiingereza; kwa kuzungumza
kiingereza ilikuwa na ishara kwamba wewe ni msomi, na hivyo kutokana na hali
hii Kiswahili kilendelea kukua polepole sana.
Kukosekana kwa vyombo vya kizalendo vya kukuza Kiswahili
Vyombo vilivyokuwa vinahusika na masuala ya ukuzaji wa Kiswahili wakati wa
ukoloni vilikuwa vimeanzishwa na wakoloni wenyewe, kwa mfano Kamati ya
Lugha ya Afrika Mashariki (Inter-Territorial Swahili Language commitee) na
Shirika la maandiko la Afrika Mashariki (East African Literature Bureau). Katika
hali kama hii ukuzaji wa Kiswahili ulikosa msukumo mkubwa wa kizalendo.
Kasumba ya kuthamini Kiingereza
Wananchi walikuwa na kasumba kwamba mtu anayezungumza Kiingereza
alichukuliwa kuwa ni mtu mwenye maendeleo na msomi, kwa hiyo hali hii
ikapelekea watu kutothamini Kiswahili na hivyo Kiswahili kudharaulika.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14
ZOEZI
Maneno kama vile tiketi, titi, stesheni na treni yaliongezwa katika Kiswahili
kipindi cha Waingereza kupitia shughuli ya___.
A Biashara
B Uchumi
C Ujenzi wa reli
D Usanifishaji
Lengo la Waingereza kukuza lugha ya Kiswahili lilikuwa ni nini?
A Kueneza dini
B Kutumia Kiswahili katika Shughuli zote
C Kurahisisha shuguli za utawala
D Kuelimisha watoto wao
Shughuli za ___ zilichangia ukuaji wa Kiswahili kipindi cha Waingereza kwa
kuongeza maneno kama vile yadi, belo na belingi.
A Kidini
B Kisiasa
C Kiuchumi
D Kiutawala
Maneno yaliyoongezeka kutokana na shughuli za kidini wakati wa Waingereza ni
pamoja na___.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15
A Belo
B Mkatukumeni
C twisti
D Rakaa
Kampuni ya uchapishaji wa vitabu (EALB) ilianzishwa mwaka gani?
A 1930
B 1947
C 1948
D 1849
Ukuaji na Ueneaji wa Kiswahili baada ya Uhuru
Shughuli mbalimbali zinazowezesha Kukua na Kuenea kwa Kiswahili nchini
Baada ya uhuru kuna harakati mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania
katika kukiendeleza na kukikuza kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na
kupendekezwa kuwa lugha rasmi 1962. Mkwaka 1964 kiswahili kilipendekezwa
kuwa lugha ya taifa na kuwa kitatumika katika shughuli zote za kiserikali na kitaifa
mfano katika elimu hususani elimu ya msingi.
Kuundwa kwa Chombo cha usanifishaji ambacho kilikuwa na kazi ya kuhimiza
maendeleo ya kiswahili, kutayarisha kamusi na vitabu mbalimbali vya sarufi na
fasihi ya lugha ya kiswahili na kuandaa wataalamu watakaoshughulikia
usanifishaji wa Kiswahili
Pia baada ya uhuru kulianzishwa Taasisi mbalimbali zitakazoshughulikia lugha ya
kiswahili. Mfano:- BAKITA, TUKI, TUMI, UKUTA, UWAVITA, Idara ya Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaamu.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16
Baada ya uhuru nchini Tanzania kiswahili kilienea kwa kasi kubwa sana. Kuna
sababu mbalimbali ambazo zilichangia kukua na kuenea kwa kiswahili hapa
nchini. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na kuteuliwa kwa kiswahili kuwa lugha
ya Taifa, Kiswahili kitumike katika Elimu, mfano kuwa lugha ya kufundishia
katika shule za msingi. Kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kukuza na kuneza
kiswahili, Kiswahili kuwa Lugha rasmi na lugha ya Taifa, shughuli mbalimbali za
kidini, shughuli za kisiasa na kiutawala na shughuli za kiutamaduni na uchapishaji
wa vitabu na majarida mbalimbali.
Kiswahili kuwa lugha ya taifa
Baada ya uhuru mwaka 1962 kamati iliundwa ili kuangalia uwezekano wa kutumia
kiswahili katika shughuli zote rasmi, mfano bungeni na shughuli zote za kiofisi.
Pia kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha ya taifa 1964 ambapo katika shughuli zote za
kitaifa zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili kilihimizwa
kutumika katika mawasiliano yote hasa katika shughuli za umma na Wizara zote,
Serikali na Bunge, kiswahili kiliendelea kupanda hadhi zaidi wakati wa Azimio la
Arusha la mwaka 1967 kwani azimio hilo lilitungwa na kuandikwa kwa lugha ya
kiswahili.
Kuundwa kwa vyombo vya ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili
Tanzania baada ya uhuru ilifanya jitihada za kuunda vyombo mbalimbali vya
kukuza na kueneza Kiswahili katika nyanja mbalimbali mfano wa vyombo hivyo
ni UWAVITA BAKITA, TUKI, Taasisi ya Elimu,TAKILUKI na Chama cha
Kiswahili Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Kutumika katika elimu
Kiswahili licha ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali,
kilipendekezwa kutumika katika shule za Msingi na kufundishwa katika elimu ya
sekondari kama somo na katika vyuo vikuu wanatoa shahada mbalimbali za lugha
ya kiswahili. Pia katika Elimu ya watu wazima ambao hawakujua kusoma na
kuandika. Watu hawa walijifunza masomo mbalimbali kwa lugha ya kiswahili na
kuwafanya watu wengi kujua kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya kiswahili
fasaha. Kampeni hii ilikuwa kwa nchi nzima ambapo walijifunza elimu ya Afya,
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17
Siasa, Kiswahili, Kilimo na ufundi kwa lugha ya Kiswahili na kuwafanya watu
wengi kuzungumza kiswahili sanifu.
Vyombo vya habari
Tangu uhuru ulipopatikana kuna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoanzishwa.
Vyombo hivi hutumika kueneza kiswahili kwa kiasi kikubwa na hufikiwa na watu
wengi licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi. Vyombo hivyo ni magazeti
na majarida mbalimbali ambayo huandikwa kwa lugha ya kiswahili lakini kuna
redio na runinga ambazo matangazo yake hutangazwa kwa lugha ya kiswahili.
Hivyo kukifanya kiswahili kuenea kote ndani na nje ya nchi.
Biashara
Shughuli za kibiashara nchini husaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na
kuwepo kwa makabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza
kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika
katika biashara hizo.
Shughuli za siasa na utawala
Tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru kiswahili kimetumika kama nyenzo
muhimu kuwaunganisha wananchi. Shughuli za kisiasa zimetumia lugha hii katika
kujiimarisha; mfano wakati wa chama kimoja, Azimio la Arusha na Mfumo wa
vyama vingi Kiswahili kimetumika kama njia kuu ya mawasiliano. Pia katika
utawala chama kinachotawala kimekuwa na harakati za kukiendeleza kiswahilli
katika nyanja zote. Ambapo kiswahili kimekuwa kikitumika katika shughuli zote
za kiutawala. Hivyo shughuli za kisiasa na kiutawala zimechangia kwa kiasi
kikubwa katika kukuza, kukieneza na kukiendeleza kiswahili.
Uandishi na uchapishaji wa vitabu
Kuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi
ambavyo vilichambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili
na utamaduni wake, mfano :- F Nkwera, Shabani Robart, Mathias Mnyapala na
Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukizi walijitokeza na wanaendelea
kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18
Shughuli za kiutamaduni
Shughuli za kiutamaduni zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya
Kiswahili. Shughuli hizo ni pamoja na harusi, misiba, matanga na sherehe
mbalimbali za kijamii ambazo zimesaidia kukiendeleza Kiswahili kwa kuwa
huwakutanisha watu tofautitofauti katika shughuli hizo, ambapo huwalazimu
kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano na kufanya kiswahili kuendelea.
