cha sheria ya misitu no. 14 ya mwaka...

40
Kitini cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002

Upload: others

Post on 29-Oct-2019

60 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

Kitini cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002

Page 2: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

Mchoraji: Kingi Kinya

Kimepigwa Chapa na C&V Marketing Communication Solution (T) LimitedP.O. Box 95092Wibu Street - KinondoniDAR ES SALAAM

LEAT, January 2013

Page 3: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

3

YaliYomoUtangulizi ............................................................................................................... 4

Sehemu ya kwanza ................................................................................................. 5

Sehemu ya pili ......................................................................................................... 5

Aina za Misitu ................................................................................................... 6

Mamlaka zinazosimamia sheria ya misitu .......................................................... 8

Mgongano wa Masilahi ...................................................................................... 12

Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Misitu .................................................................. 14

Sehemu ya tatu ........................................................................................................ 15

Mipango ya Umuduji/Utunzaji ............................................................................ 15

Uanzishaji wa Misitu .......................................................................................... 17

Sehemu ya Nne ........................................................................................................ 19

Sehemu ya Tano ....................................................................................................... 20

Fidia .................................................................................................................. 21

Hifadhi za Misitu za Vijiji ..................................................................................... 22

Hifadhi za Misitu ya Jamii .................................................................................. 24

Sehemu ya Sita ........................................................................................................ 24

Sehemu ya Saba ...................................................................................................... 26

Sehemu ya Nane ...................................................................................................... 26

Sehemu ya Tisa ........................................................................................................ 26

Sehemu ya Kumi ...................................................................................................... 27

Sehemu ya Kumi na Moja ......................................................................................... 28

Uchomaji moto ................................................................................................... 33

Mamlaka ya Ofisa Misitu .................................................................................... 33

Mgandamizo wa Makosa ................................................................................... 35

Kibali cha kushitaki na kuendesha mashitaka ..................................................... 36

Uwezo wa Ziada wa Mahakama kwa makosa dhidi ya Sheria ya Misitu ............. 36

Sehemu ya Kumi na Mbili ......................................................................................... 38

Page 4: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

4

1. UtangUlizi Mnamo mwaka 2002 Bunge la Tanzania lilitunga sheria mpya ya misitu ambayo ilichukua nafasi ya Sheria ya Misitu ya Mwaka 1959. Inaeleweka wazi kuwa misitu ni moja ya raslimali kubwa za nchi yetu.

Kama raslimali nyingine misitu ni mali ya Watanzania. Ni lazima ieleweke kuwa misitu si mali ya serikali bali ni mali ya Watanzania. Kile ambacho serikali imepewa ni dhamana ya utunzaji na uhifadhi wake kwa niaba yetu sisi wananchi wa Tanzania. Ukweli huu unasemwa na kusisitizwa na sheria hii kwani inataja raslimali zote za uhaianuwai zinazopatikana

katika misitu pamoja na rasilimali nasaba kuwa ni mali ya Watanzania ila zimekabidhiwa kwa serikali kutumiwa kwa manufaa ya Watanzania. Hivyo utumiaji wowote ule wa rasilimali za misitu ambao hauwanufaishi Watanzania unakwenda kinyume kabisa cha sheria hii na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 5: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

5

Sehemu ya kwanza Sehemu hii inazungumzia vipengele vya mwanzo ikiwa ni pamoja na jina la sheria, maana ya maneno au majina yanayozungumziwa na sheria hii.

Sehemu ya piliSheria hii inataja malengo yake makuu kuwa ni:

i. kukuza mchango wa sekta ya misitu katika uletaji wa maendeleo dumivu ya nchi yetu;

ii. Kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji mkamilifu wa wananchi katika utunzaji wa misitu;

iii. Kuhakikisha utengamano wa maumbile kupitia utunzaji wa misitu, vyanzo vya maji, na rutuba ya ardhi;

iv. Kupeleka madaraka ya utunzaji wa misitu katika ngazi za chini kabisa;

v. Kukuza ubora na uuzikaji wa bidhaa za misitu,

vi. Kukuza uratibu na ushirikiano kati ya sekta ya misitu na taasisi nyingine za umma na binafsi zinazohusiana na uhifadhi wa maliasili; na

vii. Kujenga na kuongeza uelewa wa wananchi juu ya manufaa ya kitamaduni, kiuchumi na kijamii ya uhifadhi na ukuzaji wa uwanda wa misitu nchini.

viii. Kuiwezesha Tanzania kulipia kwa ukamilifu, kuchangia na kunufaika kutokana na

juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai.

Sheria hii imegawanyika katika sehemu kumi na mbili. Sehemu hizi zinazungumzia mambo mbalimbali

yanayohusiana na misitu, kanuni za umuduji misitu, taasisi za misitu kutaja machache. Kitini hiki kinazungumzia kwa kifupi sehemu zote hizi ila kinaieleza kwa kirefu kifungu kwa kifungu sehemu ya kumi na moja

ambayo inazungumzia makosa na adhabu zitolewazo kwa kutenda makosa dhidi ya sheria ya misitu. Hii ni kuwawezesha maofisa misitu, askari, na mahakimu ambao wanasimamia utelezwaji wa sheria hii kuvielewa kwa makini vifungu vya makosa ya jinai yanayohusiana na sheria ya misitu.

Page 6: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

6

Aina za Misitu

Baada ya kutaja malengo ya sheria sehemu hii inataja aina za misitu na kusema kuwa kuna aina nne za misitu kwa mujibu wa sheria hii nazo ni:

Page 7: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

7

I. Misitu ya Taifa ambayo inajumuisha:a. Hifadhi za Misitu;b. Hifadhi ya Misitu ya Asili; nac. Misitu katika ardhi ya jumla (umma)

II. Misitu ya Hifadhi ya Misitu ya Halmashauri za Wilaya ambayo inajumuisha:a. Misitu ya halmashauri za serikali za Wilayab. Misitu katika ardhi ya jumla (umma)

III. Misitu ya kijiji ambayo inajumuisha:a. Misitu katika ardhi ya kijiji;b. Misitu ya jamii katika ardhi ya kijiji; nac. Misitu isiyohifadhiwa iliyo katika ardhi ya kijiji inayotunzwa na serikali ya kijiji

IV. Misitu Binafsi ambayo inajumuisha:a. Misitu kwenye ardhi ya kijiji ambayo inamilikiwa na mtu mmoja au watu wengi kwa

mujibu wa hati miliki ya ardhi ya kimila; nab. Misitu katika ardhi ya jumla au ya kijiji ambayo umiliki wake ni kwa mujibu wa hati

iliyotolewa kwa mtu au kampuni au ushirika kwa ajili ya kuitunza kwa mujibu wa sheria hii.

Page 8: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

8

Mamlaka zinazosimamia sheria ya misitu

Aidha, sehemu hii inaanzisha taasisi za kiserikali zenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria hii pamoja na utungaji wa sera na kanuni za utunzaji misitu. Taasisi hizi ziko katika mfumo wa watu na Idara. Taasisi hizi ni kama ilivyoanishwa hapa chini:

Page 9: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

9

a. Waziri wa Misitu ambaye amepewa jukumu la kutunga sera na kuhakikisha kuwa maofisa au watumishi wa serikali waliopewa dhamana ya kusimamia sheria hii wanatekeleza majukumu yao;

b. Mkurugenzi wa Misitu ambaye licha ya kuwa mtendaji mkuu na msimamizi wa utekelezaji wa sheria ana jukumu la kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusiana na utunzaji wa misitu; na

c. Maofisa mbalimbali ambao wameteuliwa au watateuliwa ili kuhakikisha kuwepo kwa usimamizi na utumiaji tija, mkamilifu, na wa kiuchumi wa misitu.

