annuur 1121

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1121 JAMADUL AKHEIR 1435, IJUMAA , APRILI 18-24, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Facebook:[email protected] Watakiwa kuritadi ili kuwa wananchi Kumbe tatizo ni Uislamu, kuvaa hijabu Kisingizio cha ugaidi kuendelea kutumika Magazeti yazidi kuchochea chuki, uhasama KAULI ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mheshimiwa William Lukuvi, kama ilivyonukuliwa Bungeni Lukuvi atonesha kidonda Apaza Sauti Kanisani kama Stith Ampongeza Mrema dhidi ya Uamsho Na Mwandishi Wetu na magazetini, inaleta utata unaoibua maswali mengi. Utata huo umezidi kuleta utata zaidi, pale alipoungana na kumsifu Augustino Lyatonga Mrema katika kauli yake ya kuwapakazia Waislamu wa Zanzibar, na hasa taasisi ya Uamsho kwamba inahusika na mauwaji ya Maaskofu pamoja na kuchoma makanisa. Katika maelezo yake kama alivyonukuliwa bungeni, Mrema alionesha Inaendelea Uk. 2 Lipumba, Lissu, Jussa Mama Fat’hia kasema kweli Zitto kabwe atoa kauli nzito BWANA Ismail Jussa. BWANA Tundu Lissu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi. MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba. Mufti Simba, Pengo wamekwenda kombo Uk. 2 MAMA wa Kiislamu akionyesha uso wa huzuni kutokana na madhila yanayowapata Waislamu Nairobi, Kenya.

Upload: zanzibariyetu

Post on 25-Nov-2015

875 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1121 JAMADUL AKHEIR 1435, IJUMAA , APRILI 18-24, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz Facebook:[email protected]

    Watakiwa kuritadi ili kuwa wananchiKumbe tatizo ni Uislamu, kuvaa hijabuKisingizio cha ugaidi kuendelea kutumikaMagazeti yazidi kuchochea chuki, uhasama

    KAULI ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mheshimiwa William Lukuvi, kama ilivyonukuliwa Bungeni

    Lukuvi atonesha kidondaApaza Sauti Kanisani kama StithAmpongeza Mrema dhidi ya Uamsho

    Na Mwandishi Wetu na magazetini, inaleta utata unaoibua maswali mengi.

    Utata huo umezidi kuleta utata zaidi, pale alipoungana na kumsifu Au g u s t i n o L ya t o n g a Mrema katika kauli yake ya kuwapakazia Waislamu

    wa Zanzibar, na hasa taasisi ya Uamsho kwamba inahusika na mauwaji ya Maaskofu pamoja na kuchoma makanisa.

    Katika maelezo yake kama alivyonukuliwa bungeni, Mrema alionesha

    Inaendelea Uk. 2

    Lipumba, Lissu, JussaMama Fathia kasema kweliZitto kabwe atoa kauli nzito

    BWANA Ismail Jussa. BWANA Tundu Lissu.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

    MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba.

    Mufti Simba, Pengo

    wamekwenda kombo

    Uk. 2

    MAMA wa Kiislamu akionyesha uso wa huzuni kutokana na madhila yanayowapata Waislamu Nairobi, Kenya.

  • 2 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri

    KWA jinsi mjadala wa Bunge Maalum la Katiba unavyoendelea mjini Dodoma, tuna mashaka kama i l ikuwepo nia ya dhati ya kuandikwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Hali kadhalika, kwa namna ambavyo sehemu k u b w a y a w a j u m b e wanavyowasi l isha au kutetea hoja zao ndani ya Bunge hilo, tunapata w a s i w a s i m k u b w a k a m a w a j u m b e h a o wamekwenda Dodoma kwa lengo mahsusi la kusaka mstakabali sahihi wa mhimuli au dira ya Taifa letu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo kwa miaka hamsini au mia ijayo.

    Tu n a v y o o n a , k w a namna ambavyo idadi k u b w a y a w a j u m b e wanavyowasi l isha au kuchangia mswada huu wa

    Mufti Simba, Pengo wamekwenda komboMUFTI kazi yake ni kutoa fatwa za kidini, sio katika masuala ya kisiasa. Hii ni kwa sababu siasa za nchi hii hazifuati Kitabu na Sunna. Hazifuati Shariah.

    I l a k w a u p a n d e mwingine, Mufti katika nafasi yake kama Shaaban Issa Simba, ana haki ya kutoa maoni yake na kuwa na msimamo katika masuala yanayohusu siasa za nchi. Hata hivyo hawezi kufanya msimamo huo kuwa ndio msimamo wa Bakwata anayoongoza wala kuwa msimamo wa Waislamu. Anachoweza kufanya kama kiongozi w a k i d i n i n i k u t o a miongozo ya kiujumla hasa ile ya kuwataka watu wajadiliane kiungwana huku wakizingatia amani ya nchi.

    Kwa hiyo, katika suala linaloendelea la Katiba mpya, Bakwata au Mufti wa k e , h a we z i k u t o a

    msimamo, iwe ni serikali mbili au tatu na kudai kuwa ni wa Waislamu au kuwataka Waislamu waufuate.

    K a m a a l i v y o s e m a mjumbe mmoja wa Bunge la Katiba, viongozi wa kidini watati iwa pale tu wanapopatia katika masuala ya kidini, lakini sio katika masuala haya ya kisiasa. Mjumbe huyo aligusia kauli ya msimamo wa Muadhama Kadinali Polycarp Pengo wa serikali m b i l i . M j u m b e h u y o akasema kuwa inapokuja m a s u a l a ya k i s i a s a , miongozo ya viongozi wa kidini haiwezi kufuatwa bila ya kuhojiwa kwa sababu wapo waliofikia hata hatua ya kuwa na m i s i m a m o i l i y o u n g a mkono mauwaji ya kimbari Rwanda. Na hata wao wenyewe kufanya kazi ya kuchochea na kushiriki mauwaji.

    Hamkutumwa kutunga katiba ya mipasho vijembe

    Katiba mpya, inathihirisha ni kwa jinsi gani wale magwi j i wa kutunga na kuimba nyimbo za mipasho, (si taarabu), wamefanikiwa kuathiri fikra za wajumbe kiasi cha kujisahau na kuingiza hulka hizi za mipasho, vijembe na dhihaka katika mjadala nyeti na muhimu kwa Watanzania kwa sasa.

    Imefika mahali mjumbe wa bunge la katiba, ambaye kabeba uwakilishi wa maelfu ya watu, anasimama na kupoteza muda wa bunge kwa kuibua mjadala wake binafsi wa mahusiano ya ndoa, kuolewa au kuzaa dhidi ya mjumbe mwingine.

    Wengine wanasimama na kupoteza muda wa mjadala kwa kuhubiri ilani za vyama vyao, itikadi za vyama vyao na hata sera za vyama vyao. Wengine, hasa kwa wajumbe kutoka

    Zanzibar, wamechukua fursa ya mjadala wa katiba kuzusha hisia za kaleta siasa za chuki na za kibaguzi kwa misingi ya Upemba na Uunguja, na hapo ndipo tunaposhuhudia vijembe na mipasho vikishika kasi zaidi ndani ya mjadala wenyewe.

    Lakini pia kwa upande wa b a r a , k wa k u wa w a j u m b e w e n g i w a bunge hili kutoka bara, ni viongozi na wengine wakiwa watendaji wa ngazi za juu wa serikali iliyopo ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, wanaonekana kujadili hoja ya katiba mpya wakibebwa na hisia kali za kulinda nyadhifa na nafasi zao katika mfumo uliopo, hali ya kuwa mjadala ni

    wa katiba kwa maslahi ya Watanzania wote.

    Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa, hisia na matamanio ya kimaslahi ya n a y o o n y e s h wa n a wajumbe wanaojadi l i mjadala wa Katiba mpya, ndio tatizo kubwa katika mjada mzima unaoendelea.

    Tuseme tu kwamba muelekeo uliojionyesha katika hoja hizi zilizojaa matamanio ya maslahi b i n a f s i , m i p a s h o ya mitaani, kejeli, vijembe, porojo na kina namna ya masihara, ni kero kubwa na k ichefuchefu kwa Watanzania ambao ndio wenye katiba yao.

    Haya sio yanayohitajiwa au yaliyokusudiwa na wananchi waliotoa maoni

    yao katika Tume. Kwa msingi huo, tunaona kwamba hata baadhi ya wajumbe wanaojinasibu kuwa wanatoa maoni na hoja zao katika Bunge hilo kwa niaba ya wananchi, yanat ia mushkel i wa kutoaminika.

    Hatufikiri i kwamba mipasho inayoendeleo k a t i k a b u n g e h i l o i n a y o w e k a p e m b e n i makusudio ya mjumbe kuwepo Bungeni, inatoka kwa wananachi.

    Tunachotaka ni mjadala wa hoja makini kuhusu katiba tunayoihangaikia. Watanzania hawakumtuma mtu kutoa mipasho au kuleta masihara kwenye mjadala wa katiba yao.

    Lukuvi atonesha kidondaInatoka Uk. 1

    hofu kuwa yanayotokea Zanzibar ya kuul iwa maaskofu na kuchoma m a k a n i s a Z a n z i b a r yataletwa huku Bara huku akiwanasibisha Masheikh wa Uamsho na uovu huo.

    H a d i s a s a h a k u n a k e s i i l i y o f i k i s h w a mahakamani na kufikia hatma ikionyesha kuwa waliohusika na kuuliwa askofu au kuchomwa makanisa, ni Uamsho.

    Hata hivyo, Mheshimiwa Lukuvi alisifu kauli hiyo ya Mrema na kumalizia kwa kumwahidi kuwa atasukuma masilahi yake apate kuyapata. Hata hivyo hakufafanua ni masilahi gani.

    Awali imeelezwa kuwa Waziri Lukuvi ameanza kupiga kampeni kanisani a k i wa t a k a wa n a n c h i wasikubali mfumo wa muungano wa serikali tatu, ila mbili tu.

    Tukiacha hoja nyingi nyingine alizonukuliwa kutoa kupiga kampeni hiyo, lakini inayotatiza zaidi ni pale aliponukuliwa akidai kuwa Wazanzibari wanaotaka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka Serikali i l i wa p a t e n a f a s i ya kujitangaza kuwa ni nchi ya Kiislamu.

    Na kwamba kufanya hivyo ni kutaka kuleta fujo na kusababisha machafuko jambo l i ta laowafanya Wakristo wasiendelee kuabudu kwa amani.

    N i k a t i k a k u t o a u f a f a n u z i b u n g e n i , akanukuu na kuungana na Mrema kujenga hoja kuwa

    kuna hofu juu ya Uamsho kwamba watahatarisha amani ya nchi.

    Kwamba hatari yenyewe ipo ya namna mbi l i : moja ni suala la Uamsho wanaotuhumiwa kuhusika na uchomaji makanisa.

    Na pili Uamsho huo huo kutumiwa na Chama Cha Wananchi, CUF, katika kuipigania masilahi ya kisiasa, na hasa hili la Serikali tatu.

    Baadhi ya watu wakitoa maoni yao wamesema kuwa ni matarajio yao kwamba watasikia Masheikh wa Uamsho wakitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo.

    W a m e s e m a , w a o wa n a c h o j u a U a m s h o ni taasisi ya Kiislamu i n a y o t o a D a wa h ya kuwaamsha Waislamu, hivyo kuhusishwa na vitendo vya kigaidi kama vilivyotajwa na Mrema na kutiliwa mkazo na Mheshimiwa Lukuvi, ni jambo linalochafua taasisi hiyo na Waislamu kwa ujumla.

    Japo Waislamu kwa ujumla, hasa, kupitia taasisi zao, wanatakiwa kuhoji juu ya kashfa hiyo, lakini Masheikh wa Uamsho wana dhima kubwa zaidi katika kuliweka sawa jambo hili.

    Maoni ya ujumla ya Waislamu ni kuwa, maneno ya Mrema yamewatonesha Waislamu kwa sababu ni Mrema huyu huyu wakati akiwa madarakani alikuja na madai kuwa Waislamu wanataka kulipua baa na guest houses pamoja na kutia sumu katika ulevi.

    A i d h a , n i M r e m a huyu ambaye aliendesha

    k a m p e n i k u b w a y a k u w a d h a l i l i s h a n a kuwatesa Masheikh huku akidai kuwa atawatwanga m a n g u m i w a k a t i alipowarushia tuhuma nzito, akajipa uhakimu, mtoa ushahidi na askari mnyongaji.

    N i k a t i k a k i p i n d i hicho ambapo Waislamu walishuhudia Waislamu w a k i k a m a t w a n a kupachikwa tuhuma za kutaka kulipua makanisa, harakati zilizoishia kwa kuvunjiliwa kwa mbali Baraza la Kuendeleza Usomaji wa Quran nchini (BALUKTA).

    Kwa hiyo aliyosema M r e m a , n i k a m a k u t o n e s h a k i d o n d a ambacho kimebakia kovu, na kitendo cha Waziri Lukuvi kumuunga mkono huku akileta madai kuwa Zanzibar inataka Serikali ya Kiislamu na akitumia hoja hiyo kuwatahadharisha Wa k r i s t o w e n z a k e (Kanisani), ni sawa na ile tahadhari iliyotolewa na Padri Charles Smith wa Marekani.

    Stith aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini miaka ya nyuma, al is imama Kanisani, Chuo Kikuu Dar es Salaam (Mlimani) na kuwataka Wakristo kuchukua tahadhari juu ya Waislamu, kwa maana nyingine akiwaambia kuwa wanaishi na maadui.

    Na tunajua, nini nafasi ya Marekani katika kuwapiga v i ta na kuwahujumu Waislamu duniani katika ile Crusade iliyotangazwa na George W Bush.

    Inaendelea Uk. 5

  • 3 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Habari

    Na Mwandishi Wetu

    Watakiwa kuritadi ili kuwa wananchiK U M B E t a t i z o n i U i s l a m u . H a ya ya ugaidi, Al Shabab ni kisingizio tu.