Pia katika Sherehe mbalimbali vikundi vya sanaa na muziki vinavyotumia lugha ya
kiswahili kutumbuiza. Vikundi vingine huandaa nyimbo zao kwa ajili ya kukieneza
Kiswahili.
Vyombo vya Ukuzaji na Uenezaji wa Lugha ya Kiswahili
Tangu Tanzania ipate uhuru hadi sasa kuna vyombo kadha wa kadha
vilivyoanzishwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili baadhi ya vyombo
hivyo ni hivi vifuatavyo:
BAKITA
Hii ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967
kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii Baraza ndilo mratibu
wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
BAKITA imekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuzaji na uenezaji wa lugha
ya Kiswahili kupitia majukumu yake. Majukumu ya Baraza kama
yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni haya yfuatayo:
Kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini
kote. Katika kufanya hivi Baraza lina jukumu la kuhakikisha Kiswahili
kinaendelea na kuhakikisha kuwa matumizi ya Kiswahili yanakuwa sahihi.
Kushirikiana na vyombo vingine nchini vinavyojihusisha na maendeleo
ya Kiswahili na kuratibu shughuli zao. Vyama vya Kiswahili kama vile
CHAKAMA, CHAWAKAMA vina mchango mkubwa wa kukuza na
kueneza lugha ya Kiswahili kwa kushirikiana na BAKITA. Ushirikiano wa
BAKITA na vyama hivi waweza kuwa ni wa kuto ushauri, au msaada wa
kifedha, kwa mfano BAKITA imekuwa ikiwasaidia CHAWAKAMA pale
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19
wanapokuwa wanataka kufanya makongamano nap engine wanahitaji
msaada wa kifedha, kwa hiyo BAKITA imekuwa ikiwasaidia kifedha.
Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za
kawaida. BAKITA imekuwa ikiandaa vipindi mbalimbli redioni ili
kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
Kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za
istilahi. Katiaka uundaji wa istilahi, BAKITA imekuwa ikichapisha vitabu
mbalimbali ikionesha istilahi sanifu zilizoingizwa katika lugha ya Kiswahili.
kwa hiyo kupitia jukumu hili Kiswahili kimekuwa kinakua.
Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya
serikali na yasiyo yaserikali na asasi nyingine. Kupitia tafsiri
zinazofanywa na BAKITA Kiswahili kimekuwa kikikuwa na kuenea.
Kuchapisha jarida au toleo linalohusu lugha na fasihi ya
Kiswahili. Machapisho haya ya BAKITA yanaendelea kukifanya Kiswahili
kukua kwa kuongeza msamiati mpya na hivyo watu wanaposoma
machapisho hayo wanajifunza msamiati mpya na hivyo kufanya Kiswahili
kukua.
Kushirikiana na mashirika ya kitaifa, asasi na watu binafsi, kufuatilia,
kushauri na kusimamia shughuli zinazolenga kukuza Kiswahili nchini
Tanzania.
Kutoa ushauri kwa waandishi na wachapishaji ili watumie Kiswahili
fasaha. Kwa kufanya hivi matumizi bora ya Kiswahili yanakuwa
yanaimarika.
Kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuthibitisha
vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla
havijachapishwa. Hili pia ni jamabo linaloimarisha matumizi ya Kiswahili
sanifu.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20
TAKILUKI
Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mwaka 1979
kwa lengo la kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar, ili
kutimiza lengo hilo TAKILUKI inajishughulisha na kazi zifuatazo:
Kuratibu na kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar,
kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni, kuhariri
miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti
za Kiswahili katika Nyanja zake zote, hususani katika uwanja wa sarufi na
fasihi.
Pia TAKILUKI wana kazi ya kuandaa istilahi za taaluma mbalimbali, kutoa
huduma za taaluma mbalimbali, kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa
lugha mabalimbali kwa mashirika, idara, wizara, taasisi, kampuni na watu
binafsi, kufundisha lugha za kigeni na kuandika vitabu mbalimbali vya
Kiswahili.
Pia hujishughulisha na utoaji wa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa
vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau
wengine wa Kiswahili kama vile, mashirika, wizara, taasisi, vyuo na watu
binafsi katika kuendesha shuguli za ukuzaji wa Kiswahili, mathalani
kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.
Vilevile hujishugulisha na usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya
lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari na katika shughuli mbalimbali
za serikali na za kawaida.
TUKI/TATAKI
Majukumu ya TUKI ni pamoja na kuunda sera muafaka za kustawisha Kiswahili
na pia kufanya utafiti katika lugha ya Kiswahili.
Majukumu mengine ya TUKI ni kuhariri, kuchapisha vitabu na kutawanya vitabu
na majarida ya kitaaluma katika Kiswahili.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21
Kwa sasa TATAKI inatoa shahada ya awali na uzamili katika lugha ya Kiswahili,
kwa njia hii inawaandaa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambao watatumika
sehemu mbalimbali za ulimwengu kufundisha lugha ya Kiswahili.
CHAUKIDU
CHAUKIDU ni kifupi cha Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani, makao
makuu ya chama hiki kwa sasa yapo chuo kikuu cha Wisconsin-Madison,
Marekani
Madhumuni makuu ya CHAUKIDU ni: Kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa
Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi
yafuatayo:
Kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika au
inaweza kutumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji
na utafiti wa maarifa ya aina zote, uandishi/utangazaji wa habari, uandishi
wa vitabu, uchapishaji vitabu na majarida, utayarishaji wa safari za mafunzo
katika Afrika ya Mashariki na Kati, n.k.
Kusambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho
mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta juu ya vipengele
mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili.
Kuwajumuisha wanachama kwa ajili ya kubadilishana mawazo na tajiriba
zao katika masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili (k.v. uboreshaji wa
ufundishaji, utangazaji, utafiti, uandishi, nk.) kwa njia ya KIKAO wa kila
mwaka, warsha au semina au kongamano maalumu, na hata kwa njia ya
mtandao.
Kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na
kuheshimu Kiswahili.
Kushauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili
kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda
sera muafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya
maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni,
kielimu, n.k.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22
CHAWAKAMA
CHAWAKAMA husimama badala ya Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo
vikuu Afrika Mashariki. Chama hiki kilianzishwa mwaka 2004 kwa lengo la
kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia
wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale
wanosoma Kiswahili na hata wale wenye mapenzi ya lugha ya Kiswahili pia
wanaweza kujiunga na chama hiki.
Chama hiki kina utaratibu wa kuandaa makongamano ambapo wanachama wake
kutoka nchi zote za Afrika Mashariki hupata fursa ya kukutana mara moja kila
mwaka. Pamoja na utaratibu wa chama kuandaa makongamano pia uanzishwaji
wake umeambatana na malengo kadhaa ambayo ndiyo dira inayoiongoza chama
kwa mujibu wa katiba, malengo hayo ni haya yafuatayo:
1. Kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza
vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili.
2. Kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa lugha ya kiswahili.
3. Kueneza lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi.
4. Kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha
lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama.
5. Kuwaunganisha wanafunzi wa kiswahili Afrika Mashariki na kati katika
kukikuza kiswahili.
6. Kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa
kiswahili ndani na nje ya nchi kama vile BAKITA, TATAKI, TAKILUKI,
UWAVITA, CHAKAMA, BAKIZA n.k.
7. Kuchapisha kijarida cha chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza
taaluma ya kiswahili.
8. Kuweka kumbukumbu ya wataalamu wa kiswahili kwa nia ya kuwatumia
katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23
9. Kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma ya
kiswahili.
