darasa vi kazi ya nyumbani kiswahili jina la … · ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate...

15
EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA MWANAFUNZI: _____________________ MAELEKEZO 1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi. 2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo. 3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu. SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098 Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com) “Quality Education for the New Generation”

Upload: others

Post on 26-Jun-2020

96 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

Page 1: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI

DARASA VI – KAZI YA NYUMBANI

KISWAHILI

JINA LA MWANAFUNZI: _____________________

MAELEKEZO

1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi.

2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo.

3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu.

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098

Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com)

“Quality Education for the New Generation”

Page 2: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER KISWAHILI, KAZI YA NYUMBANI MEI VI, 2020

SEHEMU A: SARUFI: Chagura herufi ya jibu sahihi na uandike kwenye kisanduku

1. Ondoa vyombo vichafu mezani. Neno lipi katika sentensi hii ni kielezi? A. vyombo B. ondoa C. mezani D. vichafu E. chombo [ ]

2. Kama angaliwahi matibabu mauti…… A. ngemfika B. simfike C. isingelimfika D. ingelimfika E. isingalimfika[ ]

3. Kauli halisi ya sentensi, Amesema kwamba hatakuja ni ipi? A. nimesema hatakuja B. haji C. hakuji D. sitakuja E. nitakuja [ ]

4. Mzizi wa neno “tunaimba” ni……. A. –tu- B. –imb- C. –imba- D. –a- E. –na- [ ]

5. Mtoto aliyeanguka jana, amelazwa hospitali. Maneno yaliyopigiwa mstari ni… A. kishazi huru B. kitenzi kishirikishi C. kishazi tegemezi D. sentensi shurutia E. kitenzi kikuu [ ]

6. Kiranja wetu alisoma risala kwa……….ya wanafunzi wote. A. adabu B. ajili C. niaba D. udhuru E. kazi [ ]

7. Wao wanashirikiana vizuri katika masomo yao. Sentensi hii ipo katika nafsi gani? A. tatu wingi B. pili wngi C. tatu umoja D. kwanza umoja E. pili umoja [ ]

8. Katika nchi yetu wanajeshi wanalinda amani na wakulima wanalima mazao ya chakula na biashara. Hii ni aina gani ya sentensi? A. sentensi sahili B. sentensi ambatano C. sentensi huria D. sentensi shurutia E. sentensi changamano [ ]

9. Sentensi ipi ipo katika hali ya mazoea kati ya hizi zifuatazo. A. Fisi hujulikana kuwa ni mnyama mwoga. B. Fisi amejulikana kuwa ni mnyama mwoga C. Fisi anajulikana kuwa ni mnyama mwoga D. Fisi akijulikana kuwa ni mnyama mwoga E. Fisi atajulikana kuwa ni mnyama mwoga. [ ]

10. Siku ya wazazi shuleni ngoma ilipigwa kwa ufanisi mkubwa sana. Sentensi hii ipo katika kauli ya… A. kutendeka B. kutendea C. kutendana D. kutenda E. kutendwa[ ]

11. Nomino ya kitenzi cheza” ni………….. A. tucheze B. chezeni C. mchezo D. chezea E. chezeka [ ]

12. …………..kumsaidia mwenzetu kwa vile hana ndugu. A. budi B. ni budi C. sio budi D. hatuna budi E. hatunayo budi [ ]

13. Niletee kisu nikatie chungwa langu. Nini wingi wa sentensi hii?.......... A. nilete visu nikatie chungwa langu B. niletee kisu nikatie machungwa yangu C. tuletee visu tukatie machungwa yetu D. tuletee kisu tukatie chungwa letu E. nipe kisu nikatie chungwa. [ ]

14. Ninasoma darasa la sita. Katika kitenzi kilichopigiwa mstari kiambishi tamati ni………. A. naso B. –na- C. nina- D. –som- E. –a [ ]

Page 3: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

15. Neno jino lipo katika ngeli ya………… A. A-WA B. KI-VI C. LI-YA D. U-ZI E. U-YA [ ]

16. Ukija kesho utanikuta nyumbani. Hii ni aina gani ya sentensi? A. sahili B. changamano C. ambatano D. shurutia E. ya adhabu [ ]

17. Kuku aliyechinjwa jana ataliwa leo asubuhi. Hii ni sentensi……….. A. ambatano B. sahili C. shurutia D. mapambano E. changamano [ ]

18. Ukwasi wake unaonekana katika mavazi yake. Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama nomino dhahania? A.wake B. ukwasi C. katika D. unaonekana E. yake [ ]

19. Baba yangu amekwenda shambani. Neno gani limetumika kama kitenzi? A. yangu B. baba C. amekwenda D. shamba E. shambani [ ]

20. Katika neno “sikujua” kiambishi kipi ni kikanushi? A. si- B. –ku- C. –ju D. a- E. –kuju- [ ]

21. Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C. kawia ufike D. asiyesikia la mkuu huvunika guu E. ngozi ivute ili maji [ ]

22. Nini maana ya kitendawili kifuatacho “ukiona njigi utadhani njege na ukiona njege utadhani njigi”…… A. maziwa na tui la nazi B. maziwa na asali C. maji na asali D. mafuta na maziwa E. tui la nazi na mafuta [ ]

23. Maana ya nahau “kumkalia mtu kitako” ni…………. [ ] A. kumuonya B. kumsumbua C. kumueleza D. kumsengenya E. kumkashfu

24. Malizia methali ifuatayo. Dau la mnyonge….. A. halikuli likakwisha B. haliishi hamu C. halisikiki D. haliendi josho E. haliendi joshi [ ]

