chuo cha biblia - spiritual life ministries ho... · web viewhii ni kweli duniani kote, kitaifa,...

434
[Front Cover] MBWEHA TALLY HO! Msingi Kwa Ajili Ya Kujenga Wanafunzi Wa Yesu Wanaojiongeza Na Wenye Maono Ya Kuigusa Dunia Nzima Kimeandikwa Na Herb Hodges

Upload: others

Post on 21-Jan-2021

12 views

Category:

Documents


4 download

TRANSCRIPT

Page 1: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

[Front Cover]

MBWEHA TALLY HO!

Msingi Kwa Ajili Ya Kujenga Wanafunzi Wa Yesu

Wanaojiongeza Na Wenye Maono Ya Kuigusa Dunia Nzima

Kimeandikwa NaHerb Hodges

Kimefasiriwa NaMch. Simon Joel Vomo

Page 2: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

[Back Cover]

Herb Hodges aliyezaliwa na kukulia jimbo la Arkansas Marekani, aliokoka siku alipotimiza miaka kumi na nane, na akaitwa kuwa mhubiri muda mfupi baada ya hapo.

Ndugu Hodges alisoma katika Chuo Kikuu cha Biblia kiitwacho Southwestern Seminary huko Fort Worth Texas, na kuhitimu shahada ya Masters of Divinity mwaka wa 1962. Alichunga makanisa kwa miaka 27 katika majimbo ya Arkansas, Texas na Tennessee. Mwaka wa 1980, Ndugu huyu akawa mwinjilisti, mwenye kufanya mikutano ya uamsho, makongamano ya Biblia, makongamano ya Maisha ya Kiroho na Ufuasi. Huduma hii imemfanya atembelee karibu majimbo yote hamsini ya Marekani.

Amesafiri sana katika nchi za nje kwa ajili ya kufundisha wachungaji na viongozi kuhusu mkakati wa kujenga wanafunzi wa Yesu wanaojiongeza na wenye maono ya kuigusa dunia nzima katika kutimiza Agizo Kuu la Kristo. Amefanya safari kwa ajili ya kusudi hilo katika nchi za nje ni zaidi ya 70.

Ndugu Hodges na Judy mkewe wanakaa mjini Memphis, jimbo la Tennessee.

ii

Page 3: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ORODHA YA YALIYOMO

UTANGULIZI.......................................................................................................................IV

SHUKRANI.........................................................................................................................VII

SURA YA 1.............................................................................................................................1

MAONO NI MUHIMU KIASI GANI?......................................................................................1

SURA YA 2...........................................................................................................................34

AGIZO LENYE KUAMUA WAJIBU WETU...........................................................................34

SURA YA 3...........................................................................................................................85

WAZO LENYE KUAMUA NJIA TUTAKAYOTUMIA..............................................................85

SURA YA 4.........................................................................................................................104

UFUNGUO ULIOKO MLANGONI MWA HISTORIA YA KANISA.........................................104

SURA YA 5.........................................................................................................................133

VINAVYOTAKIWA ILI KUFANYA WANAFUNZI.................................................................133DAWA YA DAKTARI KUTIBU TATIZO LA KUACHA AGIZO KUU....................................133

SURA YA 6.........................................................................................................................158

MPANGO WA MUNGU WA KUONGEZA...........................................................................158

SURA YA 7.........................................................................................................................177

HEKIMA YA MKAKATI WA YESU...................................................................................177

SURA YA 8.........................................................................................................................197

JINSI KIWANGO HIKI KIFANYAVYO KAZI KANISANI......................................................197

SURA YA 9.........................................................................................................................219

MANENO YAKE YA MWISHO, WOSIA WAKE..................................................................219

SURA YA 10.......................................................................................................................241

MBWEHA TALLY HO!......................................................................................................241Maana Ya Jina La Kitabu..........................................................................................241

KUMALIZIA......................................................................................................................253

MAISHA YA MBWA WA MWITUNI..................................................................................253

MUHTASARI WA KILA SURA......................................................................................264

Maswali Na Mapendekezo Kwa Ajili Ya Kujifunza Hiki Kitabu........................................270

iii

Page 4: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Utangulizi

Kanisa la kawaida mahali popote lina kundi kubwa la

“watendaji” wasiotumiwa ndani ya washirika wake. Mkristo wa

kawaida hana kazi kulingana na viwango vya Kristo vya ajira, na

yule Mkristo wa kawaida ambaye ana ajira, mara nyingi “hana kazi

ya kutosha”. Basi anatumia muda mwingi na juhudi nyingi katika

shughuli zenye kutoa matokeo madogo sana kwa habari ya kuwafikia

na kuwajenga watu. Kanisa la kawaida la Kikristo hukutana Jumapili

kwa Jumapili katika “jengo” na washirika wake ni “wasikilizaji”

binafsi, ambao ni sehemu ya “wasikilizaji” wengine. Kwa kifupi ni

kwamba, kanisa la kawaida limejaa “walioketi” ambao kusudi lao

pekee ni kuja kanisani, kusikiliza mahubiri na kuondoka,

wakitazamia kwamba mpango huo utasaidia katika kufikisha roho

zao mbinguni kwa namna fulani na kuwawezesha kuwa na maisha

mazuri kabla ya kufika huko. Kufanana kwa maisha hayo na maisha

ya Kikristo yanayo-onekana katika Agano Jipya ni kwa bahati tu.

Ni dhahiri kwamba sisi Wakristo lazima tujifunze tena Agano

Jipya, ambalo ndicho kitabu chetu cha kuongoza utendaji, na

tujilazimishe kuona mambo kama yalivyo wakati tunapofanya hivyo.

Lazima tujitangaze kuwa huru kutokana na mapokeo na desturi, na

tugundue Agano Jipya linatuambia nini juu yetu sisi wenyewe, na

kazi ambayo tumepewa na Mungu.

iv

Page 5: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mwandishi maarufu aitwaye Charles Swindoll aliandika hivi:

“Hakuna kundi katika historia lililojithibitisha kuwa na uwezo katika

utendaji kama ile timu ya uinjilisti ya karne ya kwanza – wale watu

waliokuwa karibu sana na Kristo.” Huo ni ukweli usiokanika. Kwa

nini? Bila shaka kilichochangia sana ni utaratibu ule ambao Yesu

aliutumia katika kuwafundisha. Utaratibu huo umejengwa juu ya

neno kubwa sana – “mwanafunzi”. Neno hilo linaonekana kwa

nguvu sana katika vitabu vitano vya kwanza vya Agano Jipya,

likitokea mara 269 (katika Injili ya Mathayo hadi Kitabu cha

Matendo). Linatumika kama jina na tendo. Tena, linapotumika kama

tendo, neno lenyewe ndilo amri pekee katika Agizo Kuu ambalo

Yesu aliwapa wanafunzi Wake. Alisema hivi, “Wafanyeni watu

kuwa wanafunzi”. Sasa, kwa uhalisi wa makundi makubwa ya

waamini wasioendelezwa katika kanisa la leo (tena wengi wao wako

kanisani kila tunapokutana), ni halali kwetu kuendelea kusema

kwamba tumelifafanua vizuri neno ‘mwanafunzi’? Au kwamba sisi

tumeelewa ipasavyo maana (au utaratibu) ya “kuwafanya watu kuwa

wanafunzi”? Kwa uhalisi wa kanisa kutokuwa na mguso mkubwa

kwa ujumla, pamoja na mabilioni ya watu ambao hawafikiwi na Injili

duniani siku hizi, tunaweza kweli kuendelea kuamini kwamba

tunatimiza Agizo Kuu? Sidhani.

Kurasa hizi ni mtazamo mpya na juhudi mpya za kutafsiri

kwa kifupi sana kwamba sisi ni nani kama waamini wa Kristo, na

kazi yetu kama wafuasi Wake. Ni maombi yangu kwamba Mungu v

Page 6: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

atatusumbua na kutuamsha kupitia kurasa hizi kuwa na mtazamo

mpya, kutaka kujihusisha kwa upya, na kuwa na matokeo mapya

katika kutimiza Agizo Kuu la Bwana wetu.

Ninawiwa na marafiki wengi sana na waandishi wasio na

idadi – wa kawaida na wa kanisa – kwa ajili ya mawazo tele na

mbinu ambazo zimefupishwa na kuandikwa hapa. Pia, ninawiwa na

wengi ambao wamenitia moyo kuandika vitu hivi, na wachache

ambao wamenisaidia kufanya hivyo. Ushawishi wao ninauacha

mpaka tutakapofika kwenye Kiti cha Hukumu cha Kristo, ambapo

utatathminiwa kwa ubora sana na kupewa thawabu nzuri na bora

kuliko niwezayo kuitoa mimi.

Herb Hodges - Mwandishi

vi

Page 7: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Shukrani

Haiwezekani hata kuzaliwa kama mwanadamu bila kudaiwa

sana. Kila mwanadamu anapozaliwa anakuwa na deni la pango la

miezi tisa huko alikokuwa anakaa!

Kati ya wote wenye madeni, mimi ni mmoja mwenye

kudaiwa sana, japo si kifedha. Watu wengi sana – walio hai na

walikwisha pumzika – wamechangia faida nyingi sana maishani

mwangu – hata siwezi kutaja yote. Ukweli ni kwamba siwezi hata

kulipia riba ya kile walichowekeza kwangu.

Kwa habari ya kijitabu hiki, ninawiwa sana na makundi ya

waandishi walioandika mawazo yao na kuhakikisha kwamba

nimeyapata. Ninawiwa na wahubiri, waalimu na wenzangu ambao

wametia kweli nyingi katika akili zangu, katika kipindi chote cha

Ukristo wangu. Ninawiwa na watu kama Dom Fosco, ambaye kwa

uvumilivu na uangalifu sana alihariri na kupanga upya kurasa hizi

mara kadhaa; na Clint Davis, aliyeandika sura inayohusu Utangulizi

wa Injili ya Luka (akitumia maandishi niliyotoa pamoja na kanda).

Zaidi, ninawiwa sana kwa mke wangu mpenzi Judy, anayehudumia

vile vile kama msaidizi wangu na mwandishi wangu, kwa sababu ya

kunipenda na kuniunga mkono kwa hali yake tulivu, na kwa

kuongezea hekima yake kubwa katika yangu ndogo niliyo nayo.vii

Page 8: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Ninawathamini na kuwaheshimu na kuwashukuru hao na

wengine wengi. Wamenibariki sana! Narudia kusema tena –

wamenipa deni kubwa sana. Rafiki zangu, asanteni mno.

Herb Hodges

viii

Page 9: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 1Maono Ni Muhimu Kiasi Gani?

“Mahali ambapo hakuna maono, watu huangamia.” Mithali 29:18

Katika lugha ya kiroho, “mtazamo wa KiMungu”, “hekima”,

“uwezo wa kuona”, “kuangaziwa” na “maono” ni maneno

yanayofanana kwa kiasi fulani. Maandiko mengi katika Neno la

Mungu hudhihirisha umuhimu wa maono kama hayo. Tunasoma hivi

katika Zaburi 119:18, “Unifumbue macho yangu niyatazame

maajabu yatokayo katika Sheria Yako”. Na katika Zaburi 119:130

tunasoma hivi, “Kufafanusha maneno yako kuwatia nuru, na

kumfahamisha mjinga.” Katika Yakobo 1:5 tunaambiwa hivi,

“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa

Mungu”. Katika Waefeso 1:15-19 – pamoja na mantiki yake – Paulo

ameandika mojawapo ya sala zake kuu. Ninaamini kwamba hii ndiyo

sala muhimu zaidi ambayo mwanadamu anaweza kumwombea

mwenzake. Ni maombi ya “kuangaziwa”, kitu kimoja muhimu sana

kwa ajili ya kuelewa mambo ya Mungu baada ya Kuzaliwa Mara Ya

Pili. “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuona”. Mambo mawili

ya lazima kwa ajili ya ufahamu wa kiroho ni kuzaliwa upya na

kuangaziwa.

1

Page 10: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Andiko kiongozi katika somo hili linatuonyesha kwa hali ya

kinyume jinsi ambavyo “maono” ni muhimu. Kuona kwa mtu

hutegemea “vioo” anavyotumia kuonea, kama ambavyo kusikia

kwake kunavyotegemea “chujio” analotumia kusikiliza. Tunapoanza

mafunzo haya kuhusu Agizo Kuu la Bwana Yesu kwa watu Wake, ni

muhimu sana tuelewe thamani ya maono. Tunaambiwa na Mithali

29:18 kwamba, “Mahali ambapo hakuna maono, watu huangamia.”

Huu ni mstari kamili: unafanya kazi kila mahali kwa ukamilifu

kabisa.

WAZO LA KIROHO

Kwanza kabisa, fikiri kuhusu wazo la kiroho litolewalo hapa

– wazo la “maono”. Likitazamwa katika mantiki yake, ni dhahiri

kwamba maono yanayotajwa hapa ni ya aina pekee, maalum. Hapa

kinachosemwa ni maono ya kiroho, ambayo ni maono ya maana sana

mtu anayoweza kuwa nayo.

Kila kitu huanza kwa maono. Utakuwa kama unavyoona.

Usichokiona huwezi kuwa. Utakuwa unachotazama, lakini

usichokitazama, huwezi kuwa. Yaani, kile unachotazama kwa

upendo sana, kwa kutamani, na kwa muda mrefu, ndivyo

utakavyokuwa. Utakuwa kama kitu unachokitazama.

Hili jambo ni dhahiri katika dunia ya teknolojia ya vitu vya

umeme siku hizi. Ukiacha picha fulani kwenye kioo cha kompyuta

kwa muda mrefu sana, kitajiingiza mpaka katika mfumo mzima wa 2

Page 11: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kompyuta na kuingia katika kila eneo na programu yoyote

itakayotumika baada ya hapo. Kanuni hiyo ni halisi hata kwako: Kile

unachotazama kwa muda mrefu sana kitaamua maisha yako.

Mkayun mmoja kutoka jimbo la Louisiana alikuwa anamwuza

punda wake. Mtu mmoja aliyetaka kumnunua akamwuliza hivi: “Je,

punda mwenyewe ana matatizo yoyote?” Yule Mkayun akajibu,

“Haonekani vizuri” (japo kwa lugha yake alimaanisha haoni vizuri).

Mnunuzi akasema, “Sijali sana kwa hilo. Je, anafanya kazi sana?”

Akajibiwa, “Naam, ana bidii sana katika kazi, ila, haonekani vizuri

tu” (kumbuka maana yake). Basi yule mtu akamnunua, na mwenye

kumwuza akampandisha kwenye gari la huyo bwana mpya. Alipofika

shambani kwake, alifungua nyuma ya gari lake na kumshusha yule

punda. Mara, punda akagonga mti, halafu akajigonga kwenye zizi.

Mkulima akapiga kelele kwa hasira, “Nimedanganywa! Huyu punda

ni kipofu!” Akampakia punda kwenye gari, akamrudisha kwa

mwenyewe na alipomfikisha, alipiga kelele na kusema, “Wewe

ulinidanganya kuhusu huyu punda. Punda mwenyewe kipofu.

Uliniambia uongo!” Yule mwuza punda akasema, “Hapana,

sikukudanganya. Nilikwambia vizuri kabisa kwamba, ‘punda

haonekani vizuri’!” (Bila shaka unakumbuka maana yake kwa

kikwao.)

Ndugu Oswald Chambers ambaye ni mwandishi maarufu wa

kitabu kiitwacho My Utmost For His Highest na vitabu vingine vizuri

sana vya kujisomea kwa ajili ya kukua kiroho, aliandika kwa 3

Page 12: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

utambuzi mkubwa sana, kama ifuatavyo: “Ni rahisi zaidi kumtumikia

Mungu bila maono. Ni rahisi kumfanyia Mungu kazi bila ya mwito.

Kwa sababu, hapo husumbuliwi na yale Mungu anayotaka.

Unaongozwa na akili za kawaida, ila juu yake unatia hisia za

Kikristo. Lakini kama ukisikia agizo kamilifu la Yesu Kristo hata

mara moja tu, ufahamu wa kile Mungu anachotaka kitakuwa lengo

lako tangu wakati huo na kuendelea, nawe hutaweza kumtumikia kwa

msingi wa akili zako za kawaida.” Hebu soma maneno hayo mara

kadhaa kabla ya kuendelea mbele katika mafunzo haya. Nimetumia

wino mwepesi kutilia mkazo.

Kuona kimwili ni muunganiko wa vidokezo vyenye

kuonekana (yaani, kitu halisi katika dunia inayomzunguka mtu) na

ujuzi pekee (jinsi mtu anavyotambua hivyo vidokezo vinavyo-

onekana). Kidokezo chenye kuonekana kinaweza kisibadilike

kamwe, lakini kikiisha onekana na kunasa kwenye macho ya mtu,

kinaweza kupotoshwa, kukataliwa, au kupokelewa – yaani,

kinategemea tafsiri ya mtu aliyekiona

Katika zile hisia tano za asili, kuona ni hisia mojawapo

ambayo mtu hafai kupoteza. Ralph Sockman alikuwa sahihi

aliposema hivi, “Jicho ndiyo askofu wa hisia”. Claud Monet, mchora

picha maarufu wa Kifaransa alisema hivi, “Mimi ni mfungwa kamili

wa macho yangu”. Kwa sehemu kubwa, hiyo ni kweli kwa kila mtu.

Kuona (au kutambua) ndicho kiini cha kila kitu. Kanuni ifuatayo

itakuwa kweli: Kuona hupelekea kwenye Hatua (au Utaratibu), na 4

Page 13: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Hatua zitaongoza kwenye Matokeo. Ni dhahiri kwamba katika

kanisa la Yesu Kristo tuna matatizo sana kwa habari ya matokeo. Ni

kwamba hatutoi aina ya Wakristo waliosababisha Kitabu cha

Matendo! Basi, kama tunachotoa kina upungufu, ni kwamba kuona

kwetu kuna upungufu pia.

Maono ya kiroho ni kitu gani? Tafsiri moja ya Biblia kwa

lugha rahisi inafafanua Wakolosai 1:9 kwa njia itakayotusaidia.

Paulo aliandika hivi, “Ninaomba kwamba mwone mambo kwa

mtazamo wa Mungu.” Maono ya kiroho ni kuona mambo kwa

mtazamo wa Mungu. Lakini Biblia inatuambia wazi kwamba

mtazamo Wake hautakubaliana na wa kwetu (ktk Isaya 55:10). Basi,

ni muhimu kuwepo na urekebishwaji wa dhati kiroho ili tuweze

kufikisha mtazamo wetu kwenye hali ya kukubaliana na mtazamo wa

Mungu.

Ndugu Dawson Trotman, mtu mwenye maono makubwa

kiroho, alisema hivi, “Maono ni kupata moyoni mwako kile kilicho

moyoni mwa Mungu.” Lakini, Mungu ana nini moyoni Mwake?

Mstari wetu kiongozi unajibu swali hilo kwa neno moja tu: “watu”.

Moyoni mwa Mungu kuna watu. Watu wangapi? Watu wote.

Moyoni mwa Mungu yuko kila mtu aliyeko duniani. Naye

anatazamia watoto Wake kukubaliana Naye katika jambo hili

linalomgusa sana.

Anatazamia sana kwamba watoto Wake wataigusa dunia

nzima. Basi, utume wa dunia nzima unahitaji maono ya dunia nzima. 5

Page 14: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Hii inamaanisha kwamba Wakristo wengi wanahitaji kufikishwa

mahali ambapo wataanza kuona wajibu wao wa kuibeba dunia nzima

ili waweze kuanza kuigusa kwa ajili ya Kristo.

Hebu fikiri tena swali hili: Je, moyoni mwa Mungu kuna

nini? Je, kinachotakiwa kuwa kiini cha moyo wa kila aaminiye, na

katika ndoto zake na maono yake ni nini? Mstari wetu unatoa jibu:

watu. “Mahali ambapo hakuna maono, watu huangamia.” Basi, ni

kwa nini kiasi cha 4 kwa 5 ya watu wa duniani ndiyo wamepelekewa

Injili kwa udhaifu sana, na kufundishwa kwa udhaifu sana kuhusu

yaliyomo katika Injili na mkakati wake, huku nusu ya binadamu

hawajawahi kusikia jina la Yesu kwa kiwango cha kufikia

ukombozi? Je, Ukristo uliofunuliwa katika Kitabu cha Matendo

ungevumilia hali hii? Hapana kamwe! Basi, nini tofauti kati ya

Ukristo wa Kitabu cha Matendo na Ukristo wa siku za leo, ulioko

katika kanisa? Je, Yesu wa kanisa la leo ni tofauti na yule wa kanisa

la kwanza? Hapana. Je, Roho Mtakatifu ni tofauti. Hapana. Je, Biblia

ni tofauti? Ndiyo, lakini uzuri wa hili uko kwetu, si kwa Wakristo wa

kwanza. Wao hata hawakuwa na Agano Jipya lililokamilika. Sisi

tunalo, lakini pamoja na hilo, hatujafikia karibu na jinsi wao

walivyoweza kuigusa dunia yao.

Basi, nini tofauti kati ya Ukristo uliosababisha Kitabu cha

Matendo, na Ukristo wetu sisi? Pamoja na kwamba itaonekana kama

nimerahisisha sana, mawazo yangu ni kwamba tofauti ya msingi kati

ya “Ukristo wao” na “wetu” ni mkakati. Mkakati wao ulionyesha 6

Page 15: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kutokujali kwao kujenga taasisi na kukazia zaidi kuwajenga watu.

Mkakati wao ulikuwa wa kulipuka (kuelekea nje) badala ya

kubomokea ndani. Yesu alifundisha watu kumi na mbili, “ambao

aliwaita mitume” (ktk Luka 6:13). Kwa nini akawapa jina tofauti? Ni

kitu gani kikubwa, ni kitu gani anachokazia, na anataka tuone nini

wakati mtindo Wake mkuu (hata unaweza kusema, wa pekee) wa

kufundisha uliwalenga watu kumi na mbili, na kuacha neno la

kawaida la “mwanafunzi” na kuwapa jina tofauti na la kipekee sana

la “Mtume”? Nadhani siri iko katika maana ya neno lenyewe. Ni

neno la Kiyunani linalotokana na kuunganika kwa maneno mawili

madogo. “Stolos” maana yake ni “kutuma”. “Apo” maana yake ni

“mbali na.” Hapo ndipo penye siri. Aliwajenga hao watu maalum

waliochaguliwa ili “kuwa pamoja Naye” (ktk Marko 3:14) kwa muda

aliohitaji tu kuwafundisha na kuwaingizia uzima Wake, maono Yake,

na mkakati Wake. Baada ya hapo, mpango Wake ulikuwa kuwatuma

waende mbali na eneo lao la mafunzo kiasi ambacho wangeweza, au

ingewezekana, au wangetaka kwenda. Mwongozo Wake ulikuwa:

Kuingia ndani kwa muda, lakini Kutoka kikazi! Na ukweli kwamba

orodha ya Zawadi (Watu Wenye Karama) alizotoa kwa Kanisa Lake

inaanza kwa neno “mitume” (ktk Waefeso 4:11) unaonyesha

kwamba mtume alitolewa kwa kanisa ili kuwafanya washirika na

huduma ya kanisa kuelekea nje.

Imani yangu thabiti kabisa ni kwamba, Yesu Kristo

anamtazamia kila mtu aliyeokoka atawaliwe na maono ambayo 7

Page 16: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

daima yanafanya macho yake na miguu yake kutoka nje – kwenda

hadi miisho ya dunia. Ni kweli alitupa sisi utume wa dunia nzima,

lakini lazima nirudie tena kwamba utume wa dunia nzima unahitaji

maono ya dunia nzima. Pia ninaamini kwamba maono na shughuli

yenyewe vinapaswa kuwa kitu binafsi, wala siyo kitu kinachofanywa

kitaasisi. Mkristo wa kanisa la siku hizi “asiyefanya kitu”,

asiyejihusisha katika kazi ya kugusa dunia nzima, hafikiriki na

hawezi kuvumiliwa katika mpango wa Mungu. Ninaamini kwamba

Yesu anamtazamia kila mtu aliyeokoka awe na maono na mkakati

(ambao ulionyeshwa na Yeye Mwenyewe) wa kuigusa dunia nzima

hadi miisho ya dunia na mpaka ukamilifu wa dahari!

Kumbuka kwamba Mungu anao watu wote katika moyo

Wake, Naye anatazamia sisi pia tuwe hivyo. Henrietta Mears,

mwalimu maarufu sana Mkristo, alisema hivi: “Ninapoitazama

huduma yangu, nafikiria dunia nzima. Kingine chochote

hakitamsahili Kristo wala mapenzi Yake kwa ajili ya maisha yangu.”

Mkristo asiyekuwa na maono kama hayo ni kama chombo cha

kusafiria katika anga za juu kilichopoteza ratiba yake ya safari.

Mwendo kasi wake utakifanya kufika mahali, lakini lengo lake

linaweza kufutwa kama kitakataa kufanya kazi kulingana na ratiba

yake. Sisi kama Wakristo ratiba yetu siku zote ni ile yenye kulenga

Kugusa Dunia Nzima, na mkakati wake maalum umetamka katika

Agizo Kuu la Bwana wetu. Kitu chochote kinyume cha hicho

kimetokana na mwanadamu, na hakimtoshelezi Mungu. 8

Page 17: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Ni kitu muhimu sana kutambua kwamba, Roho Mtakatifu

aliposhuka siku ile ya Pentekoste katika uwezo mkamilifu wa

ukombozi, tokeo la kwanza linalotajwa la kuja Kwake ni kwamba

“vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto” (ktk

Matendo 2:17). Mara nyingi hili limegeuzwa na kuonekana ni kitu

cha kipekee na cha siri sana kiasi kwamba kimetengwa kwa ajili ya

watu waonaji wasiokaa na watu. Sivyo. Ukweli ni kwamba hii

inapaswa kuwa kawaida ya maisha kwa Wakristo wa kiroho.

Kulingana na mantiki, hayo maono na ndoto si yale yanayotokea

wakati watu wamelala, bali ni yale yanayopatikana na kujulikana na

moyo uliojaa Roho Mtakatifu. Kwa mantiki hiyo, ndoto hizi na

maono ni ndoto za mkakati pamoja na maono yatakayopelekea

kwenye kufanya kikamilifu kabisa Agizo Kuu la Bwana wetu. Ndoto

na maono ya mikakati aina hiyo vinatakiwa kuwa vitu vya kawaida

na vya kila siku katika maisha ya Wakristo wa Agano Jipya wa

kawaida, wala si mambo ya kiajabu na kushangaza yanatokea kwa

watu fulani wachache wenye aina fulani ya maisha.

[USHUHUDA WA MWANDISHI – Nilikuwa nafundisha

kwenye mkutano wa viongozi wa kanisa miaka kadhaa iliyopita.

Nikapewa kisa hiki kifuatacho na ndugu asiyekuwa mchungaji.

Alianza kwa kunionyesha jengo lenye ghorofa kumi na nne, kisha

akasema kitu alichokuwa ameambiwa kuhusu wakuu wa shirika la

hapo.

9

Page 18: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“Lile jengo ni makao ya shirika tajiri sana. Wakati fulani

huko nyuma, viongozi kadhaa wa ngazi ya juu katika shirika hilo

walimwendea kiongozi mkuu wakamwuliza, ‘Hivi huyo makamu

wako wa kwanza ana nini juu yako kiasi kwamba inabidi aendelee

kuwepo? Mbona unamlipa mshahara mkubwa kiasi hicho wakati

hazalishi chochote?’ Yule mkuu alipowauliza maana yao,

walimpeleka hadi ofisini kwa msaidizi wake huyo na kumwambia

achungulie dirishani. Makamu wake alikuwa ameegama kwenye kiti

chake kinachozunguka, na hakikuwa kinatazama mezani. Alikuwa

ameweka mikono nyuma ya kichwa chake, na miguu ameiweka

kwenye dirisha. Hakuwa anajigusa – pengine alikuwa kalala au

alikuwa anachungulia nje. Wakamwambia, ‘Unaona tunachosema?

Hiyo tu ndiyo kazi yake, lakini analipwa mshahara mzuri sana. Kwa

nini?’ Yule mkuu wa shirika akajibu kwa upole sana, hivi:

‘Nisikilizeni kwa makini sana. Mwaka jana, huyo jamaa aliyeketi

kwenye hicho kiti katika hiyo ofisi alipata wazo lililoletea shirika hili

zaidi ya Dola milioni 85 za Marekani… Mwaka huu, ana kazi moja

tu ….’!” MWISHO WA USHUHUDA]

Wapendwa waamini wenzangu, yuko wapi mtu katika kanisa

la leo anayefikiri kuhusu wazo la Mungu la Dola milioni 85? Yuko

wapi mtu anayeona maono ya Mungu ya Dola milioni 85, au

mwenye kuota ndoto ya mkakati wa Mungu wa Dola milioni 85?

Mungu Muumbaji wa Biblia hakosi mawazo makubwa ya kiumbaji,

lakini, wako wapi watakatifu Wake wa kawaida kabisa ambao 10

Page 19: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wanaona mkakati kwa mtazamo Wake, na kupata moyoni mwao yale

ambayo Mungu anayo moyoni Mwake kimkakati?

Hebu nitaje kanuni nyingine inayohusu maono.

Hakuna maono = kushindwa kabisa;

Maono yenye mpaka = mafanikio kidogo;

Maono – mpango – matendo = ni ndoto tu;

Maono + mpango – matendo = ndoto yenye kutisha (kusikia hatia);

ila

Maono + mpango + matendo = huduma ya kiroho yenye matokeo.

Ona kwamba kipimo cha maono ya mtu ni matendo

yanayosababishwa na maono hayo. Pasipo matendo, wewe na vipawa

ulivyo navyo mnabakia kwenye kiwango cha “kuwa na uwezo wa

kufanya kitu”. Hali hiyo ni uwezo uliolala ambao haufanyiwi kazi

kamwe kupitia maono.

Myles Munroe ambaye ni kiongozi Mkristo alisema hivi

kuhusu uwezo wa mwamini kufanya kitu katika kitabu chake

kiitwacho Understanding Your Potential: “Mahali penye utajiri sana

hapa duniani si katika maeneo ya mafuta huko Kuwaiti, Iraki au

Saudi Arabia. Wala si katika machimbo ya dhahabu na almasi huko

Afrika Kusini, au machimbo ya uranium huko Urusi au katika

machimbo ya shaba yaliyoko Bara Afrika. Utashangaa tu lakini,

utajiri mkubwa sana katika dunia yetu uko mita chache tu kutoka

nyumbani kwako. Uko katika makaburi yenu. Huko chini,

kumezikwa ndoto ambazo hazikuwahi kutimizwa, nyimbo ambazo 11

Page 20: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

hazikuwahi kuimbwa, vitabu ambavyo havikuandikwa, picha ambazo

hazikuchorwa, mawazo ambayo hayakutolewa, maono ambayo

hayakufanyika uhalisi, vitu vilivyobuniwa ambavyo

havikutengenezwa, mipango ambayo haikutoka kwenye mawazo ya

mtu na makusudi ambayo hayakutimizwa. Makaburi yetu yamejaa

uwezo wa kufanya vitu ambao haukufanikiwa.

“Uwezo wa kufanya vitu unadai kwamba usikubali kutosheka

na kitu ulichofanikisha. Adui mmoja ambaye ni mkubwa sana wa

uwezo wako kufanya vitu ni mafanikio. Mafanikio kidogo huharibu

uwezekano mkubwa! Ili uweze kufikia uwezo wako kamili wa

kufanya vitu, hutakiwi kutosheka na ulichofanikisha. Pia ni muhimu

kwamba usiruhusu kile usichoweza kufanya kiingiliane na kile

unachoweza kufanya. Janga kuu maishani si kifo, bali ni maisha

ambayo hayakufikia kilele chake katika uwezo wa kufanya vitu.

“Katika kurahisisha dhana hii, hebu tutazame kitu kimoja

katika uumbaji ambacho kina nguvu sana … mbegu. Nikishika

mbegu mkononi na kuukuliza, ‘Nina nini mkononi?’ utasemaje?

Pengine utajibu kilicho wazi kabisa … ni mbegu. Lakini, ukielewa

asili ya mbegu, jibu lako linaweza kuwa uhalisi japo halitakuwa

ukweli. Ukweli ni kwamba nimeshika msitu mkononi mwangu. Ni

hivi: Katika kila mbegu kuna mti, na katika kila mti kuna matunda au

maua yenye mbegu ndani yake. Na hizo mbegu nazo zina miti

ambayo ina matunda yenye mbegu ndani yake … ambazo zina miti

yenye matunda yenye mbegu, na kadhalika na kuendelea. 12

Page 21: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Unachokiona hapa si yote. Kwa hiyo, tofauti kati ya mbegu moja na

utoaji wa chakula kama vile ngano inayoweza kulisha dunia nzima ni

kitu kinachoitwa ‘uwezo wa kufanya vitu.’ Hicho ndicho kiwango

cha tofauti kati ya unachoona na kinachowezekana.

“Kama Musa angekufa kabla hajaona kile kichaka

kilichokuwa kinawaka moto … au Paulo kabla ya kukutana na Yesu

akiwa njiani kwenda Dameski … au Ibrahimu kabla ya Isaka

kuzaliwa. Maandiko na historia vingekuwa tofauti sana. Kama

Martin Luther angekufa bila ya kuandika yale matangazo yake … au

Charles Wesley bila ya kutunga nyimbo zake … au John Wycliff bila

kufasiri Biblia katika lugha ya Kiingereza. Historia ya Kanisa

ingekuwa tofauti sana.

“Sijui ingekuwaje kama baba yako angekufa kabla

hujatungwa mimba, au mama yako kabla hujazaliwa. Dunia

ingepoteza nini kama usingezaliwa? Je, dunia itakosa nini kwa

sababu unashindwa kuishi kufikia kiwango cha uwezo wako wote?

Je, utakwenda kaburini na nyimbo, vitabu, magunduzi au dawa?”

Mimi nimetumia wino mwepesi hapa kuweka msisitizo maneno ya

mwandishi.

Je, inawezekana kwamba dhambi kuu ya Wakristo imo katika

uwezo wao wa kufanya mambo ambao haujafikiwa? Tena, uwezo

mkuu wa kufanya mambo ambao haujatumiwa katika siku za leo ni

katika eneo la kutimizwa Agizo Kuu la Bwana wetu. Yeye amekupa

wewe nafasi maalum katika Kuufikia Ulimwengu Kikamilifu, na ni 13

Page 22: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

nafasi kubwa kuliko yoyote uliyowahi kuwa nayo. Hii nafasi

haiwezekani bila ya maono kwamba inawezekana. Basi, kitu

muhimu kuliko vyote katika maisha yako ni kuwa na maono

yanayokubaliana na Mungu, na kuyafuatilia. Kwa kuwa kazi

uliyopewa inahusu dunia nzima, maono yako lazima yawe hivyo

hivyo. Je, una maono ya aina hiyo?

Sasa – watu kama wewe na mimi – wenye ubinafsi, kujijali,

wenye kujali kwao na wenye kujiona wanapataje maono ya Mungu?

Angalia kanuni hii, inayoweza kufanya kazi: habari sahihi

ukijumlisha na kuangaziwa kiroho vitaleta maono, ambayo

yatasababisha motisha, na hiyo motisha itapelekea utendaji wa

kiroho wenye matokeo. Hapo, ona kwamba maono huanza kwa

kupata habari sahihi. Sawa na ambavyo kuona kimwili kunavyoanza

kwa kuwepo kwa kivutio cha nje, ndivyo na maono kiroho

yanavyoanza kwa ukweli wa Mungu katika Maandiko na kila kitu

ambacho kinahusiana na Maandiko. “Matofali” ya kujengea maono

hayo ni: kufahamu Maandiko kiasi cha kutosha na moyo sikivu wa

kusikia Maandiko na kuyatii, halafu ufahamu wa jiografia ya dunia

na tamaduni za nchi mbalimbali, utambuzi kiroho wa matukio,

maombi, kujisomea ili kupata habari, ujuzi binafsi (“njoo uone”

katika Maandiko) wa baadhi ya maeneo ya kimisheni duniani,

ushirikiano na waamini wenye maono, kujitoa kwa ajili ya kutoa

kuhusu mambo ya umisheni, kukutana na wamishenari na Wakristo

wenye kugusa dunia, na maamuzi mbalimbali katika maisha. 14

Page 23: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Unaweza kuanza kushirikiana na Mungu katika kujenga maono ya

kiroho katika maisha yako leo. Lakini, ni dhahiri – na inasikitisha

sana – kwamba Wakristo wengi unaoshirikiana nao mara kwa mara

hawana maono kama hayo.

HALI YA KUSIKITISHA

Pili – fikiri kuhusu hali ya kusikitisha ambayo inatajwa hapa,

kwamba, “Mahali pasipo na maono.” Neno “mahali” linaweza pia

kutamkwa hivi: “popote”. Basi, haya ni maneno yanayohusu kila

mahali. Kwa lugha ya KiBiblia, nini maana ya “pasipo maono”?

Maana yake ni kwamba Mungu hatambuliwi, wala mpango Wake

mkamilifu. Maana yake ni kwamba Shetani, “mungu wa dunia hii”

ame”pofusha mawazo ya watu” wasione mambo ambayo ni ya

muhimu na yenye maana! Hawawezi kuona wala kuyaelewa mambo

haya bila ya kuzaliwa upya pamoja na kuangaziwa (ona 1Wakor.

2:9-14). Basi, hakuna mawasiliano ya kudumu baina ya mbingu na

mioyo ya watu. Hakuna biashara na kile kisichoonekana, cha milele,

cha kiroho, na ambacho ni halisi. Hakuna kumsikiliza Mungu na

kumtazama Yeye. Kwa kifupi ni kwamba, “pasipo maono” maana

yake ni kwamba watu hawamwoni “Aliye Juu na Mtakatifu, mwenye

kutamalaki Milele.” Basi, tunakuwa na mipaka na kuona maeneo

yetu madogo pamoja na upeo wetu, na mipango yetu midogo, ya

kibinafsi, ya kidhambi tu. Mtu mwenye mipaka kiasi hicho, na

mwenye mipango yenye mipaka kiasi hicho hatimaye anabomokea 15

Page 24: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ndani yake mwenyewe. Ni hivi: Kila kitu huanza kwa maono ya

kweli. Ona lile neno “kweli”. Ninalitumia kama kinyume cha

kutokuwa na maono, maono bandia na maono yenye mipaka.

Lazima tukubali – kwa huzuni sana – kwamba, watu wengi

walio-okoka wana ubinafsi, wanajipenda wenyewe na wametawaliwa

na hali ya kujilinda kwa kiwango sawa na watu waliopotea tu. Yaani,

wengi katika watu walio-okoka ni wenye dhambi (tafsiri “dhambi”

kuwa ni ubinafsi) kama waliopotea tu. Kwa nini? Hapo tena, andiko

letu la msingi linatoa jibu: Hakuna maono. Si mara nyingi tunaona

mambo “kwa mtazamo wa Mungu”. Si mara nyingi mioyo yetu

inakuwa na kile ambacho Mungu anacho moyoni Mwake – dunia

nzima ya watu mmoja mmoja waliopotea.

Mtazamo ni muhimu sana. Kuona kwa mtu hutegemeana na

aina ya vioo anavyotazamia, sawa na jinsi kusikia kwa mtu

kunavyotegemeana na chujio analotumia kusikilizia. Hebu tutoe

mfano wa kusaidia kueleweka kweli hiyo.

Mwaka wa 1877, mtaalamu wa nyota Mmarekani aliyeitwa

Percival Lowell aliushangaza ulimwengu wa sayansi kwa kutoa wazo

kwamba, kutokana na ushahidi aliokuwa amekusanya, kulikuwepo na

dalili za uhai na viumbe wenye akili katika sayari ya Mars. Nadharia

yake – kwa sehemu – ilitokana na yeye kuona vitu alivyoita

“mifereji” kwenye sayari hiyo. Wanasayansi wakabebwa na tamko

hilo kwa kishindo. Lakini, walikuwepo watu wachache ambao tangu

mwanzo walikuwa wamefahamu kwamba hiyo sayari haina mifereji. 16

Page 25: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Baadaye, Bwana Lowell alipata tatizo kubwa kiafya, lililoanza

kujitokeza. Jopo la matabibu walimpima na kugundua tatizo lenyewe.

Ugonjwa wake haukuwa umejulikana sana siku zile, basi wakauita

jina lake – “Lowell’s Syndrome”. Ishara mojawapo ilikuwa kwamba,

alipoketi muda mrefu akichunguza kitu fulani, sura na ukubwa wa

mishipa ya kupitisha damu katika macho yake ilikuwa inaonekana

kwenye hicho kitu alichokuwa anakichunguza. Basi, badala ya kuona

“mifereji” kwenye sayari ya Mars kwa njia ya darubini, alichokuwa

anakiona ni mishipa yake mwenyewe ya damu. “Alibeba” kile

alichodhani anakiona, katika kichwa chake mwenyewe. Mtazamo!

Ufuatao ni mfano mwingine tena.

Dakta Harold Lindsell, mhariri mstaafu wa jarida liitwalo

Christianity Today, alihudhuria kliniki ya macho ya Kijapani zamani

kidogo. Akiwa darasani siku moja, mkufunzi aliinua chati kwa

ghafula mbele ya darasa. Akauliza hivi: “Ni wangapi mnao-ona

namba nane?” Lindsell peke yake ndiye aliinua mkono wakati huo.

Alisema baadaye kwamba alidhani ni njama – kwamba darasa lote

lilikuwa limekusudia kumcheza shere. Lakini, mkufunzi akauliza, “Ni

wangapi mnaoweza kuona namba kumi na nne?” Kila mtu darasani

aliinua mkono! Ndipo mwalimu akazungumza na Ndugu Lindsell na

kumwambia, “Mheshimiwa! Kuna mtu ambaye amewahi kukwambia

kwamba wewe una matatizo ya kuona rangi?” Ni kwamba hapakuwa

na hila yoyote. Kila mtu siku hiyo katika lile darasa alikuwa

anasema ukweli – kulingana na alivyouona. Mtu mmoja kweli aliona 17

Page 26: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mamba nane huku wengine wote wakiona namba kumi na nne.

Mtazamo huo!

Ni hivi: Mtazamo hufunika kila kitu ambacho hakihusiki, na

kusababisha maono yatawaliwe na kile ambacho kinahusika. Kwa

hiyo ni muhimu sana.

Mwanamke mmoja alisogea karibu na Dakta G. Campbell

Morgan, mwalimu maarufu wa Biblia wa zamani. Akamwuliza huvi:

“Hivi Dakta Morgan, unaamini kweli kwamba Mungu anajali

mambo madogo madogo ya maishani mwetu?” Dakta Morgan

akamjibu kwa upole sana, hivi: “Mama. Hivi kweli unaamini

kwamba katika maisha yako kuna kitu kikubwa sana kwa Mungu?”

Mtazamo huo.

Hayo ndiyo yanayofanywa na mtazamo. Yanaondolea mbali

habari fulani au mambo fulani kuwa si ya maana, na kukuza mengine

kuwa muhimu mpaka kufikia kiwango cha “kweli”. Lakini, mtazamo

unaweza kutokana na mtazamaji mwenyewe kiasi cha kutokuwa

halisi katika hali ya kawaida kabisa. Yaani, hata unaweza usitoe

nafasi ya kitu halisi kabisa kilichopo kuonekana. Acha nikupe mfano

wa KiBiblia kuhusu mtazamo.

Sura ya kumi na tatu ya kitabu cha Hesabu ni taarifa ya

hadithi ya taifa la Israeli wakiwa Kadeshi Barnea, kusini kidogo tu

ya nchi ambayo Mungu alikuwa amewaahidi. Bila shaka walikuwa

tayari kuingia katika Nchi yenyewe. Lakini, walipatwa na hali ya

kutokuamini, wakatuma kikundi cha wapelelezi kumi na mbili 18

Page 27: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kwenda kutazama udhaifu wa nchi ile. Wapelelezi wake wakarudi na

taarifa iliyogawanyika. Wote walikubaliana kwamba nchi ilikuwa

inakaliwa na watu ambao hawakuwa na wazo la kuiachia. Halafu,

wapelelezi kumi – idadi kubwa kabisa – wakapendekeza kwamba

wasiiteke nchi kwa msingi kwamba wakazi waliokuwemo nchini

“wana nguvu kuliko sisi,” na kwamba wana wa Israeli walionekana

kama mapanzi, wakilinganishwa na majitu. Wapelelezi wawili

walitosha ushauri “wa wachache”. Wakikiri ukweli ule ule, wao

waliendelea na kusema hivi: “Hebu na tupande mara moja na

kuitwaa nchi, kwa sababu tuna uwezo kabisa wa kuiteka” (ktk

Hesabu 13:30). Ni hivi: Wale wachache walimwingiza Mungu katika

uamuzi wao, kitu ambacho wale wengi hawakukifanya. Basi,

mitazamo miwili ikaamua mashauri yale mawili yaliyotolewa:

mtazamo mmoja ulimhusisha Mungu, ule wa pili haukufanya hivyo.

Wote waliona “majitu”; wengi wao walijiona kuwa “mapanzi”.

Wawili tu ndiyo walimwona Mungu. Au basi: wengi walimwona

Mungu kupitia hao majitu, na hao wakaonekana kuwa wakubwa

kuliko Mungu. Wale wachache waliwaona majitu kupitia Mungu,

na Mungu akawa mkubwa kuliko majibu. Basi, mtazamo wao

uliamua mapendekezo yao na utendaji wao. Hapo ndipo penye

tofauti kati ya “maono” na “pasipo maono”!

Akili ya kibinadamu siku zote itakupa mtazamo wako

kulingana na maoni yako. Muujiza tu wa kuangaziwa ndiyo

utakaokupa mtazamo wa Mungu. Hapo ndipo kuna tofauti kati ya 19

Page 28: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“pasipo maono” ambayo hatima yake ni “watu huangamia”, na

“maono” ambayo kwa hiyo watu hustawi na kufanikiwa.

Jaribu kufikiri kutokuwepo na maono ya kiroho katika

madhabahu ya kanisani unapoabudu. Huna haja ya kufikiri sana

kama utatembelea makanisa mengi! 1Samweli 3:1 inasema, “Neno la

Mungu lilikuwa adimu katika siku hizo. Hayakuwepo maono ya wazi

(au, ya mara kwa mara).” Ukisoma historia ya taifa iliyotokana na

wakati huo utagundua kwamba mambo ya kusikitisha sana yalitokea

kwa sababu ya kutokuwepo na maono.

Ingekuwaje kama isingekuwepo Injili inayohubiriwa kutoka

madhabahu ya kanisa unalohudhuria? Kutokuwepo kwa kutambua

kwamba mtu amepotea pasipo Kristo? Kutokuwepo na kuamini

nguvu zenye kubadili maisha za Roho Mtakatifu? Kutokuwepo kwa

mafafanuzi ya ndani sana na wa milele wa mausia ya Mungu?

Kutokuwepo kwa mafunuo ya hazina nyingi sana zisizomalizika

zilizomo katika Neno la Mungu? Kutokuwawezesha wasikilizaji

“waishi mbinguni na duniani kwa wakati mmoja”? Kutofundishwa

kwa upana wa maisha ya Kikristo yaliyojaa Roho, yanayofuata

Neno, yaliyo na mwelekeo wa maombi, na yenye kujenga

wanafunzi? Jaribu kufikiri madhabahu “pasipo maono”.

Mchungaji: Una mashaka kiasi gani kuhusu uwezo wa kile

unachofanya sasa? Mashaka mazuri ndiyo nyundo yenye kuvunja

madirisha yaliyofunikwa na kiwingu cha mambo yanayowavutia

wanadamu. Mashaka aina hiyo ni ishara yenye kuleta matumaini. 20

Page 29: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Bila ya ukiri wa kweli kuhusu mashaka kama hayo, na uchunguzi

kwa njia ya maombi kuhusu njia mbadala itolewayo na Mungu,

madhabahu unayosimama ndani yake itadumu kutokuwa na maono.

Miaka kadhaa iliyopita, mchungaji maarufu wa Kibaptisti

alikuwa kwenye maombi ofisini mwake asubuhi moja. Alikuwa

amelala kifudifudi akimwomba Mungu upako wa nguvu za Roho

Mtakatifu juu ya huduma yake. Alimsihi Mungu tena na tena, “Ee

Bwana! Nipe nguvu Zako. Usiache nihubiri na kufanya huduma

pasipo nguvu Zako.” Kila mhubiri wa maana amewahi kuomba sala

hii kwa uzito sana na mzigo. Anasema, mara ikaonekana kama paa

juu yake limefunguka na mkono ukamshukia na kumgusa kwenye

bega. Ikawa ni kama sauti ya Mungu imezungumza ndani yake, hivi:

“Mwanangu, acha kuomba!” Alipotulia, Sauti ni kama ilimwambia

hivi, “Mwanangu! Kwa mipango yako isivyokuwa mikubwa, huhitaji

nguvu Zangu!”

Ewe Mkristo – maono yako ni makubwa kama ya Mungu,

kwa ajili ya utukufu Wake? Iko wapi mipango, ndoto, maono,

mikakati kwa ajili ya kuifikia dunia nzima – vitu ambavyo kwa kweli

vinasukuma rasilmali ya miujiza ya Mungu? Uko wapi mkakati

unaotaka miujiza endelevu ili kuudumisha? Yako wapi maono

ambayo ni makubwa kiasi kwamba rasilmali za kibinadamu (za aina

yoyote na kiwango chochote) hazina uwezo wa kuyategemeza?

Maono pekee yenye ukubwa wa umilele ambayo yeyote kati yetu

anaweza kuyahitaji yanapatikana katika lile Agizo Kuu ambalo 21

Page 30: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

tumepewa na Bwana Yesu Kristo. Kama madhabahu yako

haisumbuliwi na maneno “kuwafanya kuwa wanafunzi” na “mataifa

yote”, Mungu anawezaje kutazamiwa kuunga mkono kutoka

mbinguni? Bila kutatizwa na hilo, madhabahu ya kanisa lako ina

ubao unaosema hivi: “hakuna maono”.

Halafu, ni hatua ndogo tu kufikia kwenye viti, watu ambao

hawana maono ya kiroho ya hayo. Sheria ya maisha ya ndani ya

kanisa ni hii: “watu wako kama mchungaji alivyo”. Watu watapokea

jinsi mchungaji wao alivyo kiroho. Hebu tuseme katika mfuatano

huu, watu waketio kanisani hawana, au wamepoteza maono yao

kuhusu utukufu wa kushangaza sana wa Injili. Inakuwaje? Na

wamepoteza uzuri wa pekee wa Yesu Kristo. Inakuwaje? Na

wamepoteza maono ya ukuu na utukufu wa kazi yetu ya dunia nzima.

Inakuwaje? Na wamepoteza maono ya uwezekano wa kuigusa dunia

nzima kwa ujumbe wa Injili na uwezo wa Yesu Kristo kama

Wakristo wa kwanza walivyofanya. Inakuwaje? Mtu mmoja

amesema, na ni kweli kabisa, “Hatua kutoka aliye tayari kujitoa hadi

mtunzaji na hatimaye mzikaji ni fupi sana.”

Kwa nini washirika wa makanisa wanasisimka zaidi kuhusu

vitu vingine elfu na zaidi, kuliko kuhusu Mungu, mambo ya kiroho,

mbinguni, jehanamu, na umilele? Jibu lake: Hakuna maono, kwa

hiyo hakuna motisha. Maana, motisha hutokana na maono.

Kujifunza Injili na Kitabu cha Matendo kwa makini sana

kutadhihirisha kwamba Kanisa la kawaida la Kikristo linaendeshwa 22

Page 31: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kwa misingi ya desturi na taratibu kuliko kwa misingi ya kuangaziwa

[na Roho Mtakatifu]. Mtu mmoja – kwa mzaha tu – alisema hivi: “Ni

vizuri makanisa yafanye na kusema kila kitu kwa usahihi mara ya

kwanza, kwa sababu yatafanya na kusema kwa njia hiyo hiyo tangu

sasa na kuendelea.”

Maono yanapotoweka katika madhabahu na kwa washirika,

tuwe na uhakika kabisa kwamba hayatakuwepo maono ya kiroho

katika maisha ya kila siku. Itakuwaje ikiwa Wakristo watapoteza

kabisa maono ya nafasi yao kama chumvi na nuru (ktk Mathayo

5:14-16) katika dunia inayoharibika na yenye giza? Itakuwaje kama

sisi tutapoteza maono juu yetu kwamba ni wawakilishi wa Yesu

Kristo (ktk 2Wakor. 5:20), “katikati ya kizazi kiovu kilichopotoka,

ambacho kati yake tunang’aa kama taa duniani, tukilishika na

kulitangaza Neno la Uzima” (ktk Wafilipi 2:14-16)? Itakuwaje ikiwa

tutapoteza maono yetu juu ya daraja yetu kuu kama “mabalozi kwa

ajili ya Kristo”, tulioagizwa kusemea jambo la Mfalme wetu katika

dunia hii yenye giza na uhasama? Mbona si kitu cha kufikiri na

kukisia kabisa. Kutokuwepo na maono ni kitu kinacho-onekana

waziwazi katika madhabahu, kwa washirika, na katika maisha ya kila

siku – ukitazama tu mambo yanayotokea, kama yanavyotajwa katika

maandiko haya.

23

Page 32: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

MATOKEO YAKE, MAZITO

Hebu fikiri juu ya matokeo mazito yanayofuata hali ile ya

kusikitisha sana ya “pasipo maono”. Mahali ambapo hakuna maono,

watu huangamia.” Neno linalotafsiriwa “kuangamia” ni la Kiebrania,

lenye kushangaza sana. Yaani – limejaa maneno, na linatisha. Lina

maana kadhaa tofauti. Maana yake ni “kutokuwa na kujizuia,

kujiachilia, kuyeyuka, kuvunjika, kusambaratika vipande-vipande,

kutembea uchi, kuangamia.” Sasa, tazama matokeo ya kusikitisha

sana ya kupotea kwa maono miongoni mwa Wakristo.

Kwanza – maono yanapokuwa hayapo, watu wa jamii, wa

jumuiya, wa kanisa, wa nyumbani “huacha kujizuia”. Hayo ni

matokeo ya kiadili ya maono kupotea. Kupoteza maono husababisha

vurugu kiadili, ambapo “kila mtu hufanya kilicho sawa machoni pake

mwenyewe”. Ona kwamba, kunapokuwa hakuna utambuzi wa uhalisi

kamili, watu hufanya “yaliyo sawa machoni pao wenyewe”, wala si

kile ambacho kinaonekana kuwa makosa kwao. Kumbuka pia

kwamba “sawa” na “kosa” siku zote ni maneno tu kwa wale wenye

akili za kawaida au za kimwili. “Sawa” na “kosa” ni vitu halisi kwa

wale tu ambao wana akili timamu kiroho. “Iko njia ionekanayo kuwa

sawa kwa mtu, lakini mwisho wake ni mauti” (ktk Mithali 14:12).

Ona kwamba huyo mtu ana uhakika kwamba njia yake ni sawa –

kamwe haoti kwamba njia yake ni ya KiShetani na yenye uharibifu.

Hapo tena, tofauti ni katika ufunuo, katika maono na mtazamo wa

mtu binafsi. Inashangaza sana kuona jinsi ambavyo watu walio 24

Page 33: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

vipofu kwa mambo ya kiroho wanavyohalalisha ukweli wa kuelewa

kwao!

Kwamba watu kila mahali siku hizi wameacha kujizuia ni

kitu kinachokubaliwa na kila mmoja. Kujitawala, fujo na vurugu na

kujiamulia mambo mwenyewe ni mambo yanayozidi kuenea. Tofauti

kati ya Mwana wa Mungu na wenye dhambi inadhihirishwa hapo.

Yesu alisema hivi: “Siku zote mimi hufanya mambo ambayo

yanampendeza Baba Yangu” (ktk Yohana 8:29). Lakini, kauli mbiu

ya wenye dhambi (au kiini cha dhambi) ni: “Siku zote mimi hufanya

mambo yanayonipendeza”. Pengine atatokea msanii wa siku zijazo

atakayetengeneza sanamu au kuchora picha itakayomwonyesha mtu

wa karne ya ishirini akiwa amejikumbatia mwenyewe kwa upendo

sana, akijipiga busu mwenyewe katika kioo. Lakini, bila ya kupoteza

uzito wa hali halisi katika maneno ya utani, hebu maneno ya Shetani

aliyopewa na John Milton katika kitabu kinachoitwa Paradise Lost

yaturekebishe. Shetani alionyesha ukiri usioepukika wa wenye

dhambi wenye kufuata ubinafsi wao bila ya mipaka aliposema hivi:

“Mimi mwenyewe ndiye jehanamu”.

Miaka kadhaa iliyopita, magazeti yaliandika kisa cha

msaidizi wa fundi uchundo wa Uwanja wa Ndege wa Idlewild huko

New York, Marekani. Huyu alikuwa na miaka ishirini, naye

alimwandikia rafiki yake mmoja barua, aliyekuwa katika Jeshi la

Anga la Marekani katika jimbo la Texas. Barua ilieleza jinsi

ambavyo kijana huyo alikuwa ameachana na mchumba wake, na 25

Page 34: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

jinsi alivyopanga kuchukua ndege mojawapo ya shirika la Pan

American. Akaiba ndege aina ya DC-3 yenye injini mbili, akaanza

kuiendesha. Ikashindwa kupaa, ikaanguka, naye akafa. Habari

gazetini zilimalizika kwa maneno yake kutoka kwenye ile barua,

kwamba, “Nitakuwa nikiendesha mimi mwenyewe, kama ambavyo

nimekuwa siku zote – peke yangu.” Kisa hiki hurudiwa tena na tena,

katika mavazi tofauti, kila siku – na matokeo ni yale yale.

Kujisimamia mwenyewe ni kujiharibu mwenyewe. Mtu

anayejisimamia mwenyewe siku zote ataanguka na kuungua! Kwa

kuwa mawazo ya wanadamu hupingana sana wakati kila mmoja

anapochukuwa sheria yake mwenyewe, machafuko duniani

yanaendelea kukua na kuongezeka, na hali ya wasiwasi itokanayo

nayo. Mahali ambapo hakuna maono ya mara kwa mara miongoni

mwa watu, ambapo hakuna neno lililo wazi kutoka kwa Mungu aliye

hai, ambapo hakuna Ukristo halisi wenye maana, basi watu hutupilia

mbali vizuizi.

Pili – neno hili lenye nguvu sana la Kiebrania pia

linamaanisha “kusambaratika”. “Mahali ambapo hakuna maono,

watu husambaratika”. Hayo ni matokeo ya kijamii ya kupoteza

maono. Dhambi, inayozidi kuongezeka katika jamii yenye utovu wa

maono ya kiroho, ina nguvu ya mvutano fulani. Inawafukuza watu

watoke kwenye Kiini cha Kweli cha Uzima ambacho ni Mungu

Mwenyewe, na kwa njia hiyo kuwatenganisha wao kwa wao. Basi,

tunakuwa na dunia iliyotengana, iliyogawanyikana. Jamii huanza 26

Page 35: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“kulegea, kuyeyuka, kuvunjika, kuwa vipande-vipande”. Neno

“kugawanyika” linaelezea hali nyingi tofauti zilizomo katika dunia

yetu. Tunazo familia zilizogawanyika, mataifa yaliyogawanyika,

dunia iliyogawanyika, na watu wenye haiba zilizogawanyika. Siku

moja, daktari wa magonjwa ya akili aliingia kwenye kituo cha

mafuta akiwa na gari aina ya pikap. Nyuma alikuwa amebeba viti

vitatu. Alipoulizwa anakwenda wapi, alijibu, “Ninakwenda

kumtembelea mwenda wazimu (ambaye tatizo lake ni kuona kwamba

yeye si mmoja, bali wengi)!” Mara nyingi sana watu binafsi

wana”sambaratika”. Binti mmoja msomi wa chuo kikuu fulani

alimwambia mwenzake wanayekaa chumba kimoja, “Ninajisikia

kama Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe, inayotembea”. Mwenzake

akamjibu, “Wala hiyo si kitu. Mimi ni Vita Kuu ya Dunia,

inayotembea!” Mtu binafsi anaweza kuvumilia tatizo la aina yoyote

ile kama ameunganika ndani, lakini atashindwa na shambulio la aina

yoyote ile kama ndani yake mwenyewe kuna ubishi na hali ya

kutoelewana.