Pamoja na malengo hayo, lengo kuu la chama hiki ni kueneza Kiswahili lakini sasa
wanakienezaje? Wanachama wa chama hiki ambao ni nchi wanachama wa jumuia
ya Afrika mashariki wanakawaida ya kuandaa makongamano kwa ngazi ya kitaifa
na ngazi ya kimataifa.
Kwa ngazi ya kitaifa kila nchi huandaa kongamano kila mwaka ambalo
linawakutanisha wanachama wote kutoka vyuo mbalimbali katika nchi husika.
Katika kongamano hilo mada mbalimbali zinazohusu lugha ya Kiswahili na
mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa juu ya
maendeleo ya chama. Sasa katika mijadala kama hii inatoa nafasi ya Kiswahili
kukua kwani makala mbalimbali huandikwa ambazo pia husomwa na watu
mbalimbali. Makala hizi pia zimekuwa zikichapishwa katika majarida ya chuo
husika na pia zimekua zikichapishwa mtandaoni ambapo hutoa fursa kubwa kwa
watu wengi zaidi kuzifikia na kusoma, hivyo kwa njia hiyo Kiswahili kinakua
kimeenea.
ZOEZI
Kiswahili kilienea kwa kasi sana katika kipindi gani?
A Kipindi cha Waingereza
B Wakati wa kupigania uhuru
C Baada ya uhuru
D Kipindi cha Waarabu
Ni wakati gani ambapo Kiswahili kilitumika katika elimu?
A Kabla ya uhuru
B Wakati wa waingereza
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24
C Wakati wa waarabu
D Baada ya uhuru
Kuenea kwa kasi kwa lugha ya Kiswahili baada ya uhuru kulichangiwa na lugha
hii kuteuliwa kuwa___
A Lugha ya taifa
B Lugha ya kimataifa
C Lugha sanifu
D Lugha ya Afrika
Lipi kati haya siyo msamiati uliotokana na vita kati ya Tanzania na Uganda na
kusababisha ukuaji wa Kiswahili?
A Dikteta
B Ubia
C Nduli
D Walokole
Shaaban Robert na Mathias Mnyampala walichangia sana ukuaji wa Kiswahili
baada ya uhuru kwa njia ya___.
A Utunzi wa nyimbo
B Uandishi wa vitabu
C Siasa
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25
D Uandishi wa habari
Dhima ya kila Asasi inayokuza Kiswahili
Mafanikio na Changamoto Zinazovikabili Vyombo vya Ukuzaji wa Kiswahili
Mafanikio
Vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili vimejitahidi sana kukuza lugha ya
Kiswahili, kwa hali ya Kiswahili ilivyo sasa ni matokeo ya juhudi za
vyombo hivyo. Mafanikio ya vyombo hivyo ni pamoja na haya yafuatayo:
Machapisho ya lugha ya Kiswahili ni mengi sana nchini na nje ya nchi,
kufanya mafunzo ya Kiswahili, kukua kwa matumizi ya Kiswahili na
kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Kiswahili nchini.
Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika sehemu rasmi hasa katika ofisi za
serikali na ofisi za watu binafsi inadhihirisha mafanikio ya jitihada za
vyombo hivi kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili.
Kufundshwa kwa lugha ya Kiswahili kama taaluma kwa ngazi ya shahada ya
awali, uzamili na uzamivu. Hizi ni jitihada za TATAKI katika kuhakikisha
kunapatikana wataalamu wa lugha ya Kiswahili, hivi sasa TATAKI
wanafundisha lugha ya Kiswahili kwa ngazi ya shahada ya awali, uzamili na
uzamivu.
Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo mabalimbali vya kimataifa,
matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vikao vya Umoja wa Afrika na pia
ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika vyo mabalimbali Duniani ni
ishara tosha ya kuonesha mafanikio ya jitihada za vyombo vya ukuzaji na
uenezaji wa Kiswahili.
Changamoto
Vyombo hivi vinakabiliwa na upungufu wa wataalam. Wataalamu wengi
waliobobea katika taaluma za Kiswahili wanakimbilia nje ya nchi wakidhani
huko ndiko kuna maslahi mazuri zaidi.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26
Upungufu wa fedha za kuendeshea shughuli za ukuzaji wa Kiswahili katika
vyombo hivi pia limekuwa ni tatizo sugu. Kwa hiyo shughuli za ukuzaji wa
Kiswahili zinakuwa zinakwenda taratibu.
Taasisi hizi pia zinashindwa kujitangaza vizuri kutokana na kwamba hazina
vyombo vya habari binafsi ambavyo vingeweza kutumika kutangaza
shughuli zao. Jambo hili limesababisha vyombo hivi kushindwa kutoa elimu
ya Kiswahili kwa kutumia vyombo vya habari kutokana na kwamba
gharama za kufanya hivyo ni kubwa.
Vyombo hivi baadhi havina ofisi za kudumu, na hivyo kuhamahama jambo
ambalo linaathiri utendaji kazi wa vyombo hivyo.
ZOEZI
Kukuza ari ya kupenda somo la Kiswahili lilikuwa ni dhumuni la kuanzishwa
kwa___.
A. BAKITA
B. UKUTA
C. TUKI
D. Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
___ni chombo kikuu chenye dhima ya kusimamia shughuli za ukuzaji wa lugha
nchini.
A. UKUTA
B. BAKITA
C. TAKILUKI
D. TATAKI
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27
Baada ya uhuru kuna asasi ziliundwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili
ambazo ni___.
A. CHAUMA, TATAKI
B. CHAKIMA, TUKI
C. CHAKAM, BAKITA, TUKI
D. BAKITA, TUKI, TAKILUKI, CHAWAKAMA
Chama cha Kiswahili cha Afrika kiliundwa mwaka gani?
A. 1964
B. 1963
C. 1970
D. 1978
Ni taasisi gani ina dhumuni la kufanya tafiti za Kiswahili katika nyanja zake zote
za fasihi na sarufi?
A. Taasisi ya Elimu Tanzania
B. CHAKA
C. TATAKI
D. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
MADA YA 3 UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya
Dhana ya Uhakiki
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28
Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi
fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya
sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza
kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k
Dhima ya Mhakiki na Nafasi ya Mhakiki
Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa
msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo:
Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa urahisi;Watunzi wa kazi
za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo mhakiki
anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi kwa
kuvifafanua kwa lugha rahisi.
Husaidia ukuaji wa kazi za fasihi;Mhakiki anapoonesha ubora na udhaifu
wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na
kutunga kazi iliyobora zaidi.
Uhakiki hukuza uelewa wa mhakiki; Kwa kuhakiki kazi mbalimbali za
fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja na mambo
yanayotokea katika jamii.
Nafasi ya Mhakiki
Mhahiki ana nafasi kubwa katika kazi za fasihi, Mhakaki ndiye anafafanua kazi ya
fasihi ili hadhira iweze kumwelewa vizuri mtunzi wa kazi hiyo. Kwa hiyo hapa
mhakiki anasaidia kurahisisha mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi.
Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya
hivyo huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.
Hatua za Kufuata wakati wa Kufanya Uhakiki
Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya
hivyo huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.
Kwanza ni kuisoma kazi ya fasihi; hapa mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya
fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29
Pili ni kuainisha na kuchambua mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hiyo
katika vipengele vya fani na maudhui.
Tatu ni kutoa tathimini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.
UHAKIKI WA MASHAIRI
Shairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato
unaowasilisha mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na
hufuata utaratibu fulani.