    Ni katika ule ule mtindo wa kikafiri wa kumpa mbwa jina baya ili upate kumuuwa.

    H a y o n d i y o yanayodhihir i shwa na baadhi ya vyombo vya habari baada ya kushindwa kuficha chuki zao dhidi ya Waislamu.

    Katika kudhihirisha chuki hiyo na kuchochea u h a s a m a b a i n a ya Waislamu na Wakristo, baadhi ya vyombo hivyo vinasema kuwa tatizo kubwa kwa jamii ya Waislamu wa asili ya Somalia ni kuwa hawataki kuritadi.

    Akadai kuwa katika kukataa huko kuritadi na kubaki na mavazi yao ya hi jabu kwa wanawake na kanzu kwa wanaume, Waislamu hao wanakuwa bado hawajawa Wakenya kamili.

    K a t i k a m a k a l a moja i l iyoandikwa hivi karibuni katika gazeti la Daily Nation linalochapishwa nchini K e n y a , i m e d a i w a k u w a v i t e n d o wanavyofanyiwa jamii ya Wasomali Kenya, ni s tahiki yao kwa maslahi ya usalama wa Wakenya.

    Ikafafanuliwa kuwa pamoja na madai ya ugaidi hivi sasa ambapo msimamo wa gazeti hilo ni kuwa Waislamu hao wamedhamiria kuwafanyia ugaidi W a k r i s t o , l a k i n i inaelezwa kuwa msingi wa tatizo ni Wasomali kuwa wagumu kuritadi na kubadili mavazi yao.

    Mwandishi anasema k u w a W a s o m a l i wanaishi kwa kuvaa mavazi yao ya Kiislamu kama vile makanzu n a h i j a b u , h u k u wakiwa hawajulikani

    wanachokificha kwenye mavazi hayo makubwa.

    Makala hiyo kimsingi inaonekana kujaa chuki dhidi ya Waislamu na Wasomali, na mwandishi anahitimisha kwa kutoa w i t o k wa u t a wa l a wa Somalia kuacha kulalamika juu ya vitendo wanavyofanyiwa jamii ya Wasomali, Nairobi, bali iwahimize Wasomali kubadili Dini zao na kuwa Wakristo kama walivyo Wakenya, na wakaacha kuvaa nguo inayowaficha, yaani hi jabu na hat imaye w a k a w a Wa k e n y a kamili. (Soma zaidi Uk. 4)

    TUNDU Lissu ameendelea kuwa mtoa hoja changamoto katika Bunge la Katiba ambapo amekosoa hoja za wanaompa Mwalimu Nyerere sifa za kiungu.

    Kwa upande mwingine, Profesa Ibrahim Lipumba ametibua mambo akisema kuwa bunge linakwenda kombo hali ambayo haitaleta kat iba inayotakiwa na wananchi.

    Amesema, kumekuwa na siasa na kauli za ki-Interahamwe ambapo watu wanabaguliwa kwa kabila zao na kuchochea chuki na uhasama.

    A k a s e m a , h a l i h i y o inatokea bila ya kukemewa badala yake viongozi wakuu wa serikali waliopo bungeni hapo wanashangilia.

    Katika hali hiyo akasema, wao kama watetezi wa katiba ya wananchi, hawaoni haja ya kushiriki kujadili jambo linaloonekana kubeba agenda ya CCM wasiotaka kujali matakwa ya wananchi, lakini kubwa zaidi wasingependa kuwa sehemu ya watu wanaopandikiza chuki na hasama.

    K w a s a b a b u h i y o akaongoza wajumbe wa kundi la kutetea katiba ya wananchi kutoka nje ya bunge.

    K w a u p a n d e w a k e , mheshimiwa Zitto Kabwe ametoa kauli ya kuliweka sawa bunge ambapo baadhi

    Na Mwandishi Wetu ya watu wamekuwa wakitoa kauli za chuki na matusi badala ya kutoa hoja za msingi.

    Japo hakutaja mtu lakini jambo hilo limejitokeza kutokana na baadhi ya watu kutajana kwa majina na kukejel iana na hata kutupiana kauli za chuki na kubaguana kimajimbo (Pemba Vs Unguja) na kabila.

    Kabla ya kusimama Zitto, alizungumza mjumbe mmoja kutoka Zanzibar ambaye alimalizia hoja zake kwa kusema kuwa ukivunjika muungano, wapo watu wataenda kwao.

    Mtaenda kwenu, mtaenda , alisema mheshimiwa huyo huku akikariri kauli hiyo na kuonyesha kukasirika.

    K w a u p a n d e w a k e Mheshimiwa Bi Fathia alisema kuwa wanadau wa serikali mbili wanaodai kuwa wanawakilisha wananchi wa Zanzibar, hawasemi kweli kwa sababu ndio hao hao waliokuwa wakipinga serikali ya umoja wa kitaifa.

    Akasema, kama kuna watu wanaoweza kudai kuwa wanawasemea na kuwawakilisha wananchi w a Z a n z i b a r n i wa l e waliopigania serikali ya umoja wa kitaifa ambao kwa zaidi ya asilimia 60 walipiga kura kutaka serikali ya umoja wa kitaifa huku wana-CCM wakipita mitaani kuipinga na kusambaza propaganda chafu.

    Katika hoja zake Tundu

    Lissu alisema kuwa yeye ha jamtukana Mwal imu Nyerere bali wanaomkosea ni wale wanaompaisha na kumpa sifa za kiungu.

    A l i s e m a , M w a l i m u Nyerere sio Mungu, sio malaika wala hajakuwa mtakat i fu, ndio maana aliunga mkono hatua ya J imbo la Biafra kutaka kujitenga kutoka Nigeria.

    Na akas is i t iza kuwa kumkosoa katika jambo kama hilo, sio kumkejeli au kumtukana, bali kumpa sifa yake ya ubinadamu.

    Alisema, kama alivyosema Dr. Harrison Mwakyembe miaka 20 iliyopita, hakuna namna ya kuwa na muungano ulio imara na usio na kero; zaidi ya kuwa na muundo wa serikali tatu.

    Alisema, kukataa kuona ukweli leo kuwa zilizoungana ni nchi mbili Tanganyika na Zanzibar, na zote zinatakiwa kuonekana zipo kat ika muungano, n i kukataa ukweli ambao unasababisha huko mbele kuwa giza tupu.

    Akiongelea suala hilo, Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema kuwa msingi wa muungano ni maridhiano.

    Na kwamba kama hakuna maridhiano, mfumo wowote, iwe wa ni serikali moja, mbili au tatu unaweza kuvunja muungano.

    Kwa hiyo hoja ya msingi ya kudumisha muungano sio idadi ya serikali, bali kiwango cha maridhiano kilichokuwepo.

    Kwa maana hiyo akataka

    Lipumba, Lissu, Jussawatu wajikite katika kupata mar idhiano, kwani lau kutakuwa na kulazimishana, hata kama itakuwa ni kwa kutumia nguvu kwa kiasi gani, haitaweza kuzuiya muungano usivunjike.

    K w a u p a n d e w a k e Mheshimiwa Ismail Jussa alisema kuwa kama kuna hoja ya msingi ambayo wanatakiwa kuleta watu wanaopigania mfumo wa serikali mbili, ni kueleza ni namna gani Tanganyika itavua koti la Tanzania.

    Akitoa mifano kadhaa akaonyesha jinsi mfumo wa serikali mbili ulivyokuwa wa kinyonyaji dhidi ya Zanzibar.

    K wa m b a k a t i k a ya l e mapato yanayotajwa kuwa ni ya serikali ya mungano, ni asilimia ndogo tu inayotumika katika mambo ya muungano wa k a t i s e h e m u k u b wa hutumika katika mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Bara (Tanganyika).

    Kwa wanaoleta hoja ya udogo na kukosa rasilimali, a k a w a t a k a w a t i z a m e Singapore ilipokuwa na ilipo hivi sasa baada ya kujitenga kutoka Malaysia.

    Wakati huo huo, imetolewa kauli ya kumrudi Augustino Lyatonga Mrema ambaye anadaiwa kutoka kauli ya kuwakashifu Masheikh wa Uamsho.

    A l i p o s i m a m a k a b l a ya kutoa mchango wake, Mheshimiwa Bi Fat hia alimtaka Mrema kuomba radhi kutokana na kauli ya kuwakashifu Masheikh hao akimtaka azingatie kuwa Uamsho ni taasisi ya kidini na sio ya kisiasa.

  • 4 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Habari

    Serikali mbili zilizoboreshwa jitihada ya kutoharisha najisHUWEZI kuitoharisha n a j i s i y e n y e w e , kinachotoharishwa ni kitu kilichonajisika.

    Hiyo ndiyo hoja ya msingi kwa wanaotaka muungano wa serikali tatu.

    K w a u p a n d e mwingine inasemwa kuwa, wanaongangania uwepo wa serikali mbili wamekuwa wakija na porojo za ndekwa na propaganda za kurejea Sultan.

    Baadhi ya wananchi wanaofuatilia mjadala unaoendelea bungeni wanasema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kuwa baadhi ya wajumbe, hasa kutoka Zanzibar kuja na madai ya kurejea usultani.

    M a d a i h a y a y a kurejea sultan ni jambo l i n a l o c h e f u a k w a n i l inaonesha kufi l is ika kimawazo na hoja na pengine kuwadhania wasilikizaji kuwa hawana akili.

    A l i s e m a m s e m a j i mmoja wakati akiongea na mwandishi akionesha kukerwa na alichokiita porojo za baadhi ya watu wanaopinga ho ja za msingi kwa propaganda zisizo na mashiko.

    Amesema msemaji huyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini kwamba, ile kuwa nchi zilizoungana ni mbili, lakini sasa moja haionekani, kwa maana ya Tanganyika, bali Zanzibar pekee, hulifanya jambo lenyewe kuwa ni batili lisilokubalika.

    Ambapo tafsiri yake ni kuwa Tanganyika imekuwa ndio Tanzania wakati Zanzibar imebakia kuwa nchi.

    Na kwamba batili hiyo haiwezi kuondoka kwa kuleta porojo za kurudi sultan.

    K a m a a l i v y o s e m a mjumbe mmoja katika kujadili hoja, ni kwamba iwapo ziliungana Serikali mbili na jawabu likawa serikali mbili, maana yake ni kuwa hakuna kuungana hapo.

    Kama kuungana kupo, basi jawabu lilitakiwa kuwa tatu au moja.

    K a t i k a h a l i k a m a hiyo, maadhali jambo lenyewe limeharibikiwa, huwezi kulitwaharisha

    Na Mwandishi Wetu kwa kuongelea kuondoa kero kwa sababu huo muundo wenyewe ni kero inayotakiwa kuondolewa.

    K a t i k a m s i n g i huo, wakati baadhi ya wajumbe wa Bunge la K a t i b a wa k i c h a n g i a mjadala walisema kuwa katika mambo ambayo ni muhimu ni kwa pazia lililoificha Tanganyika kuondolewa ili Tanganyika ionekane.

    Akichangia hoja hiyo, Waziri wa Sheria wa Zanzibar, Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakari a m e s e m a k u wa h a t i yenyewe ya muungano katika kifungu cha 4 na sita inaelekeza kuwa na mamlaka tatu.

    Kwa maana ya mamlaka ya Tanganyika, mamlaka ya Zanzibar na mamlaka ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania.

    Kwa upande mwingine Mheshimiwa Abubakar akasema kuwa tatizo jingine kubwa la msingi ni kuwa maamuzi yamekuwa yakifanywa na upande mmoja wa muungano.

    Akifafanua akasema kuwa sheria zimekuwa zikipitishwa na Bunge la Jamhuri na hutajwa kuwa likishapitishwa hufanywa litekelezwe Zanzibar pia.

    Akagusia pia suala la fursa ambapo alitoa m f a n o k u wa k a t i k a Wizara za mambo ya muungano mfano wa Wizara ya Mambo ya Nje, waliohodhi nafasi ni watu wa Tanganyika.

    Akagusia pia suala la Afrika Mashariki ambapo Waziri wa masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania katika jumuiya h u w a k i l i s h a h a t a yale mambo yasiyo ya muungano kama kilimo.

    Kwa upande wake Mheshimiwa Mohamed Sanya akichangia hoja hiyo akasema kuwa hali ilivyo hivi sasa ni kwa Zanzibar kukaliwa na kuporwa mamlaka yake na Tanganyika iliyojivika Utanzania.

    Akitoa mfano akasema hata inavyoelezwa hivi leo kuwa baadhi ya kero zimeondolewa inasemwa k u w a Wa z a n z i b a r i tumeruhusiwa, akasema huko ni kudhalilishwa.

    K wa m a a n a k u wa Wa z a n z i b a r h a wa n a uwezo wala mamlaka ya kuamua juu ya mambo yao

    mpaka waruhusiwe.A k a s e m a , k a t i k a

    kul inda mfumo ul iopo wa m u u n g a n o a m b a o kimsingi unawadhalilisha Wazanzibari, kumekuwa k u k i t u m i k a n j a m a z a kuwagawa Wazanzibari ambao kwa sasa badala ya kutoa hoja katika Bunge wamekuwa wakipigana vijembe jambo linalowafanya wajidhalilishe na kujiabisha

    mbele ya wabunge wenzao.Akasisitiza kuwa, wanadai

    kuwa Wazanzibari wanataka serikali mbili hawasemi ukweli na wakitaka kujua ukweli waende wakafanye utafiti Zanzibar hapo ndio watajua kuwa Wazanzibari wamechoka na mfumo huu na hawautaki kabisa.

    Alisema, hali mbaya ya uchumi iliyopo Zanzibar hivi sasa ni kutokana na kuzibwa

    pumzi na lau itapewa fursa ya kuwa na mamlaka kamili, itachukua muda mfupi kabisa kuigeuza Zanzibar kuwa nchi ya neema, mwenyewe akisema Hong Kong ya Afrika Mashariki.