Sheria inamtaka Mkurugenzi wa Misitu kuhakikisha kuwa Halmashauri za Wilaya na taasisi zote za misitu zinashirikishwa kikamilifu katika kutoa maoni na zinaarifiwa juu ya utunzaji na uhifadhi wa misitu kwa mujibu wa sheria hii.

Page 10: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

10

Mkurugenzi amepewa mamlaka ya kutoa notisi kwa halmashauri ya wilaya au ya mji au mamlaka yoyote ile ambayo ina mamlaka juu ya msitu wowote ule ulio katika usimamizi wake pindi pale anapobaini kuwa:

a. Halmashauri au mamlaka hiyo imeshindwa kuumudu msitu huo kama ilivyoanishwa katika mpango wake wa umuduji wa misitu au kwa mujibu wa mpango wa makubaliano wa pamoja wa umuduji msitu.

b. Na pale halmashauri hiyo inaposhindwa kuzingatia vigezo na viashiria vya kitaifa au makubaliano kama hayo; na

c. Kwa kutozingatia kanuni zinazokubalika za utunzaji mzuri wa misitu au utawala bora pale vigezo na viashiria hivyo vinapokosekana.

Notisi ya Mkurugenzi yaweza kudai kufanyika kwa mambo yafuatayo:

a. kuitaka halmashauri au mamlaka hiyo kuchukua hatua zilizoanishwa katika notisi hiyo kurekebisha na kuboresha utunzaji msitu ulio katika miliki yake;

b. kuitaka halmashauri au mamlaka hiyo kutoa sababu za msingi na za kutosha za kumzuia Mkurugenzi kutokuutwaa msitu huo na kuuhifadhi yeyé mwenyewe kwa muda atakaokuwa ameutaja katika notisi;

c. Kuhamisha msitu huo na majukumu ya kuutunza na kuumudu kwa mamlaka au mtu mwingine atakayeona anafaa kwa muda atakaokuwa ameutaja;

d. kuitaka halmashauri hiyo au mamlaka hiyo kuja mbele yake kujieleza;

Baada ya hayo Mkurugenzi anapewa mamlaka yafuatayo:

• Pale ambapo Mkurugenzi anaona kuwa halmashauri au mamlaka ya utunzaji msituimeshindwa kutoa sababu za kutosha basi anatakiwa kuandaa na kuwasilisha ripoti kwa Waziri wa Misitu. Katika kutoa mapendekezo yake kuhusu utunzaji na umuduji mbovu wa msitu uliofanywa na halmashauri au mamlaka hiyo na hatua ambazo zinatakiwa kuchukuliwa ili kuumudu msitu huo vizuri.

Page 11: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

11

• Waziri baadayakupokeanakuizingatia ripoti hiyonakujiridhishakuwakutokananaumuduji mbaya uliofanywa na mamlaka au halmashauri hiyo na kwa manufaa ya umma atatakiwa kuwasiliana na Waziri wa Serikali za Mitaa ili kumuwezesha Waziri wa Serikali za Mitaa kutumia madaraka yake chini ya kifungu cha 179 cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) ya Mwaka 1982 au kifungu cha 71 cha Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) ya Mwaka 1982. Vifungu hivi vinamuwezesha Waziri wa Serikali za Mitaa kusimamisha mamlaka tajwa kuacha kufanya shughuli yoyote ile iliyotajwa na Waziri huyo. Badala yake Waziri wa Serikali za Mitaa anaweza kumtaka Mkurugenzi wa Misitu au halmashauri nyingine au mtu mwingine kuusimamia na kuumudu msitu huo.

• Pale Mkurugenzi, halmashauri au mtu mwingine anapopewa madaraka hayo basianatakiwa kuutunza msitu huo kwa manufaa ya watu wanaoishi katika miliki yake. Mapato yanayotokana na utunzaji huo baada ya kutoa gharama za utunzaji yatapewa halmashauri iliyonyang’anywa msitu na kama kutakuwa na hasara basi halmashauri iliyonyang’anywa itabeba hasara hiyo.

Inabidi ieleweke wazi kuwa halmashauri inajumuisha serikali ya kijiji au kamati yoyote ile iiyochaguliwa na serikali ya kijiji kuutunza msitu uliohifadhiwa wa kijiji.

Page 12: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

12

Mgongano wa Masilahi

Sheria ya Misitu inakataza kabisa kwa ofisa yeyote mwenye mgongano wa masilahi kushiriki kufanya uamuzi pale ambapo:

Page 13: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

13

a. yeyé au mtu wa karibu wa familia yake ana masilahi na jambo lolote ambalo anatakiwa kulitolea uamuzi au kushiriki katika kulitolea maamuzi, pamoja na kutoa ushauri, au msaada.

b. Na kama Mkurugenzi wa Misitu ndiye mwenye mgongano wa masilahi basi atatakiwa kutangaza mgongano huo kwa kumuandikia Waziri na kama ni ofisa mwingine basi naye atamuandikia Mkurugenzi.

Sheria inaendelea kudai kuwa kama msitu wowote ule umetangazwa kuuzwa au zabuni ya kuutunza na kuuvuna imetangazwa kwa mujibu wa sheria hii au sheria nyingine yoyote ile basi ofisa yeyote ambaye:

i. ana majukumu chini ya Sheria ya Misitu ambaye anapenda kuomba kupewa msitu au kuwasilisha zabuni; au

ii. ambaye anajua kuwa mwanafamilia wake wa karibu anakusudia kuwasilisha zabuni; atatakiwa kumuarifu Waziri au Mkurugenzi mara moja juu ya mgongano huo wa masilahi.

Page 14: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

14

Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Misitu

Taasisi nyingine inayoanzishwa na Sheria ya Misitu ni Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Misitu ambayo wajumbe wake wanateuliwa na Waziri wa Misitu. Waziri anatakiwa kuzingatia vigezo vifuatavyo katika uteuzi wake: utaalamu utakiwao ikiwa ni pamoja na kuhitimu na mapenzi katika nyanja zote za umuduji misitu na uuzaji wa

mazao ya misitu; uwiano wa kijinsia; kuwashirikisha watu wasio katika utumishi wa umma mmoja wao akiwakilisha halmashauri za serikali za mitaa.

Page 15: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

15

Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Misitu ina jukumu la kumshauri Waziri katika masuala yote ya utoaji wa vibali vya kutunza misitu; utangazaji wa hifadhi za misitu; mambo yanayohusiana na umuduji misitu; marejeo ya será ya misitu, na jambo lolote lile ambalo Waziri atalichagua. Ripoti yoyote ile ambayo itatolewa na Kamati hii inatakiwa kutolewa kwa umma. Kazi zote za Kamati hii zinatakiwa kuandikiwa ripoti. Waziri wa Misitu anatakiwa kuandaa ripoti ya mwaka ya utendaji itakayojumuisha taarifa ya utendaji wa kamati. Katika ripoti yake atazingatia yafuatayo:

a. tamko la mambo ambayo yaliwasilishwa kwenye kamati;b. idadi ya hoja ambazo anatakiwa kuziwasilisha kwa kamati; na c. Idadi ya mambo ambayo aliyashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Sehemu ya tatuSehemu hii inazungumzia juu ya utungwaji na usimamiaji pamoja na utekelezaji wa mipango ya kumudu au kutunza aina mbalimbali za misitu

Mipango ya Umuduji/Utunzaji Kuna aina nne za mipango ya umuduji au utunzaji wa misitu ambazo ni:• mpangodokezowaumudujiwamisitu;• mpangokamiliwaumudujimisitu• mpangowautunzajiwamsituwakijiji;na\• mpangowautunzajiwamsitubinafsi.

