annuur 1181.pdf

20
BAADHI ya wafungwa katika gereza la Guantanamo wakiswali. Juu ni gereza hilo linavyoonekana kwa nje. ISSN 0856 - 3861 Na. 1181 SHAABAN 1436, IJUMAA , JUNI 12-18, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] CCM wanaamini kuwa wananchi wataendelea kudumisha amani na utulivu kwa kuwajaza woga wa Babu Nshenga. Lakini watambue kuwa woga ukizidi sana, huzaa ujasiri usiotarajiwa wala usiozuilika. Guantanamo Dar! Aljazeera Ukerewe yazima uzushi wa ‘Jihad John’-3 Waalikeni Polisi, 'Task Force' Misikitini wajione! Mwenzao alisilimu baada ya kutesa Guantanamo OCD Nansio ajionea. Sasa ahimiza ‘Doria ya Nafsi’ ‘Ushindi lazima’ Zanzibar Woga ukizidi huzaa ujasiri Usanii wa vitambulisho upo wazi Na hapo ndipo watakapoweza kuona kasi na ghadhabu za nguvu ya Umma wakati ukifika. Tuombe amani na utulivu wa kweli na uchaguzi huru na wa haki! (Soma Uk. 16) HAIWEZEKANI Serikali ya Tanzania iachilie mambo haya yasomeshwe katika shule za Tanzania. Vipi mambo haya ya kipropaganda yenye khatari kubwa kwa nchi nzima ya Tanzania Vitabu hivi vichomwe moto Kwa nini Wizara inaruhusu kutukanwa Waislam yaendelee kusomeshwa. Kama nchi hii haina Udini, muhimu kabisa ni kupigwa marufuku usomeshaji wa propaganda za aina hii na vitabu vyote vichomwe moto leo kabla ya kesho. (Soma zaidi Uk. 7, 8) Tafrani Segerea Ustadh Salum Ally alala juu ya mti Amtaka Mwanasheria Mkuu Zanzibar Sheikh Farid aitwa kuepusha balaa MWANASHERIA Mkuu Wa Zanzibar Saidi Hassan SHEIKH Farid Hadd. Soma zaidi Uk. 20

Upload: zanzibariyetu

Post on 17-Dec-2015

1.185 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • BAADHI ya wafungwa katika gereza la Guantanamo wakiswali. Juu ni gereza hilo linavyoonekana kwa nje.

    ISSN 0856 - 3861 Na. 1181 SHAABAN 1436, IJUMAA , JUNI 12-18, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

    CCM wanaamini kuwa wananchi wataendelea kudumisha amani na utulivu kwa kuwajaza woga wa Babu Nshenga.

    Lakini watambue kuwa woga ukizidi sana, huzaa ujasiri usiotarajiwa wala usiozuilika.

    Guantanamo Dar!Aljazeera Ukerewe yazima uzushi wa Jihad John-3Waalikeni Polisi, 'Task Force' Misikitini wajione!Mwenzao alisilimu baada ya kutesa GuantanamoOCD Nansio ajionea. Sasa ahimiza Doria ya Nafsi

    Ushindi lazima ZanzibarWoga ukizidi huzaa ujasiri

    Usanii wa vitambulisho upo waziN a h a p o n d i p o

    watakapoweza kuona kasi na ghadhabu za nguvu ya Umma wakati ukifika.

    Tu o m b e a m a n i n a utul ivu wa kwel i na uchaguzi huru na wa haki! (Soma Uk. 16)

    HAIWEZEKANI Serikali ya Tanzania iachi l ie mambo haya yasomeshwe katika shule za Tanzania.

    Vipi mambo haya ya k i p r o p a g a n d a ye n ye k h a t a r i k u b w a k w a nchi nzima ya Tanzania

    Vitabu hivi vichomwe motoKwa nini Wizara inaruhusu kutukanwa Waislam

    yaendelee kusomeshwa. Kama nchi hii haina

    Udini, muhimu kabisa ni kupigwa marufuku usomeshaji wa propaganda za aina hii na vitabu vyote vichomwe moto leo kabla ya kesho. (Soma zaidi Uk. 7, 8)

    Tafrani SegereaUstadh Salum Ally alala juu ya mtiAmtaka Mwanasheria Mkuu ZanzibarSheikh Farid aitwa kuepusha balaa

    MWANASHERIA Mkuu Wa Zanzibar Saidi Hassan

    SHEIKH Farid Hadd.

    Soma zaidi Uk. 20

  • 2 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    ZIMESALIA siku chache sana kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhwani kuingia.

    H u u n i m w e z i w a k u f u n g a k a m a ilivyobainisha Qur'an iliposema:

    E n y i m l i o a m i n i ! mmefaradhishiwa swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allah.

    N a a t a k a y e k u w a m i o n g o n i m w e n u mgonjwa au yumo safarini, basi atimize hisabu katika siku nyingine. Na wale wasioweza, watoe fidia kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake.

    Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua. Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Quran kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi . Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge.

    Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika s iku nyengine. Al lah a n a k u t a k i e n i ya l i y o mepesi wala hakutakieni y a l i y o m a z i t o , n a mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allah kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru. [Al-Baqarah: 183-185].

    N i m wa k a j a n a t u tulikuwa na mgeni wetu h u y u t u n a y e t a r a j i a k u m p o k e a t e n a h i v i k a r i b u n i , M w e n ye z i Mungu akitujalia.

    Tu l i k a a n a ye s i k u zisizozidi thelathini na b a a d a ye a k a o n d o k a . H u e n d a we n g i we t u m g e n i h u y o a l i f i k a n a a k a t u a c h a k a m a alivyotukuta. Tulisahau kuwa mgeni huyu kwetu ni neema isiyofanana na kitu chochote. Na kwamba akija akaondoka bila ya Muislamu kutakasika, basi tena huyo yupo katika hasara kubwa.

    Lak in i k wa hek ma zake Mwenyezi Mungu, kila mwaka neema ya mwezi wa toba hutufikia na kupata fursa nyingine

    Karibu Ramadhaniya kujitakasa kwa ucha-Mungu.

    K w a w a l e a m b a o walikosea mwaka jana wakaiwacha Ramadhani i k a o n d o k a z a k e b i l a kui tendea haki , Bas i tusifanye makosa tena kwani bahat i wakat i mwingine haiji mara mbili.

    Ni vyema tukajiandaa m a p e m a k u u p o k e a Ramadhani na mgeni wetu huyo akija, tunahitajika tufanye mambo muhimu yafuatayo.

    K w a n z a n i k u w a wapole, wenye huruma, wanyenyekevu, kupendana na kusaidiana.

    P i l i n d a n i y a Ramadhani tunahitajika kutubu madhambi yetu kwa kumuomba Mola atusamehe yale mabaya na maovu tuliyoyatenda. Tunafahamu kuwa kwa udhaifu wa kibinadamu, katika kipindi cha mwaka mzima kama binadamu t u m e k u wa n d a n i ya dimbwi la maasi.

    Y a p o m a t e n d o tuliyotenda kwa viungo vyetu, kwa dhahiri au kwa bahati mbaya, yawe ya kutenda, ya kuona au kusikia, yote haya Ramadhani itatusaidia tuyafuta kwa sharti kuwa tuwe wakweli na tutubu katika ukweli wa kutubia.

    Hata tukishamaliza kutubia, tumeahidiwa kusamehewa na kuwa huru na mbali kabisa na madhambi. Muislamu anakuwa msafi kama siku ile ya kuzaliwa. Baada ya hapo mgeni wetu ataondoka, tunahita j i neema gani kubwa zaidi ya hii Waislamu.

    Tuangalie, ni wangapi tulikuwa nao na sasa hawapo. Hawakupenda kuondoka, lakini pia nao walikuwa wamekusuduia kuwa mwezi huu ukifika watafunga, watatubu makosa yao, lakini Mola keshawachukua.

    Basi somo hilo litoshe kwa Waislamu kujiandaa kukutana na mgeni huyu. Tu j iandae kumpokea vyema na kwa kuwa tumeshajua kuwa mgeni wetu ni mtakatifu na anakuja na neema nyingi, basi na sisi tujiandae

    kupata mafunzo ndani yake kitakatifu ili kuwa wasafi wa mwili na roho hata baada ya kuondoka.

    Tusikubali ulaghai wa dhana potofu za vunja jungu zilizobeba nafsi ya matamanio na uasi wa kidunia, zilizopandikizwa ili Waislamu wavunje imani zao na kuwa na dhamira m b a y a z a k u i p o k e a Ramadhani.

    D h a n a a m b a z o zimebuniwa ili ziwafanye Wa i s l a m u wa k u t a n e na Ramadhani wakiwa wachafu, tena uchafu wa kukusudia kufanywa kwa kuhofia kuwa ndani ya Ramadhani hakutakuwa na nafasi ya kufanya uchafu huo.

    N i u s h a u r i w e t u tujitahidi sana kuikwepa dhana hiyo ya uasi, tusiige tabia za ibilisi na shetani aliyelaaniwa.

    Sote tunafahamu kuwa Ramadhani ni ishara na alama njema na fundisho la kuwaunganisha Waislamu ulimwenguni kote katika ibada.

    B a s i W a i s l a m u wote nchini, ni vyema wakathamini somo hili, wakaungana kwa umoja wao na kusahau hitilafu zao kupitia Ramadhani hii.

    N i m u h i m u s a s a Waislamu wakajikurubisha kwa Mola wao, wakaandaa sehemu zao za ibada, masurufu ya futari na daku, kuwaomba msamaha wale wote uliowakosea, wawakumbuke yatima, wawakumbuke wagonjwa, was io j iweza , wa jane , wanaohitaji misaada, kutoa sadaka, kuwaaombea waliotangulia mbele ya haki na kila mara midomo yetu iwe ni yenye kutoa maneno safi na kumtukuza

    muumba.Shukrani zote ni zake

    Muumba wa mbingu na ardhi aliyetujaalia siku chache za mgeni wetu Ramadhan zinazompa M u i s l a m u n a f a s i ya kujisafisha na kuwa Mcha Mungu.

    Tutoe tu indhari kwa wafanyabishara wote nchini, hasa wa bidhaa za vyakula kuwa katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani, b a s i w a w a p e t a h f i f Waislamu kwa kuwauzia bidhaa kwa bei ya haki, ili kuwawezesha kutekeleza ibada hii kwa wepesi.

    Tukifanya baishara kwa uadilifu tukitanguliza mbele ucha-Mungu, utu na huruma kwa waja wa Allah, itakuwa na matokeo bora zaidi kuliko kuweka mbele tamaa ya kupata hata kwa kuwakomoa wafungaji.

    WA K I L I wa Wa i s l a m u wenye tuhuma za Ugaidi, Abubakari Salimu, amesema Serikali ina nia mbaya dhidi ya wateja wake kwa kuipiga danadana kesi hiyo ili wateja wake waendelee kusota rumande.

    Wakili huyo, ameyasema hayo Jumatatu wiki hi i akiongea na An nuur, mara baada ya Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, k u i a h i r i s h a k e s i h i y o inayowakabili Sheikh Farid Had na wenzake 23, mapaka Juni 18, 2015.

    Alisema, kutokana na mwenendo wa kesi hiyo unavyo kwenda, wanaona kama vile kuna nia mbaya ya kutaka kuichelewesha kesi hiyo kwa makusudi kwa kutumia kigezo cha rufaa yao (upande wa mashitaka) katika Mahakama ya Rufaa.

    Tunaona kama kuna nia mbaya ya kuichelewesha kesi hii, wanatumia kigezo k w a m b a k w a s a b a b u wamekata rufaa kat ika Mahakama ya Rufaa, ili pia na mambo mengine huku yasimame na hawa Waislamu waendelee kusota rumande. Alisema Wakili Salimu.

    Wakili Salimu, alisema awali katika kesi hii ya Masheikh na Waislamu, Mahakama Kuu i l isema kwamba shauri hili lirudi M a h a k a m a ya K i s u t u , ili litolewe maamuzi, na kwamba Mahakama isiseme tu kwamba haiwezi kusema chochote hivyo ikatakiwa

    Serikali ina nia mbaya-WakiliNi juu ya akina Sheikh MselemMgomo wapamba moto Segerea

    Na Bakari Mwakangwale irudi ili Mahakama iseme c h o c h o t e n a a m b a y e hatoridhika ndipo akatwe rufaa.

    Cha ajabu, alisema kwa upande wa Serikali, wao wakasema wanakata rufaa kwa maamuzi hayo ya Mahakama Kuu, akadai, hatua hiyo wanaona ni kuwa na nia mbaya ya kuchelewesha kesi hiyo, kwani imekuwa (upande wa mashitaka, Serikali) kila wakifika Mahakamani (Kisutu) wanasema kuna rufaa katika Mahakama ya Rufaa, kwa hiyo hawawezi kuendelea na chochote.

    Akifafanua kigezo hicho cha upande wa Serikali, Waki l i Sa l imu, a l isema rufaa hiyo haizui i kesi hiyo kuendelea kwani kwa vyovyote itakavyo kuwa, hata Mahakama ikisema, Mahakama Kuu ilikosea, i tabidi fa i l i l i rudishwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, na hata ikisema Mahakama Kuu ilikuwa sahihi bado faili litarudi Mahakama ya Kisutu, akahoji kulikuwa na haraka gani ya kukata rufaa.

    Wakili huyo, akasema kupigwa danadana kwa kesi hiyo ya Waislamu ni jambo la kusikitisha kwani hatua ya Serikali kukata rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu, wao upande wa utetezi wanaona sio sahihi, kwa sababu zimeshakuwepo kesi mbalimbali mfano wa hiyo, na wala Serikali haikuta rufaa.

    Kesi hizo zilikuwa ni za tuhuma za ugaidi na zilitolewa maamuzi na Mahakama Kuu

    lakini upande wa Jamhuri ya Muungano (serikali) hawakukata rufaa, si hivyo tu lakini hata nia ya kukata rufaa hawakuionyesha, lakini kwa hawa Waislamu hali inakuwa hivyo, hali hii inatia mashaka. Alisema.