    Na kwamba ikifika hapo wataweza hata kuisaidia Tanganyika nayo iondokane na matatizo yake.

    Vyombo vya habari na chuki za Usomali, UislamuNa Abuu Badriya

    Written in Kiswahili on 13 April 2014.Makala moja iliyoandikwa h i v i k a r i b u n i k a t i k a gazeti la Daily Nation linalochapishwa nchini K e n ya , i m e z u n g u m z i a k u s h a m b u l i w a , kunyanyaswa, kukamatwa na kushikiliwa Jamii ya Wasomali waishio mjini Nairobi nchini Kenya. Makala imeonyesha kwamba vitendo wanavyofanyiwa jamii ya Wasomali Kenya, ni stahiki yao kwa maslahi ya usalama wa Wakenya.

    Kwa ujumla makala hiyo inawanasibisha watu wa jamii ya Kisomali na magaidi hususan al Shaabab huku ikiwatia chuki Wakristo na watu wa Kenya dhidi ya watu wa jamii ya Wasomali wanaoishi nchini humo.

    Kama ni chuki, ni chuki, tangu awal i imewekwa wa z i h a d h a r a n i k a m a alivyotuambia Allah (SWT) katika Qur'an, kuwa chuki waliodhihirisha ni kubwa kuliko ile wanayoyaficha.

    Hata katika lugha ya Kiingereza, linatumia neno "Inciting Hatred".

    Mwandaaji wa makala hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Kwamchetsi Mokokha, a m e t a j a m a s h a m b u l i o yaliofanyika nchini Kenya na kusema kuwa tangu Kenya ilipoishambulia Somalia, yamefanyika mashambulio ya m a b o m u 8 4 k a t i k a maeneo ya Bar na kuwaua Wakenya Wakristo, Sehemu za Migahawa, Makanisani, katika magari ya matatu na katika masoko.

    M w a n d i s h i a n a o n a k w a m b a k u k a m a t w a , kushikiliwa na kunyanyaswa jamii ya Kisomali mjini Nairobi umefika wakati ambapo Wakenya wanatakiwa kulipiza Kisasi.

    Kimsingi , mwandishi anasema kwamba ihsani waliyowafanyiwa jamii ya Kisomali tangu kuanguka kwa

    utawala wa Siad Barre, Kenya iliwakaribisha wakimbizi wa Kisomali, ikawapa vyakula maelfu Wasomali, ikawapa vitambulisho na hati za kuwa Wakenya kamili huku jamii hiyo ya Kisomali ikiifanya Kenya kuwa kituo cha kupita kwenda nchi za nje au mataifa mengine, yaani Transit Point.

    M w a n d i s h i h u y o ameendelea kueleza katika gazeti hilo kuwa wengi wa jamii hiyo ya Kisomali wamesoma na kuchukua shahada zao katika vyuo vikuu vya Kenya, lakini p a m o j a n a k u f a n y i wa fadhila zote hizo, Wasomali wamekuwa si watu walio na moyo mzuri kwa taifa la Kenya na kwamba, tangu miaka ya 1962 Wasomali hao walikuwa wakitaka kujitenga na Kenya na kujiunga na Somalia.

    Mwandishi alieleza kuwa kwa muda mwingi Wasomali wakiwa na pesa zao, wakiwa si watu wa kulima mashamba na kutokuwa na majumba Kenya . Lakin i wakiwa ni watu wa kujaza fedha mifukoni mwao na isijulikane wanakozitoa.

    L a k i n i m w a n d i s h i aliloliona kuwa ni kero kubwa zaidi kwa Kenya, ni kuona jamii ya Wasomali nchini Kenya hawabadilishi Dini zao na hivyo kutokuwa Wakenya halisi.

    "Their Cushitic features have not Kenyanised, their Religion remains unchanged ". liliripoti gazeti hilo.

    A l i s e m a Wa s o m a l i wamekuwa dhaifu sana kubadi l i dini na kuwa Wakristo kama walivyo Wakenya, ambao wengi wao ni Wakristo!

    Anasema kuwa wanaishi kwa kuvaa mavazi yao ya Kiislamu kama vile makanzu na hijabu, huku wakiwa hawajulikani wanachokificha k w e n y e m a v a z i h a y o makubwa.

    M w a n d i s h i p i a analalamika kwamba jamii ya

    Wasomali Kenya hawakubali kuolewa na Wakenya na haijawahi kutokea kuripoti au kuwaarifu Polisi jaribio la mashambulio yeyote i n a y o f a n y i k a , h i v y o kutafsiriwa kitendo hicho k i m e s a b a b i s h a P o l i s i kushtuka linapofanyika shambulio.

    H i v y o W a s o m a l i wa k i s u m b u l i wa k a m a inavyofanyika sasa na kwamba huo ni ujumbe tosha kwa Al-Shabab na mashambulio yatapungua Kenya.

    K a t i k a m a k a l a ya k e ambayo kimsingi inaonekana k u j a a c h u k i d h i d i ya Waislamu na Wasomali, Mwandishi amehitimisha kwa kusema kuwa, "haipaswi Wasomali kulalamikia hatua zinayochukuliwa na maofisa wa usalama, lakini utawala wa Somalia kwa upande wake inatakiwa kuwahimiza watu wake kubadili Dini zao na kuwa Wakristo kama walivyo Wakenya, na wakaacha kuvaa nguo inayowaficha, yaani hijabu na hatimaye wakawa Wakenya kamili. Anahitimisha kwamba hiyo ni sehemu au hatua pekee inatakayowafanya kuwa Wakenya.

    Y a w e z e k a n a yaliyoandikwa na mwandishi ni maoni ya mtu, lakini yatosha kuwa j ibu kwa yanayofanywa na Serikali ya Kenya katika Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi.

    Ripota wa Al Jazeera M k e n ya m we n ye a s i l i y a K i s o m a l i , a l i w a h i kunukuliwa akisema we are not yet Kenyan huku akibubujikwa na machozi.

    H a t a h i v y o kinachodhihirika sasa kwa Wakenya wenye asili ya Kisomali na hata Wasomali wakimbizi waliopo Kenya, n i k wa m b a Wa s o m a l i wengi walioacha fikra pevu watakuwa wanajua kuwa Makafiri siyo Adui wa Al-Shabab pekee.

  • 5 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Habari za Kimataifa

    MOGADISHUSERIKALI ya Somalia imetoa wito kuitaka s e r i k a l i y a K e n y a kusitisha operesheni tata ya usalama dhidi jamii ya Kisomali huko Eastleigh, imeripoti Redio RBC ya Somalia.

    Wito huo umetolewa wiki iliyopita kufuatia taarifa iliyotolewa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri, ambapo Naibu Waziri Mkuu, Ridwan Hirsi Mohamed, alisema serikali ilishatuma barua ya malalamiko kwa serikali ya Kenya.

    Serikali ya shirikisho ya Somalia inatiwa wasiwasi

    Somalia, HRW zatoa wito kukomeshwa msako dhidi ya Wasomali

    sana juu ya msako wa polisi wa Kenya dhidi ya watu wenye asili ya Kisomali mjini Nairobi.

    Somalia imeiomba K e n y a k u b a d i l i s h a dhumuni la operesheni yake ji j ini Nairobi na ku j iepusha na hatua yoyote ya chuki dhidi ya raia wa Somalia wanaoishi nchini Kenya. Alibainisha Bw. Mohamed

    Shir ika la hak i za b inadamu la Human Rights Watch (HRW) pia ilitoa taarifa siku ya Ijumaa ikiakisi wito kwa vikosi vya Kenya kusimamisha msako wake dhidi ya Wasomali.

    Taarifa hiyo imetoa wito mahsusi wa kusitishwa ukamataji watu hovyo na kuwaweka ndani, pamoja na vitendo vya udhalilishaji na kurejeshwa watu kwao kwa nguvu na unyanyasaji mwingine.

    Watafiti wa wakimbizi wanasema kuwa kitendo cha serikali ya Kenya kuwadhalilisha watu wa jamii ya Kisomali kwa kuwafanyia mashambulizi ya kinyama, huku ikielezwa k u wa m a s h a m b u l i z i hayo yanafanywa na wa t u wa s i o j u l i k a n a , hakitawalinda Wakenya, Wasomal i au yeyote m w i n g i n e d h i d i y a

    IDARA ya polisi mjini New York Marekani, imefunga kitengo chake maalum c h a u j a s u s i a m b a c h o huwapepeleza Waisilamu ili kuchunguza kama kuna tisho lolote la ugaidi.

    Kitengo hicho kilikuwa kinatumia polisi waliokuwa wanavalia nguo za kiraia kusikiliza kisiri mawasiliano ya simu kati ya Waisilamu na hata kuzuru maeneo yanayotembelewa sana na Waislamu.

    Waisilamu hawatapelelezwa tena New YorkV y o m b o v ya h a b a r i

    nchini Marekani vinasema kuwa kitengo hicho kiliwahi kushitakiwa mara mbili kwa mbinu zao za ujasusi na pia kulaaniwa na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.

    Pia kiliwaghadhabisha Wa i s i l a m u h a s a k w a

    kuwachunguza.Mageuzi haya ni hatua

    m u h i m u s a n a k a t i k a kuondoa hali ya wasiwasi na kutoaminiana kati ya polisi na jamii ili jamii iweze kusaidia polisi kuwashika wahalifu, ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya Meya wa New York Bill de Blasio.

    mashambulizi zaidi. H a t u a y a K e n y a

    kuwarejesha Wasomali k w e n y e n c h i y a o iliyolemewa na mgogoro b i l a ya k u wa r u h u s u kuomba hifadhi itakuwa ni uvunjaji mkubwa wa wajibu wake wa kimataifa. Alisema Mtafiti Mkuu wa Wakimbizi, Gerry Simpson.

    Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Right Watch, lilisema k u w a l i m e t e m b e l e a k i tuo cha pol i s i cha Pangani huko Eastleigh na kugundua mamia ya washukiwa wakiwa wa m e j a z wa k w e n y e vyumba vilivyopangiwa kwa ajili ya watu 20.

    Taarifa ya shirika hilo ilieleza kuwa mahabusu w a m e k u w a h a w a n a sehemu ya kukaa na vyumba walivyolundikwa

    vilikuwa vinanuka mikojo na kinyesi. Taarifa hiyo ya HRW iliongeza kuwa P o l i s i wa l i k u wa p i a wanawashikilia mahabusu nje ya muda wa saa 24 unaoelezewa na sheria za Kenya bila ya kuwafikisha mahakamani.

    Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alitetea operesheni hiyo ya usalama akisema kwamba lengo lake ni kuwangoa wahalifu.

    Alisema kitendo cha kuwauliza watu wao ni nani, wanatoka wapi na kwa nini wapo Kenya si uhalifu.

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Joseph Ole Lenku, alisema zaidi ya watu 4,000 wameshakamatwa hadi sasa kwenye operesheni hiyo.

    Alisema wengi wao wameshaachiwa na 82 walirejeshwa Mogadishu na kwamba, mamia ya wengine bado walikuwa w a n a c h u n g u z w a utambulisho wao.

    H a t u a y a k u s i t i s h a mpango huo, ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi wa kituo hicho, na inaonekana kama njia moja ya kubadili mbinu za kukusanya ujasusi ambazo wengi wanasema zilichangia mashambulizi ya Septemba 9/11

    K i t e n g o h i c h o ,

    kilichoanzishwa mwaka 2003, na baadaye kuitwa, Zone Assessment Unit kilipeleleza Waisilamu hasa maeneo walikofanya kazi, kuswali, kununua m a d u k a n i n a h a t a mikahawa walikokuwa wanakulia.

    Wakuu wa kitengo hicho wanasema kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano kati ya jamii na polisi.

    Lukuvi atonesha kidondaInatoka Uk. 2Hata hivyo, wakati Mhesh imiwa Lukuvi akiwashutumu Uamsho kuwa wanatumiwa na chama cha siasa kupigania masilahi ya kisiasa, yeye pia kama alivyojieleza mwenyewe, ametumia Uwanja wa Kikr is to , Kanisa, Maaskofu na waumini wao, kupigia debe serikali mbili.

    Pengine hapa panaweza kuulizwa swali, kama msimamo wa Uamsho ni serikali tatu, na msimamo huo huo ndio wa chama fulani cha siasa, na kama msimamo wa serikali mbili ndio msimamo wa CCM, chama cha Mheshimiwa L u k u v i , n a L u k u v i anasimama Kanisani , kuwashawishi Wakristo na Maaskofu, kuunga mkono msimamo wa CCM; tatizo hapa ni watu wa dini kutumiwa na wanasiasa

    au nani anawatumia?Kama suala ni taasisi

    z a k i d i n i k u t u m i wa kupigania serikali tatu, mbona Lukuvi na CCM wanatumia Wakr is to na Makanisa kupigania msimamo wao?

    Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, Mheshimiwa wa Rais Kikwete alisema kuwa a m e c h u k u a u s h a u r i wa mtu wake wa dini anayetaka msimamo wa Serikali mbili.

    N a m t u w a d i n i a l i y e j i t o k e z a w a z i kupigania msimamo wa serikali mbili ni Mhashamu Polycarp Kardinali Pengo.

    N a h a t a m j u m b e mmoja wakati akichangia Bungeni, alisema kuwa anapingana na Kadinali

    Pengo kwa sababu kama ni kufuatwa cha kufuatwa ni masuala ya kidini, lakini katika masuala ya kisiasa hata kule Rwanda wapo Maaskofu Katoliki walipotoka wakaingia katika kundi la wauwaji na akataja baadhi yao kwa majina.

    Sasa watu wanajiuliza, kama tatizo ni watu wa dini au taasisi za kidini kutumiwa na wanasiasa katika masuala la kisiasa, mbona hi l i la Pengo halisemwi?