25. Methali ipi ni kinyume cha methali isemayo : “Chembe na chembe mkate huwa”……….. A. baniani mbaya kiatu chake dawa B. bandu bandu huisha gogo C. usiandikie mate na wino upo D. polepole ndio mwendo E. kilema si ugonjwa [ ]

26. Nahau isemayo “Shika hatamu” ina maana gani? A. ongoza B. fuata C. tangulia wakoloni D. endelea E. leta [ ]

27. Kaa huku nikae kule tumvue mshezi kofia. Tegua kitendawili……… A. ugomvi B. kula ugali C. mashindano D. mahindi E. mchezo [ ]

28. Methali ipi inalandana na hii “Sanda ya mbali haiziki”…… A. adhabu ya kaburi haijua maishi B. adui wa mtu ni mtu C. fimbo ya mbali haiuwi nyoka D. asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu E. kuuliza si ujinga [ ]

29. Huku ng’o na kule ng’o. jibu la kitendawili hiki ni lipi? A. mwanga B. elimu C. giza D. wema E. umoja [ ]

30. Nini maana ya nahau “kulala tanga” A. kulala mjini Tanga B. kulala msibani C. kulala usingizi mzito D. kulala harusini E. kulala fofofo kila siku [ ]

31. Neno “Jengo” likinyumbulishwa katika kauli ya kutendeka litakuwa neno lipi?

A. jengwa B. jengea C. jengesha D. jengewa E. jengeka [ ]

32. “Yeye hupenda sana kusoma kiswahili” katika sentensi hii ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi? A. hupenda B. Kiswahili C. sana D. yeye E. kusoma [ ]

Page 4: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

33. Katika sentensi zifuatazo ni ipi ipo katika hali ya mazoea? A. Roda alisoma gazeti la mtanzania B. Roda atasoma gazeti la mtanzania C. Roda husoma gazeti la mtanzania D. Roda amesoma gazeti la mtanzania E. Roda anasoma gazeti la mtanzania [ ]

34. “Alikuwa anajibu kihuni”. Neno kihuni limetumika kama aina gani ya maneno? A. kielezi B. kiwakilishi C. kivumishi D. kitenzi E. kihisishi [ ]

35. Mtu anayetaka msaada wa aina………nitampa. Neno linalofaa kukamilisha tungo hiyo ni lipi? A. wowote B. yeyote C. vyovyote D. yoyote E. lolote [ ]

36. “Wanafunzi wanaendelea kusoma Kiswahili ingawa hawana mwalimu”. Neno “wanaendelea” limetumika kama aina gani ya kitenzi? A. kikuu B. kishirikishi C. kisaidizi D. jina E. kitegemezi [ ]

37. Mahali pale panatisha. Neno “pale” ni aina gani ya neno? A. kiwakilishi B. kivumishi C. kielezi D. kiunganishi E. kihisishi [ ]

38. Kinyonga anatembea. Ukanushi wa sentensi hii ni upi? A. kinyonga akitembei B. kinyonga hakutembea C. kinyonga hajatembea D. kinyonga hatembei E. kinyonga hatatembea [ ]

39. Mama anapika chakula lakini baba anapanga mawe. Hii ni aina gani ya sentensi? A. changamano B. ambatano C. shurutia D. sahili E. mkanyagano [ ]

40. Kiburi si maungwana. Neno “si” limetumika kama aina gani ya kitenzi?......... A. kikuu B. kisaidizi C. mwanana D. kishirikishi E. jina [ ]

41. “Baba yangu ni mwenyekiti wa kijiji. Neno “Mwenyekiti” ni nomino ya aina gani? ….. A. dhahania B. kawaida C. pekee D. jumla E. mguso [ ]

42. Huyu ……….mwanangu mpendwa. Neno lipi ni shaihi ili kukamilisha sentensi hiyo?.... A. ndiye B. ndio C. ndiyo D. ndie E. ndiwe [ ]

43. Mbwa……….ameonekana. neno lipi linakamilisha tungo hiyo? A. aliopotea B. alipotea C. amepotea D. aliyepotea E. alivyopotea[ ]

44. Ili tuendelee……kufanya kazi kwa bidii. Neno lipi limekosekana kukamilisha sentensi hiyo? A. ni budi B. hatuna budi C. tuna budi D. kuna budi E. budi[ ]

45. Baba alilimiwa shamba na wanakijiji. Sentensi hii ipo katika kauli gani?......... A. kutenda B. kutendeka C. kutendewa D. kutendwa E. kutendea [ ]

46. Maandishi haya yanasomeka vizuri. Sentensi hii ipo katika wakati gani? A. ujao B. uliopita C. uliopo D. wa mazoea E. mtimilifu [ ]

47. “Sipendi uongo”. Sentensi hii ipo katika nafsi ipi?.... A. nafsi ya kwanza wingi B. nafsi ya tatu umoja C. nafsi ya tatu wingi D. nafsi ya pili umoja E. nafsi ya kwanza umoja [ ]

48. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ni kauli ya kutendea? A. watoto wanacheza mpira B. mpira unachezwa na watoto C. watoto wanachezeana mpira D. watoto wanachezea mpira E. mpira unachezewa na watoto [ ]

49. Baba alituambia kuwa atakwenda Dodoma. Hii ni aina gani ya kauli? A. halisi B. sadifu C. taarifa D. kiulizo E. kama [ ]