Mpango wowote ule wa utunzaji wa misitu unatakiwa kuwa na mambo yafuatayo:• maelezokamilifukwamujibuwauelewauliopowarasilimalizakiuhaiumbile(kibaiolojia),

kimazingira, kiuchumi, elimu miamba na kitamaduni za msitu husika pamoja na matumizi yake;

• maelezo juu ya malengo ya kiuchumi, kimazingira, kijamii ambayo yatafikiwa katikakuumudu msitu huo;

• kutajamaeneonavijijivinavyouzungukanamahusianoyao;• maelezojuuyamaeneondaniyamsituhuoambayoyanapendekezwakuwakandaza

matumizi kwa wenyeji ili kuwawezesha kupata mafao katika hifadhi ya msitu;• haki za jamii zawenyejiwaeneohilowalizonazona jinsiwalivyoainishanakutenga

kanda za matumizi ya msitu;• muainishowajamiiziishizokatikamaeneoyakaribunamsitunauhusianowaonamsitu

ikiwa ni pamoja na miiko na tamaduni katika kutumia na kutunza rasilimali za msitu huo;

Page 16: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

16

• Dokezo la namna, muundo wa mpango wa kuzishirikisha jamii juu ya matumizi nautunzaji wa rasilimali misitu, kanda za matumizi ya kienyeji ikiwa ni pamoja na manufaa yatakayopatikana kwa jamii hizo pale ushirikishaji wa moja kwa moja juu ya matumizi na umuduji visipowezekana;

• kanuni zinazosimamia uvunaji wa kibiashara wa rasilmali misitu ikiwa ni pamoja namipango ya kuanzisha misitu mipya au kurejesha misitu (kumisitusha).

• Kanunijuuyauhifadhinautunzajiwarasilimalimisituikiwanipamojanawanyamanamimea mwitu.

• Mapendekezo juu ya utengaji kikanda wa misitu ili kuwezesha utumiaji wa maeneolengwa ya misitu kwa malengo maalumu na muainisho wa matumizi hayo na mapendekezo ya umuduji wa kanda hizo.

• Dokezolamakadirioyarasilimaliwatunafedhazinazotakiwakutekelezampangowaumuduji na mapendekezo ya tozo na ada zitakiwazo kufikiwa; vilevile, dokezo la matumizi ya msitu na mazao ya msitu huo pamoja na mgawanyo wa rasilimali zitakazopatikana kutoka katika tozo na ada hizo na kugawiawa kwa mamlaka mbalimbali zinazohusika na utunzaji wa msitu huo.

Sheria hii inataka kutungwa kwa mipango ya uhifadhi (umuduji) wa misitu kwa aina zote za misitu.

Page 17: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

17

Uanzishaji wa Misitu

Pale ambapo Waziri anaona inafaa kutangaza eneo lenye misitu kuwa ni hifadhi ya taifa ya msitu au eneo la hifadhi ya msitu wa

serikali ya mtaa, basi sheria inataka kutengenezwa kwa dokezi la mpango wa umuduji misitu ukiwa na taarifa fupi ambayo itamuwezesha Waziri kufanya uamuzi makini kama hifadhi ya msitu wa taifa au wa serikali ya mtaa itangazwe.

Katika kutayarishwa kwake dokezo la mpango wa umuduji misitu ni lazima litilie maanani maoni ya serikali ya mtaa iliyo karibu na msitu husika, watumiaji na asasi za watumiaj wa msitu huo kutoka sekta binafsi, jamii za wenyeji wa eneo hilo na watu au asasi zinazoweza kutajwa. Takwa hili nalo linatakiwa katika utengenezaji wa mpango yakinifu wa umuduji msitu na akishirikisha

Page 18: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

18

Baada ya kupokea maoni ya wadau wote husika na kuufanyia marekebisho mpango huo, meneja wa msitu atatakiwa:

• paleambapoMkurugenziwaMisitundiyemenejawaMsitukuukubalimpangohuo

• Pale ambapo serikali ya mtaa ndiyo meneja wa msitu kuukubali kwa azimio lahalmashauri na baada ya hapo kuutunza msitu huo kwa mujibu wa mpango yakinifu wa umuduji msitu na kupeleka nakala yake kwa Mkurugenzi wa Misitu,

• Naambapowakalawa serikali,mtubinafsi, taasisi, au asasi za kiraia ndiyomenejaitakiwa kuwasilisha mpango huo kwa Mkurugenzi wa Misitu.

• Na kama Mkurugenzi wa Misitu hatamtaka meneja kuchelewesha kuuasili mpangokatika ndani ya kipindi cha miezi miwili, meneja husika atatakiwa kuasili mpango huo na kuutunza msitu huo kwa mujibu wa mpango huo.

maofisa husika wa serikali kama ambavyo Mkurugenzi wa Misitu atakavyoelekeza na serikali za mtaa katika eneo husika, Dokezo la mpango wa umuduji misitumipya wa taifa au wa serikali ya mtaa linapotolewa basi msitu husika utatunzwa na kumudiwa kwa mujibu mpango huo hadi pale mpango yakinifu wa utunzaji msitu huo utakapotungwa. Muswada (au chapisho-bichi/ghafi) wa mpango yakinifu wa umuduji msitu unatakiwa kuwekwa wazi kwa ajili ya ukaguzi na upitiwaji na watu katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya iliyo karibu na

hifadhi ya msitu na katika ofisi za serikali za vijiji vilivyo karibu na hifadhi ya msitu kwa muda wa siku sitini (60). Mpango huo yakinifu unapowekwa hadharani kwa kipindi cha siku sitini, Mkurugenzi anatakiwa kutoa taarifa ya kutosha kwa njia zote za upashanaji habari kwa umma na wadau juu ya kuwepo kwa mpango huo. Na baada ya hapo anatakiwa kufanya mkutano mkuu mmoja au zaidi wa vijiji vilivyopo katika maeneo yanayouzungka msitu huo na kuchukua maoni ya wanavijiji juu ya mpango huo.

Page 19: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

19

Sehemu ya Nne

Page 20: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

20

Sehemu hii inazungumzia hifadhi zote za misitu isipokuwa hifadhi za misitu ya vijiji na ya kijamii. Sheria inampa madaraka Waziri wa Misitu kuanzisha aina mbili za hifadhi za misitu katika eneo lolote lile la ardhi.Hifadhi hizo ni: hifadhi ya taifa ya msitu na hifadhi ya misitu ya serikali ya mitaa. Uamuzi wa Waziri ni lazima

utangazwe kwenye gazeti la serikali. Sifa za ardhi ambayo hifadhi ya taifa ya misitu inaweza kutangazwa ni hizi zifuatazo:

i. eneo la nchi ambalo limefunikwa na msitu, uliohifadhiwa au ambao unatumika kwa ajili ya uzalishaji dumivu wa mbao na mazao ya misitu unaojulikana kama hifadhi ya msitu zalishi;

ii. eneo la nchi ambalo limefunikwa na msitu, uliohifadhiwa na ambao unatumika kulinda vyanzo vya maji, udongo na uzalishaji wa mimea pori kama hifadhi ya msitu lindwa;

iii. eneo la nchi ambalo limefunikwa na misitu ambalo hutumika kwa ajili ya kulinda uoto wa asili na maeneo vutivu yenye umuhimu wa kitaifa au kimataifa na kwa ajili ya kutunza na kukuza uhaianuwai na raslimali nasaba katika hali isiyovurugwa, inayobadilika ijulikanayo kama msitu wa hifadhi ya uoto wa asili.