    Lakini wakati Lukuvi a k i w a t a h a d h a r i s h a W a t a n z a n i a k u w a wajiepushe na wanaotaka serikali tatu akidai kuwa wanataka utawala wa Kiislamu, Mwenyekiti wa B u n g e l a K a t i b a

    alimsimamisha Askofu Mstaafu wa Kanisa la A n g l i k a n a , D o n a l d Mtetemela, ndani ya Bunge kutetea Mfumo wa Serikali mbili, je, tuseme na hawa wanaotaka serikali mbili wanataka kusimamisha serikali ya Kikristo?

    Kule Arusha kulitokea mlipuko Kanisani wakafa watu. Japo zilitangulia porojo na madai kuwa mhusika alivaa kanzu na kibandiko , lakini m t u h u m i w a n a m b a moja aliyekamatwa na Polisi alikuwa na jina linaloashiria vinginevyo.

    Mpaka hivi leo hatujui kesi ile ya mtuhumiwa Victor imeishia wapi!

    K u l e Z a n z i b a r , n i kweli yaliwahi kutokea matukio ya kuchomwa

    moto makanisa na hata kuuliwa Padiri. Mpaka leo hakuna ushahidi uliwahi kutolewa na kujulikana nani walihusika!

    Lakini pia kuliwahi kutokea matukio ya utata ambapo ilidaiwa kuwa k a n i s a l i m e c h o m wa moto kule Kianga, lakini uchunguzi wa kipolisi ukaja na mambo ya utata.

    Katika mazingira haya ya utata, ukianzia na lile la Arusha ambapo h a t u a m b i w i k e s i ya mtuhumiwa Victor au uchunguzi wa Polisi , ambapo serikali iliahidi k u w a i t a f a n y a k i l a l i w e z e k a n a l o k u j u a kilichotokea; imeishia wapi, lakini tunaletewa t u h u m a z i l e z i l e z a k u w a p i g a m a d o n g o Waislamu, hii inaleta utata mwingi.

    Waislamu wanatakiwa k u w a m a k i n i n a kuyatizama mambo haya kwa undani na kwa jicho pevu.

  • 6 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Makala

    K A R I B U n a j i j i l a Jalalabad, mnamo mwaka 2001 wakati utawala wa Kiislam wa Taliban ulivyokuwa hatamuni. Hata kamera zilipigwa marufuku katika utawala huo. Taliban walikuwa washatangaza vita tukufu kwa yeyote mpinzani wao.

    M wa n d i s h i h a b a r i wa Kiengereza akiwa amevalia Burka huku akiendesha punda wake alikuwa tayari kuchukua jukumu zito la kisiri katika sehemu hii ya Afghanistan iliyokuwa ikitawaliwa na Taliban.

    Alijiingiza katika nchi kinyemela, hakuwa na kitabu cha utambulisho w a k a t i w a k u s a f i r i (paspoti) wala viza. Vipi ni jasusi wa Kimarekani?

    H a k u n a a m b a e a l i w e z a k u s e m a n a k u g u n d u a m p a k a pale yasiyotegemewa yal ipotokea . Kamera ambao alijitahidi kuificha kwa ustadi katika burka lake i l imdondoka na kuonekana na askari wa kitaliban ambae hakuwa mbali nae. Akatumia siku sita katika makao makuu ya usalama wa taifa kule Jalalabad kabla ya kupelekwa katika (chuo cha mafunzo) gereza la Kabul ambapo kitanda kilikuwa ndani ya selo chafu yenye kachumba kadogo kisicho na maji. Fikra zake zilimtuma kufanya matayarisho ya mwili wake kwa ajili ya zana mbali mbali za mateso kama za umeme, bakora, na hata kupigwa mawe mpaka kufa.

    L a b d a a l i f i k i r i a n a w a z i d i u j a n j a wataliban! Kwani Yvonne aliahidi kuisoma Quran kama ataachiwa huru. Kule kwao Uingereza, mumewe aliangua kilio kutwa kucha pindi tu aliposikia kuwa Yvonne yuko katika mikono ya Wataliban.

    Mikononi mwa TalibanAliachiwa baada ya kuahidi kuusoma Uislamu

    Na Rashid Abdallah, MUM

    YVONNE Ridley Mwandishi aliyekamatwa na Taliban kwa ujasusi kisha akasilimu.

    Taliban ni utawala wa siasa kali, nadhani watafikiri ameenda kule kwa ajili ya kupeleleza. Alisema mumewe.

    Yvonne Ridley alizaliwa m w a k a 1 9 6 8 h u k o Stanley, County Durham, U i n g e r e z a . A l i k u l i a makuzi ya Kiprotestanti katika kanisa la Uingereza. A l i k u w a m w i m b a j i mzuri tu kanisani na pia mwalimu wa mafundisho kwa watoto kanisani katika kijiji chao hicho kilichopo kaskazini mwa nchi hiyo.

    B a a d a e , a k a w a mwandishi wa habari katika gazeti la Sunday Express . Kwa miaka ipatayo kumi Yvonne a m e k u w a a k i f a n y a kazi kat ika magazeti mbalimbali yenye hadhi kama vile The Sunday Times, The Observer, Daily Mirror na Independent. M w a n a h a b a r i h u y o ambaye alishawahi kupata tuzo, pia amefanya kazi kama mrusha matangazo, mtayarishaji vipindi na pia mtangazaji katika vipindi na mashir ika tofaut i kama BBC TV na redio, CNN, ITN na Chalton TV akisafiri sana Afghanistan, I r a q n a P a l e s t i n a . Tukirudi katika tukio lake akiwa mikononi mwa Wataliban, Yvonne Ridley akaanza kuwa mkaidi. Nikawa mbaya kwa walioniteka, niliwatemea mate, mkaidi na nikagoma k u l a . K u S e m a k we l i sikuvutiwa na Uislam hata kidogo mpaka pale nilipokuwa huru kutoka k a t i k a m i k o n o h i i . Alisema.

    Mmoja kati ya wale waliomteka alimuomba awe Muislam akakataa, l a k i n i h a t a h i v y o akaahidi kama akiachwa huru ataisoma Quran. N i l i t o a a h a d i k wa Sheikh Wakitaliban kuwa nitausoma Uislam kama nikiachiwa. Nil isema hayo baada ya kuulizwa kuhusu utayari wangu katika kuukubali Uislam na nikahofia kutoa jibu la ndio au la hapana kwani iliwezekana majibu yote yakaeleweka vibaya na kutafutiwa sababu tu ya kupigwa mawe na kufa.

    Siku kadhaa baadae Yvonne aliachwa huru bila kuumizwa kwa amri ya Mullah Omar, kiongozi wa kiimani wa Taliban ambaye ni mwenye jicho moja. Kuhusu elimu na imani

    yake ya awali kuhusu Uislam, Ridley alisema Sijui kitu kwani hata nikielezea nijuayo sidhani kama naweza jaza kile kikaratasi cha stempu. Ila ningeweza kuelezea yale yote yaitwayo maovu na ubaya wa Uislam kama unyanyasaji wa kijinsia, vipi ilivyo dini chafu na mbaya iliyojaa siasa kali. Lakini baada ya kuisoma Quran katiba impayo haki mwanamke (magna carta for women) kama alivyoiita mwenyewe, Yvonne akaamua kusilimu mwaka 2003 katika majira ya joto, ikiwa ni miaka miwili na nusu tu baada ya kukamatwa kwake.

    Aliacha vileo mwaka mmoja kabla ya kusilimu. Na kwa kwel i huwa anajisikia fahari sana pale asikiapo mtu wa kwanza kus i l imu a l ikuwa n i mwanamke naye ni mke wa Mtume (Khadijah bint Khuwailid) na asikiapo kuwa shahidi (aliyekufa kwa aji l i ya dini) wa kwanza pia alikuwa ni mwanamke (Sumayya).

    Y v o n n e a n a p e n d a kuvaa hijab. Inaieleza dunia kuwa mimi sasa ni Muislam: usinipige, usiniongeleshe ovyo, usinialike katika vilevi wala nyama ya nguruwe; n a k a m a u k i h i t a j i

    tuzungumze yatupasa kuzungumza mambo ya msingi tu. Na mpaka sasa sikumbuki lini ilikuwa siku ya mwisho mtu kunitania utani mchafu, napenda waendelee h ivyo. Alisema.

    Akishangazwa na ukweli wa Q u ra n , a l i s e m a , Niliathirika sana na nilichokuwa nakisoma- hakuna hata kanukta kalichobadilishwa (katika Quran) kwa miaka zaidi ya 1400 sasa. Akilinganisha h a k i z a w a n a w a k e kutoka katika Quran na zile wanazoziita haki kule Magharibi, Ridley alinena, Kitu cha kwanza kukifatilia katika Quran kilikuwa ni sheria za ndoa, talaka na mali.

    N i k a s h a n g a z w a sana. Nilifikiri (Quran) imeandikwa na wakili wa sheria kutoka Hollywood (eneo Marekani maarufu na mahsusi kwa ajili ya matengenezo ya filamu).

    Kwa kweli, ni kutoka humu ndio wamepata wanayoyadai. Katika kut imiza ahadi yake aliyoitoa kule gerezani, i l i m b i d i a p a t e k a z i ya kuzunguuka kwa wanazuoni mbali mbali

    waaminikio wa Kiislam kwa ajili ya utafiti zaidi wa Uislam.

    Alikwenda kwa dokta Zaki Badawi kwa ajili ya ushauri na ufafanuzi; akagaiwa vitabu vingi vya Sheikh maarufu Abu Hamza Al-Masri ambae alionana nae baada ya wote kuhutubia katika majadiliano (debate) ya pamoja kule Oxford. Pia ameweza kumsikiliza na kuonana nae Dkt. Muhammad Al-Massari, kumuelezea masuala k a d h a a y a U i s l a m . Kuusoma kwake Uislam kulipelekea kuja kusema haya:

    Hii Quran imeweza kuandikwa jana kwa ajili ya leo. Inaweza kukaa pamoja na mwanaharakati yeyote wa mazingira, ni rafiki mzuri wa mazingira na ni wazo kuu kwa ajili ya karne hii ya 21, chakushangaza haijabadilika hata neno moja tangu iandikwe sio k a m a h a y a m a t a b u mengine makubwa na mazito yanayotazamiwa kuja kuleta tija.

    Badiliko lake lilikumbana na mitihani na vikwazo vigumu, yote ni tu kwa kuwa ameamua kuwa muumini mzuri wa Uislam avaaye hijab. Kulikuwa na dereva wa taxi aliyesema, Usiache bomu katika s i t i y a n y u m a n a kuuliza, Wapi ambapo Bin Laden amejificha? Ridley ameandika kitabu kilichobeba jina la In the Hands of Taliban(Mikononi M w a W a t a l i b a n ) k i l i chochapishwa na R o b s o n B o o k s h u k o Uingereza. Kitabu kingine alichotunga ni Ticket to Paradise (Tiketi Kuelekea Peponi). Baada ya kusilimu tu Ridley alienda kuhiji.akieleza yaliomsibu akiwa anahiji, Ridley alisema:

    Hija ni zoezi zuri na la kushangaza. Kwa yeyote ambaye bado hajabahatika kuhiji namuusia afanye hivyo upesi. Inakuonesha mizizi ya Uislam. Kwangu mimi jambo hili si la kusahaulika kamwe. Siku moja nilikuwa naharakisha kuwahi jamaa (swala kwa pamoja na waumini wengine) ya swala. Nikiwa napita katika mitaa yenye kona nyingi kuelekea Haraam (msikiti mtukufu wa Makkah). Walikuwa malaki kama mie tukiwahi kuielekea swala. Ikawa vurugu njiani kwa kweli- kwani kila mtu alikuwa akisukuma sukuma ili aharakishe kufika katika

    Inaendelea Uk. 8

  • 7 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Makala

    Inaendelea Uk. 12

    KILA kipindi cha historia k i l i c h o h u s i s h w a n a kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na mapatina (wenza) - vitu au watu, kwa njia yoyote ile - ama kwa kuabudu masanamu na kuyapa sifa za kiungu, au kwa kuwavisha uungu wanadamu wenzao au kuusingizia ulimwengu au vyanzo vingine vya kidunia wa kuumba - ni giza tupu. Hivi ndivyo ilivyo kwa sababu pindi imani ya Umoja au Upweke wa Mungu (s.w.t.) ikitolewa katika moyo, akili na roho huingia giza, viwango vyote hubadilika na vitu na dunia hutazamwa kwa mitizamo bandia. Hali kimaadili, kiroho, kijamii, n a h a t a k i u c h u m i n a kisayansi ya jamii ndiyo i n a y o e l e z e wa n a a ya ifuatayo ya Quran kuwa ni hali ya (jahiliyya):

    Au ( a m a l i z a o z i l e m b a ya ) n i k a m a g i z a katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone (kwa kiza kilivyoshtadi). Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na Nuru kamwe hatakuwa na nuru. (Surat An-Nur, 24:40)

    Mimi sipendi kuelezea mambo ya uongo. Isitoshe, ni upotofu ulioje kwangu mimi kuuelezea uongo wakati ukweli unaweza kuelezewa? Kwa mujibu wa maneno Yake Mwenyewe Mwenyezi Mungu (s.w.t.), Amesema hivi:

    Basi huyo ndiye Mwenyzi Mungu, Mola mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada ya (kuiacha) haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa? (Suratu Yunus, 10:32)

    Hata hivyo, ili tuliweke wazi somo hili, ninaona ni lazima niseme machache kuhusu zama za ujahiliya, yaani kabla Uislamu haujaja.