50. Nitajitahidi kufika nyumbani kwenu………….hali yangu si nzuri. A. wala B. labda C. hata D. ikiwa E. ingawa [ ]

51. Tegua kitendawili hiki. Shamba langu kubwa lakini mavuno yake ni kidogo sana. ……… A. uyoga B. nywele C. pamba D. mahindi E. manyonya [ ]

Page 5: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

52. Kamilisha methali ifuatayo. Ng’ombe haelemewi na……….. A. mzigo wake B. plau yake C. nunduye D. peme zake E. miguuye [ ]

53. Kesi haikuamuliwa vizuri kwasababu hakimu alikuwa popo. Nahau “alikuwa popo” ina maana gani? A. kuwa mgonjwa B. kuwa mlevi C. kuwa na hasira D. kuwa kigeugeu E. kuwa mbishi [ ]

54. Kamilisha methali hii. Manahodha wengi… A. chombo huenda joshi B. chombo huenda mrama C. huzamisha chombo D. huaribu safari E. wakati chombo kimoja [ ]

55. “Maji yakimwagika hayazoeleki” Methali ipi ina maana sawa na methali hii? A. la kuvunda halina ubani B. dawa ya moto ni moto C. cha mlevi huliwa na mgema D. usipojua kufa tazama kaburi E. kamba hukatikia pabovu. [ ]

56. Hatukuweza kuongea vizuri kwani mwenzangu alikuwa amevaa miwani. Nini maana ya amevaa miwani? A. amepumzika B. amekasirika C. amelala D. amelewa E. amechoka [ ]

57. Ipi ni maana ya kitendawili “ nyumba yangu imeungua mwamba wake umebaki”? A. Kaburi B. mlima C. kisima D. mfupa E. njia [ ]

58. Neno lipi linakamilisha methali isemayo………..asikifiwa tembo hulitia maji? A. mpishi B. mwashi C. mgema D. mkwezi E. mlevi [ ]

59. Jifya moja haliinjiki chungu. Methali hii ina maana sawa na ipi kati kati ya hizi zifuatazo…… A. mchagua jembe si mkulima B. kilema si ugonjwa C. kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi D. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu E. jembe halimtupi mkulima[ ]

60. “Sina hali” Nahau hii ina maana gani?...... A. nina upele B. ninaumwa C. sina ahueni D. sijambo E. sijiwezi [ ]

61. Tangu tupate uhuru hatunyanyaswi tena kama …….kabla ya kujitawala. A. inavyokuwa B. iliyokuwa C. itakavyokuwa D. ilivyokuwa E. ilivyo [ ]

62. Wingi wa maneno “mtoto huyu hana adabu” ni upi? A. watoto wale hawana adabu B. watoto hawa hawana adabu C. watoto huyu hawana adabu D. watoto wale hana adabu E. watoto wote hawana adabu [ ]

63. ……ningalionana naye japo kwa dakika moja! A. jana B. iwapo C. laiti D. labda E. ingawa [ ]

64. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ipo katika kauli taarifa? A. mzee amesema kwamba nimeshachoka kusikiliza mazungumzo. B. mzee amesema nimechoka kusikiliza mazungumzo C. mzee amesema kuwa nimechoka kusikiliza mazungumzo D. mzee amesema kwamba amechoka kusikiliza mazungumzo E. mzee amesema ninachoka kusikiliza mazungumzo [ ]

65. Neno “bwana” lina silabi ngapi? A. moja B. mbili C. tatu D. nne E. tano [ ]

66. Kitenzi kutokana na neno msomaji ni……… A. kutangaza B. kuhariri C. kupekuwa D. kukomaa E. kusoma [ ]

67. Huyu ndiye kijana…………. A. uliyomtuma B. ulimtuma C. ulituma D. uliyemtuma E. uliomtuma [ ]

68. Neno mkewe likirefushwa litakuwa “ mke wake”. Je neno nduguyo likirefushwa litakuwaje? A. ndugu yake B. ndugu yenu C. ndugu yako D. ndugu yao E. ndugu wao. [ ]

Page 6: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

69. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ni kauli ya kutenda? A. kitabu kilisomeka B. Daniel alisoma kitabu C. kitabu alisomea Daniel D. Daniel alisomewa kitabu E. kitabu kilisomwa na Daniel [ ]

70. “Niliondoka mara moja” Sentensi hii ipo katika nafsi ipi? A. nafsi ya pili umoja B. nafsi ya kwanza umoja C. nafsi ya tatu wingi D. nafsi ya pili wingi E. nafsi ya kwanza wingi [ ]

71. Mvua kubwa ilinyesha lakini watoto waliendelea kucheza mpira. Neno “lakini” limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. kiunganishi B. nomino C. kitenzi D. kivumishi E. kiwakilishi [ ]

72. Wingi wa sentensi “kazi ya balozi ni ipi? Ni upi? A. kazi za balozi ni zipi? B. kazi za mabalozi ni ipi C. makazi ya mabalozi ni yapi? D. kazi za mabalozi ni zipi? E. kazi ya mabalozi ni zipi? [ ]

73. “Mwalimu aliulizwa swali na wanafunzi”. Katika sentensi hii nani aliyetendewa jambo? A. swali B. mwalimu C. wanafunzi D. mwalimu na wanafuni E. wanafunzi na swali[ ]

74. Mkutano mkuu wa Chama wa Taifa…….mwakani. A. ulifanyika B. utafanyika C. umefanyika D. unafanyika E. ungefanyika [ ]

75. Niliwanunulia watoto wangu vitabu vyote. Neno “wangu” limetumika kama aina ipi ya maneno A. nomino B. kiunganishi C. kitenzi D. kiwakilishi E. kivumishi [ ]

76. Habari gani ndugu yangu?............hujapata nafuu bado? Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo. A. ebu B. la C. Je, D. eti E. au [ ]

77. Tulipigwa na mwalimu wetu kwasababu ya uzembe wa kutomaliza kazi tuliyopewa. Katika kitenzi “tulipigwa” mzizi wa neno ni upi?