Sehemu ya nne ya Sheria ya Misitu ya Mwaka 2002 inazungumzia misitu binafsi. Sheria inamruhsu mtu mwenye hati ya kumiliki ardhi kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Misitu ambapo msitu huo utakuwa kwa ajili ya ukuzaji bora wa misitu na uzalishaji wa mazao ya misitu kibiashara au kwa ajili ya utunzaji wa maji, au udongo, au utunzaji wa mimea pori. Makubaliano hayo yanapofikiwa mtu mwenye hati ya kumiliki ardhi hiyo haruhusiwi kuvuna au kukata misitu na mazao ya msitu bila kupata kwanza kibali cha maandishi cha Mkurugenzi wa Misitu. Makubaliano au fungamano kati ya Mkurugenzi wa Misitu na mmiliki wa

ardhi yenye msitu yana nguvu za kisheria na yanawafunga warithi wake wote ambao wanapata haki ya kumiliki ardhi kutoka kwake. Mkurugenzi naye anapewa haki dhidi ya wale wote wanaopakana na msitu huo na anaweza kuchukua hatua za kisheria kuulinda kutokana na vitendo vyovyote vile vinavyoutishia vinavyofanywa na mtu yeyote mwenye kumiliki ardhi karibu au inayopakana nao. Hatahivyo, makubaliano kati ya Mkurugenzi wa Misitu na mmiliki wa ardhi hayana nguvu ya kisheria pale yanapokiuka sheria yoyote ya nchi au mpango wa matumizi bora ya ardhi uliiokuwepo kabla yake.

Sehemu ya Tano

Page 21: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

21

Sifahizitatuzinawezakupatikanakatikahifadhiyataifayamsitu.Piahifadhiya msitu wa serikali ya mtaa yaweza kuwa na sifa hizo au zaidi.

Malengo makuu ya hifadhi ya misitu ya serikali ya mtaa ni: i. uzalishaji dumivu wa mbao na mazao ya misitu;ii. ulinzi wa vyanzo na kinga za maji, utunzaji wa udongo na ulinzi wa mimea pori, na

msitu huo hujulikana kama hifadhi ya ulinzi wa msitu ya serikali ya mtaa; iii. eneo la nchi ambalo limezungukwa na hifadhi ya msitu wa serikali ya mtaa.

Fidia

Page 22: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

22

Utangazaji wa eneo la nchi kuwa hifadhi ya taifa ya msitu au hifadhi ya misitu ya serikali ya mtaa pale unaposababisha mtu au mdau yeyote yule kupoteza ardhi yake unatakiwa kuambatana na ulipwaji wa fidia kamili na ya haki. Waziri au Serikali ya Mtaa ndio wanatakiwa kulipa fidia hiyo. Na kama mtu

au mdau huyo haridhiki na uamuzi wa kutangaza eneo la ardhi yake kuwa sehemu ya hifadhi ya msitu ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu.

Kuna aina mbili za hifadhi ya msitu ya ardhi ya kijiji ambazo ni: hifadhi tangazwa ya misitu ya ardhi ya kijiji na hifadhi rasmi ya msitu ya ardhi ya

kijiji. Hifadhi za misitu iliyotangazwa za ardhi ya kijiji ni zile ambazo zilikuwapo wakati wa kutungwa kwa Sheria hii ya Misitu. Wakati hifadhi rasmi au zilizochapishwa katika gazeti la serikali ni zile ambazo zimehifadhiwa na kupata sifa hiyo baada ya kutungwa kwa sheria hii.

Serikali ya Kijiji inapewa mamlaka ya kupitisha azimio la kuanzisha hifadhi

ya msitu ya ardhi ya kijiji. Ina uwezo wa kuwasilisha maombi kwa Mkurugenzi wa Misitu kupitia kwa serikali ya mtaa au halmashauri ya wilaya ili kuifanya hifadhi ya msitu tangazwa kuwa hifadhi rasmi ya msitu wa ardhi ya kijiji. Vilevile, kujadiliana na kuingia fungamano la pamoja la umuduji au fungamano la aina yoyote ile na Mkurugenzi wa Misitu, mtu yeyote au shirika au wakala yeyote kwa ajili ya umuduji hifadhi ya msitu wa ardhi ya kijiji. Na kuanzisha kamati ya umuduji wa hifadhi ya msitu wa ardhi ya kijiji au kuipa kamati yoyote ile ya serikali ya kijiji majukumu ya kutunza hifadhi hiyo.

Hifadhi za Misitu za Vijiji

Page 23: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

23

Kamati ya kijiji ya umuduji msitu inatakiwa kuundwa kutokana na wajumbe wa mkutano mkuu wa kijiji, kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, na mwenyekiti wake huchaguliwa kutokana na wajumbe wake. Kamati hii ni chombo kikuu cha serikali ya kijiji chenye majukumu yafuatayo;

Page 24: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

24

i. kusimamia hifadhi za misitu kijijini hapo,ii. kuripoti mara kwa mara kwenye mkutano mkuu wa kijiji, iii. kutilia maanani maoni ya mkutano mkuu wa kijiji juu ya umuduji wa hifadhi hiizo. iv. Kamati hiyo inaweza kuwashirikisha watu kama wajumbe wake katika kutekeleza

majukumu yake lakini watu hao hawatakuwa na haki ya kupiga kura pale kamati inapofanya maamuzi.

Hifadhi za Misitu ya Jamii

Sheria inawezesha kuanzishwa kwa hifadhi za misitu ya jamii. Hifadhi hizi zinaweza kuanzishwa na kikundi-jamii katika vijiji au katika maeneo yoyote yale nchini na watu wanaoishi karibu na msitu ambao wamekuwa wakiutunza au wana nia ya kuutunza kwa mujibu wa sheria na kuumiliki kiibiashara. Hifadhi ya msitu wa jamii

huwekwa chini ya uangalizi wa kamati ya hifadhi ya msitu wa jamii ambao wanakikundi huiunda. Hifadhi hii inapoanzishwa inatakiwa kuongozwa na kanuni zifuatazo:

i. kuruhusu watu wote wanaoishi katika maeneo au jirani, au wale wanaojikimu kutokana na msitu huo au wenye uhusiano mkubwa wa kitamaduni na msitu huo kujiunga na kikundi hicho;

ii. kuelewesha malengo ya kikundi hicho kwa wanakikundi au wale wote wanaopenda kujiunga nacho;

iii. kuweka utaratibu wa kuongoza kikundi ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa viongozi wake, utunzaji wa fedha, na kuongozwa na kanuni za uwazi, usawa, kutopendelea au kubagua;

iv. Kuwatia moyo wanachama wake kushiriki katika kukiongoza; nav. kutoa adhabu kwa mwanachama au wanachama kwa kuzingatia kanuni za haki za asili

yaani haki ya kujitetea na kutohukumiwa na mtu anayemtuhumu.

Sehemu ya Sita

Sehemu hii inazungumzia utaratibu wa utoaji vibali na leseni kwa ajili ya kukata au kuvuna misitu na rasilimali za misitu na kuingia katika hifadhi za misitu kufanya mambo mbalimbali. Vibali vinaweza kutolewa kwa ajili ya: i. kukata na kutengeneza mbao;

ii. kuuza mazao ya misitu ndani na nje ya nchi; iii. utafutaji na uchimbaji madini;iv. kutafuta na kuchukua mazao tajwa ya misitu;

Page 25: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

25

v. kuchuma na kuchukua mmea lindwa kwa ajili ya uchunguzi au utafiti au uzalishaji wa dawa;

vi. kujenga majengo au ujenzi wa aina yoyote; vii. kuendesha viwanda au mashine za kukata mbao; viii. kujenga barabara, reli, madaraja, au njia za ndege;

Page 26: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

26

ix. kambi kwa ajili ya watalii na upigaji picha;x. kuuza nje mazao mengine ya misitu, xi. kupanda na kukuza miti au mimea, xii. kuwinda au kuvua, kuchungia wanyama; naxiii. shughuli nyingine ambazo zinahitaji vibali.