Habari za Yuda katika Agano Jipya zinamalizika kwa maneno

haya: “Basi, mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu;

akaanguka kwa kasi akapasuka, matumbo yake yote yakatoka”

(Matendo 1:18). Kama mjuavyo, Yuda alijinyonga, na huku

kuharibikiwa kimwili pengine kulitokana na kutokufanikiwa katika

kujaribu kujinyonga, au kama matokeo ya kuvimba na kuharibika

kulikotokana na maiti yake kuning’inia kwenye kamba yake kwa 27

Page 36: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

muda mrefu. Tafsiri ya Biblia Fafanuzi inasema hivi, “Alipasuka

katikati ya mwili wake”. Pamoja na kwamba maelezo hayo

hayavutii, tunapata picha nzuri. Tafsiri nyingine inasema kwamba

Yuda “alisambaratika”. Yaani, “aliachana”. Lakini hii ilikuwa ni

tokeo la mwisho la kimwili la yale ambayo yalikuwa yametokea kwa

miaka mitatu huko nyuma. Alikuwa ameharibu kile kiini pekee –

“saruji” ya KiMungu ambayo ingeunganisha na kushikamanisha

haiba yake na kuifanya kamilifu na yenye umoja.

Kweli,“alisambaratika katikati”. Na Yuda angefaa kabisa kuwa

“mtakatifu mwangalizi” wa majira ya siku hizi. Biblia inatuambia

(ktk Wakolosai 1:17) kwamba “vitu vyote hushikamana pamoja”

katika Yesu Kristo tu. Lakini, watu wanapopoteza “Maono ya

Kuvutia Sana ya Yesu Kristo,” basi jamii inakosa nguvu za

kuunganisha, za kufanya vitu kuwa umoja, za kushikamanisha vitu

vyote.

Katika mchezo uitwao Green Pastures uliotungwa na Marc

Conally, malaika Gabrieli anaonekana akipita hapa na pale katika

kumbi na maeneo mbalimbali ya mbinguni, huku akizidi kusumbuka

kutokana na vurugu na fujo anazo-ona hapa duniani. Mwishowe

anamgeukia Mungu na kusema, “Bwana! Bwana! Inaonekana

kwamba kila kitu kilichopigiliwa ili kushikamana kinaanza

kuachana!”Watu binafsi na taasisi husambaratika wakati Kristo

anapokosa kutawala. Hayo ni matokeo ya kijamii ya upotevu wa

maono ya kiroho.28

Page 37: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Tatu – hili neno katika Kiebrania lina maana nyingine ya

“kutokuvaa” au “kutembea uchi”. Sasa – kwa kuwa kila matumizi

ya neno hili yamekuwa ya kiroho, bila shaka maana hii ni ya kiroho

pia. Tunapata uwanja mpana kiasi gani kwa ajili ya kujifunza Biblia

kama tutaona maana hii kuwa inahusu hali ya kiroho ya wanadamu.

Tafsiri kwamba “watu hawajavaa nguo” hudhihirisha matokeo

binafsi ya kutokuwa na maono. Katika Biblia – tena kwa mtiririko

dhahiri kabisa – kuokolewa kwa wenye dhambi, “kuhesabiwa haki”

kwao, ni kitu kinachoonekana kwa lugha ya wao “kuvikwa” na ile

haki yenye kulinda na kuhifadhi ya Kristo, na kuhukumiwa kwao

kunaonekana katika wao kutokuwa na mavazi na walio wazi kwa

ajili ya hukumu. Ukweli ni kwamba, katika Biblia nzima, mavazi ni

mfano wa dhambi na haki pia. Mavazi machafu mara nyingi

hutumika kama picha ya dhambi na kujihesabia haki, na mavazi safi

na meupe hutumika kama picha ya ile haki ya Kristo ifunikayo,

inayohifadhi. Ukitaka kufuatilia wazo hilo kwa upana zaidi katika

Maandiko, mafungu yafuatayo yatakuwa na maana sana kwako:

Mwanzo 3:7, 21; Zekaria 3:1-5; Mathayo 22:11-13; Luka 15:22;

Warumi 13:11-14; Waefeso 4:22-24; Wakolosai 3:5-14 na Ufunuo

19:7, 8.

Kitu kimojawapo cha kufurahisha sana katika kuwa Mkristo

ni kujua kwamba Mungu amenivika Vazi Bora Zaidi la Mbinguni –

tena, kwa gharama Yake Mwenyewe! Hili linaonekana katika

simulizi maarufu sana la John Bunyan liitwalo, Safari ya Msafiri. 29

Page 38: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Wakati yule msafiri aliyetambua hatia yake anapofika Msalabani pa

Yesu na kumwamini, mzigo wa dhambi zake unamwacha na

kuanguka, naye anainuka akiwa anasherehekea msamaha na uzima

wa milele. Ndipo anapokutana njiani na “Watatu Wenye Kung’aa”

ambao ni mfano wa Mungu baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho

Mtakatifu. Mungu Baba anamwambia msafiri huyo aliyeokoka,

“Amani iwe kwako. Dhambi zako zimesamehewa.” Mungu Mwana

anamvua zile nguo chafu alizokuwa amevaa, na badala yake,

anampa joho jipya, safi, jeupe. Na Mungu Roho Mtakatifu anaweka

alama kwenye uso wake (ambayo ni mfano wa muhuri wa Roho

Mtakatifu), na kumpa mkononi mwake gombo lililokunjwa vizuri

(ambalo ni mfano wa Biblia).

Hiyo kazi ya pili – kazi ya kumvua mwenye dhambi mavazi

yake ya kale na kumvika upya – ndiyo inayolengwa wakati andiko

letu la msingi linaposema, “Mahali ambapo hakuna maono, watu

hawana mavazi.” Tunasoma hivi katika Yohana 3:36, “Yeye

amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini yeye

asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali hasira ya Mungu inakaa

juu yake.” Mwamini anayemtumaini Kristo amefunikwa kwa haki ya

Kristo naye huepuka hasira ya Mungu kuhusu dhambi. Lakini,

mwenye dhambi asiyeamini hana nguo, na kwa hali hiyo, yuko wazi

kupatikana na kila kitu kinachotaka kumharibu.

30

Page 39: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“Mahali ambapo hakuna maono,” watu zaidi na zaidi hubaki

“bila nguo” au, pasipo ulinzi kwa kitambo na milele. Hayo ndiyo

matokeo binafsi ya kutokuwa na maono.

Mwisho, neno la Kiebrania linatafsiriwa kwa usahihi kabisa

hapa. Maana yake ni “kuangamia”. “Mahali ambapo hakuna maono,

watu huangamia.” Kweli, huruma inahitajika hapa kwa sababu,

kilicho hatarini ni “watu”. Wangekuwa wanyama au mimea, mambo

yasingekuwa mabaya sana. Lakini ni watu – kama wewe na kama

mimi. “Wanaangamia”. Katika Yohana 3:16, neno “kuangamia”

linawekwa kinyume na kuwa na “uzima wa milele”. Kuangamia

maana yake ni kuhusika milele katika kifo hai na maisha ya kufa

katika mahali paitwapo jehanamu. Hapo hapo tena, 1Wakor. 1:18

inaonyesha kwamba watu wasiokuwa na Kristo wako katika hali ya

sasa ya kuangamia. Huku kuangamia kwa watu ni matokeo ya kiroho

na ya milele ya kutokuwa na maono katika Wakristo. Watu watatu

huangamia pasipo Kristo kila sekunde, na Kanisa kwa sehemu kubwa

limepoteza maono yake! Jehanamu inajaa, na Mbingu bado ina nafasi

tele za kujazwa! Yote kwa sababu maono ya Kanisa yamechuja!

Zamani kidogo, mfanya biashara tajiri alisafiri kwenda India

kuwinda simba marara wa Bengali. Akakaa huko majuma sita.

Aliporudi nyumbani, alihudhuria ibada ya katikati ya juma katika

kanisa lake kubwa sana. Alikuta wanajadili kuhusu bajeti ya mwaka

ya kanisa. Mfanya biashara huyo alishtua kanisa zima kwa kutoa

pendekezo kwamba sadaka zote kwa ajili ya utume wa nchi za nje 31

Page 40: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ziondolewe kwenye bajeti. Mzee mmoja akauliza sababu ya

pendekezo hilo la ajabu sana. Jibu likatoka, hivi: “Ndiyo nimerudi

kutoka safari ya majuma sita huko India, na katika kipindi chote

hicho, sikuona mishenari hata mmoja.” Yule mzee akauliza tena,

“Na kusudi la safari yako hasa lilikuwa nini?” Jibu: “Nilikwenda

kuwinda simba marara wa Bengali.” Akaulizwa, “Na ulifanikiwa

kuona wangapi?” Akajibu, “Niliwaona sita.” Yule mzee akasema,

“Hiyo ni ajabu kabisa. Mimi nimekaa India miaka kumi na tatu kama

mishenari, na niliwaona wamishenari mamia kwa mamia. Lakini

mpaka sasa sijaweza kumwona simba marara mmoja wa Bengali

huko India!” Kwa hiyo, mengi sana yanategemeana na mtazamo

wetu, na maono yetu.

Maneno ya Mithali 29:18 yaliandikwa na Mfalme Sulemani,

mtu ambaye katika utawala wake, maono yalipotea. Na hapakuwa na

kushindwa kubaya zaidi katika historia ya Israeli kuliko kule kwa

Sulemani. Watu walisambaratika! Taifa liliporomoka! Ufalme

uligawanyika!

Basi, uchaguzi mbele yetu ni dhahiri kabisa: Aidha ni

“maono au mgawanyiko”! Hii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika

mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na

katika maisha ya Mkristo binafsi!

Ni lazima – na ni lazima – tumngoje Mungu katika utulivu na

maombi, tukiwa na hali ya ndani sana ya uhitaji na moyo wenye

kufundishika, na kumwomba Yeye arejeshe maono ya Utukufu Wake 32

Page 41: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mkuu sana, naya Mpango Wake mkuu mno kwa ajili yetu, na dunia!

Maono yanaporejezwa, tutagundua tena kwamba Mpango Wake

wote umefunuliwa katika Agizo Kuu la Bwana wetu, na kwamba

jukumu hapo ni “kuwageuza watu wawe wanafunzi”.

Dawson Trotman alikuwa sawa aliposema hivi: “Maono ya

kiroho ni kupata moyoni mwako kile kilicho kwenye moyo wa

Mungu – yaani, dunia!” Paulo aliomba kwamba Wakristo wa Kolosai

wapate “kuona mambo kwa mtazamo wa Mungu” (ktk Wakolosai

1:9, TLR). Kama tungefanikiwa hapo, yangekuwepo mapinduzi

makubwa sana!

“Mtu mmoja aliyeamkaAnaweza kumwamsha mwingine;

Na huyo wa pili anaweza kumwamshaNdugu yake aliyeko jirani.

Hao watatu walioamkaWanaweza kuamsha mji mzima

Kwa kugeuza hapo poteJuu chini.

Wengi walioamkaWanaweza kufanya vurugu

Kiasi kwamba hatimayeSisi wote tunaamshwa.Mtu mmoja aliyeamka,

Alfajiri ikiwa machoni mwake,HUONGEZEKA!”

33

Page 42: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 2Agizo Lenye Kuamua Wajibu Wetu

“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari.”

Mathayo 28:18-20

Tunapoondoka nyumbani, mara nyingi tunatoa maagizo yetu

muhimu sana na maelezo – mambo ambayo hatutaki watu wengine

wasahau. Mke wangu mimi huyaweka mezani au kwenye mlango wa

friji. Nini maana yake? Kwamba, hayo ni muhimu!

George Peters katika kitabu chake kiitwacho A Biblical

Theology of Missions aliandika hivi: “Agizo Kuu ndiyo taa yenye

kutuongoza katikati ya ukungu wa kibinadamu na mawazo.

Tunahitaji sana kujifunza upya na kwa undani sana Agizo Kuu. Ni

waalimu wachache sana na wafafanuzi wanaoshughulika kwa upana

sana na mafungu yanayohusu Agizo Kuu. Kanisa linahitaji kufikiri

upya na kwa uzito sana lile Agizo la kufanya watu kuwa wanafunzi.”

Mishenari mstaafu John McGee aliyefanya kazi huko Nigeria,

alisema hivi: “Kuna mengi sana katika Agizo Kuu kuliko mtu

34

Page 43: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

anavyoweza kuota, au kufikiri, au kutenda, hata kama angekuwa na

uwezo wa kuishi mara kumi.”

Katika fungu la Maandiko ambayo ni pamoja na Agizo Kuu

(ktk Mathayo 28:16-20), tunasoma kwamba “wale wanafunzi kumi

na moja wakaenda Galilaya hadi kwenye mlima ambao Yesu alikuwa

amewaagizia.” Huku ndiko kuonekana kwa Yesu kwa kipekee baada

ya ufufuo ambako kulikuwa kumepangwa kabla. Alipoonekana mara

zile nyingine zote, alikuwa anatokea tu. Bila shaka kulikuwa na kitu

fulani cha muhimu sana alichotaka kukisema au kukifanya wakati

huu. Na kweli, ndivyo ilivyokuwa! Hapa “alibandika” maagizo Yake

ya Mwisho. Kuna msemo mmoja wa kawaida sana miongoni mwa

watu wenye kutumia vyombo aina mbalimbali – “Kila Kitu

Kikishindikana, Soma Maelekezo”. Katika sura hii, tunakwenda

kujifunza na kusoma Maelekezo Yake ya Mwisho. Tutagawanya

maelekezo hayo katika mafungu mawili: Uhakikisho Ulioko Katika

Hilo Agizo, na Kazi Iliyoko Katika Hilo Agizo. Ikiwa tunataka

kuelewa na kutimiza Agizo Kuu, ni lazima tuchunguze kwa makini

sana mambo hayo mawili.

UHAKIKISHO ULIOKO KATIKA HILO AGIZO (MS. 18, 20A)

Agizo lenyewe linaanza kwa tamko la kushangaza sana

lililowahi kutolewa. Yesu alisema, “Mamlaka yote nimepewa

Mimi,mbinguni na duniani.” Hapo, sifa Yake na agizo letu

35

Page 44: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

vinategemea sentensi hiyo. Nini maana yake, na ni muhimu kiasi

gani maneno hayo?

“Mamlaka” yanayotajwa hapa ni mamlaka ya KiMungu.

Kanuni kuu katika Maandiko yote ni kwamba, “hakuna mamlaka

isipokuwa itokayo kwa Mungu” (ktk Warumi 13:1), na kanuni hiyo

inaonekana hapa pia. Katika Kiyunani, neno linalotumiwa kueleza

mamlaka ni exousia, ambalo maana yake halisi ni “kutokana na

kuwa”. Fikiri kidogo jambo hili. Maana yake ni kwamba mamlaka

yote ya lazima kutoka kwa Mungu mwenyewe yametolewa kwetu

kwa njia ya mahusiano yetu na Kristo ili kutimiza Agizo hilo.

Halafu, mamlaka hii ni mamlaka iliyotolewa. Yesu Kristo

anayo mamlaka katika Nafsi Yake, ambayo anaimiliki kwa sababu ya

kuwa Yeye. Mamlaka aliyokuwa nayo wakati wa maisha Yake hapa

duniani ilionyeshwa kwa njia nyingi zilizo wazi.

Alionyesha mamlaka Yake juu ya nguvu za asili wakati

alipotuliza dhoruba kali iliyokuwa imewatisha hata wavuvi

waliozoea, kwa neno tu la kinywa Chake na kunyoosha mkono

Wake. Alikuwa amesema na mtini nao ukakauka mbele ya macho ya

wanafunzi, waliokuwa wameshangaa sana.

Vile vile alikuwa na mamlaka juu ya dhamiri ya mwanadamu.

Kwa kutumia mazungumzo rahisi tu naye, Mwokozi wetu aliamsha

dhamiri ya mwanamke Msamaria aliyekuwa amejaa dhambi, na

kuanzisha hali ya matumaini katika nafsi yake. Wakati mwingine,

akiwa amezungukwa kabisa na kundi lililotaka kujua mambo mengi, 36

Page 45: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kwa kutaja tu jina la mtu na kumwambia ashuke kutoka kwenye mti,

aliweza kuiamsha dhamiri ya Zakayo, Myahudi aliyechukiwa na

asiyemcha Mungu, wa mjini Yeriko.

Vile vile alionyesha mamlaka makuu juu ya ile dunia ya

kiroho isiyoonekana wakati wa maisha Yake hapa duniani. Kwa neno

tu au mguso, aliweza kufukuza falme na mamlaka za uovu

zilizokuwa zimetawala maisha ya mtu.

Tena alikuwa na mamlaka ya kupendeza sana katika eneo la

udhaifu na magonjwa ya mwanadamu. Akitumia nguvu Zake bila

kutaka kujionyesha, lakini kwa ajili ya kusaidia maisha ya watu

waliokuwa wanateseka, aliwafanya viziwi wasikie, vipofu waone,

bubu waseme, viwete watembee, vilema wanyooke katika viungo

vyao, na wafu warudie uhai wao.

Hata mafundisho Yake pia yalikuwa na mamlaka. Baada ya

mafundisho Yake ya kwanza katika sinagogi fulani, watu

“walishangazwa na mafundisho Yake, kwa sababu aliwafundisha

kama mtu aliyekuwa na mamlaka, si kama waandishi” (ktk Marko

1:22, TLR). Yesu hakusita kuchukua mamlaka kamili kabisa. Alidai

kuwa na mamlaka ya kusamehe dhambi (ktk Marko 2:10). Alitoa

matamko yaliyorekebisha kanuni za Torati ya Musa, ambayo kila

mtu aliikubali kuwa ilitokana na Mungu (ktk Mathayo 5:21, 27, 33).

Hata alidai kwamba Yeye Mwenyewe ndiye angemhukumu kila mtu

(ktk Yohana 5:27).

37

Page 46: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Lakini, mamlaka inayoonekana katika madai haya si ile

mamlaka inayotajwa katika Mathayo 28:18. Yesu alisema kwamba

haya mamlaka “yametolewa” bila shaka kwa msingi wa mafanikio

Yake katika Kifo na Kufufuka Kwake. Mamlaka ambayo alikuwa

nayo wakati huo katika utukufu Wake wa ufufuo yalizidi sana yale

aliyokuwa nayo wakati wa maisha Yake. Kila aina ya mamlaka

ilikuwa Yake kwa sasa. Mamlaka hiyo alikuwa amepewa kwa amri

ya Baba Yake mbinguni. Wanafunzi walijua kwamba wao walikuwa

watumishi wa Bwana ambaye mamlaka Yake mbinguni na duniani

haikuwa na utata hata kidogo wala swali la aina yoyote ile.

Tunasoma hivi katika Warumi 1:4, “Alitangazwa kuwa Mwana wa

Mungu kwa nguvu (mamlaka) … kwa ufufuo kutoka kwa wafu”

(TLR). Hayo mamlaka ndiyo msingi wa Agizo analotoa kwa

wanafunzi Wake.

Ni dai la ajabu sana! A.T. Robertson alisema hivi: “Ni

onyesho la hali ya juu sana katika historia ya dunia, kumwona Kristo

aliyefufuka, pasipo fedha wala jeshi wala taifa, akiwaagiza kundi hili

la watu mia tano – waume kwa wake – waende kuiteka dunia na

kuwafikisha mahali pa kuamini kwamba inawezekana kufanyika,

kwa mguso na udhati na nguvu.”

Vile vile, mamlaka hii ni mamlaka anayostahili Yeye. Yesu

alisema hivi: “Mimi nimepewa mamlaka yote.” Ona kwamba hii

mamlaka hatujapewa sisi, bali kapewa Yeye. Lakini, hilo lisitupe 38

Page 47: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

hofu, kwa sababu chochote kilicho Chake ni mali ya kila mtu

aliyeokoka. Kila mtu aliyezaliwa mara ya pili ni mrithi wa Mungu

kwa sababu yeye ni “mrithi pamoja na Kristo” (ktk Warumi 8:17).

Kila kitu katika milki ya Baba ambacho kihalali ni mali ya Kristo

kwa sasa ni mali yangu pia kwa sababu ya mahusiano yangu kiimani,

au kujitambulisha kwangu kiimani, na Yeye. Chochote kilicho Chake

ni changu, si kwa sababu mimi ninastahili kuwa nacho, bali kwa

sababu mimi niko ndani Yake. Ona pia kwamba, hakupewa mamlaka

haya kwa sababu Yeye ni Mwana wa Mungu. Kama Mungu, hakuna

kitu anachoweza kuongezewa, na hakuna kitu kinachoweza

kupunguzwa Kwake. Mamlaka ambayo Yesu anadai hapa ni

mamlaka ambayo ameipata (ameistahili) kama Mwana wa Mtu.

Neno “aliyopewa” linaonyesha tendo la wakati uliopita, na bila shaka

humaanisha kukabidhiwa mamlaka hiyo siku ile alipofufuka toka

kwa wafu. Hii inakubaliana na yale maandiko katika Wafilipi 2:5-11,

yanayohusu Kunyenyekezwa na Kutukuzwa Kwake. Baada ya Paulo

kuonyesha jinsi Yesu alivyoshushwa na kunyenyekezwa, ndipo

anapodhihirisha kutukuzwa Kwake kulikofuata. “Kwa hiyo tena

Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu

Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba” (ktk Wafilipi 2:9-

11). Kwa hiyo, kutukuzwa Kwake na mamlaka Yake vilimstahili

kutokana na kifo na kufufuka Kwake.39

Page 48: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mwisho – mamlaka aliyodai kabla ya kutoa Agizo Lake Kuu

yalikuwa mamlaka yaliyoelezwa na kuwekwa wazi. “Nimepewa

mamlaka yote, mbinguni na duniani.” Maeneo hayo mawili

yanayotajwa ndiyo pekee ambayo sisi tunahusika nayo, na bila shaka

Yesu Kristo anatenda kazi katika maeneo hayo pia. “Mbinguni na

duniani.” Mamlaka yote ya mbinguni ni Yake, na mamlaka yote ya

duniani ni Yake. Anawatangazia wanafunzi Wake kwamba

“nimepewa Mimi mamlaka yote mbinguni”, mahali alipopokea “Jina

lipitalo majina yote”, mahali ambapo “ametukuzwa na kuketishwa

mkono wa kuume wa mamlaka”, mahali ambapo “ametiwa taji ya

heshima na utukufu”. Anatangaza pia kwamba “Mimi nimepewa

mamlaka yote duniani”. Hivyo, Yeye ndiye Bwana mkuu wa kote

kuwili.

Katika mchezo maarufu sana wa Shakespeare, mwandishi

Mwingereza maarufu, anaonekana Liwali wa Kent akimjia mfalme

kwa siri, akiwa amejibadilisha. Mfalme huyo Lear anamwambia,

“Unataka nini wewe?” Yule Liwali anamjibu, “Nataka nikutumikie.”

Mfalme anamwuliza, “Kwa nini?” Ndipo linatoka jibu maarufu la

Liwali wa Kent, kwamba, “Kwa sababu katika uso wako naona kitu

ambacho kwa hiari yangu mwenyewe naweza kukiita bwana”.

Mfalme akamwuliza, “Kitu gani hicho?” Liwali anajibu, “Mamlaka”.

Yesu anatoa madai halali kabisa kwamba mamlaka yote ni

Yake. Na katika mamlaka hiyo ndipo tunapaswa kutekeleza ule

mradi wa utume (na ile amri ya kufanya watu kuwa wanafunzi). 40

Page 49: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mamlaka Yake hayajapungua wala kumalizika kutokana na miaka

kupita. Basi, kwa msingi wa mamlaka hiyo, tunapaswa kutekeleza

agizo au kazi tuliyopewa katika Agizo Kuu.

KAZI ILIYOKO KATIKA HILO AGIZO (MS. 19, 20)

AMRI PEKEE KWA KANISA (KWA MKRISTO) KUSONGA

MBELE

Agizo Kuu ndiyo “amri pekee ya kusonga mbele” iliyowahi

kutolewa na Yesu Kristo kwa Kanisa Lake. Agizo Kuu ni kazi ya

kuvuna roho na utume, lakini ni zaidi ya hayo. Kuna maelezo kuhusu

Agizo Kuu la Bwana wetu katika Agano Jipya mara tano. Linatajwa

kwa njia tofauti katika Mathayo 28:18-20 (kwa maelezo yaliyo

dhahiri zaidi), katika Marko 16:15 (kwa kifupi lakini wazi), katika

Luka 24:47, Yohana 20:21 na Matendo 1:8 (kwa ufafanuzi mpana

zaidi).

Katika maelezo ya Mathayo, Kanisa la Yesu Kristo linapata

msingi kwa ajili ya kazi yake. Hakuna swali kabisa katika maneno

anayotoa Mathayo kuhusu kile ambacho Yesu alikusudia wafuasi

Wake kufanya. Si swala la hisia au kujisikia. Si kazi ya kufanywa

tutakapoona inafaa. Yesu aliacha maagizo dhahiri. Maagizo hayo ni

kamilifu (yaani, hayapitwi na wakati wala kubadilika) na ni ya mara

moja. Agizo Kuu ni la sasa hivi, na linamfunga kila Mkristo

kulitimiza wakati huu. Maneno ya Agizo hili ni maneno tendaji:

Enendeni, fanyeni watu kuwa wanafunzi, batizeni, na fundisheni. 41

Page 50: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kwa kifupi tu, Kanisa liko chini ya amri, lakini uhalisi wa hiyo amri

unaweza kuwashangaza waamini wengi.

KULIGAWA AGIZO SEHEMU SEHEMU

Ningependa kuligawa Agizo Kuu katika sehemu saba.

Muhtasari ni kama ifuatavyo: Kwanza, sisi tunawajibika kutumia kila

mtenda kazi anayepatikana (neno “ninyi” la ms. 19 liko katika

wingi). Halafu, tunatakiwa kuingia shambani (“enendeni”). Tatu,

tunatakiwa kila wakati kupanua maono yetu (“mataifa yote”). Nne,

tunapaswa kuwashuhudia wahusika (“kufanya wanafunzi”). Tano,

tunapaswa kuwahusisha walioshuhudiwa (“mkiwabatiza katika jina

la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu”). Sita, tunatakiwa

kuwaelimisha na kuwajenga waliojiunga nasi (“na kuwafundisha

kuyashika yote niliyowaamuru ninyi”). Na mwisho, tunapaswa

kutarajia Yeye kutenda kazi (“na tazama, Mimi niko pamoja nanyi

siku zote, hata mwisho wa dunia”). Bila shaka unaona sasa kwamba,

yapo mengine mengi sana kuhusu Agizo Kuu la Bwana wetu kuliko

ambavyo sisi tumekuwa tukiheshimu!

Tunapochunguza kwa makini na dhati kabisa hili Agizo,

tunagundua kitu cha kushangaza sana. Tunapata kwamba, kwa karibu

karne mbili, Agizo lilifanya kazi vizuri kabisa na kuigusa dunia

iliyokuwa inajulikana siku zile kwa haraka sana. Lakini, kitu cha

ajabu kikatokea. Kitu fulani kiliharibika kabisa. Ili kuona hilo,

ningependa tutazame kila hoja katika zile saba ambazo nimetaja. 42

Page 51: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Chini ya kila hoja, ninataka utazame vichwa vidogo viwili. Kimoja ni

“Mkakati wa Mwokozi”, na kingine kinaitwa “Mbadala wa Shetani”.

Tutafanya hivyo na kila hoja.

1. KUTUMIA KILA MTENDA KAZI

Hoja ya kwanza katika Agizo Kuu ni kutumia kila mtenda

kazi. Katika mstari wa 19, neno “ninyi” liko katika wingi, na maana

yake hasa ni “ninyi wote”.

Mkakati Wa Mwokozi

Mtu mmoja ameeleza nia ya Yesu kuhusu kutimizwa kwa

Agizo hili Kuu kwa maneno haya: “Waamini wote wanatakiwa

kuhusika, na wanapaswa kutenda wakati wote”. Kitu kimoja – licha

ya nguvu za Mungu – kilichofanya Agizo Kuu kufanikiwa sana hapo

mwanzoni ni kwamba, watenda kazi wake wote walihusishwa

kufanya huduma mahali palipotakiwa. Lengo lilikuwa kwamba kila

mwanafunzi awe mzalishaji wa wavuna roho na wafanya watu kuwa

wanafunzi kama yeye. Wote walikuwa wasemaji, waenezaji na

wainjilisti! Ukweli ni kwamba, kushiriki kulikuwa kwa kila mtu

miongoni mwao mpaka ikabidi sheria ziwekwe ili kuondoa vurugu

au kuchanganyikiwa (ona 1Wakor. 14:31). Hapakuwepo na

watazamaji miongoni mwao. Adolph Harnack, mwanahistoria

maarufu wa kanisa, alisema hivi: “Wakati kanisa liliposhinda sana

katika siku za mwanzo za Dola ya Rumi, halikufanya hivyo kwa 43

Page 52: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

waalimu au wahubiri au mitume, bali kwa wamishenari wa kawaida

kabisa.” Hili Agizo linataka huduma binafsi kutoka kwa kila

aaminiye. Wote walio viungo vya Mwili wa Kristo hawawezi

kufanya hivyo bila ya kila mshirika kufanya hivyo. Kanisa moja

katika eneo la Manhattan huko Marekani lina ujumbe ufuatao

kwenye kibao chake: “Mchungaji, --------“. “Wahudumu: Kila

mshirika.” Huo ndiyo mkakati wa Mwokozi kwa ajili ya kila mtenda

kazi kutumika.

Mbadala Wa Shetani

Sasa, tazama mbadala alioleta Shetani. Ukweli ni kwamba

Agizo Kuu lilifanya kazi. Yaani, lilifanya kazi mpaka Shetani akaona

vibaya. Lilifanya kazi vizuri sana kiasi kwamba ilimchukua miaka

200 kuondokana na kipigo alichopata na kupanga upya majeshi yake.

Hatimaye, akapambana na Agizo Kuu kwa mpango mbadala wake.

Si vigumu kuona kwamba Agizo Kuu la kwanza limevurugwa kiasi.

Limerekebishwa, na kwa karne nyingi sana, makanisa mengi

yameangukia katika mpango wa Shetani. Pigo kubwa sana la Shetani

dhidi ya Agizo Kuu lilielekezwa kwenye ile hoja ya kwanza, ya

kutumika kila mtenda kazi.

Mapema kabisa katika historia ya Kanisa, Shetani alianzisha

mgawanyo katika Kanisa. Likawa na sehemu mbili, naye akakazia

kupita kiasi zile tofauti. Walio wengi aliwaita “walei – wasiokuwa

wachungaji” na wale wachache akawaita “wachungaji – watumishi”. 44

Page 53: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Na hoja yake kubwa ilikuwa kwamba walei hawana uwezo na

hawana vipawa, na kwamba hawahusiki katika kazi halisi ya kanisa

hata hivyo. Shetani basi akasimamia ujenzi wa tabaka ya watu wa

dini walio wataalamu. Hawa wataalamu walitakiwa (1) kupigana vita

zote za kiroho, na (2) kufanya kazi zote za kiroho. Vipi shughuli ya

“walei”? Kumtegemeza na kumsaidia huyo mtaalamu kiongozi na

kulipia mpango wake kufanyika (ambapo katika Agano Jipya, watu

ndiyo mpango mkuu).

Basi, “ngazi ya kiroho” ikatengenezwa Kanisani. Juu kabisa

ya ngazi alikuwepo “mishenari”, halafu anayefuata ni mchungaji,

halafu watendaji wengine wataalamu wa kidini, na mwisho wa ngazi,

mshirika wa kawaida. Kuna mtu amesema kwamba kizazi chetu ni

“kizazi cha mtazamaji”. Mpira wa miguu una wachezaji 22 kwa mara

moja, lakini unaweza kuwa na watazamaji mamilioni wakati huo

huo! Michezo mingine ina wachezaji 18. Mpira wa vikapu una

wachezaji kumi, ngumi wachezaji ni wawili, na kuna michezo

mingine katika Olimpiki yenye mchezaji mmoja tu. Lakini michezo

hiyo yote ina mashabiki mamilioni. Mchekeshaji mmoja aitwaye

Fred Allen alisema hivi: “Kama jamii itaendelea kama ilivyo, baada

ya muda tutakuwa na dunia iliyojaa watu wenye macho makubwa

kama sahani za vikombe vya chai, na akili zenye ukubwa wa harage”

(kwa kuwa wakati wote watu wanakodoa macho, na kutumia muda

mwingi katika ushabiki)!

45

Page 54: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Matatizo Kanisani Ya Watu Kutokuwa Na Kazi, Na Kazi Kidogo

Kanisa limetengeneza matatizo mawili ya “kutokuwa na

ajira” na hayo yanaungana mkono mara zote, na kufanya mambo

kuwa mabaya zaidi. Kuna tatizo la kutokuwa na kazi kwa washirika

katika kusanyiko la mahali. Kwa kuwa mshirika wa kawaida katika

kanisa la kawaida hatimizi kazi yake aliyopangiwa na Mungu,

“mshahara” wake unapunguzwa na kuwa posho tu kwa ajili ya

kuishi. Wajibu wake hautimizwi, thawabu yake inapotea, dunia

inabakia gizani, na Shetani anatosheka vizuri sana.

Halafu kuna tatizo linalokaribiana na lile, ambalo ni mtumishi

kutofanya kazi ipasavyo. Mchungaji wa kawaida katika kanisa la siku

hizi ana kazi nyingi, lakini hafanyi kazi ipasavyo! Wakati Henry M.

Stanley aliporudi kutoka Afrika kwenye kumtafuta David

Livingstone, mwanahabari mmoja alimwuliza swali hivi: “Ni kitu

gani kilichokusumbua zaidi wakati ukiwa Afrika? Ni wale simba, au

ni nyoka?” Stanley akajibu hivi, “Wala! Walionisumbua zaidi ni

mbu!” Wachungaji wetu hawapati kuona simba na chui kwa sababu

daima wako kwenye mapambano na mbu. Wakati vita kuu za

atomiki zinapiganwa katika ulimwengu wa roho, wao wanajitahidi

kupambana na kukabiliana na mashambulizi ya mbegu ndogo ndogo

tu! Ongezeko la vitu vingi vidogo vidogo – vishughuli vingi vya

kidini ambavyo vinachokesha, pamoja na picha bandia ya huduma ya

mchungaji ambazo zimechorwa njiani mwake vinamfanya mchungaji

ashindwe kutekeleza kazi pekee ambayo Mungu amempa.46

Page 55: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Hivi karibuni nilipata taarifa kutoka Ofisi Kuu ya Jimbo

kwamba wachungaji 300 wa Kibaptisti wanaondolewa makanisani

kila mwezi. Sina uhakika na idadi hiyo, lakini najua kwamba tatizo

hilo ni kubwa sana. Pia nilisikia taarifa miaka kadhaa iliyopita

kwamba wachungaji zaidi ya elfu moja wa Kibaptisti wanaachana na

madhabahu zao. Sina uwezo wa kuthibitisha idadi hiyo, lakini najua

kwamba tatizo hilo ni kubwa sana pia. Pengine sababu kubwa ya

huko kutatizika kwa uongozi unaoitwa ni kwamba kiongozi huyo

hatosheki kwa “ajira ndogo” inayomkabili – hana kazi za kumtosha

kuridhika!

Ukristo Tazamaji Katika Kanisa

Tumetengeneza Ukristo tazamaji katika kanisa, ambao katika

huo, wachache ndiyo wasemaji, na wengi ni wasikilizaji. Kanisa

limejaa “umoja wa mashabiki” – mashabiki wa imani. Hebu fikiri

kuhusu duka la kuuza vitu jumla, ambalo lina meneja mauzo ambaye

kazi yake ni kuuza hivyo vitu na kufundisha kuhusu sifa ya vitu

hivyo na mbinu za uuzaji. Tuseme pia kwamba duka hilo lina kundi

kubwa tu la “wauzaji” ambao kazi yao kubwa ni kuwatafuta

wasikilizaji na kuwatia moyo kusikiliza tu mafundisho ya meneja

mauzo. Kingekuwa kituko cha namna gani hicho? Je, duka hilo

lingedumu kwa muda gani? Ndugu James S. Stewart wa Edinburgh,

Uskochi, alisema hivi: “Tatizo hasa la Ukristo si wasemao hakuna

Mungu wala wenye mashaka, bali ni Mkristo asiyeshuhudia, asiyezaa 47

Page 56: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

matunda, anayejaribu kuingiza roho yake mbinguni kwa njia ya

magendo, yeye mwenyewe.” Huo ndiyo mkakati wa Shetani, na zaidi

ya hayo, ametumia sana neno “ninyi” mpaka imefikia kwamba hata

hao “watumishi” si wote wanaoshuhudia!

Hebu tazama jamii ya Kikristo. Kanisa liko upande gani –

upande wa Mkakati wa Mwokozi, au upande wa Mbadala wa

Shetani? Nadhani jibu liko wazi kabisa, na linasikitisha. Ni lazima

tutazame upya Amri yetu ya Kusonga Mbele!

2. KUINGIA SHAMBANI

Hoja ya pili katika muhtasari wetu kuhusu Agizo Kuu ni

kuingia shambani kote. Neno “enendeni” ni neno tendaji, lenye

nguvu – neno linalo-onyesha kwenda au kutembea.

Mkakati Wa Mwokozi

Mkakati wa Mwokozi ni dhahiri. Katika Mathayo 13:38,

alisema hivi: “Shamba ni dunia”. Hili si shamba kwa ajili ya kanisa,

bali ni shamba kwa ajili ya kanisa lako la mahali! Yesu Kristo

anakutazamia uhusike na dunia nzima! Mifano ambayo Yesu

anatumia kusema kuhusu Wakristo na Injili imefungamanishwa

pamoja kwa kitu kimoja. Yote ina tabia ya kupenya – kuingia ndani.

Yesu alitumia mfano kama nuru, chumvi, funguo, mkate, na maji.

Nuru haina faida kama haipenyi na kufukuza giza. Chumvi haina

faida kama inabakia ndani ya chupa yake. Lazima ipenye na kuingia 48

Page 57: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

katika mboga au viazi. Mtoto mmoja mvulana alisema hivi, “Chumvi

ndiyo huharibu viazi – ukiacha kuiweka.” Funguo hazina maana

kama haziingii katika kitasa. Mkate hauna faida ukiwa nje ya mlaji,

na maji hayatoshelezi hitaji la mtu mwenye kiu kama

yasipomwingia. Vivyo hivyo, Wakristo wanatakiwa kuingia na

kupenya duniani kila mara.

“Huwezi kumtaja Mungu bila kwenda. Hakuna uzuri bila

kwenda. Huwezi kutamka neno Injili bila kwenda, na huwezi kuitii

Injili na kuwa mtumishi mzuri wa Mungu usipokwenda – kwa

masharti Yake. Ukristo ni kitu cha kwenda kwa asili yake na

msukumo – si cha kushikilia. Kila Mkristo anapaswa kuishi kikazi

(yaani, kama Mkristo) kwenye eneo la kupenya – iwe ni katika

maabara ya kisayansi, maktaba, kiwandani, shamba la matunda, kazi

ya kugawa vitu, cheo kikubwa, kwenye ndege ya kisasa, katika

hospitali ya tabibu wa magonjwa ya akili, au katika ofisi ya

mchungaji. “Dunia” yetu ni popote tulipo, penye watu. Katika Luka

10:1-3, Biblia inatuambia, “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na

wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila

mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia,

‘Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni

Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Enendeni. Angalieni, nawatuma kama wanakondoo kati ya

mbwamwitu”. Ona maeneo ambayo nimekazia kwa kutumia wino

mwepesi. Maneno hayo yamejaa! Kila Mkristo anapaswa kuwa 49

Page 58: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mwanzilishi, mtangulizi kwa ajili ya ujio wa Kristo “kila mahali

alipokusudia kwenda mwenyewe.” Wanakondoo kati ya mbwamwitu

watarajie kupona kwa muujiza tu!

Tena – neno “enendeni” katika Agizo Kuu SI AMRI.

Kulihesabu kwamba ni amri ni kuendeleza ile dhana ya “ngazi ya

kiroho katika Ukristo”. Lingekuwa ni amri, kila ambaye angekwenda

mbali ili kuihubiri Injili au kumshuhudia Kristo angehesabiwa kuwa

mtu maalum. Lakini, neno tendaji lina maana hii: “Mnapokuwa

mkienda”, au hata, “Kwa kuwa mnakwenda”. Yesu asingekosa akili

kiasi hicho, atuagize kufanya kitu ambacho tunafanya tayari! Je,

kanisa lako liko wapi Jumanne mchana saa tisa? Kwani liko

kanisani? Hapana, “linakwenda”. Swala hapa si kwamba mbona

kanisa haliendi duniani? Swala ni hili: Je, kanisa linatimiza kazi yake

linapoingia na kupenyeza?

Nilikuwa katika mji mkubwa mzuri sana katika nchi ya

kigeni fulani, miaka kadhaa iliyopita. Nilihubiri kwenye kanisa la

Kiingereza hapo Jumapili asubuhi. Nikawahi ili nipate nafasi ya

kuzungumza na watu walipokuwa wanafika ibadani. Mbona

nilishtushwa sana na watu wenyewe! Walikuwepo Wamarekani

wengi, na walikuwa wafanya kazi katika shirika la mafuta la

kimataifa, wenye mishahara mikubwa sana. Nilipowauliza jinsi

walivyokuwa wanafurahia kukaa huko, wote walilalamika kwamba

wanachoshwa na mambo yale yale kila siku. Wengi wao walikuwa

hapo kwa mikataba ya miaka miwili. Katika mahubiri yangu, 50

Page 59: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

niliuliza ni kwa nini wasijifunze lugha ya pale na wawe na

vipeperushi vyenye ujumbe wa Injili katika lugha ya pale na wafanye

umisheni, uinjilisti na kuleta watu kwa Yesu wakiwa huko. Nadhani

walipuuza wazo hilo bila hata ya kulifikiria! Ni hivi: Kuna mtu

ambaye ametuuzia wazo baya kabisa lenye kupelekea usaliti mkubwa

sana wa Yesu na Agizo Lake. Wao walikuwa “wamekwenda” (tena,

kwa kulipwa na shirika la mafuta), lakini hawakutambua wajibu wao

“wakiwa katika kwenda”.

Mbadala Wa Shetani

Shetani ameingiza mbadala wa kijanja na siri sana katika akili

za Kanisa. Maneno makuu mawili katika Injili ni “njoo” na

“enenda”. Tukisha kuja kwa Kristo (Mathayo 11:28-30, kwa mfano),

tunapaswa “kwenda na kuwaeleza” watu wote yale tuliyopata katika

Kristo. Shetani ni bingwa wa kutumia watu, na kubadili maneno.

Yeye akaingiza upotofu wa polepole kanisani, kuliondoa kwenye

“nenda ukaeleze” na kulitia kwenye “njoo usikie”. Mkomunisti

mmoja alitania Kanisa kwa maneno haya, “Kauli mbiu ya Wakristo

inaonekana ni, ‘Njooni hapa mpate ujumbe wa Mungu, mwende

mbinguni. Au acheni kuja, mwende jehanamu’!” Ndugu mmoja

aitwaye Paul Little alisema hivi, “Tatizo si kwamba Injili imepoteza

nguvu yake. Tatizo ni kwamba kanisa limepoteza walengwa wake.”

Mwingine naye akasema, “Roho Mtakatifu hawezi kuwaokoa

watakatifu na viti – lakini Kanisa limejaa vyote!”51

Page 60: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Fikiri mfano wa kimatibabu. Tuseme kwamba Wizara ya

Afya inaogopa kwamba kutatokea mlipuko wa surua. Ingefanya nini

ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo? Bila shaka ingewatenga wenye

ugonjwa huo na kuwaweka karantini wote ambao wamekwisha

upata, na kwa njia hiyo ugonjwa ungezuilika. Sasa hebu fikiri –

Wizara ya Jehanamu itake kuzuia mlipuko wa Ukristo wa Agano

Jipya. Bila shaka ingefanya kila liwezekanalo kuwatenga “wabebaji”

na kwa njia hiyo kuzuia kuenea kwake. Na hicho ndicho

kinachotokea Kanisani kwa sehemu kubwa. Tunakaa ndani ya

Kanisa kwa “mkao mtakatifu”. Timu yetu haiendi uwanjani, mahali

ambapo ili kupata ushindi mchezo lazima ufanyikie. Na kuna

wanaopenda mpango huu na uzuri wake na usalama wake. Maana,

umewahi kumsikia mchezaji aliyeumizwa akiwa hajaingia uwanjani?

Kwa hiyo, tunapanga mikakati yetu, tunafanya uchambuzi kuhusu

adui yetu, tunarudiarudia mambo na hata kulaumu wachezaji

wenzetu. Tunawaza kuhusu uanachama, mipango yetu, majengo na

fedha. Kila juma tunakuwa na “gwaride” na amri yetu kuu ni “tubaki

kama tulivyo”. Nimechanganya mifano hapo, lakini nadhani ujumbe

umefika. Daima tunaongeza shughuli zetu za kidini, tunakamilisha

mipango yetu kishirika, tunapanua na kukuza taasisi zetu za kidini,

na kuimarisha taratibu zetu kiuongozi katika dini, na yote

tunayofanya katika makanisa mengi ni kudumisha kawaida na

kujistarehesha sisi wenyewe tu! Bila shaka Shetani anafurahi sana!

52

Page 61: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kanisa la kawaida linafanya kazi kwa kufuata mpango mbadala wa

Shetani, badala ya kufuata mkakati wa Mwokozi.

3. KUPANUA MAONO

Sehemu ya tatu katika Agizo la Bwana wetu ni kuendelea

kupanua maono. Upana wa eneo letu la utendaji katika Agizo hili ni

“mataifa yote”.

Mkakati Wa Mwokozi

Hebu tujikumbushe tena – Yesu Kristo hafanyi mchezo nasi.

Anatutazamia kabisa “tukabiliane” na dunia nzima! Naye ametupa

Mpango ambao kwa huo tunaweza kufanikiwa! Je Mkristo – ni nia

yako kugusa mataifa yote kwa “kuwageuza watu kuwa wanafunzi”?

Hiyo kazi kuu ndiyo agizo la Bwana wetu. Kugusa dunia ndiyo

utume wetu. Lengo letu lazima liwe kujulisha na kugusa dunia nzima

mpaka mwisho wa nchi, mpaka ukamilifu wa dahari.

Hii hoja ya tatu katika Agizo inawezekana kuwa ndiyo ya

maana kuliko zote. Hapa ndipo motisha kwa ajili ya kuwafanya watu

kuwa wanafunzi inapotokea. Ningependa kutumia nafasi zaidi hapa

ili kuhakikisha kwamba sote tunatambua ukuu wa Agizo la kuigusa

dunia nzima. Dakta D. Martyn Lloyd-Jones alisema hivi katika

kitabu chake kiitwacho The Miracle of Grace, “Sitasita kusema

kwamba hatimaye, hakuna kipimo kamili cha ukiri wetu binafsi wa

imani kama hali tuliyo nayo moyoni juu ya shughuli ya umisheni ya 53

Page 62: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kanisa.” Mimi niongeze maneno yangu hapa kwamba, “shughuli ya

umisheni ya Kanisa” si kutuma waamini wenye mzigo maalum

kwenda nchi za mbali tu. Huanza katika moyo wa kila aaminiye, na

hutekelezwa kwa kila aaminiye kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo

anayetambua kuhusu dunia nzima, anayelemewa na dunia nzima,

anayeona dunia nzima, na mwenye kuwajenga na kuwaongeza

wanafunzi wengine wenye kuiona dunia nzima na kuigusa dunia

nzima.

Je, maono yako binafsi ni maono “makubwa kama ya

Mungu”? Je, unakusudia kufika wapi na kugusa watu? Kipimo cha

kufanikiwa kwako kama mwanafunzi wa Kristo kunaweza

kuonekana katika jinsi unavyojibu maswali haya: Je, ushawishi ulio

nao unafika mbali kiasi gani? Je, nini ukubwa wa eneo lako la

uwezo? Isaya 54:2 inasema, “Panua mahali pa hema yako, na

wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze. Ongeza urefu

wa kamba zako, vikaze vigingi vya hema yako.” Mstari huu unatoa

kauli mbiu kamili kabisa kwa ajili ya wote wanaofanya wengine

kuwa wanafunzi (yaani, wanafunzi wote wa kweli wa Kristo), na

hutoa mwito kwa ajili ya kukuza maono kusikokoma kwa kila

aaminiye, ili kuigusa dunia nzima.

Hapa tena naomba ukabiliane na swali hili: Je, nini ukubwa

wa eneo lako la uwezo na ushawishi? Je, unatenda kazi chini ya

maono kama kofia, ambapo maisha ya Kikristo yanaanza na kuishia

kwa ajili ya manufaa yako binafsi – ili uishi na upate kitu? Au je, 54

Page 63: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

maono yako ni kama mwavuli, yenye nafasi kwa ajili ya watu wawili

au watatu hivi? Au je, maono yako ni kama kibanda cha simu, yenye

nafasi ya kufunika watu kati ya watu hadi wanne? Au je, ni kama

chumba, yenye kuwaingiza marafiki kadhaa? Au pengine yako kama

nyumba, yenye uwezo wa watu kama 25 hadi 50 hivi? Au ni kama

duka kubwa, yenye uwezo wa watu mia kadhaa, na hata elfu kadhaa?

Au ni kama uwanja wa michezo, yaliyo na upana wa kutosheleza

makumi elfu? Au pengine unatamani kuwa na maono kama anga,

ambayo yanaweza kuwahusisha watu wote duniani na vizazi vyote

vitakavyokuja? Kumbuka kwamba Agizo linahitaji maono

yanayolingana na Yesu, yenye ukubwa wa Mungu, nasi tunatakiwa

tuzidi kufanana na Kristo, kwa hali hiyo kuendeleza Tabia ya Mungu

Mwenyewe. Tunakuwa “washiriki wa asili Yake ya Uungu” (ktk

2Petro 1:4) tunapo-okoka, na sehemu inayobaki ya maisha yetu

inapaswa kutumika katika kushirikiana na kupanuliwa kwa Asili

Yake ndani yetu. “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi nipungue” (ktk

Yohana 3:30). Sehemu ya huku kupanuka inamaanisha kuongezeka

katika kujitambulisha na “Kinachomsumbua” Mungu – kumjulisha

na kugusa kila mtu duniani kwa Ujumbe wa Injili Tukufu ya Kristo.

Ni dhahiri kutokana na kusoma Injili hata kwa juu juu tu

kwamba, Yesu alikuja ili kuvamia, kufahamisha na kugusa dunia

nzima. Angeweza kusema, “Mimi ni nuru ya Galilaya”, lakini

hakufanya hivyo. Alisema, “Mimi ni nuru ya dunia” (ktk Yohana

8:12). Hakusema, “Mimi ni nuru ya Wabaptisti au WaPresbiterian au 55

Page 64: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

WaMethodisti”. Hakusema, “Mimi ni nuru ya waliolelewa vema au

waliosoma vizuri au waliolishwa vizuri”. Angeweza kusema,

“Mungu aliwapenda sana Wayahudi” lakini hakufanya hivyo.

Alisema, “Mungu aliipenda sana dunia” (ktk Yohana 3:16). Yesu

alikazia tena na tena kwamba hakuwa na mpango wa kufikia

kisehemu kidogo au watu wachache – mpango Wake ulikuwa ni

dunia nzima. Yeye ndiye nuru pekee ya kiroho kwa ajili ya kila nchi

na kwa ajili ya kila mtu aliyeko katika kila nchi duniani.

Inasemekana kwamba askari wa jeshi la Napoleon walikuwa

wanabeba ramani ya dunia katika mikoba yao, pamoja na bendera ya

Ufaransa. Walikuwa ni wafungwa, mateka, watumwa wa wazo la

kuiteka dunia kwa ajili ya Ufaransa. Enyi ndugu zangu Wakristo na

dada zangu – Bwana wetu Mwenyezi ameweka maono yanayowaka

ya dunia nzima mbele ya macho ya watu Wake na amewaomba kila

mmoja kuyaruhusu yawake mpaka yachome moyo. Na haya maono

yanapaswa kushika mawazo yetu kila wakati, mipango yetu, ndoto

zetu, shughuli zetu kwa muda wote tunaoshi. Mara maono

yatakapoanza kutushika, tutatambua kwamba Yesu aliweka mpango

kwa ajili yetu – wewe na mimi kama watu binafsi – ili kutekeleza na

kukamilisha maono yenyewe. Kufanya wanafunzi wenye maono

ndiyo hilo! Unalionaje hilo?

Hebu tafakari swali hili kwa moyo wako wote. Je, Biblia na

Ukristo vilitokea katika jimbo mojawapo kati ya majimbo hamsini ya

Marekani? Hapana. Ukristo uliingizwa Marekani. Yesu hakuzaliwa 56

Page 65: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

nyumba ya jirani na kwetu, wala katika mtaa wetu. Biblia haikuwa

imeandikwa kwa Kiingereza au Kiswahili tangu mwanzo. Sisi

Wakristo wa Tanzania (au wa Afrika) ni matokeo ya wamishenari

Wakristo. Je, na sisi tumejitoa kufanya katika sehemu zingine za

dunia yale ambayo hawa wamishenari walitutendea sisi? Kama

ungekuwa mmojawapo wa waliopotea katika Bara la Asia, Afrika au

Marekani ya Latin, ungetamani mtu akuletee ujumbe wa Nuru na

Uzima? Hakika sisi Wakristo wenye ubinafsi na wenye kujali zaidi

taasisi na “makanisa ya kujikimu” lazima tutubu hasa na kuomba

huruma na msamaha wa Bwana wetu, kwa sababu tumejaribu

kumfanya Yeye kuwa mali yetu (kama Wayahudi walivyofanya)

badala ya kuruhusu atutawale na kutumiliki kabisa. Na toba yetu

lazima iwe ya kiwango cha ndani sana kiasi cha kufikia mahali pa

kusahihisha hii hali ya “Ukristo wa kibinadamu” (neno langu,

ambalo hata hivyo linapingana katika maana yake).

Ndugu John Oxenham katika kitabu chake kiitwacho Bees in

Amber, aliandika hivi:

Nasikia sauti dhahiri kabisa ikiita, ikiita,

Inaita wakati wa usiku, hivi:

Enyi mnaoishi katika Nuru ya Uzima,

Tuleteeni na sisi hiyo nuru!

Tumefungwa katika minyororo ya giza,

Macho yetu hayapati kuona,

Enyi ambao hamjawahi kufungwa wala kuwa vipofu,57

Page 66: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Tuleteeni nuru!

Haiwezekani – hamwezi kutusahau,

Sisi tulioko katika usiku wa giza kuu zaidi,

Sisi ni watu tunaozama, sisi ni watu tunaokufa,

Tuleteeni – Jamani, tuleteeni Nuru!

Sasa Mkristo, usije ukaanza kutafuta maandiko ya kunipinga

au ya kuthibitisha kwamba watu pasipo Mungu wamekufa na

hawawezi kusema hivyo! Najua hayo yote – amini hivyo! Hivyo

sivyo watu wasiomcha Mungu wanavyoishi, wanavyofikiri au

wanavyozungumza – lakini, ndivyo kila aaminiye anavyotakiwa

kufikiri! Hatuwezi kuwaeleza watu waliokufa habari za kifo, wala

hatuwezi kutazamia dalili za uhai, matendo na maneno kutoka kwao.

Wala hatupaswi kuwatazamia wao kufufuka toka kwa wafu pasipo

kuisikia sauti inayofufua wafu! Warumi 10 inaweka wazi kabisa

kwamba, hakuna tangazo kwa waliopotea pasipo waliotumwa ili

kutangaza ujumbe. Hakuna kusikia bila tangazo, hakuna imani

pasipo kusikia, na hakuna wokovu pasipo imani (ktk Warumi 10:12-

17)! Katika uhalisi, mambo yanaanzia wapi? Kwenye kutuma na

kwenye kusema! Je, kanisa lenu liko katika shughuli ya kutuma? Je,

linatumia fedha ili kutuma ili ujumbe uweze kusemwa? Uchaguzi

pekee ni kutokutii amri ya Mfalme wa Wafalme na Bwana wa

Mabwana. Je, tutajisikiaje na tutafikiri nini tutakapohudhuria mbele

ya Kiti cha Hukumu cha Kristo kama tulitumia huduma zetu

58

Page 67: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

tukikazia wale “Nyuki Wanaoua” – majengo, bajeti, miili,

vipeperushi, majigambo, na kadhalika?

Kabla ya karne iliyopita kufika katikati, Charles Kingsley

alitembelea visiwa vya New Hebrides huko Bahari ya Pacific ya

Kusini na kushangazwa na ukatili na ulaji watu vilivyokuwepo.

Aliporudi Uingereza aliandika makala kali iliyosema kwamba

serikali ya Uingereza ingefanya huduma muhimu sana kwa binadamu

kama wangetuma merikebu ya vita ili kuwaangamiza hao “washenzi”

waishie baharini kama nzi wasumbufu, kwa kuwa hawakuwa

binadamu na hakuna kitu ambacho kingeweza kufanyika ili

kuwainua kutoka kiwango walichokuwa nacho.

Lakini, walikuwepo watu wengine ambao hawakukubaliana

kabisa na tathmini ya Kingsley. Miongoni mwao alikuwepo Mkristo

aliyempenda Mungu sana, jina lake John Paton kutoka Dumfries,

Uskochi. Paton aliamini kwamba Injili ya Yesu ni nguvu ya Mungu

iletayo wokovu (ktk Warumi 1:16), na kwamba Injili ina nguvu za

kuhuisha, kuwafufua wale waliokufa katika dhambi (ktk Waefeso

2:1). Baada ya safari ndefu, Paton alifika kisiwa cha Tana huko New

Hebrides, na akiwa hatarini daima ya kuuawa, alimhubiri Kristo kwa

hao watu. Namwalika msomaji yeyote mwenye mashaka afanye

utafiti wa matokeo yeye mwenyewe. Paton alipokufa, wenyeji wa

kule walitengeneza kumbukumbu juu ya kaburi yake, iliyokuwa

imeandikwa hivi: “Alipokuja, hapakuwa na nuru. Alipokufa,

hapakuwa na giza”. Wapendwa – leo hii tunaweza kupenyeza kwa 59

Page 68: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

urahisi katika dunia nzima, kwa gharama ndogo kabisa na matatizo

madogo tu ya usafiri. “Tumeketi” juu ya rasilmali kubwa sana

ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kuwainjilisha na

kuwafanya wengi sana kuwa wanafunzi hapa duniani. Maelfu ya

Wakristo, makanisa, na watu waliopotea wangekaribisha na kuitikia

upendo wetu katika nchi za karibu na mbali, nasi mara nyingi

tunaketi tu katika hali ya kujidanganya katika makanisa yaliyokufa

na yanayokufa mahali tulipo. “Mahali ambapo hakuna maono, watu

huangamia.”