A. tuli- B. –li- C. -pig- D. –a E. –pigwa [ ]

78. Wanafunzi wale hawataruhusiwa kucheza tena uwanjani katika neno “hawataruhusiwa” kiambishi kikanushi ni kipi? A. ha-B. –wa- C. taruhusiwa D. –wa E. –ta- [ ]

79. Shangazi anatembea polepole. Neno polepole hapa limetumika kama aina ipi ya maneno? A. kitenzi B. kiwakilishi C. kivumishi D. kielezi E. kiunganishi [ ]

80. “Farida na dada yake wanapendana sana”. Sentensi hii ipo katika kauli ipi? A. kutenda B. kutendewa C. kutendea D. kutedana E. kutendwa [ ]

81. Kamilisha methali ifuatayo. Amani haiji ila kwa ncha ya………….. A. kisu B. upanga C. bunduki D. mkuki E. mshale. [ ]

82. Tegua kitendawili kifuatacho. “Blanketi la Mungu lina chawa” A. mbingu na nyota B. kichwa na nywele C. ngozi na upele D. wingu na mvua E. giza na nyota [ ]

83. Neno lipi linakamilisha methali hii; Dunia hadaa ulimwengu…………… A. mzuri B. mviringo C. mbaya D. shujaa E. mchungu [ ]

84. Samahani ndugu umenitoka. Maana ya msemo “umenitoka” ni ipi? [ ] A. nimekusahau B. umenibabaisha C. nimekufananisha D. nimekuchoka E. umeniumbua

85. Maana ya nahau “kumeza maneno” ni ipi? [ ] A. kuwa bubu B. kutoboa siri C. kuficha siri D. kunyamaza E. kuvumilia

Page 7: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

86. Sikujua kuwa maneno yale yangekuvunja moyo. Hapa “yangekuvunja moyo” maana yake ni nini? A. yangekushawishi B. yangekufurahisha C. yangekukatisha tamaa

D. yangekushtua E. yangekutia uchungu. [ ]

87. Tegua kitendawili hiki “Mwanangu ana upele mwili mzima”……… A. fenesi B. chungwa C. embe D. tango E. boga [ ]

88. Maana ya nahau “fuja mali” ni ipi? A. kuhifadhi mali B. kuiba mali C. kutafuta mali D. kutumia mali vibaya E. kutumia mali kibahili. [ ]

89. Tegua kitendawili. Mama hachoki kunibeba…….. A. miguu B. mabega C. kitanda D. kiti E. mgongo [ ]

90. Kamilisha methal hii, akili ni nywele………… A. huondoa maarifa B. kila mtu ana zake. C. hula mbivu D. si chururu E. hujaza kibaa [ ]

91. Nomino kutokana na kitenzi “nakili” ni ipi?........... A. nakala B. chukua C. kili D. sikitika E. tafakari [ ]

92. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi? Mjumbe wetu…………mchango wetu kwa mwenyekiti. A. aliahirisha B. aliwakilisha C. aliwasilisha

D. aliasilisha E. aliwasirisha [ ]

93. Wingi wa sentensi ifuatayo ni upi? Mbuzi huyu ni wangu” A. mbuzi hizi ni zangu B. mbuzi hawa ni wangu C. mbuzi hizi ni wetu D. mbuzi hizi ni zetu E. mbuzi hawa ni wetu [ ]

94. Misitu hii imepandwa na wasasi. Katika sentensi hii misitu ime…………… A. tendeka B. tendwa C. tendewa D. tendea E. tendeana [ ]

95. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ni kauli halisi? A. ameniomba nimrushie mpira ule. B. ule ndio mpira alioomba nimrushie C. nirushie mpira huo tafadhali D. alitaka arushiwe mpira huu. E. Juma aliniomba kuwa nimrushie mpira. [ ]

96. Ili nifaulu mtihani wangu………………nijifunze kwa makini. A. bidii B. ni budi C. si budi D. budi E. sina budi [ ]

97. Ipi ni sentensi iliyo katika kauli taarifa? A. tafadhali nichinjie kuku wangu B. nichinjie kuku wangu C. aliniomba nimchinjie kuku wake D. mchinje kuku huyo tafadhali

E. kwa nini unanichinjia kuku wangu? [ ]

98. Kilichomfanya…………….ni woga. [ ] A. alikimbia B. angekimbia C. kukimbia D. akimbie E. akakimbia.

99. Katika sentensi ifuatayo ni neno lipi limetumika kama kivumishi? Jana mwalimu alivaa shati nadhifu. A. nadhifu B. jana C. alivaa D. mwalimu E. shati [ ]

100. Katika neno watasoma kiambishi kinachoonesha wakati ni kipi? A. wa- B. –ta- C. –so- D. –ma E. –tas- [ ]

101. Katika neno “wananifuata” kiambishi kinachoonesha kitenzi ni kipi? A. –fua- B. –ta- C. –ana- D. –ni- E. –fuata [ ]

102. Nenda shule haraka. Neno “haraka” limetumika kama nini? A. kitenzi B. nomino C. kielezi D. kisifa E. kiunganishi[ ]

Page 8: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

103. Kama Juma anagalisoma kwa bidii anagalifaulu mtihani. Hii ni aina gani ya sentensi?........A. changamano B. shurutia C. ambatano D. ndefu E. sahili [ ]