Kibali kimoja chaweza kutolewa kwa ajili ya madhumuni yote au baadhi yake.

Sehemu ya Saba

Sehemu hii inatoa utaratibu wa jinsi biashara ya mazao ya misitu inavyotakiwa kuendeshwa. Kwa mujibu wa Sheria ya Misitu imekatazwa kwa mtu yeyote yule kuuza nje ya nchi mazao ya misitu isipokuwa baada ya kupata hati paswa kutoka kwa Mkurugenzi ihusuyo mbao au mazao ya misitu, au kuruhusiwa kwa amri ya

Waziri wa Misitu iliyochapishwa katika gazeti la serikali kuuza mbao au mazao ya misitu bila hati. Hati paswa ni lazima itaje aina ya ubora wa mbao, asili yake yaani zitokako na ubora wa kila mbao ikiwa na alama ya ubora. Sheria inasema wazi kuwa hati au leseni ya uuzaji nje wa mazao mengine ya misitu, isipokuwa mbao, itatolewa tu baada ya kuthibitishwa na ofisa husika kuwa imezingatia viwango vya ubora vilivyotajwa.

Sehemu ya Nane

Sehemu hii inazungumzia juu ya utunzaji wa miti, mimea ya pori na wanyama wa porini. Sheria inamuwezesha Waziri wa Misitu kutangaza katika gazeti la serikali mti au aina ya mti au kundi la miti katika ardhi ya jumla kuwa imehifadhiwa. Waziri atafanya hivyo baada ya kushauriana na watu, taasisi za umma na binafsi ambazo

zinauelewa wa masuala ya mazingira. Tangazo la Waziri laweza kuwa na vitofautishi na misamahakwawatunamaeneo yaardhi ya jumla. PaleWaziri anapotoa tangazohilo,sheria inakataza mtu yeyote yule kukata, kuangusha, kuharibu, au kutoa mti au mazao ya mti uliohifadhiwa katika ardhi ya jumla bila leseni kutoka mamlaka paswa.

Sehemu ya Tisa

Sehemu hii inazungumzia moto katika misitu na inakataza mtu yeyote yule, bila amri ya Waziri wa Misitu iliyochapishwa katika gazeti la serikali, kuchoma mimea yoyote ile nje ya uga wa nyumba yake, au kwa makusudi au kwa uzembe kuanzisha moto ambao anajua unaweza kusambaa na kuteketeza au kuharibu mali za mtu

Page 27: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

27

yeyote. Hivyo basi, mtu yeyote anayetaka kuchoma mimea nje ya uga wa nyumba yake au katika ardhi nyingine kama alivyoruhusiwa na mtu mwenye mamlaka hayo au ofisa misitu, anatakiwa kabla ya kufanya hivyo kutoa taarifa ya muda wa kutosha juu ya nia yake ili kuwawezesha watu wengine walio ndani ya nusu kilomita kutoka eneo analotaka kufanya uchomaji moto huo ili kuchukua tahadhari. Vilevile anatakiwa kumuarifu ofisa aliyetoa kibali hicho. Taarifa hiyo ni lazima iwe kamilifu kwa maandishi au ya mdomo, na itaje muda na wakati itakapotekelezwa.

Sehemu ya Kumi

Sehemu hii inazungumzia masuala ya fedha na uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo ya misitu. Sheria inampa Waziri uwezo wa kutangaza aina ya huduma na vibali ambavyo vitatozwa ada na mameneja wa misitu. Kibali chochote cha kukata au kuvuna mazao ya misitu kutoka katika hifadhi ya misitu, kitatolewa

tu baada ya kulipiwa ada na muombaji na au mrabaha uliotangazwa na Waziri. Waziri anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo: a) bei ya thamani ya soko inayoweza kupatikana; b) upatikanaji wa zao; c) faida ya mradi ukitilia maanani gharama na mtaji wa uwekezaji; d) kanuni za udumivu wa zao husika wakati likivunwa; na e) mambo mengine kama yatakavyokuwa yametajwa.

Sheria inakataza kutozwa kwa kilemba kutokana na kukata au kuvuna mazao ya misitu kutoka katika hifadhi ya msitu wa kijiji au ile ya kijamii unaofanywa na wanakijiji au wanakikundi isipokuwa kama ada hizo zimo ndani ya makubaliano ya jinsi ya kuitunza hifadhi hiyo.

Sheria inakwenda mbele na kutamka kuanzishwa kwa Mfuko wa Msitu wa Tanzania ambao unaongozwa na wadhamini walioteuliwa na Waziri. Vyanzo vya mapato vya mfuko huo ni hivi vifuatavyo:

i. tozo la asilimia mbili la kila ada inayolipwa kwa mujibu wa sheria hii;ii. tozo la asilimia tatu la kila kilemba kilipwacho kwa mujibu wa sheria hii; iii. kiwango chote cha pesa kinachopatikana kutokana na kuuzwa kwa mazao ya misitu

yaliyokamatwa na kuchukuliwa na serikali; iv. kipato chochote kitokanacho na mradi uliofadhiliwa na mfuko baada ya kutoa gharama

za uendeshaji; nav. pesa zozote zitokanazo na vyanzo vingine.

Page 28: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

28

Madhumuni makubwa ya Mfuko wa Misitu ni yafuatayo: i. kukuza uelewa wa umuhimu wa kulinda, kuendeleza, matumizi dumivu ya rasimali

misitu kupitia elimu ya umma na mafunzo;ii. kukuza na kusaidia kuendeleza misitu ya kijamii kwa kutunza na kulinda rasilimali

misitu ya nchi kwa kutoa ruzuku, ushauri na misaada kwa vikundi vya watu wanaotaka kujiunga katika kikundi;

iii. kukuza na kufadhili tafiti za misitu;iv. kuwawezesha Watanzania kunufaika na juhudi za kimataifa na fedha za kimataifa

zilengazo katika ulinzi na utunzaji wa rasilimali za kihainuwai na ukuzaji wa matumizi dumivu ya rasliimali misitu.

v. Kuvisaidia vikundi vya watu na watu binafsi kushiriki katika mijadala na majadiliano juu ya misitu na hasa kushiriki katika michakato inayohusiana na ufanywaji wa tathmini ya mguso/athari za kimazingira;

vi. Kuvisaidia vikundi vya watu na watu binafsi kuifuata sheria hii;vii. Kufanya mambo yote yanayohusiana na hayo hapo juu ambayo utendwaji wake

unawezesha kufikiwa kwa malengo ya sheria hii.

Sehemu ya Kumi na Moja

Sehemu hii inazungumzia makosa na adhabu mbalimbali zinazohusiana na kuvunjwa kwa Sheria ya Misitu. Kwa mujibu wa Sheria ya Misitu ni kosa kwa mtu yeyote yule asiye na kibali au ruhusa kuingia katika hifadhi ya msitu, kutenda tendo lolote lile lililoanishwa katika kifungu cha 26 cha sheria hii: kuzuia njia au barabara au

mkondo wa maji; kufunika kisiki cha mti kwa majani au udongo au kwa njia yoyote ile, kuharibu au kuondoa kisiki hicho; na kuharibu, kuchafua, kubadilisha, kuweka wigo, alama ya mpaka au notisi au ubao wa matangazo katika mti.

Sheria hii inamtwika mzigo mtuhumiwa wa kosa jukumu la kuthibitisha kutokutenda kosa. Ukatiba wa kipengele hiki ni wa mashaka kwani Katiba ya nchi yetu inataka kila mtu kutokuchuliwa kuwa na hatia na ni jukumu la mshtaki kuthibitisha bila mashaka yoyote yale ya msingi juu ya utendwaji wa kosa hilo na mtuhumiwa.