Siku ile ile Bandari ya Pearl Harbor iliposhambuliwa na

madege ya kivita ya Japani, mishenari aliyerudi kutoka Mashariki ya

Mbali alikutana na rafiki yake ambaye alikuwa hamwungi mkono

katika anachofanya, naye akimtazama kwa jicho la kejeli na

kuzungumza kwa sauti ya dharau alisema, “Ehe! Unasemaje kuhusu

WaJapani wako sasa?” Yule mishenari akamjibu kwa upole na

utaratibu, na kwa ujasiri kabisa, kana kwamba anamchoma upanga,

“Nashukuru. WaJapani wangu hawajambo, wametulia katika neema

ya Mungu. Kama unazungumza juu ya wale waliopiga mabomu meli

za KiMarekani, hao ni WaJapani wako – wale ambao wewe

unawajibika nao, lakini hukufanya chochote juu yao. Wao ndiyo

wenye kuleta matatizo yote hayo. Lakini WaJapani wangu

wanaendelea vizuri tu, wakidumu katika kumtumaini Bwana Yesu

Kristo”. Wapendwa – vipi kuhusu WaBrazili “wetu”, au WaZaramo,

au WaFipa, au WaDigo, n.k.? Vipi kuhusu WaRundi “wetu”, 60

Page 69: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

WaNyarwanda “wetu”, WaKongo “wetu” na kadhalika? Ndugu

aitwaye Frank Laubach alisema hivi: “Kama Marekani wangetumia

fedha nyingi kwa ajili ya umisheni Japani kabla ya Vita Kuu ya Pili

ya Dunia kama zilizotumiwa kujenga merikebu moja ya kivita kati ya

zile zilizozamishwa hapo Pearl Harbour, pengine hiyo vita

isingetokea kabisa.” Je, wewe unajihusisha kwa namna yoyote katika

kuigusa dunia? Je, unakwenda kama aliyetumwa ili kumfanya Kristo

ajulikane? Kama hapana, ni kwa nini?

William James ambaye ni mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu

cha Harvard Marekani, aliandika juu ya nyumba aliyoishi huko

Chocorua, jimboni New Hampshire akiwa mtoto mdogo. “Aah! Ni

nyumba ya kupendeza sana katika nyumba ulizowahi kuona. Ina

milango kumi na nne, na yote inafunguka kuelekea nje.” Ile kanuni

ya usalama inayowekwa na serikali za mitaa kuhusu majengo yetu ya

kanisa inazungumza mengi sana yenye hekima kwetu sisi. Mkristo,

kanisa, maono yanayomshika mtu, yenye kufanya kazi na milango

yote ikifunguka kuelekea nje ni kitu “cha kupendeza sana”, lakini

kwa kweli, Mkristo mwenye kutazama ndani tu, na kanisa lenye

kutazama ndani tu, inatakiwa liwe likiwa hai na ile hali yake ya

kukata tamaa, kuchanganyikiwa, kushindwa kufanikiwa, na

kushindwa kabisa!

Dunia yetu imekuwa ikipungua ukubwa kama puto ambalo

halina upepo. Ndege siku hizi zinakwenda kasi kiasi cha

kumwezesha mtu asafiri mapema asubuhi kutoka London hadi New 61

Page 70: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

York. Sijawahi kusafiri nchi za ng’ambo bila ya kukutana na idadi

kubwa tu ya wasafiri wenye kuzunguka dunia. Sauti inayonaswa kwa

redio inasikika upande wa pili wa dunia haraka sana kuliko

inavyosikika mwisho wa chumba ambapo maneno yake yanatamkwa.

Tukio linalorekodiwa na televisheni huonekana nchi za mbali wakati

huo huo linapotokea. Tunaishi katika chumba cha mbele cha dunia.

Dunia nzima imekuwa ujirani mdogo tu. Je, tunafanya nini kuhusu

jirani zetu?

[USHUHUDA WA MWANDISHI – Natazama nyuma

kwenye kanisa langu la mwisho nililochunga kwa miaka kumi, na

kujaribu kukumbuka njia tulizotumia ili kutengeneza maono ya dunia

na mguso wa dunia kwa washirika wetu.

(1) Tulitumia mpango tuliouita “weka akiba chenji yako”.

Kila mshirika alitiwa moyo kila mwisho wa kila siku kutoa chenji

yote iliyokuwa imebaki mfukoni na kuitenga kwa ajili ya umisheni,

ila abakize noti moja (au sarafu basi) ya kila kiwango. Mwezi

Desemba, tulifanya “maandamano ya umisheni” na katika hayo

tuliweka sadaka hizo zote mbele za Bwana kwamba aziongeze kwa

ajili ya kufikia mwisho wa dunia.

(2) Tulitumia mpango tuliouita “Dola Moja Kwa Juma Kwa

Ajili Ya Umisheni”. Tulimwomba kila mshirika atoe dola moja zaidi

kwa juma kwa ajili ya umisheni wa kuifikia dunia. (Mmarekani gani

ataona amepoteza kitu?)

62

Page 71: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

(3) Tulitumia mpango wa “Kamati Ya Umisheni Inayotenda

Kazi”. Tuliwachagua washirika wenye maono na roho ya umisheni,

na kuwaomba “waweke dunia mbele yetu” daima. Tulitenga ibada

kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kukazia umisheni – na

wasemaji walikuwa wamishenari (na wake zao na watoto wao), na

kusoma barua za wamishenari, maombi maalum kwa ajili ya

wamishenari “wetu”, na kadhalika.

(4) Tulitumia mpango wa “nyumba ya umisheni”. Tulikuwa

na nyumba mbili ambazo tulizitumia kuwaweka wamishenari

waliokuwa wamerudi nyumbani kupumzika na tukawaomba

“wajaze” kanisa letu kwa habari walizo nazo na ushawishi walio

nao.

(5) Tulitumia mpango wa “kutafiti dunia yetu”. Tuliomba

taarifa za kijiografia, kisiasa, kiuchumi na kadhalika kuhusu mataifa

mengi ya dunia. Sana sana tulijitahidi kujifunza kuhusu maeneo

“yaliyoiva”, yaani, ambayo yanaitikia zaidi Injili.

Katika kufafanua, tulitumia hoja kama hii. Tuseme kwamba

una shamba la matunda. Katika eneo A, mtenda kazi angevuna ndoo

tano kwa saa. Katika eneo B, kuvuna ndoo moja kunaweza kuchukua

masaa matano. Katika eneo C, hakuna cha kuvuna kwa sababu

matunda bado mabichi. Kama una wafanya kazi thelathini leo,

ungewatuma wapi? Nadhani ningetuma ishirini na tisa kwenda eneo

A ili nisipoteze matunda pale. Halafu yule mmoja ningemtuma eneo

B akafanye kinachowezekana hao, na pia kutazama eneo C. Wajibu 63

Page 72: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wa huyu mmoja ungekuwa kunijulisha wakati hayo maeneo mengine

yameiva ili niweze kuwapanga upya wale watenda kazi. Yesu alijiita

“Bwana wa Mavuno” (ktk Mathayo 9:39). Je, hajasimamia vizuri

kazi Yake? Hapana kabisa, ila – kama kawaida – watenda kazi Wake

hawajamsikiliza Yeye. Je, WEWE umekuwa ukimwomba Bwana wa

mavuno kwamba “apelike watenda kazi katika mavuno Yake”?

Kumbuka hivi: “Shamba ni dunia nzima” (ktk Mathayo 13:38).

(6) Tulitumia mpango wa “tuma mishenari”. Mimi kama

mchungaji ningetoshekaje kama Mungu angekuwa hawaiti vijana

kutoka kanisani kwangu au katika eneo langu la ushawishi kwenda

kufanya umishenari katika vituo mbalimbali duniani? Hakika

ningekuwa na mashaka na huduma yangu. Hivi karibuni tulikuwa na

mgeni nyumbani kwetu ambaye amerudi kutoka Mashariki ya Mbali

(katika nchi “iliyofungwa”). Karudi nyumbani kwa muda mfupi tu ili

atafute misaada zaidi na kuongezea ujuzi wake wa kufundisha ili

aweze kuwa “mishenari wa kawaida” (ambayo ni kichekesho maana

maono ya umisheni yamemtawala kabisa!) katika hiyo nchi

anayohudumia. Kiasi cha mwaka mmoja uliopita, alihusika sana na

kumleta kijana mmoja kwa Kristo na kumfanya mwanafunzi, na

tayari, huyo kijana amekwisha leta kumi wengine kwa Kristo – katika

nchi “iliyofungwa”! Huyu “mishenari” alimaliza chuo kikuu akiwa

na shahada ya ufundi umeme, kisha akarudi chuoni tena baada ya

miaka minne jeshini ili kujifunza sayansi ya kompyuta kusudi aweze

kupata nafasi ya kufundisha katika chuo kikuu cha nchi hiyo hiyo 64

Page 73: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mashariki ya Mbali. Ninapoandika maneno haya, amerudi tena

nyumbani, akiboresha taaluma yake ya kompyuta na ujuzi ili awe

mwalimu bora wa chuo kikuu. Kwa nini? Kwa sababu amepata

maono ya kufanya wanafunzi yenye kuigusa dunia. Aliniambia tena

juu ya safari yake katika mpango wa kufanya watu kuwa wanafunzi

(na jinsi anavyoshukuru) pamoja na kuambukizwa maono ya kuigusa

dunia yaliyokuwepo katika kanisa nililokuwa nalichunga.

(7) Tulitumia mpango wa “kutuma wamishenari wa muda”.

Sasa hivi dunia iko wazi kwa ajili ya upenyo wa umisheni wa muda

wa vikundi vidogo vidogo vya watu kutoka makanisa mbalimbali ya

nchi za Nje. Bado mlango wa dunia uko wazi. Mto wa kudumu wa

Wakristo wanaokua, wenye furaha, waliohamasika, wenye kugusa

dunia, unapaswa kuwa ukielekea kwenye maeneo mbalimbali hadi

miisho ya dunia. Baadhi ya “makanisa makubwa” yanapaswa kuwa

yanatuma haidhuru watu 200 hadi 500 kila mwaka kwenda kwenye

miradi ya umisheni ya kuzunguka dunia. Mimi binafsi nimehusika

katika safari kubwa zaidi mia moja za kimisheni huku nikiendelea na

ratiba yangu nzito kabisa nyumbani. Hivi karibuni, mlei mmoja

aliyekuwa anatembelea mji wetu aliniambia hivi: “Ningeogopa sana

kwenda nchi yoyote nje ya Marekani”. Kuogopa? Hilo halipaswi

kukaa katika akili ya Mkristo aina yoyote. Hebu jisomee 2Wakor.

11:23-33, uone ni hofu kiasi gani iliyotawala maisha ya Mtume

Paulo. Cha kusikitisha ni kwamba, rafiki yangu alikuwa anakiri

kushindwa kwa kanisa lake kumwingizia Agizo la Kristo.65

Page 74: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

(8) Tulitumia mpango wa “jifunze dini za ulimwengu”. Huu

unajieleza wenyewe, na kila ilipowezekana, tulitafuta kusikia

shuhuda kutoka kwa watu waliokuwa wahusika katika dini zingine,

wakaokoka.

(9) Tulitumia mpango wa “onyesha umisheni”. Wakati Agizo

Kuu linapolipuka katika akili ya mchungaji, kwamba ni nguvu ya

Injili, hakika atawashirikisha watu wake jambo hilo katika kila

nafasi. Atajifunza mahusiano ya kila itikadi kwa mpango huu.

“atatoa damu” ya mkazo huo katika kila mahubiri na kila nafasi

anayopata ya kutangaza Injili. Atawafanya watu wake wajue

kujitolea kwa umisheni kwa waaminio wenye maono. Yeye

mwenyewe atakwenda kwenye maeneo mengi ya umisheni kiasi

anachoweza, na kuwachukua ndugu zake Wakristo wengi kiasi

anachoweza, ili waende naye. MWISHO WA USHUHUDA]

Ewe Mkristo – je, “unaota ndoto” na “kuona maono” kuhusu

kuifikia dunia? Kwa Kiyunani – “ta ethne” – makundi yote ya watu,

mataifa yote – ng’ambo ya barabara na duniani kote. Je, Mungu

amekuvamia kwa “Shambulizi la Ramani” – ili “ubebe” dunia nzima

kwa ajili Yake? Je, unafuata mkakati wa Mwokozi, au umekubaliana

na mbadala wa kijanja sana wa Shetani?

Kongamano kuhusu Kristo na kazi Yake ya ukombozi

liitwalo “Summit III” lilifanyika mjini Chicago mwezi Desemba

mwaka wa 1986. Dakta Ralph Winter, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu

wa Kituo cha Marekani cha Umisheni Duniani, alihudhuria. 66

Page 75: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mwishoni mwa kongamano, yeye alikuwa miongoni mwa watu

wawili waliotakiwa kutoa maitikio yao kuhusu kiini na mambo

yaliyosemwa. Katika itikio lake, Dakta Winter alionyesha kwamba

maelezo yote hayakuwa yamegusia kazi ya Wakristo na Kanisa ya

kumshuhudia Kristo na kazi Yake kwa dunia. Yaani, wajibu wa

waaamini kushuhudia dunia haukuwa umetajwa.

Baada ya majibu yake, mwenyekiti wa kikao ambaye naye ni

Mkristo msomi maarufu na anayejulikana sana, alimtazama Dakta

Winter kwa macho ya kejeli na kusema, “Sawa. Tulipaswa kujua

kwamba ungetaja kitu kuhusu jambo lako unalopenda sana, ukipewa

nafasi.” Swali: Je, kuigusa dunia ni jambo wanalopenda mashabiki

wachache tu wenye mzigo, au linapaswa kuwa mapigo ya moyo wa

kila – KILA – Mkristo? Hivi kweli tunaweza kukiri kwamba Yesu

Kristo ni Bwana na wakati huo huo tupuuze wajibu pekee aliotupa

sisi kama amri ya kusonga mbele? Zaidi – je, kundi lolote la

Wakristo linaweza kujadili kwa usahihi au inavyotakiwa Nafsi na

Kazi ya Kristo bila ya kutaja kuhusu mkazo Wake kwa dunia nzima?

Ni kitu kinachotupasa sisi kutafakari maswali hayo mpaka mwisho

kabisa, kwenye kupata jibu lenye kuridhisha. Ukweli ni kwamba kila

Mkristo anapaswa kuwa Mkristo wa dunia nzima. Yeye anapaswa

kuwajibika kuwa”ambukiza” wengine, kuombea wamishenari,

maeneo ya umisheni, na Wakristo wengine, anapaswa kuivamia

dunia, anapaswa kupata na kutawanya habari, na kwa njia hiyo

67

Page 76: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kumkaribisha Mungu aongeze maisha yake kwa ajili ya kuifikia

dunia.

Rafiki zangu, dunia inawaka moto – moto wa mabadiliko,

vurugu, hofu, mapinduzi, fujo, vita – mambo yanayofaa kabisa kwa

ajili ya Injili. “Mapinduzi kila dakika” yanatokea. “Je, si kitu kwenu,

enyi wote mnaopita tu?”

Hadithi moja maarufu sana katika kitabu cha Washington

Irving kiitwacho Sketch Book ni ya mtu aliyeitwa Rip van Winkle.

Huyu jamaa alilala usingizi wa miaka ishirini – ili aepukane na hali

yake ya kutokuwa na faida, uzembe, pamoja na mke aliyekuwa

mkorofi. Alipopata usingizi na kulala, jimbo lake la New York

lilikuwa koloni la Uingereza, lililokuwa linapigania haki na uhuru wa

watu kujitawala ili kupinga ukandamizaji. Lakini, “ukandamizaji

mkubwa” ule haukumsumbua Rip, uliokuwa unamsumbua ni ule

mdogo, wa mahali pamoja, wenye ubinafsi wa nyumbani kwake.

Lakini kwa kulala mara moja tu na kwa muda mrefu, Rip

alikombolewa kutoka ukandamizaji wote. Ee Mkristo, unasikiliza

hilo? Hadithi hii ya Rip ni mfano uliofichika. Wachungaji

wanateseka kutokana na ukandamizaji mdogo, wa mahali pamoja, na

mara nyingi huingia katika usingizi uletwao na “dawa” (hakuna

maono, hakuna nguvu, hakuna kuigusa dunia) kiasi kwamba wala

hawana habari na ukandamizaji wa duniani, ambao ni utawala wa

nguvu juu ya dunia nzima unaofanywa na Shetani (ktk 1Yohana

5:19b). Sasa, ikawaje katika hadithi? Rip akalala usingizi mzito, na 68

Page 77: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

hakuamka mpaka baada ya miaka ishirini. Akiwa amelala, vita ya

Kimapinduzi ikapiganwa. Rip alipokwenda kulala, alikuwa

anatawaliwa na George wa Tatu wa Uingereza – mfalme.

Alipoamka, alikuwa anaishi katika jamhuri ya kidemokrasia, na

George mwingine – Jemadari George Washington – alikuwa

anajiandaa kutawala. Rip Van Winkle alifunga macho yake na kulala

wakati wa mapinduzi! Je, Mkristo, unasikia hilo? Mtu hawezi kujua

anachokosa akiwa amelala. Ndiyo maana Shetani anataka wewe

ujione mwenyewe – utazame kujisikia hatia kwako, ujali maombi

yako, kusoma Biblia kwako, imani yako tu, ushuhuda wako tu,

uaminifu wako tu, huduma yako tu, kanisa lako tu, dhambi zako tu,

hofu zako tu – Ukristo wa kibinadamu, wenye kutafuta kujikimu.

Amka ewe Mkristo, umtazame Mwokozi wako, utazame Biblia yako,

utazame dunia yako, utazame nafasi na fursa ulizo nazo kupitia

macho mapya kabisa!

Mbadala Wa Shetani

Turudi kwenye hoja yetu ya tatu kuhusu Agizo, katika

Mathayo 28:18-20. Tumekuwa tukitazama kwa upana sana mkakati

wa Mwokozi chini ya kichwa hiki: “Panua Maono Yako”. Sasa, hebu

kwa kifupi tutazame mbadala anaotoa Shetani hapa. Daima Shetani

anarudisha usikivu wetu kwenye mapambano yetu sisi, kujikimu

kwetu, taasisi ya mahali ambapo tunatumika (na mafanikio yake), na

kadhalika. Daima anatafuta kupunguza maono yetu yawe kitu cha 69

Page 78: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kawaida, yaendane na taasisi yetu au ubinafsi wetu, na kwa njia hiyo

wingi wa watu duniani wasipate nafasi ya kusikia hata habari za

Kristo na Injili. Yesu alitupa mpango wa kuigusa dunia nzima, lakini

tunakubali kupokea mbadala mdogo, wenye kupotosha, na usiozaa

matunda aina yoyote. Je, wewe unafuata mpango gani, mkakati wa

Mwokozi ambao kwa huo, wewe – naam, WEWE – unaweza kuifikia

na kuigusa dunia, au mbadala wa Shetani wenye kufanikisha

punguzo linalodumu la jamii ya Kikristo na kuhakikisha kwamba

mabilioni ya watu watapotea pasipo kupata habari?

4. KUWASHUHUDIA WAHUSIKA

Hoja ya nne katika Agizo Kuu ni Kuwashuhudia Wahusika.

Agizo Kuu lina maneno saba ambayo ni matendo, lakini amri pekee

ni “kuwafanya watu kuwa wanafunzi”. Katika fungu zima (Mathayo

28:16-20), neno tendaji pekee ni hilo – “kuwafanya watu kuwa

wanafunzi”. “Uinjilisti” huu ni wa aina fulani maalum – si kupata

watu “watakaokata shauri kumfuata Kristo” bali ni kupata

“wanafunzi”watakaoipindua dunia.

Mkakati Wa Mwokozi

Fikiri jambo hili kwa makini sana: Kwa kuwa ni amri ya

Yesu – Agizo Lake pekee kwa Kanisa Lake kwamba Lisonge Mbele

– bila shaka haiwezekani kuwa mwanafunzi wa kweli kama hufanyi

watu kuwa wanafunzi – kulingana na matakwa Yake na mkakati 70

Page 79: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Wake. Kipengele hiki cha “kufanya wanafunzi” si nyongeza kwenye

mpango wa Yesu, bali ndiyo amri yenyewe. Swala si kupata

“waongofu” bali ni kupata “wanafunzi”. Basi, mkakati wa Mwokozi

hapa si kuokoa roho za watu tu, bali ni kufanya watu kuwa

wanafunzi. Maana yake ni kwamba, kile ambacho Yesu alifanya kwa

wanafunzi Wake Mwenyewe, aliwaagiza nao wakafanye kwa

wengine. Walipaswa kutenda mkakati ule ule, nidhamu zile zile, na

taratibu zile zile kwa wengine, ambazo Yesu Mwenyewe alikuwa

amezitumia kwao. Rafiki yangu mpendwa: Hebu soma fungu hili lote

polepole, kwa makini sana, na katika hali ya maombi mara kadhaa

kabla ya kuendelea mbele. Tutalitazama neno ”mwanafunzi” kwa

upana zaidi hapo baadaye.

Mbadala Wa Shetani

Nini mpango mbadala wa Shetani kuhusu kufanya watu kuwa

wanafunzi? Sehemu moja ya mpango wake ni kuhakikisha kwamba

waliopotea wanaendelea kupotea, au, kuwazuia kuokoka. Sehemu ya

pili ni kuwazuia waaminio kuwa wanafunzi wenye maono ya dunia

yote, na wanaotaka kuigusa dunia yote. Au basi, kama waaminio

wakiwa wanafunzi, kusudi la Shetani ni kuwafanya wawe wanafunzi

wa wazo lao wanalopenda tu, au utaratibu wao wanaopenda tu –

mradi kitu chochote ili kuwazuia wasiwe wanafunzi wa kweli,

wanaofanana na Kristo, kama inavyotakiwa na Agano Jipya.

71

Page 80: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

5. KUWAHUSISHA WALIOSHUHUDIWA

Hoja ya tano katika Agizo Kuu ni Kuwahusisha

Walioshuhudiwa. “Mkiwabatiza katika jina la Baba, na Mwana, na

Roho Mtakatifu”.

Mkakati Wa Mwokozi

Mkakati wa Mwokozi kwa ajili ya kila aaminiye ni

kujitambulisha na Yesu Kristo kwa njia yenye kudhihirisha kifo kwa

kila kitu ambacho huyo mwamini aliishi kwa ajili yake kabla ya

hapo, na ufufuo wenye kumaanisha kwamba sasa anamwishia Kristo

tu. Kwa kubatizwa, amwaminiye Kristo anakiri kufia wakati wake

uliopita – dhambi zake za zamani, ubinafsi wake wa zamani, motisha

yake ya zamani, mtindo wake wa maisha wa zamani, jinsi

alivyokuwa anafikiri zamani – wakati wake wote wa zamani, na

anakubali kwamba sasa ana lengo na kusudi moja tu la maisha –

Kusudi lenye kutawala kila kitu na kumwishia Huyo Yesu Kristo

mtukufu. Ubatizo ni kuingia katika kaburi la maji, ambayo ni picha

ya kuingia katika kifo cha Kristo, na kufufuka tena kutoka kaburini

humo, ambayo ni picha ya kushiriki pamoja na Kristo katika

kufufuka Kwake. Basi, ubatizo hudhihirisha kujiunga kikamilifu

kabisa na kuhusika kikamilifu kabisa katika uanafunzi wa Kikristo.

Ukweli kwamba unafanywa “katika jina la Baba, na Mwana, na

Roho Mtakatifu” maana yake ni kwamba mwamini huyo anaingizwa

katika kuhusika kikamilifu katika Mpango kamili na Nafsi ya 72

Page 81: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mungu. Hakuna kitakachohifadhiwa katika maisha ya mtu kwa ajili

ya makusudi yake mwenyewe. Kifo kimefutilia mbali uwezekano

huo. Ufufuo umesababisha mwelekeo mwingine kabisa kwa ajili ya

maisha yake. Sasa, kila rasilmali na uwezo ulioko katika nafsi yake

iko kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo.

Mbadala Wa Shetani

Katika hoja hii ya Agizo Kuu, nini mbadala anaotoa Shetani?

Shetani anatafuta kusukuma mawazo ya wanadamu kwenye sehemu

mbili, ambazo zote ni zaidi ya kawaida. Kwa upande mmoja,

anasema ubatizo ni zoezi la kimwili, lisilofanya chochote rohoni, na

ambalo ni taratibu tu. Basi, halina maana yoyote. Kwa hiyo – kwa

mfano – dhehebu la Quakers halibatizi kabisa watu – kwa sababu

hiyo. Kwa upande wa pili, Shetani analeta wazo kwamba ubatizo ni

muhimu sana kuliko kitu chochote, na kwamba wenye dhambi

hawawezi kuwa na uzima wa milele wasipobatizwa. Basi – kwa

mfano – madhehebu mengi tu yanafanya ubatizo kuwa ndiyo jiwe

kuu la pembeni kwa habari ya wokovu. Hapo katikati, kuna

wanaoshikilia wazo dhaifu kabisa kwamba ubatizo ni “ishara tu – ni

mfano” – kama makanisa mengi, pamoja na WaBaptisti.

Mwanamume mmoja alifika kazini siku moja akiwa

amevimba macho na uso mzima. Mwenzake wanayefanya pamoja

akamwuliza, “Vipi? Ulipatwa na nini?” Jibu likatoka, kwa sauti

ndogo sana, “Mke wangu alinipiga”. Yule mwenzake akasema, 73

Page 82: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“Unataka kuniambia uliruhusu mwanamke tu akutendee hayo?”

Jamaa alijibu hivi, “We! Mke wangu si ‘mwanamke tu’!” Wapendwa

– tunaposema kwamba agizo lolote la Yesu ni “mfano tu”, si

tunaunga mkono upande mbadala wa Shetani? Hakuna chochote

alichowahi kusema Yesu ambacho ni “kitu tu”! Je, umeona ukubwa

wa kuungana kwako na Yesu Kristo na kuhusika kwako na Yesu

Kristo?

6. KUWAELIMISHA NA KUWAJENGA WALIOJIUNGA

Hoja ya sita katika Agizo Kuu ni Kuwaelimisha na

Kuwajenga wote waliojiunga. “Mkiwafundisha kuyashika (kutii)

yote niliyowaagiza ninyi.” Hapa tena, neno tendaji ndiyo

linalotangulia. Linaonyesha shughuli inayoendelea, ya kudumu,

isiyokoma, isiyokatizwa.

Mkakati Wa Mwokozi

Hakuna wakati wowote katika maisha yangu kama Mkristo

ambapo siwi katika kufundisha! Iwe ni kwa mfano wa makusudi,

kwa tamko la wazi, kwa kufuata mtaala ulioandaliwa, kwa ushawishi

wa kimya, katika hali iliyopangwa au isiyopangwa, mimi ninapaswa

kuwa mwasilishaji wa Yule ambaye ni uzima wangu. Kila aaminiye

anapaswa kuwa mwalimu, awe na karama ya kufundisha au asiwe

nayo. Njia za mawasiliano zilizoko leo ni nyingi mno na zenye

kutenda kazi vizuri kabisa kiasi kwamba Mkristo hana udhuru wa 74

Page 83: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

aina yoyote wa kutokufundisha. Kuna kanda za sauti ambazo zina

kila aina ya mada ya Kikristo unayoweza kutaka, zilizoandaliwa na

wataalamu wa mawasiliano Wakristo wanaomcha Mungu. Kuna

mikanda ya video ya hali ya juu sana na yenye mada nzuri tu. Kuna

maktaba kubwa sana za vitabu ambavyo vinaweza kupatikana kwa

kuazima au kununua. Kuna chapisho mbalimbali zenye makala

nyingi tu za mafundisho, na kadhalika. Nyumba ya kila Mkristo

inapaswa kuwa ghala na kituo cha kusambaza vitu hivyo vya

kufundishia. Kila Kanisa la Kikristo linapaswa kuwa kituo cha

kusambaza kweli ya Injili, kwa kutumia kila mbinu iwezekanayo na

kila mwanachama apatikanaye ili kupenya na kuingia katika mioyo,

nyumba, jumuiya mbalimbali na kadhalika, kwa ajili ya kufikisha

kweli kamili ya Injili. Kila Mkristo anapaswa kuwa makini kwa ajili

ya kufanya watu kuwa wanafunzi na kufundisha jinsi ya kufanya

watu kuwa wanafunzi, bila kikomo. Maono ya dunia nzima na

huduma kwa dunia nzima vinapaswa kuwa mbele za kila Mkristo na

kila kanisa. Nini lengo la yote hayo? Ili kila Mkristo na kila kanisa

kupata moyoni mwake kile kilicho moyoni mwa Mungu – kugusa

dunia nzima kwa kuwajenga na kuwasambaza Wakristo wenye

maono ya dunia nzima, na watakaoigusa dunia yote.

Mbadala Wa Shetani

Shetani ana mbadala gani kwa mpango huu? Kwanza,

anatafuta kuzuia mafundisho yenye upako ya kweli kuu za Biblia. 75

Page 84: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Halafu anatafuta kuwafanya Wakristo “waonja mahubiri”. Kwa hali

hiyo, hawataathirika na Ukristo wa kweli kwa sababu wamepokea

chanjo ndogo tu. Au anawafanya waaminio kuwa wachambuzi na

wachuja ukweli, wakidhani kwamba wanaweza kupambanua na

kutambua ukweli pasipo msaada wa Roho Mtakatifu. Basi,

wanajifanya wakuu juu ya kweli na juu ya mwalimu afundishaye

kweli. Neno hupokonan katika Agano Jipya, yaani “utii”, maana

yake ni “kusikia chini ya,” na picha itokanayo na neno hilo ni mtu

anayesikiliza kweli ya Mungu akiwa kwenye hali ya kudumu ya

unyenyekevu. James M. Barrie alisema hivi: “Maisha ni somo moja

refu sana, la unyenyekevu”, na ni kweli kabisa hasa katika maisha ya

Kikristo. Lakini, mkakati wa Shetani ni kufutilia mbali uwezekano

huu wa kusikiliza kweli kwa unyenyekevu, na basi kumfanya

mwamini arudie maisha yake ya kujitawala mwenyewe, kwa kujijali

mwenyewe, na kujipa umuhimu.

Mpango wa Shetani kwa ajili ya mwamini uko wazi sana kwa

Mkristo msikivu na mwenye kutambua mambo. Hebu nitumie neno

lenye kuonyesha mwisho au hatima ya mpango wa Shetani. Ni neno

“kuning’iniza mbele ya”. Shetani anafurahi sana wakati aaminiye

anapokwenda kanisani Jumapili kwa Jumapili na kuruhusu kweli

ipite mbele yake bila kuifanyia chochote. Anapofanya hivyo mara ya

kwanza, bila kupokea kwa unyenyekevu kweli hiyo iingie katika

udongo laini wa moyo mnyenyekevu, mtii na wenye kusikia,

anakuwa amepuuza kweli hiyo. Ni rahisi kuona kwamba hiyo ndiyo 76

Page 85: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kawaida ya mshirika wa kawaida kanisani Jumapili kwa Jumapili,

juma baada ya juma, mwezi baada ya mwezi, na mwaka baada ya

mwaka. Amekwisha amini kwamba kuhudhuria kanisani na

kusikiliza mahubiri NDIYO maisha ya Kikristo. Jambo hilo

likiendelea hadi mtu asiweze kukubaliana na ukweli wenyewe kwa

unyenyekevu, kuvunjika na utii katika kuomba, Mungu huingia

katika hali hiyo na kumgeuzia msikilizaji kibao. Anakuwa “mkaa

kitini” asiye na uhai, asiye na nguvu, asiye na maono katika kanisa la

mahali. Anaweza kuleta matatizo kwa kanisa na mchungaji wake –

au asilete – kutegemeana na kiwango cha kujisikia hatia kwake juu

ya jinsi alivyo. Ni hivi: Watu waliokuwa wanakwenda kanisani kila

wakati na kila mara “wakaushika” ukweli ndiyo waliokuwa na hatia

ya mawazo ya kurudi nyuma na hatimaye dhambi isiyosameheka. Ni

wale Waandishi na Mafarisayo, watu waliokuwa bora sana na wenye

kushika dini sana katika siku zao (ona Mathayo 12). Kwa hiyo,

Shetani anataka sisi tuwe “Wakristo wa kwenye foleni ya chakula”,

ambao daima wanatazama na kupima ukweli, wenye kuchagua na

kuchukua kulingana na kweli zetu tunazopenda, na wahubiri wetu

tunaowapenda na mahubiri yetu tunayopenda. Basi, hoja ya sita

katika Agizo Kuu inabatilishwa kwa mkakati mbadala wa Shetani.

Ewe Mkristo – uko upande gani? Je, unafuata mkakati wa

Mwokozi kwa juhudi zote za roho yako yenye unyenyekevu, au

“unakanyaga na kuchafua nyua za Mungu” kama msikilizaji wa siku

77

Page 86: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

zote ambaye hazai matunda kwa aina yoyote katika kutimiza Agizo

Kuu?

7. TUMTARAJIE KUTENDA KAZI

Hoja ya saba katika Agizo Kuu ni Kumtarajia Yesu Kristo

Kutenda Kazi. “Tazama, Mimi niko pamoja nanyi siku zote, hata

mwisho wa dunia”. Neno “tazama” ni baada ya neno “enendeni”.

Ahadi ya uwepo maalum wa Kristo katika mstari huu ni kwa wale tu

ambao wanatoa na kumimina maisha yao katika shughuli zote

zilizotajwa, ili kutimiza Agizo Kuu. Yaani, huwezi kudai kihalali

hiyo ahadi kama hufuati huo mpango. Hatutapata nguvu ya Agano

Jipya mpaka tutakapofuata taratibu za Agano Jipya. Basi, maombi

yetu mengi kwamba tupewe Roho Mtakatifu na nguvu Zake

yanapotea tu. Ni hivi: Tunataka hizo nguvu kwa ajili ya kitu gani?

Kwa nini tunaomba tujazwe Naye? Ni ili Mungu akubaliane na

mipango yetu? Au ni ili tukuze kujulikana kwetu? Au ni ili tupate

kiasi fulani cha mafanikio katika juhudi zetu kwa ajili Yake?

Usisahau jibu la Mungu kwa maombi ya yule mhubiri maarufu:

“Mwanangu! Huhitaji nguvu Zangu kwa mipango midogo kama

yako.”

Mkakati Wa Mwokozi

Nini mkakati wa Mwokozi? Kuhusika Yeye Mwenyewe

Binafsi katika kila juhudi za kila mtu mwenye kufanya watu kuwa 78

Page 87: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wanafunzi, na kumpaka maishani mwake na katika shughuli zake

kwa nguvu kuu za Roho Mtakatifu. Yesu alisema, “Na tazama, Mimi

Mwenyewe (neno hilo ni la mkazo sana) niko pamoja nanyi siku

zote, mpaka mwisho wa wakati.” Kila Mkristo ni mwakilishi

asiyefaa, asiyeweza, asiyetosheleza, asiye na nguvu wa Yesu Kristo,

kama hii ahadi haitimii. (Hiyo si ahadi tu, ni kitu halisi – ni ukweli).

Lakini kila mtu anayeanza katika kila eneo la utendaji anajua jinsi

ambavyo inatia moyo na kumwezesha sana wakati anapokuwepo

yule mtaalamu pamoja naye. Je, Yesu alimaanisha nini aliposema,

“Mimi Mwenyewe niko pamoja nanyi”? Alimaanisha kwamba

Uwepo halisi wa Yesu uko pamoja na yule mwenye kufanya

wengine kuwa wanafunzi. Roho Mtakatifu anaeleweka vizuri zaidi

kuwa ni “Nafsi nyingine” ya Yesu. Alimaanisha kwamba Uwepo wa

Yesu wa kudumu, unaokaa utakuwa pamoja na yule mwenye

kufanya watu kuwa wanafunzi. Hakuna wakati, hakuna hali, hakuna

mazingira ambapo mwenye kufanya wanafunzi ataishi katika

kutimiza Agizo la Kristo ambapo hatakuwa na Uwepo wa Mwana wa

Mungu Mfufuka, Mwenye Nguvu. Siku haitafika ambapo Bwana

Yesu hatakuwepo kwa nguvu nyingi sana katika maisha ya mtakatifu

Wake anayefanya watu kuwa wanafunzi. Alimaanisha kwamba

mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi anao Uwepo tendaji wa

Yesu pamoja naye wakati wote. Yesu hayuko nasi kama mwenzi

mkimya au asiyejulikana au asiyefanya chochote. Mstari wa mwisho

wa Injili ya Marko unasema kwamba “walikwenda na kuhubiri kila 79

Page 88: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mahali, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha Neno kwa

ishara” (ktk Marko 16:20, TLR). “Ishara” zinaweza kuwa za aina

mbalimbali na za hapa na pale, lakini Uwepo wa Yesu unadumu

wakati wote!

John Wesley White alisema hivi: “Ukijawa ‘enendeni

takatifu’, umejazwa na ‘Roho Mtakatifu’.” Mara nyingi watu

hutumia ahadi hii nje ya mantiki yake. Wakiwa katika mambo

magumu, wanautumia mstari huu kusema kwamba Bwana yuko

pamoja nao daima. Lakini, mstari huu si dawa kwa ajili ya nyakati

ngumu. Kuna mistari mingi sana katika Maandiko, ya kutumiwa kwa

kusudi hilo – si huu – isipokuwa kama wakati mgumu unatokana na

kutimiza Agizo Kuu. Huu mstari ni kwa ajili mwenye kufanya

wanafunzi. Yaani – kama utatamani mahali pa kumpata Yesu leo,

lazima utafute mahali ambapo wanafunzi wanazaliwa. Yeye hupita

kando ya makanisa mengi tu ambayo yanahubiri mahubiri (hata

mahubiri mazuri sana), mahali ambapo watu wanaomba (tena

maombi ya dhati kabisa), na mahali ambapo makundi yanakusanyika

(na yanaweza hata kuwa makundi makubwa sana) na kwenda Zake

kuthibitisha na kuweka upako juu ya mtu yeyote anayefanya

wanafunzi kulingana na utaratibu Wake wa Agano Jipya.

Je, ungependa kujua Yesu atahudhuria ibada wapi Jumapili

ijayo? Mtafute katika kanisa ambapo wanaandaliwa watu wenye

maono ya dunia, wenye kuigusa dunia ambao nao watazalisha

wengine wa aina hiyo. Kumbuka: Si “Wakristo wazuri” tu, kwa 80

Page 89: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

sababu huo ni Ukristo wa kibinadamu. Yesu hahudhurii na kutia

mafuta makanisa mengi na maisha ya waamini wengi kwa sababu

moyoni mwao hawana kile kilichoko moyoni mwa Mungu,

“kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi katika mataifa yote”. Kwa

upande mwingine, wakati Mungu anapoliona kanisa lenye kufanya

watu kuwa wanafunzi (kuwajenga wanafunzi kwa kufuata utaratibu

Wake na kwa kumtegemea Yeye Mwenyewe kikamilifu kabisa

katika shughuli hii), anajihusisha kikamilifu kabisa hapo. Anaingia

ndani, kulia, juu, chini na kwa kila njia anasisimka na kufurahia sana

jambo hilo – na anajiunga na kanisa hilo mara moja. Naye atakutana

na watu wa kanisani humo muda wote anaoweza kuwa hapo na

kufurahia.

Hatuhitaji uthibitisho mkubwa zaidi wa ukuu wa Agizo

kuliko kuona maneno ambayo Yesu alitanguliza na kufuatisha.

“Mimi nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” Halafu,

“Tazama, Mimi Mwenyewe niko pamoja nanyi siku zote, mpaka

ukamilifu wa dahari.” “Siku zote” – za hatari au usalama, siku za

kushindwa au za ushindi, za uhuru au kuzuiwa, za amani au za vita,

za kupanda au za kuvuna, za kujifunza au za utendaji. Hakuna siku

hata moja ambapo kweli hii haitatimia.

Wakati Fretyof Nansen, mgunduzi maarufu wa Norway

aliposafiri mwaka wa 1896 kwenda kutoboa theluji iliyoko kaskazini

mwa dunia ili kujifunza na kutafiti mwendo wa theluji hiyo, kila mtu

alijua ameingia kwenye shughuli ngumu na hatari. Alichukua idadi 81

Page 90: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kubwa tu ya njiwa wenye uwezo wa kusafiri kurudi alikotoka, na

kupeleka habari. Alipofika kila kituo kikubwa cha safari hiyo hatari,

alimwachilia njiwa mmoja akiwa na ujumbe mguuni. Kitabu cha Bibi

Nansen cha kumbukumbu nyumbani kilikuwa na maneno haya:

“Nilifurahi sana kila mara nilipomwona njiwa mmojawapo akiwa

ametua dirishani kwangu. Nilipomwona huyo ndege, nilijua kwamba

mume wangu yu hai na ananikumbuka.” Miaka elfu mbili na zaidi

iliyopita, Bwana Yesu Kristo aliyetukuzwa alimwachilia Njiwa wa

Mbinguni – Roho Mtakatifu – nafsi yake Nyingine – kuja duniani

Siku ile ya Pentekoste – kuachilia kwa Nguvu kamili ya Mungu kwa

ajili ya utimizwaji wa Mpango wa Mungu. Tunapomtii na kuona

utendaji wa Roho Wake mwenye nguvu, tunajua Yu hai na ni mzima,

na anatukumbuka, na yuko pamoja nasi akitenda kazi. Ni shauku

Yake na raha Yake kutenda hivyo wakati wote. Huo ndiyo mkakati

Wake.

Mbadala Wa Shetani

Nini mbadala wa kijanja wa Shetani hapa? Yeye hujaribu

kutupotosha ili tujenge taasisi na mambo mengine ambayo si ya

maana sana, na kwa njia hiyo kuondoa utendaji wa Roho Mtakatifu

pamoja nasi. Au, anajaribu kutushawishi kwamba tuko peke yetu

kabisa, wala hakuna anayesikia tunapoomba. Anajaribu kutufanya

tusiojua habari za Roho Mtakatifu, au kutomjali Yeye, na uwepo

82

Page 91: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wake na nguvu Zake, au kujishughulisha kutafuta ujuzi mbadala,

wenye kuwa na msingi wake juu yetu wenyewe.

Mpendwa Mkristo – unaangukia upande gani katika hili?

Agizo Kuu, au Kuacha Kukuu?

Tumelitazama Agizo ambalo linaamua wajibu au majukumu

yetu. Kumbuka, ndiyo amri ya kusonga mbele pekee aliyowahi kutoa

Bwana Yesu kwa Kanisa Lake. Lakini, Shetani siku zote anajaribu

kuupinga huo Mpango wa Mungu kwa kuhakikisha mpango wake

unatenda kazi. Popote ambapo Kanisa LINAPOTOSHWA na kuingia

katika ujenzi wa taasisi, au katika kujihifadhi, au katika kufanya

“Wakristo wazuri” tu, mkono wa Shetani ni wazi hapo. Kwa hali

hiyo, Agizo Kuu limekuwa “Kuacha Kukuu”. Jamani – wakati

haujafika turudishe Agizo Kuu mahali pake?

Nilifundisha somo hili kuhusu Agizo Kuu miaka kadhaa

iliyopita, katika darasa la wenye ndoa vijana. Mwishoni mwa somo,

mama mmoja kijana mwenye ndoa aliomba sala hii ambayo niliitoa

kwenye kanda baadaye.

Baba! Ninashukuru kwamba kuna mtu – mwanadamu –

mbinguni kwa ajili yetu wakati huu. Na kama YUPO na BADO ni

mwanadamu kweli, basi bila shaka anazo hisia za kibinadamu.

Anaweza kufurahia, kushukuru, kuumia na kuteseka. BILA SHAKA

MOYO WAKE UNASIKITIKA anapotafuta kuendeleza kazi Yake

hapa duniani, lakini anaona mwili Wake wa hapa duniani ukifuata

83

Page 92: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mkakati ambao ni KINYUME KABISA kwa kila hali, na ule mkakati

aliowapa wanafunzi Wake.

Je, ni Agizo Kuu au ni Kuacha Kukuu? Wakati haujafika

turudishe Agizo Kuu katika nafasi yake?

84

Page 93: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 3Wazo Lenye Kuamua Njia Tutakayotumia

“Mkawafanye watu kuwa wanafunzi ….” Mathayo 28:19

Kama kweli tunataka kuwa watii kabisa kwa Yesu Kristo na

kwa Agizo Lake Kuu, ni lazima tujilazamishe kuwa sahihi kabisa

katika kuelewa Agizo hilo. Hatuwezi kujiruhusu starehe ya ujinga au

kutokujua ipasavyo. Tunaishi kwa “kila neno litokalo kinywani mwa

Mungu” na hakuna mahali popote ambapo neno hilo linatufunga

kama kwa habari ya Agizo Kuu. Kwa kuwa amri pekee katika Agizo

hilo ni “kuwafanya watu kuwa wanafunzi”, maswali kadhaa muhimu

sana yanapaswa kuulizwa. La kwanza ni hili: Mwanafunzi ni mtu wa

namna gani? La pili ni, Nini maana ya kuwafanya watu kuwa

wanafunzi? Na la tatu ni hili: Tunafanyaje hilo? Siwezi kufikiri

maswali mengine ambayo ni muhimu kwa ajili ya kanisa la leo.

Vinginevyo, tunaendelea kufuata kwa ujinga kabisa “mbadala wa

Shetani” badala ya kutii mkakati wa Mwokozi.

Tumeona jinsi ambavyo maono ni muhimu kwa ajili ya

utendaji wa kiroho, na tumetazama kwa makini sana Agizo Kuu,

ambalo ndilo lenye kutupa sisi wajibu wetu. Sasa, tutachunguza

dhana au wazo lenye kuamua mbinu au njia tutakayotumia. Dhana ni

hiyo ya kufanya watu kuwa wanafunzi. Ili tuelewe dhana hiyo

kikamilifu kabisa, tunahitaji kuchunguza maneno yenye kuhusiana

85

Page 94: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

nayo. Baadhi yake yanapatikana na yanatumika katika Biblia, na

baadhi yake yanatokana na maneno yanayotumika katika Biblia na

jinsi yanavyotumiwa.

KUFANYA WANAFUNZI

Dhana inayoamua njia yetu ni uanafunzi. Yesu aliamuru hivi:

“Wafanyeni watu kuwa wanafunzi.” Maneno kadhaa inabidi

tuyatazame vizuri sana.

MWANAFUNZI

Neno moja muhimu ni “mwanafunzi”. “Wanafunzi ni watu

wanaompendeza Bwana na watu watakaoifikia dunia. Basi,

kitambulisho dhahiri cha mwanafunzi ni muhimu. Kuelewa

mwanafunzi ni nini na mwanafunzi anafanya nini ndiyo mambo

makuu muhimu kwa ajili ya kanisa. Cha kushangaza katika kanisa ni

kwamba, tunalitumia neno ‘mwanafunzi’ ovyo ovyo tu kwa uhuru,

na mara nyingi pasipo kulifafanua. Hali hiyo ni sawa na kiwanda cha

viatu kujaribu kutengeneza kitu bila vipimo au kufuata masharti.

Kitakachotokea mwisho huko ni cha ajabu sana.” (Maneno ya Bill

Hull katika kitabu kiitwacho The Disciple Making Pastor, uk. Wa

54).

Neno hili “mwanafunzi” kwa bahati mbaya sana

limepunguzwa nguvu yake katika kanisa la kisasa. Inasemekana ni

“mwongofu” hadi kuwa “aaminiye mwenye kukiri”. Kwa kawaida, 86

Page 95: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“kufanya watu kuwa wanafunzi” hufafanuliwa kuwa ni “kuleta watu

kwa Kristo”. Kuleta watu kwa Kristo ni sehemu muhimu, sehemu ya

kwanza, sehemu ya lazima katika kufanya watu kuwa wanafunzi,

lakini ni mwanzo tu. Kama utaratibu mzima utakomea kwenye kuleta

watu kwa Kristo tu, mwenye dhambi mhusika “hajaletwa” kabisa.

Katika Agano Jipya, neno lenyewe linatumiwa katika njia

kadhaa za jumla, halafu kwa maana inayozidi kulengwa. Kwanza,

linatumiwa kusema kuhusu msikilizaji wa kawaida tu. Wale wote

waliofika kumsikiliza Yesu mwanzoni mwa huduma Yake wanaitwa

“wanafunzi”. Halafu, linatumiwa kumwelezea msikilizaji aliyesadiki

– mtu ambaye anakubali kwamba kile anachosikiliza ni kweli,

ingawa anaweza asibadilishe maisha yake au mtindo wake wa kuishi

kwa sehemu kubwa. Soma Yohana sura ya 6 kwa makini sana,

ukitazama hasa mstari wa 63 hadi 66. Wale wasikilizaji wa kawaida

na ambao walikuwa wamesadiki, walipokuwa bado hawajawa

wafuasi halisi, walimwacha Yesu, “wasifuatane naye tena”. Ni hivi

wapendwa: Kanisa leo limejaa watu ambao wanatosheleza maelezo

hayo. Hawa ndiyo sehemu kubwa ya “waketi vitini” wanaojaza

makanisa yetu Jumapili baada ya Jumapili, lakini ambao hawana

nguvu na Mungu katika kubadilisha dunia, kwa sababu wao

wenyewe hawajabadilishwa kwa undani na kwa ukweli.

Matumizi ya tatu ya neno “mwanafunzi” katika Agano Jipya

yanaeleza mtu anayejifunza maisha yake yote, aliyejitolea, na

anayefuata. Haya matumizi ya mwisho ndiyo anayokusudia Yesu 87

Page 96: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

katika Agizo Kuu, na ndiyo amri yetu ya kusonga mbele. Tunapaswa

kwenda kila mahali na “kuwafanya watu kuwa wanaojitolea,

wanaojifunza maisha yao yote, na wafuasi wa Yesu Kristo.” Hii

ndiyo maana iliyo katika neno “mwanafunzi”. Mwanafunzi ni

anayeshikamana (sawa na gundi, kwa mwingine) au ni mwenye

kujifunza kwa Yesu Kristo. Pima kila neno vizuri kabisa. Tumia

muda kutafiti maneno hayo. Mwanafunzi ni mtu aliye katika

mafunzo. Au, ni kiongozi aliye mafunzoni.

Tertuliano, mmoja kati ya viongozi wa kanisa la kwanza,

aliwaita Wakristo “wanafunzi katika shule ya Mungu”. Mwanafunzi

kwanza huzaliwa, kisha hutengenezwa. Anazaliwa kwa Roho wa

Mungu akiwa na vifaa vyote vinavyohitajika ndani yake. Lakini,

lazima ajengwe, afunzwe, afundishwe na kuelekezwa ajitolee kwa

Yesu Kristo.

Waldron Scott, mtu maarufu katika kufanya wanafunzi,

aliandika hivi: “Shughuli ile ya kutengeneza hali mpya za moyo,

kupata utaalamu mpya, kuanzisha mahusiano mapya, kugundua,

kuthubutu, kutafuta, kurekebisha, kufanya upya – yaani, kujifunza –

hufanya maisha kuwa kitu cha kusisimua kama Yesu alivyoahidi.

Kama hujifunzi, ni kwamba huishi. Ni rahisi tu kiasi hicho.”

Lakini, pamoja na maneno mazuri kiasi hicho kutoka kwa

mtu wa hali ya juu hivyo, bado tunapaswa kuwa makini sana. Kuna

kitu kinachotakiwa kuongezwa katika maneno ya Ndugu Scott, hivi:

Mkazo wa huko kujifunza na kuishi unapaswa kuwa Yesu Kristo, na 88

Page 97: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

matokeo yanapaswa kuwa kufanana na Yesu Kristo kihalisi kabisa.

Mwanafunzi wa Agano Jipya amevaliwa kabisa na Yesu Kristo na

mawazo yake yote ni kwa Yesu Kristo kiasi kwamba hali yake hiyo

inameza kila jambo lingine dogo linalowezekana. Basi, naye anazidi

kuwa kama Kristo zaidi na zaidi kihalisi kabisa – anayefundisha

daima, anayehudumu daima, anayejenga maisha ya watu daima,

anayerekebisha daima kila inapotakiwa, na anayekwenda duniani

kote daima!

Basi, kuwa kama Kristo kihalisi si ile hali ya kuwa na tabia

ya upole, ya uoga, ya kutokutaka kufanya kitu ambayo tumeiruhusu

kuwepo katika kanisa la siku hizi – bila ya kufikiri. Dada Eugenia

Price alikaribia kweli muhimu sana aliposema, “Dhambi kuu zaidi ya

kanisa la leo ni kumfuga Yesu Kristo.” Sam Shoemaker, aliyesifiwa

na Billy Graham kwamba, “Alikuwa mtu wa maana kwa kanisa

kama taasisi duniani kote kuliko yeyote mwingine wa kizazi chake”

aliwahi kuandika hivi: “Si kazi kubwa ya kanisa kufanya kazi nyingi,

kuwa na orodha ndefu ya washirika, au kuchangisha fedha nyingi.

Kazi kubwa ya kanisa ni kuwatengeneza watu wenye tabia kama

Yesu Kristo – na huo si mtindo wa maisha dhaifu, wala si jinsi watu

wasivyotenda. Hawa watu watakaofanana na Kristo hawawezi

kuchongwa kutokana na makundi makubwa ya watu wa kawaida tu.

Inabidi watengenezwe mmoja mmoja.”

Hebu fananisha makanisa yetu ya siku hizi na mikakati yake,

ambayo utaratibu wake ni sawa sawa na kulipua bonge la majabali na 89

Page 98: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kutazamia kupata sanamu kadhaa zilizochongwa na kusadifiwa

vizuri. Shoemaker aliendelea kusema hivi: “Makanisa yetu

yanapaswa kupunguzwa mpaka yawe mashirika madogo yenye

uwezo wa kutoa nafasi kwa wachungaji na walei kujifunza utaalamu

mkuu wa kiroho wa kuwaleta wengine kwa Yesu na kuwafundisha.

Inaonekana kuwa ujuzi wa dunia nzima kwamba, mtu asipoweka

kazi hii kuwa ya kwanza katika maisha yake, itafukuzwa maishani

mwake kabisa mwisho wa siku. Akili zetu, hisia zetu, masaa ya siku

zetu – vyote hivyo vinapaswa kujawa na kundi maalum la watu

wakati wote – watu ambao tunatafuta kuwavuta, watu tunaotaka

kuwafundisha wachukue wajibu, watu ambao sisi wenyewe

tunawahitaji kwa ajili ya kushirikiana kiroho, na kupata msaada.”

Mtindo huo wa maisha ndiyo Yesu aliofuata, na unatakiwa kuigwa

na sisi mpaka tuujue kabisa.

Knofel Staton aliandika vizuri kabisa, kama ifuatavyo: “Nani

aliye mwanafunzi wa Yesu, na tunafanyaje ili mtu awe mwanafunzi

wa Yesu? Bila ya kuwa na picha dhahiri ya malengo yetu, tutapoteza

wakati tu mahali pamoja, na kutumia muda wetu na nguvu zetu, na

bado hatutakuwa na wanafunzi.” Neno “mwanafunzi” linatumika

mara 270 katika Injili na Kitabu cha Matendo ya Mitume. Halafu,

neno hilo halitokei tena katika vitabu 22 vilivyosalia vya Agano

Jipya. Kulikoni? Mbona neno hilo litoweke? Roho Mtakatifu

anasema nini hapa? Katika Luka 6:40, Yesu alisema hivi: “Utaratibu

ukikamilika, mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake”. Kwa hiyo, 90

Page 99: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

tutazamie maneno mengine kujitokeza yenye kuonyesha hali ya

kuendelea. Na kweli – Neno “Mkristo” linaanza kutumika. Neno

“mtakatifu” – mtu ambaye ametengwa kimaalum kwa ajili ya

kutawaliwa na Kristo – linaanza kutokea. Neno “aaminiye” – mtu

ambaye ni mwamini wa kudumu na mwenye kuendelea kumwamini

Yesu Kristo, kumshika Yeye na kufuata makusudi Yake katika

maisha yake ya kila siku binafsi – linatumika mara nyingi na mara

kwa mara.

MWENYE KUFANYA WATU KUWA WANAFUNZI

Neno kuu la pili ni neno “afanyaye wanafunzi”. Huyu ni mtu

“anayewafanya watu kuwa wanafunzi”. Huyu ni mwanafunzi

anayekomaa, maana mtu hawezi kuwa mwanafunzi wa Yesu huku

anapuuzia amri pekee ya kusonga mbele ambayo Yesu aliitoa kwa

kanisa Lake. Yaani, ni kitu kisichowezekana kuwa mwanafunzi

pasipo kuwa mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi. Afanyaye watu

kuwa wanafunzi ni mwanafunzi mwenza, anayewatafuta na

kuwaongoza wengine, huku wakijifunza pamoja.

KUFANYA MWANAFUNZI

Neno la tatu muhimu ni “kufanya mwanafunzi”. Amri ya

Yesu kwamba “mfanye watu kuwa wanafunzi” imejaa vitu vingi

sana, kutokana na mfano wa Yesu Mwenyewe, na mafundisho Yake.

Hii ni harakati ya kuwajenga watu wawe wanafunzi. Christopher 91

Page 100: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Adsit katika kitabu chake kiitwacho Kufanya Wanafunzi Kibinafsi

anafafanua jambo hilo kuwa ni “kutafuta kutimiza amri ya Agizo

Kuu kwa kufanya juhudi za makusudi kuwasaidia watu waelekee

kwenye ukomavu kiroho – kwa kutumia nguvu na maongozi ya Roho

Mtakatifu, kutumia rasilmali za kanisa la mahali, na kutumia

kikamilifu karama, vipawa na ujuzi ambao umepatikana kwa miaka

na miaka.”

Kitendo cha kufanya mtu kuwa mwanafunzi hufanywa na

mwingine, si na kitu fulani. Hufanywa na watu, si mipango.

Hufanikishwa na watu binafsi, sio taasisi. Kimsingi, kufanya mtu

kuwa mwanafunzi ni tendo la Mkristo mmoja akimgawia au

kumwingizia mtu mwingine maisha yake yote, kwa njia ya mfano,

uongozi na mahusiano. Ni uhamishaji maisha siku zote.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwasafisha wenye dhambi

na kuwafanya watakatifu kuwa wanafunzi. Kazi nyingi za kanisa –

kazi ya kichungaji, kuabudu, juhudi za kuelimishana, juhudi za

kuhamasishana na kadhalika – husababisha kusafisha wenye dhambi

kwa kiasi kidogo sana, na wala hakuna kiasi kikubwa cha kuwafanya

watakatifu kuwa wanafunzi. Unataka uthibitisho wa hilo? Rahisi

kabisa. Wakristo wengi katika makanisa mengi hawana “uzito

kiroho” wa ziada kwa ajili ya Kristo kuliko ule waliokuwa nao kabla

ya kuokoka!

Kusafisha wenye dhambi humfanya mwenye dhambi aokoke,

halafu humwingiza katika kisanduku cha kiroho cha akiba, na 92

Page 101: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

anapotokea humo anatokeza kama mwanadamu mwungwana,

aliyefugwa na kufundishwa vizuri. Kinyume chake, kuwafanya

watakatifu kuwa wanafunzi ni tendo la ujenzi mzuri wa mtu

aliyeokoka ili aweze kubadilisha dunia kwa njia kubwa sana, kwa

kuendeleza utaratibu huo huo.

Tofauti itaonekana katika mfano huu, ambao unalinganisha

kuhubiri na kufanya watu kuwa wanafunzi. Hebu tuseme kwamba

una mtu amesimama nyuma ya mstari fulani akiwa ameshikilia ndoo

ya maji. Mbele ya mstari huo, kiasi cha mita 10, kuna chupa ishirini

ndogo za maziwa. Kuhubiri ni sawa na kutupa maji kutoka kwenye

ile ndoo nyuma ya mstari, kwa matazamio kwamba kiasi fulani cha

maji kitaingia katika zile chupa. Lakini, mafanikio ya tendo hilo

yanatabirika sana: si maji mengi yatakayoingai katika zile chupa. Na

hata kama yataingia, yatafyonzwa upesi na jua kama hayatatumiwa

kwa faida. Lakini, tendo la kufanya mtu kuwa mwanafunzi ni sawa

na kwenda na ile ndoo yenye maji mpaka kwenye kila chupa na

kumimina maji ndani ya chupa mpaka ijae. Ni dhahiri kwamba

mafanikio makubwa yako hapo.

Au, kuhubiri ni kama kuchukua kifuniko cha chupa ya dawa

na kusimama dirishani katika gorofa ya tatu, na kuimimina huko

chini kwa matazamio kwamba itamwingia mtu jichoni. Lakini,

kufanya watu kuwa wanafunzi ni tendo la kumkaribia mtu na

kumtilia dawa moja kwa moja jichoni, mkiwa ana kwa ana.

93

Page 102: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Pasipo kuwa na kiwango maalum cha kufanya watu kuwa

wanafunzi, tutagawa kweli kwa ujumla na kwa wingi na kuwahesabu

watu – ingawa tunaweza kuwa tunazaa watu wachache sana wenye

maana. Kufanya watu kuwa wanafunzi kwa mtindo ambao Yesu

aliutumia kutarekebisha tatizo hilo. Wakati wanafunzi walipomsikia

Yesu akisema kwamba wanapaswa “kuwafanya watu kuwa

wanafunzi”, walitakiwa kuelewa kwamba walitakiwa kuwafanya

wengine kuwa kama Yesu alivyowafanya wao. Kufanya watu kuwa

wanafunzi ni pamoja na kufuata utaratibu mzima wa kufanya watu

kuwa wanafunzi – tangu kuongoka mpaka kufikia mtu afanyaye

wengine kuwa wanafunzi, aliyefundishwa. Hicho ndicho kiini cha

yale ambayo Kristo anatazamia kwa Kanisa Lake.

NIDHAMU

Neno muhimu la mwisho hapa ni “nidhamu”. Nidhamu ni

maeneo katika maisha yenye kudhihirisha gharama ya uanafunzi.

Hudson Taylor, mwanzilishi wa China Inland Mission na mmoja kati

ya wamishenari maarufu sana wenye maono makubwa, aliandika

hivi: “Mtu anaweza kuwa amewekwa wakfu, amejitoa na

anamaanisha, lakini hatakuwa na thamani kubwa kama hana

nidhamu.”

Je, wajibu alitooa Kristo ni wa dhati kiasi gani? Je, kanisa

limeshindwa kiasi gani kutii amri moja tu ya Agizo hilo? Je, kuna

94

Page 103: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ushahidi wowote halisi kuhusu kushindwa huko? Ninaamini kwamba

kuna ushahidi tele na wa kudumu kabisa.

[USHUHUDA WA MWANDISHI – Nilikuwa katika kikao

zamani na Mkristo mzee mwenye mvi, ambaye amekwenda

Mbinguni kupumzika zamani. Yeye na mimi tukawa peke yetu

ofisini mwake kwa muda, na hapo akaniuliza “ninafanya nini siku

hizi” katika kanisa nililokuwa nachunga. Nikamwambia, “Ninafanya

kila ninachojua ili kuwageuza washirika wa kanisa kuwa wanafunzi

wenye maono ya dunia ambao nao wanazalisha wanafunzi wengine

wenye maono ya dunia pia.” Kwa huzuni sana akanijibu, “Ndugu

Hodges, sikuwa na mafanikio yoyote katika kuzalisha

watakaozalisha wengine katika kanisa lolote nililochunga.”

Nikauliza, “Basi, ulifanya nini?” Alijibu kwa masikitiko sana,

“Niliendelea na kujitahidi kufanya kazi yote mimi mwenyewe.”

Alijihukumu mwenyewe, na ilikuwa kitu cha kusikitisha sana!

Nilikuwa nimeketi katika mgahawa mmoja nikiwa na

wachungaji watatu tukisubiri tuletewe chakula. Tukawa

tunazungumza (kwa maelekezo yangu nadhani) kuhusu kufanya watu

kuwa wanafunzi. Mchungaji mmoja mzuri tu katika kundi letu akatoa

tathmini ya ukweli kuhusu historia yake ya utumishi (na alikuwa

mchungaji mzuri tu na maarufu sana, mwenye kuamini Injili).

Alisema hivi: “Herb, ninatazama katika makanisa yangu mawili

niliyochunga kwa muda mrefu, na ninaona watu wawili tu katika kila

kanisa wanaoweza kustahili kuwa aina ya watu wale unaowataja”. 95

Page 104: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Hakuwa anazungumza kwa kulaumu au kwa hasira, bali kwa

uchungu na huzuni tu. Inasikitisha sana, lakini ndiyo kawaida!

Tukijitahidi sana, tumekuwa tukizalisha “Wakristo wazuri” ambao

mara nyingi maana yake ni watu wenye kujitazama sana ndani,

badala ya wanafunzi na wenye kufanya wengine kuwa wanafunzi

wanaogusa dunia na kuzalisha wengine. MWISHO WA

USHUHUDA]

Lengo dhahiri la Yesu lilikuwa kuzaa “wanafunzi” ambao

wangekuwa “wafanya wanafunzi”, wanaojihusisha katika kazi ya

“kuwafanya wengine kuwa wanafunzi” katika maisha yao yote na

kutekeleza zile “nidhamu” ambazo ni muhimu kwa ajili ya kutimiza

kusudi hilo.

KUFANYA WANAFUNZI KUNAKOSABABISHA HUDUMA

YA MAONGEZEKO

Halafu, Agano Jipya linaongeza jambo lingine muhimu kwa

jukumu letu. Tunatakiwa kuhusika katika kufanya uanafunzi wenye

kuzalisha huduma ya maongezeko. Ni dhahiri kwamba ilikuwa nia ya

Kristo kwamba kila mwanafunzi ahusike katika huduma ya

maongezeko. Nini maana ya maongezeko? Ni wakati wanaofanya

watu kuwa wanafunzi wanapoanza kuzaa wanafunzi wengine

wanaofanya watu kuwa wanafunzi wenye maono, na wenye kugusa

dunia. Ni hivi: Mpango wa Mungu ni kuifikia dunia kwa mtindo ule

ule uliotumika kuijaza – kwa kuongezeka. Katika Mwanzo 9:1 96

Page 105: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mungu alisema, “Zaeni mkaongezeke, na kuijaza dunia”. Kuna mtu

aliyesema kwamba hiyo ndiyo amri ya kwanza iliyowahi kutolewa

kwa mwanadamu, na ndiyo pekee aliyoitii. Agizo la Yesu la

kiinjilisti ni sawa na lile la Mungu la kimwili.

Kwa nini watu wanashindwa kuongezeka kimwili?

1. Wengine hawaingii katika ndoa, au, hakuna muungano kati

ya wanaume na wanawake. Basi, maongozeko hayawezi kutokea.

2. Wengine wana maradhi au matatizo katika sehemu

muhimu za mwili, zinazohusiana na uzazi.

3. Wengine hawaongezeki kwa sababu hawajakomaa. Sidhani

kama kuna anayefahamu wazazi wenye umri wa miaka mitatu!

Viungo vya uzazi vipo, lakini havijakomaa kiasi cha kutosha

kuruhusu maongezeko – au kuzaliana. Watoto hawazai.

Mapungufu hayo hayo yanahusika kwa ajili ya kushindwa

kuongezeka kiroho. Mahali ambapo hakuna muungano kati ya

Mkristo na Yesu Kristo kwa hali inayodumu na kuendelea,

hapawezekani kuwepo na maongozeko yoyote kiroho – labda kidogo

sana. Kuwepo kwa dhambi katika maisha ya mwamini pia kutazuia

mkakati na mpango wa maongezeko. Pamoja na hayo, kupoa kwa

Mkristo katika utoto wa kiroho kutazuia kuongezeka. Paulo alisema,

“Niliwaandikia kama watoto katika Kristo”, na Wakristo watoto

huko Korinto walikosa nafasi ya viwango vya kugusa dunia kwa

maongezeko kiroho.

97

Page 106: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Maongezeko kiroho ni maono yaliyopangwa na Mungu kwa

ajili ya kuifikia dunia yetu ya wakati huu na vizazi vyote vijavyo kwa

wale tunaowaleta kwa Yesu na kuwafundisha wakati huu. Mkakati

wa huduma ya Yesu ulikuwa wazi: Aliwatazama makundi ya watu

kupitia mtu mmoja, halafu akamjenga huyo mtu afikie makundi ya

watu. Yeye alimhudumia kila mtu aliyekuwa mbele Yake – lakini

aliwaita kwa ajili ya Ufalme Wake tu. Sisi tumepotosha kabisa

viwango hivyo katika kujenga taasisi badala ya kuwajenga watu.

Yesu alipenda kila mtu binafsi – hakika – lakini siku zote alitazama

mbele kuliko wanafunzi Wake na kuwaona watu ambao

wangewafikia na kuwafundisha (ona ktk Yohana 17:20).

Katika Matendo 2:41, 47 na 5:14, neno “akaliongeza”

linafafanua mkakati wa Mungu kihesabu, tangu mwanzoni mwa

historia ya kanisa. Lakini katika Matendo 6:1, tunasoma kwamba

“idadi ya wanafunzi ikaongezeka sana, hata kundi kubwa la

makuhani likajiunga na imani.” Halafu tunapofikia Matendo 9:31

tunasoma kwamba, “makanisa yakaongezeka sana.” Bila shaka,

kanisa halikurudi tena kwenye majumlisho madogo madogo

isipokuwa lilipotoka kwenda mstari wa mbele na kuanza tena, na

hata huko lilirudi haraka sana kwenye kuongezeka.

Watu tunaolingana umri tunapokutana na mwanafunzi

mwenzetu wa chuo kikuu au chuo cha Biblia ambaye hatujaonana

tangu shuleni, maswali muhimu huulizwa. “Vipi, umeoa/umeolewa?”

98

Page 107: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“Je, mna watoto?” “Wangapi?” “Mna wajukuu?” Na kama wahusika

ni wazee kiasi, wanaulizwa, “Je, mna vitukuu?”

Tutakaposimama mbele ya Kiti cha Hukumu cha Kristo,

pengine tutasikia maswali kama hayo hayo. “Je, una watoto? (Na

kama huna, kwa nini?)” “Watoto ni wangapi?” Halafu kipimo halisi

cha ushiriki wetu katika mpango wa Yesu unaanza. “Je, una wajukuu

– watu ambao wamekuwa Wakristo kwa sababu ya jinsi

ulivyowajenga watoto wako mwenyewe wa kiroho?” “Na je, una

vitukuu wa kiroho?” Haitaridhisha kujua kwamba tuliwahudumia

watu wengi sana, na wachache tu ndiyo wakawa wazalishaji.

Itatosheleza tu ikiwa tutakuwa tumetoa maisha yetu tukitafuta

kuwafanya wanafunzi wetu kuwa kama Yesu alivyowafanya wa

Kwake.

Ili tuwe na uhakika kwamba tunaona vizuri kiwango halisi na

kuelewa udhati wa kushindwa kufuata kiwango hicho, hebu

tumalizie sura hii kwa namna nzito – naam, hata ya kinyume kabisa.

Kitabu kiitwacho The Bridge Over River Kwai kinasimulia

habari ya kanali Mwingereza aliyetekwa na WaJapani wakati wa

Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Katika kambi ya wafungwa wa kivita

iliyokuwa katikati ya msitu mkubwa huko Burma, mamia ya

wafungwa wasio na matumaini walikaa tu wakisubiri kifo. Huyo

afisa Mwingereza akapata wazo la ubunifu ili kuinua hamasa na

kuwapa waliotekwa sababu ya kuishi. Hapo karibu na kambi, adui

walikuwa wanajenga daraja la treni. Wafungwa wakasema wao 99

Page 108: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ndiyo watakaojenga. Watafanya kazi kwa ubora na kuonyesha

WaJapani kitu ambacho kingefanywa na mafundi wa Kiingereza!

Akijitolea na askari wake kuifanya ile kazi, yule kiongozi wa

Kiingereza aliona mabadiliko katika motisha. Lengo la kujenga

daraja hilo likawa kitu kinachomsukuma, tena kizuri. Hatimaye,

daraja likakamilika na treni ya kwanza ya KiJapani iliyokuwa

imebeba vitu ikawa inavuka. Kanali huyo aliyejivunia kazi yake

aliona makomandoo wa Majeshi ya Muungano wakiwa chini ya lile

daraja, wakijiandaa kulibomoa. Kwa sababu ya jinsi alivyokuwa

amehusika kibinafsi, alipiga kelele ya kumtaarifu yule mkuu wa

Kijapani, halafu akakimbia kama mwenda wazimu kuelekea mtoni,

ili kujaribu kuwazuia wale waliotaka kulilipua daraja.

Bila shaka mfano uko wazi kabisa hapo, sivyo? Makanisa

mengi hukaa katika hali ya kukaribia kifo. Basi, viongozi wao

wanazaa mpango mmoja baada ya mwingine, ratiba baada ya ratiba,

ili kuboresha motisha na kuwapa washirika kitu cha kuwahamasisha.

Yaani, wanaingia katika mikakati ya kujikimu na kujihami, ambayo

ndiyo kawaida kabisa katika ujenzi wa taasisi. Kama hadithi

ilivyokuwa, adui anao mpango wake, na anafurahi sana kutuingiza

sisi katika “kuutimiza”. Mara nyingi tunaupokea mpango wake na

kuufanyia kazi kwa bidii kabisa. Lengo la “kujenga daraja” linakuwa

kitu kinachotusukuma kweli kweli. Mtu yeyote akisema kwamba huo

ni mpango mbadala wa Shetani, na kwamba si mkakati wa Mwokozi,

tunamgeukia kana kwamba ni adui yetu. Tumeshikwa sana na 100

Page 109: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mipango hii ya kujenga taasisi mpaka tumesahau kwamba kuna vita

kubwa zaidi kuliko ujenzi wa daraja. Kama watoto wadogo

wanaocheza michezo ya kujifanya, tunaendelea kuishi tu bila ya

kutambua kwamba tunakosa agizo halisi la Yesu.

[USHUHUDA WA MWANDISHI – Mwanzoni mwa mwaka

wa 1991 nilikaa juma zima katika kanisa moja huko Texas,

nikihubiri mikutano ya jioni kuhusu mada ambazo zinaunga mkono

mkakati huu wa kufanya watu kuwa wanafunzi, na kufundisha

kwenye ibada za mchana taratibu au hatua zenyewe. Mchungaji wa

kanisa hili alitokana na huduma ya kanisa ambalo niliwahi

kulichunga. Jioni ya mwisho, wanandoa vijana wakanijia muda

mfupi kabla ya ibada kuanza, na tulipokuwa tunazungumza, yule

mke akanipa barua iliyokunjwa. Sehemu ya barua hiyo ilisema hivi:

“Sijui kama unafahamu au vipi, lakini, mimi ni mmoja katika

wajukuu zako kiroho. Mchungaji wetu amekuwa akitufanya

wanafunzi mimi na mume wangu kwa karibu miaka minne.” Halafu

kukawa na sehemu ya maelezo binafsi, na sehemu nyingine ambapo

alifanya kama muhtasari au marudio wa mahubiri ya kila jioni kwa

juma hilo. Ndipo akaandika tena, hivi:

Asante sana kwa muda wa ziada ambao umeutumia

kutufundisha juu ya uanafunzi. Japo mimi niko kama yule ndugu

aliyekiri kwa machoni katika ibada ya mchana kwamba amekuwa

Mkristo kwa muda mrefu, lakini hakuwahi kumfanya mtu yeyote

kuwa mwanafunzi. Nimewashuhudia watu kadhaa baada ya kujifunza 101

Page 110: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

na kuwa na mchungaji wetu, lakini kwa sasa nina shauku ya

kumpokea mwanafunzi wangu wa kwanza maishani mwangu. Juma

hili limekuwa muda wa kubadilika katika maisha yangu, nami

ninafurahia jinsi ambavyo wewe umemruhusu Mungu akutumie

kunihudumia na kunihimiza na kunihamasisha. Ninapanga – na Yesu

akifanya kazi kupitia kwangu, nikufanye uwe babu-babu wa kiroho.

Asante sana kwa kuja kwako! Ni mimi dada yako na mjukuu katika

Kristo, (sahihi). MWISHO WA USHUHUDA]

Mambo halisi katika Agano Jipya yaliyotajwa katika hii barua

yanaonyesha amri ya kusonga mbele ambayo Yesu aliitoa kwa

kanisa lake. Ongezea maeneo ya kuzaa kiroho, maono ya dunia, na

taratibu halisi za kuwafanya watu kuwa wanafunzi, nawe unakuwa

umepiga hatua kubwa sana kuhusu kutimiza Agizo Lake.

Katika gazeti la chuo cha Biblia cha Kibaptisti toleo la mwezi

Mei 1983, kulikuwa na kisa cha kusikitisha sana. Majina ya

wahusika yamehifadhiwa, japo katika gazeti lenyewe yalitajwa.

“Wakati wamishenari ….. walipoandika kitabu juu ya kufukuzwa

kwao nchi ya Ethiopia, walilazimishwa kujiuliza ni kitu gani

walichoacha nyuma. Jibu likawashtua kabisa. Walitambua kwamba

walichofanya ni kumwaga mbegu tu – hawakuzipanda. Cha kushtua

zaidi kikawa utambuzi wao kwamba Wakristo kila mahali walikuwa

wanafanya makosa yale yale: wanabatiza makundi makubwa ya

watu, lakini hawafanyi watu kuwa wanafunzi. Mishenari mmoja

akasema katika ibada ya wanafunzi, ‘Hatukufanya yeyote kuwa 102

Page 111: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mwanafunzi. Tumeona watu wanaokiri imani tu. Na tunao hao katika

viti vya kanisa kila mahali Marekani, na duniani kote. Ni rahisi sana

kubatiza watu. Ni vigumu zaidi kufanya watu kuwa wanafunzi. Mimi

naona kanisa na Mungu wana mipango miwili tofauti ya utendaji.

Kanisa lina wasemaji na wasikilizaji, na wote hao hakuna anayetenda

kile Yesu alichowaitia Wakristo kuwa. Tunahitaji kuingia katika

mpango wa Mungu.”

Pengine maelezo haya yanajumlisha tatizo kana kwamba

Wakristo wote wanastahili kulaumiwa, pamoja na kurahisisha

ufumbuzi wa tatizo lenyewe. Hata kitabu hiki kina hatia katika eneo

hilo. Lakini, kinashughulikia kushindwa kwa muhimu sana katika

kanisa kwa ujumla, na kinatukumbusha juu ya mkakati mmoja tu

ambao Yesu alitoa.

Ukitaka kuanza kufanya kilicho sawa, huwi umechelewa –

yaani yale ambayo tumeagizwa kufanya. Mtu yeyote anaweza

“kurudi mwanzo kabisa” na kuanza ule utaratibu wa kuongeza.

Lakini, wengi wetu tungehitaji kujitoa wenyewe mara moja ili

kuingia katika shughuli ya kujifunza maisha na huduma ya Yesu,

tukiuliza hivi: “Alifanyaje na watu Wake?” na pia kujifunza mbinu

za kufanya wanafunzi na kuwaongeza, kama zitolewavyo katika

vitabu vingi maarufu.

Naona jeshi linalozidi kuongezeka la waongezaji wenye

maono ya dunia nzima na mguso wa dunia nzima ambao historia yao

yote ni kujitoa kwao kutimiza Agizo la Yesu la “kuwafanya watu 103

Page 112: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kuwa wanafunzi.” Mungu awapate na kuwatuma wanajeshi hao

mbele ya macho yetu

104

Page 113: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 4Ufunguo Ulioko Mlangoni Mwa Historia Ya Kanisa

“Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha, hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu. Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ‘Ile ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.” Matendo 1:1-5

Tutaanza somo hili “mlango wa mbele” wa “Matendo ya

Mitume”. Historia ya Ukristo imekuwa na mjadala si mdogo kuhusu

jina la kitabu hiki katika Biblia. Bila shaka unajua kwamba majina ya

vitabu vya Agano Jipya hayajavuviwa. Yaliongezwa miaka mingi

sana baada ya kukamilika kwa Agano Jipya. Kuna wanaoamini

kwamba kinapaswa kuitwa “Matendo ya Baadhi ya Mitume,” kwa 105

Page 114: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

sababu ni huduma za Petro, Yakobo, Yohana na Paulo tu ndiyo

zinazotajwa. Wengine wanadhani kinafaa kiitwe “Matendo Ya Roho

Mtakatifu” ili kukazia Mtendaji Mkuu na kuwaficha wale watendaji

wadogo. Lakini, kila mmoja anabakiza neno “Matendo” katika jina la

kitabu. Ona kwamba si nia, wala mipango, wala matumaini, wala

matakwa, wala mafunzo, wala tafakari, wala mahubiri ya Mitume. Ni

matendo ya mitume. Kama mitume wangekwamia kwenye hayo

tuliyotaja hapo kabla, hata kama ni moja tu, kitabu hicho

kisingeandikwa. Basi, ni maombi yangu kwa ajili yetu kwamba,

tunapofungua mlango wa mbele wa kitabu chenyewe, “tukamatwe

katika Matendo yenyewe”!

Tutaanzia kwenye mtazamo mpana wa mstari wa kwanza

kabisa wa kitabu. “Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo,

katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na

kufundisha.” Hebu niingize muhtasari wa mstari huu. Kwanza, kuna

kitabu kingine kinachotajwa hapa (“kitabu kile cha kwanza”). Halafu,

kuna mwanafunzi binafsi anayetambulishwa hapa (“Theofilo”) .

Mwisho, kuna tamko la wazi kuhusu kusudi la kuandikwa kwa kitabu

kile cha kwanza, na vivyo hivyo, tamko la kusudi kwa ajili ya

kuandika kitabu hiki cha sasa.

KITABU CHA KWANZA KINACHOTAJWA

Hebu tufikiri kuhusu kitabu kile kingine kinachotajwa hapa.

Hicho “kitabu kile cha kwanza” ni kipi? Tafsiri za Lugha Rahisi 106

Page 115: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

zinakiita “maelezo ya kwanza niliyoandaa”. Hicho kitabu cha

kwanza ni Injili kama ilivyoandikwa na Luka. Injili ya Luka ni

mojawapo katika Injili nne katika Agano Jipya. Inazo sura 24 katika

Biblia yako, na imejengwa kwenye kweli kama kumi hivi za

kihistoria kuhusu Bwana Yesu Kristo. Hizo kweli ni kama ifuatavyo:

Kuzaliwa Kwake na Bikira; Maisha Yake Yasiyo na Dhambi;

Kubatizwa Kwake; Kujaribiwa Kwake; Kubadilika Sura Kwake;

Mapambano Yake Katika Bustani ya Getsemane; Kusulubiwa na

Kufa Kwake; Kuzikwa Kwake; Kufufuka Kwake; na Kupaa Kwake.

Ili ufahamu jinsi hayo ni ya ajabu, ona cha kwanza kabisa

katika hizo kweli za kihistoria juu ya Yesu – kuzaliwa Kwake na

bikira. Kumbuka kwamba Luka alikuwa tabibu – daktari. Si rahisi

kwa madaktari kuamini uzazi wa bikira, lakini maelezo yenye

kutosheleza kabisa kuhusu kuzaliwa kwa Yesu na bikira katika

Biblia nzima yametolewa na Dakta Luka. Anatuambia mwenyewe

katika sura ya kwanza ya Injili yake kwamba alikuwa amefanya

utafiti wa habari za kihistoria kuhusu Yesu kwa ukamilifu kabisa, na

kwamba aliandika alichoandika kwa msingi wa aliyopata kwenye

utafiti. Hivyo basi, tunapata ushahidi mkubwa mwingine kuhusu

ukweli na uhakika wa habari za Yesu Kristo.

107

Page 116: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

LUKA ALIKUWA NANI, NA ALIINGIAJE KWENYE

HABARI HII?

Hivi, Luka ni nani? Na alipataje kuingia katika hadithi ya

Injili? Yeye alikuwa mtu wa Mataifa – yaani, asiyekuwa Myahudi –

na jina lake linaonyesha hilo. Alikuwa tabibu aliyeitwa “Luka, tabibu

mpendwa” katika Wakolosai 4:14. Wakati mwingine tunawaza

kwamba kila mtu katika dunia ya siku zile alikuwa mshamba, mtu

asiyekuwa na elimu, na asiyejua mengi kama tunavyojua sisi leo.

Sivyo kabisa. Luka amekosolewa mara kwa mara kuhusu kuwa

mwanahistoria na kuhusu kuwa tabibu, lakini yeye na vitabu

alivyoandika vimevunjilia mbali nyundo nyingi sana, yaani,

wakosoaji wake. Ukweli ni kwamba, katika kila hoja ya ukosoaji

inayotolea, maandishi ya Luka yamesimama vizuri na kushinda

barabara, kihistoria na hata kitabibu.

Vitabu chungu nzima vimeandikwa kuhusu Luka, kama

mwanahistoria na kama tabibu. Kwa mfano: Dakta Hobart

alichapisha kitabu kikubwa tu kinachoitwa The Medical Language

of Luke, kinachokubaliana na ubora na usahihi wa lugha ya

kitaalamu ya kitabibu katika vitabu vyake vyote viwili. Kama ilivyo

kawaida, wakati wanasayansi wanapofanya utafiti kwa kuzingatia

ukweli, hatimaye wanaifikia Biblia!

Lakini – huyo tabibu alihusikaje na uandishi wa Injili na

matetezi ya Maandiko mpaka kufikia kuandika vitabu viwili

ambavyo vinapatikana katika Agano Jipya letu? Hebu tuunganishe 108

Page 117: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

historia, ufunuo na uwezo wetu wa kufikiri kwa kifupi. Paulo na Sila

walifika katika eneo la Galatia wakati wa safari yake ya pili ya

kitume (ktk Matendo 16:6). Walipokuwa huko, inaonekana Paulo

alipata ugonjwa mbaya sana wa macho (au, ugonjwa aliokuwa nao

hapo nyuma ulilipuka mpaka kufikia hali ya hatari). Alipowaandikia

Wagalatia baadaye, alisema hivi: “Oneni jinsi nilivyowaandikia

barua kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe” (ktk Wagalatia 6:11,

TLR). Tafsiri za Lugha Rahisi zinaeleza kwa njia nyingine. Moja

inasema, “Oneni jinsi ninavyoandika herufi kubwa”. Nyingine

inasema, “Mnaona hizo herufi kubwa?” Nyingine inasema,

“Nimeandika kwa herufi kubwa kwa ajili yenu.” Kwa hiyo,

unamwona Paulo akihangaika kuandika kwenye karatasi lake,

akitengeneza ‘maherufi’ makubwa kwa sababu haoni vizuri kiasi cha

kuandika kawaida.

Katika Wagalatia 4:13-15, Paulo aliwaambia hivi, “Mnajua

jinsi ambavyo kwa udhaifu wa mwili wangu niliihubiri Injili kwenu

mara ya kwanza. Na jaribu langu lililokuwa mwilini mwangu

hamkulipuuza wala kulikataa; bali mlinipokea kama malaika wa

Mungu – naam, hata kama Kristo Yesu … Kwa sababu

ninawashuhudia kwamba, kama ingewezekana, mlikuwa tayari

kung’oa macho yenu, ili mnipe mimi.” Ona kwamba Mungu

hakumponya Paulo tatizo hili zito sana. Yeye alikuwa na kitu bora

zaidi na kikubwa zaidi kuliko kumponya Mtume Wake! Alikuwa

109

Page 118: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

anajipanga kumwita (kwa njia ya ugonjwa wa Paulo) mmoja kati ya

wasemaji Wake wakuu!

Paulo na timu yake wakasonga mbele kutoka Kusini

Mashariki hadi Kaskazini Magharibi katika “ukanda” wa Asia Ndogo

mpaka wakafika Troa, mji wa pwani uliokuwa upande wa kaskazini

wa Bahari ya Uyunani. Yawezekana alishindwa kulala usingizi

vizuri, maana hapo ndipo “Paulo akapata maono usiku. Mbele yake

alisimama mtu kutoka Makedonia, akamsihi akisema, ‘Njoo

Makedonia, ukatusaidie’.” Hapo ndipo uinjilishaji wa Ulaya Kusini

ulipoanza.

Wakati Paulo anasubiri huko Troa, alijua alihitaji kumwona

tabibu. Kuna wasomi wa Biblia wanaoamini kwamba Paulo na Luka

walikuwa wamefahamiana kabla, kwa sababu chuo maarufu cha

utabibu siku hizo kilikuwa mjini alikozaliwa Paulo. Wengine

wanapendekeza kwamba pengine Paulo aliulizia tabibu mzuri yuko

wapi, na akaelekezwa kwa Luka (ambaye kwa kweli alikuwa tabibu

mzuri sana – bingwa). Vyovyote ilivyotokea, ninaamini Paulo

alimwona Luka ili apate matibabu ya tatizo lake.

Akiwa huko, Paulo (kama kawaida) alimshirikisha huyu

tabibu Mmataifa mwenye ujuzi na akili nzuri sana habari za Kristo

na Injili Yake, na “Mungu akawasha taa” ndani ya roho yake. Dakta

Luka akaokoka na kuwa Mkristo. Aliaminishwa kuhusu dhambi zake

na kuamua kumfuata Mwokozi. Mara ile ile Paulo alianza kumfanya

mwanafunzi, lakini muda ulikuwa mfupi sana.110

Page 119: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Paulo na Sila walikuwa “chini ya amri”. Walikuwa kwenye

utume, na ratiba yao ilikuwa inapangwa na Roho Mtakatifu. Paulo

akamwambia Luka kwa upole, “Ndugu, lazima tuondoke sasa.”

Pengine Luka alijibu hivi: “Mwondoke? Mwende? Jamani, si ndiyo

mmefika tu? Tena, umeniongoza kwenye jambo kuu kuliko yote

niliyowahi kuyafahamu na kuyajua, ambalo ni uzima wa milele

katika Yesu Kristo. Ndiyo unasema lazima mwondoke sasa? Hiyo

haiwezekani!”

Lakini Paulo alipokaza juu ya jambo hilo, Luka alifikiri hali

yenyewe kidogo halafu akasema, “Je Paulo, unaonaje ukipata msafiri

mwingine katika timu yenu ya utume?” Bila shaka ari ya Paulo

iliongezeka, lakini pengine alimjibu hivi: “Kuna uwezekano mzuri

tu! Ila, itakuwaje kuhusu kazi yako ya utabibu?” Luka alijibu kwa

utulivu kabisa, “Aa! Mbona hiyo si kikwazo? Kazi yangu imekaa

vizuri. Itakuwa rahisi kuuza.” Ndipo Paulo akatambua kwamba Luka

alikuwa amemaanisha kabisa. Pengine aliuliza hivi: “Yaani

unamaanisha kwamba uko tayari kuuza kazi yako na kufuatana nasi

katika safari hii, sehemu iliyiosalia? Nashindwa kuamini.” Labda

Luka naye akajibu, “Lakini Paulo, unahitaji kuwa na tabibu wa

kudumu sasa hivi, nami ninakuhitaji kwa kadiri unavyonihitaji na

mimi. Naam – naona nitafanya hivyo!”

Je, unadhani natunga mawazo hayo? Hapana. Mpaka mstari

wa 10 wa Matendo 16, maelezo ya mwanahistoria huyo (yaani, ya

Luka) yanatumia neno “Wao” anapoandika kuhusu hiyo timu ya 111

Page 120: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kitume. Lakini unapofika Matendo 16:10 (anapozungumzia mambo

ya Troa ktk mstari wa 8), maelezo yanasema, “Mara tukakusudia

kwenda Makedonia” na ndiyo mwanzo wa sehemu za “tuka” katika

Matendo. Luka, mwandishi wa kitabu cha Matendo, alijiunga na timu

ya Paulo huko Troa!

TAFAKARI

Hebu tukatishe hadithi yetu na kuona kweli nzuri sana

zinazofaa kutafakari. Ni hivi: Tendo la kufanya watu kuwa

wanafunzi halielekei upande mmoja tu. Wakati Paulo anamfanya

Tito kuwa mwanafunzi, Tito naye anamfariji Paulo (ktk 2Wakor. 7:5,

6). Wakati Paulo anampa kijana Timoteo hekima yake ya muda

mrefu, Timotheo kijana anamhamasisha mzee Paulo. Wakati Paulo

anamfanya Dakta Luka kuwa mwanafunzi katika maisha ya Kristo,

Dakta Luka anampa mwanatheolojia Paulo ujuzi na utaalamu wake

wa kitabibu.

Je, umewahi kujiuliza mahali Paulo kama mwanadamu

alikopata mfano wake wa Kanisa kuwa ndiyo “Mwili wa Kristo”

halisi? Kibinadamu, hilo hata halifai kuwa swali. Bila shaka Luka –

kikawaida kabisa – angezungumza kuhusu utendaji kazi wa

kushangaza sana wa mwili wa mwanadamu. Pengine angefafanua hii

mashine ambayo ni mwili wa mwanadamu wakati akimtibu maradhi

yake Paulo – kama ambavyo angefanya nyakati zingine pia.

112

Page 121: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Labda siku moja alisema hivi: “Hivi Paulo, una akili kiasi

gani katika mwili wako, baada ya kichwa? Una hekima kiasi gani

katika mwili wako chini ya kichwa chako? Pengine Paulo angesema,

“Kweli sijawahi kufikiri sana juu yake, lakini bila shaka jibu sahihi

ni kwamba, ‘sina’.” Na Luka angejibu, “uko sawa kabisa. Lakini

basi, viungo vilivyoko chini ya kichwa chako vinajuaje kitu cha

kufanya kama havina hekima au akili ndani yake? Jibu ni muujiza

mwingine wa mwilini.”

Akaanza kumpa somo. “Ni kwamba una mfumo wa mishipa

ya fahamu katika mwili wako, yenye kuunganisha viungo vya mwili

na akili. Mishipa itokayo kwenye akili au ubongo hadi mwilini

hupitisha amri zitokazo kwenye akili hadi kwenye viungo vya mwili,

na kama viungo vyote viko katika hali nzuri kiafya, vinatii mara

moja na kutuma ujumbe wa kukubali kurudi kwenye akili, unaosema,

‘Sawa. Kazi unayotaka tutaitenda.’ Unaona huu mkono wangu wa

kuume ulionyooshwa? Kiganja kiko juu na vidole vimetawanyika.

Na mkono utabaki hivyo hivyo mpaka niuachie ufanye kitu kingine.

Kwa nini? Kwa sababu, muunganiko kati ya akili na kiungo uko

timamu – afya ni nzuri na unafanya kazi.”

Muda wote huo wakati Luka anazungumza, Roho Mtakatifu

anafanya kazi kwa nguvu sana katika akili ya Paulo. Ghafula

anasema hivi: “Hivyo ndivyo Kanisa linavyofanya kazi pia. Sawa na

jinsi ambavyo mwili wako ni chombo kwa ajili ya kujieleza, kanisa

nalo ni Mwili wa Kristo, na chombo kwa ajili ya Yeye kujieleza.” 113

Page 122: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Na Roho Mtakatifu anaendelea kufafanua fundisho kuhusu kanisa

kama mwili wa Kristo kwa Paulo mwanatheolojia, akipitia kwa

Luka, mishenari tabibu wa kwanza!

Muda mrefu baadaye, huyu tabibu Mmataifa – Luka –

aliyefanywa mwanafunzi kibinafsi na kwa upana sana na Paulo,

mtume mkuu wa Kikristo, alikuja kuandika vitabu viwili vya ajabu

sana ambavyo vinapatikana leo katika Agano letu Jipya. Iitokeaje

kuwa hivyo? Na inadhihirisha nini kwetu kuhusu wajibu wa kufanya

watu kuwa wanafunzi utolewao na Agizo Kuu?

Jiandae basi kupokea kweli hii kuu, ifuatayo: Ingawa Luka

aliandika vitabu viwili tu kati ya vile ishirini na saba katika Agano

Jipya, hivyo vitabu viwili ni kama moja ya nne (au robo) ya maelezo

yote ya Agano Jipya. Viliandikwa kwa ajili ya nini? Je, Dakta Luka

alikuwa na wazo lolote kwamba hivyo vitabu viwili vingekuja

kupatikana katika Biblia? Au katika Agano Jipya? Hakika hapana,

kwa sababu yeye hata hakujua kwamba “Agano Jipya” lingekuja

kuchapishwa. Basi, kwa nini aliandika hivyo vitabu viwili vya ajabu

na kushangaza sana?

114

Page 123: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

MWANAFUNZI BINAFSI ANATAMBULISHWA

ROBO YA AGANO JIPYA ILIANDIKWA KWA MTU

MMOJA!

Pili, hebu tufikiri sasa juu ya mwanafunzi binafsi ambaye

aliandikia vitabu hivi viwili. Jina lake ni Theofilo. Linatushangaza

sana. Kwa kweli, majina yanatushangaza.

Familia moja ilipata mtoto. Baada ya kutafuta jina kwa miezi

kadhaa na kuchagua jina lenye kuvutia, walimpa jina la ajabu –

“Theofilo” – baada ya kuzaliwa kwake. Rafiki yao mmoja akauliza,

“Kwa nini? Mbona baada ya kuchagua jina zuri tu mlifikia uamuzi

wa kumwita ‘Theofilo’?” Yule baba akajibu, “Tulimwita Theofilo

kwa sababu ni mtoto mwenye sura mbaya tuliyepata kumwona!”

Jina la huyu Theofilo ni muungano wa maneno mawili katika

lugha ya Kiyunani. Sehemu ya kwanza – “Theos” – maana yake

“Mungu”. Sehemu ya mwisho – “philo” – maana yake “upendo”.

Kwa hiyo, jina lake linaweza kumaanisha “mwenye kumpenda

Mungu” au “anayependwa na Mungu”. Kwa sababu ya hiyo maana,

watafsiri wengine wa Maandiko wamesema kwamba labda si jina la

mtu mmoja binafsi, bali kundi la watu. Lakini si hivyo. Mpokea

kitabu anaelezwa vizuri sana na Luka kwamba ni mtu binafsi, katika

sura ya kwanza ya Injili ya Luka.

115

Page 124: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kumbuka kwamba Injili kama ilvyoandikwa na Luka, na

Kitabu cha Matendo mwandishi wake ni mmoja, mpokeaji ni mmoja,

na vyote vina mada moja kimsingi.

Sasa, kweli kuu ya pili ni hii: Robo moja ya Agano Jipya

iliandikwa kwa mtu mmoja tu! Hapo ndipo kwenye utaalamu wa

Injili ya Kristo, tena kwa herufi kubwa kabisa! Injili ya Kristo

hukuza thamani, kusudi, maana, faida, na wajibu wa kila mtu binafsi.

Ukitaka kuona tumepotoka kiasi gani kwenye wazo na msukumo wa

Injili ya Biblia, jiulize mwenyewe swali hili: Je, umewahi kusikia juu

ya mtu yeyote hivi karibuni aliyeandika kitabu cha aina yoyote ile na

kukituma kwa mtu mmoja ili amlete huyo kwa Kristo?

Siku moja yenye jua kali ambayo haina mawingu, chukua

kioo cha kukuza maandishi na lundo la magazeti, uende nje ukafanye

jaribio. Kunja-kunja kurasa kadhaa za magazeti. Halafu, shikilia

kioo kile cha kukuza herufi juu ya hizo kurasa. Ingawa unakuza

nguvu za mionzi ya jua kupitia hicho kioo, huwezi kuanzisha moto –

ikiwa utasogeza kioo mara kwa mara. Lakini, ukikishikilia hicho kioo

kwa utulivu na kulenga sehemu moja tu na kutoa nafasi kwa hicho

kioo kukuza mionzi ile kwenye kitu kimoja, utapata nguvu za jua na

kuanzisha moto. Na moto siku zote huenea kwenye kitu chochote

kinachoungua! Katika hadithi yetu, Yesu ndiye jua, Luka ndicho kioo

cha kukuza herufi, na Theofilo ndiye sehemu iliyolengwa. Na moto

unawaka, tena, bado unaenea!

116

Page 125: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

KWA NINI LUKA ALIANDIKA HIVYO VITABU VIWILI

KWA MTU MMOJA?

Turudie swali letu la awali: Kwa nini Luka aliandika hivyo

vitabu viwili kwa mtu mmoja huyu? Je, tuna jinsi ya kufahamu hilo?

Ndiyo!

Nini hali ya Theofilo wakati Luka alipomwandikia Injili

yake? Bila shaka alikuwa amepotea, mwenye dhambi ambaye

hajaokoka. Luka anamwita “mtukufu Theofilo” (ktk Luka 1:3).

Hivyo ndivyo mtu mkuu wa Kiyunani alivyokuwa anaitwa, kwa

hiyo, huyu Theofilo alikuwa mtu mkuu wa Kiyunani, mwenye cheo

na wadhifa mkuu. Hakuna Mkristo yeyote ambaye ameitwa hivyo

katika Agano Jipya, kwa hiyo, bila shaka mtu huyu alikuwa

amepotea dhambini. Pengine alikuwa amesikia Injili kiasi fulani (ktk

Luka 1:4), lakini hakuwahi kusadiki. Kumbuka kwamba “Wayunani

hutafuta hekima” (ktk 1Wakor. 1:22), na si wepesi kukubali wazo

lionekanalo haliwezekani kwa jinsi ya kibinadamu, kama Injili

(unapoisikia mara ya kwanza). Kwa hiyo, Theofilo alishtuka na

kuhofu ukweli wakati alipoambiwa. Lakini Luka naye alikuwa mtu

wa Mataifa (yaani, asiyekuwa Myahudi), na pia alikuwa na matatizo

ya kiakili kwa habari ya Injili. Lakini, Luka akawa ameshawishika

kabisa kuhusu uhakika na ukweli wa Yesu Kristo na Injili Yake, basi,

akajitolea kuandika maelezo fasaha yenye utaratibu mzuri kuhusu

kweli za Yesu na Injili kwa Theofilo, mtu huyo ambaye hakuwa

amekubali ukweli.117

Page 126: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Basi, nini kusudi la Luka kuandika? Kumleta huyu mtu

mmoja kwa Kristo, apate kumwamini! Utafiti wa muda mrefu, kazi

ngumu na uandishi wote huo – kwa sababu ya mtu mmoja tu – ili

awe na “uhakika wa mambo hayo, ambayo alikuwa amefundishwa”.

Je, Injili ya Luka ilifanikiwa katika hilo? Ndiyo! Tunajuaje? Kwa

sababu katika mstari wa kwanza wa kitabu cha pili, Luka anaondoa

lile jina la cheo chake na kumwita “Theofilo” tu. Basi, hii kazi

kubwa ya uinjilisti ilifanikiwa kwa njia ya ajabu sana. Tabibu mmoja

Myunani, mtaalamu bingwa, alifanya utafiti kuhusu Injili kwa

ukamilifu kabisa na akamwandikia mkuu wa Kiyunani ili

kumshawishi juu ya Yesu na kumfikisha kwa Kristo na wokovu

wake. Na, ilitokea.

Basi, kwa nini Luka aliandika hii barua ya pili – Kitabu cha

Matendo (sura zingine 28 katika Agano Jipya lako)?: Kama huyo

mtu alifanikiwa kumwamini Kristo kutokana na barua ya kwanza,

kwa nini itakiwe ya pili? Ndugu zangu: Jibu la swali hili

linadhihirisha kushindwa vibaya sana kwa kanisa la siku za leo.

Kusudi la Kristo linakuwa ndiyo limeanza tu wakati mtu anapo-

okolewa! Nia ya Kristo ni kumhusisha kila mmoja katika wafuasi

Wake – waaminio wote waliozaliwa mara ya pili – katika shughuli

ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi, wenye maono ya dunia, na

wenye kuigusa dunia yote. Mpango Wake ni kwamba kila mwamini

awe mzalishaji wa wazalishaji huku akidumisha mtazamo wake wa

kutaka kufikia “mwisho wa nchi”. Nia Yake ni kwamba tufuate 118

Page 127: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mpango au mfano Wake – kuwaona watu makundi kwa njia ya mtu

mmoja, na kumjenga huyo mtu mmoja ili kuwagusa makundi. Basi,

Kitabu cha Matendo kiliandikwa na Dakta Luka ili kumtambulisha

Theofilo – katika dhana na mwenendo – aingie katika mkakati wa

kuifikia dunia wa Yesu Kristo.

Je, iliwezekana? Je, Theofilo alifanyika mwanafunzi mfanya

wanafunzi, mzalishaji wa wazalishaji? Kweli hatujui, na ni vizuri

zaidi kwa sababu, maana yake ni kwamba kila aaminiye anapaswa

kupewa nafasi zote kwa kuhusishwa kibinafsi, kuwezeshwa kibinafsi,

na kutumwa au kupelekwa kibinafsi - awe anazalisha au hazalishi.

Tunao ushahidi kiasi fulani kwamba Theofilo alishikwa na amri ya

kuwafanya watu kuwa wanafunzi maana, si tunasoma Kitabu cha

Matendo leo? Kwa hiyo, Luka aliandika kitabu kingine cha pili,

kirefu tu (sura 28 katika Biblia yako) ili kumwingizia mtu mmoja

wazo na kuteka moyo wake na kumkaribisha ashiriki katika kazi kuu

kuliko zote duniani.

Kama Roho Mtakatifu wa Mungu anaonyesha huku kuhusika

kwa hali ya juu sana katika maisha ya watu binafsi wa Agano Jipya,

wewe na mimi je, hatupaswi kuwa na kiasi kidogo cha watu binafsi

ambacho tutakuwa tunamimina na kuweka maisha yetu na maono

yetu kwao? Je, mimi sipaswi kuishi na ufahamu wenye kuwaka moto

kuhusu Agizo Kuu, na kutafuta kila njia ya kuufafanua na

kuushirikisha na makundi ya “watu waaminifu, ambao wanaweza

kuwafundisha wengine pia” (ktk 2Timotheo 2:2)?119

Page 128: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

USHUHUDA BINAFSI (wa mwandishi)

Hebu niingize ushuhuda wangu binafsi hapa. Nikiwa na

maono ambayo yamekuwa yakipanuka mara kwa mara kwa zaidi ya

robo karne, nimetumia muda mwingi sana na watu binafsi wengi

sana, na makundi madogo madogo mengi sana, na makundi mengi

sana ya wachungaji na wamishenari, na makusanyiko ya makanisa,

nikitafuta kuingiza haya ninayosema. Nimeona mafanikio makubwa

sana kiasi kwamba watu ambao nimefanikiwa kuwashawishi

wametapakaa katika sehemu mbalimbali kwa sasa katika dunia –

wakiwaleta watu kwa Yesu na kufundisha wanafunzi. Vile vile

nimeona kushindwa sana (na hata mwenyewe nimeshindwa kwa njia

ambazo hakika zilimhuzunisha Roho Mtakatifu). Ninaweza kujaza

kurasa nyingi sana kwa maelezo yenye kuthibitishwa kirahisi kuhusu

wanafunzi ambao wamekwenda ili kuzalisha aina hii ya wanafunzi

katika maeneo yao ya huduma. Wengi wao ni wachungaji (nami

nimepata fursa kubwa sana ya kuwafundisha na kuwatia moyo

wachungaji wengi zaidi na kuwatia moyo wale ambao wako katika

huduma tayari), baadhi yao ni wamishenari katika nchi za nje nyingi

tu, na wengine wengi ni “walei” wenye maono hai ya kufanya

wanafunzi mahali ambapo wanakaa, wanafanya kazi na kuabudu.

Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya fursa hii ya kipekee, nami

nimejizatiti zaidi leo kuliko wakati mwingine wowote kuhusika na

“kuwafanya watu kuwa wanafunzi”.120

Page 129: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

TAMKO LA WAZI LA KUSUDI LA KUANDIKA VITABU

VYAKE

YOTE AMBAYO YESU ALIANZA KUFANYA NA

KUFUNDISHA

Sasa tunatazama sehemu ya mwisho ya muhtasari wetu wa

Matendo 1:1 – tamko la wazi la kusudi la kuandika kitabu cha

kwanza, yaani Injili ya Luka. Luka anasema kitabu hicho kinahusu

“mambo yote ambayo Yesu alianza kufanya na kufundisha”. Ona

maneno tendaji matatu: “alianza” “kufanya” na “kufundisha”.

Maneno mawili hayo yanatupa mtazamo wa jumla wa huduma nzima

ya Yesu. Yesu ndiye mtu pekee katika historia ambaye amefanya

mlingano kati ya shauku ya KiMungu ya kufanya na kufundisha.

Katika kila huduma nyingine, iwe ya kanisa au ya Mkristo binafsi,

kumekuwepo na kutokulingana kwa maeneo hayo mawili.

Hebu fikiri kuhusu makanisa unayofahamu wewe. Mengine

yamezidisha sana eneo la kufanya. Kanuni yao ya utendaji ni kama

inawaambia hivi, “Okoka, halafu shughulika”. Wamekazia zaidi

shughuli lakini hawana mkazo kwenye mafunzo. Wako mbele

kwenye utendaji lakini wako nyuma sana kwenye kanuni na

mafunzo. Mtu mmoja alinieleza kichekesho kuhusu kanisa lake

mwenyewe kwa kusema hivi: “Ndugu, utagundua kwamba kanisa

letu lina upana wa maili 5, na kina cha robo inchi tu”. Alimaanisha

kwamba shughuli ya kukimbizana kwao inaongeza idadi ya watu 121

Page 130: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

daima katika kanisa, lakini kwamba kina chake kiroho hakilingani na

kukua kwake kiidadi.

Kwa upande mwingine, yapo makanisa ambayo yamekazia

kupita kiasi jambo la kufundisha. Daima wanalishwa Neno la Mungu

lakini hakuna mlingano unaofaa katika shughuli tendaji za huduma.

Washirika wa makanisa hayo wanaingia kwenye “kuwa na ugumu

wa moyo” ambayo ni aina fulani ya kuridhika na kujisikia

kunakoweza kupelekea majigambo na hatimaye hali ya kujihesabia

haki. Makanisa hayo yanakua kiasi cha kuridhisha, lakini Agizo Kuu

si ajenda muhimu ndani yao. Watabishana kuhusu maana ya kidole

cha tatu cha mguu wa kushoto kwenye sanamu ya Danieli, lakini

hawatajali hata kidogo mabilioni ya watu ambao bado hawajafikiwa

na Injili katika dunia yetu.

Yesu alikuwa na mlingano kamili kati ya kutenda na

kufundisha katika huduma Yake, na kila mmoja wetu anatakiwa

kutafuta hali hiyo kwa njia ya maombi katika maisha yetu na

makanisa tunayohudhuria na tunayofanya huduma.

Tunafikia kwenye neno “kubwa” tendaji katika Matendo 1:1.

Hilo ni neno “aliyoanza”. Injili ya Luka ilikuwa inahusiana na

mambo “yote ambayo Yesu alianza kufanya na kufundisha”. Hayo

matukio ya kihistoria katika maisha ya Yesu yanayotajwa mapema ni

mwanzo tu! Kama ni hivyo, yaani, kama “kitabu kile cha kwanza”

kilihusiana na mambo ambayo Yesu “alianza kufanya na

kufundisha,” basi kitabu hiki cha sasa, yaani Kitabu cha Matendo ya 122

Page 131: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mitume, kitakuwa kuhusu mambo yote ambayo Yesu anaendelea

kufanya na kufundisha. Lakini hapa tunapata tatizo mara moja.

Katikati ya sura ya kwanza ya Kitabu cha Matendo, huyo “mtendaji

na mwalimu” – yaani Yesu, anatoweka! Sasa, aliendeleaje kufanya

na kufundisha katika sura ishirini na saba na nusu zaidi kama

ameondoka machoni pao?

YESU ANAFANYA NINI WAKATI HUU?

Hebu tupanue hilo swali, hivi: Yesu anafanya nini kwa wakati

huu wa sasa? Anaendelea kufanya na kufundisha kwa kiwango cha

nia na kusudi Lake katika dunia yetu siku hizi, kama alivyofanya tu

wakati akiwa hapa siku za mwili Wake. Lakini, sasa anafanya vipi na

huku haonekani? Anafanya kwa njia ile ile aliyofuata wakati akiwa

hapa katika mwili Wake wa kibinadamu. Je, mbinu hiyo ilikuwa ipi?

Tunaiita “kufanyika mwili” ambayo maana yake ni kwamba “Neno

(logos, ‘wazo la Mungu’) alifanyika mwili, akakaa katikati yetu”.

Kwa hiyo, Mungu alishuka mpaka kiwango chetu kama binadamu

katika Nafsi ya Mwana Wake mpendwa, Yesu, na akaishi, akatenda

na kufundisha miongoni mwa watu. Je, siku hizi anatumia mtindo

gani? Huo huo kama wakati ule, ila, kuna marekebisho kidogo, kama

ifuatavyo:

1. Anakaa katika miili ya waaminio wote waliozaliwa mara

ya pili, kwa kusudi la kuendeleza utendaji Wake na kufundisha

Kwake kupitia kwao;123

Page 132: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

2. Tofauti na Yesu ni kwamba, kila mmoja wao (yaani sisi) ni

mwenye dhambi;

3. Kuna tofauti katika sifa kwa maana ya kwamba hakuna

yeyote kati yetu ambaye ni Yesu. Yeye ni Mwana wa Mungu wa

kipekee, mmoja tu.

Kwa marekebisho hayo kidogo, kila aaminiye anatakiwa

kuwa nyongeza ya Yesu Kristo kufanyika mwili! Mara tu mwenye

dhambi anapookolewa, Yesu Kristo huingia ndani kabisa ya maisha

ya mtu huyo kwa Uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu. Roho

Mtakatifu ameelezwa kama “Nafsi Nyingine Ya Yesu” na anaweza

kueleweka kwa urahisi tu kwamba ni Yesu pasipo mwili”. Basi, kila

aaminiye ni kasha lililo hai la Uwepo Binafsi wa Mwana wa Mungu,

na kusudi la msingi kwa ajili ya hilo ni ili huyo aaminiye awe

mwendelezo wa kudumu wa utendaji na mafundisho ya Yesu.

JE, YESU ALITUMIA WATU AINA GANI?

Hii inasabisha swali lingine, tena la muhimu sana. Je, Yesu

alitumia watu wa aina gani katika Kitabu cha Matendo, ili

kuendeleza utendaji na mafundisho Yake baada ya kupaa Kwake?

Cha kufurahisha ni kwamba, katika ile mistari ya kwanza ya Kitabu

cha Matendo tunapata jibu kamili la swali hilo. Mistari hiyo inatupa

picha nzuri tu ya wafuasi wa kwanza wa Kristo. Hebu tuchore picha

zao.

124

Page 133: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

1. WATU WA KAWAIDA

Cha kwanza ni kwamba, walikuwa watu wa kawaida.

Tunahitaji kukumbuka tu yote tuyajuayo juu yao kutoka katika Injili

kuona ukweli huo. Walikuwa ni mchanganyiko kutoka katika jamii,

watu wa kawaida kabisa. Wote isipokuwa mtu mmoja walitoka

Galilaya, na huyo mmoja alikuwa “yai bovu” – Yuda Iskariote.

Galilaya lilikuwa jimbo dogo lililodharauliwa sana katika Dola ya

Kirumi, na watu kumi na moja wa kwanza kabisa waliomfuata Yesu

walitoka huko. Walikuwa kundi la watu ambao “si chochote wala

lolote”, lakini akawatengeneza mpaka wakawa mashujaa Wake. Hili

linapaswa kumfanya kila mmoja wetu ajisikie vizuri sana kwa

sababu Yesu Kristo hahitaji kitu chochote kwetu kwa ajili ya

kufanikisha kusudi Lake kupitia kwetu isipokuwa kujitoa kwetu –

sisi ambao ni udongo wa kawaida tu.

2. WATU WALIOCHAGULIWA

Kinachofuata ni kwamba, walikuwa watu waliochaguliwaa.

Tazama mstari wa 2 wa Matendo sura ya kwanza. Watu Wake wa

kwanza wanaitwa “Mitume aliokuwa amewachagua”. Walichaguliwa

kwa ajili gani? Neno “mitume” linatupa kuona mambo makubwa

sana. Neno “mtume” linamaanisha “mtu aliyetumwa”. Aliwachagua

ili awatume popote alipotaka waende ili waweze kuwa, waseme na

kufanya chochote alichokitaka! Na hii ndiyo sababu alikuchagua

wewe na mimi! Ona lile neno “aliowachagua” mwishoni mwa mstari 125

Page 134: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wa pili. Kila neno tendaji la Kiyunani hutumika katika sauti tatu:

sauti ya kutenda, kutofanya chochote, na sauti ya katikati. Katika

sauti tendaji, mhusika hutenda, kama vile “Ninakimbia,”

“ninasimama,” “unatembea”, “unazungumza”. Katika kila tukio,

mada hutenda. Kutofanya chochote maana yake ni kwamba mhusika

hutendewa. Kwa mfano, “Nilikanyagwa!” Sauti ya katikati

huunganisha zile zingine mbili kiasi kwamba mhusika hutenda,

lakini kwa njia ambayo matokeo ya tendo humrudia yeye.

Sasa hili neno tendaji “waliochaguliwa” ni la sauti ya katikati

na hutupa kweli moja ya muhimu na ya kushangaza sana. Maana

yake ni kwamba, wakati Mungu alipokuchagua wewe, alikuchagua,

si kwa sababu ya wewe kufaidika – yaani upate afya, mali na furaha,

bali alikuchagua kwa ajili Yake Mwenyewe! Wewe ni Mkristo kwa

ajili ya Kristo! Uko hai kwa ajili Yake! Basi, wewe si Mkristo ili

mahitaji yako yatoshelezwe, au ili ujitosheleze mwenyewe na

kujiridhisha, bali ili utumiwe na kutumwa na Yesu Kristo kama

mwendelezaji wa utendaji Wake na kufundisha Kwake.

Nilipokuwa mvulana mdogo, baba yangu alinifundisha

kupenda mchezo wa kandanda. Kujua kwangu mchezo huo kulitoka

kwa baba, na ushindani wangu katika mchezo huo ulitoka kwa mama

yangu. Watoto wa pale mtaani walikuwa wanacheza kandanda mara

nyingi siku za Jumamosi katika sehemu iliyokuwa wazi kando ya

nyumba yetu. Nakumbuka jinsi nilivyokuwa nawakasirikia wakuu wa

timu kwa sababu, juma baada ya juma sikuwa nachaguliwa kuingia 126

Page 135: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kwenye timu, na kwa sababu hiyo, sikupata kucheza. Lakini pia

nakumbuka siku ya kwanza nilipochaguliwa kucheza. Hawakuwepo

wachezaji wa kutosha, ndipo mimi nikachaguliwa! Sikuhitaji muda

mrefu kutambua kwamba yule kiongozi wa timu hakunichagua kwa

sababu alinipenda. Yeye alinichagua kwa sababu alifikiri

kunichagua kungemsaidia ashinde mchezo.

Sijui kama mfano huo unaeleweka. Yesu Kristo ananipenda,

na hakuna ninachoweza kufanya kitakachomfanya aache kunipenda!

Hanipendi kwa kuwa ninapendeka, au ni mzuri, au nina upendo.

Ananipenda kwa sababu Yeye ni upendo – basi! Lakini,

hakunichagua kwa sababu alinipenda tu, pamoja na kwamba upendo

Wake ni mkubwa kama ulivyo. Alinichagua (pia) kwa sababu

alijisikia kwamba kunichagua mimi kungesaidia upande Wake

kushinda mchezo! Sasa je, kushiriki kwangu katika utume Wake wa

dunia nzima kunaweza kumfanya aone kwamba uchaguzi Wake

“ulistahili”? Au je, mimi “nimetulia huko Sayuni” tu, bila ya kufanya

chochote kuhusu kusudi la Kristo la dunia nzima?

Kila Mkristo asomaye maneno haya anapaswa atulie hapa na

kujiambia hivi: “Nimechaguliwa na Mfalme wa Wafalme wote!

Nimechaguliwa na Bwana wa utukufu! Je, ninatimiza kusudi Lake la

kunichagua?”

127

Page 136: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

3. WATU WALIOSADIKI

Halafu, walikuwa watu waliosadiki. Tunasoma hivi katika

Matendo 1:3, “Yesu Mwenyewe alijidhihirisha kwao akiwa hai

baada ya kufa Kwake kwa uthibitisho mwingi sana (yaani, ushahidi

usioweza kupingwa), akionekana nao kwa muda wa siku arobaini.”

Ndiyo maana baadaye, mmoja wao alikuja kuandika hivi,

“Tumeliona Neno la Uzima sisi wenyewe, kwa macho yetu” (ktk

1Yohana 1:1, TLR).

Vile vile kuna kipengele kingine cha haya maneno machache

tu kutoka Matendo 1:3 ambacho kinahitaji kutazamwa kwa makini.

Kinatokana na neno la Kiyunani “dia” ambalo maana yake “kati ya”.

Yesu “alionekana nao kati ya siku arobaini”. Hee! Mbona ni neno la

ajabu hilo! Nini maana yake? Maana yake ni kwamba kuonekana

Kwake na wanafunzi hakukuwa moja kwa moja katika siku zote

arobaini. Alionekana na kutoweka kama alivyopenda Mwenyewe

kwa hizo siku arobaini. Alitokea akaonekana, halafu akatoweka

asionekane, kama alivyopenda mwenyewe katika kipindi hicho cha

siku arobaini.

Hebu tuseme kwamba mimi na rafiki yangu tuko katika

mazungumzo mazito. Katika hali hiyo tunatazama vizuri. Lakini

ghafula, mwili mwingine unatokea katikati yetu! Wee! Kitu cha aina

hiyo kinashtua sana! Ndiyo maana ilikuwa kawaida kwa Yesu

kuanza mawasiliano Yake kwa maneno haya, “Msiogope” au “amani

iwe kwenu”. Sasa, mimi na rafiki yangu tunasahau kabisa 128

Page 137: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mazungumzo yetu na kushikwa kabisa na huyu mtu “aliyeingilia

kati”. Na hebu tuseme kwamba, tukiwa tumemkazia macho kiasi

hicho, mara tena anatoweka! Hayo ndiyo yaliyotokea mara kwa mara

katika kipindi cha siku zile arobaini baada ya kufufuka Kwake. Yesu

alitokeza na kutoweka tena na tena katika kipindi hicho.

Kitu cha ajabu hicho! Kwa nini alifanya hivyo? Alikuwa

anataka wanafunzi Wake wajue bila ya mashaka wala maswali

kwamba, awe anaonekana au haonekani, alikuwa pamoja nao wakati

wote! Na ni kweli hata siku hizi. Yesu Kristo yupo sana katika Nafsi

ya Roho Mtakatifu, kiasi kwamba anaweza kutokea katika umbo la

mwili – akitaka kufanya hivyo. Lakini kusudi Lake alilotamka ni

kwamba kila aaminiye ampe Yeye “mwili” kwa kuutoa mwili wake

kuwa “hekalu”, kuwa “Patakatifu pa Patakatifu”, kuwa mahali teule

kwa ajili ya Yesu kujionyesha Mwenyewe.

Unaonaje? Si ungesadiki kabisa kama ungemwona Yesu

kama wao walivyomwona? Kuwa mwangalifu sana hapo. Yesu

Mwenyewe alionyesha kwamba, kwa sababu ya Uwepo wa Roho

Mtakatifu, sisi ndiyo wenye faida, wala si wale waaminio wa kwanza

(ktk Yohana 16:7).

Swali: Wewe unasadiki kiasi gani kuhusu uhalisi wa Yesu?

Kuhusu uhalali wa madai Yake? Kuhusu ukweli wa nafsi Yake?

Kuhusu uwezo alio nao na mamlaka Yake? Kuhusu kusudi Lake la

utume duniani kote? Hakuna kazi kubwa ya Mungu iliyowahi

129

Page 138: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kufanyika kupitia watu wasiosadiki. Mungu na afungue macho yetu

kwa upya na kwa ukamilifu kuhusu Nafsi na kusudi la Yesu.

4. WATU WALIOPEWA AMRI

Kisha, walikuwa watu walioamrishwa. Matendo 1:2 inasema

kwamba, “Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliwapa amri”. Mstari

wa 4 unaongezea yafuatayo: “Baada ya kukutanika nao, Yesu

aliwaamuru kwamba wasiondoke Yerusalemu, bali waingojee ahadi

ya Baba, ambayo, kama alivyowaambia, ‘Mmeisikia kutoka

kwangu’.” Hiyo “ahadi ya Baba” ni Siku ya Pentekoste, siku ambapo

nguvu za ukombozi kamili za Roho Mtakatifu zilitolewa, siku

ambayo ingefuata muda si mrefu baada ya hapo.

Je, unaweza kufikiri kidogo mawazo ya mtu kama Simoni

Petro, mtu asiyetulia, asiye na subira kwa wakati huyo? Pengine

alisema hivi: “Yesu! Mbona huamui unachotaka? Umetumia miaka

mitatu kutuandaa twende, na sasa unatuambia tungoje!” Lakini,

hakuna hoja kama hiyo iliyotolewa. Kufikia wakati huu, Mitume

walikuwa wamekwisha jifunza kwamba Yesu si wa kubishana Naye.

Maana, Yeye ambaye ni Bwana Mkuu wa ulimwengu wote, yuko

sahihi wakati wote! Kanisa la leo lipate hekima kama hiyo!

Linatakiwa kutumia muda wake mwingi katika kuomba na

kuchunguza Biblia ili lisadiki kwamba linatenda kulingana na Akili

ya Kristo, halafu litumie muda wake mwingi kumtii Yeye!

130

Page 139: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Waarabu wa kale walikuwa wanazalisha aina maalum sana

ya farasi, na wakati mwingine walikuwa wanaitwa “farasi wa

KiArabu”. Hapo kwanza walikuwa wanazalishwa kwa ajili ya

kupandwa na wafalme tu. Sasa – kama sehemu ya mafunzo yao,

mfundishaji alikuwa anabeba firimbi na kamba ya ngozi kwenye

shingo yake. Kwa muda wa miezi mingi sana, farasi alikuwa

anafundishwa kuacha kufanya kila kitu akisikia firimbi ya mwalimu.

Alitakiwa kumwelekea yeye. Ilikuwa lazima kutii kikamilifu. Kukataa

kidogo tu kulihesabiwa ni kutokutii kabisa. Ndipo kwa muda wa siku

tano farasi angenyimwa chakula, na kwa siku tatu angenyimwa maji

ya kunywa. Katika kipindi hicho cha kumalizia mafunzo, alikuwa

anafungiwa katika zizi.

Siku ya mwisho, vyombo vyenye chakula na maji viliwekwa

mahali panapoonekana, kiasi cha mita kama hamsini hivi kutoka

zizini. Farasi angejitahidi kukifikia chakula na maji, kwa sababu ya

kuwa na njaa. Halafu ghafula, mlango wa zizi ungefunguliwa, na

yule farasi aliyeshangaa angeanza kuelekea kwenye vyombo vyenye

chakula na maji. Lakini akiwa anakaribia kufika, mwalimu

aliyesimama pembeni angepuliza filimbi! Farasi yule

angechanganyikiwa. Ilibidi afanye uchaguzi kwa haraka. Wa aina

gani? Je, aende kwenye vyakula na maji, au amfuate mwalimu?

Kama farasi angeendelea kwenda kwenye vyombo na kutosheleza

njaa yake na kiu yake, na kwa kufanya hivyo awe amekataa kumtii

mwalimu, basi angeanza upya mafunzo, au angetolewa katika 131

Page 140: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

utaratibu huo wa mafunzo. Kama farasi huyo angechagua kinyume

cha hisia na kujisikia kwake na kumtii mwalimu na kufuata utaratibu

wa mafunzo kwa kumwendea mwalimu kwanza, basi aliruhusiwa

kwenda kunywa maji na kula chakula kilichokuwepo.

Wapendwa: Kila siku sisi tunakabiliwa na uchaguzi kama

huo. Tutachagua nini – vyombo vya chakula, yaani kujitosheleza, au

amri za Mwalimu. Hao walikuwa watu walioamrishwa, na Yesu

anatazamia na sisi tufanye hivyo hivyo kama wao.

5. WATU WALIOTAWALIWA

Hatimaye, walikuwa watu waliotawaliwa. Katika mstari wa

4, Yesu alisema nao kuhusu “ahadi ya Baba” iliyokuwa inahusu ujio

wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuliwezesha Kanisa Lake Siku ile ya

Pentekoste.

Katika mstari wa 5 alisema hivi, “Mtabatizwa katika Roho

Mtakatifu siku si nyingi zijazo”. Tulisema Roho Mtakatifu ni kama

“Yesu asiye na mwili”. Basi, atafanya mambo yale yale, atafuata

makusudi yale yale na kujenga watu aina ile ile ambayo Yesu

alijenga, alipokuwa hapa katika mwili. Kama Yesu alitoa watu wasio

na mwelekeo na wasiosikia la mtu, basi na Roho Mtakatifu atatoa

watu aina hiyo hiyo. Lakini, Yesu hakutoa watu wa namna hiyo.

Alitoa watu waliokuwa wameandaliwa vizuri kitaaluma, wenye

ujuzi, na wenye kuhusika. Walikuwa watu ambao wangeweza

kumwakilisha Yeye katika hali yoyote. Walikuwa watu 132

Page 141: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

walioshughulikia mambo yote kuhusu Neno la Mungu na kulifanyia

kazi vizuri kabisa katika kila hali.

Na sasa, tangu Siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu ni “Rafiki

Anayekaa Nasi” aliyeko kila wakati na aliye tayari kutawala na

kututia nguvu kwa ajili ya Utume wa Bwana wetu. Je, umejazwa na

huyo Roho Mtakatifu aliye mkuu na mpole? Je, unatawaliwa na

Yeye kwa ndani ili aweze kuamua tabia yako, mwenendo wako, na

ratiba utakayofuata maishani – au unayofuata maishani?

133

Page 142: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 5Vinavyotakiwa Ili Kufanya Wanafunzi

Au

Dawa Ya Daktari Kutibu Tatizo La Kuacha Agizo Kuu

“Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile Neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.”

Luka 1:1-4

“Maana (kama inavyojulikana vizuri tu) wengi wamechukua jukumu la kupanga kwa utaratibu na kuandika maelezo (kamili) ya matendo yaliyothibitika na kutimizwa kwetu na katikati yetu, kama tulivyosimuliwa moja kwa moja na wale ambao tangu kuanza (rasmi kwa huduma ya Yesu) walikuwa mashahidi waliojionea kwa macho yao wenyewe na wahudumu wa lile Neno (yaani, fundisho kuhusu kupatikana kwa wokovu katika ufalme wa Mungu kwa

134

Page 143: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

njia ya Kristo) . Nilipoona kwamba ni vizuri na kitu cha kutamanika kwangu pia (nimekusudia), na baada ya kufanya uchunguzi kwa bidii na kufuatilia mambo yote kwa ukaribu na kwa usahihi, kuanzia mwanzo kabisa, yale mambo makubwa hadi madogo kabisa, kukuandikia maelezo yenye kufuata utaratibu mzuri, Ewe Theofilo mheshimiwa, (kusudi langu ni) ili upate kujua kweli kamili, na kuelewa kwa uhakika na kwa usalama dhidi ya makosa maelezo (au historia) na itikadi za imani ile ambayo ulijulishwa, na ambayo ulifundishwa kwa kuelezwa tu.”

Tafsiri Ya Biblia Fafanuzi

“Kwa kuwa waandishi wengi wamechukua jukumu la kuandika masimulizi kuhusu kweli ambazo zilithibitishwa miongoni mwetu, kama ambavyo mashahidi walioona mambo hayo ambao walikuja kuwa wahudumu wa ujumbe huo walivyotuambia, mimi nami, Ee mheshimiwa Theofilo, kwa kuwa nimechunguza yote kwa makini sana tangu mwanzo, nimejisikia niyaandike kwa mfululizo mzuri kwa ajili

135

Page 144: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

yako, ili uweze kujua vizuri uhakika wa mambo hayo uliyofundishwa.”

Tafsiri ya Biblia ya Williams

“Mwandishi, kwa Theofilo:- Waandishi wengi wamejitahidi kuandika maelezo ya matukio yaliyotokea miongoni mwetu, wakifuata mapokeo tuliyopewa na wale walioyaona kwa macho yao wenyewe na watumishi wa Injili. Basi na mimi kwa zamu yangu, Ee Mheshimiwa, kama mtu aliyepitia kwa makini sana mambo hayo yote, nimeamua kuandika simulizi lenye umoja kwa ajili yako, illi nikupe maarifa hakika kuhusu mambo ambayo umeambiwa.”

Tafsiri Ya Biblia Mpya Ya Kiingereza

Katika Zaburi 119:18 kuna sala hii: “Fungua macho yangu

Ee Bwana, nipate kuona mambo ya ajabu yaliyo katika sheria Yako”.

Hebu nikushauri wewe pia uombe sala hii daima unaposoma na

kujifunza sura hii. Halafu, tunasoma hivi katika Zaburi 119:130,

“Neno Lako linapoingia, linaleta mwanga; linatoa ufahamu kwa

asiyekuwa na ufahamu.” Na iwe hivyo tunapojifunza kwa pamoja.

Basi tuanze mafunzo yetu kwa kutazama kwa makini sana

mtiririko ulioko kwenye mchoro huu:

136

Page 145: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

NENO MWILI NENO MWILI NENO (weka

jina lako hapa) NENO MWILI.

Mtiririko huu unawakilisha jinsi ambavyo Injili huenea

miongoni mwa watu katika historia ya Ukristo (ktk Warumi 10:14).

Unaanzia kwa “Neno” – “Logos” – kufanyika mwili na kukaa

katikati ya wanadamu (ktk Yohana 1:14). Baada ya hapo, kila kuenea

(au kusonga mbele) ni mtindo ule ule ambao umerekebishwa kidogo,

yaani, Neno kufanyika mwili. Katika muda muafaka, kwa muujiza

wa neema ya Mungu na uwezo Wake, wokovu Wake “ulifanyika

mwili” ndani yako. Hapo, jina lako likaingia katika mtiririko kama

ilivyoonyeshwa hapo juu – na mwelekeo wako wa maisha pamoja na

kazi vikabadilika milele. Sasa, swali muhimu sana: Kwa kuwa jina

lako limeingizwa katika mtiririko huo, je, mtiririko utaendelea

kupitia kwako? Au kiunganisho hicho kitakatikia kwako

utakapokufa? Je, mtiririko unaweza kuwa kama ifuatavyo? MWILI

NENO MWILI …? Je, mtiririko uliokusudiwa kuendelea

utakomea kwako?

Hebu kabiliana na hilo swali kwa mara nyingine tena: Je,

mtirtiriko utaendelea katika historia kutokana na nafasi au sehemu

yako uliyofanya wakati ukiwa hai? Ili mtiririko uendelee na wewe,

kuna kazi ambayo lazima ujifunze, nayo imekwisha fafanuliwa na

kupangwa kwa ajili yako vizuri sana katika Neno la Mungu. Kama

utakachofanya ni kumleta mtu kwa Kristo tu, kiunganisho kinaweza

kukatikia kwa huyo mtu utakayemleta kwa Kristo. Kama utamleta 137

Page 146: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mtu kwa Kristo na kumfundisha pasipo kufahamu kikamilifu na

kutekeleza kile “kiwango” (cha kufanya wanafunzi wenye maono ya

dunia, mguso wa dunia, na wenye kujiongeza), huenda huo mtiririko

ukakatikia kwa huyo utakayemleta kwa Kristo na kumfundisha.

Ukweli ni kwamba, utamfanya kuwa “Mkristo bora” tu. Ni pale

unapomleta mtu kwa Kristo na kumfundisha kulingana na kiwango

kilichofunuliwa katika Biblia ndipo Mungu atakapohakikisha

kwamba mtiririko ule hautakatika, na wewe mwenyewe utahakiksha

kuendelea kwake kwa kuweka msingi kwa ajili ya vizazi vingi vya

baadaye.

Injili ya Luka, iliyoandikwa na mtu pekee ambaye hakuwa

Myahudi, ni kitabu kikubwa sana chenye kujaa shughuli ya kufanya

wanafunzi watakaofikia dunia nzima. Kufanya wanafunzi wenye

maono na watakaofikia dunia nzima ndicho kiwango cha kuendelea

mbele kwa Injili katika Agano Jipya. Kumbuka kwamba Luka

hakuwa mtume, hakuwa mhubiri, hakuwa mwinjilisti, wala hakuwa

hata shemasi. Luka alikuwa mtu wa Mataifa – asiyekuwa Myahudi.

Alikuwa mwanasayansi, tabibu na mwanahistoria asiyekuwa

mtaalamu ambaye aliwezeshwa na Roho Mtakatifu kuandika kitu

ambacho hakina makosa. Luka alifanya aliyofanya kwa sababu ya

kupenda shughuli hiyo. Dakta Luka ni mfano mkuu wa milele wa

kile kiwango cha NENO KUWA MWILI KUWA NENO katika

Agano Jipya. Mistari minne ya kwanza katika Injili kulingana na

Luka inafanyika utangulizi wa kitabu hicho, na ni kama iliandikwa 138

Page 147: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

baada ya kitabu chote kukamilika (kutokana na jinsi maneno

yalivyopangwa). Katika hiyo mistari, tunaona mfano mmoja mkuu

sana wa kufanya mwanafunzi upatikanao katika Biblia.

Katika utangulizi wake wa ajabu sana, Dakta Luka

anaonyesha tabia nne muhimu sana za mtu anayefanya wengine

kuwa wanafunzi, aliye na maono ya dunia na mwenye lengo la

kugusa dunia na kujiongeza. Mwanafunzi yeyote anayetaka kujua

uhalisi wa ukubwa wa maono ya Mungu yeye mwenyewe na kwa

ajili ya kizazi chake na vizazi vifuatavyo, lazima aingize tabia hizo

na kuzifanya zake katika maisha yake, na ni lazima naye azijenge na

kuzitia ndani ya kila mwanafunzi ambaye Mungu atampa.

Dakta Luka alikubali wajibu binafsi kwa ajili ya kumjenga

Theofilo. Aliingia katika utafiti mzito kwa niaba ya Theofilo.

Aliandaa vitendea kazi thabiti kwa ajili ya kumwezesha Theofilo, na

alifanya kila kilichowezekana kibinadamu kuzalisha kwa mpango wa

kudumu wanafunzi wengine wenye maono ya dunia, wenye mguso

wa dunia na wenye kujiongeza, kwa njia ya Theofilo. Soma sentensi

ya mwisho kwa makini sana, ukifikiri vizuri kabisa – “Yatafakari

ninayosema, na Bwana akupe ufahamu katika mambo yote” (ktk

2Timotheo 2:7).

WAJIBU BINAFSI

139

Page 148: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kama wewe unataka kufuata kiwango cha Agano Jipya,

lazima ukubali kuwajibika kibinafsi kwa ajili ya kuwajenga watu

kuwa wanafunzi kulingana na Agano Jipya.

Luka alianza kwa kukubali juhudi nzuri za wengine, katika

kutayarisha maelezo kuhusu maisha na huduma ya Yesu. Ingawa

wengine walikuwa wamefanya kazi kubwa na ngumu ili kuandika

masimulizi kuhusu Yesu, Luka alisema, “Niliona ni vizuri hata mimi

pia …” Roho Mtakatifu alikuwa anafanya kazi kwa njia ya Luka ili

atende zaidi ya jinsi Luka alivyoweza kufikiri. Luka aliona mtu

mmoja tu – Theofilo. Mungu aliona vizazi vingi sana – mpaka na

sisi! Luka aliandika kitabu kimoja kwa mtu mmoja. Mungu aliandaa

Injili ya ajabu sana kwa ajili ya vizazi vyote vya wakati ujao! Sisi

tunawea kuona mwanafunzi mmoja tu, lakini Mungu anaona

makundi ya watu ambao watafikiwa na kuguswa na huyo

mwanafunzi mmoja.

Historia ya Kanisa la Kikristo inathibitisha kwamba hii dhana

ya KiMungu ni rahisi sana kiasi cha akili za kibinadamu kushindwa

kuiona. Usipofanya watu kuwa wanafunzi, ni kwamba hukubaliani na

kiwango cha Yesu, na unaacha kutii amri ya Yesu. Usipowajenga

wanafunzi wako kufikia kiwango cha kuwa na maono ya dunia

nzima, kuweza kuigusa dunia nzima, na kukamilisha utaratibu wa

kufanya wanafunzi wanaoweza kujiongeza wenyewe, hujakubaliana

wala kulingana na kiwango cha Yesu – pasipo kujali mengine yote

yanayoendelea katika maisha yako! Injili yenyewe imejengwa 140

Page 149: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kwenye kukubaliana na Mungu (ktk Warumi 10:9; Mathayo 10:32,

mahali ambapo “kukiri” maana yake kukubaliana na) kuhusu sisi

kutolingana na kiwango Chake. Basi, tunaletwa na Roho Mtakatifu

kwenye kukubaliana na Mungu kuhusu jinsi anavyomwona Mwana

Wake, Yesu Kristo. Maisha yetu yote baada ya hapo yanapaswa

kuwa ni makubaliano na Mungu na mapenzi Yake. Tunapotazama

amri Yake na kiwango Chake, tunaona kwamba haitoshi kwa

Mkristo binafsi kuanza tu kuwahudumia watu, kuwa mtu mzuri kwa

watu, kutafuta kukutana na mahitaji ya watu, au kuwa mhudhuriaji

mzuri tu na mwaminifu kanisani. Lazima tuamue kati ya sisi

wenyewe (“kujikana wenyewe,” ktk Mathayo 16:24) na kukubaliana

na Mungu. Na kwa kuwa tunaambiwa kulitimiza Agizo la Yesu

“tukiwa tunakwenda”, hatupaswi kupiga hatua hata moja bila ya

kutekeleza Agizo Lake na Mbinu Zake pia.

Fikiri maneno ya Bwana wetu katika Yohana 15:16, “Ninyi

(mkazo mkubwa kabisa) hamkunichagua Mimi, bali Mimi (mkazo

mkubwa) ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka, ili ninyi (mkazo

mkubwa) mwende na kuzaa matunda (tendo linaloendelea, mkazo

mkuu) na kwamba matunda yenu yapate kudumu (kitu

kinachoendelea wakati huo huo), ili chochote mtakachomwomba

Baba kwa jina Langu, aweze kuwapa.” Je, nini kazi ya matunda? Mti

unaozaa matunda hauli matunda yake wenyewe; ni kwa ajili ya

mwingine. Sehemu moja ya tunda ni ili kuliwa, lakini sehemu

nyingine ya tunda ni ili kuzaliana. Mbegu katika tunda huendeleza 141

Page 150: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

utaratibu wa kuzalisha chakula na kupatikana kwa matunda mengine.

Je, katika embe kuna mbegu ngapi? Moja tu! Lakini, kuna maembe

mangapi katika hiyo mbegu moja? Mungu tu ndiye ajuaye!

Umeingizwa katika Ufalme wa Mungu ili uwajibike kibinafsi

kwa ajili ya mtu anayekuja. Lakini, hakuna kitakachotokea tu! Leo

utakutana na watu wengi wasiohesabika katika makundi ya maishani,

ambao wanaweza kupatikana kwa ajili ya shughuli ya kufanya watu

kuwa wanafunzi (wakiingizwa kazini vizuri, na wakipata habari

sawasawa, na kufundishwa sawasawa) – na pengine hutamjali hata

mmoja wao. Bila ya “kuona na kusikia” kwa mtazamo wa Mungu

hutaweza kutimiza wajibu wako binafsi kwa ajili ya mtu anayefuata.

Naomba nikukumbushe kwamba, lile swali “Kwani mimi ni

mlinzi wa ndugu yangu?” lilitolewa kwa Mungu kutoka moyoni mwa

muuaji wa kwanza duniani, aliyekuwa anajitetea na mwenye kujaa

chuki moyoni! Nisipojiunga na Yesu katika kuwajibika kibinafsi kwa

ajili ya kumjenga mtu anayefuata ili afikie dunia nzima, mimi

ninajiunga na mawazo ya muuaji. Jibu la Mungu kwa swali la Kaini

likawa, “Ndiyo. Wewe ni mlinzi wa ndugu yako. Tena – muhimu

zaidi – wewe ni ndugu ya ndugu yako!” Sasa, unafanya nini kuhusu

Habili wako? Hebu useme pamoja na Luka kwamba, “Niliona ni

vizuri na mimi pia. Ninachukua wajibu binafsi kwa ajili ya mtu

ambaye Mungu kanipa.”

UTAFITI MZITO142

Page 151: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kama unataka kufuata kiwango cha Agano Jipya, lazima

uingie katika utafiti mzito wa Neno kwa ajili ya mwanafunzi wako.

Yesu alisema hivi: “Ninajitakasa mwenyewe kwa ajili yao”, na

maisha yako lazima yalingane na Yake. Haitoshi tu kujifunza Biblia.

Kuna watu kila mahali ambao wamo katika kujifunza Biblia ambao

hawatawahi kumjenga mtu mmoja anayefanya watu kuwa wanafunzi

ambaye anajiongeza, atakayeigusa dunia. Kwa nini? Sababu ni rahisi

tu: mtazamo wa mwalimu wa Biblia na hata wa mwanafunzi

anayejifunza Biblia hiyo hawana maono kwa ajili ya kuigusa dunia.

Wale wanaohusika katika kujifunza Biblia hawaioni kama njia kwa

ajili ya kuifidia dunia, wala hawatengenezi mtaala kutokana na

kujifunza Biblia kwao ili kuwajenga watu watakaoigusa dunia kwa

makusudi. Badala yake, wanajifunza Biblia ili “kujua zaidi” na kuwa

“Wakristo bora zaidi”. Mpaka inafikia mahali pa kutiliwa mashaka

ikiwa kweli hayo ni makusudi mazuri na yanayofaa kwa ajili ya

Mkristo. Yanaonekana kama ni malengo ya “kuufanya Ukristo

kununulika kwa mteja”. Kibaya zaidi ni kwamba, hilo huzalisha

kuingia kubaya kwa Injili, badala ya upandaji utakaozaa, wenye

kusababisha mavuno makubwa sana ya kiroho hadi miisho ya dunia,

mpaka wakati wa mwisho kabisa. Mtu yeyote anaweza kujisomea

Biblia kwa faida yake mwenyewe. Lakini, uwezo wa kuigusa dunia

unatokana na maisha ya wale ambao kwa makusudi kabisa wanaingia

katika utafiti wa dhati kabisa kwa ajili ya kusudi la kumjua na

143

Page 152: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kumfuata Kristo kweli kweli na kumfanya Yeye ajulikane kwa

wengine.

Tazama Luka 1:3 na utazame lile neno “kuchunguza”. Hili

neno lina uzito sawa na “kutumia kwa uhalali” katika 2Timotheo

2:15, na ndiyo neno “kujulikana kabisa” katika 2Timotheo 3:10,

ambapo Paulo alimwambia Timotheo hivi: “Wewe umeyajua vizuri

mafundisho yangu, jinsi ninavyoishi, makusudi yangu, imani yangu,

uvumilivu wangu, upendo wangu na subira yangu …” Neno la

Kiyunani litumikalo katika Luka 1:3 na 2Timotheo 3:10 ni

parakolutheo, ambalo maana yake ni “kutembea na mtu mguu kwa

mguu, kufuata kwa karibu, kusikiliza kwa makini sana.” Katika

lugha ya mfano, neno parakolutheo linamaanisha kufuata kwa karibu

njia ya kifikra iliyowekwa wazi na mtu ambaye ameipitia sana,

akichunguza kila kitu na kutokuacha kugeuza jiwe lolote. Hebu

msomaji na atafakari kwa kirefu sana juu ya hiyo sentensi ya

mwisho. Na kwa mara nyingine tena, “Fikiri hayo ninayosema, na

Bwana akupe kuelewa mambo yote” (ktk 2Timotheo 2:7). Hii njia ya

kifikra katika mstari huu ni yale matukio halisi yenye kumhusu Yesu

Kristo tangu milele hadi milele. Wakati Yesu alipotoka mbinguni na

kuingia katika wakati, alianzisha njia mpya katika ardhi ngumu

yenye vingi, ya kihistoria. Kila Mkristo anapaswa kuifuata njia hiyo

kifikra na kiroho, akichunguza kila jambo ili aweze kuzalisha hayo

mambo katika maisha yake mwenyewe na kujenga kutokana na hayo

144

Page 153: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

somo na mtaala kwa ajili ya wanafunzi wake mwenyewe. Hii itahitaji

utafiti mzito.

Neno parakolutheo lina maana nyingine. Linamaanisha

“kufuatilia”. Wazo hapo ni kama vile mtoto mdogo anavyofuatisha

mchoro kwenye karatasi. Anachofanya ni kuweka karatasi nyepesi

juu ya kile anachotaka kukichora, na kwa utaratibu na uangalifu sana

anafatisha kila mstari, kila kitu kinacho-onekana. Matokeo yake ni

nakala halisi kabisa ya kile kilichokuwa kinaigizwa. Basi, Luka

anajitokeza ili kufuatisha tabia na kuzalisha moyo na shauku ya Yesu

wa Nazareti. Wakati Luka alipoondoa chombo alichotumia kuandikia

Injili ya Luka kwenye ukurasa wake wa mwisho, uzuri wa Yesu, na

ubinadamu Wake na huruma Yake kwa ajili ya wanadamu

vilidhihirishwa kwa hali ya juu sana. Kazi ya Luka iliyokamilika

haifanani na yoyote nyingine ya mwandishi wa Injili. Roho

Mtakatifu ndiye aliyeongoza kalamu ya Luka kufuatisha mfano wa

Mungu ulioko katika ubinadamu wa Yesu. Sisi nasi tunapaswa

kufuata mwongozo wa Luka katika kufuatisha tabia ya Yesu, njia

aliyofuata, na mtaala alioutumia katika kuwagusa watu – na

tunapaswa kwenda na kufanya vivyo hivyo!

Mapema kidogo tulitaja 2Timotheo 2:15. Neno la Kiyunani

linalotumiwa hapo na kutafsiriwa “kutumia kwa usahihi” linahusiana

na neno letu parakolutheo. Ni neno orthotomeo. Hebu lifikiri kidogo.

Neno lenyewe ni maneno mawili – orthos lenye kumaanisha “sawa,

sahihi,” na temno lenye kumaanisha “kukata, kugawa, kutumia kwa 145

Page 154: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

utaalamu”. Hakika, Luka alikuwa tabibu mwenye ujuzi na utaalamu

sana, ambaye alifahamu maana ya kuwa makini na kujali vitu

muhimu kutokana na kazi na taaluma yake. Luka alielewa kwamba

kama ishara moja au dalili moja ingeshindikana kuonekana,

mgonjwa wake angekufa. Alikuwa mtumiaji mwenye kuwajibika wa

ujuzi na habari na matumizi ya taaluma katika maswala ya uzima na

kifo. Naye alijua kwamba mada yake aliyokuwa anaishughulikia

wakati huo ilikuwa swala la uzima au kifo – kwenda mbinguni au

kwenda jehanamu!

Utafiti bora zaidi kihistoria unaonyesha kwamba Luka

alikuwa amefundishwa sayansi na kuelimishwa katika matibabu

katika kile chuo cha uganga kilichokuwa Tarso. Kuna wasomi

wengine wamefikia mpaka hatua ya kupendekeza kwamba Paulo,

Luka na Theofilo walikuwa wanafunzi pamoja katika chuo kikuu cha

Tarso. Basi, alikuwa amepata mafunzo bora zaidi kwa habari ya

utabibu yaliyokuwa yanapatikana wakati ule. Vyovyote vile,

yawezekana kwamba Luka, mwanafunzi bora sana wa utabibu,

alimfahamu Sauli, aliyekuwa mwandishi na mwanatheolojia stadi,

kabla ya kukutana katika Kitabu cha Matendo (ktk Matendo 16).

Inaonekana kwamba Paulo, kwa sababu ya tatizo kubwa la kiafya (na

kitabu cha Wagalatia kinaonyesha lilikuwa tatizo kubwa sana la

macho) alikwenda kutafuta msaada wa Dakta Luka. Inawezekana pia

kwamba Paulo (pengine katika kuhudumiwa) alimshirikisha Dakta

Luka Injili na habari za Kristo. Wakati Luka alipokuwa anamtibu 146

Page 155: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Paulo macho ili kurekebisha tatizo lake, Mungu Roho Mtakatifu

alipenya katika giza la upofu kiroho wa Luka na kuleta “nuru tukufu

ya Injili ya Kristo, aliye mfano wa Mungu” (ktk 2Wakor. 4:4).

“Mungu” huyo huyo, “aliyeamuru nuru ing’ae gizani”, aliangaza

katika moyo wa huyo daktari, “ili kutoa nuru ya maarifa ya utukufu

wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo” (ktk 2Wakor. 4:6)! Baadaye

kidogo, wakati Paulo alipotamka nia yake ya kuondoka Troa akiwa

na timu yake ya utume kwenda eneo lingine walilopangiwa, Luka

akaomba kuambatana naye. Pengine Paulo alisema hivi: “Lakini

Daktari, mbona una hospitali yako hapa? Huwezi kuiacha tu!” Na

pengine Dakta Luka akajibu hivi: “Hapana, ila, ni nzuri, na ninaweza

kumwachia mtu mwingine kwa urahisi tu.” Basi Luka akaiuza

hospitali yake pengine, na kujiunga na mtume Paulo katika safari

zake za kitume zilizokuwa zimesalia!

Luka ndiye mwandishi pekee wa Injili aliyekuwa amesomea

sayansi ya udaktari. Sasa, anaingiza mafunzo yake yote na utaalamu

katika kukusanya kweli za habari ya Kristo kutoka kwa wale

waliokuwa mashahidi, waliojionea mambo ya Yesu. Katika kusafiri

kwake na Paulo, na bila shaka katika safari zake binafsi, alikutana na

hao watu waliojionea mambo hayo katika Asia Ndogo, katika

sehemu mbalimbali za Palestina, na hasa huko Yerusalemu. Kidogo

kidogo, madaftari ya Luka yakaanza kujaa kutokana na mahojiano

binafsi mengi aliyokuwa amefanya. Hii ni kawaida kabisa, kwamba:

alama moja ya mtu anayefanya wanafunzi wenye maono ni daftari 147

Page 156: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

linaloendelea kujaa! Daftari la Luka liliendelea kujaa maneno

aliyosema Yesu na mambo aliyofanya. Kila alipokutana na mtu

yeyote ambaye alikaa na Yesu kwa muda fulani, au aliyekutana na

Yesu au aliyeona miujiza ya Yesu, angeuliza maswali muhimu ya

kutafiti: “Je, wewe ulimjua Yesu kibinafsi?” “Alikuwa anafanya nini

wakati ulipomwona?” “Je, Yesu alisema nini?” “Niambie kila kitu

unachojua kuhusu Yeye.” Baadhi ya watu aliowahoji kwa karibu

sana ni Petro, Yakobo, Yohana na wengine katika wale Mitume wa

kwanza. Bila shaka alizungumza na Yohana Marko kwa ukaribu

sana, ambaye naye alikuwa anamalizia Injili yake wakati huo (yaani,

Injili ya Marko). Kuna ushahidi mzito kabisa kwamba Luka alifanya

mazungumzo ya hali ya juu sana na Mariamu, mama yake Yesu.

Daktari aliandika maelezo mapana sana kuhusu kuzaliwa kwa Kristo

na bikira kuliko mwandishi yeyote mwingine wa Biblia, na

madaktari si wepesi kuamini sana kwamba bikira huzaa! Kuna

mwandishi mmoja anayeitwa William Hobart aliyeandika kitabu

kikubwa tu kuhusu lugha ya kitabibu ya Dakta Luka, na ndani yake

anaonyesha zaidi ya maneno mia nne maalum kabisa ya kitabibu

ambayo Luka aliyatumia alipoandika Injili yake na Kitabu cha

Matendo. Ni kwamba Daktari huyu aliamini kabisa kuhusu kuzaliwa

kwa Kristo na bikira kutokana na ushahidi wenye nguvu na usioweza

kupingika. Aliweza kuona na kupata habari kamili kuhusu kuzaliwa

kwa Yesu kupitia mahojiano ya moja kwa moja na Mariamu

mwenyewe. 148

Page 157: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sasa – kwa utaalamu wa hali ya juu sana kisayansi, tabibu

huyo maarufu na mwenye utaalamu aliandika simulizi lenye

mpangilio mzuri sana kuhusu maisha ya Bwana Yesu. Anatoa taarifa

yenye upana na maelezo mazuri kuhusu kuzaliwa Kwake, maisha

Yake na mafundisho, kifo Chake, kufufuka Kwake, baadhi ya

matukio katika zile siku arobaini baada ya kufufuka Kwake, na

kupaa Kwake. Ni wazi kwamba Luka alifanya juhudi kubwa sana

kutafiti kuhusu Nafsi, mafundisho, matendo na mafanikio ya Yesu.

Katika Luka 1:3, neno “kamili” linatokana na neno la Kiyunani

akribos, ambalo maana yake ni “kwa bidii, kwa makini, au kwa

uangalifu sana.” Luka alimtafiti Yesu kuanzia juu (akron – kiwango

cha juu kabisa) hadi chini (abussas – chini kabisa, shimoni). Luka

anasema, “Ee Theofilo, sikuacha kujitahidi katika kumtafiti Yesu

tangu maelezo ya hali ya juu zaidi hadi kweli za ndani kabisa.” Luka

alikuwa na uhakika kwamba amefanya juhudi zake zote kutafiti kila

kitu kuhusu maisha ya Yesu – tokea juu hadi chini.

Zile Injili nne za Agano Jipya hazikuandikwa katika utupu

usio na uchafu wowote, bali katika purukushani za kawaida za

maisha. Ingawa kila Injili imevuviwa na Roho Mtakatifu, inazo

alama pekee na vidokezo vya mwandishi wake. Yohana inasikika

kama Yohana, Marko kama Marko, Mathayo kama Mathayo –

ingawa kila mmoja anaandika kitabu ambacho ni kamilifu, na hata

ingawa kila kitabu ni juu ya Mhusika kamili. Katika Luka 1:1,

Daktari alisema kwamba maelezo yake yana mambo kuhusu Yesu 149

Page 158: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ambayo yalitimizwa na kukamilishwa mbele ya watu wa wale

aliokuwa amewahoji. Yohana ambaye ni mwandishi mwingine wa

Injili alisema katika barua yake ya kwanza kwa watu wote kwamba

hao mashahidi walikuwa wamemwona, kumsikia na kumgusa Yesu.

Hivyo, walitoa ushahidi wa mambo waliyoona, waliyosikia na

waliyogusa wenyewe. Neno “shahidi aliyeona” kwa Kiyunani,

litumikalo katika Luka 1:1 ni autoptes, ambalo ni maneno mawili

yenye maana ya “kujionea mwenyewe”. Maelezo ambayo Luka

alisikia toka kwa hao watu waliojionea kwa macho yao wenyewe

mambo hayo yalikuwa na nguvu sana kumshawishi yeye mpaka

akawa na uhakika kwamba yangeshawishi, kusadikisha na

kumtosheleza yeyote ambaye angeyatafiti mwenyewe kwa ukamilifu

zaidi. Katika Kitabu cha Matendo, anayaita “vithibitisho vingi

visivyotiliwa mashaka” au

”ushahidi usiopingika” (ktk Matendo 1:3). Anaandika Injili yake ili

kutoa huo ushahidi wenye nguvu sana utokanao na maelezo hayo.

Tena, Luka anatuambia kwamba alitafuta habari na ushahidi

toka kwa wale watumishi wa mwanzo kabisa wa Kristo, wengi

ambao walikuwa wametoa maisha yao au wangekuja kuyatoa

baadaye, kutia muhuri ushuhuda wao kuhusu Yesu kwa damu zao

wenyewe. Neno “watumishi” linalotumika katika Luka 1:2 kwa

Kiyunani ni huperetes, ambalo maana yake ni “mpiga makasia wa

chini”. Neno hili lilitumika kusema kuhusu mtumwa aliyefanya kazi

150

Page 159: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

katika merikebu, aliyekuwa anaketi mahali pa chini kabisa kwa ajili

ya kumfikisha mtu mwingine mahali alipotaka kwenda.

Mtumwa wa kwenye merikebu alipelekwa mpaka pande za

chini za merikebu hiyo na kufungwa mnyororo hapo, kwa ajili ya

kufanya kitu kimoja tu. Kazi yake pekee ilikuwa ni kumtazama yule

akida mpiga ngoma na kuvuta makasia kwa kushirikiana na wale

watumwa wengine kwa amri ya akida. Hawa “watumishi” walikuwa

wamesadiki kabisa kuhusu enzi na Nafsi ya Yesu Kristo kiasi cha

kuwa watumwa wapiga makasia kwenye ile “merikebu njema ya

Neema,” wakiishi kwa ajili ya kumtazama na kumtii Nahodha wao,

Bwana Yesu Kristo. Kusudi lao pekee lilikuwa kumfikisha mwingine

mahali alipotaka kwenda. Luka anaonyesha kwa nguvu sana kazi

hiyo yao na mtindo wao wa maisha wakati alipotafiti habari za Yesu

na kuandika hiki kitabu cha ajabu na kushangaza sana kwa ajili ya

kumfikisha mtu mmoja – Theofilo – hadi mwisho mzuri katika

maisha haya, na mwisho mzuri katika maisha yajayo. Injili ya Luka

na Kitabu cha Matendo vimejaa mfano wa mtu anayefanya watu

kuwa wanafunzi – mtu mwingine, mtu mwingine, mtu mwingine ….

Kila Mkristo anapaswa kujiona kama mtumwa aliyefungiwa katika

merikebu, anayefanya kila linalowezekana kuijua hii Injili, kufuata

maagizo yake, kutengeneza mtaala, na kujenga wanafunzi, vyote

hivyo kwa ajili ya kumfikisha mtu mwingine mahali anapotaka

kwenda – mwisho mzuri.

151

Page 160: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

VITENDEA KAZI THABITI, VINAVYOFAA

Ukitaka kufuata kiwango cha Agano Jipya, lazima uandae

vitendea kazi thabiti, vinavyofaa, kwa ajili ya kuwajenga wanafunzi

wengine. Luka aliahidi kumpa Theofilo maelezo yaliyoandikwa ya

Injili ya Yesu Kristo ambayo ni makamilifu, yenye kufuata utaratibu.

Hapa katika mstari wa kwanza Luka anatumia neno la kijeshi,

anatassomai, ambalo maana yake ni kupanga askari, au vitu, au

kweli fulani, katika utaratibu na mpango wake. Luka alitafuta

kupanga kweli kuhusu Yesu katika mpango mzuri unaofaa kama

jeshi la askari lililoandaliwa na kupangwa kwa ajili ya kuiteka dunia

nzima. Luka akamkumbusha Theofilo kwamba alikuwa ametafiti

habari za Yesu kutoka juu hadi chini na kuweka mambo aliyogundua

katika “mtiririko” au “mpangilio mzuri”. Hakuna mwanafunzi

mwenye kufikiri vizuri anayeweza kuepukana na kusudi dhahiri la

Luka la kuweka mpango mzuri katika mtaala kwa ajili ya kufanikisha

kikamilifu malengo yake katika maisha ya mtu mwingine.

Luka – kama Paulo, aliyemfanya yeye kuwa mwanafunzi –

alianza mkakati wa kuwajenga watu ambao wangeweza kutumia kwa

usahihi Maandiko (ktk 2Timotheo 2:15). Paulo alimwambia

Timotheo katika 2Timotheo 3:10 kwamba, “umeijua kabisa itikadi

yangu.” Paulo alikuwa amepanga vizuri sana kweli kuu za Injili kwa

ajili ya Timotheo, ili aweze kuzishika vizuri na kusimikwa kwa

uthabiti ndani yake, na kuzieleza kwa usahihi na ufasaha kwa mtu

mwingine. Luka alifanywa mwanafunzi na Paulo, na sasa anatoa 152

Page 161: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mfano mkamilifu mzuri kabisa wa sheria ya Yesu aliyesema hivi:

“Utaratibu ukikamilika, mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake”

(ktk Luka 6:40). Vile vile, Luka anatuonyesha katika mistari hii

mfano mkamilifu wa mwanafunzi anayetayarisha mtaala kwa ajili ya

kufanya wanafunzi wengine. Yeye “aliandaa maelezo sahihi” na

“kwa utaratibu” kuhusu kweli za Yesu kwa ajili ya kufundisha,

kuingiza kazini, kujenga na kumtuma mtu mmoja ili afikie dunia.

Mwalimu maarufu aitwaye F.F. Bruce anasema kwamba “maneno

hayo yanaonyesha mfuatano wa maelezo katika utaratibu, kimada au

kufuata matukio, badala ya maelezo tu yasiyo na mpangilio.” Kabla

ya barua hii, Luka (au pengine Mkristo mwingine) alikuwa

“amemfundisha” (Luka 1:4) Theofilo kwa ushuhuda wa maneno tu

kuhusu Yesu. Neno katecheo ni neno la Kiyunani ambalo maana

yake ni kufundisha kwa utaratibu na mpangilio, hasa kwa maswali,

majibu, maelezo na marekebisho. Luka anaonyesha umuhimu

mkubwa sana kwa ajili ya kueleza Injili kwa maneno kwa mpangilio

ili kumleta mwanafunzi kwa Kristo, na umuhimu wa kuwa na mtaala

ulioandikwa kwa mpangilio kwa ajili ya kumjenga mwanafunzi huyo

katika imani na maisha ya Kikristo na huduma.

Luka alifanya hayo yote ili Theofilo afikie kwenye ufahamu

kamili wa Yesu Kristo, na kusababisha uhakika usiotikisika juu

Yake. Alfred Plummer alifafanua neno “kwa uhakika” katika mstari

wa nne hivi: “Theofilo atajua kwamba Injili ina msingi usiovunjwa

wa kihistoria.” Sisi nasi tunapaswa kuanza kuandaa mtaala na 153

Page 162: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kutayarisha jedwali la vielelezo (hebu tazama mifano (au hekaya)

itolewayo na Yesu ambayo Luka ameiandika katika Injili yake),

kutumia kila kitu kinachofaa KiMaandiko tunachoweza kupata ili

kuwajenga wanafunzi wetu juu ya msingi usiotikisika wa Injili

tukufu ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Kuna Wakristo wengi wazuri, wenye nia njema tu, na wenye

kujua mengi sana ambao hawatalenga kumjenga mwanafunzi mmoja

mwenye maono ya dunia, mwenye kuigusa dunia, na mwenye

kujiongeza. Kwa nini? Kwa sababu, hawatajali sana juu ya jukumu

lao la kujenga (au basi kupata) mtaala unaofaa, wenye utaratibu

mzuri kwa kusudi la kufikisha mtu mwingine kwenye hatima yake ya

mwisho. Ili hata mtu wa kawaida asije kukwepa kweli hiyo, F.F.

Bruce anatukumbusha kwamba Luka alikuwa “mtu wa kawaida tu,

asiyekuwa Myahudi na asiyekuwa mhubiri”. Luka alikuwa tabibu

maarufu na mzuri sana, mwenye ratiba iliyombana sana! Lakini

alipata wakati (yaani, alitengeneza wakati) ili “kuandika kwa

utaratibu” maelezo “yenye mpangilio” kuhusu maisha ya Bwana

wetu, huduma Yake, mafundisho Yake, mambo aliyofanikisha, na

kazi Yake – kwa ajili ya mtu mmoja tu.

MPANGO WA KUDUMU WA KUZALISHA

Kama unataka kufuata kiwango cha Agano Jipya, lazima

ufanye kila liwezekanalo kibinadamu kuwa na mpango wa kudumu

wa kuzalisha wanafunzi. Kila mtu anayefanya wengine kuwa 154

Page 163: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wanafunzi, mwenye maono, lazima afanye kila linalowezekana

kibinadamu, kwa kumtegemea Mungu kabisa, kufanikisha na

kuendeleza uzalishwaji wa wanafunzi. Hawa wanafunzi lazima

waone dhahiri kwamba dunia nzima ni eneo lao la kazi, na lazima

waishi kwa makusudi kabisa ili kuigusa dunia hiyo. Mwanafunzi

yeyote mwenye maono anajua kwamba hawezi kumfanya mtu

mwingine yeyote aone kiwango au afuate lengo pasipo uwezo wa

Mungu wa kimuujiza, lakini pia anajua kwamba kama yeye

mwenyewe hatakimbia hadi kiwango cha nuru yake na uwezo wake

katika kufukuzia kiwango hicho, Mungu hatamfanya mtu mwingine

yeyote akimbie pamoja naye. Kanuni ya Agustino bado ni halisi:

“Pasipo Mungu, sisi hatuwezi; pasipo sisi, Mungu hatafanya”.

Luka ametupa mfano usioweza kusahaulika wa mtu

anayefanya wengine kuwa wanafunzi, mwenye moyo na bidii.

Alielewa kikamilifu kabisa umuhimu wa kile alichokuwa anafanya.

Luka alifanya uchunguzi kwa bidii kabisa kuhusu maisha ya Yesu wa

Nazareti, akatafuta kwa makusudi kuwa sahihi katika maelezo yake,

na alijua umuhimu wa mpangilio au utaratibu. Luka alijitia katika

kazi hiyo kwa bidii, akakusanya kweli zote zilizokuwa zinaweza

kupatikana (zilizoandikwa na za mdomo), kisha akaandika kitabu

hiki kwa mtu mmoja aliyepotea – Theofilo.

Theofilo alifanya nini na kitabu hicho? Alisadiki kabisa

kuhusu ukweli wake mpaka akakipokea, akamwamini Yule

aliyetajwa humo pamoja na ujumbe wake, na akatafuta kukihifadhi 155

Page 164: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

na kukifikisha kwa wengine. Japo kitabu hiki kiliandikiwa mtu

mmoja tu, wewe unayo nakala yake! Ni mfano ulioje huo wa

kiwango cha Yesu cha kufanya mtu kuwa mwanafunzi ili kuigusa

dunia nzima – kiwango ambacho anamwamuru kila mmoja katika

wafuasi Wake kukifuata. Amri Yake hiyo inaitwa “Agizo Kuu”.

Luka alimleta Theofilo kwa Yesu Kristo kwa kumwandikia

kile tunachoita sasa “Injili Kama Ilivyoandikwa Na Luka”. Wakati

Theofilo alipomwitikia Kristo kwa imani binafsi, Luka akaanza mara

ile ile kumfanya Theofilo kuwa mwanafunzi kwa kuandika kitabu

kingine chenye sura ishirini na nane, tunachokiita Kitabu cha

Matendo, ili kumtambulisha Theofilo kwenye wajibu na mtindo wa

Yesu wa kuigusa dunia. Ni mfano wa kushangaza vipi na wa ajabu

sana wa kile kiwango cha Mungu cha Neno kuwa mwili! Kumbuka

kwamba kiwango hiki kilitendwa na mtu wa kawaida tu aliyekuwa

tabibu ili kujikimu kimaisha, lakini ambaye kazi yake kubwa ilikuwa

ni “kuwafanya watu kuwa wanafunzi”.

[USHUHUDA WA MWANDISHI – Mchungaji mmoja rafiki

yangu aitwaye Jim Davidson alinishirikisha mfano huu, ambao nami

nakushirikisha wewe kikamilifu kabisa.

Babu yetu mzaa babu aliyeitwa Isaac Kilgore alijiunga na

jeshi la Majimbo ya Kusini ya Marekani mwaka wa 1862 akiwa na

umri wa miaka kumi na nane. Vita yake ya kwanza kubwa ilikuwa

mahali palipoitwa Shiloh. Ili upate picha ya ukali wa hiyo vita ni

kwamba, baadaye, wakati wowote askari aliposimulia jinsi vita 156

Page 165: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ilivyokuwa mbaya, alikuwa anasema hivi: ‘Yaani! Niliogopa kuliko

nilivyo-ogopa kule Shiloh.’

Mzee Izaki aliendelea, akapigana huko Chickamauga,

Chattanooga, Mlima wa Kennesaw, Atlanta, Franklin na Nashville –

kwa uchache. Zote zilikuwa vita kali. Na kwa muda, yeye alikuwa

mbeba bendera wa kikosi, na kwa maana hiyo alikuwa rahisi kabisa

kupigwa risasi, lakini alipona hata hilo. Watu zaidi ya laki sita na

ishirini elfu walikufa katika vita hizo zote. Hebu fikiri jinsi hilo

lilivyoathiri idadi ya watu leo.

Baada ya Mzee Izaki kutoka jeshini mwisho wa vita,

alitembea kwa miguu kutoka jimbo la Carolina Kaskazini hadi eneo

la Walker huko Alabama. Akaoa mara mbili na kujipatia watoto

kumi na saba. Hebu fikiri jinsi hilo lilivyoathiri idadi ya watu leo!

Na kwa kuwa hakufa vitani, alipata wazao na kuongeza vizazi.

Mmoja wao ni mimi, nami nina watoto wawili, ambao bila shaka nao

watapata watoto. Lakini je, ingekuwaje kama Mzee Izaki angekufa

vitani?

Siri ya hayo yote ni hii: Kama utapata mafunzo sahihi kama

anavyopaswa askari, na kama hutakufa vitani – na tuko vitani –

utazaa wakati wote, kizazi baada ya kizazi kwa ajili ya Yesu Kristo.

Lakini, lazima ufikiri na hili pia: Utazaa vizazi hivyo kwa ajili ya

Yesu Kristo ikiwa tu utakubali kuifia nafsi yako. Yesu alisema hivi:

‘Mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, inabakia peke yake.

157

Page 166: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Lakini ikifa, inazaa mbegu nyingi sana na kunakuwa na mavuno

mengi sana’.” MWISHO]

Je, utakubali kuwajibika kibinafsi kwa hilo na kuingia katika

utafiti mzito ili kulifanikisha? Utakubali kukuza na kutumia rasilmali

thabiti na za uhakika kwa ajili ya kuwajenga wanafunzi wa Agano

Jipya, na kujitoa mwenyewe kwa Mungu kuhakikisha kwamba kuna

uzalishaji wa kudumu katika vizazi vijavyo? Mungu anakusubiri, na

dunia ya wanadamu pia!

158

Page 167: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 6Mpango Wa Mungu Wa Kuongeza

“Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.”

Matendo 1:1-5

Kuanza kwa safari ya kiroho uliosababishwa na Siku ya

Pentekoste kukawa kumekamilika. Kanisa la kwanza lilikuwa

lisukumwe na nguvu na uwezo wa jambo hilo hadi miisho ya dunia

ya wakati ule. Petro alikuwa amemalizia mahubiri yake, akieleza

Injili ya Kufa na Kufufuka kwa Yesu na kuja kwa Roho Mtakatifu,

halafu katika mstari wa 41 wa Matendo sura ya 2 tunasoma hivi:

“Ndipo wao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa, na

siku hiyo hiyo wakaongezeka kwao kama watu elfu tatu.” Du!

Nyongeza kubwa sana! Hakuna mchungaji yeyote duniani ambaye

asingefurahishwa na kuokoka kwa watu elfu tatu kwa siku moja

baada ya kuhubiri Injili. Jali sana neno “wakaongezeka” maana

linatumika tena katika mstari wa 47 wa sura hiyo hiyo. Pitia kwa

haraka mstari wa 42 hadi 47a, halafu sikiliza sentensi hii: “Na Bwana

akaliongeza kanisa kila siku, kwa watu waliokuwa wanaokolewa”.

Umeona tena neno “kuongezeka” hapo?

159

Page 168: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sasa hebu tuone Matendo 5:14. Kisa cha kusikitisha sana cha

dhambi na hukumu ya akina Anania na Safira kimemalizika

kusimuliwa. Mstari wa 13 unasema, “Na katika waliosalia hakuna

mtu aliyethubutu kujiunga nao, ila watu waliwatukuza na kuwapa

heshima kubwa.” Ungejisikiaje kuwa mshirika wa kanisa lenye

nguvu sana kiroho kiasi kwamba watu wanaogopa kujiunga nalo?

Lakini tena katika mstari wa 14 tunasoma hivi: “Na waamini

wakazidi kuongezeka zaidi kwa Bwana, makundi ya wanaume na

wanawake.” Ile “mashine ya kuzidisha” imeharibika! Hawawezi tena

kuwahesabu kwa sababu wengi sana wanaongezwa kwa Bwana.

Sasa ona badiliko muhimu. Katika sura ya sita, mkakati wa

Mungu kihesabu kwa ajili ya kukua kwa kanisa la kwanza bila shaka

unaongezeka kwa kasi kubwa. Katika mstari wa kwanza tunasoma

hivi: “Na katika siku zile, idadi ya wanafunzi ilipozidi kuongezeka,

kulitokea manung’uniko ya Wayunani kinyume cha Waebrania, kwa

sababu wajane wao walikuwa wanapuuzwa katika huduma ya kila

siku. Unaona utaratibu huo? “Kuongezeka,” “kuhudumiwa,” na

hatimaye “kunung’unika”. Washirika wanapoongezeka kanisani,

huduma za ziada lazima zifuate, ili kuwahudumia na kuwapa

shughuli ya kufanya, na baada ya hapo – hakika kabisa kama nuru

inavyofuata giza, manung’uniko yatafuatana na maongezeko. Ni kitu

halisi kabisa kwamba watu zaidi siku zote maana yake ni matatizo

zaidi. Kwani, si hata wewe ni tatizo kwa namna moja au nyingine?

160

Page 169: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Angalia asili ya tatizo lenyewe. “Ushemasi” wa kila siku

(maana hasa ya neno ‘huduma’) ulikuwepo ili kugawa chakula, vitu

na fedha kwa idadi kubwa ya Wakristo wapya waliojikuta katika

matatizo ya ghafula kiuchumi na kijamii kutokana na wao

kumwamini Kristo. “Wayahudi wa Kiyunani” walikuwa Wayahudi

waliozungumza Kiyunani, waliokuwa wamezaliwa nje ya Uyahudi

na waliokuwa wamerudi nyumbani karibuni tu kwa ajili ya sikukuu

ya Pasaka na Pentekoste. “Wayahudi wa Kiebrania” walikuwa ni

wazaliwa wa nyumbani, waliosema Kiaramu, lugha ya Wayahudi

waliokaa Palestina. Wale wa Kiyunani walikuwa ndiyo wachache, na

wale Waebrania walikuwa ndiyo wengi.

Basi, manung’uniko yalitoka kwa wale waliokuwa wachache

(kihalali kabisa) kama hoja kuhusu wajane wao kupuuzwa katika

ugawaji wa kila siku wa vitu. “Walio wengi walikuwa wanawajali

watu wao kiasi cha kuwapuuza na kuwanyanyasa walio wachache”.

Ili kushughulikia tatizo, Mitume waliwachagua watu saba, na wote

walikuwa na majina ya Kiyunani. Hiyo ni busara, sivyo? Kutatua

tatizo na kumaliza malalamiko, watu kutoka miongoni mwa

walalamikaji walichaguliwa kusimamia ugawaji wa vitu. Tatizo

likawa limetatuliwa, “na Neno la Mungu likazidi kuenea, na idadi ya

wanafunzi IKAONGEZEKA sana Yerusalemu, na idadi kubwa ya

makuhani wakaitii imani” (Matendo 6:7). Maongezeko yalikuwa

makubwa kiasi cha kuwepo na wingi waliotoka katika ukuhani wa

Wayahudi kuingia katika jamii ya wanaomwamini Yesu huko 161

Page 170: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Yerusalemu. Ona kwamba kuanza sasa, kuongezeka ndicho kiwango

cha kawaida kwa ajili ya kukua kwa kanisa la kwanza.