    Akirejea mfano wa kesi hizo, alisema Mahakama Kuu, ilishawahi kuamua moja kwa moja kesi ya tuhuma za Uagaidi ilikuwa ikimkabili mwanasiasa Mh. Wilfred Lwakatare, ambapo alidai kuwa Mahakama hiyo ilifuta tuhuma za Ugaidi dhidi yake, lakini upande wa Jamhuri (Serikali) haikutoa taarifa ya kukata rufaa.

    Lakini akasema mbali ya kesi hiyo, aliitaja kesi iliyowahi kuwakabi l i wanachama wa Chama Cha Chadema Wilayani Igunga, Mkoani Tabora, ambapo Mahakama Kuu ilifuta mashitaka yao lakini upande wa Jamuhuri pia haikueleza nia ya kukata rufaa.

    Wakili Salumu, alisema kutokana na danadana hiyo, wanafuatilia suala hilo na kwamba wameshawasilisha maombi yao Mahakama ya Rufaa, juu ya suala hilo.

    Alisema, katika barua hiyo, wameomba mambo mawili, moja wapo ya mambo hayo, kwanza izuie hiyo taarifa ya kukata rufaa kwa maana kuwa iondolewe, ama isipo ondolewa basi rufaa husika isikilizwe haraka ili kutoka haki na mambo yaweze kuendelea katika Mahakama za chini.

    Inaendelea Uk. 4

  • 3 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Habari

    Aljazeera Ukerewe wakomesha propaganda za akina Jihad John

    Waonyesha njia. Wamwita OCD, HakimuWaislamu wasijifungie kama wauza bangiKamanda wa Polisi ahimiza Doria ya Roho

    K I T U O c h a K i i s l a m u , Aljazeera kilichopo Nansio, U k e r e we , k i m e f u n g u a milango yake kwa kila anayetaka kujua ukweli na kuvunjilia mbali propaganda chafu za kukibambikia ugaidi.

    K a t i k a h a t u a h i y o , iliandaliwa semina ya mwezi mzima ambapo msimamo na mafundisho ya Uislamu juu ya haki na wajibu wa Waislamu kwa binadamu kwa ujumla ulifafanuliwa kwa mapana na marefu.

    Masomo yaliyotolewa k a t i k a s e m i n a h i y o iliyowajumuisha washiriki 181 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, inafuta kabisa zile propaganda na dhana potofu kuwa Chuo cha Kiislamu kama Al- Jazeera , kuwa kinaweza kutumiwa kwa namna yoyote kusomesha n a k u h i m i z a j a m b o l a kuwadhuru watu.

    I l i k u l i w e k a h i l o bayana kwa vyombo vya Dola, kiserikali na kijamii, walialikwa pia washiriki na watoa mada kutoka taasisi mbalimbali zisizo za kidini wakiwemo Kamanda wa Polisi wa Wilaya, Hakimu wa Wilaya na maofisa wengine wa serikali.

    Huu ni ufunguaji milango na uwazi ambao kwa hakika ni wa kuhimizwa ufanyike k a t i k a t a a s i s i z o t e z a Kiislamu ili kuchoma moto kichaka wanakojificha watu wanaopiga propaganda chafu dhidi ya Uislamu.

    Maadhali mafundisho ya Uislamu sio biashara ya bangi, basi Waislamu wasione vibaya kuwaalika watu wengine, hasa mamlaka za kiserikali na taasisi za kijamii kuona wanachofanya na hata kutoa elimu kama alivyofanya OCD na Hakimu wa Ukerewe.

    I l ikuwa ni Imamu na Khatibu Mkuu wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mwanza Sheikh Hamza Mansour, a l i ye h u d h u r i s h a m a d a mintara fu muamala au mahusiano baina ya Waislamu na wale wasiokuwa Waislamu.

    Katika mada hiyo, Sheikh Hamza alionesha namna Mtume alivyoamiliana na wasio kuwa Waislamu kwa wema kwa kuwafanyia insafu na adala ya hali ya juu, hata wale ambao walikuwa maadui zake wa wazi kabisa.

    Ni katika hali hiyo, washiriki wa semina na Watanzania kwa ujumla wal i takiwa kujiuliza: kama Mtume (s.a.w) alikuwa akiwafanyia uadilifu, hata wale waliomtangazia uadui, vipi leo Waislamu watangaziwe ugaidi ambao tafsiri yake ni kuwadhuru watu wasio na hatia.

    Au vipi Chuo, Madrasa au shule inayoitwa ya Kiislamu, inayosomesha Uislamu, ituhumiwe kuwa inasomesha ugaidi.

    S h e i k h H a m z a

    Na Mwandishi Wetu, Mwanza

    akisherehesha mada yake h i y o , a l i w a k u m b u s h a wanasemina na Waislamu kwa jumla juu ya kisa cha mateka, aliyekuwa adui mkubwa sana wa Mtume (s.a.w.).

    Mateka huyo aki i twa T h u m a m a i b n U t h a l i aliyetangaza uadui dhidi ya Mtume (s.a.w.) kabla ya kukamatwa kwake kama mateka wakati wa vita.

    Baada ya kukamatwa m a t e k a , T h u m a m a alishikiliwa na Mtume (s.a.w) kwa muda wa siku tatu mtawalia msikitini kwake ilhali akipatiwa chakula na huduma zote za kibinadamu kwa insafu na kwa uadilifu wa hali ya juu na siku ya tatu Mtume aliamuru aachwe huru pasi kufanyiwa ubaya wowote kwa siku zote tatu za umateka wake.

    Akifafanua kisa hicho, Sheikh Hamza alisema kuwa Thumama alielekea nyumbani kwake baada ya kuachiwa huru na siku i l iyofuata akarudi kwa Mtume (s.a.w) kwa ajili ya kusilimu.

    Hata hivyo, kabla ya k u m s i l i m i s h a , M t u m e (s.a.w) alimuuliza sababu iliyomfanya asisilimu wakati alipokuwa mateka na badala yake akaja kutaka kusilimu baada ya kuwa huru.

    K w a m a e l e z o y a S h e i k h H a m z a k a m a yanavyopatikana katika vitabu vya Tarikh ya Kiislamu, Thumama alimjibu Mtume kwa kumwambia kwamba lau angelisilimu wakati akiwa mateka, watu wangelidai kwamba hakusilimu kwa imani thabiti kutoka katika moyo wake, bali amefanya hivyo kwa kutaka aachiwe huru kwa hofu ya kuchelea kuendelea kuwa mikononi mwa Waislamu akiwa mateka.

    N a k a t i k a k u j i e l e z a , T h u m a m a a k a m we l e z a Mtume (s .a .w) kwamba aliamua kusilimu kwa ridhaa yake mwenyewe baada ya kuachiwa huru kutokana na uadilifu aliotendewa na yeye mwenyewe yaani Mtume (s.a.w.) na Maswahaba zake (r.a.).

    Alisema, hakutegemea kabisa kufanyiwa wema ule

    kutokana na uadui wake a l iokuwa nao dhidi ya Uislamu na Mtume (s.a.w.).

    Kwa hiyo kutokana na utu na ubinadamu alioukuta kwa Waislamu, wafuasi wa Muhammad (s .a .w) wal iomshiki l ia mateka, ilimfanya atafakari juu ya Dini ya Muhammad na akaamua kusilimu.

    S w a l i a m b a l o k i l a mwanasemina alitarajiwa kujiuliza ni hili:

    Kama Uislamu unafundisha kuwafanyia insafu, uadilifu, utu na ubinadamu mateka wa kivita, vipi jambo la kuuwa na kujeruhi watu kigaidi linasibishwe na Uislamu, Waislamu na taasisi zao!

    Kama haya yanayodaiwa ya akina Jihad John na IS, yangekuwa na muingiliano wowote na Uislamu, basi tungeyakuta wakifanyiwa akina Thumama ibn Uthali na mfano wao, wakati wa Mtume (s.a.w).

    K w a u p a n d e w a k e Kamanda wa Jeshi la Polisi wa wilaya ya Ukerewe, Bw. Ali Muhammed alizungumzia suala la Ulinzi na Usalama ambapo aliwafahamisha wanasemina juu ya dhima ya Jeshi la Polisi katika suala la Ulinzi na Usalama wa Raia pamoja na mali zao.

    L a k i n i p i a akawatanabahisha juu ya dhima ya raia kuhusu masuala hayo kwa upande mwingine.

    Kamanda Ali aliwazindua wanasemina juu ya suala la haki na wajibu wao kwa Jeshi la Polisi kwa upande wao kama raia wa nchi hii.

    Aidha, alitumia vyema fursa hiyo kufafanua haki na wajibu wa Jeshi la Polisi kwa wananchi na kuwataka Mashekhe na Waislamu kwa jumla kudumu katika kile alichokiita 'doria ya kiroho'.

    H i y o n i p a m o j a n a kuhakikisha kuwa wanajenga hulka ya kunasihiana wao kwa wao pamoja na kuwanasihi wananchi wengine juu ya kuamrishana mema na kukatazana mambo maovu.

    Kwa upande wao kama Jeshi la Polisi aliahidi kwamba wataendelea na 'doria ya

    kimwili' katika kuhakikisha wa n a n c h i n a m a l i z a o wanakuwa katika hali ya usalama na amani.

    Kwa upande wake Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Bukindo wilayani humo Bw. Mrisho Abeid alihudhurisha mada mbili zikihusu 'Makosa ya Jinai' na 'Sheria ya Ardhi'.

    Mada ya 'Makosa ya Jinai' ililenga kuwapatia wanasemina mwangaza wa ufahamu juu matendo ya jinai ili waweze kuyatambua na kujitahidi kuyaepuka, hususan katika kipindi hiki cha zama za ulimwengu wa propaganda dhidi ya Waislamu na Uslamu kwa jumla.

    Kwa upande wa mada y a ' S h e r i a y a A r d h i Tanzania', hii ililenga juu ya kuwatanabahisha na k u w a t o l e a u f a f a n u z i wanasemina na Waislamu kwa jumla juu ya masuala mtambuka yahusuyo ardhi kama vile tafsiri ya ardhi kisheria, taratibu za kupata ardhi, umiliki wa ardhi, wajibu wa mmiliki wa ardhi, haki za mmiliki wa ardhi, jinsi ya kupoteza haki ya umiliki wa ardhi, migogoro ya ardhi, asili au chimbuko la migogoro ya ardhi pamoja na utatuzi wa migogoro ya ardhi.

    Pamoja na hayo, Bw. Mrisho Abeid aliwahamasisha Waislamu mmoja mmoja na kama kundi wajitahidi kadiri ya uwezo wao kutafuta na kumil iki ardhi , kwa munasaba wa kisheria na si kiholela au kimazoea, kwa ajili ya maendeleo yao binafsi ya kimakazi, kibiashara, kama ilivyo kwa wananchi wengine na kwa maendeleo yao kama umma kwa ajili ya ujenzi wa shule, hospitali, zahanati pamoja na vitega uchumi vingine.

    N a ye A f i s a B i a s h a r a wa wilaya ya Ukerewe, Bw. Sangarara Warioba aliwafunda wanasemina na Waislamu kwa jumla juu ya suala la ujasiriamali na umuhimu wake kwa Waislamu na kwa wanajamii wengine kwa jumla.

    Bwana Warioba alisisitiza umuhimu wa kujikwamua kiuchumi ili kujimudu kwa chakula, makazi, mavazi na kumudu kutekeleza ibada maalumu zinazomhita j i Muislamu kuwa na uwezo wa kimali kama kutoa zaka na kwenda kutekeleza ibada ya hijja.

    Akitoa nasaha zake katika semina hiyo, Sheikh wa wilaya ya Ukerewe Juma Saidi aliwanasihi wanasemina k u z i n g a t i a u t e n d a j i , uelimishaji na uchungaji wa mipaka ya Allah (s.w.).

    Kuhusu utendaji, Sheikh J u m a S a i d i a l i w a t a k a wanasemina wawe mabalozi wazuri katika jamii zao walizotoka kwa kuyatia katika vitendo yale yote waliojifunza kupitia semina hiyo katika maisha yao ya kila siku.

    Kwa upande wa suala la uelimishaji, Sheikh Juma aliwahimiza wanasemina wawafikishie Waislamu wenzao na jamii kwa jumla yale waliyojifunza pamoja na kuwataka wao wenyewe kuendelea kujifunza kutoka kwa Waislamu wenzao.

    Kwa kumalizia akawataka wa n a s e m i n a k u c h u n g a mipaka ya Allah (s.w.) popote watakapokuwa.

    Wa f a n y e h i v y o k wa kushikamana na mafundisho ya Qur-an na Sunna pamoja na kuwaasa kujiepusha na yale yote yanayopingana na viwili hivyo.

    Taasisi ya Al-jaziira Islamic Centre ( JIC) ipo kijiji cha Nebuye kata ya Ngoma tarafa ya Mumbuga wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

    Semina hi i ya mwezi mzima ni ya kumi na nne (14) ikiwa ni mwendelezo wa semina kumi na tatu zilizowahi kuratibiwa na kuendeshwa huko nyuma na taasisi hiyo kama mojawapo ya sehemu ya programu zake za kila mwaka.

    Semina ilifanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa uliopo katikati ya mji wa Nansio wilayani Ukerewe na kuhudhudhuriwa na Waislamu wapatao 181, wanaume wakiwa 98 na wanawake 83, kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na mikoa ya jirani.

    Mafunzo katika semina h i y o ya l i e n d e s h wa n a wataalamu mbalimbali wa ndani na wa nje ya taasisi hiyo waliohudhurisha mada kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba iliyopangwa ambayo ilijumuisha masomo ya elimu ya mwongozo ambayo ni Qur-an (Usomaji na Tafsiri), Hadith, Tauhiid, Fiq-hi pamoja na Sira.

    S e m i n a i l i f u n g u l i wa Ijumaa ya Mei nane (Mei 8) hadi Jumapili ya Juni saba (Juni 7, 2015).

  • 4 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Habari/Makala

    Serikali ina nia mbaya-WakiliInatoka Uk. 2Alisema, mpaka sasa kutokana na hali hiyo, wateja wake wanaoshikiliwa kwa muda mrefu sasa kwa kunyimwa dhamana, inaonekana wamepoteza muelekeo, kwani akasema hata hatua wanazo zichukua hivi sasa ni kutokana na madhila wanayoyapata.

    Alisema, hatua ya kugoma kula gerezani na kugoma kushuka katika gari kuingia Mahakamani Jumatatu wiki hii, ni miongoni mwa ishara za kupinga kunyimwa haki zao na kupigwa danadana kwa kesi yao.

    Leo (Jumatatu wiki hii) watuhumiwa wamefika Mahakamani, lakini kuna w e n g i n e h a w a k u f i k a k u t o k a n a n a s a b a b u mbalimbali, wapo ambao wanaumwa hawakuweza kufika na wengine wapo katika mgomo wametengwa, hatujui kinachoendelea juu yao. Alisema Wakili Salimu na kuongeza,

    N a h a wa wa l i o f i k a Mahakamani hapa Kisutu,

    nao hawakushuka, kutoka katika gari la Magereza ni mgomo mwingine tena huu ukiacha ule wa kula chakula, ambao ulianza na wachache wiki iliyopita.

    Alisema, migomo hiyo miwili tofauti ina maana tofaut i tofaut i kwanza wanalamikia kuona kuwa kesi yao inacheleweshwa bila sababu za msingi, lakini pia wanadai kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kusikiliza tuhuma zao kwa hivyo haikuwa sahihi wao kuletwa katika Mahakama hiyo.

    Lakini pia wametuambia kuwa madai yao waliyokuwa w a k i y a t o a s i k u z o t e ya kupat iwa mat ibabu hayatekelezwi pamoja na haja yao ya kuonana na Wanasheria Wakuu kutoka Zanzibar na Bara haijatimizwa kwa hiyo hawaoni sababu ya kuendelea na kesi yao. Alieleza kilio cha Masheikh

    na Waislamu hao.Kwa mujibu wa Wakili

    h u y o , Wa i s l a m u h a o wamedai kurejea Gerezani, Segerea kwenda kuungana na wenzao waliogoma kula, tokea wiki iliyopita jambo ambalo alidai inaongeza idadi ya wanaogoma kula kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele badala ya kupungua.

    Hata hivyo, Wakili huyo al isema kuwa Hakimu, a m e wa t a k a wa o k a m a Mawakili wa watuhumiwa hao, wanayo kila sababu ya kufika gerezani kuwaona watuhumiwa hao na kupata uhakika wa kile kinachodaiwa kugoma kula wakiwa humo gerezani.

    Kutokana na hii hali, Hakimu ameshauri tutumie nafasi yetu kwende kuonana nao na wao kama Mahakama, watachukua jukumu la kwenda kuwaona pia maana kisheria wanaruhusiwa

    k u f a n y a h i v y o , i l i kujiridhisha na kujuwa ni kweli watuhumiwa hao wamegoma kula au ni taarifa tu zinazushwa. Alisema Wakili huyo.

    Hata hivyo alisema, hatua hiyo ya kugoma kula na kuingia Mahakamani ni utashi wao kutokana na kuona kuwa hawatendewi haki, hivyo ikiwa wameona hiyo ndiyo njia ya kuweza kutoa msukumu kwa ajili ya kumaliza jambo lao, ni maamuzi yao binafsi.

    S i s i n a f a s i ye t u n i kuwashauri tu, kwamba wasigome kula, wasigome k u s h u k a k a t i k a g a r i wanapofika Mahakamani, lakini kutekeleza inabaki katika utashi wao ambao hakuna ambaye ataweza k u u i n g i l i a . H u w e z i kumlazimisha mtu mzima kula, kama anasema hataki, sasa wewe unafanyaje kwa hiyo hili ni suala la mtu binafsi

    kwa kile anachoamini inafaa katika kupigania haki yake, japokuwa sheria hairuhusu kufanya hivyo. Alisema na kufafanua.

    Kwa mujibu wa Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, imeeleza kuwa mpaka sasa (Jumanne wiki hii) idadi ya Waislamu wa l i o g o m a g e r e z a n i imefika 18, na wote hao wamewekwa katika selo ya ndani ya gereza hilo.

    Wa k a t i h u o h u o , i m e e l e z w a k u w a mtuhumiwa namba 22, katika kesi hiyo, Ustadhi Abdallah Saidi, ametolewa katika selo ya mjumuiko na wezake kutokana na kile kilichoelezwa kuwa yupo mstari wa mbele kutoa Daawa gerezani humo.

    Taarifa hizo zimesema k u w a U s t . S a i d i , alichukuliwa hatua hiyo na uongozi wa Gereza hilo tokea Juni 6, 2015,ambapo ameunganishwa katika selo maalumu ya Masheikh Faridi Had na Sheikh Mselem Ally.

    Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Rehema na amani zimfikie Mtume wa Mwenyezi Mungu.

    Kwa hakika wamezingatia wanachuoni funga kwa uwazi kuwa ni maisha ya kimaumbile hayawezi kuendelea maisha hayo i s i p o k u wa k wa f u n g a kutokana na usawa na Afya ya maumbile yetu yaliyokamili na kwa kiumbe yeyote hapana budi atakumbana na ugonjwa ambayo yatamzuia kula na kama hakufunga kwa kutaka mwenyewe.

    Hapa ndipo tunapoiona m i u j i z a ya M we n ye z i Mungu kwa kuweka sheria ya kufunga kuwa ni ibada, funga husaidia viungo katika kuvipumzisha kwa chakula kidogo pamoja na kuendeleza maisha ya kawaida kama ilivyo elimu ya kidaktari ya sasa imethibitisha kuwa funga ni kinga na ni tiba kubwa ya magonjwa mbali mbali

    Funga ni chanzo cha afya ya binadamu

    N a S h e i k h A l - s a ye d Awadh Abduladhim

    tena ya hatari magonjwa ya sasa pamoja na kuwa na kiasi kidogo cha chakula kilichopo kwenye moyo hujipanga pumzi na hufanya kazi kwa kujipumzisha zaidi na kwa mpangilio hujinyosha mapafu mawil i bi la ya kikwazo na hupungua vizuizi vya kukutana navyo moyoni hupungua mapigo yake kwa kutohitajika juhudi zote hizo zilizokubwa kwa ajili ya kusukuma damu kwenda katika moyo kwa kuipeleka msukumo wa kiasi kikubwa cha chakula na kabla ya kila kitu kwani viungo vingine hupata raha ya lazima kwa ajili ya kufanya upya wa viungo vi l ivyoharibika vipate uzima uliokamilika, n a k a m a i l i v y o k u w a uwakilishi wa chakula na uchafu wake huruhusu kipindi cha mapumziko viungo kuwa huru hapo hua upya yenyewe kwa yenyewe, na miongoni mwa mambo ambayo hayanashaka ndani yake, kwamba kila sheria katika uislam vina hukumu yake na faida zake nyingi kiasi haziwezi kudhibitiwa na akili ya kibinadamu na wala haiwezi kuwekwa kwenye elimu isipokuwa Mwenyezi Mungu ambaye ni mjuzi wa hali zote za viumbe na kwa yale yaliyo m a z u r i k wa o k wa m b a a l i v y o s e m a M we n ye z i Mungu mtukufu kwani anatu vile alivyoviumba naye ni mpole ana habari (14) Mulku lakini shina katika hekima katika kila ibada iwe kwa ajili ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mwenyezi Mungu sema hakika ya

    swala yangu na ibada zangu na uhai wangu na umauti wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu mola mlezi wa ulimwengu 162 An-aam. amesema Mtume (S.A.W) kwa hakika kila matendo hutazamwa nia na kila mtu ana alichonuia Bukhari na kwa hivyo basi ni wajibu wa kila muislam aweke lengo lake katika kila ibada ni kumridhisha Mwenyezi Mungu kwanza na mwisho na sio kupata faida ya kidunia kama hivyo ndivyo huenda ukafanikisha au usifanikishe na funga ya Ramadhani katika sheria ya kiislam ni nguzo miongoni mwa nguzo za kiislam ameifaradhisha kwa hekima yake kubwa kuziunganyisha nyoyo za waislamu kwa ucha mungu na si kwa manufaa ya kidunia ya mpito na kwa hivyo amesema enyi mlioamini imelazimishwa kwenu funga kama ilivyolazimishwa kwa watu waliopita kabla yenu ili mpate uchamungu 183 Al-bakarat funga katika uislamu sio mazoezi ya viungo, ambayo malengo yake ni kupunguza uzito wa mwili na kuiadhibu nafsi na kuilazimisha ili iwe nyepesi kukufuata na uitawale wala sio mazoezi ya kiroho kwa maana unaipa mazoezi kama huko wanako fanya mazoezi ya kihindi kwa lengo la kuongeza uzingatio au kukuza moyo au vinginevyo.

    Miongoni mwa malengo ya kidunia bali funga ni

    ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa ibada tukufu nayo ni siri kati ya mja na mola wake na Mwenyezi Mungu ndiye mlipaji wa funga amesema kila matendo ya binadamu ni yake isipokuwa funga kwani hiyo ni yangu na mimi ndiye nitakaye lipa imamu Bukhari hapo huja manufaa mwIngine yote kwa njia ya kuifuata funga au ni ya ziada tuu na moja ya manufaa hayo ni ya kidunia na hukumu ya mola mlezi ambaye wameanza kugundua juu ya funga kwa uwazi katika zama zetu hizi mpya nayo ni kupatikana afya ya kimwili na ya nafsi na badala ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumshukuru juu neema hizi zilizoongezeka katika funga juu ya neema ya kuabudu tumeanza tunajadili juu ya uwezo wa funga katika kutibu na magonjwa wakawa baadhi wanazungumzia k u h u s u k i w a n g o wanazungumzia kuhusu kiwango cha kushindwa kielimu katika kutibu kwa kutumia funga na kwamba ni tiba ya kila ugonjwa na kama ni makusudi wengine wanakanusha na wengi wao ni wale wanaotumia mali zao ovyo wao wanapinga k u wa f u n g a i n a n a f a s i yoyote ya kitiba miongoni mwa magonjwa na ni kati ya k u v u k a m i p a k a n a mapungufu akasimama mgonjwa akiwa ameduaa hajui juu ya hizi rai mbili ipi aushike na kati ya kuvuka

    mipaka au mapungufu inasimama dini ya kiislamu kwa ushupavu kwa ukati na kati wake uliozoeleka ili kuleta muongozo wake wa ukati na kati kwa ajili ya uma wa kati na kati katika hali zake zote kama alivyosema Mwenyezi Mungu mtukufu na hivyo hivyo tumewafanya uma wa kati na kati 143 Al-bakarat anasema mmoja wa madoktari waislam pamoja na kukiri kwangu kulikotimia k a m a d o k t a m u i s l a m kwamba funga husaidia katika tiba katika baadhi ya magonjwa isipokuwa mimi Siwezi kuutani kielimu kuwa ni hakika na ni maalum wakati wa mtume kabla ya zama zake kabla ya kuja mtume na hakuja mtume (S.A.W) kwa dalili ya wazi inayojulisha nafasi ya funga katika tiba na lililozuri na tuseme kwamba miongoni mwa hukumu za funga kuwa zinasaidia tiba baadhi ya magonjwa kwa masharti ya kushikamana na mpango wa chakula cha kiislam na amri za daktari anayekutibu na huu ndio muongozo wa ukati na kati katika kuifanyia kazi funga na hilo ndilo bora kwa kufuata na kuepuka kuvuka mikapa au mapungufu ambayo hupelekea maadui wa uis lamu kuwa una upungufu na hauna utukufu pale tutakapo waambia kuwa katika funga kuna tiba ya kila magonjwa tunawaambia hakuna tiba katika funga ya hivi hivi.

  • 5 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Habari za Kimataifa

    RIPOTI imefichuka kuhusu mikutano kadhaa ya siri baina ya wawakilishi wa Saudi Arabia na Israel kwa lengo la kujadili misimamo yao kuhusu Iran.

    Kwa mujibu wa tovuti ya Bloomberg, mikutano hiyo imefanyika mara tano katika kipindi cha miezi 17 iliyopita, ambapo maafisa hao wa Saudia na utawala wa Israel wamekutana kwa nyakati mbalimbali huko India, Italia na Jamhuri ya Czech.

    Tovuti hiyo imemnukuu Jenerali mstaafu katika Jeshi la Israel, aliyeshiriki katika moja ya vikao hivyo akisema, "Tuligundua kuwa tunakabiliana na matatizo na changamoto za pamoja na pia baadhi ya majibu ya pamoja."

    Aidha Alhamisi iliyopita maaf isa mashuhuri wa zamani wa Saudia na Israel walikutana katika taasisi za Council on Foreign Relations huko Washington.

    Kikao hicho kilihudhuriwa na Anwar Majed Eshki, Mshauri wa zamani wa serikali ya Saudia na Dore Gold, balozi wa zamani wa Israel ambaye nimtu wa karibu sana wa Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.

    Israel na Saudia zote kwa pamoja zinapinga kile zinachosema ni kuenea ushawishi wa Iran katika eneo la Mashariki ya Kati. Aidha pande mbili hizo zimetangaza wazi kupinga mapatano ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani.

    Hivi karibuni gazeti moja la Uingereza lilisema Israel imetangaza kuwa tayari kuipa Saudia makombora katika vita vyake dhidi ya watu wa Yemen.

    JESHI la Utawala wa Israel limewaua watoto wapatao 980 katika hujuma zake za hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza.

    Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, imekuwa ni jambo la kawaida kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kukiuka sheria zote za kimataifa kuhusu kulinda haki za watoto katika vita vyake dhidi ya Gaza.

    Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuwatetea Watoto Wapalestina, kwa mnasaba wa S i k u ya Wa t o t o Wasio na Hatia ambayo huadhimishwa Juni 4, imesema kuwa mwaka 2 0 1 4 n d i o u l i o k u wa mbaya na mgumu zaidi kwa watoto wa Gaza, kwani zaidi ya watoto 530 waliuawa katika hujuma za katili za jeshi la Israel.

    Aidha taas is i h iyo i l i sema kuwa kat ika mwaka huo, kwa wastani watoto 196 Wapalestina walikuwa wakikamatwa kila mwezi na vikosi vya Israel. Kwa ujumla zaidi ya Wapalestina 2,100, wengi wao wakiwa raia, waliuawa katika hujuma ya kutisha za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza mwaka 2014.

    Wakati huo huo taasisi za Umoja wa Mataifa zimeafikiana na taasisi za Palestina kuwa idadi ya kushtusha ya watoto waliuawa katika hujuma ya Israel huko Ghaza mwaka jana. Katika ripoti ya s ir i yenye kurasa 22 i l iyovujishwa kwa

    Watoto wanamalizwa PalestinaIsrael imeua watoto 980 Gaza

    vyombo vya habari, Jeshi la Israel limetajwa kuwa ni mtenda jinai mahiri dhidi ya watoto.

    Ripoti hiyo pia imetaja namna jeshi la Israel lilivyodondosha mabomu katika shule saba za Umoja wa Mataifa katika vita vya mwaka jana Gaza, ambapo wa t u 4 4 wa l i o k u wa

    wamepata hifadhi hapo waliuawa shahidi.

    I m e d o k e z wa k u wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, yuko chini ya shinikizo la Marekani kutoiweka Israel katika orodha ya nchi zinazokiuka haki za watoto kama ilivyopendekezwa katika ripoti hiyo.irib.

    WAZAZI wa Kipalestina wakiwa wamebeba maiti za watoto wao waliouliwa na majeshi ya Israel huko Gaza.

    CNN yafichua namna US inavyowapa mafunzo DaeshTELEVISHENI ya Marekani ya CNN imefichua kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imewapa mafunzo magaidi wa Daesh.

    Te l e v i s h e n i h i y o ya M a r e k a n i i m e s a m b a z a mkanda wa video kupitia Intaneti, ambapo ndani ya mkanda huo anaonekana Kanali Gulmurod Khalimov, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi la Tajikistan ambaye hivi sasa amejiunga na kundi la la Daesh akisema kuwa, yeye binafsi ameshiriki mara tatu katika mafunzo ya kijeshi ndani ya ardhi ya Marekani na moja ya mafunzo hayo ameyapata kwenye jimbo la Louisiana la Marekani.

    Hata Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imekiri jambo hilo. Msemaji mmoja

    wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameiambia televisheni ya CNN kwamba Kanali Khalimov, alipata mafunzo ya kijeshi katika vipindi vitano tofauti nchini Marekani na Tajikistan baina ya mwaka 2003 hadi 2014.

    Alisema, mafunzo hayo yalitolewa na kusimamiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa kile alichodai ni kupambana na ugaidi.

    Licha ya viongozi wa M a r e k a n i k u k i r i m a r a k wa m a r a k u wa n d i o waliolianzisha na kulipa mafunzo kundi la Daesh, lakini hivi sasa wameunda muungano wa kulipiga vita kundi hilo.

    Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa huo ni mchezo wa kisiasa tu wa

    JOHN Mcain aliyekuwa mgombea Urais wa Republican Marekani amekuwa kinara wa mawasiliano kati ya kundi la Daesh na Serikali ya Marekani nchini Syria.

    Mikutano ya siri Saudia na Israel ni hofu kwa Iran?

    Mar e k a n i n a k wamb a , Washington na washirika

    wake hawana nia ya kweli ya kupambana na kundi hilo.

    KAMANDA Mkuu wa Jeshi la Lebanon Jean Kahwaji ametoa shukuran zake za dhati kwa Wanaharakati wa Kiislamu wa Hizbullah nchini humo, kufuatia juhudi walizozionyesha katika kukabiliana na m a k u n d i y a k i g a i d i wakishirikiana wanajeshi w a L e b a n o n k a t i k a operesheni za pamoja katika maeneo ya mpakani mwa nchi hiyo na Syria.

    W a p a m b a n a j i w a Hizbul lah wal ianz isha operesheni za kuyasafisha maeneo ya mpakani ya al-Qalamun yaliyopo katika ardhi ya Syria tangu wiki tatu zilizopita, ambapo wamefanikiwa kuyasafisha maeneo mengi yaliyokuwa yamejaa makundi hayo.

    Kat ika hotuba yake , Kamanda Mkuu wa jeshi la Lebanon Jean Kahwaji, alisisitizia udharura wa kuendelezwa mapambano h a y o k w a l e n g o y a kuyasafisha kabisa maeneo ya mpakani mwa taifa hilo, huku akishiriautayari wa jeshi la Lebanon katika uwanja huo.

    Kahwaji alisema kuwa siasa za ndani ya Lebanon zinaviunga mkono vikosi vya jeshi hilo, ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa namna iliyo bora zaidi.

    Aidha alisisitizia udharura wa jeshi la taifa hilo kuwa m a k i n i n a k u o n g e z a kuwa, uchunguzi wa duru za usalama unaonyesha kuwa, makundi ya kigaidi yanakusudia kutekeleza vitendo vya kigaidi katika maeneo ya ndani mwa nchi hiyo kufuatia kushindwa huko mpakani.

    Inaelezwa kuwa baada ya mapigano makali katika maeneo ya al-Qalamun yaliyosababisha kusafishwa m a e n e o m e n g i n e y a kimkakati yenye ukubwa wa zaidi ya kilometa za mraba 300, kwenye miinuko ya mpakani mwa nchi mbili za Syria na Lebanon, hali ya usalama bado ni ya kutia wasiwasi katika miji na vijiji vya maeneo hayo kutokana na uwepo wa wanachama wa makundi ya Daesh na Jabhatu Nusra katika miinuko ya miji ya Arsal, Kaskazini Mashariki mwa Lebanon ambao wanaweza kufikiria kulipa kisasi.

    Ni katika mazingira hayo, ndipo Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah alisema kutokana na mazingira nyeti ya sasa ya taifa hilo la Kiarabu na eneo zima la Mashariki ya Kati, aliwataka viongozi na makundi ya siasa ya nchi hiyo kutambua mazingira hayo na kuisaidia serikali na jeshi katika kutekeleza majukumu yao ya kuimarisha usalama nchini.

    Jeshi Lebanon lawashukuru Hizbullah kwa kuwadhibiti magaidi

  • 6 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015TANGAZO

    ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

    Muda wa Kozi ni miaka miwili

    SIFA ZA MUOMBAJI:(a) Awe Muislamu.(b) Awe amefaulu masomo manne (4) au zaidi kwa kiwango cha D au zaidi katika Mtihani wa Kidato cha 4.(c) Atakayekuwa na ufaulu wa kiwango cha D au zaidi katika Lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili na Elimu ya Dini ya Kiislamu atapewa kipaumbele zaidi.

    Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 15 JULAI, 2015.Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 5,000/= (elfu tano) katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

    KOZI YA UALIMU WA LUGHA YA KIARABU, KIINGEREZA, KISWAHILI NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU NGAZI YA CHETI

    USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

    Bismillahir Rahmaanir Rahiim

    KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS COLLEGE - SAME, KILIMANJARO

    ARUSHA: Ofisi a Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu wa Bondeni, Simu: 0783 552414/0762 817640.KILIMANJARO-Moshi: Msikiti wa Riadha: 0712216490 Same Juhudi Studio mkabala naBenki ya NBC Same: 0757013344.Same: Kirinjiko Islamic Secondary School: 0784 296424/0655 676075.

    Usangi: Falhum Kibakaya: 0787 142054.

    Ugweno: Kifula shopping Centre: Yusuph Shanga: 0784 585776.

    TANGA: Twalut Islamic Centre - Mabovu Darajani: 0715 894111Uongofu Bookshop: 0784 982525.Korogwe: SHEMEA SHOP: 0754 690007.Lushoto: Mandia Shop: 0782 257533Handeni: Mafiga - 0782 105735/0657 093983.MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School: 0717 417685/0786 417685.Ofisi ya Islamic Education Panel, Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti wa Al-Amin: 0785086770/0714 097362.MUSOMA: Ofisi ya Islamic Education Panel Mtaa wa Karume, Nyumba Na. 05: 0765024623.

    SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini: 0752 180426.Kahama: Ofisi ya AN-NUUR na Msikiti wa Ibadhi: 0753 993930/0688 794040.

    DAR ES SALAAM: Ubungo Islamic High School: 0756584625/0657 350172.Ofisi ya Islamic Education Panel, Temeke - Msikiti wa Nurul Yakin: 0655144474, 0787119531.

    MOROGORO: Ramadhani Chale-0715704380

    DODOMA: Hijra Islamic Primary School: 0716 544757/0718661992.

    SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education Panel, karibu na Nuru Snack Hotel:0786425838/0784 928039.

    MANYARA: Ofisi ya Islamic Education Panel-Masjid Rahma: 0784 491196.

    KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714 717727Kibondo: Marubona Isl. SS. 0714 710802.

    LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.

    MTWARA: Amana Islamic S.S. 0715 465158/0787 231007.

    SONGEA: Kwa Kawanga karibu na Msikiti wa Nuru - 0713 249264/0683 670772.

    Mkuzo Islamic High School: 0717 348375.

    MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini- 0785 425319.

    Rexona Video mkabala na Mbeya RETCO, 0713 200209/0785 425319.

    RUKWA: Sumbawanga: Jengo la Haji Said - Shule ya Msingi Kizwike 0717 082072.

    TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566, 0787 237342.Nzega: Dk. Mbaga 0754 576922/0784 576922.

    IRINGA: Madrastun-Najah: 0714 522 122

    PEMBA: Wete Islamic Sch. 0777 432331/0712772326

    UNGUJA: Madrasatul - Fallah: 0777 125074

    Pandu Bookshop: 0777 462056 karibu na uwanja wa Lumumba.

    MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na Msikiti Mkuu: 0773 580703.

    Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

  • 7 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Makala

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-6

    Inaendelea Uk. 8

    Picha hizi mbili zimechorwa kuonesha ukhabithi wa Waarabu Waislamu. Lakini kweli picha hizi zinatokana na matokeo waliyoyafanya Waarabu? Au zote mbili zimeibiwa kutoka kwingineko na za asili hazikhusiani na Waarabu?

    Picha hii ya kushoto ya asili inakhusu ukhabithi uliofanywa Suriname, Amerika, na Wazungu Wakristo 1773. Hii ya pili ya kulia imekopiwa ili kuzua (na kupiga propaganda chafu kuwasingizia uovu) Waislamu Tanzania.

    Picha ya kwanza ni ya kuchora inazua ukhabithi ati walioufanya Waarabu Tanzania, kumbe ukweli ni kuwa inatokana na picha ya kamera inayoonesha ukhabithi walioufanya Waafrika Kongo kwa amri ya watawala wa Kibiligiji.

    Z I N A Z O F U ATA n i picha nambari 6.10 na 6.11 ambazo zimewekwa pamoja katika ukurasa wa 80 wa kitabu cha History for Secondary Schools , Form Two, 2012. Kwanza ziangalie picha zenyewe, ikisha tutazungumzia juu ya propaganda iliyotumika:

    Maana ya maelezo ya l i y o a n d i k wa k wa Kiingereza chini ya picha ya kwanza yanasema M t u m wa a k i p i g wa mboko na maelezo ya pili yanasema Mtumwa anyongwa na aachiliwa afe.

    K w a m t u y o y o t e mwenye kutumia akili yake, ataelewa moja kwa moja kuwa kuziweka pamoja picha hizi mbili si jambo la sudfa, bali ni la kukusudiwa. Ya kwanza inaonesha huyo khabithi anayemcharaza mboko mtumwa ni Mwarabu na kuiweka ya pili ubavuni mwake ni kumfanya mtazamaji mwenyewe amalize kwa fikra ya kwamba waliomnyonga mbavuni huyo mtumwa wa Kiafrika na kumwacha afe kwa maumivu mapevu ya kikatili, si wengine bali ni Waarabu Waislamu. Sasa tuangalie mchezo mchafu wa kipropaganda wenye kutumia dini kama n i k i s ing iz iyo ulivyochezwa.

    Kwanza, inasikitisha kuona kuwa waandishi wa kitabu hicho cha historia, kughushi mchoro wa yale yaliyotendeka Suriname Amerika ya Kusini, nchi ambayo ilikuwa ni koloni la Wadachi na wala sio Afr ika Mashariki na wakhusika walikuwa Wazungu Wakristo wala si Waarabu Waislamu. Sasa

    Kuadhibu Watumwaangalia tena hizo picha na zile za asili na ujiamulie mwenyewe namna na kadiri ya mchezo muovu unaochezwa na wale wenye siasa kali za kidini Tanzania.

    Picha ya kwanza ya upande wa kushoto ni ya asili, nayo imetokana na masimulizi ya John Gabriel Stedman. Picha hii, kwa tafsiri, imeitwa Mnegro aliyetundikwa ak iwa mzima kat ika mbavu zake kwa ajili ya kunyongwa Mchoro huo umetokana na maelezo ya alieshuhudia kitendo hicho huko Suriname mwaka 1773. Mtumwa huyo pichani alishindiliwa shazia au ndoana kubwa m b a v u n i m wa k e n a kutundikwa kwa ndoana hiyo. Katika tukio hilo, mtundikwa alikaa siku tatu akisononeka kabla ya kufa baada ya kupigwa rungu. Hapana shaka hayo yalikuwa mateso makubwa sana.

    Suala ambalo linafaa tujiulize hapa ni hili: Picha hii inakhusiana nini na Afrika Mashariki, kitendo ambacho hakina ushahidi wowote kuwa Mwarabu wala Mswahili kafanya Afrika Mashariki?

    K w a m t u y o y o t e a n a ye e l e wa a s i l i ya picha hizi na anayeweza k u i t u m i a a k i l i ya k e kiuadilifu, hataacha kujua kuwa hapa hapajatumika uadilifu na uelezaji wa kweli, bali zimetumika s i a s a k a l i z a u d i n i zinazotokana na Vita vya Msalaba ili kuuficha ukweli wa waliyoyafanya Waafrika na Wazungu Wakristo na kuwatupia uchafu wao Waislamu.

    N a w a u l i z a t e n a , kwanini ndugu Perazia Kaloly, Ferix Kiruthu na Cloudy Chatanda wameyafanya haya na nani waliowapa rukhsa hiyo ya kutumia propaganda hizo kuwasomeshea watoto wetu shuleni?

    Tuangalie sasa wapi imetokea na hiyo picha ya pili:

    Je, kuna shaka yoyote ile kuwa mchoraji wa picha ya juu amenyakua fikra hiyo ya kupigwa mnyonge wa Kiafrika kutokana na picha ya kamera ilioko chini yake?

    Katika picha hii ya kamera, tunayemwona

    n i M w a f r i k a n d i y e a n a y e m p i g a m b o k o Mwafrika mwenziwe, na tokeo hilo limetendeka Kongo chini ya utawala wa wakoloni wa Kibiligiji

    Wa z u n g u Wa k r i s t o . I m e a n d i k wa k w i n g i na hadi kuna kanda za filamu zinazoonesha na kuzungumzia ukhabithi wa Mfalme wa Wabiligiji,

    Leopold II (1835-1909). M f a l m e h u y u n a

    Wabiligiji walipoitawala Kongo, waliwalazimisha Waafrika kuwafanyia

  • 8 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Makala

    Picha hii inaonesha Wabiligiji na watumwa wao ambao wameshikishwa viganja vya watumwa waliokataa kufanya kazi bure na kukatwa viganja hivyo kutiwa adabu ili pia kuonesha mifano kwa wengine nini watafanywa wakikataa kuwa watumwa wa Wabiligiji.

    Wabiligiji waliwatia mpaka watoto wadogo wa Kiafrika utumwani, Kongo.

    Mwafrika kutiwa adabu na Wazungu amekatwa kiganja.

    Angalia na hii picha ya kuchora ya kerekecha inayoonesha vipi Mfalme Leopold II wa Ubiligiji alivyowazonga na kuwatia kabare Waafrika wa Kongo kama chatu.

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-6kazi kama ni watumwa wao na wanahistoria wa n a t u e l e z e a k u w a Wabiligi j i waliwauwa Waafrika wasiopungua m i l l i o n i k u m i n a k u wa m a u wa j i h a y o yanatambulikana kama ni maafa makubwa. Mauwaji ya khala ik i ya watu ambayo kwa Kiingereza huitwa genocide.

    Iangalie tena picha y a a s i l i y a k a m e r a iliyotangulia na utaona kuwa Mwafrika aliyekuwa kibaraka wa Kibiligiji, n d i y e a l i y e t u m w a kumpiga mboko mtumwa wa Kiafrika. Mzungu M k r i s t o h a o n e k a n i p i c h a n i , k wa h i v y o lawama kubwa anatupiwa nokoa wa Kiafrika kwa k u t e k e l e z a a m r i z a Mzungu za kumtendea mtumwa ukhabithi.

    Lakini picha ya kuchora inaonesha kuwa khabithi huyo mwenye kumtandika m b o k o m t u m wa wa Kiafrika, ni Mwarabu mwenyewe, ingawa hao makhabithi wa Kiarabu pia waliwatuma manokoa wao kutekeleza amri zao. Kwa hivyo, katika picha hii tunapooneshwa moja kwa moja kuwa ni Waarabu Waislamu wenyewe ndio waliowafanzia ukhabithi watumwa wa Kiafrika, lawama zetu zinawashukia Waarabu Waislamu bila ya kizuizi.

    Kama nilivyoelezea, picha hii ni ya kuchora, si ya kamera kama ya chini yake. Kwa hivyo inatokana na fikra za mchoraji . Je, unadhani mchoraji hakukusudia mtazamaji aone uchungu na ahisi chuki juu ya Mwarabu Mwislamu na hatimae kuwachukia Waislamu na Uislamu wenyewe? Kila kitu kimepangwa na wenye siasa kali za udini na wachoraji wao. Hakuna kilichochorwa kwa bahati mbaya.

    P i c h a n a a s i l i z a k e t u m e z i o n a . J e , wa n a p r o p a g a n d a z a udini walidhani kuwa kule kughushi kwao hakutatambuliwa?

    Haisikitishi tu, bali i n a l i z a k u i o n a h a l i ya masomo ya historia iliyojaa chuki dhidi ya Waislamu Tanzania ilivyo, huku wanajua fika kuwa Tanzania ina Waislamu

    Inatoka Uk. 7

    w e n g i s a n a a m b a o wameshaanza kuelewa upotoshaji huo ulivyo. Hii ni khatari kubwa sana kwa usalama wa nchi, na wa kulaumiwa hawatakuwa wengineo, ila ni wale waliojitosa katika propaganda za siasa kali za udini zinazotokana

    na Vita Vya Msalaba na kujitwika bendera ya vita hivyo visivyowakhusu ndewe wala sikio. Waku-laumiwa pia ni Serikali ya Tanzania iliyozifumbia macho propaganda hizo na kuziachilia zisomeshwe katika shule na kutia chuki katika bongo za vijana.

    K a t i k a m a a n d i s h i ya o p i a wa m e t u m i a propaganda kubwa kwa mwenye kuelewa lugha ilivyotumiwa. Kwa mfano, katika sehemu waliyoiita The psychological effect of slavery on its victims yaani: Athari ya kisaikolojia ya utumwa kwa waathiriwa, mna mengi yaliyokusudia kuficha ukweli na kuleta

    c h u k i , w a m e a n d i k a Perazia Kaloly na Ferix Kiruthu yanayofuata:

    The Arab slave traders and the Caucasians slave owners looked down upon dark-skinned people.

    Ta f s i r i : W a f a n y a biashara ya utumwa wa Kiarabu na Wakaukasian wamiliki wa watumwa waliwadharau watu wenye ngozi nyeusi.

    A n g a l i a i b a r a h i o ilivyoandikwa, kwanza katajwa Mwarabu kwa d h a m b i k u b w a y a kufanya b iashara ya utumwa, khalafu katajwa Caucasian kwa dhambi ndogo ya kumiliki.

    Je, wewe unawafahamu nani wamekusudiwa kwa jina la Caucasian?

    H i l o n i j i n a l a k ie thonol i j ia ambalo halifahamiki kwa wengi isipokuwa wasomi. Walio kusudiwa hapo ni wa jamii

    ya Kizungu. Kwa nini hawakuainisha wazi kwa kuandika Wazungu, au anataka kuwaficha?

    Ingekuwa waandishi hao wana nia nzuri ya kufundisha, wangelitumia majina yanayofahamika kwa wengi, na ikiwa kama waandishi wameamua k u t u m i a m a j i n a y a kiethonolojia kwa nini

    b a s i wa s i t u m i e k wa wote badala ya kuandika wafanya biashara wa Kiarabu wakaandika wafanya biashara ya utumwa wa Kisemiti.

    Kwa nini waighushi picha hiyo? Kwa nini wachezee maneno? Au kwa kuwataja Wazungu ingelitambulikana kuwa wao walikuwa pia ni madhalimu wakubwa na walikhusika katika udhalimu huo.

    Angalia picha zote mbili na utafakari ibara hiyo khalafu uhukumu nini agenda ya Perazia Kaloly na Ferix Kiruthu, na historia itawakumbuka kwa hayo.

    W a l i c h o k i f a n y a waandishi wa vitabu vya historia Tanzania na wachoraji wao ni kunyakua picha zenye kuonesha ukhabithi uliotendwa

    Inaendelea Uk. 12

  • 9 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Makala

    Aljazeera Ukerewe yazima uzushi wa Jihad JohnAlikeni Polisi Msikitini waone ghala la mabomu!Mwenzao alisilimu baada ya kutesa GuantanamoOCD Nansio ajionea. Sasa ahimiza Doria ya Nafsi

    Guantanamo Dar es Salaam!!!Na Bakari MwakangwaleUKIFIKA wanakuambia kabisa kuwa hapa sio M a h a b u s u . H a p a s i o G e r e z a n i w a l a h a p a sio Selo ya Polisi. Hii ni Guantanamo.

    N i l i w a a m b i a h a t a mkiniuwa msidhani kwamba mtakuwa mmefanikisha lengo lenu. Sisi mnatukamata si kwa kuiba, au tumefanya ovu lolote huko uraiani, bali mnatutuhumu kwa dhana tu, labda mseme kosa ni imani yetu na Uislamu wetu.WAISLAMU waliokamatwa kwa tuhuma za Ugaidi, wamefichua kuwa ipo Guntanamo isiyo rasmi nchini wanayoingizwa watuhumiwa kuteswa kabla ya kufikishwa Mahakamani.

    Aidha, imedaiwa kuwa Guantanamo hiyo ipo chini ya kikosi maalumu kinachojulikana kama Task Force ambacho kinafanya kazi nje ya utaratibu wa kawaida wa kipolisi.

    Hayo yamebainishwa na mmoja wa watuhumiwa hao, akiongea na An nuur, akidai kuwa Waislamu wanafanyiwa dhulma kubwa wanapokuwa mikononi mwa watu hao ambao wanajiita Task Force na kwamba unaweza usiamini ukielezwa unachofanyiwa pindi wanapokuhoji watu hao.

    Alipoulizwa kwanini a n a l e t a m f a n o w a Guantanamo, alieleza kuwa ni maafande hao, wanaoitaja sehemu hiyo kwa jina hilo mbele ya watuhumiwa, tena kwa majigambo na kwamba sehemu hiyo ipo maeneo ya Mikocheni, Jijini Dar es Salaam, na wanaeleza wazi kuwa hapo sio Polisi.

    H i l i n e n o n i w a o w a n a l i t a m k a m b e l e yetu, wanapaita hapo ni Guantanamo, na ukifika wanakuambia kabisa kuwa hapa sio Mahabusu, hapa sio Gerezani wala hapa sio Selo ya Polisi, bali wanasema hii ni Guantanamo ya Serikali. Alisema Muislamu huyo.

    A l i s e m a , k a b l a y a kukamatwa na aliposikia m a d a i y a M a s h e i k h waliofanyiwa vitendo vya kinyama, ilikuwa ni vigumu kuamini kama kweli kuna askari ndani ya Tanzania hii wanaweza kufanya mambo hayo.

    Lakini anasema, baada ya kuwa mikononi mwa watu hao, na mwenendo wao wa kuwahoji na kuwatesa watuhumiwa wa ugaidi, alibaini kuwa hawashindwi kukufanyia unyama wa aina yoyote.

    G u a n t a n a m o n i Mahabusu/gereza, lililopo Marekani, ambalo Taifa hilo hulitumia kuwahifadhi watuhumiwa wa ugaidi kutoka nchi mbalimbali kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

    Alisema, kuwa katika

    majumba hayo (Guantanamo) kuna watu wapatao tisa mpaka 12, ambao alidai kuwa ni Maafisa wa Polisi na wale wa Usalama, na kwamba hiyo ni timu maalum inayojiita Task Force.

    Al i sema, uki ingizwa humo, unawekwa mbele yao kisha wanakuuliza maswala mbalimbali kila mmoja swali lake kuhusiana na wewe binafsi pamoja na masuala

    ya Waislamu na Uislamu kwa ujumla.

    M u i s l a m u h u y o , a l iye mwenyej i wa n je ya Jiji la Dar es Salaam, aliyeshikiliwa kwa muda wa siku 20, akiwa mikononi mwa Task Force kabla ya kufikishwa Mahakamani, alibainisha kuwa, Waislamu wanaokamatwa ndani na nje ya Jiji wengi wao hufikishwa kwanza Makao Makuu

    ya Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam (Central) kisha h u p e l e k wa M i k o c h e n i (Guantamano).

    A l i s e m a , j a m a a h a o wanauliza maswali ambayo wanajua kabisa kuwa huna majibu, lakini wanataka wewe uwajibu vile wanavyotaka wao jambo ambalo mwisho wa siku watakuingiza katika kipigo tu.

    Kama ukiwaambia hujui

    wanachokuuliza, utasikia wanasema mpeleke gereji, huko ndio kuna mateso makubwa, humo gere j i moja ya zana wanayoitumia kuwaadhibu Wais lamu (watuhumiwa) ni mipini ya majembe, sio bakora, wala hupigwi kwa makofi, ni hiyo mipini na vifaa vingine vizito ndivyo vinavyotumika.

    Kuna watu wa miraba minne wanafanya shughuli h i y o , n a a n a p o a n z a kukuadhibu anachojoa shati, anapiga miguuni katika nyayo, mgogoni mpaka anatoka jasho kwa kupiga mwanadamu mwenzake. Amesema Muislamu huyo.

    Alisema, kwa kawaida ukitoka Sentro, kwenda Guantanamo, unatoka ukiwa unatembea mwenyewe, lakini ukirudi jioni kutoka huko unaitafutia miguu pa kukanyaga, kutokana na kuvimba na wakifika hapo Polisi, wanakutupa tu kama mnyama hamna cha matibabu wala huduma ya kwanza.

    Alisema, mara nyingi walipokuwa wakirudishwa Sentro katika hali hiyo ya m a u m i v u , a l i k u wa akiwafariji wenzake kwa k u wa p a m a wa i d h a n a kuwajenga kiimani kutokana na hali mbaya wanayorudi nayo kutoka Mikocheni, jambo ambalo lilisababishwa k u h a m i s h w a s e l o n a kupelekwa kituo kingine cha Polisi.

    Anasema, awali akiwa Guantanamo alipigwa sana na watu hao wanaojiita Task Force lakini wakashangaa hakuwa analia wala kupiga k e l e l e , j a m b o a m b a l o liliwashangaza na kudai kuwa yeye ni sugu.

    Hata hivyo alidai kuwa aliwajibu kwamba, wasidhani nj ia hiyo wanayotumia ya kuwatesa Waislamu ni kuwakomoa.

    N i l i w a a m b i a h a t a mkiniuwa msidhani kwamba mtakuwa mmefanikisha lengo lenu, kama mnadhana hivyo, muelewe kuwa kwa Muislamu haiko hivyo, sisi mnatukamata si kwa kuiba, au tumefanya ovu lolote huko uraiani, bali mnatutuhumu kwa dhana tu, labda mseme kosa ni imani yetu na Uislamu wetu.

    Najua nipo hapa kwa ajili ya Uislamu wangu, kwa hiyo napata faraja kila mnalonifanyia. Mimi na Waislamu wenzangu, kwetu ni kheri zaidi kuliko m n a v y o d h a n i a , z a i d i mnatuz id ish ia imani . Alisema akirejea kauli yake mbele ya Task Force.

    Alisema, kufuatia kauli yake hiyo, kuna afande aliunga mkono, akisema anachosema huyo Ustadhi ni sahihi, akiwafafanulia msimamo wa Waislamu wa Libya na Palestina, ambaye alidai amejifunza kutoka kwao alipokuwa masomoni

    Inaendelea Uk. 11

    Terry Holdbrooks Jr., ni mmoja wa Polisi Jeshi (MP) (Military Police), waliokuwa wakiwalinda, kuwatesa na kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi kule Kambi ya Guantanamo (Camp Delta, JTF Guantanamo Bay). Akiwa amefanya kazi hiyo mwaka 2003 na 2004.

    Ilikuwa ni katika usiku mmoja wa mwezi Desemba 2003 ambapo Terry anasema a l i k u w a t a y a r i k u w a Muislamu kwa kusoma maneno yaliyoandikwa kwa Kiingereza, yakisomeka:

    There is no god but God, and Muhammad is the messenger of God.

    Anasema, aliandikiwa maneno hayo katika karatasi ngumu na mfungwa mmoja yakiwa yametafsiriwa kutoka lugha ya Kiarabu kwa sabbu i l ikuwa vigumu kwake wakati huo kuyasema kwa Kiarabu.

    Anasimulia Kay Campbell kuwa Terry alisilimu baada ya kuusoma Uislamu kwa wafungwa wa Guantanamo, U i s l a m u a m b a o a wa l i aliambiwa ni dini ya vurugu na maangamizi , lak in i akakuta kumbe ndiyo dini yenye nidhamu na amani aliyokuwa akiitafuta katika maisha yake.

    Akisimulia safari ya Terry kusilimu, mwandishi Kay

    Kwenu yaweza kuwa kosa mimi kulisilimu

    Lakini mimi Terry Holdbrooks sio msalitiNi aibu kuwa na kitu kama Guantanamo

    Campbell anasema kuwa kijana Terry Holdbrooks wakati huo akiwa na umri wa miaka 29 alikuwa mmoja wa vijana wengi wa Kimarekani waliojiunga na jeshi baada ya Septemba 11, wakiwa na hasira ya kwenda kupambana na Waislamu baada ya kupigwa propaganda kuwa Waislamu ndio waliolipua majengo pacha ya World Trade Centre (WTC) na kuuwa zaidi ya Wamarekani 4000 wasio na hatia.

    Holdbrooks walked into an Army recruiters office in Arizona a year after 9/11 saying he wanted to join the Army, go kill people and get paid for it (then he) signed up for military police because it offered a bonus.

    Anasimulia mwandishi Campbel l ak imaanisha kuwa Terry aliingia jeshini katika kikosi cha MP mwaka mmoja baada ya Septemba 11 akiwa na shauku ya kuwa muuwaji wa kulipwa, akikusudia kuuwa Waislamu waliohusika na Septemba 11.

    Anasema kuwa kabla ya kupelekwa Guantanamo, w a l i p i g w a d a r a s a n a Kamanda wao wakiambiwa kuwa wanakwenda kukutana na magaidi hatari sana, magaidi wa kimataifa na hivyo wawe makini na wasiwe na chembe ya huruma

    juu yao.Remember what Muslims

    did to us. Remember who youre protecting.

    Anasema Terry, kuwa hayo yalikuwa maneno ambayo kamanda wao aliyekuwa na cheo cha sergeant alikuwa akiyarudia mara kwa mara kama kuwakumbusha kuwa wanakwenda kukabiliana na watu waliouwa Wamarekani 4000 katika September 11 na hivyo hawastahiki kuonewa hata chembe ya huruma kwa sababu ni magaidi katili.

    So Holdbrooks arrived at the hot, seared base expecting hulking killers in every cell. Anasimulia Campbell.

    H a t a h i v y o T e r r y anasema, alipofika huko na kila masiku yalivyokuwa yakienda, alikuja kuona kuwa aliyokuwa ameambiwa na makamanda wake na hali halisi, ni mambo mawili tofauti kabisa. Ni kama mbingu na ardhi.

    Akitaraji kukutana na mijitu iliyobobea katika medani ya kijeshi na kivita, a l isema al ikuja kukuta kuwa watu a l iokutana nao walikuwa madaktari, walimu wa skuli na madrasa, wa k u l i m a n a wa f a n ya biashara, maimamu wa Misikiti, madereva wa tax (tax drivers) na maprofesa wa

    Inaendelea Uk. 10

  • 10 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Makala

    Kosa kulisilimu?vyuo vikuu, huko watokako.Katika hao wanaodaiwa kuwa magaidi hatari, Terry anasema alikuwepo mtoto wa miaka 12 na mzee wa miaka zaidi ya 70 aliyekaribia kukata roho kwa maradhi ya TB (tuberculosis) iliyokuwa imefikia kilele kwa kukosa tiba stahiki.

    Hali hiyo ilimchanganya MP Terry ambaye alikuwa kazi yake ni kuwatoa wafungwa kutoka katika sero zao na kuwapeleka katika vyumba vya mahojiano na kuwarejesha. Aidha alikuwa pia katika zamu ya kuwalinda usiku na mchana.

    Kilichomshanganza zaidi anasema, watu hao hawakuonekana kuwa na fadhaa wala kukata tamaa, bali wenye moyo, ucheshi, furaha na nidhamu ya kuchunga muda wa swala.

    The detainees read their Qurans. They kept the daily schedule of prayers. They remained undiscouraged under horrendous pressure.

    Mtu anakuwaje mahali pa mateso kama hapa Guantanamo lakini abdo unamuona anatabasamu?

    Ni moja ya maswali yaliyokuwa yakimsumbua MP Terry alivyokuwa akiwaona wafungwa wake Waislamu walivyokuwa na mioyo ya kutokukata tamaa, wakiwa wenye furaha na tabasamu kila akiongea nao.

    Unakuwaje mahali pa mateso kama hapa, halafu bado unaamini kuwa kuna Mungu anayekujali, wakati anakuacha unateseka hapa Guantanamo?

    Ni swali j ingine l i l i lokuwa l ikimsumbua Terry akiwaona Waislamu wale kila ikifika muda wa swala utawakuta wanatawadha na kuswali. Nidhamu waliyokuwa nayo katika ibada zao na kudumu katika kusoma Quran.

    H i l i n i j a m b o j i n g i n e lilimchanganya MP Terry. Akawa karibu nao na kuwa akiongea nao mara kwa mara kujua walikotoka na maisha yao yalivyokuwa. Ni kupitia mazungumzo hayo, alikuja kuwajua kuwa wengi wao ni baba na waume wema katika familia zao, wasomi, lakini pia raia wema na wafanyakazi wasio kuwa na matatizo walikotoka, halikadhalika wanaolaani tukio la September 11 na kusema kuwa waliofanya uharamia na ugaidi ule ni watu katili, shambulio ambalo halikubaliki kabisa katika Uislamu.

    Unapowasikiliza watu hawa na kutizama mienendo yao, kutwa nzima, you start thinking, Was I lied to?

    Anasema Holdbrooks kwamba lazima itakujia kuwa ulidanganywa kuwa unakwenda kukutana na majitu magaidi katili.

    Hali hiyo ilimpa hamu Terry ya kusoma juu ya Uislamu kupitia internet na kisha kupata hamu ya kujua nini kipo katika Qurna ambapo alipewa Quran ya tafsiri ya Kiingereza ambayo alitumia muda wa siku tatu tu kuisoma yote.

    It took Holdbrooks three nights to read it. As a restless seeker in his teens, he had studied Christianity, Buddhism, Judaism, and never saw much sense in them. In the Quran, for the first time,

    Inatoka Uk. 9

    Terry Holdbrooks Jr.

    WAANDAMANAJI wakimchagiza Rais Barack Obama kuifunga Guantanamo.he found a religious text that meets his logical criteria.

    Ndivyo anavyosimulia mwandishi Kelly kuwa kwa mara ya kwanza Terry alikuwa ameona ndani ya Quran mafundisho yenye mantiki na yanayoingia akilini tofauti na aliyokuwa akisoma katika Ukristo, Ubudha na Uyahudi.

    It made sense from beginning to end. It doesnt contradict itself. Theres no magic. Its just a simple instruction manual for living.

    Ndivyo anavyoe leza Terry Holdbrooks mwenyewe kuwa ndani ya Quran ni vitu vyenye mantiki

    mwanzo mwisho, wala hukutani na vitu vyenye kujikoroga. Hakuna uchawi na mkanganyiko, bali ni maelekezo mepesi ya kueleweka juu ya maisha.

    Hata hivyo, mambo hayakuwa m e p e s i k wa Te r r y b a a d a ya kusilimu. Alikuja kufukuzwa jeshini ikidaiwa kuwa kachanganyikiwa. Mkewe naye akamkimbia. Alifikia kupachikwa tuhuma ya usaliti jambo lililompelekea kuandika kitabu alichokipa jina Traitor?, chenye kurasa 164.

    I may have become a Muslim, but I am not a traitor.

    Anasema Terry katika kitabu hicho kinachopatikana online kupitia www.GtmoBook.com.

    Kwamba anaweza kushutumiwa kwa kusilimu kwake, lakini labda kwa wengine huko kusilimu ndio kosa, lakini yeye sio msaliti wa Marekani.

    Kinyume chake anasema, ni aibu kwa taifa linalojinadi kwa ustaarabu kama Marekani kuwa na kambi ya mateso Guantanamo. Anasema hapo ni mahali panapofanyika mambo ambayo hutarajii afanyiwe hata mnyama, ndio maana inafikia mahali hata wafungwa pamoja na ustaarabu wao wanafikia mahali pa kugoma kula. Anataja kisa cha wafungwa 102 ambao waligoma kula kwa zaidi ya siku 100.

    I tell this story and I wrote the book so idiot-simple that anyone could read and understand that the existence of Guantanamo is something to be ashamed ofI just want to share information with people in depth and then let them make up their mind.

    A n a s e m a H o l d b r o o k s akitukumbusha kuwa wakati sisi tunajinadi kuwa tuna Guantanamo zetu huku, tujue kuwa huko kwa walimu na wakufunzi wetu, serikali inachagizwa kuifunga kwa sababu ni jambo la aibu, ushenzi, fedheha na ukosefu wa utu.

    Watu wengi wenye heshma zao katika jamii na kimataifa, wakiwemo wasomi, wanasheria, wapigania haki za binadamu, wanasiasa, watu wa dini, wameandika vitabu, makala na kufanya mihadhara kumtanabahisha Rais Barack Obama kuifunga Guantanamo kwa sababu ni jambo la kifedhuli, aibu, ushenzi lisilofaa kufanywa na watu wastaarabu.

    Akizungumzia hali ya Waislamu hivi sasa ulimwenguni, Terry ametoa wito kwa Waislamu wasiufanye Uislamu kuwa kama biashara ya bangi.

    You cant be afraid to be a Muslim in public. Tell your neighbors youre Muslim. Invite them into your home. Invite them to visit the masjid to see our secret bomb factories. If its time to pray pray. The whole world is an acceptable place to pray.

    Kwamba, Waislamu wasiogope kuweka Uislamu wao hadharani. Kama ni majirani zako wajue kuwa wewe ni Muislamu (na wanufaike na wema wa jirani Muislamu). Waalike nyumbani kwako. Waalikeni wasio kuwa Waislamu Msikitini waone (ili kukomesha propaganda kuwa kuna) viwanda vya mabomu ya kufanyia ugaidi. Ukifika wakati wa swala, swali. Ardhi yote ni mahali pa kuswalia.

    Akitoa wito rasmi kwa Waislamu wa Marekani, Terry anasema kuwa anataka lau anakuja Mtume (s.a.w) leo, basi akute Waislamu bora kabisa wapo Marekani.

    Kwa hivyo wajitahidi kwa kusoma na kuwa watu wenye kufanyiana wema miongoni mwao na kwa walimwengu, kuanzia ndani ya Marekani na nje. Kwamba Waislamu wa Marekani wana wajibu wa kufuta picha mbaya ambayo inajipaka nchi yao hivi sasa kwamba ni taifa la kibabe na mauwaji dunia nzima tena kwa watu wasio na hatia.

  • 11 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 201511 AN-NUURMakala

    Mafundisho ya Quran

    Fethullah-Gulen

    NA wape habari njema wale ambao wameamini na wakatenda matendo mema kwamba wana wao mabustani inapita ndani yake mito kila wanapopewa humo katika matunda chakula wanasema: Hiki ndicho tulichopewa huko nyuma na wanakiletewa hali ya kuwa kinafanana na wana wao humo wake walio takaswa na wao humo ni wenye kuishi mielele. [Al-Bararah 25]

    H a k i k a a ya h i i N a wa n a k i l e t e wa h a l i ya k u f a n a n a , i n a a s h i r i a kwenye kufanana, katika mtizamo wa kupata neema, na uwezesho kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

    Kufuatana na ufananizaji wa Al-Ustadh Saeed A-Nursi, neema hizi zenye kufanana huenda zikawa ni katika m i s a a d a ya M we n ye z i Mungu ya hapa duniani au ni katika misaada ya akhera. Kwa mfano: Mtu anamsifu Mwenyezi Mungu hapa duniani, maana anasema: Al-Hamdulillah anazikuta sifa hizo zinatengeneza tunda huko akhera- maana kila takbira na kila tasbihi na kila tahlili hapa, iko katika nafasi ya kokwa na mbegu zilizotawanywa na zilizopandwa katika udongo, zinazaa neema mbalimbali huko peponi.

    I s ipokuwa kunapasa kuashiria kuonyesha kitu muhimu sana katika jambo hili, nalo ni kwamba sisi hatuelewi uhusiano kati ya haya mambo mawili kwa

    ujuzi uliyokamilika.Kwa hakika ni kwamba

    sisi tunakitazama kila kitu katika ujumla wake na kwa sababu hiyo, tutabakia ndani ya mipaka ya taathira na makusudiwa yake wakati wa kusimama kwetu na uchambuzi na uundaji wa kifikra. Ila kuna mambo

    mengi sana yanayozuka k a t i k a u l i m we n g u wa sababu hizi kwa sifa ya kwamba zinasimama kwa kuudhihirisha uhakika huu ambao unatajwa na aya hii mbele ya macho yetu kwa nguvu zote.

    Kwa mfano hajasimamapo mtu yeyote kuvuna shairi

    kat ika shamba ambalo alipanda ngano pamoja na kuwa shairi na ngano ni katika jinsi moja. Na hatuvuni peasi kutoka katika mti wa tufaa wala tini kutoka katika mti wa zabibu.

    Alikuwa Mtume (s.a.w.) unamjia wahyi anayafahamu yale anayoyasema Jibril (A.S.), hawakuwa wale waliyokuwa karibu yake wanasikia kitu chochote hata kitu kidogo kilicho kama kelele za nyuki.

    Ni hivyo hivyo kushuka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu katika thuluthi ya mwisho ya usiku kwenye mbingu ya dunia na mamia ya mambo mbalimbali. Jee, tunaweza kusema kwamba sisi tunafahamu, mfano wa mambo haya katika fremu ya sababu na matokeo?

    Ni kama a l ivyosema A l - I m a m u A l - G h a z a l i : Kwa hakika sisi hatuwezi kufahamu kwa akili zetu za kidunia maana kwa akili za kimaisha, maana kwa aki l i zetu ambazo tunazitumia katika maisha yetu, mfano wa mambo haya yenye kufungamana na akhera, tukayafahamu vizuri, isipokuwa wakati tutakapoandaliwa huko

    Inaendelea Uk. 13

    Guantanamo Dar es Salaam!!!Inatoka Uk. 9katika nchi hizo kwa nyakati tofauti kuwa Muislamu wa kweli hana anachopoteza dhidi ya imani yake.Akielezea aliyohojiwa, alisema

    zaidi ilikuwa ni kuhusiana na harakati zake kwa kujishughulisha katika masuala ya Waislamu na Uislamu akihutubia mara kwa mara kuwa wanaonewa na kudhulumiwa.

    Walinieleza kuwa naonekana kila sehemu katika mikusanyiko ya Waislamu na katika Misikiti mbalimbali katika mikoa mbalimbali, sasa wakataka kujua mimi ni dhehebu gani, uwezo wa kuwepo huko kote na upata wapi.

    Niliwajibu kuwa uwezo wangu unatokana na michango ya Waislamu ndiyo inanifanya niwepo kila mahali.Alisema.

    A l i s e m a , a m e b a i n i k u w a Serikali haipendi kuona viongozi wanaokubalika kwa Waislamu, hasa wale ambao wanawaunganisha Waislamu wawe kitu kimoja katika jamii.

    Akasema, hao ndio huandamwa kwa kutafutiwa tuhuma zisizo za kweli na ukitoka inakuwa bahati yako na sio tatizo kwao kukuzuia kama unavyoona hali ilivyo kwa Masheikh wa UAMSHO na wengine.

    Alisema, akiwa huko, pia aliulizwa kuhusu Sheikh Hudhaifa, kwamba anamfahamu vipi akadai, aliwajibu kwa kuwaeleza kuwa huyo alikuwa ni kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu lakini pia alikuwa mwalimu wake.

    L a k i n i p i a wa k a n i l u l i z a namfahamu vipi Sheikh Qassim Mafuta, nikawaambia namjua kwa sababu tumesoma chuo kimoja, wakaniuliza vipi mawaidha yake, nikawaambia kwa mazingira ya sasa kwa Waislamu na Uislamu, mawaidha yake hayana lengo la kumtoa Muislamu katika dhulma inayotukabili hivi sasa Waislamu.

    Alisema.Alidai, aliulizwa pia juu ya

    Masheikh wanaohubir i kuwa kusoma ni ukafiri na kuwaghilibu

    watoto wa Kiislamu kuacha shule na vyuo ambapo aliwajibu kuwa lengo la mawaidha ya watu hao ni kutaka kuwaacha Waislamu katika

    matatizo na kuendeleza mgawanyiko miongoni mwa Waislamu kutokana na maudhui ya mawaidha yaliyo na lengo la kutaka kuwafanya Waislamu waendelee kuwa wajinga.

    Akasema, alifafanua kwamba mausatadhi hao ndio mfano wa Masheikh ambao wanaowataka Waislamu wasisome elimu nyingine zaidi ya dini, na wanawataka Waislamu wasishiriki katika harakati za kijamii na kisiasa wala wasipige kura.

    Alidai, katika kujibu na kueleza kuwa masheikh wanaohubiri imani za ki-Boko Haram (kuwa kusoma ni ukafiri), hawafai na ni wapotoshaji wa Uislamu, alishushiwa kipigo, jambo ambalo lilimfanya ajiulize maswali mengi.

    Hata hivyo, alidai kuwa kwa sasa ana hakika kuwa hizi kampeni za kuwataka Waislamu wasisome na wasijihusishe na siasa na mambo mbalimbali ya kijamii, ni mpango maalumu wa maadui wa Uislamu na Masheikh waliobeba agenda hiyo wana kazi maalum dhidi ya Waislamu.

    K a t i k a m a s i k u y a h i v i karibuni, Masheikh na Waislamu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za Ugaidi, walitoa malalamiko ya kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

    Wa i s l a m u h a o , w a m e t o a m a l a l a m i k o h a y o , m b e l e ya Mahakama ya Kisutu, wakidai kuwa walihojiwa wakiwa uchi kama walivyozaliwa, kuingiliwa kinyume cha maumbile, kushindiliwa vitu vigumu sehemu ya haja kubwa.

    Je, huu ndio utaratibu wa upelelezi mnaowafanyia ndugu zetu huku bara? Au huwa wanafanyiwa Waislamu tu.

    Alilalamika Sheikh Farid, wakati akitoa malalamiko yao juu ya unyama waliofanyiwa kabla ya kupelekwa gerezani.

    MMOJA wa watuhumiwa akionesha kovu alilolipata akiwa mikononi mwa polisi kutokana na mateso ya maafande hao kabla ya kufikishwa mahakamani.

  • 12 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 201512 MASHAIRI/MAKALA

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-6Inatoka Uk. 10na Wazungu Wakristo na vibaraka wao wa Kiafrika na kuwatupia lawama Waarabu na Waswahili Waislamu. Hakuna shaka yoyote kuwa uelekezaji wa makombora yao wenye siasa kal i za udini kuwalenga Waswahili na Waarabu, ambao ni Waislamu, kuwa k u m e f a n y w a k w a makusudi. Lengo hili la kipropaganda za siasa chafu za udini, linakwenda vipi na siasa rasmi za Tanzania zinazojigamba kila leo kuwa Tanzania haina dini?

    H a i w e z e k a n i Serikali ya Tanzania iachilie mambo haya yasomeshwe katika shule za Tanzania, ila pawe na watu wenye n g u v u k u b w a y a kuilazimisha Serikali kuwaachilia waendelee kuyasomesha hayo ya kipropaganda yenye khatari kubwa kwa nchi nzima ya Tanzania katika siku za usoni.

    La muhimu kabisa ni kupigwa marufuku u s o m e s h a j i w a propaganda za aina hii na vitabu vyote vichomwe moto leo kabla ya kesho.

    K u s e m a t u n g o j e m p a k a t u c h a p i s h e vingine venye kuelezea u k w e l i k a m i l i , n i kuendeleza usomeshaji wa kipropaganda na dhulma kubwa katika nchi inayojinata kuwa inaziheshimu dini zote kisawasawa na haina mapendeleo.

    Wasiyoyazungumzia wenye

    s i a s a k a l i z a u d i n i Tanzania

    Maudhui haya ya utumwa na biashara yake, khasa kukhusiana na Zanzibar, si mambo ya kuyafanyia maskhara. Kwa nini? Kwa sababu ni moja katika jambo lililotumiliwa vibaya s a n a : K wa n z a , n a Wamishinari na wafuasi wao katika kuupiga vita Uislamu katika A f r i k a M a s h a r i k i . Pili, kama tulivyotaja kabla, wanasiasa fulani Waislamu Zanzibar, pia

    waliyatumilia vibaya sana katika majukwaa ya siasa na kuwanyooshea vidole Waarabu peke yao kama kwamba ni Waarabu peke yao ndio walioyafanya maovu yote ya utumwa.

    Zilikuwa ni siasa za chuki zilizopindukia mipaka. Hatimaye, t u m e s h u h u d i a namna roho za watu zilivyoangamizwa 1961 na kwa wingi zaidi 1964 na kuendelea.

    N i wa j i b u w e t u tuzinduane ili tuelewe v i z u r i m a t o k e o y a l i y o w a f i k i s h a Wa z a n z i b a r i h a p a wal ipo . Inafaa pia tusomee zaidi ukweli ul ivyo wa taarikhi i n a y o k h u s i a n a n a b i a s h a r a o v u y a utumwa ili kuelewa yasiyokuwa ya kweli wanayoyakhubiri na kuyaandika wenye lengo la siasa kali za udini zisizokhusiana na mafunzo ya Yesu. (Hawa wenye) lengo la siasa zenye kutaka kuwapiga vita Waislamu na kuwakhasamisha na Wakristo katika Afrika Mashariki na kwingineko. Na katika hawa wamo pia wale Waislamu wenye kupiga debe bila ya kuujua mchezo unaochezwa. Au Wanajua, lakini wanaona kuwa ni siasa

    zenye natija kwao.Wenye s iasa kal i

    za udini hawaelezi c h o c h o t e k u k h u s u maovu waliyoyafanya baadhi ya Wazungu Wakristo. Huwaoni k u z u n g u m z i a y a Waafrika 10,000,000 ( m i l i o n i k u m i ) waliouliwa Kongo na Wabiligiji wakisaidiwa na askari wa Kiafrika. Na (hawazungumzii pia) mamilioni waliotiwa utumwani kufanya kazi mashambani, lakini wakati huo huo hujaribu kuchora picha mbovu sana juu ya Waislamu n a k u w a s i n g i z i a hata yale waliokuwa h a w a k u y a t e n d a Waislamu na kuficha mazuri waliyoyafanya. Angalia baadhi ya picha za utumwa uliofanywa K o n g o a m b a k o ukhabithi mkubwa sana ulitendwa:

    Fungua mwenyewe mtandao uandike kwa mfano Congo Slavery na utastaajabu kuona makala yalivyokuwa m e n g i k u k h u s u utumwa huko Kongo i l i p o t a w a l i w a n a Wa b e l i g i j i . K a t i k a Y o u t u b e p i a k u m e j a a m a e l e z o ya f i lamu kukhusu unyama uliofanywa na Wabeligiji.

    Askari watumishi wa Wabiligiji, Kongo akiwalinda watumwa wa kike (wakiwa wameachwa uchi wa mnyama).

    Kwa jina lako Rahimu,naanza kusimuliyaMola wetu Mkarimu,Ya Rabi nijaaliyaNikadiri kukhitimu, haya nalokusudiyaNiusifu mwezi mwema,mtukufu RamadhaniRabi peleka salamu, zende kwa wetu NabiyaMtume wetu Adhimu, Muhamadi HashimiyaNa Swahaba Akiramu, na Isilamu jamiyaNiusifu mwezi mwema, mtukufu RamadhaniYa Rabi tupe mwafaka, tufunge bila udhiyaSaumu yenye Baraka, kwako twaitaradhiyaTuifunge huno mwaka, na mwakani kwa afiya Tuufunge mwezi mwema, mtukufu Ramadhani

    Karibu wetu mgeni, kwa hamu twakungojeyaUlotukuka yakini, nuru ulivyo eneya Mtukufu Ramadhani, karibu twakupokeyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Mtakatifu adhimu, sote twakukongoweyaMwezi uliye muhimu, Mola metutunukiyaTwafurahi Isilamu, kila pembe ya duniyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Mtukufu mwezi mwema, wa sisi kunyenyekeyaMwenye kuyatenda mema, bila ya kufanya riyaTamswamehe Karima, madhambi kumfutiyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Mwezi wa nyingi faida, metukuzwa na JaliyaMwezi mwema wa Ibada, na imani kutungiyaHuondoka zote shida, nafusi zikatuliyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani Mwezi huno wa maana, ameusifu NabiyaNi bora wajulikana, kwa kheri nyingi kungiyaMwezi wa neema sana, baraka hutushukiyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Mwezi mwema wa swiyamu, wa mema kujichumiya Milango ya Jahanamu, Rahimu huifungiyaNa ya Janatu Naimu, wazi hutufunguliyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Ni mwezi wa Quraani, mwanzo kuteremkiyaAlipokuja pangoni, Jibirili kwa NabiyaIlikiuwa Ramadhan, wahayi alipokeyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Mashetani makafiri, wawi wa kuharibiyaHawawezi kuathiri, wasiwasi kututiyaHuwafungia Qahari, mbali wakatokomeyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Imo Lelatil Qadri, usiku huo kungiyaBora sana mashuhuri, kuliko elifu moyaMiezi inayo jiri, ya taqwimu Hijiriya Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Na hushuka Malaika, mbinguni wakatokeya Kwa amri ya Rabuka, duniyani kufikiya Amani hunawirika, hadi swabahi kungiyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Usiku mwema kipita, wakati huo kungiyaNa ukija kukukuta, Ibadani umengiyaHakika utaipata, Rehema yake JaliyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Haya basi Isilamu, mgeni ashaingiyaNatutimize saumu, tuifungeni kwa niya Swala zote tuzikimu, za suna na faridhiya Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Mashekhe na masharifu, wahimizeni jamiyaHima tufungeni safu, Tarawehe kuqimiyaTumlekee Raufu, kwa kuomba na kuliya Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani

    Darasani tuhimize, wenzetu kuhudhuriya Kwa wakati tufulize, misikitini kungiyaMawaidha tusikize, atatujazi JaliyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu RamadhaniHaya shime muombeni, Mola kumnyenyekeyaQuraani isomeni, kila siku juzu moya Mukiweza ongezeni, muzidi kukaririyaKongo mwezi wetu mwema, mtukufu RamadhaniNa akhiri nimefika, beti nalokusudiyaChache naloziandika, tosha kumi na tisiyaNamshukuru Rabuka, shairi limetimiya La kuswifu mwezi mwema, mtukufu RamadhaniAmina Rabi Dayani, Dua yetu kubaliyaYa Ilahi tuauni, tuepushe na udhiyaTuifunge Ramadhani, kwa furaha na afiyaTwaomba yake neema, mtukufu Ramadhani

    SWALEH SUHEIL ABEID

    MTUKUFU RAMADHANI

  • 13 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015MAKALA

    'VUNJAJUNGU', kama d h a n a n a k wa m a a n a ninayoikusudia katika makala haya, ni istilahi isiyo rasmi inayotokana na maneno rasmi mawili ya lugha yetu adhimu na aushi ya Kiswahili ambayo ni 'vunja' na 'jungu'. Maneno ambayo yamehulutishwa au kuambatishwa ama kujumuishwa pamoja na hatimaye kuzalisha istilahi hiyo is iyo rasmi, kwa muktadha wa makala haya, ambayo ni 'Vunjajungu'.

    Aghalabu matumizi ya istilahi hii hushika kasi zaidi katika kipindi hiki cha mwezi wa nane ujulikanao kwa jina la Shaaban kwa mujibu wa Kalenda ya Kiislaamu. Kwa maneno mengine, istilahi hii hutamkwa na husikika zaidi katika mwezi huu kuliko mwezi mwingine wowote k a t i k a m wa k a k u p i t i a matangazo yarushwayo na vyombo vya habari vya umma na vya watu binafsi na katika mazungumzo ya kawaida ya baadhi ya wanajamii.

    Ni nadra kusikia neno hili likitumika au kutumiwa katika miezi mingine ya mwaka kama vile Muharram, Swafar, Rajab, Ramadhaan, s h a w wa a l k wa k u t a j a michache; na pale inapotokea kutumiwa au kutumika kwake katika miezi hiyo niliyoitaja au hata katika ile mingine ambayo sijaitaja mbali na Shaaban, matumizi hayo aghalabu hurejelea ama kilichojiri au kilichotarajiwa kujiri katika kipindi cha mwezi wa Shaaban kwa k u k i f u n g a m a n i s h a a u kukihus i sha na dhana yenyewe ya 'Vunjajungu'.

    Naam, tukirejelea mada ya msingi ya makala haya ya leo neno 'vunjajungu' japo linaweza; kwa maana ya kilugha au ya msingi wa maneno yaliyotumika kuunda neno hilo; kufasiliwa kwa maana ya 'haribu chungu kikubwa' au 'uharibifu wa chungu kikubwa' ingawa hii si maana tunayoikusudia katika makala haya.

    Aidha, maana rasmi ya kikamusi neno 'vunjajungu' kama kidahizo limefasiliwa kuwa ni mdudu aina ya panzi mwenye kiuno chembamba na macho makubwa na hula wadudu wadogo.

    Maana ninayoikusudia katika makala haya, si maana hiyo ya msingi ya neno husika kama ilivyodokezwa hapo juu na katika fasili ya kabla yake bali ni ile ya kimuktadha au ya kimazingira ambamo neno hilo hutumika au hutumiwa hususan katika kipindi hiki tulichomo.

    'Vunjajungu' na hatma ya funga zetu (1)Na Abuu Nyamkomogi

    AMIR wa Baraza Kuu, Sheikh Mussa Kundecha akizungumza katika moja ya makongamano mengi yaliyofanyika ya kuwaelimisha Waislamu kuujua Uislamu wao vilivyo na kuutekeleza.

    'Vunjajungu' ni dhana inayotumiwa kumaanisha kipindi maalumu; kabla ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani au kwa maneno mengine kipindi cha mwezi wa Shaaban; kitumiwacho n a W a i s l a m u h a s a wasiojitambua kukithirisha kufanya maasi pamoja na kujikita zaidi katika ushiriki wa starehe zisizo halali kwa hofu ya kutoweza kufanya hivyo katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kwa kutambua kwamba kufanya hivyo ndani ya mwezi huo kutawasababishia waruke patupu (habaan manthuura) katika swaumu au funga zao watarajiazo kufunga katika mwezi huo.

    Ijapokuwa, kwa muktadha wa mada hi i , k i la mtu anaweza kuwa na fasili au tafsiri yake hiyo haitakosa kulihusisha suala hili na utendaji wa maasi au maovu fulani kwa namna moja au nyingine.

    Kama ilivyo desturi au ada katika kipindi hiki, kama nilivyodokeza huko nyuma, nidaa au matangazo k u h u s u ' v u n j a j u n g u ' yamekwishaanza, na naamini yataendelea, kutolewa hadi mwisho wa mwezi huu (Shaaban) yakiwavutia na kuwaraghibisha Waislamu wa sampuli niliodokeza katika fasili ya 'vunjajungu' hapo juu, wahamasike katika kuunga mkono kwa kushiriki 'vunjajungu' kwa kumuasi Allah (s.w.), kadri ya uwezo wao, katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

    Kauli kama vile zile za

    'Karibuni au Mnakaribishwa katika disko la 'vunjajungu' la kukata na shoka!'au 'Njoo uvunje jungu la mwaka nasi hadi majogoo!' na kadhalika, ni sehemu tu ya ya kauli-mbiu chache kati ya nyingi zitumikazo au zitumiwazo na vyombo vya habari na magari ya matangazo katika kuwashajiisha, aina ile ya Waislamu niliyodokeza huko nyuma, kushiriki katika mradi wao huo haramu!

    Ni katika kipindi hiki, k w a m a c h o m b e z o y a matangazo kama hayo, ndipo ambapo baadhi ya Waislamu wasiojitambua hunasa kirahisi mtego huu kwa kughururika kwa kuj i ingiza na hatimaye kuzama katika laghwu na mambo mengine kedekede ya hawaa nafsi ikiwa ni pamoja kujiingiza katika madisko ya 'vunjajungu', uzinzi pamoja na ulevi kwa kutaja machache.

    I t o s h e t u k u s e m a kwamba maasi au maovu yanayotendwa kipindi hiki si hayo tu bali nimeyataja hayo matatu kwa sababu aghalabu ndio hukithiri kwa kiwango kikubwa katika utukiaji au utendekaji wake katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

    Naam, wafungaji-tarajali wa swaumu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani wanaotanguliza mambo ya hawaa nafsi kama hayo yaliyodokezwa hapo juu na mithili yake, ni vigumu sana kuufurahia ujio wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani; japo vinywa vyao vinaweza

    kudai hivyo lakini matendo yao yanakataa; kwa kuhisi kuwa Ramadhani ni jela au kifungo kitakachowanyima 'uhuru' wao wa kutenda watakalo kama walivyozoea.

    Ndio maana, kwa kipindi hiki, Waislamu wa sampuli hii wataj i tahidi kadiri wawezavyo kujikita zaidi katika kutenda yale maovu ambayo huhisi hawatapata

    f u r s a wa l a wa s a a wa kuyatenda katika 'Jela ya Ramadhani'!

    Kwa mantiki hiyo, yumkini kabisa watu hawa hutamani mioyoni mwao 'kifungo' kiishe haraka iwezekanavyo mara baada ya 'kuanza kwake' ili waendelee kuwa 'huru' katika uzinzi, ulevi, madisko na kadhalika.

    Kumaizi ukweli wa hili hakuhitaji mtu kuwa na Stashahada au Shahada au kuwa Daktari au Profesa bali kwa kutumia akili yake ya kawaida tu (common sense) na kutumia macho yake; mara tu baada ya m wa n d a m o wa m we z i Shawwal kama taashira ya kukamilika kwa mwezi wa Ramadhani; atatambua hili kwa kuwaona wafungaji wa aina hiyo wakiuaga mwezi huo kwa cherekochereko ya madisko yao usiku huohuo wa mwandamo wa Shawwal kwa kukesha hadi majogoo, na kuusindikiza mchana wake kwa ulevi na hatimaye k u r u d i u z i n z i n i k a m a ilivyokuwa ada yao kabla ya Ramadhani.

    Huu ni msiba. Na ndio m a a n a t u n a o n a w a t u wamekuwa wakifunga, lakini lile lengo la kufunga ambalo ni kuwa wacha-Mungu, halifikiwi.

    (Mwandishi wa makala haya ni msomaji wa muda mrefu wa gazeti la AN-NUUR anayeishi jijini Mwanza.)

    Mafundisho ya QuranInatoka Uk. 11akhera kwa akili ya akhera. Wa k a t i h u o u t a w e z a kufahamu uhusiano kati ya kusema Subhanallah na kati ya kuyala matunda ya peponi, kwa sababu kila kitu kitapita huko.

    Kufuatana na kanuni za ghaibu na za nyuma ya tabia (Metaphysical), tunaona na tutafahamu kwa uwazi wote, uhusiano wa kisababu kati ya malipo na neema ambazo zinapatikana huko na kati ya kutenda hapa duniani.

    Kanuni za uhakika za Kifizikia zinazopatikana hapa haziishii hapa, zinafanya kazi huko. Kwa mfano, anasema Mtume (s.a.w.) kwamba swala zetu zitakuwa mliwazaji wetu na rafiki yetu katika makaburi yetu na kwamba mtu ataingia peponi kupitia milango yake minane ambayo ni mbalimbali na kwamba Quran itasimama ili iwe muombezi wa msomaji wake.

    Hakika neema yoyote ile, neema hiyo ama ni malipo

    ya matendo fulani au ni kusimama kwa malipo hayo au ni kwamba uwezesho wa milele huko. Ni mashuke ya mbegu za matendo mema hapa duniani.

    Kwa sababu hiyo, hayo mawili kwa mazingatio haya, yanafanana katika undani wake. Ama kwa mazingatio ya vipeo vya peponi, pana tofauti kubwa kati ya mawili hayo. Inakunjuka dunia na inavuka, kwa sababu moja lau ni matunda ya uwezo. Moja lao linabeba sifa ya umilele na jingine ni la muda. Vipeo vya ladha ya milele na jingine vipeo vya mwili. Moja lao ni wema kwa ngazi ya jicho la yakini na jingine, upole wa Mwenyezi Mungu katika kilele cha Haki ya yakini.

    (Imenukuliwa kutoka Kitabu: Miyangaza ya Quran katika mbingu ya hisia, cha Muhammad Fethullah Gullen kilichotafsiriwa kwa Kiswahili na Sheikh Suleiman Amran Kilemile)

  • 14 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia - 14

    Fatilia kuandama kwa Mwezi

    UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFACHEMSHA BONGO namba 10

    1. Taja Sura inayoelezea mwezi wa Ramadhani.2. Vita gani Waislamu walipigana katika mwezi

    wa Ramadhan.3. Ratio baina ya Waislamu na Makafiri katika

    vita vya mwanzo waliopigana Waislamu ilikuwa 1:3, 1:6, 2:9.

    4. Sala gani inayosaliwa katika mwezi wa Ramadhani tu.

    5. Katika mwezi wa Ramadhan kuna milo miwili inatakiwa kuliwa moja jua linapokuchwa na mwengine kabla ya kuingia alfajiri, milo hio ni :,

    6. Ramadhani una usiku mtukufu unaitwaje?7. Mwezi wa Hijra huandama biana ya na

    8. Kufunga kwa mwezi wa Ramadhan

    kulifaradhishwa katika mji gani?9. Asio balighi ana wajibika kufunga? Ndio au

    Hapana.10. Ramadhani humtakasa mja ..

    Ibn Sina

    Leo Ijumaa ni tarehe 24 Shaaban 1436 AH sawa na tarehe 12 Juni 2015.

    Tutaangalia kuandama kwa mwezi wa Ramadhani tarehe 17 June 2015 siku ya Ijumatano.

    Kutoka leo Ijumaa ya tarehe 12 Juni 2015 hadi kufika Ramadhani tumebakisha siku 6 tu.

    K AT I K A m a k a l a hizi za Mchango wa Wa i s l a m u k a t i k a maendeleo ya dunia, katika sehemu nyingi nilikuwa namtaja Ibn Sina na ujuzi wake wa utabibu. Aidha na mchanganyiko wa fikra zake katika asili ya maisha. Nitajaribu kuandika makala mbili tafauti juu ya Ibn Sina.

    Kwa watu wa Ulaya ni Avicenna katika k u f i c h a k u wa s i o Muislamu aonekane k u w a n i M z u n g u k u t o k a n a n a k a z i kubwa za kitaaluma alizozifanya kuanzia utibabu, falsafa, ilimu ya nyota, fizikia n.k.

    Jina lake khasa ni Abu Ali al-Husayn ibn Sina, yeye ni mzaliwa wa Afshana katika maeneo yaliokaribu na Bukhara, kaandika maandiko mengi ya kupigiwa mfano lakini kati ya kazi zake kubwa ni ile ijulikanayo kama al-Qanun fil-Tibb kita