    M t u m e M u h a m m a d (S.A.W) alikuja katika wakati ambao watu hawakujua dini ya ukweli, na kwa hiyo waliabudu masanamu ya watu hawakujua dini ya ukweli, na kwa hiyo waliabudu masanamu ya udongo, mkate na hata ya jibini kama inavyosema Qur aan:

    N a o , b a d a l a y a M w e n y e z i M u n g u , wanaabudu wasio wadhuru (wanapoacha kuwaabudu) w a l a k u w a n u f a i s h a ( w a n a p o w a b u d u ) , n a wanasema; hawa (waungu wadogo, washir ika wa Mungu! Tunaowaabudu) ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa taala ametakasika na upungufu wa kuhi ta j i mshirika) na ametukuka na hao wanaowashirikisha naye (Surat Yunus 10:18)

    Muhammad (S.A.W.) alitumwa aje kuwa Rehma kipindi cha giza cha Ujahiliya

    Walichonga masanamu ya mawe, udongo, mkate, na hata jibini, nao wakasema hivi: Hao ni waombezi w e t u k w a M u n g u , walikuwa duni kwa fikra na maadili kiasi kwamba, kama alivyoripoti Abu Dharr Al-Ghafiri kuwa, wanaweza kuketi ili kula chakula, na wakayakatakata masanamu yao vipande vipande kisha wakayala. Kisingizio pekee waliochukuwa nacho kwa u jah i l iya (u j inga) wao huo, walisema kwamba wal ikuwa wanafafanua nyanyo za mababu zao, kama inavyosema Qur aan:

    N a w a n a p o a m b i w a : fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wao husema; bal i tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu, je hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka (watawafuata vivyo hivyo kiupofu)? (Surat Al- Baqarah 2:170)

    H a t a wa l i f i k i a h a l i ya kuwazika watoto wao wanawake huku wkiwa wahi, kama inavyosema Quran:

    N a M m o j a w a o a n a p o p e wa h a b a r i ya kuzaliwa kwa msichana, uso wake husawijika, naye kajaa majuto. Akawa anajificha usionekane na watu kwa ubaya wa habari alizoambiwa (kuhusu kuzaliwa mtoto wake wa kike)! Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni (kaburini),

    ilhali bado mzima, ili afie kaburini kwa kukosa hewa)? Tazama uovu wa j ins i wanavyohukumu! (Surat An-Nahl, 16:58-59)

    Kabla ya kuja kwa Uislamu, wanawake walidharauliwa na kunyanyaswa, siyo katika nchi za Arabuni tu bali pia katika nchi za Kirumi na Uajemi (Watawala wa Sassan, huko Persia (Uajemi) mnamo miaka ya 211-651A.D.). Quran inatangaza wazi wazi kuwa wauaji hao wote watakuja kuulizwa juu ya haya:

    Na mtoto msichana aliyezikwa hali ya kuwa alikuwa hai atakapoulizwa, Kwa kosa gani aliuliwa? (Surat At-Takwiyr, 81 :8-9)

    S iku moja , baada ya kutangazwa Unabii wa M u h a m m a d ( s . a . w . ) , m m o j a w a M a s a h a b a zake alimwendea Mtume (s.a.w.), na akamhadithia alichomfanyia binti yake, kama ifuatavyo:

    E w e M j u m b e w a Allah (s.w.t.)! Nilikuwa na Binti yangu. Siku moja n ikamwambia mamake amvishe nguo, kwa kuwa nilikuwa nampeleka kwa mjomba wake. Masikini mama huyo alijua maana ya maneno hayo, hakuweza kufanya lolote zaidi ya kutii na kulia tu. Mke wangu akamvalisha binti huyo nguo nzuri, na binti mwenyewe a l i k u w a a n a f u r a h i a kwenda kwa mjomba wake.

    Nilimpeleka karibu ya kisima na nikamwambia atazame k i s i m a n i . N i k a m p i g a teke kuelekea kisimani. Alipokuwa akiangukia chini alikuwa akilia (Baba, Baba!

    K a d i r i h u y o S a h a b a a l ivyokuwa akis imul ia hadithi hii, Mtume (s.a.w) alikuwa akilia kwa kwi kwi kama vi le ni yeye aliyempoteza ndugu yake wa damu wa karibu kabisa.

    Nyoyo zilikwisha kuwa sugu. Ki la s iku shimo l i l i c h i m b wa j a n g wa n i ili azikwe hai msichana asiyekuwa na hatia yoyote. Wa n a a d a m u wa l i k u wa wakatili zaidi kuliko hata fisi. Wenye nguvu walikuwa wakiwateketeza wasio nguvu na wadhoofu. Ilikuwa ni wakati ambao unduli ulikuwa kawaida ya wanadamu, ukatili ulidhihirishwa, wenye kiu ya damu walitukuzwa, kumwaga damu kulihesabika kuwa ni sifa, zinaa ya watu wenye ndoa na wasiyokuwa na ndoa ilikuwa ni kawaida zaidi kuliko ndoa ya kisheria. Miundo ya familia ilikwisha kuharibiwa.

    Kipindi hiki cha giza n d i c h o k i l i c h o f u a t i wa na Uislamu. Na baki ya kuondosha maovu yote mengine, Mwenyezi Mungu (s.a.w) hakuacha kurudia katazo la kuua watoto wadogo, kama inavyosema Quran:

    Sema: njooni nikusomeeni

    aliyo kuharamishieni Mola wenu mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayoonekana, n a ya n a y o f i c h i k i k a n a . W a l a m s i u w e n a f s i ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki, hayo amekuusieni ili myatie akilini. ( surat Al-An`aam, 6:151)

    MAISHA YA MTUME (S.A.W). KABLA HAJAPATA UNABII.

    Mtume (s.a.w.) alilelewa c h i n i y a m a c h o y a Mwenyezi Mungu (s.w.t) na uangalizi Wake. Baba yake, Abd Allah Ibn` Abd al Muttalib alikufa kabla ya Mtume (s.a.w.) hajazaliwa, ambayo ilimaanisha kuwa aliiweka imani yake yote kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na akajisalimisha kwake kikmailifu. Alilizuru kaburi la baba yake kule Madini miaka mingi baadae, akalia sana na aliporejea alisema.

    Nilimlilia babangu na nikamwomba Allah (s.w.t) amsamehe.

    B a a d a ya k u f a b a b a yake, Allah (s.w.t) akawa amemwondoshea msaada wote wa kibinaadamu, na akamwongoza atambue kuwa hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu ( s.w.t) ambaye hana mshirika hata mmoja.

    Babu yake, Abdu al Muttalib, na ami yake abu Talib Ibn Abd` al Muttalib walimlinda kwa kiasi fulani, lakini yeye mwenyewe alikuja kutambua kuwa mlinzi wake halisi ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) nyuma ya kila tukio na kila chanzo na athari, yeye aliweza kutambua kuna mkono wa muumba mmoja tu, (s.w.t) wa ulimwengu na wa vyanzo. Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ilidhihirishwa kwake kwa njia ya umoja kiungu. Yaani, atajaribiwa katika dunia hii kwa busara, ambamo vyanzo na njia vina mchango katika kila fanikio, na kwa hivyo mtu sharti atumie vyanzo na njia za kidunia na achukue tahadhari zote muhimu ili apate kufanikisha kitu chochote. Lazima itabidi amtegemee kikamilifu Mola wake (s.w.t.) na amuombe Yeye msaada wowote, na kwa njia hiyo aonyeshe wazi kuwa ni Allah (s.w.t.) peke Yake Ndiye huumba matokeo na hutoa mafanikio.

    Baada ya kufariki babake, alianza kuitwa Lulu Yatima Isiyo, Mfano (Matchless Orphan Pearl) . Kuhusu hili, Allah (s.w.t.) baadaye. Alisema hivi:

    Na Mola wako Mlezi Atakupa mpaka uridhike. Kwani hakukukuta yatima Akakupa makazi? Akakukuta mhitaji Akakutosheleza?

  • 8 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Makala

    VIJANA wengi nchini wamekuwa wakitumia m a d a wa ya k u l e v ya kiasi kwamba mpaka taifa linachanganyikiwa kwa uwingi wa vijana kujitumbukiza katika janga hilo.

    Pamoja na juhudi kubwa kuchukuliwa kudhibiti uingizaji wa dawa hizo hapa nchini, lakini bado kabisa Serikali inaonekana k u z i d i wa u j a n j a n a mtandao wa uingizaji wa madawa hayo.

    Tunaona juhudi za vyombo vyetu vya usalama kujitahidi kudhibiti kila eneo ambalo ndio njia kuu ya upitishaji wa unga, lakini inaonekana unga bado unapitishwa kwa wingi hapa nchini.

    Kwa nini nasema hivyo, tunawaona vijana wengi katika vituo vya mabasi wakiyumba huku wengine wakijidunga na mabomba ya sindano bila hata woga wa kukamatwa na askari.

    Katika Tanzania miji mikuu ambayo inaongoza kwa utumiaji wa madawa hayo ni Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Mbeya maeneo haya yamekithiri kwa kuongoza kwa vijana wengi kutumia madawa hayo hatari ya kulevya.

    Mwandishi wa makala hi i a l ipata nafas i ya kufanya mahojiano na N u r u S a l e h H e m e d ambae ana umri wa 31 yeye alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya kwa kipindi cha miaka kumi na moja na sasa ameacha kabisa.

    Nuru amesema kuwa utumiaji wa dawa hizo alianza kutumia baada ya kuolewa na mumewe w a k i w a T u n d u r u Mkoani Ruvuma Nuru amesema mumewe ndie alie mshawishi kutumia madawa hayo mpaka kufikia kupoteza malengo yake kibao.

    Amesema kuwa baada ya kumshawishi kutumia madawa hayo yalimzowea m p a k a k u f i k i a t e j a lililo kubuhu amesema aliwambia wazazi wake k u w a a m e s h a c h o k a kuishi na mume wake huyo maana kwa sasa anataka kuacha utumiaji wa madawa.

    Wazazi walimsikiliza ikafikia ndoa yao ivunjwe na mumewe akatoa talaka ameeleza kuwa baada ya kuachika alikuja Jijini Dar

    Nuru Saleh atoa somo kwa matejaNa Mwandishi Wetu

    Nuru Salehe Hemed Mkurugenzi wa PEDDREF.

    es Salaam maana kule Tunduru unga ulikuwa haupatikani pamoja na kuacha bado alikuwa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.

    N i l i p o f i k a D a r e s S a l a a m n i l i f i k i a K a r i a k o o k wa b a b a nikawa naendeleza uteja nimeshafungiwa ndani lakini nil iruka ukuta n ikaondoka v i j iweni kubwia unga, amesema Nuru.

    Pamoja na utumiaji wa madawa hayo kuna s iku a l ikaa akai jut ia nafsi yake sasa anataka kuacha utumiaji dawa hizo maana ilifikia hatua anadharauliwa hata na watoto wadogo na mtoto wake alikuwa akicheza na wenzake wanamwambia mama yake teja.

    Alihangaika hospitali k u p a t a t i b a l a k i n i i l i shindikana kuacha baada yakushindikana hospi ta l in i n i l i funga safari mpaka Zanzibar kwenye kituo cha kulelea wanawake waliyo athirika na madawa ya kulevya kituo ambacho kilikuwa kinaongozwa na mama Fatma Sukwa.

    Amesema kuwa hiyo

    ilikuwa mwaka 2012 na alikaa huko kwa muda wa mwaka moja na miezi mitatu amesema kuwa wakati akiwa hapo alipata elimu mbalimbali kuhusu

    athari zitokanazo na dawa za kulevya.

    Ameeleza kuwa wakati akiwa huko alijifunza mambo mengi ik iwa pamoja na kuj i funza mambo ya ujasiriamali.

    Amesema baada ya muda mwingi kuwepo Zanzibar katika kituo hicho ambacho kinajulikana kwa jina la Soba House a m e s e m a b a a d a ya kupona alirudi jijini Dar es Saalam ambapo amesema alijikuta ana dhima kubwa ya kuwakomboa vijana wenzake ambao bado wapo katika janga hilo.

    A m e s e m a k u w a aliwaeleza wazazi wake kuwa anataka kuwa balozi kuwakombowa vijana wenzake wazazi wake walimsikil iza al ianza kufungua kituo cha kutoa elimu kwa vijana waliyo katika janga hilo.

    Nuru amemwambia mwandishi wa makala hii kuwa kituo hicho ambacho kipo Vijibweni wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kinajulikana kwa jina la People with D r u g D e p e n d e n c e R e l i e f F o u n d a t i o n (PEDDERF) amesema kuwa amewakusanya

    vijana wenzake zaidi ya mia moja na arobaini kati ya hao wamepata elimu pamoja na kutumia dawa na wamepona kabisa na wengine wapo mtaani wanafanya mambo yao na hawatumii tena madawa hayo.

    Nuru ameitaka Serikali kuwapa elimu vijana wote ambao wameathiriwa na dawa hizo isiangalie kwa waagiza j i tu au k wa wa u z a j i m i m i naishauri itoe elimu kwa vijana mwisho wa siku watabadilika tu amesema Nuru.

    Pia ametoa wito kwa Serikali itoe mchango kwa asasi za kiraia zilizojitolea kuisaidia katika majanga mbalimbali hasa katika k u wa k o m b o a v i j a n a maana vijana ni nguvu kazi ya taifa.

    Amesema yeye kama b i n t i w a m i a k a 3 1 amejitahidi kuwashawishi vijana wenzake mpaka kuwabadilisha si kazi n d o g o h i v y o k a t i k a zoezi hilo anakabiliana na changamoto nyingi moja ya changamoto hizo ni kutokuwa na uhakika wa kulipa pango la jengo alilokodi la kuwapa elimu vijana hao pamoja na chakula cha uhakika.

    Amewaomba wadau mbalimbali wanaoguswa n a k a d h i a h i y o ya kuliondolea Taifa hasara wa n a we a k u c h a n g i a kimoja wapo kwa nafasi yake.

    Mikononi mwa TalibanInatoka Uk. 6Haraam kwa muda. Ghafla pakaqimiwa kuwataarifu watu wawe tayari kwa swala, kila mtu alisimama na bila zogo watu wote wakajipanga katika mistari haraka. Nikaanza kufikiria hakuna jeshi lolote duniani lenye uwezo wa kujipanga vile kwa haraka. Na hivyo nikabaki nafikiria jeshi la Allah tu na moyo wangu ukitabasamu kwa mimi kuwepo ndani yake. Macho yangu huwa yanajawa na machozi kwa kufikiri hili nililoshuhudia. Ilinifanya nifurahi kuwepo katika familia hii kubwa. Pale, kulikuwa na watu kutoka mataifa tofauti, lugha tofauti na rangi tofauti.

