damu ya agano la milele - isob-bible. · pdf filevifungu vyote vya biblia vimetolewa kutoka...
TRANSCRIPT
1
Damu ya Agano la Milele
Haki ya kumiliki 2002 na Larry Chkoreff
Haki zote zimehifadhiwa.
Toleo la Kiswahili 2010
Kimetafsiriwa na kuchapishwa na:
Cistern Materials Translation & Publishing Center, Nairobi,
Kenya
Barua pepe: [email protected]
www.cisternmaterialscenter.com
Kitabu hiki ni mali ya mwandishi. Kinaweza kuchapishwa
tena, iwapo tu kitachapishwa chote, kwa ajili ya kukisambaza
bure (bila malipo). Hairuhusiwi kukibadili au kukihariri kwa
njia yoyote ile. Kikichapishwa tena ni lazima kiwe na tangazo
la miliki.
Mtindo 1.2 chapa ya Mei 2002
Mtindo 1.5 2009
Vifungu vyote vya Biblia vimetolewa kutoka The Holy Bible
in Kiswahili Bi UV052 BST/BSK 2003 published by Bible
Society of Kenya and Tanzania.
Kimechapishwa na International School of the Bible-ISOB,
Marietta, GA USA
www.isob-bible.org
2
Dibaji
Katika 1 Wakorintho 1:18-2:5 Mtume Paulo alsima
historia inadhihirisha kuwa hakuna mwanadamu aishiye
duniani bila kukumbana na hali fulani ya mateso, ugumu na
changamoto maishani, hata walio wafuasi wa Bwana Yesu.
Kwa nini?
Uasi dhidi ya Mungu ulidhihirika kupitia ukweli kuwa
Adamu na Hawa hawakutumainia Neno la Mungu pekee bali
akili zao wenyewe zilizowatenganisha na Mungu na
kuwaletea laana.
Miiba huwakilisha laana. Tulizaliwa chini ya laana za
Adamu na wengi wetu wana laana za vizazi pia. Musa
alipomsihi Mungu adhihirishe uhalisi wake, sehemu ya jibu
lake inapatikana kwenye vifungu hivi na alizungumza kuhusu
laana:
Kisha BWANA akashuka katika wingu akasimama
pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, BWANA.
BWANA akapita mbele ya Musa, akitangaza, BWANA,
BWANA, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi
wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha
upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi,
lakini haachi kuadhibu mwenye hatia, huwaadhibu watoto na
watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi
cha tatu na cha nne. Mara Musa akasujudu na kuabudu.
Yesu alituonya sote kupitia mfano kuhusu mpanzi kuwa,
hata Neno lake halina uwezo wa kutukomboa kutokana na
laana iwapo hatushirikiani Naye. Pia alizungumza juu ya
3
Shukrani
Ningependa kumshukuru mke wangu Carol kwa sababu ya
msaada wake na kwa himizo lake ili niandike kitabu hiki.
Craol alinitia changamoto ili niandike kitabu hiki Yesu
aliishinda laana vipi? Kwa kuangikwa msalabani. Na amini
kwamba tunashinda kwa njia hiyo tunapopitia kwenye
dhoruba hizi. Tunabaini kuwa hazikuwa na mamlaka juu yetu,
bali tunazitumia kubadili jalala zetu, miiba yetu, kuwa johari
kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
Kitabu cha Ufunuo ndicho Maandiko yetu kuhusu ushindi
kama utakavyosoma baadaye katika kitabu hiki. Ufunuo 21:19
inasema, Misingi ya mji huo ilipambwa kwa kila aina ya kito
cha thamani. Msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili
yakuti samawi, wa tatu kalkedoni, wa nne zamaridi.
2006
4
Yaliyomo Utangulizi .7
Sura ya 1 - Dini au Damu 14
Sura ya 2 - Je! Ilianza na Adamu? . 21
Sura ya 3 - Neema Kupitia Urithi... 30
Sura ya 4 - Mengi Kuhusu Agano la Damu 37
Sura ya 5 - Kaini na Abeli 49
Sura ya 6 - Nuhu Alipata Neema. 61
Sura ya 7 - Abramu Alipokea Neema 70
Sura ya 8 - Neema na Agano la Damu 78
Sura ya 9 - Maneno ya ushuhuda wako .. 92
Sura ya 10 - Abramu na Agano la Damu. 113
Sura ya 11 - Agano la Damu Huondoa Laana. 131
Sura ya 12 - Je! Umekuwa Mtumwa. 142
Sura ya 13 - Undani wa mahusiano... 147
Sura ya 14 - Dhoruba maishani mwako 155
Sura ya 15 Mfilisti wako ni nai? 149
Sura ya 16 - Toka lodebari hadi Yerusalemu. 161
Sura ya 17 - Agano la Damu Kusufdi lako 170
Sura ya 18 - Roho Mtakatifu. 178
Sura ya 19 - Damu ya Uponyaji .... 192
Sura ya 20 - Simba wa Yuda . ..213
Sura ya 21 - Isaya Sura ya 53 . 214
Fahirisi A - Ustadi wa Mahusiano. 216
5
Utangulizi
Je, umewahi kujipata katika hali iliyo kama moto
maishani? Je maisha yana kusisimua? Mungu aliyeumba
ulimwengu wote anataka kubadilishana mahali na wewe
kupitia agano la damu.
Danieli sura ya 3 ina hadithi ya mfalme Nebkedreza.