104. Alisema yeye hana ubaya na mtu. Neno lililotumika kama kiwakilishi katika sentensi hii ni lipi?......A. mtu B. ubaya C. hana D. yeye E. alisema [ ]

105. Wao wanahitaji kusoma vitabu vyote. Neno “wao” katika sentensi hii lipo katika nafsi gani?........

A. nafsi ya kwanza B. nafsi ya pili umoja C. nafsi ya tatu wingi D. nafsi ya umoja E. nafsi ya kwanza wingi. [ ]

106. Umoja wa sentensi “Ndege hawa wanakunywa maji” ni upi? A. ndege hii inakunywa maji B. ndege yule anakunywa maji C. dege hili linakunywa maji D. ndege huyu anakunywa maji E. ndege huyu imekunywa mamaji [ ]

107. Masalale! Tumekwisha. Neno masalale! Limetumika kama aina gani ya maneno? A. kihisishi B. kiwakilishi C. kielezi D. utenzi E. nomino [ ]

108. “Jeni amenunua gari” Hii ni aina gani ya sentensi? A. fupi B. changamano C. sahili D. ambatano E. shurutia. [ ]

109. Mtoto huyu alikuwa na bidii darasani………hakufaulu mtihani. A. hivyo B. hata lau C. walau D. angalau E. hata hivyo. [ ]

110. Alitembea…………miguu kutoka shuleni hadi nyumbani. A. kwa B. na C. wa D. cha E. pa [ ]

111. Kamilisha methali ifuatayo; kufa…………

A. ni kufariki B. kwaja C. ni kubaya D. kufaana E. ni lazima [ ]

112. Maana ya kitendawili “ tochi yangu huwaka mchana tu” ni ipi?

A. kibatari C. jicho C. meno D. maua E. jua [ ]

113. “Nazi mbovu harabu ya nzima” Methali hii ina maana sawa na ipi kati ya hizi zifuatazo?

A. nazi haivunji jiwe B. nazi ni tui la kwanza C. baada ya dhiki faraja

D. samaki mmoja akio za wote wameoza E. samaki mkunje angali mbichi. [ ]

114. Wazee wa baraza walimtaka makala amwangukie baba yake. Kama ilivyotumika katika

sentensi hii, maana ya neno “amwangukie” ni ipi? ……. A. amwokoe B. amtake

radhi C. amtulize D. amtunze E. amtimizie mahitaji [ ]

115. Methali ipi inafanana na Mganga hajigangi? A. kengele haina mgongaji [ ]

B. dalili ya mvua ni mawingu C. kilema si ugonjwa D. kinyozi hajinyoi

E. tembea uone

116. Lipi ni jibu la kitendawili kifuatacho. “nyumba yangu ina nguzo moja”?....

A. mti wa mpapai B. uyoga C. nyumba ya msonge

D. ua E. jembe na mpini [ ]

Page 9: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

117. “Siku za mwizi ni arobaini” ina maana sawa na………..

A. mchoyo hana rafiki B. hakuna marefu yasiyo na ncha

C. mwizi hushikwa kila siku ya arobaini D. mfanya mabaya huishi siku arobaini

E. mvumilivu hula mbivu [ ]

118. Maneno yapi yanakamilisha methali ifuatayo kwa usahihi? Aliye kando…………

A. amesimama wima B. anaangukiwa na mti C. haangukiwi na mti

D. hana lake jambo E. hakutakii mema [ ]

119. Tegua kitendawili hiki. Jina mizi laniita lakini silioni………. [ ]

A. jua B. mwangwi C. radi D. aina ya muungurumo E. popo

120. “Ukitaka kuruka agana na nyonga” Methali inatuasa juu ya nini?

A. nyonga ni kiuongo muhimu B. asiye na nyonga hawezi kuruka

C. tusikubali kuruka kabla ya kuuliza nyonga D. tusipopima nyonga zetu tatvunjika

E. lazima tutafakari kwa kina kabla ya kutenda. [ ]

121. “Bibi anafua nguo” “Babu anapika chakula”. Utatumia aina gani ya maneno ili kuziweka pamoja sentensi hizi?

A. kiwakilishi B kielezi C. kiunganishi D. kihisishi E. kitenzi [ ]

122. Nomino ipi ipo katika ngeli ya LI-YA kati ya hizi? A. kisu B. mti C. kichuguu D. mbuzi E. shamba [ ]

123. ……………….hatukusoma kwa bidii. Neno lipi linakamilsha sentensi hiyo? A . mimi B. sisi C wao D yeye E wewe [ ]

124. Wanafunzi wanasoma vitabu. Hii ni aina gani ya sentensi? A. changamano B shurutia C. ambatano D. sahili E. nyembamba [ ]

125. Katika neno “wanacheza” kiambishi cha njeo ni………. A. –na- B wa- C. nache- D. –a E. cheza. [ ]

126. Hapo ……….aliposimama mgeni rasmi wakati akitoa hotuba. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo? A. ndivyo B. ndiyo C. ndipo D. alipo E. ndimo[ ]

127. Wengi waliyamini maneno ya mwalimu. Neno wengi limetumika kama……….. A. nomino B. kiwakilishi C. kivumishi D. kielezi E. kitenzi [ ]

128. Nyumba imejengwa vizuri. Hii kauli ya…………….. A. kutendwa B. kutendewa C. kutendana D. kutenda E. kutendeka [ ]

129. Yeye hapendi kusoma wala kuandika. Neno “yeye” ni nafsi gani? A. I – wingi B. II- umoja C. I-umoja D. III – umoja E. III – wingi [ ]

130. Babu alisema kwamba atajengewa nyumba na mjukuu wake. Hii sentensi ipo katika kauli gani?

A. husika B. shurutia C. taarifa D. ambatano E. halisi [ ]

131. Mtoto aliyepotea jana ameonekana leo asubuhi, hii ni aina gani ya sentensi?.......... A. changamano B. shurutia C. ya masharti D. sahili E. ambatano [ ]

132. Ala kumbe! Unahitaji chakula. Kihisishi ni kipi kati ya maneno yafuatayo? A. chakula B. ala kumbe! C. unahitaji D. ala E. kumbe [ ]

133. Neno “Jicho” liko katika ngeli ya……… .A. U-ZI B. LI-YA C. KI-VI D. A-WA E. U-I [ ]

Page 10: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

134. Chausiku ni mtoto mtundu sana. Neno lililotumika kama kivumishi ni lipi? A. ni B. mtoto C. chausiku D. mtundu E. sana [ ]

135. Vijana wanaimba vizuri. Katika kitenzi “wanaimba” mzizi wa neno ni upi? A. –tu- B. –imba- C. a- D. –imb- E. na- [ ]

136. Ili tufaulu mitihani yetu…….kusoma kwa bidii. A. hatuna budi B. ni budi C. budi D. tuna budi E. kunaga budi. [ ]

137. Katika neno “sitacheza” kiambishi kipi ni kikanushi? A. –ta B. si- C. –chez- D. –a E. tacheza [ ]

138. Kama ungaliniomba kitabu kile ningalikupa. Hii ni aina gani ya sentensi? A ambatano B sahili C. shurutia D. changamano E. sahihi [ ]

139. Upele humwota asiye na kucha. Methali ipi ina maana sawa na hiyo kati ya hizi zifuatazo. A. mwenda pole hajikwai B haba na haba hujaza kibaba C. mchumia juani hulia kivulini D. penye miti hakuna wajenzi E pole pole ndio mwendo [ ]

140. Tegua kitendawili “bomu la machozi baridi….” A giza B. moshi C boga D. risasi E. panga [ ]

141. Kamilisha methali ifuatayo” fimbo ya mnyonge ni……… A. kuchapwa B. kufukuzwa C. umoja D njaa E viboko [ ]

142. Askari wangu ni mpole lakini adui wanamhara. Jibu la kitendawili hiki ni…….. A. paka B. kinyonga C. moyo D. jua E. nyota [ ]

143. Vijana wenzako wote wanafanya kazi wewe umekalia ku………tu. Nahau ipi inafaa kwa maelezo hayo? A. kufa kishujaa B. kula njama C. piga domo

D. kukata tamaa E. kukupa heko [ ]

144. Mwanzo wa methali ifuatayo ni upi…………ni silaha iliyo mkononi. A. ingali maji B. mgaagaa na upwa C penye nia D kuliko maji E hamadi kibindoni [ ]

145. Tegua kitendawili, bibi hatui mzigo wake……………. A. kobe B. nyanya C. majani D. mbarika E. siafu [ ]

146. ……….uwakamate wahalifu wote waliofanya unyama huu. Nahau ipi itatumika katika maelezo hayo? A. bega kwa bega B. fanya juu chini C punga mkno

D. tega masikio E piga makofi [ ]

147. Kamilisha methali hii; Adhabu ya kaburi……….. A. aijuaye maiti B. hakuna wajenzi C. si ujinga D. hujaza kibaba E. hufunzwa na ulimwengu.[ ]

SEHEMU B: Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Wanangu mwanishangaza, hivyo vinavyowaona,

Nashindwa mate kumeza, mavazi mnayoshona,

Ni kioo ya angaza, nguo za ndani twaona,

Hii ni tabia gani mavazi mnayovaa?

Binti yangu nakueleza, wengi jua wakuona,

Uache kujitembeza, nusu uchi kila kona,

Aibu watakubeza, watafutani we mwana

Hii tabia gani, mavazi mnayovaa?

Utu mwaupoteza, utamaduni kukana,

Kuiga sitokataza, ila iga yana maana,

Kuiga bila uliza, ni kama akili huna,

Hii tabia gani, mavazi mnayovaa?

Page 11: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

157. Ni nani anayesema maneno hayo katika shairi hili?

A. mkulima B. mzazi C. daktari D.muuguzi. [ ]

158. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi? A. moja B. saba C. nne D. tatu E. sita [ ]

159. Vina vya kati na vya mwisho katika shairi hili ni vipi? A. be, za B. ta, ni C. za, na D. nu, sho E. kit, ti [ ]

160. Mwandishi anasema anashindwa kumeza hata kitu gani? A. mate B. maziwa C. majani D. mavazi E. matendo [ ]

161. Kituo cha shairi hili ni kipi? A. aibu watakubeza, watafutani we mwana, B. wengi jua wakuona C. hii ni tabia gani, mavazi mnayovaa? D. mbona mwaniaibisha E. wadhani unapendeza [ ]