    Swala ikaanza, wote t u l i e l e w a n a w o t e t u l i u n g a n a k a t i k a muungano mzuri usio na fujo, zogo wala kelele. I l i n i h u z u n i s h a s a n a kugundua kuwa tutadumu

    vile kwa sekunde kadhaa tu, nikajiuliza kwanini tusiendelee Waislamu kuwa hivyo baada ya swala pia!

    Yvonne ni mwanzilishi w a W o m e n i n Journalism (Wanawake Wana-habari), promota wa haki za wanawake na pia ni mwanzilishi wa Stop the War Coalition (Muungano wa Vyama Kupinga Vita) na chama cha siasa cha RESPECT.

    Pia ni mjumbe katika umoja wa wanahabari wa taifa The National Union of Journalists, The Internatinal Federation of Journalists (Shirikisho l a W a n a h a b a r i l a Kimataifa) na The Society of Authors (Umoja wa Waandishi, Watunzi). Kwa sasa, anafanya kazi kama mtangazaji katika kituo cha

    televisheni kipatikanacho dunia nzima cha PRESS TV.

    P i a n i m wa n d i s h i katika kijarida cha kila siku chenye makao yake New York kiitwacho Daily Muslims. Kwa maneno y a k e m w e n y e w e a k i o n g e l e a k u h u s u kusilimu kwake, Ridley anajisifu kwa kusema Nimejiunga na familia ambayo kwangu mimi naichukulia kama ndio kubwa zaidi kwa sasa duniani bila kusahau ndio familia bora zaidi pia.

    Kama tukishikamana basi hakuna wa kutuzuia. B a a d h i y a m a s o m o y a k e y a p a t i k a n a y o kutoka katika intaneti ni kama Conversion to Islam naJourney to Islam ( Makala hii ni kwa msaada wa saidpowa.blogspot.com)

  • 9 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Makala

    Profesa Abdallah Safari anastahiki kupongezwaM A N E N O y a l i y o andikwa katika Gazeti l a M w a n a n c h i l a Alhamisi Machi 27, ni jukumu la Waislamu kuyapokea vizuri na kuyafikiria. Si hivyo tu, bali si dhambi wala vibaya kumpongeza aliyeyasema. Huyo ni Profesa Abdallah Safari; Mjumbe wa Bunge maalumu la katiba, ambaye amekubali kuivalia njuga kadhia y a M a h a k a m a y a Kadhi na kukusudia kurejesha hoja yake katika mjadala wa rasimu ya katiba.

    Kwa mara nyingine t u n a m p o n g e z a Profesa Safar i kwa hili na tunamuomba Mungu amlipe malipo makubwa hapa duniani na kesho akhera. Kwa sababu mara nyingi tumekwisha sema na kuandika kwamba uti wa mgongo wa katiba yetu mpya ni mfumo wa demokrasia na hakuna demokrasia duniani kote bila ya uhuru. Aidha hakuna uhuru muhimu k u l i k o u h u r u w a kuabudu. Ni matarajio yetu kwamba kadhia ya mahakama ya kadhi, itakuwa ni sehemu ya vipengele vya katiba ya Tanganyika. Kwa hali ilivyo kipindi hiki, ni dhahiri kwamba sio jambo la kutegemewa, na hiyo ndio sababu i n a y o t u f a n ya s i s i tukiongozwa na watu kama Profesa Safari kuanza kilio chetu upya.

    M a h a k a m a y a kadhi hapa nch in i tangu mapema ilianza kukumbwa na nuhusi kubwa kwa kupata upinzani kutoka kwa baadhi ya Watanzania wenzetu na miongoni mwao ni hawa hawa Waislamu wenzetu. Kabla ya kuanza kwa k a m p e n i ya k u d a i

    Na Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir.

    k u r e j e s h w a k w a mahakama ya kadhi, w a p o b a a d h i y a Waislamu waliojitokeza kuikosoa mahakama hii kwa sababu eti ni mahakama ya ndoa, t a l a k a , m i r a t h i n a wakfu na mfano wa hayo tu. Haina uwezo wa kuhukumu kesi za jinai; wizi, kuuwa na kadhalika, kwa maana hiyo mahakama hiyo si kamili. Wengine wakadai kwamba mahakama hii haitakuwa safi katika Uislamu kwa sababu itakuwa ikiendeshwa kwa pesa za shubuha, miongoni mwa rushwa, riba na biashara ya haramu kwa mujibu wa Uislamu. Hayo yote ni mawazo yaliyokuwa y a k i s a m b a z w a n a baadhi ya Waislamu, ambao ni dhahiri kuwa walikuwa wakitumiwa dhidi ya mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi nchini bi la ya wao wenyewe kujua kwamba wanatumiwa na wanao watumia pia hawawajui.

    Kubwa zaidi ni ile

    hujuma iliyofanywa n a B a k w a t a k w a kuwapendekeza watu fulani na fulani kuwa makadhi maalumu wa Bakwata na ilhali watu hao wenyewe hawana uwezo wa kuhukumu mambo yao kwa sababu ya uchache wao katika e l imu ya sheria ya dini ya Kiislamu. Pia wakawa ni makadhi wasio na meno kwa kuwa hawatambuliwi na katiba ya nchi na maamuzi yao yanaweza k u t e n g u l i w a n a mahakama za nchi a m b a z o z i p o k w a mujibu wa katiba.

    K a t i b a m p y a inatakiwa kuwa ni katiba ya Watanzania wote bila ya kuangalia tofauti zao za itikadi au kanda. Kinyume na hivyo itakuwa ni katiba ya kundi fulani tu la raia huku ikilitupa nje kundi j ingine ambalo kwa pamoja na lile lililomo ndio yanayo unda nchi inayo itwa Tanzania.

    Watu wa mwanzo m w a n z o a m b a o n i w a j i b u w a o kumpongeza Profesa Safari, ni Masheikh wetu walio beba jukumu la kutuwakilisha katika bunge hilo maalumu la katiba. Kwa sababu hiyo ndio kazi yao ambayo wao wenyewe wamekubali kuifanya kwa moyo mkunjufu. Katika ulimwengu wetu huu kuna watu wenye ujasiri bungeni hadi kufikia kutetea ushoga uwe ni muhimu kiasi cha kutungiwa sheria nchini. Na wengine wanapendekeza bangi iwe na uha la l i wa kulimwa, kuuzwa na kutumiwa nchini. Wala hakuna anaye weza kujitokeza na kuwapinga au kuwalaumu. Bali hao ndio wanao sifiwa kwamba ni watetezi wa haki za binaadamu na ndio wanao weza kuutetea uma na haki za uma. Kadhia ya umuhimu wa katiba

    k u t a m b u a u w e p o wa M u n g u , u h u r u wa kuabudu, uhuru wa kutoa maoni na kujieleza, kadhia ya kute tea mahakama ya kadhi kuwekewa kifungu katika katiba. Kadhia ya kuweka sheria kali ya kupinga ushoga na ndoa ya aina hiyo, kadhia ya kutetea haki za wanawake katika ndoa na kuruhusiwa wawili, watatu au wane k u o l e wa n a m u m e mmoja na mengineyo yanayo fanana na haya. Yote hayo ni dhima juu ya kila sheikh aliye kubali kubeba jukumu la kuuwakilisha Uislamu na umma wa Kiislamu katika bunge maalumu la katiba.

    A l l a h ( s . w . t . ) awasaidie ndugu zetu, m a s h e i k h z e t u n a wawakilishi wetu na awape ulimi mzuri wa kuutetea Uislamu ndani na nje ya bunge.

    Wabillah taufiq(Sheikh Abdallah

    Ahmad Bawazir-0767 215 898)

    PROFESA Abdallah Saffari (katikati). Kulia ni John Mnyika.

  • 10 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Makala

    Machi 20, 2014 Mtandao wa Kupashana Habari - Salon

    Miaka sabini iliyopita, baba yangu - Luteni Usu Eric Fletcher Waters, alikufa nchini I ta l ia akipigana n a m a - N a z i . A l i k u wa mwanaharakati wa amani, na mpinzani wa kimaadili wa vita wakati vilipoanza, lakini maovu ya Hitler yaliposambaa kote Ulaya, alibadilisha gari la wagonjwa alilokuwa akiendesha wakati London inapopigwa mabomu (na Ujerumani) akachukua kofia ya bati (helmet) na kupata kibali cha (Jeshi la Uingereza) na kujiunga na mapambano dhidi ya ufashisti. Aliuawa karibu na Aprilia katika pambano la Anzio la kivuko (muhimu kivita) hapo Februari 18, 1944. Mama yangu- Mary Duncan Waters - alibaki mwanaharakati maisha yake yote yaliyobaki, akijitahidi wakati wote kuhakikisha kuwa wanae, na wana wa wengine wote, hawakuwa na Upanga wa Damocles kupitia itikadi chukizo ziwe juu ya vichwa vyao. Mwezi uliopita, kwa hisani ya watu wa Aprilia na Anzio, niliweza kutoa shukrani kwa baba yangu ambaye sikuwahi kumfahamu kwa kuinua mnara wa kumbukumbu alipofia na kuweka shada la maua kwa heshima yake, na wengine walioanguka. Kumpoteza baba yangu kabla sijamfahamu na kulelewa na mzazi mmoja pekee, mama aliyekuwa akifanya kazi na kupigania bila kuchoka usawa na haki ilikuwa dira ya maisha yangu kwa kila njia na imekuwa msukumo wa kila nilichokifanya. Na, katika hatua hii ya safari yangu, napenda kufikiri kuwa ninatoa shukrani k w a w a z a z i w a n g u wote wawili kila wakati ninapozungumza kuunga mkono watu wa kundi lolote lile wanaonyimwa uhuru na hali ambavyo ninaamini sote sisi tunastahili.

    Baada ya kutembelea Israel i mwaka 2005 na Ukingo wa Magharibi mwaka uliofuatia, nilisononeka sana na kile nilichokiona na kudhamiria kuongeza sauti yangu katika wale ambao wanatafuta suluhisho la haki na kisheria kwa tatizo hilo - kwa Wapalestina na Wayahudi pia.

    Kutokana na malezi yangu,

    Roger Waters: Kwanini lazima niseme kuhusu Israeli, Palestina na kuisusa IsraeliMwimbaji nyota wa kundi la Pink Floyd anaelezea kwanini anaunga mkono kuisusa IsraeliNa Roger Waters

    kwa kweli sikuwa na chaguo. Mwaka 2005, makundi ya kiraia ya Palestina yalitoa mwito kwa wale wote wenye hisia njema duniani kote kuchukua hatua pale ambapo s e r i k a l i z i m e s h i n d wa . Walitutaka tuj iunge na vuguvugu lao la amani - la kususa, kuondoa raslimali na kuweka vikwazo - lenye nia ya kumaliza ukaliaji kwa mabavu maeneo ya Wapalestina, kupata haki sawa kwa wananchi wa Palestina nchini Israeli, na kutetea haki ya wakimbizi wa Palestina kurudi katika miji na vijiji walivyoondolewa kwa nguvu mwaka 1948 na 1967.

    Baada ya zaidi ya miongo miwili ya mazungumzo, jamii dhaifu ya Wapalestina b a d o i n a i s h i c h i n i ya wavamizi, huku ardhi zaidi ikichukuliwa, makazi zaidi yasiyo halali yakijengwa, na Wapalestina zaidi wanatupwa j e l a , wa n a u m i z wa a u wanauawa wakipigania haki ya kuishi katika hali ya heshima na amani, kuinua familia zao, kulima ardhi, kupania malengo yote na ya kawaida ya binadamu, kama tulivyo sisi wengine. Kutokuwa na nchi kwa Wa p a l e s t i n a a m b a k o kumeendelea kwa muda mrefu kumewafanya wawe dhaifu mbele ya mataifa yote, hasa katika maeneo waliyohamia nje ya nchi

    yao, kama sasa nchini Syria, ambako wanasulubiwa, kama watu wasio na nchi, wakimbizi wasio na uwezo, kulengwa katika utumiaji nguvu, kutoka pande zote za mzozo huo uliokithiri umwagaji damu, wakiwa wanajikuta katika hali ya taabu bila mfano na kukosa karibu kila kitu, na katika matukio mengi, hasa kwa watoto wasio na nguvu, kufa kwa njaa.

    Tunaweza kufanya nini sisi sote kupeleka mbele haki za Wapalestina katika maeneo yanayokaliwa na Israeli, nchini Israeli na walikohamia? Kwa njia hiyo, kususa, kuondoa raslimali na kuweka vikwazo ni mwamko usiotumia nguvu u n a o o n g o z wa n a r a i a umejikita katika kanuni za kimataifa za haki za binadamu kwa watu wote. Watu wote! Kwa hali hiyo, nimedhamiria kuwa mwelekeo wa kususa, k u o n d o a r a s l i m a l i n a kuweka vikwazo ni uelekeo ninaoweza kuunga mkono kikamilifu.

    N a j i s i k i a k u p e w a heshima kusimama katika mshikamano na baba yangu na mama yangu, na pamoja na ndugu zangu na dada zangu wa Palestina, na wengi wengine wa rangi zote, imani na mazingira kote duniani - ikiwa ni pamoja na idadi inayozidi kuongezeka ya Wamaerekani wenye asili

    ya Kiyahudi na Waisraeli - ambao pia wamejibu mwito huo.

    Katika zogo linaloendelea nchini Marekani hivi sasa kuhusu kususa, kuondoa raslimali na kuweka vikwazo, na jema au baya la kuisusa Israeli kitamaduni, ainisho kutoka mmoja wa mashujaa wangu, Mahatma Gandhi, limekuwa akilini mwangu. A l i s e m a k i n a b i i k u wa Kwanza wanakupuuzia, h a l a f u w a n a w a c h e k a , baadaye wanapigana nanyi, na mwisho mnashinda.