Labda umewahi kuwa dhaifu kama muumini ulipowahi
kujihisi kuwa yamfaa Mungu kukutendea muujiza. Ulisoma
katika Maandiko kuwa anakupenda na ungetaka aonyeshe
hivyo katika hali yako. Kwa kuweka chukulizi pamoja,
uliuliza Mungu akutendee muujiza na
ulitarajia akutendee. Mara nyingine
atatenda, lakini wakati mwingine, hata
unapohitaji sana hatendi.
Tunaweza kujifunza kupitia mfano
uliyoandikwa katika Yohana sura ya 6
jinsi Yesu alivyowalisha zaidi ya watu
5,000 kwa mikate mitano na samaki
wawili kwa kufanya muujiza wa kuzijumlisha na kustaajabisha
umati. Walimfikiria Yeye kuwa yule nabii aliyezungumziwa na
Musa aliyeweza kuwa mana kutoka mbinguni. Yesu akijua
kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu,
akajitenga nao akaenda milimani
peke Yake. (Yohana 6:15).
Wanafunzi walivuka
ngambo ya bahari kwa dau yao,
naye Yesu akatembea juu ya
maji na wakawasili pamoja.
Umati uliokuwa umelishwa
ulimtafuta Yesu asubuhi
iliyofuata ukitarajia kutendewa
muujiza tena. Hatimaye
6
walimpata.
Yesu akawajibu, Amin, amin nawaambia, ninyi
hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa
sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msishughulikie chakula
kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele,
ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye
Mungu Baba amemtia muhuri (Yohana 6:26,27).
Yesu aliwahimiza wajitahidi kutenda mapenzi ya Mungu.
Alijua kuwasibisha tena kutakuwa jambo lisilo la kudumu,
wala mahitaji yao hayatatimizwa ambayo yalijaa mioyoni
mwao. Yesu anataka tufanikiwe. Yesu anatamani kutimiza
mahitaji yetu, kutoka upande wa ndani hadi upande wa nje
wala sio kutoka upande wa nje hadi ndani. Yesu akawajibu,
Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini Yeye aliyetumwa
Naye (Yohana 6:29).
Yesu alianzisha mazungumzo wasiyoyatarajia kwa kuwa
alipenda kufanya hivyo. Yawezekana tunafikiri kuhusu
mahitaji ya hapa duniani naye akabadilisha nathari yetu katika
suala halisi.
Baba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa,
Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale. Yesu
akawaambia, Amin, amin, nawaambia, si Musa aliyewapa
mikate kutoka mbinguni, bali Baba Yangu ndiye anawapa
mkate wa kweli kutoka mbinguni. Kwa maana mkate wa
Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa
ulimwengu uzima. Wakamwambia, Bwana, kuanzia sasa
tupatie huo mkate sikuzote. Yesu akawaambia, Mimi ndimi
mkate wa uzima. Yeye ajaye Kwangu, hataona njaa kamwe na
yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe. (Yohana 6:31-35).
Jibu lake lilistaajabisha. Wayahudi wakaanza
kunung'unika kwa kuwa alisema, Mimi ndimi mkate
ulioshuka kutoka mbinguni (Yohana 6:41).
Pia aliwaingiza kwenye kina cha staajabu zake aliposema
Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote
7
akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu,
ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. (Yohana
6:51). Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu,
atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. (Yohana 6:56).
Yesu alikuwa akiwapa agano la damu katika Muumba
wa vyote.
Hiki ndicho atupacho mimi na wewe. Unaweza kukisia?
Mungu mwenye uwezo na utakatifu, anajitoa kukupa nafasi
wewe na mimi, watu wakosaji na walioumbwa! Alijua kuwa
agano la damu lingewaunganisha watu hawa na kuwafanya
wamoja ili wadumu ndani Yake Naye ndani yao. Alijua kuwa
kumkubali kwao kungewatimizia mahitaji yao. Ungechagua
nini, muujiza ulioweza kukuondolea matatizo ya kila siku, au
dhabihu la damu na Mungu?
Wengi wa wafuasi Wake waliposikia jambo hili
wakasema, Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye
kuyapokea? (Yohana 6:60).
Yesu alisisitiza na kuyafanya mambo yaonekane magumu
alipowauliza jinsi ambavyo wangekosewa iwapo
hawangempata kula nyama Yake na kunywa damu Yake.
Alikuwa akinena kuhusu kusulubiwa na kufufuka Kwake
(Yohana 6:62). Ni hali ya kawaida kwa binadamu kutumaini
miungu wanayoweza kuona.
8
Sura ya 1
Dini au Damu
Kwa maana mwili wangu ni
chakula cha kweli na damu yangu
ni kinywaji cha kweli. Ye yote
alaye mwili wangu na kunywa
damu yangu, atakaa ndani yangu
nami nitakaa ndani yake. (Yohana
6;55-56)
Umewahi kunyimwa mujiza?
Kama mwamini labda kulikuwana wakati mugumu
maishani ulipo hisi ingekuwa sawa kwa Mungu kukupatia
miujiza
una soma kuhusu nguvu zake za kufanya miujiza katika
bibilia. Unasoma ya kwamba anakupenda sasa unataka
uionekane kwa katika hali yako.
ukiweka haya mambo mawili pamoja unauliza miujiza
kutoka kwa mungu na unatarajia tokapo.Wakati mwingine
anafanya lakini mwingine mara mingi hafanyi.
Tutaamini vipi? ako wapi mungu wakati