162. Mstari wa tatu katika ubeti wa kwanza una mizani mingapi? A. 10 B. 16 C. 8 D. 11 E. 15 [ ]

163. Ndovu wanakimbia. Sentensi hii ipo katika nafsi ipi? A. III – umoja B. I – umoja C. III – wingi D II – wingi E. I – wingi [ ]

164. Kijana yule hapendi mzaha anapofanya kazi zake neno “yule” limetumika kama aina gani ya maneno? A. kiunganishi B. kiwakilishi C nomino D. kielezi E. kivumishi[ ]

165. Mshale umerushwa juu angani. Sentensi hii iko katika ngeli ipi? A. U- I B. LI – YA C. KI – VI D. U – WA E. U- ZI [ ]

166. Kiambishi cha wakati katika sentensi isemayo “Juma atalima shambani” ni kipi? A. a- B. –ta- C. Juma D. –li E. –ma [ ]

167. Mnyama mkali amekamatwa leo. Katika sentensi hii neno lipi limetuika kama kitenzi? A. mkali B. leo C. mnyama D. amekamatwa E. hakuna [ ]

168. Ana na Juliana ni mapacha walioungana. Katika sentensi hii neno “na” limetumika kama aina gani ya maneno? A nomino B. kielezi C. kitenzi D. kiwakilishi E kiunganishi [ ]

169. Neno “Mwanamwari” lina silabi ngapi? A sita B nne C. kumi D. tisa E tano [ ]

170. Waliondoka mapema sana kiambishi ilichopigiwa mstari kinaonesha………………….. A. mzizi wa neno B. wakati C. nafsi D. ukanushi E. rangi [ ]

171. Ufa unaonekana kabisa. Wingi wa sentensi hii ni ………….. A. maufa yameonekana kabisa B. kiufa kimeonekana kabisa C. liufa limeonekana kabisa D. nyufa zinaonekana kabisa E majiufa yanaonekana kabisa [ ]

172. Wale watakaofanya vizuri watapewa zawadi. Neno “wale” limetumika kama…………… A. kiwakilishi B. nomino C. kivumishi D. kitenzi E. kielezi [ ]

Page 12: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

173. Mtoto aliyevunjika mkono amepona. Hii ni aina gani ya sentensi? A. ambatano B. sahili C. shurutia D. aina E. changamano [ ]

Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Sera na imesikika, inatangazwa nchini,

Vijana wote hakika, wazururao mjini,

Nguvu kazi imenuka, yakutaka kijijini

Mpango wa nguvu kazi, viongozi tekeleza.

Wengi wameishaloea, hawakumbuki nyumbani,

Hujiita baharia, wakisombwa melini,

Kwa makundi hutembea, wametia vya mtoni,

Mpango wa nguvu kazi, viongozi tekeleza.

Mpango ueleweke, ni kwa yeyote nchini,

Pia na kwa wanawake, warandao mitaani,

Wasijitie makeke, eti mke wa jirani,

Mpango wa ngvu kazi, viongozi tekeleza

Viongozi wa mikoa, tekeleza kwa makini,

Wapendao kudoea, wapeleke maporini,

Wasifanye mazoea, kuzurura mtaani,

Mpango wa ngvu kazi, viongozi tekeleza

174. Ubeti mmoja wa shairi una jumla ya mizani mingapi?

A. 16 B. 12 C. 64 D. 120 E. 8 [ ]

175. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu ni vipi?

A. ma, ti B. ke, ni C. vi, o D. te, ji E. ndi, ngo [ ]

176. Neno “kudoea” kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?

A. kupelekwa maporini B. kujitia makeke

C. kufanya hila ya kupata kitu kutoka kwa mtu mwingine kwa njia ya ujanja

D. ya kutaka kijijini E. ni vijana wote hakika. [ ]

177. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi?

A. 4 B. 3 C. 5 D. 7 E. 6 [ ]

178. Kituo cha shairi hili ni kipi? A. wasifanye mazoea B. nguvu kazi imenuka

C. eti mke wa jirani D. kwa makundi hutembea

E. mpango wa nguvu kazi, viongozi tekeleza [ ]

179. Mwandishi wa shairi hili katika ubeti wa tatu anaisisitiza kuwa mpango ueleweke kwa

……nchini. A. wowote B. yoyote C. yeyote D. yote yote E. kyote kyote[ ]

Page 13: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

SEHEMU C: USHAIRI Soma shairi lifuatalo kwa usahihi. Kisha jibu swali la 31 – 35 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Kasimama kizimbani, popo anatetemeka Kaitwa mahakamani, popo kujibu shitaka, Atakiwa abaini, kwa ulimi kutamka, Ajitetee bayana, ni mnyama sio ndege.

Hakimu nakushukuru, shitaka kunisomea, Sina jadi na kunguru, ila na pundamilia, Mimi ni mnyama huru, amini ninakwambia, Tukidaiwa ushuru, kwa wanyama nalipia. Ni kweli popo napaa, na mbawa nimepata Lakini mimi nazaa, hilo halina utata, Kuwa ndege nakataa, sina undugu na bata, Nakataa katakata, mimi si ndege nasema

180. Popo anakataa kuwa si ndege kwasababu gani? A. anataga B. ana mabawa C. anazaa D. ana manyoya E. anasuka [ ]

181. “Kitendo cha kuzaaa na kunyonyesha hufanywa na viumbe ambao ni……………..” A. bata B. wadudu C. samaki D. kunguru E. wanyama [ ]

182. Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi hili huitwaje?............ A. vina B. kibwagizo C. hakimu D. mahakama E. vina vya mwisho [ ]