    Mwamko wa kususa, kuondoa raslimali na kuweka vikwazo unafikia tumaini na unaendana na alichosema Gandhi, Mkakati huo ambao kitambo kidogo ulipuuzwa kama njia muflisi ambayo kamwe isingeweza kuleta mabadiliko yoyote, sasa mkakati huo umeshika kasi katika miezi kadhaa iliyopita, na kuinua upinzani dhidi yake kama ilivyotazamiwa.

    Uondoaji wa raslimali za vyuo vikuu kadhaa vikubwa vya Marekani, mifuko ya pensheni ya nchi za Ulaya kuondoa fedha zao katika mabenki ya Israeli ambayo yanafanya b iashara na makazi haramu katika eneo linalokaliwa kwa mabavu, na tukio la kimataifa la kuachana katika njia zao, kati ya mcheza sinema Scarlett Johansson na shirika la kimataifa la kupambana na umaskini Oxfam, ni dalili za kuongezeka kwa ukinzani kuhusu ukandamizaji wa Israeli dhidi ya wazawa asilia wa Palestina, na pia, kwa miongo kadhaa ya ukaliaji wa ardhi ambayo Umoja wa Mataifa umeitoa kwa nchi ya baadaye ya watu wa Palestina.

    Na kila vichwa vya habari vinapotangaza hatua mpya ya kususa, kuondoa raslimali na kuweka vikwazo, majibu ya jazba na hasira ya wapinzani wa mwamko huo wakiwemo Netanyahu na marafiki zake wa AIPAC (mtandao wa marafiki wa Israeli nchini Marekani) wakiwa mstari wa mbele, imepanda kwa kasi. Nadhani unaweza kusema mkakati huu upo katika hatua ya halafu wanapigana nanyi.

    Baadhi wanapotosha kuhusu harakati ya kususaa, ambayo inachukua mfano wa harakati za kuisusa Afrika Kusini ya kibaguzi n a k u t u m i w a k a t i k a vuguvugu la haki za kiraia nchini Marekani, kuwa ni shambulio dhidi ya watu wa Israeli au Wayahudi kwa jumla. Hakuna kinachoweza kuwa mbali zaidi ya ukweli

    ku l iko hapo . Harakat i hizi zinatambua haki za binadamu chini ya sheria kwa watu wote, bila kujali uasili wao, dini au rangi.

    S i j i t a m b u l i s h i k a m a msemaji wa harakati ya kususa, ila, kama muungaji mkono wa dhati, na kwa kuwa ninaonekana katika fani ya muziki, nimekuwa n i k i l e n g w a n a w a l e wanaopenda kuishambulia harakat i h i i , s iyo kwa kulenga ho ja zake i la , badala yake, kwa kuashiria kuwa chuki na ubaguzi ndivyo vinavyosukuma wanaounga mkono harakati hii. Imesemwa, kikatili na kwa makosa, kuwa naunga mkono fikra ya Nazi na ni mbaguzi wa Wayahudi.

    Nilipotaja katika mahojiano hivi karibuni kuhusu mambo yanayofanana katika historia, nikisema kuwa nisingeweza kucheza sinema nafasi ya mtu wa Ufaransa ya Vichy au (utawala wa) Berlin katika vita vikuu vya pili duniani, sikuwa na nia ya kuwalinganisha Waisraeli an wa-Nazi au mauaji ya kimbari ya Wayahudi na ukandamizaji wa Wapalestina uliodumu miongo kadhaa. Hakuna mfananisho na mauaji wa kimbari, Holocaust. Wala s ikuwahi kul inganisha mateso ya Wayahudi wakati huo na taabu wanayopata Wapales t ina h iv i sasa . Kul inganisha taabu n i jambo gumu, linalovuruga na kupunguza thamani ya heshima ya kumbukumbu ya w o t e wa l i o a n g u k a , wapendwa tuliowapoteza.

    Naamini kuwa mzizi wa kukosekana kwa haki na ukandamizaji wakati wote huo ni ule ule - kuukataa ubinadamu wa mwingine. Ni hisia kali ya Sisi na Wao ambayo inaweza kutupeleka, bila kujali utambulisho wetu kiasili au kidini, kuanguka shimoni.

    Dhima tusije kusahau kuwa ukandamizaji unazaa ukandamizaji zaidi, na kuwa mti wa woga na ubaya siku zote tunda lake ni chungu. Kumalizika kwa kukaliwa Palestina, ikiwa tutafanikiwa kufikia, itakuwa ni uhuru kwa waliokandamizwa na wanaokandamiza na uhuru kutoka katika uchungu wa miaka yote hii iliyopotea, na maisha ya watu. Na hiyo itakuwa zawadi kubwa kwa dunia.

    Majivu na almasi (karata)Adui na rafikiWote sisi ni sawaMwishowe.

    WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau

  • 11 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014

    RAIS Barack Obama wa Marekani.

    Makala

    R A I S H u g o C h a v e z ambaye sasa ni marehemu alilishangaza Baraza Kuu la UM (Umoja wa Mataifa) mwaka 2006 kwa hotuba yake kali ambapo alimuita Rais George Bush wa Marekani kuwa ni shetani linalotenda kana kwamba dunia hii ni mali yake.

    Hebu tusome sehemu ya hotuba hiyo:

    Yesterday, the devil came here, right here. Right here. And it smells of sulfur still today, this table that I am now standing in front of.

    Yesterday, ladies and g e n t l e m e n , f r o m t h i s rostrum, the president of the United States, the gentleman to whom I refer as the devil, came here, talking as if he owned the world. Truly. As the owner of the world.

    I think we could call a psychiatrist to analyze yesterdays statement by the president of the United States.

    As the spokesman of imperialism, he came to share his nostrums, to try to preserve the current pattern of domination, exploitation and pillage of the peoples of the world.

    An Alfred Hitchcock movie could use i t as a scenario. I would even propose a title: The Devils Recipe.

    Kwa ufupi katika aya ya kwanza na ya pili anakusudia kusema; Shetani alikuja jana hapa, hapa hasa. Na bado pananuka kama salfa, katika meza hii ambayo nimesimama mbele.

    Jana, mabibi na mabwana, kutoka jukwaa hili, raisi wa Marekani ambaye narejea kuwa ni shetani, alikuja hapa alizungumza kana kwamba dunia anaimiliki yeye. Kweli. Kama mmiliki wa dunia

    Hiyo ndiyo hotuba kwa ufupi ya rais aliyekuwa wa Venezuela katika Baraza la Umoja wa Mata i fa . Akimzungumzia aliyekuwa kiongozi wa Marekani George Bush na kumuita shetani na akizungumza kama anamiliki dunia.

    Kwa uwelewa wangu n a h i s i z a i d i C h a v e z alikusudia kuuzungumzia uongoz i wa Marekani unaoongozwa na Bush kuwa ni wa kishetani, sababu za uongozi ule kuwa ni wa kishetani zipo nyingi na k i l a m m o j a a t a i s e m a yake kulingana na pale alipoguswa au kuumizwa.

    Utawala wa Marekani ndio unaoongoza kwa kulaumiwa kulingana na yale ambayo

    Shetani yupo Afrika MasharikiNi yule aliyefichuliwa na Chavez ndani ya UN Na Rashid Abdallah, MUM

    unawafanyia wale wasio na nguvu wakiwemo mtu mmoja mmoja na hata mataifa machanga. Tanzania kwenye mkumbo huo nasi tumo kwani tunaendeshwa vile watakavyo wao, wakisema hili fanyeni hili musifanye sisi tunabaki kutekeleza tu.

    Ni aina moja ya ushetani ambao unafanywa kwa mataifa machanga, ni hivi karibuni tu amezuia misaada kwa nchi ya Uganda kwa sababu wameweka sheria ya adhabu kali kwa yule atakaye bainika anajihusisha na mahusiano ya jinsia moja (ushoga).

    P i a t u s i s a h a u k u wa k i l i c h o p e l e k e a m p a k a Vietnam ikala k ichapo takribani miaka arobaini iliyopita ni zile siasa zake tu za kikomunisti ambazo kwa Marekani yeye zilikuwa ni siasa asizozitaka.

    Vietnam kwa sababu hiyo ikapigika kweli kweli, kuanzia silaha za kawaida, zikaja nzito hadi za sumu ambazo zimewaweka mamia na maelfu ya Wavietnam katika hali mbaya hadi leo.

    Tukisema shetani yupo Afrika Mashariki sasa hatuna maana kuwa ni shetani yule aliyemzungumzia aliyekuwa raisi wa Venezuela katika Baraza la Umoja wa Mataifa ila tunazungumzia ule uongozi alio uwacha yeye alikuwa shetani pia kaacha mashetani waongoze na uongozi wao wa kishetani wakiendelea kui tesa dunia na sasa ushetani huo unaonekana kujikita Mombasa ambapo Mashekh wanauliwa kila uchao.

    Aliiyanza Somalia kwa kuwatumia Waithopia ili

    waondoshe utawala uliokuwa unafuata mifumo ya dini ya Kiislamu, ambayo shetani anauchukia sana. Walianza na ukomunist, wameuweza kwani hauna nguvu na kwa sasa wanajihusisha zaidi na Uislamu ili wahakikishe nao wanaukata roho. Ni kama vile tu alivyopigwa Saddam Hussein si kwa sababu anamiliki mabomu ya nyuklia ila tu kwakuwa a l ikuwa na agenda ya kupora mali, kuvuruga nchi madhubuti Mashariki ya Kati na kuudhoofisha Uislamu na wakati huo huo kuijengea Israel mazingira bora ya kutamba katika eneo hilo.

    Popote alipo shetani siku zote hapana usalama na wala amani haitopatikana. Baada ya miaka mingi ya kukaa bila serikali na juhudi mbal imbal i kushindwa kutokomeza mauwaji na machafuko, Wasomal ia wenyewe wal i fanik iwa kurejesha amani katika nchi yao kwa kutumia Uislamu wao. Lakini hilo halikutakiwa na shetani anayejifanya kuwa ni mmiliki wa dunia. Akaja na kisingizio cha ugaidi akaiporomosha serikali hiyo Wasomalia wakarejeshwa k a t i k a m a c h a f u k o n a mauwaji. Kwa ksingizio hicho hicho cha ugaidi, Kenya ikatumbukizwa katika vita isiyokuwa yake-Proxy War, na kisha ugaidi sasa inaumia. Imepewa bajeti ya kuunda na kuendesha kikosi cha ATPU (Anti Terro-Police Unit), ambao kimsingi wanafanya kazi ya kishetani ya kuitumbukiza Kenya katika machafuko, lakini wamepumbazwa pamoja na serikali nzima wakijiona

    kuwa wanapambana na magaidi hatari kwa amani na usalama wa Kenya. Kumbe ni njama za kishetani kuwafanya wajiangamize wao wenyewe Wakenya kwa mikono yao!

    Wa z a z i w a C h a v e z w a l i k u w a w a a l i m u waliowahimiza watoto wao waikumbatie elimu kama njia ya kupata maisha bora. Mtoto wao wa k iume, Hugo, alijiunga na shule ya sayansi ya jeshi, ambako alikuwa na shauku kubwa ya masuala ya siasa wakati wa masomo yake. Baada ya kufuzu alijiunga na jeshi na mwaka 1983, akiwa na umri wa miaka 30, yeye pamoja na maafisa wengine wakaunda Jeshi la Mapinduzi la Bolivia 200 EBR - 200. Jina hilo lilikuwa likimzungumzia El Libertador, Simon Bolivar, ambaye peke yake aliyakomboa maeneo ya Amerika Kusni kutoka kwa viongozi wa kikoloni wa Uhispania na ambaye kanuni zake na maisha Chavez aliziunga mkono.

    Kwa kuwa hakuridhishwa na itikadi za kisiasa ambazo kwa uwazi zilipuuza mahitaji ya umma, kundi la Chavez lilifanya jaribio la mapinduzi mnamo mwaka 1992 dhidi ya rais wa Venezuela wakati huo, Carlos Perez, ambalo halikufaulu. Chavez alitupwa gerezani, lakini si kwa muda mrefu. Baadaye rais Perez alishitakiwa, na mrithi wake, Rafael Caldera, akamuachia huru Hugo Chavez mwaka 1994. Chavez alifanya juhudi za kuanzisha miungano ya kisiasa ndani ya Amerika Kusini na kukutana na v i o n g o z i m b a l i m b a l i

    akiwemo kiongozi wa Cuba, Fidel Castro. Mwaka 1996, Chavez alianzisha chama ki l ichoegemea siasa za mrengo wa shoto, The Fifth Republican Movement ili aweze kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 1998.

    Chavez alipata umaarufu k w a h a r a k a , i n g a w a mwanzoni alichukuliwa kama mtu kutoka n je . Aliugeuza ujumbe wake wa sera za kisoshalisti kuwa lugha ya watu masikini na kuikonga mioyo yao.

    Kwa mara ya kwanza baada ya kujaribu mara n n e , n a k u p a t a w i n g i mkubwa wa kura, Chavez alichaguliwa kuwa rais wa Venezuela. Bila kupoteza wakati alianza kuchapa kazi mara tu alipoingia madarakani. Serikali yake ilizitaifisha sekta muhimu za uchumi, hasa ile ya mafuta. Mapato kutokana na mauzo ya m a f u t a ya l i t u m i wa kugharamia miradi ya kijamii, kuhakikisha masikini wa n a p a t a m s a a d a wa matibabu na kulipia gharama za elimu kwa ajili ya watoto. Mwaka wa 2001 aliifanyia mageuzi sheria ya umiliki wa ardhi ili kuhakikisha a rdhi amb ay o i l i k u wa haitumiki, inatumiwa. Hadi sasa hekta takriban milioni tano zinamilikiwa na serikali na zimetengwa kwa ajili ya wakulima masikini na wafugaji wa mifugo.