Katika sura ya 9, kasi inaendelea. Sura ya tisa ni masimulizi

ya kuokoka kwa Mkristo mkuu kuliko wote – Sauli wa Tarso. Baada

ya vurugu zilizotokana na kuokoka kwake na mahubiri yake ya

kwanza kumalizika, tunasoma hivi katika mstari wa 31: “Ndipo

makanisa yakapumzika katika Uyahudi yote na Galilaya na Samaria,

tena, yakajengwa. Na, yakitembea katika kumcha Mungu na katika

faraja ya Roho Mtakatifu, yalizidi kuongezeka sana.” Kwa kuwa

sentensi yenyewe imekaa ilivyokaa, inaweza isiwe rahisi kuona

kiwango cha kuzidishwa hapa. Sasa makanisa yanaongezeka! Swali:

Je, Ukristo wa namna hiyo ulipotelea wapi? Hawakuwa na mashirika

ya kimishenari, wala kamati za kuanzisha makanisa na watenda kazi

wa kamati hizo. Hawakuwa na wamishenari wa ndani na nje ya nchi

waliokuwa rasmi, lakini makanisa yalizidi kuongezeka. Tunauliza

tena: Ukristo wa aina hiyo ulipotelea wapi?

Jibu linaweza kuonekana kwa urahisi kabisa ukifanikiwa

kuhudhuria makongamano au mikutano yoyote ya wachungaji.

Wahubiri wanaoanza kukutanika, wanauliza maswali kadhaa ya

kawaida kabisa. “Vipi, Jumapili yako ilikuwa nzuri?” Jibu: “Naam –

ilikuwa nzuri kabisa.” Swali linalofuata ni lipi? “Umekuwa na watu

wangapi walio-ongezeka?” Wapendwa: Hatuwezi kuwagusa wakazi

wa dunia hii wanaozidi kuongezeka kwa sisi kuongeza makanisa

yetu, hata kama maongezeko yetu yatakuwa makubwa kiasi gani. 162

Page 171: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kasi ya kuzidishwa haiwezi kufikiwa na maongezeko kamwe! Kuna

mtu mahali katudanganya kuhusu kitu cha muhimu sana. Mungu

ametuita kuongezeka!

Hatupaswi kupuuza thamani na umuhimu wa watu kuokoka

(au, kuongezwa) katika jamii ya Wakristo, lakini, inabidi

tujilazimishe kukabiliana na kosa kubwa sana katika taratibu zetu za

utendaji kazi kama huko kuongezeka hakutakuwa mwanzo wa kuzidi

kwa jamii ya Wakristo duniani kwa ujumla.

Amri pekee ya kusonga mbele iliyowahi kutolewa na Yesu

kwa kanisa Lake inaitwa Agizo Kuu. Kuna maneno tendaji saba

katika Agizo hilo, lakini moja tu ndiyo amri. Kuna neno moja tu zito,

lenye nguvu, ambalo ni amri moja, katika Agizo Kuu! Neno tendaji

hilo linatafsiriwa “kufundisha” ingawa hapo tena ni dhahiri kwamba

kuna jambo tunalofichwa hapa. Kwa sababu, maana ya neno hilo ni

zaidi ya kufundisha tu! Maana ya neno tendaji hilo ni “kufanya

wanafunzi”. Tunahitaji kuacha kuuliza, “Umepata maamuzi mangapi

katika ibada yako?” na kuanza kuuliza hivi: “Je, unajenga wanafunzi

wangapi?”

Kanisa la kwanza lilijizidisha kwa kutumia mfumo na

utaratibu uliokuwa umeonyeshwa vizuri na kwa ukamilifu kabisa

katika huduma ya miaka mitatu ya Yesu Kristo na wale mitume

Wake kumi na mbili. Yeye ndiye wa kwanza kufanya watu kuwa

wanafunzi, na utaratibu aliofuata lazima uchunguzwe, tujifunze,

tuufahamu na kuuiga kama tunataka kuzalisha wazalishaji kama 163

Page 172: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Yeye alivyofanya. Mimi binafsi siamini kwamba mtu anaweza kuwa

mwanafunzi bila ya kuwa mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi pia.

Kutii kwetu UBwana wa Yesu Kristo unahusisha kuweka kipau

mbele kwenye kutimizwa kwa Agizo Lake Kuu. Ninaamini kufanya

watu kuwa wanafunzi ni kitu kilichomo ndani ya mkataba wetu wa

kuwa mwanafunzi. Kama mtu ni mwanafunzi kulingana na Agano

Jipya, basi atakuwa mwenye kufanya watu kuwa wanafunzi pia.

PICHA YA MWANAFUNZI ANAYEJIZIDISHA

Sasa fungua Timotheo wa Pili sura ya 2. Katika sura hiyo,

tunapata picha saba nzuri sana za mwanafunzi, na maelezo yanayofaa

sana ya mpango wa Mungu wa maongezeko. Kwaanza, tuangalie

picha za mwanafunzi. Kila moja katika zile saba inatoa sehemu

ndogo ya picha ya mwanafunzi wa Agano Jipya.

NI “MWANA”

Kwanza kabisa, mwanafunzi wa Agano Jipya ni “mwana”

(ktk mstari wa kwanza). Yeye ni mwana wa Mungu kwa kuzaliwa

kutoka juu, lakini hapa ni mtoto wa kiroho wa aaminiye

atakayemleta kwa Kristo. Paulo alimwita Timotheo “mwanangu”

kwa sababu alimwongoza kumjua Kristo. Katika safari zake, Paulo

alifika kwenye mji ambako Timotheo alikuwa anaishi, katika safari

zake za kitume. Akakuta familia yenye wanafunzi wawili maarufu

164

Page 173: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

sana wa Agano la Kale, bibi mmoja aliyeitwa Lois, na mama mmoja

aliyeitwa Eunike (ktk 2Tim. 1:5).

Eunike alikuwa na mtoto mchanganyiko aliyeitwa Timotheo.

Baba yake alikuwa Myunani. Alipogundua jinsi kijana huyo

alivyokuwa amefundishwa Biblia vizuri, alimwongoza kwa Kristo

kwa urahisi sana. Alipoanza kumfanya kuwa mwanafunzi, akaona

uwezo mkubwa sana wa kiroho ndani ya yule kijana, ambao ulikuwa

wa kipekee sana. Paulo alipoondoka kuendelea na safari yake ya

kitume, alimtia moyo kijana huyo kukua katika mwendo wake na

Kristo. Paulo aliahidi kumwombea kila siku, na pia aliahidi kwamba

angerudi ikiwezekana.

Baadaye sana, katika safari nyingine ya kitume, Paulo alirudi

mjini kwa Timotheo. Alipomfuatilia yule kijana, ndoto zake kuu

zikawa zimetimizwa. Kijana alikuwa amekua kiroho kuliko Paulo

alivyokuwa ametazamia. Alipokaribia kuondoka, Paulo alisema,

“Sasa Timotheo, unaonaje? Ungependa kusafiri na mimi?” Pengine

Timotheo akatekewa. “Mimi? Nisafiri na wewe?” Paulo akamjibu,

“Ndiyo.” Timotheo akauliza, “Huko safarini tutafanya nini?”

Pengine Paulo alimjibu hivi, “Wewe nitazame mimi, niombee, halafu

tutazungumza usiku.” Unapokuwa Mkristo mwenye maono, huko ni

kumfanya mtu kuwa mwanafunzi!

Je, mwana au mtoto mzuri anafanyaje? Anajifunza kutoka

kwa mzazi wake, anampenda mzazi wake, anamtii mzazi wake, na

165

Page 174: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kuongeza au kukuza tabia za familia. Ndivyo na mtoto wa kiroho

anavyofanya.

NI “ASKARI”

Pili – mwanafunzi wa Agano Jipya ni “askari”. “Hakuna

apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye

aliyemwandika awe askari.” Je, askari mzuri hufanya nini?

Anaachana na mipango yake yote na makusudi yake yote, ili

kutimiza jukumu alilopangiwa. Anaingia katika mafunzo kwa bidii

na udhati mkubwa sana. Anatetea maslahi ya nchi yake. Anapigana

inapokuwa lazima. Kwa kifupi ni kwamba, yuko tayari kwa ajili ya

mapambano na kujitoa, ambavyo ni vitu muhimu kama atafanikisha

jukumu lake.

Ee Jemadari mpendwa, ulijeruhiwa vitani.

Mimi nisishangae kama nitaumizwa kidogo.

Badala yake, Ee Bwana, hebu swali langu kuu liwe

Je, nitapata kujeruhiwa vitani pamoja Nawe?

NI “ASHINDANAYE” (Mwanariadha)

Tatu – mwanafunzi wa Agano Jipya anafananishwa na

“mwanariadha” ashindanaye. Mstari wa 5 unasema hivi: “Hata mtu

akishindana katika machezo, hapewi taji, asiposhindana kwa halali.”

Imekisiwa kwamba katika Agano Jipya, mashindano ya mbio

yametajwa zaidi ya mara hamsini. Je, mwanariadha mzuri anafanya 166

Page 175: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

nini? Anajitia kabisa katika mchezo wake, anafanya mazoezi

magumu na kwa mpangilio, anapata ujuzi unaotakiwa, anajitahidi

kuwa na nidhamu kiakili pamoja na kimwili, na anafanya juhudi ili

ashinde. Mwanafunzi Mkristo hatafanya pungufu ya hapo katika

kumfuata Kristo.

NI “MKULIMA”

Nne ni kwamba, mwanafunzi wa Agano Jipya anafananishwa

na “mkulima” (ktk mstari wa 6). Je, mkulima mzuri hufanya nini?

Anafanya kazi kwa bidii. Anatifua udongo, anapanda mbegu,

analima, na anavuna mavuno aliyolima. Pia anatenga mbegu kwa

ajili ya kupanda baadaye, kuvuna, na kuongeza mazao yake.

Shughuli hizo zote zina mifano inayofanana na iliyo wazi kabisa

katika zoezi la kiroho la kuwa mwanafunzi na kuwafanya wengine

kuwa wanafunzi.

NI “MTENDA KAZI”

Kitu cha tano ni kwamba, mwanafunzi wa Agano Jipya ni

“mtenda kazi” (ktk mstari wa 15), tena, mtenda kazi bingwa. Yeye

anapaswa kuwa “mtenda kazi asiyekuwa na sababu ya kutahayari,

akilitumia kwa uhalali neno la kweli”. Ili kufanya hayo, lazima

“kujifunza ili kujionyesha kuwa amekubaliwa na Mungu”. Kama

wanafunzi Wakristo, sisi tupo ili tufanye kazi kwa bidii, sio

kuzembea.167

Page 176: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

NI “CHOMBO”

Cha sita ni kwamba mwanafunzi wa Agano Jipya ni

“chombo” (ktk mstari wa 20 na 21). Je, chombo ni nini? Chombo ni

kitu chenye nafasi, iliyokusudiwa kujaa kitu au mtu. Sisi kama

Wakristo, tumekusudiwa kumjaa na kufikisha uzima wa Kristo

Mwenyewe kwa watu. Je, chombo kizuri hufanya nini? Kinaketi

kabatini kwa mwenyewe, kikiwa kitupu na chenye kupatikana, na

kumsubiri mhusika akijaze, akipenda. Mwanafunzi Mkristo hawi

katika hali ya kujiuliza ikiwa Bwana wake anataka kumjaza au vipi.

Waefeso 5:18 inamwagiza “kujazwa na Roho”. Chombo

kikishajazwa, kinamsubiria mwenyewe akimimine. Yaani, kinasubiri

tu akitumie kama vyombo vinavyotumika. Ndivyo tunavyopaswa

kuwa na sisi kama wanafunzi wa Kikristo.

NI “MTUMISHI”

Mwisho, mwanafunzi wa Agano Jipya ni “mtumishi” au

mtumwa wa upendo. Mtumwa hana mapenzi yake mwenyewe, hana

ratiba yake mwenyewe, hana haki zake, na hana mali yake. Yeye ni

mali ya bwana wake. Lakini, hana kupungukiwa katika rasilmali.

Hazina yote ya bwana wake inatosheleza kazi yoyote ile anayoweza

kupewa na bwana wake. Ndivyo ilivyo pia kwa mwanafunzi Mkristo.

168

Page 177: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

UTARATIBU WA KUZIDISHA WANAFUNZI

Sasa, baada ya kuona picha ya mwanafunzi kama itolewavyo

katika 2Timotheo 2, hebu sasa tutazame utaratibu wa kuwazidisha

wanafunzi. Mimi nimeuita “mpango wa Mungu wa kujiongeza.” Huo

unapatikana katika mstari wa 2, pale ambapo Paulo alimwambia hivi

Timotheo: “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu [mimi] mbele ya

mashahidi wengi, [wewe] wakabidhi watu waaminifu, watakaoweza

[nao] kuwafundisha na wengine pia.” Hapo tunaona vizazi vinne vya

wanafunzi katika mstari huu mmoja: “Mimi … wewe … watu

waaminifu … wengine pia”. Kama inavyooneshwa kwenye mchoro

huu.

Watu Waaminifu Wengine

Paulo Timotheo Watu Waaminifu Wengine

Watu Waaminifu Wengine

Bila shaka unapata picha kwamba mpango huo ni sawa na kitu

kinachozidi kupanuka, sehemu ndogo ikiwa pale ambapo Paulo na

Timotheo wamesimama. Kila kitu kinaanza na “mimi” na “wewe”,

Paulo na Timotheo, na hiyo hali ya muungano inaonyesha vitu viwili

muhimu sana kuhusu kuwafanya watu kuwa wanafunzi.

(1) Umuhimu wa mtu mmoja, na

(2) Umuhimu wa mahusiano mazuri.

169

Page 178: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Ondoa yeyote kati ya hao watu wawili – Paulo au Timotheo –

na utaratibu wote unaporomoka tangu mwanzo. Hakuna kuongezeka

kunakoweza kutokea pasipo mshikamanishaji hapo mwanzo, na

wengine wa kuunganisha nguvu naye.

Paulo na Timotheo lazima wawe watu ambao ni wa sifa au

hali aina fulani na wenye msimamo kama wanafunzi, ikiwa

kuongezeka kutafanyika. Halafu, lazima wawe na mahusiano kwa

jinsi ambayo ni ya wazi, yenye kuaminika na ya kipekee. Loo!

Kanisa linahitaji kutafiti na kufanyia kazi theolojia ya mahusiano

kwa hali ya juu sana! Hiyo ni dunia nyingine nzima ambayo

haiguswi hata kidogo na kanisa kwa jumla. Kama Paulo na Timotheo

hawakuwa na mahusiano yaliyojengwa kwenye kuaminiana na

kupatikana, mnyororo ungekatikia pale mwanzoni kabisa. Lakini

kwa neema ya Mungu na kwa faida yetu sisi na vizazi vyote vya

baadaye, Paulo alikuwa balozi mzuri sana, wa kuvutia, mwenye

uwezo mkubwa wa kutenda kazi kwa ajili ya Kristo. Na Timotheo

naye alikuwa mwanafunzi mwaminifu, anayepatikana na mwenye

kufundishika kwa urahisi.

UTARATIBU HUO UNAMFIKIAJE MWANAFUNZI?

Swali: Je, Paulo “alimfikishiaje” Timotheo? Utaratibu huo

ulimfikiaje Timotheo? Yeye aliwezaje kupata hali ya Paulo mpaka

naye akaweza kuiendeleza? Paulo alisema hivi: “Mambo yale

ambayo wewe umeyasikia kwangu …” Je, ni swala la kusikia tu? Je, 170

Page 179: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mtaala ni dhana za kielimu tu, au mawazo ya kifilosofia tu, ambayo

yanawea kufundishwa darasani kutoka kizazi hadi kingine? Hapana

kamwe! Sasa basi, neno “kusikia” lina maana gani katika Agano

Jipya? Mbona kusikia kunasimamishwa ili kuonyesha kuingizwa

kwa mambo ya kiroho badala ya kuona, au kunusa au kuonja au

kugusa? Ni kweli kwamba kuna mifano kiroho inayolingana na hizo

hisia za kimwili. Basi, mbona kusikia kunatengwa na kukaziwa

zaidi? Je, yaweza kuwa ni kwa sababu kusikia ndiyo hisia ambayo

kwa hiyo utambuzi halisi huenda moja kwa moja hadi ndani ya mtu?

Katika upokeaji wa hisia zingine zote, lazima kuwe na tafsiri. Picha

zinazoonekana na macho lazima zitafsiriwe ili kueleweka kama

mawazo na dhana, ndipo zifike ndani ya mtu. Ni kweli hata kuhusu

vitu tunavyogusa, kunusa au kuonja. Lakini katika kusikia,

mawasiliano ya moja kwa moja yanafanyika. Basi, “imani huja kwa

kusikia, na kinachosikilizwa ni Neno (rhema, ujumbe muhimu,

uliosemwa kwa upendo) la Mungu.”

JE, MPANGO WA KUSIKIA UNAHUSISHA NINI?

Katika mpango wa kufanya watu kuwa wanafunzi, huko

“kusikia” kunahusisha kitu gani? Katika 2Timotheo 3 kuna mistari

miwili inayoweza kutudokeza kidogo maana yake (ms. 10 na 11).

Paulo aliandika hivi: “Wewe umejua kabisa (Paulo aliishi maisha ya

wazi kabisa mbele ya Timotheo – uwazi … kufikisha ujumbe …

mabadiliko, ndiyo utaratibu) mafundisho yangu, maisha yangu 171

Page 180: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

(mtindo), kusudi langu, imani yangu (au, uaminifu katika utendaji),

uvumilivu wangu (uwezo wa kuteseka kwa muda mrefu), upendo

wangu, subira na mateso yangu (kumbe Paulo hakumficha Timotheo

ukali wa dhiki yote aliyopata).”

Hayo ni matokeo ya kawaida kabisa ya kanuni ile inayoitwa

“pamoja naye, pamoja nami”. Yesu aliwaweka kumi na mbili ili

wawe pamoja naye” (ktk Marko 3:14). Kuwa mwanafunzi na

kufanya wengine kuwa wanafunzi ni mtindo wa maisha ambao

hunaswa zaidi ya kufunzwa. Hebu fikiri – kuna mtu anayeweza

kusafiri safari ndefu na Paulo bila ya kubadilishwa na safari hiyo?

BAADA YA MWANAFUNZI KUWEZESHWA, ANAFANYA

NINI?

Sasa basi, baada ya Timotheo “kuwezeshwa” au

“kukamilishwa” au “kufundishwa ipasavyo”, anafanya nini?

“Mambo yale uliyoyasikia kutoka kwangu mbele ya mashahidi

wengi, wewe nawe uyakabidhi hayo kwa watu waaminifu”.

Maneno mawili hapo ni muhimu sana katika kufafanua nafasi

na kazi ya Timotheo. Yeye anapaswa kukabidhi (ile imani yote,

mtindo wa maisha na kujitolea) kwa watu “waaminifu”. Hapa tuwe

makini sana. Hili ni mojawapo kati ya mambo ya hali ya juu sana

kuhusu akili ya Kikristo. Kitu hiki kinapofanya kazi sawasawa, siku

zote wanapatikana viongozi wa kizazi cha pili na cha tatu. Hii ndiyo

sababu ni muhimu sana sana kwamba mwenye kufanya watu kuwa 172

Page 181: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wanafunzi atafute tu kuingiza utaratibu huo katika watu waaminifu.

Kama wanafunzi wake watakuwa si waaminifu, mpango mzima

unaishia kwao, na vizazi vyote vya baadaye vinaweza kuachwa

pasipo uongozi wa kiroho wenye ujuzi.

Neno lingine linalopaswa kutazamwa vizuri tu ni lile neno

kuu katika mstari. Ni neno “wakabidhi”. Hapa tena, lazima tuwe

makini sana kuelewa vizuri maana yake. Ni neno la kibenki. Maana

yake halisi ni “kuweka fedha”. Unapokwenda benki kuweka fedha

katika akaunti ya kuweka fedha, unatazamia kupata faida fulani.

Ndivyo ilivyo unapofanya mtu kuwa mwanafunzi. Huwi

unayemsafisha mwenye dhambi tu ili awe safi. Unafanya uwekezaji

wa wingi na wa hali ya juu ambao utazaa faida isiyo na mwisho hadi

umilele wote!

JE, NI UWEKEZAJI AU NI MATUMIZI?

Basi, hebu niulize swali zito: Je, maisha yako ya sasa hivi ni

matumizi zaidi au ni uwekezaji? Je, unayatumia au unayawekeza?

Fikiri kwa umakini kidogo hapa. Kama unayatumia, basi matumizi

hayo ni mwisho. Hakuna faida kutokana na tendo hilo. Na ukweli

lazima usemwe. “Shughuli nyingi za Kikristo” tunazojihusisha nazo

– iwe ni kuhudhuria kanisani, kusoma Biblia, maombi, n.k. – ni

matumizi kuliko kuwa uwekezaji. Ni shughuli za “kujihami” tu

ambazo hutufanya sisi kuwa “Wakristo wazuri” badala ya kuwa

173

Page 182: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

uwekezaji ambao utaigusa dunia hadi miisho ya nchi mpaka mwisho

wa wakati. Hivyo, shughuli hizo zinasaliti Agizo la Yesu Kristo.

Timotheo alitakiwa achukue akiba yote ya maisha ya Kristo

ambayo ilitoka kwa Paulo ikamfikia yeye, naye “aiweke” katika

maisha ya watu waaminifu, na utaratibu huo haujafanikiwa mpaka

nao waweze “kuwafundisha wengine pia.” Basi, utaratibu huo

unatakiwa kuzidi kuongezeka mpaka uwe kitu kikubwa chenye

kuhusika na eneo pana zaidi na zaidi na kuwahusisha watu zaidi na

zaidi.

MIFANO YA KUONYESHA UMUHIMU NA UWEZEKANO

WA MAONGEZEKO

Hebu tutumie mifano michache ya kawaida tu ili kuonyesha

umuhimu na uwezo wa kuongezeka.

MWINJILISTI

Hebu tudhanie kwamba yupo mwinjilisti ambaye angeweza

(na kweli wapo) kuleta watu elfu moja kila siku kwa Kristo. Kama

idadi ya watu duniani sasa hivi “ingegandishwa” hapo ilipo –

asiwepo mtu yeyote kuzaliwa na mtu yeyote kufa mpaka kila mtu

afikiwe na kumfuata Kristo, muda ambao ungehitajika kufikia idadi

ya sasa ya watu duniani ni zaidi ya miaka elfu kumi na tano! Na hapa

tukumbuke kwamba, hao watakuwa wameokoka tu, si kwamba ni

wanafunzi wa Yesu.174

Page 183: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

KILA SIKU IWE YA PENTEKOSTE

Au, tuseme kwamba kila siku ingekuwa Siku ya Pentekoste,

wakiokoka watu elfu tatu kila siku. Ingechukua miaka kama elfu tano

hivi kuwaleta watu wote walioko duniani sasa hivi kwa Kristo! Na,

zingatia kwamba idadi ya watu haijanganda! Inaongezeka kwa kasi

kubwa sana. Basi, mambo yanakatisha tamaa, sivyo?

Hii ndiyo sababu lazima tufanyie kazi kanuni ile ya Biblia ya

kujizidisha. Sasa, mfano ufuatao ni wa kihesabu, wa kinadharia, na ni

kitu kisichokuwepo, lakini utatusaidia kuona uwezekano wa

kujizidisha kiroho. Tuseme kwamba mwanafunzi mmoja anayefanya

wengine kuwa wanafunzi ameguswa kabisa na kuingiziwa uwezo wa

kuwa mwalimu wa kufundisha wengine kuwa wanafunzi, naye

amtafute mwanafunzi mmoja ili amfundishe kwa mwaka mmoja kwa

njia ya kumwezesha na yeye kuwa na mwanafunzi na kumfundisha

kwa mwaka unaofuata, na hayo yaendelee hivyo hivyo bila

kubadilisha chochote katika utendaji na maongezeko, mpango huu

ungempita yule mwinjilisti “anayeokoa watu elfu moja kwa siku”

baada ya miaka 23, na (ni hoja tu) watu wote duniani wangefanywa

kuwa wanafunzi katika muda wa miaka 35. Ona tofauti kati ya

“waongofu” wa mwinjilisti na “wanafunzi” wa yule mzalishaji

mwenye maono.

Onyo: Mifano kama hii isitumike kupambanisha shughuli za

wainjilisti na wavuna roho dhidi ya wanaofanya watu kuwa 175

Page 184: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wanafunzi. Hizo ni nafasi zinazotegemeana, ambazo kila moja ni ya

muhimu. Kwa kweli ni vizuri hata nafasi hizo zote mbili

ziunganishwe katika kila mwamini anayekomaa na kuukulia wokovu.

Kwa nini kufanya watu kuwa wanafunzi kunaendelea kwa

kusuasua sana? Ukweli ni huu: Mungu amekosa watu wanaofaa na

wenye sifa za kuwa waanzilishi wa shughuli hiyo. Yaani, hakuna

wazalisha wanafunzi wa kutosha kuanzisha mpango huo duniani

kote. Lakini, hilo lisituvunje moyo. Tukiwa na maono na

mawasiliano, jambo hilo linaweza kurekebishwa haraka sana kuliko

tunavyofikiri. Tena kumbuka, mambo yanaanzia kwa Paulo kwenda

kwa Timotheo, ambaye ndiye anayefuata. Na mpango au utaratibu

mzima unategemeana na ubora, kujitolea, maono na utendaji wa hao

watu wawili wa kwanza. Kwa sababu, kikawaida, wao ndiyo mifano

inayoonekana pale mwanzoni kabisa na wenzao, pamoja na kwamba

hilo ni jambo la kutisha.

Umuhimu wa maongezeko ya kila siku ni mkubwa sana kwa

ajili ya kuhitimisha mpango mzima. Hakuna mtu anayetakiwa

kushindwa. Mkristo mmoja akishindwa kufanikisha sehemu yake ya

kuongezeka, anapunguza uwezo wa kutimiza Agizo Kuu katika

kipindi cha uhai wake kwa nusu nzima. Lakini, kama Mkristo mmoja

tu akifanikiwa (na kujizidisha), anaongeza mara mbili uwezo huo

katika kipindi cha uhai wake.

176

Page 185: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

MAONO YA KUIGUSA DUNIA NZIMA KWA KUFANYA

WATU KUWA WANAFUNZI

Ewe Mkristo, unayo maono ya kuigusa dunia nzima kwa

kufanya watu kuwa wanafunzi? Je, unawekeza vizuri kabisa ule

mtindo wa maisha ya Yesu, maono ya Yesu, na kujitolea kwa Yesu

katika maisha ya watu binafsi ili nao wawe na maono hayo hayo na

kujitolea, na kuweza kuwapa wengine? Kuna mtu ambaye amesema

hivi, kwa busara kabisa: Ili uweze kugawa maono kwa wengine,

lazima wewe mwenyewe:

Uyaone waziwazi,

Uyaseme kwa ubunifu,

Uyaonyeshe kila wakati,

Uwashirikishe watu wengine kwa bidii, na

Uyalinde kwa uangalifu sana.

177

Page 186: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 7Hekima Ya Mkakati Wa Yesu

Tunaianza sura hii kwa kutazama andiko linaloonekana si

kitu kabisa. Ukweli ni kwamba, unaweza kusoma barua ya Paulo ya

Kwanza kwa Wathesalonike mara mia bila hata ya kujali mstari huu.

Lakini – na hii ni kawaida katika Maandiko – mara nyingi Mungu

huficha hekima ya Mbinguni katika maandiko yasiyokuwa wazi

sana, na huu ni mfano mmoja. Katika mstari huu kumefichwa

utukufu wote na hekima ya Ukristo. Mstari wenyewe ni 1Wathes.

3:8, unaosema hivi: “Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi

mnasimama imara katika Bwana”.

Kumbuka kwamba Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya

Kiyunani, na uzuri mmoja wa lugha ya Kiyunani ni kwamba

mpangilio wa maneno katika sentensi hudhihirisha kama hayo

maneno yana uzito, na kama ndivyo, uzito huo ni mdogo (mfano:

Roho Mtakatifu anapandisha sauti Yake) au ni mkubwa (mfano:

Roho Mtakatifu anapiga kelele). Sasa – katika 1Wathes. 3:8, maneno

yamepangwa kwa njia kwamba neno moja limebeba mkazo, na ni

mkazo mkubwa. Mara nyingi nimewauliza watu kukisia ni neno gani

lililokaziwa, na wameshindwa. Ni hivi: Hatuwezi kwa akili zetu

kama binadamu kukisia na tukapata usahihi kuhusu Mungu. Hata

kama tutabahatisha jibu sahihi, jibu letu bado ni kosa kwa sababu

178

Page 187: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

tulikisia. Hii ndiyo sababu imetupasa kujifunza Biblia, “tukilitumia

kwa uhalali Neno la Kweli” (ktk 2Timotheo 2:15).

Neno moja ambalo limekaziwa (tena kwa mkazo mkubwa

kabisa) ni neno “ninyi”. Hebu soma mstari wote kwa sauti, ukipaza

sauti unapotamka neno “ninyi”. Je, sasa unaweza kuelewa maana

yake? Je, sasa unaona hekima na akili ya Ukristo? Je, sasa unaona

wazi kwa nini neno “ninyi” liwe ndiyo neno kuu? Hebu tuchunguze

kwa upana zaidi mpaka tupate mahali panapofaa kushika na

kufahamu.

Kuna namna mbili za maisha ambazo wanadamu wanaweza

kuzifuata. Watu wengi hawatambui injili, lakini njia moja ni mtindo

wa maisha wa Shetani, na njia nyingine ni mtindo wa maisha wa

Mwokozi. Njia moja ndiyo mtindo wa maisha wa kawaida wa

mwenye dhambi (na yawezekana kuwa ndiyo njia pekee ya maisha

ambayo mtu aliyepotea anaweza kuishi), na ile nyingine ni mtindo

wa maisha wa kawaida kabisa wa mtakatifu mtendaji. Nayatumia

maneno haya kwa makini na uangalifu sana, kwa sababu mtu yeyote

aliyeokoka anaweza wakati wowote kurejelea mtindo wa maisha wa

Shetani.

Ngoja nichore mchoro utakaotuwezesha kuona vizuri mitindo

hii ya kinyume ya maisha.

179

Page 188: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Nauita mtindo huu wa maisha wa “kutoka nje kuingia ndani”.

Haya ndiyo maisha yasiyoepukika, ya lazima ambayo ni kawaida

kwa kila mtu ambaye hajawahi kuzaliwa na Mungu. Anaishi kama

sponji – siku zote ananyonya au kufyonza vitu kutoka katika

mazingira yake kwa ajili ya faida yake binafsi. Huo ndiyo mtindo wa

maisha wa Shetani. Hilo ndilo lililomfanya Shetani kuwa Shetani,

kule kusema, “Nita”. Alirudia hilo tena na tena, akihamisha imani

yake kutoka kwa Mungu mpaka kuwa kwake mwenyewe. Hiyo

ndiyo tafsiri ifaayo ya dhambi – “Ubinafsi”. Dhambi ni “mkunjo

binafsi” wa maisha unaomfanya kila mwanadamu kugeuzia kila kitu

ndani yake mwenyewe. Dhambi ni jitihada za mwanadamu kutafuta

maana na utoshelevu katika maisha kwa ajili yake binafsi na ndani

yake mwenyewe – pasipo Mungu.

Sasa, ni lazima tukiri – japo inasikitisha – kwamba, mtu

aliyezaliwa mara ya pili anaweza pia kurejea mpaka kwenye mtindo

huo wa maisha. Kwa kuwa alichukua “mwili” na kuingia nao katika

maisha yake mapya ndani ya Kristo, wakati wowote anaweza 180

Page 189: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kujiamini mwenyewe na kutafuta kujinufaisha badala ya kumwamini

Kristo na kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Wakati Mkristo

anapoishi kwa ubinafsi, anatumbukia katika mojawapo ya makundi

mawili. Anaingia katika kundi la kuishi “kwa ubinafsi” au katika

maisha ya “kujiponya”. Kila kitu anachofanya kinamtia katika hali

ngumu ya kuishi kwa ajili ya faida yake binafsi au kwa ajili ya

kujiponya. Hata kama atasoma Biblia, aombe na kujaribu

kumtumikia Mungu, atafanya hivyo kwa sababu fulani ya kibinafsi

tu. Biblia inasema, hiyo ni hali “ya kimwili”.

Mtindo mwingine wa maisha unaweza kuonekana kwenye

mchoro huu. Upande wa kushoto unamwakilisha Yesu na upande wa

kulia ni mwamini aliyezaliwa mara ya pili.

Mtu aliyezaliwa mara ya pili anakuwa na mwenzi – Yesu

Kristo. Huyu anakuwa amehamishia matumaini yake kutoka kwenye

ubinafsi na juhudi binafsi, na kuyaweka kwa Kristo. Kumekuwepo

na hali ya kuunganika na kuwasiliana kati yake na Kristo. Maisha ya

Kristo yameingia ndani yake, na “kiini cha msimamo” ndani yake 181

Page 190: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kimehama kutoka kwake hadi kwa Kristo. Hii inaitwa “wokovu,

kuongoka, kuzaliwa tena, kuzaliwa mara ya pili” kwa lugha ya Biblia

na imani. Maneno hayo yote yanaonyesha muujiza kabisa wa Mungu

ambao unamtikisa mwenye dhambi kutoka katika kiini chake cha utu

na kumwondolea ubinafsi, na kumtia Bwana Yesu Kristo mtukufu

katikati kabisa ya maisha yake badala ya yule nafsi aliyeingiliwa na

Shetani, mwenye ubinafsi. Nasema tena, huu ni muujiza kamili wa

Mungu! Watu ambao hawajaokoka siku zote hawataelewa vizuri

kuzaliwa mara ya pili ni kitu gani. Wao wanafikiri ni mwanzo mpya

tu au kuupuuza kwamba ni ushika dini wa kupindukia. Swali la

kipuuzi: Je, mtu ambaye hajazaliwa, anaweza kweli kuelewa maisha

ya mwanadamu?

Mchoro wa pili unaonesha picha ya mtindo wa maisha

tunaweza kuuita “kutoka ndani kwenda nje” ambao ni mtindo wa

maisha wa Mungu Mwenyewe. Yesu “alijitoa mwenyewe kwa ajili

yetu” na hapo akatuonyesha jinsi Mungu anavyofanya kazi

kikawaida kabisa. Na Mkristo mtendaji huishi katika mahusiano ya

imani na Yesu Kristo, siku zote akipokea uwezo ule wa kushangaza

sana wa maisha ya kweli kabisa ya imani ya kweli. Hayo yote hupitia

kwake na kumtosheleza yeye, na kutoka na kumwendea mwingine

pia.

Sasa, hebu tusome tena ule mstari wetu. “Kwa kuwa sasa

twaishi, ikiwa NINYI mnasimama imara katika Bwana.” Wakristo

wengine hawaelewi vizuri mstari huu, kwa hiyo wanafikiri hivi: 182

Page 191: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“Ninaishi kama ninaomba vya kutosha.” Kama Mkristo, “ninaishi

kama ninasoma Biblia kiasi cha kutosha.” Au “ninaishi ikiwa

nimejitoa kabisa.” Au, “ninaishi kama mimi ni mwaminifu kabisa.”

Au, “ninaishi kama ni mwema kiasi cha kutosha.” Au “ninaishi kama

nimehamasika kabisa”. Au, “ninaishi kama ni mtendaji mwaminifu”.

Lakini, hayo maneno yote mazuri sana yana ule uwezo uliofichika

wa kugeuza maisha ya mtu huyo kurudi kwake na ndani yake tena.

Huu ndiyo ule mkunjo uliofichika sana wa ubinafsi utokanao na

mwili, na huwadanganya watu wengi sana waliokwisha okoka.

Yesu alisema hivi: “Yeye atakaye kuyaokoa maisha yake

mwenyewe (yaani, maisha ya kujitakia faida, kujijali, kujihami)

atayapoteza, lakini yeye atakayetoa maisha yake kwa ajili Yangu na

Injili, atayaokoa.” Basi kumbe, maisha yanayosimuliwa huko nyuma

ni maisha ya hasara, lakini yale maisha ya kujisahau mwenyewe,

kujitoa mwenyewe, kutojijali mwenyewe katika maelezo ya pili

ndiyo maisha yaliyo-okoka.

Sasa hebu tubadilishe michoro kidogo. Kama ilivyo kwa watu

binafsi, ni kweli pia kwa makanisa. Hata makanisa pia yanaweza

183

Page 192: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kujielekea yenyewe, yakaishi kibinafsi au kichoyo kwa ajili ya faida

yao wenyewe au usalama wao pamoja na kwamba yanakuwa katika

kutafuta watu, ila, ni kwa faida yao wenyewe ya ndani!), badala ya

kukuza na kumaliza kabisa njia zao za kujisaidia kufikia kiwango

kwamba wanasukuma na daima kupima rasilmali za miujiza ya

Mungu.

Mtindo wa maisha ya Kikristo ni kuishi kwa mahusiano, bila

ubinafsi, kwa kujisahau wenyewe, kuwafikiria wengine kiasi kwamba

Mkristo mmoja anaishi kweli ikiwa mwanafunzi wake anasimama

imara katika Bwana. Paulo alisema, “Mimi ninaishi ikiwa ninyi

mnasimama imara katika Bwana.” Basi, Mkristo anaishi katika, kwa

njia ya, kwa ajili ya, na kupitia wanafunzi wake!

Huo si ndiyo mtindo wa Yesu kabisa, na jinsi ya kuifikia

dunia? Yeye alijijenga Mwenyewe katika watu kumi na mbili kiasi

kwamba, baada ya kipindi cha mafunzo cha miaka mitatu, alisema,

“Kwaherini! Sasa maisha Yangu yako katika uangalizi wenu. Mimi

ninaishi kama mtasimama imara!” Wapendwa wangu, hiyo ndiyo

hali nzima ya kufanya watu kuwa wanafunzi.

Inasemekana kwamba “Mazoezi Humfanya Mtu

Kukamilika”. Hii kanuni imesemwa kana kwamba ni kitu

kisichobadilika, kisichoonekana, na kisichopingwa. Lakini mimi

naomba niulize swali lenye maana. Tuseme kwamba kiwango

kinachofanyiwa mazoezi si kikamilifu. Yawezekana kweli mazoezi

yote duniani yatakayofanyika yakibadili hicho kuwa “kikamilifu”? 184

Page 193: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Bila shaka hapana! Ni hivi: Mazoezi hufanya kitu kikae daima;

haimaanishi kwamba kinafanya kila kitu kuwa kamilifu. Hebu

tufafanue na kutoa maana. Bila shaka inawezekana kwamba kanisa la

Yesu Kristo limetenda kwa kufuata kanuni za kawaida na mapokeo

kiasi kwamba “kujizoeza” kwake kwote kunazidi kulikita katika

kiwango kisichokuwa kamilifu.

Kama dhana ya mafunzo haya ni sahihi, kwamba Agizo Kuu

linawakilisha “Amri ya Kusonga Mbele” ya pekee iliyotolewa na

Yesu Kristo kwa Kanisa Lake, na kama jinsi ya kuelewa Agizo hilo

Kuu kulikotajwa katika mafunzo haya ni sahihi, basi mkakati wa

kawaida kabisa wa kanisa la kawaida una makosa. Je, kujenga taasisi

badala ya kujenga watu kumechukua nafasi kubwa katika kanisa la

leo? Kumbuka kwamba maana ya “kufanya watu kuwa wanafunzi”

inatokana na njia na agizo la Yesu. Kazi Kuu anayotoa inatajwa

vizuri sana katika amri moja iliyoko katika Agizo Kuu: “Wafanyeni

watu kuwa wanafunzi.” Na njia Yake inaonyeshwa katika mkakati

Wake wa kuwashirikisha watu binafsi katika kikundi kidogo – watu

kumi na mbili.

Hebu tuulize tena swali hili. Je, Ukristo unaowakilishwa sasa

na kanisa lako ungeweza kusababisha Kitabu cha Matendo ya

Mitume? Hili swali linatia aibu, kwa hiyo halina jibu la haraka. Au

tuseme kwa njia nyingine. Je, Ukristo wa Kitabu cha Matendo ya

Mitume ungevumilia hali iliyoko duniani kwa sasa – hali kwamba

karibu nusu ya binadamu wote wanaokaa duniani bado hawajasikia 185

Page 194: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Injili (miaka elfu mbili na zaidi baada ya Kristo!) na kwamba 4/5 ya

binadamu wote wamesikia Injili kijuu-juu tu? Je, Ukristo wa Kitabu

cha Matendo ya Mitume ungevumilia hali iliyoko kanisani katika

kila nchi iliyofikiwa duniani, inayosimuliwa katika kitabu cha

Patrick Johnstone kiitwacho Operation World hivi: “Nchi hii

inahitaji sana viongozi walioelimika?” Jibu linalotia aibu la maswali

hayo yote ni “Hapana!” ya sauti kubwa sana. Sasa basi, hii mikakati

na njia za sasa vitarekebisha huku kushindwa? Mpaka kitabu hiki

kinapoandikwa, haijafanikiwa. Sawa. Si basi tuziache, na kwa ujasiri

mkubwa tupitie tena ule mkakati wa kwanza wa Yesu, na tuone ni

tofauti zipi zimetuondoa kwenye huo mkakati Wake?

Kuna maneno ya kawaida kabisa yanayotumiwa kanisani,

ambayo tumeyadhania tu. Maneno hayo ni “kama Kristo”. Nadhani

Wakristo karibu wote wangekiri kwamba lengo la maisha ya Kikristo

ni kumfanya mwamini binafsi kuwa kama Kristo. Ukweli ni

kwamba, hilo ndilo lengo la Mungu ambalo limetamkwa wazi wazi

kwa ajili ya kila mtoto Wake. Katika Warumi 8:29 tunaona kwamba

hilo limekuwa lengo na kusudi la Mungu siku zote kwamba

“tufananishwe na mfano wa Mwana Wake,” au, kutufanya kama

Kristo. Lakini tena, tumepungukiwa sana na kiwango cha Biblia

katika kufafanua maana yake. Sisi tunafafanua tu na kutoa maelezo

kwamba linahusiana na “tunda la Roho” katika Wagalatia 5:22, 23.

Lakini, nani anaweza kupingana na maelezo hayo? Kama mtu akizaa

tunda la Roho, tabia yake ya ndani ni kama ile ya Kristo bila shaka. 186

Page 195: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Lakini, hebu tufuate mfano wa matunda. Je, tunda lina jinsi ya ndani

tu, au pia lina umbo la nje? Tutumie mfano huu. Mnunuzi wa

matunda anapokwenda kutafuta malimau, anatafuta “hali ya

ulimau”? Hapana. Yeye anatafuta tunda dogo la mviringo, lenye

rangi ya manjano na ganda gumu kidogo. Yaani, limau lina umbo

lake halisi la nje, lenye kueleweka, ambalo ni tofauti na umbo la

boga, embe au ndizi. Pendekezo langu ni kwamba, tunda la Roho ni

mwanzo mzuri katika jitihada za kuwafafanua Wakristo. Je, kuwa

kama Kristo kuna umbo la nje pamoja na jinsi ya ndani?

Ngoja niliseme vizuri kwa sentensi moja tu: hutaweza

kufanya kitu chochote kitakachozidi lengo lako la kuwa kama Kristo

kuliko kuwafundisha makundi ya watu kuishi katika umoja na Yesu

Kristo kwa ndani, na kujiongeza, kujizidisha, na kuifikia dunia nzima

kwa nje. Maneno muhimu kimkakati ni “kufundisha,” (kwa kutumia

mkakati na mtaala uliotolewa na Yesu), “makundi” (kwa kufuata

ukubwa wa kikundi uliotolewa na Yesu), “muungano au umoja”

(kwa njia hiyo, kufanya maisha ya Kristo, huduma na motisha kuwa

vyetu), “kujiongeza na kujizidisha” (ambalo ni jukumu la kila mtoto

wa Mungu) na “kuifikia dunia nzima” (ambayo ni kama lengo la kila

saa kwa ajili ya kila mtoto wa Mungu). Na hayo yote yataamua

mikakati tutakayotumia kufanikisha hilo lengo.

Katika muda mtakatifu sana kihistoria unaotajwa na Yohana

19:30, Yesu alisema neno moja ambalo pengine ndiyo la maana

kuliko yote yaliyowahi kusemwa. Neno lenyewe ni tetelestai, 187

Page 196: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“imekwisha” au “ni tayari”. Kazi iliyokuwa imekwisha na

kukamilika wakati huo ni kazi ya ukombozi, neno moja

linalojumlisha kila kitu ambacho Mungu amekifanya ili kuwaokoa

wenye dhambi kabisa.

Yesu analitumia tena neno hilo katika Yohana 17:4.

“Nimekutukuza hapa duniani, nimemaliza kazi uliyonipa kuifanya.”

Je, Yesu alikuwa amemaliza kazi gani hapa? Wasomi wengi

wanasema kwamba tamko hilo pia linahusiana na kazi ya ukombozi

ambayo Yesu aliikamilisha pale msalabani, lakini sidhani. Yesu

anatumia neno la wakati uliopita, na msalaba ulikuwa bado mbele

Yake! Hapa hakuwa anasema kuhusu kazi ya ukombozi, bali kazi ya

uzalishaji. Hapa, utaratibu Wake wote wa mafunzo kwa ajili ya watu

Wake ulikuwa umekamilika. Kumbe Yesu alikuja duniani kufanya

na kukamilisha kazi mbili muhimu sana: Ukombozi na uzalishaji.

Bila kazi ya ukombozi iliyokamilishwa na Kristo kufa msalabani,

kusingekuwa na kitu chochote cha kuzalishwa, lakini tena, bila kazi

ya kuzalishwa kupitia kuongezeka kwa Wakristo, kazi ya ukombozi

ingejulikana kidogo tu, au kwa sehemu tu, au kwa hali ya chini sana

(ambayo ndiyo hali ya dunia ya leo, na hata ya kanisa la leo).

Hapa tena, swali muhimu. Nini maana ya “kuzalisha” kwa

maana ya Agano Jipya? Ni watu wangapi wanaotazamiwa kuzalisha,

na wanatazamiwa kuzalisha kiasi gani? Je, uzalishaji huo ni kufyatua

tu (kiwango cha kuvuna roho, au kuwaleta wenye dhambi kwa

Kristo) au ni kitu kinachotakiwa kusababisha maongezeko? Kama ni 188

Page 197: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

maongezeko, yawe ya ukubwa gani? Na je, malengo halali katika hili

yafikiwe vipi? Hapa tena, mbinu na njia ya Yesu viwe mwongozo

wetu.

Hebu tuchukue mfano mmoja ili tuuchunguze kwa haraka. Je,

Yesu alifuata mfano gani katika kuzalisha? Je, alizalishaje watu

watakaowazidisha wengine? Je, aliwezaje kusababisha mtazamo na

nia katika watu kumi na mbili uliopelekea dunia nzima kuguswa

mpaka sehemu za mwisho kabisa za dunia ya wakati Wake katika

kipindi cha miaka sitini tu baada ya kifo Chake? Soma tena sentensi

hii ya mwisho na uiruhusu kweli yake iingie katika akili zako.

Ruhusu swali lake lisisimue moyo wako? Ilikuwaje? Yeye aliwezaje?

Aliwezaje kusababisha mtazamo na nia? Tena, katika watu kumi na

mbili!!?? Ambavyo vilipelekea dunia nzima kufikiwa? Mpaka

miisho ya dunia iliyojulikana siku zile? Katika kipindi cha miaka

sitini tu baada ya kifo Chake? Yeye hakuwa na televisheni,

uchangishaji wa fedha, simu, njia zozote za mawasiliano ya kisasa.

Yeye alitumia mbinu ya mtu kumwambia mtu! Vipi? Ilikuwaje?

Ilitokeaje? Hakuna chochote katika mpango Wake kilichotegemea

watu wengi. Hakuna chochote katika mpango Wake kilichotegemea

mahubiri (japo aliwasiliana na watu wengi kutoa huduma,

kufundisha, na kuibua wanafunzi wa baadaye). Hakuna chochote

katika mpango Wake kilichokuwa taasisi (na hapa tunachosema ni

ukweli tu, si kwamba tunafanya tathmimi ya taasisi). Hakuna

189

Page 198: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

chochote katika mpango Wake kilichojengwa kwenye kwenda

kanisani (japo Mwenyewe alihudhuria kanisa kwa uaminifu).

Sasa basi MKAKATI WAKE ULIKUWA NINI? ALITUMIA

MBINU GANI? ALITUMIA NJIA GANI?

Pengine tutapata dokezo kwa kutazama orodha za wale watu

aliowaita “mitume” kama zinavyoonekana katika Biblia. Hebu

tuseme kwanza kabisa kwamba Yeye aliwafundisha ili awatume

mbali Naye, si ili aongeze makundi ya watu mahali alipokuwepo.

Huu mkakati haufanani kabisa na kanisa la leo hata kidogo tu,

ambalo lina tabia ya kutathmini kufanikiwa kwake (na mafanikio ya

viongozi wake) kwa kawaida kupitia kipimo. Orodha zile nne za

Mitume zinapatikana katika Mathayo 10, Marko 3, Luka 6 na

Matendo 1. Hizo orodha peke yake zinapaswa kusababisha mafunzo

mengi sana. Kuna masomo yasiyoelezeka na ya milele kutokana na

kujifunza hizo orodha tena na tena. Tuzitazame hapa.

Mathayo Marko Luka Matendo

Simoni (aitwaye Petro) Simoni (aitwaye Petro) Simoni (aitwaye Petro) Petro

Andrea Yakobo wa Zebedayo Andrea Yohana

Yakobo wa Zebedayo Yohana Yakobo Yakobo

Yohana Andrea Yohana Andrea

Filipo Filipo Filipo Filipo

190

Page 199: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Batolomayo Batolomayo Batolomayo

Tomaso

Tomaso Matayo Matayo

Batolomayo

Matayo Tomaso Tomaso

Matayo

Yakobo wa Alfayo Yakobo wa Alfayo Yakobo wa Alfayo Yakobo

wa Alfayo

Tadayo Tadayo Simoni Mzelote Simoni

Mzelote

Simoni Mzelote Simoni Mzelote Yuda wa Yakobo Yuda wa

Yakobo

Yuda Iskariote Yuda Iskariote Yuda Iskariote

Ona yaliyo dhahiri hapa. Jina lile lile linatokea mwanzo

kwenye kila orodha. Labda tuseme hivi, ni mtu yule yule, ingawa jina

halifanani kila mahali. Kwanza, “Simoni Petro” halafu “Petro”.

Turekebishe kidogo tena. Ni mtu yule yule – lakini ni dhahiri pia

kwamba si mtu yule yule! Safari ya kuhama toka kwa “Simoni”

mwenye kutawala, hadi kufikia kwa “Petro” mwenye kutawala ni

somo kubwa sana kuhusu mkakati, mbinu, njia na utaratibu wa Yesu

191

Page 200: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

katika kuwajenga wanafunzi. Je, hilo tu si ndiyo amri pekee iliyoko

katika Agizo Kuu Lake alilotupa sisi (yaani, kuwajenga wanafunzi)?

Kama ndivyo, basi tunatakiwa kufuata kwa makini sana na kwa kiasi

tunachoweza mkakati, mbinu, njia na utaratibu wa Yesu (la sivyo,

tutazamie matokeo tofauti – ambayo kwa bahati mbaya, ndivyo

imekuwa katika kanisa la siku hizi). Ni mafunzo yenye maana sana

kufuatilia tu ule utartatibu wa mafunzo ambao Yesu aliupitia kwa

ajili ya Simoni Petro peke yake. Kama mafungu yale yenye kueleza

jinsi Yesu na Petro walivyokutana, walivyozungumza na

walivyofundishana, na kama yatakuwa ndiyo kiwango kwa ajili ya

kujenga wanafunzi katika kanisa la siku hizi, basi ni rahisi kabisa

kuona kwa nini tunateseka na hali ya kutokuwa na matokeo yafaayo

(yaani, kuwa na Wakristo ambao hawajajengwa na kuwa na dunia

ambayo kwa sehemu kubwa haijafikiwa). Ingewezekana kila Mkristo

ajifunze somo hili ingekuwa vizuri sana. Kutazama utaratibu ambao

kwa huo Yesu alimaliza “Simoni” (jina lake kabla hajaokoka, lenye

kuonyesha hali yake ya kimwili) na kumwibua “Petro” (jina lake

linalotumiwa kikawaida katika Kitabu cha Matendo) ni kitu

kinachofungua macho ya mtu yeyote anayetamani kujua njia ya Yesu

katika kuwajenga wanafunzi.

Unapotazama mstari wa pili kwenye ile orodha, utaona

kwamba majina hayafanani. Ndivyo ilivyo kwa mstari wa tatu na wa

nne. Lakini –– katika mstari wa tano jina ni lile lile. Hii ni muhimu

ili kuelewa mkakati wa mafunzo aliotumia Yesu. Mstari wa sita 192

Page 201: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

hauna jina moja, wala wa saba, wala wa nane. Lakini –tena – katika

mstari wa tisa jina ni lile lile moja. Mstari wa kumi una majina

tofauti, na wa kumi na moja, na wa kumi na mbili (kama utajaza

nafasi iliyoachwa wazi na kifo cha Yuda Iskariote kwa kuandika jina

la mtu aliyechaguliwa kumrithi, yaani Matiya).

Pengine mpaka hapo tumeanza kuona njia ya msingi kabisa

iliyotumiwa na Yesu katika kujenga wanafunzi wenye maono ya

dunia nzima, wenye uwezo wa kuigusa dunia nzima, na wenye

kuzalisha wanaojiongeza kama wao wenyewe. Tunajua bila shaka

yoyote kwamba mkakati wa Yesu ulikuwa umejengwa kwenye kundi

dogo la watu kumi na mbili. Pia tunajua kwamba Yesu aliweka

“mayai” Yake yote katika hicho “kikapu” Chake kidogo sana.

Mpango Wake wote kwa ajili ya kuigusa na kuifikia dunia ulikuwa

umewekwa katika mikono (na uzalishaji) ya watu kumi na mbili!

Tena, orodha ya Mitume inaonyesha pia njia Yake katika kuwajenga

watu hao. Bila shaka Yeye (na ni dhahiri ukitazama tu) aliwagawa

watu Wake hao kumi na mbili katika makundi matatu yenye

kulingana, yenye watu wanne kila moja, na kuweka kiongozi kwa

ajili ya kila kundi. Tuna ushahidi gani kuhusu hili? Mbona ni

mkubwa tu ushahidi huo? Haiwezi kuwa ni bahati au bahati mbaya.

Watu wote katika kundi la kwanza (na hao tu) ndiyo walikuwa

wafuasi wa Yohana Mbatizaji waliokuja kumfuata Yesu kwa sababu

ya kutiwa moyo na kiongozi wao. Hao watu wote katika kundi la

kwanza ni watu wenye uwezo na machachari, kama Simoni Petro, 193

Page 202: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kiongozi wao. Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo” na

Yesu Mwenyewe! Kitabia walikuwa kama ngurumo inayotaka

kuanza kazi. Andrea bila shaka ndiye mwenye uwezo mkubwa

kuliko tunavyofikiri kwa kawaida. Yeye ndiye alikuwa mishenari wa

kwanza kufanya kazi nyumbani (ktk Yohana 1:40-42), mtenda kazi

kwa ajili ya vijana na kwa ajili ya jamii (ktk Yohana 6:8, 9), na ndiye

alikuwa mishenari wa kwanza kufanya kazi nje ya nyumbani (ktk

Yohana 12:20-22). Haiwezekani kwamba mtu mpole aliyezubaa

angeweza kufanikisha mambo yote hayo ambayo yanatajwa katika

maandiko hayo! Basi, hawa walikuwa watu wenye uwezo katika

utendaji.

Kundi la pili linaongozwa na Mtume Filipo, ambaye katika

Injili anaonekana kuwa mtu mfikiriaji, au mwanafalsafa. Na kila mtu

katika kundi lake alikuwa hivyo hivyo – Tomaso “mwenye mashaka”

na Lawi Matayo, aliyeandika Injili yenye mafundisho ya hali ya juu

sana ya Yesu. Ona kwamba Yesu hakumweka mwanafalsafa kuwa

kiongozi mkuu katika kundi Lake maana asingefanikisha chochote!

Kwa kawaida, watu aina hiyo ni wenye mashaka sana, wenye

maswali mengi, watafiti wakuu, wapinzani wakuu, wepesi kuzembea

na ni wachangiaji wakubwa kuhusu utume wa Kikristo. Lakini,

hawawezi kuwa viongozi wa kundi. Lakini, tusipuuze umuhimu na

ulazima wa watu hawa tunapotafakari hoja hii. Ni kwamba tunaona

tena jambo lingine kubwa na la maana sana katika mkakati wa Yesu.

194

Page 203: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sasa – kaa tayari. Kundi la tatu lilikuwa na wanamapinduzi

wa kisiasa tu! Kiongozi wao – Yakobo mwana wa Alfayo – pengine

ndiye alikuwa mpole kuliko wote katika kundi hilo! Pengine jina la

pili la Yuda, “Iskariote” laweza kutokana na kisu kidogo kilichokuwa

kinabebwa na baadhi ya wanamapinduzi waliokuwa wamejizatiti

kukitumia kumwua afisa yeyote wa Kirumi ambaye wangefanikiwa

kumpata katika kundi la watu (au popote pale ikiwezekana). Hili ni

jambo la ajabu. Kuna ushahidi mkubwa tu kwamba Yakobo na

Matayo (ambao wote wanaitwa “mwana wa Alfayo”) walikuwa

ndugu. Je, hili linakusisimua kiasi? Mbona mmoja (Matayo) akawa

msaliti kwa kuunga mkono Rumi, akitoa maisha yake kulipisha kodi

toka kwa Wayahudi kwa ajili ya serikali ya Kirumi, ambayo

waliichukia? Mbona yule mwingine (Yakobo) akawa mzalendo

hodari wa Kiyahudi? Je, kuna aliyeitikia maoni ya mwenzake ya

kupita kiasi? Je, uzalendo wa Yakobo ulimfanya Matayo aisogelee

Rumi? Au je, usaliti wa Matayo ulimfanya Yakobo kuingia katika

matendo ya kisiasa na kimapinduzi? Au? Hoja yoyote tutakayotoa

inadhoofishwa na ukimya wa Maandiko, lakini swali hilo linaibua

maswali na fikira sana. Yule anayeitwa “Mzelote” anatambulishwa

kwa jina lake na chama cha siasa kilichokuwa cha kizalendo sana,

chenye uasi na ukatili sana kilichoitwa hivyo hivyo. Je, ulijua

kwamba kama Simoni Mzetole angekutana na Matayo mtoza ushuru

katika hali “ya kawaida” tu, angemwua upesi sana? Ndiyo maana

nasema, Muujiza Mkuu wa Yesu haukuwa kuwalisha watu wenye 195

Page 204: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

njaa kwa kuongeza chakula, au kuwaponya wagonjwa, au hata

kufufua wafu. Kwangu mimi, Muujiza Wake Mkuu ulikuwa ni

kujenga – kwa kutumia vifaa “visivyowezekana” – kundi la Watu

Kumi na Mbili ambao wangetikisa dunia kwa Uzalishaji wa Kiroho

hadi miisho ya dunia ya siku zile! Na, kama kanisa lisingebadilisha

mkakati wa Yesu (wa kujenga watu) na kuweka kitu mbadala

kinachowafaa wao, ambacho hakika kinatokana na chanzo kingine

(kujenga taasisi zenye kujijali kwa ndani), mawimbi hayo

yaliyoanzishwa na wanafunzi yangekuwa yanaitikisa dunia mpaka

miisho yake hadi leo, na kuendelea kufanya hivyo bila kuzuiwa wala

kupungua hadi mwisho wa dahari.

