annuur 1216d

Upload: zanzibariyetu

Post on 08-Mar-2016

1.007 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1216 JAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA , FEB. 12-18, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

    Soma Uk. 4

    Kamanda MsangiMazombi hawa hapa, RB zetu hizi

    Hata mzombi unataka FBI, CIA!Dr. Shein wanusuru wananchiKila Mchunga ataulizwa hiyo siku

    Kamanda Salum Msangi

    Masheikh wasaidieni watuhumiwa hawa

    Sio magaidi lakini wanateswaAomba msaada wa matibabu

    Aweka rekodi kuendeshandege akivaa Hijab, niqab

    Aingizwa kitabu cha Guiness

    SHAHNAZ Laghari amekuwa mwanamke wa kwanza duniani wa Kiislamu kuendesha ndege akiwa kavaa mavazi ya Kiislamu.

    Sheikh Farid mgonjwa

    RAIS Dk. Ali Mohamed Shein

    Wawakilishi wateule wakiwa na vyeti vyao vya ushindi walivyopewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kushinda katika Majimbo yao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015. Baadae mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha alitangaza kufuta uchaguzi huo.

  • 2 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

    Fethullah-Gulen

    Jee Unajua?

    MASUALA1.Itaje mito mitano ilio mirefu kupita yote barani Africa. Jawabu : Nile, Congo, Niger, Zambezi, Orange2.Itaje miji 3 Africa yenye kukaliwa na watu wengi. Jawabu : Lagos, Cairo, Kinshasa.3.Taja Kiongozi wa Kiafrika aliotawala muda mrefu. Jawabu : Pail Biya4.Chuo Kikuu Kigongwe Africa ni.. Jawabu : Al-Qarawiyyn5.Mshindi wa kwanza wa zawadi ya Nobe mwenye asili ya Kiafrika. Jawabu : Max Theiler6.Raisi yupi wa Kiafrika akifariki akiwa na umri mkubwa na bado yupo madarakani? Jawabu : Bimgu (wa) Mutharika.7.Taja mnyama namba mmoja aliohatarini kutoweka barani Africa (extinct)? Jawabu : Riverine8.Kiongozi gani wa Kiafrika anayosadikiwa hakupita Shule? Jawabu : Jacob Zuma9.Itaje bridji iliorefu koliko zote Africa. Jawabu : 6 October10.Lugha rasmi kwa taifa la Afrika ya Kusini ni 11, 23, 1 Jawabu : 11

    JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 38

    CHEMSHA BONGO: 39Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

    MASUALA1.Sahaba yupi wakati wa Mtume Muhammad (SAW) alishiriki vita vyote akiwa Jamedari?2.Bunduki yenye jina gani amabayo imeleta mauaji na inaendelea kuleta mauaji mengi duniani?3.Jina jengine aliokuwa akijulikana mwanafalsafa wa Kiyunani Aristotle.4.Al-Hassan ibn Muhammad mvumbuzi aliokuja kukamatwa na kutumwa kwa Pope (Papa) Leo X kisha kubatizwa na kuwa muumini wa Kikiristo, jina lake la ubatizo akiitwa.5.Mwanamke wa mwanzo kuwa Waziri Mkuu wa Israel akiitwa.6.Mahmoud Abass kiongozi wa Kipalestina anazungumza Kiarabu, Kiengereza na lugha ipi nyengine ya kigeni? 7.Jina la Mmerekeani mweusi aliovumbua mpango wa magari ya moshi kuwasiliana na ambao hadi sasa unatumika na kuepusha ajali nyingi kutokea ni 8.Aliirejesha Jrusalem mikononi mwa Waislamu, ni shujaa yupi?9.Jina la Kiongozi wa Kiislamu kutoka uongozi wa Bani Ummaya alikuwa ni Gavana katika maeneo yote ya Afrika ya Kaskazini.10.Kimwana wa Kiyahudi aliopata kuolewa na mchezaji wa Kiriketi wa Paksitan, Imran Khan kimwana ambaye ana asili ya Kiyahudi jina lake ni nani?

    1.Watu wanaamini kuwa mwezi wa March sio mwezi wa kutokea matokeo ya Matatemeko ya Ardhi, haya sio kweli, tarehe 8 March mwaka wa 1964 sehemu ya Prince William Sound Alaska ilishudia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.2 ambao uliua watu 125 na khasara ya dolari za Kimerekani milioni 311 : http://www.livescience.com/6187-13-crazy-earthquake-facts.html2.Inasadikiwa kuwa nchi yenye kupata matetemeko ya ardhi mengi duniani ni nchi ya Japan, hufikia matetemeko ya ardhi alfu kila mwaka lakini ni matetemeko hayo mengi huwa hayana athari : http://facts.randomhistory.com/earthquake-facts.html3.Mji wa Cherrapunji uliopo nchini India ndio mji unaopata mvua kwa wingi kupita kiasi duniani; kwa mwaka hupata wastani ya milimita 26,460 za mvua : http://www.cawater-info.net/all_about_water/en/?p=16704.Nchini Phillipines kuwacha au kumtaliki mke haikubaliki kisheria. Hakuna Rais wa Marekani alioingia madarakani akiwa aliwahi kuacha mke kabla zaidi ya Ronald Reegan. Katika kila kipindi cha saa moja nchini Marekani hutolewa talaka 100 : http://www.factslides.com/s-Divorce5.Kila mwaka humwagwa uchafu baharini unaofikia kilo bilioni 6 na plastiki ndio nyingi kuliko taka za aiana nyenginezo : http://www.factslides.com/s-Pollution6.Vifo vinavyotokana na Viboko Africa ni vingi na idadi yake ni sawa kuchanganya vifo vinavyosababishwa na Simba na Mamba : http://answersafrica.com/10-interesting-facts-about-africa.html7.Kati ya nchi 54 za Kiafrika ni nchi mbili tu hazijapatapo kutawaliwa na Wakoloni nazo ni Ethopia na Liberia : http://list25.com/25-interesting-facts-africa/8.Mto mrefu duniani ni mto Nile, Afrika ndio yenye Jangwa liliokubwa likiwa sawa na ukubwa wa nchi ya Marekani, Mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu kuliko yote Africa : http://www.interesting-africa-facts.com/9.Miti ipatayo 27,000 kila siku hukatwa duniani kote katika kutengenezewa karatasi za kuendea haja (Toilet papers) : http://www.factslides.com/s-Recycling10.Bomu la Atomiki lilotupwa katika mji wa Nagasaki liliazimiwa kutupwa katika mji wa Kokura na badala yake likaangukia Nagasaki nchini Japan : http://www.factslides.com/s-Atomic-Bomb: http://www.factslides.com/s-Atomic-Bomb

    HAKIKA wale ambao wamezikufuru aya zetu punde hivi tutawaingiza katika moto, kila zitakavyoiva ngozi zao, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waonje adhabu, hakika Mwenyezi Mungu hakuacha kuwa ni mwenye kushinda, mwenye hekima kubwa. [An-Nisaa 56]

    Wafasiri wengi wakati wanapoanza kufasiri aya hii huanza kwa kuweka wazi tishio na ukubwa wa adhabu ya Jahannam,

    An nisaa: 56kwa kuitaja hadithi ya Mtume mtukufu ambayo ameipokea Ibn Omar (r.a.):

    Watu wa motoni watakuwa wakubwa ndani ya moto mpaka ni kwamba, kati ya ndewe ya sikio la mmoja wao, mpaka begani kwake kiasi cha mwendo wa miaka mia saba na ukubwa wa ngozi yake ni dhiraa sabiini na kwa hakika ngozi yake itakuwa mfano wa Jabali la Uhud.

    Na mafundisho ya jumla ya hadithi hii ni kuisifu adhabu Jahanamu na hali ya wale ambao wataingia katika adhabu hii. Mimi ninaona kuwa kunawezekana kuifahamu hadithi hii juu ya sura ifuatayo vile vile:

    Hakika mwanadamu anaendelea na anapanda kwa upande wa kiroho, kwa mfano anaona ladha, mmoja wao katika swala

    yake mara kumi zaidi kuliko kuona ladha kwako. Kwa msingi huo uwezo wake katika kupata ladha huenda ukapanda sana. Na jambo hilo hilo linapatokana katika kuhisi machungu vile vile. Na mtu ambaye amekuwa safi na kuelekea kwake upande huu, anapata maumivu kutokana kitu kidogo tu, na anakosa usingizi na huenda akazimia kwa sababu ya maumivu ya meno yake. Kwa sababu hiyo amesema mtukufu wa Mitume: Hakika mimi ninapatwa na maumivu kama wanavyopatwa na maumivu watu wawili katika nyinyi.

    Kwa msingi huo, kama yanavyozidi maumivu kwa sababu ya mkubwa wa mwili na kujaa kwake huko akhera, kwa hakika, nyongeza ya kuhisi maumivu katika Jahanamu kwa sababu ya hekima nyingi huenda hekima hizo zikaelezewa hivi vile vile. Na uhakika ni kwamba havitakuwa vikubwa viwiliwili kwa sababu ya maasia na madhambi na kufika kwake kwenye ukubwa wa majabali. Maasia na madhambi hayavikuzi na kuvipanua viwiliwili bali ni ukunjufu wa roho, ili mwanadamu aadhibiwe kufuatana na ukubwa huo. Maana kufuatana na upana huu, Jambo hilo si katika mambo yanayopingana na akili. Kwani ukunjufu wa elimu ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake na matakwa yake, sifa ambazo zimekizunguka kila kitu zinaweza kulihakikisha jambo hilo mahali popote na wakati wowote. Na sisi tunakimbilia kwenye rehma yake, iliyo pana na tunamuomba atueneze kwa rehema hiyo, na atutendee kufuatana na rehma hii pana.

    N L A G O S M P R B A K O N

    I S D G H J A A I I L I R I

    G S T T T A X U V N Q N A L

    E A S S S C T L E G A S N E

    R D N K G O H B R U R H G M

    Y C R E E B E I I M A A E C

    C A I R O Z I Y N U W S Y O

    S C P Y U U L A E T I A U N

    B V R R V M E E R H Y 1 K G

    S B Z X C A R G A A Y 11 O O

    Z A M B E Z I B B R N 2 O X

    S A I M S H A E I I U 23 H P

    S P E M B A U C T K S R N X

    6 O C O B E R N A T P M Z

    G J K F U N A J K M J G J S

    O U H A S A L E H U A R O T

    L M A D M A A M T S R A H A

    D A L H A M K I T S U N A G

    A S I I N F E M I A S V N I

    M H D L V E Y A B N A I N R

    E A W S F L F K T U L L E I

    I R A T R U E H R S E E S T

    R K B U T N K A F A M W L E

    K I R U S I R N V I Y O E W

    A S L A A G D A U R U O O A

    F A D D A D A A K 4 7 D Y R

    A L I A B I T A L I B S 5 9

  • 3 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Habari

    Mazombi hawa hapa, RB zetu hiziWAKATI Kamanda Msangi akidai kuwa hakuna mtu aliyepigwa na zombi na kuripoti Polisi, wamejitokeza watu waliowahi kupigwa na kupatiwa RB kwa ajili ya matibabu.

    Watu hao kwa nyakati tofauti, wameeleza kusikitishwa kwao na kauli ya Afande Salum Msangi, wakisema kuwa kauli yake inatia shaka kwamba huenda mazombi hao wana baraka za jeshi hilo au serikali.

    Kwa upande mwingine, wamesikitishwa na kauli ya Kamanda huyo wa polisi akitamba kuwa jeshi lake litashirikiana na vyombo vya nje kuchunguza matukio ya kihalifu Zanzibar, wakati jambo lipo wazi.

    Ni jambo la kushangaza polisi wetu kutoa kauli za kisiasa, wanapewa taarifa mpaka namba za magari wanayotumia mazombi na vikosi wanaopiga watu, leo Afande Msangi anasema watashirikiana na vyombo vya nje, kwa hiyo hata mazombi tuwaite FBI na CIA, hii si dhani ni sifa kwa polisi wetu, sana tunajidhalilisha. Alisema mtu mmoja muathirika wa vipigo vya mazombi.

    Aliyasema hayo kufuatia kauli ya Afande Msangi kuwa Jeshi la Polisi litashirikiana na taasisi nyengine za ulinzi na usalama za kitaifa na kimataifa, linafanya juhudi kukomesha vitendo vya kihalifu Zanzibar.

    Katika taarifa yake ya hivi karibuni, Jeshi la Polisi Zanzibar limewataka madaktari kuacha kuwahudumia watu wanaokwenda hospitali baada ya kupigwa na kikundi cha Mazombi bila ya kuwa na karatari ya PF3 kutoka Polisi.

    Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Salum Msangi wakati akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya jeshi hilo Kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi.

    Hapa Zanzibar wanasema kuna mazombi lakini mimi siamini kitu kama hicho, kama kuna maiti inayotembea ikapiga, hawa watu wanaosema wanapigwa mbona hawendi katika vituo vya polisi kuripoti.

    Aidha amesema, Jeshi la Polisi iwapo litambaini daktari kufanya hivyo, halitosita kumchukulia hatua, ili kukomesha vitendo vya uhalifu hapa Zanzibar.

    Alisema kuwa, taaswira ya haraka wanayoipata ni kwamba inawezekana watu wanaotendewa vitendo hivyo ni wahalifu hivyo wamekutana na wahalifu wenzao kwa hivyo wanahofia kutoa tarifa ili uhalifu wao usibainike hali inayopelekea kunungunika pembeni bila ya kuifikisha taarifa maeneo sahihi ili zifanyiwe kazi.

    Kwa mujibu wa taratibu zilizopo ni kwamba mtu yoyote anaefanyiwa kitendo cha kihalifu anapaswa kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili hatua za uchunguzi au upelelezi zifanyike ili kubaini wahalifu hao, alisema Msangi.

    Wakati Msangi akitoa kauli

    Mwandishi wetu Zanzibar hiyo, tayari watu kadhaa wameshajeruhiwa vibaya mmoja wapo ni Badru Seif Badru ambaye amechukuliwa Januari 28 mwaka huu akiwa nyumbani kwao Mji Mkongwe na kupelekwa hadi Kibanda Maiti na kupigwa vibaya kwa silaha tofauti.

    Nilikuwa nimekaa nyumbani pale Mnadani Darajani nikaona gari mbili zimesimama wakashuka watu wakiwa na silaha za jadi lakini wameshika na bunduki wamejifunika nyuso zao wakanichukua mpaka Kibanda Maiti na kuanza kunipiga hadi hali hii.

    Nikawauliza kosa langu nini? Wakanambia unajifanya unajua kusema sana.

    Unaipenda sana CUF kama ya baba yako ndio sababu ya kukupiga. alisema Badru hapo juzi.

    Januari 31,2016 majira ya saa tisa usiku vikosi vya Mazombi vilivamia maeneo ya Msumbiji na kuvunja baraza za CUF, Msikiti wa mabati na baadhi ya mabanda ya biashara ya mbao katika maeneo hayo.

    Matukio ya watu kupigwa na wanaosadikiwa kuwa ni Mazombi yameanza muda mrefu tokea wakati wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura lakini licha ya taarifa hizo kuwasilishwa katika vituo vya polisi hakuna mtu aliekamatwa kuhusiana na matukio hayo.

    Watu waliopigwa risasi usiku wa tarehe 25, 10, 2015 na kulazwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja ni Abrahman Hamza Juma (17) risasi ubavuni, Juma Kombo Juma (40) risasi ya mgongo, Issa Rajab Issa (25), risasi ya mguu na Hamad Khamis Hamad (33) risasi ya mgongo.

    Matukio mengi yanayohusishwa kufanywa na hao Mazombi ni kumpiga kijana Zubeir Makame Khamis na Suwedi Fadhili Haji wa Pwani Mchangani ambapo baadae walizipoti polisi kituo cha Lungalunga na kupewa RB. NO. Mwk4809/2015.

    Tukio jengine Jumamosi 26, 9, 2015 Shehia ya Kinuni jimbo la Pangawe majira ya saa 2 usiku watu walivamia watu waliokuwa wamekaa kwenye baraza na kuwajeruhi kwa mapanga vibaya sana ambapo baadae walikwenda kuripoti kituo cha polisi cha Mwanakwerekwe na kupatiwa RB. NO. Mwk/RB4809/2015.

    Tukio jengine ni lile la Tarehe 4. 10. 2015 wakati wafuasi wa CUF walipokuwa wakirudi mkutano wa Kizimkazi majira ya saa 12 jioni walivamiwa na kupigwa mawe ambapo baadhi ya vijana waliumia ambao walikwenda kituoni na kupewa karatasi za polisi PF3 na kwenda kutibiwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

    Waliojeruhiwa ni Said Khamis Salum (30) Makaazi wa Mgogoni RB. NO. TUNG/RB125/2015, Haji Makame Ussi (25) Mkaazi wa Shaurimoyo RB. NO. FUO/RB/68122015, Salum Machano Juma (18) Daraja bovu RB. NO. TUNG/RB/126/2015 na Salum Abdallah Suleiman (18) Mkaazi wa Fuoni RB.

    NO. TUNG/RB/126/2015.Katika mfululizo wa matukio

    kama hayo, pia baraza ya Sarayevo tarehe 1. 10. 2015 majira ya tano usiku ambapo kikundi kinachodaiwa Mazombi kilivamia baraza hiyo na kupambana na wananchi waliokuwepo hapo na kufanya uhalifu na kuondoka na mali za wananchi.

    Tarehe 2. 10. 2015 majira ya saa tatu usiku watu wawili waliumizwa baada ya kuvamiwa ambapo Mchezo Mbegu Mchezo na Yussuf Ali Chogo walipigwa vibaya na kupatiwa RB. NO. MK/RB/1179/2015. Makadara polisi.

    Tukio jengine ni kuvamia baraza za wafuasi wa Chama Cha Wananchi CUF ambapo baraza kadhaa zilivamiwa ikiwemo ile maarufu ya Commonwealth ya Michenzani ambayo ilivunjwa mara mbili na kujengwa lakini mwisho serikali iliamuru kuvunjwa baraza hiyo na badala yake kupandwa bustani katika eneo hilo.

    Mbali ya waliopigwa na kuvunjiwa nyumba zao ikiwemo Kisiwani Pemba na maeneo ya Tumbatu ambapo nyumba zaidi ya 50 zilichomwa moto ambapo watu kadhaa waliumizwa na kusababisha uhasama mkubwa kati ya pande mbili za CCM na CUF hadi leo viongozi wa dini wamekuwa wakipatanisha kwa njia za kiimani

    ili kurejesha hali ya umoja katika Kisiwa hicho cha Tumbatu ambacho kinajuliana kwa kuwa na watu wacha Mungu.

    Katika tukio hilo, mbali ya nyumba 50 kuchomwa moto, kuna watu 10 nao walikamatwa tarehe 29. 10. 2015 huko katika kisiwa cha Tumbatu na jeshi la polisi baada ya kutangazwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakidaiwa kufanya fujo.

    Watu mbali mbali wakiwemo Masheikh wamemtaka Rais Dkt. Shein kuingilia kati hali hii kabla fitna hazijachukua mkondo wake katika kipindi hiki ambacho tayari matukio kdhaa yameshaanza kuonekana ikiwemo ya kulipiziana visasi.

    Kwa mfano huko Kisiwani Pemba tayari jeshi la polisi limeshatoa onyo kali kwa watu ambao wamekuwa wakiweka alama ya x katika nyumba za wana CCM jambo ambalo kitendo hicho hakiashirii dalili njema.

    Akizungumzia suala la Mazombi ambao huvaa soksi nyeusi na kuchukua silaha na kuwapiga watu na kuwajeruhi, Msangi alisema kuwa jeshi bado linasisitiza kutotambuwa uwepo wa kikundi hicho kwa vile watu wanaofanyiwa vitendo hivyo hawatoi taarifa kwenye vituo vya polisi ili uchunguzi kufanyika.

    Masheikh wasaidieni watuhumiwa hawaMASHEIKH wametakiwa kuingilia kati dhulma wanayofanyiwa Waislamu na vyombo vya dola hapa nchini kupitia koti la ugaidi.

    Wito huo umetolewa na Bw. Jamal Yasin, mmoja wa watuhumiwa wa ugaidi ambaye alikamatwa na polisi na kuswekwa kuzuizini akituhumiwa kuwa kinara wa tukio la kuvamiwa kituo cha polisi cha Staki Shari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka jana.

    Viongozi wa Kiislamu wamekuwa wabinafsi, wanajali zaidi dunia yao, hawaoni wajibu wa kushughulikia matatizo ya Waislamu, lakini wanafungua taasisi na kuchuma na kusahau kupambana na madhila dhidi ya Waislamu. alisema Ust. Yasin.

    Aliongeza kuwa viongozi Masheikh na viongozi wengi wa Waislamu wamekuwa mstari wa mbele kutoa uchambuzi kuhusu matatizo ya Mashariki ya Kati katika vyombo vya habari, huku wao wakishindwa kushughulikia dhulma, uonevu, ukandamizaji na matatizo mengine yanayowapata Waislamu wa Tanzania wasiokuwa na hatia.

    Baada ya miezi takriban miwili ya kukaa rumande, aliachiwa baada ya kubainika kuwa hana hatia na hahusiki katika tukio hilo.

    Ust. Yasin ameeleza kuwa kwa jinsi hali ilivyo sasa, Muislamu akifuata sunna, akizoea kuvaa kilemba, kofia, kanzu fupi na akafuga ndevu, basi huyo anakuwa mashakani kwani wakati wowote anaweza kukamatwa na kuvikwa koti la ugaidi.

    Alisema, Waislamu ni Watanzania

    Na Shaban Rajab kama walivyo watu wa imani nyingine na kwamba, wana uhuru wa kuabudu vile watakavyo mradi hawavunji sheria za nchi.

    Ndio maana imejengwa dhana kwamba Waislamu ndio magaidi kwani hata polisi, humtia matatani mtu kwa alama kama hizo za kupenda kuvaa kilemba, kofia, kufuga ndevu, kuvaa kanzu au suruali fupi. Hizo ndizo alama muhimu za kamatakama ya ugaidi alisema kiaja huyo.

    Ust Yasin alisema hata wanapokamatwa watuhumiwa badala sheria kufuatwa, watu huteswa, hupigwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili wakishinikizwa kukiri makosa vile polisi wanavyotaka.

    Alisema ukishavikwa koti la ugaidi, wengi hushikiliwa gerezani kwa kipindi kirefu bila kufunguliwa kesi kigezo kikiwa ni upepelezi haujakamilika, halafu mwisho wa siku unaachiwa huru huna hatia huku tayari ukiwa na kilema au matatizo ya afya.

    Kufuatia kurundikana Waislamu wengi mahabusu katika magereza mbalimbali hapa nchini, hususan Dare Salaam na Morogoro, Ust. Yasin amewaomba Masheik kuzinduka na kulitafakari hilo kwa kina na kuchukua hatua mapema kwani hali ni mbaya sana.

    Ust. Yasin baada ya kutoka gerezani, kufuatia mateso aliyopata amepwata maradhi ambayo matibabu ni ya gharama kubwa.

    Madaktari wamebaini kwamba maradhi yake yanahitaji matibabu ya haraka ambapo kwa sasa anachoma sindano tatu kwa siku zinagharimu kiasi cha shilingi 27,000.

    Waislamu wanaombwa kumsaidia kwa kadiri watakavyoweza kuokoa maisha ya ndugu yao katika iman.

    (Kwa mawasiliano piga 0712 047 320.)

  • 4 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Maoni/MakalaAN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    WAKATI hali ya kisiasa Zanzibar ikiwa bado ni kiza kinene, ipo haja kwa viongozi wa serikali na wale wa kidini kuwa makini pale wanapotoa matamko au kauli zao juuya mkwamo huo wa kisiasa visiwani humo.

    Ni jambo lililo wazi kwamba hali ya kisiasa Zanzibar si nzuri hata kidogo tangu kufutwa Uchaguzi Mkuu visiwani humo Oktoba 28 mwaka jana. Kwa namna moja au nyingine hali hiyo inaweka rehani mustakabali wa maisha ya watu.

    Sote tunatambua kuwa pande kuu mbili zinazovutana, yaani Chama cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani upande wa Zanzibar kimepinga kufutwa matokeo hayo, kikiamini mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa mbioni kushinda katika uchaguzi huo. Na kwa ishara hiyo ya kushinda ndio maana uchaguzi ukafutwa.

    Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi, wao wanaamini kuwa taratibu za uchaguz huo zilikiukwa ndio maana ZEC ikaufuta na msiamo wa chama na mgombea Dk. Ali Mohamed Shein ni kurejewa uchaguzi huo, ambapo tayari ZEC imetangaza kuwa utarejewa Machi 20.

    CUF na mgombea wake nao tayari wamepinga hatua hiyo ya ZEC na wameshatangaza kususia uchaguzi huo wa marudio. Vyama na wagombea wao, wote wamebeba umati mkubwa wa wananchi wanao waunga mkono, kila upande ukisimamia msimamo wake.

    Sote tunatambua kuwa pamoja na juhudi za vikao vya suluhu kwa pande husika, bado utatuzi haujapatikana.

    Wakati hali ikiwa hivyo, Jumanne ya Febrari 2, BAKWATA lilieleza kuwa marudio ya uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo.

    Akizungumza na

    waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Sheikh wa BAKWATA mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, alisema Bakwata wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi huo.

    Uchaguzi huu wa marudio kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka kisiwa cha Zanzibar kuwa sehemu ya Amani na utulivu, natumia nafasi hii kuwaomba chama cha CUF kushiriki uchaguzi huu. Alinukuliwa Sheikh Alhad Salum.

    Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari, Sheikh Alhad aliongeza kuwa hata kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad, amemwandikia barua na kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani visiwani humo.

    Hata hivyo juzi Jumatano, tulijitahidi kupata ukweli kama aliyoyasema Sheikh Alhadi mbele ya waandishi wa habari kuwa Sheikh Had naye alimwandikia barua kuunga mkono kurejewa uchaguzi Zanzibar.

    Kilichotushangaza ni kwamba Sheikh Had amesema hajakutana na Sheikh Alhad na wala hakuwahi kumuandikia barua.

    Bila shaka Sheikh Alhad alitumia jina la Shekh Had, akiamini kuwa ni Mzanzibar na Wazanzibar wengi walikuwa wakimuunga mkono hatika harakati zake za kusaka maslahi ya Zanzibar kabla ya kukamatwa na kuswekwa ndani kwa tuhuma za ugaidi.

    Hivyo kwa kumhusisha na msimamo wa wale wanaoridhia kurejewa Uchaguzi wa Zanzibar, unaweza kuleta athari kwa wale wanaopinga marejeo hayo.

    Kwa staili hii tumelazimika kutoa tahadhari juu ya kauli

    za baadhi ya Masheikh, ambazo tunaona hazina tija kwa umma wala kuwasaidia Wazanzibar kupata muafaka wa kudumu kwa maslahi ya pande husika zinazovutana.

    Si vibaya na wala si tatizo kwa kiongozi wa dini au Sheikh Alhad na BAKWATA kutoa kauli juu ya mkwamo wa kisiasa Zanzibar. Ni haki yao na ndio uhuru wa mtu au taasisi kujieleza, kutoa kauli au au taarifa kwa umma.

    Tatizo ni namna ambavyo mtu anayeheshimika kama kiongozi wa dini, anaonekana kutoa kauli au taarifa yake bila kupima athari katika upokeaji wa kauli anayoitoa kwa walengwa. Lakini pia anatoa kauli isiyokuwa ya kweli ili kushawishi kwa maslahi ya msimo wake au wa upande ambao tayari binafsi ameshaonyesha kuunga mkono.

    Tumelazimika kusema haya kwa kuwa tayari tunaona kuna dalili si nzuri juu kauli za viongozi wa dini, ambazo kwa namna moja au nyingine tunaona zinakolezwa cheche za mvutano badala ya kuzipoza.

    Uchaguzi wa mwaka 2015 umetupa funzo kubwa kama taifa. Tumejifahamu zaidi kama watu na raia, na kwamba utulivu wa raia unaonekana kuwekwa katika jaribio kubwa na waweza kupotea, ustahimilivu huenda ukashuka sana na kuna baadhi ya wenzetu, si wote, maamuzi kwao ni hisia zaidi na sio mantiki. Tunavyoona sisi, na ni haki yetu kuwa na maoni, watakao haribu Amani ya nchi hii sio wananchi wa kawaida, bali viongozi wenye dhamana ya kusimamia katiba na utekelezaji wa sheria za nchi. Hao ndio waharibuji, kisha hugeuka na kuwatafuta wafanya fujo wasio kubaliana na uharibifu wao.

    Viongozi wetu nao wamejipambanua vizuri zaidi na wengi tumewafahamu rangi zao halisi. Ni hakika kwa namna moja ama nyingine, tumefikishana hapa kwasababu ya kukosekana imani, nafasi ya imani ikachukuliwa na ubinafsi na chuki.

    Kiongozi wa dini anapojitokeza na kuzungumzia tatizo lililopo Zanzibar, lazima atambue kuwa itikadi za vyama zimetawala katika nafsi za watu, utashi wa vyama umekuwa na mchango mkubwa zaidi wa kuifikisha Zanzibar hapo ilipo.

    Kiongozi wa dini anapojitokeza kutolea kauli hali ya kisiasa Zanzibar, kabla ya kutoa kauli yake awe na hakika kwamba tulipo si pazuri, hatupaswi kujivunia kiwango cha watu kutukanana hadharani, kutoheshimiana, kutokupendana, kutokuaminiana, kiwango kikubwa cha ubinafsi na chuki na kila mtu kukwepa kuwajibika kuanzia raia, wananchi hadi kwa viongozi.

    Kiongozi wa dini anapoamua kujitokeza katika vyombo vya habari na kuzungumzia suala la Zanzibar, sharti ajiridhishe kwamba kwa jinsi hali ilivyo sasa, maisha ya Wazanzibar yapo hatarini kisiasa, hivyo kuna haja ya kuchagua kauli za kutoa, zisizojenga hisia za kuegemea upande wowote na zenye kuashiria kupatikana suluhu ya pamoja, suluhu inayoweza kukubalika pande zote zinazovutana.

    Kiongozi wa dini akitoa kauli zenye mrengo wa kuegemea upande, ni hakika atakuwa ameshakwama, atachochea utengano, badala ya suluhu na akaongeza shari katika jamii.

    Utendaji katika dini unahitaji busara, uadilifu, hekma na utashi wa kiimani kuliko kisiasa.

    Kwa mtazamo wetu, Sheikh Alhadi hakupima yote haya kulingana na asili ya mzozo uliopo. Alichokifanya kama

    kiongozi wa dini, ni kufuata mkumbo wa hoja za wanasiasa wa upande mmoja wa mgogoro, badala ya hoja za kiongozi wa dini.

    Tubadilike. Fukuto lililopo Zanzibar si la kufanyia masihara. Tujifunze kuwa makini. Zanzibar imekwama. Suluhu kwa njia za hekima ndiyo itakazoikwamua. Na hekma, ni kutenda haki. Kufuata sheria zinasemaje. Laiti Alhad angetoa wito kwamba litafutwe jopo la wataalamu huru wa sheria na masuala ya katiba (nje ya CUF na CCM), watizame asili ya mgogoro na kisha kupendekeza ufumbuzi stahiki, tungemwelewa.

    Kwetu sisi, kurudiwa uchaguzi haiwezi kuwa ufumbuzi, kabla ya kuthibitisha kwamba ilikuwa halali kisheria na kikatiba kufuta uchaguzi huo. Kwa maana nyingine, uhalali wa kurudiwa uchaguzi unapatikana baada ya kupata uhalali wa kufuta uchaguzi. Lakini kwa bahati mbaya, hilo halitizamwi, halizungumzwi.

    Masheikh tuwe makini, tuepuke kufanya mzaha na maisha ya watu kwa kutumika kisiasa badala ya kutumia hekma kwa mujibu wa dini yetu.

    Kwani Masheikh si mnatuambia Quran inasema tuwe waadilifu na tutoe ushahidi wa kweli hata ikiwa juu ya nafsi zetu, jamaa zetu (na CCM yetu?)

    Masheikh wawe makini na kauli zao

    ILE kesi ya watuhumiwa wa ugaidi 43 wa ugaidi wakiwemo viongozi wa Kiislamu wakiongozwa na Sheikh Mselem Ali na Sheikh Farid Hadd, jana ilitajwa katika mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu lakini bila kuwepo Sheikh Hadd, ambaye ameelezwa kuwa ni mgonjwa.

    Wakili wa upande wa watuhumiwa Abdulfatah Abdallah alisema, watuhumiwa wote wanaokabiliwa na kesi hiyo walikuwepo mahakamani isipokuwa Sheikh Hadd, ambaye alitoa taarifa kwamba anaumwa malaria.

    Kesi hiyo iliitwa jana kwa ajili ya kutajwa na upande

    Sheikh Farid mgonjwaNa Abdul Msengakamba wa Jamhuri kama

    kawaida, wamesema kuwa upelelezi bado haujakamilika.

    Lakini wakati tunasubiri rufaa yao, sisi tumendika barua kwa Msajili wa Mahakama Kuu kumuomba aandae zile nyaraka kwa ajili ya kukata rufaa mapema iwezekanavyo, ili ijulikane kama kweli kutakuwepo na rufaa au hamna sasa tumeahidiwa kuwa zitapatikana ndani ya wiki mbili.

    Tumekubali wafanye upelelezi wa kina walete mahakani tuone kuna kesi au hakuna. Upelelezi umechukua muda mrefu. Mh. Rais ameshasema hakuna sababu ya kuchelewesha kesi kwa kisingizio cha kutokamilika upelelezi usiofika kikomo.

    Kesi imeahirishwa hadi tarehe 25 mwezi wa pili.

  • 5 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016HABARI ZA KIMATAIFA

    SHAHNAZ Laghari amekuwa mwanamke wa kwanza duniani wa Kiislamu kuendesha ndege akiwa kavaa mavazi ya Kiislamu.

    Bi. Shahnaz ameweka rekodi na kuingizwa katika kitabu cha Guiness (Guiness book of world record) kwa kuwa mwanamke wa kwanza duniani kuendesha ndege akiwa kavaa baqarda, jambo ambapo halijawahi kushuhudiwa au kuruhusiwa popote.

    Baqardani ni aina ya baibui pana linalovaliwa pamoja na niqabu, ambalo linakaribiana na vazi la burqa.

    Shahnaz ameonyesha uwezo wa kurusha ndege akiwa pekee (independent pilot) huku akiwa katika mavazi kamilifu ya stara ya Kiislamu.

    Shahnaz ambaye mwaka 2013 aliwania Ubunge kama

    Aweka rekodi kuendeshandege akivaa Hijab, niqab

    Aingizwa kitabu cha Guiness

    mgombea binafsi nchini Pakistan, ameonyesha kwamba mwanamke wa Kiislamu anaweza kufanya jambo kubwa la maendeleo na bado akaendelea kubaki katika mipaka ya dini.

    Rubani huyo kwa muda sasa amekuwa mtetezi mkubwa wa haki za wananwake wa Pakistan.

    Ukiacha shughuli zake za urubani, aidha amekuwa akijitolea kuwasaidia wanawake kwa kufungua vituo vya elimu ya bure na vituo vya kushona kwa ajili ya wanawake maskini nchini Pakistan.

    Pia hili ni fundisho kwa wale ambao wamejenga mazoea na husema kuwa katika ulimwengu wa jamii ya Kiislamu mwanamke hadhaminiwi na kupewa nafasi au kupewa cheo ilikuonyesha ubora na uwezo wao. proudpak.pk

    SHAHNAZ Laghari

    KWA mara ya kwanza Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama, amefanya ziara Msikitini akiwa Rais wa Marekani.

    Rais Obama alizuru Msikiti wa Islamic Society uliopo Baltmore Jumatano ya wiki iliyopita kwa lengo la kutetea uhuru wa kuabudu, hasa kufuatia kukithiri vitendo vya chuki na kibaguzi dhidi ya Waislamu na Uislamu.

    Taarifa kutoka White House ilithibitisha kuwa ziara ya Rais Obama, ilifuatiwa na ongezeko la vitendo vya kibaguzi na chuki, yakiwemo matamshi yasiyoridhisha dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini humo.

    Siku za hivi karibuni tulisikia kampeni za chuki zisizovumilika dhidi ya Waislamu wa Marekani, kwamba hawana nafasi katika nchi ya Marekani, alisema Rais Obama wakati akiwaeleza Waislamu wa Msikiti wa Islamic Society of Baltimore, lakini bila kumtaja mwanasiasa aliyetoa kauli hizo za chuki na kibaguzi.

    Tunatakiwa kuelewa, kushambulia imani ya mtu ni kushambulia imani zetu sote. Alifafanua Rais Obama katika ziara hiyo.

    Mwisho wa hutuba yake Rais Obama alieleza nia yake ya kudumisha uhusiano bora na Waislamu wa Marekani. Alisema jambo la kwanza ni kukumbatia utu.

    Alisema hatua nyingine ni kukumbuka ahadi ya wazee wa Marekani ya kulinda uhuru wa dini.

    Mwisho Rais Obama alisema kuwa Wamarekani wanatakiwa kuwakataa wanasiasa ambao wanaamini katika upendeleo na kuwalenga watu kwa sababu ya dini yao.

    Kwa miaka kadhaa sasa Rais Obama mwenyewe amekuwa akipambana dhidi ya madai kuwa yeye ni Muislamu aliyezaliwa nchini Kenya, imani ambayo bado inashikiliwa na baadhi ya wafuasi wa chama cha Republican.

    Hata hivyo Obama, ni Mkristo aliyezaliwa huko Hawaii, baba yake akiwa ni Muislamu msomi raia kutoka Kenya Bw. Hussein Obama.

    Hata hatua yake ya kufanya ziara yake ya kwanza akiwa Rais kuzuru Msikiti Marekani, ilitarajiwa kuibua hioja nyingi pinzani za kumhusisha na Uaislamu.

    Hata hivyo, hali haikuwa hivyo na badala yake ziara yake hiyo imevuta hisia za wengi ambao hawapendezwi na upepo wa kibaguzi nchini humo. www.dailymail.co.uk.

    Rais Obama atembelea Waislamu Msikitini

    RAIS Barack Obama alipokutana na viongozi wa jumuiya ya Kiislamu nchini Marekani hivi kribuni.

    Mjukuu wa Mandela asilimuMANDLA Mandela mjukuu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, amefunga ndoa ya Kiislamu na Bi. Rabia Clarke katika mji wa Cape Town mwishoni mwa wiki.

    Mandla na Bi. Rabia walifunga ndoa yao siku ya

    Jumamosi Februari 6 katika Msikiti wa Kinsington uliopo katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini na kufuatiwa na sherehe ya harusi iliyofanyika Jumapili jioni.

    Nina fahari na furaha kubwa kutangaza ndoa yangu na Rabia Clarke iliyofanyika Febriari 6, 2016 katika mji wa Cape Town.

    Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wazazi wa Rabia, jamaa zake na jamii ya Waislamu kwa kunipokea kwa dhati katika dini. Alieleza Mandla katika taarifa yake.

    Aliongeza kuwa ingawa yeye na Rabia wamelelewa katika mila tofauti za kitamaduni za dini, lakini ndoa yao inaonyesha kuwa wao ni watu wa kawaida. Ni wana wa Afrika Kusini.

    Kwa mujibu wa Channel ya Islam International, Mandla ambaye ni Chifu Mkuu wa Mvero, alisilimu miezi miwili iliyopita kabla ya kufunga ndoa na Rabia. Ahbaabur.blogspot.com

    MANDLA Mandela na mkewe

  • 6 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Habari

    DHULMA na dhambi ya kupora haki ya wananchi katika sanduku la kura Zanzibar, mshahara wake ni mauti.

    Ameyasema hayo Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbles Lema, akizungumzia jinsi suala la mkwamo wa Kisiasa Visiwani Zanzibar, linavyo pelekwa kwa kuiminya Demokrasia kwa lengo la kulinda maslahi ya baadhi ya watu.

    Mh. Lema alisema ukisoma historia, utabaini kwamba makundi mengi ya kigaidi duniani, yametokana na ukandamizwaji wa Demokrasia uliofanywa na Serikali zilizopo madarakani.

    Alisema, maamuzi ya kurudiwa Uchaguzi Zanzibar, badala ya kumtangaza mshindi ni kitendo ambacho hakikubaliki na kinaitia doa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, lakini pia inaashiria kuibomoa demokrasia.

    Mnafanya mzaha na Zanzibar, sawa mtafanya uchaguzi na mtashinda bila uwepo wa vyama vingine, hivi sasa manapeleka Polisi kutoka Bara na mnaweza mkaazima Polisi wengine kutoka Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), na mkajitangaza kuwa mmeshinda uchaguzi huo, lakini muelewe mtakuwa mmeharibu mustakabali wa kizazi kijacho cha Taifa hili. Alisema na kuasa Mh. Lema.

    Mh. Lema, alisema kisheria anayetakiwa kuongoza Zanzibar, baada ya matokeo kuonyesha ameshinda Uchaguzi sio Msudani ni Mtanzania, na ameshafanya kazi kubwa katika Taifa hili na hadi sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais, lakini hawataki kumpa haki yake kwa sababu wanadhani wana majeshi na wanaweza kuwazuia watu.

    Alisema, amepata kuongea na Mbunge mmoja kutoka

    Zanzibar: Mshahara wa dhambi mauti

    Watu wasipopiga kelele, mawe yataimbaNa Bakari Mwakangwale

    Chama Cha CUF, Bungeni, akasema Demokrasia inapokandamizwa na watu wanapo shuhudia uonevu, na kuona hawawezi kujitetea, ni wazi ugaidi na ujasusi utazaliwa katika Taifa.

    Aidha, alisema kuna maneno aliwahi kuyasema pia Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, wakati anapelekwa jela na Makaburu kwamba, Mtu mnyonge anapodhalilishwa na kuteswa, hafundishwi woga, bali anatafuta njia ya kufanya utetezi.

    Alisema, dhulma inayofanyika Zanzibar italeta madhara hadi Tanzania Bara, kwani uchaguzi ulikuwa halali, Rais alikua anaelekea kupatikana kwa kuzingatia maamuzi ya Wazanzibar wenyewe, lakini mwisho wa siku Demokrasia ikaminywa.

    Mnafikiri kumnyanganya Maalim Seifu Sharif Hamad, ushindi wake na wa Wazanzibar ni kutunza Muungano?, lakini muelewe hiki manachokifanya sasa ndio mna ubomoa Muungano wenyewe. Ametahadharisha Mh. Lema.

    Mh. Lema, akalitanabaisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    MAALIM Seif Sharif Hamad.kwamba, hakuna Jeshi lenye nguvu linaloweza kizuia umma uliochukia.

    Alisema, hali hiyo ikishashamiri nchini hali itakuwa mbaya katika kila sekta, kwani watalii ambao wanaingia nchini, wakizuiwa kuingia Zanzibar, ni wazi Arusha itaathirika, Serengeti itaathirika, hatimae uchumi wa nchi utayumba.

    Alisema, suala la Zanzibar ni suala la msingi kuliko pengine wanaopindisha demokrasia wanavyodhani na Bunge linapojadili mpango wa Taifa, ifahamike wanaongelea suala la maendeleo ya nchi ni lazima uongelee msingi wa nchi yenyewe kwani akadai msingi wa Taifa hili ni muhimu kuliko mpango wenyewe.

    Alisema, mwenendo wa kuzuia haki ni mbaya na ni kasumba ambayo sasa inaonekana kuendelea, hiyo ni kutokana na hivi karibuni Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kupitia Televisheni ya Taifa ya TBC 1.

    Alisema, kama hiyo haitoshi, wanafahamu kwamba wana mpango

    wa kuzima matangazo mengine, akasema bila shaka watafanikiwa kwa kuwa wako wengi na si hivyo tu akaongeza kwamba watafanikiwa kila dhambi dhidi ya haki za wananchi, lakini akaitaka Serikali kutambua kuwa mshahara wa dhambi ni mauti.

    Kila dhambi mtakayoipanga mtafanikiwa lakini muelewe kuwa mshahara wake ni mauti. Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi niwaambie kuwa tunapotengeza sheria ndani ya Bunge, wengine ni Mawaziri lakini watoto wenu hawatakuwa mawaziri, wengine mlikuwa mawaziri humu, lakini leo mnauliza maswali ya nyongeza, hizi sheria zitakuja kuwaathiri na nyinyi ama familia zenu. Alisema Mh. Lema.

    Alisema, unapotaka kutengeneza Taifa lenye misingi bora ni vyema wao kama Wabunge waliopo sasa wakajua nchi hii inahitaji kesho, (kesho) ambayo wao hawatokuwa kama hivi walivyo sasa, kwani akadai mbali ya dhana hiyo, wapo ndugu na jamaa zao ambao hawana utashi waliokuwa nao wao.

    Yesu alisema, watu hawa wasipopiga kelele, mawe haya yataimba, huko tunakoelekea watu hawatogea, haki itatafutwa kwa gharama yoyote ile. Alitanabaisha Mh. Lema, huku akinukuu maneno ya Yesu.

    Akasema, Wabunge wengi wanapokuwa Bungeni wanajiona kama Mungu watu, na kuongea wanacho taka kwa jeuri na kudiriki kuikandamiza Demokrasia, kwa kutumia Majeshi na Polisi, hata ndani ya Bunge, huku wakiwadhalilisha watu wanaotetea haki.

  • 7 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Maoni yanguSAWA, msimamo umewekwa kuwa uchaguzi utafanyika hapo Machi 20 mwaka huu. Lakini kwa jinsi tunavyoona mazingira yalivyo, hatudhani kama hakutahitajika tena kuwepo meza ya mazungumzo hapo baadae ya kutafutwa muafaka ili kuweka mambo sawa.

    Kwa jinsi misimamo ilivyo ya pande zinazosigana, hatudhani kama uchaguzi pekee ndiyo tiba ya maradhi ya kisiasa ya Zanzibar.

    Tukumbushe tu kwamba kila binadamu, bila ya kujali rika, rangi au umbo, ana haki za msingi ambazo hakuna mwenye haki halali ya kumpora.

    Wakati mwingine mtu anapodai haki yake, watawala wanaweza kumuona ni mtu hatari na anahatarisha amani na utulivu, kwa kuwa kwa namna moja au nyingine anagusa maslahi yao. Lakini kama binadamu wengine walivyo, watawala hao hao wakati mwingine wanatambua uwepo haki mbalimbali za binadamu.

    Wengine tunatambua kwamba hakuna namna Taifa kuweza kuwa na amani kama hakuna haki. Na huo ndio ukweli na uhalisia wa mambo. Wakati tukiwa tumefikishwa hapa tunajaribu kujiuliza tufanye nini?

    Mawaziri wakuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba waliwahi kuonya mwaka jana, kuwa hali ya mgawanyiko, ubaguzi wa kidini, ukabila na ujimbo, miongoni mwa wananchi inatishia umoja na utulivu wa nchi iwapo hatua hazitachukuliwa.

    Dk. Salim Ahmed Salim ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) na Jaji Joseph Sinde Warioba, walitoa onyo hilo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam, wakati walipohudhuria mkutano wa mashauriano ya amani, umoja na utulivu nchini Mei mwaka jana.

    Katika mkutano huo uliokuwa umeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation (MNF), somo kuu likiwa ni mashauriano kuhusu amani na umoja nchini, kwa nyakati tofauti viongozi hao wastaafu walisema misingi ya amani na utulivu iliyojengwa nchini inastahili kulindwa.

    Tukirejea nyuma kidogo, uzoefu unatuonyesha kuwa katika miaka ya hivi karibuni, hususan mwaka jana, viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu walitofautiana katika ahadi ya Serikali kuitambua Mahakama ya Kadhi katika Katiba.

    Suala la Muungano nalo lilisababisha mjadala mkali bungeni katika Bunge Maalum la Katiba wakati linajadili rasimu ya Katiba ya Warioba. Huku kukiwa na malalamiko mengi kutoka jamii ya Waislamu,

    Tukiendelea kuwa wakaidi Tutarejea kwenye muafaka

    wakiituhumu serikali kwa udini kufuatia nafasi nyingi za kisiasa na kiutendaji kuhodhiwa na Wakristo walio wengi.

    Wakati Dk. Salim akifungua mkutano huo uliowakutanisha viongozi wakuu wa Serikali waliopo na wastaafu, viongozi wa dini, wazee na viongozi wa vyama vya siasa, alisema na tunanukuu, Katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano Watanzania tuache ubaguzi na kubaguana kwa hisia za kiitikadi, dini, ukabila, mahali mtu anatoka, kazi anayofanya au uwezo wake kiuchumi.

    Na kamwe tusifikiri kuwa amani na umoja ni vitu ambavyo vipo tuukiona kuna amani na umoja ujue kuwa zilifanywa jitihada, tena jitihada za kweli kweli. Mwisho wa kunukuu.

    Pamoja na kwamba udhaifu katika maeneo hayo yanayomongonyoa kuaminiana katika umoja wetu kama Watanzania umekuwa ukiwekwa bayana mara kwa mara, bado tunaona serikali ikishindwa kuondoa kikamilifu udhaifu huo, licha ya kuwa ni hatari kwa Taifa siku za mbele.

    Hayo ni baadhi tu ya masuala ya kimsingi na yenye maslahi kwa umma, lakini yameendelea kubakia hewani bila kutatuliwa hadi sasa kama vile ni mambo mepesi ya kupuuzwa. Maeneo hayo yaliyoainishwa licha ya kuonekana kutakiwa kupatiwa suluhu ya haraka ili kulinda amani, umoja na mshikamano wa Watanzania, yamewekwa kiporo bila kupatiwa utatuzi wa kudumu na kuendelea kuwa tishio kwa umoja na mshikamano wetu.

    Lakini kwa sasa tupo katika tatizo jingine kubwa, ambalo kwa hakika limekuwa linabeba kundi kubwa lenye maslahi ya kisiasa na kimamlaka.

    Nalo ni tatizo la ubaguzi na chuki baina ya vyama vya siasa,

    hususan Chama Tawala cha Mapinduzi dhidi ya vyama vya upinzani hususan CHADEMA na CUF. Tatizo hili la chuki na ubaguzi katika vyama, limeonekana kushamiri na kunawiri zaidi Zanzibar kadiri siku zinavyosonga mbele, na kwa hakika udhaifu huu ndio umekuwa kiini cha kujitokeza sintofahamu ya kisiasa iliyopo sasa Zanzibar.

    Wengi tunafahamu kuwa kazi kubwa ya vyama vya siasa ni kutoa changamoto kwa chama tawala na kukosoa serikali yake pale inavyokwenda ndivyo sivyo. Lakini Lengo kuu la vyama hivi ni kushika dola na kutawala. Ni vigumu kuwa na utawala bora bila kuwa na vyama hivi mbadala katika siasa. Lakini pia ni vigumu kuwa na amani, umoja na mshikamano katika jamii bila kuwepo mfumo wa vyama vya siasa unaotanguliza maslahi ya umma badala ya maslahi ya viongozi na wanachama wa chama husika.

    Jaji Joseph Sinde Warioba, katika mkutano huo wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, alisema kuwa hivi jamii imetawaliwa na udini, ukabila na ukanda na kwamba hata viongozi hawataki kuitwa ndugu kama ilivyokuwa enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.

    Mhe. James Mbatia aliwahi kusema kuwa mahali tulipofikishwa viongozi wa dini hawaaminiani, wananchi wengi hawaaminiani, serikalini nao hawaaminiani, wachochezi wanao ondoa amani kwa kiasi kikubwa ni viongozi. Hizi ndizo zama tulizo nazo sasa.

    Lakini matatizo aliyoyaainisha Jaji Warioba, hayafui dafu kwa hili la chuki, ubinafsi na ubaguzi ndani ya vyama vya siasa kwa sasa, hasa kwa kuzingatia hali ya Zanzibar kwa wakati huu tulionao. Tujifunze japo kidogo tu, katika methali za Mfalme Sulemani, ambazo zina mafunzo makubwa na ni somo tosha

    hususan katika hali ya Zanzibar. Katika Methali zake Suleiman anatueleza kuwa, hazina za uovu hazisaidii kitu, lakini haki huokoa na mauti. Mungu hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.

    Aidha katika methali za Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu, anatueleza kuwa baraka humkalia mwenye haki kichwani, bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu. Kuwakumbuka wenye haki huwa na Baraka.

    Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu lakini fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu au kaidi.

    Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa, lakini kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu. Na pia kazi ya mwenye haki huuelekea uzima lakini mazao ya wabaya huelekea dhambini.

    Mwenye haki hataondolewa milele, bali wasio haki hawatakaa katika nchi. Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa lakini kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.

    Tuwe na yakini kwamba kijapo kiburi ndipo ijapo aibu. Ukaidi wa wenye fitina utawaangamiza. Wale wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.

    Wenye haki wakistawi, mji hufurahi, lakini waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.

    Nchi hutukuzwa kwa mbaraka za mwenye haki lakini mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.

    Pasipo na mashauri taifa huanguka lakini kwa wingi wa washauri huja wokovu. Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu.

    Methali za Suleiman zinaendelea kutupa somo kwamba atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili, lakini kwa yule atafutaye madhara, hayo yatamjia.

    Wenye moyo wa ukaidi mwisho wake atadharauliwa kwa kuwa hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu. Lakini wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.

    Umefika wakati tuamue kuachana na fikra potofu kwamba, itikadi za vyama ndio msingi wa mustakabali ya maisha ya watu. Vyama ni utaratibu tu uliowekwa na wanadamu kwa kadiri ya kiwango chao cha ufahamu, kupitia ili kupata madaraka au mamlaka.

    Ni vyema kujali zaidi matakwa ya watu kuliko maslahi ya kiitikadi katika vyama vyetu vya siasa. Tukifaulu kuondoa mazoea haya mabaya, tutajenga utamaduni mpya wa kuvumiliana, kukubali kukosoana, kushinda na kushindwa. Hapo tutaondoa mizizi ya chuki, ubinafsi na ubaguzi iliyojikita sasa. Tukifanikiwa hapa, tutaona aibu kudhulumu na tutaheshimiana.

    Shaban R. Kihara

    Dk. Salim Ahmed Salim Jaji Joseph Warioba

  • 8 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Makala

    HAKUNA Al-Qaidah wa kuingia Zanzibar kwa sababu Al-Qaidah ni hewa. Na ukisikia kuwa kuna tukio na inadaiwa kuwa ni Al-Qaida kafanya vitu vyake, hata kama limetokea tukio la kweli na limesababisha maafa, basi litizame kwa jicho la wasiwasi, udadisi na tahadhari. Uwezekano mkubwa ni mambo ya kupanga, mzaha (hoaxes) au wenyewe wanaita false flag terror attacks-au sting operations.

    Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani (U.S. Secretary of State) John Kerry alijikuta akiwa katika wakati mgumu. Ilikuwa katika mkutano na wandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Paolo Gentiloni.

    Ilikuwa ni baada ya kikao chao walichodai cha kuweka mikakati ya kupambana na magaidi wa IS (anti-Islamic State coalition) pale Rome, Italy, Februari 2, 2016, wakubwa hao walikutana na wandishi wa habari kumwaga sera zao.

    It is you who created Daesh (IS)! Mwandishi mmoja hakuweza kuvumilia, unaweza kusema unafiki uliokuwa ukimwagwa pale.

    Nyinyi ndio mliounda magaidi wa IS, alipaza sauti mwandishi huyo, ikawa zogo. Hali hiyo ilimwacha John Kerry na mwenyeji wake Paolo Gentiloni, wakiwa wamepigwa na bumbuwazi, wakibaki kwa muda wamekodoa macho. Hapo tena ikabidi polisi kuingilia kati kuzima zogo kwa kumtoa nje mwandishi.

    Hata hivyo, ujumbe ulikuwa umeshafika kwani zogo lile lilirushwa Live na Televisheni ya Taifa ya Italia (Italian state-owned television channel RAI.) halikadhalika kuripotiwa na mashirika makubwa ya habari duniani kama Reuters.

    Alichosema mwandishi huyo sio jambo jipya. Labda sasa kinachojitokeza ni kuwa imefikia mahali watu wanaamua kusema hadharani. Awali mambo haya yalikuwa yakizungumzwa katika

    Mh. LowassaFichua uongo, uzushi

    Hakuna Al-Qaidah ZanzibarLabda wapelekwe kama mazombi

    WAZIRI Mkuu mstaafu, Mhe. Edward Ngoyayi Lowassa.kiwango cha mijadala ya kisomi na machapisho ambapo ilielezwa wazi kuwa wanaoitwa ISIS na kile walichounda kama Dola ya Kiislamu katika Iraq na Syria, ni katika mkakati uliowekwa na Idara za Usalama za Marekani toka mwaka 2012. Na hiyo ikaelezwa kuwa ilikuwa ni moja ya mikakati ya mabeberu ya kuigawa Syria mapande mapande ili kurahisisha na kufanikisha malengo yao ya kibeberu na kuimarisha udhibiti wa Israel katika Mashariki ya Kati.

    Hilo lilikuja kuelezwa tena mwaka jana na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wakala wa usalama wa nchi hiyo (US Defense Intelligence Agency-DIA), Lieutenant General Michael Flynn, akisema kuwa uwepo magaidi wa IS na dola yao waliyounda, ambayo aliita Salafist principality, ni jambo lililofanywa kwa makusudi na watawala wa Washington. (Tazama pia: U.S. Created Daesh (ISIS) BY Stephen Lendman).

    Kwa hakika, kila kikundi na kila jina linalotamba katika

    vichwa vya habari kuwa ni kundi la kigaidi ni:

    US creations, or offshoots from them, used as imperial foot soldiers recruited from scores of countries, armed, funded, trained and directed to serve Washingtons pure evil agenda, its quest for unchallenged global dominance, its endless wars of aggressions, its ravaging and destroying one nation after another.

    Ndivyo anavyosema Stephen Lendman, na kwa hakika wanavyosema wasomi, wachambuzi na watafiti mbalimbali wenye kuheshimu na kuthamini usomi wao. Kwamba hawa Al Qaida, IS, Boko Haram na wengine kama hao, ni zao la mabeberu na kwamba, wanaendelea kuwepo kwa sababu mabeberu wakiongozwa na Marekani, wanaendelea kuwalisha, kuwapa mafunzo na silaha na kuwatuma kazi. Ili iwe nini? Wawe kama askari wa miguu wa Marekani (imperial foot soldiers) wa kufanikisha malengo yake likiwemo la kupora mali, kuvamia na

    kuvuruga nchi mbalimbali na kutawanya majeshi yake dunia nzima kufikia lengo la kutawala dunia (unchallenged global dominance au global hegemony).

    Kwa maana hiyo ni kwamba, kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi ni uzushi unaorembwa na kupambwa na vyombo vya habari kama vinavyolishwa habari hizo kutoka kwa maofisa wa serikali ya Washington.

    Ni uzushi kwa sababu hao wanaojidai kupambana na magadi, ndio hao hao wanaovunja Azimo la Baraza la Usalama Namba 2178 (Security Council Resolution 2178), linalopiga marufuku nchi wanachama kutoa mafunzo, vifaa, pesa na msaada mwingine wa namna yoyote kwa magaidi. Ndio vinara wa kuunda magaidi na kuwatuma kazi. (Soma: Daesh: The Enemy The US Created, Armed, And Funded.)

    Tunayaeleza haya kwa sababu, pamoja na kuwa yameelezwa sana katika vitabu na machapisho mbalimbali ya wasomi na hata kufanyiwa mijadala katika kumbi za kisomi za vyuo vikuu mbalimbali duniani, lakini bado wanasiasa wetu na vyombo vyetu habari, vinaendelea kuwatisha wananchi na kuwalisha propaganda hizo na kwa kweli kuwatia ujinga.

    Hivi karibuni Waziri Mkuu aliyejiuzulu na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA (UKAWA) Mheshimiwa Edward Lowassa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa, kama suala la Zanzibar halitatizamwa kwa makini, basi linaweza kufungua mlango kwa magaidi wa Al-Qaida. Pengine Mheshimiwa Lowassa alichokusudia kusema ni kuwa kama Zanzibar itaingia katika hali ya kuwa na vurugu, basi inaweza kuwa rahisi na magaidi nao kupenya hapo hapo.

    Niseme kuwa hakuna gaidi wa Al Qaida wa kuingia Zanzibar kwa sababu Al Qaida ni hewa. Al Qaida ni neno la Kiarabu ambalo asili yake ni maneno Data

    Na Omar Msangi

    Inaendelea Uk. 9

  • 9 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Makala Inatoka Uk. 8 Fichua uongo, uzushiBase, likitokana na orodha ya majina ya Mujahidina waliokuwa wameandaliwa na kutumiwa na Washington kupambana na Mrusi alipoivamia Afghanistan mwaka 1978-1980. Hawa baada ya vita, wengi wao waliuliwa katika ile carpet bombing Afghanistan, waliosalia walikamatwa na kupelekwa Guantanamo.

    Kwa vile wote walikuwa wakijulikana walikotoka (kutokana na ile Data Base), ilichofanya Marekani, ni kutafuta sababu ama ya kuuwa au kumkamata kila aliyepitia mafunzo ya Mujahidina kupigana na Mrusi, kule Afghanistan. Kwa hiyo linapangwa tukio inadaiwa kuwa ni Al-Qaida na wanatajwa watu. Wanakamatwa. Lakini pia ili kufanikisha mipango ya mabeberu, matukio kama Septemba 11, hutajwa kuwa ni kazi ya Al Qaidah ili kupaka picha ya jinamizi hatari la kuogofya dunia nzima. Kwa hiyo, baada ya kuwa jina hilo lishapigiwa tarumbeta kuwa Al Qaida ni magaidi, kila Marekani ilipotaka kuvamia na kupora kama ilivyofanya Iraq, ilitangazwa kuwa inawapiga magaidi. Kwa hiyo hata ilipofanya mauwaji ya kutisha na kinyama Falllujah ambapo wananchi walikuwa wakipinga uvamizi wa majeshi ya Marekani, hakuna nchi iliyoibuka kuizomea Marekani kwa sababu ikitangazwa kuwa inapiga magaidi.

    Ili kufanikisha world hegemony, lazima usambaze majeshi dunia nzima. Hili nalo Marekani inafanikiwa kwa kutangaza vita hewa ya ugaidi ambapo huingia katika nchi kama msamaria mwema wa kusaidia kupambana na magaidi. Mchezo hunza kwa kutoa mafunzo kwa vyombo vya usalama, mazoezi ya pamoja na kisha hufikia hatua ya kufungua kambi za jeshi. Ndio wameingia wamekaa. Hawaondoki tena. Kama alivyosema Prof. Michel Chossudovsky, ni upumbafu mtupu kuamini kuwa Marekani inapambana na Al-Qaida au IS na magaidi kwa ujumla na kwamba inaweza kusaidia nchi nyingine kupambana na magaidi, wakati Al-Qaidah ni creation

    ya Marekani! Akasisitiza kuwa kilichotakiwa ni watu kufichua uwongo na uzushi wa watu hawa na washirika wao pamoja na vibaraka wao. Kwamba ni waongo, wauwaji na wahalifu wa kivita.

    1. Mtu yeyote mwenye akili timamu na anayefikiria japo kidogo tu, atajua kuwa hakuna uwezekano wa gaidi kutoa Arabuni akafika Marekani na kuteka ndege akazitumia kupiga majengo pacha ya WTC katika ile Septemba 11. Lakini pia wanasayansi washaandika sana kwamba hata kama ndege ingelipiga majengo yale, isingewezekana joto lililotokana na moto wa matufa ya ndege au kishindo cha kugonga, kikayeyusha majengo yale yakaporomoka ndani ya sekunde chache kama biskuti iliyofinyangwa.

    Lakini mwandishi aliyetoa habari ya tahadhari ya Lowassa anaendelea kuwatia

    ujinga wasomaji wake kwa kuwaambia kuwa Al Qaida ni magaidi hatari na kwamba waliangusha majengo ya WTC kwa kuyagonga kwa ndege walizoteka! Ndio pale wachambuzi mbalimbali wanasema kuwa vita dhidi ya ugaidi, ni zimwi bandia linalopewa uhai kutokana na uwongo unaosambazwa na vyombo vya habari. Siku vyombo vya habari vitakapoamua kusema ukweli na kufichua uwongo, porojo za magaidi na vita dhidi ya ugaidi itakoma siku hiyo hiyo.

    Kwa bahati mbaya wandishi wengi mfano wa huyu aliyetoa habari ya Lowassa na hofu yake ya Al-Qaida, Zanzibar, hufanya kazi ya kupiga propaganda chafu bila hata ya kulipwa. Kutokana na chuki yao dhidi ya Uislamu, na maadhali kwa sasa wanaopakaziwa ugaidi ni Waislamu, baadhi

    ya wandishi ni kama wanachekelea na kulichukua jambo hili kishabiki. Wanashindwa kujua kwamba, hili la Uislamu na Waislamu ni namna ya kupita tu kufikia lengo. Na kwamba kabla ya Waislamu, Iraq, Syria na Libya, mabeberu walikuwa wakipambana na magaidi wa Nicaragua, Guatemala, El Salvador, Ecuador, Panama, Cuba, Chile, Argentina, n.k. Na hao ni Wakatoliki. Ugaidi wao ulikuwa kukataa mali za nchi zao kuporwa na makampuni ya kibeberu kutoka Marekani. Kwa mabeberu, muhimu kwako ni kupora, kuzivuruga nchi, kusambaza majeshi yao ili kufikia -unchallenged global dominance, wanayoitamani. Kama ni kupigwa vita Uislamu, ni kwa kuonekana kwamba ndio itikadi ya kuutingisha ubeberu iliyobakia baada ya kuporomoka ukomunisti.

    Kwa mchezo wa vita dhidi ya ugaidi ulivyo hivi sasa ulimwenguni, na namna majina haya Al Qaida, Boko Haram, Al Shabaab na IS yanavyohusishwa na ugaidi huo na ukweli ulivyo juu ya majina hayo, hakuna Al Qaida au Al Shabaab wa kuingia Zanzibar kama si mpango, si propaganda. Hakuna kwa sababu hiyo Vita yenyewe dhidi ya ugaidi ni hewa. Ni mambo kupanga. Ni mkakati katika kukamilisha malengo ya mabeberu.

    Walipouliwa watu mwaka 2001 katika yale maandamano ya CUF, kamanda mmoja wa polisi alisema kuwa polisi walilazimika kutumia risasi za moto kwa sababu wapo watu walikuwa wakitaka kuvamia vituo vya polisi kupora silaha. Habari hiyo ikaambatanishwa na akina mama wawili wakiwa wameshika mapanga ikadaiwa kuwa ni katika waliokuwa wanakwenda kuteka vituo vya polisi!

    Sasa wasiwasi wetu ni kuwa zisije zikatumika mbinu za mabeberu na false flag attacks zao kusingizia watu uali-Qaidah ili ipatikane sababu.

    Yasije yakafanyika ya kufanywa na mazombi, ikadaiwa kuwa ni magaidi wa Al-Qaida ili kipatikane kisingizio na uhalali wa kufanya uovu dhidi ya wananchi wasio na hatia.

    WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Paolo Gentiloni.

  • 10 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Makala

    MWAKA 1992 nilikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi wa mwanzo katika Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School), baada ya kufunguliwa rasmi, Januari 13, 1992, pale Ubungo Kibangu, Jijini Dar es Salaam. Hata hivyo tarehe hiyo ya kufungua shule, iliahirishwa hatukuanza masomo kutokana na kile tulichoelezwa kutokamilika kwa baadhi ya miundo mbinu, hivyo tarehe ya kuanza rasmi masomo ilisogezwa mbele kwa wiki moja.

    Siku hiyo ya Januari 13, 1992, ikiwa ni siku ya kwanza kuripoti Shuleni, tulikusanywa katika Msikiti uliokuwepo hapo (Masjid Aqswaa), ambapo kwa sasa ndipo palipojengwa bwalo la chakula lililobeba jengo la ghorofa tano, zikijumuisha madarasa na ofisi hivi sasa. Mazingira ya Msikiti huo yalikuwa duni sana, chini kukiwa na majamvi makuukuu, lakini tulionyeshwa madarasa tutakayosomea, yalikuwa mawili tu yasiyo na mvuto kuonyesha kwamba hii ni Shule ya Sekondari, madarasa hayo yalikuwa lilipo tenki la maji la chini ya ardhi kwa sasa, ambayo yalitenganishwa na kiofisi kidogo cha Mkuu wa Shule.

    Baada ya wiki kwisha, tulirejea tena rasmi kuanza masomo katika Shule hiyo maarufu kwa sasa, lakini idadi ile ya awali pale Msikitini ilipungu sana. Nakumbuka kutoka Mkoa wa Tanga, tulikuwa wanafunzi wawili tu na huyo mmoja nae alikuwa ni miongoni mwa wale ambao hawakurudi baada ya wiki moja. Katika moja ya mapumziko, nilibahatika kukutana na jamaa yangu huyo katika mitaa ya Jiji la Tanga, na baada ya salam nilimuuliza kwa nini hakurudi, jibu lilikuwa hakuvutiwa na mazingira duni ya Shule na miundo mbinu kwa ujumla, kisha aliniambia baada ya kurejea Tanga, alikwenda kujiunga katika shule ya Sekondari ya Popatlal, shule maarufu na yenye hadhi kubwa kwa wakati huo Jijini humo.

    Lakini pia yupo ndugu yangu mmoja, kwa sasa ni mwalimu pale shule ya Sekondari ya Kiislamu Kirinjiko (Kirinjiko Islamic High School), kwa kuwa ni mkazi wa hapa Jijini, baada ya kufanya mtihani wa kujiunga na shule hiyo (Interview), alipata hamu ya kwenda kuitafuta Shule yake. Anasema alipata taabu kuipata baada ya kila

    Ihsan Islamic Secondary SchoolShule ya kisasa ya KiislamuNa Bakari Mwakangwale

    aliyemuulizia wapi ilipo shule ya sekondari ya Kiislamu Ubungo, alisema haijui.

    Hata hivyo, anasema alibahatika kumpata mtu aliyejua ilipo, lakini alimpa tahadhari kwamba hakuna sekondari pale, bali kuna Madrasa ya Mzee mmoja wa Kichaga. (Almarhum Mzee Abdulrahman Kileo, Allah amrehem). Baada ya kufika na kuona mazingira ya pale, hakutaka kusubiri siku ya kuripoti (Januari 13, 1992) bali alienda kuchukua fomu katika Shule ya Kikristo, iliyopo Mbagala ya St. Anthon, ambayo mashaallah tokea wakati huo ilikuwa imekamilika na mvuto wa kuwa ni shule ya sekondari, ilikamilika kimiundo mbinu.

    Yapo mengi ya kuelezea namna gani wanafunzi wa mkondo wa kwanza tulivyo lazimika kushiriki katika

    hatua za ujenzi wa shule kwa namna moja au nyingine. Hakika safari ya masomo hapo Ubungo Islamic kwetu ilikuwa ya aina yake. Tulianza wengi takriban zaidi ya wanafunzi 50, lakini mpaka Novemba, 1995, tuliohitimu tulikuwa wanafunzi 39, tu.

    Leo ni takriban miaka 25, sasa tangu wakati huo, waasisi wa shule hiyo walilazimika kuanza katika mazingira hayo kulingana na hitajio la uwepo wa shule za Kiislamu nje ya Bakwata katika hali yoyote, ili kuweza kufikia malengo waliyoyakusudia.

    Nimeanza na utangulizi huo kuonyesha wapi Waislamu walipotoka katika juhudi za kumiliki shule zao binafsi kwa hali yoyote na hadi sasa, ambapo kuna shule za Kiislamu nyingi na bado zinaendelea kuanzishwa.

    Sasa wadau wa elimu katika

    jamii ya Kiislamu wamekuwa na wigo mpana wakiangalia mbele zaidi kuhakikisha shule za Kiislamu zinazoanzishwa ni zenye kukidhi haja kulingana na wakati uliopo na kuziba mapungufu yaliyopo au yaliyojitokeza katika shule zilizotangulia kuanzishwa.

    Hali hiyo imelenga kukabiliana na changamoto, ambazo sisi tulikutana nazo na kusababisha vijana wengi kulazimika kuzikimbia shule chache za Kiislamu zilizoanzishwa wakati huo na kwenda kujiunga na shule za Kikristo, kutokana na uduni wa miundo mbinu kulingana na ulazima wake wa kuanzishwa kwa wakati huo.

    Ihsan Islamic Secondary SchoolKatika kukabiliana na hali

    hiyo katika wakati huu wa Sayansi na Teknolojia, Kigamboni Educational Services Limited, imewaletea Waislamu shule ya Kiislamu ya Ihsan Islamic Secondary School, ambayo hakuna mwanafunzi au mzazi ambaye anaweza kuingia hapo kisha akaondoka kwa sababu ya kuwepo miundo mbinu inayotakikana. Shule hiyo iliyoanza kujengwa tangu mwaka 2013, ipo katika Kata ya Kisarawe Two, Tarafa ya Kigamboni na inatarajiwa kuwa katika Wilaya mpya ya Kigamboni, ikipatikana kati ya Dar es Salaam Zoo na Mwasonga.

    An nuur, ilifika Shuleni hapo na kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa Shule hiyo, lakini pia kwa sasa ni Mkuu wa Shule na Meneja, Mwalimu Hashimu Saiboko, ambaye alisema lengo la kuanzishwa Shule hiyo ni kutoa nafasi kwa wazazi ambao wanaona Shule za Kiislamu zilizopo zipo katika ubora wa chini. Kutokana na uzoefu wake katika taaluma ya Ualimu akiwa Mkuu wa Shule mbalimbali za Kiislamu Jijini Dar es Salaam, Mwalimu Saiboko, anasema kumekuwa na wazazi wengi wa Kiislamu ambao wanapenda watoto wao wasome katika Shule za Kiislamu lakini uduni wa miundo mbinu unachangia wazazi hao kutowapeleka katika Shule za Kiislamu.

    Anasema, utaona mzazi anakuja kuangalia Shule, baada ya kufahamu masuala ya kitaaluma, huangalia mazingira ya kimalazi na vikorombezo vyake, wengi huanza kukagua mabweni, vyoo, kisha mahala pa kulia chakula, unaweza

    Inaendelea Uk. 11

    MOJA ya majengo ya Ihsan Islamic Secondary School

  • 11 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 201611 AN-NUURMakala

    Ihsan Islamic Secondary SchoolInatoka Uk. 10ukajiuliza mzazi huyu anataka kumleta mwanae hotelini au aje asome?.

    Ihsan Islamic, wao wanasema hilo wamelizingatia, kwani kwa kiasi fulani wamebaini limekuwa na athari kwa kuwakosa vijana wa Kiislamu, ambao wazazi wao wakikuta hali ambayo hairidhishi huamua kutowapeleka watoto wao katika Shule za Kiislamu au watoto wenyewe kutokuwa tayari kusoma katika mazingira hayo.

    Kwa maana hiyo Sekondari ya Kiislamu ya Ihsan, imeandaliwa katika viwango ambavyo kila aina ya mzazi au mwanafunzi husika akiangalia mazigira, ataridhika na asiwe na sababu ya kutompeleka mwanae katika Shule hiyo ya Kiislamu, na kutokuwa na hofu kwamba mwanae hawezi kulala katika bweni ambalo lina mashaka mashaka, au akatoa kasoro katika sehemu nyingine yoyote.

    Kwa ujumla mazingira ya Shule yanakidhi haja kwa mwanafunzi anayetoka katika familia za kawaida na yule anayotoka katika mazingira ya kati na juu vile vile.

    Waislamu wengi ambao wanakataa kuwapeleka watoto wao katika Shule za Kiislamu, ni wale ambao wana hali nzuri za kimaisha hivyo tumewalenga wao pia. Akija hapa aridhike na mazingira ya Shule na ashawishike kumleta kijana wake hapa na kijana aliridhike na mazingira kwa ujumla. Anaeleza Mwl. Saiboko.

    Mpaka sasa kuna Mabweni yaliyo tayari kulala wanafunzi wapatao 186, ambayo yana nafasi ya kutosha, hewa safi na hata kuruhusu hali ya ufanyaji usafi kuwa rahisi zaidi kutokana na mfumo wa muundo wa ujenzi wake. Sambamba na uwepo wa nyumba za Walimu kwa kuishi familia nne.

    Kuta za ndani katika Mabweni hayo yamepakwa rangi inayoruhusu kufanyiwa usafi kwa maji pindi zinapochafuka, lakini chini kuna tailizi ambazo zinafanya muda wote mazingira kuwa safi na salama.

    Zaidi katika Mabweni hayo kumefungwa kamera za usalama katika vyumba vyote kwa lengo la kudhibiti maadili kwa wanafunzi, kwani Mwl. Saiboko anasema kwa uzoefu wake mara nyingi huwa kunakuwepo na wanafunzi wanaoingia wakiwa na tabia mbaya.

    Kwa maana hiyo, tatizo hilo huchukua muda mrefu kujua utovu wa nidhamu unaoendelea mabwenini, mpaka kuja kubaini unakuta tayari wengi wamesha

    athirika na tabia hizo. Sasa kupitia teknolojia hiyo, inalenga kukabiliana na utovu wa maadili wa aiana yoyote ambao

    haukubaliki kimaadili.Lakini pia itadhibiti utoro

    kwa wanafunzi mabwenini, na katika Mabweni hayo kuna

    chumba maalum cha Matron na Patron ambao ndio watakuwa na jukumu la kudhibiti kamera hizo na kuwa karibu na wanafunzi Mabwenini. Mbali na kuchunga maadili miongoni mwa wanafunzi, lakini pia kamera hizo zitasaidia kudhibiti wezi wa nje na wa ndani, kwani mfumo huo unarekodi, kwa kupiga picha usiku na mchana hata kukiwa na giza.

    Ama katika maeneo ya maliwato, kuna tailizi pia kuanzia chini hadi katika kuta zake, bafuni na vyooni, halikadhalika katika sehemu za kutilia udhu, kwa ujumla mazingira ni maridadi haswa na yanavutia.

    Mwl. Saiboko, anasema wameweka huduma za kimalazi yenye viwango ili kuziba gepu la wale wazazi wanaozitoa kasoro Shule za Kiislamu, wanaodai mazingira ya Shule za Kiislamu hayaridhishi.

    Tumeona hili ni tatizo, kwanza tumeona Uislamu unabezwa, hivyo tumeona ni wakati sasa pawepo na Shule ambayo inaondoa kashfa hizo kwani si kwamba Waislamu hawawezi kumiliki na kuwa na vitu vyenye ubora, ndio maana sasa ipo Ihsan. Alisema Mwl. Saiboko.

    Kauli hiyo inadhihirishwa na hali halisi ya mazingira ya Shule hiyo kwani, katika njia zote za maeneo ya Shule kutoka eneo moja kwenda lingine, mathalani kutoka jengo la utawala, kwenda madarasani, kwenda mabwenini na katika nyumba za wafanyakazi na kwengineko, kumewekwa vitofali Pleven block.

    Kwa upande wa chakula, Mwl. Saiboko anasema, watoto watakula kile wanachokula nyumbani au zaidi ya yumbani, kwa mfano kila siku ya Ijumaa wanafunzi wanakula Biriani, lakini pia wakiwa Shuleni hapo watakunywa maziwa, watakula mayai, Samaki, nyama ya Ngombe na ya kuku pia watakula Soseji, kwa ujumla suala la chakula pia lipo katika ubora uso na shaka kabisa, jambo ambalo An nuur, imeshuhudia katika Menu ya Shule hiyo aina ya vyakula hivyo.

    Kwa upande wa madarsa, tofauti na sisi tulioanza na madarsa mawili duni, hapo Ihsan, mpaka sasa kuna madarasa yaliyokamilika ya kusomea wanafunzi wapatao 280, na yaliyo katika ubora, ambapo kila darasa sakafu zake zimenakshiwa kwa tailizi, ambapo ubao wa kufundishia ni ule wa White board, zaidi

    Inaendelea Uk. 12

    Mkuu wa Shule na Meneja, Mwalimu Hashimu Saiboko.

    Moja ya madarasa ya kisasa ya shule hiyo.

  • 12 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 201612 Makala

    Ihsan Islamic Secondary SchoolInatoka Uk. 11walimu wanatumia Kompyuta iliyounganishwa na Projector katika kufundishia.

    Madarasa hayo yana uwezo wa kukaa wanafunzi 60 hadi 70, lakini kwa Ihsan, madarasa hayo yanatumika kwa wanafunzi 35, kwa kila darasa, lengo likiwa ni kuzingatia weledi zaidi wa taaluma, kwa watoto kuwa wachache darasani. Sambamba na madarasa hayo, Shule ina maabara iliyo bora, ambayo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi mpaka 40.

    Ukiangali miundo mbinu ya maji taka katika Shule hiyo, utabaini ipo katika teknolojia ya hali ya juu kabisa, kwa mujibu wa fundi wa sekta hiyo anasema maji machafu yanayotoka vyooni, bafuni na sehemu za kutilia udhu, yote yana uwezo wa kutumika kwa mara nyingine katika matumizi mbalimbali na hata kwa kunywa pia, baada ya kupitia hatua kadhaa.

    Si tu kwamba yatakuwa masafi, bali yatakuwa salama hata kunyweka na binadamu na hayatakuwa na harufu wala athari yoyote ile kiafya, hiyo ni kwa mujibu wa Teknolojia na ni kisayansi zaidi.

    Lakini sisi hapa maji hayo tutayatumia katika maswala ya umwagiliaji wa bustani za mboga mboga ambazo zitalimwa kwa ajili ya matumizi ya chakula Shuleni hapa. Alisema Mwl. Saiboko, akikazia teknolojia hiyo.