    Hugo Chavez wa Venezuela amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa saratani kwa miaka miwili ugonjwa ambao aliwahi kudai kuwa Marekani ndio wamempa. Juhudi za kuyaokoa maisha yake hazikufaulu, l icha ya kufanyiwa upasuaj i mara kadhaa nchini Cuba. Mkomunisti wa karne ya 21 akaaga dunia.

    Chavez kaenda lakini alichokisema kitaendelea kubaki na si kubaki tu pia kitaendelea kufanya kazi, kama kinavyofanya kazi sasa katika mataifa mbali mbali duniani.

    U s h e t a n i w a B u s h haukuishia kuwa ni wa kwake yeye ila pia uongozi mzima wa Maekani umekuwa ni wa kishetani kuanzia yeye Bush hadi hawa wenziwe wa sasa. Mashekhe wa Mombasa na Wasomali wamekumbwa na shetani huyu anayekula kila anachokiona ni kikwazo kwake. Shetani aliona serikali ya Kiislamu Somalia ni kikwazo kwa yake Somalia na eneo lote la Pembe ya Afrika. Akaingilia kati jambo li l i loibua kinachodaiwa kuwa ni ugaidi wa Al Shabab, jambo ambalo sasa ndio linasababisha kuuliwa Masheikh na Wasomalia nchini Kenya.

    (Email [email protected] 0773 526 254)

  • 12 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Shairi/Barua/Makala

    Ni ala ala jirani, msemo wetu wa ada, Dhamira kuithamini, ya ujirani ibada, Si kwa mseto wa dini, na mambo ya kiaqida, Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

    Kuthamini ujirani, japo kwetu ni ibada, Katu si kwa kufrani, na kukiuka aqida, Bali kwa kuuthamini, kwa kupwekesha aqida, Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

    Kushiriki Pasakani, ni kukiuka aqida, Kama hoja ujirani, kwalo bora ukadoda, kuliko kuirehani ya tauhidi aqida, Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

    Ange tutahadharini, kushiriki ushuhuda, Wa fufuko la kubuni, mithili ya maburuda, Kwalo tujitanibuni, 'tusinajisi' aqida, Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

    Twageza sira ya nani, kwa ya ujahili ada, Ya kuhuluti imani, utatu na tauhida,Jumapili Pasakani, ebu tukae baida, Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

    Ya ala ala jirani, yaendane na aqida, Yasiwe ya ujirani, dhidi ya yetu aqida, Tungamo la Pasakani, ni hilaki kwa aqida, Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

    ABUU NYAMKOMOGI -SAFARINI KAGERA.

    PASAKA SI YAKOAbtadi kwa yakini, kumhimidi Qudusu, Yu Muumba wa insani, na vyote vinomuhusu, Wahidu ulimwenguni, uwenza kwake nukusu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    Aswilani abadani, yu hana mwenza Qudusu, Kadhalika na banini, vyote kwake ni nukusu, Wenye wenza na banini, ni ajinani na nasu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki. Mushiriki wamebuni, wampachike nukusu, Eti mwana wa Manani, bin Mariamu Yesu,Aso mwana kulikoni, kumpachika nukusu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    Na Pasaka wamebuni, kuwa fufuko la Yesu, Niwombe kwa tamakuni, Injili waidurusu, Ukweli watabaini, tamamu tena si nusu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    Ishna sita funguni, kumi nane ni kisu, Kitowachoma mioyoni, hadi chini wajulusu, Nachombeza wasidhani, Mathayo wakadurusu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    Yu awagiza mjini, wanafunzi wake Yesu,Wende huko kubaini, Pasakayo kwa unasu, Hiyo ni Pasaka gani waagizwayo na Yesu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    Ufufuko kulikoni, u wapi hapo wa Yesu, Yualofufuka nani, yu kingali hai Yesu, Wagala tuelezeni, Kwa hoja za kinususu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    Chondechonde dada Shani, nawe akhui Yunusu, Jitanibuni jamani, na jambo lisowahusu, Kushiriki Pasakani, ni kufuru kwa Qudusu, Si yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

    ABUU NYAMKOMOGI -SAFARINI KAGERA.

    UJIRANI WA KUFRU !!!

    Muhammad (S.A.W.) alitumwa aje kuwa Rehma kipindi cha giza cha UjahiliyaInatoka Uk. 7Basi yatima usimwonee! Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! (Surat Adh-Dhuhaa, 93:5-9)

    Huyo Lulu Yatima Isiyo Mfano akaja kumpoteza mamake pia, katika umri m c h a n g a . B i b i A m i n a alipokufa kule Abwa akiwa na umri wa miaka 25 au 26, wakati akirejea kutoka Madina kuzuru kaburi la mumewe, mwanawe Muhammad (s.a.w.) alikuwa na umri miaka 6 tu.

    K wa h i v y o , a l i o n j a mapema uchungu wa kuwa yatima, wa kutokuwa na mama wala baba. Naam, alionja na kujifunza kila machungu, kwani ili kuja kuwafundisha watu kila kitu, na kuwa mfano wa kila aina.

    Babu yake, Abd Al-Muttalib, mkongwe wa Makka aliyeheshimika sana, akaanza kumlinda. Kwa sababu hii, Allah (s.w.t.) Alimkinga Abd Muttalib dhidi ya bahati mbaya. Alimkumbatia mjukuu wake mpendwa, na mara nyingi alikuwa akimpa kiti cha heshima nyumbani mwake.

    Alihisi kuwa Muhammad (s.a.w.) atakuja kuokoa wanadamu. Muhammad (s.a.w.) alikuwa muadilifu na mwenye tabia nzuri sana, Hata babu yake alitazamia kuwa ataupata Unabii. Naye hakuwa wa kwanza katika wahenga wake (mababu zake wa zamani) kuwa hivyo.

    Ka`ab Ibn Luayy, ambaye wengine wanamhesabu kuwa alikuwa ni Nabii, alitabiri kuwa Mjumbe wa Mwisho wa Allah (s.w.t.) atatokana na kizazi chake. Alimtaja kwa jina hasa:

    Ghafla Nabii Muhammad atakuja kujitokeza Atatoa habari, naye ni mkweli katika habari zake.

    Babu yake , Abd a l -Muttal ib, ambaye hata Abraha (Mhabeshi kutoka Ye m e n i a l i y e a z i m i a kuivunja Al-Kaaba kwa kutumia jeshi lake la tembo) hakuweza kumliza, alilia sana alipokuwa kitandani kwake akikaribia kufa. Mwanae, Abu Talib ibn Abd al-Muttalib, alipomwuuliza kwa nini analia sana, vile, Abd al-Muttalib akajibu

    kuwa: Ninalia kwa kuwa siwezi

    tena kumkumbatia mjukuu wangu Muhammad (s.a.w.). Nina hofu ya usalama wa Lulu yangu Isiyo Mfano. Ninamkabidhi kwako.

    Abu Talib aliupokea ulinzi wa Muhammad (s.a.w.), na mwanae, Ali ibn Abu Talib (r.a.) akaja kubarikiwa kuwa ni baba wa kizazi cha Nabii Muhammad (s.a.w.). Alivyokuja kuupata Unabii, Mtume Muhammad (s.a.w.) alimwambia binamu yake, Ali (r.a.) hivi: Kizazi cha kila Nabii hutokana na Nabii Yule yule mwenyewe, lakini kizazi changu kitatokana na wewe.)

    Ali ibn Abu Talib (r.a.) akaja kweli kuwa baba na mtakatifu hadi Siku ya Mwisho, kama mwakilishi wa utakatifu wa Nabii Muhammad (s.a.w.). Hii ndiyo hidaya ya Abu Talib kwa kumsaidia Muhammad (s.a.w.). Abu Talib alimlinda M u h a m m a d ( s . a . w . ) uangalifu mkubwa sana. Ibn Is-haq, miongoni mwa wanahistoria wengine na waandishi wengine wa wasifu alisimulia kuwa, aliongozana na mpwa wake hadi Syria katika msafara wa biashara alipokuwa umri wa miaka 10 au 12. Walipumzika m a h a l i k a r i b u n a Damascus, wakamwacha y e y e a a n g a l i e u l e msafara wao. Kutoka katika jumba la utawala lililokuwa jirani na pale mahali, mtawa mmoja wa Kikristo aitwae Bahira a l ikuwa ak iutazama ule msafara ulipokuwa unakuja taratibu. Alikuwa a k i u n g o j e a u j i o wa Nabii wa Mwisho; na mara nyingine alikuwa akiwachunguza wageni anaowaona. Ulivyokuwa ukija msafara wa Abu Talib, Bahira aliona kuwa wingu lilikuwa likiufuata msafara wao likitulia na kuendelea mbele kila msafara ule ulipokuwa ukisimama na kuanza kutembea tena, na saa zote wingu l i l ikuwa likimpa kivuli mtu mmoja katika msafara ule. Fikra zifuatazo zilimjia Bahira akilini mwake:

    Hii ni dalili maalumu

    y a M a n a b i i . N a b i i anayetazamiwa lazima a we m i o n g o n i m wa msafara ule.

    M s a f a r a u l e u l ipos imama kar ibu sana na jumba lake la utawala, Bahira aliwaalika wasafiri wote kwenda kula. Alipoona kuwa lile wingu lilikuwa bado limebaki linaelea kule nje, akamwuuliza Abu Talib iwapo mtu mmoja wao ameachwa yuko kule nje. Abu Talib akajibu k u wa wa m e m wa c h a mvulana kule nje i l i awaangalizie vitu vyao. B a h i r a a k a w a t a k a wakamlete huyo mtu. Alipoletwa huyo mvulana (Muhammad, s.a.w.), Bahira alimvuta Abu Talib pembeni akamwuuliza kama ana nasaba yoyote na mvulana yule. Abu Talib akamwambia kwamba: Huyu ni mwanangu. Lakini Bahira akakanusha hilo, na kusema kuwa:

    H a w e z i k u w a mwanao. Kwa mujibu wa vitabu vyetu, baba wa mvulana huyu lazima atakuwa alikufa kabla mvulana huyu hajazaliwa.

    Bahira akasema hivi: Nakupa ushauri kuwa

    umrejeshe mvulana huyu haraka sana. Mayahudi wana wivu. Wakimtambua watamdhuru.

    Hapo ndipo Abu Talib a k a t o a u d h u r u k wa wanamsarafa wenziwe alirejea Makka na mpwa wake.

    Mtume Muhammad (s.a.w.) alifanya safari ya pili kwenda Syria alipokuwa na miaka 25 akiwa na msafara wa biashara wa Khadija (r.a) mjane anayeheshimika, ambaye baadaye alikuja kumwoa. Katika safari hiyo alikutana na Bahira mara ya pili. Mtawa huyo alifurahishwa sana na kuonana huko kwa pili, yeye na Muhammad (s.a.w.) na akamwambia kuwa:

    Wewe utakuja kuwa Nabii, tena Nabii wa M w i s h o . N a t a m a n i Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ataniwezesha niishi hadi nikuone wewe umepewa Unabii nami nitakufuata wewe, nitachukua viatu vyako, na nikulinde dhidi ya maadui zako!

  • 13 AN-NUURJAMADUL AKHER 1435, IJUMAA APRILI 18-24, 2014Tangazo

    UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION ZANZIBAR INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA KHARTOUM

    STUDENTS ADMISSION 2014/2015The University College of Education invites qualified applicants to apply for first degree courses in the following specializations:Bachelor of Science with Education

    1. Physics & Mathematics 2. Chemistry & Biology 3. Physics & Chemistry 4. Computer Science & Mathematic 5.Chemistry & Mathematics 6. Biology & Geography 7. ICT

    Bachelor of Arts with Education 1. English & Kiswahili 2. English & Geography 3. English & History 4. English & Islamic Studies 5. Arabic & Kiswahili 6. Arabic & English 7.Arabic & Geography 8.Arabic & History 9. Arabic & Islamic Studies 10. Kiswahili & Geography 11. Kiswahili & History 12. Kiswahili & Islamic Studies 13. Islamic Studies & Geography 14. Islamic Studies & History 15. History & Geography 16. Counseling and Psychology.

    ADMISSION REQUIREMENTS:

    Applicants should:-1. have at least, a minimum of two principal passes at Tanzania Advanced Certificate of Secondary Education (ACSE) in the appropriate subjects or equivalent qualifications;2. be a full time student.FEES

    Tuition

    1,800,000/= (1200 US $) per annum

    Physics & MathematicsChemistry & BiologyPhysics & Chemistry Chemistry & MathematicsBiology & Geography

    1,500,000/= (1000 US $)

    Computer Science & MathematicsICTEnglish & GeographyKiswahili & GeographyArabic & GeographyArabic & HistoryKiswahili & HistoryIslamic Studies & HistoryEnglish & HistoryIslamic Studies & GeographyHistory & GeographyCounseling and Psychology.

    1,300,000/= (870 US $) per annum

    Arabic & Kiswahili Arabic & EnglishArabic & Islamic StudiesEnglish & Islamic StudiesEnglish & KiswahiliKiswahili & Islamic Studies

    Accommodation 180,000/= (120 US $) per annum

    Graduation 30,000/= (20 US $)Students Union 10,000/= ( 7 US $)Computer services 40,000/= (27 US $) per annumRegistration 40,000/= (27 US $) Medical Care 30,000/= (20 US $)Application Form 25,000/= (17 US $)Meals 1800,000/= (1200US $) OptionalStationeries 200,000/= (134 US $) Optional

    The College reserves the rights to change these fees at any time.Application forms are obtained from University College of Education- Website: www.ucez.ac.tz Academic Office, University College of Education Zanzibar at Chukwani P.O. Box 1933 Zanzibar Mobile: 0773774838 OR 0772912181 Email: [email protected] forms are also available from the following offices;- Africa Muslims Agency, MabaoniChake Chake Pemba: Tel: 024-2452337 P[Africa Muslims Agency, Tabata - Dar es Salaam: