uzazi katika utamaduni mpya mwongozo kwa wazazi wa...

80
© Spectrum Migrant Resource Centre Toleo la kwanza Juni 2009 Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongo

Upload: others

Post on 19-Jan-2020

13 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

© Spectrum Migrant Resource Centre Toleo la kwanza

Juni 2009

Uzazi katika utamaduni mpyaMwongozo kwa wazazi wa Kongo

Page 2: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 3: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

1

Kujitolea

Mwongozo huu umetolewa kwa wazazi wote wa Kongo wanaolea watoto wao nchini Australia.

“Ikiwamtotoanaishinaukosoaji,yeyehujifunzakukashifu.

Ikiwamtotoanaishinauhasama,yeyehujifunzakupigana.

Ikiwamtotoanaishinakejeli,yeyehujifunzakuwanahaya.

Ikiwamtotoanaishinauwoga,yeyehujifunzakuwanawasiwasi.

Ikiwamtotoanaishinaaibu,yeyehujifunzakuhisimwenyehatia.

Ikiwamtotoanaishinauvumilivu,yeyehujifunzakuvumilia.Ikiwamtotoanaishinahimizo,

yeyehujifunzakuwanaujasiri.

Ikiwamtotoanaishinakukubaliwa,yeyehujifunzakupenda.

Ikiwamtotoanaishinakutambulika,yeyehujifunzakuwanivyemakuwanalengo.

Ikiwamtotoanaishinauwazi,yeyehujifunzaukwelininini.

Ikiwamtotoanaishibilaupendeleo,yeyehujifunzahakininini.

Ikiwamtotoanaishinausalama,yeyehujifunzakuwanaimanikwakemwenyewena

walewaliokaribunaye.

Ikiwamtotoanaishinaurafiki,yeyehujifunzakuwaulimwengunimahalipazuripakuishi,

kupendanakupendwa.”

Asiyejulikana

Page 4: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

2

UtanguliziKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja kuhusu kumlea mtoto wako katika utamaduni mpya. Unaweza kuwa unashangaa jinsi ya kuainisha maadili ya utamaduni wako na yale yanayotumika kawaida na wazazi waliozaliwa nchini Australia. Je! watoto wako watakataa ao kusahau urithi wa utamaduni wao na lugha yao ya Kikongo? Je! watachukua fursa zinazopatikana kwao nchini Australia?

Ni kawaida kuwa na hoja hizi, lakini ni muhimu kwako kujua kwamba watoto wako wanaweza kukua watu wanaofanikiwa huko Australia, wakati pia wanajifunza desturi za utamaduni wa Kongo.

Mwongozo huu wa uzazi umeundwa kukusaidia kulea watoto wako katika nchi mpya.

Kwa kuja Australia, unaweza kukosa mwongozo kutoka kwa jamaa ambao kawaida wangesaidia uzazi wako huko nyumbani. Waweza kusita kutafuta ushauri kutoka kwa watu usiowajua ao wataalam nje ya familia yako. Mwongozo huu unapeana msaada bila kuamua njia nzuri na mbaya za kuwalea watoto wako. Tunapendekeza kwamba akina mama na baba wote wasome mwongozo huu pamoja.

Kitabu hiki cha mafunzo hukusaidia kukujulisha juu ya:

• maoni tofauti, maadili na mtindo watoto wako watapata shuleni na wakati wa kuingiliana na marafiki waliozaliwa Australia.

• Sheria za Australia kuhusu watoto, na majukumu yako ya kisheria kulinda watoto wako kutokana na madhara;

• hatua za kukua za kimwili, kijamii na kihemko ambazo watoto wako watapitia, wanapokua; na

• mazoezi ya kweli kwa akina mama na baba ya kutuatua hali ngumu ambazo zinaweza kutokea kwa vijana wako.

Jaribu kutokuwa na wasiwasi, na kumbuka kwamba wazazi wengine wengi wa Kongo-Australia ambao wamehamia Australia kabla yako, wamelea watoto wanaopendeza na waliofanikiwa na wamekuwa chanzo cha furaha na kujivunia kwa familia zao na kwa jamii nzima ya Australia.

Spectrum MRC inajaribu kuboresha huduma zetu kwa wazazi kila wakati tunapokusaidia kutulia hapa Australia. Tunatarajia majibu yako kwa mwongozo huu. Unaweza pia kufahamu juu ya huduma zingine kupitia maelezo yetu ya mawasiliano hapo chini.

Matamanio mema, Rosemary Kelada Afisa Mkuu Mtendaji

Page 5: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

3

Faharasa

Kujitolea ............................................................................................................ 1

Utangulizi ............................................................................................................ 2

Kipindicha1: Ulezi wa watoto wa Kongo-Australia katika utamaduni mpya ................ 5

Kipindicha2:Kuelewa jinsi mtoto wako hukua ....................................................... 11

Kipindicha3: Kusaidia watoto wako kukuza ujasiri ................................................ 21

Kipindicha4:Kuboresha lugha na ustadi wa kijamii wa watoto wako ...................... 25

Kipindicha5: Jinsi ya kuwasilisha hisia ................................................................. 29

Kipindicha6: Zuia vita na watoto wako ................................................................ 33

Kipindicha7: Jinsi ya kuwapa watoto wako nidhamu ............................................. 39

Kipindicha8: Kusimamia kufadhaika kwa familia ................................................... 45

Kipindicha9: Kukabiliana na vijana ..................................................................... 48

Shukrani .......................................................................................................... 57

Je! Nawezaje pata nakala ya mwongozo huu?

Unaweza kupata nakala za kuongezea za mwongozo huu kwa:

• Kuchapisha nakala kutoka kwa tovuti yetu - www.spectrumvic.org.au

• Kutembelea ofisi yetu kuu - 251 High Street, Preston, Victoria

• Kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia simu (+61) (03) 9496 0200

Page 6: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

4

Page 7: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 1 :

Ulezi wa watoto wa Kongo-Australia

katika utamaduni mpya

Page 8: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 9: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

5

Kipindi cha 1: Ulezi wa watoto wa Kongo-Australia katika utamaduni mpyaKatika kitabu hiki cha mwongozo, tunajadili maadili ya Kikongo, tamaduni na desturi kama zinavyohusiana na ulezi wa watoto.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi kubwa katika Bara la Afrika na ina idadi ya watu milioni 62. Ni nchi ya savana, mabonde na milima iliyozingirwa na mito na misitu mingi ya mvua.

Ukulima, ufugaji mifugo, uvuvi na uwindaji imekua kazi ya kimila kwa muda mrefu. Hata hivyo, wakati wa ukoloni wa Ubelgiji, jamii iligawanywa katika maeneo ya mashambani na mjini kwa tasnia ya uchimbuzi. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliundwa baada ya uhuru mnamo 1960.

Wamishenari wakristo walikuwa na athari kubwa kwenye jamii ya Kikongo na Wakatoliki walikuwa na mtandao mzuri wa makanisa, shule na hospitali. Lakini desturi za kimila zinapatikana sana na kuna dini zenye msingi wa Kikongo-Kikristo zilizoingiliana na desturi za kikabila.

Kifaransa ndio lugha rasmi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kiswahili, Lingala, Chiluba na Kongo ndizo lugha nne za kitaifa.

Maadili ya familia za kikongo

Watoto wa kongo wanathamaniwa sana na wanazingatiwa kama bima ya siku za usoni kwa wazazi. Lakini uzazi wa Kikongo ni wa kijamii kuliko kibaiolojia. Katika utamaduni anuwai wa maeneo ya mjini, marafiki na majirani wa familia wana uwezo wa kusemea watoto. Mtoto aliyezaliwa ni wa jamii nzima, ambayo inatambua karamu ya kumkaribisha ili kushukuru kuzaliwa kwake. Kukusanyika katika hafla kama hii, watu hunena methali ya wahenga wao:

“Kuzaa ni raha, kulea watoto ni changamoto”.

Kimila, utamaduni wa Kongo unathamini mahusiano na umoja zaidi kuliko fedha. Hali ya umoja ndio msingi wa familia na wa kijiji ni mahali ambapo wazazi na watoto katika jamii kubwa wanaishi, kufanya kazi na kusaidiana kwa moyo wa umoja. Hata katika maeneo ya mjini ya anuwai ya utamaduni, watu kawaida huwa na elimu ya nje na wajirani hushiriki jukumu la kutunza watoto.

Walakini, katika miaka ya hivi karibuni mawazo ya utamaduni, wakati, umoja, imani na familia zimebadilika na jamii ya kisasa ya Kikongo imejawa na wazo la pesa. Familia sasa inakuwa ya kibaiolojia zaidi kuliko ya kijamii na inaweza kushindwa kutosheleza mahitaji ya nyenzo, kisaikolojia na kijamii ya wahusika wake.

Utamaduni wa Kikongo ni kali zaidi – vijana lazima waheshimu wazee na lazima watu waheshimu wenye sheria zao.

Page 10: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

6

Hali ya kijamii ni muhimu sana kwa mtu binafsi kutoka kuzaliwa hadi kufa - hata mtoto anatendewa kulingana na kiwango chake cha kijamii. Kuwa baba ao mama ni kazi za kijamii na wazazi lazima wafuate hali yao na jukumu lao.

“Fuata hali yako, nitafuata yangu”.

Wakongo wanafikiria watu kwa msingi wa nguvu juu ya vitu ao watu. Mtu ni mdhaifu ao mwenye nguvu kuliko mwingine, kulingana na hali yake ya kijamii, jukumu na kizazi yake. Watu wa umri mmoja ni sawa kwa sababu ni wa kizazi kimoja. Wao hucheza, hushiriki chakula na kitanda usiku. Wazazi - akina baba, shangazi, akina mama na wajomba - ni wa kizazi kinachokua. Wanawakilisha ukali, maadili ya wahenga na sheria duniani. Wana mamlaka juu ya watoto wao, mpwa, yanayolazimishwa na uwezo wao wa kuwalaani.

Mamlaka ya baba juu ya watoto wake hulinganishwa kila mara na ule wa babu, ambaye ana mamlaka juu ya mwanawe, baba ya watoto. Yeye ndiye msiri wao, mlinzi, hata mshirika wao. Kukitokea kulalamika, wanaripoti kwa babu yao ambaye atatatua swala hili na baba yao.

Njia ya kimila ya kutatua matatizo ilikuwa ‘baraza’. Watu wangekutana chini ya mamlaka ya mzee wa familia ao wa jamii. Lengo la baraza lilikuwa kufikia jibu linalofaa kwa kila mtu. Inaweza kuchukua muda, lakini kufikia makubaliano ambayo yanaweza kukuza amani kati ya jamii ilikuwa inafaa kutumia wakati huo.

Nyakati za zamani, wanakijiji walishiriki mali na waliabudu mhenga sawa. Matukio ya mabaya yalifikiriwa kuwa juu ya hasira za wahenga ambao waliondoa ulinzi wao kutoka kwa mtu aliyewakosea. Ili kumrudi mtu aliyekosa, jamii ilikuwa na kutafuta njia ya kijamii kama kinaya, udhihaki, kutokubali na hata kufukuzwa.

Huko Kongo, kabila zingine ni za urithi wa kotoka kwa baba na zingine ni za urithi wa akina mama. Hii inabaini muundo wa familia na watu kwenye mamlaka. Filisofia ya waume kuwa na mamlaka umeshawishi utamaduni wa Wakongo. Hata katika utamaduni wa urithi wa kutoka kwa mama, mjomba ndiye mtu mwenye mamlaka juu ya watoto.

Waume na wake kijijini wanathamaniwa kulingana na ni nani anayebaki kijijini baada ya ndoa. Katika mifumo yote mbili, mahari kutoka kwa dada aliyeolewa inaruhusu familia ‘kumuoza’ ndugu/kaka yake.

Maadili ya familia ya Kongo inchini Australia leo

Wakati mengi yamebadilika katika vizazi vya sasa, maadili ya mila za Kongo zinaendelea kushawishi maisha ya familia. Wakati unaweza kuwa hulei watoto wako kwa njia sawa na vile ulilelewa na wazazi wako, unaweza bado kutumia mila na desturi sawa za Kikongo.

Njia za Kikongo za kulea watoto wakati mwingine ni chanzo cha mzozo wa kitamaduni nchini Australia:

• Akina baba na mama wa Kongo wana mapatano kali ya kihemko na watoto wao

Page 11: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

7

Maadili ya familia za Kikongo Maadili kamili ya familia za Kiaustralia

Wavulana wa Kongo wanapewa uhuru mwingi kuliko wasichana kuchangamana nje ya familia.

Wavulana na wasichana wanatendewa sawa

Utiifu mkali unaonyeshwa kwa wazazi, haswa baba.

Watoto huuliza wazi juu ya maamuzi ya wazazi wao

Watoto wanatarajiwa kufikia malengo ya wazazi wao ya kielimu na kitaalam

Watoto wanahimizwa kuweka malengo yao binafsi

Akina baba ndio wafanyao uamuzi Akina mama na baba hufanya uamuzi pamoja

Watoto wana jukumu la kutoa msaada wa mhemko na kifedha kwa wazazi wazee

Watoto wanahimizwa kujitegemea na hawana wajibu kwa wazazi wao

lakini akina baba kawaida huwajibika katika kuwapa watoto wao nidhamu. Hapa Australia, walimu na wengine wanaweza kufikiria akina baba wa Kongo wana tabia ya hali ya mamlaka na mhemko wa mbali, na maoni yoyote wanayoweza kutoa yanaweza kuchanganyikisha mtoto.

• Akina mama Wakongo hukuza uhusiano wa karibu na wa kukuza na watoto wao. Katika Utamaduni wa Anglo-Australia, akina mama na baba hushiriki ukuzaji na kufanya uamuzi juu ya maswala ya familia.

Kimila, watoto wa Kongo lazima watii wazazi wao kuanzia kuzaliwa hadi kufa haijalishi hali gani imetokea. Lakini mambo yanabadilika – katika jamii ya kisasa ya wakongo, wazazi wanaweza kuruhusu watoto wao wachague

taaluma, haswa wakati watoto wameenda shule, na wazazi wao hawajaenda shuleni.

Ni aibu wakati mtoto anakataa kutii na anaenda ‘njia zake’. Hii huleta aibu kwa familia na wazazi ‘hupoteza nafasi’ kati ya jamaa na jamii. “Usinifanye nipoteze nafasi ao uiletee familia yangu aibu” ni maneno ya kawaida ambayo mzazi mkongo hurudia kwa mtoto wake.

Watoto wa Kongo wako wazi kwa maadili ya Kiaustralia na vijana wanaweza kufanya uamuzi juu ya siku zao za usoni bila kuwasiliana nawe. Hata ikiwa malengo yao na hamu zao ni tofauti na zako, unaweza kuhisi kuumizwa na kukasirika na watoto wako.

Jedwali hili linafafanua baadhi ya tofauti kati ya maadili ya familia na desturi za Kikongo na Kiaustralia.

Page 12: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

8

Watoto wanatarajiwa kuonyesha kujivunia utamaduni wao

Watoto wanaruhusiwa tu kufuata mila za familia ambazo zinawapendeza

Msimamo wa kijamii wa familia uko kwa msingi wa ishara za kitamaduni za hali ya juu: • kupata masomo ya juu zaidi • kuingia katika utaalam unaohusiana na elimu

Msimamo wa kijamii wa familia ni kwa msingi wa kijamii na ishara za kiuchumi za mafanikio: • kuwa na watoto katika shule za kibinafsi • kuwa na nyumba katika mitaa ya wastani • kuwa na kazi inayolipa vizuri

Watoto wazima hubaki kuwa karibu na wazazi na huendelea kutii matarajio ya wazazi wao, pamoja na kuruhusu wazazi wao kuidhinisha wapenzi wao wa ndoa

Watoto wazima wanajitegemea kifedha na huchagua waume na wake wao wenyewe

Jamii huaibisha familia nzima ikiwa watoto hawafuati maadili ya kidini na kitabia

Jamii huhukumu watoto vibaya- sio familia ikiwa watakosa ao watakamatwa na polisi

Wazazi hutumia njia yoyote ya kuwapa nidhamu pamoja na adhabu ya kimwili.

Adhabu ya kimwili ni nadra kutumika na haihimizwi

Wazazi hawawezi kucheza na watoto wao Wazazi hucheza michezo ya ndani na nje na watoto wao kwa kawaida

Wao hutumia wakati wao na wajomba, shangazi, nyanya/bibi na babu na wazee ambao huchukua jukumu muhimu katika elimu ya kingono ambayo huonekana kama mada ‘mwiko’ kwa wazazi.

Walimu na wazazi huwafunza watoto wao elimu ya kingono

Page 13: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

9

Uzazi mzuri

Ni njia ipi bora zaidi ya kulea watoto? Kila utamaduni na kila familia una njia yao, na mwongozo huu haufanyi uamuzi wowote kuhusu njia ipi ni bora zaidi. Jambo moja la kuzingatia ni kutumia kanuni za ‘uzazi bora’. Hii inamaanisha kufanya mambo ili kusaidia watoto wako kukua, kuongeza ustadi wao na kuthibiti tabia yao. Inajumuisha kuelewa njia ambayo watoto wako hufikira, kuwafanya wakusikize na washukuru mahitaji yao mengi katika kila hatua ya kukua.

Uzazi mzuri unaweza fanywa kutangamana na kila tamaduni. Unahusisha mambo matano muhimu ambayo unaweza kufanya kwa watoto wako:

1. Peana maisha ya nyumbani salama na bila hofu; 2. Wasaidie kujifunza; 3. Wafunze jinsi ya kukabiliana vyema na mizozo; 4. Kuwa na matarajio yanayowezekana; 5. Jitunze vyema

Kuwa mfano mzuri

Kumbuka kila mara kwamba moja ya ushawishi mkubwa kwa watoto wako utakuwa wewe. Watoto wako hukuangalia na huiga jinsi wewe hufanya mambo. Fikiria juu ya wazazi wako wenyewe wakati ulipotaka kuwa tofauti nao kwa njia kadhaa, kuna njia nyingi ambazo unafanana nao. Kuwa mfano mzuri kwa watoto ni njia hakika ya kuwaweka karibu wanavyoendelea kukua.

Kutatua matatizo

Sehemu nzuri ya kuanza kuzuia matatizo ya siku za usoni na watoto wako ni kujifikiria mwenyewe na njia ambayo ulilelewa. Jiulize maswali kadhaa.

Page 14: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

10

KidoKezochamazoezi:Fanyahiinamumeaomkewako,inapaswakuchukuachiniyasaa1.

ZoeZi 1

Kufikiria juu ya jinsi unavyolea watoto wako

Jibu maswali yafuatayo juu ya jinsi unapanga kuwalea watoto wako. Jadili majibu na familia yako ao washiriki wa kikundi cha kujadili.

1. Ulitarajia nini kwa wazazi wako?

2. Wazazi wako walitarajia nini kwako?

3. Unatarajia nini kwa watoto wako?

4. Watoto wako wanatarajia nini kwako kama mzazi?

5. Unajivunia nini katika utamaduni na mila za Kikongo?

6. Ni maadili yapi ya mila na tamaduni unafikiria yanahitaji kubadilishwa ili kusaidia watoto wako kukubaliana na maisha ya Australia?

7. Uko tayari kuyabadili? Kama ni hivyo, kivipi?

Page 15: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 2 :

Kuelewa jinsi mtoto wako hukua

Page 16: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 17: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

11

Kipindi cha 2: Kuelewa jinsi mtoto wako hukua

Kila mtoto ni tofauti lakini sawa

Kama mzazi umeona kwamba kila mtoto ni wa kipekee. Ni watu binafsi, kama wewe na mke ao mume wako, na mahitaji yao hubadilika wanavyokua. Lakini kuna hatua tano muhimu za kukua ambazo sio kawaida kwa watoto wote.

Kuelelewa hatua hizi tano kutakusaidia kutambua mahitaji ya mtoto wako ya kimwili, kihemko na kijamii.

• Kuweka watoto wako kwa usalama kunamaanisha kuwa haufai kuwaumiza kimwili kwa kuwachapa kwa nguvu. Nchini Australia sheria inakataza mtu yeyote, pamoja na wazazi kutokana na kuadhibu watoto kimwili.

• Wewe na mkewe ao mumewe mnaweza kufanya kazi nje ya nyumba Wazazi wengi hujipata wakifanya kazi kwa masaa marefu na wakati wanakuja nyumbani wana shughuli nyingi zingine kama kusafisha nyumba. Waweza kuwa umechoka na kuwa na wakati mfupi wa kucheza ao kuzungumza ao kuungana na shughuli za familia wakati wa wikendi. Jadili na mume ao mke wako jinsi ya kulinganisha masaa yako ya kazi na unaweza tumia wakati gani na watoto wako.

• Katika jamii ya Australia, inafikiriwe kuwa muhimu kwa mtoto wako kuchangamana na watoto wengine wa asili zote. Kuhudhuria vikundi vya mchezo, kutembelea maktaba na kusajili mtoto wako katika shule ya mtaani ya watoto ni njia nzuri za kuanza kuchangamana na wazazi wengine na watoto wadogo.

Kiwango cha 1 – Utegemeaji

Kiwango cha 2 – Usalama na Ulinzi

Kiwango cha 3 – Upendo

Kiwango cha 4 – Utambuzi

Kiwango cha 5 – Kujielezea mwenyewe

Page 18: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

12

KidoKezo:alikawazaziwenginewaletewatotowaokuchezanyumbanimwakobaadayashule nawakatiwalikizozashule.

• Ni muhimu kwamba umsifu watoto wako wakati wanajifunza ao kujaribu mambo mapya. Haupaswi tu kuwasifu wakati wanaipata sawa. Ikiwa wanakosolewa kila mara, kukashifiwa ao kuchekewa wakati wanajaribu kufanya kitu wao wenyewe, watoto wataacha kujaribu. Watoto wako wanasifiwa na walimu wakati wanafanya jambo vizuri, wanafanya hima ao wanaonyeshe ubora katika somo ambalo limekuwa likiwatatiza. Hata wakati mtoto hafaulu shuleni, mwalimu wao atawahimiza na kuwapa mapendekezo jinsi ya kufanya vyema na kujaribu tena. Hii ni kwamba watoto wajifunze kufurahia kufanya bidii kwa jambo kama kusoma na kuandika na kuendelea kujifunza. Mara tu wanapojifunza ustadi, watapewa kitu kigumu zaidi ili waendele kuboresha. Kwa kuchukua hatua hii unawafunza watoto wako kwamba kusoma ni raha na kuwa mzuri kwa jambo kunahitaji kuendelea na mazoezi mengi. Je! wewe husifu watoto wako?

• Watoto wanaweza kuwa na nidhamu kupitia himizo mzuri. Sifu watoto wako wakati wowote wanapofanya vyema na wapuuze wanapofanya vibaya. Watahisi kuadhibiwa wakati una wapuuza. Watoto wako wanatamani kuzingatiwa nawe hata wakati ni kwa tabia mbaya. Kwa kuondoa kuwazingatia wakati mtoto wako anakosea, labda wataacha tabia mbaya.

• Walimu nchini Australia kawaida hawatawasiliana nawe wakati mtoto wako hafaulu ao anakosa shuleni. Unaweza kuzungumziwa na shule tu kwa dharura kama ajali mbaya, udhalimu ao ikiwa mtoto wako atakuwa mgonjwa akiwa shuleni.

• Utaalikwa kukutana na walimu wa watoto wako katika mahojiano ya mzazi na mwalimu. Katika mahojiano mwalimu wa mtoto wako atakupa habari nyingi juu ya jinsi mtoto wako anafanya katika kila somo shuleni na katika tabia yao katika darasa na katika uwanja wa shuleni.

KidoKezo cha Uzazi: mtoto wako mdogo hujifunza vyema kupitia michezo haswa ikiwainakuhusishaweweaowatotowengine.Kutazamaruningakunapaswakupunguzwanakusimamiwawakatiwotenamtumzima.

Page 19: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

13

ZoeZi 2 Kutimiza mahitaji ya ukuaji wa watoto wako

Fikiria hatua tatu unazoweza kufanya kupeana mahitaji ya watoto wako katika kila kiwango cha kukua.

Kiwango cha kukua Mahitaji Hatua za wewe kuchukua

Kiwango cha 1: Utegemeaji

Chakula, kinywaji, usingizi

Mfano: kulishwa kwa matiti ao chupa 1. 2. 3.

Kiwango cha 2: Usalama na Ulinzi

Kuzingatiwa kimwili, utaratibu mzuri, uhuru wa kuvumbua mazingira yao

Mfano: Weka ua unaozingira dimbwi lako la kuogelea, funza sheria za barabara 1. 2. 3.

Kiwango cha 3: Upendo

Upendo, kuingiliana kijamii, urafiki, na mapenzi

Mfano: cheza michezo kama familia na onyesha wazi upendo na mapenzi 1. 2. 3.

Kiwango cha 4: Utambuzi

Kuhisi ukiwa na mamlaka na wa muhimu, kujua ustadi, kuboresha ujasiri

Mfano: sifu watoto kwa kujaribu shuleni na katika shughuli ambazo zinawapendeza 1. 2. 3.

Kiwango cha 5: Kujielezea mwenyewe

Kuwasiliana na wengine katika hali tofauti na kupata kujua nguvu na udhaifu wao

Mfano: sikiliza watoto wako na waulize maswali juu ya jinsi wanavyojiona na wengine walio karibu nao 1. 2. 3.

Page 20: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

14

Kuweka watoto wako salama kimwili

Watoto wako kwenye hatari zaidi ya miaka ya mapema ya shule. Kuweka watoto wako salama kupitia usimamizi wa mtu mzima ni jambo unapaswa kufanya kila wakati.

Kuzaliwa hadi miaka 3

Katika miaka hii, watoto:

• Kawaida hutaka kujua na kujifunza kwa kugusa, kuhisi na uvumbuzi;

• Kuvumbua chochote ambacho kina- wapendeza, kawaida kwa kukiweka mdomoni mwao;

• Kunywa chochote (haijalishi ni nini);

• Kama vifaa vya kuchezea na vitu vingine jongevu, vyenye muziki ao kelele;

Wako kwenye hatari ya kunyongwa, kupewa sumu na kuchomeka, ao kupata ajali zingine, ikiwa wataachwa bila usimamizi.

Miaka 3 hadi miaka 5

Katika miaka hii, watoto:

• Huacha kuweka vitu midomoni mwao;

• Huhisi, hugusa na kuvumbua maeneo mapya na mawazo kidogo ao kuelewa hatari zilizoko;

• Huanza kukuza kujitawala kiasi, na huanza kufuata sheria fulani juu ya kula, kucheza na kulala.

• Hufurahia kucheza michezo nawe na hupenda kucheza wenyewe, wakiiga mambo fulani ambayo wewe hufanya kama kupika, kucheza na wanasesere na gari za mchezo.

Jeraha la ajali ndio sababu kuu ya kifo kati ya watoto nchini Australia. Ajali kama hizo hutokea mara nyingi kwa sababu hakuna tahadhari zinazochukuliwa. Kwa habari zaidi juu ya jinsi unavyoweza kulinda mtoto wako kutokana na hatari ya kimwili tembelea www.kidsafevic.com.au ambapo makaratasi ya habari yanaweza kupakuliwa bila malipo.

Kusaidia kukua kiakili na kihemko kwa watoto wako

Kutoka 0 hadi miezi 18 – Kukuza imani na kuingiliana

Kama mama wa mkongo utakuwa mawasiliano wa kudumu na mtoto wako, ili kumpa joto kitandani, mikononi mwako, kwa mikono ya wageni na mgongoni mwako. Utamnyonyesha wakati wowote anapolia. Pengo kati yako haijazwi na vitu kama chupa ya maziwa, kitanda cha mtoto, chuchu ao vifaa vya kuchezea.

Watoto hujifunza kuamini na kukuza upendo kwa wazazi wote ikiwa tu mahitaji yao yanatimizwa. Wanahitaji taratibu za kulisha, kulala, kuoga na kucheza.

Ikiwa nyumba ina mizozo, mtoto anapuuzwa, ao mama huwa mgonjwa kila mara ao anafadhaika, mtoto anaweza kuwa na upendo usio salama na wazazi wake. Hii inaweza kusababisha matatizo

Page 21: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

15

ya kudumu ya mhemko kama kutojistahi, ugumu kwa kuongea, matatizo ya kula, ukosefu wa usingizi, matatizo ya kukuza urafiki ao kuhisi kutengwa na wazazi.

Kutoka miezi 18 hadi miaka 3 – Kukuza kujitawala ao aibu

Katika mila ya Utamaduni wa Kongo, wakati mtoto wako anatembea unawacha gafla kumnyonyesha na unampeleka kuungana na kikundi cha rika yake.

Mtoto mchanga anajifunza kwamba ni mtu tofauti na wewe,kwa mfano wanaweza kujitambua kwa kioo. Kutoka miezi 18, wanaweza kuanza kuitisha vitu ao kukataa vitu kwa kusema ‘hapana’. Watoto wachanga hujaribu kufanya vitu kama kula na kunywa wenyewe. Wanaweza kusema “naweza kufanya” ao “acha nifanye”.

Katika hatua hii ni muhimu kuweka sheria wazi wakati mtoto wako anakosea haswa wakati wanatenda kwa njia zinazoweza kusababisha madhara.

Kuanzia miaka 4 hadi 6 – Uvumbuzi ao Hatia

Kukua kwa akili ya mtoto wako kutaongezeka wakati wa miaka hiyo. Ni hatua ya kwanza ambapo mtoto wako atafanya kazi mwenyewe kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mtoto wako atatumia fikira yake na kucheza michezo aliyotafakari.

Unahitaji kuhimiza mtoto wako wakati anajaribu kujifunza ustadi mpya kama kula na kijiko na

umma ao kujaribu maneno mapya. Weka sheria wazi juu ya usalama wa kibinafsi wakati wa kuvuka barabara, heshimu watu walio na mamlaka, taratibu nzuri za usafi kama kuoga na kupiga mswaki. Unaweza pia kuanza kuwafunza sheria za tabia njema kama kutodanganya ili kuepuka adhabu na kujifunza kutimiza ahadi.

Kuanzia miaka 6 hadi 9 – kukuza uwezo

Katika miaka sita, msichana wa Kikongo tayari anaitwa ‘mama mdogo’. Anaweza kuchukua nafasi ya mama yake nyumbani. Kutoka kwa mama yake, tayari amejifunza jinsi ya kutunza wadogo wake, hata baba yake.

Nchini Australia, watoto katika kikundi hiki cha umri huhusika katika ulimwengu wa nje kupitia shule. Wanatarajiwa kujifunza kusoma na kuandika, kucheza na watoto wengine na kuzungumza na walimu wao.

Watoto ambao hufanya vyema katika hatua hii hupata marafiki rahisi na hufurahia michezo ya kikundi, hufurahia taratibu za shule na hujifunza kutokana na makosa hata kama ni mbele ya wenzao. Watoto ambao hawafanyi vyema wanaweza kuepuka kwenda shule.

FKuanzia miaka 10 hadi 15 – miaka ya ujana

Kipindi hiki huanzisha kubadilika kutoka utoto hadi kuwa utu uzima. Inaweza kuwa ngumu na kusababisha hofu kwako kama mzazi na kwa familia nzima. Kijana wako sio mtoto

Page 22: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

16

tena, lakini bado hajakuwa mtu mzima. Vijana hupitia kutolewa kwa homoni za kukua ambazo husababisha mabadiliko ya kimwili kwenye viungo vya uzazi, nywele, chunusi na sauti. Homoni za kukua huathiri hisia za vijana wako. Wanaweza kujaribu tabia za hatari kama kuvuta sigara ao kuendesha gari bila leseni ambayo huonekana ya kijinga na kusababisha vita nawe.

Kila mzazi anayelea kijana anahitaji kufanya bidii kwa kuendelea kuwasiliana wazi hata wakati kijana wako haonekani kutaka kuongea nawe ao mtu mwingine kwenye familia.

Inawezakuwa kawaida kwa kijana wako kutumia wakati katika chumba chao cha kulala kuzungumza kwa simu na marafiki wao ao kuvinjari mtandao. Kumbuka hata kama mtoto wako wakati mwingine anatenda kama hakupendi kamwe, wewe bado una ushawishi mkubwa na bado anahitaji idhini yako hata kama anaonekana kukataa maoni yako.

Kijana wako atataka kutumia wakati wake mbali na familia na atahitaji uhuru zaidi ili kushirikiana na marafiki wake. Wazazi wengi lazima wajadiliane sheria mpya na vijana wao kuhusu kazi ya nyumbani kutoka shule, kutoka nje wikendi na usiku za shule, kuhudhuria kanisa ao msikiti na kile wanachoruhusiwa kuvaa.

Kijana wako anaweza kutaka kutafuta kazi ya kulipwa baada ya shule ili waweze kuweka akiba ya pesa yao. Ni jukumu lako kama mzazi kusaidia kijana wako kufanya uamuzi mzuri kuhusu mambo haya yote,na kuhakikisha kwamba maamuzi hayabadiliki na malengo ya

siku za usoni za kijana wako. Ikiwa wanataka kufanya vyema shuleni, lazima uwakumbushe juu ya umuhimu wa kulinganisha muda wanaotumia kwa kazi ya baada ya shule na ule wa masomo yao.

Page 23: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

17

ZoeZi 3

Kusaidia kukua kiakili na kihemko kwa watoto wako

Je! unatimiza vipi mahitaji ya watoto wako kwa afya ya kudumu ya kiakili na kihemko? Jibu ‘ndio’ ao ‘la’ kwa majibu yaliyoko hapo chini.

Kutoka 0 hadi miezi 18 – Kukuza imani na kuingiliana

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Wewe huongeza sauti yako karibu na mtoto wakati analia?

Wewe huangalia macho ya mtoto, humkumbatia na kutabasamu?

Wewe hurudia ao kuiga sauti ambazo mtoto wako hufanya?

Wewe huwa mvumilivu kwa mtoto wako hata ikiwa analia na hauwezi kumtuliza?

Wewe hutumia vifaa kumtuliza mtoto wako anapolia?

Kutoka miezi 18 hadi miaka 3 – Kukuza kujitawala ao aibu

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Unaelewa kwamba mtoto wako anahisia ya umilikaji kuhusu vifaa vyake vya kuchezea na wakati mwingine yuko tayari kuzishiriki?

Unaruhusu watoto wako kuvumbua mazingira yao kwa kugusa vitu tofauti?

Unahimiza mtoto wako kujiunga katika kucheza na watoto wengine?

Unajibu maswali ya mtoto wako kuhusu miili yao?

Page 24: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

18

Kuanzia miaka 4 hadi 6 – Uvumbuzi ao Hatia

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Unahimiza mtoto wako kufurahia kusoma, kucheza hadithi azipendazo na kuchora michoro yao?

Unajua kwamba watoto hujifunza kusoma na kuandika na jina lao wenyewe katika hatua tofauti?

Wewe husifu mtoto kwa kujaribu, hata kama watashindwa na jambo?

Uliza mtoto wako ni kwanini anarudia tabia fulani ‘mbaya’?

Unafundisha watoto wako kutimiza ahadi kwa kutimiza yako mwenyewe?

Unaonyesha watoto wako kusaidia watoto wengine wakati wamekasirika ao wako na hofu?

Kuanzia miaka 6 hadi 9 – kukuza uwezo

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Unatumia wakati na mtoto wako kila siku ili kumruhusu azungumze juu ya siku yake?

Unamsikiliza vizuri mtoto wako anapoonyesha wasiwasi unaoonekana ni ndogo kwako?

Unaangalia watoto wako wanapocheza michezo ya timu?

Unahimiza watoto wako kutatua matatizo yao kibinafsi hata kama suluhisho ni tofauti na zako?

Page 25: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

19

Kuanzia miaka 10 hadi 15 – miaka ya ujana

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Unaambia kijana wako unampenda na unamkubali bila kikwazo?

Unasikiliza maoni fulani ya kijana wako ambayo ni tofauti na yako?

Unahimiza kijana wako kuonyesha jinsi anavyochukua wajibu wa matendo yake?

Unasaidia kijana wako kuweka malengo yake mwenyewe na hatua ambazo watachukua kuyafikia?

Unahisi sawa kusema ‘hapana’ kwa kijana wako wakati anataka kitu?

Unafurahia mafanikio maalumya kijana wako?

Page 26: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

20

Page 27: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 3 :

Kusaidia watoto wako kukuza ujasiri

Page 28: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 29: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

21

Kipindi cha 3: Kusaidia watoto wako kukuza ujasiri

Je! kujistahi ni nini?

Kujistahi ni mkusanyiko wa imani ao hisia ambazo tunazo juu yetu. Kwa watoto wadogo, kujistahi ni juu ya jinsi wanavyohisi kukubalika na kuthaminiwa na watu ambao muhimu kwao.

Watoto ambao na kujistahi sawa huhisi kukubalikwa, kutunzwa na salama. Watoto ambao na kujistahi kulio chini huwa hawahisi salama ao sawa na washiriki wa familia yao na wanaweza kuamini kwamba hawapendwi ao hawastahili kupendwa.

Kujistahi ni muhimu kwa halinjema ya siku za usoni na furaha ya mtoto wako.

Kujistahi katika familia za Kikongo

Katika mila ya utamaduni wa Kikongo, kujistahi kwa mtoto ni kwa msingi wa jinsi familia inazingatiwa na jamii ya kawaida. Familia lazima ifuate historia ya Kongo, desturi za kimila na kidini, na inaendelea kwa njia unavyolea watoto wako.

Wahamaji wengi wa Kongo-Australia hawajakuja Australia kwa hiari yao. Wengi wao walitoroka nchi yao kama wakimbizi na wanusuru wa vita ao maongozi ya kisiasa ya kugandamiza. Ikiwa hauna chaguo la kuondoka nchi yako, hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa kujistahi kwa familia yako. Waweza kuhisi hisia hizi mbaya zikipanda ikiwa watu watakutendea tofauti ao kama mtu wasiojua katika nchi yako mpya ao ikiwa hauwezi tena kuishi kwa njia ya kitamaduni.

Familia za Wakongo kawaida hazihimizi juu ya kukuza kujistahi wa kipekee.kwa watoto wao. Nchini Australia, watu wanatarajiwa kufaulu ao kutofaulu kwa sifa zao wenyewe na wanaweza kujihukumu vibaya wakishindwa. Mtoto wako anaishi katika tamaduni ambayo kujistahi na hisia zake kuhusu kufanikiwa kwake ao kushindwa ni muhimu kwa taaluma yake ya siku za usoni.

Kama wazazi, mnahitaji kujua jinsi ni muhimu kwa watoto kukuza kujistahi.

Page 30: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

22

Jedwali lifuatalo linaonyesha mafanikio kutokana na kusaidia watoto wako kukuza kujistahi kwao.

Watotowalionakujistahikuzurimaranyingi: Watotowalionakujistahikubayamaranyingi:

• Huhisi kuthaminiwa na familia na jamii

• Hutenda kwa kujitegemea

• Hujivunia mfanikio yao

• Hukabiliana na dhiki na huendelea kujaribu

• Hukabiliana vyema na mihemko mbaya

• Huchukua wajibu wa makosa na matendo yao wenyewe

• Huhisi wamejifunza kutokana na kutofaulu kwao.

• Huhisi hawapendwi na sio muhimu katika familia na jamii yao

• Huepuka kujaribu mambo mapya

• Hulaumu wengine kwa kushindwa kwao

• Huhisi dhiki wakati mambo hayaendi walivyotarajia

• Huathiriwa virahisi na wengine

• Hujiwekea thamani ndogo kwa vipawa na ustadi wao

• Hukimbilia uhasama.

Kama mzazi una jukumu muhimu katika ukuzaji na kuboresha kujistahi kwa watoto wako. Inajumuisha kuwatendea kama watu ambao na mahitaji yao wenyewe, kuwazungumzia kuhusu tabia yao na kuwapa fursa za uzoefu.

Kuboresha kujistahi kwa watoto wako

Kuna njia kadhaa za kusaidia kuboresha kujistahi kwa watoto wako. Soma vidokezo vifuatavyo nao na familia yako.

1. Unganisha watoto wako na siku zao zamani

Ili kujenga kujistahi kwa watoto wako, ni muhimu:

• Wajue kuhusu na wajivunie urithi wa familia yao wa Kongo; • Waelewe jinsi wanavyotoshea nchini Australia na utamaduni wao; • Wawe na matumaini juu ya siku zao za usoni.

Page 31: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

23

ZoeZi 4

Kukuza majivuno katika urithi wa watoto wako na nchini Australia

Waweza kusaidia kuunganisha watoto wako na siku zao za zamani kwa kukuza majivuno yao katika urithi na maoni mazuri ya utamaduni wa Australia vile vile.

Jadili na familia juu ya hadithi, picha, vitabu, nyimbo na filamu ambazo unaweza kushiriki na watoto wako ambazo zinaweza kuongeza kuelewa kwao juu ya:

• Wazazi wako na akina bibi na babu, nyumbani asili, mizizi ya kikabila, uhamaji na makazi, furaha na ugumu uliopitia;

• mahali pako pa sasa katika jamii ya Australia na jukumu lako katika jamii ya kawaida;

• kushiriki kwako katika shughuli za kijamii, michezo, kidini na zingine;

• malengo yako na ndoto za siku za usoni kwa familia yako;

• matumaini yako kwa siku za usoni za watoto wako na jinsi zimebadilika baada ya muda;

• desturi zako za lugha na utamaduni, na ni kwa nini ni muhimu kwako na kwa washiriki wengine wa familia.

Page 32: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

24

2. Jifunze kusifu watoto wako

Watoto wako wanahitaji kusikia maoni yako ya kuwahimiza ili wahisi vizuri wenyewe. Hakuna mtoto ambaye mkamilifu kwa hivyo kumbuka mtoto wako atakuwa na nguvu na udhaifu. Uwe wazi kila mara unapowasifu na zungumza nao kuhusu maeneo ambayo wanahitaji kuboresha bila kukosoa sana.

Taja nguvu zao za kweli, haswa ikiwa wanahisi wajinga ao wana shida kujifunza kitu kipya. Wakumbushe kwamba wakati mwingine inachukua muda na mazoezi mengi kuwa mzuri kwa jambo fulani, na hautafika juu kabisa kila wakati hata ikiwa unaipenda sana. Polepole mtoto wako atajua nguvu zao fulani na udhaifu wao na ataanza kuelewa na kujiamini.

Unahitaji kutoa sana na kuwa mkarimu. Usisahau kuwasifu watoto wako kwa:

• Kusema “nakupenda, haijalishi ni nini”;

• Kuwaambia kuwa umefurahi na umebahatika kuwa nao kama watoto wako;

• Kuwasaidia kujifunza jinsi ya kutatua matatizo yao wenyewe, hata kama tatizo linaonekana kuwa dogo kwako.

3. Tambua mafanikio ya watoto wako

Wakati watoto wako wamejifunza jambo ao wamehusika katika mashindano shuleni, usisahau kuwasifu kwa kusema:

• “Kazi nzuri! Najivunia wakati unajaribu kufanya bora.”

• “Ni vyema kuona unafanya bora.”

• “Unaboresha kila wakati.”

Lakini sema tu maneno haya ikiwa ni kweli. Ikiwa utasifu watoto wako wakati hawastahili hawataelewa ni nini unatarajia kwao. Sababu ya kutambua mafanikio yako ni kuonyesha kwamba unaona thamani ya juhudi zao, na hii itawahimiza kuendelea kujaribu ao kujua ustadi mpya.

4. Kuonyesha upendo

Matendo huzungumza zaidi kuliko maneno. Kuonyesha upendo ao kuonekana na furaha wakati uko nao kunaweza kuwapa himizo sana. Unaweza kuonyesha upendo wako kwa:

• Kusikiliza maoni ya watoto wako:

• Kutumia wakati maalum nao;

• Kuhusika katika michezo na shughuli zao;

• Kuwaonyesha ishara za joto na upendo inapowezekana (tabasamu, kuwakumbatia, kushika vichwa vyao, nywele ao mgongo);

• Kuwakubalia wasaidia nyumbani na kuwasifu wanapofanya hivyo.

Page 33: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 4 :

Kuboresha lugha na ustadi wa

kijamii wa watoto wako

Page 34: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 35: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

25

Kipindi cha 4: Kuboresha lugha na ustadi wa kijamii wa watoto wako

Umuhimu wa lugha na ustadi wa kijamii

Jamii ya Australia inazingatia kujielezea na uwezo wa kuingiliana na wengine vyema. Hii hufanya iwe muhimu kwa watoto wako kuwasiliana vyema na kukuza ustadi mzuri wa kijamii.

Watoto hujifunza lugha rahisi sana katika miaka 5 ya kwanza. Hii huufanya uwe wakati bora wa kuwafunza watoto wako lugha mpya. Ikiwa wewe huzungmuza tu lugha ya kitamaduni nyumbani, huu ndio wakati wanapaswa kuwa wanajifunza Kiingereza - na ikiwa unazungumza Kiingereza nyumbani unaweza kuwa wakati mzuri wao kujua vitengo vya lugha za Kikongo na lugha zingine ungependa wao kujua.

Miaka ya mapema ni muhimu pia kwa kukuza ustadi wa kijamii. Katika mila ya Kikongo familia kubwa ndio asili na watoto wengi huingiliana tu na jamaa zao. Katika nchi mpya waweza kukosa kuwa na viunga hivi vya familia, ni vyema kujulisha watoto wako kwa watoto wengine wengi uwezavyo. Kama ilivyojadiliwa katika Sehemu ya 2, vikundi vya michezo, maktaba, shule za watoto na darasa za lugha ya Kikongo ni mahali muhimu kukutana na watoto wengine. Husaidia pia watoto wako kujifunza ustadi muhimu, kama jinsi ya kuunda siku yao na kutochelewa.

Kwa nini ni muhimu kwa mtoto kucheza?

Wazazi wanaweza kukosa kuona umuhimu wa kucheza katika maisha ya watoto wao pamoja na nyakati zinazohusisha wazazi na watoto. Je! unakumbuka nyakati ambazo ulicheza na wazazi wako? Wataalam wa kukua kwa mtoto wanatuambia kwamba kucheza na mtoto ni kufurahia; na kunaweza kusaidia watoto kujifunza.

• Ni fursa kubwa kwa mafunzo ya ihari na hufanya kujifunza kuwa raha;

• Hushawishi uvumbuzi na kutaka kujua;

• Hutoa fursa za kuingiliana na watoto wengine na kujifunza ustadi muhimu wa kijamii;

• Huhimiza watoto kukuza mapendeleo yao, ustadi na uwezo;

• Waruhusu watoto watulie, jifunze jinsi ya kufurahia, kuwa mbunifu na kutatua matatizo.

• Husaidia watoto kujifunza jinsi ya kuonyesha hisia zao.

Page 36: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

26

Jukumu lako katika mchezo wa watoto wako na ukuzaji wa lugha

Chukua muda wa kuzingatia jinsi unaweza:

• Himiza watoto wako kucheza bila kueleza makosa yao;

• Jiunge na michezo na furahia nao;

• Epuka kutawala michezo yao, na wape nafasi ya kuongoza na kufurahia wao kuwa viongozi katika michezo yao wenyewe;

• Wahimize kutumia tafakari yao na kuunda michezo mpya ya kucheza.

• Wafunze kukubadili maadili sahihi na kuyatumia wanapocheza - kama kushiriki, hakuna uhasama, kufuata sheria sawa, ushirika na uwazi.

Je! nini hufanyika wakati watoto wana ugumu wa kujielezea?

Watoto ambao na ugumu wa kujielezea wanaweza kupata dhiki ya kihemko ao kupata ugumu kukaa na watoto wengine. Unajuaje wakati mtoto wako anaonyesha ishara za dhiki? Watoto wanaopitia dhiki ya kihemko wanaweza:

• Kufadhaika na kuacha kucheza wakati hawawezi kupata njia yao;

• Kuonyesha hisia za hasira;

• Hulia virahisi na kushindwa kuacha hata ikiwa unajaribu kumbembeleza;

• Hupiga yowe ao kukuchapa ao kuchapa watoto wengine;

• Hupata ugumu kutatua mizozo;

• Hukataa kukaa na watoto wengine wa umri wa.

Watoto wanaopitia dhiki ya kijamii wanaweza:

• Kuwa kunyamaza, kuogopa, kutengwa na kujitenga;

• Hukosa ujasiri wa kujaribu shughuli mpya;

• Kukosa hamu, kuwa waoga na kudhalimiwa virahisi na watoto wengine.

Page 37: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

27

ZoeZi 5

Njia za kuboresha kujielezea kwa mtoto wako kupitia mazungumzo na ustadi wa kijamii

Zifuatazo ni vidokezo vya kuboresha kujielezea kwa mtoto wako kwa mazungumzo. Vijadili na familia yako. Wewe hufanya mambo ngapi yafuatayo?

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Husikiliza watoto wako na kuwahimiza kufafanua wanachomaanisha kwa maneno yao?

Huwauliza maswali rahisi ambayo huwahimiza kufikiria wenyewe?

Hutumia kila fursa kuwahimiza kuzungumza, kama vile kuwapeleka kwa ununuzi na kuwauliza watafuta vitu unavyotaka kununua?

Huwauliza kufafanua wanachoona na kusikia wakati wa safari kwenye treni, basi ao gari?

Hufafanulia watoto wako vitu na watu karibu nao, na kuwasaidia kujifunza kulenga, kuzingatia na kujifunza kutoka kwa hali mpya?

Huwapeleka kwa sehemu mpya kama zoo na kuwauliza kukuambia wanachoona?

Wewe huhimiza watoto wako kuboresha hisia zao na kujaribu ustadi wao wa lugha wakati wanangoja mahali tofauti (vituo vya basi, kliniki, na benki)?

Husaidia watoto wako (kuanza miezi 18 kuendelea) kuelewa kwa nini jambo moja linafuata lingine? Kwa mfano, wakati unawasha swichi, taa imewaka.

Page 38: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

28

Jewewe: Jibu‘ndio’ao‘la’

Hufunza watoto wako jinsi tabia yao inaathari? Kwa mfano, kushika visu vikali kuweza kusababisha kukatwa ao kusahau kupiga mswaki kutasababisha kuoza meno.

Kucheza michezo na watoto kukuza matamshi na ustadi wa kuzungumza?

Kuwapeleka kwa kikundi cha kucheza, darasa za lugha ao shule ya watoto wadogo?

Kuwahimiza kuzungumza Kikongo ao lugha zingine unazoweza na familia ao marafiki?

Page 39: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 5 :

Jinsi ya kuwasilisha hisia

Page 40: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 41: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

29

Kipindi cha 5: Jinsi ya kuwasil-isha hisia

Kuonyesha mihemko katika utamaduni mpya

IKatika jamii ya kisasa ya Australia, wazazi kutoka kwa asili anuwai za kitamaduni hutambua umuhimu wa kuonyesha na kuzungumza kuhusu mihemko na hisia na watoto wao.

Kimila, katika familia za Wakongo baba hastahili kuonyesha ao kuzungumza wazi juu ya mihemko, haswa wakati wa kutekeleza mamlaka yake. Wakati imani hizi zinaweza kufaa desturi za zamani za ulezi, katika jamii ya leo wataalam wa kukua kwa mtoto wanahimiza uonyeshaji wa mihemko.

Kumbuka nyuma – wewe mwenyewe ulilelewa kwa njia hii ya kitamaduni?

Hii yaweza kuwa eneo moja kubwa la tofauti kati ya utamaduni wa Kikongo na njia za kisasa za kulea watoto. Umekuja kwa jamii ambayo inatarajiwa kwamba wazazi wahimize watoto wao kuzungumza kuhusu hisia zao. Kujifunza jinsi ya kulinganisha matarajio haya machache ili kujadili hisia zako na watoto wako kunaweza kuwa tofauti sana na unachojua ao kupitia na familia yako ulipokuwa unakua. Inaweza kuwa swala lenye changamoto zaidi unalopitia kama mzazi.

Katika familia zingine za Kongo, mawasiliano ya kihemko yanaweza kuwa magumu, lakini nchini Australia ni kawaida kwa walimu na wengine

kuwauliza watoto wao waonyeshe hisia zao ao kupeana maoni yao kuhusu mambo kadhaa. Hii yaweza kuwachanganyisha watoto na inaweza kusabisha wasiwasi kati ya familia yako, haswa na vijana ambao wanaweza kuhisi kwamba kukosa mhemko kwako ni ishara kwamba huwapendi ao huwashukuru.

Weweza kujadili na watoto wako jinsi ulilelewa na wazazi wako wenyewe. Hii yaweza kumaanisha kwamba upendo na shukrani yako kwao, unaonyesha kwa njia tofauti kama kuwanunulia gari, ao kwa kupika chakula wapendacho.

Kukuza mawasiliano mazuri na watoto wako

Unaweza kuanza kukuza mawasiliano mazuri na watoto wako kwa:

• Kusikiliza na kutazama watoto wako wanapoonyesha mihemko yao kwa marafiki wao ao ndugu/kaka na dada wakubwa wao;

• Kuzungumza na watoto wako na kujifunza kuwauliza maswali;

• Kujifunza kutomkatiza mtoto wako wakati anazungumza nawe.

Hapa kuna vidokezo muhimu.

Page 42: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

30

Anza kusikiliza na kuangalia watoto wako.

1. Panga wakati wa mahali tulivu kusikiliza watoto wako. Ikiwa hauna wakati, heshimu ahadi yako ya kusikiliza watoto wako baadaye.

2. Sikiliza kamili watoto wako wana- pozungumza.

3. Ambia watoto wako kwamba unaelewa wanachosema kwa kurudia muhtasari wa kile walichokuambia.

4. Watazame machoni, tabasamu na itika wakati unaposikiliza mtoto wako.

5. Uliza maswali ambayo yanaruhusu watoto wako kujibu kwa maneno yao wenyewe kama: “Niambie kwa maneno yako mwenyewe, jinsi ilivyofanyika?” ao “Unajisikia vipi sasa?”

6. Chuchumaa na umsikilize mtoto wako mdogo ili uwe kwenye katika kiwango sawa cha kimwili.

7. Epuka kuwakosoa, kutusi, kufoka ao kuhukumu watoto wako kama washindwa. Jaribu kutumia lugha nzuri na rejelea mambo mazuri waliyofanya kila wakati.

8. Sikiliza kwa huruma kile watoto wako wanachosema, fafanua kwamba unawaelewa na kwamba uliwahi kupitia mambo kama hayo katika umri wao.

9. Jaribu kuelewa na kukubali hisia za watoto wako bila kukasirika ao kutohisi sawa nao wakati huo ao wataepuka kukuonyesha ao kukuelezea hisia zao.

Zungumza na watoto wako kwa njia ambayo itapata majibu bora:

1. Fanya mjadala na watoto wako kuanzia umri mdogo uwezavyo ili kuwasaidia kujifunza jinsi ya kuzungumza.

2. Uliza watoto wako maswali kuhusu mada zinazowahusu, kama shule, marafiki na michezo.

3. Jihusishe na shughuli za kila siku za watoto wako na uwaulize maswali juu ya shughuli hizi.

4. Tumia maneno ya himizo na sifa wakati mtoto wako ametia bidii ao ameonyesha ubora.

5. Epuka kuaibisha watoto wako ao kuwauliza maswali magumu mbele ya watu wengine.

Page 43: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

31

Kutumia ‘ujumbe wa–mimi’, sio ‘ujumbe wa-wewe’

Mojawapo ya kidokezo bora zaidi cha kuzungumza na watoto wako ni njia ambayo itasaidia ukuaji wao wa kihemko na kujistahi ni kutumia ujumbe wa ‘mimi’ badala ya ‘wewe’. Waweza kuwa hujasikia hii hapo awali lakini ni njia nzuri sana ya kuwasiliana.

Ujumbe wa-mimi: Ujumbe wa-wewe:

“Mimi sifurahi wakati unapotazama runinga bila kufanya mazoezi yako ya nyumbani kwanza.”

“Wewe ni bure na mvivu. Wewe hutazama runinga tu siku nzima na haufanyi mazoezi yako ya nyumbani."

Wakati ‘ujumbe wa-mimi’ waweza kutumiwa:

• Kushiriki maadili, hisia na mawazo;

• Kujulisha watoto wako unachofikiria na jinsi unahisi.

Jua kwamba ujumbe wa–wewe waweza:

• Kusababisha hofu na imani kwamba haupendi watoto wako;

• Kuumiza na kusisimua majibu yenye chuki na ya kujitetea

ZoeZi 6

Kutumia ‘ujumbe wa–mimi’, sio ‘ujumbe wa-wewe’

Wiki ijayo weka rekodi ya hali ambazo ulitumia ‘ujumbe wa-mimi’ na ‘ujumbe-wa-wewe’ kwa watoto wako.

Jadili na familia yako njia ipi ni bora ya kufanya watoto wako watende mema na kufurahia.

Page 44: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

32

Page 45: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 6 :

Zuia vita na watoto wako

Page 46: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 47: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

33

Kipindi cha 6: Zuia vita na watoto wakoKutatua mizozo na watoto wako ni moja ya changamoto ngumu mzazi yeyote anaweza kupitia. Ni njia ipi bora zaidi? Njia ya kimila katika tamaduni nyingi ni kuwafokea ao kuwachapa.

Wataalam wa watoto leo wanapinga njia kama hizo, wanaziona kama ni za zamani, zisizofaa na za kuumiza kwa kukua kwa mtoto kijamii, kihemko na kisaikolojia. Swala hili linajadiliwa kote kati ya wazazi katika tamaduni nyingi na kunaweza kukosa kuwa na jibu moja sahihi. Mwongozo huu haudai ukubwa wa njia moja ao nyingine. Unakuonyesha njia mbadala za kutatua mizozo na watoto wako.

Hatua sita za kweli za kutatua mzozo na watoto wako

Zoezi lifuatalo ni mfano wa kutatua mzozo kati yako na watoto wako unaotumika katika jamii nyingi za kisasa na zinapendekezwa na wataalam wa kimataifa wa watoto. Inajumuisha hatua sita na majaribio ya kufanya kwa wazazi wote na watoto kwa kuhimiza ushirikiano. Tunapendekeza ujaribu na uone kama itafanya

kazi kwako.

ZoeZi 7

Kutatua mzozo

Hatua ya 1: Elezea tatizo, mahitaji yako na ya watoto wako

Hatua muhimu zaidi katika kutatua mzozo ni kawaida kugundua kwamba tatizo lipo. Bila mtoto wako kuwepo, jadili na familia yako na/ao watu wazima wengine tatizo la nidhamu ambalo umekuwa nalo na watoto wako. Andika tatizo hapo chini.

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

…………………………………...........................................................................................

Page 48: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

34

Sasa jadili maswali muhimu kadhaa:

• Je! unasisitiza ‘ujumbe wa-mimi’ kuelezea mahitaji yako na matarajio kwa watoto wako?

• Je! unasikiliza watoto wako wakati wanajaribu kufafanua mahitaji yao ao mipango yao?

• Je! unaonyesha hisia zako mbaya (kama hasira) bila ufokaji ao kukosoa watoto wako?

• Je! unahakikishia watoto wako kwamba:

o unatafuta suluhisho kwa tatizo ambalo litatimiza mahitaji yenu wote?

o nyinyi wote mnaweza ‘kushinda’ ikiwa mtatatua swala hilo bila hasira na kujaribu kuona pande zote za tatizo?

o unasisitiza nidhamu kwa sababu kama mzazi unawajibu kwa mapendeleo yao na utawapenda watoto wako kila wakati na kuwatunza?

Hatua ya 2: Changiana mawazo ya suluhisho zinazowezekana

Sasa unahitaji kufikiria njia bora za kutatua mizozo yako na watoto wako. Chukua siku chache kufikiria juu ya tatizo uliloandika hapo juu na andika njia tano tofauti ambazo unafikiria tatizo hilo laweza kutatuliwa bila kuanzisha mzozo mwingine. Hapa kuna vidokezo muhimu:

• Epuka kukashifu ao kukosoa vikali suluhisho zilizopendekezwa na mtoto wako;

• Tafuta suluhisho mbadala kadhaa;

• Kumbuka kwamba lengo lako sio ‘kushinda’ bali kufanya kazi pamoja.

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………………...

…………………………………………………………………………………………………………...

Page 49: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

35

Hatua ya 3: Kagua suluhisho zinazowezekana

Wewe na watoto wako mnapaswa sasa kufanya kazi pamoja juu ya kile mnachofikiria ni suluhu bora za zile zilizoorodheshwa hapo juu. Kila mmoja wenu atasahihisha suluhu moja kutoka kwa majibu yako katika hatua 2, kisha jadili chaguo lako.

Kumbuka:

• Kuwa wazi wakati unakagua kila suluhu linalowezekana;

• Tathmini mjadala kwa ao dhidi ya kila suluhu;

• Uliza maswali ya kweli kuhusu jinsi kila suluhisho litatekelezwa;

• Jaribu kila suluhisho linalowezekana ili kutambua matatizo yoyote;

• Zingatia ikiwa matokeo ya kila suluhu ni sawa kwako na watoto wako.

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

Hatua ya 4: Amua suluhisho linalokubalika na nyinyi wote

Kwa kuwa umejadili suluhisho bora, amua ni gani umechagua na uiandike hapo chini. Ikiwa suluhisho mbili zinafanana, andika zote mbili. Baadhi ya vidokezo ni:

• Chagua suluhisho mnalokubali nyote wawili;

• Epuka kulazimisha suluhisho kwa watoto wako bila kuwaelezea sababu zako;

• Hakikisha kwamba nyote wawili mnaelewa matokeo ya suluhisho mliochagua.

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

Page 50: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

36

Hatua ya 5: Kutekeleza suluhisho

Jadili jinsi ya kutekeleza suluhisho mara moja baada ya suluhisho kuchaguliwa. Andika hatua za kweli hapo chini. Hapa kuna mapendekezo yanayoweza kusaidia kazi ya kukubaliana:

• Jadili ni nani anafanya nini wakati upi;

• Usionyeshe mashaka juu ya nia za watoto wako ao kusisitiza matokeo mabaya;

• Kabili watoto wako na ‘ujumbe wa-mimi’ ikiwa watashindwa kufuata makubaliano;

• Peana mapendekezo kusaidia watoto wako kuchukua jukumu lao;

• Epuka kusumbua, kujaribu kuthibiti ao kuinua sauti yako kwa watoto wako; hii itasababisha madharau na kutokea tena kwa mzozo.

…………………………………………………………………………………………………………….

…………………………………………………………………………………………………………….

…………………………………………………………………………………………………………….

…………………………………………………………………………………………………………….

…………………………………………………………………………………………………………….

…………….………………………………………………………………………………………………

Page 51: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

37

Hatua ya 6: Kagua hali

Baada ya muda unaofaa (amasiku ao wiki kadhaa) jadili na watoto wako ikiwa suluhisho imefanya kazi. Ikiwa unahitaji kufanya mabadiliko ya makubaliano, andika hapo chini. Hapa kuna maoni kadhaa:

• Ifanye iwe jambo zuri - labda wakati wa kula ao matembezi ya familia;

• Ikiwa suluhisho limefaulu, tambua juhudi na maendeleo yaliyofikiwa;

• Ikiwa suluhisho halijafaulu kikamilifu, badala ya kukataa suluhisho, fikiria juu ya mabadiliko ambayo yanaweza kuifanya iwe bora;

• Tena sikiliza vizuri kile watoto wako wanachosema;

• Kuwa wazi na mwaminifu. Kujifanya tatizo limetatuliwa wakati bado kutasababisha maswala zaidi baadaye.

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………………

Ikiwa ulipata zoezi hili kuwa ngumu ao kutofaulu, kumbuka kwamba waweza hudhuria kozi za mafunzo ya ‘uzazi katika utamaduni mpya’ ao apate ushauri wa kitaalam kutoka kwa mmojawapo wa washauri wa uzazi kwa kipiga simu (03) 9496 0200.

Page 52: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

38

Page 53: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 7 :

Jinsi ya kuwapa watoto wako nidhamu

Page 54: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 55: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

39

Kipindi cha 7: Jinsi ya kuwapa watoto wako nidhamuKama kutatua mzozo, kuwapa watoto wako nidhamu kunaweza kuwa juhudi kubwa. Kunahusisha maamuzi yasiyobadilika. Usishangae ikiwa utachanganyikiwa – wazazi wengi huhisi hivyo. Kando na ugumu huu, nidhamu ni jambo ambalo lazima ushughulikie kwa hatua fulani. Ni muhimu kujua kwamba wakati hakuna njia moja iliyokubaliwa ya kuwapa watoto wako nidhamu, kutumia nidhamu sio jambo sawa na adhabu. Nidhamu hufunza watoto wako tabia zinazokubalika, kama mzuri na mbaya na heshima ya haki za wengine. Hukuza ujasiri kwa mtoto, ikiwaruhusu kuhisi salama, kupendwa na kuweza kuthibiti matendo yao. Lakini adhabu ni ya matendo na huzingatia kuadhibu watoto kwa tabia isiyokubalika. Nchini Australia, hatua ya kisheria inaweza kuchukuliwa dhidi ya wazazi wanaoadhibu watoto wao vikali kwa kuwachapa ao kuwadhulumu.

Nidhamu ya kimila

Kama mzazi wa Kongo-Australia, waweza kuhimiza watoto wako kufuata utamaduni wako, maadili na desturi za kimila na kukuza umoja na sifa ya familia yako. Kama wazazi wengi, utatarajia watoto wako kukutii na kufuata ushauri wako wakati wa maumuzi muhimu ya maisha, kama elimu,chaguzi za taaluma na ndoa. Wazazi wengine wa Kongo-Australia bado watatumia hofu, vitisho na adhabu ya kimwili kuwapa watoto wao nidhamu. Tabia kama hizo zaweza kufaa nyakati za hapo awali na

labda zinaweza kukubalika katika nchi kadhaa lakini mambo yamebadilika katika jamii nyingi. Siku hizi, dhuluma kwa watoto na adhabu kali zinaweza kusababisha kushikwa na utawala wa kiserikali wa ulinzi wa watoto na polisi, na waweza kulazimika kujitetea kortini.

Nchini Australia, watoto wanafundishwa kwamba wana haki na hawatarajiwi kufuata masharti ya wazazi wao kiatomati. Wanafundishwa pia kwamba adhabu ya kimwili haikubaliki. Watoto wako watakuwa wazi kwa njia kama hizo za kufikiri na unahitaji kujua jinsi ujumbe huu tofauti waweza kuchanganyisha watoto wako juu ya jukumu lako kama mzazi.

Kupeana nidhamu kwenye utamaduni wa kisasa wa Australia

Nidhamu inaeleweka kwa jumla kuwa juu ya kuunda kuelewa na heshima kati ya wazazi na watoto, sio juu ya tishio la adhabu. Hii mara nyingi hujulikana kama ’uzazi mzuri’. Watoto wanatarajiwa kuelewa tofauti kati ya tabia nzuri na mbaya, kuheshimu matarajio ya wazazi wao na kukuza maadili mema na mitazamo mizuri.

Wataalam wa watoto wanapendekeza kwamba njia bora za kuwapa watoto nidhamu ni pamoja na:

• Kuwajulisha watoto athari za tabia yao;

• Kuwapa watoto umilikaji wa kukabiliana na shida hiyo;

Page 56: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

40

• Kujadili na watoto wako sheria za nidhamu;

• Kuwaruhusu watoto wako kuhifadhi heshima wao wakati hawakubaliani.

Kuwachapa watoto

Wazazi katika tamaduni nyingi wanafikiri kuwa kuwachapa watoto kunakubalika na kwamba kichapo kidogo kinaweza kumfaidi mtoto. Lakini ikiwa kuchapa ndio njia pekee ya nidhamu, yaweza kusababisha njia kali za uhasama. Watoto wanaweza kuiga tabia shuleni kwa kuchapa watoto wengine kama njia ya kutatua mzozo. Kuadhibu mtoto wako kwa kumfokea ao kumchapa kidogo kunapaswa tu kutumiwa kama njia ya mwisho, na katika dharura tu ambapo makosa ya mtoto wako kunaweza kusababisha wao ao watoto wengine kuumizwa. Jadili swala hilo la kumchapa mtoto wako na familia yako na mkubaliane ikiwa utaitumia kuwapa nidhamu watoto wako.

Kuepuka dhuluma ya mtoto

Nchini Australia dhuluma ya uzazi na kutendea watoto vibaya ni kosa kubwa ambalo linachunguzwa na vyombo vya kiserikali na katika kila jimbo na eneo. Kumbuka, dhuluma ya watoto yanaweza kutafsiriwa kwa njia nyingi. Ikiwa mtoto ameumizwa na wazazi kimwili, kisaikolojia ao kingono, hii yaweza kusababisha utawala wa serikali na polisi kuingilia. Katika hali mbaya zaidi, vyombo vya kiserikali vinaweza kuchukua watoto kutoka kwa nyumba ya wazazi wao na kuwapeleka wazazi kortini.

Kuelewa sheria za Australia za ulinzi wa watoto

Unahitaji kuelewa sheria za ulinzi wa watoto za Australia. Kumbuka, Australia ina sheria na viwango tofauti za ulinzi wa watoto kuliko nchi nyingi za Afrika.

Je! dhuluma ya watoto ni nini?

‘Dhuluma ya watoto’ ao ‘kutendea watoto vibaya’ ni wazazi kuwaumiza kimwili, kingono ao kihemko, ao mtu mzima mwingine yeyote anayetunza watoto. Dhuluma yaweza kuwa tukio moja ambalo linalosababisha kuumizwa kunachohitaji matibabu, kama kuchapa kwa mshipi, kupiga ngumi, kuitikisa ao kuchoma mtoto. Kama sivyo dhuluma inaweza kurudiwa kwa msingi wa kila siku na kusababisha athari ya kudumu ya kimwili, kiakili na kisaikolojia kwa mtoto. Kutendea watoto vibaya kunaweza kujumuisha pia kutomlisha mtoto vizuri, kuambia mtoto atoke nyumbani ao kupuuza hitaji la mtoto la joto na mavazi. Watoto pia hawapaswi kuacha wazi kwa uhasama kati ya watu wazima kwenye nyumba ya familia, ambayo baadaye inaweza kuwaathiri kisaikolojia.

Je! ni nani anawajibikia ulinzi wa watoto Australia?

Nchini Australia halinjema ya watoto ni wajibu wa pamoja wa wazazi, jamii na serikali. Maswala ya ulinzi wa watoto kawaida hushughulikiwa na wafanyikazi wataalam wa idara za jamii katika jimbo na serikali za wilaya. Polisi na

Page 57: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

41

wafanyikazi wa jamii wa serikali wanawajibika kwa kutembelea familia ili kuchunguza kila kesi na kuripoti kwa Waziri anayefaa wa serikali.

Je! matokeo ya kisheria ya dhuluma ya watoto ni yapi?

Dhuluma ya watoto inaweza kuwa na athari kubwa za kisheria. Korti zinaweza kuamuru watoto kutolewa kutoka kwa ulinzi wa wazazi wao na kuwekwa ndani ya ulinzi wa serikali. Hii inaweza kumaanisha jamaa mwingine wa familia ao familia ya walezi na serikali itaombewakulinda watoto. Katika hali za dhuluma mbaya zaidi, wafanyikazi wa ulinzi wa watoto wanaweza kuchukua mtoto anayehitaji ulinzi bila kusubiri amri ya korti. Katika hali mbaya zaidi, hata wazazi wanaweza kushtakiwa na kufungwa jela.

Athari za adhabu kali za kimwili kwa familia

Vitendo vya dhuluma ya watoto yanaweza kuwa na athari kali na za kudumu za kimwili na kisaikolojia kwa watoto. Watafiti wanatuambia kwamba adhabu ya kurudiwa ya kimwili inaweza kusababisha:

• Mtoto kutoroka, usumbufu wa kifamilia kwa sababu wenzi kutengena, ao talaka;

• Ripoti kutoka kwa majirani kwa polisi, ambao wanaweza kutembelea nyumba ili kuchunguza;

• Matatizo ya kihemko na ya kiakili baadaye maishani, pamoja na ukosefu wa ujasiri, mafanikio chache ya kielimu na tabia mbaya, na ugumu wa kuanzisha mahusiano na wengine;

• Watoto kupata matatizo ya ulemavu wa kiakili na afya mbaya ya siku zote

• Kujitenga kijamii kwa familia

Kwa habari zaidi kuhusu ukweli juu ya dhuluma ya watoto, nenda kwa wavuti ya Uanzilishi wa Australia wa Utoto www.stopchildabuse.com.au.

Ni njia ipi bora ya kuwapa watoto nidhamu?

Kuzungumza kwa jumla, hakuna njia moja sahihi ya kuwapa watoto nidhamu na kuwalea. Lakini kuna njia kadhaa za mtindo wa uzazi ambao unajumuisha njia tofauti za nidhamu. Wazazi wangependa mtindo ambao unafaa maadili yao ya kitamaduni. Bila kujali njia unazochagua, ni muhimu kwamba usibadilike.

Page 58: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

42

ZoeZi 8

Je! unachagua njia ipi ya kupeana nidhamu?

Masomo ya uzazi na saikolojia ya mtoto inaorodhesha njia pana tatu za kupeana nidhamu. Hizi zimefupishwa hapa chini.

Soma muhtasari na jadili na mke ao mume wako njia zipi ao mkusanyiko wa njia upi ambazo unatumia.

• Mtindo wa mamlaka

Wazazi wenye mamlaka wanaamini ‘utiifu kamili kwa mamlaka’. Wao huamuru ni nini watoto wao wanaweza kufanya ao wasifanye, na kuacha nafasi ndogo ya uvumbuzi na kufikiria. Tabia mbaya huadhibiwa vikali.

Ingawa inatumika bado na wazazi wengine katika jamii ya Kongo, mtindo huu haukubaliki tena ao kustahimiliwa na jamii ya Australia ao katika familia nyingi za wahamiaji.

Watoto wanaolewa kwa njia hii wanaweza kuwa kwenye hatari ya ushawishi wa marafiki wabaya, ao kufadhaika.

• Mtindo wa kupeana uhuru

Katika mtindo huu wazazi huwa rahisi, wanachukua hali ya ‘kutoa mikono’, huwa hawaweki mipaka kwa tabia ya watoto wao na huwaruhusu kujifunza kutokana na matokeo ya tabia yao. Tabia mbaya hupuuzwa ao huchukuliwa kama mchezo. Wazazi wengine hutendea watoto wao kama marafiki wao na hukataa kuchukua wajibu wakati watoto wao wamejiumiza ao wanaumiza wengine.

Watoto waliolewa kwa njia hii kwa jumla huwa wabunifu na halisi, lakini wanaweza hisi kukosa usalama na wakati mwingine kufanya uamuzi mbaya. Mara nyingi wao hupata ugumu kukabiliana na serikali na kukosa nidhamu ya binafsi kwa kusoma ao kazi ya kudumu.

Page 59: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

43

• Mtindo wa kukiri kidemokrasia

Wazazi ambao hutumia mtindo huu hupeana majukumu kwa watoto wao kulingana na uwezo wao, kuthibitisha maswala na kupeana sababu za vizuizi. Watoto huongozwa na kupewa mazoezi mengi katika kuchagua. Tabia mbaya hukabiliwa na matokeo ao kwa kutatua tatizo, kwa kuzingatia mahitaji ya mtoto. Tabia mbaya iliyozidi kwa mtoto ambaye hajitawala haikubaliki.

Mtindo unatumika sana kwenye jamii za kisasa na unafikiriwa kama muhimu kwa walimu wa Australia, wanasaikolojia wa watoto na madaktari bingwa ya watoto.

Watoto waliolewa kwa njia hii hijifunza kukubali wajibu wao kwa tabia yao mbaya, kuingiliana na wengine shuleni ao kazini, kufaulu kwa ndoa zao na kufanya chaguo zenye burasa.

Vidokezo vya kumpa mtoto wako nidhamu bora

Vidokezo vya jumla: Hapa kuna orodha ya njia ambazo zimepatikana kufanya kazi katika kuwapa watoto nidhamu. Ikiwa haujasikia juu ya hizi tayari, zijaribu na uone ni zipi zinafaa kwako.

• Kuwa thabiti wakati unapoadhibu ao kutuza watoto wako. Usibishane nao kuhusu adhabu ambayo wanapewa. Usicheke ao kutabasamu kwa mtoto wako ikiwa anakosea ao watachanganyikiwa ikiwa wanakosea hata kidogo.

• Usibadilike – wazazi wote lazima wakubali kulazimisha sheria zilizokubaliwa za nidhamu kila mara bila kushindwa.

• Wakati mtoto wako anaanza kukosea mkumbushe kuhusu sheria na athari. Kwa mfano, waweza kusema “ukiandika ukutani kwa kalamu, unajua sheria ni kwamba utalazimika kuacha kucheza na vifaa vya kuchezea uvipendavyo”.

• Adhibu ao tuza watoto wako mara moja kulingana na tabia na matendo yao. Fanya haraka kushikanisha tabia hiyo na matokeo na tumia nidhamu inayofaa.

• Komesha tabia isiyofaa kwa “hapana” thabiti, inayosemwa kwa sauti tulivu na ufafanuzi rahisi na wazi.

• Weka utaratibu wazi wa kila siku na fanya juhudi ya kuifuata.

• Usipeane chaguzi katika hali ambazo mtoto lazima afuate sheria zako. Kwa mfano, sema “ni wakati wa kwenda kitandani”....usiulize “je! ungependa kwenda kitandani”?.

Page 60: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

44

• Tumia ‘wakati wa kufikiri’ kama njia ya adhabu kali – kwa kuweka kando mahali pa mtoto wako kufikiria juu ya tabia yao mbaya kwa kipindi fulani.

• Onyesha mfano mzuri ambayo unataka watoto wako kuiga katika hali zote.

Vidokezo fulani: Watoto wanapaswa kijifunza kwamba matendo yao yana matokeo, pamoja na adhabu ikiwa watakosea. Ni wajibu wako kama mzazi kumsaidia mtoto wako kuelewa matokeo ya yale wanachofanya. Tumia jedwali lililo hapo chini kama mwongozo.