    Walimu na gharama za kusomesha mtoto IhsanKwa upande wa walimu,

    Shule imejipanga kuwa na walimu wazuri katika ufundishaji wenye ubora na uzoefu na kwamba hawatoshindwa kumpata mwalimu yoyote kwa gharama yoyote mwenye ubora na mzuri kitaaluma kwa kigezo cha kushindwa kumlipa.

    Lakini Mwl. Saiboko, anasema Waislamu wawapeleke watoto wao katika shule hiyo, na wasihofu uwezo wa kulipia ada, kwani amefafanua kuwa kwa wazazi ambao hawatoweza kumudu ada kutokana na kuwa na kipato kidogo, wameandaa utaratibu wa kupata ufadhili kwa watoto ambao utatofautina, kuna wengine wanaweza kupata sehemu ya ada na mzazi akalipa sehemu iliyobaki na kuna wengine wanaweza kulipiwa kamili na katika mpango huo kuna nafasi za wanafunzi kumi za ufadhili, kila mwaka.

    Ufadhili huo utazingatia

    uwezo wa mwanafunzi katika mtihani wa kujiunga na Shule hiyo kwa maana ikiwa mtoto amefaulu vizuri na mzazi wake hana uwezo kabisa wa kulipa

    ada, ataingizwa katika mfumo huo.

    Taaluma na maleziMwl. Saiboko, anasema

    wanatarajia kuwa katika

    mafanikio ya kitaaluma kwa kulenga vitu viwili, kwanza ni mienendo na tabia nzuri za wanafunzi watakaosoma katika Shule hiyo, mfano kwamba hawalengi kuwa na alama za A nyingi, ndio iwe kigezo cha kuwatangaza.

    Hiyo inakwenda sambamba na kutoa elimu ya maadili kwa watoto wafikie hatua ya kujitambua wenyewe katika kufuata na kuishi katika mwenendo wa maadili ya Kiislamu pasi ya kukumbushwa wajibu wao katika dini.

    Mwl. Saiboko, anasema Kampuni yao ina malengo ya kuwa na Shule ya Msingi, kidato cha Tano pamoja na Shule ya Ufundi, kwa baadae kwani wana eneo la kutosha lenye heka 33.

    Amesema, watoto watakaojiunga katika Shule hiyo wataandaliwa kusoma masomo ya sayansi zaidi kutokana na kuwepo na pengo kubwa la wanasayansi nchini. Lengo ni kila mwanafuzi atakaye pita hapo awe amesoma mchepuo wa sayansi.

    Alitoa wito kwa Waislamu kufika, Shuleni hapo na wapo tayari kupokea ushauri akiamini kuwa wao ni wadau wakubwa na ni sehemu ya kituo hicho cha Kisasa cha Kiislamu na wanapaswa kujivunia kwa namna moja ama nyingine.

    Mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ambaye tayari yupo shuleni hapo akitokea shule ya Msingi Alfalah Muslim, Zanzibar, akiwa na wenzake shuleni hapo anasema, mtazamo wa shule ni mzuri kuanzia mazingira na hata walimu, kwani wanaonekana wana ari ya kufundisha hivyo inatoa mwanga kwao kuwa shule imejiandaa katika kutoa elimu bora.

    Naye mwanafuzi aliyejitambulisha kwa majina ya Omari Kondo, ambaye amehitimu elimu yake ya Msingi katika shule ya Kiislamu ya Kirinjiko, Same, anasema kwa muda aliokuwepo hapo, ameona kuna mpangilio na utaratibu mzuri wa kuyaendea masomo yake.

    Lakini pia akasema, amevutiwa zaidi na njia za ufundishaji kuwa ni wa kisasa zaidi, na kwamba ndoto zake ni kusoma masomo ya sayansi na hapo ni masomo yanayotiliwa mkazo zaidi, hivyo ana imani kuwa ndoto zake zitatimia.

    Kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga Simu nammba:-0715 29 99 45, 0715 80 36 70 au www.ihsanschool.ac.tz, Face book-Ihsan secondary School.

    Moja ya vifaa vya kisasa vya ufundishaji.

    NJIA za kuelekea kushoto bweni la wanafunzi wa kike. Kulia kuelekea nyumba za walimu.

    Nyumba za walimu.

  • 13 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Makala/Tangazo

    P.O. Box 90042, +255 713 586 186 au 713 455 255Dar es Salaam, Tanzania

    NAFASI YA MAFUNZO YA USHONAJIChuo cha ushonaji Tanzania Islamic Centre kinawatangazia wanawake wote kuwa kinatoa mafunzo ya ushonaji (tailoring) na kudarizi (Embroidering) kwa ada nafuu sana.

    Chuo kina maadili na mazingira mazuri ya kujifunzia. Kipo Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa.

    Fomu zinapatikana hapa chuoni. Wanawake wote mnakaribishwa katika mafunzo.Wasiliana kwa simu No 0713586186 na 0713 455 255

    Wabillah Tawfiq

    Tanzania Islamic CentreManispaa ya Kinondoni

    Uislamu umekuja kuweka wazi kwamba, kushirikiana na au kufarikiana baina ya mtu na mtu au kundi na kundi kusiwepo isipokuwa kwa maslahi ya kulinda uhusiano baina yao na Mola wao! Ni uhusiano uliopo baina yetu na Mola wetu ndio unaotufanya tuwe kitu kimoja bila kujali mipaka ya nchi, bara, kabila, ukoo, hadhi au cheo cha mtu na mfano wa hayo.

    Ni kwa msingi huo, nami nimeguswa na taarifa za ndugu zetu Waislamu wanaoendelea kuteseka hapa nchini na kwingineko duniani. Waliobahatika kutoka salama kwenye mikono ya makafiri, ndio ambao wamekuwa wakitueleza hayo yaliyowakuta. Kwa hali halisi iliyopo, ni wazi kwamba, waliopo mikononi mwa hao madhalimu ni wengi na tuseme ndio majaaliwa ya Waislamu, na hatima yao pia itakuwa ndio majaaliwa vile vile.

    Hakika inauma sana pamoja na ukweli kwamba tunaamini kuna ujira mkubwa wanapata kwa Mola wetu kutokana na masaibu haya wanayopata. Poleni sana kaka na dada zangu! Poleni sana masheikh zetu Mselem Ally, Farid Had na wengineo. Nina hakika wengi wenu hamjawahi kuniona mimi, lakini mimi nakujueni kwa sura kupitia japo kwenye magazeti.

    Ni uhusiano wetu na Mola wetu ndio ambao umenituma kuandika haya niliyoandika. Sifahamu makabila yenu, koo zenu, labda vyeo/hadhi zenu na rangi zenu kwa baadhi yenu. Haya yote siyo sababu ya kuandika makala hii, bali ni Laa Ilaha Ilallah.. Hichi ndicho kiungo baina yangu na ninyi, na ndicho kiungo pekee cha kutuunganisha na au kutufarakanisha.

    Hali ni mbaya mno, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba haya mambo yako wazi kabisa kwenye magazeti. Tunaishi na

    Poleni ndugu zetu

    SHEIKH Msellem Ali. SHEIKH Farid Hadd.

    watu wa sampuli gani wasiokuwa na hisia za kibinadamu? Hawaoneshi kuguswa na haya mambo ya kutisha wanayofanyiwa binadamu wenzao, ambayo haifai kumfanyia hata mnyama.

    Tunasisitizwa kuenzi amani, upendo na mshikamano uliokuwepo. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli amekuja na kauli mbiu ya hapa kazi tu. Tunaunga mkono kauli mbiu hii, lakini ni wapi hiyo ari, nguvu na moyo wa kufanya kazi nitaupata? Kila uchao tunapata taarifa ya madhila mbali mbali wanayofanyiwa ndugu zetu, tena ya kuumiza na kudhalilisha! Lakini pia, hawa wahanga wa mateso bila hatia wanapoachiwa wanarudi na kukuta mambo yameharibika kabisa majumbani mwao, nao wamekuwa vilema wa maisha! Watatekelezaje kauli mbiu hii? Au inahusu baadhi ya watu katika jamii!?

    Imekuwa habari ya watu wa mahandaki ambao Allah mtukufu anatuambia kwamba; Wameangamizwa watu wa makhandaki Qur-an 85:04. Sababu yenyewe akaibainisha Allah ndani ya sura hiyo ya 85 katika ayah ya 8 kwamba; Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa

    wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa. Kinachofanyika sasa hivi ulimwenguni dhidi ya Waislamu, ni marudio na ndio desturi ya makafiri wa zama zote.

    Uliwashwa moto wakatumbukizwa watu kwa sababu ya kumuamini Mola wao aliyewaumba. Haya ndiyo mahusiano

    yaliyopo baina ya wanaomuamini Mola wao na wale wasiomwamini.

    Tambueni kuwa haitakaa itokee, kwamba matwaaghut wakaishi kwa amani na waislamu, wakapendana, wakaacha kuwapiga vita Waislamu. Yanayotokea sasa hivi ni marudio tu. Tusione kwamba tunaonewa, bali tusimame imara tukiwa na yakini kwamba wapo waliopata mateso mabaya kuliko haya ya kwetu, na kwamba ndio namna pekee ya kutengenezewa akhera yetu.

    Poleni ndugu zetu, Allah ajaalie kwa madhila hayo kuwa ndio sababu ya kufutiwa makossa yenu na kukupeni mwisho mwema kwa tawfiiq yake. Tambueni tuko pamoja kupitia uhusiano wetu adhiim baina yetu na Mola wetu. Nasi tunaomba dua zenu ili tufanye yale ambayo yatazidi kuboresha uhusiano wetu na Mola wetu, ambayo mlitaraji kuyafanya. Tunaamini kwamba, kinachowasibu ni uzushi mtupu. Hakuna ugaidi wala magaidi ila ni mchezo wa mabeberu.

    (Juma Jumanne, Katesh, MANYARA.)

  • 14 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016MAKALA/MASHAIRI

    UPELELEZI HADI LINI? Kwanza kongole kutoa, nibtadi kwa Raisi, Kwa kweli kuitongoa, uchelewevu wa kesi, Kelele tushapigia, jambo hili hadi basi! DPP na Polisi, Raisi mmemwelewa?

    Kwa kuwa kalisemea, hata mwadhamu Raisi, Wenda mkalichukua, kwa uzito si wepesi, Pasi na kuchakachua, au kuhujumu kesi! DPP na Polisi, Raisi mmemwelewa?

    Mmekuwa mkitoa, kila tukiwadadisi, Sababu ya kukawia, usikilizwaji kesi, Bayana mwatuambia, mu ngali mkijasusi! DPP na Polisi, Raisi mmemwelewa?

    Tumechoshwa kusikia, za isidingo 'hadisi', Kikomo zisofikia, shufu za Mashekhe kesi, Si ninyi mlofungua, nini tena mwajasusi! DPP na Polisi, Raisi mmemwelewa?

    Bilhaki unatia, mwendo huu wasiwasi, Tayari kaushakia, hata wa nchi Raisi, Hotubaye rejelea, upate picha halisi! DPP na Polisi, Raisi mmemwelewa?

    Jambo alolitongoa, ukweli limeakisi, Mwapaswa lizingatia, DPP na Polisi, Kwa kazi kulifanzia, haki ipate fanisi DPP na Polisi, Raisi mmemwelewa? ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    SHUKURANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimfikie mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kipenzi chetu Mtume (s.a.w).

    Amesema Allah (s.w) katika Surat Alfatih, amejaalia Mwenyezi Mungu njia bora kwa wale ambao aliowaneemesha, nao wapo kati ya njia mbili ya wale waliokasirikiwa na wale ambao wameielewa haki na wakapotea.

    Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, Tuongoze njia iliyonyooka njia ya wale uliowaneemesha, sio ya wale walio kasirikiwa wala ya wale waliopotea (6-7) Alfatiha.

    Na wala haitoki nje ya maana ya uwastani na ubora na kheri na ubainifu na ukati na kati uliopo kati ya pande mbili.

    Na hali ya kati na kati inakusudiwa mambo ya kheri, nayo ni kuhakikisha imani na kuamrisha mema na kukataza mabaya na hukusudia msimamo na utulivu, nayo ni kushikamana na njia iliyonyoka bila ya kupinda.

    Basi ukati na kati haukusudii kuacha faradhi au kuacha kutekeleza ibada kabisa, bali unamaanisha uwepesi

    Wamepata hasara wale walioijua haki na wakapotea

    Na Dr. Mahmoud Hasan Mahmoud

    na kuondoa ugumu katika maisha ya Kiislam, nao ni alama ya lazima. Aidha humaanisha uadilifu na hekima, basi ametafsiri Mtume (s.a.w) ukati na kati huo ndio maana ya kuchagua na hivyo basi kwani kuchagua watu waadilifu wao:-

    Amesema Mwenyezi Mungu, Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na ihsani (90) Annahl. Hivyo basi kuweka katika mizani ni ukati na kati na alama thabiti iliyodhihiri katika lango miongoni mwa milango ya Uislam katika imani na sheria na faradhi na ibada na shahada na hekima na kuamrisha mema na kukataza mabaya.

    Jihadi katika dini ya Mwenyezi Mungu na tabia na muamala na kuchuma mali na kutumia kwake na mahitaji ya nafsi na matamanio yake na kwa maana kwani ukati na kati huondoa kuwepo kwa kuzidisha na kupunguza, kutumia kwa fujo na kwa ubahili na

    mengineyo.Maisha hayabaki

    kuwa ya aina moja tu bali moja kati ya namna.

    1. Kuvuka mipaka katika mambo

    2. Kupunguza katika mambo na kuyaacha

    3. Na kati na kati ya hali hizi mbili ndiyo tunayoiita kati na kati, kwani kuvuka mipaka ni kwenda kinyume na apendavyo Allah kuwa katika mstari ulio nyoka, kama ilivyokua kuacha mambo kabisa, huo ni mwenendo wa kinyume na ubora wa mambo yenyewe.