Hatahivyo sheria inasema wazi kuwa kitendo cha mtu kukutwa katika maeneo ya hifadhi ya msitu na kifaa chochote kile kinachoweza kutumika kukata, au kuchukua zao lolote la msitu anatenda kosa. Sheria inamruhusu Mkurugenzi wa Misitu kutoa tamko katika gazeti la serikali juu ya kutokuwa kosa kwa mtu yeyote yule anayekutwa na vifaa hivi katika hifadhi nzima au sehemu yake Ni lazima tamko hilo liwekwe katika sehemu iliyo wazi kwenye

Page 29: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

29

ofisi za halmashauri za serikali za mitaa ambako hifadhi husika ipo au iko karibu yake; litangazwe katika namna ambayo ni ya kawaida katika eneo hilo ili kuwawezesha wenyeji na wakazi wa eneo hilo kupata taarifa hiyo.

Page 30: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

30

Ni kosa la jinai kwa mtu yeyote yule bila ruhusa au kibali kutoka kwa mamlaka husika na kwa mujibu wa sheria hii:

i. kuchuma, kuondoa, na kuchukua sampuli au kwa namna yoyote ile na kwa makusudi kusumisha, kuharibu au kuteketeza mimea pori iliyoorodheshwa;

ii. kuonyesha kwa ajili ya kuuza au kununua au kuwa au kumiliki mimea pori iliyooredheshwa;

iii. kuuza nje ya nchi au kujaribu kuuza nje ya nchi mimea pori au sehemu yake au mbegu zake;

Adhabu ya kosa hili ni faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi sita na kutozidi miaka miwili. Mwenyehatia anaweza kupata adhabu zote mbili za faini na kifungo. Kifungu cha 87 kinataka makosa yote yanayohusiana na wanyama pori yashughulikiwe kwa mujibu wa sheria zinazohusika na mambo ya wanyama pori na sheria nyinginezo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 88 ni kosa la jinai kwa mtu yeyote yule, asiye na ruhusa au baraka za mamlaka husika, kukutwa na mazao ya misitu, isipokuwa kama ataweza kuthibitisha kuyapata kwake kihalali au kwa namna isyo na kosa. Jukumu la kuthibitisha kutokuwa na hatia liko kwake. Adhabu ya kosa hili ni faini isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka miwili au vote kwa pamoja.

Vilevile, kama mnyama yoyote wa kufugwa akikutwa anachungwa au anaingia katika hifadhi yoyote ile ya msitu, basi mnyama huyo

atachukuliwa kuwa alichungwa katika hifadhi hiyo. Mwenye mnyama huyo atahesabiwa kuwa ndiye aliyeruhusu kuchungwa au kuingia katika hifadhi hiyo kinyume cha sheria.

Kukiuka masharti ya kifungu 84(1)(a)-(e) na 84(2)-(3) ni kosa la jinai na mtu huyo pindi akikutwa na hatia atatozwa faini kati ya shilingi elfu thelathini na shilingi milioni

moja au kifungo kisichozidi miaka miwili au kupewa adhabu ya kifungo na faini.

Kwa mujbu wa kifungu cha 85 ni kosa la jinai kwa mtu yeyote asiye na leseni au kibali kutoka mamlaka husika, kuangusha, kukata, kuharibu, kuondoa au kuuza mti uliotunzwa au kuhifadhiwa au sehemu yake kutoka katika ardhi isiyohifadhiwa. Adhabu ya kosa hili ni faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi mwaka mmoja. Mwenyehatia anaweza kupewa adhabu zote mbili yaani faini na kifungo.

Page 31: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

31

Kwa mujibu wa kifungu cha 89 ni kosa la jinai kwa mtu yeyote, asiye na ruhusa halali au sababu:i. kuvuna mazao ya misitu kwa mujibu wa sheria hii;ii. kuendesha au kusababisha kuendeshwa kwa gari na kuchukua, kubeba, kuondosha,

au kusafirisha mazao ya misitu kinyume na sheria hii;iii. kuchukua, kubeba au kuondosha kwa njia isiyo kwa chombo cha moto mazao yoyote

ya misitu kinyume na sheria hii. iv. Kutaka kuuza, kuuza au kununua mazao ya misitu kinyume na sheria hii;v. Kuhifadhi mazao ya misitu kinyume cha sheria hii;vi. Kuweka alama za ubora na viwango katika mbao yoyote ile wakati si mtu mwenye

dhamana hiyo;vii. Kuuza nje ya nchi au kulingiza zao la misitu katika mauzo ya nje, ambalo uuzaji wake

nje ya nchi unahitaji cheti husika cha uuzaji nje, bila ya kuwa na cheti sahihi cha uuzaji nje.

Dhamana au jukumu la kuthibitisha kutokuwa na hatia kwa mtuhumiwa liko kwamtuhumiwa.

Adhabu ya kosa au makosa haya ni faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja ama kifungo kisichozidi miaka miwili au adhabu zote mbili.

Kifungu cha 90 kinatamka kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote yule kufanya mambo yafuatayo:

i. kughushi, kubadilisha, kuharibu au kufuta au kuharibu stempu, alama, leseni, kibali, cheti, ruhusa, au risiti iliyotumika au kutolewa kwa mujibu wa sheria hii au kanuni, amri, au taarifa iliyotolewa au kutungwa kwa mujibu wa sheria hii;

ii. kwa udanganyifu na bila ruhusa au mamlaka halali kutumia au kutoa stempu, alama, leseni, kibali, cheti, ruhusa, au risiti iliyotumika au inayokusudiwa kutumika au kutolewa kwa mujibu wa sheria hii au kanuni, amri, au taarifa iliyotolewa au kutungwa kwa mujibu wa sheria hii;

iii. kuweka alama kwenye mbao, iwe mbao hiyo imewekwa alama na mweka alama aliyeruhusiwa au mkaguzi au hapana, au kuweka alama sawa na ile inayotakiwa na sheria hii au sheria ndogo iliyotungwa kwa mujibu wa sheria hii na kuweza kuifanya kuchukuliwa kuwa ni alama inayotakiwa na sheria hii.

Page 32: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

32

Pindi akikutwa na hatia mtuhumiwa atapigwa faini isiyopungua shilingimilioni moja na kutozidi shilingi milioni tatu au kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka miwili. Mahakama inaweza kumpa adhabu zote mbili yaani faini na kifungo.

Page 33: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

33

Uchomaji motoKifungu cha 91 kinaweka wazi kuwa mtu yeyote yule ambaye bila ruhusa halali ya kisheria:i. anawasha, au kusaidia kuwasha au kutumia au kuchochea au kuongeza mafuta katika

moto au kusababisha mambo haya kutokea;ii. anaacha bila uangalizi moto ambao bila ruhusa au kwa ruhusa amewasha au amesaidia

kuuwasha au kutumia, kuchochea, au kuongeza mafuta bila kuhakikisha kuwa moto huo umezimwa kabisa;

iii. ameshindwa kufuata au kutekeleza amri halali iliyotolewa kwake kuhusiana na Sehemu ya Tisa ya sheria hii:

ana hatia ya kosa na pindi atakapotiwa hatiani atatakiwa kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na kutozidi shilingi milioni moja au adhabu ya kifungo kisichozidi mwaka mmoja ama kupewa adhabu zote mbili.