Charlie Chaplin – mchekeshaji maarufu sana duniani –

alipokuwa hai, yalifanyika mashindano ya “Wanaofanana na Charlie

Chaplina” huko nchi ya Monaco. Bwana Chaplin alisafiri mpaka

huko, akaingia kwenye shindano hilo pasipo kujulikana, na akawa

mshindi wa tatu! Kweli najiuliza Yesu wa kweli angeshika nafasi

gani katika kanisa la siku hizi kama yangefanyika mashindano ya

“Wanaofanana na Kristo”???

Usielewe hii sura vibaya. Hakuna amri ya wazi

inayotulazimisha sisi kufuata mpango wa vikundi huo. Lakini, busara

ya kawaida tu ingeshauri kwamba, “kama Kristo” maana yake “kama

Kristo”. Hilo linaonekana jepesi kabisa, lakini ukweli wake

umeshindwa kupatikana katika kanisa. Ukubwa wa kundi la Yesu

unaonekana kuwa wa busara sana, pamoja na migawanyo yake, 196

Page 205: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

maana inatoa nafasi ya uwajibikaji, mgawanyo wa kazi, ushirika na

kadhalika. Lakini hakika, makundi hayo hayakuwa yamefungwa na

yasiyoweza kubadilika. Matokeo yanathibitisha kwamba Yesu

alikuwa Bingwa wa jinsi vikundi vinavyofanya kazi na kushirikiana.

Mbona sisi tusiwe na hekima ya kufanya hivyo? Je, kweli sisi tuna

hekima tusipofanya hivyo?

Narudia tena: wewe … na wewe … na wewe … hamtafanya

kitu kama Kristo katika maisha yenu yote kitakachozidi

kuwafundisha watu binafsi kwa kufuata mkakati wa Yesu (yaani,

“kuwafanya watu kuwa wanafunzi”) ili kuifikia na kuigusa dunia

nzima.

Je, wakati haujafika wa sisi kukagua shughuli zetu zote ili

kuhakikisha kwamba tunatimiza lile Agizo la Yesu kikamilifu, kwa

uzito na kwa mtiririko wa utaratibu unaofaa?

197

Page 206: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 8

Jinsi Kiwango Hiki Kifanyavyo Kazi Kanisani

“Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. Hivyo husema, ‘Alipopaa juu aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa.’ Basi neno hilo ‘Alipaa’, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

Waefeso 4:7-14198

Page 207: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Je, Ukristo ambao sasa unawakilishwa kanisani kwenu

ungesababisha Kitabu cha Matendo ya Mitume? Hili swali ni kali na

lenye uzito. Kuwa wazi ni kutoa jibu moja tu: Hapana! Basi, nini

tofauti kati ya Ukristo uliosababisha Kitabu cha Matendo ya Mitume,

na huu mbovu wa ajabu kabisa unaopatikana na kuonekana karibu

katika kila kanisa?

Katika kanisa la kwanza, walifuata mfano wa Yesu katika

kuwajenga watu muhimu, lakini siku hizi sisi tunahesabu watu katika

makundi. Tuna kawaida ya kupima mafanikio kwa kutazama ukubwa

na wingi wa watu. Tena, mfano tunaofuata sisi sana sana ni wa

kusafisha wenye dhambi ili waishi maisha safi. Wao walifuata mfano

wa kuwafanya watakatifu kuwa wanafunzi kwa ajili ya kuifikia na

kuigusa dunia, ingawa pamoja na hayo, maisha masafi

hayakupungua. Tunachofanya sisi ni kama kuwaweka walio-okoka

katika sanduku la kuwahifadhi liitwalo “usalama wa milele” badala

ya kila mwamini kuwekeza maisha yake yote katika watu wengine

waliokolewa ili kutengeneza wazalishaji wenye maono ya dunia

nzima, wenye kuigusa dunia nzima na kuifikia, ambao nao

watawazaa wengine wenye maono ya dunia nzima, wenye kuigusa

dunia nzima na kuifikia, ambao nao watawazaa wengine …..

Sasa – tofauti kati ya Ukristo wa mwaka wa 4BK na Ukristo

wa mwaka wa 2008BK? Je, Yesu amebadilika? Hapana.

Tunamwabudu na kumtumikia Yesu yule yule waliyemjua wao. Je, 199

Page 208: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Roho Mtakatifu ni mwingine? Hapana. Roho Mtakatifu

tunayehusiana siku za leo ni yule yule “aliyekuja” kikamilifu kabisa

katika uwezo wa ukombozi Siku ile ya Pentekoste. Je, Biblia ni

tofauti? Hapa, uwe makini kidogo, kwa sababu jibu sahihi ni

“ndiyo”. Wao hawakuwa na Biblia kamili. Walikuwa ndiyo

wanamalizia kuandika Biblia kupitia shughuli zilizoandikwa katika

Kitabu cha Matendo. Kwa hiyo, kama kuna faida ya kuwa na Biblia

kamili iko kwetu, si kwao. Je, kulikuwa na tofauti katika teknolojia au

mafanikio kwa habari ya usafiri? Aah! Swali gani tena hilo? Sisi tuko

vizuri katika kila hali – wao hawakuwa vizuri katika kila hali. Mungu

alikuwa ameandaa amani ya dunia nzima kupitia nguvu za kijeshi za

Kirumi na akatayarisha mtandao wa barabara zilizofika kila mahali

ambao ulijengwa na Warumi, lakini hayo yalikuwa machache sana

ukilinganisha na manufaa ya leo tuliyo nayo sisi. Wao hawakuwa na

simu, barua pepe, vipindi vya televisheni ili kuchangisha fedha – wao

walikuwa na “mwambie mtu”. Hawakuwa na vyombo lakini

walikuwa na KWELI MUHIMU! Lakini, na sisi pia tunazo! Sasa,

kilichowawezesha wao kuigusa dunia nzima iliyojulikana wakati ule

katika kipindi kifupi sana, wakati leo hii kiasi cha mbili kwa tano cha

binadamu wote hakijasikia kabisa Injili, na kiasi kingine cha mbili

kwa tano cha dunia nzima kimepata Injili kwa hali ya chini sana, ni

nini? Halafu, idadi ya moja kwa tano iliyobakia ina uwezo mkubwa

sana katika kila hali kuliko waliokuwa nao Kanisa la kwanza. Lakini,

kwa faida gani? Je, tofauti kati yetu na wao ni ya kujitolea? Kuna 200

Page 209: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ambao watatoa hoja ndefu na kwa sauti kubwa kabisa kwamba hiyo

ndiyo tofauti, lakini, si hiyo tu. Katika kanisa la kwanza, watu

waliokuwa wamejitoa si wengi kuliko Mkristo wa kawaida wa siku

hizi ambaye anahudhuria ibada kwa uaminifu mara tatu kwa juma

pamoja na siku maalum – lakini bado hana ushawishi wa aina yoyote

juu ya watu kama bilioni 2 nukta tatu ambao hawajasikia habari za

Kristo siku hizi. Ukristo wa Kitabu cha Matendo usingeweza

kuvumilia takwimu za jinsi hii, lakini kanisa la leo lina uwezo wa

kuendelea katika shughuli zake zote za kawaida bila hata ya kujali

hali ya kushindwa kwake iliyo kuu.

Sasa – nini tofauti basi kati ya Ukristo wa Iskanda, Rufo,

Trofena na Andoniko wa karne ya kwanza, na ule wa Jo, Suzie,

Samweli na Edwadi wa karne yetu? Mimi nasema hivi: Tofauti ni ya

mkakati peke yake. Wenzetu walitenda kazi kwa kufuata mkakati

tofauti na ule tunaotumia sisi!

Angalia mfano huu, ambao ni picha ya desturi ya taasisi ya

makanisa ya leo. Fikiri kuhusu basi lenye kusafiri kwenda mahali,

ambalo linabeba watu njiani. Kanisa ndiyo mfano wa hilo basi.

Mchungaji ni kama dereva wa hilo basi. Dereva (yaani mchungaji)

anawakaribisha abiria wapande kwenye basi (na yawezekana

wakakaribishwa na abiria wenzao pia). Wanaketi na husimama ili

kushughulikia maswala muhimu tu. Dereva (yaani mchungaji) anatoa

maelezo kuhusu vivutio vinavyoonekana njiani wakati akiwaendesha

abiria wasiofanya chochote, wenye kutazama (na pengine waliolala 201

Page 210: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

usingizi) kuelekea mahali walipokubaliana kwenda. Abiria wa

kawaida anavumilia hiyo safari, lakini kamwe hatafuti abiria

mwingine, na mara nyingi hashuhudii kuhusu jinsi anavyofurahia

basi lile, na kampuni ya hilo basi, na njia linakopitia, wala safari

linalofanya. Yaani kwa kifupi ni kwamba, mafanikio ya safari

yenyewe yako katika uwezo na ubora wa hilo basi, na utendaji wa

dereva wake. Hii ni tofauti kubwa sana sana na ule Ukristo wa

Bwana Yesu pamoja na wanafunzi wa kwanza. Ukristo wa Kitabu

cha Matendo ulikuwa ni kitu cha watu (ktk Matendo 1:8; 8:1 na 4);

haukuwa kitu cha mhubiri au kitu cha taasisi fulani.

Eneo la dunia liitwalo North Pole lina kiwango kikubwa sana

cha barafu. Wanasayansi wanatuambia kwamba barafu hiyo ikitokea

kuyeyuka basi sehemu kubwa ya dunia itajaa maji. Wakristo wengine

wanaweza kuitwa “mali ya Mungu iliyoganda”. Kama hao wote

watayeyuka mbele za Mungu na kupata joto la kutambua maono

Yake, makusudi Yake, malengo Yake, na mkakati Wake, “dunia yote

ingejaa maarifa ya Bwana, kama maji yajazavyo bahari.”

Mfano wa Mungu aliotoa ili Kanisa Lake liufuate unaelezwa

kwa uwazi kabisa katika Waefeso 4:7-14. Mada ya jumla ya fungu

hili ni karama za kiroho, lakini karama zinazotajwa hapa si zile za

aina mbalimbali ambazo kwa kawaida hutajwa katika Agano Jipya.

Orodha ya karama katika Warumi 12, 1Wakorinto 12 na 14 na 1Petro

4 ziko tofauti. Hizo ni matoleo kutoka mbinguni zinazowekwa katika

waamini na Roho Mtakatifu. Karama hizi tunazotaja hapa sasa ni 202

Page 211: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

viongozi wenye vipawa ambao Roho Mtakatifu huwatoa kwa Kanisa

Lake kwa ajili ya makusudi maalum ya jumla katika kanisa, na kwa

ajili ya kufanikisha au kutimiza malengo maalum.

Hebu nitoe muhtasari utakaotuwezesha kuona kwa ujumla

fungu zima (yaani, Waefeso 4:7-14). Fungu hili linatuonyesha mtoaji

wa hizo karama, karama zenyewe (yaani, watu waliopewa vipawa),

na malengo ya karama hizo kutolewa.

MTOAJI KARAMA

I. Mtoaji Anatajwa – mstari 8-10

Kweli kuu tatu zinatolewa kuhusu Yesu:

A. Alishuka, ms. 9, 10.

B. Alipaa, ms. 8, 9, 10.

C. Yuko juu ya vyote, ms. 10b.

II. Karama Zenyewe (Watu) Zinaonyeshwa – mstari 11

Viongozi wenye vipawa wanne (au watano) wanatajwa:

A. “Mitume”

B. “Manabii”

C. “Wainjilisti”

D. “Wachungaji waalimu”

III. Malengo Ya Kutolewa Karama Yanatajwa – mstari 12, 13

A. Ili kupata viungo kwa ajili ya Mwili, ms. 12b.

B. Ili kuwezesha viungo katika Mwili, ms. 12a.

C. Ili kutumia viungo kupitia Mwili na zaidi, ms. 12-16.203

Page 212: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Katika kile kipengele cha “Mtoaji Karama” ambacho ni mojawapo

ya maandiko maarufu sana yenye kufafanua fundisho la Nafsi ya

Kristo katika Agano Jipya, ona sheria moja inayojitokeza. Ingawa

njia ya Shetani kwenda chini ni kupanda, njia ya Mungu kwenda juu

ni kushuka. “Yeye ajiinuaye mwenyewe (kama Shetani) atashushwa,

lakini yeye ajinyenyekezaye mwenyewe (kama Yesu) atainuliwa

(kama Yesu).”

Hii orodha ya watu waliopewa vipawa (ktk mstari wa 11)

inaweza kusababisha mafundisho na mawazo yasiyo na kikomo.

Kwa mfano: Swali kuhusu zile karama mbili za kwanza ni hili: Je,

zipo katika kanisa la siku hizi? “Mtume” kama nafasi rasmi iliweza

kuwepo katika kanisa la kwanza tu kwa sababu sifa zake maalum

zilizotakiwa (yaani, kumwona Yesu na kuwa pamoja Naye)

hazipatikani kwa mwingine yeyote baada ya karne ya kwanza. Nafasi

ya “nabii” inaonekana kuwa ya Agano la Kale tu. Pia, Waefeso 2:20

inasema kuhusu mitume na manabii kuwa “msingi” wa kanisa. Siku

hizi, jengo hilo limekwisha panda sana! Kweli msingi ni wa muhimu,

lakini, ukiwa katika nafasi yake tu, si katika kuta.

Ila, kufikiri hivyo sana kusikokuwa na faida kunaweza

kutufanya tukose hoja kuu. Kuna kanuni ambayo imetajwa mara kwa

mara, kwamba, “Mfuasi ni kama kiongozi wake”. Mfuasi atakuwa

kama kiongozi wake (maneno ya Yesu Mwenyewe katika Luka

6:40). Basi, wakati Yesu alipotoa kwa Kanisa Lake viongozi wanne 204

Page 213: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wenye karama pekee na tofauti, bila shaka anatuambia waziwazi kile

anachokusudia Kanisa Lake liwe.

MTUME

Neno “mtume” maana yake ni “mtu anayetumwa kuondoka”.

Basi, anakusudia iwe hivyo kwa kanisa Lake lote (!!!), kwamba liwe

ushirika wenye kwenda na kutuma waendao. Watu wengi hujiepusha

na jukumu la kwenda kwa kubakia kwenye wazo la kutuma, lakini hii

haiwezi kupata kibali katika Agano Jipya. Vipi kanisa la siku hizi?

Limejaa watu wanaokuja – watu ambao Ukristo wao unaelezwa kwa

uaminifu wao katika kuja na kutumika. Neno “mtume” kama lilivyo

hutuambia ni kwa nini Yesu aliwachagua hao (ktk Waefeso 1:3;

Matendo 1:3). Lile neno “aliwachagua” linamaanisha kwamba Yesu

aliwachagua “kwa ajili Yake Mwenyewe”, wala si kwa ajili ya kukua

kwao, afya yao, mali yao, furaha yao, au hata utoshelevu wao.

Mkazo usiofaa umesababisha kuundwa “Ukristo unaofurahisha

wateja”, ambao ni kusoma vibaya Agano Jipya. Agano Jipya

linamwonyesha Mungu kuwa ndiye mteja, na sisi ndiyo

watoshelezaji wa matakwa Yake. Ndugu aitwaye Jim Elliott aliomba

kwa kumaanisha kabisa, hivi: “Ee Moto wa Mungu! Nifanye mimi

kuwa ndiyo mafuta!” Je, Yesu alituchagua sisi kwa ajili gani? Ili

twende mahali Yeye anapotaka sisi twende – “kuondoka” – siyo

“kukaa” – ili tuwe, ili tuseme, na kufanya chochote Yeye anachotaka.

Basi, lengo pekee lililo sahihi kwa ajili ya kila Mkristo lazima 205

Page 214: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

lihusishe mkakati wa kuifikia miisho ya dunia. Tunawezaje kuona

vikomo kwenye mkakati kama huo katika Kitabu cha Matendo?

Walijaribu kuweka mipaka kwamba kiwe kitu cha mahali pamoja,

kitu chao cha ndani, lakini Mungu alituma mateso yaliyowatawanya

kama mbegu (ambalo ni neno linalotumiwa katika Matendo 8:1; 8:4

na katika 1Petro 1:1) kwenda nje na mbali mbali kabisa katika

udongo mchanganyiko wa Dola ya Kirumi. Ee Mkristo – jihadhari,

kwa sababu mateso makubwa sana ya siku zijazo yanakaribia kulijia

kanisa la siku hizi. Uislamu wenye msimamo mkali na ukorofi

umeanza kuivamia dunia, na kilichoko njiani ni kanisa maskini na

dhaifu la Yesu Kristo. Maendeleo ya kiteknolojia na makufuru ya

sayansi na ubinadamu vimezua watesaji kila mahali. Kwa hiyo, siku

za Ukristo kukaa katika ngome yake salama kwa utulivu,

zimekwisha. Utawanyiko mwingine wa Wakristo uko njiani. Na

Mungu ndiye Mpanda Mbegu! Ni hivi: Ingawa sisi ni wagumu kwa

hiari yetu kusikia kuhusu jukumu letu la kwenda, Mungu

anamaanisha kabisa kwamba twende!

NABII

Neno “nabii” maana yake “mtangazaji” (pamoja na kwamba

ni “mtabiri” wa ukweli). Nabii ni msema kweli, si msema kitu cha

kupoza moyo. Nabii alikuwa “mtangazaji” au “mshuhuda”. Basi,

Yesu alipotoa kwa Kanisa Lake manabii wenye vipawa,

anachotuonyesha ni kwamba alikusudia kanisa Lake kuwa ushirika 206

Page 215: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wa watu wasiokoma, walio waaminifu siku zote, walio jasiri siku

zote, wenye kuzungumza siku zote. “Waliokombolewa na Bwana na

waseme hivyo.” Hii hutimiza makusudi kadhaa ya Mungu.

Humkomaza msemaji, kwa sababu mtu yeyote atafuatilia ukiri

aliotamka, hata kama ni ukiri gani. Humtukuza Mungu, kwa sababu

anakaa ndani ya sifa na shuhuda za watu Wake. Na, hufikisha Injili

kwa kila asikiaye. Mkristo asipime joto au mapigo ya moyo ya dunia

kabla hajanena – la sivyo, hatasema kabisa! Kwanza kabisa, sisi

husema kwa Mungu, na kuhusu Mungu, na kwa ajili ya Mungu. Basi,

hatupaswi kunyamaza kimya kamwe. “Ninaamini, hivyo nimesema.”

Manabii, wahubiri, waalimu na viongozi wa kanisa lazima waseme

kwa ukamilifu, kwa uwazi na kwa ujasiri – na waamini wote vivyo

hivyo!

MWINJILISTI

Neno “mwinjilisti” maana yake ni “msema mema,” yaani,

mtu ambaye “anamsema vema” Yesu kwa watu, na watu kwa Yesu.

Injili inakiri habari mbaya sana kuhusu Shetani na mbinu zake

mbaya, mwanadamu na hali yake ya dhambi na utendaji wake,

Mungu na itikio Lake takatifu kinyume cha dhambi, na kuzimu kama

makazi ya mwisho kabisa ya mwenye dhambi anayejiona na

kujifikiria mwenyewe. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, kanisa

limetangaza habari mbaya mara nyingi zaidi na kwa nguvu sana

kuliko ambavyo limetangaza Habari Njema. Ujumbe mkuu na wenye 207

Page 216: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

nguvu zaidi katika Maandiko unaitwa “Injili” – euaggelion – “Habari

Njema”. Hakuna mtu aliyepokea habari njema kweli kweli mpaka

ajisikie vizuri kuhusu Mungu, kuhusu Yesu, kuhusu Roho Mtakatifu,

kuhusu yeye mwenyewe, kuhusu wokovu wake, kuhusu hali yake ya

sasa na ya baadaye, na kuhusu matokeo ya mwisho kabisa ya mambo

yote. Mungu analikusudia Kanisa Lake kuwa tukufu na lenye ushindi

katika kueleza kwake habari njema.

MCHUNGAJI MWALIMU

Halafu neno “mchungaji mwalimu” linatoa kweli ya mwisho

kuhusu kile ambacho Mungu anatazamia kwa Kanisa Lake. Neno

“mchungaji” maana yake “mtunza mifugo” na linaeleza anakusudia

watu Wake waongoze. Ili kuongoza, Mkristo lazima ajue kwa uwazi

na kwa uhakika yeye ni nani, ana nini, anakwenda wapi, jinsi ya

kufika aendako, kusudi lake leo na kila siku ni nini, na jinsi ya

kufanikisha kazi yake. Mtu yeyote anayejua mambo hayo kwa uwazi

na uhakika anaweza kumwongoza mtu mwingine. Neno “mwalimu”

linaonyesha kwamba Yesu anakusudia Kanisa Lake kuwa ushirika

wenye kueleza ukweli, kufundisha na kulisha. Na hii ndiyo kazi ya

kila aaminiye. “Kwa njia zote” (ktk 1Wakor. 9:22) – neno la papo

kwa papo, ushuhuda ulioandaliwa, mafundisho rasmi na mahubiri,

ugawaji wa maandiko, vitabu, magazeti, barua ( na Mungu yuko juu

sana kwa uandishi wa barua), kanda za sauti na video, redio na

televisheni, kuonana uso kwa uso au kwa umbali – lengo la Mkristo 208

Page 217: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

linatakiwa kuwa ni kushawishi, kugeuza, “kuwavuta baadhi” kwa

shughuli zozote anazofanya.

Hizo ndizo karama zikionyeshwa; basi, kazi, wajibu na jinsi

ya kanisa kuwa wazi na dhahiri kabisa.

MALENGO YA KUTOA KARAMA HIZI

KUPATA VIUNGO

Tunapaswa “kuujenga” Mwili wa Kristo kwa kutumia hawa

watu wenye vipawa na wafuasi wao watakaopatikana. Hivyo,

kiwango kipya cha kupata watu lazima kitumiwe na kanisa. Masharti

yote ya kuwapata watu lazima yatumike mara moja na kanisa. Kila

kitu katika “mkataba” wa Kikristo lazima kitamkwe na kukubalika

tangu mwanzo kabisa – wakati wa kukata shauri – yaani, kujikana,

kubeba msalaba (hayo ni masharti ya “pale pale mlangoni”, si

nyongeza kwa kuwa mtu amekomaa), kuishi nje kama mtu alivyo

ndani, kujisomea Biblia kwa ajili ya kujijenga na kwa ajili ya

kutumika, kuabudu na maombi ya mapambano, na kadhalika. Na

hayo hayawezi kufanyika sehemu ya maisha kwa mafunzo ya saa

moja kwa juma, au masaa mawili, au matatu kwa juma.

Je, katika uinjilisti wetu, ni wapi penye kiwango na utendaji

kwa ajili ya kumkataa kijana tajiri yule aliyekuwa anapenda mali

yake? Kiwango hiki cha hali ya juu sana kilitumiwa na Yesu katika

kumwondoa mtafutaji muungwana, wa dhati aliyekuwa anataka 209

Page 218: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kujua cha kufanya (hebu jisomee Mathayo 19:16-26 kwa makini

sana). Tena ujue kwamba swali la huyu kijana – “Nifanye nini kizuri,

ili niweze kuwa na uzima wa milele?” – Yesu aliulizwa mara mbili.

Mwanasheria (“mtaalamu” wa Torati ya Musa) aliliuliza katika Luka

10:25 katika mantiki tofauti kabisa. Na hakuna wakati wowote

ambapo Yesu alitoa jibu ambalo wengi wetu tungelihesabu kuwa ni

“mpango wa wokovu unaofuata utaratibu”. Yeye aliweka “kipimo

cha katikati” pale mwanzoni kabisa – penye mlango wa kuingilia!

Ni hivi: Neno “amini” ambalo linatumika kirahisi sana na sisi

kueleza njia ya wokovu, ni muungano wa maneno mawili ambayo

maana yake ni “kwa uzima”, au “kuishi kwa”. Unavyotenda ndivyo

unavyoamini! Mengine yote ni mazungumzo tu ya kawaida kabisa,

“si lolote si chochote”, maneno mazuri tu ambayo yamejaa “kelele na

ghadhabu, yasiyo na maana yoyote ile”. Huu ni Ukristo wenye

kujadili lakini hautendi. Ni Ukristo wenye “kujitukuza” bila ya

kwenda, wenye “kufurahia” lakini usiotii, wenye kujitakasa

wenyewe kwa ajili ya usafi lakini kamwe haujimimini wala kujitoa

kwa ajili ya ushindi. Hujitokeza ili kujaza kanisa (Jumapili asubuhi)

lakini haujimwagi ili kujaza na kugusa dunia mpaka pande za

mwisho kabisa za nchi … Lazima tutaje waziwazi kama sharti la

kuingia kwamba, Kuzaliwa Upya (kitu kinachofanywa na Mungu tu)

lazima kufuatwe na Maisha Mapya) ambayo pia yanatendwa na

kuwezeshwa na Mungu pia). Basi, tunahitaji kuwapata wanachama

wapya katika kanisa la siku hizi, wanachama wenye kuelewa 210

Page 219: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mafunuo kamili ya Yesu. Kwa kawaida si inatakiwa mwenye kutia

sahihi karatasi yoyote asome na kuelewa mkataba mzima kabla ya

“kutia sahihi”?

KUWEZESHA VIUNGO

Halafu, kila mshirika anapaswa “kuwezeshwa” kwa ajili ya

kazi yake binafsi ya “huduma” (ktk 4:12a). Sentensi hii ina neno

moja pana sana na lenye mafafanuzi makubwa katika Agano Jipya.

Ni neno “kuwakamilisha” ila, maana kamili ya neno hilo si rahisi

kuipata. Kuna tafsiri moja ya Biblia inayosema kwamba hao watu

wenye karama au vipawa wametolewa kwa kanisa ili

“kuwawezesha” washirika. Nyingine inasema “kuwapa vitu vyote

wanavyohitaji”. Kitu kimoja ni hakika kwa tafsiri yoyote ile:

Wakristo wote – bila kukosa, bila kupendelewa, na bila kutengwa –

wanapaswa kuwezeshwa hivyo, kupewa kila wanachohitaji. Mfumo

wa taasisi yenye kutazama ndani ya kanisa la siku hizi ni kwamba,

mchungaji ndiye mchezaji pekee kwenye jukwaa, na “walei –

washirika” wanaachiwa kazi za hapa na pale kama wasaidizi wa

jukwaani, wahusika na taa na walinzi. Mfumo huu lazima

ubadilishwe mpaka ifikie mahali ambapo mchungaji atakuwa ndiye

“mwezeshaji” wa watu, na watu wawe ndiyo watumishi. Kusudi la

wazi kabisa lililotajwa hapa la kuwawezesha washirika ni ili kila

Mkristo aingie katika “kazi ya huduma”. Ni hivi: Siku ile ulipo-

okoka uliitwa kuingia katika huduma! Kanisa lingekuwa jeshi 211

Page 220: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kubwa, lenye ushindi sana, lenye kupenya, lenye kusonga mbele,

lenye kuimba, na lenye kelele za shangwe kama wangejua hilo! Dada

Eugenia Price alisema hivi: “Dhambi kuu kuliko zote ya kanisa la

siku hizi ni kwamba, limefanikiwa kumfuga na kumdhoofisha yule

Simba wa Yuda.” Tumezuia vitisho vyote, hatari yote na uwezekano

wa kufia Ukristo visitokee katika Ukristo. Basi, michezo au tamasha

za muziki ndiyo zenye kuweza kutoa changamoto, msisimko na hali

ya kujali kuliko kusonga mbele kwa Kanisa la Yesu Kristo.

Neno “kuwezesha” au “kukamilisha” ni neno kubwa.

Ukijifunza neno hilo katika Agano Jipya utashtuka na kushangaa.

Kwa Kiyunani, neno hilo ni “katartismon”. Kipande chake ni neno

“artis” na maana yake ni “fundi stadi”. Kumbe kazi ya kila

mchungaji mwalimu ni kumfanya kila mwamini aliye chini ya uwezo

wake kuwa fundi stadi katika kulitumia, kulielewa, kuliishia,

kutawaliwa nalo, kuhudumia, n.k. kwa kutumia Neno la Mungu. Kazi

hii ilimla Yesu sana, kama mkakati kwa ajili ya Watu Kumi na Mbili

katika mafunzo kazini ya muda wote, kwa karibu, katika kipindi cha

miaka mitatu tu. Hapo tena – nini maana ya neno “kama Kristo”?

Tukiondolea mbali Mkakati Wake, na kuondoa Agizo Lake Kuu, na

kupuuza Mfano aliotoa, kwa nini sisi tulalamike kuhusu hali ya

kanisa na ya dunia? Ni kwamba tunaishi na tulichotengeneza

wenyewe. Kumbuka kwamba Utambuzi hupelekea Taratibu, na

Taratibu kupelekea Matokeo. Kama kilichotokana na mfumo mzima

212

Page 221: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

ni kibaya, (na hakuna awezaye kukana kwamba sivyo), basi

Utaratibu wetu lazima una makosa.

Angalia tena lile neno “kuwezesha”. Utafiti unadhihirisha

kwamba lilikuwa neno la kawaida kabisa lililotumika katika dunia ya

Kiyunani ya karne ya kwanza. Na lilikuwa na maana nyingi

mbalimbali.

(1) Kutuliza mji uliokuwa umetengana.

(2) Kutibu kiungo kilichokuwa kimeteguka.

(3) Kuendeleza viungo fulani vya mwili kwa mazoezi.

(4) Kumrejeza mtu kwenye hali yake ya kawaida.

(5) Kuwapatanisha marafiki ambao walikuwa wametengana.

(6) Kumwezesha mtu au kitu kwa ukamilifu kabisa, kwa ajili

ya kusudi fulani.

(7) Kuweka mambo kwa utaratibu, au kupanga vitu vizuri.

(8) Kuelekeza kitu kwenye mkono wa maendeleo.

Kabla ya kuachana na orodha hiyo kwa haraka, hebu tazama

kila neno na ulifafanue kulingana na maelezo ya kazi ya viongozi wa

Mwili wa Kristo. Halafu, tafsiri kila neno katika maisha na

mwenendo wa wafuasi wote, kwa sababu wanafunzi watakuwa kama

mwalimu wao (ktk Luka 6:40).

KUVITUMIA VIUNGO

Basi, zile nafasi za kawaida zilizozoeleka za “wachungaji” na

“washirika – walei” lazima zibadilishwe. “Walei” wanakuwa ndiyo 213

Page 222: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

askari walioko mstari wa mbele (wenye silaha kamili, wenye

ufahamu kamili, na wenye utendaji kamili), na “wachungaji” na

mkutano wa kanisa lote, wapo kwa ajili ya kuwaunga mkono. Ndugu

Charles Colson alikuwa sahihi kabisa alipoandika hivi: “Kila mmoja

wetu kama waamini lazima tujione kama watumishi wa Injili. Sisi si

wahudhuriaji wa kanisa tu, walaji wa mambo ya kiroho.” Mkristo

ambaye hana huduma binafsi yenye kupelekea mguso wa dunia yote

kwa nguvu ni mfano potofu wa Mkristo. Lengo ni kumtumia Mkristo

kila wakati katika kuishi maisha ya Kikristo na kupenya na kugusa

dunia nzima kwa mkakati wa Yesu. Halafu tena, kujengwa kwa

wanafunzi wenye kujizidisha, wenye maono ya dunia na wenye

uwezo wa kuigusa dunia ndicho Kipau Mbele Kikubwa (kama katika

Agizo Kuu). Ili kanisa liweze kurekebisha mawazo potofu yake,

lazima lianze uandikishaji tofauti, liwe na uwezeshaji tofauti na

mpya, na liwe na utumaji mpya na wa tofauti. Mungu na afungue

macho ya mioyo yetu na kuijaza nuru (ktk Waefeso 1:17-19)!

Kumbe basi – kusudi la sasa katika ushirika wa waaminio ni

“kuwawezesha watakatifu”. Hii inahitaji mafunzo ya hali ya juu, ya

kikamilifu kabisa, kwa kila mwamini. Hatimaye, kusudi kuu ni

“kulijenga kanisa” – kihali, kwa kulijenga kwa ndani, na kwa idadi,

kwa kulipanua kutoka nje. Nje kwa kiasi gani? Kila kanisa lazima

lione kwamba wajibu wake ni mpaka “mwisho wa nchi”. Kwa hiyo,

lazima liongeze uwezo wake – watendaji, mapato, mipango, mikakati

na utendaji wake – hadi mwisho kabisa wa nchi. Kumbuka kwamba 214

Page 223: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mwangaza unaong’aa mbali zaidi hung’aa kwa nguvu zaidi

nyumbani.

MIFANO YA USHIRIKA WA WAAMINIO WA MAHALI

PAMOJA

Tumalizie mafunzo haya kwa kuonyesha michoro miwili ya

mifano ya ushirika wa waaminio walioko mahali pamoja. Mfano

mmoja ni ule wa kawaida katika makanisa yetu mengi, na ule

mwingine ndiyo ufaao, tunaosema juu yake katika maelezo yetu.

Kusanyiko/Waamini

Viongozi

Watendakazi

Mchungaji

Katika mfano wa kwanza, washirika ni watu wengi – waamini

wasiotosheka – wasikilizaji, watazamaji, waunga mkono. Wakati hali

ya kujitoa inaposhuka na kuwa nzito kidogo, yule aliyejitoa zaidi

Dunia

215

Page 224: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

katika ushirika anafanywa kiongozi. Kadiri huko kujitoa kunavyozidi

kuwa kwa hali ya juu (sana sana katika kanisa la mahali pamoja peke

yake), wafanya kazi wa kanisani wanaanza kupatikana. Halafu, yule

aliyejitoa kuliko wengine wote kanisani ndiye anaonekana kufaa

kuwa mchungaji! Bila shaka upotofu wa huu mfano ni dhahiri. Basi,

uzito wa mwili wote na majukumu yake yote unatulia juu ya

mchungaji. Mchungaji anabeba majukumu yasiyohesabika katika

mwili au kundi hilo, na wakati mwingine ndiye anayeona au

kushughulikia majukumu ya nje ya mwili au kundi. Mipango

maalum inawashawishi wale washirika waliojitolea kabisa

kujihusisha na kazi zile “maalum” za kuleta watu kwa Yesu, kufanya

utume, huduma za kawaida katika jamii na kadhalika. Lakini mzigo

wa utendaji, mafanikio na hatimaye kuifikia dunia nzima

humwangukia mchungaji zaidi.

Matokeo ya mfano huu ni matatu:

(1) Uongozi uliovunjika moyo kabisa. Zaidi ya wachungaji

elfu moja kila mwaka wanaacha huduma. Wengine zaidi ya mia tatu

kila mwezi wanaondolewa kwa nguvu kwenye madhabahu. Je hilo

linatutia aibu? Kama hapana, linapaswa kututia aibu! Na, linaweza

kurekebishwa kabisa.

(2) Wanachama wa kanisa ambao kwa sehemu kubwa ni “wa

kimwili” (yaani, wenye ubinafsi, wanaotaka kujitosheleza wenyewe).

Katika mfano huu, washirika hawajui kazi nyingine isipokuwa

kuhudhuria kanisa, kuwa waaminifu kwa taasisi yao (au dhehebu 216

Page 225: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

lao) na kutathmini mapato. Je, ni ajabu kwamba wanazidi kuwa

kimwili?

(3) Dunia inayobaki bila kushuhudiwa. Sehemu kubwa ya

binadamu duniani aidha hawajasikia kuhusu Jina la Yesu kabisa, au

wamesikia “kidogo” tu. Ukristo wa Kitabu cha Matendo

ulishughulika na hali iliyokuwa mbaya zaidi, wakaibadilisha kabisa

kwa muda mfupi sana. Hali iliyoko inaweza kubadilishwa vivyo hivyo

hata leo, lakini si kwa kuendeleza mfano huo mbovu.

Mfano ule wa pili ni kama kinyume kabisa cha ule wa

kwanza.

Mchungaji

Watendakazi

Viongozi

Kusanyiko/Waamini

Dunia

217

Page 226: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Katika huu, mchungaji ndiye mwenye kuwajibika kwanza kabisa.

Nafasi yake ni ya kuwajibika, si ya heshima! Wajibu wa nafasi kama

hiyo ni mkubwa zaidi sana kuliko heshima au sifa yoyote inayoweza

kupatikana kutokana nayo. Ukweli ni kwamba hiyo inaweza kuwa

kama sheria: nafasi yoyote katika mwili inayopelekea kuendelea

kukua kwa sifa ya kiongozi wake (kimafanikio, na kadhalika) itiliwe

mashaka kabisa katika Ukristo! Mwili hutafuta kuonekana,

kutambuliwa, kutuzwa – na hilo ni eneo moja tu la udhaifu ambalo

mwili umerithi! Mwili hauwezi kuaminiwa na aina ya pongezi na sifa

zinazotolewa kwa viongozi “maarufu” katika michezo au siasa.

Wajibu wa kwanza wa mchungaji katika mfano huu ni

kuwawezesha na kuwaambukiza watenda kazi pamoja naye maono

ya kufanya watu kuwa wanafunzi, ili kuifikia dunia nzima. Maono

haya ya kawaida na ya wote yanapaswa kuamua huduma ya kila

mtenda kazi kanisani, na kupanga malengo yake kwa ajili ya

wanafunzi ambao yeye anawajenga. Mchungaji pia anawajibika

katika kuwawezesha na kuwaambukiza viongozi maono yake, lakini

sasa ana fursa pekee. Viongozi kwa wakati huu “wanawezeshwa

mara mbili” kwa kupewa maono ya kawaida na mkakati – kutoka

kwa mchungaji moja kwa moja, na kutoka kwa watumishi wa kanisa.

Basi, mchungaji, watumishi wa kanisa na viongozi watakuwa na

umoja katika kuwawezesha watakatifu wote kwa ajili ya kazi yao ya

huduma. Wakati matarajio hayo yanapofanyiwa kazi, “mafuta ya

ziada” yataondoka, na “vijana tajiri” watahama. Lakini, macho, 218

Page 227: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

midomo, masikio, mikono, magoti na miguu ya mwili wenyewe

vitakuwa vinaona, vinasema, vinasikia, vinatenda, vinapiga magoti

na kutembea katika muungano kamili kabisa – siku zote kuelekea nje

hadi mwisho wa dunia. Ushirika wa mahali pamoja ndiyo mahali pa

msingi pa huduma (ingawa huduma nyingi hufanyikia hapo). Ndicho

kituo chenye nguvu kwa ajili ya huduma. Watu pale wanaonyesha na

kumshirikisha Kristo popote walipo, na kwa makusudi kabisa

wanajenga mikakati kwa ajili ya wao binafsi kupenya hadi mwisho

wa nchi.

Nini matokeo wakati mfano wa pili unapokuwa halisi? Hapa

tena, matokeo ni matatu.

(1) Viongozi walio na msisimko na waliotosheka walioko

duniani.

(2) Waamini “wa kiroho” wanaozidi kuongezeka (ambao

Kristo ni wa muhimu kwao, wanamheshimu Mungu,

wamejazwa Roho na ni watakatifu wanaogusa dunia).

(3) Dunia kuzidi kushuhudiwa.

Mikakati kwa ajili ya kufanyia kazi mfano huu wa pili imo

katika Amri na Mfano wa Yesu, na Amri na Mfano wa Waefeso sura

ya 4. Lakini, lazima tuwe waangalifu sana. Mwisho wa siku,

makusudi ya Mungu yanategemea kutimizwa kwa makusudi Yake ya

sasa. Je, wewe binafsi unafundishwa kwa utendaji wa karibu kabisa

wa kazi za kuifikia dunia? Je, wewe unawajenga wengine – kwa

karibu, kwa kuwapa kazi za kuifikia dunia?219

Page 228: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 9Maneno Yake Ya Mwisho, Wosia Wake

“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Waefeso 4:7-14

George Orwell, mwandishi maarufu wa kitabu kiitwacho

1984 na Animal Farm, aliwahi kuandika hivi: “Sasa tumezama

kufikia kiwango ambacho wajibu wa kwanza wa watu wenye akili

timamu ni kurudiwa kusemwa mambo ambayo ni ya kawaida.”

Katika kanisa la siku hizi, kilicho kawaida ni kitu chenye kuleta

mapinduzi na mabadiliko sana. Hakuna kitu kinachopuuzwa sana

kama lile agizo “dhahiri” au la kawaida la Yesu. Tunapotaja kitu

hicho kwa mara nyingine na kufanyia kazi, kanisa linatikiswa hadi

misingi yake.

Agizo la Yesu lilitajwa katika kila Injili nne na katika Kitabu

cha Matendo ya Mitume. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni

maendelezo ya habari zinazosimuliwa katika Injili. Kitabu chenyewe

kimeandikwa kwa mtiririko mzuri na kinafuata utaratibu wa

kijiografia ambao unaonekana kwa urahisi sana, utaratibu

220

Page 229: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

unaopatikana katika Matendo 1:8: “Yerusalemu … Uyahudi …

Samaria … mwisho wa nchi.” Kitabu cha Matendo kinaweza

kugawanywa katika sehemu tatu kubwa (sura ya 1 hadi 7; ya 8 hadi

12; ya 13 hadi 28), huku sehemu ya kwanza ikionyesha jinsi kanisa

la kwanza lilivyoendeleza huko Yerusalemu ile kazi ambayo Yesu

aliianzisha (ktk Matendo 1:1). Sehemu ya pili inahusiana na

maendeleo ya Injili katika Uyahudi na Samaria, na sehemu ya

mwisho inahusu kuendelezwa kwa Injili hadi “mwisho wa nchi”.

Mstari wa nane katika Matendo moja unayo maneno ya

mwisho ambayo Yesu Kristo aliyazungumza kwa wanafunzi Wake,

muda mfupi tu kabla hajapaa kwenda mbinguni. Injili ya Luka na ya

Yohana inadhihirisha kwamba mara ya kwanza Yesu alipokutana na

wanafunzi Wake baada ya kufufuka, aliwaagiza kuwa mashahidi

katika mataifa yote. Alirudia agizo hilo mara moja tena jioni hiyo

hiyo. Akalirudia tena baadaye pale mlimani Galilaya, kama

ilivyoandikwa katika Mathayo 28. Na sasa, yuko nje ya mji wa

Yerusalemu, siku arobaini baadaye, muda mfupi tu kabla ya kupaa

Kwake. Hivyo basi, agizo hilo linapaswa kuwa dhahiri kabisa kwetu

sisi. Lakini, swali moja litafunua kwamba hatujajali sana agizo hilo.

Je, unaigusa dunia nzima kwa kiasi gani katika mambo unayofanya,

unayofikiri, unayosema, au unayotayarisha? Ni hivi: Yesu alishikwa

sana na jambo la kuhusisha dunia nzima, lakini mtulivu sana kuhusu

mbinu au njia. Sisi tumefanya kinyume! Tunakwenda kongamano

221

Page 230: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

baada ya kongamano kujifunza kuhusu mbinu, lakini tunaepuka kule

kuhusika kwenyewe, ambako ndiyo muhimu.

Amri ya Yesu ilidai matendo. Agizo Kuu halikutolewa ili

watu wajifunze tu. Ni mpango wa utendaji. Katika somo hili,

tutalitazama tena, tukitumia Matendo 1:8 kama msingi wetu. Lakini

swali kubwa ni hili: Je, utakuwa tayari kupatikana katika kila hatua

kwa ajili ya kutimizwa kwa Agizo Kuu?

MKAKATI KWA AJILI YA KUENDELEZA INJILI

Kwanza, tunaona katika tamko hili Mkakati kwa ajili ya Injili

kuendelea kuenea. Mkakati upo katika neno “shahidi”. Hili ni neno

muungano lenye mambo mengi ndani yake. Neno la asili kwa

Kiyunani ni “martutia”, ambalo bila shaka si neno kimya. Neno hilo

limezaa neno la Kiingereza “martyr” yaani, “shahidi mfia imani”.

Kumbe basi, mtindo wa maisha unaotokana na neno hili ni kuishi

maisha yenye kujihatarisha katika utendaji. Kuwa “shahidi mfia dini”

ni mradi wa kuishi au kufa.

Dada mmoja aitwaye Virginia Owens aliandika hivi: “Kuwa

Mkristo ni nafasi ya ajabu sana – si ya salama. Mtu hamfuati Kristo

akiwa anatembea katikati ya barabara iendayo kwenye kuheshimika.”

Mwanatheolojia mmoja, aliyekuwa ameanza kuelewa “nafasi ya

kupita kiasi” ya Ukristo aliandika hivi: “Hebu tukusanye Agano

Jipya zote zilizopo, tuzipeleke kwenye kiwanja mahali au juu ya

mlima, halafu, wote tukiwa tumepiga magoti, mmoja wetu aseme na 222

Page 231: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mungu hivi: ‘Kichukue Kitabu hiki tena. Sisi binadamu, kama

tulivyo sasa, hatufai kushughulika na kitu kama hiki.

Kinatuhuzunisha tu.’ Wazo langu ni kwamba, sawa na wakazi wa

Gerasi, tumwombe Kristo ‘aondoke kwetu’.” Hao waandishi wawili

wameanza kuelewa dai la Yesu kwamba tuwe “mashahidi wafia

imani”.

Neno hilo “martus” linatokea zaidi ya mara 30 katika Kitabu

cha Matendo, na ni miongoni mwa maneno makuu kitabuni.

Hutujulisha kwamba tunapaswa kusahau mawazo yoyote ya mtindo

wa maisha unaotilia maanani “usalama kwanza”. Tazama mifano

ifuatayo.

Mkulima alikwenda kuwinda na mbwa wake porini, maili

nyingi mbali na nyumbani. Akagundua kwamba amesahau kopo la

kumlishia mbwa wake chakula. Aliweka bunduki yake chini na

kumwambia mbwa wake akae hapo mpaka arudi. Alipokuwa

amekwenda, moto wa pori ukatokea, na yule mbwa akafa. Baadaye,

mkulima yule aliukuta mwili wa mbwa wake – ulioungua kabisa –

kando ya bunduki yake. Kwa huzuni sana alisema, “Siku zote ilibidi

niwe mwangalifu katika ninachomwambia mbwa wangu afanye, kwa

sababu angefanya hivyo hivyo.” NDUGU WAKRISTO, Yesu Kristo

anataka na sisi tujali sana kuhusu kufanya anachosema mpaka

tusahau kuhusu moto wa porini unaowaka.

223

Page 232: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Profesa mmoja wa sayansi ya viumbe alitaja kanuni moja ya

sayansi siku moja darasani. Alisema hivi: “Kujihami ndiyo sheria ya

kwanza katika nguvu za asili.” Mwanafunzi mmoja Mkristo

akamwambia baada ya darasa akiwa anatabasamu, “Inashangaza

sana kuona tofauti kati ya nguvu za asili na neema. Sheria ya kwanza

ya nguvu za asili ni kujihami, lakini katika neema, sheria ya kwanza

ni kujitoa.” SAWA KABISA!

Jionee hali ya kujitoa mwenyewe ya Kalvari iliyo kiini cha

neema ya Mungu, halafu ukumbuke kwamba kanuni ya kwanza ya

uanafunzi wa Kikristo inapatikana katika maneno haya ya Yesu:

“Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike

msalaba wake, kisha aje anifuate.” Kujikana mimi mwenyewe maana

yake ni kujiambia yale maneno aliyosema Petro kwa habari ya Yesu

wakati alipomkana: “Sijawahi kumsikia kabisa mtu huyo. Simjui mtu

huyo mimi!”

Ndugu mmoja aitwaye Bruce Morgan aliandika hivi: “Tatizo

la Wakristo ni kwamba hakuna mtu anayetaka kuwaua tena.” Dada

Eugenia Price alikariri wazo hilo aliposema hivi: “Dhambi kubwa

ya kanisa ni kwamba LIMEMFUGA Yesu Kristo na kumfanya

mpole.”

224

Page 233: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Aina ya ushahidi ambao unatajwa katika Matendo 1:8 ni wa

asili dhahiri kabisa kiasi kwamba unatuingiza katika matatizo kila

wakati (lakini pia unaleta furaha ya daima ndani yetu, na huambatana

na miujiza ya daima pia).

Mkutano wa mamia ya viongozi wa kidini kutoka Marekani

yote ulifanyika, na ajenda kuu ilikuwa hii: “Tunawezaje kutumiwa ili

kulirejeza taifa hili kwa Mungu?” Kila mhudhuriaji alipewa nafasi

jioni moja kutoa jibu lake kwa kifupi. Kiongozi mmoja – Mmarekani

Mweusi – aliinuka na kusema hivi: “Wapendwa. Wakristo wa

Marekani hawatapata tena uwezo wa kuigusa jamii hii mpaka

wapoteze hofu yao ya kifo.” Akakaa chini. Watu wengi

waliohudhuria mkutano huo walisikika wakisema kwamba pengine

jibu bora kuliko yote katika mkutano huo lilikuwa la huyo ndugu.

Miaka mingi iliyopita, mhubiri maarufu mishenari aliyeitwa

Robert Wilder alitembelea Chuo kidogo kiitwacho Hope huko Jimbo

la Michigan ili kuhubiri katika ibada ya wanafunzi kuhusu utume wa

dunia nzima. Akaweka ramani kubwa sana ya India mbele ya kanisa,

na akaweka kimulimuli mbele ya hiyo ramani. Katika mahubiri yake

alitamka kwamba kila mara kimulimuli kilipowaka, mtu mmoja wa

India alikuwa anakufa pasipo kusikia habari za Kristo. Siku hiyo,

Kristo na maono Yake ya dunia nzima aligusa moyo wa mwanafunzi

mmoja aliyekuwa karibu kumaliza hapo chuoni aliyeitwa Samuel 225

Page 234: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Zwemer. Maono hayo yalipowaka moyoni mwake, alimwomba

Mungu amweke mahali pagumu kabisa duniani.

Muda si muda, alianzisha makazi katika Kisiwa cha Bahrain

huko Ghuba ya Uajemi, katikati kabisa ya jamii ya dunia ya

Kiislamu. Kisiwa hiki ni maarufu. Zwemer akaanza kuchapisha na

kugawa vipeperushi vya Injili, japo hakuwa amepata kibali cha

serikali ya Kiislamu ya mahali pale. Katika kipindi cha juma moja,

binti wawili wa Zwemer – mmoja wa miaka minne na mwingine wa

miaka saba – walikufa kwa sababu ya magonjwa na joto kali la

mahali pale. Samuel Zwemer akaomba wakuu wa Bahrain ruhusa ya

kuzika miili ya binti zake, lakini alinyimwa kibali kwa madai kwamba

walikuwa Wakristo, na miili yao ingenajisi ardhi ya pale. Zwemer

akakata rufani na akapata ruhusa – kwa sharti kwamba yeye

mwenyewe achimbe makaburi. Alifanya hivyo, na baada ya maziko,

aliweka jiwe la kumbukumbu lililosema, “Amestahili Mwanakondoo

aliyechinjwa, kupokea utajiri.” Huo ndiyo mtindo wa kishujaa wa

kutoa kila kitu hadi kufa, ambao Yesu alitaka watu waishi.

Shirika moja la zamani kidogo lililohusika na kutuma

wamishenari lilituma wamishenari sabini kwenda nchi ya Kamerun,

ambayo ni “kiungo” muhimu kati ya Afrika magharibi na Afrika

kusini na kusini kati. [Waislamu kwa sasa wanajitahidi sana kujaribu

kuipata Kamerun.] Katika hao sabini, sitini na nane walifia huko.

Wastani wa uhai wao baada ya kufika huko ilikuwa miaka miwili na 226

Page 235: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

nusu! Inasemekana wengi wao walisafiri pamoja na majeneza yao,

wakijua kwamba uwezekano wa kurudi ulikuwa mdogo! Yesu alitaka

mtindo huo wa maisha wa kishujaa, wa kutoa kila kitu hadi kufa!

Familia moja ya kimishenari ilikwenda Uchina kuhubiri Injili

huko, chini ya “shirika la utume wa imani”. Walikwenda kama

waalimu wa shule za kawaida. Waliporudi, walirudi kama

wamishenari wa kawaida likizoni – wakiwa na boksi lenye picha na

vitu mbalimbali vya kuonyesha. Walipomaliza kuonyesha maonyesho

yao na kutoa maelezo yao, kipindi cha maswali na majibu

kikatolewa. Mshirika mmoja wa kanisa alisimama na kuuliza hivi:

“Mlipokuwa huko hamkuogopa kwamba mnaweza kufia huko?” Jibu

la baba wa familia ile ya wamishenari lilitoka, hivi: “Hapana,

maana KABLA HATUJAENDA TULIKWISHA KUFA.” Hii ndiyo

maana ya neno “martus” au “shahidi mfia imani”.

Mchungaji Charles Crowe wa KiMethodisti alikuwa

anaendesha gari lake mjini Chicago, kwenye mzunguko wa

barabara, kama alivyokuwa anafanya mara nyingi tu. Jengo la

kanisa lake lilikuwa maarufu sana hapo mjini kuwa ndiyo lenye

kilele kirefu katika makanisa yote ya Marekani Kaskazini. Juu yake

ulikuwepo msalaba mkubwa sana. Siku hii asubuhi, wakati

Mchungaji Crowe anapita mbele ya jengo hilo, aliona kundi kubwa

tu la watu wamesimama kando ya barabara mbele ya jengo, na wote 227

Page 236: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

walikuwa wanatazama juu. Akainama kwa makini katika gari lake na

kutazama juu aone walikuwa wanatazama nini. Akaingia kwenye

eneo la kuegesha magari, akaharakisha kuweka gari lake katika

sehemu yake ya kuweka gari, kisha akaharakisha kwenda mbele ya

kanisa na kujiunga na waliokuwa wanatazama juu.

Juu ya msalaba palikuwa na mpaka rangi mwenye ndoo ya

rangi. Alikuwa amefungiwa msalabani, na kwa utaratibu alikuwa

anapaka rangi ule msalaba, akielekea chini. Msalaba wenyewe

ulikuwa unayumba kwa utaratibu kila alipopaka rangi. Watu

walikuwa wanatazama kazi yake hatari. Baada ya muda, Charles

Crowe aliondoka kwenye lile kundi la watu na akaanza kuelekea

ofisini kwake hapo kanisani. Mara Roho Mtakatifu akamwambia,

“Mwanangu! Umepita hapo mara nyingi, na hapajawahi kuwepo

mtu yeyote njiani akitazama juu kwenye ule msalaba. Nini

kilichofanya tofauti leo? Ni hiki: LEO, MSALABA ULIKUWA NA

MTU JUU YAKE! Siku zote, dunia itasimama kuona wakati mtu

mkweli atakapokuwa msalabani.”

Leo hii kanisa linaambiwa na dunia maneno yale ambayo

Tomaso alisema kuhusu Yesu katika mashaka yake na kutokujua:

“Nisipoona alama za misumari mikononi Mwake, na kutia kidole

changu katika alama hizo … sitaamini.” Wanatafuta kujitoa bila

maonyesho kwa Mkristo ambaye Kristo ndiye kiini cha maisha yake,

la sivyo, hawataamini.228

Page 237: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Pengine ni vizuri tutulie kidogo hapa na kujikumbusha

kuhusu mbadala pekee wa mtindo huu wa maisha ya Kikristo. Yesu

alisema hivi: “Yeyote atakayeokoa (linda, tetea, hifadhi) maisha yake

atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu

atayapata.” Sehemu ya kwanza inafafanua ule mtindo wa maisha

wenye kufikiri usalama kwanza, mimi ndiyo wa muhimu, nijiokoe

mwenyewe kwa gharama yoyote ile. Sehemu ya pili inafafanua ule

mtindo mwingine wa maisha – wa kuwekeza, wa kutojijali, wenye

kujali wengine, wa kuwajenga wengine, uliojawa na Kristo – ambao

ndiyo mtindo wa maisha wa Mkristo.

Wasafiri wawili walinaswa na tufani ya barafu walipokuwa

wanasafiri sehemu ya kaskazini. Walipokuwa wanakabiliana na hiyo

dhoruba, walimkuta mtu amegandia kwenye barafu, wakadhani

amekufa. Mmoja akasema, “Nina matatizo ya kutosha kujisaidia

mwenyewe. Nasonga mbele.” Yule mwingine akasema, “Siwezi

kumpita binadamu mwenzangu katika hali hii wakati bado ana pumzi

hata kidogo tu ya uhai.” Akainama na kuanza kumpa joto yule mtu

kwa kumsugua kwa bidii sana. Hatimaye yule mtu akafungua macho

yake, akarejelea uhai wake, akapata nguvu na kutembea pamoja na

yule mtu aliyemsaidia. Walipoendelea na safari, walikuta nini?

Walimkuta yule mtu aliyeamua kujishughulikia mwenyewe na

kujitafutia usalama wake akiwa amekufa kwa baridi katika barafu.

229

Page 238: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Yule Msamaria Mwema alihifadhi maisha yake mwenyewe

kwa juhudi zilizohitajika kumwokoa yule mtu mwingine. Msuguano

ule ulisisimua damu yake na kumfanya hai. Sheria haibadiliki wala

haishindwi: “Yeyote (Mkristo au kanisa) atakayeokoa maisha yake

atayapoteza; na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu

atayapata.”

Mwandishi maarufu aitwaye C.S. Lewis alifanikiwa kunasa

uzuri na msisimko wa maisha ya Mkristo katika kitabu chake cha

“Chronicles of Narnia” kwa kumfanya mtu mmoja katika sehemu

iitwayo The Last Battle (Vita ya Mwisho) aseme hivi: “Afadhali nife

nikiwa napigania taifa la Narnia kuliko kuzeeka na kuwa mjinga

nyumbani, na pengine nishindwe kutembea mpaka nitumie kiti na

mwishowe nije kufa tu.” Rafiki zangu. Tutakufa kwa namna moja au

nyingine. Kujitoa kwa Kikristo ni kwamba, “Kristo atukuzwe katika

mwili wangu, katika uhai wangu au kwa kifo changu.”

Kwa maneno mengine, Yesu anasema hivi: “Ee mwamini!

Wewe ndiye ushahidi wangu, vitambulisho vyangu, hoja zangu,

wasifu wangu, mwenezaji wangu, matangazo yangu.” Na Msalaba

ndiyo kiini cha uwakilishi wowote wa Kristo. Mtu mmoja aitwaye

George Bernard Shaw aliuliza hivi: “Je, ni lazima Kristo asulubiwe

katika kila kizazi kwa kuwa tu dunia haina ubunifu?” Jibu kwa swali

lako, mheshimiwa, ni, “Ndiyo” nasi tunapaswa kuwa wale

230

Page 239: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wanakondoo wasiojijali wenyewe. “Ninyi ndiyo mashahidi wangu

wafia imani.” Huo ndiyo mkakati wa Injili kusonga mbele.

CHANZO CHA USHUHUDA WA INJILI

Pili, tunaiona asili au chanzo cha ushuhuda wa Injili. Asili

yake inaonekana katika matukio matatu ya neno “nanyi”. “[Nanyi]

Mtapokea nguvu baada ya Roho Mtakatifu kuwashukia [ninyi], nanyi

mtakuwa mashahidi wangu.” Maneno “nanyi” na “juu yenu” yako

katika wingi. Agizo limetolewa kwa Mwili wote wa Kristo na

linatimizwa na kila kiungo cha huo Mwili. Wewe Mkristo mpendwa,

unahusika kabisa – kikamilifu kabisa – katika mkakati wa Yesu.

Wewe ni asili au chanzo cha ushuhuda wa Injili.

Ona kwamba neno “nanyi” linazidi kutajwa kwa Roho

Mtakatifu mara tatu katika mstari huu. Hii si kwamba inapunguza

nafasi na jukumu Lake; bali huongeza wajibu wako. Hao “nanyi” ni

akina nani? Si malaika, si watu wasiokuwa wa kawaida, si watu

maalum. Andiko linadhihirisha “nanyi” hao katika mistari

inayofuata. Matendo 1:2 inawataja kabisa kwamba, ni wale “mitume

ambao Yesu alikuwa amewachagua”.