    Kutekelezwa mambo kwa moyo safi pasina shaka wala uchafu wowote wa kitabia na chuki ya moyo, kufanya jambo pasi na kuwasha moto wa uadui na bugudha, hupelekea kusafika kwa jamii kutokana na matatizo na magomvi na unafiki na tabia mbaya na ugonjwa na umimi na kujipendelea mwenyewe. Tukiacha hayo kuna faida kubwa na nyingi tu za kuneemeka kila mmoja.

    Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, inatoa wito kwa Waislamu kuchangia huduma za malazi kwa Masheikh Farid Had, Mselem Ally na Waislamu wengine waliopo katika gereza la Segerea Jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za Ugaidi.

    Hakika kwa kila atakae toa atakuwa amejiwekea akiba isiyo oza, mbele ya Mwenyezi Mungu.

    Unaweza kuchangia kupitia Namba zifuatazo:-0655, 0767, 0789, 0774/ 74 52 88.

    Katibu Ustadhi Ally Mbaruku.

    Shura ya MaimamuKamati ya Maafa

    Kalamu nimeishika, kuwauliza vijana, Majibu yenu nataka, msijefanya khiyana, Uhuni sitautaka, nijibuni kiungwana, Siku hii Valentine, maanaye hasa nini? Kichwani natatizika, nahitaji mbayana, Mwenye hoja za hakika, za mambo ya Valentina, Wazi apate 'niweka, kwa marefu na mapana, Siku hii Valentine, asiliye hasa ni nini? Wapendwa mnopendeka, wapenzi wa Valentina, Nipeni basi hakika, nini hasa Valentina, Yu dada anotajika, au siku ya fitina, Siku hii Valentine, lengole hasa ni nini?

    Arubashara 'kifika, Februari kwa sana, Idhaani hunadika, i siku ya Valentina, Kesho kutwa kwa hakika, Jumapili mtaona, Siku hii Valentina, tarehe hii kwanini?

    Huvutwa na kuvutika, si wazee si vijana, Wenye anuwai rika, na jozi zisolandana, Wapate 'kuserebuka', pasi na soni kuona, Siku hii Valentine, mseto huu wa nini? Libasi zinovalika, ahamaru tena sana, Dukuduku lanishika, kunako yake maana, Kwa wale mnojivika, nijuzeni yake mana, Siku hii Valentine, wekundu huu wa nini?

    Upendo unosifika, katu si wa kuoana, Kwa nduni watambulika, ya uzinifu kufana, Mwishoni huathirika, kwa 'ngoma' wengi vijana, Siku hii Valentine, hatimaye hasa nini?

    Vijana mlolimbuka, vipenzi wa Valentina, Nyote ninawaalika, mlo na hoja mwanana, Mezani hoja naweka, nangojea mbayana, Siku hii Valentine, wa kunifunda ni nani?

    Upambe sitautaka, uso na hoja za mana, Japo utoke kwa kaka, au dada Amina, Sitaupa mlahaka, nakujuzeni bayana, Kaditama nimefika, kalamu naweka chini.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    SIKU YA VALENTINE ! (MASWALI YA TAFAKURI)

  • 15 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Makala

    NI jambo lililo dhahiri kwamba teknolojia ya habari imechochea kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo na kuifanya dunia kuwa kama kijiji. Aidha kushamiri kwa utandawazi kwa namna moja au nyingine kumechochewa na kupevuka sayansi ya mawasiliano duniani. Internet, video telecommunication, whatsap, twitter, facebook, instagram, email nk. Zote hizo ni nyenzo za mawasiliano ambayo ni ya haraka na ya wakati zaidi, ambayo ni matokeo ya kukua kwa sayansi na teknolojia ya mawasiliano.

    Simu ya kiganjani na kompyuta ni vifaa ambavyo vinatumika zaidi kufanyika mawasiliano hayo kwa watu. Matumizi ya vifaa hivi yamekuwa yakiongezeka kila uchao kwa kuwa ni njia pekee rahisi na ya uhakika ya kuwasiliana binadamu. Pamoja na kwamba matumizi ya simu na kompyuta yamekuwa makubwa kwa kuwa ndio njia pekee rahisi na nyepesi inayokidhi haja kwa wakati katika sekta ya mawasiliano kwa sasa, kiasi kwamba watu wengi wanatumia vifaa hivyo kujiletea maendeleo, lakini kuna matatizo yake.

    Kizuri hakikosi kasoro. Wataalamu wanaeleza matumizi ya muda mrefu ya simu za mkononi yana madhara kwa mwanadamu. Imebainika kuwa matumizi ya simu za mkononi ambayo huambatana na kutumika sumaku na mionzi (electronic radiations) na kusababisha madhara katika mwili wa binadamu. Mawimbi ya simu huambatana na mionzi ambayo hunasawa na sumaku, jambo ambalo kwa mtumiaji wa simu, anayeongea kwa muda mrefu anaweza kuathirika na mionzi hiyo, jambo ambalo huleta madhara makubwa kwa afya ya mwanadamu. Baadhi ya athari zinazoweza kupatikana ni kama vile kupungua uwezo wa ubongo kuhifadhi mambo, kuhisi uchovu, kukosa usingizi, saratani, uvimbe wa ubongo, utasa na ugumba. Ndio maana hata wataalamu wa masuala ya mionzi wanashauri kuwa usiweke simu karibu na moyo au eneo la kiuno. Inashauriwa pia kuwa simu iwekwe kwenye mfuko ambao hauko katika nguo, ili athari zake mbaya zipungue.

    Tuwe makini simu za mkononi hatari kwa watotoNa Shaban Rajab Hata hivyo wataalamu

    wamebainisha kuwa watoto ndio wanaoathirika zaidi na simu za kiganjani.

    Watoto wanakabiliwa hatari kubwa ya kuathirika kiafya kutokana na matumizi ya simu za kiganjani. Athari zinazopatikana kutokana na mionzi ya microwave radiation (MWR) inayotumika katika vifaa visinyoungwa kwa waya (wireless devices), hasa kwa watoto na vichanga ambavyo havijazaliwa (mimba) zimeleta hofu kubwa. Ingawa takwimu kushabihiana kati ya saratani na MWR zimebainika. Kutokana na uchunguzi wa L. Lloyd Morgan, Bingwa wa sayansi wa Environmental Health Trust na vyuo na wenzake, alitoa chapisho lilijulikana kama Journal of Microscopy and Ultrastructure mtandaoni Julai 15. Mwanasayansi huyo alieleza kuwa watoto wanakabiliwa na hatari kubwa ya kiafya kutokana na matumizi ya simu za kiganjani kuliko watu wazima. Walichunguza umri wa watoto waliotumia simu hizo kuanzia mwaka 2009 hadi 2014, sambamba na takwimu za mionzi ya simu, nyaraka za serikali, maelekezo ya watengenezaji wa simu na machapisho kama hayo. Watoto na mimba wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupata madhara katika miili, ikiwa ni matokeo ya MWR katika simu za kiganjani, kwa mujibu wa Morgan na wenzake.

    Imeelezwa kuwa kiwango cha mionzi ya MWR kupenya kwa watoto ni kikubwa kuliko kinachopenya kwa watu wazima, kwasababu tissue za ubongo kwa watoto zinaruhusu zaidi kupenya mionzi hiyo na mafuvu yao ni membamba na ukubwa wake pia mdogo zaidi. Uchunguzi huo umeonyesha kuwa watoto wanapatwa zaidi na mionzi ya MWR kuliko watu wazima. Iligundulika kuwa tissue za ubongo za mtoto zinanyonya mionzi ya MWR zaidi ya mara mbili kuliko ubongo wa mtu mzima na uchunguzi nyingine zilibainisha kuwa ute wa mifupa (bone marrow ) wa mtoto unanyonya mionzi ya MWR mara kumi zaidi kuliko wa mtu mzima.

    "Ubeligiji, Ufaransa, India na serikali za nchi nyingine zinazojali zaidi zimepitisha sheria na kutoa tahadhari kuhusu watoto kutumia vifaa

    vya kisasa (wireless devices) walibainisha wataalam hao.

    Tahadhari hizo pia zimepewa uzito mkubwa na nchi kama vile Uswisi, Austria na Canada ambako hutolewa tahadhari kwa umma kuhusu hatari ya matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa watoto na mabarobaro walio katika kundi la umri wa chini ya miaka 16. Waliandika kuwa mionzi ya MWR imekuwa haibadilishwi kwa miaka 19. Pia waligundua kuwa watengenezaji wa simu za kisasa (smartphone) walibainisha kiwango cha umbali mdogo kabisa kutoka mwilini, ambao bidhaa zao lazima ziwekwe kwa hiyo umbali wa kisheria wa kuweza kupata mionzi ya MWR haujaongezwa. Kwa kompyuta za laptop, umbali wa kisheria kutoka mwili ni sentimeta 20 (sawa na inchi 7.8).

    Waandishi hao walieleza kuwa matokeo ya sasa ya madhara ya mionzi ya simu yamekuja kufuatia dhana potofu kwamba uharibifu wa tissue kutokana na kupata moto simu ndio madhara pekee yaliyokuwa yakifikiriwa kuweza kutokea katika simu za kiganjani. Wataalamu wanasema kundi hili huathiriwa zaidi na mionzi ya kielektroniki na nguvu za sumaku au magnetism. Wanasema watoto ambao wanatumia simu za mkononi hukabiliwa na hatari mara tano zaidi ya kupata aina mbalimbali za uvimbe wa ubongo. http://www.webmd.com/children

    Katika ripoti nyingine iliyochapishwa na gazeti la Daily Telegraph, uchunguzi uliofanywa na wasomi wa Sweden umebaini kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 huathirika mara tano zaidi

    na mionzi hatari ya simu za mkononi kwa kuwa mfumo wao wa ubongo bado unastawi. Katika uchunguzi wao umebaini kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka 12 wanapaswa tu kutumia simu za mkononi iwapo kuna jambo la dharura. Kutokana na kuwa wanaadamu leo hawana budi ila kutumia vyombo vya kielektroniki kama vile simu za mkononi katika maisha yao ya kawaida, wataalamu hivi sasa wanafanya utafiti wa kina ili kutafuta njia za kukabiliana na madhara ya mwili kwa mwanadamu pale anakabiliana na mionzi ya kielektroniki na nguvu za sumaku. Kutokana na madhara mengi yaliyopo katika utumizi wa simu za mkononi, wataalam wanashauri kuwa watoto wa umri wa chini ya miaka 16, wasitumie simu na watu wazima wanaozitumia, basi matumizi yake yawe ya wastani. Kimsingi simu ya mkononi ni kifaa cha mawasiliano wakati wa dharura na kwa ajili ya mazungumo yanayopaswa kuwa mafupi.

    Kama kuna mjadala mrefu, inashauriwa kutumia simu za mezani au kukutana ana kwa ana kuliko kufanya mjadala kwa simu na kutumia muda mrefu, jambo ambalo husababisha madhara yanayopatikana katika mawasiliano ya aina hiyo na kuhatarisha maisha.

    Tunafahamu kwamba kupevuka teknolojia katika sekta ya habari na mawasiliano ni kwa maslahi ya watu, hasa kurahisisha na kuboresha maisha. Lakini pia hakuna anayependa kuhatarisha afya yake. Kwa msingi huo ni vyema tukajifunza katika matumizi sahihi ya vifaa hivyi vya kiteknolojia, ili ziwe na manufaa kwetu badala ya kutudhuru.

  • 16 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1437, IJUMAA FEB 12-18, 2016Makala

    KUJIFUNZA na kuyafanyia kazi mafunzo mema yenye maslahi na maisha ya mwanadanu ni jambo jema na lenye manufaa kwa wanadamu, wawe ni Waislamu au wasiokuwa Waislamu

    Mafunzo yanayopatikana katika Sunna za Mtume Muhammad (s.a.w) yamekuwa sehemu ya chemchem ya ufahamu na yenye manufaa kwa wanadamu kama ilivyokusudiwa.

    Yote tunayoyapata kutoka katika Sunna za mAwalimu wetu, Mtume Muhammad (s.a.w) ni mafunzo yenye faida kwa wanadamu, iwe ni faida ya nafsi au faida katika mwili au faida katika maisha kwa ujumla. Kuna hekma kubwa katika mafunzo hayo.

    Kutoka kwa Al-Baraa Bin Azib kwamba Mtume (s.a.w) kasema; utakapofika wakati wa kulala, tawadha kama udhu wa swala, kisha lala upande wako wa kulia, kisha sema: Allahumma aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu wajhiya Ilayka, wa aljaatu dhwahriy Ilayka, raghbatan wa rahbatan Ilayka, laa maljaa wa laa manjaa Minka illa Ilayka, aamantu bi-Kitaabikal-ladhiy Anzalta, wa bi-Nabiyyikal-ladhiy Arsalta

    Ewe Allah, nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu wewe na nimeuelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulichokiteremsha na Mtume wako uliyemtuma.

    Kusoma dua hiyo au kutamka maneno hayo, ni sawa na kuyafanya yawe ni maneno yako ya mwisho kwani utakapokufa utakufa katika Fitwrah (Uislam) [Al-Bukhar na Muslim] .

    Ni jambo jema kwa Muislamu kuamini na kuyafuata mafunzo haya kadiri iwezekanavyo, kwani hakuna msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake Muhammad (s.a.w).

    Mjumbe ambaye hasemi kwa matamanio yake ila ni wahyi (ujumbe) kutoka kwa Mola Muumba.

    Anasema: Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio

    Hekima ya kulalia upande wa kulia

    funuliwa. [An-Najm: 3-4].Basi hebu tuone hekma ya

    kulala upande wa kulia.Ubongo (Brain) sehemu

    yake huwa upande wa kulia na ndio ambao unauongoza moyo ulioko upande wa