Mashairi yapo ya aina mbili:
1. Mashairi huru
2. Mashairi ya arudhi
Mashairi ya arudhi
Haya ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa
mashairi. Arudhi/kanuni hizi ni pamoja na:
1. Kugawika kwa shairi katika beti
2. Beti kuwa na idadi maalum ya mishororo.
3. Mishororo ya ubeti kugawika katika vipande
4. Mishororo kuwa na ulinganifu wa mizani
5. Shairi kuwa na urari wa vina
6. Shairi kuweza kuimbika / kuwa na mahadhi au mapigo.
7. Kuwepo kwa kipokeo katika shairi
8. Kuwa na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwala
9. hairi kuwa na utoshelezo wa beti / kujisimamia kimaana.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30
Mashairi huru
Pia hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiozingatia
lazima ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu huweza kuwa:
1. Lugha ya muhtasari
2. Lugha yenye mahadhi
3. Lugha ya kisanii iliyo na mafumbo na taswira
4. Mara nyingine hugawika katika beti.
5. Mishororo kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)
Sifa za Mashairi
Mashairi huwa na sifa maalum zinazoyatambulisha kama kazi ya kishairi, yawe ya
kimapokeo au kimapinduzi.
Sifa hizi ni kama vile:
1. Mashairi hutumia lugha ya mkato / muhtasari
2. Ni sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundi
3. Huwa na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi beti.
4. Hutumia lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na
jazanda.
5. Mashairi huwa na sifa ya kuweza kuimbika hivyo shairi ni wimbo na wimbo
ni shairi.
Dhima ya mashairi
1. Kupasha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvuto
2. Kuelimisha na kuzindua jamii.
3. Kuendeleza na kukuza kipawa cha utunzi.
4. Kuhifadhi msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31
5. Kuburudisha hadhira na wasomaji.
6. Kuwasilisha hisia za ndani za mtu na mawazo
Hatua za uhakiki wa mashairi
1. Soma shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumla.
2. Soma shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali
na kuchunguza maana ya kila mojawapo
3. Pitia maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu
yanayotarajiwa.
4. Soma shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu
maswali.
5. Toa majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririko.
Vipengee vya Uchambuzi Wa Mashairi
1. Anwani/kichwa cha shairi – Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au
sentensi moja. Anwani ni kidokezo muhimu cha kinachozungumziwa katika
shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa moja, fumbo, kinaya, kibwagizo
au sehemu ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina anwani, basi lipewe anwani
inayoafikiana na maudhui au dhamira kwasentensi isiyozidi maneno 6.
2. Maudhui – Haya ni masuala makuu au mambo muhimu yanayohusu
mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi. Kwa
mfano: malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k. Maudhui
hung‟amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa kilichomo katika shairi.
3. Dhamira / shabaha - Ni lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake.
Dhamira ya mtunzi huwa ni ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji
kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi katika shairi. Mfano: Baada
ya kusoma shairi, unaweza kung‟amua mtunzi alitaka kusisitiza kauli
kuwa uongozi mbaya haufai, misitu ni uhai n.k. Dhamira hutokana na
mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa yake.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32
4. Mbinu na tamathali za lugha - Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi
zilizotumiwa na mshairi katika shairi. Mfano:Mazda / ziada / zidi -
kurefusha maneno;enda kuwa enenda. Inksari / muhtasari - Ni kufupisha
maneno;aliyefika kuwa alofika. Utohozi – Mbinu ya kugeuza msamiati /
maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika kana kwamba ni ya
Kiswahili. Mfano: Time - taimu; One – Wani. Mbinu hii vilevile
huitwa ukopaji au uswahilishaji.
ZOEZI
Mfano wa kazi za fasihi andishi ni___.
A Ngonjera, nyimbo na methali
B Ushairi, riwaya na tamthiliya
C Riwaya, maigizo na tamthiliya
D Hadithi, ngano na tarihi
Moja wapo ya dhima ya mhakiki kwa wasomaji wa kazi za fasihi ni___.
A Kumsifia mwandishi
B Kuelimisha hadhira
C Kusaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi
D Kumkosoa msomaji
Umuhimu wa mhakiki katika kazi ya fasihi ni pamoja na___.
A kuwakosoa waandishi
B Kuwaelimisha wasomaji
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33
C kushawishi wasomaji
D kufichua maovu ya waandishi
Ni kitendo gani kati ya hivi hakifanyiki katika uhakiki?
A Kubeza
B Kutathmini
C Kutoa maoni
D Kuainisha
Kipi kati ya hivi hakifanyiki katika uhakiki wa mbinu ambazo msanii ametumia
kuwasilisha kazi yake?
A Mtindo
B Msimamo
C Matumizi ya lugha
D Muundo
Taarifa Muhimu za Mwandishi wa kila Kitabu
Mwandishi wa fasihi ni mtu anaeweza kubuni kazi ya fasihi na kuiweka katika
maandishi. Unaposoma kazi za fasihi ni lazima ujue taarifa muhimu za mwandishi
wa kazi hiyo, ambazo ni jina, kwa sababu kila utakapokua unajibu swali ni lazima
utaje jina la mwandishi wa kitabu. Falsafa na utamaduni kujua msimamo wake, na
muundo kujua mpangilio wa matukio, mtindo kujua upekee wake na matumizi ya
lugha.
ZOEZI
Ni kipengele gani amacho huelezea mwelekeo wa ujumla wa mawazo ya
mwandishi kuhusiana na jambo fulani?
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34
A Falsafa
B Mtindo
C Mtazamo
D Msimamo
Mwandishi wa fasihi ni nani?
A Mtu naeweka habari katika maandishi
B Mbunifu wa kazi za fasihi na kuweka kimaandishi
C Mtu anaenakili maandishi
D Mwanafasihi
Kipengele kinachotoa taarifa ambayo hubeba mawazo ya mwandishi ni ___.
A Dhamira
B Mtindo
C Falsafa
D Mtazamo
NI muhimu kujua falsafa ya mwandishi___
A Kujua siasa yake
B Ili kujua msimamo wake
C Kubaini kufaulu na kufeli kwake
D Ili kujua matatizo yake
Zifuatazo si taarifa muhimu kufahamu kuhusu mwandishi
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35
A Desturi
B Msimamo
C tamaduni na mila
D Umri na lugha
MADA YA 4 KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Utungaji wa Mashairi
Mambo ya Kuzingatia katika Utungaji wa Mashairi
Utungaji/uandishi wa kubuni ni ule unatokana na hisia ambazo zinamsukuma
mtunzi ili atunge kazi yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo
vinamsumbua akilini na kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka
aliwasilishe wazo lake ili hadhira ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi
hukosa usingizi na hivyo hulazimika kuamka na kuandika kile kinachomsukuma
akilini mwake.
Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu
kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona,
kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja.
Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo
lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – je ni ya golori au
la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?
Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au
nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au
uturi? Je, ananuka mdomo?
Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko
wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini?
Akikugusa bega unajisikia nini?
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36
Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni chungu au tamu?
Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina
ukakasi au uchachu?
Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya
ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni
sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?
Uzoefu wa Mwandishi
Uzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu.
Mwandishi ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni
matatizo gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani
umekutana nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011)
kuna baadhi ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana
nailoni na je kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?
Uchunguzi/utafiti
Uchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio
bila kuongopa. Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa
wasomaji wa kazi zake.
Uchunguzi ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje,
anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na
wenzane na mazingira yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi
kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na
akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.
Mwandshi baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi
yake. Hapa sisi tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika
hatua ya utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya
hapo tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo
yatatuwezesha kutunga mashairi.
Dhana ya shairi
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37
Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti
za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa
huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.
Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana
halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi
ijapokuwa hazikuandikwa
Mashairi yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya
maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo
kadhaa yanayotakiwa kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:
1. Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.
2. Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti
ileile mwishoni mwa sentensi.
3. Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.
4. Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo vya aina tatu:Kituo
cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika
kila ubeti;Kituo cha kimalizio – ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno
yake hubadilika ubeti hadi ubeti;Kituo nusu bahari – ni mstari wa mwisho
ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi
ubeti.
Katika mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe
na maana kamili.
Vipengele vya fani katika mashairi
Vipengele vya fani katika shairi ni pamoja na:
Jina / anwani
Mandhari
Wahusika
Muundo –tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38
Mtindo – pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima
cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.
Vipengele vya Maudhui kati mashairi
Vipengele vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo,
mtazamo, na dhamira za mwandishi.
Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza,
kufundisha, kuburudisha, kukosoa, na kadharika.
Baada ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.
ZOEZI
Mtiririko wa maelezo ya shairi ambayo hutolewa kwa kuzingatia utangulizi, kiini
na mwisho huitwa___.
A Muwala
B Kituo
C Beti
D Urari wa mistari
Ni jambo gani la kuzingatia katika utunzi wa shairi ili kuweza kuchochea hisia za
wasomaji?
A Muwala
B Urari wa vina
C Lugha ya kishairi
D Taswira
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39
___hutokana na jambo linalojadiliwa katika shairi na huzingatiwa katika utunzi.
A Anwani ya shairi
B Beti
C Muundo
D Mizani
Utungaji unatokana na___.
A Mawazo ya mhakiki
B Mazingira yanayomzunguka mwandishi
C Mawazo ya mwandishi
D Mawazo ya watu
Silabi zinazounda mistari ya beti za mashairi huitwa___.
A Beti
B Vina
C Kichwa cha shairi
D Mizani
MADA YA 5 UANDISHI
Uandishi wa Insha za Kiada
Insha ni kifungu cha maandishi kilichoandikwa kutokana na mtazamo wa
mwandishi katika kujadili juu ya mada fulani. Mwandishi anaweza kuandika
kuipinga mada hiyo au kuishadidia mada hiyo. Kuna aina mbili za insha, insha za
kaida (zisizo za kisanaa) na insha za kisanaa.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40
Insha za kaida ni insha zinazotumia lugha ya kawaida kuelezea mambo
mbalimbali katika jamii, mfano juu ya mazingira, uchumi, biashara, historia n.k.
Muundo wa Insha za Kaida
Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:
1. Kichwa cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika
insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k
2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya
maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda
kuyajadili katika insha yako.
3. Kiini cha insha; katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile
unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa
kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
4. Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini
cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika
insha.
Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha
Taratibu za uandishi zinapozingatiwa insha pia itasomeka vizuri na pia itakuwa na
mtiririko mzuri wa mawazo.
Epuka kutumia vifupisho vya maneno visivyo rasmi.Uandishi wa insha ni
suala rasmi, kwa hiyo katika uandishi wake inatakiwa kuzingatia kuepuka
kutumia vifupisho ambavyo sio majumui yaani havijulikani. Kwa mfano
maandishi kama, xamahani (samahani), ckatai (sikatai) na mengine
yafananayo kama hayo ni lazima yaepukwe katika uandishi wa insha.
Andika utangulizi unaovuta umakini wa msomaji. Hiki ni kipangele cha
muhimu sana, msomaji anapoona kwamba kwenye utangulizi hakuna kitu
kinachomvutia hataendelea kuhangaika kusoma insha hiyo.
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41
Andika kiini cha insha kwa mpangilio mzuri Unatakiwa kuandika insha
yako katika mpangilio mzuri huku kila wazo kuu likipewa aya yake na
kuwepo na mtiririko mzuri wa mawazo.
Andika hitimisho la insha likiwa linahitimisha mawazo
yaliyokwishajadiliwa katika kiini.Hakikisha unapofanya hitimisho epuka
kudokeza wazo jipya ambalo linazua mjadala mpya, hakikisha hitimisho
lako linabeba mawazo uliyokwisha yajadili katika insha yako na wala
yasiwe mawazo yanayotoka nje ya kile ulichokijadili.
ZOEZI
Muundo wa insha ya kiada huwa na vipengele vingapi muhimu?
A Sita
B Vitano
C Vinne
D Vitatu
Ni sehemu gani katika muundo wa insha za kiada huonesha mapendekezo ya
mwandishi kuhusiana na jambo lililojadiliwa?
A Kichwa cha insha
B Hitimisho
C Kiini cha insha
D Utangulizi
Fasili ya maneno muhimu hutolewa katika kipengele gani ndani ya insha ya kiada?
A Kiini cha insha
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42
B Hitimisho
C Utangulizi
D Kichwa cha insha
___ni sehemu katika muundo wa insha ya kiada ambayo hubainisha kwa undani
jambo linalozungumziwa.
A Kiini cha insha
B Hitimisho
C Kichwa cha insha
D Utangulizi
___huzingatia wazo kuu la insha ya kiada na wakati mwingine kupigiwa mstari.
A Kiini cha insha
B Utangulizi
C Kichwa cha insha
D Hitimisho
Uandishi wa Insha za Kiada
Uandishi wa Hotuba
Hotuba ni insha ambayo hutoa maneno halisi ya mzungumzaji/kiongozi
anapozungumzia hadhira, kuhusu jambo fulani. Insha ya hotuba huandikwa katika
hali ya usemi halisi na mwandishi hatakiwi kuweka alama za kunukuu anapoanza
insha yake.
Hotuba inaweza kutolewa na kiongozi wa kisiasa, utawala, kidini, kikundi, shirika
fulani, daktari, n.k. Hadhira katika hotuba husheheni wageni waalikwa,
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43
wanachama, wafuasi, wananchi, n.k ambao wanahusishwa katika mada
inayorejelewa katika hotuba hiyo.
Muundo wa Hotuba
Hutuba inakuwa na muundo ufuatao:
Anwani
Anwani, mada au kichwa cha hotuba hurejelea mada ya hotuba. Pia mada inaweza
kutaja hadhira.
Hotuba ya Waziri wa Afya kuhusu madhara ya ukimwi kwa wananchi.
Hotuba ya Mwalimu Mkuu kwa Wazazi
Utangulizi
Anza hotuba yako kwa kuwatambua waliohudhuria KIKAO (hadhira).
Wataje kwa majina/vyeo vyao kuanzia yule wa cheo cha juu hadi wa chini,
mabibi na mabwana. Kumbuka kwamba hauhitajiki kuwasalimia.
Kuwatambua kwa majina pekee kunatosha.
Jitambulishe kwa hadhira yako hasa ikiwa unazungumzia hadhira isiyokujua
au wageni.
Tanguliza mada yako.
Kwa mfano:
Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Mbunge, wanachama wa kikundi hiki
cha Mazingira, mabibi na mabwana. Ni matumaini yangu kwamba nyote mu
buheri wa afya. Mimi ni mwakilishi wa Kikundi cha Mazingira na jioni ya leo
kuna jambo muhimu ambalo ningependa sote tulifahamu ili kuboresha mazingira
yetu kwa …
Kiini
Hakikisha kuna mtiririko wa hoja kuanzia mwanzo hadi mwisho
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44
Ujumbe wako wote unapaswa kuwa katika usemi halisia wala si wa taarifa.
Tamati
Hakikisha kwamba mwisho wa hotuba yako unatambulika.
Unaweza kumaliza kwa shukurani
ZOEZI
Kipi kati ya hivi siyo kipengele katika muundo wa hotuba?
A Muhtasari
B Kiini
C utangulizi
D Tamati
___ni sehemu katika muundo wa hotuba ambapo msisitizo na shukrani hutolewa.
A Hitimisho
B Kichwa cha hotuba
C Utangulizi
D Kiini
Shukrani katika hotuba hutolewa katika kipengele gani kati ya hivi?