183. Popo alitakiwa kujitetea bayana, usemi “kujitetea bayana” una maana gani? A. kujitetea waziwazi B. kujitetea kwa kificho C. kujitetea kwa aibu D. kujitetea kwa mabano E. kujitetea wasiwasi [ ]

184. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi? A. moja B. nne C. mbili D. kumi E. tatu [ ]

185. Kila mstari katika ubeti wa pili una mizani mingapi? A. nane B. kumi na mbili C. saba D. kumi na sita E. mine [ ]

Soma habari ifuatayo kwa usahihi kisha jibu swali la 41- 45 kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Hapo zamani palikuwa na kijana mmoja aliyeitwa Majaliwa. Majaliwa alifahamika sana kwao Mahama

kwa sababu ya uhodari wake wa kukimbia. Kila mtu alisema kwamba Majaliwa alishika usukani katika

mbio. Aliweza kukimbia kwa kasi sana umbali mrefu bila kuchoka. Kwa ajili hiyo aliteuliwa kuwa

mmoja wa watumishi wa mfamle wa Mahama. Mfalme alitumtia Majaliwa kupeleka habari haraka

sehemu mbalimbali. Vijana wa rika la Majaliwa walimtania kwa kumwita “Farasi wa mfalme” kutokana

na kazi hiyo.

Page 14: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

Siku zote Majaliwa alifanya juu chini kufanya kazi zake kwa kuzingatia muda. Hali hiyo ilimfanya azidi

kupendwa na mfalme. Siku moja mtoto wa mwisho wa mfalme alishikwa na maradhi. Alitibiwa na

waganga wengi lakini hakupona wala kupata ahueni. Hali hiyo ilimfanya mfalme kukosa raha kabisa.

Mganga mkuu wa mfalme alimshauri mfalme wajaribu kupata dawa kutoka kwa mganga Fundi.

Mganga Fundi alikuwa anaishi nchi ya Ngalaba. Kutoka Mahama hadi Ngalaba ilikuwa ni safari ya

siku nne kwenda tu. Mfalme alimtuma Majaliwa aende huko. Majaliwa alielekezwa njia ya kufika

Ngalaba. Siku ilipowadia Majaliwa alianza safari alfajiri. Alikimbia kutwa nzima. Alasiri alifika kwenye

mto. Alikunywa maji na kupumzika kidogo. Baada ya kuvuka mto alikutana na mzee mwenye

kibiongo. Yule mzee na vijana wawili walikuwa wakichunga ng’ombe wengi sana. Majaliwa alipigwa

na butwaa kuwaona ng’ombe wengi vile. Majaliwa alimuuliza Yule mzee “iji ng’ombe jose ni ja

kweni?” Yaani hawa ng’ombe wote ni wa nani? Kwa bahati mbaya Majaliwa hakujua Kiswahili na

yule mzee mchungaji hakujua lugha ya Majaliwa. Kwa hiyo hawakuweza kuelewana. Yule mzee

akamwambia Majaliwa “sikuelewi” Majaliwa akaendelea na safari yake akiamini kuwa wale ng’ombe

wote ni mali ya mtu aliyeitwa Sikuelewi. Majaliwa akajisemea moyoni “Ama kweli sikuelewi ni tajiri.

Ng’ombe wote wale!”

MASWALI

186. Kwanini Majaliwa alifahamika sana kwao Mahama?...............................................................

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………

187. Majaliwa alipewa jina gani la utani na vijana wa rika lake?.......................................................

………………………………………………………………………………………………………………

188. “Majaliwa alishika usukani katika mbio” usemi huo una maana gani?

…………………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

189. Ni nani aliyemshauri mfalme kuwa wajaribu kupata dawa kutoka kwa Mganga fundi?............

………………………………………………………………………………………………………………

190. Mganga fundi alikuwa anaishi katika nchi gani?......................................................................

………………………………………………………………………………………………………………

Page 15: DARASA VI KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · Ni methali ipi inafanana na hii “udongo upate ungali maji”.. A. uchungu wa mwana aujua mzazi B. siku za mwizi ni arobaini C

EPUKA COVID – 19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

Kamilisha simu ifuatayo kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Mwandikie simu ya maneno matano dada yako Joanitha Mkomazi anayetumia anuani ifuatayo: S.L.P 2010 Arusha. Kumjulisha kuwa aje haraka mama yenu amelazwa. Jina lako ni Yohana Mkomazi JOANITHA MKOMAZI S L P 2010 ARUSHA

191. ………………………………………………………….

192. ………………………………………………………….

193. …………………………………………………………

194. ………………………………………………………….

195. …………………………………………………………. SEHEMU E: UFAHAMU Soma habari ifuatayo kwa makini kasha jibu swali la 41 – 45 kwa kujaza nafsi zilizoachwa wazi. Luka na Maria wamezaliwa na Job na Lisa. Baba yake Lisa huja mara kwa mara kuwasalimia na anapokuja huwa anakuja na Miki ambaye ni mtoto wa Zabloni. Zabloni ni kitinda mimba kwa akina Lisa. MASWALI 196. Lisa ni……………………..yake Zabloni. Kulingana na habari hii.

197. Zabloni anamwitaje Luka ambaye ni mtoto wa Lisa?........................

198. Baba yake Lisa anaitwa nani kulingana na habari uliyoisoma?.............

199. Miki anamwitaje Maria?...................................

200. Kutokana na habari uliyoisoma inaonekana kuwa Lisa ni………..wa Job.