Kifungu cha 91(2) kinatamka wazi kuwa mtu yeyote yule ambaye kwa makusudi na kwa kinyume cha sheria anawasha moto katika hifadhi ya msitu, shamba la misitu, miti iliyomea, mche, vichaka, viwe au visiwe ni vya asili anatenda kosa la jinai na pindi akikutwa na hatia atapewa adhabu kama ilivyoanishwa na kifungu cha 321 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Mamlaka ya Ofisa MisituKwa mujibu wa kifungu cha 93 ofisa yeyote yule aliyeidhinishwa, ofisa wa misitu au askari polisi anaweza kudai mambo yafuatayo: i. kutolewa kwa leseni au kibali chochote ambacho kinamuwezesha huyo kufanya jambo

lolote kwa mujibu wa sheria hii; ii. kumtaka mtu yeyote, pale ambapo ana sababu ya msingi ya kumshuku mtu huyo

kuwa na mazao bila uhalali ya misitu, kusimama na kutoa maelezo juu ya kuwa kwake na mazao hayo. Ofisa huyo anaweza, bila ya kuwa na hati ya ukaguzi ila kwa kuzingatia masharti ya kifungu hiki, kumkagua mtu, mzigo, kifurushi, gari, boti, ndege, hema, au jengo lilo chini ya miliki au usimamizi wa mtu huyo pale ambapo mazo hayo yanashukiwa kuwekwa au kuhifadhiwa; Masharti ambayo ofisa anatakiwa kuzingatia yameanishwa na kipengele cha 93(2) (a)-(b) nayo ni kuwa (a)madaraka haya hayatatekelezwa na walinzi wa misitu au polisi chini ya cheo cha inspekta; na (b) na yatatekelezwa na maofisa ambao wamepewa mamlaka hayo na kifungu hiki mbele

Page 34: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

34

ya mashuhuda/wajulizi wawili huru. iii. kuzuia kuondolewa au kuchukua na kuzuia mazao hayo ya misitu au mifugo pale

kunapokuwa na hisia kuwa kosa dhidi ya sheria hii limefanywa hivi karibuni. Vitu vingine anavyoweza kuvizuia au kuvitwaa ni ndege, boti, magari, mashine, vifaa na zana ambazo zilitumika katika kutenda kosa hilo. Ofisa huyo anatakiwa kuandika ripoti juu ya utwaaji wa mali hizo na kuikabidhi kwa hakimu aliye karibu naye.

iv. Kumkamata bila hati mtu yeyote ambaye ofisa huyo ana kila sababu ya kumshuku kwamba ametenda au ameshiriki katika kutenda kosa dhidi ya sheria hii pale mtu huyo:• atakapokataakutajajinanaanuaniyakeaupaleanapotajajinanaanuaniambayo

ofisa anashuku kuwa ni ya uongo; • anapokuwanasababuzamsingizakuaminikuwamtuhuyoanawezakukimbiaau

kutoroka.

Pale ofisa yeyote yule anapotumia madaraka yake kwa mujibu wa kifungu hiki basiatahakikisha kuwa anampeleka mtu huyo mahakamani.

Kifungu cha 94 kinataka kupelekwa katika Kituo cha polisi kilicho karibu kwa kitu au zao la misitu liliokamatwa kwa mujibu wa kifungu cha 88 au 90 na baada ya hapo kupelekwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa meneja wa hifadhi ya msitu aliye karibu. Ripoti ya uchukuaji na uwekwaji wake itatolewa kwa ofisa mkuu wa polisi mwenye mamlaka juu ya eneo hilo.

Kitu au zao la misitu lililowekwa chini ya uangalizi wa polisi au meneja wa hifadhi ya msitu litabakia katika uangalizi huo hadi pale kosa hilo litakapokuwa limefikishwa mahakaman au linapogandamizwa1 au pale uamuzi wa kutokushitaki unapotolewa.

Endapo kitu au zao la misitu lililokamatwa ambalo linaweza kuoza au kuharibika, basi meneja wa hifadhi ya msitu anatakiwa na kifungu cha 94(3) kuamuru cha kifaa au zao hilo kuuzwa au kuharibiwa na pale linapokuwa limeuzwa, fedha zitakazopatikana zitawekwa na kutumiwa au kushughulikiwa kwa mujibu wa kifungu cha 94(2).

Kama mwenye kitu au mali iliyokamatwa atashindwa kutokea au atatokomea na kuacha mali yake kwa muda wa siku thelathini, Mkurugenzi wa Misitu au ofisa husika anaweza kuuza mali hiyo na fedha itakayopatikana itatumika kulipa gharama zilizotumika na kiasi kilichobaki, kama kipo, kitawekwa katika Mfuko wa Misitu.

Page 35: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

35

Mgandamizo wa Makosa

Kifungu cha 95 kinazungumzia mgandamizo wa makosa. Kwa mujibu wa kifungu hiki pale ambapo Mkurugenzi wa Misitu au ofisa ambaye ameruhusiwa na Mkurugenzi wa Misitu, kwa taarifa iliyotangazwa katka gazeti la serikali, ataridhika kwamba mtu ametenda kosa dhidi ya sheria ya misitu anaweza kugandamiza kosa hilo na

kukubali kupokea kiasi cha pesa na zao la msitu, kama lipo, ambalo kwalo kosa limetendwa.

Kiwango cha pesa kinachoweza kulipwa ni lazima:i. kisizidi mara tano ya faini ya juu ambayo inatakiwa kulipwa kwa mujibu wa sheria kwa

kosa hilo;ii. ijumuishe faini zote na vilemba vilivyotakiwa kulipwa au ambavyo vingelipwa kama

tendo hilo lingekuwa limefanyika kisheria;iii. kama zao la msitu husika katika kosa hilo limeharibika au kuumizwa au kutolewa

wakati wa utendaji wa kosa, ajumuishe kiwango cha fedha kisichozidi thamani ya zao la msitu;

iv. ajumuishe gharama zinazokubalika ambazo Mkurugenzia ameingia katika ukamataji, utunzaji, uhifadhi au uondoaji wa vitu vilivyoshikwa kwa kutenda kosa hilo.

Inabidi ieleweke kuwa mamlaka ya kugandamiza makosa kwa mujibu wa kifungu hiki yatatekelezwa tu pale ambapo mkosaji anakiri kutenda kosa au makosa hayo kwa maandishi katika fomu iliyoidhinishwa kwa mujbu wa kifungu hiki. Vilevile, ni kuwa mamlaka haya yanatumika tu pale ambapo thamani ya zao la msitu ambalo kwalo kosa

limetendwa au uharibifu uliofanywa hauzidi shilingi milioni mbili.

PaleambapoMkurugenziauofisamwenyemamlakayakugandamizamakosaanatekelezamamlaka yake kwa mujibu wa kifungu cha 95 anapokea fedha kutoka kwa mkosaji anatakiwa kumpa risiti ambayo inatakiwa kuwa katika fomu iliyo katika mundo uliotajwa na sheria. Baada ya hapo Mkurugenzi au ofisa huyo anatakiwa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Mkurugenzi au afisa tawala wa wilaya husika ambapo kosa hilo lilitendwa juu ya yeyé kutumia madaraka ya kugandamiza kosa.

Fedha zote ambazo zinapatikana kutokana na kugandamiza kosa zinatakiwa, baada ya kuondoa gharama zilizotumika zinazokubalika, kupelekwa na kuwekwa katika Mfuko wa Misitu.

Page 36: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

36

Kosa linapogandamizwa, ugandamizaji wake ni utetezi tosha juu ya mashitaka ambayo yanaweza kuletwa juu yake kutokana na utendwaji wa kosa hilo. Anachotakiwa kuonyesha ni kuwa kosa hilo ni lile ambalo yeyé alishikwa nalo na likagandamizwa na Mkurugenzi au ofisa husika.

Kibali cha kushitaki na kuendesha mashitaka

Katika nchi yetu mtu mwenye mamlaka ya kushitaki mtu kwa kosa la jinai ni MkurugenziwaMakosayaJinai.Polisinaowanamamlakahayolakiniwanafanyakazi hiyo chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai. Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai anaweza kuingilia kesi yoyote ile ya jinai na kutaka kuiendesha

yeyé mwenyewe au kuindoa mahakamani.