A Anwani
B Utangulizi
C Hitimisho
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45
D Kiini
___ni kipengele cha muundo wa hotuba ambacho hurejelea mada ya hotuba.
A Tamati
B Anwani
C Kiini
D Utangulizi
Muundo wa hotuba una sehemu___.
A Nne
B Tano
C Tatu
D Sita
Uandishi wa Risala
Risala ni hotuba fupi inayosomwa mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi fulani la
watu hasa hasa wanafunzi, wafanyakazi, washiriki, wanachama, mafundi n.k ili
kutoa maelezo ya haja zao mbalimbali na mahitaji yao au kuonyesha msimamo wa
kundi hilo kwa kiongozi.
Muundo wa Risala
Utanguizi
Cheo cha kiongozi anayehusika
Kundi linalowakilishwa
Kiini
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46
Maelezo ya hali halisi ya maswala na msimamo wa kundi linalowakilishwa.
Mapendekezso na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa.
Hitimisho
Shukrani
Tanbihi: Kama vilivyosemwa awali risala ni hotuba fupi lakini inachukua mambo
muhimu tu na kuyaeleza. Hivyo risala yenyewe huwa ni maelezo ya muhtasari kwa
jambo linalohitaji maelezo marefu Katika hotuba. Utungaji wa risala unahitaji
uangalifu sana na lugha ya heshima iliyo wazi kueleweka kwa kiongozi.
Mfano wa risala:
Ndugu Mgeni rasmi, Walimu, Wanafunzi wenzetu, Wazazi, Wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne, tunayo heshima na furaha kubwa ,
kukukaribisha ili ushiriki nasi katika siku hii muhimu na kusikia mafanikio
mbalimbali kwa kipindi chote cha masomo yetu hapa shuleni.
Shukrani zetu za pekee na za dhati ziende kwa uongozi mzima wa Shule na
walimu wetu wote kwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wa kutufundisha, hivyo
tumefundishika vyema; kwasababu tupo tofauti sana na tulivyokuja hapa mwezi
januari 2009.
Ndugu mgeni rasmi, tulianza kidato cha kwanza tukiwa wanafunzi 120; wasichana
60 na wavulana 60. Mpaka leo tunapohitimu tupo wanafunzi 90; kati yao wavulana
ni 43, na wasichana 47. Wengine wameshindwa kuhitimu nasi siku ya leo
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ujauzito na kuhama shule.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema wa Baraka kwa ulinzi wake
kwetu hadi leo hii tunahitimu kidato cha nne.
Ndugu mgeni rasmi, elimu hii ya kidato cha nne imetupatia msingi mzuri wa
kujiunga na Elimu ya juu, pia imetujengea uwezo mzuri wa kujitambua na kufikiri,
kufanya kazi vizuri na kufanya maamuzi sahihi; pia imetuwezesha sisi wanafunzi
kupata elimu ya mambo mbalimbali kupitia masomo tunayo fundishwa hapa
shuleni, mfano; tumepata elimu ya uraia, historia ya mambo mbalimbali katika
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47
nchi yetu na dunia kwa ujumla, pia tumeweza kupata uelewa kuhusu afya na
magonjwa, usalama katika mazingira yetu, Kilimo, Maumbile ya nchi, hali ya
hewa, misitu, na viwanda. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kusoma vitabu
mbalimbali kwa lengo la kupata ujuzi wa kuinua uchumi wetu wa taifa.
Ndugu mgeni rasmi, mafanikio hayo yamepatikana kwasababu ya ushirikiano
mzuri kati yetu na walimu wetu. Tangu tujiunge na shule hii tukiwa kidato cha
kwanza tumefanya majaribio na mitihani ya mara kwa mara jambo lililo tusaidia
kuinua taaluma yetu.Tunawashukuru sana walimu wetu, tuna waahidi kufanya
vizuri katika mitihani yetu ya Taifa ya kidato cha nne mwaka huu, na Mungu
awabariki sana.
Ndugu mgeni rasmi, tumepata changamoto mbalimbali wakati wa maisha yetu ya
kielimu hapa shuleni, kama ifuatavyo;
Ndugu mgeni rasmi, tuna changamoto ya upungufu wa vitabu vya kiada na ziada;
hii imepelekea kushindwa kujisomea vizuri, kwani kitabu kimoja kinatumiwa na
wanafunzi zaidi ya ishirini (20).
Ndugu mgeni rasmi, changamoto nyingine ni upungufu wa vifaa vya maabara, hii
inapelekea kuchangia kifaa kimoja, hivyo tuna tumia muda mwingi sana kujifunza
na kumuelewa mwalimu.
Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa walimu, hasa wa
masomo ya sayansi; hii imepelekea kutomaliza „syllabus‟ kwa wakati.
Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa samani za shule, kama
vile; madawati kwa ajili ya wanafunzi, viti na meza kwa ajili ya walimu; hii
imepelekea baadhi ya wanafunzi wenzetu kukaa wawili kwenye dawati moja.
Ndugu mgeni rasmi, maji ni changamoto hapa shuleni, kwani shule haina kisima
cha maji, hii imepelekea shule kununua maji kwa gharama kubwa, ambayo
hayatoshelezi mahitaji ya shule, kama vile usafi; hususani kwa upande wa vyoo,
bila kuwa na maji ya kutosha tutapata magonjwa ya mlipuko, kama vile
kipindupindu.
Ndugu mgeni rasmi, changamoto ya vifaa vya michezo; kama unavyojua kuwa
michezo ni afya, shule yetu ina upungufu mkubwa wa vifaa vya michezo kama
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48
vile; mipira ya miguu, pete na mikono, pia hatuna milingoti ya chuma kwaajili ya
magoli ya viwanja vya michezo yote tunayocheza hapa shuleni.
Ndugu mgeni rasmi, tunashukuru uongozi wa shule hii, walimu na wazazi ambao
wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya shule yetu; kwa
upande wa masomo ya sayansi; shule imeweza kutenga chumba kimoja cha darasa
kitumike kama maabara japo kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa.
Ndugu mgeni rasmi, tunayo matumaini kwamba maombi yetu umeyasikiliza na
utayaatekeleza, maana tunajua kwamba wewe unaweza kupitia Hlimashauri unayo
isimamia, asante sana.
Mwisho tunaomba msamaha wa dhati toka moyoni mwetu kwa Walimu,
Wanafunzi wenzetu na Wazazi pale tulipoenda kinyume na matazamio yenu,
kwani watu wakiishi pamoja tofauti lazima ziwepo, tunatumaini mtapokea
msamaha wetu, nasi hatuna jambo lolote baya kwenu.
Ndugu mgeni rasmi, tuna kushukuru sana kwa kufika katika Mahafali yetu, kwani
tunatambua kuwa unamajukumu mengi ambayo umeyaacha na kuwepo hapa
kwaajili yetu.
ZOEZI
Muundo wa risala una sehemu kuu nne. Ni ipi kati ya hizo hukazia malengo ya
risala?
A Kiini cha risala
B Hitimisho
C Utangulizi
D Mwanzo wa risala
Ni kipi kati ya hivi hutajwa katika utangulizi wa risala?
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49
A Shukrani
B Jina la mwandishi
C Salamu
D Msisitizo wa malengo
___sio mojawapo ya kipengele cha muundo wa risala.
A Utangulizi
B Shukrani
C Hitimisho
D Kiini
___ni sehemu katika muundo wa risala inayoonesha malengo ya risala.
A Hitimisho
B Utangulizi
C Kiini cha insha
D Mwanzo wa risala
Risala ya kidato cha nne ilionekana kuwa bora zaidi kwa sababu
walizingatia___wa risala.