UmriWatoto wanachoelewa

Njia ya nidhamuNjia za adhabu zinazofaa

Chini ya miaka 2Kuelewa kidogo ao kukosa kuelewa athari za tabia yao

Kuzingatia tabia bila kuacha

Tumia kuvuta mawazo kuzingatiwa na mtoto mbali na tabia zisizokubalika

Miaka 2-4Kuanza kuelewa athari za tabia yao

Weka sheria rahisi kabisa

Ondoa mtoto kutoka hali hiyo

Wapeleke nyumbani

Wakati wa kufikiria

Kuchapa kidogo

Miaka 5 na kuendelea

Elewa athari za tabia yao

Fafanua sheria na athari wazi

Toa ufikiaji wa vifaa vya kuchezea, Runinga ao michezo kwa muda mrefu

Page 61: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 8 :

Kusimamia dhiki kwa familia

Page 62: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 63: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

45

Kipindi cha 8: Kusimamia dhiki kwa familia Kuwalea watoto wakati mwingine inaweza kuwa hali ya kufadhaisha. Ingawa hiyo huleta furaha na msisimko, mara nyingi huambatana na dhiki bila kujali umri wa watoto wanaohusika. Wakati dhiki inaweza kuwa athari nzuri, kuzidi kwake kunaweza kufanya maisha ya familia kuwa ngumu na hata kuwafanya washiriki wa familia wagonjeke. Kujifunza kukabiliana na dhiki hii ni ustadi muhimu kupata kwako.

Dhiki na familia za wahamaji

Maisha ya familia wakati mwingine yanaweza kuwa na dhiki zaidi kwa familia za wahamiaji. Kuna sababu kadhaa:

• Waweza kupata dhiki kutokana na hali zako za uhamiaji Australia. Waweza kuwa ulikuwa mkimbizi, kutenganishwa na familia kubwa, kupitia mateso ya kisiasa ao athari za vita, ao kushiriki aibu juu ya matukio mabaya huko Afrika. Dhiki zaidi zinaweza kusababishwa na ubaguzi, ugumu ambao Wakongo wengine wa Australia wanao katika kupata ajira ao utaalam unaolipa vyema, na kwa uhusiano mbaya wa vyombo vya habari ao mitazamo ya jamii.

• Wazazi wako wanaweza kuwa wamelelewa tofauti, kutumia njia tofauti za kuonyesha mihemko na kutekeleza nidhamu. Watoto wako wenyewe wanaweza kukosa kukubali njia za akina babu. Wanaweza kutaka

kufuata tamaduni za kisasa, ambazo husisitiza kujitegemea, kutuza ujasiri na kuhimiza utafutaji wa furaha ya kibinafsi.

• Wakongo wengi hurudi nyuma kwenye uzazi wa kitamaduni ambao unaweza kuwa umeisha kwenye jamii za kisasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hii yaweza kufanya matatizo yaliyoelezewa hapo juu yawe mbaya zaidi.

• Bila jamaa na marafiki wa Kongo ambao ulikuwa nao, watoto wako wanaweza kukosa vielelezo vya jinsi ya kutenda katika familia ya Kikongo.

• Waweza kuwa hauna washirika wengine wa familia ili kukusaidia kuondoa shinikizo kwako wakati wa dhiki kuu.

• Kimila, wazazi wengi wa Kongo huzingatia makosa ya watoto wao kama chanzo cha hatia ao aibu.

• Kujitolea huku kwingi ambao unafanyia watoto wako - kufanya kazi kwa muda mrefu ili kuwapa kiwango cha juu cha maisha ao kulipa karo- kunaweza kumaanisha una wakati mfupi wa kukaa nao. Hii yaweza kusababisha watoto kuhisi kudharauliwa na wazazi kuhisi kutoshukuriwa na watoto wao.

Lakini usife moyo. Utamaduni wa kimila na kisasa wa Kiafrika unaosisitiza nidhamu kali ya familia, umoja wa familia na elimu umesaidia vijana wengi wa Kongo-Australia kutoshea vizuri na kufikia ufanisi mkubwa.

Page 64: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

46

Kuwaelewa watoto wako

Kuelewa jinsi watoto wako wanakua kunaweza kusaidia kukabiliana na dhiki ya familia. Unahitaji kutambua kwamba:

• Watoto wako ni wa kipekee na tabia, mahitaji, vipawa, uwezo na udhaifu tofauti tofauti;

• Wao hukua kwa muda tofauti kimwili, kihemko, na kiakili;

• Ni upendeleo na sio vyema kulinganisha watoto wako kila mara na wengine hata katika familia yako.

• Hauna wajibu kwa tabia ya watoto wako unawajibu kwa kufundisha watoto wako kuwajibika kwa matendo yao wenyewe.

Tazama mahitaji yako mwenyewe

Waweza kuhitaji kuzingatia maoni yako ya maisha ya familia. Kuna mabadiliko ambayo waweza kufanya ambayo yatakusaidia kupunguza dhiki. Kwa mfano:

• Kubali ustadi na nguvu zako za uzazi;

• Usijilaumu kwa makosa ya watoto wako;

• Haupaswi kuhisi hatia kuhusu kuchukua muda wa kupumzika wako mwenyewe.

• Hasira yako ambayo haijathibitiwa inaweza kufanya dhiki kuwa mbaya zaidi na kusababisha watoto wako kuiga tabia yao ya hasira na hata kukosa heshima ao kuasi.

• Unapaswa kujaribu kutatua hali za dhiki kabla hajazidi.

Kupunguza dhiki na kuthibiti hasira

Jaribu kukuza njia zako mwenyewe za kuthibiti dhiki. Njia yako ya kukabiliana na dhiki itakuwa na athari kwa watoto wako, ndoa yako na, labda, afya yako.

Kama vile dhiki ni tabia ya kawaida kwa maisha ya kila siku, lengo halipaswi kuwa kuiondoa kabisa lakini kujifunza jinsi ya kuthibiti dhiki vyema.

Page 65: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

47

ZoeZi 9

Kujadili njia za kuthibiti dhiki

Zifuatazo ni mapendekezo bora kadhaa ya kuthibiti dhiki. Jadili na familia yako jinsi waweza tumia njia hizi.

1. Fanya mazoezi wakati unahisi kuwa na dhiki, kwa mfano, kutembea.

2. Kumbuka kwamba hauko peke yako. Jaribu kupanua mtandao wako wa kijamii. Jadili hoja zako na wazazi wengine wa Kongo wanaopitia dhiki ya kifamilia.

3. Fanya washiriki wengine wa familia wawe marafiki wako bora. Jadili maswala nao. Usijaribu kukabiliana na matatizo na dhiki za familia peke yako.

4. Tafuta suluhisho zinazowezekana. Angalia unaweza kubadilisha nini kama mzazi. Tambua ni nini unaweza kufanya kuepuka ao kupunguza dhiki katika familia yako. Kuwa mvumilivu na kukubali.

5. Usiwe msumbufu sana kwa dhiki. Usiongeze chumvi kwa swala hilo linalosababisha dhiki. Ichukulie kama sehemu kawaida ya familia.

6. Ikiwa unapata shida kukabiliana nayo, tafuta msaada wa kitaalam, msaada na ushauri kutoka kwa wataalam wa uzazi.

Page 66: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

48

Page 67: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

Kipindi cha 9 :

Kukabiliana na vijana

Page 68: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 69: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

49

Kipindi cha 9: Kukabiliana na vijanaMafunzo ni njia ya kimila ya wakongo ya kujifunza na kufunza – kwenda kufunzwa ni mpito.

Kulingana na desturi za kabila yako, wavulana wadogohuenda katika kambi ya mafunzo msituni kwa mwaka moja ao mbili. Kuenda mafunzoni kumaliza kutojua kwa mvulana na utata wa kingono na kukuza kutaka kujua kwao katika hatua hii. Wanafunzwa juu ya maadili ya kimila, maarifa na njia na ndoa.

Baada ya kwenda mafunzoni, wanarudi kwa jamii yao kama wanaume walio tayari kuoa na tamasha huandaliwa kwa heshima yao.

Kwa utofauti, wasichana hupokea mafunzo yao katika kijiji ao msitu ulioko karibu.

Kwenda mafunzoni huzuia mkurupuko wa shida za kijamii na kisaikolojia ambazo zinaweza kuhatarisha jamii kwa jumla.

Mpito kutoka utoto hadi utu uzima unaweza kuwa tofauti kwako na kijana wako huko Australia.

Wewe na watoto wako mtahisi kutokuwepo kwa washiriki muhimu wa familia, kama akina babu. Umeidhinishwa kusisitiza wajibu wa mzazi kama vile msemo huu wa Kongo unavyosema: “wazazi wapya katika nchi mpya”.

Unaweza kuwa ulipitia changamoto nyingi wakati ulipotoroka nchi yako, kama kuishi miaka mingi mafichoni msituni kama watafutaji ukimbizi.

Changamoto za uzazi na vizuizi vingine vya kukabiliana nazo. Kama vile Wakongo wengi walivyopitia ugumu wa kambi za wakimbizi unaweza kunyumbuka kama vile methali ya kikongo inavyosema: “macho ambayo yameona juu ya mlima hayawezi kuogopa miteremko ya kwenda chini”.

Je! Mzozo wa vizazi ni nini?

Kuwalea vijana ni moja ya kazi ngumu ambayo mzazi yeyote anaweza kupitia. Mizozo mara nyingi husababisha matokeo yanayoweza hata kusumbua familia zenye raha kabisa.

Mzozo kati ya vijana na wazazi wao – na wakati mwingine vijana na akina babu – mara nyingi hujulikana kama ‘mizozo ya vizazi’. Hufanyika katika familia kutoka kila tamaduni na katika kila nchi, lakini familia za wahamiaji hupitia shinikizo zaidi. Kama vile tofauti kati ya vizazi, familia za wahamiaji lazima wakabiliane na mitazamo tofauti ya kitamaduni juu ya jinsi ya kuwalea vijana.

Wakati unakabiliana na ugumu, sio kama haiwezekani. Fungu hili litakusaidia kuelewa tatizo hilo bora. Inamalizia na maoni fulani jinsi ya kuboresha mawasiliano na vijana wako na kupata ushirika bora kutoka kwao.

Page 70: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

50

Mahitaji maalum ya familia za wahamiaji

Kabla tuangalie jinsi bora ya kukabiliana na mzozo wa vizazi, ni muhimu kuelewa shinikizo nyingi zinazokumba familia yako.

• Unaweza kuwemo familia kubwa ambao huwapa akina babu, shangazi na wajomba, ndugu/kaka na dada wajibu wa jumla kwa kulinda watoto.

• Kama sivyo, unaweza kuwa hauna washiriki wengine wa familia wa kutegemea hata kidogo na waweza kushindwa kupata ushauri kutoka kwa wazazi ambao na uzoefu wa jinsi ya kukabiliana na miaka migumu ya watoto.

• Waweza kuwa na familia kubwa na kupata ugumu wa kupata nyumba kubwa ya kuwapa vijana nafasi ya kutosha wanavyotaka.

• Kunaweza kuwa na shinikizo la ziada kwa watoto wahamiaji kwa sababu kuwapa fursa kunaweza kuwa mojawapo ya sababu za wewe kuchagua kuhamia Australia.

Uhamiaji unajumuisha uhuru, furaha na fursa mpya, lakini pia inaweza kujumuisha gharama zinazoweza kumudika.

Page 71: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

51

Kwa nini mzozo wa vijana ni kawaida?

Jambo muhimu zaidi kwa vijana ni ‘kutoshea’ katika marafiki na vijana wengine. Ni wakati wa maisha ambapo vijana wanahitaji kuunda utambuzi wao wenyewe mbali na uthibiti wa jamaa na wewe kama mzazi wake. Hii yaweza kusababisha tabia ya uasi na kukataa kukusikiliza na kukutii.

Katika hamu yao ya kujitegemea vijana mara nyingi huonyesha tabia ambayo waweza kuona kama uasi:

• Vijana wanaweza kutaka usiri mwingi na hufahamu sura yao, haswa katika uwepo wa jinsia tofauti.

• Wao huhisi shinikizo la kubadili utamaduni wa hali ya juu katika sura na tabia yao. Wanaweza kubadili mavazi yao, huanza kuzungumza Kiingereza pekee, na hukataa kufuata tamaduni na mila za kawaida za Kiafrika..

Uzuri na ubaya wa familia za uhamiaji

Uzuri Ubaya

Fursa bora za elimu kwa watotoUwazi kwa maisha ambayo husababisha wasiwasi na mila zako

Kujifunza utamaduni mpyaMzozo kuhusu jinsi ya kuwalea watoto na ni kiwango kipi cha uhuru wanapaswa kupata

Mfumo bora wa ustawi wa jamii, mapato ya juu na pesa zaidi ya kutumia kwenye familia

Gharama za juu kwa kulea watoto

Usawa kwa wanaume na wanawake, akina mama na baba

Kuelewa tofauti kuhusu jukumu na mamlaka ya akina baba na mama kati ya wanaume na wanawake kwa jumla

Uhuru kutoka kwa kutarajiwa kufuata ‘njia za kale’ katika kulea watoto wako

Kuchanganyikiwa juu ya njia bora ya kuwalea wototo wako ili wasisahau utamaduni wako na utamaduni wa mababu zao

Page 72: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

52

Athari za mzozo mbaya ya kifamilia

Familia nyingi hukabiliana vyema na mzozo wa vizazi. Lakini ikiwa mzozo ni mbaya sana na kukosa kutatuliwa, unaweza kusababisha kuvunjika kwa familia. Katika hali mbaya zaidi mzozo unaweza kusababisha:

• Watoto kutoroka nyumbani ao kukamatwa na polisi;

• Familia yako kuhisi shinikizo la kurudi kwenye nchi yako asili kwa sababu watoto wako wamepoteza ‘mizizi ya kitamaduni’ na wamechanganyikiwa juu ya utambuzi wao wa kikabila;

• Uhasama kati ya wazazi na watoto;

• Watoto kusema matusi ao kuonyesha tabia isiyo na heshima kwa wazazi;

• Watoto kutumia dawa za kulevya na pombe ao kuiba kutoka kwa wazazi;

• Watoto kudanganya kwa wazazi, kukosa darasa ao kufanya vibaya shuleni;

• Wazazi kuchezea kamari ao kutumia wakati mwingi kazini ili kuepuka kuwepo nyumbani.

Sababu zinazojulikana za mzozo

Kuna sababu kadhaa za mzozo wa vizazi zinazojulikana kwa tamaduni zote.

ZoeZi 10 Sababu ya kawaida ya mzozo wa vizazi

Soma orodha ifuatayo ya sababu zinazojulikana za mzozo kati ya wazazi na vijana. Sahi-hisha zile ambazo zimetokea katika familia yako. Je! una mpango wa kusaidia familia yako kukabiliana nayo? Jadili kila swala na mume ao mke wako na panga jinsi ya kukabiliana na kila tatizo.

Sababu zinazojulikana za mzozo

Je! hii imefanyika katika familia yako?

Je! una sheria zilizokubaliwa?

1. Kwenda nje usiku bila ruhusa

2. Mabinti wako kukataa kutii sheria za familia isipokuwa kama ndugu/kaka zao watatii sheria hizo pia

3. Kukataa kuhudhuria tukio maalum za kidini, kitamaduni ao familia

Page 73: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

53

Sababu zinazojulikana za mzozo

Je! hii imefanyika katika familia yako?

Je! una sheria zilizokubaliwa?

4. Kukataa kula chakula cha kitamaduni

5. Kuvaa mavazi yasiyofaa ao kuchagua marafiki usiowakubali

6. Kuwa na rafiki mvulana ao msichana

7. Mtoto wako anaweza kutaka kuoa mtu kutoka kwa jamii ya nje ya Afrika

8. Kuepuka kazi ya shule na kusomea mitihani na kuacha shule

9. Uvutaji sigara ao kunywa dawa za kulevya na pombe

10. Kukataa kuzungumza ao kujifunza lugha ya kitamaduni na kutotaka kujua mila za utama-duni

Vidokezo vya kupigana na mzozo

Mzozo na vijana hauwezi kuepukwa lakini wakati unakabiliwa vyema, inaweza kusababisha mahusiano bora ya kifamilia.

Kuna njia zingine za kijumla ambazo unaweza kutumia ambao zitakusaidia kukabiliana na kushinda mzozo na vijana wako:

• Usibadilishe sheria na matarajio ya familia juu ya jinsi unavyotaka watoto wako kutenda;

• Weka mfano mzuri kwa watoto wako kwa kuzungumza kuhusu sheria hizo kabla wawe vijana, ili wajue cha kutarajia;

• Jifunze njia mpya za kuwasiliana na watoto wako kwa kuwa wazi na kwa kuwazungumzia kuhusu ugumu sawa ambao ulipata kama kijana;

• Zingatia mahitaji na hisia za watoto wako wakati unafanya maamuzi kuhusu familia;

Page 74: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

54

• Jifunze jinsi ya kuonyesha hasira na mihemko nyingine bila kusababisha machozi, lugha ya matusi ao uhasama;

• Chagua ni sehemu zipi za utamaduni mpya unaweza kuiga na ni zipi za kutunza za utamaduni wako asili. Andika orodha. Hakikisha wewe na familia yako mnakubaliana juu ya sheria za kitamaduni na mila ambayo unataka familia ifuate;

• Kuwa wazi kuhusu kiwango cha kushiriki ambacho unataka katika familia yako kutoka kwa babu za watoto na washiriki wengine wa mbali wa familia;

• Hakikisha sheria hizi mpya za familia zinajadiliwa vyema na zinaeleweka na washiriki wote wa familia ambao wazazi wote wanakubali kutotatanisha wengine wakati wa kutekeleza sheria hizi.

Vidokezo fulani

Hapa kuna sababu kadhaa za mzozo wa familia kutoka Zoezi 10 na vidokezo kadhaa za kuzishinda.

Kwenda nje usiku bila ruhusa

Haijalishi watoto wako wanadai nini, familia nyingi bila kujali asili ya kitamaduni huwa hawaruhusu watoto wao kwenda nje wakati wowote wanataka.

Unapaswa kuweka sheria na kutobadilika. Kwa mfano, unaweza kuamuru watoto wako wawe nyumbani wakati fulani ao kwamba wanaweza kwenda nje na ndugu, dada, jamaa ao rafiki unayemwamini. Njia nyingine ni kwamba unaweza kuamua kwamba wanaweza kwenda nje tu wenyewe mchana.

Sheria tofauti kwa wana na binti

Ikiwa utakubali wana wako waende nje usiku, usishangae ikiwa mabinti wako watataka uhuru sawa. Unaweza kuheshimiwa na kutiiwa zaidi na wana na mabinti wako ikiwa utawatendea sawa.

Ikiwa unapendelea sana wana wako na mkali kwa mabinti wako, hii inaweza kusababisha matatizo na mabishano.

Page 75: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

55

Kuwa na rafiki mvulana ao msichana

Usishangae ikiwa hii itafanyika na usihisi usumbufu sana. Panga wakati wa kuijadili na watoto wako. Wasikilize na uonyeshe hoja zako kwa njia tulivu na upendo. Zungumza juu ya maadili ambayo ungependa wafuate na jinsi zimekusaidia katika ndoa yako. Jadili changamoto za kihemko ambazo mahusiano yanaweza kuwaletea.

Jadili athari za kuwa na mahusiano ya ujana kwa mfano. jinsi yanaweza kuathiri kazi ya shule.

Kukataa kuhudhuria tukio la kidini, kitamaduni ao familia

Hii ni njia wa mtoto wako ya kuonyesha kuchanganyikiwa kwao kuhusu utambuzi wao wa kikabila. Jadili urithi wako wa kitamaduni na watoto wako na waelezee kwamba katika ulimwengu wa sasa, kuweza kutembea bila wasiwasi kati ya lugha mbili na tamaduni ni faida.

Ikiwa watakata kukubali utamaduni wako, usihisi msumbufu sana; watoto kawaida hujivunia urithi wao wakati wanafikia utu uzima. Kwa kuhisi msumbufu sana, waweza kuwalazimisha katika nafasi ambayo wanakataa mara moja kuhisi kushambuliwa nawe.

Kuchagua marafiki ambao hukubali

Jaribu kutohisi msumbufu sana kwa hali hii ya kawaida. Usitoe maoni mabaya juu ya marafiki wa watoto wako. Jadili na mume ao mke wako ikiwa marafiki hao wanafaa.

Wape watoto wako sababu nzuri kwanini marafiki wao hawafai na jaribu kuwashawishi kuliko ‘kuweka sheria”. Kumbuku, watoto wanaweza kukupa changamoto ikiwa utawaambia wasihusiane na mtu kwa sababu tu ya rangi ao dini.

Page 76: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

56

Kukataa kusoma kile unachopenda ao kushindwa kusoma kwa bidii

Wahamiaji wengi hutamani kwamba watoto wao wawe wanafunzi wazuri, lakini huwa haifanyiki hivyo kila mara. Kulazimisha watoto wako kusoma haitafanya kazi. Unahitaji kuunda mazingira sawa na kuweka mfano mzuri, kama kuzungumza kuhusu shule kutoka wakati wanaanza, sio tu katika miaka ya mwisho. Kuwa na vitabu nyumbani, kujadili maswala ya sasa kusoma vitabu na kununua magazeti bora huonyesha mfano mzuri kwa watoto.

Kuchukulia masomo yao kuwa muhimu sana na kuwakumbusha kwamba mafanikio shuleni hutokana na juhudi na uvumulivu ili kwenda katika chuo kikuu. Zingatia shule yao na zungumza na walimu wao mara kwa mara. Zungumza na watoto wako kuhusu jinsi itakuwa vyema kuendelea na elimu yao, ukiwaelezea jinsi elimu itaunda nafasi nzuri za kazi maishani mwao.

Kulazimishwa kutafsiria wazazi

Hii yaweza kusababisha watoto wako aibu kubwa na hata dhiki. Watoto wako wanaweza kufikiria kwamba mtu unayemzungumzia anafanya uamuzi kwamba familia ni jinga.

Usiwatumie watoto wako kukutafsiria wakati inahusisha maswala ya kibinafsi ao ya siri; tumia mtafsiri mtu mzima ao mtaalam wa kutafsiri kila mara.

Wasaidie watoto wako kuelewa sababu za wewe kujua Kiingereza kidogo. Hakikishia watoto wako kwamba unajaribu kujifunza lugha hiyo.

Page 77: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

57

Uvutaji sigara ao kunywa dawa za kulevya na pombe

Usishangae ikiwa mtoto wako atajaribu kuvuta sigara, dawa za kulevya ao pombe. Hii hufanyika kutoka kwa kila asili ya kitamaduni. Jibu sio kuwaficha watoto wako kutoka kwa jamii ya Australia ili kuepuka hatari hiyo, kwani hii haiwezekani.

Ni muhimu kujadili matatizo yanayoweza kutokea kwa kuvuta sigara, kunywa dawa za kulevya na pombe. Anza mapema iwezekanavyo kwani watoto wako wamekomaa kuelewa. Unapaswa kuanzisha sheria kwa familia nzima. Kwa mfano, unaweza kukataza pombe nyumbani mwako ikiwa ni jukumu lako la kidini.

Usibadilike na usitumie vibaya dawa na pombe wewe mwenyewe. Ni vigumu sana wewe kutarajia mtoto wako kutokunywa, kuvuta sigara ao kutumia dawa za kulevya ikiwa wewe mwenyewe hufanya hivyo.

Ikiwa unafikiria mtoto wako anaweza kuwa anatumia dawa za kulevya ao pombe, ichukulie vikali na uone daktari wako ao mtaalam wa afya. Ni wajibu wako.

Page 78: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

58

ShukraniMwongozo huu uliandaliwa kutumia mapendekezo yaliyopokelewa kutoka kwa wazazi wa Kongo ambao walishiriki katika vikundi na darasa za malengo ya uzazi. Shukrani kwa wafanyikazi wa Spectrum’s Parenting, Clovis Mwamba na Albert Muyunga, ambao alipanga vikundi vya uzazi kwa washiriki wa jamii ya Wakongo.

Ningependa kumshukuru Meneja wetu wa Makazi na Huduma za Familia, Sonia Vignjevic na Dk Khairy Majeed ambao ni wachangaji wakuu kwa muundo na utafiti wote ambao umesababisha kufanikiwa kwa masafa haya ya miongozo ya uzazi. Dennis Glover pia anashukuriwa kwa uhariri wake.

Spectrum Migrant Resource Centre ilifanya kazi kwa kushirikiana na jopo la washiriki wa jamii ya Wakongo na utaalam katika nyuga za kijamii na uzazi. Mwisho, ningependa kuwashukuru watu hawa kwa kupeana maoni ya kitamaduni katika yaliyomo; Antoinette Vumilia, Bijoux Ilondo Botuna, Christian Konkwe Tshiloko, Debora Immaculée Gbemina, Désiré Botuna, Dieudonné Musangu, Jean-Bovet Kandolo, Jean Claude Mutombo, Jocelyne Mamona, Josephine Zita Nyarubibi, Léonard Mathurin Kabemba, Marguerite Kiembe Mujinga, Martine Muyunga, Ndayi Sido na Pastor Peter Bondole.

Serikali ya Jumuiya ya Australia kupitia Idara ya Familia, Makazi, Huduma za Jamii na Maswala ya Kindani (Fahcsia) walikuwa na maono ya kupeana fedha kwa mradi huu kupitia Mpango wa kufadhili mradi wa Majibu ya Kawaida. Maoni yaliyoonyeshwa katika toleo hili ni yale za mwandishi pekee na hayawasilishi maoni ya Waziri ao Fahcsia.

Rosemary Kelada Afisa Mkuu Mtendaji

Page 79: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja
Page 80: Uzazi katika utamaduni mpya Mwongozo kwa wazazi wa Kongoethniccouncilshepparton.com.au/wp-content/uploads/2019/03/Congolese_Swahili.pdfKama mzazi mpya mhamaji, waweza kuwa na hoja

www.spectrumvic.org.au1800 700 712

Spectrum MRCDarebin Office251 High Street,Preston, 3072Phone: 03 9496 0200Fax: 03 9484 7942

Spectrum MRCMoreland Office13 Munro Street,Coburg, 3058Phone: 03 9384 7900

Spectrum MRC Employment, Education & TrainingBroadmeadows Office1/1100 Pascoe Vale Road,Broadmeadows, 3047Phone: 03 9301 7400

Spectrum ImmigrationPreston Office59A Roseberry Avenue,Preston, 3072Phone: 03 9470 2311

Spectrum MRC Offices1800 770 712Email: [email protected]