Ni kutokana na ukweli huu kifungu cha 96 kinawawezesha Mkurugenzi wa Misitu au ofisa husika kufungua na kuendesha mashitaka juu ya makosa dhidi ya sheria hii pale wanapopata ruhusa au kibali cha Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Uwezo wa Ziada wa Mahakama kwa makosa dhidi ya Sheria ya MisituKwa mujibu wa kifungu cha 97(1) pale mtu anapokutwa na hatia ya kutenda kosa dhidi ya sheria hii, mahakama imepewa uwezo wa, licha ya kutoa adhabu iliyotajwa na sheria hii, kutoa amri zifuatazo:

i. kwamba kibali chochote kilichotolewa kwa mtu huyo chini ya sheria ya misitu kifutwe na mtu huyo hasistahili kupewa kibali kingine chochote kwa kipindi kitakachotajwa na mahakama;

ii. kwamba zao la misitu lililokamatwa kutokana na kukiuka sheria lichukuliwe na meneja wa hifadhi ya msitu. Meneja wa hifadhi ya misitu anaweza kuuza au kuondoa zao hilo kwa namna atakayoona inafaa;

iii. pale zao la misitu linapokuwa limeharibiwa au kuumizwa katika kutenda kosa, mtu aliyekutwa na hatia atakiwe kumlipa meneja wa hifadhi ya msitu fidia ya thamani ya zao hilo;

iv. na kama mali ya serikali au halmashauri ya serikali ya mtaa imeharibiwa au kuumizwa katika utendwaji wa kosa hilo au kuhusiana na utendaji wa kosa, mkosaji amlipe Mkurugenzi wa Misitu au Ofisa Mtendaji Mkuu wa halmashauri ya serikali ya mtaa husika fidia yenye thamani ya mali iliyoharibiwa;

v. kwamba mkosaji aliyetiwa hatiani amlipe meneja wa hifadhi ya msitu kiwango kiwezacho kufikia mara kumi ya malipo ya kilemba/mrabaha au ada ambazo kama

Page 37: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

37

kitendo hicho kingekuwa kimeruhusiwa kisheria zingelipwa;vi. na kama kosa hilo linahusiana na kukaa, kulima au kuchunga katika hifadhi ya misitu

bila ya kuwa na haki au kibali, mkosaji huyo aondoe jengo, uzio/boma, vibanda, mazao, mifugo, katika muda utakaotajwa na amri hiyo; na kuwa jengo, uzio/boma, mazao au mifugo iwe mali ya serikali na Mkurugenzi aiuze au kuigawa kwa namna anayoona inafaa;

vii. kwamba mwenye hatia amfidie meneja wa hifadhi ya msitu gharama na matumizi ya fedha aliyoyafanya katika kutwaa, kuhifadhi na kutunza na kuondoa zao lolote la msitu au bidhaa na vitu vingine vilivyochukuliwa na serikali kwa kuhusiana na kosa hilo.

Kifungu cha 97(2) kinatamka kwamba licha ya matakwa ya kifungu cha 97(1)(b), Mkurugenzi wa Misitu au ofisa yeyote mhusika, atatakiwa kuuza au kuondosha zao lolote la misitu lililokamatwa kwa mujibu wa sura ya 11 ya sheria hii kwa kwa jinsi atakavyoelekeza katika amri ya jumla au lengwa.

Kifungu cha 97(3) kinaagiza kuwa fedha zozote zile zilizolipwa au zitakazolipwa kwa Mkurugenzi au kupatikana kwa kuuza mali yoyote kwa mijibu wa kifungu cha 97 ni lazima ziwekwe katika mapato ya jumla ya serikali.

Kifungu cha 98(1) kinatoa kinga kwa maofisa wahusika pale ambapo tendo au matendo yao yaliyofanywa kwa nia nzuri wakati wa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria hii kutokushitakiwa au kubeba dhamana ya kosa wao binafsi.

Kinga kwa Maofisa wa Misitu

Kifungu cha 98(2) kinatamka kwamba katika mashitaka yoyote yale ambapo nia nzuri juu ya ofisa mhusika ya utekelezaji wa mamlaka au uwezo aliopewa inapokuwa inatiliwa mashaka au kuwa hoja, basi ofisa mhusika atatakiwa tu kuonyesha kuwa alikuwa akifanya kazi zake kwa mujibu wa sheria hii. Baada ya hapo jukumu au wajibu wa kuthibitisha visivyo utahamia kwa mtu anayekataa kuwapo kwa nia njema.

Kifungu cha 99 kinampa Mkurugenzi wa Misitu uwezo wa kutoa zawadi ya isiyozidi nusu ya thamani ya faini ambayo inatozwa kwa kila kosa kwa mtu yeyote yule aliyetoa habari zilizosabisha kutiwa hatiani kwa mkosaji. Kwa mujibu wa kifungu cha 100 hakuna kifungu chochote cha sehemu ya 11 ya sheria

Page 38: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

KITINI CHA SHERIA YA MISITU NO. 14 YA MWAKA 2002

38

hii ambayo inaizuia serikali au mtu yeyote kushitaki ili kupata fidia kutiokana na hasara au uharibifu alioupata kutokana na kosa lilofanywa chini ya sheria hii.

Sehemu ya Kumi na Mbili

Sehemu hii inazungumzia vipengele vya mambo mengineyo kama vile utoaji wa notisi ikiwa ni pamoja na kutoa notisi kwa mtu binafsi na kama mtu hapatikani basi kwa njia ya barua, au kubandika notisi katika sehemu ya wazi iliyo karibu na eneo au nyumba anayokaa, ofisi za serikali ya mtaa iliyo karibu na eneo lake au

kuichapisha katika gazeti la serikali. Notisi hiyo inaweza kuwa katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza.

Sehemu hii vilevile inazungumzia juu ya umuhimu wa kutumia kila njia ifaayo katika utoaji wa habari au taarifa ili kuwezesha umma kuipata na kuifanyia kazi.

Aidha, inazungumzia juu ya uwezo wa mtu yeyote aliyeruhusiwa na Mkurugenzi wa Misitu, baada ya kutoa notisi ya saa arobaini na nane, kuingia pewa uwezo wa kuingia katika ardhi yoyote isiyokuwa na nyumba ambayo matumizi yake ni kwa ajili ya makazi tu. Mtu huyo anatakiwa kuingia katika ardhi hiyo katika muda unaofaa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Sehemu hii pia inazungumzia juu taratibu ambazo mtu anayetaka kufanya utafiti katika masuala ya misitu au mazao ya misitu anatakiwa kuzifuata ikiwa ni pamoja na kuomba na kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Misitu.

Waziri wa Misitu anapewa uwezo wa kutunga kanuni na sheria ndogo kuhusiana na hifadhi ya msitu, mbao, au mazao ya misitu ili kuwezesha kutekelezwa vyema kwa matakwa ya sheria hii.

Page 39: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria
Page 40: cha Sheria ya Misitu No. 14 ya Mwaka 2002mamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/KITINI-CHA-SHERIA.pdf · juhudi na hatua za kimataifa katika kulinda na kukuza uhaianuwai. S heria

Chama Cha Wanasheria Watetezi Wa Mazingira (LEAT)

Mikocheni B, Barabara ya WariobaMtaa wa Mazingira, Kitalu namba 428S.L.P 12605, Dar es Salaa, Tanzania

Simu: +255 (22) 2780859, Faksi: 255 (22) 2780859

Barua pepe: [email protected], Tovuti: http://www.leat.or.tz

iSBn: 978-9987-648-36-8