A Urefu
B Ufupi
C Mtindo
D Muundo
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50
UANDISHI WA KUMBUKUMBU/TAARIFA ZA VIKAO
1. Taarifa za kikao
Kumbukumbu za kikao ni muhtasari wa mambo yaliyojadiliwa na kukubaliwa
katika kikao. Ni muhimu kuandika kumbukumbu za kikao ili kusaidia na
kurahisisha utekelezaji wa mambo yaliyoamuliwa. Pia kumbukumbu za kikao
hutumika kwa ajili ya marejeleo kwa vizazi vya baadaye.
Namna ya kuandika kumbukumbu za kikao
Katika kuandika kumbukumbu mwandishi hana budi kuzingatia mambo
yafuatayo:
(a) Kichwa cha kumbukumbu
Kichwa cha kumbukumbu kioneshe kuwa kikao kinahusu nini, kilifanyikia
wapi na tarehe gani.
(b) Mahudhurio
Mwandishi anapaswa kuandika orodha ya majina ya watu waliohudhuria kikao
na wasiohudhuria. Kama kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza
mahudhurio yatakuwa na majina ya waliohudhuria tu.
(c) Uteuzi wa viongozi
Iwapo kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza wajumbe hupaswa kuteua
viongozi wa kikao hicho ambao ni Mwenyekiti na Katibu kabla ya kuanza kwa
kikao. Kikao hakiwezi kuanza pasipo viongozi wa kusimamia mijadala yote
katika kikao husika.
(d) Ufunguzi wa kikao
Baada ya kuteua viongozi, Mwenyekiti aliyeteuliwa hufungua kikao rasmi na
kuanzisha mijadala ya kikao cha siku hiyo na siku zijazo hadi itakapokuwa
vinginevyo
(e) Ajenda
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51
Hapa huandikwa ajenda zilizojadiliwa kwenye kikao. Mambo yaliyojadiliwa
katika kila ajenda yaandikwe kwa muhtasari. Kwa kila ajenda kauli ya
kukubaliwa au kukataliwa itamkwe wazi.
(f ) Mengineyo
Hapa huandikwa ajenda ambazo hujitokeza katika kikao lakini hazikupitia kwa
Mwenyekiti na zinastahili kujadiliwa kama ajenda.
(g) Yatokanayo
Hapa huandikwa mambo ambayo yamejitokeza katika kikao na hayana
uhusiano na ajenda za kikao. Kwa mfano masuala mtambuka kama mjumbe
kulipia gharama za kikao,taarifa ya dharura inayoweza kumfanya mjumbe
aondoke kabla ya kikao kuahirishwa, n.k
(h) Kuahirisha kikao
Baada ya majadiliano ya ajenda, Mwenyekiti huahirisha kikao. Mwandishi wa
kumbukumbu azingatie muda kikao kilipoahirishwa.
Baada ya kikao mwandishi apitie tena kumbukumbu hizo na aziandike vizuri na
kuzihifadhi kwa ajili ya marejeleo ya kikao kijacho. Kumbukumbu hizo zitiwe
saini na Mwenyekiti na Mwandishi (katibu) kisha wakati wa kikao kingine
zisambazwe na kusomwa na wajumbe wa mkutano. Baadaye zithibitishwe na
wajumbe na Mwenyekiti na atie saini ya kuthibitishwa huko.
Ufuatao ni mfano wa kumbukumbu za kikao kinachofanywa kwa mara ya
kwanza:
KUMBUKUMBU ZA KIKAO CHA KWANZA CHA WANAFUNZI WA
KIDATO CHA NNE KUHUSU MAHAFALI KILICHOFANYIKA TAREHE
5/4/2017 KATIKA UKUMBI WA SHULE KUANZIA SAA 4:00 ASUBUHI
HADI SAA 6:00 MCHANA.
(a) Mahudhurio
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52
Waliohudhuria (orodhesha majina yao)
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Wasiohudhuria (orodhesha majina yao)
-
-
-
-
-
-
-
-
-
(b) Uteuzi wa viongozi
Kiranja wa darasa aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kikao na katibu wake ni
kiranja msaidizi. Wajumbe wote walikubaliana na uteuzi huo.
(c) Kufungua kikao
Kiranja wa darasa ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho
alifungua kikao mnamo saa 4:00 asubuhi kwa kuwaeleza wajumbe madhumuni
ya kikao hicho.
(d) Ajenda
- Siku na mahali pa mahafali
- Mgeni rasmi
- Zawadi
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53
- Michango ya sherehe
- Uteuzi wa kamati
Siku na mahali pa mahafali
Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuwa mahafali yafanyike
jumamosi ya pili kabla ya kuanza kwa mitihani ya kitaifa ili kuwawezesha
waalikwa wote kuhudhuria lakini pia kutoa muda wa kutosha kwa wahitimu
kujiandaa kwa mitihani yao.
Kuhusu mgeni rasmi
Wajumbe walikubaliana kuwa jukumu la kutafuta mgeni rasmi apewe mkuu wa
shule.
Kuhusu zawadi
Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kuwa zawadi zitapangwa na kuamuliwa
na kamati itakayoundwa.
Michango ya sherehe
Kikao kiliazimia kwa pamoja kuwa ili kupata pesa za kufanikishia mahafali kila
mjumbe apewe fomu maalumu itakayoandaliwa ili kuchangisha toka kwa
ndugu, jamaa na marafiki kiasi chochote atakachoguswa mtu kuchangia.
Uteuzi wa kamati
Wanafunzi wafuatao walichaguliwa ili wafanye mipango ya kuandaa na
kusimamia sherehe ya mahafali yao. Wanafunzi hao ni;
- Mtungi
- Baraka
- Mujuni
- Byoma
- Shukuru
- Sikudhani
- Kachacha
- Stumai
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54
- Tamasha
- Kaitaba
Wajumbe hao walikubaliana na uteuzi huo na wakaahidi kupeana majukumu.
(f) Mengineyo
Wajumbe walisisitiza kwamba kamati ifanye mipango kwa kuzingatia kwamba
muda uliobaki ni mfupi. Walipendekeza kwamba kufanyike mkutano wa
kuwapatia wajumbe taarifa kuhusu mgawanyo wa majukumu.
(g) Yatokanayo
Mjumbe mmoja aliwaburudisha wajumbe kwa vinywaji na nyama choma ya
mbuzi katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
(h) Kuahirisha kikao
Mwenyekiti aliahirisha kikao kwa kuwaomba wajumbe wengine wawe na
ushirikiano kwa wenzao katika kufanikisha mahafali hayo. Kikao liahirishwa
saa 6:00 mchana. Kikao kijacho kitakuwa 12/4/2017 kuanzia saa 9:00 mchana
hadi saa 12:00 jioni.
Mwenyekiti…………………….Tarehe…………………………........
Katibu………………………….Tarehe……………………………….
Ikiwa kikao kinafanyika kwa mara ya pili:
Kikao cha pili na kuendelea huwa na muundo ufuatao:
1. Kichwa cha kikao
2. Mahudhurio
3. Kusomwa na Kuthibitishwa taarifa za kikao kilichotangulia
4. Kufungua kikao
5. Ajenda
6. Mengineyo
7. Yatokanayo
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 55
8. Kuahirisha kikao
9. Majina & saini za viongozi
ZOEZI
Kumbukumbu za mkutano huchukuliwa na nani?
A Mwenyekiti
B Mjumbe
C Walioalikwa
D Katibu
Tarehe ya mkutano huandikwa katika kipengele gani wakati wa uchukuaji wa
kumbukumbu za mkutano?
A Ajenda
B Mahudhurio
C Mengineyo
D Kichwa cha kumbukumbu
Kichwa cha kumbukumbu za mkutano hutaja mambo yafuatayo isipokuwa___.