Ni hivi wapendwa: Mitume wote walikuwa wanaume. Hii

haipunguzi nafasi ya wanawake, inaongeza tu jukumu la wanaume.

Roho Mtakatifu bila shaka alitazamia matatizo ya historia ya Kikristo

– kwamba ingekuwa rahisi kabisa kwa wanaume kukimbia wajibu

wao na kuwaachia wanawake. Kwa hiyo , siku hizi katika makanisa 231

Page 240: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

yetu tuna vikundi vya umisheni vya wanawake. Mungu ashukuriwe

kwa ajili ya wanawake wanaojali na wanaomcha Mungu, lakini hili

ni jukumu la wanaume kimsingi! Ni hivi: Ukifanikiwa kumpata

mwanamume, kiongozi aliyewekwa na Mungu katika idara ya msingi

katika jamii, unakuwa na nafasi bora sana ya kumpata kila mtu

mwingine katika eneo lake la utawala. Lakini ukimpata mmoja wa

watu wake kwanza (mke, watoto) unaweza kushindwa kumpata huyo

kiongozi au wengine katika eneo lake.

Zamani kidogo Ijumaa Kuu moja usiku, jengo la kanisa

liitwalo People’s Church huko mjini St. Paul jimbo la Minnesota,

Marekani, lilishika moto. Ilikuwa baada ya usiku wa manane na

idara ya zimamoto ilizuiliwa na barafu katika juhudi zake za kuuzima

moto. Walipokuja kufanikiwa, jengo likawa limeungulia chini.

Asubuhi iliyofuata, washirika wa kanisa hilo na wanamji ule

walianza kukusanyika pembeni mwa lile jengo lililokuwa bado

linafuka moshi. Jengo lenyewe lilikuwa aina fulani ya makumbusho

ya picha za kidini pamoja na jengo la kanisa, hivyo lilikuwa maarufu

sana kwa utalii.

Nyuma kabisa ya madhabahu ilikuwepo picha ya kuigiza ya

“Kristo Anayesihi” – sanamu kubwa ya marumaru iliyokuwa na

urefu wa futi nane, iliyoandaliwa na mchoraji maarufu Mdenish

aliyeitwa Thorsvalden. [ZIADA: Mishenari maarufu wa India

aitwaye Stanley Jones alikuwa anatembelea mji wa Copenhagen, 232

Page 241: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Denmark miaka mingi kabla. Mwongoza watalii akawa amewapeleka

kwenye Kanisa moja la Kikatoliki huko Copenhagen, mahali ambapo

sanamu ya hiyo picha tunayosema, ilikuwepo. Sanamu yenyewe

inamwonyesha Yesu akiwa amesimama, uso umetazama chini,

mikono imefunguliwa kwa dunia. Imetokana na Mathayo 11:28,

kwamba, “Njooni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na wenye

kulemewa na mizigo mizito, nami nitawapa pumziko.”

Sasa, walipokuwa wanaondoka hapo, yule mwongoza watalii

aliuliza, “Je, kuna yeyote aliyefanikiwa kuuona uso wa Bwana Yesu”

Jones akajibu, “Tungewezaje kuuona? Umeinamia chini.” Yule

mwongoza watalii akajibu kwa sauti ya chini ya unyenyekevu,

“Ndiyo hivyo Mzee. Ukitaka kuuona uso wa Bwana, lazima kwanza

upige magoti miguuni Pake!” MWISHO WA ZIADA]

Sasa, lile jengo la kanisa lilipoungua, ile sanamu ilianguka

na sakafu na kutumbukia shimoni katika vyumba vya chini ya ardhi.

Siku ya pili yake, masaa ya asubuhi, baadhi ya watu wa kanisa

walipata ruhusa ya kushuka na kuingia katika magofu ya kanisa ili

kuona kama kuna vitu vya thamani vilivyopona moto. Wakaikuta ile

sanamu, imepata alama za moto na majivu na moshi kidogo, lakini

haikuwa imeharibika isipokuwa kipande kikubwa kilichobomoka

kutoka sehemu ya sanamu kusimamia. Wakaiacha ipoe, halafu

mchana ule wakaibeba taratibu kutoka huko chini na kuiweka

pembeni ya barabara. Wakapanga watu sita kusimama kuilinda ili

wapitaji na watazamaji wasiiharibu, halafu wakarudi tena chini 233

Page 242: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kutafuta vitu vingine.Waliporudi tena baada ya muda, kundi la watu

lililokuwepo halikuwa linatazama tena lile jengo lililoharibiwa.

Badala yake, walikuwa wanatafuta nafasi katika huo mviringo, wote

wakiwa wanajaribu kuitazama hiyo sanamu maarufu.

Hebu niufanye huo mfano kuwa wa kiroho, ili kutilia mkazo

jambo moja. Ni hivi: Yesu alikuwa katika hilo kanisa kwa muda

mrefu tu, lakini alikuwa “amefungiwa minyororo madhabahuni,” na

watu wa mtaani walikuwa hawajapata kumwona. Ni wakati tu kanisa

liliposhika moto na kuungua (!) na baadhi ya watu wa kanisani (!)

kumchukua na kumweka pembeni ya barabara (!) ndipo “watu wa

nje” walipoweza kumwona kwa mara ya kwanza kabisa! Wewe,

mwamini wa Kikristo, ndiye asili au chanzo cha ushuhuda wa Injili.

MADA YA USHUHUDA WA INJILI

Halafu, mstari wetu unatuonyesha mada ya ushuhuda wa

Injili. Yesu alisema hivi, “Ninyi mtakuwa mashahidi WANGU.”

Ushahidi wetu haupaswi kuelekea kwenye kanisa, au dhehebu, au

itikadi, au fundisho, au ukiri fulani, au taratibu fulani. Unapaswa

kumwelekea Kristo. Ni fursa yetu nzuri tu kumweleza Yeye kama

alivyojieleza Mwenyewe katika Neno Lake, kwamba ni Mwokozi

mwenye Kukomboa (ktk Matendo 1:3), kwamba ni Bwana Mfufuka

(1:3 tena), na kwamba ni Mfalme Anayerudi (ktk 1:11). Mada hiyo

haina mwisho! Tena, ni kweli kuu yenye kuvuta usikivu kabisa.234

Page 243: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Picha kwenye ukuta wa jumba la maonyesho ya sanaa huko

Ujerumani ni mfano mzuri wa sehemu hii ya kazi yetu. Picha hiyo

inamwonyesha Martin Luther, Mjerumani maarufu aliyeleta

Matengenezo ya Kanisa, akiwa anahubiri katika mimbari ya kanisa

la Kijerumani. Mkononi mwake ameshika Biblia, na kwa mkono

mwingine amenyoosha kidole, na mdomo wake uko wazi kana

kwamba anatangaza kitu. Anaihubiri Injili. Unaweza kumwona

mhubiri na wasikilizaji wake katika picha hiyo. Lakini ukitazama

kwa makini sana, utaona kitu cha kushangaza. Hakuna msikilizaji

wake hata mmoja anayemtazama mhubiri ambaye ni Martin Luther!

Ukifuata mahali wanapotazama, unaona kitu cha kufurahisha sana.

Pembeni mwa lile jengo, kuna umbo dhahiri japo liko mbali la Yesu

Mwana wa Mungu – na kila jicho hapo linamtazama Yeye.

Wanamsikiliza Luther, lakini wanamtazama Yesu!

Hayo ndiyo matokeo tunayotaka ya kumshuhudia Kristo

kwetu. Tunamtangaza Yeye, Naye anajitambulisha mwenyewe

kupitia ushuhuda wetu. Basi, usikivu wa kila “msikilizaji” hatimaye

unamwelekea Yeye.

UPANA WA USHUHUDA WA INJILI

Mstari huo pia unadhihirisha upana wa ushuhuda wa Injili.

Ona kwa makini sana maneno yake ya kumalizia – “Nanyi mtakuwa

mashahidi Wangu katika Yerusalemu NA Uyahudi wote, NA 235

Page 244: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Samaria, NA mpaka sehemu za mwisho za dunia.” Sasa tuchambue

kidogo.

Watu wa karibu ni kazi yetu – “Yerusalemu”;

Watu jirani ni kazi yetu – “Uyahudi”;

Watu waliopuuzwa ni kazi yetu – “Samaria”;

(Samaria ni mfano wa watu unaowachukia kabisa, unaowabagua); na

Watu wanaofuata ni kazi yetu – “mpaka mwisho wa nchi”.

“Yerusalemu” huwakilisha hali yako ya karibu. “Uyahudi na

Samaria” huwakilisha hali yako ya jirani, na “mwisho wa nchi”

huwakilisha maeneo ya kimataifa yanayokuzunguka. “Yerusalemu”

huwakilisha ushuhuda wa mjini kwetu, “Uyahudi na Samaria”

huwakilisha ushuhuda wa nchi yetu, na “mpaka mwisho wa nchi”

huwakilisha ushuhuda wa dunia yetu.

Halafu, ona kwa makini sana kwamba si swala la “aidha au”

kuhusu watu hawa. Ni swala la “pamoja na”. Yesu Kristo

anatutazamia tuishughulikie dunia nzima – kweli kabisa, na kwa

dhati kabisa! Kwa njia gani? Kwa kujifunza na kufuata ule mkakati

wa kufanya watu kuwa wanafunzi ambao kwao tunaona makundi ya

watu kwa njia ya mtu mmoja, na kumjenga huyo mtu awaguse hao

wengi – ambao ndiyo mkakati aliotumia Yesu na wale Kumi na

Mbili aliokuwa nao.

Kitabu cha Matendo ya Mitume ni kimoja katika vitabu

vichache sana vya Biblia vyenye kujipanga vizuri. Sura ya kwanza

hadi ya saba huonyesha ushahidi wa wanafunzi wa kwanza huko 236

Page 245: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Yerusalemu. Sura ya nane hadi kumi na mbili katika Uyahudi na

Samaria, na halafu sura ya 13 hadi 28, “mpaka mwisho wa nchi”.

Kipimo cha kweli cha nguvu na uwezo wa Mwili wa Kristo

katika mahali pamoja ni hiki: Je, ushawishi wake unafika mbali kiasi

gani? Mungu kwa hakika kabisa analitazamia kanisa la mahali

kushugulikia dunia nzima! Maana, Yesu aliweza kufanya hivyo na

watu kumi na mbili, na alifanikiwa kabla ya kuwepo kwa siku,

televisheni, na teknolojia aina zote. Yeye alikuwa na waeleza watu

tu! Lakini, aligusa dunia nzima ya siku Zake kupitia kundi Lake hilo

dogo, la watu wa hivi hivi.

Siku hizi tunafikiri kwamba lazima tuwapate watu wa jamii

zetu nyumbani kabla ya kuanza kushughulika na wale tulioagizwa

kuwafikia duniani. Lakini, mpango huo ni kinyume. “Nuru ing’aayo

mbali zaidi inang’aa kwa nguvu sana karibu na nyumbani.” Kila

kanisa linapaswa kuwa na mpango daima jinsi linavyoweza kufikisha

Injili katika sehemu nyingi duniani kwa haraka kiasi iwezekanavyo,

na lengo lake linapaswa kuwa kuwajenga wanafunzi ambao wana

maono ya dunia, watakaoigusa dunia nzima hadi mwisho wake, hadi

ukamilifu wa dahari. Mungu alisema hivi: “Niombeni, nami nitawapa

ninyi mataifa kuwa urithi wenu, na sehemu za mbali za nchi kuwa

mali yenu” (ktk Zaburi 2:8, TLR). Sasa, kwa nini hatujapata watu wa

mataifa kuwa urithi wetu, na sehemu za mwisho za dunia kuwa mali

yetu? Sababu pekee pengine ni kwamba, hatuombi! Ni dhahiri kabisa

kwamba kanisa kwa ujumla halina kwenye moyo wake kile kilicho 237

Page 246: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

moyoni mwa Mungu. Vipi kuhusu kanisa lenu? Kuhusu kanisa lako?

Vipi wewe mwenyewe?

Ona pia kwamba, mstari wenyewe unasema, “katika

Yerusalemu na Uyahudi yote, na Samaria, mpaka mwisho wa nchi”.

Si swala la “aidha au” bali ni “pamoja na”. Tunapaswa kuwa

tunashuhudia mahali pote hapo kwa wakati mmoja, na pote

tunapaswa kupahifadhi na kupabeba moyoni. Kivipi? Kwa kujenga

maono kwa ajili ya dunia nzima, halafu kwa kuwajenga watu wa

kutekeleza maono hayo. Upana wa eneo letu la kazi ni dunia nzima.

SIRI YA USHUHUDA WA INJILI

Hatimaye, maneno ya Yesu yanadhihirisha siri ya ushuhuda

wa Injili. Alisema, “Mtapokea nguvu, baada ya Roho Mtakatifu

kuwajilia juu yenu.” Njia nzuri ya kumfikiria Roho Mtakatifu ni

kwamba, Yeye ni Yesu pasipo mwili. Roho Mtakatifu ni mbadala wa

Kristo hapa duniani, akifanya aliyokuwa anafanya, na kuendeleza

kazi Yake.

Mvulana mmoja alimwuliza mama yake, “Mama! Mungu

analetaje mvua?” Baadaye akawa kama amekumbuka, na kujibu

swali lake mwenyewe. “Usijali, ninajua tayari. Yeye anamwambia

Roho Mtakatifu afanye hivyo. Roho Mtakatifu ndiye anayefanya kazi

yote!” Roho Mtakatifu ndiye Nafsi Mtendaji katika Uungu. Siku hizi,

Yeye ndiye hufanya kazi yote!

238

Page 247: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Halafu fikiria kuhusu neno “nguvu”. Neno la Kiyunani

linalotumiwa hapa ni “dunamis”, ambalo limezaa neno la Kiingereza

“dynamite” au baruti. Lakini, kiunganisho hicho kinaleta tatizo la

msingi kwetu. Kwa kawaida baruti ni kitu chenye mlipuko mkubwa.

Basi, tuna kawaida ya kutazamia nguvu za Mungu kulipuka kwa hali

ya juu sana kama kiwakilishi cha ahadi ya Yesu. Tatizo ni la aina

mbili: kwanza, hakuna hali ya kulipuka katika Injili; na pili,

Wayunani walikuwa hawana baruti. Baruti iligunduliwa na Alfred

Nobel mwaka wa 1866, ambaye ndiye mwanzilishi wa Tuzo za

Nobel. Basi, kulitafsiri neno hilo kwa msingi wa neno letu la

Kiingereza la baruti kunaweza kutupotosha kidogo, kuwafanya

Wakristo watazamie “mlipuko” badala ya kumruhusu Roho

Mtakatifu kutengeneza na kuzaa ubora na tabia ya utulivu na utendaji

iliyokuwepo katika maisha na huduma ya Yesu.

Nguvu ya Matendo 1:8 ni

Nguvu ya kubadilisha tabia,

Nguvu ya kuangaza,

Nguvu kwa ajili ya mawasiliano,

Nguvu kwa ajili ya utendaji wa dhati, endelevu.

Ni nguvu ya kushuhudia, pamoja na kuwa nguvu katika

kushuhudia. Kuna mtu anayefafanua nguvu ya tabia kuwa ni

“onyesho lenye nguvu la haiba ya mtu” na hiyo ndiyo tafsiri nzuri ya

nguvu za Mungu. Ni onyesho lenye nguvu la haiba ya Mungu – jinsi 239

Page 248: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Mungu alivyo. Linaweza kuwa kitu mlipuko, lakini mara nyingi

huonekana kama ushawishi ulioko ndani kabisa katika tabia ya mtu,

na kusadiki kunakomgusa yeye na wengine wanaomzunguka. Kazi

ambazo Yesu aliahidi kwamba zingefanywa na Roho Mtakatifu ---

Kusadikisha (ktk Yohana 16:7-11);

Kuangaza (ktk Yohana 16:13-16),

Mawasiliano (ktk Yohana 15:26), na

Kuifikia au kuigusa dunia (ktk Matendo 1:8)

-- zaidi sana katika eneo la ushawishi wenye nguvu kuliko

eneo la maonyesho au madhihirisho “mlipuko”.

Ona kwamba nguvu hii “inapokelewa”. “Mtapokea nguvu”.

Haipatikani kama malipo ya kazi, inapokelewa. Haifikiwi kwa juhudi

zozote, inapatikana. Haihitajiki kipawa kikubwa sana ili kupokea

chochote. Watu matajiri na maskini kabisa wanaweza kupokea kitu

chochote kitolewacho. Bila shaka mtu anakipokea tu. Mungu anataka

sana kukupa wewe nguvu ya Roho Mtakatifu – lakini kwa masharti

Yake na kwa ajili ya makusudi Yake tu. Yeye amekuagiza ujazwe na

Roho Mtakatifu, nafsi pekee ambayo ni nguvu za Mungu.

Tunasoma hivi katika 1Yohana 5:14 – “Huu ndiyo ujasiri

tulio nao katika Yeye, kwamba, tukiomba chochote kulingana na

mapenzi Yake, anatusikia.”

Kwa kuwa ametuagiza tujae Roho Mtakatifu, tuna uhakika

kwamba ni mapenzi Yake. Basi, tukae katika hali ya kutazamia

daima na kumwomba daima atujaze kwa Roho Wake, na tumpokee 240

Page 249: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

tu katika utimilifu Wake. Ndipo kwa ujasiri kabisa tutaweza kujua

kwamba Nafsi ya Roho Mtakatifu siku zote “anasafiri nasi” popote

tuendapo, mradi tu tunaishi kutimiza Agizo Kuu la Bwana wetu.

241

Page 250: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Sura Ya 10Mbweha Tally Ho!

Maana Ya Jina La Kitabu

Najisikia vizuri kupata nafasi ya kujibu swali hili, kwa sababu

kazi yote ya Yesu kwetu inapatikana katika jibu nitakalotoa. Hebu

kwanza nifafanue mfano uliozaa jina la hiki kitabu.

Mbwa wanapokuwa katika kundi, wanakimbia pamoja na

kufanya moja au mengi katika haya manne yafuatayo:

1. Watalala.

2. Watajihami kwa manufaa ya usalama wao.

3. Kama hawatishiwi, watakaribisha wanachama

wapya katika kundi lao.

4. Watapigana wao kwa wao.

Lakini, kuna kitu cha kutilia maanani, nacho ni hiki: HAYO YOTE

WATAFANYA MPAKA MBWEHA APITE!

Sasa – “kanisa” ni nini? Ingawa tafsiri nitakayotoa hapa ni

dhaifu, isiyopendeza na nyepesi sana, kanisa ni Wakristo katika

vikundi, wanaokimbia pamoja. Theolojia imejaribu kueleza kanisa

kwa njia ya hali ya juu zaidi kidogo inaposema kwamba “ni

kusanyiko au ushirika wa waamini waliozaliwa mara ya pili na

242

Page 251: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

walioitwa, walio katika Yesu Kristo, walioungana pamoja kwa ajili

ya malengo ya kiroho yanayofanana.” Tafsiri yangu mimi ni nyepesi

tu na rahisi kabisa na yenye kueleweka, lakini inaeleza hicho hicho.

Lakini, kosa kubwa la maana au tafsiri zote hizo si mfano bali ni

utendaji halisi. Makanisa mengi hayakimbii. Kweli “yanakimbizwa”

(utasikia watu wakisema, “analiendesha kanisa lake”, au, “hao ndiyo

wenye kuliendesha kanisa hili”. Au, “kanisa hili linaendeshwaje?”),

lakini hayakimbii! Yanaendeshwa kama mitambo inavyoendeshwa,

au kama biashara inavyoendeshwa, lakini yenyewe hayakimbii

kufukuzia lengo ambalo yamepewa.

Haya – turudi kwenye tafsiri yetu. Kanisa ni Wakristo katika

kikundi, wanaokimbia pamoja. Wakristo wanapokimbia pamoja

katika vikundi (na ndivyo ilivyo), watafanya moja au mengi katika

haya manne yafuatayo.

1. Watalala. Andiko linalofaa kabisa kusomewa makanisa

mengi kabisa ni hili: “Amkeni enyi mlalao, mfufuke kutoka kwa

wafu.” Miaka mingi iliyopita, mishenari aitwaye John Halsy

aliandika maneno haya, mazito kabisa:

Kama ningekuwa mwandishi mwenye kutamani kujulikana

kwa kuandika kitabu kifupi kuliko vyote, ningewaendea baadhi ya

washirika walio katika makanisa yetu maarufu ya mjini, yaliyotulia,

niwaombe kibali chao kuandika maelezo ya kile wanachomfanyia

Kristo na kufanya kwa ajili ya dunia. Historia hiyo ingekuwa fupi

kweli kweli! Pengine herufi moja au mbili tu zingetosha kueleza kila 243

Page 252: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

kitu kinachofanywa na wengi wao kwa ajili ya Bwana aliyewanunua,

na kwa ajili ya dunia inayoangamia! Kuna andiko ambalo linaweza

kuwapa starehe sana baadhi ya watu wanaoitwa Wakristo. Ni hili –

‘Sisi tulioamini tunaingia katika pumziko.’ Lakini kumbuka kwamba

hilo ni pumziko la mtenda kazi baada ya kazi, si pumziko la mvuvi

kutokana na kazi. Ila, nina andiko lingine la kuweka pamoja na hili –

‘Ole wao waliopumzika huko Sayuni!’ Ndiyo! Ole, kwa sababu hiyo

starehe ni mwizi anayeiba hali ya kujisikia hatia, ikiwaibia waamini

na makanisa nafasi yao ya kushiriki pamoja na Kristo katika

shughuli iletayo raha kuliko zote duniani.

Ufufuo au kupaza sauti kuamsha watu si vitu vibaya katika

kufafanua hitaji la Wakristo wengi na makanisa mengi. Ninasema

hivyo kwa aibu kubwa sana, kwa sababu mimi mwenyewe binafsi

nimelala katika sauti za baragumu nyingi sana kutoka mbinguni,

zilizotolewa ili kuniita niende mstari wa mbele kwenye makabiliano

na mapambano mapya. Lakini, ukweli unabaki pale pale kwamba

makanisa mengi yenye kukiri Jina la Kristo na kusema kwamba

yamejipanga na kuungana na Ukristo ule uliosababisha Kitabu cha

Matendo ya Mitume kuandikwa, yamekufa kama makaburi. Huku

yakiwa yamelewa sana na dawa ya ubinafsi, na kuzoea sana (na

kupenda sana pia) Ukristo usiokuwa na msalaba, na yenye shauku ya

kuufanya Ukristo kupendwa sana na kuwa maarufu, wao (na sisi pia)

huonekana kama hawana mwelekeo kabisa katika kumfuata Bwana

Mkubwa (au, kama ndugu Mkristo mmoja mpendwa alivyosema, 244

Page 253: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“kumfukuzia Kristo hasa hasa”) au kufuata “Kusudi lile Kuu (ambalo

ni kuifikia dunia nzima) au kutekeleza ule Mpango Mkuu (yaani,

“kufanya watu kuwa wanafunzi” kwa kiwango cha Kristo na kwa

kufuata mkakati Wake). Kwa hali hiyo, wanalala tu.

[MZAHA KIDOGO – lakini wenye lengo la kufikisha

ujumbe.]

Jamaa mmoja alisema hivi, “Kama watu wote wanaolala

kanisani wangepangwa mstari – wangejisikia vizuri zaidi!”

Mwingine ametafsiri mahubiri kuwa ni “mtu mmoja

akizungumza katika usingizi wa mwingine”.

Mama mmoja alimpigia simu mchungaji wake saa tisa usiku

akasema, “Mchungaji! Nina tatizo kubwa sana. Shida yangu ni

kwamba sipati usingizi, hivyo silali kabisa. Naomba unihubirie

kidogo!” (Yaani, akisikiliza mahubiri anapata usingizi.)

Uzuri ni kwamba hivyo ni vichekesho, ingawa “wakalia vitu

kanisani” mara kwa mara hufanya hayo kuwa kweli. Ila sasa,

tunapofikiri uhalisi wa kusikitisha sana wa Wakristo kuishi maisha

yao kwa kujitakia mema na kujihudumia au kujihami, na makanisa

nayo yakielezwa kwa uwazi kabisa na kwa uhalali kabisa kuwa ni

“majitu yaliyolala” (ingawa ukweli ni kwamba si hivyo, na

inasikitisha sana kwa sababu, watu wengi hata hawajui hilo jitu

linapaswa kufanya nini au linaweza kufanya nini au lingeweza

kufanya nini kama limeamka kabisa na kwa ukamilifu. Basi,

wanaelewa kwa udogo sana jinsi ambavyo kanisa limelala kweli), 245

Page 254: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mbona hayo yanakuwa kama hukumu badala ya kuwa vichekesho.

Kwamba kanisa ni “jitu lililolala” ni wazo la Shetani kabisa.

Sasa, tufikie sehemu ya pili ya kanuni zile tulizotaja.

2. Watahakikisha usalama wao wenyewe. Fikiri tofauti kubwa

iliyo kati ya kujihami na kuishi tu, na huduma ya kweli. Tofauti hiyo

mara nyingi haionekani kwa sababu kwa kawaida makanisa hujitia

katika mpango ambao ni mchanganyiko wenye kupooza, ambao

unatoka katika hayo mawili. Wana “ibada” na wanatoa “nafasi za

kuhudumu” lakini je, matokeo yanakaribia utendaji na matokeo

yaonekanayo katika Kitabu cha Matendo ya Mitume? Huduma ya

kweli ina kujitolea, kujihatarisha na hali ya kutokujua kilicho mbele,

na masharti yake yanapangwa na Yeye anayesimamia shughuli

yenyewe. Wakati mtu anapoingia katika huduma ya kanisa la siku

hizi, anainuliwa kwamba ni “Mkristo wa kipekee sana,” lakini

mambo kama hayo yanaonyesha tu ujinga na kujipenda kwa

mwamini “wa kawaida”. Labda tuulize swali hapa – je, Mkristo wa

kawaida ndiye mbaya katika wazuri, au ndiye mzuri katika wabaya?

Vyovyote vile, kanisa la kawaida ni wazi kwamba liko kwenye

kujihami, likihesabu kondoo zaidi ya kuwalisha na kuwawezesha

kondoo ili watumwe kwenda kama ‘kondoo katikati ya mbwa mwitu’.

Kanisa la kawaida linajihusisha sana na majengo, bajeti, vipeperushi,

idadi ya watu na Biblia – vitu ambavyo, ingawa ni vizuri sana

vinapotumiwa sawasawa, husababisha “kifo” vinapokuwa lengo kuu. 246

Page 255: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Hivyo ni (au vinaweza kuwa) vitu muhimu vinavyoshikika kanisani,

lakini kuchukuliwa navyo ni hatari kwa habari ya Makusudi Halisi ya

kanisa. Kanisa linalojihami ni wazo la Shetani kabisa.

Tuangalie sehemu ya tatu.

3. Kama si tishio kwao, mbwa katika kikundi watakaribisha

wanachama wapya. Wakati mwingine, makusudi nyuma ya kutafuta

washirika wapya kanisani, kukua kwa kanisa na “mikutano ya

uinjilisti” yanahitaji kuchujwa vizuri kabisa. Makusudi ni rahisi sana

kupotoshwa na kuharibiwa kama yanakuza au kutukuza majina ya

watu na kuonyesha mafanikio ya viongozi binafsi pamoja na

mashirika au madhehebu au taasisi zinazo-ongozwa nao. Ile hali ya

kujilinda na uhasama wa baadhi ya viongozi ni dalili ya kutambua

kwao makusudi yao mchanganyiko yaliyoko nyuma ya wao

“kujenga” majengo, taasisi, taratibu, makundi ya watu na kadhalika.

Hakuna kusudi la mtu yeyote lililo safi kabisa, lakini kukua kwa

kanisa kunaweza kukuza sifa ya mtu na kuficha hali ya kujipenda na

kujisifu ya ndani, japo matangazo yatolewayo ni kwamba kuna nia

safi na shauku safi kabisa ya “kumtumikia Bwana”. Sikuzote mwili

uko karibu sana, na ni kitu hatari kilichojificha katika ngozi laini

sana ya hali ya kiroho. Hapo ninakiri udhaifu wangu pia, na kusema

ukiri wa wachungaji wengi walio wakweli na wacha Mungu ambao

nimewafahamu. Ninajua makanisa mawili madogo sana ambayo

yalijikuta katika jamii zenye kukua haraka. “Wazee” waliokuwa 247

Page 256: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

katika makanisa hayo waliitikia kukua kwa makanisa hayo kwa njia

za ajabu sana. Kote, viongozi walimwambia mchungaji wao, “Inabidi

tuwe makini sana kuhusu hawa watu wapya wote wanaokuja maana,

ikiendelea hivi, tutapoteza utawala wa kanisa letu.” (!!!) He! Hivi

kweli, hali hiyo ya kujijali, kujifikiria na kujihami inaweza kudumu

katika kanisa “linalokua”? Je, hoja kama hizo zinaweza kutoka kwa

viongozi wa kanisa? Kila kiongozi mwenye cheo chochote kanisani

au wadhifa amewahi kukabiliana na mambo kama hayo katika

uongozi – na pengine yeye mwenyewe yuko hivyo. Hii ni namna

moja tu ya sura ambayo mwili unaweza kuvaa. Kwa kawaida, mwili

aidha unapenda utendaji au unapinga, na viongozi wa kiroho na

washirika waaminifu kanisani wanalengwa na Shetani ili

kusababisha maonyesho kama hayo, ya tabia ya mwili. Baada ya

zaidi ya miaka arobaini katika huduma, nimegundua kwamba lazima

kila mara nijitahidi kuuweka mwili “chini ya mamlaka”, na

kuuhesabu (Warumi 5:6, 11; Wagalatia 2:20).

Lakini kumbuka mahali mambo yanapobadilika katika ule

mfano wetu: MPAKA MBWEHA APITE! Mbweha akipita, na

aonekane wazi kabisa na wale mbwa, hawapati nafasi hata ya kulala.

Hawatashughulika na kujihami tena. Watawapokea wanachama

wapya katika kundi lao wanapokuja, lakini mbwa watakaokuja ni

wale walioko tayari kuingia katika mpango wa kumwinda yule

mbweha na kujiunga na wale mbwa wengine wote watakaohusika.

Ingawa mbwa wenyewe wanaweza kugongana kwa nguvu zaidi na 248

Page 257: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mara nyingi zaidi kuliko mwanzo, hawataona vidonda vyao na

uvimbe wao – kwa sababu wana mambo makubwa zaidi ya kufanya

kuliko kungurumiana, kubwekeana na kutaka kuumana. Mbweha

akiwa anaonekana, mbwa hao watakimbia kwa pamoja wakiwa na

maono yanayofanana na makusudi pia.

MBWEHA NI NINI?

Je, mbweha ni nini kwa Mkristo na kwa ushirika wa

waaminio? Mimi binafsi nahesabu kuwa kitu muhimu cha kufukuzia

katika maisha ya Mkristo ni Yesu Kristo. Kazi kubwa katika maisha

ya Kikristo ni “kumfuata Yesu” au “kumtafuta Yeye kwa bidii zote”.

Kwangu, hilo ndilo la mwisho kabisa. Lakini, utaratibu uliowekwa

kwa ajili ya kuwaingiza wafuasi wengine ndiye huyo mbweha

ambaye Yesu alimweka mbele ya wanafunzi Wake ajulikanaye kama

“Agizo Kuu”. Viongozi wa Kikristo wana kawaida ya kuweka

mbweha wadogo ili “watu wao” wawafukuzie – vitu kama

mahudhurio, michango kwa ajili ya bajeti, mambo ya ujenzi,

mikutano ya uamsho ya mara kwa mara, na mikazo mingine

mbalimbali. Lakini hao “mbweha wadogo” wanaweza “kuharibu

mizabibu”! Wanakuwa ndiyo kiini kikubwa na malengo makubwa,

wakielekeza usikivu wa waaminio katika shughuli na mipango

ambayo inawasaidia wao zaidi kuliko kuifikia dunia.

Wakulima kadhaa walikuwa wanapoteza muda wao wakijisifu

juu ya mbwa wao wa kuwindia. Mmoja akasema, “Nadhani mbwa 249

Page 258: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

wangu anaweza kusikia harufu ya miaka hamsini iliyopita.”

Mwingine akasema, “Acha mchezo bwana. Hakuna mbwa

anayeweza kusikia harufu ya zamani hivyo.” Yule aliyetangulia

akasema, “Nadhani mbwa wangu anaweza.” Mwindaji wa tatu

akasema, “Ninajua jinsi ya kupata ukweli. Nakumbuka Baba yangu

akisema kwamba nilipokuwa mtoto mdogo palikuwa na mbweha

mzee aliyekuwa anapita chini ya nyumba yetu kila jioni. Ni miaka

arobaini na zaidi sasa. Si twende mpaka pale tuone kama mbwa

wako anaweza kunusa hiyo harufu?” Basi, wakampakia mbwa

kwenye gari na kwenda mpaka hiyo nyumba ya zamani.

Wakamfikisha pembeni mwa nyumba hiyo na wakamzungusha mpaka

kandoni. Mara yule mbwa akaanza kupiga kelele na kuonyesha dalili

za kunusa na kufuata – akijivuta kwa nguvu atoke kwenye kamba

iliyokuwa imemfunga. Mwenye mbwa akamwachia. Mara, mbwa yule

akakimbia mbio, akavuka uwanja uliokuwa mbele ya nyumba.

Alipokaribia kama yadi ishirini mbali na nyumba, mara aliruka juu

kama futi sita! Mtu mmoja akasema, “Huyo mbwa ana matatizo

gani?” Yule mkaazi wa pale akajibu, “Hana matatizo yoyote. Miaka

arobaini iliyopita, hapo mahali kulikuwa na uzio, na yule mbweha

alikuwa anarukia hapo!” Yule mbwa akaendelea kulia na kunusa

huku akivuka ule uwanja. Mara akakata kulia na kufuata njia kando

ya nyumba. Yule mkaazi wa zamani wa pale akasema, “Miaka

arobaini iliyopita kulikuwa na kichaka hapo na miti, na yule mbweha

alikuwa anaizunguka. Kweli, mbwa wako ananusa njia ya yule 250

Page 259: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

mbweha wa zamani.” Mbwa akaendelea kwenda pole pole akinusa

na kulia mpaka akapotelea kabisa. Wale wawindaji walikuwa

wanamwangalia sana huyo mbwa, hawakuona akitoweka. Hatimaye

mmoja akasema, “Hebu tumfuate, tuone atatufikisha wapi.”

Wakafuata kweli, lakini pamoja na kumtafuta sana kila mahali,

hawakumpata. Baada ya kumsaka mchana kutwa, ilibidi waachilie

mbali shughuli hiyo, wakitumaini kwamba mbwa yule angerudi

mwenyewe baadaye. Lakini haikuwa hivyo. Mbwa akawa amepotea,

na hawakuweza kumpata popote. Baada ya kusubiri majuma kadhaa

na kuendelea kumtafuta hapa na pale, na kuuliza, walikata tamaa na

kuachilia mbali msako wao.

Miaka miwili baadaye, muda mrefu tu baada ya kuachilia

mbali kumtafuta mbwa na baada ya kupoteza matumaini, yule

mwenye mbwa akapigiwa simu jioni moja. Mpiga simu akasema,

“Je, hapo ni nyumbani kwa Reks, mbwa mwindaji?” Mwenyewe

akasema, “Ndiyo – alikuwa akikaa hapa, lakini amepotea kwa muda

wa miaka kama miwili hivi. Wewe nani, na kuna nini?” Akajibiwa

hivi: “Ni hivi mzee. Maelezo yangu yatakushangaza. Mimi ni meneja

wa duka kubwa sana katika mji wa New York. Nimemtambua mbwa

wako kwa jina na anwani yako uliyomwekea shingoni. Hapa dukani,

amekaa analinda vazi la ngozi ya mbweha la zamani, na

nimeshindwa kumtoa.” Mwenye mbwa akaacha kushangaa, akaifikiri

kidogo halafu akasema, “Mheshimiwa. Unaweza kumrudisha mbwa

wangu kwa gharama zangu?” Yule mwenye duka akasema, 251

Page 260: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

“Nimefikiri hilo, na nimekwisha fanya utafiti, na gharama yake ni

kubwa sana.” Mwenye mbwa akauliza, “Hiyo ngozi yenyewe ina

thamani gani?” Mwenye duka akajibu, “Ni dola 65”. Baada ya

kufikiri kidogo, mwenye mbwa alisema hivi, “Basi mzee, naomba

unitumie hiyo ngozi, halafu uache duka lako wazi kwa dakika tano tu

kesho”.

Wapendwa – wakati umefika – kwa ajili ya Mungu na kwa

ajili ya Kristo na kwa ajili ya mabilioni ya watu waliopotea, na kwa

ajili ya ushirika wa waaminio, na kwa ajili ya kila kitu kilicho kweli

na kizuri na chema, kwetu sisi kurudi hadi “nyumbani kwetu” kiroho,

tupate tena kunusa ile harufu ya zamani (yaani, Agizo Kuu) – harufu

ambayo itakuwa na thamani na maana zaidi sana kuliko hivi vitu

vingine tunavyofukuzia – dunia na mwili – na kuanza kumfuata

Mbweha Mkuu.

Huyo Mbweha Mkuu ni nani? Ni kuifikia dunia yote. Dunia

Yote. Kuifikia dunia yote kwa ukamilifu wake wote. Ndiyo Mbweha

Mkuu wa Kristo – aliyewaagiza watu Wake wamfukuze. Kila

Mkristo anapaswa atazame kwa makini sana na kwa muda mrefu

sana huyo Mbweha Mkuu kila siku ya maisha yake. Kumtazama

huyo Mbweha kwa muda mrefu kutapelekea kuelewa mambo kadhaa

muhimu. La kwanza ni maono. Lingine ni mkakati. Lingine ni

maongezeko yaliyohamasishwa, dhana ambayo bila shaka ilikuwa

na sehemu muhimu katika kutokea kwa Kitabu cha Matendo. Na kitu

cha mwisho ni kuelewa Ufikiaji Dunia Yote kwa ukamilifu, - lengo 252

Page 261: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

la kuifikia dunia nzima, na lengo la ufikiaji ambao utakuwa kamili –

yaani, wenye kuhusisha kila njia iliyoagizwa na kufunuliwa, ili

kukamilisha kazi yenyewe.1

1 Hakuna chochote kilichosemwa katika hii sura fupi ambacho kinapaswa kuhesabika kuwa kinyume cha kanisa kwa namna yoyote ile. Tayari kuna kulipiga kanisa kwa kila namna – mimi sitaki kuwa na hatia ya kuongeza. Ila, tahadhari hii ichukuliwe kwa uzito wake. Kanisa tukufu la Mungu – Mwili na Bibi Arusi wa Kristo, Jengo la Mungu, “nguzo na msingi wa ukweli” linahitaji kuongeza idadi ya washiriki wenye kuomba, kwenda, kutoa na kuunga mkono mkakati huo kuliko wakati mwingine wowote. Lakini, kusudi mbadala au utaratibu bandia (“mbweha wadogo”) vitaharibu utukufu wa kanisa na kuliruhusu lilaumiwe kihalali kabisa, na kukataliwa na wengi. Tunaomba Mwili wa Kristo umpe Yeye kitu tendaji kabisa kwa ajili ya kutimiza Agizo Kuu! Tunaomba Bibi Arusi wa Kristo ampende Kristo sana kiasi kwamba kule kutajwa tu kwa Agizo Kuu kusukumwe na pendo la Kristo kulitimiza! Tunaomba Jengo la Mungu liwe Hekalu la kutosha kabisa kumwonyesha Mungu wetu kwa dunia nzima!

253

Page 262: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

KumaliziaMaisha Ya Mbwa Wa Mwituni

Wale watu ambao nimepata nafasi na fursa ya kufanya kazi

nao katika kufanya watu kuwa wanafunzi, na utaratibu wa kuifikia

dunia ni miongoni mwa Wakristo wenye motisha kubwa niliowahi

kuwafahamu. Mfano mzuri sana ni mwanafunzi kijana aitwaye Ian

Bowers. Amekuwa akisonga mbele na kuendelea katika ufahamu wa

kuwafanya watu kuwa wanafunzi na kujihusisha kwa miaka kadhaa

sasa. Wakati fulani aliwahi kutunga shairi kuhusu mfano wangu wa

“Mbweha huyo!” Nimelisoma mara kadhaa. Niliomboleza wakati

ujumbe wa shairi hilo uliponifikia na kunigusa moyoni. Kwa kibali

chake, ninamalizia kitabu changu kwa shairi hilo. Naomba na wewe

ubarikiwe kama mimi nilivyobarikiwa.

Maisha ya mbwa wa mwituni ni rahisi tu,

Ingawa si maisha ya starehe.

Hebu nitoe mtazamo mpya

Maana tunaishi maisha ya uhitaji.

Hayo mahitaji yanaonekana kututawala

Na kusimamia maisha yetu.

Lakini kila siku ninajiuliza

Ikiwa mahitaji hayo si uongo tu.

Ni hivi: Kila siku ni yetu ya kushinda

254

Page 263: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Hatuna ratiba yoyote ya kufuata.

Lakini, hili hitaji hutujia

Hitaji la kulala.

Katika uwanja au chini ya mti wa kivuli

Au chini ya mbingu iliyojaa nyota

Unatamani maisha ya mbwa

Unapotuona tumelala hapo chini.

Ila, usiache kuendelea na hadithi yangu sasa.

Sikiliza, na usikie vizuri sana.

Ugundue kwamba maisha ya mbwa anayelala

Ni hatua moja tu kutoka Jehanamu.

Maana nikiamshwa tu kwa dakika

Kitu fulani hujigusa ndani yangu

Nami nina njaa – njaa sana

Hitaji langu ni kula.

Mjini nitapata takataka kidogo

Msituni nitapata mnyama mdogo

Lakini nikisha tosheka

Ninarudi haraka tu kulala usingizi.

255

Page 264: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Na kwa hili wala sikutishwa

Nilihesabu kuwa ni hazina ya dhahabu

Wakati mbwa mvivu kuliko mimi

Alipokaribishwa kundini.

Je, bado ni maisha ya mbwa

Yanayotamaniwa na moyo wako?

Rafiki yangu, hujui hata kidogo

Maana, kuna zaidi ya hayo.

Hatimaye kisa changu kitakuwa dhahiri sana

Maana, sasa pokea mwanga

Upande mbaya wa maisha ya mbwa mwitu

Ni hitaji la kupigana.

Lakini, kupigana kwa sababu gani? Nikuulize sasa

Je, waweza kuniambia wakati

Wa kuinuka kinyume cha mbwa mwenzangu

Au pengine kumkomeshea maisha yake?

Yeye ni mbwa mwenye ngozi na mkia

Anayo meno na macho ya kuona

Lakini lazima athibitishe kwamba yeye ni bora

Au wakati mwingine ni mimi.256

Page 265: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Basi, unguruma na ubweke, na ung’ate

Kiburi chetu kutosheleza

Mmoja atashinda hii vita ya kijinga

Na inawezekana hata mmoja akafa.

Na vita inapokuwa imekwisha

Sikuzote ni hasara, hakuna faida

Na kile tulichothibitisha

Ni kwamba mbwa wanaweza kuwa na kiburi sana.

Sidhani kama ni sahihi kusema

Kuna hitaji la kupigana

Nadhani badala yake ni kwamba tunakosa la kufanya

Na tuko hatua moja tu kutoka kwenye kufa.

Je, unasikiliza kwa makini?

Rafiki yangu, unasikiliza kweli?

Maana hadithi yangu haijaisha.

Sasa ndiyo tu imeanza.

Kuna hitaji moja ninalokubali

Tena nasema pasipo aibu

Huyu mbwa mwitu anapenda, na hata anaishi257

Page 266: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kwa ajili ya kukimbiza au kufukuza.

Lakini si kukimbiza tu, rafiki.

Ni kukimbiza ambako ni kuzuri sana

Kukimbiza kwenye kuhamasisha maisha yangu

Na kunakoshika akili yangu.

Si wale mbweha wadogo.

Hao nimewahi kuwafukuza wote.

Wao ni rahisi kuwashika na kuwamaliza

Nikawa nimechoshwa upesi nao.

Siku moja ikatokea

Kamwe sitasahau

Kulitokea harufu fulani hewani

Nikapata hamu kubwa.

Nikainua pua yangu angani

Nikasimama kwa miguu yangu

Ndipo nikawaona wale mbwa wengine

Wakiwa tayari kama mimi.

Kiongozi wetu ni Salvadori

Wa kikundi chetu cha mbwa kumi na mbili258

Page 267: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Ngozi yake ilikuwa manjano kabisa

Na michirizi myekundu mgongoni.

Huyu ndiye mliyekuwa mnamsubiri

Ndivyo alivyosema, huku macho Yake yaking’aa

Huyu ndiye mbweha ambaye mkimshika

Hakika itagharimu maisha yako.

Inueni pua zenu hewani

Inuseni hiyo harufu

Jifunzeni muijue vizuri,

Jifunzeni muijue vizuri.

Na wakati msipoweza kuniona

Inuieni pua zenu juu

Pateni hiyo harufu na kuifuata

Mjue kwamba nipo.

Nikahisi moyo wangu unaongeza mapigo

Shinikizo la damu likaongezeka

Kadiri hiyo harufu ilivyozidi kuwa na nguvu

Nguvu zaidi.

Halafu bila ya maonyo259

Page 268: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Kama radi ya umeme

Kiongozi wetu akageuka na kujitupa

Kuelekea katika giza la usiku.

Tulisimama kidogo tu

Na kutazamana machoni

Tukajua gharama itakayotukabili

Lakini hatukujua zawadi tutakayopata.

Na kama ni kumshika huyo mbweha,

Hatukupaswa kukawia zaidi.

Maana kazi ilikuwa ni kubwa sana

Harufu ilipoanza kupotea.

Lazima ibakie kwenye pua yetu

Kusudi letu lazima liwe wazi

Tutamshika huyu mbweha mwenye nguvu

Kauli mbiu yetu itakuwa HAYA TENA – MBWEHA

HUYO!!

Pua zangu zikapanuka, misuli zangu zikakaza

Nikaruka kutoka mahali pangu

Miguu yangu ya mbele ikakutana na ardhi

Na mbio zikawa zimeanza.260

Page 269: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Lakini rafiki yangu, usifikiri unajua

Nilichokuwa ninakimbilia

Zawadi haikupatikana katika mbweha

Ilikuwa kitu kingine zaidi.

Sikuwa naendeshwa na hitaji

La kulala au hata kula chakula

Badala yake, nilikuwa nimetawala kabisa

Kilichokuwa kinanishikilia hapo kwanza.

Je, unasikiliza kwa makini sana?

Je, rafiki yangu, unasikiliza?

Zawadi ni hii: Maisha sahihi

Niliyoishi kulingana na kusudi.

Ningepumzika nile, ningepumzika nilale

Uchovu uliniambia wakati wa kufanya hivyo

Lakini nguvu zilipokuwa zinanirudia tu

Ufukuzaji uliendelea.

Kwa habari ya kupigana, jifunze kweli hii

Hatukuwa tena na nafasi!

Tulikuwa tumepata changamoto ya maisha261

Page 270: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Yenye kushika akili yetu.

Maana hatukufukuzia kitu bure tu

Yaani mbweha tusiyemwona

Tulijua yeye ni mjanja

Basi, tukafukuza kwa mkakati.

Hatukuhukumu wala kutishia

Wageni waliokuja kundini

Tuliwashirikisha maono yetu kwa ujasiri

Na kuwaingiza pia katika kumtafuta.

Hii njia, hiyo zawadi kuu

Mbwa wengine hawakuiona

Na wengine waliingia katika mbio

Isingekufa na mimi.

Sasa jifunze hili somo la mbwa mzee

Jifunze vizuri, vizuri sana

Kwa kila mbwa anayekufa

Watatu zaidi wajiunge.

Kwa hiyo usifikiri unaniona sasa

Mbwa dhaifu anayekaribia kufa262

Page 271: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Nuru yangu itang’aa bado

Hata nitakapovuta pumzi yangu ya mwisho.

Kwa sababu nimewafundisha

mbwa wengine wa mwitu

Na nimewafundisha hilo vizuri sana

Nimewafundisha jinsi ya kuinua pua zao

Nimewafundisha jinsi ya kunusa.

Kitu kingine nilichowafundisha

Cha muhimu zaidi sana

Nimewafundisha wote mkakati nilioishi na kuufuata

“Ukimbiaji”.

Sasa mmesikia hadithi yangu.

Je, ulisikiliza kwa makini?

Je, unatamani maisha ya mbwa

Ambayo ni hatua moja tu kutoka Jehanamu?

Changamoto iko mbele yako

Je, utaongeza mfumuko?

Nenda uingie katika mbio

Kimbia na wewe, na UKIMBIE VIZURI!

- Mtunzi ni Ian Bowers263

Page 272: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

FAHIRISI

264

Page 273: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Muhtasari Wa Kila Sura

Sura Ya Kwanza Maono Ni Muhimu Kiasi Gani? (Mithali

29:18)

I. Dhana Ya Kiroho

A. Umuhimu Wa Maono

B. Maana Ya Maono

II. Hali Ya Kusikitisha

A. Hakuna Maono Madhabahuni

B. Hakuna Maono Katika Viti

C. Hakuna Maono Katika Maisha Ya Kila Siku

III. Matokeo Yake Mabaya

A. Watu Huacha Kujizuia – matokeo ya kiadili ya

kutokuwepo kwa maono

B. Watu Husambaratika – matokeo ya kijamii ya

kutokuwepo kwa maono

C. Watu Huwa Tayari Kuhukumiwa – matokeo ya

kibinafsi ya kutokuwepo kwa maono

D. Watu Huangamia – matokeo ya kiroho, ya milele ya

kutokuwepo kwa maono

Sura Ya Pili Agizo Lenye Kuamua Wajibu Wetu (Mathayo

28:18-20)

I. Uhakikisho Nyuma Ya Agizo Lenyewe265

Page 274: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

A. Mamlaka Ya KiMungu

B. Mamlaka Iliyotolewa

C. Mamlaka Stahili

D. Mamlaka Iliyofafanuliwa

II. Wajibu Katika Agizo Lenyewe

A. Amri Ya Kusonga Mbele Ya Pekee Kwa Kanisa (Kwa

Mkristo Pia)

B. Kuligawa Agizo

1. Watenda Kazi Watumiwe

2. Kuingia Shambani

3. Kupanua Maono

4. Kuwashuhudia

5. Kuwaingiza Kazini Wanaopatikana

6. Kuelimisha Na Kuwajenga Walio Kazini

7. Kumtazamia Yeye (Bwana) Kutenda Kazi

C. Je, Ni Agizo Kuu Au Ni Kupuuza Kukuu?

Sura Ya Tatu Wazo Linaloamua Njia Tutakayotumia

(Mathayo 28:19)

I. Kufanya Wanafunzi

A. Mwanafunzi

B. Mwenye Kufanya Wanafunzi

C. Tendo La Kufanya Wanafunzi

D. Nidhamu Husika266

Page 275: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

II. Kufanya Wanafunzi Kunakosababisha Huduma Ya

Kujizidisha

Sura Ya Nne Ufunguo Ulioko Mlangoni Mwa Historia Ya

Kanisa

(Matendo 1:1-5)

I. Kitabu Cha Kwanza Kinatajwa

A. Injili Kulingana Na Luka

B. Luka Alikuwa Nani, Na Aliingiaje Katika Hadithi?

C. Kweli Za Tafakari

1. Mfano Wa Kanisa Kama “Mwili Wa Kristo”

2. Luka Aliandika Vitabu Viwili Vya Ajabu

II. Mwanafunzi Binafsi Anatajwa

A. Moja Ya Nne Ya Agano Jipya Iliandikwa Na Mtu

Mmoja!

B. Kwa Nini Luka Aliandika Vitabu Hivi Viwili Kwa

Mtu Mmoja?

C. Ushuhuda Binafsi

III. Tamko La Wazi Kuhusu Kusudi La Kuandika

A. Yote Ambayo Yesu Alianza Kufanya Na Kufundisha

B. Je, Yesu Anafanya Nini Sasa?

1. Anaendelea Kufanya na Kufundisha

2. Kila Aaminiye Ni Chombo Hai Cha

Kuhifadhi Uwepo Wake267

Page 276: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

C. Je, Yesu Alitumia Watu Aina Gani?

1. Wa Kawaida

2. Waliochaguliwa

3. Walioamini

4. Walioamriwa

5. Waliotawaliwa

Sura Ya Tano Vinavyotakiwa Ili Kufanya Wanafunzi, au

Tiba Ya Daktari Kutibu Kuacha Kukuu

(Luka 1:1-14)

I. Wajibu Binafsi

II. Utafiti Wa Dhati

III. Vyanzo Sahihi

IV. Uzalishaji Unaodumu

Sura Ya Sita Mpango Wa Mungu Wa Kuongeza (2Tim. 2:2)

I. Picha Ya Mwanafunzi Mwenye Kuongeza Wanafunzi

A. Ni Mwana

B. Ni Askari

C. Ni Mwanariadha (mkimbiaji)

D. Ni Mkulima

E. Ni Mtenda Kazi

F. Ni Chombo

G. Ni Mtumishi268

Page 277: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

II. Utaratibu Wa Kuongeza Wanafunzi

A. Mpango Unamfikiaje Mwanafunzi?

B. Nini Kilichomo Katika Mpango Wa Kusikia?

C. Mwanafunzi Akisha Wezeshwa, Anafanya Nini?

III. Mifano Yenye Kuonyesha Umuhimu Na Uwezo

A. Mwinjilisti

B. Siku Ya Pentekoste “Kila Siku”

C. Kuongezwa Fedha

D. Maono Ya Kuifikia Dunia Kwa Kufanya Wanafunzi

Sura Ya Saba Hekima Ya Mkakati Wa Yesu (1Wathes.

3:8)

Sura Ya Nane Jinsi Kiwango Hiki Kifanyavyo Kazi

Kanisani

(Waefeso 4:7-14)

I. Mtoa Vipawa

A. Alishuka

B. Alipaa

C. Yuko Juu Ya Vyote

II. Vipawa Vyenyewe

A. Mitume

B. Manabii

C. Wainjilisti269

Page 278: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

D. Wachungaji Waalimu

III. Malengo Ya Kutolewa Kwa Vipawa Hivi

A. Kupata Viungo

B. Kuviwezesha Viungo

C. Kuvitumia Viungo

Sura Ya Tisa Maneno Yake Ya Mwisho, Wosia Wake

(Matendo 1:8)

I. Mkakati Kwa Ajili Ya Kuenea Kwa Injili

II. Chanzo Cha Ushuhuda Wa Injili

III. Mada Ya Ushuhuda Wa Injili

IV. Upeo Wa Ushuhuda Wa Injili

A. Hali Yako Inayokukabili

B. Mazingira Yako Hapo Ulipo

C. Eneo Lako Kimataifa

V. Siri Ya Ushuhuda Wa Injili

270

Page 279: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

Maswali Na Mapendekezo Kwa Ajili Ya Kujifunza Hiki Kitabu

Kwa ajili ya Sura ya Kwanza, “Maono Ni Muhimu Kiasi Gani?”

1. Toa maana mbili za maono ya KiMungu.

2. Nini matokeo yanayofuata, wakati watu wa Mungu

wanapokuwa hawana maono?

Kwa ajili ya Sura ya Pili, “Agizo Lenye Kuamua Wajibu Wetu”.

1. Nini kazi saba za Agizo Kuu? Ngapi katika hizo ni amri?

2. Ni mpango gani mbadala ambao Shetani ametoa chini ya

kila kazi, katika hizo saba?

Kwa ajili ya Sura ya Tatu, “Wazo Linaloamua Njia

Tutakayotumia”.

1. Toa maelezo kuhusu kila moja katika maneno haya:

“Mwanafunzi,” “Mfanya Wanafunzi,” “kufanya

Wanafunzi,” na “Nidhamu”.

2. Nini tofauti kati ya Ukristo wa kawaida, wa kuhudhuria

kanisani, na maisha ya Kikristo yenye kuzaa huduma ya

maongezeko?

Kwa ajili ya Sura ya Nne, “Ufunguo Ulioko Mlangoni Mwa

Historia Ya Kanisa”.

1. Toa maelezo mafupi kuhusu utaratibu wa kufanya

wanafunzi wa Paulo hadi Luka hadi Theofilo.

271

Page 280: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

2. Tuna ushahidi gani kwamba Theofilo “alishika” huo

mkakati na “kukimbia nao”?

Kwa ajili ya Sura ya Tano, “Vinavyotakiwa Ili Kufanya

Wanafunzi, au

Tiba Ya Daktari Kutibu Kuacha Kukuu”

1. Orodhesha na kueleza kwa kifupi mambo manne ambayo

Dakta Luka alifanya, na mwanafunzi Theofilo.

2. Nini umuhimu wa kila hatua katika utaratibu mzima? Je,

mfanya wanafunzi anaweza kupunguza hata moja katika

hizi na kutazamia mafanikio katika kufanya wanafunzi?

Je, ni hatua ngapi katika hizi ambazo wewe unafanyia

kazi kwa sasa kwa ajili ya kufanya mwanafunzi?

Kwa ajili ya Sura ya Sita, “Mpango Wa Mungu Wa Kuongeza”.

1. Nini picha saba za mwanafunzi katika

2Timotheo sura ya 2? Je, ndiyo

imekamilika, au ni pendekezo tu?

2. Eleza kidogo ule mkakati wa vizazi katika

2Timotheo 2:2, ukionyesha kilicho cha

lazima ili “kuhakikisha” maongezeko ya

vizazi vinne.

Kwa ajili ya Sura ya Saba, “Hekima Ya Mkakati Wa Yesu”.

1. Eleza hekima ya mkakati wa Yesu kiutaratibu,

alipowafundisha Mitume Wake kumi na mbili.

272

Page 281: CHUO CHA BIBLIA - Spiritual Life Ministries Ho... · Web viewHii ni kweli duniani kote, kitaifa, katika mahali pamoja, lakini sana ni kweli katika Kanisa la Yesu Kristo na katika

2. Je, unaamini maelezo ya mfumo yaliyotolewa katika hii sura

kuwa ni ya msingi, au ya bahati mbaya, au ya kubahatisha tu

katika mkakati wa Yesu?

Kwa ajili ya Sura ya Nane, “Jinsi Kiwango Hiki Kifanyavyo Kazi

Kanisani”.

1. Je, mkakati wa kufanya wanafunzi kwa vizazi ziaid ya kimoja

unaweza kufanya kazi katika kanisa la siku hizi? Kivipi?

2. Fafanua kidogo yale maelezo ya mipango miwili

yaliyotolewa katika sura hii – mfano wa kawaida na ule

utolewao na Waefeso 4:7-14.

Kwa ajili ya Sura ya Tisa, “Maneno Yake Ya Mwisho, Wosia

Wake”.

1. Ni neno gani moja katika Kitabu cha Matendo

linalodhihirisha mkakati wa Mungu kwa ajili ya kuenezwa

kwa Injili? Nini maana zake mbili? Nini uhusiano kati ya hizo

maana mbili za neno hilo?

2. Nani aliye katika “kundi la watenda kazi” wa Mungu, na

wanapaswa kufanya kazi katika maeneo gani?

3. Watenda kazi watafanikishaje kazi hiyo?

Kwa ajili ya Sura ya Kumi, “Haya Tena, Mbweha Huyo!”

1. Fafanua ule mfano wa “Mbweha”.

2. Je, mfano huo ni wa kweli kulingana na mambo uliyoona

katika kanisa la mahali?

3. “Mbweha Mkubwa” ni nini? 273