A Tarehe
B Gharama
C Mahali
D Muda
“Waliohudhuria ni wanafunzi 3 wa kidato cha 3B.” Sentensi hii hubainisha nini?
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 56
A Ajenda
B Kichwa cha kumbukumbu
C Mengineyo
D Mahudhurio
Hoja zitakazorejelewa katika mkutano huitwa___.
A Mapendekezo
B Maazimio
C Maafikiano
D Ajenda
MADA YA 6 : UFAHAMU
Ufahamu wa Kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni
uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo
kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri
wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata
kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.
Kujibu Maswali ya Habari Uliyosikiliza
Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata
maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 57
Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna
zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia
kila anachokisema.
2. Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza
jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
3. Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya
muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.
4. Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono,
kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi
huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
ZOEZI
___ husaidia kupata maana ya maneno na misemo ili kujibu maswali ya habari
unayoisikiliza.
A Kusikiliza kwa makini
B Matumizi ya neno
C Wazo kuu
D Msomaji
Ni kipi afanye msikilizaji ili aweze kubaini mawazo makuu katika habari
anayoisikiliza?
A Kuuliza maswali
B Kusikiliza kwa makini
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 58
C Kufuatilia ishara
D Kuandika
Ipi siyo ishara ya mwili inayotoa maana katika kujibu maswali ya habari
inayosikilizwa?
A Kukaa kimya
B Kupepesa macho
C Kutingisha kichwa
D Kutingisha mabega
Inapaswa kuzingatia vidokezi vya maana ili kujibu maswali ya habari uliyosikiliza.
Ipi si kazi ya vidokezi vya maana?
A Kutofautisha
B Kuhitimisha
C Kuonesha mtiririko
D Kurahisisha
Yafuatayo hufanyika katika ufahamu wa kusikiliza, isipokuwa:
A Kuzingatia ishara
B Kuandikwa kwa ufupi yasemwayo
C Kuzingatia vidokezi vya maana
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 59
D Kuzingatia matini
Kufupisha Habari
FIli kuandika ufupisho mzuri wa habari uliyoisikiliza yafuatayo hayana budi
kuzingatiwa; kusikiliza habari kwa makini ili kuielewa vizuri, kuandika mawazo
makuu yanayojitokeza katika kila aya, kuyaunganisha mawazo makuu na
kuiandika habari kwa maneno yako, kuhesabu idadi ya maneno kama inazidi na
kuandika idadi hiyo mwisho wa ufupisho upande wa kulia chini kidogo.
ZOEZI
___ yapaswa yaunganishwe ili kuandika ufupisho mzuri wa habari.
A Mawazo makuu
B Maneno magumu
C Maneno ya kila aya
D Matamshi ya mzungumzaji
___siyo jambo la kuzingatiwa katika kuandika ufupisho unaofaa wa habari
iliyosikilizwa.
A Uunganishaji wa mawazo makuu
B Vidokezo vya maana
C Mawazo makuu
D Idadi ya maneno
___hupatikana baada ya kuyatambua mawazo makuu na kuyafupisha.
A Nafsi
B Kiini cha habari
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 60
C Kichwa cha habari
D Njeo
Katika kufupisha habari uliyosikiliza kipi katika haya ni cha kuzingatia?
A Ishara za mwili
B Aya
C Matamshi ya mzungumzaji
D Mawazo makuu
Katika ufupisho wa habari uliyosikiliza ni muhimu kubainisha___.
A Njeo
B Kichwa cha habari
C Swali
D Nafsi
Ufahamu wa Kusoma
Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu
cha habari, kitabu au gazeti.
Kujibu Maswali kutokana na Habari ndefu uliyosoma
Jibu maswali kutokana na habari ndefu uliyosoma
Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:
Uelewa wa msamiati na
Uelewa wa matini
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 61
Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati
uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka
vilevile matini yote hataeleweka.
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu
inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa
analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini
mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za
uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na
endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya
mwandishi.
3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa
zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya
maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema
maana ya mwandishi.
4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele
anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari
aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.
Kufupisha habari
Kufupisha habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache
lakini bila kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza.
Ufupisho wa habari huwa na sifa hizi:
1. Huwa ni mfupi kuliko habari ya mwanzo
2. Huwa na ujumbe uleule uliokuwa katika habari ya mwanzo
3. Hujumuisha mawazo makuu yaliyodondolewa kutoka kwenye habari ya
mwanzo
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 62
4. Mawazo haya sharti yapangwe katika mtririko wenye mantiki
Hatua za kufuata katika kuandika ufupisho
Ili kuweza kufanikiwa kufupisha habari kwa ufanisi hatua zifuatzo sharti zifuatwe:
Kuisoma au kuisilikiza habari kwa makini ili kuielewa vizuri
Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya
Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari
hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupostosha maana ya habari ya
kwanza.
Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi
iliyotakiwa.
Kama muda unaruhusu pitia tena habari ya mwanzo na pitia tena ufupisho ili
kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.
ZOEZI
___ni ujumbe wa msingi katika habari unaopaswa kuzingatiwa.
A Ishara
B Misemo
C Mawazo makuu
D Lugha ya mwandishi
Nini huweza kuhafifisha maana ya mwandishi katika habari ikiwa
hakitazingatiwa?
A Aina ya insha
B Urefu wa insha
C Alama za uandishi
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 63
D Idadi ya maneno
Mbinu gani itaepusha kutoka maelezo marefu na yasiyohitajika wakati wa kujibu
maswali ya habari ndefu uliyosoma?
A Kujibu kwa ufupi
B Kuwa mtulivu
C Kuelewa swali
D Kusoma kwa makini
___ siyo mojawapo ya vidokezo vya maana vinavyotumika katika kuhitimisha
habari.
A Hivyo
B Hatimaye
C Hata hivyo
D Kwa hiyo
Msomaji afanye nini ili asome habari ndefu kwa ukamilifu bila kuruka baadhi ya
aya na kujibu maswali yake?
A Kuwa mtulivu
B Kujibu kwa ufupi
C Kuelewa swali
D Kusoma kwa makini
Kufupisha Habari ndefu uliyosoma
Ili kuweza kuandika ufupisho wa habari ndefu uliyoisoma hatua zifuatazo sharti
zifuatwe, kusoma habari kwa makini na kuielewa vizuri, kubaini mawazo makuu,
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 64
kuandika ufupisho wa habari kwa maneno yako, kuhesabu idadi ya maneno na
kupunguza yaliyozidi na kupitia tena habari ya mwanzo na ya mwisho kama muda
unaruhusu. Aidha ufupisho wa habari huwa ni mfupi na una ujumbe uleule wa
habari ya mwanzo.
ZOEZI
Zifuatazo ni hatua za kufuata ili kuandika ufupisho wa habari, isipokuwa:
A Kuisoma habari kwa makini
B Kuandika ufupisho kwa maneno yako
C Kuhesabu maneno
D Kubaini mawazo makuu
___ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache bila kupotosha
ujumbe wa habari ya kwanza.
A Kufupisha habari
B Ufahamu
C Uandishi
D Insha
Ipi ni hatua ya mwisho ya kuzingatia katika kuandika ufupisho wa habari
uliyosoma?
A Kuhesabu idadi ya maneno
B Kutambua mawazo makuu
C Kusoma kwa makini
KIDATO CHA NNE 2019
Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 65
D Kuandika idadi ya maneno
Kipi kati ya hivi ni muhimu kujumuishwa katika ufupisho wa habari ndefu
uliyosoma?
A Viunganisha
B Misemo
C Vielezi
D Mawazo makuu
Maneno yaliyozidi katika ufupisho hupunguzwa baada ya___.
A Kuhesabu idadi ya maneno
B Utambuzi wa mawazo makuu
C Kubaini mawazo makuu
D Kuandika idadi ya maneno
top related